Simulizi : Salhat
Sehemu Ya Nne (4)
****** ****** ******
Alionekana mwanamke mmoja aliyeweza kukaa katika kiti kikubwa cha kifalme kilichoweza kurembwa na kupambwa kwa nakshi nakshi za dhahabu.
Hapo aliketi mwanamke mmoja ambaye alimtazama Eddy na kumwambia.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nafikiri unatambua kazi baba yako Sadick aliyoweza kunipatia kabla ya kifo chake na maneno hayo hayakuwa ya kwake Bali ya Sultan Samir baada ya Sultan Sayid kufa.......Sasa basi kwa kuwa mmeshawapata wale wote ambao wanatakiwa kuikomboa dunia kwa adhaa Kubwa itakayokuja Siku za mbeleni cha kufanya ni kila mtu ajitambue sasa uwezo alionao na jinsi gani anaweza kuufanyia kazi uwezo huo" alizungumza mwanamke yule ambaye alikuwa mama yake Eddy hivyo Eddy kusema ya kuwa Salhat ni ndgu yake hakuweza kukosea kwasababu ni mtoto wa mama yake mdogo.
"Sawa malikia"
"Nasma na Sheilah nataka kuwapongeza kwa kazi nzuri ambayo mmeifanya ya kuweza kumpata Johnny........ila kuna tatizo juu ya hilo"
"Tatizo gani??? Walidakia wote kwa pamoja.
"Mapenzi!!!! Mapenzi yataleta kizaa zaa sana ns kusababisha damu zisizo na hatia kumwagika na pia kusalitiana ninyi kwa ninyi"
"Kivipi aliuliza Eddy.
"Mimi nampenda yule Polisi......Johnny anapendana na Salhat huyu Sheila itabidi apendane na Edrick ili tusisababishe damu" alizungumza Nasma.
"Lau kama ingekuwa ni urahisi namna hiyo basi ninyi msingehitajika.....tambueni ya kuwa lazima kuna mmoja atakuja kugeuka na kuwa mbaya wenu na yote hayo ni kutokana na mapenzi laiti kama ningelikuwa namfahamu basi ningewaambia mkamuuwe kwani atasababisha matatizo makubwa sana" aliendelea kuongea Malikia yule aliyeonyesha kusikitika na kuhofia usalama wao
Edrick akiwa hapo alikumbuka kilichotokea baina ya Akram na Johnny kwa Siku ya leo.
Hapo hapo aliweza kupata picha.
****** ******* ******
Ilifika mpaka saa4 usiku bado Salhat hakuweza kurejea nyumbani Johnny hakuweza kulala kabisa alikuwa njee ya nyumba karibu kabisa na geti kama mlinzi ili aweze kumfungulia Salhat mlango wakati huo nao Grace alikuwa akimtafuta kwa kupita chumba hadi chumba huku akilitaja jina lake.
"Atakuwa ameenda wapi??? Aliuliza Grace huku akiendelea kupanda gazi za juu lakini alishtuka baada ya kuona mlango uko wake kwenye kile chumba ambacho aliweza kumfungia Sarah ndani.
Alipanda ngazi haraka haraka na alipofika alifungua mlango kwa spidi zote.
Hatimaye ilisikika honi getini na Johnny alisimama pembeni huku mlinzi akienda kufungua geti aliingia Salhat akiwa amebeba marboro nyeusi Johnny alimfuata kwa kasi Sana.
"Umetoka wapi usiku huu na umebebe nini hapo?? Alafu yule mwanaume ni nani uliyeweza kuondoka naye??? Aliuliza Johnny.
Akram aliingia na kumjibu.
"Kwani na wewe ni nani wa kumuuliza maswali yote hayo???
"Mimi ndiye niliyemuajiri hapa kwahiyo kila atokapo lazima aache taarifa hapa na achukue ruhusa hapa". Aliongea Johnny kwa Sauti.
"Sawa kwa hayo Masaa machache ambayo nimekaa naye unataka nikulipe shilingi ngapi??? Aliuliza Akram na kuanza kutoa pesa katika pochi yake.
"Huyu mbwaa anaongelea nini???? Alizungumza Johnny na kumfuata Akram Kisha akampiga ngumi moja safi kabisa iliyomfanya adondoke chini na damu zianze kumtoka mdomoni.
Jay!!!!!! Aliita Salhat.
Na kufanya neno hilo likapate kujirudia rudia kichwani mwake kwani Sauti hiyo aliweza kuifananisha naya Salhat alipokuwa mdogo.
"Akram uko salama eeee!!! Aliuliza Salhat ambaye tayari alishakuwa chini na kuanza kumpapasa usoni ambako alikuwa akitoa damu.
Johnny alienda akamshika mkono kisha akaanza kumburuza kwa kumuingiza ndani huku akitoa order kwa mlinzi ya kuwa amtupe Akram njee.
Wakati hayo yakiendelea Badra alikuwa juu ya ghorofa akitizama kwa chini alitabasamu na kucheka sana huku akisema.
"Kumbe udhaifu wake ndo huo" aliendelea kucheka huku akifinya finya vidole vyake dizaini ya kama anatafuta mbinu sasa.
Akram alimuingiaza Salhat ndani ya chumba chake kisha akamfungia mlango na kutoka njee wakati huo nao Grace bado alikuwa kama kichaa huku akijiuliza Sarah yuko wapi na ni nani aliyeweza kutambua ya kuwa Sarah yuko hapo.
Alikimbia chumbani kwake kisha akainua simu na kupiga.
Kulikucha asubuhi na ndiyo kwa Mara ya kwanza kabisa Johnny kuamka asubuhi kuliko watu wote.
"Mpumbavu kabisa huyu usiku mzima anamuwaza huyo pusii kama yuko salama wakati mimi Ndiyo mume wake mm ndiye nitakayemuowa sasa anamjali yule wa nini??
Alianza kufanya mazoezi akiwa na mawazo mengi sana kichwani na asijue ya kuwa tayri alishaweza kufanya mazoezi kupitiliza.
"Kuna nini Leo hapa ndani??? Aliuliza Ashura baada ya kuona vitu ambayo hata yeye alishndwa kuvitafsiri .
"Madam Grace ahitaji kelele kabisa na Badra yuko chumbani kwake yeye anakunywa wala hana hata wasiwasi tatizo ni kwa Johnny.
Ameamka Leo kabla ya watu wote hapa mm nimeamka saa 11 na 30 namkuta anafanya mazoezi hadi sasa saa3 asubuhi afanyi zoezi lingine zaidi ya hilo hilo moja tu.......hata ukimuita aitiki zaidi ya kukutolea tu macho na kutingisha kichwa.
Salhat baada ya kusikia maneno hayo aliwahi hadi chumba ambacho alikuwa akifanyia mazoezi Johnny.
"Jay!!! Aliita Salhat ila Johnny aliendelea na kufanya zoezi lake.
"Dada Fatna kaniambia kwanzia asubuhi hufanyi zoezi lingine lolote tofauti na hilo na sasa hivi ni saa3 embu acha kwanza na uwende ukanywe chai. Alizungumza Salhat na kujaribu kuushika mkono wa Johnny ambaye aliutoa mkono huo na kuendelea kufanya zoezi lile.
"Sasa nimfanyaje ashuke mungu wangu..........anaumia eti" alizungumza Salhat kwa Sauti ya chini ila Johnny aliweza kuisikia vizuri kabisa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Salhat alitizama na kuona chupa ya chai aliifunua na kwenda kukaa mbele ya Johnny kisha akamwaga chini kwa kumuonyesha Johnny baada ya hapo aliuweka mkono wake mbele Kisha akaanza kuilaza ile chupa ya chai design kama anataka kuimwagia Mkononi mwake ila ghafla alisimamishwa na Akram.
"Unataka kufanya nini kwaajili ya huyu mpuuzi ambaye hajali kabisa kuhusu wewe?? Alifoka Akram.
'Kipi tena kimekuleta hapa?? Aliuliza Salhat huku akimtazama Johnny.
"Ile Siku Ndiyo Leo hivyo lazima twende sasa hivi alizungumza Akram na kuweka chupa ya chai chini.
Johnny alijifanya anaendelea zake kufanya mazoezi.
"Jay ntawahi kurudi Leo sawa.....kwahiyo toka basi hapo alafu unywe chai chakula cha mchana na cha usiku nitakuja kukuandalia mm mwenyewe alisema Salhat na kuondoka.
Johnny akishikwa sana na hasira kisha akaanza kupiga juu kabisa bila kujali ya kwamba angeweza kuharibu na kutokujua amekimbia kwa kiasi gani na kwa masaa mangapi.
Badra alikuwa juu akimtizama John Kisha akaanza kuteremka chini tartibu kabisa kwa sura ya Salhat Mara ajinadilishe na awe Grace. Aliendela na mchezo ule wa kujibadilisha badilisha hadi alipofika karibu kabisa na chumba cha Johnny alitabasamu kisha akasema.
"Sijui nianze na sura ipi"
Badra alitabasamu kisha akaenda kwa sura ya Grace.
"Johnny inatosha sasa naomba uache sasa kufanya mazoezi.....hayo uliyoyafanya yanatosha kabisa alizungumza Badra ambaye alikuwa tayri katika sura ya Grace.
Johnny alitoka na kuondoka eneo lile kisha akaelekea chumbani kwake.
Badra alicheka kisha akasema.
"Sasa nitaanza kutumia sura za uwapendao ili nikupate wewe......leo usiku nahitaji kulala na wewe Jay" alisema na kutabasamu.
Baada ya muda mwingi kupita alikuwa Johnny nyumbani huku akiwaza kwa Mara ya pili tena Salhat ameweza kuchukuliwa na mwanaume mbele yake.
Alitikisa kichwa chake na ghafla mlango wake ulifunguliwa na aliingia Grace ndani.
"Unaendeleaje sasa???
"Naendelea vizuri"
"Unaonekana kama huna furaha kabisa kwanini??? Aliuliza Grace.
"Basi tu sijisikii vizuri Leo"
"Labda twende........."
"Grace Tafadhali niache niko na mawazo mengi sana naomba uniache kwa Leo" alizungumza Johnny Kisha akavuta shuka lake na kugeukia upande wa pili.
"Sawa Mimi natoka kidogo ila nitachelewa kurudi pia Leo nilikuwa naomba ulale na Mimi" alisema Grace.
"Nilale na wewe????? Aliuliza Johnny kwa mshangao mkubwa kabisa.
"Sijamaanisha kufanya mapenzi namaanisha kulala tu na wewe mpaka pale utakapo kuwa sawa" alisema Grace na kumtizama Johnny ambaye alionyesha kuwa na wasiwasi.
"Johnny inamaana hujawahi kulala na mwanamke hata mmoja??? Aliuliza Grace kwa mshangao.
"Nani kasema nimelala nao wengi tu alisema huku akitizama pembeni na kumfanya Grace atambue kabisa ya kuwa Johnny hajawahi kulala na mwanamke mwingine.
Sawa me naenda alisema na kumbusu Johnny mdomoni kisha akondoka zake.
Alipofika mlangoni sura yake ilibadilika na alikuwa ni Badra
"Haaa yani hajawahi kulala na mwanamke yoyote siamini macho yangu.....hapana siwezi kumuacha akalala na mwanamke yoyote tofauti na mimi lazima Mimi niwe mwanamke wa kwanza kulala na Jay" aliongea na kubadili sura yake ikawa ya Salhat.
Naamini Salhat na Grace wote watachelew kurudi hivyo nitatumia muda huo kulala na Johnny.
***** ***** *****
Alioneka Grace akiwa katika maeneo ya baharini huku akiwa amevalia nguo zilizomfanya asiweze kutambulika kwa urahisi kabisa.
Alipita kijana mmoja na yeye alikaa kando yake kisha akachukua gazeti na kujifanya anasoma.
"Yule mtoto tayri ametoroka na nihatari kwa maisha yangu naya kwenu pia....yule binti tuliyeweza kumtengenezea kesi nahisi yeye ndiye aliyeweza kumtorosha yule mtoto hivyo cha kufanya ni kumuuwa yule mtoto kisha ummalizie mbali Salhat kwani hao wote ni hatari kwa maisha yetu"
"Nimekuelewa lakini sass nitampataje huyo mtoto??? Aliuliza Kijana yule aliyeenda kwa Jina la Dany.
"Nahisi Salhat anajua mahali alipo Sarah hivyo nilimtuma Casim amfuatilie…...….… chukua pesa kidogo kama kianzio na ukimaliza kazi hiyo basi nitakumalizia pesa iliyobaki" alizungumza na kuinuka kisha akaondoka eneo lile.
****** ****** ****
Johnny akiwa amejilaza chumbani kwake ghafla alishtuka kutoka usingizini na kuita Salhat!!!!!!!
Tukio la kumuwa Salhat akiwa mdogo liliweza kujirudia tena kichwani mwake.
"Ni nini hii alizungumza na kutoka kitandani haraka haraka kisha akavaa suruali yake akabeba Shati na hapo alikutana na Badra aliyetaka kukibadili sura ya Salhat lakini alishindwa baada ya kumuona Johnny.
"Unaenda wapi Johnny???? Aliuliza Badra ambaye alikuwa amejiandaa kwa tendo la mapenzi.
Johnny aliondoka bila kusema kitu na kitu hicho kilimkera sana Badra nakuanza kujipiga makofi huku akisema naichukia sana hii sura niliyo nayo naichukia sana hii sura.
***** ******* ****
Johnny alijikuta anaenda tu kwenye njia ambayo hata yeye hakuweza kujua kwann kapita njia hiyo ila wakati anaendesha gari aliliona tukio ambalo Salhat anagongwa na gari aina ya Lori.
"Hapana siwezi ruhusu kilichotokea kwa Salhat kitokea tena kwa Salhat huyu hapana siwezi" alizungumza Johnny na kuongeza mwendo wa gari.
Barabarani nako Alioneka Akram akiwa na Sarah katika upande mwingine hiyo ni kutokana na kumuacha pale kisha kwenda kumchukua Sarah ambaye aliomba amuone.
Baada ya Sarah kumuona Salhat alijikuta akitabasamu kisha kuanza kuelekea barabarani kwaajili ya kwenda kumkumbtia Salhat ambaye na yeye aliifunua mikono yake kwaajili ya kumkumbatia wakati huo alionekana Casim akiwa ndani ya Lori Kubwa na kusema.
"Nitawamaliza wote kwa dakika moja" alikata Simu na kumtizama Sarah ambaye alienda akamkumbatia Salhat kisha wakaanza kurudi wote kwa pamoja na hapo Casim aliwasha gari.
Huku nako Akram alianza kuyasikia mapigo ya moyo yalipiga kwa kasi sana. Alitizama huku na huko kwaajili ya kujua mapigo hayo anayasikia kwa wapi hatimaye alifanikiwa kumuona Johnny kwa mbali akipiga kelele wakati huo nao Edrick Sheilah na Nasma walipata mshtuko ambao wote walijua watu wako matatizo.
"Salhat"
"Johnny"
Walitizama na kupotea.
Salhat alishtuka baada ya kulio gari likiwa linakuja kwa kasi na limebakiza sekunde chache tu kufika pale walipo alimsukuma Sarah's na kubaki yeye njiani ila ghafla na yeye alisukumwa na kuangukia upande mwingine.
Tayari Johnny alishafika eneo lile na Lori lile liliweza kumgonga kwa kiasi kidogo tu kwani tayari Edrick Sheilah na Nasma walikuwa kwa nyuma walizuia Lori lile lisiende kasi kwa nguvu zao za kijini.
"Jayyyyyy!!!!! Aliita Salhat kwa Sauti na kumfuata Johnny ambaye damu zilianza kumtoka.
Salhat aligeuka na kulitazama Lori lile kwa hasira likiwa limesimama pale ghafla lilianza kupasuka vioo na matairi yakaanza kulia milio ya kupiga pancha.
"Eddy kamsaidia Salhat kwani awezi kujicontrol na itakuwa mbaya kama atagundulika mapema namna hii" alizungumza Nasma ambaye alimfuata Johnny.
"Salhat punguza hasira Salhat aliita Edrick lakini tayari macho ya Salhat yalisha badilika kabisa rangi na aliyefanikiwa kuona hivyo ni Casim ambaye alishashuka ndani ya gari na kutaka kukimbia lakini alishindwa kujielewa baada ya kuona miguu yake imekuwa mizito"
Wakati huo nao Akram alianza kuyasikia maumivu ya kichwa ambayo alishindwa kuyaelewa yametoka wapi.
"Salhat" aliita eddy huku akiendelea kumshika na kwenda kumzuia.
"Nakwambia nipishe alitoa Sauti ya ukali na kumfanya Edrick apepee mbali na pale alipokuwa kwani ulitoka upepo mkali kabisa.
Salhat alipomfikia Casim alimshika kwa mkono mmoja kisha akasema kufa nakwambia kufa.
"Sheila tutafanyaje juu ya Salhat kabla watu hawajaja???? Aliuliza Nasma.
Akram alisogea mpaka sehemu aliyoko Salhat na Casim kisha akauchuku mkono mmoja wa Salhat na kuushikisha moyoni mwake na hapo alianza kutulia na hatimaye kumuachia Casim kisha akarudi mbio mbio kwa Johnny.
Akram na yeye baada ya kufanya hivyo alihisi ametulia sasa alienda mpka sehemu aliyoko Johnny kisha akambeba mbio mbio hadi kwenye gari lake kisha akaondoka naye katika eneo lile na kumpeleka hospitalini.
Nyuma ya gari Salhat alikuwa akiweweseka huku akimuita Johnny kila saa.
"Salhat Niko salama shida unalia sana bhna" alizungumza Johnny kwa Sauti ya chini na ya utulivu.
"Sasa kwanini lakini ukafanya hivyo??? Na huyo mbwaaa huyo nitamkamata tu ila Johnny usijali utafika tu salama" alijibu Salhat.
"Akram ongeza mwendo zaidi" aliongea Salhat.
****** ****** ****
"Unaongelea nini wewe?? Umemgonga mwanaume gani???? Aliuliza Grace.
"Nafikiri ni Johnny lakini mimi sikumuona yeye alijitokeza mbele ila hajaumia sana"
"Hivi unadhubutu kusema hajaumia sana nani Johnny ambaye umemgonga nakuapia Casim chochote kikimkuta Johnny nakuuwa" alizungumza Grace na kukata Simu kisha mbio mbio akaingia kwenye gari lake na Badra na kuelekea hospitalini ambako tayri alishaweza kupata ya alipopelekwa.
"Umeshindwaje wewe???? Aliuliza Dan.
"Huwezi kuamini yule mwanamke lazima ni mchawi kwani vioo vya gari vilipasuka na gari matairi ya gari yote yakabust bado haikutosha wakati nashuka ili nitoroke miguu yote ikawa mizito kisha akaja huyo mwanamke wa kumuuwa akiwa amebadilik macho yake yalikuwa ya rangi ya blues yote yani huwezi kuamini" alizungumza Casim.
"Umeshamwambia Grace???
"Bado ila nilimwambia niliona kitu cha ajabu lakini hakutaka nimuelezee yeye anauuliza sana kuhusu huyo Bwana wake"
"Ahaaaa hivyo siyo na Dan umeshamwambia??? Aliuliza Dan..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"We ni kichaa nini unaniuliza nini na Ndiyo unaona nakwambia sasa hivi kwamba yule mwanamke ni mchawi" aliongea Casim.
"Well nimekuuliza hivyo kwasababu Mimi siyo Dan aliongea Edrick na kuonyesha sura yake halisi.
Casim alimkumbuka Johnny na kuanza kuogopa.
Sikuwa na mpango wa kukuuwa lakini lazima nifanye hivyo ili siri hii ibaki kuwa siri alizungumza na kutabasamu.
***** ***** *****
"Samahani ni nani ndugu wa karibu wa huyu mgonjwa??? Aliuliza dactari.
"Mimi hapa" alijibu Salhat.
"Wewe ni nani wake????
Salhat alifikiria kwa dakika kadhaa kisha akasema.
"Mimi mke wake....huyo ni mume wangu" alizungumza Salhat na kumfanya Akram ashangae na kumtizama Salhat.
"Sawa" tunakuomba u sign hapa aliongea dactari na Salhat alifanya vile alivyoambiwa na wakati huo huo alingia Grace.
"Vipi hali ya mgonjwa mimi ni mke wake" aliongea Grace.
"Samahani mke wake tayari ameshasign sisis hatukutambui wewe" alizungumza nesi na hapo hapo Grace alimgeukia Salhat aliyekuwa akimtazama tu.
Grace alimtizama Salhat pasina kuongeo neno lolote lile.
Baada ya Siku tatu kupita.
Johnny aliweza kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yake kuonekana imeanza kutengamaa.
"Yuko wapi Salhat???? Aliuliza Jay baada ya kufika.
Grace alimtazama tu bila kusema neno kisha akamwambia
"Aliondoka na yule mwanaume wake sasa wanasiku 2 hajajaj nyumbani"
Johnny aliung.ata mdomo wake kwa hasira na kutizama pembeni ambako Badra alikuwa amekaa na kumtizama tu.
**** ***** *****
Johnny akiwa amelala usiku dirisha lake lilifunguliwa na hatimaye aliweza kuingia Salhat ambaye alitoroshwa na Edrick gerezani baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha juu yake na kurudishwa tena mahabusu.
Salhat aliingia mpaka ndani ambako alimuita Johnny kwa Sauti ya chini.
"Jay....Jay..... Jay....!!!!
Johnny alifungua macho yake.
"Sal........."
"Shshshhs sitaki mtu yoyote atambue ya kuwa Mimi Niko ndani hapa" alizungumza Salhat.
"Uliondoka na mwanaume gani na ulikuwa naye wapi??? Aliuliza Johnny.
"Nafikiri huu siyo muda mzuri wa kumuliza mwanamke wangu maswali kama hayo alizungumza Edrick na kutabasamu huku akimfanya Johnny nayeye acheke.
"Nilijua umeondoka na yule mwanaume mwingine na yule kwanza ni nani eti?? Aliuliza tena Johnny.
Salhat alimpa ishara ya Eddy aondoke kisha amuache na Johnny.
Baada ya Eddy kuondoka Salhat alimkumbatia Johnny huku akilia na kuzungumza maneno Haya moyoni.
"Siwezi kukwambia ya kuwa Grace ndiye aliyehusika na hayo yote kwani utaniona ya kuwa Mimi simpendi Grace" alizungumza Salhat kimoyoni ila wakati huo Johnny hakuwa akimsikiliza Bali akilihisi Joto la Salhat mwilini mwake.
Baada ya dakika 5 kupita.
Johnny alikuwa amejilaza mapajani mwa Salhat.
"Kwahiyo bado tu hujampata aliyehusika na hayo??? Aliuliza Johnny.
"Hapana" alijibu na kuangalia pembeni.
"Mbona kama unaniongopea??? Aliuliza Jonny.
"Hamna kweli" alizungumza Salhat huku akiendelea kusema.
"Siwezi kukwambia ya kuwa Grace anahusika na hilo hata kidogo kwani sitaki niwe chanzo cha ugomvi baina yenu ukizingatia Mimi Niko tofauti na ninyi" maneno hayo Johnny aliweza kuyasikia na kisha akasema.
"Grace!!!!!!!! Aliuliza kwa Mshangao sana.
"Hapana mbona Mimi sijaongea lolote alisema Salhat.
"Ahaaaa sawa nlihisi kama umesema jina la Grace" alizungumza Johnny ambaye hakutaka Salhat atambue ya kuwa anauwezo wa kumsikia hata akiwa kwa umbali wa kilomita ngapi.
**** ****** ******
Salhat alifika ngomeni kisha akatoa heshima kwa Malikia ambaye alifurahi sana baada ya kumuona Salhat.
"Hatimaye sasa imekuwa rahisi baada ya kukupata wewe natumaini hata mama yako Samia huko aliko atakuwa na furaha baada ya na wewe kufika mahali ambako ndipo palipokuwa chimbuko la mama yako" alizungumza Malikia huku akimwagia mwagia maji ambayo aliyaandaa kwaajili yake.
Baadaye waliweza kupata muda kwa wao wawili tu wakiwa wamekaa na kuongea.
"Vipi kuhusu Johnny????
"Bado sijamwambia kuwa Mimi ni Salhat kwani naamini nitamkumbusha Yale ambayo ameyasahau na pia Mimi ndiye niliyemuulia mama yake nikiamini amemuuwa mama yangu kimakosa hivyi nahitaji kukaa mbali nayeye kisha ayaanze maisha mapya" alisema Salhat na machozi kwa mbali yakianza mteremka.
"Salhat utaweza kufanya kia kitu katika hii dunia lakni huwezi kuuficha moyo wako au hisia zako mbele za yule umpendaye wewe na Johnny tayri imeshandikwa mtakuwa pamoja katika kuisaidia dunia"
"Kama ulivyosema imeandikwa katika kuisaidia dunia lakini siyo kuijenga familia hivyo Mimi sipo tayri kumwambia ya kuwa Mimi ndiye Salhat" alizungumza Salhat huku akiifikiria sura ya Johnny kichwani mwake.
***** ******* ****
Zilipita Siku 7 bila ya Johnny kumtia machoni Salhat hata alipojaribu kumtafuta kwa kutumia Sauti yake bado ilikuwa vigumu kwa yeye kumpata sasa alibaki nyumbani na dirisha akiwacha wazi huku akiamini ya kuwa ipo Siku moja Salhat ataweza kurudi tena na kuwa wake.
Aliweza kuikumbuka kauli ya mwisho ya Salhat kwamba ahitaji kumwambia yeye ya kuwa Grace anahusika na hayo yote kwani anaweza akahisi yeye anafanya hivyo kwaajili ya kuwachoganisha au kutaka apendwe yeye.
"Kama Grace ameweza kufanya hivi basi siwezi kumuacha hai kabisa lazima nitapambana naye kwa hali yoyote ile mpaka pale nitakapo hakikisha umepata adhabu unayostahili" alikula kiapo Johnny.
Akram alisimamishwa katika ofisi ya mkuu wa kituo na kuombwa kujibu shtaka la kutoroka kwa Salhat kwani Mara nyingi alionekana karibu naye. Hivyo alisimamishwa kazi mpaka pale ushahidi utakapo patikana kama aliweza kumtorosha basi adhabu Kali zitachukuliwa dhidi yake.
Akram alitoka katika kituo cha Polisi huku akitabasamu.
"Kwa kuwa Salhat yuko salama Mimi sijali hata kuhusu kazi yangu najali sana maisha yake kuliko kitu chochote kile". Akram alipanda gari lake kisha akaondoka zake eneo lile wkati huo nao Mkuu wa kituo alitoka na askari mmoja kisha akampa ishara ambayo askari huyo alimpa heshima na kuingia ndani ya gari kisha kuanza kumfuatilia Akram.
***** ***** ****
Johnny akiwa anachapa chapa round katika chumba cha Grace huku akifanya upekuzi kama kuna uwezekano wa yeye kupata kitu chochote kile ambacho kinaweza kikawa ushahidi mbele ya mahakama akishtuka baada ya kuguswa begani mwake.
"Unatafuta nini ilikuwa ni Sauti ya Grace.....
"Hakuna nilikuwa napanga panga chumbani kwa mke wangu mtarajiwa amah nimefanya vibaya??? Aliuliza Johnny......
"Hapana siyo vibaya kwni Siku Si nyingi tutaanza hata kushare miili yetu alizungumza Grace hku akianza kumpapasa kifuani johnny ambaye alisisimka baada tu ya kuguswa eneo hilo.
Grace baada ya kuona hivyo alimgusa zaidi akiamini ya kuwa Johnny anaweweseka kwa midadi ya mapenzi.
Lakini la hashaa!!! Sicho kilichokuwa kikimfanya Johnny asisimke kwani Kila Johnny anapohisi Jini yuko karibu naye basi huwa anapata msisimko wa ajabu kabisa.
Alimshika mkono Grace Kisha akamtizama kwa makini sana na kumlaza kitandani hku akiwa amemgeuza chini.
Alianza kumpapasa papasa mgongoni mwke huku akiifungua cheni yake na kutoa unga kidogo ambao aliweza kuupaka mkononi mwake alipomshika mgongoni.
Grace alipiga kelele za ajabu sana.
"Nini mbona kelele tena aliuliza Johnny.
"Hamna" alizungumza na kuanza kupita mbal na Johnny hatimaye akakimbia kabisa katika chumba cha Grace.
Alipofika mbele kidogo alibadilika na kuwa Badra ambaye alianza kuguguma kwa maumivu makali aliyoweza kuyapata.
Alitizama kulia na kushoto na baada ya kugundua hakuna mtu alipotea kimazingara.
Johnny alitabasamu tu kwani alimuona na tayri alishagundua ni Badra huyo.
"Ahaaa unatumia sura ya Grace ili ulale nami alicheka na kusema.
Siyo vigumu kwa Mimi kukutambua wewe muuwaji wa niwapendao hata ukija kwa sura ya nani harufu yako ya kijini haiwezi kupotea puani mwangu.
**** ***** *****
Johnny akiwa amekaa huku anatizama TV na Badra akiwa amekaa pembeni yake huku akimtungia sheria kichwani bila ya kujua ya kuw Johnny anamsikia.
"Leo lazima nifanye mapenzi na wew najua ukiiona sura ya Salhat hapo huwezi bisha kwa chochote...... Na nitamfanya Grace achukiane na Salhat mpaka mmoja wao amuuwe mwezie alafu atakayebaki akafie polise.....mchezo ni ule ule.
Johnny alicheka tu kimoyo moyo na hap hpo alipata wazo na kusema ya kuwa inawezekana pia aliyesababisha kifo cha Mr and Mrs Joseph ni Badra kwa sura ya Grace.
Haya sasa hii vaa vaa sura za watu kwa Badra hatimaye itaanza kumtokea puani na ni baada ya Johnny kuhisi yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya baba na mama Salhat.
Ulikuwa usiku ambao Salhat alikuwa ngomeni huku akiwa mwingi wa mawazo sana juu ya Johnny ambaye hakupata kumuona Malikia alisogea hadi karibu naye na kumgusa begani kisha akakaa kando yake.
"Unajua huna tofauti sana na mama pale alipoweza kumpenda baba yako alijizuia sana lakini mwisho wa Siku alishindwa na akaamua kuufuata moyo wake....kwani aliweza kuacha kila kitu na kuelekea duniani ambako aliishi maisha ya shida baada ya Badra kuingilia mapenzi baina yao wawili.
"Madam Badra??? Aliuliza kwa mshangao.
"Ndiyo......ngoja nkuhadithie kidogo vile navyoyafahamu maisha ya wazazi wako" alizungumza Malikia na kuanza kumuelezea Salhat.
***** ****** ****
Jay na yeye akiwa amekaa chumbani kwake huku akimini ya kuwa Badra atakuwa kwa sura ya Salhat na ghafla dirisha lilifunguliwa na aliingia Salhat mwenyewe ambaye alionekana akiwa na furaha Kubwa sana baada ya kumuona Johnny.
Alielekea mpaka sehemu Johnny aliyoko kisha akamkumbatia kwa nguvu sana wakati huo Johnny alikuwa akicheka akiiamini ya kuwa yule ni Badra na wala siyo Salhat wake.
"Jay!! Aliita Salhat akiwa mgongoni mwake huku akisema.
"Naamini ya kuwa nimekutesa sana kwa Siku ambazo sikuweza kuja kukuona lakini kumbuka ya kuwa Mimi Si chochote bila ya wewe....na nakuahidi ya kwamba kwanzia sasa na kuendlea Mimi nitapambania penzi langu juu yako na sitamruhusu mwanamke yoyote yule akuchukue wewe kwani ndvyo mama yangu alivyofanya kwa baba yangu"
Johnny alijikuta akihisi tofauti kabisa na hata machozi yakianza kumtoka alimtoa Salhat mgongoni mwake kisha akaanza kumfuta machozi.
"Salhat...... Aliita Jay na kumtizama lakini ghfla alijiwa na wazo la kusema ya kuwa huyo siyo Salhat wake.
Alimkumbatia tena kwa nguvu kisha akaichukua Sindano yake ambayo aliitayarisha akiamini yakuwa ni Badra kisha akamchoma mgongoni ambako
Salhat alikosa nguvu na kudondoka chini kisha akaanza kujiburuza buruza pale chini kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Na wakati huo nao Badra Ndiyo alishakaribia mlango wa Johnny alibadilisha sura yake hadi ikawa ya Salhat lakini wakati akifanya kitendo hicho Nasma aliweza kumuona akiwa na Sheila.
"Amefanya nini huyu???? Aliuliza Sheila.
"Na Salhat yuko ndani na Johnny na anataka amwambie kuwa yeye ni jini Leo ikitokea Badra kaona basi hatutaweza kuyatimiza malengo yetu. Aliongea Nasma ambaye alipotea.
Na hapo hapa alirudi na Eddy.
Walitizamana wote watatu kisha wakapotea kwa pamoja.
"Jay!!!! Jay!!!!! Aliita Badra na Johnny alienda kumfungulia mlango akiamin ya kuwa ni Salhat aliyekuwa akimuita.
Alimkumbatia kwa furaha sana na kwa nguvu hali iliyomfanya Badra ahisi raha kupitiliza huku na yeye akimkumbatia huku akilihisi joto lile.
"Ulikuwa wapi Salhat??? Aliuliza Johnny huku akimshika mikono yake.
"Nilienda kumsalimia mama bila kukuaga kwasababu alikuwa mgonjwa ila kwa sasa anaendlea vizuri" alizungumza Badra.
"Salhat kwa hichi utakachokiona hapa ndani usishtuke nitakuelezea kila kitu alizungumza Johnny kisha akamuachia mwanya kidogo Badra aone kipi kilichopo ndani.
Badra baada ya kuitizama aliacha macho yake pale pale.
Na Jay na yeye aligeuka kisha akatizama mahali Badra anapotizama.
Alishangaa baada ya kutokumuona Salhat akimini ya kuwa ni Badra ambaye alikuja kwa sura ya Salhat.
"Hapana Badra alikuwa hapa!!! Alijikuta ameropoka bila ya kujua ya kuwa aliyekuwa pale ndiye Badra.
"Unaongelea nini Johnny?? Aliuliza Badra na kumfanya Jay ashtuke kidogo kwani Salhat anamuitaga Jay na hakuna Siku hata moja alishawahi kumuita Johnny ila Johnny hakulitilia maanani kabisa.
"Hamna" alisema Jay.
Na hapo hapo Badra alienda akamshika kwa nyuma kisha akaanza kumfungua vifungo Jay.
"Unataka nini Salhat???
Badra alianza kumbusu shingoni na kuendelea kumpapasa kifuani kwake kwa pupa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Johnny aligeuka na kuanza kumzuia lakini alishindwa hatimaye na yeye alijikuta akianza kumpapasa kwa hali ambayo siyo ya kawaida na kuanza kumrarua nguo alizokuwa amezivaa Badra.
Eddy aliingia akiwa na Nasma pamoja na Sheilah.
"Tufanyaje sasa???? Aliuliza Sheilah.
Ila wakati huo tayri Nasma alishaenda na kutaka kumshika Badra ila alishndwa baada ya kupigwa shoti na kudondokea ukutani.
"Nasma kuwa makini.....Badra siyo Jini wa kawaida" alizungumza Eddy.
"Tufanyaje sasa??? Jay haruhusiwi kufanya mapenzi na msichana yoyote tofauti na Salhat.
"Kwani nguvu na uwezo alionao unaweza ukapotea na tukashindwa kuikomboa dunia" aliongea Sheilah.
Fanyeni vile muwezavyo wasifanye mapenzi kwa dakika10 ntakuwa nimeshamleta mtu ambaye anaweza akaistopisha hii. Alizungumza Eddy na kupotea.
Nasma Alitizama na kuona picha ya Salhat alienda na kuidondosha kwa nguvu na kufanya Johnny ashtuke kwa kiasi kikubwa sana alielekea sehemu picha ilipo.
"Salhat picha yako imedondoka hii ni ishara...... Kabla hajamalizia kuongea Badra alimsimamisha kisha kuipeleka mikono yake kifuani mwake. Na kuendelea kumbusu.
Sheilah alifungua na kuyafunga makabati kwa kasi sana na kumfanya tena Johnny ashtuke kwa kiasi kikubwa sana.
Ila Badra aliendelea kumchombeza.
"Mpumbavu huyu ndo aelewi alisema Nasma na kutoa upepo mkali mdomoni mwake ambao ulianza sasa kusambaratisha vitu pale ndani na madirisha yakaanza kujifunga na kufungua.
Badra alitaka kumshika tena ila Johnny alimsukuma kitandani kisha akamuuliza.
"We ni nani???? Aliuliza John na kumtazama Badra ambaye alikuwa kitandani mwake.
"Jay!! Aliita Badra na Johnny alimfuata na kumtizama kwa macho makali sana ambayo yalimfanya Badra anaanze kuweweseka .
Nasma walipashana mikono na Sheilah wakiamini ya kuwa hapo tayri wameshamaliza kazi.
"Nakuuliza wewe ni nani....mbona unaifanya nakutamni sana eti" alizungumza Johnny na kuutoa mkanda wake katika suruali yake.
"Anafanya nini tena huyu!? Aliuliza Nasma kwa mshangao.
Johnny alimvuta Badra karibu kisha akamfungua vifungo vya sketi yake na kuanza kupandisha juu sketi yake.
"Mungu baba mungu baba anataka kufanya nini huyu???? Aliuliza Nasma ambaye sasa alianza kushika kichwa chake.
"Hapana usiingize.... Hapana bhna huyo siyo Salhat..... Tafadhali nakuomba usiingize" aliendelea kuomba Nasma ukifikiri kuna Aliyekuwa akimsikia
Ghafla mlango ulifunguliwa na aliingia Akram.
Badra alisimama na kuvaa sketi yake vizuri kisha akatafuta Shati na kujifunika upande wa juu ambako alibakia na sidiria tu.
Akram alimfuata Johnny na kumpiga Ngumi kisha akamshika mkono Badra na kuanza kumtoa njee akiwa katika sura ile ile ya Salhat.
Johnny alianza safari ya kutoka njee ila alipotazama chini aliiona sura ya Salhat iliyokuwa imepasuka kioo na alisita kupiga hatua.
Akram alimfikisha njee kisha akaanza kumpiga vibao Salhat.
Unawezaje kunisaliti Salhat unawezaje Salhat??? Aliuliza Akram na kumfanya Badra ashindwe kuelewa huyo ni nani na anamahusiano gani na Salhat.
Akram alipanda kwenye gari lake na kuondoka.
Alicheka sana kwani wote walikuwa na Edy ndani ya gari.
"Mmama mpuuzi sana huyu" alizungumza Akram.
"Yuko wapi Salhat?? Aliuliza.
"Hali yake ni mbaya kutokana na sindano aliyochomwa na Johnny akidhani ni Badra ila mama anamtafutia dawa tunaweza kwenda wote tukamtizama" alisema Eddy.
**** ***** ****
Ngomeni nako hali ya Salhat iliendelea kuw mbaya kwani hakuacha kutetemeka na alianza kubadiika rangi sasa.
"Tufanye nini juu yake??? Aliuliza Nasma.
"Dawa nilizompa hazijamsaidia mtu pekee anayeweza kuiondoa Sumu hiyo ni Johnny pekee yake pia kuitoa hii sindano kwani yeye pekee Ndiyo anajua ni maneno gani aliyazungumza pindi alipokuw akimchoma.....na kama Badra ameanza kuitumia sura ya Salhat basi itakuwa hatari kwa Salhat pamoja na Johnny. Kwani Johnny anaweza kumuuwa Salhat bila kutambua na kutoa siri nzito kwa Badra bila kujua ya kuwa siyo Salhat"
***** ***** ****
Johnny akiwa anapit alishangaa baada ya kumuona Badra akiwa amekaa kwenye television huku akitizama TV.
"Hapana haiwezekani kwa sindano ile niliyomchoma alitakiwa sasa hivi awe amebadilika rangi lakini mbona yuko kawaida kabisa" alijiulza Johnny.
Na hapo hapo alianza kuyafananisha matukio tukio la Salhat kuingia kupitia dirishani na tukio la Badra kuingilia Mlangoni.
Sasa alikumbuka hata Mara ya kwanza Salhat aliingilia dirishani.
"Hapana haiwezekani siyo Salhat wangu" alizungumza na kuanza kukimbilia ndani.
Johnny alirudi ndani kwa haraka zaidi huku akianza tizama sehemu ambayo Salhat alidondokea.
"Salhat wangu siyo Jini hata kidogo yule siyo Salhat wangu....lakini kwanini sasa alipitia mlangoni?? Alianza kujiuliza maswali kibao huku akijikuna kichwa chake alitoa Simu yake na kumpigia Eddy.
Simu wala haikupokelewa.
**** ***** ****
Sasa tufanyaje aliuliza Akram ambaye alishatambua kila kitu kuhusu Salhat
"Hapa ni Johnny apatikane na ikitokea akafikisha Siku NNE akiwa katika hali hii basi atafariki" alizungumza Malikia.
"Hapana simuhitaji Johnny sihitaji anitambue ya kuwa mimi ni Salhat hata kidogo wala sihitaji ajue ya kuwa mimi ni Jini" alizungumza Salhat ambaye kidogo hali yake ilianza kutengamaa lakini siyo kupona kabisa.
Eddy alimtazama Salhat na kushusha pumzi ndefu.
Muda kidogo aliweza kukutana na Johnny ambaye alionekana akiwa mwingi wa mawazo alipomuona alimkimbilia na kumuuliza.
"Salhat yuko wapi??? Yuko salama!!! Yupo katika hali gani?? Kama unajua mahali alipo Tafadhali nipeleke" alizungumza kwa dakika moja tu tena haraka haraka.
"Sijamuona Salhat Nina kama Siku wiki kwanzia ulivyopata ajali sijamuona tena machoni pangu" alizungumza Eddy na kumfanya Johnny aanze kuwaza.
"Moyo wangu na akili yangu inafikiri kabisa Salhat yupo matatizoni na natambua ya kuwa akili yangu haiwezi nidangaya ila kila ninapoitafuta Sauti yake siipati kabisa sijui sasa yuko wapi? Alizungumza Johnny na kuketi chini katika kiti.
Huku nako Akram akiwa amekaa alianza kutafsri tendo lile la ajali ya Johnny.
" ni kweli kwamba alimuona Johnny kwa mbali sana lakini ghafla tu kwa sekunde chache tayari alishaweza kufika eneo lile Salhat alilokuwepo na kumuokowa ikiwa tu yeye aliyekuwepo karibu alishindwa.
Itakuwa pia anauwezo wa kukimbia kwa kasi sana alizungumza Akram huku akimgusa baba yake ambaye bado hali yake haikuwa imetengamaa hospitalini hapo.
***** ***** *****
Zilipita Siku mbili na Johnny hakukaa kwa kutulia kabisa nyumbani kila Mara amtazamapo Badra anapata shauku ya kumuuwa mapema lakini alijizuia kwanza Siku hiyo akiwa nyumbani huku akiwa anazisikiliza Sauti tofauti tofauti mpaka pale atakapoiweza kuipata ya Salhat.
Hatimaye aliweza kuisikia Sauti ile alisimama kisha akayafunga tena macho yake na kuanza kusikiliza kwa makini Sauti ile.
"Sitaki Jay ajue chochote kuhusu mimi......sitaki kumbukumbu zilizofutika ziweze tena kurudi kwaajili yangu.....sitaki kumtonesha kidondo kilichoweza kupona tayri na ajue ya kuwa mimi ndiye Salhat niliyeweza kumuuwa mama yake....hivyo hata kama ni kufa kwaajili ya Sumu hii Niko tayr.....na.......
Kabla hajaendelea kusikiliza zaid Grace alimuita na kumfanya masikio yake yaume kwa kiasi Fulani kwani alikuwa akivuta Sauti ya mbali sana na Sauti ya Grace iliweza kutoka karibu yake kabisa.
"Johnny zimebaki Siku 10. Kabla ya ndoa yetu umejiandaaje?? Aliuliza Grace.
"We andaa kila kitu mimi Niko na vitu vya muhimu navifuatilia" alizungumza Jay na kuchukua ufungue wake wa gari kisha akavaa koti na kuondoka zake eneo lile.
Alipanda ndani ya gari na kutaka kuisikiliza tena ile Sauti lakini hakuweza kuisikia tena.
"Huyu mpumbavu Grace huyu.......Salhat... Siamini macho yangu kwamba we ndiye Salhat wangu! Nitakuokowa kwa kila namna usijali nitayasaidia maisha yako sitahitaji tena nikupoteze kwa Mara nyingine na nishindwe kukusaidia kama nilivyoshindwa mwanzo. Alizungumza Jay.
**** ***** ****
Hali ya Salhat iliendelea kuwa mbaya na sasa alibakiza Masaa machache kabla ya kumaliza Siku nne huku nako Jay alikuwa amekaa chumbani kwake huku akitizama saa ile.
"Edrick Tafadhali nakuomb uje unichukue na unipeleke kwaajili ya kumsaidia Salhat wangu Tafadhali alizungumza huku akiendelea kuzunguzunguka tu ndani pake.
Yalibaki Masaa matatu mawili na hatimaye likabaki lisaa limoja ambalo sasa zilianza kukatika Dakika huku nako hali ya Salhat iliendelea kuwa mbaya.
"Salhat" aliita Eddy ila bado Salhat alitingisha kichwa akimaanisha ya kuwa ahitaji mtu aende akamuite Johnny.
Zilibaki dakika10 na wote walikuwa wakitizamana.
"Hapana mtanisamehe alizungumza Nasma na kupote eneo lile.
"Ta...fa....dha....li......mzuieni....asiende.....kwa Ja....Jay....ta.....fa .....kabla hajamalizia kauli yak alianza kukoho damu.
Eddy na yeye alipotea.
Hatimaye Eddy alirudi akiwa na Nasma pamoja na Johnny.
Johnny alipofika tu alimkimbilia Salhat mahali aliko kisha akamtizama mikono yake alimgeuza nyuma na kufungua kibegi chake ambacho alimwaga vitu vyake chini kisha akamgeuza Salhat nyuma ambako alimchoma sindano alitoa dawa yake na kumwagia kwenye kisu kidogo alichoweza kuja nacho alizungumza maneno kidogo kisha akachomoa sindano ile na baada ya kuchomoa alimwagia tena dawa ile kwenye kisu ambacho kwa wakti huo kilikuwa kikitoa moshi mkali sana.
Alimchomea sehemu ambayo aliweza kumchomea sindano na Salhat aliweza kutoa Sauti ya maumivu ambayo ilimuuliza sana Johnny kwani machozi yalikuwa yakimtoka huku akikumbuka ya kuwa Mara ya kwanza ni yeye aliweza kumchoma kisu na kumfanya apoteze maisha na sasa tena amemchoma sindano yenye sumu.
Kwa usiku mzima Johnny alikuwa akimuhudumia Salhat ndani ya chumba chake pale alipohisi baridi aliweza kumfunika kwa mashuka ambayo yalikuwa ya ngozi aliyoweza kuyakuta ngomeni pale pale. Alipohisi joto basi alimfunua na kaunza kumpepea huku maji y moto yakiwa jikono ambayo aliyatumia kumkandia Salhat.
Uliingia usiku wa manane hatimaye pakaanza kukucha kabisa huku bado Johnny akiendelea kumuhudumia Salhat.
Kulikucha na Eddy aliingia ndani.
"Johnny ni vizuri kama sasa utaweza enda kupumzika na mini nikusaidie kumtazama Salhat"
"Hapana mimi nitakaa hapa hapa" alijibu Johnny huku akimfunika vizuri Salhat.
Zilipita Siku mbili mchana na usiku Jay akiwa anamuhudumia Salhat pasina kufunga kbisa macho yake.
Uliingia mchana wa Siku ya tatu hatimaye ukaingia Jioni ambako sasa Salhat alianza kujisikia aliyafunua macho yake taratibu kabisa na hapo alikutana na uso wa Johnny wenye tabasamu.
"Unaendleaje?? Unajihisi vizuri sasa aliuliza Johnny huku akianza kumpapasa Usoni kwa kumpima joto lake.
Nahisi umepona sasa alizungumza Jay na kutabasamu.
Salhat Alimtizama na kuupeleka mkono wake shavuni kwa Jay alishtula baada ya kugundua ya kuwa Johnny ni wa moto sana.
"Mbona we ni wamoto sana??? Aliuliza Salhat kwa Sauti na kufanya watu waliokuwa njee waje ndani kumtizama.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Salhat unaendeleaje??? Aliuliza Akram ambaye aliweza kufika saa hiyo hiyo.
"Jay mbona ww ni wamoto sana embu naomba sijui ni maji ya baridi naombeni na............ Kabla hajamalizia kuongea Jay alishika mkono na kumwambia.
"Kwakuwa wewe uko salama na mimi Niko salama pia" alizungumza Jay na kutabasamu hata hakuchukua sekunde 3 alizidiwa na kudondokea mabegani mwa Salhat.
Watu walianza kuita Johnny huku wakianza kutafuta njia gani bora wanaweza kuitumia ili kumsaidia Johnny.
Kitendo kile kili mnyima raha kabisa Akram ambaye hakukuwa na furaha baada ya kuona hakuna mtu ambaye anamjali hata kuhusu yeye watu walikuwa wakihangaika na Johnny wengine walimkanyaga na wala hawakutambua hilo kwani mawazo yao yote yalikuwa kwa Jay.
Alipoteza furaha kabsa na akajiona hana dhamani yoyote mbele ya Johnny kwani hakuna mtu aliyekuwa akimjali yeye kama mwanzo.
Alitoka ndani na kuendelea kutembea taratibu taratibu huku akikumbuka jinsi gani watu walikuwa wakimjali Johnny Hata Siku ambayo Grace aliweza kumuuliza yeye ni nani mpka ampige Johnny wake. Akakumbuka na Siku Salhat aliyoweza kusema ya kuwa Johnny ni mume wake....aliendelea kucheka na kutabasamu baada ya kufika karibu aliupiga mti Ngumi kwa hasira na kufanya damu zimtoke mkononi.
Akram aliondoka akiwa mwiingi wa hasira sana.
Huku nako alionekana Salhat akiwa amepitiwa na usingizi pembeni kabisa ya Jay ambaye bado fahamu zake azikumrejea.
Wakati huo Sheilah, Nasma Malikia pamoja na Eddy walikuwa hapo wakiwatizama wote wawili.
Malikia aliwaomba watoke njee na wawaache katika hali ile.
Walipofika njee kila mtu alitabasamu kwa design yake
"Akram yuko wapi??? Nasma alikuwa wa kwanza kugundua ya kuwa Akram hayuko eneo lile.
"Atakuwa huku huku" alizungumza Sheilah.
Malikia alifunga macho kisha akayafungua na kusema.
"Hayupo hapa yuko barabarani na anaendesha gari kwa kasi sana hii ni kutokana na hasira alizonazo embu Nasma kuwa makini kwanza na Akram ili kama yeye atakuwa shida mbeleni tuweze kummaliza sasa" alizungumza Malikia na kumpa amri hiyo Nasma ambaye alitoa heshim ana kuondoka eneo lile.
**** **** ****
Yuko wapi Johnny aliuliza Grace aliyekuwa amerudi nyumbani baada ya kutokuonekana kwa Siku kadhaa.
"Sitambui maana Mara nyingi huwa huwaga hatoki chumbanj kwake na hata akiondoka huwaga haagi mtu ila nahisi Leo Siku ya NNE sijamuons kabisa.
"Atakuwa na shida gani kwani hata simu yake apokei" alizungumza Grace na kuendelea kupiga simu wakati huo nao Badra alikuwa akipita na akiyasikia malalamiko Yale.
Huku nako Johnny alikuwa na Salhat huku akimtazama tu.
"Hata Siku moja sikutegemea ya kuwa ninauwezo wa kukutana nawewe tena katika dunia hii hii tena ukiwa hai.....unajua......"
Kabla hajaendelea kuzungumza Salhat alimuwekea kidole mdomoni akimaanisha aache kuongea.
Johnny aliacha na kutabasamu tu.
"Jay inabidi uendee nyumbani sasa kwni ikitokea Badra akakutafuta na akakukosa anaweza akaanza kuhisi jambo juu yako"
"Lakini sasa Mimi sitaki kurudi duniani kwasasa bado sijamaliza hamu ya kukaa nawe" alijibu Johnny.
"Jay mimi nitakuja kukutembelea Leo usiku"
"Umeahidi na usipokuja hatutaelewana hapo" alijibu Jay na kusimama kisha akasema nataka ww unipeleke duniani.
Salhat alicheka kisha akaenda akamshika mkono alafu akapotea naye wakatokea karibu kabisa na gari lake.
"Salhat" aliita tena Jay na kumshika Salhat mikono kisha kumsogeza karibu kabisa na gari lake na kumfanya aliegemee.
"Nini?? Aliuliza Salhat baada ya kuona ya kuwa Johnny anamsogelea zaidi.
Johnny alitabasamu na kumbusu mdomoni kisha akamtizama na kumbusu tena na tena na tena.
"Jay!!!! Aliita Salhat baada ya kuona sasa mabusu yanazidi.
"Unajua ndoa yetu tayri imeshapitishwa hata mbingu sasa imebaki wewe tu kunitimizia mimi haja zangu kama......alizungumza na kuanza kumuangalia kifuani kisha akaanza kumfungua kifungo cha shati alilovaa.
"Mjinga wewe huna adabu alizungumza na kumpiga kibao Jay mkono ambao ulikuwa ukitaka kufungua kifungo cha shati aliloweza kulivaa.
"Kwahiyo utaki siyo aliuliza Jay kwa Sauti ya utulivu.
"Sitaki nini??? Aliuliza Salhat.
"Aaaaaaahhhhhhh we nmbie tu utaki basi me nitakuelewa" aliongea Johnny.
"Unaongelea nini wewe???
Johnny alisogea nyuma na kumuachia nafasi Salhat.
"Sawa me naenda alizungumza na kugeuka zake huku akiangua kicheko bila Salhat kumuona.
"Jay aliita Salhat ila pia Sauti ya Grace nayo ilisikika hapo hpo.
Ulikuwa wapi Johnny unajua nimekutafuta sana eti" alizungumza Grace na kwenda kumkumbtia Johnny kwa nguvu.
"Niko salama Grace sasa unaweza kuniachia" alizungumza na kujitoa mikononi mwa Grace.
Alipogeuka nyuma hakumuona tena Salhat.
Alimfungilia Grace mlango wa gari na Grace aliingia kisha Jay akawa anazunguka huku akitizama kama anauwezo wa kumuona Salhat.
Aliingia hadi ndani ya Gari na kuanza kuwasha gari lake.
Huku akiendelea kutafuta tafuta.
"Ameenda wapi huyu mwanamke alizungumza Johnny kwa Sauti ya manung.uniko.
"Unamuongelea nani Jay aliuliza Grace.
"Hamna alijibu huku akiendelea kutafuta tafuta. Aliliondoa gari na kwa mbali alimuona Salhat akiwa nyuma ya mti mmoja mkubwa huku akiwatizama.
Jay hakuwa na chakufanya zaidi ya kumtizama tu na kuondoka na gari lake akiwa na Grace.
**** ***** *****
"We taira toka hapo mbele yangu" alizungumza Akram akiwa ndani ya gari huku akimpigia honi Nasma aliyekuwa mbele ya gari lake.
"Sitoki wewe huruhusiwi kwenda popote pale kwni utasababisha matatizo makubwa sana kwanza najua unataka kwenda kwa Johnny sikuruhusu"
"We mwanamke ni kwambie Mara ngapi ya kuwa Mimi siendi huku unakosemea we"
.
"Sasa kama huendi kwann hutaki twende wote?? Aliuliza Nasma
"Aise toka hapo eti nitakugonga..nakwambia".
"Nigonge ila hapa sitoki nimpewa kazi na Malikia ya kuhakikisha usalama wa Johnny" alijbu Nasma.
"Mpumbavu kabisa huyu anakuja kutaja jina la Johnny katika nyumba yangu Mimi" alizungumza Akram na kuwasha gari lake Kisha kuliendesha kwa kasi kwa kumuelekea Nasma ambaye alikaa kabisa chini siyo kusimama tena.
Chupuchupu amgonge alisimamisha gari na kutoka ndani ya gari.
"We mwanamke alizungumza Akram na kwenda kumshika Nasma mkono kwaajili ya kumtoa hapo ila alishtuka baada ya kugundua ya kuwa Nasma alizimia.
"We......we......wewe......amka embu" alizungumza huku akimshika Nasma kwa kumpiga vibao Nasma vya shavuni.
"Sasa huyu mbona ananisababishia matatizo alizungumza Akram na kumbeba kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake.
Alimlaza ndani ya chumba chake na kuanza kumuhudumia.
Zilipita dakika 7 na bado hakukuwa na hali yoyote ya matarajio.
"We Mpumbavu embu amka hakunaga mtu anazimia kwa dakika zote hizo alizungumza na kuanza kumuasha Nasma ambaye alikuwa akizungumza moyoni ya kuwa hawezi kumuacha Akram akaenda popote.
"Si nimeshakwambia sikuruhusu wewe uende mahali popote alizungumza Nasma na kujiamsha kitandani.
"Ahaaa tayri umeshaaamka Mimi niko busy na mambo yangu sasa nataka kuondoka" alizungumza na kuanza kuondoka Ghafla alipofika mlangoni alishngaa Baada ya mlango kujifunga ufunguo ulichomoka na moja kwa moja ulielekea kwa Nasma.
"Nimeshakwambia huendi mahali na huwezi kubishana na mimi kwani Mimi ninauwezo mkubwa kukuzidi" aliongea na kuushika ufunguo kisha kusimama kitandani
"Ila sidhani kama kuna mwanaume anayeweza kushindwa nguvu n mwanamke alizungumza Akram na kumfuata Nasma kisha akamnyang.anya ufunguo na kumuonyeshea.
Nasma aliinama na kuanza kumng.ata mguu wake
"We mwanamke we........Akram aliweza kuuachia ufunguo ule kisha akaanza kukitoa kichw cha Nasma kilichokuwa kikimng.ata mguuni mwake.
Nasma aliukimbilia ufunguo na kuuchukua Kisha akamwambia.
"Kama wewe ni mwanaume sasa uchukue"
Alizungumza na kuutupia ufunguo katikati ya kifua chake.
"Unafikiri huko kuna nini mpaka nisichukue..... Alizungumza Akram na kusogea mbele zaidi.
"Haya chukua" alizungumza Nasma na kujisogesa kifua mbele"
"Hivi unafikiri siwezi kuchukua siyo" alizungumza Akram na katika sintofahamu alijikuta tayri mkono wake umeshaingia katika kifua cha Nasma ambaye alibaki ameduwaa na kutoa macho tu ilikuwa sawa sawa na Akram kwani hata na yeye alijikuta tu katika hali ya kushangaza ameshaufikisha mkono wake huko.
****** ******* *******
Huku nako yalikuwa majibizano baina ya Johnny na Grace.
Johnny zimebaki Siku NNE kabla ya ndoa yetu lakini wewe hujishughulishi kabisa na kitu chochote.
"Sasa wewe unataka nijishughulishe na nini.?? Aliuliza Johnny aliyekuwa akielekea chumbani kwake.
"Jay mpaka sasa hujajitafutia nguo ya harusi lakini wewe unaona simple tu me nahitaji twende wote shopping kwaajili ya kukutafutia wewe nguo ya harusi" alizungumza Grace.
"Grace unataka Siku hiyo nivae nguo ngapi kwa mfano??? Tayari nimeshakwambia ninayo Suti ya harusi na ukiendelea kunisumbua zaidi....utajikuta uko mwenyewe Siku hiyo ya harusi"
Alizungumza Johnny aliyeondoka na wala Si kuingia tena ndani ya chumba chake.
"Unamaanisha nini wewe unaposema ya kuwa nitajikuta mwenyewe.........unaonana na mwanamke mwingine sindiyo.....Salhat huyo ndiyo anakufanya wewe unione Mimi sifai tena ikiwa unakaa kwangu unalala kwangu na kuvaa kwangu sindiyo" alizungumza Grace na kumfanya Jay ageuke kisha akamwambia.
"Hutakaa unione tena ndani ya nyumba yako......na sahau kuhusu ndoa" alizungumza Johnny na kutupa koti lake chini kwa hasira.
"We Johnny nakwambia rudi hapa...... Unaondoka sindiyo... Utajuta nakwambia utajutaaaaaa.........alizungumza kwa hasira na kuingia ndani ya chumba cha Johnny kisha akaanza kutupa tupa vitu.
Badra alikuwa pembeni akitizama tu na kusema.
"Ni sinema gani hii Johnny amenichezea alijizungumzia Badra na kumtizama Grace.
"Sasa itanibidi na Mimi nianze kucheza sinema zangu ili zikutane katikati.
baada ya mtafaruku mkubwa kutokea baina ya Grace na Johnny ambaye aliondoka nyumbani hapo.
Badra aliweza kuingia katika chumba cha Grace na kwenda kumbembeleza huku akimwambia asijali wala asihofu Jay ni wakwake tu ila ameondoka kutokana na hasira tu.
***** ****** ****
Huku nako kila mtu alikaa upande wake wa kitanda Akram alionekana akitizama mkono wake ambao uliingia mahali ambko siyo sahihi hata kidogo. Upande mwingine nao Nasma alikuwa akigusa gusa vimikono vyake huku akiwa ameushikilia ufunguo mkononi mwake.
Akram alisimama na kumfuata kisha akanyoosha mkono.
"Nini??? Aliuliza Nasma.
"Nipe ufunguo nataka nitoke" alijibu Akram.
"Huwendi mahali Malikia......
"Nimeshakwambia siendi huko alafu Nasma....... Alizungumza na kumnyooshea mkoni ambao ulielekea kifuani kwa Nasma.
Alimeza mate kisha akamwambia.
"Nipe ufunguo"
Nasma alisimama na kwenda kufungua mlango kisha akamwambia tutaenda wote.
***** **** *****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Johnny aliingia katika nyumba moja ya Kubwa ya kitajiri na kila alipopig hatua kulikuwa na wafanyakazi walioweza kumpa heshima kwa kuinamisha vichwa vyao aliingia kisha akakalia sofa moja Kubwa sana.
Alikuja mfanyakazi mmoja na kumtoa viatu alivyokuw amevaa. Jay aliwasha TV na kuletewa juice.
Aliipokea na kuweka mezani kisha kuendelea kutizama TV yake. Akiwa pale alifikiria jambo kidogo kisha akatoka na kuelekea chumbani kwake ambako alifunga macho kisha akaanza kuitafuta Sauti ya Salhat baada ya kuipata aliita kwa Sauti ya utaratibu kabisa na kumfanya Salhat kule aliko kutabasamu.
"Jamani tutaendelea kuzungumza baadaye kuna mahli naenda aliongea na kuwaacha Eddy pamoja na Sheilah kisha akapotea eneo lile.
"Huyu sasa hatujamalizia kuongea anaenda kwa bwna wake" alizungumza Eddy na kumtizama Sheilah ambaye alitabasamu tu na kuzungumza kidogo tu.
"Napenda sana nikiwaona pamoja"
Eddy Alimtizama tu.
Huku nako Salhat alitokea katika nyumba ile aliyokuwapo Jay.
"Huku wapi huku?? Aliuliza Salhat.
"Kwetu"
"Kwetu?!!!! Alirudia neno lile kwa mshangao.
"Ndiyo kwetu"
"Sijaelewa unachokimaanisha ukisema kwetu" alirudia tena kuuliza akihitaji maelekezo zaidi Salhat.
Jay alimvuta kwa ukaribu na kumkunbatia kwa nyuma huku akimwambia.
"Namaanisha hapa ni kwetu Mimi na wewe.....pamoja na familia tutakayoweza kuitengeneza tutaishi hapa" alizungumza Jay.
Salhat alibasamu na kumgeukia Jay.
"Yani wew unawaza sana kuzaa badala ya kuwaza jinsi gani tunaweza yakabili matatizo yatakayoweza kuikumba dunia" alizungumza Salhat.
"Dunia ni Mimi na wewe bila mm n we wala kusinglikuwa na dunia lazima tuwaze kwanza maisha yetu kabla hatujawaza maisha ya watu wengine tofauti na sisi" alizungumza Jay na kumshka mkono Salhat kisha akaenda kukaa kitandani na kumfanya Salhat akae juu ya mapaja yake.
"Salhat"
"Abee"
"Nahitaji tujenge familia yenye amani na upendo kam haya yote yataweza kuisha"
"Sawa unahitaji tuzae watoto wangapi???? Aliuliza Salhat.
"Wowote wale Mungu atakayeweza kutujalia hata kama ni 9"
"Watoto Tisa???? Hapana !!!! Haaaa!!!!
"Sasa kwani wewe unawaza nini na pesa ipo ya kuwalelea" alizungumza Jay.
"Siwazi pesa yani wewe uniingize miye leba mara9, unataka nifie uko au???
"Mbona wenzako wanazaa mpaka12 na hawafi" alijibu Jay.
"Sitaki labda watano nizae Mimi na wanne umalizie wew e" alijibu Salhat.
"Ahaaa kwahiyo na Mimi nizae" alizungumza Jay.
"Sindyo"
"Mshenzi sana ww na adabu huna Mimi nawazalia wapi hao watot kwa mfano aliuliza Jay.
"Usijali ukifikia muda wa kuzaa Mimi nitakuonyesha uzalie kwa wapi" alizungumza Salhat.
"Hivi unaongea ujinga gani hapa" alizungumza Jay na kusimama kitandani huku akimuachia Salhat ambaye alisimama.
"Sasa kinachokukasirisha ni nini kwa mfano aliuliza Salhat akimfuata Jay.
"Unanikera bwana unasema Je Mimi nizae" alizungumza Jay.
"Sasa kwani na wewe htaniwi jamani" alizungumza Salhat aliyekwenda mbele ya Johnny na kusimama kisha akamshika mikoni yake.
"Yaishe basi name wewe mbona hivyo nisamehe basi alizungumza na kumtoa mikono Jay aliyokuwa ameikunja.
"Jay yaishe basi alizungumza na kumpiga busu la mdomo "nisamehe" alimbusu tena na tena hadi Jay alipoweza kuiweka mikono yake nyuma yake kisha akambusu.
"Ingelikuwa sikupendi ningekuacha Leo kama nilivyomuacha Grace"
"Unamaanisha nini unaposema umemuacha Grace na ndoa ni kesho kutwa tu"
Jay Alimtizama kisha akaitoa mikono yake.
****** ******
"Grace huwezi amini ya kuwa kinachomfanya Johnny asikutake ni Salhat" alizungumza Badra.
"Hata Mimi natambua ya kuwa Salhat ndo chanzo cha yote Hata nimemwambia Mara nyingi tu akae mbali na Johnny lakini hanielewi wala hanisikii.
"Grace sitaki kuaibika Mimi sitaki kabisa kupata aibu mjini hapa lazima tufanye vile utakavyoona inafaa lakini uolewe la sihivyo Mimi nitaondoka nikuwache wew na aibu zako"
"Sasa mama nifanyaje?? Aliuliza Grace.
"Kiburi cha Jay ni Salhat lakini endapo Salhat atakufa basi lazima arudi tu kwako" alizungumza Badra.
"Huyu mpuuzi huyu nilimtengenezea kesi Mara ya kwanza akaikimbia ila kwasasa hivi sitakuacha mzima Salhat sitakuacha mzima" alizungumza kwa hasira na huku nako Badra alicheka na kutabasamu tu huku akizungumza kimoyoni.
"Kwa upande wa Grace nimeshamaliz sasa natakiwa nimtafute Salhat" alizungumza kimoyomoyo huku Alimtizama Grace na kutikisa kichwa chake ishara ya kuwa anamuonea huruma sana.
Huku nako yalikuwa mahojiano baina ya Salhat na Jay.
"Lakini Jay ulivyofanya Si vyema" alizungumza Salhat.
"Kwani wewe unashida gani?? Mimi sikumpenda Grace na hata yeye alitambua tena nilikuwa naye kwaajili ya kulipiza kisasi changu juu yake"
"Lakini huwezi kutumia moyo wa mtu katika kuutekeleza shida zako Jay.....kila kitu kinaweza kupata repair lakini siyo moyo wa mtu hujamfanya vyema kabisa Grace"
Jay alitafakari kwa muda kisha akasema
"Ni kweli sijamtendea haki Grace kwani yeye ni tofauti kabisa na mama yake Badra ila sasa yeye ndiye aliyekuwa njia pekee ya mimi kumfuata Badra.......pia kitu kingine ni kuwa ninauhakika Grace hakuhusika na mauji ya wazazi wako Bali ni Badra ili yeye anipate mimi hivyo lazima akuteketeze wewe na Grace" alizungumza Jay na kusimam kisha akaelekea dirishani na kusema.
"Badra muda wako sasa umefika lazima niyatete maisha ya Grace kama fadhila ambazo niliweza kuutumia moyo wake. Alizungumza Jay.
Siku hiyo aliweza kukutana na Grace katika bar ambayo walikaa kisha akaanza kuzungumza.
"Grace nafanya Haya yote kwaajili yako kwani naamini ya kuwa wewe ni tofauti na mama yako ambaye aliweza kuniuliwa watu wangu wa dhamani pamoja na baba yako Mr matata"
"Unaongelea nini wew???? Aliuliza Grace akionekana kushangaa kutokana na maneno aliyoweza kuambiwa na Johnny.
**** **** ****
Huku nako alionekana Nasma aliyekuwa akimchuachua kwa kutumia dawa bab yake Akram kuanzia mikononi kwani aliweza kupararaizi.
Akram alikuwa akiziweka nguo nyingine za baba yake kwani kila Mara huwa anamletea nguo nyingine kumvisha kisha humchukua video kila Siku iitwapo leo huku akiamini ya kuwa Siku baba yake atakayoweza kuamka basi atakuwa akimshukuru yeye kwa kuwa alikuwa akimjali sana alipokuwa hospitalini.
"Nasma nikusaidie kidogo" alizungumza huku akichukua dawa ile na kuminyia mikononi mwake kisha na yeye akaanza kumpaka mkono mwingine.
"Nasma" aliita tu baada ya kuanza kuupapasa mkono wa baba yake.
"Abee"
"Imepita miaka mingi sana baba yangu akiwa katika hali hii hata katika graduation yangu hakuweza kuhudhuria katika dunia hii hakuna mtu ninayemfahamu zaidi ya baba yangu pekee" alizungumza huku akiyazuia machozi yake yasitke.
"Na shuleni ulisomaje??
"Ni katika hali ya kushangaza sana kutokana na akili nilizo nazo basi nilimpata mfadhili ambaye sijawahi onana naye hadi sasa wala mfadhli huyo hajawahi kuzungumza na mimi"
"Ni wa jinsia gani???
" wa kiume" alijibu Akram.
"Ametokea nchi gani????
"Mara nyingi nilipoweza kuwauliza wale ambao wnapoke fedha kwa mfadhili wangu walisema mfadhili wangu hahitaji kujiweka wazi mbele yang.....lakini yeye ni mtu mweusi tena mtanzania hadi sasa namtafuta unajua kwann??? Aliuliza Akram.
"Hapana" alijibu Nasma.
"Katika maisha yangu napenda kuwafahamu ndugu zangu zaidi na zaidi nikimuweka baba pembeni nahisi ya kuwa huwenda na yeye akawa ni ndugu yangu ndyo maana haitaji kujitambulisha kwangu" aliangalia huku akicheka.
"Bora hata wewe unababa......mimi na Sheilah tuliokotwa na Malikia ambaye tunaishi naye sasa Sheila alikuwa wa kwanza kupatikana kisha nikapatikana na mimi katika mazingira yaliyo tofauti.......mara ya kwanza kuingia katika ngome ile nilikuwa mpweke sana na mkimya wa ajabu Eddy pamoja na Sheilah Ndiyo walioweza kuniambia maneno ambayo yalinifanya nikabadilika sana na nikawa faraja kwao"
"Kwahiyo wewe humjui baba wala mama yako wala wewe ni nani??? Aliuliza Akram.
"Hapana kwasababu mimi Sikuwa Jini Bali binadamu ila baada ya kuona nateseka dunia ni Malikia aakaamua kunibadilisha hadi Jini ili niweze kuishi naye huku" alizungumza Nasma.
"Kumbe binadamu anaweza kubadilishwa kuwa Jini ???
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndiyo lakini ni hatari sana kwa mara ya kwanza nilipoweza kuwa Jini sikuweza kushika kitu chochote kile katika mkono wangu wla sikuweza kuonekana tena katika macho ya kawaida kama nilivyozowea hivyo niliona kama wamenipa mzigo mzito sana na kuwachukia zaidi lakini miaka ilivyozidi kwend niliweza kuyazoea mazingira na hadi sasa nayafurahia sana kwani nimekutana na watu ambao upendo wako ni mkubwa sana juu yangu" alizungumza Nasma na kuyafuta machozi yake ambayo yaliweza kudondokea katika mkono wa baba yake Akram.
**** ****** *******
Grace alirudi nyumbani akiwa kama kichaaa nywele zake zilikuwa tifutifu sana kila alipokuwa akikumbuka Yale yote aliyoweza kuambiwa na Jay aliishiwa nguvu kabisa na hatimaye aliweza kudondoka chini.
****** ******* ******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment