Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

ROHO ILIYORUDI KUANGAMIZA - 5

 





    Simulizi : Roho Iliyorudi Kuangamiza

    Sehemu Ya Tano (5)



     Akiwa ameshaingia katika geti la hospitai hiyo kabla hajaivuka kaunta, Mwarami naye akawa nyuma.

    "Heri umewahi"

    Wakaongozana moja kwa moja mpaka katika wodi ya Jabir.

    "Niwie radhi kwa kuhartibu usingizi wako ndugu. Ila hali inazidi kuwa tete na mauzauza yanazidi kuongezeka mpaka nyumbani kwangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akamuhadithia yote yaliyotukia chumbani kwake. Jabir akionesha kuzidi kushangaa jambo hilo. Hakujua chochote cha kuwasaidia watu hao walionesha kuhamanika kwa mambo yaliyokuwa yakiendelewa.

    Mambo yaliyokuwa yakifanywa na Jenifa.

    "Nahitaji twende alipokuwa akiishi Jenifa"

    "Dada yangu!" Jabir aklishanbgazwa na sauti hiyo thabiti iliyomtoka Regina "huoni kama ni usiku na kesho ndiyo nilikuwa naruhusiwa, kwanini usingesubiri basi mpaka kesho?"

    "Unataka nife?" Aliuliza kwa wahka kiasi na macho ya hasira yakawa yamemtoka pima "ni lazima twende usiku huu"

    Regina akamgeukia Mwarami.

    "Huyo dada wa mapokezi hapo atatusaidia kupata joho la kitabibu na kutuwezesha kutoka nje ya geti bila maswali" alimgeukia tena Jabir kisha akahamia tena kwa Mwarami "inaonesha ni mwenye njaa" akapiganisha kidole chake cha kati na kile gumba na kusema "ukipenyeza tu rupia kidogo haongei kitu"

    Mwarami akatoa tabasamu na Regina naye akalipokea.

    Dakika chache baadaye, Regina akarudi akiwa na vazi la kitabibu. Akamtupia Jabir begani, akamwambia

    "Vaa hilo na tutatoka hapa kuelekea alipokuwa akiishi Jenifa"

    Nusu baadaye wakawa katika barabara ielekeayo Mbatini baada ya kumpita yule mlinzi wa getini bila maswali. Jabir akasema

    "Nyumba yake ipo ndani ndani gari haiwezi kufika"

    Wakashuka na kuanza kukatiza mitaa mpaka pale walipoifikia nyumba ambayo Jabir alisema

    "Ni hapa"

    Haikuwa nyumba yenye kuonesha uafadhali wa kipesa au afadhali ya maisha ni nyumba iliyotangaza umasikini na njaa kali kwa yoyote aliyeishi ndani ya nyumba hiyo.

    Lakini Regina aliifahamu.

    Aliitazama kwa makini nyumba hiyo na mtaa ilipo alijihakikishia ni yenyewe na wala mawazo yake hayakumdanganya. Haikuwa na umeme.

    Walipobisha hodi ya tatu, ndipo walisikia sauti uya kiuchovu kutoka chumbani ikiitikia. Wakiwa bado wamesimama hapo hapo mlangoni, waliisikia sauti ike ikitokea dirishani.

    "Nani wewe?"

    Jabir akaitikia "ni mimi shangazi"

    Mlango ulipofunguliwa, mbele yao akasimama mwanamke wa makamo aliepoteza nafasi huru ya kuitwa kijana. Alikuwa akiwasaili wageni hao kwa kuwatazama kwa zamu lakini alimfahamu au kumkumbuka jabir peke yake. lakini Regina alimfahamu labda yeye hakumkumbuka Regina.



    ...



    Baada ya kukaribishwa ndani Regina aliendelea kushangazwa na nyumba hiyo. Aliifahamu vizuri na alikuwa mwenyeji sana hapo kipindi cha nyuma.

    Wakakaribishwa katika makochi kuu kuu ya nyumba hiyo huku wakisaidiwa kuonana na mwanga wa kibatari kilichowashwa mwanzo na Bi Faudhia na kuwekwa juu ya stuli.

    "Shangazi huyu ndiye yule mama niliyekutana naye akiwa na marehemu binamu yangu Jenifa katika mazingira ya kutatanisha"

    Jabir alikuwa ameshamueleza kila jambo lililotukia shangazi huyu ambvaye inasemekana ndiye mama wa Jenifa.

    Bi faudhia akaanza kulia. Alilia kwa uchunbgu kutokana ana kuhisi kama aliyetoneshwa kidonda chake kilichoanza kupona. Bi faudhia alimpenda sana Jenifa, nadhani kuliko kitu chochote. Ndiyo maana kila alipojaribu kukumbuka tukio lililomkuta binti yake, alitokwa na machozi. Tumbo la Bi Faudhia lilinuna kutoa mtoto. Mimba tano alizozitoa ya sita ikatoka na kizazi. Wanaume walimkimbia kutokana na kutowatimizia haja yao ya kupata mtoto. Aliumia sana mpaka pale alipompata Jenifa akiwa mlangoni pake. Akaanza kuhadithia kifo kibaya kilichopokonya uhai wa Jenifa.

    "Ilikuwa jumapili katika shamba la kaka yangu. Alikutwa amenyofolewa kichwa na wala hakikuonekana kichwa hicho. Alikuwa uchi kama alivyozaliwa" akaanza upya kulia. Ilibidi wanyamaze na kusubiri ili waone kitakachoendelea katika simulizi hiyo. Regina aliendelea kuchanganyikiwa kwa kuwa hakufahamu ni vipi Jenifa aingiliane na kumbukumbu zake za hapo zamani. Nyumba hiyo aliifahamu na Bi faudhia alimfahamu, ni vipi salome aingiliane na Jenifa?

    Kikawa kitendawili kizito kwa Regina.

    "Mtoto mwenyewe hakuwa wangu ila nilimpenda kama niliyemzaa mwenyewe. Jenifa wangu wamemuonea jamani. Mama yake alimtupa na kijibarua kisicho na maana yeyote na watu wabaya wamemuaa bila sababu yeyote"

    Bi Faudhia alilia kwa uchungu na kilio kikapamba moto. Ni hapo jambo la kushangaza likatukia. Regina naye akapaza sauti yake kwa kilio huku akishika papi zake. Hakuna ambaye hakuacha kushangaa kati ya Jabir na Mwarami.

    'Sawa inawezekana kukosa mtoto kwa mama huyu kunasababisha kumtonesha kidonda Regina, sasa ndio alie kwa uchungu namna hii?' Mwarami akajiuliza.

    Mwarami hakufahamu siri nzito aliyoificha Regina katika uvungu wa moyo wake. Hakufahamu ni nini kilifanya alie baada ya kusikia hadithi hiyo inayomuhusu Jenifa.

    Regina akaomboleza.





    Regina aliomboleza kwa kuwa kila kilichoongelewa hapo kilimgusa. Licha ya kumgusa pia vikamuumiza. Vilimuumiza kwa kujua kuwa Jenifa ndiye mtoto wake.



    Hapo zamani kipindi cha miaka ishirini na sita iliyopita, Regina alikamata ujauzito akiwa shuleni. Regina huyu wa mwangani sio yule afanyaye mambo yake gizani. Hivyo haikuwa rahisi hata kwa rafiki yake, Batuli kufahamu undani halisi wa Regina. Tumbo lake dogo likamsaidia kutoonesha mimba iliyojikita ndani yake kwa miezi mitano. Akakimaliza kidato cha tatu.



    Ilimbidi kukaa nyumbani mpaka atakapojifungua akamalizie masomo yake ya sekondari.



    Baba na mama yake wote walikuwa wakimsikitikia kwa jambo hilo. Alikuwa ni binti wa pekee kwao, hivyo hata ukali wa baba yake ukapungua kwake alipokosea. Licha ya Regina kusamehewa yote hayo na jambo hilo kutochukuliwa kiuzito na familia yake yeye akapanga jambo la kusikitisha.

    "Nitazaa na kumtupa"



    Regina aliumizwa na hisia za kukataliwa na baba wa mtoto aliye ndani ya tumbo lake. Kijana yule aliyempa moyo wake wote alicharuka na kuwa simba aliyejeruhiwa alipoambiwa kuwa

    "Kelvin, nina ujauzito wako"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo ikawa pia ndio mwisho wa kumuona Kelvin.



    Regina hakutaka mtoto wake apate shida. Alifanya utafiti wa wapi atakapompeleka mara baada ya kumzaa. Wapi atakapomtupa iwe sehemu salama.

    'Faudhia'



    Jina la dada wa jirani likampitia. Alimfahamu dada huyo kwa mbali tu wala hajawahi kukaa pamoja wakazungumza. Alifahamu historia yake kupitia kwa msichana wao wa kazi.



    "Aliolewa kwa kuwa kwao masikini. Hawana kitu shoga. Yaani dhiki imewakithiri na kuwakuna kama sio kuwaadhibu mwenzangu"

    Huku wakigongeana Sadah akaendelea kuongeza udambuudambu kwa mbwembwe "wazazi wakamshinikiza aolewe aondoe baa la njaa nyumbani mwenzangu. Kumbe bi dada hana kizazi. Amezaliwa hivyo tangu kwa mama yake. Bi shosti anatafuta mtoto kwa tabu yule"

    Regina akaitikia kwa masikitiko

    "Masikini!"

    Sadah akaendelea kumwaga mchele "ndio basi mwenzangu yaani dada wa watu anapata tabu mpaka basi"



    Ilikuwa ni kumbukumbu iliyompitia ghafla tu kichwani. Kumbukumbu ya miezi mingi iliyopita. Ni hapo akaona kuwa ni sehemu sahihi ya kumpeleka mtoto atakayemzaa.



    Siku zikaenda haraka miezi ikahesabika hatimaye masaa na uchungu ukamkamata. Alikuwa peke yake nyumbani, hivyo bahati ya nyota ya jaa iukawa upande wake. Alijikongoja taratibu mpaka hospitali kwa msaada wa dereva taksi na kuingia mpaka wodini.

    Akajifungua mtoto wa kike.



    Alirudi nyumbani peke yake. Mkononi alikuwa na kijikaratasi alichokinunua kutoka kwa daktari aliyedondoka sahihi na muhuri wa uongo kwa malipo madogo ya fedha kwa hongo. Mtoto alikuwa ameshamuacha kwa Faudhia.



    Baba na Mama yake walisikituishwa kutokana na jambo hilo. Lakini wote wakaendelea kuwa na hekima na kusisitiza kuwa yote ni mipango ya mungu.

    Hawakujua.



    Jioni yenye ubaridi mzuri uliofurahisha ukamfurahisha zaidi Faudhia. Si ubaridi tu pekee uliomfurahisha ni hicho alichokikuta mlangoni kwake.

    Kikapu chenye mtoto.



    Alikuwa ni mtoto wa kike aliyeachwa na barua iliyofungwa kwenye nepi yake. Barua iiyosomeka





     Baba na Mama yake walisikituishwa kutokana na jambo hilo. Lakini wote wakaendelea kuwa na hekima na kusisitiza kuwa yote ni mipango ya mungu.

    Hawakujua.



    Jioni yenye ubaridi mzuri uliofurahisha ukamfurahisha zaidi Faudhia. Si ubaridi tu pekee uliomfurahisha ni hicho alichokikuta mlangoni kwake.

    Kikapu chenye mtoto.



    Alikuwa ni mtoto wa kike aliyeachwa na barua iliyofungwa kwenye nepi yake. Barua iiyosomeka



    -naomba radhi kwa kitendo cha kinyama nilichokifanya kwa binti yangu. Lakini sikuwa na jinsi kuliko kumlea bila malezi mazuri. Hii ni zawadi yangu kwenu kwa uhitaji wa mtoto. Naamini kuwa mtamlea vile ambavyo mtoto wenu angepaswa kulelewa kwenu. Naomba mumpende mtoto huyo na kumchukulia kama mtoto wenu. Msiogope na msije mkadhani ipo siku nitakuja kumchukua.

    Ahsante.



    Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Faudhia kumpata mtoto huyo. Ilikuwa ni furaha zaidi kwa Mumewe aliyeanza kupoteza imani ya kufa asiwe japo na mtoto. Alimpenda mke wake lakini hakuwahi kujisikia vibaya kwa mkewe kukosa mtoto. Maneno ya dada zake na mama yake yalimkarahisha.

    "Mtoto huyu atawanyamazisha sasa"



    Akapanga yeye na mkewe waigize mtoto huyo ni wao kwa kuwa wazazi wake na mume wa Faudhia walikuwa wakiishi Maswa, Shinyanga. Hivyo wangeamini kuwa Faudhia amejifungua hivi karibuni. Wote kwa pamoja wakafurahi ujio wa Faudhia nyumbani kwao.



    Kitendawili kikaendelea kubaki kichwani mwa Faudhia, Regina na Mwarami kutofahamu juu ya kifo cha Jenifa ni nani amehusika. Kitendawili kikubwa kikazidi kumuumiza kichwa Regina, ni vipi Jenifa amfanyie Mauzauza?

    ...



    Regina akiwa anelekea ofisini kwake ndani ya gari yake alikuwa ni mwenye mawazo sana. Aliwaza mengi juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea



    Pembeni ya kiti chake kulikuwa na gazeti lililo na picha ya maiti ya Kilaza aliyenyofolewa moyo wake na damu nyingi zikiendelea kumvuja kutoka katika tundu lile.

    Ilikuwa ni picha iliyotisha sana.



    Aliingia ofisini akiwa na mawazo sana. Alimpita katibu muhtasi wake aliyeonekana kuwa ana jambo la kumwambia.



    "Niache kwanza Subira"



    Akiwa amekaa kwenye kiti chake nyuma ya meza pana Subira akawa anaingia na bahasha mkononi.



    "Nimeikuta juu ya meza yangu wakati naingia ofisini bosi na wala sifahamu imefikaje wakati ofisi zilikuwa zimefungwa"

    Ilikuwa ni kauli ya Subira iliyomfanya Regina kutumbua macho pima.

    "Iko wapi?"

    Ilikuwa ni sauti ya hofu iliyomvamia ghafla Regina. Alinyanyuka kitini na kumtumbulia macho Subira, katibu muhtasi wake. Subira akampatia bahasha ile aliyoishika yeye mkononi. Regina akaipokea kwa pupa na kuichana haraka haraka. Bahasha juu iliandikwa Salome.



    "Regina. Najua unafahamu fika kila jambo ulilofanya juu yangu. Kifo changu umekisababisha wewe. Hujui kwa undani juu ya kifo changu. Ukanihukumu kwa sababu unazozijua wewe. Sikupenda kutembea na baba yangu lakini machoni mwa watu nilionekana kufurahia hali ile. Kitu ambacho sikuweza kumwambia kila mtu ni kuwa baba yangu Mzee Kilaza, aliniroga. Sikuwa na akili zangu kutokana na hali iliyokuwa ikiendelea juu ya kurogwa na baba yangu. Sikupendezwa na tabia ya Mzee Kilaza ndio sababu nilianza kumuua yeye. Watafuata vibaraka wako kisha jitayarishe kwa ujio wangu. Jitayarishe kwa kifo chako. Salome Kilaza"

    Barua hiyo iliyoandikwa kwa wino wenye rangi nyekundu, ikamtetemesha sana Regina. Ujasiri na ukatili wa Regina ukapotea. Alihisi machozi yakimponyoka. Kope zake zikalowa mashavu yakawa chapachapa.

    Alikuwa akitetemeka.



    Hali hiyo ilimtisha sana Subira. Kumuona bosi wake akilia halikuwa jambo la kawaida. Anamfahamu Regina kwa muda mrefu. Mwanamke mwenye rojo mbaya na asiye mwepesi kucheka wala kuonesha wazi hisia zake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakika leo amepatikana! Akajinong'oneza kwa kicheko cha ndani kwa ndani.



    Alimsogelea regina aliyejibweteka kwenye kiti chake kama gunia na kuanza kuishiwa nguvu kwa hali ya taharuki iliyomkumba. Subira akaitwaa ile barua kutoka mkononi mwa Regina.

    Akaisoma.



    Kilichoshangaza kwa upande wa subira, alipomaliza kuisoma barua ile, alikuwa akistaajabu kwa furaha. Alishika midomo yake huku furaha ikiwa wazi juu ya uso wake. Kwa furaha aliyoshindwa kujizuia kwayo, alimkumbatia Regina.



    Regina akiwa katika hali ya kulia kwa huzuni, alishitushwa na hali aliyokuwa akiifanya Subira. Hakuelewa kwanini alikuwa akifurahi na kufikia hali ya kurukaruka.

    Regina akamuuliza wa hali ya hasira iliyomkumba ghafla.



    ...



    Abdi babu akiwa na wenzake ndani ya bar wakipata bia mbili tatu, waliendelea kutumia pesa kama walivyokuwa wakijigamba. Hawakupenda tena kufanya kazi kwa kuwa walizozipata kwa mama Regina, zilitosha.

    Abdi Babu na wenzake sita alioendelea kudumu nao katika kazi hiyo haramu, walijitanua na kujulikana sana katika jiji hilo la mwanza.

    "Babu kula pesa achana na machangu kaka" Christian akamwambia kwa sauti ya kuilevi huku akigida pombe kali na kufuta bilauri yake.

    "Achana na mimi" akamjibu kwa kebehi baada ya kubeua akamalizia "hujui kuwa huu ndio urithi wetu?"

    Wote kwa pamoja wakacheka kilevi kisha wakaendelea kutafuna nyama pamoja na kunywa pombe.

    Asubuhi wakati ambao wahudumu wa guest ya Coloured Guest house wakiendea chumba namba 12 alichokuwa amelala Abdi Babu na kimada wake tangu jana usiku, hawakutoka wakikimbia kwa madaha tena kama zamani. Wengi walikimbizana na kupiga yowe la hofu hivyo wakawa wanajikwaa kuokoa roho zao.

    "Amekufa"

    Mmoja ndiye akapata walau nguvu ya kuzungumza. Meneja wa guest ile akakiendea chumba kile kilichotokea mauaji.

    Taswira ya chumba haikutamanisha.

    Abdi Babu alikiacha kitanda na kwenda kuikumbatia sakafu. Uti wa mgongo ulikuwa wazi mbele ya macho ya kila aliyemuona. Ngozi ilichanwa na kufunuliwa wazi na kuachwa wazi kama zipu. Kichwa hakikuepo shingoni. Ni nani ambaye angeuona utumbo ulionyofolewa nje wakati Abdi babu alilalia tumbo? Damu nyingi na nzito chumba kikawa kama mto wa damu uliosimama.

    Regina akaanza kupokea taarifa za vifo vya vijana wake.

    "Subira?" Subira akasimama kukifanya alichokuwa akikifanya, akamtazama Regina huku tabasamu na hali ya kucheka ikiwa mlangoni mwa midomo yake. "Yaani wewe mimi unafurahia matatizo yangu?"

    Subira akaonesha mshituko wa kushangazwa na swali alilouliza Regina akamuuliza kwa kustaajabu.

    "Mama! Yaani kupandishwa kwako cheo kumekuwa jambo la hudhuni na matatizo hata nisifurahi?"

    Kupandishwa cheo?

    Barua hiyo ikazidi kumchanganya Regina kwani mara baada ya kumpokonya Subira mara ya pili aliporudia kuisoma, haikuwa ile iliyoandikwa kwa mkono kwa wino mwekundu na iliyojaa vitisho. Hii ya pili iliandikwa kwa mashine na ilikuwa na ujumbe wa kumfanya kila mwenye dhiki afurahi. Ujumbe wa kupandishwa cheo kutoka uwakili wa mahakama ndogo ya wilaya na kwenda kusimamia ya mkoa pamoja na ongezeko la mshahara zaidi ya asilimia thelathini halikuwa jambo dogo. Hakufurahi kama ilivyotegemewa.

    Regina alizidi kuona kizungumkuti katika mambo hayo yaliyokuwa yakizidi kuendelea kutokea. Swali lililozidi kumuumiza kichwa ni jinsi gani barua hiyo iliingia ofisini kwake. Akamuita subira aliyekuwa anatoka ofisini kwake.

    "Subira embu.."

    Kelele za simu ile ya mezani, ikamfanya anyamaze.

    "Halo"

    "Ndio Regina" ilikuwa sauti ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bwana Maafudha. "Umeipata barua yako kutoka ofisini kwangu?"

    Hapo Regina akakumbuka kuwa barua ile ilitoka moja kwa moja kwa mkuu wa mkoa huo, akajibu haraka haraka

    "Ndio mkuu"

    "Sasa basi mheshimiwa amekuchagua wewe ushike nafasi hiyo jana jioni tulimtuma kijana wetu lakini hatukukuta wala katibu muhtasi wake zaidi ya mtu mgeni ofisini kwako ila ni vizuri kama utakuwa umeipata na hivyo utaanza kazi rasmi mara baada ya kuapishwa"

    "Sawa ahsante"

    Simu ikakatwa.

    Swali la pili likaongeza mlolongo wa maswali ndani ya kichwa cha Regina.

    'Mtu?' Akamgeukia Subira kwa uso uliojaa ghadhabu "wewe jana ulitoka ofisini kwako saa ngapi?"

    "Muda wa kawaida mama"

    "Imekuaje umuachie mtu kiti chako ofisini na wewe usionekane?"

    "Hapana mama mimi mbona sijatoka jana" macho ya hofu yakiwa yamemtoka pima, akaendelea "kweli vile mama nakuapie"

    "Nenda ukafanye kazi zako"

    Subira akamuacha Regina akiwa katika taharuki.

    Subira akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zinazomuweka katika ofisi hiyo, alimjia msichana.

    "Karibu"

    "Ahsante dada Subira"

    Subira akapatwa na mshangao. 'Amaenifahamu vipi?' Hakumuuliza kwanza akataka afahamu ni msichana mwenye shida gani.



     Subira akamuacha Regina akiwa katika taharuki.

    Subira akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zinazomuweka katika ofisi hiyo, alimjia msichana.

    "Karibu"

    "Ahsante dada Subira"

    Subira akapatwa na mshangao. 'Amaenifahamu vipi?' Hakumuuliza kwanza akataka afahamu ni msichana mwenye shida gani.

    "Wewe ni nani? Na nikusaidie nini?"

    Yule msichana alicheka kwa kebehi na kumjibu Subira kwa dharau

    "Jina langu si muhimu sana kwako lakini naamini mama Regina ana shida sana ya kuniona kwa sasa tafadhali naomba nimuone"

    "Hapana" Subira akajibu kwa hakika iliyo thabiti "siwezi kukuruhusu kumuona bosi wangu kama utambulisho wako haujakamilika"

    Akawa anaendelea na kushughulika na kile alichokuwa akikifanya mbele ya kioo cha kompyuta.

    Hata sikuelewa nini yule msichana alimfanya Subira. Aliingia bila Subira kuzungumza wala kumtazama alipokuwa akipita kuelekea katika ofisi ta Regina.

    Regina alishituka kukutana na msichana huyu ndani ya ofisi yake. Huyu ndiye msichana aiyemfahamu kama Jenifa.

    Jenifa ambaye ni mzimu wa Salome.

    Jenfa akazungumza.



    ...



    Wakati ule mwili wa Jenifa uliobeba roho ya Salome ukiingia ndani ya ofisi ya Regina, midomo yake Jenifa ilikuwa imepambwa kwa tabasamu pana alipokuwa akishuhudia mshangao wa hofu uliomkumba Regina alipomuona akuiingia.

    Akamsalimu

    "Habari yako Regina"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nani amekuruhusu kuingia ofisini kwangu?"

    Jenifa akacheka kicheko cha kuudhi. Akazungumza

    "Huna haja ya kuogopa ila ninakuja kukutoa ukungu wa juu ya kifo kilichomkumba Jenifa"

    Hapo Regina akafahamu anautazama uso wa Jenifa lakin anazungumza na Salome. Akajiuliza kwanini Salome anapenda kuutumia mwili wa Jenifa kuyafanya hayo anayoyafanya. Kabla hajazungumza Jenifa alikuwa ameshajikaribisha kitini na akamjibu Regina alichokuwa akikiwaza.

    "Ni heri niutumie mwili wa Jenifa ili kukusuta kwa kitendo ulichokifanya juu yangu mie nisie na hatia. Regina nakuahidi lazima nilipize kisasi juu yako hata ikiwaje. Mimi si mtu hai bali ni mzimu so usidhani kuwa nitakufa mara ya pili kama ukiwa na nia hiyo"

    Jenifa mwenye kuongozwa na roho ya Salome ndani yake akazungumza.

    "Sasa nadhani sina wakati mkubwa wa kupoteza ni muda wa kukueleza kile kiulichonileta. Kukueleza juu ya kifo cha Jenifa"

    Regina alikuwa amechanganyikiwa lakini hakuna alichoweza kukifanya zaidi ya kuendelea kuduwaa kwa hofu.

    Jenifa mwenye roho ya Salome akaanza kueleza kisa kizima cha kilichomuhusu Jenifa mwenyewe.

    Ilikuwa ni jumamosi tulivu ndani ya isamilo lounge. Jenifa akiwa na jamaa aliyenawiri pesa akanukia na kuvutia vilivyo. Huyo akawavuta warembo wengi kumtazama na wengine kudiriki kumuonea wivu Jenifa. Wenye yao wakasonya na kumponda Jenifa kuwa hakuwa wa hadhi yake.

    Jenifa hakuwajali.

    Yeye na Brown walipishana miaka isiyozidi minne, hivyo wakawa na ndoto siku moja kuja kuwa mke na mume.

    Ikawa ni ndoto aliyoiota Jenifa peke yake.

    Ukweli ni kwamba Brown hakuwa mwanaume ambaye Jenifa alimdhania. Mwanaume ambaye hakuwa ametulia na msichana mmoja. Brown aliitwa majina mengi yote yakimaanisha uzoefu wake juu ya kubadilisha wasichana.

    Jenifa alikuwa ndani ya mlolongo wa wasichana wengi aliowapanga Brown. Brown hakujali umri wa msichana aliyetembea naye, alichojali yeye ni kuridhisha mwili na nafsi yake. Hivyo miongoni mwa wasichana wote alikuwa pia na wanawake waliomzidi umri. Wanawake wasio na tofauti na mama zake.

    Brown hakujua pia miongoni mwa wanawake wale, mmoja wao alimuhusu sana kwa ukaribu Jenifa.

    Siku hiyo ikawa ya raha sana kwao. Jenifa alikunywa na kula vitu ambavyo hata hajawahi kukutana navyo katika maisha yake. Jenifa akaona kuheshimiwa na kupendwa kuliko wanawake wote kwa siku hiyo. Akaiona thamani ya mapenzi pale alipobembelezwa kwa sauti ya kimahaba na Brown. Naye akadeka kwa aibu na kujichekelesha pasipo sababu. Siku hiyo wakafanya vitu vya kushangaza kana kwamba ndio kwanza walikuwa wanaanza mapenzi.

    Hawakuwa peke yao ndani ya siku hiyo.

    Pembeni meza ya tatu kutoka walipokaa hapo kulikuwa na kibaraka aliyetumwa kufuatilia nyendo zote za Brown. Brown alikuwa akilelewa na kupewa kila alichokitaka kutokana na penzi alilokuwa akilitoa kwa mwanamke mmoja aliyemzidi umri.

    Watoto wa mjini hujiita mario.

    Yule kijana alizidi kufuatilia kwa umakini huku akipiga picha eneo alilokaa Brown na Jenifa kwa uangalifu ili asigundulike hila zake. Akafanikiwa kukusanya data za kutosha na kuondoka baada ya kuhakikisha kuwa Brown na Jenifa wameenda kulala chumba fulani katika hoteli hiyo.

    Akarudi kwa aliyemtuma

    "Mama, nimefanikiwa"

    Kibaraka yule aliyefahamika kwa jina la Mwarami, alikuwa akitoa taarifa kwa Regina. Regina ndiye mwanamke aliyekuwa akimpa jeuri na kiburi Brown. Ndiye mwanamke aliyemzidi brown zaidi ya miaka kumi na minne. Hakuona ubaya kutoa penzi lake kwa kijana yule mtundu.

    Alikuwa na wivu sana juu ya penzi la Brown. Alichokipata kutoka kwa kijana yule aliyefahamu sehemu hatari za kumuamsha kihisia aliapa kumuangamiza atakayemsogelea. Ni hapo ndipo alianza kuwa katili. Ni hapo ndipo alipofahamu juu ya kumwaga damu. Alikuwa tayari na pesa hivyo aliamini juu ya pesa hakuna kinachoshindikana.

    Regina akaijibu simu ya Mwarami.

    "Sawa nakuhitaji ofisini tujue nini tunafanya juu ya huyo baradhuli"

    Regina akaingia chuki juu ya damu yake bila kujua.

    Walichopanga Mwarami na Regina katika kikao cha siri, likawa ni jambo zito kuelezeka. Damu ya Jenifa ndiyo walitaka kuimwaga. Mapenzi yakamuendesha Regina kutamani kuwa mtu katili kuliko kawaida.

    Ndivyo ilivyokuwa saa tano baadaye

    Jenifa akiwa njiani kurudi nyumbani kwao alihisi akifuatiliwa na gari iliyokuwa ikitembea taratibu pembeni yake. Alijitahidi kupunguza mwendo nayo ikapunguza. Akajilaumu kuchelewa kurudi kutoka katika starehe zake na Brown. Aliogopa na kutamani kukimbia lakini miguu ikakataa. Kutoka kwenye lile gari, Mwarami akashuka akiwa amepambwa na tabasamu baya la kishetani usoni mwake.

    Hakumjua wala hakuwahi kuonana naye hapo kabla.

    Walimvamia Jenifa wakiwa watu watatu na kumuingiza ndani ya gari kwa fujo. Alikuwa akijaribu kujizuia lakini hakuna kilichowezekana kwa vipande hivyo vya watu walioshiba kimazoezi. Walimchukua Jenifa mpaka pembezoni kidogo mwa mji wa mwanza kuelekea maswa.

    Walimtupa kwenye msitu mmoja huko baada ya kumbaka na kumfanya kitu ambacho si rahisi kukieleza kwa kuandika ukaelewa.

    Jenifa alikatwa mikono huku akilia kwa uchungu, akatolewa miguu yake yote miwili na kunyofolewa nywele zake ndefu kuvutwa na mashine ya kusagia mpaka ilipofika mwisho na kutoka na ngozi ya kichwa. Ubongo ukatapika kwa nje. Wakaona adhabu hiyo haikutosha baada ya Jenifa kupoteza maisha kwa uchungu ule wa kuvutwa nywele za kichwa wakakinyofoa kabisa kichwa chake.

    Wakiwa wamevaa gloves maalumu, mwarami na wenzake wakaingiza kiwiliwili cha jenifa ndani ya mfuko wa cement na kurudi nao mjini. Huko wakaelekea moja wa moja mpaka alipokuwa akiishi Brown na kumtupia mzoga wa mwili wa Jenifa mlangoni mwake. Wakatokomea.

    ...

    Muda wote ambao Regina alikuwa akisikiliza hadithi hiyo alikuwa akilia kwa kuomboleza. Hakika alihisi uchungu wa ajabu usiolezeka moyoni mwake. Alihisi hatia kuliko hatia ambayo alikuwa akimpatia Salome.

    Yeye alitembea na mwanaume wa Mtoto wake hivyo hawakuwa na tofauti yeyote na Salome kutembea na Baba yake. Sura ya Jenifa nayo ikalowa machozi. Machozi ya Jenifa yalikuwa yakitoka damu na sio maji kama machozi ya binadamu wa kawaida. Regina akamsihi Jenifa

    "Tafadhali salome, usiniue. Naomba radhi kwa yote niliyowahi kuyafanya kwako na kwa Jenifa mwanangu. Naomba nisamehe salome"

    Jenifa akapotea sasa taswira ya Salome ikawa wazi mbele ya Regina. Salome hakuwa akilia tena bali alikuwa akicheka kicheko kisicho na ladha yeyote kuitwa kicheko. Hakikuwa kicheko cha furaha.

    "Nitakuua regi.."

    Akiwa anazungumza hayo huku akimuinukia na kumfuata pale Regina alipo, Salome aliona nafsi ya mtu mwingine nyuma ya Regina. Nafsi ile aliifahamu na kumfanya asite kuitoa roho ya Regina kwa wakati huo.

    Alikuwa ni Batuli.

    "Salome mwanangu"

    Batuli alizungumza wa hali ya utulivu huku machozi yakimtiririka. Regina hakumuona batuli hivyo alibaki akiduwaa akimshangaa Salome aliyekuwa akiduwaa. Batulia akaendelea

    "Tafadhali naomba usamehe kama mimi niivyokusamehe. Naomba upumzike kwa amani na uachane na visasi"

    Batuli akatoweka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Salome naye akawa analia na kukaa kitini kwa kubweteka kwa hofu. Regina akiwa anashangaa yote yanayoendelea akashuhudia Salome akitoweka bila kumfanya chochote

    Regina akapona.

    ...

    Mwarami hakuamini kile alichokisikia kutoka kwa Regina. Alibaki akiduwaa na kukiri hakika Regina amekamatika. Lakini bado alikosa imani juu ya maisha yake pamoja na Regina kwa kuwa ni usiku wa siku hiyo alipokea ujumbe wa kitisho juu ya kifo alichoahidiwa na Salome.

    Akazidi kuomba mungu iwe kama alivyohadithia Regina. Kuwa Salome alipotea kumuacha akiwa hai. Lakini utata ukabaki kwanini Salome amuache baada ya kuduwaa kama aliyeona kitu fulani kilichomtisha mbele yake na kumfanya alie?



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog