Search This Blog

Sunday 19 June 2022

ROHO MKONONI - 5

 





    Simulizi : Roho Mkononi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Akiwa ameushikilia mguu vilevile aliachia ngumi ile moja kwa moja kwenye korodani za Rambo. Yowe kubwa likamtoka Rambo wakati akijirusha na kutua chini, safari hii Husna hakungoja asimame! Akamrukia kwa miguu yake miwili, akatua tena katika nyeti. Husna akafanya kitendo ambacho kila mwanaume anatambua kuwa hawezi kukihimili kikitokea!! Akaanza kumsigina Rambo kwa kutumia kisigino chake katika nyeti zake, Rambo akapoteza fahamu!! “UPO CHINI YA ULINZI TULIA HIVYO HIVYO!!” wakati Husna akiamini amemaliza kazi alisikia sauti ikimuamrisha!! Akatulia tuli. Mapigo ya moyo yakiwa juu, damu nayo ikizidi kumtiririka.

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MKE alitii amri ya mumewe, kweli baada ya kuzungumza na maaskari ambao aliwaamuru kumfuatilia Ndayanse kisha kumpatia taarifa, akaiweka simu katika mfumo wa kimya!! (Silence mode). Hapa sasa amani ikatawala, mume na mke wakafurahia ndoa yao bila bughudha aina yoyote. Majira ya saa nane usiku, baba Vicy alihitaji kwenda uani kujistiri haja ndogo. Aliposhuka kitandani akapapasa huku na kule hakuyapata makubadhi yake. “Mama Vicy simu ipo wapi?” “Juu ya meza hiyo!!” Assistant super retendant Seba alipapasa na kuipata, akabofya kitufe kimojawapo ikawaka akamulika na kuyapata makubadhi yake, lakini ni muda huo huo alipoona ujumbe katika simu. Akajiahidi kuusoma akishatoka uani. Lakini azma yake haikutimia akajikuta katika kiherehere cha kujua kuna nini kinaendelea. Huenda ni vijana wake. Akafungua!! Kweli akakutana na jina la kijana wake likiwa limetuma ujumbe. ”Tupo katika hatari, wenzangu wawili wamekufa. Chamanzi huku. Msaada wa haraka tafadhali” Ule mkojo uliomtoa kitandani ukakoma ghafla, akatumbua macho na asijue kama ameyatumbua. Ujumbe ule ulimtisha na kumshtua. Hakuelewa maana yake kwanza, akabaki kusimama wima. Mkewe akahoji hakujibiwa. Akaamua kuiwasha taa ya pale ndani. Mama Vick akamshuhudia mumewe akiwa ameganda kama aliyepigwa shoti, akajitanda kanga yake haikumkaa vyema mwilini aliposimama ikaanguka na hakufanya jitihada zozote za kuiokota akasalia uchi wa mnyama. “Kuna nini babaa!!” alihoji huku akizungusha mkono wake katika kiuno cha mumewe. Mguso huo ukarejesha fahamu za Seba. “Meseji mke wangu!!” alisema huku akimkabidhi simu mkewe. Upesi upesi mama Vicky akmaliza kuusoma ujumbe ule. “Sasa ni akina nani hawa.” “Vijana niliowaagiza wakamfuatilie Inspekta Ndayanse!!” alijibu kama anasuta!! Mkewe akabaki kimya huku akiwa ana simu mkononi. “Mbaya zaidi hapatikani tena. Halafu ujue hiyo ishu ilikuwa nje ya utaratibu wa kazi, yaani ofisi haitambui jambo hilo.” Aliendelea kuzungumza, akiwa bado kimya. Mara akaichukua ile simu kutoka kwa mkewe, akapiga namba fulani na kutoa amri za kiaskari. Kisha akavaa nguo zake za kiraia na kumuaga mkewe. Kwa kinyongo mke akamkubalia!! Assistant super retendant Seba akaondoka. Akiwa njiani akapokea taarifa kutoka mahali alipoagiza apatiwe taarifa zile. Zilikuwa taarifa juu ya namba ile ya simu iliyomtumia ujumbe. Ni wapi ilikuwa inapatikana. Akawachukua vijana wengine wane, wakaelekea eneo la tukio. Wakati wapo njiani ilikuwa saa nane na nusu usiku!!

    Laiti kama usingekuwa ujasiri wa Ben, askari kijana ambaye baada ya kutoka kichakani kujistiri haja ndogo alishuhudia wenzake wawili wakiwa wamefyatuliwa risasi. Mlio huo mkubwa aliusikia tangu akiwa kichakani hivyo akajibanza na kujikaza asipatwe hofu na kuishia kupiga kelele. Baada ya tukio lile alinyata na kuifikia ile gari, akachukua simu na kisha kujificha chini ya gari lile kisha akautuma ujumbe wa simu kwa Seba juu ya hatari waliyokutana nayo. Wakati anamalizia kutuma, mwanga wa simu yake ukaakisi katika macho ya Rambo ambaye alikuwa anamtafuta baada ya kuwaua wenzake wawili. Ni hapa Ben alivyoamua kutimua mbio….huku akidhani kuwa adui pekee ni Rambo ambaye anamkimbiza, huku nyuma ya nyumba anakutana na kizaazaa kingine, anapigwa ngwara na kutua mikononi mwa Husna ngumi jiwe!! Hii inakuwa safari yake ya mwisho pale anaporushwa hewani na kisha bunduki isiyokosea shabaha ya Inspekta Ndayanse ilipoondoa uhai wake!! Wakati ujumbe unasomwa na Seba, Ben na askari wengine wawili walikuwa wameuwawa tayari!! Uwanjani walibaki watu wachache sana. Wakazidi kupungua baada ya Husna kumsambaratisha Inspekta Seba, kisha Fonga na Joyce kuruhusiwa kutimua mbio. Hatimaye uwanja ukabaki na watu wawili tu wanaoweza kutikisa. Rambo na Husna, mpambano wa ana kwa ana!! Wakati huo Beka akiwa ametawanyika akiwa hana uwezo wake wa kufikiri wala nguvu za kukimbia!! Husna wakati anamalizia mpambano wake kwa kuzisigina korodani za Rambo kisha amkabili Beka ndipo alipoisikia sauti ya kuamrisha kiaskari. “UPO CHINI YA ULINZI!!”

    HUSNA akajaribu kucheza kwa hisia, akadhani mtekaji yupo mmoja, akajaribu shambulizi lake la shukrani ya punda. Husna akajirusha upesi kinyume nyume!! Pigo lake lilikuwa sahihi, lakini lenye madhara makubwa. Ni wakati huo alipokutanisha macho yake na sura ambayo aliwahi kukutana nayo wakati akiwa rumande katika kituo cha polisi Msimbazi. Akajaribu kulitambua jina lake. Akalikumbuka!! Alikuwa anatazamana na ‘Roho ya paka’. Askari ambaye alizisikia sifa zake wakati yupo jela, kuwa huwa hana utani na ana roho ngumu ya kikatili sana. Husna hakungoja muda mrefu upite ili aweze kugundua ukatili wa yule bwana. Bunduki yake ikakohoa kidogo. Husna akatokwa na yowe kubwa huku akikosa uwezo wa kusimama imara!! Risasi ilikuwa imelisambaratisha goti lake, Husna akalia kilio kikubwa wakati huo yule askari alikuwa akimsogelea huku akitabasamu!! Alipomfikia akamfanya kma mpira wa miguu, akaachia teke kali likausambaza uso wake, naye akatawanyika kama Beka. Damu zikasambaa kutokea mdomoni na katika paji la uso. Ama kwa hakika huyu alikuwa ni roho ya paka!! Baada ya pigo lile yule askari akamsogelea Rambo, akamfyatua teke moja kumpima kama yu hai ama la!! Rambo akagumia kwa maumivu huku akionekana kuwa yupo katika dakika za mwisho za uhai wake. “Seba!!” alisikia sauti ikimwita kuelekea sehemu moja pembeni kidogo ya eneo lile. Upesi akatoa pingu zake akawaunganisha Rambo na Husna!! hatua mbili akamtambua mheshimiwa mbunge Beka!! Huyu naye akamtia pingu kwa usalama!! Kisha akaelekea kuutambua mwili uliokutwa kichakani. Alikuwa ni Inspekta Ndayanse ambaye katika mapambano hayo alijiita Inspekta X. hakuwa katika fahamu zake na alikuwa amejilaza katika namna ya kustajaabisha kama mtu asiye na mifupa. “Mpelekeni katika gari huyu!!” aliamrisha, askari wakavaa mipira mikononi na kumtwaa Ndayanse. Zoezi la kukagua eneo lile likaendelea huku simu za ulinzi zaidi zikipigwa makao makuu!! Hali ilikuwa tete sana. Husna akakata tamaa ya kujiokoa tena, akakiri kuwa kisicho ridhiki hakiliki. Huku akibubujikwa damu mdomoni akaiona tena milango ya gereza ikifunguka ili aweze kuingizwa tena. Safari hii aliamini kesi ilikuwa kubwa kuliko!! Husna akajiona hana thamani yoyote duniani, akaamua kufanya jambo ambalo litamuhukumu upesi kuliko kupitia msoto wa rumande kisha jela. Alifikiria atafanya nini huku ana pingu mkononi. Na ndipo alifika yule roho ya paka!! Akainama kuwanyanyua wale watu wasiokuwa na uwezo wa kunyanyuka. Hii ikawa nafasi ya mwisho ya Husna kufanya maajabu!! Roho yake akaiweka rehani!! Roho ya paka, alipoinama tu kuwanyanyua Husna akatumia mkon wake mmoja uliokuwa huru akaishika nguo ya Seba kisha kwa mguu wake mmoja uliobaki salama na nguvu kiasi akamzoa mtama Seba. Kwa sababu hakutergemea tukio hilo akaenda chini, mahesabu sahihi kabisa. Shingo ya Seba katika mdomo wa Husna. Akaunganisha meno yake na kuukamata mshipa mkubwa wa damu shingoni akayaunganisha meno yake kwa ghadhabu. Roho ya paka akageuka roho ya fisi!! Akaanza kupiga mayowe ya uoga na uchungu. Askari waliopeleka mwili wa Inspekta Ndayanse garini hawakufanikiwa kuiskia sauti ya mkuu wao. Katika tukio hili Beka naye akajikuta anapata uhai, akabeba jiwe huku akiwa na pingu zake ili aweze kushambulia. Alipolinyanyua jiwe ili amshambulie Seba, jiwe likamzidi uzito akapinduka nalo na kuanguka huko kama kifurushi cha kokoto. Akapoteza fahamu!! Husna akaendelea kumdhibiti Seba ambaye alikuwa akijaribu kujirusharusha bila mafanikio. Mshipa ulikuwa katika meno ya Husna. Askari wale waliporejea walimkuta mkuu wao katika hali mbaya mikononi mwa Husna!! Wakamuamuru Husna amwachie lakini hakumwachia, wakaamuru tena hakutii amri. Hatimaye wakafyatua risasi!!

    *****

    MAJIRA ya saa kumi na mbili na nusu Betty na Isaya walikuwa macho tena!! Betty akaamua kutumia fursa ile kuzungumza na Isaya juu ya alichokuwa anakifikiria katika kichwa chake. Mazungumzo ambayo yalileta mtafaruku na msuguano wa nafsi kwa nafsi. Isaya akajiweka makini kumsikiliza Betty “Isaya!! Nakupenda sana mpenzi wangu, na sipendi kuona ukihangaika siku moja. Katika hili siwezi kujieleza sana nadhani unanielewa tayari!!....kuna jambo ambalo naona sio haki hata kidogo nikiacha kukushirikisha kuhusu mimi. Hasahasa jana usiku, nadhani ulishangaa sana nilivyosisitiza uvae kondomu. Kuna jambo napenda ulijue ili usiwe na kinyongo na mimi. Ujue nilipotekwa nilibakwa, niliumia sana hakika, nilibakwa mara mbili na hao watekaji. Sasa sijui kama wapo salama ama la! Na nisingeweza kukaa kimya nikuangalie Isaya ukifanya mapenzi na mimi bila kinga. Nd’o maana niliamua kukusisitiza juu ya kinga mpenzi wangu Isaya. Kitu kingine mimi nilihitaji kwenda kupumzika nyumbani kidogo ili niyasahau haya yaliyotokea……..” akasita na kumshangaa Isaya jinsi alivyoingiwa na hofu kutokana na maelezo yake. “Isaya kuna nini?” alimuuliza. Lakini Isaya akajifanya kutabasamu, mara abofye simu iliyozimika, mara ajikune ndevu!! Isaya hakuwa sawa. “Ehe! Umesema unataka kwenda nyumbani, hivi ni wapi vile!!” alihoji Isaya. “Mwanza!!” alijibu Betty. “Lakini haupo sawa Isaya!!” “Yeah si unajua sijawasiliana na mzee mpaka muda huu na sijui lolote kuhusu Kindo. Nd’o nataka niwasiliane nao kwanza maana mzee wangu bwana!!” alijilazimisha kuchangamka!! Betty akaguna! “Basi utanieleza baadaye mpenzi au vipi?” alikatisha Isaya kish akarejea kitandani. Akajifunika shuka gubigubi, alipoyafumba macho mara akaanza kuiona filamu ambayo kama ingewezekana ingerudishwa nyuma na ifutike kabisa. Isaya alikuwa katika choo cha kulipia, akajifungia kama anayetaka kujistiri na haja kubwa. Akatoa pakiti ya kondomu mfukoni. Akatoa na wembe mfuko mwingine, akakata chuchu za kondomu zote pakiti tatu. “Unaniletea ujanja wa kijijini mimi!! Nitumie kondomu? Unaumwa nini? Ngoja kama ni mimba ainase mi nitahudumia kwani nini?” alisema Isaya kwa sauti ya chini huku akizihifadhi zile kondomu tena. Akautupa ule wembe kisha akaondoka kurejea kule chumbani, akamuta Betty anamsubiri. Ili mchezo wake uende vizuri kabisa akazima taa. Kisha akavaa kondomu zake zilizotolewa chuchu ya mbele, Betty akaamini Isaya alikuwa amevaa Kondomu lakini haikuwa hivyo Isaya hakuwa amevaa kondomu na kama ni mimba basi angenasa!! Lakini haikuwa kwa sababu ya mimba, Betty alikuwa katika harakati za kumwokoa Isaya lakini Isaya akaleta ujanja wa mjini akazitoboa kondomu zote tatu kabla ya kujamiiana na Betty. Sasa amejifunika shuka gubigubi akiwaza upuuzi alioufanya, hakika aliuogopa Ukimwi. Sasa anasikia kuwa amefanya mapenzi bila kinga na mtu aliyebakwa!! Labda la kubakwa halishangazi sana lakini uhalisia ni kuwa Betty alikuwa muathirika wa gonjwa la Ukimwi. Isaya matatani!! Mara simu yake ikaita. Ndipo akakumbuka kuwa katika kuibonyezabonyeza wakati Betty akimsimulia alikuwa ameiwasha pasipo matarajio. Akashtuka na kuitazama, Betty alikuwa ameishikilia. “Ni mama anapiga!!” Betty alimwambia huku akimkabidhi. Isaya akaichukua kisha akaipokea. “Mama!!” aliita Isaya. “Heeee!! Nani wewe…..” alihoji mama mtu. “Mama mi Isaya jamani au.” “Isaya mwanangu mimi ama!! Isaya si wamemuua mwanangu..” alijaribu kutulia mama na kujieleza. “Mimi Isaya mama au unaota….” Alihoji Isaya. Mara simu ikakatwa bila kuagwa na mama yake. Alipojaribu kupiga simu yake ikawa inatumika…akabaki kustaajabu!!

    ***** MZEE Akunaay akajiuliza iwapo apokee simu ya mkewe ama la!! Ikaita mara ya kwanza, kisha ikaita tena mara ya pili. Akaona kukaa kimya wakati mwingine badala ya kuwa jibu huzua maswali mengine zaidi. Akafikiria kitu, akaiwasha luninga na kuweka sauti ya juu. Akaisogeza simu katika luninga ili aweze kuipokelea hapo na kujifanyayupo katika kelele hawezi kuongea wakaelewana. Akafanya mawazo yake yalivyomtuma akaweka sauti ya juu. Kisha akapokea simu akiwa jirani na luninga. Ni hapa ndipo likatokea tukio mfano wa muujiza. Ile sauti ya luninga ikiwa juu na mama Isaya naye akapaza sauti sasa yakawa mashindano. LUNINGA : Mwili wa Inspekta Ndayanse uliojeruhiwa vibaya sana upo katika chumba cha wagonjwa mahututi chini ya uangalizi wa madaktari wakati majeruhi mwingine mheshimiwa Beka akiendelea vizuri.

    MAMA ISAYA: Isaya amenipigia simu mume wangu, Isaya kwa namba zake mwenyewe. Uuuuwi!! Isaya wangu eeeh….Isaya Isaya namtaka Isaya wangu!!!

    Ndayanse amejeruhiwa vibaya, Beka anaendelea vizuri!!! Isaya yupo hai hajafa na amepiga simu!! Mzee Akunaay akalegea taratibu, simu ikaanguka chini kisha yeye akafuata. Akapoteza fahamu!!



    UPANDE MWINGINECHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Akunaay anayedhani mtoto wake amekufa anapata taarifa mbili asubuhi, Isaya yu hai lakini Beka naye yupo hai pia!!anapoteza fahamu. Upande wa Isaya amepagawa baada ya kupasua kondomu na kufanya mapenzi na Betty anayedai kubakwa!!!!

    SASA ENDELEA!!!

    LUNINGA : Mwili wa Inspekta Ndayanse uliojeruhiwa vibaya sana upo katika chumba cha wagonjwa mahututi chini ya uangalizi wa madaktari wakati majeruhi mwingine mheshimiwa Beka akiendelea vizuri.

    MAMA ISAYA: Isaya amenipigia simu mume wangu, Isaya kwa namba zake mwenyewe. Uuuuwi!! Isaya wangu eeeh….Isaya Isaya namtaka Isaya wangu!!!

    Ndayanse amejeruhiwa vibaya, Beka anaendelea vizuri!!! Isaya yupo hai hajafa na amepiga simu!! Mzee Akunaay akalegea taratibu, simu ikaanguka chini kisha yeye akafuata. Akapoteza fahamu!!

    ****

    DEREVA wa taksi alikuwa amekunja sura yake sijue nini cha kufanya, kama kubembeleza alikuwa amebembeleza sana pasi na mafanikio yoyote, mteja wake hakutaka kusikia lolote lile. Alikuwa akipiga mayowe huku akinena kikabila. Dereva alilazimika kufungulia redio yake katika gari huenda ataweza kupambana na kilio cha mama yule. Katika nafsi yake dereva alikiri kuwa mteja wake yule wa kwanza kwa siku hiyo alikuwa kiboko kwa kulia!! Redio haikufua dafu, mama alikuwa analia kwa dakiku kumi kisha ananyamaza kwa sekunde kadhaa. Wanyakyusa kwa kulia hawajambo!! Dereva alijisemea huku akiendelea kuendesha gari kwa makini. Hatimaye wakafika mama yule alipohitaji!! Akamshusha baada ya kuwa amelipwa pesa yake. Aliposhuka chini tu akaanzisha kilio cha juu zaidi, alilia huku anatembea mwendo fulani ambao hauna uelekeo rasmi. Watu wakawa wanaduwaa tu!!

    “Mume wangu uuuuuuwi!!! Ino weeeee Inoooooo……uuuuwi Inooooo!!” aliendelea na kilio hicho hadi katika mlango wa nyumba aliyoifahamu. Bahati nzuri alikuta watoto wakiwa wameamka wakijiandaa kwenda shuleni. Walipomuona wkamtambua. Mama Saidi!!! Mke wa Inspekta Abrahiman Inocent Ndayanse, ama kwa jina lake la uficho. Inspekta X. Kilio kikapanda juu zaidi baada ya mwenyeji wake kutoka nje. Huyu alikuwa mama Vicky, mkewe Assistant Super Retendant Seba!!

    “Inoooo wangu eeeeeeeh Inoooooo!!!” hapa sasa alilia huku akirukaruka kama ambaye anahangaika kupambana na mkojo uliombana haswa! Mama Vicky akabaki kuduwaa asielewe nini kinaendelea hapo. “Hebu mama Said, njoo huku…” mama Vicky alimshika mkono na kumkokota kuelekea ndani. Maana pale nje majirani walianza kutazama onyesho la bure kabisa.

    Baada ya kubembelezwa sana mama Said akanyamaza. Ni hapa alipoelezea juu ya taarifa ya habari aliyoisikiliza asubuhi ya siku hiyo. Taarifa juu ya mumewe kuwa chini ya uangalizi wa madktari katika chumba cha wagonjwa mahututi.

    “Amekuwaje hadi akafikishwa huko!!” mama Vicky mke wa Seba aliuliza huku akili yake ikimtuma kuwa Inspekta Seba huenda amefumaniwa mahali na kupokea kipigo kitakatifu kilichomfikisha hapo.

    “Mama Vicky yaani hujui kuwa hata mumeo hajulikani kama yu hai ama amekufa uuuuuuwi!!!!” mama Saidi akapiga mayowe tena ya kuduwaa. Mama Vicky alimshangaa mwanamke mwenzake kwa hiyo kauli yake, aliamini kuwa hajui anachokisema labda. Lakini kabla hajafikiri zaidi akaikumbuka meseji ambayo mumewe aliipokea usiku ule na hatimaye kutoweka nyumbani!! Hapa sasa akailewa vyema kauli ya mke wa Inspekta. Hatimaye kila mmoja akawa kama mwenzake. Lakini mke wa Inspekta akapiga hatua moja zaidi, alipoona kuwa mama Vicky hajui lolote na mumewe hayupo nyumbani. Akakimbilia kituo cha polisi kilichokuwa mita kadhaa mbele. Huku akazua mtafaruku wa aina yake asieleweke ni nini anataka. Akajisahau kuwa polisi sio sehemu ya utani. Wakamkamata na kumweka ndani!!

    Mwisho wa kelele zake!!

    ****

    ULIKUWA mshtuko mkubwa sana kwa jeshi la polisi. IGP aliipokea taarifa hii akiwa nyumbani kwake baada ya vijana wake kushuhudia waliyoyashuhudia. Mheshimiwa mbunge aliyedhaniwa kutekwa, Inspekta Abrahimn, Assistant Super retendant Seba. Wote katika utata wa uhai wao. Kila mmoja akwa amejeruhiwa vibaya na wote wakiwa wamepoteza fahamu. Askari watatu vijana akiwemo Ben wakikutwa wamepoteza maisha. Kijana mmoja asiyejulikana akikutwa ameuwawa pia, huku vijana wengine wawili mmoja mwanaume na mwingine mwanamke wakiwa katika hali mbaya sana!! Aliyeshambulia hakujulikana hadi muda huo. Ajabu ni kwamba katika eneo hilohilo, siku iliyopita vijana wawili waliotambulika kwa majina ya Kindo na Jose walikutwa wamekufa kwa kupigwa risasi. Nyumba ile ikafahamika kuwa ni mali halali ya mbunge wa Geita mjini Akunaay Zingo. Lakini tatizo hakuna tukio hata moja lililotokea ndani ya nyumba kwa taarifa zilizokuwepo wakati huo, kila kifo kilikuwa nje ya nyumba, kila majeruhi alikutwa nje ya nyumba ile. Ajabu!! Mheshimiwa akahitajika kituoni ili aweze kutoa maelezo japo kidogo kama lipo ambalo analifahamu. IGP akaikabidhi kesi ile kwa Inspekta Mushi. Akahitaji upelelezi wa kina na kila taarifa ipelekwe kwake moja kwa moja!!! Hilo lilikuwa tukio lakitaifa. Wabunge wawili wa chama tawala kuhusishwa katika kesi moja, tena mmoja kati yao ni waziri wa ulinzi na usalama, mheshimiwa Akunaay Zingo. Mushi akaingia kazini!!

    ****

    BAHATI ilikuwa upande wake fahamu zilimrejea kabla muda wa kusafisha chumba haujafika. Alijishangaa kwa muda na kisha akagundua kuwa alipoteza fahamu baada ya taarifa fulani ya kutisha!! Alipigiwa simu na mkewe na aliona taarifa ya habari yenye utata. Akasimama na kujinyoosha kisha akaangalia huku na kule akakutana na simu yake. Akakuta simu zisizojibiwa ishirini. Akaifungua na kukutana na jina la Isaya, mke wake na wabunge zaidi ya wanne. Alipoona namba za wabunge akakumbuka juu ya Beka, mbunge aliyetoweka kwa kutekwa na sasa amepatikana. Hapohapo akamkumbuka Inspekta X, askari ambaye aliagizwa kwa ajili ya kumuua Beka. Kwa sababu Beka yu hai maana yake ni kwamba hakufanikisha azma yake. Utata!! Akunaay akaamua kuizima simu yake ili ajipe muda kidogo wa kufikiri juu ya nini kinapaswa kufanyika muda huo. Hatua ya kwanza ikawa kuhama nyumba ile ya wageni kabla hajaanza kutafutwa. Hilo hakulipa nafasi ya kupata majibu mawili, jibu lilikuwa ndiyo. Akaondoka!! Hakumweleza mtu yeyote na wala hakumuaga mtu yeyote kuwa anaondoka. Aliyafanya hayo yote kimyakimya!!

    ****

    Isaya alizidi kuvurugwa baada ya kupokea simu kuwa Kindo, yule rafiki yake alikuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi. Isaya akakumbuka kuwa alikuwa akijaribu kumpigia Kindo simu bila mafanikio hapo kabla. Hapa sasa akatambua kwa nini amahisiwa kuwa amekufa. Huenda kuna mtu alitumwa kumuua yeye akiwa anampeleka huyo Jose katika nyumba yao ya Chamanzi na sasa amemuua Kindo badala yake. Mapigo ya moyo yakapiga kwa nguvu, akasahau kidogo kuhusiana na Betty na taarifa yake ya kubakwa. Isaya akawa amevurugwa hasa!! Akampigia baba yake simu bila mafanikio, simu ilikuwa inaita tu bila kupokelewa. Mama yake alikuwa analia tu huku na yeye akilalamika kuwa alikuwa anampigia simu bila kupokelewa. Hali ambayo ilizidisha wasiwasi. Walipojipa muda kuwa ni yeye atakuja kuwapigia haikuwa hivyo, mzee Akunaay alikuwa amezima simu tayari. Alipopotea hewani mzee Akunaay alielekea anapopajua yeye, na hata alipoibuka alikjua mwenyewe. Lakini ilileta mastaajabiko ya aina yake huku kuibuka huko kukizua utata mpya kabisa ambao haukuwa ukifahamika hapo kabla.

    ***

    ILIKUWA kesi ya aina yake yenye muunganiko wa kisa ambacho ni kama kilikuwa kinakaribia kutoa jibu lakini walisubiriwa wahusika fulani waweze kusema neno kwa ufupi na upelelezi uweze kukamilika. Hii ilikuwa ni kesi nzito sana ambayo ilikuwa imechukua nafasi kwa siku chache zaidi kupita kesi nyingine zote zilizokuwa na utata katika siku za nyuma. Mbunge aliyetekwa nyara tayari alikuwa amerejewa na fahamu, kijana asiyejulikana jina lake alikuwa anaelekea kupona kabisa japo asingeweza kuzalisha tena, nyumba iliyozungukwa na janga kuu lililojitokeza ni ya mheshimiwa mbunge ambaye ni rafiki wa Beka aliyekuwa ametekwa, huyo mbunge hiyo ilikuwa ni siku ya nne hajulikani alipo. Katika lugha ya kipelelezi mbunge wa Geita mjini Akunaay Zingo alitakiwa kupatikana aweze kusema neno kutokana na janga hilo. Msako ukaanza kimya kimya!! Ulinzi mkubwa uliwekwa kwa kijana asiyekuwa na jina!! Beka alichukuliwa kama msamaria mwema tu ambaye alikuwa ametekwa na kijana yule akishirikiana na yeyote yule ambaye atamtaja katika maelezo yake, ulinzi ukawekwa katika hospitali ambayo wahusika hawa walikuwa wamelazwa. Inspekta Mushi alikuwa makini sana na kila jambo!!

    BAADA YA SIKU MBILI

    Mheshimiwa Beka akiwa chini ya ulinzi alikuwa ana uwezo wa kuongea vizuri kabisa. Na sasa alikuwa na uwezo wa kutoa majibu kutokana na lolote lile ambalo atahojiwa. Inspekta aliyepewa jukumu hilo la kuipeleleza kesi ile alikuwa katika ofisi yak akingojea kuianza shughuli hiyo kwa kumuhoji mheshimiwa Beka. Kwa huyu walitaka mwanga tu kujua ilikuwaje akatekwa kwa siku hizo chache ama la ilikuwaje akkutwa eneo la tukio akiwa hoi kiasi kile. Inspekta alitegemea majira ya saa nne asubuhi kama daktari alivyosema kuwa atakuwa ameruhusu mgonjwa wake kutolewa hospitali, lakini ilikuwa inakimbilia saa tano na dakika ishirini. Inspekta Mushi akaamua kupiga simu eneo husika kuuliza kulikoni. Huku akakutana na habari nyingine nzito ya kushangaza. Mheshimiwa Beka alikuwa amezidiwa ghafla na alikuwa amerudishwa chumba cha wagonjwa mahututi. Mushi akaduwaa, ni yeye alitoka kumjulia hali Beka siku iliyopita wakacheka pamoja. Leo hii amerejeshwa chumba cha wagonjwa mahututi!!! Ilishangaza. Akastaajabu kwa muda bila kukubaliana kabisa na hali halisi, hakutaka kujiaminisha kuwa hali kama ile inaweza kuwa ya kawaida. Akafanya mawasiliano na vijana wake baada ya robo saa ili waweze kuelezea kwa kifupi hali ya usalama ilivyokuwa. Wakamueleza kuwa tofauti na spika wa Bunge na wabunge wengine wawili kuja kumjulia hali mheshimiwa Beka, hakuna kiumbe mwingine aliyeruhusiwa kuonana na mheshimiwa, kuhusu wale wagonjwa wengine kwa upande wao hakuna kabisa aliyekuja na kujitambulisha kama ndugu yao. “Mheshimiwa zaidi ya hayo pia muda mchache uliopita yule binti aliyepigwa risasi mbili na vijana wetu amefariki na hakuweza kusema neno lolote, inaonekan risasi ilimvunja mfupa halafu mwanzo alikuwa amevunjwa goti hivyo alipoteza damu nyingi sana. Jitihada zimegonga mwamba.” “Jina lake limeweza kufahamika!!” “Hapana afande hakusema neno lolote hadi anapoteza uhai.” “Seba anaendeleaje na Ndayanse!” “Seba bado amelala bosi na Ndayanse ni kama tahira hivi japo amepararazi, hiyo ni kwa mujibu wa daktari” Mazungumzo yakaishia hapo na simu ikakatwa!!

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MAJIRA YA saa sita mchana ujio wa mzee wa makamo ghafla katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ulishangaza watu wengi. Haukuwa muda wa kusalimia wagonjwa lakini yeye akalazimisha apewe nafasi hiyo. Alikuwa ni mzee wa makamo kiasi, nguo zake zikiwa zimechakaa na akiwa na majeraha kadha wa kadha. Alikuwa akihangaishana na walinzi kuhusu kuingia kwake katika hospitali hiyo, mzee huyo alikuwa kama amepagawa. Akilia kwa kutaja jina Beka!! Alilia kwa uchungu haswa!! Kila mmoja akashangaa. Polisi wakapewa taarifa hiyo juu ya mzee wa maajabu!! Wakamkabili na kumuuliza kulikoni, ni hapa ndipo baadhi yao walipoanza kuitambua sura yake kwa mbali. “Wametaka kuniua mimi uuuuuwi!!! Beka weeeeee Bekaaaaa!! Beka!!” mzee aliomboleza kwa uchungu mkubwa. Polisi wakamvuta kando na kuhoji kulikoni, lakini mzee hakuwa katika utulivu!! “Nataka anieleze kwa nini anatalka kuniua mimi!! Anieleze uuuuwi!!” alilia zaidi na zaidi. Polisi wakamwona kuwa ana umuhimu kwao. Hasahasa walipomtambua zaidi kuwa ni mbunge wa Geita mjini aliyekuwa ametoweka siku mbili nyuma!! Bila kujulikana ni wapi alipokuwa. Mzee Akunaay akatiwa chini ya ulinzi, akahifadhiwa katika karandinga ya polisi. Wakati karandinga ile inatoweka pale kituoni. Mheshimiwa Beka naye alimalizia mkataba wake wa kuvuta pumzi duniani!! Akakata roho! Uchunguzi ukaonyesha kuwa alikosa hewa barabara!! Kitimtimu!!

    ****

    KITUO CHA POLISI

    MAELEZO ya mzee Akunaay kituo cha polisi yakelezea juu ya kutekwa kwake na watu asiowafahamu na kisha kumbuluza vichakani. Wakamweleza kuwa asiwalaumu wao bali mzee Beka ndiye aliyewatuma, japo hakuwaambia sababu moja kwa moja ila walihisi kuwa Beka alikuwa anamwonea wivu kwa cheo chake cha uwaziri, hivyo kwa kumuua yeye huenda raisi angeweza kumteua yeye kuchukua nafasi hiyo. Mzee Akunaay aliyaeleza yale kwa uchungu!! Hasa hasa alivyoelezea jinsi kijana wake alivyokoswakoswa kuuwawa baada ya kuwa amemwagiza kwenda kutazama nyumba yake ya Chamanzi!!

    “Maskini weee!! Sijui angeenda mwenyewe ingekuwaje wangemuua Isaya weeee!!” alianza kulia tena mzee Akunaay. Isaya alikuwa nje pamoja na mama yake wakisubiri kuona nini kitajiri baada ya maelezo hayo ya mzee Akunaay. Isaya akiwa amesahau kwa muda juu ya mchezo alioufanya kwa Betty ambaye alimweleza kuwa alibakwa. alipokumbuka jambo hili, ghafla akamkumbuka Betty na mazungumzo yake siku moja kabla. Betty aliitambua picha ya mzee Beka wakati wa taarifa ya habari. Akamweleza Isaya kuwa ni mzee yule aliyekuwa amemteka na kumbaka. Baada ya mzee Akunaay kumaliza kuhojiwa huku maelezo yake mengi yakiwa hayana ushahidi, tukio pekee lililokuwa na ushahidi ni kifo cha Kindo na Jose ambapo ni kweli simu yake ya kumuagiza Isaya ilikuwa imerekodiwa. Isaya akapata nafasi ya kuzungumza na yule mpelelezi na kumueleza juu tukio la marehemu Beka kumteka nyara pia mchumba wake na kisha kumbaka. Isaya aliamini kuwa ni Betty pekee awezaye kumwokoa mzee Akunaay na kuuthibitishia umma kuwa mzee huyu hana hatia. Inspekta Mushi alivutiwa sana na maelezo ya Isaya, maana alikuwa akihitaji sana mtu yeyote ambaye yupo hai aweze kuelezea tukio lolote lililotokea ndani ya nyumba ya mzee Akunaay. Hili lilikuwa tatizo kubwa sana. Kesi isingeweza kwenda hivihivi bila kupatikana mtu mmoja wa kuzungumzia hali ya ndani ya nyumba na nje kabla ya mauaji ya kutisha. Maana askari aliyetegemewa kuelezea chochote alikuwa amepararaizi na hakuweza kuzungumza hadi siku hiyo, kuna madhara makubwa yalikuwa yamejitokeza katika uti wake wa mgongo na kuithiri akili yake. Huyu alikuwa ni Inspekta Ndayanse. Vijana watatu waliotegemewa waliuwawa mapema eneo la tukio. Msichana aliyekutwa hoi na kupigwa risasi na maaskari baada ya juhudi za kumsalimisha Assistant super retendant Seba ambaye alikuwa ameng’atwa meno na binti yule kushindikana, sasa alikuwa amefariki. Beka naye alikuwa amefariki!! Assistant super retendant, fahamu zikiwa hazijamrudia. Sasa linaibuka jina la Betty!! Ni hapa ndipo ilipofufuka ile kesi ya binti kutekwa, jitihada za polisi zikagongwa mwamba kumpata. Sasa amepatikana na inasemekana alikuwa ametekwa na marehemu Beka!! Betty akahitajika kwa namna yoyote kituo cha polisi. Aweze kuthibitisha kutekwa na kisha kubakwa, na huenda atakuwa na maneno ya kuongezea juu ya kutekwa kwake. Na maneno hayo yangeweza kuwa mwanga mkali wa kesi hiyo ya aina yake iliyohusisha watu wengi na wenye vyeo vyao serikalini.



    MOROGORO MJINI

    WAKATI ULIOPO

    ILIKUWA ni kawaida ya Fonga kutoka nje kwa ajili ya kununua chakula na mahitaji mengine wakati Joyce alikuwa mtu wa kukaa ndani tu katika nyumba ya kulala wageni ambayo walikuwa wamepanga kwa malipo ya juma moja. Hata siku hii ya aina yake ambayo Fonga alikuwa ameagizwa vitumbua na maandazi ilifanana na siku nyingine zote zilizopita. Joyce ambaye alikuwa ameridhia hatimaye Fonga kuwa mpenzi wake bila kipingamizi japo waliahidiana kuwa watakapopata uhuru waende kupima afya zao, alikuwa amejibweteka kitandani huku kanga mpya aliyonunuliwa na Fonga ikiwa haijamstiri vizuri mwili wake. Fonga aliifikisha alichoagizwa huku akimtengea Joyce vitumbua na soda ya kopo ambayo ilikuwa chaguo la Joyce. Joyce hakuwa na haraka ya kula, aliendelea kujivinjari kitandani kwa dakika kadhaa kisha akainuka na kuisafisha mikono yake kabla hajaanza kusosoa alicholetewa. Alipokua akinyanyua kitumbua cha pili kutoka katika gazeti ambalo lilitumika kufunga vitumbua vile alivutiwa na alichokiona. Aliona jina linalofanana na la rafiki yake kipenzi, Betty. Kwanza hakutilia maanani kuisoma habari ile ndefu inayoambatana na jina la Betty. Lakini mara umakini ukaongezeka baada ya kuona jina jingine, Isaya mara akaona Beka na kisha Akunaay. Hapa kitumbua hakikulika, akamwita Fonga na kumwonyesha juu ya ile habari. Fonga naye akavutika kuisoma. Ilimuhusu Betty ambaye alingojewa kwa hamu kumwezesha mzee Akunaay kubaki huru kwa ushahidi wake thabiti kuwa alibakwa na mzee Beka ambaye ni marehemu tayari. Baada ya kuisoma wote wawili wakabaki kimya!! Joyce akiwa kimya akistaajabu kuwa kumbe Betty yu hai! Lakini akizizima baada ya kusikia kuwa rafiki yake huyo alibakwa na Beka, kama Beka alimbaka bila shaka hakutumia kinga, na Betty ni muathirika hivyo aliondoka na virusi kiuhakika. Na baada ya hapo akamwingilia Joyce kimwili, japo alitumia kinga. Joyce aliingiwa na baridi kali!!! Baridi ya uoga. Uoga wa kujitambua kuwa yu marehemu mtarajiwa. Fonga yeye alikuwa kimya akisubiri kauli ya Joyce ambaye ndiye alikuwa na uchungu wa dhati juu ya rafiki yake huyu.

    DAR ES SALAAM

    SIKU MBILI NYUMA

    JOYCE na Fonga walikuwa katika nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya chini kabisa mathalani ‘mbavu za mbwa!’. Fonga akiwa na uzoefu wa simulizi kadha wa kadha alizopata akiwa gerezani kutoka kwa wafungwa wa kesi za ujambazi na unyang’anyi alijifunza namna ya kukwepa mkono wa dola ama adui kwa kujihifadhi mahali ambapo hatarajii unaweza kujihifadhi. Joyce akawa mtiifu akafuata kila alichoelekeza Fonga. Ni katika nyumba hii ya kulala wageni yenye hadhi duni, Joyce na Fonga walifungua begi ambalo kila dakika lilikuwa mgongoni mwa Joyce baada ya kulitwaa katika nyumba ya Akunaay ambayo ilisemekana Betty alikuwa ametekwa. Pesa hizo alizitoa Beka kwa hiari yake baada ya mambo kumuwia magumu. Hizo zilikuwa pesa kwa ajili ya malipo ya vijana wake baada ya kumaliza zoezi zima la kufanikisha kumteka Betty na hatimaye Joyce kuingia mikononi mwake kama mpenzi wake. Fonga ambaye alikuwa amerejea katika hali yake ya kawaida alizihesabu pesa zile na kufikia makadirio ya shilingi milioni kumi na nane Pesa nyingi sana kwa wakati huo. Fonga akatabasamu na kujaribu kumshirikisha Joyce juu ya pesa zile lakini uso aliokutana nao haukuonyesha kujali kuhusu pesa hata kidogo. Joyce aliamini kwa kuzifurahia pesa zile ni kufurahia moja kwa moja aidha kifo ama kupotea kwa rafiki yake kipenzi, Betty. Joyce hakutaka kuonyesha unafiki wowote mbele ya Fonga bdala yake alimwambia moja kwa moja kuwa hana furaha bila Joyce.

    Tabasamu la Fonga likayeyuka na kisha akajawa na mashaka na fadhaa. Akamtazama Joyce usoni, hapa akapata neno la kusema. “Joyce mpenzi wangu, umekuwa shuhuda tangu mwanzo tumejaribu tukiwa bega kwa bega kumtafuta Betty, usidhani ninafurahia kumkosa lakini tazama hali ilivyokuwa Joy, kama asingekuwa Husna huenda tungekuwa tumekufa na asingepatikana wa kutambua nini kimemsibu Betty. Sikia Joy hapa kitu cha msingi ni kuangalia namna nyingine ya kumtafuta Betty lakini kwa wakati huu hatutakiwi katika mji huu Betty. Nawajua polisi vizuri, nadhani nilikusimulia mkasa ulionikumba hadi nikafungwa jela. Sasa tujiweke mbali huku tukiangalia hatua kwa hatua ya tukio hili kabla hatujaamua tena kuingia kumtafuta Betty. Kitu kimoja ambacho unatakiwa kujua ni kwamba kwa sasa hivi tukijitokeza hadharani ujue kabisa tuna kesi ya kujibu. Kesi ya kumteka nyara mheshimiwa mbunge na mauaji yote yaliyotokea mbele ya macho yetu nasi tutahusishwa. Sasa jiulize hivi tukiwekwa rumandfe tutakuwa na uwezo gani tena wa kumtafuta Betty?” Fonga alimaliza kutoa maelezo hayo, akanyanyua uso na kumtazama Joy, sasa alikuwa amebadilika na maneno yale yalikuwa yamemuingia haswa. Wakabadili mada!! Mwisho wakafikia makubaliano. Asubuhi iliyofuata wakadamka alfajiri na kukwea mabasi yaendayo Morogoro. Joyce na Fonga wakawa wakimbizi katika nchi yao wenyewe.

    WAKATI ULIOPO

    Wakiwa na siku mbili mjini Morogoro maeneo ya Kihonda ambapo walikuwa wamejihifadhi kwa mara nyingine katika nyumba ya kulala wageni ndipo linatokea tukio la Joyce kukutana na habari kuhusiana na Betty. Sasa yu kimya na Fonga anangoja kauli yake!! Joyce anatumia dakika kadhaa kufikiria, hapa unamrudia mlolongo wa matukio yote. Hasahasa tukio la kujitoa muhanga kwa ajili ya rafiki yake kipenzi na kumfichia siri nzito juu ya gonjwa lake hatari. Kisha akakumbuka pia alikuwa na mtihani wa kumzuia Betty asije kumwambukiza Isaya Ukimwi, na hapohapo alikuwa na jambo zito kabisa mkononi mwake, elimu. Alihitaji kuitetea elimu yake ipasavyo. Sasa alikuwa anakaribia kupoteza kila kitu alichokuwa anajaribu kukitetea.

    1. Penzi la Isaya; hili alijipa asilimia miamoja kuwa hana uwezekano wowote wa kulipata, na hakuwa na haja na penzi la mwanaume ambaye baba yake anajishirikisha na vitendo viovu. Joyce alikumbuka yule bwana aliyewateka na kumfyatua risasi Mark alidai kuwa aliagizwa na mzee Akunaay kufanya yale yote ambayo alikuwa anayafanya. Joyce akakiri kuwa Isaya hakuwa riziki yake.

    2. Masomo; licha ya kwamba alikuwa anayo ruhusa kutoka chuoni na angeweza kurejea na kupokelewa, lakini angeweza vipi kusoma bila kuwa na amani moyoni, angeweza vipi kusoma wakati Fonga amemwambia kuwa na wao watakuwa na kesi kubwa ya kujibu iwapo tu watatiwa mikononi mwa polisi. Hili nalo likazua utata.

    3. Kudumisha urafiki wake na Betty, hili nalo akaliona likielekea ukingoni. Maana ilionekana dhahiri kuwa Betty yupo tayari kusimama upande wa kumkomboa baba mkwe wake yaani mzee Akunaay ambaye gazeti lile lilitaja kuwa kauli ya Betty pekee nd’o ambayo itamuweka huru moja kwa moja huku kesi ikibaki kwa marehemu mzee Beka. Joyce yeye alikuwa kinyume na Betty japo hawakuwa wameonana na kuzungumza, lakini Joyce hakuwa upande wa Akunaay, masikio yake hayakumdanganya hata kidogo. Hata Fonga alikuwa shahidi wa kulitambua jina la Akunaay japo hakuwa ametambua kama ndiye baba yake Isaya. Joyce akauona kwa mara ya kwanza upinzani wa waziwazi dhidi ya rafiki yake iwapo tu ataendelea na utetezi wake kwa mzee Akunaay. Hapa ndipo Joyce akakiri kuwa wahenga hawakuwa wanafiki waliposema mshika mbili moja humponyoka lakini huenda hii ingeweza kuwa heri kwake. Yeye alitakiwa kusimamia katika msemo wa ‘mtaka yote kwa pupa hukosa yote’. Naam! Joyce alikuwa anaelekea kukosa kila kitu alichojipangia yeye. Hapa pia akakiri kuwa ‘mipango si matumizi’. Alichopanga yeye kimeshindikana kutimia. Anafanya nini sasa? Alijiuliza na aliamini kuwa hata Fonga ambaye alikuwa kimya alikuwa akingojea kauli yake!!! Ghafla Joyce akazungumza. “Fonga, nadhani nirejee Dar es salaam. Ujue huyo Akunaay akiwa huru na kisha agundue kuwa tunatambua siri yake atatusumbua sana, nadhani unajua kuwa ni waziri hivyo atatufanya lolote atakalo. Fonga sitaki huu uwe mwisho wa elimu yangu sitaki kabisa maisha yangu ya uyatima yaishie hapa. Lazima nifanye kitu hapa.” Alizungumza kwa hisia kali Joyce. Fonga akamtazama Joyce kisha akamjibu, “Usemalo Joyce ilimradi unaona lipo sahihi, nalibariki. Lakini nakusihi kuwa makini sana na kauli zako huko uendapo. Usijiumeume, kama ni kusema sema kweli. Neno moja nakusihi, kabla hujaenda huko lazima uundwe uongo mtakatifu! Uongo mtakatifu..” alisita Fonga kisha akamtazama usoni Joyce, kisha akaendelea “neno kuwa ‘tulimteka Beka’ liondoke kichwani mwako, neno ‘tulienda na Beka Chamanzi’ liondoke kabisa maana litakufunga…” “Sasa naenda kusemaje kule jamani!!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tupa shutuma zote kwa marehemu, kiri jambo moja mbele ya hadhara kuwa marehemu aliwahi kuwa mpenzi wako, lakini mlitengana. Baada ya rafiki yako kutoweka ukaamua kumwona kwa msaada wowote iwapo itabidi. Ni hapo ndiupo ulipotambua kuwa kuna jambo anajua kuhusu tukio hilo. Baada ya kukubali kurudisha mahusiano akahitaji kufanya mapenzi na wewe na hapo ndipo mlipotekwa na watu msiowajua. Sasa hapo unaweza kuendelea na simulizi ya Chamanzi, wakati wa kuzungumza jifanye hujui lolote kuhusu mimi. Wala humtambui Mark, lakini kikubwa mtambue yule mwanaume aliyedai ametumwa na Akunaay kumuua mzee Beka na kisha kuwaua ninyi wote. Ulifikia hapo elezea ukombozi kutoka kwa Husna ambaye haufahamu anahusika vipi katika huu utata. Hapo utakuwa umeunda uongo mtakatifu kabisa na utakuweka mahali salama. Cha msingi kumbuka kucheza na maneno, usiwe muoga na usiwe muongeaji sana.” Fonga alimaliza kutoa nasaha zake. Akamkatia Joyce fungu kubwa kwa ajili ya safari hiyo. Siku iliyofuata akaondoka kurejea jijini Dar es salaam kukutana na mtihani mkubwa katika maisha yake!! Mtihani wa kupingana na Betty kwa mara ya kwanza katika maisha yake!!

    ****

    WAKATI Joyce akimezeshwa uongo mtakatifu na kamanda Fonga. Jijini Dar es salaam, Isaya alimpa Betty kila alichokuwa anataka ilimradi tu amtetee mzee wake na aweze kuachiwa huru. Akaunti ya Betty ilikuwa ina shilingi milioni kumi kwa ajili tu ya neno lake moja kuthibitisha kuwa alitekwa na Beka na kisha kubakwa na katika kubakwa Beka alimtaja Akunaay kuwa atamuua baada yake. Kauli zake hizi zingemweka pabaya marehemu Beka na kujikuta lawama na aibu vikimfuata kaburini. Maswali makuu japo hayakuwa yamepata utatuzi, Inspekta Ndayanse ambaye amepararaizi alifuata nini Chamanzi, Assistant Super retendant naye alifuata nini kule. Mkewe alisema kuwa alipigiwa simu na Ben, Ben sasa ni marehemu. Huu ukawa utata, akaongezea kuwa kabla ya hapo alipigiwa simu na mke wa Ndayanse. Mke wa Ndayanse alipoulizwa akadai ni wivu ulimtuma kuhisi Ndayanse anaenda kwa mwanamke mwingine. Huyu hakuwa na msaada mkubwa!! Nani wa kuunganisha matukio haya sasa. Lipatikane jibu sahihi. Akunaay alichokuwa anajaribu kukikwepa ni kuingia katika mlolongo huu wenye utata. Sasa alitakiwa Betty athibityishe kuwa wakati Beka anambaka alimweleza mipango yake kuhusu kumuua Akunaay na kisha ile nafasi ya uwaziri apewe yeye baada ya kifo cha waziri huyo. Sasa Betty amepokea pesa na anatakiwa kusema uongo mwingine mtakatifu pia!!! Joyce amemezeshwa uongo wa kujilinda na Betty naye amemezeshwa uongo wa kumlinda Akunaay.



    HEKAHEKA ZA MWISHO USIKU JIJINI DAR ES SALAAM.

    KIGIZA kilikuwa kimetanda na kuongezeka makali yake kutokana na shirika la umeme kuwa katika mapumziko katika usambazaji huduma!!! Umeme ulikuwa umekatika. Giza hili liliwaruhusu machangudoa kubadili muda wa biashara yao badala ya kuwa usiku sana wakausogeza hadi kuwa saa mbili tu za usiku!!

    Na muda huo tayari walikuwa kazini.

    Giza hili lilisababisha baadhi ya maeneo kuwahi kunyamaza na kuwa tulivu hali ambayo ilimstaajabisha Joyce. Aliishutumu saa yake kuwa huenda inamdanganya!! Lakini ilibakia kuwa kweli ni saa mbili za usiku. Joyce akarejea kitandani, akaichukua simu yake na kuendelea kubofya hapa na pale pasi na sababu ya msingi!! Ilimradi tu kubofya. Wakati akiendelea na mchezo huo ndipo akakumbuka kuwa siku iliyokuwa inafuata alikuwa na jukumu kubwa moja, la kutumia uongo mtakatifu ili kumwingiza Akunaay matatani na kisha yeye kubaki huru. Alipokumbuka jambo hili akakumbuka kuwa alikuwa akijitayarisha pia kupambana na rafiki yake kipenzi. Jina la Betty likamshambulia ghafla kichwani mwake, kana kwamba analisikia ama kulifikiria kwa mara ya kwanza. Joyce akainuka na kukaa kitako. Akaangaza huku na huku akakutana na chupa yake ya maji ya kunywa, akaitwaa. Akaginda mafunda mawili makubwa.

    Funda la tatu akasukutua na kisha akaenda kutema katika choo cha ndani kwa ndani. Huko huko akapata wazo la kujimwagia maji, alikuwa anahisi uchovu. Akafungulia bomba la maji, akatoa nguo yake moja iliyobaki mwilini. Akaoga!! Baada ya hapo akili yake ikamtuma kwenda kumtafuta Betty.

    Alikuwa amevamiwa na fikra za ghafla kuwa itakuwa jambo la ajabu na la aibu sana yeye kugombana na rafiki yake kipenzi ghafla bin vuu mahakamani ama popote pale wakati walikuwa hawajaonana siku nyingi. Aliamini kuwa hali ya kutukanana ama kukwazana na Betty ambaye aliukwaa Ukimwi kwa ajili yake ingeweza kuyaathiri maisha yake kifikra milele.

    Na kama angeathirika kifikra bila shaka hata elimu yake isingekuwa na maana tena. Ndio!

    Angeweza vipi kusoma ilhali amekosana na mwanamke ambaye alikuwa shujaa wake hadi hapo alipofikia? Angeweza vipi kupata maksi za kumvusha kwenda hatua nyingine wakati akili yake itakuwa imelala usingizi wa pono? Jibu likawa hapana!!

    Kama ni kugombana na Betty basi wagombane wao kwa wao wakiwa wawili tu! Na kisha wapate suluhisho wakiwa wawili hivyo hivyo. Hilo likawa jibu sahihi kwa Joyce!! Akaufungua mlango, akatoka nje!! Wakati huu alikuwa amejivika hijabu na nikabu!!

    ***

    Aliyafuata mawazo yake, akaingia mitaa kadhaa kisha akatwaa teksi na kuamuru impeleke chuo kikuu cha Dar es salaam. Joyce alikuwa ameamua kumvamia Betty ambaye aliamini kwa namna yoyote atakuwa nyumbani kwa Isaya. Alipoikanyaga ardhi ya chuo kikuu ambacho bado alikuwa ni mwanafunzi lakini si mwanafunzi huru akajisikia kutetemeka na ni hapo alipogundua kuwa alikuwa anaogopa sana!! Lakini kwa sababu ulikuwa ni usiku haikumsumbua sana hali ile. Akapenya huku na kule hadi alipozifikia Hosteli alizokuwa akiishi Isaya!! Akawauliza watu wawili katika namna ya kuwafanya wasiingiwe shaka, mmoja hakujua lolote. Mwingine akamueleza Joyce kuwa Isaya alihama na hakuwa akiishi tena pale hosteli japo mizigo yake ilikuwa katika chumba chake kilekile. Ni huyu aliyemwelekeza Joyce nyumba ambayo Isaya alikuwa akiishi kwa wakati ule. Hata kabla hajamaliza kumuelekeza tayari Joyce alikuwa ameitambua nyumba hiyo ambayo Isaya aliwahi kumpeleka wakati wa urafiki wao. Joyce akashukuru kisha akaondoka tena na kutwaa taksi nyingine. Akaelekea Sinza!! Wazo lake likiwa lilelile kuzungumza na Betty na kuwa na msimamo mmoja kabla hapajapambazuka na kukutana mahakamani!!

    Foleni za hapa na pale hazikusumbua sana mara kwa mara dereva alikuwa mjuaji wa kuhama njia huku na kule, na kadri alivyokuwa anahama aliwapa akili na madereva wengine kumfuata kwa nyuma ili wawahi kufika. Walipofika Sinza Mori, Joyce akashuka na kufanya malipo. Hapo akaanza kwenda kwa mwendo wa miguu hadi akaifikia nyumba ambayo aliamini kuwa kama Isaya yumo basi na Betty atakuwa humo. Sijui itakuwaje nisipomkuta??

    Halafu hata Fonga sijamwambia kama nakuja huku!!

    Tabia mbaya kweli Joyce!! Alijisema!! Hatimaye akalifikia geti, akabonyeza kengele. Ikaita sana bila geti kufunguliwa!!

    Akabonyeza tena mara ya pili na mara ya tatu ndipo geti likafunguliwa!! Aliyelifungua hakufanania na mlinzi wa getini.

    “Nikusaidie nini dada!!” aliuliza huku akionyesha kutishwa na uvaaji wa Joyce. “Namuulizia Isaya!”

    “Isaya? Wewe ni nani?”

    “Rafiki yake tu!!”

    “Muda huu hauwezi kuonana naye dada labda kesho.”

    “Nina mazungumzo naye kuhusiana na baba yake, usiponiruhusu kuingia na kesho mambo yakimuharibikia akijua ulinizuia atakuua.” Joyce alitisha.

    “Mambo ya baba yake….aaah kwani ukiniambia mimi kuna ubaya.?”

    “Ok! Nimeinakiri sura na sauti yako, nitakukumbusha wakati anataka kukuua kwa uzembe wako wa kushindwa kuniruhusu nionane naye.” Alisema kwa hasira kisha akaanza kuondoka.

    “Dada samahani njoo basi kwanza, njoo!!” sasa alibembeleza yule kijana. Joyce akasimama lakini hakugeuka wala kurudi nyuma.

    “Unasemaje? Ishu ni moja tu unamuita ama la!”

    “Njoo, namuita.” Alijibu, sasa Joyce alirejea getini. Yule bwana akapiga simu. Akatoa mael;ezo mafupi, hatimaye Isaya akatokea akiwa anasindikizwa na wanaume wengine wawili waliojazia vifua vyao. Joyce akawatambua mara moja kuwa hao waliwahi kuwa walinzi wa mheshimiwa Akunaay Zingo. Walinzi wa baba yake Isaya. Wanamlinda hadi Isaya!! Maajabu!!

    “Ondoa nguo yako hiyo usoni tafadhali” waliamuru walinzi wale, wakati huo Isaya akiwa nyuma yao. “Isaya, nahitaji kuzungumza na wewe…”

    “Aaah Kidoti!!” Isaya alihamaki hatimaye!! Ni ujio ambao hakuutegemea hata kidogo kwa wakati huo, akawasukuma walinzi pembeni akamkabili Kidoti. Sasa Joyce aliweza kuondoa nikabu yake. Akkaribishwa ndani, akaingia katika chumba ambacho alikuwa yeye na Isaya pekee.

    “Isaya, sihitaji maongezi na wewe nahitaji kuzungumza na Betty kwanza, naamini upon aye na kama hayupo basi sidhani kama nahitaji kusema neno na wewe kwa sasa.” Joyce alizungumza huku akiwa amemkazia macho Isaya. “Betty aaah!! Yupo mbali lakini sio hapa.”

    “Kama hakuna uwezekano wa kuzungumza naye nd’o kama nilivyosema. Sioni pia umuhimu wa kuzungumza na wewe. Naweza kwenda Isaya.”

    “Lakini umesema kuna mambo wataka kuzungumza kuhusu mzee wangu Kidoti.”

    “Sikusema kama hayo mambo nahitaji kuzungumza na wewe Isaya, nahitaji kusema na mkwe wake. Kama hayupo basi haina haja ya mimi kuwa hapa.” Alijibu Kidoti huku akianza kuifunga tena nikabu yake. Isaya akabaki kuduwaa asijue nini cha kusema.

    “Hebu ngoja kidogo Joyce!! Alisema Isaya kisha akatoka nje na alirejea dakika mbili baadaye. Hakuwa peke yake, sasa alikuwa na Betty ambaye alikuwa mchangamfu!!

    Joyce akaruka mbiombio na kwenda kumkumbatia Betty, Betty japo hakuiona sura ya Joy ambaye alikuwa amejitanda nikabu tayari, lakini alipomkumbatia tu na kuinusa harufu yake, machozi yakamtoka papo hapo. Kama walivyokumbatiana siku ambayo Joyce na Betty wanaonana kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam ilikuwa hivi hivi siku hii. Isaya na wale walinzi wakabaki kuwashangaa. Baada ya kupeana ple za hapa na pale waliomba faragha.

    Walinzi wa Isaya wakatoka na kuwaacha Joyce na Betty huru waweze kuzungumza.

    ***

    Isaya Akunaay na wale walinzi wa baba yake walikuwa katika chumba kingine cha siri, huku walikuwa wakifuatilia tukio linaloendelea katika chumba walichowaacha Betty na Joyce. Picha zilikuwa zinaonekana na sauti ilisikika vyema japo walikuwa wakijaribu kunong’onezana. Maskini wasichana hao hawakujua kama walikuwa wametegewa mitambo ile. Joyce akamweleza kwa makini na tahadhari juu ya wao kumteka Beka na hatimaye Akunaay kuagiza Beka auwawe ilimradi aweze kuwa huru.

    “Yaani aliagiza Beka afe na sisi wote tuliokuwa tumetekwa tuuwawawe. Akunaay ni muuaji Betty, wewe ni rafiki yangu na sijawahi kukuficha kitu chochote maishani mpenzi wangu, asingekuwa Husna mimi ningekuwa marehemu lakini ningekufa nikiwa nakusaka wewe mpenzi…Betty nilipagawa nilipoona kanga yako pale chumbani mpenzi. Nikajua wamekuua, nilifadhaika sana.” Wakati akiongea haya, Betty alikuwa akitokwa na kilio cha kimyakimya, alimtazama Joyce kama shujaa wake. Hakuwahi kujua kama Joy aliweka maisha yake hatarini kiasi kile kwa ajili yake. Sasa alikuwa akisikia mambo ya ajabu, jinsi Joy alivyojiweka katika mdomo wa kifo kwa ajili ya urafiki.”

    “Joyce, mimi nilitoroka na sikuwahi kujua kwa nini nilitekwa, mimi nikadhani ni mapedeshee wangu wamenifanyia mtimanyongo kumbe Beka alikuwa anakutaka kimapenzi? Jamani watu wabaya sana, mimi hakunifanyia ubaya wowote hadi nikashangaa…” kabla hajamaliza Joyce akamkatisha, “Lakini magazetini wanasema umebakwa na Beka??”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Joyce, kama usivyoweza kunificha jambo lolote kuhusu wewe nami siwezi kukuficha. Joy mimi sijabakwa, hilo la kubakwa naweza kuwa nililiunda bahati mbaya tu kwa ajili ya ukombozi. Ujue nini Joyce nilijikuta nampenda Isaya, sikutaka na yeye awe katika ile orodha. Basi nilikuwa sijawahi kumpa penzi langu. Nd’o kwa mara ya kwanza baada ya mimi kutoroka nikakutana naye faragha akataka mambo. Nikamwonea huruma nikamlaghai kuwa Beka alinibaka na kunitesa, nikamlazimisha atumie kondomu. Si unajua wanaume tena wanavyopenda kujihakikishia tu usalama wakishikwa hamu zao. Ndo Isaya kuvaa kondomu mwenzangu.” Betty naye alimsimulia Joyce. Joyce aliposikia neno kondomu akajipa imani kuwa afadhali Isaya hatakufa kwa Ukimwi!! Hakujua Isaya alijiwekea ujanja ujanja wake akapasua kondomu. Mazungumzo yakaendelea!! Joyce na Betty wakajikuta wamekuwa wamoja.

    “Mimi nina pesa za kutosha tayari, nitaharibu ushahidi kisha naenda zangu Ukala.”

    “Nami pia nitasema niyajuayo….” Joyce alimalizia.

    Na hapo chumba kikawa kimya!!

    Huku katika chumba cha akina Isaya waliokuwa wakifuatilia filamu hiyo moja kwa moja, kila mmoja alikuwa akitetemeka. Hawakuamini watoto wa kike wanaweza kuficha siri nzito kama ile. Isaya alikuwa amepagawa, kwanza hakujua orodha aliyoizungumzia Betty ni ipi, kwasababu kama kujitoa kwenye orodha ni kutumia kinga, basi yeye alikuwa kwenye orodha bado. Na pili akajiuliza ni kwa namna gani baba yake ameweza kuwa gaidi kiasi hicho na kufikia hatua ya kuagiza watu wamuue mzee Beka na kisha wawaue wote waliomzunguka?? Kichwa kikamuuma Isaya!! Mara akalegea zaidi alipobaini kuwa Betty na Joyce wameamua kuwa kitu kimoja na kumsaliti mzee Akunaay. Isaya akapoteza fahamu!!

    Wale mabaunsa wawili wakakimbilia kule chumbani, mlango ukapigwa teke. Ukaachia wenyewe. Bunduki mbili ziliwatazama akina Joyce. Kisha ikabaki moja baada ya mmoja wao kuihifadhi kiunoni. Akaanziwa Joyce kupigwa teke la mbavuni kisha Betty akakutana na vibao vitatu vikali usoni.

    “Pumbavuu zenu kabla hamjaenda kupeleka umbea wenu mahakamani mnaanza kufa kwanza shenzi type!!” alikaribia yule mlinzi huku akishusha mkong’oto matata kwa wasichana wale. Joyce na Betty hawakupata nafasi ya kujitetea hata kidogo. Yule jamaa ni kama alikuwa amevurugwa na madawa mabaya kichwani na aalikuwa akitambua vyema wapi pa kupiga ili kuleta maumivu makali. Bila shaka alikuwa amesomea mambo hayo!!

    Sasa Joyce alikuwa akiamini kuwa lazima atakufa na Betty alikuwa amepoteza fahamu na damu zikimvuja mdomoni na katika fuvu la kichwa alikuwa amepasuliwa kwa kitako cha bunduki!! “Tu….sa..me..ee.e..hatu….ta….h atu..se…mi teena..” alilalamika Joyce kwa sauti ya chini huku akitema damu. “Fonce usimsikilize msichana wewe wajinga hawa watamchoma mzee.” Alisisitiza baunsa aliyekuwa na bunduki!! Fonce akawa katika kuandaa pigo la mwisho.

    “Namvunja shingo huyu….” Fonce akajiapiza. Sasa alikuwa amenuia. Lakini hakuweza kupiga hatua yoyote mbele!! Kabl;a hajasikia amri matata.

    “Tulia kama ulivyo ama tetemeka kidogo nisambaratishe matako yenu mbwa nyie!!” Fonce badala ya kutii amri akatetemeka na kugeuka nyuma. Ebwana eee!! Kumbe kuna watu wehu kuliko Fonce na wakisema wanamaanisha, bunduki ikakohoa. Kama alivyodai ni kweli alimaanisha. Akafyatua matako magumu ya Fonce. Risasi ikapenya hadi katika sehemu zake za siri ikampasua vibaya. Alipata nafasi ya kulia kama mtoto mdogo lakini hakuamka kamwe!! “Na wewe tetemeka tena nikuhanithi bloody fool!!!” amri nyingi isokuwa na utani hata kidogo ikatoka. Utaweza kufanya lolote wakati aliyeambiwa atasambaratishwa amekiuka masharti na kusambaratishwa kweli? Wakati haya yanatokea ilikuwa yapata saa nne na nusu za usiku!!



    Yule mlinzi aliyesalia alikiri kuwa amekamatika, mwenzake hakuwa na uhai tena pale chini alipokuwa na damu ilikuwa imetapakaa.

    Uoga wa kufanywa kama alivyofanywa mwenzake ukamtawala na kujiuliza huyo aliyemwekea kipingamizi cha kutotikisika alikuwa amejidhatiti vipi hadi awe na amri kuu kiasi kile, lakini tatizo hakuruhusiwa walau kugeuka na kuuliza jambo lolote lile. Mtekwaji akaamua kuvuta subira zaidi huenda akili ilikuwa haijapata utulivu.

    “Nyinyi ni akina nani na mlihitaji nini kutoka kwa wasichana hawa!!” sauti ikakoroma tena.

    “Walinzi wa nyumba hii.”

    “Na mlikuwa mnataka nini kwao?” swali jingine. Yule mlinzi kimya.

    Ukimya wake ukasababisha apigwe na kitako cha bunduki mgongoni, akatokwa na yowe la hofu.

    “Tulitaka watuambie….” Alijibu huku akitetemeka.

    “Wawaambie kitu gani?” akaulizwa na kukaa kimya tena.

    “Zedi!! Mtoe mtu wetu tuondoke naye, huyo mwingine hatuhusu!!” alizungumza yule aliyeikamata bunduki, mwenzake akapita kwa umakini mkubwa sana. Akamtambua Joyce. Akamsikiliza mapigo yake ya moyo, bado alikuwa hai!! Akajaribu kumzoazoa, akazidiwa uzito. Akachukua simu yake na kuanza kubofya bofya.

    Mlinzi akamuona jinsi alivyojisahau, sasa akaamua kucheza pata potea, alikiona kivuli cha bunduki iliyokuwa imemuelekea na aliamini mshika bunduki alikuwa hamtilii maanani ten na badala yake anasimamia zoezi lile la mwenzake kubeba maiti.

    Mlinzi hakupoteza dakika zaidi, akarusha teke farasi katika mahesabu ya kuipata ile bastola akitumia kivuli chake.

    Barabara!! Akaipata vyema, alijua kuwa hawezi kupambana na watu wawili kwa pamoja, na alitambua pia akifanya kosa la kuikimbilia ile bunduki na akaikosa basi atakuwa amehalalisha kifo chake. Hapo akajirusha na kumfikia Zedi akampiga teke la tumbo, simu aliyokuw ameshika ikaruka na kusambaratika kisha akamkaba shingo yake vyema kama anayekaribia kuua.

    “Ukifyatua navunja shingo yake!! Sina utani.” Sasa mlinzi aliweza kukoroma. Yule mtekaji aliyeitwa kwa jina la Joshua aliingiwa na kiwewe, hakujua yapi ni maamuzi sahihi. Kweli Zedi alikuwa amewekwa katika kabali ya aina yake, kabali ambayo imewekwa kiufundi kabisa.

    Wakabaki kutazamana huyu anatazama mdomo wa bunduki na mwenzake anatazama macho yanayotazangaza harufu ya kifo!! Hali ikawa tata kwelikweli.

    Hofu iliyotanda usoni mwa Joshua ikampa upenyo yule mlinzi kutawala na kisha kuamrisha apendavyo, Joshua akatii ili kuulinda uhai wa rafiki yake.

    Lakini mkwara huu haukudumu sana, hatimaye macho ya Zedi yakapata uhai, alimuona kwa mbali Jaguda akinyata akiwa na bunduki yake mkononi. Zedi akajipongeza kuwa ujumbe alioutuma sekunde chache kabla ya kugeuziwa kibao na yule mlinzi ulifika, na kuhusu suala la umakini hakuwa na wasiwasi hata kidogo dhidi ya Jaguda nd’o maana hata hapo ametumiwa ujumbe wa kuja kusaidia kuubeba mwili wa Joyce na bado amekuja kwa umakini mkubwa.

    Ewalaa!! Alikuwa sahihi, risasi iliyolengwa vyema ilisambaza mguu wa yule mlinzi aliyekuwa akigeuka huku na kule akiwa amemweka kabalini Zedi. Mlinzi akarushwa pembeni na Zedi akaanguka chini huku akipumua kwa fujo.joshua akachanganyikiwa hakujua ni nani aliyerusha risasi ile, lakini Zedi akawahi kumtoa hofu kwa ishara akimweleza kuwa ni Jaduda.

    “Nyie ni akina nani?” sauti ya kike hatimaye iliuliza. Alikuwa ni Joyce.

    “Ooh!! Umezinduka, sisi ni vijana wa Fonga kuwa na amani. Tuliwekwa kwa ajili ya kuangalia usalama wako jijini hapa, tupo nawe tangu uliposhuka Ubungo!! Unaweza kusimama?” alijibu Zedi, huku akijaribu kusimama tena. Yule mlinzi alikuwa anaugulia chini bado kwa maumivu!! Na bunduki mbili zilikuwa zinamtazama.

    Joyce alihisi kama msumari wa upendo ukipasua anga ya moyo wake, yaani licha ya magumu yote anayopitia bado Fonga yupo naye bega kwa bega!! Kwa mara nyingine tena alikuwa amesimama upande wake na alikuwa ameokoa maisha yake, maana bila Fonga hakika angeuwawa. Alisikia maneno ya yule mlinzi ambaye ni marehemu tayari, alitaka kumvunja shingo.

    Yule bwana mwenye Bunduki, alinyanyua simu yake na kumpigia Fonga. Akaiweka katika spika za nje.

    “Bosi wangu nipe habari!!”

    “Kama ulivyohisi bosi haukuwa umekosea, alitekwa na walikaribia kumuua. Tunachoshukuru tuliwahi kabla ya pigo la mwisho.”

    “Wacha weee!! Ni akina nani hao, vipi anaweza kuongea…” aliongea kwa papara Fonga. Joyce akawa anajisikia hatia ikimtawala kwa kumpuuzia Fonga na kujifanya yeye anaweza kila kitu bila msaada wa Fonga!!

    “Kwa sasa hali si shwari hapa, tupo eneo la tukio ngoja baadaye kidogo. Cha muhimu malizia malipo yetu mkuu maana ni kama vile tumemaliza kazi.”

    “Usijali, weka imani kama tulivyoanza tumalize hivyohivyo!! Kesho nakuja jijini. Nadhani mnadai milioni na nusu!!”

    “Bila shaka bosi wangu!!” alijibu Joshua kisha akakata simu. Na wakati huohuo zikaanza kusikika vurugu na michkato kadha wa kadha getini kisha vishindo kuizunguka nyumba ile.

    “mmekwisha wanaharamu wakubwa nyie!!” mlinzi aliyekuwa pale chini aliwaambia akina Zedi huku akicheka kwa dharau.

    Kitu ambacho hawakujua ni kwamba yule mlinzi ambaye walikuwa wamempuuzia kwa sababu hakuwa na uwezo wa kusimama wala kupambana tena, akiwa pale chini alifanikiwa kubonyeza kitufe fulani ambacho ni maalum kwa ajili ya ulinzi na usalama. Kitufe kile hupeleka taarifa kwa shirika la ulinzi lenye dhamana ya kulinda nyumba ile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa ulinzi ulikuwa umewadia tayari!! Na bado walikuwa ndani ya nyumba ile. Wasingeweza kupita wakiwa na Joyce begani ama vyovyote vile, hivyo walitaka kuweka usalama kwanza kabla hawajapita.

    Joshua na Zedi wakiwa na silaha mkononi walinyata hadi nje. Huko wakakutana na mzunguko mkali katika nyumba ile. Kupitia upenyo wa dirisha Jaguda naye aliona viwiliwili. Hapo akafyatua tena miguu ya yule mlinzi, kisha akaiweka sawa bunduki yake, akapitisha dirishani akamfyatua mwanaume mwenye mavazi ya ulinzi ambaye alikuwa getini. Risasi ile ikamtupa hadi nje. Wenzake wakabaki kuduwaa wasijue ni wapi shambulizi hilo limetokea. Jaguda alifanya vile ili wahamaki kisha kujiweka pamoja aweze kujua idadi yao, kuhusu nje hakuwa na mashaka dhidi ya Joshua na Zedi.

    Lahaula!! Walikuwa wengi sana!!

    Hapa Jaguda akaamua kutumia ile kauli ya kila mmoja na aiokoe nafsi yake, akanyata kutoka nje akiwaacha Joyce, Betty na yule mlinzi katika hali zao tete.

    Aliwakuta wenzake wakiwa wameduwaa mlangoni katika hali ya kuviziana na maadui wale.

    Songa mbele!! Alimrisha Jaguda!! Na hapo ukazuka mpampano wa kurushiana risasi, kila mmoja katika ustadi wa aina yake!! Walinzi kutoka shirika hilo ambao hawakuzoea kupambana kwa bunduki walikosa umakini hivyo kumpa fursa Zedi na Jaguda kuwaangusha mmja baada ya mwingine.

    Walipolifikia geti ndipo Joshua alipatwa na shabaha ya kifua, Zedi aligeuka na kukutana na uso wa aliyemdungua Joshua. Bila kungoja alimfyatua risasi nne za kichwa kwa hasira na kisha wakatokomea wakimwacha Joshua akihaha kutafuta pumzi za mwisho.

    Zedi na Jaguda wakatoweka!!

    Joshua akaaga dunia !!

    Huku ndani yule mlinzi akiwa hawezi kutumia tena miguu yake alijivuta kuelekea chumba kingine lengo lake likiwa moja tu kujipatia bunduki mapema ili aweze kuwamaliza Joyce na Betty ili atokomeze ushahidi ambao unaweza kumuweka matatani, akajivuta kiujasiri huku akiugulia maumivu makali katika miguu yake isiyokuwa na uhai.

    Naam!! Akapishana na mwili wa Isaya!!

    Naanza na huyu bwege!! Alijisemea huku akizidi kutambaa kuelekea katika chumba alichoamini kuna silaha anayoweza kuitumia kuangamiza upesiupesi kabla hao walinzi ambao baadhi yao wanamtambua hawajaingia ndani!!

    Akakifikia chumba akahangaika hadi akafanikiwa kufungua!!! Akaangukia ndani na kuzidi kujikongoja akalifikia sanduku akavuta!!

    Haswaa akakutana na bunduki!!

    Akaiweka katika kiwambo cha kuzuia sauti,tayari kwa kuua kimyakimya!! Akauma meno yake kukabiliana na maumivu kisha akaanza tena kutambaa tayari kwa kufanya maanagamizi na kupoteza ushahidi!!

    Alikuwa anaitetea nafsi yake kwa kuondoa nafsi za watu wengine!!

    Kisha kesi ibaki kuwa majambazi walifanya mauaji kisha wakatoweka na kumwachia majeraha makubwa mlinzi wa mbunge aliye rumande,bwana Akunaay!!!!



    Joshua na Zedi wakiwa na silaha mkononi walinyata hadi nje. Huko wakakutana na mzunguko mkali katika nyumba ile. Kupitia upenyo wa dirisha Jaguda naye aliona viwiliwili. Hapo akafyatua tena miguu ya yule mlinzi, kisha akaiweka sawa bunduki yake, akapitisha dirishani akamfyatua mwanaume mwenye mavazi ya ulinzi ambaye alikuwa getini. Risasi ile ikamtupa hadi nje. Wenzake wakabaki kuduwaa wasijue ni wapi shambulizi hilo limetokea. Jaguda alifanya vile ili wahamaki kisha kujiweka pamoja aweze kujua idadi yao, kuhusu nje hakuwa na mashaka dhidi ya Joshua na Zedi. Lahaula!! Walikuwa wengi sana!! Hapa Jaguda akaamua kutumia ile kauli ya kila mmoja na aiokoe nafsi yake, akanyata kutoka nje akiwaacha Joyce, Betty na yule mlinzi katika hali zao tete. Aliwakuta wenzake wakiwa wameduwaa mlangoni katika hali ya kuviziana na maadui wale. Songa mbele!! Alimrisha Jaguda!! Na hapo ukazuka mpampano wa kurushiana risasi, kila mmoja katika ustadi wa aina yake!! Walinzi kutoka shirika hilo ambao hawakuzoea kupambana kwa bunduki walikosa umakini hivyo kumpa fursa Zedi na Jaguda kuwaangusha mmja baada ya mwingine. Walipolifikia geti ndipo Joshua alipatwa na shabaha ya kifua, Zedi aligeuka na kukutana na uso wa aliyemdungua Joshua. Bila kungoja alimfyatua risasi nne za kichwa kwa hasira na kisha wakatokomea wakimwacha Joshua akihaha kutafuta pumzi za mwisho. Zedi na Jaguda wakatoweka!! Joshua akaaga dunia !!

    ***

    Simu kutoka kwa Joshua na vijana wake ilikuwa faraja sana kwa Fonga. Akajipongeza kwa imani yake ndogo dhidi ya Joyce. Ni kweli Joyce alionekana kuwa msichana mwenye msimamo lakini hilo halikutosha kumshawishi Fonga kuwa binti yule atakuwa salama. Akaamua kutumia kiasi fulani cha pesa kutoka katika kitita walichokitwaa katika nyumba ya Mzee Akunaay ambapo Beka aliwakabidhi, pesa ile ikafanya kazi, sasa amepokea simu ambayo imemfanya asijutie kuitoa pesa ile. Joyce alikuwa matatani, hivyo asingechukua hatua za mashaka kama zile bila shaka binti yule angeuwawa. Fonga baada ya kumaliza mazungumzo yale, sasa alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kuingia tena jijini Dar es salaam ili aweze kuwa karibu na Joyce ambaye kwa taarifa ni kwamba alikuwa amejeruhiwa, lakini alikuwa hai. Hapakuwa na mzigo mkubwa wa kubeba! Fonga akazihifadhi zile pesa vizuri huku akizitenganisha mafungu kwa mafungu iwapo kuna lolote baya litakalotokea safarini. Baada ya hapo akaingia kitandani, akautafuta usingizi katika namna ya kuwaza jinsi atakavyoishi na Joyce kama mkewe, akafikiria amani itakavyotawala ndani ya nymba na namna ambavyo atajitoa kwa asilimia mia moja kwa ajili ya msichana anayempenda. “Tena vile yeye msomi!! Anakuwa akienda kazini na mimi naenda kazini, eeh!! Hizi pesa hapa tunafungua biashara yaani hata kama ni kaduka kadogo, mi naenda dukani yeye kazini, nikiwahi kurudi nyumbani mi napika kwani nini? Si ninampikia mke wangu!! Baada ya miezi mitatu tukikubaliana anabeba mimba, hapo tunatafuta msaidizi wa kazi. Tena nitakuwa makini sana maana hawa wasaidizi nd’o huwa wanasababisha ndoa zivunjike yaani, naenda kumchukua mshamba huko kijijini namweka pale…halafu akijifungua sasa mtoto tunamwita nanii…..tuna….” Usingizi ukamtwaa!!

    Simu ilimkurupua kwa mlio mkali majira ya saa kumi na nusu alfajiri, upesi akaingia kuoga. Wakati akiingia bafuni ndipo akagundua kuwa alilala na kuacha luninga ikiwa inapiga kelele bila kuizimisha. Akasonya kidogo kisha akaingia bafuni. Akasafisha kinywa na mwili wake. Saa kumi na moja na nusu alikuwa akimalizia kuchomekea shati katika suruali yake. Akatupa na miwani yake ya jua machoni, alipotanabai kuwa bado kuna giza akaipandisha katika paji la uso. Akaweka begi mgongoni, akaanza kujikongoja kuelekea kituo cha mabasi yaendayo Dar es salaam. Akafanikiwa kulipata gari la kwanza kabisa, akajitwalia tikiti yake. Akachukua nafasi. Saa kumi na mbili kamili, basi likaiacha ardhi ya Msamvu Morogoro!! Safari ya kuelekea jijini Dar es salaam. Kero zikaanza baada ya abiria ambaye anafaa kuitwa mzee alichukua siti upande wa kushoto wa Fonga.

    “Haujambo mjukuu wangu!!”

    “Shkamoo mzee” alisalimia Fonga.

    “Marahaba, naomba nikae dirishani kidogo halafu nitakupisha.” Alisihi yule mzee. Fonga hakutaka kuhoji kulikoni. Akampisha maana alizijua vyema tabia za wazee, kadri umri unavyozidi kwenda wanakuwa wakorofi na wepesi kulalamika.

    Mzee akatoa kimfuko chake, akachomoka na redio maarufu kwa jina la ‘mkulima’ akafungulia huku akiutupa nje waya ambao bila shaka ulitumika kama antenna. Redio ilikuwa inapiga kelele, ajabu mzee hakukerwa.

    “Hiki kipindi cha matukio, mjukuu wangu kikinipita nakosa amani kabisa.” Mzee aliongea kwa furaha. Fonga akatamani kuhama nafasi ile lakini tikiti yake haikuruhusu. Mzee hakujihangaisha kuurekebisha masafa zaidi, akaendelea kutega sikio kwa makini.

    “Eee Mungu wee watu wanauwawa jamani, Tanzania tunaelekea wapi jamani. Looh..yaani enzi zetu..basi tu.” alilalamika peke yake mzee na sasa Fonga aligundua kuwa kinywa chake kilitoa harufu mbaya vilevile. Akajikaza na hakumjibu chochote mzee. Hadi ulipojiri muda wa mzee kuwa rafiki wa karibu!!

    Kila jambo katika maisha lina maana, ilimradi tu wewe uitambue hiyo maana na tilie maanani katika jambo hilo.

    Mzee alikuwa sawa kabisa kuzitafsiri zile kelele kama habari murua, naam!!

    Fonga akasikia habari iliyomshtua, na hakusikia tena zile kelele alizokuwa anasikia awali. Ilikuwa habari kuhusiana na mtoto wa mheshimiwa mbnge na vifo vingine vya kushangaza.

    Mwandishi alikuwa akitoa taarifa moja kwa moja kutoka eneo la tukio. Mtoto wa mheshimiwa Akunaay aitwaye Isaya, mlinzi, wasichana wawili, na wanaume wengine wasiofahamika pamoja na walinzi kutoka kampuni ya Simba security wamehusishwa katika tukio hilo ambalo wakazi wa Sinza wanalihusisha na uhasama unaosemekana kuwapo kati ya kambi ya marehemu mzee Beka na mheshimiwa Akunaay ambaye yupo rumande. Fonga alijikuta akivua miwani yake.

    “Vipi mwanangu!! Yaani hizi siasa hizi. Zinamaliza vijana wetu ona…halafu wakuu wenyewe hawana habari kabisa.” Alizungumza yule mzee huku akimtazama Fonga. Sasa Fonga hakuhisi tena ile harufu kali kutoka katika kinywa cha mzee.

    “Sasa hao wote wamekufa ama?” hatimaye aliuliza.

    “Watakuwa wamekufa maana bunduki zimekutwa eneo la tukio, yaani mjukuu wangu kuwa uyaone, bunduki haina lelemama yaani ikifyatuka imefyatuka, tuulize sisi tuliopigana vita ya Kagera. yaani Nduli na jeshi lake waliomba msamaha..” mzee alianza kumchanganyia habari Fonga aliyepagawa. Fonga alijikuta akilegeza kifungo kimoja baada ya kingine. Hali ilikuwa tete.. “Ujue huyo kijana ninasoma naye.” Fonga alimpoteza maboya yule mzee ambaye alionekana kumshangaa kwa hofu iliyomkumba. Mzee akatikisa kichwa akimsikitikia.

    “Hamna redio nyingine wanaweza kutangaza?” sasa Fonga aliitamani redio.

    “Ahh mjukuu wangu mmoja anaitwa Yakobo, mkorofi huyo aliivuta sijui wapi yaan kwa sasa inashika redio moja tu, nikifika Chalinze kuna fndi mmoja anaitwa Kakele, nitampatia anitengenezee, mafundi wa Msamvu matapeli sana hawa, wanaweza kunibadilishia vifaa hawa siwaamini lakini Kakele safi sana yule kijana. Tukifika Chalinze nitamwita akusalimie kidogo.” Mzee alileta mashairi mengi yaliyomtia hasira, swali dogo la ndio na hapana alilijibu kwa insha!! Tena vile hakuwa anaongea upesiupesi, basi ilimgharimu Fonga dakika kadhaa kusikiliza.

    Wazee bwana!!

    ***

    Mzee Akunaay akiwa rumande aliweza kutabasamu tena baada ya kuwa mwenye hofu siku kadhaa nyuma.

    Naam! Alikuwa na haki ya kutabasamu. Maana aliamini kuwa hiyo ilikuwa siku yake ya mwisho kuugulia rumande, ushahidi wa Betty pekee ulitosha kumuhukumu marehemu Beka huku yeye akitoka nje akiwa huru tena mwenye heshima tele. Alikuwa akipanga zawadi ya kumpa Fonce, mlinzi wake kwa kufanikiwa kuondoa uhai wa mzee Beka kwa wakati muafaka. Maana bila Beka kuuwawa hali ingekuwa tete kwa namna yoyote ile. Kifo cha Beka kilifukia mengi sana.

    Nampa nyumba ya Chamanzi!! Akunaay Zingo alifikia maamuzi hayo. Akamfikiria na wakili wake pamoja na maaskari wanaomvujishia siri, hawa pia akawapangia fungu lao. Hali ya kutojitambua na kuwa kama zezeta ya Inspekta Ndayanse ilimsababisha amtoe katika mgao.

    Ndio!! Atamgawiaje mwendawazimu chochote!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakupatwa na usingizi tangu majira ya saa tisa, alikuwa akiwaza na kuwazua namna ya kurejea tena uraiani. Hatimaye mwanga wa jua ukapenya na kuingia katika selo. Akauita mwanga wa matumaini. Mida ikazidi kusogea, na hofu ikaanza kutawala maana alitarajia Betty atatoa ushahidi wake mapema sana na yeye mheshimiwa kuachiwa huru kutoka katika kesi ile ya kuteka nyara. Majira ya saa mbili asubuhi yule askari ambaye huvujisha siri kwa Akunaay alipita kumtonya.

    “Mwanao Isaya haeleweki kama ni mzima ama la! Fonce amekufa na Nigga haeleweki kama yu hai ama la, Betty naye mahututi haijulikani kama atapona, na wengine kibao wamefia nyumbani kwako Sinza…..mzee kesi inakuwa ngumu hii. IGP yupo eneo la tukio na ile dhamana iliyotarajiwa imefutwa na usishangae ukihamishwa leo hii hii na huu kuwa mwisho wa mimi kuonana na wewe kirahisi kama hivi…” alimaliza yule askari kisha akatoweka pale. Ama!!

    Ilikuwa kama askari alivyodai!! Muda si mrefu wakafika askari wengine wazito katika vyeo, Akunaay akahamishwa huku akikemewa.

    “Huna mamlaka ya kuzungumza chochote muheshimiwa!!” alipigwa pingu katika mikono yake!! Akaongozwa kwa ulinzi wa mitutu mitatu ya bunduki. Akatupwa gereza la Segerea kama mahabusu!! Akunaay hakuamini kama ile ndoto yake ya kulala nyumbani kwake siku hiyo ilikuwa imeyeyuka. Aliduwaa na ni kitu ambacho hakukitarajia, kwani hakuamini kama alikuwa na mpinzani yeyote yule tena baada ya kifo cha Beka na vijana wake wote. Amani ikatoweka rasmi!!

    ***

    Majira ya saa nne hospitali ya taifa ikawa katika kuhangaika na miili zaidi ya kumi. walinzi wa mzee Akunaay, mtoto wa Akunaay, wasichana wawili, wanaume wasiofahamika, na walinzi lukuki kutoka Simba security!!

    Fonga alikuwa nje ya hospitali iliyokuwa imewekewa ulinzi mkali sana kama walivyokuwa mashahidi wengine waliotaka aidha kutambua ndugu zao ama basi tu kushuhudia kilichojiri. Fonga hakuitoa miwani yake usoni, aliamini kuwa hakuwa salama bado na wakati wowote angeweza kuingia matatani. Macho yake yalikuwa makini kupepesa huku na kule.

    “Hapa mzee Mushi kwa kesi kama hizi mbona wamemfikisha …” kijana mmoja alisema huku akionekana kufurahia kulitaja jina la Mushi. Jina la mpelelezi wa kesi hiyo.

    Inspekta Mushi!! Kufikia saa tano walinzi watano walithibitika kuuwawa kwa risasi, mlinzi mmoja wa mzee Akunaay aliyefyatuliwa risasi ya matako yeye alikuwa amekufa kitambo sana. Huyu aliitwa Fonce. Wasichana wawili ambao kila mtu alitaka kuwatambua vyema bado walikuwa hai lakini katika hali tete. Mtoto wa mbunge alikuwa amerejewa na fahamu!!

    Simu ikapigwa kwa Inspekta Mushi, na baada ya muda alikuwa katika chumba alichokuwa amelazwa Isaya. Alitarajia kupata mwangaza upesi kabla majanga hayajaendelea. Huku akakutana na kituko cha mwaka. Isaya hakuwa akisema neno la ziada zaidi ya kauli mbiu yake baada ya kuzinduka. “Baba, mimi nakufa…..Baba, mimi nakufa!!” Aliulizwa maswali mengi lakini hakuna alichoweza kujibu zaidi ya kuimba wimbo ambao anaujua yeye mwenyewe. Inspekta Mushi akapagawa!! Isaya akapigwa sindano ya usingizi, wakitaraji kuwa akiamka atakuwa sawa kwa ajili ya mahojiano. Habari zikavuja chinichini na kumfikia Fonga kuwa Isaya hajielewielewi. Habari hii ikazidi kuyafanya mawazo yake yazidi kumpwaya!!

    Saa sita mchana, habari kutoka chumba kingine. Mzee Seba yule aliyeng’atwa na Husna ngumi jiwe, marehemu Husna alikuwa anaweza kuongea tena!!

    Inspekta Mushi akaamua kuanza naye. Huku hakupata lolote la maana, Seba alidai kuwa huenda Ndayanse anajua kitu. Lakini Ndayanse alikuwa amepararaizi na hajielewi kabisa. Inspekta Mushi akachoka tena!!

    Wakati huohuo akaelezwa kuwa Nigga alikuwa amerejewa na fahamu tena. Kama amri ya IGP ilivyodai kuwa asingojewe mtu afe na ushahidi, inspekta Mushi alitimua mbio. Ana kwa na na Nigga. Huku akapata mawili matatu!!

    Nigga alikuwa mlinzi wa Akunaay, na wakati wa tukio walikuwa katika kumwelekeza Betty cha kusema kama ushahidi, wakavamiwa ghafla na yakatokea hayo yote.

    Majira ya saa kumi na moja jioni, kile kilichongojewa na wengi kikajiri. Betty alikuwa amefumbua macho huku Joyce akiwa na timamu zake kabisa. Inspekta Mushi akiwa na vifaa vya kurekodia alifika eneo lile. Akaomba kupishwa azungumze na Joyce. Joyce kama alivyokaririshwa na Fonga akautema uongo mtakatifu kisha akaelezea tukio la kumtafuta Betty hadi hatimaye kufikwa na mswaibu yale. Maelezo yake yalikuwa yamenyooka sana. Ni katika maelezo haya inspekta akagundua kitu. Upesi akawaagiza vijana wake. Naam! Wakakipata alichokuwa anataka, ni kamera zilizokuwa zimetegwa katika chumba ambacho yalifanyika mauaji. Hakika Joyce alikuwa sawa!! Tukio zima likaonekana.

    Mazungumzo yake na Betty katika namna ya siri ambayo hawakujua kama ni siri yalikuwa ushahidi tosha!!

    Ushahidi wa kumfunga Akunaay. Katika video hiyo akaonekana yule aliyemuua Fonce, na hapa likatokea tukio ambalo liliwafanya wanaume waliokuwa wakiitazama video ile wakiri kuwa Joyce alikuwa msichana wa shoka. Alionekana Nigga, yule mlinzi wa mzee Akunaay akiwa na bunduki.

    Akihaha huku miguu yake ikiwa imelemaa na ikivuja damu kwa wingi. Akaufungua mlango ambao Joyce na Betty walikuwa hoi. Akafika na kuzidi kujikongoja ndipo ghafla Joyce akamrukia, risasi aliyotaka kufyatua ikaishia ukutani. Baunsa asiye na miguu timamu akapalangana lakini Joyce aliyekuwa amejeruhiwa vibaya alionekana kuwa na nguvu mpya.

    “Nini kilijiri hadi ukapata nguvu hizo?” Mushi alimuuliza Joyce majira ya usiku wakati akiwaelezea tukio kwa tukio.

    “Nilimsikia akinitukania mama yangu na mama yake Betty, matusi ya nguoni.” Alijibu Joyce kwa hisia. Mkanda ule ukaendelea Joyce akizidi kutapatapa huku na kule, sasa yule baunsa alikuwa anaanza kumzidia, ndipo akatokea mtu mwingine akiwa na sahani kubwa ya udongo. Alipoonekana sura Joyce akastaajabu.

    “Isaya!!” Mkanda ukamwonyesha Isaya akimbamiza yule mlinzi na sahani kichwani, hapo akalegea na kumwacha Joyce kipoteza fahamu na Isaya akaanguka chini. Baada ya hapo hakuna kilichoendelea hadi walipoonekana askri wakiitoa miili ile ndani ya chumba kile.

    ***

    Ushahidi wa Betty, ulikuwa wa kuhitimisha tu filamu hii ya aina yake. Tayari ilishajulikana mbivu na mbovu. Katika maelezo yake hakuthubutu kujitaja kama muathirika wa Ukimwi lakini Joyce alimweleza kuwa kila kitu kipo wazi katika ule mkanda. Hivyo kwa shingo upande akakiri kuwa ameathirika. Na alimdanganya Isaya kuwa alibakwa ilimradi tu asiweze kumwambukiza.

    Matukio yakaunganishwa!!

    Upelelezi yakinifu ukafanyika wakati huo watuhumiwa wote wakiwa rumande. Nigga baada ya kugundua kuwa hakuwa na ujanja alilazimika kukiri kuwa mzee Akunaay anahusika katika kifo cha mzee Beka na jinsi alivyoshiriki katika mauaji hayo.

    Baada ya majuma matatu!! Wakati Joyce na Betty wakiachwa huru huku mtu aitwaye Fonga akisakwa pia kwa mauaji baada ya mkanda ule kumwonyesha yule bwana aliyemuua Fonce akitaja jina la Fonga kama mtu aliyewaagiza na hata simu iliyopigwa ilisikika. Mzee Akunaay alishtakiwa kwenda jela miaka arobaini na tano!! Kwa kesi takribani kumi na tatu tofauti tofauti huku kubwa kabisa ikiwa ya mauaji ya aina mbili. Murder (Mauaji ya mtu wa kawaida) na Assasination (Mauaji ya kiongozi katika serikali)…….na makosa mengine kumi na matatu.

    *****

    KIHITIMISHO!!!

    Betty hakuendelea tena kuishi katika jiji la Dar es salaam, alijiondokea akiwa na pesa aliyokuwa amelipwa na Isaya na kuhifadhi katika akaunti yake. Akaamua kwenda Ukala kisiwani alipozaliwa huku akijiaminisha kuwa mtaji aliokuwanao ungetosha kuleta mabadiliko kiuchumi katika kisiwa cha Ukala. Joyce akabariki safari hiyo!!

    JOYCE akiwa chuoni siku chache baadaye, majira ya usiku alipata mgeni wa siri. Huyu alikuwa ni Fonga!! Aliadamana na wanaume ambao Joyce alizikmbuka sura zao, hawa walikuwa ni Jaguda na Zedi!!

    Wanaume walioagizwa na Fonga na hatimaye kuiokoa roho ya Betty na Joyce. Fonga aliongea kwa uchungu mkubwa sana akisikitika kumkosa Joyce kama mkewe, akamshukuru kwa wakati wote waliokuwa pamoja, akasihi kwa hakuna mtu hata mmoja wa kuhusudu mauaji yake isipokuwa Joyce pekee kwa sababu ni yeye ajuaye kwa nini aliua. Joyce aliguswa sana, na kwa mara ya kwanza kutoka moyoni akamkumbatia Fonga na kumbusu midomoni.

    “Nakupenda sana Fonga!!”

    “Nakupenda pia japo nitakuwa mbali nawe Joyce.”

    “Fonga pliiz..” alisihi Joyce na hapa Fonga akaamua kumweleza kusudi lake. Kusudi la kuhitaji mtoto wa kumbukumbu kutoka kwa Joyce. Joyce hakupepesa macho, akakubali!! Angeanza vipi kukataa kwa yote ambayo Fonga alikuwa amemtendea hadi dakika hiyo? Hakika ilikuwa ngumu.

    Baada ya juma moja wakakutana faragha!! Wakatimiza walichokubaliana!!

    Fonga akamwachia milioni nane kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

    “Nimekuachia roho yangu mikononi mwako, itunze roho hiyo!!” alizungumza huku akilishika tumbo dogo la Joyce Kidoti, Kisha akatoweka. Haswaa!!

    Hawakukosea, majibu baada ya siku kadhaa!! Joyce akanasa mimba ya mwanaume ampendaye baada ya Isaya ambaye alikuwa amethibitishwa kuwa ameathirika akili yake ama kwa lugha fupi, Isaya alikuwa kichaa!! Kichaa anayesema maneno matatu tu! ‘baba, mimi nakufa!’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    HATA baada ya kurejewa na fahamu Inspeka Ndayanse ambaye alikuwa amepooza mwili mzima aliishia kutupwa gerezani kwa vitendo vyake vya kiasi!! Inspekta Seba alirejea kazini tena baada ya miezi kadhaa!!!

    WAKATI hali ikiwa shwari mjini kisiwa cha Ukala kilikuwa kinamalizia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa hisani ya Betty!!! Betty ambaye siku za kuishi zilikuwa zinahesabika!!

    MWISHOOOOOO

    TOA MAONI YAKO TAFADHALI!!!

0 comments:

Post a Comment

Blog