Simulizi : Binti Kipofu
Sehemu Ya Pili (2)
"Bossi sidhani kama atakuwa akimfahamu Rickson. Alizungumza Daudi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa tumfanyaje?? Aliuliza Adrian.
" Inabidi tumfuatilie zaidi Saruni kwani inavyoonekana hat huyu anatumiwa na Saruni bila kujua y kuwa anamfanyia kazi Rickson " alizungumza Adrian akimtizama Alice aliyekuwa amelowa damu mwili mzima.
"Ili tumpate Rickson inabidi tumtumie Saruni na ili tumpate Saruni inabidi tumtumie Alice" alizungumza Adrian.
*** *** *** ****
"Ndivyo alivyoweza kuniambia ya kuwa kama nafikiria mali zipo kwa Tropina basi nimefeli" alizungumza Frank akimpa maelezo hayo Adrian.
Baadaye alionekana Adrian akiwa ameweka kalamu mdomoni mwake huku akijizungusha katika kiti cha ofisini.
"Kama mali haziko kwa Tropina basi zitakuwa ziko kwa Larry...... Lakini hapana Larry umri alionao hawezi kuandikishwa mali hizo hivyo basi mwenye nazo ni Vanessa......lakini Vanessa hawezi kuwa na hizo mali kwasababu bado yuko chini ya upelelezi wa kifo cha mumewe pamoja na ndugu zake.....sasa mali zipo kwa nani?? Alijiuliza Adrian.
Au zipo chini yngu nini??? Hahahaha huyu mwanamk mjinga kweli hivi wananifanya mimi nateseka siku zote kumtafuta nani mwenye mali ukute zipo chini ya jina langu......ngoja.... Ngoja......ngoja.....lazima nimtafute wakili wa familia anipe majina ya wana familia.
Aliinua simu yake na kupiga.
"Hallo samahani naweza kuzungumza na mwanasheria Josephat" alizungumza Adrian.
**** **** **** ****
"Nachotakiwa kufanya ni kuhamisha mali zote chini ya jin la Adrian mpaka kwenye jina lako kwani ikitokea Adrian akifahamu ya kuwa kwa miaka yote hiyo mali zilikuwa chini yake wakati akihangaika kuzitafuta basi atazichukua kiulaini sana" alizungumza Vanessa.
"Lakini mama" alizungumza Vikram.
"Rickson inabidi uokoe mali za Baba yako mkwe, mke wako pamoja na bwashe wako kwani mimi najua ipo siku moja nitatoweka duniani na kumfuata mme wangu kipenzi sitaki kufa katika hali ya mashaka nikiwa sijui maisha ya wanangu yataishia katika hali ipi ikiwa mimi na tamaa zangu za kimwili ndizo zilizoweza kuchangia haya yote yatokee katika familia yangu. Alizungumza Vanessa mpaka machozi yakiwa yanamtoka.
" Mama ni sawa nimekuelewa nani salama pia" alizungumza Vikram au Rickson ambaye aliweza kufahamika tangu mwanzo alipoweza kuingia tu katika nyumba ya kina Vanessa.
***** ***** *****
"Wewe ni nani??? Aliuliza Josephat .
"Naitwa Adrian mume wa Vanessa nilikuwa nataka kujua mali zote zipo chini ya nani??? Aliuliza Adrian.
" sawa nipe dakika tano alizungumza wakili yule huku akizitafuta document zenye kuonyesha ni nani anamiliki mali zile.
Huku nako Vanessa alikuwa akimpigia simu lakini nmba ilikuwa busy.
"Tufanyaje yuko busy anazungumza na simu nyingine? Alizungumza Vanessa akimtizama Vikram.
"Alafu sijihisi vizur kabisa nahisi kuna kitu kikubwa kitatokea kwa siku ya leo"
"Kitu gani aliuliza Vikram"
***** ******
"Mali zote za bwana Miller Molell zipo chini ya Adrian Kivuyo kwanza mwaka 2012 mpaka leo hakuna mabadiliko yoyote yaliyoweza kufanyika lakini kwann unaniuliza ikiwa wewe ndyo bwana Adrian na sahihi zako zinaonekana hapa" aliuliza wakili.
"Hapana haina shida naomba uniandalie hiyo original nakuja kuchukua sasa hivi" alizungumza na kukata simu kisha akainuka na kutaka kuondoka ofisini lakini alirudi nyuma n kuitizama picha ya Tropina
"Nikirudi hapa tena ukuta huu utakuwa na picha yangu na siyo ya kwako tena" alizungumza na kuufungua mlango wake kisha akaondoka.
"Inabidi tuelekee huko huko ofisini hatuwezi kusubiri zaidi" alizungumza Vanessa na kubeba pochi yake kisha haraka haraka akashuka akiwa na Vikram.
"Larry...... Larry....."
"Nini......mbona tunashtuana jaman" alizungumza huku akitoka ndani ya chumba chake.
"Twende haraka"
"Wapi??? Aliuliza Larry.
" wewe twende "
"Vanessa mm sijavaa nguo subiri nikavae"
*hapana tutachelewa*
"Basi nikachane hata nywele" alizungumza Larry.
"Wewe twende alizungumza huku akimshika Larry mkono na mbio mbio kumburuta.
" bwashe viatu...viatu..... " alizungumza huku akutokomelea mlangoni.
***** ******
"Sikutegemea kama utawahi kufika mapema hivi....karibu sana alizungumza mwanasheria yule akimkaribisha mtu.
Hatimaye aliingia kijana mmoja ambaye aliweza kuutegemea ujio wake.
"Naomba unifuate huku tafadhali alizungumza josephat lakini ghafla mlango wa ofisi yake ulifunguliwa kwa pupa na kwa haraka zaidi.
" Vanessa "!!! Aliita kwa mshangao huku akiwatizama Vikram na Larry walioweza kuvaa kiatu kimoja kimoja.
"Kuna shida gani mbona mmekuja hivyo?? Aliuliza tena Josephat.
**** **** ****
Baada ya muda kidogo alionekana akitoka Larry akiwa ananung.unika huku akijaribu kuificha mguu wake mmoja ambao hauna kiatu usionekana.
" Unashida gani mbona unatembea hivyo?? Aliuliza Vanessa.
"We niache bhana..... Yuko wapi Rickson?? Aliuliza Larry.
" Nafikiri anamalizia malizia kusign tutangulie kwenye gari" alizungumza Vanessa alitoka njee ya ofisi ile.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"At least sijakosa vyote amah kwa hakika Mungu yupo upande wangu....naamini mali zote sasa wamemmililisha Rickson ambaye nakwenda kumfahamu siku ya leo kisha kumuangamizia mbali siku baada ya leo. Alizungumza Adrian ambaye tayari alishafika katika ofisi ile na aliweza kuyasikiliza maelezo yote yaliyoweza kutolewa na Vanessa.
Alitoka katika kordo ile aliyoweza kujificha kisha akautizama mlango wa mwanasheria Josephat.
Alianza kupiga hatua kuelekea mbele ya mlango ule wakati ndani ndipo alipokuwa akimalizia malizia kusign karatasi Rickson au Vikram.
Hatimaye alitembea mpka kubakiza hatua chache tu kuufikia mlango ule.
Ghafla aliweza kupita mtu na kujikwaa hali iliyomfanya kahawa aliyoweza kuibeba amwagie katika nguo ya Adrian.
" jamani samahani" alizungumza huku akijaribu kutoa kitambaa chake mfukoni na kuanza kumpangusa.
Wakati huo nao Vikram aliweza kuufungua mlango pasina kutambua ya kuwa kuna uwepo wa Adrian.
"Inatosha alizungumza Adrian huku akiitoa mikono ya mtu yule katik mwili wake na kuyageuza macho pamoja na mwili wake tena katika mlngo wa mwanasheria Yule. Wakati anageuza mwili wake ndyo wakati ambao Vikram alimalizikia kupita nyuma yake kisha akaendelea na safari zake. Adrian alifungua mlango ule na kuingia ndani hapo alimkuta yule kijana wa kwanza ambaye alitangulia kufika kabla ya Vanessa. Alitabasamu huku akiamini ya kuwa ni Rickson.
" Rickson " aliita kwa bashasha Kubwa na kijana yule aligeuka pamoja na wakili.
"Nani wew?? Aliuliza wakili au mwanasheria.
" Naitwa Adrian mume wake Vanessa "
"Ahaaaa samahani sana lakini leo wamekuja kumbadilisha mridhi wa mali na......."
"Natambua na kuelewa vyote kwahiyo Rickson ndo anasign sasa hivi??? Aliuliza ili awe na uhakika.
"Inamaana hujapishana naye hapo mlangoni?? Aliuliza wakili.
" Nani huyo??? Aliuliza Adrian kwa kuhamaki.
"Rickson"
"Kwahiyo huyi siyo Rickson aliuliza tena Adrian akiwa kama mtu ambaye haamini kile alichoweza kuambiwa.
Adrian alitoka njee haraka haraka kwaajili ya kwenda kumuona Rickson lakini yuko pale aliliona gari la Vanessa likitoka katika eneo lile huku akibahatika tu kuona kivuli cha mtu kwni lilikuwa mbali na upeo wa macho yake.
Adrian alitaka alifuata lile gari lakini alijipa akili ya kuwa CCTV camera za kituo hicho zitakuwa zinafanya kazi.
" sina haja ya kuwakimbiza na wewe kwa gari kwani kabla haujashuka ndani ya gari mimi tayari nimeshaweza kukutambua ya kuwa wewe ni nani??? Alicheka na kuzitazama CCTV camera za eneo lile huku alisema.
"Sawa tuone utajificha mpaka lini???
***** ***** *****
" unatafuta nini kwenye droo yangu?? Hilo lilikuwa swali la Tropina lililoweza kwenda moja kwa moja hadi kwa Frank.
"Tropina aliita Frank huku akilifunga kabati la Tropina na kuweza kuweka karatasi moja katika tumbo lake kisha kufunika kwa nguo yake ya juu huku akiamini ya kuwa Tropina amuoni kwasababu ni kipofu.
" Nilikuwa nakutafuta sana kuna kitu nilitaka nikwambie" alizungumza Frank
"Ndoo ufungue droo yangu ya siri Frank?? Aliita Pinah.
Frank alishtuka baada ya kusikia jina lake limetajwa tena katika mdomo wa Pinah.
" Vipi unashangaa ya kuwa unafahamika sindiyo...... alizungumza Pinah huku akielekea kwenye kochi lake na kukaa.
**** **** ****"
"Nini CCTV camera hazifanyi kazi???? Alizungumza Adrian kwa mshangao.
" ndiyo iliharibika toka juzi Ila leo ndiyo ataletwa fundi kwaajili ya kuweza kuweka kila kitu katika hali ya kawaida kama mwanzo.
"Sasa kwanini usingeniambia mapema mpaka nikamuacha akaenda kwanini hukuniambia" alilalamika sana Adrian
"Me nilijua mmezunguza na Vanessa ndo maana nikamuona yeye ame........." Kabla hajamalizia sentence yake Adrian aliweza kumdaka na maneno kwa juu.
"Umeona sura yake?? Aliuliza Adrian.
" Sura ya nani mbona sikuelewi??? Aliuliza tena Josephat.
"Rickson Rickson sura yake umeiona???
Wakili yule aliweza kufikiria kidogo kisha akajibu.
" sidhani maana alikuwa amekaa kofia na haikuwa rahisi mimi kumtambua Ila mguuni alivaa kiatu kimoja.......Ila tofaut na jina hilo Larry alikuwa akimuita jina lingine.
"Jina gani hilo??? Aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.
" sijui ata alikuwa anamuitaje lakini sikuwa attention sana na yeye bali jinsi y kuweza kuandaa hatimiliki nyingine. Alizungumza Josephat
"Hiyo hapo ni business kadi yangu na ina namba zangu kama utakumbuka hilo jina lingine basi utanipigia" alizungumza na kuanza kutoka njee.
"Samahani lakini mguuni alikuwa amevaa kiatu kimoja tu yeye pamoja na yule Mdogo wake Tropina wa kiume"
"Larry!!! Aliuliza kwa mshangao.
"Ndiyo ni Larry"
"Kingne unachokumbuka zaidi ya hicho??
"Hamna"
"Basi sawa ukiweza kulikumbuka hili jina unipigie"
"Ndiyo nimekuelewa...... Alafu pia kuna mahali unatakiwa usign alizungumza huku akiwa anapekenyua pekenyua mafaili mengineo.
***** ******* ******
" Alice akiwa katika mateso makubwa aliweza kuyafumbua macho yake na bado alikuwa amekaa gizani huku akiwa amefungwa kamba mwili mzima.
"Haya wajinga wananipotezea time............
......siku zinaenda eti na nahitajika kumaliza kazi niliyiweza kupewa kabla mwezi wa 12 haujafika......natakiwa kumtafuta Rickson inavyoonekana hata Adrian amtambui nani ni Rickson sasa itanibidi Saruni anikutanishe na Rickson alizungumza Alice huku akiweza kuibinya Pete yake iliyoweza kuwa kwenye kidole chake na kutoa kisu kidogo sana
Alianza kukata kamba huku akizungumza.
" Adrian baada ya yote haya kuisha lazima ulipe kwa hichi ulichoweza kukifanya.
***** ****** *****
"Inavyoonekana huku ndani siku hizi kuna mambo yanaendelea ambayo mimi sishirikishwi kabisa" alizungumza Tropina aliyekuwa akishuka chini ya ngazi baada ya Vanessa Larry na Vikram kurud nyumbani.
"Nimechoka sana naomba nikajipumzishe alizungumza Vanessa na kupanda zake ngazi.
" nahitaji kwenda kulala" alizungumza Larry na kupanda na yeye juu sasa alibki Vikram na Tropina.
"Na wewe unaenda kufanyje??! Aliuliza Tropina.
" kupeleka hatimiliki ndani" alijibu na kupanda ngazi.
"Haya na wewe Tropina unafanya nini?? Alijiuliza mwenyewe huku akiwatizama wanavyopanda ngazi kama wagonjwa.
"Kuna shida gani leo mbona hivyo???? Alijiuliza Tropina.
***** ****** *****
hatimaye kulikucha.
Vikram alifungua mlango wake na ghafla alishangaa baada ya kuona watu wanatoka n mabegi katika chumba cha Tropina.
" kuna shida gani tena......Pinah.....Pinah...!!!!!
"Nini mbona unaita hivyo??? Aliuliza Tropina.
"Nilihisi hauko salama.....mbona mabegi ynapakiwa unaenda wapi?? Aliuliza Vikram.
" Siyo mabegi yngu yangu tu" alizungumza huku akimpa ishara ya kuw atazame na chumba cha Larry.
"Bwashe unaenda wapi na begi.......mbona kubaa hivyo?? Aliuliza Vikram.
"Huwaga tunatabia ya kwenda picknick kila mwanzo wa mwez au mwisho wa mwez" alijibu Vanessa aliyekuwa akitoka na begi lake mkononi.
'Jiandae tunaenda wote " alizungumza Tropina na kushuka.
Hatimaye baada ya maandalizi sasa walipanda gari moja na kuondoka zao.
Hatimaye siku imefika ya kuweza kuwasambaratisha wote kwa pamoja kama nilivyoweza fanya kwa Mr Miller Baba yenu. alizungumza Adrian.
"Haloo!!!! Ndyo wametoka hakikisha inakuwa ajali na hakuna mtu yoyote yule ambaye anatakiwa afahamu kuwa siyo ajali"
Baada ya Adrian kupiga simu na kutoa maelezo yale aliweza kuinua tena simu yake na kupigia mtu mwingine!!!
"Haloo naomba uniandalie majeneza matatu ya watu wazima na moja la mtoto mwenye miaka9. Alipomaliza alikata simu.
" sitaki mje mnilalamikie ya kuwa sikuwekea umakini miili yenu pindi mlipoweza kufariki. Alicheka na kuingia ndani ya nyuma ile huku aliita wafanyakazi wa nyumba ile na kutoa amri ya kuwa nyumba ipambwe na kiandaliwe chakula kizuri kwni tutapokea habari njema ndani ya masaa matatu ya mbeleni.
*** *** ***
Waliweza kupanda gari moja huku Vikram akiwa anaendesha gari na pembeni yake akiwa amekaa Larry. Nyuma alikaa Vanessa na Tropina.
"Hivi wewe huwezi kutulia" alizungumza Tropina akimzungumzia Larry.
"Anaongea na nani?? Aliuliza Larry.
" anayehangaika kwenye gari ni nani kama siyo wewe " alijibu Tropina
"Nimehangaikaje aliuliza Larry huku akiendelea kufungua fungua baadhi ya sehemu kwenye gari hilo.
Tropina alimtizama bila kusema neno. Baada ya kumaliza kufanya hivyo alitoa begi lake na kuanza kula popcorn ndani ya gari akatoa na juice yake na kuendelea kunywa. Tropina alimtizama tu bila kusema neno lingine lolote lile.
Alipomaliza kula sasa alianza kucheua ndani ya gari.
" Larry sipendi mimi huo usumbufu wako" alizungumza Vanessa.
"Nimefanyaje?? Aliuliza Larry na kutoa baadhi ya piza zilizoweza kuwa kwenye begi lake.
" unataka kufanyaje?? Aliuliza Tropina.
"Kula pizza" alijibu huku akifungua boksi lile la piza.
"Siyo ndani ya gari yangu..... Utoke njee ukalie huko" alizungumza Tropina na kuchukua boksi lile la Pizza.
"Nilijua tu lazima utabutreat vibaya kwasababu gari ni la kwako....alizungumza Larry na kukaa kwenye gari sasa alifungulia mziki kwa sauti ya juu kabisa kisha akaanza kuimba na kucheza ndani ya gari lile.
Baada ya dakika kadhaa alionekana Tropina akielekea upande wa gari wa mbele na kwenda kufungua mlango akamtoa njee Larry.
"Kaa hapo usubirie gari lako kisha ufanye yale yote uyatakayo kwenye gari lako. Alizungumza Tropina na kutoa kitambaa chake kisha akaanza kufuta futa sehemu aliyokuwapo Larry.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nilijua we ni mchoyo sana na vitu vyako alizungumza Larry aliyekuwa njee ya gari la Tropina. Tropina aliingia ndani ya gari kisha akaufungua mlango. Larry alienda akagonga kwenye kioo cha gari upande alioweza kukaa Vanessa. Vanessa alishusha kioo cha gari.
" kwahiyo unaniacha hapa mwenyew mpaka walete gari......shuka bhana Vanessa " alizungumza Larry na Vanessa alimtizama bila kusema neno lolote lile alichukua kipochi chake pamoja na miwani yake kisha akashuka ndani ya gari huku akimtizama Larry.
Aligonga tena kioo cha Tropina na Tropina alishusha kioo cha gari.
Alimtizama na kumwambia ampatie simu yake ameisahau ndani.
Tropina aliiona simu chini kisha akainama na kuokota simu. Wakati huo anainama Larry aliweza kumkonyeza Vikram na Vikram alimpa poa katika ishara ya kidole.
Larry alichukua simu yake na kutoka pale.
Alivyorudi nyuma alikutana na Vanessa.
"Kwanini umeamua kufanya hivyo hivi unawezaje kumuuza dada yako kwa mwanaume"
"Siyo mwanaum yule ni mume wake............ni vizuri kama watapata muda wote kwa pamoja wa kuzoeana kabla ya Tropina kumfahamu ya kuwa ndo Rickson'
" kwahiyo ndo plani yenu??
"Siyo yangu mimi niya mkwe wako" alijibu Larry
"Vanessa inabidi turudi nyumbani au tufatute sehemu nyingin kwaajli ya kwenda kuifidia siku ya leo garama zote zitakuwa juu yangu" alizungumza Larry.
"Siyo juu yaki bali juu ya Tropina"
"Kivipi nitalipia mimi kila kitu" alizungumza Larry.
"Utalipia wewe kwa ATM card ya Tropina..... Unafikiri sikukuona ukiuchukua?? Aliuliza Vanessa akitangulia mbele.
" Dah imekuwaje huyu naye mpaka akaona. Aliuliza huku akiitoa atm card ya Tropina kwenye mfuko wake wa suruali.
***** ****** ****
Adrian akiwa nyumbani aliweza kupokea simu.
"Boss Tropina ameweza kumshusha Larry pamoja na Vanessa ambao hao wameingia kwenye gari lingine"
"Wote wanatakiwa kufa kwa siku ya leo hakuna ruhusa ya yoyote kubaki hai" alizungumza Adrian.
"Gari gani ambalo uliweza kukata break zake kwa udogo?? Aliuliza Adrian.
" alilopanda Tropina " alizungumza Daudi.
"Sawa gonga hilo gari aliloweza kupanda Vanessa na Larry hilo na Tropina wakiweza kushika break kila saa nyaya itaendelea kuachia na hatimaye itakatika kabisa" alizungumza Adrian kwa kujiamini huku akiwa juu kabisa ya nyumba ile na kutazama jumba lile huku akisema.
"Hatimaye yamebaki masaa machache tu niwe mmiliki wa nyumba hii baada ya kupitia matatizo na kasheshe nyingi sasa hatimaye nimefanikiwa.
" hongera Adrian hongera sana" alizungumza kwa kujipongeza huku akinywa wine aliyoweza kuwekewa kwenye glass.
**** **** *****
"Mbona unanitizama kisha unatabasamu sana?? Aliuliza Tropina baada ya kumuona Vikram anatabasamu.
" naweza nikaushika mkono wako??? Aliuliza Vikram ambaye tayari alishauchukua mkono wa Tropina na kuushika.
"Na kwnini uushike?? Aliuliza huku akijaribu kuutoa mkono wake.
" japo kwa siku ya leo uache kuwa mkaidi na ufanye vile nitakavyo mimi tafadhali!! Alizungumza Vikram na kuushika tena mkono wa Tropina.
"Lakini sasa si unaendesha?? Aliuliza Tropina baada ya kukosa sababu ya kutoa mkono wake tena.
"Usijali naweza kuendesha pia kwa mkono mmoja"
"Lakini sheria ndogo ya barabara kifungu namba.............."
"Nakuja na kukuelewa vizuri kabisa kwamba wewe ulisomea sheria marekani ngazi ya degree na uliondoka na wastani wa A ya 94 kwahiyo kaa kimya nimekuomba" alizungumza Vikram na kumfanya Tropina anyamaze.
*** **** **** **
Gari lililoweza kupaki pembeni likiwa linamsubiria Vanessa na Larry wamalize kula ili waondoke eneo hilo nyuma yake kulikuw na gari Kubwa aina ya scania aliloweza kuwepo Daudi ndani yake huku akiwa subiria wote wapande kisha waondoke.
Alimuona Vanessa pamoja na Larry wakija katika uelekeo wa gari lao.
"Vanessa......... Nimesahau atm card ya Tropina ndani" alizungumza Larry na kurudi ndani wakati huo wote Daudi alikuwa akijitengenezea hivyo hakuweza kumuona Larry akirudi ndani ya hotel ile. Alipomaliza kuvaa koti lake pamoja na mask usoni aliweza kumuona Vanessa akipanda ndani ya gari hivyo kuamini ya kuwa wote wameweza kupanda ndani ya gari.
"Wameshapanda" alitoa taarifa hiyo Daudi kwa Adrian.
"Hakikisha ufanyi makosa ligonge hata zaidi ya mara tatu sitaki mtu yoyote atoke hai. Nahitaji marehemu tu. Alikata simu.
Larry aliweza kufika ndani ya hotel ile na kuelekea moja kwa moja hadi kwenye meza waliyokuwapo na kuweza kuacha Atm card pale.
Alipofika tu alishngaa baada ya kuona ashiki Atm card bali mkono wa mtoto wa kike uliyoweza kuikamata Atm card ile.
"We mtoto toa mkono wako" alizungumza Larry akimtizima.
Binti yule alimtizama kisha akacheka. "Mimi na wewe nani atoe mkono kwenye mkono wa mwenzke" aliuliza huku akimtizama Larry.
"We ni kichaa nini toa mkono wako kwenye Atm card yangu" alizungumza Larry kwa a hasira huku akimtizama Queen ambaye ni Mdogo wake na Winnie.
"Sikujua kama huwaga unapoteza kumbukumbu kwa haraka namna hiyo" alizungumza Queen huku akimsogelea kwa karibu.
"Kumbukumbu za nini embu toa mkono wako" alizungumza Larry akijaribu kuivuta atm card yake.
Queen alitoa mkono wake kisha akazivuruga nywele zake na kumtazama Larry ambaye alishtuka baada ya kumuona.
"Mungu wangu kumbe ni yule kichaa" alizungumza kwa mshtuko hadi akadondoka chini na kuweza kuidondosha Atm card yake.
"Inavyoonekana huyo yuko busy na mambo yake huku ndani mpigie simu dereva mwingine kisha umuelekeze mahali alipo aje kumchukua sisi tutangulie kuna mahali nataka kwenda kwanzia sasa" alizungumza Vanessa na dereva yule alifanya kama vile alivyoweza kuagizwa baada ya kumaliza aliliwasha gari na kuliondoa eneo lile.
Daud na yeye baada tu ya kufika mbali kidogo na yeye aliwasha gari na kuanza kulifuata.
**** ***** *****
Huku nako safari iliweza kuendelea baina ya Tropina na Vikram.
"Lakini njia hii siyo ya.........."
"Shshshsh alizungumza Vikram kwa kumbinya mkono Tropina alioweza kuushika
Nilikuomba unyamaze unaweza ukafanya hivyo" alizungumza akamgeuzia na uso wake ulioweza kujaa Tabasamu.
Tropina aliweza kutizama chini kwa aibu na kwakukumuiba iba Vikram ambaye alicheka na kuuchukua mkono wa Tropina zaidi kisha kuusogeza katika lipsi zake na kuubusu taratibu.
Kwa upande wa Vanessa Lori lile liliweza kusogea karibu zaidi na gari lake huku nako Vikram alikanyaga break lakini alishangaa baada ya kuona ya kuwa break haishiki.
Ni baada ya Vikram kushindwa kukanyaga break huku nako Lori likiweza kusogea kabisa kwa ukaribu gari aliloweza kupanda Vanessa.
"Kuna shida gani mbona umeshindwa kukanyaga break" aliuliza Tropina baada ya kuwa na wasiwasi.
"Hpana ni bobo la Larry ndo nililikanyaga badala ya break" alisema huku akilisogeza bobo lile kwa mguu"
"Nilidhni break imekatika tena wakati tumeshaitengeneza" alizungumza Tropina.
Tropina aliweza kugundua wa kwanza ya kuwa nyaya za break ile ilibaki kidgo tu kuachia baada ya kuinama na kuokota simu ya Larry wakati ule ambapo Larry alimuomba ampatie hivyo waliweza kwenda kwa machanica na kabadilisha break kisha kuendelea na safari yao.
***** ***** *****
"Hilo Lori mbona kama linatufuatilia?? Alizungumza Vanessa baada ya kuona ni muda mrefu sana Lori liko nyuma yao.
" Punguza mwendo na ulipishe kwa kukaa upande mwingine tuone alizungumza Vannesa akimuamrisha mfanyakazi wake.
Mfanyakazi au dereva yule aliweza kufanya kama vile alivyoweza kuamrishwa au kuelekezwa na Vanessa.
Lakini Lori lile nalo liliweza kupunguza mwendo na kuhamia upande ule ambao gari la Vanessa liliweza kuhamia.
Dereva alitizama mbele na aliiona ishara ya kuwa huko waendako kuna mteremko mkali ndo maana Lori hilo linawafuatilia mpaka wafike mahli hapo kisha awasababishie ajali.
"Adrian" alizungumza Vanessa huku akipiga mkono wake kwa hasira kwenye kiti cha dereva.
"Madam Vanessa njoo siti ya mbele kisha jifunge kwa kutumia mkanda nitakuonyesha kitu cha kufanya. Alizungumza maneno hayo na Vanessa aliweza kufanya kama alivyoweza kuambiwa.
Hatimaye waliweza kufika sehemu ambayo sasa walihitajika kupunguza mwendo kwasababu tayari wameshafika eneo lenye mteremko mkali.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dereva yule aliweza kuongeza mwendo zaidi na kumfanya Daudi na yeye aanze kujiandaa kuongeza mwendo
" huyo dereva kichaa nini hata mfanye nn hamuwezi kuondoka mkononi mwangu salama.
Alizungumza Daudi
Kabla hajafikia hazima yake alishangaa baada ya kuona gari nyingine ndogo moja ilikuja kwa mwendo kasi na kuingia katikati yao.
" Ni mjinga gani huyo?? Alianza kulalama Daud huku akitafuta upande wa pili apite ili aweze sasa kuligonga gari la kina Vanessa lakini gari lile nalo liliweza kuingia pia upande huo huo wa pili.
"Huyu mjinga" alilalama Daud.
Huku akijaribu tena kuhamia upande mwingine na wakati anahamia upande mwingn gari lile lile nalo likahamia upande ule.
"Nini kinaendelea?? Aliuliza Vanessa.
"Nahisi huo ni msaada alizungumza dereva huku akijitahidi kuendesha kwa ustadi wa hali ya juu ile gari lisiweze kuporomokea kwenye mteremko huo.
Mkono ulioweza kushikilia pipi alafu wa kike uliweza kutoka ndani ya gari lile kisha ukampa ishara dereva wa Vanessa aongoze mwendo zaidi.
Dereva yule aliweza kutoa ishara ya ndio.
"Jishikilie vizuri zaidi tunahitaji kuongeza mwendo ili kujisaidia alizungumza dereva yule na kumfanya Vanessa aweze kujishikilia kwa nguvu zaidi.
Ndani ya gari lililoweza kuingilia katikati yao uliweza kuonekana mkono ukifungulia mziki na kupunguza mwendo katika gari hilo hali iliyoweza kufanya Daudi ajikute ameigonga bila kupenda kwake na kufanya gari lile liweze kwenda mbele kidogo.
" Sorry sweety ilisikika sauti ya kike ikizungumza huku ikilipapasa lile gari.
Wakati huo nao Daud aliweza kuongeza mwendo zaidi ili aweze kupita upande mwingine kwa haraka zaidi na kuweza kulifikia lengo lake akiwa katika harakati hizo pembeni yaliweza kuja magari mengine madogo mawili na moja liliweza kupita kwa mwendo kasi zaidi huku lingine likikaa upande huo huo na kutoweza kuondoka huku akipunguza mwendo kama gari lililoweza kuwa mbele ya Daud.
"Wakina nani hawa?? Alijiuliza Daud na kupunguza mwendo kwenye scania yake kwa ajili ya kuweza kupiga simu na kutoa taarifa.
Wakati huo yule msichana aliyoweza kuwa ndani ya gari alitoa tena ishara nyingine kwa dereva wa Vanessa ya kuwa alifuate gari hilo lililokuwa likija kwa kasi.
Dereva wa Vanessa na yeye alitoa mkono njee na kumpa ishara ya kuwa ameelewa.
" Ni wakina nani hawa?? Aliuliza Vanessa.
"Siwafahamu lakini kwa kuwa wanatusaidia cha kufanya ni kufuata kile wakitakacho" alizungumza na wakati huo dereva wa gari lile alishaweza kuwa mbele yao.
"Gonga wote nimekwambia gonga wote mpka ulifikie hilo gari la Vanessa" alizungumza Adrian kwa hasira sana.
"Ndyo mkuu" alijibu Daud na kuligonga gari lile lililoweza kuwa mbele yake hali iliyofanya liendee mbele na ligonge gari la Vanessa kidogo kwa nyuma.
Dereva aliyekuwa mbele kabisa ya msafara huo alitoa ishara ya dereva aongeze mwendo huku na yeye akaongeza mwendo wa gari.
"Madam naongeza mwendo zaidi"
"Fanya chochote utakachoweza nahitaji kutoka hapa nikiwa hai" alizungumza Vanessa na dereva yule aliweza kutoa heshima kisha akaongeza mwendo zaidi.
Daudi aliendelea kuligonga gari lile ili aweze kulifuata gari la Vanessa lakini alishindwa ni baada ya gari lile la tatu lililoweza kukaa pembeni nalo kuweza kwenda mbele hivyo akawa anauhitajika wa kugonga magari mawilu kabla hajalifikia gari la Vanessa pia akajaribu kuhamia upande mwingine yanamfuata yote kwa pamoja.
Alishikwa na hasira sana kwani hakuwa na jinsi tena zaidi ya kuendelea kupambana na yale magari huku akiliona gari la Vanessa kwa mbali likipotelea.
"Ujinga gani huu............alibaki akizitizama plate namba za gari hilo na kuzikariri tu. Ghfla alishngaa baada ya kuona yameongeza mwendo kisha yakatawanyika alipotazama mbele tayari walishaweza kumaliza ule mteremko na gari la Vanessa wala halikuweza kuonekana tena.
" Leo nimekufa" alizungumza huku akishika simu yake na kutaka kupiga simu tena.
"Huku ni wapi aliuliza Vanessa baada ya kuona wanaingia katika geti la tatu sasa na hawafiki huko wanakopelekwa hatimaye geti la tano liliweza kufunguka na waliingia kwa magari yao baada ya hapo alishuka kijana mmoja makamo yake ya Rickson na kwenda kuufungua mlango wa gari sehemu aliyokuwapo Vanessa.
Vanessa aliweza kutoa mguu wake njee ya gari kwa wasiwasi mkubwa sana kwamaana alishindwa kuelewa ni wapi ameletwa.
" Naitwa Jimmy Johns wengi wanapenda kuniita Jimmy boy" alijitambulisha kijana yule.
"Njia ni hii tafadhali naomba unifuatwe na usiwe na wasiwasi"
"Nyie ni watu wa nani??? Aliulza Vanessa.
Kabla Jimmy hajajibu swali lake simu yake iliita.
" ndyo bosi yuko salama Ila kidogo ameumia kwenye paji lake la uso"
Baada ya kusikia malalamiko ya nguvu kwenye simu aliitoa karibu na masikio yake kisha akaiweka mbele kidogo ya uso wake.
"Samahani boss haitajirudia tena.......nampa madam Vanessa simu.
Vanessa aliweza kupokea simu ile kwa mashaka kidogo huku akimtizama Jimmy.
"Halo" alizungumza Vanessa.
"Rickson!!!!!! Alijikuta ameita jina hilo kwa mshangao mkubwa sana na kushindwa kuamini.
'Umeenda kufanya nini huko?? Aliuliza Tropina baada ya kumuona Vikram akirudi kutoka sehemu tofauti na aliyokuwapo yeye.
" twende picnic acha uwivu wako " alizungumza Vikram huku akimshika mkono Tropina aliyoweza kuvaa kapero ili kuficha sura yake asiweze kugundulika.
***** ***** *****
Vanessa aliweza kuingizwa ndani ya jumba lile la kifahari na alikuwa upande wa hospital ndogo iliyoko ndani pale.
Aliingia msichana mmoja ambaye aliomba samahani kwa kuchelewa.
"Naitwa Kim Kardashian. Wengi wanapenda kunifupisha na kuniita Kim.
Alizungumza huku akitungua koti lake la kidocta na kulivaa.
"Nitakutibu sasa Madam Vanessa"
"Wewe ndo yule wa kwenye gari?? Dereva wa Vanessa alijikuta akiuliza.
Kim alicheka akimaanisha ndo yeye.
" Obama yuko wapi?? Aliuliza Jimmy
"Alirudia kwaajili ya kwenda kuangalia usalama wa Larry si unajua ni kazi yake Ila nilimuomba backup baada ya kuhisi nitazidiwa.
*** *** *** ***
"Larry" aliita Adrian kwa mshangao mkubwa sana baad ya kumuona.
"Nini umeona mzimu nini mbona umeshtuka hivyo??? Aliuliza Larry ambaye hakuwa akifahamu chochote kilichoweza kutokea kwa siku hiyo.
**** **** *****
" Chumba kimebaki kimoja tu" alikuwa mhudumu wa hotel hiyo ya Palace alitoa maelezo.
"Hapana tunataka viwili" alizungumza Tropina.
"Pinah.............Mimi sitaweza tena kuzunguka na wewe nachukua chumba hicho hicho kimoja kilichoweza bakia kama wewe unataka kwenda kutafuta kingine nenda.
Alizungumza Vikram na kutoa Atm card yake mfukoni kisha akalipia chumba kile.
" huwendi wewe?? Aliuliza Vikram akimtizama Tropina aliyekuwa akijishauri.
Hatimaye aliamua kutembelea na kumfuata Vikram.
"Kuna vyumba?? Ilikuwa sauti ya mmoja kati ya watu watatu walioweza kufika pale
" ndiyo vipo" alijibu muhudumu yule.
Tropina alitaka kumrudia Ila Vikram alimshika mkono na kumpandisha juu ya ngazi ili kuelekea mahali chumba kilipo.
Wakati hayo yakiendelea alionekana mtu aliyekuwa akiwatizama kwa umakini huku akicheka.
Mtu yule aliweza kuelekea mpaka pale reception baada ya kufika aliweza kupatiwa pesa ambzo alizigawa na kumpatia mhudumu yule kisha kumshukuru na kuondoka zake.
"Haloo........ Jimmy.........yap nilikuwa hapa boss aliniomba nimsaidie apate chumba kimoj a tu" alizungumza kijana yule huku akiondoka katika hotel ile.
"Sasa mbona chumba ni kimoja na bafu na choo?? Aliuliza Tropina.
"Inamaana hujawahi ingia katika vyumba vya hotel?? Aliuliza Vikram.
" Nani kasema?? Alizungumza Tropina huku akionyesha kuwa na wasiwasi juu ya Vikram.
"Usiogope sitakufanya chochote kile bila ridhaa yako.... Wewe ingia bafuni ukaoge mimi nashuka chini kwenda kuagiza msosi"
"Kuna haja gani ya kushuka mbali kote huko si upige tu simu utoe order utaletewa" alizungumza Tropina
"Nitawezaje kukaa hapa kwa kutulia wakati we utakuwa uko bafuni ukioga na kama unavyojua watu hawaogagi na................."
"Basi yaishe unaweza kwenda" alizungumza Tropina huku akifungua begi lake na kuchukua mswaki pamoja na taulo.
"Huko pia kuna kuwaga na taulo" alizungumza Vikram.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Najua"
"Sasa kama unajua hilo umelibeba la nini?? Aliuliza.
" amm.....amh
.......... Sipendagi ku share na mtu " alijibu na kuingia ndani akiwa na hasira.
"Uuuwwwhhhh nitaumbuka leo inabidi nijitahidi na asigundue ya kuwa ni mara yngu ya kwanza kufika hapa" alizungumza Tropina.
****** ****** ******
"Adrian" aliita Larry.
Adrian alikata simu yake aliyokuwa akijaribu kumpigia Daudi ambaye hakuwa akipokea simu wala kujibu msg.
"Naam"
"Kama simu yako ina credit unaweza ukanipatia nikampigia mtu? Aliuliza Larry.
"Yas sure"
Kabla Larry hajapokea simu ya Adrian na kupiga simu aliyokuwa akiitaka simu yake iliita.
"Basi ahsanteh" alijibu na kupokea simu yake huku akianza kurud kwenye chumba chake.
"We Vanessa inamaana........
Larry alisita kidogo na kushindwa kuelewa kisha akauliza " Ww ni nani unaongea?? Nani.......................Nani mama yangu amepata ajali???
Baada ya kusikia hivyo Adrian alishtuka sana na kucheka akiamini ya kuwa kazi yake imeweza kukamilika japo kwa kiasi fulani.
***** ****** *****
Wakati huo nao Vikram aliweza kurud ndani ya chumba kile cha hotel kwa kuufungua mlango ule kwa kutumia mgongo wake kwani alikuwa amebeba vinywaji na Glass.
Wakati huo nao Tropina alikuwa akijipaka mafuta huku taulo likiwa kwenye kifua chake.
"Pinah" aliita Vikram na kuweza kugeuka huku akidhani ya kuwa bado yuko bafuni.
Tropina aliweza kugeuka kwa wasiwasi na kujikuta taulo aliloweza kuweka kifuani likadondoka chini kisha akabaki kama alivyoweza kuzaliwa.
Glass pamoja na pombe aliyoweza kubeba Vikram ziliweza kumponyoka na kudondoka chini kisha miguu yake ikamuishia nguvu kujikuta akizifuata glass chini.
Tropina alibaki akipiga kelele huku akiinama na kuokota taulo lake kwa nguvu kisha kukimbilia bafuni na kwenda kujifungia huko.
****** ***** ******
Huku nako alioweza kuonekana Alice aliyekuwa akijiib iba kuingia katika nyumba ya Kina Tropina pasina walinzi wowote kufahamu hilo aliweza kuingia na hatimaye aliingia katika chumba cha Tropina. Alipofika alianza kukagua kagua chumba hicho kama vile aliyekuwa akitafuta kitu fulani aliweza kuchukua kifaa chake cha mawasiliano kisha akakiwekaa masikioni mwake.
"Mnanipata?? Aliuliza huku akikitengenezea vizuri.
" ndiyo ndiyo ilijibu sauti ya kiume. Mtu huyo hakuwa mbali na sehemu ile ya nyumba ya kina Tropina.
"Unaweza ukaweka sasa" alizungumza kijana yule ambaye jina lake ni Calvin.
"Sawa" alijibu Alice na kuweza kutafuta ni sehemu gani nzuri ambayo anaweza kuweka camera katika chumba kile.
Aliweza kuweka katika shelfu moja la nguo lililoweza kuwa karibu pande moja ya kuta za chumba hicho.
"Hapo je?? Aliuliza
" hapo imekaa vizuri Agent Veronica " alijibu Calvin baada ya kuweza kukiona chumb chote cha Tropina.
Alice ambaye jina lake la ukweli ni Veronica alipotaka kuondoka aliiona picha ya Vikram katika chumba kile aliisogelea picha ile kisha akaanza kuishika huku akitabasamu.
"Nmekumiss sana eti Vikram naamini baada ya kupatikana kwa Rickson hatimaye tutaweza kuwa pamoja kama mwanzo tukila kwa pamoja tukicheza pamoja na kufurahi.......na mwisho wa siku nitaweza kukwambia neno ambalo nimekuwa nalo moyoni pindi tu nilipoweza kukuona" alizungumza Alice kimoyomoyo kisha akaichukua picha ile na kuondoka nayo.
***** ***** *****
Larry aliweza kufika katika hospital aliyoweza kuletwa Vanessa baada ya kupata matibabu yote ili kuepusha watu kuwa na mashaka ya juu ya wapi alipoweza kutibiwa.
Huku kim Kardashian akiwa ni docta wa hospital ile.
"Imekuwaje kuwaje hiyo mpaka ukapata ajali?? Aliuliza Larry aliyeweza kuongozana na Adrian ambaye alishindwa kuelewa ajali gani hiyo mbona ameumia sehemu kidogo tu ya kichwa hapo hapo simu yake iliweza kuita alipotizama aliona JENEZA.
" Samahani kidogo" alizungumza na kutoka njee ya pale.
"Tayari nimeshayatuma majeneza yanakuja huko nyumbni"
"Hapana siyataki tena mwambie ayarudishe na asiyafikishe kabisa nyumbani.
" Sasa niyapeleke wapi??!! Aliuliza muuza majeneza.
"Yakae hapo hapo kazini kwako kwani pesa zako si tayari nimeshakulipa" alizungumza Adrian na kukata simu.
"Huyu mjinga Daud kwanini hapokei simu na mbona hakuna taarifa yoyote ya gari kupata ajali.......... Ngoja inamaana hata Tropina na yeye ni mzima" alinyanyua simu yke na kumpigia tena Daud.
"Halo boss........ Ni kwamba.......... Alice..... Alice......."
"Nini tena?? Aliuliza Adrian kwa kuhamaki.
"Hayupo pale tulipoweza kumfungia.......yani namaanisha ametoroka.....kiti kipo pekee yake"
"What???? Hivi wewe unafanya shughuli gani mpaka hayo yote yakatokea yani wewe ni bure kabisa ni bure wewe.......mtafute huyo Alice kabla hajaenda kituo cha polisi na ikiwezekana umuuwe" baada ya kumaliza kuzungumza hayo alikata simu na ghafla iliita simu na jina lilikuwa la Alice.
"Halo!!!
***** ***** *****
Hatimaye usiku uliweza kuingia na alikuwapo Tropina pamoja na Vikram wote wakiwa kimya kabisa huku kila mtu akila chakula chake kivivu na bila kumsemesha mwenzk Ila waliweza kuibiana kwa kutizamana
" Mmmhhhh" aliguna Vikram akijitayarisha kuongea
"Hujaona chochote" alizungumza Tropina
Vikram alitingisha kichwa ishara ya ndiyo.
"Sawa........hata hivyo nashangaa ni kipi kilichoweza kukushangaza wakati ni mara ya pili unaniona"
"Naam" aliitikia Vikram na kukumbuka yakuwa siyo mara yake ya kwanza kumuona Tropina akiwa uchi alishawahi kuingia ndani ya chumba cha Tropina na wakati huo Tropina alikuwa akitoka bafuni na alipofika alitoa taulo lake na kuanza kujipaka mafuta.
"Ahaaaaa" alijibu Vikram na kuufunga mdomo wake.
"Me nitaenda kutafuta chumba kingine wewe utalala hapa mwenyew"
Kwanini??? Aliuliza Tropina.
"Naam"
"Unashangaa nini sasa??? Aliuliza Tropina na kusimama kisha kuelekea alipokaa Vikram.
Vikram alianza kujisogeza na kutaka kutoka katika kochi lile.
" unashida gni wewe mbona kama unaniogopa?
"Hamna" alijibu Vikram.
"Haya nisogelee" alizungumza Tropina huku akimvuta karibu Vikram.
Alianza kufungua vifungo vya shati la Vikram.
Vikram alimshika mkono.
"Unashida gani wewe mjinga?? Aliuliza Vikram na kumtazama Tropina.
"Wewe umelewa eeeee" alizungumza Vikram huku akimshika Uso Tropina na kumpandisha uso juu.
Aligundua ya kuwa Tropina amelewa.
Alimshika na kumuinua kwenye kiti kisha akaanza kumpeleka kitandani.
"Sitaki huko mimi sitaki" alizungumza Tropina huku akijivuta na asitake kuelekea kitandani.
"Tropina embu acha kunivuta tafadhali twende ukalale" alizungumza huku akiendelea kumvuta Tropina ambye alikuwa na yeye akijivuta kutoka mikononi mwake.
Bahati mbaye wote waliweza kudondokea kitandani huku Vikram akiwa chini na Tropina akiwa juu yake.
Vikram alianza kumtoa Tropina juu yake
"Vikram aliita Tropina na kumfanya Vikram aache zoezi lile alilokuwa anataka kulifanya.
Tropina baada ya kumtazama alitabasamu.
" nini?? Aliuliza Vikram
"Nataka nilale kifuani kwako kwa siku ya leo unaweza ukafanya hivyo? Alizungumza Tropina.
Aaaammmmhhhhh sawa alijibu Vikram huku akimsogeza kitandani vizuri Tropina aliyekuwa bado hajalala kitandani vizuri.
Vikram aliweza kumlaza vizuri kitandani kisha akakiweka kichwa cha Tropina kifuani mwake.
Tropina aliweza kupanda tena juu ya mwili wa Vikram.
" Pinah hivyo utanipa shida mama yangu usiku lalia tu kifua changu" alizungumza huku akitaka kumtoa katika mwili wake Tropina.
"Sitaki kwanini mimi nilalie kifua tu nataka nikulalie kote Rickson... Wewe ni mume wangu..... Ninahaki zote juu ya mwili wako" alizungumza na kujilaza vizuri katika mwili wa Vikram.
Vikram hakuweza kuzungumza neno lolote zaidi ya kuweza kuweka mikono yake kiunoni mwa Tropina kisha akatabasamu tu huku akimbusu Tropina kwenye paji lake la uso.
Ghafla Tropina alisimamisha kichwa chake.
"Nini tena??? Aliuliza Vikram baada ya Tropina kuinua kichwa chake.
Tropina alijisogeza juu zaidi kabisa y uso wa Vikram.
" nini shida mama yangu?? Aliuliza tena Vikram.
Tropina alitabasamu na kumtazama machoni Vikram kisha akamwambia.
"Funga macho nikupe kitu"
Vikram alifanya kama alivyoweza kuagizwa.
Vikram baada ya kufunga macho alihisi kuna kitu kimeweza dondoka juu ya kifua chake.
"Pinah.....Pinah....
Pi" aliamua kufungua macho yake baada ya kuona kimya. Alimkuta Pinah akiwa tayari amezidiwa na pombe na hatimaye alilala kabla hajampa kile alichokuwa akitaka kumpa.
Vikram alicheka tu kisha akamlaza pembeni na kutoa shuka juu ya kitanda alafu akamfunika.
Alipotaka kuondoka alishngaa baada ya kushikwa mkono.
"Unaenda wapi??? Aliuliza Pina.
" Nakuja we lala kwanza " alizungumza Vikram.
Pinah alitingisha kichwa kisha akageukia upande mwingine na kulala.
*** **** *** ***
"Unajua sielewi elewi imekuwaje mpaka kwanza ukaondoka mwenyew" aliuliza Larry alipokuwa akimpandisha mama yake ngazi na kumuelekeza chumbani kwake.
"Nataka kupumzika maana umeniuliza maswali mengi sana ambayo mengine siyaelewi kabsa" alizungumza Vanessa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa haaaa"
"Nini tena?? Aliuliza Vanessa.
" Nilisahau kumjulisha Tropina kuwa.......... "
"Yuko na mume wake muache usimwambie chochote" alizungumza Vanessa.
"Sawa"
Maneno yale mfanyakazi mmoja wa nyumba ile aliweza kuyasikia hatimaye aliweza kuingia jikoni na baada ya kuhakikisha hakuna mtu alipiga simu.
"Haloo......ndyo......Vanessa amesema ya kuwa Tropina leo yuko na mume wake.......gari lake Niliweza kuliwekea GPRS kwahiyo mtaweza fahamu liko wapi na pia mkampata Rickson" alizungumza na baada ya hapo aliweza kukata simu.
"Daniel!! Aliitwa na hatimaye aliweza kushtuka na kugeuka na kwa haraka.
"Umemuona Diana??
" hapana" alijibu Daniel aliwa na wasiwasi ya kuwa kuna uwezekano wa kuwa alisikika.
"Wewe.... Aliita Daniel na kumfanya mfanyakazi mwenzak asimame.
" Nini????
"Hujasikia chochote kile??
" Kama nini?? Aliuliza akionekana kutokumuelewa
"Oky nenda" alijibu Daniel
Mfanyakazi yule aliweza kupiga hatua chache na hatimaye na yeye alitoa simu yake kisha akapiga.
"Ndyo nimesikia ya kuwa Tropina yuko na Rickson leo.....
Wameondoka na gari la Tropina.......sawa" alijibu mfanyakazi yule na kukata simu yake.
Jina lake ni Sikitu huyo alikuwa mfanyakazi wa Siri wa Adrian ambaye lolote liwezalo kutokea lazima amtaarifu.
**** **** *****
"Ndyo naelekea huko walikoelekea kwani agent Daniel ameweza kumsikia Larry pamoja na Vanessa wakizungumza hivyo....... Tafadhali naomba backup kwni tunaenda mkamata gaidi la kimataifa na wote tunamuelewa vizuri Rickson mambo gani aliyoweza kuyafanya na yakatikisa dunia. Ila ni vyema kwanza kama tutaweza kumfahamu Rickson kbla ya kumkamata ili tusije tukakuta tunamkamata ambaye siye Alikata simun na kuweza kuongeza mwendo.
Wakati huo Rickson alikuwa njee ya hotel huku akipata pata upepo wa mahali pale.
" Siku ya leo itakuwa fupi sana nani kwasababu Niko tu na Pinah........huyo mjinga kaondoka nini mbona simuoni alizungumza huku akiendelea kutizama tizama mbele yake.
"Mr Ricky" aliita kijana yule ambaye umri wake uliweza kuendana na Rickson na ndiye aliyeweza kufanya Rick akapata chumba kimoja na Tropina.
Walikaa kwa pamoja na hatimaye walianza kuzungumza.
"Kitambo kidogo hatujaonana" alizungumza Lewis.
"Ni kweli vipi wazima wote nyumbn?? Aliuliza Vikram.
" ndiyo na wamekumiss sana si unajua ni miaka mingi huwajapata kukuona"
"Ni kweli baada ya tukio lile kutokea sijawahi kufikaga tena nyumbani"
"Ila wanafuraha sana kwasababu maisha yako kwa sasa yko salama na wamesema wapo tayri maisha yao yawe hatarini Ila ya kwako yaendelee kuwa katika hali ya usalama kwani uliweza kuwasaidia sana na kuonyesha hivyo me nimejitolea maisha yangu kwaajili yako"
Mazungumzo yale yaliweza kuendelea kwa kitambo kidogo na baada ya hpo alionekana Vikram akipanda ngazi taratibu kabisa huku akiwa anakumbuka sauti ya mtoto Mdogo ikimuita.
"Kaka......kaka...Rickson......tafadhali unaweza kunisaidia" kumbukumbu zile ziliweza kuambatana na milio mingi ya risasi ghafla akaumbukumba mlipuko mkubwa sana ulioweza kutokea"
Rickson alijikuta hawez kutembea na anataka kudondoka lakini alidakwa na Tropina.
"Kwanini umechukua muda mrefu kurudi ndan......na mbona upo katika hali hiyo....kipi kimetokea huko njee" aliuliza Tropina huku akijitahidi kumbeba Rickson na kumpeleka chumbani.
Wakati huo Lewis alikuwa akikitizama chumba kile alichokuwepo Vikram.
"Nitaweka umakini zaidi katika maisha yako kama Baba yako alivyoweza kuweka umakini juu ya familia yangu na hatimaye akaweza kupoteza maisha kwaajili ya kumlinda mke wangu ambaye alikuwa mjamzito" aliongea Lewis kisha akaingia ndani ya gari lake na kuongezea zaidi.
"Nitabaki hapa nikikulinda mpaka kesho ulale salama Rickson" alizungumza Lewis.
Ghafla simu yake iliita.
"Halo!!! Jimmy......siwezi kuja leo kambini namlinda Rickson tutaonana kesho pakishakucha nitaondoka" Alikata simu.
Alice alishaweza kufika maeneo yale huku akimpigia simu Danielle.
"Nimefika tayari ni katika hotel ya ............................" Aliweza kutoa taarifa ni wapi walipo.
Nitaingia kwenda kutafuta ni chumba kipi walichopo ili niweze kumfahamu Rickson nyie mkija ni kumkamata tu. Alikata simu na kutoka ndani ya gari aliangalia kulia na kushoto baad ya kuona hamna mtu anayeweza kumuona alivaa kofia na kuishusha chini zaidi hivyo ilifanya sura yake isiweze kuonekana lakini wakati akiyafanya yote hayo aliweza kuyafanyia mbele ya gari la Lewis ambaye alibaki akimtizama Alice.
"Anashida gani huyu??? Alijiuliza huku akiendelea kumfuatilia kwa macho hatimaye aliweza kupotelea katika macho yake baada ya kuingia ndani ya hotel ile.
Lewis akiwa anaendelea kunywa juice yake aliweza kushtuka baada ya kukumbuka ya kuwa aliweza kuona bastola katika mwili wa Alice na ilikuwa nyuma ya mgongo wake.
" hivi kwanini nilikuwa mjinga" alizungumza na kutoka ndani ya gari lake kisha kuelekea mahali ambako Alice aliweza kutokomea.
Wakati huo ndni ya chumba alikuwapo Tropina pamoja na Vikram aliyeweza kujilaza kifuani mwake.
Vikram machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakimtoka na hatimaye usingizi ulimpitia akiwa katika hali ile.
Tropina aliweza kumnyanyua na wakati anamnyanyua ndyo wakati ambao Alice alikuwa akipanda magorofa na kuelekea katika chumba alichokuwa Tropina na Vikram huku nako Lewis akipanda ngazi kwa haraka zaidi kwaajili ya kuweza kuelekea chumba walichopo.
Alice aliweza kupanda taratibu kabisa huku akihakikisha ya kuwa hakuna mtu yoyote yule anayeweza kumuona yeye wakati huo nao Daniel alikuw nyuma na akija na baadhi ya maaskari.
Baada ya Tropina kumuweka kitandani Rickson aliweza kuingia chooni kwaajili ya kujisafisha wakati akiufungua mlango wa kuingia ndipo napo Lewis alifungua mlango wa kuingia ndani ya chumba kile. Alipotizama dirishani alifanikiwa kuuwona mkono mmoja hivyo akaamini ya kuwa muuwaji Huyo ndo anapanda alimtizama Rickson ambaye uso wake ulikuwa huko huko dirishani hivyo angeweza kuonekana kwa ukaribu zaidi wakati Alice ndo anachomoza kichwa chake tayari lewis alishafanikiwa kuiona switch ikiwa karibu na yeye na alizima taa hivyo Alice hakufanikiwa kumuona Rickson wala kugundua ya kuwa kulikuwa na mtu kitandani bali aliiona mwanga umewashwa katika mkono wa mtu ambaye aliweza kuuwash karibu na uso wake.
Lewis alichukua kiberiti chake cha gesi na kuweza kukiwasha na kukizima karibu na uso wake hivyo kufanya Alice aweze kumuona yeye kwa mawenge mawenge baada ya hapo alitoka njee na Alice aliingilia dirishani na kumfuata Ila wakati anaukaribia kuufikia mlango wa kutoka njee ndipo Tropina na yeye aliweza kuufungua mlango wake na kutoka njee ya chooni pasina kutambua chochote hapo nako Rickson aliweza kuyafumbua macho yake baada ya kuwa na hisia ya kuwa kutakuwa na mtu mwingine tofauti na Tropina.
Walikimbizana mpaka njee ya jengo la hotel baada ya kufika hapo Lewis aliweza kuvua koti lake huku akipambana na Alice aliyekuwa akihitaji kuiona sura yake. Alice hakuwa na uwezo mkubwa juu ya Lewis hivyo kila alipoweza kujaribu kupambana naye alijikuta akipigwa tu. Lewis baada ya kulivua koti lake aliweza kulishika kwa mikono miwili na hatimaye aliweza kumfungia nalo mikononi kisha akamuweka kwenye kibambaza na kumtazama.
"Nani kakutuma??? Alimuuliza Alice ambaye alikuwa akijitahidi kufurukuta ili atoke mikononi pale.
Aliweza kumpiga teke Lewis sehemu muhimu kabisa za mwili wake na kumfanya amuachilie Alice alitumia upenyo huo kwa kumpiga tena teke jingine na kumfanya adondoke chini mazima.
Alice alikimbia huku akijitahidi kulifungua koti ambalo aliweza kufungiwa nalo mikononi mwake Lewis na yeye aliweza kuamka na kuchukua simu yake mkononi kisha kumpigia Rickson.
Rickson hakuweza kupoke simu hiyo kwani alikuwa amelala na Tropina pia simu ilikuwa silence.
Lewis alimpigia tena Jimmy na kabla Jimmy hajapokea simu alishtukia amepigwa na kitu kichwani mwake hali iliyomfanya aanze kusikia kelele za kama filimbi iliyoweza kupulizwa masikioni mwake na kumfanya asikie sauti ya Jimmy kwa mbali San.
" haloo...halow
.......Lewis" aliita Jimmy baada ya kusikia kimya.
Lewis aliweza kudondoka chini n hapo aliweza kumuona Daniel aliyekuwa amempiga na nondo nzito kichwani mwake.
Lewis akijitahidi kusimama kwaajili ya kupamba na Danielle aliweza kuligwa teke jingine na kumfanya adondoke mbali na simu aliyoweza kushika bila Alice na Danielle kuelewa ya kuwa kuna mtu anayeweza kuwasikiliza kupitia simu aliyoweza kuipiga Lewis.
"Nafikiri Lewis yupo kwenye matatizo alisema Jimmy akimwambia Doctor Kim.
Waliinuka wote kwa pamoja na kuweza kuwasha simu yao moja ambayo sehemu yoyote Lewis alipo wanaweza kumfikia.
"Mpigie boss simu" alizungumza Jimmy akipokea simu ile kutoka kwa Docta Kim na kuingia ndani ya gari wote kwa pamoja.
"Hapokei simu yake" alizungumza Doctor Kim
"Unafikiri atakuwa salama??? Alijiuliza huku akimtizama Jimmy aliyekuwa yuko kwa mwendo kasi kwaajili ya kuliondoa gari eneo lile.
**** ***** ***
Rickson aliamka tena na kuelekea moja kwa moja hadi dirishani kwake ambako akijaribu kutazama kwa chini kama kuna usalama kwni alijikuta tu ghafla hana tena usingizi. Baada ya kuhisi hali ya usalama aligeuka nyuma na kumtazm Tropina aliyekuwa kapitiwa na usingizi wakati yeye akitizama nyuma yake alikuwa akipita Danielle pamoja na Alice wakiwa wanamburuta Lewis aliyekuwa kalowa damu mwili mzima.
Labda kwasababu nimelala naye kitanda kimoja ndo maana sina usingizi alijisema na kucheka mwenyewe.
" na mwanamke mwenyew wala hana hata wasiwasi ya kuwa amelala na mwanaum amelala usingizi tena com4table kabisa me ndo nahangaika tu hapa mwenyewe" alitingisha kichwa chake kisha akatizama njee ambako alifanikiwa kuviona vivuli vya watu wawili wakiburuza kitu huku akiamini ya kuwa ni walinzi wanaburuza uchafu na kuutoa njee ya hotel ile alirudi kitandani lakini aliiona simu yake iliyokuwa karibu na Tropina aliinua mikono yake na kuanza kupeleka karibu na simu yake Tropina aliushika mkono wake na kuulalia akimini ya kuwa Rickson alihitahi aulalie mkono wake Rickson alitabasamu tu na kujikuta akimtizama na kucheka hivyo hakuwez kuichukua tena simu yke aliyafunga macho yake na kumsogeza Pinah karibu kisha akalala tena kwa mara nyingine.
**** **** ****
Vanessa akiwa katika chumba chake aliweza kuingia Larry.
"Kuna shida gani?? Aliuliza Vanessa.
" Huyo mtoto wako ajaja??? Aliuliza Larry.
"Adrian!!
" ndiyo "
Vanessa alimtizama Larry bila kumsemesha kitu.
"Nini mbona unanitizama kwa mimacho mikali hivyo?? Aliuliza Larry.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Unaelekea wapi na huo mto pamoja na shuka lako?? Aliuliza Vanessa.
"Since mtoto wako bado hajaja ntalala hapa leo na wewe kwasababu unaumwa sitaki uzidiwe.......na sitakagi kushare chochote na yeye kwahiyo nimekuja na mto wangu pamoja na shuka hivyo nitalala kwenye kochi tu. Alizungumza na kuelekea kwenye kochi.
Baada ya kupanda na kujifunika Vanessa alizima taa
" weeeee Vanessa.....washa taa mimi naogopa giza" alizungumza Larry aliyeweza kushtuka sana baada ya taa kuzimwa kwa muda mfupi tu akioneka ni mwoga sana akiwa gizani.
Vanessa alimtizama Larry bila kuzungumza chochote na kubaki akimtizama Larry ambaye moyo wake ulikuwa ukimdunda kwa haraka sana.
***** ***** *****
Jimmy na doctor Kim waliweza kufika eneo alilokuwapo Lewis.
"Hakuna signals kabisa alisema Jimmy akijaribu kukiweka chombo kile katika hli ambayo ingeweza kuleta signal.
" hiyo imeleta alizungumza na Jimmy na ghafla alinyamaza.
"Yuko wapi sasa?? Aliuliza Dr Kim.
"Imezima chaji" alisema Jimmy.
"Sawa inabidi tufanya jitihada za kumtafuta Lewis atakuwa ndani ya hotel hii hii. alizungumza Dr Kim na kushika njia yake huku nako Jimmy akitafuta pa kuelekea.
" mfunue tumone" alizungumza Danielle.
Alice aliweza kutoa kitambaa kilichokuwa juu ya uso wa Lewis na kuweza kumuona.
"Mpige picha kisha umtumie mkuu na umwambie tumemaliza kazi" alizungumza Daniele na Alice aliweza kutoa simu yake kisha akampiga picha Lewis. Mwanga wa simu yake uliweza kumfanya Jimmy ausikie na kuuona kutokana na kutoa sauti.
"Nafikiri nimewapata" alizungumza Jimmy akimpa taarifa Dr Kim.
"Sawa nimekupata......kuwa makini" alizungumza na kuanza kuitizama simu yake ambayo iliweza kumpa signal mahali alipo Jimmy.
Jimmy aliwez kupita na simu ya Alice kisha akampiga sehemu ya shingo Daniele na kumfanya azimie hapo hpo bila hata kuchukua dakika kisha akapotelea gizani hali hiyo ilitokea kwa haraka sana hali iliyomfanya Alice ashindwe kuelewa ni upepo au ni nini kimemtokea mbona ghafla sana. Ghafla vilisikika ving.ora vya police vikija eneo lile hali iliyomfanya Dr Kim ajifiche kwni vilikuwa vikielekea kule alipokuwa akielekea yeye. Jimmy na yeye baada ya kusikia ving.ora vile vya polisi aliweza kumtazama chini Lewis ambaye alishindwa kujua amsaidiaje.
Huko nako Rickson aliyafumbua macho yake baada ya kusikia ving.ora vya polisi aliamini hali si shwari hakutaka kumuamsha Tropina hivyo alienda akachungulia dirishani na hapo aliweza kuliona gari la Lewis.
"Lewis atakuwa kwenye matatizo" alizungumza na alipotaka kutoka Tropina aliamka.
"Kuna nini??? Aliuliza
Rickson alitoa kitambaa kwenye suruali yak kisha akamfuata na kumshika nacho usoni.
" hakuna tatizo wewe lala"
Tropina aliponusa tu harufu ya kitambaa kile aliweza kulala hapo hapo.
Alichukua simu yke na hapo alikutana na missed call pamoja na msg ya Dr Kim.
"Tunahisi Lewis yupo kwenye matatizo hivyo tunaelekea kumsaidia"
"Shit...... Aliwasha simu yake na hatimaye aliweza kuziona signal tatu tu ya Obama iliyokuwa iki move ka speed kisha akaona ya Dr Kim pamoja na Lewis.
Jimmy anashid gani mbona sioni signa l yake. alizungumza huku akifungua begi lake na kutoa mavazi mengine ambayo aliyavaa na kwenda kufungua dirisha lake Ila alipofika aliona tayri kuwa limeshafunguliwa. Alitizama chini na tayari kulikuwa na watu wachache tu pale. Alishukia kupitia dirishani pale taratibu kbisa pasina mtu yoyote kumuona.
Wakati huo Lewis alikuwa ameishikilia simu yake mkononi mwake ni baada ya kuiokota tena.
Polisi waliingia na kumkamata kisha wakaondoka naye bila Alice wala Danielle kupand gari hilo.
Wao wlipanda gari la nyuma na kuwafuata nyuma wakati huo Danielle alikuw akijishika sehemu aliyoweza kupigwa na Jimmy.
Wakati huo Rickson alishafika na kuweza kumuona Lewis akipandishwa katika gari la polisi wala hakumuona Alice.
Wakati wakipanda Obama alishafika na gari lake eneo lile hata na yeye tukio lile aliweza kuliona.
Dr Kim pamoja na Jimmy na wao pia waliona.
Kwa walivyomuona waliamini ya kuwa uwezekano wake wa kupona ni Mdogo sana.
Ghafla Jimmy aliweza kumuona Dr Kim aliyekuwa akimfuata Rickson ambaye na yeye aliweza kuonekana na Obama aliyekuwa akishuka kwenye gari na kumfuata Rickson.
Wote waliweza kukutana sehemu moja.
" tufanyaje??? Aliuliza Obama.
"Namuhitaji Lewis atakama ni marehemu namuhitaji" alizungumza Rickson kisha wakitizama na kuanza kupanga plan kumchukua Lewis kabla hajafikishwa huko polisi.
Rickson akipanda gari moja na Obama alafu Dr Kim akapanda gari la Jimmy na kisha Jimmy akionekana kutokomea kwa kukimbia.
Waliweza kuwasha gari wakiwafukizia polisi kwa nyuma pasina mtu yoyote yule kufahamu hilo. Walipoweza kuondoa gari lao hap hapo liliweza kuingia gari jingine na alishuka Adrian pamoja na Daud.
Adrian alipokea kofia ambayo alipewa na Daud kisha akaivaa na kuishusha chini kabisa ili kuficha sura yake.
"Haaaaaaaa hivi wewe umeelewa kilichotokea hapa?? Aliuliza mtu mmoja au mmoja kati ya wale wateja katika ile hotel akimuuliza mwenzake.
" Me pia sielewi nilisikia ving.ora vya polisi ndo nikafika hapa lakini wamesema eti waliyemkamata ni.......alitizama kulia na kushoto kama kuna atakayemsikia wakti huo Adrian masikio yake yalikuwa sambamba na mazungumzo yao.
"Eti gaidi la kimataifa..........alafu kabla ya kusikia ving.ora vya polisi alizungumza huku akitizama kulia na kushoto kama kuna anayeweza kumsikia tena.
" Ki ukweli me nilikuwa njee muda wote ila sitaki kuwa shahidi.....alikuwa binti mmoja na kijana mmoja walimpiga sana huyo jamaa wanayesema ni gaidi alafu walimuita Ric....Ric........
"Rickson!! Alidakia Adrian kwa mshangao.
Mama yule aliweza kushangaa na kushtuka huku akijaribu kumtazama Adrian aliyekuwa amefunika uso wake.
" Rickson sindiyo wametaja hilo jina"
Alitingisha kichwa ishara ya ndiyo.
Adrian na Daud waliondoka hotelin pale kisha wakapanda ndani y gari.
"Tuelekee wapi???? Aliuliza Daud.
" Namtaka Rickson lazima tumchukue mikononi mwa polisi kabla hajafika kituoni"
"Sawa" alijibu Daud.
Alice akiwa ndani ya gari na Daniele aliweza kushtuka kitu.
"Kuna nini??? Aliuliza Danielle.
"Waambie wasimama hao wa mbele......Gaidi Rickson aliokota simu yake sasa anaweza akafuta kila kitu na tukose ushahidi juu yake.
Wala hakuwa amekosea kitu Alice. Lewis wakati huo alishaweza kuirestore simu na ilikuwa imefikia Asalimia 58.
Gari lilisimamishwa na Alice aliweza kushuka chini na Danielle haraka haraka wakiiwahi simu ambayo tayari ilishaingia 87? .
" kuna nini?? Aliuliza askari mmoja aliyekuwa amekaa na Lewis ambao wao waliamini ya kuwa ni Rickson.
Alipofika alimshusha yule askari chini kisha akaiona simu ikiwa mikononi mwa Lewis. Lewis alimtizama na kutabasamu tu kwani simu ilishafikisha asilimia 95.
Alice aliichukua simu ile huku akijaribu kuizima na bado asilimia ziliendelea kusoma mikononi mwake.
Danielle alichukua na kutoa betri lakini tayari zilishabaki asilimia 1 tu simu kumalizima kurestore hivyo ilifika 99?.
Lewis alicheka tena safari hii alicheka kwa sauti Kubwa iliyoweza kupenya masikioni mwa Alice na kumkasirisha zaidi.
Alice alienda akamtoa ndani ya gari la polisi na kumdondosha chini kisha akaanza kumkanyaga na mabuti aliyoweza kuyavaa.
Askari waliweza kutoka na kuanza kumshika Alice ili asiweze kumpiga Lewis.
Walikuja askari wengine wawili na kumchukua Lewis kisha kumuingiza ndani ya gari la polisi kisha mmoja akakaa na mbele kwa dereva na mwingine akakaa na Lewis.
Gari liliwashwa huku likimuacha Askari mmoja aliyekuwa amemshikilia Alice pamoja na Daniele.
"Acha ujinga tafadhali alizungumza Daniell na kuingia ndani ya gari huku akifuatiwa na yule askari pamoja na Alice ambaye jin lake halisi ni Veronica.
Baada ya msafara wa polisi kuwafuata nyuma na kuweza kulifuata gari moja lililoweza kutangulia na Lewis.
Walionekana watu wawili chini walioweza kuvuliwa nguo zao na kubaki na bukta pamoja na flana wakiwa wamezimia huku vikionekana viatu vya vyeusi vya mtoto wa kike maeneo yale.
Akipiga simu.
No.1 imeisha tuingie plan no 2.
" Sawa" alijibu mtu mmoja ambaye aliweza kuongeza kasi ya mwendo wa pikipiki yake na huyo alikuwa Jimmy.
"Sasa haya magari mawili nayafanyaje??? Alijiuliza Dr Kim huku akijaribu kuchakachua akili yake.
****** ******* *******
Aliweza kuhamisha gari moja na kulipeleka kichakani ambako hakuna mtu atakayeweza kufahamu ya kuwa kuna gari eneo hilo.
Aliweza kulirudia gari lingine kisha akaweka muziki na kuweka spidi za kutosha kisha akawasha gari na kuondoka eneo lile
Aliweza kulipita gari lakina Daud pasina yeye kutambua ya kuwa ameweza kulipita gari la maadui wengine wanaoweza kumuwinda Rickson.
Daudi alishtuka baada ya gari lile kupita kwa mwendo kasi sana.
" huyo aogopi kufa au" alizungumza kimoyomoyo ghafla alishtuka baad ya kuona plate nama za gari lile.
"Boss" aliweza kumuita Adrian ambaye alikuwa katika mawazo mazito sana..
"Gari gari......plate namba za hilo gari lililoweza kupotelea mbele ndo lile gari ambalo liliweza kunizuia mimi nisimuuwe Vanessa.
" liko wap hilo gari??? Aliuliza Adrian.
"Limepita hapa kwa kasi"
"Na wewe ukiwa wapi mpaka likupite kwa kasi namna hiyo eti?? Aliuliza kwa ukali Adrian na kumfanya Daudi aongeze mwendo kwaajili ya kufukuzia gari ambalo tayri lilishaweza kufika mbali sana na upeo wa macho yake.
***** ***** ****
" Linaelekea wapi hilo gari?? Aliuliza askari mmoja aliyekuwa ndani y gari la Kina Alice.
"Kwanin?? Aliuliza Alice.
" njia ya kuelekea kituoni siyo hiyo" alizungumza na kufanya Alice atizame njee kwa makini.
"Wanaelekea wapi hawa?? Aliuliza askari mwingine aliyekuwa askari wa karibu sana na Inspector George Pesambili aliyeweza kuwa classment wa Tropina.
" Mnajua tukifanya uzembe akija Inspector George hatuna cha kujitetea weka king.ora na uombe backup waje kutusaidia kwa haraka zaidi haturuhusiwi kumpoteza huyo Rickson.
Ndyo alijibu Askari mmoja na kuweza kuweka king.ora cha polisi juu huku akipiga simu kwaajili ya kuweza kuwataarifu askari wengine.
"Mbona hafiki huyu??? Aliuliza Rickson.
" Lewis hali yake inaazidi kuwa mbaya" alizungumza Obama.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo hapo Jimmy aliweza kutokea kisha akawapita na pikipiki kwa kasi huku akiwa ishara ya vidole vitatu ya kuwa kila kitu kipo sawa.
"Nahitajika kurudi nyumbani kabla Pinah hajaamka na kunikosa ndani kwahiyo tutafanya kwa haraka zaidi" alizungumza Rickson na kuongeza mwendo wa kwenye gari.
alipoweza kufika mbele aliongeza mwendo zaidi.
"Ongeza na wewe mwendo" aliamuru askari wa karibu na inspector George.
"Ndiyo" alijibu na kuongeza mwendo zaidi.
"Fanya hata kuwapita hao askari wapumbavu hatutakiwi kumpoteza Rickson.................Danielle!!!
" naelewa kaa kimya" alizungumza Daniele na kutaka kuongeza mwendo ghafla gari lao liliweza kugongwa kwa nyuma na kufanya ligonge gari lililoweza kuwa mbele yake alilokuwa anataka kulipita.
Alishuka ndani ya gari Dr Kim kisha akaenda kushika upande wa nyuma ambako aliweza kupagonga alibinua Pete yake ambayo aliweza kuivaa mkononi na kufanya itokee ncha aliweza kulitboa tairi lile mara tatu kisha akairudishia Pete yake katik hali ya kawaida kabisa.
"Ooohhhh samahani....
Samahani jaman..
Bahati mbaya tu alizungumza huku sura yake akiwa ameificha na alishuka Alice pamoja na Danielle wakiwa na askari.
Imekuwaje mpaka ukagonga gari inamaana huoni au??? Alizungumza Alice kw hasira.
" Samahani " alizungumza na kwenda kwenye gari lake kisha akatoa business card na kumpatia Alice.
"Namuwahi mama yngu ni mgonjwa garama zote za uharibifu nitalipia alizungumza na kuelekea kwenye gari lake kisha akaliwasha na kuliondoa eneo lile.
" Sisi tutatangulia alizungumza askari mmoja na kish kwenda kupanda kwenye gari lao kwaajili ya kuondoka lakini walishanga baada ya kuona ya kuwa tairo lao la nyuma pia lina pancha.
Dr Kim alifungulia mziki baada ya kuondoka eneo lile huku akikumbuka ya kuwa aliweza pia kuharibu gari la askari hivyo alishaweza kupunguza misafara miwili.
"Jimmy..........clear huku nimesafisha"
"Oky nimekupata" alijibu Jimmy na kupunguza mwendo wa pikipiki yake baada ya kupita gari lililoweza kumbeba Lewis aliweza kukaa nyuma yake polisi waliowez kumfuatia walishangaa baada ya kuona pikipiki iko mbele yao na inatawala Barabara nzima.
"Ni nini mbona unayumba yumba??? Aliuliza afande Thobias aliyekuwa na ukaribu mkubwa na inspector George.
" nashindwa kuelewa kuna pikipiki ngap mbele yangu maana kila nikijaribu kukwepa kwa upande mwingine naiona tena.
Afande Thobias alipoweza tazama mbele hata yeye alishindwa kuelewa.
Hapo hapo simu yake iliita.
"Hakikisha ya kuwa mnampata Rickson kwani akipotea tutakuwa tumechokoza nyuki kwenye mzinga wake kuliko apoteee piga risasi mpaka wafe wote" alitoa amri hiyo Alice.
"Sawa" alikata simu.
"Pigeni risasi wote" alizungumza na kutazama mbele ambako alibaki mdomo wazi wala hakukuwa tena kitu chochote "
"Wameenda wapi???? Aliuliza afande Thobias na kufanya maafande wengine na wao watazame mbele.
****** ****** ****
" Vikram...... Vicky.......aliita Tropina baada ya kumkosa Vikram kitandani. Wakati huo nao Vikram alikuwa akirejea chumbani kupitia njia ile ile aliyoweza kutoka nayo bila kujua ya kuwa tayari
Tropina na yeye alikuwa akimtafuta.
"Ameenda wapi huyu??? Aliuliza huku akielekea dirishani ambapo Vikram alikuwa na yeye akingilia.
Alipoweza kukaribia kufika dirishani simu yake iliweza kuita hivyo aliifuata na wakati huo nao Rickson aliweza kutokea dirishani.
"Mmmhhhh mbona Vanessa ananipigia simu sasa hivi kuna tatizo aliuliza huku akipokea simu.
" haloo"
Rickson aliweza kuingia ndani kwa utaratibu kabisa kisha akaingia bafuni pasina Pinah kuhisi chochote kile.
Baada ya kumaliza kuzungumza na mama yake alikata simu na Rickson alitokea bafuni.
"Wewe!!! Aliita kwa mshtuko.
" nini!!!
Umetoka wapi??? Aliuliza Tropina
"Kwani huku wapi?? Aliuliza akifunga taulo lake.
" nimekutafuta na kukuita sana lakini hukuitika"
"Siitikagi nikiwa uwani" alizungumza Vikram na kuendelea kupiga hatua za mbele.
"Lakini mbona niliingia...........
" uliishia bafuni.....Ila mimi nilikuwa uwani" alizungumza Vikram .
"Ila" Tropina alibaki akijiuliza huku akimtizama Vikram.
"Nataka kubadilisha nguo vipi nitoe tu" alizungumza Vikram.
Tropina alishtuka na kugeukia upande mwingine hapo aliona dirisha likiwa wazi.
Alinyoosha mkono dirishani na hapo Vikram aliweza kuona alibaki akimtizama tu Tropina kwa makini sana huku sura yake ikiwa imebadilika.
Alikumbuka ya kuwa mara ya mwisho alimuona Vikram akiwa ameamka na alipomuliza kwanini alimwambia arudi kulala.
***** ****** ******
Kulikucha na hakukuwa na mtu yoyote yule kitandani.
Tropina alipiga simu.
"Vicky umeenda wapi tena?? Aliuliza Tropina.
" aaaammmmhhhhh kuna rafiki angu wa kiume nimekuja kukutana naye asubuh asubuhi hii kwasababu anamatatizo kidogo..... Wewe tangulia nyumbani tutakutana"
"Lakini......haloo.... Haloo
....mbona amenikatia simu kwa haraka hivyo. Na tumaini yuko salama.
alizungumza Tropina huku akikaa kitandani.
**** **** *****
" unazungumza upumbavu gani??? Mnawezaje mkampoteza mtu ambaye tayari alikuwa mikononi mwenu.aliuliza inspector George
"Samahani mkubwa kidogo tulichezewa mchezo ambao ulituweka katika hali ya sintofahamu" alijitetea Tobias
"Huo upuuzi ndyo ambao sitaki kuusikia mlienda zaidi ya maaskari 6 lakini mkashindwa kumfikisha mtu mmoja tu kituoni nyie ni wajinga kabisa tena mtapata adhabu wale wote mlioweza kwenda huko" alizungumza inspt. George
Hapo hapo simu yake iliita.
"Haloo........ndyo mkuu.......nitalifanyia umakini jambo hilo.....naahidi unipatie wiki moja tu nitamleta Rickson"
**** **** ***
"TUMEJITAHIDI kufanya kila tuwezalo lakini bado amepotea tena mikononi mwetu" alizungumza Veronica ambaye ni Alice.
"Yani nyie wote watatu pamoja na maaskari lakini hakuna kitu mmefanya mnazubutuje kuzidiwa ujanja na mtu mmoja......Calvin's"
"Naam mkuu"
"Wewe ulikuwa wapi????
" Samahani mkuu nilikuwa mbali kidogo na jiji hili.....nil......."
"Nyamaza mpuuzi ukubwa wewe........ Serikali inawahudumia nyie kwaajili ya kumpata Rickson ni zaidi ya miaka 4 sasa na bado tu mnashindwa akili na mtu mmoja" alizungumza mtu ambaye alionekana ndiye mkuu wa shughuli hiyo.
"Daniel umekaa katika nyumba ile kwa mwaka wa tatu sasa lakini hauna taarifa kamili juu ya Rickson ilihali wote walioko pale ndani wanamfahamu umeenda kula tupale sindiyo???
" hapana " alijibu Danielle
"Na wewe huu ni mwaka wa pili uko na mahusiano na Saruni lakini hata sura ya Rickson huifahamu kazi yako ni kustarehe naye tu basi sindiyo"
"Hapana mkuu shida ni kwamba ni wasiri sana Saruni ni msiri kila siku namuuliza kama ana ndugu yoyote katika maisha yake lakini huwaga anasema hana ndugu yoyote hivyo inakuwa vigumu mimi kumuuliza direct anaweza akanigundua" alizungumza Veronica.
***** ****** *****
Chumba alichokuwepo Lewis baada ya kupatiwa matibabu zlisikika kelele na kuwa fanya wote waliokuwa sebleni wakijadili jambo waanze kukimbia na kuelekea chumba hicho.
"Imekuwaje tena"
"Amefanyaje???
"Lewis!!
Kila mtu alizungumza lile lililoweza kumtoka mdomoni mwake.
Dr Kim alielekea mpaka pale alipo kisha akaanza kumtazama machoni na kusikilizia mapigo yake ya moyo.
Alidondosha kipimio chake chini na miguu ikamuishia nguvu.
" nini" aliuliza Vikram.
"Tuambie ni nini?? Aliuliza Jimmy.
" hawezi akawa amekufa bhana" alizungumza Obama na kwenda kuyasikiliza mapigo ya moyo ya Lewis.
Na yeye alibaki akikodoa macho tu.
"Embu sogea alizungumza Jimmy na kusikiliza mapigo ya moyo.
" imekuwaje??? Aliuliza Vikram huku na yeye akipiga hatua za kwenda mbele na kumtizama Lewis.
****** ***** ****"
"Imekuwaje mbona kichwani umefungwa hivyo?? Aliuliza Tropina baada ya kumuona Vanessa na wakati huo Adrian na yeye ndipo alipokuwa akirudi nyumbni.
" unajua ikitokea ya kuwa unamfuga mbwa ambaye anajaribu kujitutumua na kutaka kuwa juu yako basi mbwa huyo hana faida tena kwako cha kufanya ni kumuonyesha tofauti ya kuwa yeye ni mbwaa na wewe ni mmilili wake. Alizungumza Vanessa na maneno hayo Adrian aliyasikia na yalimkera sana kisha akaanza kurudi alipoweza kutokea.
"Adrian.........
Jana uliondoka hospital bila kunijulia hali na sasa hivi pia unataka kuondoka bila kunijulia hali.......... .........
Sidhani kama uwepo wangu wa kuendelea kuwa hai na katika hali ya usalama imekuridhisha wewe" alizungumza Vanessa.
"Sasa kama unajua uwepo wako haujaniridhisha unaniuliza ya nini??? alizungumza Adrian na kutokomea zake mlangoni.
" mpuuzi mkubwa huyo.......... Sijawahi kushindwa na mwanamk wala sitawahi kushindwa na mwanamke lazima nitakuuwa tu hata kama ni kwa mikono yangu mimi mwenyewe nachukia sana kauli ya kuitwa mbwa katika maisha yangu " alizungumza Adrian na kuweza kufuta chozi moja lililoweza kudondoka kutoka machoni pake.
***** ***** ****
Alice aliweza kukutana na Saruni na safari hii alienda akiwa na sura ya kazi kabisa. Saruni aliamini ya kuwa yeye ndiye anayeweza kamtumia Alice ili kumsaidia Rickson pasina kufahamu ya kuwa yeye ndye anayeweza kutumika kwaajili ya kumpata Rickson.
"Imepita wiki sasa hata wala sijakutia machoni ulikuwa wapi????
" Busy kumtafuta Rickson " alijibu huku akimtizama.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mbona umeshtuka Kaka yake Rickson............... We ulifikiri ya kuwa unanitumia mimi....
........hapana wewe huwez kunitumia mimi bali mimi nakutumia wewe kwa ajili ya kumpata Rickson.........sasa nimetumia njia ya kubembeleza mpaka nimechoka sasa naona ni vyema kama nitatumia force kwasababu tayri nina uhakika ya kuwa unamfahamu Rickson...
Saruni alishngaa baada ya kuona wamekuja wanaume wawili na kuweza kumfungia kamba kitandani alipoweza kujilaza.
'Na unajua kwanini sikuwahi kukwambia chochote kuhusu Rickson ni kwasababu nilishakutambua toka mwanzoni na nilijua siku hii itatokea Ila ni bahati yako kwasababu usingeweza kujitambulisha leo wewe malaya basi kesho ungekipata. Alizungumza kwa hasira sana Saruni.
" ohoooo sorry sana natumaini ya kuwa huna taarifa jana Niliweza kumpiga huyo Rickson wako na ninauhakika kaa sehemu nilizoweza kumpiga haponi"
"Nani Rickson??? Rickson wangu?? Namaanisha Mdogo wangu mimi umempiga wewe??
" ndyo Mdogo wako wewe nimempiga mimi tena siyo kwamba nimempiga bali nimemuuwa" alimwambia taratibu kabisa kwenye masikio yake.
"WeWe mbwa chochote kile kikimtokea Rickson Mdogo wangu...... Naapa kwaajina la Mdogo wangu nitakuuwa na kukutawanya vipande vipande"
"Hivyo sasa ndo hauwezi kwasababu tumeshakufunga hapa" alijibu Alice.
"Unauhakika gani ya kuwa umenifungaa?? Aliuliza Saruni na kutabasamu ghafla aliweza kuwapiga vikumbo wote wawili na kuweza kutokomea dirishani.
" ni hatari kama ataondoka salama kwasababu tayri ameshatutambua sura zetu na ataweza kwenda kumtaarifu Rickson kama bado yuko hai basi tumeisha wote. Alizungumza Alice na kukamata bastola kisha na yeye akatoka katika chumba kile na kumfuata Saruni.
Saruni aliweza kukimbia kwa kujificha na wakati huo mguu wake mmoja ulikuwa ukivuja damu hivyo hali hiyo ilikuwa rahisi Alice kufuatilia damu na kuelewa kaelekea wapi.....
Saruni aliweza kuelekea katika kibanda cha simu kwaajili ya kumpigia Rickson ambaye simu yake iliita bila kupokelewa.
Alipiga tena na tena huku Alice akizidi kusogelea karibu na maeneo yale.
Ni baada ya Saruni kuweza kuondoka mikononi mwa Alice kisha kuelekea kwenye kibanda cha simu kwaajili ya kumpigia simu Rickson.
*** *** ***
Mbona mapigo yake ya moyo hayadundi?? Alijiuliza Rickson ambaye alihisi kuishiwa nguvu mwili mzima.
***** ***** ****
Tafadhali pokea simu Rickson tafadhali..... huwez ukawa umekufa eti ukaniacha mimi duniani nilimuahidi Baba Mdogo ya kuwa nitakulinda na sitaruhusu kitu chochote kibaya kitokee juu yako..........haloo!! Rickson Rickson....
"Kaka Saruni wamemuuwaa Lewis ........Lewis amefariki dunia wamemuuwa wakidhani ni mimi.... Alilalama Vikram huku machozi yakimtoka.
" hivyo wamemuuwa Lewis wakijua ni wewe....... Huyu mwanamk mpumbavu sana mjinga sana huyu.....alilalamika Saruni.
"Mwanamk gani!!!! Aliuliza Vikram.
" Rickson maish yangu kwasasa yako hatarini sana natamani hata nikutane na ww ili nikwambie maneno machache ambayo yatakusaidia wewe katika kupambana na adui wako lakini...................
Ghafla ilisikika milio ya risasi katika simu aliyoweza kuiweka masikioni Vikram.
"Bro....bro........Kaka" aliita Vikram.
Kwasauti ya mbali sana na iliyoweza kujaa uchungu wa kifo ilisikika ikiyazungumza maneno haya ya mwisho.
"Yule mwanamk...... Yu...le....mwanamk..... A.....a.....a!!!! Kabla hajamalizia kulitaka neno hilo zlisikika kelele nyingine za risasi.
" kuna nini tena?? Aliuliza Jimmy ambaye tayri alishasimama pale alipo na kumfuata Rickson.
"Kipi tena kimemtokea Saruni??? Aliuliza Dr Kim.
Alice baada ya kumaliza kumuuwa Saruni aliweza kwenda mpaka pale alipo ili kuthibitisha kama tayar ameshaweza kupoteza maisha.
Alipofika alikutana simu ikiwa inaning.inia aliichukua simu ile na kuweza kuirudishia vizuri huku watu walio weza kusikia milio ya risasi zile walijitahid kukimbia kadri wawezavyo ili waokoe maisha yao.
***** ****** ****
"Bwashe yuko wapi leo ndo tunafungua shule nahitajik kwenda" alizungumza Larry.
"Aliondoka na kuniacha asubuhi asubuhi kisha akaniahidi ya kuwa atawahi kuja nyumbni lakini simuoni hat simu nikipiga hapokei.
Alijibu Tropina aliyeonekana kuwa na wasiwasi kidogo juu ya Rickson.
" Sasa nitafanyaje nimebakiza masaa machache tu ya kubaki nyumbni.
"Kwani we unataka ufanyaje?? Aliuliza Tropina
" kuna mambo nahitaji kuzungumza naye kabla sijaondoka"
"Mambo gani??? Aliuliza Tropina.
" mambo ya watoto wa kiume na wewe " alijibu Larry na hapo hapo simu yake iliita.
"Namba ya nani hii?? Aliuliza huku akipokea simu.
" halooo.......nani???...............nini.......yule mzimu hapana namaanisha Queen.
Alimtizama Tropina na kisha kuingia ndani ya chumba chake.
"Yuko wapi Rickson namaanisha Vikram?? Aliuliza Vanessa.
Tropina alitabasamu tu kisha akamjibu.
"Sikuweza kurudi naye kwani aliniacha yeye akaelekea kwenye mishe mishe zake"
"Ni sawa pia alijibu Vanessa huku akielekea chini.
"Unaelekea wapi?? Aliuliza Tropina.
**** **** ***
" Bado kabisa hajatengamaa yani hata tukimvizia usiku na kuzima taa akiwa amelala anaamka saa hiyo hiyo huku akiomba taa iwashwe na tukiichelewesha kuiwasha basi anaweweseka sana jasho linamtoka na muda mwingne pia pumzi humuishia" maneno hayo aliweza kuzungumza mwalimu ambaye aliweza kupewa kazi ya kumuwekea umakini Larry awapo shuleni.
******* *********
"Unajua tatizo la mtoto wako Larry bado nimeshindwa kulifanyia ufumbuzi kabisa kwanini chanzo cha nini kilitokea mpaka yeye akawa anaogopa giza namna hiyo huwenda tungepata dawa kupitia chanzo hicho" aliweza kuzungumza docta wa Larry.
Alionekana Vanessa akiwa anatoka katika hospital ile huku akiwa mnyong.onyefu zaidi aliweza kukumbuka usiku wa siku hiyo ya kuwa alizima taa lakini ghafla Larry aliweza kuinuka na kusema taa iwashwe huku akiwa ametota kwa jasho.
"Nitafanyaje kipenzi changu juu ya udhaifu wako huo?? Alijiuliza Vanessa na hapo alikumbuka kauli ya docta kwamba iwapo ataweza kuufahamu ukweli ilikuwaje mpaka Larry akafikia katika hatua hiyo basi kutamsaidia yeye kupata dawa.
" hiyo ni siri ya familia siwezi kuiweka hadharani hata kidogo kwani sitakuwa nimemsaidia mwanangu bali kumkandamiza kabisa.
***** ***** ******
"Ushahidi wowote ule ulioweza kpatikana eneo la tukio?? Aliuliza George
" hatukuweza kupata ushahid wowote tofauti na kumpata Rickson mwenyewe "
"Upumbavu gani huo??? Alifoka insp Georges.
Happ hapo aliweza kuletwa Alice aliyekuwa akibishana na maaskari walioweza kumshika baada ya kufanya tukio la mauaji.
Insp. Huyu hapa alichukua simu ya Rickson. Alizungumza Thobias.
Na kumfanya Alice amtazame huku nako George akimtizama Alice.
" Lazima niende nikaichukue maiti ya Kaka yangu hawezi kuzikwa na manispaa ilihali mimi Niko hai na nikishaweza kuipata basi watajuta kwa kosa la kuweza kunichokoza wenyewe. alizungumza Vikram aliyekuwa akiyauma meno yake kwa hasira mara simu yake iliita na aliyekuwa akipiga simu ni Tropina alishindwa kupokea na hatimaye iliweza kukata tena..
****** ******* ********
"Sawa mimi nimekuelewa lakini ndo hivyo hairuhusiwi kupiga risasi hovyo na kuwashtuwa wakazi wa eneo husika hata kama ni Askari hivyo atakaa kwa masaa5 ndani ndipo aweze kutoka. aliongea George aliyekuwa na Calvin.
" Sawa " alijibu Calvin.
*by the way nahitaji simu aliyoweza kuichukua kwani kesi hii ipo mikononi mwangu na sijaweza kupewa taarifa yoyote ya kuwa nimewekewa wasaidizi wengine wa siri" alizungumza George
"Sawa nitaweza kuileta lakini simu ile haina ushahidi wowote ule kwani aliweza kui restore. Alizungumza Calvin akimpa taarifa zaidi George.
" Haina shida wewe ilete hivyo hivyo tu "
¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥
Siku mbili ziliweza kupita bila Vikram kupiga simu nyumbn wala kupokea simu tena pale alipoweza kuona wanamsumbua alizima simu baada tu ya kutuma msg ya kuwa yeye yuko salama.
Vikram alikuwa katika sehemu mahalumu ya makaburi aliyoweza kuyaandaa baada ya kuwazika Saruni na Lewis.
"Boss Rickson.....
Kama wewe utaacha hili lipite mimi sitaweza kuwacha hili lipite lazima walipe kwa hichi walichoweza kukifanya. Alizungumza Jimmy kwa hasira.
"Tumeshaitengeneza hili Bomu?? Aliuliza Vikram akimuliza Obama.
" tayari "
"Saruni na Lewis hamuwezi kwenda wenyewe mbinguni nitawaletea watu wengi zaidi watakaoweza kuwa na ninyi huko mbinguni.alizungumza Vikram huku sura yake ikiwa imekunjamana kwa hasira.
***** ****** ***
Katika makaburi ya manispaa lilikuwapo kundi Kubwa la maaskari walikuwa wakipiga picha sehemu kaburi lilipoweza kufukuliwa na hapo ndipo alipozikwa Saruni lakini haikuwapo tena maiti yke askari wengine waliweza kuwauliza maswali wahusika wa mahali pale.
" Mliyeweza kumkamata na kuweza kumpiga sidhani kama ni Rickson " alizungumza George akimtizama askari wake Thobias.
"Lakini huyo ndye si ulimsikia yule binti
............."
"Huo ni mchezo alioweza kuchezewa kwani walishaweza kumuona na kumfanyia mchezo huo Ila ninauhakika ya kuwa alimuacha Vikram ndani......umeshaweza kufuatilia CCTV camera za chumba kile??
" Ndiyo Ila walisema CCTV hazijaweza kurecord tukio lolote lile la uwepo wa Rickson "
"Huyu ni mjanja sana na hatuwezi kumkamata kirahisi kama tunavyoweza kufikiria" alizungumza George huku akitizama chini ambako aliomba kitambaa na kuokota mfuniko wa kalamu.
"Sijui kama utaweza kusaidia huu katika upelelezi aliuliza na kumtazama machoni Thobias.
Ghafla ilisikika milio mikubwa ya milipuko karibu kabisa na eneo lile na hapo hpo ziliweza kusikika milio ya hofu na uwoga wa watu.
" ni nini?? Waliuliza askari ambao wengine walishaweza kujificha huku Thobias na George wakiwa wamesimama na kusikilizia mlio huo.
"Mbona kama mbona kama.......... Alishindwa kumalizia George.
" Huo ni mlio wa bom...... .... Rickson hamjamuuwa nimewaambia na mmemuulia ndugu yake wananchi sasa watakipata" alizungumza Kwa hasira sana George huku akielekea eneo lile.
Maaskari waliokuwa karibu n sehemu bomu lilipoweza kusikika waliweza kutoka na kuelekea huko huku George akiwa wakwanza kuongoza msafara huo.
Kam George alivyoweza kubunia ni bomu lililoweza kulipua kiwanda cha nguo kilichokuwa karibu na eneo lile la manispaa.
Watu wengi walishaweza kufurika eneo lile ili kutizama kipi kinaendelea baada ya kusikika mlipuko huo.
**** ***** *****
"Nini??? Kiwanda changu??? Huyo ni huyo mpuuzi Rickson nasema huyo ni Rickson....... Atafutwe eti atafutwe na aletwe hapa" alitoa maagizo mkuu ambaye aliweza kupigiwa simu na Alice na kupewa taarifa za kuungua kwa kiwanda chake.
"Mr. Harlan amesema atafutwe Rickson tena apelekwe kwake" alimpa taarifa hizo Calvin.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hivi kwanini Rickson anafanya hivyo eti kwanini anauwa watu tu kila pale apendapo?? Ni wangapi wamekufa kwenye hiyo ajali?? Aliuliza Calvin.
" wamekufa watu kumi na mbili tu "
"Mbona kiwanda kile kinawafanyakazi zaidi ya 50 imekuwaje wakafa 12 tu aliuliza Calvin.
" bado sijapata maelezo zaidi"
***** ***** *******
"Saruni hatimaye wameshaweza kukufuata wewe pamoja na Lewis huko mlipo.................wamefariki wangapi? Aliuliza Vikram
" Wamekufa 12 tu wale tulioweza kuwapanga" alijibu Jimmy.
"Mali je?!!
" Tumeweza kuteketeza kiwanda chote na kila kilichomo ndani ya kiwanda hicho" alizungumza Jimmy.
"Hasara ya bei ngapi imeingia?? Aliuliza tena Vikram.
" Ni kama million 400 hivi"
"Mr Harlan natumaini ya kuwa sasa atakaribia kuwa kichaa na kwakuwa hajui mahali nilipo basi atataka kulipiza kupitia Tropina hivyo ulinzi uongezwe zaidi na watu wawe makini.
"Inamaana wewe hurudi huko??
" nitawezaje kurudi wakati kwasasa natafutwa sana na sitaki Tropina ajue chochote kuhusu mimi kwani sitaki kuwaingiza kwenye matatizo " alizungumza Vikram ambaye simu yake iliita tena alikuwa ni Tropina hivyo hakuwa na uwezo wa kuipokea.
"Kwanini hapokei simu yangu aliniahidi kuwa angewahi kurudi lakini wiki imepita sasa hata simu yangu hapokei nafikiri atakuwa salama alizungumza Tropina aliyekuwa akikitazama chakula alichoweza kupatiwa.
"Madam Tropina...... Japo ujaribu kula sasa kwanzia jana mchana ujala japo ujaribu kidogo tu" alizungumza Diana.
"Hapana Niko salama tu......nahisi kushiba sihisi kabisa kula chochote.
"Lakini kwanzia jana................"
"Dee sihitaji kelele tafadhali toka njee" aliongea kwa hasira.
Diana aliweza kutoka njee akiwa na chakula chake mikononi mwake.
"Nipe hicho chakula.....alizungumza Vanessa na kupokea chakula kile kisha kuingia ndani ambako Tropina alikuwapo.
**** ***** *****
Vikram alikuwa akitizama picha ya Tropina kwenye simu yake huku akitabasamu.
" Mke wangu siwezi kuja kwasasa japo nimekumiss sana nilihitaji tupate muda mwingi kwaajili ya kukaa na kukwambia ukweli wote juu ya maisha yangu. Hapo hpo simu yake iliita na alikuwa ni Alice.
"Hello Alice......hapana siko busy sana......tuonane sasa hivi......sawa nitafika tu.....wapi hapo......sawa nakuja Ila pesa ya kula juu yako. alizungumza na kukata simu.
**** **** ****
Vikram aliweza kufika katika sehemu husika aliyoweza kuitwa na Alice wakati huo nao Tropina alihisi kuwa Vikram atakuwa kwa Winnie hivyo alifunga safari ili aelekee nyumbani kwa Winnie.
Alice na Vikram waliweza kumaliza kula na sasa Vikram alienda kununua ice cream kwaajili ya kumpelekea Alice.
Tropina aliweza kumuona Vikram na aliamuru gari lisimamishwe alishuka akiwa na furaha baada ya kumuona Vikram ghafla furaha yake iliweza kuisha baada ya kutizama mbele yake na kumuona Vikram akipeleka ice cream kwa mwanamke mwingine tofauti na Winnie.
Aliinua simu yke na kumpigia Rickson. Rickson alitoa simu yake na baada ya kuona ni Tropina alikata. Tropina alipiga tena na Rickson alikata na hatimaye akazima simu yake.
"Ni nani huyo??? Aliuliza Alice.
" aaaammmmhhhhh hamna ni mtu tu ananisumbua" alijibu Vikram.
Na maneno hayo Tropina aliweza kuyasikia Tropina aliyafuta machozi yake yaliyoweza kudondoka ikiwa ndyo kwa mara ya kwanza baada ya kifo cha Baba yake kutokea.
Aliingia ndani ya gari lake na Alice aliweza kumuona.
Unatizama nini?? Aliuliza Vikram akitaka kugeuka nyuma.
"Hamna" alijibu Alice huku akimgeuza Vikram asimuone Tropina.
"Ohooooo huyu sasa kajitafutia matatizo alizungumza Dr Kim huku akimpigia simu lakini haikupatikana.
Aliwasha gari na kumfuata nyuma Tropina aliyeamuru gari ligeuzwe na liweze kuelekea nyumbni.
Maneno ya " aaaahhhmmmm hamna ni mtu tu ananisumbua " pia kitendo cha kumpigia simu Rickson kisha akakata hatimaye akazima kabisa.
Alipishana na Adrian na aliweza kumpiga kikumbo huku sura yake ikiwa iko chini.
"Ni nini huyu??? Aliuliza Adrian akitembea mbele lakini alisimama baada ya kupiga hatua mbili na kuweza kutoa chozi katika mkono wake.
" Ngoja.................nani analia??? Yani Huyu kipofu leo analia!!! Hahahaha itabidi nitafute hicho chanzo cha yeye kulia nilidhani hana uwezo wa kulia tena....
Hahahahaha.....aliendelea kucheka Adrian na kurudi ndani huku akihairisha safari yake.
'Unatatizo gani?? Aliuliza Vanessa.
"Nahitaji kupumzika tu sihitaji kelele tena kwasasa" alizungumza Tropina na kwenda kujitupia kitandani kwake.
"Sawa" alijibu Vanessa huku akimvua koti alilokuwa amelivaa akamvua viatu kisha akamtoa hereni na kumuwekea mto kichwani alafu akamfunika na shuka.
***** ***** ****
"Unamaanisha nini?? Nani??? Pinah kaniona nikiwa na Alice!!
" Ndiyo" alijibu Dr Kim.
"Kwahiyo alivyokuwa akinipigia simu alikuwa pale pale"
"Ndyo na ulivyokata na kuzima simu pia alikuona nahisi pia hata maneno uliyoweza kuyazungumza kayasikia" alijibu Dr Kim.
Rickson alikumbuka maneno aliyoweza kumwambia Alice.
"Nitafanyaje sasa?? Aliuliza Vikram kwa huzuni.
Kila mtu alipandisha mabega ishara ya kwamba hafahamu kipi anatakiwa kufanya.
" Nimpigie amah?? Aliuliza Vikram
"Sidhani kama atapokea" alijibu Jimmy ambaye alikuwa wa mwisho kuondoka pale.
"Au niendee tu mwenyewe......hapana.... Larry.... Larry kwanza nizungumze naye alipiga simu lakini ilikuwa imezimwa.
" Mungu wangu................ Ameenda shule alafu nilisahau sijazungumza naye kabisa......... Nimpigie Vanessa....... Uuuwwwhhhh hapana siwezi zungumza naye.
***** **** ******
"Umeweza kufuatilia taarifa zote za huyo mwanamk wake?? Aliuliza Mr Harlan
" Ndyo ni mtoto wakwanza katika familia yao. Wamezaliwa wawili tu kwako yeye na Mdogo wake wa kiume ambaye anamiaka 9.
"Sitaki kufahamu wako sita tisa au mia moja wanamiliki mali za pesa ngapi??
" kampuni moja inayouza magari makubwa tu.....kampuni nyingine inahusika na maswala ya bandarini.......kampuni moja ya sheria pamoja na kampuni inayohusika na maswala ya madini ya tanzanite, ruby pamoja na Almasi jumla ya mali zote hizo ni............."
Kampuni ya madini inagharimu shingapi??
"Kama million 300"
"Nataka ilipuliwe na kila kilichopo ndani kisitoke hata kimoja viungulie vyote huko ndani alafu nione Rickson atachukua hatua gani" alitoa amri hiyo Mr Harlan.
"Sawa mkuu" alijibu mfanyakazi wake wa karibu anayekwenda kwa jina la Denise.
***** ***** ****
"Mbona umerudi wewe nani anamlinda Tropina?? Aliuliza Jimmy.
" Kwani wewe nani anamlinda Vanessa?? Aliuliza Dr Kim.
"Vanessa hana shida wala hawezi fuatiliwa na Mr Harlan lakini Tropina na Larry lazima.... Hivi umemuona Obama akiwa katika mavazi ya ualimu.
" kivipi??
"Kazi yake si kumlinda Larry sasa si yuko shuleni imebidi aende kuomba kazi ya ualimu na ameweza kuipata alafu ujanijibu umeamucha na nani Tropina.
" Rickson leo lazima aende akabembeleze hivyo nimepata muda wa kupumzika. Alijibu Dr Kim aliyekuwa anafungua friji na kutoa kinywaji cha baridi.
Njee ya dirisha la Tropina alikuwa Vikram aliyekuwa akijadili aende au asiende ndani.
"Unafanyaje hapo? Aliuliza Vanessa aliyeweza kumuona Vikram.
" Mama! Aliita Vikram kaa aibu.
**** ***** ****
"Zimepita dakika 30 na sioni maendeleo yoyote"
"Unamaanisha unahitaji huo mlipuko utokee usiku huu? Aliuliza Denis.
" kama unaswali uliza hilo ni jibu"
"Sawa nimekuelewa" alijibu Denis na kuondoka eneo lile.
**** **** *****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ulikuwa wapi?? Nakwanini unakuja nyumbani kwa kuiba iba??
" aaaammmmhhhhh..................... Mama............"
"Leo umeonana na mwenzako?? Aliuliza tena Vanessa.
" ammmhh hapana....namaanisha ndiyo "
"Sasa hapo jibu ni lipi?? Aliuliza Vanessa.
" Ndiyo lakin hatujazungumza.............yani wala mimi sijamuona yeye Ila ....
Nliambiwa tu na unajua........ Ki ukweli mimi sijamuona na simu yake ni kwamba"
"Vikram sielew unachokizungumza labda Tropina ndo ataelewa kwahiyo unaweza ukaenda tu. Alizungumza Vanessa na kufungua mlango.
" Sawa" alijibu Vikram na kuelekea mlangoni kwaajili ya kutoka.
Vanessa alifunga mlango wake na Vikram taratibu alianza kupiga hatua za kivivu kuelekea katika chumba cha Tropina.
Alipofika alijikohelesha na kujitengenezea kidogo.
"Pinah....... Ammhhh.....hapana hiyo siyo nzuri. Nitaanza
" nimekuja kukuomba samahn kwa kukukatia simu "
Hapana hapana nianzaje sasa.
"Sina mahusiano yoyote na yule mwanamke mimi"
Wakati akiyazungumza maneno hayo Tropina alikuwa mlangoni na alikuwa akicheka.
"Sasa nimeshamalza zaidi ya dakika tano kwa kufikiria cha kumwambia inanibidi niingie ndani mimi ni wakiume.
Tropina alirudi nyuma ya mlango ulifunguliwa lakini ghafla simu yake iliita.
" Hallo!! Kim Sawa nakuja " alizungumza Vikram na kuufunga mlango wa Tropina kisha kuondoka zake.
Tropina alifungua mlango wake na aliweza kumtizama tu kwa mbali Vikram akiwa anaishilia kwa mbali.
"Vicky" aliita Tropina ambaye happ hapo sura yake iliweza kubadilika.
"Mr Harlan....... Sawa nakuja sasa hivi" alijibu Vikram na kukata simu yake.
Aliwasha gari lake kwa haraka haraka na kuondoka nalo.
'Umemuona alovyoingia ndani?? Aliuliza mlinz mmoja aliyeweza kushtuka kwa uwepo wa Vikram.
"Sidhani kweli" alijibu mfanyakazi mwingine.
**** **** ***
Bossi kuna simu yako hapa.
"Nani anapiga?? Aliuliza Mr Harlan
"Private no" alizungumza mfanyakazi wake wa kike.
"Hahahahaha nilijua tu atanitafuta" alizungumza Mr Harlan akimruhusu mfanyakazi wake aipoke.
"Haongei"
"Nipatie"
Mr Harlan aliweza kupokea simu yake halo.
"Hasara ya million 300 siyo Kubwa kama hasara ya million 900 ya biashara yako ya nchini Uganda kwahiyo usitake nimfuate mwanao nchini Paris alafu nimfanye mke wangu"
"Wewe achana na binti yngu Rickson achana na binti yangu nakwambia"
alizungumza Mr Harlan.
"Basi usije ukajaribu kugusa mtu mwingine tofauti na mimi kwasababu na mimi nitamshik mtu mwingine tofauti na wewe" alikata simu baada ya kumaliza kuzungumza maneno yake
"We Rickson wwe....wewe mtoto"
Mpumbavu mkubwa huyu ananikatia simu mimi huyu mshenzi....... Fanya hivi mpigie simu Denise na umwambie aache hiyo kazi niliyompatia.
"Ndyo boss" alijibu mfanyakazi yule wakike ambaye jina lake aliitwa Aisha.
*** *** ***
"Tunafanyaje sasa?? Aliuliza Dr Kim
" naamini kila kitu kitakuwa salama hawezi lipua tena kampuni ya madini naamini hivyo " alijibu Vikram aliyekuwa akisubiria simu ya Mr Harlan.
"Huyo anapiga simu" alisema Jimmy na Vikram alipokea.
"Sawa nimeacha kufanya kila kitu na wewe itabidi unirudishie nusu ya hasara uliyoweza kunisababishia" alizungumza Mr Harlan.
"Hasara....hasara.....unaongelea hasara gani....... Unaweza kuirudishia uhai wa Kaka yangu nirudishie uhai wake na mimi nitakupa hata billion 300"
"Ngoja Kaka ako.................. Unamuongelea nani?? Saruni kauwawa?! Aliuliza Mr Harlan aliyekuwa hana taarifa yoyote ya kifo cha Saruni.
" Usijifanye unashangaa na kwamba ufahamu chochote Harlan nakwambia utalipia kwa hili utalipia" alizungumza na kukata simu.
"Sidhani kama Harlan anahusika na kifo cha Saruni" alizungumza Rickson.
"Sasa kama siyo yeye ni nani?? Aliuliza Jimmy.
" inamaanisha unaadui mwingine tofauti na Harlan? Aliuliza Dr Kim.
"Mmeweza kupata chochote cha huyo mwanamke aliyekuwa akitembea na Kaka yangu?? Aliuliza Vikram.
" Hapana nani kwamba inashangaza maana hata simu ya Saruni haina namba yake wala picha hata moja mpaka nakuwa na mashaka juu ya huyo mwanamke" alizungumza Dr Kim.
"Pia mara ya mwisho Saruni alinambia anaenda kwa huyo mwanamke" alizungumza Vikram.
"Hivyo tunatakiwa sasa tuanze kumtafuta huyo mwanamke" alizungumza Jimmy.
"Nafikiri hivyo lakini kwanini sasa amuuwe kwa risasi nyingi namna ile alafu kesi si iko police lakini hatuwezi kuifuatilia kwasababu wanakuhitaji wewe" aliendelea kuongea Jimmy.
Hatimaye wiki tatu ziliweza kupita na hakukuwa na mawasiliano yoyote baina ya Rickson na Tropina.
Siku moja Tropina akiwa anatizama zake njee kupitia dirishani kwake aliweza kumuona Vikram lakini alihisi ni mawazo yake tu kwani mara nyingi sana huwa anazidi kumuona kila mahali aendapo.
"Nimechoka na hizi ndoto za mchana mimi alizungumza na kufunga dirisha lake.
"bado anahasira na mimi nitafanyaje sasa?? Alijiuliza Vikram.
Aliweza kuzunguka na kuingia ndani.
Tropina alikuwa akishuka ngazi na alimuona tena Vikram.
Alijua ya kuwa ni mawazo yake tu.
Alimpita Vikram na kwenda kukaa.
" Pinah " aliita Vikram.
"Aaahhhh sipendi unifuate fuate bwana tafadhali niache na maisha yangu...wewe sasa hivi unakula raha na mwanamke mwingine alafu kivuli chako kinanisumbua mimi" alizungumza Tropina kwa sauti huku akidhani anachokiona ni kivuli cha Vikram.
Vikram alimfuata mpaka alipokaa kisha akakaa chini yake na kumshika mkono huku akitabasamu.
Alitoa Pete kisha akamvalisha kwenye kidole chake.
"Pinah...mimi siyo kivuli mimi ni Rickson mimi ni Rickson wako" alizungumza huku akimpapasa sehemu ya mapaja yake.
"Kweli wewe ni Rickson wangu?? Aliuliza Tropina.
" ndyo"
"Hapana najua tu ni mawazo yangu wala Vicky wangu hayuko hapa" alizungumza Tropina na kugeuka zake upande mwingine.
Adrian alikuwa akipita pale.
"Adrian Niko na nani hapa?? Aliuliza Tropina.
" unaniuliza inamaana humuoni Vikram mwenye mapaja yako ahaa kumbe wewe kipofu basi huyo ni Vikram maana naona hata harufu yake tayari imeshakupotea" alizungumza Adrian na kuendelea kutembea.
"Ricky" aliita Tropina kwa furaha bila kujua ya kuwa ni hatari kwasababu Adrian yuko pale.
Adrian baada ya kusikia jina hilo alisimama na kugeuka nyuma ambako macho yake yaligongana na Vikram aliyekuwa akimtizama na wakati huo nao Tropina alijawa na furaha na alitaka kutamka tena jina lile kwa kumuita hivyo macho ya Vikram na Adrian yalikuwa mdomoni mwake.
Tropina aliita
"Vicky!!!! Na hapo ndo ikiwa msaada wa Vikram na Adrian asigundue chochote kile.
Adrian alihisi kitu lakini hakuweza kusema jambo wakati huo Tropina alikuwa amemkumbatia Vikram aliyekuwa akimshukuru Mungu kwa kuweza kuitwa Vikram kwa mara ya pili na siyo Rickson.
Adrian alitoka njee na kupanda gari lake.
" mbona kama nilisikia amesema Ricky! Alijishangaa mwenyewe lakini akajiaminisha ya kuwa huwenda yeye ndyo amesikia tofauti.
"Ngoja nimtafute Winnie" alizungumza Adrian na kupiga simu.
"Mbona umekuwa kimya sana" aliuliza Adrian.
"Nawaza jinsi gani naweza kumpata Rickson.....lakini bado sina njia." Alisema Winnie aliyeonekana amepowa sana kimawazo.
"Kwahiyo unakaa tu nyumbani bila kufanya chochote na unasema hujui cha kufanya??
" sasa nitafanya nini mimi?? Nitafanya nini??
"Ili kumpata Rickson lazima umteke Tropina" alishauri Adrian.
"Kweli??? Aliuliza Winnie
" Sasa unanjia nyingine tofauti na hiyo?? Aliuliza Adrian.
"Sina"
"Basi mteke Tropina na uache ishara yoyote ambayo Rickson anaweza akatambua ya kuwa wewe ndiye umemchukua" alizungumza Adrian.
"Lakini mbona Tropina hamfahamu Rickson sidhani kama njia hiyo itasaidia" alizungumza Winnie.
"Juzi hadi wamelala naye chumba kimoja wewe umekaa kaa tu"
"Nani kalala na nani??? aliuliza kwa hasira na kusimama Winnie.
"Usinikurupukilie mimi kuwa makini na maneno yako na huwa sipendagi kelele kabisa" alizungumza Adrian akimuonya Winnie Aache kelele zile ziliweza kumfanya Queen aliyekuwa ndani ya chumba chake atoke njee na kutizama ni nini shida mbona kuna kelele.
"Ni nani Huyo anayepiga kelele hapa" Alijiuliza na kuweza kuwachungulia kwa chini tu lakini hakubahatika kuiona sura ya Adrian kwasababu alikuwa amempatia mgongo alipotaka kushaka na kwenda kumtazama zaidi simu yake iliweza kuita aliyoiacha ndani ya chumba chake.
"Ni yule handsome wangu" alizungumza na kukimbilia simu yake.
"Haloo..... Larry.....nimekumiss sana eti" alizungumza Queen.
"Hivi wewe huendagi shule?? Aliuliza Larry.
"Naendag Ila huwa ninakwenda na kurudi sipendi boarding kabisa" alizungumza Queen.
"Kwanini???
" Sipendi kukaa mbali na nyumbani kwani huwa nikirudi kuna shughul nafanya ya kukuza kipaji changu" alizungumza queen.
"Kipaji chako?? Kipaji gani hicho?? Aliuliza Larry.
" huwa na design mavazi na kuyashona mwenyew nitatengeneza tena nguo yako kisha nitakuletea shuleni"
"Kwanini uje ww utatuma tu mimi nitapokea"
"Kwnini hutaki uje kwani unamwanamk mwingine tofauti na mimi?? Aliuliza Queen
"Sina mimi.....alafu kwanza unamaanisha nini mimi nipo shule ya wanaume kwahiyo"
"Hamna nilitaka tu kujua kama unamwanamk kumbe hauna" alizungumza Queen.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Na kwanini unataka kujua? Aliuliza Larry
"Kwasababu mimi ni mwanamke wako"
"Mwanamk wangu??? Hahahaha unanichekesha wewe, mimi sitakagi wanawake wanaongea kama wewe, alafu sitakagi mwanamke mchafu mchafu kama wewe na anayejitongozesha mwenyewe" alizungumza Larry.
"Sawa nitaanza kupunguza kuongea..........nitaacha uchafu......na sitajitongozesha kwa mwanaume mwingine tofauti na wewe...... Hapo je si utakuwa mpenzi wangu" aliuliza Queen.
"Hahaha" Larry alibaki akicheka tu na kumfanya Queen na yeye acheke. Wakati akifanya hivyo aliweza kuonekana na Obama ambaye hakuwa mbali na eneo lile kwani kazi yake ilikuwa ni kumlinda Larry.
Alicheka kisha akaondoka eneo lile huku akimuacha larry aendelee kuzungumza na simu yake aliyomuomba kwaajili ya kuipigia familia yake kama alivyosema.
**** **** ****
Tropina akiwa ndani na Vikram huku akiwa amelalia kifua cha Vikram na akiwa anapapasa mikono yake.
Huku Vikram akiwa anapapasa nywele zake kichwani.
Calvin akiwa ndani ya chumba ambacho kulikuwa na camera zilizoweza kutegwa katika nyumba nzima ya Tropina.
Alishngaa baada ya kuona Tropina akiwa na mwanaume ndani ya chumba chake alichukua simu yake na kumpigia Alice.
"Veronica nimeshampata Rickson yuko chumbani kwa Tropina" alizungumza Calvin.
"Una uhakika ni yeye?? Aliuliza Alice.
"Piga picha unitumie" alisema Alice na kukata simu.
Picha iliweza kuingia na aliifungua.
"What?? Vikram!!
" Halo huyo siye usimpigie simu mtu yoyote yule subiri nakuja" alisema na kukata simu kisha akawahi kuja eneo lile.
"Ni nani huyo kwanini unasema siyo Rickson? Aliuliza Calvin.
" huyo ni Vikram wangu. Alisema Alice.
"Vikram wako?? Aliuliza Calvin kwa mshangao.
" Huyu mwanamke huyu mpuuzi huyu?? Alizungumza Alice na kuchukua simu yake kisha kumpigia Vikram.
Vicky simu yake iliita na aliitizama kabla hajaipokea.
"Anataka nini huyu?? Alijiuliza kisha akimtizama Tropina aliyepandisha macho yake juu na kumwangalia.
" Ni nani??
"Aaaammhhh hamna mtu alisema kisha akaiweka silence.
" Vikram unakata simu yangu.....alizungumza Alice na kupiga tena simu yake.
"Pinah....naenda kupokea simu alafu nitarudi" alizungumza Vikram na kusimama.
Alitoka njee na kufunga mlango.
"Haloo"
"Vikram nahitaji nikuone sasa hivi......Niko maeneo ya ................"
Baada ya kumaliza kuzungumza alikata simu.
"Anashida gani huyu mbona ameongea kwa haraka hivyo? Alijiuliza na kujikuta amesahau kila kitu kuhusu Pinah kisha akaondoka katika nyumba hiyo.
Pinah aliweza kutizama dirishani na alimuona Vikram akiondoka kwa haraka baada tu ya kuwasha gari.
" uliniahidi ya kuwa utarudi lakini umeondoka bila kuja kwangu " alichukua simu yake kisha akampigia mfanyakazi wake.
"Mfuatilie Vikram anapoenda na unipe details zote" Baada ya kumaliza kuongea alikata simu na kuelekea zake kitandani kwaajili ya kujilaza.
Alice aliweza kusikia kila alichoweza kukizungumza Pinah na kuongea.
"Tuone sasa unataka kumchukua Vikram wangu......nitakuonyesha Tropina kuwa Vikram ni wa kwangu na ananipenda mimi" Baada ya kumaliza kuzungumza aliondoka zake.
"Hii ni drama gani naiona hapa" Alijiuliza Calvin na kumtizama Tropina kwenye screen.
Vicky aliweza kukimbia hadi eneo aliloweza kuambiwa afike.
Hapo hapo aliingia Alice ambaye alienda kum kumbatia Vikram baada ya kumuona.
"Vipi uko salama?? Aliuliza Vikram huku akiendelea kumpiga piga mgongoni wakati huo kijana aliyeweza kutumwa alimuona hivyo Tropina alikuwa akipiga picha kwa kila tukio.
Wakati huo Alice alikuwa akitabasamu huku akimini ya kuwa kila akifanyacho kitapelekwa kwa Tropina.
Vikram alimchukua na kwenda kumpandisha katika gari lake.
" Ni vizur kama nitakupeleka nyumbni"
Alice alichukua simu yake na kumtumia mama yake msg.
"Uko nyumbani"
"Ndiyo, unakuja nyumbani? aliuliza mama yake.
" hapana siji nyumbani lakini nilikuwa nataka nikuombe uka chongeshe ufunguo wa nyumbani sasa hivi"
"Kwanini sasa hivi?? Aliuliza mama yake.
" ww fanya hivyo na hakikisha ya kuwa unafunga mlango kabla ya kuondoka " alimalizia kutuma msg na kujilegeza.
Vicky aliweza kufika na kumtoa ndani ya gari huku akiwa amemshika kiuno na kumtembeza taratibu bila kujua ya kuwa Alice anafanya hivyo kwa makusudio yake.
"Halo wako wapi?? Aliuliza Tropina.
" Sawa fuatilia kila kitu "
Wakati alipokuwa akizungumza na simu ndipo Vikram alipokuwa akigonga mlango wa kina Alice lakini baada ya kuona hamna mtu aliamua kumpeleka katika chumba chake.
"Madam Tropina amemuingiza chumbani kwake" alitoa taarifa mtu yule na kumfanya Tropina ashushe pumzi ndefu kisha akakata simu.
"Yani huyu mbwa huyu anapata maisha yote mazuri hivyo alafu bado anamsaliti Madam wangu natamani atanipewa ruhusa ya kumulia mbali huyu mpuuzi" alizungumza na mfanyakazi yule jina lake Patrick.
Tropina aliitoka njee ya nyumba yake na kumfuata Patrick akiwa amepanda taxi.
"Tropina mmemuona wapi?? Aliuliza Vanessa.
" ame ame ame....amepanda taxi " alijibu Diana akiwa katika hali ya mshangao kwani kwa mara ya kwanza kabisa Tropina alipanda taxi.
"Taxi!!!!! Alishngaa Vanessa.
**** **** **** ***
" Namuhitaji huyu kipofu hapa haraka sana" alitoa taarifa hizo Winnie akiwa taarifa hizo vijana wawili.
"Huyu si Madam Tropina.....binti kipofu huyo?? Aliuliza kijana mmoja kwa mshtuko mkubwa.
" ndyo ni yeye" alijibu Winnie.
"Me siwezi hiyo kazi kuingiza mwili wangu katika mdomo wa mamba hapana" alisema kijana mmoja na kuondoka.
Winnie alimpiga bastola na kumuulia hapo hapo.
"Na wewe je utaweza kuifanya au huwezi aliuliza Winnie ikiwa tayari bastola iko kichwani mwake.
Aligeuka na kumtizama mwenzake akiwa chini kisha akamtizama na Winnie.
" nitafanya hivyo " alijibu kwa uwoga wa hali ya juu.
***** ***** ******
Alionekana Alice akitoka ndani ya chumba cha Vikram akiwa na taulo tu na kujinyoosha nyoosha huku akijishika sehemu za mwili wake.
"Huyu mjinga" alizungumza Patrick na kutaka kwenda Ila Tropina alimshika bega.
"Madam" aliita Patrick.
"Shshshsh shshshsh...... "
Patrick aliufunga mdomo wake baada ya kuamrishwa kunyamaza.
Alirudi ndani na kumtizama Vikram aliyekuwa amepitiwa na usingizi kwenye kochi. Alivaa nguo zake na kumwagia maji Vikram.
"Aaaahhhhh jamani samahani ungevua hiyo nguo ya juu ntakusaidia" alizungumza huku akimvua nguo ya juu.
"Usinishike nitavua mwenyewe" alizungumza Vikram na kutoa mikono ya Alice mwilini wake alivua shati lake.
"Ntaenda kukuanikia alizungumza Alice na kuchukua shati la Vikram.
Alianza kujisogeza karibu na yeye na Vikram alimwacha ndani na kutoka zake njee bila kujua ya kuwa hiyo ndiyo ilikuwa nia ya Alice.
" Huyu Alice anakichaa nini ananishika shika mwili wangu...alizungumza Vikram huku na yeye akijishika kifuani mwake.
"Kwahiyo baada ya ku enjoy sasa mnatoka njee huku mkiwa mnajishika shika miili yenu" alizungumza Tropina na kuamua kuondoka zake.
Wakati akiondoka ndipo napo Vikram aliyageuza macho yake lakini hakumuona mtu yoyote yule.
"Nilimuahidi Pinah ya kuwa sitaondoka lakini nimeondoka bila kumwambia chochote...... Itakuwa nimemuumiza tena kwa kiasi kikubwa sana hivyo nitamnunulia kitu kizuri kwaajili ya kumuomba msamaha" alijisema na kutabasamu.
Mama yake Alice aliweza kugongana na Tropina na kufanya funguo zake zidondoke.
Tropina aliinama na kuokota fungue zile kisha akampatia na kutoa heshima alafu akaondoka zake.
"Huyu sura yake siyo kama ya ngeni kwangu nahisi nimewah kumuona mahali" alizungumza mama yake Alice na kuelekea nyumbani.
Tropina akiwa njiani na dereva wake aliomba ampeleke sehemu ambayo kutakuwa na vinywaji vya kileo.
Patrick alifanya hivyo na Tropina alipofika alianza kunywa pombe taratibu kabisa huku akikumbuka vitendo vile alivyoweza kuviona kwa siku hiyo.
"Haloo......ndiyo usijali nitamchukua kirahisi sana kwasababu pia amelewa kwa siku ya leo" alizungumza kijana yule aliyeweza kubaki akitoa taarifa kwa Winnie.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***** ****** ******
"Jimmy embu nitizamie signal ya Tropina nashindwa kuelewa yuko wapi kwa sasa" alizungumza Dr Kim.
"Wewe ulimuachaje........ammmhh simu yake imezima hivyo signal hatuwezi kuipata gari lake nalo signal yake inaonekana iko nyumbani......tofauti na hapo uliweka wapi tena cheap? Aliuliza Jimmy.
Katika baadhi ya pear ya viatu vyake alizungumza Dr Kim.
" sidhani kama atakuwa amevivaa leo alijibu Jimmy.
"Umemtafuta Rickson? Aliuliza Jimmy.
" Nitawezaje kufanya hivyo lazima atanilaumu me nilijua atakuwa naye siku nzima ndo maana nikaondoka nikiamini yupo katika hali ya usalama. Alizungumza Dr Kim.
"Sawa subiri" alizungumza Jimmy na kumpigia Rickson aliyekuwa katika duka moja la vito vya thamani akichagua cheni kwaajili ya Tropina
"Yes halow..........Tropina..... Haonekanije?? Aliuliza kwa mshangao hapo hpo iliingia simu nyingine.
"Hallo.......Obama unasemaje"
"Samahani bossi uko nyumbani? Aliuliza Obama.
" kwanini unaniuliza?? Aliuliza Vikram.
"Ni kwamba Larry haonekani shuleni na tumeshindwa tambua kaelekea wapi sasa nikahisi atakuwa amerudi nyumbani.
"Unaongelea nini wewe?? Aliuliza Vikram ambaye sasa alianza kuchanganyikiwa. Embu subiri Nimpigie Vanessa.
Vikram aliunganisha simu na kumpigia Vanessa lakini simu yake haikupokelewa.
Aliamua kumpigia tena Jimmy.
" uko wapi wewe??
"Niko nyumbni tajiri" alijibu Jimmy bila wasiwasi.
"Vanessa yuko wapi?? Aliuliza Vikram.
" Madam Vanessa..... Madam Vanessa alikuwa akizungumza huku akitafuta signal yake.
"Kwanini mnafanya upuuzi eti na mnatambua kabisa Mr Harlan bado anatufuatilia nasema hivi hao watu wapatikane haraka sana tena mara moja na endapo mtu akamkosa mtu ambaye nilimkabidhi nitawauwa wote" alikata simu baada ya kuzungumza kwa hasira huku akiwaacha wote wakiwa katika hali ya kutetemeka.
"Inabidi nimpate Larry, Rickson ataniuwa kabisa " alizungumza Obama huku akiendelea kumtafuta Larry pamoja walimu waliokuwa usiku ule shuleni.
"Tunafanyaje sasa?? Aliuliza Dr Kim.
"Mimi nafuatilia signal ya simu ya Vanessa" alizungumza Jimmy na kuondoka mbio mbio.
"Jimmy" aliita Dr Kim na kuondoka tena baada tu ya kufika kambini hapo muda si mrefu.
Rickson aliinua simu yake na kupiga tena kwa Tropina bado namba haikupatikana......alipiga simu kwa Vanessa na iliita tu bila kupokelewa.
"Ni kipi kimetokea tena jamani inabidi niwahi kwenda nyumbni" alizungumza na kuongeza mwendo wa gari lake.
Wakati huo Patrick alienda msalani kidogo kujisaidia aliporudi kwenye meza aliyomuacha Tropina hakumuona.
"Madam Tropina atakuwa kaenda wapi Alijiuliza na kutizama kulia na kushoto lakini hakuona mtu.
Hapo hapo simu yake iliita.
" Nani huyu ananipigia?! Alijiuliza na kupokea simu.
"Haloo.........Vickram ......unasemaje!?
"Usikate hiyo simu na usiondoke hapo mlipo" alizungumza Vikram na kupanda gari lake huku aki locate ni wapi simu hiyo imeweza kupokelewa.
"Anashida gani huyu kwanini ananiamrisha nisikate simu... Alijiuliza Patrick lakini hakupata maana yake aliiweka simu yake mfukoni mwake na kuendelea kumtafuta Tropina"
"Samahani nilimuacha bossi wangu hapa ambaye ni kipofu sijui kama mmemuona?? Aliuliza meza ya jirani ambayo haikuwa mbali na meza aliyomuachia Tropina.
" Yule binti aliyekuwa anakunywa kwenye mezaa hiyo hapo pembeni......amevaa gauni jekundu....kofia nyeusi..... Viatu....
"Huyo huyo umemuona ameelekea wapi?? Aliuliza Patrick.
" amevaa gauni jekundu alafu ni mwanamke?? Aliuliza mlevi yule na kumfanya Patrick asimame huku akimtizama kwa hasira.
"Si nakuuliza ni mwanamk??
" ndyo ni mwanamke " alijibu Patrick na kuanza kuondoka akiamini ya kuwa hana lolote la kumsaidia.
"Ameelekea kwenye vyoo vya kike alipita hapa akanipush kidogo nimwage pombe yangu akaelekea kule....au kule siyo chooni?? Aliendelea kuuliza
Patrick aliwahi kwenda katika choo cha wanawake na alipofika hapo aliita Madam Tropina Alisikia mlio wa maji ishara ya kuwa kuna mtu chooni alijisogeza mbali kidogo na eneo lile huku macho yake ykiwa hayabanduki kwenye mlango wa choo.
Dakika tano zilipita bila Tropina kutoka njee.
" Madam anafanyaje?? Alijiuliza na hapo hapo Vikram aliingia.
"Yuko wapi Tropina aliuliza Vikram.
" Unataka kujua yuko wpi ili nini?
"Napendaga kujibiwa swali nililouliza" alizungumza na kumtazama Patrick kwa macho yaliyokuwa mekundu.
Patrick alinyooshea mkono wake chooni.
Vikram alikimbilia chooni na kugonga Alisikia mlio wa maji yaliyokuwa yakichuruzika.
"Pinah tafadhali fungua mlango tuongee" alizungumza Vikram akigonga mlango..
Hapo hapo aliingia Dr Kim aliyeweza kupata maelekezo ya kuwa Patrick aliondoka kisha Tropina akamfuata nyuma kwa tax baada ya dakik 30 kupita.
Alipofika alitoa heshima kwa Vikram na kugonga mlango.
"Halo samahn nahitaji kutumia toilet unaweza ukafungua.......Hallo....... Tropina" aliita Dr Kim Ila bado palikuwa kimya.
"Ameingia saa ngapi?? Aliuliza Dr Kim.
" zimeshapita kama dakika 7 na hatoki alijibu Patrick na kumfanya Vikram aanze kuvuta kitasa kwa force.
Dr Kim alimshika na kumpa ishara ya asifanye chochote hapo hapo alikuja muhudumu wa hotel ile pamoja na baadhi ya Wateja baada ya kusikia vishindo
"Tafadhali tumaomba ufunguo wa ziada wa hapa kuna mtu ameeingia huku ndani na ameshindwa kutoka sasa tunahisi hayuko katika hali ya usalama. Alizungumza Dr Kim na muhudumu yule aliweza kukimbia haraka haraka na kwenda kuleta ufunguo mlango ulifunguliwa na watu walishtuka baada ya kuona damu ikiwa imechanganyikana na maji baada ya maji kujaa katika sink kisha kulifuata tofali lililokuwa chini ya pale likiwa limetapakaa damu.
Vikram aliishiwa nguvu miguuni na karibia adondoke lakini aliweza kushikwa na Dr Kim.
Watu waliokuwa ndani ya hotel ile walianza kupiga kelele na njee alionekana David mfanyakazi wa Adrian akicheka na kuondoka eneo lile.
****** ***** ******
Kwa upande wa Obama waliokuwa wakimtafuta Larry na walimu pamoja na wanafunzi baadhi walioamua kujiunga kwaajili ya kumtafuta Larry.
Ghafla zilisikika kelele za wanafunzi wawili waliokuwa wakiwaita walimu.
Obama alikimbia na kuelekea kwenye kelele hizo alipofika aliwasogeza wanafunzi na hakuamini macho yake kwa kile alichoweza kukiona.
Lilikuwa jabali Kubwa chini nililoweza kulowa damu huku likiwa na kipisi cheupe cha nguo aliyokuwa ameivaa Larry kwa siku hiyo.
Obama aliishiwa nguvu na kukaa chini huku akijilaumu kwa kumuacha Larry mwenyew aongee na simu.
**** ***** *****
Kwa upande wa Jimmy aliweza kuelekea mpaka mahali signal ilipokuwa ikionekana.
"Mbona ni duka la nguo alizungumza na kutembea mbele kuelekea kwenye duka hilo kwa haraka sana.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" samahani alizungumza Jimmy na kumuonyesha picha ya Vanessa kwenye simu yke.
"Mtu huyu yuko wapi?? Aliuliza Jimmy.
"Simu yake aliweza kuiacha hapa lakini yeye alitoka kidogo na kuelekea kwenye hoteli ile kwahiyo nilikuwa natafuta mtu wa kumuacha hapa ili nimpeleke simu yake" alizungumza muhudumu yule.
"Ahaaa ndiyo amenituma nije nimchukulie simu yake kwahiyo unaweza kunipatia alichukua simu ya Vanessa na kuelekea kule alikoweza kuelekezwa.
Alipofika aliliona kundi la wanawake watatu wakiwa wamekaa sehemu moja huku kiti kimoja kilichokuwa na pochi juu kikiwa hakina mtu aliamini ya kuwa Vanessa atakuwa pale.
Alijitengenezea vizuri koti lake kisha akaivaa miwani yake na kusogea mahala pale.
" hellow warembo....... Alizungumza baada tu ya kufika na kufanya wanawake wale waanze kujigusa gusa nywele kwa kujitengenezea.
"Naweza nikakaa hapa aliuliza kimtego.
" ndiyo unaweza" alizungumza mwanamke mmoja.
"Hpana hpo tayari kuna mtu ni mama Tropina"
"Ahaaa ameelekea wapi?? Aliuliza Jimmy.
" Kuna Baba alikuja hapa akamchukua na kuelekea naye ndani kule" alionyesha sehemu aliyowez kuelekea Vanessa.
Ghafla walipiga kelele.
Jimmy aligeuka na kuutazama upande ambao inasemekana Vanessa alielekea huko.
Alitoka mtu mmoja aliwa amejaa damu mwili wake wote mpaka usoni zikiwa zimemrukia rukia na akiwa ameishikilia cheni ya Vanessa mkononi.
Jimmy aliweza kutoa macho yake baada ya kuiona cheni hiyo kwani alikumbuka mwenye cheni hiyo ni Vanessa.
Jimmy aliwez kukimbia na alipofika alimvaa mzima mzima mtu yule bila kumsemesha neno lolote.
**** **** *****
Adrian alikuwa usiku nyumbani mwake akiwa anapata wine taratibu kabisa huku akiweza kucheka na kujipongeza kwa usiku huo hapo hpo simu yake iliita.
"Nani huyu ananipigia simu mimi wakati huu mzuri alizungumza Adrian na kutoa simu yake mfukoni.
"Winnie" alipokea simu yake.
"Nini??? Aliuliza Adrian kwa mshangao na kudondosha chini glass aliyokuwa akiitumia.
Ni baada ya Adrian kupokea simu ambayo iliweza kumshtua.
"Unamaanisha nini eti unaposema kuwa mtu uliyemtuma kashindwa kumkamata huyo kipofu! Sasa embu ngoja subiri" alizungumza Adrian na kukata simu yake.
Akimtafuta Daud kwenye simu yake.
"Wewe ulisema nani kamuuwa nani??
" Tropina ameuwawa na yule mtu aliyetumwa na Winnie.
"Ulimuona akimuuwa? Aliuliza Adrian.
" hapana lakini baada ya mlango wa choo alichokuwa ndani kufunguliwa kulikuwa na tofali lenye damu hivyo lazima atakuwa ameuwawa" alijibu Daud.
"Mshenzi mkubwa wewe na akili hauna.......huyo aliyetumwa na Winnie mwenyewe alikuwa njee ya choo akimsubiria Tropina lakini hakutoka mpaka alipowasili dereva wake alafu"
"Inamaana Tropina yuko wapi sasa?
" hilo swali unamuuliza nani mpumbavu wewe nimesema sitaki habari za kwamba yuko hai namtaka akiwa marehemu haraka sana " alizungumza kwa hasira Adrian na kutupa simu yake chini kwa hasira.
Diana aliweza kumsikia kwa yote aliyokuwa akiyazungumza alishtuka sana na haraka haraka aliweza kuondoka eneo lile akiwa na matunda aliyokuwa akiyaleta kwaajili ya Adrian.
Maneno yale hakuwa ameyasikia yeye tu pekee yake hata Danielle aliweza kuyasikia.
"Kwanini anataka kumuuwa Tropina?? Alijiuliza na kuondoka akiwa mnyonge sana.
Baada ya kufikiria takribani dakika tatu aliichukua simu yake na kumpigia Alice.
"Veronica inabidi umtafute Tropina mahali alipo umsaidie"
"Kafanyaje?? Aliuliza Alice aliyekuwa akipata kinywaji baridi.
" Adrian anataka kumuuwa inabidi umuokowe Tropina"
"Adrian anataka kumuuwa Tropina?? Aliuliza kwa mshangao.
"Nitakuelekeza yuko wapi na itabidi uende kumsaidia wewe na Calvin me siwez kutoka hapa nitamfuatilia Adrian kwa kila atakapokwenda.
Alice alikata simu na kumpigia Calvin haraka haraka lakini simu ikiwa inaita ghafla yaliingia mawazo mengine kichwani.
" Tropina ndiye atakayenifanya mimi nishindwe kuwa na Vikram hivyo hii ni nafasi nzuri ya mimi kuitumia kwaajili ya kummalizia mbali Tropina.
Hpo hapo simu yake ilipokelewa.
"Halo" aliita Calvin lakini Alice alikata simu ile. Kisha akacheka na hapo hpo iliingia msg kutoka kwa Danielle akimuelekeza ni wapi alipo Tropina.
"Waoooooo bravo!!! Alizungumza Alice akiachia Tabasamu pana mdomoni mwake kisha akaweka kinywaji chake mdomoni na akanywa taratibu kabisa.
**** ***** ****
Embu nipisheni ilisikika sauti ya mlevi mmoja aliyekuwa hotelini pale.
" haaa damu na maji.......yule mwanamke atakuwa ameuwawa na yule aliyemfuata nyuma "
Vikram alimfuata mlevi yule.
"Nani alimfuata nyuma?? Aliuliza Vikram na wakati huo kijana yule aliyetumwa na Winnie alishusha kofia yake kisha akatafuta njia nyingine kwaajili ya kupitia na kuondoka eneo lile.
"Si yule aliyevaa gauni jekundu na kofia........"
"Ameanza tena alizungumza Patrick na kumtizama Vikram.
" eeeeee huyo huyo alifuatwa na nani?? Aliuliza Vikram.
"Alifuatwa na huyu kijana alizungumza huku akimnyooshea mkono Patrick.
" Nilijua hakuna atakachokizungumza alisema Patrick akimtizama mlevi yule.
"Tofauti na huyu hakuna mwingine?? Aliuliza Vikram.
" atakuuliza tu yule aliyevaa gauni jekundu na kofia nyeusi hakuna atakachokizungumza cha maana alizungumza Patrick.
"Yule mwanamke aliyevaa gauni jekundu na kofia nyeusi" alirudia mlevi yule.
"Nilisema sikusema?? Aliuliza Patrick akitizama mlangoni ambako aliona mtu akiondoka eneo lile.
Watu waliachana naye wakiamini ni mlevi na hana msaada wowote.
" ndyo ni Huyo" alijibu Dr Kim.
"Kabla ya kufuatwa na huyu alifuatwa na kijana mmoja aliyekuwa amekaa pale" alinyooshea mkono alipokuwa amekaa kijana yule aliyeagizwa na Winnie.
Patrick alikumbuka ni kweli pale alikuwa amekaa mtu mmoja aliyekuwa amevaa kofia na kufunika nyuso yake.
Dr Kim alienda mpka pale na hapo aliweza kuona picha ikiwa imedondoka chini. Aliinua na ilikuwa ni picha ya Tropina.
Patrick alianza kuwatizama wote usoni.
"Mbona hamniulizi kaenda wapi?? Aliuliza mlevi yule na kumfanya Vikram amuulize.
" Kaenda wapi???
"Hata na yeye alikuwa hapa hapa na wakati mnafungua mlango na yeye alikuwa hapa hapa sasa kama angekuwa alimuuwa asingebaki hapa"
"Kwahiyo unataka kusemaje?? Aliuliza Vikram.
" Hili ni tofali la hapo juu inamaana yule binti mwenye gauni jekundu labda aligundua anafuatiliwa ndo maana akayafungulia maji hapa alafu wakati anatoa hilo tofaul ndo likiwa linamuumiza mikono ndo maana tukaona damu" alizungumza mlevi yule na maneno yake yaliweza kuwashangaza wengi kila alichokuwa akikizungumza ndicho kilichokuwa kimetokea.
"Kwahiyo huyo mtu yuko wapi?? Aliuliza Patrick.
" Hata wewe umemuuona akitoka njee" alizungumza mlevi yule.
Na Patrick alikumbuka kweli alimuon mtu akitoka njee.
"Kwanini sasa hukusema mapema?? Alifoka Patrick.
" kwani wewe uliniuliza mapema?? Aliuliza mlevi yule huku akisema anataka pombe nyingine.
"Kim muwekee umakini huyu mtu naenda kumtafuta Pinah" alitoa amri hiyo Rickson na kumpa ishara Patrick amfuate nyuma.
"Twende nikakununulie kinywaji alisema Dr Kim akimshika mkono mlevi yule na kumpeleka mezani kwaajili ya vinywaji zaidi.
***** ****** *****
Kwa upande wa Obama walikaa chini wanafunzi wote huku pamoja na walimu wakilia kwa kuamini ya kuwa Larry ameshaweza kupoteza maisha.
" sasa mwili wake uko wapi?? Aliuliza mwalimu mmoja baada ya kugundua hakuna mwili wa Larry.
"Mwili wa nani?? Ilisikika sauti ya mtu akiuliza.
Wote waligeuka nyuma na kutizama ni sauti ya nani baada ya kumuona kelele ziliweza kuzidi zaidi alikuwa Larry aliyeweza kuchafuka kwa damu mwilini mwake huku nguo yake ya juu ikiwa imeraruka.
" Mzuka?? Walipiga kelele wanafunzi na kuanza kukimbia.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hawa ni washenzi nini?? nani Mzuka!!? aliuliza Larry na kuelekea moja kwa moja hadi kwenye lile jabali lenye damu.
" Huyu mwanaharamu kaniharibia nguo yangu alilalamika baada ya kuona kipisi cha nguo yake chini.
"Ulikuwa wapi?? Aliuliza Obama kwa mshangao.
" Nilisikia kitu kikigusagusa begi langu la shule ndo nikafuata mlio kumbe alikuwa ni paka ndo tukaanza kimbizana naye kani kwarua kwarua lakini nimemuuwa" alisema Larry na kufanya wale walioweza kumsikia akiyazungumza hayo maneno washike mioyo yao.
****** ***** *****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment