Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

WANAWAKE NI WAUAJI ?! - 3

 







    Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?!

    Sehemu Ya Tatu (3)





    [["Mwanangu vipi kuhusu yule binti naona siku zinaenda na wewe uko bussy sana wala huoneshi kujali kama awali, ooohoo angalia wasije kuwahi wenzako!"]

    ["Daah, baba bwana... Mbona siku bado ila nitajitahidi basi wiki hii nimtafute mshenga tuandike barua ipelekwe au unasemaje baba"]

    [["Akaah mimi sio muoaji shauri yako mwanangu ila kumbuka alivyokusaidia yule binti..!"

    ["Nakumbuka baba"]

    [["Basi ufanye hima kama utashindwa kumtafuta huyo mshenga basi itabidi uje huku tukutafutie"]]

    ["sawa baba"]

    Yalikuwa ni maongezi kwa njia ya simu baina ya Kamishna Shebby pindi alipokuwa ndani ya ofisi yake pale gerezani akizungumza na babaake ambae ni mzee Mwinchande aliyekuwa nyumbani muda huo na kumkumbushia swala la kumuoa Dk Asha.

    Ukweli jambo la mr X ndilo lililomchanganya sana Shebby na kusahau jambo la ndoa kwa wakati huo huku akiumia kila alipokumbuka vifo vya askali wenzake na kuzidi kupata motisha ya kumtafuta mr X.



    Kesho yake majira ya asubuhi na mapema Kamishna Shebby mara baada ya kufanya mawasiliano ya siri na Cj4 kama ilivyokuwa kawaida na taratibu yao waliyojiekea na kupeana riport zote muhimu walizozibaini katika mikakati yao ya siri juu ya mr X, ndipo Shebby alipomuelekeza Cj4 kuwa ataelekea huko hotelini kukutana tena na Hussein akitaka ampe kazi itayofanya awe anatoka mara baada ya kusikia kuwa tokea siku alipomuacha hajatoka kwenda popote kutembea wala hakukuonekana dariri za mtu yeyote kutaka habari zake wala wale maspy wa mr X.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kweli majira ya saa nne asubuhi Shebby aliwasili pale hotelini na kukutana na Hussein bubu.

    "Karibu baba karibu sana"

    alikaribisha Hussein akiwa mwenye furaha pindi alipofungua mlango na kumkuta aliyemgongea kuwa ni Kamishna Shebby

    "Ahsante sana baba"

    alijibu Shebby na kuingia ndani.

    "sasa baba ilikuwa nije kesho lakini nimekuja leo kwa sababu frani zitazofanya nikuongezee muda wa kuendelea kuwepo hapa lakini nilikuwa naomba unisaidie jambo moja"

    "Usijali baba, usijali kabisa nakusikiliza na kabla hujasema naamini niko tayari kama litakuwa ndani ya uwezo wangu"

    alijibu na kukaa vizuri Hussein huku akimuangalia na kumsikiliza Kamishna Shebby kwa umakini mkubwa.

    "Sawa mzee wangu, ni hivi... Kipindi nilipokuwa nauguza jeraha la mguu nilitokea kupendana na binti ambae ndie alikuwa daktari wangu alienisaidia kwa kiasi kikubwa sana hadi nikafikia hatua hii ya kuwa kama awali..."



    "Ndio baba endelea"

    "Sasaa, nilimuahidi kuwa nitafanya mpango wa kujitambulisha kwao ili tufanye taratibu za kufunga ndoa na kuwa mke na mume.... sasa Shida yangu baba nakuomba wewe uwe mshenga wangu unisaidie kuandika barua ya posa nikupeleke hadi nyumbani kwao na wewe ndie utayeingia na kunitambulisha sambamba na barua."

    "Mh! mwanangu lakini mbali na kukutibu tu umechunguza tabia yake kiumakini?"

    "Kwa hilo baba sina shaka"

    "Haya mwanangu mimi kwako sina pingamizi kwa hilo, fanya tuiandike hiyo barua na hata leo hii ukitaka unipeleke niko tayari kwa hilo kwa moyo mmoja ila nasaha zangu kwako ziko palepale usiwaamini wanawake wala usiwachukie kumbuka kuwa Wanawake ni Wauaji"

    aliongea Hussein na kumfanya Shebby atabasamu na ndipo alipotoka na kurejea tena akiwa na bahasha sambamba na karatasi na kwa msaada wa Hussein wakaanza kuiandika barua.



    * * * * * *



    "Mamaaa, mamaa, mama kaa tayari tayari leo usitoke kwenda popote"

    "Kivipi Asha mwanangu mbona ratiba zako sizielewi!"

    "mama bwana, ni hivi... yule mchumba niliekwambia barua yake inakuja leo"

    "Hee, ni wewe kweliii Asha au mwengineee"

    "Ni mimi mama mbona huamini!?"

    "Mh! unajua toka uliponambia siku ile nilichukulia mzaha kwa itikadi zako za kutojichanganya na watu, sasa sijui imekuwaje kuwaje hadi ulikubali kuacha shughuli zako na kumtibu mgonjwa yule tena ukidiliki kukaa kwao kwa zaidi ya miezi miwili na kama haitoshi unarudi na kuniambia ndio mchumbaako? au mlikuwa mnafahamiana muda mrefuu!!!"

    "hahaha hapana mama ni mapenzi tu, basi si unajua wewe ndie mama na wewe ndie baba. Ikija barua ijibu malizana nao bhaasi ahhaha"

    "Hahahaaa haayaa mwanangu nimekuelewa"

    Yalikuwa ni mazungumzo ya dk Asha akiwa na mamaake ndani ya nyumba moja ya kifahari ambayo walikuwa wanaishi wao wawili tu yaani mama na mwana.

    Haikujulikana kama yule mama alikuwa na watoto wengine ama laah, lakini mara nyingi pale alikuwa anaishi na Asha ambae yeye alikuwa mtu wa kutoka mno na alihakikisha mamaake anakuwa ni mwenye furaha siku zote.



    Baada ya masaa matano kupita yule mama akiwa amekaa sebuleni mara alarm ya mlango iligongwa na alipoinuka kufungua alikutana na mlinzi wao wa getini akiwa kasimama mlangoni.

    "Samahani mama, kuna mzee furani anahitaji kuonana na nyinyi vipi nimruhusu apite?"

    "Mruhusu tu"

    "Sawa Asante mama"

    alijibu mlinzi na kukimbilia tena getini na kumruhusu kuingia ndani ya jengo huyo mzee aliyemzungumzia ambae alikuwa ni Hussein bubu mara baada ya kuoneshwa nyumba husika na Shebby ambae alikuwa kasimamisha gari mita hamsini na eneo lilipokuwa geti la kuingilia kwa kina Asha.

    "Habari mama"

    "Salama karibu"

    alijibu yule mama ambae alikuwa na mwili wa wastani mara baada ya kusalimiwa na Hussein na kumruhusu akae.



    Hussein hakuchelewa kujielezea kilichomleta pale na yule mama hakuonesha kupinga wala kuwa na maswali mengi zaidi ya kukubali na kuipokea ile barua

    "Ahsante sana mama kwa ukarimu wako, vipi lakini mzee bado hajarudi kazini.?"

    "haha Hapana usijali mzee kwa bahati mbaya hatunae siku nyingi"

    "Oooh pole sana mama"

    alijibu Hussein na kunyanyuka akijiandaa kuaga mara baada ya kupewa tarehe ya kuja kuchukua barua ya majibu lakini kabla hajaaga alikumbuka kitu frani

    "samahani mama hivi unaitwa nani.?"

    "Ahaa mi naitwa Zena Hamisi Kidongo"

    alijibu huku akiwa katabasamu yule mama lakini ikawa tofauti kidogo kwa Hussein mara baada ya kulisikia lile jina.

    "ZENA HAMIS KIDONGO!!?"

    "Eeeh kwani vipi baba mbona umeonesha kulishangaa kidogo jina langu baya sana nini?"

    "Hapana mama, hilo jina sio geni sana labda nikuulize unamfahamu Mariam Hamis Kidongo"

    "MARIAM? Haah!! huyo ni Marehemu dadaangu kabisa we umemjuaje na alifariki miaka mingi sasa"



    alistaajabu yule mama na kumuangalia kwa makini Hussein ambae alijikuta anakaa chini kabisa akiwa kapigwa na bumbuwazi zito usoni mwake na machozi kuanza kumtoka akiikumbuka barua ya mariam iliyomuelekeza kuhusu ugonjwa wake na habari juu ya mtoto wake wa kike ambae alikuwa anaitwa Asha na kuanza kuamini kuwa huyu aliyekuja kumchumbia huenda akawa ni mwanae kabisa kwani hata jina alilotajiwa na Shebby pindi walipokuwa wanaandika barua ni Asha Hussein

    "Zenaa.. Oooh! Mi naitwa Hussein.. aaagh ndioooo Hussein Bakari... Hussein yule wa dadaako Mariam"

    aliongea huku machozi yakimtoka Hussein kama mtoto

    "Haa! Ina maana wewe ni Shemeji Hussein tuliyesikia umefungwa maisha sijui Kunyongwaa aaagh Ashaaaaaaaa ni mtoto wako aliekuachia dada!!aaaaaaaa Munguuuuu"

    alistaajabu yule mama na kuangusha kilio kilichomstua Asha mara baada ya kusikia anaitwa na kuanza kushuka haraka juu alipokuwa na kufika sebureni ambapo hakuamini alichokuwa anakiona na hakujua kisa na mkasa mpaka mamaake na yule mzee ambae alijua ni mshenga kugalagala chini wote wakiwa wanalia kwa uchungu mithili ya familia moja iliyopokea taarifa ya kifo cha ghafra kwa mtu waliyempenda na kumtegemea.



    "Mamaa .. maaamaa!!! Vipi nini kimetokea tena?"

    alifika haraka pale sebureni Asha huku akiuliza kwa mshangao na kumuinua mamaake ambae hakuwahi kumuona akiwa analia kwa uchungu kiasi kile tangia apate fahamu zake mara baada ya kurudi kutoka India alipokuwa amepelekwa akiwa bado mdogo na wafadhili walioishi nae kwa zaidi ya miaka kumi kabla ya kufariki kwao nae na alipofuzu masomo yake ya udaktari hakutaka kuendelea kubaki nje zaidi ya kurejea nyumbani Tanzania ambapo alipokelewa na mamaake yule ambae alimuonesha mapenzi kama mtoto wake wa kumzaa mbali na ukweli kuwa mamaake mzazi hakuwa yeye.



    "Mamaa mamaaa hebu nyamazeni basi mnambie nini kimetokea! Eti we mzee umeleta habari gani tena iliyomkosesha furaha mamaangu?"

    aliuliza kwa hasira Asha na kumuangalia Hussein bubu ambae yeye aliacha kulia kwa sauti na kukaa kitako akimtazama Asha akiwa haamini kama hii leo anakutana na mwanae ambae hakuwahi hata kum beba akiwa mtu mzima tena mrembo na asilimia kubwa alifanana na mamaake ambae alikuwa mwanamke wa kwanza kumpenda kwa dhati Hussein mbali ya kuwa alikuja kumtenda vibaya.

    "Asha, hapana mwananguuuu.... Usiongeeee kwa sauti hiyooooo... aaaaaaah Najua itakuwa ngumu kuelewa harakaharakaaa mamaaa .. ila huyo mzee unayemuona mbele yakooo ndiee....ndieeeee.... ndie babaako Mzaziiiiii....hiiiii"

    aliongea kwa kujikaza kisabuni yule mama mbali ya kuwa alikuwa na uchungu mzito moyoni mara baada ya kujitonesha kidonda cha kumkumbuka marehemu dadaake.

    "Whaat!! Mamaaa!!?.."



    alitaharuki Asha na kugeuka kumtazama Hussein kwa mshangao wa hali ya juu na kumtazama tena mamaake ambae sasa nae alikaa kitako na kuanza kujifuta machozi kwa kanga huku akimuangalia mwanae Asha ambae alikuwa bado kataharuki.

    "Asha mwanangu, huyo ni babaako.. Huyo ndie Hussein babaako ambae tulikuficha ukweli miaka yote ila leo nitahadithia kila kitu na yoote ambayo huenda hata Shemeji Hussein hukuyajua... naomba Asha unisikilize kwa umakini sana mwangu."

    aliongea kwa uchungu Zena huku akijifuta tena machozi ambayo yalikuwa hayakomi kumtoka na kumfanya Asha aungane nao na kukaa kabisa pale chini huku upande wake wa kushoto alionekana Hussein na kulia kwake alionekana mamaake ambae ni Zena.

    "Asha... Asha kwanza naomba utambue mimi si mamaako mzazi, nimeumia sana leo na naikumbuka sana barua ya dada aliyoniachia sambamba na maneno yake ambayo yote yalisafiri na maji mara baada ya mafuriko siku chache baada ya kifo chake kabla hawajaja wale wafadhili kukuchukua kwa msaada ulipokuwa darasa la nne baada ya kupita miaka sita ya maisha magumu na maajabu yako shuleni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanangu japo ilionekana sahihi kukuacha uende kulelewa na watu wengine tena ukiwa na umli wa miaka kumi tu na japo faida yake nimeiona na naiona mapaka sasa unanilea lakini ukweli nimeenda kinyume kabisa na maagizo aliyoniachia dadaa ambae ni mamaako. aaagh! Hussein unisamehe sikuwahi kumleta Asha wala kumwambia ukweli ambao dada alinisisitiza pindi atapokua nimwambie...

    Eee Mungu nisamehe lakini sidhani kama nimechelewa, naahidi sasa nitawaambia ukweli wote nilioujua kuhusu Asha Dada na Hussein."

    sauti ya mkwaluzo iliyoonesha dhahili imebeba maumivu mazito kutoka moyoni ilisikika ikitoka midomoni mwa Zena na kumfanya hata Dk Asha aanze kulengwa na machozi huku Hussein bubu yeye ndio kabisa alibaki kaganda kama sanamu akili na masikio yote aliyaelekeza kwa Zena japo macho muda wote yaliganda kwa Asha.

    Alimeza funda la mate Zena huku akirekebsha sauti yake kwa kukohoa kidogo kwa kujikaza kiume na kuanza kusimulia kisa chote kilichokuwa nyuma ya pazia juu ya maisha ya Mariam na Asha.



    * * * * *

    (MIAKA 23 ILIYOPITA)

    <<<<====>>>>

    ..................Simulizi Ya Zena....................

    ^^^

    Sintoisahau ile siku dada aliponipigia simu akiwa anaongea kwa shida sana akinisihi niende haraka kwake kwa sauti ambayo ilinitisha na kunipa wasiwasi hali iliyonipelekea niache shughuli zote nilizokuwa nafanya nyumbani na kukimbilia kituo cha daladala pasi na kumuaga yeyote wala kumsubiri mama ambae alikuwa ameenda kwenye shughuli ya harusi ya mtoto wa rafikiake mwananyamala,

    nilisimama kituoni na muda mfupi ilitokea daladala iliyokuwa inaelekea kule nilipokuwa naenda ambako ndipo alipopanga dada Mariamu na mara baada ya daladala ile kusimama kituoni nilipanda na baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari ilifika kwenye kituo nilichokuwa nashuka na kushuka huku nikitembea mwendo wa haraka haraka kumuwahi dada ambae nilikuwa najua kuwa anaumwa lakini sikuwahi kuwaza kama ugonjwa aliokuwa anatuambia ungeweza kumzidia na kumfikisha katika hali mbaya kiasi kile kama nilivyotafsiri kupitia sauti yake niliyoisikia simuni muda mfupi.



    Sikuamini pindi nilipoingia ndani moja kwa moja na kumkuta mtoto wa dada ambae ni Asha kipindi hiko akiwa na miaka minne tu akiwa analia pale chini huku akimtingisha mamaake aliekuwa amelala huku nzi wengi wakiwa wamemjalia sehemu ya koo na mdomo ameuacha wazi ulimi kiwa umemtoka mithili ya mtu aliyekuwa amebanwa na kitu shingoni.



    'Daaadaa!!....daadaaaa..!' Niliita kwa uchungu na kumsogelea pale chini huku machozi yakinitoka nikiwa sielewi nini kimempata dadaangu kufikia katika hali ile ya kushindwa hata kuitika na kubaki akinitazama tu huku macho yake yakitokwa machozi mfululizo na kunijengea imani ni kiasi gani alikuwa anapata maumivu makubwa sana ya ugonjwa ambao hadi dakika huo nilikuwa sijaujua hadi pale nilipojitutumua kumuinua kwa lengo la kumrudisha kitandani kabla sijafanya taratibu za kuita gari ya kumuwahisha hospitali na hapo ndipo niliposhangaa kuona uchafu uliokuwa unatoka chini kidogo ya shingo ya dada karibu na eneo la bega tena ajabu ulikuwa unatokota kadri alivyokuwa anataka kujaribu kusema kitu ama kumeza mate na kunifanya nitaharuki na kugundua sababu za nzi wengi kumzonga dada Mariamu.

    'Aaaaaaaah..daadaangu nini tena kimekupata?!!'

    Nilijikuta najisemea mwenyewe huku machozi yakinitoka kila nilipokuwa namuangalia na Asha alivyokuwa analia tena huku akiwa kashika bakuli ya plastiki mkononi akitingisha miguu ya mamaake bila kujali uwepo wangu.



    "maamaaa tata ujiiii... mama ujiiiii.."

    Sauti na maneno ya Asha yalizidi kuniliza na kubaini kuwa zaidi kilichokuwa kinamliza Asha ni njaa na ilionesha wazi hakukupikwa chochote siku hiyo toka asubuhi na masikini ya Mungu mtoto mdogo kama Asha ambae bado akili yake ilikuwa haijakomaa, hakuwa anajua nini kimempata mamaake hadi wamekaa na njaa muda wote na hakuwa na chochote cha kufanya kwa umli wake zaidi ya kumtingisha kwa kumuamsha mamaake apike basi huo uji ambao niligundua ndio kilikuwa chakula kikubwa alichokizoea yule mtoto.

    Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kutoka kuomba msaada kwa majirani mara baada ya milango mengine miwili ya ile nyumba iliyokuwa na vyumba vitatu tu alipopanga dada kuonekana makufuri yakining'inia na kuashiria wahusika hawakuwepo na kwa bahati mbaya hata wale majirani niliowafata ambao asilimia kubwa niliwakuta wanawake baada ya waume zao kuwa kwenye mishughuliko hawakuweza kabisa kunipa msaada.

    Hali hii ilinishangaza mno kwanini wale majirani wamekuwa na roho mbaya kiasi kile kwani kila niliyemfata kumuomba tena huku nikiwa nalia kama mtoto alionesha kunihurumia na nia ya kunisaidia lakini nilipomuelekeza nyumba yenyewe basi hubadilika na kuzuka sababu nyengine tofauti huku wengine wakidiriki kunicheka kabisa na kunitajia kiasi kikubwa cha pesa kama nitakuwa nataka msaada wao.



    Nilihumia na sikujua sababu za msingi kwanini waltu wa pale walimchukia sana dadaangu na kushindwa kunisaidia walau kumbeba kumfikisha barabarani stendi ya Taxi kwani kiukweli eneo lile alipokuwa anaishi dada hakukuwa na njia ya kuruhusu gari lolote kufika hata bajaji.

    Sikuwa na jinsi nilijikaza tena kiume na kupiga moyo konde nilikimbia kama mwizi ama kichaa moja kwa moja hadi pale stendi na kuwaita vijana wawili ambao nilipatana nao kiasi furani cha pesa na kukubaliana nami kwenda kum beba huyo mgonjwa kumleta kwenye Taxi ambayo nayo niliongea na dereva wake aliekubali kutusubiri.



    Nilitangulia ndani na kumfunika dada vizuri hususani sehemu za juu kuuficha uchafu uliokuwa unavuja na kutoa harufu kali kwa kitenge changu ambacho nilijifunga kiunoni na kujikuta nabaki na skin tight ndefu ambayo awali nilikuwa siwezi kutembea mtaani nikiwa nimevaa yenyewe tu pasi na kujifunga walau kanga ama kitenge lakini siku hiyo nilijikuta najisahau kabisa kwa kuchanganyikiwa na laiti kama nisingekuwa na walau hiyo skin tight basi hata uchi kabisa ningetembea pasi na kujijua wala kujihisi.



    Lakini kila nilipokuwa namuangalia dada alinionesha machoni kuwa kuna jambo anataka kunambia lakini anashindwa na nilipomtazama kwa makini alinipa ishara kwa kuangalia kwenye dressing table yake na kuniangalia mimi, alifanya vile kama mara tatu ndipo nilipoenda kuangalia hapo kwenye dressing table kuna nini na nilipekuwa kuangalia ndipo nilipoiona bahasha kubwa ya barua ikiwa imeandikwa jina langu kwa nje na ndipo nilipomuangalia dada ambae aliniashilia kwa macho kuwa ndio hiko kitu alichomaanisha lakini kwangu sikuona umuhimu wa kukaa chini kuanza kusoma barua wakati dadaangu amelala anateswa na maumivu makali..!!

    Nilichofanya niliitumbukiza kwenye handbag yangu ile barua na

    kuwaruhusu wale vijana waingie ambapo walipoingia niligundua mshtuko wao na adha ya harufu ya ajabu waliyokutana nayo mule ndani ambayo mimi sikuihisi nilipoingia hadi pale nilipojionea kidonda cha dada kilichokuwa kinavuja uchafu na hata hivyo sikukerwa hata chembe kwa ile harufu zaidi ya kuniongezea simanzi.

    "Dada, mzima huyu?"

    "Aaagh! Fanu maswali gani hayo? we kamata huko tum bebe tumpeleke.... unauliza mzima!! sasa toka lini mtu aliyekufa akawa anatoa ukoromo?"



    maneno ya kijana wa mwanzo yalinichoma sana japo sikuweza kujibu chochote lakini niliumia sana kuona dadaangu kipenzi akifananishwa na maiti angali yu hai kwa kigezo cha ile harufu..!?

    Aaaaah!! ama kweli wanaadamu tunakufuru kubwa.

    Afadhali kauli ya yule mwenzake aliyemjibu kidogo ilinifurahisha japo sikuipenda pia kwani dadaangu alikuwa hakoromi bali alikuwa anaugulia maumivu makali aliyokuwa anayapata lakini kile kidonda ndicho kilichokuwa kinaifanya sauti yake kusikika kama mkoromo kutokana na kutokota kwake kadri alivyokuwa anachezesha koromeo.

    Nilimnyanyua na kum beba Asha ambae bado alikuwa kashikilia bakuli lake akilia na kutoka nae nikiwa nyuma ya wale vijana waliom beba dadaangu Mariam na sikukumbuka hata kufunga mlango zaidi nilikuwa makini na kumshika Asha ubavuni nilipom beba kutokana na kulia kwake na nilipandwa na hasira zaidi mara baada ya kupita hatua chache kwa majirani wale ambao walininyima msaada awali na kuwakuta wameeka vigenge vya umbea kwenye baraza zao huku macho yao yakiwa kwetu na tolipofika karibu walinyamaza na kuishia kutututazama na tulipopita ndipo waliangua kicheko kikubwa kwa pamoja.

    '''HEEHEEEEEE KAPIMEEEEEEEE'''



    Nilitamani nirudi nikachambane nao lakini nilishindwa na kubaki nimefura hasira iliyochanganyika na maumivu mpaka tulipofika pale stendi ambapo kila aliyetuona hakuacha kutushangaa wakati dada alipokuwa aningizwa kwenye ile Taxi nami nikamnunulia soda na Keki mbili Asha mara baada ya kumalizana na wale vijana,

    na hapo kidogo kelele za kilio cha mwanangu Asha zilipungua pindi tulipoingia kwenye ile Taxi na kumueka mbele huku mimi nikikaa nyuma na kumpakatia dada ambae sauti aliyokuwa anaitoa iliyo mithili ya ukoromo ilizidi kuongezeka na kuniumiza zaidi kwa kugundua kuwa maumivu yanazidi mwilini mwa dadaangu kipenzi.



    Nilimuamuru dereva kutuwahisha mwananyamala hospitali na kumpigia simu mama muda uleule gari ilipoanza kutoka na kumuelekeza hali ya dada huku nikimficha juu ya kidonda cha ajabu kilichokuwa shingoni kwa dada kwa kujua kuwa mamaangu anakuwaga na uoga unaoambatana na presha ya kushuka hasa anapomuona mwanae anaumwa sana ama kazidiwa hivyo hata ile kauli yangu kuwa nampeleka hospitali ilitosha kumstua kule aliko na mara baada ya taxi yetu kufika hospitali mwananyamala niliwakuta tayari mama na baadhi ya rafiki zake waliokuwa kwenye shughuli wakiwa na nyuso za huzuni getini huku mamaangu akiwa peku kabisa licha ya kuwa alitoka nyumbani akiwa amependeza na zaidi alivaa viatu ambavyo alinunuliwa na dada Mariam.



    Ilibidi nishushe kioo na kuwapungia kuwaelekeza kuwa Taxi wanayoitazama inayoingia sasa ndiyo niliyomo na kweli walianza kuifatilia hadi iliposimama ndani ya ile hospitali na ndipo mama alipoingia kumchungulia dada pindi nilipomuacha na kwenda kuwaita manesi ambao walikuja haraka na kitanda cha matairi kwa nia ya kuja kum beba dada.

    Moyo uliniuma sana nilipotoka na kumkuta mama akiwa analia huku ameshikwa na wale shoga zake na manesi wa mwananyamala sitoweza kuwasahauuu..... aaaaaagh nakumbuka jinsi walivyokuwa wanampakia dada kwenye kitanda kile mithili ya mzigo mbali na kelele za ukoromo wa maumivu na kusababisha kile kitenge nilichomtanda kwa kuziba eneo lile la jeraha kufunuka na kudondoka na hapo kila mtu aliyekuwa jirani alistaajabu kushuhudia ule uchafu ambao hata mimi nilishangaa kuona umezidi mara dufu huku lile tundu likiwa si dogo kama nilivyoona awali bali liliongezeka na ilitaka moyo sana kulitazama.

    ''"Aaaaaaaaaaaaaaaaaaagh, Mariaaaaamu Mwananguuuuuuuuu"''

    Sintoisahau kauli hii ya mama angu.. mamaetu kipenzi aaagh,

    Sikujua kabisa kama ile siku niliyomuambia 'mama umependeza sana leo umekuwa kijana kabisa' asubuhi yake pindi aliponiaga anakwenda kwenye shughuli ya harusi ya rafiki ake wa miaka mingi Mwananyamala kama itakuwa ndio siku yetu ya mwisho kucheka pamoja....!



    Aaaaah sikuwaza wala kuhisi kama ipo siku mamaangu atanitoka ghafra namna ile tena mbele ya macho yangu na watu wengi kiasi kilee aaaah, masikini Zena mimiii nitalia na nani na tulizaliwa wawili tu na dadaangu ambae ndio nae alitoa ukoromo wa sauti ya juu uliotokea kwenye lile tundu na kurusha uchafu mwingi sambamba na damu mithili ya bomba mara baada ya kitenge kilichokuwa kinaburuza na kukanyagwa na nesi kudondoka na mama kupiga ule ukelele uliopelekea kuanguka chini.

    aaaaaaaaaah kwanini hamkunambia ndugu zangu kama mmepanga kuondoka pamoja kwenye ulimwengu wa mauti na kunifanyia suprize iliyoutesa moyo wanguuu na kuniachia upweke wa milele!!??...... aaaaaaaaaaah

    Nilijikuta nami nawasindikiza mama na dada kwa kupoteza fahamu pindi nilipokuwa nashuhududia vifo vyao ambapo mama alitapatapa na kukata roho pale chini muda mfupi baada ya kudondoka huku dada Mariam nae alimalizikia muda mfupi baada ya kutoa ule mkoromo mkubwa mithili ya firimbi uliorusha mafunda ya uchafu na damu.

    Sintosahau maneno ya yule daktari alipokuwa ananipa maelezo ya uthibitisho wa vifo vya ndugu zangu siku moja baadae pindi nilipopata fahamu na kuruhusiwa wodini.

    Alinambia kuwa kifo cha mamaangu kilisababishwa na presha iliyoshuka ghafra kupita kiwango vilevile dadaangu Mariam kifo chake kilisababishwa na kansa hatari ya koo.

    Sintosahau kabisa hata mara baada ya ndugu na majirani kuungana nami hospitali na kuchukua maiti kurudisha misiba ile ya kihistoria moyoni mwangu mpaka nyumbani na baada ya taratibu za mazishi kukamilika hatimae mama na dada wote walizikwa siku moja na makaburi yao yalifatana. aaaah! Mungu awaeke mahali pema.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku moja kupita baada ya mazishi ilibidi nitoke na vijana wa kiume wachache sambamba na mzee wetu wa mtaa tuliokuwa tunaishi tuliyezoea kumwita babu japo hakuwa na undugu wa damu na sisi lakini alikuwa jirani mwema na alisifika kuwa mzee mwenye busara sana.

    Safari yetu ilikuwa ni kule alipokuwa anaishi dada Mariam kwa niaba ya kukusanya vitu vyote lakini hatukuamini baada yakufika na kukutana na habari za uvamizi na wizi uliotokea siku moja iliyopita ambapo vitu vyote muhimu vya dada viliibiwa na chumba kubaki cheupe mithili ya mtu aliyehama.

    Japo ilituuma lakini tulipiga moyo konde na kushukuru tu, kwani iwapo tumempoteza mtu kabisa sembuse hivo vitu?

    tuliwaaga wale wenyeji tuliowakuta kwenye vile vyumba viwili ambavyo siku ile nilipokuja kumchukua dada vilikuwa na makufuri tu.



    Yule mzee alinisaidia kuongea na wale majirani visilani mara baada ya kumuhadithia mkasa ulipoanzia ambapo kwa busara zake aliweza kuambua sababu kuwa kumbe dada Mariam alikuwa ni mtu wa kujiona ona sana kipindi anaishi pale na mashoga zake watatu waliopanga pamoja huku mmoja wao akiwa si mwanamke bali ni shoga kabisa tena mbaya zaidi waliitumia ile nyumba kama dangulo la kuingiza wanaume hali iliyokuwa inawakera sana majirani kwa vile kujiona kwao, kutoshiriki kwenye misiba ya wenzao na matatizo mengine huku wakiwa ni watu wenye nyodo nyingi na ndio sababu kuu za kuwachukia wote na kuwatenga. Hapo kidogo nilielewa lakini bado sikulidhika na yale waliyonionesha lakini niliamua yote kuyapuuza na kurudi nyumbani sambamba na yule mzee na wale vijana.



    ulipita mwezi mmoja baada ya kumaliza matanga ndugu wote walitawanyika na kuniacha nikiwa na mwanangu Asha mtoto wa marehemu dada bila msaada wowote wa kimalezi zaidi ya kuniachia maneno ya pole na maisha mema na huo ndio ukawa mwanzo wa maisha mapya ya misukosuko na mazoea baina yangu na Asha.



    Lakini kabla hazijaanza tabu na misukosuko ambayo sikutaraji kama yatatukuta mimi na mwanangu yule niliumizwa na kulizwa na kitu kimoja ambacho nilikikumbuka mwenyewe baada ya kusahau kwa muda mrefu..... Kitu chenyewe ni barua, barua ambayo ilionesha wazi kwa nje ilinihusu mimi, barua ambayo sikujua imebeba nini hasa ndani yake, barua ya mwisho ambayo muandishi wake nilijua kama hatoniandikia tena barua nyengine milele, ila kwa barua ile niliweza kuihisi sauti yake akiongea pindi nilipokuwa nasoma hati ya maandishi yake, barua toka kwa marehemu dada Mariam ambayo licha ya kupotea kwake kutokana na janga kubwa la mafuriko ya mwaka lililokuja kutokea wiki chache baada ya kuisoma lakini maneno yake yaliendelea kuishi akilini mwangu kila nilipomkumbuka yeye ama nilipomuangalia Asha.

    Barua yenyewe ilikuwa hivi................



    ^..................................................................................^

    Mdogo angu Zena, naandika barua hii nikiwa na maumivu makali sana sehemu za shingo na kifua hususani kooni na hivi sasa uvimbe ambao awali ulikuwa kwa ndani lakini sasa umezidi kutokeza nje ya shingo, najua muda wowote unaweza kupasuka na kuimaliza safari yangu ya hapa duniani kuianza safari mpya kwenye ulimwengu wa ahadi kwa kila mja aliyeumbwa.

    Uvimbe huu si wa jipu la kawaida bali ni ugonjwa ambao nimeuficha kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na aibu na kutopenda niwatie majonzi mapema lakini kwa kuwa sasa naona ule wakati wa kuumbuka umefika nimeamua kukuweka wazi ukae ukijua kinachoniua ni nini..

    Hiki kinachonitafuna Zena ni Kansa.



    Kansa ambayo imesababishwa na wadudu wabaya waliotoka kwenye mbegu za mwanaume nisiyemjua ambae kumbe alikuwa na ugonjwa m baya sehemu zake za kutungia mbegu nami bila kujua nilijikuta nazipokea mdomoni kwa kumnyonya uume wake mpaka anafika kilele kinywani mwangu nikijua nampagawisha ili nimchune vizuri kumbe nilikuwa naeka lehani maisha yangu mara baada ya bakteria hatari ambao sijawahi kuota kama wapo walipoingia na kueka makazi pembeni ya koo langu kutokana na ukweli huwezi kutema chote kile kichofika kwenye ulimi na hiyo ndio ikawa mwanzo wa tatizo ambalo nilikuja kugundulika tayari nimechelewa.



    Ni aibu lakini nimeamua kutubu kwa kukuandika ukweli huu mdogo angu Zena nakusihi kama nawe una tabia ya kunyonya tupu za wanaume kwa kuamini ndio unamkoleza nakusisitiza acha haraka tabia hiyo na hili uje kumfunza hadi mtoto ninayemkabidhi kwako baada ya kifo changu.

    Narudia Zena kumbuka kinachoniua dadaako na simjui ni mwanaume yupi aliyeniachia hawa bakteria walioshindika kutokana na kuwafanyia mchezo huu karibu kila mwanaume niliekutana nae kimwili kasoro mwanaume wangu wa kwanza na yule wa pili ambae ndie baba halali wa mtoto huyu nae ni shemeji ako niliyemuacha kimakosa mimi mwenyewe baada ya kumsaliti sana ambae ni Hussein.



    Zena nakukumbusha pia hata utapoolewa ukiwa na mumeo usikubali kumuacha awe anakunyonya tupu yako mpaka unafika kishindo kwani kuna hatari kubwa ya magonjwa ya ajabu kupitia sehemu za siri si kwa mwanaume wala mwanamke ambayo mengi hayajaibuka ila leo hii mimi nimekuwa mfano wa mavuno ya tabia hizi chafu ambazo asilimia kubwa ya vijana si wa kike si wa kiume wanafanya haya kila siku ilihali sehemu husika zipo. Basi waambie wataokusikia habari za kifo changu labda utasaidia kuwaokoa baadhi yao japo najua wengi watakupuuza na hata wataokaidi basi waache waendelee ila wajue yanaweza kuwakuta kama yaliyonikuta mimi kwani hizi ni zama za mwisho wasiige mafunzo ya kishetani yanayosambazwa kwenye mikanda ya ngono.

    Kifo kinauma sana hasa kifo cha dhihaka kama hiki... Dawa pekee ya haraka niliyoambiwa na daktari ni kukata sehemu inayoshambuliwa lakini sasa mimi nashambuliwa koo maana yake hata nikikatwa haitakuwa tiba.



    Huo ndio ukweli Zena najua mwanangu hatolelewa na babaake wala hajawahi walau kushikwa mkono na babaake ambae wote tunajua maisha yake anayamalizia gerezani.

    Basi nakuomba pindi utapokuwa unamlea Asha mlee katika maadili tofauti sana Zena mdogo wangu na uwe unampeleka walau mara moja kwa mwaka gerezani akamuone babaake kwani taarifa za uwepo wake naamini anazo.

    Kumbuka Zena kumbuka mpeleke Asha madrasa akajifunze elimu ya dini.

    Naamini kifua chake kitapojaa imani na jina la mungu litapokaa kinywani naamini atafauru majaribu mengi ya kishetani na kamwe hatokuwa mwanamke muuaji kama walivyo wanawake wengi wa leo nikiwemo mimi na wewe kwa kitendo chako cha kutoa mimba zaidi ya mara mbili tulipokuwa shule.

    Nakusihi nawe utubu mdogo wangu na uzingatie usije kumpa mtu mwengine amlee Asha naogopa asije kuharibika na kuwa mwanamke muuaji akaja umiza wanaume kama mimi nilivyomuumiza babaake.



    Kwa heli Mdogo angu,

    mimi natangulia....

    Mungu akipenda tutaonana kwenye ulimwengu wa mauti pindi nawe utapokuja mwaka wowote.



    ^................................................................^



    Barua ya dada ilifufua msiba upya moyoni mwangu huku nikilia kwa uchungu sana kwani hata mimi nilikuwa na tabia hiyo ya kunyonya tupu za wanaume lakini daaaah! kumbe harufu na uchafu ule ambao ulikuwa unatokota shingoni mwa dada ni kansa ya koo?!!

    Tena chanzo chake ni mchezo ambao hata mimi nilikuwa ni mmoja wa wachezaji wake...!! aaagh nilipogundua na kukumbuka mateso ya dada hadi pale alipotoa mkoromo mkubwa tena sauti ikitokea kwenye tundu lililokuwa linarusha uchafu wa usaha na damu hadi kufa kwake.... Nami kuanzia muda huo niliapa kamwe sitoruhusu mwanaume aninyonye utupu wala mimi kumnyonya utupu na kuahidi kuutumia mdomo wangu kwa kula, kunywa na kuramba vile vilivyohalalishwa tu.



    Lakini mwezi mmoja baadae lilitokea janga la mvua iliyosababisha mto uliopita jilani na pale tunapoishi kufurika na maji kupasua kwenye makazi ya watu ikiwemo nyumba yetu majira ya usiku ambapo nilichobahatika ni kujiokoa mimi na mwanangu Asha niliyeachiwa na dada na hapo ndipo tulipogeuka wahanga wa mafuriko tulioishi katika kambi maalum uwanja wa taifa baada ya kupoteza makazi kwa zaidi ya miezi miaka miwili.

    Serekali yetu imejaa hila na rushwa kwakweli japo machoni na midomoni haiko hivyo kwani baada ya kupewa ile kambi kipindi cha janga lile na kutusaidia miezi michache ya awali, ndipo walipotutelekeza kabisa na hapo nami nikakata shauli baada ya kumpata bwana ambae alitukaribisha kwake kabla ya kumuhama baada ya manyanyaso na kumuonesha chuki za wazi mwanangu Asha ndipo nilipopanga maeneo ya uwanja wa fisi na kujiajili kwa kuutumia mwili wangu. aaaag Moyo unaniuma sana kwa nilichofanya kwani nilimpeleka Asha kwenye shule ya watoto walio kwenye mazingira magumu sana na yatima na kumuacha kwa muda huko mwanangu Asha si kwa lengo kuwa simpendi bali kwa kumueka mbali na mazingira yale ambayo nilijua yatamuharibu kisaikolojia pindi atapokuwa anaona mamaake kila siku nalala na wanaume tofauti tofauti.



    Siku zilikwenda huku kipato changu kikiongezeka na kuwa namtembelea mara kwa mara mwanangu Asha ambae alikuwa anazidi kunipenda siku hadi siku na pia nilizidisha mapenzi kwake hasa baada ya kipaji chake cha elimu kuonekana kwa wafadhili wa kihindi miaka minne tu tokea aishi pale na alipata bahati ya kupendwa na wale watu ambapo zilifanyika taratibu za kuondoka nae kwenda kumsomesha huko japo awali nilitaka kukataa lakini kwa ushauri wa watu na walimu wake sambamba na kalatasi za serikalini na kuhakikishiwa kuwa mwanangu hawezi kupotea na hii ni kwa faida yetu wote pindi atapofanikiwa huko kwani hata mimi nilishindwa kumlea hadi nikampeleka pale ndipo akiwa na miaka kumi tu niliweza kuvunja vunja zaidi yoote niliyoagizwa na dada Mariam juu ya Asha na hiyo ndio safari ya mafanikio yaliyokuja kuibuka na kufaidi matunda ya mwanangu Asha na kwa bahati mbaya dawa nilizokuwa natumia nisipate mimba ziliniletea madhala pale nilipohitaji mtoto nilishindwa kabisa kubeba mimba na nilipochunguzwa nilihakikishiwa haitawezekana kubeba mimba na ndio sababu hadi leo sina mtoto yeyote zaidi ya mwanangu Asha ambae siku zote aliamini mimi ndie mamaake mzazi.



    <<<===>>>

    .............................

    * * *



    Kipindi Zena akimalizia simulizi yake iliyowafanya Hussein bubu na dk Asha kubaki wanadosha machozi kwa uchungu mkubwa huku wakiwa wameshabadilisha kila aina ya mikao wakimtazama Zena bila kujua kumbe mlango ulikuwa unagongwa muda mrefu sana na walichostushwa ni baada ya kufunguliwa na kusikia viatu vya mtu akiingia pale sebureni na walipogeuka wote walimshuhudia Kamishna Shebby akiwa amesimama baada ya kuingia tena akiwa amestaajabu kupita kiasi kwa kile alichokuwa anakiona watu wamekaa chini wameyaacha makochi na zaidi wote walikuwa wanalia.



    "Vipi Asha?! samahani mama kwa kuingia pasi na ruhusa.. vipi mzee wangu mbona sielewi kwema??"

    aliongea kwa taharuki Kamishna Shebby na kusogea pale walipokaa kina Hussein baada ya mama mdogo wa Asha kumruhusu kwa ishara nae akae tu sofani huku nao wakijizoazoa kuketi vizuri kwenye masofa wakiwa bado na nyuso za huzuni.

    "Vipi mzee wangu, umenitisha sana baada ya kuchelewa Asha.. Mama nini kimetokea hapa?"

    aliuliza Shebby huku akiwatazama machoni ndipo Hussein alipoanza kumsimulia kisa kizima na kumfanya Kamishna Shebby abaki ameduwaa.



    "Kha!! Ina maana Asha ni mwanao!!! yaani kumbe wewe niliyekutuma ni baba Mkwe!? Eee Mungu mbona siamini.."

    "Amini hivyo baba, mimi ni mama mdogo tu wa Asha na huyu ndie babaake kweli kabisa wala sio utani hata mimi siamini kama leo hii tumekutana"

    aliongea Zena kwa majonzi

    "BABA"

    Kwa mara ya kwanza Hussein masikioni mwake aliisikia sauti ya mtoto wa kike akimwita baba tena mtoto ambae hakuwahi kuilea hata mimba yake, walijikuta wananyanyuka kwa pamoja Asha na Hussein na kukumbatiana kwa nguvu huku wote wakilia lakini kilio cha sasa kilikuwa ni cha furaha.

    "sikuwahi kufikiria hiki kitu jamani babaangu pole sana kwa yaliyokukutaa"

    "Aaaah! mwanangu usinipe pole mamaaa nisamehe sana mimi nilichelewa kujua uwepo wako aaa"

    Ilikuwa ni furaha ya baba na mwana kujuana huku Zena na Shebby wakiwa wamekaa wakiwaangalia na kumshukuru Mungu kabla nao hawajasimama na kuungana nao pamoja kuwafariji.



    Baada ya kuliwazana na kila mtu kurejea katika hali ya kawaida huku furaha ya aina yake ikiwa kwenye moyo wa kila mmoja ndipo Asha aliposimama na kumshukuru sana Kamishna Shebby kwa ukalimu aliomuonesha babaake huku akimuomba babaake (Hussein) kuanzia siku hiyo afanye makazi yake pale kwenye ile nyumba wakti pia akimtafutia makazi mengine mazuri ya kuishi lakini ajabu Hussein alikataa na kumwambia Asha maneno ambayo hakuyatarajia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Asha mwanangu nakupenda sana na nimefurahi mno kukujua, lakini wewe ni mwanamke na sasa upo mbioni kuolewa na mwanangu wa hiyari ambae nataraji atakuwa mkwe wangu mwema siku zote, kwa sasa furahia kuwepo pale mpaka mtapooana ndipo kwa amri ya Mkwe wangu ndipo nitatoka na kukaa sehemu nyengine mtayojadili kwa pamoja nikae lakini si kwa amri wala matakwa yako binafsi."

    Maneno mazito ya Hussein yalitosha kuutafsiri moyo wa Asha kiasi gani babaake alikuwa na mapenzi mazito na mchumbaake hivyo alikubaliana na mawazo ya babaake ila alimuomba Kamishna Shebby amruhusu basi alipie yeye gharama za pale hoteli na kwa mapenzi ili mradi mpenzi wake alidhike Shebby alikubali.



    Baada ya hayo kumalidhika ndipo Hussein alipomuomba Asha alete kalamu na karatasi kwa niaba ya kuijibu ile barua tena mbele ya Shebby mwenyewe ambae awali alitaka awapishe nje ili wajadiliane vizuri lakini Hussein alimzuia na Zena alikuwa radhi Hussein amalize kila kitu.

    "Nimekuja kama mshenga na sasa naichana bahasha na kuijibu barua kama baba, Asha mwanangu taja mahali yako ya Ndoa."

    "Mh! baba si utaje wewe tu"

    "Hapana wewe ndie unayeolewa"

    "sawa basi mi.... mi Elfu kumi tu inatosha"

    "Safi sana mwanangu"



    alijibu Hussein na kuendelea kuandika na alipomaliza alimkabidhi Shebby palepale.

    "Mwanangu tuachane na mambo yote barua hii ifike nyumbani ukitaka kuoa hata kesho njoo nitatoa mimi hiyo elfu kumi ya Asha japo ni katika pesa zako ulizonipa, hakuna gharama nyengine zaidi ya hiyo elfu kumi huku kwetu"

    alisisitiza Hussein na kumshangaza mno Shebby lakini ukweli ndio ukawa hivyo na lilikuwa jambo geni kabisa kwa mila na desturi za kibantu barua kujibiwa mbele ya muhusika wa kiume na kumkabidhi yeye moja kwa moja.



    Baada ya hapo ndipo Hussein na Shebby walipoondoka huku wakiwaacha Zena na Asha wakiwa nusu wameamini nusu hawajaamini kwa kilichotokea siku hiyo.



    * * * * * *

    MKESHA WA MAWAZO



    ^^^^^^^^

    HUSSEIN BUBU

    ______________

    Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu kwa Hussein kupata usingizi kwani muda wote mawazo yalimpeleka mbali sana huku akiwa haamini kama leo yuko huru na kumbe yule daktari bingwa Asha aliyesaidia kumtibu mtu aliyemsaidia yeye kwa moyo ni mwanae na kwa uwezo wa Mungu alifanya kazi ya kumsaidia jeraha baya alilopata Shebby mpaka amepona kabisa na kujikuta wanakuwa wachumba?

    Alijikuta anageuza msikiti chumba cha ile hotel mala baada ya kujiazinia mwenyewe na kuanza kusali usiku kucha ambapo kila alipopumzika aliomba dua na kumshukuru Mungu na kuendelea kusali.



    ("Aaaaaah! kweli Mungu wewe ni Mkubwa sana na mwenye sifa za kipekee, Nakuomba kama ulivyonitendea muujiza wa kutoka jela na ukafanya kunikutanisha na mwanangu ambae nilijua habari zake nikiwa jela na kukata tamaa ya kumuona tena, basi baba nakuomba kama ulivyofanya hayo yote basi iwe hivyo na kwa Mr X niweze kumjua na kulipa kisasi kwa mikono yangu")

    Na hiyo ndio ilikuwa dua kubwa ya Hussein bubu katika nafsi yake kila alipopumzika na kumshukuru Mungu na alisali huku mawazo yake hayo ambayo alikuwa nayo toka jela yakijirudiarudia akilini mwake



    ^^^^^^^^^^^

    KAMISHNA SHAABAN

    ___________

    Si Hussein tu, mambo yalikuwa hivyo pia kwa Kamishna Shebby ambae nae alikosa lepe la usingizi kwa kufikiria mengi sana huku akivuta picha siku ya kwanza anakutana na Hussein bubu.

    ("Daaah! Mungu kweli wa ajabu na ameeka siri nzito sana katika maisha ya kila kiumbe yalivyo mbele kutokana na mzunguko anaomuonesha kabla daa.... Yaani kumbe muda wote natoa msaada kwa mtu ambae imeandikwa ndie baba mkwe wangu!!! ")

    aliendelea kuwaza Shebby

    ("Nina sababu zote za kumtafuta mshenzi mr.X na kulipa kisasi bado niko sahihi kwa hili")

    aligeuka Shebby pale kitandani na kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya mto na kumtumia txt Cj4 akimjuza kila kitu kilichotokea kule walipopeleka posa ambacho awali hajamjuza.

    )('So huyo mkeo mtarajiwa Hussein kumbe ni babaake?')(

    iliingia sms ya Cj4



    na Shebby kumjibu ndipo sms ya Cj4 ilipoingia nyengine

    )('Kuwa makini sana na mchumbaako hupaswi nae kumwambia habari zozote za mipango yetu')(

    ))('Sawa lakini kwanini unasema hivyo')((

    )('Kumbuka upo kwenye mchezo na mr X sasa usikubali uchezeshe na mr X kwenye huu mchezo ila wewe ndie umchezeshe mr X ktk huu mchezo na hapo tutamshinda.. Kumbuka kama Hussein bubu tumemumtoa kama chambo harafu mwanae kumbe ni mchumbaako nina shaka hili mr.X analijua na isije kuwa na huyo mchumbaako akawa anachezeshwa na mr X kwenye huu mchezo pasi na yeye kujijua')(

    SmS ya Cj4 ilimfanya Shebby ashushe pumzi na kuirudia mara mbilimbili huku moyoni akikili kuwa kuna upana mkubwa sana wa kimbinu na fikra baina yake na Cj4



    DOKTA ASHA

    ______________



    Kwa upande wa Dokta Asha yeye ilikuwa tofauti kidogo, naweza kusema yeye ndie alikuwa na mawazo mazito pengine kuliko wote.

    Alijikuta anagalagala kitandani akigeuka huku na kule kuulazimisha usingizi ambao ulimuhama kabisa kutokana na mawazo mengi yaliyoibuka kichwani mwake mara baada ya kuujua ukweli na kuonana na babaake.

    Muda wote maswali mazito yasiyo na majibu kamili yalizidi kuandama kichwa cha Asha na kumnyima amani ya kusinzia usiku kucha.

    ("Hivi kwanini lakini imekuwa hivi? aagh! Kwanini sasa?

    Aaaaaaaaaa!!? Kumbe Mungu Yupo? leo ndio Nimeamini lakini Kwanini?!!")



    alijiuliza maswali haya Asha mara nyingi kupita kawaida huku akijipigapiga kichwa chake na kadri alivyokuwa anajiuliza ndivyo hasira zilivyozidi kumshika na kuvimbisha kifua chake na hapo ndipo alipoamua kunyanyuka kwa style ya aina yake nusu sarakasi kwa jinsi alivyoizungusha miguu na kujibetua kiwiliwili akitegemea kichwa kabla ya kujirusha na kutua nje ya kitanda tena akiwa kasimama mbele ya dressing table yake ndogo anayotumia kujiremba na hapo ndipo alipoisukuma kuisogeza pembeni na ukutani pale kulipozibwa na dressing table kulionekana picha yake mwenyewe lakini ajabu alipoiondoa ile picha kulionekana batani kama za simu ambazo alitumia kuingiza namba alizozijua mwenyewe na hapo hapo kwa ajabu pale aliposimama kulipokuwa na dressing table kulipoanza kudidimia kwenda chini taratibu akishuka kama lifti na hatimae Asha alibukia kwenye chumba kimoja kidogo sana kilichokuwa na Kompyuta screen touch maalum za kisasa zikiwa kwenye kila upande wa kuta za kile chumba pamoja na kiti kimoja sambamba na mashine special za kuscan huku taa za rangirangi zikiwa zinawaka muda wote na Kompyuta zote zilikuwa on.



    Alikaa harakaharaka huku akili zake zikiwa na mawazo mazito ndipo alipoandika ujumbe uliosomeka.

    'NATAKA NIKUONE'

    na kusimama akihema huku akizunguka zunguka kusubiri jibu lakini mara jibu lililokuja alipolifungua liliustua zaidi moyo wake ambalo liliandamana na picha ya babaake aliyemjua siku hiyo tu tena ujumbe ulisema

    'KWANZA MALIZA KAZI YA KUIONDOA ROHO YA HUYU'



    "Whaat..!!?"

    alitaharuki Asha na kushindwa kujua aujibu vipi ule ujumbe na akiwa anatafakari mara ujumbe mwengine uliingia na alipousoma ulimpa maelekezo husika sambamba na kumuonesha picha ya hoteli ambayo alifikia Hussein na kona zote za ulinzi wa ile hoteli.

    ('I can't do this')

    aliwaza Asha na kufungua ripoti za nyuma alizokuwa anatumiwa sambamba na picha juu ya watu ambao mission zake alizimaliza na kiasi cha pesa alichokuwa anatumiwa.

    Moyo ulimuuma na kujutia kwanini amekubali kushawishika na kazi za mtu ambae hakuwahi kumuona hata siku moja katika maisha yake?

    Kulikuwa na siri nzito sana moyoni mwa dk Asha juu ya safari ya maisha yake nchini India ambayo hakukuwa na yeyote anayeijua zaidi yake yeye mwenyewe.



    ...................

    (^((^((^(((^^"Aaaagh!! Kweli nyie WANAWAKE NI WAUAJI hatari sana tena msiorudi nyuma WALA KUFIKIRIA hasa pale mnapopewa nafasi ama amri huitumia vizuri ili mzidi kuimanishwa na muonekane bora kuliko wanaume. Ila KUMBUKA kuwa wewe si wa kwanza kutumiwa na mr.X na laiti UNGEMJUA YAKINIFU huyo anaekutuma kesho anaweza kukuua hata wewe endapo atasikia upo kwenye mazingira hatarishi na maisha ya siri yake..... hahahahaaaa tatizo WANAWAKE HAMFIKIRII hah haha Ila nami nakwambia hii uliyoipata leo ni bahati kubwa sana ni bora tu uitumie lakini nakuahidi ukiniacha hai lazima nije kukutafuta na utalipa Damu zote zilizovuja leo.

    Naapa sitokuja kukuacha hai kama leo utaniacha hai na umwambie mr.X asijidanganye MWISHO WAKE UPO na atakufa kifo kibaya na cha mateso aaghhh.." ^^)))^)))^))^))^)

    .................



    Ilimjia kichwani sauti hii ambayo aliiongea Kamishan Shebby kumwambia yule Ninja wa kike kule Mkuyuni pindi alipobong'onyolewa mguu, hii inamaanisha kumbe dk Asha ndie yule ninja aliyetumwa Mkuyuni na ni kibaraka wa mr X lakini kilichomuuma leo ni kuujua ukweli juu yake harafu kutomjua Mr X

    "WHO FUC** ARE YOU..!!!?"

    alipiga kelele za hasira Asha na kupiga teke kile kiti kilichokuwa mbele yake na kukipaisha hadi kwenye screen moja ya computa na kuivunja palepale.



    Hayo ni maajabu machache sana kati ya mengi aliyokuwa nayo Dokta Asha.

    Mzuri wa sura na umbo lakini nyuma ya pazia ni hatari sana ana nguvu na trick za kila aina za kimafia.

    Ukweli yeye ni Muuaji wa Kimataifa wa siri anayetumiwa na Mr X muda mrefu na kashawaua wengi sana nyuma ya pazia waliojaribu kumpekenyua Mr.X kwaajili ya kumchafua.



    Yeye ndie yule Ninja wa Mkuyuni na mr X ndie aliyesababisha kumueka jilani na Kamishna Shebby mara baada ya kumuarifu atautumia mtandao wake kumshawishi babaake Shaaban ambe ni mzee Mwinchande pasi na kujua chochote akubali kumwita yeye ambae kwa nje dunia ilimjua kama daktari awe tabibu namba moja na Mr X huyohuyo ndie aliyemtupa ajenge mahusiano na Kamishna Shebby ili aolewe nae na iwe rahisi kumdhibiti na kujua mbinu zote zitazopangwa juu yake kwani Shebby ndie alionekana mwenye kihelehele cha kumjua sana mr X.

    Lakini mbali na hayo yoooooote Ukweli ni Kwamba Dk Asha hakuwahi kuongea ana kwa ana na Mr X wala kumuona.

    Na ndio kitu kikubwa kilichokuwa kinamuumiza sasa... lakini kwanini miaka yote anafanya kazi na kuwasiliana na mtu asiyemjua ?

    kaanza anza nae vipi na wapi hadi imefikia kuamini na kumtumikia hali ya kuwa hamjui ?

    Imekuaje awe na sifa ya udaktari bingwa lakini kumbe pia ana sifa ya uuaji?

    Hakika maisha ya Asha yalibeba maswali mengi sana ambayo kama hujayasoma na kuyajua maisha yake nyuma ya pazia yalivyokuwa basi hutoweza kuwa na majibu yake.



    ''I hate You Mr X.... I'll Find You..... and I'll Kill You''

    aliongea kwa hasira kwenye mike moja maalum iliyoconnectiwa na mitambo yake iliyokuwa mule ndani Asha na kuituma moja kwa moja kwa Mr X na hapo ndipo alipoanza kuvunja vunja computa na kuharibu kile chumba chake cha siri huku akilia kwa uchungu lakini mara majibu yalirudi kwenye kompyuta moja ambayo alikuwa bado hajaivunja na alipoyafungua alistaajabu baada ya kusikia sauti ya Mr X ambayo mara nyingi huwa inaeditiwa juu kwa juu pindi inapotumwa na kila siku hua inabadilika badilika na safari hii ilikuwa nzito na ilianza kwa kicheko kikubwa sana kumuonesha Asha Mr X jinsi gani anajiamini na amemdharau sana licha ya kwamba alikuwa Ninja mmoja hatari mno asiyejulikana.

    ' '''hahahahahahaaaa Asha wewe ni mtoto mdogo sana ambae huna mbinu hata robo ya kunitambua zaidi ukijieka wazi utakuwa ndio Umejiangamiza mwenyewe hahahahaaa, Ukitaka kupambana na mimi na wewe itakubidi ufanye zoezi kama nililokuagiza umwambie Shebby afanye hahaha, tulia kwenye mchezo wetu Asha nakupa siku saba tu kama nilivyompa babaako Hussein miaka ile na uanze kuhesabu kuanzia Kesho.



    Kumbuka wewe ni nyota wa mchezo wangu wa Vipofu.

    wewe ni Kipofu wangu mzuri kati ya vipofu wangu wengi wanaocheza mchezo huu wa pamoja unaonieka salama mpaka sasa na kunifurahisha kila ninapoutazamaa hahahaaaa Asha Hussein pole sana, ni bora ungejiengua mapema kipindi kile nakusajili katika Mchezo wangu.

    Umekaa na kukua katika mchezo huu na umekomaa nao Asha utawezaje kutoka? hahahahaaa kama ulikuwa Huujui Mchezo niliokuweka ucheze basi unaitwa Mchezo Wa Vipofu uliounza pindi tu ulipoingia kwa mara ya kwanza ndani ya ndege iliyokufikisha India ukiwa na wafadhili wako niliowaua miezi michache baadae hahahahahahahaaaaaaaa My Name is Mr X huwezi kucheza na mimi kwani nilishakupofua miaka mingi huna macho Asha.

    hahahahahahahaaaa'''''''

    Ilimalizikia ile sauti kwa kicheko kilichomfanya Asha abadilike zaidi na kubinuka sambasoti mara alipoikwanyuma kwenye umeme ile computa na kuibamiza chini kwa hasira na hapo ndipo alipojibinua tena na kufungua sehemu moja kulipokuwa na kijimlango chengine na ndipo mbele yake alitazamana na mavazi yake ya kazi sambamba na silaha zote.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "We tumia macho yako mimi natumia hisia zangu...Lazima Tuone Kati ya mimi Kipofu na wewe Mwenye Macho nani Atashinda Mchezo"

    aliongea maneno haya Asha na kuanza kuvaa mavazi yake ya kazi kwaajili ya kuianza kazi ya kupambana na Mr X kutoka kwenye Mchezo wa Vipofu.



    *<>*<>*<>*<>*<>*

    ^ ^ ^

    - MIAKA 17 NYUMA -

    -------------------------------

    MCHEZO WA VIPOFU

    ( ASHA HUSSEIN )

    ___

    _______________



    Akiwa haamini kama kweli ni yeye leo hii yupo kwenye ndege ile kubwa ambayo ilikuwa inachana mawingu angani huku pembeni yake amekaa na bwana mmoja raia wa India akiwa na mkewe mwenye asili ya Kizungu, aliendelea kugeuka geuka na kuwatazama watu wale aliowajua kama mr & mrs Rajesh ambao hawakuisha kumuonesha tabasamu mtoto yule wa makamo waliyemjua kwa jina la Asha Hussein.



    Safari ilikuwa ni nzuri na salama kwao na muda wote Asha aliwaza maisha aliyomuacha mamaake na kujiapiza kamwe hatoenda kuichezea bahati ile iliyomuangukia miguuni mwake pindi atapoanza masomo yake nchini India kama ilivyokuwa nia na madhumuni ya wale watu ambao walikuwa ni wafadhili waliojitolea kwenda kumsomesha kwao hasa kutokana na uwezo wa ajabu wa akili waliougundua kuwa nao yule mtoto pindi walipokuwa na ziala ya kuwatembelea na kuwasaidia watoto wasomao kwenye shule ambazo zilitokana na mfuko wao walio-share na serikali ya Tanzania zilizowajumuisha Yatima na watoto waishio kwenye mazingira magumu ili wapate elimu.



    Akili za Asha na uwezo wa kufauru alama za juu hususani masomo ya sayansi ndio kilikuwa kivutio kikubwa kwa wale wafadhili kufata taratibu na kumchukua kwa niaba ya kwenda kumuendeleza kwao ambapo waliamini ndipo kuna elimu bora zaidi itayoweza kumuinua kipaji chake hususani katika sekta ya utabibu kwa vile alivyofauru sana Biology na maneno yake mwenyewe alipoulizwa anataka kuwa nani mara zote Asha alijibu kuwa Doctor.



    Ndege waliyounganisha kutokea SA iliwasili ktk jiji la Mumbai baada ya safari ndefu ambapo wasafiri walianza kushuka na kwa mara ya kwanza mboni za Asha ziliweza kuitazama Mumbai na kukanyaga ardhi ya India akiwa na miaka kumi tu, huku akiwa anashangaa ukubwa wa ule uwanja na ndege kubwa nyingi ambazo zilikuwa tofauti na zile alizoziona Dar se salaam Tanzania.

    Walitembea taratibu huku akigeuka geuka nyuma kuangalia ule uwanja Asha alikutanisha tena macho na baba mmoja muafrika aliyemuonesha tabasam na kumkumbuka kuwa walionana toka uwanja wa ndege Tanzania na alimpatia zawadi ya kimdoli cha bata pindi alipokuwa ndani ya ndege kabla haijaruka DsM na hapo Asha nae alitabasam na kumpungia yule mtu.



    Walifika nje ya uwanja na kuingia kwenye gari moja ya kisasa aina ya Hummer milango sita iliyokuwa inawasubiri wenyeji wake ambapo kwa Asha alikuwa anajionea maajabu tu lakini ndio ulikuwa ukweli bibi na bwana Rajeesh walikuwa watu wenye pesa sana.

    Lakini walipoanza kuondoka yule bwana muafrika nae aliingia kwenye taxi na kumuamuru dereva aifatilie ile Hummer taratibu ila achunge asiwe anaikaribia sana.



    Na kweli aliweza kuifatilia ile Hummer hadi ilipofika eneo husika na kusimama nje ya geti moja kubwa na kwa upande wa yule bwana wa kiafrika aliyekuwa kwenye Taxi alimuamuru dereva apitilize kwenye ile njia asisimame.

    hadi baada ya mwendo mfupi alimuamuru aingie kwenye Hoteli moja iliyokuwa jirani na kule walipoiacha ile Hummer na baada ya yule bwana kumlipa ujila wake yule dereva taxi aliondoka na kumuacha mteja wake akiingia kwenye jengo la lile hoteli hadi sehemu ya mapokezi.



    Kulikuwa na siri nzito yule bwana iliyomfanya afike india na muda mwingi katika kila stage anayopiga kuna mtu alikuwa anachart nae na kumpa maelekezo kunachoendelea.

    )(' Weldone, kazi nzuri Tyga andaa mbinu ya kuwa nae ndani ya mwezi mmoja')(

    Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwenye simu ya yule bwana aliyeitwa Tyga pindi alipokuwa ndani ya chumba cha hoteli ile mara baada ya kumaliza taratibu zote za malipo.

    )('Woryout Boss')(

    alijibu kwa kifupi na kuendelea kukichunguza kile chumba pande zote na baada ya kulidhishwa nacho alitupia kibegi chake kidogo alichokuwa nacho kitandani sambamba na Kapelo aliyovaa kisha akavua nguo zote na kubaki na bukta ndogo na hapo alianza kujinyoosha kwa kufanya mazoezi ya ajabu ya kujipinda pinda na kila kiungo kilijigosha hadi alipokuwa anajipinda kukawa kimya bila kugosheka kiungo ndipo aliporidhika na kuingia bafuni kuoga.



    Aliporudi alikuta simu yake ikiwa imeingia ujumbe wa picha na video uliomfanya atabasam na mara alipoufungua alianza kushuhudia garden huku camera ikionesha kuchukuliwa bila utulivu lakini haikumzuia kuona mazingira machache hadi sehemu za ndani za nyumba moja ya kifahari huku akisikia sauti za watu waliokuwa wanaongea na mtoto aliyebeba ile kamera mpaka pale alipokiona chumba alichokuwa anakaribishwa yule mtoto na mara aliona kitanda kipindi hiko sasa kamera ilitulizwa na hapo ndipo alipomuona mtoto Asha akikaa pale kitandani baada ya kuelekezwa mazingira ya chumba chake na bafu.

    ("Good baby, soon Asante kwa ushilikiano wako")

    aliongea yule jamaa na kuzitazama picha muhimu zilizotumwa na kuyasoma mazingira ya nyumba ya bwana Rajeesh na chumba cha Asha.



    Wakati hayo yakiendelea kwa bwana Tyga upande wa Asha baada ya kuoneshwa mazingira na mrs Rajeesh muda wote yeye alikuwa na ule mdori aliozawadiwa na yule baba wa kiafrika ambae hakuwa anamjua pia hakuwa anajua ule mdori ni nini hasa.

    Hata Rajesh na mkewe walichukulia ile kama zawadi na walijua ule ni mdori kama ilivyo midori mengine bila kujua mdori wa Asha uliotengenezwa kwa mfano wa bata ni mdori maalum uliokuwa na uwezo wa kutuma mawasiliano ya sauti na picha huku ukirekodi kwa video kamera maalum zilizotengenezwa kama macho ya ule mdori huku kwenye upande wa mdomo wa mdori kwa ndani kulikuwa na memori maalum iliyounganishwa na kinasa sauti huku wire mwengine uliokuwa upo ndani ya ule mdori ukiwa na kadi special inayoconnect vyote na kutuma signa kwa wahusika wa ule mdori.



    Mara nyingi Asha alipenda kucheza na mdori wake kutokana na kukosekana mtoto saizi yake wa kuongea nae kwenye nyumba ya Rajesh kipindi akingojea nafasi ya kupelekwa shule kama alivyoahidiwa na hali ile ilimfanya azunguke nae karibu kila kona ya nyumba na kuwasaidia watu wamiliki wa mdori kuzidi kuchukua picha muhimu za jengo ile kupitia mdori ule wa bata.



    Baada ya wiki mbili Asha alipewa habari za kupata shule na aliambiwa angejiunga nayo siku tatu zijazo.

    Habari ile ilimfurahisha sana na siku ya siku ilipofika mr. Rajesh pamoja na mkewe waliingia kwenye gari sambamba na Asha kumpeleka kwenye hiyo shule maalum ambayo huko watu walikuwa wanasomea lengo tu.

    Yaani kama unataka kuwa daktari wa mifupa basi utasome udaktari wa mifupa kama unataka kuwa daktari wa moyo halkadhalika utasomea ndoto yako hiyo basi ilimradi lazima baada ya miaka kumi utakuwa professional kabisa.



    Lakini siku hiyo walipokuwa njiani kuelekea kwenye hiyo shule ambayo ilijitenga kidogo na jiji la Mumbai na hata njia ya kufika kwake ilikuwa lazima ukatishe kwenye msitu mmoja wa serikali ambao ulikuwa kimya sana ndipo unaibukia kwenye milima ilipokuwa hiyo shule ambapo kulikuwa na majengo mengi makubwa na hostel za wanafunzi.

    Nia na madhumuni ya chuo kile kuwa mbali na jiji ni kuwapa wanafunzi muda wa kusoma na kutuliza akili zao na hata Rajesh alipendezewa na shule ile na kuamini itamfanya Asha asome na kutimiza malengo yake.

    Katika hali ambayo hawakuidhania wala kuitarajia bwana Rajesh alipokuwa anakaribia kumaliza kile kieneo chanye msitu mara mbele yake kwenye kona alilikuta roli likiwa limeharibika tena limeziba bara bara lakini punde tu aliposimama walitokea vijana watatu wakiwa wamejifunga vitambaa usoni na kuanza kulishambulia gari la mr Rajesh na kuharibu haribu matairi yote na kuyatia pancha.



    "Msiniue jamani msituue semeni mnataka sh ngapi niwape tafadhalini"

    aliongea Rajesh baada ya wale vijana kuacha kurindimisha risasi na kuwaamuru wote waliokuwa ndani ya gari ile watoke nje.

    kwa Asha ilikuwa ni kilio na mikojo kuanza kumtoka kwa hofu na kujilaumu kwanini amekubali kuja kwenye nchi ambayo kumbe haina amani hata kidogo,

    alikuwa hakuwahi kusikia milio ya risasi ikipigwa live hapo kabla zaidi ya kuangalia kwenye picha za kivita.



    Lakini Mbali ya Rajesh kujitahidi kujitetea na kuitetea familia yake haikutosha kuwatia moyo wa huruma wale watu ambao walionesha walikuwa hawahitaji pesa za Rajesh zaidi walianza kummiminia risasi tano za kifua palepale na kumpeleka Rajesh chini mbele ya macho ya mkewe na Asha.

    "Nehiiiiiiiiii"

    alipiga kelele mke wa Rajeshi na kumlalia mumewe aliyeanguka chini muda mfupi huku damu nyingi zikiruka na kutapakaa eneo lile lakini nae alipigwa risasi ya kichwa na hapo ndipo alibaki Asha akilia huku akiwa kafumba macho kwani alijua tu lazima na yeye auliwe na wale watu na hakuweza kujitetea vyovyote kwani hakuweza kuzungumza kihindi wala kiingereza chake kilikuwa cha kitoto sana kile cha kutajisha lakini Rajesh ilikuwa rahisi kuongea nae kutokana nae kujua kiswahili japo rafudhi yake haikuwa nzuri.



    Lakini akiwa kachuchumaa amefumba macho Asha akilia kwa uchungu huku mwili ukiwa umekufa ganzi ndipo mara alisikia muungulumo mwengine wa gari ikija kasi na kufunga breki karibu na gari yao iliyoshambuliwa na hapo ndipo aliposikia milio ya risasi ikirindima mfurulizo na vioo vya gari vikipasuka kwa zaidi ya dakika tatu na kumfanya azidi kutetemeka kwa hofu na kujikojolea zaidi huku akiwa hajui nini kinaendelea.

    Lakini baada ya ukimya alisikia sauti za viatu na hatua za mtu akimsogelea na hapo alijua sasa ndio mwisho wake hivyo alisali kwa na kutulia akijiandaa kuisikia risasi ikipenya mwilini mwake lakini ajabu haikuwa hivyo alishangaa kuhisi akishikwa bega na huyo mtu baada ya kumsogelea zaidi.

    "Inuka binti Usiogope"

    aliisikia hii sauti iliyomfanya ageuze shingo kumuangalia muhusika ambapo hakuamini hata kidogo mara baada ya kuiona sura ambayo haikuwa ngeni machoni mwake.



    ~ SIKU MOJA KABLA ~

    ______________



    ["Ndio bosi ni Holt Mandu Academy, sawa kabisa nimeielewa na leo ndio nakutana na vijana niliopanga nao issue na ili waone tofauti nawalipa asilimi 60 kabisa katika makubaliano.... sawa bosi hilo halina shida kabisa andika kabisa The Game is Over"]

    alionekana Tyga akiongea kwa simu akiwa chumbani mwake kule hotelini na baada ya hapo alitoka nje na kukodi taxi kama kawaida mpaka maeneo ya kusini mwa jiji la Mumbai aliposshuka na kuingia kwenye bar moja huku muda mwingi alionekana kuwa bussy na simu.



    Alifika na kukutana na jamaa mmoja baada ya kusalimiana alimpa ishara amfate na hapo ndipo walipoelekea usawa wa kauta na kufungua kilango kilichotokea kwenye kiukumbi kidogo kirefu kilichokuwa kinawaka taa zenye mwanga hafifu huku kikiwa na milango mingi pande zote.

    Baada ya mwendo kidogo ndipo yule mwenyeji wake aliyekuwa na asili ya ki Asia alipofungua moja ya mlango uliowakutanisha kwenye ukumbe mwengine ambao kulionekana watu wakijidunga wengine wakifanya mapenzi bila kujali huku moshi wa marujuana ukiendelea kufuka kwenye vinywa vya wale watu.

    waliachana nao na kufika mbele ya mlango mmoja ambao juu yake Tyga aligundua kumetegwa kamera kimtindo.

    Baada ya mwenyeji wake kubonyeza alarm sauti ilisikika kutokea kwenye kitasa kilichokuwa na spika ikiwaruhusu waingie na huko walikutana na Bonge la mtu (mnene sana) aliyekuwa kakaa kwenye kiti cha kuzunguka huku mwili wake ukiwa umepigwa machata ya michoro ya ajabu ajabu.

    "Umeleta Advance?"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliuliza yule bonge pindi Tyga alipotoa bahasha ya khaki iliyovimba ambayo ndani yake kulikuwa na noti za dollar mia mia karibu vibunda kumi na kila kibunda kimoja kilikuwa na noti mia.

    "Safi sana hahahaaa. umefanya nikupe vijana wangu wa daraja A hahaha Zanjili, Jackson, Vijay, nyinyi ndio mtafanya kazi tuliyotoka kuijadili na huyu jamaa kesho"

    aliongea yule kibonge mara baada ya kuchana bahasha na kuzihesabu zile pesa.

    Baada ya kila kitu kuwa sawa Tyga alikabidhiwa funguo za gari ambayo ndio alitakiwa atokee nayo eneo la tukio na kisha alipewa bastora mbili ndogo zilizojazwa risasi za bandia.



    "Mchezo ni mwepesi sana na utachukua dakika kumi tu, wewe itakubidi uwe makini kuifatilia gari yao pindi itapokuwa inatoka mpaka kukaribia ile kona subiri kama dakika tano then unatokeza mkuku na kumuhadaa binti unayemuhitaji kwa kuwapiga risasi za kifua vijana wangu wataojifanya wamekufa ili kumtoa hofu bint ndipo utadondosha bahasha yetu yenye hele zilizobaki na utokomee eneo lile then mchezo uliobaki watajua vijana wangu jinsi ya kuumalizia."

    alitoa maelekezo ya mwisho yule kibonge na kupeana tano na Tyga aliyeikubali moja kwa moja ile mbinu na kuondoka.



    Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kesho yake kumbe kuanzia muda mr Rajesh akiwa na mkewe na Asha wakitoka tayari Tyga alikaa sehemu husika na mara gari ya mr Rajesh ilipoanza kutoka aliifata nyumanyuma hadi yote yaliyoenda kutokea pale na yeye ndie aliyekuja kumuhadaa Asha kama muokozi wake baada ya kuwapiga risasi za uongo wale watu waliojiziba nyuso na kuangusha bahasha iliyokuwa na salio pale chini kisha kumfata Asha aliyekuwa ameinama chini ya gari ya mr Rajesh ambae alishafariki na mkewe kisha akamshika bega Asha ambae alipogeuka Tyga alimuonesha tabasamu kama alivyomfanyia siku ile aliyomzawadia mdori wa bata na siku waliposhuka uwanja wa ndege wa Mumbai na muda huo ilikuwa mara ya tatu wanatazamana uso kwa uso na mtoto Asha.



    * * * * * *



    "Usiogope bint ni salama sasa"

    aliongea tena Tyga kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijua ndio anaielewa kiufasaha sana mtoto Asha na kumuinua pale chini na kumkumbatia.

    Hakuwa na jinsi Asha zaidi ya kumkumbatia yule baba (Tyga) aliyegeuka kuwa mkombozi wa maisha yake muda ule huku akifarijika pia kusaidiwa na mtu aliyemuona tangia uwanja wa ndege nchini kwao (Tanzania) na aliamini moyoni mwake kuwa Mungu ameamua kumuonesha muujiza ambao hakuwahi kuuota wala kusimuliwa hata siku moja kama upo.



    Yaani anawapoteza wenyeji wake waliojitolea kumchukua tangia huko kwao katika mazingira ambayo hata kama asingeuwa na wale watu bado aliamini angekufa kwa kuuawa hata na wanyama wakali katika msitu ule kwa kukosa muelekeo wapi aende vipi aombe msaada nani angemuelewa ikiwa hajui kihindi hata kidogo? tena mbaya zaidi alisikia sifa za ubaguzi za watu weusi tokea yupo shule..!

    Lakini leo hii anasaidiwa na mtu wa kwao kabisa baada ya kumfariji tena kwa maneno ya lugha ya Kiswahili.



    "Pole sana mtoto usiogope haya twende haraka tuondoke hapa kabla hawajaja wengine"

    aliongea Tyga na kumshika mkono Asha ambae awali alisita na kugeuka kutazama walipolala wafadhili wake mr&mrs Rajesh

    "Tuwachukue babaaa na mamaa"

    "Hatutaweza binti wameshakufa hao"

    ndivyo alivyojibiwa na Tyga ambae alimshika mkono nae Asha alimfata hadi kwenye gari aliyokuja nayo Tyga na kuingia ndani yake ambapo gari ilichekechwa na kugeuzwa kiufundi palepale na kuanza kurudi ilipotoka huku Asha akiwa hajui wanapoenda lakini hakuacha kuchungulia nyuma kupitia kioo cha ndani cha ile gari akiwa haamini kama kweli maisha ya watu wenye hela zao aliotokea kuwapenda na kuwazoea wiki chache tu alizokaa nao kama ndio kweli yameishia pale msituni.



    Hakuna aliyejua kilichoendelea baina yao baada ya kufika maeneo ya mbali na eneo la msitu huku Asha akiwa hana la kufanya zaidi ya kumsikiliza yule aliyeamini ni muokozi wake chochote atachomwambia.

    "Unaitwa nani binti?"

    "Asha"

    "Ooh! Asha nani?"

    "Asha Hussein"

    "Sawa mimi unaweza kunita Uncle Tyga"

    "Anko Taiga!!"

    "Eeh, Uncle Tyga ni mfanyabiashara wa Tanzania ninaezunguka hapa India na kwengineko, nilikuona kwenye ndege si ndio wewe?"

    "Eeh, Uncle Tyga"

    "Basi usiwe na wasiwasi sawa eeh"

    "Sawa lakini naomba nisaidie unirudishe kwetu"

    "Hilo halina tatizo Asha kwani huku uliokuja nao wale kina nani?"

    "Wafadhili walinichukua ili wanisomeshe na ndio walikuwa wananipeleka shule"

    "Oooh! pole sana kumbe unapenda kusoma?"

    "Ndio"

    "sasa kama anatokea mfadhili mwengine akachukua nafasi ya wale waliokufa ili akusomeshe huku, utakuwa tayari tena kurudi nyumba?"

    "Hapana kama nitapatiwa shule napenda sana nisome"

    "Basi vizuri"

    Ndivyo walivyoanza kuzoeana baina ya Tyga na Asha kipindi hiko gari ilikuwa katika High Way speed kali na kuanza kuliacha jiji la Mumbai huku Tyga akimsemesha semesha Asha ambae mwishoe alipitiwa na usingizi na baada ya gari kutembea kwa zaidi ya masaa manane tena kwa speed ya nguvu hatimae waliingia katika jiji la Delhi ikiwa tayari majira ya usiku.

    aliamshwa Asha na kumfata mwenyeji wake mara walipofika kwenye nyumba moja ya kizamani ambayo ilionesha ilikuwa haikaliwi na mtu kwa muda mrefu hasa mara baada ya kuingia ndani na kukuta mazingira yalivyo.



    "Karibu Asha utakuwa unakaa hapa kwa muda na habari njema ni kwamba nimelifikiria sana swala lako na nimezungumza kwa ujumbe wa simu na bosi wangu ninayefanya biashara zake kuwa yuko tayari kushika nafasi za wale wafadhili na atakusomesha hadi pale unapohitaji mwenyewe na kukuhudumia kwa kila kitu"

    habari hizi ziliukonga moyo wa Asha na kujikuta anasahau matatizo yalliyotokea muda mfupi na kumpigia magoti Tyga kwa kumshukuru.

    "Hapana usinishukuru sana mimi. Utamshukuru vizuri bosi wangu siku ya kumuona"

    "sawa Uncle Tyga, kwa hiyo nitasoma?"

    "Utasoma Asha"

    "Lini Uncle"

    "Kesho jioni nitakupeleka kwenye hiyo shule ni nzuri na ni salama zaidi ya ile waliyokuwa wanakupeleka wale, si umeona mwenyewe njiani kulikuwa na majambaza..?"

    "Ndio Uncle"

    "Basi usijali Asha, si umesema unataka kuwa daktari"

    "eeh"

    "Basi huko utakuwa zaidi ya daktari na hii ni kwa mujibu wa bosi wangu ambae kumbuka ndie msaada mkuu kwako"

    alisisitiza Tyga na kumpatia Asha mfuko uliojaa nyama za kuku wa kukaangwa sambamba na mikate ya maziwa huku mfuko mwengine ukiwa na Juice kubwa ya matunda.



    Na huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana kwa Asha na Tyga ambae mpaka muda huo hakumuambia Asha jina halisi la huyo bosi wake ambae Asha nae alimjengea moyo wa upendo na ukarimu kabla hata hajamuona huyo bosi na aliamini kuwa ndie mkombozi wake wa elemu ambayo alidhani kashaikosa pindi aliposhuhudia wafadhili wake wakiuawa.



    * * * * *



    Siku mbili baadae Tyga akiwa sambamba na Asha ndani ya gari majira ya jioni walifika eneo moja lenye mitimiti mingi baada ya mwendo mrefu na kufika kwenye geti moja lililoandikwa kwa lugha ya kijapani na kuingia mara baada ya kufunguliwa na walinzi walioonekana eneo lile.

    Asha hakujua kama pale anapoletwa ndio shule kwenye hadi baada ya kuambiwa na Tyga ashuke kwani wamefika shule.

    Mazingira hakuyaelewa kwani hayajakaa kishuleshule na hakukuonesha dariri ya watu kufika mara kwa mara eneo lile kutokana na kupooza kwake.

    Lakini ukweli ukabaki kuwa pale ndio shule penyewe alipoahidiwa na bosi wa Tyga kuwa atasomeshwa bure mpaka atimize ndoto zake.



    Hali ya mazingira awali yalimuia ugumu sana kutokana na uchache wa wanafunzi ambao asilimia kubwa walikuwa wanawake lakini siku hadi siku alianza kuyazoea na kuyapenda masomo ambayo walikuwa wanafundishwa pale shuleni na walikuwa wanalala pale pale huku zile siku za mwisho wa wiki alikuja Tyga na kumtembelea huku akimletea zawadi mbalimbali kutoka kwa bosi wake ambae sasa na Asha alimtambua kwa jina la mr X.

    "Msalimie sana mr X uncle mwambie nampenda sana nashukuru kwa msaada wake"

    yalikuwa ni maneno ya Asha siku moja mara baada ya kuletewa zawadi nyingi na Tyga huku akimwambia zimetoka kwa bosi wake ambae ni mr X na Asha alizidi kumpenda na kumuhusudu mr X kupita maelezo kwa kuamini ndie mfadhili wake na mtoa msaada kwa yote yale yanayofanikishwa na Tyga bila kujua kumbe yupo katika mchezo wa vipofu alioingizwa na mr X na kupofuka pasi na kujitambua Asha.



    Ile shule mbali na kuwa na walimu wachache waliokuwa wanadeal na swala la mifupa ya binaadamu tu lakini ilikuwa na mazoezi mengi kila siku ya viungo na walimu wakubwa wa mazoezi walikuwa wajapan na huu ndio ukawa mwanzo wa Asha kujifunza ushupavu pasi na yeye kujua huku akiendelea na masomo ya mifupa ya binaadamu bila kusahau practical kibao walizifanya pale shule na baada ya miaka miwili ugeni wote ulimtoka Asha na akawa mzuri sana kwenye mazoezi ya viungo na kutokana na kuwa bado msichana aliweza kuwa mwepesi zaidi hali iliyomfurahisha sana Tyga aliyekuwa anaenda pale mara kwa mara.



    Baada ya miaka mitano Asha alimaliza mafunzo pale na wakati huo tayari alikuwa na umri wa miaka kumi na tano ndipo alipohamishwa na kupelekwa kusini kabisa mwa India na Tyga na huko ndipo mchezo mzima ulipoanza mara baada ya kukutanishwa na mzee mmoja Ninja wa Kijapani ambae alijiekea makazi kusini mwa India na haikujulikana alifahamiana vipi na mr X zaidi ya maelekezo tu aliyopewa Tyga kuwa ampeleke Asha huko.



    "Kwanini nalazimika kufanya hivi Uncle Tyga?"

    "Kwa sababu ya usalama wako wa baadae Asha na msaada kwa bosi"

    "Usalama kivipi Uncle na msaada gani tena kwa bosi?"

    "Dunia sasa kuna watu wabaya sana Asha, si unakumbuka kilichotokea kwa mfadhili wako wa kwanza bwana Rajesh?"

    "Ndio"

    "sasa pale kama ungekuwa na taaluma nyengine zaidi ya kulia ungeweza kumsaidia na kumuokoa na ndivyo ilivyo kwa mfadhili wako huyu hadi ameamua kujificha kwa kuogopa watu wabaya wanaomfatilia kila siku wakitaka wamjue na wamuue"

    "kwanini sasa Uncle?"

    "kwa sababu watu wabaya sana na wana wivu hasa kwa watu wema wanaosaidia wengine."



    "Daaah!! kama ni hivyo Uncle nami niko tayari kabisa kulipa fadhila na kumlinda bosi mr X kwa watu wote wabaya sitokubali nae wamuue kama Rajeesh"

    "sasa itakubidi uvumilie na ukubali haya mafunzo na huyu babu tutakuwa pamoja siku zote, shika simu hii ongea na mama"

    aliongea tena Tyga na kumtolea Asha simu na kumshangaza mno baada ya Tyga kuipiga na kuzungumza na mama mdogo wa Asha aliye Tanzania.

    Hili ndio jambo kubwa ambalo Asha hakuwahi kujiuliza Tyga alianza vipi mawasiliano na mamaake lakini ni kwamba Tyga miaka yote alikuwa na mawasiliano na mama Asha na kumliwaza juu ya maendeleo ya mwanae japo kwa upande wa mama mdogo wa Asha alikuwa anajua anaongea na walewale wafadhili ambao walimchukua mwanae kwenda kumsomesha India.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    (MIAKA 10 BAADAE)

    ............



    Ilikuwa ni ndani ya uwanja wa Ndege wa Mumbai walionekana wasafiri wakipanda ndani ya ndege ile kubwa iliyokuwa inafanya safari zake moja kwa moja mpaka bara la Afrika ktk nchi yaTunisia.

    Ndani yake alionekana msichana mrembo sana Asha akiwa kakua sasa tofauti na alivyoingia kwa mara ya kwanza kwenye ule uwanja miaka kumi na tano iliyopita.

    Safari hii hakuwa na mtu mwengine yeyote katika safari yake, hata yule mtu aliyewahi kumpa mdori miaka ile na kuja kugeuka ndugu yake wa pekee mara baada ya kumuokoa katika shambulizi lililopoteza nafsi za watu waliomfadhili na kumfikisha katika ile nchi, pia nae hakuwa nae kwenye ile ndege safari hii.



    Akiwa anaendelea kujisomea kitabu huku akiwa haamini kama leo hii amekuwa Daktari Special wa mifupa na mishipa ya binaadam tena akiwa na vyeti vya uthibitisho kutoka kwenye chuo kikubwa sana India ambacho kiukweli hakuwahi kabisa kusomea hiko chuo japo ni kweli alikuwa na ujuzi mkubwa wa kutibu mifupa iliyovunjika na kuifanyia uparation kuiunga samba na mifumo ya mishipa yote ya mwili wa binaadam.

    Hakujua mbinu gani zilitumika katika kumsaidia kupata kile cheti kilichoonesha alidumu kwenye kile chuo tangia angali na miaka kumi lakini alikumbuka maneno ya Tyga pindi alipokuwa anamuaga na kumpa jukumu la kuhakikisha usalama wa bosi wake Mr.X unakuwa mikononi mwake.



    {{'''"Asha, kumbuka wewe ni Lady Ninja uliyevaa kivuli cha Dokta kwaajili ya ulinzi wa siri na usalama wa bosi wetu Mr X ambae kuna maadui ndani ya ngazi ya serikali wanamuinda kutokana na kuwafichua watu wabaya na kuwasaidia kwake wanyonge.

    Nakukabidhi nafasi yangu niliyodumu kwa muda wa miaka ishirini sasa nikiwa kama mlinzi wa siri wa Mr X.

    Sidhani kama tutaonana tenahuku ninapoenda ila nategemea utafanya vyema na kulipa fadhila kwa bosi mr.X ... Namba yako ya siri ni 9121 ktk code maalum utayokuwa unawasiliana nae mkuu"''}}

    {"sawa Uncle Tyga, vipi nitaonana nae sasa maana natamani kumuona pia nimshukuru mbele yake."}

    {{"Utamuona lakini kwanza inabidi umuoneshe kivitendo mission yoyote atayokupa ambayo itahatilisha maisha yake hakikisha unaimaliza haraka kabla haijawa tatizo, naamini ukiweza mission tatu atakuamini zaidi na utakutana nae ana kwa ana. Kuna kiasi kikubwa cha pesa ushawekewa kwenye account yako.

    Mama tayari anaishi kwenye nyumba maalum aliyoijenga mkuu kwa kupitia jina lako ila hii siri ya huku ibaki kwenye kifua chako, kumbuka kile kiapo unatakiwa kila mtu akujue wewe ni Daktari bingwa wa mifupa lakini usikubali kuajiliwa popote. Safari njema My Lady Ninja"''}}



    Aliyakumbuka maneno haya aliyokuwa amezungumza na Tyga mara ya mwisho pindi alipofuzu mafunzo ya udunguaji wa Kininja na kupewa jalibio la kustukiza mara baada ya siku moja kutelekezwa kimakusudi na Tyga na kumuacha katika balaa kwenye kundi la wahuni zaidi ya 25 lakini aliweza kuwadhibiti na kuwavunja vunja wote lakini mwishoni alipotaka kuondoka eneo lile ambalo lilikuwa nyuma ya bustani moja kulipokuwa na Bar na kambi ya siri ya kuuza madawa ndipo ghafra alitokea Ninja ambae alisumbuana nae sana kupambana nae ili kuokoa maisha yake mbali na kwamba yeye Asha hakuwa na nguo zake za kininja wala silaha na alishatoka kupambana na watu zaidi ya ishirini lakini aliweza kula sahani moja na yule Ninja hadi baada ya nusu saa alipoanza kuzidiwa mbinu Asha ndipo yule Ninja alimuacha Asha baada ya kuona ameanza kumzidi huku nae akiwa kakiona cha mtema kuni kutoka kwa yule binti na hapo alikubali na kumsogelea kisha alijifunua uso na kumshangaza Asha baada ya kugundua kuwa alikuwa anapambana na Uncle Tyga.

    Ndipo Tyga alipomwambia maneno hayo ya kuagana nae kisha alipotea kwa kutumia uchawi wa Kininja mbele yake.

    Alitabasamu Asha wakati akikumbuka yale kipindi hiko ndege ilikuwa tayari iko angani ikikata mawimbi na kuzidi kuliacha bara la Asia.



    * * * * * *



    Na kweli Asha mbali na kupokelewa kwa shangwe pindi alipounganisha ndege kutoka Tunisia mpaka Jijini Dar, Tanzania alipomkuta mamaake ambae ni Zena akiwa na wapambe kadhaa waliokwenda kumpa sapoti hususani sifa aliyorudi nayo ilimfurahisha sana wazili wa Afya wa Tanzania kwa kuona wataalam wanazidi kuongezeka nchini, lakini kitendo cha Asha kukataa ajira yoyote nchini na kutangaza kuwa atajiajili mwenyewe yaani awe anakodiwa kwa kazi maalum itayowashinda madaktari wa pale hususani maswala ya mifupa na mshipa basi atakuwa radhi kusaidia lakini si kuajiriwa kabisa na kuwa mfanya kazi wa kila siku.



    Kauli hii kila mtu aliielewa anavyojua yeye lakini hakuna aliyejua nini kinaendelea nyuma ya pazia ya maisha ya Asha na kwa kutumia kode maalum aliyokuwa anawasiliana na mr X aliweza kupata maelekezo yote muhimu na siri ya nyumba ile hususani chumba chake ambacho kumbe kilikuwa na sehemu maalum iliyotengenezwa kwa mfumo wa lifti na chini yake ndipo kulikuwa na chumba cha mawasiliano na maelekezo juu yake nini afanye kuhusu usalama wa bosi wake ambae alimpenda na kumuhusudu kama muokozi wake mbali ya kuwa hajawahi kumuona katika miaka yote toka afahamu uwepo wake.



    * * * * * *



    Ikiwa ni miezi mitatu imepita tangia arejee nyumbani Tanzania huku akiendelea na mawasiliano ya siri na bosi wake ambae siku zote hakuwahi kufikiria sana wala kuhoji sababu za kujificha kwake ama kutopenda kuzungumza nae ana kwa ana.

    Kila akikumbuka wema aliofanyiwa na Uncle Tyga kule india hadi alivyomuokoa na kumsomesha hata kumuunganisha na kuaminiwa na bosi wao kuchukua nafasi yake ndivyo alivyozidi kumpenda mr.X na mara zote usiku aliingia kwenye chumba chake cha siri na kuwasiliana nae na ndipo siku hiyo alipokutana na ujumbe wa picha ya kijana askali magereza pamoja na maelezo kiurefu yaliyosema.....



    ^^^

    ^^Huyo ni Shaaban Mwinchande, Kamishna wa polisi na mkuu wa gereza la Nyato lile la wafungwa wenye makosa makubwa nchini.

    Babaake ni adui wangu mkubwa na sasa anamtumia mwanae ili aweze kujua nilipo kwaajili ya kuniangamiza^^

    ^^Picha hii ya chini huyu ni mzee mganga wa muda mrefu anaitwa Mnyungunyungu, aliwahi kuwa rafiki angu miaka ya nyuma lakini baadae akawa msariti kwa tamaa na kujiunga na mzee Mwinchande babaake huyo Kamishna Shebby anayetaka kunijua kwa udi na uvumba na kuniua^^

    ^^Sasa My Lady Ninja location ya tukio ni Mkuyuni Morogoro

    huko utakutana na mzee huyu unayemuona hapa chini... Anaitwa Aly77 namba zake ni hizo yeyey ndie anayechunga usalama wangu pale na ndie alietuma taarifa za huyo kijana aliyeenda kunitafuta kwa mzee Mnyungunyungu ambae ni kweli kuna baadhi ya taarifa zangu muhimu ila Aly77 ameshamdhibiti mzee Mnyungunyungu na huyo Kamishna kaondoka huko, lakini najua lazima atarudi tena kutaka habari zangu toka kwa mtoto wa mzee Mnyungunyungu ambae ni huyu umuonae sasa kwenye picha, yeye ndie mganga wa pale anayejua fununu zangu na ni hatari kwa maisha yangu kama atabaki hai na kuzitoa siri kwa maadui zangu. ^^

    Kazi kwako Lady Ninja okoa maisha yangu.^^



    ^^^

    Baada ya kuupata ujumbe ule na kuzirusha zile picha kwenye Memory yake, Asha aliandaa mavazi yake ya kazi na kuyaweka kwenye begi dogo kisha usiku uleule aliandika ujumbe mfupi na kuuacha mezani akimuarifu mamaake pindi atapoamka kuwa amepata dharura kisha alitoka na kuingia kwenye gari yake ndogo ya kifahari taratibu safari ya Morogoro Mkuyuni ilianza.



    Kwa kutumia code alizopewa aliweza kuwasiliana na huyo mzee aliyeitwa Aly77 ambae ndie aliyemuekea sumu maalum iliyokuwa inamtafuna mganga Mnyungunyungu taratibu hadi kufikia kuwa hoi bin taaban.

    Miaka yote alijichomeka pale kijijini yule mzee ambae alionekana mcha Mungu kutokana na tabia yake ya kupenda kuswali na kuvaa kanzu na kibaraghashia kumbe nyuma ya pazia hakuwa hivyo alikuwa anafanya kazi ya mtu ambae alikuwa anamsaidia kipato na kuiwezesha familia yake pia mzee Aly77 ndie alikuwa baba mzazi wa Tyga na alijitolea kufanya kila kitu kwa mr X mara baada ya kusaidiwa miaka iliyopita pindi mwanae alipopata ugonjwa m baya uliotakiwa asafirishwe India nae kwa kukosa uwezo alijikuta anapita huku na huko kuomba msaada ndipo alipokutana na msaada wa mr X kupitia mwana mama Mrembo ambae alisafiri na Tyga hadi India pamoja na babaake na huko waliishi mwaka mzima mara baada ya oparation na siku zote yule mama aliwasisitiza kuwa msaada ule walipatiwa na Mr X na hiko kikawa chanzo cha yule mzee kumuhusudu mr X hasa baada ya kuambiwa kuwa mwanae ambae ni Tyga atasaidiwa zaidi na mr X kusomeshwa nchini Japan hadi atimize malengo yake nae mzee Aly alipewa kisa kizima kama alivyopewa Asha na Tyga juu ya kujificha mr X lakini yote hayo mzee Aly hakujali wala hakuwa na haraka ya kumjua huyo mr X zaidi ya kuwasiliana nae kwa simu zenye code maalum, na kupewa maelekezo muhimu huku kila mwisho wa wiki pesa iliingizwa kwenye account yake.



    Na safari hii waliunganishwa sambamba mzee Aly77 na Dokta Asha katika mission ile ya kuisambaratisha familia ya Mzee Mnyungunyungu ili Kamishna Shebby na wenzake wasije kujua siri zozote kuhusu Mr. X

    Na hivi ndivyo mchezo ulivyokuwa unachezwa katika location ya Mkuyuni ambao Mr X ndie alikuwa mtengenezaji na mtazamaji na aliishia kufurahi na kujisifu kwa vile ambavyo mambo yalianza kutokea Mkuyuni kwenye mchezo ambao wachezaji wake walitumia akili na mbinu nyingi lakini kwake yeye aliuita Mchezo wa Vipofu.



    Haikuwa shida kwa Asha baada ya kuwasili usiku wa manane Mkuyuni na kukutana kwa siri na mzee Aly77 ambae alimpa maelekezo yote muhimu na zaidi kuhusu simu fake waliyopiga na kumuhadaa mganga yule mtoto wa Mnyungunyungu kwa kudhani kuwa anaongea na mteja wao wa siku nyingi juu ya kukutana kesho kwa niaba ya dawa ambazo sharti lake lazima aamke asubuhi sana akaziandae na kutokana na hali ya mazingira ya pale kijijini watu kuchelewa sana kuamka huo utakuwa wasaa mwepesi kwa Lady Ninja kufanya kazi yake ya kummaliza kwani endapo kina Shebby wakirudi na kuongea na yule bwana basi ajue fika tayari siri ya maisha ya tajiri wao mr X yatakuwa hatarini sana kwani waliamini pia Shebby anafanya kazi ile kwa shinikizo la babaake bwana Mwinchande ambae kwa maelekezo waliyopewa na mr X ni kuwa Mwinchande ni adui ake anayemtafuta miaka mingi ili amuue baada ya kumfichua ubaya wake kipindi akiwa polisi mkubwa na hivyo ameeka kisasi ambacho kinapitia mgongoni mwa mwanae anaejua kuwa mr X ni mtu m baya kutokana na hadithi za uongo alizopandikizwa na babaake (Mzee Mwinchande).



    Kazi ilikuwa kama kumsukuma mlevi kwenda kilabuni ama kumfungulia mlango wa choo aliyebanwa na tumbo la kuhara,

    yaani namaanisha kazi ilikuwa nyepesi mno kwa Lady Ninja kumuondoa duniani mtoto wa mzee Mnyungunyungu pindi tu alipoingia kibandani mwake bila kujua kwa juu kuna LadyNinja anamuinda na pindi alipokua wanainama yule bwana ili akae hapo hapo Lady Ninja Asha alijiachia kiwiliwili na kunining'inia mithili ya popo huku mikono yake kwa speed ya hatari ilifanikisha kupora panga dogo aliloshika yule mganga na kumkata eneo la koromeo huku mkono mwengine akimzuia kwa kumnusisha unga wa dawa frani zilizomfanya yule mganga ashindwe kupiga kelele na kubaki anatapatapa kwa krusha miguu akiwa amekaa amezuiwa kichwa na Lady Ninja huku ameshikishwa kipanga kilichonasia shingoni mwake wakati koromeo lililokatwa liliendelea kurusha damu mithili ya bomba la maji.

    Ndipo hapo aliporidhia yule muuaji na kumuachia kichwa baada ya kuona damu zimepunguza kasi ya kuluka hapo nae alijikunja tena Lady Ninja na kujiachia chini ambapo alitumia dawa maalum za uchawi wa Kininja kisha akatoweka kimaajabu eneo lile.



    Alisikilizia kwenye maficho yake ya siri kwa siku mbili huku akipewa taarifa na mzee Aly77 kuhusu kinachoendelea baadae na hapo akapata habari za kuja tena kwa Kamishna Shebby na kuziwasilisha kwa code maalum ya mr X kupitia simu yake iliyofungwa chipu ambayo haisomi kwenye mtandao mwengine wowote wa kawaida.

    )('Sikia My Lady Ninja, hao watu wamenizidia ubaya sasa nami ni mtu mwenye huruma sana lakini muda mwengine sina jinsi kwa kuwa ni maadui na wamenianza, sasa hakikisha unaua wote wataojifanya kimbelembele, tena usije kumuacha mjukuu wa Mnyungunyungu huyo kijana ndie mrithi wa kila kitu hapo.. ili kuwazuia kabisa hao askali hakikisha na huyo humuachi hai pia Askali wote watakaotaka kukuzuia ua mara moja kasoro Kamishna wao Shebby yeye mpe onyo na umwambie kama anataka kupambana na mimi basi akafanye mazoezi ya kusimama juani na kukamata kivuli chake')(

    Ndivyo ujumbe wa mr X ulivyosomeka na hapo ndipo Lady Ninja alipoweka mtego wake wa pili palepale msibani juu ya mti mkubwa kwa zaidi ya masaa 12 bila kusinzia wala kupepesa jicho akiwa kabanisha juu ya tawi moja lililokuwa usawa wa kile choo akiamini lazima yule mjukuu wa Mnyungunyungu aliyepewa amri ya kumuua iwe isiwe atakuja tu pale chooni kujisaidia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * * * *



    Na kweli Kipindi kina Kamishan Shebby na st,sirjent Kimaro wanaondoka muda mfupi baada ya shughuli ya mazishi kumalizika ndipo yule kijana akiwa na ndoo yake mkononi aliingia bafuni kwa lengo la kujisaidia haja Kubwa na hapohapo kwa mtindo wa ajabu na aina yake Lady Ninja aliweza kukirusha kitanzi maalum cha waya ambao aliuunganisha kwenye mashine ndogo aliyoifunga juu ya tawi la pili alipokuwapo na kweli kile kitanzi kilifika usawa wa shingo ya yule kijana na kabla hajapiga kelele kwa mstuko Lady Ninja aliwahi kutight kitanzi kwa kutumia ile machine na kuanza kuzidi kuzungusha skurul iliyokuwa ikiukusanya ule waya kwenye mviringo wake wa ile machine.



    Na hivyo ndivyo alivyokuwa ananyongwa yule kijana na Lady Ninja Asha aliyekuwa kalala juu ya tawi la ule mti na kumpandisha juu yule kijana kupitia wire uliotight barabara shingoni mwake na pindi alipofika usawa alioutaka Lady Ninja alichomoa kamba nyengine ya Katani na kuifunga juu ya tawi baada ya kutengeneza kitanzi kisha akampachika shingoni yule kijana ambae tayari alishakuwa marehemu na kuulegeza tena ule waya wake kwa kutumia ileile mashine yake maalum na baada ya hapo alimvua kitanzi cha waya na kumuacha akining'inia kwa kitanzi cha kamba ya katani.



    )(("Nimemaliza kazi Bosi"))(

    aliwasiliana na mr X, Lady Ninja Asha pindi aliposhuka kwa style ya kipekee pale juu ya mti pasi na kuonekana na kuingia kule maporini kwenye makutano yake ya siri na mzee Aly77.

    ))("Weldone My Lady Ninja, Ushawekewa Mil, 200 kwenye account yako, lakini Umebakiza mtu mmoja ambae hana budi nae auawe")((

    )(("Nani bosi"))(

    ))("Mzee Aly77")((

    )(("Aliy77!!? si mwenzetu huyu?"))(

    ))("Kuna kitu bado hujaelewa Lady Ninja, ila ni muhimu ufanye hivyo kwa sababu ya usalama zaidi na uhai wa siri yako kama Dokta Asha huna budi kummaliza huyo babu kwani anaweza kustukiwa na hana mbinu wala si mwepesi kupambana kama wewe kutokana na hali yake pia hutakiwi kuwa na share kwa kazi hii kuanzia sasa kila kitu utaongoza mwenyewe Lady Ninja")((

    )(("Sawa bosi, nasubiri signal yake ya kukutana nami nimalize mchezo"))(

    ))("All the Best My Lady")((



    Na hayo ndio majibu aliyoyapata Lady Ninja Asha kutoka kwa Mr X mara baada ya kumjuza kilichokuwa kinaendelea na ndipo aliposubiri signal ya kukutana na mzee Aly77 ili atimize agizo la bosi wake ambae ni Mr X.



    Na kweli baada ya muda mzee Aly77 alimtumia signal maalum Lady Ninja na kukutana pale kwenye kimsitu huku mzee Aly77 akiwa anahema mno kuonesha ni mtu aliyekuwa anakimbia kwa hofu pia.

    "9121, Toweka eneo hili mara moja kuna msako unaendelea, yule Kamishna Shebby amekuja na polisi wengi sana uuuphh daah! Toweka haraka hapa si salama sasa mi nataka nirudi wasije kunitafuta harafu wakakosa kuniona uuuppph"

    aliongea huku akitweta mzee Aly77 lakini katika hali ambayo hakuitarajia palepale Lady Ninja Asha alichomoa kisu na kumkita kifuani kwa Nguvu.

    "AAAAAAAAAAGHH.."

    Alitoa ukelele wa maumivu mzee Aly77 na kuanguka chini na muda uleule Lady Ninja alisikia sauti za miguu ya watu wakikimbilia eneo lile nae bila kupoteza muda aliruka beki mfurulizo kurudi nyuma mpaka usawa wa miti mingi mikubwa ambapo alidanda danda kwa speed ya Ajabu na kuibukia juu ya mti mmoja ambao aliamini isingekuwa rahisi kuonekana.

    Hapo aliwashuhudia askali wengi wakiongozwa na Kamishna Shebby wakija mkuku eneo lile alipotoka ambapo alimuacha mzee Aly77 akiugulia maumivu pale chini akiwa bado hajakata roho.



    Lady Ninja alifungua zipu ya mfuko uliojengewa na sambamba na mavazi yake na kutoa kifaa kimoja kimoja ambpo alipomaliza kuviunganisha ilionekana bunduki kubwa ya udunguaji ikiwa kamili.

    Na hapo ndipo alipojieka sawa na kuanza kumlenga mzee Aly77 mara alipoona amepakatwa na Kamishna Shebby akilazimishwa kusema kitu.

    Alisogeza lenzi na kumjaza vizuri kabisa sehemu za kichwa mzee Aly77 na papo hapo alifatua risasi iliyofumua kichwa cha mzee Aly77 mbele ya kamishna Shebby kabla hajatoboa siri yoyote.



    Kitim tim ndio kilianzia pale Kamishna Shebby alipotoa ukelele na kuwaamuru vijana wake wakae makini watafute alipo mdunguaji, lakini bila presha wala papara Lady Ninja Asha aliendelea kumtungua askali mmoja mmoja na kuzidi kumchanganya Shebby hasa pale alipomshuhudia rafiki ake kipenzi st,sajent Kimaro akipoteza maisha na kuingia kwa kiza kilichowafanya washindwe kuona vizuri, lakini kwa Lady Ninja mambo yalikuwa mepesi kwani alivaa miwani maalum ya kuonea usiku.

    )("Amebaki mwenyewe Shebby bosi")(

    alichart kimtindo pale juu ya mti na mr X

    (("Huyo mvunje mguu tu inatosha ili asikufate lakini hakikisha unampa Onyo nililokwambia"))(

    Msg ilirudi na kipindi hiko Shebby alikuwa anahangaika akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa kwa hasira akimtukana muuaji huku akimlaumu kwa kuua watu wasio na hatia na kumlazimisha kama kweli anajiamini basi asijifiche bali ajitokeze wapambane.

    Kipindi akiyasema hayo Shebby na kutupa bastora yake alikuwa maeneo ya mti uleule aliokuwa Lady Ninja Asha ambae aliamua sasa kushuka kwa kutumia kamba maalum aliyoinasisha kwenye lile tawi huku akitoa kicheko cha dhalau.

    Na hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza Kamishna Shebby kukutana na Lady Ninja Asha kabla hajageuka kuwa Dokta wake na hatimae kuwa mke mtarajiwa.





    Baada ya mabishano ya Shebby na Lady Ninja hadi kufikia kumpiga risasi ya mguu na kuchomoa bastora ndogo iliyokuwa na risasi maalum yenye kisindano kidogo ambacho mtu akichomwa nacho kikagusa karibu na fuvu la kichwa basi kinapoteza kumbukumbu zote muhimu ambazo muhusika alikuwa anazifikiria na kumpoteza.

    Alifanya hayo yote kwa niaba ya usalama wa mr X.

    Aliamini mr X ni mtu mwema anayewindwa na wabaya siku zote.

    Hakujua kama amepofuliwa na kile anachojua ama kuona kuhusu mr X sivyo hivyo kabisa.

    alimpiga risasi ya ile sindano kichwani Shebby ambae alipoteza fahamu palepale.



    * * * * * *



    Baada ya Lady Ninja kumaliza na kuzima kabisa tukio lililotaka kuvumbua siri na ukweli wa bosi wake ambao hata yeye aliyeulinda hakuujua wala hakuwahi kumfikiria sivyo bosi wake ambae mbali na kutoonana nae lakini alimuheshimu siku zote na kufata matakwa ya kile alichoamrishwa nae kutokana na vile alivyosaidiwa na kujengwa kiimani juu yake tangia anaokolewa kwenye msuko suko kule India bila kujua kuwa yote ilikuwa mipango.



    Baada ya kurudi kama kawaida yake siku hiyo hiyo aliingia kwenye kile chumba chake cha siri na kukuta ujumbewa Mr.X kuwa akae tayari muda wowote atapigiwa simu kwa niaba ya kwenda kumtibu Kamishna Shaaban kupitia mbinu ambayo hakufafanuliwa zaidi ya kuambiwa kuwa Mzee Mwinchande ameshatekwa kiakili na kuaminishwa yeye tu (Asha) ndie atayeweza kumtibu vizuri mwanae kutokana na kuchanganyikiwa kwake baada ya kupata taarifa ya tukio.

    ))("Kumbuka Lady Ninja, kinachokupeleka pale sio kumtibu tu, bali ni kujieka karibu na ile familia kama alivyowahi kujieka Aly77 kwenye familia ya Mnyungunyungu. nawe jichomeke na umtibu kwa umakini sana pia fanya kila mbinu hadi aanze kukupenda na ukifanikiwa kumteka kimapenzi utakuwa umemaliza kazi kwani utaelewa kila kitu kama kutakuwa na ubaya unasukwa juu yangu naamini utanisaidia mapema")((

    Ndivyo alivyoagizwa na Mr X mara baada ya kuwasiliana nae kwenye kile chumba chake cha siri kisha alitoka na kweli alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akihema na kumuomba afanye msaada wa moyo wake ili kuweza kumsaidia mtoto wake ambae ameshambuliwa huko Mkuyuni.



    Taarifa zile alizipokea kwa masikitiko makubwa Lady Ninja ambae sasa alijivisha kivuli na kuwa Dokta Asha kisha akamuaga mamaake na kwenda kukutana na mgonjwa yule ambae babaake alimtangazia kumlipa dau nono ili tu ahakikishe mwanae anarudi na kuwa kama zamani.



    Na kweli Dokta Asha alikuwa mtaalam sana wa maswala yale na alikuwa na cheti cha kimataifa.

    Alimtibu Kamishna Shebby kwa moyo wa kivuli cha Dokta Asha lakini akiwa anatega makucha kama Lady Ninja jasusi wa mr X.

    Siku zilienda na alizidi kumuonesha mapenzi mgonjwa wake na kumyeyekea mno hali iliyofanya afauru kuanza kumteka akili yeye Shebby mpaka wazazi wake wakatokea kumpenda Asha na kuombea aolewe na mtoto wao bila kujua kiundani Asha ni nani.



    Kama walivyosema wahenga 'Mapenzi hayajalibiwi' na ndivyo ilivyokuwa kwa Asha mara baada ya kuzidi kuwa karibu na Kamishna Shebby ndivyo alivyojikuta anazidi kumpenda kweli na moyo wa huruma kuanza kumjia kila alipomuona akilalama kupoteza kwake kumbukumbu na mara nyingi alitamani amsaidie kwani alijua yote yanayomsibu lakini alipokumbuka kiapo alichoapa mbele ya Tyga kuhusu kutii na kufatwa matakwa ya mr X, ilimlazimu aache kama ilivyo japo kuna muda alikuwa anaumia kweli juu ya Shebby na kupelekea hadi machozi kumtoka.

    Na ndipo usiku mmoja ambao ndio ulikuwa wa mwisho kuwepo pale kwa mzee Mwinchande alipokata shauli na kuamua kumtibu Shebby akiwa kwenye usingizi mzito baada ya kumchoma sindano maalum ya usingizi na kufanikisha zoezi la kumtoa kisindano kilichokuwa kichwani mwake kilichomfanya asiwe na kumbukumbu vizuri.



    Lakini usiku huo huo aliporudi katika makazi yake ndipo alipokutana na ujumbe mwengine kutoka kwa Mr X ukimlazimu afanye haraka kuzuia ujio wa mtu mmoja ambae alisahauliwa kuwa ni adui mkubwa wa mr X ambae anakuja jijini na askali mmoja shupavu kwa niaba ya kumchunguza wapi alipo Mr X.

    ))("Fanya Mbinu unayojua wewe Lady Ninja kuhakikisha huyo mzee hafikishwi jijini akiwa hai")((

    alituma agizo mr X sambamba na docoment zenye maelekezo zaidi kuhusu huyo mzee ambae alikuwa na urafiki na mzee Mwinchande ambae nae ni adui wa mr X kwa mujibu wa maelezo aliyokuwa anampa Asha.

    )(("Worry out I'll do my Best"))(

    alijibu ujumbe ule Asha na kuchomoka kama kawaida yake usiku huku akiacha ujumbe mezani swala ambalo mamaake aliyekuwa anaishi nae alishalizoea japo hajawahi kuhisi vibaya mwanae anaendaga wapi na kufanya nini zaidi alimuombea arudi salama na kukubali pale alipokuwa anajibiwa kifupi tu na Asha pindi alipomuuliza mara nyingi alisema 'nimepigiwa simu ya dharula, nimeona haina haja ya kukusumbua usiku'

    Na kutokana mwanae alikuwa special kwa utabibu wa mifupa wala hakuhoji zaidi yule mama ambae ni Zena.



    Signal maalum za satelite zilitumwa na kuonesha kidoti cha gari iliyokuwa imem beba mzee Cyplian kupitia saa aliyovaa Asha pindi akiwa kwenye gari yake ndogo aina ya Toyota Crester nyeupe akielekea Morogoro na alipokaribia Chalinze signal ilionesha gari husika inakaribia maeneo yale na kwa mwendo inayotembea ingetumia dakika ishirini tu kufika pale na hapo ndipo alipoisogeza gari yake maeneo ya Shelly na kushuka kisha akaelekea ile njia ya Tanga huku akiwa makini na kupiga hesabu ya mbinu ambayo alipanga kuitumia na kwa hesabu zake haraka haraka ziligota pindi alipoiona basi moja iliyokuwa inatokea Tanga na kusimama pale juu maeneo ya Polisi Chalinze na ndipo alipoisogelea na kujichanganya na vijana waliokuwa wanauza matunda kisha kimakusudi alidondosha pochi yake na kumfanya ainame kuiokota ndipo alipobonyeza pete yake maalum ya mionzi mikali na kuirengesha usawa wa ringi ya taili za mbele kulipoingia waya za breki na kuzikata pasi na mtu yeyote kujua na wakati huo pia alipoangalia saa yake signal ilimuonesha ile gari iliyom beba mzee Cyplian imebakiza dakika tano tu kupita pale Chalinze.

    ("Camoon, go, go, go")

    aliwazia na kujisemea moyoni Lady Ninja ambae safari hii alivaa mavazi ya kiislam hususani kwa wale washika dini na wenye itikadi kali kwani alivaa hadi nikabu usoni mwake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kweli mara ile gari ilianza kuondoka kwa mbembe sekunde zile zile na ile gari aliyokuwamo mzee Cyplian ndio ilikuwa inafika eno lile na kilichofuta pale ni kishindo na honi nyingi mara baada ya dereva wa basi kushindwa kulicontrol basi lake kwa kukosa breki na kukata kona huku akiyagonga magari mengine na kulikosakosa lile alilokuwamo mzee Cyplian.

    Kipindi hayo yote yakitokea Lady Ninja alikuwa makini sana tena kama sie yeye vile aliwashuhudia hadi polisi wakifika maeneo yale kudumisha usalama na ndipo nae alipoanza kusogea upande wa chini huku akijiapia hawezi kuondoka hadi ahakikishe mzee Cyplian amepoteza maisha pale na ndipo alipokuwa anaangalia kule ilipotokomea gari iliyombeba muhusika aliona aliona dariri zote za kufauru mission yake hasa pale alipomuona kijana ambae aliamini ndie dereva wa mzee Cyplian akiwa anavuja damu huku kachanganyikiwa akili.

    Alikutana nae macho kwa macho na alishangaa kuona macho ya yule askali dereva akiwa anamtazama kwa kumshuku mno na hapo alinyanyuka kumfata kule alipokuwa anaenda, nae Lady Ninja alijiandaa kumlipua kwa mionzi iliyokuwa kwenye pete yake lakini kama bahati yule askali ambae alikuwa ni Cj4 alidondoka na kupoteza fahamu kipindi hiko Lady Ninja aliingia kwenye gari yake na signal ilikuja toka kwa mr X kuwa mission yake imeenda vizuri na ndipo hapo aliwasha gari yake taratibu na kuanza kuondoka huku akimuwazia yule askali ni mtu mwenye mbinu kiasi gani hadi alimtilia shaka kuhusika na ajali ile ambayo ingekuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kusema eti imetengenezwa.

    Na hapo ndipo alipokuwa njiani alipokosana kugongana na Jeep ambayo alipoiona tu alitabasam kwani aliijua vizuri kuwa ni ya mumewe mtarajiwa ambae ni Kamishna Shebby na alifanikisha kutoka maeneo yale na alipofika mbele kutokana na fikra juu ya askali yule aliyezimia kule aliona ni vyema apoteze ushahidi kabisa mara baada ya kusimamisha gari maeneo ya kibaha ambapo alimpa lifti bint mmoja na walipofika Kibamba aliipaki gari njia panda ya kijiji cha Hakipo.

    "Samahani dada, naomba ukae hapa huku ukikanyaga kanyaga breki nataka kucheki huku nyuma kama taa inawaka maana hiyo display sielewi imekuaje sasa."

    Aliongea Asha na kumfanya yule binti mpenda lifti kukaa kwenye kiti cha usukani bila kujua ni trick ya yule mtu nae alianza kufanya kama alivyoagizwa lakini Asha alipozungukia nyuma tua aliwasha mionzi yake hatari iliyomulika lile gari kwa dakika moja na papo hapo ilianza kuwaka moto huku akiwa amelock milango yote alianza kuondoka taratibu eneo lile na kumuacha bint wa watu akiteketea garini.



    "NOOOOO"

    Alizidi kupiga kelele Asha mara baada ya kutoka kwenye mawazo mazito na kukumbuka mission ile ya mwisho aliyomfanyia mr. X kupelekea kuua watu wengi wasio na makosa kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja aliyemgeuza kuwa kipofu kiakili na mawazo juu yake pasi na kujitambua na leo hii alitaka akamuue mtu ambae anajua fika alikuwa ni babaake mzazi.



    Aliumia sana Asha mara baada ya kukumbuka yote yale yaliyopita na kujikuta akilia kwa uchungu mno na kuijutia nafsi yake.

    "Nilikuamini sana Mr X, siku zote nilijua wewe ndie mtu muhimu kwangu na umejitolea kufanikisha maisha yangu kuwa bora kumbe ulikuwa na vitu unavitaka toka kwangu na ulijua fika mimi ni nani na kwanini unanitumia. aaah!! Umenifanya kipofu wako kwa muda mrefu sana.. Nadiriki kusema wewe ni zaidi ya SHETANI. Ndio wewe ni Shetani Mr X shetani mkubwaaa na lazima Ufe kikatiri..."

    Alinung'unika Asha huku akigugumia kwa maumivu na kuhisi kama nafsi zote za watu alizozikatisha uhai zimesimama mbele yake zikimshutumu na kumzomea.



    Ukweli hakupanga mwenyewe kuwa na mahusiano na Shebby japo baada ya tendo lile la kikubwa walilofanya siku moja ndio lilichochea kasi zaidi na ashki ya kumpenda kweli Shebby.

    "Nimeua weeeengi wasio na hatia kwa ajili ya Shetani mmoja!!? hapana sikubali kwa hili hata kidogo lazima Nilipe vifo vya watu wote japo nilivitenda mwenyewe kwa mikono yangu lakini nina sababu zote za msingi. LAZIMAAAAAA.."

    Alizidi kupayuka mwenyewe Asha kwa hasira huku akizidi kupiga mateke vitu vilivyokaa jilani yake na kuchomoa connector zote zilizofungwa chumbani kwake zilizokuwa zinamuwezesha kuwasiliana na Mr. X baada ya Connector zote kuzima signal zenyewe automatic mara baada tu ya mr X kutuma ujumbe ule wa sauti akimcheka kwa nguvu na ndipo alizima kabisa mitambo yote iliyokuwa inamuunganisha na Asha.



    Lengo la Mr. X ni kusambaratisha kila aliyekuwa na kisasi nae na hapo alitumia akili nyingi kutengeneza mchezo ule wa vipofu ambao wachezaji walimuhusudu bila kujua wanaomuhusudu ndie adui yao waliyepaswa wapambane nae na kwa kuwa walikuwa hawalioni hilo ndio maana mchezo wake akauita wa vipofu.

    Alifikiria mateso mazito aliyokumbana nayo babaake.

    Alikumbuka vifo vya wafadhili wake na kugundua kuwa yote ilikuwa ni trick ya kuingizwa ktk mchezo na Mr X akimtumia Tyga ambae pia aliamini kuwa amehadaika na mchezo wa Vipofu aliokuwa anaucheza mr X lakini kitu kimoja hakujua kabisa Asha kama yule mzee Aly77 aliyemuua kule Mkuyuni ni baba mzazi wa Tyga.



    Alivalia mavazi yake ya kazi Usiku ule ule alikaa tayari kwa ajili ya kuianza kazi ya kumsaka Mr X na alijua wapi aanzie japo hakujua wapi amalizie.

    "I Must Find You Mr. X"

    Alijiapiza Asha baada ya kuyatinga mavazi yake ya Kininja na silaha zake zote muhimu usiku huo huo aliharibu kila kitu kilichokuwa kinamuunganisha na mr X mule ndani kisha akafanya uchawi wake wa Kininja na mara ulitokea moshi wa ajabu mule ndani akatoweka na kuibukia nje ya nyumba yao ambapo style aliyotembea nayo sasa hivi ilikuwa tofauti kabisa na awali kwani alienda mwendo wa haraka mno na sehemu zengine aliweza kudanda kwenye mistimu na kupita juu ya nyaya sa umeme pasi na kuonekana.



    Asikwambie mtu hakuna Ninja aliyekamilika asiyekuwa na mazingaombwe na ndivyo ilivyokuwa kwa Lady Ninja Asha ambae alifundishwa mambo mengi na mzee wa Kijapani ambae alikuwa ni Full Ninja Master na aliyatii mafunzo na kuyafata kwa moyo wote huku uvumilivu akiuweka mbele na hiyo ndio ikawa sifa ya uwezo wa ajabu aliokuwa nao leo hii.

    Aliamua sasa kujitolea maisha yake kupambana na mtu asiyefahamika anayetumia akili nyingi huku akiwa na wafuasi wasiofahamika.

    Alijua ni hatari lakini alijiamini pia hakuifikiria kabisa ndoa yake iliyo mbeleni yeye na Kamishna Shebby wala hakuona umuhimu wake kwa wakati huo zaidi ya umuhimu wa kukatisha uhai kwa mtu aliyeamini ni Shetani aliyepindukia Mr X.



    Safari yake ya wizi wizi usiku ule huku jiji likiwa limepoa kabisa ilimpeleka hadi maeneo ya mbagara na mbele yake aliliona jengo kubwa la hoteli ambayo alipangiwa babaake pale.

    ("Lazima nifanye mbinu nimuhamishe hapa baba kabla huyu Chizi hajatuma kinyago wake mwengine aliyempofua kuja kumaliza azma yake")

    Aliwaza Lady Ninja Asha na kutoa tena ile dawa yake ya unga maalum ambayo akiishika kwa style maalum aliyofundishwa na kutamka maneno ya Mzimu wa Kininja aliyoyajua mwenyewe, basi hupotea na kuacha moshi mdogo eneo lile na hutokea mahala ambako alikukusudia akilini kabla hajafumba macho na kusema yale maneno.

    Na ndivyo ilivyokuwa ambapo Asha alinuia na kuieka akilini picha ya nyuma ya hoteli ile ili iwe rahisi kuingia kimya kimya lengo kuu likiwa ni kumuhamisha babaake pale hotelini na kumpeleka sehemu nyengine ambayo aliamini inaweza kuwa salama ili amuondoe kwenye Rada ya Mr X.



    * * * * * *



    Kwa upande wa Cj4 yeye alikuwa ndani ya nyumba moja iliyokuwa jilani na ile hoteli alipokuwa amepangiwa Hussein babu bubu huku muda wote alikuwa makini mno na kila kitu kilichokuwa kinaendelea hotelini pale mara baada ya kutega kamera maalum ya kijeshi kwenye usawa wa dirisha lake na kuchukua upande wa V ya hoteli ile kwa mbele, pia kamera nyengine aliitega kwenye chumba cha guest iliyokuwa upande wa nyuma ya hoteli ile na kwa jinsi alivyoitega ilikuwa ngumu mno mtu kuona ama kujua na kwa kutumia kamera hizo mbili aliweza kurekodi kila kilichokuwa kinaingia na kutoka kwenye ile hoteli kwa kutumia compyuta yake aliyoiconect na zile kamera.



    Usiku huo kama kawaida alikuwa anawascan watu aliokuwa anawatilia shaka na kuchukua picha zao pasi na wao kujua kila aliyekuwa anaingia au kutoka mule hotelini na kwa kutumia compyuta yake maalum aliyoiconect na zile kamera.

    Vilevile kitu kilichozidi kuzipa upekee zile kamera za Cj4 ni setting zake za moja kwa moja pindi inapommulika mtu yeyote mwenye silaha ama silaha yoyote ilikuwa inatuma Alarm kwenye compyuta yake na kumpiga picha muhusika na kutuma moja kwa moja kwa mtaalam Cj4.



    ("Mh! kila kitu kipo sawa, mbona huu mchezo Mr X hauvagai au kashaustukia...!! Camoon Mr X")

    aliwaza Cj4 pindi alipokuwa anacheki cheki jengo la hoteli hususani usawa wa ghorofa kilipokuwa chumba cha Hussein ambako napo kulifungwa kamera kwa siri na Kamishna Shebby ambayo ilikuwa inaonesha kinachoendelea mule ndani na kutuma moja kwa moja kwa Cj4 na kwenye simu ya Kamishna Shebby.

    Yote hayo walifanya kwaajili ya usalama wa Hussein bubu na kumtega Mr X kwa kumtumia Hussein bubu kama chambo pale hotelini kwani walijua kuwa shabaha iliyobaki kwa Mr X ni kwa Hussein bubu tu na akifanikiwa kumuua na huyo atakuwa kamaliza kila kitu na kamwe hakutakuwa na sababu ya kumtaja wala kumzungumzia tena.

    Lakini yote yale yalikuwa yanaendelea pasi hata na Hussein mwenyewe kujua japo na yeye alikuwa na kiu na shauku ya kumuua Mr X na kila siku alikuwa anasali ili utokee muujiza amuue kwa mkono wake Mr X.



    Lakini Cj4 akiwa amejipumzisha baada ya kuangalia kona zote kuwa ni salama mara Alarm ilibeep ktk kompyuta yake kumuashiria kuna hatari katika zone moja ya eneo alilotegesha kamera na hapo ndipo kwa speed alifungua kuangalia na alimshuhudia mtu aliyevaa mavazi ya Kininja akiingia kinyemera kwenye nyuma ya jengo la hoteli kulipokuwa na bustani kubwa na tayari alishaua walinzi wawili pasi na eneo la mbele ya Hoteli kujua chochote.

    "Karibu kwenye Mchezo wee Mbuzi"

    aliongea kwa Hasira Cj4 na kuchukua Kisu chake kikubwa kilichokuwa na dira kwenye mpini wake sambamba na wire maalum wa silva kwa niaba ya kwenda kuoneshana kazi na yule Ninja aliyeamini ametumwa na Mr X na alienda pale kwa niaba ya kumaliza kazi aliyotumwa na Mr X nayo ni kummaliza Hussein babu bubu.



    Ndipo muda ule ambo Cj4 anatoka na kuanza kupita Kikomando akichanganya na Uninja ndani yake alishangaa alipokuwa anakaribia kwenye ile bustani kukukuta kuna timbwili limeibuka lililomshangaza mno na lililomfanya kwanza ajibanze sehemu kulishuhudia mwisho wake utakuaje.

    Naam lilikuwa ni Timbwili la Maninja wawili tena wote wakiwa wamevaa mavazi meusi yanayofanana sana.

    Hali hii ilimchanganya Cj4 na kuamua kubanza pale kwenye moja mti uliokuwa kwenye ile bustani huku akiwa haelewi wapi ametokea Ninja mwengine wakati awali alimuona mmoja na je yule Ninja mwengine ni nani na kwanini wanapigana pale? Pia kati ya wale Maninja wawili yupi Ninja mwema na yupi Ninja m baya?



    Alijiuliza maswali haya Cj4 ambayo hakujua majibu yake na alijua ni ngumu kujua majibu yake hadi atapozidiwa Ninja mmoja ndipo ataangalia yule mwengine atachukua maamuzi gani akimmaliza mwenzake, kama atachukua maamuzi ya kupanda kwenye hoteli kwa nia ya kwenda kummaliza Hussein bubu basi atadeal na huyo kwani ni mbaya lakini kama atachukua hatua ya kuondoka basi huyo atakuwa Ninja ambae hana chuki na mtu yeyote bali huenda kaja kutoa msaada kwa Hussein bubu ama alikuwa na kisasi na yule Ninja mwengine ambacho kaja kumlipizia.

    Lakini pia alijiuliza Cj4 kama kuna Ninja kati ya wale anapigana kwa niaba ya kumtetea Hussein ni Ninja gani huyo? maana mission ya usalama wa Hussein ipo katika mikono yake na mikono ya Kamishna Shebby sasa huyo Ninja ametokea wapi? ama hakika Cj4 alipata mtihani wa maamuzi kipindi akiangalia ule mpambanu lakini pia aliamini katika moja ya mawazo yake basi kuna wazo sahihi kabisa kuhusu wale maninja waliokuwa wanaendeleza kasheshe pale bustanini.



    Mapigano makali ya wale maninja huku mmoja akiwa mwepesi sana kuruka na kukwepa vidubwana alivyokuwa anarusha mwengine ambavyo vilikuwa vikimkosa vinazunguka na kurudi kwenye mikono ya mrushaji wake na katika harakati zile mara Ninja yule aliyekuwa anaruka mno alipokitwa na kile kidubwana kimoja maeneo ya tumbo mara baada ya Ninja mwenzangu kumzidi ujanja mdogo katika urushaji na kumsababishia akwepe tofauti na kuingia kwenye kumi na nane za Ninja mrusha vidubwasha.

    Hapo sasa Cj4 kuna kitu alianza kukigundua baada ya yule Ninja aliyechomwa kile kidubwasha mithili ya msumeno wa round kuanza kuzidiwa kutokana na maumivu na kumpa nafasi ya kushambuliwa zaidi na Ninja mwenzake mpaka ikafikia sasaameanguka chini hana ujanja huku mkono mmoja ameshikilia pale tumboni mwake ndipo yule Ninja alipoanza kumsogelea na kumsimamia mbele yake huku akimwambia maneno ambayo Hussein yalimsaidia kuwatofautisha wale Maninja na kumjua m baya ni yupi mwema ni yupi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na wakati yule Ninja akimtambia kwa maneno makali mwenzake aliyekuwa katika hali mbaya tena akimtambia zaidi kwa kuamua kuvua maski ile ya Kininja inayoficha uso na kumuwezesha Cj4 kumuona sehemu za Kisogo na kugundua yule ni Ninja dume tena alionekana kichwa chake kikiwa na mchanganyiko wa nywele nyeupe na nyeusi kuonesha kuwa yule ni Ninja mwenye umli mkubwa yaani sio kijana japo alionekana bado strong na mwenye mbinu kwa vile alivyomuona akipambana.

    Hapo sasa Cj4 alimshuhudia yule Ninja mzee akichomoa lile panga lake kubwa la Kininja kwa niaba ya kummaliza Ninja yule aliyezidiwa kwa kuchomwa na kidubwasha ambae tayari Cj4 aligundua kuwa ndie Ninja mwema na hapo aliona itakuwa uzembe mkubwa kuacha Ninja yule mwema auawe mbele ya macho yake wakati ana uwezo wa kutoa msaada na aliamini anaweza kumdhibiti yule Ninja mzee baada ya kumsoma toka awali alipokuwa anapambana na Ninja mwenzake na alizigundua mbinu alizomshindia Ninja mwenzake ambae aliamini pia ingekuwa si mbinu zile za ujanja ujanja basi hata yule aliyejeruhiwa angeweza kumdhibi.

    Alichungulia Cj4 na kupiga mahesabu ya haraka pindi yule Ninja aliponyanyua panga kwa dhumuni sasa la kummaliza mwenzake bila huruma ambae alikuwa na dariri zote za kukata tamaa na kusubiria kifo na hapo ndipo Cj4 alipoinunua ile kesi kwa style ya kipekee na ajabu.



    * * * *





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog