Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

DEMU WA FACEBOOK - 2

 





    Simulizi : Demu Wa Facebook

    Sehemu Ya Pili (2)



    Huku kwa upande wa Peter siku zikionekana kwenda taratibu sana kwa jinsi alivyokuwa na hamu ya kuonana na kimwana Husna aliyeaminika katika ubongo wake kuwa ni binti mrembo sana na anayetoka katika familia ya kitajiri sana, kwa upande wake yeye Husna binti fukara wa kutupwa aliyedanganya kuwa ni mototo wa kitajiri aliona siku zikiwa zinakimbia kwa kasi kubwa sana na alikuwa hajajua bado atatumia uongo gani kumlaghai Peter ili awe nae katika mapenzi kwani aliamini kwa umbo lake na sura yake mbovu kamwe kijana mtanashati Peter asingeweza kusimama naye hata dakika moja kwa ajili ya mazungumzo kwani kwa dakika chache alizopata nafasi ya kumuona siku ile ya ugomvi alimuona kuwa ni mtu wa mashauzi ambaye vijana wa mjini wanamuita ‘sharobalo’ ni hapo moyo wake (Husna) ulikuwa umependa kwa dhati na kwa mara ya kwanza. Mara ya kwanza katika maisha yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ulikuwa usiku wa siku ya ijumaa masaa machache kabla haijaingia siku ya jumamosi ambayo haswaa ndio ilikuwa siku kamili ya miadi aliyotoa kwa Peter, akili ilikuwa imewaza nini cha kufanya na sasa alikuwa amechoka sana, taratibu akiwa kitandani kwake na simu yake mkononi aliamua kuingia katika mtandao wa kijamii wa facebook,hakuwa na jipya sana wakati huu zaidi ya kulitafuta jina la Peter Isuti na kumjulia hali na kama yupo hewani waweze kupiga stori mbili tatu za hapa na pale na hatimaye waweze kulala.



    HUSNA: Mambo vipi mume??

    PETER: Poa mpenzi wewe hujalala jamani au ulikuwa unapika leo

    HUSNA:hapana jamani nilikuwa nimelala lakini nikakuota imenilazimu kuamka ili nikujulie hali

    PETER:Asante jamani mpenzi wangu wewe, vipi kuna joto au baridi huko??

    HUSNA:Mh!! Hebu tuachane na hayo kwanza kesho ndio tutaonana lakini samahani itakuwa jioni sana kuna kazi nitakuwa namsaidia baba ofisini na siwezi kuondoka kabla hazijaisha si unajua tena. (Husna aliendelea kuwa muongo)

    PETER: Pole my dear,usijali lakini mimi hata ukiniambia saa nane usiku mi nipo tayari

    HUSNA: Mh!! Unavyoupenda usiku wewe, anyway nilikuwa nimesahau kukwambia nahofia kuonana nawe eneo la wazi kwa kweli yaani rafiki zake daddy wakiniona tu hiyo ni kesi habari zitamfikia baba, na mimi sipendi kumkera hata kidogo

    PETER: So niambie ni wapi utakuwa confortable kabisa sitaki uwe na hofu hata kidogo

    HUSNA: Naomba utafute lodge nzuri na ya kistaarabu na wewe pia uwe mstaarabu na uniheshimu mwenzio sipendi kukwazwa mwisho wa siku.

    PETER: Usijali Husna nitatimiza yote yale unayoyataka hata usiwe na hofu hautajuta kukutana nami, yaani umeniteka ile mbaya motto.

    HUSNA:Hivi Peter ukikutana nami nina sura na umbo baya utafanyaje au ndio kunikimbia??

    PETER: Haitatokea hata siku moja kwangu mimi, sijapenda sauti wala sura yako ni moyo tu umenituma kuwa nawe katika penzi wala hizo picha zako hazina maana kwangu (kawaida ya wanaume kujidai wanajua kupenda wakati hakuna lolote)

    HUSNA:Kama ni kweli hayo unayoyasema basi kesho tutaonana Peter nakupenda sana mie. Nakupenda namaanisha!!!

    PETER: Haunizidi mimi na kesho ndio utaamini ninachokuandikia na kusema

    HUSNA: Haya naisubiri hiyo kesho kwa hamu tuone nani anampenda mwenzake zaidi na nani muongo kwa mwenzake!!!

    Hatimaye walimaliza kuchat wawili hawa baada ya Husna kudanganya kuwa alikuwa ameitwa na baba yake kwenda kumsaidia kazi kwenye kompyuta mara moja katika ofisi ndogo iliyopo nyumbani kwao.

    Usiku ulikuwa mfupi sana na hatimaye ikafika asubuhi, kichwa kilizidi kumuuma Husna, alikuwa kama anaumwa tena ugonjwa mbaya kabisa wa Malaria unaopigwa vita hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.

    Haikuwa kawaida yake kuwa mnyonge kiasi kile hata siku moja.

    Vijana wa pale mtaani kwao Husna hawakuhitaji elimu ya kwenda darasani kufahamu kuwa Husna alikuwa amekumbwa na tatizo flani. Ilikuwa ni kawaida yake yeye (Husna) kuwakwaza watu wengine lakini sio yeye kukwazwa,sasa kwa asubuhi hiyo na yeye yalikuwa yamemkumba watu walitamani sana kufahamu ni nani huyo mkali alikuwa amefanikiwa kumtibua mwanadada huyo mapepe na mkorofi lakini pia hawakupata jawabu lolote.

    "Mwajuma ndala ndefuuu!....Mwajuma ndala ndefuu!" zilisikika sauti za watoto kutoka madirisha ya nyumba za majirani wakimtania Husna lakini hata hakujibu lolote neno, haikuwa kawaida yake hata kidogo kufumbia macho suala kama hilo, laiti kama angekuwa katika hali ya kawaida angeufungulia mdomo wake uweze kutoa matusi ya nguoni na kama angepata fursa ya kuwagundua wanaomtania hivyo basi angetoa onyo kwa kutoa kipigo kikali.



    Jumamosi hii hakuwa Husna yule aliyezoeleka.



    Alikuwa Husna mpole sana na mnyenyekevu kuliko!!!

    "Shogangu mwenyewe huyo Husna wa ukweli looh! Umeupara shoga unaenda wapi? Umejishetua mwenyewe looh!!" ilisikika sauti ikimwambia Husna lakini hakuweza kusikia kutokana na mawazo yake. Mawazo ya kukutana na Peter.

    "Sio mpango wala nini shoga yangu yaani nakupa masalam unayapo tezea kihivyo" alianza kulalamika mtu yule. Sauti yake ikihangaika kusikika vyema.

    "Aah! Jamani Mwamvua ni wewe, samahani sijakusikia jamani… yaani kuna mambo yamenichanganya we acha tu mwenzangu..nisamehe bure mie" aligutuka Husna na kujibu salamu ile ya yule aliyemsalimia

    "Aah! Kamanda wangu nini cha kukuchanganya wewe tena hapa mtaani steringi wangu" alihoji kijana yule wa kike ambaye alionekana kama ametoka kutumia madawa ya kulevya muda si mrefu sana.

    "We acha tu! Sijui hata nianzie wapi kukueleza" alijibu Husna huku akisogea pembeni kwenye kivuli na yule msichana akamfuata ili kujua kulikoni.

    Husna mcharuko alikuwa amefikwa. Kama ni maji sasa yalikuwa shingoni.

    Je aseme ukweli kuwa amedanganya facebook ama aendelee kuwa mbishi.

    Nguvu ya penzi itazungumza. Ile nguvu inayoua ubongo wa mwanadamu kabla hajafa.



    * * *

    Mchakato wa kuchukua chumba ulikuwa umekamilika. Baada ya kufundishwa mambo kadha wa kadha kule chumbani sasa alikuwa anajiamini!!!

    Ule wakati ukawa unasubiriwa!!



    Peter alikuwa makini kabisa katika geti la hoteli ya Lamada,tayari shilingi elfu hamsini ilikuwa imemkatika mfukoni kwa kuchukua chumba katika hoteli ile iliyopo maeneo ya Ilala Boma, aliamini huenda chumba kile alicholipia hakikuwa hadhi ya mwanadada mrembo Husna ambaye alimtarajia jioni hiyo. Ile picha na nyodo za Husna zilikuwa zinamteketeza.

    Hakutaka kuchafuliwa katika nguo zake alizoamini zimempendeza sana na kwa hakika alikuwa amependeza nywele zilizotoka kuoshwa na kuwekewa mawimbi (waves),suruali nyeusi ya kitambaa dizaini ya modo, shati ya mikono mirefu rangi ya pinki iliyochomekewa vyema ikisindikizwa na kiatu cheusi mguuni huku kijitai kifupi kikinin'ginia kifuani. Marashi yalitawala eneo alilokuwa amesimama, macho yake yote yakiwa yanatazama getini huku mikono yake ikisubiri kupokea simu kwamba Husna amefika.

    "Helow honey umefika wapi?" Peter alituma ujumbe katika simu ya Husna baada ya kuona kimya kimekuwa kikubwa sana.

    "Sorry nipo ndani ya gari nimekaribia kufika" alijibiwa.

    "Umepanda ya Mbagala au Temeke" aliuliza Peter.

    "Ooh! Sorry natumia 'private car' ya mshua" alijibiwa tena.

    Ujumbe huo ulirudisha uoga wa Peter na kumtetemesha sana kijana huyu wa kisukuma.

    "Mama yangu hivi kweli na private car (gari binafsi) ana hadhi ya kulala na mimi sembuse kunishika mkono dah? Naumbuka leo mie,kwa nini sikuchukua chumba Kempisk?" alianza kujilaumu Peter huku akiwa hajui hata chumba cha Kempiski kilikuwa kinagharimu bei gani. Akiwa bado anaumia kwa mawazo mara simu yake ikatoa mlio mfukoni, haraka haraka akaitoa kama vile angeiacha ingeweza kulipuka!!! hakuwa mwingine jina likatokea likimaanisha Husna.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Helow at Lamada already! Where are you boy" ilisikika sauti nyembamba ya kike katika simu ya Peter. Sauti ile ikaupasua moyo wake!! Hofu ikatanda.

    "Yes aah! Iam nipo hapa getini where are you" alijichanganya Peter kwa uoga, kiswanglishi kikachukua nafasi. Hakupata jibu simu ikawa imekatwa naye akabaki kujifuta jasho ambalo lilikuwa limeanza kutiririka katika mgongo wake kutokana na hofu kutanda katika moyo wake. Akiwa anajiandaa kupiga simu ili aweze kutoa maelekezo vizuri mbele yake macho yake yalikutana na kitu ambacho kilisitisha zoezi la kupiga simu, kadri alivyozidi kuduwaa ndivyo kitu kile kile kilizidi kumsogelea zaidi.

    "Mh! Anakuja kwangu au!??" Peter alijikuta anajiuliza.

    "Hapana hawezi kuwa anakuja kwangu" alijipa jibu mwenyewe.

    Wakati akizidi kuamini kwamba mwanamama yule hakuwa akielekea upande wake lakini ujio wake ulizidi kumshangaza

    “Au amelewa nini huyu mdada” Peter alijisemea kwa sauti ya chini aliyoamini hawezi kusikia muhusika mkuu. Mwendo wa yule binti haukueleweka, miguu haikujulikana kama inaelekea kusini kasikazini mashariki ama magharibi. Peter akawa mtazamaji.

    Kiwiliwili kikazidi kusogea kumfuata!! Akataka kukipisha akiami hausiki nacho. Chenyewe kikazidi kumwelekea. Mazito!!!!

    “Mh!! Hata sijakosea nakuja kwako baby boy Pira (Pita)” alishangaa kusikia yule binti alikuwa anakuja kwake. Jinsi alivyotamka jina lake kwa kulitilia nakshi za kisasa. Peter akatweta. Hofu!! Mauzauza!! Amekamatika!!

    “Aah!! Sorry na karibu sana kwani wewe ndio Husna au?” alihoji Peter akiwa bado anamshangaa binti huyu.

    “What do you think!! kwani” badala ya kujibu swali huyu binti naye akahoji.

    Peter hakujibu bali akaanza kujiumauma bila mantiki yoyote ile. Ni kama vile hakutegemea ujio ule kwa namna ile ya kushangaza. Akajaribu kuongea mdomo ukawa mzito. Akajaribu kukohoa akagundua kuwa anajikoholesha. Akataka kucheka, tabasamu likagoma kutokeza, akawa kama amewekewa silaha ya moto na anaamriwa kusalimu amri. Lakini sasa hapakuwa na silaha yoyote mbele yake. Pagumu hapa!!! Peter mtegoni!!





    Baada ya kama dakika tatu ndio Peter akaupata ujasiri wa kumkaribisha mgeni wake yule aliyemtegemea.

    “Hili eneo ni salama kwa gari langu” alihoji kabla hajahalalisha suala la kuingia chumbani huku akizungusha funguo zake katika kidole chake cha mwisho kwa madaha sana

    “Eeeh! Ndio wamenipa uhakika,mi mwenyewe ni mgeni sana maeneo haya yaani kwa kifupi maeneo ya Guest huwa sitembelei sana ni kwa ajili yako nimekuja huku” alijibu kwa kirefu Peter hata majibu yasiyohitajika kwa swali lile.

    “Owwwwwwwk!!!!!” alijibu yule binti Husna huku akiunyanyua mguu wake na kama vile mwanamitindo wa kimataifa akaanza kuikanyaga ardhi kwa nyodo zote akimfuata Peter ambaye alikuwa bado hajiamini sana. Huku nyuma ikasalia mitetemeko ya makalio ya binti huyu. Hakuna aliyejali!!!

    Alipokatiza pale mapokezi kila jicho liliutazama mguu wake. Waliokuwa bize wakaacha shughuli zao wote jicho kwake. Hakuwa na muda wa kuwashangaa alishazoea watu kumshangaa.

    “Eeeh!! Karibu,karibu sana hapa ndio nyumbani…….aah! samahani sio nyumbani hapa ndio pale uliponiambia tukutane” alijieleza Peter wakati binti Husna anajitawala katika kitanda kilichokuwa pale ndani kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

    “Nimekaribia” alijibu binti Husna huku akijiondoa kinguo alichokuwa amejitanda na kubakia na sidiria pekee katika upande wa kifua chake. Chini kanga moja ikaendelea kutesa

    “Hauhisi joto na hayo manguo yote Peter jamani nakuonea huruma mie hebu yavue na uzime taa inaongeza joto…na vile sipendi kiyoyozi mie basi tabu” alipokuwa tayari ameondoa nguo yake ya juu dada huyu alimwambia Peter maneno hayo huku bila hiyana akimsogelea na kuanza kumwondoa tai kisha kumfungua vishikizo vya shati yake kimoja hadi kingine na huku akitumia kucha zake ndefu kuchomachoma kifua cha Peter ambaye mapigo ya moyo yalikuwa juu sana na hakuna alichoweza kuongea wala kufanya pingamizi la aina yoyote hadi alipoachwa kifua wazi kabisa.

    Khanga nyepesi kabisa aliyokuwa amevaa mwanadada huyu na jinsi alivyokuwa anakaa hovyo hovyo, mapaja yakachungulia nje. Mapaja ya kuvutia sana. Hayakuwa tepetepe bali magumu na yasiyokuwa na misuli kama mkimbia riadha hali hii ilisababisha tamaa kumjia Peter kwa kasi mno, ujasiri ukamwingia ghafla akawa amemzoea binti yule mbele yake ambaye wamejuana kupitia mtandao wa kijamii wa facebook.

    Pasipo kusita Peter kama vile ametumwa baada ya kuzima taa alimvagaa na kuanza kumpiga mabusu huku na yeye binti akimtekenya hapa na pale Peter hadi akawa hoi. Ile hali ya kuwa hoi Peter hakuwahi kukutana nayo kabla. Alizoea kuwavagaa tu wasichana na kumaliza haja zake sasa leo alikuwa amekutana na jambo geni kabisa. Mara ulimi upenye katika sikio lake. Anakakamaa kama anakata roho!! Mara kucha zizame katika mbavu zake anaruka kama amepigwa shoti!! Mara ulimi unahamia karika shingo yake na meno ya kichokozi yanamg’ata kimapenzi anazizima kama anayeimba wimbo wa taifa. Akiwa hajakaa sawa mara binti anapenyeza mikono huku na huko Peter anapiga mayowe bila kujitambua. Hatimaye Peter akawa hoi. Hakuna alichotaka kingine. Sasa alihitaji tendo kwani yule binti angeendelea kidogo tu basi Peter na ujanja wake angejikuta akiwapa kazi wahudumu kufua mashuka siku inayofuata!!!

    Peter akajikakamua hatimaye binti chini mjanja wa mjini juu yake!!!

    “Please no no no no Peter usitake kunikera unaniaminije na mimi nakuamini vipi?” aliuliza swali la maana sana binti ambalo lilimfadhaisha sana Peter kwani licha ya kupenda kufanya mambo yake kwa uhakika leo hii alikuwa amesahau kuingia na kinga kwa ajili ya kutetea afya yake. Maajabu!!

    “Aaah!! Samahani baby nimejisahau likini mimi nakuamini wewe asilimia zote Husna” aliongea Peter maneno ambayo kiasi flani ni ucheshi kwani hajawahi kumwona binti huyo lakini anasema anamuamini asilimia mia(haka kamchezo bana hakana mjanja).

    “Kama waniamini hata mimi najiamini lakini naogopa mimba!!” alidai binti yule

    “Nilishakwambia mpango wangu ni kukuoa sasa unahofia kitu gani tena mimi nafanya kazi na nitakuhudumia mpaka unajifungua” alidanganya Peter ili aweze tu kupewa anachotaka” ukiwa

    “Hapana kwa leo mpenzi tutumie kinga” alisisitiza

    “Haya sipendi kukukera baby wangu kwa hiyo nifate hapo dukani!!” aliuliza Peter wakati jibu alikuwa nalo.

    “Samahani kabla haujaenda ni aina gani ya Condom tafadhali”

    “Salama condom, salama studs, salama tatu bomba, dume, yaani yoyote tu!! Au vipi” alijibu bila wasiwasi Peter.huku akiwa wima yeye na miguu yake yote mitatu wima !!!

    “Whaaaaat!!! Yaani unasema yoyote tu!! Unanichukuliaje mimi unadhani na mimi ni wa uswahilini, hapana huo uchafu hauingii katika mwili wangu nasema..kama umenidharau kiasi hicho naomba niondoke.” Alikuwa mkali ghafla yule binti. Maajabu !! mara akaanza kujiliza. Peter akaenda kumbembeleza.

    “Eeh!! Jamani Husna kwani ni ipi unayotaka? Mpenzi wangu..niambie basi baby wangu !!”

    “KAMASUTRA HIGH QUALITY CONDOMS peke yake ndio naweza kutumia (msomaji hiyo ni aina ya Condom inauzwa mara nyingi katika Supermarket shilingi nyingi tu za kitanzania na kawaida unakuta zipo mbili) sio nyingine” alijibu kwa mashauzi makubwa dada yule huku akiirekebisha weaving yake kichwani. Iliu menza kuvurugika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Peter mdomo wazi kama toto dogo likiwa limejikojolea !! hajui aina hiyo ya Condom. Hata baadhi ya wasomaji hawaijui. Zetu Salama tatu bomba na Dume huku g wawawa kavukavu biula soksi.

    “Ok! Nitaenda kuchukua kwenye gari yangu nilinunua kwa ajili yako nisubiri” aliaga binti yule na kutoweka akimwacha Peter akiwa na hamu kubwa ya kumfaidi. Peter bado matamanio yalikuwa juu sana !!

    “Dah! Facebook imenipa binti mrembo kiasi hichi mh!! Yaani ikifungwa nitaumia sana moyoni na maisha nitaona kama hayaendi…kiulainii najilia vilivyo bora Peter mimi!!” Peter alikuwa anajiongelea wakati huo akiwa tayari uchi wa mnyama akimsubiri Husna na hizo Kamasutra zake.

    Baada ya kama dakika saba alisikia mlango unafunguliwa.

    “Umerejea Husna wangu!!!” alihoji Peter lakini hakujibiwa na badala yake akaja kutanabai tayari alikuwepo mtu kifuani kwake, kwa hisia za kimwili alikuwa uchi wa mnyama,Peter hakuwa na hiyana kwa hamu alizokuwa nazo akaanza shughuli na cha kushangaza hakukumbuka hata kuulizia condom iliyokuwa imefuatwa. Otokali sa ua jinsia ya kike lilikuwa limeufunga ubongo wa Peter.

    “Mh! Kuna watu humu duniani wazito jamani amakweli usipime uhondo wa kitabu kwa kuangalia kava…” alijiwazia Peter alipousikia uzito wa yule binti. Lakini hakupoteza muda zaidi wa kujali ule uzito. Sasa alikuwa amepania kumkomesha!!!

    Peter hakujali kuwa ametumia Condom au hapana alijisikia faraja na raha tele kufanya mapenzi na Husna,walikuwa katika giza lakini alikuwa tayari ana picha ya mrembo matata aliyekuwa amemwona pale nje wakati anaingia hadi akaingia ndani, mapozi yake aliyoyafanya pale ndani yalimzidishia Peter hamu huku kumbukumbu za kucha zilizomfinya finya wakati alipokuwa anavuliwa nguo zikimfanya amng’ang’anie bila kuwa na wazo la kumuachia bila kuwa na wazo lolote la kumuachia Peter alipata raha isiyo kifani.

    Dhambi ya asili!!



    * * *



    Malezi aliyoyakosa kwa mzazi wake wa kike (mama yake), tangu akiwa na miaka mitatu, udhalilishaji aliofanyiwa baba yake kutokana na kuombaomba hapa na pale ili aweze kupata japo chakula cha kumkimu yeye. Na kubwa zaidi ilikuwa kumbukumbu mbaya ya kifo cha baba yake kwa kupigwa mawe baada ya kusingiziwa kuwa ameiba kuku ya jirani yake jambo ambalo halikuwa kweli hata kidogo. Picha hiyo kamwe aikufuti kichwan kake. Kila alipokuwa na akili zake timamu.

    Ni masumbufu hayo yaliyompelekea binti mrembo wa wastani kwa jina Mwamvua kuamua rasmi kuingia katika maisha ambayo hakuyategemea maisha ya kujiachia kwa lolote jambo ili aweze kupata pesa kidogo kwa ajiri ya chakula.

    Alianza kwa kuwa anaosha vyombo katika migahawa, mara kufua nguo za wanachuo katika hosteli mbalimbali jijini Dar es salaam, akatembeza karanga, maji ya kufunga kwenye mifuko. Alilala nje, alilala mitaroni, alipigana sana na watoto wenzake. Hadi akakomaa kabla ya wakati na akaanza kufanya mapenzi. Anakumbuku bikra yake ilitolewa katika choo cha kulipia usiku wa manane.dio alipiga kelele sana. Lakini tatizo pale palikuwa ni Kariakoo. Nani angejali???

    Maisha akaendelea.sasa alikuwa hana tena cha kuogopa.

    Akaamua ule upenyo uwe biashara. Kwa kuwa alikuwa mrembo.biashara ikawa inamlipa.

    Kujiuza aliifanya kama kazi yake kama vile imehalalishwa,aliifanya mchana na hata usiku hakuofia hata kidogo kusemwa na watu pale mtaani. Na hata wao pia walimtambua, matumizi ya madawa ya kulevya yaliiharibu kabisa akili yake na kuondoa aibu yote kichwani mwake. Mwamvua hakujijari hata kidogo kwani hakujaliwa na mtu yeyote tangu akiwa mtoto mdogo.

    Alikuwa ni Mwamvua huyu huyu aliyekuwa mmoja kati ya watu wachache katika eneo la Kinondoni ambao hawakumuhofia Husna na visa vyake kwani hata yeye pia maisha yalikuwa yamemuwia magumu hivyo kwa namna yoyote ile angeweza kupambana na Husna kama ungetokea mtafaruku wowote lakini kwa bahati nzuri hawakuwahi kugombana.



    Katika siku hii Mwamvua akiwa ametoka katika kijiwe kimoja kujidunga madawa ya kulevya alikutana na Husna katika hali isiyokuwa ya kawaida,bila kuficha chochote kwani hakuwa na mbinu nyingine ya ziada ya kuweza kukutana na Peter katika njia ya amani ambayo itamridhisha hisia zake zilizokuwa zinamsumbua kwa majuma kadhaa sasa.

    “Husna hilo mbona suala dogo sana dada yangu,yaani ndio umeumia hivyo na kuishiwa raha kabisa” Mwamvua alimwambia Husna baada ya kumaliza kutoa maelezo

    “Sasa nitafanyaje ndugu yangu na muda ndio huo unawadia sijui bado masaa mangapi”

    “Una pesa ya mafuta??”

    “Kama shilingi ngapi vile Mwamvua eeh1!!” aliuliza kwa shauku kubwa Husna.

    “Elfu kumi hivi inatosha si unajua yanabakia na mafuta kidogo ya kwangu kuingilia katika biashara yangu” alijieleza Mwamvua.

    “Inapatikana hiyo bila wasiwasi sasa tunafanyaje mpango mzima??”

    “We ni mjanja sana lakini kwa hili lazima uwe mpole sana unisikilize mimi mwalimu wa haya mambo” Mwamvua alijieleza kwa majigambo kiasi fulani na kweli ilibidi Husna awe mpole sana hadi alipopewa maelekezo yote naye akafuata



    Mida ya saa moja usiku tayari Husna alikuwa ndani ya gari pamoja na Mwamvua katika siti mbili za nyuma na aliyekuwa anaendesha alikuwa ni mzee mmoja wa makamo ambaye safari nzima alikuwa kimya sana hadi walipokaribia katika hoteli ya Lamada ndipo akampisha Mwamvua akaukamata usukani na kumalizia safari.

    “Sasa wewe tulia mimi nikaanzishe mchezo kazi yako wewe kumalizia tu sawa,haya baki hapa na dereva,na wewe mbaba usije ukaleta longolongo kwa dada yangu maana Na wewe huna dogo” Mwamvua alitoa maelekezo hayo kwa Husna pamoja na dereva huku akiondoka kwa madaha na mkononi akiwa ameikamatilia simu aina ya Iphone ndani yake pakiwa na Line ya Husna tayari kwa shughuli ambayo kwake aliamini ni ndogo na ya dakika chache sana.

    Husna alikuwa amepooza bila papara zozote akisubiri komando Mwamvua afanye mambo.

    Baada ya dakika kama thelathini Mwamvua alirejea, akiwa hana wasiwasi wowote, akamvuta Husna akatoka nje.

    “He! Dereva yuko wapi tena!!!”alihoji Mwamvua

    “Nimembutua huko ananiletea upuuzi wa kuniita mi mbaya hivi hanijui eeh!!” alijibu Husna akiwa amekunja sura. Hali hii ilimfanya awe mbaya zaidi.

    “He!! Sasa tunarudije nyumbani leo,si…..”

    “Nimemnyang’anya mapema tu mbona!!” alijibu kwa jeuri Husna hata kabla Mwamvua hajamaliza kuzungumza.

    “Kama unao funguo hakuna ubaya kamanda wangu sasa sikiliza tayari mambo yote huko ndani na taa nimezimisha tayari ni wewe tu usimsemeshe we mvagae umalize haja zako..ametepeta hana akili tena pale…tafadhali usiongee lolote, usiogope!! Fanya kweli” alitoa maelezo hayo Mwamnvua na bila kusita Husna akiwa ndani ya khanga moja alijongea katika chumba alichokuwa ameelekezwa na Mwamvua.

    Kimavazi alifanana kabisa na Mwamvua kasoro umbo tu!! Ndio wote walikuwa wa miili mikubwa lakini kasoro ilikuwa moja tu Mwamvua alikuwa mrembo!!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * *



    Peter akiwa bado anaufurahia uhondo wa penzi la Husna pale ndani mara ghafla alisukumwa pembeni baada ya kuwa amemng’ang’ania Husna kwa muda mrefu kisha Husna akatoka nje mbio mbio akimwacha Peter peke yake pale ndani akibaki anashangaa na asijue la kufanya. Hata hivyo hamu ilishaisha tayari. Huo ndio ubaya wa wanaume!!!

    Peter alitegemea kuwa huenda Husna ameondoka na atarejea tena lakini pia hakuwa na hofu hata kama asingerejea kwani tayari hamu ya kwanza ilikuwa imeisha na ilichukua dakika kadhaa kuitafuta tena. Peter akiwa bado anasubiri pale ndani mara simu yake ilitoa mlio ulioashiria kuwa kuna ujumbe umeingia kwenye simu yake

    “Peter siamini kama tumefanya bila kondom mwenzio sijawahi hata siku moja maishani mwangu na nilikwambia kabla” ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Husna.

    “Aah! Shauri zake bana kwani nilimlazimisha kuja?? huyu anataka kuniuzia mimba isiyokuwa yangu kirahisirahisi kwanza yeye motto wa kizito akipata hiyo mimba anatoa fasta tu” alijipa ujasiri huo Peter na kuamua kuacha kumjibu Husna ujumbe wake.

    “Mimi ndio kidume bwana unajidai matawi ya juu haya sasa hiyo laki na nusu iko wapi,yaani kilaini nimemchinja mtoto wa kike na maringo yake yote nimejimegea kiulaini kabisa mi ndio Peter kidume wa ukweli, na akijichanganya mara ya pili nampeleka guest za buku tatu Kigogo…kumbe mtoto laini kabisa…ila mzito huyo!!” alijitamba

    Peter akiwa peke yake akivaa nguo zake.



    * * *



    Husna alikuwa hana utani hata kidogo alipopata hofu juu ya kufanya mapenzi bila kutumia kinga ndani ya muda mfupi mtoto wa kike akajitambua kuwa tayari ameshika ujauzito, hakushtuka sana japo alipata mawazo yaliyomchanganya kidogo. Je Peter atakubaliana na ujauzito ule??? Ndio lilikuwa swali kuu kichwani mwake.

    “Yaani amkatae mtoto wake heeee!! Ndio atanijua mimi Husna ni nani na kwa nini sipendeki hapa mtaani” alijipa moyo Husna akiwa kitandani kwake siku tatu baada ya kugundua kuwa yu mjamzito.



    Tabia yake ya kuchat katika mtandao iliendelea kama kawaida lakini kila alipomtumia ujumbe Peter hakuwa akimjibu wakati alishuhudia akitoa maoni (Comments) yake katika status za watu wengine mara kwa mara.

    “Peter hivi ni kwa nini hutaki kuonyesha ushirikiano kwangu tangu nikubali kukupa mwili wangu, kwa nini Peter unanifanyia hivi unakuwa binadamu wa aina gani wewe lakini usiyekuwa na shukrani wala huruma kwa binadamu mwenzako? Kwa nini haukujali thamani ya mwili wangu?? Kwa hiyo nilikuwa mjinga kujitoa kwako eeh!! Haya endelea na ukimya wako lakini tambua kuwa nina mimba yako ulinipa siku ile pale Lamada asante” Husna alimwandikia ujumbe mrefu Peter bila kujalisha aidha ataujibu ujumbe ule au la alichoamini ni kwamba ameupata na ameuelewa.

    Ni kweli Peter aliupata ujumbe ule!!

    Jasho jembamba lilimtoka Peter hakuamini alichokisoma kutoka kwa Husna.



    “Mh!! Mimba mapema hivi, hee!! Halafu nipo shule dah! Nikimuendekeza huyu mtoto anaweza kuniharibia shuleni huyu. Halafu maskani sitaeleweka kabisa na mama anaweza hata kupoteza uhai akisikia sisomi tena” aliwaza hayo Peter huku akiwa bado anaitazama meseji aliyotumiwa.

    “Hapa natakiwa kufanya maamuzi magumu sana ya kujiondoa katika mtandao ili kumkwepa huyu binti, kwani facebook kitu gani bwana najiondoa tu,huu msala ukiisha narudi hii facebook ipo tu!!



    * * *



    Zilikuwa zimepita wiki nne tangu Peter aamue rasmi kujiweka mbali na Husna. Alikuwa amebadilisha namba yake ya simu huku akiwa anaiweka mara chache sana kila anapotaka kuongea na mama yake au ndugu wengine kijijini kwenye mtandao wa facebook ndio alikuwa ameamua kujitoa kabisa. Ilimradi tu kumkwepa Husna na mimba yake.

    .Ilikuwa ni siku ya jumatano akiwa amerejea kutoka shuleni na kuingia katika chumba chake, siku hii aliamua kuiweka laini yake aliyokuwa ameihifadhi siku nyingi bila kuitumia, hazikupita dakika mbili mara simu yake ikaingia ujumbe.

    “Mambo vipi wewe mbona umeuchuna sana siku hizi?? Hata kwenye usokitabu (facebook) huonekani kabisa mtu wangu au umejitoa nini??” ilikuwa meseji kutoka katika namba iliyohifadhiwa kwa jina Asha Scooby. Peter alikuwa anamfahamu!!!

    Palepale bila kupoteza muda kwa papara zake za kupenda wasichana aliangalia salio na kugundua kuwa ana kama shilingi mia tano katika simu yake akaamua kumpigia Asha.

    “Asha mambo vipi habari za siku nyingi dah!! Tangu siku ile unirushe pale saluni hadi leo dah!! Vipi lakini” alianza kuongea Peter.

    “Aah!! Kaka siku ile simu yangu ilizimika si unajua mambo ya chaji tena na umeme wetu huu wa hapa bongo..nisamehe lakini mkali wangu” alijibu kwa mbwembwe binti yule kutoka upande wa pili.

    “Poa nipe story nyingine mbona hauonekani katika mtandao lakini?” aliendelea dada yule.

    “Aah!! Kazi zinanibana sana lakini hivi karibuni nitarejea..nimeamua kujipumzisha kidogo si unajua tena majuku..tunategemewa wengine”

    “Haya mkaka mimi kesho naingia pande za kigogo hapo kwa dada yangu hivi ndio kitaa chako eeh!! Au we unakaa wapi??” ilihoji sauti ile kwa pozi.

    “Kama kawaida ndio hapo hapo napatikana kesho nzima nitakuwepo kama unakuja uje kweli usinirushe kama siku ile mrembo..ukiulizia raisi wa Kigogo utaelekezwa kwangu usiache aisee” alijieleza Peter. Akijisifia kwa upande mwingine.

    “Hamna sasa hivi simu yangu iko full machaji na makila kitu usiogope mkaka wa ukweli” ilisisitiza sauti ile ambayo Peter aliamini ni ya Asha.

    “Basi mimi nitakusubiri kwa hamu kubwa Asha” alimaliza maongezi Peter na kumuaga Asha huku tayari akiwa ametawaliwa na furaha. Tamaa kama kawaida yake!!

    “Na huyu nae akijichanganya napiga kama kawaida halafu nampotezea kama Husna, kwani Husna ameishia wapi na mbwembwe zake za kutisha sembuse huyu!!! Ooh!! Nina mimba sijui hatukutumia kinga …hiyo mimba anataka niichukue mimi au?? Chizi kweli..hivi kumbe na watoto wa kishua wanakuwa machizi hivi…” alijipa kichwa Peter na kujiona kidume hasa hasa.

    Siku iliyofuata majira ya saa sita mchana tayari Peter alikuwa amjiegesha katika katika mgahawa uliokuwa na wateja wachache kabisa ili aweze kupata fursa nzuri ya kukutana na Asha. Mfukoni alikuwa amejiweka tayari kwa lolote.



    * * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Husna alikuwa amekerwa na ukimya uliokuwa unafanywa na Peter na sasa baada ya mwezi mzima kuwa umepita aliamua kuingia rasmi katika mapambano makali na Peter.

    “Nilimfahamu kabla hajanifahamu, nimefanya naye mapenzi bila yeye kugundua leo hii anajidai mjanja nitamuonyesha mimi ni nani hana ujanja wowote wa kunizidi mimi hata kwa mbali shenzi zake.” Alijihakikishia Husna huku akinyanyua simu yake akaitoa laini yake ya kawaida na kuipachika ile aliyoitumia kuongea na Peter huku akijifanya kuwa yeye ni Asha Scooby.

    “Yaani akiipata meseji hii hapa lazima achanganyikiwe nimeshagundua ana papara sana huyu mkaka lakini mimi ndio nimependa tayari na lazima na yeye anipende kwa sababu tayari nina mtoto wake tumboni hana ujanja” wakati anautuma ujumbe ule Husna alijipa matumaini hayo na hakuwa amekosea kwani baada ya masaa kadhaa mbele alipokea simu kutoka kwa Peter. Karata sahihi kabisa.

    “Tayari kaipata meseji na amejileta kwenye mkenge mwenyewe” alisema Husna kabla hajapokea simu ile kutoka kwa Peter.

    Kama kawaida yake alimchangamkia Peter kwa sauti ileile aliyotumia siku alipomzuga Peter kuwa yeye ni Asha wa facebook. Bila kugundua kuwa anadanganywa Peter wa watu alikubali haraka haraka na kujua ni bahati nyingine inakuja mbele yake tena kwa bei rahisi.

    Laiti kama angejua anazungumza na Husna!!!!........



    Husna hakuwa na uoga tena na wakati huu hakuhitaji msaada kutoka kwa Mwamvua kwani aliamini hata akiwa mwenyewe mtihani huu angeuweza.

    Majira ya saa tano asubuhi Husna tayari alikuwa ameshuka kutoka katika daladala aliyokuwa amepanda kutokea Kinondoni kuelekea pale Kigogo.

    “Aliniambia Mini Best Bite eeh!! Yeah!! Bango lake hilo hapo afadhali” alisema kimoyomoyo Husna huku akiipata furaha kubwa moyoni mwake kwani alijua angepoteza muda mwingi sana kuitafuta sehemu hiyo.

    Takribani mita miambili mbele alifanikiwa kuona sehemu hiyo aliyoelekezwa, ilikuwa na madhari mazuri kiasi chake kutokana na mtaa wa Kigogo ulivyo.

    Hapakuwa na kelele sana zaidi ya muziki uliokuwa katika sauti ya wastani tu ukitambaa eneo lile kuwaburudisha wateja ambao wengi wao walikuwa wanakunywa pombe na wachache sana walijidunga soda.

    Husna alichukua nafasi yake pembezoni kabisa mwa eneo la ndani la mahali hapo na kuagiza maji ya kunywa madogo ambayo aliyafungua na kuanza kunywa.

    “Habari dada yangu” alisalimiwa Husna na muhudumu wa pale ndani

    “Poa tu vipi??”

    “Salama tu!! Tukuhudumie nini jikoni” aliuliza muhudumu yule huku akiikunjakunja mikono yake.

    “Kuna mbuzi……”

    “Ndio anapatikana wa kuchoma, mchemsho ama..….nikutengenezee kiasi gani dada”

    “Hee!! Wewe mbona unajiwahi hivyo mimi nimeulizia kama yupo, jibu ndio au hapana mambo ya unitengenezee kiasi gani baadae nitasema mimi” alijibu Husna huku akimkazia macho yule dada.

    “Samahani dada eeh!! Kwa hiyo tutengeneze kiasi gani labda”

    “Ushanichefua nipishe nitakuita baadae” alimaliza mazungumzo Husna na kuanza kubonyeza simu yake bila sababu za maana, muhudumu akiwa haamini alichokisikia alijiondokea zake kwa aibu.

    Husna alikuwa tatizo !!!



    * * *



    Tangu afike pale majira ya saa sita alisubiri kwa masaa mawili hadi saa nane bila dalili za mtu yeyote kufika pale hadi alipopokea ujumbe kutoka kwa Asha kuwa hatafika eneo lile kwani mama yake ameugua ghafla.

    “Aaah!! Shiiiit!! Upuuzi huu sasa nimejipanga muda wote huo halafu hajaja, hapana siwezi kutoka hapa hivi hivi ngoja nitafute wa kupumzikia kwa leo” aliwaza Peter baada ya kupokea ujumbe ule wa Asha.

    “Yes yes yes….ngoja nimwite Lucia yule pale dakika mbili tu amefika na anavyopenda ngono yule sasa hivi ndani ya nyumba kidume najichinjia mtoto mtamu kabisa” alipata jibu la wazo lake Peter na punde tu alituma ujumbe ambao jibu lake lilikuwa furaha kwake.

    Kama alivyotaraji ndani ya saa zima aliingia binti aliyemtegemea wakakumbatiana kisha wakakaa na kumuita muhudumu aweze kutoa huduma kwa binti huyo.

    Mapozi waliyokaa wawili hawa hayakuhitaji ushahidi wa chumbani kujua hawa ni wapenzi tena wazoefu sana mara binti alimshika kidevu Peter mara ampige vikofi vya kizushi na mengineyo mengi wanayofanya wapenzi walioshibana na wa siku nyingi.

    Muhudumu kama alivyoagizwa alipeleka huduma kwa binti yule.

    “Peter ngoja niende uani mume wangu halafu tuondoke jamani pameanza kuniboa hapa” Lucia alimwambia Peter ambaye bila kikwazo alimkubalia. Tayari walikuwa wamemaliza vinywaji vyao.

    Wakati wawili hawa wakionyeshana mapenzi ya hapa na pale. Watu baadhi wasiokuwa na shughuli za kufanya walikuwa wanawatazama, aidha kwa matamanio ama kwa dharau kwa jinsi wanavyovunja tamaduni za kitanzania. Ni mtu mmoja tu ambaye kazi yake yeye ilikuwa kuwatazama wawili hawa. Japokuwa ilikuwa ni kazi yake lakini alikuwa anaumizwa sana. Kazi sasa akaanza kuiona ngumu. Huyu alikuwa ni Husna

    Maneno aliyoongea Lucia yalimfikia Husna pale alipokuwa hata kabla ya wenyewe kuingia tayari alikuwa ameagiza wali na alikuwa ameumaliza kwani ni muda mrefu sikio lake lilikwepa mawimbi ya muziki na kupokea kwa uzuri kabisa mawimbi nyororo ya sauti za wawili hawa (Peter na Lucia). Akili ya Husna ilikuwa inafanya kazi kwa kasi sana alihisi asipokuwa makini ataibiwa mpenzi wake na ilikuwa lazima kufanya jambo lolote ilimradi amlinde mume wake huyo ambaye alitaka kujaribu kumkwepa.

    “Huyu mshenzi anaweza kuniibia hivi hivi na ni suala la aibu sana mimi kuibiwa mbele ya macho yangu yaani ni aibu kwangu na kwa huyu mtoto niliyembeba humu tumboni haiwezekani huko huko anapoenda tunamalizana, kumshikashika kote kule bado hajaridhika hapana imetosha kwa kweli” aliongea kwa sauti ya chini Husna huku hasira ikimkaba kooni. Haraka haraka aliposikia yule binti anaaga kwenda chooni na yeye alienda huko huko baada ya sekunde kadhaa na mahesabu yake yalienda sawia kabisa,akiwa ameshika simu yake akibonyeza hapa na pale bila kuangalia mbele lakini alijua wapi anapoenda ndio akakutana na yule dada (Lucia) kwa upande wa Lucia ilikuwa bahati mbaya wakati kwa Husna ilikuwa makusudi kabisa kugongana na yule binti

    “He! We vipi mbona umenigonga yaani unatembea hata hauangalii mbele ona sasa” aligomba Lucia baada ya kugongana na Husna

    “We Malaya vipi wewe, yaani unajitembeza vibaya hapa unanigonga halafu unanikaripia, mshenzi mkubwa tena changudoa wa shilingi miambili wewe, mwanaizaya mkubwa” alilipuka kwa mvua ya matusi Husna, matusi ambayo yalisaidia kupunguza hasira zakekidogo. Lengo kuu likiwa kumhamasisha yule binti naye akasirike.

    Wakati huo bado walikuwa pale eneo la choo

    “Nini??? Unaniita Malaya unanijua vizuri wewe ngoja nikufunze adabu yako sasa.” Alijibu kiubabe Lucia huku akionekana dhahiri kuwa yupo tayari kwa shari yoyote, kwa Husna ilikuwa kama sherehe kwa ni ugomvi na matusi vilikuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku.

    “Saaafiii!!! Amejiingiza ninapotaka sasa na nilivyo na hasira haki ya mama yangu aliyenizaa namchakaza huyu kiumbe na huyo Malaya wake nahakikisha hawaendelei tena na hizo starehe zao lazima nipiganie penzi langu” aliwaza Husna huku akisubiri Lucia ajilete mbele yake.

    Wakati Lucia anajiandaa kumkabili Husna mara ghafla alishtushwa na kufadhaishwa na kitendo cha Husna kumuunganisha mikono yote miwili kwa kutumia mkono wake mmoja wa kuume alijaribu kufurukuta lakini hakuweza kujinasua, mikono aliyokutana nayo ilikuwa imara sana, kisha Husna akachota maji yaliyokuwa maalum kwa ajiri ya huduma za bafu na choo maji na kummwagia mwilini…Lucia akapiga yowe la hofu, nguo zake zikawa tepetepe,pozi likamwishia Lucia akabaki ameduwaa, hakuamini kinachotokea wakati Husna aliondoka kwa kasi eneo lile akimwacha Lucia kidomodomo kikiwa kimemuisha kwani hakuwa na la kufanya Husna alikuwa mbabe zaidi yake

    "Ukome waume wa watu malaya wewe na ole wako nikufumanie tena.." Husna alibwatuka kwa ghadhabu wakati anatoweka. Lucia hakujibu chochote alikuwa anatetemeka kwa aibu aliyokuwa ameipata.

    Kama vile mtoto yatima. Alijongea hadi pale alipomwacha Peter.

    "Lucia nini kimekusibu malaika wangu" Peter alimpokea Lucia kwa bumbuwazi hilo aliporejea pale akiwa kama kituko amelowana mwili mzima

    "Nani malaika wako,naomba hela ya kupanda teksi nirudi kwetu sasa hivi! No diskasheni" alijibu kwa ukali Lucia huku akiwa hana hata chembe ya tabasamu,uso wake ulikuwa umejikunja sana kwa hasira na aibu

    "Kwani kuna nini jamani"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nenda ukamuulize mkeo hilo swali mimi sina jibu la kukupa mwanaume mzima unachungwachungwa na hawara zako nyoo!" aliendelea kujibu kwa jazba Lucia. Peter hakuwa na ujanja kwa kuepusha watu kujazana eneo lile alichomoa shilingi elfu kumi akamkabidhi Lucia ambaye alitoweka eneo lile huku dhahiri aibu ikiwa imemjaa usoni. Akachukua taksi akatoweka kuelekea napopajua mwenyewe.

    Kwa Husna ndio kwanza mchezo ulikuwa umeanza.

    "Na leo lazima nijue ni wapi we mshenzi unapoweka mgongo wako, nakwambia Peter mimi ndio Husna na nikisema utaoa ni kweli utaoa, yaani kirahisi rahisi unijaze mimba halafu uniache kwenye mataa hapana kwa kweli hapa nakomaa na wewe mwanzo mwisho" Husna alijiapiza hivyo macho yake yalipomwona Peter akiondoka eneo lile akiwa mnyonge kabisa. Husna kwa mbali alianza kumfatilia Peter aliyekuwa anaenda kwa mwendo wa miguu taratibu kabisa.



    Peter alikuwa ameitoa kwa uchungu sana shilingi elfu kumi yake kumpatia Lucia bila hata kulala naye kwa siku hiyo,na kabla ya kutoa pesa hiyo tayari alikuwa ametumia shilingi elfu kumi nyingine kwa malipo ya chakula na vinywaji walivyokuwa wamekunywa yeye pamoja na Lucia.

    "Dah! Buku teni imeondoka mfukoni hivi hivi huku inacheka mh! Inauma kudadeki,hapa naingia geto full kupiga usingizi hadi pakuche. Hiyo pesa bora ningenunua walau unga na dagaa vikae pale geto kwangu" aliwaza Peter huku akijikongoja kuelekea katika chumba alichokuwa amepanga maeneo flani katika mtaa wa kigogo,Peter alikuwa anapigia mahesabu pesa ambayo haipo tena mkononi mwake.

    "Sasa huyu Lucia naye amekuwaje? Mbona amerudi amelowana halafu anadai nimuulize mke wangu sasa yupi huyo tena amekuja kunipeperushia tetere wangu? ah! au......" Mawazo ya Peter yalikatishwa ghafla na macho yake kuona kwa mbali sura ambayo haikuwa ngeni machoni pake.

    "Mh! Nina bahati kweli ya kuonana na huyu dem sasa mara ya tatu,leo mkimya hana hata kasheshe loh! Kuna watu dunia si mchezo yaani mdada kama yule anakuwa mtu wa shari kiasi kile 'anyway' umbo lake linaruhusu maana Mungu akikuumba we mbaya lazima akupe na njia ya kuutetea ubaya wako...dah! Lakini cha kufurahisha na yeye hapo eti ana boyfriend halafu pia ataolewa na atazaa dah! wanaume bwana!! Yaani mimi hata kwa dawa yaaani hata kama napewa pesa silali chumba kimoja na kontena kama lile ..bora unipasue kichwa kwa hali ile" alimaliza Peter kwa kucheka huku akigonganisha mikono yake,macho yake yalikuwa hayajakosea alikuwa amemwona Husna msichana ambaye alikuwa amepata nafasi ya kumshuhudia katika fujo mara mbili. Husna alikuwa anatembea kwa mwendo wa taratibu sana akielekea mahali ambapo Peter naye alikuwa anaelekea lakini yeye Husna alikuwa kwa mbali.

    "Sijui nimpige tena picha niweke facebook? Mh! Lakini akigundua yanaweza kunikuta nikaaibika mtoto wa kiume tena hapa mtaani kwetu wanavyonikubali itakuwa nuksi sana..kwanza likizo yangu ya facebook bado haijaisha.." alijiuliza na kupata muafaka Peter kisha akaamua kuachana na Husna na kuendelea na safari yake akaihifadhi simu yake aliyotaka kuitumia kumpiga picha.

    Peter alikiri kimya kimya kuwa hata yeye alikuwa anamuogopa yule binti!!



    *****



    Macho ya Husna yalikuwa chonjo sana yakifuatilia kila nyendo anayopitia Peter kwa umakini kabisa bila kupoteza hata sekunde tatu kukwepesha Husna alimshuhudia Peter alipogeuza shingo mara mbili kumwangalia na kuwa kama amemfananisha,kwa umakini bila kugundulika alipunguza mwendo na kujifanya amepokea simu ambayo hata ilikuwa haijapigwa.

    Lengo la Husna lilikuwa kujua mahali ambapo Peter anaishi ili aweze kuanzisha vita rasmi na baba wa mtoto aliyetegemea kuzaliwa baada ya miezi kadhaa, baba huyo akuwa mwingine bali ni Peter huyohuyo. Peter siyejua lolote!!!

    Wakati akiwa na simu sikioni aliendelea kufuatilia hatua za bwana Peter kwa mbali kabisa hadi akafanikiwa kumwona akiingia katika geti la mbao, kwa spidi kali kama mgonjwa wa kuhara anavyowahi chooni kila anapohisi mambo kuharibika ndivyo Husna alivyowahi katika lile geti na kuweka jicho lake pale mlangoni bila uoga …."VAMPIRE" lilisomeka jina hilo lililoandikwa kwa kutumia chaki katika mlango wa chumba alichoingia Peter.

    "Hongera Husna nakukubali" alijisemea Husna huku akiubetua mdomo wake na kufanana na mkongwe wa muziki wa taarabu na ngoma za asili Bi.Kidude binti Baraka.

    Husna aliondoka kwa shangwe sana katika mtaa wa Kigogo pembeni kidogo ya kata ya Magomeni, hakika alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa ameshinda tena kwa kishindo michezo miwili kwanza alifanikiwa kumzuia Peter asimsaliti kwa binti waliyekuwa naye pale Bar na pili aliweza kutambua ni wapi Peter anaweka mgongo wake kila usiku.

    Ndani ya gari litokalo maeneo ya Buguruni Husna alikuwa amesimama akiwa na furaha tele na hata viti vilipobaki wazi hakutaka kukaa aliendelea kusimama hivyo hivyo hadi alipofika Kinondoni na kushuka baada ya kuwa amelipa nauli, tayari ilikuwa imetimu saa moja na nusu usiku.

    Hakuwepo wa kumuuliza kwanini amechelewa kurudi nyumbani kwani vituko vyake vilikuwa vimewashinda na walikuwa wamevizoea tayari. Mama mwenyewe hakuwa na hofu na mwanaye kwani aliamini hakuna mwanaume wa kumzuzua na katu hakuwahi kutegemea kusikia habari za Husna amekutwa na mwanaume mahala fulani!! Hata mama alitambua kuwa wanaume hutazama kitu gani hadi kufikia hatua ya kumsumbua msichana.

    Kama malkia vile Husna alijitawala na kuingia hadi chumbani kwake na kujitupia kitandani na baadaye kujiandaa na kuingia bafuni kuoga kisha akarejea tena kilichofuata akatoka nje na kuelekea dukani aliporejea alikuwa na kinywaji aina ya Sayona mkononi, moja kwa moja chumbani mwake alipoifungua na kujipongeza kwa ushindi wake wa ugenini. Siku hiyo usiku hakujumuika na familia kwa mlo wa usiku.

    "Sina kazi ya kufanya mie nitamfatilia hadi nimjue nje ndani mwanaume huyu, kama ni nauli ni bora nigharamike lakini Peter abaki kuwa wangu yaani ni hapo tu Kigogo haki ya Mungu mara tatu kila wiki nitakuwa nahudhuria Kigogo" alijiapiza Husna huku akinywa Sayona yake taratibu. Jeuri yake ilitokana na pesa alizokuwa akitumiwa na ndugu zake ambao kimaisha wapo juu kidogo.





    ***



    Peter aliendelea na tabia ya kuacha kujibu meseji zote za Husna pia hata simu yake hakuwa tayari kupokea. Tabia hìi iliendelea hadi Husna alipokoma kutuma meseji na kupiga simu.

    "Kwisha habari yake kumbe alikuwa ananizuga tu mimba ya wapi mbona yupo kimya sasa" aliwaza Peter baada ya kuona ukimya wa Husna unazidi katika simu yake pia katika mtandao wa kijamii wa facebook.



    Kama ilivyo starehe ya Peter, leo hii alikuwa mwenye furaha na alikuwa amesahau jinsi Lucia alivyopepea na kumwacha kwenye mataa. Sasa alikuwa na kifaa kipya kutoka Mwanza ambacho ndio kwanza kilikuwa kinasubiri siku kadhaa zipite kitimize mwezi mmoja jijini Dar.

    Huyu alikuwa ni Doreen, binti aliyekuwa ametoka jijini Mwanza na kuhamia Dar es salaam kimasomo.

    Ilimchukua Peter siku tano za wiki kumlaghai na kumwonyesha binti huyo raha ya jiji la Dar es salaam ambapo ndio alikuwa amekanyaga kwa mara ya kwanza tangu azaliwe. Mara Msasani Beach, Mlimani City, Coco Beach, Chuo kikuu cha Dar es salaam, na sehemu nyinginezo. Binti kachanganyikiwa akajiona yupo katika pepo na Peter ndiye malaika mlinzi wake. Sasa malaika na mtu wake walikuwa nyumba ya kulala wageni!!! Kiliwapeleka nini? Hayo walijua wao!!

    Malaika huyu kwa jina la Peter alidumu na furaha kwa dakika takribani thelathini kabla mambo hayajaharibika. Hali ikawa tete.

    Kelele zilisikika katika chumba namba 18 alichokuwa Peter na msichana wake wa siku hiyo.

    "Mh! Hivi ni hapa au?" Peter alimuuliza yule binti ambaye alikuwanaye pale ndani. Nani amjibu mwenzake wakati mlango umefungwa.

    "Mi sijui jamani" alijibu huku akiwa ameishikilia kanga yake vyema kifuani isidondoke. Nguo nyingine hazikuwa mwilini.

    Peter kwa haraka alikimbilia katika tundu dogo lililokuwa katika kitasa cha mlango wa chumba hicho. Akachungulia!!!

    "Mama yangu we naniii wewe njoo uone mh! Njoo haraka sijui ni nini leo ndio leo" aliongea kwa sauti ya chini Peter akimwambia binti waliyekuwa naye. Jasho jembamba lilikuwa linamtoka licha ya feni kuwa inapuliza pale ndani,taulo iliyokuwa katika kiuno chake tayari ilikuwa imeanguka na hakujua imeanguka saa ngapi........

    Peter uoga ulikuwa umemkumba katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu kama saba wa jinsia ya kike walikuwa wanapiga kelele kwa fujo pale mbele ya mlango wa chumba chake,akiwa bado haamini kuwa walikuwa wanamaanisha mlango wake mara mlango ulianza kugongwa si katika hali ya shwari bali shari tena shari kubwa sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Peter hakuelewa walitaka nini pale. Akawa anatetemeka, hisia za kufanya uzinzi zikawa zimetoweka tayari hakuwa na hamu tena, mapaja meupe ya msichana aliyekuwanae hapo chumbani hakuyatamani tena alimuona kama mikosi tena mikosi mikubwa kwake.

    "Umeangusha taulo Peter" binti yule alimwambia Peter aliyekuwa hajielewi bado. Haraka haraka aliinama akaikota taulo lakini hakuirudisha kiunoni bali aliitupia kitandani badala yake akachukua suruali yake akaivaa haraka haraka akawa amesahau kuvaa Boxer,yule binti naye akafanya hivyo hivyo,kisha kwa kutetemeka Peter akawa anauendea mlango

    “Umesahau kuvaa boxer baby!!” yule binti akamkumbusha Peter. Peter akageuza tena akataka kuvua suruali mara akataka kuvaa boxer juu ya suruali. Alikuwa amechanganyikiwa.

    Akaamua kuahirisha vyote akaificha boxer chini ya godoro!!! Akauendea mlango akafungua kidogo

    "Niwasaidie nini jamani!!..." alihoji Peter kwa wasiwasi huku akipepesa macho huku na huko, akiwa bado hata hajamaliza vizuri kuongea mara mmoja kati ya wanawake waliokuwa pale nje akausukuma mlango, Peter alipojaribu kumzuia na yeye alisukumwa kidogo aanguke akawahi kushika ukuta. Na kama vile msukumaji alijua kila kilichokuwa kinatendeka pale ndani alimvamia yule binti na kumbeba mzegamzega kama wafanyavyo wacheza mieleka. Akamsogeza nje, Peter alitaka kuingilia akakutana na jicho kali la mwanamama aliyemsukuma awali. Peter akaogopa!!!

    "Jamani ni nini kwani, kwani nimefanyaje…" aliuliza yule binti huku akiwa amebebwa juu juu.

    “Utaelewa tu si unataka majibu!!!” aliongea mwanamke mwingine huku akimdaka na kumweka chini

    "Mshenzi mkubwa tena mwendawazimu unajua tu kuchukua waume za watu sivyo utatueleza vizuri" alijibu kwa hasira mwanamke yule aliyekuwa amejazia mwili wake.

    "Mimi ni mgeni huku jamani!"

    "Mgeni! Eti unasema we mgeni, nyie ndio nilikuwa nawatafuta...sasa leo tunamalizana hata mimi nilikuaga mgeni" alidakia mwanamke mwingine huku akituliza kibao cha nguvu katika mgongo wa yule binti hadi akatoa kilio kikali kilichoashiria maumivu.

    Peter alikuwa ameduwaa tu hata asijue la kufanya wanawake wote mbele yake walikuwa wanasema yao tena kwa sauti ya juu huku wamemshikia viuno.

    Umati ulianza kuongezeka kwa kasi,tayari palihisiwa kuwa na fumanizi katika nyumba ile ya kulala wa wageni pale kigogo.

    Waswahili hawana dogo jamani!!!



    ***

    Husna alikuwa katika mizunguko ya hapa na pale katika mtaa wa Kigogo katika kutimiza wajibu wake wa kumpeleleza Peter mienendo yake na maisha yake kwa ujumla.

    Siku hii ilikuwa njema sana kwake kwani alifanikiwa kugundua kitu kingine kikubwa sana kuhusu Peter, macho yake kama kawaida yalikuwa yanaonyesha ushirikiano mkubwa sana katika msako huo kwani hayakumdanganya hata kidogo, ndani ya shati nyeupe ya mikono mirefu, tai ya bluu shingoni, suruali rangi ya bluu na kiatu cheusi ndio mavazi aliyokuwa amevaa kijana huyu aliyetelemka katika gari litokalo Mtongani kwenda Kawe katika kituo cha Kigogo au maarufu kama 'njia panda' laiti kama mavazi yake yangebaki kuwa hivyo basi angeweza kufanania na mfanyakazi wa benki ya Barclays ama hata diwani wa kata flani kijijini lakini muhuri uliokuwa katika shati lake uliosomeka Jitegemee Secondary School 'JKT' ulimshusha hadhi na heshima zote akabaki na jina la 'wakusoma' huyu alikuwa Peter akiwa ametoka shule kabla ya muda. Makubwa!!! Kumbe …kumbe…

    Peter alikuwa mwanafunzi!!!!

    "Dah! Mungu wangu kumbe ni kianafunzi! He! Watu wengine waongo jamani mh! Sasa hapo alinidanganya ili iweje!!!" aliduwaa Husna kwa sauti ya chini huku akimlaumu Peter kwa kuwa muongo na kujisahau kuwa yeye ndiye bingwa wa uongo.

    "Au ninamfananisha jamani!!" alijiuliza lakini hakuwa akimfananisha yule mbele ya macho yake alikuwa ni Peter mwenyewe.

    "Lakini jukumu langu ni kumfatilia huyu kiumbe hebu ngoja nitimize wajibu, awe mwanafunzi asiwe mwanafunzi huyu ndiye aliyenipa mimba na si mwinginealiapiza Husna huku akitafuta maficho ili aweze kumuona mume wake vizuri.

    Mara!!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "He! He! He! Peter mume wangu nani huyo uko nae tena jamani kwa nini unakuwa malaya kiasi hicho mume wangu jamani magonjwa jamani magonjwa Peter Wangu!!!" Husna alijikuta akilalamika mwenyewe baada ya kumuona Peter akiwa na msichana wanaongozana kuelekea pale anapoishi. Machozi yalimlenga!!!

    "Lazima nijue mwisho wao hawa he! Yaani mh!" aliongea Husna huku aking’ata kidole chake cha shahada

    Wivu ulichukua nafasi yake!!! Wivu kwa mtu asiyemtambua!!! Wivu kwa Peter

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog