Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SIONDOKI MPAKA NIFE - 2

 





    Simulizi : Siondoki Mpaka Nife

    Sehemu Ya Pili (2)



    Usiku ulikuwa mkubwa wenye hali ya baridi kali ndani ya jiji a Arusha. Kikao cha viongozi wa serikali kiliwekwa ndani ya hoteli maarufu katikati ya mji huo maarufu wa kitalii. NGURUDOTO hotel ndani ya chumba maalumu cha siri kulikuwako na waheshimiwa wazito wa serikali. Mkurugenzi wa usalama wa taifa Bw. Johnson Kimati alikuwa ametunishaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kitambi chake kilichogusa meza iliyozungukwa na watu wa tano wengine wenye nyadhifa zao kubwa serikalini. Yule pale alikuwa Twaha Nasibu, yeye alikuwa katika idara nyeti ndani ya kitengi cha usalama wa taifa kuchunguza makosa ya jinai. Wale wengine watatu waliobaki mmoja alikuwa amechafuka vyeo kwa kutunukiwa kuwa mkuu wa mapolisi kanda maalumu ya mkoa wa Arusha akiwa kama mwenyeji wa kikao hicho alitambulikana kwa jina la Rashid Fungafunga alikuwepo pia mkuu wa jeshi la Polisi Bw Donald Nyanda na wa mwisho yeye ni mkuu wa polisi kanda ya mkoa wa Dar es salaam Bw. Tunu Kazinja. Mwanamke pekee jasiri aliyebahatika kukaa pamoja na wanaume kujadili mambo mazito ya kitaifa. "Ndugu zangu hii ni aibu" Bw Donald Nyanda alizungumza. Alizungumza kwa sauti ya upole isivyo kawaida yake. Johnson Kimati naye akadakia huku akiwaangalia wajumbe wa kikao hicho kwa zamu. "Majirani zetu hawatatuelewa kabisa katika hili" alinyamaza kuwatazama kuona kama alichozungumza kimewaingia, akamalizia "wataona kama sisi tunawafuga majambazi kwa kuwa wapo kwetu" "Lakini jamani" Kila mmoja akamgeukia Twaha aliyeonekana kama mdogo kwao. "Kwanini hili jambo msiniachie mimi kama tulivyopanga katika vikao vya awali? Bado sijashindwa japo muda unakwenda ila nipo mbioni kuwapata majambazi hayo" Johnson akamkatisha. "Unaongea nini Twaha? Miezi mitatu sasa imepita hakuna kunachoendelea. Unafikiri tunahitaji kuonekana sisi wazembe katika hili?" Akawageukia wenzake na kuona kuwa aliungwa mkono katika hilo baada ya kuona kila mmoja akitabasamu na kutingisha vichwa vyao kwa ishara ya kukubaliana naye "Jeshi la polisi halipo tayari kubeba lawama kutoka kwa majirani zetu, mimi naona bora tuwashirikishe wenzetu Interpol katika hili ili watusaidie" Nyuso za kila mjumbe zikaonekana kusawajika ghafla na kuchukizwa. Moyo wa Twaha ukalipuka kwa furaha baada ya kuona sasa Johnson ameharibu. Kiongozi wa kikao hicho mkuu wa jeshi wa polisi, Donald Nyanda yeye akasema "Johnson umeharibu mwanzo mzuri sasa unatufanya tuone kuwa Twaha alikuwa sahihi kuomba kuachiwa operation hii" Alinyamaza na kukohoa kiasi kisha alimtazama kila mmoja kwa tuo. Akamalizia "ninachoomba tumpe muda Twaha wa kulimaliza jambo hili kisha baada ya wiki moja Twaha tutaomba utukabidhi watuhumiwa" Uso wa Twaha uling'aa kwa tabasamu lililochanua uso wake na kufanya uonekane uliopendeza kama mtoto mdogo. Twaha akazitoa zile picha zilizochorwa na askari wa kimataifa walioletwa na nchi ya kenya kusaidia msako huo. Picha ambazo zilichorwa kutokana na vivuli viivyotolewa kutoka kwenye kamera za benki ile pamoja na maelezo ya askari waliobahatika kuona sura za kikundi cha majambazi waliokwenda kuiba benki. Picha hizo kama hazikuwa sawia na sura halisi kabisa na za Fredy, Maliki na Titus basi zilifanana sana. Kila mmoja ndani ya kikao hicho alizitazama picha hizo na mkuu wa polisi kanda ya mkoa wa Arusha Rashid FungaFunga akawatia moyo wenzake. "Wanaonekana ni vijana wadogo sana. Hawana ujanja sana kuzdi jeshi la polisi la Tanzania, lazima watakamatwa hivi karibuni" Kila mmoja akaunga mkono na kupatiwa nakala za picha hizo zilizotolewa kwa rangi kabisa. Kikao kikafungwa huku Twaha akiamini kuwa kila mmoja katika kikao kile alikuwa ni sawa na yeye aliyetafuta haki ya kutetea maslahi ya kulinda amani ya taifa. Hawakujua pia wapelelezi wa kimataifa pia walitoka kutoka Kenya na kuhamia Tanzania kuendesha msako huo. Jambo ambalo katika kikao kile walilikataa na kuona kuwa walikuwa wakilitia aibu jeshi la polisi la Tanzania. Twaha akaingia kazini kwa mori na kuapa kuwa ni lazima awapate majambazi hao. Alishindwa kulala na kula vizuri kwa muda mrefu. Hata kuonana na binti yake ilikuwa ni kwenye simu tu. Simu yenye uwezo wa skype. Hata hivyo waliwasiliana mara. Chache sana. ... Kazi ya kumtafuta mpelelezi aliyekuwa akiifuatilia kesi yao haikumuingia akilini kama ambavyo alikuwa akiwaza kumtafuta msichana aliyekutana naye mara chache tena katika kumbi za starehe. Akili ya Titus ilisumbuliwa sana na Agape. Jina alilomfahamu Agape ni Isabella. Mawazo yaliyoganda kichwani mwake ni Isabella. Hata jioni aliposhindwa kuvumilia kuganda na kuendelea kuumizwa na mawazo ya Isabella aliamua kwenda zilipo hostel za Ifm. Hostel ambazo alimuacha Agape usiku wa jana. Alipokelewa na baadhi ya wasichanaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ waliokuwa wakijisomea nje ya hostel hizo. "habari zenu?" "nzuri karibu" alikuwa Irene rafiki mwingine wa karibu wa Nadia. Rafiki ambaye alikuwa akilala chumba kimoja na Nadia. Chumba ambacho pia alikaribishwa Agape kulala kutokana na pombe nyingi aliyoifakamia katika kumbi ya starehe. "naomba mnisamehe kuwakatisha masomo yenu, ila nina shida fulani" alinyamaza kusikiliza kama angepata nafasi ya kuuliza. Irene ndiye alijibu "uliza tu kaka." "kuna msichana anaitwa Isabella anakaa katika hostel hizi, naweza kuona naye?" irene alimgeukia jirani yake waliyekuwa wakisoma pamoja "isabella? Unamfahamu?" mwenzake yeye akajibu "hapana simfahamu" Titus akarahisisha swali hilo kwa kuwaambia kuwa "hapana jana usiku nilikutana naye katika hotel ya Jb alikuwa na wenzake wawili niliwarudisha mishale ya saa nane ya usiku hapa" irene akaonekana kukumbuka kuwa aliyekuwa akizungumziwa hapo ni msichana anayemfahamu yeye huenda akawa ni Agape. Huenda hata mmoja kati ya rafiki zake wawili wa msichana waliokuwa wakitajwa mmoja wao alikuwa ni Nadia. Wakati akiwaza hayo Nadia na Agape walikuwa wakizishuka ngazi za ghorofa ya hostel yao. Irene akaropoka "tena hao wanashuka" Titus alipogeuka, alimuona Agape. Alibumbuwaa kwa muda akitazama uzur wake. Zikiwa zimebaki hatua chache wasogeleane, pia Agape alimuona Titus. Alimtambua Titus kama kijana aliyemsaidia na kuyaokoa maisha yake. Furaha iliyomfanya akenue na kutabasamu ni sababu iliyomfanya Titus kutabasamu pia akiamini kuwa Isabella (ambaye ni Agape) amemkumbuka. Aliamini zile zilikuwa ni pombe tu. Waliposogeleana, wote kwa pamoja walikumbatiana kwa furaha. Furaha iliyomfanya Moses kuropoka "oh isabella wangu siamini kama ungenikumbuka" jambo lililomshangaza Agape na kuchukua hatua ya kushangaza na kumsukumia mbali Titus Titus alistahimili asianguke japo alikuwa karibu kuanguka baada ya kuikwaa meza aliyokuwa akiisomea Irene. Jambo hilo lilikuwa la kushangaza. Kwa kuwa hakuna aliyefahamu kwanini Agape afanye hivyo. Nadia akasema kwa sauti ya kumshangaa mwenzake "Agape?" Macho yakiwa yana mawasiliano ya karibu kabisa na kila kiungo juu ya uso wake. Alikuwa katika hali ya kutofahamu "Unafanya nini?" Agape alikuwa akimtazama Titus akijiuliza kwa mshangao wa wazi. "Huyu ni nani? Kwa nini ameniita jina langu la zamani?" Hakuna aliyemjibu maswali yake. Kwa kuwa alikuwa akiwasiliana na nafsi yake. Sauti aliyokuwa akiisikia kichwani bado iliendelea kumnong'oneza. 'Lakini huyu ndiye aliyeniokoa pale kilwa road, huyu ndiye' alikuwa akimtazama Titus kwa muda mrefu huku Titus naye akiwa tayari amesimama sawa lakini pia naye alikua akijiuliza juu ya jina halisi la Agape. Wazo lake halikuzunguka peke yake kichwani mwake kisiri siri likatoka nje na kuwasilishwa kwa mdomo. "Agape?" Kila mmoja akawa amenyamaza kusubiri asikie atakachozungumza Titus "wewe unaitwa Agape?" Agape aliitika kwa kutingisha kichwa tu huku uoga ukiwa umevaa hisia zake. Uoga wa hatia iliyomtafuna ndani kwa ndani. Hatia ya kumsukuma mtu ambaye huenda wasiyefahamiana. Hatia ya kumkumbatia mvulana ambaye alianza kuhisi kuwa amemfananisha. Akataka kusema samahani lakini mdomo ukawa mzito. Akataka kukimbia lakini akaona angeonekana mwehu. Akasimama kusikiliza aichotaka kuzungumza Titus. Titus akaendelea kwa mshangao naye akiwa ameandamwa na hatia kudhani huenda labda amemfananisha. Akamkumbatia msichana aliyemfananisha. Basi kama angemfananisha asingekuwa amekosea sana. Agape labda angekuwa pacha wake Isabella na Agape angemueleza wapi atakapompata Isabella. 'jamani huku si kufanana' aliropoka mpaka akasikika. "Kufanana? Nani na nani wamefanana?" Ikawa kama sinema ya bure kati ya Agape na Titus waliokua wakijibizana kwa kutumia mswaada uliovuta hisia za Nadia na Irene baada ya sofia kuondoka. "Wewe unayeitwa Agape" "Ndiyo mimi naitwa Agape, nimefanana na nani?" Agape alimjibu Titus kwa kuona kama alikuwa kama anamchelewesha kung'amua kilichokuwa kinamtatiza kichwani. "Hapana" "Hapana nini kaka yangu?" Agape akawa ameghafirika moyo na kuiharibu sura yake pia. Titus alinyamaza kwa muda akijaribu kutafakari jinsi ya kulitengeneza swali lake na kuliweka sawa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ 'Unamfahamu ..' Akaropoka "hapana" akaendelea kuwaza 'wewe na Isab..' Akaona sasa ni sahihu "anha ! Okey unamfahamu msichana anaitwa Isabellah? Ni ndugu yako?" Alipoona Agape kuwa anachelewa kujibu akaendelea "mumefanana sana" "Mimi pia naitwa Isabella kwa jina langu la ubatizo" Furaha dhahiri ikachanua juu ya uso wa Titus. Alijihisi mwepesi na kutamani kumkumbatia tena. Hakukumbuka kabisa ni huyo aliyemsaidia katika ajali a gari pale Kilwa road. Hakujua kuwa huyo ndiye aliyempa kilema cha maisha kwenye mguu wake, na kumbariki kovu la milele. "Tuliwahi kukutana kenya uankumbuka, ulikuwa na stress sana pale club ukaniagiza tusker nikashangaa sana mrembo kama wewe na .. naaa.." Hakuona Tabasamu waa kitu cha kumshitua usoni mwa Agape. Akahisi huenda bado alikuwa hajafahamika. Aliobgea kwa furaha akiamini kuwa asilimia mia moja Agape ndiye Isabellah waliyekutana kenya. Lakini Isabellah bado hakumkumbuka yote aliyosema aliyaelewa vizuri lakini Agape kilichomchanganya zaidi ni huyu malaika aliyekuja kwa sura tofauti. Huyu kijana aikutana naye kenya ndani ya club ya usiku katikati ya jiji la Nairobi akiwa na mawazo ya kuachwa na Venance. Lakini huyu ndiye huyu huyu aliyemuokoa kutoka katika kifo pale alipokoswa koswa na gari. Sasa huyu ni nani? Kwanini Mungu amlete kwake kipindi cha matatizo tu? Moyo wake ukaanguka ghafla na kunyong'onyea katika huba zito na Titus. Ni hapo alipopat ujasiri wa kumsogelea Titus na kuinua mguu mmoja wa suruali aliyoivaa Titus, akalitazama kovu kubwa lililoonekana kwa wazi kabisa kutokana na ukubwa wa mshono wake. Titus akiwa ameduwaa aisjue kwanini na lengo la Agape kufanya hivyo, ni saa ngapi asishangae papi zake zikivamiwa na kuanza kunyonywa mate na Agape? Titus akalipokea tukio hilo kwa furaha huku naye akizungusha mikono yake kwenye mgongo wa Agape na kukumbatiana bila aibu wakaanza kunyonyana ndimi zao hadharani bila aibu. Nadi na Irene kutokana na aibu iiyowakumba ghafla walijikooza kinafki. Agape akajibandua mikononi mwa Titus akiwa na tabasamu pana huku machozi yakimtiririka mfululizo. Akamuuliza "Ulikuwa wapi siku zote?" "Isabellah! Bado..." Agape akamnyamazisha na kumueleza "Tafadhali naomba uniite Agape kuanzia sasa" "Sawa Agape unajua bado npo njia panda?" "Kwanini?" "Kwanini ulipofunua mguu wangu nilioumia, ukaanza kuninyonya denda?" "Unakumbuka chanzo cha ajali uliyoipata?" "Ndiyo" "Ni nini?" "Nilikuwa namuokoa msichana fulani aliyekuwa anakaribia kugongwa na gari lililopoteza muelekeo, kwa hiyo?" Agape alijibu huku akitabasamu. "Msichana yule uliyemuokoa ni mimi na niikuja.." Kwa furaha ya ajabu, Titus akauliza kwa sauti ya ghafla "Unasema?" "Ndiyo, ni mimi na nilikuja hospitali nilipokuacha, sikukukuta ulienda wapi?" "Ni hadithi ndefu naomba nipate muda mrefu na wewe tuzungumze Agape" "Usijali mpenzi" Titus alijitambulisha kwa Agape rasmi na kufahamiana vizuri. Nadia na Irene walibaki na hadithi kichwani mwao huku usoni mshangao usiowakauka baada ya Agape na Titus kuondoka pamoja kusikojulikana. Maisha ya mapenzi yakaonekana kuwa magumu sana kwa upande wa Agape. Alikuwa na sababu nyingi za kuona uzito juu ya mahusiano mapya aliyoyaanzisha. Mahusiano ambayo yameanza ghafla. Mahusiano aliyoyaanza huku moyoni bado akiwa na kidonda cha mapenzi. Wakati ambao ameachana na Venance sio muda mrefu kiasi cha kusema kuwa amemsahau kabisa. Mawazo mengi juu ya Venance, aliamini akiwa na Titus ndiye atakayemsahaulisha alipotoka na alivyoumizwa. Hakuwaamini kabisa wavulana. Aliwaona wavulana ni wanyanyasaji. Wavulana ni makatili na wenye roho za kinyama. Ingekuwa hiari yake, angeangamiza kizazi chote cha hao wanaojiita wavulana. Lakini alikaa na chuki hiyo moyoni mwake hata alipokuwa ameanzisha mahusiano na Titus. Titus alijitahidi kumpa Agape kila alichotaka kwa kuwa alimpenda sana. Sawa Titus alikuwa ana roho ya kinyama. Mlenga shabaha asiyekosa chambo chake. Lakini alianguka kimapenzi kwa Agape. Ujasiri wote alio nao akaegea kwa Agape. Mapigo yake ya moyo, yalipiga kasi mara mbili zaidi ya kawaida kila alipokuwa akikutana na Agape. Agape ndiye mwanamke aliyepata bahati ya kupendwa na kuwa wa kwanza kwa Titus. Tofauti yao ikawa katika uaminifu ndani ya moyo wa Agape. Titus alipokuwa akimtoa out kutembea, akajinong'oneza 'hata Venance alianza hivi hivi' Titus alipokuwa akimletea zawadi kadha wa kadha, akazikumbuka nyingi alizowahi kupewa na Venance. Lakini hiyo haikusababisha kuondoa penzi zito alilonalo moyoni mwake juu ya Titus. Alimpenda Titus kwa moyo wake wote lakini hakumuamini asilimia zote. Kitu cha ajabu, Titus hakuwahi kumpeleka nyumbani kwake au kwao anapoishi. Titus hakuwahi kuizungumzia familia yake wala hakujua kama titus angekuwa na familia kwa kuwa hakuwahi kusikia kama ana ndugu. Alishamshuhudia mara nyingi Titus akijitenga pembeni alipokuwa naye pamoja na kwenda kupokea simu mbali kidogo. 'Kwanini? Kuna analolificha' alijiambiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ mwenyewe kwa uchungu, huku akimuona kama Venance. Venance hakumruhusu kuishika simu yake wala kufahamu simu alizokuwa akipigiwa. Akatabasamu kwa hasira alipomkumbuka Venance "Aha ha mjaluo yule!!?" Akacheka alipoukumbuka weusi wake na sura iliyomvutia. Titus aliporudi, alijkaribu kumuuliza "Ni simu ya ofisini" Titus akajibu na kuinyanyua glass ya pombe na kuigida kwa mkupuo mmoja. "Lakini mpenzi" Agape akazungumza kwa huba. Titus alipogeuza uso wake kumtazama Agape, Agape akaachia tabasamu na kuendelea kuzungumza "Kama ni simu ya ofisini, ndio ukaongee mbali na mimi? Au.." alizungumza kwa mahaba zaidi huku akichezea chezea eneo la shindo ya Titus. "Mimi sipaswi kufahamu chochote kinachokuhusu?" Titus akatabasamu zaidi lakini tabasamu hafifu. Alijiona yupo katika mtego wa kuisaliti kambi yake ya uharamia. Lakini hakuwa tayari kujibu chochote na Agape hakuendelea kuuliza pia. Kuna wakati simu yake titus haikupatikana hata siku mbili na hata walipopanga wakutane, yeye akabadilisha sehemu ghafla mara baada ya Agape kufika eneo lile. Yote hayo Agape akavumilia huku mapenzi ya dhati yakitafuna hisia zake. Hakujua sababu ya kumpenda Titus kiasi hicho wala hakujisumbua kujiuliza 'mapenzi hayaulizi kwa nini' Akajiambia kimoyomoyo. Hakuona umuhimu wa kuendelea kumfuatilia. Akaona kuwa anajiumiza japo kila siku mambo ya ajabu ndiyo yalizidi kuibuka katika mapenzi yao. Kuna siku asipatikane kabisa. Siku nyingine asipatikane wiki nzima. Hata alipouliza, hakuna la maana aliloambiwa. Akajiona mpumbavu kumpenda mtu kama Titus. Mtu asiye na muda kwa mpenzi wake, mtu asiyejali hisia zake, "nitamuacha, huenda ana mwanamke mwingine" akajiwazia kwa uchungu, machozi yakimfariji. Alipojaribu kuchunguza kama mawazo yake yalikuwa sahihi au lah! Akajiona mpumbavu pale ambapo mitego yake yote haikunasa. Ukweli ni kwamba Titus akili yake yote ilikuwa kwenye kazi. Kazi ya siri, siri kama baba yake. Titus moyo wake ulikuwa mzito na macho yalifungwa kutazama wasichana. Hakumuhitaji mwingine zaidi ya Agape. Agape akalifahamu hilo ndio maana akaanza kumuamini Titus. Mwanaume anayeamini atakayemuoa. Akapata wazo. Wazo la kumtambulisha Titus kwa baba yake. Alipanga naye wakaelewana kuwa ni lazima Titus akapafahamu anapoishi Agape. Agape akategea siku ambayo baba yake yupo nyumbani ndiyo ampeleka. Bila kumpa taarifa, alimchukua Titus na kumkaribisha kwao Masaki. Titus akastaajabu mandhari nzuri ya nyumbani kwa mzee Twaha. "karibu mpenzi, ngoja nikamcheki dad" kwa sauti nyororo akasema Agape huku kwa mwendo wa madoido ya furaha akiingia ndani ya kasri lao. ... Kazi bora ya Titus ikaanza kuingia doa. Hakujali tena kiasi gani serikali ilikuwa ikimtafuta usiku na mchana bila kupumzika. Hakujali tena kila alichoambiwa na Maliki. Akafanya alichoona ni sahihi. Simu alizopigiwa na Maliki na kwenda kuongelea pembeni pale alipokuwa amekaa na Agape, hakuna cha maana alichomjibu Maliki bali kumwambia "Sina muda kwa sasa naomba tufanye hiyo ishu kesho" Akaikata simu na kuizima kabisa. Hata pale alipoona hofu inazidi kumtafuna, akaamua kwenda alipoitwa na kukutana pamoja na washirika wenzake. Ajenda nzito ya kikao, ikawa ni kumuangamiza mpelelezi aliyepewa kesi yao. Taarifa na sifa ambazo walipatiwa kuhusu mpelelezi huyo ni zaidi ya Joram Kiango. Walilijua jina lake la kazi Mzee wa Analojia, lakini halisi hawakulifahamu. Kichwa kikawauma pia kwa kua hata baba yake na Maliki hakuwa na picha ya Twaha. Ile aliyokuwa nayo haikuwa na ubora wa kuweza kumtwambua mzee huyo. Lakini kilichowapa matumaini baada ya kusikia kuwa ni mzee. "Tutammudu" Wote wakajiambia kwa kujipa moyo. Lakini baada ya kujadiliana hapo, alipotoka Titus hawakumuona tena na wala hawakuweza kuelewana kwenye simu. Ikambidi Maliki kuanza kumfuatilia Titus kufahamu nini kinamfanya kuwa hivyo. Aliweza kushirikiana na Fredy na baadaye kugundua kuwa aliyekuwa akimchanga Titus ni mwanamke. Mwanamke mrembo aliyemtamanisha hata Maliki. Aliwaona Titus akiwa pamoja na Agape, katika fukwe moja huko bagamoyo. Moyo wake ukaingiwa na tamaa. Tamaa ya kutaka kummiliki Agape. Kikwazo kikawa ni Titus. Akawaza jambo. Jambo lenyewe halikuwa zuri juu ya urafiki alio nao na Titus. Lazima kumchukua Agape, ingemuuma sana Titus na kuanzisha chuki baina yao. Mwanzo alipokuwa akikaa peke yake, alihofia kumpoteza rafiki yake wa siku nyingi ambaye ni Titus kwa sababu ya msichana. Lakini kadri alivyokuwa akimnfuatilia Agape, ndipo alipofahamu kitu cha pekee alichobarikiwa nacho Agape, nacho ni uzuri. Uzuri uliochanganya kamanda wake Titus, na kuihasi kambi. Naye akavutiwa sana na Agape. Akaapa ni lazima ampate Agape kwa gharama yeyote. Kwanza alipanga kufanya wazo lake kuwa siri kubwa ambayo Titus hatogundua chochote juu ya mipango yake ya kumteka Agape kimapenzi. Pili hakujali uhai wa Titus endapo angegundua njama zake za kumchukua Agape. Akacheka kimoyomoyo alipokuwa juu ya ghorofa moja ya fukwe ya bahari pembezoni mwa bahari ya hindi. Siku hiyoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ hakufanya hila zozote. Alirudi katika nyumba waliyokuwa wakikaa huko mbweni. Nyumba waliyonunua kwa kiasi kikubwa cha pesa mara baada ya kuiba zile fedha benki. Nyumba yenya ulinzi mkali na wa kutosha kila kona. Ulinzi wa teknolojia na si watu. Hawakuamini watu kwa kuwa watanzania njaa ziliwasumbua. Ukimpa pesa kidogo hatoacha kueleza siri zote anazozifahamu. Ndio sababu wakaweka mitambo madhubutu ya kuikinga nyumba yao na silaha yeyote ikiwemo bomu. Pia nyumba hiyo ilikuwa na chumba maalumu cha kutazama mazingira yote yaliyokuwa yakizunguka nyumba hiyo. Pia kulikuwako na kamera zilizofungwa nje kuona kwa umbali mrefu eneo zima la nyumba hiyo. Kamera ambazo zilikuwa na uwezo wa kuona kitu chochote kutoka nyumba ilipo mpaka kilometa kumi zaidi. Walijidhatiti kwa kiasi kikubwa bila kamera hizo kuonekana wala ulinzi wao kutojulikana. Akiwa chumbani kwake, Maliki mawazo yakawa zaidi kwa Agape. Hakumjua jina, uzuri wake ulitosha kunmchanganya. Fredy alifahamu kuwa Maliki ana mawazo. Hakutaka kumuuliza ni yapi labda aseme mwenyewe. Yeye Fredy hakuwa mtu mwenye makuu. Alipenda kuwa mtu mwenye kufanya kazi yake kwa ufanisi bila kuchanganya na kitu chochote. Alipomuona Maliki akiwa katika hali ya mawazo, akatoka na kurudi katika kile chumba chenye ulinzi. Maliki naye alitoka na kwenda katika kile chumba alichomo Fredy. "Hoya niaje?" "Shwari leo vipi? Upo sawa?" Fredy akauliza "Yah niko poa" Maliki akajibu na kuendelea "sasa, embu mcheki kwenye simu Tito uakuambie alipo" "Poa" Alikuwa amewaza jambo jingine baya zaidi. Fredy akawa ameshamaliza kuongea na Titus na kumgeukia Maliki "Yupo slipway" "Poa" Ni pale pale ambapo Maliki alipokuwa amemuacha Titus na Agape. Alirudi kwa kutumia gari yake yenye vioo vyeusi vitupu. Akaiegesha mbali kidogo na maeneo hayo ili titus asiione. Alipokaribia katika maeneo hayo, akamuona Agape yupo peke yake. Akatazama huku na kule hakumuona Titus. Akazidi kuangaza zaidi akamuona akiogelea katika bwawa dogo mbali na alipo Agape. Akamuita muhudumu aliyekuwa akipita karibu yake. "Naomba peni na karatasi" Muhudumu yule alitoka na kurudi na vitu alivyoagizwa na Maliki. Maliki baada ya kupatiwa, aliandika ujumbe fulani na kumrudishia yule muhudumu. Akamwelekeza alipokuwa amekaa Agape "Naomba umpelekee yule binti pale" Muhudumu akawa ameondoka kumfuata Agape alipokuwa amekaa. Eneo ambalo alikuwa amekaa Titus ni mbali kidogo na msongamano wa watu. Alikuwa yeye peke yake. Akakitoa kitambaa chake na kukipulizia dawa yake ya usingizi huku akitabasamu. ... Twaha alikuwa na kipindi kigumu sana katika kazi hii ya kutafuta wezi wa mabilioni ya pesa katika akaunti ya benki kuu ya Kenya. Kipindi ambacho alikuwa amepewa kuwakamata wezi hao, zilibaki siku tatu pekee. Na Bw johnson ambaye ni mkuu wake wa kazi alikwisha mpigia simu mara tatu kumuuliza kuhusu maendeleo ya kazi aliyopewa. "Bado mkuu" Kila siku jibu likawa hilo. Mara alipokata simu akaingia katika tafakuri nzito huku michoro ya picha ya Maliki, Titus na Fredy ikiwa juu ya meza yake pana. Akaitazama mara mbili mbili na kushindwa kuelewa ni wapi walipojificha watu hao. Alishazunguka kila kona ya jiji akijaribu kuwauliza watu kadhaa kisiri siri lakini jibu la watu walioulizwa likazidi kumvunja moyo. Walikuwa hawaeafahamu kabisa watu hao. Kuna wengine walimponda hata huyo ambaye alikuwa amewachora "Mbona kama katuni" Kiufupi hawakuielewa michoro hiyo. Kuna wakati alitamani kulia kutokana na ugumu wa kazi aliyoiomba ifanye yeye. Alirudi nyumbani akiwa mchovu na asiye tamani kufanya chochote kwa siku hiyo zaidi yua kutafakari jinsi ya kuwakamata watu hao. Titus na Agape walikuwa sebuleni wakibadilishana mate ghafla mlango ulifunguliwa bila hodi wala kengele ya getini hawakuisikia. Hivyo Twaha alikuwa ameamua kuiacha gari yake nje huku akiwa na nia kuwa atatoka tena baadaye. Twaha pia hakujua kama Agape angekuwa nyumbani kwa wakati huo. Alitaka kuwapita bila kutazama kwenye makochi walipokuwa wamekaa Agape na Titus. Agape ndiye alimshitua Baba yake "Baba" Twaha akaonekana mwenye mawazo mazito. Alipogeuka kule alipoitwa na sauti ya mwanaye, sura ya kwanza aliyokutana nayo ni ya Titus. Titus akamsalimia kwa heshima huku Twaha akiitika kwa kigugumizi. Aliitazama sura ya Titus kwa makini akiwaza ni wapi aliwahi kukutana nayo. Mwisho kabisa aliwaomba akapumzike baada yaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kutopata jibu sahihi. Aliona huenda ukawa ni uchovu wa kazi yake nzito. Alipoingia chumbani, ndipo Agape na Titus waipopanga kutoka na kwenda slipway. Slipway huko ndipo Maliki alipowaona na kuwarudia mara ya pili.



    Baada ya Agape kupokea ujumbe ulioandikwa kwenye kipande cha karatasi na kukabidhiwa na muhudumu wa hoteli hiyo, aligeuka nyuma kumtafuta aliyekiandika.

    "Naweza kukupeleka madam" muhudumu alizungumza kwa utii bila kufahamu nini ambacho kilikuwa kinaenda kutokea. Agape akamtazama Titus, Titus akawa bado anachezea maji. Alinyanyuka na kuongozana na muhudumu aliyekuwa bado amesimama.

    "Nipeleke"

    Hatua chache wakafika eneo la peke yake, alipokuwa amekaa Maliki. Tabasamu pana lilikuwa limeunakshi uso wa Maliki. Alisimama kumkaribisha Agape. Agape hakutaka kukaa. Kwanza mtu huyo alikuwa mgeni machoni pake na pili hakupenda kumpa tabu Titus kumtafuta eneo hilo atakapomkosa alipokuwa amekaa. Maliki akamruhusu muhudumu yule kwenda na kumwambia aje kuchukua oda baadaye.

    "Sawa mkuu"

    Akaondoka. Agape akakaa huku akiwa ametawaliwa na wasiwasi. Hakukaa kwa kujiachia ila kimtegomtego kama kwamba ataondoka muda wowote. Baada ya hatua nyingi alizozipiga yule muudumu na kuwaacha peke yao, Maliki akapanga kutekeleza lile lililomfanya kumuita hapo Agape. Alinyanyuka tena akijifanya kwenda kuagiza vinywaji Agape hakujua hila za Maliki. Maliki alipoona Agape hajageuka, alikifunua kitambaa chenye dawa ya kulevya na kuibana vyema juu ya pua ya Agape. Agape akarusha mikono akapiga piga miguu chini hatimaye nguvu zake zikamsaliti. Akalegea na kusinzia papo hapo. Wala hakuwa mzito. Alimbeba kama wapenzi waliopo kwenye mahaba mazito. Kutokana na kulegea kule kwa Agape, kila mtu aliamini kuwa amelewa chakari. Alimuingiza ndani ya gari lake aliloliacha hatua chache kutoka alipotoka. Akazipachika gia na kuliingiza gari barabarani kuelekea maeneo ya mbweni. Huko mbweni kulikuwako na nyumba yake ya siri ambayo si Fredy wala Titus alikuwa akiifahamu. Ilikuwa ni nyumba ya siri yenye ulinzi wa kutosha pia. Hakukuwa na mtu zaidi ya muhudumu mmoja wa kike. Muhudumu huyo hakuwa muhudumu pekee bali ni mmoja kati ya watu hatari sana katika moja ya kikundi cha baba yake Maliki. Akamuingiza Agape ndani ya chumba nadhifu na kumtupa juu ya kitanda kipana chenye futi sita kwa sita. Maliki akatabasamu na kulitaja jina la Titus mara kadhaa. Akasikitika kwa kutingisha kichwa kisha akatoka ndan ya chumba kile.

    "Habari yako Suleya?"

    "Salama kaka, mgeni wetu amefanyaje?" Msichana yule mrembo aliletwa na baba yake Maliki kwa minajiri ya kuwa mpenzi wa Maliki. Maliki hakulifahamu hilo wala hakuvutiwa naye. Pia Suleya hakumpenda kijana huyo kwa kuwa hakuwa mmoja kati ya wavulana aliowahi kuwatamani. Pia hakuwahi kuhisi kitu kinachoitwa mapenzi ndani ya moyo wake, ndio maana akaja na ujumbe wa kuwa ametumwa kumlinda. Maliki akacheka aliposikia hivyo lakini hakuwa na jinsi kwa kuwa alimuamini Suleya kwa kuwa alimfahamu ukakamavu na nguvu zake. Akakubali.

    "Yule ni wifi yako"

    "Sasa mbona yupo katika hali ya kubebwa kuna jambo limetokea" Suleya akahamaki. Maliki akatabasamu na kumshika bega kwa liwazo

    "Hapana Sule imenilazimu kumpa madawa ya kulevya ili asinisumbue"

    "Bado sijakuelewa" akaonesha kutohitaji kujua zaidi juu ya msichana yule ambaye ni Agape akaingiza mada nyingine "nikuletee chakula?"

    "Hapana acha niende kwa washikaji zangu"

    "Msalimie Titus" suleya aliwahi kumuona Titus akiwa na Fredy pamoja na Maliki. Alimuhusudu sana na ndiye aliyemfanya kutomtamani Maliki na kumpenda yeye. Mara nyingi alikwisha mfikishia salamu hizo kupitia kwa Maliki, Maliki akapuuzia wala hakuchukulia kiuzito. Akatoka huku akimuachia maagizo.

    "Hakikisha huyu msichana hakusumbui na asitoke humu ndani"

    "Okey"

    Maliki akatoka na kuelekea alipo Fredy.



    ...



    Titus hakuoga kwa muda mrefu, kwa kuwa alikuwa akimtazama Agape mara kwa mara alipokuwa amekaa. Tangu aingie ndani ya bwawa hilo alishamtazama zaidi ya mara tatu, mara ya nne alipoibua kichwa chake hakumuona. Akaangaza katika kaunta, Agape hakuwepo. Wasiwasi ukavaa mapigo yake ya moyo na kuanza kumuenda mbio. Alitoka ndani ya maji na kwenda katika kitanda alichokuwa amelala Agapa akiota jua na kujifuta maji kwa taulo huku akiendelea kumtafuta Agape. Alizivaa nguo pale pale na kuanza kuzunguka kila kona ya eneo zima la Slipway, Agape hakuonekana. Simu yake pia haikupatikana.

    "Ameenda wapi?"

    Akiwa amejiinamia na kukishika kichwa chake ndani ya tafakuri nzito juu ya kitanda alicholala Agape hapo mwanzo, alikuja yule yule muhudumu aliyetumwa kumuita Agape.

    "Kaka mmeamua kuja kukaa huku?" Hakuona uso wa Titus akadhani ni Maliki. Titus alipoinua kichwa chake akaona kuwa si Maliki aliyemtuma kumuita yule msichana aliyekuwa amekaa katika kitanda alichokiwa amekaa Titus.

    "Oh samahani nimekufananisha"

    Akiwa bado kwenye mawazo Titus akahisi jambo. Akakumbuka kuwa yule muhudumu amesema 'mmekuja kukaa huku' ina maana anafahamu katika kitanda hicho alikuwa amekaa nani mwanzo. Akamkimbilia alipokuwa anaondoka

    "Samahani kuna jambo nataka kukuuliza" Titus akasema huku akipumua kwa nguvu.

    "Niulize tu mkubwa"

    "Katika kile kitanda alikuwa amekaa msichana fulani, umemuona maeneo haya"

    "Ndiyo"

    moyo wa Titus ukalipuka kwa furaha huku macho yake yakiwa na shahuku ya kujua ni nani.

    "Na mimi nilikuwa namtafuta yule kaka aliyenituma nimuite maana aliniambia nirudi tena aniagize vinywaji"

    "Yupoje?" Akauliza kwa kuhamaki.

    "Mweupe, mweupe hivi kama mwarabu"

    "Ahsante, ahsante"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Titus akafanya haraka kuondoka na kurudi mbweni. Wasiwasi ulikuwa umemtanda na kufanya mapigo yake ya moyo kumuenda kasi sana. Akafika mbweni baada yua mwendo mrefu kwa kasi ya gari na tamaa ya kufika haraka ikamfanya apaone ni karibu. Akapandisha ngazi harakaharaka mpaka vyumba vya juu alipokuwa na hakika atamkuta Fredy pekee, alichokitarajia si kama alivyodhani. Alikuwako na Maliki pia. Mwanzo mawazo yake yalimuhakikishia hizo ni njama za Maliki. Alikuwa akihema juu juu. Maliki na Fredy wakamgeukia na kumuuliza kwa pamoja

    "Hoya vipi?"

    Titus hakujibu kitu. Maliki akamfuata mpaka pale alipo Titus akiwa ameishika picha fulani. Tumempata mpumbavu anayetutafuta. Akaitupa ile picha mikononi mwa Titus.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog