Simulizi : Binti Kipofu
Sehemu Ya Nne(4)
Vikram alizinduka kutoka kitandani na kumtafuta Tropina kwa kumuita wakati huo nao Vanessa na yeye alizinduka baada ya kumwagiwa maji na Diana.
"Madam nahofia usalama juu ya Tropina amechukua bastola na kuondoka baada ya kupokea simu yako.
" Tropina kaondoka aliuliza Vikram kwa mshangao na mshtuko.
Wakati huo nao yalionekana magari ya polisi yakiwa njiani kuelekea katika eneo la tukio.
Naye Tropina alikuwa mlangoni katika jumba lile aliloweza kuelekezwa na Alice.
Ndani alikuwa Larry na Alice.
Alice alidondosha bastola chini na kusema nimemaliza kazi.
"Hivi unafikiri utaondoka hapa ukiwa hai?? Aliuliza Larry na kuiokota bastola aliyoweza kuitupa Alice kisha kufyetua risasi.
" ooopppsss sorry nilisahau kumbe nilizitoa zilizobaki alizungumza Alice na kuendelea kupiga hatua za kuondoka pale.
Larry aliitupa ile bastola chini kisha akaanza kumfuata Alice aliyekuwa akimcheka.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Larry alitizama pembeni na aliweza kuona chuma kikiwa karibu naye alikufuata na kukishika hapo hapo aliingia tropina na kumwambia usiguse kwa mikono yako.
"Ooooopppsssa sorry umechelewa kidogo tu ungeweza kumzuia lakini tayari ameshakishika sasa tufanyaje? Aliuliza Alice akimtizama Tropina aliyeenda na kukichukua kile chuma kilichokuwa mikononi mwa Larry kisha kukipangusa kwa kitambaa chake.
" Umeshika kipi kingine?? Aliuliza Tropina.
"Na mbona unadamu aliuliza Tropina akimfuta futa Larry.
" Tropina amemuuwa Daniel alisema Larry na kunyooshea Mkono pale alipo Daniele aliweza kuchakazwa kwa risasi yeye pamoja na Mr Harlan.
Aligeuka na kuja kwa hasira paka pale alipo Alice kisha akampiga kibao.
Alimrudia Larry kisha akamwambia.
"Toka njee ya hapa.....alafu usahau kama ulishawahi kufika hapa mtu yoyote yule akikuuliza kuhusu mahali nilipo Mimi mwambie haufahamu.....na kingine mtunze Vanessa kwaajili yangu mimi, sawa haya nenda njee"
Lakini Tropina.
Alianza kubisha larry ila Tropina alimshika kisha akamwambia
"Siku zote katika maisha yako ujuwe ya kuwa dada yako kafanya hivi kwasababu anakupenda sana" alisema Tropina na kumpiga busu la paji la uso.
"Waoooo jamani mapenzi mazito kati ya Dada na mdogo wake....embu ngoja nione Leo Dada mtu atafanya nini kwaajili ya kumuokowa mdogo wake ambaye anakwenda kuwa muuwaji kwa jumla ya watu watatu" alizungumza Alice na kukaa.
Tropina alielekea mpaka pale zilipo zile maiti kisha akaanza kuzishika sehemu zilizokuwa zikutoa damu na kujipaka katika mavazi yake aliyoweza kuyavaa.
Larry alibaki akilia na kumtizama Dada yake.
"Toka hapa" alisema Tropina kwa kufoka na Larry alielekea katika njia ya mlango kisha Kuondoka zake hapo hapo aliingia Tobias.
"Madam!! Aliita kwa mshangao.
" kwanini nguo zako zinadamu?? Aliuliza Tobias.
Mfuate Larry mchukue kisha muondoke bila kutumia gari fanya haraka
Alisema Tropina.
"Vipi kuhusu wewe sasa??? Aliuliza Tobias.
" fanya vile nilivyoweza kukwambia"
"Sawa" alisema Tobias na kumuachia ufunguo wa gari kwa kuutupa chini kisha kuelekea kule Larry alipoweza kuelekea.
"Hiyo bastola hiyo mdogo wako ameishika.... Alizungumza Alice akimtizama Tropina aliyekuwa akimtizama kwa hasira sana.
" kama Huniamini sawa usiiguse" Alisema Alice.
Tropina alisogelea na kuiokota kisha akaanza kuipangusa kwa kitambaa kingine baada ya hapo aliigusa na kuitupa mbali na zilipokuwa zile maiti katika upande mwingine.
Kisha akaitoa bastola yake.
"Hiyo ya kwani ninauhakika kwamba Haina risasi ila yakwangu miye inayo na najua utakuwa umeshapiga simu polisi na kuwataarifu nimewauwa watu wawili ili kuonyesha ya kuwa nimewauwa hao nataka nikuuwe na wewe ili nikiipata adhabu iwe ya haki" alizungumza Tropina na kuikoki bastola.
Hapo hapo vilisikika ving.ora vya polisi Alice alimkimbilia Tropina na kuishika bastola aliyoweza kuishika na kujifyetulia risasi ya bega baada ya hapo alianza kujigongeza katika zile kuta za nyumba ile huku akipiga kelele.
"Tropina usiniuuwe.......Tafadhali saidia maisha yangu alizungumza na kuendelea kujigongeza zaidi.
Tropina alimfuata na kumshika kichwa kwa kumzuia na wakati huo huo polisi waliingia na alivyokuwa akionekana Tropina aliweza kuonekana ya kuwa alimshika ili ambamize zaidi na zaidi.
Alice baada ya kuona polisi wamefika alijiangusha chini na kujifanya amezimia.
" anamuectia nani huyu mbwaa" alizungumza Tropina na kutupa bastola Yale chini kisha kumtazama alice aliyekuwa chini ya sakafu.
Hapo hapo aliingia Vikram na Vanessa na baada ya kumuona Tropina amechafuka damu waliamini ya kuwa Tropina ndiye aliyeweza kuuwa. Vanessa miguu yake ilimuishia nguvu na kudondoka chini.
Alice alibebwa na machela pamoja na maiti ya Danielle ikiongozana na maiti ya Mr Harlan mpambe wa Mr Harlan aliweza kuona tukio hilo alipiga simu na kutoa taarifa.
"Mr Harman, baba yako ameweza kuuwawa na mwanamke" alizungumza mfanyakazi wa Mr Harlan.
Baada ya Tropina kufikishwa kituo cha polisi hakukuwa na mjadala tena hata dhamana haikuruhusiwa juu yake kwani tayari alishakuwa na kesi zaidi ya moja.
Aliingia Gorge katika chumba cha mahojiano na alimkuta Tropina akiwa amekaa kw utulivu sana.
Alimtizama bila kusema neno lolote na hatimaye alikaa katika kiti kilichokuwa mbele ya Tropina.
"Pinah nakujua tangu ulivyokuwa mdogo japo kuwa watu wengi wanaamini ya kuwa wewe ni mkorofi lakini natambua huwezi kuuwa mtu kwani hata mende ulikuwa unaogopa kumuuwa niambie nani kauwa??
Tropina alicheka kisha akasema.
" Miaka mingi imepita sana na Kuna mambo mengi yametokea juu yangu yanayonifanya nibadilike" alizungumza Tropina.
"Sawa najua hutaki kuzungumza ukweli ila Mimi nitaipambania haki yako niamini kwahilo" alisema George na kuinuka hapo hapo aliweza kuingia Vikram.
"Pinah" aliita na kwenda kumkumbatia Tropina ambaye baada ya kumuona Vicky alianza kulia.
"Usijali kila kitu kitakwisha usijali nitakutoa hapa siwezi kukuacha uteketee huku hiyo ilikuwa ahadi ya Vikram juu ya Tropina.
" Tunahitaji tumuhamishe mtuhumiwa" alizungumza Tobias na kuwapa ishara ma afande wenzake wawili waende kumchukua Tropina.
"Lakini kwnini sasa? Na mnampeleka wapi?? Aliuliza Vikram.
" Yeye anahusika na mauji ya zaidi ya watu wawili hivyo hatuwezi kumuacha hapa kwani ameshakuwa muuwaji hatari"
"Vicky me sitaki kwenda" alizungumza Tropina na kuelekea nyuma ya Vicky.
"Lakini....... "
"Haina cha lakini tena hiyo Tafadhali madam Tropina hapana namaanisha mtuhumiwa Tropina ongozana nasi. Alizungumza Tobias na kuamua kumfuata Tropina mwenyewe aliyekuwa amekaa nyuma ya Vicky na kuanza kumvuta.
" Huoni ya kuwa umemfunga pingu na unamvuta zinamuumiza alizungumza Vicky kwa sauti ya ukali na hasira iliyowafanya wote washtuke.
Kisha akamgeukia Tropina.
"Pinah" aliita Vikram kwa sauti ya upole.
"Sitaki Mimi sitaki kwenda mahali.....sijauwa Mimi Vicky" alizungumza na machozi yakimtoka.
"Najua ujauwa wal huwezi kuuuwa niamini Mimi kama nitashindwa kukutoa kwa kutumia sheria basi nitakutoa kwa njia nyingine nakuahidi hilo"
Tropina alitikisa kichwa kwa ishara ya sawa na Vikram alimbusu mdomoni huku machozi yakimtoka.
"Hivi hamuwezi kufungua hizi pingu?? Aliuliza Vikram.
" hatutaweza yeye anahukumiwa kwa kesi ya mauaji ya wtu zaidi ya watatu na kesho atasomewa mashtaka hayo mbele ya mahakama kwahiyo Tafadhali tunamuomba mtuhumiwa wetu" alizungumza George aliyeweza kufika eneo lile.
"Vicky" alibaki akiita tu Tropina na machozi yakimtoka.
"Usijali nimeahidi nitakutoa na nitafanya hivyo" alizungumza Vikram na kutoka njee ya chumba kile Tropina ndiye aliyebaki akipiga kelele na kuita Vikram.
"Sitaki kubaki huku Mimi.... Vicky please usiniache"
***** ****** *****
Vanesa alielekea moja kwa moja hadi kwenye chumba cha Alice aliyekuwa amelazwa huku akicheka baada ya kuona ya kuwa game lake limeenda vizuri aliacha kutabasamu baada ya uso wake kukutana na uso wa Vanessa aliyekuwa amevimba kwa hasira.
"Mshenzi mkubwa wewe unawezaje kuja katika maisha ya wanangu na kuwaharibia furaha yao walioweza kuipata ndani ya muda mchache.... Aliuliza vanesa huku akimnyonga Alice shingoni.
Alitizama pembeni na aliona kabati dogo ambalo lilikuwa la kuwekea vitu kwaajili ya wagonjwa.
Alienda na kuliinua wakati huo nao Alice alishainuka kitandani huku akikohoa kwa kuishika shingo yake.
" Nikikuuwa wewe utaacha kumcontrol Vikram kwa kile ulichoweza kumuwekea Larry katika mwili wake na Vikram ataweza kumuokoa Tropina polisi " alizungumza Vanessa akiwa amelinyanyua kabati lile dogo na kuanza kumfuata Alice aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuona ya kuwa anazidiwa na Vanessa.
Vanesa alilirusha lakini Alice aliweza kulikwepa ila lilimpata kidogo katika Mkono wake ambao aliweza kujipiga risasi na kumfanya alie kwa uchungu na damu nyingi zikitoka.
Hapo hapo waliingia manesi ambao walianza kugonga mlango ili ufunguliwe na waweze kuingia ndani.
"Unalia kwa maumivu hayo madogo sana wakati sisi umetusababishia maumivu makubwa hivyo unawezaje kuja na kuharibu familia yangu kwa kiasi hicho unawezaje?? Aliuliza Vanessa na kuona kisu kikiwa chini yake alikiokota na kuanza kumfuata Alice kwaajili ya kumuuwa ila hapo hapo mlango uliweza kufunguliwa kwa funguo nyingine za ziada na waliingia manesi pmoja na walinzi walioweza kumshika Vanessa na kumnyang.anya kisu kile.
Alice ndiye aliyeweza kubaki akilia kwa maumivu huku akisema.
" huyu ni kichaaa huyu mpelekeni polisi atatakaje kuniuwa Mimi?? Aliuliza Alice aliyekuwa akizitizama damu zilizokuwa zikimtoka katika Mkono wake.
***** ****** ****
Nyumbani alikuwa Larry aliyekuwa akizunguka katika chumba chake hpo hapo mlango wake uliweza kufunguliwa na macho yake yote yaliweza kuelekea mlangoni na kutizama ni nani huyo anakuja katika chumba chake aliingia Vikram.
"Bwashe aliita Larry na kwenda kumkumbatia huku akilia machozi.
" Mama na Dada wote wamekamatwa namaanisha Vanessa wangu pamoja na Tropina wote wamekamatwa" alirudi Larry akiwa analia sana hakuwa mtu mkubwa ambaye angeweza kukabiliana na changamoto moto hizo alikuwa mtoto tena mtoto sana mwenye umri wa miaka 10 tu.
"Larry mama hatolala kituoni nitaenda kumtoa sasa" alizungumza Vikram.
"Na Dada je???
" Tropina hawezi kutoka kwa urahisi hivyo na nikishindwa kumtoa kwa kutumia sheria basi nitaivunja sheria"
"Lakini Dada yangu hakuuwa ni yule mwanamke yule mwanamke wa Adrian yule mfanyakazi wake yeye ndiye aliyesababisha yote hata yeye alinifanya Mimi.........." Larry hakumalizia kuzungumza kwikwi zilimkaba na machozi yakaanza kumtoka.
"Natambua yote kwanza kunakitu kipo katika mwili wako nahitaji kukiondoa ili niweze kuwasaidia wote hao wawili nahitaji kukiondoa kitu hicho katika mwili wako, Dr Kim aliita Vikram na aliingia Dr Kim ndani.
" Larry chochote kile utakachoambiwa kufanya na Dr Kim hakikisha unafanya hii ni kwaajili ya kusaidia maisha yako na mama pamoja na Dada sawa "
.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Larry alitikisa kichwa na kusema hata akisema nivue nguo mbele zake nitavua"
Vikram alitabasamu baada ya kuyasikia maneno hayo na akamgonga Larry kwenye kichwa.
"Kuwa na adabu wewe hujui ya kuwa akikuona wewe ni sawasawa na ameniona Mimi.....fanya kila kitu isipokuwa kuvua hiyo suruali" alizungumza Vikram na kucheka na hata pia Larry alicheka.
Vikram alitoka njee na kicheko cha Larry kiliishia kuwa machozi Dr Kim alimtizama na yeye pia machozi yaliweza kumtoka.
"Chochote kile kitakachoweza kutokea hakikisheni Larry hatoki njee ya chumba chake ili asiendee kusababisha matatizo zaidi. Alizungumza Vikram kwa kumpa taarifa Patrick pmoja na wafanyakazi wengine.
" haloo Jimmy umeshampata wakili wa Tatu........Sawa hakikisha unapata mawakili ambao wataweza kusaidia kesi hii na kama ikishindikana nimeshakwambia pia tafuta vijana wa kumtorosha Tropina kwahiyo fanya vyote kwa wakati mmoja .
Alikata simu na kumpigia simu mtu mwingine.
"Please I need ur help (Tafadhali nahitaji msaada wako) baada ya kuzungumza maneno hayo alikata simu.
****** ***** *****
Asubuhi asubuhi na mapema ya siku hiyo ilionekana ndege kuwasili iliyoweza kutoka nchi za njee na alishuka msichana mmoja aliyeweza kunyoosha shingo yake.
"Waoooo so this is Tanzania (waooo kumbe hii ndo Tanzania" alivaa miwani yake kisha akateremka mpka chini na kutoka njee kabisa ya uwanja wa ndege.
"Welcome sisters Mary" (karibu sister marry ) alikuwa ni Jimmy aliyeweza kumkaribisha Sister Mary.
"Thanks you (nashukuru)
" This way please, ( Njia hii Tafadhali) alizungumza Jimmy na kuonyesha njia.
Ilikuwa asubuhi ya saa nne na Vanessa akiwa katika kikao cha board member wa kampuni ya Precious mineral limited Company.
"Tayari tumeshagundua ya kuwa wewe na mwanao nyote nini ni wauwaji hatutaki kuongozwa tena na wauwaji tunaomba ujihudhuri katika nafasi hiyo uliyonayo na hatutaki Tropina tena aendelee kuwa wakili wa kampuni hii kwani ni muuwaji na kwa kilichoweza kutokea hatuna imani tena na ninyi alizungumza Mr mpalila.
" Ni sawa Kuna kingine mnachoweza kukihitaji?? Aliuliza Vanessa akiwa mpole kabisa.
"Mtoto wako alitaka kutukata katika hisa zetu million3 kwaajili ya kusema ya kuwa ni usumbufu sasa na sisi tunahitaji million3 kwaajili ya kupunguziwa usumbufu alizungumza na wengine walitikisa kichwa ishara ya ni kweli
Mzee mmoja aliwatizama kisha akatikisa kichwa na kumuangalia Vanessa aliyekuwa hana maneno mengi bali alionekana kuwa mwingi wa mawazo.
" kama nyie mnazihitahi hizo million3 Tatu zichukuweni nyie ila Mimi sipo tayari kufanya hivyo" alizungumza mzee yul na kutoka njee.
"Secretary uza hisa 8 kati ya zile 68 kisha uwapatie pesa wanayoitaka" alizungumza Vanessa na kuondoka zake.
Mr mpalila alicheka akiamini ya kuwa sasa uongozi anauchukua yeye hivyo anahitajika kununua hisa hizo8 zitakazo uzwa hivyo atakuwa na share nyingi kuwazidi wengine.
Vanessa alifika katika kampuni ya Magari na kesi yote sasa ilimuangukia Tropina huku Adrian akiwa mstari wa mbele kabisa kutaka alipwe pesa kwa kuweza kukatwa hisa zake kwa kosa ambalo siyo lake.
Vanessa alicheka baada ya kuona Adrian anataka kulipwa fidia.
"Kwahiyo Unataka kusema ya kuwa Tropina ndo anahusika na kuingizwa kwa magari ambayo hayana viwango?? Aliuliza Vanessa.
" Ndiyo kama aliweza kuuwa watu watatu atashindwaje kufanya hivyo ili azichukue tu hisa zangu?? Alizungumza Adrian.
"Sawa....secretary kwenye hisa 57 mpe hisa zake 5 ambazo uliweza kuuza alafu Kuna kingine?? Aliuliza Vanessa
" Nahitaji kulipwa fidia ya million40 kama kosa la kuitwa Mimi msaliti ilihali ni binti yako au nikafungue kesi nyingine mahakamani kumuhusu" alisema Adrian.
"Sawa, secretary toa hisa zote na mlipe yoyote atakaye ziuze tu" alisema Vanessa na kuondoka zake.
**** ***** *****
Muda wa mahakamani ulifika na Tropina alikuwa ameshikwa na maaskari wawili waliokuwa wakimpeleka mahakamani huku pingu zikiwa mikononi mwake.
Alipelekwa hadi mbele kabisa na hapo aliweza kumuona mama yake Larry pamoja na Vikram walioweza kumtabasamia.
Tropina alitabasamu na kutaka kuwafuata lakini alizuiliwa na Tobias George alimpa ishara ya amuachie na alifanya hivyo Tropina alienda na kumkumbatia mama yake Vanessa aliyekuwa akilia kisha akamkumbatia mdogo wake na Vikram wake.
Vanessa alimshika Tropina mikono huku akijizuia machoz yasimtoke.
"Pinah nitauza kila kitu mpenzi wangu kila kitu tulichoweza kuwa nacho kwaajili ya kukufanya wewe usiwe hapa tena" alizungumza na kumtazama mikono ambayo tayari ilishakuwa na alama ya pingu na damu zikiwa zinamtoka.
"Mama niko salama Mimi usijali kuhusu Mimi Vikram atanitoa" alizungumza na kumtazama Vikram.
"Dada aliiita Vikram.
Tropina alitabasamu na kutaka kuinama kwaajili ya kumshika mdogo wake ila aliambiwa muda umeisha alihitajika sasa akasimame kizimbani kwaajili ya kusomewa mashtaka.
Tropina aligeuka nyuma na kuondoka huku akiacha majonzi makubwa mbele ya familia yake.
"Mimi ni wakili wa familia kwahiyo lazima niitete kesi yake" alizungumza Josephat
"Tayari nimeshaandaa wanasheia wengine kwaajili ya kuweza kumsaidia Tropina na wewe ni wa familia lakini siyo mwanasheria wa Tropina" alizungumza Vikram.
"Vicky tumuache tu namuamini sana Josephat atatusaidia katika hili"
"Lakini mama aliita Vikram.
" Vikram tuingie mahakamani alisema Vanessa na kumshika Vikram Mkono kisha kuenda naye ndani.
Josephat alimtizama Adrian na kutabasamu kisha akaelekea ndani ya mahakama .
Baada ya kufika Tropina aliweza kusomewa shtaka kwa kosa la kumuuwa Winnie lakini ilitajwa siku nyingine kwaajili ya kusomewa mashtaka yake yote siku ya mahakamani hapo kisha hakimu akatoa amri ya watu waondoke mpaka siku ya kesho ambayo angeweza kusomewa mashtaka yake yote.
***** ***** *****
Ilfila siku nyingine na Tropina aliweza kupelekwa tena mahakamani Alifikishwa na mashtaka yote yaliweza kusomwa kwa kosa la mauaji.
"Mshtakiwa Tropina livingstone unashtakiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kosa la kufanya mauaji ya watu watatu.
1. Winnie Bariki mwenye umri wa miaka 23
2.Harlan Singh mwenye umri wa miaka 49 huyu ni mwenyeji kutoka India na ndiye aliyeweza kununua uraia wa Tanzania
Na watatu ni
" Rickson Miller mwenye umri wa miaka 24...
"Rickson aliuliza kwa mshangao Tropina na kumtazama Rickson ambaye na yeye aliweza kusimama akiw na Vanessa pamoja Larry.
Hakimu alimtizama Tropina na kuendelea.
" Rickson Miller mwenye umri wa miaka 24 huyu wote tunamfahamu kutokana na matendo mengi ya kigaidi aliyoweza kuyafanya hivyo uliweza kumficha gaidi na hivyo kesi zote zinazomuhusu Rickson zitakuwa juu yako" alisema hakimu na kugonga mezani.
Tropina ndiye aliyebaki akiwa haamini baada ya kusikia shtaka la Tatu na la mwisho.
Vikram alisimama na kutoka njee ya mahakama.
"Dr Kim ulishakipata kile kitu katika mwili wa Larry"
"Hapana bado sijapata kukiona nimetafuta mwili mzima na bado sijapata kukiona nashindwa kujua kiko wapi labda tujaribu kufanya tena jaribio kwa Mara nyingine. Alijibu Dr Kim.
" sasa sihitaji kumpoteza Larry kwaajili ya Tropina wala sihitaji kumpoteza Tropina kwaajili ya Larry " alizungumza Vikram baada ya kukata simu.
"Huyu ni Alice tu huyu ni Alice"
"Jimmy uko wapi?? Alipiga simu tena kwa Mara nyingine.
" Dr Kim ameshindwa kufahamu wapo kpo hicho chombo katika mwili wa Larry hivyo nahitaji upate remote control ili niweze kuwasaidia wote kwa pamoja" alizungumza Vikram aliyekuwa amechanganyikiwa.
***** **** *******
"Bwashe mbona Danielle amekuja kuwa Rickson namaanisha amekuja kuwa wewe, alafu hakimu amesema wewe ni gaidi wa kimataifa sijui umeuwa...unajua..."
"Larry ingia ndani ya gari nataka kuzungumza na Vikram"
Alizungumza Vanessa akimpatia Larry pochi yake aweze kuingia nayo ndani.
"Madam Vanessa imekuwaje Daniele akaja kuwa sijui Rick nini imekuwaje hiyo?? Aliuliza Patrick.
" ingia ndani ya gari kwanza" alisema Vanessa na Patrick alitikisa kichwa ishara ya sawa na kuelekea ndani ya gari.
"Imekuwaje hii mbona siwaelewi imekuwaje Danielle akawa wewe, alafu wanaposema wewe gaidi wanamaanisha nini aliuliza Vanessa.
" Mama ni story ndefu sana na pia kwasasa sina muda wa kuelezea zaidi nahitaji kufanya kitu juu ya Tropina.
Alizungumza Vikram na kupanda ndani ya gari lake kisha akaondoka zake.
**** ***** *****
Ilikuwa ni siku ya kununua hisa zilizokuwa zikiuzwa katika kampuni zote mbili kampuni ya Magari pamoja na kampuni ya madini
Kiwango cha pesa kilitajwa kwaajili ya kuuzwa hisa hizo na katika mkutano huo aliingia sisters Mary na kukaa katikati yao kisha akawapa salamu na kutazama mbele kinachoweza kuendelea.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ni nani huyo aliuliza Mr mpalila akimuuliza Adrian ambaye na yeye alionekana kutomtambua.
Baada ya dakika 10 alionekana Mary akiwa njee ya jengo lile la kampuni ya kina Tropina akipokea salamu kutoka kwa washirika wengine.
Adrian na yeye alisogea zaidi akiwa na Mr mpalila na kumtazama sisters Mary ambaye alionekana mkarimu sana.
"Hello if am not mistaken ur Adrian?? ( habari kama sijakosea utakuwa Adrian? Aliuliza sister Mary na kuachia bonge la Tabasamu.
****** ***** ****
" Ni nini hiki kinataka kutokea tena katika maisha yangu matumaini yangu yote yameweza kupotea kabisa alikuwa akizungumza Tropina huku akitizama kucha zake ghafla walikuja mabinti watatu na kuanza kumpiga bila sababu yoyote ile.
****** ******
"Mkashindwaje kununua hisa zile na pesa niliwapatia ?? Aliuliza Alice .
"Kuna sister mmoja alikuja na huwezi kuamini amenunua hisa zote za makampuni yote Yale mawili na yeye ndiye amenunua hisa zote na hisa zake ndo nyingi kuliko za watu wote hivyo yeye ndiye atakayekuwa bossi wa makampuni yote Yale. Hapo hapo msg ziliweza kuingia katika simu zao.
" namba ya nani hii?? Walijikuta wameuliza wote kwa pmoja.
"Ninashida na wewe Tafadhali tuonane kesho saa9 mchana hotel ya palace view" msg zote ziliweza kusema hivyo.
Alice aliwatizama tu bila kusema neno lolote lile.
***** ***** ******
Bossi nimetafuta hadi naelekea kuwa kichaa sijaona chochote kile alizungumza Jimmy.
"Mungu wangu sina budi zaidi ya kujidhihirisha sasa kuwa Mimi ni Rickson ili Tropina akapate kuokoka"
"Unazungumzia nini wewe, hata ukijidhihirisha bado Tropina atafungwa tu kwasababu Kuna mauaji mengine ya Winnie Mr Harlan pamoja na Danielle, Rickson kumbuka unategemewa na watu zaidi 3000 Kuna kampuni ziko chini yako sisi pia tumejitolea maisha yetu kwaajili yko iweje wewe Leo utake kutoa maisha yako kwaajili ya mwanamke ambaye hata ukifanya hivyo haitasaidia" alizungumza Jimmy alitikisa mwili Vikram.
"Jimmy sina kitu cha kufanya zaidi ya hicho ili Alice aache kufanya vyote hivyo ni Mimi kuwa gerezani nikishakuwa gerezani basi atatulia na maisha yake Tropina Larry pamoja na Vanessa hawataweza kuteseka tena juu yangu"
"Lakini kwanini unakata tamaa mapema hivyo bado tunapambana Vikram na ukitaka msaada basi inabidi ukubali kupoteza kimoja kwaajili ya kukipata kimoja"
"Unamaanisha nin?? Aliuliza Vikram.
" kati ya Tropina na Larry lazima mmoja wao apoteee kama hutafanya hivyo basi unauwezo wa kuwapoteza wote kwa pamoja na wewe mwenyewe kama utajipeleka gerezani hutakuwa umesaidia bali umemsababishia matatizo Vanessa ya kuwaza tena kuhusu wewe" alizungumza Jimmy na hapo hapo Vanessa aliingia.
"Kuna nini tena hapa?? Aliuliza baada ya kuingia.
" madam Vanessa, Vikram anataka kwenda kujisalimisha kama............."
"Jimmy embu nenda njee" alisema Vikram na kumkaribisha Vanessa ndani.
"Kipi kinaendelea, nimetoka kuzungumza na mwanasheria josephat amesema nimlipe pesa nyingi kidogo kwaajili ya kumsaidia Tropina, Ndiyo nimetoka ku draw pesa bank alizungumza Vanessa na kuweka begi lake pembeni.
"Mama hilo begi lote ni pesa anazozihitaji huyo mwanasheria? Aliuliza Vikram kwa mshangao.
" ndyo, nimekuja tuzungumze kuhusu wewe Rickson kwnini umeuwa watu wengi hivyo?? Aliuliza Vanessa.
****** ***** *****
"Umefanya kazi nzuri sasa vizibitisho hivi hapa vyote kesho kutwa hakikisha vinafika mahakamani alizungumza Alice aliyeweza kumtizama Josephat pembeni yake na kucheka.
Mwanasheria yule alitoa kitu mfukoni mwake na ilikuwa ni cheni Larry aliyoweza kupatiwa na Danielle kabla ya kifo chake alimtizama Alice na kutabasamu baadaye kidogo aliweza kukutana na Adrian na hapo alimpatia cheni ile na Adrian alimpatia pesa zilizoweza kuwa kwenye begi.
"Siwezi kukuamini hivyo lazima niwe na silaha ya kujiami pindi utakapotaka kunisaliti basi niweze kujitetea" alizungumza akiishika cheni ile iliyokuwa bado iko ndani ya mfuko mweupe mwepesi.
Vanessa aliweza kupeleka pesa zote zile alizoweza kuagizwa na Josephat huku akiwa anapigwa picha bila yeye mwenyewe kufahamu
"Lakini kwanini umetaka tukutane kwenye eneo kama hili lenye giza kiasi hichi utafikiri tunafanya biashara haramu" alizungumza Vanessa huku akijaribu kulitazama eneo lile.
"Ha...ha...mna alijibu kwa wasiwasi Josephat na Vanessa alimsogelea zaidi.
" Iwe hivyo ila ikiwa tofauti na hivyo hutaaamini kile nitakachokifanya juu yako" alizungumza Vanessa na hapo hapo alitoka ndani ya gari Vikram na kumfungulia mlango huku akimtizama Josephat aliyekuwa akitetemeka.
"Mama sina imani juu yake ninamashaka sana juu ya mwanasheria huyo" alizungumza Vikram.
"Hata Mimi nahisi hivyo lakini hakuna cha kufanya tena kesho ni siku ya mahakamani hatuwezi kumbadilisha. Alizungumza Vanessa.
" Hivi nimeota ama nimeona si walisema Rickson amekufa na huyu huyu aliyetoka njee ni nani?? Alijiuliza Josephat huku akikumbuka ya kuwa Mara ya mwisho nyumba nzima na Mali za Vanessa zipo chini ya jina la Rickson.
"Ni vizuri kama utakaa kimya na kama kipo unachokifahamu dunia haikijui basi ukae hivyo hivyo kimya ili usifupishe siku zako" aliongea Alice na kutabasamu huku akikabithiwa camera ya picha zilizoweza kupigwa.
Alimlipa pesa mpiga picha yule kisha akaondoka zake.
****** ***** *****
Ulikuwa usiku na Larry akijiandaa kulala ghafla alianza kusikia maumivu ya kichwa na kujikuta anajigonga gonga katika kuta za nyumba yao huku akipiga kelele na kumfanya Diana atoke chumbani kwake kisha kwenda moja kwa moja hadi kwa Larry.
"Nini shida?? Aliuliza Diana na kuanza kumshika Larry mikono yake kisha kumvutia sehemu ya uwazi hivyo ilikuwa vigumu yeye kujipigiza kichwa baada ya kusikika kelele watu wote waliweza kukimbilia katika chumba cha Larry.
Kelele zile pia Vanessa aliweza kuzisikia baada ya kufikishwa nyumbani na Vikram.
" mbona huyo ni Larry?? Aliuliza Vanessa na kuanza kukimbia kuelekea ndani huku Vikram akimfuata nyuma.
"Ni nini huyu?? Aliuliza Vanessa na kuanza kumshika Larry aliyeweza kuponyoka tena na kuanza kuelekea ukutani alishikwa tena kwa Mara nyingine na Vikram kwa Mkono mmoja.
Vikram alitoa simu yake na kumpigia Alice
" nimekwambia acha unachokifanya" alizungumza kwa hasira sana Vikram.
"Nilikutumia msg ya kuwa nataka tuonane saa4 asubuhi ila mpkaa saa4 hii usiku ujajibu wala ujaja unajifanya unatafuta njia ya kuwaokoa aya muokowe huyo nikuone" alizungumza Alice na kugusa sehemu flan katika remote hali iliyomfanya Larry angue kilio kikubwa sana kilichowafanya wote washtuke.
"Alice nimekwambia achaaaaaaa.....nakuja sasa hivi niambie uko wapi?? Aliuliza Vikram.
" Sawa harakisha basi... Unajua nipo wapi kwahiyo njoo" alizungumza Alice na kuzima remote yake hapo hapo Larry alidondoka chini na kuzimia.
****** ***** ******
Vikram aliingia mpaka ndani kwenye nyumba ya Alice alipofika alimpiga Alice kibao na kutaka kuondoka.
"Ongeza hatua moja nyingine na uone kipi kitamtokea Larry" alizungumza Alice na Vikram alisimama pasina kupiga hatua yoyote ile.
"Hivi Unataka... ...... Nakuuliza unataka nini eti"
Alice alisema remote chini kisha akaanza kumfuata Vikram taratibu kabisa na kumwambia.
"Hivi inamaana ujui kweli nataka nini kutoka kwani Rickson, na kutaka wewe.......wewe ndyo nakutaka" alizungumza Alice kwa utaratibu masikioni mwa Vikram huku akimpapasa sehemu za kifua.
Vikram aliishika mikono ya Alice kwaajili ya kuitoa lakini mbele aliiona remote hivyo alijua njia pekee ya kumsaidia Larry na kuipata hiyo remote lakini asingeweza kwenda kwa mkupuo kwani Alice angeweza kumuwahi.
Alimgeukia Alice na kuanza kumpapasa nywele zake taratibu huku akimgeuza upande wenye remote na kuanza kumtembeza taratibu kabisa huku akimpulizia upepo sehemu za shingoni wakati mambo hayo yakitendeka picha zilikuwa zikipigwa pasina Vikram kutambua hilo.
Na alikuwa mpiga picha mwingine tofauti na yule wa mwanzo.
Vikram alitumia kila mbinu awezayo katika kumnogesha Alice katika mapenzi ili tu aweze kufika mahali remote control ilipo ili aweze kuichukua alipofika karibu na kwenye kochi ilipo remote alimsukuma Alice kwenye kochi lile kisha akamfuata taratibu huku akifungua vifungo vyake vya shati Alice aliamini ya kuwa Vikram yupo tayari kulala na yeye Vikram alimpandia kwa juu na taratibu kabisa na kuanza kuvuta remote control aliyokuwa ameikalia huku Alice akipitisha mikono yake katika mwili wa Vikram. Baada ya Vicky kuipata remote alitoka katika mwili wa Alice na kuitupa chini kisha akaikanyaga kanyaga huku akimtizama kwa hasira sana Alice.
"Kwa ulichoweza kukifanya juu ya Tropina sitakusamehe hata nikifa Leo mzimu wangu utakufuata tu, unawezaje ukamuuwa Danielle alafu useme yeye Ndiyo Mimi , unafikiri ya kuwa nitakana mahakamani kwamba Mimi siyo Rickson siwezi kufanya hivyo, Unataka Tropina anichukie Mimi na aone sina msaada juu yake sindiyo......sasa kwakuwa umeamua hivyo Mimi nitaenda na Tropina huko huko unakotaka kumpeleka" alizungumza Vikram.
"We....we...... unawezaje ukaenda na kusema wewe ni Rickson..... Vikram nimefanya hivyo kwasababu yako, yote niliyoweza kuyafanya ni kwasababu yako Vikram kukuweka wewe katika hali ya usalama"
"Usalama?? Usalama gani ulioweza kuniweka wewe!?? Unasababisha matatizo kila kukicha katika maisha yangu alafu bado unaniambia maswala ya usalama....... Najuta sana kukutana na mtu kama wewe katika maisha yangu, Tafadhali kama tutazaliwa tena kwa maisha ya pili baada ya haya katika dunia nyingine naomba tusikutane kabisa" alizungumza Vikram na kuondoka zake.
"Vikram wewe, Vikram njoo hapa.....Vikram" aliita kwa sauti ya kubwa lakini haikuweza kumfanya Vikram asite kwenda atakapo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sina njia nyingine ya kuitumia zaidi?? Nitafanyaje?? Mimba mimba!! alizungumza n kushika tumbo lake natakiwa niwe na mimba ili kumzuia Rickson asiende mahakamani Alice alikimbia ndani kabatini na kufungua droo yake nzima iliyokuwa na vipimo vya mimba. Alikichukua kimoja na kuelekea chooni kwaajili ya kulima kama anamimba au laa.
Alipopima majibu yalikuja hana mimba.
" Pumbavu" alizungumza na kurusha kile kipimio cha mimba kule.
" natakiwa niwe na mimba lakini sin mpaka sasa hivi nifanyaje sasa?? Alijiuliza Alice aliyekuwa kama kichaa kwani choo kizima kilijaa vipimo vya mimba.
***** ****** *****
Vikram alirudi nyumbani kwa kina Vannesa na ilikuwa ni usiku sana alielekea mpaka chumbani kwa Vanessa lakini hakukuwa na mtu hapo hapo alimuona Diana akitoka katika chumba cha Tropina.
"Mama yuko wapi?? Aliuliza Vikram.
Diana alishusha pumzi ndefu na kuonyeshea katika chumba cha Tropina.
Vikram alianza kupiga hatua na Diana alimsemesha
" Rickson, namaanisha Vikram hakuna msaada wowote ambao naweza kuwasaidia hata kama ni kutoa maisha yangu nataka kuwasaidia" alizungumza Diana.
"Usijali Diana kesho kila kitu kitaisha nakuahidi hivyo" alizungumza Vikram na kumshika Mkono.
Aliingia ndani katika chumba cha Tropina na kumtizama Vanessa alimfunika vizuri na shuka kisha akatoka na kufunga mlango.
Alielekea mpaka chumbani kwa Larry aliyekuwa amejipumzisha huku akiweweseka na kuita
"Dada.....dada.....bwashe anakuja kukusaidia usiachie hyo kamba" alikuwa akizungumza ndotoni na Vikram alimfuata kisha akamshika begani kwa kumtuliza na Larry alilala tena.
Vikram alimtizama kichwani na alikuwa ameumia kwa kiasi kikubwa sana alitoka njee kisha akarudi na boksi la huduma ya kwanza alitoa pamba na taratibu alianza msafisha huku akimpuliza kichwani ili asipate maumivu wakati huo machoz yalikuwa yakimtoka.
******* ****** *****
Ilikuwa ni siku ya mahakamani tena sema yalibakia masaa manane kabla ya watu kuelekea mahakamani huku vichwa vingi vya habari vya magazeti vya siku hiyo vikiwa vimejaa habari hiyo tu. Watu wengi walikaa attention wakisubiria masaa hayo.
Alionekana Queen akiwa ameingia ndani ya chumba cha Dada yake Winnie.
"Dada sitaweza kumsamehe yule aliyehusika na mauaji yako hata kama sheria itashindwa kumpatia adhabu Mimi siwezi shindwa kumpatia adhabu alizungumza Queen akilitizama gazeti lililoweza kupambwa na picha za watu watatu Vanessa, Tropina pamoja na Alice kwani ilikuwa ni siku pia ya Vanessa kusomewa mashtaka yake ya kutaka kufanya jaribio la kuuwa.
***** ****** ******
Tropina akiwa mahabusi alisiikia namba yake ikiitajwa na alihitajika kuelekea kule alipoweza kuitwa alienda na alipatiwa bahasha..
" nani kaleta hii?? Aliuliza Tropina.
"Sijui Mimi imeletwa na mbaba mmoja tu na kusema upatiwe wewe kisha akaondoka. Alizungumza askari gereza na kumtapatia.
Tropina aliichukua na kuifungua baada tu ya kuona kilichopo ndani yake aliweza kuidondosha bahasha
Tropina alitoa zilikuwa ni picha Vikram akiwa na Alice kwanzia siku ya kwanza alivyoweza kulala naye.
"Mbona hapa ni kwenye chumba changu?? Aliuliza Tropina akiwa haamini.
Inawezekanaje hii?? Aliuliza tena.
Alice alituma picha za mwanzo alizoweza kumpiga Vikram alipokuwa akizungumza na Vanessa pale alipoweza kugonga mlango alichanganya na picha za Jana yake usiku kwa pamoja.
Alimimina zote chini na kutazama zote kwa kuchambua hapo chini aliweza kuiona tape recorder aliiplay na alianza kuzisikia sauti za ajabu.
" wanafanya nini hawa?? Aliuliza Tropina na kujikuta hakun mtu wa kumsaidia kujibu.
Aliitupa na kuanza kuikanyaga kanyaga kwa kuipasua kabisa kwani hakuhitaji kuzisikia sauti zile katika masikio yake.
***** Saa 9 alasiri ******
Watu walianza kuongozana Mahakamani hapo huku wengi wakiwa ni waandishi wa habari wakimpiga picha Vanessa aliyeingia mahakamani hapo akiw na Larry pamoja na Vikram.
Huku Alice akiingia na Adrian pamoja na mzee Mpalila.
Amri ilitolewa watu wasimame juu kwni hakimu alikuwa akiingia.
"Yuko wapi Tropina?? Aliuliza Vikram wote waligeuka nyuma na kutizama lakini hakukuwa na mtu.
Hakimu alikaa na kuwaruhusu watu wakae.
" mtuhumiwa yuko wapi?? Aliuliza hakimu baada ya kukaa.
Wote walitizamana na hapo hapo aliletwa Tropina aliyekuwa amefungwa bandage katika mikono yake.
"Nini kimetokea?? Aliuliza Vanessa na kuanza kumfuata Tropina lakini alizuiliwa na maaskari.
"Samahani, mtuhumiwa aliweza kujiumiza yeye mwenyewe masaa machache yaliyopita ya siku ya Leo kwa kupiga nondo za mahabusu kutumia mikono yake hivyo ikabidi tumpeleke hospitalini ndo maana tumechelewa.
Hakimu aliyasoma mashtaka kwa Mara ya pili na aliulizwa kama anayakubali au anayakataa mashtaka.
Alimtizama Vikram kabla ya kujibu swali na Vikram alimpa ishara ya kukataa mashtaka.
" Ndiyo nayakubali mashtaka yote isipokuwa limoja tu" alizungumza Tropina na kurudisha macho yake kwa Vikram.
"Unamaanisha nini?? Aliuliza hakimu huku kila mmoja akimtizama Tropina.
" anataka kufanyaje huyu?? Aliuliza Alice akimtizama Tropina kwa makini.
"Namaanisha nakubali nimeuwa wote hata kama sijauwa ila kesi ya kumuuwa Rickson nakataa kwasababu Rickson hajafa yuko hai na yuko mbele ya macho yangu" alizungumza Tropina.
"Unaongelea nini?? Aliuliza tena hakimu na kumfanya Adrian ashangae kwni yeye anatambua ya kuwa tayari Rickson ameshauwawa.
" namaanisha Rickson ni huyo apo" Tropina alinyoosha Mkono sehemu aliyoko Vikram na kufanya watu wote wamgeukie Vikram aliyekuwa haongei chochote kile zaidi ya kumtazama tu Vikram.
"Huyu mtoto anafanya nini?? Aliuliza Vanessa na kutaka kumfuata Tropina lakini alizuiliwa na Vicky..
" Mama ni salama tu hata hivyo nilikuwa nataka kufanya hivi hata kabla hajafanya yeye alizungumza Vikram na kunyoosha mikono yake mbele ya George akihitaji akamatwe.
Hakimu alibaki akiwatizma tu na kushindwa kuelewa ni maigizo gani yanaonyeshwa hapo .
Kesi ilipigwa tarehe tena baada ya wiki moja ndiyo ingeweza kusikilizwa.
Tropina alitolewa wa kwanza katika mahakama hiyo na Vanessa alimfuata.
"Umefanya nini eti??
" mama usikae karibu na yeye yeye na Alice wote wapo kitu kimoja na Ndiyo chanzo ch haya yote yaliyoweza kutokea katika familia yetu"
"Wewe nani kakwambia hivyo....nani kakwambia utumbo huo?? Aliuliza kwa kugomba Vanessa.
" Larry Mimi si Dada yako chochote kile atakachoweza kukizungumza Vikram na akwambie ukifanye kataa usifanye chochote atakachoweza kukwambia ukifanye"
"Kwanini sasa?? Aliuliza Larry.
" Muamini Dada yako sawa" alizungumza Tropina.
"Lakini hata na yeye ni bwashe wangu sasa" alizungumza Larry akiwa kama ahitaji kufanya kile Dada yake anachokizungumza.
"Larry" aliita Tropina na ghafla alihisi kizunguzungu.
"We acha kumjaza mdogo wako ujinga wako huyo aliyekwambia hayo maneno yote ni mtu ambaye hakutakii mema hivyo ukirudi tena mahakamani kataa na useme Vikram siyo Ricskon maana yeye pekee ndiye msaada wako" alizungumza Vanessa na kumshika Larry Mkono kisha Kuondoka naye.
Vikram na yeye aliweza kufungwa pingu na kutolewa mahakamani.
Vanessa alienda mpaka alipo Vikram na kuanza kumpapasa usoni uku akimwambia kila kitu kitakuwa salama.
Tropina alikumbuka ya kuwa mikono yake hakujipiga mwenyewe kwenye nondo za mahabusu bli mahabusu wakike wawili waliweza kufanya kazi hiyo na baada ya kufanya hivyo alichukuliwa na kupelekwa hospitalini ambapo Alice aliingia ndani ya chumba alichokuwapo.
"Uliupata mzigo nilioweza kukutumia" aliuliza Alice
Tropina alisimama na kutaka kumfuata lakini alikuwa amefungwa kwa pingu katika kitanda alichoweza kulala.
"Tulia......taratibu kabisa.... Punguza hasira nikuelezee ilikuwaje.......unakumbuka siku ile usiku Vikram alivyokutumia msg na kukwambia uwende kwenye chumba chake usiku huo huo alinitumia msg na kuniambia.
" Alice mke wangu njoo chumbani kwa Tropina Leo nimekipamba kwaajili yako na Tropina nimemwmbia aendee katika chumba changu atakaa huko mpaka pale tutakapomaliza mambo yetu"
"Usiniambie Mimi huo ujinga wenu, Vicky anihusu tena Mimi" alizungumza Tropina.
"Na unajua ni nani aliyenambia nifanye yote hayo ni Vicky ili Mimi na yeye tuweze kuishi katika maisha ya amani na raha inabidi wewe ukae mbali na Mimi pamoja na yeye...na kwakuwa unampenda huwezi kusema mahakamani kuwa yeye ni Rickson bli utakubali yote na mchezo utaishia hapo" Alice alizungumza hivyo na hapo ndo ukawa mwisho wa kumbukumbu za Tropina.
"Vikram sitakusamehe hata kidogo nitakuteketeza kama ulivyoweza kuiteketeza familia yetu. Alizungumza Tropina na kupelekwa mpaka kwenye gari ya polisi kwaajili ya kupelekwa mahabusu huku nako Vikram akipandishwa katika gari lile lile.
" Pinah " aliita Vikram.
"Usidhubutu kuniita jina langu" alizungumza Tropina na kumtazama kwa macho makali Vikram.
Vikram alitabasamu tu na kubaki akimtizama Tropina aliyekuwa akitizama chini.
"Ninafuraha kwa kuwa kwasasa nipo karibu na wewe utakachokula wewe Ndiyo nitakachokula Mimi, utakapolala wewe ndipo nitakapolala Mimi na.........."
"Nitakapo fungwa Mimi Ndiyo utakapofungwa wewe" alizungumza Tropina na kumfanya Vikram atabasamu.
"Alafu hata sijui unamchekea nani??? Maaskari waliokuwa ndani ya lile gari nao ilibidi wacheke tu.
" Ni mke wangu huyu" alisema Vikram akiwaambia maaskari.
"Nani mke wa nani???
" wewe hapo" alizungumza Vikram.
"Mimi siyo mke wako"
"Lakini mbona kila mtu anafahamu kuw wewe ni mke wangu"
"Nani anafahamu?? Aliuliza Tropina.
Vikram alirudisha macho yake kwa maaskari na hakuna hata mmoja aliyeweza kujibu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" unaona hakuna mtu anayeweza kujua ya kuwa Mimi na wewe ni mke na mume" alizungumza Tropina n kutabasamu.
"Lakini tayari wameshafahamu baada ya kuwaambia" alizungumza Vikram akicheka.
"Ni kweli kumbe nyie ni mke na mume nilikuwa sinaga uhakika" alizungumza askari mmoja.
"Umeona eeee" aliuliza Vikram na kumsogelea karibu Tropina aliyemsogelea na kumuuliza umeona nini??
Vikram alimtizama na kumbusu mdomoni.
"We mshenzi nini??? Aliuliza Tropina na kutaka kumpiga Vikram kwa kutumia mikono aliyoweza kufungwa nayo pingu.
" Tulia Pinah utajiumiza" alizungumza Vikram akiishika mikono ya Tropina, Tropina alimtizama Vikram na kuweka mguu wake katika sehemu za Vikram.
"Ammmhhhh hiyo mbaya hiyo, baadaye usije lalamika unakosa watoto wakati mambo uliyaharibu mwenyewe" alizungumza Vikram na kumfanya Tropina ashushe mguu wake na kutoa mikono yake katika mikono ya Vikram kisha kukaa kwa kutizama pembeni.
Maaskari waliokuwapo ndani walicheka na hata George aliyekuwa upande wa mbele wa gari nayeye aliweza kucheka kwa kutabasamu tu.
***** ***** *****
"Kimetokea nini sasa nilitegemea Vikram atakana kuw yeye siyo Rickson lakini hajapinga chochote" alizungumza Alice akiendelea kuishikashika mikono yake aligeuza macho yake na hapo aliweza kukumbuka kitu na kutabasamu alielekea mpaka upande wa jikoni alifungua mlango na kuanza kusikitika alikuwa ni mama yake na Alice aliyeweza kudhoofika mwili baada ya kukaa bila kula takribni siku nne.
"Niliwezaje kusahau ya kuwa uko huku jamani mama.....lakini leo nimekukumbuka kwanza inabidi ule nahisi Leo ni siku ya pili hapana ni siku ya nne jamani umewezaje kuvumilia mateso yote hayo....ila walisema mwanamke anaweza kukaa siku 7 sijui niongezee nyingine Tatu ili nitizame kauli hiyo ni ukweli kweli au wanadanganya....
Lakini hapana ninashida na wewe sana nahitaji ule...vizuri ushibe kabisa kwani wiki ijayo kuna kazi inabidi unisaidie kuifanya" alizungumza Alice akitembea tembea maeneo yale.
****** ***** *****
Ilikuwa ni asubuhi na mapema na askari walionekana wakiwa njiani kuelekea katika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu na msamaria mwema.
Walipofik walikuta kundi kubwa la watu likiwa limezingira sehemu hiyo.
George aliweza kupewa maelekezo na Tobias.
"Hakuna aliyeweza kushuhudia tukio hilo ila walisema walimuona akiwa amedondoka tu hivyo wanasema amejiuwa.
George alifika na kugeuza mwili ule wa marehemu alikuwa ni mpiga picha ambaye aliweza kupiga picha usiku ule ambao Vanessa alimpatia pesa Josephat.
Aliweza kuiona camera baada ya kumgeuza aliichukua camera ile na kuanza kutizama ndani.
Alishtuka na alichoweza kusema baada ya kutizma kwa sekunde 50.
"Andaeni magari tunaenda kumkamata Vanessa"
"Vanessa!!! Aliuliza Tobias kwa mshangao.
George alimpatia kamera na kushusha pumzi ndefu.
Tobias aliipokea na kuanza kutazama kile kilichokuwa ndani ya camera ile. Zilikuwa ni picha alizoweza kupigwa wakati akimpatia Josephat pesa.
" hii inamaanisha nini?? Aliuliza Tobias.
"Pale tutakapo wakamata wote wawili lazima wataelewa kipi kimetokea" alizungumza na kuamuru baadhi ya maaskari wauchukue mwili wa marehemu na yeye akapanda gari pamoja na maaskari wengine wawili kwaajili ya kuelekea nyumbani kwa Vanessa.
***** **** *****
"Hii kazi ninayoifanya niya hatari sana japokuwa inanitengenezea pesa za kutosha naamini pale tu nitakapomaliza kutoa ushahidi wa uwongo mahakamani basi lazima Alice atahitaji kuniuwa hivyo lazima niwe na silaha yoyote ile itakayomuwezesha aache kufanya hivyo" alizungumza Josephat na kuigusa pen yake juu iliyokuwa inauwezo wa kurecord sauti ya mtu.
Hapo hapo aliweza kuingia Alice.
"Alice umekuja? Aliuliza akiw na wasiwasi.
"Ndiyo nimekuja kwani Kuna shida ya mimi kuwa hapa? Aliuliza na kukaa kwenye kiti huku akimtizama Josephat.
" hapana Hamna" alizungumza na kukaa.
Pen yake iliweza kuanza kurecord kila asemacho Alice.
"Nafikiri na wewe pia utakuja kukamatwa ukifika polisi cha kufanya ni kumlimbikizia kesi hiyo Vanessa alafu nione kama Tropina atakuwa na wakumsaidia tena" alizungumza Alice.
"Lakini Alice kwanini umefanya yote hayo, umewauwa watu wote hao na kumsingizia Tropina.....bado haijatosha unahangaika pia na mama yake kwa kumbambikizia kesi ya mauaji ambayo umeyafanya wewe alizungumza Josephat.
" wewe punguza mdomo, kwanza niyafanyayo mimi hakuna yoyote yule anayeweza kufahamu ya kuwa Mimi ni muuwaji kwamaana nimtengeneza mazinga ya kesi zikawaangukia watu wengine "
"Lakini kwanini umeyafanya yote hayo?? Aliuliza Josephat.
" kwaajili ya mapenzi yangu kwaajili ya mapenzi mazito niliyonayo juu ya Vikram ambaye Anampenda Tropina " alizungumza Alice kwa hasira na kupiga meza hali iliyofanya kalamu ile iliyokuwa ikirecord idondoke chini na kumfanya Josephat ashtuke na kutazama chini.
Alice alimtizama na kutia mashaka kidogo juu yake
Lakini wala hakujali.
*** *** *** ***
"Vanessa yuko wapi?? Aliuliza George baada ya kufika katika nyumba ya Vanessa.
" Unamtakia nin?? Aliuliza Larry aliyekuwa akishuka katika ngazi.
"Naitwa Inspector..........
"
"Nakufahamu, nimekuuliza Vanessa unamtakia nini???
"Tunahitaji tumpeleke kituo cha polisi kwaajili ya mahojiano kuhusu kifo cha mtu mmoja kilichoweza kutokea Leo saa4 asubuhi" alizungumza George.
"Nani kafa tena?? Aliuliza kwa kuhamaki Vikram.
Tobias alitoa camera na kumpatia Larry ambaye alishtuka baada ya kuziona zile picha.
" Mama yangu hayupo" alizungumza na kuwarudishia camera yao uku akiwasukuma watoke njee.
"Nani hayupo?? Aliuliza Vanessa aliyeweza kutoka chumbani kwake pasina kutambua habari zozote zile.
**** *** ****
Mahabusu aliyoweza kuwekwa Tropina iliyofuata basi aliwekwa Vikram.
" Pinah" aliita Vikram na kumtazama Tropina.
Pinah aliyageuza macho yake na kumtizama Vikram kisha akayarudisha chini.
"Kuna kitu nahitaji kukwambia Tafadhali unaweza ukasogea kwa hapa?? Aliuliza Vikram.
"We zungumza hata hapa nakusikia"
"Nop.....sogea karibu na Mimi nataka nikwambie kitu cha siri sana sihitaji mtu mwingine asikie" alizungumza Vikram.
"Sitaki" alijibu Pinah.
"Pinah nahitaji kukuelewesha kile kilichoweza kutokea juu yangu na Alice Tafadhali njoo karibu na Mimi.
" sihitaji kusikia chochote kwaamaana huyo Alice ameshaniambia kila kitu Haina haja tena" alizungumza Tropina na kugeukia upande mwingine huku akijizuia machoz yasimtoke.
"Aaaaahhhh...... Aaaaahhhh........aaahhhh alipiga kelele Vikram na kumfanya Tropina ageuke nyuma na kutizama kipi kimetokea juu yake.
Vikram Vicky, uko salama.....walinzi.......nyie polisi" alipiga kelele Tropina akihitaji waje wamsaidie Vicky aliyeonyesha kubanwa pumzi.
Vikram alimshika Mkono na kukaa chini katika sero yake hali iliyomfanya naye Tropina akae chini waliweza kutenganishwa na nondo tu.
"Niko salama bhana acha kelele" alizungumza Vikram.
"Mpumbavu wewe alizungumza Tropina na kutaka kunyanyuka lakini Vikram alimshika vyema mikono yake.
" nisikilize Tafadhali nisikilize mimi, alizungumza Vikram.
"Siku ile uliyosema ya kuwa ulipata msg na Mimi nilikwambia uwende nyumbani kwangu siyo kwli kwni na Mimi nilipokea msg kutoka kwenye namba yako na uliniambia nije chumbani kwako........................................ Vikram aliendelea kujielezea mbele ya Tropina huko nako alionekana Vanessa akiwa katika chumba cha mahojiano.
Aliletewa picha ya marehemu na kuulizwa.
"Unamfahamu huyo kijana???
" Simfahamu" alijibu Vanessa.
"Sasa kwanini kwenye camera yake Kuna picha zako pmoja na wakili wako?? Aliuliza George.
"hilo swali siyo la kuniuliza Mimi muulizeni huyo aliyepiga picha" alijibu Vanessa
"Lakini tayari ni marehemu sasa?? Aliuliza Thobias.
" Ndiyo mfanye mbinu ya kumfufua awajibu hilo swali au mmoja wenu afe aende akamuulize hilo swali popote alipo" alizungumza Vanessa kisha akasema.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sitazungumza tena nahitaji wakili wangu"
"Hapo hapo aliweza kuingizwa pia Josephat akiwa na pingu mkononi.
" Josephat?? Aliita kwa mshangao
"Kama wewe, huta zungumza basi huyu atazungumza alisema George na kumtazama Vanessa.
****** ****** *******
" lakini aliniambia.........."
"Pinah..... Niamini Mimi vyote nilivyoweza kukwambia ni ukweli, ukwli tena ukweli mtupu" alizungumza Vikram.
"Kwahiyo umelala naye Mara moja tu? Aliuliza Pinah.
" Ndyo hiyo hiyo moja tu, sijafanya tena na yeye Mara nyingine " alizungumza Vikram na kumtazama Tropina.
"Unasema moja tu unafikiri ni raha, wewe ni mume wangu hupaswi kulala na mwanamke mwingine hata kidogo hata kama ni kwa sekunde1" alizungumza Tropina.
"Ndiyo natambua hilo ndo maana nakutaka radhi, lakini kama asingelinifunga kitambaa ningejua siyo wewe, nakuapia ungemkuta marehemu kule ndani na kila alichoweza kukitumia vyote nilivitupa kwenye dustbin na kununua vipya" alizungumza Vikram.
"Sawa" alijibu Tropina.
"Pinah"
"Abee"
"Ye walah siyo mtamu kama wewe" alizungumza Vikram na kumfanya Tropina atabasamu na kuona aibu kisha akatizama chini.
**** ***** *****
"Nahitaji kujua kati ya Daniel na Vikram yupi ni Rickson maana sielewi kabisa usikute nafurahia kuwa niko salama na mali zote zitakuwa zngu pindi haya mambo yatakapoisha ukute Rickson yupo hai na bado ni mmiliki wa mali hizo hapokuwa Sister Mary ameniamini na kufanya kampuni ya Magari iwe juu yangu bado simuamini mtu......Daudi nataka ufuatilie na unipe majibu nani ni Rickson je ni Danielle au Vikram?
" Ndiyo boss " alijibu Daudi na kutoka ndani ya hotel aliyokuwa akiishi Adrian baada ya Kuondoka katika nyumba ya Vanessa.
Daudi baada ya kutoka alipiga simu mahali.
"Bossi, inavyoonekana bado Adrian anamashaka juu ya Vikram kwani amenituma nichunguze.......Ndiyo....... Sawa nimekuelewa" alikata simu Daudi na kufungua lifti ili ashuke.
"Mpumbavu huyu Adrian nimemsaidia kwa kiasi kikubwa mpaka hapo alipoweza kufikia lakini bado anajaribu kutaka kunichunguzia Vikram wangu" alizungumza Alice kwa hasira baada ya kumfanya Daudi awe kwa upande wake na kumlipa pesa nyingi zaidi ya Adrian amlipavyo.
**** **** ****
"Huyu taira anazungumza nini hapa?? Aliuliza Vanessa akitaka kumkwida Josephat.
" lakini madam Vanessa ni ukweli ulinipatia pesa nikusaidie kumsingizia kuwa Vikram ni Rickson ili mtoto wako akapate kuachiliwa huru pia uliniambia sheria kama itashindwa kumsaidia mtoto wako ambaye ni muuwaji basi nitafute vijana kwaajili ya kumtorosha hapa kituoni. alizungumza Josephat na kumfanya Vannesa ashike kichwa chake.
"Mungu wangu, Mungu wangu,....huyu katuni anaongea uwongo gani hapa?? Niambie Alice amekulipa kiasi gani mpaka Unataka kuyaharibu maisha ya binti yangu vyote nilivyofanya juu yako pamoja na kuitendea mema familia yako Leo unanilipizia mabaya" Vanessa aliinuka kwa hasira na kutaka kumvaa tena Josephat.
Alizuiliwa na maaskari kisha akatolewa njee ya eneo lile.
"Nafikiri sasa tutaweza kuzungumza vizuri, Huyo camera man aliuwawaje?? Aliuliza George.
Wakati ananipatia pesa aliweza kumuona huyo camera man yeye alinitaka Mimi niondoke na kusema ya kuwa atamfuatilia camera man mwenyewe,hivyo niliondok na sikujua kama Vanessa angeweza kumteketeza namna hii" alizungumza Josephat huku akisikitika n kufuta machozi yake ya uwongo na ukweli.
George alimtizama kisha akamtizama na Tobias aliyekuwa akimtizama kwa makini sana Josephat.
"Natumaini anadanganya alizungumza George.
"Hata Mimi" alijibu Tobias.
"Mahali walipoweza kukutana ni mbali sana na eneo lililoweza kutokea mauaji na katika njia hiyo hakuna sehemu yoyote ya kujificha hivyo asingeweza kukimbia umbali mrefu hivyo" alizungumza George.
"Na kingine kama Vanessa alishaweza kumuona ni mpiga picha asingeweza kumuuwa kisha akaondoka bila kuchukua camera" aliongezea Tobias na kumfanya George aache kutembea.
'Nini shida???
"Lazima tutafute ukweli Mimi nitaenda tena eneo la tukio wewe itabidi uwende sehemu waliyoweza kukutana Jana usiku na hakikisha unapata ushahidi hata mmoja tu nahisi Kuna kitu hakiendi sawasawa" alizungumza George.
"Pia ni vizuri kama tunamfahamu huyo Alice kwani ni zaidi ya Mara Tatu Vanessa anatamka jina hilo" alizungumza Tobias na kuondoka.
Bahati mbaya ni kwamba wakati wakiyazungumza hayo yote Alice aliweza kuyasikia akiwa na Daudi.
"Hawa viherehere wawili hawa?? Alizungumza kwa hasira sana na kuelekea alipokuwa akielekea.
****** ****** ****
" Vipi unaumwa mbona sura yako inaonekana namna hiyo? Aliuliza Vikram.
"Sijielewi hata nahisi tu kizunguzungu kila wakati na mara nyingine nahisi kichefuchefu pia nahisi ni malaria" alijibu Tropina
"Unaonekana kuchoka sana sidhani kama ni malaria pekee yake, unahitajika kupata vipimo zaidi, akija askari yoyote nitamuomba hilo kabla ya wewe kupelekwa mahakamani. Alizungumza Vikram akimpapasa uso Tropina.
" Niachieni msinipelekepeleke mimi" alizungumza Vanessa aliyekuwa akiletwa katika sero aliyokuwapo Tropina.
Aliingizwa sero ya mbele yao na kufungiwa huko.
"Vanessa!! Aliita Tropina kwa mshangao na kusimama.
" mama" aliita Vikram na yeye pia kwa mshangao.
"Huyu ng.ombe Josephat ametusaliti" alizungumza Vanessa na kukaa chini.
Tropina na yeye alihisi kizunguzungu na kutaka kudondoka lakini aliweza kudakwa na Vikram aliyekuwa sero ya jirani yake.
**** **** *****
Larry alikuwa nyumbani mwenyewe huku akiwa kama mtu asiyeweza kuelewa kipi kimeikumba familia yao.
"Larry, inabidi japo utumie hata juice tu kwanzia asubuhi hujatumia chochote kitu" alizungumza Diana.
"Shangazi kila mtu aliyekuwa karibu nasi wote wametugeuka na wote Ndiyo waliyoweza kusababisha matatizo haya mazito katika familia yangu ona sasa hivi kila mmoja yupo gerezani nimebaki Mimi tu, hata Mimi naamini muda si mwingi nitawafuata walipoweza kuelekea kwani sina wa kumtegemea tena. Alizungumza Larry kwa kulia.
" usijali nipo hapa kwaajili yako na nitafanya kila kitu niwezacho kwaajili ya kuwasaidia kama Kuna mahali nitaweza kuweka msaada nakuahidi......Sasa kula japo kidogo alizungumza Diana.
"Hapana sihitaji chakula" alizungumza Larry.
"Sasa kama hutakula na kupata nguvu ya kuipigania familia yako unafikiri nani ataweza kuifanya kazi hiyo" ilikuwa ni sauti ya Queen aliyeweza kuingia katika chumba cha Larry.
Larry alibaki akistaajabu baada ya kumuona Queen.
Queen alienda akaichukua juice aliyoweza kuishika Diana na kumpatia Larry.
"Haya kunywa hiyo fanya haraka" alizungumza na kumshikishia mkononi.
"Bado hunywi tu" alizungumza Queen na kuchukua glass ile kisha kumuwekea mdomoni.
Larry alianza kunywa taratibu kabisa hata katika uso wke nao Tabasamu liliweza kuonekana japo kwa mbali sana huku usoni kwa Queen kukionekana machzo yaliyokuwa yakitaka kumtoka machoni.
***** ***** ****
Alice alitoka kwa mkuu wa kituo baada ya kuzungumza naye na mkuu huyo aliweza kumsndikiza mpaka njee hapo alikutana macho kwa macho na Inspector George.
"Natumaini ombi langu utalifanyia kazi alizungumza Alice.
" nitalifanyia kazi wala usijali alizungumza mkuu huyo wa kituo na kumwambia George.
"Nafikiri ni vizuri kama utawatenganisha na uwaweke kila mtu katika sero yake"
"Sifikiri kama Kuna haja tena ya kufanya hivyo kwani, Vanessa pamoja na Vikram wanatoka sasa" alijibu George.
"Kwanini watoke?? Aliuliza kwa kuhamaki Alice.
" Kwa kuwa Vikram siyo Rickson na Vanessa siyo muuwaji" alijibu.
"Vikram natambua siyo Rickson, lakini Vanessa ni muuwaji" alizungumza Alice.
"Inawezekana ukawa shahidi wa kutosha kwa tukio hilo kwani mteja wangu Mimi hajahusika na mauaji yoyote sasa unavyong.ang.ania ya kuwa kauwa Kuna uwezekano mkubwa ulikuwa eneo la tukio" alizungumza Mwanamke mmoja aliyeweza kuvalia nguo zuri zilizoweza kumkaa vizuri mwilini mwake akionekana hana asili ya kitanzania kabisa bali mtu aliyeweza kuchangia damu ya kitanzania aidha kwa baba au mama.
"Naitwa mwanasheria Lucresia Antony, sidhani kama unanifahamu ila Mimi ni Dada yake na huyo unayesema muuwaji hivyo ninahitaji dakika 10 za kuzungumza na wewe ili unielezee kwanini unasema ya kuwa dada yangu ni muuwaji ilihali hakuna udhibitisho unaoonyesha hivyo?? Baada ya kuzungumza maneno Yale aliachia Tabasamu mwanana asubuhi ile na kufanya jua ling.aalo angani liendelee kuonyesha uzuri wake.
Wakili Lucresia alitizama nyuma yake na kulikuwa na gari jeusi lililoweza kupaki pembeni ndani yake akiwa Jimmy pamoja na Dr Kim ambaye alimkonyeza na kumpa ishara ya dole gumba.
George alibaki akitabasamu na kumtizama Alice.
" Tafadhali ukishamaliza kuzungumza nayeye nilikuwa pia na mazungumzo na wewe kuhusu background yako kwani nimejaribu kufuatilia lakini haieleweki kwani ninyi mko mapacha , na kama ni mapacha mbona hamfanani na ikawaje katika familia moja mabinti wote mkapewa jina moja la "Alice" alizungumza George na kumfanya Alice ashtuke.
Alice aliwatizama wote kwa wakati mmoja kisha akacheka.
"Wewe cjui wakili.. Kwasasa sina muda hivyo inabidi uweke appointment juu yangu kama unahitaji kujua ukwli wa nani muuwaji, na wewe I don know ni Inspector au officer.... Inavyoonekana Unataka kunichunguza sana ila sina muda kwasasa unaweza kutana na mama yangu yeye atakujibu yote" baada ya kumaliza kuzungumza aliondoka na kuwaacha pale.
"Waoo anaujasiri kiasi gani huyu?? Aliuliza Lucretius na kumtazama Alice.
Wakati huo Vikram pamoja na Vanessa waliweza kufunguliwa katika sero zao.
Vikram alienda na kumshika mikono Tropina.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Pinah inabidi uniamini sasa kwakuwa nahitaji kukutorosha hapa kwani tutachukuwa muda mrefu kuupata ukweli na utaendelea kutesekea hapa na hilo sihitaji kabisa niweze kuliona tena....... Hivyo kila utakachoambiwa mahakamani ukijisikia kukubali wewe, kubaki ukijisikia kukataa wewe kataa ili hukumu itolewe juu yako na siku watakayohitaji kukupeleka gerezani Ndiyo siku nitakayokutorosha sawa"
Tropina alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo na kutabasamu.
"Pinah, mama yako atakutoa hapa nitatumia mbinu yoyote ile na kuhakikisha nakutoa hapa. Alizungumza Vanessa.
" Sawa mama" alijibu Tropina na kufuta machozi
"Njia ni hii Tafadhali alizungumza officer mmoja kwa kuweza kuwaelekeza njia Vanessa na Vikram.
Vikram aliikamata tena mikono ya Tropina na kuibusu zaidi.
" nitakutoa hapa" alizungumza Vikram na kuondoka huku akimuacha Tropina katika majonzi mazito
"Vicky" aliita Pinah.
"Nakuamini na nakupenda sana sana sana sana sana mpaka naumwa" alizungumza Tropina na kucheka.
Vikram alirudi na kisha kumbusu Tropina mdomoni kupitia nondo zile ndogo za mahabusu ile.
**** **** ****
"Hivi wanafikiri Mimi ni mpuuzi kama hao, hahahaha najua mtataka kumtorosha Tropina na Mimi nawahakikishia ya kuwa atakufa kabla hilo halijatokea" alizungumza Alice na ghafla alihisi kutapik na aliweza kukimbilia kwenye sink na kwenda kutapikia huko.
Alitoka akiwa anajifuta futa mdomo wake.
"Nimekula nini Leo mpaka natapika Hivi? Alijiuliza Alice akichukua ki taulo chake na kujikausha .
Ghafla aligatuka na kuachia Tabasamu.
" uuwwhh isije ikawa ni mimba sasa....lazima nikapime alizungumza na kuchukua kipimo chake cha mimba kisha kuelekea chooni tena.
***** ****** *****
"Mbona hichi chumba Leo kinanukia harufu ya tofauti kabisa?? Aliuliza Vanessa baada ya kuingia chumbani kwa Larry.
" harufu gani?? Aliuliza huku akimfuata nyuma mama yake.
"Harufu ya tofauti kabisa alirudia tena Vanessa na kumgeukia Larry.
"Nini!!! Aliuliza Larry.
"Jana ulikuwa na mgeni chumbani kwako?? Aliuliza Vanessa na kumtazama Larry aliyeeonekana kuweweseka na kumjibu Vanessa.
'Ha...ha....Hamna... Hata mulize Diana" alizungumza Larry.
"Pinah yuko wapi?? Aliuliza Larry
" bado yupo gerezani "
"Hivi hakuna njia nyingine ya kumtoa Tropina?? Aliuliza Larry.
" ipo ila itahatarisha maisha yetu mpaka tuweze kumpata Tropina alizungumza Vanessa.
***** **** ******
"Kwanini umetaka tuonane?? Aliuliza Vikram baada ya kukutana na Alice.
Alice alichomoa barua na kumpatia Vikram.
" nini hiyo?? Aliuliza Vikram.
"Fungua" alizungumza Alice na kutabasamu.
Vikram baada ya kuona aliweza kushtuka sana na kumuuliza.
"Inamaana una mimba?? Aliuliza Vikram.
" Ndiyo Vickam, nina mtoto wako nimeweza kumbeba mtoto wako tumboni mwangu" alizungumza Alice na kuchukua Mkono wa Vikram huku akitaka auweke katika tumbo lake.
"Hapana, haiwezi ikawa ni ukwli, hapana hii haiwezekani, alirudia Vikram akiwa haamini.
" kwanini isiwezekane Vikram ni kweli ninamtoto wako na ni vizuri sasa kama wote tutaamua kuacha kila kitu kinachoihusu Tropina na familia yake kisha tuanze maisha yetu mapya" alizungumza Alice.
"Hapana siamini hilo" alizungumza Vikram na kupiga simu.
"Kim upo hospitalini?? Aliuliza Vikram.
***** **** ****
" vipi umeweza kupata vile nilivyoweza kukuagiza?? Aliuliza Adrian.
"Ndiyo" alijibu daudi na kumpatia bahasha ya kaki aliyoweza kuuingia nayo ndani.
Adrian alipekuwa kila kitu kisha akaanza kucheke.
"Kweli kabisa yani nilikuwa naishi na mtu nyumba moja na nikashindwa kutambua kumbe Danielle ni Rickson.
Alizungumza na kucheka Adrian aliyeweza kuamini ya kuwa Daniel ni Ricky baada ya kuletewa vizibitisho hivyo.
***** ****** *****
" anaujauzito wa wiki1 na siku 2" majibu hayo aliweza kuyatoa Dr Kim akimtizama kwa hasira sana Alice usoni aliyekuwa akitabsamu.
Rickson aligeuka na kumtizama Alice aliyekuwa akitabasamu.
**** ****** *****
Tropina akiwaa mahabusu alikuja Wakili Lucretius.
Tropina altizama na kukaa chini kwenye kiti.
"Hello, naitwa wakili Lucretius Antony ni wakili wa kujitegemea, naomba uniamini Mimi kwasababu nakuwa wakili wako na nitakupambania.
alizungumza Lucretius.
Pinah alimtizama kwa makini kwanza kisha akatabasamu.
" sawa " alijibu na kuendelea kumtizama machoni Lucretius aliyekuwa akikwepesha Macho yake.
****** ***** ****
Vikram alielekea mpaka mahabusu akiwa katika hli ambayo haikuwa nzuri.
"Vicky" aliita Tropina na kwenda kumkumbatia Vikram aliyekuwa haongei.
"Unashida gani mbona uko hivyo?? Aliuliza Tropina.
" Hamna" alibu Vikram na kuachia Tabasamu la uwongo.
"Niambie umemuonaje wakili wa Leo?? Aliuliza Vikram.
" aaaammmmhhhh wa kawaida tu, Lucretius ni mtu ambaye nilisoma naye chuo kimoja cha sheria USA na sikuwa nikiptna naye kutokana na mambo yetu ya kike"
Wakati akiyazungumza hayo Vikram aliyakumbuka maneno y Dr Kim ya kuwa Alice anamimba.
"Pinah" aliita tena Vikram.
"Kuna shida gani mbona uko hivyo?? Au Kuna kitu tena Alice amekifanya?? Aliuliza Tropina na kumshika mikono Vikram.
" Alice.........alizungumza Vikram na kabla hajamaliza kuongea Tropina alimdakia.
"Naapa kwa jina la Mungu nikitoka hapa mtu wa kwanza kumuuwa ni Alice, huyu mwanamke atafanya mikono yangu iwe na damu, siwezi kumuacha hai hat kidogo, naapa nitamteketeza" alizungumza Tropina.
"Pinah usiseme hivyo" alizungumza na kuchukua mikono ya Tropina.
Tropina aliitoa mikono yake na kusema.
"Nitamuuwa naaapa nitamuuwa siwezi kuishi na yeye kwenye dunia moja ukizingatia alilala na wewe, akamuuwa Danielle, akazifilisi kampuni zetu tulizoweza kuzipambania, siwezi muacha hai naapa siwezi muacha hai"
Vikram alishindwa atafanyaje kwani sasa yeye alikuwa katika hali ngumu na kushindwa kuelewa afanye nini hakutaka Tropina akae jela lakini pia hakuhitaji Alice auwawe kwani tayari anamtoto wake
******* ****** *******
"Hakuna njia nyingine ya kumtoa Tropina gerezani, ni kumtorosha tu" alizungumza Lucretius.
"Wewe umemtolea wapi huyu?? Aliuliza Vikram baada ya kumtoa pembeni Jimmy.
" ni miongoni mwa wale watu ambao wataweza kumtorosha Tropina hivyo nimeshangaa baada ya kujua ya kuwa amekuwa tena wakili " alizungumza Jimmy.
"Sawa ila Pinah amenambia niwe makini naye sijui kwanini?? Aliuliza Vikram.
"Sawa nitakuwa naye makini" alizungumza Jimmy.
***** ***** ******
Mbona Vikram hajaja mpaka sasa tayari zimeshabaki siku 4 kabla ya mahakama na Vikram hajaja kabisa. Alizungumza Vanessa.
"Siku ya mwisho aliyokuja hapa hakuonekana kuwa sawa kabisa, Patrick's umekuja naye?? Aliuliza Tropina.
" Ndiyo mlete ndani nahitaji kuzungumza naye"
"Sawa, ngoja nikamuite
Baada ya masaa machache Patrick alirudi katika kituo cha polisi na aliweza kufunguliwa geti kwaajili ya kutaka kuonana na Tropina.
Alitoa simu yake na kumpatia Tropina. Tropina alizitizama picha zile na kutabasamu.
" kwahiyo ananidanganya Mimi kuwa atanitoa hapa wakati anakuwa na wakati mzuri na huyo mwanamke wake mwingine. Alizungumza huku akitizama picha zilizokuwa kwenye simu ya Patrick.
"Patrick nahitaji unisaidie kitu kidogo" alizungumza Tropina.
Baada ya muda kidogo alikuja Wakili Lucretius na kutaka kumuona Tropina.
"Sihitaji huyu awe tena wakli wangu wala sihitaji wakili yoyote yule katika kesi yngu" alizungumza Tropina na kuondoka.
"Pinah"
Officer sitahitaji tena kuonana n huyu mwanamke na siyo wakili wangu tena" alizungumza na kurudi ndani.
Alitoka njee na kumpigia simu Jimmy kisha akamuelezea kile kilichoweza kutokea kwa Tropina.
Wakati huo Vikram alikuwa hospitalini tena na Alice aliyekuwa akilalamika ya kuwa tumbo lake linamuuma.
"Sioni shida yoyote ile ila nahitaji apunguze msongo wa mawazo kama hata fanya hivyo basi ataweza kumpoteza mtoto wake. Alizungumza dactari mwingine aliyeweza kwend katika hospital yake.
"Vikram simu yake iliita na aliipokea.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Halo..........Kwanini.......sawa" alijibu Vikram n kukata simu.
***** ***** *****
Vikram aliweza kuonana na Lucretius.
"Kwanini amekataa??
" Sikuwaga na mahusiano mazuri na yeye lakini sidhani kama ndicho kilichoweza kumfanya yeye akatae wakili"
"Sawa nitaenda Mimi" alijibu Vikram na kushuka ndani ya gari lake.
Alikaa katika meza kwaajili ya kumsubiria Tropina ambaye alipoweza kumuona tu alisema.
"Officer huyu naye sitataka kuonana naye alizungumza Tropina na kurudi ndani.
"Pinah....Pinah" aliita Vikram ila officer aliweza kumshika na kumwambia atoke njee.
Vikram alipiga simu na kumtafuta Vanessa.
"Mama, nahitaji uje kituoni nashngaa Tropina amekuwaje" alizungumza Vikram na kumsubitua Vanessa ambaye aliwasili hapo baada ya dakika7.
"Kuna shida gani??
" nashindwa kuelewa Tropina hataki tena wakili wala haitaji kuonana na Mimi " alizungumza Vikram.
"Imekuwaje aliuliza Vanessa na kuingia ndani ya kituo cha polisi.
" nahitaji kuonana na mwanangu alizungumza Vanessa.
"Amesema haitaji kuonana na mtu mwingine yoyote yule tofauti na Patrick hivyo tutafanya vile atakavyo" alizungumza George na kuwaomba watoke njee.
Vanessa alipanda gari pamoja na Vikram kisha wakaondoka wakati hayo yote yanatokea Alice aliweza kuyaona.
"Nina habari nzuri lazima ni share na yeye" alizungumza Alice na kutoa bahasha yake ya kaki alicheka na kushuka katika gari lake kisha kuanza kuelekea Polisi.
Alice aliweza kuingia mpaka ndani ya kituo cha polisi.
"Unataka nini aliuliza George.
" nahitaji kuonana na Tropina" alizungumza Alice.
Ameshatoa taarifa kwamba haitaji kuonana na mtu yoyote yule alizungumza Tobias.
"Lakini ukimwambia kuwa ni Alice hawezi kukataa. Alizungumza Alice.
" ameshasema......."
Alizungumza Tobias lakini George alimwambia.
Fanya vile atakavyo ili atambue ya kuwa Tropina haitaji kuonana na mtu. Alitoa amri hiyo George na Tobias alitoa ishara ya Ndiyo na kuelekea mahabusu.
George alisogeza kiti na kukaa juu ya meza huku akimtizama Alice.
Tobias alirudi akiwa mwenyewe.
"Nafikiri umeona kuwa haitaji kuonana na mtu" alizungumza George na kusimama kutoka kwenye meza kisha kutizama upande ambao aliweza kutoka Tobias.
Tropina alikuwa nyuma yke baada ya kufika alikaa na kumtizama Alice aliyekuwa akitabasamu tu.
"Hello Tropina alizungumza Alice na kucheka.
Tro Pinah alimtizama na kuomba watu waliokuwa pale waweze kutoka njee.
" unaendleaje, vipi mazingira ya huku yakoje?? Aliuliza Alice.
"Nenda kwenye kile kilichoweza kukuleta hapa" alijibu Pinah.
"K, sawa kama unahitaji iwe hivyo ila ni kwamba nina habari nzuri hivyo nahitaji kushare na wewe alizungumza Alice na kuifungua pochi yake kisha kutoa bahasha na kumpatia.
Tropina aliipokea na kufunguwa ndani ambako aliweza kutoa ultrasound.
Alimtizama Alice na kutazama karatasi ile.
" I namaanisha nini?? Aliuliza Tropina huku Mkono wake mmoja ukiishikilia vizuri nguo yake aliyoweza kuivaa kwa hasira alizoweza kuzipata.
"Vipi inamaana umekuwa kipofu tena au, hiyo ni picha ya mwanangu, hapana namaanisha mtoto wake Vikram, yani Mimi na Vikram tunatarajia kupata mtoto"
Tropina alijitahidi kuzuia machozi yake yasimtoke.
"Kwahiyo?? Aliuliza Tropina.
" kwahiyo, inamaana huelewi Mimi na Vikram tunaenda kuowana wewe utabaki huku huku na utafia hukuhuku kwasababu Vikram hawezi muacha mtoto wake ateseke kwaajili yako" alizungumza Alice.
"Ahaaaa ndo alikwambia hivyo?? Aliuliza Tropina na kusimama huku akiiondoka zake
" Unafikiri nakuongopea Mimi na Vikram tayari tumeshajadiliana swala la ndoa na nitakuletea kadi ya ndoa, Vikram atakuwa mume wangu Mimi wala hawezi kuwa mume wako" alizungumza Alice
"Sawa tuone mwanaum mwenye ndoa atawezaje kufunga ndoa nyingine, na nikusaidie kitu kingine siyo wewe pekee mwenye mtoto wa Vikram" alizungumza Tropina na kuelekea ndani.
"Anaongea nini huyu?? We kichaa wewe Tropina nakuapia Vikram ni wangu na nitafanya chochote kile kumpata Vikram alipiga teke kiti alichoweza kukalia Tropina baada ya Kuondoka.
" Tobias wewe unafikiri nin?? Aliuliza George aliyekuwa akitizama na Thobias.
"Naweza nikasema huyu mwanamke ni chanzo cha yote haya yanayotokea kwa Tropina na familia yake hata kama hatuna ushahidi" alizungumza Tobias.
"Shida ni kwamba Tropina ataki kuwa muwazi kwangu laukama angeniambia Mimi kila kitu basi ningejua jinsi gani ningeweza kumsaidia. Alizungumza George.
" hata hivyo zimebaki siku chache tu kabla ya kesi kusikilizwa na Tropina ahitaji tena wakili" alizungumza Tobias na kumtazama Alice aliyekuwa akiishilia.
Tropina alipofika ndani ya mahabusu alichanachana ile ultrasound iliyoweza kuletwa na Alice.
"Vikram unanisaliti Mimi kwaajili ya haka katoto pamoja na mama yake aliyesababisha yote hay kwenye familia yngu, naapa sitamuacha hai mmoja kati yenu nitawauwa wote" alizungumza Tropina huku akipiga piga moyo wake uliokuwa ukiuma sana.
**** **** ****
Vikram alikuwa pamoja na Vanessa.
"Mama sihitaji kumpoteza mtoto wangu lakini pia sihitaji kumpoteza Tropina, nashindwa kujua nifanyaje?? Aliuliza Vikram aliyekuwa akilia.
" Naelewa Vikram Naelewa ya kuwa kwasasa unawakati mgumu, mtoto wako ni wa muhimu sana lakini pia Tropina ni muhimu kwako kwa kuwa ni mwanamke unayeweza kumpenda, Alice amekuacha bila ya chaguo na nia yake amefanya hivyo ili uweze kuachan na Tropina na kuweza kuwatenganisha kabisa. Alizungumza Vanessa.
"Mama nafikiri kumuuwa Alice ili Tropina awe huru" alizungumza Vikram.
"Hapana kumbuka anamtoto wako huwezi kufanya hivyo kwasasa"
"Lakini vipi kuhusu Tropina sasa itakuwaje kuhusu yeye" alizungumza Vikram.
"Vicky hatuna njia nyingine zaidi ya kumtorosha Tropina" alizungumza Vanessa.
"Sasa mama nitawezaje tena kumwambia Tropina kwmba Alice anamimba hawezi kunisamehe kwa kila kitu alizungumza Vikram.
" nitakusaidia kuongea naye" aliongezea Vanessa aliyekuwa akimfuta machozi Vikram na kumlaza katika mapaja yake huku akimpiga piga mgongoni.
"Kila kitu kitaisha Vikram nakuahidi" alisema Vanessa.
******** ********* *******
Vanessa alihitajika kuonana na Tropina lakini Tropina alikataa.
Ila baada ya muda aliweza kutoka njee.
"Kwnini hutaki kuonana na mtu hata mmoja?? Aliuliza Vanessa.
"Umekuja kufanya nini hapa??
" Kesho ni siku yako ya kwenda mahakamani kuwa makini sana uwapo pale alafu pia Kuna tatizo dogo limetoke ............ammmhhhh Alice anamimba ya Vikram hivyo"
"Unasemaje tatizo dogo ....unaona ni tatizo lidogo hilo?? Aliuliza Tropina akiwa analia.
" natambua ni tatizo kubwa ila Vikram hana la kufanya kama unavyojua ya kuwa ilikuwa ni bahati mbaya "
Alizungumza Vanessa.
"Kama anataka nimsamehe mwambie aitoe hiyo mimba, mwambie hiyo mimba aitoe ndo nitamsamehe" alizungumza Tropina.
Vanessa aliinuka na kumpiga kibao.
"Unadhubutuje kusema hivyo, unafikiri ni kitu kirahisi mzazi kumuuwa mtoto wake?? Aliuliza Vanessa kwa hasira.
Alice ndiye aliyeweza kufanya yote hayo lakini huwezi kumuadhibu Vikram kwa kumwambia amuuwe mtoto wake asiyempenda ni Alice lakini siyo alichoweza kukibeba Alice, unawezaje kuona ya kuwa wewe Ndiyo unateseka mwenyewe wakti wewe na Alice mnampa wakati mgumu Vikram, hivi utajisilkiaje pale ambapo utaambiwa umuuwe mtoto wako mwenyewe, ni sawa naweza nikawa sikuwa mama mzuri kwako lakini sijakufundisha tabia ya kutojali roho za watu wengine hasa kwa mtoto mdogo kama huyo ambaye hana hatia" alizungumza Vanessa na kutoka njee huku akimuacha Tropina akiwa analia.
"Pinah aliingia Vikram aliyekuwa amesimama pembeni ya mlango na kuweza kuwasikia walichokuwa wakikizungumza na kumfuata Pinah.
" Pinah alita Vikram na kumshika Mkono.
Tropina aligeuka na kumpiga kibao.
"Kwanini umefanya hivyo tena.......kwanini umempa mimba huyo mwanamke kwanini??? Aliuliza Tropina aliyekuwa akililia kifuani kwa Vikram.
"Pinah, sikutegemea iwe hivyo.....ila........"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kati ya mimi na Alice unampenda nani?? Aliuliza Tropina
" mke wangu, unajua kabisa ya kuwa katika maisha yangu nakupenda wewe, nakupenda wewe tu Tropina sina mwanamke mwingine "
"Kudhibitisha hilo ka muuwe Alice nenda kamuuwe" alizungumza Tropina.
"Pinah siwezi kufanya hivyo sasa kwani kila nikihitaji kumuuwa anatafuta njia nyingine ya kujisaidia..."
"Sawa huwezi kumuuwa Alice, huyo mtoto wako aliyoko tumboni kwa Alice muuuwe"
"Pinah ni mtoto Wang yule na anaumuhimu katika maisha yangu"
"Ahaaa kwahiyo Unataka kusema Mimi sina umuhimu tena katika maisha yako sindiyo? Aliuliza Tropina na kuiachia mikono ya Vikram aliyokuwa ameishika.
"Sijamaanisha hivyo Tropina.. Nilikuwa namaanisha.........."
"Basi Haina haja ya kunidanganya tena sawa nimeshatambua ya kuwa mtu mwenye thamani sasa katika maisha yko ni Alice pamoja na mtoto wake sawa nimekuelewa tena vizuri sana, sasa endelea na maisha yako na Mimi nitaendelea na maisha yangu" alizungumza Tropina na kuondoka zake
"Pinah. ...Tafadhali nisikilize.... Tropina" aliita Vikram bila mafanikio yoyote Yale.
****** ******* ******
Larry alikuwa usiku kitandani akiota Ndoto ya kutisha sana na alibaki akiweweseka usiku na hatimaye aliweza kupiga kelele na kuamka.
Ndoto hiyo hata Tropina aliweza kuipata alipokuwa mahabusu
"Mama" alisema hivyo tu na hatimaye kuliweza kukucha na jengo la mahakama likionekana.
Mashtaka yaliweza kusomwa kwa Mara ya pili tena na aliulizwa kama ana wakili yoyote yule anayeweza kuisimamia kesi yake.
"Hapana sina" alijibu Tropina kwa ujasiri.
Na Je unayakubali makosa yako?? Aliuliza hakimu kwa Mara nyingine.
"Ndiyo nayakubali yote na sina kipingamizi hivyo naiomba mahakama yako iweze kutoa adhabu juu yangu haraka iwezekanavyo" alizungumza Tropina na kufanya watu walioweza kuhudhuria pale waweze kumshangaa
"Sawa ombi lako limekubaliwa na baada ya lisaa limoja hukumu itapita juu yako" alizungumza hakimu na kusimama.
Vanessa alimtizama Tropina na kutoka njee huku Vikram akihitaji kumsogelea Tropina ambaye alisema haitaji kusogelewa na mtu huyo.
"Hii ni drama gani inayoendelea hapa" alijiuliza Larry ambaye macho yake yliweza kugongana na Queen aliyekuwa akimtizama tu.
Masaa hayo yaliweza kuisha na sasa ilibaki wasaa wa hakimu kutoa hukumu.
"Kutokana na ushahidi ulioweza kutolewa katika upande wa mshtaki pmoja na vidhibitisho ambavyo vinaonyesha ya kuwa Tropina livingstone amehusika na muaji ya watu hao watatu pamoja na kuweza kumficha gaidi la kimataifa Rickson Miller mahakama hii inamuhukumu kifungo cha kunyongwa hadi kifo.
Tropina alishtuka na kujikuta anashngaa ni kipi kimemtokea.
Kwa mshtuko alioupata Vanessa alidondosha pochi yake.huku Larry magoti yakimuishia nguvu na kudondoka Vikram aliweza kusimama tu alipoweza kukaa na kubaki akimtizama hakimu.
Alice alikuwa akicheka sana moyoni mwake.
Queen macho yake yaliweza kumtizama mtu mmoja na kuchezesha midomo yake kwa hasira sana.
" hukumu hii imepitishwa Leo tar.....mwez.....na mwaka ...... Na adhabu hiyo itafanyika kesho saa9 mchana hivyo mtahitajika kuja kushuhudia tukio hilo. Alizungumza hakimu na kugonga mezani akimaanisha hukumu imepita.
Vanessa akiwa amesimama aligeuka na kumtizama Alice aliyeweza kumchekea na kumpungia Mkono wa bye bye.
"Vicky huwezi kumuuwa mtoto wako mwenyewe kwani utajihisi uchungu siku zote za maisha yako ila Mimi nitakusaidia" alizungumza Vannesa na kuokota pochi yake kisha akatoa bastola na kutaka kumpiga Alice aliyekuwa akielekea mlangoni.
"Mama acha" alizungumza Vikram lakini tayari Vanessa alishaweza kufyetua risasi ambayo iliweza kumpata ya Mkono.
"Mama wewe silaha yako chini walizungumza maaskari walioweza kuwa pale wakimtaka Vanessa afanye hivyo.
Vannesa alipiga risasi nyingine na hpo hapo Alice alichukua bastola iliyokuwa pembeni yake na kumpiga Vanessa risasi za kutosha mbele ya mahakama.
" mama!!!! Aliita Tropina ambaye hakuweza kuamini kipi kimeweza kutokea kwa mama yake.
Alice alienda kukamatwa ila alisema
"Nilikuwa najilinda nyie hamuoni ya kuwa alitaka kuniuwa" alizungumza Alice na kufanya aachiwe na maaskari.
Tropina alisimama na kumtazama Alice aliweza kumnyooshea kidole ila kabla hajazungumza aliweza kuzimia mikononi mwa Vicky.
Hali hiyo haikuweza kumshtua Tropina mwenyewe bali hata Larry aliyekuwa kazimia dakika chache zilizopita.
Alice alitoka njee ya mahakama na kuondoka Vikram alianza kumfuata nyuma huku akiwa anachomoa bastola yake.
Jimmy alimuwahi na kumzuia.
"Usitake kufanya kitu cha kipumbavu, Tafadhali muache kwanza tutizame hali ya Vanessa Larry pamoja na Tropina nampigia simu Kim ajiandae kuwapokea. Alizungumza Jimmy aliyekuwa akimtuliza Jimmy na kutoa ishara kwa Lucretius amzuie asifanye kitu chochote cha kipumbavu.
Vanessa aliweza kuingizwa chumba cha emergency kwaajili ya matibabu zaidi na Dr Kim.
" Kim muwekee umakini Vanessa, hakikisha unamsaidia kwa hali yoyote ile" alizungumza Vikram.
"Dr, aliita nesi aliyeweza kumuingiza ndani Vanessa.
Alitikisa kichwa ishara ya kwamba amefariki.
" unamaanisha nini?? Aliuliza Vikram akimsogelea Nesi yule.
"Amefariki" alisema nesi na maneno hayo yaliyoweza kumfikia Larry ambaye alishazinduka.
"Nani kafa?? Aliuliza Larry na kusogea pale.
Mwili wa Vanessa uliweza kutolewa ukiwa umefunikwa mpaka juu.
Larry aliwazuia na kwenda kufunua ili kudhibitisha je ni kweli au anaota.
Alilishika shuka na kufunua hapo aliweza kukutana na uso wa Vanessa uliokuwa umefunga macho yake, mdomo wake pamoja na pumzi zake.
" mama, mama..... Embu amka acha kufanya hivyo unavyotaka kufanya kwasasa...... Amka eti fumbua macho yako"
"Nini kinaendelea hapa?? Aliuliza Tropina ambaye na yeye aliweza kuzinduka na aliletwa na askari akiwa na pingu mkononi.
" Kwanini unalia?? Aliuliza Tropina na kutembea mbele zaidi kwaajili ya kuona kipi kinachoendelea.
***** ****** *****
"Mama nilihitaji unisaidie kitu lakini sasa mambo yote yameenda sawia kama nilivyokuwa nahitaji ila kwasasa kimebaki kitu kimoja tu ndoa, ndoa yangu na Vikram ndicho kilichoweza kubaki na itabidi nimtumie Larry ili aweze kunisaidia kwahilo" alizungumza huku akimlisha chakula mama yake na Alice ambaye alikitema na kumtemea.
"Mimi nakusaidia hapa usife wewe unaniona Mimi mjinga? Aliuliza Alice.
" Nani anahitaji msaada wako niuwe niuwe kama ulivyoweza kumuuwa mume wangu pamoja na mwanangu Alice niuwe, ila nakuhakikishia ya kuwa ipo siku ipo siku yako tu utalipa kwahaya yote nakuahidi " alisema mama yake Alice na kumfanya Veronica acheke sana.
***** ***** ****
"Kwanini Tropina alianguka, anashida gani Mara kadhaa amekuwa akihisi kizunguzungu na....... Kabla hajamaliza kuzungumza Tropina alitokea.
" Dr hizo ni information zangu sitopenda mtu yoyote yule aweze kuambiwa" alizungumza Tropina na kuondoka zake akiwa amefungwa pingu Mkononi.
Vikram alisimama na kumfuata Tropina.
"Pinah........
" toka mbele ya uso wangu..... Sihitaji kuina sura yako na sihitaji ukae katika nyumba yetu nahitaji uondoke..... Alizungumza na kuondoka zake Tropina huku akimpush Vikram.
Larry aliweza kuyaona yote Yale na hakuwa na lakusema.
"Larry..... Aliita Vikram na kutaka kumfuata.
"Usinisogelee mtu mbaya sana wewe ulisema utamsaidia mama yangu pamoja na dada yangu lkini hujafanya chochote mama yngu amekufa Leo na dada yangu anakufa kesho, huna chochote ulichoweza kukifanya" alizungumza Larry huku akimtupia lawama Vikram na kuondoka zake.
Vikram miguu ilimuishia nguvu n kujikuta anataka kudondoka lakini alizuiliwa na Jimmy.
"Mfuate Larry hakikisha afanyi kitu chochote cha kijinga....nitaenda kumtoa Tropina Leo usiku haijalishi itakuwa hatari kiasi gani ila nitamtoa Leo usiku andaa watu wote wale ambao tuliweza kuwapanga" alizungumza Vikram
Jimmy alitoa heshima na kuondoka zake.
"Vikram nafikiri hii inaweza ikasaidia alizungumza Dr Kim na kumpa faili la Tropina aliyekataa faili lake asipewe mtu yoyote yule.
Vikram alifungua na kutabasamu baada ya kusoma faili lile.
" Tropina anamimba ya miezi miwili na siku 10 hivyo ukipeleka hii Mahakamani lazima watasogeza tukio la kunyongwa mbele na hiyo itachukuwa miaka mitatu au mitano mpaka pale mtoto atakapo kuwa hivyo tutatumia njia hiyo kumtorosha" alizungumza Dr Kim.
"Kwahiyo Tropina anamimba yangu namaanisha anamtoto wangu mimi,"
"Ndiyo"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Basi Alice naenda kumuuwa mtoto wa Tropina ananitosha Mimi kabisa" alizungumza na kuondoka huku dr Kim akimfuta na kumzuia asifanye hivyo.
**** **** *****
Kulikucha asubuhi na watu waliweza kuwasili katika nyumba ya Vanessa kwaajili ya kujiandaa na taratibu za mazishi.
Larry alikuwa amekaa tu hku akiitizama maiti ya Vanessa iliyokuwa mbele ya macho yake.
Hpo hapo aliweza kuletwa Tropina akiwa na pingu Mkononi picha nyingi ziliweza kupigwa na waandishi wa habari hku wengine walianza kumsogelea na kumuuliza maswali.
"Toa mwili wako mbele ya macho yngu" alizungumza Tropina akimwambia mwanahabari mmoja aliyekuwa kasimama mbele ya macho yake.
Aliweza kutoka na Tropina alielekea mpaka mahali ulipoweza kulazwa mwili wa mama yake.
Akiwa pale Alice aliweza kuja na yeye eneo lile alitaka kumfuata lakini aliweza kushikwa Mkono na Larry huku akimpa ishara ya kuwa asiendee Alice aliweza kuongozana na Adrian pamoja na Mr mpalila.
"Alice, wewe ndiye uliyeweza kusababisha umauti wa Vanessa inawezekana je ukaja tena kwenye mazishi yake??
Alice alianza kulia.
" Madam Vanessa ni bossi wangu Mimi na haijalishi alitaka kuniiuwa Mimi nilipokuwa hospitalini lakini nilifuta kesi juu yake, sikuhitaji kuwa na kinyongo juu yake pia najisikia vibaya sana kwamba mwisho wa siku niliweza kuyatoa maisha yake wakati nikiyatetea maisha yangu natamani hata muda urudi nyuma ili nimruhusu yeye anipige risasi Mimi ili asiweze kupoteza maisha"
"Na ni kipi chanzo cha ugomvi wenu?? Aliuliza mwingine.
" alikuwa akinihisi vibaya kwamba Mimi namchukulia mume wake Adrian ndyo maana akawa anayafanya yote hayo.......nilijitahidi kumwambia Mara nyingi niwezavyo lakini hakutaka kunisikia yeye alihitaji kuniiuwa tu" alisema Alice na kuendelea kulia.
Wakati akiyazungumza yote hayo Tropina alikuwa akilia na machozi mengi yakimtoka huku akiwa amekunja ngumi kwa hasira.
Ghafla alihisi kichefuchefu na alielekea pembeni kwenda kutapika wakati hayo yakitendeka Alice aliweza kuliona hilo na alikumbuka Tropina alimuliza.
"Unafikiri wewe pekee ndiye mwenye mimba ya Vikram??
Alikumbuka usemi huo na hapo hapo akasema
" hapana haiwezekani"
"Kipi kisichowezekana aliuliza mwanahabari mmoja.
" hapana Tafadhali nimechoka nahitaji kwenda kuona mwili wa marehemu.
Alizungumza na kusonga mbele akimfuata Tropina alipoweza kuelekea.
Wakati akifanya hivyo Vikram alikuwa pembeni akimtizama kisha akaiweka silence bastola yake na kumfuata nyuma Alice.
Alice aliweza kuelekea hadi jikoni na kumtafuta Tropina. Vicky aliweza kumuweka target na kutaka kumshambulia lkini ghafla alizuiliwa na mtu akiw nyuma yake.
"Hata Mimi nataka afe lakini siyo kirahisi hivyo" alizungumza Diana.
"Sihitaji kabisa kumuona mbele ya macho yngu huyu mwanamke ameniendesha sana sihitaji tena kumuona mbele ya macho yangu" alizungumza Vikram na kutaka kumpiga tena..
"Natambua ila tambua ya kuwa Vanessa hakuhitaji wewe ufanye hivi kwaajili ya mtoto wako kumbuka Alice ana mimba yako"
"sijali tena kwani Tropina anamimba yangu tena anamtoto wa kiume siwezi kumuacha hai huyu" aliendelea kujielezea Vikram.
"Unafikiri Vanessa hakujua ya kuwa Pinah alikuwa na mimba yako alitambua hilo, ila hakutaka wewe ufanye hivi kwani utauwa kiumbe kisichokuwa na hatia" alizungumza Diana.
"Lakini........
" Vikram, fanya vile Vanessa alivyohitaji ufanye Tafadhali " aliomba Diana na kuanza kuichukua bastola ile mkononi mwa Vikram aliyeweeza kudondoka chini na kulia kwa hasira na kwa kigugumizi.
Waliweza kwenda kumzika Vanessa na wakati wote huo Vikram aliweza kujificha ili Tropina asiweze kumuona wala Larry.
"Ni wakati wa kuweka mashada kama hatua ya mwisho ya kumsindikiza marehemu alale salama"
Alizungumza padri na wa kwanza kuweka ua alikuwa Larry kisha akafuatiwa na Tropina huku nyuma yake akiwa Vikram.
"Unafanya nini hapa?? Aliuliza Tropina baada ya kumuona.
" Tafadhali naomba tumalize msiba wa mama kisha tutaenda kuzungumza mambo mengine pembeni. Alizungumza Vikram.
"Sihitaji Tafadhali ondoka alizungumza Tropina na kutupa shada la mauwa.
" sihitaji kukuona hapa Tafadhali ondoka toka... Toka" Tropina alianza kumfukuza Vikram.
"Tafadhali achaaa" alizungumza Larry kwa sauti ya ukali.
"Sihitaji mtu wa kumsumbua mama yngu kwasasa hivi Tafadhali nawaombeni" alizungumza Larry akitizama Tropina na Vikram.
"Sasa mwambie huyu aondok.....
..." Hakuweza kumalizia sentensi yake na aliweza kuzimia kifuani kwa Vikram.
"Pinah" aliita Larry na kusimama katika kaburi aliloweza kulikalia.
"Usiogope Larry yuko salama, ni kutokana tu na hali aliyonayo" alizungumza Vikram.
"Hali gani?? Aliuliza Alice.
Vikram alimtizama kwa hasira kisha akatabasamu na kumwambia.
" ana mimba yangu, namaanisha anamtoto wangu Mimi yani mtoto wetu Mimi na yeye"
Alice alishtuka baada ya kusikia maneno hayo.
Baadaye pembeni alikuwa akihangaika huku na kule
"Hapana haiwezekani......... Siwezi muacha akawa na mimba ya Vikram kwani Vikram hatonijali tena Mimi inabidi nifanye kitu juu ya hiyo mimba yake"
***** ***** *****
Muda wa mahakama ulifika na ulikuwa ni wakati wa Tropina kuweza kunyongwa.
Tropina moyoni alijiongelea.
"Alice unafikiri nitakufa kizembe hivi......sahau hiyo...haiwezi kuwa kirahisi namna hii" alisema Tropina na kutabasamu.
"Samahani samahani hamuwezi kufanya hivyo kwasasa" alikuwa ni Vikram aliyeweza kuwasili na Dr Kim.
"Kwanini??? Aliuliza hakimu.
" ana mimba yangu, hivyo hamuwezi kumuuwa mwanangu yeye hana hatia yoyote ile" alizungumza Vikram na kutoa bahasha ya kaki kisha kumpatia hakimu ambaye alizipitia na kuwapitishia wazee wa baraza la mahakama.
Baada ya kujadiliana kwa dakika 7 hakimu alisimama mbele ya muhadhara.
"Kutoka na kizibitisho kilichoweza kuletwa hapa basi atakaa gerezani kwa miaka 7 kisha adhabu hii itafanyika juu yake" alimaliza kuzungumza hakimu na kuondoka zake.
"Umeona Alice hiyo, najua imekuumiza roho sasa nataka nikwambie utanitambua vizuri, nitamtumia mwanaum unayempenda wewe kukuumiza wewe" alizungumza na kutabasamu huku akimtizama Alice aliyekuwa akiweweseka.
Tropina alishushwa katika kitanzi kile na kuanza kupelekwa mahabusu tena kabla ya kupelekwa gerezani.
"Kwanini hukuniambia ya kuwa una mimba yangu? Aliuliza Vikram.
" Sikukwambia? Aliuliza Tropina na kutabasamu. Ni kwasababu sitaki kuwa na mtoto na mwanaum kama wewe. Alizungumza Tropina
"Unamaanisha nini unaposema hivyo?? Aliuliza Vikram.
" namaanisha tumbo langu haliwezi kubeba uchafu wako hivyo nitaitoa muda siyo mrefu "
"Pinah kuwa makini na maneno yako, huyo ni mtoto wangu Mimi"
"Hata Mimi najua ni mtoto wako Ndiyo maana nataka nimtoe"
"Pinah usidhubutu kufanya jambo lolote lile na ukichaa juu ya mtoto wangu nakuapia sitakusamehe, sitakusamehe kabisa" alizungumza Vikram na kumsogelea Tropina kwa makini.
"Alice Ndiyo anaweza kuuweka uchafu huo tumboni mwake lakini siyo katika tumbo langu Mimi nakuhakikishia nitautoa ujauzito huu" alizungumza Tropina na kuondoka.
" Nakuapia ukijaribu kufanya hivyo sitakuacha mzima Pinah kumbuka hilo" alizungumza Vikram na machozi mengi yakimtoka huku akimfuata Dr Kim.
"Kim hakuna njia yoyote ya kumtoa mtoto wangu tumboni kwa Tropina amesema atamuuwa" alizungumza Vikram.
"Hapana bado mdogo sana haitawezekan wala hakun mama atakaye hitaji kumuuwa mtoto wake"
" lakini Tropina kasema hivyo, kasme atamuuwa"
Alice aliweza kusikia maneno Yale na aliweza kukumbuka siku aliyokuwa na mimba na aliweza kumwambia lakini Vikram alimpleka kwa Dr na baada ya kudhibitisha hilo alimwambia atoe mimba
"Kwahiyo mimba yangu Mimi ulihitaji uitoe ila mimba ya Tropina hutaki aitoe sindiyo" alizungumza kwa hasira Alice.
Wakati huo Tropina alikuwa ndani ya defender na aliweza kushika tumbo lake huku akisema.
"Nitakutenganisha kidogo na baba yako hii ni kwaajili ya usalama wako mwanangu utanisamehe kwa hilo, na naamini sasa Alice atahitaji wewe utoke tumboni mwangu ila nimeshaandaa njia za kukupambania. Alizungumza Tropina na kutabasamu
Larry akiwa nyumbani huku akitizama picha ya mama yake Vanessa.
Aliingia Queen na kukaa pembeni yake Larry aliinua macho yake na kumtazama tu bila kusema neno lolote lile.
Queen aliichukua mkono wa Larry na kuushika huku akimpa ishara ya kuwa yuko salama.
Hapo hapo waliweza ingia wanafunzi wenzake kwaajili ya kumpa pole huku Collin's akiwa kiongozi wao.
Alimtizama Queen aliyekuwa kakaa karibu kabisa na Larry kwa uwivu na kumtazama Larry kwa hasira sana.
Queen alimtizama na yeye kwa hasira huku kukionekana kama Kuna kitu kilichoweza kuendelea katikati yao.
Baadaye kidogo Queen akiwa ametoka chumbani kwa Larry baada ya kupumzika alikutana na Collins aliyeweza kumpita lakini Collin alimuita.
"Kwanini unajifanya kama vile hunitambui na hakuna chochote kilichoweza kuendelea baina yetu??
Queen aligeuka na kumtizama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza tena kupiga hatua.
"Kama hutakaa karibu na Mimi na kuachana na Larry basi kile kilichoweza kutokea siwezi wacha kumwambia Larry" alizungumza Collins.
"Kwamba nilikubusu nikidhani ni yeye, msubiri kidogo amke kisha umfuate na kumwambia alizungumza Queen na kuondoka.
" siwezi mwambie hapo tu lazima niongezee"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Lakini hakuna kingine nilichoweza kukifanya zaidi ya hicho tu, sikufanya kingine" alizungumza Queen kwa kuhamaki.
"Ndiyo najua hatujafanya kingine lakini nitamwambia hatukuishia hapo tena nitamwambia ya kuwa unajifanya uko karibu naye ili kumteketeza yeye kama Dada yake alivyoweza kumteketeza Dada yako, alafu unanishangaza sana hivi Dada yako.......... ."
"Collins!! Aliita Queen kwa hasira.
" waoooo kumbe unalifahamu jina langu.
Queen alimsogelea tena kwa ukaribu zaidi.
"Dada yake Larry hajafanya kitu chochote kile kwa Dada yangu.......namaanisha WiFi yangu Mimi hajafanya chochote wala kutenda chochote kwa WiFi yake......na kitu kingine, huo mdomo wako huo uuchunge kwamaana huwezi kujua nina uwezo wa kufanya nini juu yako, usitake kujua nikichukia huwa nafanya nini,? Alizungumza na kurudi nyuma kisha akaondoka zake.
" Sawa tuone, itakuwaje siwezi kukuachia wewe kwa Larry hata kidogo" alizungumza Collins na kuondoka mazungumzo hayo Larry aliweza kuyasikia yote alirudishia mlango wake na kurudi kitandani.
****** ***** ****
"Hivi ni kweli kabia Tropina anataka kutoa mimba ya Vikram, hapana najua hawezi kufanya hivyo haijalishi ya kuwa anamchukia Vikram kiasi gani hawezi kufanya hivyo kwani hakuna mama anayeweza kumtoa uhai mtoto wake hivyo Tropina Kuna game analolicheza kweli? Alijiuliza huku akipelekea red wine yake katika mdomo wake na kutabasamu.
****** ***** *****
"Umetoka wapi?? Alikuwa mama yake Queen aliyekuwa amekaa kwenye kochi na kuzimaa taa kwani tayari ilishakuwa saa mbili usiku.
" ammmmhh mama kwanini umezima taa? Aliuliza Queen huku akijishika shika nguo yake.
"Nimekuuliza umetoka wapi??? Alirudia tena swali lile mama yake Queen.
" Zena, embu muache mtoto Tafadhali achana naye kabisa" alizungumza baba yke Queen.
"Lakini wote tunajua kuwa ametoka wapi? Alizungumza Zena.
" Ndiyo tunaelewa lakini muache mtoto, Queens elekea chumbani kwako ukapumzike.
Queen alitoa ishara ya kukubali kwa kichwa kisha akaondoka zake.
"Queen aliita Zena.
" sitaki tena nikuone unaenda kwenye nyumba ya wauji, tena sitaki kabisa hayo mazoea uliyoweza kuyaanzisha na huyo Larry nafikiri tumeeleewana.
Queen hakusema neno zaidi ya kuendelea kuelekea ndani kwake.
"Kwnini umesema nimuache huoni ya kuwa anachofanya siyo sahihi?? Aliuliza Zena.
" Natambua siyo sahihi wala umri wake hauruhusu kufanya hivyo ila inabidi tumuache kwa sasa kwani yeye amechanganyikiwa zaidi yetu na hapo alipo hajui kama anachofanya ni sahihi au siyo sahihi"
Wakati huo Queen aliingia ndani na aliweza kukumbuka tukio Flani ambalo hawezi kulisahau.
Siku ya tukio alipokuja kukamatwa Larry na yeye hakuwa mbali na nyumba ya kina Larry hivyo alimuona akitolewa kwa geti la nyuma na kuingizwa kwenye gari alimuamuru dereva wake alifuatilie nyuma na ndipo alipoweza kufika katika jumba lile alimuacha dereva wake katika gari kisha yeye akaingia huko ndani na alipoweza kufika alikuta Alice akizungumza na simu na kuhitaji mtu afike eneo lile kisha alipoweza kutizama Larry kalala chini mbele yake kidogo aliweza kuziona maiti nyingine mbili.
Hpo hpo aliweza kulipa watu wale pesa na kusema Larry atolewe katika mfuko ule ulioweza kuletwa.
Queen aliamua kutoa simu yake na ku record video hivyo kila kilichoweza kuendelea kabla ya kuja Tropina na baada ya kuja ameweza kuki record katika simu yake kumbukumbu zake ziliishia hapo kisha akarudisha tena kumbukumbu zake baada ya kukaa kitandani kwake na kuchukua mto ambao aliweza kutoa kikaratasi kidogo cha daftari.
Baada ya kusikika ving.ora vya polisi aliweza kukimbilia katika gari lake baada ya dereva wake kuja kumchukua na kuondoka naye eneo lile alipofika nyumbani alitoa simu yake na kutoa memory iliyokuwa na ushahidi huo na baadaye aliweza kuziona taarifa za habari zikimshtumu Tropina kwa kuuwa watu.
Aliichukua memory yake na kuelekea kwa Josephat lakini alishindwa kumpatia baada ya kumkuta akiwa na Adrian na Alice wakizungumza namna gani wanaweza kummalizia mbali Tropina kwani hana ushahidi. Hivyo alirudi nyumbani bila kusema chochote kile wala kumwambia mtu yoyote yule juu ya kile alichonacho .
Kulikucha asubuhi na ilikuwa ni siku ya kuweza kumuhamisha Tropina kutoka kwenye mahabusu na kupelekwa gerezani kwanza kwaajili ya kutumikia kifungo cha miaka 7 kabla ya adhabu ya kifo.
Larry aliweza kuwasili akiwa na Jimmy ambaye kwasasa ndiye aliyekuwa mlinzi na dereva wake.
Hawezi ruhusiwa kuzungumza na mtu yoyote kwasasa kwasababu tunamuhamisha.
"Sawa tutakuwa nyuma yenu tukiwafuata mpaka huko mnakompeleka kwani tunamaongezi naye ya muhimu sana.
George alikubali na gari za polisi zilikuwa mbele huku ya kwake ikiwa iko nyuma na Larry.
" kitu gani hicho cha muhimu unachotaka kumwambia Dada yako?? Aliuliza Jimmy.
Larry hakuzungumza kitu zaidi ya kushusha pumzi ndefu na kutizama vidole vyake.
***** ****** *****
"Bossi huyu hapa na yeye ni mmoja kati ya wafungwa wa gereza lile" alizungumza Dr kim aliyekuwa akimpa taarifa hizo Vicky.
"Nataka umlinde huyu......alitoa picha ya Pinah na kuweka mezani.
" haswa haswa kijana wangu Mimi aliyetumboni mwake kila wiku ntakuwa nakupa laki2 kwa kumlinda yeye"
Hakuwa mmama wala msichana bali mwanamke mwenye makamo ya kati.
"Picha yake Ndiyo hii,?? Aliuliza na kuikamata picha ya Tropina.
" Ndiyo huyo na kingine sitaki ajue kuwa unamlinda wala sitaki atambue kuwa Mimi nimekuweka wewe kama mlinzi wke nimeshaongea na afisa mmoja hivyo ataletwa kwenye gereza yako Tafadhali umuwekee umakini" alizungumza Vikram .
"Na tayari nimeshakufungulia account na nimeweka million1 hiyo ni pesa ya kumlinda kwa wiki tano za mwanzo kwani siwezi muacha akamzalia kijana wangu gerezani hivyo hatakaa hata kwa miezi 6 maneno hayo aliyaongelea rohoni tu.
"Kwanini unahitaji kuonana na Mimi?? Aliuliza Tropina.
" Vikram alinambia una mimba yake??
"Huyu mwanaum ni mpuuzi nini, alinung.unika chinichini.
" kwahiyo??? Aliuliza Tropina.
"Usiitoe hiyo mimba ni Mjomba wangu Mimi tena wa kiume uruhusiwi kufanya hivyo" alizungumza Larry
Pinah alimtizama na kumuuliza.
"Ndicho kilichokuleta?? Aliuliza Tropina.
" Kingine nahitaji kujua kwanini yule secretary wa Adrian aliwauwa wale wawili, alafu mbona Josephat nilimpa cheni ambayo nilipewa na Danielle kabla hajafa nimeenda polisi wamesema hakuna ushahidi wa namna hiyo, alafu nimekuta picha za mama akiwa anampa begi jeusi walizosema Kuna pesa ndani na........'
"Huwezi elewa kwasasa hivi mambo ni mengi sana unatakiwa urudi shule mengine yote yaliyoweza kubaki nitayafanya Mimi" alizungumza Tropina.
"Nitawezaje kurudi shuleni sasa na wewe bado uko huku hata sielewi kipi cha kufanya juu yako"
Larry aliita Tropina na kumshika mikono,
"Elimu ni kitu muhimu sana katika maisha yako na yangu pia kwa ujumla, tazama sasa ziko wpi Mali baba na mama walizoweza kuzichuma zote hazipo tena mikononi mwetu, lakini tizama elimu yangu hakuna yoyote aliyeweza kunichukua kutoka kwangu"
"Hiyo elimu yako imekusaidia nini sasa mbona upo gerezani sasa na umehukumiwa kunyongwa? Aliuliza Larry.
"Sikuwa na ushahidi wowote ule wala uwezo wa kujitetea kwani ni kesi ya mauaji, ila nakuhakikishia nitamaliza hii kesi na wewe nataka uniahidi kitu kimoja tu kwaajili ya kumlinda Mjomba wako na kurudisha mali zetu basi inabidi ufanye vitu viwili" alizungumza na kumtizama larry aliyekuwa akimtizama kwa makini.
Baada ya muda Larry alionekana kutoka katika gereza hilo huku akiwa mwingi wa mawazo sana.
Gari la Vikram liliweza kuingia pale pale.
"Umezungumza na Pinah, amekwambiaje kuhusu mtoto wangu, bado tu anataka kumtoa?? Aliuliza Vikram kwa mkupuo.
" Mwache afanye kile atakacho" alizungumza Larry na kuondoka.
"Unamaanisha nini bwashe? Aliuliza Vikram.
" Alice ndo chanzo cha yeye kuwa gerezani alafu pia na Alice anamtoto wa kiume, nimeongea na dada yangu na nimeshaelewa kila kitu uliwezaje kumleta mwanamke mwingine chumbani kwa Dada yangu na ulale naye alafu nguo yake ya ndani ukampa Dada yangu. Alizungumza Larry kwa hasira.
"Pinah amekwambia nini?? Aliuliza Vikram kwa mshangao.
Larry alimtizama bila kusema neno na kwenda kupanda kwenye gari kisha Jimmy akawasha gari akimtizama Vikram aliyekuwa akielekea sero.
" Umemwambia Larry, kwnini amebadilika ghafla na anasema ufanye chochote ukitakacho kwaajili ya mtoto wangu?? Aliuliza Vikram.
"Ndo kilichoweza kukuleta hapa?? Aliuliza Tropina.
" Ndiyo"
"Sawa nimemwambia vile nilivyoweza kujisiikia kumwambia" alizungumza na kuinuka zake.
"Lakini umemdanganya Pinah ilihali mimi nilikwambia ukweli kila kitu nilikwambia zile nguo za Alice nilizitupa na nikaenda kununua zingine kwanini sasa wewe, umemdangany Larry, au Unataka Larry anichukie Mimi kama wewe unavyoweza kunichukia mimi? Aliuliza Vikram kwa sauti ya upole sana ambayo ilimfanya Tropina adondoshe machozi na kuelekea ndani ya gereza.
***** ***** ****
Larry akiwa ndani ya gari aliweza kukumbuka maneno aliyoambiwa na dada yake cha kwanza ni Kukaa mbali na Vikram na kujifanya anamchukia ili Alice asiweze tafuta mbinu yoyote ile ya kumteketeza Mjomba wake kwa kumtumia yeye, na kitu kingine anahitajika kusoma ili azikomboe kampuni zao.
" Sawa Dada nitafanya vile utakavyoo kwaajili ya mjomba wangu n kwaajili ya kile alichoweza kukiacha baba na mama...bwashe utanisamehe nahitaji kufanya hivi kwaajili ya kumlinda mtoto wako" baada ya kuzungumza hayo kimoyomoyo alisema kwa sauti.
"Kesho nitarudi shuleni nahitaji unifanyie maandalizi ya vitu vidogo vidogo kabla ya Kesho"
"Sawa" alijibu Jimmy na kutuma msg kwa Dr Kim.
"Kamchukue Vikram , sidhani kama ataweza kuendesha gari"
Dr kim aliisoma na kutoka katika chumba chake cha ki Dactari.
Alipotoka tu aligongana uso kwa uso na Alice aliyekuwa akitaka kuingia ndani.
"Dr. Kim nahitaji kuzungumza na wewe, kwamaana mume wangu Vikram amenambia wewe ni dactari wake kwahiyo dactari wa mume wangu ni dactari wangu pamoja na mwanangu"
Dr Kim alimtizama bila kusema neno lolote lile bali aliufungua mlango wake kwa hasira na kumwambia.
"Ingia ndani"
"Anashida gani huyu Dr mbona anaonekana kama hanipendi alizungumza na kumfuata nyuma huku akijiuliza kwann hapendwi na Dr Kim.
***** ****** **
" Kesho narudi shuleni na wew inabidi ufanye hivyo " alizungumza Larry aliyekuwa amekaa sehemu moja na Queen.
"Sawa nitafanya hivyo" alizungumza Queen aliyekuwa ameshikilia kikaratasi kile chenye memory.
"Utakuwa unakuja kunitembelea siku za jumapili?? Aliuliza Larry.
" eeeeeyhhhh, nije shuleni kwenu? Aliuliza kwa kutahamaki.
"Ndiyo au Kuna mtu unamuogopa??
" ha...Hamna....Hamna......nitakuwa nakuja usijali kuhusu hilo" alizungumza Queen huku akiwa anawasiwasi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Queen"
"Abee"
Larry aliingiza Mkono wake mfukoni kisha akatoa cheni na kusogea mpaka nyuma ya Queen na kumvisha cheni ile.
"Najua sisi bado wadogo sana na umri wetu hauruhusu kufanya au kuongea chochote nitakachoweza kukizungumza hapa"
Unamaanisha nini?? Aliuliza Queen na kutaka kugeuka ila Larry alimzuia asigeuke.
Alikaa nyuma yake na kupitisha mikono yake katika tumbo la Queen kisha akamkumbatia kwa kuikutanisha mikono yake na kuweka kidevu chake katika bega moja la Queen.
"Nakupenda sana Queen na sihitaji nikupoteze wewe kwa Collins, sihitaji nipate shida na mateso kama anayoyapata Bwashe wangu juu ya Dada yangu"
"Larry, kuhusu Collins........."
Larry alimpiga busu kwenye bega lililomfanya Queen ashindwe kuongea.
"Najua niliwasikia mkiongea, sitopenda tena unifananishe na mwanaum yoyote yule tena haswa haswa Collins"
"Sawa sitafanya tena hivyo, ila nahitaji kuonana na Pinah unaweza ukanipeleka huko kabla ya kwenda shule kesho? Aliuliza Queen akitizama Mkono wake uliokuwa na kikaratasi alichoweza kuhifadhia memory.
" Sawa" alijibu Larry na kumpapasa vidole Queen aliyeweza kutoa Mkono wake kwani Ndiyo uliokuwa na memory.
***** ***** *****
"Nilisikia Unataka kutoa mimba, unafikiri Mimi nitaamini hilo, wataamini hao hao wajinga watakaoweza kukuamini ila siyo Mimi tena nataka nikuhakikishie ya kuwa hiyo mimba utaitoa tu iwe Unataka au hautaki kwasababu hatuwezi kuwa wote na watoto wa kiume kwaajili ya Vikram. alizungumza Alice na wakati huo Queen alikuwa amefungua mlango kwaajili ya kuingia ndani na wakati huo aliweza kuweka record kwenye simu yake wakati anapozungumza na Tropina aweze kurecord kwani pia ingeweza kusaidia katika upande wa ushahidi kama kesi itarudiwa tena pindi atakapokataa rufaa ya kesi.
" Unajua Larry na yeye aliweza kumuuwa mama yangu?? Alizungumza Alice.
"Unamaanisha nini unaposema kuwa Larry kamuuwa mama yak?? Aliuliza kwa hasira Tropina.
" shshshs punguza sauti, siyo kwamba ameshamuuwa lakini atakwenda kumuuwa kama wewe ulivyoweza kumuuwa Danielle na Mr Harlan pamoja na Winnie kwaajili ya mimi kumpata Vikram, basi Larry na yeye atamuuwa mama yangu ili akae gerezani kama wewe " alizungumza Alice.
"Unataka nini tena kutoka kwngu?? Aliuliza Tropina.
"Kitu kimoja tu kwani hicho cha pili kitatokea baada tu ya wewe kufanya hicho cha kwanza. Alizungumza Alice na kucheka kwa dharau.
" unahitaji nini???
"Mwanao afe mwanangu abaki hai, hivyo tu...... Alijibu Alice na kutoa vidonge kisha akampatia Tropina.
"Ni vidonge vya kutoa mimba hivyo nakupa siku Tatu Leo kesho na kesho kutwa kama hutatoa hiyo mimba basi utamuona Larry akiwa nyuma yako" alizungumza na kwenda kufungua mlango ambako alikutana na Queen aliyejifanya alikuwa akiingia ndani saa hiyo hiyo.
Alienda mpaka kwenye kiti na kukaa.
Tropina alimtizama kwani alionekana kuwa na wasiwasi.
"Queen!!! Uko salama wewe?? Aliuliza Tropina.
" Ndiyo me naenda" Alisema na kusimama kwenye kiti alichokuwa amekaa.
"Lakini Unaonekana unawasiwasi sana Kuna chochote ulichoweza kukisikia aliuliza Tropina wakati huo Queen alikuwa akiishilia mlangoni.
Alipofika njee alikutana na Alice mbele ya macho yake kabla hajazima record yake.
" Ulisikia nini wewe mtoto?? Aliuliza Alice na kumfanya Ashtuke Queen aliyekuwa akitaka kuisave record yake.
"We ulitaka nisikie nini?? Aliuliza Queen akijikaza.
" Ni bora kama umesikia ukakae kimya usije ukapeleka kiherehere chako kuisababishia familia yako matatizo" alizungumza Alice.
"Hivi unafikiri kila mtu anakuogopa au? Aliuliza Queen na kumsogelea kwa karibu.
" Mama na baba yngu wote wako juu ya miaka 40 hata wakifa sasa hivi hawna maana tena kwamaana wameshaishi maisha ya kutosha dada yangu tayari uli................ Tafadhali usinitibue" alizungumza Queen na kuelekea kwenye gari ila kabla gari halijaondolewa alifungua kioo na kumwambia.
"Ikitokea Larry akakatwa ata ukucha wake bila ridhaa yake utanitambua Mimi ni nani??
"Hahahahaha haka katoto ka nani kana ujasiri hivi" alizungumza Alice na kusogea kwa karibu.
"Kama unadhani nakutania jaribu sasa kuugusa hata unywele wake hapo ndo ambako utajua ya kuwa kwenye lile Jumba hukuwa wewe Larry na Tropina pekee yake bali Kuna mtu aliwasili pasina mwaliko wako" alizungumza Queen na kucheka kisha akamwambia dereva twende polisi nataka kesi ya mauaji ya Dada yangu irudiwe tena.
"Ndiyo madam"
Queen alimshika tena bega Alice kisha akacheka na kumuaga kwa kuendelea kumcheka.
"Mungu wangu anasemaje huyu eti kwenye Jumba nini?? Aliuliza tena Alice aliyeshindwa kuzungumza alipiga simu na kumwambia Daud.
" hilo gari linalotoka hapa gerezani wagonge na uhakikishe ya kuwa wamepoteza maisha na hakikisha huachi ushahidi wowote ule. Alikata simu na kuanza kuvuta kumbukumbu kama vile alihisi Kuna chuma kimeweza kukanyangwa lakini alipotaka kwenda Tropina aliweza kufika hivyo hakuwaza tena. Haiwezekani kama kungekuwa na ushahidi angeweza kuuleta kituo cha polisi au anataka kunitengenezea kesi nini. Aliuliza Alice na kutizma pale alipokuwa kulikuwa na CCTV camera hivyo wakati anagombana na alichukuliwa kama akifa mtu wa kwanza kuhisiwa ni yeye.
"Tropina itakuwa kamwambia afanye hivi ili Mimi niingie matatizoni. Alichukuwa simu yake na kumpigia Daud.
" Naona ametuma mtu aweze kutufuatilia alizungumza derev wa Queen.
"Nilijua tu lazima aingie kwenye mtego alisema Queen na kutabasamu.
"Nitajitahidi kuyaokowa maisha yako jifunge mkanda Vizuri wakati huo Daudi tayari alishaweza kumfikia Queen.
Lakini aliweza kuwapita na kutabasamu.
" mbona hatugongi tena?? Aliuliza kwa hamaki.
"Nafikiri ameshagundua" alizungumza dereva wa Queen jina wale walimuuita Jacob.
Alice alitoka njee na kupiga tena simu kwa mtu mmoja.
"Mpe huyo mwanaharamu simu" alizungumza kwa hasira sana na mtu alipokea simu.
"Tropina unamtumia Queen ani trick Mimi sasa siku zimepungua nakupa na Kesho kama hujanywa hivyo vidonge vya kutoa mimba basi utamuona Larry" alikata simu Alice.
"Anaongelea nini huyu?? Aliuliza Tropina aliyemtizama askari aliyeweza kuleta ile simu na kuisave bossi aliamini ni njia moja na Alice.
"Naomba nimpigie simu mdogo wangu Larry nahitaji kuongea naye kabla hajaenda... . "
"Mfungwa nambari 4747 unahitajika" alizungumza askari mmoja na kumfanya Tropina amfuate.
Alikuwa ni Larry.
"Umekutana na Queen hapo njee?? Aliuliza Tropina.
" hapana kwani ameshafika hapa?? Aliuliza Larry kwa mshangao.
"Ndiyo na nahisi aliyasikia mazungumzo yangu na Alice"
"Alice?? Huyo muuwaji bado anakuja hapa?? Aliuliza kwa hasira Larry.
" Larry shida siyo hiyo bali nahisi alipotoka njee kile alichoweza kukisikia kutoka kwa Alice au vile ulivyoweza kumwambia kipi kilitokea siku ya tukio itakuwa kamwambia Alice na Alice anafikiri labda yeye alikuwapo......hata sielewi ila maisha yake sijui kama yatakuwa salama" alizungumza Tropina
"Pinah unaongea pasina kuweka pumzi sikuelewi, Alice alikuja kufanya nini hapa"
"Amekuja kuniambia nitoe mimba kama mpaka kesho nitakuwa na mimba basi atakutengenezea na wewe kesi kama mimi...Larry kuwa makini ukiwa shuleni usitoke ukaenda popote wala usishike chochote kwa mikono yako ni vizuri ulitumia gloves kila wakati" alizungumza Tropina.
"Ndiyo nimekuelewa" alijib Larry na kutoa kitu mfukoni kwake.
"Nilifanya kama ulivyoweza kuniagiza" alizungumza Larry na alipofungua mfuko vilikuwa vidonge sampuli ya vyakuharibu mimba lakini hivyo vilikuwa vya kuongeza uzito wa mtoto.
"Sawa.... Kuwa makini" alisema Tropina na kumkumbatia mdogo wake kisha akaondoka zake .
***** ***** ******
Larry alifika hapa na kuniomba nimpe vidonge vya kutoa mimba alizungumza Dr Kim.
"Larry" alisema kwa mshtuko na kutokuamini Vikram.
"Ndiyo ila sijampa vya kutoa mimba nimempa vya kumkuza mtoto hivyo.........halo....halo......boss" aaaiiiishshshsh ameshakata simu tena.
"Jimmy uko na Larry hapo?? Alimpigia simu Jimmy.
" ndyo "
"Mpe simu"
"Sawa"
Jimmy alimpa simu Larry ambaye alishusha pumzi ndefu kabla ya kupokea simu.
"Halo"
"Larry, mimba ya Tropina ikitoka nakuapia nitaenda kukufungulia mashtaka sitakuacha mzima" alizungumza Vikram na kukata simu.
"Ukishanifikisha shule utaondoka na sitahitaji tena kukuona.
" kwnini?? Aliuliza Jimmy.
"Kwasababu Mimi na bossi wako ni maadui kwanzia sasa" alisema Larry na kutabasamu tu huku akimini ya kuwa amefanya kazi nzuri.
"Ni nini?? Aliuliza Alice.
"Larry kanunua vidonge vya kutoa mimba na kampelekea Tropina, Sijui kwanini wanataka kumfanyia hivyo mwanangu? Alizungumza Vikram kwa uchungu sana.
" lakini Vicky hata mimi nina mtoto tena wa kiume kama alionao Tropina "
"Tena wewe kama siyo hii mimba wewe Alice wewe ningekwisha kuuwa zamani sana, na usifikirie Mimi nitampenda huyo mtoto wako wala wewe nitamchukia kwasababu amezaliwa na mama wa kipumbavu kama wewe, na mtoto wangu kwa Tropina akifa sababu ni wewe pia kumbuka hilo" alizungumza Vikram.
"Sasa unaenda wapi??
Aliuliza Alice.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Naenda kufungua kesi juu ya Larry kwa kutaka kumuuwa mtoto wangu ili Tropina akamatwe na awekwe katika ulinzi asiweze kumtoa mtoto wangu "
"Anaongea nini huyu, wewe Vikram... Rudi hapa nakwambia alisema Vikram
Aliichukua simu na kupiga tena.
" hakikisha anaitoa hiyo mimba sasa hivi hakuna tena kusubiri mpaka kesho aitoe sasa hivi hivi ikiwezekana itoe hiyo mimba wewe mwenyewe nitakupatia pesa nyingi sana" alizungumza na kukata simu
Afisa yule aliyekuwa mkuu wa gereza kwa upande wa wanawake alielekea mpaka gereza alilokuwa akikaa Tropina na wenzke wawili alitoa ishara na wote waliweza kumvamia na kuchukua vidonge alivyokuwa akivishika pasina uwepo wa mtu ambaye alipewa hela kwaajili ya ulinzi wa Tropina.
Baada ya kumaliza kumpatia dawa ile waliondoka na kumuwekea kitambaa mdomoni kilichoweza kumfanya kelele zisifike mbali huku akiguguma kwa maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Vilionekan vidonge vya aina nyingine vikiwa chini hivyo haikuweza kugundulika ni vidonge vipi ameweza kupatiwa.
Vikram alifika gerezani ili kutoa taarifa hizo lakini alishangaa baada ya kuiona ambulance ikiwa imesimama pale.
"Hapana hii haiwezekani" alizungumza na kushuka ndani ya gari lake. Alipofika karibu na gari lile mgonjwa aliweza kuletwa na alikuwa ni Tropina aliyekuwa akimiminika damu kwanzia sehemu kiuno na kushuka chini.
"Amefanyaje huyu, mtoto wangu yuko wapi?? Aliuliza Vikram.
" Samahani lakini tumekuta vidonge hivi pembeni yake na damu nyingi zikimtoka watu wanasema ni vidonge vya kutoa mimba. alizungumza afisa mmoja wa jela.
"Kwa....kwa.....kwahiyo mi...mi....mimba imetoka??
" wewe huoni damu nyingi hivyo hawezi kuwa na mimba tena hapo anawahishwa hospitalini kusaidiwa maisha yake. Alizungumza afisa yule na Vikram alikumbuka ya kuwa Dr Kim alimuhakikishia ya kuwa amempa vidonge vya kuongeza uzito wa mtoto aliye tumboni.
Alivichukua vidonge vile na kuondoka navyo wakati huo nao ambulance ilishaweza Kuondoka gerezani pale.
Alipofika mpaka hospitalini kwa Dr Kim alitupa vile vidonge mezani.
"Hivi vidonge ndo ulimpatia Larry sindiyo?? Aliuliza Vikram kwa hasira sana.
" Ndiyo Kuna tatizo kwani?! Aliuliza Dr Kim
"Box uliloweza tolea hivi vidonge naliomba" alizungumza Vikram na Dr Kim aliinama na kufungua droo yake ndogo kisha kutoa boksi na kuweka hapo juu meza.
Vikram alilichukua na kumuuliza.
"Hizi ndo dawa za kukuza mimba au za kutoa mimba?? Aliuliza kwa hasira
Dr Kim alilichukua boksi lile na kulitizama.
" heeee" alishnga na kufunguwa tena droo yake lakini hakukuwa na boksi lingine.
"Hilo limetoke wapi huku, Mimi nauhakika nilimpa vidonge la boksi jingine" alizungumza Dr Kim.
"Kwahiyo hili likatokea wapi huku, Kim siwezi kukusamehe kwa kumuuwa mtoto wangu, ondoka ndani ya ofisi yangu na sikuhitaji tena wewe kama dactari wangu" alizungumza Vikram na kuondoka zake akiwa na boksi lile dogo.
Alice alikuwa pembeni tu na kutabasamu huku akiwa ameshikilia boksi lingine mfanano na lile aliloweza kuondoka nalo Vicky.
"Wewe ukiwa dactari wangu Kuna vitu nikikwambia ufanye hutaweza kufanya hivyo na utamwambia Vikram sasa hii Ndiyo nzuri ya kumtafuta Dr nimpendaye miye. Alicheka kisha akatoka eneo lile
Wakati huo wote Dr Kim alikuwa akiwaza na kutafakari inawezekana akawa amempa Larry dawa tofauti na zile alizoweza kumpa.
Wakati huo Tropina alikuwa hospitalini na chumba chake kikiwa kimefungwa na kufunikwa kwa mapazia mekundu.
Mlango wa nyuma wa chumba hicho kilifunguliwa na aliingizwa mgonjwa mwingine aliyekuwa akivuja damu sana.
Tropina aliweza kuamka pale alipokuwa amelala katika kitanda kile kisha akampandisha Diana aliyekuwa akitokwa na damu.
" Dr atakuwa salama kweli? Aliuliza Tropina na kukumbuka ilikuwaje.
Wakati akiletwa katika gereza ile tayari alishaweza kuzungumza na mkuu wa gereza ambaye yupo katika upande wake na kila kilichoweza kutokea baina ya Alice na yeye mkuu wa jela aliweza kuyaona na kuyashuhudia hivyo waliweza kutafuta damu nyingi ili pindi atakapojidai ametoa mimba basi ziwepo damu za kutosha lakini Diana na yeye aliomba asaidie katika hilo kwani ana mimba ya Adrian ambaye aliweza kumbaka na aihitaji kabisa hivyo mimba yake ingeweza kumsaidia Tropina asigundulike ya kuwa hakutoa mimba kama hawatakut ushahidi wa kutosha. Hivyo waliweza kukubaliana naye kwani Diana aliomba sana.
Wakati hao wakipanda kuja kumvamia Tropina na kumuulia mbali mwanaye basi alitoa vile vidonge vya protein na kuviweka pembeni yake huku vya kutoa mimba akawa amevificha mbali na pale.
Hivyo walivyoweza kuja na kumnywesha dawa ile pembeni alishandaa bobo la damu hivyo aliweza kulimwaga baada ya sekunde kadhaa kupita ya kunyweshwa dawa zile.
"Diana utakuwa tu salama wala usihofu" alizungumza Tropina akimshika mikono Diana aliyekuwa akilia kwa uchungu sana.
Baada ya muda mwingi kutokea alitoka dactari aliyeongozana na mkuu wa gereza huku Tropina akionekana kuwa kitandani na kujifanya bado hajapata fahamu.
"Dr mwanangu?? Aliuliza kwa hamaki Vikram.
" samahani mtoto amefariki ila mke wako tumejaribu kumuokowa na tumefanikiwa kufanya hivyo... Baadhi ya sehemu za mwili za mtoto wako nitawaambia manesi wakuandalie kisha ufanye taratibu za mazishi.
Vikram machzo pamoja na hasira zote kwa pamoja ziliweza kumpanda na kujikuta anapinga ngumi kuta za hospitalini.
*** **** ****
Larry akiwa darasani huku anasoma Collin alikuja na kumsogelea kwa ukaribu zaidi.
"Natumaini hujaziona hizi habari kwasababu kwanzia uje unajifanya ya kuwa unasoma sana"
Alitoa ipad yake na kuweka mezani kisha Larry akayatoa macho yake na kupeleka kwenye ile I pad.
"Ahaaaa wewe ndo unasikia hapo sasa hivi Mimi nilishajua hayo kabla hata ya Jana" alizungumza na kurudisha macho yake kwenye daftari lake
"Dada ako ametoa mimba, yani familia yenu yote ni ya wauaji,sihitaji ukae karibu na Queen utamsababishia matatizo" alizungumza Collins.
"Sawa akisema Queen mwenyewe nikae mbali naye nitafany hivyo lakini kama hatasema wewe siyo mtu wa kuniambia Mimi nikae mbali naye kwani huna undugu wowote na Queen" alizungumza Larry na kusimama eneo lile kisha akaondoka zake.
"Mpumbavu huyu" alizungumza Collins na kupiga dawati kwa hasira sana.
*** **** *****
"Pinah, umemfanya nini mtoto wetu, kwanini umeamua kumtoa katika tumbo lako, sawa nakubali Mimi Ndiyo mwenye makosa lakini hukupaswa kumfanya mwanangu alipie kwa dhambi zangu, kwanini sasa umefanya.hivyo kwanini unanifanya Mimi nikuchukie Tropina, amka na uongee na mimi nimekwambia amka?? Alizungumza Vikram na kuanza kumsukuma sukuma Tropina aliyekuwa amejifanya ya kuwa amezimia lakini aliweza kumsikia kwa kila kitu alichokuwa akikizungumza.
Dr aliingia ndani na kumuamur Vikram atoke njee ya chumba kile Vikram alikuja kutolewa na baadhi ya maaskari wa eneo lile walioweza kumleta Tropina.
Tropina alikaa kitandani na kuanza kulia kwa kumsikitikia Vikram ambaye aliweza kuongea maneno ya kuumiza moyo wake.
" Anakupenda sana mume wako na hili uliloweza kumwambia limeweza kumuumiza sana" alizungumza Dr yule akimtizama Tropina aliyekuwa bado analia.
***** ***** ****
Larry alikuwa sehemu tulivu akijisomea na ghafla alihisi Kuna ujio wa mtu nyuma yake.
"Larry umemfanya nini mtoto wangu, kwanini umeamua kumtenganisha mtoto wangu katika tumbo la mama yake?? Aliuliza Vikram akiwa amejaa hasira na machozi mengi yakiwa yanamtoka.
Larry alitizama pembeni kidogo kisha akayarudisha macho yake kwa Vikram.
" Sihitaji uke wenza kwa Dada yangu na pia sihitaji kumuona Mjomba angu akizaliwa akiwa gerezani wakati huo baba yake yuko njee na mwanamke mwingine ambaye anamtoto mwingine, sihitaji Mjomba angu atambue ya kuwa mwanamke unayeishi naye wewe ndiye aliyeweza kusababisha kifo cha bibi yake na ndiye aliyesababisha mama yake akawa gerezani na yeye akazaliwa gerezani, ndomaana nimeamua kufanya hivyo " alizungumza na kusimama zake akihitaji Kuondoka.
"Larry unajua nilikuamini, nilikuamini tena nikakuamini sana sikutegemea kama ungeweza kumpatia Dada yako vidonge vya kuweza kutoa mimba na kumtoa mtoto wangu Mimi , Sasa hapo tofauti yako na Alice iko wapi wewe ni muuwaji na yeye ni muuwaji pia tofauti yenu iko wapi nakuuliza?? alizungumza Vikram na kulia kw kupiga kelele.
" Sawa yeye ni muuwaji na Mimi ni muuwaji nimelipiza kwa kile Alice alichoweza kukifanya "
"Alice kafanya nini katika huyo mtoto au mtoto wangu kawakosea nini nyinyi, Vanessa aliniambia makosa ya mtu mwingine usimpe adhabu mtu mwingine lakini ona ulivyoweza kufanya...... Mtoto wangu ni mdogo kabisa hata hajazaliwa unawezaje kumfanyia hivyo unawezaje?? Alizungumza kwa ukali na kupiga piga miguu yake chini kwa hasira.
" Sawa hajafanya chochote lakini tayari nimeshamuuwa na kama Kuna mwingine aliyeweza kubaki katika tumbo la Dada yangu na yeye nitamuuwa pia" alizungumza Larry na mbele yake aliweza kumuona Queen ambaye baada tu ya kusikia maneno Yale aliweza kuidondosha chakula alichoweza kukibeba kwaajili ya Larry
"Sawa nitakusamehe kwa yote uliyowahi kuyatenda katika maisha yangu lakini siyo hili cwezi kukusamehe hata siku naingia kaburini" alizungumza na kuondoka zake Vikram.
Sasa alibaki Queen na Larry.
Larry aliweza kumtizama Queen aliyekuwa akimsogelea taratibu kabisa.
"Anachokizungumza Vicky ni kweli eti....unaweza ukafanya hivyo?? Hapana namaanisha umempa vidonge Tropina vya kutoa mimba?? Aliuliza maswali mfululizo.
Larry aliweza kukumbuka ya kuwa dada yake alimtaka Siri hiyo iwe ya kwao tu wala asimshirikishe mtu mwingine yule.
Larry alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo na Queen alimpiga kibao.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Queen" aliita tena Larry lakini aliambulia kibao kingine.
"Mwanaume mbaya sana wewe unawezaje ukafanya hivyo eti, unawezaje?? Aliuliza Queen.
" Sihitaji tena mahusiano na mwanaum kama wewe, na wala hutkaa unione tena mpaka siku ya kifo changu " alizungumza na kuondoka.
"Queen" aliita Larry lakini haikusaidia.
Queen alielekea mpaka kwenye gari lake kisha baada tu ya kufunguliwa mlango na dereva wake liliweza Kuondoka.
***** ****** ******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment