Simulizi : Usinibanie
Sehemu Ya Nne (4)
BAADA ya siku moja tu toka niokolewe na kina Omar nyumbani kwa Mzee Nurdin nikapokea simu toka kwa Tausi. "Halo..Jhemapele Tausi!" alimaanisha kuwa naitwa Tausi.
Kwanza nilichanganyikiwa kuisikia sauti yake, netiweki ya
mbongo ilianza kuwa luzi. Ilikuwa ikiingia na kutoka, nahisi
aligundua kuwa nimepagawa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kilichotokea ni kwamba sikujua niheme kwanza au niongee
kwanza maana hamu ya kuongea ilikuwepo, wakati huo huo pumzi zilikuwa zimenibana. Kuja kutahamaki simu ikawa imekatika, nikaruka hewani mtu mzima. Muito uliendelea kwa muda bila kupokelewa, mwisho simu ikakatika.
Baada ya myda mfupi, akaruka yeye hewani, nikaipokea fasta.
"Komatitapel?" Nilimuuliza tena jina lake kwa lugha ya
kifaransa. "Tausi binti Nurdin" Nikashusha pumzi ndefu,
kabla sijajitambulisha akaniambia kuwa amepata habari za
Hoza.
Nikasita kwanza kujitambilisha ili nimhoji na kuzijua hizo
habari za Hoza. Nilihisi mwili unaishiwa nguvu pale
alipokuwa akiniambia kuwa Hoza ni mpenzi wake na muda ule yuko naye! Kwanza nilitoa kicheko cha masikhara, ila kwa sauti aliyoendelea nayo sikuhisi kama alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akitania.
Nikajikaza kiume, nikamwambia kuwa nataka kuongea naye, nikijua wazi kuwa hakuna namna yeyote ya yeye kuwa na Hoza kuwa kuwa mimi ndio Hoza. Na isitoshe ilikuwa ni muda ambao sio rahisi kwa Tausi kuwa karibu na mwanaume yeyote. Ilikuwa inakaribia saa tano za usiku.
"Haloo!" Ilisikika sauti ya kiume wakati Tausi aliponiambia
kuwa anampa mpenzi wake Hoza aongee na mimi. Nilijihisi
nikitetemeka na kushindwa kuongea, nikakata simu. Simu
ikaita tena nikaipokea. Nikajikuta nikiongea Kiswahili "We
nani?"
"Shemeji, mbona huongei na mpenzi wangu Hoza? Si umesema kuwa ni ndugu yako, au sio Hoza huyu?" Naye akaniongelesha kwa Kiswahili. Donge likanishika nikajihisi machozi yakinitoka, ila sikujua nalilia nini.
Ikasikika tena sauti ya kiume, "haloo, mbona huongei?"
Nilijikuta nikimpa tusi ambalo nilikuwa na muda mrefu
sijalitumia, ila cha ajabu wala halijamuuma. Najua
halijamuuma kwa kuwa aliamua kunicheka.
"Tusi la kizamani namna hiyo umelipata wapi wakati we
unajifanya hujui vizuri Kiswahili?" Nikajihisi kutetemeka
huku jasho likinitoka. Simu bado ilikuwa sikioni.
"Kama hukuhitaji mawasiliano na mimi nduguyo Hoza ulikuja kufanya nini? Kuanzia sasa hatutakupigia tena simu na wewe usijaribu kuipiga tena namba hii, sawa Mfaransa koko?"
Liliongea jamaa kwa majivuno ya hali ya juu.
Baada ya maneno hayo simu ilikatwa na sikuwahi kuipata tena hewani namba hiyo hadi leo hii. Nilibaki nikizunguka huku na kule bila kujua kinachonizungusha na wala sikujua
nilichokuwa nikikiwaza.
Kimsingi nilikuwa nazunguka zunguka tu kama mchaga
aliyeunguliwa na duka lake alilokopea hela Saccos.
Mara simu yangu ya mkononi ikaita tena nikaanza kuitafuta
ilipodondokea, nikaja kuikuta imejibana katikati ya mashuka bila mimi kujua kuwa ilifikaje. Nikaiona ni namba ngeni, nikaipokea. Kwa namna nilivyoipokea kwa pupa endapo yangekuwa ni maji ningepaliwa!
"Koma savaa" nilikimwaga Kifaransa kabla sijapokewa na
kicheko toka upande wa pili wa simu.
"Umegeuka mfaransa kaka?"
"Nani?"
"Biskuti imeyeyuka kwenye glasi yako ya maji!" Iliniambia
sauti ya kike toka upande wa pili wa simu.
Nikashusha pumzi ndefu, nilijua fika kuwa simu hiyo
inamaanisha nini. Ilikuwa ni simu ya kikazi. Nilipoangalia
saa ilikuwa yakaribia saa sita na robo za usiku!
Nikajimiminia pegi kadhaa za whisky ili ubongo ukae vizuri
kidogo, nikavaa haraka haraka, nikajilodi silaha na kuanza
safari ya kwenda kwa mkuu.
"Tausi ushakufa, tutaonana kuzimu!" nilijisemea sio kwa
sababu kazi niliyokuwa nikielekea kuifanya ilimuhusu Tausi
bali nilikuwa nikijilazimisha niamini kuwa Tausi amekufa ili
akili iweze kufikiria mambo mengine.
Hii ndio njia ambayo huwa naitumia kumtoa mtu akilini,
lakini kwa Tausi iligoma. Kila nikijilazimisha akilini
nimuone yuko kwenye jeneza, namuona akiniangalia kwa mahaba.
Tena nilikuwa namuona kwa picha iliyokuwa wazi utafikiri
alikuwepo pale, nilimuona kifuani alivyo na mvuto, nilimuona sehemu za tumboni na namna alivyotanuka baada ya kiunoni.
Niliamua kutumia njia mbadala, nikafungulia muziki kwa sauti ya juu na kujilazimisha kuuimba wimbo ulio hewani kwa sauti kubwa nikiufuatisha lakini wapi.
Muda si mrefu nilikuwa ofisini kwa mkuu. "Namba tatu,
sifuri, moja," mkuu wa kazi aliniambia akiniangalia usoni
kwa makini. Ilikuwa ni kazi ya Mzee Nurdin, ameingia kwenye mtego hivyo ilitakiwa akakamatwe katikati ya uhalifu wanaoutarajia kuufanya.
Mkuu akanipa taarifa zote, aliniambia kuwa usiku ule
watakuwa wakiwasafirisha watoto kuwaleta Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapandisha ndege.
Akili yangu ilifanya kazi kwa haraka sana, nikajua kuwa ni
mojawapo ya fursa chache sana zinazoweza kupatikana.
Nikamuonyesha dalili fulani mkuu nikitegemea matokeo fulani.
Mkuu aliponiangalia akaanza kuhisi kuwa siko sawa na ndio
kitu nilichotaka akiamini, akaniuliza zaidi ya mara tatu
nikamwambia kuwa niko sawa sawa.
Unajua kwa nini? Ukimwambia kuwa hauko sawa, atakupa namna ya kulitatua tatizo lako kisha utatakiwa ukaifanye kazi uliyopangiwa. Ila ukimwambia kuwa uko sawa sawa, hawezi kukuruhusu kwenda kazini kama anakuona huna dalili za kuwa uko sawa.
Mkuu akaniamuru nikapumzike, akampa jukumu mtu mwingine.
"Naenda kwa Tausi" nilijisemea moyoni.
Nilijua ulinzi usingezingatiwa kwa kuwa akili ya Mzee Nurdin isingekuwepo pale nyumbani kama mambo yangekuwa yameharibika barabarani.
"Mkuu ningependa nijue kila hatua" niliomba. Nikapewa namba maalum za kuwasiliana na watu watakaokwenda kwenye hiyo operesheni ya kumliza ba mkwe! Wakati natoka ofisini kwa mkuu ilikuwa yapata saa nane, usiku!
Niliendesha gari kwa kasi kuelekea kwa Mzee Nurdin. Kwa kuwa tayari nilikuwa tayari niko kikazi sikuwa na sababu ya kurudi kwanza nyumbani. Baada ya muda nilikuwa nikikaribia kwenye himaya ya Mzee Nurdin.
Nikazima taa nikawa naliendesha gari gizani kwa mwendo wa taratibu ambao haukuwa ukitoa kelele. Nikaliegesha gari
mbali kidogo na nielekeapo. Hali ya hewa ilikuwa imetulia
sana, labda ni kutokana na muda wenyewe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaanza kutembea taratibu kwa tahadhari kubwa, nilitembea hadi karibu kabisa na ukuta wa kwa mzee Nurdin. Nilikuwa nimebeba mkoba ambao ndani niliweka mkasi maalum wa kukatia ukuta, vifaa vya kuundia mabomu ambayo hayana madhara na
kimtungi kidogo cha gesi.
Ndani ya begi pia kulikuwa na kemikali kadhaa za kuniwezesha kutimiza kazi yangu. Pia bastola yangu ilikuwa mkononi.
Vingi kati ya hivyo nilivipata wakati nikihudhuria kozi
maalum ya kijeshi nchini Marekani iitwayo CRT.
Nilivyokuwa nikimhadithia rafiki yangu mmoja alishangaa
kusikia kuna mkasi maalum wa kukatia ukuta. Mikasi hiyo ipo na inatumiwa sana kwenye operesheni za uokoaji kwenye majeshi yanayoendeshwa kisasa, inakata ukuta kama karatasi.
Nikasogea hadi kwenye ukuta, nikaukata tundu kubwa ambalo linaweza kumfanya mtu akapita kwa kuinama. Nikaingia ndani nikikimbia hadi kwenye giza giza hadi karibu na dirisha la Tausi, nikapiga simu kuulizia operesheni inaendaje.
Nikaambiwa kuwa kila mtu yuko kwenye nafasi yake wakisubiri amri. Nikawatakia kila la heri. Nikawa pale chini nasubiri taarifa, kidogo nikapata ishara fulani kupitia simu yangu.
Nikafanya mawasiliano, nikajulishwa kuwa vijana wa Mzee
Nurdin wameshakamatwa na watoto waliokuwa wakitaka
kuwasafirisha, na tayari kuna kikosi kimetumwa ili kumchukua Mzee Nurdin.
Nikatambaa hadi chini ya dirisha la Tausi, lile lile
nililokuwa napigiaga chabo, nikajiinua taratibu. Kulikuwa na mwanga hafifu, lakini niliweza kuona vyema ndani. Tausi
alikuwa amejilaza kitandani, nikaanza kupata hisia mbaya.
Nilikuwa namuona kama amechoka choka, nikawa nahisi kuwa Hoza wa bandia ameshafanya mambo.
Hasira zilinipanda sana, nikajihisi natetemeka. Lakini
sikufanya pupa. Nikatulia kama dakika kumi hivi nikasikia
mlio wa gari linaloingia kwa Mzee Nurdin, nikajua akili zote
za walinzi zitakuwa getini.
Nikakimbia na kupanda bomba kuelekea juu ya nyumba ya Mzee
Nurdin, kama hesabu zangu zilivyonipa, mlinzi akawa
anaangalia getini. Nikaingia chini haraka haraka, nikabetua
kitasa na kuingia chumbani kwa Tausi.
Sikuwa na muda tena wa kuremba, nikatoa pamba na kuimiminia
kemikali kidogo. Nikamkandamizia puani, akahangaika kidogo
kisha akapitiwa na usingizi. Nikatulia kusikilizia hali ya
hewa.
Nikasikia watu wakiongea ongea kisha kukawa kumetulia,
nikawa nayasikia maongezi kwa mbali. Nikatoka kuchungulia,
kulikuwa shwari. Nikarudi ndani nikamuweka Tausi begani kama
kiroba.
Nikapanda nae juu kupitia zile ngazi, nikamuweka karibu na
geti kisha nikatoka kuchungulia. Yule mlinzi wa juu, alikuwa
bado kaganda kuangalia getini. Nikamtua Tausi chini.
Nikamnyatia mlinzi kisha nikamzimisha, kwa mapigo mawili ya
nguvu, akatulia chini kimya.
Nikamrudia Tausi, nikamuweka begani nikaanza kushuka nae
hadi chini. Kufika chini, nikategesha bomu pale chini. Bomu
hilo huwa linatoa mlio mkubwa sana lakini halina madhara.
Nikamuweka begani Tausi na kuendelea na safari yangu gizani
huku mbwa wa Mzee Nurdin wakitusindikiza. Inaelekea walikuwa
wamenimisi sana! Nikajibana, kwenye kagiza fulani
nikisubiria bomu langu, huku nikiwa nimeachama midomo, pia
nilimtanua midomo Tausi.
Mlio mkubwa ulisikika ghalfa, nikakimbia hadi kwenye tundu
la ukuta nililolitengeneza. Nikamuegesha Tausi, nikatoka
kisha nikamvutia nje. Nikamuweka begani na kukimbia naye
hadi kwenye gari, nikamuweka kwenye siti ya nyuma. Nikapanda
gari na kutoka nalo kwa kasi.
Wakati naiangalia saa yangu ilikuwa yapata saa kumi kasoro
alfajiri, nilikuwa nakaribia kuingia kwangu Boko. Baada ya
kuingia ndani nilimbadilisha nguo Tausi, nilimvalisha traki
suti yangu baada ya kumfuta futa, nikamlaza kitandani
nikisubiri azinduke.
Muda huo nikaanza kufanya mawasiliano na watu waliokuwa
kwenye operesheni, wakaniambia kuwa Mzee Nurdin bado
anashikiliwa lakini imefanywa ni siri kubwa sana, wanaojua
ni watu wachache sana.
Nilirudi chumba alichokuwemo Tausi, nikawa pembeni yake
nikimwangalia. Nilikuwa na hamu ya kujua hali ikoje nyumbani
kwa Mzee Nurdin lakini sikutaka kuchukua hatua yeyote
kufutilia.
Nilikuwa nasubiria kwa hamu kumuona Tausi wangu, kwa kweli
sikuweza kuvumilia kusikia yuko na mwanamme usiku ule. Na
kama ningemkuta, nadhani ningeua.
Wakati nikiwaza hayo, Tausi alifumbua macho akawa kama
anayeota. Nilimuacha kwanza aangaze angaze ili akili yake
ikae sawa. Akajiinua na kukaa chini akiwa anafinya finya
macho, akageuka akanitazama. Tukakutana macho kwa macho.
"Tausi!" Nilimuita. Tausi hakujibu kitu, alikuwa kama bado
anaota. "Hapa uko kwa kaka yangu, walikufuata jana usiku
kwenu. Waliamua hivyo kwa kuwa nilitaka kujiua baada ya
kusikia una mwanamme mwingine."
Tausi akawa bado yuko kimya akinitazama, nilitamani kujua
anachofikiria lakini nilihisi kuwa anatafakari maneno
niliyomwambia.
"Hoza!" Hatimaye aliniita.
"Tausi" Nilimchukulia juisi na kumpa Tausi, akaipokea. Kabla
ya kunywa, aliniangalia kwa muda. Akanywa kisha akarudi
kujilaza. Sikumuelewa kwa muda ule, nikaanza kuingiwa na
hofu. Alitulia kimya pale kitandani.
Niliamua kufanya mawasiliano mbadala, nami nikajilaza
pembeni yake nikamkumbatia. Tukawa kimya! Zilipita takribani
dakika arobaini tukiwa vile vile, japo sikujua anachowaza
lakini nilikuwa na uhakika kuwa hanichukii, bado ananipenda.
"Hoza, ni kweli ulitaka kujiua?" Ni swali la ghafla
lililonifanya nijihisi ubaridi, ilikuwa ni ngumu kumdanganya
Tausi wangu ila ilibidi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siwezi kuishi bila wewe Tausi, ulikuwa na nani?"
"Baba na msaidizi wake mmoja."
Akili yangu ilianza kuzunguka, mambo mengi yakipita
kichwani. Tausi alinielezea mkasa mzima kuwa iligundulika
kuwa nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tausi, hivyo
mpango ulikuwa nisingiziwe kesi.
Kwa kifupi mpango wa Mzee Nurdin ulikuwa ni kunipoteza,
hivyo mawasiliano yote aliyokuwa akiyafanya Tausi yalikuwa
yakidhibitiwa ili tu Hoza nikamatwe na kupotezwa.
Wakati ananihadithia yote hayo hakuwa akinitazama usoni, ila
sauti yake nyororo iliutuliza moyo wangu. Tatizo lililobaki
ni kuwa ningemwambiaje ukweli kuhusu mimi?
Na angeuchukuliaje ukweli huo? "Unaonaje tukienda kuoga?"
Nilichombeza nikiwa na lengo la kuomba mambo kiaina.
Tausi akajiinua taratibu, nikainuka haraka zaidi.
Nikamnyanyua na kumpeleka bafuni. Nikaanza kumvua traksuti,
kisha nami nikavua nguo zangu. Tukawa kama tulivyozaliwa
bafuni mule.
Niliduwaa nikiukagua mwili wa Tausi ambaye alishindwa
kunikazia macho akawa ananiangalia kwa aibu. Nilifarijika
sana moyoni nikajisifu kwa uharamia nilioufanya,
nikamsogelea na kumkumbatia huku mkono mmoja ukibonyeza
kuyaruhusu maji yatiririke kwenye miili yetu.
Kilichobaki ilikuwa ni kusuguana kulikopitiliza, na hata
tulipotoka bafuni hakuna aliyemsemesha mwenzake, tukajilaza
kitandani tukijifunika shuka kubwa.
Nilishtuliwa na mlio wa simu, alikuwa ni Mkuu. Haikuwa
kawaida kwa Mkuu kupiga simu muda kama ule, hivyo nikaanza
kujiuliza maswali yasiyo na idadi. Kumtupia jicho Tausi,
naye akawa ameshtuka ananiangalia kwa jicho la kwa nini
hupokei hiyo simu?
Nikaifuata na kuipokea, mkuu aliniuliza maswali kama matatu
hivi lakini uzito wake ulinifanya nitokwe na jasho kwenye
paji la uso.
Kimsingi alikuwa akinihoji kama niliona pilika zozote kwa
Mzee Nurdin kuwa kuna watu wanamfuatilia Tausi, kabla
hajanitaarifu kuwa ametekwa na watu wenye mbinu za kijasusi.
Akaniambia kuwa tukio hilo lilipishana muda kidogo sana na
muda aliokwenda kuchukuliwa Mzee Nurdin kwa ajili ya
mahojiano.
Baada ya Mkuu kukata simu, nilijikuta bado nimeishikilia ile
simu mkononi nisijue jambo la kufanya kwa haraka haraka ila
sikupata presha sana kwa kuwa mtu aliyeteuliwa kulifuatilia
suala hilo naujua uwezo wake.
"Vipi?" Tausi aliniuliza akiwa anajiinua kitandani.
Nikamdanganya kuwa aliyepiga simu ni kaka.
"Kuna kitu unanificha Hoza, na bora nikisikie toka mdomoni
mwako kuliko nikikisikia kwa mwingine. Kwa maana
sitakusamehe" aliniambia Tausi akionesha kuwa hana masihara
hata chembe.
Nilibaki kimya nikimtazama, nilijaribu kupata picha endapo
angeniacha, nikajihisi maumivu makali sana moyoni. Nikampa
mkono, akaushika. Nikamwinua, akanyanyuka. Nikammiminia
mabusu mfululizo huku mikono yetu ikiwa imeshikana vyema.
Tukaanza michezo michezo yetu, huku tukifurahi kisha
nikamwambia tutoke tukatembee ufukweni. Akanitania kuwa
tutembelee majini sio ufukweni, nilicheka lakini
nilimwelewa. Nikampa bukta na fulana moja nyepesi, nami
nikabadili tukatoka.
Baada ya muda mchache tulikuwa katikati ya maji tukiendelea
na mchezo wetu uliopelekea kuonja mahaba ya ndani ya maji,
shughuli ilikuwa tamu usipime! Kwa muda wote aliokuwa pale
kwangu, Tausi alikuwa akiyafaidi mapishi yangu. Alionekana
kufurahia mno.
Nakumbuka kilichoniponza. Jioni iliyofuatia nilimchukua
Tausi tukaenda kukaa ufukweni jua lilipokuwa likikaribia
kuzama. Tausi alikuwa ametulia akinisikiliza kwa umakini,
ambacho nilitaka kumwambia.
Nilimwambia ukweli! Nilimwambia kuwa aliyekuja siku ile ni
mimi na sina kaka. Nilimwambia wazi kuwa mimi ni afisa
upelelezi ila nilimficha kuwa nilikuwa pale kwao kumpeleleza
baba yake.
Nilichomwambia ni kuwa, nilikuwa likizo nikaamua kwenda pale kwa Mzee Nurdin ili nipate nafasi ya kuwa naye. Nikamueleza
kuwa niliwahi kumuona siku moja uwanja wa ndege, nikavutiwa
naye. Nikaamua kuchunguza habari zake nikagundua kuwa yeye
ni nani na anakaa wapi.
Nilimweleza mengine mengi na ni kwa kiasi gani nampenda na
sitaki kumpoteza katika maisha yangu. Muda wote huo Tausi
alikuwa akiniangalia tu kama anatizama sinema ya kihindi.
Nilishindwa kujua anafikiria nini ila alikaa kimya kwa muda
mrefu.
Nilijaribu kumshika, lakini hakutaka nimshike. Alisema nimpe
nafasi kwanza akili yake iweze kupembua maneno
niliyomwambia, niliogopa. Baada ya muda mchache, Tausi
aliinuka taratibu na kuanza kuondoka akiongozea nyumbani kwangu.
Nikainuka na kuanza kumfuata nilichanganyikiwa kwa kweli.
Tausi alirudi moja kwa moja hadi chumbani, akabadili nguo.
Alivaa nguo nilizomnunulia mchana ule, akajiandaa kama ana
safari fulani, kisha akakaa kitandani.
Nilimfuata nikaishia mlangoni nikimwangalia nisijue ni lipi
la kumwambia, sikujua anawaza nini kwa muda ule. Ila alikuja
kuniambia neno moja tu, "mimi na wewe basi!"
Nilijikuta machozi yananidondoka japo sikuwa nalia.
"Ni heri kumuona mwanamume akikata roho kuliko kumuona
akitoa machozi!" nilimwambia kwa huzuni nikimkazia macho.
Nilimwambia, "toka nipate akili timamu, hata mama yangu
mzazi hajawahi kuliona chozi langu. We ndio mwanamke wa
kwanza kuliona chozi langu, sitakubali utoke katika maisha
yangu!"
Tausi aliniangalia kwa muda, alionekana mwenye huzuni sana.
Nilipoendelea kumwangalia nilimshuhudia akiangua kilio,
nilimsogelea nikakaa pembeni yake.
Alilia kwa muda kisha akageuka kunitazama, moyoni nilijawa
na huzuni lakini sikulia tena. Nilijikaza kiume tukabaki
tunaangaliana. "Huwezi kuamini ninavyokupenda Hoz.. sijui
sasa nikuiteje?" Tausi aliniuliza.
"Niite Musa, nimeamua nijivue niwe halisi."
"Ok, nitalizoea taratibu. Nakupenda sana Musa, lakini siwezi
kukuamini tena!" Maneno ya Tausi yalikuwa ni kama msumari wa
moto moyoni mwangu, yalinichoma na nikaumia haswa.
Nikajaribu kumwelezea sana kuhusu namna nnavyompenda lakini
kwake ilikuwa ni kazi bure, aling’ang’ania msimamo wake kuwa
mimi na yeye basi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mara zote nilikuwa nikiambiwa kuwa maaskari hawaaminiki, na
mimi nilijiapiza kuwa sitakuja kufanya urafiki na askari.
Tazama leo, mpelelezi ndio amekuwa mwanamme wangu wa kwanza" alisema Tausi akilia.
Nilijaribu kumwelewesha sana lakini haikusaidia, maswali
aliyokuwa akiniuliza yalinivunja nguvu. Mfano aliniuliza
kuwa atajuaje kama sikumtaka yeye ila nimchunguze baba yake.
Alinielezea kuwa baba yake alishahisi kuwa mimi ni
mpelelezi, na tayari alishamuonya kuhusu tabia za askari na
akaniambia kuwa askari hatuna mapenzi ya kweli.
Nilijihisi napata homa kali, sikuwa na pointi tena za
kujitetea kwa kuwa Tausi alionekana kudhamiria kunifungia
milango ya mapenzi. Nikajilaza kitandani nikisubiri hatima
ya yote, sikuwa na nguvu tena ya kumshawishi Tausi.
Ila kikubwa nilimpa muda wa kutafakari maneno niliyomwambia.
Nilikuwa nimefumba macho nikiongea taratibu, ilikuwa ni kama
namkumbusha Tausi mambo tuliyoyafanya pamoja, niliyachagua
yale yaliyokuwa yakisisimua. Nilimsikia akishusha pumzi
ndefu, nikaendelea na simulizi zangu.
Nilimwambia hadi jinsi nilivyokuwa silali bila ya kumpiga
chabo, nilipofikia hapo nikamsikia akijizuia kucheka.
Sikujali japo nami nilijizuia kucheka, niliendelea
kumhadithia hatua kwa hatua hadi nilipobambwa mara ya kwanza
nikapigana na walinzi.
Mwisho nikaanza kumuelezea namna nnavyojisikia moyoni
kutokana na uamuzi wake, uamuzi ulionifanya nijihisi kama
mtoto yatima anayekimbiwa na mama yake. Kufikia hapo Tausi
akausogeza mkono wake na kuushika wangu, akauvuta na
kuukumbatia.
Nikawa nalihisi joto la mwilini mwake. Nikaona kuwa ulikuwa
ni wakati muafaka kuiacha miili ibembelezane na kuchukua
nafasi ya midomo. Nikamvutia kitandani. Akaanza kunipa
ushirikiano wa kutosha.
Tukawa tumezama mapenzini huku maneno yakiwa hayanikauki
mdomoni, nilimsihi asije kulivunja penzi letu. Tulipomaliza
Tausi alikuwa amelala kifuani kwangu.
Aliufungua mdomo na kuniambia maneno niliyoyaelewa japo
yaliniumiza sana, alinihakikishia kuwa ananipenda na
anaamini kuwa penzi langu ni la kweli. Lakini tusingeweza
kufikia tunapotaka kwa kuwa kwanza baba yake asingekubali
tuoane, akaniambia wazi kuwa hadhani kama kuna mtu
anayechukiwa na baba yake hapa duniani kuliko mimi.
Pili kwa yeye isingekuwa rahisi yeye kuniamini kama
ningeendelea kuwa katika kazi yangu ya upelelezi kutokana na
mambo anayoyasikia na kuyasoma kuhusu wapelelezi. Ila
aliniambia kuwa atabaki kunikumbuka katika maisha yake yote
na hadhani kama kuna mwanamume ambaye angeweza kunitoa
katika moyo wake.
Pamoja na kuwa maneno hayo yalinifariji lakini sikuwa
nahitaji kumpoteza Tausi, nilikuwa naumiza kichwa ni njia
gani itakayonibakizia Tausi wangu. Tulilala tumekumbatiana
kwa nguvu sana usiku ule.
Naukumbuka vizuri usiku ule, joto la Tausi nililihisi hadi
moyoni mwangu. Kila nilipofikiria kuwa ile ndio ilikuwa ni
mara yangu ya mwisho, moyo uliniuma sana. "Sikubali"
nilijisemea usiku ule.
Tuliendelea kulala vile vile pamoja hadi ilipofika asubuhi.
Tausi akawa anataka kwenda kwao, nilimsihi asubiri giza
liingie. Akaniuliza swali gumu kuwa ningemrudisha kama
nilivyomchukua? Nikamwambia hapana, ningemrudisha kivingine.
Ila kwa namna ambayo atakuwa salama. Nikarudia tena
kumwambia namna ninavyompenda, ila alinikatiza kabla
sijamalizia.
"Usifanye mambo yale magumu, nielewe mpenzi" aliniambia
akinibusu mdomoni na kuufanya mdomo wangu uhisi ganzi!
Baadae kidogo Tausi akaniambia kilichonishangaza,
sikutegemea kama angenifikiria jambo lile. Akaniomba iwe
zamu yake kunipikia, nikamuuliza unaweza? Akabaki anacheka,
akaniambia subiri uone.
Tausi akaingia jikoni, mi nikawa msaidizi wake. Nikawa
nasaidia kukatakata vitunguu, mara niambiwe lete chumvi basi
ilikuwa raha tu. Kikubwa nikawa nasubiri kitakachotoka kama
utamu wake utafanana na Tausi? Tausi ana tabu kweli, unajua
alichokuwa amevaa? Alivaa kagauni fulani kafupi, kepesi na
kanaonyesha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa nikisisimkwa kila nikimuangalia japo nilikanunua
mwenyewe, mtoto huyu mvuto wake umepitiliza yaani utadhani
ni binti jini! Uzalendo ukanishinda, ikabidi tuliweke kando
kwanza suala la kupika likawa ni suala la kupikana humo humo
jikoni.
Baada ya kuhakikisha presha zimeshuka, zoezi la kupika
likaendelea huku Tausi akinionyeshea viwango vya jikoni.
Siku hiyo tuliinjoi sana, nilijitahidi kupata raha kwa
kadiri ilivyowezekana pamoja na kumpa raha za kutaka
kumkomoa ili abadili uamuzi wake.
Nilimuomba afikirie tena kuhusu uamuzi wake, ila nilimwambia
asinijibu pale pale. Nilipomwona anakosa raha nikabadilisha
maongezi nikampa stori za kumchekesha chekesha. Akarudi
kwenye ’mudi’! Baadae muda wa kuondoka ukawadia!
Tukaanza kujiandaa, mpango ulikuwa ni kwenda na Tausi hadi
karibu na nyumbani kwao kisha ningemuacha na watu ambao
tayari nilikuwa nimewapanga. Kila nilipomwangalia Tausi,
nilijihisi kuwa ni mwanamume mwenye bahati mno.
Ni aina ya msichana ambaye hata ukimuhonga gari ukawa
unatembelea daladala huwezi kujilaumu. Watu hao niliowaandaa
wangemfikisha Tausi hadi nyumbani kwao kwa madai kuwa
walimuokota akiwa kapoteza fahamu nje ya mji.
Kila kitu kilikuwa kimepangwa vyema. Sikutegemea kufeli kwa
kuwa watu niliowaandaa walikuwa ni kina mama wawili maaskari
na mzee mmoja. Pia nilitumia ’uchawi wa kizungu’, pesa!
Wote hao sikuwaambia ukweli ila niliwadanganya kuwa Tausi ni
demu wangu, lakini kwao geti kali hivyo kwa kuwa
nilimtorosha nikachelewa kumrudisha ingekuwa kesi nzito. Utu
uzima dawa, walinielewa vyema japo walikuwa wakininanga
kizamani. Eti kwa nini usitoe posa, unaendekeza uhuni tu?
Wazee wengine bwana!
We unafikiri ningemtangulizia posa Mzee Nurdin hata nafasi
ya kuongea na Tausi ningeipata? Si Mzee Nurdin angeona
namletea uchuro tu? Baada ya kumaliza kujiandaa, tulitoka
kwa kutumia gari la rafiki yangu.
Sikutaka kutumia gari langu kutokana na sababu maalum. Tausi
alizifunga tu nywele zake kwa nyuma, akavaa gauni kama lile
alilovaa siku ile nilipomchukua. Kuna kitu nilitaka
nisikihaditie lakini ngoja tu niwaambie.
Unajua alipomaliza kuvaa kama nilivyomchukua, lile gauni
lilimuonyesha umbile lake vyema. Na kila nilipomtazama,
mawasiliano kichwani yakaanza kupotea kama netiweki ya simu
mbovu. Tukakata kiu tena.
Muda mfupi baadae tukawa tukiingia barabara ya Bagamoyo
ambako jioni ile hakukuwa na foleni kabisa. Kagiza kalikuwa
kameshamiri.
Niliingia barabara hiyo kuu nikiendesha huku mpenzi wangu
Tausi kanilalia begani na mkono wake ukiwa pajani kwangu
akinifariji, dunia yote ilikuwa yangu. Muziki laini ulikuwa
ukiunguruma garini huku Lionel Richie akifanya vitu vyake
vya kiutu uzima. Kwa kweli ukijipanga pepo inashuka hapa
hapa bongo!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment