Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SIONDOKI MPAKA NIFE - 3

 





    Simulizi : Siondoki Mpaka Nife

    Sehemu Ya Tatu (3)



     Ilikuwa ni picha ya Twaha. Titus akaitazama na kuiona sura ya uzee na iliyopoteza matumaini ya kuishi. Hakuikumbuka. Akaitupa mezani na kushika paji la kichwa chake huku akiuma meno.

    "Oya vipi?"

    Maliki akafahamu kuwa hayupo sawa. Ndio maana akamuuliza.

    "Dah! Unajua" akapiga kite cha hasira juu ya meza pana iliyobeba kompyuta mbili kubwa.

    "Kuna demu nilikuwa naye sasa katoweka katika mazingira ya kunitatanisha sana mwanangu"

    "Kumbe ndio alikuwa anakufanya utuhasi kamanda wangu?" Fredy akaropoka bila kufahamu chochote kilichokuwa kinaendelea. Hakujua kama Maliki alikuwa anahusika.

    "Bwana enhee! Potezeeni hizo ishu tuongee kuhusu huyu mdudu"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maliki akaropoka kwa hasira. Ukimya mfupi ukatanda kila mmoja asiwe na sauti kwa Maliki. Titus akawepo ndani ya jengo hilo kimwili, mawazo na roho yake haikuwepo hapo. Ndio maana hata alipokuwa akipewa nakala ya picha ya Twaha kukaa nayo, hakuweza kumgundua kabisa kama huyo ni yule aliyekutana nae nyumbani anapoishi Agape. Kwanza hata siku alipokutana naye, hakuinakili vyema sura ya Twaha, ndio maana alipopewa picha hakuitambua. Akaiweka kwenye mfuko wake akijitia kuendelea kusikiliza. Kila Maliki alipokuwa akimgeukia Titus, alimuona kuwa mwenye mawazo sana. Ghafla Titus akakifanya kitendo ambacho Maliki alikitarajia. Kunyanyuka na kuondoka katikati ya mazungumzo yao. Fredy alibaki akishangaa Maliki alicheka kwa tuo bila kuonesha meno. Titus alitoka mpaka nje asijue wapi anaenda. Maliki naye alitoka na kumuacha Fredy akiendelea kushangaa matukio ya ajabu wanayoyafanya wenzake. Maliki alipiga simu kwa Suleya.

    "Huyo mtu wangu ameamka?"

    "Ndiyo ila amekaa kula tangu ulipomuacha"

    "Kwa hiyo unaniambia nini?"

    "Nikuambie nini vipi Maliki? mtu wako amekataa chakula"

    "Nakuja"

    Baada ya kukata simu, aliufungua mlango wa chooni na kutoka. Akakutana na Fredy akiwa amesimama mlangoni kwa minajiri ya kutaka kuingia. Uso wa Fredy ulionekana ni wenye wasiwasi sana. Akamuuliza.

    "Vipi mbona hapa?"

    "Nimebanwa sana na mkojo mshikaji wangu"

    Lakini hakukuwa na ukweli wowote juu ya sauti yake iliyotetemeka. Maliki akatabasamu kwa kebehi na kuona kuwa ameanza kufuatiliwa. Akajiuliza

    'Kama nimemteka mwanamke wa Titus kwanini anifuatilie huyu mpumbavu?'

    Akacheka tena, kisha akaondoka. Alirudi katika kile chumba cha mitambo ya ya ulinzi. Alikuta kikome cha kahawa ambacho bila shaka alikuwa akinywa Fredy. Akautumbukiza unga wa sumu kwenye kahawa ile na kutoka.



    ...



    Baada ya dakika chache baadaye, Agape aliamka. Alikuwa anapata shida sana katika kupumua na pia alihisi anakosa nguvu ya misuli katika shingo yake. Alijinyoosha nyoosha kila upande mpaka misuli ya shingo yake kutoa mlio. Chumba alichokuwemo kilikuwa kina giza. Akapiga kelele za kuomba msaada.

    "Nisaidieeni"

    Hakusikia chochote kilichokuwa kikitembea. Alijaribu kutembea ndani ya giza hilo hakugusana na chochote wala hakujua ulipo mlango wa kutokea. Hewa safi ya kiyoyozi ilikuwa ikibadilisha hali ye hewa ndani ya chumba hicho. Alikaa kimya kwa muda akiitafakari sehemu aliyopo akaanza upya kupiga kelele.

    "Anybody here" aliongea kimombo "pease help me" nadhani alifahamu au alihisi lazima waliomteka walikuwa wanafahamu yeye ni mtoto kutoka katika familia yenye uhafadhali wa kimaisha. Akahisi labda mtekaji alikuwa anataka kiasi fulani cha pesa kutoka kwa baba yake, ndio maana akaropoka tena

    "Nieleze basi unataka nini, najua unanisikia"

    Taa zikawashwa. Alishuhudia vioo vikamtazama. Akiwa hajakaa vizuri akasikia sauti ya viatu vyenye kisigino kirefu kikitembea kuingia ndani ya chumba hicho chenye ukuta wa vioo. Akajaribu kuvunjaa kioo kwa kukipiga teke kwa nyuma yake kioo kimoja kikaachama na mwanamke mwenye asili ya kiaarabu akaingia.

    "Huwezi kukivunja kioo hicho usijisumbue"

    Suleya alizungumza akiwa na taswira ya tabasamu la kinafki. Alibeba sahani pana yenye aina ya chakula chenye hadhi ya juu. Akamtupia kama mbwa kwa kumsukumizia na miguu yake. Agape akiwa anatokwa na machozi naye akakipiga teke sahani ya chakula kile na kukimwaga kabisa. Suleya akatoka ndipo akazungumza na Maliki wakati ule wakati Maliki anampigia simu.

    "Yupo wapi?"

    Baada ya dakika chache baadaye Maliki alikuwa ameingia ndaniya nyumba aliyomuihifadhi Agape.

    "Yupo kwenye chumba chake"

    Maliki akaenda kuonana na Agape akiamini akirudi atakutana na mzoga wa Fredy.



     Mlango wa chumba alichomo Agape,

    ukafunguliwa. Agape akashituka sana

    kukutana na mtu mwingine mwenye asili

    kama ya yule mwanamke aliyetoka.

    Wote walikuwa ni waarabu. Huyo

    alimtambua kwa kuwa alikuwa na

    kumbukumbu mara ya mwisho alikuwa

    slipway. Akajiuliza taratibu huku

    akimtolea macho ya hasira Maliki

    'Nipo wapi hapa? Nilizimia kwa muda

    gani?'

    Hisia zake zikamuongoza kudhani kuwa

    alikuwa mbali na Tanzania.

    'Sasa niko wapi?'

    Akabishana hata na nafsi iliyomwambia

    ukweli. Akaanza kulia kwa uchungu

    huku akimuambia Maliki.

    "Mnataka nini kwangu? Baba yangu

    atawapa chochote mnachokitaka

    naomba mniruhusu kuongea na baba"

    Maliki akacheka kipumbavu na

    kumfanya Agape kujiona mjinga.

    Akaamua anyamaze. Maliki akamsogelea

    pale alipo na kuanza kuzichezea nywele

    zake Agape. Agape akamtemea mate.

    Maliki akayafuta na kuyalamba huko uso

    wake ukiwa umegandwa na tabasamu la

    kejeli. Dakika chache baadaye uso wa

    Maliki ukavaa hasira na kuuuvuta mkono

    wake na kukiachia kibao kikali juu ya

    shavu laini la Agape. Agape alitoa kilio

    cha uchungu na kumalizia na kwikwi

    mfululizo. Akamtemea tena mate Maliki

    mchezo ukawa ni ule ule, maliki

    akajipangusa kisha akayalamba. "Ujue

    wewe ni msichana mzuri sana, hupaswi

    kupigwa ukaumizwa kiasi unachotaka"

    akiwa anamshikashika shavu "naomba

    utii ninachokueleza bila shuruti"

    Tabasamu la kifedhuli likizidi

    kung'ang'ana juu ya papi zake Maliki.

    "Naomba uniambie mnataka nini

    kwangu?"

    "Hatuhitaji pesa kutoka kwa baba yako,

    hana pesa ya kutupa"

    "Basi nijuze mnahitaji nini kwangu

    tafadhali niachieni" Agape alilalama

    huku akijinyonga nyonga kama

    anayetaka kufungua kamba za mikono

    alizofungwa.

    Maliki akajinyanyua na kumuacha Agape

    peke yake pale alipo. Alitoka na kumpa

    maelekezo Suleya juu ya ulinzi mkali wa

    Kumlinda Agape. Suleya bado alikuwa

    katika giza la kutofahamu kuhusu

    Agape. Hakufahamu sababu ya Maliki

    kumteka nyara Agape. Wala hakumjua

    Agape. Akatamani kumuuliza, lakini

    misingi yake ya kazi haikumruhusu.

    Maliki akaondoka. Alirudi katika nyumba

    yao aliyomuacha Fredy. Huko nako

    alimkuta Fredy. Fredy akipumua huku

    akiinywa kahawa yae na kutafuna

    kashata. Tabasamu la dhihaka

    likamponyoka Fredy alipoutazama uso

    wa Maliki. Uso uliosawajika na

    kustaajabu nini kimetokea. Kichwani,

    Maliki aliwaza jinsi ambavyo aliweka

    sumu ile isiyomuacha mnywaji wake

    japo kwa dakika kumi zaidi.

    "Nini kimetokea?"

    Kwa dhihaka zaidi Fredy akainywa

    kahawa ile na kuutoa ukelele wa raha

    baada ya kunywa kinywaji hicho

    "Haaaa!!!"

    Maliki alishindwa kujizuia kutoonesha

    hasira zake. Akazikunja ndita zake kwaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hasira na kusonya. Uhasama juu ya

    Maliki na Fredy ukawa wazi. Lakini Fredy

    hakuonesha kutojali. Hakufahamu nini

    kilikuwa kinatokea ndio maana aliweka

    ulinzi mkubwa juu ya kila akifanyacho

    Maliki. Alishagundua Maliki si rafiki tena.

    Maliki akaingia ndani hakuchukua muda

    zaidi na baadaye kutoka nje.

    Hakumuaga Maliki.

    ....

    Kulala katika kulala kwa Twaha,

    hakukuwa kawaida kama siku zote

    alivyokuwa akilala. Alilala zaidi ya muda

    ambao alijizoesha kulala siku zote.

    Twaha alipoingia kulala chumbani kwake

    na kumuacha Agape na kijana fulani

    sebuleni, hakuamka mpaka saa sita ya

    usiku. Kijana aliyekuwa na binti yake

    ndio kijana aliyemuota ndani ya ndoto

    zake. Ndoto ambayo ilimfanya aamke

    ghafla huku akitweta. Huenda bila ndoto

    hiyo Twaha asingeamka. Haijulikani

    kwanini alilala kwa muda mrefu kiasi

    hicho. Ila ndoto hiyo bila shaka ndiyo

    iliyoharibu usingizi wake. Ndoto ya

    nyoka mkubwa mwenye sura ya kijana

    anayemfananisha na kijana ambaye

    anamtafuta kwa udi na uvumba kisha

    nyoka huyo akammeza binti yake wa

    pekee. Furaha yake iliyobaki baada ya

    mke wake kufariki. Ni hapo alipomezwa

    na nyika akashituka na kuamka akiwa

    amelowa jasho. Akaikumbuka sura ya

    yule kijana aliye na umbo la nyoka.

    Alipoikumbuka kwa makini, alikumbuka

    ni moja kati yua picha za watuhumiwa

    anaowatafuta. Alifungua mtoto wa kabati

    lake na kutoa bahasha iliyohifadhi picha

    za watu ambao anawatafuta. Picha ya

    Titus ikawa ya pili. Tabasamu fulani raha

    likampitia. Alishuka mpaka sebuleni

    hakumkuta Agape binti yake. Akaamua

    kuipiga simu ya Agape haikupatikani.

    Wasiwasi ukamuingia. Alianza kuhisi

    huenda wale pia wamemteka kutokana

    na kumuhisi anawafuatilia. Akaipiga

    simu ya mkuu wa kazi hiyo.



     Maliki hakwenda mbali alipokuwa ametoka nje. Nia yake ikawa ni kumfuatilia kila anachokifanya Fredy. Wasiwasi wake mkubwa ni kama angeitoa siri hiyo kwa Titus kama yeye ndiye muhusika wa kumteka Agape. Alikaa akisikiliza kila anachoongea na anachokifanya Fredy. Hakuwa na madhara yeyote. Kwani aliiteketeza dakika nyingi bila kusikia kama fredy alipokea simu wala kupiga, akaamua kuondoka. Bila kufahamu Fredy alikuwa anafahamu uwepo wake chini ya dirisha nje ya ukuta wa chumba alichomo. Alikiona kichwa cha maliki kikinyanyuka na kurudi tena chini kupitia kioo cha kompyuta yake aliyokuwa akitumia. Alitumia wakati huo alipomuona akiondoka kuipiga simu ya Titus, iliita bila kupokelewa mpaka ilipokatika. Akarudia zaidi ya mara nne mwisho majibu yakaja kuwa simu imezimwa.

    "Huyu naye"

    Akaropoka huku akijinyanyua kwenye kiti. Hali ya uoga ikamtafuna kiasi cha kupanga kukimbia nyumba. Wakati ambao Maliki anaiweka sumu kwenye kahawa yake aliona. Hivyo aliamini kabisa kitu ambacho Maliki anakificha ni kikubwa sana na kulinda thamani ya uaminifu wake kwa Titus. Ndio maana alipanga kuitoa roho yake. Hakumjua Agape, ila aliamini Agape ni mtu anayemuhusu Titus. Hakufahamu uhusiano wao, lakini kumwambia Titus aliamini kungekuwa kutatua tatizo ambalo Maliki analificha. Tatizo ambalo limeweka roho yake rehani. Alivyopambanua mambo kwa kina ndipo akaona uzito wa jambo linalomkabili. Alilichukulia kikawaida lakini alipokumbuka alipokutana kwa mara ya kwanza na Maliki asingeamini hata leo kama Maliki angewaza hata siku moja kumuangamiza.

    "Kwanini aniue?" Akashika kiuno mara aikunje ngozi ya chini ya midomo yake "lazima nifahamu nini kinaendelea"

    Akashusha pumzi nzito na kuizima kompyuta. Akairudia simu yake aliyoitupa juu ya meza na kuipiga simu ya Titus, ilikuwa inapatikana na ikapokelewa. Sauti ilikuwa ya Titus

    "Uko wapi mshikaji wangu?"

    "Nipo njiani kuna mtu namtafuta Fredy kuna tatizo?"

    "Hapana ila kuna jambo nafikiri ni muhimu ukalifahamu"

    "Jambo lipi?"

    "Si vyema tukazungumza kwenye simu"

    "Poa nakuja"

    Damu ya Fredy ikazunguka kwa kasi ndani ya mishipa yake na kupeleka kwenye moyo. Akahisi kukosa nguvu kila alipolifikiria jambo hilo. Moyo wake ukakataa kabisa kukaa ndani ya nyumba hiyo. Akazishuka ngazi kutoka juu chumba chenye mitambo kilipo. Kabla hajaufungua mlango wa kutoka nje alipofika ukumbini, akasalimiwa na mdomo wa bastola. Bastola iliyoshikwa vyema na Maliki. Maliki hakuonesha mzaha kabisa katika hilo. Alikuwa akicheka kifedhuli na kiushindi. Fredy akaiona taswira mbaya aliyokuwa haifahamu kutoka kwa maliki. Matumaini ya kuishi hakuwa nayo tena. Aliamini hata siri aliyotaka kuitoa kwa Titus isingemfikia.

    'Nani atamfikishia Titus ujumbe niliotaka kumwambia? Nani atafahamu uovu wa Maliki?'

    Akiwa anawaza hayo mwili wote ukiwa unamtetemeka ndipo wakati ambao Maliki akafanya kitu cha ajabu mbele ya uso uliopoteza matumaini wa Fredy.



    ...



    "Unafanyaje kazi kizembe Twaha?"

    "Mkuu nilikuwa nimechoka sana sikuweza kumjua kabisa mkuu"

    "Sasa unafikiri nitakusaidiaje zaidi ya kuwatafuta umuokoe na mtoto wako?"

    "Nilikuwa natoa taarifa tu mkuu" "au umeshindwa kazi nikupe askari wengine?"

    "Hapana mkuu nitalishughulikia hili mwenyewe"

    Maongezi ya Twaha yakahitimishwa na kukatwa kwa simu. Twaha akazishusha pumzi ndefu na kuwaza aanze wapi kumtafuta kijana ambaye amemuona kwa mara moja tu na asijue wapi atampata kumuuliza kuhusu alipo mtoto wake. Machozi yaitaka kumtoka alipokumbuka wosia ambao marehemu mke wake alikuwa akimuasa mara kwa mara

    "Mume wangu kazi yako ni ya hatari unaweza kutuletea matatizo baba Agape"

    Yeye hakujali akajibu kishababi

    "Anha mimi kama simba wa nyumba nina haki ya kuinda familia yangu"

    Sasa leo yote yakajirudia kama mkanda wa video. Alimkumbuka sana mke wake. Alihisi kububujikwa na machozi kwa kuwa mwanaume aliyekaa mara ya mwisho na Agape ndiye mwanaume anayemtafuta usiku na mchana. Ndiy huyu anayeitazama picha yake tena na tena kujihakikishia kuwa kama ndiye yule aiyeiba mabilioni ya pesa katika benki kuu ya kenya.

    "Pumbavu"

    Akaitupa picha ile chini na kukipiga piga kichwa chake kwa viganja vyake. Akili yake ikamuongoza kwenda chuoni. Chuo cha Diplomasia. Alivaa haraka haraka hata gari yake akaiendesha kwa mwendo wa kasi. Dakika 30 zikawa nyingi na kukutana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma na Agape.

    "Unamfahamu kabisa Agape?"

    "Ndio mzee" alikuwa ni rafiki yake wa hapo Diplomasia aliyejulikana na wengi kwa jina la Gunga. Alikuwa ni rafiki wa karibu wa Agape ambaye Twaha alitambulishwa na baadhi ya walimu wake Agape.

    "Sasa mwenzako amepotea"

    "Amepotea?"

    Macho makubwa ya Gunga, yakazidi kuwa makubwa kutokana na hilo aliloambiwa na Twaha.

    "Ndiyo. Ndiyo maana nipo hapa kukuuliza kama unafahamu chochote"

    "Hapana mzee wangu ila"

    Akiwa ameinamisha kichwa chini akijaribu kutafakari jambo. Alitoa simu yake kwenye kimkoba alichokipachika kiunoni na kushikiliwa na mkanda.

    "Ila..?"

    Twaha akauliza kwa shahuku.



     Gunga naye akajibu huku akiendelea kupekua kitu kwenye simu yake.

    "Pale Ifm.. Agape.. Agape ana rafiki yake mkubwa"

    Akanyamaza kwa sekunde na kumkera Twaha aliye na shahuku ya kufahamu nini alikuwa akisema.

    "En enhee!" Gunga akashituka kwa kusema "namba yake hii hapa" akampa simu Twaha. Juu ya kioo chake namba ilikuwa ni jina la Nadia.

    "Nadia?"

    "Ndiye huyo rafiki yake mkubwa wanazunguka naye kila sehemu. Huyo lazima atakuwa anajua wapi alipo Agape"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Twaha akaihifadhi namba ya Nadia kwenye simu yake. Akajaribu kuipiga ikawa haipatikani.

    "Shit!"

    Akapiga kite cha hasira. Alikuwa na wasiwasi mkubwa huenda Nadia asifahamu alipo Agape. Mawazo yakamtuma kudhani yule aliyekuwa akimtafuta usiku na mchana amegundua Agape ni binti yake. Akajilaumu kwanini hakupoteza japo dakika chache za usingizi wake kumsikiliza binti yake. Ona sasa. Ona sasa anashindwa kula na kufanya chochote kwa sababu ya binti yake kupotea. Ona sasa anaanza kuwatafuta watu wawili ambao wote ni muhimu kupatikana wakiwa hai. Au lah! Mmoja akiwa amekufa mwingine akiwa hai. Huyo aliyetakiwa kuwa hai ni binti yake maiti iwe ya yule kijana. Machozi yakachota mboni zake akatamani kuyadondosha, akakumbuka kuwa yu karibu na kijana mdogo saizi ya mwanaye. Akasahau hata kumuaga Gunga akatoka mbio kulifuata gari yake.

    "Kwa hiyo mzee unaelekea Ifm?"

    "Ndio kijana wangu. Acha nikamuangalie huko"

    "Sawa basi hujaniachia namba yako ya simu"

    "0..6..5..4..8..4..6..0..8..4"

    "Sawa kama kuna lolote nitakujulisha mzee"

    Twaha akawa ameshaingia ndani ya gari na kulitekenya, injini ikaitika. Aliliingiza barabarani kwa mwendo wa fujo sana. Kutokana na foleni pale eneo la bandari barabara ile ile ya kilwa, ikapandisha mori ya Twaha. Mara auume meno, apige selo kwa fujo dakika ishirini baadaye gari zikaanza kutembea. Alitukana kila tusi pasina mtu kusikia chochote alichokuwa akiongea. Akakatiza mitaa ya posta na kuipita steers na kukifikia chuo kikuu cha uadhili wa fedha Ifm. Akaiegesha gari pembezoni kidogo mwa ukuta wao.

    "Sasa nianzie wapi? Au.."

    Akiwa amejitokeza nje akaona wanafunzi kadhaa wakiwa wanapita pita. Wengine wakiingia ndani ya geti la Ifm na wengine wakitoka. Akaona kabla hajamuita mmoja wao kumuulizia huyo Nadia, apige ile namba tena.

    "... Haipatikani"

    Sauti kwenye spika za simu ikampandisha zaidi hasira Twaha. AKapiga ngumi nzito juu ya bati la gari yake. Akaropoka kwa hasira

    "Pumbavuu"

    Akaunda tabasamu hafifu baada ya kumuona msichana pembeni yake.

    "Habari yako binti"

    Yule msichana hakuwa na kawaida kabisa ya kusimamishwa akasimama. Ila taswira ya Twaha, ikamfanya asaliti kawaida yake. Sura yenye hekima na umri ukiwa umemtupa mkono. Akajisemea mwenyewe 'labda ana shida na mtu humu ndani'

    "Shikamoo"

    Akamsalimu Twaha, huku Twaha akijaribu kuilazimisha furaha usoni mwake.

    "Naomba kukuuliza"

    Yule msichana alimsogelea Twaha huku akitingisha kichwa kwa kukubali kumsikiliza.

    "Sijuhi unamfahamu Nadia?"

    "Nadia Chopa?"

    "Sijuhi ndiye mimi simfahamu"

    "Ndiye maana hapa hakuna Nadia mwingine maarufu zaidi yake. Najua na nimemuacha.. Oh! tena huyo anakuja"

    Akamuonesha alipokuwa Nadia. Nadia alikuwa akikatiza barabara na kuja usawa ambao wao walikuwa wamesimama. yule msichana akamuita Nadia

    "Nadia una mgeni"

    Nadia akasimama na kumsalimu Twaha.

    "Habari yako Nadia"

    "Salama tu"

    "Mbona simu yako haipatikani tangu asubuhi?"

    Nadia akashituka na kubetua midomo yake kwa dharau. Hilo Twaha hakulijali

    "Wewe umepata wapi namba yangu?"

    Nadia akauliza tena kwa dharau. "Mimi ni baba yake Agape sijuhi unamfahamu?"

    Hapo Nadia akashituka na kuishika midomo yake kwa viganja vyake. Aibu ikamkamata na kuyafinya macho yake. Akaomba radhi kwa Twaha kana kwamba alikuwa amemtukana.

    "Usijali binti yangu namtafuta sana mwenzio na sijuhi wapi alipoelekea na wasiwasi juu ya watu wabaya"

    "Mimi mwenyewe baba nachanganyikiwa kwa kuwa alikuja mchumba'ake hapa dakika chache tu zilizopita kumtafuta nikipiga simu yake haipatikani sijuhi atakuwa wapi Agape"

    Twaha akaelezea mazingira ya mwisho ambayo aliachana na Agape na yeye kwenda kulala. Akaeleza kuwa alikuja na kijana, akauelezea muonekano dhahiri wa Titus. Hapo Nadia akaropoka

    "Huyo bila shaka ndiye Titus Mchumba'ake"

    Twaha akalipukwa na mapigo a moyo na kunyamaza kimya kwanza. Kisha akarudi ndani ya gari yake na kutoa bahasha yenye picha za wahalifu wote anaowatafuta, ya Titus nayo ilikuwa miongoni mwa picha hizo.

    "Ni huyo ndiye mchumba'ake?"

    "Di diii! Duh! Ndiye huyu huyu. Dah baba wewe mchoraji nini? Maana umempatia kweli"

    "Sasa unapafahamu kwa huyu kijana? Maana huenda yupo huko au namba zake za simu?"

    "Hapana baba sina chochote kati ya hivyo viwili mara nyingi alikuwa akija anakuja na Agape mwenyewe"

    Matumaini ya kumpata Agape kwa wakati huo yakazidi kufifia kwa kuwa aliamini kuwa Agape yupo mikononi mwa watu wabaya ambao huenda wamemteka Agape kumpunguza kasi ya kuwatafuta. Akaachana na Nadia na kurudi nyumbani kwake Masaki. Juu ya kaunta ya vinywaji vyake vikali akaichomoa pakti ya sigara zake na kuiwasha moja iliyobakia. Akamimi kilevi cha jack daniel akisubiri simu kutoka kwa watu waliomteka mwanaye. Aliamini muda wowote wangepiga.



    ...



    Mlio wa risasi uliofyatukia begani kwake Fredy, Titus aliusikia na alimuona Fredy wakati akianguka mbele ya Maliki aliyeshika bastola.

    "Nini kimetokea?"

    Titus akalishika bega la Fredy lililokuwa na jeraha ya risasi.

    "Huyu mpumbavu anataka kutuchoma tuje kukamatwa, sogea nimmalizie"

    Akawa amempiga kikumbo Titus na kuikoki tena silaha yake akitaka kumfyatulia risasi nyingine Fredy. Fredy akiwa amekunja sura kwa maumivu ya kuvunjika mmoja katika mifupa ya bega lake, akalirusha teke lililompata barabara Maliki sehemu zake za siri. Maliki akagugumia kwa maumivu ya teke lile hata kumfanya kuidondosha silaha yake aliyoiweka kiwambo cha kuzuia sauti. Titus akawa amemfuata tena Fredy na kuzuia jeraha lake Fredy kwa shati lake alilolivua na kulifunga juu ya bega la Fredy.

    "Ngoja nikupeleke hospitali Fredy"

    Kulikuwako na hospitali yao maalumu humo humo ndani ya nyumba. Walikuwa na daktari wao aliyehusika na kuwahudumia pale walipopata matatizo yeyote ya kiafya. Fredy hakutaka hayo yote roho yake ikawa inamsukumu kumwambia kile alichokifahamu kwa kuwa alijua Maliki alikuwa na nia naye mbaya. Hivyo muda wowote Maliki angemuangamiza kama asingemuambia mapema Titus kuhusu ubaya wa Maliki. Titus akiwa ameshamfikisha Fredy katika chumba cha daktari na kumuweka juu ya kitanda akataka kuondoka. Fredy akamvuta Titus shati. Titus akamgeukia na kumwambia

    "Usijali utapona ni jeraha dogo tu"

    "Lakini nina la muhimu la kukuambia."

    Titus akamgeukia na kusimama pembezoni mwa kitanda chake alicholala Fredy.

    "Maliki si mtu mzuri na ndiye aliyemteka msichana ambaye nadhani unamtafuta yupo..."

    Dokta wilson bila kufahamu umuhimu wa habari aliyokuwa akipewa Titus na Fredy, akawa amemdunga sindano ya usingizi. Titus akajaribu kumuamsha Fredy, Fredy akawa amelala fofofo.

    "Dokta umemfanya nini?"

    "Samahani Titus sikujua kama mlikuwa mkizungumza kutokana na kumuona alikuwa anahitaji huduma haraka nikaona heri nimpe dawa ya usingizi niweze kuitoa risasi iliyopo mwilini mwake"

    Titus akatoka mbio mpaka pale alipomuacha Maliki hapo mwanzo.

    Hakumkuta.

    Maliki akamuona jinsi ambavyo Titus alikuwa anamtafuta pale nje na kila kona ya nyumba. Akawa amejibanza ndani ya ua kubwa lililopo karibu na dirisha a chumba cha daktari. Titus akarudi tena ndani kumuachia maagizo Dokta Wilson.

    "Tafadhali natoka naomba usitoke ndani ya hiki chumba mpaka fredy atakapoamka"

    "Bila shaka Titus"

    "Yaani umlinde huyu hata Maliki asimguse"

    "Sawa nimekuelewa"

    Titus akawa ametoka kama amechanganyikiwa hakujua wapi anaenda lakini aliingia ndani ya gari lake na kutoka nje. Akakumbuka kuwa Malikia aliwahi kumtambulisha kwake msichana anayeitwa Suleya. Akaitafuta namba ya suleya kwenye kitabu chenye orodha ya namba za simu. Namba alikuwa nayo. Akaipiga.

    "Uko wapi kwa sasa Suleya?"

    "Labda unijulishe kama unataka kuonana na mimi lakini si kukuelekeza wapi nilipo"

    "Sawa mimi nipo bunju tunaweza kuonana?"

    "Tukutane kule mwabepande"

    Sauti nyororo ya Suleya ikaishia hivyo kwenye spika zilizokuwa zikitoa sauti na kupenyeza ndani ya masikio ya Titus. Sauti hiyo ikapenya moja kwa moja mpaka ndani ya kilindi cha moyo wake. Titus akajitahidi kuepuka mawazo ambayo alikuwa akiyawaza kwa wakati huo na kuyarudisha katika mipango mipya aliyo nayo ya kumpata Agape. Simu ile hawakuwa wawili tu hewani. Maliki pia naye alijumuika katika mazungumzo yao pasina kuongea chochote. Jambo hilo Suleya hakufahamu kama simu yake kuna mchezo amefanyiwa hata kila simu iliyokuwa ikiingia ilipita pia moja kwa moja kwa Maliki. Malikia akaiandaa sumu yake na kuingia ndani ya chumba cha dokta wilson. Alipoufungua mlango, dokta wilson alikuwa anashugulika kumuwekea Fredy kifaa cha kumsaidia kupumua. Akachomwa na sindano ya Maliki iliyobeba dawa yenye sumu yenye uwezo wa kuutoa uhai wa mtu haraka. Dokta Wilson akadondoka kama gunia pale pale. Maliki akakichomoa kifaa kile kwenye pua ya Fredy na kutokomea zake baada ya kumchoma na yeye sindano nyingine yenye dawa ile ile iliyomuangusha Dokta Wilson.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Titus alienda mpaka katika eneo la mwabepande alipotakiwa kukutana na Suleya. Huko alikaa dakika chache na kusikia mngurumo wa pikipiki alipokuwa amekaa katika eneo la wazi. Akageuka nyuma yake na kumuona Suleya. Akasimama na kumfuata mpaka pale alipokuwa akimpa kiasi chake kama malipo yule dereva wa pikipiki.

    "Habari yako Suleya"

    Suleya akamkumbatia Titus na kumpiga mabusu mawili shavu la kushoto na kulia, kisha akaitikia salamu yake

    "Nzuri Titus naomba uzungumze haraka kidogo"

    "Mnh! Mara ngapi ulikuwa ukinisumbua tukutane?"

    Suleya hakujibu kitu akatoa tabasamu hafifu la fedheha.

    "Sasa leo nimejileta mwenyewe ukipenda nichinje ukitaka nitafune mzima mzima"

    Titus akatumia hila za kumlaghai kimapenzi kwa kutumia udhaifu aliokuwa nao Suleya na alifahamu. Alishawahi kukutana mara tatu na Suleya kila mara walipokutana Suleya alikuwa na kila dalili za kumtaka kimapenzi Titus. Alimng'atia papi za midomo yake mara amkonyeze huku akijitia ni bahati mbaya, akatumia hila hizo kufahamu kille alichokisema Fredy. Hakujua kama Suleya ndiye aliyemuhifadhi Agape ndani ya chumba cha siri katika nyumba ya siri ya Maliki. Allichokifahamu kuwa Suleya ni mtu wa karibu sana na Maliki. Hivyo kukaa naye karibu kwa kutumia udhaifu wake wa kumtaka kimapenzi angepata chochote cha kumsaidia katika utafiti wake wa kumpata Agape.

    "Ndiyo lakini bosi wangu asiponikuta nyumbani itakuwa shughuli nzito"

    Suleya akammanisha Maliki ndiye bosi wake lakini hakutaka kuwa wazi alikuwa akifanya kazi wapi au anakaa wapi na bosi wake ni nani hata Titus alipojaribu kunchunguza.

    "Dah! Basi sawa kama umekataa kabisa kunipa ushirikiano. Lakini.."

    Titus akamuingizia maneno yake na kumuacha Suleya bado hajaelewa nia ya Titus kumuhitaji wala alichokuwa akizungumza hivyo hakufanya haraka ya kuondoka.

    "Sasa Tito ulikuwa unasemaje, mbona unajiuma uma?"

    Titus akacheka kidhaifu na kumtazama kimahaba Suleya. Midomo yake akailamba na macho akayalegeza, kwa mitego hiyo akaamini kuwa isingekuwa ngumu kwake kupata alichokuwa akikitafuta.

    "Tunaweza kuwa pamoja usiku wa leo?"

    Suleya akaguna aliposikia jam bo hilo. Akili yake ikafanya kazi kwa wepesi na kukumbuka vizuri ukatili ambao angefanyiwa na Maliki endapo asingemkuta nyumbani. Endapo Agape angetoroka ingekuwa tiketi yake ya kifo. Akatamani kumkatalia Titus lakini pia alitamani sana kuwa pamoja naye usiku huo. Kwani alikuwa akimpenda kwa muda mrefu sasa. Hiyo ndiyo bahati, bahati ya pekee kuona Titus amejileta mwenyewe bila yeye kutangaza udhaifu wake. Akafikiria ni mnara ngapi Maliki alikuwa anakuja mida ya jioni katika nyumba ile.

    'Mara chache sana'

    Akajiambia kimoyomoyo. Akaugeuza uso wake na kumtazama tena Titus kisha akatabasamu.

    "Sawa nitakuona saa tatu usiku, ache niende"

    Titus alifurahi sana. Saa ya ushindi akaiona ipo karibu naye. Akamzawadia tabasamu Suleya tabasamu Maridhawa na kumtandika busu safi juu ya papi zake. Suleya akaondoka kurudi nyumbani huku bunju.



    ...



    Maliki baada ya kumuua Dokta Wilson na Fredy, alitoka ndani ya nyumba hiyo na kuelekea kwa Suleya alipomuhifadhi Agape. Huko alienda akiwa anaamini kabisa hatomkuta Suleya. Aliamini kwa simu aliyopokea Suleya kutoka kwa Titus ni lazima kwa sasa wangekuwa maeneo fulani wakijivinjari au Titus akimchota jambo fuani. Alihema kwa nguvu na kumfanya kuonekana kama mtu aliyekimbia mbio za marathoni. Huyo ndiye Maliki aliyeongozwa na hisia na kuutandika mlango wa nyumba yake hiyo ambayo haikujuikana na mwingine yeyote labda Agape na Suleya. Agape hakufahamu huo nje kulifananaje wala hakujua wapi alipo. Watu pekee aliozoea kuwaona ni mwanaume na mwanamke wenye asili ya kiarabu. Alijaribu kuvunja vioo japo afahamu mlango wa kutokea lakini hakuweza. Pale alipotazama kwa makini na kuamini kuwa ndipo mlango ulipo hapakuwa pale. Hapakuwa pale kwa kuwa alipojitokeza tena Suleya ni nyuma yake. Chumba hicho kilikuwa kinazunguka bila kufahamu kama kinazunguka. Chumba maalumu kwa ajili ya mateka. Suleya alikuwa amewahi sekunde kadhaa kabla Maliki hajaingia kwa ghadhabu ndani ya nyumba hiyo.

    "Suleyaa!"

    "Maliki"

    "Kumbe upo? Ulienda wapi?"

    Suleya alitoa macho ya mshangao na kuhisi mkojo ukitaka kujipenyeza katika sketi yake aliyoivaa. Hakuwa na jibu sahihi kwa kuwa hakujua kwanini Maliki alimuuliza hivyo. Maliki akaona uoga juu ya uso wa Suleya. Akajua fika Suleya ameshakutana na Titus. Akataka kufahamu walizungumza nini na Titus.

    "Ulikuwa wapi nakuuliza?"

    Alimkaba koo na kumfanya Suleya kushindwa kuhema vizuri. Akamtingisha tingisha pale kisha akamuachia. Suleya alikohoa mfululizo na kupokea kibao kizito kutoka kwa Maliki

    "Utanijibu ulikuwa wapi?"

    "Usiniadhibu tafadhali"

    "Sema ulikuwa wapi?"

    Suleya akanyanyuka akiwa na damu nzito iliyokuwa ikimvuja kutoka mdomoni. Uso wa Suleya ukatazamana na mdomo wa bastola ya iliyoshikwa sawia kabisa na mkono wa Maliki huku uso wake Maliki ukiwa umejitenga mbali na mzaha.

    "Najua ulipokuwa, ni kwa mshenzi Titus"

    Jina la titus likaamsha ufahamu wa Agape. Alitumbua macho kwa nguvu akitazama uso wa Maliki uliojaa taswira nzima uya roho mbaya na unyama alionao. "Sasa usiposema mlizungumza nini nakuua wewe na huyo mshenzi wako atafuata"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog