Simulizi : Roho Iliyorudi Kuangamiza
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Regina alijitahidi kumsihi asilie, lakini haikusaidia. Batuli aliyasema mengi. Alimlaani vya kutosha Salome na Kilaza. Aliwalaani kila laana mbaya unayoijua hapa duniani. Regina akatabasamu kwa kuwa naye alipanga hivyo hivyo, kama alivyokuwa akiropoka ropoka ovyo Batuli. Batuli alitamani kusikia siku moja Kilaza na Salome walizipoteza pumzi zao kwa kifo cha kusikitisha sana. Damu yao haikuwa na faida kwa kizazi chochote kile. Regina akampiga piga mgongoni huku bado tabasamu likiwa pambo zuri usoni mwake. Yeye alipanga kuwaangamiza wote. Alipanga kuanza na Salome, kisha angefuata Kilaza. Alihofia angepoteza urafiki wake na Batuli, lakini kumbe Batuli naye alikwisha tia sahihi ya kifo cha watu hao wawili. Hivyo alikuwa huru sasa kufanya lolote. Baada ya Batuli kunyamza kulia. Batuli alimuhadithia yote Regina yaliyotokea. Alianza pale Kilaza alivyompiga, akaondoka asijue wapi anaelekea. “alikuja kukutana na mimi. Alinitisha tisha kuwa eti akimjua anayemfundisha kiburi mke wake atamfanya kitu mbaya” Regina alimwambia. Batuli akashagaa, akamalizia mpaka leo sababu iliyomfanya aondoke kabisa nyumbani. “…uliponipigia simu ndipo niliposikia Karim akifungua Geti. Gai yake ilikuwa ndiyo inaingia. Nilisimama dirishani nikitegemea kuwa alikuwa peke yake, kumbe alimpitia Salome shuleni. Niliumia sana wakati Salome alipokuwa akishuka huku akimbusu baba yake mdomoni” Regina akacheka kicheko cha kishetani na kibaya; akamwambia “wewe Batuli, Salome yule si baba yake tena ni mpenzi wake embu acha kujifariji kama uliwahi kuzaa katika maisha yako kuanzia sasa” Batuli naye alicheka kwa karaha,. akamaliza mpaka alipompiga kwa kumkuta anaongea na simu na baada ya kujua anaongea na Ragina. Ndipo naye aliamua kuondoka nyumbani kwake. Regina alitabasamu tena, akamfariji “usijali rafiki yangu, wewe si rafiki tu pekee, sasa ni ndugu yangu” walikumbatiana kwa pamoja, huku Batuli akianza upya kulia. Dakika chache baadaye Regina alimuaga Batuli kuwa alikuwa na miahadi ya kukutana na mshirika wake mmoja maeneo ya mjini. Batuli akaiona hiyo ilikuwa ni fursa ya pekee kufanya lile jambo alilopanga kulifanya. Jambo alilopanga aifanye ili aweze kupumzika kwa amani.
Regina akatoka kwenda kuonana na washirika wake. Washirika wa siri katika mipango yake ya siri. Aliwaita washirika kwa kuiweka siri iwe siri asiiache uchi siri yake isiwe siri tena. Kwa hiyo hata Batuli hakufahamu siri yeyote ya Regina. Hivyo Batuli asingethubutu kudiriki kuwaza alilotaka kufanya mpaka ashuhudie jambo alilolipanga Regina. Lakini pia, laiti kama Regina angefahamu alichokipanga Batuli! Regina asingethubutu kumuacha peke yake hata kwa dakika chache. Batuli akatimiza lile alilopanga kulitimiza kabla ya jua kuzama. Batuli akayakatisha maisha yake kwa kujinyonga. Ikawa mwisho wa simulizi za Batuli. Batuli aliyejinyonga kwa maumivu yakutendwa na mume aliyetembea na mtoto wake mwenyewe wa kumzaa. Aliiandika barua fupi kwa wote waliomfahamu. Ikasomeka hivi.
Nimeuchukua uamuzi mgumu wa kuyatoa maisha yangu baada ya kuona thamani ya maisha ikipungua. Uovu uliokuwa ukitendeka mbele ya macho yangu uliniumiza sana nafsi. Uovu baina ya Kilaza mume wangu na Salome binti yangu. Regina rafiki yangu usilie kwa jambo hili, sikupenda nikubebeshe mzigo wa kuishi nami tena katika maisha yako. Naomba uwe jasiri katika hili, kama ulivyo siku zote katika maisha yako. Nimeyatoa maisha yangu kwa kupenda mwenyewe. Kifo changu kisihushishwe na mtu yeyote wala tabia yeyote. Muishi kwa amani wakati ambao sitokuwepo tena duniani. Mimi Batuli Carlos. Barua akaiweka chini ya stuli aliyoipindua baada ya kujining’iniza juu ya kitanzi alichokifunga juu ya panga boi iliyoshikiliwa na chuma kigumu juu ya mbao iliyoezekea bati. Batuli akawa amekufa akiwa bado anaipenda dunia na famili yake pia.
…..
Regina alipanga kukutana na Mwarami pamoja na Erick katika mgahawa ule ule. Ilikuwa ni jioni kiasi, lakini halikuwepo giza kubwa lililomfanya ashindwe kumuona Erick; ama kumkumbuka. Alikuwa amekaa karibu na vile viti walivyokaa siku za nyuma walipokutana kwa mara ya kwanza. Erick hakumuona Regina, kwa kuwa Erick alimpa mgongo. Regina aliwahi kumuona Erick kwa kuwa alimuona tangu akiwa ndani ya gari yake. Alimgusa bega Erick akageuka “oh! Regina karibu” aliinuka akimuelekeza pa kukaa. Regina alipokaa muhudumu yule yule alikuja huku akiwa na tabasamu. “karibuni wateja wangu” akiwa anamuangalia Regina “nikuhudumie nini leo mama?” Regina alitabasamu pia kwa kuwa alimkumbuka “Kama kawaida tafadhali” Regina alipendezwa na juice ya ukwaju na ubuyu. Regina akauvunja ukimya “Erick kuna jambo nataka nikuulize” Erick akaonesha utayari wa kulipokea kwa tabasamu fupi kisha akajibu “ndiyo uliza bila shaka” Erick alitegemea iwe hivyo. Akadhani huenda swali alilokuwa akitaka kuuizwa ni ‘hivi Erick una rafiki wa kike ama mchumba?’ alikaa tayari kutayarisha tabasamu la ushawishi kisha akatafakari jibu la kumpa ‘hapana mpenzi nimtoe wapi wanawake wenyewe nyie siku hizi mnaumiza tu nafsi zetu’ lakini kwa upande wa Regina, akafarijika. Akaendelea “kuna jambo nataka nikushirikishe.” Alinyamaza kumpa muda wa kulitafakari jambo hilo; baada ya kupokea juice aliyoletewa. Alipoinywa funda moja akamtazama Erick aliyekuwa akimtazama na yeye pia Erick akawa anamtazama kwa maii ili aione aibu dhahiri liyotawala Regina. Ingetoka wapi kwa mwanamke huyu mwenye uso wa mbuzi? Mwanamke katili? Kama aliitafuta angeitafuta kwa muda mrefu asingekutana nayo hata kwenye sauti yake. Regina akaendelea kwa sauti ya taratibu iliyojaa umakini “nataka tushirikiane kumuuwa yule mzee uliyeniona naye hapa siku ya kwanza” likawa jambo la kumshangaza sana Erick akahisi kama amepaliwa na maji aliyokuwa akinywa huku akimsikiliza Regina “unasema!?” Regina akatabasamu kifedhuli, akajibu huku akijitia kucheka “nilijua ni lazima utashangaa. Nijibu kwanza unaweza kutekeleza jambo hili?” likawa jambo lingine zito kwa Erick. Hata hivyo mawazo ya kimapenzi yakamtoka Erick. Akakumbuka alivyoteswa na Kilaza akakumbuka alivyotishwa kufanyiwa kitu kibaya na yule mbabe wa mahabusu. Akakumbuka alivyoliwa na mbu usiku kucha akiwa amelala huku amesimama, alilala sasa basi? Akasonya. Akajiambia ni lazima amfanyizie. Akakumbuka siku alipokuwa amelala kwa rafiki yake aliyeamua kumuhifadhi, aliwahi kujiapia ipo siku akifanikiwa kuwa na pesa kama za Kilaza atamfanyia kitu kibaya. Sasa ile siku si ndiyo hii hapa? Ile siku aliyokuwa akiingoja imejileta yenyewe, ikisindikizwa na malaika wa shetani. Regina, mwanamke aliyedhani amekuja kwake kimapenzi, kumbe amekuja na ujumbe wa kuuwa. Potelea mbali huu ndio wakati wangu wa kulipiza kisasi. Akatafakari mpaka jinsi atakayomuua. Akacheka kwa raha jinsi alivyokuwa akiona maono ya Kilaza atakavyokuwa akimsihi asimuue. Jinsi ambavyo Kilaza atakuwa chini ya miguu yake akilamba sori ya kiatu chake. “bila shaka Regina. yatatukia lini mambo hayo?” Regina hakuwa na mashaka na kila alichokuwa akipanga. Alikuwa na uhakika kwa hadithi aliyoambiwa na Erick, hadithi ya kuwekwa ndani kwa kosa la kumtongoza Salome; kwa habari hiyo Erick asingeweza kukataa. Akatae wakati Regina alisokomeza kikombe hicho cha mauaji na mkate wa pesa zilizoshiba? Asingekuwa kijana mwenye njaa na fedha, endapo angekataa pesa hizo alizotajiwa. Ujira wa shilingi milioni kumi na tano. Regina akiwa anamalizia kupanga njama zaote za jinsi ya kummaliza Kilaza; naye Mwarami akajiokeza kati kati yao. Erick alipigwa na butwaa kumuona mwarami kati kati yao. Erick alimfahamu Mwarami, Mwarami hakumsahau hata chembe Erick. Wote kwa pamoja hawakutegemea kukutana sehemu kama hiyo.
Erick alifurahi kumtambulisha Mwarami kwa Regina. Huku akiwa anachekacheka “Regina, siamini. Huyu ndiye Yule rafiki yangu niliyekuwa nakuambia katika ile hadithi” ikawa kitendawili kwa Regina kukumbuka. Erick akang’amua hilo akaendelea “huyu ndiye Yule aliyenisaidia baada ya kutolewa mahabusu, nilipotupwa na Kilaza; umeshasahau?” Erick aliuliza baada ya kutambulisha huku akiwa na furaha ya ajabu. Mwarami naye akawa amepigwa na bumbuwazi. Bumbuwazi ya ilikuwaje Erick, mjinga mjinga kufahamiana kwa karibu na huyu mwanamke katili? Lakini Regina naye alikumbuka jambo hilo akalipuuza. Aliona wakati umekwisha kwenda na alikuwa amepanga awahi kurudi nyumbani kuzungumza na rafiki yake, Batuli. Laiti kama angejua. Angejuwa kuwa alikuwa akimfikiria marehemu Batuli, asingethubutu kufikiria, kuendelea japo kuzungumza salamu na Mwarami. Jambo usilolijua, ikabaki sawa na usiku wa giza. Regina akaendelea kutabasamu na Erick, mpaka alipomruhusu aondoke; ili aweze kuzungumza na Mwarami. Alipenda kuwagawa kwa mafungu, katika siri zake ili kila jambo liende kisiri siri. Erick alipoondoka, Mwarami baada ya kupokea kinywaji chake; Regina akauvunja ukimya. “sina muda mwingi sana wa kukaa hapa, nina ugeni nyumbani” Mwarami alitingisha kichwa kwa maana kuwa amemuelewa “hivyo kilichonifanya nikuite ni kwamba ninahitaji umfuatilie Yule kijana aliyetoka hapa” kana kwamba alikuwa amesahau jina lake. Mwarami akamuuliza “nani? Erick?” Regina akatabasamu “ndiyo. Huyo huyo. Kila anapokwenda na kila anayekutana. Kuna jambo nimeamua kumshirikisha kwa kumtega ili nione kama atafudhu kuingia katika himaya yangu” Mwarami naye akacheka kivivu kikohozi kikavu kikampitia “sawa mama bila shaka” wazo la Regina halikuwa la vijana hawa wenye njaa kama walivyokuwa wakifikiria. Wazo la Regina lilikuwa ni kulindwa bila wao wenyewe kujuwa. Regina alitabasamu kinafki alipoagana na Mwarami na kuingia ndani ya gari yake. Aliichukua simu yake na kumpigia Erick “umekwishafika nyumbani kwako?.... vizuri, sasani hivi… lengo la kukupigia simu ninahitaji hiyo kazi usiifanye haraka…. Ndiyo chukua muda mwingi kumfuatilia nani na nani anakutana naye… ndiyo, pia kila anayeongea naye hakikisha unafahamu wamezungumza nini.. nitakutafuta kesho jioni kwenye akaunti yako ya pesa za mtandao” simu ilipokata aliingiza gari barabarani kwa mwendo wa kakakuona. Akiwa anaendesha taratibu kichwa chake kilikuwa katika tafakuri nzito. Alitafakari jinsi alivyojiingiza katika vita na Kilaza. Alikuwa na uhakika kilaza si mzembe amtishe na asitimize jambo baya alilomuhaidi tena ikiwa Batuli ameondoka nyumbani kwake. Lazima nifahamu anapanga mipango gani ili niweze kummaliza vizuri yule fedhuli. Lazima nimuwahi mimi kabla hajaniwahi, Regina alijiwazia. Alipofika getini kwake alikutana na mlinzi akiwa anatoka kama aliyechanganyikiwa asijue wapi anelekea. Regina alichomoka garini kwake na kuanza kutimua mbio. Hakumbuki ni muda gani alitoka ila alipokuja kujitambua ni pale alipoanguka pamoja na yule mlinzi. Mlinzi alikumbana na kichuguu huku Regina akimparamia mgongoni na kuanguka pamoja. Wote kwa pamoja walikuwa wakihema.
"Vipi wewe!?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nime..nimem..mhm..mkuta ame..ameji..amejinyonga"
Kisha akakohoa mfululizo huku macho kayatumbua. Alikuwa ni mlinzi wa getini wa Regina. Regina akahamanika kwa hofu na hasira
"Wewe pumbavu mbona sikuelewi" akamzaba kibao kwa jazba "embu acha pupa. Niambie nani kajinyonga?"
"Yule rafiki yako mama"
"Whaaat!!!?"
Regina aliyatoa macho pima asijue kuwa alichosikia ni kitu cha kweli kabisa. Alinyanyuka na kuanza kukimbia kurudi ndani. Alipitiliza moja kwa moja chumbani alipokuwa akilala Batuli, akapokelewa na mwili wake uliokuwa ukining'inia. Regina alipiga ukunga wa nguvu na kulia kwa uchungu.
"Batuli kwanini umefanya hivi rafiki yangu!!"
Alilia akaomboleza muda mrefu mpaka akaishiwa nguvu. Baadaye baada ya kupiga simu katika hospitali ya mkoa pamoja na polisi, hawakuchelewa kutoana na hadhi yake mjini.
Mwili wa Batuli ukatolewa pale juu na kufunikwa shuka jeupe. Wanausalama walikuja pale nyumbani kwa Regina na kumuhoji maswali ya hapa na pale. Maswali yalikuwa ni mengi na mwisho akawajibu kiuvivu.
"Aliondoka nyumbani kwa mumewe kwa kuwa alikuwa na matatizo katika ndoa yake"
Hakuona umuhimu wa kumueleza afisa usalama aliyekuja, juu ya rafiki yake kuja kuishi ndani kwake na si kwa mumewe. Kisha waliondoka na mwili siku hiyo kuupeleka mochwari, msiba ukawa kwa Regina. Watu waliomfahamu Batuli walihudhuria akiwemo Kilaza pamoja na Salome. Hasira na chuki alizokuwa nazo Regina, moyo wake ulitamani unyofoke kifuani pake. Alitamani awameze lakini nafsi yake ikamnong'oneza
'Sasa si wakati muafaka'
Akajikaza kumaliza kipindi hicho kigumu cha msiba. Baadaye siku ya tatu, Batuli akazikwa katika makaburi ya kanisa la TAG huko Nyegezi.
Hakuona umuhimu wa kumueleza afisa usalama aliyekuja, juu ya rafiki yake kuja kuishi ndani kwake na si kwa mumewe. Kisha waliondoka na mwili siku hiyo kuupeleka mochwari, msiba ukawa kwa Regina. Watu waliomfahamu Batuli walihudhuria akiwemo Kilaza pamoja na Salome. Hasira na chuki alizokuwa nazo Regina, moyo wake ulitamani unyofoke kifuani pake. Alitamani awameze lakini nafsi yake ikamnong'oneza
'Sasa si wakati muafaka'
Akajikaza kumaliza kipindi hicho kigumu cha msiba. Baadaye siku ya tatu, Batuli akazikwa katika makaburi ya kanisa la TAG huko Nyegezi. Huko vituko vikaendelea kutokea. Salome alilia kwa uchungu. Alijigalagaza kwenye vumbi akaita mama haikusaidia. Regina akabetua midomo yake kwa kebehi na dharau huku moyoni akijiambia
'Unafki' hakuna ambaye alifahamu nini kilimpata Salome hata ulipofika wakati wa kurusha udongo katika kaburi la mama yake? Yeye akataka kuingia mzima mzima. Ikawa ni simanzi kwa waombolezaji bali kwa Regina ikawa ni maigizo. Ukweli wote yeye aliufahamu.
Wakazika
zikapita siku, miezi ikayoyoma na miaka ikakatika bado Regina alikuwa na kisasi moyoni mwake. Aliapa ni lazima atimize. Akaisuka mipango yake ikasukika na kuona sasa baada ya miaka mitatu tangu amfukie rafikiye, ndio ulikuwa wakati wa kutimiza lile alilolikusudia. Si auwaye kwa upanga atakufa kwa upanga? Basi adhabu iliyomstahili mtu kama Salome ni kifo. Kifo cha kusikitisha na kuhudhunisha sana.
Akiwa ofisini kwake kabla hajaitafakari kesi inayomkabili waziri mkuu wa zamani, kesi ambayo amepewa yeye jukumu ya kuisimamia; akawa anawaza juu ya kumuangamiza salome. Aliwatafakari vijana wake, hakuona kipingamizi mbele ya pesa. Akapiga funda moja la kilevi kilichokuwa ndani ya glass, kisha akabeua kwa shibe hatimaye akajinyanyua kwa madaha. Akaitupa simu yake ya mkononi mkono wa kulia na funguo za gari mkono wa kushoto, kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo.
Alielekea benki.
Akachomoa kiasi kikubwa cha fedha kisha akarudi ofisini. Huko akaiandaa picha ya salome mezani na kitita kile cha pesa. Akanyanyua mkonga wa simu ya mezani na kubonyeza bonyeza nambari kadhaa kisha akaweka sikioni. Upande wa pili ulipopata uhai, naye akazungumza.
"Naomba uje na timu yako ya watu sita"
Kisha alikata simu.
....
Baada ya Batuli kuondoka nyumbani kwa Kilaza, walijihisi wapo huru zaidi. Lakini shida ilikuja kwa Kilaza. Kilaza alijihisi mpweke na hatia ndani ya moyo wake. Kilaza licha ya mambo yote aliyyokuwa akimfanyia Batuli, lakini umbali wake na Batuli ukamtafuna moyo. Alianza kuyaona makosa aliyokuwa akiyafanya na mwanaye. Ikawa kama ndio kwanza wamefunguka macho na kuona mabaya yao.
"Nimefanya nini sasa?" Akajiuliza kwa nguvu katika hali ya hasira "jamii itanielewaje Kilaza mimi?"
Aibu pia ikamkamata na kuona endapo Batuli akisema sababu ya kukimbia ndoa yake.
Akiwa chumbani peke yake, akadondosha machozi. Salome ndio akazidi kujitanua katika nyumba hiyo na kuwa mke rasmi. Alienda huku na kurudi kule kwa maringo bila kuwa na hofu. Zamda na wafanyakazi ndani ya nyumba hiyo wakasikitika kwa hali hiyo. Maisha yakaendelea japo ufusa huo haukuvumilika machoni mwa mtu mwenye busara na aibu. Ndipo ikafika ile siku. Siku chache tangu Kilaza atoke kuonana na Regina. Simu ya mkononi ya Kilaza ikapata uhai. Juu ya kioo cha simu ya Kilaza ilikuwa ni namba ya Regina.
"Habari yako!?" Kilaza aliitikia. Baada ya sekunde chache baadaye alipoisikiliza sauti ile ya upande wa pili, akatoa sauti ya hamaniko "unasemaa!?" Midomo ikaanza kumtetemeka na kuiondoa simu sikioni.
Ilikuwa imeshakatwa.
Alilia kutokana na taarifa hizo alizozipata kutoka kwa Regina. Taarifa za msiba wa Batuli. Taarifa za kuwa Batuli amejinyonga. Hakika ilikuwa hudhuni kubwa sana.
Kilaza na Salome wakahudhuria katika msiba kama kawaida na ndiyo siku ambayo Salome akaanza kufanya vituko pae msibani. ile haikuwa hali ya kawaida machoni mwa mtu aliyekuwa akifahamu kila kitu. Lakini kwa wengine wangegundua labda ni uchungu tu wa kumpoteza mama. Dawa zile alizofanyiwa na Kilaza zilianza kupoteza nguvu siku nyingi ndio maana akamuona Kilaza hakuwa akimridhisha tena. Ndio maana alianzisha uhusiano na George mwanafunzi mwenzake. Ndio maana hata siku hiyo ya msiba alihisi hatia kubwa kusababisha Batuli, mama yake kufariki. Aliomboleza akiomba msamaha mara kwa mara huku akiwaacha wengine njia panda wasijue alikuwa akiomba msamaha wa nini. Dawa hizo zilipoteza nguvu yake kwa kuwa Kilaza hakufuata tena masharti ya mganga baada ya kuupata utajiri. Kufungwa alikofungwa Salome, kukaanza kufunguliwa. Salome akaanza kutambua alichokuwa akifanyiwa na baba yake. Aliona sasa kiulikuwa ni kitendo cha aibu. Hata msiba ulipomalizika na kumzika Batuli, Salome bado alikuwa akilia kila siku. Maisha ya Salome yakawa ni ya hudhuni kila mara na kumfanya adhoofu mwilli wake kwa hudhuni.
Salome akavimaliza vidato, akajiunga na chuo cha muhimbili kuchukua masomo ya vipimo kwa kutumia mionzi. Huko nako akamaliza na kuamua kurudi nyumbani mwanza. Akiwa mwanza, akapata kazi katika hospitali ya mkoa. Baada ya miezi sita akiwa kazini, siku moja akiwa anatoka kazini na kuelekea nyumbani, alikutana na vijana wapatao kumi na wawili. Vijana waliomfanyia kitendo cha kinyama na aibu. Walimbaka kwa zamu mpakaa akatokwa na damu nyingi sehemu zake za siri kisha akazimia. Wakamlisha Cement na kumuingiza sime lenye makali kotekote kule sehemu zake za siri na wao kutokomea.
Siku ya kwanza ofisini kwake, Salome hakuonekana. Wafanyakazi wenzake walipojaribu kumpigia simu nayo haikupatikana. Walijiuliza nini kilichomkuta mwenzao hawakupata jibu. Siku ya pili mmoja wa wafanyakazi wenzake na Salome, alipokuwa akipita kutoka ofisini karibu na jalala moja lililopo kilomita moja kutoka ofisini kwao, alikuta wakiwa wamejazana wakishangaa jambo. Ndipo akasogea jirani na eneo hilo. Akautazama mwili uliolala juu ya dampo hilo ukiwa uchi na umeanza kuvimba. Hakika Salome alikuwa amebadilika sana kutokana na kifo kile kilichomkuta. Hakuna ambaye angeweza kumkumbuka lakini mfanyakazi yule mwenzake, aliweza kumng'amua. Alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana. Ndipo akapiga simu ofisini kwao na kuja kuuchukua mwili wa mwenzio. Hakuna ambaye hakuacha kulia katika kitengo kile alichokuwa akifanyia kazi Salome. Wengi walilia kwa uchungu kumpoteza mtu kama Salome. Licha ya kumpoteza mtu mcheshi mkarimu na mpole pia walimpoteza katika hali ya kuhudhunisha sana. Unyama aliofanyiwa Salome, hakuna ambaye angedhani kama kungekuwako na mtu mwenye roho ya kumfanyia hivyo mtu asiye na hatia.
Salome akazikwa mwili, roho yake ikabaki duniani. Roho yake ilirudi kuangamiza kila nafsi iliyohusika katika mauaji yake. Kilaza alishirikia katika mazishi ya mwanaye yeye ndiye alianza kulipa kisasi hicho.
Hakuna ambaye alifahamu mzuka uliozuka katika jalala la vichaa kuwa hakuwa binadamu kamili bali ni roho iliyouvaa mwili wa mwanadamu. Roho iliyojaa visasi na chuki kwa yale iliyofanyiwa hapo mwanzo. Ni roho iliyojibadilisha taswira na kuivaa taswira ya msichana mrembo. Midabwada aliyoibuka nayo katikati ya wawendawazimu, akaivua pembezoni mwa barabara ielekeayo Igoma. Akaibukia katika bar moja jirani na ilipo ofisi ya Kilaza baba yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Msichana mrembo, mwenye midomo iliyopakwa rangi nyekundu. Akaibusu chupa ya kilevi kwa ustadi kwa kugida kinywaji kilichomo ndani ya chupa hiyo, macho yake yaliyorembuka yakijitupa huku na kule kwa madaha. Kope zake ndefu zikifunga zisingekuwa na tofauti na zile zikonyezazo. Gauni lake refu lenye rangi nyekundu lilijichora sambamba na mwili wake uliovimba pembeni na kuchomoza zile bastola zake na makalio yaliyovimba. Akaikunja nne kwa kuinua mguu wake wa kulia na kuupandisha juu ya mguu wa kulia huku akichezesha kiatu chake kirefu chenye rangi ya damu mzee chenye kisigino kirefu. Alikuwa mweupe, mweupe haswa. Nywele zilizodondokea mgongoni zikaongeza uzuri huo na kuwa sanjari na malaika.
Huyo akawa Salome mpya kati kati ya watu waliomfahamu marehemu Salome aliyefariki katika kifo cha kuhuzinisha na kusikitisha. Hiyo ndiyo roho iliyojivika ndani ya mwili wa msichana huyo mrembo. Alikuwa hana shaka muda mchache mbele, angemuona baba yake, Mzee Kilaza.
Bia ya kwanza ikaisha muhudumu akaileta ya pili huku akiinywa taratibu. Ilikuwa ni ajabu kwa salome kuwa mpenzi wa kunywa pombe, lakini mwili wa mtu aliyemchukua ulikuwa ni bingwa kwa unywaji wa pombe. Mwili huo na taswira ulikuwa ni wa mwanamke aliyefariki miaka mingi iliyopita. Alikuwa ni mwanamke aliyependelea sana kunywa pombe mpaka pale mauti yalipomkuta. Yeye pia alikufa katika kifo cha kusikitisha sana. Yeye mwanamke huyo alifahamika kwa jina la Jenifa. Alikutwa amekufa akiwa bafuni kwake na tundu la risasi iliyofumua vibaya komwe lake. Mwisho wa Jenifa ukawa wa kusikitisha na ulioteka vyombo vingi vya habari. Salome alimfahamu vizuri Jenifa. Japo hakuwahi kuwa karibu naye, lakini alikwisha soma habari kwenye gazeti moja lililoandika juu ya kifo chake. Kipindi hicho yeye akiwa bado mdogo sana.
Kabla hajaimalizia pombe hiyo ya pili, vinyweleo vikamsimama na ndani ya nafsi yake akasikia sauti za mabishano
"Sipo tayari kuvumilia huo upumbavu nimesema ni lazima huyo mwanamke auwawe leo kabla jua halijazama"
ilikuwa ni sauti ya Kilaza ikibishana katika hali ya utulivu sana. Salome akazidi kusikiliza
"Yeye ndiye amehusika katika kifo cha mwanangu Salome, ameniharibia sana familia na maisha yangu naomba mfanye juu chini mkamilishe hiyo mipango"
Kisha akiwa anatazama kule ilipo ofisi ya baba yake, Salome alimuona Kilaza akitoka huku akiongea na simu. Alikuwa akielekea kwenye gari yake. Salome akafanya jambo la kushangaza lililomshangaza muhudumu aliyekuwa akimuhudumia.
Alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
...
Kilaza akiwa anatoka ofisini kwake katika hali ya kughabidhika, alikuwa anazungumza na mtu muhimu kwenye simu yake. Alikuwa akijaribu kumpa maelekezo ya kufanya juu ya Regina. Hasimu wake wa muda mrefu ambaye aliona kuwa muda unakwenda bila analolipanga kutimia. Akiwa ndiyo kwanza anaikata simu na kuitia mfukoni mwake, mbele yake akachomoza mwanamke mrembo. Ilikuwa ni bahati mbaya iliyodhamiriwa na msichana yule, Kilaza pamoja naye waligongana na kikumbo hicho kuwadondosha mpaka chini. Kilaza alisimama na kumpa pole binti yule aliyekuwa akigugumia kwa maumivu. Alijaribu kusimama akajitia kudondoka tena. Alijitia kujikwaa kumnasa Kilaza, Kilaza akanasa baada ya kuingia tamaa.
Kilaza alimkongoja mwanamke yule mpaka kwenye gari yake. Baada ya msichana huyo mrembo kuingia ndani ya gari ya Kilaza, kilaza akaipasha moto injini na kuzipachika gia.
"Pole sana"
"Ahsante Kilaza"
Mshituko.
Mshituko wa ghafla ukamkumba Kilaza. Si kwa kuwa tu alitajwa jina lake ba msichana yule ambaye alikuwa hamfahamu, bali pia muonekano wa msichana yule uliobadilika badilika kwenye sura yake. Kuna wakati ilikuja sura ya Salome na kuna wakati ikarejea ile ya Jenifa.
Kilaza hakufika hata kilometa 2 akaisimamisha gari ghafla pembezoni mwa hifadhi ya barabara jirani na kituo cha polisi cha Mwatex.
"Wewe ni nani? Na kwa nini unanichezea"
Akauliza kwa jazba. Salome akacheka kicheko kisicho cha kibinadamu. Kicheko kilichorindima na kuvuma katika masikio ya Kilaza na kurudia rudia kama mwangwi. Uoga ukaivaa roho ya Kilaza. Wazo likampitia kichwani mwake
"Kimbia"
Mshituko wa ghafla ukamkumba Kilaza. Si kwa kuwa tu alitajwa jina lake ba msichana yule ambaye alikuwa hamfahamu, bali pia muonekano wa msichana yule uliobadilika badilika kwenye sura yake. Kuna wakati ilikuja sura ya Salome na kuna wakati ikarejea ile ya Jenifa.
Kilaza hakufika hata kilometa 2 akaisimamisha gari ghafla pembezoni mwa hifadhi ya barabara jirani na kituo cha polisi cha Mwatex.
"Wewe ni nani? Na kwa nini unanichezea"
Akauliza kwa jazba. Salome akacheka kicheko kisicho cha kibinadamu. Kicheko kilichorindima na kuvuma katika masikio ya Kilaza na kurudia rudia kama mwangwi. Uoga ukaivaa roho ya Kilaza. Wazo likampitia kichwani mwake
"Kimbia"
Ikawa kama sauti iliyozungumza kwa nguvu kwani hata Salome akamuuliza
"Unataka kukimbia? Hutatoka salama humu ndani" akacheka tena kwa tuo na kumwambia "kwa bahati mbaya napenda kukutarifu tu kuwa itatoka maiti yako na si wewe ukiwa mzima"
Dakika chache baadaye kilichotokea, hakikupaswa kutazama bali kusimuliwa kama hivi nikuambiavyo. Kucha ndefu zilizoanza kumchomoza Salome kwenye vidole vyake, zikawa na makali kama kisu. Mkono wa Salome ukachimba moja kwa moja kwenye kifua cha Kilaza na kuchomoka na moyo wake Kilaza uliokuwa bado katika hali ya kudunda. Damu nyingi zilimvuja Kilaza huku nyingine zikitokea mdomoni na puani. Kilaza alitupa mikono yake hewani ndani ya gari hilo na kufurukuta kiasi kisha akatulia. Alinyamaza kimya, ukimya wa milele.
Baada ya Salome kumaliza kilichomleta kwa Kilaza, Baba yake; akatoweka. Alitoweka huku akiacha ujumbe kwenye kijikaratasi alichomsihikisha Kilaza mkononi mwake. Kiaratasi hicho kiliandikwa kwa damu na si wino.
"Salome is back" aliandika kwa lugha ya kigeni akimaanisha kuwa salome amerudi. Akapotea kama upepo eneo hilo huku gari la Kiaza likiwa limesimama eneo hilo hilo la kituo cha polisi cha Mwatex.
...
Regina akiwa ofisini kwake akijiandaa kutoka, akapokea ujumbe katika simu yake. Ujumbe wa kutisha uliomfanya asitoke ofisini kwake na kurudi kitini mwake. Jasho lilimtoka na kuhema kwa hali ya kasi sana.
"Baada ya Kilaza kuingia kuzimu hakikisha wewe unajiandaa usife kabla hujatubu. Salome"
Aliusoma tena na tena akijihakikishia kuwa hajasoma vibaya ujumbe huo.
'Salome!? Ni nani anapanga kunichezea? Ina maana juu ya mambo niliyoyafanya yameshavuja?'
Kiti chake kilikuwa kikubwa, kila alipojigeuza bado alihisi alikuwa haenei. Kiyoyozi kilibadilisha hali ya hewa ndani ya ofisi yake, lakini jasho lilikuwa likimchuruzika kwa hofu. Alitafakari kuwa Salome amekwishafariki na je huyo aliyejimtumia ujumbe ni yupi? Hakuelewa.
Akajipa nguvu za kusimama mpaka aliposogelea mlango wa kutoka nje ya ofisi yake. Simu yake ikaita.
"Mama Regina"
Ilikuwa ni sauti ya Mwarami aliyehamanika kutokea upande wa pili wa maongezi.
"We mwarami vipi?" Regina naye akapatwa na hofu.
"Kilaza, mama" akatulia kama anayemeza funda la mate "amekufa kifo kibaya sana hapa Mwatex. Kwenye kifua kuna tobo kubwa na moyo wake umekutwa nje"
Ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Regina. Baada ya simu ya Mwarami kukatika, akajaribu kuipitia tena ule ujumbe wa ulioingia punde.
"..Baada ya Kilaza kuingia kuzimu"
'Mungu wangu! Ina maana Kilaza amefariki kweli?'
Jasho likazidi kumtoka. Wasiwasi ulimvaa wala hakujua jambo la muhimu la kufanya. Alielekea kwenye gari yake huku akiwa na mawazo tele yaliyomtia hofu. Salome akamtia wazimu. Salome aliyerudi kulipiza kisasi kutoka katika kifo. Salome aliyeanza na Kilaza, baba yake. Regina akaipachika gia baada ya kuipasha moto injini na kukohoa kiasi. Aliingiza gari barabarani kwa mwendo wa taratibu kuitafuta barabara ya igoma kuelekea Mwatex. Alitaka kujihakikishia mwenyewe juu ya tuhuma hizo za kifo cha Kilaza. Dakika chache akiwa jirani na kituo cha mwatex, alishuhudia umati mkubwa wa watu waliokusanyika sehemu moja.
'Bila shaka ndiyo pale' akainong'oneza nafsi yake. Kabla hata hajafika eneo lile akiwa na mawazo ya kule aendako, alikanyaga kwa nguvu pedeli za breki ya gari yake tairi zikalalama na kuserereka kwa fujo barabarani hapo. Watu kadhaa walipiga kelele walioshuhudia tukio hilo.
"Toba!!"
"Unauua wewe mwanamke" mzee mmoja akasema ka uchungu.
Alikuwa ni msichana aliyepita mbele ya gari ya Regina. Regina alitumbua macho pima aliposhuhudia yule aliyemgonga, akiruka hewani na kujitupa mpaka chini huku asitoke damu waa chochote kilichoitwa mkwaruzo au kuchubuka. Regina alishuka garini na kumfuata yule msichana.
Hakumjua.
"Umeumia?"
Regina akamuuliza kwa hofu. Yule msichana hakulalama kwa maumivu wala kuonesha dalili kama alikuwa ameumia. Yule msichana alisimama huku akitabasamu. Regina alikua akimuangalia kwa huruma akiwa na hofu huenda atakuwa ameumia.
"Labda nikupeleke hospitali? Inawezekana umeumia kwa ndani ufahamu"
"Hapana usijali mama Regina, nipo salama"
Mshituko.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umeniitaje binti?"
Sasa Regina akawa amemuachia pale alipomshika akawa anamtazama kwa uso wa kazi. Yule msichana bado akawa akitabasamu.
"Nakuuliza wewe binti" alimtazama moja kwa moja kwenye mboni zake "umenifahamu vipi jina langu?"
Kimya
Wakiwa bado wamesimama kama mita 50 kutoa pale walipokusanyika watu waliokuwa wakitazama tukio lile la mauaji ya Kilaza, kukatokea mtafaruku kiasi kule kwenye ule mkusanyiko kiasi cha watu kukimbizana ovyo.
Virungu vya askari wa kutuliza ghasia.
Ving'ora vya gari la wagonjwa vikasikika gari hilo nalo likawa limeshafika. Mmoja kati ya wakimbiaji kutoka kule kwenye mkusanyiko, alimpita pale pale aliposimama Regina na yule msichana. Alikuwa ni kijana anayemfahamu yule msichana aliyesimama na Regina.
"Jenifa!!"
Ulikuwa ni mshituko uliompata baada ya kumuona Jenifa eneo lile kiasi cha kumfanya kupoteza fahamu papo hapo. Regina hakuelewa. Alimtazama Jenifa kisha akamtazama yule kijana aliyelala pale ardhini. Alipouinua tena uso wake kumtazama Jenifa, Jenifa hakuepo.
Kaenda wapi?
...
Baada ya tukio lile, Regina alizidi kuchanganyikiwa. Hakuweza tena kuendesha gari peke yake kutokana na matukio ya mauzauza yaliyoanza kumtokea. Mwarami alikuwa nyuma ya stering akiindesha gari ya Regina.
"Ilinishangaza sana Mwarami"
"Sasa mama unadhani atakuwa ni Salome?"
"Sielewi Mwarami" akiwa ameshika paji la kichwa chake kwa hali ya kuchanganyikiwa, akamalizia "huyu kijana ninayekuambia tunamfuata hospitali, alimuita kwa jina la Jenifa na hata sura haikuwa ya Salome"
"Sasa mama kwanini uwe na wasiwasi?"
"Wasiwasi wangu juu ya jina langu. Amelifahamu vipi na anataka nini kwangu kama ni huyo Jenifa nisiyemfahamu mimi"
Wakawa wamekaribia katika hospitali aliyompeleka yule kijana aliyezimia mara baada ya kumuona Jenifa. Uzuri alimkuta alikwisha amka. Baada ya salamu, Regina alikuwa na kiu na shahuku ya kufahamu juu ya lile tukio pale barabarani.
"Anha unajua dada yangu kilichonifanya nizimie, yule msichana ni nduhu yangu. Mtoto wa mjomba wangu Dastan. Amefariki zaidi ya miaka sita iliyopita. Kifo chake kilileta sana utata katika familia na kushangaza wengi waliomfahamu, nimeshishtushwa sana kumkuta akiwa pale tena hai" akawa amenyamaza huku akiwaacha hoi wale wasikilizaji. Yeye akaendelea "kwani wewe unamfahamu vipi Jenifa!? Na yuko wapi sasa hivi?"
Hakupata jibu lolote kutoka kwa Regina kwa kuwa Regina alikuwa amechanhanyikiwa sana. Mwarami ndiye alimjibu
"Aliyeyuka"
"Unaona? Ule ni mzimu. Ule ni mzimu kabisa" yule kijana akasema kwa wahka huku macho kayatumbua pima.
Regina hakuweza kuunganisha kisa chochote na kupata picha halisi ya mambo yanayomtukia. Akiwa chumbani kwake hata chakula hakikumpita, alikuwa amejiegesha huku mkono ameulaza juu ya paji la uso wake kiuvivu.
Baadaye ikaja taswira mbaya ya siku ya kifo cha Salome. Hakuwepo siku hiyo, lakini alishuhudia vyema kama mkanda wa sinema. Kabla haijamalizika filamu ile ya kutisha alishituka na kuamka. Moyo ulikuwa ukimuenda mbio na jasho jingi likimtoka. Akatambua kuwa si ndoto ile ndiyo ilimfanya ashituke kwa hali ile ya kuogofya. Juu ya paji lake la uso aliuhisi unyevunyevu. Unyevunyevu mzito. Akajipangusa na kutazama unyevu ule.
Damu.
Akazitazama damu hizo na kutazama labda eneo hilo juu ya paji lake la uso kulikuwa na jeraha. Hakuwa nalo. Akasimama na kuwasha taa akajitazama kwenye kioo kipana na kirefu alichokipachika ukutani. Damu hazikuwepo na jeraha hakuliona.
Inashangaza.
Hofu ikamvaa na kujiuliza kuwa ni mambo gani hayo yaliyokuwa yakimkuta. Akaogopa sana. Alijaribu kuangaza juu ya dari la chumbani kwake, hakuona kitu.
Wazo pekee lililompitia kichwani kwake, "salome aliyekuja kwa taswira ya Jenifa" akaona si sahihi aendelee kukaa ndani ya chum ba hicho bila kulitafutia ufumbuzi jambo hilo. Ufumbuzi angeupata hospitali kwa jabir aliyemfahamu Jenifa kiundani.
Akatoka chumbani kwake na kuliwasha gari kuelekea hospitali. Akiwa ndani ya gari akampigia Mwarami.
"Kama nilivyokueleza hali inazidi kuwa mbaya kwa upande wangu"
Alizungumza kwa hofu huku akiwa anaifuata barabara ielekeayo katika hospitali ya mkoa. "Naomba tukutane kwa Jabir ili niweze kufahamu kwa undani kumuhusu huyu Jenifa"
Kisha akaitupiua kwenye simu yake kwenye kochi la pembeni, akaendelea kukanyaga pedeli ya mafuta.
Akiwa ameshaingia katika geti la hospitai hiyo kabla hajaivuka kaunta, Mwarami naye akawa nyuma.
"Heri umewahi"
Wakaongozana moja kwa moja mpaka katika wodi ya Jabir.
"Niwie radhi kwa kuhartibu usingizi wako ndugu. Ila hali inazidi kuwa tete na mauzauza yanazidi kuongezeka mpaka nyumbani kwangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akamuhadithia yote yaliyotukia chumbani kwake. Jabir akionesha kuzidi kushangaa jambo hilo. Hakujua chochote cha kuwasaidia watu hao walionesha kuhamanika kwa mambo yaliyokuwa yakiendelewa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment