Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?!
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Asha kufanya mazingaombwe yake na kuyayuka then kuibukia pale bustanini, alistaajabu kuona maiti mbili za walinzi na alipocheki kwa mbele alimuona Ninja kama yeye akisota mpelampela kuelekea usawa wa chumba kile cha Hussein bubu kwenye ghorofa la ile hoteli.
Alijua sasa tayari kumekucha, na kama ilivyokuwa kwenye mawazo yake kuwa mr X lazima kuna kipofu wake atamtumia kuja kufanya ile kazi baada ya yeye kuikataa na kujua kuwa amejua hadi kufikia kumzimia mitambo ya mawasiliano kati yao alijua sasa na yeye ni miongoni mwa adui wa mr X na yule Ninja katumwa kuja kufanya ile kazi akimaliza lazima atumwe kwake pia hivyo akaona ule ndio wasaa na kwakuwa amewahi lazima kapambane nae.
Aliruka beki kavu mfurulizo Lady Ninja Asha na kumzuia kwa mbele yule Ninja ambae nae alikuwa hajategemea ujio wake lakini alijua kuwa yule kaja kumzuia kufanya kazi muhimu aliyotumwa na hapo ndipo kasheshe likaanza.
"Wee ni Muasi, Lazima Ufe leo hapa hapa ni bora umejileta"
aliongea yule Ninja lakini Lady Ninja hajajibu chochote zaidi alianza kumshambulia kwa mateke ya angani mfurulizo hadi akaanza kumrudisha nyuma japo nae yule Ninja hakuwa wa mchezo.
Pambano lilikuwa kali sana na ikafika sasa Asha alikaribia kummudu yule Ninja lakini mara yule Ninja akabadili mapigo na kuanza kutumia 'Invisible Knifes'.
Ni visu special vidogo sana vya duara vyenye meno makubwa sita ambavyo hurushwa kwa uchawi wa kininja na kama huujui uchawi huo hata kidogo kamwe huwezi kukikwepa hata kimoja lakini uzuri japo Asha yeye hakuwa na vile visu lakini alikumbuka mafunzo aliyopata kwa yule babu wa kijapani kule India na maelekezo ya maneno ya kichawi anayopasa kutamka pindi anaporushiwa 'Invisible Knife' na Ninja yeyote na jinsi ya kuvikwepa.
Na ndivyo alivyofanya Asha kwa wepesi wa ajabu aliweza kuvikwepa kwepa vile visu kwa kubinuka binuka huku nae akijaribu kupeleka mashambulizi lakini kwa bahati mbaya kisu kimoja kilimpata mara baada ya yule Ninja kumzidi ujanja na kumuhadaa kwa kumtishia kisha akamtokea upande wa pili na kuvirusha vitatu kwa mpigo na hapo ndipo Lady Ninja Asha alishindwa kuvikwepa vyote.
"Hhahahahahahaha"
kilisikika kicheko cha yule Ninja na kuendelea na pambano huku Lady Ninja akiwa na maumivu makali sehemu za chini ya tumbo kutokana na kunasiwa na kile kisu lakini alijitahidi kupambana ili kumzuia yule Ninja asiende kumuua babaake.
Alizidi kuelemewa Asha na yule Ninja kibaraka wa mr X hasa kutokana na kutoneshwa palepale na yule Ninja na kuzidi kukisukumia ndani ya nyama zake za tumbo kile kisu kidogo kilichonasia na hatimae Lady Ninja alikosa kabisa nguvu na kuanguka chini.
"Hahahahahaaa 9121 Lady Ninja, sikuwahi kutegemea kama utakuja kuwa msariti kiasi hiki."
Alicheka kwa dharau yule Ninja na kuongea kwa uchungu huku akimsogelea taratibu Asha pale alipoanguka.
"Wewe ni kipofu uliye kwenye Mchezo wa Mr X hujui ukweli wowote, kama unaniua tafadhali Niue mimi tu lakini si babaangu, tafadhali huyo uliyetumwa kumuua ni babaangu tafadhali sana badala yake niue mimi"
aliongea huku akisota sota kurudi nyuma Lady Ninja Asha hakuwa na ujanja wowote, maumivu yalimzidia hakuweza kupambana tena, alikuwa tayari kufa yeye lakini si babaake aliyemjua siku moja tu kabla ya matatizo yote yale.
"Aaaahaaa, vizuri sana kumbe ni babaako hahahahaha yaani hata kama isingekuwa amri ya mr X lakini kwa vile nimejua babaako basi lazima ningemuua tu, na Nitamuua ila kwanza naanza na wewe"
alijibu yule Ninja mara baada ya kusikia kumbe Hussein bubu aliyetumwa akamuue ni baba wa Lady Ninja.
"Lakini mbona unataka kufanya unyama kwa mzazi wangu ambae hana hata muda toka arudi Uraiani? mbona huna huruma wewe...! hebu fanya ingekuwa mzazi wako wewe ungejisikiaje?"
"Ahaaaaa Umeongea vizuri sana Lady Ninja, wewe ni mtoto mdogo kwenye vita vya wanaume lazima utoe mikojo... Umeongea vizuri sana, labda nataka ukumbuke vile ulivyoasi na kumuua babaangu. Ulitegemea na wewe babaako atabaki mzima? Laiti ningejua kama mtoto ninayempa msaada siku zile ndie atayekuja kumuua babaangu basi ningekuua palepale India ulipomwaga mikojo ya hofu"
aliongea safari hii yule Ninja akiwa kasimama jirani kabisa na Asha ambae alisota mpaka kwenye ukuta wa jengo na hakuwa na pa kuendelea zaidi.
Muda wote Asha alipigwa na butwaa mara baada ya yule Ninja kuongea maneno yale, hakufahamu ni babaake gani aliyemuua ila kauli ya kusaidiwa India ndio iliyomstua zaidi na zaidiiii.... ni pale yule Ninja alipoamua kuvua mask yake iliyokuwa inaficha uso na kumfanya Asha azidi kutaharuki japo yeye hakuvua ya kwake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"AAAH!! UNCLE TYGA..!?"
"Ndio Mimi Mtoto wa Mzee ALY77"
Aliongea Ninja Tyga huku akichomoa kisu kikubwa cha kininja kwaajili ya kummaliza kabisa Asha ambae aliamua kufumba macho baada ya mwili wote kufa ganzi na kukumbuka kuwa ni kweli alimuua mzee Aly77 lakini ilikuwa ni agizo toka kwa Mr X na hakuwahi kujua kama ni babaake na Tyga ambae aliagana nae miaka michache iliyopita kule India.
Lakini ghafraaaaaaaaaaa alishangaa Asha kusikia ukelele wa maumivu kutoka kwa Uncle Tyga uliomfanya afumbue macho na hakuamini alichokuwa anakiona mbele yake juu ya ujio wa kidume ambae alikuwa hajavaa Kininja wala nguo za sare ya aina yoyote iliyomtambulisha yeye ni nani, huku chini alimuona Uncle Tyga akiwa ananyanyuka kwa hasira na usoni damu zikimvuja hali iliyomfanya Asha ashangae zaidi asijue kapigwapigwa vipi sekunde zile chache na yule mtu ambae alisimama mbele yake na alipomuangalia kwa umakini kwa jinsi alivyosimama tu... Aliamini huyu ni zaidi ya Ninja.
Na huyo si mwengine bali ni Cj4.
Na kweli kile alichokifikiria Lady Ninja Asha na ndivyo ilivyokuwa kwani mbali na mbinu, uzoefu na ujanja aliokuwa nao Tyga katika maswala ya upiganaji na uninja lakini kwa Cj4 alionekana bado kabisa hajaiva kutokana na mapigo aliyokuwa anapelekewa hata yeye mwenyewe Tyga alishangaa.
"Nani wewe unaingilia ugomvi usiokuhusu!!?"
alilalama Tyga mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili na kutema mate yaliyochanganyika na damu nyingi sambamba na meno mawili ya mbele mara baada ya kupokea nakozi za ajabu kutoka kwa Cj4 aliyakuwa anamchanganyia mapigo matatu kwa wakati mmoja.
"NANI WEWE!!!?"
Aliuliza tena kwa kufoka Tyga huku akijizoazoa tena pale chini damu zikizidi kumvuja baada ya swali la awali kutojibiwa kwa mdomo zaidi ya kupelekewa mateke mfurulizo ya angani ambayo alifanikiwa kuyapanch yote lakini alistaajabu pindi yule mtu ambae hakumjua alipotua chini tu ghafra alimfatua mguu kwa kumchalaza na wire furani uliomvinga na kumchota mtama Tyga na kudondoka kama gunia la viazi.
Alisimama na kujikaza kiume Tyga huku akirudia rudia kuuliza lile swali ambalo Cj4 hakunyanyua mdomo kumjibu zaidi alimjibu kwa mkong'oto wa hali ya juu uliopelekea sasa Tyga kuona nyota nyota.
Wakati mwanaume Cj4 akiendelea kumfunza adabu Tyga kwa kumuonesha vita vya kiume ndipo Lady Ninja Asha alipotumia ule uchawi wake wa Kininja na kufanikiwa kuondoka eneo lile na kutokea upande wa pili ambapo alitembea hivyo hivyo japo alikuwa na maumivu makali sehemu zile alizoumizwa na Tyga hususani pale tumboni kulipokuwa na kile kisu cha kininja.
Huku nyuma bado Tyga alizidi kudhibitiwa na Cj4 na hatimae alizimishwa kwa kupigwa kata ya shingo iliyopelekea kuteguka ule mshipa uliopitia nyuma ya sikio na kupoteza fahamu.
"The Game is start, Mr X you are the Next..."
aliongea Cj4 huku akiwa kamkanyaga kifua Tyga pale chini alipopoteza faham na kuchomoa kijiantena kilichokuwa katika saa yake kubwa ya mkononi ambayo pia ilikuwa kama simu na hapo ndipo alipotuma location za mawasiliano kwa Kamishna Shebby na signal ilipofika tu alipiga simu muda ule ule bila kuchelewa kutokana na yeye kule alipokuwa alikuwa kwenye usingizi wa mawenge kutokana na mawazo ya ndoa yake na Asha pia vile alivyojua kuwa Hussein bubu ni baba mkwe wake.
["Muangalie usoni atakuwa ni mwanamke tu, Nakuja sasa hivi"]
aliongea Shebby kwa njia ya simu mara baada ya kupata signal maalum ya Cj4 na kupewa taarifa kwa ufupi kilichojili.
Na kweli baada ya pale CJ4 alimnyanyua Tyga ambae alikuwa kapoteza fahamu na kutimka nae kwa umakini eneo lile hadi mahala ambapo aliamini pametulia wakati huo signal iliyokuwa inampa mwelekeo Kamishna Shebbyikiwa on.
Nusu saa baadae Shebby alifika pale na gari ndogo akiwa mwenyewe walimpakia Tyga na kuondoka nae kuelekea maeneo ya Kongowe njia iliyoelekea gerezani kwa Shebby na huko walipanga kumuingiza kwenye gofu la nyumba moja ya zamani iliyokuwa haishi mtu yeyote ili wamfungie mule kwaajili ya kumuhoji juu ya Mr X.
"Kumbe walikuwa wawili?"
aliuliza Shebby pindi wakiwa njiani
"Yah! walikuwa wawili ila mmoja nimemuacha aende"
alijibu Cj4
"Kwanini sasa?"
"Kwa sababu alikuwa mwema"
"Mwema?! Kivipi wakati nae ni Ninja"
"Kwa sababu ni Ninja wa kike"
"Cj4 umefanya kosa huyo wa kike ndie nilikuwa namtaka haswaaaaa nina imani ndie aliyetushambulia Mkuyuni"
Alilalalma Shebby baada ya kusikia kumbe walikuwa wawili lakini Cj4 amemzalau wa kike na kumuacha aende.
Aliumia Shebby kwani hasira zake kuu ni kumjua yule Ninja wa kike ili amuue kwa mkono wake kama alivyomuahidi siku ile endapo atamuacha hai.
Lakini kwa Cj4 alishagundua kitu kutokana na kusikia maongezi ya yule Ninja na kuhisi kwa asilimia tisini kuwa mchumba wa Shebby waliyeenda na Hussein bubu kukutana nae ndie yule Ninja aliyemsaidia pale lakini hakutaka kumwambia haraka Kamishna Shebby kwa kuwa alijua kuwa yule Lady Ninja alitumiwa kimakosa na Mr X kwa kuwa alikuwa katika mlolongo wa watu waliotakiwa kupotezwa na Mr X.
* * * * * *
Alirudi Asha na kufanikiwa kuibuka chumbani kwake pasi na mtu yeyote kujua.
Alijiangalia kwenye kioo cha chumbani kwake mara baada ya kuvua mask yake ya Kininja na kuchukua sindano aliyoichoma dawa ya kuzuia maumivu na kujidunga eneo lile la tumboni.
Na bada ya nusu saa maumivu yalikata kwa nguvu ya ile dawa hapo ndipo alipochojoa mavazi yake ya kininja na kubaki na nguo ya ndani kisha alichukua visu maalum vya oparation vilivyokuwa chumbni kwake mule na kujituliza mbele ya kioo na kuanza kujichana huku akijibinya kwa nguvu kuondoa kile kisu kwenye nyama zake za tumbo.
Kitendo alichokuwa anakifanya Asha kilikuwa si cha kitoto kwani ilihitajika ujasiri wa hali ya juu sana kufanya kama alivyokuwa anafanya Asha tena huku akijiangalia kwenye kioo mpaka akafanikiwa kutoa kile kibisu cha kininja kilichonasia kwenye nyama za tumbo lake.
Baada ya hapo Lady Ninja Asha alianza kujishona taratibu sehemu ile ya jeraha kwa umakini mkubwa mpaka akafanikiwa kumaliza kabisa na kubaki na alama ya mshono eneo lile la chini kidogo ya tumbo.
Ndani mwa Dk, Asha ilikuwa nusu ya hospitali kwani kila kitu muhimu kilikuwepo na aliandaa haya yote kwa kujua kuwa katika kazi zake siku moja inaweza kumpata balaa na kujisaidia mwenyewe na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo.
Alijifunga bandage yenye dawa maalum eneo lile la mshono na kuizungushia kiunoni ambapo ilibana vizuri kisha alisafisha eneo lote lililokuwa na dam dam na kujilaza chali kitandani akiwaza nini hatma yake ya baadae na huyo Mr. X
("Hivi yule aliyenisaidia ni nani hasa? Na kwanini alikuja eneo lile Mh! Inaonekana ni mtu hatari sana tena sana lakini kwanini alikuwepo pale? Au anajua kinachoendelea pale ? Natamani ningemjua nimuulize lakini sidhani kama anaweza kuwa salama kwangu")
Aliendelea kuwaza Asha akiwa pale kitandani wakati huo tayari ilikuwa inaingia alfajiri na maumivu ya mshono yakaanza upya na kumuongezea zaidi mawazo kwani alijua kabisa vile visu vinakuwaga na sumu ndani yake pindi vikiingia kwenye nyama ya binaadam.
Japo aliweza kukitoa lakini aliamini tayari mwilini mwake ana sumu ya Invisible knife na itakuaje endapo atajulikana kuwa na jeraha atadanganyaje? au hiyo ndoa kama itapangwa haraka ataolewaje...?
Alifikiria Asha na kujiuliza maswali haya yaliyomfanya chozi limtoke kwa mara nyengine.
Hakujisikitikia yeye kama atakufa mapema kwa sumu iliyo mwilini mwake bali alisikitika endapo atakufa kabla ya kumuua Mr X.
"Twambie nani Mr X na wapi alipo?"
lilikuwa ni swali toka kwa Kamishna Shebby akimuuliza mateka wao yule ambae ni Tyga.
"Sijui unazungumzia nini"
alijibu Tyga kwa kujiamini mbali na kuwa uso wote ulikuwa umechakaa hata hakuweza kuona vizuri kutokana na uvimbe na damu zilizokuwa bado zinamvuja.
"Narudia twambie wapi Mr X alipo na ni NANI??"
"Nimeshasema sijui unamaanisha nini wala sijawahi sikia hiko kitu"
bado aliendelea kutia ngumu Tyga wakati huo Cj4 alikuwa anasikia kile alichokuwa anajibu Tyga lakini alimuacha Shebby aendele kumuhoji huku upande wake binafsi alikuwa na mtu mmoja akimuhabarisha kinachoendelea nae si mwengine ni mkuu wa majeshi tu.
"Nani Mr X??????"
"SI-JU-I"
Mabishano yaliendelea ambapo safari hii Cj4 aliamua kutoka kule nje alipokuwa na kurudi speed hadi kwa Tyga bila kumuuliza kitu chochote alichomoa kisu chake cha kikomandoo na alipomfikia Tyga tu alikamata sikio na kulikata lote palepale mbele ya Kamishna Shebby aliyekuwa anatumia maneno mengi kumuhoji Tyga.
"Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhhhhh"
Alipiga yowe la maumivu Tyga mara baada ya Cj4 kumpangusa sikio na kulieka mbele yake pasi na huruma.
"Sasa Muulize tena kama atakuwa hasikii vizuri au haelewi nakuja baada ya dakika kumi kumalizia la upande wapili"
Aliongea Cj4 na kunyanyuka tena kwenye sehemu ile waliyoiandaa mapema kipindi wanasuka mchezo wao wa kumnasa Mr X hivyo ndani ya lile gofu haikumaanisha tu waliingia kwa dharula ama walibahatisha. bali walikuwa walipaandaa mapema kwa kujua lazima Mr X atatuma mtu wake wa kummaliza Hussein bubu.
Kitendo cha Cj4 kumkata kwanza sikio Tyga bila kutumia muda wa kubembeleza kumsemesha wala kumuuliza kidogo kilimstaajabisha Shebby ambae yeye hasira zake muda wote zilikuwa kwa Ninja wa kike ambae Cj4 alimuacha aende.
Maumivu yalikuwa makali sana kwa Tyga lakini bado msimamo wa kumficha Mr X ulikuwa palepale hali iliyomtia hasira zaidi na Shebby aliyeamua kumzibua sehemu za sikio zilezile zilizokuwa zinarusha damu na kupelekea Tyga kupoteza fahamu.
"Huyu atasema kweli?"
aliuliza Shebby kwa kuhisi kuwa yule mateka wao anaonesha yuko tayari kabisa kufa kuliko kusema ukweli kuhusu mr X
"Kwa kuwa ana mdomo atasema tu kile anachokijua kweli, ukimshindwa utanambia nije nimsemeshe"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alijibu kwa kujiamini Cj4 na kuingia tena mmule ndani alipozimia Tyga.
Lakini alipokuwa anamsogelea kumkaribia pale chini alisikia mlio wa kitu mithili ya alarm ya saa ya kimulimuli ikibeep kwenye mavazi ya Tyga ambapo alimpekua harakaharaka ndipo alipostuka baada ya kugundua kumbe kwenye lebo ya nyuma ndani ya kola ya gwanda ile ya kininja aliyovaa Tyga kulikuwa na maneno madogo ambayo kumbe yalishonewa na wire wenye signal maalum za bomu la kuendeeshwa na rimoti... Yaani lile vazi zima la Kininja lilitengenezwa kwa nyuzi maalum za baruti nyeusi ikiwa na maana combat aliyovaa Tyga lilikuwa ni bomu.
Hii ilimstua na kumshangaza Cj4 kwa kuhisi kuwa hata yule Ninja mwenyewe hakuwa anajua kama amevaa bomu muda wote na sasa namba zake zimeingizwa kwenye systim na rimoti imewashwa na ishaanza kuhesabu japo pale haikuwaonesha itahesabu kwa dakika ngapi.
"Tokaaaa Shebby Rukia nje harakaa Tokaaaaa"
alikimbia Speed kutoka nje Cj4 na kumkamata Kamishna Shebby kuruka nae kwa nje ya ile nyumba pindi alipokuwa anashangaa Cj4 alipokuwa anampigia kelele za kutaka arukie nje wakimbie eneo la kile kibanda.
Waliangukia mita kumi na lile gofu huku Shebby akiwa bado haelewi, Cj4 alimshika tena mkono na kuanza kukimbia nae pamoja kuelekea mbali zaidi na lile gofu.
"CJ....Vi....."
alitaka kuongea kitu Shebby lakini kabla hajamalizia alistushwa na kishindo cha mlipuko kutokea nyuma yao na alipogeuka hakuamini kuona gofu lile alilokuwemo mateka wao likisambaratika kwa moto.
"Shiit Cj4 ina maana umeamua kumlipua!!?"
aliuliza kwa mshangao Kamishna Shebby pindi alipokuwa anashuhudia ule mlipuko uliowasha moto ghafra kule kwenye gofu walilomfunga mateka wao Tyga.
"Huu sio muda wa kuuliza Kamishna bado tupo kwenye mchezo wa Mr X japo na sisi tumeanzisha mchezo wetu ndani yake tuondoke hapa haraka."
aliongea Cj4 na kukimbilia kule ilipo gari yao sambamba na Shebby na kujitoma ndani yake ambapo safari hii dereva alikuwa Cj4 mwenyewe.
"Lakini kwa nini umemlipua?"
"Mimi sie niliyemlipua ila ni Mr X mwenyewe"
"Mr X?? Kamlipua lipuaje sasa"
"Kwa kutumia akili za siku nyingi kabla hajatafuta wachezaji nyota wa kuucheza mchezo wake"
majibu ya Cj4 si kwamba yalikuwa yanamsaidia Shebby kutatua maswali aliyokuwa nayo, bali ndio kwanza yalikuwa yanampa maswali mapya ambayo yalikuwa yanamuonesha mwanga jinsi ya kutafuta majibu pasi na kuuliza tena.
"So what is Next..?"
aliuliza Shebby japo alihisi wanaenda kwa Hussein bubu ila alitaka kujua kama itawalazimu wamuhamishe ama waendelee kumtega palepale lakini jibu la Cj4 lilizidi kuonesha tofauti baina ya KOMANDOO wa JESHI na KAMISHNA wa POLISI.
"Next mimi nitadili na Hussein wewe pitiliza alfajiri hii hii kwa mchumbaako na umuhamishe pale anapoishi haraka kwa usalama zaidi"
"Mchumbaangu? Ina maana dokta Asha?"
"Ndio hivyo, all the best Kamishna"
Alijibu maneno haya Cj4 wakati huo tayari gari ilifika pale Mbagara karibu na ile hoteli kulipoonekana kun mkusanyiko wa watu na maaskali polisi hususani sehemu ile ya nyuma kwenye bustani.
Alishuka Cj4 na kumuachia usukani Shebby ambae alikuwa bado anayatafutia ufumbuzi majibu ya maswali ya Cj4 huku akipiga gia kuelekea kwa mchumbaake kwa kufata kauli ya mtu aliyeamini kwa moyo mmoja kuwa amemzidi mbinu na akili ya vita.
Lakini ukweli ni kua Cj4 alibaini mchezo uliotegwa na Mr X kwa wale Maninja wake hasa alipowaona wanapambana usiku wake sare zao zilishabihiana karibu kila kitu na kubaini kuwa matereo ndio yaleyale na system ndio ile ile hivyo kuna uwezekano mkubwa na yule Ninja mwengine akalipuliwa na mavazi yake ambayo aliamini wazi kuwa hajui kama ni bomu.
Na kwa kuwa alihisi kwa asilimia kubwa kuwa yule Ninja ni mchumbaake Shebby aliyevaa kivuli cha Dokta Asha na yote hayo aliyabaini kupitia maongezi yao wenyewe pindi walipokuwa wanapambana bustanini.
Hivyo aliamini kama asipoenda mtu kumtoa kule basi maisha yake nayo yatakuwa hatarini.
* * * *
Aliamka asubuhi ile Asha na kujichoma tena sindano ya kuua maumivu kabla hajatoka kuelekea chini akiwa na maana ya kufanya mazoezi ya kutembea kwa kupandisha ngazi na kutroti kidogo ili kukipa shurba kidonda chake kibichi kisijivute na kumfanya astukiwe na watu kama alikuwa na jeraha mwilini mwake.
Alivaa full tracksuit na kwa jinsi alivyokuwa anatembea kwenye ngazi mara baada ya kutoka chumbani kwake ilikuwa ni vigumu mno kumtambua kama ana jeraha la mshono mwilini mwake.
Mazoezi ya kupanda na kushuka ngazi yaliendelea wakati huo bado mamaake alikuwa hajaamka na kutoka chumbani kwake.
Akiwa anafanya yale mazoezi mepesi ya kupanda na kushuka vingazi mulemule ndani bado mawazo yalikuwa mengi sana kichwani mwake Asha hususani kuhusu kifo cha Mr X.
Hakuwahi kumuona alivyo wala kujua wapi alipo hata historia yake alikuwa haijui zaidi alichojua kipindi cha nyuma kuwa mr X ni mtu mwenye kutetea haki za watu na kuwasaidia na kuwafichua wabaya na ndio sababu ya kuwa na maadui waliokuwa wanataka afe ili akosekane mtu wa kuwafichua na kusaidia wengine.
Awali aliamini hayo lakini sasa ameujua ukweli kuwa wote waliokuwa wanamtafuta mr X kwaajili ya kumuua walikuwa sahihi kabisa.
Lakini ugumu unakuja ni kugundua picha halisi ya mr X na jina lake halisi ama hata wadhfa aliowahi kuwa nao kwani ingesaidia kumgundua na kumpata kiurahisi.
"Mwisho wako unakuja... Mwisho wako ndio huu, Mwisho wako unakuja , Mwisho wako ndio huu"
aliongea haya maneno Asha kwa hisia huku akiwa kama anaimba pale alipokuwa anapandisha ngazi na kushuka.
Lakini mara akiwa bado anapandisha na kushuka pale kwenye ngazi ndipo aliposikia mlio wa kitu cha alarm ukitokea chumbani kwake kama vile alivyokuwa anasikia Cj4 na kumfanya Asha asijue Alarm ile ni ya nini kwa kuwa yeye hajawahi kuset alarm yenye mlio kama ule.
Alianza kupandisha taratibu kurejea chumbani kwake kuangalia hiyo alarm ilikuwa ya nini, lakini akiwa anapandisha kabla hajaufikia mlango wa chumbani mwake alijikuta moyo unamuenda mbio na kusita kuingia kwanza na kusimama mlangoni kusikilizia akiwa anajishauli inapotokea hiyo alarm na kupata hisia ni pale kitandni alipozivua nguo zake za Kininja usiku aliporudi na hapo kidogo alijipa moyo kuwa hakuna kitu kibaya na ndipo alipotaka kufungua mlango lakini Hamaaaaaadiiiii.......!!! Alirushwa yeye na Mlango baada ya mlipuko wa ajabu kutokea ghafra mule chumbani na kumstua hadi mamaake aliekuwa analala chumba cha chini.
''Aaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhh''
"Ashaaaa!!! Ashaaaa Ashaaa Mwananguuuu Jamaaaaniii msaadaaa...
Motoooo Moootoooo"
alipagawa Zena huku akimbuluza Asha kwa nje kumtoa pale alipodondokea na kwa bahati nzuri alidondokea kwenye Sofa huku ule mlango uliofatuka kwa mlipuko na kurushwa sambamba nae ukiwa umedondokea sakafuni na hapo ndipo moto ulianza kukamata zuria pale chini taratibu.
"Jamani msaaadaaaaaa aaaaaah"
alipiga yowe Zena lakini kumbe mlinzi pale getini alishatimua mbio muda mrefu mara baada ya kishindo kizito kilichosikika upande ule wa juu ya nyumba chumbani kwa Asha sambamba na fungu la moto lililofumuka angani mithili ya wingu na kushuhudia hadi vigae vilivyokuwa upande ule vikifumuka kwa mlipuko ambao uliwatisha hadi majirani na wapita njia waliokuwa karibu na eneo lile.
Akiwa anahangaika mwenyewe Zena kumvuta Asha huku akiogopa hali ya usalama mule ndani mara baada ya moshi kuanza kutanda hususani na ule moto ulioshika zuria kuzidisha kasi yake ya uwakaji, alizidi kuchanganyikiwa Zena na kulia kama mtoto mdogo hasa kila alivyomtazama Asha alikuwa kalegea mwili mzima hasemi wala hatazami.
"Ashaaaa mwaanaaanguuuu Ashaaaaa amkaa mamaaaa"
hakuweza kum beba kutokana na umli na nguvu chache alizokuwa nazo Zena lakini hakuweza kumuacha pia alijitahidi kumnyanyua sehemu za juu na kumbuluza vivyo hivyo kuelekea mlango wa kutokea nje mara baada ya kuona msaada umeenda kombo.
Lakini mara ghafra mlango ulifunguliwa kwa nguvu na mwanaume aliingia huku akiwa kachanganyikiwa mno haamini kile alichokuwa anakiona.
"Ashaaaaaa ASHA Wanguuu"
alitoa ukelele wa maumivu na mshangao Kamishna Shebby mara baada ya kuingia na kumkuta Zena akimkokota Asha aliyekuwa katika hali mbaya huku sehemu zake za chini ya tumbo kukionekana damu kumvuja kwa wingi.
"Mama Tangulia haraka nje kabisa Usishike hilo geti la mlangoni niachie mimi"
alinena Shebby na kutoa tahadhari ile huku akimnyanyua Asha mara baada ya kuona cheche zikizidi kwenye socket za umeme mule ndani na ule moto wa kwenye zuria ulianza kudaka masofa na mapazia makubwa yaliyokuwa Dirishani pale Sebuleni.
Alinyanyuka huku akiwa kam beba Asha Kamishana Shebby na kutoka nae haraka haraka na kuelekea alipopaki gari kule nje na kumkuta Zena akiwa kasimama huku ameeka mikono kichwani.
"Mama ingia kwenye gari twende mamaaa"
aliongea Shebby kwa sauti ya kazi zaidi kutokana na uchungu aliokuwa nao na kumfanya Zena afungue mlango wa nyuma na kutangulia kukaa pindi Shebby alipomuingiza Asha na kumlaza huku mapajani mwa Zena, ndipo baada ya kuufunga mlango Shebby alizunguka upande wake haraka na kuingia ndani ya gari kuondoka eneo lile ambalo tayari moto ulianza kuwa mkubwa kule kwenye ile nyumba na watu walianza kuzongea huku wengine wakipiga simu sehemu za usalama wa zimamoto kitu ambacho Zena na Shebby hawakukikumbuka wala kujali zaid walichanganyikiwa na hali aliyokuwa nayo Dokta Asha.
("Mr X MR X lazima nikuue lazima nikuue na Ninja wako malaya wako unayemtumia lazima nae Nimuueee Lazimaaa damu ya mchumbaangu ilipwe hata kama atabaki hai..")
aliwaza moyoni Shebby huku akiendeesha gari speed kuwahi hospitali kuokoa maisha ya mchumbaake kipenzi, mkewe mtarajiwa, thamani ya moyo wake hasa alipokuwa anakumbuka alivyotibiwa mguu wake, mwanamke aliyeamini ndie mke bora wa kumuoa kutokana na sura yake ya bashasha, upole na upendo wa dhati aliomuonesha kipindi anamtibu.
Nae si mwengine ni Dokta Asha ambae mpaka muda huo Shebby hakujua kuwa yule ndie Ninja wa kike aliyekuwa anatumiwa na Mr X.
* * * *
Kelele za watu pamoja na ving'ora vya polisi vilivyokuwa vinasikika upande wa chini ya jengo la Hoteli ile ndio zilizomsababisha Hussein bubu aamke alfajiri ile na kuelekea usawa wa dirisha la chumba chake kile alichopangiwa na Shebby kwenye ile hoteli.
Alishangaa sana mara baada ya kuona umati wa watu wengi sambamba na polisi wakiwa eneo la bustani kubwa iliyokuwa nyuma ya ile hoteli usawa wa vyumba vile vya upande aliokuwepo.
(He!! Nini tena kimetokea?")
alijiuliza mwenyewe kimoyo moyo baada ya kuona kuna ambulance iliyokuwa inapakia miili ya watu wawili iliyokutwa imeuawa mahala pale pa bustani alfajiri ile hali iliyomstua zaidi Hussein na kuamua kuvaa nguo zake harakaharaka ili apate kwenda kule chini akajionee mwenyewe kilichokuwa kinaendelea.
"Nini kimetokea hapa?"
alimuuliza swali bwana mmoja baada ya kushuka chini na kupenya penya kwenye jopo la watu mpaka alipofika nyuma ya yule bwana aliyekuwa amesimama sehemu za mbelembele kulipozungushiwa warning tape za police kutoruhusu mtu yeyote kusogea eneo lile la tukio zaidi ya wana usalama waliokuwa wanafanya kazi yao ya upelelezi na utafiti wa kina kujua kilichowasibu wale maiti waliokutwa pale.
"Kuna walinzi wameuawa hapa"
alijibu yule bwana
"Walinzi...!!"
alitaharuki Hussein
"Eee, bwana walinzi wamevamiwa na watu wasiojulikana na kuchomwa na vitu vya ncha kali shingoni kila mmoja"
"Kwani walikuwa wangapi?"
"wawili"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"na walinzi wengine je?"
"Wengine walikuwa upande wa mbele kule naona hawajasikia wenzao wlipokuwa wanauawa"
"Duh! kwa hiyo hao majambazi wamefanikiwa na kuiba?"
"Dah! ndugu yangu hata mimi mwenyewe mpita njia tu sio msemaji wa hoteli wala polisi we sikiliza tu fatilia utajua kila kitu"
Alijibu yule bwana mara baada ya kuona maswali ya Hussein yanazidi kuwa mengi.
Aliangalia huku na huko Hussein huku akiwa na maswali ya wale watu waliovamiwa upande ule wa nyuma ambao ulinzi ulikuwa mchache kutokana na kutoonekana kuna thamani kubwa ya kuchukua zaidi eneo lile lilikuwa kama la kupumzika wageni tu, tofauti na eneo la mbele ambapo pia kulikuwa na parking kubwa ya magari na ndio kulikuwa na mashine za ATM na milango ya kuingilia mule hotelini.
("sasa hawa majambazi gani wamevamia na kuua watu upande huu huku kukionekana hakuna madhara menggine yoyote upande wa mbele? Mh! itakuwa visasi tu hivi sio bure")
aliwaza Hussein huku anaangaza macho huku na huko na mara alipogeuka kwaajili ya kuondoka pale kuna mtu alimuona upande wa pili aliyemstusha kidogo macho yake.
("Haa!..!>>!)
alipigwa bumbuwazi huku akiwa haamini kama mtu anayemtazama pale ndie au sie na kuanza kusogea haraka ili avuke barabara eneo lile la upande wa pili kumuwahi kabla hajaondo kwani ni mtu ambae alikuwa anamkumbuka vizuri sana na alipomuona moyo wake ulistuka na kubadilisha mapigo kwani hakuwahi kufikiria kama atamuona tena mtu yule ambae sasa alikuwa mita chache tu mbele ya macho yake.
Alikuwa ni Cj4 nae alishamuona Hussein muda mwingi tu japo alijifanya kutomuona na katika hali ya kumzuga na kumpoteza maboya alisubiria roli moja ambalo lilikuwa linapita pale barabarani pindi lilipowaziba tu baina yao alizunguka haraka na kuingia kwenye ile nyumba ya wageni ambayo ndio alikuwa amefikia na kupandisha juu chumbani kwake mpaka dirishani na kuanza kumuangalia Husein ambae sasa alionekana kutamtafuta.
("Mh!! kaendea wapi sasa yule kijana!!?")
alijiuliza Hussein kipindi akitafuta na kutomuona Cj4 ambae alichokuwa anakumbuka yeye ni kwamba alikuwa mfungwa mwenzake kule gerezani ambae nae alikuwa na mkasa kama wake na hata alipoingia gerezani kwa mara ya kwanza alikuwa na maneno kama yale yale aliyoyaamini yeye kuwa Wanawake ni Wauaji lakini kilichokuja kumshangaza baada ya kuzoena nae alikuja kutoweka kwa kutoroka jera na jitihada zilifanywa za kumtafuta lakini hadi anatoka gerezani alikuwa hajapatikana wala hata dariri za kuonekana kwake.
("Mh! mbona maajabu haya, au mzimu!!)
alijisemea moyoni Hussein mara baada ya kuona hakuna hata dariri ya uelekeo wa yule mtu aliyekuwa amekusudia kumfata pale na kuamua kugeuza kurudi tena kule hotelini.
Lakini wakati wote huo Cj4 alikuwa anamtazama Hussein na kumfanya atabasam kw vile Hussein alivyoonekana kuhaha kwa kumtafuta yeye bila kujua ameelekea wapi wala kutambua kama yuko nae pale kila siku.
* * * *
Kwa speed ya hatari yenye umakini wa ajabu Kamishna Shebby aliweza kuiingiza gari mpaka hospitali kuu ya Jeshi la polisi Kilwa road na pindi gari iliposimama walikuja watu wa machera haraka haraka kutokana pia na kuitambua gari ile ilikuwa ya nani na aliposhuka tu ndio kabisa huduma za kumtoa Asha garini zilifanywa haraka sana na kwa umakini mkubwa.
Alionekana kudata Kamishna Shebby huku akiwa anazunguka zunguka wodini pindi Asha alipoingizwa chumba cha upasuaji bada ya kutolewa taarifa kuwa alirushwa na mlipuko hivyo madaktari walihisi huenda pia kuna vyuma au vibati vimeingia mwilini mwake hususani sehemu ya tumbo kulipooneaka kuvuja damu kwa wingi.
("Ama zako ama zangu.. ama zako Ama zangu..")
alirudia rudia Shebby maneno haya huku akiimaliza korido na kurudi mwanzo akifika mwisho anarudi tena mwanzo huku kichwa kakiinamisha wakati huo Zena alikaa kwenye viti vya kusubiri wagonjwa akilia kwa uchungu.
Baada ya nusu saa alitoka Dokta mmoja kwenye chumba cha upasuaji.
"Vipi Dokta?!"
aliuliza Shebby kwa mshtuko huku akiwa na shauku ya kujua kilichoendelea kwenye kile chumba cha upasuaji.
"Usijali mkuu, maendeleo ni mazuri tu inaonesha zaidi alipata mshtuko wa moyo uliosababisha presha kuwa chini sana lakini hana majeraha makubwa wala mwilini mwake hakuna kipande chochote cha chuma au chenye ncha kali, kwa sasa wanarekebisha mshono aliokuwa nao ambao ndio ulifumka na kumsababishia damu nyingi kuvuja"
majibu ya yule Dokta yalishusha presha aliyokuwa nayo awali Shebby kwa kiasi kikubwa na ndipo alipomfata na mama (Zena) kumuelezea lile na kumtoa wasiwasi kisha alimuachia kiasi cha ths laki moja kwa niaba ya dharula yoyote itayojitokeza pale nae aliahidi kurudi baada ya muda mfupi ujao.
Alitoka na kuingia kwenye gari huku mawazo yake kichwani yakiwa kwenda kukutana na Cj4 ambae alizidi kumuona mchawi wa mbinu kwa kugundua vitu ambavyo yeye hakuvifikiria.
Lakini akiwa njiani alikumbuka vizuri maelezo ya yule daktari pindi alipotoka chumba cha upasuaji na alipoyafikiria vizuri maneno yake kuna kitu kimoja kilianza kumchanganya na kutoelewa.
("Mshonooo, mshonooo. Mh!! mbona sikumbuki kama Asha aliwahi kuwa na mshono. mshonooo!!.. mshono gani tena huo?!!")
aliwaza Shebby na kujiuliza mwenyewe pindi alipokuwa njiani baada ya kukumbuka vizuri maelezo ya yule daktari.
* * * *
"Huwezi amini Cj yaani kabla hata sijafika kwenye ile nyumba kwa macho yangu nilishuhudia mlipuko upande wa juu na nilipoingia sikuamini hali niliyomkuta nae Asha .. Daaah!! Mr X naamini nitapomuua nitapata thawabu Dah!"
aliongea Shebby mara walipokutana kwa siri na Cj4.
"Kwa hiyo mchumbaako vipi?"
"Mungu amesaidia nimemuacha hospitali kwa matibabu zaidi ila kuna kitu sijakielewa"
"Kipi hiko?"
"Nimeambiwa jeraha lililokuwa linavuja damu tumboni kwa Asha ni la mshono.."
aliongea Shebby kauli ambayo Cj4 aliichekecha harakaharaka na kupata uhakika sasa kua mtoto wa Hussein ambae ni mke wa Kamishna Shebby ndie yule Ninja aliyemsaidia usiku baada ya kuchomwa na kisu cha kininja tumboni hivyo alijua mshono unaozungumziwa pale laima atakuwa amejishona mwenyewe usiku uliopita na kutokana n msukosuko wa bomu umefumka.
"Sasa neno Mshono limekuchanganya nini? mbona mi naona kawaida."
alijibu Cj4 kwa kumzunguka Shebby kwani hakutaka kabisa agundue mapema mchumbaake ni nani.
"Sikia Cj, sijawahi kumuona na mshono Asha wala hajawahi kunambia hiko kitu."
"hahahaha, tatizo Shebby unapanik mapema, nataka ukumbuke kuwa mshono unamaanisha sehemu ambayo iliwahi kufumka ikazibwa upya. sasa unajuaje kama kipindi cha nyuma mchumbaako aliwahi kufumka sehemu hizo?"
"Mh! sasa ndio uachie na kuvuja damu?"
"Inawezekana kishindo kilikuwa kikubwa.. Ila mi nataka nikushauri kuwa fanya jitihada mapema tu umuoe Asha"
"Mh! Cj mi naona kwanza tumalize hili la mr X"
"Hapana, unajua mr X anatumia akili na mambo yake mengi aliyaeka kwenye mipango kabla hayajatokea. sasa ili akuchanganye anataka kudili kwanza na watu uwapendao. Ndio maana nakwambia muoe kwanza Asha mueke jilani harafu hapo sasa hata mr X mwenyewe utakuwa umeshamzunguka"
Ushauli wa Cj4 hakuutarajia kabisa Kamishna Shebby lakini hakutaka kuupinga kwani moyo wake tayari ulikuwa unamuamini sana Cj4 na kumkubali hivyo aliongea na wazazi wake ambao walikubali lifanyike hilo jambo haraka hususani mzee Mwinchande limpongeza mno mwanae kwa maamuzi aliyofikia lakini kwa kile kilichotokea kwa Asha Shebby alizificha taarifa zile nyumbani kwao kwa kuogopa kuwatisha pia kwa kuzingatia ushauri wa awali aliopewa na Cj4 na hata Hussein babu bubu hakuambiwa kilichompata mwanae zaidi ya kuja kusikia habari za nyumba kuwaka moto huku akidanganywa ni kwa shoti ya umeme kipindi ambacho wakazi wote (Zena na Asha)
hawakuwepo pale nyumbani.
* * * * *
Siku ileile masaa machache baada ya Shebby kuondoka Asha alirejewa na fahamu wakati huo tayari madaktari walikuwa wamemaliza kumshona vizuri sehemu ile ya chini ya tumbo kulipoachia.
Kutokana na kupungukiwa damu ililazimika kuongezewa chupa nne za damu na usiku huo alilala pale wodini huku upande wa Shebby alihaha na kufanikiwa kuwakodia nyumba nyengine nzuri maeneo ya jilani na ile hoteli aliyopngiwa Hussein kwa kujua kuwa pale amewaeka kwenye usalama kwa uwepo wa rada za Cj4.
Baada ya kila kitu kuwa sawa upande wa Cj4 siku hiyo asubuhi na mapema alitoka kinyemela pale alipokuwa anaishi pasi na kumuarifu Shebby na alielekea kule hospitali akiwa amevaa sare zake za kipolisi zilizomtambulisha kama Inspecta na kufanikiwa kuingia wodini kumuona mgonjwa ambae siku hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kuruhusiwa.
Hakukuwa na vizuizi wala maswali mengi pindi alipotaka kukutana na yule mgonjwa, ila kukaibuka mstuko na taharuki kubwa kutoka kwa yule mgonjwa ambae ni Asha pindi alipokutanisha macho na Cj4 ambae nae alistuka kidogo baada ya yale macho kuyakumbuka vizuri siku ile ya ajali ya kule chalinze ambayo ilipelekea kupoteza kwa maisha mtu muhimu aliyetakiwa kuhojiwa juu ya upelelezi wa kum baini Mr X.
Asha alijitahidi kuificha hali ile ya mstuko wake machoni lakini Cj4 alimgundua vizuri sana na kwake yeye hakuonesha mstuko wowote machoni zaidi ya kumsogelea na kumpa pole kabla hajaanza kumuuliza maswali ambayo Asha alibaki kama bubu asijue aanzie wapi kuyajibu.
"Hebu nambie unajua nini zaidi kuhusu mr X, wala usinifiche ila nataka unijuze mr X alikupa neno gani la mwisho pindi ulipoasi?"
Aliuliza Cj4 kwa sauti ya chini sana lakini iliyosikika vizuri masikioni mwa Asha na kubaki anababaika aanzie wapi na hapo ndipo Cj4 alipomuachia kikaratasi cha namba za mawasiliano kisha akatoka taratibu na kumuacha Asha ametumbua macho kwa taharuki.
("Khaa! huyu si ndio yule Afande wa Chalinze? kajuaje kama niko hapa? kajuaje mambo yangu na Mr X?")
alijiuliza maswali haya Asha ambayo alijua fika kuwa hakuna mtu wa kumfata moja kwa moja akampa majibu yale bila yeye mwenyewe kuyatafutia ufumbuzi kupitia yule yule mtu.
Baada ya masaa mawili Kamishna Shebby nae alifika pale hospitali na kufanya utaratibu wa kuwatoa na kuwapeleka kwenye makazi mapya aliyowatafutia.
"Mama kwa sasa mtakuwa hapa kipindi tunafanya taratibu za kumaliza hili suala la ndoa, nataka Mungu akitujaalia tulifanye hata wiki ijayo"
"Wiki ijayo?"
"Eeh mama"
"Atakuwa kashapona vizuri kweli!?"
aliuliza kwa mshangao yule mama kutokana na kuona mambo yamekaa jilani sana tofauti na alivyodhani baada ya Asha kupatwa matatizo
"Kwa hilo usijali mama, kama yeye alivyoniuguza na tukakaa wote hadi kuwa wachumba basi nami nitamuuguza tukiwa wote kama mtu na mkewe, naamini Mungu ndie anayetupangia tukutane aktika vipindi vigumu vya mataaizo kama hivi"
aliongea Shebby maneno ambayo Zena aliyaelewa na kukubali
"Lakini naomba mjitahidi baba asijue kama ana mshono mwanae mtamchanganya"
aliwakumbushia nao walikubali jambo lile na Hussein bubu hakuambua kujua ukweli juu ya kilichompata Asha zaidi ya kujua makazi mapya na kuingojea hiyo siku ya kumuoza mwanae kwa udi na uvumba.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa upande wa Asha ilikuwa ngumu sana kwa kumtazama tu ukagundua kuwa ana jeraha mwilini mwake kwa jins vile alivyokuwa anajichangamsha na kujiweka lakini kuna kitu kimoja kilimuumiza akili zake na kuufanya usiku ule wa kwanza kwenye yale makazi mapya kuwa mgumu sana upande wake na si kwa sababu ya kufikiria juu ya ndoa bali ni kwa sababu ya ule ujio wa askali ambae anakumbuka alionana nae siku ile aliposababisha ajali iliyopelekea kifo cha mzee Cypilian.
Alishangaa kila alipomuangalia Shebby hakuonesha dariri zozote za kumstukia zaidi alipowahi kumuuliza juu ya mshono kule hospitali nae alijibu aliwahi kweli kufanyiwa upasuaji mdogo wa kidole tumbo (appendex) wiki za karibuni na alifanya siri ili asimtie hofu mamaake na uongo huo Shebby aliuamini kabisa.
Usiku huo Asha hakuwa na jinsi ilibidi amtafute hewani yule askali na kweli alipopiga tu zile namba Cj4 alipokea na baada ya kujua anayeongea nae alimuuliza swali lile lile na Asha hakuwa na jinsi ilibidi aongee yote anayoyajua na kumpa lile neno la mwisho aliloambiwa na mr X ambalo lilikuwa sawa kabisa kama alilowahi kuambiwa amwambie Shebby.
* * * *
Mipango ya ndoa ya Kamishna Shebby na Dokta Asha ilizidi kushika kasi kwenye vichwa vya wanafamilia ambapo kwa upande wa mzee Mwinchande na mkewe ilikuwa ni zaidi ya furaha na walifanya utaratibu na kuongea na sheikh mkuu wa jiji la Dar ndie aje kuwa mfungishaji Ndoa hiyo ambayo Mwinchande alipania kuifanya iwe ya kipekee sana japo mipango yake ilikuwa ni ya muda mfupi.
Na hatimae baada ya maandalizi yote kukaa katika mstari (kuwa sawa) Kamishna Shebby alikutana tena kwa siri na Cj4 siku moja kabla ya ndoa kwa maongezi maalum.
"Sikia Shebby, kesho ni siku kubwa sana na muhimu katika kujua muelekeo wa Mr X"
aliongea Cj4
"Kivipi kiongozi"
"Kumbuka neno la mwisho la mr X uliloambiwa na yule Ninja."
"Yap nakumbuka lile fumbo"
"sasa kwa kuwa kesho kutakuwa na wageni wengi kwenu wanaokutambua nina wasiwasi kutakuwa na ugeni wa Mr X pia kwa kuwa anakutambua. Na hii ndio inanifanya na mimi kuja kwenye hiyo sherehe lakini hakuna atayejua kama nimekuja zaidi yako lakini pia nawe hutoniona kama nimekuja lakini nitakuja."
alichanganya maneno Cj4 na kumfanya Shebby akubali lakini asijue maana halisi ya maneno yale zaidi alipata picha kuwa kuna uwezekano kweli mr X akahudhulia hiyo sherehe au akatuma mtu wake kwaajili ya kuwamaliza katika hiyo sherehe ya harusi iliyotarajiwa kufanyika kesho yake.
"Kitu chengine Shebby umepangaje kuhusu Hussein akitoka hapo hotelini?"
aliuliza Cj4
"Nimepanga nikamnunulie nyumba sehemu salama."
alijibu Kamishna Shebby kauli iliyopingwa na Cj4
"Hapana Shebby, hakuna nyumba iliyo salama kwa Hussein kabla ya kifo cha Mr X"
"sasa Unanishauri vipi kiongozi"
"Inabidi ukae na wazazi wako uwaombe waishi na Hussein pale kwenu kidogo hiyo itakuwa salama kwake"
"Kwa hiyo unananambia Hussein akaishi nyumbani ndo itakuwa salama?"
"Ndio hivyo nionavyo"
"Sio kama nitasogeza maadui wanaomuinda nyumbani?"
"Hapana Shebby, hiyo ndio njia ya msingi"
"sawa kiongozi"
Kamishna Shebby alikubali tena swala la pili lililotolewa na Cj4 na kuagana huku wakitakiana kila la kheri hiyo kesho yake ambapo Cj4 atakuja kwa ngazi maalum ya kuwachunguza wageni wataofika ili apate kumtambua Mr X.
* * * * *
Wageni na viongozi mbalimbali waliendelea kumiminika katika ukumbi maalum uliokodiwa kwa niaba ya sherehe za kuwapongeza bwana Shaaban Mwinchande na bibi Asha Hussein kwa muungano wao wa kimwili na kuwa kitu kimoja kama ilivyo katika maandiko yaani mke na mume.
Ilikuwa ni majira ya saa kumi jioni mara baada ya ndoa iliyofungwa majira ya saa nne asubuhi katika Msikiti mkubwa kabisa jijini chini ya Sheikh mkuu.
Ilikuwa ni furaha sana kwa kila mtu hususani Hussein yeye muda wote alikuwa na leso akifuta machozi kwa kutoamini kama leo amefanikiwa kumuoza mwanae kwa mtu ambae alitokea kuwa chachu ya yeye kutolewa jera.
Ilikuwa ni furaha kwenye sherehe ambayo kweli ilikuwa ya kipekee na wageni walikuwa wengi sana kuanzia viongozi wastaafu waliokuwa na urafiki mkubwa na mzee Mwinchande miaka hiyo pamoja na viongozi wa usalama hususani jeshi la polisi na magereza.
Bila kusahau wageni wengine tu waalikwa ambao wao hawakuwa na wadhifa wowote nchini.
Akiwa amekaa upande maalum kulipotegwa kwa wazazi wa kiumeni na wale wa kikeni Hussein muda mwingi alikuwa na furaha lakini kila anapogonganisha macho na mamaake Kamishna Shaaban alijikuta anapata mshtuko muda mwengine ambao hakujua unatokea wapi lakini alikuwa anaupotezea.
Kuna wakati hasa ule wa kula keki na kupiga picha ndio kabisa Hussein alizidi kuushangaa moyo wake kuongeza mapigo kila anapoangaliana na yule mama hasa wakati walipokaa pamoja na mzee Mwinchande, Zena na yule mama Shaaban alijikuta kama anatamani kumuuliza kitu lakini hakujua ni kitu gani na kuishia kujichekesha tu.
kulikuwa na wapiga picha waalikwa tofauti tofauti kwenye ule ukumbi na mmoja wapo kati ya wale wapiga picha alikuwapo Cj4 ambae ilikuwa ni vigumu sana kutambulika kwa mtu yeyote aliyekuwa anamjua hapo kabla kwa ule muonekano alioingia nao pale.
Hata Shebby alipokaa na mkewe jukwaa kuu kusikiliza nasaha za hapa na pale kutoka kwa wazazi na watu wengine, macho yake muda mwingi yalikuwa yanaangaza huku na huko ndani ya ukumbi kwa lengo la kumuona Cj4 lakini hakufanikiwa kumgundua japo alikuwa jilani nae muda wote kwani wapiga picha walikaa mbelembele ya eneo la tukio ili kuweza kuchukua na kupiga picha vizuri.
Muonekano wa Cj4 siku hiyo alikuwa na Mustachi mkubwa tu sambamba na miwani ambayo kwa nje ni kama ya macho lakini haikuwa hivyo na hata mustach aliokuwanao ulikuwa wa bandia.
Alichokuwa anafanya kwa kutumia ile kamera Cj4 ni kurekodi video huku akiwachukua karibu wageni waalikwa hususani wale wastaafu wote nia na madhumuni pindi atapoondoka akirudie kuikagua kwa umakini ile video apate kumjua mr X kwani aliamini kivyovyote mr X lazima angekuja mwenyewe sehemu ile ya ukumbi na iwapo atakuja basi amani itatawala lakini iwapo mr X asipokuja aliamini kuna tukio lolote lingeweza kutokea hivyo muda wote alikuwa makini kwa hayo yote mawili Cj4.
Kwa jinsi mambo yalivyoenda vizuri pale ukumbini hakukuwa na aliyegundua wala kuhisi kama yule bibi harusi ana jeraha la mshono tumboni na hiyo ilibaki siri ya watu wachache tu japo wengi walisikia tukio la kuungua kwa nyumba ya Dokta Asha.
* * * * *
Sherehe ziliisha majira ya usiku sana na kutokana na sababu maalum fungate la Shebby na Asha lilipangwa kufanyika palepale kwenye Jumba kubwa la kifahari la mzee Mwinchande.
Nyumba ile nyengine aliyokodi Shebby ililipiwa na kukabidhiwa Zena kuwa nyumba yake huku kwa upande wa Hussein bubu alijumuika pamoja na wazazi wa Kamishna Shebby kwaajili ya makazi ya muda pale kwenye jumba la Mwinchande kipindi ambacho Kamishna Shebby atapokuwa anamtafutia makazi rasmi ya kudumu.
Alfajiri na mapema ndani ya jengo la mzee Mwinchande kwa mara ya kwanza Hussein bubu alijiona kweli yuko huru mara baada ya kulala katika chumba kikubwa chenye mandhali ambayo hajawahi hata siku moja kulala tokea kuzaliwa kwake mpaka pale alipofikia.
Usiku huo alimshukuru sana Mungu kwa yote yaliyoendelea na aliendelea kumuomba kama ilivyokuwa kawaida yake kuwa amsaidie aweze kumtendea muujiza alipe kisasi kwa kumuua Mr X kwa mikono yake.
Japo kwa akili ya kawaida ilikuwa ni kazi ngumu na ni kitu kama cha kufikirika tu kutokana na wengi waliokuwa mashupavu na uwezo wa vita kushindwa walau kumjua mr X sembuse Hussein ambae kashaanza kujiishia umri umemtupa mkono harafu aweze kumuua?
Lakini kwa Mungu Hussein aliamini hakuna linaloshindikana aliamini kabisa imani thabiti na kumuomba kila siku japo alijua kuua ni dhambi lakini kwa dhambi ya kumuua Mr X aliiomba na kuikubali kwa moyo mmoja kuliko kumuacha hai.
"Aslaam alaykum"
alisalimia mzee Hussein asubuhi ile pindi alipotoka na kumkuta Mzee Mwinchande upande wa sebuleni ambapo alikaa kwenye mswala akisoma qur'aan baada ya kusali sala ya alfajiri.
"Waaleikum salaam warahma tullah wabarakatul"
alijibu kiurefu kabisa Mzee Mwinchande kwa rafudhi maridhawa ya kiarabu kuonesha jinsi gani dini imelala kwenye ubongo wa Mzee Mwinchande.
Moyoni Hussein alijisikia faraja sana kukutana na familia ya wacha Mungu kama ile na akiwa maeketi kwenye moja ya sofa akimtazama babaake Kamishna Shebby akisoma qur aan kwa utulivu kabisa na kumliwaza Hussein japo alikuwa hajui tafsiri yake na alipata imani ya kumuelewa vizuri Kamishna Shebby kwanini kawa mtu tofauti mwenye roho nzuri, kumbe kwa sababu amelelewa na watu wenye imani na kuishika dini.
Akiwa ametabasamu pale sebuleni mara alimuona kwa mara nyengine mamaake Shebby ambae rich ya kwamba nae umli kidogo ulisogea lakini pindi anapokutanisha nae macho moyo wake unastuka sana na hadi muda mwingi alipuuzia na hakujua kwanini lakini safari hii asubuhi mara tu aliposikia sauti ikimsalimia na kuinua kichwa chake kuitikia huku akimtazama akili yake ilimletea picha iliyomfanya apigwe na bumbuwazi hadi yule mama alishangaa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitamani kumuuliza kitu palepale lakini ulimi wake ulikuwa mzito na kubaki kimya lakini akilini tayari ilikuja picha ya mwanamke aliyewahi kumpenda miaka mingi.
Picha ya mwanamke aliyemuamini kupita kiasi.
Picha ya mwanamke aliyeweka doa katika historia ya maisha yake mpaka kufikia pale alipo.
Picha ya mwanamke huyo iliyomjia akilini haikuwa picha ya mwanamke yeyote mwengine bali ni picha ya Zainabu.
Mwanamke aliyeuteka moyo wa Hussein na kumuonesha mapenzi ya dhati yaliyomfanya awali Hussein ajione yeye ndie mwanaume bora kuliko wote lakini mwisho wa siku mwanamke huyo ndie aliyekuja kutoa kauli iliyomfanya Hussein miaka yote abaki na imani kuwa wanawake ni wauaji.
Alimtazama mama Shebby mke wa mzee Mwinchande na kwenye macho yake aliweza kuiona taswiera ya Zai wake aliyesingiziwa alimuua mwenyewe sambamba na mtoto wao wa kiume ambae aliushuhudia mwili wake ukiwa umekatwa kichwa na viganja ambavyo vilikutwa mifukoni mwake.
Lakini hata hivyo aliamua kulipotezea lile wazo kichwani na kumuomba Mungu kimoyo moyo amuondolee akili ya kumuwaza sana Zai kwani kuna muda aliamini kabisa Zai amekufa lakini kuna muda pia hakuamini na alihisi kuwa Zai hajafa ila waliyemuulia pale ni mtoto wake kipenzi aliyekuwa na miezi mmne tu.
Lakini japo alijitahidi kupotezea bado kuna vitu akiviona kwa yule mama ambae yeye hakuonesha kumjua Hussein hapo kabla hata kidogo, vilimfanya amkumbuke sana Zai mke wake na kitu kikubwa kwanza ni uvaaji wa Kiremba.
Jinsi ambavyo alikuwa akimtazama mama Shebby ule ufungaji wake kiremba cha kitenge ulimfanya pia amkumbuke sana Zai ambae nae alipenda sana kufunga kiremba tena kwa mtindo wa kipekee ambao wengi walikuwa hawafungi vile na ajabu mtindo ule wa mkewe Zai kwa mara nyengine aliukuta kwa mama Shaaban.
Kitu cha pili kusoma (kuimba) qaswida hasa nyakati za asubuhi.
Hili nalo aliligundua kwa mama Shebby siku hiyo asubuhi alipoonana nae tena na kumshangaa kupita kiasi alikuwa anatembea huku akiimba qaswida jambo ambalo hata mkewe Zai ndio alikuwa analipenda sana.
Lakini mbali na sababu hizo pia kulikuwa na sababu nyengine akizifikiria zinamkatalia kuwa mama Shebby si Zai na moja ya sababu hizo ni umri wa Shebby ambae uliandikwa kwenye daftari maalum siku wanafungishwa ndoa kuwa Asha alikuwa na miaka 29 anakaribia 30 jambo ambalo lilikuwa sahihi kabisa kwani alipokuwa anapelekwa jera baada ya kuhukumiwa barua ya mchumbaake wa zamani Mariam ilionesha kuwa tayari Asha ana miaka mitatu na yeye amekaa miaka 26 gerezani.
Lakini kwa upande wa Kamishna Shebby yeye umri wake ulionesha ni miaka 28 jambo ambalo lilikuwa tofauti kabisa kwani miaka hiyo 28 ndio kwanza alionana na Zai Arusha na hakuwa na mtoto wala hata alivyokutana nae mwaka uliofuata baada ya kushinda mitihani aliyopewa na Zai alimkuta ni bikra yaani yeye ndie alikuwa mwanaume wake wa kwanza kwa hiyo aliamini wazi kuwa Zai hakuwahi kuwa na mtoto mwenye umri mkubwa kama Shebby kwani mtoto wao kipenzi wa pekee aliyezaa na Zai alichojua aliuawa miaka 26 iliyopita.
Kwa kigezo cha umri wa Shebby kilimuondoa kabisa kwenye mashaka ya kumfananisha mamaake Shebby na aliyewahi kuwa mkewe ambae bado hakuwa na uhakika kama alikufa au mzima bi Zainab.
* * * * *
Usiku baada ya sherehe zile kuisha na watu wote kutawanyika alionekana Cj4 ambae alikuja na pikipiki moja iliyomtambulisha kama mpiga picha kutoka ofisi ya wazili wa mambo ya ndani na hata kitambulisho alichokuwa amevaa kilionesha hivyo na kila aliyemuona aliamini hivyo kutokana na kumtambua muhusika wa kile kitambulisho na muonekano wa Cj4 hakuna aliyemtilia hofu hadi wakati anaondoka pale ukumbini.
Safari yake ilimpeleka hadi sehemu moja pembeni ya barabara kulipokuwa na daraja na kusimamisha pikipiki ile nyuma ya gari moja ndogo iliyokuwa imeegeshwa pembeni na kushuka lakini aliachana na ile gari yeye alienda moja kwa moja hadi chini ya barabara uvunguni mwa lile daraja ambalo lilikuwa limekauka maji, na alipotoa simu yake ya mkononi kumulika mule uvunguni alionekana mtu mmoja ambae alifanana nae sana jinsi alivyojiweka, akiwa kafungwa kamba mikono na miguu huku mdomoni kazibwa na plasta kubwa.
"Good mr, kazi imeisha kama nilivyokuahidi siwezi kukudhuru kwa kuwa mimi si mtu m baya ila ukitaka kuujua ubaya wa mtu upoje uende ukatoe siri kuwa aliyekwenda kwenye ile sherehe ya harusi hukuwa wewe."
aliongea Cj4 na kumtoa plasta ile iliyokuwa mdomoni mwa yule jamaa aliyekuwa na kitambi kiasi sambamba na mustachi mkubwa.
Alibakia anahema tu yule bwanakipindi Cj4 akimfungua zile kamba na alipomaliza alimrudishia kitambulisho chake sambamba na funguo ya pikipiki kisha akatoa memory iliyokuwa ndani ya ile kamera na kumkabidhi kamera tupu.
"Zingatia ndugu niliyokwambia"
aliongea Cj4 na kutoka mule darajani huku yule bwana akiwa amesimama haamini hadi pale aliposikia gari ikiwashwa na kuondoka ndipo nae alipotoka mbio kule na kuwasha pikipiki yake na kuondoka.
Baada ya kufika ndani ya chumba chake alichokodi kwenye ile guest Cj4 alianza kubadilisha muonekano wake kwa kuondoa ule mustach wa bandia na kuanza kubambua mfuko wa plastik maalum uliobanwa tumboni mwake na kumuonesha kama aliyekuwa na kitambi cha wastani pindi alipovaa shati ile kubwa sambamba na kikoi.
Mara baada ya kumaliza kupambua vitu vya bandia mwilini mwake ndipo alipotumbukiza ile memory kwenye compyuta yake na kufungua mafaili ya video alizoshoot kwenye ile sherehe ya harusi ya Shebby ndipo kwa umakini mkubwa Cj4 alianza kufatilia matukio na nyuso za watu aliokuwa anawachukua ili kuhakikisha na kubaini kwa mbinu zake za kikomando kati ya wale wageni waliohudhulia pale nani alikuwa Mr X.
Alitulia kwa umakini mkubwa Cj4 kutazama yale matukio yaliyokuwa yanaendelea kipindi cha shughuli ile lakini kadri alivyokuwa anaangalia bado hakuona tofauti kwa mtu yeyote wala kupata taswira nani kati ya wale watu waliokuwepo kwenye ile shughuli ni Mr X?
Aliangalia hadi mwisho bila kumuhisi mtu yeyote aliyeoneka kuwa na utofauti furani ambao ungemsaidia kumtambua mr X na ndipo alipoamua kuianzisha upya safari hii akipunguza speed ya utembeaji wa picha na kueka ule wa taratibu na kiminato (slow motion)
Aliangalia tena kwa umakini mno wakati huo kila hatua aliyoichukua na mwishoe aliimaliza tena hadi mwisho bila kupata picha wala taswira ya kumjua huyo mgeni aliyeamini kuwa lazima atakuwepo kwa kuwa kauli za mr.X zenye mafumbo mazito kwake Cj4 aliweza kuyatatua kiasi yale mafumbo na kujua lazima Mr X atakuwa kwenye mzunguko wa maisha ya Kamishna Shebby iwe katika ngazi ya jeshi la polisi ama kwa marafiki wakuu wa babaake mzazi mzee Mwinchande kutokana nae alikuwa ni moja ya askali wakubwa enzi hizo hivyo alikuwa na mtandao wa karibu na watu wengi ambamo Cj4 aliamini lazima miongoni mwao atakuwa ndie Mr X.
Lakini safari hii alipofika mwisho kuna kitu kimoja alikiona akagundua hakipo sawa.
Hapo ndipo alipoanza kurudisha nyuma na kueka slow motion zaidi vile vipande vya Hussein bubu na kuna kitu akaanza kukibaini na kukitilia shaka.
Ni vile Hussein muda mwingi alionekana alikuwa anamuangalia sana mamaake Kamishna Shebby tena kwa kumuiba iba.
Alikaa vizuri Cj4 na kumzoom Hussein sehemu za macho yake na kugundua kuwa kuna kitu alikuwa anakifikiria ama anakifananisha kwa jinsi alivyokuwa anamtazama mamaake Kamishna Shebby.
("Mh! hapa hapa ndipo pa kuanzia.")
alijiambia akilini Cj4 na kumsogeza kwa karibu mamaake Kamishna Shebby sehemu za uso na kumplay katika slow motion kumchunguza vile alivyokuwa anamuangalia Hussein na hapo napo kuna kitu alikisoma kuwa mama Shebby hakuweza kabisa kumuangalia Hussein hata kwa sekunde kumi, na mara alipogonganisha macho na Hussein aliyakwepesha kiujanja na kugundua sehemu alipoyaelekeza ni upande aliokaa mumewe ambae ni babaake Kamishna Shebby.
"Mh!"
Aliguna Cj4 na sasa alianza kumzoom babaake kamishna Shebby ambae ni mzee Mwinchande lakini kila alivyoitafuta tofauti yoyote kutoka kwa mzee Mwinchande kwa kile alichokiona kwa Hussein na mama Shebby hakuweza kuona chochote kutoka kwa Mwinchande.
Alimueka katika slow motion ile ya chini kabisa lakini muda wote aligundua kuwa mzee Mwinchande alikuwa na furaha na muda mwingi alionekana yuko bussy na kile kilichokuwa kinaendelea ukumbini hususani kuwatzama bibi na bwana harusi.
Alirudia tena Cj4 kwa upande wa Hussein na mama Shebby walivyokuwa wanapelekeana macho na hapo aliikumbuka vizuri story ya Hussein juu ya maisha yake yaliyopita mpaka anaingia jera na kuanza kupata hisia inawezekana Hussein akawa anamfananisha mama Shebby na mkewe ambae ilisemekana alimuua.
"Hapa hapa kuna alama ya Mr X."
alijisemea mwenyewe Cj4 lakini kila alipotaka kumshuku babaake Shebby alijikuta moyo unakuwa mzito kukubali japo akili ilianza kumpeleka huko.
("Inawezekanaje huyu akawa ndie mke wa Hussein? Mh! ila pia inawezekana na kama ndio nina mashaka na babaake Shebby akawa ndie Mr X. ilaaaaa.... Agh! Nina wasiwasi na hapa hapa")
aliwaza na kujisemea moyoni Cj4 na kujilaza kitandani wakati huo tayari ilikuwa alfajiri.
"Mzee Mwinchande upo katika mstari wangu wa mashaka. Hii sasa itakuwa mission yangu peke yangu."
alitamka maneno haya Cj4 na kueka nia sasa mtu atayedili nae katika kumchunguza ni baba wa Kamishna Shebby ambae ni mzee Mwinchande, na hili alipanga kulifanya bila kumwambia hata Kamishna Shebby ambae ndie aliyekuwa anashirikiana nae katika mission zao za siri juu ya kumtafuta na kumnasa Mr X.
* * * * *
"Ibada ni jambo jema sana mzee mwenzangu."
"Kweli kabisa."
"Mwenye kufanya ibada hujieka jilani na Mungu na kujilinda na Sheitwaan"
"Naam."
"Mimi na mke wangu kama unavyotuona, sisi ni waislam safi kabisa na kila siku tunafanya ibada na ndio sababu nyumbani kwetu kuna amani na ndoa yetu imedumu miaka mingi."
"Daah! kweli kaka hongereni sana."
"Ahsante lakini hata wewe si mzee kama unaamua."
"Kuamua kivipi kaka."
"Amua uoe ili upate utulivu si unajua ng'ombe hazeeki maini?"
"KUOA!? hahahaa hapana kaka mimi maisha yangu nitayamalizia hivi tu."
alijibu Hussein bubu huku kipindi akizungumza na Mzee Mwinchande pale sebuleni majira ya mchana.
Mzee Mwinchande alikuwa anamuelezea Hussein habari nyingi nzuri na jambo kubwa alikuwa anamsisitiza juu ya imani yake kwa Mungu.
Maneno ya mzee Mwinchande yalizidi kumfanya Hussein amsome kuwa ni mtu mmoja mzuri sana na moyo wake ulifanana na wa Kamishna Shebby kwa vile alivyoonekana mwenye kujali na kuthamini wengine.
"Hivi unajua vizuri kusali?"
aliuliza mzee Mwinchande
"Mh! hapana kiukweli nimesahau dua nyingi sana za kusoma wakati unasali"
alijibu Hussein bubu.
"Basi mi nataka kuanzia leo uwe unajiunga nami tusali pamoja hususani alifajiri na usiku ndio mida mizuri sana kusali na kuomba"
aliongea mzee Mwinchande huku akipekua chini ya screen kubwa iliyokuwa ukutani pale sebuleni ambapo kwa chini kulijengewa kama kikabali maalum cha kuhifadhia vitabu na hapo alitoa kitabu kimoja kilichoandikwa SALA NA MAFUNZO YAKE, kisha alimkabidhi Hussein.
"Hiki kitabu kitakusaidia sana katika kujua kusali sala zote za kiislam."
"Asante sana kaka, daah! Nashukuru kwa kweli kwa kuonesha kunijali."
alijibu kiunyenyekevu Hussein wakati huo mke wa mzee Mwinchande alikuwa anashuka ngazi akitokea sehemu za juu ya nyumba yao na kama kawaida yake Hussein alipokutanisha tena macho na mama Shebby moyo ulimripuka tena na safari hii kuna kitu chengine alikiona ambacho kiliustua zaidi mtima wake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alibaki amemkodolea macho mama Shebby ambapo kikubwa alichokuwa anshangaa Hussein ambacho alikigundua ni alama ya baka la mstari mweusi juu ya paji lake la uso eneo lilipoanzia nywele kuota.
Alama hii safari hii aliiona vizuri baada ya ushungi aliojifunika mke wa mzee Mwinchande (mama Shebby) kufunuka bahati mbaya na alikuwa hajavaa kiremba kama ilivyokuwa kawaida, na hata chanzo cha kuvaaga kiremba Zai ilikuwa ni kwasababu ya kuficha baka la mstari pale juu ya paji la uso ndio maana ufungaji wake Kiremba ulikuwa wa kipekee sana, sasa imekuaje na mama Shebby nae awe na mitindo ya kufunga kiremba kama Zai harafu kumbe na yeye ana baka la mstari mweusi?
("Mh! hapana sasa nina wasiwasi")
alijisemea moyoni Hussein na kumuaga kwanza mzee Mwinchande akizuga kwenda chooni lakini ukweli hakuwa na haja yoyote zaidi alienda kukaa kufikiria kile alichokuwa amekiona pale nyumbani kwa mkwewe Kamishna Shebby.
("Inakuaje kuaje mama Shebby afanane vitu vingi na mke wangu Zai? au ni kweli yeye huyu! Eee Mungu naomba unisaidie nipande ufumbuzi wa uhakika wa hili suala")
aliwaza na kuomba kimoyo moyo Hussein pindi alipokuwa chooni akilifikiria sana lile jambo na alijaribu kukumbuka mambo mengi aliyokuwa anayapenda mkewe Zai kipindi hiko ili iwe rahisi kuzidi kuyapima na kuyafuatilia kwa mama Shebby kama kuna uwezekeno wa kufananisha mambo mengine zaidi.
("Mh! lazima nifanye hivi nione, ina maana kama kweli huyu ni yuleyule Zai mke wangu basi naamini babaake Shebby ndie adui angu Mr X mwenyewe. Mh!! lakini sasa mbona babaake Shebby haoneshi hata chembe kama ana moyo m baya? hafanani hata kidogo na vitendo vya mwana izaya Mr X.")
aliendelea kufikiria Hussein na hatimae alitoka kule chooni na kurudi sebuleni alipokuwa Mzee Mwinchande na kuendelea na maongezi yao.
"Basi inshaallah mzee mwenzangu, wewe tulia kisome kwa umakini sana hiko kitabu tuwe tunajumuika wote hapa kuswali suna za usiku na faradhi ya alfajiri"
"Nashukuru kaka, usihofu."
* * * *
Siku zilienda huku fukuto likizidi kufukuta kifuani na kichwani mwa Hussein juu ya kumtilia mashaka siku baada ya siku mama Shebby ambapo safari hii kila ile tabia sugu aliyokuwa anaikumbuka kuwa Zai alikuwa nayo alibaini kuwa hata mamaake Shebby alikuwa nayo na hii ikazidi kumpa uhakika wa asilimia nyingi kuwa akitafutacho ndicho akionacho.
Lakini uzito wa kuamini hilo unakuja pale kila jinsi alivyomtazama mzee Mwinchande alkuwa hafanani kabisa kuwa ni mtu mwenye moyo wa kikatiri na roho mbaya kama alivyo mr X kwani kama kweli mamaake Shebby ni Zai basi bila shaka babaake Shebby ni Mr X na hata akiwa siye bado Zai atajua wapi alipo kwa kuwa katika maneno ya mwisho ya mke wake Zai kabla hajapoteza fahamu baada ya kupigwa na kitu kizito siku ile walipovamiwa na Ninja wa mr X pindi walipokuwa wanaelekea kwa baba mkubwa ambae alikuwa mganga mzee Mnyungunyungu.
Lakini bado swali lengine lilikuja kichwani mwa Hussein bubu kama basi yule atakuwa Zai harafu yule mzee Mwinchande asiwe Mr X hivi usalama wao ungekaakaa vipi miaka yote hadi wanafikia pale wakati yeye tu aliponzwa kwa kuishi na Zai tena alikuwa mkewe kabisaa lakini bado Mr X alimfanyia matukio makubwa na wote waliokuwa na habari walau za tetesi kuhusu mr X waliuawa.
Sasa inakuaje kwa mtu anayejua kila kitu kuhusu mr X akaachwa hai hadi muda ule wakati mr X mwenyewe bado yu mzima?
Maswali yalikuwa mengi sana kwa Hussein babu bubu na kila alipoamka na kuwa anasalishwa na mzee Mwinchande yeye mawazo yake yalihama kabisa akiwa haamini kile akifikiriacho na mara akawa anaamini lakini bado akawa anaomba Mungu azidi kumpa uyakinifu zaidi katika lile swala na kila siku alitamani kumuuliza mama Shebby jina lake harisi ni nani lakini alishindwa wala hakujua aanzie wapi.
Baada ya siku saba fungate la kinyumbani nyumbani la Dokta Asha na Kamishna Shebby liliisha na kufanikiwa kuondoka na mkewe kuishi kwele yale makazi aliyoandaliwa na serikali kule karibu na gereza ambapo kulikuwa na nyumba za kisasa zilizojengwa na serikali kwa niaba ya makamishna wote nchini.
Na ulipotimu ule usiku ambao Shebby aliondoka Hussein bubu alipatwa na ndoto ya maajabu sana........
'''''''''
(^^"Tumuue tu mke wangu.^^")
(("^^ Hapana mume wangu kwa adhabu ya awali imetosha mbonaa!?^^"))
(^^"Hapana mke wangu atatusumbua huyu tusipofanya haraka."^^)
(("^^Mh ! sidhani kwani wewe unatakaje^^")
(^^"Vizuri, chukua dawa hii ujitahidi ifike kwenye chakula atachokula au maji atayokunywa hapo ataanza kumung/unyuka taratibu na hatochukua miezi mitatu atakufa"^^)
(("^^Haya ila moyo unaniuma daah!^^^"))
(^^"Usiumie Zai mke wangu"^^)
''''''''''
"Hee!"
alikurupuka Hussein mara baada ya kumuota mama Shebby na mzee Mwinchande wakijadili suala la kumuua.
Alikaa kitandani huku akihema na kuifikiria ndoto ile na pale pale lilimjia wazo atoke anyate kuelekea juu chumbani kwa mzee Mwinchande na Zai lakini hakujua aende kufanya nini ila alijikuta moyo unamsukuma atoke aende huko.
Aliangalia saa ilikuwa ni saa saba za usiku ndipo alipoanza kufungua mlango na kunyata taratibu kuelekea kule juu kulipokuwa na chumba cha mzee Mwinchande na mkewe.
Katika hali ya ajabu na mshangao mkubwa Hussein pindi alipokaribia tu kumbe muda huo mzee Mwinchande na mkewe walikuwa hawajalala wala hawakuwa chumbani zaidi walukuwa kwenye korido moja ya kisasa pale juu iliyotengenezwa kwa niaba ya kupumzika na kula kipupwe cha upepo wa bahari.
Kilichomstua zaidi Hussein si kutolala kwao bali ni maneno waliyokuwa wanaongea.
"Unaona Zai mke wangu, hii picha ya video ni siku ilee, hapa nahisi ndio alikugundua na kujifanya anaenda chooni kujisaidia kumbe kufikiria tu kwa kile alichoanza kukihisi. Nilikwambia mapema mke wangu, sasa acha kwanza nimpofue ili iwe rahisi kumpoteza jumla"
aliisikia vizuri kauli hii ya mzee Mwinchande iliyomfanya agande kwa mshtuko wa hasira na maumivu ya ajabu baada ya kujua ukweli sasa kumbe yule ni kweli Zainab mkewe na mzee Mwinchande ni Mr X.
Alianza kunyata taratibu Hussein bubu huku mapigo yake ya moyo yakienda kasi kupita kawaida akiwa haamini kabisa kama kweli leo hii amemtambua adui yake kwa mtindo ambao hakuwahi kuufikiria hata siku moja wala kuuota.
Alifanikiwa kufika mwisho wa ngazi taratibu na kuendelea kunyata kwa umakini mkubwa na kilichomsaidia zaidi alikuwa pekupeku ambapo mara alipofanikiwa kuukuta mlango wake na kuingia ndani tu aliufunga taratibu na ndipo alipofanikiwa hata kushusha pumzi ambayo alikuwa kaibana muda wote alivyokuwa ananyata kurudi mara tu aliposikia sauti ya mzee Mwinchande na mama Shebby ambae sasa aligundua kuwa ni Zainab yule yule mke wake wakijadili juu ya kumuua.
"Uuuuuphhhhhhhhh"
Alihema kwa nguvu Hussein huku akiwa kaegemea ukuta wa pale chumbani pindi alipoufunga mlango na kujikuta akisota kwa mgongo taratibu mpaka akakaa kitako pale chini huku mikono kiwa ameiweka kichwani.
("Heeee! Mungu kumbe muda wote niko katika chaka la Simba mla watu aliyevaa ngozi ya kondoo? hapana aaa uuupphhhh")
aliongea moyoni Hussein huku machozi yakimtoka akiwa anasugua sugua mikono kwa nguvu pale chini lakini mara aligundua kitu kilichomfanya ainuke haraka na kuzima taa kisha kujilaza kitandani moja kwa moja na kujifunika mwili wote.
("Huyu ni mshenzi mwenye mbinu nyingi sana, kama aliweza kunitegea kamera chooni nadhani hata humu chumbani kamera haikosi, sasa hapa inabidi niwe makini kabla hajawahi kunistukia kama nimemstukia ili niweze kumuua kiurahisi. Lakini nitamuua ua vipi mshenzi huyu? Aaaah.. Kivyovyote lazima nimuue. Naamini Mungu aliyeniotesha haya na kunnikutanisha nae ndie atayeniongoza na kunionyesha njia rahisi ya kummaliza huyu mshenzi loh! Kumbe mr X ni babaake kijana aliyenisaidia kutoka jera? au isije kuwa ndie Mwinshehe wangu?")
aliwaza Hussein na kufika mbali zaidi mara alipotia shaka isije kuwa na Kamishna Shebby akawa ndie Mwinshehe, jina la mtoto wake alieuawa akiwa na miezi minne tu.
("Zainabu...Zainabu...Zainabuu Mke wangu kumbe hukufa? aaaagh! Wanawake ni Wauaji kweli aaaaagh, au kwa sababu uliniona masikini Zai, si ungenambia tu nikuache uende salama nami nibaki salama...!!! Aaaaagh! Eeeeh Mungu kwaniniii Kwaniniiiiiiiii??!!!")
aliendelea kusema na moyo wake Hussein huku machozi yakimtoka mfurulizo na moyo kumuenda mbio kupita kawaida.
Mwili wote wa Hussein bubu ulibadilisha homon ghafra na kuanza kutetemeka kwa hasira mithili ya mgonjwa wa homa aliyemwagiwa maji ya baridi.
("Aaaagh! Zaiiii...Zaiii... Zaii!!!!? siaminiiiii aaaaaaaaaaaagh. Wanawake ni Wauaji..... Wanawake ni Wauaji..... wanawakeeeee!?")
(..........................) (.......................) (......)
(..."Zai ulijua kumbe ile barua ni ya nani lakini ulikanusha Zai? aaagh! Ulinipa moyo nipuuze kumbe kila kitu ulijua... aaagh! umemgeuka mumeo kwa ajili ya tamaaa kwa mtu baradhuli na katili kama huyu? Eti Mr X. aaaaagh! Samson alimuamini Delila kuwa mwanamke anayempenda bila kujua kumbe Delila anatumiwa kumchunguza na maadui zake. Yaliyokuja mkuta Samson mwanaume yeyote kweli yanaweza kumkutaaa. Zai!!!? Lazima nawe ufe")
Uchungu na mawazo aliyokuwa nayo Hussein uliendelea hadi pale alipostuliwa baada ya mlango kugongwa.
"Nani?"
aliuliza Hussein kwa sauti iliyojaa mikwaruzo.
"Swalaaa swalaaa.. Salaaa. swala ni bora kuliko usingizi"
aliisikia sauti ya Mzee Mwinchande akimuamsha waende wakasali na kugundua kuwa tayari ilitimu alfajiri.
("Kum**aako lazima Nikuue Mshenzi wewe.")
aliongea moyoni kwa hasira na kushuka pale kitandani hussein na kuwasha taa ili ajiandae kwaajili ya kuungana na adui yake katika kumuomba Mungu (kusali) pamoja.
* * * * *
"Mme wangu, mme wangu Nakupenda sana"
"Hata mimi nakupenda sana mke wangu Asha"
"Lakini sidhani kama nastahili upendo huo"
"Kwanini usistahili sasa! Unastahili kabisa na una haki nikupende zaidi ya hapa"
"Kweli?!"
"Kweli kabisa mke wangu. Kwanini unaniuliza hilo?"
"Kwa sababu nina wasiwasi."
"Wasiwasi!!? wasiwasi gani tena mke wangu.. Ondoa wasi kabisa Asha siwezi kuja kukutenda kwa mwanamke yeyote yule. Kwako mimi nimefika kabisa kama ni meli imetia nanga."
"Najua ni rahisi kusema hivyo kwa sasa, lakini sidhani kama kila siku utasema hivyo. Naamini kuna siku utanichukia kupita kiasi na nina wasiwasi utaniua."
"WHAT!!?"
Alistuka Kamishna Shebby baada ya kusikia kauli ile ya Asha pindi walipokuwa wanazungumza alfajiri ile wakiwa kitandani.
"Asha baby, mbona leo umeamka ukiwa na maneno makali sana?"
"Kwasababu ya maumivu baby"
"Maumivu? yapi tena"
"Ya mshono tuu"
Alizuga Asha pindi alipotaka kumwambia ukweli Kamishna Shebby juu ya yote ambayo hakuyajua kuhusu yeye lakini alijikuta anaamua kumkwepa baada ya moyo wake kuwa mzito ghafra na kushindwa jua aanzie wapi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Pole sana baby, sasa maumivu yako ya mshono ndio yasababishe nikuchukie? niache kumchukia mshenzi mr.........."
alisita Shebby baada ya kutaka kuropoka juu ya mr X na kukumbuka kauli na ushauri wa Cj4 kuwa asimzungumzie wala kumtaja Mr.X hata kwa mkewe ama wazazi wake bila kujua huyo anayemficha anajua mengi zaidi ya anavyomuona.
"Unasema umchukie Mr..!!? mr. ndio nani?"
aliuliza kimakusudi Asha na kuzidi kumpoteza kisaikology Shebby aliyeamua kutunga uongo wa palepale ambao Asha alijifanya kuukubali.
Maisha yao mule ndani kila mmoja alikuwa na siri ambayo mwengine haijui na mtu aliyekuwa anawaunganisha kwenye hiyo siri kila mmoja hajui kama mwenzake huyo mtu anamjua ama anawasiliana nae, na wote kwa pamoja walimuamini sana huyo mtu na kumsikiliza kutokana na mioyo yao kukiri kuwa huyo mtu amewazidi kila kitu kuanzia mbinu hadi uwezo wa kupambana kimwili.
Na hakuwa mwengine huyo mtu bali ni Komandoo aliyeaminiwa kati ya makomando kutoka Jwtz naye ni Komando Jumanne au Cj4. ambae sasa nae aliwaingiza kwenye mchezo Shebby na Asha baada ya kugundua siri ambazo aliona ili apate majibu inabidi acheze mwenyewe mchezo kama alioutengeneza Mr X ule wa vipofu lakini tofauti yeye aliwaweka vipofu rafiki zake, watu asio na visasi nao na kwa sababu maalum zenye faida kwao wote
Siku hiyo tofauti na siku zote Kamishna Shebby alitoka alfajiri sana majira ya saa kumi na moja kasoro na baada ya Kamishna Shebby kutoka tu ndipo Asha alipoamka haraka na kuchukua simu yake na kupiga tena ile namba ya siri aliyopewa na Cj4 kule hospitali kwa shauku akiwa anataka ushauri kwa Cj4 nini afanye juu ya ukweli anaouficha kwa mumewe juu yake na mr X.
["Hallow kaka Inspekta"]
aliongea Asha mara baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
[["Lady Ninja, leta ripoti ulichopata."]]
ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Asha ashushe kwanza pumzi baada ya kuona yule mtu ambae yeye alikuwa anadhani ni Inspekta kuwa anajua mengi sana kuhusu yeye hasa baada ya kusikia anamwita Lady Ninja.
["Naomba unisaidie ushauri kwani natamani kumwambia ukweli mume wangu lakini nahisi huu ukweli unaweza kuwa ndio mwisho wa upendo baina yetu isitoshe nami nampenda kweli sasa. msaada tafadhali huu uongo unaniumiza nafsi"].
[["Hupaswi kuwa na haraka kumwambia sasa, unachotakiwa uwe unakwenda mara kwa mara kule kwa wakwe zako naamini sasa Mr X rada yake haipo kwenu kwanza ipo kwa babaako."]]
aliongea Cj4 na kumpa maelekezo yale Asha ambae aliyakubari kwa moyo mmoja na baada ya kukata simu alianza kutafakari yale maneno ya Cj4 kuwa kwanini Mr X sasa hana habari na wao bali ataendelea kwanza kudeal na Hussein ambae ni babaake aliyekuwa kule kwenye Jumba kubwa la mzee Mwinchande?
("Mr X sawa anadeal na babaangu, lakini kwanini Inspector ananambia niende mara kwa mara?! Mh!! nina wasiwasi na haya maneno kitaalam kama anamaanisha mr X hayuko mbali na pale..!")
aliwaza Asha baada ya kukata simu.
Wakati huo nae Shebby alikuwa njiani akienda huko huko kwa Cj4 kama kawaida toka amefariki Kimaro na kupona kwake mguu hakutaka kabisa kuendeeshwa hata alipobembelezwa na serikali kutokana na heshima aliyokuwa ametunukiwa lakini alikataa katakata na alifanya hivi kutokana na mission zake za siri sambamba na Cj4.
Shebby akiwa kwenye gari yake mawazo yote alifikiria sana mazungumzo ya mkewe na aliona kama kulikuwa na kitu cha zaidi alichotaka kusema yule mwanamke lakini alighairisha ghafra na kuzuga story nyengine na kumbe Shebby hata alivyokuwa anamuitikia haikumaanisha alikuwa hajastukia kama kuna kitu Asha alikuwa ameficha lakini alichofikiria kwa nini anaficha?
Lakini kwa kuwa alikua na mtu wanaesaidiana kwenye mission yao ya kumnasa mr X na kwa sababu ya kuamini huyo mtu ana uwezo mpana sana wa mbinu na fikra aliamua kwanza kukutana nae alfajiri amuelezee na kile alichokuwa anakihisi yeye ili wapate ufumbuzi zaidi wa mambo.
Ulikuwa ni ujanja wa Cj4 alioutengeneza kwa Shebby na Asha na sasa ilikuwa ni yeye tu anawacontrol wote wawili pasi na kujitambua wenyewe.
Asha ametoka kuongea nae na mara alipokata simu hazikupita dakika ishirini na Shebby nae aliingia.
* * * *
"Asalamu alykum bwana, swala muda ndio huu Mwenyezi Mungu anatuamuru tuamke tumuombe nae atatujibu..."
aliongea mzee Mwinchande mara baada ya Hussein kufungua mlango na kutoka.
"hahaaa Kweli kabisa daah!"
alijibu Hussein kwa kujichekesha machoni lakini moyoni alikuwa na hasira kupita kifani juu ya mzee Mwinchande baada ya kumgundua kuwa ndie alikuwa mr.X mwenyewe.
Lakini kilichomsaidia Hussein ni vile jinsi alivyoweza kuyaficha ya moyoni na kuvaa uhalisia wa kitu tofauti kabisa na hii kwa kuwa alijua mtu hatari mr X yupo mbele yake kwa hiyo itakuwa hatari zaidi kama akiwahi kugundua yaliyo moyoni mwake.
Walisimama sehemu ile ya kusalia na mzee Mwinchande alisimama mbele yake akiwa ndie Imam (kiongozi wa sala) huku Hussein bubu akisimama nyuma ya mzee Mwinchande akiwa maamuma (muongozwaji wa sala) na hapo ndipo Mwinchande alipofungua sala.
"Allaaaaaaaahu Akbaaar." (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)
alitamka mzee Mwinchande na Hussein aliongoza vile japo moyo ulimuuma na kujikuta machozi yanaanza kumdondoka tena kipindi Mwinchande akisoma pale mbele kuiongoza sala yao.
("Yaaani nakubali kabisa kusalishwa na adui yangu? Yani eti nimuombe Mungu pamoja na adui yangu tena yeye ndie awe ananiongoza kumuomba Mungu? hapana... Hapanaaa")
aliongea mwenyewe Hussein moyoni mwake huku akimuangalia mzee Mwinchande kwa hasira pale mbele akijaribu kutafakari nini amfanye ili aweze kutimiza azma yake na nafasi aliyoiomba zaidi ya miaka ishirini?
Nafasi ambayo aliona ndio ile leo hii iko mbele yake na mr X adui yake aliyesubiri muujiza wa kumjua utokee kwa miaka mingi na sasa imekuwa hivyo yuko mbele yake na amempa kisogo.
("Inawezekana bahati hii nisiipate tena akaja kuniwahi huyu mshenzi.")
alifikkiria tena Hussein huku akigeuka geuka kutazama maeneo yale yalivyokaa kaa akiwa kama mwenye kutafuta kitu wakati sala ilipokuwa inaendelea na alijua kwa upande wake lile jambo la kugeuka geuka tayari lilikuwa lishamuharibia sala lakini aliona yuko sahihi kwani hawezi akasalishwa na shetani harafu hiyo sla ifike kwa Mungu.
Aliamini kabisa mr X ni shetani wala hapaswi kabisa kuishi na aliamini kuwa asingeweza kuendelea kuvumilia kwa siku tatu zaidi bila kustukiwa na mr X kilichokuwa moyoni mwake.
Na katika kugeuka geuka kwake hatimae alibahatika kukiona alichokuwa anaaangaza angaza macho kukitafuta na hakikuwa chengine bali ni kipande cha chuma kilichokuwa kinatumiwa kwaajili ya kupasulia nazi na alikiona jana yake usiku pindi yule mfanyakazi wa ndani alipokisahau kukirudisha sehemu husika mara baada ya kukitumia kipindi akiangalia filam kwa sebuleni na kukisahau juu ya sink dogo karibu na mlango wa jikoni nyuma kidogo na eneo walilokuwa wanasali.
("Shabbashhhhhh, najua hii yote ni Mungu amemfanya yule bint kukisahau na kunikumbusha mimi nikitumie kama silaha ya kummaliza adui wa watu aliyesimama mbele yangu")
aliongea Hussein wakati huo walikuwa wamesimama tena baada ya lakaa (sujuda) ya kwanza ambapo mzee Mwinchande akiwa hana habari aliendelea kusoma kwa madaha kabisa taratibu bila kujua wala kuhisi nini kinaendelea nyuma yake ambapo Hussein bubu alikuwa ananyata taratibu sana kinyume nyume hadi kulipokuwapo kile chuma na kukikamata kwa nguvu na kuanza kunyata tena kumsogelea mzee Mwinchande huku mapigo yake ya moyo yakizidi kasi kadri alivyozidi kupiga hatua hadi alipofika mita chache kabisa na kujiandaa kwa nguvu zote kumshambulia adui yake.
("Leo ndio Historia inaandikwa.")
aliongea kimoyo moyo na kujihesabia mwenyewe Hussein lakini mara ghafra alistuka kusikia sauti ya miguu ya mtu akishuka ngazi kwa haraka kutoka juu kuja kule sebureni tena akiwa anakimbia.
"Mume wanguuu Mume wanguuuuuu Babaaaaa......"
alikuwa ni Zainab mamaake Kamishna Shebby akikimbia kuwahi kule chini mara baada ya kuona kinachotaka kutokea kupitia kwenye screen yao maalum iliyokuwa chumbani inayoonesha maeneo ya nyumba ile kupitia kamera ndogo zilizotegwa kila kona kwaajili ya usalama na kurekodi kila kinachoendelea mule ndani.
Lakini pindi anatoa ule ukelele kumpa tahadhari mzee mwinchande ambae alikuwa anajiandaa kusujudu ndipo Hussein bubu alipowahi kwa kumtandika vyuma vya kichwa mfurulizo na kwa nguvu zote.
"KUFAAA KUFAA KUAFAA"
Alipiga kelele Hussein kipindi anamshambulia mzee Mwinchande kwa nguvu zote mpaka walipodondoka pale chini ambapo kwa sekunde zisizozidi arobaini tayari damu nyingi zilikuwa zinamvuja mzee Mwinchande aliyekuwa anapapatika sebule nzima huku Hussein bubu akiwa kamng'ang'ania bado anampelekea dozi ya kutosha kwa kumpiga kwa nguvu na kile chuma hali iliyosababisha sasa damu kuwa inamrukia Hussein na mbaya zaidi alianza kupasua hadi fuvu la kichwa.
"Hoooooooooooooooooooooooooooooooooo..."
alipiga kelele na kuanguka pale mwisho wa ngazi Zainab huku akiwa haamini kile alichokuwa anakiona kikitokea mbele ya macho yake.
"Uuughhhhrrrrr..Ughhhrrrrrr.."
alikoroma koroma kwa nguvu Mwinchande kila Hussein alivyokuwa anamporomeshea kipigo cha kihistoria.
"Kufaaaaaaa Mshenzi weweee kufaaaaaaaa, Kufaaaaaaa"
alikuwa nusu kapagawa Hussein na alizidi kupata nguvu pindi alipokuwa anatoa dozi kwa mzee Mwinchande ambae sasa alionesha wazi tayari alikuwa anamalizikia roho huku akiwa amepasuka vibaya sehemu za kichwani na paji la uso damu zikiwa zimetapakaa sehemu ile ya kusalia hadi maeneo ya jikoni katika kikirikakara zilizokuwa zinaendelea.
Kelele za Zainab na Hussein ziliweza kumuamsha dada wa kazi aliekuwa chumba cha chini karibu na jiko ambapo alipotoka hakuamini kile kilichokuwa kinaendelea mara baada ya kumshuhudia Hussein bubu akiwa anamshambulia kwa nguvu zote mzee Mwinchande pale chini huku kwa mbele maeneo ya ngazi zilizoelekea vyumba vya juu alionekana mamaake Kamishna Shebby akiwa ameanguka huku kaishiwa nguvu akilia bila kutoa sauti.
Ubaya wa nyumba ile ilivyotengenezwa ni kuwa na vioo vya tinted pia madirisha yalikuwa hayafunguliwi kutokana na AC iliyokuwa inawashwa masaa 24 na kama ukitaka upepo halisia unapandisha sehemu za juu kabisa, na kwa sababu hiyo hata walinzi waliokuwa nje hawakujua chochote kilichokuwa kinaendelea ndani.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
["Hlloooo, halloooooo, halooo kakaa shebiiii babaaa hukuuu aaaah muwahi babaaaaanakufaaaa... "]
aliongea huku nae akilia yule msichana wa kazi mara baada ya kukimbilia tena ndani mwake na kuamua kumpigia Kamishna Shebby kumpa taarifa ili awahi kuja kutoa msaada kwa kile kilichokuwa kinaendelea pale.
"HAHAHAHAHAHAHAHAAAAA"
alicheka kwa nguvu Hussein mara baada ya kuona Mzee Mwinchande katulia na kaacha kupapatika.
"hahahahahahahahahahaaaaa"
Alicheka tena huku safari hii akimpiga piga kwa nguvu sehemu za mdomo na kuanza kumvunja meno bila kujali hata zile damu zilizokuwa zinamrukia huku akiwa na Furaha ambayo toka anaingia Jera hajawahi kufurahi kwa nguvu Hussein kama siku hiyo.
"ASANTE BABA MUNGU"
Aliinua kichwa juu na kushukuru Hussein bubu kwa kuona ile ndoto yake na maombi kuwa aje kumuua Mr.X kwa mikono yake muda ule ilikuwa imetimia na hatimae kweli Mzee Mwinchande ambae ndie alikuwa Original MR.X aliuawa kwa mikono ya Hussein babu bubu baada ya usumbufu wa zaidi ya miaka 28.
Baada ya Hussein Kuhakikisha hakuna Jipya tena kwa Mr X aliinua uso wake na kumtazama mama Shebby pale chini ambae alikuwa amekosa nguvu kabisa hakuweza hata kunyanyuka zaidi ya kuwa anasota kuelekea juu ya ngazi zile kwa hofu huku akilia mara baada ya kumuona Hussein amenyanyuka kwa hasira na macho yote alikuwa kayaelekeza kwake.
* * * * *
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment