Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SIRI YA FURAHA - 2

 





    Simulizi : Siri Ya Furaha

    Sehemu Ya Pili (2)



    Watu pekee waliokuwa karibu na bwana Lamos walikuwa walinzi wa kampuni ya ulinzi ya ‘Ultimate Security’ ambao mara kadhaa walikuwa wakipangwa kulinda nyumba yake. Muda wote Lomos alionekana akiwa na kiu ya maisha kwani alikuwa hapatikani dukani kwake huku akijitahidi kutafuta uwezekano wa kupanua biashara yake katika mikoa tofauti. Mbali na mambo hayo alikuwa akisafiri mara kadhaa kuelekea jijini Hong Kong nchini China ambako alikuwa akinunua bidhaa alizokuwa akiziuza dukani kwake.

    Siku moja ya Jumamosi ya kwanza mwezi wa nane wakati Lamos akiendelea na zoezi la kukagua hesabu za mauzo ya duka lake, alionekana mama mmoja ambaye alikuwa amembeba mtoto pamoja na rambo ndogo mkononi mwake. Mama huyo aliyekuwa akitembea taratibu katika mitaa hiyo ya Kariakoo alionesha dalili ya kushtuka kabla ya kuelekeza kwa makini macho yake katika bango kubwa lilikuwa katika duka moja eneo hilo la Kariakoo, mtaa wa Msimbazi. Bango hilo lililokuwa limeandikwa ‘Lamos Maputo Traders’, lilimshtua mama huyo ambaye hakuwa mwingine zaidi ya mkewe wa zamani wa Lamos, mapigo yake yake ya moyo yalimwenda mbio ghafla. Alikuwa ameshtushwa na jina la biashara la duka hilo ambalo lilikuwa la mume wake wa zamani ambaye alimtoroka na kumwacha na mtoto wao. Akiwa bado hajatulia vizuri alianza kutembea taratibu akijongea katika duka hilo huku akiwa na shauku ya kumfahamu mmiliki wake.

    Baada ya sekunde kadhaa alikuwapo ndani ya duka hilo lililokuwa likiuza vifaa vya magari huku akiwa amebaki ametoa macho huku mdomo wake ukiwa wazi akionesha mshangao pasipo kuongea jambo. Alikuwa amemwona mumewe wa zamani bwana Lamos Maputo akiwa katika droo kubwa ya fedha ya duka hilo, mkononi alikuwa na fedha nyingi alizokuwa akizihesabu. Hakuna aliyemwona mama huyo katika hali hiyo kwani wateja pamoja na wauzaji wa duka hilo walikuwa katika harakati za kuwahudumia wateja waliokuwepo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ Maputo….. wewe baba Veronika au nimekosea?” alisikika mama huyo baada ya kushangaa kwa sekunde kadhaa. Sauti kubwa aliyoitoa ilimshtua kila mtu aliyekuwapo katika duka hilo akiwapo Maputo mwenyewe ambaye aliinua kichwa chake huku akionekana kushtuka kidogo. Mara baada ya kuinua kichwa chake macho yake yaligongana na mkewe wa zamani, mwili wake ulisisimka ila baada ya sekunde kadhaa alikuwa sawa huku akitazamana na mwanamke huyo ambaye alianza kutokwa na machozi. “wewe mwanamke ni nani mbona sikufahamu?” alisikika Lamos Maputo kwa hali ya kujiamini kwa asilimia zote. “Ina maana umenisahau mimi baba Vero…. Ah! Na hivi vitu umepata wapi we mwanamme msaliti?” alisikika mama huyo huku akiwa na hasira na alionekana akitaka kujongea eneo la ndani la wauzaji alikokuwapo mumewe wa zamani.

    Lamos alionekana kugundua kuwa mkewe wa zamani alitaka kuingia eneo la wauzaji alilokuwapo na zaidi alitambua kuwa alikuwa na sekunde kadhaa ili ajiokoe kutoka katika tatizo la kuaibika. Alisimama eneo alilokuwapo na kumwoneshea ishara mlinzi aliyekuwa eneo la mlango mwa duka hilo. Mlinzi huyo alitii ishara hiyo kabla ya kuingia haraka katika duka hilo. “ eya! Mtoe huyo mwanamke simuelewi anachoongea na zaidi simfahamu…..” Baada ya maelezo hayo mlinzi huyo alimkamata mama huyo kwa nguvu kabla ya kuanza kumvutia nje. Alipiga kelele za kuomba kuachiwa lakini hakusikilizwa, mlinzi huyo alimvuta mpaka nje ambako mama huyo aliishia kuanza kutoa kauli za kumtukana Lamos ambaye hakujali na tayari alitambua jibu la jambo hilo.

    Alikuwa hasira kidogo ambazo zilipotezwa na furaha aliyokuwa nayo. Alikuwa amegundua mwanaye alikuwa mzima wa afya na kwa umbali aligundua kuwa alifanyiwa upasuaji katika kichwa chake kwa vile alilona kovu dogo.

    Alitambua mkewe wa zamani hangeweza kuondoka eneo hilo kama angeendelea kuwapo dukani kwake. Alimwita kijana wake mmoja kati ya watano walikuwapo dukani hapo kabla ya kusikika “ sasa sikia mimi naondoka ila hakikisha unamfuatilia mwanamke huyo anayepiga kelele nje mpaka ujue eneo analoishi naona kanidhalilisha ila asigundue kama unamfuatilia…. Mimi naondoka” alimalizia Lamos Maputo aliyekuwa na ufunguo wa gari lake mkononi kabla ya kuanza kutembea akielekea nje ya duka lake. Mara baada ya kutoka nje huku mkewe akiendelea kumtukana ilhali watu kadhaa wakiwa wanajongea eneo hilo alionekana kutojali. Mkewe huyo wa zamani alipojaribu kumsogelea Lamos, mlinzi wa duka hilo alimzuia na alishindwa kumfuata zaidi aliishia kumshuhudia Lamos akiondoka na gari lake la kifahari eneo hilo

    Baada ya Lamos kuondoka mama huyo alionekana kuishiwa nguvu huku akiongea peke yake taratibu. Alianza kutembea taratibu kuelekea katika kituo cha mabasi huku akionekana mwenye hasira. Wakati akiendelea kuelekea katika kituo hicho cha mabasi ya Kimara, nyuma yake alionekana kijana wa bwana Lamos Maputo akimfuatilia. Kijana huyo walipanda gari moja na safari ilianza kuelekea Kimara. Mama Veronika akiwa na hasira hakujaribu hata kumwangalia mtu yeyote aliyekuwa karibu yake zaidi alitamani afike haraka nyumbani kwake kwani huko aliamini angeenda kupumzika. Baada ya dakika arobaini na tano alikuwa akishuka kwenye daladaa aliyopanda na bila kupoteza muda alianza kutembea kwa haraka akielekea nyumbani kwake pasipo kujua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kijana wa Lamos. Kijana huyo alimfuatilia mpaka eneo ambalo mama huyo alikuwa akiishi na mwanaye pasipo kugundulika. Ili kupata uhakika wa jibu la kumpa bosi wake alihakikisha mpaka chumba alichokuwa akiishi mama huyo.

    Baada ya zoezi hilo alipanda daladala kurudi tena Kariakoo ili kuendelea na shughuri za biashara ya bosi wake. Tayari alikuwa ameshamwambia bosi wake juu ya kazi ya kumfuatilia mama Veronika aliyokuwa ameitoa. Lamos alionesha kufurahia taarifa hiyo huku akimwahidi zawadi kijana wake huyo. Majira ya jioni wakati wa kufunga maduka Lamos alirudi tena katika duka lake mtaa wa msimbazi, Kariakoo. Lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha anapelekwa na kijana wake eneo ambalo mkewe wa zamani alikuwa akiishi. Baada ya jambo hilo alijua angeandaa taratibu nyingine za kumpata mtoto wake Veronika aliyekuwa na mwaka mmoja na nusu wakati huo. Kijana wake alimpeleka mpaka eneo ambalo mama Veronika alikuwa akiishi na majira ya saa mbili nusu usiku walikuwa wakiondoka na gari jingine la Lamos eneo la nyumba hiyo. Lamos alitumia gari hilo jingine ambalo halikuruhusu mtu wa nje kumwona mtu wa ndani ili asigundulike.

    Majira ya saa tatu usiku, kijana wa Lamos alikuwa akishuka katika gari la bosi wake katika maeneo ya Magomeni tayari kwa kuelekea nyumbani kwake. Alikuwa amepewa kiasi cha shilingi elfu hamsini kutokana na kazi aliyokuwa ameifanya. Lamos tayari alikuwa ameshatambua jambo la kufanya wakati huo na alihitaji subira ya wiki mbili ili kukamilisha adhma yake na zaidi hakutaka kugundulika na mtu katika zoezi alilolipanga. Baada ya wiki mbili alionekana maeneo ya Manzese huku akiwahitaji watu wa kumkamilishia kazi yake ndogo. Baada ya saa kadhaa alimpata kiongozi wa kundi moja la wahalifu waliojiita ‘Tuliochoka’. Bila kupoteza muda alimweleza kiongozi huyo kuwa alitaka vijana wa kundi hilo wafanikishe zoezi la kumteka mwanaye aliyekuwa akiishi na mama yake maeneo ya Kimara. Jambo hilo halikuwa gumu kwa kiongozi wa kundi hilo ambaye aliahidi kulifanyia kazi ndani ya siku tatu. Ahadi yake ilifuata baada ya kiongozi huyo kuoneshwa nyumba ambayo mwanaye Lamos aliishi na mama yake.

    Siku ya Jumatatu ya katikati ya mwezi wa nane majira ya saa nane usiku, zilionekana teksi mbili zikiegeshwa mbele ya nyumba ya mama Veronika. Walishuka vijana wanne wanne kutoka katika kila gari wakiwa wameongozwa na kiongozi wao wa kundi la ‘Tuliochoka’. Walikuwa na mavazi ya rangi nyeusi huku wakiwa na mapanga mikoni mwao ilhali wengine wakiwa na shoka mbali na vitu hivyo walivaa vinyago vilivyozuia mtu kuona sura zao. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amebeba chupa ya damu ya binadamu ambayo ilikuwa na damu, mkononi wake mwingine ulikuwa na kisu kilichokuwa kinang`aa sana. Bila kupoteza muda walitembea kabla ya kuujongea mlango wa chumba alichokuwa akilala mama Veronika. Bila kupoteza muda kijana mmoja wa kundi hilo alikikata kitasa cha mlango mara mbili huku akitumia shoka lake hatimaye mlango huo ulifunguka. Bila kupoteza muda kiongozi wao akiwa na kisu mkononi huku akiwa ameiweka chupa ya damu katika koti lake alikuwa wa kwanza kuingia katika chumba hicho.

    Nyuma yake alifuatwa na vijana watano ilhali wengine walikuwa wamebaki nje. Kiongozi huyo aliwasha taa ya chumba hicho kabla ya kusikika kelele ya mama Veronika ambaye alikuwa amekaa kitandani huku akiwa na hofu kwani alisikia kelele za kuvunjwa mlango. Taswira ya chumbani kwake ilimpa hofu na ghafla alijikuta akiamini kuwa eneo hilo halikuwa na usalama. “tulia mwanamke kwa usalama wako vinginevyo tutamwaga damu yako isiyo na hatia…..” baada ya kauli hiyo kutoka kwa kiongozi wa kundi hilo mama huyo alitulia lakini alikuwa akitetemeka kupindukia na haja ndogo ilikuwa imemtoka pasipo kujitambua.

    “mtoeni haraka kitandani…” alisikika kwa mara nyingine kiongozi wa vijana hao wa kundi la `Tuliochoka`. Bila kupoteza muda vijana wake wawili walimvuta kwa nguvu mwanamke huyo aliyekuwa na nguo za kulalia na kumtoa kitandani. Mama huyo alisimama katikati ya vijana hao wawili huku akiendelea kutetemeka kupindukia. Kiongozi wa kundi hilo alimsogelea mwanamke huyo kabla kuonekana akimshika mkono wake wa kushoto. Mwishoe alitoa bomba la sindano ambalo lilikuwa na dawa ndani yake. Alilitikisa bomba hilo kabla ya kuishia kumchoma katika mkono wa mwanamke huyo ambaye alipiga kelele kidogo ila alipooneshwa mapanga alinyamaza ghafla. Mara baada ya zoezi hilo kiongozi wa kundi hilo alicheka kabla ya kuelekea kitandani ambapo mtoto wa mama huyo, Veronika alikuwa bado amelala. Alimfunua shuka alilofunikwa mtoto huyo kabla ya kuanza kukitembeza kisu mwilini mwa mtoto huyo. Jambo hilo lilimchanganya mama yake ambaye alitamani kupiga kelele lakini panga lililokaa katika koo lake wakati huo alilooneshewa na kijana mmoja lilimkatisha tamaa ya kufanya jambo lolote.

    Kadri sekunde zilivyozidi kwenda mama huyo alihisi kuishiwa nguvu huku macho yake yalionekana kuwa mazito kama alihitaji kulala wakati huo. Huku akihusisha sindano aliyochomwa na jambo hilo alijitahidi asilale ili kujua jambo ambalo watu hao walitaka kulifanya kwa mwanaye. Alijitahidi kutoa macho kumwangalia mtu ambaye alikuwa akiendelea kutembeza kisu mwilini mwa mwanaye lakini kadri sekunde zilivyoenda alijiona akishindwa zoezi hilo. Baada ya dakika mbili alianguka chini kama mzigo na tayari alikuwa katika usingizi mzito. Kiongozi wa kundi hilo la `Tuliochoka` aliwaonesha vijana wake ishara na bila kupoteza muda walimbeba mama huyo na kuanza kutoka naye nje kwa kasi. Mara baada ya kutoka naye nje walimpakiza katika teksi su

    Kiongozi wa kundi hilo alipoona mama wa mtoto huyo amelala, alitambua huo ulikuwa muda muafaka wa kumchukua mtoto huyo wa Lamos kirahisi. Kabla ya kumchukua alitoa chupa ya damu ya binadamu aliyokuwa nayo kisha aliitoboa chupa hiyo akitumia kisu. Damu iliyotoka katika chupa hiyo aliielekeza kwenye kitanda hicho na kuisamba kila sehemu. Baada ya zoezi hilo alitoka akikimbia na mtoto huyo. Aliongoza mpaka katika moja ya gari kati ya magari mawili waliyofika nayo, mara baada ya kuingia katika gari hilo waliondoa gari zao kwa kasi eneo hilo.

    Baada ya dakika kumi magari yao yalionekana katika foleni Ubungo yenye makutano ya barabara nne. Mara baada ya upande wa magari ya barabara ya Morogoro kuhurusiwa, gari la kiongozi wa kundi hilo akiwa na mtoto wa Lamos liliongozwa kufuata barabara ielekeayo Posta. Gari jingine liliongozwa kufuata barabara ya ielekeayo Buguruni huku likiwa na mama Veronika ambaye bado alikuwa katika usingizi mzito. Majira ya saa tisa na nusu kiongozi wa kundi la `Tuliochoka` alikuwa nyumbani kwa Lamos akimkabidhi mtoto wake ambaye alikuwa ametekwa maeneo ya Kimara.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kumi magari yao yalionekana katika foleni Ubungo yenye makutano ya barabara nne. Mara baada ya upande wa magari ya barabara ya Morogoro kuhurusiwa, gari la kiongozi wa kundi hilo akiwa na mtoto wa Lamos liliongozwa kufuata barabara ielekeayo Posta. Gari jingine liliongozwa kufuata barabara ya ielekeayo Buguruni huku likiwa na mama Veronika ambaye bado alikuwa katika usingizi mzito. Majira ya saa tisa na nusu kiongozi wa kundi la `Tuliochoka` alikuwa nyumbani kwa Lamos akimkabidhi mtoto wake ambaye alikuwa ametekwa maeneo ya Kimara. Baada ya mazungumzo mafupi Lamos alimlipa kiongozi huyo kiasi cha milioni mbili kama walivyokuwa wameahidiana na kiongozi huyo aliondoka. Lamos akiwa na furaha, alimchukua mtoto wake huyo ambaye alikuwa bado na usingizi. Alimpeleka mpaka katika chumba maalumu ambacho alikuwa amekiandaa kwa ajili ya mtoto huyo. Chumba hicho kilikuwa kikubwa huku kikiwa na vitu vingi vya watoto, zilikuwapo baskeli kadhaa za watoto, magari pamoja redio zilizokuwa zikitoa kelele tofauti.

    Lamos Maputo alikuwa na furaha ya kumpata mtoto huyo ambaye ndiye pekee alikuwa kikwazo cha furaha yake. Alitaka kumlea mtoto huyo katika misingi ya masharti aliyopewa na mganga wake wa jadi bwana Karamaj Sankar aliyekuwa raia wa India. Alitaka kumlea katika misingi ya masharti hayo kwani alielewa mwishoe mwanaye hakupaswa kufanya mapenzi wala kuolewa katika maisha yake. Hakuwa na hofu huku akiwa na mikakati kadhaa ambayo aliipanga kuitumia katika kumwandaa mtoto wake huyo pekee kuwa mrithi wa utajiri wake.

    * * * * *

    Mama Veronika alizinduka kutoka katika usingizi mzito majira ya saa nne asubuhi huku akiwa amechoka sana. Alikuwa pembezoni mwa bahari ya hindi katika fukwe ya Kigamboni. Ndani ya sekunde kadhaa alionekana akifikicha macho yake kama vile mtu ambaye alikuwa hajitambui. Baada ya dakika moja alisikika akianza kulia kwa nguvu kama mtoto mdogo. Wakati akiendelea kulia alikuwa akilitaja jina la mwanaye ambaye alidai alikuwa ameuawa. Kelele hizo ziliwafikia wahudumu wa hoteli moja iliyokuwa karibu na eneo hilo la ufukweni ambao walianza kujongea eneo hilo huku wakiamini mtu huyo alikuwa mwehu. Walipofika eneo hilo wahudumu hao waliokuwa watatu walitulia na kuanza kumsikiliza mwanamke huyo aliyekuwa akilia kwa uchungu huku akionekana kuishiwa nguvu kabisa.

    Wahudumu hao walimuhurumia mwanamke huyo kabla kumsaidia kwa kumbeba na kumpeleka katika hoteli waliyokuwa wakifanyia kazi. Huko walimwambia mwanamke huyo apumzike wakati ambao walikuwa wakiongea na bosi wao juu ya mkasa wa mwanamke huyo. Baada ya muda mfupi wa mazungumzo bosi huyo alikubali kumsaidia mwanamke huyo kumfikisha nyumbani kwake kwa vile alikuwa akitarajia kuelekea maeneo ya Kimara kufuata mahitaji ya hoteli hiyo. Mama Veronika alikuwa ametulia wakati huo huku akionekana kukata tamaa ya kila jambo, kwani alikuwa akiamini mwanaye pekee alikuwa amefariki kwa kuuawa usiku wa siku hiyo.

    Majira ya saa sita na nusu aliondoka na bosi wa hoteli hiyo ambaye alikuwa akielekea maeneo ya Kimara na gari lake dogo la mizigo. Wakati wote akiwa kwenye gari hisia za kifo cha mwanaye ndizo zilizokuwa zikiendelea kuongezeka na hakutamani kufika eneo alilokuwa akiishi. Kila alipokuwa akimkumbuka kiongozi wa watu waliomvamia usiku wa siku hiyo alikuwa akiwaza juu ya kifo cha mwanaye tu. Alikumbuka jinsi kiongozi huyo alivyokuwa akikitembeza kisu chenye ncha kali katika mwili wa mtoto wake na aliamini lazima alimuua mwanaye. Baada ya saa moja walikuwa maeneo ya Kimara huku wakijongea taratibu katika nyumba ambayo mwanamke huyo alikuwa akiishi. Mwonekano wa nje ya nyumba aliyopanga ndio ulimfanya mama huyo aanze kulia tena kwa sauti. Kulikuwa na kundi kubwa la watu waliokuwapo eneo hilo ambao walionekana kukizunguka chumba cha mama huyo.

    Mara baada ya gari alilokuwapo kusimama alishuka akilia kwa sauti huku akikimbia kuelekea katika chumba alichopanga ambacho kilikuwa kimezungukwa na watu wengi. Watu waliokuwapo nje ya nyumba hiyo walishtuka kumwona ilhali wengine walianza kumwogopa. Huku akisukumana na watu kadhaa aliongoza mpaka ndani ya chumba chake ambako alienda kuwaona watu wengine kadhaa ambao hakuwajali. Alielekeza macho yake katika kitanda chake akiwa na imani ya kuweza kumwona mwanaye. Haikuwa hivyo, aliishia kushuhudia damu zilizokuwa zimetapakaa katika eneo la kitanda hicho. Huku akilia kwa uchungu alikimbia na kupanda katika kitanda hicho kabla ya kuanza kuyakumbatia mashuka hayo huku akilia kwa uchungu.

    Watu waliokuwapo walipata mshtuko kidogo kwani walikuwa wakiamini uwezekano wa kuuawa kwa Mama Veronika na mwanaye. Mara baada ya kufika nyumbani kwake hapo huku akionekana kumlilia mwanae, waligundua uwezekano wa jambo baya lililokuwa likiendelea. Mchungaji Sigismund Leopold ndiye aliyekuwa wa kwanza kumfuata mwanamke huyo katika kitanda chake wakati akiendelea kulia huku akiwa ameshika mashuka yaliyokuwa na damu. Aliongoza naye wakitoka katika chumba hicho huku akifuatwa na watu kadhaa waliofika eneo hilo.

    Walikuwa wakihitaji kujua juu ya jambo lililokuwa limetokea mpaka wakati huo, Mama huyo aliwasimulia juu ya kila jambo lililokuwa limetokea usiku wa siku hiyo baada ya kuvamiwa na watu aliooamini walikuwa majambazi. Baada ya taarifa hiyo ndefu waliyoipokea, watu hao wakiongozwa na mchungaji Sigismund Leopold waliondoka eneo hilo wakiwa na lengo la kwenda kutoa taarifa hizo katika kituo cha polisi cha Kimara. Taarifa hizo zilikuwa za mara ya pili baada ya nyingine kutolewa kabla ya Mama Veronika kurudi nyumbani kwake. Askari hao hawakuruhusu jambo lolote kuchukua nafasi zaidi ya upelelezi walioahidi kuwa walishaanza kuufanya wakati huo.

    Wakati wa jioni Mama Veronika aligoma kabisa kulala nyumbani kwake hivyo mchungaji Sigismund aliamua kumtafutia chumba kimoja kilichokuwa katika kanisani alilokuwa akiliongoza. Mama huyo alimshukuru mchungaji huyo huku akiwa na amani kidogo tofauti na ilivyokuwa awali. Usiku wa siku hiyo alikuwa na mawazo tele huku akimuwaza mwanaye ambaye aliamini alikuwa ameshauawa. Hakuwaza kumfuata baba wa mtoto huyo kumpa taarifa zozote kwani aliamini hakuwa mtu mwema hata kidogo. Alikuwa akimwomba Mungu ili watu waliomuua mwanaye wakamatwe na zaidi alihitaji kujua sababu zilizowafanya wamuue mtoto huyo.

    Siku iliyofuata iliisha pasipo taarifa zozote, muda wote mama Veronika alikuwa katika chumba alichopewa kanisani hapo. Hakula chakula hata kidogo na mfariji wake alikuwa mchungaji Sigismund ambaye mara kadhaa alimtembelea katika chumba hicho na kumtuliza na zaidi alimweleza wasubiri upelelezi uliokuwa ukufanywa na jeshi la polisi. Hatimaye muda wa wiki mbili ulipita pasipo kupatikana kwa taarifa zozote za mtoto huyo waliyeamini alikuwa ameuawa. Jeshi la polisi lilitoa taarifa yake rasmi ya kuamini kuwa mtoto huyo, Veronika aliuawa siku ya tukio baada ya chumba walichokuwa wakikaa na mama yake kuvamiwa na watu ambao hawakujulikana. Jeshi la polisi pia lilihurusu yafanyike mazishi ya kumbukumbu ya mtoto huyo na zaidi walidai walikuwa wakiendelea na upelelezi.

    Misa ya mazishi ya kifo cha mtoto huyo, Veronika ilifanyika katika makabuli ya Mbezi Luis na mara baada ya zoezi hilo mama wa mtoto huyo bado aligoma kurudi nyumbani kwake na alihitaji kufanya kazi za kanisa na kuishi katika eneo hilo. Kanisa halikuwa na pingamizi juu ya suala hilo na mama huyo alihurusiwa kuanza kuishi rasmi kanisani hapo. Baada ya siku kadhaa alionekana akianza kurejewa na faraja iliyopotea kwa muda mrefu na taratibu alianza kuchangamka tofauti na ilivyokuwa awali. Alikuwa akifanya kwa bidii kazi za kanisa kila siku na kila mtu aliziona bidii za mama huyo ambaye taratibu alianza kubadilika na kuonekama kama mrembo ambaye hakuwahi kuwa na mtoto. Mazingira mazuri yenye maua ambayo yalionekana eneo la kanisa hilo yaliwapa shauku wengi ambao hawakuwahi kuiona taswira hiyo kabla. Walipokuwa wakiuliza juu ya mtu ambaye alikuwa akitengeneza mazinngira hayo walikuwa wakijibiwa kuwa ni Mama wa Kanisa, jina ambalo watu wengi wa kanisani walipenda kumwita kutokana na kutumia muda mwingi kufanya usafi wa kanisa hilo. Nyakati za jioni mama Veronika alikuwa akijumuika na waimbaji wengine wa kanisa hilo katika mazoezi ya kwaya, hakuwaza jambo jingine wakati huo zaidi ya kumtumikia mwenyezi Mungu.

    Baada ya mwaka mmoja Mchungaji Sigismund Leopold raia wa Ujerumani ambaye alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano, tayari alikuwa ametimiza miaka mitano ambayo alipaswa kulitumikia kanisa lake nchini Tanzania kama alivyopangiwa. Wakati huo alikuwa amebakiwa na miezi mitano ili aondoke Tanzania. Mbali ya kuwa kumbuka ndugu zake nchini Ujerumani, kuna jambo lililokuwa likimtatiza kichwani ambalo alihisi lingekuwa kikwazo kwake kutoweza kurudi nchini Ujerumani. Mchungaji Sigismund alikuwa katika matamanio mazito kwa mwanamke wa kitanzania ambaye alikuwa tayari kumuoa. Mwanamke huyo alikuwa tofauti na alivyokuwa akimtegemea awali kwani alikuwa mrefu kiasi huku akiwa na umbo lenye sifa za urembo. Rangi yake ya maji ya kunde na upole wake ambao kila mtu aliutambua ndivyo vitu vilivyomchanganya kabisa na hakuwa tayari kumkosa mwanamke huyo.

    Mwanamke huyo aliyekuwa anamchanaganya mchungaji Sigismund hakuwa mwingine zaidi ya mama Veronika au mama wa kanisa kama alivyokuwa akiitwa wakati huo huku akiwa mcha Mungu siku zote akiwa kanisani hapo. Jambo hilo lilikuwa linamuumiza kichwa kwani alikuwa mwoga wa kuongea na wanawake kuhusiana na mahusiano toka akiwa mtoto mdogo. Hakuwa na hofu juu ya sheria za kanisa lake hilo ambazo hazikumzuia yeye kuoa. Mchungaji Sigismund alikuwa mtulivu kwa muda mrefu na mwishoe aliamua kutoa jambo hilo lililokuwa moyoni mwake kwa mwanamke huyo. Ilichukuwa muda kwa mama Veronika kuelewa jambo hilo aliloelezwa na mchungaji Sigismund kwani alihisi alikuwa akijaribiwa. Jambo hilo lilimchanganya kabisa mchungaji huyo baada ya kuona hajibiwi na mwanamke huyo na zaidi alishindwa kuendesha hata misa za majuma mawili mfululizo huku akiwapa jukumu wasaidizi wake kuongoza misa hizo. Baada ya wiki mbili na nusu mama Veronika aliamua kuufungua moyo wake na kumkaribusha mchungaji Sigismund. Alichukua uamuzi huo baada ya kugundu mchungaji huyo alikuwa amebadilika ghafla na aliamini jambo aliloelezwa. Uamuzi huo ulifuata pia baada ya kuwapo kwa mazungumzo kadhaa baina ya waumini ambao hawakujua sababu ya Mchungaji wao kutokuwa sawa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa furaha kwa mchungaji Sigismund Leopold baada ya kukubaliwa na mwanamke huyo na kudhihilisha furaha yake alifikisha ujumbe huo kwa wazee wa kanisa hilo ambao walibariki uhusiano huo uliokuwa ukielekea kwenye harusi. Hatimaye katika misa ya juma hilo mchungaji Sigismund Leopold alitangaza jambo ambalo waumini hawakulitegemea. Alitangaza harusi ambayo alitarajia kufunga na mwanamke wa kitanzania, watu wengi walilipokea tangazo hilo hilo huku wakiibariki harusi hiyo ilikuwa baina ya mchungaji huyo na mama wa kanisa. Harusi hiyo iliyokuwa faraja kwa waumini walioshangilia kwa namna tofauti huku wakiwa na furaha ilipangwa kufungwa katika tarehe ya mwisho ya mwezi wa kumi na mbili ambayo ilikuwa siku ya kumwaga mchungaji huyo.

    Siku zilisogea hatimaye harusi hiyo ambayo watu wachache walikuwa wakihisi ilikuwa ndoto ilifungwa ikiwa sambamba na sikukuu za kumuaga mchungaji huyo ambaye alikuwa kipenzi cha waumini wengi. Mwishoe ndoto za mchungaji Sigismund Leopold zilitimia kwani tarehe tatu ya mwezi Januari alikuwa na mkewe wakielekea nchini Ujerumani. Walikuwa katika ndege ya shirika la British Airlines na baada ya saa kadhaa walikuwa wakitarajia kufika nchini Ujerumani wakifikia katika jimbo la Stuttgart. Ndege yao ilikuwa ikitarajiwa kupita jijini Cairo nchini Misri kabla ya Uingereza na mwishoe Ujerumani. Walikuwa na furaha na zaidi mchungaji Sigismund ambaye alikuwa amemficha mkewe juu ya sherehe kubwa ambayo ndugu zake walikuwa wameiandaa kwao katika jimbo la Frankfurt. Alitambua furaha ya ndugu zake ilitokana na jinsi walivyomkubuka na zaidi hatua ya kuoa aliyoifikia iliyokuwa kikwazo kwa muda mrefu kwa ndugu zake hao.





    Mwishoe ndoto za mchungaji Sigismund Leopold zilitimia kwani tarehe tatu ya mwezi Januari alikuwa na mkewe wakielekea nchini Ujerumani. Walikuwa katika ndege ya shirika la British Airlines na baada ya saa kadhaa walikuwa wakitarajia kufika nchini Ujerumani wakifikia katika jimbo la Stuttgart. Ndege yao ilikuwa ikitarajiwa kupita jijini Cairo nchini Misri kabla ya Uingereza na mwishoe Ujerumani. Walikuwa na furaha na zaidi mchungaji Sigismund ambaye alikuwa amemficha mkewe juu ya sherehe kubwa ambayo ndugu zake walikuwa wameiandaa kwao katika jimbo la Frankfurt. Alitambua furaha ya ndugu zake ilitokana na jinsi walivyomkubuka na zaidi hatua ya kuoa aliyoifikia iliyokuwa kikwazo kwa muda mrefu kwa ndugu zake hao.

    * * * *

    Lamos Maputo alifurahi sana baada ya zoezi la kumpata mtoto wake kufanikiwa hakuwaza jambo lolote zaidi ya mafanikio kwa wakati huo. Tayari mtoto wake huyo pekee, Veronika alikuwa amemtafutia mfanyakazi wa kike ambaye jukumu lake likuwa ni kumlea. Mwanaye huyo hakuhurusiwa kutoka nje hata siku moja na jambo hilo lilifanikiwa kwani watu wengi wa mtaa ambao Lamos alikuwa akiishi hawakujua kama alikuwa na mtoto. Kila siku alikuwa na ratiba ya kurudi nyumbani kwake mara mbili ua zaidi kwa lengo la kumwangalia mwanaye huyo aliyempenda sana.

    Baada ya miaka miwili na nusu wakati mwanaye huyo mwenye afya njema akiwa na miaka minne, Lamos alianza kufikiri jinsi ya kumsomesha mtoto huyo ambaye wakati huo alipaswa aungane na watoto wenzie kwa ajilia ya masomo ya chekechea lakini alipowafikiria watoto wa kiume hakukubaliana na jambo hilo. Hakuhitaji mwanaye ajenge urafiki wowote na watoto wa jinsia hiyo. Hivyo aliwaza jambo nyingine, aliwaajiri walimu watano wa kike ambao kwa wakati tofauti walikuwa wakifika nyumbani kwake na kumfundisha mwanaye. Wakati huo alikuwa na mafanikio makubwa ikiwapo nyumba ya kifahari iliyojenga Mbezi Beach zaidi alikuwa na maduka mengine kila mkoa wa nchini ambayo yalikuwa yakitumia jina la `Lamos Maputo Traders`. Tayari jina lake lilianza kuwa midomoni mwa watanzania ambao walikuwa wakimwongelea Lamos kama tajiri aliyekuwa akipanda kiuchumi kwa kasi kila siku iliyokuwa ikipita. Bado alikuwa akiagiza bidhaa zake alizoziuza kutoka Hong Kong nchini China na Dubai nchini United Arabs Emirates (U.A.E). Wakati huo mara kadhaa alikuwa akisafiri kwa ndege kuelekea mikoa tofauti kwa lengo la kuhakikisha ufanisi wa biashara zake.

    Jambo lililomfurahisha lilihusiana na taarifa alizopewa na walimu waliokuwa wakimfundisha mwanaye kwani alielezwa mwanaye alikuwa na akili sana na zaidi uwezo mkubwa wa kufikiri. Mbali na jambo hilo kuwa faraja kwa Lamos alikuwa akiwaza jinsi ambavyo mtoto wake huyo angeeanza elimu ya msingi. Bado alikuwa hahitaji mtoto huyo awe karibu na watoto wa kiume hata kidogo. Hatimaye alifikisha umri wa miaka saba tayari kwa kuanza elimu ya shule ya msingi, Lamos Maputo aliwaza tena jambo. Alienda katika shule ya kimataifa St. Mary na huko alifanikiwa kumshawishi mkuu wa shule hiyo jambo. Alimweleza mkuu wa shule hiyo kuwa mwanaye alikuwa na matatizo makubwa kiafya yaliyosababisha azimie kila wakati na alihitaji mwanaye awe mwanafunzi wa shule hiyo lakini awe anasomea nyumbani kwake na kufanya mitihani na wenzie kipindi husika.

    Mkuu wa shule hiyo alielewa jambo hilo hasa baada ya kuelewa kuwa mtoto huyo angefundishwa na walimu wengine mbali na walimu wa shule hiyo. Furaha yake iliongezeka baada ya Lamos Maputo kulipa ada yote kwa ajili ya mwanaye huyo ambaye angekuwa akifika shuleni hapo kwa ajili ya kufanya mitihani tu. Hayo ndiyo maisha mapya ambayo Veronika aliyaanza katika elimu yake ya shule ya msingi. Wakati huo Lamos alimjengea mwanaye huyo darasa katika nyumba yake pamoja na maktaba ndogo ambavyo aliamini vingemsaidia. Aliwaajiri walimu wengine wa kike watano kwa ajili ya kumfundisha mwanaye huyo na zoezi hilo lilianza. Maelezo aliyopewa kutoka kwa walimu wa mwanaye huyo bado yaliendelea kumfariji kwani alielezwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa sana.

    Jambo hilo lilijidhihirisha katika mtihani wa muhula kwanza wa shule ya kimataifa ya St. Mary, Lamos alisimamisha shughuli zake za kila siku na alikuwa akimpeleka mwanaye katika shule hiyo ya kimataifa ili afanye mtihani. Muda wote wakati mtihani ukiendelea alikuwa akimsubiri mwanaye nje ya darasa ambalo walikuwa wakifanyia mtihani. Kila mtihani Veronika alikuwa wa kwanza kutoka katika chumba cha mtihani na jambo kubwa alilokuwa akimweleza baba yake alidai mitihani ilikuwa mirahisi sana. Hatimaye mitihani hiyo iliisha na ndoto za Lamos juu ya mwanaye kutosogelewa na mtoto yeyote wa kiume zilifanikiwa kwa asilimia kubwa kwani Veronika hakufahamiana na mtoto yeyote.

    Baada ya mwezi mmoja Lamos alipokea ripoti ya matokeo ya mwanaye iliyomfurahisha kwani alikuwa ameongoza darasa lake kwa alama za juu sana tofauti na watoto wengine aliofanya nao mtihani. Jambo hilo lilimfurahisaha sana na aliamini njia aliyokuwa akiitumia ilikuwa sahihi na alipanga kuitumia mpaka Veronika akimaliza elimu yake ya juu. Miaka ilisogea huku Veronika akisoma shule nyumbani kwao na kufanya mitihani ya shule ya kimataifa ya St. Mary. Lamos Maputo hakujaribu kufikiri wala kutamani kuoa hata kidogo, mara kadhaa mwanaye alimuuliza maswali juu ya mama yake, alimjibu alifariki wakati akizailiwa na kumwacha akiwa mtoto mdogo. Hakuwa tayari kuvunja masharti ya mganga wake wa jadi, Karamaj Sankar yaliyokuwa sababu ya uwezo wake kifedha na jina kubwa lililokuwa siyo geni masikioni mwa watu nchini kwa wakati huo.

    Kadri upeo wake wa kufikiri ulivyozidi kuongezeka kutokana na kukua kwake, Veronika alikuwa akiushangaa mfumo aliokuwa akiutumia wa kusoma nyumbani tofauti na wenzie. Alipomuuliza baba yake juu ya suala hilo alikuwa mkali na aliogopa kumpeleleza zaidi. Aligundua pia kuwa baba yake alikuwa hapendi awe karibu na watoto wenzie wa kiume. Jambo lililomshangaza zaidi lilihusiana na pole alizokuwa akipewa na walimu wake mara kadhaa wakati akifanya mitihani ya shule yake. Alikuwa akizipokea kauli hizo za walimu wake waliokuwa wakijua alikuwa na matatizo ya kumzia na zaidi baba yake alimtaka asijaribu kuwaeleza kama alikuwa mzima.

    Jina lake bado lilikuwa gumzo kwa wanafunzi wa shule yake kutokana na uwezo wake darasani kwani alikuwa akiongoza darasa lake toka akiwa darasa la kwanza. Wanafunzi wenzie walihitaji kumfahamu zaidi Veronika lakini ilikuwa vigumu kutokana na ulinzi aliokuwa akiupata kutoka kwa baba yake. Muda wote alikuwa na baba yake ambaye mara kadhaa alisafiri naye kuelekea nchi tofauti kwa vile alikuwa akihofia kumwachia uhuru mwanaye huyo. Hatimaye Veronika alimaliza shule ya msingi na kufauru vizuri katika mtihani wake wa mwisho. Baba yake Lamos Maputo alimtaka mwanaye aendelee na elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari ya St.Mary. Alifanya hivyo kwani aliamini Veronika angeendelea kusoma kwa mfumo alioutumia awali na jambo hilo lilifanikiwa. Veronika alianza elimu ya sekondari huku akisomea nyumbani kama awali na kufanya mitihani katika shule ya St. Mary.

    Wakati huo baba yake aliwahurusu rafiki zake wa kike ambao walikuwa wakimtembelea mara kadhaa lakini jambo hilo halikusaidia hata kidogo. Wakati huo Veronika alikuwa amekua na kutambua mambo mengi, alikuwa akitamani kuwa karibu na wavulana isivyo kawaida. Muda mwingi alikuwa akijifungia chumbani kwake na alikuwa akipenda kuangalia tamthilia za mahusiano. Tabia yake hiyo iliyokuwa kwa kasi ndiyo iliyomfanya apende kuwasiliana na wanafunzi wa kiume ambao alibahatika kupata namba zao kupitia kwa wanafunzi wa kike waliokuwa wakifika nyumbani kwao. Mmoja wa wanafunzi hao wa kiume aliopenda kuwasiliana nao sana alikuwa ni Rashid Kagu. Alikuwa ni kijana aliyemvutia sana katika maongezi ya simu na ujumbe mfupi kupitia mtandao kwa vile alikuwa na kompyuta chumbani kwake, namba ya kijana huyo aliihifadhi kwa jina la Rehema. Alifanya hivyo kwa vile alikuwa akimhofia baba yake ambaye alikuwa akiikagua simu yake kila mara. Hata wavulana wengine alihifadhi namba zao kwa majina ya kike ili baba yake asigundue. Veronika alikuwa akiwasiliana na Rashid Kagu pasipo kumfahamu kwa vile hakuwahi kupata nafasi ya kuwa karibu na wanafunzi wenzake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye ulifika wakati ambao alianza kufanya mtihani wa muhula wa kwanza wa kidato cha tatu, ni kipindi ambacho alipanga kufahamiana na Rashid Kagu aliyekuwa rafiki yake mkubwa kupitia njia ya simu. Siku ya kwanza iliyokuwa Jumatatu walikuwa wakianza na mtihani wa hesabu. Kama ilivyokuwa kawaida baba yake Lamos Maputo alikuwa nje ya chumba cha mtihani akimsubiri mwanaye. Muda wote wakati mtihani ukiendelea Veronika alikuwa akimuwaza Rashid Kagu, kijana aliyemvutia kupitia mazungumzo ya simu. Siku hiyo tofauti na ilivyokuwa kawaida yake ya kutoka mapema katika chumba cha mtihani, Veronika alimaliza mtihani mapema lakini alibaki amekaa akiwa na lengo la kuhakikisha anamfahamu Rashid Kagu siku hiyo.

    Baada ya masaa matatu mtihani huo uliisha na watu walianza kutoka taratibu kutoka katika chumba hicho baada ya kukusanya mitihani yao. Veronika alitulia kidogo kwani alitambua kuwa Rashid alikuwa akimfahamu tofauti na ilivyokuwa kwake kwani hakumfahamu. Alitulia kwa sekunde kadhaa na alianza kuangalia huku na huko katika chumba hicho cha mtihani ili kujaribu kumwona mtu ambaye angemfuata. Marafiki zake wa kike walipita na kumsalimia sehemu aliyokaa lakini shauku yake ilikuwa kwa Rashid. Hatimaye alianza kukata tamaa ya kukutana na kijana huyo kwani darasa hilo lilibakiwa na wanafunzi watatu tu, wawili walikuwa wakiweka sawa vifaa vyao tayari kwa kuondoka na mmoja alikuwa ameinama katika meza aliyokuwa amekaa huku akionekana kama alikuwa akichora kitu kwani kulikuwa na rangi kadhaa katika meza yake.

    Baada sekunde kadhaa wanafunzi hao wawili walitoka na alibaki mmoja ambaye alibaki ameinamia meza yake akiendelea kuchora. Veronika alivuta pumzi ndefu na kuanza kusukuma meza yake akiwa na lengo la kuondoka huku akiwa amekosa amani kabisa.

    “ hey! Vero, unaenda wapi wewe? Aah! Halafu ulishaniahidi kunitafuta leo vipi?” alisikika kijana aliyekuwa ameinamia meza yake awali, wakati huo alikuwa akitembea taratibu kujongea eneo alilokuwa Veronika ambaye alianza kuondoka katika chumba hicho cha mtihani. Mshtuko ndiyo uliompata Veronika kwani aligeuka na kumshuhudia kijana nadhifu kimavazi na mwonekano wa sura yake ulitimiza ukweli wa utanashati wa kijana huyo aliyetambua alikuwa ni Rashid. Alimkimbilia kijana huyo na wote walikumbatiana kwa furaha. Walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu kwa muda mrefu na wakati huo walikutana rasmi.

    Rashid naye akiwa ameelekeza macho yake katika paji la uso wa Veronika aligundua mambo mengi zaidi kwani msichana huyo alikuwa ni mzuri tofauti na vile alivyokuwa akimdhania. Alikuwa mweupe na mwembamba akiwa mrefu kama yeye na zaidi alibainisha moyoni mwake kuwa msichana huyo alikuwa mrembo haswa. “ nina zawadi yako Vero……” alisikika Rashid huku akimkabidhi msichana huyo bahasha kubwa ya kaki iliyoonekana ilikuwa na kitu. “ahsante Rashid… nashukuru…..” aliipokea na kuiweka pembeni yake kidogo katika eneo lililokuwa na vifaa vyake vya shule. Walitazamana tena kabla ya kukumbatiana kwa nguvu, walibaki wametulia kwa namna hiyo kwa muda mrefu na kila mmoja aliamini walikuwa zaidi ya marafiki na hisia za upendo zilipenya katika miili yao iliyosisimuka na mioyo iliyo iliyoonekana kusuuzika majeraha ya upweke waliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

    Kwa jinsi walivyokuwa kila mtu akili yake haikuwa sawa na walibaki wamekumbatiana kwa sekunde kadhaa. Hawakugundua hata sauti ya makanyagio ya viatu vya bwana Lamos Maputo ambaye aliingia katika chumba hicho na kuonekana akiwashangaa huku akiwa na hasira kupindukia, jasho lilikuwa likimtoka kupindukia. Alivuta pumzi ndefu kabla ya kujiweka sawa, alikuwa tayari kwa kufanya jambo hatari. Alijongea kwa kasi eneo hilo walilokuwawapo kabla ya kumpiga na ngumi Rashid kwa nguvu. Karaha hiyo iliwapeka chini Rashid na Veronika, kabla hawajasimama Lamos alimvamia tena kijana huyo na kuanza kumpiga mateke mfululizo. “sorry dad, usimpige nitakwambia kila kitu dad usimpige…”alisikika Veronika akilia kwa uchungu lakini baba yake hakusikia maelezo hayo





    “sorry dad, usimpige nitakwambia kila kitu dad usimpige…”alisikika Veronika akilia kwa uchungu lakini baba yake hakusikia maelezo hayo. Baada ya dakika moja ya kumpiga, Lamos alitulia kidogo na wakati huo Rashid alikuwa akitokwa na damu usoni ambayo ilitapakaa eneo alikuwa amelala. Lamos akiwa na hasira aligeuka na kumpiga kofi mwanaye ambaye naye alianguka chini. Alisimama kwa taabu huku akiwa analia, aliishika bahasha aliiyopewa na Rashid pamoja na vifaa vyake alivyokuwa akifanyia mtihani. Alibaki ametulia huku akimwangalia kwa huruma Rashid aliyekuwa mtulivu wakati huo. “ kijana usijaribu kumfuatilia tena mwanangu, vinginevyo…….” Alisikika Lamos akiongea kwa jazba kabla ya kuvuta pumzi ndefu ”….. nita nita nitakupoteza usimfuate mwanangu kabisa kijana..”. Alimshika mkono Veronika na kuanza kumvuta kwa nguvu wakiondoka eneo hilo la darasani hapo. Veronika akiwa ameshika bahasha aliyopewa na Rashid pamoja na vifaa vyake alivyokuwa akifanyia mtihani alianza kutembea huku akimwanagalia Rashid aliyebaki eneo la darasani hapo huku akiwa amezungukwa na kiasi kikubwa cha damu.

    Lamos Maputo alimvuta mwanaye huyo mpaka katika gari lake aina ya Mercedez Benz ambalo mara baada ya kumpakia mwanaye alipanda kwenye gari hilo pia na kuliondoa kwa kasi katika eneo hilo la shule. Alikuwa na hasira juu ya kila jambo alilokuwa amelishuhudia ambalo hakuwahi kulifikiria kama lingeweza kutokea kwa mwanaye hata siku moja. Alikuwa na hasira juu ya kijana aliyemwona na mwanaye kupindukia. Wakati huo aliwaza kutafuta mbinu ya kuhakiksha Veronika hakai karibu na wavulana tena wala kuwasiliana nao. Jambo la kwanza alilolifanya mara baada ya kufika nyumbani kwake alimnyang`anya mwanaye huyo simu, alichukua pia komputa ya mwanaye huyo iliyounganishwa mtandao pamoja na televisheni iliyokuwa chumbani kwake. Veronika alilia kwa uchungu juu ya tukio hilo na aliamini mwisho wa mawasiliano kati yake na Rashid, kijana aliyempenda ulikuwa umefika. Alikuwa amezoea kumpigia simu na mara kadhaa na walikuwa wakiwasiliana kupitia mtandao akitumia kompyuta aliyokuwa nayo chumbani kwake. Hata tamthilia kadhaa alizozoea kuzitazama aliamini mwisho wake ulikuwa umefika.

    Akiwa na hasira hakutaka kula kabisa siku hiyo zaidi alijifungia chumbani kwake akilia. Baba yake hakujali juu ya jambo hilo, alionekana kuwa na jazba juu ya tabia ya mwanaye. Majira ya saa sita usiku akiwa na hofu juu ya afya ya Rashid, aliikumbuka zawadi aliyopewa na kijana huyo. Aliifuata bahasha kubwa ya kaki aliyopewa kabla ya kuifungua akiwa na shauku ya kuona kitu kilichokuwapo ndani. Alishtuka mara baada ya kufungua bahasha hiyo na machozi ya furaha ndiyo yaliyoanza kumtoka huku akiwa haamini macho yake juu ya zawadi aliyoiona. Zilikuwa picha zake zilizokuwa zimechorwa kwa mkono kama vile zilipigwa kwa kamera, picha moja ya kawaida ilikuwa ya Rashid Kagu aliyeonekana akiwa nadhifu. Ni wakati ambao Veronika alikumbuka awali alipomwona Rashid akiwa ameinamia meza na kuonekana akichora kitu. Picha moja ilionekana ilichorwa siku hiyo hiyo wakati ambao Veronika alikuwa akiendelea na mtihani. Picha nyingine tano zilichorwa katika kipindi cha nyuma wakati Veronika akiwa shuleni hapo kufanya mtihani, picha moja wapo ilimwonyesha akishuka kwenye gari ilhali baba yake akiwa pembeni. Picha nyingine ilimwonesha akikumbatiana na baba yake mara baada ya kufanya mtihani wake.

    Picha hizo zilimfanya atambue kipaji cha hali ya juu alichokuwa nacho Rashid Kagu lakini pia alijikuta akigundua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kijana huyo kwa muda mrefu. Picha ya Rashid Kagu ndiyo aliyoiangalia kwa muda mrefu na hakuichoka hata kidogo. Alizificha picha hizo chini ya godoro la kitanda chake na alitulia kidogo akioneakana kuwa na faraja. Baada ya dakika kadhaa alianza kulia tena, hofu juu ya afya ya Rashid iliongezeka na hakutambua jambo lolote lililokuwa likiendelea. Siku iliyofuata kama ilivyokuwa kawaida baba yake alimgongea akiashiria aamke na kujiandaa kwa ajili ya kwenda shule ili kuendelea na mitihani. Veronika alitii wito juu ya jambo hilo, aliamka na kuanza kujiandaa. Wakati huo alikuwa na shauku ya kuhitaji kujua kama Rashid angeenda shuleni. Mara baada ya kujiandaa aliondoka na baba yake nyumbani hapo na kuelekea shuleni huko aliendelea na mtihani kama kawaida lakini aliingiwa na hofu zaidi moyoni mwake. Rashid Kagu hakuwa mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakifanya mtihani siku hiyo. Alijitahidi kuangaza macho huku na huko kumwangalia lakini hakufanikiwa kumwona. Hakuelewa jambo lolote lililokuwa likiendelea kwa kijana huyo. Hatimaye alimaliza mtihani huo na kwenda kuungana na baba yake kabla ya kuondoka shuleni hapo.

    Hatimaye Veronika alimalizia mitahani yote pasipo kumwona tena Rashid. Baada ya mtihani huo, shule yao ilifunga na yeye alikuwa nyumbani kwao muda wote. Mara kadhaa rafiki zake wa kike walimtembelea nyumbani kwao lakini nao walionekana kuto tambua jambo lolote lililookuwa likiendelea dhidi ya Rashid Kagu. Hatimaye shule nayo ilifungua na yeye aliendelea na masomo yake nyumbani kwao kama baba yake alivyotaka. Alikuwa amepoteza matumaini dhidi kijana aliyekuwa akimpenda, Rashid na mara nyingi alikuwa akiitazama picha yake ambayo ilishaanza hata kuchakaa. Mara kadhaa alikuwa akilia huku akiwa ameikumbatia picha hiyo. Rafiki zake wa kike walipomtembelea nyumbani kwao wakati huo ambao shule ilikuwa imefungua walimpotezea matumaini kabisa. Walimweleza kuwa Rashid hakurudi tena shuleni na hawakuwa na taarifa zozote juu yake. Veronika aliendelea na mfumo wake wa shule huku akimkumbuka Rashid kila siku, kijana aliyekuwa chaguo la moyo wake.

    * * * *

    Baada ya miaka minne Veronika alikuwa amemaliza elimu ya sekondari huku akiwa amefauru vizuri mtihani wake wa kidato cha sita. Wakati huo alikuwa hataki kusoma tena nchini na alitaka kuondoka ili kupata uhuru wa mambo yake. Aliwaza hivyo kwa vile alikuwa amechoka kufuatiliwa na baba yake katika kila jambo alilokuwa akilifanya. Mpaka wakati huo hakubahatika kumwona Rashid, kijana aliyeuteka moyo wake. Jambo hilo lilimfanya awe akijifungia chumbani kwake na kulia kwa uchungu huku akiwa ameikumbatia picha ya Rashid ambayo kwa wakati huo ilikuwa imechakaa sana. Wakati huo alikuwa hamtamani mwanamume wa aina yeyote na muda wote alikuwa akiamini angekuja kukutana na Rashid ambaye alijitahidi kumtafuta lakini hakuweza kufanikiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Suala la Veronika kugoma kusoma chuo kikuu cha nchini lilimchanganya sana bwana Lamos Maputo ambaye moyoni hakuwa tayari kumwona mwanaye akiondoka nchini na kwenda kusoma nchi nyingine. Aliandaa mikakati kadhaa akiwa na lengo la kuona mwanaye akisoma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Aliamini mwanaye angesoma katika chuo hicho angeweza kumfuatilia na zaidi angeweza kusoma akitokea nyumbani kwake. Hatimaye majina ya watu waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu yalitoka na Veronika alikuwa amechaguliwa kujiunga na vyuo vitatu tofauti kikiwapo chuo kikuu cha Dar es salaam. Bwana Lamos aliona ndoto za mwanaye kusoma nchini zilianza kutimia, pasipo kumjulisha juu ya jambo lolote mwanaye alianza kumwandalia mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kujiunga chuo kikuu.

    Baada ya zoezi lake hilo lililochukua siku kadhaa alimwita mwanaye na kumweleza juu ya adma yake ya kuona akisoma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mambo yalikuwa tofauti kwani Veronika alikataa na aliona bora asiendelee na shule. Hakuwa tayari kusoma katika chuo kikuu cha nchini hata kidogo. Bwana Lamos alidhani mwanaye angebadili uamuzi huo lakini haikuwa hivyo. Hatimaye vyuo vilifunguliwa lakini Veronika hakuwa tayari kwenda kujiunga na wanafunzi wenzie wa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ulipita mwezi mmoja akiwa nyumbani kwao na mara nyingi alikuwa akijifungia chumbani kwake. Kwa muda wote huo hakujaribu kuongea na baba yake hata kidogo, alikuwa akimkimbia baba yake kwani hakutaka kuongea naye.

    Jambo hilo lilimuumiza sana kichwa bwana Lamos ambaye aliamua kukubaliana na uamuzi wa mwanaye aliyekuwa akitaka kwenda kusoma nje ya nchi. Hatua hiyo ilifuata baada ya kulifikiria sana jambo hilo. Wakati huo alikuwa amepata njia ambayo aliamini angeitumia ili kuendelea kumlinda mwanaye dhidi ya wanaume. Hakumweleza mwanaye juu ya uamuzi huo aliokuwa ameufikia, jambo alilofanya alitafuta chuo nchini Uingereza na alifanikiwa kupata nafasi ya mwanaye katika chuo cha Cambridge kilichopo katika mji wa Cambridge . Akiwatumia vijana wake kadhaa alifanikiwa kupata nafasi ya mwanaye katika chuo hicho chini ya shahada ya biashara na masoko ambayo alikuwa akiihitaji.

    Baada ya kukamilisha kila jambo alimweleza mwanaye juu ya hatua hiyo aliyokuwa ameichukua ya kumtafutia chuo nchini Uingereza. Veronika alifurahi juu ya taarifa hiyo na alijiona yuko huru baada ya kuishi kama mfungwa kwa kipindi kirefu cha masomo. Wakati akiwa na furaha juu ya hatua ambayo baba yake alikuwa ameichukua alikuwa haamini vizuri kama baba yake alikuwa amebadili uamuzi wake wa awali. Moyoni bado alikuwa akihisi uwezekano wa baba yake kuendelea kumfuatilia akiwa nchini Uingereza lakini hakujali juu ya jambo hilo. Tarehe saba mwezi Januari alikuwa kwenye ndege ya shirika la Ethiopia Airways akielekea nchini Uingereza. Alikuwa na furaha kupindukia kwani aliona mwanzo wa ndoto zake kukamilika ulikuwa umefika. Ndani ya ndege hiyo aliyokuwapo alikaa na mwanafunzi mwenzie mmoja ambaye alikuwa akielekea chuo kikuu cha Oxford. Furaha yake iliongezeka zaidi kwani hakusindikizwa na baba yake na alijihisi yuko huru kupindukia. Hakuwahi kupata nafasi ya kuwa huru kama ilivyokuwa siku hiyo. Muda wote alikuwa akifuatiliwa na baba yake kwa kila jambo alilokuwa akilifanya. Hata safari kadhaa za nje ya nchi alizowahi kusafiri alikuwa akiongozana na baba yake.

    Ndege hiyo aliyopanda ya shirika la Ethiopia Airways ilipita katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia, walikaa kwa saa kadhaa na safari iliendelea huku wakipita katika jiji la Algiers nchini Algeria. Majira ya saa tatu usiku walikuwa wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London. Mbali na uchovu aliokuwa nao, haukuifikia furaha yake ya kusoma nje ya Tanzania. Mara baada ya kushuka kwenye ndege hiyo alipokelewa na maofisa watatu wa chuo kikuu cha Cambridge na safari ilianza wakielekea katika hoteli waliyokuwa wamepangiwa. Katika msafara huo alikuwa na wanafunzi wenzie zaidi ya ishirini walikuwa wakitoka nchi nyingine tofauti ambao walifika nchini humo siku hiyo. Baada ya saa moja walifika katika hoteli waliyopangiwa na chuo iliyokuwa katika kitongoji cha Old Windsor jijini hapo. Walikabidhiwa vyumba kwa ajili ya kulala siku hiyo na walielezwa siku iliyofuata wangeanza safari kwa kutumia gari kuelekea katika mji wa Cambridge uliokuwapo kaskazini mwa jiji hilo.

    Baada ya siku tano tayari alikuwa amesajiliwa na chuo kikuu cha Cambridge huku akiwa amepangiwa kukaa katika hosteli za chuo hicho zilizopo katika kitongoji cha Harningsea kilichopo kilometa kadhaa kutoka chuoni hapo. Alikuwa akitumia usafiri wa treni za kasi kuhudhuria masomo yake katika chuo hicho kila siku. Veronika alikuwa na furaha kwa vile alijiona huru tofauti na alivyokuwa nchini Tanzanaia. Jambo lililomfurahisha zaidi ni marafiki wengi aliowapata kwa muda mfupi tofauti na matarajio yake. Rafiki zake wengi walikuwa wakimsifia kwa uzuri aliokuwa nao. Alikuwa akifurahi sana kwa vile wakati huo alijitambua alikuwa mzuri haswa. Tofauti na wakati akiwa nchini Tanzania watu wachache waliwahi kumsifia kuwa alikuwa mzuri. Uthibitisho wa jambo hilo ulienda sambamba na usumbufu alioanza kuupata kutoka kwa wanaume ambao walimhitaji awe na uhusiano nao. Siku zote alikataa ombi hilo lililothibitisha uzuri wake na aliwataka wanaume hao waishie kuwa marafiki.

    Veronika alikuwa akitamani kuingia katika mahusiano lakini alipokuwa akimkumbuka Rashid Kagu alishindwa kukubaliana na ombi hilo. Siku zote alikuwa akiamini angekuja kukutana na kijana huyo ambaye bado alikuwa moyoni mwake. Mara nyingi alikuwa akiziangalia picha alizochorwa na Rashid zaidi ya miaka minne iliyokuwa imepita. Wakati huo picha ya Rashid ilikuwa imechakaa kabisa kwani alikuwa akiiangalia kila siku kabla ya kulala kwake.

    Siku moja ya Ijumaa akiwa amemaliza vipindi vyake vya juma zima, majira ya saa tisa alasiri alionekana akitoka katika eneo la chuo hicho wakati huo alikuwa akielekea katika kituo cha treni ili asafiri kurudi katika hosteli za chuo za Harningsea ambako alikuwa akiishi. “hey Vero! Please wait for me…” ( Tafadhari Vero nisubiri……) sauti hiyo ilimshtua jambo lililomfanya ageuke haraka kabla ya kumshuhudia kijana mmoja mzungu ambaye alikuwa akikimbia kuelekea eneo alilokuwapo. Veronika alisimama na kumsubiria na baada ya sekunde kadhaa kijana huyo alifika eneo alilokuwa amesimama Veronika, “ Sorry, my name is Craig and I got this for you miss….. remember true love never dies, he can be your true lover…” ( samahani, jina langu ni Craig na nina huu mzigo wako….. kumbuka upendo wa kweli haufi, anaweza kuwa mpenzi wako wa kweli) alimaliza kijana huyo kuongea huku akiwa amemkabithi Veronika bahasha iliyokuwa ya rangi nyeupe na alianza kuondoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog