Simulizi : Siri Ya Furaha
Sehemu Ya Nne (4)
Kijana huyo aliyekuwa amevaa kofia, alijifunika koti lake kichwani na Veronika aliamini alikuwa amelala. Hakujali juu ya jambo hilo na alibaki mtulivu katika siti yake huku akisubiria safari hiyo iianze.
Baada ya nusu saa safari hiyo ilianza, ni wakati ambao Rashid aliyekuwa uwanjani hapo alionekana akiiangalia ndege hiyo ikipaa angani huku moyoni akiumia kwani alihisi alikuwa akitenganishwa na mtu muhimu sana katika maisha yake. Mara baada ya ndege hiyo kuzamia, aliingia katika gari lake kabla ya kuondoka akiwa na lengo la kurudi katika kitongoji cha Yelling ambako walikuwa wamepanga. Alijipa faraja juu ya upweke aliokuwa nao lakini aliamini jambo hilo lingepata ufumbuzi baada ya muda mfupi kwa vile mapumziko waliyopewa na chuo yalikuwa ya miezi miwili.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuwapo angani kwa dakika kama kumi Veronika alimshuhudia kijana aliyekuwa pembeni yake akijifunua koti alilojifunika. Alipata mshtuko kidogo mara baada ya kijana huyo kujifunua koti hilo, huku akiwa bado amevaa kofia. Alikuwa akimtazama kijana huyo kwa ubavu na hakufanikiwa kumwoana vizuri zaidi ya hisia kali zilizotawala kichwa chake. Mshtuko wake uliongezeka zaidi mara baada ya kijana huyo kutoa kofia yake na kumgeukia Veronika kabla ya kuanza kumtazama. Kijana huyo hakuwa mwingine bali ni Moses ambaye Veronika alishamhisi alipojifunua koti lake. Mapigo yake ya moyo yaliongezeka katika wakati ambao walikuwa wakitazamana pasipo kuongea jambo.
“hi! My love, you look good” (hi! Mpenzi umependeza) ilikuwa sentensi ya kwanza kutoka kwa Moses ambayo hakujibiwa na Veronika ambaye alionekana kukosa amani ghafla katika safari yake hiyo. Moses hakukata tamaa aliendelea kumwongelesha Veronika ambaye baada ya muda mfupi alikosa uvumilivu na alianza kubishana na kijana huyo huku akimweleza kuwa hakuwa na mpango wa kurudiana naye. Moses hakujali juu ya jambo hilo kwani alikuwa na mipango kadhaa kichwani mwake. Aliwaza kuja kukaa nchini kwa siku kadhaa ili kufanya ushawishi wa kurudiana na mpenzi wake huyo.
Mpaka wakati huo alikuwa amemfuatilia sana Veronika na mwishoe alifanikiwa kugundua mrembo huyo alikuwa akisafiri na shirika hilo la ndege. Hakupoteza muda kwani naye aliamua kuilipia siti iliyofuatana na Veronika akiwa na lengo la kumfanyia ushawishi ili warudiane.
Baada ya masaa kadhaa Veronika alikuwa kimya tena, hakutaka kuongea tena na mwanamume huyo ambaye hakukata tamaa. Walisafiri kwa masaa kumi huku wakiwa wamepita katika jiji la Cairo nchini Misri kabla ya kukaa kwa muda mrefu katika uwanja wa ndege wa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Majira ya saa kumi na nusu alfajiri ndege hiyo waliyopanda ilikuwa ikitua katika uwanjwa wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa jijini Dar es salaam. Wakati huo Veronika alipata amani moyoni mwake kwani aliamini ilikuwa vigumu kwa Moses kumpata akiwa nchini. Hiyo ilitokana na ulinzi mkali aliokuwa akiupata kutoka kwa baba yake akiwa nchini.
“Moses, you have a chance to love another woman and don’t waste you time chasing me because I’m in love with Rashid” (Moses, unayo nafasi ya kumpenda mwanamke mwingine na usipoteze muda wako kwa kunifuatilia kwa sababu nampenda Rashid) alisikika akiongea Veronika wakati akiwa anasimama tayari kwa kushuka katika ndege hiyo. Ilikuwa ni wakati ambao abiria waliokuwa katika ndege hiyo walihurusiwa kuanza kushuka.
Moses hakujali hata kidogo maelezo hayo aliyopewa na Veronika na aliwaza kuwapo nchini kwa siku kadhaa ili aendelee kumfuatilia mrembo huyo. Abiria walianza kushuka na Moses alikuwa anamfuatilia Veronika kwa umakini huku akiwaza kuhakikisha anaifahamu sehemu aliyokuwa akiishi.Hakupata taabu kwani alikuwa na vielelezo vyote muhimu vilivyomhurusu kuwapo nchini kwa siku kumi na nne. Baada ya dakika arobaini na tano alikuwa katika sehemu ya mapokezi akimsubiria Veronika atoke kwa vile alikuwa na mizigo yake kadhaa ambayo alikuwa hajaipata. Tayari alikuwa amekodi teksi ya kumfuatilia Veronika sehemu ambayo alikuwa akielekea. Katika eneo hilo alilokuwapo kulikuwa na watu wengi na hakuweza kufanikiwa kumhisi mtu yeyote kama ndugu yake Veronika.
Baada ya dakika tano Veronika akitoka eneo hilo akiwa analivuta toroli dogo lililokuwa na mizigo yake, ni wakati ambao Moses alimgundua baba yake Veronika. Alimshuhudia mwanamume huyo mtu mzima akimkimbilia Veronika kabla ya kuonekana wakikumbatiana kwa muda mrefu. Baada ya sekunde kadhaa mzee huyo aliwaoneshea ishara vijana wake saba ambao walionekana kama walinzi wake huku wakiwa wamevaa suti nadhifu. Vijana hao walibeba mizigo ya Veronika na taratibu walianza kutembea kuelekea nje ya eneo hilo. Huko waliishia kupanda katika magari matano ya kifahari yaliyokuwapo uwanjani hapo. Moses alimshuhudia Veronika na baba yake wakipanda katika gari la tatu, hakupoteza muda alielekea katika teksi aliyoikodi kabla ya kumwamuru dereva ayafuatilie magari hayo na ikawa hivyo.
Dereva huyo alitekeleza agizo hilo na walikuwapo barabarani kwa muda wa saa moja na robo kutokana na foleni ya magari iliyokuwapo barabarani kabla ya kuishia katika nyumba moja ya kifahari iliyokuwapo Masaki. Veronika akiwa na msafara huo aliingia katika nyumba hiyo ambayo Moses aliamini ndio ambayo mrembo huyo alikuwa akiishi na familia yake. Aliyachunguza vizuri mazingira ya eneo hilo kabla ya kumweleza dereva wa gari hilo ampeleke katika hoteli ya Movenpick. Jambo hilo lilichukua nafasi na majira ya saa tano asubuhi Moses alikuwa amelala katika moja ya chumba cha hoteli hiyo ya kifahari kutokana na uchovu aliokuwa nao.
Siku iliyofuata alianza zoezi la kumfuatilia Veronika ambalo lilikuwa gumu kupindukia. Nyumba hiyo ya bwana Lamos Maputo ilikuwa na ulinzi mkali na zaidi hakufanikiwa kumwona Veronika akitoka katika nyumba hiyo. Kwa siku kumi mfululizo alikuwa akishinda karibu na geti kuu la nyumba hiyo akiwa na imani ya kukutana na Veronika lakini hakufanikiwa. Mara chache alimwona Veronika akitoka katika nyumba hiyo huku akiwa katika pamoja na baba yake ambaye alitembea na walizi muda wote. Wakati huo akiwa amebakiwa na siku nne za kuwapo Tanzania alihisi zoezi hilo lingekuwa gumu kama angeendelea kuishia kukaa karibu na geti hilo akimsubiri Veronika. Mbali na taarifa kadhaa alizozipata za ukali wa bwana Maputo juu ya watu wanao mfuatilia mwanaye, hakujali juu ya jambo hilo.
Siku iliyofuata majira ya saa mbili alielekea mpaka katika geti kuu la nyumba hiyo ambako alikutana na walinzi wanne waliokuwa eneo la getini la nyumba hiyo. Aliwaeleza lengo lake la kuhitaji kukutana na bwana Lamos Maputo ambaye alidai alikuwa na miadi naye asubuhi ya siku hiyo. Aliamua kuhitaji kukutana na mzee huyo kwa vile aliamini hangehurusiwa kuingia kama angehitaji kumwona Veronika. Walinzi hao walimpigia simu bwana Lamos Maputo na kumweleza juu ya jambo hilo. Tajiri huyo alishangaa juu ya maelezo hayo na aliahidi kutoka nje baada ya ya muda mfupi.
Zilipita dakika kumi kabla ya mzee huyo ambaye sura yake ilionesha hakuwa na huruma kuanza kutembea akitoka nje. Alikuwa amevaa nguo zake za kulalia huku akiwa na shauku juu ya mtu aliyedai kuwa na miadi naye. Mara baada ya kufika eneo la getini Moses alimsalimia mzee huyo kwa lugha yake ya kiingereza na bwana Lamos Maputo alijibu salamu hiyo mara baada ya kutafsiriwa na mlinzi wake mmoja. Alipoulizwa shida yake Moses alimweleza kuwa alifika eneo hilo akiwa na lengo la kumwona Veronika aliyedai alikuwa rafiki yake wa Karibu. Bwana Lamos Maputo alipandwa na hasira za ghafla huku akionekana kurudia tabia yake ya miaka mingi wakati Veronika akisoma Sekondari. Akiwa hajajibu kitu alimwamuru mlinzi wake mmoja aende akamwite Veronika na baada ya dakika tano msichana huyo alikuwapo eneo hilo. Alikuwa na mshtuko mkubwa ambao hakuuonesha, lakini alitambua wakati huo jambo ambalo lingefuata kwa Moses ni karaha. Hata Moses alipomsalimia, Veronika hakujibu na alikuwa akimtazama kama vile alikuwa hamfahamu. “unamfahamu huyu mpuuzi” aliuliza bwana Lamos Maputo kwa ukali swali ambalo alijibiwa haraka. “noo! Dad simfahamu hata kidogo kwani ni nani?” alisikika Veronika akijibu huku akitikisa “ok! Rudi ndani mwanangu mpendwa, huyu leo atanitambua” alisikika bwana Lamos Maputo katika wakati ambao Moses alikuwa akiwaangalia pasipo kutambua jambo walilokuwa wakiongea.
Veronika alianza kutembea taratibu akielekea ndani ya nyumba yao huku akiwaacha eneo hilo. Wakati akitembea alikuwa akigeuka mara kadhaa kumwangalia Moses na alimwonea huruma sana kwa vile alimfahamu vizuri baba yake ambaye hakutaka wanaume wamfuatilie hata kidogo. Mara baada ya Veronika kuzamia katika nyumba yao bwana Lamos Maputo alisikika “wewe kijana unajifanya mmarekani na hujui kiswahili kumbe umekuja kumfuatilia mwanangu, sasa leo utatutambua” alikurupuka kabla ya kumpiga kichwa usoni kilichompeleka mpaka chini. Aliwaoneshea ishara walinzi wake ambao kwa kasi ya ajabu wamlivamia Moses eneo hilo la chini alilokuwa ameanguka kabla ya kuanza kumshushia kipigo cha nguvu. Walimpiga kwa viatu vyao vya kiaskari walivyokuwa wamevaa bila huruma huku mmoja wao akionekana kutumia kitako cha bunduki yake kumpiga kijana huyo sehemu tofauti za mwili wake.
Moses alilia kwa uchungu juu ya kipigo hicho alichokipata na damu ilikuwa imezunguka eneo hilo katika dakika mbili tu walizokuwa wamempiga. Wakati huo Veronika kwa umbali alionekana akiangalia tukio hilo kupitia dirisha la chumba chake kilichokuwa ghorofa ya kwanza ya nyumba hiyo. Baada ya kuona mpenzi wake huyo wa zamani akipigwa kisawasawa aliumia moyoni pia aliamua kwenda kujilaza kitandani kwake ili asishuhudie tukio hilo. Baada ya dakika tano Bwana Lamos Maputo aliwaelekeza walinzi wake waache zoezi hilo, alijivuta toka mbali na kumvamia kijana huyo kwa kumpiga kwa teke tumboni kabla ya kusikika. “hakuna mtu atakaye muoa mwanangu…ataishi kama mimi pumbavu”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo Moses alikuwa amezimia, bwana Lamos aliwaamuru walinzi hao wamtoe eneo hilo la nyumbani kwake haraka iwezekanavyo na jambo hilo lilichukua nafasi. Walinzi wawili walimpakiza Moses katika siti za nyuma za gari moja aina ya Mercedez Benz kabla ya kuliondoa kwa kasi eneo hilo. Waliongoza mpaka katika fukwe ya bahari ya hindi ambako walienda kumwacha Moses kabla ya kurudi katika eneo lao la kazi. Moses alizinduka majira ya saa kumi jioni akiwa katika hospitali ya Aga Khan huku akiwa amezungukwa na watu kadhaa ambapo mmoja wao alijitambulisha kama balozi wa Marekani nchini Tanzania.
Walimweleza kuwa watu kadhaa walimchukua katika fukwe ya bahari ya Hindi akiwa katika hali mbaya na walipomchunguza waligundua alikuwa raia wa Marekani kutokana na vitambulisho alivyokuwa navyo. Watu hao waliomsaidia ndio waliotoa taarifa katika ubalozi wa Marekani nchini juu ya kukutwa kwake akiwa ameumia katika fukwe ya bahari ya Hindi. Moses alikuwa ameshonwa nyuzi sehemu tofauti za mwili wake na mkono wake wa kushoto ulikuwa umevunjika, alikuwa na maumivu makali sana ambayo yalisababisha auchukie uamuzi wake wa kuja Tanzania. Maofisa wa jeshi la polisi walipomhoji juu ya jambo lililotokea hakutaka kueleza ukweli huku akidai alikuwa amevamiwa na kundi la vibaka wakati akiwa katika fukwe hizo za bahari ya Hindi.
Aliamini kumtaja bwana Lamos Maputo kuwa alihusika na suala hilo kungefungua ukurasa mwingine wa kisheria na zaidi asingeweza kumpata tena Veronika mwanamke aliyekuwa wa ndoto zake. Hakutaka kuwaeleza askari ukweli pia kwa vile hakuwa na hamu na Tanzania tena na alihitaji kurudi kwao nchini Marekani haraka. Alimwomba balozi wa Marekani nchini amsaidie kumwandalia safari yake aliyopanga kusafiri siku nne zilizofuata. Balozi huyo alielewa jambo hilo na aliwagiza wafanyakazi wake kuhakikisha wanamtafutia tiketi kijana huyo ili arudi nchini Marekani.
Siku hiyo ilipofika majira ya saa nane mchana gari moja la ubalozi wa Marekani nchini lililonekana likitoka katika hoteli ya Movenpick likuwa na Moses ambaye bado alikuwa akiumwa huku akiwa amefungwa bandeji sehemu tofauti za mwili wake ilhali mkono wake wa kushoto ukiwa umevunjika. Majira ya saa kumi na moja tayari alikuwa safarini kuelekea Marekani akitumia usafiri wa shirika la ndege la British Airways. Ndoto zake wakati huo zilikuwa juu ya jimbo la Illinois katika kitongoji cha Chicago ambako alikuwa akitokea. Alikuwa ameikumbuka sana familia yake lakini kichwani hakuwaza kuacha kumfuatilia mwanamke aliyempenda, Veronika mbali na kipigo alichokuwa amekipata.
Alikuwa ameikumbuka sana familia yake lakini kichwani hakuwaza kuacha kumfuatilia mwanamke aliyempenda, Veronika mbali na kipigo alichokuwa amekipata.
* * * *
Rashid alikuwapo katika kitongoji cha Yelling kilichopo katika jimbo la Cambridge, wakati huo alikuwa akichora katuni ya michezo iliyokuwa ikitoka kila siku ya Jumamosi katika gazeti la The Sun. Alikuwa akiwasiliana na Veronika ambaye alikuwepo nchini Tanzania, siku zote alikuwa akipigiwa simu na mrembo huyo. Alikuwa akihofia kumpigia kwa vile alitambua kama bwana Lamos Maputo angetambua jambo hilo wangepata matatizo katika uhusiano wao. Huku akiwa analipwa fedha za kutosha na gezeti la The Sun alilokuwa akifanyia kazi, alikubwa na tatizo ambalo alikuwa akilihofia mwisho wake. Bi. Jane ndiye aliyekuwa kikwazo kwani alifikia hatua ya kumweleza kuwa alimtaka awe mpenzi wake. Jambo lililomuumiza sana kichwa, mwanamke huyo alitishia kutuma picha za Veronika akiwa na Moses kwa bwana Maputo kama angegoma kutekeleza ombi hilo.
Alijitahidi kumkwepa mwanamke huyo huku akimpa ahadi za uongo zilizokuwa zikimfariji. Wakati huo alikuwa akimsubiria kwa hamu Veronika ili wajue jambo la kufanya. Tayari Bi. Jane alishaanza kujenga mazoea ya kumtembea Rashid katika nyumba waliyokuwa wamepanga na Veronika katika kitongoji cha Yelling. Siku zote hakuutambua ukweli juu ya nyumba hiyo huku akimini kuwa alikuwa akiishi Rashid peke yake Baada ya miezi miwili Veronika alirudi nchini Uingereza na kwenda kuungana na Rashid kwa ajili ya mwaka kwa pili wa masomo yao.
Alikuwa na furaha kuungana na mchumba wake kwa vile alimkumbuka sqna baada ya kuwapo katika mapumziko yake ya muda mrefu nchini Tanzania. Jambo ambalo lilikuwa likiumiza kichwa cha Veronika lilihusiana na Moses. Alikuwa na mashaka kwa kiasi kikubwa juu ya uhai wa kijana huyo. Kila wakati alipokumbuka jinsi alivyopigwa na walinzi wa nyumbani kwao waliokuwa wakiongozwa baba yake alikosa raha kabisa. Kwa kiasi kikubwa alihisi alikuwa akihusika na tukio hilo ambalo hata hivyo halikuweza kubadili msimamo wake juu ya upendo aliokuwa nao kwa Rashid. Alijaribu kumtafuta Moses kwa kutumia namba yake ya simu aliyokuwa akiitumia akiwa chuoni hapo lakini alikuwa hapatikani. Jambo hilo lilimpa hofu kidogo kwa vile tayari masomo yalikuwa yameshaanza chuoni hapo na hakufanikiwa kumwona Moses.
Wakati huo Veronika alikuwa akitambua juu ya kila jambo lililomhusu Bi. Jane, mwanamke aliyetumwa na baba yake kumchunguza. Alitambua juu ya jitihada za mwanamke huyo aliyekuwa na ndoto za kumpata Rashid. Hakujali juu ya jambo hilo huku hofu aliyokuwa nayo kwa miaka mingi moyoni ikianza kumtoka. Alijitambua kuwa alikuwa mtu mzima wa kupanga mambo yake mwenyewe na zaidi aliichukia tabia ya kufuatiliwa na baba yake ambayo siku zote hakufanikiwa kupata sababu ya jambo hilo.
Siku moja ya mwisho wa juma majira ya saa moja usiku bi. Jane alionekana akishuka kutoka kwenye teksi ya kukodishwa kabla ya kuanza kutembea taratibu akijongea nyumba ambayo siku zote alikuwa akiamini alikuwa akiishi Rashid peke yake. Mawazoni alitawaliwa na mambo mengi huku akiwa na imani ya kulala na kijana huyo kwa usiku mzima. Alikuwa amemfuatilia kwa muda mrefu sana lakini siku hiyo aliamini ndoto ya kuwa na kijana huyo ingetimia. Huku akiwa amebeba mkoba wake mdogo katika bega la kushoto, mkono wake wa kulia alibeba mfuko uliokuwa na zawadi tofauti alizomnunulia Rashid.
Kadri alivyozidi kujongea katika nyumba hiyo iliyokuwapo katika kitongoji cha Yelling ndivyo ambavyo hata mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakienda kasi. Hatimaye aliufikia mlango wa nyumba hiyo na kuugonga mara kadhaa pasipo kufunguliwa. Hakujali juu ya jambo hilo kwa sababu alikuwa tayari mwenyeji wa nyumba hiyo, aliamua kufungua mlango na kuingia kwa vile mlango huo ulikuwa umeegeshwa. Mara baada ya kuingia katika nyumba hiyo alipokelewa na mandhari nzuri ya sebule hiyo ambayo alikwisha izoea. Jambo moja lilimshtua na alihisi lilikuwa tofauti na jinsi ambavyo alikuwa akiifahamu nyumba hiyo. Aliuona mkoba wa mwanamke ukiwa umewekwa katika sofa mojawapo lililokuwa katika chumba hicho lakini zaidi kulikuwa na viatu vya kike vilivyovuliwa sebuleni hapo.
Jambo hilo lilimshtua na alihisi Rashid alikuwa na mwanamke siku hiyo katika nyumba yake. Alivua viatu vyake vyake vya wazi kisha aliuweka mkoba wake katika meza moja iliyokuwapo sebuleni hapo pamoja na mfuko uliokuwa na zawadi za Rashid. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio, wivu ndio uliokuwa umetawala kichwani mwake. Alianza kutembea taratibu huku akinyata kuelekea katika chumba ambacho alitambua kilikuwa cha Rashid. Mapigo yake ya moyo yaliongezeka zaidi kila alipozidi kukisogelea chumba hicho kutokana na kelele alizosikia ambazo zilimuumiza moyoni. Mara baada ya kuufikia mlango huo alijikaza na kuufungua taratibu, ni wakati ambao aliumia zaidi kabla ya kuurudisha taratibu mlango huo pasipo kuonwa na watu waliokuwa katika chumba hicho.
Alikuwa amemshudia Rashid na Veronika wakiwa katika wakati wao, aliumia sana juu ya jambo hilo lilomfanya aanze kutokwa na machozi pasipo kujitambua. Alianza kutembea kwa kunyata kurudi eneo la sebuleni ambako alikuwa ameacha vitu vyake. Alipofika sebuleni hapo aliuchukua mkoba wake pamoja na mfuko aliofika nao kabla ya kuvaa viatu vyake vya wazi na kutembea haraka kuelekea nje. Baada ya sekunde kadhaa alikuwa nje ya nyumba hiyo akitembea haraka huku akilia kwa sauti. Hasira alizozipata zilimkaa shingoni kama vile alikuwa amemfumania mume wake na mwanamke mwingine.
Kulipa kisasi kwa kuwaumiza Rashid na Veronika ndio jambo lilomkaa kichwani. Aliwaza kuifanya kazi aliyotumwa na bwana Lamos Maputo kiufasaha ili kuwaumiza watu hao. Kwa jinsi alivyozifahamu hasira za tajiri huyo aliamini angetosha kuutuliza moyo wake. Alipanga kuanza kumfuatilia Rashid na Veronika ili aongeze idadi ya picha za kumtumia bwana Lamos Maputo kwa vile kwa wakati huo aligundua watu hao walikuwa wapenzi. Baada ya saa moja na nusu alionekana akishuka katika teksi moja tayari kwa kuelekea katika nyumba yake iliyokuwa katika kitongoji hicho cha Dullingham.
Akiwa nyumbani kwake alituliza akili yake kabla ya kuanza kuandaa kamera yake tayari kwa kuanza kuwafuatilia Rashid na Veronika. Wakati huo hakuwa na huruma hata kidogo huku akijilaumu kwa kukiuka masharti aliyopewana bosi wake bwana Maputo ya kuhakikisha anatoa taarifa zozote za kimahusiano zilizomhusu Veronika. Siku iliyofuata asubuhi na mapema alielekea chuo kikuu cha Cambridge huku akiwa na fedha za kutosha pamoja na kamera iliyokuwa kila kitu kwake. Hakupata taabu kwa vile alikuwa anayafahamu vizuri mazingira ya chuo hicho. Majira ya mchana zoezi lake lilianza kuzaa matunda kwani alifanikiwa kumpiga Veronika picha na Rashid wakiwa wamekumbatiana kabla ya kupanda gari lao na kuelekea katika moja ya mgahawa wa chuo. Hakupoteza muda naye aliwafuatilia nyuma kwa teksi ya kukodi kwa vile alitambua wakati huo walikuwa wakielekea kupata chakula cha mchana.
Baada ya dakika kumi alikuwa na kamera yake katika mgahawa huo huku akijificha na kofia yake aliyokuwa ameivaa. Akiwa na muda mfupi wa kuwapo katika mgahawa huo bi. Jane alifanikiwa kuwapiga picha nyingine wakati wakilishana chakula. Aliendeleaza zoezi lake mpaka katika kitongoji cha Yelling walikokuwa wakiishi. Hakuishia hapo, siku iliyofuata aliendelea na zoezi hilo katika wakati ambao aliridhika na picha alizokuwa amezipata. Tayari alikuwa na picha zaidi ya thelathini ambazo alizipia wakati Veronika akiwa na uhusiano wa kimapenzi na Moses pamoja na hizo alizozipata wakati huo.
Siku hiyo akiwa nyumbani kwake alikunywa pombe kwa kiasi kikubwa huku akijipongeza kwa kazi aliyokuwa amefanya. Aliamini zoezi hilo lilikuwa la maana kwa bwana Lamos Maputo aliyegharamia fedha nyingi kumlipa ili amfuatilie mwanaye. Siku iliyofuata iliyokuwa ya Jumamosi hakuwa na kazi kubwa zaidi ya kuzituma picha kwa tajiri huyo. Picha zote alizituma kwa bwana Lamos Maputo akitumia anuani yake ya barua pepe ambayo alipewa awali ili aitumie kutoa taarifa zozote zilizokuwa zikimhusu Veronika. Mara baada ya zoezi hilo alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia tajiri huyo akiwa na lengo la kumweleza juu ya hatua hiyo aliyokuwa ameifikia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu ya tajiri huyo iliita kwa muda mfupi kabla ya kupokelewa na kusikika sauti nzito ya bwana Lamos Maputo. “eeh! Bi. Jane unaendeleaje nchini Uingereza na je una jipya kuhusu mwanangu?” alisikika tajiri huyo aliyekuwa akiongea haraka.
“ndiyo bosi, nimekutumia uchunguzi wangu kupitia anuani yako ya barua pepe”
“kuna jambo lolote baya linalomhusu Veronika, maana sasa naingia kwenye mkutano mkubwa” alisikika bwana Lamos Maputo ambaye kwa wakati huo alikuwa akijiandaa kuingika katika ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro hotel ambako kulikuwa na mkutano wa matajiri wakubwa wa Afrika uliokuwa ukihusu uwekezaji.
“usijari bosi kila kitu nimekutumia” alisikika bi. Jane katika hali ya kumtuliza bwana Lamos Maputo. “ ok! Namtuma kijana wangu akachukue kila kitu ulichonitumia” alisikika bwana Lamos upande wa pili kabla ya kukata simu yake.
Bi. Jane alipiga kelele za furaha juu ya jambo hilo na alitambua lengo lake lilikuwa limefanikiwa. Wakati huo alitaka Veronika na Rashid wajue juu ya jambo hilo. Alitambua wange changanyikiwa kusikia picha za uhusiano wao zilikuwa zimetuimwa kwa bwana Lamos Maputo. Kwake jambo hilo lilimpa amani na zaidi alikuwa akiifikiria hatua ambayo bwana Lamos Maputo angeichukua pasipo kupata jibu. Alikodi teksi akiwa na lengo la kuelekea katika kitongoji cha Yelling ambako aliamini angewakuta kwa vile siku hiyo ya Jumamosi walikuwa hawaendi chuo. Baada ya masaa mawili alikuwa akitembea taratibu kujongea katika nyumba yao waliyokuwa wamepanga. Gari lao aina ya Ferrari lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba hiyo lilimpa jibu kuwa watu hao walikuwepo nyumbani hapo.
Hakugonga mlango wa nyumba hiyo ambao ulikuwa umeegeshwa na mara baada ya kuingia alimshuhudia Rashid akiwa amekaa sehemu moja na Veronika ambaye alikuwa anamchezea nywele zake ilhali wakisikiliza muziki uliosikika kwa sauti kubwa katika sebule hiyo waliyokuwapo. “ naona mnakula raha za dunia vijana” ilikuwa sauti ya bi. Jane iliyomtoa Veronika kutoka mikononi mwa Rashid aliyekuwa akizichezea nywele zake. Aliposimama na kumwona mama huyo alirudi eneo alilokuwa amekaa na Rashid pasipo uoga “kama unavyoona mwanamke au unataka uwe wewe” alijibu Veronika kwa kejeli zilizompandisha hasira bi. Jane ambaye hakuchelewa kuanza kulielezea kila jambo lililokuwa linaendelea juu ya picha alizokuwa amewapiga pamoja na zile zilizomhusu Moses. Rashid alipata mshtuko huku akiwa na hofu tele juu ya bwana Lamos Maputo ambaye alishawahi kumpiga akiwa kidato cha tatu kwa kuwa na uhusiano na mwanaye.
Hali ilikuwa tofauti kwa Veronika ambaye alionekana kutojali jambo hilo. Hata bi. Jane alipowaonesha picha alizowapiga bado hakuonesha mshtuko alionekana kuwa tayari kwa jambo lolote ambalo lingefuatia.
Hali ilikuwa tofauti kwa Veronika ambaye alionekana kutojali jambo hilo. Hata bi. Jane alipowaonesha picha alizowapiga bado hakuonesha mshtuko alionekana kuwa tayari kwa jambo lolote ambalo lingefuatia. Mwishoe mwanamke huyo aliondoka huku akiwa amemwacha Rashid katika hofu kupindukia, wakati huo alikuwa akiwaza kukimbia kwa vile alitambua bwana Lamos Maputo angemuua. “Rashid unanipenda?” alisikika Veronika akimuuliza Rashid muda mfupi baada ya bi. Jane kuondoka. “ndiyo nakupenda lakini…” kabla hajaendelea alikatishwa “… lakini nini hakuna kosa tunalolifanya nina umri wa miaka ishirini na tatu na ninatambua mema na mabaya… naomba uniahidi kama utakuwa na mimi siku zote za maisha yako” alisikika Veronika katika sauti iliyokuwa ya chini kidogo. “ok! Nakuahidi nitakuwa na wewe Veronika siku zote” alisikika kabla ya kuonekana wakikumbatiana.
Ratiba zao za siku hiyo walizivunja ghafla na walishinda nyumbani kwao huku wakijadili mambo tofauti ya maisha yao ya baadaye. Kila mmoja aliahidi kuwa na mwenzie mbali na jambo lolote ambalo lingetokea kutokana na nguvu ya kifedha ya bwana Lamos Maputo. Kuna wakati Rashid alikuwa akitokwa na machozi kwa vile hakuwa tayari kumkosa mwanamke huyo aliyekuwa akimpenda sana katika maisha yake. Hatimaye ilitimia saa moja jioni, walikuwa hawajala kwa siku nzima na simu ya Veronika ilikuwa imewashwa kwa vile walikuwa wakitarajia kuwa bwana Lamos angepiga simu muda wowote. Haikuwa hivyo kwani mpaka inatimia majira ya saa nne na nusu usiku hakuna simu yoyote iliyopigwa iliyohusu picha zao zilizokuwa zimetumwa na bi. Jane. Walianza kusinzia ilhali wakiwa wamekumbatiana eneo hilo la sebuleni huku wakiwa hawana imani ya jambo lolote kutokea siku hiyo. Majira ya saa saba kamili usiku hisia zao zilichukua hatua, simu ya Veronika ilianza kuita na kuwashtua kwa vile walishaanza kupitiwa na usingizi.
Veronika aliichukua simu yake haraka na kuitazama kabla ya kulishuhudia jina la baba yake kama mpigaji. Alishtuka kidogo na kumfanya Rashid naye asogelee simu hiyo kabla ya kugundua ilikuwa imepigwa na bwana Lamos Maputo. Simu hiyo iliita pasipo kupokelewa na Veronika, baada ya sekunde kadhaa ilipigwa tena na wakati huo alijikaza na kuipokea. “haloo! Naongea na Veronika Lamos Maputo?” ilisikika sauti ya mtu mmoja upande wa pili sauti ambayo hakuitambua hata kidogo. “ndiyo mimi unasemaje…. Halafu mbona umetumia simu ya baba yangu?” “ok! Naomba utulie na unisikilize kwa makini kuna jambo limemtokea baba yako…”
* * * *
Bwana Lamos Maputo aliwasili nyumbani kwake majira ya saa nne na nusu usiku baada ya kushinda katika mkutano mkubwa uliokuwa ukihusu uwekezaji ambao uliwahusu wafanyabiashara wakubwa. Mpaka wakati huo akiwa anatokea katika ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro hotel hakuwa na amani kwa siku nzima. Alikuwa akiwaza juu ya taarifa alizokuwa amezipata kutoka kwa bi. Jane ambaye alimweleza kuwa alikuwa amemtumia vielelezo kadhaa vilivyomhusu mwanaye juu ya maisha aliyokuwa akiishi nchini Uingereza. Mara baada ya kushuka kutoka kwenye gari lake alianza kutembea haraka kuelekea katika sebule ya nyumba yake.
Kichwani alikuwa akiwaza kuona vielelezo aliyokuwa ametumiwa na bi. Jane kwa kutumia anuani yake ya barua pepe. Tayari alikuwa amemwagiza kijana wake mmoja atembelee anuani yake ya barua pepe na alitarajia kuona kila kitu kikiwa sawa. Mara baada ya kuingia katika nyumba hiyo ambayo siku zote alikuwa akiishi peke yake aliongoza mpaka katika ofisi yake ndogo ya nyumbani hapo. Alifanya hivyo kwa vile kijana aliyempa jukumu la kuitembelea anuani yake ya barua pepe alimweleza alikuwa ameweka picha katika ofisi yake. Alikuwa na shauku ya kuziona picha hizo ambazo hakupewa maelezo yake hata kidogo.
Alipofika katika ofisi hiyo aliichukua haraka bahasha ya kaki iliyokuwa juu ya meza kabla ya kukaa kwenye kiti. Aliifungua bahasha hiyo haraka kabla ya kuanza kuangalia picha zilizokuwapo ndani ya bahasha hiyo. Baada ya sekunde kadhaa alianza kuvuruga nywele zake kama mtu aliyekuwa amechanganyikiwa, hakuamini hata kidogo matukio aliyokuwa akiyaona katika picha hizo zilizokuwa na maelezo kadhaa. Alihisi utajiri wake uko hatarini kwa vile mrithi pekee wa mali zake alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi ambayo siku zote alimuepusha nayo. Alimkumbuka mganga wake wa jadi bwana Kamaraj Sankar ambaye alimpa uatajiri huo kabla ya kujihisi akichanganyikiwa ghafla. Hasira zake zilimpanda zaidi alipoiona picha za kijana mmoja ambaye alimpiga miezi kadhaa iliyokuwa zimepita kwa kushirikiana na vijana wake ambaye naye alionekana kuwa na uhusiano na mwanaye, Veronika. Kuua ndio jibu alilowaza kuwafanyia vijana wawili waliokuwa wakitembea na mwanaye na kumrudisha Veronika Tanzania lilikuwa ni jambo la pili alilotaka lichukue hatua ndani ya siku tatu.
Alitoka akikimbia kuelekea nje ya nyumba yake kabla ya kuishia kupanda gari lake la kifahari aina ya Bentley Continental GTZ, aliliondoa kwa kasi isiyo ya kawaida hata walinzi wake waliposhuhudia jambo hilo walifungua geti la nyumba hiyo haraka. Wakati huo akili yake ilikuwa haijatulia kwani alikuwa akiwaza kufika nchini Uingereza. Alilikimbiza gari lake akiwa na lengo la kuelekea uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiwa njiani alikuwa akilitaja jina la mwanaye ambaye alikuwa amemuudhi kupindukia. Alikimbiza gari lake pasipo kujali sheria za barabarani, huku akiwaza kusafiri alikuwa hajachukua hata pasipoti yake ya kusafiria.
Hasira zake zilizopelekea kasi ya gari lake ziliishia katika makutano ya barabara, eneo la Ubungo. Akiwa anatokea Mwenge hakutazama hata kidogo taa zinazoongoza eneo hilo. Wakati huo taa nyekundu ilikuwa ikiwaka kuzuia kupita magari yote yaliyokuwa yakitokea Mwenge. Bwana Lamos Maputo hakutazama taa hiyo zaidi ya kuendesha gari lake hilo kwa kasi kabla ya ajali mbaya kutokea. Akiwa anawaza kufika uwanja wa ndege, ndoto zake zilizimwa na lori la mizigo lillilokuwa kasi huku likitokea upande wa Kimara wa barabara hiyo. Ajali mbaya ilitokea na gari lake liliburuzwa kwa umbali mrefu baada ya kugongwa katika ubavu wa kulia ambao alikuwa amekaa akiliendesha gari hilo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya saa mbili bwana Lamos Maputo alikuwa amelazwa katika chumba maalumu huku akiwa mahututi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Madaktari na wauguzi walionekana katika pilika pilika za kuokoa maisha ya tajiri huyo lakini ukweli waliutambua kuwa jambo hilo halingewezekana. Bwana Lamos alikatika mguu wake wa kulia katika eneo la tukio huku mguu wake wa kushoto ukiwa umevunjika vunjika kwa kiasi kikubwa. Alikuwa na majeraha mengi katika sehemu tofauti za mwili wake likiwapo kovu kubwa kichwani. Mbali ya kupiga kelele juu ya maumivu makali aliyoyapata mbavuni, bwana Lamos alionekana akiwaeleza wauguzi na madaktari kuwa alimhitaji mwanaye haraka sana.
Tayari vyombo ya habari vilianza kusikika vikielezea ajali hiyo ambayo uchunguzi wake wa awali juu ya chanzo cha ajali hiyo ulipangwa kuanza kutolewa siku iliyofuata. Tayari maelezo kadhaa yaliyotolewa na mashuhuda wa ajali hiyo yalionesha bwana Lamos Maputo ndio alikuwa kiini wa ajali hiyo ambayo iliwajeruhi kidogo watu waliokuwapo kwenye Lori la mizigo. Matajiri kadhaa walikuwapo eneo la hospitali kuu ya taifa huku wakufuatilia maendeleao ya kiafya ya tajiri mwenzao ambaye alikuwa gumzo Afrika kwa mambo kadhaa. Moja wapo likiwa uwezo wake wa kifedha ambao ulidhihirishwa na uwekezaji wake aliokuwa ameufanya katika nchi tofauti za Afrika. Jambo kubwa zaidi lilihusiana na maisha ya tajiri huyo ambaye hakuwahi kuoa wala kuhisiwa kufanya mapenzi katika maisha yake.
Majira ya saa nane usiku mambo kadhaa yalikuwa yamechukua hatua, madaktari walikuwa wamemkata bwana Lamos Maputo mguu wake wa kushoto baada ya kuamini mguu huo haungepona zaidi ulikuwa ukimwongezea maumivu tajiri huyo. Rafiki zake wa karibu walikuwa wamewasiliana na viongozi wa chuo kikuu cha Cambridge juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea. Chuo hicho kilitoa ushirikiano na kuahidi kuwa Veronika angesafiri kwa usafiri wa ndege siku iliyofuata akitumia shirika la ndege la British Airways ambalo ndege yake ilikuwa ikiondoka siku iliyofuata asubuhi. Veronika pia alikuwa ameelezwa juu ya ajali aliyokuwa ameipata baba yake ingawaje hakuelezwa juu ya ukweli wa hali mbaya aliyokuwa nayo.
Siku iliyofuata hali ya bwana Lamos Maputo ilionekana kuzidi kuwa mbaya zaidi na madakari walionekana wakijitahidi ili tajiri huyo aonane na mwanaye aliyekuwa akimtaja kila wakati. Kwa zaidi ya mara tatu alihangaika kama vile alitaka kukata roho lakini haikuwa hivyo. Saa tatu na nusu usiku lilionekana gari la polisi likikimbizwa kwa kasi kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Gari hilo lililokuwa likipigwa vingora vya hatari lilifuatwa nyuma na gari mbili aina ya Mercedez Benz ambazo zilitokea katika uwanja huo wa ndege. Katika gari la katikati kati ya hayo matatu, alikuwapo Veronika ambaye alikuwa amekumbatiwa na Rashid huku akilia kwa sauti. Alikuwa akifarijiwa na mpenzi wake huyo kwa muda wote wa safari yao ya ndege lakini hakupata faraja hata kidogo. Baada ya dakika ishirini na tano magari hayo yakiwa kwenye kasi yaliegeshwa mbele ya hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili. Madaktari kadhaa waliokuwa na watu tofauti maarufu nchini wakiwamo viongozi wa ngazi za juu walijongea katika gari hilo kabla ya kumpokea Veronika wakati akishuka.
Veronika alishikwa mkono na madaktari wawili walioanza kutembea naye kwa kasi huku wakidai kuwa alipaswa kumwona baba yake haraka iwezekanavyo. Alitembea huku akiendelea kulia akiwa amemwacha Rashid nje ya hospitali hiyo na watu kadhaa waliompokea. Baada ya dakika tano alikuwa katika chumba alicholazwa baba yake kilichokuwa na madaktari zaidi ya kumi na mbili. Alishtushwa na hali mbaya aliyomwona nayo baba yake huku akiwa amekatwa miguu yote miwili na jambo hilo lilimfanya aanze kulia zaidi kwa nguvu kabla ya kumfuata baba yake na kumkumbatia.
Madaktari walikaa kando wakishudia jambo hilo, wakati huo bwana Lamos Maputo pia alikuwa akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata na zaidi alikuwa akiongea kwa taabu sana. Tajiri huyo alinyoosha mkono kuwaoneshea ishara madaktari hao waondoke katika chumba hicho na jambo hilo lilichukua nafasi kwa sekunde kadhaa na chumba hicho kilibaki tupu. Veronika aliendelea kumwangalia baba yake kwa uchungu kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo. Bwana Lamos ambaye alikuwa akitokwa na machozi alimwangalia mwanae kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanza kusikika akiongea kwa taabu. “nisamehe mwanangu, naamini nitakuachia kazi kubwa duniani kutokana na kosa kubwa nililolifanya katika maisha yangu kwani naamini nakufa….. Biashara zangu hazikuwa za halali hata kidogo kwani nilifanikiwa kutokana na masharti ya mganga wa jadi, masharti ambayo unapaswa uyarithi na mali zangu…” alisikika akiongea na kumfanya Veronika apunguze kulia na kutulia kidogo. “Nilipewa masharti ya kibiashara ambayo unapaswa uyarithi pia”,
“Sharti la kwanza, toka leo mpaka mwisho wa maisha yako huhurusiwi kuolewa wala kufanya tendo la ndoa” alisikika bwana Lamos akitoa kauli iliyomshtua Veronika. “ndio maana siku zote sikupenda uwe karibu na wanaume kwa vile nilijua utayarithi mashari haya na mali zangu “Sharti la pili, halikuhusu kwa vile hauna mtoto ungekuwa na mtoto naye alipaswa kurithi mali hizi baada yako kwa misingi ya kutooa au kuto kuolewa” alitulia kidogo katika wakati ambao Veronika alikuwa ametulia pia akiwa haamini mambo aliyokuwa akiyasikia
“onyo ukikiuka masharti hayo basi utafilisika na kuwa mwehu, kama utashindwa masharti hayo na kuhitaji kuyatengua basi utapaswa uende…uende… uende…” Veronika alikuwa amechanganyikiwa huku akiwa amemtolea macho baba yake akiwa na lengo la kusikia eneo ambalo angepaswa kutengua masharti hayo lakini ghafla tajiri huyo alianza kupatwa na kwikwi huku akiwa ametoa macho, baada ya sekunde kadhaa alianza kujiviringisha kitandani hapo huku akitoa sauti ambazo Veronika hakuzitambua. “dokta! dokta! Nisaidie nisaidieni” Alipiga kelele Veronika zilizowafanya madaktari waingie kwa kasi katika chumba hicho kabla ya kuanza kumhudumia bwana Lamos. Madaktari wengine walimwongoza Veronika nje ya chumba hicho ambako alienda kukutana na Rashid na watu wengine wengi waliokuwapo.
“Dokta! dokta! Nisaidie nisaidieni” Alipiga kelele Veronika zilizowafanya madaktari waingie kwa kasi katika chumba hicho kabla ya kuanza kumhudumia bwana Lamos. Madaktari wengine walimwongoza Veronika nje ya chumba hicho ambako alienda kukutana na Rashid na watu wengine wengi waliokuwapo.
Huku akilia alikuwa na hofu ya maisha yake mapya ambayo angeyaanza endapo baba yake angefariki. Hakutamani hata kidogo afariki. Alimhitaji baba yake awe hai ili watengue masharti hayo magumu ambayo aliamini asingeyaweza katika maisha yake. Wakati huo alikuwa analia huku akiwa amekumbatiwa na Rashid ambaye alikuwa akimfariji. Baada ya dakika kumi Veronika aliishia kuzimia baada ya taarifa za kifo cha baba yake zilizotolewa na daktari mkuu mbele ya umati watu waliokuwa wamejaa nje ya mlango huo wengi wao wakiwa matajiri na viongozin wa ngazi za juu wa nchi.
Wauguzi walimpa huduma ya kwanza na baada ya muda mfupi alizinduka na kukutana na hadithi ileile ya kifo cha baba yake. Msiba huo ulihamishiwa nyumbani kwa bwana Lamos Maputo ambaye alitawala vyombo vya habari. Ingawaje hakuwa mwingi wa misaada ila sifa zake kutoka serikalini zilitokana na uwekezaji wake wa kiwango cha juu uliokuwa ukisaidia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.
Taratibu za mazishi zilifanyika na bwana Lamos Maputo alizikwa siku mbili baadaye jijini Dar es salaam. Msiba wake urihudhuriwa na watu wengi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi. Jina la bwana Lamos Maputo, mbali na kuwa jina maarufu kutokana na uwezo wake kifedha lilitarajiwa kuanza kusahaurika miongoni mwa watanzania. Hisia za wengi zilikuwa zimehamia kwa Veronika Lamos Maputo ambaye alianza kutajwa kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchini na Afrika kwa ujumla kutokana na urithi alioupata kutoka kwa baba yake. Muda wote wakati wa tukio hilo la mazishi na baada, Veronika hakuwa na amani hata kidogo, alikuwa na mawazo ambayo hakuna mtu aliyepata kujua juu ya jambo ambalo lilikuwa bado likimsumbua mrembo huyo aliyefiwa na baba yake.
Baada ya wiki mbili Rashid alianza kumshauri warudi nchini Uingereza kuendelea na masomo yao ya chuo. Jambo hilo lilichukua muda kubadili mtazamo wa Veronika ambaye alionekana akiichukia shule ghafla. Muda wote alikuwa akiwaza juu ya masharti magumu ya kibiashara ambayo aliachiwa na baba yake. Mwishoe alisafiri na Rashid kurudi nchini Uingereza kuendelea na masomo. Baishara zake zote zilikuwa chini ya bwana Alex George, mmoja wa tajiri aliyekuwa karibu na marehemu Lamos Maputo. Bwana Alex alichaguliwa na matajiri wenzake ambao walikuwa wakimsisitiza Veronika arudi chuo.
Hatimaye walijumuika na wenzao kuendelea na masomo katika chuo kikuu cha Cambridge, wakati huo mambo yalikuwa tofauti. Veronika alikataa kabisa kukaa na Rashid katika nyumba yao waliyopanga katika kitongoji cha Yelling. Mrembo huyo aliamua kupanga nyumba nyingine katika kitongoji cha Croxton huko aliamini asingeweza kuvunja sharti la kufanya mapenzi lililokuwa kubwa katika masharti ya kibiashara aliyopewa na baba yake. Veronika alikuwa mnyonge hata maendeleo yake kitaaluma yalianza kushuka kadri siku zilivyokuwa zikienda. Mbali na utajiri aliokuwanao huku akitembelea gari la kifahari aina ya BMW alikosa amani juu ya maisha yake kwani kila siku aliamini masharti aliyopewa yangemshinda.
Rashid aliingiwa na mashaka ya ghafla juu ya mchumba wake ambaye alibadilika mambo mengi kwa wakati huo. Alikuwa hampigii simu na mara kadhaa alikuwa hapokei simu akimpigia. Hisia zake zilianza kumwingia akihisi huenda Veronika alikuwa katika harakati za kumwacha. Mbali na gari la kifahari aliloachiwa aina ya Ferarri pamoja na nyumba ya kifahari aliyopangiwa, Rashid aliona havitoshi kwa vile alikuwa akimhitaji Veronika na sio vitu hivyo. Aliamua kuanza kumpeleleza Veronika katika nyumba yake aliyokuwa akiishi katika kitongoji cha Craxton huku akihisi huenda alikuwa amerudiana na Moses ambaye alikuwapo chuoni hapo. Baada ya uchunguzi wake wa wiki mbili hakuna jambo alilofanikiwa kugunda zaida ya unyonge aliokuwa nao Veronika.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliendelea kujipa matumaini huku akihisi huenda mrembo huyo alikuwa bado na mawazo ya kifo cha baba yake. Wakati huo hakufanikiwa kula naye chakula, kuongea naye kwa muda mrefu hata alipokuwa akimwambia anampenda hakujibiwa mara kadhaa. Jambo lililomshangaza zaidi Veronika alikuwa akimwekea fedha za matumizi kila baada ya wiki mbili katika akaunti yake ya benki na alipomshukuru alikuwa hajibiwi. Rashid aliamua kuanza kupanga jambo, alitaka kuishi na mchumba wake kama walivyokuwa awali. Aliamini kwa kufanya hivyo angemwondoa kutoka kwenye dimbwi la mawazo alilokuwa nalo. Aliwaza kumtembelea siku ya Jumamosi iliyokuwa ya mwisho kwa mwezi wa tatu. Siku hiyo ilikuwa maalumu kwa maonyesho ya sanaa yaliyokuwa yakifanyika katika chuo chao lakini aliamini Veronika asingeenda kutoka na jinsi alivyokuwa. Siku husika ilipofika majira ya kumi jioni, Rashid alionekana akitoka na gari lake katika nyumba aliyopanga akiwa na lengo la kumfuata Veronika katika kitongoji cha Croxton alikokuwa akiishi. Kichwani alikuwa akiwaza kwenda kulala na mchumba wake huyo ambaye hakubahatika kuwa naye karibu kwa muda mrefu. Alikuwa akiamini jambo hilo lingerudisha ukaribu wao ulioanza kupotea.
Baada saa mbili ya kuwapo barabarani hatimaye Rashid alifika katika nyumba aliyokuwa amepanga Veronika. Alipoegesha gari lake majira hayo ya jioni, alishuka katika gari hilo na kuanza kutembea kuelekea katika mlango mkubwa wa nyumba hiyo. Wakati akiendelea na zoezi hilo Moses Malcolm, kijana ambaye alikuwa akimpenda pia Veronika alionekana kwa mbali kama vile alikuwa akimfuatilia Rashid. Kijana huyo, mtoto wa familia ya kitajiri alikuwa akimwangalia Rashid kwa kutumia darubini huku akiwa katika gari lake aina ya Cadillac, hatimaye aliliondoa gari lake kwa kasi pasipo kugundulika.
Rashid aliugonga mlango wa nyumba hiyo mara kadhaa lakini haukufunguliwa. Alipojaribu kuufungua aligundua mlango huo ulikuwa wazi, mwishoe aliingia na kukutana na taswira ambayo hakuitarajia hata kidogo. Veronika alikuwa amelewa huku akiendelea kunywa pombe kana hana akili nzuri. Kulikuwa na chupa kadhaa za pombe kali zilizokuwa mezani katika sebule ya nyumba hiyo huku chupa kadhaa za pombe hiyo zikiwa hazijatumika. Akiwa na mshtuko Rashid alimsogelea Veronika aliyekuwa amekaa chini katika sebule hiyo huku akionekana kama alikuwa akiangalia kitu. Alipojongea karibu aligundua mrembo huyo alikuwa akiangalia picha yake Rashid, alimshtua kwa kumshika bega kabla ya Veronika kuanza kusimama huku akipepesuka.
“Rashid…. Nakupenda sana, kwa nini unaniacha?” alisikika Veronika kwa sauti ya kilevi huku akimkumbatia Rashid. “umeanza lini kunywa pombe aah!” alisikika Rashid akiwa na jazba kabla ya kuanza kumwongoza Veronika kuelekea chumbani kwake. Baada ya dakika tano alifanikiwa kumfikisha mrembo huyo chumbani kwake. Alikaa kando yake huku akimweka sawa, wakati huo Rashid aliwaza mambo mengi ambayo aliyakosa kutoka kwa Veronika kwa muda mrefu. Aliamini muda huo ulikuwa muafaka kujumuika na mchumba wake huyo na alifanya hivyo.
* * * *
Moses Malcolm tayari alikuwapo nchini Uingereza kuendelea na shahada yake ya muziki na filamu. Tayari alikuwa amepona mkono aliokuwa amevunjika pamoja na majeraha kadhaa aliyoyapata miezi kadhaa akiwa nchini Tanzania kumfuatilia Veronika kabla ya kupigwa na marehemu Lamos Maputo akishirikiana na walinzi wake. Tayari alikuwa na taarifa za kifo cha tajiri huyo ambazo zilimuumiza kidogo zaidi alimwonea huruma mwanamke aliyekuwa anampenda, Veronika. Kichwani alitawaliwa na mawazo ya ushindi na aliamini lazima angempata Veronika kwa wakati huo. Hakuwa tayari kumkosa, aliwaza kutumia gharana yeyote ili kuhakikisha anampata Veronika.
Mara baada ya kupata taarifa za kurudi Veronika kutoka Tanzania kwenye msiba wa baba yake, alianza kumfuatilia nyendo zake kwa ukaribu sana kabla ya kugundua alikuwa akiishi katika kitongoji cha Croxton. Wakati huo alipata faraja kwani aligundua mrembo huyo hakuwa karibu na Rashid tena na jambo hilo lilimpa faraja ya kumpata. Siku moja ya mwisho wa mwezi wa tatu alipanga kwenda kumtembelea Veronika katika nyumba aliyokuwa akiishi. Kwenye gari lake alikuwa na Craig, rafiki yake wa karibu kwa muda mrefu. Mara baada ya kufika katika nyumba hiyo walimshuhudia Rashid akiingia nyumbani hapo kwa Veronika. Moses alipandwa na hasira juu ya tukio hilo ambalo lilimuumiza sana moyoni. Baada ya kubadilishana mawazo na Craig kwa muda mfupi walimua kufanya jambo. Walipanga kumteka Veronika akiwa nyumbani kwake hapo na kumhamishia sehemu nyingine ili Moses aweze kuwa na Veronika kinguvu katika usiku wa siku hiyo.
Jambo hilo lilichukua nafasi, majira ya saa tano usiku vijana saba waliokuwa wamevaa vinyago waliivamia nyumba hiyo na kumteka Veronika huku wakimfunga Rashid pingu na kumwacha katika nyumba hiyo akimlilia mchumba wake. Wakati huo Veronika pombe ndio ilikuwa ikianza kumtoka taratibu kichwani. Hakupata wakati wa kurudiwa na fahamu vizuri kwani watu hao waliomteka walimchoma sindano ya usingizi iliyomfanya alale. Waliendesha kwa kasi gari zao walizofika nazo awali katika nyumba hiyo, hawakuwaza kwenda mbali zaidi ya nyumbani kwa Craig aliyekuwa akiiishi katika kitongoji hicho cha Croxton. Huko walikuwa wakisubiriwa na bosi wao, Moses ambaye alipanga kutimiza adma yake kwa Veronika usiku huo.
Baada ya dakika arobaini na tano gari lao liliegeshwa katika nyumba aliyokuwa akiishi Craig na bila kupoteza muda walimshusha Veronika ambaye bado alikuwa amelala. Waliongozana na mrembo huyo mpaka katika chumba ambacho Moses aliwaelekeza. Hatimaye vijana hao walilipwa fedha zao kwa kazi hiyo waliyokuwa wameifanya kabla ya kuondoka wakiwa na furaha. Akiwa peke yake katika nyumba hiyo Moses alipiga kelele akishangilia juu nya ushindi aliokuwa ameufikia. Hakupoteza muda alielekea katika chumba walichompeleka Veronika kabla ya kutimiza ndoto zake.
Majira ya saa kumi mbili asubuhi Veronika alishtuka kutoka kwenye usingizi mzito. Alionekana akiinyosha mikono yake kutokana na uchovu lakini ghafla alipomwona Moses akiwa amelala kando yake alishtuka sana na kushuka katika kitanda hicho haraka. Alipojipapasa kidogo aligundua tayari alikuwa ameangamia, alikuwa amevunja sharti ambalo baba yake alimlithisha na utajiri wake. Sharti ambalo hakupasa kufanya mapenzi katika maisha yake. Ghafla alihisi maumivu makali kichwani mwake na baada ya sekunde kadhaa alipoteza fahamu na kuanguka chini kabla ya kuanza kujiviringisha kama mgonjwa wa kifafa.
Alijiviringisha kwa muda mrefu katika wakati ambao Moses alikuwa ameamka huku akishangaa juu ya jambo lililokuwa linaendelea. Alimwogopa kabisa Veronika ambaye alikuwa ametoa macho kama vile alikuwa akitaka kufa. Baada ya dakika kadhaa alitulia kidogo na kusimama kabla ya kuanza uhalibifu katika nyumba hiyo. Alivunja vyombo vya thamani pasipo kujali na zaidi alikuwa akiongea lugha ambayo Moses hakuwahi kuisikia katika maisha yake. Alipojaribu kumshika Veronika kwa lengo la kumzuia, alishangazwa na nguvu alizokuwa nazo kwani alikuwa na nguvu zisizo za kawaida. Hatimaye Veronika aliondoka katika nyumba hiyo huku akiwa amemwonya Moses asijaribu kumfuata. Mambo aliyokuwa akiyafanya yalimpa jibu Moses kuwa mrembo huyo alikuwa kichaa. Alirudi akikimbia ndani ya nyumba ya Craig akiwaza kufanya jambo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment