Simulizi :Roho Za
Kishetani
Sehemu Ya Tatu (3)Alikuja hapa Mango akiwa na imani ya kufanikiwa kumpata mwanadada wa kustarehe naye, mwanadada ambaye hata kama yuko tayari kwa lolote na kwa yeyote lakini asiwe na uwazi sana katika kuitangaza biashara hiyo. Mara kadhaa aliwahi kuhudhuria kumbi ambazo vikundi vya taarabu vilikuwa vikitumbuiza. Huko alikuta idadi kubwa ya waliofurika ni wanawake, tena wanawake wazuri, wenye sura za kuvutia na maumbo ya kutamanisha.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadhi yao walikwenda humo kwa minajili ya kujiburudisha tu na muziki lakini wengine walikuwa na dhamira mbili, muziki na kuwanasa wanaume wasiopitwa na vipendezavyo. Mara kadhaa Muganyizi hakukosa kupata wanawake katika kumbi hizo.
Ndiyo maana, usiku huu, akiwa na kitita cha kutosha mifukoni mwake aliamua kuingia hapo Mango Garden kusaka wa kumliwaza.
Alikwenda dirishani na kulipa kisha akaingia taratibu, mikono mifukoni huku akiangaza macho huku na kule ukumbini. Wingi wa watu, na watu wenyewe wengi wao wakiwa ni wanawake ilikuwa ni taswira halisi iliyompa matumaini ya kufanikisha azma iliyompeleka hapo.
Lakini hakuwa na haraka. Alikwenda moja kwa moja kaunta na kuagiza bia. Akanywa akiwa hapohapo kaunta huku akiwatazama waimbaji wa kikundi cha taarabu na mashabiki wa kike waliocheza wakinengua kwa umahiri kama vile hawana mifupa nyongani.
Saa nzima baada ya kuingia humo hakuwa yule Muganyizi wa awali. Huyu alikuwa ni Muganyizi mwingine, Muganyizi ambaye pindi bia zaidi ya tatu zinapotambaa katika mishipa yake ya damu, uchu wa kujipatia mwanamke humwingia nafsini.
Katika kiti hiki kirefu alichoketi, alikuwa na majirani wawili, kushoto na kulia, wote wakiwa ni wanawake wenye mvuto mkubwa mbele ya mwanamume mpenda wanawake wazuri. Mara mbili, tatu aliwaona wakitoka vitini na kujimwaga jukwaani. Na yeye akawa miongoni mwao japo hakuwa hata na chembe ya ujuzi wa kucheza muziki. Ni kama vile alikuwa akirukaruka bila ya mpangilio, lakini hakuna aliyechunguza nani anacheza vipi.
Kila mtu, hususan wanaume walicheza kila mmoja kwa namna yake, na ilionyesha dhahiri kuwa sio muziki wao. Yeye alikuwa miongoni mwa wanaume wachache waliohudhuria onesho hilo na akawa miongoni mwa wachache vilevile waliojimwaga jukwaaani 'kurukaruka.'
Lakini kwa kuwa haikuwa fani yake, mara alirudi kitini na kuendelea kugida bia. Zaidi aliishia kukodoa macho kwa wanawake walioonekana kumudu uchezaji wa muziki huo. Ndio, alivutiwa na uchezaji wao na zaidi, huyu mmoja ambaye minenguo yake iliyavuta macho ya wengi.
Alikuwa ni mwanamke, ndiyo. Lakini hakuwa ni mwanamke kama wanawake wengine walioingia ukumbini humo. Alikuwa na sura nzuri, umbile la kuvutia na mavazi yaliyompendeza. Kadiria mwenyewe uzuri wa mwanamke mzuri. Licha ya mavazi yaliyompendeza, licha ya uzuri wa sura na umbo lake, pia alimudu kuvitumia viungo vyake kucheza kimahiri jukwaani. Kwa ujumla alijua kucheza taarabu.
Muganyizi alimpenda, Muganyizi alimhitaji. Laki tano zilizogawanywa katika mifuko ya suruali yake zilimvimbisha kichwa. Akajiona kuwa yeye ndiye mwanamume, zaidi ya wanaume wote waliokuwa ukumbini humo.
Akawa katika zoezi la kumwinda.
Wimbo ulipokwisha yule mrembo alikwenda kaunta na kuagiza maji. Hakukuwa na nafasi za kukaa hivyo yeye, kama wengine wengi alibaki amesimama na kuendelea kugida maji yake. Ni hapo ndipo Muganyizi alipoamua kuijaribu bahati yake. Akamsogelea na kumgusa bega.
Mrembo huyo alishtuka na kugeuka. Wakatazamana.
“Hongera, mrembo,” Muganyizi alimwambia huku akiachia tabasamu la kirafiki. “Nimewaona wengi wakicheza, lakini tuweke uongo pembeni, wewe ni zaidi yao.”
Mwanamke yule naye alitabasamu. “Asante ,” hatimaye alijibu kwa sauti ya kudekadeka, akiyaepuka macho ya Muganyizi ambayo kwa uzoefu wake, akiwa ni mwanamke gwiji dhidi ya wanaume wakware hakushindwa kuyatambua matamanio dhahiri katika macho ya Muganyizi.
Aibu za bandia zilizojikita katika macho ya mwanamke huyo ilikuwa ni hatua moja mbele kwa Muganyizi katika kuifanikisha azma yake. Ulimi wake ukawa mwepesi kutamka chochote kile alichokidhamiria.
Akauteremsha mkono na kumshika kiganja. Akakitomasa kidogo. Tabasamu la mwanamke huyo likachipua tena huku akiunyofoa mkono wake kistaarabu.
“Mrembo, nadhani maji hayataikata kiu yako. Pata bia moja mbili uchangamke.”
Mwanamke huyo alimtazama tena Muganyizi, safari hii kipembepembe, macho yake ya kichawi yakijizungusha huku na kule kwa namna ivutiayo.
Muganyizi hakumpa nafasi zaidi, alimshika tena mkono na kumwambia, “ Tusogee pembeni, hapa kuna msongamano mkubwa wa watu.”
Walizunguka kidogo ukumbini humo na kwa bahati nzuri wakafanikiwa kupata sehemu ya kukaa. Muganyizi akaagiza bia. Mwanamke akashusha bia mbili kooni mwake huku akipokea 'mashairi' kutoka kwa Muganyizi, 'mashairi' ambayo hayakuwa mageni masikioni mwake.
Huyu hakuwa mwanamume wa kwanza kumtongoza akimtaka mapenzi. Wengi walishamwambia hivyo na wapo waliokubaliwa na kuna ambao hakuafikiana nao. Huyu Muganyizi alikuwa ni miongoni mwao na hakuwa na sababu ya kumkatalia ombi lake. Hakuwa na mume, hakuwa na hawara mwenye uzito wa juu nafsini mwake, hivyo hakukuwa na mtu ambaye angemwuliza “Leo kwa nini umerudi usiku wa manane?” “Leo kwa nini 'umelala nje'?” au “Kwanini leo umelewa?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa huru. Huru kuutumia uhuru wake. Hivyo hata pale Muganyizi alipomwambia waondoke, hakukaidi. Alikuwa tayari kwa lolote kama pia alivyokuwa tayari kwa yeyote.
Hawakwenda Malick Hotel. Muganyizi alikodi teksi hadi eneo la Mkwajuni ambako alikodi chumba katika gesti moja iliyokuwa haitofautiani na Malick Hotel kwa ubora wa vyumba. Wakausukuma usiku huo wakifanya kila waliloweza katika kuziridhisha nafsi zao, wakitumia nguvu na maarifa hadi Muganyizi akajikuta akiropoka, “...Tina...we ni mwanamke...ni mwanamke mzuri...umekamilika kila idara... usiniache...naomba uwe mke wangu...”
*****
TINA alipotoka nyumbani, Magomeni Mapipa saa mbili usiku, dhamira yake kuu ilikuwa ni kwenda Mango Garden, Kinondoni ambako kulikuwa na burudani ya kundi moja maarufu la muziki wa taarabu, kundi ambalo yeye binafsi alitokea kulipenda sana.
Ndani ya mkoba wake kulikuwa na shilingi elfu kumi na tano tu, fedha alizotarajia kuzitumia kwa kulipa kiingilio mlangoni na kujipatia bia mbili, tatu na pia kwa ajili ya usafiri wa kumrudisha nyumbani, Magomeni.
Hakuwa na miadi na mwanamume yeyote. Kilichomtoa nyumbani na kumleta hapo ni muziki. Hivyo alipoingia, mara kwa mara alikuwa akicheza muziki na akichoka huketi na kunywa bia. Aliagiza bia moja tu, ilipokwisha hakuagiza nyingine. Akazama katika kuburudika na muziki. Akacheza kwa raha zake.
Ni wakati alipohisi kiu ndipo alipotoka kwenye mkusanyiko wa watu na kwenda kuagiza maji kaunta. Wakati akinywa taratibu ndipo alipohisi kuguswa begani na alipogeuka akakutana na sura ya mtu asiyemfahamu. Kilichofuata hapo ndicho kilichowafanya wajikute wakifikia mbali zaidi kiuhusiano.
Tina alikuwa ni mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, kituo chake cha kazi kikiwa ni Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Alikuwa ni askari polisi. Katika umri wake wa miaka ishirini na minane bado hakuwa na haraka ya kuolewa. Alijua ipo siku atapata mtu ambaye moyo wake utaridhia kuolewa naye.
Kitu ambacho hkauwa tayari kukifanya ni kuwa na uhusiano wa mapenzi na mfanyakazi mwenzake. Baadhi ya askari wa pale makao makuu, hususan wale waliokuwa wakimzidi wadhifa walikuwa wakimwandama kwa maneno haya na yale kuhusu mapenzi. Hakuwa tayari kukubaliana nao japo akiwa ni mwanadamu, na akiwa ni mwanamke kama wanawake wengine alikuwa na mchemko wa damu na kuna wakati alijikuta akimhitaji mwanamume.
Hii ilikuwa ni miezi mitano tangu alipoachana na bwana aliyekuwa naye awali. Na waliachana baada ya bwana huyo kutokuwa mtulivu katika masuala ya wanawake. Alibadili wanawake bila ya kujali. Ni hicho kilichowatenganisha, na kuanzia wakati huo hakuwa na mwanamume yeyote, zaidi aliamua kutokuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwanamume katika kuepuka kile alichokiona kuwa ni kuumiza moyo wake.
Aliamini kuwa na uhusiano wa mapenzi ni kujitia kitanzi. Je, ikitokea huyo bwana naye akawa na tabia kama za yule waliyetengana miezi mitano iliyopita? Ni wazo hilo lililomfanya aamue jambo moja tu; kama mwanamume atamtaka, na moyo wake ukaridhia, basi kitakachofanyika ni kuzitumia saa kadhaa kwa starehe na baada ya hapo kila mmoja anashika njia yake. Uhusiano unafia hapo.
Huyu mwanamume aliyemjia baada ya kutoka kucheza muziki jukwaani, alimwona kuwa ni mwanamume mwenye mvuto kiasi chake. Alikuwa ni mtanashati, na tabasamu halikukauka usoni pake. Isitoshe, mtiririko wa maneno wakati akimtongoza, ulikuwa wa kipekee na ambao ungeweza kumfanya mwanamke yeyote 'ngangari' alegee na kutepeta kiasi cha kujikuta akikubaliana naye kama zuzu.
Kitu kingine cha ajabu ni kwamba, kila walipokutanisha macho, Tina alihisi kusisimkwa mwili, hali ambayo hakukumbuka ilimtokea lini kwa mara ya mwisho. Ni mwanamume mwenye mvuto wa kipekee; kwa nini asistarehe naye?
Kwa nini asijiliwaze naye wakati naye ni binadamu kama binadamu wengine? Kwa nini asiburudike na mwanamume huyu mzuri ilhali yeye, Tina, ni mwanamke kama mwanamke yeyote mwingine mwenye kuweza kupandwa na shetani la ashki, shetani ambalo kutulizwa kwake ni pale tu anapopatikana mwanamume rijali?
Jibu lilipatikana haraka kichwani mwake. Jibu rahisi. Uhuru. Hakuwa na ndoa iliyombana asiwe na hawara. Isitoshe, uaskari wake hakikuwa kikwazo cha kufanya mapenzi na raia. Cheo chake cha u-koplo kilikuwa na nguvu kwa wakati wake. Kilikuwa na nafasi yake. Siyo kila wakati. Haukuwa u-koplo wa kuingilia maisha binafsi ya 'koplo.' Kama hakuna sheria iliyombana askari polisi kuoa au kuolewa na raia asiye askari, vipi askari azuiwe kuwa na hawara asiye askari?
Alikuwa huru. Huru, kuutumia uhuru wake. Ndiyo, alikuwa huru kustarehe na mwanamume aliyempenda kwa dhati au kwa unafiki. Usiku huu, huyu Muganyizi ndiye aliyeuteka moyo wake.
Walipoingia gesti, Tina akiwa na kiu kubwa ya kufanya mapenzi, alitumia juhudi na maarifa yote aliyojaaliwa, bia tano zilizosambaa katika mishipa ya damu yake zikiwa ni changamoto kubwa katika zoezi alilokabiliana nalo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni katika patashika hiyo, ndipo alipomsikia Muganyizi akibwata: “...Usiniache...Naomba uwe mke wangu...”
Yalikuwa ni maneno ambayo hayakumwingia akilini Tina. Kuolewa, kwake lilikuwa ni jambo ambalo lingehitaji kujadiliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) au Mchungaji pamoja na Baraza la Wazee wa Kanisa. Hakuwa na sababu ya kutopenda kuolewa, zaidi ni kuepuka kutawaliwa, kudhibitiwa.
Aliwahi kuwaona wanawake wenzake wakinyimwa ruhusa na waume zao pindi walipotaka kwenda mahali fulani. Mke hakuruhusiwa kwenda Mango peke yake kama hivi alivyofanya Tina. Na sio suala la kuhudhuria matamasha ya burudani pekee, la. Hata kama angetaka kwenda mahali pengine hususan nyakati za jioni au usiku, ingemlazimu kumwomba ruhusa mumewe. Na hapo kulikuwa na mawili; kukubaliwa au kukataliwa.
Ni hayo yaliyomfanya aufikirie mara mbili, mbili uamuzi wa kuolewa. Kitu kingine kilichomfanya asikimbilie kuolewa ni umri. Alijiona kuwa bado umri unamruhusu kuzifaidi raha za duniani. Ndiyo kwanza alikuwa anafikisha umri wa miaka ishirini na mitano ya kuzaliwa. Kwake, huo ulikuwa ni umri mzuri wa kuendelea 'kutesa.'
Hivyo, haya maneno aliyoambiwa na Muganyizi yaliingilia sikio moja na kutokea la pili. Alichokifanya, badala ya kutamka lolote, ni kuongeza juhudi ili kumteka zaidi Muganyizi. Awe mshindi katika zoezi walilokabiliana nalo.
“Nakupenda sana Tina,” Muganyizi alitokwa tena na kauli, safari hii zikiwa ni sekunde chache tu baada ya Tina kujing'atua kifuani pake na kujitupa pembeni huku akimtazama kwa namna iliyoonesha kuridhika kwa zoezi lililopita.
“Hata mie nakupenda,” Tina alinong'ona. “Umenichosha sana . Una pumzi mwanaume wee!”
Hiyo ilikuwa ni kauli iliyomvimbisha kichwa Muganyizi. Akahisi kurejewa na nguvu upya, nguvu za kuendelea kuvitesa viungo vyake katika namna inayoburudisha na kusisimua, kupitia mwili huu mwororo, unaong'ara na kujazia kila palipostahili. Mwili wa mrembo Tina.
Mara akamvuta na kumkumbatia. Akambusu shavuni kabla hajauzamisha ulimi kinywani mwake huku mkono mmoja ukitambaa mgongoni na kushuka chini hadi nyongani ambako ulitulia kwa muda.
“Hapana, labda baadaye...” Tina alimzuia pindi naye alipoupenyeza mkono hadi mahala fulani mwilini mwa Muganyizi na kuyabaini mabadiliko fulani yanayosisimua.
Na ilikuwa ni baadaye.
Saa kumi na moja alfajiri, Tina alihisi yuko katika dunia nyingine. Alipumua kwa mfumo wa ajabu na wa kipekee. Alitumia pua na mdomo uliokuwa wazi akihema kwa sauti iliyoweza kumfikia yeyote ambaye wakati huo angekuwa nje ya chumba hicho, kando ya dirisha 'akijiumiza' kwa kutega masikio.
Safari hii, Muganyizi akichukulia kuwa ni kipindi cha 'lala salama' alihakikisha anamwonyesha Tina uwanaume wake. Akatumia nguvu na akiba ya ujuzi aliokuwa nao.
Dakika kadhaa baadaye, walikuwa katika sura tofauti, wakionekana kuridhika kwa kila walichokifanya. Ni wakati huo ndipo Muganyizi aliposema, “Naamini kama utakuwa mke wangu, maisha yetu yatakuwa na neema tele...” Ukafuata mlolongo mwingine wa maneno ya kusihi, akionyesha ni jinsi gani ametokea kumpenda Tina kwa kiwango kikubwa.
Bado Tina alikuwa mgumu. Akatoa kisingizio cha kujiendeleza kimasomo, akidai kuwa alihitimu elimu ya kidato cha sita kiasi cha mwaka mmoja uliopita.
Muganyizi alikuwa king'ang'anizi. “Kusoma, utasoma tu,”alimwambia. “ Hilo sio tatizo. Gharama zote za masomo nitashughulikia. Muhimu kwako ni kuwa mke wangu. Hayo mengine ni mambo madogo sana kwangu. Ulitaka kuchukua kozi gani?”
“Uandishi.”
“Uandishi wa habari?”
“Ndiyo. Nataka kuwa paparazi.”
“Kwanini umeamua kuchukua fani hiyo?”
“Basi tu. Nimeipenda.”
“Kwanini usisomee uhasibu au hata fani ya hoteli?”
“Uhasibu siuwezi. Nilitokea kuzichukia hesabu tangu nikiwa primary. Na mambo ya hoteli siyapendi.”
Muganyizi alitikisa kichwa akiashiria kukubaliana na maneno ya Tina. Kisha likamtoka: “Kwa hiyo nd'o umeamua kufanya kazi ya kufuatilia maisha ya watu; utauawa!”
Tina alicheka kisha akasema, “Ni kawaida. Wangapi wamefanya kazi hiyo hadi wanastaafu na hawajauawa? Naweza kuikwepa kazi hiyo lakini nikafa kwa mambo mengine. Kufa ni kufa tu.”
Ukimya wa muda mfupi ukapita. Kisha tena Muganyizi akaibuka: “Okay, usijali. Nitalipa. Ni kiasi gani? Zinaweza kuzidi laki tano?”
“Sijui. Lakini zinaweza kufika.”
“N'talipa,” Muganyizi alisisitiza. “Laki tano siyo pesa za kusumbua akili ya mtu anayejua kusaka pesa. Na siyo kwamba nitazitafuta. Ninazo!”
Ukimya wa muda mfupi ulitawala, kisha Muganyizi aliongeza: “Leo, kitu kama saa saba mchana tukutane popote utakapoona panafaa, nikupe zawadi.”
“Zawadi?”
“Ndiyo, zawadi yako kwa faraja uliyonipatia. Na pia nitakuwa na mengine ya kukwambia. Nitakueleza kwa sababu ni wewe pekee uliyetokea kuniliwaza na kuniondolea machungu moyoni.”
Tina alionekana kushangazwa na maneno ya Muganyizi. Akasema, “Muga, hauko wazi katika maneno yako. Ungenieleza vizuri, nikuelewe.”
Muganyizi alikohoa kidogo. “Nitakueleza, muda wa kufanya hivyo uta'potimu,” alisema. “Kwa kifupi leo ni siku ambayo moyo wangu utatakasika kwa kiasi fulani huku Watanzania wengi wakishangaa, wengi wakikata pumzi kwa namna ifurahishayo na wengi vilevile wakiomboleza.”
Bado Tina hakumwelewa, na alizidi kushangazwa na maneno yake. Akabaki kaduwaa.
Mara, kama aliyepagawa, Muganyizi akacheka kwa sauti, japo haikuwa sauti kubwa. Hata hivyo, kicheko hicho hakikuficha uchungu na hasira iliyohifadhiwa katikati ya mtima wake. Macho yake yalitangaza bayana kutokuwa na amani moyoni mwake.
Kama alivyokizua kicheko hicho, ndivyo pia alivyokikata. Badala yake, kwa sauti ambayo pia ilionesha kuwa kuna jambo zaidi ya jambo moyoni mwake, akasema, “Hatutajali...ndiooo...hatutajali! Hatutajali wala kuumia mioyoni kwa vifo vya Watanzania wachache kati ya mamilioni, wakati serikali haikujali wala kuumia pale Watanzania wengine, na familia zetu walipoteketezwa...walipouawa kikatili na wakimbizi wanaolelewa na taifa hili.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mara nyingine kicheko kikamtoka, lakini safari hii Tina hakuhitaji hata sekunde tano za kutafakari kama kilikuwa ni kicheko cha furaha au kicheko cha uchungu.
“Ni kipi hasa unachokizungumza?” Tina alimwuliza, moyoni akiamini kuwa kuna jambo zaidi lililofichika katika maneno ya Muganyizi.
Huku akivaa nguo harakaharaka Muganyizi akamjibu, “Nitakueleza.”
“Lini, leo?”
“Ndiyo.”
“Muda gani?”
“Sasa hivi.”
Alimweleza, na alimweleza kila kitu. Hakusita kuropoka kuwa siku hiyo, na siku ya Jumapili kwa kutumia sumu kali aina ya PAK mamia ya Watanzania wasiopungua mia moja watakufa ndani ya majengo yenye ofisi mbalimbali na pia waumini wengi watakufa ndani ya msikiti na kanisa wakiwa kwenye sala. Na wala hakuuona umuhimu wa kuihifadhi zaidi moyoni, hoteli iliyowaficha katika kipindi chote hiki cha mkakati wao.
Aliitaja!
Yalikuwa ni maelezo ya kusisimua masikioni na akilini mwa Tina. Yalimsisimua, yakamtisha na kumtia hasira. Yale mapenzi yote kwa mwanamume huyu yaliyeyuka mithili ya kipande cha barafu ndani ya tanuru la moto. Akamwona Muganyizi kama shetani. Akajilaumu kwa kudiriki hata kumchojolea nguo. Kwa ujumla alimchukia kwa kiwango kisichokadirika huku pia kiwango fulani cha woga kikiwa kimeganda moyoni mwake.
Kwa dakika chache woga ukamtawala, na dakika chache nyingine nafasi hiyo ikatwaliwa na hasira pamoja na uchungu. Mwisho wa hayo yote ni ujasiri wa kipekee uliotwaa nafasi.
Ikamjia taswira ya jinsi raia wasiokuwa na hatia watakavyokufa vifo wasivyovitarajia, wakiwa wametoka nyumbani na kuja labda kwa shughuli fulani katika ofisi fulani ndani ya jengo fulani.
Kuna ambaye atakuwa ofisini, kompyuta mbele yake akitekeleza majukumu ya kazi yake. Ghafla atainamia meza na kukata roho. Mwingine atakuwa akiifuata lifti ya jengo ili apande. Hataifikia. Ataanguka ghafla sakafuni na kuanza kutokwa damu nzito na povu zito mdomoni, masikioni na puani kabla ya kufa muda mfupi baadaye.
Katika msikiti fulani waumini watakuwa katika sala, lakini ghafla, mmoja, mmoja wataanguka chini na kufa katika hali itakayoshangaza na kutisha. Kama vile haitoshi, ndani ya kanisa moja napo kutazuka tukio la ajabu. Huenda kwaya itakuwa ikiimba katika kuwasilisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa washarika au huenda kasisi atakuwa madhabahuni akihubiri na huenda pia waumini wote watakuwa wamesimama, wakiimba mapambio kwa nguvu na furaha huku wakipiga makofi na vigelegele.
Chochote kile kitakachokuwa kikiendelea kanisani humo kitasitishwa ghafla, na badala yake, mmoja baada ya mwingine wataanguka huku povu lililochanganyika na damu likiwatoka vinywani, puani na masikioni. Dakika kama tano baadaye ndani ya kanisa hilo hakutakuwa na kiumbe aliye hai! Kila aliyekuwa hai muda mfupi uliopita, akishangilia kwa kuimba nyimbo za kusifu atakuwa sakafuni, maiti!
Yatakuwa ni maafa makubwa sana , aliwaza. Siyo chini ya watu mia moja au mia mbili watakaopoteza maisha ndani ya siku tatu tu!
Haiwezekani! alijisemea kimoyomoyo. Ndiyo, hakuwa tayari kuliachia tukio hilo lifanyike, akishuhudia.
Wakati huo anga ilizidi kutakata. Ilitimu saa 11:30. Kwa mujibu wa Muganyizi, operesheni ingeanza kutekelezwa saa 4 asubuhi ya siku hiyo katika majengo yenye ofisi za taasisi mbalimbali. Kesho yake ambayo ingekuwa ni Ijumaa, msikiti mmoja uliokusudiwa ungefuata, na Jumapili ndipo zoezi lingehitimishwa kwa chupa ya mwisho kufunguka kanisani.
Sasa kila sekunde ilipopita, chuki dhidi ya Muganyizi ikazidi kujiimarisha moyoni mwa Tina. Lakini hakutaka kuchukulia pupa. Aliamini kuwa pupa ya aina yoyote ingetoa matokeo mabaya, jambo ambalo hakutaka litokee.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment