Search This Blog

Sunday 19 June 2022

DEMU WA FACEBOOK - 4

 





    Simulizi : Demu Wa Facebook

    Sehemu Ya Nne (4)



    “Mambo vipi wadada nyie yaani hapo mnadhani sitawajua kwa taarifa yenu nimewajua kitambo sana” aliongea Peter alipowafikia huku wakiwa bado wamempa mgongo. Alikuwa akijilambalamba papi za midomo yake. Mtindo uliokuwa maarufu kipindi hicho.

    “Mh!! Peter hebu patishia sisi kina nani tukupe unachotaka” alijibu mmoja wa wasichana wale pale gizani kwa sauti iliyolegea sana.

    “Mh! Sauti nishaijua mbona yaani umejitahidi kubadilisha lakini wapi imeshindikana pole yako nanihiii! Alijibu Peter.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aah!! Vipi unao wengi unaogopa kusema jina utaumbuka eeh!!” alisema yule msichana mwingine.

    “dah!! Mmeniweza ngoja niwe muwazi haya jamani jitambulisheni na karibuni sana Kigogo mmeandikisha majina kwa mwenyekiti wa mtaa au ndio kimya kimya tu” alisema Peter huku akitupia na utani kidogo mwishoni. Mmoja akacheka, mwingine. Kimyaa!!

    * * *

    Husna na Mwamvua walikuwa wameamua kweli kupambana na Peter waliyeamini kuwa hana lolote la kuwatisha zaidi ya ile mimba, licha ya kwamba Husna alikuwa anampenda Peter kiukweli ukweli toka moyoni lakini aliamini kwa kukaa kimya na kumfumbia macho Peter basi hata malipo ya hilo pendo lake asingeyapata na mwisho wa mambo yote angeambulia maumivu ya kuzaa mtoto asiyekuwa na baba hapa duniani pia heshima yake ingeshuka kwa kiwango kikubwa sana na kuonekana dhaifu sana. Ni hayo yaliyomfanya aamue kuendelea kupigania penzi lake kwa vitendo na sasa alitaka atambulike kwa Peter kuwa ni yeye huyu huyu Husna kutoka facebook na sio kama ile picha anayoiona kila siku ya mrembo wa tija katika mtandao mwenye maisha bora sana pengine kuliko wasichana wote waliopo katika mtandao huo wa kijamii unaounganisha mamilioni kwa mamilioni ya watu dunia nzima.

    Wazo la Husna la kumfata Peter mpaka kwake lilikubaliwa kwa moyo mkunjufu na Mwamvua ambaye tayari alikuwa amepandwa na pepo wa shari.

    Jioni ya siku hiyo tayari walikuwa ndani ya mtaa wa Kigogo ndani ya mavazi yao aina ya baibui yanayovaliwa kwa wingi sana katika nchi ndogo ya Zanzibar, mavazi hayo yaliwapendeza kwa vigezo viwili kwanza walikuwa waumini wa dini ya kiislamu na pili Husna alikuwa mnene wakati Mwamvua alikuwa ana umbo. Wote ndani ya baibui walitaka kufanana.

    Walijinywesha taratibu soda walizokuwa wameagiza katika duka mojawapo jirani kabisa na barabara ya lami iendayo magomeni. Majira ya saa moja usiku waliondoka eneo lile na kuingia ndani zaidi hapo Kigogo safari yao iliishia jirani na anapoishi Peter, bahati nzuri walikuta geti lipo wazi na walimshuhudia Peter akiwa amejiachia mbele ya mlango wa nyumba yake alikuwa kifua wazi na masikioni alikuwa na ‘earphone’ akisikiliza mziki taratibu.

    “Mh!! Ana kifua kizuri jamani” Husna alimwambia Mwamvua

    “Tafadhali mapenzi yako weka pembeni tumekuja kazini na ni hayo mapenzi tunayapigania wewe uyapate sasa ukijidai wewe ndo bingwa wa mapenzi hii shughuli nitakuachia mwenyewe..shoga tafa tena tafaa!!!” aliongea kwa ukali Mwajuma akimwambia Husna. Bingwa wa mabingwa akakaa kimya. Husna alikuwa amepata mbabe wake!!

    “Yaishe shoga nimepitiwa mwenzako” alijitetea Husna.japo Mwamvua hakujibu kitu alionyesha kuwa amemuelewa. Punde wakiwa sehemu waliyoweza kumuona Peter na yeye asiweze kuwaona walimshuhudia akiurudishia mlango wake na kuondoka taratibu kutoka pale akiwa tayari amevaa shati lake hali iliyoonyesha anaenda mbali japo sio sana. Dakika kama tano baadae ndipo Husna na Mwamvua walipojikongoja haraka haraka hadi pale alipokuwa anaishi na kujidai kuwaulizia watoto waliokuwa pale kuwa Peter yuko wapi nao wakajibu kuwa ametoka muda si mrefu.

    “Akija mwambie tumekuja hapa wanafunzi tunasoma naye tunamsubiri pale hivi sawa” Mwamvua aliwaambia watoto wale huku akiwaonyesha watakapokuwa.

    “Haya!!” walijibu kwa pamoja huku wakiendelea kucheza.

    “Huyooo anajileta mume wako mwenyewe” Mwamvua alimwambia Husna alipomuona Peter akija huku ameongozana na watoto wawili.

    Baada ya jitihada za Peter kujaribu kubashiri wawili hawa ni akina nani kugonga mwamba aliamua kuwaambia wajitambulishe.

    “Kama umeshindwa kutufahamu basi utatujua kesho darasani” aliambiwa Peter na wasichana wale wawili.

    “Aah!! Jamani msinifanyie hivyo warembo mbona nitashindwa kulala mie” alibembeleza Peter.

    “Sikia Peter sisi tuna ujumbe wako na hapo hapo kuna majina yetu ukishausoma utatuletea majibu kesho darasani sawa mtanashati wetu” sauti nyororo ya msichana aliyekuwa anaongea mara kwa mara ilimueleza Peter.

    “Haya jamani kama mmeamua hivyo poa tu lakini sio vizuri lakini mi nishawajua na yasingekuwa hayo mabaibui ningewajua hadi majina yenu” alijibu Peter huku akitazamana na wawili hawa waliokuwa kama ndugu kutokana na kufanana katika mavazi yao.

    “Usijali kesho utatufahamu,……tena sio kesho ni leo leo kama vipi utatupigia au sio” alisema Mwamvua huku akimkabidhi Peter kibahasha kidogo na baadaye wakaaga na kuondoka zao.

    “Mh! Atakuwa demu gani huyu au ni Lilian anaomba msamaha nini!!! Kama sio yeye basi atakuwa Neema huyu tayari amewashwa ananitaka, dah!! Mara awe Violeth yule dem wa kisomali amenijibu duh!! Itakuwa shangwe hapo mtoto wa watu naenda kujilia vyangu……..ebwana nina nyota na hawa jinsia tofauti na yangu sijui nimpe nani shukrani kwa hilo ni maza au ni walionileta mjini lakini na jina pia linachangia kwa kiasi chake” njia nzima kuelekea pale kwake Peter alizungumza na kichwa chake.

    “Haya watoto video kesho sawa watoto wazuri”

    “aaah!! Kaka Peter umetudanganya” walilalamika wale watoto kwani walikuwa wamepewa ahadi na Peter muda mfupi uliopita kuwa watawashiwa luninga na kuangalia kadri wawezavyo kwani Peter alikuwa na mikanda mbalimbali iliyowavutia sana.

    “Haya kesho kuanzia asubuhi”alidanganya Peter huku akiwa na uhakika kabisa kuwa atakapoamka asubuhi kuwahi shule watoto wale watakuwa bado wamelala,kwa kusikia hivyo kama kawaida watoto wakadanganyika na kuondoka zao wakimwacha Peter akijifungia ndani ya chumba chake

    Hamu kubwa ya Peter ilikuwa kujua ni binti gani aliyeutuma ujumbe ule kwake usiku ule,matumaini yake yakiwa yameegemea kwenye furaha hakuwa na wasiwasi wowote ule

    “Sasa sijui ndio honey, darling, sweetheart au mpenzi maana hawa mabinti na vijimaneno vyao mh!! Vinakosha hivyo jamani” alijisemea Peter huku akiwa amefungulia redio yake kwa sauti ya chini na wimbo wa “Endless love” ukiwa unakonga nyoyo taratibu, huku feni ikimpepea na kujihisi yuko katika hekalu la kifalme huko Swazilandi kwa mfalme Mswati (12).

    Taratibu huku akitabasamu na kuzisahau shida zote. Aliufungua ujumbe alioletewa na wale wasichana!!!

    Mikono haikutetemeka na mapigo ya moyo yalikuwa kawaida tu!! Alishazoea mambo haya.

    Ghafla!!!

    “Mama yangu!!!!! Nini tena hiki sasa” alipiga kelele Peter huku akitetemeka sana mikono yake, ghafla feni ikakosa umaana tena, joto kali likauvagaa mwili wake, jasho ikawa inatiririka kwa kasi kubwa mno, macho ya Peter yalikuwa yamemtoka mithili ya mruka sarakasi maarufu hapa nchini maarufu kwa jina la ‘Wabogojo’. Alijaribu kugeuka huku na huku huenda kuna mtu ameshuhudia yote yaliyotokea lakini hakuwepo mtu yeyote yule chumba kizima alikuwa peke yake.

    Akatamani kupiga kelele. Sauti ikakwama!!! Akataka kukimbia lakini miguu ikawa mizito.

    Peter akajiuliza dalili za kuzimia ni zipi huenda anakaribia kuzimia. Lakini aliendelea kusubiri azipoteze fahamu kwa muda lakini haikutokea. Aliendelea kuutambua ukweli!!

    Ilikuwa ni picha iliyochorwa na mtu ambaye hakuwa na utaalamu wowote wa kuchora bali alitumia akili ya kuzaliwa kujaribu kuufikisha ujumbe alioutaka yeye, kwa akili ya kawaida kabisa ya kibinadamu ukiiona ile picha lazima utagundua mchoraji alimaanisha nini kwa mchoro ule.

    Alikuwa ni mwanamke mwenye tumbo kubwa ambalo bila shaka mchoraji alimaanisha ni mimba na ili kusisitiza hayo mbele ya lile tumbo aliandika ‘ina miezi mitatu sasa’ halafu ili kudhihirisha kuwa ujumbe ule haujapotea njia chini yake aliandika ‘ni mimi 07677790**’ Peter hakuwa na haja ya kuiingiza ile namba tena kwenye simu yake ili ajue ni ya nani kwani kwa sasa alikuwa anaitambua vyema na ilikuwa amenasa katika ubongo wake, ilikuwa ni namba ya Husna.

    “Wamepajua kwangu tena basi nimekwisha nasema sina ujanja mimi Peter sasa nitamshirikisha nani mie anielewe?? aah!!” Peter alijikuta anatoa machozi bila kupigwa

    “Wamepajua kwangu tena basi nimekwisha nasema sina ujanja mimi Peter sasa nitamshirikisha nani mie aah!!” Peter alijikuta anatoa machozi bila kupigwa

    Peter hakuwa na ujanja tena kwa kilichotokea pale.

    “Ina maana yule pale ni Husna amekuja na mabaibui yale nisimfahamu au vipi? Ningejua nisingeenda pale waliponiambia wale watoto sasa hapa mama atanielewaje hapo akisikia nimefukuzwa shule kwa sababu ya wanawake dah!! Nimelikoroga mimi Peter” alizidi kujilaumu Peter baada ya kuanza kuona mambo yanazidi kuwa magumu upande wake.

    Akili ya Peter ilichoka kuwaza na kichwa kilimuuma sana licha ya kujaribu kunywa tembe mbili za Panadol alizokuwa nazo pale ndani bado hakujua siku inayofuata itaanzaje na itaishaje, aliamini kuwa siku hiyo haitaisha bila kuwa na kimbwanga kingine

    “Nisingekuwa na mtihani kesho mi nisingeingia shuleni kwa kweli maana wakiniibukia pale shuleni najua ndio masuala ya kunilaza polisi mtoto wa kiume na ninavyopaogopa duh!! Haki ya Mungu ningekuwa na Bunduki ningeua mtu mimi aaaaaaargh!!” alisema kwa jazba kali Peter.

    Majira ya saa saba usiku usingizi ulimpitia na kushtuka saa kumi na mbili, kila alipofikiria kuhusu yanayomtokea Peter alikuwa anakata tamaa ya kila kitu katika mipangilio ya ratiba zake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mi sitaki tena mambo ya madem dem ona sasa yanayonikuta hata washkaji wakisikia watanishusha thamani kabisa, sitaki mademu nasema sitaki tena” alijiapiza Peter huku akitia dawa katika mswaki wake tayari kwa kwenda kusafisha kinywa chake.

    Baada ya kumaliza kuswaki na kuosha mwili wake Peter alivalia nguo zake za shule na kuondoka zake kuelekea kituo cha mabasi huku akiwa amekata tamaa na kutawaliwa na wasiwasi mkubwa moyoni, njia nzima hakutaka kuangaliana na watu usoni kwani alihisi anaweza kukutana na akina Husna muda wowote.

    Peter akaanza kuishi maisha ya kidigidigi!!!

    “Peter vipi kaka una homa za vipindi nini?? Maana wiki mbili zilizopita ulikuwa umenyon’gonyea halafu baadae ukawa poa tena na leo hauko kawaida kabisa ndugu yangu kuna nini??” rafiki yake Peter aliyemuona katika hali ile alimuuliza.

    “Ah!! Hangover tu hizo si unajua tena masuala ya kuruka kwanja tena mpaka asubuhi” alidanganya kiujasiri Peter.

    “Dah!! Kaka na wewe na kuruka mziki haujambo lakini sasa wewe unachekesha maana wenzako wanaruka mziki na kupiga pombe wanakuja shule wamechangamka sana mwenzangu wewe unalegea kweli au hofu ya hako kamtihani” alihoji yule rafiki yake.

    “Ah!! Na kenyewe kana ugumu wake lakini sio ka kuniumiza kichwa kiasi hichi” alijibu Peter kwa mkato huku akionekana kuna jambo kubwa limemkwaza katika maisha yake.

    Wakati huo walikuwa waapo mstarini wakisubiri matangazo ya hapa na pale ili waweze kuingia darasani tayari kwa kuanza ratiba za siku hiyo.

    Baada ya matangazo huku moyo wa Peter ukiwa bado haujapata kutulia alijiwahisha darasani na kuchukua nafasi yake, hakutaka bughuza yoyote, alichukua kidaftari kidogo akawa anapitia pitia kwa mara ya mwisho kabla ya kuanza kufanya mtihani uliotarajiwa kuanza baada ya muda mfupi.

    Pale kwenye karatasi palikuwa na mengi sana ya kusoma lakini Peter alikuwa haoni lolote lile pale mawazo ndio yaliyomtawala kwa kiasi kikubwa sana, mawazo ya kuumbuka hadharani. Hadi mwalimu alipoingia na kuwaamuru wafunike kila kitu kinachohusiana na mtihani Peter hakuwa amesoma lolote lile hivyo aliingia kuufanya mtihani ule kichwa kichwa tu.

    Ndani ya dakika kumi Peter alikusanya mtihani wake na kutoka nje akiwaacha watu midomo wazi kwani wao waliuona mtihani mgumu sana na ulihitaji muda kufikiria tofauti na Peter aliyetumia dakika chache sana. Wanafunzi wakaamini kuwa mwenzao mtihani ameuweza.

    Peter akatoka nje na kujipeleka chini ya mwembe!! Hakujali kama alikuwa ameufanya vibaya mtihani ama la!! Akiwa bado amekaa chini ya mwembe alimwona msichana aliyekuwa anamfahamu. Taratibu Peter akaanza kumfuata baada ya kumpigia mluzi naye akasimama.

    “Hivi Aneth ushawahi kusikia au unajua lolote kuhusu mimba maana kuna mtu nabishana naye kweli tangu jana ananibishia kweli!!” Peter alimuuliza binti aliyekuwa kidato cha sita wakati huo uilikuwa wa mapumziko ya kwanza majira ya saa nne asubuhi.

    “Ndio mimi msichana tena kidato cha sita kwa nini nisijue vitu vya kawaida kama hivyo jamani….kwani anakubishia nini???” alijibu kwa kujiamini sana msichana huyo kisha na yeye akauliza swali, binti yule alikuwa akiona fahari kuzungumza na Peter.

    “Yaani tunabishana lakini ni ujinga mtupu dada yangu ila tusaidie hivyovhivyo kwa kweli ili nijue mimi ndio sijui au yeye” alianza kujin’gatan’gata Peter, hakutaka kuusema ukweli.

    “Niambie na mimi nakusikiliza na nitakujibu ndani ya uelewa wangu”

    “Hivi mimba inapofikia miezi mingapi ndio inagoma kutoka yaani ‘arbortion’ ni mwezi wa kwanza hadi wa tatu, wa tatu hadi wa sita au wa sita hadi wa tisa eeh!! Ndio hicho kitu tulikuwa tunabishana na jamaa yangu” aliuliza Peter huku akiwa ametawaliwa na aibu usoni.

    “Mh!! Mna mambo nyie wakaka dah!! Lakini ni swali zuri lakini sio mwende kujaribishia kwa wasichana wenu sio vizuri sawa Peter”

    “Mimi siwezi hata siku moja kwanza sina hata huyo mpenzi, hayo mapenzi mie siyataki kwa sasa, mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa Aneth yaani mimi ni heri kuwa kama nilivyo” alijibu kwa hisia kali Peter jambo ambalo hata Aneth alilielewa.

    Maigizo ya wanaume!!! Aliwaza Aneth.

    “Mh!! Peter nawe mwongo kweli ina maana na wewe unataka kunidanganya kuwa huna mtu hapa shuleni au ndio kusema mimi siyasikii mambo yako jinsi unavyogombaniwa na wasichana kuanzia form one hadi sisi wa kidato cha sita” alijieleza huyo msichana huku akiwa hajajibu swali la Peter.

    “Hapana sio kweli kwani mimi nina nini cha kunitofautisha na wengine hadi nipendwe???” alihoji Peter huku naye akiwa amesahau kama kuna swali anatakiwa kujibiwa. Wote wakawa wamehama mada.

    Wakiwa wanaendelea na maongezi yao huku wakiwa wamehamisha mada ya utoaji mimba na sasa walikuwa wanaongelea mambo binafsi, mara kwa mbali kabisa Aneth aliona watu watatu wakionyeshana kama ishara flani ambazo kwa vyovyote vile zilikuwa zinawahusu wao (yeye na Peter) kwani watu wale walikuwa wanawanyooshea vidole kutokea mbali.

    “Ndio tabu sasa ya kusimama na watanashati kama wewe maana tayari wakezo wameanza kuwa na wivu usiokuwa na maana ona tayari uvumilivu umewashinda waambie waache hizo” Aneth alimwambia Peter ambaye alikuwa amewapa mgongo hao watu waliokuwa wanawanyooshea vidole

    “Kwani nini tena Aneth jamani” alihoji Peter kwa mshangao huku akijaribu kuwatambua kwa mbali wasichana wale.

    Hakuwa akiwafahamu!!!

    “Huyo hapo anakuja subiri umuulize mwenyewe lakini na nyie ma-handsome mnaboa kwa kweli” alilalamika Aneth huku akibetua midomo yake.

    Peter alipogeuza shingo yake alimuona mtoto mdogo ambaye kwa makadirio alikuwa kidato cha kwanza au cha pili alikuwa anatembea haraka haraka kuelekea pale Peter na Aneth walipokuwa wamesimama. Peter akaingiwa wasiwasi kwa mbali. Akamuwaza Husna lakini ile hali ya wale wasichana kumnyooshea vidole ilimtoa hofu.

    “Hapo kameagizwa kakuite hakuna la ziada hapa” alisema kwa hasira Aneth kwani tayari na yeye alikuwa amevutiwa na Peter.

    “Hata sikajui haka kadogo huwezi amini, ya nini kuandikia mate na wino upo??” alisema kwa kujiamini sana Peter wakati huo yule mtoto alikuwa amebakiza hatua chache kuweza kuwafikia

    “Shkamoo kaka…….shkamoo dada” alisalimia mtoto yule.

    “Marahabaa” walijibu kwa pamoja Peter na Aneth.

    “Eti kaka wale wakina dada wameniambia kwamba wewe ndio kaka Peter!!!!” alianza kujieleza yule mtoto , huku akijiuma uma vidole vya mikono yake kwa aibu.

    “Haya toa kwanza vidole mdomoni mtoto mzuri……eheeee!! Hapo sawa sasa…..ndio mimi ni kaka Peter” alijibu Peter.

    “Nilikuwa nimetumwa kwako” aliendelea yule mtoto huku Aneth akimrekebishia kora ya nguo yake vyema.

    “Ndio mtoto mzuri mwalimu nani amekutuma??” aliuliza kwa sauti ya upole na ukarimu Peter huku Aneth akiwa kimya.alisubiri kuwa shahidi!!

    “Mh!! Unajishaua eti mwalimu yaani wewe Peter wewe tunatakiwa tupate muda tuongee sana ili tushauriane mambo fulani hivi” alidakia Aneth.

    “Hii hapa” badala ya kujibu chochote Yule mtoto alimpa Peter bahasha ya kaki ukubwa wa A4. Kabla Peter hajaipokea Aneth akaikwapua.

    “Haya asante mtoto mzuri wewe nenda mama sawa”

    “Haya dada!!” Aneth aliagana na yule mtoto, Peter alikuwa anaduwaa huku akiwa ametoa tabasamu hafifu akisubiri ni kitu gani Aneth anataka kufanya na ile bahasha.

    “Vipi nikusaidie kufungua au vipi”

    “Fungua tu!! Unadhani mimi nina hofu basi!!!” alijibu Peter.

    “Hapana kwa kweli sitaki kujipa presha zisizokuwa na msingi fungua mwenyewe kadi zako hizo za wakupendao” alisema Aneth huku akimpa Peter ile bahasha.

    “Haya ngoja nifungue na wewe ujionee yaliyomo najua ni upuuzi mtupu” alisema Peter huku akiifungua bahasha kwa kuichana taratibu. Hakutaka Aneth aelewe ndani kuna nini kwanza, akaingiza jicho moja na kuchungulia

    “Nini nini jamani Peter umekuwaje Peter, Peter mamaaaa!!!” alipiga kelele Aneth, Peter alikuwa ameanguka chini na kutulia tulii akiwa na bahasha yake mkononi, kelele za Aneth ziliwafikia watu wengi na ndani ya dakika tano pekee hadi baadhi ya waalimu walikuwa wamefika pale, Aneth alikuwa kama mwendawazimu vile kila swali lilikuwa kwake.

    “Amekuwaje?, ni nani?, hiyo bahasha ya nini?, kwani ameangukaje?” yalikuwa baadhi ya maswali aliyoulizwa Aneth na kushindwa kujibu hata moja kwani wingi wa maswali yale ulizusha kelele, kelele zikamjaza hofu, wenye busara zao walikuwa wanampepea Peter kwa kutumia madaftari na wengine walikuwa wamevua mashati yao wote dhumuni lao likiwa kumpepea Peter aweze kuzinduka pale alipokuwa ameanguka. Peter hakuzinduka mapema!!

    Mwalimu wa zamu aliamuru Peter abebwe haraka apelekwe katika Zahanati iliyopo pale shuleni huku ile bahasha aliyokuwa nayo mkononi ikichukuliwa na mwalimu wa zamu na kuelekea nayo ofisini. Lilikuwa jambo lililofanywa haraka sana!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Maskini utakuwa ni msiba huo hapo dah!!” baadhi ya wanafunzi walisikika wakisema wakati kundi la wanaume likiwa limembeba Peter juu juu kuelekea Zahanati. Wasichana wao hawakuwa na la kufanya zaidi ya kulia kwa fujo kana kwamba Peter amekufa tayari. Peter alikuwa anapendwa sana!!! Laiti angesikia vilio hivi angejua ni jinsi gani anasumbua vichwa vya akina dada wengi.

    * * * *

    Vita waliyokuwa wameianzisha Husna pamoja na Mwamvua dhidi ya Peter ilikuwa ni vita hasa hasa vita iliyohitaji ushindi kutoka upande mmoja kwa namna yoyote ile kibaya zaidi upande wa Peter alikuwa anapambana na maadui wengi tena asiowafahamu, wote kwa pamoja Husna na Mwamvua lengo lao lilikuwa kumdhihirishia Peter kuwa wao sio watu wa kuchezea na kamwe asizoee kuwadharau wanawake kwa kujali masilahi yake binafsi.

    Peter alikuwa ametolewa kafara ili na wengine wajifunze kupitia yeye.

    Usiku mmoja baada ya kumtumia tena namba za simu waliona hiyo haitoshi hata kidogo kumkomoa na kumuadabisha Peter hivyo usiku huo huo Husna alimpa wazo Mwamvua kuwa wafanye mpango wa kumtumia Peter picha ambayo yeye (Peter) anaamini kuwa ni ya Husna ambayo ilikuwa katika mtandao wa kijamii wa facebook. Kwa Mwamvua hilo halikuwa tatizo hata kidogo kwani alikuwa na channel mbalimbali tofauti za kila aina.

    “Umesema shida ni internet café si ndio hivyo” alisema Mwamvua baada ya kumsikiliza Husna kwa makini sana.

    “Ni hilo tu shoga yangu nadhani akiipata hiyo picha ndio atachanganyikiwa na kujua tupo nae karibu kiasi gani la sivyo atazidi kuleta dharau.” alisisitiza Husna ambaye kwa wakati huu jina lake mtaani lilikuwa limefifia kwa sababu lilikuwa halisemwi semwi tena hovyo kama ilivyokuwa hapo awali

    “Hivi pale kwa Alex si kuna hiyo sijui internet café??” aliuliza Mwamvua.

    “Ndio ipo kwani unamjua mtu pale!!” alijibu kwa mtindo wa swali Husna.

    “Amini usiamini huyo Alex mwenye hicho kijengo ndio mwanaume wangu wa kwanza namaanisha ndio kanitoa usichana wangu” alisema Mwamvua kwa sauti ya chini.

    “Kwa hiyo pale ni kama kwangu japo yote hayo yamepita!!!” alimalizia.

    Mapokezi waliyoyapata pale internet café yalitosha kabisa kumpa jibu kwamba Mwamvua hakuwa na utani wowote ni kweli yeye na Alex walikuwa kitu kimoja. Mwamvua hakupoteza muda sana alijieleza shida yake na kama vile mteja mwenye haraka sana alihudumiwa kwa umakini mkubwa shida yake.

    “Hapo vipi Husna imekaa vizuri au badobado” Mwamvua alimuuliza Husna wakati akiitazama picha.

    “Hapo imependeza sana tayari tosha kabisa” alikubali. Kama vile wamelipia mamilioni kuitengeneza ile picha walitembea kwa maringo na kuondoka pale.

    “Mh!! Shoga nawe ukaweka picha nzuri kiasi hichi..ujue kwa upande mwingine Peter tunamuonea bure!!” Mwamvua alimwambia Husna wakati wakiitazama ile picha ya mwanadada akiwa ameketi kihasarahasara mapaja yote nje. Husna akajichekesha!!!

    “Mwamvua chukua bahasha jamani sasa utatembea na picha hivyo” Alex alimkumbusha Mwamvua wakati anaondoka, Mwamvua alirejea na kuichukua bahasha akaitia ile picha ndani yake na kujiondokea wakiongozana na Husna aliyekuwa amependezea ndani ya mavazi ya baibui ambayo kwa hali halisi yalikuwa yamelifanya umbo lake baya kuonekana lina mvuto kiasi cha kukidhi haja ya mtazamaji.

    Siku iliyofuata asubuhi na mapema Husna kama vile alikuwa amepewa ajira ya kudumu tena yenye kipato kikubwa alidamka na kujiandaa, akaanzia kwa kaka yake akamwomba nauli. Akapewa!! Akaenda kwa mama yake akamwomba ya vocha akapewa!! Akazijumlisha zikawa zinamtosha kwa siku hiyo!! kisha akampigia simu Mwamvua.

    “Hee!! Shoga mwenzio nilikuwa nimepitiwa na usingizi na usingepiga simu hapa saa tatu ndio ningeshtuka, biashara jana ilichanganya sana mwenzangu nilikamatika kwa mzungu mmoja basi mi hoi, ngoja niamke sasa nijiandae tuweze kwenda kwenye hiyo shughuli yenyewe” Mwamvua alimjibu Husna kwenye simu kwa sauti ya kizembezembe. Biashara ya uchangudoa!!!

    “Haya usichelewe lakini basi maana mwenzio nipo wima wima nasubiria hilo sekeseke nimejiandaa tangu zamani ujue” Husna alisema kwa haraka haraka halafu akakata simu.

    Baada ya saa zima wawili hawa ambao walikuwa wameshibana waliongozana wakipeana stori za hapa na pale hadi kituo cha daladala walipofanikiwa kupata gari lililokuwa wazi sana wakajichukulia siti ya watu wawili wakakaa. Marashi aliyopulizia Husna ndio yalitawala ndani ya gari lakini kwa sura na umbo lake basi watu wote wakamlaani Mwamvua wakidhani ndiye aliyeleta balaa hilo!!!

    Kimya kilitanda safari nzima kila mmoja akiwaza lake lakini hawakusahau kuwaza kilichowapeleka, hakika walikuwa na shauku sana ya kumtenda Peter.

    Kwa sababu ilikuwa asubuhi sana basi hawakupata usumbufu mkubwa wa foleni kwani mida hiyo magari mengi yanakuwa hayajaingia barabarani hasahasa ya watu binafsi kwani hayo ndio mengi kuliko ya abiria hivyo ndani ya dakika kama thelathini gari lilisimama kituo cha uhasibu na kuwashusha hapo abiria wanne, wawili kati yao wakiwa Husna na Mwamvua wote wakiwa na miwani za jua katika nyuso zao. Bila kupoteza muda kama vile wana miadi ya maana sana walianza kujikongoja kuelekea katika geti la kuingilia shule ya upili Jitegemee (J.K.T).

    “We mtoto wewe njoo hapa mara moja” Mwamvua aliita kwa ukali akimkaripia mwanafunzi aliyekuwa anataka kuvuka barabara.

    “Shkamoo dada” Yule mwanafunzi alienda mara moja na kuwasalimia Husna na Mwamvua.

    “Marahaba mbona unavuka barabara bila kuangalia kushoto na kulia ukigongwa na gari utamlaum nani” Mwamvua alimkaripia mtoto yule licha ya kwamba barabara ile ilikuwa ni ya njia moja yaani “one way” ambayo haiitaji kuangalia kushoto na kulia wakati wa kuvuka, lakini kwa sauti kali ya Husna mtoto yule hakujibu chochote zaidi ya kuinama chini.

    “Haya unasoma wapi wewe”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nasoma Jitegemee” alijibu kwa ukakamavu.

    “Ahaaa!! Kumbe ni hapo mbele tu haya unaenda wapi sasa hivi”

    “Naenda shuleni lakini nampitia kwanza rafiki yangu hapo mbele” alijibu kwa uoga.

    “Hapana utachelewa nenda shuleni sawa halafu unamfahamu Peter anasoma hapo shuleni kweni ni kaka mmoja mrefu hivi………” kabla hajaendelea kujieleza mtoto akawahi kujibu kwa njia ya swali

    “Raisi wa Kigogo???” aliuliza yule mtoto haraka haraka hata kabla hajamaliza swali lake Mwamvua.

    “Yeye huyo yukoje raisi wa Kigogo”

    “Anaitwa Peter ninakaa naye kule kigogo anasema yeye ndio raisi wa Kigogo” alijieleza kwa ufasaha, huku akifurahia kutoa maelezo yale.

    “Ndio huyo huyo yaani huyu kaka yangu haishi visa kwa kweli yaani anajiita raisi dah!! Haya tuachane na hayo ni kwamba yule ni mdogo wangu sasa nina mzigo wake nataka nikupe umpelekee sawa”

    “Sawa lakini dada sasa hivi wako darasani hadi wakati wa mapumziko..wenyewe wanaingia asubuhi sana sio kama sisi” alijibu yule mtoto wa kike.

    “Haya hiyo saa nne uje hapa hapa utatukuta pale chini ya mti ule pale unaoonekana pale, uje uchukue umpelekee halafu nitakununulia chai sawa” alitoa maelekezo hayo Mwamvua wakati Husna akiwa maskini wa maneno kimya kikimtawala zaidi

    “Sawa dada” alijibu yule mtoto

    “Yaani Ramla nataka huyo Peter ashangae yaani hajui kama nimekuja huku Dar atacheka huyo” alizuga Mwamvua kuongea na Husna huku akiwa amembadilisha jina ili kumtoa wasiwasi yule mtoto na kumpoteza kabisa. Kama Peter akimuuliza jina basi ataambulia kujibiwa kuwa ni Ramla.

    Hawakuwa na haraka na hata wangekuwa vnayo hawakuwa na pa kwenda hivyo wawili hawa walijisogeza kwanza katika mgahawa wa chuo cha uhasibu (T.I.A) ambapo walikuta chai bado haijawa tayari, bila kujalisha utupu wa matumbo yao yaliyohitaji chakula cha moto waliagiza soda za baridi wakaanza kujinywesha taratibu hadi chai ilipokuwa tayari wakahudumiwa na kuendelea nayo takribani saa moja na nusu walikuwa wako pale ndani wakijilisha taratibu sana huku kichwani wakiwa na nia yao.

    Baada ya mlo huo walijisogeza hadi chini ya ule mti waliomuelekeza Yule mtoto awakute.

    “Hivi katakuja kweli kale maana watoto wa Dar na wao siku hizi heshima hakuna zaidi ya shkamoo shoga!!!” aliuliza Husna.

    “Ndio hawana heshima lakini mbele ya kitu pesa wana heshima sana lazima katarudi kale hakana pesa ya chai leo” alijibu Mwamvua. Ilipojiri saa nne na dakika kadhaa yule mtoto alirejea hayakuwepo maongezi marefu sana yule mtoto alipewa ile bahasha pamoja na shilingi elfu moja kwa ajili ya chai kwake yeye ulikuwa ujira mzuri sana kwani haikuwa kazi yenye ugumu wowote kumtafuta mtu maarufu kama Peter pale shuleni hivyo ilikuwa bahati ya kipekee mno.

    Mwamvua na Husna hawakukubali kupitwa na lolote jambo walifatilia kwa makini hadi walipoona tukio zima la Peter kupewa ile bahasha bkisha baada ya kuifungua akaanguka palepale, hawakutaka kujua nini kitaendelea tena pale wakatoweka kwenda kujipongeza.

    “Akiamka kutoka pale chini atajua nini cha kufanya kuyaepuka haya pumbavu zake” aliropoka Husna huku wakiondoka. Peter akiwa hajitambui tayari!!

    “Utamuua mumeo shoga halafu uanze kunililia hapa” alitania Mwamvua akimwambia Husna halafu wote wakacheka na kugonganisha mikono yao. Ushindi kwa mara nyingine!!! Vita nyepesi!!!

    ****

    Ilimchukua Peter masaa matatu kuweza kurejewa na fahamu zilizopotea baada ya kuwa ameshuhudia picha aliyozoea kuiona katika mtandao wa kijamii wa facebook, ni picha aliyoitamani akaisifia, akaitaka kimapenzi, ile picha ikampa namba ya simu, akaanza kuwasiliana nayo, ile picha ikaonekana inaishi maisha ya kifahari. Mara Peter akaingia katika uhusiano wa kimapenzi na picha. Ikafika siku ya kuonana na ile picha. Picha ikafika. Baada ya kuonana sasa ile picha inalalamika kuwa ina mimba. Na sasa ile picha ipo mbele yake!!!! Hofu, wasiwasi tena shuleni na ni usiku mmoja tu ulikuwa umepita tangu aletewa barua iliyokuwa imeambatanishwa na namba ya Husna bila maelezo mengine tofauti na picha iliyochorwa ikimuonesha mwanamke mjamzito na maandishi mbele yake kuwa ni mwezi wa tatu sasa.

    Hata ungekuwa wewe!!! Yangekukuta haya!!

    “Msimuulize kitu tafadhali” sauti ya mwalimu wa zamu ilisikika kwa chini ikiwaasa wanafunzi waliokuwa wamemzunguka Peter wasiulize chochote kwa kuhofia kwamba ile picha ilikuwa ina ujumbe mzito sana kwa Peter ambao laiti kama angekumbushwa angeweza kuzirai tena labda kwa muda mrefu zaidi ya hayo masaa matatu. Peter aliyasikia maneno hayo hata kabla hajauliza chochote kuhusu uwepo wake katika eneo lile ambalo tayari alikuwa amelitambua kuwa ni zahanati.

    Akili yake ilivuta kumbukumbu zote za nini kilichotokea muda mfupi uliopita akaikumbuka picha!! Picha ya Husna, picha ile ilimshtua maana hakuitegemea. Ni jana usiku walikuwa nyumban i kwake na sasa wamefika shuleni. Hakuna pa kukimbilia tena!! na hakika aligundua ni kwa nini yuko pale katika kitanda kile. Tofauti na mawazo ya watu kwamba ataanza kuuliza ni kwa nini yuko pale Peter hakuuliza kitu kwa muda kama wa dakika ishirini alikuwa anashangaa shangaa pale ndani.

    “Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe” ndio maneno aliyosema Peter baada ya kimya cha muda mrefu kupita. Maneno hayo yalimchoma kila mtu na hapakuwa na swali zaidi majibu yote yalikuwa nje kwamba Peter alikuwa amefiwa na aliyekufa ndio yule aliyekuwa kwenye ile picha kutoka kwenye bahasha.

    “Pole sana Peter haya yote ni ya kidunia pole sana” Mwalimu mkuu msaidizi alimwambia Peter baada ya kuwa ameruhusiwa kutoka hospitali.

    “Ah!! Hawa!!! Umekufa dadangu...nilikusihi sana acha kujirahisisha na wanaume, Hawa nikakusihi usome ona sasa!! Ona Hawa umekufa, mimba mimba mimba najua tu umetoa mimba!!” alilalamika Peter. Mara wanafunzi wenye mioyo myepesi wakaanza kulia.



    Kapu la michango likapitishwa, hata wale waliokuwa wabahili walichanga visenti vyao. Kisa? Husna anaolewa!!! Nani asiyemjua Husna!! Kila mtu alikuwa anamfahamu mitaa ya Kinondoni shamba na mitaa ya jirani. Na hata mbali pia alijulikana Kigogo, Kurasini, Kariakoo, Tegeta, Posta, Ilala..pote huku aliwahi kuzusha matafrani.

    Kwanini wasimjue?? Michango ikawa michango!!.

    “Mimi nitatoa turubai!!”

    “Mimi nitaleta kreti nne za bia”

    “Kuhusu Muziki niachieni mimi”

    “Nina kikundi changu cha mnanda nitakileta bure.”

    “Picha zote za mnato (still picture) nitapiga mimi”

    “Ukumbi nitapamba mimi.”

    “Fungate niachieni mimi nt’awapeleka Zanzibar”



    Haya yote yalikuwa maneno ya baadhi ya wadau waliojitolea kuidhami harusi hii!!

    Maajabu!! Kumbe Husna alikuwa anapendwa kiasi hiki!! Alishangaa mama yake.

    Si mama yake pekee hata wadau wengine walishangaa maana walidhani kuwa Husna alikuwa anachukiwa..lakini kinyume chake kikawa kuwa binti yule alikuwa anapendwa na hata waliomchukia hawakuwa wakimaanisha kutoka katika mioyo yao.



    Sasa shughuli ilibarikiwa kufanyika.

    Husna akapewa kitchen party!! Makubwa haya jamani!!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaungana akinamama wakongwe wakamfunza jinsi ya kuishi na mwanaume jinsi ya kuilinda ndoa yake…..



    Haya ile siku iliyokuwa inangojewa ikawadia!!! Ni wewe tu na macho yako!! Nani wa kukudai kiingilio?? Kama hukupata muda wa kwenda kushuhudia basi usinisumbue mimi niliyeenda!!

    Lakini kutokana na ukarimu wako. Na suikivu kaa kimya nikusimulie kile kilichotokea mitaa ya Kinondoni shamba.



    Siku hii maeneo ya Kinondoni jambo la kuvutia na kushangaza lilikuwa linasubiriwa, watu wengi walikuwa wamemiminika chini ya turubai, nyuso zao zilikuwa katika namna mbili, mshangao na furaha. Hakuna aliyekuwa anasikitika, hii ilimaanisha kuwa hapakuwa na msiba eneo lile bali jambo la furaha.

    ilikuwa ni harusi ambayo iliteka hisia za wengi, binti ambaye hawakutegemea kama atakuja kuolewa sasa ilikuwa siku yake ya kuitwa mke.

    Nyimbo za taarabu zilitawala eneo lile huku wanawake wakiwa wametingiana kanga zao zilizojaa vijembe, mara ‘utajiju’, ’umefulia mama’, ’sanamu la michelini’, ‘Choo cha kike’ ‘wa kuolewa utakuwa wewe’ na mengineyo ilimradi burudani. Ni maandishi yaliongea, kama hujui kusoma basi hii vita ilikuwa haikuhusu.

    Macho na masikio ya watu yalikuwa kwa watoto waliokuwa wanacheza kiduku na wengine walioimba kaswida kiustadi, mwenye kikundi cha mnanda aliendelea kuwatumbuiza wageni wasiokuwa rasmi na wale waliodhani kuwa wao ni rasmi katika shughuli hiyo.



    Katika kundi hilo kubwa lililokuwa limejumuika kufurahi ni mama mmoja tu aliyekuwa amenyong’onyea sana licha ya kwamba mtoto wake ndio alikuwa anaolewa lakini alijilazimisha kutabasamu,mama yake na Husna alikosa raha kwani hata siku moja hakuwahi kumuona mkwelima wake (Peter) mara zote aliishia kuonyeshwa picha hivyo hakuamini kama mtu huyo yupo duniani au ndio aibu za watu kudai michango yao waliyotoa kwa hali na mali kufanikisha sherehe hii.

    Alikuwa amejikunyata ndani ya vitenge vyake vya kupendeza akisubiri aibu itakayomkumba. Alikuwa kama aliyemwagiwa maji ya baridi!!!

    “Mama Husna mwanao amempata wapi yule kaka dah!! Pale kweli kala dume, ni mume wa ukweli ameng’ara kweli……” mama Husna aliambiwa na mwanaume aliyetoka kumpamba Peter.

    “Mh!! Wanajuana wenyewe mwanangu utawaweza vijana wa sasa????” Alijibu mama Husna kwa upole sana. Hakuwa na uhakika hata kidogo na mwanaye.



    Harufu kali ya pilau na mazagazaga mengine ilitawala eneo lote lile kwa uzuri kabisa, mchango ulikuwa ni mkubwa sana uliotolewa hivyo harusi ilifana sana, suala la chakula halikuwa tatizo hata kidogo, ratiba ilisomwa na bibi harusi alitakiwa kuingia ukumbini saa kumi adhuhuri akiongozana na bwana harusi kutokana na ratiba punde tu baada ya kufika wao ndipo chakula kingeanza kuliwa.

    Hadi kufikia saa tisa na nusu bado walikuwa hawajatokea wawili hawa wala wasindikizaji wao, ukumbi uliokuwa umejengwa kwa mabanzi imara ulikuwa umefurika, watu walikuwa bize kila mtu na lake kutokana na sekta waliyopangiwa na kamati husika.

    Hakika ilikuwa vyema na kupendeza kuitazama harusi hii. Kama uliikosa!!! Basi tusiulizane!! Au ngoja niendelee kukusimulia!!

    Muda ulizidi kusogea mbele na shamra shamra za kumsubiri bibi harusi na bwana harusi zilizidi kuongezeka, vigelegele miluzi na mbinja zilizidi kuvuma kwa fujo kila gari yoyote iliyoingia pale watu walidhani ndio wahusika wenyewe.

    Dakika zilizidi kusogea na hatimaye saa kumi ikawadia, watu walianza kulalamika chinichini kuwa walikuwa na njaa. Vile viduku vikaanza kufifia, mnanda ukalala, miduara ya taarabu ikapungua urefu.

    Kina mama wasema sana makoo yakawakauka, wakawa kimya. Kila mmoja analalamika njaa. Tena wale wasiochanga ndio walilalamika sana!! vituko!!

    Mateja nao waliojumuika pale kujipooza njaa zao waliponda sana utaratibu huo wa kucheleweshewa chakula. Ni kama vile walikuwa wamelipia huduma ile.

    Hakuwepo wa kujibu tuhuma hizi. Kila mmoja alikuwa anamrushia mzigo mwenzake, na aliyerushiwa mzigo naye hakudumu nao aliurusha kwa mwingine.



    Malalamiko haya yaligeuka maana yake baada ya nusu saa kila jicho liligeuka kujionea nini kinatokea meza ya wageni rasmi ilisimama pia lilikuwa jambo la kushangaza sana na kila mmoja hakulitegemea aina hiyo ya maharusi kuingia ukumbini hawakuwahi kuiona kamwe na ndio ilikuwa mara ya kwanza, ulikuwa msikemshike wa hali ya juu.

    Hali tete!! Nani hakutaka kuona mbele, kila mmoja kumsukuma mwenzake.

    Njaa zikasahaulika!! Ngoma za mnanda nazo zikaachwa katika upweke. Wale wacheza viduku wakasimama wima!!!!

    Fahari ya macho!!!

    Ilikuwa mshikemshike nguo kuchanika…….



    * * *



    Kilikuwa kikao cha dharula. Tena dharula kubwa.

    Wanajeshi wawili wenye vyeo tofauti vinavyotambuliwa na serikali za vichwa vyao walikuwa katika majadiliano ya dharula sana.

    Wanajeshi hawa walikuwa ni wa jinsia ya kike mmoja akiwa Bregedia Mwamvua na Luteni Husna. Nyota nyingi zilitawala mabega yao!!

    Walikuwa wanajadili juu ya vita iliyokuwa inaelekea mwishoni. Maadui wote walikuwa wameangamizwa. Adui moja ambae katika mazungumzo haya alitambuliwa kwa jina la uficho ‘Raisi”.

    Maajabu kumbe hawa wanajeshi walikuwa wanataka kumpindua Raisi. Na hatua waliyokuwa wamefikia ni kumteka. Tayari walikuwa wamefanikiwa!! Sasa hatua iliyofuata ni kuichukua nchi!!!

    Raisi huyu alikuwa wa nchi ya Kigogo. Raisi wa Kigogo!!! Peter Isuti mjukuu wa Mioyo.



    Brigedia Mwamvua aliongoza maongezi!!

    “Sikiliza Husna, huyu mtoto tukisema tu tumpeleke kwenye ndoa za serikali atatuzidi ujanja. Na atapata upenyo wa kutupiga bao.”

    “Kwa hiyo tunafanyaje sasa…” alihoji Husna.

    “Kule serikalini, mara wataomba vyeti vya kuzaliwa..we unacho sawa je Peter..”

    “Hata mimi sina shosti..” Aliingilia Husna. Mwamvua akaduwaa.

    “OK!! Sio mbaya sana….kwa namna yoyote serikali watataka kila mmoja aape kuwa hajalazimishwa katika ndoa hii..hapa napo tutaumbuka. Peter atakukana. Ubabe wake huwezi kuwaletea polisi watakuvunja miguu wewe.”

    Husna kimya!!!

    “Lakini bado hakijashindikana kitu!!!.”

    “Mh!! Shoga ujue kule nyumbani sherehe zimeanza..”

    “Najua ndio..sasa unataka twende kwenye sherehe ama…we vipi.” Aliwaka Mwamvua.

    Husna kimya!!!

    “Twende huku nishapata wazo!!! Mtoto mdogo kama yule ana nini mbele yangu..” alimaliza maongezi Mwamvua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ****



    Peter alibakia pale chumbani kwa muda mrefu kidogo hadi baadaye alipoingia msichana ambaye alimfahamu vizuri sana kwani ni mara nyingi sana aliweza kubambana naye kwenye matukio mbalimbali, alikuwa amelembwa sana lakini urembo haukuonekana kubadili hali yake. Binti yule alikuwa hajapendeza lakini kidogo alikuwa tofauti na aliyezoea kumuona.

    Aliingia pale ndani akiwa ameongozana na kundi la wasichana wawili waliokuwa na uzuri wa wastani, baada ya kumsalimia pale walimpiga maswali machache huku wakimuita shem yaani shemeji, alijua kwanini wanamuita shem ni kwa ajili ya uhusiano wake na Husna lakini ambacho hakujua ni kuwa Husna ni yupi kati ya wale wasichana.

    Labda Husna yupo nje?? Ama labda Husna ni rafiki yake huyu binti…..Mariam!! alikumbuka jina hilo liliwahi kutambulishwa mstarini siku binti huyo akiambatana na mama yake walileta malalamiko juu ya mimba. Na kweli alikiona kitumbo kikiwa kimevimba. Hakika alikuwa na mimba…..

    Ni siku hiyo walipomwachia namba ya Husna.

    Inamaana inamaana!!!...aliduwaa Peter. Kwa mbali akahisi kutetemeka.

    Baada ya kama nusu saa wasichana wawili waliaga na kumwacha mmoja ambaye tangu waingie pale ndani hakuwa ameongea neno lolote, Peter hakutaka jambo linaloitwa kwamba yule ndio Husna litokee hapana hakuwa tayari kuwa katika mahusiano na binti yule hata kuwa naye chumba kimoja aliona sio sawa.

    Kashkashi zake alizifahamu fika na kitendo cha kuthubutu kukwaruzana naye kingeweza kuleta matatizo.

    “Peter……” alijikakamua yule msichana na kuzungumza, sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwa Peter, hakika yule alikuwa ni Husna, lakini Peter alidhani amefananisha.

    “Umenijuaje” aliuliza Peter kwa uoga.

    “Mimi ni mkeo Husna kwa nini nisikujue!!!!!” alijibu Husna kwa jeuri. Peter alibaki anamshangaa binti yule alidhani anatania lakini hapakuwa na utani yule ndio alikuwa Husna halisi. Peter alitamani kupitia ukutani lakini hizo zilikuwa ni ndoto tu isingewezekana.

    Peter aliamua kupambana aweze kutoka pale ndani lakini alitua katika mikono kakamavu ya Husna.

    “Unataka kukimbilia wapi?” aliulizwa huku akiwa ameunganishwa mikono yake miwili vyema kabisa.

    Peter akathubutu kujitoa kwa nguvu.

    Husna alikuwa makini akarusha kofi moja likampata Peter usoni barabara…..akayumbayumba.

    Hapa akaiukumbuka ile picha ya yule kondakta aliyepigwa na huyu huyu Husna hadi akaanguka chini.

    Peter akatamani kupiga mayowe ya kuomba msaada….

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***HAYA SASA….PETER mikononi mwa HUSNA ORIJINOOOOO….

    ***Wapo chumbani….PETER amejaribu kukurukakara..amejikuta mikononi mwa HUSNA…….Bingwa wa mapambano ya ana kwa ana….



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog