IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS
*********************************************************************************
Simulizi : Ahadi Ya Ndotoni
Sehemu Ya Kwanza (1)
Jeska alitembea kwa mwendo wa taratibu akiwa amepoteza muelekeo wa maisha yake, alijiona ni kiumbe asiye na thamani. Pamoja na uzuri aliojaaliwa na Muumba, bado alikuwa kiumbe chenye mikosi. Hakuamini uzuri aliojaaliwa na Mungu amekuwa kiumbe wa kuchezewa na wanaume.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wazo lake lote lilikuwa kujiua ili kujiepusha na walimwengu ambao wamekuwa hawaoneshi ushirikiano naye. Alikuwa ameisha kaa na wanaume zaidi sita ambao wote walimuahidi kumuoa, lakini mwisho wa siku ilikuwa kutendwa na kushindwa kuelewa tatizo ni nini.
Katika mitihani ya maisha Jeska amejikuta akibakwa kila alipokuwa akijaribu kutoka ili kutuliza mawazo, mara ya mwisho alibakwa na wanaume zaidi ya sita ambao hawakutumia kinga. Kwa hali ile aliamini anaweza kuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi.
Kupima aliogopa kwani aliamini angekufa kwa presha, kimuonekano alijikatia tamaa akawa si mtu wa kujiheshimu tena. Mawazoni mwake alijua huenda Mungu alimuumba ili aje amtese, tokea ajali mbaya ya moto iliyochukua uhai wa wazazi wake wote pamoja na ndugu zake akiwa na umri wa miaka saba.
Baada ya vifo vya wazazi wake waliofia ndani ya nyumba, Jeska alichukuliwa na ndugu wa baba yake na kumlea, huku wazazi wake wakiwa wamemuachia mali nyingi. Lakini kwa bahati mbaya walioachiwa kumlea walihodhi mali yote na mwisho wa siku alifukuzwa kama mbwa baada ya kuhoji mali za baba yake.
Tokea hapo Jeska alianza kuonja adha ya maisha, pamoja na kufukuzwa na ndugu wa baba yake na kutishiwa kuuawa kama atataka kujua mengi zaidi. Siku zote Mungu hamtupi mja wake aliangukia katika mikono ya wazazi wa shoga yake. Ambao walimchukua na kumuahidi kumsomesha mpaka mwisho wa elimu yake.
Jeska alishukuru Mungu na kuwaza kusomea sheria akifika chuo kikuu ili siku moja alirudishe mali iliyochuliwa na ndugu wa baba yake. Maisha kwake yalikuwa mazuri yaliyomfanya asahau mateso ya ndugu wa baba yake, aliweza kumaliza vizuri kidato cha nne kwa kupata matokeo mazuri na kumuwezesha kujiunga na kidato cha tano. Akiwa kidato cha tano huku umbile alilojaaliwa na Mungu likizidi kupendeza na kutamanisha wanaume wakwale.
Siku moja hakuamini aliposhtuka usingizini na kumkuta baba wa shoga yake aliyemuheshimu kama wazazi wake akiwa juu ya mwili wake akimbaka. Jeska aliumia sana na kulia kwa uchungu. Lakini baba wa shoga yake alimbembeleza na kumuomba aifiche siri ile yupo tayari kumfanyia chochote katika maisha yake hata kumnunulia gari.
Jeska hakutaka kuisambalatisha familia ile kwa kuogopa kumsema baba wa rafiki yake kwa mkewe, aliamua kufa na siri moyoni ambayo ilikuwa ikimla siku hadi siku hata kupoteza uwezo wake darasani. Kila alipomuona baba wa shoga yake moyo ulipasuka na kujikuta akikimbia chumbani kwake na kuanza kulia.
Aliona kama ni uonevu kwa upande wake, wazazi wake wote wamekufa kwa mpigo ndugu waliobaki kumlea wakidhurumu mali. Na mwisho wa siku mtu aliyemtegemea kuyaokoa maisha yake amegeuka kiumbe mbaya kumbaka bila ridhaa yake. Kitendo kile kilimla sana Jeska kiasi cha kupungua siku hadi siku huku akiwaweka wenyeji wake katika njia panda wasijue Jeska anaumwa nini.
Kila walipomuuliza aliishia kulia na kuamini kauli yake huenda ikawa bomu litakalo isambaratisha familia ile. Siku zote alimuomba Mungu ampe ujasiri ili weze kuyakabili majaribu yale, Edna shoga yake muda wote alikuwa karibu yake kumdadisi kutaka kujua shoga yake amekubwa na tatizo gani ambao linaweza kutafuliwa na familia yake.
Kila alipoulizwa alisema hana tatizo lolote bali hujikuta akikosa amani kufikilia jinsi wazazi wake walivyokufa ghafla kabla hawajamtengenezea mazingira ya kujitegemea. Mama Edna na Edna walimuweka chini na kumpa mifano mingi ambayo ni mitihani ya wanadamu, mama Edna alimueleza.
“Jeska mshukuru Mungu, usipige teke fadhira zake, ni bahati kupata sehemu salama kama hii. Ni wangapi wamefiwa na wazazi wao lakini leo hii wanahangaika na kuishiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi.”
Kauli ile ilimfanya Jeska aangue kilio na kuamini hata yeye katika mawazo yake aliamini walio ndani ni salama kuliko wanaozurula. Lakini akili yake ilibadilika na kuamini watu wachache wenye uwezo huwa na huruma ya mamba kukuchekea kumbe wanakutamani kukutafuna utakapoingia kwenye maji kama alivyofanya baba Edna.
Alijuliza ni wangapi wamo katika mikono inayoonekana salama kumbe kuna watu wenye roho ya mamba kuwatafuna watu huku machozi yakiwatoka, wakiamini wanawaonea huruma kumbe na furaha ya kutafuna minofu na kiumbe kisicho na hatia.
Kilio chake kilizidi kuwaweka njia pana na kuanza kumdadisi upya.
Ndoto zake za kuwa daktari zilifutika na kuzihamishia kuwa mwanasheria mkubwa sana ambaye ataweza kuwasaidia wote waliodhulumiwa mali zao na ndugu wa mume wakiwemo yatima na wajane.
Kingine alichokifikiria ni kuanzisha NGO’S ya sheria atakayotoa huduma kwa bei ya chini hasa ikiwalenga wanyonge. Usongo aliokuwa nao na uchungu wa kudhulumiwa mali zake na kumfanya kuishi maisha ya kubahatisha kuishia kuangukia katika mikono ya wabakaji.
Mwezi wa tatu toka abakwe na baba Edna aligundua mabadiliko katika mwili wake, siku zake za hedhi hazikuonekana. Pia maumivu ya kichwa na mwili kuchoka vilimtia wasiwasi. Mabadiliko yale mama Edna aliyaona, wasiwasi wake mkubwa ulikuwa malaria.
Ilikuwa siku ambayo Jesca aliamka na kushindwa kwenda shule, kichefuchefu kilikuwa kikali sana kilichofanya atapike kila chakula alichokula asubuhi ile. Baada ya kuona dalili zote za malaria, alimpeleka hospitali, Jesca ambaye hakuwa anaelewa kilichokuwa kikiendelea, alipoulizwa na daktari alimueleza anavyojisikia.
Alichukuliwa vipimo vya malaria, majibu yalikuja hana marelia. Ilibidi kichukiliwe kipimo cha mkojo, ambacho kileleta majibu. Daktari hakutaka kumpa majibu wakiwa wote alimtoa nje Jesca ili ampe majibu mama yake.
Jesca hali ile ilimtisha japo anajua virusi vya ukimwi vinapimwa kwa damu, wasiwasi wake huenda ameathirika baada ya kubakwa na baba Edna.
Ndani daktari alimueleza majibu ya vipimo yanavyosema.
“Mama binti yako vipimo vinaonesha ni ujamzito.”
“Eeh!?” Mama Edna alishtuka kusikia vile.
“Ndiyo, binti yako anaujauzito wa miezi mitatu.”
“Mtumee, mtoto huyu!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama Edna alishika mkono mdomoni na kujikuta akikumbuka miezi mitatu ya nyuma hali ya Jesca ndani ilibadilika na kuwaweka katika sifahamu. Aliamini kama Jesca amefikia hatua ya ufuska lazima atamuambukiza mwanaye Edna ambaye amekuwa naye karibu zaidi.
Wazo la kumfukuza lilikuwa gumu, kwa kuhofia jamii ingemtazama vibaya, alipanga akitoka pale amueleze mume wake, nini wafanye kutokana na tabia za chui za Jesca kujificha katika ngozi ya kondoo ya upole na ukimya.
Alitulia tuli huku akiwa amehama kimawazo na kushtuliwa na daktari.
“Mama nafikiri umenielewa?”
“Nimekulewa baba, asante.”
“Nafikiri hili swala si la kulitolea maamuzi mazito, kwani siku hizi mabinti zetu wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na Mafataki. Wasiwasi wangu asiwe ameambukizwa ukimwi tu.”
“Mmh, hapo ndipo nachanganyikiwa.”
“Basi mama kakaeni naye chini muulizeni kwa utaratibu lazima mwenye ujauzito atamtaja. Kama kuna ushahidi mfungulieni mashtaka.”
“Nashukuru baba kwa ushauri wako.”
Mama Edna akiwa amechanganyikiwa kidogo, alitoka na kumpitia Jesca aliyekuwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea ndani.
“Twende zetu.”
Jesca alinyanyuka na kumfuata mama yake aliyekuwa anatoka nje ya hospitali bila kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea mule ndani.
Jioni ya siku ile baada ya kurudi baba Edna mkewe alimwita na kumueleza kilichotokea hospitali, Jesca alijisogeza kwa kujificha nyuma ya mlango ili asikie mama atamueleza nini baba na nini atakijibu juu ya kilichoelezwa hospitali.
“Za saa hizi mume wangu?”
’Nzuri, vipi za hospitali?”
‘Mmh, si nzuri,” kauli ile ilimshtua Jesca na moyo kuanza kwenda mbio na kujiuliza huenda wazo lake la kuathirika ni kweli. Mwili ulimtetemeka na kumuomba Mungu amuepushe na janga lile.
“Mbona unanitisha kuna habari gani?”
“Jesca ni mjamzito,” kauli ile ilimshtua Jesca na kushika kifuani kwa hofu huku akipiga ukelele wa chini.
“Mama yangu weee nimekwisha.”
“Eeh!?” Mzee Ezekiel alishtuka.
“Ndiyo, usishituke habari ndiyo hiyo, mtoto mbaya tunamuona mkimya kumbe ana mambo ya chini chini. Unafikiri atamfundisha nini Edna kama siyo kuwa malaya kama yeye.”
Maneno yale makali yalikuwa msumari wa moto kwenye moyo wa Jesca binti yatima asiye na kosa lolote ambaye ukimya wake ulikuwa umemponza sawa na mshumaa kuwaangazia wengine huku unateketea.
“Mke wangu taratibu, Jeska ni mtoto wetu kama Edna hivyo tumchukulie kama ni Edna amekosa na wala si mtu baki.”
“Hata angekuwa Edna nisingefurahia upuuzi huo?”
“Sifurahii na pia ningemkanya kama nitakavyo mkanya Edna, hatuwezi kuwabangua kwa vile Jeska sasa hivi ni binti yetu.Umeisha mueleza tatizo lake?”
“Bado, kwa vile nilikusubiri kwanza wewe kabla ya kumueleza mwenyewe, ili nijue tutalitatua vipi.”
“Basi kazi hiyo niachie mimi,” baba Edna aliuchukua mzigo ule kwa kuamini kabisa huenda muhusika ni yeye japo hakuwa na uhakika kamili.
Mzee Ezekiel alikubaliana na mkewe, kabla ya kubadili nguo alimtuma Edna amwite Jeska aliyekuwa nyuma ya mlango akilia kwa majuto ya ujauzito alioupata baada ya kubakwa na mzee Ezekiel. Edna alimkuta nyuma ya mlango akitokwa na machozi na macho kuvimba.
“Jeska vipi mbona kila siku umekuwa mtu wa majonzi ndugu yangu?” Edna alimuuliza kwa sauti ya huzuni.
“Basi tu, naona huu ni mwaka wangu,” Jeska alisema kwa sauti ya kilio huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Jeska una nini tena jamani?”
“Nina imani naishi kimakosa.”
“Jeskaaa!!”
“Kila balaa linaniandama mimi, unafikiri kuna umuhimu wa kuendelea kuishi?”
“Jamani Jeska maneno gani hayo ya kusema ndugu yangu.”
“Sina mengine zaidi ya hayo, kilichobakia ni utekelezaji, likitokea usishangae ila ujumbe nitakuachia.”
“Mama yangu, Jeska unataka kufanya kitu gani Mungu wangu hebu muondoe pepo wa mauti kwenye moyo wa Jeska. Jeska usifanye hivyo hata siku moja bado una nafasi kubwa ya kuishi na kutatua matatizo yako”
“Edna, umri wangu ni mdogo lakini matatizo yanamzidi mtu aliyeishi miaka mia moja. Kama nitaendelea kuishi nafikiri kuna balaa kubwa zaidi”
“Kwani kuna nini tena Jeska”
“Ipo siku utajua”
“Basi baba anakuita naomba umueleze yanayokusumbua,” Edna naye machozi yalimtoka kwa hofu ya maamuzi mazito ya Jeska.
Jeska aliongozana na Edna mpaka sebuleni alipokuwa amekaa mzee Ezekiel, alishangaa kumuona Jeska akitokwa na machozi na macho yamemvimba.
“Jeska, una nini tena mama?”
“Basi tu baba.”
“Hebu njoo hapa binti yangu mpenzi.”
Jeska alisogea pembeni ya mzee Ezekiel, ambaye kabla ya kuzungumza naye alitoka naye nje na kwenda naye kwenye bustani. Walipofika alimuuliza kwa sauti ya upole.
“Jeska una tatizo gani?”
“Mama ameisha kwambia?”
“Una rafiki wa kiume?”
“Sina baba.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Una..na..taka kuniambia au una uhakika una mimba?” Mzee Ezekiel aliuliza kwa sauti ya kigugumizi.
“Mimi sijui mama ndiye aliyeambiwa majibu yangu.”
“Sasa unalia nini wakati hujajua kama una ujauzito?”
“Si mama kakwambia na hali yangu ilikuwa na kila dalili za ujauzito.”
“Mmh, unaweza kuwa wa nani?”
“Sijawahi kukutana na mwanaume hivi karibuni zaidi yako.”
“Kabla yangu umepita muda gani?”
“Mwaka wa tatu sasa.”
“Mmh, makubwa, unataka kuniambia ujauzito ni wa kwangu?”
“Labda wewe unaweza kumjua mtu mwingine zaidi yako au wa roho mtakatifu.”
“Mama yako ameisha kuuliza ujauzito wa nani?”
“Ataniuliza vipi, toka tumetoka hospitali hana habari na mimi.”
“Sasa sikiliza, nitafanya mipango kuitoa hiyo mimba ili uendelee na masomo.”
“Sawa,” Jeska alikubali.
“Akikuuliza mama yako mweleze ni ya kijana mmoja kondakta wa daladala.”
“Sawa baba.”
“Ila kesho nina safari ya kikazi kwa wiki nzima nikirudi tutaitoa, ila naomba iwe siri yako”
“Sawa baba.”
“Shika hii pesa itakusaidia kwa vitu vya hamu,” alimpa laki moja.
“Asante baba.”
Baada ya makubaliano walirudi ndani, sebuleni alikuwa Edna na mama yake. Jeska alipitiliza chumbani kwake kulala, hakuwa na hamu na kitu chochote kwa siku ile.
Mzee Ezekiel na mkewe walikubaliana Jeska asiguswe kwa lolote bali apate msaada kama sehemu ya familia.
Baada ya makubalino yale, Edna alimueleza mama yake uamuzi mzito aliotaka kuuchukua. Mama Edna alishtushwa na habari zile, alimfuata Jeska aliyekuwa chumbani amejilaza akilia.
“Jeska...Jeska mwanangu amka mama.”
Jeska alinyanyuka huku macho yakiwa yamemvimba kwa kulia, mama Edna alishtuka na kuamini uamuzi mbaya wa Jeska yeye ndiye muhusika kwani alionesha kumtenga toka walipotoka hospitali bila kumpa majibu muhusika.
Mama Edna alishtuka hali aliyomkutanayo Jeska ilimshtua sana.
“Jeska mwanangu mbona hivyo mama?”
“Hapana kawaida?”
“Unaumwa?”
“Hapana.”
“Sasa nini?”
“Kawaida tu mama.”
“Hapana Jeska mwanangu najua jinsi gani nilivyokukosea.”
“Hujanikosea mama.”
“Si kweli Jeska, nakiri kufanya kosa, kwanza naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea.”
“Mama hujafanya kosa lolote.”
“Ni vigumu kuliweka wazi lililokusibu moyoni mwako, naweza kusema baada ya kutoka hospitali mimi kama mzazi nilijikuta nachanganyikiwa na kushindwa kuamini nilichoambiwa hospitali na jinsi nilivyokuwa nakuamini.”
“Ni kweli mama, mimi ndiye mkosefu kwa tukio lililotokea wa kuomba msamaha ni mimi.”
“Hapana Jeska, napenda kukueleza kitu kimoja, sisi ni wazazi na wajibu wetu ni kuwatunza ninyi. Hivyo lazima tukasirike mnapokosea kuonesha jinsi gani tusivyokubaliana na yaliyotokea. Lakini mwisho wa yote ni kukusamehe kwa vile imeisha tokea.”
“Sawa mama nimekusikia, lakini nimeisha yatia doa maisha yangu.”
“Hapana Jeska, kukosea ni sehemu ya kujifunza. La muhimu ni kumtafuta huyo mwenye mzigo huo ili tujue nini majaliwa baada ya mtoto. Ila malezi yako na hali yako bado itabakia mikononi mwetu.”
“Sawa mama.”
“Nani mwenye mzigo huu?”
“Konda wa daladala”
“Mmh, haya...yupo wapi?”
“Siku hizi simuoni wala hajui kama siku tulipokutana aliniachia ujauzito huu.”
“Umekutana mara ngapi.”
“Mara moja ilitokea kama ajali, yaani najuta,” Jeska alisema kwa sauti ya kilio ambayo ilionesha kweli anajua. Lakini alifunika kombe mwana haramu apite.
“Sawa, basi tuliza mawazo tutailea mimba na mtoto akizaliwa vile vile tutamlea na ukijifungua tutaendelea kukusomesha.”
“Nitashukuru mama.”
“Basi mama naomba usilie na kujiona umefanya kosa kubwa, la muhimu ni kujifunza kutokana na makosa. Usifanye chochote kibaya cha kujizuru, sawa mama.”
“Sawa, nitafanya hivyo mama yangu.”
“Basi twende ukale.”
“Sijisikii kula mama.”
“Hapana nyanyuka mwanangu mzuri.” Mama Edna alimbembeleza Jeska huku alimshika mkono na kunyanyua, Jeska naye hakutaka kumbishia mama yake alinyanyuka na kutoka naye nje.
* * *
Siku zilikatika huku Jeska akiendelea kumeza mfupa wa siri nzito juu ya ujauzito aliopewa na baba Edna. Alijitahidi kuzuia hali yake kila akiwa shuleni ili wasimgundue kama mjamzito kutokana na kusinzia kila wakati na kichefuchefu.
Siku ya nne toka ingundulike mimba ya Jeska, maswali ya wanafunzi wenzake juu ya hali yake yalimnyima raha wapo waliodiliki kumwambia.
“Jeska tuna wasiwasi huenda wewe ni mjamzito.”
Maneno yale yalimchanganya na kumnyima raha, alijikuta akiona siku haziendi muda alioelezwa na baba Edna amsubiri unachelewa. Wazo la haraka lililoingia kichwani mwake , kwenda kuitoa ile mimba kwa vile pesa za kutolea alikuwa nazo.
Jeska baada ya maneno ya chini chini ya kumfikiria mjamzito, alipanga siku ya pili wakati wa mapumziko atoroke kwenda kutoa ujauzito. Siri ili ilibakia moyoni mwake kwa kuogopa kuwashirikisha watu wengine.
Siri ili ilibakia moyoni mwake kwa kuogopa kuwashirikisha watu wengine.
Baada ya kufika alikutana na daktari ambaye walikubaliana kiasi cha pesa kwa ajili ya kazi ile. Jeska alipanda kitandani kwa ajili ya kutolewa mimba, daktari alianza mara moja kufanya kazi yake ya kumsaidia Ziraili mtoa roho kutoa roho ya kiumbe kisicho cha hatia.
Katika utoaji wa mimba mambo hayakwenda kama alivyozoea damu ilimtoka nyingi sana. Mganga alichanganyikiwa hali ya Jeska ilikuwa mbaya sana, cha kwanza kukifanya kilikuwa kufanya kazi ya ziada ya kuzuia damu ambayo ilitokana na makosa ya utoaji mimba.
Baada ya kufanikiwa kuzuia damu hali bado ilikuwa mbaya sana kutokana na kupoteza damu nyingi. Daktari alimuhamishia katika chumba kingine ili kumpumzisha akipata nguvu aende kwao. Dokta alifanya siri ikiwemo kumpelekea chakula cha kumpa nguvu, Jeska alikula kwa shida baada ya kula alimdunga sindano ya usingizi ili apumzike kwa muda kabla ya kiza kuingia ili aende kwao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majira ya saa mbili dokta alimtoa Jeska ambaye afya yake haikuwa nzuri alitembea kama mtu aliyelewa. Alimkodia gari hadi kwao na kumueleza dereva akiisha mshusha tu asisubiri kitu atimue zake kukwepa ushahidi. Jeska alipofikishwa kwao baada ya kuteremka kwenye gari, gari liliondoka bila kujua kama amefika salama. Jeska alitembea kizunguzungu kikiwa kikubwa sana hakuweza kufika mbali alianguka chini.
Wapita njia ndiyo waliomuona amelala chini pembeni ya geti la nyumba moja. Watu walimshangaa binti mwenye nguo za shule ambaye alionekana akitokwa na damu kwenye miguu hata siketi yake nayo ilikuwa imelowa damu. Kila mmoja alisema lake wengi waliamini huenda amebakwa.
Mmoja kati ya wale watu alimtambua Jeska na kuwaeleza yule ni msichana wa nyumba iliyokuwa mbele yao. Mmoja wa watu waliokuwa pale walikimbia kwenda kugonga mlango na kuwaita waliokuwa ndani. Wa kwanza kutoka alikuwa Edna, baada ya kupewa taarifa zile alikimbilia kwenye kundi la watu waliokuwa wamemzunguka Jeska aliyekuwa hajitambui.
Hata bila ya kumtambua vizuri nguo na viatu alijua ni Jeska, aliangua kilio kilichowashtua waliokuwa ndani. Mama Edna alifika kwenye tukio na kukuta Jeska amelala chini hajitambui damu zikimtoka chini kuonesha kuna kitu kibaya kafanyiwa.
Kwa haraka walimbeba juu juu na kuchukua gari mara moja alikimbizwa hospitali.
Alipofikisha uchunguzi wa haraka ulionesha alifanyiwa zoezi la utoaji mimba uliofanyika vibaya na kusababisha kutokwa na damu nyingi sana zilizosababisha kupoteza nguvu.
Ilifanyika huduma ya haraka kuyaokoa maisha ya Jeska kwa kuongezewa damu na kutibiwa majeraha aliyopata wakati wa kutoa mimba.
Mama Edna alitaka kujua kama zoezi alilofanya Jeska la utoaji wa mimba lilifanikiwa.
“Eti baba alifanikiwa kuitoa mimba?”
“Ndiyo mama, vipimo vinaonesha mimba imetoka.”
“Mungu wangu mbona mtoto huyu ana mazito hivi, nilimuonya asiitoe japo baba yake hakumjua lakini sijui shetani gani aliyemvaa na kufanya mauaji ya kiumbe kisicho na hatia.”
“Poleni sana.”
“Hatujapoa baba na hospitali iliyofanya hivi lazima tuishitaki.”
“Nafikiri kuna umuhimu wa kufanya hivyo.”
Daktari aliwaomba warudi nyumbani wakapumzike kwani hakukuwa na madhara zaidi waliamini damu atakayo ongezwa itamsaidia kumrudisha katika hali yake ya kawaida. Ila walishauriwa kumpima virusi vya Ukimwi kwa usalama zaidi wa afya yake.
Baada ya kutolewa wasiwasi mama Edna na Edna walirudi nyumbani huku wakizidi kumuombea dua ili atoke salama. Njiani Edna tukio la Jeska alilimsukasuka moyoni kiasi cha kumfanya akose raha, maneno ya Jeska kukanusha ujauzito ule siyo wa konda ina mtu ambaye hakutaka kumtaja ulimsumbua sana.
Aliamua kumueleza mama yake maneno ya Jeska kuhusiana na ujauzito ule, baada ya kukaa kimya alimwita mama yake ambaye naye alikuwa katika dimbwi la mawazo.
“Mama.”
“Unasemaje Edna?”
“Unajua kuna vitu vinanichanganya.”
“Vitu gani?”
“Kuhusiana na ujauzito wa Jeska.”
“Kinakuchanganya nini?”
“Kuhusiana na mtu aliyempa ujauzito.”
“Sasa nini kinakuchanganya?”
“Usiri wa mtu aliyempa ujauzito na inaoneka haikuwa ridhaa yake.”
“Edna mbona mimi kaniambia kila kitu.”
“Si kweli mama alikudanganya.”
“Kanidanganya kipi?”
“Aliyempa mimba si konda?”
“Si konda! Kama si konda ni nani na kwa nini unasema si kwa ridhaa yake?”
“Mama Jeska anasiri nzito moyoni mwake, ameniambia kuwa ameamua kukudanganya kwa vile anakuheshimu sana.”
“Sasa kama ananiheshimu kwa nini anidanganye?”
“Alinieleza kuwa umdhaniaye ndiye kumbe siye.”
“Alikueleza maana ya usemi wake?”
“Alisema atanieleza siku moja kama kuna kitu kitashindikana na kama kikifanikiwa basi siri hiyo atakufa nayo moyoni mwake.”
“Mmh, mbona mnanitisha, unataka kuniambia kuna mtu aliyempa ujauzito hataki tumjue?”
“Ndiyo, inavyoonekana na kitu alichokipanga kukifanya ni kutoa ujauzito kama sikosei, kwa vile umetoka siri itabakia moyoni mwake.”
“Sasa unataka kuniambia ni nani aliyempa ujauzito kwa kukisia?”
“Mama, nimemuuliza maswali mengi ashakumu si matusi ilifikia hata kumuuliza ujauzito huo labda ni wa baba.”
“Alijibu nini?”
”Alikataa.”
‘Sasa mbona anatuchanganya?”
“Lakini mama naomba Jeska akitoka hospitali kaa naye na kumuuliza kwa kituo atakueleza siri iliyomoyoni mwake juu ya ujauzito kuna mengi inaonekana yamejificha.”
“Mmh, haya.”
Walipofika nyumbani walioga na kula chakula cha usiku ambacho hawakuwahi kula kutokana na taarifa ya kushtusha ya Jeska.
***
Jeska alizinduka hospitali majira ya saa saba usiku na kukupepesa macho yake, jicho lake lilitua kwenye chupa ya damu iliyokuwa imebakia robo kumalizika. Alivuta kumbukumbu na kukumbuka alikwenda kutoa mimba lakini tokea hapo hakukumbuka vizuri kama alitokewa na nini.
Alijiuliza pale ndipo hospitali aliyokwenda kutoa mimba au wapi, lakini taratibu alikumbuka kutokwa na damu nyingi wakati wa utoaji wa mimba kiasi cha kuhamishwa chumba kingine. Pia alikumbuka kama alipandishwa kwenye gari kwenda nyumbani lakini zaidi ya hapo hakukumbuka kitu chochote.
Mazingira ya hospitali yalimchanganya yalikuwa masafi tofauti na kule alipolazwa baada ya kutolewa mimba, kilikuwa chumba kama cha kawaida lakini pale palionekana hospitali ya ukweli. Akiwa katika kutafakari macho ametizama juu, daktari aliingia na kukuta Jeska karudiwa na fahamu. Alimsogelea hadi kitandani na kumsemesha.
“Jeska,” alimwita.
“Abee.”
“Pole sana.”
“Asante,” alijibu kwa sauti ya chini.
“Unajisikiaje?”
“Bado.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tatizo bado nini?”
“Kizunguzungu na uchovu wa mwili.”
“Ooh, pole sana, mh, tatizo kubwa ni nini?”
Swali lilikuwa gumu kwa Jeska kusema kilichosababisha kufanya vile, alibakia bubu akikapua macho. Daktari aligundua uzito wa swali lake, alimuuliza kwa kulifumbua zaidi.
“Nini kilichosababisha utoe mimba ikiwa wazazi wako walikuwa tayari kuitunza hiyo?”
“Nimeamua kuitoa kwa vile nataka kusoma.”
“Kwani ungejifungua usingesoma?”
“Nina imani nisingesoma kwa vile nisingeweza kuwatumikia mabwana wawili mtoto na elimu.”
“Ungejua hivyo usingejiingiza katika mapenzi ukiwa mwanafunzi.”
“Najua utasema hivyo, si kila kosa likitokea linamhusu mtendaji.”
“Una maana gani?”
Saa kumi na mbili asubuhi Edna na mama yake walifika hospitali kumjulia hali Jeska, walipofika walikwenda wodini na kumkuta Jeska akiwa anaongezwa chupa ya damu nyingine.
Wakati wanaingia alikuwa amejipumzisha, bahati nzuri walikutana na daktari wa zamu.
“Vipi baba?”
“Aah, salama tu mama mgonjwa anaendelea vizuri, hata usiku alipozinduka nimezungumza naye mengi”
“Kuna mwanga wowote ulioupata?”
“Mmh, kwa kweli binti ni msiri sana, nimembembeleza na kunieleza atanieleza baadaye.”
“Mmh, mtoto huyu msiri sana.”
“Ni kweli inaonesha ana vitu vingi moyoni mwake vinavyomuumiza.”
“Sawa baba wacha na sisi tukajaribu labda tutaambulia.”
Waliagana na daktari aliyekuwa akielekea ofisini kwake kujiandaa kurudi nyumbani. Walipofika pembeni ya kitanda cha Jeska, kabla ya kumuamsha alifumbua macho mwenyewe.
“Jeska.”
“Abee mama, shikamoo.”
“Marahaba mwanangu unaendeleaje?”
“Mmh, sijambo kidogo.”
“Pole Jeska,” Edna alimsalimia.
“Asante Edna.”
“Mmh, mwanangu kwa nini siku hizi unanificha?” Mama Edna alimuuliza Jeska.
“Kukuficha lipi mama?”
“Eti mimba si ya konda wa daladala?”
Jeska hakujibu alinyamaza kimya kwa kuamini akikataa ataulizwa ni nani, lakini aliamua kujibu.
“Ndiyo mama.”
“Ya nani?”
“Japo najua nitaonekana sina adabu naomba kwa hili mzazi wangu niachie mwenyewe maadamu ujauzito umetoka.”
“Jeska mbona unatuzunguka, kwa nini usimseme ikiwezekana tumfungulie mashtaka.”
“Nakuombeni tuacheni na hilo.”
“Au baba yako?”
Kauli ile ilimshtua Jeska ambaye alikuwa bubu mara moja,
“Haiwezekani litokee tatizo zito kama hili ukae kimya kama ni baba yako sema na akirudi atanitambua.”
“Mama mbona hivyo umeambiwa ni baba?” Edna alimtetea baba yake.
“Mama mbona umekwenda mbali hivyo, baba afanye hivyo ili iwe nini?”
“Kwani si mwanaume, Jeska basi naomba umtaje la sivyo nitajua ni baba yako,” mama Edna alikuja juu.
“Nitamtaja ngoja nimalize matibabu utamjua tu.”
“Sawa, lakini lazima nimjue na pia nataka kumjua aliyekutoa ujauzito wako, tukiachia hali hii hata mwenzako Edna akipata atakimbilia huko. Hata wewe usingekutwa na balaa hili tusingejua.”
“Mama hebu niacheni nimalize matibabu nitawaeleza kila kitu bila kuwaficha.”
“Sawa.”
Baada ya makubaliano Jeska alipewa chai na kunywa kisha walimuacha na kurudi nyumbani. Siku ile ndiyo siku aliyokuwa akirudi Mzee Ezekiel baba yake Edna, baada ya kufika alielezewa yote kuhusiana na kilichomkuta Jeska.
“Mnasema ametoa mimba?”
“Ndiyo, na kazua mapya kuwa mwenye ujauzito ule si konda,” mama Edna alimwambia mumewe.
“Etii! Kamtaja nani?” aliuliza kwa mshtuko.”
“Amesema akimaliza matibabu ataweka kila kitu hadharani.”
“Mmh, sawa tutamsikiliza.”
Mzee Ezekiel baba Edna alipumua baada ya kusikia hakutajwa, lakini alipanga kabla familia yake haijakwenda hospitali mchana awahi kumuomba Jeska asimwambie mtu hata kwa kumuhamisha hospitali ili tu ibakie siri yao wawili.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment