Simulizi : Salhat
Sehemu Ya Tano (5)
Hku nako Salhat aliweza kumuelezea Eddy yote yaliyoweza kutokea juu ya Grace huku wakiamini ya kuwa kwa % zote Badra ndiye anayehusika na hayo yote.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ila hamuwezi kumuhukumu Badra moja kwa moja kwasbabu tu alikuwa akitumia sura ya Grace" alizungumza Malikia.
"Sasa tufanyaje???? Aliuliza Salhat.
"Mumfuatilie Badra na Grace kwa umakini zaidi alizungumza Malikia.
Eddy alitingisha kichwa kumaanisha ya kuwa amekubalina na hiyo aliloweza kulizungumza Mama yake.
Sasa kazi ilianza ya kumfuatilia Badra pasina yeye mwenyewe kujua.
Usiku mmoja wa Giza alionekana Badra akitoka katika nyumba huku akinyata kuelekea njee pasina mtu yoyote kujua ila kwa bahati mbaya kwa Siku hiyo Salhat alikuwa pamoja na Eddy huku walimtizama mahali anapoelekea.
Alipofika njee alipanda gari na moja kwa moja alielekea katika nyumba moja baada ya kuingia ndani ya dakika2 alitoka tena njee huku akitizama kushoto na kulia aliingia ndani ya gari lake akaliwasha kish akaondoka eneo lile.
Salhat Alitizama na Eddy kisha wakaelekea ndani na ndipo waliposhtuka baada ya kukutana na damu zikiwa nyinyi chini.
***** ****** *****
Kulikucha Asubuhi na Badra alielekea mezani kwaajili ya kupata kifungua kinywa alipofika alikaa na kuanza kuvuta chai alimimina kisha akaweka sukari na kisha akaanza kukoroga chai yake ila alisita na kupandisha macho juu hapo macho yake yaligongana naya Grace.
"Unashida gani???? Aliuliza Badra.
Hapo hapo taarifa ya habari ilirushwa kuhusiana na kijana aliyekutwa ameuwawa ndani ya nyumba yake kwa kusambuliwa na risasi na mtu asiyejulikna.
Badra Alitizama tu kawaida kisha akaendlea kunywa chai yake.
"Mama unafikiri nani atakuwa muuwaji maana hata ushtuki"
"Sasa nishtuke huyo kwa kupigwa risasi na wanaopigwa mapagwa na kuwekwa kwenye salflet wafanywaje???? Alizungumza Badra ambaye alionyesha kutokujali kwa tukio hilo.
Hapo hapo aliingia Jay na kukaa.
"Johnny umerudi???? Aliuliza Badra kwa furaha sana.
"Ndyi nimerudi kuna mtu wa muhimu niliweza kumfuata hapa ndani na siwezi kuondoka kabla sijampata mtu huyo alizungumza huku akimtizama Badra na kuachia tabasamu ambalo lilimfikia Badra na kujikuta kicheka Cheka huku anatazma chini.
"Mpuuuzi mkubwaaaaa huna Siku nyingi utalipa kwa Yale yote uliyoweza kuyatenda yalikuwa maneno ya Jay juu ya Badra.
Katika wodi namba 87 alikuwapo Nasma aliyeweza kuyaleta maua mazuri yenye kunukia katika chumna hicho.
Aliweza kuyaweka katika mtungi kisha akaelekeza macho yake sehemu ambayo alitabasamu baada ya kumuona Mgonjwa wa wodi ile.
"Baba unaendeleaje aliuliza huku akielekea mahali alipoweza kulazwa mgonjwa alikuwa baba yake Akram IGP Saidi ambaye mpaka sasa hakijulikani ni kitu gani kiliweza kumkuta na kumfanya yeye awe katika hali hiyo ya kuparalize.
**** **** ****
Mwili wa aliyeweza kuuwawa na Badra uliweza kuchukuliwa na askari wa polisi kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Mwili huo haukuweza kufahamika mara moja ya kuwa ulikuwa na mahusiano na nani kwani askari waliobaki hawakuweza kutambua chochote kile kilichokuwa kikiweza kuendelea baada ya mambo kuwa magumu basi Akram aliweza kurudishwa kazini kwa sharti la kuwa awatafute wauwaji na pia Salhat aje mikononi mwa polisi.
Akram alitingisha kichwa na Mara moja aliianza kazi yake.
Aliweza kuelekea hadi katika nyumba ambayo alikuwa akikaa mtu yule alifunua funua kwaajili ya kutafuta ushahidi wowote lakini hakuona kitu chochote kile.
"Embu ingieni hicho chumba kingine kutafuta alisema Akrama akiwaamuru polisi wawili waweza kwenda katika chumba kilichokuwa kinafuata kwaajili ya kutazama kama kutakuwa na ushahidi wowote ule.
Baada ya askari wale kufanya vile alivyosema. Aliingiza mkono wake mfukoni kisha akatoa cheni ambayo alikumbuka maneno ya Salhat.
"Badra ndiye aliyeweza kumuuwa na nilishuhudia kwa macho yangu ila nimeshindwa kujua ni nani huyo aliyemuuwa nani kwasababu gani???
Aliidondosha ile cheni pale kisha akaelekea na yeye kwenye chumba ambacho aliwaambia watu watangulie.
***** ****** ******
Badra aliweza kuzisikia Sauti za mvutano zikiwa pembeni kabisa ya chumba chake aliweza kufungua mlango Kisha akaangalie ni nini hicho??.
Alipofungua mlango macho yake yaligongana na ya Akram ambaye alijitambulisha kama polisi Kisha akamuhitaji aongozane naye kwa uchunguzi zaidi.
"Kwani nimefanya nini???
"Unashatakiwa kwa kosa la kufanya mauaji.
"Mauaji unaongelea nini wewe......mauaji kwani mimi nimemuuwa nani??? Aliuliza Badra.
"Kama unapinga shtaka lako unaweza kumuita mwanasheria wako lakini kwasasa nahitaji wewe ulipe ushirikiano jeshi la polisi. Alizungumza Akram kisha akataka kuweka pingu mikononi mwa Badra ambaye alisema nitaenda.
"Kuna nini hapa??? Aliuliza Grace aliyekuwa ametoka matembezini.
Alielezewa na askari mmoja kwannn mama yake yupo chini ya ulinzi.
"Hapana mama yangu hawezi kufanya hivyo" alizungumza Grace.
"Basi hayo maelezo na wewe utakuja kuyatoa mahakamani aliongea Akram na kuanza kumburuta Badra ambaye aliitoa mikon ya Akram kisha akaanza kutembea.
"Mama usijali nitampigia simu wakili wetu na atafika hapo usijali kabisa alizungumza Grace huku akipiga simu na kuanza kuomba msaada.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Huyu naye hajui y kuwa mama yake Si mwema kwa upande wake yeye bado anataka kumtetea tu" alizungumza Jay alikuwa pale akiwa amejibanza na Ashura.
***** ****** *******
Badra aliweza kuachiliwa baada ya Masaa kadhaa kupita alirudi nyumbni na moja kwa moja akaelekea bafuni mwake.
"Mpuuzi gani huyo anayediriki kutumia sura yangu amah kwa hakika sitoweza kumuacha hai sitoweza kumuacha hai??? Alizungumza Badra kwa hasira sana kupasua kioo kilichokuwapo pembeni ya anako ogea.
***** ***** *****
"Ni sawa ushahidi umekamilika ila kuna kitu kidogo kinanipa mashaka" alizungumza Akram.
"Kitu gani???? Aliuliza Nasma.
"Kwani Jini akibadilika na kuja katika sura ya mtu mwingine fingerprints zake huwa niza tofauti?? Aliuliza Akram.
"Sijakuelewa umezungumza nini???
"£aaahhhhh basi tu kwanza huwezi nielewa......ila Nasma ungeenda ukapumzike sasa kwani umekaa muda mrefu na mimi nitamtizama baba" alizungumza Akram.
"Hapana wewe usijali tena nasikia burudani sana nikifanya vitu vyote hivi kwani katika maisha yangu sijawahi hata Siku moja kumuwekea umakini mtu hivi hivyo najifunza mingi kupitia baba na ukizingatia sina mpango wa kuolewa na Jini Bali binadamu hivyo nataka nijifunze kufanya kazi nyingi kadri ya uwezo wangu" alizungumza Nasma huku akimfuta futa Mr Saidi na kitambaa cha maji ya moto miguuni mwake.
"Akram!!! Aliita Nasma.
"Kwa kumtizama baba ndani ya wiki hii lazima ataamka tu kwasababu namfanyia masage kila saa namchuwa na dawa yak namsagia matunda lazima ataamka tu na kilio chako cha miaka14 sasa kitapungua"
Akram alitabasamu na kuendelea kumtizama Nasma. Ghafla simu yake iliita.
"Salhat nakuja!!! Alikata simu akiwa na furaha kisha akaondoka bila kusema neno lolote kwa Nasma.
Nasma alihisi kuumia moyo but alitabasamu tu akiamini ya kuwa ipo Siku moja Akram ataweza kuyabadili mapenzi yake yaliyoko kwa Salhat kisha akayaweka juu yake.
Aliyafuta machozi yake kisha akazungumza.
"Baba nitakuangalia vizuri sana na kuhakikisha ya kuwa utaamka kwa gharama yoyote ile kwani napenda sana kuiona furaha ya Akram" alizungumza Nasma na kuendelea kumkanda na kitambaa kile cha moto.
******* ******* ******
Grace akiwa tena katika chumba cha mahojiani ilitolewa cheni na kuwekwa mezani na Akram.
Cheni hii ni ya kwako na ilipotea Siku ile ulipofanya tukio kwahiyo huwez kukataa.
"Nakwambia hivi sijauwa..... Kwanza udhibitisho gani ulionao kwamba cheni ni ya kwangu??? Aliuliza Badra kwa ujasiri.
Akram aliyatoa makaratasi ambayo yaliweza kudhibitisha ya kuwa mmiliki wa cheni ile ni Badra.
"Cheni yangu siyo hiyo" aliongezea Badra.
Bali ni hii alizungumza na kutoa cheni nyingine ambayo ilikuwa mfanano kabisa na ile aliyokuwa nayo Akram hivyo ikamuwia vigumu Akram kupata ushahidi wa kumfunga. Aliweza kuachiliwa tena huru kwa zamana.
Akiwa ndani ya gari lake alianza kuvuta kumbukumbu ya kuwa Alikuw nayo usiku ule na aliweza kuivua baada ya kutoka matembezini kisha akapitiwa na usingizi baada ya kuchoka sana hivyo alilala fofofo na cheni ile aliweza kuicha juu ya dressing table yake sasa imefikaje kule.
"Lazima kuna mjinga anayetaka kucheza na akili yangu lazima kuna mpuuuzi anayetaka kumijaribu mimi uwezo na nguvu nilizonazo sasa sitaweza kumuacha hai mtu yoyote yule anayenitengenezea mimi uadui wa namna hii" alizungumza Badra akiwa ndani ya gari lake.
****** ***** ******
Nasma ni hatari kwa maisha yako kama utaelekea huko katika ukoo wa Abandandi.
"Lakini sasa huko Ndiyo kwenye dawa pekeee ya kuweza kumsaidia baba yake Akram" alizungumza Nasma.
"Sijasema itamponyesh bali itaweza kumsaidia kwa asilimia chache sana" aliongezea Sheilah.
"Hizo hizo chache zinaweza mfanya Akram akafarijika zaidi" alizungumza Nasma.
"Lakini Nas........"
"Nimesema naenda na hii iwe Siri baina yetu" aliongea Nasma na kuendlea kumkanda baba yake Akram huku akisema.
"Baba sasa utatoka katika hali hiyo uliyonayo ni kesho tu nitaelekea huko" alizungumza Nasma.
****** ****** ******
Siku iliyoweza kufuata Alioneka Badra akiwa anatoka tena njee usiku huu aliweza kuonekana na Ashura na moja kwa moja Ashura alimpigia simu Jay na kumpa taarifa hizo.
Ila wakati akitoa taarifa hizo Badra aliweza kumsikia alitabasamu tu kisha akaendelea kuondoka zake maeneo yale kwani ndicho alichokuwa akikihitaji.
Wakati huyo akiondoka alionekn Badra akiwa chumbnai mwake tena akiwa amelala fofofo na hiyo ni baada tu ya kunywa maji pamoja na dawa zilizokuwa pembeni yake.
Sasa hapo ndipo ambapo hata sisi tunashindwa kuelewa ni yupi Badra wa kweli ni yule aliyetoka njee au ni huyo aliyeweza kulala ndani.
Ila tutaelewa tu tuendelee.
Wakati akitoka njee alipanda gari lake na kutokomea eneo hilo huku akisema moyoni mwake.
"Leo Ndiyo mwisho wako.......alizungumza huku akilitizama gari la Jay lililokuwa likija nyuma yake". Na kucheka kwa nguvu sana.
Alifika mahali kisha akapaki gari na hapo hapo aliweza kuteremka alikuja mtu mmoja Kisha akatoa pesa na kumpatia wakati akifanya yote hayo aliweza kuchukuliwa video pasina yeye mwenyewe kujua kwani aliiamini ya kuwa tayri ameshaweza kumuacha mbali sana Jay.
Baada ya kuchukua pesa kijana yule aliweza kuondoka ila hakufika mbali Badra alitoa bastola na kumpiga za mgongo baada ya hapo alienda akachukua fedha zake kisha akauweka mwili yle kwnye malboro alafu akaenda kuuchimbi mahali na kusema.
"Sasa nimekumaliza tuone tena kama na hapa utaweza kutoka"
Alihisi kama kuna mtu nyuma yake na hapo aligeuka kwa haraka wala hakuona mtu. Ila alihisi kuna mtu baada ya kusikia kijiti kimevunjika maeneno Yale.
Ni kweli alikuw Jay ila alisaidiw na Salhat ambaye alitokea chap kisha kupotea naye.
"Kwanini unaenda kufanya kazi hiyo mwenyewe hujui ya kuwa ni hatri laiti kama angekukamata basi angekuuwa" alizungumza Salhat akimtizama Jay aliyekuwa akitabasamu.
"Kumbe ulikuwa ukinifuatilia nyuma nyuma??? Aliuliza Jay.
"Aunt Ashura Ndiyo alinipigia Simu ya kuwa wewe umeamua kumfuatilia Badra pkee yako ikabidi nikufuate.
Waoooooo kumbe unamashaka juu yangu sindiyo?? Aliuliza Jay huku akimfuta Salhat ili amkumbatie.
**** **** *****
Kulikucha asubuhi na Grace aliende kumuamsha Badra.
"Amka Mama umelala sana......"
"Nitaamka Aliongea Badra.
Grace alisimama na kutaka kuondoka Ila alisita baada ya kuona viatu vikiwa na rangi tofauti.
"Mama ulienda wapi mbona viatu vyako vichafu na hata miguu yak?? Aliuliza Grace.
"Nilitoka kidogo alijibu Badra na kuendelea kuvuta usingizi.
"Nani kweli ulitoka kidogo kwenda kufanya mauaji kisha ukarudi kulala ilikuwa Sauti ya Akram iliyoweza kumshtua Badra kutoka usingizini.
Akram alitabasamu kisha akamwambia ushahidi sasa umekamilika huna pa kukimbilia" alizungumza Akram.
"Wanaongelea nini hawa??? Aliuliza Badra ambaye alionyesha kutokujua wala kuelewa chochote kile.
Badra alifikishwa katika chumba cha mahojiano na hapo alikaa huku akishindwa kuelewa ni kitu gani knaendelea kutokea katika maisha yake.
Aliingia Akram huku akimchekea Badra ambaye alikuwa katika dimbwi la mawazo ila alipohisi kuna uwepo wa mtu alitoka huko aliko kisha akamtizama Akram.
"Badra hapana mtuhumiwa naomba tuendeee moja kwa moja kwenye kesi ya kuwa ulikuwa wapi usiku wa Jana??
"Nilikuwa kitandani nimelala na sijui kipi kilichoweza kuendelea kwani nilipotoka kwenye part moja kwa moja nilielekea kitandani kwangu na kulala kwahiyo hicho mnachokizungumza hapa siwaelewi aliongea Badra baada ya kumuona Jay akiingia ndani.
"Johnny embu waambie hawa watu ya kuwa mimi siwaelewi kipi wanachokizungumza hapa" aliongea Badra
"Huelewi nini sasa hapo Badra alizungumza Jay huku akielekea sehemu aliyoko Badra.
"Unamaanish nini kuongea hivyo?? Aliuliza Badra baada ya kutokuelewa ya Kuwa Jay kazungumza nini.
Jay alipofika karibu na yeye alitoa simu yake kisha akamuonyesha video ambayo aliweza kurecord tukio lizima la Jana usiku.
"Sasa hapo utasema huelewi nini tena aliuliza Jay akamtizama Badra.
"Nimesema siyo Mimi wala sijui ni nani huyo aliyeweza kuitumia sura yngu katika kulifanya hilo jambo" aliongea Badra.
Hapo hapo aliweza kuonyeshwa tena video nyingine alipokuwa akibadilika na kuwa katika sura ya Grace na Salhat.
"Utakataa tena?? Aliuliza Jay akimtizama Badra kwa hasira.
"We ni nani??? Aliuliza Badra akimtizama Jay.
Hahahaha Jay alicheka tu kisha akamsogelea karibu zaidi Badra na kumwambia.
"Bado tu unashindwa kunielewa mimi ni nani??? Aliuliza Jay kisha akamsogelea na kumwambia.
"Hata Salhat bado tu umeshindwa kumtambua ni nani??? Aliuliza Jay na kumsogelea karibu zaidi.
Badra!!! Aliita kwa Sauti ya juu kabisa na kumfanya Badra amkumbuke mtoto wa kiume ambaye ndiye aliyeweza kumsambaratisha Salhat.
"Hapana haiwezekani siyo wewe!! Alizungumza na kusimama.
"Vizuri kama umenikumbuka sasa kwani Mimi ndo huyo unayemfikiria na Salhat ndo huyo pia unayemfikiria.
"KKwahiyo umekuja kulipiza kisasi kwa kutumia sura yangu.....basi umeshindwa kwani huniwezi na Mimi siyo mtu wa kawaida kama unavyofikiria Alizungumza Badra na kucheka.
"Hata Mimi natambua ya kuwa wew siyo mtu wa kawaida ndy maana nimekuja hapa kuwa saidia polisi" alijibu John.
"Haya tuone utawasaidia vipi polisi" aliongea Badra na kutaka kupotea lakini kila alipojitahidi kupotea alishindwa.
"Umenifanya nini?? Aliuliza Badra.
"Ulisema wewe siyo mtu wa kawaida ila ukashindwa kutambua ya kuwa hata mini siyo mtu wa kawaida alisema huku akiiutoa unga unga Fulani kwenye cheni yake kisha akamuonyesha Badra.
"Hapanauwezi nifanyie hivyo uwezi ninyang.anya nguvu zangu",
Johnny alimwagia na kilichosikika nikelele tu.
**** ***** ******
Baada ya wiki mbili kupita mmbo yalikuwa safi kabisa kwani Badra aliweza kutuhumiwa kwa kesi zote tatu za mauaji na kufanya Salhat awe huru tena.
Maisha baina ya Jay na Salhat yalizidi kusonga mbele huku Akram akiwa bado hajarizika kwa hukumu iliyoweza kupita juu ya Badra kwani kuna vitu alivihisi haviendi sawa kabisa.
Hivyo kila Mara alikuwa akikutana na Salhat na kumwambia mashaka yake kwani alihisu lazima kuwe na mtu mwingine tofauti na Badra ambaye aliweza kumcheze Badra.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanini kila Siku unasema Badra siye aliyeweza kuyafanya matendo yote hayo??? Aliuliza Salhat.
"Kuna matendo ambayo nikiyaweka kwa usawia hayaingiliani kabisa kwasbabu....kabla hajaendelea kuzungumza kitu kingine hapo hapo alipigiwa simu na daktari.
"Baba" ndilo jina aliloweza kulitamka kisha akaondoka na kumuacha Salhat
Alifika hospitalini na moja kwa moja aliweza kuingia katika chumba cha baba yake. Baada ya miaka 14 sasa kupita hatimaye baba yake aliweza kuyafungua macho yake na kuyafunga tena huku akiyapepesa kulia na kushoto.....
Akram aliingia akiwa na furaha sana huku akimkunbatia Baba yake.
"Baba ni Mimi mwanao Akram baba" alizungumza na machozi yakimtoka wakati huo upande wa pili alionekana Nasma akiwa amechubuka chubuka mwili mzima na mwili wake ukivuja damu.
Sheila aliweza kwenda kumpokea huku akilalamika kwann aliweza kwenda katika ukoo ule wa mashetani.
"Sheilah sasa baba ameweza kufungua macho yake na naamini ya kuwa Akram atakuwa mwenye furaha sana.
"Mimi naongelea kuhusu wewe.....wewe unaongelea kuhusu mwanaume ambaye hata hajali kuhusu wewe"
"As long as Akram yuko na furaha basi ni faraja yangu" aliongea Nasma akitabasamu hatimaye alizidiwa na kushindwa kutembea akadondoka chini.
***** ******* *******
"Jay nakushukuru sana kwani umeweza kunisaidia kwa kiasi kikubwa sikuweza kuamini ya kuwa Mama yangu Badra anaweza akawa na roho mbaya kiasi hicho hata hivyo yote na yote yeye bado ni mama yangu na ninampenda sana" alizungumza Grace huku akililia kifuani kwa Jay.
"Usijali Grace nakuahidi kukuwekea ulinzi Siku zote za maisha yangu.....na Leo kama unahitaji nitakusindikiza ukamuone mama yako"
"Kweli Johnny"
"Ndiyo alijibu Jay na kutabasamu.
***** ****** *****
Ki ukweli ni kwamba Badra hakuweza kuhusika na mauaji yoyote Yale ambayo aliweza kuwekwa gerezani Bali kuna mtu ambaye aliweza kuufahamu mchezo huo na akatumia njia hiyo ili kujikwepesha yeye katika mikono ya polisi.
Badra akiwa gerezani alikuwa mwingi wa mawazo huku akiwaza ni nani huyo ambaye ameweza kumtengenezea yeye kesi na kucheza na sura yake.
"Lazima atakuwa Salhat hakuna mtu mwingine zaidi ya Salhat hao Ndiyo walioweza kunifanyia mimi hivi ili walipize kisasi chao. Alijiaminisha hivyo Grace.
Na hapo hapo aliweza kukumbuka ya kuwa Badra aliyeweza kumuuwa yule mtu wa pili alikuwa na Bangili mkononi ambayo alianza kufikiria ya kuwa hiyo bangili aliweza kumuona nayo nani.
Hapo hapo ulionekana mkono wa mtu uliokuwa umevalia Bangili ile ukisukuma moja kati ya geti zilizokuwa kwenye gereza lile na kuingia ndani.
"Salhat alisikika mtu akilitaja jina hilo.
Aligeuka Salhat na kutabasamu ni baada ya kumuona Akram.
"Hapana usiinuke......umekuja kunisalimia au!?? Aliuliza Akram.
"Hapana nimekuja kumuona Badra" alizungumza Salhat.
"Badra!!! Aliuliza Akram kwa mshangao kidogo na kumtazama Salhat.
"Mmmmhhh sawa" alijibu Akram na kuanza kumuelekeza Salhat.
"Badra akiwa pale aliambiwa kuna mgeni wake na mgeni Huyo alikuwa ni Grace.
Badra baada ya kumuona Grace alienda kumkumbatia na kisha akalia kwa machoz huku akimlilia mtoto ambaye aliweza kumlelea kama mtoto wake.
Grace alikaa chini huku akiyafuta machozi yake na kumshika mama yake mkono.
"Mama usijali mimi naamini hujafanya chochote na ninahakikisha kukutoa hapa" aliongea Grace na kumtizama mama yake ambaye alikuwa akiyatoa machozi tu.
Grace mwanangu alizungumza Badra na kuiinua mikono ya Grace juu huku akiwa ameshika.
"Mimi siyo.........kabla hajamalizia kuzungumza hapo hapo alishtuka na kukumbuka ya kuwa mtu aliyekuwa akiitumia sura yake alikuwa amevaa bangili na bangili hiyo aliweza kuionana mikononi mwa Grace sasa alishamkumbuka ya kuwa mtu ambaye alikuwa akihitaji kumkumbuka ni Grace.
Alimtizama Grace kwa macho makubwa na Grace Alimtizama.
"Kuna nini mama mbona unaniangalia hivyo??? Aliuliza Grace baada yakuona ya kuwa Badra anamtizama kwa macho makali.
"Grace unawezaje kunifanyia hivi??? Aliuliza Badra.
"Nimekufanyia nini kwani?? Aliuliza Grace.
"Wew ndiye uliyeweza kuwauwa watu wote wale kwa kutumia sura yangu sindiyo??? Aliuza Badra.
Grace Alimtizama kisha akatabasamu.
"Ni wewe sindyo" aliuliza tena Badra na wakati huu alimpiga kibao Grace.
.
Jay aliweza kuona na akaamua kuelekea ndani ambako kungeweza kumchukua dakika mbili kabla ya kufika huko.
Aliweza kufika na alishangaa baada ya kukutana na damu chini alipomtizama Grace alimkuta amelowa damu mwili mzima.
"Grace kipi kimekutokea mbona umelowa damu hivi?? Aliuliza Jay ambaye alipoangalia kwa umakini zaidi aliweza kumuona Grace akiwa ameshika bastola na aliuona mwili wa Badra ukiwa pale chini. Hpo hapo aliweza kuingia Akram na Salhat ambao na wao walijikuta wameshangaaa tu baada ya kukuta hali ambayo siyo ya kawaida ndani pale.
**** ***** *****
Baada ya kumzika Badra kwa heshima Kubwa hatimaye walikuwa wakitoka makaburini huku akionekana Jay kuwa karibu zaidi na Grace na Akram kuwa karibu zaidi na Salhat.
Huku Sheila akiwa karibu na Eddy ila Nasma alikosa wa kuwa karibu naye hivyo alijiondokea akiwa amenyong.onyea kwa mbali Akram alimuona na aliona Si vyema anavyofanya kwani Nasma kila Siku ndo mtu pekee ambaye anamtizama baba yake na anafanya baba yake anazidi kutengemaa zaidi.
"Samahani kidogo alizungumza Akram na kumuacha Salhat aliyekuwa akimsubiri kwa kusimama.
Nasma aliita Akram baada ya kumfikia karibu.
Nasma alifuta machozi yake kisha akageuka.
"Abeee" aliitika Nasma huku akiweka tabasamu usoni mwake.
"Ammmmhhhh unaendeleaje??? Aliuliza Akram.
"Vizuri tu alijibu Nasma.
"Unaelekea wapi sasa hivi nataka nikupeleke?? Aliuliza Akram.
"Naelekea hospitalini"
"Akram twende alizungumza Salhat na kumfanya Akram ageuke.
"Sawa nakuja" alimjibu Salhat na kumgeukia tena Nasma.
"Umesema unaenda hospitali"
"Usijali weww unawaza kwenda naye mimi nitaenda hospitalini mwenyewe alizungumza Nasma na kugeuka zake kisha akaendelea na safari zake.
Akram alishaweza kutambua ya kuwa Nasma anampenda sana tena Sana lakini hakutaka kujionyesha ya kwamba anajua kwani yeye hampendi na ahitaji kumuumiza hata kidogo.
Nasma alipofika mbele zaidi aliweza kukaa pembeni kisha akaanza kulia kwa Sauti akiwa hapo alishangaa baada ya kumuona Akram mbele yake alijikuta ameshindwa kujizuia na kumkumbatia kwa nguvu sana.
Wakati huo huo nao alionekana Akram akiwa ndani ya gari na Salhat.
Nasma alikuwa amekumbatiwa na Akram mwenyewe ila kwa upande wa Salhat alikuwa na Grace pasina kutambua ya kuw amechukua sura ya Akram na alikuwa akiendesha gari huku akisema.
"Siwezi kukuachia Johnny hata Mara moja kwani mimi ndiye niliyehusika na mauji yote hayo na hakuna atakayeweza kutambua mpaka pale ambako nitamaliza mchezo huu na Leo Ndiyo Siku ya mwisho ya maisha yako hapa duniani. Alizungumza Grace kimoyomoyo huku akimtizama Salhat na kutabasamu.
Simu ya Salhat iliita na aliipokea.
"Haloo.....Grace!!!! Aliita kwa mshangao na kumfanya Grace asimamishe gari kwa wasiwasi.
Sawa nimekuelewa.alizungumza huku akimtizama Grace pasina kujua ya kuwa siyo Akram.
"Nini mbona umeshika brake kwa haraka hivyo??? Aliuliza Salhat akikata simu yake.
"Hamna....nimekusikia ukitaja Grace"
"Ndiyo Johnny kaniambia hamuoni Grace kwahiyo alikuwa ananiuliza kama tumeondoka naye.
"Ahaaa hivyo sivyo" alijibu Grace na kuanza kuliendesha gari. Ghafla simu ya Salhat iliita tena na wakati huo Salhat alibaki akiitizama Simu na kumtizama Grace.
"Kuna nn tena????
"Simu yako iko wapi??? Aliuliza Salhat.
Grace alijifanya kujipapasa kama vile anaitafuta.
Salhat alimuonyeshea kwenye Simu yake kuwa jina la Akram ndilo linalompigia simu.
Salhat aliipokea ili kuisikilizia Sauti ila kabla hajisikia Grace alimnyang.anya na kuichukua simu kisha akaiweka masikioni yeye.
"Uko na Grace???? Lilikuwa swali lililoweza kutoka kwa Akram.
"Haloo....halooo...halooo" aliendelea kuita Akram baada ya kuona hakuna mtu anayeongea alihisi mtandao utakuwa unasumbua hivyo aliikata simu na kuendeelea kuendesha gari lake.
Salhat aliingiwa na mashaka kidogo huku akimtizama Akram feki aliyekuwa akimuendesha.
Nasma alifikishwa hadi hospitalini kisha Akram akamshika mkono wake na kuanza kuelekea ndani ya Hospitali hiyo ilikuwa furaha Kubwa sana kwa Nasma kwani alihisi kufarijika moyoni mwake.
Siku zilienda na kila Mara Grace aliweza kuzitumia sura zao hadi kuwachanganya wao kwa wao wasielewane kisha yeye atatumia wasaa huo vizuri kumtengenezea kesi Salhat na yeye aishie gerezani au kumuuwa kwa kupitia sura ya mtu mwingine.
Siku moja Nasma alikuwa ndani ya chumba cha wodi na Akram ambaye alikuja kumtembelea baba yake ambaye aliweza kufumbua na kuyafumba macho yake tu hadi wakati huo.
Akram alitoka njee kidogo kwaajili ya kwenda kumchukua Salhat aliyekuwa amefika hospitalini hapo na yeye akitaka kumuona baba yake.
Hivyo ndani alibaki Nasma na Baba yake Akram.
Grace aliingia mpaka ndani ambapo alipofika tu aliijibadilisha sura yake na kuwa ya Salhat kisha akapiga hatua za kwenda mbele.
"Nasma" aliita Grace kwa sura ya Salhat.
"Ahaaa Salhat..... Akram ameenda njee kukuchukua kumbe ulikuwa umeshafika maeneo ya karibu na nani kakuelekeza hapa?? Ngoja nimpigie simu nimwambie ya kuwa umeshafika" aliinua simu yake na kutaka kumpigia lakini ghafla alishtukia kibao kilichoweza kushuka katika upande wake wa kushoto wa shavu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alibaki akimtizama Grace na kusema Salhat.
"Iwe Mara ya mwanzo na ya mwisho kumfuata fuata Akram kila mahali anakoenda Akram ananipenda mimi hata wew hilo unalitambua kwanini unamng.ang.aniza akupende wewe. ......kila Mara Akram ananiambia ya kuwa wewe umekuwa kero kwa upande wake kila Siku uko hospitalini kama nesi ilihali yeye tayri ameshamuandaa nesi wa kumlea baba yake hivyo kaa mbali naye usipende kujisogeza karibu na yeye hilo ni onyo umenisikia wew kahaba unayejitongozesha kwa Akram"
Neno lile la kuitwa kahaba liliweza kujirudia takribani Mara tatu katika kichwa cha Nasma. Nasma alikimbia na kutoka njee ya Chumba kile Grace alitabasamu na kumuangalia mzee Saidi ambaye alionekana kukasirishwa na maneno ya Salhat huku akiyatoa macho makubwa sana
Hapo hapo mlango ulikuwa ukisukumwa na aliichukua sura ya Nasma kitendo hicho Mzee Saidi alikiona lakini hakuwa na nguvu ya kuongea wala kuonyesha chochote kile.
"Nasma mambo" alisalimiwa na Salhat.
Lakini Grace Alimtizama tu na kutoka njee huku akimpiga kikumbo.
"Anashida gani huyu?? Aliuliza Akram akimshangaa Nasma kwani hiyo tabia hakuwahi kumuona nayo.
Nasma alikimbilia chooni na huko alilia sana baada ya muda alirudi katika chumba kile na hapo alimkuta Akram akikita chungwa na kumkamulia Salhat kwenye glass kisha kumnywesha mdomoni. Alikumbuka Yale Yale maneno aliyoweza kuambiwa na Grace huku akiamini ni maneno aliyoweza kuambiwa na Salhat.
Alirudishia mlango wake taratibu kabisa kisha akaondoka zake.
**** **** ******
Siku iliyofauta.
Nasma akiwa yuko hospitalini aliingia Akram ndani akaleta Machungwa kisha akayaweka pembeni bila salamu.
"Akram" aliita Nasma lakini kutokana na alivyogeukiwa na Akram Alitizama tu chini bila kusema neno.
"Nataka nimuweke nurse hapa kwahiyo sitaki ung.any.anie kukaa hapa" alisema na kutoka njee baada tu ya kufika njee alibadilika na alikuwa ni Grace wala siyo Akram.
Wakati huo nao Alioneka Salhat akija na msichana mmoja pamoja na Akram.
Waliingia ndani ya chumba na Nasma aliyafuta machozi yake kitendo kile Akram alifanikiwa kukiona lakini hakukitilia maanani hata kidogo.
"Nasma unaendleaje humu ndani"
Nasma Alimtizama tu na kuona ya kuwa anamuenjoy lakini akamjibu tu.
"Salama"
Nasma Alimtizama mgeni yule ana kuelew kabisa ni nurse.
Alichukua pochi yake na kuweka vitu vyake vidogo vidogo ambavyo havikuwa ndani ya pochi.
"Salhat alisema ya kuwa ni vizuri kama tutamleta msaidizi hapa kwani unatumia Siku zote saba ukiwa hapa mwenyewe na unachoka sana kwahiyo nimekuletea msaidizi kwamba ukitaka kwenda nyumbani utaenda kisha..........
"Haina haja ya kujielezea" alizungumza Nasma kisha akaweka mkoba wake begani.
"Nimeshampatia juice ya maembe sasa hivyo kaa baada ya Masaa mawili kisha umkamulie juice ya machngwa....ndani ya hayo Masaa mawili uchukue kila nusu saa kumkanda miguu na mikono yake kwa maji ya vuguvugu utakayoyachemsha kwemye ile hitter pale.
"Usimpatie juice ya mapapai wla tikitiki kwani humuumiza tumbo ukitaka kumpatia ndizi iweke kwanza kwenye maji ya moto kisha ikipata moto umpondee na kumpa kila anywapo juice hukaa baada ya dakika thelathini kisha ataachia haja. Toa Mpira kisha muite docta am badilishe alizungumza nasma kisha akawapisha wote na kuondoka zake.
Akram alibaki akiwa amesimama mpaka machozi yakamtoka kwani hakuwahi kutegemee kama kuna mtu hata Siku moja ataweza tambua baba yake anapenda nini hapendi nn na mtu atakayeweza kumjali baba yake kwa kiasi hicho.
Hata yeye ni baba yake lakini hakuweza kutambua kipi baba yake anapenda na kipi hapendi .
Alitaka kufungua mlango kwaajili ya kumfuata Nasma lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa njee akiamini ya kuwa aliyefunga ni Nasma lakini siyo aliyefunga ni Grace na alikuwa pembeni tu ya hapo mlango ni.
Nasma alikuwa akitembea huku machozi yakimtoka na na hatimaye aliamua kukimbia na kuondoka kabisa karibu na eneo hilo.
Akram alijitahid kupiga simu lakini haikupokelewa alikuwa akizungumza usiku kucha kumtafuta Nasma kwani hata nyumbni pia hakuelekea.
Kulikucha asubuhi bila mafanikio yoyote Yale.
"Unajua mimi sikuongea kwa ubaya kwani nilihitaji na yeye apate muda wa kupumzika sasa yeye akanichukulia vibaya" alizungumza Akram akimuelezea Sheilah Eddy Jay pamoja na Salhat.
"Jay Si unaweza kumtafuta embu mtafute basi."
"Sasa hivi makelele ni mengi sana nitaumia sana masikioni mimi" alizungumza Jay.
Akrama Alimtizama Jay huku machozi yakamtoka kisha akapiga magoti na kusema Tafadhali naomba unisaidie kwahilo"
Watu wote wlimshangaa Akram hata Jay alishangaa na kwenda kumuinua
"Me nilikuwa nakutania kwanni sasa ukafanya hivyo" alizungumza Jay kisha akayafumba macho yake na kuanza kumtafuta Nasma.
Jay alimshika mkono na kuingia ndani ya mawazo yake hivyo kila ambacho anachokiwaza Johnny yeye anaweza kukisoma na kukiona pia.
Walitumia muda mwingi sana wakiwa katika hali hiyo hadi majasho yakaanza kuwatoka wakimtafuta Nasma.
Sheila na Eddy na wao walishikana mikono wakitizama kama wanaweza kumpata Nasma.
Salhat aliendelesha kuwafuata Akram na Jay kwa kitambaa cha maji ya baridi.
"Rudi nyuma" alizungumza Akram.
"Wapi??? Aliuliza Akram.
"Juu ya huo mti mrefu nahisi kama Nasma yuko hapo kwani nimeona chozi lake likidondoka"
Jay alifanya alivyoambiwa na ni kweli alikuwa Nasma katikati ya msitu akilia.
"Twende" alisema Akram na kuyafumbua macho yake.
Walishikna mikono watu wote watano kisha wakapotea.
Wakti hayo yote yakitokea Grace alikuwa akiwatizama.
"Wpauuzi hawa nitatafuta njia yoyote ya kuwatenganisha lazima"
Grace aliweza kuondoka huku akisema.
"Inabidi nipate nguvu zaidi kwaajili ya kuweza kuwafanya wote hawa kupambana"
***** ***** *****
Waliweza kufika katikati ya msitu ambako Nasma alikuwa juu kabisa.
"Nani kawaambia mje huku nyie?? Aliuliza Nasma baada ya kuwaona chini.
"Nasma nimekutafuta sana eti!! Kwanini umekuja huku??? Aliuliza Akram.
"Kwani wewe umefuata nini huku we ondoka zako Si uko na Salhat hapo unataka nini tena kutoka kwangu??? Aliuliza Nasma.
"Wewe usijaribu kukimbia tena me Sitakuwa na muda wa kukutafuta zaidi mpaka sasa masikio yangu ynauma alizungumza Jay.
"Haya tuondokeni Nasma atakuja na Akram mwnyewe alizungumza Salhat kisha akamshika mkono Jay na kupotea naye wakati huo nao Sheilah alipotea na Eddy naye alimshika bega Akram na kuondoka zake.
Alibaki Nasma aliyekuwa akimtizama Akram na kupindisha mdomo wake.
"Nasma kwanini ulichukia kiasi kile jamni, me niliona ya kuwa ni vyema nikikuletea msaidizi ili na wewe upumzike lakini wewe ukachukulia hasira na kuondoka tu"
"Kwanini hukunipa ya kuchagua jibu nwenyewe ukaja Mara ya kwanza na kuniambia ya kuwa niondoke na nising.ang.anie alafu Mara ya pili ukaja na Salhat na kunifanya ya kuwa unakuja....... Alizungumza Nasma.
"Unaongelea nini wewe mbona sikuelewi?? Aliuliza Akram akiwa hajamuelewa ni kipi alichoweza kukizungumza Nasma.
Nasma Alimtizama tu bila kusema neno lolote lile.
***** ******* *******
Salhat alikuwa na Jay huku wakiwa wamekaa katika kochi moja na Salhat akiwa amemlalia Jay kifuani mwake.
"Jay"
"Naam"
"Unajua kuna vitu sivielewi juu ya Grace"
"Unamaanisha nini?? Aliuliza Jay.
"Kuna Siku nilimuona akitoka nyumbani usiku na alichelewa kurudi sana..... Alafu pia kama kuna kitu nilikiona lakini nilishindwa kuelewa" aliongezea Salhat.
"Hapo sijakuelewa hata ulichokiongea"
"Namaanisha nilipokuwa namfuata nyuma......."
Kabla hajamaliza kuzungumza aliingia Grace.
Salhat alihitaji kuamka lakini Jay alimzuia na kumkalisha pale pale.
"Ammmhhh basi me nilikuwa natak nitoke kidogo tu" alizungumza Grace.
"Usijali wala usiombe ruhusa unaweza ukaenda popote utakapo kwani wew siyo mtoto tena" aliongea Jay na kumfanya Grace atabasamu aliondoka huku akimtizama Salhat aliyekuwa kifuani kwa Jay wakati huo.
Salhat nilikuwa naomba nitumie gari lako Mara moja kwani la kwangu limeisha mafuta. Aliomba Grace.
"Lakwangu pia halina mafuta Grace" aliongea Salhat.
"Tumia la kwangu" aliongea Akram na kumpatia ufunguo uliokuaa juu ya meza.
Grace aliuchukua na kutabasamu baada ya kufika mbali kidogo aliutupa ufunguo huo na kuongea kwa hasira.
"Mpuzi wew........... Umejitoa katika hili Leo lakini hutoweza kujitoa tena kwa Siku za mbeleni nakuapia kwa hilo" aliongea Grace kwa hasira na kutoka njee.
***** ***** ******
Akram alikuwa polisi huku akiendelea kufanya kazi zake akiwa pale alihisi amemuona Grace akiwa njee ya kituo cha polisi.
"Grace amekuja kufanya nini hapa? Alijiuliza na wakati huo alitoka njee ilia mfuate Grace na ajue anashida gani.
Alimuona Grace akiingia katika chumba kimoja na Akram alimuona.
"Huko ameenda kufanya nini??" aliuliza na kumfuata lakini alshngaa baada ya kupamiana na Salhat akitoka huko.
Alitizama ndani ya kile chumba na hakukuwa na mtu mwingine tena ndani ya kile chumba.
"Mbona kama nimemuona Grace akiingia huku" aliuliza Akram kwa kushangaa.
Hata Grace alishngaa kwani yeye ndiye aliyeingia na kutoka kwa sura ya Salhat.
"Una.....una.....unamaanisha nini wewe??? Aliuliza Grace baada ya kujua ya kuwa alionekana.
"Nimemuona Grace kabisa akiingia ndani huku" alirudia tena Akram.
"Itakuwa hujaona vizuri mimi ndiye niliyeweza kuingia ndani wala Grace hayupo hapa" alijiby Grace akiwa katika sura ya Salhat.
Akram alifikiria kwa muda kisha akaona ni sawa tu.
Grace Alimtizama kwa hasira na kutazama pembeni kisha akazungumza
" Kwanini kaniona huyu kichaaa sitaweza kufanya tena kile ambacho kimenileta hapa".
Akram bado alikuwa akiwaza huku akimtizama Salhat kwa sura nyingine kabisa.
**** ***** ****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika ukoo wa Abandandi Malikia aliweza kupatiwa taarifa za kuuwawa kwa Badra ambaye alikuwa mtoto wa Malikia wa koo hiyo.
"Kwa kile walichoweza kukifanya sitaweza kuwasamehe hata mmoja.......kwanzia Leo na kuendelea tunatangaza vita juu ya binadamu wote wanaoishi duniani kwa kosa la kumuuwa princess wa ukoo wetu" alitangaza vita hivyo Malikia wa abandandi na kufanya Majini wote wliokuwa kule wapige vigelegele kwa kushangilia vita ambavyo wanataka kuanzisha na binadamu.
Katika miliki ya Malikia ya ukoo wa Sultan aliweza kuzipata habari hizo.
Alijua sasa wakati wa vita vimeanza hivyo watu wote wale walipaswa kuwa makini katika kuhakikisha ya kuwa maisha ya binadamu yanakuwa salama kabisa.
****** ****** ******
Johnny alikuwa ndani huku akitizama TV na Grace aliyekuwa amevalia gauni fupi sana huku akiwa ameketi katika hali ambayo ingeweza kumtamanisha mwanaume yoyote yule ambaye angeweza kumuona.
Jay alikaa pale huku akitizama TV lakini baada ya kuona ya kuwa Grace anaanza kuyafanya mmbo ambayo alishaelewa ya kuwa anahitaji kitu basi alisimama na kuanza kuondoka zake.
"Jay" aliita Grace na kuinuka pale alipokuwa amekaa na kumfuata Johnny.
Alipofika akimkumbatia kwa nguvu na kuanza kumbusu shingoni.
"Unashida gani wewe?? Aliuliza Jay akijitahidi kurudi nyuma lakini Grace alimng.ang.ania na kuendelea kumbusu zaidi huku akianza kuvua nguo yake ya juu.
Jay aliishika kwaajili ya kuhitaji kuirudisha lakini akiwa anafanya hivyo Salhat aliingia ndani na kujua ya kuwa Johnny alikuwa akimvua nguo ya juu Grace.
Wote waliacha baada ya kumuona Salhat. Grace aliishusha nguo yak chini vizuri kisha akamtizama Salhat.
"Me sijafanya chochote alizungumza Jay huku Salhat akimtizama shati lake ambalo liliweza kutoka vifungo wakati wa purukushani na lipsi zilizowez kubaki katika Shati lake.......
Baada ya kujitizama alishindwa kuzungumza kitu akabaki tu.
"Ni kweli lakini sijafanya kitu" alirudia tena neno hilo huku akimtizama Salhat aliyekuwa akidondosha machozi.
Alitoka njee na kuwaacha pale
Jay alimgeukia Grace na kumwambia.
"Nikirudi nisikukute tena hapa" alizungumza kwa hasira na kutoka njee kwaajili ya kumfuata Salhat.
Grace alicheka na kusema "huwezi kunifukuza mimi ndani ya nyumba yako unatakiwa umfukuze Salhat kwani yeye ndiye aliyeweza kuyaingilia mapenzi yetu"
**** ***** ****
Alionekana Grace akiwa anapita katika kimsitu kidogo na kuelekea sehenu ambayo ilikuwa tofauti kabisa na mazingira ya kawaida akiwa anaelekea huko huku akiwa amekamata kuku mwekundu mkubwa na akiwa amevalia nguo nyekundu zote.
.
Akiwa anakaribia kufika huko ambako alikuwa akielekea vilianza kusikika vimilio vya kama mtu anapiga Ngoma na kuchezea kengele aliweza kufika katika kijumba kidogo kilichoweza kuzindikwa na majani tu. Aliingia na hapo alikuwepo mganga mmoja mwanamke aliyeweza kucheka baada ya kumuona Grace.
"Nafikiri mambo yako yameenda sawa"
"Ndiyo ila bado nguvu ulizonipa hazijaweza kutosha nahitaji nguvu zaidi ya kuweza kufanya mambo mengi zaidi" aliongea Grace na kutabasamu.
"Unataka nguvu gani tena??? Aliuliza mganga yule huku akimpapasa kuku yule".
.
Grace alitabasamu na kuifikiria sura ya Salhat kichwani mwake .
Huku nako alionekana Akram akiwa amenunua cheni barabarani na akielekea hospitalini.
Alipofika alimkuta Nasma akiwa amelala katika mkono wa baba yake aliokuwa akiukanda. Alimtoa kitambaa kilichokuwa mikononi mwake kisha akakiweka pembeni na kumuinua katika kiti kisha akaweza kwenda kumlaza katika sofa lililokuwa eneo lile..
Alisimama hapo na kuanza kumkagua uso wake huku akitabasamu na kuchekacheka pasina yeye mwenyewe kujua ya kuwa anafanya hivyo.
Alihisi mlango umefunguliwa na aligeuka nyuma kutizama.
Aliingia dactari ambaye alimuomba waongee njee kidogo.
"Hali ya baba yako imezidi kuwa nzuri na kutengamaa kabisa hivyo nilikuwa naona ni vyema kama ungeweza kumpeleka nyumbani akapate Huduma ndogondogo natumaini ata endelea kuwa sawa. Alizungumza dactari huku aki sign sign makaratasi na kumpatia Akram.
"Alafu pia mke wako ni mwanamke mzuri sana amekaa kwa kipindi kichache tu na baba yako lakini ameweza kufanya akawa katika hali nzuri ......alafu nilitaka kukushauri ya kuwa mumpatie muda mwingi wa kupumzika kwani anatoka wodini saa5 usiku na Saa11 tayri ameshafika hiyo pia ni mbaya kwa afya yake" alishauri dactari na kumpa maelekezo zaidi ya zile karatasi alizoweza kumpatia.
**** ***** *****
Huku nako Alioneka Grace akiwa ndani ya gari lake na kumpigia Simu mtu ambaye hatukuweza kufanikiwa kumtambua ni nani.
Baada ya kumaliza kuzungumza aliyohisi ni sahihi kwake alikata simu kisha akasema
"Nasma nikianza na wew itakuwa vizuri zaidi kwani nahitaji kujua kama hizi nguvu nilizoweza kupatiwa Leo zinafanya kazi amah lah" alitabasamu na kuongeza mwendo wa gari.
Aliweza kuingia katika wodi ya baba yake Akram akiwa katika sura ya Akram na dactari alimuona kisha akaamua kumfuata.
"Bwana Akram" aliita dactari na kumfanha Grace aache kufungua mlango kisha kumtizama dactari.
"Kuna ulichosahau tena??? Aliuliza.
"Hapana kwani kuna shida yoyote?? Aliuliza Grace aliyekuwa hana taarifa ya kuwa Mzee Saidi tayri ameshampelekwa nyumbni mwake.
"Namaanisha tayri umeshaondoka na baba yako na wodi hiyo tayri tumeshampatia mgonjwa mwingine kwahiyo Si ruhusa kwa wew kuingia tena ndani hapo" aliongea Dactari na kumfanya Grace ashtuke na awe na wasiwasi wa kushindwa kujibu ya kuwa alikuwa anafuata nini.
"Nimekuelewa dactari ila nilisahau simu yangu ndo nimeirudia" alizungumza Grace.
Na wakti huo huo alitokea nesi mmoja na kumpa Simu ya Akram huku akisema
"Nilikutunzia"
Grace alichukua na kumshukuru Kisha kuaga ya kuwa anaondoka. Alikuwa akitoka huku akilalamika kwani mipango yake yote ya Siku hiyo iliweza kufeli.
Alianza kuelekea kutoka njee na wakati huo huo Akram wa kweli alikuwa akirudi ili kuja kuichukua simu yake na katika mlango huo huo wa kuingilia Ndiyo mlango ambao Grace alikuwa akiutokea. Wakiwa wamekaribiana kukutana ghafla walipita manesi waliokuwa wakikimbiza mgonjwa katikati yao na kufanya wasionane.
Akram alifika na docta alimuuliza.
"Umesahau nini tena kingine???
"Unamaanisha nini unaposema kingine?!! Aliuliza Akram aliyekuwa hajamuelewa docta alichokuwa akikizungumza.
Ghafla alikuja nesi na kusema "docta unaweza ukaenda Mimi nitazungumza naye"
Dactari aliondoka na kuwaacha hapo wala hakuwa nesi Bali ni Grace aliyoweza kujibadili katika umbo lile baada ya kumuona Akram akiingia ndani.
Dactari akiwa anaelekea kwenye chumba cha wagonjwa kwaajili ya kwenda kuwahudumia alishangaa baada ya kumuona tena nesi yule.
"Nesi Carolina umefikaje huku na nilikuacha na Akram??
"Nani huyo!! Mimi nilishaachana na Akram baada tu ya kumpa Simu yake pale pale ndo nikaja huku kwa wagonjwa" aliongezea Nesi huyo.
Docta Alimtizama na kukumbuka ya kuwa alimuona Akram akiwa na Carolina sasa hivi imekuwaje huyo aseme ya kuwa hayuko naye?? Alimtizama kwa kupepesa macho yake ila baadaye alijipiga kichwa chake huku akisema.
"Haka kapombe nilikokanywa asubuhi asubuhi kananifanya naona wtu Mara mbili mbili"
****** ****** ******
Jay akiwa amekaa nyumbani mwake ghafla alianza kuzisikia kengele za ajaby ajabu zilizokuwa hazieleweki kichwani mwake.
"Ni nini tena hii??? Aliuliza baada ya kuona ya kuwa kelele hizo haziachi kuzisikika.
Baadaye akiwa amekutana na Eddy aliweza kumueleza na hata Eddy alishindwa kumpa ufafanuzi juu ya hilo.
"Unazisikia sasa?? Aliuliza.
"Hapana"
"Basi muda mwingine ukizisikia ziwekee umakini sana na uhakikishe unatambua ni sehemu gani zinatokea kisha umkariri huyo mtu sura yake labda inamaana Kubwa sana kwa upande wetu" alitoa ushari huo Eddy na Jay alikubaliana nao.
******* **********
Nasma akiwa ndani ya nyumba ya Akram alimkuta Akram akiwa mwingi wa mawazo Sana.
"Akram.......Akram...... Akram!!!! Aliita zaidi ya Mara mbili na Akram alishtukia huko kwenye mawazo yake.
"Unashida gani maana hata nimekuandalia chai hujanywa mpaka imepoa? Aliuliza Nasma na kukaa karibu naye.
"Unajua kuna vitu vinazidi kunichanganya changanya na sivielewi"
'Kivipi?? Aliuliza Nasma.
"Jana kama vile nimejiona mimi alafu nashindwa kuelewa nimejionaje"
Nasma alicheka tu na kumtizama
"Sasa kama ulijitizama kwenye kioo Kwanini usijione?? Aliuliza akiwa bado hajamuelewa Akram.
"Hapana naamaanisha nilipoenda hospitalini kama nilipishana na mtu kama mimi lakini sikumuwekea mkazo"
"Sasa hiyo itakuwaje....au labda mlizaliwa mapacha?? Aliuliza Nasma.
"Sidhani"
"Si ulisema aliyekuwa akikulipia wewe kila kitu ni mfadhili ambaye humfahamu basi labda atakuwa ndo huyo" alishauri Nasma na kushangaa baada ya Akram kuganda kwa sekunde kadhaa huku akimtizama
"Nini mbona unanitizama hivyo?? Aliuliza huku akijishika shika uso wake.
Akram alimkumbati na kumwambia.
"Kweli wewe unaakili ni sawa yule atakuwa ndo yule mfadhili aliyekuwa akinilipia mimi ada na kila kitu yule atakuwa ni ndugu yangu maana amefanana na mimi kwa kila kitu" aliongea akram na kuchka.
Lakini nyuma yao alikuwa Grace aliyekuwa amejibanza kordo moja na kucheka baada ya kusikia wakiongea upuuzi wao.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila Nasma alihisi kuna uwepo wa mtu ndani hapo lakini hakutilia maanani aliendlea kulifurahia kumbatatio hilo..
***** ***** *****
Huku nako katika ukoo wa Abandadi uliweza kuletwa mwili ya Badra uliokuwa umeoza vibaya sana na hata kutoa harufu Kali kupitiliza.
Mama yake alikuja akamtizama mwanaye ambaye mwili wake tayri ulishaanza kulia na wadudu wa ardhi huku akisema.
"Lau kama wangelikuwaa kama Jini basi ningekurudishia uhai tena lakini waliweza kukugeuza binadamu kisha wakakuuwa.
Alimchkua mdudu mmoja aliyekuwa akipita katika mwili wa Badra na kumtupia mdomoni mwake kisha akamtafuta na kusema.
"Nitawatafuna wote walioweza kukufanya wew katika hali hii kama mdudu huyu alivyoweza kuuutafuna mwili wako" alikuwa kiapo Malikia wa Abandadi
***** ****** ******
Jay akiwa anarudi zake nyumbni aliweza kuiona gari ya Akram ikiw imepakiwa pembeni kabisa.
Alimpigia Simu kumuuliza yuko wp lakini simu yake haikipokelewa ni kutokana na kwamba Akram alikuwa polisi huku akimuhoji mtuhumiwa mmoja juu ya kosa lililoweza kumfikisha yeye mahli pale.
Jay alikiona kinjia ambacho kilikuwa kikielekea katika restaurant moja iliyokuwa karibu na eneo lile.
Alipoweza kukaribia restaurant ile alishangaa baada ya kumuona Akram akiwa amepiga magoti na ameishikilia Pete ya uchumba alitaka kumvika Salhat.
"Huyu mbwa anawezaje kufanya hivyo ilihali anatambua ya kuwa Salhat ni mke wangu mimi" aliongea kwa hasira sana lakini hasira zake zote ziliisha baada ya kumuona Salhat akimpa mkono Akram ishara ya kuwa amvike Pete hiyo na baada ya kuvikwa alimpiga busu na watu waliokuwa pale waliweza kushangilia na kuwpa hongera.
Jay alianza kurudi nyuma taratibu taratibu na hatimaye alianza kutembea kinyonge katika eneo lile.
Akram Alitizama na Salhat kisha wakacheka kwa pamoja kwani waliweza kumuona.
Wakati huo nao lilionekana gari la Salhat likipaki maeneo Yale na hatimaye alishuka.
"Huyu Jay huku akaja kufanya nini ??? Alijiuliza akipiga hatua za kwende mbela kupitia kinjia kile kile alichokuwa akirudia nacho Jay
Unafikiri kipi kitafuata pale ambapo Jay ataweza kugongana na Salhat ilihali ya kuw aliyemuacha akivishwa Pete ni Salhat.
Zikiwa zimebaki hatua chache sana kabla ya watu hao kukutana simu ya Salhat iliweza kuita na wakati akiinama katika pochi yake kwaajili ya kuitizama simu yake.
Jay aliweza kumpita pasina kumuona Salhat wala Salhat kumuona Jay.
"Haloo" ilikuwa Sauti ya Akram.
"Uko na Jay??? Aliuliza Akram.
"Hapana sipo naye" alijibu Salhat.
"Nimekuta mised call yake nimejaribu kumpigia lakini hapokei Simu sasa sijui Kwanini alafu katika moyo wangu nahisi maumivu sana nahisi kuna jambo litakuwa limemtokea Jay" alizungumza Akram.
Gari lake nimeliona sehemu flani hivi na mimi Ndiyo napanda kwenda kummuangalia usijali nitakupa taarifa zaidi alizungumza Salhat na kukata Simu.
Alishangaa baada ya kutokea sehemu ambayo alishindwa ielewa ikoje.
"Jamani mbona kama niliona kuna nyumba hapa na kama kulikuwa na kelele za vigelegele alijiuliza Salhat baada ya kukuta vichaka chichaka tu visivyoweza kueleweka.
Alipogeuka nyuma na kuitizama njia aliyotokea hakukuwa na njia tena Bali manyasi nyasi tu.
"Hivi ni kwamba naota au Ndiyo naona" alijiuliza bila kupata jibu.
Ila ngoja nitadhibitisha alianza kurudi nyuma na kwenda kutizama kama angeliweza kuliona gari la Jay tena lakini hakukuwa na gari jingine tofauti na lake.
Alisimama kwa muda akitafakari ni kuwa yuko kitandani amah lah.
Aliweza kurudi nyumbani na kabla hajafika ndani aliweza kuiona Pete chini ambayo ilimvutia na kutaka kuichukua lakini ghafla Grace alitokea.
"Unataka kuivaa??? Aliuliza huku akimtizama kwa machl ambayo yalimfanya Salhat atingishe tu kichwa kama zezeta flani ambaye aliweza kukubaliana na kile alichoweza kuambiwa na Grace.
"Nipe mkono wako" alitoa amri hiyo Grace na Salhat alifanya kama vile alivyoambiwa afanye.
Grace alimvalisha huku akicheka na kutabasamu zake baada ya hapo alimwambia unaweza kwenda kwenye chumba chako ukapumzike kisha ndo utoke baada ya dakika tano Jay yupo sebleni.
Salhat alitikisa kichwa kisha moja kwa moja akaanza kuelekea chumbani akiwa katika hali ya kutokujielewa wala kutokujitambua.
Grace alitabasamu kisha akaikunja mikono yake mbele ya kifua chake na kuelekea sebleni alipo Jay.
Baada ya Salhat kurejea katika ufahamu wake wa akili aliweza kutoka chumbani na kuelekea sebleni ambako alimkuta Jay amekaa huku glass moja ikiwa mezani.
Alielekea mpaka kwenye kochi aliloweza kukaa Jay na yeye akakaa huku akiwa amekishika kichwa chake.
Aliinua glass iliyokuwa iko mezani na kuipeleka mdomoni akiamini ni maji.
Alitema baada ya kugundua ni pombe.
"Jay" aliita kwa kustaajabu
Jay Alimtizama tu bila kusema neno.
"Mbona hii ni pombe.....umeanza lini tena kuanza kunywa pombe??? Aliuliza Salhat.
Jay aliivuta glass yake na kuanza kuipeleka mdomoni.
Salhat alimnyang.anya na kuiweka pembeni.
"Inamaana hujanisikia nilichokuuliza au??? Aliuliza tena Salhat.
Jay alisimama na kuanza kuondoka zake
"Johnny" aliita tena na kwenda mbele yake.
Ghafla simu yake iliita.
"Haloo....Akram" alipokea simu hiyo na Jay alimnyang.anya kisha akaiweka masikioni mwake.
"Vipi hali yake??? Anaendlea vizuri??? Mbona bado me moyo wangu unaniuma sana??? Aliuliza Akram baada ya kuona hakuna mtu anayemuitikia aliita.
"Salhat!!! Haloool!!! Salhat!!!!
"Akram" aliita Jay kwa Sauti ya utaratibu.
"Ni wewe Jay… unashida gani Leo mbona moyo wangu unaniuma sana na nahisi maumivu Haya ni moyo wako. Kuna tatizo lolote" aliongea Akram.
"Tafadhali naomba ukae mbali na Salhat wangu.....yeye ni mke wangu nakuomba hilo"
"Mbona sikuelew unamanisha nini??? Aliuliza Akram lakini ghafla simu ilikatwa.
"Unashida gani wewe......na Kwanini umemamwabia Akram maneno hayo" alizungumza Salhat.
Lkini Jay alitoka hpo na kuelekea katika chumba chake.
"Grace unatambua ni kitu gani kimemkuta Jay??? Aliuliza Salhat.
Grace alitingisha kichwa ishara ya kwamba hajui ilihali anaelewa mchezo alioweza kuucheza peke yake.
Kwani kwasasa aliweza kuongezewa nguvu zaidi na angewez hata kugawanyika Mara mia moja kwa sura zozote zile alinazoweza kuzitaka yeye.
****** ******** *******
Akram akiwa amerudi nyumbanu aliweza kupokelewa mkoba wake na Nasma kisha yeye akakaa sebleni huku akiushika moyo wake na kujiongelesha mwenyewe.
"Kwanini Jay kaniambia maneno ya namna hayo mimi" alibaki akijiuliza tu pasina kupata jibu lolote lile.
Kesho yake aliweza kumpigia simu Salhat wakutane mahali na Ndivyo ilivyokuwa.
"Kuna shida gani mbona jana Jay ameniongelesha hivyo? Aliuliza Akram.
"Hata mimi sielewi kwani Ndiyo kwa Mara ya kwanza namuona Jay akiwa katika hali hiyo chaajabu ni kuwa nikimuuliza hanijibu"
"Inawezekana kuna kitu kiliweza kutokea jana wakati alipokuwa akipiga simu kwani majira ya saa 9 alikuwa wapi??? Aliuliza Akram.
"Kwa kweli mimi sijui maana hanisemeshi chochote kile" alizungumza Salhat alifikiria tukio la jana ila alihisi ni mawenge yake tu hivyo hawezi kumwmbia mtu akamuelewa kwani ni kitu ambacho hakiwezekani.
Mida ilienda na nyakati zikaweza kusonga mbele Akram alikuwa akirudi nyumbani alishangaa baada ya kukuta nyumba katika hali ambayo alishindwa kuelewa ni kipi kimetokea mpaka nyumba ikawa katika hali ile ya kuvurugika vurugika kila mahali.
"Nasma alianza kuita na kukimbilia katika chumba cha baba yake hapo alimkuta baha yake akiwa katika hali ya taharuki na kutaka kuzungumza jambo lakini alishindwa.
"Baba kipi kimetokea??? Aliuliza Akram akimuuliza baba yake ambaye alijitahidi kuzungumza lakini alishindwa.
"Nasma yuko wapi Tafadhali baba jitahidi uniambie mahli alipo Nasma" alizungumza Akram huku akiwa anatoa machozi.
Baba yake yye alijitahidi kumuonyesha kwa sign za machoni lkini Akram hakuweza kuelewa.
Hatimaye mzee Saidi alijitajihidi hadi akauinua mkono wake na kumuelekezea Mahali alipo Nasma.
Alielekezea upande wa bafuni kisha akaushusha mkono wake baada ya kuhisi maumivu makli sana.
Akram alienda na kuufungua mlango wa nguvu. Alishtuka baada ya kukuta mavazi ya Nasma yakiwa yameraruliwa raruliwa na kuchanika vibaya sana huku Nasma akiwa ameshalia va kutosha na sasa alibaki akiguguma tu huku akijikumbtia mwili wake.
Akram alivua Shati lake kisha akamvalisha na kumtoa taratibu kabisa hadi kumpeleka chumbani kwake ambapo alimklisha kitandani na kumuuliza.
"Nani kafanya hivi???? Aliuliza huku akiwa mwingi wa hasira na jazba.
Jay akiwa nyumbani kwake anatizama TV aliingia Akram akiwa na hasira sana na alipofika hakuzungumza na yeye zaidi ya kumuinua kwenye kochi na kumpiga ngumi.
Eddy alikuwa maeneo Yale alisimama kisha akaenda kumzuia Akram aliyekuwa akijitahidi kutoka mikononi mwake.
Grace na yeye alimfuata Jay aliyekuwa yuko chini huku damu zikimtoka mdomoni.
"Nakwambia hivi kaa mbali na Nasma kama kuna chochote kinachokukera juu yangu pambana na mimi lakini usije ukamguse tena Nasma kwamaana sitakucha mzima Jay" alizungumza kwa hasira Akram kisha akajitoa mikononi mwa Eddy na kuondoka zake.
"Anaongelea nini huyo?? Aliuliza Jay aliyekuw hafahamu ni kipi chanzo cha kupigwa kwake.
Grace Alimtizama kwa hasira sana Akram aliyekuwa akipotelea mbele ya macho yake.
"Mshenzi wewe unkuja kumpiga Jay wangu kwajili ya huyo Nasma kisa tu nilitumia sura ya Jay kuja kujifanya nahitaji kum baka sindiyo ......sasa nitakuonyesha adhabu ya kumpiga Jay wangu" alizungumza kimoyomoyo huku akimtizama Akram aliyekuwa akipotea.
Alitokea Salhat ambaye Alimtizama kwa hasira sana kisha na yeye akarudi alikotoka kwani aliweza kuja na Akram kwa pamoja.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hivi ni nini kinaendelea mbona siwaelewi.....Jay kuna tatizo gani baina yako na Akram???
Jay Alimtizama tu kisha akainuka na kuondoka zake eneo lile.
Unafikiri kipi kitafuata baada ya Jay kusimama na kuondoka zake....
MWISHO
0 comments:
Post a Comment