Simulizi : Usinibanie
Sehemu Ya Pili (2)
HASIRA zilinipanda kichwani nikajiona nadhalilika mwanamume mimi, niliona wazi kuwa nakosewa adabu. "Nimchape vibao nini?" Nilijikuta nikiwaza kwa haraka haraka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bahati nzuri akaingia mmojawapo wa watumishi wa mule ndani,
cha kushangaza Tausi hakuufurahia ujio ule. Akamdakia,
"sihitaji usumbufu, nina shauri muhimu na Hoza. Waambie na
wenzio!"
Yule mtumishi akatoka harakaharaka na kuishia zake
nje. Nikashusha pumzi ndefu kisha nikatulia kwa muda ili kuipa
nafasi hekima ichukue mkondo wake. Akili ilipotulia
nikamjibu. "Mimi sio mtunzi wa mashairi, huwa naandika
kilichopo moyoni wangu. Samahani kama nimekukwaza" nilimjibu kwa upole lakini kwa chuki kubwa.
Niliojiona nimedharaulika sana mwanamume mimi, lakini Tausi
hakuonyesha kujali kabisa. "Unaweza kuniambia
uliyemwandikia?" aliniuliza akiniangalia usoni.
Mapigo ya moyo yalibadilika ghafla. Laiti kama angetokea
daktari pale na kunipima presha, kwa hakika ningepelekwa
wodi ya wagonjwa mahututi kwa jinsi mapigo hayo
yalivyoongezeka.
Huyu mtoto sijui vipi? Anaongea na mwanamume akimtazama
usoni. Sijui kaitowa wapi tabia hii, ila kwa mimi
sikumshangaa kutokana na kusafiri nchi kadhaa. Ni tabia za
kizungu!
Nilishusha pumzi ndefu nikamkazia macho na kumjibu kwa upole lakini kwa kujiamini. "Sidhani kama itasaidia nikikwambia Tausi, niliyemwandikia ameshayasoma na anajijua ila sitamruhusu anijibu kwa maneno kwa kuwa hataweza
kunitamkia!"
Mchezo ukageuka ghafla, nikamwona Tausi anapoteza ujasiri
wake. Macho yake yalianza kubadilika rangi na kuwa mekundu
yakifunikwa na utando wa machozi. Nikaacha kumtazama kwa
kuwa alishindwa kuendelea kuangaliana na mimi wakati
nilitaka aniangalie nikimpa vidonge vyake.
Nikaendelea kumwambia "Nahisi ana mwingine ampendaye, moyo unaniuma lakini nafurahi kwa kuwa ameshazijua hisia zangu kwake. Mara zote nikimwangalia, natamani nimkumbatie lakini sidhani kama nitakuja kupata ruhusa yake!" .
Tausi akanikatisha "Nenda tafadhali Hoza, naomba uniache
nipumzike."
Kwa sauti aliyoitoa nilijihisi mwili unasisimkwa
na kupoteza ujasiri wake. Nikamwangalia usoni, hakuwa akionyesha kuwa ananiambia niondoke kwa nia mbaya, ila maneno yangu yalikuwa yakimchoma. Akageuka na kuanza kuondoka akiniacha nimesimama.
Nilijikaza mtoto wa kiume nikamuita. "Tausi!"
Akasimama bila kunigeukia, "unasemaje?"
"Nahitaji bado kuongea na wewe, ukipata muda naomba unifikirie!"
Tausi akageuka kuniangalia. Akasimama kwa muda akinitumbulia macho. Baada ya kimya kifupi, mrembo Tausi alishusha pumzi ndefu akaniuliza kwa sauti yake laini. "Huogopi?"
"Naamini sifanyi kosa, sidhani kama natakiwa kuogopa!"
nilimjibu kwa kujiamini.
Tausi alitabasamu, kisha akageuka na kunijibu akiwa
anaondoka. "Nishakuelewa unachotaka kuniambia."
Akaishia na kuniacha nimesimama kama sanamu ya kwenye duka la nguo kasoro sikutoa pozi. Mwanamume nikatoka taratiiibu nikiwapita watumishi na wambeya
wengine waliokuwa wakisubiri nje ili waniulize kuwa
nimeitiwa nini na Tausi.
Kweli watu wanapenda wenzao wakipatwa na matatizo,
walifurahi sana nilipowaambia kuwa niliitwa kusemwa kutokana
na kuchelewa kufanya usafi.
Nilipotoka pale nikaanza kufanya usafi haraka haraka, kisha
nikarudi kibandani kwangu na kujifungia ili nipate
kuutafakari mwenendo mzima wa maongezi yangu na Tausi.
Nilihisi mambo kama vile yameharibika, mara nyingi msichana
akishajua kama umemzimia inakuwa ngumu sana kumnasa kama yeye hakutaki. Nilijiona kuwa natakiwa kufanya uamuzi wa hatari sana na wa haraka, nilijua wazi kuwa Tausi hawezi
kuamua kunikubali hata kama ananipenda kutokana na hali
yangu.
Inabidi nifosi goli! Hakika Tausi alikuwa ameanza kuuogopa
ujasiri wangu, nilimuona kuwa katikisika hivyo sikutaka
kumpa nafasi ya kuutafuta tena ujasiri wake ulioyeyuka.
Usiku ulivyoingia, nilienda moja kwa moja hadi dirishani
kwake na karatasi langu mkononi, wakati huo hakuwa ameingia
chumbani kwake, nikampenyezea. Karatasi hiyo niliiandika
hivi....
‘Nitaingia humu chumbani usiku sana tupige stori’
Karatasi lile lilipeperukia pembeni kidogo ya kitanda,
karibu na dirishani. Nilitulia pale nikisubiri kumwona
atalichukuliaje suala lile.
Tausi alipoingia chumbani, akalikuta lile karatasi. Moja kwa
moja akaliendea na kuliokota, akawa analisoma. Nilimuona
akiwa na hofu kubwa akiangaza angaza huku na kule ili ajue
karatasi lile limeingiaje mule ndani.
Alikuja hadi dirishani, nikainama chini ili asinione.
Akaanza kulikagua, alijisahau kuwa dirisha la kuzuia mbu
halikuwa limefungwa vizuri nami nilitumia upenyo huo
kupenyeza lile karatasi kisha nikalifunga.
Baada ya kushindwa kujua karatasi lile limeingiaje akabaki
pale kitandani akiwaza. Sikujua alikuwa akiwaza nini.
Nilikuwa nataka kuusoma mwenendo wake, kama angetoa taarifa kwa walinzi au angeuchuna.
Kuuchuna kwake kulimaanisha kuwa yuko tayari kuhifadhi siri.
Lakini vile vile yawezekana kuwa amekaa kimya kwa kujua
kwamba sina uwezo wa kufanya nilichoandika.
Ilipofika saa nane kasoro, myumba yote ilikuwa kimya. Ni
mbwa na walinzi tu waliokuwa wakiranda randa. Inaelekea hata
wale mbwa walikuwa wananishangaa kutokana na mizunguko yangu ya usiku kwa usiku, wangekuwa binadamu wamgeshatoa umbeya.
Sijui mapenzi yana nini? Nilikuwa na ujasiri wa ajabu kuweza
kufikiria kufanya lile nililokusudia. Nilimchungulia Tausi,
hakuwa amelala. Ananisubiri? Mwanaume nikaanza kunyata
nikiizunguka nyumba, nikaliendea bomba linalopandisha maji
kwenye tenki.
Nikaanza kulikwea taratibu hadi juu. Juu ya nyumba ya Mzee
Nurdin kuna sehemu ya kupumzikia, pia kuna mlango ambao
nilipoufungua kitasa chake kwa kutumia waya nilikutana na
sehemu yenye gazi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliteremka na ngazi taratibu nikatokea kwenye chumba kimoja
chenye giza nene. Nilitulia kwanza ili macho yangu yazoee
lile giza. Japo nilikuwa nina tochi ndogo, lakini huwezi
kuwasha katika mazingira yale.
Macho yalipolizoea giza, niliona sehemu ulipo mlango mdogo.
Nikanyata kuulekea huo mlango, nilipotoka nikakutana na
korido ndefu ambapo mbele yake kulikuwa na mlango mkubwa
sana. Hakukuwa na mlango mwingine wowote ulioonekana katika mwanga ule hafifu.
Nilipotazama kwa makini niliona dalili za kuwepo mlango
mwingine mdogo mita chache kutoka pale niliposimama.
Nikatabasamu! "Huyu mzee ni mjanja sana!" nilijisemea
moyoni.Unajua katika mazingira ya kawaida ukitokea tu lazima
mawazo yote yatakuwa kwenye mlango ule mkubwa na ndipo huwa kunawekwa ulinzi mkubwa.
Nilicheza na kitasa cha kale kamlango nikaufungua,
nikatokeza kwenye kikorido kifupi chenye milango minne
tofauti. Nikajua ni vyumba vya kulala. Nilianza kupiga
hesabu kutokana na madirisha yalivyokaa kwa nje nikakihisi
chumba cha Tausi. Nikaanza kutembea nikinyata kuuelekea
mlango niliouhisi kuwa ni wa chumba cha Tausi.
Hapo sasa ndio akili ikaanza kunirudia. Wasiwasi ulinijaa,
jasho jembamba likaanza kunitoka lakini nikajipa moyo kuwa
hata nikishtukiwa poa tu, nitamwambia mkuu kuwa nilikuwa
naichunguza ile nyumba.
Nilipougusa mlango wa Tausi, nikagundua kuwa uko wazi.
Nikausukuma polepole na kuchungulia, Tausi alikuwa amepitiwa na usingizi akiwa kakaa kwenye kitanda huku amejiegemeza ukutani. Niliingia taratibu na kujiegemeza pembeni ya mlango nikimwangalia.
Mapigo ya moyo wangu yalienda kwa kasi ya ajabu, nilikuwa
sijui nifanyeje. Kwa akili ya haraka haraka nilijua kuwa
endapo angeshtuka, cha kwanza angepiga kelele. Nikajivua
kamba ya urembo ambayo nilikuwa napenda kuivaa mkononi,
nikaidondosha chini kisha nikaondoka.
Ilipofika asubuhi niliendelea na taratibu zangu kama
kawaida. Nilifanya kama vile hakikutokea kitu usiku wake.
Nilipomaliza usafi nikakaa kwenye eneo langu la kujidai na
paka wa Tausi. Kila nilipochungulia pale dirishani kwenye
eneo la Tausi, sikumuoana Tausi.
Nilianza kuingiwa na wasiwasi. Baada ya muda kidogo
nilimuona Tausi akiwa anajongea mbele yangu. Niliingiwa na
hofu sana lakini nilijikaza kwa kutabasamu ili kuficha hofu
niliyokuwa nayo. "Hivi wewe Hoza, una akili kweli?"
Alinianza kwa swali la kebehi.
"Sina akili hata moja Tausi," nilimjibu bila kusita hata
nukta. Tausi alikaa kimya kwa muda kabla ya kutoa kicheko
kilichoambatana na mhemo.
"Ulimtuma nani kuleta hii kamba yako?"
"Niliileta mwenyewe!"
"Thubutuuu!" Tausi alisema huku akicheka kwa kebehi
akinirushia kamba yangu. Niliiona kama bahati ya mtende,
nikamwambia kuwa kama anabisha aende nayo, usiku nitaifuata
kama nilivyoileta. Naye eti akakubali, sasa sijui nae
alikuwa na hamu tuonane usiku au alikuwa anabisha kiukweli
ukweli.
Malaika ’mzima jua’ akafanya kazi yake, giza likatawala
katika uso wa dunia na watu katika himaya ya Mzee Nurdin
wakawa wamelala. Kitu ambacho nilikuwa nimekigundua wakati nikiongea na Tausi asubuhi ni kwamba alikuwa ameondoka kabisa ile hali ya kuwa mimi ni mfagizi wao. Alikuwa akinichukulia kama mwanamume anayemfukuzia.
Jambo hilo lilinipa mzuka sana, nikajiona nimepiga hatua kubwa sana kuelekea kumpata Tausi.
Usiku ulipoingia, mwanamume nikapitia njia yangu ile ile.
Ila kabla sijaianza safari yangu nilimchungulia Tausi
nikamkuta yuko macho anasubiri aone ’uongo wangu’.
Nilipofika mlangoni, sikuhangaika na kuufungua mlango wake,
niligonga taratibu. Mlango ukafunguliwa, tukakutana uso kwa
uso na Tausi. Tausi hakuweza kuuficha mshangao wake, nami
nilijihisi kuwa mzunguko wa damu umeongezeka kasi mara dufu.
Tukabaki tunatazamana kwa muda.
Ghalfa akili ikamrudia Tausi akanivutia kwa nguvu ndani.
"Una hatari sana wewe! Umeingiaje?" Nilikuwa natabasamu tu
nikimuangalia Tausi. Alikuwa kavalia suruari ya kulalia na
shati lake vilivyomkaa sawa sawa. Nikamuuliza kimoyomoyo,
"Mbona hujanivalia lile gauni lako la hudhurungi
linaloonyesha yaliyomo?"
Tausi alibaki kimya akinishangaa, nami nilibaki nikimtazama
usoni. Nadhani alishangaa nilivyovaa, nilivaa suruali ya
’traksuti’ nyeupe, juu nilivaa fulana nyepesi nyeupe ya
mikono mirefu ambayo ilionyesha mabonde na milima ya mwili
wangu.
Nilikuwa msafi haswa tena wa kukaribishwa kitandani.
Tulikaa kimya kwa muda tukitazamana, sio yeye wala mimi
ambaye alipata kauli ya kutamka. Taratibu tabasamu lilianza
kutoweka usoni kwa Tausi, nami nikafunika meno yangu
yaliyopangana mithili ya punje za mahindi.
Nilishusha macho yangu kuitazama midomo yake nikahisi kuwa
inahitaji kitu fulani. Nikasogea hatua moja mbele, tukawa
tunatazamana kwa ukaribu sana. Nikaupeleka mkono wangu
kumshika shavuni, nikimpapasa. Midomo yetu ikakutana kisha
ndimi zikasabahiana.
Niliuzungusha mkono wangu kiunoni kwake, nikauhisi mwili
wake ukitetemeka, ukivaibreti kama uliopigwa na shoti ya
umeme. Miili yetu ilikuwa ikibadilishana joto na kuifanya
akili yangu ishindwe kufikiri wala kuiona hatari ya mimi
kuwa mule ndani usiku ule.
Ghafla Tausi akanisukuma na kujitoa kwenye mikono yangu,
alibaki akinitazama huku anatweta. Akaniambia kwa sauti
laini iliyojaa mihemo. "Ondoka Hoza!"
Nilimwangalia kwa sekunde kadhaa, kisha nikageuka na kuanza
kuondoka. Tausi akanishika bega nikageuka na kumwangalia.
"Umekasirika?"
Sikumjibu kitu, nilibaki nikimwangalia tu kwa
upole, akanivuta na kunipiga busu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nami sikufanya ajizi nikampelekea, tena zima-zima. Baada ya
muda tukawa tunatazamana. "Ahsante kwa busu lako, mimi
naenda!" Nilimwambia Tausi nikigeuza na kuanza kuondoka.
Wakati navuka mlango nikamsikia akisema kwa sauti ya
kunong’ona "I love you." Nikarudi ndani. "Unasema?" Akabaki
akiniangalia huku akitabasamu. "Toka hapa! Kama hujasikia
basi!" Nilicheka kidogo na kutoka kupitia njia yangu ile
ile.
*********
Naukumbuka usiku ule, kwa kweli sikupata usingizi wa moja
kwa moja. Na hata nilipopata usingizi ndoto zilikuwa ni
kuhusu mabusu ya Tausi tu.
Najua unaweza kuniona bwege kwa kutofanya kweli katika usiku ule, lakini ngoja nikudokolee siri za wanawake hasa warembo kama Tausi.
Hutakiwi kuwa na papara, kuuteka moyo wa Tausi ni kitu
kikubwa kuliko kufanya nae mapenzi. Wanaume wengi hudhania kufanya mapenzi ndiyo uhakika kuwa unapendwa. Mtachekwa!
Siku iliyofuatia Mzee Nurdin, baba yake Tausi alirejea toka
safari yake akiwa na msafara wake kamili. Ulinzi
uliimarishwa mara dufu na sheria zikaanza kuzingatiwa,
ilikuwa ngumu sana.
Zilipita siku kadhaa bila ya mimi kumuona Tausi, moyo wangu uliniuma sana.Nilihisi kuwa hata yeye alikuwa na wakati mgumu kama mimi.
Mawazo kuhusu kazi iliyonipeleka pale hayakuweza kabisa
kuitoa akili yangu katika fikra juu ya Tausi. Nikaanza na
kuingiwa na woga wa kuharibu kazi, nikakumbuka mambo ya
Ngoswe katika kitabu cha ’Penzi Kitovu cha Uzembe’.
Lakini nilijipa moyo kutokana na uwezo wangu mkubwa wa
kuutumia upungufu wangu kama njia ya kupatia ushindi. Kila
mpango nilioupanga sikuona kama ungeleta manufaa au katika
kazi yangu ya kumpeleleza Mzee Nurdin ama katika kumsogeza
karibu tabibu wa moyo wangu, Tausi.
Siku moja baada ya kufikiria kwa kina, nikaamua kufanya
jambo la hatari, nikaamua kuwa liwalo na liwe. Lazima
nionane na Tausi! Siku hiyo niliamua kuwa katika hali ya
kivita haswa, nilivaa pajama jeusi, fulana nyeusi na raba
nyeusi.
Niliamua kuwa mtu wa gizani. Niliamua pia kuifanya
safari hiyo mapema sana mara baada ya giza kuingia.
Nilitembea taratibu kuielekea njia yangu ya kuingilia ndani
kwa Mzee Nurdin.
Nilipanda taratibu kwenye bomba kuelekea
juu. Nilipofika tu juu nikashtushwa na sauti ya miguu
inayotembea, nikatulia na kuangaza katika giza lile.
Nilimuona mlinzi mmoja akirandaranda huku mkononi amekamata bunduki.
Nikatulia kwanza!
Yule mlinzi alizunguka zunguka kisha akawa anaelekea kwa mbele ya sehemu ile ya kupumzikia ambayo ukisimama unaona hadi getini, akawa kanipa mgongo.
Nilinyata kwa haraka hadi kwenye kigeti cha kuingilia ndani,
nikakuta kimeegeshwa tu. Nikakifungua taratibu na kuanza
kushusha ngazi kwa tahadhari kubwa. Sikufika moja kwa moja
kwenye kale kachumba ka giza, niliishia kwenye gazi nikawa
nakikagua kwa macho kwa kukichungulia. Nikakiona kuwa ni
kitupu. Nikasimama kulitazama lango kubwa, safari hii
lilikuwa wazi.
Nilimuona mlinzi mmoja akiwa kasimama sambamba na ukuta
karibu na lango lile. Pia kutoka pale niliweza kuwaona
watumishi wa ndani wakizunguka huku na kule. Nikabaki
nikipiga hesabu za kuweza kuufikia ule mlango mdogo ambao
huwa ninapitia. Tena kuufikia bila ya kuonekana na yule
mlinzi na watumishi.
Kwa kuangalia zile pilika pilika za watumishi nikajua kuwa
yalikuwa ni maandalizi ya chakula cha jioni, kwa hiyo nikawa
nasubiri kuwaona Mzee Nurdin na familia yake wakipita. Baada
ya muda pilika zilitulia, nikamuona Tausi akipita.
Nilijikuta nikitabasamu! Kisha mama yake na Mzee Nurdin nao
wakipita.
Macho ya mlinzi yalikuwa yakiwasindikiza, nikapita haraka kuuendea mlango wangu. Kuugusa ukawa umefungwa!
Nikarudi spidi na kujituliza pale gizani nikitafakari cha kufanya.
Akili moja iliniambia nirudi, nyingine iliniambia nisonge
mbele.
Wakati nimekaa nafikiria cha kufanya, niliuhisi ubaridi
fulani kwenye ule ukuta niliouegemea ambao ni tofauti na
ubaridi wa ukuta wa kawaida. Nikajaribu kuugonga-gonga.
Ulikuwa ni ukuta wa chuma!
Nikatoa tochi ndogo yenye mwanga hafifu na kuanza kuukagua
ukuta ule wa chuma. Nikaviona vitufe kadhaa kama vya lifti
za kwenye majengo marefu. Baada ya kuvisoma kwa muda
nikagundua kuwa ule ni mlango, nikajawa na shauku ya kuujua
ni mlango wa kuelekea wapi?
Nikabonyeza kitufe cha kufungulia, lango likafunguka. Mbele
kulikuwa na ngazi kadhaa, nikashuka taratibu kuzifuata hizo
ngazi. Chini nikakutana na korido ndefu sana, nikatulia kwa
muda ili kuona kama kuna harakati zozote. Kulikuwa kimya
mno!
Nikaanza kutembea kuifuata ile korido kwa uangalifu. Baada
ya kutembea kwa takribani dakika tano nikatokea kwenye
chumba chenye milango mitatu tofauti. Mmoja ulikuwa ni
mkubwa, miwili ilikuwa ni midogo.
Nikaanza kuvichunguza vitasa, nikauhisi mlango mmojawapo
kati ya ile midogo miwili una hadhi ya juu na haufunguliwi
mara kwa mara. Nikauchagua huo, nikaukorokochoa na funguo
zangu malaya, ukafunguka. Nikaingia kwa tahadhari kubwa,
nikakutana na ngazi zinazopandisha juu ambako nilikikuta
choo.
Kilionekana kuwa ni choo cha mtu binafsi, na kilikuwa
kimefungwa kwa ndani. Nikakifungua na kutoka nje, nikakutana
na sebule kubwa ya kifahari. Kwa kuiangalia haraka haraka
ile sebule haikuwa ngeni kwangu! Nikaanza kuvuta kumbukumbu.
Jibu nililolipata sikuweza kuliamini, ni ofisini kwa Mzee
Nurdin! Sikuamini kwa sababu kutoka ofisini kwa Mzee Nurdin hadi nyumbani kwake ni mwendo wa zaidi ya robo saa kwa gari!
Inakuwaje? Nilianza kuikagua taratibu sebule ile kwa macho,
nikahakikisha kuwa ndio yenyewe. Nikaanza kufanya upekuzi wa nyaraka mbalimbali pale sebuleni na ndani ya ofisi yake.
Nilitoa kopi nyaraka kadhaa ambazo nilidhani kuwa
zingenisaidia kwa upelelezi wangu, pia nilinyonya mafaili
kadhaa toka kwenye kompyuta yake baada ya kufanikiwa
kuzibomoa namba zake za siri. Nikayaweka kwenye flash diski
yangu.
Wakati najiandaa kuondoka nilipata wazo ambalo lilinifanya
niingiwe na hofu kwa sekunde kadhaa. Nikaangaza kona zote za
ofisi ile, nikakikuta nilichokitarajia. Kamera! Mambo yote
niliyokuwa nikiyafanya yalikuwa yakirekodiwa na kamera ile!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilifikiria njia ya kufanya bila jibu.
Niliwaza kama kuna watu walikuwa wanafuatilia ina maana hadi pale nilishajulikana na sikuwa na ujanja wa kufanya lolote!
Akili ikaanza kuzunguka nikipanga na kupangua namna ya
kujinasua bila kuharibu uwepo wangu pale nyumbani kwa Mzee
Nurdin.
Nilijua nikiharibu tu na Tausi nimemkosa. Nikaanza kukosa
raha. Nilishusha pumzi ndefu, nilipopata wazo. Nikarudi
kwenye kompyuta za ofisini kwa Mzee Nurdin, nikaanza
kuifungua moja baada ya nyingine.
Hatimaye, nilifanikiwa kupata inayohifadhi rekodi
zinazochukuliwa na zile kamera za ulinzi. Nikaipapachua na
kukitoa kisehemu cha kuhifadhia kumbukumbu kisha nikaizima.
Niliporidhika kuwa kila kitu kiko sawa nikaanza safari yangu
ya kurudi huku nikiwa na mawazo mawili mawili, nipite kwa
Tausi ama la! Nilifanikiwa kurudi hadi kwenye kale ka chumba
ka giza, nilibaki pale nikipiga hesabu za kutoka.
Kutokana na vitu nilivyobeba haikuwa busara kwenda kwa
Tausi. Tatizo kubwa alikuwa yule mlinzi mwenye bunduki
anayelinda sehemu ya kupumzikia iliyo juu ya nyumba ya Mzee
Nurdin.
Nilikuwa najaribu kupiga hesabu ili kwa vyovyote ilivyo
niepuke mapambano, japo najiamini kwa ufiti nilionao haikuwa
ni jambo jema kutoa ujumbe kuwa umetokea uvamizi.
Nilianza kunyata taratibu nikizipanda ngazi za kuelekea juu,
hadi nilipolikaribia geti. Nikamuona yule mlinzi ametulia
katikati ya geti. Nikakaa pale ngazini nikimkodolea macho
yule mlinzi mnoko ambaye hakuwa na dalili yeyote ya kuondoka getini.
Zilipita takribani saa mbili ndipo mlinzi yule alipotoka
pale getini kufanya mzunguko mdogo. Nikaitumia fursa hiyo
kutoka kwa haraka ila kwa tahadhari kubwa. Nikatembea na
ukuta, nikalidandia bomba na kuseleleka kushuka chini bila
kufanya kelele.
Nikanyata na kurudi kwenye kibanda changu nnachoishi.
Nilikuwa nimepiga hatua moja kubwa sana! Nilitumia usiku ule
kuzipitia nyaraka zote nilizozitoa kopi kule ofisini kwa
Mzee Nurdin, nilivinakili vitu muhimu nilivyovitaka kisha
makaratasi yale nikayaweka kwenye sufuria ndogo na
kuyaunguza.
Nilibaki na flash diski na kile kiboksi cha kuhifadhia
kumbukumbu cha kwenye kompyuta. Inabidi hivi vifike kwa
mkuu!
Siku iliyofuatia kulikuwa na pilika zisizo za kawaida hivyo
kila mtu akawa anajiuliza kuwa ni nini kimetokea ila jioni
yake tukapata taarifa kuwa wasaidizi wa Mzee Nurdin
wanashikiliwa na polisi.
Wakati kila mtu akitafakari kuhusu mambo yale, ilikuja gari
la polisi, tukakusanywa wafanyakazi wote kasoro walinzi.
Akilini nilijua kuwa ni nini kinaendelea. Tukapelekwa hadi
kituo cha polisi ambacho sijawahi kukijua kabla kwa
mahojiano, akawa anachukuliwa mmoja mmoja.
Ilipofika zamu yangu kupelekwa nilishangaa kujikuta uso kwa
uso na chumba kitupu. Wakati nashangaa akatokea mkuu, nyuma yangu. "Umepata nini?"
Mara moja niliitambua sauti yake, wakati huo alikuwa
akielekea kukaa kwenye kiti kilicho mbele yangu. Nikampa
taarifa zote. Nikamwelekeza nilipoficha flash diski na kile
kiboksi cha kompyuta.
"Sasa nimeanza kupata picha, nilishangaa kwa biashara
anayoifanya anawezaje kupata fedha nyingi za kufadhili
shughuli za chama," alisema mkuu akizunguka-zunguka kwenye
kiti.
Pia alinidokeza kuwa wale waliokuja kutuchukua hawakuwa
askari wa kawaida na pale ni kituo bandia cha polisi ambacho
huwa wanakitumia kwa operesheni kama hizo. Nikarudishwa kwa wenzangu ambako kila mtu alikuwa akilalamika kivyake.
Biashara kubwa alizokuwa akizifanya Mzee Nurdin za magendo, kusafirisha nyara za serikali na mbaya zaidi kusafirisha watoto nje ya nchi. Ila kwa watu alikuwa akijulikana kama mfanyabiashara wa mazao ya kilimo akimiliki pia viwanda vya usindikaji.
Ila taarifa iliyomwacha hoi zaidi mkuu ni ile kwamba kuna
watu wazito katika taasisi nyeti ambao wako katika orodha ya
malipo ya Mzee Nurdin. Kuna maofisa wakubwa katika jeshi,
idara ya usalama wa taifa, mahakama, polisi, ikulu, ndani ya
chama tawala na ofisi ya bunge. Hao wote hutumika kumlinda
na kumfikishia taarifa zote muhimu.
Tuliachwa pale kituoni na mapolisi feki kadhaa.
Tukasikia
mlio wa gari linaloondoka, nikajua kuwa wanafuata vitu
nilivyowaelekeza. Kichekesho alikuwa yule bosi wangu mnoko,
toka tukamatwe ye alikuwa analia tu akilalama. Eti hastahili
kukamatwa kwa kuwa yeye ni mtumishi mtiifu wa Mzee Nurdin.
Tuliachiwa kesho yake alfajiri kwa kurudishwa na lile lile
gari. Wakati tunashushwa pale nje kwa Mzee Nurdin, nilimuona
Tausi amesimama akituangalia.
Uso wake ulikuwa umejaa huzuni kubwa, ila sikutaka hata
kumtazama. Niliinama chini na moja kwa moja niliongozea
kibandani kwangu ambako sikukuta chochote kati ya vile vitu
nilivyowaelekeza. Nikajua kazi imefanyika!
Pamoja na kufurahia kuwa nimefanikisha jambo kubwa sana,
upande mwingine nilikuwa nasononeka kwa kuwa mazingira ya
kumbinjukia Tausi yangekuwa ni magumu sana. Sio kwamba
ningeshindwa kubinjuka, bali endapo ingetokea kugundulika
mchezo wangu basi mzigo wote wa yaliyotokea ungekuwa ni juu
yangu. Nifanyeje?
Siku moja wakati nimekaa kwenye eneo langu la kazi,
nikamuona Tausi amekaa sehemu ile aliyokuwa akutumia
kunichungulia. Tukakutanisha macho. Akafungua dirisha na
kutupa kifurushi kidogo, aliniangalia kwa muda kisha
akaondoka pale dirishani. Nilienda kwa kasi hadi pale
dirishani, nikakiokota na kukifungua. Ilikuwa ni simu ya
Nokia 3310, maarufu kama nokia ya jeneza.
Ilikuwa na chaja yake na tayari ndani kulikuwa na laini na
salio la kutosha. Lilikuwa limehifadhiwa jina moja tu,
’Ndege’ alikuwa akitania kutokana na jina nililompa katika
shairi langu nililomwandikia siku ile. Kwa shauku nikaanza
kuipiga namba hiyo ya ’Ndege’ simu iliita hadi ikakatika.
Ghafla akapiga yeye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Inaelekea una kiu sana, hata dakika haijapita?" Nilijikuta
nikiishia kucheka tu nikishindwa kutoa jibu ila nilifurahi
kupita kiasi. Tulianza kuwasiliana karibu kila dakika labda
kwa kupiga au kwa ujumbe mfupi, ila tuliboresha sana
uhusiano wetu.
Nikaanza kujihisi nahitaji penzi la Tausi, nilihisi kuwa
naye ana haja hiyo. Ila niliogopa msemo wa ’mvumilia mbivu
hula mbovu’. Nikaanza chombeza chombeza, naye akielekea
kibra!
"Lini utanipa penzi Tausi?" nilijikuta nikiulizia. Tausi
alicheka sana hadi nikajihisi nimechemka kumuuliza swali
hilo. Nikawa mpole, tena mdogo kuliko kidonge cha piriton.
Siku nzima nilikosa raha kutokana na kitendo kile cha
kikatili alichonifanyia Tausi binti Nurdin, nilijihisi kama
nimeachwa bila nguo.
Niliamua kuizima simu ili nipate muda muafaka wa kufikiria
nini cha kufanya, kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kujiona
mjinga, ilibidi nijipe nafasi ya kujitia ujasiri.
Usiku uliingia bila kuwasiliana tena na Tausi, nikalala
kinyonge nikijikunyata kama kinda la njiwa. Nilikuwa Musa
Njiwa hasa, Musa mtoto wa Njiwa. Nikawazia kuwa ni kweli
majina huwa yanajidhihirisha.
Asubuhi ya siku iliyofuatia, nilijidamka asubuhi sana
nikazifanya kazi zangu zote na kurudi katika kibanda changu
na kurudi kulala.
Ilipofika saa nne asubuhi, mlango wangu uligongwa.
Nikakurupuka kwenda kuufungua, nikakiona nilichokitegemea,
kiongozi wangu wa kazi. "Twende kuna kazi, unalala lala
sana. Mzembe sana wewe" alianza kubwabwaja bila breki.
Niliamua kukaa kimya bila kumjibu chochote kwa maana maneno
yote yaliyokuwa karibu na mdomo wangu ni matusi matupu, huku
moyo wangu ukiwa umejaa chuki. "Ipo siku yake tu ataingia
kwenye anga zangu" nilijisemea moyoni.
Wakati najifikiria jamaa likawa linaendelea na mineno yake
ya kukera, nilichokifanya nikurudi ndani na kuvaa raba
zangu. Nikatoka na kumfuata kwa nyuma kwa kuwa muda wote
alikuwa mlangoni akinisubiri utafikiri askari anayemsubiria
mfungwa atoke mahabusu.
Tuliongozana mkukumkuku akinipeleka hadi kwenye lango la
nyumba kubwa. Tausi alikuwa amesimama akiwa katika hali ya
kutoka, pembeni yake amesimama binti mmoja mtumishi wa mle
ndani.
"Utampeleka bosi kufanya manunuzi yake, huko acha uvivu
uvivu wako" lile jamaa liliendeleza gubu. Nilimwangalia kwa
jicho kali huku nikishusha pumzi ndefu, jamaa linanitoa
nishai mbele ya mtoto bwana?
Tausi alitangulia kwenye gari bila kunisemesha akifuatiwa
kwa nyuma na yule mtumishi. Wakati huo dereva alikuwa
ameshawasha gari. "Kanichunia nini?" Nilijiwazia huku
nikilijongelea gari na kuingia.
Safari ilianza taratibu kila mtu akiwa kimya, hakuna
aliyekuwa na la kumwambia mwenzake japo tumetoka nyumba moja ukiondoa mawasiliano ya siri kati yangu na Tausi hakuna
aliyekuwa na mazoea na mwenzake zaidi ya kuonana kwa juu
juu.
Tausi alikuwa kimya akiangalia mbele bila kusema neno wala
kumwangalia yeyote kati yetu, na kwa jinsi ilivyokuwa
ilionekana kuwa dereva alikuwa na ratiba kamili ya safari.
Tulipita katika maduka mbalimbali lakini yote aliteremka
Tausi na yule binti mtumishi. Mara ya kwanza nilitaka
kuteremka akanizuia kwa kuniambia kuwa akihitaji niteremke
ataniambia.
Nilihisi ananinyanyasa kisaikolojia, ila kilichonikera zaidi
ni kitendo cha yule dereva kunicheka kwa kuniona kuwa mimi
ni kimbelembele.
Nilitamani kumtukana kwa kuwa ndio lugha inayonipunguziaga
hasira. Tukahama toka Posta, tukaelekea maeneo Mnazi Mmoja.
Gari likaegeshwa mbele ya benki iliyokuwa mtaa wa Lumumba
katika jengo la Ushirika, yule binti akataka kuteremka na
Tausi.
"We subiri kwenye gari na vitu. Hoza twende!" Mapigo ya moyo
yaliongezeka spidi nisijue yule binti alitaka nimsindikize
benki kwa ajili gani. Akawa ametangulia mimi niko nyuma
yake.
Kufika mlango wa benki akapitiliza, nikaendelea kumfuata kwa
nyuma. Akawa kama anaelekea kupanda lifti, akakata kona
kuzielekea ngazi lakini hakuzipanda kwenda juu akawa
anateremka.
Kama kawaida niliendelea kumfuata kwa nyuma kama mbuzi
anayepelekwa machinjioni, tukafika chini tukatokeza kwenye
maofisi mengi. Tausi aliongozea kwenye ngazi nyingine
inazopandisha juu.
Tulitokea nyuma ya jengo la Ushirika kwenye mtaa wa Kipata,
akasimamisha teksi akaingia mlango wa nyuma, na mimi
nikamfuata humo humo kwenye siti ya nyuma. "Wapi dada?"
Dereva aliuliza.
"Hotel yeyote iliyo karibu" akajibu Tausi.
’Kama hoteli yeyote si tuingie hii hapa mbele yetu?’
nilidakia mazungumzo. Dereva wa taksi aliniangalia jicho la
kuniambia ’acha uchawi wewe’
"Dah kweli. Samahani kaka, lakini nitakupa hela kidogo"
alitamka Tausi akionyesha alimwelewa. Tukaingia hotelini.
Tukafanya taratibu za haraka haraka, tukapata chumba.
Mpaka muda huo sikujua lengo la Tausi lilikuwa ni lipi,
lakini cha mwisho nilichoamini ni kuwa kaamua kunisusia
penzi lake. Nilipowaza hilo nilijihisi mwili ukisisimka
kujiandaa na kukabiliana na zawadi ya penzi la kushtukiza,
nguo ikawa haikai vizuri tena. Tukaingia ndani, tukajifungia
mlango.
Mwanamume nikaanza kutetemeka bila kujijua, nikajihisi
napata tumbo la kuhara. "Sijui nitoke kidogo nikamnywee
konyagi?" Nilijiuliza kwa haraka haraka. Nilijikuta mawazo
ya kihama huku na kule.
Kutahamaki Tausi alikuwa amenisimamia mbele yangu
akiniangalia usoni. "Umenikasirikia?" Aliniuliza kwa utulivu
akiwa ananitazama usoni.
"Hapana ila nilifadhaika sana ulipoamua kuniche.."
nikakatizwa na mdomo wake ambao tayari ulikuwa umeshafika
mdomoni kwangu. Nilijiona dhahiri kuwa nazidiwa, Tausi
alianza kuutawala mchezo.
Nikaona ni jambo la hatari kumruhusu mpinzani akutawale
mchezoni. Mwanamume nikaanza kupiga ’kaunta ataki’ au kwa
lugha fasaha mashambulizi ya kushtukiza. Nikawa namgusa zile
sehemu zitakazomfanya apoteze kasi yake.
Nilianza kumtoa kitambaa cha kichwani alichokitumia
kuzistiri nywele zake, nikaanza kuzichezea nywele zake
taratibu nikimpiga busu masikioni na kushuka taratibu hadi
shingoni. Nikamuona akianza kuhema kama mgonjwa wa pumu.
Tausi alianza kuhema kwa shida akitetemeka, nikajua sasa
nimeudhibiti mchezo. Nikamlaza pole pole kitandani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nakupenda sana Hoza" aliniambia akihema. Nilimwangalia kwa
makini, hakuonyesha masihara akitamka maneno yale.
Mambo yote toka tuliache gari pale mbele ya benki
yalituchukua takribani dakika kumi na tano, nikaona kuwa
bado naweza kulifanya nilitakalo kwa muda uliobakia.
Nikajipa tena dakika tano za ’shoo gemu’.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment