Simulizi : Roho Iliyorudi Kuangamiza
Sehemu Ya Pili (2)
“Hapana Daktari, hii si sahihi” Kilaza akakataa. “ninahitaji kuongea na Salome binafsi, na asiingie mtu mwingine yeyote wakati nipo katika mazungumzo naye” daktari alikubali huku akimpa maelekezo mafupi muuguzi wa kike kuendelea kuweka mazingira yatakayowafanya watakaoingia wasihisi tofauti yeyote.
“Amekufa?” daktari alipotoka chumbani alipomlaza Kilaza, aliulizwa kwanza na Batuli hata kabla hajamaliza kuufunga mlango. Alitabasamu kidogo kisha akauweka uso wa faraja.
“Hapana mama, mzee amepata matibabu mazuri lakini kwa sasa amepumzika” akiwa kama aliyesahau jambo akalikumbuka baada ya kunyanyua kidole juu kabla ya kuuinamisha uso wake na kuyafinya macho. “Ameniambia anahitaji kuongea na Salome, sijuhi ni nani kati yenu?” alipitisha kidole kwa Zamda kikapita kwa Batuli kikasimama kwa Salome aliyekuwa ameduwaa huku akisema
“Mimi” Salome akayahamisha macho yake kwa mama yake, Batuli. Daktari hakuwaruhusu wajadiliane chochote akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu mzee ana bahati sana, sumu aliyokunywa ilikuwa mbaya sana” alijua tu kwa kusema hivyo angekatishwa kwa kauli ya mshangao
“Sumu!!!!”
Akatabasamu kidogo kabla hajajibu uongo mwingine “Ndiyo ni ile sumu ya kuua wadudu wa mashambani inatisha sana”
Batuli aliangua kilio, Zamda na Salome wakiwa na kazi ya kumbembeleza. Daktari hakuwa hata na chembe ya huruma kwa kweli. Alichochea uongo, kwa pesa alizonogeshwa nazo. Aliongeza “Salome naomba uingie haraka ili apate muda wa kupumzika tafadhali”
Salome alinyanyuka akimuacha Batuli chini akigala gala kwa kulia huku yeye akiingia chumbani. Batuli naye alinyanyuka baada ya kusikia hivyo, akitaka kuingia.
“Hapana mama naomba usubiri kwa muda kidogo” Daktari alimzuia. Ilikuwa ngumu Batuli kukubali kirahisi. Aliyatumbua macho, akibinua midomo, akatanguliza kifua mbele tayari kwa kuigia “Mama tafadhali, naomba uheshimu hospitali; ufuate taratibu unazoelekezwa” Batuli akabwatuka
“Wewe kijana naona hunijui, unanieleza mume wangu amekunywa sumu halafu nitakuelewaje unaponikataza kuingia halafu unamruhusu mtoto?” Daktari alijibu kwa kutetea dili lisiharibike kwa Kilaza
“Mgonjwa ana hali mbaya sana lakini ameomba kuzungumza na mtoto tu kwanza naomba usipoteze muda wa kumuhudumia mumeo umruhusu mtoto aingie kisha utaratibu mwingine utaendelea baada ya Salome kutoka” hapo Batuli alikubali kwa shingo upande. Salome akapita chumbani.
Salome alitembea kwa uoga kama aliyekuwa akiiogopa ardhi. Muuguzi wa kike aliyekuwa akirekebisha shuka iliyomfunika Kilaza alitamani kumcheka Salome aliyelowa kwa machozi. Hakumcheka kwa sababu Salome alikuwa akilia. Hakumcheka kwa sababu alifahamu hayo yalikuwa maigizo. Hakucheka kwa kuwa Kilaza alikuwa akitabasamu taratibu, kabla Salome hajafika hivyo kumfanya yeye acheke. Wala hakucheka kwa kuwa alichekeshwa na ulichodhani kimemchekesha.
Muuguzi huyo alicheka, kumuona Salome akiwa ndani ya nguo za kulalia. Nguo ambazo alizivaa wakati ambao anaenda kuufungua mlango uliobishwa wakati ule Batuli na Kilaza wakiwa wamemfuata kujua kulikoni.
Salome alitembea kama watawa kanisani, mikono kaikunja kwa adabu. Lakini hatua chache fupi zilimfikisha mbele ya uso wa baba yake(Kilaza) uso ulioonesha maumivu, kuumwa na huruma iliyopitiliza.
Salome aliogopa kumshika. Muuguzi alimsaidia kumuamsha kwa upole kama aliyeunguwa na mafuta ya moto; ‘ukimgusa vibaya utamumiza’.
Kilaza aliweza kuigiza haswa.
Aliyafumbua macho yake kwa shida na kuona chozi la chungu lililomshuka Salome. Aliendelea kuigiza kama aliyeugulia kweli maumivu. Alisema kwa shida baada ya kumpiga ukope muuguzi yule atoke nje
“Salome mwanangu, haya yote ni kwa sababu yako” aliuchezesha ulimi na kuwa kama mzito; uliomfaya aonekane kama kibogoyo. Salome alimshika mkono baba yake na kumlilia kwa uchngu
“Baba nisamehe, sitomwambia mama, usife baba” maneno yote ya hudhuni yakamtoka. Kilaza alikohoa mfululizo kama aliyepaaliwa. Hakuzungumza chochote. Aliendelea kukohoa. Hiyo ilikuwa ni moja ya njama zake, kumuongeza maumivu Salome. Alijua akiwa katika hali hiyo. Hali ya utete kama anayekaribia kukata roho, Salome hataweza kukubali kujiona yeye ndiye chanzo cha kifo cha baba yake. Chanzo kwa kutoa siri? Siri tu? Ambayo angeweza kuificha kwa kuokoa maisha ya baba yake? Siri ya kubakwa na baba yake jamani? Salome pia aliapa kutomwambia mtu yeyote.
Aliijua vyema hali halisi ya nyumbani kwao. Ugumu wa maisha mara atakapokufa baba yake, Kilaza; ulianza kumtia joto la karibu kama kuzimu. Hapana asingekubali kuwa mpumbavu kiasi hicho. Asingekubali kutoa siri leo aje kuteseka milele. Alijua jambo lile lilikuwa la siku moja tu hivyo baba yake angeamka angekuwa ameshamsamehe na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Lakini pia hakuwa mpumbavu kukubali endapo Kilaza angemtaka tena kimapenzi. Aliapa pia kutomruhusu kabisa kuuchezea mwili wake. Lakini alijiuliza kama asipomueleza mama yake ni wapi atakapokimbilia. Atakapoimbilia endapo mchezo wa baba yake ukikomaa? Alikiri kwa kujinong’oneza, kuwa yeye ameshakomaa sasa, na amepevuka, hivyo atamdhibiti.
Ni aibu iliyoje ikisikika mtaani. Alijiwazia kwa uchungu, akiwa anatoka chumbani alipolazwa baba yake(Kilaza). kikohozi hicho kilimfanya muuguzi yule atoke mbio, hata akampiga kikumbo nusura kumdondosha Salome aliyekuwa akitembea huku akiangalia nyuma alipolala Kilaza.
Baada ya masaa machache Kilaza aliruhusiwa na kurudi nyumbani.
Alirudi na mfuko uliojaa dawa zisizo na maana. Ilikuwa yapata jioni, saa kumi na mbili. Salome hakuwepo nyumbani. Alimkuta Batuli chumbani kajiinamia kwenye kabati. Alipougeuza uso, Batuli alikuwa amechoka kwa tafakuri nzito. Mawazo yaliyomfanya hata asimsikie Kilaza aliyemkumbatia kwa nyuma na kupitisha mikono yake mpaka tumboni akilipima joto la mkewe. Alishituka kidogo kisha akazungumza
“Salome ananichanganya sana mume wangu”
Hapo hali na uso wa Kilaza ukabadilika tena. Tabasamu pana likapotea, ukaja uso wa hudhuni. Akauliza kiunyonge lakini kwa kudadisi
“Kuna nini tena mke wangu” alilingojea jibu kwa hamu huku jasho la uoga likimchuruzika.
Batuli alikaa kwanza chini ili amueleze vizuri mumewe. Lilikuwa ni jambo ambalo yeye binafsi alilichukulia kiuzito kiasi. Hakuwepo mtu wa kuwasumbua sebuleni walipokaa. Utulivu uliomfanya Kilaza akaipenda hali hiyo.
Batuli alianza kumsimulia kuwa, waliporudi nyumbani, Batuli hakusubiri hata watulie kwanza.
Alimuuliza Salome hata kabla hajakaa, Hapa Batuli akawa anamsimulia Kilaza jinsi ambavyo alimuuliza Salome
“Hukunimalizia kuhusu huyo mtu aliyeingia chumbani kwako jana usiku” Salome hakuwa na la kujibu kwa kuwa aliapa kutomwambia hata mama yake. Lakini pia hakutunga uongo wa kuziba hiyo siri anayoipanga kuificha.
Hilo likawa ni kosa.
Akamjibu huku akiwa anaogopa kumtazama Batuli “Niliposhituka nilihisi kama ilikuwa ni ndoto tu mama. Ule uzito haukuepo tena wala sikuona mtu juu yangu, sielewi kuwa kilikuwa ni kiumbe gani”
Batuli akatoa tabasamu lililopwaya, tabasamu la hasira. Aligundua uongo wa Salome kuna jambo baya ambalo analificha. Ni lipi basi? Ndiyo hilo lililomuumiza kichwa. Hapo hapo Kilaza naye akatoa tabasamu la raha. Raha ya ushindi.
Alijua hiyo ni kufanikiwa kwa njama zake za kumtisha Salome asiitoe siri yake kwa mtu mwingine. Hivyo alifanikiwa.
Akawaza ‘usiku tena’.
Udenda ukamtoka kwa tamaa za utajiri zilizochanganywa na tamaa za kimwili. Alimshika mkewe kwa mahaba huku akimuuliza kwa upole
“Sasa mke wangu unadhani au kufikiri ni nini kinaendelea” aliuliza kwa mtego akijuwa fika jibu la Batuli litamsaida kuendeleza njama zake. Batuli naye akajaa kwenye mtego, akajimwaga mwaga.
“Mume wangu na wasi wasi wale mabinti wale wakina Husna ndiyo wanamharibu mtoto wetu”
Kilaza aliiona hoja iliyotolewa na Batuli haikuwa na mashiko, hivyo akaipuuza baada ya kusimama. Alipofika njia ya kuelekea chumbani akiwa ameliweka shati lake begani alisema “Swala la Salome niachie mimi, nitalifuatilia kiundani. Lisikuumize kichwa”
Angalau kauli ya Kilaza ikampa matumaini mapya Batuli, naye akapata uhai akajinyanyua kumfuata Kilaza.
Usiku mwingine wa manane Salome kama asivyotegemea, alishangaa kukibeba kiumbe kizito juu ya mwili wake. Kiumbe hicho kilikuwa kikimtomasa tomasa hapa na pale, huku na kule kumpandisha ashki.
Salome akanyong’onyea kama kuku mwenye kideri.
Alikwishafahamu aliyekuwa akimfanyia mchezo huo mbaya. Chozi likamtoka kwa huzuni akishindwa kujitetea. Sauti ya Kilaza ikapata uhaiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nafikiri utazoea Salome bado kitambo kidogo tu hutapata tena maumivu haya” ilikuwa ni sauti ya kubembeleza na iliyokera. Kilaza akaivua khanga ya Salome aliyojifunga rubega, akaitupa kusikojulikana. Matiti yaliyoanza kusimama dede, chuchu zake zilikuwa zimezama katika midomo ya Kilaza.
Alizinyonya kama zilikuwa zikitoa chochote.
Salome aliendelea kulia bila kufanya chochote cha kujinusuru. Siku ya pili kilaza akambaka Salome. Ukawa ni mchezo ulioendelea mara kwa mara usiku wa manane. Mchezo ulioanza bla Salome kupenda baada ya siku chache baadae Salome mwenyewe alikuwa akitabasamu kwa furaha kila ulipofika muda huo.
Si rahisi kwa kuelezea, ila Salome alimpenda zaidi Baba yake(kilaza) kuliko mwanaume yeyote duniani. Upendo usio na maana kati ya baba na mwana. La hasha! Ni upendo kati ya mpenzi na mpenzi. Upendo uliozaa wivu kwa mama yake. Wivu ambao Salome aliona Batuli, mama yake alikuwa akifaidi muda mwingi na mpenzi wake, kuliko yeye aliyekuwa akikutana naye kimwili usiku tu.
Hakuona tena aibu hata kama ingetokea nafasi ya kumtambulisha mbele za watu, kuwa Kilaza ni mpenzi wake. Masikini Salome, kumbe hakujua. Hakujua kama akili yake imechezewa kidogo, ikacheza kweli. Soda ya kopo aliyoletewa na Zamda, mshirika mkubwa wa Kilaza, ikiwa imefunguliwa; iliwekwa madawa.
Madawa kutoka kwa mganga yule yule wa Kilaza.
Ilibidi iwe hivyo ili mambo zaidi yasiharibike. Katika beseni lililojazwa maji, kwa mganga huyo; Kilaza alimuona Salome akiwa chumbani peke yake akiwaza jinsi gani ya kumwambia mama yake. Kwa hali hiyo aliona ushauri wa mganga ulikuwa ni sahihi. Ushauri wa kumuwekea limbwata ili ampende zaidi. Masharti yakaongezeka, tofauti na yale ya mwanzo. Kilaza aliambiwa kuwa ni lazima Salome atafanya njama zote ili mama yake aondoke pale nyumbani na yeye ammiliki Kilaza moja kwa moja.
Hilo likamshitua Kilaza, lakini hakujali, aliendelea kusikiliza.
“Utajiri utakaotisha, utawatisha wengi. Batuli atajinyonga kwa aibu ya wewe kutembea na binti yako” Ghafla mganga akashituka pia kabla hajaendelea na kile alichokuwa akikisikiliza ndani ya kibuyu alichokishika.
Sauti ile ya mzimu kutoka katika kibuyu cha mganga, iliongea lugha isiyoeleweka. Lugha aliyoielewa mganga peke yake. Sauti ambayo haikuwa hata na chembe ya mzaha. Sauti iliyokuwa ikijirudia rudia kama mwangwi.
Mganga aliisikia lakini Kilaza hakuielewa.
Mara Kilaza alishuhudia Mganga akitoa macho ya mshangao na yeye akapatwa na hamu ya kujuwa kinachoendelea. Nini ambacho mganga alisikia.
“vipi babu” aliita jina ambalo halikumfaa mganga, kutokana na umri wake mdogo; lakini alimuita babu kutokana na kazi yake. Kazi ya uganga. Hivi kwani ni lazima mganga wa kiume aitwe babu au mjukuu wa babu? ama wa kike aitwe bibi? Hilo ni swali ninalojiuliza mara kwa mara. Lakini majibu ambayo yalikuja kichwani mwangu mara kwa mara ni kudhani kuwa labda ni hali ya kuvuta wateja kwa majina ya kuogofya.
Mganga hakujibu aliendelea kusikiliza huku macho kayatoa kama anayenyongwa na kukosa pumzi. Ilikuwa ni habari mbaya sana kwa hapo baadae. Lakini pia mganga alikatazwa asimwambie chochote Kilaza.
Sauti ilipokatika mganga naye alishusha pumzi.
Si pumzi iliyomchosha kwa kutembea mwendo mrefu, si pumzi iliyosababishwa kwa kuwa alipanda kilima kirefu pia wala hakuwa amefanya kazi ya kubeba kitu kizito, ila yale aliyoyasikia tu yalitosha kumchosha.
Kilaza aliondoka kwa mganga bila kupata lolote la maana.
Japo alikuwa na mawazo sana. Mawazo ya kwanini mganga hakumueleza ile sauti ilizungumza nini. Licha ya kumuona mganga akiwa katika hali ya uoga unadhani akili yake ingetulia? Baada ya kurudi nyumbani, Hali ile ya kunyata usiku ikaendelea. Ukawa ni mchezo alioupenda pia. Ila sasa hakufanya tena kama mwanzo. Hakumuwekea tena madawa ya kulevya Batuli, ili asiweze kuamka mpaka asubuhi.
Hilo likawa kosa. Kosa alilofanya kiuzembe. Laiti kama angejua? Siku moja akiwa ananyata kumtoroka Batuli, Batuli naye alinyata kwa kufumbua jicho moja; kumfuatilia, wapi Kilaza alikuwa akienda usiku wa manane mara kwa mara, tena kwa kunyata? Hali hiyo ilimfanya ahisi kuna jambo ambalo lilikuwa likiendelea. Jambo lililomfanya moyo wake, kwenda mbio kuliko kawaida.
Hilo likawa kosa. Kosa alilofanya kiuzembe. Laiti kama angejua? Siku moja akiwa ananyata kumtoroka Batuli, Batuli naye alinyata kwa kufumbua jicho moja; kumfuatilia, wapi Kilaza alikuwa akienda usiku wa manane mara kwa mara, tena kwa kunyata? Hali hiyo ilimfanya ahisi kuna jambo ambalo lilikuwa likiendelea. Jambo lililomfanya moyo wake, kwenda mbio kuliko kawaida.
Japo kiyoyozi kilibadlisha hali ya hewa na kuwa ya ubaridi, lakini jasho lilimchuruzika kwa kuogopa kile ambacho alihisi. Hisia hizo mbaya, zilianza tangu siku alipohisi amewekewa kitu kibaya katika kinywaji alichokunywa usiku wa jana. Usiku ambao ulikuwa mrefu pia kwa Salome, aliyechelewa kuamka asubuhi yake. Hata alipoulizwa kwanini? Salome alijibu ‘kuna mtu aliingia humu ndani jana’ na pia Kwa sababu nguo za Kilaza hazikuwahi kufuliwa na mfanyakazi yeyote. Hivyo, hata lile doa la damu nzito iliyoanza kuganda kwenye suruali yake ya usiku, Kilaza alipoamka na kwenda kumbaka Salome kwa mara ya kwanza, Batuli ndiye alikuwa wa kwanza kuliona.
Hakujua kwa mara moja, ila aliunganisha matukio. Tangu Salome alipopata kigugumizi cha kushindwa kumueleza nani aliingia chumbani kwake. Hospitali alipokataliwa kuingia. Mpaka suruali ya Kilaza aliyoivaa siku moja tu kuikuta na damu sehemu ya mguu, bila yeye mwenyewe kuwa na jeraha lolote.
Hivyo leo alipanga kujua nini kilikuwa kikiendelea kwa macho yake ama kusikia kwa masikio yake mwenyewe. Kilaza hakuufunga mlango ili iwe rahisi atakaporudi asipate shida ya kuufungua.
Ikamsaidia pia Batuli kuamka, naye alianza kunyata taratibu, baada ya kulitupa shuka kitandani. Alisimama kumchungulia Kilaza alipokuwa akielekea. Hakuwa amefika mbali, hata mwisho wa safari ambayo Batuli aliitegemea. Hivyo ilimbidi kuchukuwa kitambo kidogo mpaka atakapofika anapopatarajia. Kilaza alitembea kwa kunyata, bila kuwa na haraka. Kuna muda aligeuka nyuma, kutazama kama alikuwa akifuatiliwa.
Alipokuwa akitazama nyuma, Batuli naye alijficha asionekane. Mwiso wa safari yake ndefu, kwa mwendo ule wa kunyata, uliishia katika mlango wa chumba cha Salome. Mapigo ya moyo wa Batuli yalienda mbio kuliko mwanzo. Aliwaza kwenda na fujo kushuhudia kitu ambacho Kilaza alikifuata kwa Salome usiku huo. Nafsi yake ikamkataza. Alitamani kulia, machozi yakagoma. Aliamua naye kunyata taratibu kwenda kusikiliza nini kilikuwa kikiendelea katika hiko chumba.
Batuli naye hakuwa na haraka ya kuufungua mlango wa chumba cha Salome. Kwa kuwa kicheko cha huba kilichomtoka Salome, kikampa muda mwingi wa kusubiri zaidi. Alijua alichokuwa akisubiri ndio maana hakuchoka. Hakuchoka kusubiri hata wakati ambao sauti ya Kilaza iliyobembeleza ikaitikiwa na ya Salome iliyopwaya hazikusikika kabisa. Mwili wake Batuli ulitetemeka kwa hasira.
‘mwanangu? Mwanangu niliyemzaa mwenyewe jamani?’ uchungu uliomfanya akumbuke ile siku alipong’ata mito, haikung’atika. Akamfinya mkunga, haikusaidia. Aliita mama, haikupunguza uchungu. Leo mwanaume yule yule aliyemzalisha mtoto huyu Salome, mwenyewe Batuli alipenda kumuita mama; leo wapo chumbani kama mke na mume, Wakiivunja amri ya sita? Amri iliyoamriwa na mwenyezi mungu katika vitabu vya dini ya kikristo. Haikuwa rahisi kukubali kwa kile alichokisikia kwa masikio yake mwenyewe.
Lakini je? Masikio yanamdanganya? Ikawa ni sauti iliyomsuta nafsi yake iliyojibembeleza kwa uchungu. Alijuta kuzaa. Lakini ni nani afahamuye yale mambo yajayo? Si alitamani na kupenda muda mrefu mwenyewe kuitwa mama? Chozi likamtoka akalia kama mtoto. Sauti ya kilio chake haikuwa kubwa sana, lakini ilizidi kuongezeka kila mara Salome naye alipokuwa akilia.
Tofauti yao wote ilikuwa hapa.
Salome alilia kwa huba na raha ya mapenzi aliyoyapata kutoka kwa Kilaza, lakini Batuli alilizwa na uchungu ulioukamata roho yake, uchungu uliomkaa kooni kama aliyemeza tonge la ugali lililohitaji maji mengi ili liweze kushuka.
Aliwaza mengi ya kufanya.
Aliwaza kuingia ili awaharibie kitendo wanachofanya, nafsi yake ikamshauri apuuzie. Aliwaza ajiue usiku huo huo kwa kunywa sumu ya panya ama kujinyonga; pia akajicheka kwa dharau huku akiwa ndani ya kulia. Akajinong’oneza kwa dharau ‘sasa nitakuwa nimemkomoa nani’ aliwaza aondoke usiku huo huo, aende popote alipokuwa akipajua. Kwa kuwa kulikuwa na marafiki zake wengi tu ambao wangemkaribisha kwa mikono miwili muda wowote ambao angewagongea, lakini hakuwa na la kuwajibu endapo angeulizwa imekuwaje na mabegi ya nguo usiku wa manane?.
Alijihisi aibu na kudhalilishwa. Alijihisi kukosa thamani mbele ya walimwengu. ‘kwanini mimi? Kwanini familia yangu? Eh! Subhanahallah’ alizidi kulia kila alipofikiria jinsi alivyompenda mwanaye na jinsi mume wake alivyompenda tangu siku ya kwanza walipokutana. Licha ya mapenzi hayo ya kifamilia lakini lilikuwa ni jambo la kusikitisha na la kishenzi baba kutembea na mtoto wake, tena ndani ya nyumba ya familia.
Batuli alihisi mikosi iliyoing’ang’ania maisha yake, hakuikuta ukubwani. Mikosi ya kuikosa elimu ya chuo kikuu kama alivyotegemea, akabebeshwa mimba na mwanaume aliyempenda akidhani hiyo ingekuwa furaha na upendo wake ukazidi kuongezeka kumbe ndo kwanza mwanaume huyo alilisubiri na yai aliloliangua litotoe kifaranga amtafune na kifaranga mwenyewe baada ya kumkinai kuku.
Alikaa muda mrefu akiwa hata amesahau kinachoendelea. Alishitushwa na kitanda kilicholalamika kwa sauti za ajabu ajabu
‘wamemaliza’ akajisemea.
Alinyanyuka mbio kurudi chumbani. Aliapa kuwa hiyo ilikuwa ni siku mbaya katika maisha yake kuliko yoyote iliyowahi kumpita duniani. Ni siku ya kipekee aliyowahi kuumia nafsi kuliko siku yoyote tangu kuzaliwa kwake. Batuli akamchukia Kilaza, akaichukia na damu yake (Salome) pia.
Alitamani ambwatukie Kilaza aliyekuwa akinyata na kuufunga mlango wa chumbani taratibu kama mwizi, lakini pia nafsi bado ilimkataza. Koo likajaa donge la uchungu, likashushwa na lita za mate.
Usingizi ukampitia karibu na asubuhi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hiyo, hakuthubutu kumsalimia Kilaza aliyejitahidi kumchangamkia tangu alipoamka hata wakati alipomuandalia chai. Hakujali tena kuchelewa kuamka kwa Salome kama mwanzo, alijifanya kama hajui kitu. Muda mwingi aliutumia akilia chumbani ndani ya shuka lake alilojifunika gubi gubi. Kilaza aliyaona mabadiliko, lakini hakuwa na wasiwasi na tabia yake aliyokuwa akiiona kama starehe. Aliona hali hiyo mpya Batuli ni nzuri sana kwa kumpa mwanya wa kutosha zaidi kujivinjari na Salome.
Siku kadhaa baadaye, Salome alipanga njama za kumfukuzisha Batuli(mama yake) ndani ya nyumba. Hayakuwa mawazo yaliyopendeza, ila yalimpendeza binafsi. Alitamani kumiliki, milki ya mwili wa Kilaza(baba yake), moja kwa moja.
Alijisikia vibaya, kumuona Batuli akimfuta chakula kilichochafua papi za Kilaza. Batuli naye alifanya hayo kwa uchungu huku akitazama jicho baya alilotazamwa na bintiye. Salome hakupedezwa tena na Kilaza kunyata usiku wa manane, kama mwizi; katika zile safari zao za huba usiku wa manane.
Salome hakuwa na umri uliozidi miaka kumi na sita. Hakuwa mwanamke hata astahili kuolewa na mwanaume yeyote licha ya Kilaza baba yake. Lakini dawa alizokunywa na mapenzi moto moto, alidiriki hata kutamani kupanga njama za kumuua mama yake.
Angemuua vipi? Alijiuliza sana.
Hakutaka kuacha ushahidi wowote wa kumkamatisha. Wala polisi wamshuku kuwa yeye ndiye muhusika wa mauaji hayo. Angeiweka wapi sura yake? Sura itakayochukuliwa kiukatili na wanajamii watakaomuona kama muuaji? Muuaji wa mwanamke aliyemleta duniani? Mwanamke ambaye ni mama? Wangapi hawana mama? Sio Twahiya niliyemuandika katika kile kitabu cha KIJAKAZI, alimlilia mama yake ambaye hakumlea? Kwanini Salome yeye? Kwanini asimpende mama yake? Kwanini asimpende kama mama yake alivyompenda? Salome alifahamu fika jinsi gani Batuli alimpenda. Ndiyo maana pia inanifanya nihisi muda mwingine ndiyo sababu ya Salome kuwa na jeuri kiasi kile. Lakini Salome aliazimia kufanya hivyo. kufanya unyama ili roho yake iridhike. Alitamani kuwa mmiliki na siyo mwizi.
“Mwizi?”
“Ndiyo. mwizi wa mapenzi. Kuiba penzi la baba yake na kumdhulumu mama yake. Aibu iliyoje”
Usiku baada ya kurudi kutoka disko walipokuwa, alijaribu kuongea na Husna, rafiki yake. Alimuuliza kuhusu sumu zinazoweza kuuwa haraka bila ya muathirika kuomba hata maji. Alimuuliza bila kuweka wazi juu ya maswali mengi ya kiutatanishi. Husna naye hakuwa na muda wa kuchunguza chochote kuhusu utata wa maswali hayo. Alijibu kiuchovu huku sauti yake ikiwa inapotelea kati kati ya usingizi mzito. \
Usingizi uliomezwa na pombe kali aliyoinywa na yule bwana wa kimakonde mwenye ‘pesa chafu’ pale jolly club
“kuna ya panya, papasi, mende na viboroto”
Hata alipopakosea hakuparekebisha. Alianza na kukoroma hata mashine ya kusaga haikufua dafu. Baada ya kumaliza maongezi na Husna, maongezi ambayo alichong’amua ni sumu ya panya, mende, kiroboto na papasi; aliamka na kwenda kuzima taa ili walale. Ilikuwa yapata saa nane na dakika chache.
Kumbe wakati Salome alikuwa akiingia, Batuli alimsikia. Batuli alinyata mpaka mlangoni katika chumba cha Salome kusikiliza maongezi yao. Batuli hakuwa akijiamini tena. Hakujiamini yeye na maisha yake. Alikuwa na hisia zote kuwa ni lazima ipo siku Salome atasahau kuwa yeye ni mtoto na yeye(Batuli) ni mama yake.
Aliamua kurudi chumbani kwake kwa kunyata mwili wote ukiwa unamtetemeka. Alipofika hakulala kwanza. Alikaa kitandani akitafakari kuhusu mazungumzo ya Salome na Husna.
“Sumu?” alijiuliza. Anataka kumuua nani? Aniue mimi? Kwa sababu ya mapenzi? Mapenzi ya yeye na baba yake? Salome atakuwa amepandwa na wazimu. Wazimu nitakaousubiri niuone mwisho wake. Aibu iliyoje jamani? Mtoto yule nimzae mwenyewe leo atamani kuwa mke mwenzangu? Zaeni muone jamani. Nilitamani mtoto, mtoto wangu anatamani kuwa mke mwenzangu. Masikini Batuli mie. Nimekukosea nini Mungu wewe? Salome aliyeniachisha ndoto zangu leo anataka kuzifuta kabisa?”
Hapo hapo ule unyevu unyevu unaoitwa machozi ukakosa uvumlivu ukachuruzika kutoka jicho moja yakipokelewa na la pili mashavu yakalowana chapachapa. Batuli alihisi dunia nzima ikimzomea. Ikimzomea kwa kitendo cha Kilaza na Salome wanachokifanya usiku wa manane. Ufuska walioufanya gizani wakizani ni siri yao wawili, kumbe wangejua? Batuli alihisi hata siku ile ya kwanza alipoona Salome amechelewa kuamka, haikuwa siku yao ya kwanza alipatwa na hisia kuwa mchezo huu ulianza muda. Mchezo wa Kilaza kumtoroka usiku na kwenda kuzini na Salome. Mchezo wa Kilaza kumuwekea madawa ya kulevya katika juice na maji ili apotelee usingizini. Salome mtoto wao wa kumza wao wenyewe. Laana gani hii jamani?
Mvua iliyonyesha ikamfanya kupitiwa na usingizi. Usingizi uliomfanya aamke saa tano asubuhi, tofauti na kawaida yake. Kama alivyotegemea, aliwakuta Salome na Husna mezani. Salome alitoa tabasamu maridhawa. Kama ungekuwa na Shahuku ya supu, supu iliyonakshiwa kwa harufu na viungo mbalimbali kufanya inukie; angeparamika kwa kujibu tabasamu hilo kwa tabasamu pia. Batuli alikwishazoea hivyo vyote. Salome alimsalimu akiwa ameshika uma iliyonasa kipande cha sosejina bakuli lililojaa supu, likimzomea. Batuli alijibu salamu hiyo kwa sauti iliyopwaya. Sauti iliyogonga kengele ya hatari, kichwani mwa Salome. Husna naye alimchangamkia Batuli bila kuwa na hatia yoyote lakini tabasamu lake la kheri likaonekana baya mbele ya uso wa batuli.
Salome alimsalimu akiwa ameshika uma iliyonasa kipande cha sosejina bakuli lililojaa supu, likimzomea. Batuli alijibu salamu hiyo kwa sauti iliyopwaya. Sauti iliyogonga kengele ya hatari, kichwani mwa Salome. Husna naye alimchangamkia Batuli bila kuwa na hatia yoyote lakini tabasamu lake la kheri likaonekana baya mbele ya uso wa batuli.
Batuli alimchukia Husna.
Alimchukia kwa kuwa alijua ndiyo chanzo cha tabia chafu za Salome. Tabia za kumuhonga Karim mlinzi, ili atoroke usiku. Tabia za kurudi usiku wa manane akiwa amelewa. Tabia chafu za kutoonekana shule kwa muda wa miezi miwili. Alijuwa lazima Husna alikuwa anajuwa.
Anajua alipokuwa anaenda Salome.
Salome alikuwa akiaga anaenda shule, lakini walimu shuleni waliwasiliana na Batuli kulalamika Salome alikuwa haonekani shule. Hata hii ya kutembea na Kilaza, baba yake inawezekana ni Husna ndiye amemfundisha. Husna pia itakuwa ameiga mchezo huu mchafu kutoka kwa mama yake, Mwamtumu aliyekuwa anajiuza katika mahoteli makubwa makubwa.
Wakiwa katika kuendelea kuburudika na supu Salome alishitushwa na sonyo lililoponyoka Batuli kwa ghadhabu.
“He! Mama. Kwema?” Salome aliuliza.
Batuli alihisi amekabwa na nyama aliyoimeza ghafla bila kushushia na ile supu. Macho ya Batuli yalikuwa yakimtazama yeye. Akajihukumu Masikini, kwa hukumu asiyoistahili. Ndiyo! Nasema hakuistahili kwa sababu hakujua kinachoendelea. Kwa kuwa pombe na wanaume ndiyo ilikuwa familia iliyomliwaza Husna. Wengi walimuona Salome kama ni rafiki yake wa karibu sana(yeye Husna). Lah! Haikuwa hivyo. Husna alichukuwa muda mwingi kumdanganya Hashimu ili amnunulie simu nzuri ya bei kubwa. Alijiuliza ni lini atamiliki gari nzuri ya kutembelea. Husna alikuwa mkubwa kwa Salome zaidi ya miaka miwili. Hivyo akachukulia mawazo ya Salome ni ya kitoto. Mawazo ya kwenda beach siku za sikukuu na mawazo ya kununua nguo mpya.
Husna hakupaswa kuhukumiwa kutokana na makosa ya Salome. Uhuru wake Husna anaoupata wa kwenda popote anapopatakakwa muda wowote hakumuazima Salome pia. Hakuwahi kumshauri waende disko wala warudi usiku sana huku wakiwa wamelewa, si unajua mambo ya mziki yakinoga? Husna angeshangazwa pia kuwa Salome mwenye upole na uso usiotofautiana na malaika kama angekuwa anatembea na baba yake.
Hivyo hakujua hilo pia.
Husna hakujua mawazo ya Batuli aliyaogopa macho yake yaliyokaza kama anayetaka kumtoa mtu roho. Batuli akaketi kati kati yao, akiwa anawatazama kwa awamu. Alimtazama Salome kisha Husna; kama aliyekuwa akiwaibia. Aliitazama supu kama uchafu usiotamanisha. Alijua huo ni mtego wa Salome. Atakuwa ameweka sumu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sumu ya kuniua nimpe uhuru. Alihisi chozi likitaka kumponyoka mtesi wake amdhihaki. Hakuiruhusu hali hiyo. Hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake. Kawaida ya kumuulizia Mwamtumu shoga yake. Hakuwauliza Husna na Salome habari za shule kama ilivyo kawaida. Hali hiyo ikamkosesha raha Husna, asijue ni nini kinaendelea.
Hakumuelewa Salome aliyekuwa akimnyali mama yake. Kitendo cha dharau. kumpandisha na kumshusha kwa macho yasiyo na adabu. Hakuelewa kwa nini Batuli hakugusa chochote hapo mezani, wala kuongea chochote. Husna supu aliyoifurahia ikamtumbukia nyongo. Supu iliyopata tabu kukata kilevi japo kwa ndimu nyingi na pili pili. Lakini kwa hali aliyokuwa nayo Batuli, hali ya kisirani kisichoeleweka ikamfanya akitafute kilevi kilichojifanya kibishi kutoka; akakiri hakikuepo tena kichwani.
Alimtazama Batuli kwa jicho la kuibia, wakati aliposimama kunawa mikono. Ilikuwa ni sawa na kipindi cha vichekesho vilivyomfanya kidogo kicheko kimponyoke. Ilikuwa ni hali mpya na ya kushangaza ndani ya nyumba ya Kilaza. Alimkuta Batuli naye akimtazama Salome, huku kaubinua mdomo. Alipomaliza akazuga kwa kukohoa. Wote wawili walipopata uwepo wao mezani, Husna akajifanya kama hakuona jambo lolote. Alishukuru baada ya kuhakikisha yuko sawa.
“Asante mama” alimtazama Batuli. Batuli aliitika kiupweke
“Umetosheka? huongezi?” Batuli alinyanyuka akitaka kumuongezea supu nyingine. Supu iliyofunikiwa kwenye hot pot ya tofauti na ile iliyo wazi. Salome akaropoka
“Hapana mama hiyo ni ya kwako yetu tumeshamaliza” Batuli akalitoa tabasamu la dhihaka. Alichokuwa akikitafuta akakipata. Akapata uhakika kuwa Salome alidhamiria kumuangamiza. Kichwa chake kikapwita kwa kengele ya hatari. Kengele iliyomtahadharisha kuwa makini.
“Mama nashukuru nimeshiba sana usijali” Husna alijbu kwa hali ya kutoelewa. Naye akapatwa na wasiwasi. Wasi wasi ulioanza tangu Salome alipozitenga supu hizo katika vyombo viwili tofauti. Wasiwasi uliofuatiwa na Salome kuingia jikoni na sio kama ilivyozoeleka ni kwa mtumishi maalumu wa jikoni. Wasiwasi uliohakikishiwa na kuamka na gubu isiyoelezeka ya Batuli asubuhi hiyo. Halafu ikamaliziwa na kuwa wasiwasi ulokamilika kwa vitendo alivyovishuhudia mezani hapo. Macho ya dharau baina ya mama na mtoto na supu aliyotengewa mama hakuruhusiwa kunywa mtu mwingine. Yaani hata alipotaka kuinywa baada ya kuisifia ilikuwa tamu sana, alikatazwa.
Kuna nini? Alijiuliza bila kupata jibu. Akaaga kuondoka, Salome akanyanyuka kumsindikiza. Batuli aliendelea kubaki mezani mpaka aliporudi Salome. Alipopita Swaumu, mtumishi wa jikoni; ulimi wa Batuli ukapata uhai.
“Swaumu” Batuli aliita’
“Bee! Mama” Swaumu alikatisha safari ya jikoni na kurudi mezani, alipo Batuli. “Swaumu” aliita tena kama vile Swaumu bado hakuwa amefika alipoitwa. “Hii supu ya leo nani ameiandaa” Batuli aliuliza huku akimuangalia Salome kama alikuwa akimuuliza yeye.
Swaumu naye akapatwa na wasiwasi wa kujibu haraka haraka. Batuli akarudia tena
“Nakuuliza Swaumu, supu ya leo ni nani ameiandaa?” Salome akajibu baada ya kuona Swaumu akiogopa
“Nimeiandaa mimi” Batuli akacheka. Kicheko kisicho na dalili yeyote ya kuitwa kicheko.
“Sawa. Swaumu nenda kaendelee na kazi”
Swaumu aliitikia kwa kichwa na kutaka kuondoka. Kabla hajapiga hatua nyingine yeyote, Batulia alimuita tena
“Ila Swaumu” Swaumu akageuka “tafadhali kama umeshindwa kazi ya kuniandalia chakula changu, niambie niajiri mtu mwingine, sintokula chakula alichoandaa mtu mwingine zaidi yako na utakuwa ukionja chakula unachopika kabla sijala mimi. Hiyo itakuwa ni kazi mpya itakayokuongezea mshahara mwingine zaidi. Ila hakikisha unakuwa makini na chungu chako huko jikoni”
Swaumu alijibu akiwa na tabasamu pana usoni. Aliondoka sasa kwa mwendo wa kama anayetaka kukimbia. Salome alikwishaelewa njama za Batuli, hivyo hakuwa na furaha tena; japo alitabasamu kinafki. Batuli naye alimtazama salome, huku tabasamu lisilofaa kuitwaa tabasamu likimzomea.
Mchana wote wa siku hiyo, Batuli alishinda kwa rafiki yake waliyesoma naye sekondari. Rafiki yake wa pekee. Rafiki aliyemfanya kama ndugu yake. Rafiki waliyeshibana katika shida na raha. Ilipotokea shida, walilia wote, kwenye raha wakacheka pamoja. Rafiki aliyehisi maumivu ya Batuli, naye akatokwa na chozi hata kabla Batuli hajalia. Rafiki aliyetumia muda mwingi na uwezo alio nao kutatua tatizo lililomkabili Batuli mpaka alipohakikisha limeisha. Urafiki wao haukukoma hata Batuli alioshindwa kuendelea na masomo kutokana na mimba aliyoipata. Mimba aliyoipata kutoka kwa mchimba madini. Yeye rafiki mwenyewe hakumjua muhusika. Hakumjua kwa kumuona. Lakini habari yake alipoisikia kwa mara ya kwanza, aliyetambulishwa kwa jina lake Kilaza, alionekana kama mtumishi aliyetumwa na mungu kumsaidia Batuli. Aliyemsaidia katika mavazi ya shule. Malazi mazuri, kutoka katika kibanda chenye mwanga wa kibatari mpaka nyumba yenye umeme wa nguvu ya jua. Batuli hakukosa chakula katika laka zote tatu muhimu kwam binadamu. Batuli hakulelewa katika maisha mazuri kama ulivyo uzuri wake. Batuli aliishi kwa shida tofauti na wengi walivyomfikiria. Unadhifu wa Batuli ulimuweka karibu na marafiki ambao ni watoto wenye uwezo nyumbani kwao kama rafiki yake. Batuli alimpoteza mama yake(Tausi) akiwa ameimaliza elimu yake ya msingi. Ugonjwa usioeleweka ulimfuta tausi katika uso wa dunia. Hadithi yake pia ikasahaulika. Hata kidogo alichomuachia Batuli. Batuli akaporwa. Ile hadhina ndogo iliyowekwa bank ndugu wenye tamaa ya mali wakaichukua kiujanja kwa kumlaghai batuli kuweka sahihi katika kitabu cha bank. Fedha zote zikakombwa. Hata kile kibubu kilichohifadhiwa fedha za mchezo, unaojulikana kama upatu, kilichofichwa chini ya uvungu, kilipasuliwa ndugu wenye tamaa wengine wakazichukua zilizobaki. Batuli akubaki na chochote. Ndugu waliosutwa kwa kitendo walichokifanya walikataa kuishi naye. Batuli akachukuliwa na kulelewa na mjomba wake aliyebakia jijini Mwanza. Mjomba hakuwa mjomba, mjomba mwenye malezi mazuri. Mjomba alikuwa mlevi kupindukia. Mjomba hakulijua daftari la Batuli wala kikao cha wazazi shuleni kwa akina Batuli. Mjomba hakufuatilia maendeleo ya mtoto hakushughulika na chochote. Mjomba alikuwa maarufu mwanza nzima. Hakuna ambaye hakumfahamu Makulupuko. Japo halikuwa jina alilopewa na wazazi wake. Jina lake la nyumbani alijulikana kama Adamu, makulupuko akabatizwa katika vilabu vya pombe. Ni nani asiyejua kama gongo ni mbaya? Asiyejua kwamba gongo imekatazwa? Asiyejua jina la ubatizo la kilevi hicho ni Haramu? Basi kwa kuwa Adamu alifahamu, ndio maana alikurupuka kila alipohisi harufu ya wakuda. Wakuda ni askari waliopenda kumsulubisha kwa virungu vya miguuni, kisha kumchomoa pesa ndogo na kumuachia huru. Makurupuko ama Adamu yeye na halmashauri yake ya kichwa, akawaita askari hao wakuda. Ikawa sababu ya kumuita makurupuko hata kusipo na sababu ya kukurupuka. Huyo ndiye mjomba wa Batuli. Aliyeshinwa kulipa japo pesa ndogo a shule ya kata, aliyofauli Batuli. Mjomba aliyeshindwa hata kujua batuli alikula nini? Na alipata wapi chakula? Hata habari ya Batuli kufukuzwa shule na baadae kujifungua mtoto wa kike aliipata baada ya kutoka mahabusu. Mahabusu alipokaa kwa muda wa mwaka mzima bila kesi yake kusikilizwa. Machozi yalimchuruzika Batuli, wala hayakukoma. Rafiki yake akastaajabu. Rafiki yake aliyejulikana kama mama Regina. Hakuwa na mtoto kama nilivyotanguliza mwanzo. Alipenda kuitwa Mama kwa heshima aliyopenda iwe hivyo. Jina lake aliitwa regina. Mtu mkubwa sana katika jiji la mwanza. Serikali ilimuheshimu, wahalifu wakamuogopa. Alikuwa ni mtunza haki ya aliyeonewa kwa kusimamia sheria na ushaidi uliokamilika. Huyu alisome sheria chuoni. Kazini akatunukiwa cheo cha kuhukumu waliotuhumiwa katika makosa mbalimbali. Yeye akaitwa hakimu ofisini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alistaajabu kuyaona machozi ya Batuli. Baada ya kuhisi labda yangekuwa mwisho, tangu Batuli alipompata Kilaza. Machozi yaliyomuhuzunisha hata akajizuia asilie kama zamani. Si unajua ukubwa dawa? Alimshika Batuli mgongoni na kumliwaza kwa upole “Batuli rafiki yangu, mbona sikuelewi? Tangu umefika unalia tu.” Batuli hakunyamaza. Sauti ya Regina kama ilikuwa imetoa tamko la kufungulia machozi ya Batuli. Machozi yaliyotoka kama bomba. Batuli hakunyamaza alimkera sana Regina. Regina alikuwa na shahuku ya kujua kilichomsibu Batuli. Alipania kumjua aliyemfanya Batuli lie. Kwanini amlize rafiki yake? Rafiki aliyempenda kama ndugu. Rafiki aliyeumia na yeye akaugulia maumivu. Wakaitwa mapacha shuleni na mitaani wakapendwa. “regina rafiki yangu” Batuli akaipata sauti yake. Unadhani aliweza kuendelea kuongea? Angeupataje uwezo huo? Uchungu uliomkalia kooni ungemuachia saa ngapi? Kilio kikawa kilio na yeye. Kilio kilichomchosha Regina na kumucha alie mpaka achoke, ndiyo amueleze kilichomsibu. Kati kati ya kilio Regina aliambulia kulisikia jina la “salome” mara “Kilaza” ila hakuelewa chochote. Hakuelewa ni nini kimeipata familia ya rafiki yake. Aliyeshika nafasi kubwa katika maisha yake kiuwepo tu au hata kumfikiria mara kwa mara katika mawazo yake. “batuli naomba unyamaze unieleze ni nini kimeipata familia yako” alimchoka sasa. Muda wote kulia tu? Kama kulia si angeyamaliza machozi yake huko kwake? Lakini kwa kuwa Batuli naye alikuwa amelia kwa muda mrefu. Hata machozi yakawa yamemkauka. Sasa akawa tayari kuzungumza yote. Ilikuwa hadithi asiyoijua mwanzo wake. Lakini aliianza alipojua kana kwamba hapo ndio mwanzo wake na kuielezea kama aliyeijua kiufasaha. Hadithi iliyoanza kwa tabia chafu za Salome kutoonekana shuleni. “Ni Husna yule mtoto wa changudoa Mwamtumu ananiharibia Bini yangu” akaongeza kwa kunogesha chumvi bila kuonja ladha yake. Hakujua kama ilizidi ama ilipungua. Akaendelea mpaka alipoanza kuona salome akichelewa kuamka “haikuwa kawaida yake ndiyo maana nikapatwa na wasiwasi. Nilimbana nijue nini kimemsibu, akaanza simulizi za ajabu ajabu” hadithi ikaanza kumvutia regina. Alikohoa kikohozi kikavu kilichomdhihirishia Batuli kuwa anasikilizwa kwa makini. Aliendelea “akaniambia mtu kuhusu kuingia chumbani kwake ndiyo nilipoanza kugundua na vitu vingine vingi….” Alieleza yote mpaka alipogundua kuwa, Salome alikuwa akilala na baba yake, Kilaza. Hata vitendo vya dharau ya Salome. Vilisababishwa na Kilaza. Siku hizi Salome alikuwa akichelewa kurudi. Batuli alihisi huenda, hata ile safari ya ghafla ya Kilaza; kutoka nje ya mji haikuwa ya kweli. Huenda alijificha pembezoni mwa mji wa mwanza, akitafuna kuku wa kukaangwa na bia kadhaa akijivinjari na Salome. Ndio maana Salome sasa akawa kama mgeni nyumbani. Nani anayejua ukweli? Labda alikuwa akimtembelea kilaza mpaka huko alikojificha? Hakuna ambaye angeujua ukweli kama Kilaza alikuwa nje ya mji kweli ama Lah!. Lakini Batuli alikuwa amekwishakosa imani na familia yake. Imani ndogo iliyomfanya ahisi ukweli kama alivyohisi. Imani iliyomfanya aunganishe vipande vya hadithi hata ionekane hadithi ya kusikitisha. Simulizi ilyomfanya Regina kulengwa na machozi. Simulizi iliyomfanya Regina kumchukia Salome ‘mimba ya Salome ndiyo ilimfanya rafiki yangu kufukuzwa shule na kumfanya ashindwe kutimiza lengo lake kielimu’ Regina alijinong’oneza. Akamchukia pia Kilaza.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment