Search This Blog

Sunday 19 June 2022

MCHEZA FILAMU ZA NGONO - 2

 





    Simulizi : Mcheza Filamu Za Ngono 
    Sehemu Ya Pili (2)





    Gibson akaonekana kuanza kujisahau kabisa, mara kwa mara alikuwa akifanya mapenzi na Katie hotelini. Alimsaliti sana Prisca lakini katika hayo yote ambayo



    alikuwa akiyafanya, yalikuwa yakimpatia fedha nyingi kwa kumridhisha Katie kwa namna ambayo alikuwa akiitaka.

    Kuanzia hapo hakukuwa na siri tena, mapenzi yao yakajulikana kwa kila mfanyakazi wa kampuni ile ya Utalii katika mbuga ya wanyama ya Mikumi. Mara kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mara walikuwa wakitoka na kwenda katika sehemu nyingine mbalimbali, kimuonekano wa nje, Gibson alikuwa amekwishaanza kubadilika.

    Siku ambayo waigizaji walitakiwa kurudi nchini Marekani ikafika lakini Katie hakutaka kurudi, bado alikuwa akihitaji muda zaidi wa kutanua na Gibson ambaye



    alionekana kuwa kama mpenzi wake wa dhati.

    Akili ya Gibson ilikuwa ikifanya kazi sana na mara kwa mara alikuwa makini sana na kila kilichokuwa kinaendelea katika maisha yake. Kwanza hakutaka



    kuonyesha mabadiliko yoyote yale kwa mpenzi wake, Prisca, kila siku alikuwa akimjali huku kila alipokuwa akirudi nyumbani kwake alikuwa akikaa nae karibu



    sana.

    Ilikuwa ni vigumu sana kwa Prisca kugundua kama Gibson alikuwa ameanza kutoka nje ya uhusiano wao katika kipindi hicho. Mapenzi yalikuwa yameongezeka



    hasa na hii ilitokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikuwa akikipata kila siku.

    “Bado miezi miwili mpenzi nikajifungue” Prisca alimwambia Gibson ambaye akaonyesha tabasamu pana.

    Gibson akaanza kulishaika tumbo la Prisca, tabasamu likaongezeka usoni mwake, maneno ambayo aliambiwa na Prisca yalionekana kumfurahisha kupita



    kawaida. Bado alikuwa akitamani kupata mtoto katika maisha yake, kila siku alitamani kuitwa baba.

    “Nitafurahi nikimuona mtoto wangu. Ninapenda kuiona damu yangu” Gibson alimwambia Prisca.

    Huo haukuwa mwisho wake wa kuendelea kuwa pamoja na Katie, mahusiano yao yalikuwa yakiendelea kama kawaida huku wakiendelea kusafiri sehemu



    mbaimbali na kufanya kila kitu kama wapenzi.

    Bado Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi, moyo wake ulikuwa ukiendelea kumuamini Gibson kupita kawaida. Hata alipokuwa akihoji kuhusu fedha nyingi



    ambazo alikuwa akizipata, majibu ambayo alikuwa akipewa yalionekana kumridhisha kwa asilimia mia moja.

    “Kuna safari tunatakiwa kwenda kesho” Gibson alimwambia Prisca.

    “Safari ya wapi tena?”

    “Mbuga ya Ngorongoro. Kuna wazungu wamepanga kwenye ile hoteli yetu wanataka tuwapeleke huko” Gibson alimwambia Prisca.

    “Na mtarudi lini?”

    “Bado sijajua. Nafikiri bosi akituambie siku ya kurudi, nitakutaarifu simuni” Gibson alimwambia Prisca.

    Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, bado moyo wake ulikuwa ukimuamini Gibson kupita kawaida, kwa moyo mmoja akakubaliana nae. Gibson



    akaonekana kuwa na furaha, hadi kipindi hicho hakuamini kama kweli Prisca alikuwa akikubaliana nae na wakati alikuwa akimsaliti.

    Kiukweli, hakukuwa na safari ya Ngorongoro kama alivyomwambia Prisca bali alikuwa akitaka kupata siku tatu mfululizo kuwa pamoja na Katie. Mapenzi ya



    Katie yakaonekana kumlevya kupita kawaida, fedha ambazo alikuwa akipewa mara kwa mara na mwanamke huyo wa kizungu zikanekana kumteka kupita



    kawaida.

    Safari hii, Kati akalipa kiasi cha dola elfu moja mia tano kwa ajili ya Gibson na kumkabidhi bosi wa kampuni ile. Wote kwa pamoja wakaanza kuelekea Arusha



    ambako huko wakala sana raha na kisha kuelekea visiwani Zanzibar. Katika kila kona ambazo walikuwa wakienda, walikuwa wakipeana mapenzi ya dhati huku



    Gibson akijitahidi kufanya ngono na Katie, ile ngono ya uhakika ambayo ilikuwa ikimchanganya sana Katie.

    Walikaa Zanzibar kwa siku mbili na ndipo wakarudi tena Morogoro.Gibson hakutaka kumwambia Katie kama alikuwa na msichana ambaye alikuwa akiishi nae



    kwa wakati huo, alichokisema yeye ni kwamba alikuwa akiishi peke yake na wala hakuwa na uhusiano na msichana yeyote yule.

    “Kwa hiyo utanioa?” Katie alimuuliza.

    “Muda wowote ukitaka” Gibson alimwambia Katie ambaye akaonyesha tabasamu pana la furaha.

    Katie hakutaka kuendelea kukaa sana Tanzania, alichokifanya kwa wakati huo ni kumuachia kiasi cha dola elfu kumi Gibson na kisha kuelekea nchini Marekani



    huku akiahidi kuwasiliana nae kila siku.

    Maisha ya Gibson yakaanza kubadilika, kila mtu mtaani alionekana kushangaa lakini wala hakuonekana kujali. Shida ambazo walikuwa wamezipitia zikaonekana



    kubaki kuwa kama historia ambazo zingekumbukwa tu vichwani mwao.

    Bado Prisca hakuonekana kufahamu sehemu ambazo fedha zile zilipokuwa zinatoka kwani kila alipokuwa akiuliza, majibu ambayo alikuwa akipewa hayakuwa



    yakieleweka sana. Gibson hakutaka kubadilika, bado mapenzi yake kwa Prisca yalikuwa yakiendelea vile vile, alikuwa akimpenda kupita kawaida huku



    akimfanya kuwa na furaha kila siku.

    Mawasiliano kati yake na Katie yalikuwa yakiendelea mara kwa mara kwa siri, alikuwa akipigiwa simu na kuongea nae, alikuwa akitumiwa zawadi mbalimbali



    pamoja na fedha nyingine nyingi.

    Gibson hakutaka kumsahau rafiki yake, Richard ambaye alikuwa amempa ushauri mkubwa wa kutembea na Katie, mtu huyo ndiye ambaye alionekana mtu



    ambaye alikuwa na ushauri mkubwa katika maisha yake.

    “Sasa si unaona bahati hiyo. Ulikuwa unaogopa nini sasa?” Richard alimuuliza Gibson.

    “Unajua nilikuwa nimefunikwa na ujinga. Asante sana Rich”

    “Usijali. Wewe ni rafiki yangu, hautakiwi kuwa na wasiwasi” Richard alimwambia Gibson.

    “Asante sana. Ila kuna safari nataka unisindikize” Gibson alimwambia Richard.

    “Safari ya wapi tena?”

    “Kuelekea Dar es Salaam”

    “Kufanya nini?”

    “Kununua gari. Nataka niwe na gari kwanza kabla ya kujenga nyumba” Gibson alimwambia Richard.

    “Dah! Yaani umeshafika huko. Kweli ulikuwa na bahati”

    Siku mbili zilizofuata, wakasafiri kuelekea jijini Dar es Salaam ambako wakarudi na gari aina ya Opa. Kuanzia hapo maisha ya Gibson yakabadilika kabisa.



    Kwanza akaacha kazi na kuanzisha biashara zake kubwa. Maisha yake yakahamia jijini Dar es Salaam. Katika kipindi hiki hakutaka kuishi na Prisca kama mpenzi



    wake bali akaanza kuishi nae kama mke wake baada ya kufunga ndoa huku wakiishi pamoja na mtoto wao wa kiume, Genuine.

    “Mwaka umepita bila kukuona mpenzi” Gibson alikuwa akichati na Katie katika mtandao wa Bearshare

    “Nafahamu mpenzi. Mambo yamekuwa mengi sana. Ila ningependa uje huku ukae nami japo mwezi mmoja tu” Katie alimwambia Gibson.

    “Mimi kuja huko?”

    “Ndio. Kwani kitu gani kinashindikana?”

    “Tatizo viza. Ubalozi wenu unasumbua sana”

    “Usijali. Nitakutumia kadi ya mualiko. Kila kitu nitashughulikia mimi mwenyewe” Katie alimwambia Gibson.

    “Sawa”

    Kuanzia hapo, Gibson akaanza kujiandaa na safari ya kwenda Marekani kuonana na mpenzi wake, Katie. Maandalizi yake yakaanza kuwa ya chini chini ila



    mwisho wa siku akaamua kumwambia Prisca juu ya safari hiyo.

    “Kwa hiyo unakwenda kufanya nini huko?”

    “Kuna watu fulani nakwenda kuonana nao kwani nataka kufungua kituo cha watoto yatima. Mimi kama mimi siwezi, ninahitaji sana msaada kutoka kwa watu



    wengine. Ninakwenda huko kuonana nao, kama mambo yatakwenda vizuri, nafikiri watanisaidia kiasi fulani cha fedha na ndipo nitaanza kufungua kituo hicho”



    Gibson alidanganya.

    “Kwa maana hiyo hao watakuwa kama wafadhili?”

    “Yap. Hiyo ndio maana yangu mke wangu” Gibson alimwambia Prisca.

    Siku zikaendelea kukatika huku mawasiliano ya siri kati yake na Katie yakiendelea kama kawaida. Waliwasiliana kwa meseji huku wakati mwingine

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakiwasiliana kwa maongezi kwa kutumia mitandao mbalimbali.

    Kila mmoja akaonekana kuwa katika mapenzi ya dhati lakini kwa Gibson akaonekana kuishi kwa tahadhali ili mke wake kipenzi asiweze kufahamu kitu chochote



    ambacho kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.

    “Nitakufanyia saplaizi kubwa sana mpenzi” Katie alimwambia Gibson.

    “Niambie mpenzi. Ipi hiyo?”

    “Mbona una haraka? Wewe njoo tu uje uione” Katie alimwambia Gibson.

    Kuanzia hapo akili ya Gibson haikuweza kutulia, kila wakati alikuwa akiifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameambiwa na Katie. Alishindwa kufahamu ni kitu



    gani ambacho alikuwa ameandaliwa. Alitamani aondoke haraka na kwenda nchini Marekani, akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikiendelea kufikiria fedha tu.

    Alikuwa na fedha nyingi sana lakini bado alikuwa akihitaji zaidi na zaidi. Ndoto za kuwa tajiri mkubwa ndizo ambazo zilikuwa zikitawala kichwani mwake kwa



    wakati huo. Alihakikisha anakuwa na Prisca mpaka pale atakapoona amechukua fedha nyingi sana kutoka kwa msichana huyo ambaye kwake alionekana kutoka



    katika moja ya familia za kitajiri nchini Marekani.

    “Mmmh! Huyu msichana ameniandalia nini? Mbona ameushtua sana moyo wangu? Haiwezekani, ngoja niende” Gibson alijisemea.

    Siku ya kupanda ndege ikawadia na kama kawaida alifika uwanjani katika muda husika na kupanda ndege ya shirika la American Airways. Kwa wakati huo akili



    yake ilikuwa ikifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameandaliwa na mpenzi wake, Katie.

    Moyoni hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ingemletea matatizo makubwa, hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea hata Prisca kufahamu kile



    ambacho alikuwa amekifuata nchini Marekani, hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea kujuta kutembea na Katie huku saplaizi hiyo ndio



    ikimuwekea kifungo cha kuonana na Prisca kwa kipindi kirefu kijacho.



    Katika kipindi cha kurudi nchini Marekani, Katie hakuonekana kuwa na furaha kabisa, muda mwingi alikuwa akimfikiria mpenzi wake, Gibson ambaye alikuwa



    amemuachana nchini Tanzania. Ukweli wa moyo wake, hakutaka kabisa kurudi nchini Marekani, bado alikuwa akihitaji muda wa kukaa na Gibson mpaka pale



    ambapo nafsi yake ingeridhika kabisa.

    Alikuwa akirudi nchini Marekani kwa kulazimishwa tu kwa sababu uzinduzi wa filamu yao mpya ulikuwa ukitaka kufanyika katika hoteli ya Grand Evenue



    ambayo ilikuwa katika jiji la Hollywood nchini Marekani. Ndani ya ndege mawazo yake wala hayakumuisha hata kidogo, bado alikuwa akiendelea kumfikiria



    mpenzi wake, Gibson.

    Mapenzi na Gibson yakaonekana kumteka kupita kawaida, shughuli ambayo alikuwa akiipata kitandani kipindi cha nyuma ilimfanya kumuamini Gibson kwamba



    angekuwa mfariji wake wa maisha katika mambo yote ya kitandani.

    Ndege ilichukua zaidi ya masaa thelathini ndipo ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy uliokuwa katika jiji la New York.



    Mabosi wake walikuwa katika uwanja huo wakimsubiri, pale alipowasili, safari ya kuelekea nyumbani kwake kuanza.

    Kuanzia hapo maisha yake yakawa ni kuendelea kuigiza kama kawaida. Uzinduzi wa filamu yao ile ulipofanyika, kila mmoja akabaki na mshangao, ilionekana



    kuwa filamu nzuri ya ngono ambayo ingeuza sana duniani.

    Kila mtu alikuwa akimmwagia sifa Katie kwa ushiriki wake mzuri ambao alikuwa ameigiza ndani ya filamu ile ya ngono. Kwa mashabiki wa filamu zile,



    aliwathibitishia kwamba alikuwa bora, na ubora wake ungeendelea zaidi ya pale.

    Mwezi ukakatika, bado mawasiliano yake na Gibson yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Walionyeshana kujaliana na kusikilizana, mapenzi moto moto ya



    simuni na mitandaoni ikaonekana kuwateka kupita kawaida.

    Katie hakusitisha misaada yake ya kifedha kwa Gibson, mara kwa mara alikuwa akimtumia kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilikuwa kikiyabadilisha maisha ya



    Gibson ambaye alikuwa akiishi na mkewe, Prisca bila Katie kufahamu kitu chochote kile.

    Mara nyingi sana Katie alikuwa akipata wazo la kuja nchini Tanzania lakini mipango yake yote ilikuwa ikiingiliwa na filamu mbalimbali ambazo alikuwa



    akitakiwa kuigiza. Wazo moja likamjia kichwani mwake, alijiona kuwa na uhitaji wa kuwasiliana na Gibson na kumwambia kwamba alitakiwa kwenda nchini



    Marekani.

    Wazo lake hilo wala halikupata vikwazo kichwani mwake ila alikuwa akisubiria muda maalumu wa kumwambia Gibson juu ya wazo lake ambalo aliamini



    kwamba lingemfurahisha kupita kawaida.

    Miezi mingine sita ikakatika na kufikisha mwaka mmoja, Gibson bado alikuwa katika kichwa chake, filamu, kwake hazikuonekana kuwa na faida yoyote ile,



    alijiona kuwa na uhitaji wa kumuona mpenzi wake huyo ambaye hadi katika kipindi hicho alikuwa amemkumbuka kupita kawaida.

    Akaona lingekuwa jambo zuri sana kama angeandaa saplaizi fulani kwa ajili ya mpenzi wake huyo. Kila aina ya saplaizi ambayo alikuwa akiiona kufaa kichwani



    mwake alikuwa akiingana nayo, mwisho wa siku akafikiria kuhusu kufunga ndoa na Gibson.

    Kwake, wazo hilo la saplaizi yake likaonekana kupitishwa kwa nguvu zote kichwani mwake. Akamtaarifu Gibson juuya saplaizi ambayo alikuwa amemwandalia



    bila kumwambia ni aina gani ya saplaizi hiyo.

    Alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na marafiki zake kuhusu harusi yake ambayo angefunga muda wa siku chache zijazo. Kila mtu akaonekana kushtuka,



    hawakuamini kama kungekuwa na mwanaume ambaye angediriki kumuoa Katie na kumruhusu kuendelea na kazi yake ya kuigiza filamu za ngono.

    Kila mtu akataka kumfahamu mwanaume huyo ambaye alikuwa akitaka kufunga ndoa na Katie. Magazeti mbalimbali nchini Marekani yakaanza kuchapisha



    taarifa ile jambo ambalo lilimfanya kila mtu kuwa na hamu ya kuiona harusi hiyo ikifanyika.

    “Am getting married soon (Ninaolewa hivi karibuni)” Katie aliwaambia marafiki zake huku akionekana kuwa na furaha.

    “Who is going to marry you? (Nani anakwenda kukuoa?)”

    “Gibson”

    “Who is he? (Ndiye nani?)

    “The man I met in Africa. Dont you remember him? (Mwanaume niliyekutana nae Afrika. Hamumkumbuki?)” Katie aliwauliza.

    “A driver? (Dereva?)

    “Yeah! He is the one (Yeah! Ndiye yeye)” Katie alijibu huku akionekana kuwa na furaha.

    Mipango ya harusi bado ilikuwa ikifanyika, tarehe ya kufunga ndoa ikatangazwa, kila mtu akatamani japo kumuona mwanaume huyo ambaye alikuwa amejitoa



    mhanga kwa ajili ya kumuoa Katie.

    Marafiki zake wakaweka oda za zawadi mbalimbali kutoka kwenye maduka tofauti tofauti kwa ajili ya Katie. Katie hakutaka kutulia, kila siku alikuwa mtu wa



    kumwambia kila rafiki yake juu ya harusi ambayo alikuwa akitaka kufunga.

    Alikuwa na hamu ya kumwambia Gibson juu ya ile saplaizi ambayo alikuwa amemuandalia lakini akaona isingekuwa jambo zuri kama angemwambia. Katie



    alikuwa akichukulia kila kitu kuwa kawaida, alikuwa akimpenda sana Gibson, hakuwa tayari kumuona akiondoka mikononi mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakupewa taarifa na Gibson kama alikuwa ameoa. Alimchukulia kuwa mvulana wa kawaida ambaye alikuwa akiishi maisha ya peke yake. Kwa wakati huo



    alijiona kuwa na uhitaji wa kuwa na mume, nae aitwe mke wa fulani jambo ambalo lingemfanya kufurahi kupita kawaida.

    Wazo la kuacha kuigiza filamu za ngono bado hakuwa ameamua kama angeacha au la, ila kitu ambacho alikiona ni kuongea na mume wake huyo na kupata



    uamuzi kama alitakiwa kuachana nalo au aendelee nalo.

    Siku ambayo Gibson aliingia nchini Marekani, Katie alikwenda kumpokea uwanja wa ndege. Ile kuonana tu, wote wakaanza kukimbiliana na kukumbatiana.



    Wote wakaonekana kuwa na furaha, watu ambao walikuwa akimfahamu Katie, wakaanza kumpiga picha kwani kitendo cha kumuona mtu mashuhuri kama yeye



    lilikuwa jambo adimu sana nchini Marekani.

    “I missed you (Nilikukumbumba)

    “I missed you too. You look very cute (Nilikukumbuka pia. Unaonekana kuwa mzuri)” Gibson alimwambia Katie na kisha kumkumbatia tena.

    Wakalifuata gari ambalo alikuja nalo Katie na kisha kuondoka nalo mahali hapo. Kila mmoja kwa wakati huo alikuwa na furaha kupita kawaida, kipindi cha



    mwaka mmoja ambacho walikuwa wamekaa bila kuonana kilionekana kuwa kipindi kirefu sana.

    Walipofika nyumbani, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuingia bafuni, wakachezeana mpaka wakachoka, wakafanya mapenzi mpaka kulala juu ya makochi huku kila



    mmoja akiwa kama alivyozaliwa.

    “It’s suprise moment now (Sasa ni muda wa saplaizi)” Gibson alimwambia Katie mara baada ya kutoka bafuni kuoga.

    “Dont worry. Let’s eat (Usijali. Tule kwanza)” Katie alimwambia Gibson.

    Japokuwa walikuwa wakila lakini bado Gibson alikuwa na kimuemue cha kutaka kufahamu ni aina gani ya saplaizi ambayo alikuwa ameandaliwa. Muda wote



    alikuwa mtu wa kujichekesha tu lakini akilini mwake alikuwa akijaribu kuweka kila aina ya saplaizi ambayo alikuwa akiidhania.

    “Au anataka kunipa kampuni? Mmmh! Sasa ni aina gani ya saplaizi hiyo?” Gibson alijiuliza lakini hakupata jibu lolote.

    Walitumia mida wa dakika thelathini mpaka kumaliza kula ambapo hapo wakapelekan mpaka kitandani. Yaani, kwa ujumla siku hiyo ilikuwa ni siku ya kufanya



    mapenzi tu. Miili yao ilikuwa imekumbukana kupita kawaida, hawakufikiria kitu chochote zaidi ya kufikiria ngono tu.

    Katika kila hatua ambayo ilikuwa ikiendelea mahali hapo, Gibson hakuweza kukumbuka kwamba alikuwa amemuacha mke nchini Tanzania ambaye alikuwa



    amemzalia mtoto mmoja, kwa wakati huo mawazo yake yalikuwa yakifikiri ngono na saplaizi tu.

    Walichukua masaa mawili, wakawa hoi tena. Miili yao ikachoka kupita kawaida, hawakupata hata nguvu ya kunyanyuka, wakajikuta wakilala mpaka



    waliposhtuka saa moja na nusu usiku.

    “Give me some more (Nipe nyingine zaidi)” Katie alimwambia Gibson huku akianza kumshika shika kifuani.

    Gibson hakuwa na jinsi, akili yake ilikuwa ikifikiria mambo mengi kwa wakati huo. Utajiri na fedha nyingi kutoka kwa Katie ndicho kilikuwa kitu ambacho



    alikuwa akikihitaji kwa namna yoyote ile. Alifanya nae mapenzi mpaka pale ambapo hamu yote ilionekana kuisha mwilini mwa Katie.

    “Nataka tufunge ndoa. Utakuwa tayari?” Katie alimuuliza Gibson.

    “Kufunga ndoa! Nipo tayari. Hata sasa hivi” Gibson alimjibu Katie kiutani.

    Katie akatabasamu. Kichwa cha Gibson kilikuwa kikifikiria kwamba mpaka wafunge ndoa basi ingewachukua hata miezi sita, hakujua kama jibu lile alilolitoa



    kiutani lilionekana kumfurahisha sana Katie.

    Katie akasimama, akaanza kufurahia kupita kawaida. Gibson akainuka na kuanza kufurahi pamoja nae. Katie akaona huyo haitoshi, akanyanyua simu yake na



    kuwaataarifu marafiki zake kwamba kulikuwa na uhakika wa kufunga harusi siku mbili zijazo kama alivyowaambia.

    “Marafiki zangu wamefurahi sana. Wameahidi kuhudhuria harusi yetu kesho kutwa” Katie alimwambia Gibson huku akionekana kuwa na furaha.

    Siku ambayo alikuwa ameitaja Katie ikaonekana kumshtua Gibson, hakuamini kama Katie alikuwa amemaanisha kwa asilimia mia moja kile alichokuwa



    amekisema na wala hakuwa na utani wowote ule moyoni mwake.

    “Umesema lini?” Gibson aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Kesho kutwa. Hii ndio saplaizi ambayo nilikuwa nimeandaa kwa ajili yako. Tufunge ndoa na kuwa mume na mke” Katie alimwambia Gibson ambaye



    akaonekana kuchoka.

    Hapo ndipo picha ya Prisca ilipoanza kujengeka kichwani mwake, hakuishia kumfikiria Prisca bali akaanza kumfikiria na mtoto wake, Genuine. Kwa kiasi fulani



    Gibson akaonekana kukosa amani, akakaa kochini.

    “Mbona umebadilika ghafla?”

    “Hapana. Umenishtukiza sana” Gibson alijibu.

    “Kweli?”

    “Ndio”

    “Sasa hiyo si ndio maana ya saplaizi. Yaani ushtuke kama ulivyoshtuka” Katie alimwambia Gibson ambaye mawazo yake yalikuwa nchini Tanzania tu.

    “Sawa. Tutaoana kama ulivyotaka ila kwa masharti kadhaa”

    “Masharti gani?” Katie aliuliza huku akimsogelea Gibson na kumlalia kifuani.

    “Sharti la kwanza.........” Gibson alisema huku Katie akiwa kimya akimsikiliza.

    “Kwanza ndoa yetu nataka iwe ni ya mkataba. Hii ni kwa sababu nitataka zaidi kujilinda mpenzi” Gibson alimwambia Katie.

    “Hilo si tatizo, ndoa hizo ndizo ambazo huwa tunafunga huku. Kuna kingine?” Katie alimuuliza Gibson.

    “Ndio. Tena mengi tu. Vipi kuhusu watoto?”

    “Si la kuongelea kwa sasa, hilo linatakiwa kuongelewa ndani ya ndoa” Katie alijibu.

    “Ndani ya ndoa! Hii ni mipango ambayo yatupasa kuipanga Katie”

    “Nafahamu. Ila unaonaje kama mpango huo tukiupangia ndani ya ndoa?” Katie aliuliza.

    “Hakuna tatizo. Na vipi kuhusiana na kazi?”

    “Kazi gani?”

    “Unafikiri nitakuwa nikikaa tu ndani bila kufanya chochote kile? Hapana, hayo si maisha. Inanipasa niwe na kazi ya kunifanya kuwa bize” Gibson alimwambia



    Katie.

    “Hilo si tatizo. Nitakutafutia” Katie alimwambia Gibson.

    Wote wawili wakawekeana makubaliano na kufikia muafaka. Kitu ambacho alikifanya Katie kwa wakati huo ni kuwa makini sana, kila wakati alikuwa akimbana



    sana Gibson ili asiweze kuangalia sana televisheni wala kusoma magazeti.

    Vyombo vyote vya habari kwa wakati huo vilikuwa vikiitangaza harusi hiyo huku maneno ‘MUIGIZAJI WA FILAMU ZA NGONO’ yakiwa yametawala katika



    kila chombo cha habari ambacho kilikuwa kikiandika kuhusiana na harusi ile.

    Katie hakutaka kabisa Gibson afahamu kile ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha yake, hakutaka kabisa ajulikane kwamba alikuwa muigizaji wa filamu



    za ngono ambaye alikuwa akivuma sana.

    Alitaka kwanza afunge nae ndoa na hatimae aje kufahamu baadae sana kwamba alikuwa akijihusisha na filamu zile ambazo kadri siku zilivyokuwa zikizidi



    kusogea mbele na ndivyo ambavyo zilizidi kupata mashabiki zaidi.

    Gibson akawa akishinda ndani, alikuwa akiisubiria siku hiyo huku aone ni kitu gani ambacho kingeendelea. Mawazo yake kwa wakati huo hayakuacha kuifikiria



    familia yake ambayo ilionekana kuwa muhimu sana katika maisha yake.

    Kwa kitendo chake cha kwenda kufunga ndoa na Katie kilionekana kuwa kama usaliti mkubwa katika ndoa yake na Prisca. Gibson hakuwa akifahamu kitu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    chochote kile kuhusiana na maisha halisi ya Katie, kwake alionekana kuwa msichana tajiri sana lakini wala hakuwa akijua siri ya utajiri wake ule.

    Gibson akaanza kuufikiria utajiri ule, kichwa chake wala hakikuweza kutulia, kwa sababu alikuwa mchaga, ubongo wake ulikuwa umetulia kwa kufikiria fedha



    tu. Siku ya kwanza ikakatika na ya pili kuingia. Marafiki mbalimbali wa Katie walikuwa wakifika nyumbani pale na kisha kuongea na shemeji yao mtarajiwa,



    kila mmoja alionekana kuwa na furaha.

    Watu ambao hawakuwa karibu na Katie hawakuweza kumfahamu Gibson kabisa kwani hata waandishi wa habari hawakuwahi kumuona mwanaume huyo



    ambaye kwao alionekana kuwa na moyo wa kujitolea kufunga ndoa na msichana ambaye alikuwa maarufu kwa kuigiza filamu za ngono.

    Siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa ikawadia, Gibson akawa ndani ya suti kali katika sehemu ambayo walitakiwa kufunga ndoa na Katie. Mahali hapo wala



    hakukuwa na idadi kubwa ya watu, ni watu hamsini tu ndio ambao walikuwa wamekusanyika katika harusi hiyo ambayo ilimgharimu Katie kiasi cha dola laki



    moja, zaidi ya shilingi milioni mia mbili za Tanzania.

    Ndoa ya mkataba wa kudumu wa miaka mitano ikafungwa na mkataba huo kusainiwa mbele ya watu hao ambao walikuwa wamekusanyika ndani ya uwanja huo



    mdogo wa nyumba ya Katie iliyokuwa hapo New York katika mtaa wa kitajiri wa Buttlefly 56th.

    Harusi ikafungwa na hatimae Gibson na Katie kuwa mume na mke. Kwa Katie ilionekana kuwa furaha kubwa lakini kwa Gibson ikaonekana kuwa kama tatizo



    kubwa katika maisha yake. Hakujua ni kitu gani ambacho kingetokea pale ambapo mke wake wa Tanzania, Prisca angesikia kwamba alikuwa amefunga ndoa na



    mwanamke wa kizungu nchini Tanzania na kumsaliti.

    Wanandoa wakaondoka kuelekea katika kisiwa cha Bahamas kwa ajili ya kula raha tu. Walikaa huko kwa takribani mwezi mzima, wakarudi tena jijini New York



    kwa ajili ya kuendelea na maisha yao kama kawaida.

    Waandishi wa habari wakazipata picha za Gibson na kuanza kuzitoa katika vyombo mbalimbali vya habari, hapo ndipo watu walipogundua kwamba mume wa



    Katie alikuwa mtu mweusi tena aliyesadikiwa kutoka barani Afrika.

    Kila mtu ambaye aliziona taarifa za harusi ile akaonekana kushangaa, hawakuamini kama kungekuwa na mtu mwenye ngozi nyeusi ambaye angekubali kuwa na



    mwanamke ambaye alikuwa akiigiza filamu za ngono.

    Kuigiza filamu za ngono kilikuwa ni kitendo ambacho kilikuwa kikiendelea kuwa siri kubwa katika maisha ya Katie, hakutaka mumewe ajue kile ambacho



    kilikuwa kikiendelea. Hakujua ni nani ambaye alimfuata Gibson na kumueleza kile ambacho alikuwa akiendelea kukifanya, kilichomshtua zaidi ni pale aliporudi



    nyumbani na kumkuta Gibson akiwa katika muonekano wa tofauti.

    “Why didn’t you tell me before? (Kwa nini hakuniambia kabla?)” Gibson aliuliza huku akionekana kukasirika.

    “Tell you what? (Kukwambia nini?)” Katie aliuliza huku akijifanya kushangaa.

    “That you are a porn movie star (Kwamba wewe ni muigizaji wa filamu za ngono)” Gibson alimwambia Katie.

    “Who told you that? (Nani alikwambia hayo?)”

    “Just wait for me right here (Nisubiri hapa)” Gibson alisema na hapo hapo kuanza kupandisha katika ghorofa ya juu kulipokuwa na chumba chao.

    Katie alibaki akizunguka zunguka pale sebuleni alipokuwa amesimama. Kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mtu ambaye alikuwa amemwambia Gibson kile



    ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha yake, kwa wakati huo, akaonekana kuwa na wasiwasi, hakujua Gibson angeamua uamuzi gani.

    Gibson akarudi mahali hapo huku mkononi akiwa na gazeti la New York Times ambalo lilikuwa likitoka mara tatu kwa wiki nchini humo. Akalitupa gazeti juu



    ya meza, picha ya Katie pamoja na picha yake zilikuwa zikionekana kabisa mbele ya gazeti lile.

    “Tell me about this (Niambie kuhusu hii)” Gibson alimwambia Katie.

    Katie akalichukua lile gazeti na kuanza kuliangalia vizuri. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumdunda, hakujua ni maneno gani ambayo alitakiwa kumueleza



    mume wake huyo ili kuiokoa ndoa yake ambayo ilikuwa imedumu kwa miezi miwili mpaka muda huo.

    “Tell me about this (Niambie kuhusu hiki)” Gibson alimwambia Katie, kwa wakati huu, aliongea kwa sauti ya juu iliyoonyesha ukali.

    “It is true (Ni kweli)

    “Good (Vizuri)” Gibson alisema na kuanza kupanda juu ghorofani.

    “Please Baby...Let me explain (Tafadhali mpenzi...acha nifafanue)” Katie alimwambia Gibson huku akiwa amemshika suruali pale kwenye ngazi za kupandia juu.

    “What do you want to explain to me? Do you want to tell me that you have been fucked with all men around this fucking City? Do you want to tell me that you



    are a Porn movie star who cheats to her husband and speaks rubish on his back? What do you want to tell me? (Unataka kunifafanulia nini? Unataka kuniambia



    kwamba umefanya mapenzi na wanaume wote ndani ya jiji hili? Unataka kuniambia kwamba wewe ni mcheza filamu za ngono ambaye anadanganya mume wake



    na kuongea uchafu nyuma yake? Unataka kuniambia nini?)” Gibson aliuliza huku akionekana kukasirika kupita kawaida.

    Kutokana na hasira ambazo alikuwa nazo katika kipindi hicho, mishipa yake yote ya mwili ilikuwa imemtoka, alikuwa akitetemeka kwa hasira huku meno yake



    yakigonganagongana tu. Hakuwa akiamini kwa wakati huo kwamba msichana ambaye alikuwa amefunga nae ndoa alikuwa ni mcheza filamu za ngono ambaye



    alikuwa akivuma sana kwa kipindi hicho.

    “I am not a Porn movie star (Mimi sio muigizaji wa filamu za ngono)” Katie alisema huku akilia.

    “Then, who the hell are you? (Kwa hiyo wewe nani?)”

    “Gibson’s wife (Mke wa Gibson)” Katie alisema kwa sauti ya chini.

    “Thats fucking rubbish (Huo ni uchafu)” Gibson alisema na kisha kuendelea kupanda ngazi.

    Breki ya kwanza ilikuwa ni kitandani, akajilaza, mwili ulikuwa ukimtetemeka kupita kawaida. Moyo wake ulikuwa ukijuta sababu zilizompelekea kwenda



    nchini Marekani na kukubali kumuoa Katie. Hapo ndipo alipopata majibu juu ya mambo ambayo alikuwa akifanyiwa na Katie kama kunyimwa uhuru wa



    kuangalia televisheni na hata kusoma magazeti.

    Katie akaingia chumbani hapo na moja kwa moja kuanza kumfuata Gibson kitandani pale alipolala na kumlalia mgongoni. Katie alikuwa akilia kwa kwikwi,



    alionekana kuwa na sura ambayo ilikubali kwamba alikuwa amekosa ila kwa wakati huo alikuwa akihitaji msamaha.

    “I was a porn movie star but I am not a porn movie star (Nilikuwa muigizaji wa filamu za ngono lakini kwa sasa mimi sio muigizaji wa filamu za ngono)” Katie



    alimwambia Gibson.

    Gibson hakuongea kitu chochote japokuwa kwa hali fulani maneno yale aliyoongea Katie yakaonekana kuanza kumuingia. Katie akaanza kumpapasapapasa



    Gibson mgongoni hali ambayo ikaanza kumuweka Gibson katika hali mbaya.

    Katie hakutaka kutulia, aliendelea zaidi na zaidi, ndani ya dakika tano, Gibson alikuwa radhi kwa kila kitu. Hasira zote ambazo alikuwa nazo juu ya Katie



    zilikuwa zimemtoka na tamaa ya kufanya mapenzi ikiwa imeanza kumuingia.

    “I need you (Ninakuhitaji)” Katie alimwambia Gibson na kisha kukipeleka kinywa chake kinywani mwa Gibson, kilichofuata hapo ni kubadilishana mate na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kisha kuanza kufanya tendo la ndoa.



    Maisha hayakuwa ya shida tena, umasikini ambao alikuwa ameupitia pamoja na Gibson ukaonekana kutokujirudia tena katika maisha yao. Kwa wakati huo kila



    kitu kilionekana kubadilika kabisa. Walikuwa na fedha za kutosha, walijenga nyumba ya kifahari huku wakiwa na magari mawili ya kifahari.

    Hawakuishia hapo, pia walikuwa na miladi mbalimbali ambayo ilikuwa ikiwaingizia kiasi kikubwa cha fedha. Mapenzi yao yaliendelea kama kawaida,



    hakukuonekana kama kulikuwa na mtu ambaye alimchoka mwenzake, walionekana kuzidi kupendana kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.

    Prisca hakujua fedha zile zilitoka wapi, kila alipokuwa akiuliza, alipewa majibu ambayo wala hayakuonekana kuridhisha japokuwa baada ya muda fulani



    akaonekana kuyaamini. Hakujua kama fedha zile ambazo zilikuwa zikitumika kuwatengenezea maisha yao zilikuwa zikitoka kwa msichana ambaye alikuwa



    muigizaji mashuhuri wa filamu za ngono na ndiye ambaye kwa wakati huo alikuwa akimuibia penzi lake kutoka kwa mume wake, Gibson.

    Maisha yakaendelea kusonga mbele, furaha yao ikaongezeka zaidi na zaidi, mtoto wao mpendwa, Genuine alikuwa akiwafanya kuwa karibu sana. Kutokana na



    fedha ambazo walikuwa nazo katika kipindi hicho, wakaanza kujulikana jambo ambalo likaanza kuwaweka katika listi ya watu mia moja ambao walikuwa na



    fedha nyingi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

    Maisha yaliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo Gibson akaelekea nchini Marekani huku akisingizia kwamba alikuwa akienda kukutana na wafadhiri wa



    kituo cha watoto yatima ambacho alikuwa akitarajia kukifungua jijini Dar es Salaam.

    Prisca akaonekana kuridhika, katika maisha yake alikuwa akiwajali sana watoto yatima, aliwapenda kupita kawaida kwani alijua fika kwamba walikuwa wakiishi



    katika mazingira magumu na ya tabu kupita kawaida.

    Akampa baraka zote mume wake kwamba aende na arudi salama ndani ya nchi ya Tanzania ili waendelee na maisha yao kama kawaida. Moyoni hakujua, hakujua



    kwamba mume wake alikuwa akienda kukutana na saplaizi ambayo ilionekana kubadilisha kila kitu katika maisha yao.

    Wiki ya kwanza ikakatika, japokuwa alikuwa ameahidiana na mumewe kwamba wangewasiliana lakini haikuwa hivyo, Gibson akaonekana kuwa kimya sana.



    Hakukuwa na mawasiliano ambayo yalikuwa yakiendelea, kila alipokuwa akitafutwa, hakuwa akipatikana.

    Baada wiki mbili kupita hapo ndipo alipokutana na taarifa ambayo ilikuwa imemchanganya kupita kiasi. Mwanamke ambaye wala hakuwa akifahamiana nae



    akamfuata nyumbani pale na kisha kumuonyesha picha ambazo zilikuwa zikimuonyesha Gibson akiwa ndani ya suti huku pembeni yake kukiwa na msichana



    ambaye alivalia shela.

    Kwa jinsi picha ile ilivyokuwa ikionekana, wala hakukuwa na kitu cha kujiuliza kama pale kulikuwa na tukio gani ambalo lilikuwa likiendelea, lilionekana kuwa



    ni tukio la harusi kati ya watu hao wawili.

    Prisca akajihisi akikosa nguvu, miguu ikaanza kumlegea na kujikuta akikaa kochini. Hakuweza kuiamini picha ile, akahitaji picha nyingine zaidi na zaidi,



    akaonyeshewa zaidi ya picha ishirini jambo ambalo lilimfanya kuumia zaidi.

    “Mungu wangu! Gibson” Prisca aliita huku akiziweka zile picha mezani.

    Tayari akaonekana kuchanganyikiwa, hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa amekiona kwa wakati ule. Machozi yakaanza kumtoka, hapo ndipo



    alipogundua sababu ambayo ilimpelekea Gibson kutokuwasiliana nae kwa kipindi kirefu tangu aelekee nchini Marekani.

    “Umezitoa wapi hizi picha?” Prisca aliuliza huku akionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.

    “Kwenye mtandao. Hivi kwanza unamjua huyo mwanamke?” Mwanamke yule aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Fatuma aliuliza.

    “Hapana”

    “Pole sana shoga yangu. Mwanamke huyu ni mcheza fiamu za picha za ngono nchini Marekani” Fatuma alimwambia Prisca maneno ambayo yakaonekana



    kumshtua zaidi.

    Prisca akaonekana kuchanganyikiwa zaidi, akashindwa kuvumilia kukaa mahali pale, alichokifanya kwa wakati huo ni kuondoka kuelekea chumbani huku akiwa



    na baadhi ya zile picha. Akajifungia na kuanza kulia, alilia kwa uchungu, hakuamini kama kweli Gibson angeweza kufanya kitu kama kile, kufunga ndoa na



    mwanamke wa kizungu.

    Kilio chake hakikuweza kumsaidia chochote kile, aliendelea kulia zaidi na zaidi lakini ukweli bado ukabaki kuwa pale pale kwamba Gibson alikuwa amefunga



    ndoa na mwanamke wa kizungu ambaye alikuwa mcheza filamu za ngono, Katie.

    Siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ilijaa maumivu kuliko siku zote katika maisha yake. Akatoka chumbani na moja kwa moja kuelekea katika sehemu ya



    kuegesha magari na kuchukua gari moja aina ya Verosa, akamuweka Genuine kwenye kiti kingine na kisha kuwasha gari na kuondoka mahali hapo.

    Akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikimwambia afanye kitu kimoja tu, aondoke na kuelekea nyumbani kwa wazazi wake ambako huko angewaambia kila kitu



    ambacho kilikuwa kimetokea na kuwaoyesha zile picha na kuwa kama ushahidi kwake.

    Alipofika, akamchukua Genuine na kuanza kuingia ndani ya nyumba yao. Alipogonganisha macho yake na wazazi wake, akaanza kulia, kila kitu kikaanza



    kujirudia ndani ya kichwa chake.

    “Kuna nini tena?” Mzee Steven alimuuliza binti yake.

    Prisca hakutoa jibu la swali lile, akabaki akilia zaidi na zaidi. Katika kipindi hicho alijiona kutokuwa na nguvu za kuongea hata mara moja, alikuwa akijiskia



    kulia zaidi na zaidi tena kwa uchungu mkubwa.

    “Prisca. Kuna nini kimetokea?” Mama yake, Bi Magreth aliuliza.

    Prisca hakutoa jibu lolote lile, alichokifanya kwa wakati huo ni kuwaonyeshea wazazi wake picha zile ambazo alikuwa ameletewa na Fatuma. Wazazi wake



    wakazichukua na kuanza kuangalia picha moja baada ya nyingine.

    “Mmmh!” Mzee Steven alisikika akiguna.

    “Hii inawezekana kweli” Bi Magreth aliuliza huku akiziangalia vizuri picha zile.

    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiamini kile ambacho alikuwa akikiona katika picha zile, waliziona kuwa kama picha za kutengenezwa ambazo mtu yeyote



    mwenye ujuzi wa kuzitengeneza angeweza kuzitengeneza.

    Chini ya zile picha kulikuwa na jina la mtandao ambao picha zile zilikuwa zimechukuliwa jambo ambalo likamfanya mzee Steven kuchukua laptop yake,



    akaiunganisha na internet na kisha kuanza kuufungua mtandao ule.

    Picha ambazo alikuwa akiziona katika mtandao ule zilikuwa ni picha zile zile ambazo walikuwa nazo mikononi na huku nyingine zikionekana kuwa mbaya zaidi



    ambazo zilidhihirisha kwamba watu wale walionekana kuwa mume na mke ambao walikuwa wameingia katika ndoa.

    “Hivi inawezekana kwa Gibson kufanya vitu kama hivi?” Mzee Steven aliuliza huku akionekana kushangaa.

    “Inawezekana na ndio maana amefanya hayo” Bi Magreth alijibu.

    Kitu walichokifanya mahali hapo ni kuondoka na kuelekea nyumbani kwa mzee Lyimo ambaye alikuwa baba wa Gibson. Kwa kutumia usafiri wa gari lao,



    walitumia muda wa dakika thelathini wakawa wamekwishafika, wakateremka na kuanza kuelekea katika nyumba hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda wote huo Prisca alikuwa akiendelea kulia, bado mawazo yake yalikuwa kwa mume wake ambaye aliamua kufanya jambo lililomshtua kupita kawaida.



    Hamu ya kuwa ndani ya ndoa ikanekana kuanza kumtoka moyoni, hakutamani kurudi nyumbani kabisa.

    “Mmmh! Inawezekana kweli kwa Gibson kufanya haya?” Mzee Lyimo aliuliza huku akionekana kushtuka kupita kawaida.

    Tayari picha zile zikaonekana kumshtua kupita kawaida, hakuamini kama mtoto wake, Gibson alikuwa ameamua kuoa nchini Marekani na wakati alikuwa na



    mke pamoja na mtoto mdogo ambaye alikuwa na miezi kumi tu.

    “Mmmh!” Mama yake Gibson, Bi Yustina aliguna.

    Kila mmoja akaonekana kutokuelewa sababu ambazo zilimfanya Gibson kuamua kufanya uamuzi ule ambao ulionekana kumuumiza kila mtu aliyeziangalia



    picha zile. Prisca bado alikuwa akiendelea kulia kupita kawaida, moyo wake ukaanza kupatwa na majeraha ya mapenzi, mtu ambaye alikuwa akimuamini ndiye



    ambaye alikuwa amekuja kumuumiza.

    “Inaniuma sana” Prisca aliwaambia huku akiendelea kulia.

    “Pole sana Prisca”

    “Sijaumia kwa yeye kuoa mwanamke mwingine tu bali nimeumia pia kwa aina ya mwanamke aliyemuoa” Prisca aisema.

    “Eeeeh! Kwani unamjua?”

    “Hapana”

    “Sasa ni mwanamke wa aina gani?”

    “Mcheza filamu za utupu”

    “Unasemaje?” Wazazi wote wanne walisema kwa pamoja.

    “Ndio. Ni mcheza filamu mzuri wa utupu duniani” Prisca aliwaambia.

    Maneno hayo ndio ambayo yalionekana kuwachanganya zaidi na zaidi, wakaona kwamba kijana wao tayari alikuwa amepotea njia kwa uamuzi ule ambao



    alikuwa ameufanya. Taarifa kwamba msichana ambaye alikuwa amemuoa alikuwa mcheza filamu za ngono ilionekana kuwaumiza na kuwakasirisha kupita



    kawaida.

    Walichokijua ni kwamba kule alipokuwa akifanya kazi Gibson, mbugani ndipo ambapo kulikuwa na uwezekano wa kukutana na mwanamke yule, walichokitaka



    kwa wakati huo ni kuwasiliana na mtu yeyote kutoka katika kampuni ile aliyokuwa akifanyia kazi kwa ajili ya kutaka kuufahamu ukweli.

    “Nina namba ya rafiki wake wa karibu, Richard” Prisca alisema.

    Hapo ndipo mawasiliano na Richard yalipoanza. Kitu ambacho alitakiwa kukifanya Richard ni kutoka Morogoro na kuja jijini Dar es Salaaam kwa kutumia



    usafiri wa ndege na gharama zote zilikuwa juu ya Prisca.

    Ndani ya masaa kadhaa, Richard alikuwa katika nyumba hiyo ya mzee Lyimo. Kitu cha kwanza walichokifanya ni kumkabidhi Richard picha zile na kuanza



    kuziangalia. Richard akaonekana kushtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona kwa wakati ule.

    “Umeshtuka nini?” Mzee Lyimo alimuuliza.

    “Kuona picha hizi” Richard alijibu.

    “Yaani unajifanya kama haujui chochote kile”

    “Yeah! Sikujua kama angefanya kitu hiki” Richard aliwaambia.

    “Kwa hiyo ulikuwa ukijua kwamba ana mwanamke?”

    “Hapana. Ila nilijua kwamba anakwenda nchini Marekani kwa sababu aliniaga” Richard alisema.

    “Alipokuaga alikwambia nini?”

    “Kwamba anakwenda kukutana na wadhamini wa kituo cha watoto yatima ambacho anataka kuanzisha” Richard alidanganya.

    “Kwa hiyo haujui chochote kuhusu mwanamke huyo?”

    “Sijui” Richard alijibu.

    “Hapana. Kuna kitu unafahamu tu. Naomba utuambie ili tujue pa kuanzia. Unajua limekwishakuwa suala kubwa sana hili” Mzee Lyimo alimwambia Richard.

    Richard hakutaka kutoa siri ya kitu ambacho kilikuwa kinaendelea. Alikuwa akikataa kuzungumza kitu chochote mpaka pale alipobanwa sana na ndipo akaanza



    kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika kipindi cha nyuma.

    Prisca akaonekana kushtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa Richard, hakujua kama Richard nae alikuwa akifahamu kila kitu japokuwa



    alikuwa mtu wake wa karibu kuliko marafiki wote wa Gibson.

    “Kwa hiyo ukanisaliti? Ukawa unafahamu kila kitu ila haukutaka kuniambia?” Prisca alimuuliza Richard kwa sauti ya ukali.

    “Nilihofia. Nilichokuwa nikitaka kukiona ni kuona kwamba Gibson anafanikiwa na kutoka kwenye maisha aliyokuwa anaishi. Niliamini kama angefanikiwa,



    hata mimi rafiki yake wa karibu ningefanikiwa pia. Na hiyo ndivyo ilivyokuwa” Richard alimwambia.

    “Unamaanisha hata hizi fedha zote alizokuwa akizipata Richard zilitoka kwa mwanamke huyu?” Mzee Lyimo aliuliza.

    “Ndio. Hebu jifikirieni hapo, kama ningeamua kumwambia Prisca juu ya hili, unafikiri hizi fedha wangezipata? Unafikiri Prisca angekuwa muelewa.



    Niliiangalia hali yao, ilikuwa hali mbaya, Prisca alikuwa mjauzito ambaye alikuwa akihitaji kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya matunzo. Kitendo cha msichana



    Katie kuja katika maisha ya Gibson niliona kuwa kama muujiza ambao wala haukutakiwa kuachwa kutokea. Na kweli, baada ya kumkubali Katie kisiri,



    mafanikio yakaja. Najua kwa kufanya hivyo nimekuumiza sana Prisca ila jua nilifanya hivyo kwa sababu sikutaka uishi maisha ya tabu mara utakapojifungua.



    Mshahara wa Gibson haukuwa ukitosheleza” Richard alimwambia Prisca.

    Wote wakaanza kumuelewa Richard, maneno ambayo alikuwa ameyaongea yakapenya masikioni mwao na kutulia katika akili yao. Ni kweli alionekana kuwa



    msaada mkubwa sana kwa Prisca kwani kama angeamua kusema ukweli, Prisca angekuwa kwenye hali mbaya katika kipindi kile cha ujauzito.

    “Kwa hiyo haukufahamu kama huyu binti alikuwa mcheza filamu za ngono?” Mzee Steven aliuliza.

    “Sikufahamu kabisa na ninadhani kwa sababu mimi si mpenzi wa filamu hizo” Richard alijibu.

    “Shukrani sana. Umeamua kuwa mkweli. Sasa tuambie kwamba hakukwambia kama alikuwa anaenda kufunga ndoa na msichana huyu?” Mzee Lyimo aliuliza.

    “Hakuniambia kabisa. Kitu ambacho aliniambia ni kwamba alikuwa ameandaliwa saplaizi na mwanamke huyo, nadhani harusi ndio ilikuwa ni saplaizi yenyewe.



    Nina uhakika kwamba Gibson ameoa huku akiwa hataki kuoa. Naamini hilo” Richard aliwaambia

    “Unawasiliana nae?”

    “Hapana. Nimejaribu kumuandikia barua pepe zaidi ya tatu, naona kimya” Richad alijibu.

    “Dah! Sasa ataweza kurudi nchini Tanzania?”

    “Ataweza. Gibson anachokiangalia kwa mwanamke yule ni fedha tu, hakuna kingine cha zaidi. Mitego yake yote ameiweka katika fedha tu kwani anajua kwamba

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mwanamke yule ana fedha nyingi” Richard aliwaambia.

    Waliendelea kumuuliza maswali mengi na Richard alikuwa akijibu kwa ufasaha sana bila kusema kwamba yeye ndiye alikuwa amemshinikiza Gibson kutembea



    na Katie.

    Maisha yakaendelea zaidi na zaidi, kila siku Prisca alikuwa mwanamke mwenye huzuni, japokuwa alikuwa na fedha za kutosha lakini fedha hazikuwa na thamani



    kwake, thamani kubwa ilikuwa ni Gibson ambaye alikuwa na mapenzi yake ya dhati moyoni mwake.



    Je nini kitaendelea?

    Je wazazi wa pande zote mbili wataamua nini?

    Je maisha ya Gibson yatakuwaje nchini Marekani?

    Je ndoa yao itadumu?

    Hapa ndipo hadithi inapoanza rasmi.



    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog