Search This Blog

Sunday 19 June 2022

MCHEZA FILAMU ZA NGONO - 3

 





    Simulizi : Mcheza Filamu Za Ngono 
    Sehemu Ya Tatu (3)







    Miaka saba ilikuwa imekwenda sana tangu kipindi kile ambacho mvulana Daniel alipokuwa ameangukia katika mapenzi ya msichana Katie katika kipindi kile

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ambacho walikuwa wakiishi mitaani. Katika kipindi hiki hakuwa nchini Marekani tena, alikuwa akitembea katika nchi mbalimbali kama baharia ambaye alikuwa



    akifanya kazi katika meli kubwa ya Metropoza iliyokuwa ikizunguka sehemu mbalimbali duniani.

    Picha za Katie alikuwa akiziangalia mara kwa mara, alimkumbuka sana msichana huyo kutokana na uzuri mkubwa ambao alikuwa nao, alimkumbuka kwa kila



    kitu japokuwa alijua fika kwamba msichana huyo kwa sasa alikuwa akiigiza filamu za ngono ambazo zilikuwa zikimuingizia fedha za kutosha.

    Alikuwa amefanya kazi ya ubaharia kwa miaka zaidi ya saba, uzoefu wake mkubwa ambao alikuwa nao Daniel ndio ambao uliwafanya hawa nahodha wa meli



    hiyo kumpa uongozi huku akimlipa kiasi kikubwa cha fedha.

    Daniel alikuwa akiyakumbuka vizuri maisha yake ya nyuma ambayo alikuwa ameishi zamani, yalikuwa maisha ya shida ambazo kila siku zilikuwa zikimpelekea



    kutafuta fedha maishani mwake pasipo kujali ni aina gani ya shida ambazo angeweza kukutana nazo.

    Maishani mwake alipenda sana maendeleo, alitamani pia kuwa na msichana Katie ambaye alikuwa akimfahamu toka walipokuwa wadogo, wakicheza wote na



    kufanya mambo mengi pamoja. Katika kipindi kile, japokuwa Katie alikuwa akijitahidi kutokumuonyeshea mapenzi ya wazi lakini Daniel alikuwa na uhakika wa



    asilimia mia moja kwamba msichana yule alikuwa akimpenda sana.

    Kwake, kitendo cha Katie kujiunga na uigizaji wa filamu za ngono ukaonekana kumuumiza sana lakini hakujua ni kitu gani ambacho alikuwa akitakiwa



    kukifanya zaidi. Kama kumshauri, alikuwa amemshauri sana lakini Katie hakuonekana kubadilika.

    Daniel alikuwa na uhakika kwamba katika kipindi hicho Katie hakuwa akikumbuka kitu chochote kile ambacho kilikuwa kimepita katika maisha yao. Ingawa



    alikuwa akiendelea kufanya kazi ya ubaharia lakini akili yake wala haikuacha kumfikiria Katie ambaye kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo alikuwa



    akiendelea kunawili.

    Kwa kipindi hiki, Daniel alikuwa mnyonge sana japokuwa alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha, maisha yake katika kipindi hiki hayakuwa nchini Marekani tena,



    alikuwa akiishi nchini Uingereza katika jiji la Newcastle ambako huko alikuwa amenunua nyumba kubwa na ya kifahari.

    Fedha ambazo alikuwa amezipata katika ubaharia wake ndizo ambazo akaamua kufungulia mghahawa ambao ulikuwa ukitumiwa sana na wachezaji wa mpira



    wa klabu ya Sunderland ambao walikuwa wakifika sana mahali hapo kwa ajili ya kupata kifungua kinywa na hata chakula cha jioni hasa mara baada ya kutoka



    mazoezini.

    Ingawa maisha ya Uingereza hakuyapenda sana kutokana na baridi lakini akaamua kuvumilia tu. Kwake alijiona kuwa mtafutaji ambaye alitakiwa kukaa sehemu



    yoyote ile katika dunia hii mpaka pale ambapo angebadilisha maisha yake na kuishi kama tajiri mmoja mkubwa nchini hapo na kurudi nchini Marekani na



    kununua nyumba na maisha ya kifahari kuanza rasmi.

    Maisha ya Daniel yalikuwa yamelenga mambo mengi sana, hakutaka kutumia fedha zake vibaya, alikuwa akiishi nchini Uingereza kama mgeni tu na hivyo kuna



    siku angehitaji kurudi nchini kwake. Kutokana na kuanza kuingiza fedha nyingi, wasichana mbalimbali wa hapo Newcastle walikuwa wakipenda kumfuatilia



    kwa lengo la kuwa nao lakini Daniel hakukubaliana nao, kazi yake ilikuwa ni kutembea nao kwa zamu na kuwaacha tu.

    Maishani mwake hakutaka kuwa na msichana yeyote yule zaidi ya Katie ambaye bado alikuwa akiigiza filamu za ngono kama kawaida yake. Miezi ikakatika na



    ndipo hapo Daniel aipojiona kuwa na utayari wa kurudi nchini Marekani kwa ajili ya kuendelea na maisha katika nchi hiyo huku tayari akiwa ameingiza zaidi ya



    kiasi cha paundi milioni tano.

    Kitu cha kwanza mara baada ya kufika nchini Marekani ni kuanza kufungua biashara nyingi ambazo zilionekana kumuingizia fedha na kisha kuanza kumtafuta



    Katie simuni. Msichana huyo hakuwa akipatikana kabisa jambo ambalo lilimfanya kuendelea kumtafuta zaidi na zaidi. Ingawa alikuwa akiiangalia mikanda ya



    filamu ya Katie ambayo alikuwa akiigiza akifanya mapenzi na wanaume mbalimbali lakini bado alikuwa akihitaji kuwa nae katika maisha yake.

    Baada ya kipindi kirefu kupita, Daniel akaja kupata taarifa ambayo ilionekana kumshtua sana, taarifa ambayo ilimfanya kuchanganyikiwa kupita kawaida. Katie



    alikuwa akitarajia kufunga ndoa, aliuhisi moyo wake ukichomwa na msumali wa moto na kisha tundu hilo kumwagiwa tindikali.

    Hakuziamini taarifa zile jambo ambalo likamfanya kutembelea katika website ya Katie na kuangalia. Kile ambacho alikuwa amekioa katika magazeti mbalimbali



    nchini Marekani kilikuwa sawa sawa na kile ambacho alikuwa amekikuta katika website ile.

    Daniel akajiona akikosa nguvu kabisa, akaanza kupiga hatua kuelekea katika kochi na kisha kutulia. Mawazo yakaanza kumuandama kichwani mwake. Katika



    maisha yake, hakuona kama kulikuwa na mtu ambaye alitakiwa kumuoa Katie na kuishi nae tofauti na yeye, jambo lile likaonekana kumtia hasira sana.

    Alichokifanya ni kuanza kupeleleza juu ya mwanaume ambaye alikuwa akitarajiwa kufunga ndoa na Katie. Alijitahidi kumtafuta zaidi na zaidi lakini hata picha



    yake akashindwa kuipata mpaka siku ya harusi ilipofika na watu hao kufunga ndoa.

    Daniel akaonekana kuchanganyikiwa zaidi, alijua fika kwamba ndoto zake za kutaka kuishi na Katie hapo baadae zilitakiwa kufutika kunzia muda huo. Kila siku



    alikuwa akishinda chumbani akilia huku picha za Katie ambazo alipiga nae kipindi cha nyuma walipokuwa mitaani utotoni zikiwa mikononi mwake.

    Mapenzi yake yalikuwa makubwa kwa Katie, alimpenda sana kuliko msichana yeyote katika dunia hii. Alimuona kuwa msichana ambaye alihitaji thamani kubwa



    sana katika maisha yake. Hakuwa radhi kuwa na msichana mwingi, msichana ambaye alikuwa akimpenda na kumhitaji alikuwa Katie tu.

    Alipokuja kuiona picha ya Gibson kwamba ndiye alikuwa mume halali wa Katie, Daniel akapigwa na mshangao. Kwanza akaanza kumwangalia vizuri Gibson



    huku akijaribu kujilinganisha nae, hakuwa akifanana na Gibson hata kidogo.

    Hapo hapo akaanza kumchukia Gibson, hakujali kama Katie ndiye ambaye alikuwa amemtongoza Gibson na hatimae kuoana, yeye alichokuwa akikijali kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo ni kuendelea chuki kwa Gibson tu huku ngozi ya Gibson kuwa nyeusi ndicho kilikuwa kitu ambacho kilimkasirisha zaidi na zaidi.

    Daniel hakuwa radhi kumuona Gibson akila raha pamoja na mwanamke ambaye alikuwa akimpenda tangu utotoni, hakuwa radhi kuona Gibson akila raha na



    msichana ambaye alikuwa amefanya nae mapenzi sana mitaani, hakuwa radhi kuona Gibson akila raha na msichana ambaye alikuwa akiishi nae kwa karibu zaidi



    ya mtu yeyote, kitu alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuyarudisha mapenzi ambayo yalikuwa yamepotea na kusahaulika tu.

    Hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kuyarudisha mapenzi ya Katie kwake zaidi ya kufanya kitu kimoja tu, cha kumuua Gibson. Aliamini kwamba kama



    asingefanya hivyo, basi kwake lingekuwa jambo gumu sana kuweza kumpata Katie ambaye alionekana kuwa kwenye mapenzi mazito na mwanaume huyo.

    Alichokifanya ni kuanza kuandaa mipango kabambe, mipango ambayo ingemmaliza Gibson na kisha kumsahaulisha katika kichwa cha Katie na baada ya hapo



    angeweza kumfuata Katie na kumwambia juu ya jinsi alivyokuwa akiendelea kujisikia ndani ya moyo wake, amkubalie, amuoe na hatimae kutimiza ndoto yake



    ambayo alikuwa akiiota kila siku.

    Alichokifanya ni kuwakodisha vijana ambao walitakiwa kuucheza mchezo ule kwa makini sana bila kukosea sehemu yoyote ile. Vijana wakakubaliana nae kwa



    malipo makubwa ambayo wala hayakuonekana kuwa tatizo kwa Daniel ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na fedha za kutosha.

    Sehemu ambayo ilitakiwa Gibson auawe ilikuwa ni Texas, jiji ambalo kwa kiasi fulani lilionekana kuwa kama jangwa. Kila kitu kikapangwa, vijana wakaomba



    siku mbili za kujiandaa na hatimae baada ya hapo kukamilisha kila kitu.

    “Kwa hiyo baada ya kumteka tumuue au tukusubirie wewe umuue?” Kijana mmoja alimuuliza Daniel.

    “Nataka kumuua mimi mwenyewe. Tena kwa mkono wangu” Daniel aliwaambia.

    “Sawa sawa. Usijali. Tutakamilisha kila kitu” Kijana yule alimwambia Daniel na kisha kuondoka.

    *****

    Maisha ya mapenzi bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa wapendanao, Gibson na Katie. Walikuwa na ukaribu mkubwa sana huku kila siku wakiwa



    wanatawala vyombo vya habari nchini Marekani. Bila kupenda, Gibson akaanza kuwa maarufu nchini Marekani jambo ambalo lilimpelekea kuanza kujulikana



    kila sehemu hasa katika nchi nyingine.

    Bado malengo yake yalikuwa ni yale yale, kwa msichana Katie, kitu ambacho alikuwa akikihitaji ni kupata fedha tu. Alikuwa amekwishagundua kwamba Katie



    alikuwa na fedha nyingi, hivyo alijitahidi kuonyesha kila kitu hasa mapenzi ya dhati ili mwisho wa siku apate kile ambacho alikuwa amekipanga kukipata.

    Katie akaonekana kuanza kubadilika, akajifanya kuacha kuigiza filamu za ngono jambo ambalo likaonekana kuwakasirisha watu wengi nchini Marekani ambao



    walikuwa na kiu ya kutaka kumuona akiigiza filamu zile.

    “Sasa tufanye nini?” Bwana Donald, mkurugenzi wake alimuuliza.

    “Nitakuwa nikiigiza kama kawaida” Katie alijibu.

    “Sasa akiziona itakuwaje?”

    “Usihofu. Nitakuwa namwambia kwamba hizo zilikuwa filamu za zamani ambazo zilikuwa zimekwishatengenezwa hata kabla ya kukutana nae” Katie alijibu



    huku akitabasamu.

    “Utaweza kweli kumshawishi hadi akubaliane nawe?”

    “Ndio. Mwanamke atabakia kuwa mwanamke, hatosema kitu chochote kwa mwanamke, atakubaliana nami tu” Katie alijibu.

    Alichokifanya baada yakufika nyumbani ni kumsubiri Gibson atoke kazini na ndipo hapo alipomwambia kila kitu kilichokuwa kinaendelea. Japokuwa Gibson



    alijifanya kuumia lakini akakubaliana nae jambo ambalo lilimfanya Katie kumpa mapenzi moto moto.

    “Au tufanye kitu kimoja ili kukupa uhuru” Gibson alimwambia Katie.

    “Kitu gani?”

    “Wewe igiza tu filamu zako. Ila nataka kukuwekea sharti moja tu” Gibson alimwambia Katie.

    “Sharti gani?”

    “Hakikisha cd hizo hazionekani machoni mwangu. Yaani kama ukitaka kuziangalia ziangalie kwa siri. Umenielewa mke wangu?” Gibson alimuuliza Katie.

    “Nimekuelewa mpenzi na ninashukuru kwa ruhusa yako. Nakuhakikishaia kila kitu kitakuwa kama ulivyoniambia” Katie alimwambia Gibson ambaye akili yake



    ilikuwa ikifikiria fedha tu na huku akiwa ameshaanza kutuma fedha kisiri katika akaunti yake iliyokuwa nchini Tanzania.

    ******

    Vijana watatu wakajipanga vilivyo huku lengo lao katika kipindi hicho likiwa ni kukamilisha kazi ambayo walikuwa wamepewa na Daniel ya kumteka Gibson na



    kisha kumpeleka sehemu ya siri ambako huko wangempigia simu bosi wao na kisha kumueleza kila kilichoendelea.

    Wakaandaa bunduki zao, walikuwa wamejiandaa na utekaji nyara ambao mara kwa mara ulikuwa ukifanyika sana nchini Marekani hasa kwa watoto wa watu



    wenye fedha na watekaji hao kudai kiasi kikubwa cha fedha.

    Walichokuwa wameelekezwa ni mahali ambapo kulikuwa na uwezekano wa Gibson kupatikana na kisha kumpeleka sehemu yoyote ile ambayo kusingekuwa



    rahisi kwa Katie kuweza kuwasiliana nae mpaka pale atakapouawa na mkono wa Daniel.

    Mipango ilikuwa imekamilika kabisa, saa 4:18 asubuhi, gari aina ya Mc Lloyd lilikuwa limesimama mbali kidogo na nyumba kubwa aliyokuwa akiishi Katie na



    Gibson katika mghahawa mmojawapo wa Mc Donald. Vijana wale waliendelea kusubiri zaidi na zaidi huku kengo lao likiwa ni kutaka kumuona Gibson akitoka



    ndani ya nyumba ile kwa ajili ya kufanya kile ambacho walikuwa wametumwa.

    Saa 6:24, gari ndogo aina ya Ferrari yenye viti viwili ikaanza kutoka ndani ya nyumba ile. Vijana wale wakatoka katika mghahwa ule na moja kwa moja kulifuata



    gari lao na kuingia ndani. Wakaanza kulifuatilia gari lile kwa mwendo wa taratibu uliojaa angalizo kubwa.

    Bunduki zao zilikuwa tayari, walikuwa wamejiandaa kwa kitu chochote kile ambacho kingetokea mahali hapo, kitu ambacho kingewafanya kutofanikisha



    mpango ambao walikuwa wameupanga kuufanya kwa wakati huo.

    Waliendelea kulifuata gari lile la kifahari mpaka lilipoingia katika duka moja kubwa la nguo ambalo lilikuwa likitumika sana na masupastaa au na watu ambao



    walikuwa na fedha nyingi na za kutosha. Vijana wale hawakutaka kuingia, wakasubiri nje huku wakiwa garini mwao.

    Muda ulikuwa ukizidi kwenda zaidi na zaidi lakini hakukuwa Gibson na Katie hawakuweza kutoka ndani ya duka lile, waliendelea kusubiri zaidi na zaidi na



    baada ya dakika arobaini na tano, wakawa wanatoka huku mikononi mwao wakiwa na mifuko miwili mikubwa ambayo waliipeleka ndani ya gari lao na kisha



    kuingia na kuanza kuondoka mahali hapo.

    Vijana wale hawakutaka kusubiri mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuwafuatilia kwa mara nyingine tena. Waliendelea kuwafuatilia zaidi na zaidi mpaka



    kufika katika barabara ya mtaa wa Vikingstone ambako hakukuwa na magari mengi kabisa na kisha kulipita gari lile na kulisimamisha gari lao mbele na



    kuteremka kwa kasi ya kikomandoo.

    Katie ambaye alikuwa katika usukani alibaki akiwa amepigwa na mshangao mkubwa ulioambatana na mshtuko, hakuonekana kufahamu ni kitu gani ambacho



    kilikuwa kinaendelea mahali hapo, hata kabla hajajua afanye kitu gani, vijana wale wakawa wamekwishalifikia gari lile na kuvivunja vioo vya dirishani kwa



    kutumia vitako vya bunduki zao.

    Hawakutaka kuuliza kitu chochote kile, kutokana na kutokuwa na uwepo wa watu katika barabara ya mtaa ule wa kifahari iliwafanya kuwa na uhuru mkubwa



    wa kuwafanya chochote walichotaka kufanya. Mara ya kwanza Gibson alitaka kuonyesha ubabe lakini alipoziona bunduki mbele ya macho yake, akatulia.

    Wakateremshwa garini mule na kisha kupelekwa katika gari lile walilokuja nao vijana wale na kisha safari ya kuelekea katika sehemu ambayo walitakiwa



    kuwapeleka kuanza kwa wakati huo. Muda wote Gibson na Katie walikuwa wakitetemeka kwa hofu, watu ambao walikuwa nao ndani ya gari lile walionekana



    kuwa watu wenye roho mbaya ambao muda wote walikuwa wakinuka damu.

    Gari likachukua barabara ya Melville 46 na kisha kuanza kuelekea katika mji wa Baldwin huku lengo lao kubwa katika kipindi hicho ni kwenda kwenye jiji la



    Texas ambalo lilikuwa katika upande wa mashariki wa jiji hilo la New York karibu kabisa na mji wa Greenvale.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwendo wa gari lao haukuwa wa kasi sana, walikuwa wakizihofia kamera za barabarani ambazo zingewafanya kuwafuatilia zaidi endapo mwendo wao



    ungeonekana kuwa wa kasi zaidi tofauti na magari mengine. Waliendelea na safari ile kwa muda wa dakika kumi na ndipo hapo walipochukua barabara ya magari



    yaendayo kasi ya Hoy Hills huku wakiwa na dakika thelathini kabla ya kufika katika jiji la Texas.

    Muda wote huo, hakukuwa na mtu ambaye aliufungua mdomo wake, wote walikuwa kimya kabisa ndani ya gari lile. Katie alitamani kuuliza juu ya kitu



    ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo lakini hakupewa jibu lolote lile zaidi ya wote kupewa onyo la kutokuongea kitu chochote kile.

    Huku gari likiendelea kwa mwendo wa kasi ya zaidi ya kilometa themanini kwa saa, simu ya kijana mmoja katika ya vijana wale watatu ikaanza kuita

    “Mko wapi?” Sauti ya Daniel iliskika.

    “Tupo katika barabara ya Hoy Hills” Kijana yule alijibu.

    “Mko nae hapo?”

    “Ndio. Tupo nao wote”

    “Ina maana hadi Katie?” Dany aliuliza huku sauti yake ikisikika kujaa mshangao.

    “Ndio bosi’

    “Hapana. Huyo msichana simuhitaji kabisa. Mshusheni arudi zake. Ila mshusheni katika sehemu ambayo hamtoonekana kirahisi” Daniel alisema.

    Kila kitu ambacho Daniel alikuwa ameamuru kwa wakati huo ndicho ambacho kilitakiwa kufanyika kwa haraka sana, tena bila ya kuulizwa swali lolote lile.



    Gari lilipofika katika kituo cha mafuta, Katie akateremshwa na kisha kuanza kupelekwa bafuni ambako kijana mmoja alikuwa pembeni yake akiigiza kuwa kama



    mpenzi wake ili kuwaondoa wasiwasi watu wachache ambao walikuwa wakipishana nao.

    Walipofika chooni, Katie akafungwa kamba katika bomba la maji na kisha kijana yule kurudi garini na kuendelea na safari yao huku Gibson akizidi kutetemeka



    kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda mbele.

    Baada ya dakika zaidi ya arobaini wakaingia katika jiji la Texas ambalo lilikuwa likionekana kuwa kama jangwa. Jiji hili ndilo ambalo lilikuwa limepakana kwa



    ukaribu sana na nchi ya Mexico na watu wengi ambao walikuwa wakiishi katika jiji hilo walikuwa wakitoka katika nchi hiyo huku muda mwingi wakiwa



    wanavaa makofia makubwa ya Malboro huku wakijulikana sana kwa jina la Cow Boys.

    Hali ya hewa haikuwa ya baridi sana kama ilivyokuwa jijini New York, kutokana na sehemu kubwa kuwa jangwa, hali ya joto ndio ambao ilikuwa ikitawala sana



    hasa katika nyakati hizo za mchana. Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na jumba kubwa bovu bovu na kisha kumuingiza humo.

    Gibson akatulia ndani ya jumba lile ambalo lilionekana kuwa na hadhi ya kujengwa katika sehemu kama ile ya jangwa huku vijana wale wakiwa nje



    wakimsubiria Daniel ambaye alikuwa amewataarifu kwamba ni lazima angefika mahali hapo haraka iwezekanavyo.

    Ndani ya dakika hamsini, gari la kifahari aina ya Penina 11 likaanza kuingia ndani ya eneo hilo na kisha Daniel kuteremka huku akiwa amevalia suti nyeupe na



    macho yake yakiwa yamefunikwa na miwani ya mwanga. Akawasalimia vijana wale huku uso wake ukionyesha kuwa na furaha na kisha kukabidhiwa bunduki na



    kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jumba lile.

    Uamuzi ambao alikuwa ameuweka Daniel kwa kipindi hicho ulikuwa ni uamuzi mmoja tu ambao wala haukuhitaji hata ushauri kutoka kwa mtu yeyote yule,



    hakutaka maelezo yoyote yale, kadri alivyokuwa akipiga hatua kuufuata mlango wa jumba lile na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyokuwa zikizidi kumpanda.



    Kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Katie, alimuona Gibson kuwa kiziuzi kikubwa kwa yeye kuwa na msichana yule ambaye alikuwa akimpenda kuliko



    mwanamke yeyote yule.

    “Hakuna maelezo, hakuna maswali na wala hakuna mahojiano, hapa ni kuua tu” Daniel alisema huku akiwa amekwishaingia ndani ya jumba lile huku mkono



    ulioshika bunduki ile ukimtetemeka kwa hasira kali. Mtu ambaye alikuwa akimwangalia katika kipindi hicho, alikuwa Gibson ambaye alikuwa akitetemeka



    kupita kawaida.

    “Ninakuua” Daniel alijisemea huku akimnyooshea Gibson bunduki ile.

    “Paaaaa...paaaaaa...paaaaa...” Risasi zilisikika zikitoka katika bunduki aliyoishika Daniel huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.





    Katie alikuwa chooni huku akiwa amefungwa kamba mikononi mwake na kisha ile kamba kufungwa katika bomba. Muda mwingi alikuwa akipiga kelele za



    kuomba msaada lakini wala hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifika mahali hapo na kumsaidia.

    Katie hakutaka kukata tamaa, aliendelea kupiga kele zaidi na zaidi. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikimfikiria mume wake ambaye alikuwa ametekwa



    na kupelekwa asipopafahamu. Alitamani kuifungua kamba ile na kisha kuichukua simu ambayo ilikuwa mfukoni mwake lakini kitu kile kilionekana kuwa



    kigumu kufanyika.

    Tayari mambo yakaonekana kuwa magumu kwa upande wake, kamwe asingeweza kuendelea kupiga kelele kama asingeonyesha jitihada za kutaka kujisaidia yeye



    mwenyewe. Alichokifanya mahali hapo ni kuanza kuzifungua kamba zile kwa kutumia meno yake.

    Japokuwa mara ya kwanza kazi ilionekana kuwa rahisi sana lakini baadae ikaonekana kuwa ngumu tofauti na hisia zake. Alijitahidi kufungua zaidi na zaidi,



    alichukua zaidi ya dakika thelathini na ndipo ambapo kamba zile zikafunguka.

    Akaanza kuugonga mlango wa choo kile, aligonga zaidi mpaka pale ambapo muuzaji wa mafuta alipokuja na kisha kuufungua mlango wa choo kile. Nywele za



    Katie zilikuwa zimevurugika sana, zilikuwa timtim kama chizi. Akaanza kuelezea kile kilichokuwa kimetokea na kisha kupiga simu polisi.

    Kila mwananchi ambaye aligundua kwamba mwanamke yule aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Katie, wengi wakatamani kutaka kupiga nae picha,



    uadimu wa kukutana na masupastaa waliokuwa wakiishi nchini mwao ndio ilikuwa sababu mojawapo iliyomfanya kila mmoja kutaka kupiga picha na Katie



    japokuwa alikuwa katika hali mbaya.

    Ndani ya dakika tano, polisi wakaingia mahali hapo na kisha kuanza kuchukua maelezo ya awali ya Katie na kisha kumpakiza garini na kuondoka nae. Garini,



    Katie hakuwa na amani, alikuwa akimfikiria mume wake ambaye alikuwa ametekwa na watu ambao wala hakuwa akiwafahamu.

    Maswali mfululizo yalikuwa yakijikusanya kichwani mwake juu ya watekaji wale ambao walikuwa wamemteka mume wake mpendwa. Hakujua kama mpaka



    katika kipindi hicho Gibson alikuwa mzima au alikuwa ameuawa. Amani haikupatikana moyoni mwake, muda wote alikuwa akitokwa na machozi tu.

    Alipofikishwa katika kituo kikuu cha polisi cha New York, akaanza kutoa maelezo kwa kirefu zaidi. Katika kila kitu ambacho alikuwa akikieleza mahali hapo,



    polisi mmoja alikuwa akiandika katika faili lake ambalo lilikuwa mezani. Kila kitu kilipokamilika, akaruhusiwa kuelekea nyumbani huku mapolisi wakianza



    kazi yao.

    Katie akarudi mpaka nyumbani, moyo wake ulikuwa katika maumivu makali kupita kawaida. Hisia kwamba Gibson alikuwa ameuawa zikaanza kumjia kichwani



    kitu ambacho kikamfanya kuwa na wasiwasi kupita kawaida. Muda mwingi alikuwa akilia tu, miezi sita ambayo alikuwa amekaa na mume wake ulionekana



    kuwa muda mfupi sana, alikuwa akihitaji kuwa nae zaidi na zaidi mpaka pale ambapo mkataba wa ndoa yao ungeisha na kufikiria ni kitu gani ambacho



    kingeendelea maishani mwao.

    Katie hakutaka kubaki kimya, akaanza kuwataarifu marafiki zake na ndugu zake na kisha kuwaelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea jambo ambalo



    liliwafanya wafike nyumbani hapo kwa ajili ya kumfariji. Hakujua ni nani ambaye aliwapata taarifa waandishi wa habari, lakini ndani ya nusu saa tayari



    walikuwa wamekwishafika nyumbani hapo na kisha kuanza mahojiano nae.

    Katie hakutaka kuficha, akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea bila kuficha kitu hata kimoja. Kila mmoja akaonekana kushangaa, utekaji wa



    mtu mkubwa haukuwa umefanyika kwa kipindi kirefu sana nchini Marekani, utekaji ambao ulikuwa ukifanywa mara nyingi ulikuwa ni wa watoto tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lengo la watekaji wala halikueleweka kabisa, waandishi wa habari, polisi pamoja na watu wengine ambao walikuwa wamesikia kila kiichotokea wakaonekana



    kushangaa kupita kawaida. Tayari kukaonekana kuna namna, tena kitu ambacho walikuwa wamekifikiria zaidi ni kwamba watekaji hao walikuwa wamekwenda



    kumuua Gibson.

    ‘Hata kama watamuua....nitataka kuuona mwili wake” Katie alisema huku akilia kama mtoto na ndugu, marafiki zake wakimfariji.

    ******

    Milio mitatu ya risasi ilikuwa imesikika mahali hapo, uso wa Daniel ulikuwa ukionyesha tabasamu pana kama njia mojawapo ya kuonyesha kwamba tayari



    alikuwa amekamilisha kile ambacho alikuwa ametaka kifanyike mahali hapo.

    Gibson alibaki kimya huku akitetemeka, hakuamini kama risasi zile tatu ambazo zilikuwa zimepigwa, zilikuwa zimepita pembeni yake. Haja ndogo tayari



    ilikuwa imekwishamtoka, alikuwa akitetemeka kwa hofu kubwa. Japokuwa alikuwa na miaka zaidi ya ishirini lakini hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza



    kuusikia mlio wa risasi.

    Gibson akaanza kujipapasa kuona kama kweli hakukuwa na risasi ambayo ilikuwa imepenya mwilini mwake, mwili wake ulikuwa vile vile, wala haukuwa



    umejeruhiwa kwa risasi yoyote ile jambo ambalo lilimfanya kumwangalia Daniel ambaye uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana.

    “Kama nikitaka kukuua, naweza kukuua sasa hivi, tena ndani ya sekunde moja tu. Ila ukiona risasi imepita pembeni yako, basi jua sitaki kukuua” Daniel



    alimwambia Gibson ambaye alikuwa kimya huku akizidi kutetemeka.

    Daniel hakutaka kuendelea kumnyooshea bunduki Gibson kitu ambacho kilimfanya kuiweka kiunoni mwake na kisha kuanza kumsogelea. Tayari Daniel



    alikwishaona kwamba kama angeendelea kuishika bunduki ile basi kusingekuwa na maelewano yoyote yale ambayo yangeweza kufanyika mahali hapo, aliona



    kuwa na uhitaji wote wa kuweza kuificha bunduki ile kutoka mbele ya Gibson ili waweze kuongea vizuri na kufikia muafaka.

    “Nimekuacha kwa sababu moja kubwa” Daniel alimwambia Gibson ambaye bado alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi na kuendelea.

    “Kitu kikubwa ambacho ninakitaka kutoka kwako, achana na Katie. Yule ni msichana wangu ninayempenda sana kutoka moyoni. Ninapoongea sasa hivi, nataka



    uachane nae” Daniel alimwambia Gibson.

    “Itakuwa ngumu sana” Gibson alimwambia Daniel.

    “Kwa nini?”

    “Mkataba wa ndoa yetu haujakwisha kabisa. Ndio kwanza miezi sita imekatika” Gibson alimwamba Daniel.

    “Hata kama. Ninachotaka uachane nae tu. Nitakupa ofa kama utaweza kufanya hivyo ndani ya wiki moja” Daniel alimwambia Gibson.

    “Ofa gani?”

    Hilo ndilo swali ambalo Daniel alikuwa akitaka kulisikia kutoka kwa Gibson. Alijua fika kwamba Gibson alikuwa akimpenda sana Katie ila aliona kuwa kama



    alitaka watu hao watengane basi ilikuwa ni lazima afanye kitu kimoja kikubwa, atumie fedha tu.

    Kumfuata Katie na kumrubuni kwa fedha ili aachane na Gibson lilikuwa jambo gumu sana na hii ilikuwa kwa sababu msichana huyo alikuwa na kiasi kikubwa



    cha fedha. Gibson, kwake ndiye ambaye alionekana kuwa mtu mzuri ambaye angeweza kuyazima mapenzi aliyokuwa nayo kwa Katie kama tu angeweza



    kumuahidi kiasi fulani cha fedha.

    “Nina dola milioni kumi. Nataka uachane na Katie tu” Daniel alimwambia Gibson.

    Gibson akajiona kama kutokusikia vizuri kile ambacho alikuwa ameambiwa, alimwangalia Daniel mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kile ambacho



    alikuwa ameambiwa mahali pale. Akaileta kalkuleta ya kichwani mwake, akazibadilisha fedha zile katika thamani ya fedha za kitanzania, zilikuwa zaidi ya bilioni



    ishirini, yaani angepata zaidi ya shilingi bilioni ishirini tu endapo angefanikisha kuachana na Katie.

    Ofa ile ikaonekana kuwa nzuri kwake, hakuamini kama mwisho wa siku angeweza kupata kiasi kikubwa namna ile kwa kufanya kitu kidogo tu, cha kuachana na



    Katie. Tamaa ya fedha ambazyo alikuwa nayo ikazidi kuota mizizi moyoni mwake, alikuwa radhi kumfanyia Katie kitu chochote isipokuwa kumuua endapo tu



    angeahidiwa kiasi cha fedha kama kile ambacho alikuwa ameahidiwa.

    Hakutaka kujiona chizi, hakutaka kujiona kutokuwa na bahati, ofa ile ilikuwa ni vigumu sana kukatalika moyoni mwake, na si kwa yeye tu bali hata kwa



    Watanzania wote ambao walikuwa wakikaa nchini Tanzania. Kumuacha Katie kwake wala hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile.

    “Ofa imekubalika” Gibson alimwambia Daniel maneno ambayo yalimfanya Daniel kutabasamu zaidi.

    “Ila inakubidi kuwa makini” Daniel alimwambia Gibson.

    “Umakini gani?”

    “Nitazituma fedha katika akaunti yako, nataka ndani ya wiki, kila kitu kiwe kimefanikiwa, usipofanikisha ndani ya wiki. Nitakuua. Umesikia?” Daniel



    alimwambia Gibson.

    “Ndio”

    “Ok! Kumbuka ni ndani ya wiki tu” Daniel alisisitiza.

    “Sawa”

    Daniel akaonekana kuwa mwenye furaha zaidi, alionekana kufurahia sana kwa kuwa Gibson wala hakuonekana kuwa mgumu kuikubali ofa ile. Alichokifanya



    mahali hapo ni kutoa karatasi na kumkabidhi Gibson na kisha kuandika akaunti yake ya benki ambayo angependa fedha hizo ziingizwe.

    “Mbona namba hii ngeni machoni mwangu?” Daniel aliuliza mara baada ya kuiona namba ambayo Gibson alikuwa ameiandika.

    “Hiyo ni namba ya akaunti yangu ya nchini Tanzania. Nataka nikiachana nae tu nirudi nchini Tanzania. Au wazo baya hilo?” Gibson aliuliza.

    “Wazo zuri. Tena zuri sana” Daniel alimwambia Gibson na kisha kumruhusu kuondoka mahali hapo kuelekea garini tayari kwa kurudi jijini New York pamoja



    nao.

    Muda wote Gibson alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kila siku maisha yake alikuwa akiyaona kuwa na bahati kubwa. Alikumbuka kwamba



    alikuwa amesoma katika shule za kawaida sana na wala hakufikiria kama angekua tajiri, lakini kwa sababu ya mapenzi tu, yakamfanya kuwa tajiri nchini



    Tanzania.

    Huku akiendelea kuumiliki utajiri mkubwa, kiasi kikubwa cha fedha ambazo angeweza kukiingiza kwa miaka mitatu, alikuwa akikiingiza ndani ya masaa



    machache tu, yaani pale ambapo angemwambia Katie kwamba ule ndio ulikuwa mwisho wa mahusiano yao, kwa maana hiyo wangeachana na kurudi nchini



    Tanzania.

    Walipita katika njia nyingine kabisa mpaka kutokea jijini New York ambako wakamuacha. Gibson akaanza kutembea kuelekea katika stesheni ya treni na kisha



    kupanda treni na kuelekea nyumbani kwake, pembeni mwa jiji hilo la New York. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kufika



    nyumbani na kumwambia Katie kwamba asingeweza kuendelea nae tena na hivyo mkataba wa ndoa yao uvunjwe haraka iwezekanavyo.

    “Mmmh! Nitaanzia wapi sasa hadi kumwambia tuvunje ndoa?” Gibson alijiuliza.

    “Ila poa. Nitajua nimwambie nini” Alijijibu mwenyewe.

    *****

    Gibson akaingia ndani, waandishi wa habari ambao walikuwa ndani ya eneo la nyumba hiyo kwa ajili ya kumhoji Katie wakaanza kumsogelea huku wakiviweka



    mbele vyombo vyao vya kuekodia sauti. Kila mwandishi akaonekana kumshangaa Gibson, wakati huo habari ilikuwa ikiripotiwa kwamba alikuwa ametekwa, je



    kwa nini alikuwa mahali hapo muda huo? Je aliwatoroka watekaji au walimuacha? Na kama walimuacha bila kumjeruhi, lengo lao la kumteka lilikuwa nini?

    Kila mwandishi ambaye alikuwa akijiuliza maswali hayo hakupata jibu, mtu pekee ambaye angewapa majibu ya kutosha na kuridhisha alikuwa mmoja tu,



    Gibson. Gibson hakutaka kuongea kitu chochote kile, alichokifanya ni kuendelea kupiga hatua mpaka ndani ya nyumba yake.

    Katie, ndugu zake na marafiki zake wa karibu wakashtuka, hawakuamini kama Gibson alikuwa akiingia ndani ya nyumba ile kwa wakati ule na wakati alikuwa



    ametekwa masaa kadhaa yaliyopita. Katie akashindwa kuvumilia, akainuka, akaanza kupiga hatua kumfuata Gibson, alipomfikia, akamkumbatia kwa furaha.

    Katie akashindwa kuyazuia machozi yake ya furaha, yakaanza kumtoka huku akiwa bado amemkumbatia Gibson. Gibson akaanza kumbembeleza Katie kwamba

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwa wakati huo hakutakiwa kuhofia kitu chochote kile kwa sababu alikuwa amerudi akiwa mzima wa afya kama alivyokuwa ametekwa.

    Katie akamjitoa mwilini mwa Gibson na kisha kuanza kumwangalia kwa mtindo wa kumchunguza. Alikuwa akimwangalia kwa makini kama alikuwa



    amejeruhiwa au la. Mwili wake ulikuwa vile vile, hakukuwa na jeraha lolote lile.

    “What happened to you? (Nini kilikutokea?)” Katie alimuuliza Gibson.

    “I ascaped (Nilitoroka)” Gibson alijibu.

    “Thank you Jesus! I was just worring about you. Where did they take you to? (Asante Yesu! Nilikuwa nikihofia kuhusu wewe. Walikupeleka wapi?)” Katie



    alimuuliza Gibson.

    “They planned to take me to Texas but when we arrived Shealbon, five kilometre to Texas, I ascaped? (Walipanga kunipeleka Texas lakini tulipofika Shealbon,



    kilometa tano kabla ya kuingia Texas, niliwatoroka)” Gibson alijibu.

    “How did you escape? (Ulitoroka vipi?)”

    “I fought them (Nilipigana nao)

    “Sure? (Kweli)

    “Yeah” Gibson alijibu.

    Waliendelea kuongea zaidi na zaidi huku Katie akishindwa kabisa kuificha furaha yake ambayo alikuwa nayo, muda wote alikuwa pembeni ya mume wake



    akimkumbatia tu, alishindwa kumuachia, aliona kama angekaa mbali nae kidogo basi angeweza kuondoka mikononi mwake kitu ambacho hakuwa akikitaka



    kitokee.

    Kichwa cha Gibson kilikuwa kikiwaza kitu kingine kabisa, hakuyafikiria mapenzi hata kidogo, kitu ambacho alikuwa akikifikiria sana kwa wakati huo ni fedha



    ambazo alikuwa ameahidiwa na Daniel kama angefanikiwa kuvunja ndoa yake na mkewe, Katie.

    Mpaka kufika kipindi hicho wala hakujua angeanzia wapi, alimuona Katie akiwa na mapenzi ya kweli sana kwake jambo ambalo ilikuwa ni vigumu sana



    kuufanya uamuzi ule ambao alikuwa ameambiwa kuufanya ndani ya wiki moja. Mapenzi ya Katie ndio ambayo yalikuwa yakimuweka katika hali ngumu ya



    kuufanya uamuzi ule.

    Dhahiri alionekana kuwa katika wakati mgumu kuufanya uamuzi ule lakini kiasi cha fedha ambacho alikuwa ameahidiwa kilikuwa ni kiasi kikubwa sana



    ambacho angeonekana kuwa mjinga sana kama asingekifanya kile ambacho alikuwa ameambiwa kukifanya.

    Usiku, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Daniel na kufikiria kile ambacho alikuwa ameambiwa kukifanya. Japokuwa mke wake, Katie kwa wakati huo



    alikuwa kwenye wakati mgumu wa kumtaka mume wake wafanye mapenzi lakini kwa Gibson wala mawazo yake hayakuwa yametulia kabisa, hakujisikia kabisa



    kufanya kitu hicho.

    Katie hakutaka kutulia, alikuwa akimpapasapapasa mumewe mpaka pale hamu ya kufanya tendo lile ilipomshika na kuanza kufanya. Kwa kipindi kile, tendo lile



    wala halikuwa na utamu wowote kwa upande wa Gibson, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Daniel tu, hasa kitita ambacho alikuwa ameahidiwa kukipata pale



    atakapokamilisha kuvunja mkataba wa ndoa na Katie.

    Siku ya kwanza ikakatika, bado Gibson alikuwa kwenye wakati mgumu sana kukamilisha mpango ambao alikuwa ameambiwa na Daniel kuukamilisha. Muda



    mwingi alikuwa akionekana kuwa mpole, furaha ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma ilikuwa imepotea kabisa.

    Katie akaonekana kuwa na wasiwasi, kamwe hakutaka kumuona mume wake akiwa katika hali ya unyonge jambo ambalo alikuwa akimuuliza sana lakini Gibson



    alikuwa akimficha kwa kumwambia sababu nyingine ambazo wala hazikuwa na maana yoyote ile.

    Siku ya pili ilikuwa imekwishakatika na ya tatu kuingia. Bado Gibson alikuwa akiendelea kujiuliza ni sababu gani ambazo angezisema ili kuuvunja mkataba wa



    ndoa ambao walikuwa wamewekeana katika kipindi walichooana. Kwa Gibson, mambo yalionekana kuwa magumu sana, kila alivyokuwa akimwangalia Katie



    na kuona jinsi alivyokuwa akimpenda, alijiona kufanya kosa kubwa sana kama angeamua kufanya hivyo.

    Siku ya nne ikaingia, ya tano na hatimae wiki nzima kukatika. Bado Gibson alikuwa kwenye wakati mgumu, wasiwasi wa kuuawa tayari ukaanza kumuingia



    kama ahadi iliyotolewa na Daniel endapo asingeweza kukamilisha kile ambacho alikuwa amemwambia. Siku moja baada ya wiki ilipoingia, akashtukia akipigiwa



    simu na namba ngeni, alipoipokea, alikuwa Daniel.

    “Umefikia wapi?” Sauti ya Daniel ilisikika ikiuliza.

    “Bado sijaanza kazi. Nahofia utanigeuka” Gibson alimwambia.

    “Kukugeuka! Kivipi?”

    “Kama nikikamilisha kufanya ulichoniambia, halafu fedha haujaniingizia, hauoni tatizo hilo?” Gibson alimuuliza.

    “Ok! Nakuingizia nusu ya fedha. Utakapokamilisha, nakumalizia” Daniel alimwambia Gibson.

    “Hapo utakuwa haupo sawa. Ziingize zote kabisa”

    “Sasa nitaingizaje fedha zote na wakati kitu ninachokitaka hakijafanyika?”

    “Sasa na mimi nitauvunjaje mkataba wa ndoa na wakati fedha zangu hazijamaliziwa?”

    “Ok! Kwa hiyo nikiingiza zote utakamilisha kila kitu?”

    “Ndio”

    “Sawa. Nakwenda kukuingizia leo hii hii. Na ninataka kazi ifanyike ndani ya masaa ishirini na nne. Umenielewa?” Daniel aliuliza huku sauti yake ikiwa



    imebadilika na kuwa ya hasira zaidi.

    “Nimekuelewa”

    Ndani ya masaa mawili, meseji ikaingia ndani ya simu ya Gibson kumtaarifu kwamba kiasi cha dola milioni kumi kilikuwa kimeingizwa ndani ya akaunti yake.



    Gibson hakuamini kama kweli fedha zile zilikuwa zimekwishaingizwa kwenye akaunti yake. Kazi ilikuwa imebakia moja tu kwa wakati huo, kuuvunja mkataba



    wa ndoa yake na Katie.

    Siku hiyo ofisini hakukukalika hata kidogo, muda wote alikuwa akifikiria ni kwa namna gani angeweza kufanya kile ambacho alikuwa amekipanga kukifanya.



    Akaanza kupekua katika kabati la mafaili yake na kisha kutoa karatasi kadhaa ambazo zilikuwa zikionyesha ni kiasi gani cha fedha alikuwa amekituma nchini



    Tanzania.

    Tayari yeye binafsi alikuwa amekwishatumia zaidi ya dola elfu sabini nchini Tanzania ambazo zilikuwa sawa na shilingi milioni mia na hamsini. Tayari kwa



    wakati huo alijiona kuwa na fedha za kutosha na hii ilionekana kutosha kabisa kurudi nchini Tanzania.

    “Nitaanzisha timbwili nyumbani” Gibson alisema.

    “Yaani leo hakulaliki mpaka mkataba uvunjwe” Gibson alijisemea na kuanza safari ya kuelekea nyumbani.

    Siku hiyo alionekana kupania kile ambacho alikuwa amekipanga kukifanya, hakutaka kuendelea kuishi na Katie tena kwa kuwa alikuwa amekwishaingiziwa kiasi



    kikubwa cha fedha katika akaunti yake. Hakujua ni aina gani ya maumivu ambayo angeyapata Katie, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo kilikuwa



    fedha tu.

    Alipofika nyumbani, akaegesha gari na kuteremka huku akianza kuelekea ndani. Alichokifanya hapo ni kujifanya kuwa na wasiwasi mkubwa mno kitu ambacho



    kilionekana kuwashangaza hata wafanyakazi wa ndani. Gibson siku hiyo alionekana kutokujiamini kabisa, alikuwa akionekana kuwa na mashaka makubwa sana



    usoni mwake.

    Hata Katie aliporudi nyumbani hapo, bado Gibson alikuwa akiigiza kuwa katika hali ile ile, hali ya kuwa na mashaka makubwa. Katie alipomuuliza sababu,



    hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kuonekana katika hali ile ile ambayo ilikuwa ikimtia wasiwasi Katie.

    “Kuna nini mpenzi?” Katie aliuliza kwa sauti ya unyonge.

    “Nimepokea simu ya kifo” Gibson alijibu.

    “Simu gani tena?”

    “Ya kifo. Nimeambiwa nijiandae kufa. Muda wowote ninauawa kuanzia sasa hivi. Aina ya kifo changu kitakuwa ni kama cha John F. Kennedy, kufyatuliwa risasi



    kadhaa za kichwa” Gibson alisema huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Hapana mpenzi, hautakiwi kuwa na wasiwasi kabisa. Ngoja niwapigie simu polisi” Katie alimwambia Gibson.

    “Hapana mke wangu. Ni lazima niondoke hapa”

    “Uondoke? Uelekee wapi tena?”

    “Nyumbani, Tanzania”

    “Kufanya nini?”

    “Nafikiri nitakuwa salama kutoka katika mikono ya watu hawa wanaonitafuta” Gibson alijibu.

    “Mbona umechukua uamuzi wa haraka sana?”

    “Ndio hivyo mke wangu”

    “Kwa hiyo utaniacha mimi mwenyewe? Utakubali kukaa mbali nami?” Katie aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Inawezekana. Najua haya yote yanatokea kwa ajili yako, kama ningekuwa nimemuoa mwanamke wa kawaida nadhani haya yote wala yasingenitokea kabisa.



    Nilitekwa, nikatoroka, leo hii napokea simu ya kifo, nadhani maisha yangu yapo ukingoni kama nitaendelea kuishi katika nchi hii ya ugeni” Gibson alisema.

    “Kwa maana hiyo unataka tuachane?” Katie alimuuliza Gibson.

    Gibson alibaki kimya, swali ambalo alikuwa ameulizwa likaonekana kuwa gumu kujibika, akayapeleka macho yake usoni mwa Katie, Katie alikuwa amebadilika



    sana, macho tayari yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba muda wowote ule machozi yangetiririka mashavuni mwake.

    “Mbona kimya tena? Kwa maana hiyo unataka tuachane?” Katie alimuuliza tena.

    “Kama inawezekana” Gibson alijibu.

    “Haiwezekani. Haiwezekani hata kidogo. Hapa mpaka mkataba uishe” Katie alimwambia Gibson maneno ambayo yalionekana kumchanganya.

    Kwa haraka sana mawazo yake yakahamia kwa Daniel, tayari kukataa kwa Katie kulionekana kumsababishia kifo kutoka kwa Daniel ambaye alikuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    amekwishamuingizia kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake. Gibson akaonekana kuchoshwa na jibu la Katie ambaye alianza kulia.

    “Kuvunja mkataba wa ndoa. Haiwezekani kabisa” Katie alimwambia Gibson katika kipindi ambacho simu ya Gibson ilikuwa ikiita, alipoichukua na kuiangalia,



    ilikuwa namba ya Daniel, namba ambayo ilikuwa ikimtia wasiwasi.

    “Umefikia wapi?” Daniel alimuuliza Gibson.

    “Bado kwanza” Gibson alijibu kwa sauti ya chini ambayo alihakikisha Katie asikii.

    “Sawa. Una masaa mawili tu. Usipokamilisha. Tunakuja kukua humo humo ndani” Daniel alimwambia Gibson na kisha kukata simu huku akimwacha Gibson



    akitokwa na kijasho chembamba kilichojaa wasiwasi.



    Tayari mambo yalikwishaanza kuwa magumu kwa Gibson, simu ambayo alikuwa ameipokea kutoka kwa Daniel ikaanza kumtia kiwewe kupita kawaida.



    Hakutulia, muda wote alikuwa amkimsisitizia Katie kwamba ilikuwa ni lazima wauvunje mkataba wa ndoa yao ili aweze kuikoa nafsi yake ambayo ilikuwa



    ikisakwa sana.

    Baada ya kulalamika sana, Katie akakubali kishingo upande. Moyoni mwake ilikuwa imemuuma kupita kawaida, mapenzi yake makubwa bado yalikuwa kwa



    Gibson ambaye kwa wakati huo alitaka wavuje mkataba wa ndoa wa miaka mitano ambao walikuwa wameandikishiana.

    Walichokifanya ni kuelekea mahakamani ambako huko mkataba ukavunjwa. Ingawa Gibson alikuwa akifanya hivyo lakini moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita



    kawaida. Nguvu ya fedha ndio ambayo ilikuwa imempelekea kufanya kitu kama kile ambacho wala hakuwa akitaka kukifanya.

    “Nitarudi Tanzania tu. Tena haraka iwezekanavyo” Gibson alijisemea.

    Alikaa nchini Marekani kwa siku mbili zaidi huku akionana na Daniel ambaye alikuwa akimpa pongezi kwa kile ambacho alikuwa amekifanya, na baada ya hapo,



    akakata tiketi na kurudi nchini Tanzania kwa kutumia ndege ya American Airlines.

    Ndani ya ndege hakuwa na raha hata kidogo, kwanza akili yake ilikuwa ikimfikiria sana Katie ambaye alikuwa amemuacha katika hali ya unyonge mkubwa huku



    akiwa amemuumiza kupita kawaida. Ukiachilia na Katie, pia mawazo yake yalikuwa yakimfikiria mke wake aliyemuacha nchini Tanzania, Prisca pamoja na



    mtoto wake, Genuine.

    Gibson hakujua kama Prisca alikuwa amekwishajua kilichoendelea au la. Kitu ambacho alikuwa akitaka kukifanya mahali hapo ni kuusoma mchezo tu. Kwanza



    angeangalia Prisca angempa mapokezi gani, hapo ndipo ambapo angegundua kwamba siri ilikuwa imevuja au bado iliendelea kuwa siri.

    Alitumia zaidi ya masaa ishirini katika ndege ile na ndipo ndege ilipotua katika uwanja wa Mwl Julius Nyerere huku ikiwa ni saa tisa usiku. Kwa sababu ilikuwa



    ni usiku sana, Gibson hakutaka kurudi nyumbani, alichokifanya ni kwenda kulala kwenye hoteli ya New African.

    Usiku wala hakulala, kichwa chake kilikuwa kikiwafikiria watu wawili kwa wakati huo. Kwa Katie, alijiona kufanya uamuzi mkubwa na mgumu kufanyika,



    kuna wakati mwingine alijiona bora amefanya uamuzi ule kwani ulikuwa na manufaa kuliko kuendelea kuishi na mwanake huyo ambaye alikuwa akicheza



    filamu za ngono.

    Katika kichwa chake, kwa wakati mwingine alikuwa akimfikiria sana mke wake, Prisca. Hakujua mwanake huyo angesema kitu gani hasa mara baada ya kuishi



    nchini Marekani kwa zaidi ya miezi sita bila kuwasiliana nae. Akili yake ikaanza kufikiria uongo mbalimbali ambao alitakiwa kumwambia Prisca mara baada ya



    kufika nyumbani kwake.

    “Nitamdanganya tu, wanawake ni rahisi sana kuukubali uongo” Gibson alijisemea.

    “Mmmh! Lakini miezi sita bila mawasiliano! Hivi kama isingekuwa Daniel si mpaka mwaka ungetimia bila kufanya mawasiliano na Prisca. Kweli nilifanya kitu



    kibaya sana” Gibson alijisemea na kisha kupatwa na usingizi huku ikiwa imetimia saa kumi na mbili alfajiri.

    Alikuja kuamka ikiwa saa saba mchana muda ambao aliagiza chakula na kuletewa chumbani na kisha kuanza kula. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa



    kikifikiria namna ya kumwambia Prisca ili aweze kumuelewa. Ni kweli kwamba alitunga uongo mbalimbali lakini kwa wakati ho, kila uongo ambao alikuwa



    ameutunga ulionekana kutokufaa, yaani aliuona kuwa uongo wa kitoto.

    Ilipofika saa tisa, akajitoa mhanga na kuanza kuelekea nyumbani kwake. Kadri gari ilivyokuwa ikizidi kusogea na ndivyo ambavyo wasiwasi ulivyokuwa



    ukimshika zaidi na kuufanya moyo wake kududa kupita kawaida.

    Alichukua dakika thelathini hadi kufika nyumbani ambako akateremka ndani ya taksi na kisha kumlipa dereva na kuanza kulifuata geti la nyumba yake. Mapigo



    yake ya moyo yakazidi kudunda zaidi na zaidi kana kwamba kulikuwa na hatari kubwa mbele yake. Alipolifikia geti, akabonyeza kengele na mlinzi kuja



    kufungua.

    “Karibu sana kaka” Mlinzi alimkaribisha huku akimpokea begi.

    “Subiri kwanza. Shemeji yako yupo?” Gibson aliuliza hata kabla hajaingia ndani.

    “Hayupo. Aliondoka kwenda kwa wazazi wake” Mlinzi alimjibu.

    “Dah! Toka lini?”

    “Mwezi wa tano huu” Mlinzi alimjibu Gibson jibu ambalo likaonekana kumtia wasiwasi.

    “Duh! Kwa nini sasa?”

    “Nilimsikia Rehema akisema kwamba kisa kilikuwa picha”

    “Picha gani?”

    “Hakutaka kuniambia”

    “Ok! Rehema mwenyewe yupo?”

    “Ndio” Mlinzi alijibu.

    Gibson akaanza kupiga hatua kuingia ndani na kisha kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni. Kwa wakati huo alikuwa akitaka kuongea na Rehema ambaye



    alikuwa mfanyakazi wa ndani na kisha kumuuliza kuhusu picha ambazo mpaka hapo zikaonekana kumchanganya.

    “Picha gani?” Gibson alimuuliza Rehema.

    “Kuna picha alipewa zikionyesha kwamba ulipiga na mzungu” Rehema alijibu.

    “Sasa kupiga picha na wazungu si kawaida sana hasa unapokuwa Marekani au Ulaya. Kipi hasa kilichomfanya kuondoka hapa nyumbani?” Gibson aliendelea



    kuuliza.

    “Hizo hizo picha”

    “Picha?”

    “Ndio. Ulipiga ukiwa na mwanamke wa kizungu ambaye alikuwa amevaa shela la harusi huku wewe ukiwa umevaa suti, yaani lilionekana kuwa tukio la



    kufunga ndoa” Rehema alimwambia Gibson ambaye akabaki kimya.

    Tayari kila kitu kiichoendelea nchini Marekani kikaonekana kujulikana kwa Prisca, kwa maana hiyo kama Prisca aliweza kuujua ukweli basi iliwezekana hata



    wakwe zake na wazazi wake walikuwa wakiufahamu ukweli. Kitu alichokifanya mahali hapo ni kutoka nje, kuchukua gari na kisha kuanza kuelekea nyumbani



    kwao huku akioneknana kuchanganyikiwa.

    Tayari kwa wakati huo alijiona kufanya makosa makubwa, asingeweza kuelekea nyumbani kwa kina Prisca bila wazazi wake, alichokuwa akikifanya kwa wakati



    huo ni kumfuata baba yake, mzee Lyimo pamoja na mama yake ili waweze kuelekea nyumbani kwa kina Prisca kwa ajili ya kumuombea msamaha kwa kila



    kilichotokea nchini Marekani.

    “Umefanya upumbavu mkubwa sana” Mzee Lyimo alimwambia Gibson kwa sauti ya juu.

    “Nafahamu baba, nafahamu kwamba nimefanya kosa kubwa lakini ninahitaji kusamehewa pia kama ambavyo ninaomba msamaha” Gibson alimambia baba yake.

    “Yaani umetutia doa hata sisi wenyewe. Tumeonekana tumekulea katika maisha ya ajabu ajabu. Eti unaondoka hapa na kuelekea Marekani kufunga ndoa, tena na



    mwanamke malaya ambaye anacheza filamu za ngono. Huo ni ujinga sana” Mzee Lyimo alisema maneno ambayo yalimfanya Gibson kushtuka.

    Hapo ndipo alipogundua kwamba wazazi wake walikuwa wakifahamu kila kitu kilichoendelea na hadi kazi ambayo Katie alikuwa akiifanya ilikuwa



    imekwishagundulika. Kwake, tayari mambo yakaanza kuonekana kuwa magumu, alijua fika kwamba kwa hatua ile ambayo alikuwa amefikia, ilikuwa ngumu



    sana kwa Prisca kuweza kumsamehe.

    Gibson akaanza kueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake pamoja na Katie, wazazi wake walikuwa kimya huku wakimsikiliza kwa



    makini kwani walihitaji kufahamu kila kitu kuona ni kwa namna gani wangeweza kuwaelezea wazazi wenzao ili kukubaliana nao na kumsamehe Gibson.

    “Kwa hiyo ukaamua kuvunja mkataba wa ndoa?” Mzee Lyimo alimuuliza.

    “Ndio. Niliamua kuuvunja kwa sababu nilijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kuja Tanzania na kumuona mke wangu na mtoto wangu. Kamwe nisingeweza



    kukaa zaidi bila kuwaona wao” Gibson alidanganya.

    Gibson, mzee Lyimo na mama yake, Bi Yustina wakaanza kuelekea nyumbani kwa mzee Steven huku lengo lao likiwa ni kumuombea msamaha kijana wao



    ambaye alikuwa ameamua kutubu dhambi zake juu ya kile ambacho alikuwa amekifanya nchini Marekani.

    Walipofika nyumbani kwa mzee Steven, wote wakateremka na kuanza kuelekea getini kisha mlinzi kuwafungulia na kuanza kuingia ndani ya eneo la nyumba



    hiyo. Wakaanza kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni ambao wakaugonga na kukaribishwa ndani.

    Mzee Steven na mkewe, Bi Magreth walikuwa sebuleni hapo, walipowaona wazee wenzao wanaingia, wakawakaribisha kwa furaha lakini mara walipomuona



    Gibson akiingia pamoja nao, wakabadilika kabisa. Nyuso za furaha ambazo walikuwa nazo zikawa zimekwishabadilika kabisa, walionekana dhahiri

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kutokumpenda Gibson kwa wakati huo. Hata pale Gibson alipowasalimia, hakukuwa na mtu aliyeitikia.

    Wakakaa kochini na kisha kuanza kuongea na baadae kumpa ruhusa Gibson kuongea. Ila kabla hajaanza kuongea, Prisca akaitwa mahali hapo, alipomuona mume



    wake, akaanza kulia. Prisca alikuwa mgumu kubembelezeka, alizidi kulia zaidi na zaidi huku Gibson akiangalia chini kwa aibu.

    Prisca alilia kwa muda mrefu, aliponyamaza, Gibson akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake na Katie tangu kipindi kile walipokutana



    kazini. Gibson alikuwa mkweli, ila katika sehemu moja tu hakutaka kuwa mkweli, hakutaka kuwaeleza wazazi wake kwamba alikuwa amevunja mkataba wa



    ndoa kwa sababu alipewa kiasi kikubwa cha fedha, alichokisema yeye ni kwamba alivunja mkataba wa ndoa kwa sababu alijua kile alichokuwa akikifanya



    kutokuwa kizuri, hivyo alihitaji kurudi nyumbani kuishi na mkewe aliyekuwa akimpenda.

    Alipomaliza kuelezea kila kitu akaanza kuomba msamaha. Ilikuwa ni ngumu sana kwa Prisca kumsamehe Gibson kwa sababu kile alichokuwa amemfanyia



    kilikuwa kitu kibaya sana kilichomuumiza moyo wake. Yalipita masaa mawili huku Gibson akiomba msamaha huku akilia kama mtoto na ndipo Prisca akaamua



    kumsamehe tena huku msaada wa wazazi wao ukiwa umesaidia kwa asilimia kubwa.

    Baada ya hapo, Gibson akaamua kuishi na mke wake, Prisca kwa amani, hakutaka kusikia kitu chochote kutoka kwa mwanamke Katie. Moyoni mwake hakujua



    kabisa, hakujua kwamba alikuwa amemjeruhi sana Katie, na hivyo muda si mrefu kuanzia hapo angetaka kulipiza kiasi kwa kile kilichotokea. Huko Marekani,



    Katie alikuwa amebadilika, alikuwa kama mbogo aliyejeruhiwa huku akimtafuta mtu aliyemjeruhi.

    Baada ya hapo, maisha yataanza kubadilika, huzuni itaingia, hasira za Katie zikabadilisha kila kitu, furaha ikawa huzuni na majonzi. Kwa Gibson hilo wala



    hakulitambua, alikuwa akiendelea kuishi na Prisca huku akijua kwamba yeye na Katie yalikuwa yamekwisha, kumbe ilikuwa tofauti kabisa kwani ndio kwanza



    mambo yalikuwa yakianza tena ngoma ikiwa mbichi kabisa...na kama gazeti, ndio kwanza ulikuwa umeanza ukurasa wa kwanza.



    Je nini kitaendelea?

    Je Katie atafanya nini kudhirisha hasira zake?

    Je maisha yataendelea kuwa ya furaha kwa Gibson na mkewe, Prisca?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog