Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

ROHO ILIYORUDI KUANGAMIZA - 3

 





    Simulizi : Roho Iliyorudi Kuangamiza

    Sehemu Ya Tatu (3)



     Lakini Batuli alikuwa amekwishakosa imani na familia yake. Imani ndogo iliyomfanya ahisi ukweli kama alivyohisi. Imani iliyomfanya aunganishe vipande vya hadithi hata ionekane hadithi ya kusikitisha. Simulizi ilyomfanya Regina kulengwa na machozi. Simulizi iliyomfanya Regina kumchukia Salome ‘mimba ya Salome ndiyo ilimfanya rafiki yangu kufukuzwa shule na kumfanya ashindwe kutimiza lengo lake kielimu’ Regina alijinong’oneza. Akamchukia pia Kilaza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilaza aliyemuona kama mmoja wa mitume, kati ya kumi na wawili; aliyetumwa na mungu. Mtume aliyetumwa, kulitimiza neno lake kuwa; hatowaacha watoto wake wateseke kamwe. Regina alipitia mafundisho mbalimbali ya kanisani, hivyo aliyajua hayo. Kumbe ni mlaghai aliyekuja kwa roho ya malaika, Alijisemea. Mwanaume anayetaka kumsononesha rafiki yake, Batuli. Kwa hadithi aliyoisikia hakufaa kuwa Kilaza yule aliyemfahamu mwanzo. Habari zilizokera na kuchefua kwa mtu aliyelelewa katika maisha ya ucha mungu. Kama yeye. Kitendo cha kutembea na mtoto wako uliyemzaa mwenyewe? Ni aibu iliyoje? Alipatwa na chuki kila alipomfikiria Kilaza. Chuki zilizomfanya atamani kumtafuna mzima mzima, kama angekuwa na uwezo huo. Alitamani kumfanyia jambo zito. Jambo litakalompa kilema cha maisha. Kilema ambacho kitamtoa chozi kila akikitazama, kulipa chozi la thamani, la rafiki yake. Akaisuka mipango yake taratibu huku akizungusha macho yake yaliyong’ara kwa hasira. Macho yaliyoonesha akiwa katikati ya fikra nzito. Ilipita miaka mingi tangu rafiki hawa wawili watengane wasiishi pamoja. Lakini hiyo haikuwa sababu ya Batuli hata asahau hasira ya rafiki yake. Hakusahau Regina alivymchoma Salim na bikari, alipokuwa akimsumbua sumbua yeye(Batuli), mara ngapi wanaume waliyoogopwa shuleni walipigana na Regina kwa madai kuwa walipimana nguvu na mwanamke huyu wa shoka? Akakumbuka hata ile siku ambayo regina aliuvaa ugomvi wake, akapigana na kile kikundi cha wanawake wenye maneno machafu na kuogopwa na shule nzima. Urafiki wao kipindi hicho ndipo ulipoota mizizi. Urafiki uliokomaa hata ukawafanya wadhaniwe kuwa ni mapacha wasiofanana. Urafiki wa kweli, mfano wa kuigwa. Batuli aliupata ulimi wake, huku akiwa katikati ya kilio “Regina, unataka kufanya nini katika hili?” aliuliza kwa uoga. Mawazo yaliyomtoa Regina katika ulimwengu huu wa kawaida, yakamfanya asisikie hata alichoulizwa. Regina aling’ata papi za midomo yake kwa hasira. Aliwaza ni adhabu ipi atakayompatia Kilaza, ikamstahili shetani kama yeye. Akatabasamu kwa karaha kama aliyekuwa akimuona Batuli alipokuwa akimtazama. Ukweli ni kwamba Regina hakuona wala kusikia chochote kilichomzunguka kwa wakati huo. Batuli alimgusa taratibu huku akiendelea kumuuliza taratibu. Regina hakujibu chochote, alitabasamu tu kumridhisha Batuli ahisi kuwa yupo pamoja naye. Lakini akamshauri jambo “Rudi nyumbani na umuadhibu Salome ukiwa kama mama, siku nyingine akifanya kitendo cha dharau mbele yako. Vitendo vinavyoenda kinyume na maadili nyumbani kwako ni wewe mwenyewe mwenye una nguvu ya kuvikemea. Hakuna ambaye ataweza kuirekebisha nyumba yako pasipo wewe kuchukuwa hatua” angalau Batuli akaipata guvu iliyomdhihaki mwanzo. Nguvu iliyokuja baada ya kuupuza mshangao wake, kutokana na ushauri alioupata kutoka kwa Regina. Ushauri usio wa kawaida na alivyomzoea rafiki yake. Alimjua ni mtu wa kulipiza kisasi. Mtu asiyekubali kushindwa na kuacha mambo yaishe kirahisi rahisi, hivi hivi. Kumbe hakujua. Hakujua mipango ya regina ilikuwa sawa na alivodhani na kumjua tangu mwanzo. Lakini sasa Regina hakuwa mwepesi wa kuropoka kabla hajachuku hatua. Regina alikuwa mtu hatari. Alishirikiana na vikundi vya watoto wahuni kufanya uhuni. Regina alichukua hatua ya kupanga kumwaga damu. Ilikuwa ni hatua ya kutisha lakini ni mipango aliyoitaka ichukue muda mrefu mpaka atakapobaini ukweli kwa macho yake mwenyewe. Kazi yake ikamwaathiri. Kila kitu katika maisha yake sasa, kikawa ni lazima kifanyike kwa ushaidi uliokamilika. Aliona alichowaza kinafa



    SEHEMU YA NNE

    Salome akapendeza machoni mwa wanafunzi wenzake. Wanafunzi wakampenda kutokana na unadhifu alio nao, pamoja na uzuri aliobarikiwa. Wasichana wenzake wenye imani ndogo wakaongeza mapenzi kwa wapenzi wao, wasije kuibiwa. Hakuna mwanaume aliyeshindwa kujizuia kugeuza shingo yake, pale Salome alipokuwa akipita. Salome akawa Salome kweli. Kifua chake kikabeba vichuchu vilivyosimama na kunogesha kila nguo aliyovaa na kuwa kivutio tosha kwa wengine. Miguu iliyonawiri na kujaa kiubora hata ikaitwa miguu ya bia. Ngozi yake laini iliyoteleza hata ikipakwa mafuta ya kawaida, ilimeremeta sana. Ilikuwa ni ngozi iliyozoea kupigwa na Air condition muda wote. Nyumbani kila sehemu ipo, kwenye gari la anko Salimu ipo; hata darasani ilikuwepo pia. Hiyo ikamfanya ngozi yae kuto kuathiriwa na miale mikali ya jua. Kati ya wanaume waliomtolea Salome macho ya uchu, alikuwako kijana mmoja asiye na uwoga. Kijana aliyeujuwa utajiri, pia akalelewa katika maisha ya kifahari. Utajiri wa baba yake, Mzee Rutashobya. Mzee mwenye viwanda vya sukari huko Kagera. Kila Muhaya alimfahamu mzee huyu. Serikali ikatambua msaada wake. Alisaidia mkoa wa Kagera kusambaza sukari katika kila kona ya mkoa huu. Sukari yake pia ilipenya hata mpakani mwa Tanzania na Uganda, pale mtukula ikaelekea na nchi nyingi kama kenya pia. Rwanda na Burundi pia ikafika. Utajiri ulioanza kama masihara kwa ndoto iliyompata usiku wa manane. Ndoto aliyoiota ikiwa ndiyo kwanza, faida yote aliyoipata kutoka katika uvuvi; aliitumia yote kwenye msiba wa baba yake. Ilikuwa ni siku chache tu zilizopita, alitoka kumzika baba yake bila msaada wa ndugu yeyote. Baba aliyemuachia urithi wa mashamba ya kahawa, migomba na miwa. Lakini yeye alichagua kuanzisha kiwanda cha kutengeneza sukari. Aliiona adha ya wananchi wa mkoa huo, kusubiri sukari kwa muda mrefu iliyokuwa ikitoka mjini Dar es salaam. Bidii ikamfikisha leo katika tabasamu pana akitazama nyumba ya kifahari iliyozungukwa na msitu wa maua yaliyopendeza. Mbele ya nyumba hiyo aliegesha magari mbalimbali ya kutembelea tu. Yale ya kazi aliyaegesha sehemu maalumu ya maegesho yake kilipo kiwanda chake cha sukari. Alikuwa na utajiri wa kumfanya acheke. Utajiri wa upendo kutoka kwa mwanamke mrembo wa kichaga, Lizana. Utajiri wa watoto watatu wa kwanza akiwa ni George akifuatiwa na wadogo zake wa kike wawili; Dorice na Cecilia. Basi Salome hakulikataa ombi la George. George aliyeteseka nafsini mwake kutokana na hisia zilizomtesa muda mrefu. Nafsi iliyoteseka tangu alipomuona Salome kwa mara ya kwanza. Nafsi iliyopoteza subira, tangu salome alipoipoteza miaka kumi na saba na leo akisheherekea miaka kumi na nane. Kikwazo kikawa ni dini. George alilelewa katika misingi thabiti ya dini yake ya kikristo. Rutashobya, baba yake; alipewa uzee wa kanisa katika kanisa la kkkt kijijini kwao Kiziba. Salome pia, Kilaza baba yake; alikuwa ni muisilamu mwenye siasa kali, walijulikana kama Sunni. Lakini hisia alizonazo Salome, hazikujali jambo hilo. Usishangae. George akauvunja ukimya baada ya kumkabidhi kadi ya birthday. Akamchombeza maneno fulani. Maneno yaliyomlegeza Salome asijali tofauti zao za dini. George alifanikiwa. Dini haikuwa kipingamizi cha kuzuia hisia zao. Yalikuwa ni mapenzi motomoto. Mapenzi ya George yakazidi yale aliyoyapata kutoka kwa Kilaza. Kilaza alikuwa mvivu kumfikisha anapopataka. Salome alijilalamikia nafsini mwake “huu ni uzee ama? Raundi moja tu jamani?” ilikuwa kila baada ya Kilaza kutimiza haja zake na kutokomea. George akawa mwanaume wa shoka aliyekata kiu ya Salome. Salome pia hakuwa tayari kumpteza George kwa mwanamke mwingine. Akajiapiza. Shule nzima nayo ikafahamu uhusiano wao. Wanawake wakamuogopa George kama ukoma, waliogopa kumgusa. Waliogopa kuongea naye hata kuwa karibu naye. Salome alitisha kila alipokuwa akipita. Alikuwa ni mzuri mwenye nuru ya ukatili isiyojificha.

    ********************************************

    Alishusha pumzi ndefu baada ya tafakuru iliyomezwa na uvuguvugu wa kahawa ya maziwa. Kahawa aliyoletewa na katibu wake. Baada ya kuinywa kwa funda moja tu, kikombe kikawa cheupe. Aliinamisha kichwa chini mara akakilaza kisogo chake juu ya kiti, hiyo yote akiwa katika kuwaza. Mara wazo la kitoto likampitia Regina, alipokuwa nyuma ya kiti chake ndani ya ofisi kubwa ya kifahari. Wazo la kumfuatilia Salome kila hatua katika mienendo yake. Alitaka kufahamu kuwa, kama Salimu ni kweli alikuwa akimpeleka shule, ama hisia za Batuli zilikuwa zikiendana na ukweli. Hisia zilizomfanya ahisi huenda hata Kilaza hakuwa mkoa wa pili alipoaga ghafla kuwa anaenda kikazi. Ama alipokuwa akihisi, hata kuchelewa kwa Salome kulisababishwa na kule kujivinjari kwake na Kilaza katika hoteli yoyote ya kitalii katika jiji hili hili la Mwanza. Batuli alijuwa Salome hakumuogopa tena, wala Kilaza hakuwa na upendo wowote kwake. Hivyo walikuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hawana uoga wa kwenda kufanya ufuska wao mbali na jiji hilo Mwanza. Regina akamuahidi kumsaidia

    kujuwa ukweli. Ukweli ambao yeye mwenyewe pia alitamani kuujuwa. Aliuinua mkonga wa simu yake iliyojisahau mezani kwake, na kuzungusha tarakimu kadhaa. Sauti ya kiume iliyoitika kiupweke, ilisikika upande wa pili. Alikuwa ni Mwarami. Mwarami yule kibaka mzoefu aliyeajiriwa na Regina kwa kazi ya kupeleleza matukio yaliyo nje na ofisi ya Regina. Kibaka aliyetafutwa na wananchi kwa uchu wa kuiangamiza roho yake, ambaye ndiye rafiki mkubwa wa hakimu huyu katili. Alipeleleza matukio makubwa yaliyompatia pesa nyingi Regina lakini yeye Mwarami alifanya kwa ujira kiasi. “kijana saa saba sasa.. jana usiku ulikuwa wapi aise?” aliuliza kwa ghadhabu baada ya Mwarami kupokea tusi. “owh! Mama, Regina huyo” ilikuwa ni sauti iliyokwaruza kama spika mbovu iliyopoteza nyaya zake. Kisha aliendelea baada ya kuinakili sauti ya Regina “si unajua mambo ya club, nimechoka sana. Pia hatukuwa na miahadi ya kukutana leo ndio maana sikuona sababu ya kuwahi kuamka” Regina alisonya, kisha aliendelea kutoa agizo la sababu ya kumpigia simu ya ghafla “kuna jambo nataka unisaidie” alisema “…unaifahamu shule ya St mary’s iliyopo kule mjini.. enhe! Hiyo hiyo karibu na sheli.. nisikilize basi… kuna binti yupo pale nahitaji msaada wako… sasa unadhani msaada gani tena? Umfuatilie mpaka nitakapokuwambia basi … ndiyo, picha zake zote zinazofaa kwa habari ni muhimu; kwa hiyo nahitaji sana uwe muangalifu na nina imani ile kamera unayo bado?.. pitia ofisini kwangu kuchukuwa ile gari ndogo, kazi ianze leo. Ujue ni gari gani huja kumchukua shuleni, na wapi huelekea baada ya kutoka shuleni na anakutana na nani awapo matembezini na popote pale… sawa kabisa vitu kama hivyo…. tangu lini ukaniuliza ujira? njoo tuyajenge, kisha utaniorodheshea mahitaji yako yote mengine… fanya haraka” simu ilikatika kisha alishusha pumzi nyingine mfululizo na kupata akili mpya. Akili ya kumtuma kijana wake mwingine kumfuatilia alipo Kilaza. Hakutaka kumshirikisha Batuli katika hili hivyo alikuwa muangalifu katika kumchimba Batuli mpaka ajue kilaza alimuaga anaelekea wapi. Hakutumia simu yake ya mkononi. Alizungusha tena tarakimu kadhaa, mkongo ukiwa sikioni. Simu iliita, mara ikapokelewa na sauti ya Kilaza ikiwa upande wa pili. Regina alihamaki na macho kumtoka pima. Sauti ya kilaza ilisikika upande wa pili wa chombo ikiendelea kukoroma “halo halo…” regina aliamua kuitikia akijaribu kutengeneza uchangamfu ili Kilaza asijaribu kushitukia chochote. “enhee halo shemeji.. za masiku?.... mimi ni Regina jamani umesahau hata sauti yangu? …. Ndiyo… mungu wangu kumetokea nini shemeji” alijitia kama hajui jambo lolote “hapana hakunieleza lolote… sawa shemeji … nakusubiri” kisha simu ilikatwa na kilaza. Regina jasho likamtoka. Hakujua Batuli, alikuwa katika hali gani wakati huo. Aliitazama ile simu ya mezani kama vile ingeweza kutoa majibu ya kile kinachoendelea, lakini haikuwa hivyo. Alikuwa na uhakika ingekuwa kosa kubwa sana kumtumia japo ujumbe mfupi wa maneno, Batuli kwa sababu hata alipompigia simu ilipokelewa na Kilaza. Akiwa katika kuhamanika huko, mara Mwarami aliingia. Chapu chapu Regina alimpa maelekezo mafupi, baada ya kuona kazi haikuwa ndefu na ngumu kama alivyotarajia. Kwa kuwa haikuwa na haja ya kumpigia mwingine wa kumfuatilia Kilaza. Nguvu zake sasa alizielekeza kwa Salome ili aweze kumnasa Kilaza pia. Mwarami alimpa moyo Regina kazi ingefanyika sawia na mipango ingekuwa ni ya siri kubwa. Mwarami na Regina waliagana baada ya kukabidhiwa kitita fulani cha pesa na kuondoka. Regina akiwa amesimama akimtazama Mwarami wakati akitoka, mara Kilaza pia aliingia. “shemeji sijachelewa sana?” Kilaza alikuwa katika haraka wala hakujali mshangao uliotawala uso wa Regina. Regina hakuitaji Kilaza ainakili sura ya Mwarami. Hivyo ilikuwa ni sababu ya kumfanya aduwae kama aliyeataka Mwarami apae na atoweke katika ofisi hiyo. Alizuga kama hakuna lilitokea. Alijibu kwa shida kama aliyepatwa na ububu “ndi..i.i..yo shemeji” huku tabasamu la kinafki likiudhihaki uso wake. Kilaza na Regina walitoka mpaka nje, katika mgahawa mmoja wa kifahari huko mjini, kuzungumza kwa kinagaubaga. Ingewachukuwa muda kurudi. Hivyo Regina alimuaga katibu wake kuwa asingerudi kabisa siku hiyo. Regina akatumia gari ya Kilaza, yake akiwa ameliegesha ofisini hapo hapo. Anayo magari mengine mawili nyumbani kwake. Gari ya Kilaza ikalamba lami.



    Regina hakuitaji Kilaza ainakili sura ya Mwarami. Hivyo ilikuwa ni sababu ya kumfanya aduwae kama aliyeataka Mwarami apae na atoweke katika ofisi hiyo. Alizuga kama hakuna lilitokea. Alijibu kwa shida kama aliyepatwa na ububu “ndi..i.i..yo shemeji” huku tabasamu la kinafki likiudhihaki uso wake. Kilaza na Regina walitoka mpaka nje, katika mgahawa mmoja wa kifahari huko mjini, kuzungumza kwa kinagaubaga. Ingewachukuwa muda kurudi. Hivyo Regina alimuaga katibu wake kuwa asingerudi kabisa siku hiyo. Regina akatumia gari ya Kilaza, yake akiwa ameliegesha ofisini hapo hapo. Anayo magari mengine mawili nyumbani kwake. Gari ya Kilaza ikalamba lami.

    Walifika mgahawani wakiwa hawajazungumza chochote tangu mwanzo wa safari. Kilaza akiwa amefura kwa hasira. Hasira iliyoshindwa kujificha na kuvimbisha mdomo kama ulioficha mnofu. Regina yeye hakuwa na la kuongea, kwa sababu yeye alikuwa hapo kumsikiliza Kilaza. Walipofika iliwabidi kusimama. Kilaza aliangaza huku na kule kuchagua viti vilivyo pembezoni mwa mgahawa huwo. Sehemu ambayo imetulia. Sehemu ambayo midundo ya mziki wa marehemu Marijani, ingewafikia kwa mbali sana. Kilaza alimshika mkono na kumuelekeza Regina pa kukaa. Wakiwa bado wanatazamana mhudumu wa kike alikuja na kuwahudumia, kisha aliondoka na oda ya wali na samaki mbili pamoja na maji mawili makubwa ya kilimanjaro. Wote kwa pamoja walikuwa wapenzi wa chakula hicho. Regina ndiye aliuvunja ukimya huwo kwa kulitupa swali mezani. “shemeji! Batuli amefanyaje tena?” swali hilo lilionesha kumpa shida sana Kilaza, kulijibu. Kinywa chake kilitafuta mwanzo mzuri. Hatimaye kikapata uhai, baada ya kutafakari kwa muda “hivi Regina” alikatishwa na kikohozi kikavu kilichopita kooni mwake. Kisha aliendelea “rafiki yako(Batuli) ana akili timamu kweli yule?” kabla Regina hajajibu mhudumu alirudi na kitoroli cha kusukuma, kilichobeba sinia la chakula lililobeba sahani mbili za wali na samaki, kisha maji baridi na bilauri mbili za udongo. Mgahawa uliwakirimu vizuri wateja wake, hata huduma ikawa nzuri tofauti na migahawa mingine iliyo pembezoni mwa mji. Regina alianza kwa kung’ata mnofu wa samaki, kisha akakumbuka kuwa ilikuwa zamu yake kuzungumza “sijakuelewa shemeji una maana gani?” Kilaza alijitia kucheka tabasamu lililojenga hali ya karaha na mfadhahiko. Aliacha kula, mikono akiwa ameifunga kwa pamoja na kuiweka chini ya kidevu chake. Mikono yake ikiwa imeegemea muhimili wa meza pekee. Sura yake ikaingia katika umakini kwa kile ambacho alifikiria kukizungumza. Alianza “Batuli amenishangaza sana. Sikutegemea kama angekuwa na akili za kipumbavu kiasi kile. Akili za kushikiwa. Juzi usiku shemeji..” ladha ya chakula mdomoni mwa Regina haikuwepo tena. Hadithi aliyoianzisha Kilaza ikamvutia, ikamfanya hata kususa uma na kisu kilichoanza kukata mnofu mwingine wa sato aliyebaki upande mmoja tu wa nyama. Naye akawa katika umakini wa kumsikiliza. Kilaza naye alikuwa, katika kuendelea kuipanga hadithi yake iwe tamu. “..nilimuaga kuwa naelekea kazini huko mwadui kama ujuavyo? Cha kunishangaza niliporudi leo nyumbani, nilikuta hali ya kustaajabisha sana nyumbani kwangu. Batuli alikuwa analia peke yake chumbani” Ilikuwa majira ya saa saba mchana. Batuli alikishindwa chakula akipendacho. Chakula alichoandaliwa na Swaumu kijakazi wake. Batuli alirudi chumbani kwake baada ya kuhisi uchungu uliomkaba kooni, ulitaka kumporomosha machozi yake tena. Uchungu ambao uliletwa kila alipokuwa akikumbuka vitendo alivyokuwa akifanywa na binti yake mwenyewe wa kumzaa, na kipenzi mumewe Kilaza. Aipokuwa katika kulia huko, ndipo mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa taratibu. Ulifunguliwa taratibu kama vile muingiaji alikuwa katika mipango ya kutaka kumdhuru aliye kuwako ndani. Batuli aliunyanyua uso wake na kukutana na uso wa Kilaza ukitabasamu. Kilaza akastaajabu kumkuta Batuli akilia. Alimfuata kwa kiunyenyekevu kama vile alikuwa na mapenzi ya kweli basi. Kama vile alikuwa anajuwa kuwa Batuli alikuwa anajuwa anang’ong’wa. Hivyo naye ndipo akazidisha mapenzi ili Batli afute kile alichokuwa akidhania. Batuli aliuputa mkono wa Kilaza kisha alisimama kwa jazba. Machozi yalizidi kumtoka huku akilia kwa kwikwi. Maneno yakaanza kumporomoka bila kujali ukali wa sauti yake “hivi kilaza mume wangu nimekukosea nini mimi? Kilaza humuogopi Mungu wewe? Kilaza ni nini unaifundisha jamii na wengine watakapogundua kitendo unachokifanya?” kilaza akiwa bado katika kushangaa, hakuelewa ni nini Batuli alikuwa anamaanisha. Alimfuata akimshi wazungumze CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/taratibu ili waelewane “tafadhali Batuli nyamaza kwanza kulia ili nifahamu umekumbwa na nini ili niweze kukuelewa. Halafu zungumza taratibu” Batuli aliiputa kwa mara ya pili tena mikono ya Kilaza kisha alihamia ulipo mlango “nasema sitaki!” aliropoka kwa nguvu haswa. Kilaza alibaki akimtazama. Batuli akaendelea “ni nani asiyefahamu humu ndani wewe unalala na mwanao(Salome)? ni nani asiyefahamu hata siku ile tulipokupeleka hospitali ulicheza mchezo na Zamda, wa kujifanya unaumwa ili Salome asinieleze siri zako? Umekosa nini kwangu Kilaza? Nakuuliza?” alimfuata akiwa anampiga piga kifuani. Mara ardhi ikampokea Batuli kwa heshima. Ikamng’oa jino lake la mbele. Damu nazo zikaisalimia zulia la manyoya. Kilaza alimpiga kibao cha ghafla. Kibao kilichomuangusha mpaka chini Batuli. Kisha naye Kilaza alipata sauti “huu upuuzi umeupata wapi? Umeichoka ndoa?” akiwa amemuinamia Batuli aliyekuwa akilia kwa maumivu na damu nyingi zikimchuruzka kutoka mdomoni. Ndipo hapo simu ya Regina ilipoingia. Regina alisikia Batuli akilia. Kilaza alimueleza yote hayo Regina, kama aliyekuwa akishangazwa na jambo hilo. Alijitetea. Haikuwa kawaida Batuli kumshuku hata alipokuwa akirudi usiku wa manane. Iweje leo anishuku natembea na binti yangu? Salome? Nimekosa wanawake? Yupo anayetaka kuharibu ndoa yangu, yupo anayemwambia haya mambo ya kipuuzi Batuli. Regina alishusha pumzi nzito kisha alimuuliza “sasa wewe unadhani ni nani?” kilaza alijibu kwa kubwatuka. “nitamjua Regina” alinyamaza kuruhusu pigo hil la maneno limuingie vizuri Regina, huku akimuangalia Regina kama alikuwa akimtisha “na nikimjua ama zake ama zangu” regina akacheka kwa dharau, naye akajinong’neza ‘huna adabu. Umekuja hapa kunitisha kwa upumbavu wako? Au kwa sababu unajua mimi ni rafiki pekee wa karibu wa Batuli? Na mimi nikikumata kwenye kumi na nane zangu nitakachokufanya utajuta’

    hawakuongea tena mpaka sahani zao zilipokuwa nyeupe kabisa. Kilaza ndiye alikuwa wa kwanza kuaga. Regina aliitika kwa kichwa akiwa ameshikilia upande wa mwisho wa samaki. Alipokuwa akitembea kulifuata gari ake, Kichwa cha Kilaza kiliwaza mengi. Kuna lolote analolijua? Kwanini amenijibu kwa jeuri kiasi kile? Anajiamini kwa cheo chake? Nitakachomfanya yule fedhuli atajuta. Hawezi kuanza kuichokonoa ndoa yangu nikiwa namtazama. Lazima amkumbuke bibi wa bibi yake mwaka huu. Aling’ata papi zake, kwa meno ya juu yaliyong’ata za chini kwa hasira. Aliitekenya gari yake aina Mitsubishi, nayo ikaitika kiuvivu na kuingia barabarani kama iliyokuwa haitaki vile. Regina naye hakuendelea tena na yule samaki aliyebaki mifupo tu. Aliagiza juice ya rozela iliyochangwa na ubuyu. Aliipenda sana. Alipokuwa katika kutafakari. Akitafakari vitisho vya Kilaza, bila shaka aliamini lipo jambo litakaloenda kutokea. Ni jambo lipi? Litatokea muda gani? Wakati akiwaza, ndipo simu ya Mwarami nayo iliingia. “ndiyo mwarami… sipo ofisini …. Hapa mjini katika ule mgahawa wetu… ndiyo huo huo… nini? .. safi umepata picha za kutosha?... sawa njoo hapa nilipo basi” alijichekea mwenyewe. Lakini kwa kuwa alitazamana na sura ya kijana mgeni katika macho yake, alicheka kama aliyefurahishwa na sura ya kijana huyo aliyekuwa akitabasamu mbele yake. Kicheko kikazidi pale yule kijana alipombinyia kijicho chake kimoja. Mara yule kijana alisimama kumfuata alipo Regina. He! Anakuja?. Yule kijana aliinuka kumfuata. Regina alimtazama akisubiri afike. Hakuwa mwanamke aliyeogopa wanaume. Alijiamini sana na hakujidharau kwa kuwa eti yeye ni mwanamke. Mawazo ya Kilaza yakapotelea hewani kwa muda. “Habari yako?” yule kijana alinyoosha mkono kwa ishara ya kusalimiana. Tabasamu la Regina halikumbanduka, aliitika huku akimkaribisha “nzuri.. karibu” kijana huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Erick, alikaa kwenye kiti alichokiacha Kilaza. “sijui nianzie wapi dada yangu?” alianza. Regina alimuita muhudumu amsikilize Erick. Baada ya muhudumu kuondoka na oda ya maji makubwa ya Kilimanjaro, Regina aliupata ulimi wake. “anzia tangu uliponiona katika huu mgahawa” Erick akacheka, kisha akakohoa kusafisha koo. “unajua dada yangu wewe ni mzuri sana?” Kwa sura hii iliyoanza kuzeeka? Huyu kijana ananitafuta nini? Ndio njama za Kilaza hizi? mbona bado mapema? Regina alijiuliza huku akitabasamu kinafki kumridhisha. Akamjibu “nafahamu. Ndicho kilichokuleta?” “hapana ninakusikitikia sana” alisimamisha maongezi pale alipoletewa kinywaji chake. Alimshukuru muhudumu, na kufakamia bilauri ya maji kwa funda moja. Kisha aliendelea “yule mzee uliyekuwa naye hapa namfahamu vizuri sana” macho yakamtumbuka Regina kama yalikuwa yanataka kumtoka. “unamfahamu vipi?” aliuliza kwa tamaa ya kumjua Kilaza. Alifahamu kuwa akipata pa kumuanzia Kilaza, itakuwa rahisi kumuangamiza. “yule mzee ni kiwembe hatari” Regina akajitia kutokuelewa, aliuliza “kiwembe? Kivipi?” Eick alicheka kisha aliyabwaga yote. Erick ni kijana aliyekuwa akiishi mtaa wa pili karibu na nyumba anayoishi Kilaza na familia yake. Salome alimuhusudu sana kila alipokuwa akimuona. Tembea yake akitembea. Ongea yake ya mapozi akiongea na rafki yake Husna. Hata akicheka. Ndipo siku moja alipoamua kumtolea uvivu. Akamfuata. “salome mimi nakupenda” Erick hakufahamu kama ilikuwa ni utoto wa Salome ama ni nini kwa kipindi hicho. Alishangaa siku moja akiwa kibarazani kwake akipunga upepo, huku akijisomea gazeti la udaku. Mapolisi watatu walimjia na mzee aliyemfahamu kuwa ni Kilaza, baba yake Salome. Walimtia pingu bila kujua kosa wala kuambiwa na kumuweka kwenye landrover yao huku akiwa na singlendi tu. Hakuruhusiwa kumuaga yeyote. Wala kuufunga mlango wake. Kila alipokuwa akiuliza kosa lake, alijibiwa kwa mabuti ya uso. Mpaka alipofika mahabusu, uso wake ulichakaa kwa damu nzito zilizoanza kugandana. Alipelekwa katika kituo cha mabatini. Hakujua chochote, kama mwanzo alipochukuiwa. Lakini alivuliwa kila alichonacho na kubaki na suruali pekee. Akatupwa lupango. Alikaa mule ndani kwa muda wa wiki mbili bila mshitaki wake kutokea, ili apadishwe kizimbani. Ndipo siku moja polisi mmoja wa kike, alimtoa kama aliyekuwa akimchukulia maelezo. Kumbe akaenda kumpa mwanga wa maelezo ya kesi yake. Ndipo alipojua kuwa, Kilaza alikuwa akitembea na binti yake. Polisi huyo alifahamu kuwa Kilaza alikuwa akitembea na binti yake, kwa sababu yeye alikuwa kimaa wake. Alimuacha polisi huyu kutokana na penzi alilopata kwa binti yake, Salome. Mama huyu wa kinyakyusa aliongea kwa masikitiko makubwa, lakini alimuahidi kumtoa Eick. Jioni wa siku iliyofuata, Eick alitoka Mahabusu akiwa bado na bumbuwazi. Aliduwaa kusikia kuwa, Salome alikuwa akitembea na Kilaza, hakuamini. Aliporudi nyumbani, hakukitamani chumba chake. Kilikuwa kimevunjwa na kubakiziwa godoro tu. Chumba kilikuwa cheupe kama alivyohamia na kupewa ufunguo na mzee mbekaye kwa mara ya kwanza. “hizi ni hila za Kilaza” alijisemea kwa uchungu, huku machozi yakimtiririka. Alihama mtaa huo, usiku hou huo; akielekea kwa rafiki yake Emmanuel, aliyekuwa akiishi mbali na mtaa huo. Ikawa hadithi mbaya iliyomuhakikishia Regina, kuwa Kilaza kweli alikuwa akitembea na binti yake. Alimuuliza Erick “uliendelea kumfuatilia Salome?” “wee! Hapana unataka nife?” alihamaki, kisha aliendelea “Yule jamaa ameweka walinzi wa kutosha wa kumfuatilia yule demu” Regina alimpa bussiness kadi yake “tafadhali naomba unitafute baadae, kuna jambo nataka tuongee. Hapa nilipo, kuna mgeni namsubiri ana jambo nyeti anataka kuzungumza na mimi”. “hamna shida sister, ila yule jamaa hafai kuwa na mrembo kama wewe” neno hilo la mrembo ndiyo lilimfurahisha zaidi Regina. Erick akaondoka Mwarami akaingia.



     Regina alimpa bussiness kadi yake “tafadhali naomba unitafute baadae, kuna jambo nataka tuongee. Hapa nilipo, kuna mgeni namsubiri ana jambo nyeti anataka kuzungumza na mimi”. “hamna shida sister, ila yule jamaa hafai kuwa na mrembo kama wewe” neno hilo la mrembo ndiyo lilimfurahisha zaidi Regina. Erick akaondoka Mwarami akaingia.

    Mwarami alikuja akiwa na kijimkoba. Bila shaka kijimkoba hicho kilikuwa na kamera ya kazi. Waliita kamera yaazi yeye na Regina pekee. Haikumchukua muda kumuona Regina, mgahawani. Sehemu waliyokuwa wakikutana mara kwa mara katika vilkao vyao nyeti. Hata kile kikao cha mwisho cha kumuangamiza meya wa jiji la mwanza, Joram Mperembe; kazi waliyotumwa na mpinzani wake, ambaye alikuwa hawara wa Regina, kilifanyika katika mgahawa huo ho. “mbona leo umebadilisha makazi Mama, Regina?” Mwarami alimuuliza huku akiwa anajifuta jasho. Hakujibu haraka haraka. Utamu wa juice ulimkolea mpaka kisogoni. “ah! Kuna mpuuzi mmoja alidhani mimi mgeni kiwanja hiki” akimmanisha Kilaza. Aliendelea “ndiyo alinileta hapa, sasa nikaona tumalizie hapa hapa maongezi na wewe” mhudumu yule yule, aliyewahudumia wageni wote wa Regina, alikuja tena kumuhudumia Mwarami “nakunywa Sparleta” Mwarami alijibu, muhudumu akaondoka. Regina aliendelea “enhee nipe habari, shushu wangu” alimtania. Utani uliosindikizwa na tabasamu la bashasha. “mama ujumbe wa leo utaufurahia kwa kweli. Kale katoto sikutegemea kama kageweza kuwa kanatembea na mtu mkubwa hivi hapa mjini” Mwarami aliongea hayo, huku akiwa anapekua pekua kwenye begi lake kama anayetafuta kitu “mama bwanaa…! Picha? Picha nimepiga za kutosha tu. Ila yule mtoto ni Budege kwa kweli” Regina alionyesha kutoelewa. Aliendelea kumkazia macho bila kuongea chochote. “yaani zoa zoa yule binti. Kwa leo tu..” Aliyakatisha maongezi yake yaliompa hamasa kubwa Regina ya kusikiliza kwa makini. Alikuwa ameinama, alipoinuka akainuka na kamera. Kisha akaendelea “enh…e! picha hizi hapa.” Alimpatia kamera aina ya digital yenye screen inayoonyesha picha zote zilizopigwa. Regina akiwa anaendelea kuzitazama picha kwa makini, Mwarami alikuwa akiendelea kuzungumza “huyo ni mwanafunzi mwenzake. Walikuwa wamekaa kimahaba mahaba muda wote walipokuwa kituoni. Huyo kijana ni mtundu sana. Mara amshike chuchu mara ambusubusu, anaonesha hana uoga na mach ya watu wazima” Mwarami aliungumza kila tukio kila pica iliposogezwa mbele na Regina. Ilipofika kwenye picha nyingine, Mwarami alitabasamu kumuona Regina ameshtukana hakuendeea kuzipeleka haraka haraka kama za mwanzo. Alisema kwa bashasha “Sasa huyo mwanafunzi alipoondoka ndipo likaja gari la huyo jamaa yake mwingine na gari yake ni…” kaba hajamalizia. Regina aliropoka “Mitsubishi” Mwarami alimtazama kwa mshangao Regina. Akajiuliza, ina maana mama ananituma kazi huku akiwa ananifuatilia? Ina maana hii kazi kaniwekea mtego? Ikambidi kuuliza “umejuaje” kwa hamaki, Regina alijibu kama aliyejawa na shahuku. Shahuku ya kutamani kumwambia yote kwa wakati mmoja. Alimjibu kiufupi “huyo mpuuzi aliyeniweka hapa, ndiye huyu hapa pichani” Regina alimuonesha upya Mwarami kamera yenye picha ya Kilaza na Salome wakiwa wameshikana viuno kama wapenzi. Mwarami naye aliishangaa picha hiyo kama si yeye aliyekuwa ameipiga. “Mwarami” Regina aliita. Mwarami aliuinua uso wake, kamera ikiwa mkononi “kazi yetu imeanza sasa” Regina alimueleza yote kuhusu jambo hilo. Alimueleza tangu siku ya kwanza alipokutana na Kilaza karibu na mti wa mkungu, pale shuleni kwao. Batuli akiwa ana ujauzito ambao bado haukuanza kuliathiri shati lake kwa kutunishwa na kitambi cha ujauzito. Akamuleza yote kuhusu Batuli alipoachishwa shule kwa sababu ya mimba aliyoipata kutoka kwa Kilaza. Batuli akaolewa akiwa na binti wa kike aliyempa jina, Salome. Mpaka alipoamua kumueleza kuwa binti huyo pichani na huyo mzee ni mtu na baba yake. Mwarami hakuamini. Macho yalimtoka kama aliyepokea habari za kutisha. Aliuziba mdomo huku akiangaza huku na kule kama ni siri ambayo haikupaswa kusikika kwa mtu mwingine. Alimuinamia Regina kama anayemnong’oneza “mama Regina? unasema kweli?” Regina hakutoa sauti alitimngishia kichwa hukua akitabasamu kwa raha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********************

    Kilaza alipotoka katika mkutano wa vitisho na Regina, alinyoosha mguu mpaka shule aliyokuwa akisoma Salome. Alimkuta Salome ameshajichokea, yupo peke yake kituoni. Hakujuwa kuwa muda mfupi alikuwako na mvulana anayejaribu kutingisha penzi lake kwa Salome. Hakujuwa pia kuna mtu mwingine alikuwa katika kazi ya kumfuatilia Salome. Alikuwa huru kwa kuwa aliona muda ulikwisha kwenda. Kituoni hakukuwa na mtu na magari yalipita kwa kupishana dakika nyingi nyingi. Hivyo alimtandika busu, la kwenye papi zake, Salome bila aibu na Mwarami naye aliichukua picha hiyo bila ajizi. Kilaza alikuwa akiyachezechezea mashavu ya salome kama aliyekuwa akimbembeleza hivi. Salome alipoonesha tabasamu naye alijilegeza kwa huba. Kiuno kikatwaliwa katikati ya mikono ya Kilaza iliyompeleka kwenye gari. Salome alilegea haswa. Alilegea kama changudoa yeyote aliyeopoa bwana la kizungu. Ila ukweli haukuwa hivyo. Kilaza aliyempiga mabusu kadha wa kadha ni mzazi kabisa wa Salome, aliyeyapokea mabusu hayo kwa furaha. Gari likachomoka kwa mwendo wa taratibu bila pupa. Kilaza alikuwa akiendesha gari huku akiwa hana furaha, Salome anagundua hali hiyo iliyomkumba Kilaza. “mpenzi. Kuna nini?” msikilize huyu msichana asiye hata na chembe ya aibu. Si huyu ndiye alikuwa akimlilia Kilaza mara kwa mara kana kwamba ni baba yake. Huyu huyu Kilaza aliyekuwa akiitwa baba hapo zamani naye akaitikia “ndiyo mwanangu kipenzi” leo anaitika bila hata haya “acha tu darling, kuna mpumbavu kashitukia dili letu” macho yakamtoka pima Salome “dili letu? lipi?” ina maana Salome amekwishaona ni halali kutembea na baba yake kama mpenzi? Ina maana amesahau kuwa kitendo wanachokifanya ni kosa la jinai? Hivi hajui vitendo wanavyofanya ni sawa na dili? Sasa anashanga nini kusikia dili? Kilaza akaona uvivu kujibu akanyamaza. Salome aliuvunja ukimya “Kilaza” aliita kwa kukosa heshima kabisa. Lakini si ni yeye mwenyewe, Kilaza alikwishamvunjia heshima tangu mwanzo?. Kilaza alimgeukia, kisha aliyarudisha macho tena barabarani. “nakuuliza kuna nini?” Salome alipatwa na ghadhabu. Kilaza naye alijibu kivivu “salome unanichosha akili yangu, natafakari kuhusu Regina. Regina amekwishamueleza yote mama yako; kuhusu mimi na wewe ni wapenzi” Salome akamkatisha Kilaza kwa kicheko cha kebehi “sasa wewe una wasiwasi gani? Kwani tatizo nini akiondoka? Mimi sikutoshelezi? Au sio wewe unayenisifiaga mimi ni mjuzi kuliko mama yangu?” Kilaza alicheka kwa karaha, hukumjibu kitu. Alipiga selo baada ya kusimama mbele ya geti kubwa la jumba lake la kifahari. Karim alilifungua geti hilo kwa rimoti, huku akiwa ndani. Salome ndiye alikuwa wa kwanza kushuka na kuingia ndani. Kilaza alichelewa chelewa kidogo kisha naye alishuka na kuingia ndani. Hakusimama sebuleni alipokaribishwa chakula na Swaumu, alielekea moja kwa moja chumbani kwake. Chumbani alimkuta Batuli akiwa amesimama dirishani akiongea na simu. Batuli alipomuona Kilaza ameingia, alishituka na kukatisha maongezi. “ulikuwa unaongea na nani?” kilaza aliuliza huku akimfuata alipokuwa amesimama. “Regina” Batuli alijibu. Jina hilo likapandisha hasira zaidi ya Kilaza. Hasira iliyoinua mkono mzito wa Kilaza na kumzaba kibao Batuli. Batuli akaibusu ardhi tena. Alinyanyuka akiwa amekwishalowa machozi mashavuni mwake. “niuue.. niuue nakuambia” Batuli aliinuka na hasira akimfuata Kilaza, kifua mbele. Kilaza alimsukumiza ukutani Batuli akapigwa mweleka akaanguka chini. Akainuka tena akimfuata kama guruwe lisiloona linapooelekea. “nakuambia niuue sio unanitesa tesa. Kila mtu anafahamu ufuska wako unaoufanya na Salome. Na huyo malaya kama ni mimi ndiye nimemzaa akanyonya ziwa langu” alikuwa akiongea kwa uchungu, huku akiyashika matiti yake na kuyatingisha juu chini “…miezi tisa. Nakuapia kwa jina la mama yangu Tausi. Kilaza…” aliapa kwa kupitisha kidole chake shingoni “….atakufa kifo kibaya sana na atajuta” hayo yote Salome alikuwa akiyasikia chumbani kwake, akayapuuza. “Kilaza mimi naondoka. Ukipenda talaka yangu utanipa usipopenda inshaallah. Baki na malaya wako asiye hata na aibu kutembea na baba yake” hilo nalo halikumtisha Kilaza, alicheka lkwa kebehi “ondoka bwana. kibiriti ngoma wewe, kafie mbele huko” kauli hiyo ikamfanya Salome atabasamu. Huku nje wafanyakazi wa hapo nyumbani walikwishazoea mambo hayo kwa sasa. Lakini walipokuwa nje wakipiga hadithi za hapa na pale walishangazwa kumuona Batuli akiwa na begi kubwa uso umemvimba. “mama, mama unaenda wapi?” Swaumu alimfuata Batuli akimsaidia mzigo. “acha tu Swaumu naenda ninapopajua”

    Batuli alitoka kwa huzuni. Alisimama huku akiiangalia nyumba aliyomuacha Kilaza na Salome wakiwa ndani; akiwa analia kwa uchungu. Aliyameza mate yaliyojikusanya kama fungu na kulimeza funda kubwa, zito ‘gudu’ likapata shida kupita kooni mwake. Aliingalia nyumba iliyopendeza kwa nje huku ndani ikiwa imeoza kama mwili wa binadamu. Mwili ulionawiri nje, ndani ukiwa umebeba utumbo uliobeba uchafu wa kila aina. Zamda alisimama huku akimuangalia Batuli, alimsikitikia. Karim alihuzunika, Swaumu akamwaga chozi. Wote walimpenda Batuli kwa kuwa aliishi nao vizuri. Aliishi nao muda mrefu tangu Salome akiwa bado mdogo sana. Hivyo Swaumu na Zamda bado walikuwa mabinti pia. Karim aliikumbuka siku ile alipookotwa naye, Batuli pale dampo la jirani na soko kuu; akichakula chakula uchafu kutafuta vyuma chakavu. Hakika ni uchungu mkubwa. Chozi lisilo na adabu, likashindwa kustahimili kuulinda uanaume wake. Alilia kwa uchungu pia. Wote kwa pamoja walimuaga mpaka alipotokomea mbali na macho yao. Kilaza aliyaona yote kupitia dirisha la chumbani kwake. Naye roho ilimsuta lakini aliivaa roho ya shetani. Roho isiyojali, kwani nini? Alijiuliza. Sijamfukuza.. kaondoka mwenyewe, alibishana na nafsi yake nzuri iliyokuwa ikimsuta kwa roho ya kifedhuli aliyokuwa nayo. Alishuka chini na kutoka nje. Kilaza aliamuru kila mmoja kurudi kazini kwake chini ya utawala wa mke mpya Salome. Salome aliyetawazwa kutoka katika utoto na kuwa mke. Jambo hilo lilifanyika kwa muda wa dakika chache mara tu baada ya Batuli kuondoka. Salome alifurahi kutambulishwa hivyo mbele ya wafanyakazi wote wa humo ndani. Watakoma sasa, alijinong’oneza. Hakuna aliyeshangaa kwa kuwa wote walikwishafahamu. Ni ngumu kuamini kama hili jambo linaweza kutokea, ila amini usiamini hili jambo lipo na ni kawaida kabisa kwa dunia ya sasa. Si kwa Salome tu anayeweza kfurahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na baba yake; wapo vijaa wa kiume wanaotembea na mama zao wazazi, hiyo haikushangaza zaidi?. Batuli alielekea kwa Regina akiwa na begi lake la nguo tu. Hakuchukua chochote kutoka katika mali walizochuma wakiwa pamoja na Kilaza. Regina alimpokea kwa picha. Picha za Kilaza na salome wakipigana mabusu kedekede. Ile ambayo Kilaza alimshika kiuno Salome, ikamponyoka Batuli. Miguu yake ikakosa nguvu ya kukibeba kiwili wili chake. Batuli akadondoka kama gunia ‘puu’ Regina hakuwa akimtazama. Kishindo kilimshitua na kugeuka haraka kama aliyesikia mlio wa risasi. Alikimbia kumuokota, Batuli hakuwa amezimia kabisa. Ilikuwa ni presha iliyomfanya akose nguvu na kudondoka bila kupenda. Jambo la Kilaza na Salome lilimpatia ugonjwa ambao hakutegemea kuupata katika maisha yake. Presha, ni ugonjwa ambao aliuona unawapata watu wenye mawazo mengi na matatizo ya dunia. Kwa raha alizozipata kwa Kilaza; kula vizuri, kulala vizuri na maisha yaliyopendeza kwa kutazama ama kuhadithiwa hakuna siku ambayo alidhani angeyaacha maisha yale na kwenda kuhifadhiwa na rafiki yake. Kitu kilichomuuma zaidi na zaidi mtoto wake wa kumzaa mwenyewe ndiye aliyemfukuza ndani ya nyumba. Ilikuwa ni huzuni iliyomtiririsha muda wote machozi mengi. Regina alijitahidi kumsihi asilie, lakini haikusaidia. Batuli aliyasema mengi. Alimlaani vya kutosha Salome na Kilaza. Aliwalaani kila laana mbaya unayoijua hapa duniani. Regina akatabasamu kwa kuwa naye alipanga hivyo hivyo, kama alivyokuwa akiropoka ropoka ovyo Batuli. Batuli alitamani kusikia siku moja Kilaza na Salome walizipoteza pumzi zao kwa kifo cha kusikitisha sana. Damu yao haikuwa na faida kwa kizazi chochote kile. Regina akampiga piga mgongoni huku bado tabasamu likiwa pambo zuri usoni mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog