Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

CHANGUDOA - 5

 





    Simulizi : Changudoa

    Sehemu Ya Tano (5)



     Taarifa za Msiba wa Salim zilimshitua sana meneja wa hoteli ya Wanyama. Meneja huyo mfupi mwenye tumbo kubwa na mwenye upara kichwani mwake, alikuwa akitiririkwa na jasho jingi Mara baada ya kuletewa taarifa za mauaji ya mwanaume mmoja ndani ya chumba kimoja katika hoteli hiyo.

    Muhudumu huyu aliyekuwa akiendea chumba kile kwa minajiri ya kufanya usafi, ukimya ulimshangaza mpaka majira yale ya saa tano; saa ambayo mteja wa chumba katika hoteli hiyo alipaswa kuondoka katika chumba chake kupisha usafi. Akapata ruhusa ya kutumia ufunguo wa akiba kutoka kwa meneja ambaye bado hakujua nini kilikuwa kimetendeka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wahudumu wamekuwa wakipata ruhusa ya kufungua milango ya vyumba vya wateja wao pale tu wanapohisi kama mteja husika ameondoka na ufunguo wa chumba. Ni hapo muhudumu yule alipoingia na kushituka alipokuta damu nyingi sakafuni huku mwili wa mteja wao mwenye asili ya kiarabu umelala juu ya kidimbwi hicho kilichokauka.

    Alipiga kelele za woga.

    Meneja wa hoteli alipoelezwa kuwa muuaji yawezekana akawa ni mwanamke changudoa alikataa kwa kuwa yalikuwa ni mauaji ya kutisha. Mtu pekee aliyetoa ushuhuda ni yule kijana wa mapokezi na kumkumbusha meneja wake kuhusu yule changudoa wa Jana usiku.

    "Umesahau vipi bosi, wakati huyu jamaa alijitetea kuwa yule mwanamke ni mkewe?"

    "Sasa nimekumbuka aisee"

    Akajishika shika kidevu, huku baadhi ya wafanyakazi na wapangaji wakijitahidi kujipenyeza chini ya mikono thabiti ya walinzi waliokuwa wakiwazuia kushuhudia kile ambacho kimetokea ndani ya chumba kile. Baadhi ya askari nao walikwishaitwa na askari hao hawakuja peke yake kana kwamba waliitwa pamoja waandishi wa habari na walikuwepo.

    Habari zikasambaa na muuaji mwanamke ambaye iliaminika kuwa ni changudoa, akawa anatafutwa. Hakukuwa na picha ambayo ingesaidia kumuonesha mwanamke anayetafutwa lakini kulikuwa na mchoro ambao wachoraji kutoka katika kitengo maalumu cha polisi, walifanya kazi yao kwa msaada wa meneja wa hoteli ile na muhudumu kutoka mapokezi. Msichana aliyechorwa hakika alikuwa ni changudoa lakini hakufanana na Nadia labda kwa asilimia kumi tu. Msichana aliyechorwa alikuwa amevaa wigi lenye rangi ya dhahabu kipensi kifupi kilichonesha mapaja yake na kitopu kifupi kilichoonesha sehemu kubwa ya kitovu chake na shanga. Msichana huyo kama asingekuwa katika muonekano wa kuigiza basi labda angefanana kwa kiasi Fulani na Nadia ambaye kwa sasa mchakachaka huo ukiendelea alikuwa akinywa supu ya mbuzi na chapati bar ya jirani na mwananyamala hospitali. Hakuna ambaye aliweza kung'amua kwa kuwa hakuwa yule ambaye jana usiku alikuwa na nywele na huyu alikuwa amesuka kilimanjaro. Walikuwa ni Nadia wawili tofauti.

    Habari ya kifo cha Salim na bila kuchukuliwa kitu chochote ikamshitua sana afisa wa polisi ambao walikuwa wakisubiri mambo mengine makubwa zaidi kuendelea kwa kuhisi huenda muuaji huyu ametumwa na kulipwa na watu wenye kisasi na huyu mtu aliyeuwawa mwenye asili ya kiarabu.

    Gumzo katika jiji zima ikawa ni habari juu ya changudoa muuaji aliyeingia na kuua wanaume bila kuchukua chochote. Wanaume waliogopa hadwa wale wazinzi wachukuao vimada katika uwanja wa fisi na maeneo yote wapatikanapo aina hiyo ya madadapoa. Tofauti kwa upande wa pili, wanawake wenye ndoa zao walifurahi kwakuwa wanaume zao wangetulia.

    ...



    Simu ya Nadia iliita akiwa bado anapata supu yake pamoja na chapati. Juu ya kioo cha simu yake jina la Majid lilikuwa likielea hewani

    "Nimeipenda kazi yako mwanangu, nimepata taarifa"

    "Sawa mzee bado bi Faudhia na Rashid"

    "Haha binti yangu kuhusu faudhia tayari Mungu amemfundisha adabu ameshatangulia kuzimu lakini Rashid nitakupa mbinu kwa kuwa amerudi juzi tu kutoka south na nimemuona mjini lakini naamini kifo chake ninapaswa kushiriki kwa asilimia zote"

    "Sikujua kuhusu faudhia"

    "Na pia hujuhi kuhusu Rashid kuwa hata pale ulipokuwa ukikaa ni sehemu ya Rashid"

    Jambo hilo likanshitusha sana Nadia na kuuliza kwa wahka

    "Unasemaje babamdogo? Pale kwa mzee Kumba?"

    "Kabisa, Kumba ni mshirika wa Rashid na ndiye wanauza pamoja madawa ya kulevya ambayo ulitumwa kuyasafirisha na kuwatoroka wale vibaraka wa Kumba pale uwanja wa ndege"

    "Wewe umeyajuaje haya yote?"

    "Nilikufuatilia muda mrefu tangu nilipoingia mjini na nilikujua kutokana na kuingia karika mitego niliyokuwa nimemtegea Rashid sikujua kuwa naua ndege wawili kwa jiwe moja"

    "Oh! Sawa nitakuona saa ngapi?"

    "Usiku nitakuja geto kwako na kuanzia sasa usiwe unatoka katika viwanja vya machangudoa ili usije ukakamatwa katika msako wa changudoa muuaji"

    Nadia akacheka kwa dhihaka kicheko kilichopokelewa na Majid wakacheka pamoja kisha Nadia akakata simu.

    ....

    Ni vipi Kumba akatae kuwa pamoja na James katika mipango michafu ya kutaka kumdhulumu Rashid ikiwa amebanwa sehemu mbaya? Hakuwa na ujanja wowote. Mzigo hakuwa naye hivyo akawa anafuata kila anachoongozwa kama mbuzi wa hitima. James na Kumba wakawa washirika wa karibu baada ya makabiliano yao kule msituni.

    Kutokana na kuupoteza mzigo ule wa madawa ambao ulikuwa ni mali ya james na Reginald siku chache mara baada ya tukio lile la kule msituni kupita na asiwe na habari zozote kuhusu Nadia, mzee Kumba alichukuliwa na watu wasiojulikana ambapo alikuwa nyumbani kwake akisubiri taarifa mpya juu ya kupatikana kwa Nadia kutoka kwa vijana wake waliopoteza mzigo ule.

    Watu hao walimchukua Kumba akiwa amevalishwa mzura mweusi asione aendako pamoja na kuingizwa katika gari ambalo hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia sauti za watu waliokuwa wakicheka na kupiga soga za hapa na pale kana kwamba hawakuwa na mateka ndani yao. Watu hao wengine walikuwa wakivuta bangi na Kumba aliisikia na aliifahamu kwa kuwa alikuwa anakaa na watoto wakihuni kutoka magomeni.

    "Mnanipeleka wapi? Niachieni niachieni jamani"

    Mzee Kumba alilalama lakini akiwa na hofu katika sauti yake. Hakuwa akijua huyu aliyemchukua sasa kama ni James ama Reginald. Akanaswa kibao

    "Nyamaza mshenzi wewe"

    ilikuwa ni sauti mbaya iliyokwaruza kama muongeaji huyo alikuwa na kikohozi ambacho hakutaka kukitoa. Kweli Kumba alinyamaza pamoja na uzee wake. Izee huo wa kimjini mjini haukuwatisha vijana wale washenzi walioanza kumchezea chezea mzee kumba ndevu mara kifua na wakaenda mbali zaidi na kunshika makalio

    "Leo naanza mimi sio kila siku muanze nyinyi tu"

    Alisikika kijana mmoja akilalamika huku mzee Kumba akiendelea kuchezewa makalio yake. Mzee Kumba alijisikia vibaya kudhalilishwa kwa namna hiyo, akamuomba Mungu kama itawwzekana amnusuru katika kazia hii na aache kabisa uanaharamu wa madawa ta kulevya. Mzee Kumba akadondosha chozi la uchungu

    "Unalia!!?" Mmoja alizungumza kama aliyetaka kucheka na kisha akacheka kwa sauti ya juu huku gari likiendelea kutembea "Mzee kama wewe huwa unalia? Kumbe na umafia wako wote huwa unaliaga? Leo basi ndio mwisho wa mateso yako lazima cnn wakutangaze kwa tutakachokufanya"

    Mzee Kumba aliogopa sana na kuhuzunika moyoni mwake. Mara gari ikasimama na Mzee Kumba alishushwa ba mikono ya watu wasiopungua watatu.

    "Songa mbele wewe"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mzee Kumba alirembea kwa kujikokota mpaka sehemu fulani na kusikia sauti za ndege waliokuwa wakilia kama ishara ya kumtambulisha kuwa yupo msituni. Hapo akaikumbuka ahadi ya James kuwa atanirudisha tena hapa ba kuitoa roho yake endapo tu kati ya masharti yake yasipotimizwa, hali hiyo ilimtisha sana Mzee Kumba.

    Alipovuliwa soksi ile kubwa ya kichwani, ni hapo aliposhuhudia taswira ya Reginald akiwa anatabasamu tabasamu baya kuliko yote aliyowahi kuyaona, mdomoni mwake ikining'inia sigara kubwa yenye moshi mzito.

    Mzee Kumba alizungusha macho kutazama huku na kule hakuona cha haja zaidi ya msitu mnene uliofunikwa na miti mingi huku pembeni akiwa amesimamiwa na vijana walioshiba na kujazia vifua, mzee Kumba akakiona kifo chake kipo karibu kuliko pumzi alizonazo.

    “kumba hii kazi tumeanza muda mrefu mimi na wewe lakini sasa naona unataka tuvunjiane heshima”

    “kwanini Reginald ndugu yangu?”

    “mimi sio ndugu yako kwa kuwa sifahamu kwanini unapanga njama za kunidhulumu haki yangu unajuwa kuwa cha mtu hakiliwi?” Reginald aliyatoa macho yake makubwa kwa hasira zilizojionyesha dhahiri usoni mwake “Sitaki hadithi nataka changu”

    Kumba alijiona ni mwenye mkosi kwani hazikupita siku nyingi tangu alipochukuliwa na James mpaka katika msitu ule ambao hakuufahamu vyema. Uoga ulimvaa na alikuwa akitetemeka kama mtoto mdogo, Reginald alinyoosha mkono kama anayetaka kupokea kitu Kumba akasema

    “Mzigo umepotea ndugu lakini namsubiri Rashidi atakaporudi tufanye mipango ya kukurudishia pesa zako”

    “Rashid arudi mara ngapi wakati yupo mjini” Reginald akafoka kwa hasira akamgeukia kijana wake na kuzungumza “Nipatie silaha yangu”

    Baada ya kukabidhiwa bastola yake ndogo Reginald aliikagua kama ina risasi za kutosha na kumtazama tena mzee Kumba

    “Mzee nadhani wewe si mgeni katika hizi kazi zetu na huu ni mshahara wa yeyote anayekiuka mkataba wa biashara yetu”

    Kilichosikika ni kikohozi tu kutoka katika bastola ile na mara mzee Kumba alidondoka chini kama gunia na kuanza kurusha miguu kama mwenye degedege huku damu nyingi zikimtoka kwenyee koo yake pale risasi ilipoingia na kutoboa koromeo lake. Dakika chache baadaye ukawa ni mwisho wa hadithi za Kumba.



     Kifo cha mzee Kumba hakikutoka nje ya msitu ule hata kwa umbali wa sentimita.Reginald baada ya kumaliza kazi ile, alifukia maiti yale kule kule msituni huku siri ya mauaji hayo ikibaki vifuani mwa vibaraka wake Reginald pamoja naye binafsi. Ukawa ni mwisho wa biashara kati ya Rashid na mfanyabiashara Reginald aliyetimkia Dubai kusubiri upepo wa mambo machafu ya kesi ya madawa ya kulevya unaomkabili Rashid upite bila kutajwa na hata kama atatajwa asionekane nchini. ....



    SIKU KADHAA NYUMA



    Rashid akiwa amefika eneo ambalo liko wazi akiuacha msitu ule uliomsaidia kumuhifadhi baada ya kutoroka jela, alikuwa katika barabara kubwa lakini ipitayo magari machache. Kulikuwa kuna nyumba chache zilizokuwa mbali mbali kutokana na eneo hilo kuonekana wazi si eneo la makazi ya watu wengi. Aliamua kwenda kuigonga nyumba iliyokuwa ikimtazama bila kujali ilikuwa ni saa ngapi kwa wakati huo. Baada ya kugonga mara tatu, sauti ya mwanamke ikampokea kwa lugha ya ki- xhosa ambayo Rashid hakuielewa, hivyo alikaa kimya.

    Msichana yule hakufungua mpaka alipouliza tena kwa lugha ile ile na majibu yakawa ni yale yale ya ukimya mpaka Rashid alipoamua kuzungumza kwa lugha ya kiingereza aluyomaanisha "sifahamu unachozungumza binti, nifungulie unikaribishe kikombe cha kahawa napigwa na baridi nje" Msichana yule akaingiwa na imani na kufungua mlango usiku Ule wa manane ikiwa wazazi wake wamelala. Hakuitambua taswira ya Rashid wa wakati huyo aloyefichwa na Giza Nene lakini alishaioba sura ya rashid anayetafutwa kwenye taarifa ya habari. Kwa kuwa hakuwasha taa, aliiendea swichi na kuiwasha taa ile iliyoleta mwanga. Msichana yule ambaye hakupungua wala kuzidi miaka 18 kulingana na jumbo na jinsi alivyoonekana alishituka sana wakati anampelekea chain ya moto Rashid pale alipokuwa amekaa. Mwanzo alihisi amekosea lakini kadri alipomtazama kwa maji ni ndipo aligundua kuwa hakuwa amekosea ila ni kweli huyu ndiye yule atafutwaye kwa kutoroka polisi.

    Wasiwasi uliomkuta binti yule Rashid aliufahamu hakuona tena sababu ya kupoteza muda na pia hakutaka kuifanya haraka ya kupoteza ushahidi. Dakika chache baadaye akamnyonga yule binti kwa mikono yake na kutoka ndani ya nyumba ile kabla wazazi wa yule binti hawajaamka na kushituka. Rashid aliondoka ndani ya nyumba ile akiwa na silaha Mona kisu kikubwa aina ya sime alichokikuta huko jikoni alipouburuza mwili wa mwanamke yule.

    Alikuwa akikimbia na kukimbia huku akitazama nyuma kana kwamba alikuwa akifuatiliwa na mtu, ghafla alianguka alipoiacha barabara na kuingia eneo Mona la vichakani. Aliumia kiasi na kuchubuka chubuka mara baada ya kudondoka pale. Mara baada ya kukagua sehemu ile aliyoanguka, alitambua kuwa ilikuwa ni barabara reli lakini hakuitambua ni reli ielekeayo wapi, akazidi kusonga nayo mpaka kufika eneo moja ambalo ilionekana ni kama stesheni ya treni. Kulikuwa na mwanga mkali wa taa zilizotowa mwanga huo huku abiria wakiwa wengi wenye mabegi yao wake kwa waume na watoto. Kuna waliokuwa wanelala na kuna ambao walikuwa wakitembea huku na kule sigara zilizokuwa zikipasha moto mapafu yake zikiwa midomoni mwao.

    "Nitaanzia hapa hapa japo sijuhi niendako" Kwa wakati ule hakuna aliyemtambua Rashid kutokana na usiku kuwa mkubwa pamoja na ila mmoja kuwa na nawenge ya safari yakiwa yamebaki Massa nachache mtu safari itokeayo mjini Capetown ipite pale na kuelekea moja kwa moja Msumbiji Huo ukawa mwanzo wa safari ngumu ya Rashid. Safari ambayo ilimlazimu kulala chini ya vitu na muda mwingine ilimlazimu hata kulala chini ya miguu ya wangu pale bwana titii alipokuwa akipita na kukagua tikiti zake. Alifanikiwa kuvuka mpaka wa nchi ya frika kusini na nchi nyinginezo mpaka mwisho wa treni ile iliyoishia Msumbiji.

    Ndani ya treni ile si kwamba hakuwa akila chochote. Alikutana na baadhi ya watu waliozamia kama yeye na wengine wenye mioyo ya huruma na kuwapatia juisi pamoja na mikate na kisha kuwaficha kwa pamoja mpaka mwisho wa safari ile. Mwisho haukuishia pale japo Rashid alibadilisha nguo alizozichukua katika kamba ndani ya nyumba ile aliyomuua binti yule wa kisouth, lakini alikuwa akinuka kwa kuwa hakuwa ameoga kwa kipindi kirefu na ukizingatia alitoroka kupitia katika bomba la maji machafu.

    Walifika msumbiji baada ya siku tatu huku tayari ikiwa imeshafika jioni. Mmoja wawazamiaji ndani ya treni ile, aliwakaribishwa wenzake nyumbani kwake alipokuwa akiishi, hapo ndipo Rashid alipoweza kubadilisha tena nguo na kuoga huku akiliacha sime lile akiamini kuwa hakuna kikwazo kingine huko aendako, kisha aliwahadithia wenzake yaliyomkuta na kila mmoja naye kuhadithia yaliyomkuta lakini Rashid akabaki katika midomo yao kama mtu aliye na roho ngumu sana kutoroka na kufanikiwa kuvuka boda ya nchi yenye ulinzi mkali kama afrika ya kusini "Ndugu wewe una Mungu aisee" mmoja wa wale vijana wanne akaropoka huku akimtazama Rashid kwa mastaajabu. Haikuwa ngumu tena Rashid kuingia Tanzania japo hakuwa na pasipoti wala chochote mkononi mwake kunthibitishia yeye ni raia wa nchi hiyo. Askari mbali mbali walizibwa macho na midomo yao kwa pesa kidogo ambazo Rashid alipatiwa kumsaidia huko njiani kwa ajili ya safari ba chakula na yule mmoja wao aliyewakaribisha waTanzania wawili katika ntumba yake. Hivyo Rashid alitobozea huko mtwara na hapo ukawa mwanzo na hasira zake kupanda juu ya Mzee Kumba. Ni wakati huo Rashid akiwa anaigusa Dar es salaam pale Mbagala ndipo Majid alikutana naye kama bahati mbaya. Majid alikutana na Rashid kama bahati mbaya kutokana na Majid ilimuibukia tu tamaa ya kwenda kutazama mpira wa Azam huko katika kiwanja chao kilichopo chamanzi japo haikuwa kawaida yake na ndipo yeye aliweza kumuona Rashid lakini Rashid hakuweza kuntambua Majid kwa kuwa yeye hakuwa huru kutokana na kujificha jificha asionekane kutokana na kuwa mtu anatetafutwa.

    Gari aliyoipanda ilikuwa ni ya nwenge ili akashukie Magomeni na kuelekea kule kwa mzee Kumba. Hiyo ilikuwa ni siku chache baada ya Salim kufariki. Majid akamuungia tela mpaka mwisho wa safari ya Rashid. Akafahamu uwepo wa Rashid Dar es salaam hakuwa na tamaa ya kutimiza lengo lake kwa kukurupuka akarudi alipofikia na kupanga mipango yake upya. Rashid akiwa amebadilisha miondoko na muonekano wake ili watu wa eneo lile wasimfahamu, lakini yupo aliyemtilia shaka huyu ni yule kibaraka wa Reginald ambaye naye aliwekwa maeneo hayo jirani na nyumba ya mzee Kumba kuchunguza kila kinachoendelea na hivyo naye kumfikishia taarifa Reginald uwepo wa Rashid mjini. Rashid naye baada ya kuhakikisha Kumba yupo magomeni hiyo hiyo, hakuwa na papara ya kumfuata akiwa amejipumzisha lakini laiti kama angefahamu hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho kumuona mzee Kumba, angepita japo kumsabahi. Kwani siku hiyo ndiyo ile siku ambayo vijana wa Reginald walimchukua mzee Kumba na kwenda kumuua mzee Kumba kule msituni. .... Majid kila alipofikiria namna ya kumuangamiza Rashid hakuiona kwa kuwa kama angemtumia Nadia basi lengo lisingetimia na mipango yao ingeharibika hivyo alipata shida sana kukaa akiwa na mawazo mengi baada ta kumyona Rashid akiwa amerudi. Akaona jambo la mwisho ni kumchomea kwa askari. Rashid alikuwa ni mtu anayetafutwa kama kitu chochote cha haramu hivyo habari ya kuonekana kwake Tanzania ingeshambuliwa na kuchukuliwa kama jambo la dharula ndani ya jeshi la polisi.

    Majid akajichekea kimoyomoyo alipokumbuka shauri hilo alilolipitisha katika halmashauri ya kichwa chake na kuona kuwa linafaa. Alisuburi siku inayofuata na hivyo alimpigia simu Nadia kumpa mipango hiyo bila kujua Nadia naye alikuwa amempangia mipango mingine na yeye pia. "Nina uhakika Majid alishirikiana na Rashid kumuua baba yangu hivyo nitahakikisha namuua kabla na mimi sijafa nikasalimie wazazi wangu" lakini hayo yalikuwa ni mawazo ya Nadia aliyofikiria kabla ya kuipokea simu ya Majid iliyompa mipango mipya ya kumkamatisha Rashid. ... Rashid akiwa maeneo hayo hayo ya Magomeni siku ya pili tangu aingie Tanzania, alishituka kusikia king'ora cha gari ya polisi kilichotokea upande wa kusini mwa mtaa aliokuwepo lakinu hakujiwekea tahadhari ya juu ya jambo lolote litakaloenda kutoke na mara alishangaa kuona askari wawili wakiume walioshuka na kukimbilia pale alipo yeye, walimuoneshea bastola alipokuwa amesimama jirani na ntumba ile aliyokuwa akilelea watoto yatima.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuwa na ujanja mwingine kwa kuwa upande wa kaskazini gari aina ya difenda lenye askari ambao hawakuvalia sare zao ndio lilikuwa kikiegeahwa mita chache kutoka pale alipo. Alinyoosha mikono juu na mmoja wa askari wale alienda mpaka pale aliposimama Rashid na kunfunga pingu. Wakati huo ambao wanamkokota Rashid taratibu huku watu wakiwa wamejaa kama ujuavyo maeneo hayo ya uswahilini alisikika msichana aliyekuwa akipiga kelele kama aliyewehuka akilalama "Nakufaaaa nisaidieni jamani nakufaa mie mwenzenu" Alikuwa ni Nadia aliyekuwa akikimbia huku Majid akimfuata kwa nyuma bila kutambua hila za Nadia. Wananchi wale walipowapisha bibi na bwana yule, bibi yule ambaye ni Nadia alianguka miguuni mwa askari huku akitweta kwa uchovu huku akimuoneshea kidole Mahid aliyekuwa amesimama akiwa ameshika kiuno akimtazama Nadia kwa mastaajabu. Ni wakati huo Rashid alikuwa ameshapakizwa kwebte difenda na yule askari aliyevalia sare zake akamuuliza Nadia "Vipi wewe?" "Anataka kuniua ana bastola kiunoni mwake, anataka kuniua huyu mzee" Nadia alikuwa akizungumza hayo huku akimtazama Majid aliyechanganyikiwa asijue cha kufanya. Askari wale wawili nao wakatoa bastola zao

    "Mikono juu, nasema mikono juu" Majid alinyoosga mikono yake juu akiwa amelowa asiamini kitendo alichokifanya Nadia. Majid naye alitiwa pingu huku akintazama Nadia aliyekuwa akiondoka eneo lile akiwa na tabasamu pana usoni mwake.

    "Shit" Majid akaropoka



    MWISHO!!!!!

0 comments:

Post a Comment

Blog