Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SALHAT - 3

 







    Simulizi : Salhat

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Maisha baina ya Jay na Grace yaliendelea huku Jay akionekana kuendelea kutafuta mbinu zaidi za kumteketeza Badra ambaye alikuwa safarini sasa kwa takribani miez6.



    Huku wakiendelea kuzozana na Grace kuhusu swala la Pete ya uchumba.



    Siku hiyo akiwa anatizama habari hapo ndipo aliposhtuka na kujikuta akilitaja jina la "Salhat"!!!



    Johnny alishtuka sana baada ya kupata habari hizo na hapo hapo alianza mbio haraka haraka kuelelea mahali ambako ilielekezwa hospital aliyoweza kupelekwa Salhat.



    Alipishana na Grace ambaye aliweza kumleta juice na bila kumsesha chochote.



    "Anashida gani huyu alijiuliza na hakujipatia hata majibu ilibidi na yeye aingie sebleni na kutazama kipi kilichoweza kumfanya Johnny akawa katika hali ile.



    Zilizokuwa zikirushwa hewani ni habari za Salhat ambaye alihitaji hukumu ya kuuwawa na baada ya kuona ya kuwa lengo lake halijatimia basi aliamua kujikata mishipa yake mikuu ya damu na sasa hali yake ipo hatarini.



    ****** ********



    Walionekana mabinti wawili wakiwa njee ya hospitali hukuwakijadiliana kuhusu swala la Salhat.



    "Unajua kabisa hatuwezi kumsaidia kwani tutakuwa tunaingilia kazi ya Edrick na hairuhusiwi" alizungumza binti yule.



    "Lakini sasa Nasma unaelewa kabisa ya kuwa Salhat ndyo kila kitu katika sisi yeye pekeee ndyo anayeweza kuurudisha tena ukoo wetu wa Sultan"



    "Yote kwa yote Sheilah sisi haturuhusiwi kumsaidia yeye na pia kazi yetu sisi ni kumtafuta mwendano wake.....hata hivyo mpka sasa Salhat ajaomyesha tukio lolote lile la kushngaza bado yeye ni binadamu na bado hatujatambua ni lini Atarudi katika umbo lake la kijini tena"



    "Yote uyasemayo ni sawa lakini ikiwa yeye ndyo tunayemtizamia kama mkombozi hatuwezi kumuacha akapoteza maisha yake lazima tufanye jambo juu yake..." Aliongea Sheilah.



    "Ila bado nakusisitiza sisi siyo Edrick"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tambua Edrick yupo katika adhabu kwa kosa na kulala na binadamu na hakuna mwingne wa kumsaidia isipokuwa sisi...wote tunatambua ya kuwa hakuuhusika na mauaji ila hawa wapuuzi binadamu wanatoa hukumu pasina kuufahamu ukweli"



    "Sasa tutamsaidiaje???? Aliuliza Nasma.



    "Nifuate Mimi" alijibu na kutoweka pia na yeye alitoweka.



    Johnny aliweza kuingia akiwa katika hali ya haraka zaidi aliweza kupishana na Akram pasina hata mmoja kumtambua mwenzake kwani kila mtu alikuwa busy katika harakati zake.



    Akram alitoka njee kwaajili ya kwenda kutafuta damu ambayo itaweza kuwekwa tena katika mwili wa Salhat kwani alivuja damu nyingi sana.



    "Docta.....mgonjwa huyu anahitaji damu kwa haraka zaidi na tukizidisha kwa dakika kumi atapoteza maisha" maelezo hayo aliyatoa nesi mmoja kumpatia Dactari William.



    "Umeshapiga simu katika bank ya damu???



    "Ndyo ila wamesema blood type 0- wameishiwa"



    "IGP Akram umeshampa taarifa hizo???



    "Samahani damu yangu ni type hiyo naweza kumchangia ilikuwa ni sauti ya Johnny iliyoweza kupenya katikati mwa nesi na docta William ambao hawakupoteza muda hapo hapo walimchukua Johnny.



    Baada ya dakika kadhaaa kupita alionekana Johnny akiwa amelala huku akiitizama upande wa kushoto ambako aliiona sura ya Salhat iliyoweza kujaa makovu mdomo uliokauka sana na nguo iliyoweza kulowa damu.



    "Salhat......!!! Aliita kimoyo moyo na kumtizama Salhat.



    "Samahani sana kwa kuchukuwa muda mwingi kabla ya kuja kukusaidia nisamehe sana Salhat" aliongea huku machozi yakimtoka na kumtazama Salhat ambaye hakuwa amerejelewa na fahamu zake.



    Baada ya kumaliza kutoa damu Johnny alindoka bila kusema neno lolote lakini alishangaaa kwani alihisi anaanza kuzisikia sauti za watu wakizungumza.



    "Hapana siwezi kukubali mtoto wangu afe nitambana kwaajili ya kutafuta hiyo pesa hata kama ni kwakuiba" alizungumza mama mmoja.



    Na johnny aliweza kumsikia alitoa check kisha akamuuliza mwanao anadaiwa kiasi gani???



    Maka yule alimtizama Johnny na alitaja kiasi cha fedha.



    "Lakini wewe umejuaje mbona Mimi haya maneno nimeyazungumza kutoka moyoni, na hakuna anayefahamu ya kuwa aliyelazwa hapa ni mwanangu???



    "Hapana hujayaongelea mbona me nimekusi......... Johnny hakuweza kumalizia sentensi yake na hapo alikumbuka ya kuwa pindi alipokuwa mdogo alikuwa na uwezo wa kusikia kitu chochote kile mtu anachokizungumza kutoka moyoni ila uwezo huo ulipotea tu ghafla akiwa anawaza Yale aliingia Akram akiwa na kundi la watu takribani 12 alioweza kuwaleta ili wamsaidie kutowa damu kwaajili ya kuwekea Salhat bila kugundua ya kuwa tayari alishapatikana mtu wa kumuwekea damu.



    Johnny alitaka kuwasikiliza wale watu ili ajue kama ni kweli anawasikia au laaahhh......!!!! Alipojaribu kuwasoma mmoja baada ya mwingne aliweza kuzisikia sauti zao zikizungumza ila alipotaka kumsoma Akram alishangaa baada ya kuhisi kelele masikioni mwake wala hakujali aliondoka zake.



    ****** ********



    Baada ya siku kadhaa kupita hali ya Salhat ilirejea katika na aliwekewa umakini mkubwa sana hospitalini hapo huku akifungwa pingu mkono mmoja pamoja na mguu mmoja huku vitu vyenye ncha Kali vikiwekwa mbali na yeye masa24 walikuwa askari wawili ndani wa kike kwaajili ya kuutizama usalama wa Salhat.



    Hatimaye waliweza kupitiwa na usingizi na Salhat alitizama pembeni akaona kisu kilichoweza kukatia matunda alitamani kisu kifike karibu na yeye na katika hali ya kushngaza alishngaa baada ya kuona kisu kimefika pale alipo alishtuka na kutizama kulia na kushoto akihisi anaota au hicho kisu kimewezaje kufika pale.



    Alikitizama na kusema kisu kirudi pale.



    Kisu kiliweza kurudi pale alipoweza kukielekeza.



    Aliitizama Meza moja na meza ile iliweza kusoge hadi karibu na mahali alipo yeye......sasa alifanya kama mchezo ambao uliweza kumfurahisha aliwabeba askari wale kwa macho na kuwapeleka chooni huku akiendelea kufurahia.



    "Pingu funguka nazo zilifunguka.......pingu jifunge na ndicho kilichoweza kutokea.



    "Kitanda jizungushe kitanda kilianza kujizungusha na kumfanya Salhat awe na furaha"



    "Mpuuzi huyu anaagiza tu vitu anafikiri sisi hatuchoki au ?? Alianza kulalamika Nasma aliyekuwa akizungusha kitanda pamoja na Sheila.



    "Usilalamike Nasma, Edrick atalipa kwa hili".



    "Kitanda simama" aliongea Salhat na kitanda kilisimama.



    Alicheka sana tena sana huku akijifariji ya kuwa anafanya mmbo ya ajabu bila ya kujua kuwa hakuwa akifanya yeye Bali majini wawili waliokuwa ndani ya hospitali ile.



    Salhat alikitizama kile kisu kisha akakishika na hapo hapo akaainua mkono wake ambao ulikuwa bado na bandage.



    "Tutafanyaje Sheila???



    "Hatuwezi kumnyang.anya kwasabbu bado hatuna nguvu za kutosha"



    "Sasa kwanini anataka kujiuwa kila SAA??? Aliongea Nasma huku wakitizamana na Sheilah.



    Salhat alikiinua kisu juu na kukishika kisha akaakishusha kwa kasi sana"





    Salhat alitaka kukishusha kile kisu mkononi, ila ghafla alisikia pingu ikililia mkononi mwake na kuunganishwa na kitanda. Alikuwa ni Akram aliyeweza kumfunga pingu kisha akakichukua kile kisu na kumtazama.



    "Unajua tayri uko na kesi ya jaribio la kutaka kujiuwa na bado unataka kujiuwa tena??? Alimuuliza huku akipanga vitu vizuri vilivyokuwa vimevurugika ndan.



    "Yani huyu natamani hata nimng.ate kama siyo afisa wa polisi hapa huyu mpuuzi angejikata tena. Alizungumza Nasma na kutaka kwenda kumpiga Salhat.



    "Huna uwezo wa kumshika binadamu na wewe njoo tukae kwa hapa tupumzike kwanza......alishauri Sheila na kukaa zake.



    Nasma alimtizama Salhat kwa hasira na kurudi alipoketi Sheilah na yeye akakaa zake.



    "Sikuwa nataka kujiuwa wasiwasi wako tu...... Nilitaka kupasua hili tunda" alijielezea Salhat na kuishika pingu aliyofungiwa mkononi.



    Akram alimtizama na kwenda kulichukua lile tunda kisha akalikata katikati na kumpatia kipande kingne.



    "Na umewezaje kuvurugua hapa hivi ndani ya dakika kadhaa?? Aliuliza Akram.



    "Magic!!! Alijibu Salhat na kutabasamu na hiyo ndyo ilikuwa Mara ya kwanza kwa Akram kumuona Salhat akitabasamu.



    "Magic??? Aliuliza Akram.



    "Ndyo......., unataka nikuonyeshe?? Aliuliza Salhat.



    Akram alitingisha kichwa akimpa ishara ya kuwa ndyo.



    "Hapana jamani... Me nimechoka Sheilah nenda wewe" alizungumza Nasma.



    "Wewe ndyo mdgo inuka hapo" aliongea Sheila na Nasma alifanya akama alivyoagizwa.



    "Naweza kukuvutia lile kabati lije hapa" aliongea Salhat.



    "We mpuuuzi nini?? Mbona anaagiza tu vitu vizito ukiambiwa ww usukume hilo kabati utaweza au ni kuwatesa tu wenzako!! Eeeee!!!!



    "Hakuna anayekusikia zaidi yangu we mburutie hilo kabati hadi lifike hapo anapotaka aliongea Sheila na kumtizama Nasma aliyekuwa kavimba kwa hasira sana huku akimtizama Salhat.



    ***** ****** *****

    Siku zilipita na hatimaye zikasonga mbele hadi Siku ya mahakama ikafika na Salhat sasa alituhumiwa kwa kesi mbili kesi ya kwanza ni kuwauwa wazazi wake na kesi ya pili ni ya kujaribu kutaka kujiuwa alisomewa mashtaka yote akakubaliana nayo akapewa kifungo cha miaka 32 jela. Ila aliruhusiwa kukataa rufaa ndani ya miezi mitatu kama hajaridhika na hukumu iliyotolewa.



    Salhat aliyaanza maisha yake mapya gerezani akiwa na mfungwa namba

    103 na tripu hii hakuna aliyedhubutu kumuonea kwani kila Mara Sheila na Nasma walikuwa msaada kwa upande wake.



    Akiwa anaota zake jua njee aliweza kuitwa na kuambiwa ana wageni wake. Alishangaa na kushtuka kwani hakuna aliyekuwa akimfahamu zaidi ya wazazi wake sasa wageni gani tena hao walioweza kumtembelea hadi gerezani?



    Alitoka akiwa na mashaka makubwa sana na ndipo alipokutana na sura mbili ngeni kabisa machoni pake.



    Wote walijitambulisha na mmoja alikuwa wakili aliyesema amekuja kumsaidia katika kesi yake.



    "Wewe unanijua mm???? Salhat alimuuliza wakili yule.



    "Hapana??? Alijibu wakili yule.



    "Basi nimeuwa na sihitaji msaada wowote kutoka kwa mtu yoyotd tule....kwani hii ndyo adhabu ninayostahili. Na we shida yako nn??? Aliuliza Salhat akimgeukia yule mwingne ambaye aliweza kuja na wakili yule aliyejulikana kwa jina na Benny yeye alikuwa wakili maarufu sana na mwenye sifa kibao.



    "Mimi ndiye niliona hujatendewa haki hivyo nilitaka tu kukusaidia" alizungumza.



    "Kama huko na fedha nyingi na unahitaji kusaidia watu basi usisaidie waalifu jaribu kuwasaidia yatima wajane pamoja na wazee. Baada ya kumaliza mazungumzo yake alisimama na kurudi zake ndani.



    Wakili Benny aliweza kutoka njee na mwenzke na hapo lilikuwa limepaki gari lililoonekana kuwasubiria na baada ya kuwaona vilishuka viatu vya kiume vikiwa vinatembea tembea vikitamani wafike pale alipo yeye.



    "Imekuwaje???? Alikuwa ni Johnny aliyeweza kufanya mchezo huo ili Salhat kesi yake irudi tena mahakamani na adhibitishe hana hatia.



    "Prf Johnny amekataaa kata kata tena kabisa" alizungumza Wakili Benny.



    "Kwanini usiendee wewe mwenyewe labda atakubali!!! Alishauri wakili Benny.



    Johnny alitizama gerezs lile na alishindws cha kuongea akabaki akishusha tu pumzi ndefu.



    Akiwa anapanda ngazi kwaajili ya kuelekea kule aliweza kupishana na Akram na hapo hapo aliweza kusikia kelele zisizoeleweka masikioni mwake zilizokuwa zikimuumiza ila baada ya Akram kupita kelele zile ziliisha. Alimtizama Akram kwa nyuma lakini hakumjadili sana hapo hapo simu ya Grace iliingia lakini hakuipokea alikata na kuendelea kuzama ndani ya gereza.



    Aliweza kufika na kukaa kwaajili ya kumsubiria Salhat ambaye na yeye alianza kuja kuelekea pale taratibu kabisa.



    Ghafla sms iliingia kwenye simu yake na ilikuwa ikisema

    "Mama anakuja Leo airport anakusubiri ukampokee" ulikuwa ni ujumbe ambao alikuwa akiuusubiri kwa takribani miezi6, ili aweze kulipiza kisasi chake.



    Alisimama na kupiga ngumi meza huku akisema mama Grace. Mlinzi aliyekuwa pale aliweza kulisikia hill neno la mwisho pekee yake.



    Wakati Johnny akifungua mlango kwaajili ya kutoka na kuondoka na hapo Ndipo mlango wa Salhat ulikuwa ukifunguliwa kwaajili ya kuingia ndani pale.



    Hivyo walipishana na hakuna hata mmoja aliyeweza kumuona mwenzke akiingia wala akitoka.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yuko wapi??? Aliuliza Salhat aliyekuwa na furaha usoni mwake.



    "Ameondoka!! Alijibu Askari aliyekuwa pale.



    "Kaenda wapi???? Aliuliza Salhat



    "Iliingia msg kwenye simu yake kisha nkasikia jina Grace tu alafu akaondoka kwa haraka" alieleza askari yule



    Salhat aliishia kutabasamu tu kisha akaanza kuyakumbuka matukio ya nyuma ambyo Mara nyingi yalipotokea matukio kati yake na Grace, johnny alijali zaidi kuhusu Grace.



    Aliirudi gerezani akiwa na mawazo sana huku nako Johnny aliendesha gari akiwa na hasira ya hali ya juu huku akikumbuka jinsi gani familia yake ilivyoweza kuteketezwa na Badra. Alipaki pembezoni mwa barabara na kupiga kelele ambyo wale majini waliweza kuisikia kisha wakasema.



    "Tumempata huyo ni Johnny" alizungumza Sheila na harakaharaka alishikana mkono na Nasma kisha wakapotea kwa pamoja.



    Huku nako Akram alikuwa ofisini kwenye kikao lakini alibaki katika hali ya mshngao.



    "Kuna tatizo gani IGP Akram.



    "Nahisi kama nimesikia Sauti ya mtu akipiga kelele" alizungumza Akram.



    "Kuna aliyesikia sauti hiyo??



    Wote waliokuwepo kwenye kikao walitingish kichwa ishara ya kwamba ni hapana.



    "Basi samahanini" aliongea Akram na kuendelea kuandika notes ndogo ndogo ndan ya kikao hicho.



    Lakini ni kweli Akram aliweza kuisikia sauti hiyo na ilikuwa ni ya Johnny ambaye alikuwa mbali sana na hapo alipo yeye"



    Johnny alikuwa wa kwanza kufika kabla ya Grace na alisimama huku akitizama katika sehemu ambayo ndiko walipokuwa wanatoka wasafiri.



    Akiwa amesimama pale kwa sekunde kadhaa aliamua kuinua simu yake kisha kutafuta jina la Grace kwaajili ya kumpigia lakini alibaki akiduwaa na kushangaa sehemu moja baada ya kuona viatu ambavyo viliweza kuvalia miguu ambayo mpaka Leo na hata kesho hatoweza kuisahau. Alitabasamu kidharau kisha akasema "Badra" alipandisha macho yake juu na hapo alikutana na tabasamu zito la Badra lililokuwa likimuelekea yeye na bila hiyana Johnny na yeye alilirudisha tabasamu hilo.



    "Nilifikiri hutaweza kunikumbuka since tumeonanaga Mara moja tu tena kwa Masaa kadhaa" alizungumza huku akimkumbatia Johnny.



    "Nakutambua hata ukipita gizani kwa harufu yako na haswa mwendo wako" alijibu Johnny.



    "Mmhh kwa mwendo wangu?? Aliguna na kushangaa kidogo kisha akauliza.



    "Ndiyo miguu yako siwezi kuisahau, alizungumza Johnny na kukaza macho kisha kumtizama Badra ambaye alishtuka na kumshangaa.



    Johnny aliachia tabasamu na kumfanya Badra na yeye acheke.



    "Aise lakini we unafaa kuwa mwigizaji umenishtua eti!! Alizungumza na kuishika moyo wake.



    "Ila sikutani Mimi naongea ukweli" alizungumza Johnny na kutabasamu kisha akampokea begi lake na kuanza kuongoza njia. Badra wala hakutaka kuwaza sana juu ya hilo alimtizama Johnny kwa nyuma na kuanza kutabasamu.



    "Kijana mzuri sana huyu" alizungumza na kutabasamu bado tabia yake ya kupenda kijana wadogo wala hakuiacha. Tayri alishamtamani Johnny bila kujua ya kuwa ni hatari kwa upande wake.



    ***** ******* ****







    Akram aliweza kukutana na Salhat ambaye alikuwa kasharudi tena katika hali yake ile ya kutokucheka na mtu wala kula chakula chochote kile.



    "Mbona hakuwa hivi?? Aliuliza Akram akiwauliza maaskari baadhi waliokuwa hapo.



    "Alibadilika tu baada ya kuja mkaka flani hivi aliyetaka kumuona lakini aliondoka kabla hawajaonana"



    "Mkaka??? Aliuliza Akram kwa mshangao.



    "Ndyo"



    "Mbona ameandika hana ndugu huyo kaka ametokea wapi?? Aliuliza Akram.



    "Namaanisha itakuwa ni mpenzi wake maana alivyotoja njee Salhat.... Alikuja akiwa na furaha baada ya kumuulizia nilimwambia alilitaja jina Grace kisha akaondoka kwa haraka......kwanzia hapo ndo amechukia mpka Leo hii chakula chenyewe ameanza tena kataa kula" alijibu Askari yule aliyekuwa akimuelezea taarifa hizo Akram.



    "Mpenzi wake!!!!!! Alirudia kwa mshangao sana tena kwa Sauti ya juu.

    Alimtizama Askari yule na kumtizama Salhat aliyekuwa ndani ya fensi ya gereza akiwa amejikumbatia tu huku akizungukwa na dactari mmoja pamoja na wafungwa wenzake waliokuwa wakimfarji japo ale kidogo tu.



    **** **** ****



    "Sheilah unauhakika huyu ndye Johnny mwenyewe tuliyekuwa tukimtafuta??? Aliuliza Nasma



    "Nina uhakika ndye kwani unakumbuka tulivyoambiwa na Malikia Zay, kwamba tutamtambua kwa kuwa atapiga kelele kwa uchungu na pia katika shingo yake anaalama, sasa cha kufanya ni kumkagua katika shingo yake" alizungumza Sheila.



    "Tutawezaje sasa kufanya hivyo... Wakati hatuna uwezo wa kumgusa binadamu yoyote?? Aliuliza Nasma.



    "Na hapo ndo kasheshe maana mashati yake yote yanakola......



    "Nimekumbuka tutaingia bafuni aliongea Nasma na alitazamwa na macho makali na Sheillah hata yeye alimtizama na kutazama chini.



    "Lakini hakuna njia nyingne tofauti na hiyo au wakati anavaa nguo" aliongezea Nasma na kumtazama Sheilah ambaye walikubaliana na hilo.



    ****** ****** *****



    Ulifika usiku na Johnny aliweza kujiandaa kwaajili ya kuelekea bafuni alikuwa akiishi katika nyumba moja na Grace pamoja na Badra lakini alikuwa akikaa chumba chake pekee yake.



    Alikuwa na hisia Kali sana hivyo alihisi kuko na watu maeneo Yale tena aliweza kuelewa ya kuwa siyo mmoja Bali wawili hivyo aliacha kuvua nguo Zake pale kisha akaingia bafuni huku akisema kimoyo moyo "na ona Leo Badra kaja kutembelewa na majini wenzake sasa ngoja niwaonyeshe"



    Alizungumza na kumwagia unga unga ambao aliutoa kwenye cheni yake iliyokuwa na kidani cha love aliupuliza tu.



    "Sawa twende sasa bafuni" aliongea sheilah.



    "Sawa"



    "Na ufunge macho" aliongezea Sheilah.



    "Sasa nikifunga macho nitaonaje alizungumza Nasma na kumtizama Sheila.



    Kisha wakapotea wote kwa pamoja zilisikika kelele tu na baada ya muda walionekana wakiwa sehemu tofauti na pale walipotarajia ya kuwa wataamka.



    Walikuwa ndani ya chupa ambayo iliweza kuwekwa na Johnny juu kabisa ya mti ambao ilikuwa vigumu kwa mtu kuweza kupanda hadi kufika huko alikowaeka.



    "Ni nini hii jamani??? Aliuliza Nasma.



    "Hapana sitaki kuamini ya kuwa sisi ndo tayari tumeshakamatwa na kufungiwa ndani ya chupa.....hapana jamani bado sijaishi hata duniani miaka mingi" alizungumza Nasma na ghafla alishtukizia kibao cha kichwa.



    "Usiongee upuuzi hapa,..... Tutafute njia ya kutoka hapa?? Aliongea Sheilah.



    "Na nivigumu sana kutoka hapa mpaka Edrick amalize kifungo chake ndyo atakuwa na uwezo wa kujua tuko hapa au mpka Huyo mkaka atuonee huruma na aje atutoe mwenyewe" aliongea Nasma.



    "Akuonee huruma....embu subiri na alijuaje ya kuwa sisi tuko pale mpka akaweza kutukamata?? Walitizamana wote na ghafla Nasma alibaki akiwa ameshangaa sehemu moja.



    Sheila alipeleka macho yake pale na ndipo alipokuta chupa nyingi tu zikiwa na majini wenzao.



    "Inamaana tulikosea yeye siyo Johnny Bali mkamata majini hapa hatutoki tena"!! Aliongea Nasma na kushusha uso wake chini.



    ***** ***** ****



    John akiwa anapita sebleni na Sigland yake aliyoweza kuivaa huku umbo lake likiwa limechoreka vizuri kabisa ndani ya sigland yake.



    "Uuuuwwhhh huyu kijana ni mzuri jamani hajatofautiana sana na Naseeb kama niliweza kumkosa Naseeb basi huyu siwezi kabisa kumkosa" aliongea kimoyo moyo akiamini hakuna aliyeweza kumsikia ila Johnny alisikia kila kitu na akabaki akicheka tu huku akiipeleka juice yake mdomoni tararibu kabisa.



    "Nafikiri Badra nimeshapata njia nzuri ya kukuuwa wewe......itakuwa vizuri kama kisasi changu kitalipwa na Grace" alitabasamu na kuondoka eneo lile.



    ***** *****



    Maisha ya Salhat yalibadilika kwa kiasi kikubwa kabisa hakuna tena mtu wa furaha na tendo hilo lilimuumiza sana Akram ambaye alijikuta akimuonea huruma sana Salhat.



    Siku moja akiwa amekaa huku anamtizama Salhat aliyekuwa amekaa juani huku wenzake wakicheza tu.



    Akram alishtuka baada ya Salhat alipomgeukia na kuiona sura ile ile ikiwa katika mavazi mengine kabisa.



    Alifuta macho yake na kumtizama tena.



    Aliona mavazi yenye kung.aaa na yakiwa yamesheheni nakshi nakshi zenye dhahabu tupu huku kofia ya kimalikia iliyoweza kupambwa vizuri na madini ya almasi ikiwa kichwani mwake.



    Alishtuliwa na mtu na alipogeuka na kumtizama tena alimuona katika nguo za kawaida za jela tu.



    Alijipiga kichwa chake na kuamini ni ndoto za mchana hizo. Wakati huo akimgeukia tena yule aliyemshtua..



    "Mgeni wake Salhat kaja!! Alizungumza Askari Yule.



    "Jinsia yake??? Aliuliza Akram.



    "Ni mwanaume" alijibu Afande yule.



    "Nitaenda Mimi wala usimuite Salhat" alijibu kisha akaondoka eneo lile na kuelekea sehemu ambayo wageni huja kwaajili ya kuwatizama wafungwa.



    "Salhat hayuko tayari kuzungumza na wewe unaweza ukaondoka" aliongea Akram akiwa katika sura ya kutokuonyesha mzaha kabisa.



    "Umemwambia nani kaja lakini" ilisikika Sauti ikiuliza huku ikipuliza kucha zake kwa kutoa uchafu.



    "Nimesema Mimi siwezi kukuruhusu wewe ukamuona Salhat"



    "Kwa kuwa wewe ni nani hadi unikataze mm??! Iliulizs Sauti ile kwa hasira kisha ikaonekana sura ya mtu ambaye alisimama na kukutanisha macho yake na Akram alikuwa ni Edrick.



    "Nafukiri hakuna kifungo chochote cha sheria kinachokataza mtu asimuone mhalifu eti kwasababu IGP ataki" alizungumza wakili William aliyeweza kuongozanan na Edrick.



    "Sheria yangu inaniruhusu ikiwa nitakuwa na hofu juu ya mfungwa wangu" alizungumza Akram.



    "Ni sawa lakini Mimi siyo mtu baki......Mimi ni mpenzi wake tuma askari wako akamwambie Salhat ya kuwa Mpenzi wake, mume wake mtaraji Edrickson yuko hapa anamsubiria" alizungumza kwa msisitizo huku akimtizama Akram ambaye macho yao yaliweza kukutana tena na kuna kitu Johnny aliweza kugundua juu ya Akram. Akabaki akimtizama juu mpaka chini.



    "Kuna shida gani?? Aliuliza Akram baada ya kugundua ya kuwa Edrick anamtizama sana.



    "Hamna" alijibu Edrick na kutizama mlangoni ambako aliingia Salhat akiwa na tabasamu pana kisha kumkumbatia kwa furaha sana huku machozi yakimtoka kitendo kile Johnny aliweza kukiona na kilimkisesha raha hivyo aliitizama malboro yake ambayo aliweza kubeba chakula kwaajili ya Salhat na document alizoweza kuziandaa ili Salhat assign na kesi irudishwe tena mahakamani.



    Aliteremka ngazi zake pole pole huku akiyakumbuka maneno ya Edrick mwambie mpenzi wake mume wake mtarajiwa..... Kisha akakumbuka vizuri kitendo cha Salhat kuja kwa furaha na kumkumbatia mpaka machozi yakatoka alipanda ndani ya gari lake na kuushika moyo wake uliokuwa ukipiga kwa kasi wakati hayo yakiendelea katika mwili wake Akram aliweza kuyasikia mapigo Yale ya moyo na kuanza kuyafuata yanapotokea na wakati anatoka Edrick alimtizama sana Akram.



    Akram kila alipozidi kupiga hatua ndivyo alivyozid kusikia mapigo yale ya moyo kwa ukaribu zaidi.



    Alipokaribia kufika na kuweza kuona anayasikia kwa mtu gani. Ilingia pikipiki na kumzuia Akram asiweze kumuona Johnny aliendelea kusogea kwa ukaribu zaidi na alipofika kumuona Johnny alipandisha kioo chake na kuondoa gari lake hivyo Akram hakubahatika kumuona.



    Alipotoka tu liliweza kutoka gari jingine lililokuwa likinfuatilia nyuma nyuma Johnny bila yeye mwenyewe kujua.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Tusameheane kidogo jina la wakili ni Benny na siyo William.



    Johnny aliweza kuondoka katika gereza lile pasina kujua ya kuwa yuko mtu aliyekuwa akimfuata kwa nyuma.



    Akram alisimama tu na kutazama gari lile lililokuwa likipotelea katika usawa wa macho yake.



    Wakati hayo yakiendelea Edrick alikuwa nyuma yake hata yeye alifanikiwa kuliona gari lakini hakufanikiwa kumuona mwenye gari.



    Alifunga macho yake na kuanza kuwatafuta Sheilah pamoja na Nasma kwa hisia lakini alishikwa na hasira baada ya kuwaona wako kwenye chupa.



    "Shenzi!!! Alizungumza na neno hilo Akram alilisikia alitaka kushuka chini ili aweze kulifuata gari lile kisha atambue ni nani aliyekuwa pale lakini aliitwa na wakili Benny hivyo hakubahatika kumuona Johnny.



    ***** ***** ****



    Johnny alifika chumbani kwake na kwa hasira alitupa document zake kitandani huku akili yake ikirejea kumbatio la Salhat mwilini mwa Edrick alishikwa na hasira zaidi na kujikuta akipiga ngumi ukutani hadi mkono ukachanika na damu zikaanza kutoka.



    Badra aliingia ndani na kumkuta Johnny damu zikiwa zinamtoka mkononi aliweza kumuweka kitandani kisha akachukua kiboksi cha Huduma ya kwanza na kuanza kumuhudumia huku akimpuliza na kumuuliza ni nini shida.



    Johnny alimtizama kwa hasira na baadaye alijua ya kuwa hasira Zak hazitamsaidia kitu zaidi ya kufanya mmbo yake kwenda mrama.



    "Hamna kitu" alijibu Johnny na kuutoa mkono wake mkononi mwa Badra.



    Badra alimshika tena mkono na kisha kumwambia atulie hawezi kujifunga bandage mwenyewe.



    Johnny alitaka kukataa lakini kwa mbali aliweza kuvisikia vishindo vya viatu alitambua kabisa huyo ni Grace.



    Alitabasamu kish akajisemea moyoni.



    "Mchezo unaanza sasa"



    Aliketi chini kisha akampa mkono Badra.



    "Sawa" alijibu na kuachia tabasamu mwanana lililomfanya Badra akiri ndani ya moyo wake kwamba Johnny ni mzuri kama Naseeb.



    Johnny alifungua vifungo vya juu ya shati lake na kufanya robo ya kifua chake kionekane. Aliweza kufanya hivyo makusudi kabisa huku akisikilizia viatu vya Grace vilivyokuwa vikikaribia maeneo hayo.



    Badra alibaki akimtizama Johnny kifuani kwake huku akiendelea kumfunga taratibu na wakati huo Johnny aliyafunga macho yake akijifanta hatambui ya kuwa Badra anamtazama kifuani kwake.



    Grace alifika pale kisha akasimama na kumtizama Badra kwa hasira ambaye bado alikuwa amezamisha mawazo yake katika kifua cha Johnny.



    "Mama!! Aliita Grace kwa hasira na kumfanya Badra ashtuke kisha kudondosha bandage.



    "Unafanya nini hapo??? Aliuliza Grace.



    "Namfunga Johnny........."



    "Tofauti na hicho unafanya kipi kingine??? Aliuliza Grace akiwa na jazba.



    "We Grace unafanya nini hivyo kwanini unamfokea mama kwa kiasi kikubwa namna hiyo......Mimi ndiyo nilimuomba mama anifunge bandage kwasababu nimeumia kama nimekosea basi nisamehe Mimi lakini usimgombeze mama" alizungumza Johnny kwa kujifanya anamtetea Badra ambaye aliweza kufumaniwa na mwanaye akimtizama mkwewe.



    "Hapana sijamaanisha hivyo Johnny, nilikuwa......" Kabla hajamaliza kuongea Johnny alimpa ishara ya anyamaze.



    "Sawa nimekuelewa hukumaanisha hivyo...........mama aliita na kumshika mikono Badra ambaye aliweza kuweweseka mwili mzima.



    "Nisamehe Mimi mama yangu, kwa kitendo cha Grace kukufokea naamini ya kuwa hakupaswa kukufokea na kile alichokitenda siyo sahihi kabisa, hivyo nakutaka radhi badala yake" alizungumza kwa ustaarabu wa hali ya juu .



    "Ona jamani.....ona mpaka anavyoomba msamaha kwa kosa ambalo siyo lake hadi kanitetea Mimi mbele ya Grace yani huyu kijana ni mkarimu sana" aliendelea kumsifia moyoni bila kujua ya kuwa Johnny alimsikia kwa kila anachokizungumza.



    Johnny aligeuza sura yake na kumtizama Grace aliyekuwa amefura kwa hasira akimtizama Badra bila kusema chochote kile.



    "Hata usipoongea kitu ......tayari sura yako inaongea" alizungumza Johnny kimoyomoyo.



    ***** ****** ****



    "Kusema kweli Mimi sikumbuki chochote ila nakumbuka ya kuwa nilimchoma kisu baba" aliongea Salhat.



    "Kumbuka kwa ufasaha zaidi ulichoma kisu??? Aliuliza wakili Benny.



    "Salhat!! Aliita Akram na kumtizama.



    "Embu amini ya kuwa hujawauwa wazazi wako kisha uvute kumbukumbu kwasababu unaamini umewauwa ndomaan hukumbuki chochote tofauti na hicho" aliongea Akram.



    "IGP Akram......kuna mwanamke amekuja kuonana na Salhat" alitoa taarifa askari mmoja Salhat aliweza kushangaa na kutazama na wakili pamoja na Akram.



    "Mwambie aingie ndani". aliongea Akram na hatimaye mwanamke yule aliweza kuletwa ndani.



    Alikuwa nama yake na Sarah aliyeweza kumkumbatia Salhat baada ya kumuona huku machozi yakimtoka.



    Baada ya muda walikuwa wawili tu katika chumba kile.



    "Salhat... Hata watu wote waamini ya kuwa wewe ni muuwaji wa wazazi wako ila Mimi bado naamini na nitaendelea kuamini ya kuwa huusiki na chochote katika hilo" alizungumza mama Sarah.



    Pia kitu kingne ni kwamba Siku ile ya tukio Sarah na yeye alitoka nyumbani usiku na kusema ya kuwa anakuja kukaa na wewe amsuburie baba yako atoke katika uvuvi kisha ampatie samaki.....lakini hakuwahi kurudi nyumbani mpaka Leo hii ninavyoongea na wewe...nimejaribu kutafuta hata maiti yake lakini nimeikosa kabisa na sitaki kuleta taarifa hizi polisi kwasababu watasema ni wewe tena ndiyo utakuwa umehusika na mauaji ya Sarah" alizungumza mama Sarah na machozi mengi.



    "Kwahiyo Sarah na yeye hujamuona aliongea kwa kigugumizi na machozi Salhat.



    "Sina imani ya kuwa amekufa nahisi aliweza kushuhudia mauaji na Sarah pekee ndiye atakayekuwa anajua nani muuwaji basi atakuwa amekamatwa na wauwaji hao.. Aliendelea kutoa maelezo.



    "Mama....kama Sarah yuko hai basi nitapambana hadi kumrudisha katika mikono yako na hata kama amekufa nitalipa kisasi chake na kuuleta mwili wake mikononi mwako" alizungumza Salhat.



    Mama Sarah alitingisha kichwa tuu kwani alijikuta akishindwa kuongea na kusindikizwa na machozi.



    Alimshika Salhat mikono.



    "Sipendi kabisa kukuona hapa laiti ningelikuwa na uwezo basi ningeweza kumkodisha wakili mpaka amalize hii kesi yako au kama kungekuwa na uwezekano ningefungwa Mimi badala yako....ona vile walivyoweza kuyaharibu maisha yako......ona vile mikono yako ilivyojaa alamaa na malenge lenge kila mahali....uso wako uliokuwa umejawa na tabasamu mwanana hatimaye binadamu wameweza kuupoteza......" Aliyazungumza maneno hayo kwa uchungu sana mama Sarah.



    ***** ****** *****



    "Kitu cha kufanya ni kumtafuta kwanza Sarah yeye ndye atakayeweza kuyakomboa maisha yako" aliongea Edrick.



    "Na tutampata wapi ndo tatizo?? Aliongezea Benny.



    "Lakini kwa kuwa Salhat yuko njee kwa dhamani mpaka mwezi unaofuata inabidi yeye ndye aweze kutupeleka maeneo ambayo ulikuwa ukipenda kukaa naye na hii ishu haitakiwa mtu yoyote kujua kwani kama yuko hai Sarah tutayahatarisha maisha yake" alizungumza Akram.



    Salhat alitingisha kichwa ishara ya ndiyo.......



    Wote waliingia ndani ya gari kisha wakaanza safari kwa pamoja.



    Wakiwa ndani ya Gari.



    Edrick alimtizama Akram huku akiwa ameshikilia juice yake aliamua kumwagia kwenye kola kidogo kisha akatoa hang a chief yake na kuanza kumfuta futa huku akimfunua katika shingo yake. Hatimaye alifanikiwa kuiona alama ambayo iliweza kumuanisha jambo flani.



    **** ***** ***



    "Nyie ni wapuuzi kweli tuliwap kazi ya kumfuatilia Johnny ambaye atakuwa Mwenza wake Salhat lakini nyie mnawafuatilia wakamata majini mpaka na nyie mnakamatwa" alilalama Edrick baada ya kuwatoa Sheila na Nasma katika mtego ule walioweza kuwekwa na Johnny.



    "Nimeshafanikiwa kumpata....."



    "Jamani ahsante mungu kama umeshafanikiwa kumpata inamaana kazi yetu imeisha sasa na sisi tutapewa nguvu na uwezo mkubwa kama majini wengine." Alizungumza Nasma aliyeyaona macho makali ya Edrick.



    Aliufunga mdomo wake kwa kutumia mkono wake.



    "Umempata nani???? Aliuliza Sheila.



    "Nimempata msaidizi wa Johnny....... Kupitia yeye itakuwa rahisi kwa nyie kuweza kumfahamu partina wake na Salhat... Kwani ni miaka mingi imepita tutakuwa tunamtafuta mtu kwa jina kumbe kabadili jina"



    "Hapo sijakuelewa unavyosema umempata msaidizi wa Johnny"



    "Nawza nikasema siyo msaidizi bali huyo anaweza kutambua kujua wapi mahali alipo Johnny na hata akipata shida yoyote yeye pia anaweza kutambua ya kuwa Johnny yuko kwenye matatizo kama ilivyo kwangu na kwa Salhat" alielezea Edrick.



    "Hapo nimekuelewa kwahiyo tukitaka kuzipata habari zote za Johnny sasa tutamfahamu Johnny kumpitia huyo! Aliongea Sheilah na kutabasamu huku akisema..

    "ni vizuri kwasababu tumepata pa kuanzia sasa"



    " na vipi kuhusu Salhat??? Aliuliza Nasma.



    "Bdo tunaendelea na kes.........



    "Hapana namaanisha nguvu zake za kijini bado 2 hazijamrejea?? Aliuliza tena Nasma.



    "Hapana labda tukishampata Johnny ndo tutajua kipi cha kufanya juu ya Salhat" alitoa maelezo hayo Edrick.



    ***** ****** ****



    Johnny akiwa nyumbnai aliweza kuisika Sauti ya mtoto ikilia katika masikio yake.



    "Ni nani huyo jamani Si anyamaze ananiumiza Mimi akili na masikio yangu kila saa naisikia Sauti yake tu" alilalamika Johnny baada ya kuwa anaisikia Sauti hiyo kila saa na asijue ni ya nani nakwa kusudio gani.



    Hiyo ilikuwa ni Sauti ya Sarah aliyekuwa ndani ya jumba lile lile Kubwa huku akiwa amefungiwa katika chumba chenye Giza tororo na hapo uliweza kuonekana mwanga dhaifu kisha vikasikika Sauti ya viatu vikikanyga na kuelekea kule alipo,yeye.



    "Mambo Sarah!!! Na hiyo ilikuwa ni Sauti ya Grace.



    "Vipi unaogopa eeee!!! Aliuliza huku akiinua uso wa Sarah uliokuwa umechafuka damu.



    Grace alitabasamu Kisha akageuza macho yake na kumpigiza sura Sarah aliyeweza kutoa kilio tena kilichoweza kupenya katikati ya masikio ya Johnny trip hii Johnny aliiwekea Sauti hiyo umakini kidogo na kugundua ya kuwa mtoto huyo hakuwa akipigwa Bali akiteseka hakujali sana aliendelea na mmbo yake.



    **** ***** ****



    Huku nako Edrick alimtizama Akram na kuelewa kabisa njia pekee ya kumpata Sarah ni kumpata Johnny na njia pekee ya kumpata Johnny ni Akram sasa ataanzaje kumwambia Akram juu ya hayo na Akram na yeye hazihivii kabisa.



    "Nielekee wapi sasa?? Aliuliza Akram.



    "Nimekwambia hivi tulipeleke mahali ambako moyo wako unataka kwenda, sehemu ambayo moyo wako unataka kwenda ndiyo sehemu Sarah alipo" aliongea Edrick.



    "Kivipi???? Aliuliza.



    "Wewe twende tu....mahali moyo wako unataka kwenda.....kumbuka nimekwambia.....



    "Umesema moyo...moyo....moyo au unafikiri sijakusikia na usinipelekeshe hivyo Mimi ni IGP wa polisi. Alizungumza Akram na kuwasha gari.



    Baada ya muda alizima na kusema.



    "Hapa ndiko mahali moyo wangu umenmbia nije" aliongea na kuteremka ndani ya Gari kisha akacheka.



    Edrick aliteremsha kioo na kulikuwa ni kituoni kwa polisi.



    "Hii kazi jamni itakuwa ngumu kama hatutampata Johnny" alijikuta ameropoka jina hilo bila kutegemea



    "Johnny" alilirudia jina hilo Salhat na kujilazimisha tabasamu usoni mwake kisha baada ya sekunde kadhaa akakunja tena sura yake.



    "Unashida gani na wewe.....unamfikiria yule professor mpuuzi sindiyo" aliongea Edrick na kumtizama Salhat kisha akatoka kwenye gari na kubamiza mlango.



    "Na huyu takataka mwingne na yeye anatuleta sisi kituo cha polisi....mbona kazi ngumu hivi na huyo Johnny sasa Si ajitokeze" aliendelea kulalama na kutizama kituo cha polisi huku akikuna kichwa chake.



    ***** ***** *****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Johnny akiwa anatembea zake kando kando mwa ufukwe wa habari huku akisikiliza muziki wa tararibu kabisa kwa mbali yake alionekana kijana ambaye alichomoa kisu na kumtazama Johnny kisha akatizama picha iliyokuwa kwenye mfuko wake wa sweta aliyoweza kuitoa na kufananisha sura ya kwenye picha ya Johnny.



    Aliinua simu yake na kupiga mahali kisha akasema.



    "Nafikiri nimeshampata sasa ulisema nimuuwe au.....!!!?? Aliuliza kijana yule aliyeoonekana hakuwa akihitaji utani kabisa pindi inapokuja kazi yoyote ilimradi iwe² na pesa ndefu.



    Akram akiwa ofisini kwake roho yake ilianza kumuenda mbio na akashindwa kujielewa kwann alijitahidi kujizuia lakini alijikuta akitoka njee kabisa ya kituo cha polisi kisha kuelekea sehemu ambayo hata yeye hakuelew ni wapi anapoelekea.

    Ila wakati anaondoka Sheila n Nasma walikuw eneo lile hivyo na wao waliamua kumfuata.



    Akram alielekea hadi baharini ambako alikuwepo Johnny aliyekuw amejifunika na sweta lake Kubwa huku kijana yule akichomoa kisu chake kidogo na tartibu kuanza kumfuaya Johnny.



    Akram alifanikiwa kuliona tukio hilo na haraka haraka alianza kukimbilia upande ule aliokuwepo Abdul aliyetaka kuuwawa.



    Mtu yule tayari alishaweza kumfikia Johnny ambaye alikuwa busy na kutembea huku akiendelea kusikiliza miziki yake.



    Akram alichomoa bastola na kumpiga Kijana yule bila hata yeye kutaraji hpo alimfanya Johnny ashtuke na kutoa earphone zake masikio.........alipotazama chini aliweza kumuona mtu mwenye damu. Ghafla watu waiingia eneo lile na kufanya wamzunguke.



    "

    Johnny alitoka tartibu taratibu bila mtu yoyote kutambua..



    "Sasa Shaeilah....kwa msongamano huo tutawezaje kweli kumtambua Johnny??? Aliuliza akiwa na mashaka makubw sana.



    Ghafla alikuja mtu aliyefunika uso wake na kumpatia Nasma Kisha akamwambia "peleka pale akapewe Huduma ya kwanza." Baada ya hapo aliondoka na kupanda kwenye gari lake kisha akaondoka zake.



    "Huyu na yeye ananituma tuma tu Mimi hapa" alilalama Nasma na kuanza kupiga hatua za kuelekea mbele ila baada ya kupiga hatua kama 3 alisimama na kugeuka nyuma ambako alikutana uso kwa uso na Sheila.



    "Haa ameniona alitamka Nasma"



    "Ametuona alitamka" Sheila



    Hivyo walijikuta wametamka vyote kwa pamoja.



    "Wewe mdada kimbizeni hiyo 1st aid mtaongea baadaye" alizungumza mmoja kati ya wale waliokuwa wakimpatia huduma kijana yule aliyetaka kumchoma kisu Johnny.



    Nasma na Sheila walibaki wakishangaana hadi alipokuja mtu mmoja na kuchukua kiboksi cha huduma ya kwanza kisha akaondoka huku akilalama



    "Watu wengine wajinga wajinga kweli yani......mnaona mtu anakaribia kufa badala ya mlete mlichoambiwa nyie mnatizama tu"



    Nasma alimshika Sheila kwa pamoja wakaanza kupiga kelele wote wakishangilia na kufurahia baada ya kuona sasa wanaonekana.



    "Subiri yuko wapi Johnny???? Aliongea Sheilah na waliachiama mikono kwa pamoja na kuanza kuelekea kule walipokuwa binadamu wakimpa huduma ya kwanza mtu yule aliyeweza kupigwa bastola.



    "Embu tupisheni tupisheni walizungumza huku wakijipenyeza.



    "Sisi ni madaktari tupisheni tunataka tumtazame mgonjwa" aliongea Nasma na watu wlifungua njia Nasma akamshika mkono Sheilah kisha wakapenya wote kwa pamoja mpaka walipomfikia Mgonjwa Nasma aliinama kisha akambinua na kumtizama mgongoni kwenye shngo ili aone Je kuna hiyo alama lakini hakuwa nayo.



    Alitikisa kichwa akimpa ishara Sheila kwamba siye na kitendo kile Akram alikiona akauliza

    "Amekufah???



    "Hapana hajafa" aliongea Nasma.



    Wakiwa hapo Mara mtu mmoja akauliza "yule aliyekuwa anatakiwa kuchomwa kisu yuko wapi???



    "Nlimuona akimpatia huyu docta kiboksi cha Huduma ya kwanza kisha akaondoka" alijibu mwingne aliyeweza kufanikiwa kumuona Johnny.



    Nasma alisimama mbio mbio na Sheila kisha wakatimua mbio na kuanza kufuatilia lile gari la Johnny.



    Lilishafika mbali sana na upeo wa macho yao hata namba za gari hakuna aliyeweza kuzishika hata kidogo.



    Walipotazama nyuma waliona watu wote macho kwao hivyo wangeshindwa kupotea na kutokea barabarani kwani wngewatisha binadamu.



    ****** ****** ****



    Johnny baada ya kufika katika chumba chake alisimama na kupiga ukuta ngumi kwa hasira hapo hapo Simu yake iliita.



    "Haloo hakuna mlichoweza kukifanya mtu mliyemtuma ni Bure kabisa kwani ameweza kupigwa risasi kabla hajafanya lile nililotaka nifanyiwe". Johhnny ndye aliyeweza kuagiza watu waje wamchome kisu yeye kwani alitaka kutengeneza ugomvi Kubwa baina ya Badra na Grace lakini ilishindikana baada ya Akram kutokea na kuharibu mipango yake.



    "Na huyo mpuuzi ni nani.....ni nani yule aliyeweza kumpigs risasi Mimi mtu niliyemwagiza" alizungumza akitaka kujaribu kusikiliza Sauti ya Akram..



    Alifunga macho yake na kuanza kuzipeleka hisia zake baharini.



    Huko alisikia maneno ya watu wakisema.



    "Atpona tu kwamaana amepigwa risasi ya mguu ila wewe uliyempiga wewe ni nani??? Aliuliza mwanamke mmoja.



    Johnnny aliweza kutega sikio ili asikie ni nani huyo aliyeweza kufanya hivyo.



    Ila alijikuta masikio yake hayasikii chochote zaidi ya kelele zilizoweza kuyaumiza masikio yake.



    "Ni nani huyo kwann siwezi kumsoma kile anachofikiria?? Alijiuliza Johnny bila kujipatia jibu lolote lile.



    Na hapo alianza kukumbuka ya kuwa kuna Siku alipokuwa hospitalini akiondoka baada ya kumaliza kumtolea Damu Salhat alishimdwa kumsoma mtu na masikio yake yaliuma Siku pia alipokuwa akitoka kituo cha polisi masikio yake yaliuma na Leo tena masikio yake yanauma hivyo hivyo na kupiga piga kelele za ajabu.



    "Ni nani huyo???? Alijiuliza Johnny na kujikuta akitamani afahamu ni nani huyo ambaye yeye anashindwa kumsoma kile anachokifikiri kabla ya kukiwaza.



    ***** ***** ****



    "Mnasemaje????!!!! Aliuliza kwa mshangao sana Edrick.



    "Mnatambua kabisa ni vigumu kiasi gani kumpata Johnny lakini bado mkabahatika kupata nafasi ya kumjua yeye ni nani ila nyie mkaichezea..



    "Siyo kuichezea aliongea Nasma.



    "Ila.harufu ya pafyumu yake siyo ngeni katika mapua yangu Nina hakika ya kuwa tayri tu nilishawahi kukutana naye somewhere lazima hiyo......ila usijali nitampata hata kwa kutumia harufu tu" aliongea Nasma.



    Na hapo hapo Sheilah alibaki katika hali ya mshangao.

    "Ni yule aliyeweza kutukamata sisi kisha akatufungia katika chupa.....ni yule mkamata majini aliweza kuzungumza Sheilah.



    "Ndyo ni yule harufu yake ni ile ile" alidakia Nasma.



    "Mkamata majini?????!!! Aliuliza Edrick kwa mshangao mkubw sanaa tu.



    "Sheilah we mpeleke" aliongea Nasma na kupotea.



    "We" aliita sheilah lakini alikuwa tayari ameshachelewa.

    Alimtizama Edrick na kumchekea naye Edrick alimrudishia kicheko feki kisha akamkamata na kumwambia huwezi nikimbia kama Nasma nipeleke huko. Alizungumza Edrick na kumfanya Sheila amtazame tu na kuacha kucheka tena.



    Hatimaye walifika katika nyumba ya kina Grace kwa njee na Sheila alimuonyeshea na kumwambia nyumba ndo hii kaahiyo unaweza kwenda aliongea hivyo na hatimaye alipotea.



    "Hawa nao ni wajinga tu yani wanaogopa binadamu lakini inanibidi niwe makini" alijizungumza.



    "Unafanya nini hapa???? Ilisikika Sauti ikiuliza iliyokuwa ikitokea nyuma yake.

    Edrick aligeuka na hatimaye walikutana uso kwa uso alikuwa ni Jay.



    "Kwani we unafanya nini hapa??? Aliuliza Edrick na kugeuka zake kisha akaanza kuitizama nyumba ya kina Grace.



    "Nakuuliza tena unafanya nini hapa???? Aliuliza Jay.



    Edrick alitaka kugeuka na kumsemesha jambo lakini aliacha hapo hapo baada ya kumuona Grace akitoka njee ya geti ya nyumba ile aliyokuwa akiitizama.



    "Haaaa Johnny Leo umeleta mgeni....sasa mbona humuingizi ndani karibu ndani....haaa Edrick karibu ndani jamani" alizungumza Grace na kumtizama Johnny ambaye akili yake yote ilirudi nyuma na kukumbuka kumbatio aliloweza kulipata kutoka kwa Salhat.



    'Siy.........kabla hajamaliza zungumza Edrick alimdakia kwa juu.



    "Ndyi Shemeji tulikuwa tumesimama hapa kidogo akinionyesha mazingira ya njee basi kwa kuwa na wewe umefika waweza nionyesha mazingira ya ndani" alizungumza Edrick na kumlamata Grace mkono kisha akaondoka naye eneo lile.



    Jay alimfuata nyuma baada ya Edrick kuingia ndani walikuwa wamekaa mezani na Jay macho yake hayakubanduka usoni kwa Johnny aliyekuwa akimsoma kile alichokuwa akikuzungumza ndani ya Kichwa chake.



    Johnny unashida gani mbona unamtizama hivyo mwenzko aliuliza Grace baadaya kuona Johnny macho yake yote yako kwa Edrick.



    Edrick alisema wala usimuwaze huyo mm nimeshamzoea wewe tuendelee kula tu.



    Edrick alimtizama Johnny na kutabasamu tu huku akisema.



    "Huyo ndye Johnny sasa anakula tu raha hapa kwa Grace yani atakuwa anamiliki jumba Kubwa lote hilo yani huyu anabahati lakini shida ni kuwa anakaa kwa mwanamke. Alijiongelesha moyoni na ghafla Johnny alisimama na kuipiga meza ya chakula makofi kisha akamwambia.



    "Huwezi fikiria kingine wewe tofauti na hicho unachokifikiria sasa?? Aliuliza Johnny kwa hasira na kuanza safari ya kuondoka ila aliposimama tu alikutana uso kwa uso na Badra ambaye alimuachilia tabasamu ambalo jay na yeye alilirudisha tabasamu hilo.



    Edrick alisimama na kumfuata Jay.

    "Nimelipenda shati hili naliomba aliongea Edrick na kuanza kumfunua Jay ili aweze kuaminu ndo yeye amah siye.



    "Wewe ni kichaa nini??? Alijibu Jay na kuanza kujifunika zake.



    Sasa wakaanza kukimbizana hadi kwenye chumba cha Jay ambako hatimaye Edrick alimkamata na kumfungua vifungo viwili vya shati kisha akamgeuza na kumfunua shingoni alidhibitisha ndiye ila ghafla na yeye Edrick alijikuta yuko chini na Jay akiwa juu yake.



    "Salhat mzima??? Aliuza swali hilo kwa Sauti ya utulivu kabisa huku akiwa anamtizama Edrick machoni ambaye aliamini ya kuwa Johnny anauliza swali hilo akiwa serious.



    Alitabasamu kidogo kisha akamjibu.



    "Ndyo mzima na nashukuru kwa wakili uliyeweza kumleta kwani anatusaidia sana ila bado kuna tatizo juu ya kesi hiyo" aliongea Edrick.



    "Tatizo gani hilo??? Aliuliza Johnny.



    "Sarah's" alijibu Edrick na kurudia tena "Sarah"



    "Sarah???? Alirudia Jay ikiwa kama swali na ghafla aliingia Badra ambaye alifunga macho yake baada ya kuwaona wakiwa wamekaliana juu na Johnny akiwa amevulika Shati lake na mpaka mgongo wake ukiwa unaonekana kwa kiasi kikubwa zaidi.



    "Hamna kitu" walijibu wote kwa pamoja lakini walivyotazamana walivyokaliana kila mtu alimrusha mwenzke na kukaa kivyake.



    "Hamna kitu lakini....walirudia tena kwa pamoja.



    "Hata Mimi sijasema kama kuna kitu" aliongea Badra na kutoka njee kisha kuwachaa.



    Wewe ndo sababu aliongea Edrick na kutoa mto kitandani kisha kaanza kumpiga nao Johnny ambaye na yeye alianza kusimama na kuanza kujikinga.



    "Basi urafiki wao rasmi ulianza hapo"...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***** ****** ****



    "Sasa tutafanyaje juu ya Salhat??? Aliuliza Sheilah.



    "Chakufanya hapa ni kumfanya Salhat amfuate Johnny tena kwa haraka zaidi kwani Johnny akilala na mwanamk mwingne tofauti na yeye itaweza kumfanya Salhat asiwe na nguvu zozote za kijini na tutakuwa hatuna faida tena kwani hata miaka yote tuliyokuwa tukimtafuta Johnny tayari itapotea tu.

    Alielezea Edrick.



    "Kasheshe ni kwamba Johnny na Salhat havipandi kabisa na hii ni kutokana na Grace" alizungumza Sheilah.



    "Basi tumuuwe Grace" aliongea Nasma na alijishtukia baada ya kuona amepigwa jicho na Sheila.



    "Nilisahau kumbe haturuhusiwi kuuwa kiumbe kisichokuwa na hatia......sasa tufanyaje???? Aliuliza Nasma.



    "Hilo ndyo swali na kujiuliza??? Ila ninachokifahamu ni kuwa Johnny anauwezo wake wa kumsikia mtu yyte chochote kile anachozungumza sasa nitatumia uwezo huo ili kumfanya awe karibu na Salhat" aliongea Edrick.



    "Na kwakuwa Salhat anaweza kufanya chochote juu ya Sarah basi tutumie njia hii kwaajili ya kuwaweka pamoja" alishauri Nasma na wote wakamgeukia huku wakimuuliza kwa shauku.



    "Njia gani????



    Alitabasamu Nasma na kutengenezea nywele zake vizuri.



    ***** ****** ****



    Ndani ya jumba Kubwa kabisa la kina Grace.

    Johnny alikuwa akielekea chumbani kwake ila umeme ulikatika ghafla baada ya yeye tu kukaribia kwenye chumba chake ila kutokana na mbalamwezi kuwa Kubwa haikumpa shida yeye kufungua mlango wake.



    Alishngaa baada ya kuona kuna mwanamke kwenye chumba chake alitizama njee kwenye mlango wake nakuuwacha wazi huku akisema mchezo umekwisha.



    Alijiaminisha kwa asilimia zote kuwa aliyoko ndani ya chumba chake ni Badra hivyo alitaka kumchonganisha tena.



    Alielekea mpka mahali alipo kisha akapitisha mikono yake katika tumbo dogo na kuikutanisha mbele ya kitovu kishaakaanza kumkwangua kidogo sehemu za tumbo huku akimlalia begani ila wakati akifanya hivyo akajikuta anakumbuka Siku ya kwanza kabisa kumshikaa Salhat eneo lile aliweza kutoa kamlio kadogo ambako hata hapo pia alikasikia.



    Johnny alishtuka na ghafla taa ziliwashwa hapo hapo aligeuka nyuma na Johnny alikutana uso kwa uso na Salhat alishtuka na kusema Salhat!!!!!!



    Huku nako katika chumba cha Ku control umeme wa nyumbs nzima alionekana Nasma akikung.uta mikono yake huku akisema show inaanza sasa hapa mpka tuondoke na moyo wa Johnny katika hii nymba.



    Sheila n Edrick walimpigia makofi ya kumpongeza Nasma.



    Huku nako walibaki wkitizamana tu bila hata mmoja kumsemesha mwenzke.



    Salhat aliamua kuuvunja ukimya kwa kujitambulisha.



    "Naitwa Salhat na mimi ni mfanyakazi katika hii nyumba nimeletwa kwaajili ya kuhakikisha chumba chako na cha Grace kinakuwa katika hali ya usafi mpaka siku mtakapoingia katika ndoa. Aliongea maneno hayo na wala Johnny hakuyajali kabisa alimfuata Salhat na kumkumbatia barabara huku akijizuia machozi yake yasitoke.



    Wakati wakiendelea katika hali hiyo huku nako alionekana Grace aliyekuwa akija katika chumba cha Jay ambacho mlango ulikuwa wazi kabisa.





    Wakiwa katika hali ile ile. Hapo hapo ilisikika Sauti ya Grace ambaye alijikwaa kidogo na kupiga kelele.



    "Uuuewhhhh ni nini hiki alisema Grace na baada ya kujikwaa na kumfanya Salhat ajitoe katika mwili wa Johnny ambaye bado alikuwa amemkumbatia pasina kujali chochote.



    "Johnny aliita Grace kisha akaelekea pale alipo na kumbusu Johnny mdomoni mbele ya Salhat.



    "Umerudi saa ngapi aliuliza Grace.



    "Muda siyo mrefu alijibu Johnny na kuitoa mikono ya Grace katika mwili wake..



    Salhat alitoa heshima na kuondoka ila alipofika mlangoni Grace alimuita.



    "Salhat"



    "Ndyo mama" alijibu Salhat.



    "Usiniite mama niite Mrs Johnny" alizungumza Grace.



    "Ndyo Mrs Jay" aliongea Salhat.



    "Umeshamuandalia mume wangu maji ya kuoga?? Alizungumza Grace.



    "Ndyo Mrs Johnny"



    "Umesha piga pasi nguo zake safi na kufua nguo chafu??



    "Ndyo Mrs Jay" alijibu



    "Sawa kazi nzuri" alijibu Grace kisha akaanza kumfungua vifungo vya shati la Johnny ambaye alishindwa kumzuia asifanye hivyo.



    "Unaweza ukaondoka sasa maana tunataka tuoge kwaajili ya kujiandaa na mapenzi ya usiku" alizungumza Grace.



    Salhat alitoka kisha akaufunga mlango na kuwaacha ndani.



    Johnny alimtizama Grace na kushikwa na hasira huku akikunja ngumi yake ila akuongea neno lolote lile juu yake.



    Usiku ulifika na Johnny akiwa kitandani kwake alianza kukisikia kilio cha Sarah sasa alaimua kuinuka na kufuatilia ili ajue kilio kile kinatokea wapi??



    Akiwa anafuatilia kilio kile mdogo mdogo ghafla alishikwa begani na mkono wa kike pale alipokuwa anakikaribia chumba kile.



    "Unaelekea wapi Johnny??? Ilikuwa Sauti ya Badra.



    Jay aligeuka kwa tabasamu zito kabisa huku akimtizama Badra.



    "Hamna Badra nilikuwa natizama tizama nyumba hii kwani kuna maeneo mengi ambayo siyafahamu kabisa" alijielezea Johnny huku akipiga hatua za kumsogelea Badra ambaye alianza kurembua na kujilegeza.



    "Badra umechafuka hapa" aliongea Jay na kumtoa Badra uchafu uliokuwa juu kabisa ya kitovu chake.



    Badra aliweza kusikilizia baada ya kushikwa juu na kubaki akiguguma......



    Jonnny alizidi kumsogelea Badra ambaye alikuwa akihema kwa staili ya nguvu kabisa na hatimaye alijikwaa baada ya kujikanagisha miguu yake na kabla hajafika chini Jay aliweza kumdaka kwa kumshika kiunoni na hapo hapo aliingia Salhat.



    Na kuwakuta katika hali ile Jay alimtizama Kisha akamtizama Badra aliona endapo atamuachia basi atajipiga vibaya sana katika kichwa chake.



    Hivyo alimuinua taratibu kabisa na kumuweka sawa.



    Badra aliirudishia vizuri nguo yake ya kulala na kumtazama Salhat.



    "Tayri nimeshaandaa kitanda chako madam" alitoa heshima na kugeuka.



    "We binti?!!!! Aliita Badra na kumfanya Salhat ageuke.



    "Kwahichi ulichokiona hapa usimwambie Grace"



    "Ndyo mama" alijibu na kuondoka zake.



    Johnny alimtizama na kujikuta anafanya mmbo ambayo Salhat hatoweza kuwa karibu na yeye.



    ***** ****** *****



    Salhat aliita Johnny na kumfuata.



    Salhat alisimama na kumtizama Johnny.



    Chumbani kwangu hujatandika kitanda alisema Johnny na kumsogelea karibu Salhat ambaye alimpita na kuelekea chumbani alipofika alishangaa baada ya kukuta chumba kimevurugika kabisa.



    Aligeuka nyuma na kumtizama Johnny ambaye alipandisha mabega juu na kumtizama Salhat kisha akaenda kukaa kwenye kochi akaweka laptop yake kwenye mapaja yake na kuendelea kuitizama huku akicheka na kusema moyoni.



    "Furaha yangu ni nikikuona karibu yangu" alisema huku akimtizama Salhat ambaye aliongea moyoni ya kuwa.



    "Nitamuuwa huyu mpuuzi anataka kunifanya Mimi punda wake hapa katupa tupa hivi vitu yani huyu.....alisema na kumtizama Jay aliyemtizama na kumpa ishara ya Afanye kazi.



    Aliinama na kumuokota mdoli mmoja ambaye aliifananisha sura yake na Johnny kisha akaanza kuifinyanga huku Johnny akiwa anamtizama tu.



    ******* ******* *****



    "Yuko wapi Salhat??? Aliuliza swali hilo Akram baada ya kukutana na Edrick.



    "Yupo kazini kwaajili ya kumleta Sarah" alijibu Eddy.



    "Kazini wapi???? Aliuliza tena Akram.



    "Mahali moyo wako ulipo" alijibu Edrick na kuondoka zake kisha kumuacha Akram pale.



    "Mahali moyo wangu ulipo?? Alijiuliza na kumtizama Edrick ambaye tayri alishapotea kabisa katika macho yake.



    **** **** ****



    " mama kesho ni Siku yangu ya kuvalishwa Pete na Johnny nataka nipendeze kuliko wanawake wote watakao kuja eneo hili" aliijinadi Grace.



    " Sawa " alijibu mama yake na kuendelea kutizama tv.



    "Mbona kama hujafurahia mm kuvishwa Pete na Johnny???



    "Nakwann nisifurahie mafanikio ya mwanangu??? Wewe nenda kajiandae tu" alijibu Grace na kusimama zake.



    Najua unamtaka Johnny lakini Johnny ni wangu na siwezi kumruhusu mwanamke yoyote yule amchukue Johnny wngu aliongea na kuanza kuondoka zake huku akimpigia simu Johnny na kumuuliza yuko wapi ili waende shoping kwa pamoja.



    **** ****** ****



    Mlango wa gari ulifunguliwa na alitoka Johnny ndani ya gari hilo baada ya Grace kumuona alimfuata na kumpiga busu la mdomoni wakiwa katika hali ile Salhat alitoka ndani ya gari akiwa anatizama chini huku akiwa ameshikilia mkoba wa Grace.



    Kila Mara Johnny amuonapo Salhat akiwa na Grace basi huwa anaishiwa pozi kabisa la kufanya chochote kile kwani anampenda sana Salhat na ahitaji kabisa amuumize Salhat.



    Grace alimtizama na kumfuta futa mdomo Johnny ambaye alikuwa akitizama pembeni tu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya hapo waliingia ndani ya shopping na Grace alikuwa akibadili nguo huku Salhat na Johnny wakiwa wamekaa sehemu moja.



    Johnny alikuwa akimtizama Salhat ambaye aliamini amechukia kwa kitendo kile cha yeye kumpiga busu Grace.



    Alikuwa akizishika shika kucha zake.



    Johnny htimaye aliingia ndani ya akili yake na kukuta Salhat awazi chochote zaidi ya matukio ambayo aliyaona yeye akiwa na mama yake Grace pamoja na Grace mwenyewe.



    Alimshika Salhat mkono ambao aliutoa na kutizama pembeni Johnny alimshika tena lakini Salhat alitaka kuutoa baada ya kuona ameshindwa alisimama na kutaka kumng.ta Johnny mkono ambao aliuzuia na kumtizama Salhat ambaye tayri alishaanza kulia.



    Johnny aliangalia chumba ambacho Grace alienda kubadili mavazi.



    Alimshika mkono Salhat kisha wakaingia katika henga moja ambayo ilikuw na nguo nyingi na hapo Johnny alimuweka Salhat ukutani kisha akairudishia henga ile ya nguo.



    "Salhat" aliita Johnny na kumtizama Salhat ambaye kwikwi ndiyo zilikuwa zikipokezana katika mdomo wake.



    Johnny aliyatizama machozi ya Salhat na kupeleka mdomo wake mashavuni kwa Salhat kisha kuyanyonya machozi Yale kupitia Wake.



    Salhat alitulia na kwikwi ziimuisha sasa wakabaki kutizaman tu machoni.



    "Salhat aliita tena Johnny na kuinua sura ya Salhat ambayo tayari ilishaacha kutoa machozi.



    "Salhat" aliita tena kwa Mara nyingine na safari hii Salhat aliitikia kwa Sauti nyororo kabisa iliyojaa bashasha.



    "Abeee"



    Sauti hiyo iliweza kupenya mpaka katika moyo wa Johnny ambaye aliushika moyo wake na kumtizama Salhat huku akisema.



    "Sauti yako hiyo jamani"



    Salhat alitabasamu na hatimaye alicheka.



    Yuko wapi Johnny??? Ilisikika Sauti ya Grace ikiita.



    Johnny aliyarudisha macho yake kwa Salhat kisha akamuiba busu la mdomo kwa sekunde kadhaa kisha akamwambia maneno Haya.



    "Haijalishi nitawek mahusiano feki na wanawake wangap lakini tambua ya kuwa mwanamke ninayempenda Mimi ni wewe.....kama ilivyokuwa moyoni mwako kwamba unanipenda Mimi", alizungumza hivyo na kumbusu tena Salhat ambaye safari hii alimshika kiunoni na kumsogeza karibu kbisa na kifua chake baada ya kumaliza kufanya hivyo aligeuka nyuma na kuanza safari ila aliuweka mkono wake katika tumbo dogo la Salhat kisha akambinya kidogo na kumuacha Salhat akiutoa mlio kidogo kabisa wa mahaba.



    Hatimaye ikifika usiku na ulikuwa wasaa kabisa husika wa kuvalishwa pete kwa Grace.



    Yuko wapi Johnny?? aliuliza Mc.



    "Anamalizia kuvaa atakuja muda siyo mrefu aliongea Edrick ambaye alikuwa pamoja na Sheila pamoja na Nasma.



    "Nasma ulifanya kama tulivyokuagiza??? Aliuliza Edrick.



    "Mimi ndiyo Nasma we tuliane hapa mtashangaa bwana harusi mtarajiw kakacha"



    Ndani ya chumba cha Johnny ulisikika mziki mdogo tu tena wa chini na wataratibu kabisa uliokuwa chumbani hapo alionekana Johnny akiwa amemshikilia Salhat huku akicheza naye.



    "Johnny" unaitwa bwana alizungumza Salhat ambaye alimtizama Johnny aliyekuwa hataki kumuachia.



    "Sawa dakika mbili za mwisho alizungumza Johnny na kuendelea kumshikilia vyema Salhat aliyekuwa akitaka kujitoa mikononi mwake.



    Johnny alimsogeza kwa karibu zaidi kisha akaanza kumpiga mabusu ya sehemu mbali mbali za mwili. Salhat alijitoa na kumwambia.



    "Mrs Jay anaweza akakufuata huku na akitukuta katika hali hii atachukia sana"



    Johnny alimuachia na kumtizama.



    "Mrs Jay yupi???? Alimtizama na kuvuta koti lake.



    "Basi usichukie nilikuwa nakutania tu" alisema Salhat na kuanza kumvalisha Jay koti vizuri.



    Jay aliendelea kumpiga busu Salhat ambaye alikuwa akirudi nyuma nyuma.



    Salhat" aliita Jay.



    "Abee"



    "Utakubali kuwa mke wangu tena mke wangu pekee yangu? Aliuliza Johnny.



    "Ndiyo ila najua ya kuwa wewe huwezi kuwa mume wangu pekee yangu" aliongea na kummalizia kumtengenezea koti.



    "Salhat" aliita tena Jay.



    "Will u Merry me??? Aliuliza Jay.



    Wakati huo nao Edrick akiwa akipiga stori na Sheila pamoja na Nasma na bila kumuona mtu Grace alipita na kuelekea juu ya chumba anachokaa Salhat.



    "Ndyo" alijibu Salhat na ghafla Jay alipiga magoti chini kisha akatoa Pete na kumvalisha Salhat aliyekuwa haamini macho yake.



    Salhat alimuinua Johnny na kumkumbatia kwa furaha sana na wakati huo mlango wa Johnny ulifunguliwa na Grace.





    Akiwa tayari ameshafungua mlango aliitwa na mama yake Badra.



    "Grace"



    'Abee"



    "Kwanini umetoka tena ukumbini??? Aliuliza Badra.



    "Johnny hayupo ndiyo maana nimekuja kumtizama anafanya nini. Alijibu Grace.



    "Hata Mimi nilipanda kwaajili yake ila nilijisikia vibaya ikabidi nirudi ndani kwanza kwaajili ya kujiweka fresh" alizungumza Badra.



    Grace alifungua mlango na tayri alimkuta Johnny akiwa amesimama mlangoni.



    "Ulikuwa unafanya nini muda wote huo??? Aliuliza Grace.



    "Nilikuwa namalizia surprise yako nashangaa kwann umekuja hapa??



    "Muda umefika ndo maana nimekuja" alizungumza Grace.



    "Sawa twende" aliongea Johnny na kumshika Grace mkono kisha kuondoka naye eneo lile ila wakati anaondoka alisikia Sauti ya mtoto ikisema.



    "Nisaidie nisaidie Tafadhali......Tafadhali nisaidieni huku ni giza naogopa"

    Johnny alisimama na kuanza kuisikiliza Sauti ile kwa umakini zaidi alitizama juu kabisa na kuangalia Sauti inapotokea baada ya hapo aliendelea kupiga hatua za mbele. Wakati hayo yakiendelea Edrick Sheilah na Nasma waliweza kuutizama mlango ambao Johnny aliutizama.



    "Nafikiri mlango ndo ule" aliongea Nasma na kisha kupotea.

    Huko walimkuta Sarah ambaye alikuwa akilia kwa Sauti ya kuomba msaada baada tu ya kuona watu, walimchukua kisha wakaondoka naye eneo lile.



    *** *** **** ***



    Siku ile ilipita nahatimaye pakakucha asubuhi yake na Salhat alikuwa jikoni akiandaa kitafunio cha asubuhi baada ya kumaliza alibeba kisha akapeleka chumbani kwa Grace ambaye alikuwa bado amelala baada ya kumaliza kumuandalia aliondoka hapo kisha akaelekea chumba cha Johnny ambaye alimkuta amelala alitenga breakfast pembeni kisha akakaa kitandani na kuanza kumpapasa Johnny usoni ambaye alikuwa amelala.



    Alitabasamu tu kisha akachukua shuka na kumfunika vizuri alipokuwa anataka kuondoka alishikwa mkono na Johnny na kumvutia kitandani kwake.



    "Umeamkaje???? Aliuliza Johnny.



    "Salama tu na wewe???



    "Hata Mimi salama pia" alijibu Johnny na kumvuta Salhat karibu zaidi.



    "Johnny niache sijafunga mlango mimi Mrs Jay anaweza akaja" alijisema Salhat.



    Johnny alimuachia na kumtizama.



    "Umenuna kisa nimesema Mrs Jay??



    "Mara ngapi nakwambia sitaki kabisa kusikia ukimuita mtu jina ambalo nilakwako wewe ndiyo mke wangu Mimi"



    "Lakini wa kivuli" alijibu Salhat.



    Johnny alimtizama na kuinuka kitandani ambako alikuwa amekaa.



    "Mara ngapi ninakwambia......sitaki uniletee chai asubuhi asubuhi hapa ndan?? Eeehhh kila Siku nakwambia sipendi mayai unipikie chapati lakini hunisikii" alizungumza Johnny.



    "Unaongelea kuhusu nini wewe mbona..........kabla hajamalizia sentensi yake alimuona Badra na hapo Johnny alimkonyeza.



    "Salhat"



    "Ndiyo madam Badra"



    "Fanya vile Johnny apendavyo aliongea Badra na kumshika bega Johnny.



    Salhat alimtizama na kumtizama Johnny ambaye alimtizama na kuona kabisa ya kuwa Salhat ajapendezwa na kitendo kile.



    "Sawa ngoja nikapike hicho ukitakacho" alisema Salhat na kuinua Sinia kisha akaondoka zake.



    Johnny alimshika mkono na kumwambia.



    "Acha hapo hiyo utatengeneza Siku nyingine" alisema Johnny na kuanza kuchukua Sinia alilolibeba Salhat.



    Salhat alilivuta Sinia na kuondoka zake.



    Johnny alimtizama na kutabasamu kwa mbali.



    "Badra" aliita Johnny na kumfuata.



    "Kipi kimekuingiza ndani kwangu asubuhi hii?? Aliuliza Johnny na kumtizama Badra.



    Badra alimsogelea karibu zaid kisha akaanza kumpapasa kifua.



    "Johnny unajua wewe ni mzuri sana na Mimi mara nyingi napenda sana vijana wabichi wabichi kama wewe kwani bado damu yangu inachemka"



    "Unaongelea kuhusu nini Badra?? Aliuliza Johnny huku akijua kabisa Grace yuko maeneo hayo ya pale pale na anawasikia.



    "Grace ni wakike na Mimi ni wakike pia raha unazompa Grace basi na Mimi nazihitaji raha hizo Tafadhali bhana nipatie raha hizo hata kwa Siku moja tu Mimi nitarizika" aliyazungumza maneno hayo Badra na kuanza kumsogelea Johnny ambaye alikuwa akirudi nyuma na ghafla aliingia Grace na kuita.



    "Mama!!!!!!!!! Aliita kwa hasira na kuchuku chungu cha uwa hapo pembeni kisha kumpiga nacho cha kichwa na kumfanya nyingi zimtoke kichwani..



    Johnny alimfuata Grace kisha akamnyang.anya chungu kile cha uwa na kumwambia acha kufanya hicho unachokifanya aliongea Johnny na kutabasamu nyuma yake huku akisema.



    "Bado hata haijafikia robo ya vile ulivyoweza kuvifanya juu yangu Badra bado nitahakikisha unamwaga damu nyingi kabla ya kukupelekea kuzimu na kukuuwa mwenyewe" aliongea Johnny moyoni na kuendelea kutabasamu.



    ****** ******* *******



    Badra alikuwa hospitalini akifanyiwa matibabu zaidi.



    Akiwa pale hospitalini



    "Grace huwezi nifanyia ujinga Mimi yani unipige kisa mwanaume ambaye hata wewe wala hakupend anampenda mwanamke mwingine kabisa tofauti na ww na unahisi anakupenda wewe" alizungumza Badra na kutabasamu tu huku akisema sasa nitakuonyesha kwamba Mimi ni nani??? Aliendela kula kiapo Badra na kuyauma meno yake kwa nguvu sana.



    ***** ****** *****



    "Grace ni vyema kama utaenda kumtizama mama yako hospitalini kwani yuko hospitalini" alizungumza Aisha ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani pale.



    "Siendi mahali Mimi anawezaje kumtaka mwanaume wangu kimapenzi, Mimi nitafanya chochote kile juu ya Johnny nipo tayari hata huyo apoteze maisha"alizungumza na kubwia juice yake na wakati huo nao Salhat alikuwa pale ma maneno hayo aliyasikia.



    Alimtizama Grace kwa hasira sana na ghfla Grace alidondosha Glass ile cheni kwa kusema anashangaa tu ghafla imemuunguza na hajui moto huo umetoka wapi ikiwa juice ilikuwa ya baridi.



    ***** ****** ****



    Akram kwa upande wake alionekana akiwa katika chumba cha mahojiano na Sarah.



    "Je ulishuhudia mauaji???



    Sarah alitikisa kichwa akimaanisha Ndiyo.



    "Ulishuhudia mauaji ya watu wangapi??? Aliendele kuuliza Akram.



    "Watatu......baba Salhat mama Salhat pamoja na mzee Ngoroba ambaye alikuwa usiku huo na baba Salhat" aliongea Sarah.



    "Unaweza ukaniambia ilikuwaje??? Aliuliza Akram.



    Salhat alianza kuvuta kumbukumbu zake na kukumbuka ilikuwaje.



    Baada ya Salhat kutumwa kiko na baba yake cha mzee Ngaboko.



    Yeye alitaka kwenda alikuwa akiwasili pande zile lakini alishangaa baada ya kuona watu wawili na mwanamke mmoja wakija eneo lile walimbeba mzee Ngaboko kisha wakamchoma kisu baba yake Salhat.



    "Nani huyo aliyemchoma kisu kati ya hao watatu????



    "Huyo mwanamk ambaye mpaka sasa sura yake ipo akilini mwangu" aliendelea kuzungumza Sarah



    "Eheee ikawaje???



    "Alivyomaliza kumchoma alimuacha pale kisha wakaelekea katika nyumba ya kina Salhat na huko alimwagia mafuta ya taa ndani baada tu ya kumuuwa mama yake Salhat.



    "Kwahiyo unataka kusema ya kuwa walimuuwa mama yake Salhat kabla ya kuchoma kibanda??? Aliuliza Akram.



    "Ndiyo"



    "Walimuuwa na nini??? Aliuliza Tena Akram.



    "Na kamba walimnyonga hadi kufa na hatimaye wakamwaga petrol na kuchoma nyumba" alijielezea Sarah.



    "Na hizo picha zilipigiwa wapi???



    "Hata Mimi sifahamu ila mara ya mwisho niliweza kuona ya kuwa kuna kijana mmoja alileta camera yake na kuanza kuwaonyesha kama amepiga picha vizuri.



    "Sawa na wewe walikukamata???

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nilisikia wakisema ya kuwa kesi hiyo wamemuandalia Salhat....... Na kwakuwa Salhat ni rafiki yangu ninayempenda siwezi kuachia hivi hivi hivyo nilitaka kwenda kumpa taarifa Salhat na hatimaye waliweza kunikamata na kuniweka katika chumba chenye Giza ambacho nimewahi kuiona sura moja tu kwanzia niingie katika hicho chumba"



    "Sura ya nani??? Unaweza ukatuambia ni nani???? Aliendela kuuliza Akram.



    "Simtambui jina lake ila Niko na uwezo mkubwa wa kuichora sura yake"



    Hatimaye vililetwa vitu vya kuchorea na Sarah aliaanza kuchora.



    Sarah aliweza kuchora na baada ya kumaliza kuchora sasa ampatia Akram mchoro ule.



    Akram aliutazama mchoro ule kisha akamtazama na Sarah aliyekuwa akitizama zake chini.



    Baada ya kumaliza kufanya hivyo Salhat baadaye aliingia ndani na kumkumbatia Sarah kwa uchungu mkubwa kabisa huku akiyafuta machozi yaliyokuwa yakitoka machoni mwa Sarah.



    **** ***** ****



    Grace akiwa ndani ya chumba chake aliingia Johnny aliyetaka kujua anaendeleaje kihali.



    Alimkuta Grace akiwa busy huku chumba kikiwa kimejaa majarida.



    "Johnny mume wangu afadhali umekuja njoo uangalie Leo nimetumiwa majarida kutoka kampuni mbalimbali zinazopamba maharusi......embu angalia na wewe ipi ni nzuri ambayo itaweza kutufanya sisi tupendeze kabisa" aliongea maneno hayo Grace ambaye alionekana kutokujali kabisa kuhusu hali ya Badra.



    "Hivi unaelewa ya kuwa kama kesi hii ingeenda mahakamani umefungwa.....lakini tumeshindwa kufanya hivyo kwasababu ni mama yako lakini wewe hujali kabisa kuhusu yeye badala ya kuwaza hali ya mama yako ikoje wewe unawaza maswalaa ya ndoa ambayo bado hayana umuhimu kwa sasa na maisha ya Badra. Aliongea Jonny na kumtizama Grace ambaye alionekana kutokuelewa kile Johnny alichoweza kukizungumza.



    "Johnny nataka tufunge ndoa mapema nataka uniowe mapema ili uwe mume wangu pekee yangu kwasababu sipendi kushare vile vitu nivipendavyo Mimi na watu wengine.



    Johnny alimfuata na kumtikisa mabega huku akisema

    "Grace amka na utoke huko uliko lala sasa hivi tunaongelea hali ya mama hapa hatuongelei maswala ya ndoa" alizungumza Jay.



    "Nimesema sitaki kujua kitu chochote kile kuhusu yeye nataka kujua uhusiano wetu.....nataka kujua ndoa yetu imefikia wapi kwasasa na utaratibu mwingine wa maandalizi ya harusi. Aliongea Grace huku akiendelea kufanya vitu vingine kabisa.



    "Haloo wew ndiye mpambaji ukumbi???Ndiyo sawa......basi Niko na sherehe yangu ya Harusi unaweza kuja na unmbie kwamba nitapambaje hapa nyumbani kwetu hadi pa pendeze"



    Baada ya Johnny kuona kabisa anazungumza na mwanamke ambaye hajali kuhusu hicho anachokizungumza yeye aliondoka zake.



    Baadaye alikuwa jikoni na Salhat huku akilalamika.



    "Yani li mtu naliambia kuhusu hali mbaya aliyonayo mama yake yeye wala hata hawazi ndo kwanza anazungumza vitu ambayo havip kabisa akilini mwangu Mimi" alizungumza Jay.



    "Ni sawa kama haviko kwenye akili yako kwenye akili zake vipo vitu hivyo....cha kuangalia hapa ni hali ya madam Badra kwanza kisha tutatizama swala la ndoa baadye kidogo baada ya hili kuisha" alishauri Salhat aliyekuwa akiandaa chakula jikoni kwa kuosha mboga mboga.



    Johnny alimsogelea kwa ukaribu zaidi na kumkumbatia kwa nyuma kisha akalaza kichwa chaka kwenye began moja la Salhat.



    "Salhat unajua hata Mimi sipendi kufanya vitu ambavyo vinaweza kukuacha wew na kovu lakini kuna vitu navihataji katika familia hii nahitaji kulipiza kisasi hivyo nitafanya chochote kile kuhakikisha ya kuwa kisasi chngu kimetimia" aliongea na kuendelea kujikumbatisha zaidi kwa Salhat ambaye alimshika mikono yote miwili kisha akamwambia.



    "Usijali kuhusu hilo popote pale patakapohitajika msaada wangu basi utaniambia na Siku utakayojisikia kunielezea kipi kilitokea katika maisha yako mpaka ukafikia kuwa na kisasi kizito namna hiyo basi pia nitakusikiliza.



    Wakati hayo yakiendelea aliingia Ashura na kukuta Johnny kamkumbatia Salhat kwa nyuma.

    Salhat alitaka kujitoa lakini Johnny hakutaka kabisa.



    "Mama",aliita Johnny kwa kumuita Ashura ambaye makamo yake yalishaweza kwenda mbali sana.



    "Salhat ndo mwanamke nimpendaye na ndiye nitakayeweza kufunga naye ndoa bila kujalisha nitapitia vikwazo ama mateso mangapi kwaajili yake nitafanya chochote juu yake" maneno hayo yalitoka kinywani mwa Jay.



    Ashura alitabasamu kisha akaelekea mpaka mahali alipo Salhat na Jay.



    Aliwashika wote katika sura zao kisha akasema



    "Mapenzi yake yakapate kuwa na nguvu zaidi ya Naseeb na Samia.......na mimi nataka kuwa hakikishia ya kuwa tripu hii sitaacha tena Badra asababishe Yale yaliyoweza kutokea miaka ya nyuma" kiapo hicho alikikula Ashura au Aisha na kutabasamu zake.



    ****** ********* ********



    "Lakini huyu ni tajiri maarufu sana hapa Tanzania tutaanzaje anzaje kwanza kumshatki.....pili kama ni mtu wa dezain hii lazima tuwe na ushahidi wenye uhai nachomaanisha anaweza kusema sisi tumemtengeneza Sarah aseme hivyo. Alizungumza Akram huku akiwa ameishikilia picha ya Grace mkononi iliyokuwa imechorwa na Sarah.



    "Unamaanisha nini sasa, na unajua imebaki wiki moja tu kesi irudi mahakamani??? Aliuliza Edrick.



    "Kutafuta ushahidi ambao uko hai kwafano alama za vidole vyake sehemu yoyote ya tukio" aliongea Akram.



    "Sawa" alijibu Eddy au Edrick baada ya kupata maelekezo hayo kutoka kwa Akram.



    Baadaye kidogo alionekana Salhat akiwa sokoni huku akichagua chagua vitu bahati mbaya alidondosha nyanya wakati anachagua na nyanya hiyo iliokotwa na mkono wa kike kisha kumpatia.



    "Halo naitwa Sheila" alijitambulisha Sheila ambaye aliweza kujitokeza mbele ya Salhat.



    Salhat alimshukuru na kuupokea mkono wake.



    "Me naitwa Salhat" alijibu Salhat.



    "Nashukuru kukufahamu Salhat....... Then unachagua nyanya za nini??? Aliuliza Sheilah.



    "Nyanya za kupikia" alijbu Salhat.



    "Naweza kukusaidia kufanya hvyo kwasababu mimi pia ni muuzaji hodari wa mboga mboga hivyo najua kuchagua" alijibu Sheilah na kuanza kumchagulia nyanya Salhat.



    Alimaliza kumchagulia na baada ya hapo alimpatia nyanya zake sasa walianza kuondoka huku wakipiga stori mbili tatu za kuulizana kazi wanazofanya wakiwa wanaendelea mbele walimkuta msichan ambaye alikuw aknyang.anyway vitu vyake na vibaka walimsaidia na vibaka wale walikimbia.



    "Vipi Dada pole jamani pole.....umeumia kwani??? Aliuliza Sheilah.



    "Hapana nashukuruni sijaumia sana ila wamechukua pesa zangu zote" hiyo iikuwa Sauti ya Nasma



    "Usijali nitakupa nauli ya kufika mpaka kwenu alijitolea Salhat huku akimkung.utakung.uta Nasma.



    "Nashukuru........nashukuru sana" alijibu Nasma na kutabasamu.



    ***** **** *****



    "Mmeshafanya vile nilivyowaambia" aliuliza Edrick.



    "Kila kitu tayari na kuna kitu nimehisi juu ya Salhat" alizungumza Nasma.



    "Kama nin??? Aliuliza Eddy.



    "Kama vile nguvu zake za kijini zimeshamrudia" alisema Nasma.



    "Umejuaje wewe????? Aliuliza tena Eddy.



    "We elewa vile nakwambia Salhat nguvu zake zimeshamrejea" alimjibu Nasma.



    Na wote walibaki wakimtizama tu maana sasa hakutaka kuwaelezea ni jinsi gani amemtambua ya kuwa Salhat tayari amesharudia nguvu zake za kijini"



    ****** ****** *****



    Salhat alikuwa akitembea huku akiwa amefura kwa hasira ni baada tena ya kumkuta Grace kifuani kwa Johnny aliyekuwa akijibebisha mwenyewe.



    Alitembea kwa hasira sana na baada ya kufika alivioa vyombo vichafu juu ya meza alipokuwa akivifuata kwa hasira kabla hajavigusa vikombe vile vilipasuka puuuuuhhhh!!!!!



    Alishtuka na kurudi nyuma na wakati huo Grace alikuwa akija eneo lile na Johnny.



    "Umefanya nini hapo???? Aliuliza Grace kwa ukali.



    "Samahami Grace" alisema Salhat.



    "Mara ngapi nakukataza kuniita Mimi Grace alisema Grace na kumpiga kibao Salhat ambaye alilishika shavu lake na wakati huo nao Johnny aliufinyanga mkono wake kwa hasira sana na akabki akiyauma meno yake.



    Salhat aligeuza uso wake kwa hasira na kumtizama Grace



    "Usinitizame Mimi na macho hayo" alisema Grace na kutaka kumpiga kingine lakini kibao kile hakikuweza kusogea mbele kwani mkono wa Grace ulikuwa kama umezuiliwa na mtu kwa nyuma ilihali hakukuwa na yoyote Johnny alitaka kusogea mbali lakini kwa bahati nzuri tayri IGP Akram alifika pale na kumzuia mkono wake kisha akamuuliza Salhat kama yuko salama.



    "Niko salama" alijibu Salhat na kutizama chini huku akishika sehemu aliyopigwa kwenye shavu.



    Akram alisogea mpaka pale alipo kisha baada ya kufika aliiutoa mkono wa Salhat na kuanza kumpuliza usoni pake.



    Baada ya Johnny kuhisi anashindwa kuvumilia alienda na akatoa mkono wa Akram kisha akamuweka Salhat nyuma yake.



    "We nani???? Na umefuata nini katika nyumba hii na unahaki gani ya kumshika mke wangu mtaraji??? johnny alijikuta ameuliza swali ambalo halikupasa kuuliza mbele ya Grace

    Ila Grace alitabasamu akiiamini ya kuwa mke mtarajiwa ni yeye.



    "Na wewe ni nani wa kuuniuliza Mimi maswali hayo??? Aliuliza Akram na kumsogelea karibu Johnny.



    "Unataka kunifahamu Mimi ni nani???? Aliuliza Johnny kisha aksema Mimi ndiye mmiliki wa nyumba hii na Ndiyo mmliki wa mwanamke uliyemgusa" alizungumza Johnny kwa hasira na kufanya Akram ahisi kelele kelele za ajabu masikioni mwake na alipomtazama Johnny alijikuta anaiona sura nyingine kabisa ikiwa katika mavazi ya mfalme Fulani aliyafikicha macho yake na kutizama tena hapo kwa pamoja sasa



    Alimuona Johnny pamoja na Salhat wakiwa wamevaa mavazi ya mfalme na malikia.



    "We ni nani???? Aliuliza tena Akram kwa mshangao mkubwa.



    "Nimesema hivi huyu mwnamke hapa hivi aliongea na kumshika Salhat.



    Ni................





    Johnny akitaka kuelezea umuhimu wa Salhat katika maisha yake ghafla ilitokea Sauti kwa nyuma ya mwanaume na kusema.



    "Ni Shemeji yake hivyo lazima amlinde kwa lolote libaya litakaloweza kumtokea" alizungumza Eddy na kwenda kuutoa mkono wa Johnny katika mkono wa Salhat.



    Grace alimsogelea Johnny na kumuuliza kama yuko salama.



    "Na wewe ni nani?? Wa kuingia katika nyumba hii kisha ukaanza kujibizana na mume wangu Mimi??? Aliuliza Grace kwa hasira.



    "Utanitambua baadaye Mimi ni nani lakini siyo sasa kwasababu muda wa kunitambua bado haujafika" aliongea Akram kisha akamtizama Salhat na kumwambia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nifuate" Salhat aliutoa mkono wa Edrick kisha akatoka njee kumfuata Akram kitendo kile kilimkera sana Johnny na alielekea kwenye chumba chake kisha akapigiza kwa kuufunga mlango wake kwa nguvu.



    Aliitoa mito kitandani na kuitupa tupa chini kisha akavuta shuka kwa hasira na kuikumbuka tena sura ya Akram.



    ***** ****** ******



    "Nafikiri muda umefika sasa wa Mimi kurudi nyumbani ili show niliyoweza kuipanga nikiwa hapa ikapate kuanza" alizungumza Badra aliyekuwa akimalizia kuweka vitu vyake katika mkoba wake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog