IMEANDIKWA NA : SALMA R. RAMADHANI
*********************************************************************************
Simulizi : Binti Kipofu
Sehemu Ya Kwanza (1)
Walionekana wafanyakazi walioweza kuvalia gauni nyeupe fupi wakijipanga mstari katika jumba Kubwa la kifahari kuelekea mlangoni.
"Madam anakuja kila mtu akae vizuri" alizungumza mmoja wa wafanyakazi hao akiwatahadharisha wenzake ambao na wao walianza kujiweka vizuri kwa kutengenezea tai zao. Hapo hpo liliingia kundi la wanaume saba walioweza kujigawa katika magari matatu yaliyoweza kuwapo eneo lile.
Vilisikika viatu vilivyokuwa vikitoka ndani ya jumba lile Kubwa la kifahari wote waliinama chini ishara ya kutoa heshima alitoka mwanamama mmoja aliyeweza kuyavalia miwani yake baada tu ya kujitokeza mbele ya wafanyakazi wake.
Aliirudishia pochi yake vizuri mkononi kisha akaanza kupiga hatua za kuelekea mahali magari yalipo. Akiwa anaelekea huko alisimama baada ya kuhisi ya kuwa kuna mtu anakuja nyuma yake.
Aligeuka nyuma na hapo aliweza kukutana na mkono wa kiume uliokuwa ukilikunja shati lake vizuri mkononi na kutengenezea saa yake vizuri mkononi.
Adrian aliita mwanamk yule ambye makamo yake yalionekana kusogea mbele.
Adrian alitabasamu kisha alipoweza kufika karibu naye alimpiga busu la mdomo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umeamkaje kipenzi changu Vanessa?? Aliweza kuuliza Adrian ambye kwa umri alionao hakupaswa kumuita Vanessa kipenzi bali mama au aunt.
Walishikana mikono na kuelekea mahali magari yalipo Adrian alitaka kuingia gari la kwanza lakin watumishi waliweza kumzuia.
'Kwanini mnanizuia kupanda??! Aliuliza kwa sauti ya ukali sana hadi kumfanya Vanessa ashuke kwenye gari aliloweza kulipanda.
" kuna shida gani hapo??? Aliuliza Vanessa.
Mtumishi mmoja alitoa heshima kisha akaanza kuzungumza.
"Madam Tropina amesema leo atapanda gari hili kwahiyo boss Adrian hatopanda gari hili Leo"
"Hivi huyo kipofu ananitafutia nini Mimi?? Hajui ya kuwa Mimi ndiye Baba mwenyenyumba hii"
"Nyumba ipi hiy? Ilisikika sauti laini na ya utaratibu na kwa sauti ya juu ikiuliza swali hilo.
Vilionekana viatu vyekundu simple vilivyowezwa kubebwa na suruali nyeupe chini iloyoweza kupanda hadi kiunoni, kiuno hicho kilikuwa chembamba kilichoikaa vyema suruali hiyo shati jekundu lililoweza kuchomekewa ndani ya suruali hiyo nyeupe.
Adrian alimtizama juu mpaka chini kisha akakosa neno la kuongea juu yake.
Tropina aliweza kupiga hatua hadi kufika pale Adrian alipo.
"Mwambie mama yako akununulie gari la kuzurura nalo mtahani lakini siyo utumie gari la pesa aliyoweza kuitafuta Baba yangu alizungumza Tropina kisha akaufungua mlango wa gari kwa nguvu na kumgonga Adrian pajani ambako alianza kugutaguta kwa maumivu aliyoweza kuyapata huku akishika paja lake gari liliwashwa na hatimaye aliweza kuondka zake.
Vanessa aliweza kwenda kumkimbilia Adrian na kumpa pole huku akijaribu kumgusa gusa na kutizama gari aliloweza kuondoka nalo Tropina.
Adrian aliyauma meno yake kwa hasira huku akiona kabisa ya kuwa Tropina anamfanyia dharau na makusudi.
Alirudi ndani kwa hasira sana huku nyuma akifuata na Vanessa. Baady ya wote kuingia ndani ya nyumba mbele yao aliweza kujitokeza mfanyakazi mwenzao Diana aliyekuwa wa vituko kila kukicha baada ya kufika pale aliweza kuyarudia maneno ya Tropina huku akitembea na akiwa ameyafunga macho yake. Ghafla Vanessa aliweza kutoka ndani na Diana aliinama chini akijifanya ya kuwa anafagia zake.
***** ******** *******
Katina upande mwingine alikuwa mwengine aliyeonekana ya kuwa alikuwa akimsubiri mtu aweze kufika eneo lile kwni alikuwa akiitizama saa yake na kutizama upande wa juu wa barabara.
Aliitoa simu yake kisha akaipiga.
"Mbona hapokei simu alizungumza huku akiendelea kupiga cmu ghafla akiwa pale aliweza kusikia mlio wa pikipiki ukiwa unakuja eneo lile.
" kila cku namwambia aache kukimbiza pikipiki hivyo lakini Vikram huwa asikiagi mtu kbisa" alilalamika Alice pikipiki ile ilipofika karibu na yeye iliweza kusimama na Vikram aliweza kushuka juu ya pikipiki ile.
Alianza kuitoa helmemt aliyoweza kuivaa lakini kabla haijamtoka yote kichwani liliweza kupita gari na kuwamwagia maji machafu hali iliyoweza kumfanya Vikram aache kutoa helmet yake.
"Huyu...................... Anajifanya haoni amah nini" alilalamika huku akitaka kuwasha pikipiki yake kwaajili ya kumfuata lakini Alice alimzuia.
"Achana naye bhana alizungumza Alice aliyeonekana siyo mpenda shari kabisa.
" adhabu mwenyezi Mungu aliyoweza kumpa inatosha"
"Adhabu gani??
" ni kipofu huyo lakini anadharau sana watu........pia hapatani kabisa na wanaume na anamiliki kampuni Kubwa Kubwa zote Africa hiyo ni kutokana na mali aliyoweza kuachiwa na Baba yake. Alizungumza Alice aliyeonekana kumfahamu vizuri sana Tropina.
****** ******* *******"
Upande mwingine alionekana mtoto mdogo makamo yake miaka 9 akiwa amesimama njee ya shule huku akitizama muda wake.
"Mbona dada Tropina hajafika mpaka sasa alizungumza huku akiweza kutoa tablet yake na kuanza kumtafuta dada yake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Larry unafanya nini hapo??? Aliuliza madam wake aliyekuwa akimfuata Larry
"Unajua dada yako akikukuta njee ya geti atagomba ingia ndani mpaka aje"
Ghfla aliweza kupigwa kikumbo na gari na kudondoka chini hapo hapo mlango wa gari aina ya Noah nyeusi ulifunguliwa kisha Larry akatekwa na gari kuondoka eneo lile.
Wakati gari hilo likiondoka ndo gari la Madam Tropina liliweza kufika pale.
Mwalimu alijitahidi kusimama ilihali alikuwa na majeraha mengi huku walimu wengine wakitoka njee baada ya kusikia kishindo kikubw baaada ya sekunde kadhaa kupita.
"Umefanyaje??????
" Larry katekwa.!!!!
Ndyo kauli aliyoweza kuitoa na kauli hiyo iliweza kupenya hadi katikati ya ngome za Tropina aliyekuwa akishuka ndani ya gari lake. Mguu wake mmoja ndyo uliokuwa umeteremka tu na hkushusha tena mguu mwingine.
**** yalipitaa masaa7 *******
Na hakukuwa na habari zozote juu ya Larry Vanessa ndiye aliyekuwa akiweweseka kwani ndye mwanaye wa mwisho na kitinda mimba wake.
"Nimesema nitatoa pesa yoyote ile mwanangu tafadhali mtu asimdhuru na naomba mnipigieni simu nmba zangu ni
........... Aliweza kutoa nmba zake na hapo hapo aliingia Tropina na kusema.
" hakuna hela yoyote itakayoweza kutolewa mahali popote kwasababu nmekufungia account zote na wale walioweza kumchukua Larry nawazidishia masaa7 mengine muwe mumeshamrudisha Larry nyumbani na siyo shuleni tena kwani nimechoka kutembea" baada ya kusema hyo aliondoka na kupanda ngazi
Adrian alimtizama sana kwa hasira.
"Waaandishi wa habari nisikilizeni Mimi achaneni na hiyo BINTI kipofu kwasababu tangu ajali ya kifo cha bba yake anaishi kama mnyama na siyo binadamu tafadhali naomba mnipigieni simu nmba zangu tayri nimeshaweza kuzitoa kiac chochote ntawapa nyie mlioweza kumteka.
Waaandishi wa habari walimtizama tu bila kusema neno lolote kwani mwenye kauli ya mwisho ni Tropina na siyo yeye.
**** **** *****
Bossi tufanyaj??? Ilikuwa sauti ya afande mmoja akimuuliza mkuu wake.
" tufanye nini sasa ikiwa hata ndugu hakuna aliyeweza kureport ya kuwa ndugu yao ametekwa huyu Tropina sijui anaroho ya namna gani.......sisi tuendelee tu kula ma apple alizungumza huku akitupia kipande cha apple mdomoni mwake na kutabasmu huyo alikuwa mkuu katika kitengo cha polisi idara ya ulinzi na usalama miaka yake haikupishana na Tropina hata kidog pia alikuwa clasament wake hivyo tabia za Tropina aliweza kuzifaham jina lake aliweza kuitwa George pesambili.
"Ila ndani ya masaa3 watamrudisha wenyewe na kama hawatamrudisha basi hii nchi itachafuka ndani ya dakika20 tu na Larry atakuwa amepatikana ,kwahiyo sisi tuendeleeni kula jamani.
***** ****** *******
" halooo alionekana Adrian akipokea simu.
"Nawaambia ndani ya hayo masaa7 kaeni kimya alafu tuone kama hatobadilisha mawazoyake muuweni kisha mumtumie picha tutamuuza hata akiwa marehemu alizungumza huku akiwa anahasira sana.
Baada ya kugeuka nyuma tu aliweza kukutana uso kwa uso na Tropina aliyekuwa nyuma yake.
"Kama nimeshindwa kuwapa pesa akiwa mzima mnafikiri akiwa marehemu nampeleka wapi???? Nakupa masaa3 kama hajarudi hapa utanijua Mimi ni nani? Alizungumza kisha akageuka nyuma na kuondoka zake.
Adrian aliirusha simu yake chini kwa hasira kwani game lake tayari limeshaweza kugundulika.
Aliyauma meno yake kwa hasira sana huku akimtizama Tropina aliyekuwa akishuka chini.
" nakwambia ipo siku yako ipo siku yako maana upofu haukutoshi ww bado unaakili sana" aliyazungumza hayo Adrian.
** ** ** ** **
Huku nako alionekana Vikram akiwa anaelekea nyumba moja kwani aliweza kupatiwa mzigo aupelekee pale kutoka katika kampuni yao.
Alipofika alikuta ni kimya sana ndani hapo alipogusa mlango uliweza kufunguka hivyo alianza kuingia ndani taratibu kabisa na kwa umakini wa hali ya juu kabisa.
Alisikia kelele zilizokuwa zikitoka kwenye TV aliweza kusogea hadi kribu pale alimkuta Larry akiwa anacheza game.
"Wewe wenye nyumba wako wapi??? Aliuliza Vikram
Larry alimtizama bila kumjibu chochote kile.
" wewe mtoto si ninakusemesha"
"Inamaana Mimi sina muonekano wa kumiliki nyumba???
Vikram alimtizama akaitizama na nyumba kisha akamtizama tena.
" wewe mtoto nakuuliza bba yako yuko wapi???
"Kaburini"
*sawa na mma yako*
"Anaweweseka knitafuta Mimi" alijibu Larry.
Vikram alimtizama kisha akamuuliza dada yako yuko wapi.
"Ananisikiliza nikicheza Game" alijibu Larry
Vikram alimpiga kwenzi la kichwa.
"Mpumbavu kabisa mtoto huna adab wewe mimi ni wakiume siyo dada yako"
Larry alimgeukia na kumtizama kisha akamuuliza.
"Hivi unanijua Mimi ni nani???
" mtoto uliyekosa adabu tena unabahati Leo siko kwenye mood ya kupiga watoto niambie bba na mama yko wako wapi???
Larry alimkazia macho tu.
"Usinitizame Mimi" aliongea huku akimsukuma kichwa Larry
"We mkaka kwanini unanisodola"
*kwasababu wewe ni wakiume lakini mjinga" alijibu Vikram
Ujinga wangu uko wapi???
Akiwa anataka kumjibu Larry ghfla Larry aligusa kitufe cha video bahati mbaya na kufanya taarifa zake za kutekwa ndizo zilizokuwa hewani.
"Wewe mtoto hapa ni wapi??? Hapana namaanisha hapa ndo nyumba uliyotekewa??
" ndyo" alijibu Larry kisha akauchukua mzigo alioweza kuuleta.
"Niliwaambia sitaki bugger naitaji sandwiche"
Vikram alianza kurudi nyuma na bahati.aligongana na mtu.
"Kaka mtekaji Mimi hata sijui kama mmemteka mtu kwanza Mimi ni bubu huwaga sioni kwahiyo naomba niondoke.
Alipopiga hatua ya mbele zaidi alikutana mwingine.
" Kaka jambazi nawaapia ya kuwa kwetu hatuna mali kabisa na Mimi ni kiziwi jamni sioni"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mimi sijawahi kuona kiziwi asiyeona bali kipofu"
Vikram alibki akitizama tu bila kusema neno.
Ndyo Mimi ni kiziwi na bubu sioni.alizungumza Vikram nakuanza kuondoka.
"Uncle kwahiyo ukitoka hapa unaenda kumwambia dada ya kuwa nimetekwa katika nyumba hii?? Aliuliza Larry
" hako katoto katakuwa kanawasemesha nyie siyo Mimi" alisema Vikram.
"Uncle Vikram naongea na wewe"
"Vi.....vi.....Vikram amelijuaje jina langu?? Alijkuta akiropoka na kuwauliza magaidi wale.
" hapna kwanza mm siitwi Vikram bali Joseph " alianza kuondoka lakini ghfla alivutiwa ndani na jambazi mmoja.
"Tropina ndo amekutuma cndyo?? Aliuliza huku akitoa kisu chake
"Unaongelea nini wewe.....mimi hata simjui huyo mwanamke ni nani mimi nimekuja kuleta order kama mlivyoagiza kwenye kampuni yetu.
Alipo alijitetea Vikram akimtizima Larry ambaye alikuwa akicheka.
Baada ya muda kupita wote walikuwa ndani ya chumba kimoja huku Vikram akiwa anahangaika huku na kule.
" we Kaka si ukae" alisema Larry.
"Tena wewe nyamaza unadhubutuje kusema ya kuwa mimi nikae ilihali nimetekwa na yote ni wewe chanzo kwani walikuwa tayari wameshaniachia lakini wewe kwa ujinga wako ndo umenisababishia haya....tena ningelijua hichi kitambulisho ningekificha wala usingeweza kulitambua alizungumza huku akiendelea kuzurura ndani ya chumba kile
.........lakin ngoja we si umesema dada yako ni mtu mwenye pesa sasa kwnini asitoe sisi tuachiliwe.
" ameshasema hatoi hela na anawapa masaa3 tu wawe wamenirudisha"
"Huyo dada ako kichwa chake hakina tofaut na chakwako maana wewe umekaa kabisa na game unacheza utafikir hujatekwa au hawa majambazi siyo wakali nini?? Aliuliza na kumfanya Larry acheke.
" unacheka nini wewe mjinga?? alizungumza na kumpiga kichwa chake.
"Hivi mbona unanichukulia mimi wakawaida sana majambazi wenyew hata kuninyooshea kidole hawajazubutu lakini wewe tangia uje unanipiga tu" aliuliza Larry
"Sasa unataka nikuchukulie wewe wa special kwani umeumbwa kwa maji. Mitoto mingine mijinga kweli na huu ujinga itakuwa umejifunzia kwa hyo mpumbavu dada yako ambaye hataki kutoa hela sisi tuachiwe"
"Sisi tuachiwe au mimi niachiwe......nitaachiwa mwenyewe wewe tafuta njia ya kutoroka mwenyewe" aliongea Larry.
"Muone huyu mpuuzi" aliongea Larry na kumsukuma tena kichwa Larry.
***** ****** *******
Alice alionekana akiwa anaokota mafaili yaliyoweza kudondoka chini kutoka katika kabati moja.
Mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na aliingia Adrian akiwa amevimba kwa hasira.
Alice alimpa heshima bila kusema kitu kisha akaanza kutoka njee akiwaa anapiga hatua za kutoka njee Alisikia mlio uliomfanya ageuke nyuma na kukuta Adriana ameweza kupiga ngumi picha ya Tropina iliyokuwa ndani ya ofic hiyo hadi damu zikaanza kumtoka.
Alice alirudi kisha akatoa kitambaa chake na kuanza kumfuta damu zilizokuwa zikitoka katika mkono wake.
"Huyu mpuuzi kipofu huyu" hyo ndyo maneno aliyoweza kuyasikia Alice akilalama Adrian.
Simu yake iliita na aliutoa mkono wake kwa Alice kisha akamtaka atoke njee.
"Nani........ Kijana gani.......Vikram.....na nyie mmemuweka ndani waachieni wote alafu hakikisheni ya kuwa mnamrudisha hadi nyumbani mimi nitawalipa kwa kazi yenu" baada ya kumaliza alikata simu.
Aliitizama picha Kubwa ya Tropina aliyoweza kuipasua ikiwa chini kwa hasira sana.
******** ******* ********
Larry pamoja na Vikram waliweza kupelekwa hadi nyumbani na kuwekwa njee ya geti kisha wakaondoka zao.
Baada ya kufika pale tu walitoka walinzi wanne njee na kuanza kumfungulia Larry kitambaa alichoweza kufungwa machoni waliweza kulichukua begi lake walimtizama Vikram aliyekuwa akihangaika kujifungua kamba aliyoweza kufungwa mkononi lakini alishindwa.
"Hivi inamaana mimi sionekani au?? Aliuliza baada ya kushindwa kufungua kamba aliyoweza kufungwa nyuma.
" Vikram natumaini tutaonana zaidi aliongea Larry kisha akatoa amri ya asifunguliwe kamba bali apelekwe katika kampuni yake.
"Nyie mnanipeleka wapi?? Aliuliza Vikram ambaye alikuwa akivutwa na asijue ya kuwa anapelekwa wapi.
" aise nyie ni majambazi tena amah wewe mtoto waambie waniachilie hawa watu akiendelea kuzungumza Tropina alikuwa akitoka njee baada ya kuzisikia kelele ambazo hazikueleweka masikioni mwake.
Alipokanyaga mguu wake mmoja njee ya geti na ndipo mguu mmoja wa Vikram uliweza kuingizwa ndani ya gari alipoweza kuutoa mguu wa pili na mguu wa Vikram nao uliigizwa ndani ya gari kisha mlango ukafungwa.
"Ni kelele zanini hizo?? Aliuliza Tropina na wote wlitoa heshima kwa kuinamisha vichwa vyao.
Kwa mtu yoyote ambaye angefanikiwa kumuona Tropina kwa mara ya kwanza wala asingeliweza kuamini ya kuwa yeye ni kipofu kwani macho yake yalikuwa wazi na aliweza kuyapepesa kwa jinsi atakavyo pia nyumba anayoishi yeye alitembea pasina kupata muongozo wa mtu yoyote yule wala kutumia fimbo ya kipofu kama watumiavyo vipofu wengine. Aliweza kumtambua kila mmoja kwa harufu pamoja na sauti yake kwani alikuwa na uwezo mkubwa wa kukariri kitu.
" mpelekeni kwenye kampuni yake" alitoa kauli hiyo Larry na watu wawili waliweza kupanda ndani ya gari baada ya kutoa heshima na kuliondoa gari eneo lile.
"Hivi mimi natoa amri ya kuulza na wewe unatoa amri ya aondolewe eneo hili?? Aliuliza Tropina aliyeweza kumgeukia Larry.
" kwasababu ni mgeni wangu mimi nani Shemeji yangu mimi wewe hakuhusu" alijibu na kuelekea ndani.
"Shemeji" alirudia neno lile huku akishindwa kulielewa.
**** **** *****
Vikram akiwa na Alice huku akimuhadithia mmbo yote yaliyoweza kutokea.
"Siamini macho yangu kwamba katika duniani bado kuna watu wanateka watu kwaajili ya pesa badala watafute zao.........lakini na ndyo nimeona maajabu ya mtu kutekwa alafu akarudishwa nyumbani kwao bila hata senti tano.
Dah kweli duniani watu wanaonyesheana ubabe balaa alizungumza huku akicheka.
" unabahati ya kuwa ulitekwa na mtoto wa kitajiri ndo maana ukaachiliwa ukiwa hai kama sivyo tungekuw tunaomboleza hapa alimalizia kuzungumza kisha akainuka alipokuwa amekaa na kuutizama mwezi juu kwani walikuwa wamekaa njee katika nyumba ya kina Alice aliyoweza kupangisha Vikram ambaye alikuja kuwa rafiki mkubwa sana wa Alice.
"Vikram" aliita macho yake yakiwa juu ya mwezi.
Vikram aliitika kisha akasimama alipokaa na kumfuata Alice kisha kumtizama anatizama nini na yeye akaweza kuutizama mwezi.
"Mama yangu huniambiaga ya kuwa pindi unapoona mwezi umeng.ara namna hii basi omba kitu chochote kile juu ya mwezi huo na maombi yako yataweza kujibika kwa haraka zaidi"
"Na wewe unaamini hilo??!! Aliuliza Vikram.
" ndyo kwani mara niombpo basi kile ninachokiomba huweza kutimia"
Vikram alitingisha kichwa kisha akaikutanisha mikono yake na kuutizama tena mwezi kisha akasema.
"Eeehhhh mwezi naomba imni hii aliyonayo huyu binti basi imtoke"
"Vikram acha utani embu omba kile unachoweza kukihitaji katika maisha yako na ufunge macho.
Vikram pamoja na Alice waliweza kfunga macho na wote wakaomba vile wavipendavyo katika maisha yao.
Alice alikuwa wa kwanza kumaliza kisha akamtizama Vikram na kusema kimoyomoyo.
" natumaini utaomba kile nilichoweza kukiomba mimi"
***** ****** ******
Vikram akiwa anakuja katika kampuni ya kusambaza vyakula alishangaa baada ya kuona ya kuwa takribani wafanyakazi wote wanamnyooshea vidole yeye.
"Kuna nini tena leo huku jamn" alijiuliza huku akitizama kulia na kushoto kma mtu mwingine tofauti na yeye.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijikaza akatembea hadi alipofika counter ambako nako James aliyekuwa mhudumu wa hapo na rafiki yake kipenzi na yeye alibaki akimtizama.
"Kuna nini leo jamaa angu?? Au nimekosea kuvaa nini mbona mnanitizama hivyo?
Kabla hajajibiwa swali lake aliingia director wa kampuni hyo ya Japhary Food & Fast supply.
" Vikram nikuone ofisini mara moja" alitoka amri hiyo huku akitembea kinyonge na kuingia ndani ya ofisi yake.
"Eeeeheeee mungu wangu jana tu niliomba nipate kazi yenye ubora leo naitwa kufukuzwa kazi heri hata nisingalimuamini Alice yeye ndo chanzo cha yote hayo" alilalama huku akiendelea kuingia ndani.
Baada ya mud kidogo yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoka ndani ya ofisi ya Director akiwa amenyong.onyea sana na akitembea kama mtu aliyeweza kushindwa maisha.
"Imekuwaje tena Baba mbona unatembea hivyo na nilisikia habari nzuri kukuhusu wewe" aliuliza James akimtizima Vikram.
Vikram alidondosha begi lake chini kisha akaanza kushangilia kwa furaha kutokana na taarifa alizoweza kuzipata.
Baady alionekana Alice akiwa anazungumza na simu.
*kwahiyo unasema umeambiwa uwe una suppy sandwich katika nyumba ya Madam Tropina pekee yako na utakuwa ukipeleka kwa gari ambalo umenunuliwa naye na mshahara wako umeongezwa........mmmhhhh hivi unauhakika ni Madam Tropina mwenyeww ndo katoa kauli hiyo?? aliuliza tena Alice.
"Mimi huyo Tropina simjui namjua yule mtoto maana ndo nilitekwa naye kwasababu nilimtreat vizuri tukiwa kule labda ndomaana Tropina akaamua kunipa ofa hiyo"
****** ********* *****
Alionekana Vikram akiwa amevaa suti yake nyeusi na akiwa anashuka ndani ya gari jeuc baada ya kuendeshwa aliweza kushuka na boksi dogo aliloweza kilibebea tumboni alionyeshwa mlango wa kuingilia na wafanyakazi waliokuwa mlangoni.
Alipoingia ndani aliweza kushangaa kwani nyumba iliweza kumeremeta kwa vito vya dhamani huku asilimia Kubwa ikiwa ni dhahabu palikuwa mchna lakini taa ziliwezwa kuwashwa ndani kwaajili ya kuleta mwanga mzuri utakaoweza kuwavutia watu.
Akiwa anaendelea kushangaa na kutembea tembea pale ndani aliweza kumuona msichana mmoja akiwa anakuja eneo lile.Alisimama pale na kumtizama msichana kutokana na alivyoweza kumvutia kwa kumuona kwake tu ila sasa hakuwa msichana bali Tropina.
Aliweza kumpita Vikram.
"Wewe Binti inamaana hujaniona au ni dharau?? Aliuliza bila kujua ya kuwa hapo anajitafutia matatizo.
Tropina aligeuka na Vikram aliamini ya kuwa Tropina anamuona.
" nimekuja hpa kwa Mara ya kwanza ila kidogo nyumba hii inanichanganya yule kichaa mdogo yuko wapi..... Sijui hata anaitwaje tena lakini katoto kamoja kana kama miaka9 au 10 yuko wapi??
"Hivi hayo maswali unamuuliza nani?? Aliuliza Tropina baada ya kuona kuwa mtu hyo anajifanya hamfahamu.
" we ni mjinga nini kwani hapa ndani tuko wangapi zaidi ya mimi na wewe aaaaaaiiiiiiiishshshshsh hii nyumba itanishinda kama wanaokaa humu ndani wanadharau hivyo sasa huyo Tropina ninaye ambiwa si atakuwa balaa" alizungumza Vikram
"Unadhubutuje kusema Tropina pasina kutanguliza Madam" aliuliza Tropina baada ya kuhisi ni dharau.
"Madam wa nini........wamuite hao anaowalipa mshahara kwanza mimi kumuita mwanamke Madam siwez.... Kwanza nahangaika kuongea na taira badala nitafute mtu mwenye akili timamu humu ndani" alizungumza na kugeuka nyuma huku alianza kuita heloow jamn kuna mtu anayeweza kujielewa humu ndani.
Aaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhhhh zilisikika kelele kutoka nyuma ya Vikram na hiyo ilikuwa sauti ya Tropina.
Ni baada ya Tropina kupiga kelele
Sasa endelea
Wafanyakazi wote walikuwa njee waliweza kuingia ndani na waliokuwepo ndani waliweza kusogea mpaka eneo ambalo kelele zile ziliweza tokea hata Larry na yeye aliweza kufika baada ya kumuona tu Vikram alitambua kabisa ameshaharibu.
"Kelele za nini wewe kipofu?? Aliuliza Vanessa aliyekuwa akitoka chumbani kwake na Adrian.
" ki.....ki.....kipofu!!! Vikram aliweza kulirudia neno lile kwa mshangao na kurudisha macho yake kwa Tropina ambaye alikuwa akishusha pumzi na kuzpandisha kwa nguvu zaidi.
Walinzi kadhaa waliweza kumkamata Vikram.
Tropina aliweza kusogea kwa hisia mpaka pale alipo kisha akapandisha mkono wake juu na kumpapasa kwanzia kifuani hadi kupanda juu ambako aliweza kugusa uso wake.
Baada ya walinzi kuona tu ameguswa usoni walimuachia na kusogea mbali kidogo huku kila mmoja aliyekuwa pale aliweza kufunga macho yake kwni walijua kitakachofuata ni nini na wakati huo nao Larry aliweza kusema tu
"Ohoooo na kujiziba mdomo wake huku akifunga jicho moja na kuacha lingine wazi.
Vikram akiwa bado anashangaa shangaa na anashindwa kuelewa kwanini watu wanafanya vile ghafla alianza kuhema kama mtu aliyekosa muelekeo na mtu aliyehitaji kupiga kelele aliweza kumtizama Tropina kisha kushusha macho yake chini ambko tayari kiwiko cha mguu wa Tropina kilishaweza kutembelea sehemu muhimu kbisa ya mwili wake kwa kumpiga na kiwiko hicho.
Vikram aliitoa mikono ya Tropina usoni mwake kisha akaushusha mguu ule ambao uliweza kumpiga sehemu zake kisha akajishikilia sehemu zake na kuanza kupiga kelele huku akiruka ruka na kuweza kumkanyanga mfanyakazi mmoja ambye alikuwa na kidonda cha mguu hali hiyo ilimfanya mfanyakazi yule na yeye aanze kuhangaika huku mguu wake mmoja ukiwa juu kwa bahati mbaya katika hangaika hangaika yak na yeye aliweza kugusa chombo kimoja kilichokuwa na ua na kukifanya kidondoke chini na kupasuka wakati huo bado Vikram alikuwa akihangaika kwa maumivu na aliweza kurudi hadi pale kwenye chombo kilichoweza kupasuliwa na kilikuwa na maji pasina kujua aliweza kuteleza na kujikuta akielekea moja kwa moja hadi sehemu aliyokuwapo Tropina ambye alikuwa akitabasamu tu alipofika karibu na yeye Tropina alimkwepa na kumfanya aende mzima mzima hadi kwenye ncha ya meza ambayo iliweza kugusa pale pale alipokuwa akilia kwa maumivu. Baada ya kuumia tena aliweza kusimama hapohapp pasina kusema neno lolote bli kumtizama Larry na kuweza mate tu.
****** ***** *****
Alice alikuwa akimalizia kumkanda na kuweka maji pembeni huku akimtizima Vikram aliyekuwa akijikagua kwenye kioo.
"Huyu kichaa huyu mwanamk nitamuonyesha tu kwakweli siwezi kuliacha hili likapita tu kwanza amenigusa sehemu ambayo hakuna mwanamk aliyewahi kuigusa mjinga huyu mpuuzi kabisa mshenzi kasoro robo"
"Unajua Vikram upunguze utani wako kwni unafanya mmbo ambayo yanahatarisha maisha yko alafu wewe unaona umefanya mambo ya maana sana" alizungumza Alice.
"Sasa mimi ningejuaje yakuwa yeye ni kipofu kipofu gni macho yke yanakuwa wazi huyo atakuwa anajiekitisha tu" alilalama Vikram
"Vikram"
"Ww ngoja utaona"
"Vikram usitake kushindana na mtu usiyemfahamu wewe ndiye unayemuona kama mwanamke lakini yeye ni zaidi ya mwanamk na usipende kushindana naye kwani yeye hapendi kushindwa hivyo utabaki kujiumiza tu " alizungumza Alice.
"Hpana lazima nimkomeshe tu ni kwasababu yake yeye mimi Nina vidonda mwili mzima hadi sasa hiv.......... Alafu huku alikonipiga huku inabisi kesho nikapime uckute vitu vimehamia kwingine maana sijisikii vizur kabisa ogaoa mimi ni wakiume lakini nahic kutapika" alilalama Vikram ambaye alionekana kutokutaka kbisa kumuelewa Alice.
"Kesho atanitambua hyo kichaa" alizungumza na kusimama alipokuwa amekaa.
Wakati huo upande wa pili nako kiapo hicho ndicho alichokuwa akikiapa Tropina.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unajua Larry alitumia sauti yangu kwaajili ya kufanya wewe uamini ya kuwa mimi ndye niliyekupa hiyo kazi sasa utajua kufika hapa na kwanini umeniita mimi sina akili utalipa kwa hilo ngoja kesho asubuhi pakuche.
*** *** *** ***
Larry akiwa ndani kwake Adrian aliweza kuingia.
Larry alimtizama tu bila kusema neno lolote lile.
Alikaa kitandani ambako Larry alikuwa amekaa huku akicheza game lake.
" aaaammmmhhhhh Larry mwanangu unaendeleaje??.... Maana baada ya tukio la kutekwa lililoweza kutokea nilikuwa busy sana Ila sasa hivi ndo nimepata muda vipi kuna sehemu yoyote uliyoweza kuumia??
Larry aliweza kutabasamu kwa kupindisha mdomo wake pembeni kwa dharau kisha akazungumza.
"Sku zote mbwaa awezi kumbwekea mwenye nyumba"
"Unamaanisha nini"
"Huyo mbwaaa aliyetuma watu wanitekee mimi ndyo mwenye nyumba wake hivyo hawezi kubweka wala kuniuma mimi kwani siku akifanya hivy ndo cku atakayoweza kutambua ya kuwa Tropina ni nani. alijibu na kumtazama machoni Adrian ambaye alikuwa akilivuta shuka kwa hasira.
" kuna shida gani mbona umelikusanya shuka hivyo?? Aliuliza kwa kumuinyoy.
"Hpana hmna....... Since uko salama sasa nafikiri mimi niendee sasa nikajipumzishe.......na wewe hakikisha unalala mapema kwani muda umeenda" aliinuka na kuelekea mlangoni ambako baada ya kufika Larry aliweza kusema
"Sawa" kisha akaplay mdoli ambaye aliweza kulia kama mbwaaa.
Adrian alifunga mlngo kwa hasira na kufanya Larry atabasamu huku akikasirika baada ya Adrian kutoka ndani pale.
Aliinuka na kutoa shuka ambalo aliweza kulitandika kitandani alipoweza kukaa Adrian. Alilitupa na kulichana chana huku akilikanyaga kanyaga kw hasira na kusema.
"Ngoja utaona huna miaka mingi" alizungumza huku akiitizama na picha ya mama yke kisha akasema.
"Utaondoka katika nyumba hii siku si nyingi"
***** ****** *******
Kulikucha asubuhi na wakati Vikram anakuja ktika nyumba ile aliweza kumkuta Tropina getini.
"Huyu kichaa asubuh asubuhi kilichomsimamisha getini ni nini??? Alijiuliza huku akiendelea kuiendesha pikipiki yake kwa nguvu alipofika getini aliisimamisha na kufanya itimue vumbi.
" Madam imekuwaje asubuh asubuhi umesimama getini?? Aliuliza huku akitoa helment yake kichwani na kutabasamu.
"Vicky" aliita Tropina.
Vikram aligeuka kulia na kushoto kisha na kutizama kama kuna mtu mwingine nyuma yake.
"Samahani yani mimi ndo umeniita Vicky ?? Aliuliza kwa mshangao.
" ndyo..... Vicky........"
"Huyu mshenzi ananiitaje mimi Vicky jina la kike" aliongea kimoyomoyo huku akinyoosha mkono wake kama anataka kumpiga.
"Hakikisha unakuwa makini zaidi kwani ndyo siku yako ya kwanza kuwa kazini na huo mkono wako unamuinulia nani"
Vikram aliushusha mkono wake na kumtazama kwa makini machoni.
"Pia usipende kunitizama kwa ukaribu namna hiyo sina myu yoyote ninayeweza kufanana naye katika dunia hii.
" ndiyo Madam " alijibu Vikram.
"Sawa ni vizuri kama utanifuata sasa" alizungumza na kuanza kuonyesha njia.
Alipokuwa akipanda ngazi za kuelekea ndani kwake aliweza kusimama.
"Unataka nini wewe?? Aliuliza Tropina.
" huyo wa nyuma yako ni mfanyakazi wangu mimi wa kuniletea sandwich na hausiani na wewe kwa nmna yoyote ile Vikram nifuate mimi.
Vikram aliweza kuchekelea na kupiga hatua za kwenda mbele huku akimshukuru Mungu wake kwa kuwa hayupo tena mkononi mwa Tropina.
"Larry" aliita Tropina.
"Naama mwanamke"
"Nitakulipa mara 10 yake ya mshahara ulioweza kumpatia na unipatie mimi Vikram"
"Hpana huyu ni mfanyakazi wangu mimi simuuzi kwa ntu yoyote"
"Kabisa aliongezea Vikram huku akitabasamu na kumwambia.
" sir Larry embu twende huko unakotaka twende" alizungumza na kuanza kumpepea Larry kwa mikono yake
Tropina alichukia sana huku akiapa hawezi kumuacha Vikram kwa Larry kwani anahitaji awe chini ya mikono yake.
"Najua unatamani sana mimi niwe chini yako ili unipelekeshe nitakavyo lakini nakuapia hutaweza timiza hilo.
"Huyo dada yko king.ang.anizi sana sindiyo" aliuliza Vikram baada ya kuingia kwenye chumba cha Larry.
"Alafu anaonekana kama kichaa kichaa...... Hivi unauhakika ya kuwa dada yako ni kipofu??
" unachotakiwa kufanya katika hii nyumba ni kuhakikisha ya kuwa huzozani na Tropina kwni yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho katika hii nyumba nimekusaidia leo lakini sitaweza kukusaidia kila siku kwahiy kuwa makini" alizungumza Larry.
"Sawa" alijibu na kukaa kwenye kochi.
"Wewe hujaja kukaa hapa kawaambie waniandalie chai"
"Yani wewe unanituma mimi!!! Aliuliza kwa mshangao.
" sawa kama hutaki nakurudisha kwa Tropina"
"Hapana cjasema sitaki bali nimekuuliza tu kwahiyo umesema waandae chai sawa boss mtoto naenda kuwaambia unahitaji tu chai pekee yake"
**** ***** ****
"Mara ngapi nawaambia muwe makini lakini....!!! Alikuwa akifoka Adrian kwenye simu wakati huo Alice alikuwa akiingia ofisini hapo aliyatenga mafaili huku alijitahidi kuweza kusikia kile kilichokuwa kikiongelewa katika cmu ile.
Alifungua mlango na kuanza kutoka njee baada ya hapo aliweza kuingia moj kati ya kordo iliyokuwapo katika ofisi ile na kupiga simu yake.
***** ***** ****
Vikram akiwa anatoka katika chumba cha Larry aliweza kumuona Tropina akija eneo lile.
" huyu kichaa anafuata nini huku lazima nimkwepe asinione maana anaweza akanisababishia matatizo mengine" alizungumza huku alijibambaza ukutani karibu kabisa na mlango.
Tropina aliweza kufika hadi eneo lile kisha akaufungua mlango.
Vikram alianza kucheka akiamini ya kuwa Tropina hajamuona.
"Sikuwa nakuja kwa ajili yako kwahiyo kuwa na amani" aliongea n kuingia ndani.
"Oky hata hivyo nilisahau ya kuwa ww cy kipofu kwasababu sijawahi onaga kipofu kama ww" alijibu Vikram na kuondka zake
Maneno Yale Tropina aliweza kuyasikia aligeuza shingo yake tu na kufunga mlango.
**** **** *****
"Unawaza nini??? Lilikuwa ni swli lililoweza kutoka kwa Alice na moja kwa moja kwenda kwa Vikram.
" Namfikiria Tropina maana nashindwa kumuelewa"
"Tayar umeshagombana naye tena"
"Hapana mbona Ila niwaza kama kweli ni kipofu au lah"
"Na kwann unawaza hivyo kwni ww unamuonaje??
" anawezaje kutambua mtu akiwa mbele yake yani wafanyakazi wa ndani anawatambua wote na hat mtu akipita tu mbele yke hata kama yuko kwa umbali kwa hatua 7 anamtambua kabisa hapo ndipo ambapo nashangaa"
"Uwezo wke ni mkubwa sana na yeye si wakawaida kama vipofu wengine ndo maana unaona hivyo hata hivyo hakuzaliwa kipofu"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa ikawaje akawa kipofu? Aliuliza Vikram.
" alipata ajali ya gari yeye pamoja na Baba yake Baba Yake alifariki dunia Ila yeye aliweza kupata majeraha sehemu nyingi sana za mwili wake hivyo kufanya hata macho yake kutoweza kuona tena" alielezea Alice.
"Alipata ajali???
" ndyo na ajali hyo ilitokea siku aliyokuwa akiendaa chuo kwaajili ya kusherehekea mahafali yake baada ya kumaliza kusomea degree ya sheria USA.
"Kwahiy walikuwa wanaelekea airport??
" kabisa"
"Na katika gari hilo walikuwa wangap?? Aliuliza tena Vikram
" ilikuwa Noah yenye nmba za usajili T.............,
Hivyo walikuwa familia nzima isipokuwa mdogo wake na mama yake waliokuwa kwenye gari lingine "
"Hao ndugu zake wko wapi???
" aaaaaaiiiihhhhhh wewe mbona unauliza sana jamani walikufa wote isipokuwa yeye tu pekee yake yeye tu pekee yake"
"Na......."
"Hapana......sihitaji swali tena juu yake"
"Moja la mwisho naapia alisema Vikram.
"hakuna uwezekano wa yeye kuona tena"
*hakuna ajuaye report zake kwasababu nisiri yake na daktari wake " alimalizia Alice.
"Natumaini ya kuwa anaweza akapata uwezekano wa kuona tena"
"Kama uwezekano huo ungelikuwepo basi tayri angeshaweza kuona kwani yeye ni tajiri mkubwa sana hawezi kushindwa na matibabu"
Vikram alitingisha kichwa.
"Vikram kwanzia nikufahamu wewe kwamara ya kwanza ndyo naiona sura yako ya serious sijui ya huzuni hiyo"
"Hamna basi tu" alijibu Vikram kisha akaingia zake ndani.
"Anashida gani huyu?? Alijiuliza Alice bila kupata jibu.
Kesho yake asubuhi Vikram aliweza kuingia tena ndani ya nyumba na kipindi hiki alikuwa akiyakumbuka maneno yote aliyoweza kuambiwa na Alice.
Huku akiyajumlishia na matukio kadhaa aliyoweza kuyaona ndani ya nyumba ile.
Alimuona Tropina akiwa dirishani huku akipunga upepo katika dirisha hilo na alikuwa mwingi wa mawazo.
Alisimama n kuanza kumtazama akiwa pale na kwa mara ya kwanza kabisa Vikram alijikuta akimtizima Tropina kwa muda mrefu na kujikuta akitabasamu pasina yeye mwenyewe kujua.
Ghafla aliguswa shati na aliposhtuka alikuta ni Larry. Alimtizama akatabasamu kisha akayarudisha tena macho yke kwa Tropina.
Baady alionekana Vikram akiwa ndani na Larry.
" hivi wewe leo umeona nini kwa dada yangu kilichokuvutia hivyo hadi unacheka tu mpaka sasa hivi?? Aliuliza Larry kwa hasira.
"Hamna"
"Unanijibu hamna na unaendelea kucheka?? Ninaenda kumwambia dada yangu" alizungumza huku akianza kutembea kuelekea njee.
Vikram alimvuta na kumrudisha ndni kisha akamkalisha kwenye kochi.
"Acha kiherehere mtoto wa kiume wewe....... Sasa huyo dada yako utamuowa wewe?? Aliuliza Vikram.
" kwni we ndo utamuowa??
"Mjinga wewe unaniona mimi siyo mwanaum au.......naweza kumuoa hata sasa hivi nikitaka"
Larry alisimama na kucheka sana tena sana
"hivi ukimuangalia dada yangu unaweza kumuingiza kwenye kundi la wanawake ww.....labda wewe humjui huyu kipofu vizuri kwanza mwanaum atakaye muowa yeye yeye ndo atakuwa kaolewa siyo yeye kaowa .... hakuna hata hiyo. dada yangu mimi hawezi kumpenda mtu hivi kama mtu anamchukia hata mama yake aliyemzaa unafikiri atakupenda wewe kwanza ww angalia tu nilivyotekwa alisema hatoi hata kumi na nasikia alifunga account zote za mama ili asitoe hela sasa kama hajali ndugu zake ww unafikiri anaweza kujua hata mapenzi ni nini?? Aliuliza Larry.
" kwani wewe unajua mapenzi ni nini au unabwata tu hapa na ww aliongea huku akimpiga kibao cha kichwa.
"Sawa mm sijui wewe unayejua jaribu bahati yko" alizungumza Larry huku akikusanya mto wake kwenye kochi na kukaa vizuri.
****** ****** ******
Adrian alikuwa bar huku akipata kinywaji chake na akitizama saa yake kama vile alikuwa akimsubiria mtu ambaye aliweza kuchelewa kufika.
Wakati akiendelea kuutizama muda wake pembeni yake aliweza kuonekana msichana mmoja aliyekuwa pembeni yake huku nywele zake zikiwa za rangi ya blue na zikiwa zimeweza kumfunika mpaka mbele kabisa ya uso wake nywele hizo ziliweza kuishia katika nyusi kisha zikapokelewa na miwani mikubwa meusi ambayo ilimfanya kutokutambulika kwa mapema zaidi. Alikuwa akimtizama Adrian mara zote.
Hapo hpo aliweza kuja Vanessa. Na baada ya Binti yule kuona hivyo aliweza kuondoka pale huku akiwa anapiga simu akitoka njee ya bar ile.
**** **** ****
Uliingia usiku na Vikram alikuwa akiendelea kutembea tembea katika nyumba ile ghafla aliweza kupita karibu kabis na chumba cha Tropina kilichokuwa wazi.
"Amenda wapi huyu kichaa alijiuliza huku akiingia ndani ya chumba kile aliweza kuziona picha za Tropina tangu alipokuwa mdogo akiwa katika mapozi mbalimbali picha zile ziliweza kumvutia na aliweza kuchomoa moja picha moja ghafla Tropina alitoka bafuni akiwa na taulo.
" mbona umewahi kuja hivyo Diana? Aliuliza Tropina akiamini ya kuwa ni Diana.
Aliweza kufungua taulo alilokuwa nalo na wakati huo ndo macho ya Vikram yalikuwa yakielekea mahali sauti ilipoweza kutokea.
Aliyerudisha macho yake kwa haraka zaidi na kutaka kudondoka kwa presha aliyoweza kuipata.
"Nani ww? Aliuliza Tropina baada ya kuhisi ya kuwa aliyokuwapo ndni ya chumba chake siyo Diana.
"Nauliza nani yuko ndani?? Alifoka kwa sauti na hapo ndipo Diana alipokuwa akiingia ndani ya chumba hicho huku akiwa na juice mkononi mwake.
Alihitaji kumuita Vikram Ila kabla hajalitamka jina hilo tayari Vikram alishafika pale na kumziba mdomo huku akifumba na kufumbua fumbua macho yake Diana alishtuka na kujikuta glass inamponyoka mkononi mwake il kabla haijafika chini tayr Vikram aliweza kuidaka wakati huo nao mkono wa Tropina ulikuwa ukielekea mahali alipokuwa Vikram alipoweza kukaribia kuugusa mgongo wa Vikram.....Vikram aliweza kupinda kidogo tu na kufanya mkono wa Tropina ushike uso wa Diana.
" mjinga wewe saa zote nakuuliza kama ni wewe kwanini ukakaa kimya?? Aliuliza Tropina akiutoa mkono wake ambao ulikuwa kidogo tu uushike mkono wa Vikram uliokuwa umeuziba mdomo wa Diana.
Vikram alimshikisha glass yake kisha akamkonyeza kumpa ishara ya akae kimya huku akitoka njee ya chumba kile.
Tropina naye aligeuka nyuma baada ya kutoka njee Vikram's kisha akacheka na kukasirika hapo hpo aliyachukua mafuta yake na kuyabinyia mkononi kwa hasira zaidi.
**** **** **** ****
Alice alikuwa ndani kwao huku akipika chakula cha usiku wa siku hiyo. Ghfla alihisi kuisikia sauti ya Vikram akizungumza na mama yake sebleni kwao.
Aliacha kila kitu jikoni kisha akatoka kwenda sebleni ambko alikuwapo Vikram.
Baada ya muda kidogo wote walikuwa njee huku Vikram akipata kinywaji chake cha shark.
"Unaonekana ya kuwa leo unafuraha sana"
"Aaaammmmhhhhh mimi hamna bhna" alizungumza Vikram na kucheka.
"Hamna na unacheka tena!! Au leo Madam Tropina kakufurahisha??
Alicheka na kuweza kukumbuka yale yaliyoweza kutokea usiku huo.
" hamna"
"Oooohhhyyy kila nachokuliza wanijibu tu hamna bora nikalale maybe kesho tunaweza tukaongea vizuri" alizungumza Alice na kuingia zake ndni.
Vikram alibaki njee akicheka cheka tu huku akigusa gusa kopo lake la shark.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku nako ndni ya chumba chake Tropina alikuwa dirishani huku akipata red wine na akiwa anapinga upepo alitabasamu tu baada ya kuhisi ya kuwa amekumbuka kitu kilichoweza kumfanya afanye hivyo.
**** ***** ****
Vanessa akiwa chumbani kwake akionekana kutafuta tafuta kitu ambacho bado hakufanikiwa kukipata.
"Zimeenda wapi??? Alijiuliza mwenyew huku akiendelea kuchambua chambua makaratasi mengine.
" kuna shida gni??? Aliuliza Adrian aliyekuwa akiingia ndani ya chumba hicho.
"Natafuta hatimiliki za kampuni yangu ya magari"
"Ahaaaa"
"Umenionea?? Aliuliza Vanessa.
"Sifikiri kweli" alijibu Adrian na kuanza kuvua koti lake la juu.
"Lakini Nina uhakika ya kuwa niliweka hpa hatimiliki sasa nani atakuwa amechukua na chumba hich tuko wawili2.
" kwahiy kwa maelezo yako mimi ndyo muizi" alizungumza Adrian.
"Baby jaribu kuelewa nacho kizungumza sijsema kuwa ww ni muizi"
"Kama ndani tuko wawili na hatimiliki zako hauzioni alafu hujanipa ruksa ya kuzichukua means kabisa ww unanishukia ya kuwa mimi ni mwizi"
"Adrian mimi mbona sijalitamka neno hilo lakini"
"Ndyo maana sikuwa nahitaji kuishi katika nyumba hii kwasababu hakuna anayenijali mimi hata watoto wako wote wananiona mimi kama takataka kwasababu ya nini sina chochote mimi nachomiliki kwa jina langu"
"Adrian kwngu mimi nakuona ni mume wangu tena nakuheshimu sana Ila wanangu wote wanakuchukia wewe kwasababu wananichukia mimi pia wakihisi ya kuwa mimi ndyo chanzo cha kifo cha Baba yao na ndugu zake kwasababu usiku wa kabla ya ajali niligombana na mme wangu kwaajili yako na watoto waliweza kuusikia ugomvi huo kwahiy wanakinyongo juu yako na yangu pia" alijielezea Vanessa aliyeonekana kukolea katika penzi la Adrian.
"Hii nyumba ni miliki yako na mume wako aliyekuwa marehemu na kwakuwa amefariki nyumba yapaswa kuwa yngu na yko lakini katika hati ya nyumba umeandika majina ya watoto wako tu....kampuni zote na viwanda navyofanyia kazi vyote vinamajina ya wanao hakuna hata kiwanja ulichowahi kununua kwaajili yangu unanifanya mimi kama chombo cha starehe tu umalizie haja zako katika mwili wangu" alifoka Adrian.
"Adrian tafadhali kuwa mpole mbona hivyo hatimiliki ya kampun magari ndyo nilikuwa naitafuta niangalie nitafanyaje mpaka iwe ya kwko punguza papara tafadhali" aliongea Vanessa kwa kumbembeleza.
"Mjinga mkubwa wewe utaondoka katika hii nyumba kama ulivyoweza kuja huna utakachokiongeza wakati ukiondoka wala utakachoweza kukiongoza" aliyazungumza maneno Yale Tropina kisha akageuka nyuma akiwaa active na kuelekea katika chumba chake alipofika karibu na chumba chake alishtuka kidgo kisha akauliza.
"Nani ww??
"Inaonekana kwanzia jana umepoteza uwezo wako wa kutambua watu"
"Unaongelea nini wewe?? Aliuliza Tropina na kuendelea kuelekea chumbani kwake.
" Tropina " aliita Vikram.
"Vicky!!!!!! Mimi siitwagi kihuni hivyo"
alizungumza Tropina.
"Hata mimi siitwagi kihuni hivyo" alijibu Vikram kimoyomoyo n kumwambia
"Sorry Madam Tropina ni kwamba sijazoea Ila kwanzia sasa nitazoe"
"Kwanini useme kwanzia sasa??
" kwasababu mimi ni mfanyakazi wako root zako zote za kwenda safari yoyote ile nitakupeleka nitakuandalia kila kitu katika upande wa chakula nitafanya kazi yoyote utakayoweza kuniamrisha kufanya"
"Piga magoti mbele yangu na unishike viatu vyngu" aliamrisha Tropina
"Unasema!!!!!! Alijikuta anazungumza kwa sauti Kubwa sana na kufanya watu waliokuwa karibu na maeneo yale waweze kusogea zaidi sehemu ile.
" ujasikia au kiburi......nimekwambia piga magoti chini kisha unishike viatu vyngu " alizungumza kwa sauti ya juu.
Vikram aliweza kutizama kulia na kushoto ambako tayri kulishaweza kujaa watu hadi wafanyakazi wa njee nao waliweza kuingia ndani.
Vikram alianza kushuka chini na hatimaye alipiga kbisa magoti chini kisha akashika viatu vya Tropina akiwa mwingi wa hasira.
Baada ya Tropina kuona matakwa yake yametimilizwa basi alimwambia nifuate Vikram akiwa bado yuko chini alitizama mbele yake na macho yake yalikutana uso kwa uso na Larry aliyeonekana kumtazama tu kwa macho ya huruma.
**** **** *****
"Huyu mwanaharamu mwanamke huyu......laanatulah huyu.......shetani hana bahati nasema hana bahati mjinga mkubwa kabisa ananidhalilisha mimi nitalipiza nitalipiza naapa" alikuwa akizungumza Vikram kwa uchungu mkubwa kbisa baada ya kuonyesha dhahiri ya kuwa kitendo kile kimemkera sana.
Wakati akiyazungumza hayo kwa upande Wake. Tropina alikuwa akitabasamu na kusema tuone kama unauwezo wa kunikomoa.
Alionekana Vikram akiwa bado anahasir y kile kilichoweza kutokea usiku.
Akiwa pale Alisikia akiitwa.
"Bwashe"
Aliweza kugeuka nyuma baada ya kusikia sauti hiyo kwni alikuwa akifanya mazoezi.
"Bwashe!!! Alirudia neno lile kwa mshangao na kumtazama larry.
" kwani nimefanya vibaya kukuita hivyo ? Aliuliza Larry huku akikaa katika kibenchi kilichopo pale.
Vikram alirudi kuendelea kupiga pushap zake huku akiendelea kukumbuka jinsi alivyoweza kupiga magoti mbele ya Tropina.
"Eti bwashe" aliita tena Larry kwa kumsogelea karibu zaidi sikioni.
Vikram aligeuka na kumtazama larry.
"Hahahaha Larry alicheka na kumwambia.
" nahitaji msaada wako kidogo"
Baada ya muda kidogo wote walikuwa ndani ya gari huku wakitizama njee.
Vikram alimtizama Larry na kutabasamu.
"Hivi ni akili zako au!!
We ni bwashe wangu inabidi unisaidie bhna. Alizungumza Larry na kumtizama Vikram.
" sawa " alizungumza Vikram kisha akateremka ndani ya gari na kutengenezea suti yake vizuri huku akiwekea tai vizuri.
Alitizama mbele na ilikuwa ofisi ambayo alikuwa akifanyia kazi Adrian.
**** **** ****
"Diana sasa hivi saa ngapi?? Aliuliza Tropina.
" Saa3:46 Madam Tropina "
Mlango wa gari ulifunguliwa na alitoka ndani Vikram na Larry.
"Larry umetoka wapi saa tatu hii??
" hyo ni mambo yangu hayakuhusu" alijibu Larry na kuondoka zake.
"Na wewe Vikram??
" mimi nini Madam Tropina ?
"Kwanini umechelewa kuja leo kazini??
" ahaa kumbe nimechelewa kuja leo.....kwni mpendwa me ni mfanyakazi wako?? Aliuliza Vikram...... Ahaaa nilisahau ya kuwa jana nilikwambia mimi nitakuwa mfanyakazi wako..... Nimebadilisha mawazo sitaki tena" alizungumza Vikram.
"Kwanini hutaki tena?? Aliuliza Tropina.
Vikram alimsogelea karibu zaidi na kumuelezea masikioni Tropina alitikisika na kutaka kudondoka Ila Vikram aliwahi kumdaka kwa kumshika kiuno kisha akamsogelea masikioni zaidi na kumwambia.
"Ukitaka nifanye kazi zako basi itabidi uniombe nifanye kazi chini yako na nitafanya vile ninazozitaka miye" baada ya kumaliza kufanya hivyo alimbinya kiuno kidogo kisha akamsimamisha vizuri alafu akampulizia upepo usoni na kuondoka zake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tropina alisimama na kujikuta anashangaa.
"Diana"
"Ndyo madam"
"Umeona kile alichokifanya huyu?? Aliuliza kama vile aelewi. Alihisi kizunguzungu na kutaka kudondoka lakini Diana aliweza kumshika mkono. Ila alishtuka na kuutoa mkono Wake.
" samahani Madam alizungumza na kutoa kitambaa chake kisha akaweza kumfuta sehemu ambayo amemshika.
*** *** *** ****
"Unazungumzia nini unaposema amekuja hapa?? Aliuliza Adrian.
"Hata mimi nilishindwa kumuelewa lakini alipofika alimpigia simu Tropina na Tropina alidhibitisha hilo akasema nimpe kile anachokitaka"
alizungumza mfanyakazi wa Adrian aliyejulikana kwa jina la Mbise.
"Na ukampa"
"Ndyo kwasababu Madam Tropina kasema nimpatie lau kama nisingempatia basi unajua kipi kingefuata" aliongea mbise.
Adrian alishikwa na hasira na kutazama kiboksi ambacho kilikuwa kitupu na hakukuwa tena na kitu ndani yake.
**** **** *****
Ndani alionekana Larry akiwa anatabasamu tu huku akimtizama Vikram aliyekuwa akicheza Game.
"Bwashe"
"Yeah"
"Nataka nikushukuru kwa kuweza kunisaidia kwa siku ya leo kwani umenisaidia sana"
"Oky alijibu Vikram na kuendelea kucheza zake game.
Ghfla mlango ulifunguliwa na aliingia Vannesa.
" Vikram nifuate" alizungumza na kutoka pale.
Vikram alishangaa kwani ndiyo mara ya kwanza kabisa kwanzia aingie katika ile nyumba kuitwa na Vanessa.
Aliweza kumfuata na Vannesa aliweza kuelekea hadi katika chumba chake. Baada ya kuingia ndani Vanessa aliweza kufunga mlango.
Hatimaye nusu saa iliweza kupita Vikram akiwa ndani ya chumba kile huku Larry akiendelea kuzurura zurura njee ya chumba cha mama yake.
Hatimaye aliweza kutoka akiwa mpole kabisa.
"Bwashe bwashe!! Kuna usalama huko?? Aliuliza akiwa anamshika mkono.
Mama yake alitoka njee na kumtazama larry. Larry alimtizama mma yake bila kusema neno lolote kisha akamshika mkono Vikram na kutembea naye taratibu taratibu hadi kumpeleka chumbani kwake.
**** **** **** ***
"Vikram" aliita Alice baada kutokumuona Vikram kwa siku hiyo.
"Vikram......Vikram" aliita Alice huku akigonga mlango wa chumba cha Vikram.
"Ni kwamba leo hajaja au" Alijiuliza huku akijaribu kuufungua mlango ambao uliweza kufunguka.
Aliweza kuingia ndani na alimkuta Vikram ndani akiwa amekaa tu huku akijikumbatia miguu yake.
"Vikram unashida gani ww?? Vipi unaumwa?? Eeee unajisikiaje?? Aliuliza Alice ambaye alishindwa kutambua ya kuwa hakuwa Vikram pekee yke ndni.
" muache hana shida atakuwa salama tu pindi atakapopata maamuzi sahihi" hiyo ilikuwa sauti ya Larry aliyekuwa amekaa kwenye kochi.
Alice aliweza kugeuka na hapo alikutana na macho ya Larry aliyekuwa amekaa kihuzuni huku akishika tama.
"Boss Larry!! alizungumza kwa mshangao.
" wewe unanifahmu mimi?? Aliuliza Larry huku akimtizama Alice ambaye alionekana kushtuka baada ya Larry kumuuliza swali hilo.
"Ammmmhhhh naitwa Alice Peter mimi ni secretary wa boss Adrian kwahiyo naifahamu kidogo familia yenu"
"Larry" aliita Vikram.
"Ndyo bwashe"
"Twende nyumbni" alizungumza Vikram.
"Una uhakika lakini?? Aliuliza Larry.
" ndyo alizungumza huku akisimama kutoka kitandani pale.
Vikram aliita Alice.
"Niko salama Niko salama kabisa tutaonana kesho nikiwa Niko sawa nitakuja" Vikram aliongoza njia ambako chini kulikuwa na wafanyakazi wawili wakiume waliokuwa wakimsubiria Larry kwaajili ya kumpeleka nyumbn.
Vikram alifunguliwa mlango na hatimaye aliingia ndani ya gari hilo kisha akashuka Larry na yeye akaingia baada ya hapo mlango ulifungwa na kisha wafanyakazi hao wakaingia ndani ya gari na kuliondoa eneo lile.
"Bwashe!!! Alice aliweza kulirudia neno lile huku akiwa bado hajapata maana sahihi kabisa.
Tropina akiwa anapata kinywaji chake karibu kabisa na dirisha lake kama ilivyokawaida yake.Siku hiyo aliweza kulkumbuka tukio moja kabla ya yeye kuwa kipofu na kabla ya Baba yake kufariki dunia.
Akiwa Binti wa miaka 17 alipokuwa akimalizia elimu yake ya sekondary basi Baba yake aliweza kumzawadia cheni ambayo aliweza kumwambia ya kuwa cheni hyo aliweza kupatiwa na mama yake pindi tu alipomaliza masomo yake ya secondary kama alivyoweza kumaliza yeye. Na pia kupindi hicho Mdogo wake Larry alikuwa na miaka miwili tu hivyo bado alikuwa Mdogo sana Ila walikuw wakiishi maisha ya furaha yeye pamoja na Baba na mama yake.
" nimeyamiss maisha yale" aliweza kutamka na machozi yakaweza kumtoka ghafla alihisi kunamtu nyuma yake na alipogeuka kidogo aliweza kushtuka na kutaka kudondoka Ila Vikram aliweza kumdaka tena kwa mara ya pili akiwa amemshika mkono wake mmoja wa kulia kisha akamvuta na kumfanya adondokee kifuani kwa Vikram ambaye aliweza kuyafunga macho yake na kuyafumbua.
"Unashida gani leo mbona kila uhisipo uwepo wangu wajidondosha makusudi kwa kujua kabisa ya kuwa nitakudaka eeehhhh" aliuliza Vikram na kufanya Tropina ajitoe kifuania mwake.
Alipotaka kumpiga kibao Vikram alimdaka mkono wake na kumwambia
"Ka mkono kalaini kama haka kanapaswa kumpikia mumeo na kujipendezesha mwili wako kwaajili yake siyo kupiga piga wanaume"
Tropina aliutoa mkono wake na kuweka glass chini ambayo tayri kinywaji chake kilisha mwagika.
Tropina alitabasamu na kumpapasa Vikram usoni.
"Vick" aliita kwa sauti ya upole na utaratibu kabisa.
"Naam" aliitikia kwa maringo lakini aliweza kurejelewa na kumbukumbu ya kuwa mara ya mwanzo pia aliweza kushikwaga hivyo hivyo ni kilichofata ni kiwiko katika kiwanda chake cha uzalishaji.
Wakati akirejesha akili yake tayari alishakutana nacho. Alimeza mate mafundo mawili kisha akaanza kuhangaika ndani hapo huku akigugumilia maumivu.
"Mjinga wewe kabisa na usije ukajaga kunilaumu mimi kwa kukosa watoto" alijikuta ameropoka Vikram pasina hata yeye kutambua kwani aliendelea kuyasikilizia maumivu yake.
**** ***** *****
Kulikucha asubuhi na hali ilikuwa shwari ndani ya nyumba huku watu wakiwa mezani kwaajili ya kupata kifungua kinywa.
"Bwashe njoo ukae tunywe chai" alizungumza Larry.
"Bwashe!! Aliirudia kauli ile Tropina na kuwafanya watu waiwekee umakini.
" hivi umemuita Vikram bwashe" aliuliza Vanessa.
Adrian na yeye alimtizama Vikram huku kipisi cha mkate kikiwa kipo mdomoni mwake.
"Aaaaahaaaaaa kuna demu mmoja namfuatilia na yeye ni Kaka yake kwahiyo ni bwashe wangu" alipotezea Larry kinamna hiyo.
"Demu!!! Wote watatu waliongea kwa mshangao.
"Sasa nyie wawili mnashangaa nini Vanessa na Adrian kwani hamuelewi nini.....wakushangaa hapa ni huyu mwanamk Tropina maana ndo hajui kitu kabisa zaidi ya kuamrisha watu na kuwapelekesha atakavyo.......we Tropina demu maana yake mwanamke namaanisha WiFi yako" alizungumza Larry kwa msisitizo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umri wako?? Aliuliza Tropina.
" miaka 9"
"Huoni ya kuwa wewe ni Mdogo sana hupaswi kuanza hayo mmbo" aliongea Tropina.
"Umri wako??? Aliuliza swali hilo Larry.
" 24" alijibu Tropina
"Huoni kwamba umri wako umeenda na kwasasa unatakiwa ujiingize kwenye mahusiano?? Aliuliza swali hilo Larry.
Tropina aliweka uma chini aliokuwa anautumia kulia mayai na kusimama katika kile kiti kisha akaanza kuongoza kwenda ndani.
Ghafla akiwa anatembea alihisi maumivu kichwani mwake na kama vile anaona mwanga hafifu mbele yake hakuchukua hata sekunde kadhaa alijikuta amedondokea mikononi mwa Vikram.
Wote waliweza kuinuka kutoka katika viti huku maneno yao mdomoni yakiwa ni
"Tropina"
Adrian alibaki akiwa amekaa huku akiwatizama wengine walioweza kusimama kwaajili ya Tropina.
"Embu mpigie simu docta wake aje amuangalie fanya haraka" alitoa amri hiyo Vanessa huku akimpa ishara ya Vikram ampeleke ndni ya chumba chake.
Larry alielekea moja kwa moja hadi kwenye simu ya mezani.
"Vanessa namba ya dactari wake mimi sina kichwani.....nimpigie wa kwangu au?? Aliuliza
" Mjinga kama Baba yako tu" alizungumza Vanessa na kuelekea kwenye simu ile ya mkononi alipofika aliandika namba il kabla hajapiga alimtizama Larry na kusema.
"Nahisi namba hizi niza dactari wangu"
"Ndyo unaakili kama za mume wako" alijibu Larry na kuondoka zake.
"Huyu mtoto mshenzi huyu anamjibu nani?? Aliuliza Vanessa na kungata mdomo Wake.
**** **** *** ***
Alice akiwa ameingia ndani ya ofisi ya Adrian aliweza kuweka faili alizoweza kuzileta mezani kisha baada ya kufanya hivyo alianza kutazama kulia na kushoto alipohisi hakuna mtu alichomoa cheap moving camera katika maziwa yake kisha akaweka katika shelfu moja ambalo lilikuwa na kitabu kimoja kikubwa aliweza kukisogeza kisha akaweka camera pale alishika masikio yake kwani tayari alikuwa akisikik kwa kila akifanyacho.
" halo.......ndiyo bossi.......sawa"
Baada ya kumaliza kufanya kile alichokuwa akikifanya alijitengenezea kisha akatoka njee ambako mlangoni alikutana na Adrian na baada ya kumuona Adrian aliweza kushtuka.
Adrian alimtizama na kutizama ofisini kwake.
"Kuna tatizo kwni??? Aliuliza.
" hakuna bali nimeweka mafaili ya ile kazi ya jana ofisini kwako"
"Oky sawa" alijibu Adrian.
"Alafu leo umechelewa sana kuja ofisini? Aliuliza Alice.
" aaaaahaaaaaa huyo kipofu leo alidondoka nyumbni ndo nimeacha wanamshughulikia huko nahisi docta wake atakuwa amekuja"
"Kwahiy ujui kilichomdondosha??
" Hajawahi hata dondokaga ndo mara ya kwanza kabisa namuona kwamba na yeye anaumwaga kwanzia nimfahamu aaahhhhhh alicheka kidogo kisha akasema. "Tropina eti na yeye leo anaumwa!! Alifungua mlango wa ofisi yake akaingia ndani huku akicheka.
***** ****** *****
Walionekana Larry Vanessa na Vikram wakiwa njee ya chumba cha Tropina.
Huku Larry akimtizama mama yake.
" Vanessa "
"Abee"
"Eti na wewe leo unajali kuhusu huyo mwanamke huko ndni"
"Nani anajali kuhusu nani?? Aliuliza Vanessa.
" Vanessa anajali kuhusu Tropina " alizungumza Larry.
"We kinachokuzungusha hapa ni nini?? Aliuliza Vanessa.
"mimi.......hamna............mimi mbona Niko hapa kwaajili ni njia ya kuelekea kwenye chumba changu na hapa kuna upepo mzuri ndo maana nazungukia hapa" alijielezea Larry.
"Mmmmmhhhhhhhh aliguna Vanessa akimtizama Larry.
Wakati huo Vikram alikuwa akizunguka zunguka huku vidole vyake vikiwa mdomoni mwake hakuweza kuvitoa kabisa.
" bwashe" aliita Larry lakini bado kulikuwa kimya.
"Bwashe aliita tena
" Baba!!! Vikram eeehhhh"
Vikram aliweza kushtuka na kumtizama Larry.
"Usijali atakuwa salama tu " alizungumza na Vikram alitingisha kichwa huku akiendelea kuvipishanisha vidole vyake mdomoni.
Mlango ulifunguliwa na docta alitoka njee.
"Vipi anaendeleaje walijikuta wameuliza wote kwa pamoja.
" anaendelea vizuri tu kidogo alipata mshtuko tu ndani ya..........."
"Doctor Helen wewe unaweza ukaenda tu" ilikuwa sauti ya Tropina aliyeweza kutoka huku akiwa amefungwa kitambaa cheupe machoni mwake.
"Mbona imekuwa hivyo?? Aliuliza Larry.
"Umemfanyaje??? Aliuliza Vanessa.
" macho yake yameanza kupona sindiyo?? Aliuliza Vikram na wote walimgeukia na kuona swali lake ndiyo lenye maana.
"Macho yake yamepona??? Waliulza Vanessa na Larry.
"Hpana lakini kuna.......... Kabla docta Helen hajamalizia kuzungumza.
Tropina alimuomba aondoke.
" eheee na nyie mnafanya nn hapa??
"Baada tu ya kutoka ndani hali yote ya hewa imebadilika bora niende kwenye chumba changu" alizungumza Larry na kuondoka zake.
"Aaaaiiishshshshshsh Larry kazungumza ukweli hali ya hewa y hapa imebadilika" alimalizia kuzungumza Vanessa na kuondoka.
"Eheee na wewe" aliuliza Tropina na sasa alibki Vikram pekee yake.
"Nipo hapa kwaajili yako nataka kufahamu macho yak kwanini yamefungwa hivyo?? Aliuliza Vikram pasina wasiwasi wowote .
"Na wewe ni nani mpaka uniulize mimi hivyo? Aliuliza Tropina
" mtu anayejali kuhusu wewe niambie kwann umewekewa hiyo machoni?? Aliuliza tena Vikram huku akimshika Tropina mikono yake na kumfanya asisimuke.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tropina alijikuta anashindwa kuongea hivyo alikohoa na kuitoa mikono yake alafu akaingia ndani ya chumba chake kwa kupamiana na sofa lake kisha akaufungua mlango wake kwa uwoga.
Vikram alibaki akigonga mlango njee ili afunguliwe na Tropina lakini hakuweza kufunguliwa.
****** ***** *****
"Anaendeleaje huyo??? Aliuliza Adrian baada ya kumpigia simu Vannesa.
" nilizungumza na dactari wake na alinambia ya kuwa kidogo Tropina anaweza akawa na uwezo wa kuanza kuona lakini atahitaji kufuata masharti aliyoweza kupewa basi kuna uwezekano wa yeye kupona kabisa" alizungumza Vanessa kwa furaha.
"What akapona kuwa kipofu??? Aliuliza kwa sauti ya juu na mshangao ambayo iliweza kupenya hadi masikioni mwa Alice ambye na yeye alijikuta amesimama kwa pale alipokuwepo.
" vipi mbona kama umeshtuka aliuliza Vanessa baada y kuhisi hivyo.
"Hamna hapana ni taarifa nzuri hizo mbona alizungumza Adrian.
" basi sawa baadaye nitawahi kuja nyumbni leo pia kwamaana sina kazi nyingi"
Adrian alikata simu kuchukua koti lake haraka haraka kisha akaanza kutoka njee ya ofisi yake Ila mlangoni alikutana na Alice.
"Boss Adrian unaelekea wapi?? Aliuliza kimtego.
" nitarudi kesho leo sitakuja tena ofisini" baada tu ya kumaliza kutoa maelezo hayo aliweza kuondoka zake.
**** **** ***** ***
Tropina akiwa ndani kwake maneno aliyoweza kuyakumbuka yalikuwa ya Vikram tu na maneno hayo yalimfanya ajikute anatabasamu na kucheka huku akikifungua kitambaa kilichokuwa machoni mwake alichoweza kufungwa na docta Helen baada ya kumaliza kufanya hivyo sasa alichukua kioo kidogo kilichokuwa pembeni yake na kuanza kukielekeza machoni mwake huku bado maneno ya Vikram yakiwa yanajirudia kichwani mwake.
*** *** **** ****
Alionekana binti mmoja akiwa anaelekea katika hotel moja huku akiwa anatizama kulia na kushoto kama kuna mtu yoyote yule anayemtizama yeye Binti huyo aliweza kuonekana akiwa anamfuatilia Adrian siku kadhaa zilizoweza kupita baada tu ya kuondoka pale alipomuona Vanessa akija kuzungumza na adrian ndani ya hotel. Kama bado mtakuwa na kumbukumbu.
Aliweza kufika reception kisha akatoa maelezo fulani na kuondoka zake eneo lile baada ya kuelekezwa njia.
Hatimaye alipanda lifti na kuelekea katika chumba kimoja ambako aliingiza Master card na kufungua aliingia ndani na kukuta chumba kikiwa kimepambwa vizuri kabisa huku maua ykiwa yanamueleza mahali pa kwenda.
Alianza kuyafuata na hatimaye alikuta meza ikiwa na glass mbili zenye red wine ndani yake.
Ghafla aliweza kukumbatiwa nyuma na mikono ya kiume ambayo iliweza kuonekana mbele ya tumbo lake.
Mwanaum huyo aliitoa kofia yake na kumbusu begani huku akimfanya na msichana yule na yeye atoe kofia yake kisha akaelekea mezani na kumkabidhi glass moja na yeye akachukua moja na kuweka mdomoni. Hapana shaka huyu alikuwa Alice.
Alice aliweza kugonga cheers na kunywa wine yote.
"Hope sasa utakuwa tayari kuniambia kila kitu ilisikika tu sauti ikizungumza huku akiwekea glass chini baada na yeye kumaliza kunywa alafu akachukua barafu iliyoweza kuwa katika glass nyingin aliyoweza kuiandaa.
Aliweza kuutoa ulimi wake njee kisha akaiweka barafu ile mdomoni mwake alafu akasimama na kwenda nyuma ya Alice ambako aliweza kuishusha kola yake kwa chini kidogo kisha kuanza kuweka ulimi wake wenye barafu katika shingo ya Alice aliyekuwa akiing.ata meno yake kwa raha aliyoweza kuisikia yeye mwenyewe.
" Madam Tropina anauwezekano wa kupona macho " alizungumza Alice na kumfanya mvulana yule aache kile alichokuwa akikifanya kwa kushtuka na kuyatoa macho yake makubwa.
"Unamaanisha nini unaposema ya kuwa Tropina anaanza kupona upofu??.
*** *** *** ***
Tropina aliweza kutoka njee ya chumba chake ambako aliweza kuhisi kuna uwepo wa Vikram mahali pale.
"Vicky!!!! Vicky!!!! Aliita tena kwa mara nyingine lakini hakuyasikia majibu yoyote.
Aliweza kutizama huku na kule pale alipohisi hamna mtu anayeweza kumuona.
Alitabasamu kisha akatizama chini na upande ambao Vikram alikuwa amejiegesha na hatimaye akapitiwa na usingizi.
Aliinama na kuanza kumtazama huku akiutizama mdomo wa Vikram na kuzungumza moyoni mwake.
" amah kwa hakika Vicky ni mzuri tangu siku ya kwanza ambayo nilimuona".
Sasa Tropina alianza kukumbuka ni siku gani ya kwanza aliweza kumuona Vikram.
Aliweza kukumbuka siku yakwanza kabisa Vikram alivyoweza kupishana na Vikram aliyekuwa amekuja kwa mara ya kwanza kabisa katika nyumba yake.
Alitabasamu na kuendelea kumtizama Vikram vizur. Ghafla Vikram aliweza kuyafumbua macho yake na hapo Tropina alishtuka kidgo adondoke.
"Umenishtua wewe" alizungumza huku akiiushika moyo wake.
"Unaniona?? Aliuliza Vikram.
" Nakuonaje na mimi ni kipofu?? Alidanganya Tropina.
"Dactari alisemaje kuhusu macho yako sasa kwanini aliyafumba?? Aliuliza Vikram.
Tropina aliweza kukumbuka vile dactari alivyoweza kumwambia.
"Tropina inabidi uwe makini na afya yako kula vile vyote nilivyoweza kukushauri ule pia punguza mawazo na dawa nilizoweza kukupatia hakikisha ya kuwa unazitumia kwa muda muhafaka kabisa kama hutoweza kufanya hivyo basi macho yako yatapoteza uwezo wa kuona na utakuwa kipofu sasa wa kweli siyo ku act tena" hayo yalikuwa maneno ua docta Helen.
Alimtizama Vikram na kumwambia
"Alinifunga na kunambia ya kuwa macho yangu yanaweza yakapona kama nitakuwa nakunywa dawa na kufuata maelekezo yote aliyoweza kunipatia"
Vikram alimshika mikono Tropina kisha akamuita.
"Pinah" Baada tu ya kutamka jina hilo Tropina alijikuta jina hilo likiji rudia rudia kichwani mwake huku akiwa kama vile anamkumbuka mtu ambaye alikuwa akimuitaga jina hilo.
Haikuwa kwake tu bali hata kwa Vanessa aliyekuwa akiyasikiliza mazungumzo yale.
Alirudia kulitamka jina lile Pinah huku akimkumbuka mtu ambaye alikuwa akimuitaga Tropina kwa jina hilo.
"Usijali kuhusu macho yake utapona na utaweza kuona tena kama ulivyokuwa ukionaga"
"Wewe ni nani??? Aliuliza Tropina.
"Unamaanisha nini ukiniuliza mimi nani, me ni Vikram..............imekuwaje kwani ni kwamba umepoteza kumbukumbu au Tropina unajisikiaje?? Aliuliza kwa kuhamaki Vikram.
"No....Niko salama tu kidogo ulivyoniita mara ya kwanza kumenishtua" alizungumza na kusimama pale alipokuwa ameweza kuchuchuma kisha akaanza kuingia ndani ya chumba chake akiwa kama mtu aliyeweza kubeba magunia mazito katika kichwa chake au amefungwa minyonyoro mizito miguuni mwake hiyo ni kutokana na jinsi alivyoweza kutembea.
"Pina si kifupi cha Tropina au mbona huyu kama kashtuka sana utafikiri nimeongea kitu cha kutisha sana" alilalama Vikram huku akisimama zake.
"Kuna shida gani mbona Vanessa na Tropina kama wameshtuka sana baada ya kusikia jina Pina?? Hilo swali alikuwa akijiuliza Larry.
" anyway hayanihusu hata hivyo nilikuwa napita tu ndo nikasikia" alizungumza Larry na kuelekea chumbani kwake.
**** **** ****
Adrian akiwa ofisini kwake ujumbe uliweza kuingia katika cmu yake. Aliweza kuusoma na baada ya kumaliza kuusoma alipiga simu.
"Hakikisha kazi hiyo unaifanya usiku wa leo........na hakikisha unaifanya kwa umakini mkubwa zaidi alisisitiza Adrian na kukata simu yake huku akisema
" Tropina natumaini huo mchezo unaufanya sasa mwisho wake ni leo" alizungumza na kucheka.
Wakati akiyafanya hayo yote alikuwa akionekana kutokana na camera iliyoweza kutegeshwa na Alice.
Mtu yule aliichukua simu yake kisha akapiga huku nako ofisini simu ya Alice ilikuwa ikiita Alice aliwatizama wafanyakazi wenzake akawaona wako busy na kula chakula cha mchana kwa pamoja hivyo alitoka na kwenda njee kwaajili ya kuzungumza na simu hiyo.
"Mbona umechukua muda mrefu hivyo kupokea aliuliza mtu yule baada tu ya Alice kupokea simu.
"Saruni kwanini unanipigia simu sasa hivi jamani na unajua Niko kazini??
"Hata mimi nataka nikupe kazi pia alijibu na hatimaye sura yake iliweza kuonekana alikuwa mrefu na mweupe ambaye kila nguo ambayo angelitaka kuivaa isingeliweza kumchukiza hata kidogo nywele zake ziliweza kuweka mawimbi mengi kichwani hivyo kumfanya azidi kuvutia zaidi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kazi gani sasa hiv nipo kazini nitakutafuta baadaye" alizungumza Alice.
"Hpana naihitaji hiyo sms iliyoweza kuingia katika simu ya Adrian kwani najaribu kumzoom ili nisome hiyo msg lakini maandishi hayasomeki kwasababu camera iko kidogo mbali na yeye"
Baada ya dakika tano kupita msg iliweza kuingia katika simu yake.
"Waooo ndo maana nakupendaga sana Alice we mshapu sana"
Hapo hapo simu iliweza kuita na alipokea.
"Ndyo nimeiona basi ujiandae vizuri usiku wa leo kuna mahali nataka tuendee ili nikupongeze kwa kuifanya kazi hii vizuri sana" alizungumza Saruni.
**** **** **** ****
"Hallo............ndiyo nimeshafika eneo lenyewe" alizungumza kijana mmoja ambaye na yeye aliweza kuhusika juu ya utekaji wa Larry jina lake ni Daudi.
***** **** *****
Katika upande mwingine alionekana Saruni akiwa ndani ya gari na simu yake iliita
"Haloo!!!........nini......hpana mpaka hapa vile demu wangu alivyoweza kufanya inatosha sasa kaangalie record za mke wako Tropina mwenyew mimi naenda zangu kujivinjari" baada ya kumaliza kuzungumza hivyo alikata simu.
"Huyu Rickson huyu anataka kunifanya mimi kama mfanyakazi wake mjinga kabisa huyu" alizungumza Saruni na hatimaye aliweza kumuona Alice akija eneo lile huku akiwa amevlia gauni lenye kumpendeza mwilni wake.
Saruni alitoka njee kisha akaufungua mlango wa gari na Alice alpoweza kufika aliingia ndani ya gari kisha Saruni akafunga na safari ya kutoka pale ikaanza.
**** **** ****
"Nafikiri kila kitu kipo vizuri sasa unaweza ukaingia sasa hakikisha ya kuwa unalipata hilo faili lenye recodr zote za afya yake" alizungumza Adrian na kukata simu.
"Tuone sasa hivi ni kweli wewe ni kipofu au una act kuwa kipofu ili unikamate mimi kwa urahisi zaidi"
Haya sasa unafikiri kipi kitafuata baada ya Adrian kuanza kuwa na hisia ya Tropina anaweza akawa anaigiza kuwa kipofu???
Hatimaye Daudi aliweza kuingia ndani ya hospital ile kwa kutumia mlango wa nyuma ambao uliweza kufunguliwa na nurse mmoja aliyeweza kushirikiana na Adrian katika hilo alitangulia mbele na Daudi aliweza kumfuata nyuma alipofika mahali aliweza kukihifadhi kiti cha kubebea wagonjwa alikitoa kisha akamtaka Daudi akae pale kisha ampeleke kama mgonjwa kwani ulinzi ulikuwa mkali sana kwa wakati huo.
Hatimaye alifanikiwa kuingia hadi ndni kwa docta Helen baada tu ya kufika ndani alianza kuingia kwenye droo zake na kuanza kutafuta file la Tropina kwa umakini zaidi alitafuta zaidi ya dakika 10 lakini hakuweza kulipata ghafla alihisi kuna mtu anakuja katika chumba kile aliweza kukimbilia ndani ya kordo moja iliyokuwa ndani ya ofisi ile ya Helen.
Aliingia docta Helen mwenyew kisha akatoa faili moja katika droo yake iliyokuwa pale ndani ghafla simu yake iliita
"Haloo.......ndyo...... Huzioni.....embu subiri nije nikupe" alikata simu baada ya kuyazungumza maneno yale kisha akatoka ndani ya chumba kile baada tu y yeye kutoka njee Daudi alitoka pale alipoweza kujificha kisha moja kwa moja akalielekea faili lile na kulifunua.
Alitabasamu baada tu ya kuliona lina jina la Tropina pamoja na picha yake. Aliitoa simu yake ya mkononi kisha akaanza kuzipiga picha zile document na baada ya kumaliza alitizama kulia na kushoto kama kuna aliyeweza kuwa akimuona baada ya kugundua ya kuwa hakukuwa na mtu alijitengenezea vizuri kisha akatokea mlangoni na kuacha zile documents pale. Baada tu ya yeye kuondoka docta aliingia kwa kucheka na ghafla simu yake iliita.
"Hallo.......ndyo niliweka file fake hapa mezani kama ulivyonitaka nifanye hivyo kisha nikajifanya simu imeeita na kutoka njee alafu nikawa namchungulia kwa njee alivyokuwa akipiga picha documents fake.
" usijali documents original zipo salama kbisa alizungumza huku akilitoa faili lingine lenye rangi ya kijani na kuliweka juu ya lile faili lenye rangi nyekundu.
Alikata simu kisha akachukua faili original lenye recodr zote za ukweli kuhusu Tropina na kuenda kuweka katika droo nyingine ambayo alihisi kwa hapo documents zitakuwa salama..
Baada ya kumaliza kufanya hivyo basi alitoka njee ya chumba chake na kuzima taa.
"Huyu mjinga anazima taa aliambiwa kuwa ndani yuko mwenyewe au!?? Ilikuwa sauti iliyokuwa inatoka pembni kabisa mwa kabati moja alipoweza kujificha muda mrefu.
" aaaaiiishshshshshsh nimekaaa sana kwa muda mrefu eti " alizungumza huku akielekea kwenye document original ambzo docta Helen aliziweka huko akiamini ya kuwa ni salama.
Aliweza kuwasha tochi ya simu yake na kuzitizama alizipiga picha kisha akalirudishia faili lile pale na kutokomea kwa kupitia dirishani.
**** **** **** ****
Vanessa alikuwa ofisni kwake na yeye baada tu ya kuweza kupatiwa copy ya faili la Binti wake Tropina kisha akaanza kuyapitia maelezo yote yaliyoweza kuwa ndani yake.
Ghafla mlango wake ulifunguliwa na aliingia Adrian.. Alisogea mpaka alipo Vanessa kisha akampiga busu
"Kuna nini mbona leo umekuja ofisini kwangu asubuh?? Aliuliza Vanessa akimtizama Adrian.
Adrian aliingiza mkono wake mfukoni kisha akatoka na tiketi ambazo aliweza kumpatia Vanessa.
" waoo tiketi za kwenda kutizama move" alizungumza tu baada ya kuziona na kuzisoma.
**** **** **** ****
"Unafanyaje sasa?? Aliuliza Tropina baada ya Vikram kukaa juu ya mapaja yake.
" wewe ni mbishi sana ma mimi natamani upone kabisa kwahiyo kama sitakulazimisha kukupaka hizi dawa hutaweza kupona.
"Sawa yote kwa yote nani anawekewaga dawa kwa style hii unayoweza kunifanyia mimi hapa?? Aliuliza na kumtazama Vikram aliyeweza kuwa juu ya mapaja yake.
Ghafla aliingia Diana na kuwakuta katika hali ile.
"Ammmh Madam Tropina una mgeni wako"
"Ni nani huyo?? Aliuliza Tropina.
" Ni nani wa nini huruhusiwi kabisa kufanya chochote sasa nahitaji kukupaka hii dawa ya machoni na unajua unatakiwa upumzike ndani ya dakika30 bila kufanya chochote na muda wa kupaka dawa ndo huu..... Kamwambie Tropina amelala aje baada ya masaa 2 aliongea Vikram lakini ghafla vilionekana viatu vya kiume vikiingia katika chumba cha Tropina.
"Waaaaoo nashangaa sana maana anayejibu si Tropina alizungumza mtu yule aliyeweza kuingia ndani pale.
Tropina alishtuka tu baada ya kumuona mtu huyo na alisima ma kwa wasiwasi mkubwa hadi kufanya Vikram aweze kudondoka na kupigisha matako yake chini.
Baadaye kidgo alionekana Vikram akiwa na Larry juu kabisa ya ngazi kisha wakiwa wanatizama sebleni.
" ni nani huyo?? Aliuliza Vikram.
Larry alisunya kisha akasema
"Namchukiaga mimi huyo askari simpendi kbisa awe bwashe wangu lakini dada akimuonaga anachekaga chekaga tu" alizungumza Larry
"Utaamini dada yako amenidondosha chini kwaajili ya huyo mwanaum alafu ajapaka dawa mpaka sasa hivi" alizungumza Vikram akiwatizama walivyokuwa wakicheka kwa pamoja.
"Tufanyaje sasa?? Aliuliza Larry.
" Tropina anahitaji azitumie dawa kwa muda muhafaka asiongeze wala asipunguze......nani hatari kwa afya yake kama atafanya hivyo lakini muangalie mwenyew hata awazi kabisa kipi kitamtokea alizungumza kwa sauti ya huzuni kabisa huku akiutizama mkono wake ulioweza kubeba dawa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliamua kurudi zake ndani akiwa amenyong.onyea.
"Huyu naye katok wapi jamani!! Ona anamfanyia bwashe wangu mpaka anataka kunitoa machozi mimi." Alizungumza na kupanda juu alipoweza kuelekea Vikram.
Alikuwa James aliyeweza kuwa inspector katika kituo kilichopo ndani ya jiji la dar es salaam.
Ghafla alishuka Larry kisha akasimama mbele yao.
"Unashida gani wewe mtoto aliuliza Tropina baada tu ya kumuona.
" wewe alizungumza kwa kumuita James.
"Ahaaa naitwa inspector James.
"Sitaki kujua kama wewe ni inspector au generali lakini usije ukampenda dada yngu maana mimi sitaki wewe uwe bwashe wangu"
"Unazungumza nini wewe?? Aliuliza Tropina baada ya kuona ya kuwa mdogo wke ameongea maneno mazito.
" na wewe alimgeukia Tropina "
.
"Mimi nini?? Aliuliza Tropina.
" Simtaki mimi huyu kama bwashe wangu kwahiyo uruhusiwi kumpenda hata kidogo na nakupa dakika mbili malizia kuongea upande chumbani kwako ukawekewe dawa" alimalizia Larry.
"Haka katoto kana mcomand nani eti.......haka katoto"
Kabla hajamalizia kuongea tayari Larry alishaweza kuzungumza kwa sauti ya juu.
"Wewe alafu usiniite haka mimi ni Kaka yko tena wa kiume na mimi ndyo kama Baba ndani ya hii nyumba nikikwambia kitu cha serious usinichukulie pouwa kabisa kwnza panda juu uwende ukapakwe dawa na wewe ndugu inspector cjui afande naomba uwende" alizungumza Larry huku akimtizama Tropina.
"Haka............."
"Shshshsh haya haraka panda juu" alirudia tena Larry.
Tropina aliisimama kisha akimtizama Larry na akaamua kupanda zake juu kwa hasira.
James na yeye hakuwa na la kufanya zaidi na yeye kuondoka eneo lile.
"Mmmhhhh mmmmmhhh mmmmhhhhh mmmmhhhhh kumbe nalelea simba ndani ya nyumba atakayeweza kuja kunizuru baadaye alizungumza Adrian baada ya kuona tukio hilo.
'Nilidhni Tropina ndyo kuchukua tabia ya Baba yake lakini hpana ni Larry na hii ni mbaya kwa upande wangu kwni anauwezo wa kunimaliza siku siyo nyingi endapo nikimuacha na yeye aendelee kuwa mkubwa inabidi nimtafutie kitu kizuri kwaajili yake. Alizungumza na kucheka baada tu ya kukumbuka tena tukio lile.
Ni baada ya Rickson sasa kupiga simu.
"Halo!! Ndyo kila kitu nimeshakiweka tayari alizungumza Rickson na kukata simu yake.
**** ***** *****
Tropina akiwa ndani ya chumba chake huku akikumbuka maneno aliyoweza kuambiwa na Larry.
" Hivi haka katoto kalikuwa kanam gombeza nani hivi!!! Na kwanini.....hivi" alizungumza huku akiendelea kuyarudia maneno Yale.
**** **** ****
Alionekana Vannesa akiwa Adrian wakiwa wanaelekea katika jumba la sinema baada.
"Vanessa...... Naelekea uwani kidogo naomba unisubiri ndani ya dakika moja" alizungumza kisha akaondoka eneo lile. Alianza kuelekea maeneo ya uwani lakini alipofika mlangoni alikata kona na kuelekea sehemu nyingine kabisa ambako Vanessa hakuweza kumuona Ila yeye aliweza kumuona.
"Haloo.... Hakikisha unafanya kile nilichoweza kukwambia" alizungumza Adrian kisha akakata simu yake na kutoka akiwa anajitengenezea kama vile alikuwa uwani.
Alimshika mkono Vanessa kisha akaondoka naye na kuelekea kwenye jumba la sinema.
*** *** *** ***
Alice naye alikuwa ndani ya chumba cha ofisi cha Adrian akitafuta kitu ambacho aliweza kuelekezwa na Saruni. Alipekuwa kila mahali lakini bado hakuweza kufanikiwa kbisa. Alikata tamaa na kuamua kupiga simu.
"Halo mimi sioni hicho ulichonituma nikutafutie" baada ya kuzungumza hivyo alikata simu na hatimaye alikutana na mfanyakazi mwingine wa eneo lile macho kwa macho. Alishtuka na kumtazama kwa wasiwasi.
"Nini hicho ambacho umekitafuta na hujakipata?? Aliuliza mfanyakazi yule ambaye kwa mara ya kwanza aliweza kutowa package baada tu ya Vikram kuja na kuchukua akisema ametumwa na Tropina na yeye ni mumewe jina lake aliitwa Alphonse.
Alibaki akicheka tu huku akimtizama Alphonse.
**** **** **** ****
"Vikram" aliita Tropina aliyekuwa amejilaza katika kiti chake baada tu ya kupakiwa dawa machoni mwake na kuweza kufungwa.
"Naam"
"Hivi kwnini unajli sana kuhusu mimi ilihali mimi sijali kabisa kuhusu wewe na pia nakufanyia mengi mabaya"
"Me sijali kuhusu chochote kile ukifanyacho juu yangu....najali tu kuhusu usalama wako alizungumza Vikram.
" lakini watu wengi wananichukia mimi sina kutokana na tabia niliyonayo huwa sipendi watu kabisa na nadharau sana wanaume pia sijali kabisa kuhusu utu hata wa mtu kutoka katika familia yangu " alizungumza Tropina.
"Naamini hayo yote yameweza kutokea kutokana na watu walioweza kukuzunguka vitendo walivyoweza kuvifanya juu yako ndivyo vilivyosababisha wewe ukawa hivyo" alijibu Vikram.
"Vikram nashukuru kwa kuwa wewe pekee ndiye unayeweza kunielewa mimi jinsi nilivyo" alizungumza Tropina aliyeonyesha sura ya huzuni.
"Usijali kuhusu mimi kwani napenda sana kutambua vitu vyote vinavyoweza kumkabili mke wangu ili asinipe shida wakati nitakapo kuweka ndani" aliongezea Vikram.
"Vikram kwanini unapenda kuniita mimi mke wako?? Aliuliza Tropina.
"Kwasababu wewe ni mke wangu kweli....." Alijibu Vikram kisha akamfunika na kumwambia.
"Usizungumze chochote sasa nakuhesabia dakika zilizoweza kubaki ili nikutoe hiyo dawa ya machoni"
Tropina aliitikia kwa kutingisha kichwa ishara ya sawa au ndiyo.
**** **** **** ****
Kwa upande mwingine alionekana msichana mmoja aliyekuwa ameshuka ndani ya ndege na kupokelewa na kundi Kubwa la ma bodyguard pamoja na mzee mmoja aliyekuwa ameenda kimakamo na akiwa amevalia nguo za bei ghali sana hapana shaka ya kuwa huyo alikuwa Baba wabinti yule.
"Winnie karibu tena Tanzania mwanangu" alizungumza mzee yule na kumkumbatia.
"Thanks dady" alijibu kwa furaha sana na kumkumbtia
"Yuko wapi mume wangu Rickson mbona hajaja kunipokea aliuliza Winnie.
"Nilifikiria ya kuwa baada tu ya kufika hapa utaweza hata kuniulizia kuhusu mimi ndugu yako lkini cha ajabu umeanza kumuulizia Rickson" ilikuwa sauti ya Binti wa kike makamo yake yakiwa takribani miaka8.
"Waooo Queen Mdogo wangu nimekumiss sana alizungumza na kwenda kumkumbatia Mdogo wake huyo kwa furaha.
" yuko wapi mama?? Alimuuliza Mdogo wake.
Mdogo wake Huyo aliweza kunyoosha mkono mahali mama Yake alipo.
**** ***** *****
Alionekana Winnie akiwa anaingia katika nyumba moja Kubwa ya kifahari huku akiita "Rickson..... Rickso....mkeo nimerudi uko wapi wewe?? Aliendelea kuita kwa sauti ya juu. Ghafla alikutana na viatu mlangoni hapo.
" Rickson hayupo nyumbni " ilikuwa ni sauti ya Saruni aliyeongea akiwa hana utani kbisa ndani yake.
"Waooo Shemeji Saruni......nimekumiss kweli na nimefurahi kukuona" alizungumza Winnie.
"Kama umeshamaliza kuongea nakuomba urudi nyumbni kwenu hapa Rickson hayupo"
"Hapa ni nyumbani kwa mume wangu huna ruksa ya kuniambia niondoke mimi nitakuja wakati niutakao na kuondoka wakat niutakao pia" alijibu Winnie na kuendelea kuiingia ndani huku akiita Rickson.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mpendwa labda nikusahihishe tu hii nyumba siyo ya Rickson bali ya kwangu na Rickson kwani ni mali ya Baba yetu.... Na unaposema ya kuwa wewe ni mke wa Rickson unakosea kwani mke wa Rickson na wahalali siyo wewe labda aamue tu kukufanya wewe kimada na sidhani kama mkewe atakubali kwani ni mkali sana"
"Unaongelea nini wewe?? Aliuliza Winnie.
"Ukishamaliza kupiga kelele huko ndani wakati unatoka funga huu mlango kwasababu naondoka sasa hivi kwenda kumuona Shemeji yangu Pinah" aliongea Saruni na kuondoka zake.
"Anazungumza nini huyu??? Alijiuliza Winnie huku akimtizama Saruni aliyekuwa akiingia ndani ya gari.
**** **** **** ***
Baadaye Saruni alikuwa ndani ya gari na Rickson.
" Huyu mwanamke katokea wapi jaman mpaka huku?? Aliuliza Rickson ambaye sura yake bado haikuweza kuonekana.
"Unamuulza nani sasa na uliyataka mwenyewe?? Aliuliza Saruni.
" lakini bro mimi nilikuwa nafanya utani kwaajili ya kuisaidia kampuni yao na kumtunzia heshima yeye sasa inakuwaje yeye achukulie serious laiti ningelitambua ya kuwa itakuwa hivi basi ningeondoka na zile karatasi za ndoa mimi" alizungumza Rickson.
"Kaka Saruni sasa nifanyaje??? Aliuliza Rickson.
*** *** *** ***
"Nitafutie historia ya huyo mwanamke kwanzia siku yake aliyozaliwa hata siku atakayokufa kama itawezekana" yalkuwa ni maneno ya Winnie na hatimaye akakata simu. Mbele yake alisimama kijana mmoja alimpatia picha kisha akamwambia.
"Nitafutie huyo mwanaum popote pale alipo jina lake anaitwa Rickson"
****** ******* *******
Vikram akiwa ndani ya chumba cha Tropina huku akikagua kagua baadhi ya vitu vilivyomo ndani ya chumba kile hatimaye alikutana na karatasi moja ikiwa pembeni ya kitanda anachoweza kulalia Tropina.
"Ni nini hii?? Aliuliza huku akianza kusoma karatasi lile.
" mbona karatasi ya ndoa hii" aliendelea kuuliza huku akiitizama.
"Vikram kwnini unaisoma hiyo karatasi lilikuwa swali la Tropina lililoweza kwenda moja kwa moja hadi kwa Vikram.
Tropina alielekea moja kwa moja hadi sehemu aliyopo Vikram kisha akamnyang.anya ile karatasi na kwenda kufungua droo yake akaiweka vizuri na kuifunga akaelekea hadi kwenye friji ndogo iliyokuw ndani ya chumba chake akatoa shark mbili kisha akachomoa glass mbili na kumiminia wakati wote huo akifanya hayo mmbo Vikram alibaki akimshangaa huku akihisi ni kwamba anaota au ni nini!!!
Tropina aliketi na kuanza kunywa kinywaji huku akiwasha TV na kumwambia karibu kinywaji.
" unashida gani mbona unantizama hivyo?? Aliuliza akikunja nne na kuielekea TV zaidi. "Unashangaa nini ndo kwamba umeniona leo nikifanya hivi amah!?? Ghafla!!!!!!!
Alishtuka na kujikuta ametema kinywaji alichokuwa amekiweka mdomoni na kumtazama Vikram aliyekuwa bado anashangaa.
" Tropina unaona??? Nna uhakika ya kuwa unaona Tropina una........kabla hajaongea zaidi Tropina aliweza kwenda hadi sehemu alipo kisha akamfunga mdomo............... Huku akijilaumu kwnini amefanya vile mpaka Vikram akaitambua Siri yake.
***** ***** *****
"Bossi Adrian nimejaribu kuitafuta kama ulivyoweza kuniambia lakini bado tu nimeshindwa kuutambua mahali alipoweza kuuficha ndani ya ofisi kwake.. Alizungumza Daudi.
" hivi wewe lini utaifanya kazi kwa ufasaha zaidi!! Hakuna kazi uliowahi kuifanyaga kwa usahihi hata kidogo" aligomba sana Adrian.
"Sitaki kujua utatumia njia gani nachohitaji mimi ni huo muhuri uupate"
"Unauongelea muhuri gani?? Aliuliza Vanessa na kumfanya adrian abaki akicheka na kukosa cha kuzungumza.
**** **** *****
Katika nyumba ya Tropina leo aliweza kuingia Winnie.
" yuko wapi huyo kipofu wenu!! Yuko wapi huyo mwanamke?? Alizungumza kwa sauti sana na kumfanya Vikram na Tropina waweze kutoka ndani na kuyakatisha mazungumzo yao.
"Mbwa gani huyo anaingia kwa kubweka nyumbni kwangu?? Aliuliza Tropina aliyekuwa akishuka chini ya ngazi.
Aliitoa ishara ya aachiliwe kwani tayar alishakuwa chini ya walinzi.
" yuko wapi huyo kipofu aliuliza.
"Inaonekana unamtafuta mtu usiyemfahamu ndo maana unabweka bweka na kutupigia kelele" alizungumza Tropina na kwenda kukaa kwenye sofa.
Winnie alimtizama na alipoweza kurudisha kumbukumbu zake nyuma kwa kuwa tayri alishapitia historia yake aliweza kumtambua .
"Yuko wapi mume wangu Rickson??? Aliuliza Winnie.
" Ricky!!!!!! Aliitika kwa sauti Kubwa na ya mshangao
"Ww nani??? Aliuliza Tropina.
" Mimi mke wake nilifunga naye ndoa Paris mwaka huu mwezi wa 5 yeye ni mume wangu wa ndoa nani halali yngu "
"Ahaaaa kumbe mwaka huu........me nilifunga naye ndoa nikiwa na miaka 9 na baada ya kuona hiyo haitoshi tukafunga ndoa nyingin nikiwa na miaka18 na Rickson 20 mpaka sasa ndoa yetu inamiaka 6 sasa wewe uliwezaje kufunga ndoa na mwanaum wa mtu?? Aliuliza Tropina na kumsogelea karibu zaidi Winnie.
" na huyo unayemuulizia mwsho wa mimi kumuona ni akiwa na miaka11 sijawahi kumuona mpka leo kwahiyo unaweza ukarudi ulipotoka alizungumza Tropina na kusimama.
Unasimama unaenda wapi wewe kipofu " alizungumza Winnie akiwa amezishika nywele za Tropina.
"Bwashe unaona mke wako anapigwa nenda ukamsaidie kumuondoa yule kichaa"
"Mimi niende pale hapan.........kwanza hayo ni mmbo ya kike hatupaswi kuyaingilia alizungumza Vikram huku akipanda juu ya ngazi.
Ghafla aliingia Vanessa na kuzishika nywele za Winnie kisha kumtupia mbali kabisa.
" uko salama binti yangu?? Aliuliza Vanessa na kuanza kumpapasa papasa na kumtengenezea nywele Zake
Huyu mbwa huyu alizungumza na kuanza kumfuta tena Winnie kisha akaanza kumpiga lakini alizuiliwa na Adrian.
"Wewe mwanamk unanipiga unanijua?? Alizungumza Winnie.
" wewe kuwa na heshima na mama yangu kabla ya kumuita mwanamk tazama umri wako na umri wke" alizungumza Larry.
" ahaaahhhaaaaa mnajifanya mnanguvu na midomo sana sasa nitawaonyesha" alizungumza Winnie na kuanza kuondoka.
Kabla hajafika mbali zaidi Alisikia mruzi.
"Wewe sikujui umetokea wapi jin lako nani na kipi kilichokufanya ukajiamini mpaka ukafika hapa lakini nataka kukwambia ya kuwa usijaribu kutaka kuwasha njiti ya kibiriti kwenye kiwanda cha gas huuwez mlipuko wake"
Ni baada ya Tropina kuanza kutishiana na Winnie juu ya Rickson.
Sasa tuendelee Winnie aliondoka akiwa na hasira ya hali ya juu.
"Mpumbavu huyo Rickson yuko wapi mtafuteni popote alipo nahitaji kumjua" aliongea Tropina.
"Me nitamtafuta niachie hilo mimi" aliongea Vikram aliyekuwa akishuka juu ya ngazi baada tu ya Winnie kuondoka.
Adrian alimtizama Vikram kisha akamtazama Vanessa na Larry waliokuwa bado na hasira juu ya Winnie.
**** **** ****
"Lakini ulivyofanya siyo vizuri utaweza je kwenda nyumbani kwa mtu na kuleta vurugu siyo hata nyumbani kwa mtu bali nyumbani kwa mke wa aliyeweza kukusaidia unafikiri Rickson atakubaliana na wewe kupitia hilo?? Alizungumza mama yke Winnie aliyekuwa akimtizama Winnie aliyekuwa akifanyiwa matibabu usoni mwake baada ya kuparuzwa na kucha.
"Mama Rickson ni mume wangu mimi"
"Unajua kabisa kampuni ya Baba yako ilikuwa hatarini pamoja na watu walikuwa wakikushushia heshima yko yeye aliitunza na kuilinda kampuni ya Baba yako kwanini wewe leo unataka kumuharibia maisha yake na mke wake??
"Rickson ni mume wangu mimi siwezi muachie yule kipofu" .
**** **** ****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kazi niliyokuwa nikiifanya siku zote ni sawasawa na sifuri tu kumbe bado kuko na mtu anayeweza kumulikii hizi Mali zote kwamaana hata nikiwauwa hawa wote bado mimi sitapata kitu kwasababu mali zote ziko chini ya huyo mjinga KIPOFU ambaye tayari anamume hata nikimuuwa mali zote zitaenda kwake. Cha kwanza ni kumtafuta huyo Rickson. Aliongea kisha akanyanyua simu na kupiga mahali.
"Haloo kuna kazi mpya naomba tukutane njee ya ofisi yangu baada ya dakika 20 kupita" alikata simu baada ya kuzungumza hivyo huku akisema "Rickson umetokea wapi wewe??" Alipiga meza yake kwa hasira.
Huku nako alionekana Saruni akiwa anamtizama Rickson.
"Nilikwambia mimi sinilikwambiaga lakini huyo mwanamke siyo mtu wa kumsaidia ona sasa kila mtu anakutafuta wewe"
"Sasa bro nitafanyaje nahitajika kumsaidia Tropina zaidi alafu huyo naye sijui katoka wapi alilalama Rickson.
*** **** **** ***
" Tropina nimejaribu kutafuta habari kumuhusu Rickson lakini hakuna chochote nilichoweza kuambulia kwani hana data zozote zile wala picha yake hata moja" alizungumza Vikram .
"Huyo mpuuzi lazima apatikane lazima aletwe hapa eti mume wangu mume gani kubuhu namna hiyo anaowa owa tu wanawake wengi awatakao ananiletea shida mimi na hao wanawake zake" alizungumza Tropina kwa hasira.
"Lakini Tropina huna uhakika kama ni kweli Rickson anafanya hivyo au lah unajua si vizuri kumuhukumu mtu" aliongea Vikram ambaye alinyamaza baada ya kuyaona macho makali ya Tropina.
*** **** **** ***
"Madam ile picha uliyoweza kunipatia imepotea katika mazingira ambayo hata mimi nimeshindwa kuyaelewa.
" unazungumzia nini unaposema ya kuwa picha imepotea katika mazingira usiyoweza kuyaelewa?? Aliuliza Winnie kwa kufoka.
Wakati huo ulionekana mkono uliokuwa umeshika picha na kiberiti cha gas kisha akakiwasha na kuiunguza ile picha.
"Hakuna atakayeweza kunifahamu mimi mpaka nimalize kile kilichoweza kunifanya mimi nikauficha uso wangu mbele za watu" baada ya picha kumalizia kuungua aliikanyaga chini kisha akayapuliza majivu yale na kuyafanya yasambaratike.
**** **** ****
"Ni vigumu sana kumpata Rickson kwasababu hakuna data zozote juu yake" aliongea Vikram.
"Yule mwanamke atakuwa anajua kila kitu kuhusu huyo mpuuzi Rickson lazima niendee kwake" alizungumza Tropina.
"Vicky!! Twende"
"Wapi ......ahaaa kwa huyo mwanamke mimi siendi huko naenda kwa dactari Helen kuchukua dawa zako maana naona ya kuwa unajali sana kuhusu huyo mume wako Rickson badala ya afya yako"
"Vicky samahani kwa hilo lakini nataka nipambane na hili hadi liishe"
"Sawa alijibu Vikram na kuchukua koti lake kisha kutoka njee alipofika njee alikutana na Larry aliweza kumpa maelezo kisha akaondoka zake.
Tropina alitoka njee na alipomkaribia Larry aliweza alishangaa baada ya kumuona ya kuwa anamfuata.
" mbona unanifuata??? Aliuliza Tropina.
"Ww hujaona bwashe akinipa maelezo kuhusu wewe.......... Hata hivyo utaonaje na wewe ni kipofu twende huko unakoenda natakiwa kukurudisha nyumbani salama" alizungumza Larry na kutangulia ndani ya gari.
Tropina alimtizama Vikram aliyekuwa akielekea kwa miguu hospital kwani hapakuwa mbali sana na hapo.
*** **** ****
"Yuko wapi huyo king.ora wenu" hilo lilikuwa swali la kwanza baada tu ya Tropina kuingia katika nyumba ya Winnie.
"Samahani king.ora ni nani?? Aliuliza mfanyakazi wa ndani.
Tropina aliweza kujisahau na kujikuta amenyooshea mkono picha ya Winnie iliyokuwa sebleni.
" nimeshafika niambie kipi kimekuleta hapa kwetu wewe kipofu?? Alizungumza Winnie aliyekuwa akishuka katika ngazi.
"Waooo kumbe ndo unanukaga vibaya hivyo ukiwa umetoka kitandani aaiiisshshsh hujaoga kabisa wewe ndiyo umekurupuka hivyo kutoka kitandani. Alizungumza Tropina aliyekuwa kabana pua.
" wewe kipofu aliongea Winnie na kuanza kunusa gauni lake la kulalia
"Unaongelea nini??
"Inamaana hujasikia ulivyoambiwa au......Unawezaje mtoto wa kike ukalala mpaka saa 4 asubuhi alafu unanuka harufu hivyo jana usiku ulioga kweli wewe? alizungumza Larry.
" na wewe ni nani wa kumwambia dada yangu hivyo " aliuliza Queen aliyekuwa na yeye kaamka huku nywele zake ndefu zikiwa zimevurugika kichwani.
"Uuuwwwhhhh mzimu" Larry alipiga kelele na kukaa nyuma ya dada yake huku akitoa kichwa chake kumtizama Queen.
***** ***** ****
"Itakuwa vigumu kumpata kwasababu hakuna mtu anayemtambua" alizungumza Tropina.
"Na yule mwanamke kichaa?? Aliuliza Vanessa.
" atakuwa anaifahamu sura yake Ila nimemuomba picha hata yeye hana anasema aliyokuwa nayo imepotea"
"Kwanini sasa ikapotea?? Aliuliza Vanessa.
Wakati wote huo larry alikuwa kimya akifikiria jambo.
" huyo ndugu yako mbona kama kadumbukia kwenye wimbi la mawazo " alizungumza Vanessa
"Sasa mimi nitajuaje na sioni" alizungumza Tropina na kusimama zake.
Larry aliinuka na kuelekea chumbani kwake bila kusema neno lolote.
"Huko mlikoenda umemfanyaje Mdogo wako?? Aliuliza tena Vanessa.
Alifika katika chumba chake kisha akaufungua mlango wake na kuingia ndani ambko alimkuta Vikram akiwa anacheza game.
Alielekea moja kwa moja hadi kwenye kitanda kisha akakaa akiwa ameshika tamaa huku anawaza.
"Ww dogo njoo tucheze game" alizungumza bila kumtazama Larry machoni
" We bwashe " aliita Vikram na kugeuka.
"Kuna nini mbona hivyo.....kipi kimetokea niambie. Alizungumza na kumsogelea karibu zaidi.
" nafikiri Tropina siyo kipofu namaanisha Tropina anaona sasa" alizungumza huku akikumbuka jinsi Tropina alivyoweza kunyooshea mkono picha ya Winnie.
"Kwahiyo ni hicho tu hakuna kingine kilichotokea???
Larry alitingisha kichwa akimaanisha hapana.
"Bwashe inamaana wewe unajua y kuwa Tropina anaona?? Aliuliza Larry.
***** ***** ****
Siku moja Winnie akiwa yuko shopping ghafla alitokea mtu pembeni yake na kumuuliza habari yake.
" nani wewe?? Aliuliza.
"Natumaini umesoma vingi kuhusu Tropina kwahiy huwez acha kunitambua mimi ni nani?? Alizungumza Adrian na kutowa miwani yake machoni.
Unafikiri kipi Adrian amekifuata kwa Winnie.......
Vipi kuhusu Vikram atamwambia ukweli Larry ya kuwa dada yake siyo kipofu....
Adrian aliweza kurudi nyumbani na sebleni alikuwepo Tropina aliyeonekana mwingi wa mawazo Adrian alitabasamu kisha akaelekea mahali alipo.
"Tropina" aliita Adrian na kukaa na wakati huo nao Vanessa alikuwa akishuka kutoka katika chumba chake.
"Nini"
"Nataka tuzungumze juu ya Rickson maana sielew ni kipi kimetikea juu yenu.
"Hayo ni matatizo yangu hayakuhusu" alijibu Tropina na kugeukia upande mwingne.
"Lakini hayo unayoweza kusema ni matatizo yako yanaharibu kampuni kwani yanaishushia hadhi na heshima yule mwanamke amekuja leo ofisini na kuleta vurugu sana na hali hii ni mbaya kama waaandishi wa habari watapata taarifa hizi....pia wawekezaji wakisikia wanaweza wakatoa hisa zao na kusababisha kampuni kudondoka au kuelekea mikononi mwa mtu mwingine kabisa" aliongea Adrian.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tropina aligeuka na kumtazama.
"Sasa mimi nifanye nini?? Aliuliza Tropina.
" uniambie kila kitu juu yako wewe na Rickson na mlianza mahusiano wap kwasababu Winnie alisema ameshafunga naye ndoa sasa isije
Ikaw wewe ndy uliyeweza kuchukua mume wa mtu" alizungumza Adrian.
"Sijui chochote kuhusu Adrian kwani hata picha yake siifahamu lakini naweza nikasema mm ndiye wa kwanza kufunga ndoa na Adrian tena ya serikali kwani Baba aliniletea karatasi na kuniambia ni sign ni za mtu ambaye ataweza kunisaidia kwa kiasi kikubwa pindi niwapo shidan"
"Tuone hizo hati za ndoa" alizungumza Adrian huku akiaamini ya kuwa Tropina ameweza kunasa kwenye mtego wake na anahitaji msaada wake.
"Vicky!! Aliita Tropina.
" mmmhhh" aliitikia Vikram aliyekuwa kwenye dimbwi la mawazo.
"Unaweza nenda nisaidia kuniletea kile cheti cha ndoa?? alizungumza kwa kuuliza na Vikram akaenda
" lakini Adrian me naweza sema namtambua Rickson hawezi kufunga ndoa kwa mara ya pili na naamini y kuwa mume wangu hakufanya chaguo baya juu ya Rickson. Alizungumza Vanessa.
"Vanessa hakuna anayeweza kumfahamu Rickson kwa sasa mwisho wa kumuona ni akiwa na miaka9 Ila sasa anazaidi ya miaka 20 watu wanabadilika....tunachoangalia hapa ni kutunza heshima na wadhifa wa kampuni zetu. Alizungumza Adrian na wakati huo Vikram alikuwa akishuka huku akiwa ameshikilia document.
Adrian alizungumza kimoyomoyo hatimaye sasa kiburi na jeuri chako kitakwisha nyaraka hizo zikiingia mikononi mwangu basi ni umekikaribia kifo chako. Alizungumza huku akipokea cheti kile cha ndoa.
Alikikagua na kuuliza.
" original kiko wapi......ili pindi Winnie atakaposambaza y kuwa wewe umemnyang.anya mume wake tunabidi kuonyesha udhibitisho original kabisa y kuwa wewe n mke halali wa Rickson na Winnie ndiye aliyeweza kuiba mume wa mtu. Aliongea Adrian.
"Unamaanisha nini ukisema hicho siyo original?? Aliichukua cheti kile na kuanza kukisoma akiwa amejisahau.
"Sas na huo upofu wako hapo utaweza kusoma?? Alizungumza Vikram kama kumtahadharisha asije akafanya kile anachotaka kukifanya.
" hata kwa kukipapasa naweza gundua kama ni chenyewe au ni photocopy alizungumza Tropina kwa kufanya watu wasielewe kile alichoweza kuelekezwa na Vikram.
"Kwann nani kaenda kukitoa photocopy Alijiuliza mwenyewe.
" Vikram hakuna kingine labda mimi sijawahi kbisa kukitoaga photocopy sasa nani kakichukua original Alijiuliza kwa mshangao.
"Kwahiyo huna original ya cheti cha ndoa??? Aliiuliza Adrian.
" Siyo kwamba sina mimi ndiyo nilikuwa nacho lakini nashngaa kimekuwaje kikawa photocopy??
"Rickson labda ndo anacho original?? Aliuliza Adrian.
" hapana cheti cha ndoa kilitengenezwa kimoja tu na nilikuwa nacho mimi tu wala Rick hana kabisa alizungumza kwa mshangao na kuwa fanya watu wote washangae.
***** ****** ******
"Bado hujafanya kitu hata tukikiteketeza hiki feki bado hatufahamu original iko wapo hivyo hakuna tutakachokuwa tumekifaya" alizungumza Winnie.
"Cheti alikuwa nacho yeye lakini anasema hat yeye anashngaa kuona copy. Alijielezea Adrian.
" una uhakika lakini ukute yeye ndiye amekificha original alafu anasema afahamu mahali kilipo?? Aliuliza Winnie.
"Hapana Tropina azungumzagi uwongo ndiyo maana watu wengi wanamchukia huwa akisema hapana ni hapana kweli hakuna atakayeweza kuja na kabadilisha mawazo yake.
"Sasa kam ndo hivyo cheti original kachukua nani??? Aliuliza Winnie huku akimtizama Adrian ambaye alikuwa na yeye akifikiria.
***** ***** *****
Kama kawaida ilionekana mikono iliyokuwa imeshikilia cheti kile cha ndoa huku akisema.
" Pinah anataka kufanya kitu ambacho atakuja kujutia mbeleni hichi cheti ni cha umuhimu San katika maisha yake na ya kwang huyo alikuwa ni Rickson akizungumza baada tu ya kuweka lamination katika cheti kile.
*** **** *****
"Bwashe" aliita Larry.
"Unajua ile siku uliposema nimpeleke yule kipofu"
"Kuwa na heshima na mke wangu wewe yule ni dada yako"
"Hata hivyo nilishasahau ya kuwa siyo kipofu tena na hapa nazungumza na mme wake......kwenye ile nyumba ya yule dada aliyekuja hapa alafu akasema cjui mke wake na Rickson kuna katoto kadogo kadogo ka kike nilikaona sasa nashangaa mpaka ucku nikilala nakaona tu hata nikitizama TV nikicheza game hata nikikuangalia wewe...........
Kabla hajamalizia neno lake alipigwa na mto na Vikram.
" Ukome unataka kuniona mimi kama mwanamke mjinga wewe " alizungumza Vikram.
"We si ungeniacha nimalizie?? alizungumza Larry.
" umalizie huo ujinga wako?? Aliuliza Vikram na kusimama Zake
"Na ndyo maana"
"Nini?? Aliuliza Vikram.
"Unampenda mke watu" alizungumza Larry.
"Huyu mjinga anazungumza utumbo wake mbele yangu" alijibu Vikram na kuanza kukimbizana sana na Larry ndni pale baada ya kukimbizana na kupigana kutumia mito baada ya dakika tano wote walikuwa wamechoka huku wakiwa wamejilaza kitandani.
Larry alikilalia kifua cha Vikram.
"Toa kichwa chako hapo hichi siyo kwaajili yako" alizungumza Vikram aliyekuwa anahema kwa nguvu.
"Nataka nijue dada yangu na yeye akiwa analala hapa atasikia raha gani*
Walicheka wote kwa pamoja.
" bwashe aliita larry kwa umakini.........dada yngu na mama yangu ndiyo ndugu zangu pekee walioweza kubaki katika dunia hii sitaki baya lolote lile liwapate .. Japokuwa watu wa njee wanaweza sema ya kuwa sisi hatupendani lakini ukweli kutoka moyoni tunapendana sana na endapo mmoja wetu atakumbwa na tatizo basi huwa tunafadhaika sana moyoni na ku act hatumjali mbele za watu.....dada yangu ndiye ninaye huyo huyo mmoja sina mwingn.. Sitaki aje aishi maisha ya shida au ya karaha pindi nitakapokuwa Niko mbali naye nataka kumkabidhi kwako kwani naamini ya kuwa atakuwa salama na wewe pia tayar umeshaeza kuelewa tabia zake kuhusu Rickson nitamtafuta na nitamuomba akuachie wewe dada yangu kwani mimi naamini utaweza kumtunza.
Wakati Larry akiyazungumza maneno hayo mazito Pinah alikuwa njee akimsikia mdogo wake kwa yale aliyoweza kuzungumza alijkuta machozi yanamtoka na kushindwa kuvumilia ilibidi aondoke zake eneo lile Ila maneno yale pia hakuweza kuyasikia mwenyew hata Adrian aliyasikia.
"Nataka ufunge ndoa na dada yangu haraka iwezekanavyo nitamuwekea karatasi za zangu za shule nyingi kisha katikati nitaweka karatasi ya ndoa najua hawezi kusoma zote hivyo atasign na tayari atakuwa mke wako"
Adrian aliweza kuyasikia maneno yale mazito yaliyoweza kumchanganya kichwa.
"Kwa kuwa Tropina ni kipofu ata sign na mali zote tena zitaenda kwa Vikram hapana hii haitakiwi itoke kabisa hapana" alizungumza Adrian huku akihisi kama vile anaelekea kuwa kichaa. Alitoka na kupiga simu anapopafahamu yeye.
"Larry" aliita Vikram.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ikitokea Rickson ni mtu ambaye unamjua nani wa karibu na wewe kabisa Ila ameamua kujificha kwaajili ya kuweka mambo yote sawa. Bado tu utaweza mfanya dada yako nimuowe mimi??? Aliuliza Vikram
***** ****** *****
" ni nan huyo Vikram?? Aliuliza Winnie.
"Ni kijana mmoja anayeishi pale nyumbani sifahamu kwao ni wapi wala historia yake yoyote Ila anatakiwa kumuowa Tropina kesho"
.
"Waooo ni sawa alafu Rickson atabaki wa kwangu" alizungumza Winnie .
"Unaakili wewe atakuwaje wa kwako na bado cheti cha ndoa original hatufahamu kiko wapi ili tusipaje shida mara mbili ya kuja kutafuta tena cheti hiki kingine cha ndoa inabidi tufanya maamuz mazito sana.alizungumza Adrian na kutabasamu.
"Hata akiwa mtu mwingine tofauti n wewe siwez kumpa dada yangu mimi nakutaka wewe tu" alizungumza Larry kwa kumaanisha.
**** **** ****
"Sasa unataka tufanyaje?? Aliuliza Winnie tena.
" Vikram ndo tatizo Kubwa sana kwasasa inabidi tumfanye aondoke katika ile nyumba " alizungumza Adrian.
"Sawa mimi nitatafuta hicho cheti cha ndoa original na kukisambaratisha" alizungumza Winnie kisha akainuka na kuondoka zake.
***** **** ****
"Unawaza nini?? Lilikuwa swali na Vikram lililoweza kwenda kwa Tropina.
" nashindwa kuelekea imekuwaje mpaka nikawa na photocopy y cheti cha ndoa ilihali nilikuwa nacho original na ninani huyo atakuwa amekuja kukichukua cheti hicho?? Aliuliza Tropina.
"Labda uyo mume wako ndiyo ameamua kuja kukichukua"
"Ricky!!! Aliuliza kwa kustaajabu.
" ndyo Rickson" alizungumza Vikram.
"Na kwnini aje kukichukua sasa?! Aliuliza Tropina.
" kwasababu unataka kufanya kitu cha kijinga bila kumshirikisha yeye " alijikuta akizungumza kwa hasira Vikram.
"Sasa ndo uzungumze kwa hasira hivyo n sauti ya juu hata ungeongea taratibu ningekuelewa" alilalama Tropina akimtizama Vikram aliyekuwa akimtizama yeye.
**** ***** *****
"Cheti cha ndoa unacho wewe?? Aliuliza Vanessa akiwa ofisini kwake huku akionekana kumtazama mtu.
" ndiyo mama" alijibu Rickson aliyeweza kufika ofisini kwa Vannesa.
"Kuwa makini na cheti kile kwani ndicho cha umuhimu zaidi ambcho hata sisi tukifa bado Adrian na tamaa zake hataweza kuzipata mali za mume wangu"
**** ***** ****
Aliingia Winnie akiwa na ameongozana na mwanaume mmoja ndani ya nyumba ya kina Tropina.
"Kilichokuleta hapa" aliuliza Tropina baada ya kumuona.
"Watu wanaposema ya kuwa una tofauti Kubwa sana na vipofu wengine hapo naamini umejuaje ya kuwa nimefika hapa??
"Ungesema kilichokuleta ingependeza Zaidi. Alizungumza Vanessa aliyekuwa akishuka chini baada tu ya kutoka katika chumba chake.
" ohoooo mama Tropina nimekuletea mkwe wako huyu hapa " alizungumza Winnie akimnyooshea kijana aliyeweza kuja naye.
"Nini??? Nan??? Aliuliza Tropina baada tu ya kumpandisha na kumshusha mtu yule kwa kumtizama.
Hakuwa Rickson bali mwanaum mwingine ambaye alipanga kumleta kwaajili ya kuweza kummalizia mbali Vikram pia kwaajili ya kuweza kutafuta cheti original cha ndoa baina ya Tropina na Rickson.
Vanessa alimtizama kisha akacheka.
" ngoja huyu huyu.....ni nani umesema?? Aliuliza tena.
"Rickson nimeona nimrudishe kwenu ili aweze kulipia fidia za kupoteza muda wangu pamoja na kunidhalilisha" alijielezea Winnie.
Vanessa alimtizama kisha akacheka.
"Eti wewe ni nani?? Aliuliza kwa kumsogelea karibu zaidi kijana yule.
" Rickson mama hunikumbuki miaka mingi imepita kweli hata hivyo naona sana aibu nakuja katika familia hii nikiwa katika hali hii" alizungumza Rickson fake aliyoweza kutengenezwa kwaajili ya kufanya kazi ya Adrian pamoja na Winnie.
"Hata kama imepita miaka mingi vipi lakini sauti yako siwez kuisahau......sasa niambie wewe ni nani??? Aliuliza Vanessa kwa sauti ya ukali sana.
" Ni sawa tu aseme Winnie anataka shingapi kama fidia na Rickson apelekwe chumbani kwangu" hiyo ilikuwa kauli ya mwisho ya Tropina na kuingia ndani.
Wakati huo hayo yakiendelea Adrian alikuwa amesimama mlangoni na kutabasamu baada ya kuona ya kuwa dili lake limeweza kufanikiwa.
Baada ya dakika kadhaa kupita walikutana tena
"Nilihisi itakuwa kazi ngumu lakini imekuwa nyepesi sana kuliko nilivyoweza kufikiria" alijipongeza Winnie kwa kunywa juice ya mango aliyoweza kuiweka kwenye glass.
"Tropina siyo mjinga kiasi hicho na hizo millions 3 alizokupa kwake ni kitu kidogo sana lakini kinachonishangaza kwanini amemkubali Frank kwa haraka hivyo?? Aliuliza Adrian.
" we hujui ya kuwa ni kipofu kwahiyo hata harufu yake hawez ikumbuka kwani zaidi ya miaka 10 naa hawajaonana" alijibu tu kwa urahisi Winnie.
"Hata mimi naomba iwe hivyo" alizungumza Adrian.
*** *** *** ***
Alionekana Tropina akiwa ameshikilia plaizi huku akiifuta futa na kuitazama kwa umakini huku akiicheka.
"Yani wewe unaletwa na wewe unaleta tu kichwa chako kama boga hapa sasa lazima uniambie nani kakutuma na million tatu zangu utazirejesha tu Frank. Alizungumza Tropina baada ya kuweza kufuatilia historia nzima ya Frank aliyeweza kuja na kujitambulisha kama Rickson.
***** **** ****
Winnie akiwa anarudi nyumbani kwake alishtuka baada ya kuviona viatu vyeusi vikiwa vimekaa katika ngazi yake alipandisha macho yake mpaka juu na hapo aliweza kukutana uso kwa uso na Rickson.
" Rickson aliita na kutaka kuelekea kule juu alipo lakini alimpa ishara ya asipande.
"Mimi sina mahusiano na wewe tena kwasababu tayar umeshachukua million tatu kwaajili ya kusign karatasi za talaka na umesha sign tayr... Sasa nachohitaji umuache mke wangu pekee yake tafadhali mwache Pinah wangu, na ninaomba ukamchukue yule taira wako uliyempeleka nyumbani kwao. Alizungumza Rickson na kuanza kuondoka.
" Rickson wewe ni mume wangu eti kumbuka tumeowana tukiwa......"
"Wewe umesahau ya kuwa umesha sign karatasi za talaka Leo?? Aliuliza Rickson
"Zilikuwa ni feki wala hazikuwa original"
"Ni kweli wewe uliziweka feki Ila mimi niliweka original......taarifa za kuwa wewe utafanya kitu kama hicho tayar nilishakuwa nazo toka jana hivyo nilikuandalia original na kukuwekea kwenye document zako kisha zile feki nikazichoma moto.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana hapana Rickson wewe ni wangu eti hupaswi kufanya hivyo mimi ni mke wako, alilalama Winnie.
Alifungua pochi yake kisha akatoa zile karatasi n kudondosha zile pesa alizoweza kupatiwa chini alizichana Chana ila sasa Rickson aligeuka na kumtizama kisha akamwambia.
" umesahau ya kuwa hizo ni copy original uliziacha kwa mke wangu !!! Aliuliza huku akimtizama Winnie aliyekuwa akiweweseka kwa kushindwa kuelewa afanye nini.
*** *** **** ***
"Utalala chumba kimoja na Vikram kwamaana bado nimeshindwa kukuamini kwanza. Alizungumza Pinah.
" usijali kila kitu kimeenda vizuri sitaki nikuforce ukumbuke bali vut kumbukumbu taratibu na hatimaye moyo wako utaweza kukwambia ya kuwa mimi ni nani kwako alizungumza Frank bila kujua ya kuwa tayari ameshafahamika.
"Umefuata nini tena??? Aliuliza Vikram baada ya kumuona Tropina.
" utalala na huyu leo mpaka kesho tutamuandalia sehemu nzuri ya kupumzika" aliongea Tropina.
"Nani??? Huyo??? Alale wapi??? Aliuliza maswali mfululizo Vikram.
" kwa leo tu tafadhali alizungumza Vikram.
"Yuko wapi??? Alikuwa akimtafuta mtu Larry.
" unamtafuta nani??? Aliuliza Vikram.
"Nimeambiwa huyo Rickson kaja hapa leo ndyo namuulizia yuko wap??? Aliuliza Larry.
Vicky alimpa ishara ya kugeuka na kumtazama.
Larry alipiga ukunga na kelele baada tu ya kugeuka nyuma.
Ni baada ya Larry kumuona Frank na kupiga ukunga.
"Nini wewe?? Aliuliza Tropina.
" huyu sokwe kutokea wapi huku ndani?? Mbona mbaya hivi?? Alafu ngoja anafanya nini kwenye chumba cha bwashe angu??
"Huyo siyo sokwe huwezi kuona ya kuwa ni mtu na huyo ndyo mume wangu Rickson. Alizungumza Pinah.
" Hivi unauhakika ya kuwa Rickson ndo huyu?? Aliuliza tena Larry.
"Usiniulize maswali mm kwanza wewe hayakuhusu kwani ni mume wako?? Alizungumza Tropina kwa sauti.
" haijalish Ila sitaki kuishi na sokwe huku ndani sitaki wajomba zangu wawe na lisura kama lake....nakwambia hivi mtatalikiana....si mzee aliwaozesha sasa mimi navunja ndoa na kesho naleta karatasi za talaka " alizungumza Larry na kuondoka.
"Huyu cjui Ana majini......tena hayo aliyonayo ni mahurani hivi anafikiria nani ataweza kumkubali huyo sokwe mtu" alizungumza Pina baada tu ya kuingia kwenye chumba chake mlango uligongwa.
"Nani tena huyo??? Alijiuliza huku akienda kuufungua.
" Vicky!! Aliita kwa kutahamaki.
"Nilishakwambiaga sipendi unifupishie hilo jina linakuwa la kike"
"Wewe unashida gani mbona umekuja na blanket chumbani kwangu???
" wewe unafikiri nani anaweza kwenda kulala na yule sokwe...wewe umtoe chumbani kwako umlete kwngu!!
"Hata kama lakini ungeenda kulala kwa Larry" alizungumza Pinah.
"Baada ya kuona sokwe mtu kashtuka na mlango ka funga hivyo sitaki kumsumbua bwashe wangu...... Hata hivyo sitakugusa popote kwasababu sipendag kulala na mwanamk ambaye amevaa nguo nyeusi wakati wa usiku" alizungumza Vikram kisha akaenda kitandani na kujilaza.
"Sasa na kwanini ulale kitandani ungelala chini" alizungumza Pinah
"Kwanini nilale chini
" kwasababu hapa ni chumbani kwangu"
"Nani kampeleka yule sokwe chumbani kwangu......kama hutak lala kitandani lala kwenye kochi" alizungumza Vikram na kujifunika shuka.
Tropina alimtizama na kutizama kwenye kochi akaona ni bora tu apande zake kitandani.
"Kafunge mlango" alizungumza Vikram.
"Wacha kunituma tuma najua kipi cha kufanya" alizungumza Pinah huku akielekea mlangoni kwenda kuufunga.
Alirudia kisha akashusha gauni lake la kulalia chini.
"Nishakwambia sipatanag na manguo meusi kwahiyo usijiangaishe"
"Na nivizuri ukiwa hupatani nayo maana ukinigusa popot pale nitakumaliza leo usiku" alizungumza Pina akiwa mito katikati ya kitanda kisha akalala.
Vikram alitabasamu na kuchukua mto.
"Nini?? Kwanini umetoa?? Aliuliza kwa mfululizo Pinah.
" siwezi kulala bila kuegemea mto" alizungumza Vikram na kutabasamu.
Pinah aliweza kuchukua mito miwili iliyobakia na kuipandisha juu huku akimtizama Vikram.
"Nini tena??
" huwa napendaga kulalia mito miwili" alizungumza na kuchukua mto mwingine wa pili.
Tropina aliamka na kukaa kitandani akimtizama Vikram.
"Nini...unataka nichukue na huu mtu mwingine au" alizungumza na kukaa kitandani.
Tropina aliamka na kuchukua mto uliobaki kisha akavuta na shuka na kuelekea kwenye kochi aliweka mto kisha akalala na kujifunika na shuka juu huku akitizama juu.
"Waooo afadhali umeacha kitanda maana nisingeweza vumilia. Alizungumza Vikram na kujilaza katikati ya kitanda.
Tropina alimtizama na kutizama zake juu kisha kulikumbatia shuka lake na kulipandisha juu zaidi ya kifua chako.
Frank alikuwa njee ya chumba kile akijitahidi kusikiliza walichokuwa wakizungumza lakini alishindwa kuelewa na kusikia pia kilichokuwa kikizungumzwa.
Aliichukua simu na kumpigia Winnie ili ampe taarifa ya kile kinachoweza kuendelea pale.
Wakati anatoka Vanessa aliweza kumuona na kumfuata nyuma nyuma.
Baada ya muda kupita Vikram alikuwa amekaa chini akimtizama Tropina ambye alikuwa amemuweka kitandani alimtizama kisha akaanza kumshika nywele zake kwa kutengenezea vizur kwa kuziingiza ndani ya kofia ya kulalia.
"Pinah umekuwa mkubwa na umeendelea kuwa mzuri sana" alizungumza huku akitabasamu.
Aliinuka na kuelekea kwenye kochi Ila alipopiga hatua kadhaa alirudi tena na kuinama kisha akampiga picha Tropina na kumpiga busu la paji la uso kisha akamfunika vizur na kuondoka kuelekea kwenye kochi.
Tropina aligeuka upande mwingine na kuyafumbua macho yake kisha akatabasamu na kufumba tena macho yake
Asubuhi kulikucha na Vikram alikuwa wa kwanza kuamka alitoka njee akiwa ameshikilia shuka lake na akiwa na Tabasamu mwanana usoni mwake.
"Wewe....... Bwashe...... Umetokaje huko??? Aliuliza Larry aliyeweza kumuona Vikram.
'Shshshsh wacha kelele kwani ni mpaka Vanessa ajue nimelala wapi leo? Alizungumza Vikram.
"Sasa umemfanyaje dada yangu? Aliuliza Larry.
Vikram alitabasamu tu baada ya kukumbuka busu aliloweza kumbusu usiku Tropina.
"Mbona unatabasamu eti kwanini unatoka mwenye chumba cha dada yangu na shuk lako"
"We ulitaka nilale na yule sokwe ndani.......embu ngoja hivi umeniuliza kweny chumba cha dada yako.....ni umesema dada yako au nimekosea" alirudia huku akicheka kwani ndiyo mara ya kwanza kumsikia Larry akimuita Tropina dada.
Larry alimtizama tu bila kujibu chochote.
**** **** ****
Watu wote wakiw wako sebleni kwaajili ya kupata chakula ulitangazwa ujio wa Winnie ambao ulimfanya Vanessa ashtuke.
"Anataka nini huyo mwanamk? Aliuliza Vanessa huku akimpa ishara ya Vikram aondoke pale alipo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Winnie aliingia na kuanza kuita Rickson
"Nini unapiga kelele ni kwamba humuoni Rickson au?? Aliuliza Vanessa akimtizama Frank.
Winnie alinyamaza baada ya kugundua kuwa tayari alishampeleka Frank asimame kama Rickson pale.
Alishindwa kuzungumza zaidi baada ya kumuona Adrian.
"Nitamtoa njee" alizungumza Adrian na kumshika mkono Winnie kisha kuanza kumtoa njee ya pale.
"Unashida gani ww?? Aliuliza Adrian.
" Rickson... Rickson.... Ame"
"Sasa ongea vitu vya kueleweka maana sikuelew Rickson original au huyo feki uliyeweza kumleta?? Aliuliza Adrian.
Winnie aliweza kumuelezea kila kitu.
"Sasa huyo Rickson ameyajuaje hayo yote mpaka akaweka karatasi ambazo ni original?? Aliuliza Adrian huku akijaribu kutafakari.
"Na kwanini hataki sura yake itambulike .....nahisi atakuwa ni mtu ambaye anafahamika namaanisha mtu wa karibu na sisi" alizungumza Adrian.
"Embu nielekeze umbo lake likoje na sura yake pia labda naweza kumtambua" alizungumza Adrian.
"Mara nyingi hupenda kuficha sura yake kwa kuvalia kofia hivyo sura yake siitambui vizur Ila nikimuona nitamfahamu"
"Sasa uliolewaje na mtu ambaye huitambui sura yake huna tofauti na Tropina???
" Niliweza kuiona sura yake siku moja tu na ndyo siku aliyoweza kuniowa baada ya hapo aliondoka na picha yake aliweza kuidondosha na ndipo nilipoiokota kwanzia siku hiyo sikubahatika kumuona tena niliposikia amekuja Tanzania ndipo nikaja na Kaka yake ndye aliyeweza kuniambia ya kuwa ameshaowa mwanamke mwingine.
"Basi huyo Kaka yake tukimfuatilia tutaweza tambua wapi alipo Rickson" alizungumza Adrian akitabasamu na kumtizama Winnie aliyekuwa akizing.ata kucha zake.
***** **** ****
"Sign hizo karatasi" alizungumza Larry baada ya kupokea karatasi hizo kutoka kwa mwanasheria wake.
"Zanin??? Aliuliza Frank.
" kwni jana hukunisikia nilivyosema utasign karatasi za talaka au"
Alizungumza Larry na kumtizama Frank huku Tropina akimtizama Frank.
Franck alimtizama Adrian ambaye alimpa ishara ya asign huku akitabasamu.
Frank alikumbuka ya kuwa tayari alishaonana na Adrian na pia aliweza kufundishwa sign ya Rickson baada ya Adrian kuchukua karatasi za Rickson alizoweza kusign kwenye cheti cha ndoa.
Frank aliichukua karatasi zile.
"Unataka kufanya nini??? Aliuliza Tropina.
"Naona kama familia yenu haijaridhika na mimi hivyo nataka niwaache muendelee na maisha yenu" alizungumza Frank huku akichukua kalamu na kuanza kupeleka kwenye karatasi za ndoa .
"Subiri alimsitisha tena Tropina.
" Ni sawa kama atasign kwasababu sitaki kuwa na ndoa na mtu nisiyemfahamu" akifikiria Tropina kisha akasema.
"Sign"
"Wewe.....wewe.... Subiri........" Alizungumza Vikram aliyekuwa akiingia ndani na Vanessa kwa wakati huo.
"Bwashe nilikuwa nakusubiria sana.....hizi hapa sign wewe.....karatasi za ndoa" alizungumza Larry na kutoa karatasi zingine za ndoa.
"Huyo anafanya nn aliuliza baada ya kupokea karatasi za ndoa kwa Larry.
" nimemwambia sitaki amuowe dada yangu hivyo kakubali na anasign karatasi za talaka"
"Na kwanini asign!? Aliuliza Vikram kwa kutahamaki.
"Ili wewe uowane na Tropina"
"Hapana sitaki" alizungumza Vikram.
"Na kwanini hutaki aliuliza Tropina akiamka.
Vikram alizichukua zile karatasi za talaka kwa Frank.
"Unashida gani tena bwashe?? Aliuliza Larry kwa kutahamaki.
Vanessa alichukua zile karatasi na kuzichana kisha Vikram akaziokota na kweda kumpa mfanyakazi huku akimwambia kazichome jikoni.
"Mna nini nyie wawili?? Aliuliza Larry.
"Nini kinaendelea aliuliza Tropina baada ya kushindwa kuelewa ni nini kinatokea.
'Kwanini mmechana sasa........naomba zile zilizobaki wakili" alizungumza na kutaka kuchukua nyingine..
Vanessa alizichukua tena.
"Nini shida" aliuliza wakili.
"Sitaki kuona karatasi za talaka hapa kwangu ataolewa na Rickson na siyo mwanaume mwingine huyo ndiye aliyechaguliwa na Baba yake na lazima nitimize ahadi ya mume wangu" alizungumza Vanessa.
"Sawa atasign tu nakwambia" alizungumza Larry.
"Kama unataka laana msainishe hizo karatasi"
"Sasa ataolewaje na Vikram kama hata sign hizo karatasi za talaka Vanessa??
"Ww acha hivyo hivyo me sitaki kumuowa tena?? Alizungumza Vikram.
"Kumuowaje tena?? Aliuliza Larry.
Vikram alishindwa kujibu swali la Larry.
"Kwasababu ameshaolewa" alizungumza Vanessa kumtetea Vikram.
"Ndiyo kwasababu ameshaolewa" alirudia Vikram.
Larry alimtizama Vikram na kumtazama Vanessa kisha akaondoka eneo lile.
"Bwashe!! Aliita Vikram lakini alijishtukia kisha akanyamaza kwani Larry alimtizama tu bila kusema neno lolote.
Tropina na yeye aliwatizama kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake.
Alibaki Vikram akiwa katika hali ya sintofahamu huku Adrian akimtizama kwa uso wa uchunguzi zaidi machoni bila kutambua ya kuwa Vanessa alikuwa akimtizama yeye kwa uso wa hasira sana.
Tropina alipofika ndani alitupa vitu vyote vilivyokuwepo juu ya meza yake kwa hasira kisha akaanza kuvikanyaga kanyaga kwa hasira na kutoa mito ilikuwapo kitandani kisha kuirusha rusha katika chumba chake.
Vikram aliona siyo wasaa mzuri wa kuongea na Tropina hivyo alienda katika chumba cha Larry ambako alipokelewa na mvurugiko wa vitu chumbani hapo glass zilizoweza kuvunjwa kabati TV radio kila kitu alichokishika mkononi mwake alitupa. Alielekea moja kwa moja hadi kwenye pc ya Vikram iliyokuwa chumbani kwake. Aliishika na kutaka kupasua ghafla Vikram alitokea
" Bwashe hiyo acha" alizungumza Vikram
"Hiyo ina vitu vingi sana vya maana huko utaharibu"
Larry alimtizama na kuishusha chini lakini ghafla aliibamiza chini.
"Hata dada yangu ni mtu wa muhimu sana kwangu lazima na mimi nikuumize ww kama ulivyoniumiza mimi" alizungumza Larry na kumtazama Vikram.
Vikram aliinama mpaka chini kisha akaiokota laptop yake kwa simanzi Kubwa sana na akainuka.
"Mbona kama bwashe unataka kulia?? Aliuliza Larry akimtizama Vikram machoni.
Vikram alikuwa akiitizama laptop yake iliyoweza kupasuka tayari huku akiipapasa papasa.
Larry alimtizama kisha akaichukua ile laptop.
"Leta nitaenda kukutengenezea" alizungumza Larry na kuichukua laptop ile mikononi mwa Vikram aliyekuwa bado akiitizama laptop yake jinsi ilivyoweza kuvunjika.
"Bwashe.... Bwashe aliita Larry akimtizama Vikram usoni.
" embu nenda chumbani kwako kwanza alafu ukapunguze hasira" alizungumza huku akimburuta na kuanza kumpeleka chumbani kwake. Ghafla alisikia kelele ya vitu kupasuliwa kwenye chumba cha mama yake.
"Huyu Vanessa na yeye anashida gani?? Aliuliza huku akijaribu kuchungulia chumbani kwa mama yake.
Alimuungiza ndani Vikram na kumfungia mlango wake lkini alifungua na kwenda kuchukua PC yake na vitu ambavyo aliona nivya muhimu.
" bwashe unaweza sasa ukaendelea kupunguzia hasira chumbani kwako" alizungumza Larry na kuondoka lakini hakupiga hata hatua mbili ulisikika mshindo ambao ulimfanya Larry aogope hadi kuushika moyo wake kwa kishindo hicho.
"Mungu wangu huyo mbona hasira zake ni nyingi sana hivyo amedondosha nini kikubwa hivyo?? Alijiuliza huku akiwa amekaa chini"
"Mungu wangu computer yangu computer yangu niliiisahau chumbani kwake" alizungumza Larry na kuacha kila kitu alichokuwa amekibeba huku akiaamini ya kuwa ni vitu vya maana sana na kwa upande wako.
Alipoweza kuufungua mlango wa chumba cha Vikram alijikuta computer yake chini ikiwa imepasuka pasuka na Vikram aliimazia kwa kuikanyaga kanyaga.
"Bwashe hiyo ungeiacha.....hiyo usingeipasua alizungumza huku akilia machozi.
"Wewe lakini si ulinambia ya kuwa nimalizie hasira zangu huku........sasa mbona unalia?? Aliuliza Vikram huku akianza kuokota okota vipisi vya computer ile.
***** **** ******
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" nahis kuna kitu juu ya Vikram" alizungumza Adrian aliyekuwa akizungumza na mfanyakazi wake Daudi.
"Kwahiyo nifanyaje aliuliza Daudi.
" umepata nini juu ya Saruni........ Alishakutan na Rick ?? Aliuliza Adrian
"Hapana ila nahisi anakutanaga na yule mfanyakazi wako wa kike....simkumbuki vizuri Ila nilimpiga picha" alizungumza na kutoa simu yake
"Alice!!! Aliita Adrian kwa hasira.
" mara zote nilikuwa nikiwaza ya kuwa nani atakuwa ananifuatilia na kutoa taarifa zangu kumbe ni huyu Alice......hivyo basi inaonekana Rickson ananifahamu mimi vizuri sana" alizungumza na kutabasamu.
"Daudi!! Aliita Adrian.
"Namuhitaji huyu msichana leo hii hii"
Daud aliichukua simu yake kisha akatoa heshima na kuondoka Zake.
**** ***** ****
Alionekana Saruni akiwa ndani ya nyumba yake huku akizungumza na Rickson.
"Sasa kwanini usijitambulshe tu?? Aliuliza Saruni na swali hilo lilienda moja kw moja kwa Rickson.
"Vanessa amenambia nisifanye hivyo kwani nitayaingiza maisha yangu hatarini kabla ya kuyaingiza maisha yao. Alizungumza Rickson ambaye bado sura yake haikuweza kuonekana.
*** *** *** ***
" Bwashe..... Bwashe aliita Larry akimtafuta Vikram.
"Bwashe"
"Naaam"
"Heeeeee ni nani huyo?? Aliuliza Larry na kugeuka nyuma.
Alishtuka baada ya kugeuka nyuma.
"Wewe sokwe!!!! Unafikiri nakuita wewe??? Shindwa na ulegee namuita Vikram Vikram ndiye bwashe wangu siyo wewe"
"Sawa niwe sokwe nyani au tumbili....ndiyo tayri nimeshakuwa mume wa dada yako na mimi ni bwashe wako alafu tena uuchunge huo mdomo wako maana mali zote zipo chini ya mke wangu mimi na mimi ni mume wake kwahiyo kuwa makini na mdomo wako" alizungumza Frank.
"Unaongea nini wewe sokwe.......nani kakwambia mali zote zipo chini ya Tropina ndo kilichokuleta hapa na kujifanya ya kuwa wewe ni Rickson" alizungumza Larry na kucheka.
"Mali zote zipo chini ya ............." Kabla hajamalizia kuzungumza aliingilia Tropina haina haja ya wewe kumwambia huyo kwamba mali ziko chini ya nani kwasababu yuko hapa kwaajili ya yangu na siyo ya mali sindiyo Rick! Alizungumza Tropina akitabasamu.
Larry aliamua kuondoka zake akiwa ameshikilia laptop ya Vikram mkononi.
"Huyu naye kaenda wapi leo!!?? Alijiuliza akielekea ndani ya chumba chake.
" sihitaji kujua kuwa wewe ndiye Rickson amah lah Ila huwa sipendi kabisa mtu yoyote yule amkasirishe Larry wala Vanessa natamaini ya kuwa umeelewa.
Baada ya dakika kadhaa kupita Alice aliweza kukamatwa na kupelekwa katika nyumba ya Daudi huko nako alieleka Adrian.
"Eheeeee niambie nani anakutuma wewe kunifuatilia mimi alizungumza huku akiuvua mkanda wake na kumtazama Alice aliyeweza kuchafuka damu na akiwa amefungiwa katika kiti.
Alice alimtizama tu bila kusema neno.
"Niambie ni Tropina sindiyo au ni Larry...... Aliuliza Ila Alice hakuzungumza chochote kile zaidi ya kumtazama tu kwa hasira Adrian.
" Me nakusemesha wewe unanitizama namna hiyo?? Aliuliza na kumchpa na ule mkanda kwa upande wa bakoli.
Alice alibaki akiguguma kwa maumivu makali sana bila kutoa sauti njee.
***** ******* ***
"Unafanyaje aliuliza Vikram.
" natizama tizama picha zako huku bwashe...... Mbona kama haya Maeneo siyo ya Tanzania haya uliyopigia picha?? Aliuliza Larry.
"Nime edit hizo" alijibu Vikram.
"Hakikisha unafungua kila kitu kwenye hiyo computer" alizungumza Larry akiendelea kupekua laptop ya Vikram.
Ghafla alikutana na picha zilizoweza kumshutua.
"Bwashe huyu msichana ni nani?? Aliuliza baada ya kuona Vikram akiwa katika picha na binti mmoja.
" ahaaa huyo......ni mke wangu mimi" alijibu Vikram akiendelea kupekuw pekuwa computer ile aliyoweza kuinunua kwaajili ya
Larry ka kuendelea kuifungia Zaidi.
"Ni huyu binti eti nakuulizia? Aliuliza tena na kumuonyesha Vikram.
" ndiyo ni mke wangu huyo Pinah" alijibu na kutabasamu.
"Rickson" aliita Larry na Vikram aliitikia kwa kumtazama na kumuachia Tabasamu mwanana.
"Are u Rickson??? Aliuliza tena kw Mara nyingine na hapo ndipo Vikram alipoweza kushtuka na kujikuta ya kuwa tayari amesha yazungumza yale yaliyoweza kuwa Siri kwake.
"Wewe ni nani eti??? Na kwanini umepga picha na dada yangu enzi za usichana wake??? Ngoja ngoja hilo swali siyo sahihi....
Inamaana we ni Rickson hapana namaanisha wewe ni Rickson wa ukweli???
Vikram alimtizama Larry kisha akaitikia..
" yes am Rickson "
Larry alimtizama kwa furaha na kujikuta machozi yanamtoka huku akiwa amemkumbatia.
"Unashida gani wewe?? Aliuliza Tropina baada ya kuufungua mlango wa chumba kile walichoweza kuwepo.
"Hamna tatizo" alijibu Vikram huku akimtoa Larry katika mwili wake.
"Vikram ninashida na wewe mara moja" alizungumza Tropina.
"Sawa nakuja" alijibu Vikram aliyekuwa akipambana na mikono ya Larry iliyokuwa ikitaka kumkumbatia tena.
Tropina alimtizama Larry na kuuliza.
"Huyo yuko salama lakini??? Aliuliza Tropina.
"Hana shida yuko tu kwenye emotional basi" alijibu Vikram na kumlaza Larry kitandani huku akimfunika.
"Bwashe" aliita Larry.
"Mmmhhh" aliitikia Vikram akimtizama.
"Lakini Unauhakika ni wewe Rickson"
"Ndyo ni mimi Ila hupaswi kumwambia Tropina chochote kwani atachukia sana kama taarifa hizi ataweza kuzipata kupitia kwa mtu mwingine" alijibu Vikram
"Sawa nimekuelewa..........
...haya nenda mke wako anakuita" alizungumza Larry.
"Ndiyo mke wangu ananiita" alijibu Vikram na kuondoka chumbani pale.
Aliingia katika chumba cha Tropina na kumkuta Tropina anamtizama.
"Kuna shida yoyote kwani mbona unaniangalia hivyo??? Aliuliza Vikram.
" ammmmhhhh....... Aaammmhhhh
......... Tropina alishindwa kuzungumza na kujikuta anaishia tu kumtazama Vikram bila kusema neno lolote.
Vikram aliweza kuelewa kipi alichokuwa akitaka kukisema Tropina
Alisogea karibu na kumfanya Tropina na yeye aanze kusogea kwa kurudi nyuma.
"Nini unataka mbona unanisogelea? Aliuliza Tropina.
Vikram alianza kucheka akimtizama Tropina.
" unacheka nini???
Vikram alimtizama kisha akacheka tena.
"Nakuuliza unacheka..............kabla hajamalizia neno lake Vikram alishaweza kusogea pale na kumvuta karibu na yeye kwa kumshika kiuno chake.
" una......una......una........ Maneno yaliweza muisha Tropina hiyo tu ni baada ya kifua chake kukutana nacha Vikram huku akiwa ameshikiliwa kiuno chake Barabara.
"Una......"
"Shshshsh shshshsh" Vikram alimtaka anyamaze kwa kuweka kidole chke kwenye lipsi nene za Tropina na kumfanya Tropina aishiwe maneno huku akibaki kutoa pumzi njee na ndani macho yake yaliyoweza kulegea yakimtizama Vikram aliyekuwa akimtizama kwa macho makavu na yenye tamaa ya kitu fulani juu ya mwili wake.
Vikram aliyashusha macho yake chini hadi kwenye lipsi za Tropina na kuanza kupitisha kidole chake katika lipsi hizo huku akikagua rangi ya mdomo iliyoweza kumkaa vizur am mdomoni hapo.
Ghafla vilisikika viatu vikiwa vinakuja eneo lile na kuwatoa katika hali hiyo.
Aliingia Diana akiwa na kikombe cha kahawa.
"Samahani nahisi nimeingia wakati mbaya alizungumza Diana na kuanza kuondoka.
" hapana mbona huyu alikuwa anaenda aya nenda wewe " alizungumza Tropina huku akimsukuma Vikram.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vikram aliondoka.
"Mshenzi huyu anazubutuje kunitoa mm njee.....mwanamk gani huyu hana hata adabu mbele ya mume wake" alilalama Vikram huku akiondoka eneo lile.
***** ****** ****
Wakati hayo yote yakiendelea Frank alikuwa akiwatizama kila hatua waliyokuwa wakiweza kufanya ndani ya ile nyumba pasina kutambua ya kuwa hata yeye kila alichokuwa akikifanya na kuzungumza kilikuwa kikijulikana kwani alikuwa akifuatiliwa zaidi na Vanessa.
***** ***** *****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment