Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

ROHO ILIYORUDI KUANGAMIZA - 1

 



     IMEANDIKWA NA :  STALLONE JOYFULLY





    *********************************************************************************





    Simulizi : Roho Iliyorudi Kuangamiza

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Wewe unadhani ungekutana naye kwa mara ya kwanza; ungekuwa na ujasiri wa kumtazama tena? La hasha! Usingethubutu nakuambia. Hakuwa msichana mwenye hadhi ya kuitwa msichana, wala kumtazama kama ulikuwa na nia hiyo. Kifua chake kilipoteza ile sura ya usichana, yaani matiti hayakuepo kabisa. Alikuwa na vijindimu tu vilivyotunisha blazia na kuweka ishara ya usichana katika mwili wake. Nywele zilizokosa wembe kwa kipindi kirefu na kusababisha kuzoa uchafu wa kila aina. Blazia aliyoivaa nayo ilipoteza rangi yake ya asili. Japo tangu ilipoopolewa katika sagura sagura ya mitumba katika soko lolote lile la mitumba, ilikuwa imefifia, lakini sasa haikujulikana uasilia wake kabisa. Yeye aliiokota baada ya kupoteza thamani mwilini mwa aliyeitupa na kuwa kama sadaka jalalani hapo. Mabaka ya uchafu yaliyochukiza kutazama na kupendeza miongoni mwa wachafu wenzake. Ilikuwa imeraruka upande mmoja wa titi lake, hali iliyosababisha moja wapo kuchungulia nje.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walimshangaa wasiomjua mtu huyu, asiyeeleweka na kuzuka katikati ya vichaa waliozuka na kufanana na mizuka.

    Katikati ya mizuka hiyo ndipo alipozuka mzuka huyu Salome. Lakini kwa mimi ninayemfahamu Salome, si huyu aliyenifanya niandike kitabu hiki nilichokiita ROHO ILIYORUDI KUANGAMIZA. Salome hapo mwanzo hakuwa Salome katikati ya vichaa waliomjua salome kama chokoraa Lome. Salome aliiangamiza miaka ishirini na miwili ya starehe na anasa katika ufahari wa mzee Kilaza.

    Mhitimu wa chuo cha udaktari mkoani mwanza pale Bugando.

    “Ni miongoni mwa malaika waliosahaulika duniani na kuishi katikati ya binadamu kama sisi” wanafunzi wenzake walinong’onezana kwa siri. Msichana mwenye asili ya kisukuma aliyechanganya na damu ya kijapan. Unaweza kutabiri mwenyewe urembo msichana huyu.

    Ni huko ndipo kisa hiki cha kusisimua kilipoanzia. Kisa cha daktari mrembo kuokotwa dampo ameuwawa kinyama. Sime lililopenyezwa sehemu zake za siri na kulishwa nusu kilo ya saruji, baada ya kubakwa na kundi la wahuni; ndiyo sababu ya kifo chake.

    Taarifa ya magazeti yaliyouzika sana siku hiyo yalipambwa hivyo. Hakuna aliyefahamu ukweli wa sakata hili la kutisha lililotokisa jiji zima la Mwanza. Jiji lililotoa sauti moja na kuwa kama mwangwi na kukera masikio mengine yaliyosikia sauti hii zaidi ya mara moja.

    “Mauaji, mauaji, mauaji”

    Yalikuwa ni mauaji ya kutisha lakini yalitisha zaidi kwa mashuhuda wasioshuhudia alivyouwawa, kuongeza utamu wao zaidi ili hadithi yao inoge. Waliosimuliwa walisisimka vinyweleo mpaka nywele zikawasimama.

    Habari hii ikaifikia kila sikio ndani ya jiji la mwanza hata nje ya mikoa ya jirani. Lakini yupo aliyeipokea habari hii kwa uso wa huzuni. Huzuni ya kinafki. Huzuni ya fulani na fulani wasifahamu kama anafurahia mauaji kama anavyowahukumu wauaji. Yeye alikaa nyuma ya kiti cha heshima, akilinda haki ya waliodhulumiwa sheria, huku yeye akishikilia ufunguo wa kuvunja sheria hiyo kigaidi zaidi.



    Watu kumi na wawili walitumwa kumbaka Salome, pia walifanikiwa kuitoa roho yake. Walitimiza agizo la mama Regina.

    Yeye Regina aliitwa mama kwa kupenda mwenyewe, japo hakuwa na uchungu wa mtoto hata mmoja. Kukosa mtoto, hakumlaumu Mungu kwa sababu anazozikumbuka mwenyewe.

    Regina anakumbuka fika jinsi alivyozitoa mimba nyingi akiwa kipindi cha sekondari na hivyo ile ya mwisho iliyotolewa vibaya kumsababishia kutoka na kizazi chake.

    Waliotumwa pia wao wenyewe hawakujuwa sababu ya agizo hilo la kinyama. Lakini begi lililotuna fedha za kigeni dola ishirini na tano elfu, lililosusa kushikilia reli za zipu na kuwa kama lililoachama likiwazomea, fedha nje nje zikiwadhihaki kwa uchu; Hiyo ilitosha kutohoji chochote badala ya kutekeleza walichotumwa.

    Watu hao wakatili walitimiza unyama wote kwa Salome.

    Walipomaliza kumtenda vibaya Salome, waliambaa ambaa gizani na kupita vichochoroni wasionekane.

    Dakika chache kabla ya roho kumtoka Salome. Salome aliapa. Aliapa roho yake itarudi kuangamiza na kulipa kisasi kwa kila roho iliyoshiriki kuitoa yake. Aliapa atalipiza kisasi kwa mkono wake mwenyewe. Aliapa ataangamiza wanaume waliomtesa akiwa hai. Chuki iliyosababishwa na baba yake.

    Mzee Kilaza aliyembaka na kumpotezea usichana wake, kipindi hicho akiwa bado hamjui mvulana. Siku kadhaa, Mzee Kilaza akamzoesha mchezo huo mchafu, naye akaupenda.

    Salome akauzoea.

    Salome akiwa kimada mpya wa Mzee Kilaza, jina la baba likapotea mdomoni mwake. Mama yake Salome, Batuli mke wa Kilaza hakuwa na lolote analolifahamu.

    Hivyo Kiapo cha Salome kilitimia mara roho yake ilipomtoka. Roho hiyo ilichagua mabadiliko ya kimuoekano katika mwili wake, ili iwe rahisi kulipiza kisasi chake. Isiwe rahisi wanaomfahamu wamng’amue.

    Hivyo maisha ya roho hiyo yalianza kuishi juu ya dampo hilo tangu siku mwili wake ulipotupwa katika jalala hilo, nje kidogo ya mji wa Mwanza.



    Labda ndugu yangu utakuwa unajiuliza ilikuwaje Salome aliuwawa kinyama kiasi kile. Kabla sijaendelea, ningependa ufahamu asili ya ROHO ILIYORUDI KUANGAMIZA ili kulipiza kisasi; Nikuhadithie yaliyotokea hapo mwanzo.

    Kipindi hicho Batuli bado binti. Kipindi embe zilizosimama kifuani mwake hazikuanguka kwa kubinywa binywa na mvulana huyu kisha Yule, kuangalia kama zimekwishaiva. Akiwa ameimaliza miaka tisa siku chache zilizopita, ndipo alipogundua baba anayeishi naye si baba yake mzazi.

    Baada ya kuchoshwa na maswali kuhusu asili yake naye akaamua kumtupia mzigo huo mama yake.

    “Mama. Baba yangu yuko wapi?”

    “Tangu lini mwanangu ukaniuliza wapi alipoenda baba yako?” huenda mama yake hakuelewa. Hakuelewa nini Batuli alikuwa akizungmza kutokana na umri wake kuonekana mdogo kuliko swali alilolilenga kuliuliza.

    Batuli akamsahihisha kwa kuweka wazi swali.

    “Mama nataka nimfahamu baba yangu halisi”

    Ikawa sawa na shambulio ambalo hakulitegemea. Mama huyu wa kisukuma aliyezaliwa na kukuwa ugenini, katika kijiji cha Bagamoyo. Kwa mara ya kwanza alihisi nafsi yake kukosa ushirikiano kamili na akili.

    Aliikumbuka ile siku ambayo alihisi ilikuwa sawa na bahati ya ngekewa. Alipoiokota pochi yenye fedha za kigeni. Alikuwa ana haha kuificha mara akatokea ‘mchina mmoja’ alisema hivyo Tausi, mama yake Batuli.

    Mchina huyo alikuwa kama aliyewehuka na lugha isiyoeleweka, japo alizungumza Kiswahili. Kilikuwa ni Kiswahili kibovu sana.

    “Pochi yangu nimedondosha”

    hapo Tausi akang’amua shida yake. Aliitoa pochi na kumpatia bila kujua ilikuwa ina kiasi gani cha fedha. Kabla mchina Yule hajatia neno lolote, Tausi aliwageukia wachuuzi walioleta ndoo zao zilizojaa vibua.

    Siku chache baadae, mchina alirudi katika lile genge la Tausi kumshukuru. Alienda kwa lengo la kumshukuru, lakini bila kutarajia lengo lingine likaibuka. Lengo ambalo kwake binafsi lilikuwa ni zaidi ya ngumi ya kushitukiza.

    Hakuupata ulimi wake kiufasaha, japo kutoa salamu.

    Kama ujuavyo wasukuma walivyobarikiwa. Minofu iliyoongeza kilo za nyama nyuma ya makalio yao. Miguu iliyofinwangwa na kufinyangika na mfinyanzi asiye na mpinzani, rabana. Mashavu yaliyojaa na kubarikiwa vishimo vinavyoitwa ‘dimples’ na wenzetu wa ng’ambo na kuongezewa nakshi na ule mwanya uliopamba tabasamu lilelile lililomrudisha mchina huyu aliyedhani kuwa anaenda kwa nia ya kumshukuru tu.

    Kiukweli Tausi alikuwa amebarikiwa kiuno chembamba kilichobeba tumbo dogo lisilo na dalili yoyote ya kitambi cha hasara. Kifua kilichobeba viembe viwili vidogo vilivyokaribia kuiva na kughasi mioyo ya wakware wasiovumilia tamaa zao na kufanya kifua kilichomfanya aitwe mrembo.

    “Nikusaidie nini” kha! Hivi unajua ‘mchina’ bado alikuwa amesimama. Alisimama akimkagua muda wote? Alianza kiunoni akapanda kifuani. Usoni kulikuwa na taswira ya malaika aliyesahaulika duniani. “Haha!! usimcheke mchina tu hata wewe ungemuona Tausi huenda ungezubaa zaidi ya mchina huyu”

    Tausi alikuwa ameshasimamisha wateja watatu na mchuuzi mmoja wa samaki akimsubiri ‘mchina’ azungumze.

    “Nataka kutoka na wewe usiku wa leo” Mkalimani wake alifanya kazi nzuri ya kumfundisha Kiswahili fasaha. Mchina huyo aliyefanana na wachina ila asili yake ni Japan aliyejibatiza jina la Carlos. Jina aliloliona ni jepesi kuliko lile lake la asili, ambalo linaweza kukukata ulimi wako ukiambiwa ulitamke.

    Tausi alitingisha kichwa kwa ishara ya kukubali kisha aliwageukia wateja wake.

    Hapo baadaye Tausi na carlos wakashibana. Starehe zikawa chachu ya penzi lao kukuwa maradufu siku za usoni. Ule urojo pale forodhani katika visiwa vya unguja. Kuku mzima wa kupaka pale Bagamoyo. Usisahau zile safari zisizoisha kwenda kuangalia filamu mpya ya Rhino Race na rafikiye Bow, filamu iliyoteka watu kipindi hicho katika majumba mbalimbali ya sinema. Ukiachilia mbali yale mabwawa ya kogelea aliyoyazoea kwa kucheza na maji katika hoteli mbalimbali za kifahari.

    Starehe hizo zote zikamtunuku Tausi ujazito.

    Ujauzito ulioleta mushkeli pale Carlos alipowehuka siku aliyoambiwa kuwa yeye ndiye muhusika wa ujauzito huo.

    Kipindi cha juma la mwisho katika siku, Carlos na Tausi wakiwa bado wanaponda raha katika hoteli ya kitalii yenye hadhi kubwa ulimwenguni na duniani kote Sheratoni, Tausi akiwa pembezoni mwa bwawa dogo la kuogelea, akila upepo mwanana huku akimumunya kipande cha mwisho cha ndimu baada ya kufyonza vitatu alivyovitupa kihasara juu ya sahani ya bati; ndiyo ilikuwa ile siku ambayo Carlos alikata mguu wake kuja hotelini hapo.

    Taarifa hizo zilimjia Tausi katika kijikaratasi kidogo kilichohifadhiwa kiheshima kwenye bahasha yenye nembo ya hoteli hiyo na kuletwa ikiwa juu ya sinia na mhudumu mtanashati mmojawapo kati ya wengi walioajiriwa hapo.

    Barua hiyo ilisomeka hivi-: Sina nia mbaya ya kukimbia ujauzito niliokupa ila sipo tayari kuona ukiteseka na damu yangu huku nikiwa kifungoni. Tausi mimi Carlos sikuwa mkandarasi wa kweli kama nilivojitambulisha kwako hapo mwanzo. Kazi yangu halisi ni ya ujambazi na kupora mali za watali wengine naomba unitunzie siri hii mpaka nitakapopata nafasi nyingine ya kuja Tanzania. Kadi hiyo ina kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazoweza kukusaidia kuanza nazo maisha na mtoto wetu. Usishangae kuandika kiswahili sahihi rafiki yangu Ben amenisaidia tafsiri. Wako nikupendae kwa dhati Xuu lyan chi, Carlos

    Barua hiyo ikanifanya pia na mimi moyo wangu upasuke, pah! Kwa kugundua kitu kipya. Kitu ambacho kimemfanya Carlos kujiita Carlos. Ukiachilia lile jina lake alilopewa na wazazi wake. Kazi yake ya ujambazi ilimfanya ajiite Carlos kutokana na ukatili alionao. Huko nchi za ughaibuni palipata kutokea gaidi mmoja aliyesumbua jeshi la polisi kwa kuuwa maelfu ya watu kinyama bila huruma.

    Yeye pia aliitwa Carlos.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara Tausi akataka kusimama, miguu ikakosa ushirikiano. Muhimili wa pekee aliupata kwa kuegemea ngazi iliyozama majini mwa bwawa hilo. Alichanganyikiwa kwa kweli.

    Barua hiyo ilimfikia pamoja na fedha zilizohifadhiwa kwenye kadi ya Atm sawa, lakini moyo wake tayari ulimuhitaji zaidi carlos kuliko mali na fedha. Carlos aliiteka akili yake kwa muda mfupi kisha kuitupa bila thamani. Thamani aliyompa Carlos hakutegemea kama angeweza kumtenda hivyo.

    Ikawa mwisho wa kumuona Carlos mpaka leo Batuli akiwa na miaka tisa huku akitaka kumjua baba yake. Hiyo ikawa ni hadithi fupi ambayo Tausi alimuhadithia Batuli kuhusu baba yake aliyemkimbia kabla hajazaliwa.

    …….

    2

    Turudi sasa katika mkasa wa kisa kizima cha roho iliyorudi kuangamiza kilipoanzia. Ilikuwa ni miaka mingi imepita, mara baada ya Tausi kufariki na kumuacha Batuli; kisha Batuli naye akapata mtoto aliyemuita Salome.

    Usiku uliorindima mingurumo ya radi na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kwa hasira, ilimziba masikio Salome. Ilimziba asisikie chochote, zaidi ya kumpa usingizi mzito usio na ndoto ya maana. Ndoto iliyoaanza na kupata gari la kifahari, iliyoishia akiwa katikati ya reli huku treni ikija kwa kasi ikitaka kumsaga saga. Ni wakati huo, aliposhituka na kukuta mapigo ya moyo yakimuenda mbio huku sehemu aliyoweka kichwa kuwa kama kidimbwi cha maji.

    Yalikuwa majasho ya uwoga.

    Akaidharau hali hiyo akarudi tena kulala. Huku nje ya chumba chake, kukiwa kuna mtu ambaye alikuwa akinyata kwa kuuwendea mlango wa chumba alicholala. Salome akiwa ameimeza miaka kumi na mitano juzi tu, alitamanisha wengi.

    Ila huyu aliyekosa adabu na kupata uwezo wa kuingia katika kasri la Mzee Kilaza, sijuhi alijiamini nini.



    Akaidharau hali hiyo akarudi tena kulala. Huku nje ya chumba chake, kukiwa kuna mtu ambaye alikuwa akinyata kwa kuuwendea mlango wa chumba alicholala. Salome akiwa ameimeza miaka kumi na mitano juzi tu, alitamanisha wengi.

    Ila huyu aliyekosa adabu na kupata uwezo wa kuingia katika kasri la Mzee Kilaza, sijuhi alijiamini nini.

    Alikuwa na lengo la kutikisa milki ya mzee huyu hatari?. Ina maana hakusikia japo kwa majirani juu ya ukatili wa bosi huyu kijana; ukatili uliofananishwa na unyama? Mavazi yake pia yakanifanya nijiulize. Suruali nyeupe ya kulalia, kifua wazi? Alitokea nyumbani kwake? au ni yule mlinzi kichaa wa mapenzi aliyeitwa Karim. Kutokana na tamaa aliyo nayo kwa mtoto wa bosi wake, alitaka kukiotesha nyasi kibarua alichokipata kwa ngama?

    Maana mara kadhaa siku za nyuma alimsumbua Salome kwa maneno yake ya kipuuzi. Hata alipotishiwa atasemewa kwa baba, hakuacha kumtazama na kummezea mate. Kama ni hivyo, tamaa zake zilizidi mipaka. Pia hata sijuhi akikamatwa kitu gani atafanywa.

    Mtu huyo ambaye bado sikumjua, aliufikia mlango akitazama huku na huko.

    Kitasa nacho kikashikwa, kikafunguliwa kiustadi, kikatii kubembelezwa kisitoe sauti; mlango ukaachama. Kutokana na mwanga hafifu wa mwanga wa mbalamwezi ulimsaidia kuona aendako huyu aliyeingia huku akinyata kama mwizi sasa alikuwa kama kivuli tu na si kiwili wili tena.

    Usingizi uliomteka salome haukumpa japo ndoto, kuwa chumba alicholala hakuwa peke yake tena. Angejuwa yupo mtu wa pili anayemtazama, asingethubutu kuitupa khanga yake kuikaribisha baridi ya kipupwe cha usiku. Joto ndiyo lilimfanya aache maungo yake wazi bila hiyana.

    Joto hilo lilaaniwe kwa nguvu zote.

    Hiyari ikashinda utumwa. Yale mapaja yaliyokatika kutoka chini ya kalio na kuishia katika magoti, miguu iliyovimba kwa kufinyangwa kiustadi ikafinyangika; yote hayo yalikuwa nje mbele ya kiumbe hichi kilichoshiba. Kiwili wili chake pekee baada ya msaada wa mwanga wa mbalamwezi ndiyo imenilazimu kusema kiumbe kilichoshiba baada ya kukiona kifua kilichovimba na kuwa kama kalio la mtoto mdogo aliyebarikiwa umbo na mikono iliyokatika kimazoezi.

    Kiwiliwili kile hatimaye kikapata uhai. Kikaanza kujisogeza mpaka kilipo kitanda cha salome “Kha! Yupo uchi” akili ya mfedhuli huyu ikaropoka. Ninaweza kusema ni kama vile nilikuwa na uwezo wa kipekee kusoma mawazo yake mara baada ya kumuona akishituka kwa macho ya tama.

    Wakati alipoanza kuipapasa ngozi laini ya Salome, ndipo salome pia alihisi akipapaswa. Salome akashituka. Kitu cha kwanza alichowaza kichwani kwake ni jinamizi. Ilimlazimu kuwaza hivyo kwa sababu si binadamu pekee, asingekuwako hata paka ambaye angeweza kuruka ukuta wa nyumba hiyo.

    Ulinzi ulikuwa mkali kupitiliza.

    Nyaya zilizowekwa shoti ya umeme na mbwa wenye njaa kali wakiranda randa huku na huko. Kabla hajawaza kupiga kelele nyingine, mikono yenye nguvu ilikwisha ivamia midomo yake. kisha jamaa huyo alitimiza haja ya tamaa zake. Purukushani ndogo hafifu alizoziweka Salome, hazikumsaidia kushindana na mtu huyu mwenye minguvu hatari.

    Kwa mara ya kwanza salome akabakwa bila kumjua mvulana yeyote yule.

    Maumivu yalikuwa makali kwa sababu hakuwahi kufanya hivyo kabla. Pia ilichangiwa na kufanya kitendo ambacho hakuwa tayari. Kisha akiwa katika kulia lia bila kutoa sauti kwa maumivu aliyoyapata, taa ikawashwa. Mbakaji huyo alimfunga mikono kwa kamba na miguu, midomo akatumia shuka kumziba sauti isitoke. Yeye mbakaji alikuwa kama alivyozaliwa kama alivyo Salome. Salome alitazama mapaja yake damu zilichafua mpaka shuka pia. Mbakaji alitumia kipande cha khanga kilichosauliwa pembeni na Salome kwa minajiri ya kulifukuza joto. Akaivaa suruali yake nyeupe wala asilione lile doa jekundu lililo nyuma ya mguu wake wa kushoto. Ilikuwa ni damu ya Salome.

    Kisha aligeuka kuutazama uso wa Salome. Binti mdogo asiye na hatia yoyote. Binti aliyekuwa akilia kwa sauti ya kwi kwi. Ambaye yeye mwenyewe alitoka kumfanyia kitendo cha kifedhuli punde tu. Haikuwa sura ngeni kwa Salome. Macho yakamtoka pima nusu kumdondoka. Mtu huyo naye alimkazia macho bila haya huku akiuweka uso usio na ladha yoyote ya ubinadamu.

    “Baba” Salome aliropoka.

    Kibao kimoja tu kilimkatisha kauli iliyoishia kwenye papi zake. Chozi lililomtiririka kwa fujo likamshuka na kumchafua mashavu. kwikwi nayo ikasikika kwa mbali. Hatimaye nikagundua huyu fedhuli asiye na haya, ndiye huyu aliyetamani kula kuku na mayai yake ni huyu huyu ndiye aliyemtoa aliyemtoa.. Salome katika kiuno chake mwenyewe, mzee asiye na aibu Mzee Kilaza, mzee tajiri mwenye ufahari ulioletwa baada ya kuchimba madini kwa muda mrefu.

    Hakuwa mzee kiumri ila pesa zikamfanya aitwe mzee kwa heshima ya masikini kuizoea na kuiabudu pesa ya Kilaza. Mimi nikiwa mmoja wa vijana masikini nilietumbukia katika shimo na masikini wenzangu tukiabudu pesa za kilaza bila kuwa na uhakika zilipotoka. Mzee kilaza akaipata sauti yake baada ya kuirekebisha kwa kikohozi kifupi; kisha alisema kama anayenong’oneza.

    “Hii ni siri, mama yako asifahamu endapo nikijua nitakufanya kitu ambacho hutanisahau hata tukikutana kuzimu”

    Salome alinyamaza kulia huku akimkazia macho kama aliyepoteza jambo juu ya uso wa baba yake. Mzee Kilaza aliendeleza na maongezi “Nitakukabidhi chochote utakachohitaji ila kuanzia leo wewe utakuwa mke na si mtoto tena. Siri hii asifahamu mtu yeyote ukimjumuisha mama yako” Mzee kilaza akakazia.

    Nafikiri hata ingekuwa wewe ungekosa ule ujasiri unao kufanya ukajiamini mara kwa mara. Uso wa Mzee Kilaza haukuwa na mzaha hata chembe. Wema ulijitenga, na roho mbaya ikamtawala. Alitumbua mimacho yake mibaya kama fundi saa aliyepoteza sukurubu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliyabinya binya matiti ya Salome, huku akitabasamu kifedhuli kisha alikazia vitisho vyake “Salome usifanye kosa ukajuta, usimueleze mtu yeyote siri hii” kisha akamfungua kamba aliyomfunga. Wakati mzee Kilaza akitoka chumbani kwa Salome alikuwa na uhakika kuwa hakuna ambacho kingeharibika kwa sababu vitisho alivyompa Salome vilitosha kumtisha yeyote hata aliyejitia kiburi.

    Ila mwendo ulikuwa ni wa taratibu kama asiyejiamini. Moyo ulimsuta? Ina maana wazo la kumuwekea madawa ya kulevya Batuli katika kahawa aliyoinywa haraka haraka, usingizi nao ukaja haraka haraka pia, hatimaye yeye mwenyewe akalitupa pembeni shuka alilojifunika nalo baada ya kuhakikisha Batuli amekwishalala; hapo moyo haukumsuta bado? Hatua za kunyata kutoka chumbani kwake mpaka chumba alicholala Salome; moyo haukumsuta kipindi hicho bado? Moyo wake haukuwa hata na chembe ya haya kwa kuwaza kufanya kitendo cha aibu kama hicho. kitendo kinachoonekana sawa na laana kwa jamii.

    Hapana lipo jambo. Ipo namna ya mzee huyu aliyepata heshima kufanya kitendo hicho cha kumvunjia heshima. Nani anajuwa anachowaza? Nani anajua sababu ya kufanya alichofanya? Ilikuwa tamaa ya mwili? najua ndio kitu ambacho ungejibu. Lakini ningekuuliza Batuli hakumtosheleza? Batuli alikosa nini ambacho Salome alikipata? Si ni yeye aliyemvunja usichana wake kipindi kile anasoma kwa mimba aliyompatia kwa kumlaghai na ile nokia mayai aliyompatia kule SHAMSI GUEST HOUSE? Au hata alishakwishazisahau zile sifa alizommwagia Batuli kuwa ni fundi wa kukisakata kiuno. Hata akaapa atamtafuta kungwi aliyemfanya kua hivyo, amlipe vinono kwa kumfanya apate vinono? Sasa leo imekuwaje akamuona Salome anafaa zaidi ya Batuli? Salome aliyemfuta kinyesi, Salome aliyemkojelea akamchapa? Kipindi kile hata akakimbia majukumu ya kumlea asirudi hata wiki mbili kabisa kutokana na utundu alionao Salome? Hakika huyu mzee alikosa haya katika uso wake ni si ajabu hata katika mzunguko mzima wa damu yake.

    Mwendo ukawa mrefu kutoka kitandani mpaka alipokifikia kitasa. Alipokishika na kutaka kukifunga, sauti ya Salome ikapata uhai.Sauti ya kinyonge iliyotolewa kwa hali ya uwoga ikamsimamisha Mzee Kilaza.

    “Baba kwanini umeamua kunifanyia hivi?”

    Masikini Salome. Macho yakafumba kwa lita za machozi zilizonasa kwenye kope zake. Mdomo ukawa mzito kuendelea kuongea, baada ya donge zio kulinasisha koo lake. kilio kikaanza upya. Kilaza akageuka, huku Tabasamu lile la shetani likiwa juu ya uso wake. Tena naweza kusema lilikuwa ni tabasamu baya zaidi ya lile la shetani.

    “Unataka kufahamu?” aliuliza kwa kejeli huku akijitia kama anayetaka kucheka. Salome hakuitikia, aliendelea kulia. Mzee Kilaza alirudi kitandani alipo Salome kumueleza haya, kwa dharau “Salome wewe ni binti mzuri, hivi nikuulize? wangapi wanakutamani huko nje?”

    Yarabi msikilize huyu Mzee. Alikosa japo soni kuzungumza ufedhuli na mtoto wake wa kumzaa? Mikono yake isiyo na adabu ikiwa matembezini katika kifua cha Salome.

    “kuna ubaya gani mimi baba yako nikaonja japo ladha yako kidogo kama afanyavyo mama yako, aonjapo mboga zake jikoni?” aliendelea “Salome, wewe ni mtu mzima sasa. Unahitaji kuwa na maisha yako binafsi kama ungekuwa ukiishi huko Ulaya. Kwanini usinifurahishe bila ghasia nikakupa ile nyumba ya kule Kinondoni? Hauhitaji gari nzuri ya kutembelea? Salome nakuahidi ukinifurahisha, nitakupa zaidi ya hivyo vyote”

    Salome akaupata ulimi wake akamuuliza “Hivi baba, kweli wewe ni baba yangu wa kunizaa kabisa?”

    Salome akawaza pamoja nami. Binafsi na mimi nilianza kupatwa na mashaka na mzee Kilaza kuwa baba mzazi. Nikasubiri kusikia jibu atakalotoa “Mimi sikupata mimba, hilo swali ni vyema ukamuulize mama yako, mke mwenzio” Mzee Kilaza alipotaka kunyanyuka swali lingine likamkalisha

    “Sikujua kama mtu niliyekuheshimu unaweza kunifanyia kitu kama hiki. Ulikosa malaya wengine huko nje?” mzee kilaza alijitia kama anayesikitika kisha alimsogelea Salome karibu kabisa na sikio lake na kumnong’oneza

    “Haya ni masharti ya utajiri, hutaki kuishi vizuri wewe” kisha alimtazama Salome aliyelowa kwa machozi. Kisha alicheka kicheko cha kebehi kilichomfanya Salome ashindwe kujizuia kulia. Mzee Kilaza alitoka chumbani humo akimuacha Salome bado akilia.

    Unadhani usingizi ulimpata Salome? Wa mang’amung’amu haukuepo hata ulipobembelezwa. Ungekujaje kwa kitendo alichofanyiwa? Kitendo cha kudhalilishwa sawa na cha kinyama. Kitendo kilichomfanya ajihisi hana thamani nyingine tena duniani.

    Labda usingizi huo ungekuwa umepotea njia.

    Kichwa kilijaa mawazo yaliyomporomosha machozi kila wakati. Mawazo yaliyomfanya afikirie kujiua muda mwingine katika usiku huo.

    “Ndiyo heri nife nipumzike kuliko aibu nitakayoipata” alijinng’oneza kwa huzuni. Aibu ya kubakwa na baba yake mzazi. Kilaza mwenye uwezo wa kuwa hata na wake zaidi ya wawili kama angeamua, kama aliona Batuli hakumridhisha. Mara akawaza “Nimwambie mama” ile sura ya baba yake Kilaza ikampitia na kumkumbusha kile kitisho

    “Hii ni siri ambayo hata mama yako hapaswi kuifahamu”

    Sauti hiyo iliyotisha ikagonga kichwani mwake. Akiwa katika lindi hilo la mawazo yasiyo na majibu, usingizi usio na taarifa ukampitia bila apointment.

    Asubuhi mezani Kilaza akiwa na Batuli wakinywa chai alikuwa ni mwenye wasiwasi. Wasiwasi uliomfanya kukaa tayari kwa swali au jambo lolote litakalotokea. Yeye alihisi Batuli anamvizia, hivyo na yeye akawa katika kumvizia Batuli bila Batuli kujua kama Kilaza huyu anayeifurahia kinafki chai aliyomtengea, anamuwaza yeye.

    Kilaza hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake. Alikaa kimtegomtego kama mwizi anayevizia kukaba. Leo hakumuulizia Salome kama alivyokuwa akifanya sikuzote. Hakuongeza sukari kulalamika kama ni ndogo. Yai alilokaangiwa kwa kunogeshwa na viungo mbalimbali lisionekana kama limeungua halikumtia tamaa ya kulimaliza. Jasho lililomtoka lilikuwa jepesi, lilikuwa ni lile jasho la uoga.

    Sasa aliogopa nini na yeye alijitia kidume? Nilitamani kucheka kumuona Kilaza mzee mwenye ujasiri kazini akiinamia kikombe saa zote kama mtu aonaye aibu. Mara chache chache akauinua uso wake kumuibia batuli kama alikuwa akimtazama. Batuli hakugundua chochote kwa mumewe, hata kikombe kilichotetemeka kwa mikono iliyomtetemeka Kilaza.

    Akili ya Batuli nayo haikuwa katika chai ya mezani. Kilaza hilo hakuligundua. Saa pana ya ukutani iliyoonyesha ni saa tano asubuhi, ikamfanya Batuli ajiulize mambo mengi.

    “Huyu mtoto siku hizi ana nini? Mbona anataka kuniletea balaa kwa baba yake” alijisemea kwa sauti ya chini iliyomfanya Kilaza kuwa makini kusikiliza anachoongea. Alipatwa na wasiwasi juu ya Salome. Kwa sababu haikuwa kawaida yake kupitiliza muda wa kuamka.

    Batuli alinyanyuka kwa ghafla baada ya sonyo lililomponyoka kumtangulia. Kwa mara ya kwanza Kilaza naye aliuvunja ukimya



    Akili ya Batuli nayo haikuwa katika chai ya mezani. Kilaza hilo hakuligundua. Saa pana ya ukutani iliyoonyesha ni saa tano asubuhi, ikamfanya Batuli ajiulize mambo mengi.

    “Huyu mtoto siku hizi ana nini? Mbona anataka kuniletea balaa kwa baba yake” alijisemea kwa sauti ya chini iliyomfanya Kilaza kuwa makini kusikiliza anachoongea. Alipatwa na wasiwasi juu ya Salome. Kwa sababu haikuwa kawaida yake kupitiliza muda wa kuamka.

    Batuli alinyanyuka kwa ghafla baada ya sonyo lililomponyoka kumtangulia. Kwa mara ya kwanza Kilaza naye aliuvunja ukimya

    “unaenda wapi?” Batuli hakusimama. Kilaza naye alinyanyuka kumfuata Batuli kuzuia chochote kitakachotokea ili siri yake isifichuke. Japo kwa vitisho alivyompa Salome usiku ule baada ya kumbaka, alijua akibanwa sana anaweza akaropoka. Alijua ni lazima Batuli atakuwa anaenda chumbani kwa Salome. Na ndiyo ile sababu kuwa na mawazo mengi hata akasahau kuweka sukari kabisa katika chai, na ndiyo sababu hata ikamfanya akaunguza lile yai na kuwa jeusi kabisa hata likautisha ulimi.

    Alihisi Batuli amegundua alichokifanya usiku? Ama ni hisia tu, basi jasho likamtoka, likakata hakujali; yeye aliendelea kumfuata.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Batuli una nini wewe, mimi si nakuita?”

    Batuli alizimaliza ngazi za kuelekea chumbani kwa Salome. Hatua ndefu ndefu zilizoongozana na mapigo ya moyo ya Kilaza zilimfanya amfikie Batuli kabla hajakishusha kitasa cha mlango wa Salome.

    “We mwanamke leo una nini?” Batuli hakujibu alifura kwa hasira kama mdudu aliye tayari kutema sumu muda wowote. Kilaza yeye akavaa ujasiri ujasiri ukampendeza. ‘kama atakuwa amegundua, ni saa ngapi? Alikwishaonana na Salome kabla? Mbona amekuwa na hasira na mimi hivi leo?’ akiwa katika kujiuliza Kilaza.

    Batuli aliupata ulimi wake huku akifoka ki kike. “Huyu mtoto ameanza tabia mbaya baba Salome, huenda anaenda disko usiku huyu. Haiwezekani hii leo siku ya tatu mimi ndiye nimtengee chai halafu aje kunywa saa sita ya mchana. Nani amemzaa mwenzake humu ndani?”

    Kilaza alicheka kwa kebehi baada ya kikohozi kifupi cha kusafisha koo kumpitia.

    “Sasa mke wangu jambo hilo ndiyo likufanye ufure kama kobra aliyepoteza mayai yake” sasa alicheka na kumfanya Batuli naye kulipata tabasamu lake

    “Nilikuja mbio mbio nilidhani labda umehisi amelala na mwanaume” alinyamaza kama aliyekuwa akikumbuka jambo. Batuli naye alimkazia macho kama anayesubiri aendelee. “Sijuhi ningemfanya nini huyu ambaye angeniharibia binti yangu” wakati Kilaza akimaliza kuongea hivyo, Salome alifungua mlango wake. Alikuwa amejifunga shuka tu. Baada ya kuwasalimia wazazi wake huku akifuta tongotongo kwa kiganja, alisema

    “Mama kuna jambo nahitaji kuongea na wewe”

    kisha alirudi chumbani bila kuongeza chochote.

    Kilaza aliganda kama sanamu akimtazama Batuli, aliyekuwa anamtazama ampishe yeye apite. Kilaza alipotaka kuingia yeye kwanza, Batuli akamuuliza kwa mshangao

    “Wewe baba Salome umeitwa wewe? Embu tulia kwanza nikazungumze na mtoto bwana nijue ana tatizo gani siku hizi. Unajua muda mwingine atashindwa kueleza matatizo yake ikaleta madhara baadaye?”

    Kilaza alitamani kubisha kutumia mabavu kwa nafasi yake ya ubaba, lakini macho makali ya Batuli yakamsuta kufanya hivyo. Batuli akaingia baada ya kufunga mlango, ila nyuma Kilaza hakuondoka.

    Alisimama akitegesha sikio mlangoni kusikia yatakayoendelea humo ndani. Kilaza alifahamu fika Salome alikuwa na nia ya kumwaga mchele hadharani. Alijua kama siri yake ingekuwa hadharani, ingemchukua muda mrefu kusahau majuto yatakayompata. Majuto ya kufutwa kwa kizazi cha Kilaza vizazi kwa vizazi kwa vifo vya ghafla visivyo na tiba.

    Ni kipindi hicho mapigo ya moyo yalipomuenda mbio na kujuta kuelekezwa kwa mganga yule. Alimlaumu kimoyomoyo rafiki yake Abdallah kumuelekeza kwa mganga mwenye jicho moja la mbuzi na mwenye uso wa kutisha.

    Aliyetisha yeye mwenyewe na sehemu aliyokaa.

    Mganga aliyempa masharti magumu baada ya yeye kwenda na shida ya kutaka utajiri. Utajiri kupitia katika mgodi wake wa dhahabu huko Mwadui. Masharti aliyoyaona mepesi kila alipoona taswira ya utajiri mbele ya uso wake.

    “Utembee na Salome mtoto wako kwa muda wa siku thelathini na damu ya mkeo iwe sadaka kwa mizimu. Utakuwa tajiri utakayejiogopa mwenyewe na kuogopwa na dunia nzima kwa heshima utakayopata”

    sauti ya mganga ikapotelea katika kicheko kibaya kilichotisha zaidi ya kicheko cha shetani. Kicheko kisicho na asili yoyote hapa duniani labda kuzimu, katika makazi ya shetani mwenyewe.

    Utajiri wa kutetemesha makapuku kadhaa katika jiji la mwanza, alikuwa nao. Lakini pesa aliyoitaka bado hakuipata. Heshima aliyoihitaji pia ilikuwa ndogo. Alitamani kuangukiwa miguuni na raisi wa nchi akimuomba msaada wa kifedha kama sio ushauri wa kiuchumi kama afanyavyo katika safari zake nje ya nchi.

    Alitamani kuitetemesha dunia kwa fedha zisizo hesabika na kuwa hazina idadi zilizowekwa katika benki mbalimbali duniani. Alitamani aishi juu ya sheria, sheria isimpinge chochote kuhusu biashara yake. Huyo ndiye Kilaza aliyewaza ujinga huku tabasamu la heri ya maisha likimpitia katika papi za midomo yake.

    Kilaza alimkubalia kwa moyo mmoja mganga huyo huku mwenyewe akiongeza kwa kusema

    “Hata ungehitaji damu ya baba yangu ningekuletea kichwa chake kikielea ndani ya beseni lililojaa damu yake”

    Aliona kwa nini aendelee kumtunza mzee wake aliyepoteza meno mengi kutokana na uzee alionao? Kikongwe anaetembea kwa msaada wa mkongojo wake, fimbo ya mpera. Aliyepoteza mboni zake hata kabla Kilaza hajamaliza elimu yake ya msingi.

    Aliona utajiri ulikuwa ni afadhali, kuliko vyote alivyo navyo.

    Akiwa katika mawazo ya mganga, ndipo aliposikia Salome akizungumza

    “Mama, Baba bado yupo hapo nje?”

    Salome aliuliza kwa sauti ya chini kama aliyenong’oneza.

    “Hapana mwanangu alitaka kuingia nikamfukuza. amerudi zake chini kuendelea na chai. Salome mwanangu una nini mama” Batuli alimuuliza Salome kwa upole na upendo wa mama ukimbembeleza, Hali iliyomfanya Salome kuanza upya kulia licha ya Batuli kumshuhudia macho yaliyo mekundu na kuvimba kwa kulia.

    Kilaza alitamani kuingia kumtisha Salome asiropoke, lakini nafsi yake ikamkataza. Akatamani kufanya jambo lakini lipi lingefaa? Kumtisha Salome ili kulinda siri yake? Kulinda heshima yake? mikono iliishia kushika kitasa bila kukishusha wala kufanya chochote. Alikazia sikio mlangoni lakini hakusikia chochote. Chumba kikatawaliwa na ukimya uliozidi kumtisha Kilaza.

    ‘anamnong’oneza?’alihisi hivyo.

    Heri Zamda mfanyakazi aliyekuwa na jukumu la kuhifadhi bustani katika kasri yake alipita, alitokea katika moja ya vyumba vya wafanyakazi ndani ya nyumba hiyo wa ajili ya kuingia kazini rasmi.

    Aimfuata na kumwambia jambo.

    Laiti kama dakika chache mbele Kilaza angeendelea kusubiri, angeisikia sauti ya Salome. Salome aliyekuwa akimwambia mama yake

    “Mama jana usiku kuna mtu aliingia chumbani kwangu”

    Yeye Kilaza aliupoteza muda mwingi kupanga mbinu za kuharibu mazungumzo ya Batuli na Salome. Alimfuata Zamda na kumwambia kuwa amfuate Batuli chumbani na ahakikishe anakuja naye chumbani kwao huku yeye akiigiza kama mtu aliyedondoka na kifafa.

    Ulikuwa ni mchezo wa kitoto uliofanywa na mtu mzima, ujinga ulioje.

    Chumbani kwa Salome, Batuli aliyatoa macho yake, kama aliyeambiwa habari za msiba. Ilikuwa ni ngumu kuamini, nyumba yenye ulinzi mkubwa, kama hiyo ya tajiri Kilaza; mtu kuruka ukuta uliozungushiwa nyaya za umeme na kulindwa na mbwa wakali ukimuacha mbali yule mlinzi aliyeupoteza usingizi wake takribani miaka ishirini iliyopita katika kazi yake.

    Salome akiwa bado anamtazama Batuli, aliuhisi mdomo wa mama yake ukipoteza staha, na kuwa kama mtu aliyekaribia kuropoka.

    “Mama usipige kelele basi subiri nikumalizie” uvumilivu tena haukuwepo, Batuli bado hakujisikia kunyamaza. Uso wake ulijaa maswali, maswali yaliyojibiwa na machozi ya Salome. Batuli aliponyanyuka, Salome akakishika kipande cha khanga kilichokaribia kumvuka

    “Mama, sasa unaenda wapi jamani”

    Batuli alishindwa kupiga hatua yoyote. Khanga iliyokaribia kumvuka ilikuwa imeshikwa upande wa pili na Salome isije kumuhadhiri. Alirudi kukaa huku akitweta kama mgonjwa aliyepoteza kauli. Ingawa kifaa cha kubadilisha hali ya hewa kutoka joto na kuleta ubaridi, kikiwa katika kazi yake kama kawaida, lakini Batuli alichuruzika jasho lililomlowesha.

    Kwanini Batuli alikuwa katika hali hiyo? Hali ya kuchanganyikiwa kabla ya kuelezwa mtu aliyeinga alikuja kufanya nini? kwani Batuli alikwisha mjua aliyemtembelea Salome chumbani humo usiku wa manane? Kama ingekuwa Hawa na Husna waliokuwa wakitoroka disko na kuona nyumba hiyo ndiyo kama sehemu ya kuja kufichia makucha yao kwa wazazi wao; ambao ni mashoga wa Batuli?

    Lah! Hayo yote hayakuwa kichwani mwa Batuli.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuwaza hata moja kati ya hayo yote, Batuli aliikumbuka kauli ya Kilaza Mumewe

    “..nimetoka mbio nikijua Salome amelala na mwanaume humu ndani”

    Batuli aliwaza kumuita mumewe, nafsi ikamkataza. Aliwaza atoke akampige na ufagio ule wa chuma, yule mlinzi aliyeanza uzembe, pia getini alipaona mbali. Aliamua kukaa na kumsikiliza Salome.

    “Mama jana usiku wakati nimelala nakumbuka nilizima taa kabisa, sasaghaflanilihisi uzito wa mtu kifuani kwangu kwa sababu usingizi ulikuwa mzito sikuweza kushituka mapema mpaka alipotaka kuanza kunibaka ndiyo….”

    Batuli akamkatiza kwanza

    “We salome! nieleze vizuri unanichanganya, umefanya nini na ni nani aliyeingia humu ndani”

    Wakati Salome akiutafuta ulimi wake, Mlango ulipoteza nguvu, na msukumaji alikuwa akija kwa kasi.

    Ulifunguliwa kama pazia la sinema, kwa kweli Zamda alijuwa kuigiza. Alisahau hata kusalimia alichokumbuka ni kuita

    “Mama, mama…. Baba”

    Huku akionyesha mkono wake nje ya chumba. Zamda alikuwa ni mtu mcheshi na mtundu aliyepitiliza, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo ghafla alipongia chumbani kwa Salome, hakuna ambaye angekataa kama kweli Zamda amechanganyikiwa.

    Laiti kama ungeuona Batuli alivyochanganyikiwa usingestahimili kuvumilia kukibana kicheko chako. Alitamani kurudi kumuuliza Salome maswali mengi alitamani kutoka nje basi mwisho aliishia kati kati ya chmba akienda huku akirudi kule mikono ikishikilia kipande cha khanga kilichokosa uvumilivu wa mikikimikiki ya mwili wa Batuli.

    Kilitaka kuanguka tu iwe afadhali kwake.

    Salome pia alichanganyikwa kupitiliza, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kutoka chumbani kabla ya Batuli baada ya Zamda kuzimaliza ngazi. Kilaza alikuwa chini mapovu megi yakimvuja mdomoni.

    Kilaza alikuwa muigizaji mzuri.

    Alijilaza kama aliyepoteza roho yake katika mwili. Aliziba pua zake, akijifanya kama aliyekuwa akipumua kwa shida pia. Hakujigusa, hata aliposhikwa akajilegeza kama mlenda. Mtu wa kawaida ungesema ameshakufa. Batuli alilia huku machozi yakimtiririka kwa kasi. Salome alichanganyikiwa zaidi. Alijiuliza mengi, yasiyo na majibu. Kwa pamoja wakisaidiana na yule mlinzi walimpeleka Kilaza hospitali kutokana na hali ile ya jabu.

    ‘inawezekana ni sababu ya kutaka kutoa siri ya baba kunibaka kwa mama ndio wametaka kumuua baba? Kwani ni wakina nani?’ yeye Salome ndiye aliyewaza mawazo ya kunichekesha zaidi. Sasa kwani alifahamu ni wakina nani waliifahamu siri ya Kilaza kumbaka zaidi yake mwenyewe? Sikujua kwa nini aliwaza hivyo.

    Mawazo yake yakakatishwa na daktari aliyewaomba wampishe ili aendelee kumuhudumia mgonjwa. Wakati huo huo Kilaza alifungua jicho kidogo kuchungulia hali ya chumba huku kukiwa hakuna aliyemuona. Alihakikisha kila mtu amekwisha ondoka huku akiwa amebaki na daktari tu, alimvuta shati Daktari. Hakushituka wala kuogopa kuona macho yaliyomtoka pima daktari. Aliuona mshangao na uoga ulimfanya atabasamu kwa kejeli. Alimnyamazisha asipige kelele yeyote, kisha alimueleza uongo mfupi tu ambao aliuziba kwa kitita cha pesa kitakachomaliza kiu ya Daktari huyo wa kichaga

    “Tafadhali usimueleze mtu yeyote siri hii kuwa sina tatizo ila unaweza kuwaambia tu ni sumu niliyoinywa kutoka kwenye maji ya kunywa niliyokunywa pale nyumbani”

    Alitoa kitita cha noti kikubwa kilichomtoa udenda daktari huyo. Daktari alikubali haraka haraka, akificha kitita hicho kwenye soksi zake ndefu; huku akitingisha kichwa chake kama aliyechanganyikiwa

    “Sawa mheshmiwa hakuna tatizo, yote yataenda sawa” yeye akatoka huku akiwa amemuachia mashine ya oksijeni puani, kuwatisha zaidi walio nje.

    “Hapana Daktari, hii si sahihi” Kilaza akakataa. “ninahitaji kuongea na Salome binafsi, na asiingie mtu mwingine yeyote wakati nipo katika mazungumzo naye” daktari alikubali huku akimpa maelekezo mafupi muuguzi wa kike kuendelea kuweka mazingira yatakayowafanya watakaoingia wasihisi tofauti yeyote

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog