Search This Blog

Monday 20 June 2022

SITAISAHAU FACEBOOK - 1

    https://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/11/sitaisahau-facebook.html


    IMEANDIKWA NA : EMMY JOHN PEARSON

    *********************************************************************************

    Simulizi : Sitaisahau Facebook

    Sehemu Ya Kwanza (1) 


    “Isabela….Isabela…” nilisikia sauti ya mwanamke ikiniita, niligeuka mara moja maana sauti ile ni kama niliwahi kuisikia mahali. Lakini sikukumbuka ni wapi. Giza totoro lilinizuia kuweza kumtambua mtu yule aliyeniita kwa ufasaha kiasi kile tena gizani.Nilianza kujiuliza iwapo nirejee nyuma kurudi kumtafuta ama niendelee mbele ambako pia sikuwa na uhakika ni wapi. Manyunyu ya mvua yalikuwa yamenilowanisha hasa na nguo yangu ilikuwa imeshikana na mwili. Nilikuwa natetemeka huku michubuko kadhaa katika mwili wangu ikiniwashawasha. Kilikuwa kitendawili aidha niende mbele ama nirudi nyuma kuifatiliza hiyo sauti.Ile hali ya kujiuliza niende mbele ama nirudi nyuma ikanifanya niwe kama naigiza igizo lisilokuwa rasmi.“Isabelaaaa!!!.” Iliita tena sauti hii. Sasa ilisikika dhahiri kuwa sauti ile ilikuwa katika kulia, mwenye sauti ile alikuwa katika uchungu mkubwa na bila shaka aliuhitaji sana msaada wangu. Nilitamani kuitika lakini midomo ikawa mizito. Nilipolazimisha kuitika nikawa kama nanong’oneza, sauti haikutoka. Koo lilikuwa limekauka sana. Hapo ndipo nikagundua kuwa nilikuwa na kiu sana.Nikiwa bado katika kigugumizi mara nikasikia kama hatua za mtu ama mnyama zikikatiza taratibu. Mara moja nikajiziba mdomo wangu, pumzi zangu zisiweze kusikika kwa huyo mtu. Sikuamini hata kidogo kwamba huyo anaweza kuwa yule mwanadada aliyekuwa ananiita kwa jina langu, maana huyo alisikika kutokea upande mwingine na wala sio huu aliosikika huyu anayekatiza. Nikaamua kutulizana.Baada ya muda pakawa kimya, kwa tahadhari kubwa nikaanza kunyata kwa kutembelea vidole kwa mbele vya miguu. Moyo ulikuwa katika mwendo kasi ambao hapo kabla sikuwahi kuufikiria.Moyo wangu ulikuwa katika majuto makubwa na tamaa yangu ilikuwa inaniponza sasa. Pesa nisizozitolea jasho zikawa zimenifikisha katika maluweluwe haya. Maluweluwe ya kutisha. Ulimwengu ukawa unanihukumu.Nilimfikiria yule dada aliyekuwa ananiita, nilielewa kabisa kuwa nilikuwa namfahamu lakini swali likaja.Anaitwa nani?? Ni wapi tulionana??Baada ya dakika thelathini za kutangatanga katika kipori hicho kidogo hatimaye niliifikia barabara.Ilikuwa ni barabara ya vumbi ukubwa wake ulikuwa unatosha gari kupita bila wasiwasi. Nikaamua kuifata barabara ile ili niweze kutoka eneo lile la hatari kabisa. Niliifata barabara ile kwa urefu mkubwa sana…miguu ilichoka lakini sikuwa tayari kukubali kukaa chini. Hata kama ningelia kwa wakati ule isingesaidia kitu nilikuwa katika hali ngumu sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/MIEZI SITA NYUMAMaisha ya chuo yalikuwa yamenipiga haswa, mwalimu Nchimbi ambaye ni mama yangu mzazi naye alikuwa ameungana na waalimu wenzake katika mgomo wa nchi nzima dhidi ya masilahi finyu ya waalimu hivyo hakuwa na senti yoyote ya kuweza kunisaidia, baba naye alizidi kupata umaarufu katika vilabu vya pombe kwa kucheza na kuimba hovyo baada ya kuwa amegida za kutosha.Kaka yangu alizidi kuchanganywa na madawa ya kulevya huku dada yangu mkubwa akiwa bize na ulokole aliouamini kuliko hata mume wake waliyezaa naye watoto watatu. Sikuwa na mtu yeyote wa kumwomba msaada kwani kaka yangu mwingine ambaye kidogo alikuwa anajiweza alikuwa haambiliki wala hashikiki mbele ya mke wake halafu kibaya zaidi mke wake tayari tulikuwa tumegombana.Mkopo wa asilimia ishirini niliokuwa napokea ulikuwa unaishia katika kulipa madeni.Maisha yalikuwa yameniwia magumu sana, na marafiki hawakuwa na kikubwa cha kunisaidia.Muda wangu mwingi nilikuwa naupoteza katika kusoma vitabu na pia kuperuzi mitandao ya kijamii, facebook ukiwa namba moja. Picha zangu ziliwafanya watu wengi wasiweze kuamini kuwa nina matatizo lakini ukweli nilikuwa naujua mimi binafsi.Kawaida ya wavulana walikuwa hawaishi kutoa maombi yao ya kuwa wananipenda lakini nilijaribu kuwakwepa kwani niliamini kuwa kujiingiza katika mahusiano ni sawasawa na kujiongezea matatizo katika maisha yangu kwani wanaume hawaaminiki hata kidogo.Kila mwanaume huwa ana mbinu zake za kumuingia msichana, na mimi kama msichana nilikuwa nimezikariri na kumwelewa mwanaume iwapo anakaribia kunitongoza ama la. Lakini kati ya wanaume wote aliibuka mwanaume mwingine naweza kumuita wa ajabu kupita wote. Yeye alikuwa hatabiriki leo mara anaelekea kwenye mapenzi mara kesho siasa, akisema leo kuhusu mpira wa miguu basi siku nyingine ataleta masuala ya dini.Jina lake lilisomeka kwa kifupi kama Dk. Davis. Na kamwe sikuwahi kulijua jina lake kamili zaidi ya kujua kuwa anaitwa dokta davis. Kwa kuwa ule ni mtandao wa kijamii sikuwa na haja ya kumjua sana, haikuwa na maana yoyote ile.Picha za dokta Davis zilikuwa za kawaida sana na hakuonekana kama ni mtu anayeweza kuwa na msaada wowote. Ule udokta wake nikauchukulia kama ule wa kutafuta sifa facebook.Haikupita siku bila Davis kunitumia ujumbe, sikumtilia maanani sana.Siku moja majira ya jioni, nikiwa nimekaa chumbani kwangu, hasira zikiwa zinafukuta kichwani baada ya wanachuo wenzangu tuliokuwa tunaishi hostel moja jijini Mwanza, kunisimanga kuwa silipii umeme halafu ni bingwa wa kuutumia. Kwanza nilitaka kuulaani umasikini lakini nikahisi nitakuwa nauonea. Nikaanza kumlaani mwalimu Nchimbi, mume wake, baba na babu zao kwani niliamini kama wangefanya kazi kwa bidii bila shaka wangeupiga kikumbo umasikini.Laana zangu, ambazo nilitaka kuzifikisha hadi kwa mizimu yao zilikatishwa na mlio katika simu yangu. Ulikuwa ujumbe umeingia. Niliogopa kuufungua maana niliamini ni watu wanaonidai. Nilitamani kuzima simu lakini nikakukumbuka kuwa nilikuwa nimem-bip mama yangu dakika saba zilizopita na alikuwa hajanipigia bado.Nikapiga moyo konde nikaufungua ule ujumbe.“Umepokea Tshs. 66,666 kutoka kwa Magreth Pearson. Salio lako jipya ni 66,666”Zile laana zikakoma mara moja, mawazo yote yakahamia katika simu yangu. Nikausoma vyema tena ule ujumbe. Ulikuwa upo sahihi. Nilipoangalia salio langu kweli lilikuwa lieongezeka.Nikajiuliza huyu Magreth ni nani. Jibu halikupatikana.Nikazungusha kichwa huenda yupo mtu nilikuwa namdai jibu likawa hapana ni mimi nilikuwa nadaiwa.“Huenda ni mtu kakosea kutuma!!!” likaja wazo hilo. Likachukua nafasi kubwa. Mara moja pepo la tamaa likaniingia nikamwomba msamaha kimoyomoyo huyo aliyetuma kimakosa. Kisha nikazima simu. Sikuwa nataka tena habari za mwalimu Nchimbi huko kijijini Makambako.Upesi upesi nikakimbilia katika vibanda vya kutolea pesa nikawasha simu na kuitoa ile pesa upesi.Kisha kwa mara nyingine nikazima simu tena.Kitu cha kwanza niliwakata kidomodomo wanachuo walionisemasema. Nikalipia umeme!!!!Heshima kidogo ikarudi!!! Usiku huo nilipika pilau, pilau yenye hadhi ya kuitwa pilau.Najua iliwauma!!! Nilifanya makusudi!!!Kesho yake baadhi wakawa marafiki zangu tena.Baada ya siku tatu nikaiwasha simu yangu. Hapakuwa na meseji yoyote iliyoingia ikilalamika juu ya kukosea kutuma pesa!!!!Sikuhangaika kujiuliza kulikoni.*******Ile pesa ilipokwisha nikarejea kwenye msoto kama ilivyo ada, nikawa najiliwaza katika mtandao wa kijamii wa facebook.Kama kawaida Dokta Davis, alikuwa amesheheni katika kisanduku cha kuhifadhi ujumbe.Leo Davis alikuwa na topiki nyingine kabisa, Dokta Davis alikuwa anazungumzia biashara ya mtandao.Biashara ya mtandao?? Nikajiuliza…cha kushangaza kabla sijamuuliza hilo swali tayari alikuwa amenipa majibu.Akaniuliza kama napenda kufanya biashara.Kidogo nisimjibu maana kwa picha zake biashara kubwa kwake labda ya kuuza ubuyu karanga za kuchemsha. Sasa anataka kufanya biashara gani na mimi?? Nilijiuliza na kupatwa hasira kidogo. Lakini kwa kuwa sikuwa na kazi ya kufanya nikaendelea kuchat naye lakini vinginevyo nisingemjibu upuuzi wake aliotaka kuniambia.“Unaweza kuvuna hadi milioni mbili…si lazima iwe mwisho wa mwezi!!!.” Ujumbe wake ulisema. Mh!! Macho yakanitoka, nikaingiwa na dharau kabla ya kuendelea na mazungumzo hayo.“Kivipi??” nilimuuliza ilimradi tu..“Kirahisi sana.” Alijibu. Sikuridhika na jibu lile nikambambika maswali mfululizo hatimaye Davis akanitumia kwa kirefu ni biashara gani hiyo aliyotaka kufanya nami na kwanini anichague mimi.Baada ya dakika mbili nilikuwa nimemaliza kuusoma ujumbe mrefu wa Dokta Davis. Nilikuwa natetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa katika mwendokasi wa kutisha sana. Macho yalikuwa hayafumbi bali yanaitazama simu yangu!!! Nilikuwa simuoni Dokta Davis lakini nilikuwa katika TAHARUKI!!!!!SIKUAMINI!!!!!(Biashara ya mtandao)Kilichonishangaza zaidi ni faida iliyoandikwa na Dokta Davis. Sikuipinga lakini mtaji wake haukuonekana kabisa, swali likawa ni biashara gani hii isiyohitaji mtaji lakini ina faida kubwa kiasi hiki??Nilitaka kumuuliza lakini nikakumbuka kuwa tayari aliita biashara ya mtandao.Shida zilizokuwa zikinikabili sikutegemea kuwa naweza kumruhusu roho wa kukataa anitawale.Mara moja nikakubaliana na Davis kuwa naweza kuifanya biashara ya mtandao. Sikutaka hata kidogo kukumbuka kuwa katika biashara huwa kuna faida na hasara.“Lakini tunatakiwa kuonana sasa itakuwaje!!! Au hakuna mkataba?” nilimuhoji.“Keshokutwa kama ukiwa na nafasi njoo unipokee Airport, haitakuwa mbaya kama utakuja na rafiki yako mmoja anayejua kuongea kiingereza kiasi.” Alinijibu.Siku hiyo ikapita, lakini haikumalizika bila maajabu mengine.Ilikuwa saa moja jioni. Sikuwa na mpango wowote wa kupata pesa, ujumbe ukaingia kwenye simu yangu.“Nitumie namba yako ya akaunti kuna kipesa kidogo nataka nikuwekee ili mtumie kama nauli kuja uwanja wa ndege kunipokea. Nilishangazwa na meseji hiyo kutoka katika namba ambayo hakika haikuwa ya mtandao wa Afrika mashariki. Bila kuuliza nikajibu ujumbeule lakini haukuweza kwenda, simu yangu haikuwa na salio la kutosha.Ni kama vile upande wa pili ulitambua hilo. Simu ikaanza kuita nikapokea. Alikuwa Dokta Davis, nilimtajia namba za akaunti yangu kwa ufasaha. Ilikuwa mara ya kwanza kusikia sauti yake.Sio siri dakika kumi zilikuwa nyingi ukaingia ujumbe kuwa pesa tayari imewekwa. Sikukumbuka kufunga mlango nilikaza mwendo hadi ‘ATM’ nikaiweka kadi yangu huku nikiwa siamini kama ni kweli ama la.“Salio lako ni 666,666” macho yalisoma tarakimu hizo, nilitumia mkono wangu kuzihesabu moja baada ya nyingine huku nikijiuliza kuwa hiyo ni elfu sitini ama laki sita? Jibu lilikuwa laki sita. Kijasho!!Niliondoka ATM na shilingi laki mbili. Kinyago gani angenibabaisha pale chuoni? Mimi ndio mimi.Usiku mzima nilikuwa naitafakari pesa na kazi niliyoahidiwa na Dokta Davis. Nilianza kujiuliza ni nani ambaye anafaa kuwa nami katika msafara wa kwenda kumpokea mtu huyu muhimu, Dokta Davis. Niliwachambua marafiki zangu mmoja baada ya mwingine, hatimaye nikamchagua Mariana. Huyu alikuwa ni rafiki yangu hasa, lakini tatizo kiingereza kilikuwa kinampiga chenga..nikamsikitikia sana kwa kuikosa nafasi hii hadimu. Mwishowe nikamchagua Happy ambaye hatukuwa karibu kivile lakini alikuwa ana vigezo. Vigezo alivyotaka DavisCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/MCHEZO RASMI UKAANZANdege ilitua muda ambao dokta Davis alikuwa amenieleza kabla, alitupigia simu baada ya kuwa ameshuka na tukafuata maelekezo ya jinsi ya kuonana naye.Happy alikuwa mkimya sana kwani hakuwa akijua mengi hivyo aliniachia mimi majukumu yote.Hatimaye tukaonana na Dokta Davis. Kwa jinsi alivyokuwa muonekano wake na sisi basi ilimpasa yeye aje kutupokea sisi na wala si sisi kwenda kumpokea yeye. Lakini ndio hivyo ni sisi tulienda kumpokea yeye.Lafudhi yake ilikuwa na mchanganyiko wa kiingereza cha Afrika magharibi na Marekani. Alikuwa na mwili mdogo tu usiokuwa na chochote cha kuvutia sana. Hakuonekana kuwa mtu mwenye pesa.“Happy, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi.” Nilimtambulisha Happy kwa Davis bila kumwambia kama tulikutana facebook. Nikamtambulisha na Happy huku tukienda kwenye taksi iliyotuleta.“Nipeleke hoteli nzuri kabisa.” Alizungumza Dokta. Nami bila kusita nikamuelekeza dereva kwa kiswahili hoteli nzuri ya kifahari. Moyoni nilikuwa na wasiwasi bado kama Dokta Davis atazimudu gharama za hoteli hiyo. Muonekano wake bado ulikuwa kikwazo kwangu. Hakufanania kabisa kumiliki pesa nyingi!!Alipolipa kwa mfumo wa dola bili za hoteli alinikata wasiwasi wangu!!!Hapo kabla nilikuwa sijawahi kuingia hoteli yenye hadhi kama ile. Nilikuwa nashangaa shangaa tu pale ndani, sikujua ni wapi mlango unafunguliwa, sikuona mahali pa kuwashia taa baada ya kuingia ndani, na ilinishtua kengele iliyopiga kelele baada ya kuwa mlango haujafungwa vizuri. Hata Happy naye nilimwona akishangaa shangaa, lakini Davis alionekana mzoefu sana wa sehemu kama hizi. Heshima ikaanza kujengeka.Tulizungumza mengi sana na Davis, alitawala maongezi kutokana na maswali aliyokuwa anatuuliza. Tulimweleza maisha magumu tunayopitia pale chuoni. Alisikitika sana na kuulaani umasikini.****Siku hiyo alitupatia shilingi laki moja kwa ajili ya nauli za kurudi chuoni kila mmoja ya kwake. Happy alipagawa nayo kila mara alirudia kusema asante huku Davis akimwambia asijali ni hali ya kawaida.Nilipofika hostel niliyokuwa ninanishi nilitamani kila mtuanitambue Isabella nilikuwa nina shilingi ngapi mfukoni. Nilifika ndani na kujibweteka huku nikijisikia mwanamke mwenye bahati kupita wote. Nani wa kunisumbua!!Nilimkumbuka John Paul, huyu alikuwa ni mpenzi wangu ambaye licha ya kuachana bado nilikuwa nampenda. John aliniacha kisa sikuwa na pesa, aliniacha kwa sababu umasikini ulikuwa damuni mwangu, huenda John alidhani naweza kumwambukiza umasikini, John akaniacha na kuunda uhusiano na msichana wa kitajiri, aliyekuwa anamiliki gari yake mwenyewe na kila mara alibadili nguo za bei ghari. Aliitwa Jesca.Niliumizwa sana na hali ile ya kuachwa na John, nilijipa moyo kuwa siku moja nami nitapata bahati ya kupendwa tena. Lakini bahati mbaya kila aliyekuja alionekana kuwa ni mdanganyifu.Yale matendo ya kejeli aliyonifanyia John, niliamini sio kwa kupenda kwake bali msukumo kutoka kwa Jesca yule binti wa kitajiri.Hasira ikanipanda maradufu sasa nikauona ule wakati wa kulipiza kisasi ulikuwa umefika.Wakati wa kumwonyesha John kuwa sasa nina pesa!!! Nikawaza kumiliki gari, nikawaza kuwa mwanadada asiyepitwa na vazi lolote jipya. Na kubwa zaidi nikamuwaza Dokta…..dokta Davis.Nikamjengea picha kaka huyu iwapo atakuwa mpenzi wangu, kwanza nitakuwa na amri juu ya pesa zake, na pili nitakuwa Mrs. Davis. Lolote analofanya lazima nishirikishwe.Mh!! Itawauma kweli Isabella nina mchumba kutoka Marekani. Nilijisemea huku nikitabasamu.Zile picha za dokta Davis ambazo mwanzoni niliziona kuwa hazina mvuto sasa nikaziona kuwa hazina mfano dokta akawa dokta kweli. Uchafu gani mwingine wa kunisumbua humo facebook?? Nilijiuliza. Kisha nikagundua nilianza kujengeka kiburi kichwani!!!Usingizi ulinipitia nikaja kushtuka saa kumi na mbili asubuhi.Ni kama niliamka wakati sahihi. Dokta akapiga simu.“Mchukue gari ya kukodi, mwambie dereva tutamtumia sikunzima.” Alitoa maelekezo hayo Davis. Nikafuata maelekezo.Baada ya saa zima nilikuwa katika gari la kukodi.Kabla ya kwenda kwa dokta nikaamua kwanza kulipa kisasi, nikamuamuru dereva twende chuo. Bahati ilikuwa upande wangu, ile nashuka kwenye gari kwa mbwembwe zote. Karibia wanafunzi kumi niliosoma nao darasa moja waliniona.Macho yao yalionyesha kutoamini nami sikuwajali.Nikajizungusha zungusha hapo kisha nikamwamrisha dereva, tukaenda kumchukua Happy. Huku nyuma najua niliacha gumzo!!!Tulipofika nyumbani kwa Happy, Happy hakuwepo!!! Nikajaribu kupiga simu yake, haikupokelewa. Niliwauliza majirani wakadai kuwa alitoka lakini hawajui kama alirudi ama la.Anachezea bahati huyu!! Nilijisemea.Nikapanda ndani ya gari. Safari ya kwenda kwa dokta ikafuata.Maajabu nilimkuta Happy akiwa amefika tayari!! Alikuwa na dokta wakinisubiri.Mchomo wa wivu ukanishambulia na kunijeruhi moyoni, nikaanza kuhisi zile ndoto zangu zimeanza kufifishwa. Happy alinisalimia akiwa na tabasamu mwanana. Dokta akiungana naye kutabasamu. Nami nikajilazimisha nikatabasamu!!!“Kesho nitarejea nyumbani mara moja….kuna dharula imejitokeza. Lakini kitu kimoja nahitaji mfanikiwe kupitia mimi.” Alianza kutueleza dokta, tukiwa ndani ya gari la kukodi. Kisha akaendelea, “Nitarejea hivi punde tu!! Na nikiwa huko nitakuwa nawasaidia, msisite kunieleza lolote nami nitawasaidia, hata mimi kufika hapa nilikuwa nasaidiwa kwa hiyo ni zamu yangu kusaidia.” Aliongea kwa ukarimu mkubwa.Kwa mahesabu ya harakaharaka zile dola thamani yake ilikuwa milioni sita za kitanzania. Hizo ndizo Dokta alituachia tugawane.Kwangu mimi ilikuwa kama ndoto ya mchana!!!Siku iliyofuata dokta huyu wa ajabu akarejea huko anapojuayeye!! Hakutaka kusindikizwa uwanja wa ndege.Ile hali ya kumshuhudia Happy akiwa na Dokta Davis ilinitia mashaka sana na kuhisi kwamba muda wowote ule nitanyang’anywa tonge mdomoni. Hivyo nikalazimika kuchukua tahadhari na kuanza kumpeleleza Happy kujua iwapo ana mawasiliano ya ukaribu na Davis ama ni wasiwasi wangu tu.Niliamini kabisa Davis alikuwa ni mali yangu na si ya mtu mwingine hivyo, Happy kama alitaka kunizunguka basi alikuwa hanitendei haki hata kidogo.Ilikuwa siku tulivu ya jumamosi nikiwa chumbani kwangu. Chumba ambacho kwa sasa kilikuwa na mabadiliko kidogo tofauti na awali. Simu yangu iliita alikuwa ni dokta Davis. Nikapokea.Dokta alizungumza mengi huku kubwa zaidi akinigusia kuhusu biashara tuliyozungumza. Ni hapo ndipo nikaikumbuka biashara ya mtandao. Siku tulivyochat naye katika mtandao wa facebook huenda sikumuelewa vyema. Sasa alikuwa ananielewesha vyema ni jinsi gani mimi nitahusika katika biashara hiyo inayolipa mamilioni mengi kwa muda mfupi.“Sasa hapo biashara hiyo inafanyikaje? Huo mtandao uko vipi?.” Nilimuuliza kwa utafiti. Kwani hakuwahi kunielekeza moja kwa moja juu ya biashara hiyo ya mtandao.“Umeuliza swali hili wakati muafaka sana. Nilitaka kukueleza kuwaumependekezwa kuwa mwakilishi wetu katika nchi yako. Hongera sana.” Aliniambia na kabla sijauliza chochote aliendelea, “Ni lini utapata walau siku nne za kuwa free uweze kunitembelea huku niweze kukupa maelekezo zaidi?”“Wewe upo wapi??” Nilimuuliza.“Lusaka Zambia, lakini tutakutana Ndola.”“Ndola ndio wapi?.” Nilijawa na maswali mfululizo.“Mkoa mmoja hapahapa Zambia.”“Kwa sasa nipo free sana. Hatujaanza kuwa bize.” Nilimjibu huku nikiwa nafurahia mazungumzo hayo.“Waweza kukimbia mara moja kuja huku ofisini kwetu kwa ajili ya kusaini mikataba?.” Aliniambia, nikacheka kimya kimya yaani yeye Zambia alipaona karibu sana eti ananiambia nikimbie mara moja.“Naweza ila…”“Usijali mambo ya nauli na kila kitu kampuni itakulipia. Kesho zitaingizwa kwenye akaunti yako.”Ni hilo haswaa nilitaka kumuulizia na sasa alikuwa amenipa jibu tayari.Baada ya kukata simu ile nilitamani sasa kila mtu aitambue furaha yangu, nipo chuo mwaka wa pili napata kazi nje ya nchi, mshahara zaidi ya milioni mbili. Nani kama Isabella.mara nikamsahau Happy aliyekuwa anakisumbua kiichwa changu.Nikafumba macho, nikatamani sana kumshrikisha mwalimu Nchimbi ambaye ni mama yangu mzazi lakini nikaona ni mapema sana, nikataka kumwambia Happy lakini nikahisi huyo alikuwea mpinzani wangu katika kumuwania Davis. Nikakaa kimya sikumwambia mtu yeyote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Siku moja kabla ya kuondoka nilizungumza na kiongozi wa darasa letu Class Represenative ‘CR’ kuhusu kazi zitakazokuwa zinatolewa darasani awe ananiandika kuwa nipo japo sitakuwepo, mwanzoni alinikatalia lakini nilipotoa noti moja baada ya nyingine hadi zikafika noti kumi nyekundu alilainika na kugeuka kibaraka. Tena akawa mzungumzaji mkuu!! Pesa bwana!!(Safari ya Zambia)Kesho yake asubuhi nilikuwa katika basi la kampuni ya Abood kuelekea Mbeya kisha Tunduma halafu safari ya kwenda Ndola. Kusaini mkataba!! Mkataba nisioufahamu!!Nilijihisi kama malikia na lilikuwa kosa kubwa sana kujaribu kunifananisha na mwanafunzi yeyote wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino ambacho nilikuwa nasoma. Hata wale wa huko Dar pia hawakutakiwa kufananishwa na mimi Hakuna ambaye angeweza kukaa ngazi moja na mimikwa sababu wengi wao waliishi kwa kutegemea mkopo sasa mimi nilikuwa nina pesa yangu na kubwa zaidi nilikuwa naingia kazini. Hao watoa mikopo ningepata fursa ya kukutana nao nadhani ningekuwa na jeuri ya kuwashushiamvua ya matusi.Nikiwa safarini kuelekea Mbeya nikitokea mjini Dodoma baada ya safari ndefu kutoka Mwanza siku iliyopita, tulipofika Makambako nilianza kuifikiria familia yangu niliwaza kumjengea mama yangu nyumba ya kifahari kisha nimtoe baba yangu katika ulevi sugu kwa kumuwekea pombe za kisasa ndani. Hizo niliamini zitamnenepesha badala ya kumkondesha. Wadogo zangu waliokuwa wakisoma shule za kata nao nadhani walitakiwa kusoma shule zenye hadhi ya mshahara nitakaokuwa napokea dada yao. Tena wote nawapeleka shule za bweni!!! Nilijiapiza huku pua zangu zikinusa kwa mbali harufu nzuri ya sabuni ambayo nilitumia asubuhi kuoga katika hoteli ya kifahari mjini Dodoma.Nilitoa tabasamu hafifu kisha nikaendelea kuuchapa usingizi.Nilifika Mbeya salama. Dereva teksi wa kwanza niliyekutana ndiye alipata bahati ya kuniendesha msichana ambaye nilikuwa na malengo makubwa kama mimi. Alitakiwa kujisifu kama angekuwa kichwani mwangu.Alinifikisha hadi hoteli maridadi yenye hadhi ya kulaliwa na watoto wa vigogo na vigogo wenyewe. Nililipia na kulala hapo kesho yake mapema nikawa Tunduma halafu mwisho ikafuata safari ya Ndola. Hata ule uchovu haukusumbua mwili wangu.Ndani ya basi tulilokuwa tumepanda walikuwepo watu mchanganyiko. Hakuna aliyekuwa na hadhi kama mimi. Yaani nilikuwa najisikia kuwa na uwezo hata wa kuamuru basi hilo lisimame na likasimama lakini sikufanya hivyo.Majira ya saa kumi na moja jioni kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilikanyaga ardhi ya nchi tofauti na Tanzania. Isabella ndani ya NdollaMwanzo wa safari ya kwenda Marekani!!! Nilijiwazia hivyo.Nilitegemea kuhangaika sana baada ya kuwa nimeshuka pale kituoni. Lakini la!! Haikuwa hivyo. Nilipotelemka tu. Nilitumia dakika moja tu kushangaa wanawake wawili waliokuwa wamependezea katika mavazi yao ya suti walinipokea begi langu dogo huku wakinisalimia kwa nidhamu kubwa sana.Niliwajibu kwa tabasamu, sasa nilianza kuamini kuwa Dokta Davis atakuwa ni mtu mkubwa sana. tofauti na mwonekano wake.Niliongozwa hadi katika gari aina ya Noah, nilitaka kuingia humo lakini nikaambiwa hilo ni kwa ajili ya mizigo. Nikacheka moyoni huku nikiwaza kuwa laiti kama ningepewa hilo gari. Chuo wangekoma!!Mh!! Mzigo gani sasa?? Nilijiuliza. Hakuwepo wa kunijibu.Baada ya hapo nikapelekwa katika gari iliyokuwa na milango sita.Hapo nikafunguliwa milango nikaingia ndani. Niliokutana nao mle ndani wote walikuwa na nyuso zilizong’aa tofauti na ule wa dokta Davis. Japo walikuwa weusi na sura zao zikitangaza roho flani hivi isiyokuwa na ukarimu sanalakini walitabasamu.Naishi kama mfalme nchi za watu?? Mwalimu Nchimbi natamani ungeyaona haya goodbye umasikini!!!! Nilijitamba kichwani mwangu huku nikikaa vyema na kuzijibu salamu za watu pale ndani.Safari ikaanza. Sikuwa naujua mji hata mmoja lakini safari nayo haikuwa fupi.Nilitamani sana niulize kuwa pale ni wapi lakini ningeanza kumuuliza nani?? Hilo likawa swali. Laiti kama dokta angekuwepo hapo sawa.Nikiwa bado nashanga shangaa hapa na pale mara mwendo ulipungua kisha honi ikapigwa. Geti likafunguliwa na watu waliovaa nguo nyeupe sana. Gari zikaanza kuingia, yetu ikiwa ya pili kuingia.Tulipotaka kushuka milango ilifunguliwa na akina kaka wenye kila sababu za kuitwa watanashati na wanamazoezi. Nikazidi kuvimba kichwa kwa mema haya niliyokuwa natendewa.Nikiwa bado sijafungua kinywa kuzungumza tangu nijibu salamu garini, walinifuata akina dada watatu wakanielekeza kwa ishara za mikono niwafuate. Sikuwa na kipingamizi niliwafuata. tuliingia katika chumba kilichokuwa na mvuto hata kwa yule asiyejua ubora wa chumba. Lakini mimi nilikuwa naujua ubora niliambua.“You have to re-dress madame” (Unatakiwa ubadili mavazi yako).Waliniambia kwa pamoja. Sauti zao tamu zilinikonga moyoni.Wakanipa maelekezo na baada ya dakika kadhaa nilitoka mle ndani nami nikiwa nang’ara katika mavazi meupe sana.Nilikuwa nimependeza sikuhitaji kumuuliza mtu.Sasa tukarejea katika magari tena. Mi nilijua tumefika mwisho kumbe lile lilikuwa geti la kwanza tu.Mwendo wa dakika tano tukashuka tena. Tukaingia geti jingine kubwa. Hapo tukatelemka na kuanza kutembea juu ya kapeti jekundu.Red kapeti!!! Niliwaza. Nikafanya tabasamu.Nikiwa juu ya lile kapeti nikajihisi kuwa na hadhi ya Rihanna, Beyonce ama Lady Gaga. Kisa tu nipo juu ya zulia jekundu.Hapa kama ni kazi nimepata!! Nilijiaminisha.Nilikuwa makini katika kulikanyaga lile zulia jekundu, sikutaka kuonekana mshamba katika hilo. Nilijilazimisha kutembea mwendo wa kilimbwende wakati niliamini kuwa iwapo nitathubutu kuingia katika mashindano ya ulimbwende basi nitashika nafasi ya mwisho ama sitapata walau kigezo cha kusimama jukwaani kama mlimbwende. Maana nilikuwa cha ufupi na nilikuwa na dalili ya kuwa kibonge.Niliongozwa hadi katika chumba kikubwa sana, kila kitu pale ndani kilikuwa cheupe kasoro ngozi yangu ambayo ilifanya kama uchafu pale ndani. Sikujali!!!“Utalala hapa ndani…na hawa watakuhudumia.” Nilipewa wakinamama wawili kwa ajili ya kunihudumia. Umri wao sidhani kama unatofauti sana na wa mwalimu Nchimbi yule mama yangu mzazi. Lakini matabasamu yao ni kama walikuwa na miaka kumi na nane.Ungekuwa wewe ungejisikiaje. Mwenzako nilijisikia kama malkia.Nilipata huduma zote za msingi hadi nilipopitiwa na usingizi na kuamka siku iliyofuata. Baada ya kuwa nimeoga na kupewa nguo nyingine nyeupe tena nilikaribishwa kifungua kinywa.Ilikuwa kufuru nyingine tena niliyoweza kuishuhudia. Meza ilikuwa imesheheni kila aia ya makorokoro. Kazi kwako mlaji kujihudumia. Kiaibuaibu nikajinyima kula nilivyovitamani nikala nilivyovizoea. Na ushamba pia ulichangia. Kuna vyakula sikuelewa kama vinaliwa kwa kijiko ama uma, harufu yake nzuri ikabaki kunisurubu. Nikaogopa kujaribu!!!Majira ya saa tano asubuhi niliongozwa tena kuelekea katika ile gari ya milango sita. Nikaingia humo kwa namna ileile kama malkia. Safari yetu ikaishia katika sehemu nyingine ya kifahari. Sikuwa naielewa nchi ya Zambia hivyo sikujua lolote.“Mukuba Hotels.” Hilo ndilo neno nililoweza kulisoma baada ya kuunyanyua uso wangu juu. Sikujua maana ya Mukuba. Lakini bila shaka zilikuwa lugha za huko kwao. Hii hoteli ama jumba la kifalme!! Nilijiuliza.Tuliingia hadi ndani huku mimi nikiwa mfuata mkia nisiyejua lolote linaloendelea mbele. Baada ya kukatiza kona kadha wa kadha sasa tukakutana na mlango ulioandika kwa maandishi yenye rangi ya dhahabu!! Dr. Davis. Moyo wangu ukapiga kwa nguvu. Paa!!Ina maana Davis anaishi hapa? Nilitamani kuuliza ila nikasita.Nikiwa nasubiri ajitokeze mtu kwa ajili ya kubisha hodi ili tuweze kuingia ndani maana sikuona mahali pameandikwa ‘PULL/PUSH’ mara mlango ule wa vioo ulianza kufunguka wenyewe.tukaingia ndani.Sasa tulikuwa watu watatu pekee!! Wale wawili baada ya kuingia ndani pamoja nami wakatoka nje. Bila kusema neno!!Sasa nikabaki peke yangu.Kiti cha kuzunguka kilichokuwa kimegeuziwa ukutani kikazungushwa taratibu. Vazi la suti likanisabahi, kisha uso ukanyanyuka.“You are most welcome!!” Alinikaribisha. Kisha akatabasamu. Alikuwa anafanana na Davis lakini sikutaka kuamini. Labda ndugu yake au au au…“Ndo mimi mbona unashangaa.” Aliniwahi. Ni kama alijua nilichokuwa nawaza. Alikuwa ni Davis. Sauti yake ilikuwa ileile.Nikachukua nafasi. Bila kusema lolote alibonyeza kitufe mara kikashuka mfano wa kitrei cha kuwekea vyombo.“Unatumia kinywaji gani.” Aliniuliza mimi nikiwa bado nashangaa.“Aaaah!! Chochote.” Nilijiumauma.Akabonyeza vitufe kadhaa, kikaondoka na kurejea tena baada ya dakika tano.Maajabu ya nane ya dunia. Kile kitrei kilikuwa na glasi mbili za juisi. Akatwaa moja akanipatia. Sijawahi kuona tangu nizaliwe!!“Asante.” Nilimshukuru. Hakujibu.Dokta Davis aliyekuja Tanzania hakufanana hata kidogo na huyu. Huyu alinuka pesa tena pesa nyingi.“Karibu Ndolla Zambia, hii ni ofisi yangu ndogo ya huku, nyingine ipo Lusaka, Accra na kubwa zaidi ipo Washington.” Alinielezea kwa sauti iliyojaa ujivuni. Lakini alikuwa amechangamka!!Nilikuwa makini kumsikiliza.“Isabela…. .”“Abee!!.” Niliitika.“Kampuni yangu imeamua kufanya kazi na wewe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Nashukuru sana Dokta.” Nilishukuru, hakujali hilo akaendelea“Unauchukia umasikini?.”“Nauchukia kuliko niavyoweza kujielezea.” Nilisisitiza.“Na….anyway..unaenda sana kanisani.”“Aaah!! Kiukweli ni mara chache chache.”“Kwa nini?.”“Aaah!! Mambo huwa yanakuwa mengi sana.”“Ok!! Achana na hayo…Isabella kazi uliyopata hapa ni kazi nyepesi na kila mwezi itakuingizia shilingi milioni sita laki sita na elfu sitini na sita kila mwezi.” Alizungumza Dokta bila wasiwasi, alimanusura nipoteze fahamu. Mwili ukawa wa baridi. Nikajaribu kujishtua huenda ninaota, haikuwa hivyo. Hali ile ilikuwa halisi.Nilikuwa Zambia na nilitangaziwa dau hilo kubwa.“Unawazungumziaje wanaume kwa ujumla?.” Davis hakujali ule mshtuko wangu akanitupia swali jingine, bila shaka milioni sita kwake si lolote si chochote.“Aaah!! Kiaje labda” Nilimuuliza huku nikifinya finya mikono yangu.“Vyovyote vile lakini hasahasa katika kazi ya mapenzi.”“Viumbe waongo, wasiokuwa na huruma, wanyanyasaji na…”Nilishindwa kuongea nilikuwa nimemkumbuka John, mwanaume aliyeamua kuachana nami kisa sina pesa. Sasa hapa nazungumzia juu ya kupata pesa.“Labda ukiambiwa uwape adhabu utatoa adhabu gani kwao.”“Dah!! Sijui watoweke duniani…aaah!! Sijui ila nawachukia wanaume wenye tabia hii.” Nilimjibu huku nikilegeza koo kwa kugida funda mbili za juisi ile. Ilikuwa tamu sana. sijui tunda gani lile!!!“Safi sana…kumbe kazi utaiweza kabisa lakini lazima kwanza ubadili kwanza mawazo yako hayo ya kuombea wanaume watoweke. Lengo la kampuni yangu mimi ni kuwabadili wanaume kuacha na mfumo huo wa unyanyasaji na pia kuwafunza wanawake kuepukana na vishawishi vya wanaume wadanganyifu. Tunaamini kuwa utaweza kutuwakilisha vyema katika nchi yako. Ukimuelimisha msichana mmoja kwa siku basi ujue umeielimisha jamii kubwa sana.” Aliongea kwa umakini mkubwa huku akiwa amenikazia macho. Nilikwepesha kutazamana naye.“Nitaweza hata usitie shaka.” Niliikubali kazi. Zikaangushwa karatasi nne mezani nikasaini mkataba mnono.“Baadaye kidogo pesa ya utangulizi itaingizwa katika akaunti yako.” Alimaliza Dokta.Tunaweza kuzunguka zunguka kidogo uitazame ofisi yangu. Lilikua ombi la Dokta nikakubaliana nalo.Tulizunguka kona tofauti tofauti. Nilikuwa nikimtazama Davis kwa kuibia ibia na yeye pia alifanya hivyo. Yale mawazo ya kumfanya awe mpenzi wangu yakawa yananisumbua akili nilitamani kumwambia lakini mdomo ukawa mzito.Laiti kama nikiwa naye!! Hata hii ofisi pia itakuwa mali yangu!! Niliwaza.*****MWANZAUlikuwa usiku wa kipekee sana kwangu, ndio kwanza nilikuwa nimerejea jijini Mwanza, kwa usafiri bora wa ndege. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Sijui niseme mara ya pili!! Maana mama alinihadithia kuwa nilipokuwa mtoto niliwahi kupanda ndege!!!Baada ya kushuka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere bila kuwa na wa kunipokea sasa hapa uwanja wa ndege wa Mwanza nilihitaji mtu fulani ajue kuwa nimekuja na ndege!! Huyo mtu ni nani kama sio John!!!Nilimwomba John afike kunipokea. Nilifanya hayo makusudi ili kumkomoa kwa ubaya alionifanyia. Ubaya wa kuniacha na kuwa na mahusiano na msichana mwingine.Ni kweli John alikuwa amenitenda vile lakini John bado alikuwa moyoni mwangu. Nilikuwa nampenda sana John. Walikuwepo wanaume wengi lakini nafasi ya John bado nilikuwa sijaona wa kumrithisha.John aliposikia nakuja na ndege hakusita kunikubalia. Labda ili athibitishe kwamba kweli nimekuja na ndege ama la. John alinipokea huku akinipapatikia, niliifurahia hali hiyo. Tulichukua taksi iliyotufikisha katika hoteli yenye hadhi ya juu ya La kairo jijini Mwanza tukajipatia chumba. Chumba cha bei ya juu kabisa!! Sikuwa na wasiwasi kuhusu pesa!!Wakati huo John tayari alikuwa amemdanganya mpenzi wake wa wakati huo Jesca kuwa hatarejea chuoni siku hiyo kwa kuwa kuna rafiki yake anaumwa. Ameenda kumsalimia.Usiku majira ya saa nne, tayari tulikuwa tumelia sana baada ya kukumbushiana yaliyopita. John akaniomba msamaha nami sikusita kumsamehe. Kilichofuata hapo ni kurejesha hisia za zamani na kuanza kushambuliana, kila mmoja akijitahidi kuamsha hisia za mwenzake, baadaye kidogo. Vita!!!Vita ya miili. Kila mmoja akitamani kuibuka mshindi, hapakuwa na mwamuzi. Wakati vita hiyo ikiendelea ikaanza kusikia kama sauti ikiniongelesha kwa kabila kama kihehe vile, lakini sikuweza kuielewa lakini niliwahi kuisikia mahali. Ni kweli niliwahi kuisikia mahali, lakini sasa sikuwa nakumbuka ni wapi. John alikuwa bize, huenda alikuwa akifurahia peke yake. Nilitamani kumwambia John azisikilize zile sauti lakini hakuweza kunisikia alikuwa ulimwengu mwingine.John alipokoma, na sauti zile nazo zikatoweka. Ni kama vile zilikuwa kando ya dirisha zikitusemesha ama zikinisemesha.“John walikuwa wanasemaje?.”“Nani?. Hao wahudumu ama.?” Aliuliza kwa utafiti.“Hapana!!!anyway acha ilivyo.” Nilimaliza mjadala.John hakuuliza zaidi.Nilielekea bafuni kujisafisha, kisha nikarejea tena pale kitandani. John alikuwa amesinzia. Sikuwa na hamu naye tena bali nilizitafakari zile sauti zilikuwa zikisema nini.Lakini kama John , hajazisikia basi hakuna sauti yoyote!!! Nilijipa moyo.Asubuhi John alikuwa wa kwanza kuamka. Aliingia aliwatoni akajisafisha na kuniamsha. Nami nikafanya kama alivyofanya kisha tukaondoka. John akaelekea alipopajua nami nikaelekea chuoni.Zile sauti nilizozisikia usiku ule sikuzikumbuka tena. Nilichokumbuka ni kwamba mimi na John tulikumbushia enzi.******Sikuweza kujua ilikuwa ni saa ngapi, lakini niliamini ilikuwa ni usiku tena usiku sana. Kuna sauti zilikuwa zimezungumza nami, tena kwa lugha ninayoielewa, zilikuwa sauti zenye furaha sana.Nikiwa bado natafakari sauti hizo zilizungumza nini na mimi. Mara simu yangu iliita. Alikuwa ni rafiki yangu wa darasani. Nikajiuliza kulikoni. Nikaipokea simu.“Isabella, Isabella….Jenipher jamani. Jenipher!!”“Amekuwaje tena. Eh!! Nambie.”“Jenipher yupo hoi hospitali hapa.” Alijitahidi kuongea bila taharuki lakini alisikika akitetemeka. Baada ya pale hata kabla sijamjibu, simu yake ilikatika.Nilipojaribu kumpigia hakupatikana. Nikajilazimisha kulala, huku nikiamini kuwa lile ni tatizo la kawaida tuAsubuhi palipopambazuka, taarifa ilikuwa nyingine, taarifa ya kushtua nafsi!! Jenipher msichana aliyekuwa akiishi na huyo rafiki aliyenipigia usiku uliopita.alikuwa amefariki baada ya jitihada za madaktari kugonga mwamba.Ilikuwa habari ya kusikitisha sana kwani kilikuwa kifo cha ghafla mno.Sikuzikumbuka zile sauti za usiku ule zilikuwa zinasema nini na mimi.Sasa nikawa nawaza juu ya msiba huo!! Msiba wa ghafla!!Mwili wa marehemu uliagwa katika viwanja vya Raila Odinga. Kila aliyehudhuria alijawa na simanzi, hasahasa kutokana na kilio cha mama mzazi wa binti yule ambaye alikuwa haishi kumlilia mwanaye huyo wa pekee aliyefanikiwa walau kufika chuo kikuu.Tofauti na watu kuwa na majonzi niliweza kubaini sura ya mtu mmoja ilikuwa na hofu kuu. Huzuni ikiwa mbali naye.Huyu alikuwa ni John. Sikujua kwa nini alikuwa katika hali ile. Niliyalaumu macho yangu kwa kumtazama vile huenda alikuwa sawa lakini hapana nafsi haikuridhika.Muda wa kuaga ulifika ilianza familia ya marehemu iliyoungana nasi pale chuoni, kisha wakafuata wanafunzi wa kike. Nilinyanyuka na kuungana na msafara mrefu uliokuwa na nia moja ya kumsindikiza marehemu.Jua kali lilikuwa likinisumbua sana na kunifanya nitokwe jasho sana, si mimi pekee niliyelalamika bali na baadhi ya wasichana waliokuwa nyuma yangu nao walilalamika. Lakini mwendokasi wa foleni haukuwa mbaya tuliamini kuwa muda si mrefu kila mmoja atakuwa amemuaga marehemu.Kwa akili zangu timamu nilisikia mivumo kwa mbali sana. Sikuwa nimesinzia ili nijilaumu kwamba ni ndoto. Hapana nilikuwa najitambua kabisa. Mivumo ile ilikuwa mithili ya mkutano wa injili unaofanyika mbali kiasi na wanatumia spika kubwa kuhamasisha watu wengi waweze kusikia. Kisha sauti hizo kutwaliwa na upepo kisha kurudishwa. Sikuweza kusikia maneno yote na hata hayo niliyoyasikia yalikuwa nusunusu. Nilitaka kumuuliza aliyekuwa mbele yangu lakini bahati mbaya hatukuwa tukifahamiana. Lakini wa nyuma yangu nilikuwa namfahamu nikaamua kumuuliza kama kuna kitu anasikia.“Eti dada unasikia nini?.” Nilimuuliza.“Sijui hata kuna nini huko mbele hata dah!! Jua kali kweli.” Alinijibu nje kabisa ya swali nililomuuliza. Nikameza mate kulainisha koo langu, alikuwa amenikera.Ghafla nikagundua kuwa foleni ile ilisimama, sasa nikagundua kwa nini yule binti alinijibu vile. Kumbe hakunielewa kabisa.Kimyakimya nikamsamehe!!!Foleni ile haikuweza kusogea mbele, nilikuwa bado katika kutafakari,kulikoni ghafla ilitawanyika. Haikuwa foleni tena bali purukushani. Kila mmoja akataka kutazama kilichopo mbele. Mwanzoni ilikuwa foleni ya wasichana lakini sasa ulikuwa mchanganyiko wa jinsia zote. Kila mmoja akijitahidi kwa kadri anavyoweza kutazama mbele kuna nini.Nilikuwa mmoja kati ya walioparangana na kufanikiwa kuona mbele. Alikuwa ni Jesca , aidha kwa hiari ama lazima alikuwa amekumbatia ardhi isiyokumbatika. Alikuwa ametulia tuli kumaanisha labda amekipenda kitendo kile. Tulibaki kushangaa kwamba kuna nini kimetokea. Wasichana tukiwa katika mshtuko wanaume walijiongeza wakavua mashati yao na kuanza kumpepea Jesca. John akiwa mstari wa mbele kumtetea huyu mpenzi wake kutoka katika hali aliyokuwanayo.Niliweka kando hasira na chuki dhidi ya binti huyo ambaye kwa maksudi alininyang’anya tonge mdomoni kwa kumchukua mpenzi wangu John kutoka katika himaya yangu.Niliuvaa ubinadamu, huruma ikanishika.Jesca hakutingishika hata kidogo. Sasa alibebwa mzega mzega hadi akawekwa katika kivuli. Zoezi la kumpepea liliendelea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Yule mwanadada mwingine aliyekuwa ametulia tuli katika jeneza na yeye alikuwa amesahauliwa kwa muda. Cha ajabu hata mama yake mzazi naye macho yake yalikuwa yakifuatilia kwa ukaribu tukio la Jesca kuanguka.Sio maajabu haya!!!!Harakati za kumpepea Jesca ziliendelea hadi gari ya huduma ya kwanza ilipofika eneo lile. Jesca alipakizwa na gari ikaondoka kwa kasi huku ikipia ving’ora vya kuashiria hatari ama dharula.Nilifanya ishara ya msalaba na kumkabidhi Jesca kwa Mungu kutokana na tatizo lililomsibu.Zoezi la kuaga liliendelea tena upesi upesi. Wakati huu sikumuona tewa John. Bila shaka aliongozana na mpenzi wake alyekuwa amekumbwa na maswahibu.Ile kufikiria kuwa Jesca ni mpenzi wa John. Wivu ukanipiga kikumbo nikajisikia vibaya. Nikahisi kuwa naonewa. Kisha nikaukumbuka usiku wangu wa mwisho na John. Ulikuwa usiu wa kipekee….na…na……na usiku wa kwanza kusikia sauti zile zisizokuwa na maana. Sauti za maajabu.Sasa zinamaanisha nini? Hilo lilikuwa swali. Nje kabisa ya uwezo wangu kujibu. Lakini nani hasa wa kunijibia????Baada ya taatibu zote za kuuaga mwili kufanyika. Zilifuata taratibu za kifamilia. Kuondoka na mwili wao.Mwili ambao ulikuwa umeagizwa kuja kusoma kwa lengo la kuisaidia familia hapo baadaye mwili huu sasa ulikuwa unarejeshwa nyumbani kwa ajili ya kuzikwa. Inauma sana.Baada ya watu kusambaa niliwasha simu yangu kwa ajili ya kumpigiaJohn na kumjulia hali Jesca. Lakini kabla sijapiga, iliingia simu ya Dokta Davis. Nilishtuka kwanza maana ile kazi niliyoagizwa hata siku moja nilikuwa sijaifanya. Nikaanza kutunga uongo kisha nikapokea simu.“Pole sana na kazi!!! Usijali utazoea. Naona unachoka sana hata kupiga simu inakuwa tabu. Bila shaka ulifika salama na kazi uliianza mara moja." Aliongea bila kuweka kituo Dokta Davis. Nilibaki kujichekeshachekesha, kisha nikakiri kuwa kazi inaenda vizuri sana.“Safi sana …safi sana.” Alinisifia Dokta. Nikajisikia vibaya kwa kuwa nimemdanganya.Tulizungumza mengi huku akinisihi niangalie akaunti yangu maana kuna pesa ilikuwa imeangulizwa.Taarifa hiyo ilikuwa furaha sana kwangu. Kiukweli nilikuwa napenda sana pesa.Nilipotoka pale eneo la viwanja vya Raila Odinga nilijivuta taratibu hadi nikazifikia ATM, nikazama ndani nikadondosha kadi yangu. Nikatazamana na akaunti yangu ikiwa imekenua, kunifurahisha mimi. Milioni tatu, laki sita na elfu sitini na sita zilikuwa zimeongezeka katika akaunti yangu. Nilitabasamu mwenyewe, huku nikichomoa kadi yangu. Sikuwa na haja na pesa kwani kwenye pochi yangu laki moja na nusu ilikuwa inasubiri matumizi yangu.Nilipokuwa natoka katika kituo hicho cha kujichotea pesa. Nilianza kuwaza kuhusu umaarufu. Wanafunzi mia nne wa darasani kwetu pekee kunifahamu hilo niliona kama halitoshi. Nilihitaji walau nusu ya chuo waweze kunifahamu. Sikupata muda wa kufikiria kuwa sifa haziliwi wala hazinenepeshi.Mawazo yangu hayo yasiyokuwa na maana sana yaliingiliana na mlio wa simu.“Isije ikawa taarifa mbaya…” niliwaza.Nikaipokea simu nimsikilize shemeji yangu alikuwa akisema nini. Huyu alikuwa ni rafiki yake na John.“Pole shemeji yangu…” Aliniambia kwa sauti iliyokata tamaa.“Mh!! Asante..bana ndo mipango ya Mungu.” Nilimjibu.“Haya bwana mi ndio naelekea huko kumpa kampani mshikaji.”Kumpa kampani mshkaji?? Mshkaji gani tena hapa. Nilijiuliza. Sikupata jibu simu ikawa imekatwa.Baada ya dakika kadhaa nilikuwa katika taksi nikielekea maeneo ya Kijiweni ambayo ndio nilikuwa naishi. Hapakuwa na foleni kama kawaida hivyo baada ya dakika chache nilifika chumbani kwangu. Njaa ilikuwa imenishika, sikudumu sana pale ndani nilivua viatu vyangu vya kufunika na kuvaa vya wazi kisha nikatoka. Kuelekea kwenye mgahawa kupata chakula.Nikiwa katika mgahawa niligundua kuwa kuna kitu napungukiwakatika himaya yangu. Simu!!!Nilikuwa nimeisahau kwenye pochi yangu.Sikutilia maanani sana kwa kuwa tayari nilikuwa najua ni wapi ipo.Nilijikita katika kusubiri chakula huku nikifanya tathmini ya hapa na pale juu ya kazi ya kipekee hiyo niliyokuwa nimepata kutoka nchi za kigeni. Ilikuwa ni kazi moja ya kipekee sana iliyokuja katika maisha yangu wakati muafaka kabisa.Nikiwa katika kuiwaza hiyo kazi, nikakumbuka ‘umaarufu’ na wenyewe pia nilikuwa nautaka kwa namna yoyote, siwezi kuimba mziki, sijui kuigiza. Sasa nitakuwaje maarufu!!!Pesa, pesa ndio kila kitu. Pesa zitanipa umaarufu. Nikiwa kimya hivihivi kila mtu atajilinganisha na mimi wakati mimi nipo matawi mengine kabisa. Niliwaza hayo!!!Au nigombee uraisi wa chuo?? Nilijiuliza. Nikakatishwa na chakula kilicholetwa mbele yangu. Hivyo sikupata nafasi ya kutafakari majibu.Baada ya saa zima nilirejea chumbani. Moja kwa moja katika mkoba wangu. Simu ilikuwepo. Nikaitwaa nikajilaza kitandani.Nikatazama kama kuna mtu alinipigia.Yeah!! John alikuwa amepiga na wengine watatu, mama pia akiwemo. Nikawapanga katika orodha nianze na yupi. Niliamini nikianza na mama hatutamaliza maongezi maana tulikuwa na mengi ya kuzungumza.Nikaamua kuanza na John. Nilipopiga simu ikawa inatumika, nikaamua kumpigia mama.Tulizungumza mengi huku akiniahidi kuwa siku inayofuata atanitumia shilingi elfu ishirini za kitanzania kwa ajili ya matumizi pale chuoni.Kidogo nicheke kwa sauti kubwa lakini nikajibana kucheka.Pesa ninayotumia kwa nauli ya siku moja, leo hii mama anataka anitumie kwa ajili ya matumizi. Kichekesho!!!Wakati naendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale mama. Simu ya John nayo ilianza kuingia. Nikamdanganya mama kuwa salio limeisha nikakata simu nikamtwangia John huku nikiwa bado nakitafakari kielfu ishirini cha mama.John hakuwa anaongea, lakini nilisikia kwa mbali vilio vya kwikwi. Kuna nini? Nilijiuliza.“Halo, halow…John.” Niliita sikujibiwa.Niliendelea kumsikiliza, alikuwa kimya, nikakata nikampigia rafiki yake. Yeye alipokea upesi tu!!“Vipi upo na John?”“Nimeachana naye muda si mrefu, amechanganyikiwa kabisa.”“Amechanganyikiwa? Kwa nini?.” Nilimuuliza kwa wasiwasi.“Dah!! Yaani amezinguana na madaktari huko hospitali hatakikuamini kabisa.”Simu hii ilizidi kunichanganya. Nikajikadiria majibu yangu, ina maana John ana Ukimwi ama? Mungu wangu nimekwisha!!! Nilihamaki.Suala la kusikia John, kuzinguana na madaktari, amechanganyikiwa. Utata!!!Sasa na mimi nikaanza kuhaha, kana kwamba niliyoyawaza ni sahihi.Upesi nikanunua muda wa maongezi nikampigia tena rafiki yake John. Nikamsihi anieleze nini kimetokea.Bila kusita akaanza kunieleza. Mwishowe nikapata jibu kamili. John hakuwa ameathirika na UKIMWI bali mshtuko. Jesca aliyeanguka wakati wa kuaga mwili wa marehemu viwanja vya Raila Odinga na yeye amefariki.Cha ajabu na kushtua hakuna ugonjwa wowote uliohusika katika kifo hicho. Nilifadhaika nikakaa chini, sikukumbuka hata kuaga tayari nilikuwa nimekata simu.Mbona hivi vifo vinakuja mfululizo kiasi hiki?? Nilijiuliza na hakuwepo timamu yeyote wa kunijibu.Jesca naye kama ilivyokuwa kwa aliyetangulia aliagwa na wanafunzi uwanja uleule wa Raila Odinga. Halikuwa jambo la kushangaza bali lilimezwa na huzuni. Haikuwa mara ya kwanza vifo kutokea katika maisha ya chuo, lakini hiki kifo cha Jesca kilikuwa cha ghafla mno. Iliuma sana!!!****Wiki mbili zilikatika tangu Jesca aache simanzi kubwa katika chuo cha Mtakatifu Agustino. Nilikuwa karibu sana na John nikimfariji kwa kumpoteza mpenzi wake. John kwa kiasi kikubwa sana alifurahia ukaribu wangu kwake. Kiasi kikubwa upweke ukawa unatoweka.USIKU WA MANANEKila kona ya jijini Mwanza ilikuwa imetulia, upepo ulikuwa unavuma kiasi cha kuyumbisha miti midogomidogo iliyoota pembezoni mwa barabara. Magari machache yalikuwa yakiipa usumbufu barabara ya lami ambayo ilikuwa katika mapumziko baada ya suluba ya mchana.Gari dogo aina ya Corolla ilipata hitirafu ambayo ilionekana kuwasumbua vichwa abiria waliokuwa ndani yake. Kila mmoja alionekana kumsukumia mwenzake mzigo wa kutafuta suluhu ya ya gari hilo. Wale abiriawatatu wote walikuwa wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Augustino.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baada ya muda wa kujadiliana hatimaye mwanafunzi mmoja aliyetambulika kwa jina la Joseph alivua shati lake akaweka pembeni akaingia katika ufundi. Wenzake wawili walitulia wakimtazama.Baada ya dakika kadhaa mwanafunzi mmoja alibanwa haja ndogo. Taratibu akajivuta kichakani. Sijui kwanini aliamua kukitafuta kichaka cha mbali wakati usiku ulikuwa mnene na hapakuwa na watu wakipita hovyo. Alikifikia kichaka taratibu akaanza kuifungua zipu yake tayari kwa kukidhi haja yake ya wakati huo.Ghafla aliiachia suruali yake na kutazama mbele katika namna ya kukodoa huku akiwa na hofu kuu. Alikuwa akitetemeka huku akifanya namna ya kushtua kama anatisha kitu kibaya kinachomkabili. Nilitamani sana kujua ni nini hicho mbele yake lakini nikaendelea kuwa mtazamaji wa filamu hiyo ya ajabu.Kisha kama aliyesukumwa akaanguka chini. Akawa anajaribu kupambana kwa kujirusha huku na huko. Alikanyagakanyaga lakini hakufua dafu. Alirusha mikono hewani, bado alionekana kukabwa ipasavyo.Ghafla nikajiona kuwa mtu wa ajabu sana, kwa nini nashuhudia jambo hili na sitoi msaada wowote. Nikataka kupiga kelele. Lakini koo lilikuwa limekauka.Kwanza ni filamu!! Nilijiambia tena.Mara yule kijana akatulia tuli. Nami hapo nikashtuka!!!!Ndoto!! Ndoto mbaya.Nilikuwa nimeung’ata kwa meno upande wa kitanda. Nilikuwa natokwa jasho na nilikuwa naunguruma kama mbwa mwenye ghadhabu anayejiandaa kubweka.Nilihisi kama maumivu kwa mbali katika bega langu.Taharuki!! Kamwe sijawahi kuota ndoto kama hii!! Mbaya sana.Nilitazama saa ilikuwa saa tisa usiku. Giza nene nikiwa peke yangu kitandani.Nilisimama nikafanya ishara ya msalaba. Nilikuwa natetemeka. Na nilivyokuwa muoga wa filamu za kutisha, basi nilikuwa sikamatiki kwa hofu.Nilikuwa nimebanwa na mkojo lakini nilipaogopa sana chooni. Nikaamua kurejea kitandani. Mkojo ukazidi kunibana. Sasa nikajiona kuwa bwege, nina choo ndani halafu naogopa kukitumia.Ni ujinga kujikojolea kitandani wakati kuna choo ndani ya nyumba!!!Nikaiuweka uoga kando nikaenda bafuni. Nikachuchumaa niweze kukojoa, nikahisi maumivu kiunoni.Mh!! Nimelala vibaya ama!! Nilijiuliza huku nikijilazimisha kuchuchumaa.Nilipochuchumaa ndipo nikagundua kuwa nanukia marashi yasiyokuwa ndani ya chumba changu. Hilo pia nikalipuuzia.Nikamaliza haja zangu nikarejea kitandani. Nikajidhihaki kwa hofu ya kijinga niliyoiruhusu initawale.Usingizi ukanipitia. Sikuota tena!!!!Asubuhi majira ya saa mbili nikashtuka usingizini. Ilikuwa siku ya jumamosi, nikaamka kuwahi saluni kutengeneza nywele.Kabla ya kufika saluni nilipita hotelini nikapata kifungua kinywa.****Niliwakuta wateja wawili tu hapo saluni, hivyo mahesabu yangu yalikuwa sawa, sikuwa nimechelewa sana.Nilisubiri kidogo zamu yangu ikafika. Baada ya mimi kuanza kuhudumiwa walimiminika wateja wa kutosha.Kila mmoja na haja yake.Saluni huwa ni eneo zuri sana kwa wale wabahili wa kununua magazeti ya udaku, kujipatia habari nyingi burebure tena kwa uhakika kwa sababu hata nafasi ya kuuliza maswali huwa inapatikana.Penye wengi pana mengi. Na sasa tulikuwa wengi pale saluni. Mara kimya kikatawala alipoingia mwanamke mnene. Sikuwa namjua jina lakini haikuwa mara ya kwanza kumwona.Baada ya kimya hicho ambacho uswahilini kinaitwa ‘jini kapita’ wote tulilipuka na vicheko.Hata yule mama mnene na yeye alilipuka kwa kicheko kikubwa. Kisha tena akauvaa uso wake wa awali.“Mnacheka wakati watu tuna msiba” Alikoroma, nusu akimaanisha na nusu ukionekana dhahiri kuwa ni utani.Wengine wakacheka na wengine wakakaa kumsikiliza.“Halafu mjue sitanii jamani.” Alikazia kisha akaendelea, “Basu ametutoka.”“Basu? Basu ndio nani?.” Mwanamke moja aliuliza.Nami nikapatwa na kihoro cha kuuliza. Nikajizuia lakini sikuweza.“Basu huyu wa BBA (Bachelor of Business Administration).” Niliuliza.Mama yule mnene kumbe na yeye alikuwa mwanafunzi. Akaiunga mkono kauli yangu. Kwa kueleza kuwa ni mwanadarasa mwenzake.Basu alikuwa amekufa!!!Nini kimemuua jamani, si juzi tu alikuwa anacheza mpira kwenye haya mashindano ya FAWASCO? Niliuliza.Msomaji mashindano ya FAWASCO ni mashindano ya michezo mbalimbali huwa yanafanyika chuoni SAUT. Na katika mashindano haya watu wengi walitokea kumfahamu Basu kutokana na umahiri wake uwanjani.Yule mama mnene akashusha pumzi kabla ya kujibu kwa sauti ya kunong’oneza.“Ameng’atwa shingoni huko Nyegezi Kona. Amekutwa kwenye mawe huko.”“Niniiii!!!!.” Kila mmoja wetu alishtuka kwa namna yake. Wahudumu walisimamisha walichokuwa wanafanya wote wakamgeukia mama mnene. Hakuna kauli aliyobadilisha alimaanisha alichokisema.Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yanaenda kasi. Ile mashine kichwani ikageuka mzigo. Nikahisi kizunguzungu.Alichokizungumza yule mama kilifanana na hali fulani halisi, ilikuwa ni hali gani na kwa nini nilikuwa natetemeka? Nilijiuliza. Sikupata jawabu. Nikafumba macho nikakumbuka saa nane usiku!!!!NDOTO!!! NDOTO YA KUTISHA!! Ndoto iliyonipelekea kushituka nikiwa na maumivu makali. Na si maumivu tu. Nilikuwa nimekiuma kitanda kwa nguvu sana. Na…na …..na nilikuwa nakoroma kwa hasira. Kama Mbwa!!! Nilikuwa kama mbwa!!!Hiki nini!! Nilitaharuki kwa hofu. Sikusema kitu chochote, niliulazimisha utulivu!!! Lakini moyoni hapakuwa na amani.Inamaana nimekiota kifo cha Basu? Nilijiuliza. Bado sikupata jibu.Nilivuta kumbukumbu ya sura ya Basu, nikamfananisha na yule mhanga wa kwenye ndoto.Hofu!!! Alikuwa mtu mmoja.Nikapiga ukelele wa hofu.“He Mungu wangu nimemuunguza dada wa watu.” Yule muhudumu alipiga kelele huku akizima mashine.Hakugundua kuwa nilikuwa dunia nyingine kabisa tofauti na hiyo aliyokuwa anadhania.Alinimwagia maji akaniosha nywele. Sikujali ubora wa kazi, nilikuwa nimehamakinika. Akili ilimuwaza Basu.Kama amekufa kifo cha kufanana na kwenye ndoto maana yake nini?Au nataka kuwa mtakatifu??? Nilijiuliza. Huku nikiamini moja wapo ya dalili za kuwa mtakatifu ni kuyajua yanayokuja kupitia ndoto.Mh!! Utakatifu gani huu lakini hata kanisani penyewe siendi?? Nilitengua mawazo yangu.“Dada nakuita jamani!!.” Sauti ya yule muhudumu ilinishtua. Inavyoonekana alikuwa ameniita mara nyingi sana.Nilikuwa sipo kawaida na niliombea sana wasiitambue hali hii.Simu yangu ikaita nikaitoa kuitazama alikuwa ni Dokta Davis.Nikapokea na kuiweka sikioni.“Samahani nipo saluni.” Nilimsihi.“Usijali nilikuwa nakutaarifu ukatazame salio katika akaunti yako.”“Hamna shida.” Nilimjibu na kukata simu.(Kovu la ajabu mgongoni)Nilipotoka pale saluni nilitaka niende kwanza nyumbani kwangu lakini nikaona kwanza nipitie benki kutazama salio.“Laki sita elfu sitini na sita na mia sita sitini na sita.” Hiki ndio kiasi kilichokuwa kimeongezeka katika akaunti yangu. Sikushtuka sana safari hii, nilikuwa nimeanza kuizoea pesa hii kubwakubwa.Sikuwa na haja yoyote ya kutoa pesa kwani bado nilikuwa na pesa nyingi ndani. Niliingia katika bajaji iliyokuwa imenileta nikamuamuru anipeleke Kijiweni, huku ndipo nilikuwa naishi.Tulipoifikia kona ya kijiweni nilitelemka na kuliendea duka la madawa nikachukua dawa za kutuliza maumivu.Nilipofika chumbani nikanywa na kujipumzisha kidogo kwa minajiri ya kuoga baada ya dakika kadhaa. Nilikuwa bado nawaza kuhusu kifo cha Basu kwa kung’atwa, lilikuwa jambo la kushangaza sana. Na kilikuwa kifo cha kustaajabisha, kivipi afe kama ndoto yangu ya usiku? Nilijiuliza sana. Sikupata jibu. Nikajitia imani kuwa hizo ni ndoto.Suala la kwamba ninaandaliwa kuwa mtakatifu lilinisaidia kupungaza hofu.Lakini utakatifu gani sasa huu wa kuupata bila kwenda kanisani??Kwani watakatifu wote walikuwa wanaenda kanisani!! Nilijiuliza. Kisha nikaukatisha mgogoro huu wa nafsi kwa kumpigia simu John, nilizungumza naye kidogo akaniambia yupo njiani kuelekea Nyegezi kona kutazama maiti ya Basu.Aliposema jina hilo nikashtuka lakini hakugundua kwa sababu hakuonyesha wasiwasi na wala hakuuliza swali.“Basu…Basu amekufa?” Nilijifanya sijui lolote. John akanieleza stori ileile kama mama mnene wa kule saluni aliyosema.Nikaingia katika fumbo, sikumjua mfumbuzi!!!Nikapitiwa na usingizi!!!****Nilikuwa nautazama sasa umati wa watu ambao sikuelewa ni shughuli gani walikuwa wakiifanya. Sikuwatilia maanani sana na wala sikujuaeneo lile ni wapi. Mara nikamuona mtu ambaye ninamfahamu. Nilitamani kumuita lakini niliamini kwa zile hekaheka alizokuwa nazo wala asingeweza kunisikia. Nikapuuzia!!Sikujua nilikuwa nimejikita katika shughuli gani lakini kuna jambo nilikuwa nafanya.Mara nikamwona tena yule mtu ambaye nilionekana kumfahamu, sasa alikuwa katika mtafaruku. Wenzake wote walikuwa wakimpigia kelele katika namna ya kupingana. Alikuwa peke yake na hakuna aliyemuunga mkono. Mara wenzake wakaanza kumzonga sasa hayakuwa mabishano tena bali ugomvi. Mtu mmoja anachangiwa na watu zaidi ya kumi. Ugomvi ukawa ugomvi. Kuna jambo walikuwa wanalazimisha. Jambo hilo huyo mmoja hakuunga mkono kabisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baada ya kuzidiwa mara yule mtu akawaponyoka. Akaanza kukimbia. Alikuwa anakimbia huku akiangalia nyuma. Nilikuwa natabasamu nikimtazama maana alionekana kuwa na hofu kuu.Alipogeuka mara ya kwanza lilikuwa kundi la watu watano wakimfukuza, akazidi kukimbia, alipogeuka tena walikuwa watatu, akajitahidi kujitetea kwa kuendelea kukimbia, wakabaki wawili. Safari hii hakugeuka.Alipokuja kugeuka sasa alikuwa amekaribia kukamatwa. Lakini cha kutia moyo alikuwa anakabiliwa na mtu mmoja tu. Japo alikuwa amechoka lakini hata huyu aliyekuwa anakabiliana naye alikuwa anahema juu juu. Walikuwa wanatazama kama majogoo yanayofanyiana ubabe.Mara jogoo lililokuwa linamkimbiza jogoo mwenzake likamrukia yule mkimbizwa. Wakaanguka chini, ugomvi ukazuka.Wakagalagana hapo chini kwa namna ya kuchekesha. Nami nikawa nacheka.Mara yule mtu niliyekuwa namfahamu akaangushwa vibaya. Halafu yule aliyemuangusha akachomoa kisu kidogo, upesi akamchana nacho mgongoni. Akatoa ukelele wa uchungu na hofu.Kuchanwa huko kukawa kumemrejesha upya katika ugomvi. Sasa alikuwa na nguvu kamilifu. Yule aliyekuwa na kisu alipojaribu kumchana tena akawa amechelewa mkono wake ukadakwa, kisha kikafanyika kitendo cha sekunde kadhaa tu cha kuikamata shingo ya mwenye kisu na…na….na…“Mamaaaaa!!!” Nikakurupuka usingizi!!Nilikuwa nimelala masaa sita. Niliyapikicha macho yangu huku na huko niweze kuangalia vyema mbele.Ukungu ulikuwa umetanda. Nikajipikicha zaidi nikaweza kuona, na sasa niliweza kusikia. Mlango ulikuwa unagongwa kwa nguvu. Fahamu zikanirejea vizuri, nikauendea bila hata kuulizia nikafungua.Alikuwa ni jirani yangu.“Kakasirika kweli John dah!! Amegonga mlango, kapiga simu yakohupokei.” Alinieleza huku na yeye akionekana kukasirika.Nilipiga mwayo mrefu kisha nikamuuliza kuwa alikuja saa ngapi. Akanijibu. Kisha akajieleza shida aliyokuwa nayo nikamsaidia . akaondoka!!!*****Sikuweza kuhudhuria msiba uliomuhusu Basu, akili yangu ilikuwa imechoka sana. Baada ya harakati za hapa na pale nilijipikia chakula kisha nilipomaliza nikalala tena.Mara hii mlango ulipogongwa nilisikia vyema kabisa. Nikasimama na kwenda kumfungulia. Alikuwa John na ilikuwa saa tatu usiku.John alikuwa amefanya mfano wa hasira usoni, nililitambua hilo na sikuwa na haja ya kumuuliza kwa nini amekasirika.Baada ya kuzungumza naye dakika kama kumi hivi huku nikijiweka karibu naye. Alilainika na uso wake ukaunda tabasamu.Tulizungumza mengi na mpenzi wangu huyu wa zamani. Na kama vile tulikuwa tumeambiana kwa pamoja tukageukiana tukakumbatiana kwa nguvu. John alikuwa analia.Nilijua kuwa anamlilia Jesca, sikutaka kumuuliza najua angelia zaidi. Nilichofanya ni kuzidi kumkumbatia, viatu vikabaki sakafuni, sasa tukawa kitandani. Lugha iliyozungumzwa ilikuwa lugha ya mapenzi.John alikuwa mtulivu kama aliyesafiri kwenda ulimwengu wa mbali. Nikaitoa shati yake akawa amebakiwa na singlendi. Nikataka kuitoa na ile.“Ngoja nikaoge kwanza baby…” aliniambia kwa sauti nzito yenye kutamanisha.Nikatulia nikamtazama naye akanitazama.“Twende wote pliiz.” Nilimsihi. Hakujibu chochote nikajua kuwa maana yake ni kwamba twende.Nikaziondoa nguo zangu, nikajivika upande wa kanga.“He!! Sa na hiyo singlendi waipeleka bafuni kufanyaje tena!!!” Nilimuuliza John baada ya kumuona akiingia na ile singlendi bafuni.“Si haujataka kunivua sa mi ntafanyaje?.” Aliniuliza kitoto. Nikatabasamu, nikamwendea, akakimbilia upande mwingine wa chumba nikamfata tukawa kama tunagombana. Japo hatukutumia nguvu sana!!!“Ukiweza kunivua nakubeba mgongoni!!” Alinipa motisha nikazidisha juhudi. Nikaitoa nikawa mshindi.Mshindi kubebwa mgongoni!! Ikumbukwe hiyo.Mimi ndiye mshindi, mgongo mali yangu.John akachuchumaa nikawa nyuma yake.Ile nataka kupanda mgongoni nikaona kitu cha ajabu.Kovu!!! Kovu bichi!!! Kovu katika mgongo. Kovu la kuchanwa na kisu!!“Mamaaaaa!!” nikapiga kelele. John akasimama. Tayari nilikuwa katika kona ya chumba nikiwa natetemeka sana!!!“Sabe sabe!! Umekuwaje…” aliniuliza huku akinisogelea. Nikawa namkimbia, lakini wakati huu haukuwa mchezo tena nilikuwa katika hofu ya ukweli. Nilikuwa namuogopa John.John alinisihi niache utani!!! Lakini sikuwa natania. Nilikuwa katika kumaanisha.Hali ilikuwa tete. John alikuwa ananitisha.Nikiwa katika kumkimbia John. Sasa aligundua kuwa kuna jambo limenisibu. Akanifuata kwa kasi. Akanivagaa. Nikajilazimisha kujitoa mikononi mwake huku nikipiga kelele. Ghafla akaninasa vibao viwili.Sasa hapo ndio nikachanganyikiwa mwenzenu na kuamini kuwa dunia imefika mwisho. Nililia huku nikimtaja mwalimu Nchimbi.Lakini cha ajabu na kukera huyo mwalimu Nchimbi hata hakuwa akinisikia.Iliniuma. John akaniongeza vibao vingine viwili. Sasa yale maumivu akili ikasogeleana.“John una damu!! Una damu!!”“Damu??” aliniuliza.“Mgongoni umekuwaje wewe.”“Mgongoni pamekuwaje kwani…alilalamika huku akijipapasa”Maajabu mengine jamani!. Mkono wake haukuwa na damu. Akanigeukia.Nikatamani kuiaga dunia niende likizo mbinguni. Hakuwa na kovu. Mgongo laini kabisa wa kiume ukatazama nami. Nikaruka mita kadhaa.Akapoteza uelekeo kuniona naruka vile nikataka kukimbia nje.Akanidaka kanga yangu. Kanga ikateleza ikauacha mwili.Shanga nane za rangi tofauti zilizokishika vyema kiuno changu ndio pekee zilizosalia katika mwili wangu. Sasa John alikuwa amebaki na kanga mkononi mimi nikiwa nina shanga kiunoni. Nusu nilikuwa nje na nusu nilikuwa ndani.Swali likavamia kichwa changu.Nikimbie na shanga kiunoni kwenda nje ama nirudi chumbani kwa John huyu wa maajabu!!! John niliyemuhisi kuwa sasa ni ………….Nikabaki katika kizungumkuti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog