Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

BINTI KIPOFU - 5

 







    Simulizi : Binti Kipofu

    Sehemu Ya Tano (5)





    Tropina akiwa gerezani huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo ghafla aliweza kuguswa begani na Diana aliyeweza kuja kumtembelea.



    "Diana vipi uko salama??



    " Ndiyo ila Vikram naamini anaweza akawa kichaa anakunywa pombe usiku kucha na amemfukuza Jimmy Jana baada ya Jimmy kumnyang.anya pombe pia Dr Kim na yeye aliweza kumfukuza sababu alimpa Larry vidonge vya kutoa mimba yako kama amiinivyo yeye'



    "Diana jaribu kumsaidia Vikram asinywe kwa kiasi hicho anaweza akapoteza maisha eti kabla hajamuona mtoto wetu, embu mwambie aje nataka kuzungumza naye inabidi nimwambie ukweli kwni sihitaji kumpoteza zaidi"



    "Hata Mimi nafikiri hivyo ni vizuri" alizungumza Diana na kuondoka baada ya muda alionekana Vikram akiwa amekaa na Tropina aliyeeonekana kulewa sana



    "Vikram kwanini unakunywa pombe na unajua sipendi nikikuona unakunywa pombe" alizungumza Tropina na kumtazama Vikram ambaye Alicheka kidogo na kumtizama kwa hasira.



    "Hivi unajua nataka nikufanye nini kwasasa Hivi...nataka nikunyonge na nikuuwe kama ulivyoweza kumuuwa mtoto wangu ila sitaki kufanya hivyo kwani itakuwa umewahi kupoteza maisha hivyo utakaa mpaka miaka 7 iishe kish unyongwe nikishuhudia......mwanamke mbaya sna wewe hata baada ya kumtoa mtoto wangu bado unahitaji talaka? Aliuliza Vikram.



    " talaka??? Aliuliza Tropina kwa mshangao.



    "Sawa nitafanya kama vile unavyotaka sindiyo ulichoweza kuniitia hapa sawa tutafanya hivyo" alizungumza Vikram na kutoa karatasi kisha kumpatia Tropina.



    "Wewe Vikram nani kakwambia Mimi nimedai talaka?? Aliuliza Tropina.



    "Usijifanye ya kuwa hujui nani kafanya hivi wakati ni wewe mwenyewe ndiye uliyeweza kutuma mwanasheria katika nyumba yngu umeona kumtoa mtoto wangu haitoshi sasa Unataka na talaka tena wakati unajua kabisa kwenye dunia hii sina kingine kilichoweza kubakia zaidi ya wewe na Larry lakini oneni mnavyoyachezea maisha yangu oneni mnavyoyachezea maisha yangu" alizungumza kwa hasira na kumwambia Tropina.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sign sasa sindiyo unachoweza kukihitaji. Alimpa karatasi kwa nguvu Mkononi.



    Tropina alishngaa baada ya kutoweza kumuona tena Vikram.



    " Ndiyo nilijua ya kuwa nitarejea katika hali yangu ya ukipofu lakini nilihitaji sura yko iwe sura ya mwisho ambayo ningeweza kuiona kabla sijawa tena kipofu Vikram nashukuru kwahili nitakaa na sura yako hii mpaka pale nitakapoweza kufanyiwa operations kwa Mara nyingine... Na kwa Mara nyingine pia natamani nitakapofungua macho yangu basi wewe uwe wa mwanzo kukuona ila sitapenda nikuone kwa sura hii yenye udhuni" alizungumza Tropina na kuchukua biki kwa kutumia hisia zake kisha kutaka kusign karatasi zile ila karatasi zile aliweza kuzigeuka na upande ambao alitakiwa kusign ukakaa juu na kumuelekea Vikram aliyekuwa akitetemeka kwa hasira



    Vikram alichukuwa karatasi zile na kumgeuzia ili azisign bila kugundua wala kushtuka chochote.



    Tropina jiandae tunakuhamisha gereza. Ilikuwa sauti ya mkuu wa gereza kwani asingeweza kukaa tena pale pindi mimba yake ingeendelea kukuwa basi ingefahamika hakutoa mimba.





    'Mnampeleka wapi aliuliza Vikram na kusimama.



    "Sorry, tunamuhamisha gereza kwani kutokana na tukio la kutoa mimba aliloweza kulifanya litamuhadhiri kisaikolojia kama atabaki hapa. Alizungumza mkuu wa gereza.



    " kwahiyo mnampeleka gereza la vichaa amah, afisa kutoa mimba siyo kwamba ni kichaa Pinah siyo kichaaa" alizungumza Vikram.



    "Hapana hatumpeleki gereza la vichaa, tunampeleka gereza lingine tu la kawaida......... Tropina kachukue kila unachoona cha dhamani na utoke kwaajili ya kuelekea huko"



    Pinah alitingisha kichwa chake kisha akasimama na kusogeza kiti chake kwa hisia na kuvuta kumbukumbu alikujaje hapo ndani.



    Alipiga hatua Tatu za kuelekea mbele na hatimaye aliweza kuzifikia nondo za pale na kuanza kutafuta komeo taratibu pasina mtu yoyote yule kugundua.



    Baada ya muda alionekana akiwa ndani ya defender yeye pamoja na baadhi ya wafungwa wenzake na mkuu wa gereza aliloweza kutoa naye akisema na kumwambia dereva



    "Hilo gari linaloweza kutufuatilia hakikisha unalipoteza bila yeye mwenyewe kutambua hilo"



    "Ndiyo" alijibu na kuongeza mwendo pamoja na kuingilia magari kadhaa ya mbele huku akiweka mlio uliweza kufanya magari yaliyokuwa yako mbele yaweze kumpisha na kurudi nyuma. Hatimaye Vikram alishindwa kuwafuata baada ya magari kadhaaa kuingilia mbele yake.



    "Pumbavu kabisa, nilijua tu hiki kitatokea....alizungumza na kupiga gari lake.



    " Pinah kitu gani unakifanya na uhitaji Mimi nikifahamu?? Aliuliza Vikram aliyeanza kupigiwa honi watu wakihitaji apishe njia. Aliwasha gari lake na kuligeuza kisha kurudi alikoweza kutoka.



    **** **** **** ****



    "Ndiyo ameweza kupelekwa gereza la vichaa na huko ataka mpaka miaka yake 7 iishe kisha atatimiliziwa hukumu yake" alizungumza afisa ambaye alikuwa kitu kimoja na Alice.



    "Sawa kazi nzuri ila inabidi na wewe sasa nikufanyie mbinu uelekee huko huko kwani Kuna kazi ya mwisho sasa nahitaji ukanisaidie kumalizia. Alizungumza Alice na kukata simu.



    " kitu kilichoweza kubaki ni Mimi kuolewa na Vikram ili niwe mke wake halali, hivyo inabidi talaka itokee katikati yao" alizungumza Alice na kucheka.



    Wakati huo ndani Vikram alikuwa akinywa pombe na kushikilia karatasi ambazo aliweza kumpatia Tropina a sign.



    "Mwanamke mjinga sana huyu...anaaamini sana watu wengi Ndiyo maana kila mara anakuwa kwenye matatizo alizungumza na kuzichomoa zile karatasi ndani.



    Zilikuwa karatasi Tatu ya kwanza ilikuwa ya Precious mineral limited na karatasi ya pili iliweza kuandikwa T&L Company huku ya Tatu ikiwa imeandikwa Guardian. Hivyo karatasi zote mbili zilikuwa za umiliki wa kampuni zote mbili alizoweza kuzinunua tena Vikram kwaajili ya Tropina na Larry na karatasi ya tatu ikionyesha nani atakuwa mlinzi wa kampuni hizo pamoja na mtu ambaye anaweza akatoa maamuzi katika Maisha yao.



    Hapo hapo msg iliweza kuingia katika simu yake na ilisomeka hivi.



    " tayari nimeshaweza kuandaa talaka feki pamoja na watu ambao wameshaweza kuzi sign talaka hizo" baada ya kumaliza kusoma msg hiyo aliichukua kinywaji chake na kuweka mdomoni huku akisema.



    "Alice najua ndiko utakapo kimbilia"



    **** **** ****



    Huku nako Larry alikuwa amepanga foleni akielekea kwenda kusign kwaajili ya kujisajili kufanya mtihani wa darasa la nne wa kitaifa. wenzake wote waliweza kusign karatasi moja ila alipofika yeye mwalimu alimtizama na kutoa karatasi Tatu sehemu nyingine kisha akampitia asign.

    Alizitizama na kutaka kusoma ila mwalim alizificha na kumwambia sign haraka wengine wanakusubiria wewe Larry alisign zote pasina kuzisoma na baada ya hapo ilisogezwa karatasi walyokuwa wakisign watu wote na kuambiwa sign na hapa.



    Alisign na kuondoka zake ila alipofika mbele kidogo alijiuliza kwanini ame sign karatasi nne wakati wenzake wame sign moja moja tu. Alimuona mwalimu akizirudishia karatasi zile Tatu katika bahasha ya kaki na kuzifunga kisha kusimama na kumwambia mwalimu mwingine awa signishe yeye akatoka njee.



    Larry alimfuata taratibu pasina mwalimu kugundua chochote na mbele aliweza kukutana na Vikram aliyekuwa akimsubiri.



    Alitoa bahasha ile na kumkabithi Vicky.



    Vikram alimshukuru na kutoa bahasha ndogo kisha akampatia.



    "Kama Kuna mtu mwingine tofauti Mimi ataweza kuja hapa na kukwambia umsignishe Larry basi naomba unipigie simu na uniambie karatasi hizo zinahusu nini Mimi nitakuongezea pesa. Alizungumza Vikram.



    " Haina shida mkuu hiyo Haina shida kabisa " alizungumza mwalim ambaye alionekana kupenda pesa sana.



    Larry alimtizama Vikram na kutabasamu.



    "Nilifikiri kweli kwamba hutakuja tena kuniona kama ulivyoweza kuzungumza na hutanisamehe kwa kunidanganya kwaajili ya wewe na dada yangu nitasoma sana tena sana" alizungumza Larry na kufuta machozi yake.



    Vikram alitoa atm card na kumpatia yule mwalimu akitaka ampatie Larry.



    Larry aliweza kuondoka baada ya kutokuwa na mashaka kwenye karatasi ambazo alisign.



    *** **** **** ****



    Tropina aliweza kupelekwa katika gereza jingine na huko alishngaa baada ya kumkuta Diana na kuweza kuisikia sauti yake.



    "Diana" aliita kwa kuhakikishana Diana alimkimbilia na kumkumbatia



    "Umefuata nini huku?? Aliuliza Tropina.



    "Nimekuja kukuweka umakini wewe pamoja na mwanao kwani madam Vanessa aliniomba nikutunze sana ikitokea yeye hatakuwepo tena duniani.



    Alizungumza na kumkumbatia zaidi.



    ****** ***** ******



    Alice aliweza kuja katika nyumba anayoishi Vikram ni nyumbani kwa kina Tropina na aliingia moja kwa moja hadi katika chumba anacholala Vikram akimtafuta.



    Alimtafuta bila ya mafanikio na aliziona karatasi katika meza iliyokuwa chumbani hapo.



    Alizishika na kuziinua kisha kuanza kuzisoma kwa pamoja.



    Alicheka na kuchukua simu yake kisha akampigia mtu.



    " haloo Haina haja tena ya kwenda kwani tayari wameshaweza kuachana" alizungumza Alice na kutabasamu.



    Wakati huo kulikuwa na camera ndogo iliyoweza kurecord mambo yote pale ndani.



    Vikram alikuwa sehemu nyingine akiwa na laptop yake huku akicheka na kuendelea kunywa pombe taratibu kabisa.



    Hapo hapo aliweza kuingia kijana mmoja na kutoa karatasi zingine kisha akampatia Vikram.



    "Hapo hata huyo unayefunga naye ndoa hawezi gundua ya kuwa ni feki" alizungumza kijana yule.



    "Ni sawa kwa kuwa kila kitu ni feki pia nilihitaji wewe uwe padri au unasemaje?? Aliuliza Vikram na kutoa pesa kisha kuziweka mezani.



    " katika pesa hakuna kitu kinachoweza shindikana" alizungumza na kuzichukua pesa zile kisha kuweka mfukoni.



    Vikram aligeuka nyuma baada ya kuhisi Kuna mtu anaweza kumfuatilia na hapo aliweza kutoka kijana mmoja aliyeweza kushusha kofia yak mpaka chini na kufanya uso wake usiweze kuonekana.



    Vikram alimtizama na kuweka tena pombe yake mdomoni na kuinywa taratibu kabisa.



    Alitoka njee na kukata kona huko naye aliyekuwa akimfuatilia na yeye aliweza kukata kona lakini hakumuona tena. Ghafla aliweza kuwekewa kisu shingoni mwake.



    "Nani kakutuma unifuatilie?? Aliuliza Vikram.



    " Ni Mimi Jimmy" alizungumza Jimmy.



    Jimmy aliitoa kofia yake na hapo sura yake iliweza kuonekana.



    "Oohhh Jimmy"



    "Sorry boss" alizungumza na kuanza kuondoka zake.



    "Jimmy, aliita Vikram na kumsogelea..... Samahani nataka kukuomba msamaha kwa kile kilichoweza kutokea ...unajua nilikuwa na hasira sana ndomaana nikazungumza maneno Yale yote ila kwa kweli nataka niwaombe radhi hata Dr Kim na yeye" alizungumza na kumshika mikono Jimmy.



    "Jimmy msamehe bossi wako Tafadhali nsamehe basi" alizungumza na kuanza kumkonyeza Jimmy ambaye Alicheka.



    "Nitakusamehe lakini kwa kufanya kitu kimoja kwaajili yangu" alizungumza Jimmy.



    "Sawa, nitafanya"



    "Uache kunywa pombe na turudi nyumbani......" Alizungumza Jimmy.



    "Sawa bossi" alijibu Vicky na wote walicheka kwa pamoja.



    ***** ***** *****



    Siku zilisonga mbele na miezi nayo ikatembea na sasa ilishafika miezi 7 tangu Tropina awe gerezani huku akionekana kukamata gazeti ambalo lilikuwa na picha ya Alice pamoja na Vikram katika siku ya ndoa yao iliyoweza kipita miezi mitano au minne ya nyuma.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiy hiyo pia ilikuwa ni siku y kufanya mtihani kwa darasa la nne mtihani wa taifa kwaajili ya kuingia darasa la tano mwakani huku njee alikuwapo Jimmy ambaye ndiye aliyekuwa mlinzi wa karibu kwa Larry pasina mtu yoyote kufahamu



    Ilikuwa alfajiri ya saa12 wanafunzi walipoweza kuamka na kuanza kujiandaa.



    Huku ikiwa imetimia miezi 9 kwa upande wa Tropina na kutegemea kuzaa muda wowote ule huku mimba ya Alice ikiwa ya miezi 7 na akiwa anasubiria miezi miwili ya mbeleni kwaajili ya kujifungua.



    Adrian akiwa amerud tena katika nyumba ya kina Larry na Tropina na safari hii akiwa mmiliki wa kampuni ya T&L company aliyoweza kuachiwa aitunze na kuiwekea umakini na sister Mary pasina kutambua yakuwa anaiwekea umakini kampuni ambayo bado ipo mikononi mwa Tropina.



    Alice akiamini ya kuwa kila kitu kimeisha na sasa ni mke halali wa Vikram akiendlea na maisha yake.



    Vikram aliweza kufungua kituo chke kidogo cha kulelea watoto yatima wazee wajane pamoja na watu wasiojiweza.



    Tropina akiwa gerezani ghafla alianza kuhisi maumivu makubwa sana tumboni mwake na Diana alikuwa pembeni yake hivyo aliweza kumsikia akiguguma.



    Hapo hapo simu iliweza kuita kwa Larry.



    "Dada yako anakwenda kujifungua Leo pia zinahitajika pesa za kutosha kwani kama haitowezekani kujifungua kwa njia ya kawaida basi tunahitaji pesa ya operations kwani Dr aliyekuwa akimtembelea hapa alisema Kuna uwezekano mkubwa sana wa Tropina kizaa kwa njia ya operations" alizungumza mkuu wa jela ambaye alihama na Tropina kutoka katika jela ya kwanza hadi kuingia naye katika jela ya pili.



    "Sawa nipe account namba zako nakutumia sasa hivi" alizungumza Larry na kukata simu.



    Akitizama atm card aliyopewa na Rickson haikuwa na pesa za kutosha.



    Alipiga simu yake ambayo iliweza kumuamsha Vikram aliyekuwa amelala kwenye kochi.



    "Haloo .......nani anaongea?? Aliuliza Vikram



    " Bwashe naomba unitumie million 10 kwenye account yangu" alizungumza Larry.



    "Million 10?? Aliuliza kwa mshangao na kuamka.



    " pesa nyingi hivyo za nini?? Aliuliza Vikram.



    "Tafadhali maisha ya watu wawili yako mashakani naomba unitumie hiyo pesa" alizungumza Larry.



    "Sawa nakutumia sasa hivi" alikata simu Vikram kisha akatoka njee na kumpigia simu Jimmy.



    "Uko hapo maeneo ya shule.......Kuna pesa namtumia Larry nataka ufuatilie matumizi ya hiyo pesa kwani ninawasiwasi sana" alizungumza Vikram na kukata simu kisha akaingia kwenye menu ya mpesa kwaajili ya kutuma pesa.



    Hapo hapo baada ya Larry kupokea pesa ile alipiga tena simu na kwa umakini zaidi Jimmy alikuwa akimfuatilia.



    Muda kidogo liliingia gari na hapo hapo alishuka mkuu wa gereza na kwenda kuchukua atm card ya Larry iliyokuwa na pesa kisha Kuondoka nayo.



    "Imeingia hapa defender ya polis na Larry ametoa atm card nashindwa kuelewa.



    "Embu fuatilia kwa makini inawezekana Tropina Kuna tatizo ameweza kulipata" alizungumza Vikram na kurudi chumbani kwake kisha akaelekea bafuni haraka haraka.



    Hpo hpo simu ya Alice iliita na alipokea.



    "Nini!!! Nani anamimba??



    " Mara zote alikuwa akikaa ndani na sero yake ilikuwa tofauti na ya kwetu ila Leo wamemtoa hapa na mimba yake ni kubwa tena nahisi anaenda kujifungua" alizungumza afisa ambaye alikuw chini ya Alice tangu alipokuwa kwenye gereza la kwanza.



    "Jua wanampeleka hospital ipi.....huyo mtoto lazima afe" alizungumza na kusimama zake kitandani kisha kwenda kuvaa nguo zake kwaajili ya kuondoka wakati huo nao Vikram alitoka bafuni na kuelekea kwenye kabati yake huku akichambua chambua nguo kwa kuzitupa huku na kule haraka haraka.



    Alice alihisi ya kuwa Vikram ameshagundua.



    "Vicky, unawahi kwenda wapi mume wangu?? Aliuliza Alice.



    " Hata Mimi sijui ila ninahisi nitapata habari za kushtusha hivyo nahitaji kufanya haraka"



    hapohapo simu yake iliita.



    "Haloo boss sifikiri kama naona sahihi ila nina uhakika ya kuwa huyo mwenye mimba mbele yangu ni Tropina na anaingizwa hospitalini kwaajili ya kujifungua alimaliza kuzungumza Jimmy na kumfanya Vikram akumbuke maneno ya Larry.



    " Kuna watu wawili wanahitajika kusaidiwa"



    Mtoto wangu alisema neno hilo Vikram na kutoka njee ya chumba kile.



    "Vicky!!! Aliita Alice na kuanza kumfuata nyuma.



    Vikram ghafla aliweza kujikwaa na kudondoka chini Vikram akishangaa kwani ilikuwa ni ghafla sana na aliweza kubiringita kwanzia juu ya ngazi hadi chini.



    " Alice" aliita Vikram na kumfuata Alice akiyekuwa chini huku akiguguma kwa maumivu.



    Hapo hapo msg iliingia kwenye simu yake na kusoma jina la hospital aliyoweza kupelekwa Tropina.



    "Njoo nisaidieni kumbeba huyu tumpeleke hospital" alizungumza Vikram na walinzi kadhaa waliingia ndani na kumtoa njee Alice.



    ***** ***** ****



    Hospitalini baada ya kuzidiwa kwa Tropina aliweza kuhamishwa kutoka labour mpaka Katika chumba cha operation wakati huo nao Alice aliweza kuletwa na machela na kupelekwa chumba hicho hicho cha operations.



    "Pinah" aliita Vikram na kumshika Mkono Tropina aliyekuwa amejawa na jasho mwili mzima.



    "Ricky" aliita Tropina kwa shida sana.



    "Usijali utatoka ukiwa salama kila kitu kitakuwa salama" alizungumza Vikram na kuuachia Mkono wa Tropina aliyeweza kuingizwa chumba cha operations.



    "Anashida gani huyu?? Aliuliza Dr aliyeweza kumpokea Alice.



    " anamimba ya miezi saba na ameweza kudondoka juu mpaka chini ya ngazi" alizungumza Vikram.



    "unauhakika ni ya miezi saba"



    "Ilikuwa inaelekea miezi 8" alizungumza Vikram.



    "Sawa embu, subiria hapa tumtizame hali yake pamoja na mtoto"



    "Vikram aliita Alice na kumshika Mkono.



    "Usijali utakuwa salama" alizungumza na na wote waliweza kuingizwa katika chumba kimoja hku wakitenganishwa na pazia Vikram's alikuwa njee huku akishika kichwa chake na kukikuna Kuna.



    Hapo hapo iliweza kuingia simu ya Larry.



    "Larry usiwe na wasiwasi, fanya mtihani kwa umakini zaidi Mimi nitamtizamia Tropina na Mjomba wako"



    "Dada angu atakuwa salama lakini?? Aliuliza Larry



    " Ndiyo yuko salama" alijibu Vicky.



    "Walisema ataingizwa operations kama.........."



    "Hapana hajaingizwa theater yoyote ile wewe kuwa makini katika mtihani wako atajifungua salama" alizungumza Vikram na kukata simu.



    Larry alishusha pumzi ndefu kisha akaanza kuelekea katika chumba cha mtihani.



    Masaa matatu yalipita na hakukuwa na Dr wala nesi yoyote aliyeweeza kutoka katika chumba cha operations.



    "Jimmy ni saa tatu sasa na hakuna chochote kile kilichoweza kutokea kwanini hatoki mtu hata mmoja Mimi nitaingia ndani. Alizungumza Vikram na kutaka kuingia ndani mbele ya macho yake aliweza kukutana na manesi wawili walioweza kushika watoto wawili wadogo na wote ni wa kiume.



    Aliwatizama wote kwa pamoja na kutabasamu.



    " Watoto wangu hawa" alizungumza na kutabasamu.



    "Huyu ni mtoto wa mwanamke Tropina alizungumza nesi mmoja na Vikram alimtizama kisha akatabasamu.



    " na huyu ni wa Alice " alizungumza nesi mwingine na aligeuza macho yake kwa mtoto mwingine.



    "Ni wazuri wote na wanafanana sana, ila huyu kafanana sana na Larry pamoja na Mimi na mama yake" alizungumza Vikram na kutabasamu.



    "Tafadhali tunaomba tuwapeleke sehemu husika. alizungumza nesi yule.



    " Huyu wa Tropina andika Rickson na huyu wa Alice andika Vikram " alizungumza Vikram na kucheka sana huku akijisifia na kusema ni watoto wangu eti.



    Hapo hapo walitoka madactari wawili.



    "Tropina na Alice wanaendeleaje??



    " Tropina bado hajapata fahamu na Alice yeye pia bado hajapata fahamu ila anaweza akaamka muda wowote kutoka sana na pia kwa mtoto wa Tropina anaonekana kama alipokuwa tumboni kwa mama yake aliweza kunywa Yale maji machafu hivyo tunahitaji kumfanyia matibabu zaidi na kwa upande wa mtoto wa Alice pia ametoka akiwa mdogo sana mimba yake haikuweza kukamilika hivyo pia mtoto wake anaweza akapoteza maisha kama hatutaweza kumuwekea umakini. Alizungumza Dr.



    "Sasa unazungumza nini mbona sikuelewi?? Aliuliza Vikram na Tabasamu lake liliweza kupotea usoni.



    Manesi walipoweza kufika katika chumba cha kuweka watoto mmoja wao aliweza kuchanganya.



    "kasema mtoto wa Tropina tumuandike Vikram alafu mtoto wa Alice tumuandike Rickson " alizungumza nesi mmoja.



    "Hapana bhna amesema mtoto wa Tropina tumuandike Rickson alafu wa Alice tumuandike Vikram" alizungumza nesi aliyekuwa amembeba mtoto wa Tropina.



    "Hapana wa Alice tumuandike Rickson alafu wa Tropina Ndiyo Vikram" alizungumza nesi aliyeweza kumbeba mtoto wa Alice.



    "Sawa ila sina uhakika" alizungumza nesi yule na kuandika jina la Vikram kwa mtoto wa Tropina.



    Hivyo watoto wakawa wamebadilishwa kwa njia hiyo.



    Baada ya muda kidogo Vikram alikuwa nyuma ya kioo akiwatizama watoto wake ambao waliweza kubadilishwa pasina yeye kutambua.



    "Sitaacha jambo lolote baya liweze kuwatokea ninyi.....nitawasaidia kwa njia yoyote ile na kuhakikisha ya kuwa mpo katika hali ya usalama" akiwa anazungumza maneno hayo ghafla mtoto wa Alice aliyeweza kuandikwa jina la Rickson alianza kuweweseka weweseka kitanda hapo.



    "Nesi, docta.....nesi" aliita kwa sauti na manesi waliweza kufika pale na kuanza kuingia ndani ya chumba kile cha kuhifadhia watoto.



    Vikram alitaka kuingia lakini aliweza kuzuiliwa na madactari walioweza kumchukua mtoto haraka haraka na kumpeleka katika chumba cha operations zaidi kwani hata nayeye pia aliweza kunywa maji machafu yaliyoweza kuwa tumboni mwa mama yake wakati huo nao Tropina aliweza kupata fahamu na neno la kwanza lilikuwa ni



    "Mtoto wangu" alisimama katika kitanda kile na kuanza kutoka njee taratibu kabisa huku akijitahidi kuvumulia maumivu kwani bado alikuwa na mshono katika tumbo lake.



    Alipiga hatua huku akiugulia maumivu katika tumbo lake aliweza kujikongoja na kutembea kwa kutumia vibambaza taratibu kabisa mpaka alipoweza kumuona Vikram akiwa njee ya chumba cha operations tena huku akizunguka zunguka kulia na kushoto. Ghafla waliweza kuonana.



    Alimfuata na kumchukua taratibu.



    "Rickson......mtoto wetu yuko wapi?? Aliuliza Tropina.



    Vikram alimkumbatia na kumwambia usijali kila kitu kitakuwa sawa...subiria kidogo tu ataweza kuja hapa hawezi kuondoka na kutuacha sisi nyuma" alizungumza Vikram na kumkumbatia Tropina.



    "Mtoto anayeumwa ni mtoto aliyeweza kuandikwa Rickson' alitoa majibu nesi mmoja aliyeweza kumletea majibu Vikram aliyeweza kuuliza ni mtoto yupi anaumwa.



    " anamaanisha nini?? Aliuliza Tropina.



    "Mtoto wako nilisema aandikwe Rickson kisha mtoto wa Alice wamuandike Vikram ili kuweza kuwatenganisha. alizungumza Vikram na ghafla damu zilianza kutoka tena katika tumbo la Tropina aliyekuwa ameshonwa muda siyo mrefu.



    Vikram aliweza kumbeba na Tropina alizimia hapo hapo.



    " Dr....Dr aliita Vikram kwa kasi sana wakati huo Jimmy alikuwa akirudi ndani ya hospital baada ya kutumwa na Vikram.



    "Ni nini tena?? Aliuliza Jimmy na kumsaidia Vikram kufungua mlango wa chumba alichokuwa amelala Tropina baada ya kutoka chumba cha Operations.



    Jimmy aliweza kuleta nguo mbili za watoto wadogo tena mfanano alizoweza kuagizwa na Vikram.



    Wakati huo katika chumba cha watoto alionekana mtoto wa Tropina akifumbua macho yake na kuanza kulia huku katika shingo yake upande wa kushoto alikuwa na alama nyeusi ndogo iliyokuwa mfanano na alama ya Larry na hiyo ndiyo sababu Vikram aliweza kusema ya kuwa anafanana na Larry.



    Larry akiwa amemaliza mtihani wa kwanza aliweza kutoka njee na kuwa na mashaka sana ghafla aliweza kuitwa na mwalim ambaye ni mshirika wake na Rickson.



    Alitoa simu yake mfukoni na kumuonyesha picha ilikuwa ni picha ya mtoto mdogo aliyoweza kuituma Rickson na kutaka Larry afanye mtihani akiwa hana mashaka yoyote yale pia aliusindikiza na ujumbe mfupi.



    " amefanana na wewe, na Mimi pamoja na dada yako"



    Larry alitikisa kichwa na kutabasamu.



    "Kwaajili ya Mjomba wangu nitafanya vizuri sana kuhakikisha ya kuwa siiharibu hii siku yake ya kuzaliwa.



    Wakati huo Vikram alimpiga mtoto wa Tropina picha akiamini niwa Alice na kusema



    " Sina cha kufanya kingine juu yako mwanangu, Tafadhali muombe kwa Mungu ndugu yako na yeye awe salama kama ulivyoweza kuwa wewe " alizungumza Vikram na hapo hapo aliitwa.



    " Wewe Ndiyo baba wa Rickson"



    "Ndyo Mim mtoto wangu anaendeleaje?



    " yuko salama kabisa kwa sasa na hali yake ni nzuri ila anahitaji muda zaidi wa kupumzika pia tunampatia hewa kupitia mitungi ya oksijen ila baada ya muda mfupi atarejea katika hali yake na tutatoa mipira hiyo" alizungumza Dr.



    "Je naweza kwenda kumuona?? Aliuliza Vikram.



    " Ndiyo ila kwa dakika chache tu"



    "Na mama yake je??



    "Sawa ila usimtembeze utachukua kigari na kumuweka hapo alafu utampeleka akamuone mtoto wke.



    " Sawa Dr ahsante" alizungumza Vikram na kutoka katika chumba cha kuwatizama watoto na kuelekea katika chumba alichokuwa amepumzishwa Tropina.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Amepona eeeee sasa ngoja nikamuuwe Mimi mwenyewe" alizungumza Alice na kuvaa koti la ki dactari kisha kuelekea katika chumba ambacho alikuwa amelazwa mtoto wake lakini pasina ya kutambua.



    Alipofika mtoto aliweza kufumbua macho yake na kuachia kitabasamu kwa mbali sana.



    "Unanichekea Mimi?? Aliuliza Alice na kutoa mpira ule wa oksijen aliokuwa akiutumia mtoto yule baada ya kuona hapati shida katika upumuaji alimziba pua na mdomo wake kupitia mikono yake na hapo hapo mtoto aliweza kutupa tup miguu yake kwa sekunde kadhaa na hatimaye aliweza kuacha kufanya hivyo.



    Alice aliurudishia mpira ule na kutabasamu kisha kuanza kuelekea njee ghafla akiwa mlangoni aliweza kumuona Tropina na Vikram wakiwa wanakuja katika chumba alichoweza kusimama mlangoni.





    Miaka ilieenda na hatimaye miaka mitatu ilipita na alionekana Alice akitoka katika kituo cha polisi hapo hapo aliweza kuja Thobias na George.



    "Mkuu nimepata ushahidi zaidi siku ya tukio hivyo ningependa kesi hii irudiwe tena," alizungumza George



    "Haina haja" alijibu mkuu wa kituo.



    "Kwanini??? Aliuliza George.



    " kwasababu tunakuhamisha kituo cha kazi na unaelekea mbeya" alizungumza Mkuu wa kituo hicho.



    "Unamaanisha nini sasa... Na tayari nimeshaweza kuandaa ushahidi mwingine wa......"



    George sitaki ubishani na wewe Tafadhali Tobias muandalie vifaa vyake na aondoke. Alizungumza mkuu wa kituo na kutoka na Alice aliyeweza kumtizama George na kutabasamu kisha akaondoka eneo lile.



    George alitizama ushahidi ambao aliweza kuuandaa aliitupa chini na kuukanyaga kanyaga kisha akaondoka kwa hasira.



    ***** **** ****



    "Miss Queen ni kwamba nimetizama hospitalini na hakuna ushahidi wowote kuwa Alice aliweza kumuuwa Mtoto wa Tropina kwani hakukuwa na record yoyote iliyoweza kurecord tukio hilo...pia nimejaribu kuwalipa ma nesi kama Kuna kitu chochote kiliweza kutokea wakati ule na wote wamekiri hakuna kitu chochote kibaya kilichoweza kutokea wala sign ya mtu yoyote yule aliyekuwa akihitaji kumuuwa mtoto yule.



    Alitoa maelekezo hayo Jacob msaidizi wa Queen.



    " ndo hivyo siyo?? Aliuliza Queen aliyeeonekana kukuwa baada ya miaka mitatu kupita.



    "Ndiyo" alijibu Jacob.



    "Sawa"



    "Na graduation ya Larry ni siku ya Ijumaa baada ya kumaliza mtihani wake wa mwisho siku ya alhamic. Alizungumza Jacob.



    Queen alimtizama na kumwambia.



    " nani alikutuma ukafuatilie taarifa hizo? Aliuliza Queen na kuonekana kuchukia baada ya kutajwa jina la Larry.



    Aliingia chumbani kwake na kukaa kitandani.



    "Mpumbavu huyu nani kamuliza kuhusu Larry" alizungumza Queen na kutupa tupa mito iliyoweza kuwa kitandani kwake.



    ******* ****** ******



    Larry alikuwa katika chumba chake huku akitizama picha ya Queens.



    "Vipi umemmiss aliuliza rafiki yake Larry



    "Hamna...alisema Larry na kuweka simu yake mfukoni.



    " atakuja siku ya graduation yake?? Aliuliza tena.



    "Hawezi kuja" alizungumza Larry.



    "Kwahiyo hukuwahi kumwambia ukweli wowote ule juu yako na Stellar?? Aliuliza rafiki yake Larry huyo walimuita Godlisten.



    " Nilimpigia simu lakini hakupokea nilipokwenda kumuona nyumbni kwao wazazi wake waliweza kunifukuza na nilipopiga tena simu wala hakupokea hivyo hata nimwambie nini awezi nielewa kwasababu alikuta Stella akiwa ananibusu alafu Queen akichukia ni mgumu sana kuelewa " alizungumza Larry na kutabasamu.



    "Ila naamini ya kuwa atakuja tu kwaajili yako na ipo siku ataelew kuwa Stellar alitumwa na Collins kwaajili ya kuharibu mapenzi yenu" alizungumza Godlisten.



    ****** ****** ********



    "Kwanzia sasa utaitwa Jacky na utakuwa ni msaidizi wangu Mimi katika kupambana na Rickson au Vikram vyovyote vile ajiitavyo na kufanya alipe kwa kifo cha baba yangu" alizungumza Harman.



    "Ndiyo" aliitikia mfanyakazi aliyekuwa wa Mr Harlan na sasa kawa mfanyakazi wa mtoto wa bossi wake.



    ***** ****** *******



    Tropina akiwa ndani ya gereza lake aliweza kuja Patrick aliyeeonekana kubadilika kabisa



    "Nilidhani umeweza kunisaliti na kukimbia na pesa zote" alizungumza Tropina.



    "Hapana siwezi kufanya hivyo madam Tropina nimeshaweza kuandaa kila kitu ulichoweza kuniagiza Philippines na Kuna mtu tayari anaishi kwa jina lako kwa miaka mitatu sasa hivyo ukienda haitakuwa na shida yoyote ile juu ya uwepo wako" alizungumza Patrick.



    "Sawa, siku ya Kuondoka ni Ijumaa usiku baada ya graduation ya Larry kuisha nataka Mimi niwe zawadi yake. Alizungumza Tropina huku mkuu wa gereza akiwa pembeni pamoja na Diana.



    ***** ****** ****



    "Jimmy, na Kim

    Kila mtu atafanya kitu kama tulivyoweza kupanga siku ya ijumaa.



    " Kim utamtorosha Tropina na kumchukua kwenye gari lako, Jimmy utamchukua Larry na Mimi nitamchukua Millerstone baada ya hapo Lucretius unajua unatakiwa uwe wapi na hakikisha rubani uliyempata kwaajili ya kuwahamisha nchi awe msiri sana" alitoa maelezo hayo Vikram na kusema.



    "Kila mtu awe makini na Alice endapo atatambua tu hili basi mchezo mzima umekwisha Mimi nitajua cha kufanya mpaka Tropina aweze kuhudhuria kwenye graduation ya Larry" aliongezea Vikram na kuwatizama.



    ****** ***** ******



    Millerstone alikuwa mkubwa mwenye miaka mitatu sasa.



    "Dady" aliita Millerstone na kumpokea Vikram.



    "Umeamka salama?? Aliuliza Vikram.



    " Ndiyo'



    "Na Alice?? Aliuliza Vikram.



    " Sijui limelala hata sielewi" alizungumza Millerstone.



    "Kwanini, humpendi mama yako?? Aliuliza Vikram.



    " Simpendi tu" alizungumza Millerstone na hapo hapo Alice alikuwa akishuka katika ngazi.



    "Millerstone mwanangu umeamka salama? Aliuliza Alice na Millerstone alibinua mdomo wake.



    " Miller Mara ngapi nimekwambia uwe na heshima kwa mama yako kwanini hutakagi hata kumsalimia?? Aliuliza Vikram aliyeweza kumsogeza Millerstone mbele ya macho yake.



    "Haya nenda kamsalimie mama yako" alizungumza Vikram na Millerstone alisogea mpaka alipo Alice.



    "Shikamo Alice" baada ya kumsalimia alirudi kwa baba yake.



    "Umeona?



    " bado "



    "Sawa twende leo baba ako akakuogeshe" alizungumza Vikram na kumbeba mwanaye kisha kupanda naye juu ambako alikutana na Adrian.



    "Millerstone hujambo? Aliuliza Adrian wala Millerstone hakuangaika kumjibu.



    " haka katoto kako kana kiburi kama Larry vile" alizungumza Adrian na kuondoka zake kuelekea kazini.



    Waliokuwa bafuni katika sink Vikram akimuogesha mtoto wake aliweza kumtizama sehemu ya pembeni ya shingo ambapo ndipo kulipokuwaga na alama ya mwanzo aliyoweza kuifananisha na Larry.



    "Miller" aliita Vikram



    "Dady"



    "Unajua kwanini unaalama katika shingo yako ya kuunguwa?? Aliuliza Vikram.



    " hapana "



    "Mimi na mama yako tulikuwa tukikugombania wewe na kwa bahati mbaya maji ya moto aliyokuwa ameyashika mama yako yaliweza kukumwagikia shingoni ulipokuwa na siku mbili baada ya kuzaliwa kwako, niliamini ya kuwa utaweza kupoteza maisha kama ndugu yako lakini namshukuru Mungu kwa kuwa hakuweza kuwachukua wote alizungumza Vikram na kutabasamu.



    " baba "



    "Naam"



    "Hivi Alice na Adrian wana mahusiano gani?? Aliuliza Millerstone.



    " kwnini unaniuliza hivyo??



    "Hamna" alijibu na kucheka.



    "Millerstone wewe ni mjanja sana na unaakili japo kuwa ni mtoto mdogo naamini ukifikisha miaka 5 basi utakuwa na uwezo mkubwa kuliko mtu mzima mwenye umri wa miaka hata 40....na hiyo ni kwasababu wewe wa......."



    "Mtoto wa baba Vikram's" alimalizia Millerstone na kutabasamu huku akiachia dimpozi zake katika mashavu yake.



    **** **** *****



    "Nina uhakika ya kuwa siku hiyo pia Vikram anapanga kunitorosha hivyo sitataka kuingia katika mikono yake hakikisha unafanya kila kitu kwa usahihi" alizungumza Tropina.



    "Sawa madam Tropina" alijibu Patrick.



    "Patrick unauhakika utaweza kulimudu hili?? Aliuliza Diana.



    " Ndiyo msijali kwani nimeandaa mpango kabambe ambao Vikram hata weza kugundua chochote kile mpaka pale ninyi nyote mtakapo ondoka " alizungumza Patrick akiwa na uhakika.



    Hatimaye cku yenyewe ili wadia na katika uwanja wa ndege ziliweza kuonekana ndege nne za private zikiwa zimepaki kila moja katika eneo lake.



    "Ndege ya kwanza alikuwapo Jacky ambaye aliweza kumuweka mtu pale na rubani, ndege ya pili alikuwa Lucretius aliyekuwa na rubani wake ndege ya tatu alikuwapo Patrick aliyeweza kuwa na kijana mmoja kisha akimpatia maelezo kipi kifanyike pamoja na rubani akiwa eneo lile ndege ya nne alisimama kijana mmoja aliyeeonekana kusikiliza mziki akiwa anatafuna bublish zake taratibu kabisa bila wasiwasi wowote.

    Hapo hapo simu yake iliita na aliipokea.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Yes boss...niko kwenye location" alizungumza na kukata simu wakati huo nao alionekana Queen akikata simu na kutazama nguo zake alizoweza kuziweka kitandani



    Simu yake iliita tena.



    "Unataka nini tena Jacob Aliuliza Queen.



    " ammmhhhh ni kwamba ammmhh............. Hapo hapo ilisikika sauti ya Larry



    "Queen kuliko kutuma mtu aje aangalie naendeleaje unaonaje ukija kuniona Mimi......nakusubiria saa12 jioni sherehe itaisha pindi ikiisha tu nitakusubiria bustanini sitatoka hapo mpaka pale utakapo kuja" baada ya kuzungumza hivyo alikata simu.



    "We...Larry......wewe....." Aliita lkini simu ilikatwa.



    "Hyu mpumbavu nini anampangia nani muda wa kwende?? Alijiuliza Queen na kuzitizama tena nguo zake.



    " unafikiri itasaidia?? Aliuliza Larry aliyeeonekana kuwa mtu mzima sasa kwani alishaweza kufikisha miaka13.



    "Ndiyo atakuja nina uhakika kwa hilo" alizungumza Jacob ambaye aliweza kumuuza Queen kwa Larry.



    ****** ****** ******



    "Tropina kutoka kama mgonjwa ndo itakuwa njia rahisi ya sisi kwenda kumtorosha kutoka hospital kwahiyo ifikapo saa11 hakikisha unamchoma sindano hii Tropina au unamuwekea kwenye chakula baada ya kula tu ataanza kuhisi kuumwa hivyo watampeleka hospital wakidhani ni sumu na hapo Dr Kim utaweza kuingia katika jopo hilo na utamchoma sindano hii ambayo itaondoa sumu yote mwilini....kumbuka zikishapita dakika 49 kama hajadungwa sindano hii basi atapoteza maisha kwahiyo kuwa makini, kwa upande wako Jimmy baada ya sherehe kuisha wewe utamchukua Larry natambua ni mbishi sana hivyo utamnusisha madawa ya usingizi na moja kwa moja utampeleka mahali ilipo ndege ambapo utamkuta Lucretius hapo....na Mimi nitamchukua Millerstone na kumleta huko huko" alimaliza kuzungumza Vikram na kutaka kila mtu aifanye kazi yake kwa usahihi.



    ***** ****** ****



    Haina haja ya sisi kujisumbua ya kuwa nitatokaje hapa naamini Vikram ameshaandaa njia zote na baada ya kunichukua Mimi hap ndo plan yetu inatakiwa ianze ya kuweza kunitorosha mimi na Larry katika mikono yake" alizungumza Tropina akimpatia taarifa hizo Patrick.



    "Kwahiyo utakula hicho chakula chenye sumu?? Aliuliza Diana.



    " Ndiyo kwani Ndiyo njia pekee ya mimi kutoka hapa na ndivyo alivyoweza kunijulisha Vikram " alizungumza Tropina.



    "Lakini Mimi sitaingia kwenye matatizo kweli? Aliuliza mkuu wa jela.



    " hapana bali unaweza ukafungwa kwa miezi7 tu kisha watakuachia na hapo utaenda kuchukua pesa zako bank kama tulivyoweza kukubaliana. Alizungumza Tropina.



    "Sawa"



    ****** ******* *****



    "Jacky, natumaini umeshaandaa vijana wa kwenda kusababisha ajali ya moto katika gereza lile na kumtorosha Tropina kwa Mimi kuingia ndani na kujifanya namsaidia ili asiweze kujua ya kuwa nimepanga iwe hivyo, Larry Naye baada ya kumaliza graduations yake na atakapoweza kutoka tu fanya aone mauaji na pale atakapoanza kuweweseka na kuto kujua kipi cha kufanya basi utajitokeza na kwenda kumsaidia alafu huyo mtoto wa Vikram huyo ni wakutekwa" alizungumza Harman na kutabasamu.



    **** ***** ****



    "Millerstone muage mama" alizungumza Vikram na kumtaka Millerstone afanye hivyo.



    "Mnaenda wpi?? Aliuliza Alice.



    " Tunaelekea kwenye graduation ya Larry, vipi wewe huendi?? Aliuliza Vikram



    "Hapana"



    "Ahaaa Hatimaye umekuwa sasa na hutaki tena kujionyesha kwenye magazeti kwamba unaionea huruma familia ya Vanessa" alizungumza Vikram na kuondoka na mtoto wake.



    "Siyo kwamba sijui unachotaka kwenda kukifanya leo Vikram huwezi kufanya hivyo unavyoweza kutak kukifanya" alizungumza Alice na kupiga simu yake.



    "Daudi ....umeweza kufanya kama nilivyoweza kukuagiza....sawa kazi nzuri" alikata simu na kurudi ndani kwake ambko alielekea bafuni na kuingia kwenye sink la kuogea huku akitizama sindano iliyokuwa pembeni yake.



    "Tuone atapona na nini ilihali sindano ya yenye dawa ninayo Mimi" Alicheka sana Alice na kusema mwisho kabisa.



    "Vikram unaamua kumuuwa kipenzi chako mwenyewe"



    Vikram alipanda ndani ya gari akiwa na mtoto wake Millerstone na alipokuwa ndani ya gari alifungua begi lake na kutoa sindano ambayo baada ya kuitizama alitabasamu na kuirudisha alipoweza kuitoa.



    Aligeuka na kumtizama Millerstone ambaye alionekana akiwa katika mawazo mazito.



    "Miller......Miller....

    Millerstone" aliita Vikram kwa sauti na hapo ndipo alipoweza kushtuka.



    "Unawaza nini?? Aliuliza Millerstone.



    " dady, tofauti na Alice hakuna mwanamke mwingine unayempenda?? Aliuliza Millerstone na swali hilo lilimfanya mpaka dereva wa gari na yeye ashangae.



    "Kwanini umeniuliza hivyo mtoto wangu" aliuliza Vikram na kumsogeza karibu Millerstone.



    "Hapana nilitaka tu kujua" alijibu.



    "Yupo, tena Ndiyo nataka ukakae naye uko Thailand pamoja na Mjomba wako Larry tunayeenda kumuona leo" alizungumza Vikram.



    "Basi vizuri...baba"



    "Naam"



    "Usije ukalala na Alice" alizungumza Millerstone.



    "Unamaanisha nini?? Aliuliza Vikram ambaye hakuweza kumuelewa mwanaye.



    "Namaanisha kufanya naye mapenzi na ukitaka kufanya hivyo basi tumia kondom alizungumza Millerstone.



    Dereva aliyekuwa akiendesha alishtuka na kusimamisha gari siyo yeye tu hata Vikram alishangaa mtoto wke anazungumza nini.



    'Miller unajua sikuelewi unachokiongea alizungumza Vikram na kumtazama mwanaye vizuri usoni.



    Millerstone hakuzungumza chochote tena baada ya kuzungumza maneno hayo.



    Wakati huo watahiniwa wa darasa la saba walihitajika kuingia ukumbini wakiwa na ndugu zao.



    Mr Mpalila aliweza kufika akiwa na mkewe kwaajili ya kijana wao Collins.



    Collins alimsogelea na kumwambia.



    "Sijui wasaa wako nani atatoka mbele kwaajili yako kwasababu hun baba huna mama wala Dada hata Queen naye hawezi kufika. Alizungumza Collins kwa ujasiri na aliweza kupita na wazazi wake



    Godlisten alimshika Mkono Larry na kumtuliza alipotizama aliona watahiniwa wenzake wakiwa na ndugu zao pembeni yao. Kwani walihitajka kuingia mmoja mmoja ukumbini wakiwa na wazazi au walezi wao.



    Watoto wote waliweza kupita mbele na ndugu zao na Larry ndiye aliyekuwa mtoto wa mwisho kuweza kuingia ukumbini alitizama viti vitatu vyote vilikuwa kwaajili yake.



    " Larry Livingstone" aliita jina hilo mwalim na kumtaka aingine pamoja na watu wawili ukumbini pale.



    Larry alitizama nyuma na hakukuwa na mtu yoyote yule ambaye aliweza kumfahamu.



    Mawazo yaliweza kumjia kama vile anamuona mama yake pamoja na dada yake wakija pale alipo kwaajili ya kumsindikiza ukumbini.



    "Larry livingstone Tafadhali ingia ndani ya ukumbi pamoja na wazazi walezi au ndugu zako wawili" alirudia mwalim yule na Larry alianza kujisogeza hatua za mbele alsikia minong.ono ya chini kwa chini.



    "Baba yake na mama yake wote wameweza kufariki na dada yake yuko gerezani anatumikia kifungo cha miaka7 kabla ya kunyongwa........

    Yuko pekee yake hana ndugu tena katika dunia hii mpaka namuonea huruma" alizungumza mmama mmoja aliyekuwa akimsemesha mwenzake.



    "Larry livingstone.... Huna mtu yoyote wa kukusindikiza wewe hata ndugu yako wa umbali kidogo? Aliuliza mc.



    " hapana nipo mwenyewe alijibu Larry " na kuanza kuelekea ukumbini.



    "Nipo Mimi nitamsindikiza ukumbini alizungumza Godlisten ambaye tayari alishaingia ukumbini na kusimama akitaka kuelekea alipo Larry ili amsindikize na yeye aje akae alipoweza kukaa.



    " Msipate tabu sana tumeshawasili" ilikuwa sauti ya Vikram iliyoweza kumfanya Larry adondoshe machozi na kumfuata pale alipo.



    "Samahani kwa kuchelewa bwashe" alizungumza Vikram na kumpiga piga mgongoni Larry.



    "Bwashe!!! Alirudia kauli ile kwa mshangao Millerstone.



    " Miller msalimie Mjomba wako huyu utaenda kuishi naye Thailand " alizungumza Vikram.



    "Kwahiyo ni wewe tu mwenyewe hakuna mtu mwingine? Aliuliza Mc.



    " inamaana huoni tuko wawili hapa?? Aliuliza Vikram na kumuonyesha Millerstone aliyekuwa amembeba.



    "Tofauti na huyo? Aliuliza Mc.



    "Hapana" alijibu Vicky na kumshusha Millerstone chini.



    "Lakini wanahitajika watu watatu. Alizungumza Mc.



    " we.........kabla hajamaliza kuzungumza Vikram alisikia sauti ikimdakia kwa nyuma.



    "Nipo.........samahani kwa kuchelewa" alikuwa ni Queen aliyeweeza kuvaa shati jeupe, sketi ndefu ya njano yenye mauwa meupe, kiatu cheusi kirefu na koti lirefu leusi aliloweza kulivaa kwa juu bila kuliingiza ndani ya mwili wake na kipochi chake cheupe.



    Watu walioweza kuwepo pale walishngaa ujio wa Queen kwani tayari alishaweza kujizolea umaarufu kutokana na kuwa model katika kutangaza bidhaa mbali mbali kupitia nguo alizoweza kazi design mwenyewe



    Aliwapita wote na kuelekea kwenye kiti kukaa huku akivaa miwani yake meusi.



    "Nafikiri tumekamilika tunaweza tukaenda kukaa sasa? Aliomba ruhusa Vikram na Mc alimtizama Collins ambaye alionekana kutaka kumuhaibisha Larry mbele ya umati wa watu lkini mbinu yake hiyo haikuweza kukamilika.



    Majira yaliweza kwenda na sasa ilishaweza kuingia saa11jioni.



    Vikram alitoka ukumbini kidogo na kumuachia Millerstone Queen.



    "Eti wewe ni nani? Aliuliza Miller.



    " naitwa Queen"



    "Hapana namaanisha kwa Mjomba wangu wewe ni nani yake?? Aliuliza tena Miller.



    Queen alimtizama Larry ambaye alikuwa akimtizama kwa makini akionekana kusubiria jibu.



    " Ni rafiki yangu " alijibu Queen.



    "Rafiki yako......aliuliza Millerstone na kumtazama Larry aliyekuwa akishuka pumzi baada ya kusikia jibu hilo.



    " kwanini unamchukia uncle wangu?? Aliuliza Miller.



    "Nani kasema namchukia? Aliuliza Queen.



    " Sasa acha kujifanya kam unamchukia ingali unampenda" alizungumza Millerstone na kumuacha Queen katika hali ya kuweweseka na kushindwa kutoa jibu.



    Larry alitabasamu na kumtazama Millerstone huku akitabasamu zaidi na kutikisa kichwa chake.



    Queen ndiye aliyebaki akiweweseka na kumtazama Millerstone kwa makini.



    "Mbona mko katika hali hiyo?? Aliuliza Vikram....... Ahaaaa haka katoto kameshaharibu mazingira eeeeehhh......haya mtoto wake Vikram umemwambia nini shangazi yako? Aliuliza Vicky.



    Wakati huo Tropina akipewa chakula ambacho anatambua kabisa kina sumu ndani yake kwaajili ya kula. Ndiyo wakati ambao mabomu yalishaweza kuanzwa kuwekwa katika gereza lile pasina mtu yoyote yule kufahamu wala kutambua hilo.



    ***** ****** ******

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo alionekana Queen akiingia katika bweni la Larry na bweni hilo hulitumia mwenyewe kutokana na matatizo yake kutokuta giza hivyo basi mama yake aliweza kuomba atengenezewe bweni lake mwenyewe kw pesa yake mwenyewe ili asiweze kuwapa wenzake shida pindi watakapokuwa wakitaka kuzima taa.



    Alifungua kipochi chake kisha akatoa cheni ndani yake iliyoweza kuonekana ya dhamani sana aliitizama na kutafuta pa kuiweka sehemu ambayo Larry angeweza kuiona kwa urahisi zaidi.



    Ghafla alihisi Kuna mtu anakuja kule alipo aliweza kuzima taa na kujificha pembeni ya kabati.



    Larry aliweza kuishika switch iliyokuwa mlangoni na kuwasha taa lakini alishtuka kidogo na kuzungumza.



    "Sijawahi kuzimaga taa iwe mchana asubuhi au jioni" alizungumza hivyo na kuelekea katika kabati lake ambapo pembeni tu alikuwa amejificha Queen.



    Alitoa shati lingine na kuvua lile alilokuwa amelivaa. Alilitupa chini kisha akaondoka zake.



    Baada ya Queen kuhisi hakuna tena mtu ndani pale. Alitoka alipoweza kujificha na kuokota lile shati.



    "Ameanza lini huu uchafu wa kutupa nguo chini? Wakati Mara nyingi yeye ndiye aliyekuwa akinikemea Mimi na kuniambia ya kuwa hapendi wala hataki uchafu? alizungumza Queen na kuanza kulikung.uta shati lile huku akianza kutafuta sehemu ya kuweza kuiweka.



    Alilinusa shati lile na kusema.



    " bado tu hajabadilishaga aina ya pyafumu na alisema haipendi hii pafyumu nilivyoweza kumletea.



    Ghafla alihisi kukumbatiwa na mtu nyuma yake.



    "Queen.... Nilikumiss sana ..sana... Sana tena zaidi ya sana........ Nashukuru kwa wewe kuja kuniona Mimi hapa kwasiku ya Leo" alizungumza Larry n Queen aligeuka na kutoa mikono ya Larry katika mwili wake.



    "Usinishike shike Mimi" alizungumza na kutupa shati katika kitanda cha Larry kisha kuanza Kuondoka.



    "Kwahiyo hicho ulichoweza kulileta kwaajili yangu unaondoka nacho tena?? Aliuliza Larry.



    " nani kasema nilikuletea wewe...... Hii nitampatia mtu bora zaidi ya wewe" alizungumza na kutoka njee lakini alirudi tena ndani baada ya kuisahau pochi yake.



    Alitaka kuishika pochi yake lakini Larry aliwahi kuichukua.



    "Nipe pochi yangu" alizungumza Queen na kuanza kuirukia pochi yake kwani alikuwa mfupi kwa Larry.



    "Nataka tuongee kuhusu Stellar" alizungumza Larry.



    "Mwone alivyokuwa mjinga huyu.. Sitaki kuongea na wewe kuhusu mwanamke wako"



    "Lakini Queen yule siyo mwanamke wangu Mimi"



    "Niliona akikubusu usikate" alizungumza Queen.



    "Kweli sikatai lakini kama ulivyoweza kuona yeye ndiye aliyekuwa ananibusu mimi siyo Mimi nilikuwa nikimbuss yeye" alizungumza Larry.



    "Ulimshika mikono nilikuona" alizungumza Queen.



    "Ngoja nikuonyeshe ilivyokuwa alizungumza Larry na kutupia pochi kitandani kisha kumsogeza Queen karibu na yeye akaichukua mikono yake na kuweka juu ya mabega yake.



    "Unaona yeye alikuwa akibusu Mimi Mimi nilipokuwa naitoa mikono yake namna hii huku akinibusu wewe ndipo ukaingia na kuhisi Mimi nakusaliti....lakini Queen unajua kabisa siwezi kufanya hivyo kwasababu nakupenda kutoka ndani ya moyo kabisa na unatambua hilo ila Collins ndiye anayafanya yote hayo ili kuweza kukupata wewe, Tafadhali naomba unielewe" alizungumza Larry



    "Unauhakika ya kuw nilipowaacha hamkufanya chochote? Aliuliza Queen.



    " kufanyaje chochote na uliona kabisa Mimi niliweza kukufuata wewe" alizungumza Larry



    "Sawa"



    "Umenisamehe?? Aliuliza Larry.



    " Ndiyo yameisha lakini akikubusu tena sitamuacha hai"



    "Wala sitamruhusu afanye tena hivyo" alizungumza Larry na kumbusu Queen mdomoni.



    Queen alimtizama kisha akatabasamu na kuamua kabisa kutumia romance kwa siku hiyo zaidi ya mabusu ya kawaida.



    ***** **** ****



    Dr Kim hakikisha unafika muda muhafaka na unamuwekea umakini Tropina.... Ili umchome dawa kabla hajafariki pia utambue ya kuwa Alice ameshaweza kugundua kuhusu tunachokifanya kwahiyo wewe utasaidiana na Jimmy Mimi nitamchukua Millerstone pmoja na Larry na tutakutana Airport.



    Alikata simu Vikram na kuanza kujiuliza.



    "Huyu Miller na uncle wake wameenda wapi?! Alijiuliza Vikram na kuanza kuwatafuta



    Wakati huo alionekana Calvin akiwa maeneo yale na aliweza kupiga simu na kuzungumza na Harman.



    " nafikiri nina weza nikamchukua Millerstone sasa kwani yuko mwenyewe na baadaye nikamrudia Larry kwa kumfanya yeye ampate Millerstone.



    Dr Kim alishafika na Jimmy eneo lile la gereza huku wakisubiri muda wowote kwanzia saa hiyo liweze kuingia gari la Huduma ya kwanza kwaajili ya kumchukua Tropina na kuondoka naye. Ili na wao waweze kufanya mipango mingine.



    "Jimmy.....unamuona yule mtu pale?? Aliuliza Dr Kim baada ya kumuona mtu maeneo ya njee ya gereza akiwa anadondosha dondosha vitu huku akionekana mwenye wasiwasi.



    " Nani huyo?? Aliuliza Jimmy na kuanza kutazama kw makini.



    "Yule pale"



    "Nafikiri ni mtu wa Alice ameshamtuma cha kufanya ni kutumia plan B hakuna njia yoyote ile, mtaarifu Vikram awahi kuwaleta airport Mimi nitaenda kumchukua Tropina na kumtorosha wewe washa gari kwa haraka zaidi na ukae standby.



    Jimmy alishusha kapero lake na kuelekea moja kwa moja hadi katika lango kuu la Gereza kabla hajafika ving.ora vya kuja kwa ambulance viliweza kufika eneo lile.



    Hivyo alihairisha safari yake na kukata kona ambako aliweza kukutana na mtu yule ambaye kama walivyoweza kuhisi wao ni kwamba ametumwa na Alice, lakini haikuwa hivyo alikuwa ni mtu wa Harman.



    Baada tu ya kukutanisha macho yao Jimmy alihisi kumjua mtu yule lakini hakuwa na kumbukumbu ya kuwa amemuona wapi.



    Jacky or Denis aliweza kumpita na kuelekea mbele Jimmy alijitahidi kuvuta kumbukumbu na hapo hapo aliweza kukumbuka ya kuwa Jacky ni mfanyakazi wa Mr Harlan



    Alipogeuka amtizame tena hakuweza kumuona.



    Aliinua simu yake na kupiga.



    " haloo.....bossi nafikiri tuna tatizo kubwa zaidi...yule mfanyakazi wa Mr Harlan alikuwa hapa gerezani na Kuna vitu alionekana kuvidondosha Ndiyo navifuatilia......aligutuka baada ya kukutana na kitu kilichoweza kumshtua.



    "Umeona nini?? Aliuliza Vikram aliyeoneka bado kumtafuta Millerstone.



    "Nafikiri ni bomu" alizungumza na kutazama mbele zaidi.



    "Cyo bomu ni mabomu" alizungumza baada ya kuona mengine yakiwa yamejipanga..nitajitahidi kwenda kumuokowa Tropina kabla mabomu hayajalipuka. Alikata simu baada ya kuzungumza hayo na kumpigia tena simu Dr Kim aliyekuwa ndani ya gari.



    **** **** *****



    "Samahani kidogo naomba utangaze jina la Larry na Millerstone kwani nashindwa kuelewa wameelekea wapi? Alizungumza Vikram akiendlea kupapasa macho



    Hapo hapo alikuja Godlisten na Millerstone.



    " Umemtolea wapi huyu? Aliuliza Vikram na kumtizama Millerstone kama Kuna popote pale alipoweza kuumia.



    "Niko salama" alizungumza millerstone.



    "Larry yuko wapi??



    " nilimuona akipanda kuelekea bwenini kwake lakini imeshapita nusu saa sijamuona tena"alizungumza Godlisten



    "Sawa nitizamie huyu mtoto na usiende popote pale wala usimpatie mtu yoyote yule"



    "Sawa"



    Vikram alianza safari ya kuelekea katika uelekeo bwenini.



    **** **** ****



    Alice alikuwa juu kabisa ya Jumba la kina Tropina huku akipata red wine.

    Simu yake iliita na aliipokea.



    "Haloo........ndo anapakizwa ndani ya ambulance? Aliuliza Alice.



    " Haina shida maana dawa nimeshaweza kuibadilisha na kuweka sumu zaidi hivyo atakufa tu........ghafla aliisikia milipuko ya kupokezana ndani ya simu yake.



    "Haloo.....halooooo

    .." Aliita Alice na kusema



    "Mbona kama milio ya bomu hiyo?? Alijiuliza na kupiga tena simu lakini namba haikuweza kupatikana.



    "Ni nini hiyo?? Alijiuliza tena na kushuka kisha kuelekea chumbani kwake kwaajili ya kuvaa nguo



    ***** **** *****



    Vikram aliweza kufika katika bweni anayokaa Vikram kabla hajagonga mlango mlango uliweza kufunguliwa na alitoka Queen.



    Ambaye alimpa heshima kwa kuinamisha kichwa chake na kuondoka huku akitngenezea nywele zake.



    Larry na yeye alitoka na macho yake yaliweza kugongana na Vikram ambapo baada tu ya kumuona alianza kujichekesha.



    " bwashe, umekuja kufuata nini huku?? Aliuliza akitizama tizama chini.



    "Wewe umetumia kinga?? Aliuliza Vikram.



    "Naam" aliitika Larry.



    "Nakuuliza umetumia kinga?? Alirudia tena swali lile Vikram.



    "Kinga....... Ndiyo....nimetumia" alizungumza Larry na kufuta futa mikono yake katika suruali yake.



    "Sijapenda hii tabia yako ya Leo, na sitopenda itokee tena umenielewa? Aliuliza Vikram



    " Ndiyo nimekuelewa....nimeelewa" alizungumza Larry na kushusha pumzi ndefu.



    Vikram alimtizama kwa makini na Larry alikuwa akikwepesha macho yake



    "Jiandae wewe pinah na Millerstone mtaenda Thailand na mtaenda kuishi huko mpaka pale nitakapoweza kupata ushahidi wa kudhibitisha ya kuwa Tropina hana hatia" alizungumza Vikram na Larry alitikisa tu kichwa chake.



    ***** ***** ****



    Baada ya kusikika milipuko ile kwa pamoja yote pamoja na gari la Huduma ya kwanza kuweza kuungulia ndani.



    "Njee kidogo kulikuwa na gari jeupe lililoweza kupaki na ndani ya gari hilo alikuwepo Tropina ambaye alikuwa akilalama maumivu ya tumbo na hapo hapo aliweza kuzimia.



    Alikuwa ndani Patrick pamoja na mkuu wa gereza ambaye waliweza kuliona gari likiteketea na ndani ya gari hilo alikuwa Diana aliyeweza kutaka Tropina aende kwa gari jingine na yeye aweze kupakiwa katika gari la Huduma ya kwanza kama mgonjwa ili kama Alice atahitaji kufanya chochote basi kisiweze kumfanya Tropina akashindwa kuchomwa dawa ya tiba.



    " tunafanyaje sasa?? Aliuliza mkuu wa gereza jiba lake aliitwa Nurath.



    "Nitaenda kuchukua tiba ya Tropina natumaini watakuwa wameiacha ndani ya gari" alizungumza na kushuka katika gari lile kisha akashusha kofia ya sweta lake na kulifunga moja kwa moja akaelekea katika gari waliloweza kuja nalo Jimmy na Dr Kim ambao walionekana kuchanganyikiwa baada ya kushuhudia tukio lile kulipuka kwa gereza pamoja na gari aliloweza kupanda Tropina kama walivyoweza kudhani wao.



    Aliingia ndani ya gari kupitia upande wa nyuma na kuona begi dogo ambalo mwanzo alikuwa amelibeba Vikram alipokuwa ndani ya gari na Millerstone kabla hawajaelekea kwenye graduation ya Larry.



    Alifungua na hapo alikuta sindano mbili alishindwa kuelewa ni ipi ya dawa na ipi siyo ya dawa hivyo alizichukua sindano zile na kuondoka zake wakati akiyafanya hayo aliweza kuonekana kupitia camera ndogo iliyokuwa ndani ya gari lile.



    Aliweza kurudi kwenye gari lile na mwanzo na gari hilo liliweza kuwashwa na kuondoka eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vikram alipigiwa simu na kupewa taarifa zile.



    "Unamaanisha nini unaposema ya kuwa gari alilokuwa ndani Pinah limelipuka?? Aliuliza Vikram na wakati huo alikuwa pembeni Larry aliyekuwa akicheza na Millerstone nyuma ya gari.



    " kipi kimetokea kwa Tropina tena?? Aliuliza Larry na Vikram aligeuza gari kisha akaanza mbio kuelekea uelekeo wa uliopo gereza.



    Wakati huo Millerstone alikuwa akimtizama baba yake pamoja na uncle wake.



    "Tropina ni nani?? Aliuliza Millerstone akimtizama Larry ambaye alishaonekana kutaka kulia katika uso wake.



    " Ili kumpata Larry hatuwezi kwenda mbali na hapa kwani lazima atakuja na hiyo itakuwa njia raisi ya kumchukua alishauri Nurath.



    "Sawa basi tufanye hivyo"



    "Vipi kuhusu hiyo sindano mchome basi" alizungumza Nurath



    "Nashindwa kuelewa ipi ni ya dawa kwani haziwezi kuwa zote mbili ni dawa lazima moja hapa iwe sumu na katika dakika 40 tumebakiza 15 za kumchoma sindano na dakika 20 za kufika airport lasihivyo ndege itaondoka na kutuacha nyuma" alizungumza Patrick akizitizama sindano zile.



    **** **** ****



    "Ndiyo nimefanya vile ulivyoweza kunielekeza ila lile gari lililoweza kumchukua Tropina nimeshindwa kugundua limeelekea katika uwepo upi" alizungumza Jacky aliyeeonekana kufahamu ya kuwa Tropina alikuwa katika gari jingine.



    "Huo Ndiyo upuuzi nisiotaka kuuasikia, namuhitaji Tropina Larry pamoja na hako katoto ukishindwa kuniletea hat mmoja wao basi ujiandae kufa" alizungumza Harman na kukata simu.



    "Inabidi nielekee tena katika gereza hilo ili kuhakikisha ya kuwa nampata hata mmoja wao haswa Tropina na huyo mtoto" alizungumza Harman na kuomba aandaliwe gari kwa haraka zaidi.



    Vikram alifika na kushuka ndani ya gari lake huku Larry akimshusha Millerstone na kuanza kutembea naye kwa haraka haraka kwaajili ya kutizma wapi alipo Tropina Dada yake.



    Patrick aliweza kurudi na aliweza kumuona Larry akiwa amemshikilia Millerstone.



    Alimsogelea kwa karibu na kumgusa bega alipoweza kugeuka tu alimpulizia spray usoni mwake na kumfanya Larry azimie mikononi mwake kutokana na watu walikuwa ni wengi pamoja na majeruhi hakuna aliyeweza kuliona tukio lile tofauti na Millerstone aliyekuwa ameshikwa na Larry Mkono.



    "We unamfanyaje.... Kabla hajamaliza kuongea na yeye aliweza kupuliziwa spray ile kisha akadondokea mikononi mwa Nurath aliyekuja kumsaidia.



    Alimbeba Millerstone na kuelekea naye hadi ndani ya gari aliloweza kuja nalo Vikram kisha akaufungua mlango na kutoka njee kwa kumfuata Patrick aliyekuwa na Larry mikononi mwake.



    Tukio lile pia liliweza kurecodiwa pasina yeye kutambua hilo.



    Vikram akiwa pale aliweza kupitwa na mtu aliyeweza kufunika sura yake na alipomaliza tu kupita Vikram alihisi Kuna mabadiliko ndani ya mwili wake hapo hapo alishangaa baada ya kuhisi Kuna ubaridi ndani ya tumbo lake alipoweza kutizama aliiona damu ikichuruzika katika ubavu wake wa kushoto.



    Jimmy na yeye aliweza kumfikia na alipotazama Mkononi mwa Vikram aliiona damu.



    " nini shida?? Aliuliza na kuweza kumtazama tumboni Vikram.



    "Mtafute Millerstone na Larry uwaweke usalama" alizungumza Vikram na kurudisha macho yake katika gari lililoweza kuunguwa kwa kiasi kikubwa na maaskari wakizuia watu wasielekee ndani pale.



    Dr Kim alifika pale.



    "Larry yuko wapi?? Aliuliza dr Kim.



    " muwekee umakini boss Mimi ninaenda kuwatafuta Larry na Miller "



    "Kivipi" aliuliza Dr Kim na hapo aliweza kuliona jeraha la Vikram.



    "Mungu wangu" alisikika akisema hivyo.



    Na wakati huo yule aliyeweeza kumchoma kisu Vikram alikitizama kisu alichoweza kumchoma nacho Vikram na kusema.



    "Hii Ndiyo njia pekee ya mimi kuifahamu DNA yako" alikuwa Harman na alitabasamu tu.



    Kwa upande mwingine alipokuwa Patrick na Nurath sasa zimebaki sekunde 60 tu eidha wamchome au apoteze maisha.



    "Tufanyaje aliuliza Patrick??



    Zimebaki sekunde chache tu alizungumza Patrick.



    Nurath aligeuka nyuma na kufungua sindano moja kisha kumchoma sindano ya paja Tropina kwa nguvu na kumiminia ile dawa pale.



    " kwanini umefanya hivyo je kama ni sumu?? Aliuliza Patrick na hapo hapo hali ya Tropina ilianza kubalika kwa kuweweseka zaidi na kuwa kama mtu mwenye degedege





    "Tufanyaje sasa?? Aliuliza Patrick na hapo hapo Tropina aliweza kuacha kufanya vil na kutulia kimya.



    " Madam Tropina.... Madam Pinah" aliita Patrick na hapo hapo kumbukumbu za Larry ziliweza kumrudia au kupata fahamu.



    "Ghafla Pinah alipiga chafya na mapigo yake ya moyo yalianza kudunda tena.



    " Nini kimetokea? Aliuliza Larry na kumtazama Tropina aliyekuwa akihema kama kawaida.



    Wote waliweza kushusha pumzi ndefu na Nurath aliweza kuishika mikono yake ambayo ilikuwa ikitetemeka.



    "Yuko wapi Millerstone? Aliuliza Larry.



    " nimemuacha ndani ya gari Vikram atamkuta huko" alizungumza Patrick.



    "Na vipi kuhusu Tropina kwanini amekuwa hapa tena na alikuwa amekufa, itabidi nimpigie simu Vikram na nimwambie yuko hai atakuwa anamtafuta sana"



    "Tafadhali usimpigie" alizungumza Patrick.



    "Kwnini??



    *** ***** *****



    Vikram alikuwa katika machela huku akiingizwa katika chumba cha matibabu haraka haraka na Millerstone akiwa nyuma na Jimmy.



    Baada ya kuingizwa ndani ya chumba cha matibabu Dr Kim aliweza kujitambulisha kama Dr wa Vikram na kuingia na yeye katika chumba alichoweza kuingizwa.



    " Uncle wako Larry nani amemchukua?? Aliuliza Jimmy.



    "Kachukuliwa na mtu mmoja tu hivi lakini haonekani kama mtu mbaya"



    "Huyo mtu mbaya na mzuri unamtambuaje? Aliuliza Jimmy.



    " kupitia uso wake" alijibu Millerstone na hapo hapo aliweza kuingia ndani Alice aliyeeonesha kutota kwa jasho.



    "Yuko wapi Vikram?



    Millerstone alimtizama na kwenda kukaa kwenye kiti kisha akakunja mikono yake



    Walifika Airport Patrick, Tropina aliyekuwa bado kazimia, Nurath pamoja na Larry.



    Waliitoa machela iliyoweza kumbeba Tropina na kuanza kuiburuza kuingiza airport kupitia upande wa nyuma pasina mtu yoyote yule kufahamu.



    Wakati huo Nao Lucretius aliweza kupigiwa simu na Jimmy kisha akapewa taarifa zile za kuuwawa kwa Tropina kama walivyoweza kudhani wao.



    Aliweza kupita upande ule ule wanyuma aliokuwa akija Larry pamoja na wenzake huku wakimfunika Tropina na shuka ili asitambulike.



    Waliweza kupishana na Lucretius aliyeonekana kuwa na haraka zaidi bila kutambua wala kuwajua.



    Hatimaye Tropina aliweza kuingizwa katika ndege moja kati ya nne ambazo ziliweza kupakiwa pale airport na ziliweza kuondoka ndege mbili kwa wakati mmoja na kila moja ikichukua njia yake.



    Harman aliweza kufika na kuona ndege zile.



    " kati ya hizi mbili Kuna moja yuko Tropina fuatilia information zao na utambue zinaelekea nchi gani" alizungumza Harman na kuwasha gari kisha kuliondoa eneo lile.



    ****Baada ya miaka 2 kupita*****



    Alionekana Queen akiwa anatembea shopping huku akisukuma kigari cha mtoto mdogo aliyekuwa ndani ya kigari kile na Pembeni yake akiwa Collins pamoja na Millerstone.



    "Aunt" aliita Millerstone ambaye umri wake ulishaweza kufikia miaka5.



    "Yes" alijibu Queen.



    "Uncle Larry atakuja lini Mimi simpendagi huyu hata kidogo" alizungumza na kumtupia macho Collins.



    "Usijali atakuja siku siyo nyingi pamoja na baba" alizungumza Queen na alipotazama mbele ghafla aliiona mtu anayeweza kufanana na Larry akimtizama.



    "Embu mtizame V Mara moja nakuja" alizungumza Queen na kuelekea eneo lile aliloweza kupotelea mtu yule aliyeweeza kumfananisha na Larry.



    Aliweza kumfuata na alianza kumtafuta Hatimaye alimuona akimpa mgongo alimfuata na kumgeuza alipogeuka wala hakuwa Larry tena.



    "Samahani nimekufananisha alizungumza Queen na kutafuta tafuta.



    " Mbona kama nilimuona Larry" alizungumza Queen na kugeuka tena nyuma kumtazama mtu yule alipoweza kuishilia kijana yule alitizama nyuma na hapo aliweza kumuona Larry.



    "Nashukuru alijibu Larry na kutoa pesa kisha akaamua kuondoka zake.



    "Sifikiri kama unafanya maamuzi mazuri na dada yako akisikia hayo lazima atakasirika" alizungumza bodyguard ambaye aliweza kuwapeleka katika ncho nyingine na yeye ndiye aliyekuwa rubani wa ndege.

    Huyo walimuita Amani.



    "Ni vizuri sasa ukakaa kimya na asigunduwe chochote kile alizungumza Larry na kutoka njee ya shopping ile.



    "Ila sas kama ni demu wako mbona anamtoto ni wanani?? Aliuliza Amani.



    Larry aligeuka na kumtizama kwa hasira Amani ambaye aliweza kumpisha na kwenda mbele.



    Aligeuka tena na kutizama eneo la shopping ambalo alikuwa Collins akimshika shika mtoto yule huku akitabasamiana na Queen.



    *** **** ****



    Kwa upande wa pili alionekana Sister Mary akiingia katika kampuni ya Precious Mineral limited.





    "Mpigie simu na umwambie namuhitaji hapa alizungumza sisters Mary na kukaa katika kiti baadaye kidogo alikuja Mr mpalila na kutoa salam kwa Sister Mary.



    " Mbona ghafla hivyo?? Aliuliza Mr Mpalila.



    "Niletee documents zote za kazini, pesa zilizoweza kuingia, kutumika pamoja na matumizi yake" alizungumza Sister Mary na kumtazama Mr Mpalila ambaye aliweza kushtuka baada ya kuambiwa maneno hayo.



    "Mbona haraka hivyo?



    ***** **** ****



    Larry aliweza kurudi katika Jumba kubwa la kifahari na hapo aliweza kupishana na Harman.



    " umetoka wapi mbona umekuwa mnyonge hivyo?? Aliuliza akiwa ameishika juice.



    Larry alimtizama na kuingia zake ndani.



    Amani alikuwa nyuma yake huku akiweka headphones zake masikioni na kumpita Harman.



    "Mbona mnanipita tu kunashida gani eti? Aliuliza Harman.



    Amani aliendelea na safari zake bila kugeuka kokote pale.



    ***** ****** *****



    Alice akiwa ndani ya Jumba la kina Tropina na akiwa anakunywa red wine yake huku akionekana mtu pembeni yake aliyekuwa anamshika Mkono na baada ya hapo aliweza kusimama na kwenda nyuma yake akimshika shika mwili wake.



    " Lakini unajua ni mwaka sasa tangu Vikram aondoke bila kumuaga mtu yoyote yule mpaka nashindwa kuelewa amepatwa na nini huko alikoweza kwenda na alienda na yule Dr Kim pamoja na Jimmy pia aliondoka akiwa kama mtu aliyeweza kupata habari za kushtusha" alizungumza Alice na ilisikika tu sauti ikimwambia.



    "Kila kitu kitakuwa sawa, hata mimi naomba asirudi kabisa kwasababu sasa npata muda mwingi wa kuwa na wewe" alizungumza mtu yule na kumbusu Alice ambaye alionekana hana furaha naye.



    **** **** **** ****



    "Aunt....." Aliita Millerstone akiwa anaingia na ndani na Queen pamoja na mtoto mdogo wa kike jina lake waliweza kumfupisha na kumuita Vee.



    'Yes" aliitika Queen.



    "Hivi hujawamiss wazazi wako?



    " hata kama nimewamiss sina budi kukaa mbali na wao, kwani muda mwingine itabidi ukae mbali na watu uwapendapo ili kumkinga pia umpendaye......ni kama baba yako alivyoweza kufanya "



    "Kukaa mbali na Tropina ili ahakikishe ya kuwa anakuwa katika hali ya usalama dhidi ya Alice? Alizungumza Millerstone.



    "Yap......ni vigumu sana kukaa mbali na umpendaye lakini muda mwingine kwaajili ya usalama wake basi inabidi ufanye hivyo alizungumza Queen.



    "Aunt, Je Tropina anampenda baba yangu?? Aliuliza Millerstone.



    " Sanaa tu..... Mpaka nawaombea Mungu siku moja akapate kuwapatia furaha kama waliyoweza kuwa nayo mwanzo kabla ya kutokea mambo yote hayo " alizungumza Queen.



    "Hata Mimi nakuombea wewe na uncle Larry pia mkapate kurudiana na kumlelea Vee kwa pamoja" alizungumza Millerstone.



    "Miller unajua wewe ni mdogo lakini uwezo wako wa akili ni mkubwa sana......natamani kama ungekuwa mtoto wa Tropina" alizungumza na Miller alishusha pumzi ndefu.



    "Hata Mimi hicho ndicho ninachoweza kukiomba nikapate kuwa mtoto wa mtu mwingine tofauti na Alice......Mimi simpendagi hata" alizungumza Millerstone na hpo hapo Vee alimka na kuanza kulia.



    "Heeee Vee analia" Alizungumza na kuanza kumbembeleza pale pale alipokuwa kwenye kitanda chake.



    Collins aliweza kuyasikia mazungumzo na alichukia sana baada ya jina la Larry kutajwa katikati ya mazungumzo hayo.



    "Queen nilishakwambia siwezi kukuachia tena Larry wewe nitakufanya mke wangu tu" alizungumza Collins na kuondoka ndani pale alipoweza kujificha pasina kuonekana.



    Iliweza kupita miaka Mingine Mitatu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na ilikuwa ni katika ukumbi mkubwa ulioweza kuandaliwa vizur kwaajili ya mashindano ya nguo zilizoweza ku designiwa.



    Waliweza kupita ma model mbali mbali wakionyesha mitindo ya nguo walizoweza kuzivaa huku watu wakizikagua na kuweza kuzipa maksi.



    Hapo aliweza kuonekana Collins akiwa ameongozana na watoto wawili wa kwanza akiwa wa kiume na wapili wa kike.



    Waliweza kufika mahali fulani katika meza ndogo na kukaa.



    "Vee....mama yako atakuwa MSHINDI me namuaminia sana japo kuwa ni pambano lake la mwanzo" alizungumza Collins akimsemesha mtoto wa kike ambaye umri wake ulikuwa wa miaka4 huku Millerstone akiw na miaka 7.



    Alimtizama Millerstone bila kumjibu kitu na Millerstone alimtizama tu Collins.



    Wakiwa pale katika Jumba lile vilionekana viatu vile vya kiume sampul mbili vikija eneo lile la maonyesho.



    Walipofik waliweza kukaa nyuma ya meza waliyoweza kukaa na katika hali ya kushangaza tu.



    Vee aligeuka nyuma na hapo aliweza

    Kukutanisha macho yake ni mmoja kati ya wale walioweza kuingia ndani na kumfanya atabasamu.



    Alirudishiwa Tabasamu lake na Collins aliweza kugeuka na kumuona Vee akitabasamu.



    Aligeuka na kumtizama huyo anayefanya Vee acheke ni nani.



    Alishtuka baada ya kumuona na kusema Larry.



    Millerstone na yeye aliweza kuyageuza macho yake na hapo waliweza kutazamana.



    Katika upande mwingine alionekana mtu akipiga simu akiwa anatoka airport.



    "Haloo ........sijachelewa sana nahakika nitawahi katika maonyesho hayo kabla hayajaisha.



    Ilikuwa ni sauti ya kiume huku akiongozana na watu wawili mmoja akiwa wa Kike na mwingine wa Kiume.



    "Waooo niliimiss Tanzania" alizungumza kijana mmoja na kutabasamu huyu alikuwa Jimmy akitumia pipi yake y kunyonya baada ya kutoka airport.



    Pembeni yake alikuwa Dr Kim akiwa ameshikilia begi jeusi na akiivaa miwani yake usoni huku mbele yao akiwa Vikram ambaye alikuwa akitengenezea suti yake vizuri.



    Waliweza kupita njia ya kushoto na katika upande wa kulia viliweza kuonekana viatu vya kike vilivyoweza kupambwa na almasi vikiwa vinatembea huku vikiongozwa na viatu vingine viwili kimoja cha kike na kingine cha kiume.



    "Hello......sawa tupo njiani kuja katika shoo hiyo" alizungumza na kukata simu.



    Aliacha Tabasamu kidogo na kusonga mbele.



    Patrick kila kitu kipo sawa.? Aliuliza



    "Ndiyo madam kila kitu kipo sawa" alijibu Patrick ambaye alionekana akiwa na msichan mwingine pembeni yake ambaye hakuweza kuonekana kabisa.



    Aliyekuwa wa kwanza kuwasili ni Vikram ambaye aliweza kukaa meza ya mwisho pasina mtu yoyote yule kufahamu kuwa amewasili mahali hapo.



    Wakati huo nao alionekana Larry akiwa chooni huku Miller na yeye akiingia chooni.



    Larry alimtizama Millerstone ambaye aliweza kumpita na kuelekea sehemu nyingine kwaajili ya kuweza kujisaidia baada ya kumaliza kutumia choo aliweza kutoka na kwenda kujisafisha kisha akaelekea mlangoni kwaajili ya kutoka.



    "Vip......tumelingana umri nini?? Aliuliza Larry akigeuka kumtizama Millerstone.



    " Anayejifanya hakujui na wewe jifanye haumuoni" alizungumza Millerstone na kufunguwa mlango kisha akaondoka.



    "Ahaaa bado tu genius" alizungumza Larry na kugeuka katika kioo baada ya kujitengenezea Nywele zake.



    Alivuta pumzi ndefu na alipokuwa akitoka alikutana uso kwa uso na Collins aliyesimama mbele yake.



    "Unataka nini?? Aliuliza Larry



    " nataka urudi ulikotoka Tafadhali usiharibu ndoa yangu pia usiharibu furaha ya familia yangu, Queen anaishi vizuri sasa Tafadhali naomba urudi ulikotoka na usimfnye Queen aipoteze furaha yake" alizungumza Collins.



    "Nawezaje nikawa furaha ya mke wa mtu? Anyway niko hapa kwaajili ya shughuli zangu cjaja hapa kwaajili ya mke wa mtu" alizungumza Larry na kumpush kisha akaondoka zake.



    "Pumbavu nini, hata Mimi najua wameoana sasa anamwambia nani?? Aliuliza Larry na kuelekea ukumbini tena.



    Nyuma ya ukumbini alionekana Queen akiwa amekaa kwenye kiti huku mikono yake ikiwa inatetemeka.



    Collins alikuja na kumshika mikono yake.



    " Collins " aliita Queen na kutabasamu.



    "Mbona una wasiwasi sana"



    "Unajua ndo Mara ya kwanza naonyesha design zangu kwa public naogopa sana maybe wanaweza wakawa hawajazipenda alafu..............."



    Collins alichuchuma kisha akamshika mikono Queen.



    "Sawa nitakupeleka jukwaani kama pia unaogopa macho ya watu ila niahidi mimi kwamba chochote kile kitakachoweza kuonekana mbele ya macho yako kisikufanye wewe ukaacha kuweka umakini kwa kile kinachoweza kuendelea. Alizungumza Collins na Queen alitikisa kichwa na kumshika mikono Collins kwa nguvu.



    ****** ***** ******

    Alice alionekana akitoka katika chumba cha guest huku akilalamika juu ya mwili wake.



    " hivi nitaendelea kutumika mpaka lini? Alijiuliza na kuondoka eneo lile.



    Baada tu ya kuweza kutoka aliweza kutoka mwanasheria Josephat akitabasamu na kusema



    "Kila siku unazidi kuwa tu mzuri kitandani ndo maana siishiwa hamu na wewe nashukuru Mungu niko na video ambayo inanifanya Mimi ni stareheke na wewe kila saa na wakati niutakao.



    Alitabasamu na kurudi katika chumba alichoweza kutokea kwani alikuwa na taulo kiunoni tu.



    ***** ****** *****



    Vikram aliweza kusimama kwaajili ya kutoka njee na hapo aliweza kushngaa baada ya kusimama kwani aliona mtu mbele yake.



    Macho yake yaliweza kukutana na Tropina ambaye na yeye aliweza kushngaa baada ya kumuona Vikram kwani hakutegemea kumuona pale.



    Pinah aliweza kujikaza na kumpita Vikram kama vile amfahamu wakati huo Vikram aliweza kukumbuka matukio ya nyuma siku ambayo gereza liliweza kuunguwa na katika ambulance waliweza kupata mwili uliokuwa umeungua vibaya sana na kusemekana ni wa Tropina, Pia Ndiyo siku ambayo hakuweza tena kumuona Larry katika macho yake bali aliweza kuviona vipande vipande vya video katika gari lake pamoja na la Dr Kim.



    Alikumbuka Kuna mtu alimrudisha Millerstone katika gari na kuondoka zake, pia alikumbuka dawa aliyoweza kumpatia Dr Kim Kuna mtu aliweza kuingia ndani ya gari na kuichukua baada ya tukio.



    "Kama nilivyoweza kufikiri Pinah hajafa......bado yuko hai...na niliwaza tu siku moja atarudi kulipiza kisasi na kisasi chke kitakuwa pia juu yangu. Alijizungumzia na kutabasamu kisha akatoka njee kabisa ya jengo kwaajili ya kwenda kupunga upepo.



    Kuna mtu alikuwa nyuma yake na kupiga simu



    " yupo kabisa huku juu gorofani anapunga upepo " alitoa maelezo hayo na kukata simu.



    Wakati huo nao alionekana mtu akikata simu na alikuwa Harman akiwa anaendeshwa na Jacky.



    "Siku ya Leo itakuwa siku kubwa sana" alizungumza Harman na kutizama njee ya gari lake.





    **** ***** **** ****

    Stejini aliweza kusimama mc na kuweza kumkaribisha mtu ambaye angeweza kuja kumtaja MSHINDI wa siku hiyo.



    "Naomba nimkaribishe Mrs Harman Singh" alitamka Mc na Pinah aliweza kusimama katikati ya watu ambao waliweza kumpigia makofi na Patrick alimshika Mkono kwaajili ya kum escort apande ngazi.



    Watu waliokuwa pale wengine walianza kumsifia kwa uzuri wake huku wengine wakianza kumfananisha na Tropina kwa mbali sana kwani aliweza kubadilika kwa kiasi kikubwa.



    "Mrs Harman" alirudia kauli ile Vikram na kupatwa na hasira ghafla alimuona mwanae Millerstone akionekana pamoja na Vee huku Millerstone akiwa amekaa huku akitizama sehemu moja tu.



    Vikram alipeleka macho yake katika meza aliyokuwa akiitizama Millerstone na alimuona Larry.



    "No wonder, hata yeye atajifanya hatufahamu alizungumza Vikram na kutabasamu.



    Tropina aliishika karatasi ile na kumpa Patrick ambayo aliifungua akaisoma na kumnong.oneza kitu masikioni.



    " Samahani kidogo siwezi kuwaambia ni kwamba mgeni wetu rasmi yeye ni kipofu hivyo hataweza kulitaja jina mwenyewe'



    "Yani bado tu ana act" alizungumza Vikram na kusimama ila kabla hajatoka njee Harman alikuwa akiongozana na Jacky wakiingia ukumbini.



    Alishngaa kwa muda na kusema hii mbaya hii.



    Aliimpa Dr Kim ishara na Dr Kim aliweza kuinuka na kumpa ishara Jimmy ambaye aliweza kuinuka na kumfuata Dr Kim.



    Walienda mpaka meza waliokuwa Vee pamoja na Millerstone kisha Dr Kim akakaa nyuma ya Millerstone huku Jimmy akikaa nyuma ya Vee.



    "Jimmy, Kim.....yuko wapi baba yangu aliuliza Millerstone akitabasamu.



    Jimmy alimkonyeza na kupisha kidogo kimwanya kidogo ambacho kiliweza kumfanya Vikram aonekane.



    Vikram alimpa Hey na kumuachia Tabasamu.



    " Vee, baba kaja" alizungumza Miller.



    "Nataka kwenda kwa uncle" alizungumza Vee na kutaka kusimama



    "Hpana embu tulia kwanza kwa dakika 3 kisha utaenda kumuona alizungumza Dr Kim na kumpandisha katika kiti.



    Wakati huo wote macho ya Vikram hayakubanduka katika mwili wa Harman.



    " amekuja kufanya nini hap?? Alijiuliza na hapo aliweza kumuona akimchekea Larry ambaye hakuwa na shughuli naye.



    "Mshindi wa siku ya Leo ni Queen Collin's" alizungumza Tropina na kuachia Tabasamu huku taa zikiwa zimewashwa upande ambao walikuwa wakimsubiri Queen atoke.



    Aliweza kutoka akiwa na Collins katika upande wake wa kushoto.



    "No wonder, si mke na mume nilijua tu watakuja pamoja lakini siyo kwa kushikana namna hiyo" alizungumza Larry akionekana kuwa na uwivu mkubwa juu ya Collins na Queen.



    Queen alipofika karibu na Tropina aliweza kushangaa baada ya kumuona Tropina akiwa katika hali y kugeuka ili kumuuliza Collins aliweza kumuona Larry akiwa anakunywa red wine huku akionekana kuwa na hasira juu yake.



    "La....la.....la.........." Hakuweza kumalizia kuzungumza na kwa mshtuko alioweza kuupata aliweza kuzimia mikononi mwa Collins.



    Vikram alitoa ishara ya Millerstone pamoja na Vee waweze kutolewa huku yeye akipanda jukwaani na kutaka radhi kisha kuchukua ua kutoka kwa Tropina ambaye alitakiwa kumpatia Queen na kusema.



    "Samahani kwa kilichoweza kujitokeza....Queen ni mjamzito ndo maana hali kama hii huwa inamtokea Mara kwa Mara.. ...alienda akampokonya Tropina medali ambayo pia alitakiwa apewe Queen na kuondoka nayo.



    Alienda akamshikika Collins bidhaa zile kisha akambeba Queen na kutoka naye ukumbini.



    Larry alisimama kwenye kiti kwa hasira na kutoka njee huku Amani akimfuata njee.



    Wakati huo Harman alikuwa akizungumza moyoni.



    " Kwa miaka mitatu nimekuwa nikipigana nawe katika jimbo la Kashmir ukanishinda Mimi na ukamshinda baba yangu, lakini sasa pambano letu limehamia Tanzania na tayari niko na mwanamke umpendaye pamoja na huyo bwashe wako, unafikiri utanishinda tena.. alizungumza na kuishika glass yake kwa nguvu mpaka ikaweza kupasukia mikononi mwake.



    ***** ***** ****



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa asubuhi na mapema na watu wote walikuwa mezani huku ukimya ukiwa umetawala.





    Huku akionekana Vee pamoja na Millerstone wakitizama sehemu moja.



    "Wewe Uncle, kwanini umekuja kwetu na mabegi yako kwani huna kwen?? Aliuliza Vee.



    " Nani kakwambia hapa ni kwenu? Aliuliza Larry aliyekuwa akila yai la kukaanga kwa kutumia kijiko pmoja na kisu.



    "Mama yngu aliniambia hii ni nyuma ya ............."



    "Vee nyamaza" alizungumza Queen kwa kumtaka mwanaye anyamaze.



    "Umefuata nini huku?? Umekuja tena kumsumbua aunt wangu? Aliuliza Millerstone.



    "Nafikiri baba zenu hawajaambia kwamba nyumba hii ni ya nani, na mnapaswa kuwa na adabu kwani Mimi ndiye mmiliki wa nyumba hii na mnatakiwa mniheshimu kama sivyo wote mtaondoka na kuniachia nyumba yangu........... Alafu naona hauli nipe mimi hayo mayai yako" alizungumza Larry akichukua sahani ya Vee ya mayai.



    "Wewe ni mlaku sana" alizungumza Vee na kuchukua sahani ile ya mayai.



    "Mimi Ndiyo mwenye nyumba nimesema nipe hayo mayai" alizungumza Larry na kuyachukua kwa nguvu kwa Vee.



    Vee alianza kulia huku akiyataka mayai yake.



    "Sitaki kelele nyamaz" alizungumza Larry kwa sauti kubwa na ya hasira hali iliyomfanya Vee anyamaze kwa muda kisha akaamua sasa kufungulia sauti ya kilio.



    "Pumbavu haka katoto kana kelele.....toka njee nenda kalilie huko alizungumza Larry na kumfuata Vee kisha kuanza kumvuta Mkono



    Larry" aliita Queen kwa ukali na kumchukua mtoto wake.



    "Kama unahasira na Mimi malizia hasira zako juu yngu lakini siyo kwa binti yangu Mimi" alizungumza Queen na kupiga magoti huku akimshika shika Vee na kum bembeleza.



    "Usijali mama ataenda kukuandalia mayai mengine sawa" alizungumza Queen na kumfuta mwanaye machozi kisha akaondoka naye.



    Larry alirudi mezani na kuendelea kula mayai yale aliyoweza kum nyang.anya Vee.



    "Kula na haya sasa" alizungumza Miller na kumsogezea mayai kisha akaondoka zake.



    "Hata mkikataa wote nakula" alizungumza Larry na kumiminia mayai yale katika sahani yake kisha akairudisha sahani ile kwa hasira mezani pale.



    Alice alisimama akaondoka kisha akasimama Collins na kuondoka Hatimaye alibaki Larry na Vikram.



    "Mbona wew huondoki?? Aliuliza Larry



    "Wacha kujiumiza mwenyewe, kwani kujifanya unawachukia watu ambao unawapenda ni kujitesa mwenyewe" alizungumza Vikram na kutoka mezani pale.



    Baada tu ya Kuondoka machozi yaliweza kumtoka Larry aliyekuwa amejaza mayai katika mdomo wake.



    Vikram alimuona na kutoka eneo lile.



    ****** ****** *****



    "Patrick nataka uwe makini na Vikram kwani Vikram siyo mwanaume wa kuamini kirahisi ya kuwa Mimi siyo Tropina wala sioni lazima adhibitishe yote hayo" alizungumza Tropina na kuweza kukumbuka ya kuwa baada tu ya Harman kuingia ukumbini aliweza kuonana na Vikram ambaye alionekana kushtuka na hapo hapo aliweza kuwatuma watu waka wawekee ulinzi Miller pamoja na Vee.



    "Alafu Kuna kitu kimoja nitakifuatilia mwenyewe" alizungumza Tropina na kutizama pembeni.



    Patrick aliweza kutoa ishara ya sawa kwa kutikisa kichwa chake na hapo hapo aliweza kuja msichana ambaye kwa Mara ya kwanza aliweza kuonekana akiingia airport na Pinah pmoja na Patrick



    "WiFi.... Aliita na kutabasamu.



    " Ndiyo "



    "Lini nitaenda kumuona kaka Harman sijamuona takribni miaka mitatu sasa na niliweza kumuona kwa masaa machache tu katika events ile lakini alipotea" alizungumza Jacintah.



    "Usijali kwa kuwa anapafahamu nyumbani basi atakuja tu...au atatupigia simu ila kwasasa yuko busy na anamambo ya kuyafanya alizungumza Pinah na kumshika mikono Jacintah.







    ****** ***** ********



    " Millerstone na Vee nahitaji mnisikilize haswa haswa Miller.........alizungumza Vikram aliyekuwa amempakata Vee.



    "Hamta enda shule? Alizungumza Vikram.



    " Kwanini uncle?? Aliuliza Vee.



    "Uncle wako anataka nyie msome hap hapa nyumbani nitawaletea walimu wa kuwafundisha hapa na nitawatengenezea chumba kidogo kwaajili ya maktaba yenu"



    "Dady......kuna tatizo lolote lile juu yetu.... Ulipotea ndani ya miaka minne alafu Jana pia kama sikuwa nilikuelewa Kuna mtu yoyote anakutishia wewe kupitia sis?? Aliuliza Millerstone.



    " nashukuru Mungu kwa kuwa wewe ni mwepesi wa kuelewa alizungumza Vikram na kumshika mikono Millerstone.



    "Sasa kwa kuwa umeweza kulitambua hilo inabidi umuwekee makini ndugu yako" alizungumza Vikram na Millerstone alitikisa kichwa.



    Larry alikuwa pembeni na maongezi Yale aliweza kuyasikia



    "Kama tunavyofahmu ya kuwa Vikram aliweza kupotea ndni ya miaka minne na alivyoweza kurudi tu Jana Leo kuwaambia watoto wake hivyo" alizungumza Larry



    "Watoto wake?? Aliuliza Tropina.



    " Millerstone na ile taka taka nyingine ya Collins " alizungumza Larry na kuonyesha kuchukizwa.



    "Unamaanisha Vee"



    "Huyo huyo bhna kwani mpaka umtaje jina? Aliuliza Larry na kuonyesha kuchukizwa kisha kuanza Kuondoka.



    "Sasa unaenda wapi na hatujamalizia kuzungumza? Aliuliza Tropina lakini Larry alishaweza kufika mbali sana.

    " Amani kuwa makini na huyu pindi awapo pale anaweza akamuwekea hata sumu yule mtoto kwa kumchukia tu" alizungumza Tropina.



    ****** ****** *****



    Ilikuwa asubuhi na mapema sana ya siku nyingine na alionekana Alice kunyata kwa kuingia ndani.



    "Umetoka wapi sasa hivi?? Aliuliza Vikram aliyekuwa juu ya ngazi akimtizama Alice.



    Alice alishtuka na kusimama pale pale.



    " ammhhh Vikram" aliita Alice na kuanza kujichekesha.



    "Swali langu ni jepesi sana, umetoka wap?? Aliuliza tena.



    " ammmhh nilienda kwenye party ya rafiki yangu, tulikaa sana huko sasa usiku ulivyoweza kuingia ndo nikaona bora nilale huko huko " alizungumza Alice.



    "Kwanini nilivyoweza kukupigia ulikata simu na Hatimaye ukazima?? Aliuliza Vikram akishuka katika ngazi.



    " ammm kulikuwa na kelele na nivyokuwa nikitafuta sehemu nzuri ya kuzungumza na wewe simu ilizima chaji" alizungumza Alice.



    "Okay, simu ilizima chaji?? Aliuliza Vikram na kutabasamu kisha akanuna hapo hapo.



    " Anglia ulichoweza kukupambania kikawa ni zero kwani siku nikigundua unanisaliti japo kwa mawazo tu tunaachana alizungumza Vikram na kupanda ngazi zake kuelekea juu.



    Wakati upande wa ndani sehemu ya kupigia mswaki alionekana Vee akiwa anapiga mswaki ghafla mlango ulifunguliwa na aliingia Larry.



    Kisha akachukua mswaki na kuenda kupiga mswaki upande wa pili ambapo haukuwa mbali na pale alipo Vee.



    "Lione linaamka sasa hivi" alizungumza Vee na Larry aliyasikia maneno Yale na kumgeukia.



    "Wewe unasema nani livivu?? Aliuliza Larry akiwa na mswaki mdomoni.



    " Hamna alijibu Vee na kujiosha uso wake.



    "Nilichafu kweli linaongea na mswaki mdomoni " alizungumza Vee na Larry aliyatema mapovu ya mswaki yaliyokuwa mdomoni mwake kisha akautupa mswaki na kuufuata



    "Wewe" alizungumza na kumsukuma kichwa





    "Mama" aliita Vee na kuanza kulia.



    "Lione lilivyo lijinga kama baba yake" alizungumza Larry na kumsodola kichwa zaidi hapo hapo aliingia Queen.



    "Unamfanyaje binti yangu wewe? Aliuliza na kumsukuma Larry pembeni.



    Huku akimchukua mwanaye na kumtoa pale juu alipokuwa amekaa kwaajili y kupiga mswaki.



    " Nani kakupandisha huku juu?? Aliuliza Queen.



    "Collins alinipandisha na kuniambia anaenda kuchukua mswaki wake tuje tupige wote" alizungumza Vee na kujifuta machozi yake.



    "Larry unashida gani na mtoto wangu lakini, hivi huwezi kumchukulia mtoto huyu kama wa kwako na uache kumfanyia haya unayoyafanya" alizungumza Queen.



    "Siwezi kuwa na mtoto mjinga kama huyu maana ningeshamtupiaga mtoni siku nyingi........Kaone kalivyo" alizungumza Larry na kuanza Kuondoka.



    "Ndo maana hata hujasukutua meno yako.......mchafu sana wewe" alizungumza Vee na Queen alimziba mdomo.



    "Kaone kalivyo ka baya kama baba yake" alizungumza Larry na kutoka njee .



    "Vee msikilize mama yako.....

    Kaa mbali na Larry, usimsogelee wala usijibizane naye chochote sawa"



    "Na kama akinisodoa tena kichwa.



    " Utamwambia mama wala usimjibu chochote sawa "



    "Ndiyo mama" alijibu Vee na kumkumbatia mama yake.



    Wakati huo Collins alikuwa amekaa mahali Akicheka na kusema.



    "Nitakufanya wewe umchukie Larry kupitia mtoto wenu mwenyewe na mwishoni nikishindwa nitamuuwa mimi lakini atakuwa Larry kwasababu yeye ndiye mwenye kumchukia Vee. Alitabasamu tu.



    Uliikuwa ni muda wa mezani na Larry alikuwa akitizama na Vee aliyekuwa akimtizama tu.



    " usinitizame na hayo macho yako mabaya nitakutoboa sasa hivi Mimi" alizungumza Larry na kuendelea kula.



    Vee alimtizama kwa macho makali bil kumjibu chochote kile.



    'Usinitizame Mimi hivyo" alizungumza Larry.



    Vee aliendelea kumtizama na Larry aliinua kijiko na kutaka kumpiga nacho cha kichwa.



    "Mama" aliita Vee na Larry aliacha.



    "Unafikiri Mimi namuogopa huyo mama yako, mjinga wewe" alizungumza Larry na kuondoka mezani pale akimuacha Vee na wakati huo nao Queen alikuwa akija eneo la kulia chakula na walipishana na Larry.



    "Uko salama Vee?? Aliuliza Queen baada ya kufika



    "Alitaka kunipiga na kijiko" alizungumza Vee na mama yake alimshika kichwani.



    "Larry kwanini Unataka kujenga uadui na mtoto wako mbona umebadilika hivyo eti" alijiuliza Queen na hatimaye aliweza kupata ujumbe katika simu yake.



    Aliufungua na kuusoma ujumbe ule kisha akamtizama mwanaye Vee aliyekuwa akila wali.



    ******* ***** ******



    "Daudi nitkupa chochote kile utakachoweza kukitaka lakini Kuna mtu nahitaji unisaidie kumfanyia kitu alizungumza Alice akimpapasa Daud







    " utanilipa kiasi gani?? Aliuliza daudi.



    "Daud tumeanza kufanya kazi kwa miaka mingapi mpka usiniamini kwa kiasi kikubwa hivyo, wewe fanya kazi na baada ya kuisha kazi nitakulipa" alizungumza Alice.



    "Unajua umeshanifanya nimemsaliti Adrian ambaye pesa yake alikuwa akinilipa nyingi na Mimi nikawa nakuletea information zake sasa Adrian akirudi na Mimi nitarud kwake" alizungumza daudi.



    "Sawa, tuone kama utaweza kufanya hivyo kwani nitamwambia siri zake zote ulizoweza kuniambia" alizungumza Alice na kuanza kumpapasa kifuani Daudi.



    "Unataka nini?? Aliuliza Daudi na kutoa mikono ya Alice.



    " kwahiyo Unataka kuniambia ya kuwa sikuvitii kabisa " alizungumza Alice na kuanza kutoa nguo yake ya juu.



    "Una......una....... Alitaka kuuliza lakini aliacha kuzungumza baada ya Mkono wake kugusishwa kifuani.



    ****** ****** *****



    Queen aliweza kuja nyumbani saa 4 usiku na Larry alikuwa juu kabisa ya gorofa akipata unywaji.



    " Yani Ndiyo anarudi nyumbani usiku huu, si ajabu ametoka kwa mwanaume mwingine baada ya kumuacha Collin's na mwanaye. Alizungumza Larry na kushuka kwaajili ya kumfuata.



    Alipishana naye katika ngazi na Queen alimpita bila salamu.



    "Wewe" aliita Larry na Queen aligeuka kumtizama.



    "Umetoka wapi sasa hiv? Aliuliza Larry



    " Nimetoka kazini" alizungumza Queen na kuendelea kupanda ngazi.



    "Kazi gani hiyo ya kurudi usiku wa manane? Aliuliza Larry na kumfuata juu.



    " nimeshakwambia Nimetoka kazini nafikiri inatosha ukijua hivyo" alizungumza Queen.



    Larry alienda na kumshika Mkono.



    "Hapa ni nyumbani kwangu mwisho wa kurudi ni saambili usiku ukizidisha nenda katafute nyumba ya kurudi hata saa10 usiku alizungumza Larry na kutupa Mkono wa Queen kisha kuingia ndani kwa hasira.



    Collins alikuwa pembeni na aliweza kutabasamu baada ya kuona tukio lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni baada ya Larry kumtaka Queen awe akirudi nyumbani upesi na mapema.



    Wakati hayo yakiendelea Vikram aliweza kuyaona na baada ya Queen kupanda juu alijitokeza Collins na kutabasamu.



    Vikram aliendelea kumtazama na hapo hapo ujumbe mfupi uliingia katika simu yake aliweza kufungua na ulikuwa ujumbe ambao ulimfanye atoke njee na kuchukua gari lake kisha Kuondoka.



    Hakuna mtu yoyote aliyekuwa akiweza kutambua utajiri aliokuwa akiumiliki Vikram kwani alionekana mtu simple sana na anayefanya kazi za kawaida tu.



    ***** ***** *****



    Katika nyumba aliyekuwa akikaa mama yake Alice walionekana watu watatu wakija huku wakigonga nyumba ile baada ya miaka mitano kupita.



    "Mama yake na Alice anashida gani,ni miaka mitano sasa bila hata salamu" alizungumza mwanamke yule ambaye aliweza kuja na mwenzake.



    Waligonga bila ya mafanikio yoyote Yale na walipoona kimya sana na baada ya kusubiri kwa masaa mengi waliamua kubeba virago vyao na kuondoka .



    Hawakufika mbali sana waliweza kuonekana na jirani ambaye alikuwa karibu na eneo lile



    "Mmekuja kumtafuta mama yake na Alice? Aliuliza



    " ndyo "



    "Siku hzi hakai hapa tena anakaa kwa binti yake huko alipoweza kuolew na wala hajawahi kujaga kutusalimia kwanzia alivyoenda" alizungumza jirani yule.



    "Unapafahamu huko aliko tunahitaji kwenda"



    ****** ****** ******



    "Umetoka wapi?? Aliuliza Millerstone aliyekuwa akijisomea barazani.



    " baba yako yupo? Aliuliza Alice.



    Millerstone alimtizama kwa macho makali kisha akarudisha macho yake katika kitabu chake alichokuwa akikisoma.



    "Si ninakuuliza baba yko yup.......Vee njoo njoo" aliita Alice na Vee alimsogelea



    "Uncle yuko wapi? Aliuliza Alice.



    " Sijui Mimi nilivyoamka sijamuona " alizungumza Vee.



    "Amelala njee kama wewe ulivyoweza kulala njee ila Kuna tofauti yeye alienda kufanya kazi na wewe unajua ulichokifuata" alizungumza na kusimama kisha Kuondoka.



    "Haka katoto kangekuwa siyo ka kwangu ningekavunjilia mbali....mbona kana penda sana kunifuatilia........ngoja kwanini Vikram hajalala nyumbani ameenda kulala wapi?? Alijiuliza na kuchukua simu yake kisha kupiga haraka haraka.



    ***** ****** *****



    " Bossi bado tu umeshindwa? Aliuliza Jimmy



    "Nashindwa kujua nifanyaje tena kwamaana kuingia kwa Harman hapa Tanzania nina uhakika Kuna kitu atataka kufanya tu na kwa kuwa anahisi Mimi nahusika na mauaji ya baba yake lazima atake kulipiza kisasi tu kupitia familia yangu, hivyo Millerstone, Vee pamoja na Queen nitawaketa hapa.

    Alafu kitu kingine mtafute mtu atakayeweza kumfuatilia Collin kwa makini nijue ratiba zake zote ndani ya siku nzima" alizungumza Vikram



    "Majibu ya DNA yametoka" alizungumza Dr Kim na kutoa karatasi la majibu.



    "Haiwezekani hii, kwamba yule siyo Tropina......hpana Harman siyo mjinga hata kidogo mpaka akae karibu na yeye....... Kama harman hatataka kumuachia Tropina basi Kuna njia ya kutumia. alizungumza Vikram.



    " lakini pia mbona ni kipofu kama cyo Tropina?? Alijiuliza Jimmy.



    "Siyo kipofu yule, anaweza akawadanganya wote ila siyo Mimi" alizungumza Vikram.



    Na kukumbuka siku ya kwanza kuonana naye aliweza kushtuka sasa kama ni kipofu angewezaje kujua mimi niko mbele yake na kingine hata ajiite nani yeye bado ni Tropina. Alijizungumzia moyoni Vikram.



    ***** ****** ******



    Wakati huo Tropina alikuwa katika jumba moja kubwa huku akifikiria siku ambayo aliweza kumuona Vikram akitizamana na Harman.



    "Kwanini Harman na Vick walitizamana namna ile" aliendelea kujiuliza na ghafla alisiikia sauti ya Vicky ikilitaja jina lake.



    "Amepajuaje hapa?? Alijiuliza Tropina na kushusha pumzi ndefu kisha kuelekea katika huko aliko Vikram.



    " yuko wapi huyo mume wako?? Aliuliza Vikram.



    "Samahani, ila ningeweza kwanza kukutambua wewe ni nani kabla ya kukwambia mume wangu yuko wapi" alizungumza Tropina na kusogea mbele zaidi.



    "Me naitwa Phina, ni mke wa Harman" alizungumza Tropina na kumfanya Vikram acheke.



    "Eti Phina...alirudia kauli ile na kutabasamu zaidi............mfikishie taarifa hii Harman.........Mimi siyo mjinga kama anavyofikiri yeye na endapo atamgusa mtu yoyote yule katika familia yangu na Mimi nitamuumizia familia yake tena nitaanza na wewe mke wake" alizungumza Vikram na kuondoka.



    "Anashida gani huyu?? Alijiuliza Tropina na kumtizama Vikram akiishilia eneo lile.



    " sijawahi kumuonaga katika sura hii kabla "



    ***** ****** *******



    Alionekana mama yke na Queen akiwa anakuja katika nyumba ya kina Larry akiwa na ghadhabu sana.



    "Yuko wapi huyo baba wa huyo mtoto wako ........ Kumbe umekuja kukaa huku kwaajili ya Huyo mpuuzi yuko wapi?? Aliingia ndani Zena kwa jazba na mlangoni alikutna na Vee.



    "Yuko wapi huyo baba yako? Alimuuliza Vee ambaye alibaki akimtizama.



    "We nani?? Aliuliza Vee na hapo hapo Millerstone alitokea.



    " Vee nenda chumbani kwako "



    "Kwanini?? Aliuliza Vee



    "Na wewe yuko wapi huyo baba yako mpuuzi?? Aliuliza Zena.



    " Kama umemfuata baba yangu au baba yako na Vee wote hawapo hapa ndani labda uende urudi baadaye" alizungumza Millerstone na kumshika Mkono Vee kisha akaanza kuondoka naye na wakati huo nao Larry alikuwa akiingia ndani baada ya kutoka kwenye mihangaiko yake.



    Ghafla macho kwa macho na mama yake Queen.



    Alisitisha atua zake na ghafla alishanga baada ya kumuona mama yake Queen akiwa anakuja kwa jazba sehemu aliyoko aligeuka nyuma kutizama kama Kuna mtu nyuma yake lakini hakukuwa na mtu alipogeuka tu alikutana na kibao cha mama yake na Queen.



    Alipotaka kumpiga kingine Amani aliweza kumzuia na kumshika.



    "We mama unashida gani?? Aliuliza Larry.



    "We uliona ulichokifanya ni sahihi..... Sindiyo........ukamtenganisha binti yangu na familia yake kwaajili ya huyo laana wako.....alafu unakuja tu bila hata kuja na kututaka radhi"



    "Unaongelea nini wewe?? Aliuliza Larry aliyekuwa hajamuelewa Zena.



    " Ngoja nije nikupige kibao kingine kisha utaelewa ninachokimaanisha alizungumza Zena na kutaka kujitoa mikononi mwa Amani.



    "Mama" aliita Queen na kumsogelea.



    "Ahaaa nawaona sasa pamoja waza..............." Kabla hajamalizia kuzungumza Vikram alitokea.



    "Larry hajui chochote kile unachotaka kumwambia na ni bora kama utaondoka kimya kimya bila kuongeza neno lolote lile katika mdomo wako kwani utaifufua kesi yako" alizungumza Vikram na Zena alijitoa mkononi mwa Amani



    Alimtizama Larry na kumnyooshea Mkono alipofika mbele kidogo Vee alikuwa amesimama Millerstone alipita katikati yao na kumfanya Vee adondoke chini.



    Queen alimfuata mwanaye na kumuinua kisha Kuondoka naye wakati huo huo naye Larry alipanda juu ya ngazi kwa hasira na kuelekea kwenye chumba chake.



    "Uko salama?? Aliuliza Vikram akimuuliza mwanaye Millerstone.



    Alitikisa kichwa ishara ya kwamba yuko salama.



    Baada ya muda kidogo alionekana mtu akigonga mlango katika chumba anacholala Amani pamoja na Larry.



    Amani alienda akafungua mlango kisha akaingia ndani Queen aliyeweza kuja na bakuli kubwa kidogo akiwa ndani ameweka barafu pamoja na kitambaa cheupe.



    " Hii utachukua na kuweka sehemu ambayo mama aliweza kukuumiza" alizungumza Queen kwa upole na kuanza Kuondoka.



    "Siwezi kushika kitu cha baridi Mimi kwhiyo kazi hiyo utaifanya wewe kwani mama yako ndo chanzo" alizungumza Larry na Queen aliweza kuinama na kuweka barafu katika kitambaa kile.



    "Mimi nawapisha kidogo" alizungumza Amani na kutoka njee.



    Queen alianza kumuwekea barafu ile katika upande alioweza kupigwa kibao na ghafla Larry alitoa mlio wa kuumia na kumfanya Queen aache kile anachoweza kukifanya huku mkono wke ukiwa unatetemeka.



    "Vipi nimekuumiza aliuliza kwa sauti ya upole na kumfanya Larry abaki akimtizama sana machoni na kujifuta akimsogelea zaidi na taratibu kabisa huku Queen akiyafumba macho yake na kushika kitambaa kile kwa nguvu.



    "Hapana, maji hayo ni ya baridi" alizungumza Larry na kurudisha uso wke nyuma kisha kumfanya Queen akibaki na aibu.



    "Sawa ngoja nikatafute bonge lingine ambalo cyo la baridi sana alizungumza na kusimama ila Larry alimshika Mkono na kumsogeza mpaka karibu na ukuta.



    Kisha akaanza kumpapasa nywele zake.



    " Queen, kitu gani kibaya niliweza kufanya juu yako mpka mama yako anasema nimerudi na sijaenda kuwataka radhi? Aliuliza Larry na katika uso wa Queen aliona umebadilika.



    Queen alikumbuka ya kuwa msimamo wke wa mwanzo ulikuwa ni yeye aweze kuolewa na Larry hata miaka10 ingepita pasina Larry kurejea Tanzania basi angeendelea kusubiri lakini uliweza kubadilika baada ya siku moja mtoto wke Vee kuweza kunyakuliwa mikononi mwake na watu wasioweza kujulikan alipkuwa akipiga kelele za kuomba msaada ndipo alipoweza kwenda Collins na kuwafuata na gari watu wale baada ya dakika 10 kupita alirudi akiwa na mtoto lakini katika hali mbaya ambayo ilimshtua kila mmoja mwili wak uliweza kujaa alama za visu na aliweza kupelekwa hospitalini na akiwa pale aliweza kumuomba Queen kama atatoka salama basi akubaliane naye kufunga ndoa pindi umri ukifika.



    Queen aliweza kukubaliana na hilo.



    Wakati akiyakumbuka hayo machozi yalikuwa yakimtoka na Larry alibaki akimshangaa.



    "Sihitaji umchukue Vee kutoka kwangu, kwani pindi nitakapokwambia Vee ni mtoto wako basi hutataka akae na Mimi kwasababu ya Collins. Alijizungumzia kimoyomoyo na kutoa Mikono ya Larry katika mwili wake kisha akatoka njee ambako aliweza kupishan na Collins aliyeweza kumuona akitoka katika chumba cha Larry.



    ****** ***** ****



    " Jacky, namuhitaji Millerstone katika ngome yngu kwasababu ndo kitu cha dhamani na cha pekee ambacho anacho Vikram. Alizungumza Harman.



    "Ndiyo bossi" alijibu Jacky na kumtazama Calvin ambaye alishindwa kuelewa .



    "Jacky, inamaana Danielle hakuwa Rickson bali Vikram au mbona Me sielewi" alizungumza akikuna Kuna kichwa chake.



    ***** ****** *****



    "Bwashe najua ya kuwa unatambua basi niambie ni kipi hicho kama hamtataka kuniambia basi nitaenda kwa mama yake Queen mwenyewe" alizungumza Larry.



    "Nafikiri ni vizuri kama kitu hichi utaweza kukisikia kwa Queens mwenyewe mpe muda kidogo na atakwambia yeye mwenyewe" alizungumza Vikram na kutoka njee.



    Wakati huo Millerstone alikuwa akipita pale



    "Miller njoo" aliita Larry na Millerstone alikuja.



    "Najua wewe ni muelewa sana na baba yako hawezi kukuficha kitu chochote kile kwahiyo nahitaji uniambie ukweli" alizungumza Larry.



    "Nikikwambia utaniamini?? Aliuliza Millerstone Larry alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo.



    "Basi usimchukie Vee, na vitu vyote unavyovifanya juu yake kwaajili ya kumuumiza uache"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuzungumza hivyo aliondoka zake.



    "Huyu mshenzi nini Mimi namuuliza swali na laana anamuingiza yule kichaa kwnye mazungumzo yetu.

    Alizungumza Larry na kutazama pembeni ghafla alishtuka na kuonekana kama kukumbuka kitu hivi.



    " hapana haiwezekani " alizungumza kwa sauti kubwa sana.



    Kipi kitatokea je Larry atakuwa na uwezo wa kutambua kuwa Vee ni mwanaye. Na vipi kuhusu mpango wa Harman juu ya Millerstone je atafanikiwa.



    Usikose sehemu ifuatayo siku baada ya kesho.



    Pia Leo imewez kuwa hewani mapema kwasababu Hamna umeme hivyo nahofia saa inaweza ikafika alafu cm ikiwa imezima chaji.





    Ni baada ya Larry kusema hpana haiwezekani kwa sauti ya juu.



    "Hii nyumba bado Ina mende, huyo si mende huyo?? Alijiuliza na kuanza kupanda juu ya ngazi haraka haraka.



    Queen akiwa katika kampuni ya Precious mineral limited akiw kama model wa kampuni hiyo kwa kutangaza madini ya dhamani kupitia cheni hereni na viatu mbalimbali vinavyoweza kutengenezwa na kampuni hiyo.



    Simu yake iliita na alipotazama alikuwa ni Larry.



    " samahani kidogo alizungumza Queen na kutoka njee ya jukwaa alilokuwa akipiga picha.



    "Haloo"



    "Uko wapi?? Aliuliza Larry.



    "Unashida gani na Mimi kama huna kitu cha maana Mimi nakata simu" alizungumza Queen na kukata simu.



    "Sasa kata uone haka katoto kako nitakafanya nini Leo? Alizungumza Larry.



    " haya unasemaje??



    "Nimekuuliza uko wapi kwanzia asubuh sijakuona? Aliuliza Larry.



    Queen alishusha pumzi ndefu kabla ya kumjibu.



    ****** ******* ******



    Alionekana Millerstone akiwa na Dr Kim katika jumba la shopping huku Miller akichagua baadhi ya vitu.



    Katika jumba hilo hilo Tropina alikuwa eneo hilo akiwa na Jacinta.



    Ghafla alihisi mapigo ya moyo wake yanaenda mbio na kama anahisi kitu hata Millerstone alihisi hivyo hivyo katika upande wake na aliweza kushika moyo wake.



    " Young master Kuna shida yoyote ile?? Aliuliza Dr Kim.



    "Moyo wangu unaenda kasi sana"



    "Embu nione" alizungumza dr Kim na kumshika kifuani Millerstone.



    "Mbona hauna tatizo lolote embu ngoja nikakuletee maji kwenye gari kisha unywe" alizungumza kim na kutoka njee.



    Millerstone aliendelea kushika baadhi ya vitu ambavyo alihisi vinamfaa. Huku akiushika moyo wake.



    Nyuma yake alionekana Jacky akiwa amevalia mavazi meusi na kufunika uso wake vizuri alitoa kitambaa na kumiminia madawa Flani yakiyokuwa kwenye chupa.



    Alipiga hatua za mbele na kuelekea mahali alipo Millerstone ambaye alihisi kama Kuna mtu nyuma yake.



    Alitabasamu kidogo tu kisha akamwaga vitu baadhi vilivyokuwa katika shelfu lile alilokuwepo na kufanya watu wote wageukie mahali walipo na ikawa ngumu kwa Jacky kwenda kumteka kama alivyoweza kukusudia.



    Jacky alirudisha kitambaa chake mfukoni na aliporudisha macho yake kutizama alipoweza kumuona Millerstone hakuweza kumuona tena.



    Alitizama huku na kule lakini hakukuwa na mtu zaidi ya wahudumu walioweza kufika pale na kurudishia vitu vilivyoweza kudondoka.



    Alianza kumtafuta na wakati huo Millerstone aliichukua kapero moja iliyokuwa ndani ya jumba lile na kuweka pesa ya kofia ile chini kisha kuanza kumkwepa Jacky aliyekuwa akimtafuta.



    Aliweza kupita nyuma ya Tropina aliyekuwa akikabidhi vitu kwaajili ya kulipia na Tropina aliweza kuhisi kitu fulani ambacho kilimfanya ageuke na atizame mlangoni ambako aliweza kumuona mtoto mdogo akiishilia mlangoni na hapo Dr Kim aliweza kutokea na kumshika Mkono akiwa bado anashangaa aliweza kumuona tena mtu akipita eneo lile lile na kutoka njee huyo alikuwa ni Jacky.



    "Nakuja" alimwambia Jacintah na kutoka njee kwaajili ya kwenda kutizama ni kipi kinaendelea.



    Alipofika ndipo gari lilikuwa likiondoka eneo lile huku Millerstone akitoa kofia yake na kutizama njee ambako aliweza kuonana na Tropina kwa Mara ya kwanza na kuhisi kitu ndani ya moyo wake hivyo hivyo pia kwa Tropina.



    "Mtoto wa Vicky, kwnini kila nimuonapo nahisi kama anaukaribu na Mimi zaidi ya kuw na uhusiano na Vikram?? Alijiuliza na aliweza kumuona Jacky akipiga piga mateke gari lake ambalo liliweza kuonekana kuwa na pancha.



    Alivua miwani na kumtazama Jacky kwa makini Jacky aliweza kugeuza macho yake na alipoweza kukutana macho kwa macho na Tropina alianza kuwa na wasiwasi.



    ***** ***** *****



    " Unaongea upumbavu gani wewe,?? Umeshindwaje kumkamata Millerstone unajua kwa hichi ulichoweza kukifanya lazima tutalipia sasa jiandae kwa kile Rickson atakachoweza kukifanya" alizungumza Harlan na kukata simu.



    ****** ****** ******



    "Nini??? Aliuliza Vikram kwa sauti kubwa na hapo hapo akasimama katika meza yake.



    " Huyu mjinga huyu, sitamuacha hai..... Nitamuonyesha tu" alizungumza Vikram na kutoka njee ya chumba chake.



    "Kuna nini mbona unahasira hivyo?? Aliuliza Larry aliyekuwa amekaa kwenye kochi.



    " Embu nifuate" alizungumza Vikram na kuingia chumbani kwake ambako aliweza kumfuata.



    Alifungua droo yake na kutoa bastola yake kisha akampatia Larry ambaye alianza kuuliza.



    "Ya....ya....yanini. .alafu bwashe hiyo si bastola?? Aliuliza Larry.



    " sitaweza kuwalinda watoto wote kwa wakati mmoja hivyo hii utamlindia Vee. alizungumza Vikram na kutoka njee.



    "Lakini sijakuelewa" alizungumza Larry na kumfuata nyuma.



    "Maisha ya Queen na Vee nayaacha mikononi mwako Mimi nitawekea umakini maisha yako Millerstone, Tropina pmoja na Mimi mwenyewe"



    "Namaanisha kwanini Mimi nimlinde huyo mtoto wakati anababa yake?? Aliuliza Larry.



    " Larry acha kuwa mjinga na uweke umakini hichi nilichokwambia" alizungumza na kuicock bastola nyingine kisha akaondoka.



    "Bwashe........ Kuwa makini huko uendako alizungumza Larry na Vikram alitikisa kichwa na kutoka.



    ***** ***** ***



    Hivi unakumbuka siku ile niliyokuadithia ya kuwa ndgu wa mama Alice walikuja kumuona".



    " eeeehh nakumbuka"



    "Niliwapeleka mpaka Katika nyumba anayoishi Alice, baada ya kufika tu walianza kuniuliza eti nimewapeleka wapi mbona yule siyo Alice wao"



    "Hapo sijakuelewa mbona" aliuliza mmama aliyekuwa akipigiwa stori



    "Walimkana na kuondoka zako......pia hata Mimi nahisi kama siye yeye ila sina uhakika" alizungumza mama yule.



    "Unamaanisha nin??



    " Mara ya kwanza alipoweza kuhamia hapa alikuja na binti ambaye alinitambulisha ni mwanaye anaitwa Alice lakini baada ya miaka miwli nilipoweza kumuona huyo Alice alikuwa amebadilika sana mpaka nikashangaaa. ....lakini tatizo siyo hilo.



    "Sasa tatizo ni lipi mbona unanipa umbea nusu nusu" aliuliza mama yule kwa kulalamika.



    "Alipoulizwa kuhusu mama yake alisema eti alisema anaenda kijijini...." Alizungumza mama yule.



    "Kijijini si alisemaga anaishi naye siku ile tulipoweza kumuuliza" aliuliza tena.



    "Ndo tushngae wote sasa mama Alice kaenda wapi maana kijijini kwao hayupo na kwa mwanaye pia hayupo" wakiwa wanapiga umbea huo ghafla waliweza kuja watu watatu ambao walikuwa wamevalia nguo aina ya kampuni moja na kuelekea katika nyumba ya mama Alice na kugonga mlango.



    "Heeeeeee hawa wakina nani tena?? Waliulizana na kuamua kuwafuata kwa kupnda ngazi chache tu.



    " habari za saa hizi naitwa Emanuel Mimi ni mtendaji katika kampuni ya Gold, tulikuwa tumekuja kumuulizia Mr Anderson au baba Alice kama yuko nyumbani kwake lakini tunaona kimya"



    "Baba yaliyoko hapa ni mazito kwa maana sasa hata mke wake hajaonekana ndani ya miaka3" alizungumza mama yule.



    "Basi itabidi tukafikishe taarifa hii polisi kwani Kuna documents za muhimu aliweza kuondoka nazo kabla ya kuacha kazi miaka mitano iliyoweza kupita" alizungumza Emanuel na kuondoka na wenzake wawili



    "Hivi kweli baba Alice yuko wapi?? Aliuliza na walibaki wakitizamana.



    ******** ******** ********



    Wakati huo kituo cha polisi vilionekana viatu pear mbili vikiingia.



    " Inspector George siamini kama tumerudi tena na tumepewa kesi ya faili lile lile tuweze kulifanyia kazi" alizungumza thobias na kutabasamu..



    ***** **** ****



    "Nini kesi ya Winnie inarudiwa tena?? Aliuliza Alice baada tu ya kuzipokea habari hizo.



    Ni baada ya Alice kuweza kupata mshtuko baada ya kuzipata taarifa za kuwa kesi inafunguliwa upya.



    Taarifa hizo pia ziliweza kumfikia Tropina ambaye aliweza kutabasamu na kusema sasa Haina haja ya kujificha tena. Alizungumza na kutabasamu wakati huo nao.



    Alionekana Adrian akitoka viwanja vya ndege huku Daudi akiwa mbele yake.



    Aliweza kufika katika nyumba ya kina Tropina na aliingia ndani ila alishtuka sana baada ya kukutana macho kwa macho na Larry.



    "Ohoo ndo umerudi Leo?? Aliuliza Larry na kutabasamu huku akibweka kama mbwa mbele ya Adrian kisha Kuondoka zake eneo lile.



    " we.. We....we.....mtoto njoo hapa" alizungumza Larry akimuita Vee.



    "Nini? Aliuliza Vee baada ya kufika mahali alipo Larry.



    " Ntakuzibua kibao Mimi siyo mama wala baba yako wa kukucheke chekea, umeshakunywa chai?? Aliuliza Larry.



    "Bado sasa kama mm sifikii mezani na siwezi kufungua chupa? Aliuliza Vee.



    " hivi huyu mama yako anaakili kweli, anaondoka tu bila kukupatia kitu chochote.....alafu sikia nakupoozea Leo tu usifikiri ni kila siku......aunt

    Aliita Larry baada ya kuona mfanyakazi anapita.



    "Hakikisha asubuhi akishaamka Vee awe amekunywa chai" alizungumza Larry na kumwambia Vee twende huku.



    ***** ****** ******



    "Mama Jane njoo uone" alizungumza jirani wa mama Alice.



    "Kuna nini tena aliuliza mama Jane baada ya kufika eneo lile.



    " Kwa mama Alice maaskari wamekuja" alizungumza mama Aisha.



    "Heeeeeee mwenzangu embu twende tukaangalie" alizungumza mama Jane na kutangulia



    "Afisa Kuna usalama hap? Aliuliza mama Jane.



    " nyie ni jirani zake?? Aliuliza Thobias.



    "Ndiyo"



    "Kuna documents za muhimu za kampuni ya Gold Ndiyo zimekuja kutafutwa hapa hivyo tuna search warrant tu hatuna kitu kingine tulichoweza kukifuata" alizungumza Tobias.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Afande , samahani nakuomba Mara moja" alizungumza afisa mmoja na Tobias aliweza kuingia ndani.



    Ulikuwa ni upande wa jikoni ambako waliweza kukuta kamba ikiwa chini ya kiti kilichokuwa jikoni pale.



    **** ***** *****



    "Nini wameelekea Nyumbani kwa mama?? Aliuliza Alice baada ya kupata taarifa hizo na hapo aliweza kukumbuka ya kuwa sehemu ya jikoni aliacha ushahidi wa kuonyesha dhahiri ya kuwa Kuna mtu alikuwa mateka ndani ya nyumba ile.



    " Mungu wangu, Mungu wangu, naelekea kuwa kichaa alizungumza Alice baada ya kupokea simu kutoka kwa mwanasheria Josephat.



    Akiwa pale pale aliweza kumuona Tropina mbele ya macho yake na hapo ndipo alipoweza kushtuka na kudhani mzimu.



    "Vipi kama vile umeona mzimu" alizungumza Tropina na kumfuata karibu Alice aliyekuwa akitetemeka Tropina aliendelea kumsogelea na hatimaye aliweza kudondoka chini kwa uwoga.



    "We nani?? Aliuliza Miller na kutokea mbele ya Tropina kisha kusimama katikati yao.



    Macho yake yalipoweza kugongana naya Tropina walijikuta wote wakitizamana kwa sekunde kadhaa bila hata mmoja wao kusema nenololote.



    Miller aliinama na kumuokota Alice kisha akamgeukia Tropina na kumwambia.



    " umefuata nini kwetu?



    "Tangu lini mwenye nyumba akaulizwa amefuata nini katika nyumba yake?? Aliuliza Tropina na kumsogelea Alice aliyekuwa akiogopa zaidi.



    " Pinah" aliita Larry na kushuka ngazi huku Amani akiwa nyuma yake na alipoweza kufika alitoa heshima na hapo hapo Adrian alishtuka sana na yeye baada ya kumuona Tropina pindi alipokuwa akitoka jikoni na juice chakula chake Mkononi.



    Aliweza kuidondosha sahani ya chakula chini na kupasuka.



    Tropina Alicheka na kumtazama kwa makini.



    "Kwa kipindi kirefu hatujaonana Adrian"



    Miller alimtizama Adrian na mama yake kwa makini kisha akamtizama tena Tropina alipoweza kumtizama kwa makini aliweza kukumbuka ya kuwa siku moja alipoweza kuingia katika chumba cha baba yake aliweza kukuta gazeti ambalo lilikuwa likitangaza kifo na juu ya gazeti hilo ilikuwa picha ya Tropina pia katika laptop ya baba yake picha nyingi zipo za mwanamke huyo.



    Alipotizama mlangoni aliweza kuwaona wafanyakazi wa nyumba ile wote wakiwa mlangoni na kuchungulia ndani huku wakiteta jambo fulani Tropina tu alipoweza kuwageukia wote walipiga kelele na kudondoka chini. Alipogeuka kumtazama Millerstone na yeye aliweza kuweweseka na kudondoka chini.



    ****** ******* ******



    Nlimtuma mtu wa kumfuatilia Collins na ameweza kunipa ratiba yake ya siku nzima zote hazina shida ila Kuna picha moja tu ambayo nimeweza kushtuka kidogo alizungumza Jimmy na kutoa picha moja.







    Vikram alipotazama alishindwa kuielewa.



    "Hii mbona siielewi" aliuliza na Jimmy akamjibu.



    "Kipindi cha nyuma Vee aliweza kutekwa na watu watatu na mmoja kati ya watu hao ni huyu" alizungumza Jimmy.



    "Kwahiyo Unataka kusema kuwa Collins anaweza akawa amehusika na utekwaji wa Vee kisha akajifanya kumsaidia?? Aliuliza Vikram na Jimmy alitikisa kichwa.



    "Bossi Kuna tatizo" alizungumza Dr Kim na kutoa gazeti ambalo liliweza kutoka siku hiyo.



    "Nani huyo kaandika habari zangu?? Aliuliza Vikram na kushtuka zaidi.



    Katika upande mwingine alionekana mwandishi wa habari akiwa anapita pita mitaani huku akiwauliza watu maswali juu ya taarifa hizo.



    Gazeti hilo pia liliweza kumfikia Harman ambaye alilikusanya kusanya na kulitupa mbali kabisa



    " Kwahiyo ameshajisafisha jina lake sasa na anaonekana shujaa wa Tanzania , Rickson sitakuacha mzima kwa kuniulia baba yangu siwezi kukuwacha mzima hata kidogo lazima na Mimi nikuulie mtu unayempenda sana katika Maisha yako ili na wewe uhisi maumivu na uchungu kama nilivyoweza kuhisi Mimi...........



    Aliinua simu na kupiga



    "Halooo change the plan...... Sikahitaji haka katoto kakiwa hai muuuwe na ukishindwa kufanya hivyo basi nitakuuwa wewe" alikata simu.



    "Calvin sasa hivi ni kumuuwa wala siyo kumteka tena" alizungumza Jack.



    ******* ******* *******



    Wakati wa pita pita za Larry akiongozana na Vee pamoja na Millerstone baada ya kutoka matembezi.



    Jacob rafiki wa Larry aliweza kumuona.



    "Larry"



    "Jacob" aliita Larry na kwenda kumkumbatia.



    "Aise ulikuwa wapi wewe mbona ulitukimbia tu baada ya kuharibu?? Aliuliza Jacob.



    "Kuharibu nini ??? Aliuliza Larry



    " Acha basi kujifanya haujui sasa hivi huwezi kukamatwa tena na polisi umri umeend bhana " alizungumza Jacob.



    "Unaongelea nini mbona sikuelewi"



    "Namaanisha.........."



    "Uncle Larry..... Tuwahi nyumbani Mimi njaa inaniuma alikatisha mazungumzo hayo makusudi kabisa na kuanza kumvuta Larry ambaye alimshika Vee Mkono na kuondoka naye



    "anafanana na baba yake kweli, lakini mbona Larry anavyoniuliza kama vile hatambui ya kuwa Vanessa ni mtoto wake? Alijiuliza lakini aliamua kuondoka baada ya kuona hana la kuzungumza.



    Walipokuwa ndani ya gari Larry alikuwa na mawazo sana kwani hiyo ni kauli ya pili kuambiwa kuwa baada tu ya kuharibu aliweza kukimbilia.



    " Millerstone" aliita Larry.



    "Yea Uncle"



    "Kuna kitu chochote unakijua na Mimi sikifahamu?? Aliuliza Larry



    **** ***** ****



    Wakati huo alionekana Tropina akiwa na Nurath ambaye alikuwa mkuu wa gereza na aliweza kumsaidia kutoroka.



    " samahani ni kwaajili yangu ndo maana ukakosa kazi"



    "Hapana siyo kwaajili yako bali kwa wale walioweza kutega mabomu"



    "Hivi bado tu hajapatikana ni nani aliyeweza kutega mabomu?? Aliuliza pinah



    " hapana bado hajapatikana lakini serikali yetu bado inaendelea kumtafuta.



    Wakati Tropina anachukua glass ya maji kwaajili ya kunywa glass iliweza kudondoka chini na kupasuka hapo hapo alihisi mapigo yake ya moyo yanaenda kasi sana.



    Alimtizama Nurath na kutazama glass chini.



    Hata kwa Rickson pia picha ya mwanaye Millerstone iliweza kudondoka chini na kupasuka.



    "Ni nini hii?? Aliuliza Vikram na kwenda kuokota picha ya mwanaye Millerstone hapo hapo mapigo Yake yamoyo pia yaliweza kwenda kwa kasi sana.



    Akichukua simu yake na kumpigia Larry.



    " yes hello...



    "Yuko wapi Millerstone??



    " Anaongea na simu, alafu mbona alisema anakupigia ww na anamaongezi ya Siri na wewe ndo akatoka ndani ya gari "



    "Katoka ndani ya gari?? Hakikisha unamrudisha na mrudi nyumbani sasa hivi, Vee yuko wapi??



    "Niko naye"



    "Fanya haraka mrudi nyumbani.....Kuna mahali nitawaleta mje kuishi kwanza kwa muda"



    "Sawa" Larry alikata simu na kushuka njee ya gari hapo hapo simu yake iliita alikuwa ni Tropina.



    "Uko salama wewe?



    " ndiyo"



    "Embu mpigie simu, Vikram umuulize kama yuko salama kisha uniambie" alizungumza Tropina.



    "Bwashe nimeshaongea naye sasa hivi Ndiyo amesema nimchukue Miller.....

    ........ Aligotea hapo na mbele ya macho yake alimuona Millerstone akivuka barabara huku gari jeusi likija kwa kasi sana na kumgonga kisha kumrusha pembezoni tena mwa barabara



    " Millerstone alisikika akiita Larry kwa sauti na simu ya Tropina iliweza kudondoka chini huku nako Vikram aliweza kudondoka alipokuwa akishuka ngazi.



    Gari lile liliweza kupitiliza na kuondoka zake.



    ***** ***** ****.



    Alice akiwa nyumbani alikuwa na mashaka sana moyoni mwake na hapo hapo waliweza kuingia maaskari wa polisi



    "Tafadhali tunaomba uongozane nasi hadi katika kituo cha polisi tuna maswali kidogo tunahitaji kukuhoji juu ya kutokuonekana kwa mama na baba yako ndani ya miaka 5, hivyo ongozana nasi"



    Alionekana Vikram akiwa eneo la hospital njee ya chumba cha operations huku akijaribu kuzunguka kulia na kushoto katika eneo lile, na Larry akiwa amemshikilia Vee mikono aliyekuwa akilia.



    Hapo hapo aliweza kuingia Tropina ambaye alienda akamkumbatia Vikram aliyekuwa akijitahidi machoz yasimtoke lakini alishindwa kufanikisha hilo na kujikuta akilia mbele ya Tropina aliyekuwa na yeye akilia.



    Hapo hapo aliingia Queen aliyeonekana kushindwa kutembea na kudondoka kila atembeapo.



    "Millerstone yuko wapi??



    " yuko katika chumba cha operations bado madactari hawajatoka njee" alizungumza Larry.



    "Ni makosa yangu yote haya ni makosa yangu huwenda ningekwambia ukweli basi Millerstone asingetoka kwenye gari na kuja kunipigia simu Mimi" alizungumza Queen.



    "Ukweli gani huo?? Aliuliza Larry na kumshusha Vee kisha kumsogelea Queen.



    " Kwmba Vee ni. ................"



    "Mlango uliweza kufunguliwa na alitoka nesi mmoja akiwa anakimbia mbio mbio Mara akatoka tena wa pili.



    " Ni vipi hali ya mwanangu?? Aliuliza Vikram na kumng.ang.ania nesi mmoja.



    "Hali yako bado siyo nzuri ameweza kupoteza damu nyingi sana hivyo Tafadhali nahitaji kwenda kuchukua damu Zingine" alizungumza nesi na kukimbia haraka haraka.



    Nesi wa kwanza aliweza kurudi na chupa tano za dripu kisha akafungua na kuingia ndani, nesi aliyeweza kufuata na yeye aliweza alikuja na chupa Tatu za damu na kuingia nazo ndani.



    "Mungu wangu mtoto wangu' Ndiyo kauli ya mwisho iliyosikika ikitoka mdomoni mwa Vikram kabla ya kudondoka na kuzimia mwilini wa Tropina.



    Jimmy alitizama chumba kile cha operations kwa hasira na kufuta machozi yake.



    " Utanitambua Leo" alizungumza na kutoka njee.



    "Jimmy...

    Jimmy alibaki akiita Tropina aliyekuwa akijaribu kumpepea Vikram.



    Tropina alitoa simu na kumpigia Patrick.



    " Muwekee ulinzi Jimmy hakikisha afanyi chochote cha kipuuzi"



    "Ni kipi kinaendelea jamani" aliuliza Adrian baada ya kuwasili katika hospital ile na kukuta wote wakimtizama vibaya.



    "Larry, yuko wapi Dr Kim?



    " Yupo huko ndani kwenye chumba cha operations"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***** ***** *****



    Mwisho wa kumuona baba yako Mr Anderson ilikuwa ni lini??



    "Alipoaga anakwenda kazini hakurudi mpaka Leo" alijibu Alice.



    "Na mwisho wa kumuona mama yako ni lini???



    " alipoondoka na kusema ya kuwa anarudi kijijini kuwasalimia ndugu zake"



    "Je ulimpigia simu na kumuuliza ya kuwa amefika??



    " nilijaribu kufanya hivyo lakini namba niliambiwa haipatikani "



    "Inavyosemekani ni kwamba usiku wa tar. 23/07/2012 majira ya saa 3 usiku baba yako aliweza kuonekana maeneo ya dukani akinunua vocha na kuelekea nyumbani.........kisha baada ya masaa mawili kupita ulionekana ukitoka katika nyumba yenu, Je unaweza kujielezea kupitia hilo"



    "Kitu ninachokumbuka ni kuwa baada ya baba yangu kuondoka nyumbani sikuweza kumuona tena, na mara kadhaa nilipokuwa nikimuuliza mama yangu kuhusu baba hakupenda kabisa nahisi atakuwa alikuwa na mwanamke mwingine na ndo maana hakurudigi nyumbani" alizungumza Alice.



    "Una uhakika na unachokizungumza?? Aliuliza Tobias.



    " Ndiyo nina uhakika"



    Tobias alitoa picha na kumuonyesha Alice ambaye aliweza kushtuka baada ya kuziona picha zile.



    "Unawafahamu hawa??



    " Ndiyo huyo ni Dada yake mama yangu na huyo mwingine ni mdogo wake" alizungumza Alice, na picha zilikuwa ni za wale wanawake wawili walioweza kuja kutoka kijijini na kuja kumuona Alice pamoja na mama yake.



    "Wako wapi??



    "Walikuja kunisalimia na hatimaye hawakukaa hata ndni ya masaa matano nao walirudi kijijini tena niliweza kuwapatia nauli Mimi"



    "Inavyosemekana watu hawa baada ya kuja kukuona wewe, hawajarudi tena kijijini wala hawaonekani" alizungumza Tobias



    "Je uliweza kuwapigia simu na kuwauliza kama wamefika??



    " hapana sikuweza kuchukua namba zao, lakini sikuelewi unaposema ya kuwa na hawa nao hawajafika kijijini" alizungumza Alice.



    "Na hapo ndo hata Mimi nashindwa kukuelewa ya kuwa unazungumzia kijiji kipi walichoweza kwenda watu hawa baada tu ya kuonana na wewe Alice



    ***** ****** ****

    Ghafla zilianza kusikika kelele za ajabu ndani ya chumba cha operations.



    Vikram alienda akafungua mlango na kuingia ndani.



    "Ongeza tushtue mapigo ya moyo" alizungumza Dr Kim na kuanza kumshtua mapigo ya moyo Millerstone kwa kutumia vipimio maalumu vya kufanyia kazi hiyo.



    "Ongeza zaidi" alizungumza Dr Kim



    "Lakini imeshafikia 78" alizungumza Dr.



    Vikram alienda akamsogeza pembeni na kuongeza yeye mwenyewe mpaka 100.

    Dr Kim alimshtua na kumshtua lakini ghafla mapigo ya moyo yaliweza kusimama.



    "Ni nini hiyo?? Aliuliza Vikram na kumtazama Millerstone aliyekuwa amewekewa mipira katika mdomo wake pamoja na kushonwa sehemu nyingi katika kichwa chake.



    Alipomtizama Dr Kim , Dr Kim alitoa ishara ya kuwa Millerstone ameshafariki.



    " hapana, mwanangu hawezi kufa aliniahidi mwenyewe ya kuwa akiwa mkubwa lazima aninunulie gari sasa unasemaje amekufa na bado hajaninunulia gari. Alizungumza Vikram na kuchukua mashine ile ya kushtulia moyo kisha kuanza kumpiga nayo Millerstone katika sehemu za moyo wake



    Alifanya zaidi ya Mara saba wala hakukuwa na majibu yoyote Yale bado Millerstone alikuwa kimya.



    "Tangaza muda wa kifo kisha mtoeni huyo apo" alizungumza Dr mmoja na kuanza kuelekea njee.



    Vikram aliendelea kumshtua mapigo ya moyo Millerstone na ghafla yaliweza kurudi na machine ilianza kuonyesha kupanda kwa mapigo ya moyo.



    Dr Kim alimsogeza pembeni Vikram kisha kuyafunua macho ya Millerstone na kutabasamu.



    "Tunaomba mtoke njee sasa alizungumza nesi na Tropina alienda akamchukua Vikram.



    Aliyekuwa akilia huku akisema.



    " umefanya vizuri mwanangu, umefanya vizuri Millerstone "



    Baada ya dakika mbili waliweza kutoka madactari watatu pamoja na manesi wanne wote wakionyesha sura za Tabasamu.



    "Millerstone sasa hivi yuko sawa, ila"



    "Nini tena kim? Aliuliza Vikram kwa wasiwasi.



    " Kuna kitu kidogo tunahitaji kutoka kwa mama yake ili aweze kuwekewa yeye" alizungumza Dr Kim



    "Hivi Alice yuko wapi?? Aliuliza Vikram na kuwageukia watu waliokuwa eneo lile.



    Wote walikuwepo isipokuwa Alice.



    Hapo hapo vilisikika viatu vikija kwa kasi eneo lile.



    " mtoto wangu yuko wapi,anaendeleaje mtoto wangu?? Aliuliza Alice.



    "Umekuja wakati mzuri ongozana na Dr Kim Kuna kitu anahitaji kutoka kwako. Alizungumza Vikram na Alice alipomtizama aliona ameshikiliwa Mkono wake na Tropina.



    " Nafikiri mama wa mtoto amekuja mimi ninaenda " alizungumza Tropina na kuanza Kuondoka bila kujua ya kuw yeye ndiye mama halisi wa mtoto yule.



    Miller aliweza kutolew katika chumba kile cha operations na kupelekwa katika chumba cha kawaida akiwa bado hajapata fahamu.



    Vicky alimshika Mkono Tropina kisha akauliza



    Jimmy yuko wapi???



    Mbele ya macho yake alionekana Jimmy akiwa amechafuka damu mwili mzima na akiwa ameparuliwa paruliwa.



    "Jimmy , umetoka wapi?? Aliuliza Vikram na kuanza kumsogelea huku Queen, Collin's, Larry pamoja n Adrian wakisimama katika viti walivyokuwa wamekaa.



    Aliingia Patrick na kutoa heshima kwa Tropina pamoja na Vikram.





    "Patrick" aliita Adrian kwa mshangao..



    Patrick aliweza kukumbuka ya kuwa baada ya kupigiwa simu na Tropina aliweza kumfuata na alipotaka kuingia katika nyumba moja kubwa ya kifahari alimzimisha kwa kumpiga na kitako cha bunduki kisha akamfungia katika cage moja na aliweza kumleta mbwaa kisha akamwambia.



    "Mfanye huyo ni adui wako na umuuwe"



    Wakiwa eneo lile lile aliweza kupitishwa mama mmoja na kukimbizwa ICU mwanamke huyu alikuwa ni Dada yake na mama Alice aliyeonekana kujaa udongo mwili mzima na kuhema kwa shida sana lakini hakuna aliyeweza kumtambua.



    ***** **** ***



    "Unasemaje hajafa?? Aliuliza kwa mshangao Harlan na kutupa simu yake baada tu ya kupokea ujumbe huo.



    ***** ***** *****



    Dr Kim aliweza kumuita Vikram ndani ya chumba cha Dr.



    " Kuna nini tena mbona umeniita"



    "Kile tulichokuwa tukitaka kukichukua kutoka kwa Alice tumeweza kukichukua lakini shida ni kwamba DNA haziendani"



    "Kivipi"



    "Millerstone siyo mtoto wa Alice"



    "Unamaanisha nini?? Aliuliza Vikram na kujikuta amesimama katika kiti.



    " Nataka nichukue damu yako na yake niangalie kama zinafanana DNA " alizungumza Dr Kim



    "Kwahiyo Unataka kusema Millerstone siyo mtoto wangu?? Aliuliza kwa hasira Vikram.



    Baada ya muda aliweza kutoka njee akiwa mnyonge sana.



    Kila mtu aliyekuwa amekaa kwenye njee aliweza kumtazama.



    " Shemeji kimetokea nimi eti mbona umerudi katika hali hiyo?? Aliuliza Queen



    Jimmy.

    Aliita Vikram na Jimmy aliweza kusogea.



    "Vee, Larry, Queen na Tropina wapeleka katika nyumba yangu huko watakuwa salama zaidi na pia kesho nitamuhamisha Millerstone hapa na kumpeleka katika nyumba yangu, yeye ni mtoto wangu tu wala hana baba mwingine, wala sitaruhusu mtu yoyote yule amchukue kutoka kwngu" alizungumza Vikram.



    "Ndiyo"



    "Mimi nitabaki hapa na Vikram pamoja na Millerstone nyie mnaweza mkaenda tu' alizungumza Tropina



    "Kuna mahali naenda nitakuja kumwangalia Millerstone baadaye alizungumza Alice na kusimama.



    " ww Alice aliita Adrian na kumfuata huku Collins akiwa amebaki pale.



    "Collin's kwaajili ya usalama wa maisha yako na wewe wafuate wenzako" alizungumza kwa upole Vikram.



    "Hpana Mimi ninakazi kidogo Nahitaji kuimalizia ofisini Kwahiyo naondoka sasa Hivi" alizungumza na Kuondoka.



    "Kuna shida gani?? Aliuliza Tropina



    " Pinah, hata kama Millerstone hatakuwa mtoto wangu, siwezi muacha akaenda kwa baba mwingine " alizungumza Vikram na kutoa machozi



    "Haitawezekana Millerstone akawa siyo mtoto wako, ni mtoto wako yule" alizungumza Tropina na kumkumbatia Vikram.



    ***** ***** *******



    Adrian akiwa nyumbani ghafla maaskari waliweza kuingia.



    "Adrian tunahitaji uwepo wako polisi kwaajili ya maswali kidogo juu ya kifo cha Winnie" alizungumza Inspector George na kumwambia.



    "Unastahili kukaa kimya mpaka pale utakapoweza kufika polisi pia una haki ya kuita mwanasheria kama kesi hii itakubana "



    Dr Kim aliweza kuingia katika chumba alichoweza kulazwa Millerstone aliyekuwa bado hajazinduka na Pembeni yake alikuwa Vikram pamoja na Tropina wakiwa wamemshika Mkono huku Tropina akionekana kupitiwa na usingizi.



    Dr Kim alimpa ishara Vikram ambaye alimka na kumfuata Dr Kim.



    "98% Millerstone ni mwanao lakini kwa alice ni 3% zinazonyesha Millerstone ni mwanaye, hivyo Alice siyo mama wa Millerstone"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sasa mama wa Millerstone ni nani?? Aliuliza Vikram.



    " Wewe ndo ukumbuke wapi na wapi uliweza kufanya shughuli alizungumza Dr Kim.



    "Tofauti na Alice na Pinah sijawahi kulala na mwanamke mwingine, ngoja unamaanisha Millerstone ni mtoto wa Pinah?? Aliuliza na yeye alikosa jibu.



    Wakati huo nao alionekana Millerstone akitikisa Mkono wake ambao uliweza kushikwa na Tropina na kumfanya Tropina azinduke.



    " Millerstone!! Aliita Tropina kwa furaha



    "Mama" aliita Millerstone na kutabasamu huku akimfanya Tropina adondoshe machozi na kufurahia kuitwa jina hilo.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog