Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

AJIRA TOKA KUZIMU - 1

 



    IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA





    *********************************************************************************



    Simulizi : Ajira Kutoka Kuzimu

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Aliitazama nchi hii kwa mbali sana, aliyekuwa mkuu wake alimuonyesha kwa kutumia kidole kimoja. Ilikuwa ina rangi ya bluu hii ndio ilikuwa nchi kubwa aliyokuwa ameagizwa kumfanyia kazi yake ambayo hakuwa ameshurutishwa kuifanya bali kwa hiari yake mwenyewe. Baada ya kuelekezwa vyema katika nchi hii sasa alimuelekeza vi-nchi vingine vidogo vidogo ambavyo havikuwa na ukubwa wa kutisha. Majina yake mengi yalikuwa ya kigeni lakini yalieleweka na kukaa vyema katika kichwa cha kijana huyu aliyekuwa anaelekezwa. Alitikisa kichwa juu na chini kuashiria kuwa anaelewa somo alilokuwa anapewa.

    Mkuu wake aliyefahamika kwa jina la Tuntufye Kanyenye ama kwa kifupi Tuntu alitoa tabasamu ambalo kwake lilikuwa bora lakini linatia karaha ukilitazama. Tabasamu hili lilimaanisha kuwa alikuwa na imani kubwa na kijana huyu aliyekuwa anaagizwa katika nchi hii ya bluu na nyingine ndogo ndogo.

    “Nakutakia safari njema yenye mafanikio….” Tuntu alimtamkia kijana wake huku akimpapasa kichwa chake katika hali ya kubariki. Baada ya hapo akampulizia marashi fulani katika nguo zake. Halafu akamtwaa na kumnyanyua juu juu tayari kwa kumrusha katika dunia hiyo. Hofu ikaanza kumtawala kijana huyu akawa anatetemeka ujasiri aliokuwanao ukaanza kuyeyuka akawa anatweta kwa hofu lakini tayari alikuwa katika mikono hii mibaya yenye nguvu. Akiwa bado katika uoga mara alirushwa kwa nguvu zote akauacha ule ulimwengu akawa anaelekea katika ulimwengu mwingine. Alikuwa anarusha miguu huku na kule lakini aliishia kuipatia majeraha hewa ambayo ilikuwa katika kila sehemu.

    Kwa takribani dakika tano nzima alikuwa hewani na sasa alikuwa anakaribia kutua katika nchi hii ya bluu. Uoga ukamzidi akajikunyata akauziba uso wake kisha akapiga kelele kubwa sana za uoga huku akijaribu kukwepa asitue eneo lile aliloliona kuwa la hatari sana.

    Jasho kali lilikuwa linamtoka, alikuwa peke yake chumbani alikuwa amekaa kitako katika kitanda chake cha futi tano kwa sita. Alikuwa anatetemeka. Taa ilikuwa imezimwa akasimama aweze kwenda kuiwasha lakini akajihisi kuwa alikuwa katika kutetemeka, akarudi akaketi tena. Alikuwa ametoka kuota ndoto mbaya sana ambayo hajawahi kuiota kabla. Alijaribu kupikichapikicha macho yake ili aweze kuona kama aliyoyaota yalikuwa ndani ya chumba kile lakini hapakuwa na mfano wa kitu kama hicho pale ndani. Kwa unyonge akarejea kitandani akauchapa usingizi tena.

    Palipokucha hakuwa na kumbukumbu tena kama usiku ule alikuwa ameota ndoto mbaya. Aliamka akiwa na amani tele. Alijisikia mwenye nguvu za kustaajabisha!!

    Hakujua kama alikuwa ameingia katika utumwa

    Utumwa wa bila kujua.



    ****



    Hassan alikuwa anazipitia post za hapa na pale katika mtandao wa kijamii wa facebook katika namna ambayo hakuwahi kuifanya hapo kabla. Alizitazama post za mapenzi hasa hasa za wasichana, hakujalisha kama ni warembo ama la. Hakuwahi kufikiria kuwa siku moja anaweza kuwa kama alivyo.

    “Beatrice Cosmas” alilisoma jina hilo na kulirudia mara kwa mara, “Saint Augustine Mwanza” akakisoma na hicho chuo alichokuwa anasoma dada huyu.

    “Nipo njiani nakuja Dar yeyote aje kunipokea jamani” hatimaye akaikariri na ile post aliyoweka dada huyu mnene katika picha akiwa na mwanya na macho ya kuvutia.

    Hassan aliingia katika inbox ya dada huyu akamkaribisha Dar huku akimwomba ampe nafasi ya kumpokea mara atakapofika. Beatrrice akazuga kujizungusha zungusha na kumwomba Hassan namba yake ya simu na kuahidi kumpa taarifa baada ya kufika. Hassan bila kinyongo alimpatia namba yake ya simu huku akitoa tabasamu.

    Hassan aliingia katika shughuli zake huku akiwa ameanza kusahau kama alikuwa na ahadi ya kupokea simu yoyote ile mpya. Ilikuwa kama bahati ya kipekee baada ya kuwa amepokea malipo baada ya mauzo ya mzigo wake wa samaki.

    Wakati anaingia katika gari lake aina ya GX 100 alikutana na mlio wa simu yake, ilikuwa namba mpya, aliitazama kisha akabonyeza kitufe cha kupiga. Simu ikaita kidogo ikapokelewa na sauti nyembamba ya kike.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hassan jamani…nimekupigia simu muda mrefu kweli!!!”



    “we nani??”



    “Jamani mi Beaty!!!”



    “Beaty yupi tena”



    “Wa facebook…”



    “aaah!! Beatrice wa Mwanza eeeh!!”



    “Ndio mimi, tupo Mbezi vipi unakuja kunipokea kweli?”



    “Poa nakuja!!” alijibu Hassan upesi. Kisha akafanya upesi akakabidhi biashara yake kwa vijana wake akaingia garini akawasha gari na kutokomea kwa kupitia njia za panya hadi akafika Ubungo stendi.



    Zilikuwa zimepita dakika tano tangu gari la Zuberi kutoka Mwanza liingie hapo stendi na kushusha abiria. Beatrice hakuwa na uhakika kama Hassan atakuja kweli ama la!!! Aliposhuka akajaribu kuipiga simu ya Hassan haikupokelewa, akajaribu tena haikupokelewa akaanza kukata tamaa. Akiwa anatafuta uwezekano mwingine wa kutoka pale stendi mara simu yake ikamwonyesha kuwa Hassan alikuwa anapiga. Akapokea haraka haraka. Kabla hajaongea simu ikakatwa, akahisi Hassan amebip, akapiga kite cha karaha, akatazama salio kisha akataka kupiga. Akashtukia ameguswa begani, alipogeuka akakutana na sura ngeni kabisa ikamtupia tabasamu, hakujibu lile tabasamu badala yake akashangaa.

    “Hassan Tembo…..” akajitambulisha kwa jina lake analotumia kule facebook.

    “Mambo!!!” alisalimiwa katika hali ambayo ilionyesha kuwa Beatrice bado alikuwa katika mshangao.

    “Poa…vipi za safari pole sana na karibu Dar”

    “Asante mh!! Yaani kule facebook unaonekana mkubwa kweli mh!! Facebook ina mambo” Beatrice aliyasema hayo kwa kebehi. Maneno hayo yakamuumiza Tembo, akahisi amedharauliwa sana, lakini kabla ya kujibu chochote alimtazama kwa kuibia ibia Beatrice kuanzia chini, akakutana na viatu vyenye mtindo wa kisasa lakini vikiwa vimechakaa kutokana na kuikanyaga sana lami na kuvaliwa mara kwa mara, bila shaka hakuwa na viatu vingi, gauni lake kwa mahesabu ya haraka haraka lilikuwa halifiki hata shilingi elfu kumi na tano, kichwani alikuwa na wigi huku nywele zake halisi zikichungulia kwa mbali na kuutangaza uchakavu wake.

    Mkononi alikuwa na mabangili ya bei chee huku akiwa amevaa na kicheni kilichopauka kikiwa na maneno I LOVE U…usoni hakuwa na mng’aro wa utajiri huku mkoba wake uliochakaa ukiutangaza umasikini wake kama sio ubahili.

    “Mh!! Hana lolote huyu hebu ngoja…sijui na yeye nimwambie kuwa picha zake za facebook anaonekana mrembo?? Yaani anaonekana ana pesa kumbe hana maana yoyote” alijisemea Tembo huku usoni akizuga kutabasamu.



    “Kwa hiyo unaelekea wapi sasa hivi, twende basi”



    “Mh!! Asante Hassan usijali na asante kwa kuja mi nishafika hivyo, tutaonana facebook baadaye basi!!” Beatrice alijaribu kumkwepa Tembo, naye akaligundua hilo. Moyoni mwake aliitambua dharau ya Beatrice akaahidi kumkomesha na kumkata kidomo domo.



    “Wapi sasa unaelekea sasa hivi!!” Tembo aliuliza huku akijua fika kuwa yule binti hakuwa na pa kwenda.

    “Nitaenda hapo Magomeni ila kuna mtu namsubiri”:.alijibu.

    “Basi twende nikusindikize!!”



    “Asante Hassan..usijali hata” alizidi kukwepa Beaty.



    “Poa basi ngoja mi nirejee maskani yangu” alisema Tembo.



    “Poa basi ngoja nikusindikize kidogo” Beaty akawa amejibu bila kujua kuwa amefanya kosa kubwa sana. Walisogea mbele kidogo, Hassan mtoto Mama Tembo akatoa funguo za gari akabonyeza. Gx 100 ikapiga kelele za kujitoa loki, akafika akaegemea ile gari akaanza kuagana na Beaty tena. Wakati huu sasa Beaty akatoa tabasamu la ukweli. Mara akawa muongeaji sana. Tembo akajua tayari amemuingiza kwenye kumi na nane.

    Wasichana kwa tamaa!!!

    Lakini hakujua Beaty anajiingiza katika domo baya wakati huu!!



    “Mh!! Huyu shoga yangu mwenyewe sijui haji??” Beaty akaanza kujiongelesha ilimradi tu kufikisha ujumbe. Tembo akamwambia kuwa kama haji waondoke naye, binti akaingia mkenge akakubali, milango ikafunguliwa, akakutana na marashi ya aina yake huku mziki ukisikika kwa mbali sana kutoka katika santuri iliyokuwa katika redio, hiyo ni baada ya gari kuwashwa. Beaty akabweteka katika siti ya nyuma, Tembo akakataa kuendesha gari hadi alipohamia siti ya mbele. Safari ya kutoka ikaanza.



    Tayari Beaty alikuwa amesahau kuwa alisema kuwa Tembo ni mdogo sana, sasa alikuwa anamwona kuwa ni mkubwa tena mtanashati. Tembo alikuwa kimya sana huku akitikisa kichwa kufuatana na mdundo wa mziki uliokuwa unaendelea.



    “B twende tukapate msosi kwanza au vipi”



    “Poa tu twende” alikubali haraka haraka Beaty. Tembo akafurahi na nafsi yake.



    “Atanikoma na hatanisahau!!!” aliapa kimya kimya Tembo huku akiiendesha gari kuitafuta Kinondoni. Na hatimaye akaifikia Best Bite, akapaki gari wakaingia katika mgahawa ule maarufu jijini Dar es salaam.

    “Chipsi mayai….” Akaagiza B, muhudumu akamwambia hakuna orodha hiyo ya chakula. Tembo akacheka kimoyo moyo akagundua kuwa Beatrice alikuwa na ujanja wa facebook tu, wala kimaisha halisi hakuwa na ujanja wowote. Hata chakula kilivyoletwa Beatrice hakujua jinsi ya kutumia uma na kisu , kuzitumbua chipsi na paja la kuku lilokuwa mbele yake.

    Kwa mara nyingine tena Tembo akausoma ushamba wa Beatrice!!!!

    Kwisha habari yake!!!!!! Akajisemea huku akistaajabu huo ujasiri alikuwa ameutoa wapi.



     ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kutafuna mifupa ya kuku wa kisasa wanaokuzwa kwa kutumia madawa makali lakini ikatiwa viungo na kuonekana kuwa bora kwa mwanadamu. Tembo alikuwa akimsikiliza Beaty atasema nini, na tayari ilikuwa saa nne na dakika kadhaa usiku.

    “Kwa hiyo twende Magomeni au sio..ni Magomeni ipi kwani??” aliuliza Hassan Tembo huku akijichokonoa na kijiti katika meno yake.

    “Mh!! Sijui watafungua geti sasa hivi maana mh!!” alizungumza kama anajisemea vile Beaty. Tembo akajichekesha kwa kulazimisha.

    “Kwani wewe unaenda wapi sasa hivi??” aliuliza huku akizungusha funguo za gari lake huku na huko.

    “Naelekea nyumbani pande za Mbagala hivi”

    “Dah!! Vipi anakusubiri mke nini??” aliuliza huku akijichekesha

    “Hapana nipo na mwanangu mmoja tu sijaoa bado” alijibu kwa kujiamini.

    “Mhh!! Kumbe una mtoto Hassan…” alihoji Beatrice..

    “Hapana mwanangu yaani rafiki yangu mmoja hivi… mi sina mtoto wala!”

    “Mh!! Afadhali maana presha ishaanza kunipanda” Beaty akatokwa na kauli iliyomfanya Tembo atabasamu.

    “Kwani wewe ni lazima uende nyumbani leo???” akamhoji

    “Mh!! Wala sio lazima maana hawajui kama nimefika..sasa nisipoenda nitaenda wapi?” alijibu na kujiuliza. Tembo hakusema lolote akaingia garini na Beaty akaingia. Tembo akawasha gari hadi Kinondoni kwa Manyanya, gari yake ilipolifikia geti la CHICHI HOTEL geti lilifunguka bila msaada wa mlinzi. Beaty akaduwaa, Tembo akashuhudia hali hiyo, akajiaminisha moyoni kuwa tayari amemteka Beaty na ushamba wake.

    “Elfu hamsini Deluxe” alitajiwa bei ya chumba akazama mfukoni akahesabu hizo noti akamkabidhi binti mweupe wa haja aliyekuwa na tabasamu muda wote pale mapokezi.

    Kisha kwa ishara akamwita Beaty, kama msukule Beaty akamfuata hadi chumba namba kumi na nane. Tembo akachomeka kikadi akaufungua mlango. Beatrice hakuwa na ujanja wowote, Tembo akawa kiongozi Beaty akawa mfuasi.

    “Mh!! Siamini kama nalala na wewe leo, yaani mh! Umevunja rekodi kabisa, sijawahi kulala na mwanaume sehemu kama hizi… yaani tumekutana mara ya kwanza tu dah..” Beaty alizungumza huku akikishangaa kile chumba. Tembo hakumjibu badala yake akapenyeza mkono wake kiunoni mwa Beaty na kisha akamtekenya kidogo, Beaty akaanza kujichekesha kama bwege.

    Kwisha habari yake!! Akajisemea Tembo, kisha akamrusha kitandani.



    Bila kutegemea walioga wote, walicheza wote na mwisho wa siku wakajikuta wamefanya mapenzi nani aliyejiuliza kuhusu mimba na maambukizi ya magonjwa, jibu lilikuwa jepesi tu HAKUNA.



    Palipokucha Tembo alimsindikiza Beaty hadi nyumbani kwao. Ile kushuka kwenye gari na kuambiana kwaheri huo ndo ulikuwa mwisho wa Tembo kuonana na Beaty japo walikuwa wanawasiliana. Hadi Beaty anarejea chuoni hakuwahi kumtia tena Tembo machoni. Kule facebook hakujibiwa chochote alichouliza, hatimaye akachoka akajiweka pembeni.

    Na huo ukawa mwanzo wa Tembo Hassan kujielewa kwamba alikuwa amefanya jambo ambalo hakuwahi kulitegemea.

    Hakuwa na wasiwasi!!!

    Beatrice akajipa moyo kuwa mambo yameishia pale, kuwa amedanganywa tu na mwanaume na bahati mbaya wamefanya mapenzi… hakujua Tembo yu kazini hakujua balaa aliloachiwa!!!



    *****



    Tembo Hassan aliitazama kwa dharau picha ya msichana mmoja akiwa yupo pamoja na mpenzi wake, walikuwa wamekumbatiana kimahaba huku wote wakiwa na tabasamu halisi kutoka moyoni.

    “I love my husband jamani” picha ile iliandikwa hivyo kwa juu. Tembo akakereka sana kuona maneno yale, akamtazama vyema yule msichana. Paja jeupe la kuvutia, macho mazuri!!



    “Clara Clara Clara!!!!” aliita kwa sauti ya chini ile picha kana kwamba ilikuwa inamsikiliza, halafu akamaliza akaihifadhi katika simu yake. Kabla ya kuifunga simu yake aliamua kufungua profile ya Clara akaanza kuipitia hatua kwa hatua.

    “Reading novles” alikuta maneno haya katika vitu ambavyo vinamvutia Clara mojawapo likiwa hilo la kusoma riwaya.

    Tembo kwa akili ya haraka haraka akamkumbuka mdau mmoja wa facebook kwa jina la Ibarahim Gama. Huyu alikuwa ni mtunzi mahiri ambaye mara chache Tembo huwa anapata nafasi ya kupitia simulizi zake zinazopendwa na watu wengi katika mtandao wa kijamii. Tembo alizikumbuka kichwani mwake jinsi simulizi hizo ambavyo huwa zinaiteka akili yake.

    Ghafla bila kujua anachokifanya aliingia katika mtandao wa kijamii wa facebook, akaingia katika kundi la simulizi moja baada ya jingine. Kona ya riwaya, Uwanja wa simulizi, Stori za mapenzi na sitosahau, Tungo zetu kisha akamalizia na kurasa ya George wa hadithi stories. Huko kote akakuta kuwa Clara ni mdau na anazifuatilia simulizi kwa ukaribu.

    Hapahapa! Akajisemea Tembo kisha akaandika “Kaa mkao wa kula kusoma simulizi zangu kuanzia kesho” watu wengi waliitazama kama utani na hawakuamini kabisa kuwa Hassani Tembo alikuwa na uwezo wa kuandika simulizi. Lakini wakamjibu kuwa wanangoja simulizi hizo.



    Tembo alipofika nyumbani alifungua maboksi kadhaa akakutana na vitabu vya simulizi vya kiingereza na Kiswahili. Akavichukua vyote viwili akavilinganisha. Akachagua cha kiingereza, akakisoma kikamvutia sana. Akatulia tuli akaanza kukitafsiri katika lugha ya Kiswahili, siku iliyofuata akadondosha katika makundi simulizi hii. Maoni yakawa mengi, sifa zikamiminika, wanawake walikuwa wengi waliomsifia Tembo kwa mwanzo mzuri, wanaume walikuwa wachache, jambo hilo lilimvutia sana. Alikuwa katika mawindo, Hassan Tembo!!

    Hakuwa na shida na wanaume. Lengo lake lilikuwa ni hao hao wanawake na mawindo yake yalikuwa kwa Clara. Hadi inafika sehemu ya sita ya simulizi yake hii ya kuiba kutoka katika kitabu cha kiingereza na kuitafsiri kuwa ya Kiswahili bado Clara alikuwa hajajitokeza lakini tayari mawindo yake yalikuwa na wateja wengi sana ambao walikuwa wamejiingiza katika kutaka kumjua sana zaidi ya pale facebook.

    Huku Tembo akidhania kuwa Clara hakuwa akifuatilia simulizi zake, haikuwa hivyo Clara alikuwa naye bega kwa bega. Siku hii Tembo akaamua kumtag Clara katika simulizi zake.

    “Asante Tembo kwa kunitag hadithi yako yaani imenigusa kweli hii simulizi yaani haya mapenzi acheni yaitwe mapenzi” Clara alimuandika meseji Tembo. Kabla ya kuijibu Hassan alitabasamu kidogo halafu akafikiria nini cha kumjibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tembo:Usijali dear….imewagusa wengi sana!! Na ndiyo nia yangu mimi

    Clara:Ikiwa inaendelea uwe unanitaarifu basi

    Tembo:Usijali….ntakuwa nakutaarifu

    Clara:Mh!!!!natamani uimalize yote nijue mwisho wa huyu mkaka maana dah!! Sipati picha.

    Tembo: Mambo mengi sana ujue natamani kuwa naandika sana sema muda tu

    Clara: Haya kaka hongera kwa kipaji sipati picha wifi si atakuwa anafurahia sana, kila siku unamuhadithia, nikija Dar nitakutafuta unisimulie au unipe kitabu nijisomee.

    Tembo: aah!! Wala hapendi hadithi, kwani we upo wapi? Halafu kitabu sijatoa bado ila nitatoa.

    Clara: Mwanza nipo chuoni huku lakini Dar ndo nyumbani.

    Tembo: Huwa nakuja Mwanza mara kadhaa siku nikija nitakutafuta.

    Clara: Nitafurahi sana yaani sana tu…pliz usiache kunitafuta kama kweli ukija.

    Tembo: usijali dadangu sitaacha nipatie namba yako kama hutajali…maana facebook sio pa kuamini sana unaweza uingie au usiingie.

    Tembo akapewa namba ya simu!!!

    Mtego unaelekea kunasa!!



    *****



    Basi liliiliwaza stendi ya Mwanza iliyokuwa katika upweke mkubwa kutokana na kukosa mabasi mengi katika muda huo wa usiku.

    Abiria mmoja baada ya mwingine walishuka kutoka katika basi lile. Walipomalizika kabisa alisimama abiria ambaye huenda ni maksudi ama kukwepa vurumai aliamua kuwa wa mwisho kushuka. Alikuwa hana dalili ya nywele katika kichwa chake kilichofanana rangi na uso wake mweusi. Mgongoni alikuwa na kibegi kidogo cheupe kilichorandana na kiatu chake mguuni, hakuonekana kuwa mgeni sana wala mwenyeji sana, usoni alikuwa na miwani kubwa nyeupe iliyomkaa vyema.

    Alipofika chini aliusabahi mji huu kwa kuvua miwani yake na kufanya mfano wa toba ya kiislam. Kisha alipiga hatua kadhaa mbele hadi akakifikia kibanda cha chipsi.

    “Zege na mishkaki mitatu!!” aliagiza kwa sauti ya wastani lakini yenye amri ndani yake.

    “Poa braza”

    Baada ya dakika kumi na tano Hassan Tembo alikuwa akifanya mashambulizi ya hatari katika viazi mviringo vyenye mayai pamoja na mishkaki.

    “Nipatie na Fanta baridi”

    Punde aliletewa akaigida kwa fujo zote kisha akalipa kilichostahili akasimama na kuondoka bila kuaga.

    Alitembea haraka haraka kama mwenyeji hadi katika kituo cha mabasi, kulikuwa na baridi kali sana kutokana na msimu wa mvua uliokuwa ukiendelea, kila mtu alikuwa na koti ama sweta lakini Tembo hakuwa na chochote kile zaidi ya fulana yake. Baridi lilianza kuushambulia mwili wake kwa fujo akajihisi kama hana hata hiyo fulana.

    Taratibu akiwa katika kujikunyata akaichukua simu yake akaingia katika orodha ya majina akaligusa jina la Clara, akabonyeza kitufe cha kupiga simu ikaanza kuita iliita mara tatu ikapokelewa.

    “Nani wewe??” sauti ile ilihoji.

    “Aaah!! Jamani si tunasalimiana kwanza au??”

    “Bwana eeh!! Sema wewe nani??” ilitoa karipio sauti ile iliyokuwa katika usingizi.

    “Hassani hapa…”

    “Yupi?”

    “Tembo…”

    “Aaah!! Jamani Tembo samahani jamani….nisamehe bure miee” sauti ya Clara ikabadilika ikawa katika kubembeleza. Tembo akakenua meno.

    “Usijali nimeona kuondoka kimya kimya sio ishu….nipo hapa Mwanza kesho naweza kuondoka kurejea Dar es salaam….”

    “Jamani Tembo wewe tabia mbaya upo wapi kwani njoo basi kwangu walau nikuone tu”

    Tembo aliunda tabasamu jingine maridhawa kisha akamuuliza Clara ni wapi anapoishi.

    “Huku panaitwa Nyamalango sijui unapajua. Karibu na chuo kikuu cha mtakatifu Augustino”

    “Hapana nielekeze labda naweza kuja”

    Clara akamuelekeza Tembo, hadi akaelewa.

    Akabaki kusubiri kama atakuja ama laa.



    Ile hali ya Clara kuzungumza na Tembo ilimsababisha ajikute akizifikiria simulizi baadhi za Tembo ambazo amewahi kuzisoma. Nyingi zikiwa za mapenzi motomoto. Ile baridi ikaamsha mshawasha katika mwili wa Clara, kifua chake kipana kikaanza kuwasha alijaribu kuzikuna nyonyo zake lakini haikusaidia kitu alikuwa anazifanya zizidi kuwasha. Mwili ukawa unamsisimka bila kujua sababu haikuwa kawaida yake kabisa kukumbwa na hali kama hii. Baridi likazidi kujikusanya na kuutesa mwili wake. Alikuwa peke yake kitandani.

    Mara simu ikaita hakutaka kuipuuzia alipokea. Alikuwa ni Hassan Tembo tayari akiwa maeneo jirani na chumba cha Clara.

    “Nakuja bab….aaa!! Hassan” alijiumauma Clara huku ule muwasho ukizidi.

    Muwasho ulihitaji mkunaji!!!

    Haya yalikuwa maajabu ambayo hakuwahi kuyapata hapo zamani. Kuzungumza na mtu kwenye simu kisha anakuwa katika hali ile???

    Ilistaajabisha!!



     ****



    KITU cha kwanza baada ya Tembo kuingia katika chumba cha Clara. Binti alilalamika kuwa ana kiu ya kumsikiliza Tembo akimsimulia mojawapo ya hadithi zake za mapenzi. Tembo akatabasamu kisha akamtazama Clara usoni, akamkazia macho kwa sekunde kadhaa, macho ya Clara yalikuwa yamejirembua tayari, lakini ile kutazamwa na Tembo yalikaribia kufumba kabisa, Clara akajikuta anachukua kidole chake kimoja na kukitumbukiza mdomoni akaanza kukimung’unya kama pipi.

    Tembo akajikoholesha, macho ya Clara yakafumbuka. Tembo alitaka kumkabili binti yule pale kitandani lakini alikuwa ana hofu moyoni mwake.

    “Nisogee ama utanisikia nikiwa nasimulia nikiwa huku!!” Tembo akauingiza mtego.

    Clara naye akatumia nafasi ile kujifaidisha.

    “Hassan!! Usiku huu bwana…sogea unisimulie nifaidike mwenyewe!! Peke yangu yaani…” alijibu kwa sauti nyororo. Tembo akajikuta anatabasamu tena, akasimama na kuelekea mahali alipokuwa ameketi Clara.

    Kitandani kwake!!

    Tembo akachukua simu yake akafungua sehemu ya picha, akaitafuta ile picha ya Clara kutoka facebook akiwa amemkumbatia mpoenzi wake na kisha kujisifu kuwa anampenda sana. Tembo akaamua kumchokonoa.

    “Mumeo akinikuta humu si itakuwa msala?”

    “Tembo ulihudhuria ndoa yangu ama…. Please!! Mi nd’o mwenye hiki chumba na nimekukaribisha….” Alijibu Clara huku akionyesha kukereka na wasiwasi wa Tembo. Lakini wakati huo huo aliushangaa moyo wake!!

    Deniss alikuwa kila kitu katika maisha yake, alikuwa rafiki, mpenzi na mume mtarajiwa!! Hakuwahi kutarajia kuwa ipo siku atakutanisha macho yake na kisha kuanguka katika hisia na mwanaume mwingine, lakini sasa amenasa kwa Tembo. Hawana hata saa zima tangu waonane lakini mwili wa Clara umechemka, unawasha na unahitaji huduma.

    Kazi kwelikweli!!

    Hassan akiwa pembeni ya Clara alianza kusimulia simulizi yake moja ambayo aliiba kutoka lugha ya kiingereza na kuileta katika Kiswahili. Hata kabla hajafika mbali Clara akaingilia kati.

    “Mhh!! We Hassani wewe mjanja kuna mahali unasoma, ndio kuna mahali unasoma nd’o unanisimulia….” Clara alilalamika ilhali kiuhalisia kabisa Tembo hakuwa akisoma mahali popote.

    “Aaah!! Wala sisomi Clara..”

    “Kama kweli hausomi ngoja nikubambe sasa…” clara akasimama na kupiga hatua kuiendea swichi ya kuzima na kuwa sha taa, wakati anatembea, upesi Tembo akamtazama na kubaini kuwa Clara alikuwa ameumbika haswa!! Na mbaya zaidi alikuwa amevaa kanga moja tu!!

    Wanawake!!!!

    Clara akaizima taa, kwamba Tembo asimulie wakati wakiwa gizani.

    Ile simulizi ikabadilika baada ya Clara kurejea pale kitandani…. Ilikuwa ni simulizi ya binti wa kitajiri alivyoangukia katika penzi la mtoto wa kimaskini. Vikwazo vingi vikataka kuliua penzi lao lakini uimara wao ukalisimamisha tena…..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kadri Tembo alivyosimulia Clara naye akazidi kuwashwa….

    Unawashwa halafu hausemi!! Clara usiwe mjinga, usiwe mjinga!! Sauti ya ndani ikamwambia Clara…

    Kweli akajiona mjinga sana, akamwangukia Tembo huku akiitoa kanga yake mwilini. Kanga ikaanguka, akavua na blauzi yake.

    Na hapo likamtoka neno moja

    “TEMBO NIKUNE!!”

    Clara alikuwa katika hisia ambazo hajawahi kuzipata maishani akiwa na mwanaume yeyote yule

    Hisia kali za kimapenzi!!!



    Bila kujijua labda ama kwa kuzidiwa na hisia Clara alijikuta akiuvaa uhusika wa yule binti wa kwenye simulizi aliyeitwa Sarah akamkumbatia Hassan kwa nguvu sana, Hassan naye akajikuta amevaa uhusika wa yule mtoto wa kimaskini wa kwenye simulizi aliyekuwa na jina la George. Clara akajikuta anatokwa na machozi, machozi hayo yakatambaa katika mabega ya Hassan, mara bila kunong'onezana wakajikuta wanatazamana, kila jicho lilikuwa kama aidha linaanza kuupata uhai ama linaupoteza uhai wake, Clara na Tembo walikuwa katika hali ya mahaba. Maajabu kweli!!! Mahaba ya siku moja tena dakika kadhaa!! Ilikuwa inashangaza.



    Tembo akawa wa kwanza kuusogeza mdomo wake katika shavu la Clara lakini ghafla Clara kama vile kuna ugomvi alikwepesha shavu na kuziruhusu papi za mdomo wake zichukue hadhi hiyo. Papi zilipokutana na ndimi zikachomoza zikaanza kugombana kwa sekunde kadhaa kabla ya kuachana bila kuachanishwa. Ni wakati huo ambao ndimi zilikuwa katika ugomvi wa kusisimua ndio Tembo alipata nafasi ya kuzitomasa chuchu nzuri kubwa zilizojaa vyema kifuani mwa za Clara.

    Mpapaso huo wa Hassan Tembo ukazua kizaa zaa sasa walikuwa wameachiana lakini Clara alikuwa katika muwasho wa aina yake na sasa alihitaji kukunwa, na kweli alihitaji kukunwa sio kwa kutumia gunzi ama kucha zake yeye mwenyewe maana kweli alitegemea kucha zake zitakidhi haja lakini zilikuwa zimeshindwa. Clara akamtumbulia Tembo jicho la haja, haja ya mapenzi. Tembo akalitambua hilo.

    Mwanga ungeweza kuwa shuhuda pekee wa tukio hili la aina yake, lakini tayari Clara alishaufukuza mwanga chumbani. Basi giza likabaki kutazama yatokeayo, uzuri wa giza ni kwamba likiona mambo halimwambii mtu yeyote!!.



    Kitanda kikatwaliwa na watu wawili, chaga zikahimili uzito na sasa ulikuwa unasubiriwa ujasiri wa hizi hizi chaga kuwazuia wawili hawa wasiangukie uvunguni iwapo wataanza kutingishika!!!

    Kweli wakaanza kutingishika kwa fujo!!

    Zilifanikiwa kuhimili na zilistahili pongezi.



    Asubuhi sana Tembo alikuwa yupo macho siku hii ilikuwa ni jumatatu hiyo ikimaanisha kuwa jumapili Clara na Tembo walikesha. Clara alipoamka Tembo alikuwa ameoga na kuvaa tayari kwa kuondoka. Clara alimwonea Tembo aibu lakini Tembo alijidai hajalishtukia hilo akazuga kuchangamka, hatimaye Clara naye akawa na furaha akaungana na Tembo kufurahia madhambi waliyofanya usiku uliopita

    Laiti kama Clara angejua madhara ambayo yangetokea baada ya tukio hili, hakika asingemkaribisha Tembo chumbani kwake na kulala naye kama wapenzi wa siku nyingi!!!

    Hilo lilikuwa kosa kubwa lililoyabadili maisha yake!!



    ****



    Wiki nzima ilikuwa inakamilishwa na siku hii ya jumapili, siku hii ilikuwa ya saba tangu Clara alale na Tembo bila Deniss ambaye ni mpenzi wake kushtukia mchezo huu. Chaga za kitanda zingekuwa na uwezo wa kusema zingekuwa za kwanza kumshtaki Clara kwa Deniss kwani zilikesha zikipiga mayowe siku hiyo ya tukio.



    Siku hii ilianza kama jumapili nyingine, tofauti ilikuwa moja. Clara hakuwa na ari ya kwenda kanisani siku hiyo, basi hakutaka kujilazimisha akaghairisha kwenda, kingine ni kwamba alichelewa kuamka tofauti na kawaida, hilo halikumpa shida kwa kuwa hakuwa na mambo mengi ya kufanya hapo chumbani kwake. Saa nne kasorobo ilimkutia Clara akiwa bado kitandani alihisi njaa kwa mbali hilo pia halikumsumbua.

    Mkojo ndo kitu ambacho baada ya kujizuia sana sasa alikuwa amesalimu amri alikuwa ameamua kwenda msalani.

    Aliporejea ndo mkanda huu hapa ukaanza, ni kama simulizi na ilikuwa hivi. ….Clara alijirudisha tena kitandani kumalizia makombo ya usingizi wake, safari hii hakupata nafasi ya kusinzia akaanza kupata muwasho kwa mbali sana, muwasho huu katika ncha za matiti yake ulikuwa mtamu na wa kipekee, alikuna kwa pozi huku akiviringisha viringisha katika viganja vyake ncha za chuchu zake, hali kama ile ikatambaa hadi katikati ya miguu na penyewe alisogeza kidole kimoja mara viwili hatimaye vitatu mwasho ulikuwa umeongezeka.

    Alizidi kujikuna kwa juhudi zote lakini ikashindikana, Clara alitaka kuusingizia ugonjwa wa U.T.I lakini alighailisha baada ya kugundua kitu flani cha tofauti, mara taratibu zikamvaa hisia za kufanya mapenzi, alijikuta katika hisia zilizomfanya Tembo ajilie vitu bila gharama yoyote. Clara alipalangana kuzishinda lakini ilishindikana. Deniss mpenzi wake alikuwa anasoma huko Dodoma, Tembo aliyekata kiu yake siku saba zilizopita tayari alikuwa Dar es Salaam, machozi ya uhitaji yakaanza kumtoka Clara, alikuwa anahitaji huduma kwa udi na uvumba!!!!

    Muwasho ule haukujali kilio chake, ukazidi kumhangaisha!!

    Clara akaanza kutetemeka mwili wake hasahasa sehemu za mapaja.

    “Nini hiki jamani….nini hiki…” alilalamika akiwa anajiviringisha huku na kule pale kitandani.

    Clara alikuwa anazidi kujifaragua huku na huko akihangaika mithili ya kuku anayetaka kutaga na mahali pake pa kutagia kuna kitu mithili ya kunguru. Hakujua atafanya nini. Alitamani kupiga kelele lakini kelele hizo zingesaidia nini?? Akagundua hazina maana akatulia akijaribu kujikaza. Lakini hakufanikiwa. Aliyaunganisha meno yake akayaumanisha kujaribu kupambana na hali ile lakini bado hali ilikuwa tete. Akarusha rusha miguu, akaikanyaga kanyaga shuka lakini wapi ilikuwa kazi bure!!!



    Clara akajilazimisha kusimama akafanikiwa, akahisi kutetemeka, mikono yake ikawa inatetemeka, Hakuwa katika hali ya kuanguka lakini alikuwa kama mtoto mdogo anayejifunza kutembea akiwa katika hatua za awali kabisa. Hakujua anaelekea wapi lakini ni kama alikuwa anaufuata mlango, alipoufikia akakishusha kitasa ukafunguka, hakukumbuka kuufunga wakati anapiga hatua moja baada ya nyingine kutoka nje. Alipofika nje alitazama huku na huko akavutiwa na mlango uliokuwa nusu wazi nusu umefungwa, akili yake ikamwagiza kwa amri kali kuufuata mlango ule, akajikongoja sasa alikuwa kama bibi kizee kwa jinsi alivyoukunja uso wake, alipoufikia mlango alijifikiria kwa nusu dakika, alitaka kubisha hodi lakini akahisi anachelewa. Akausukuma na kuzama ndani.

    KILICHOTOKEA HUKO!!!!.....



     Alikuwa ni Joshua Joseph, wanachuo wa SAUT Mwanza walizoea kumuita baba mchungaji, alikuwa na tabia za kipekee, haikujulikana mara moja kama chanzo kilikuwa ni kusomea shule za wamisionari kwa muda mrefu ama ni malezi aliyoyapata kutoka kwa baba na mama. Hakuwa mtu wa mambo ya kidunia, starehe alizipiga kikumbo na kuyafuata yaliyompeleka hapo chuoni.

    Masomo!!!, alikuwa si mpenda michezo sana hata hivyo dhahiri shahiri alikuwa amezishinda tamaa za ngono, hakuwahi kuonekana kushawishika kumpenda msichana yoyote na hakuwa na dalili ya kummwagia sera binti yeyote licha ya kuwa na mwonmekano wa kuvutia.

    Baba mchungaji alikuwa mhudhuriaji mzuri sana wa makongamano ya injili, na mara kadhaa alikuwa akiwaelimisha vijana wenzake kubadili mienendo yao. Wapo waliobadilika na kuna wengine yaliingilia sikio hili na kutokea la pili huku wakimchukulia Joshua kama punguani aliyedondokea hapo chuo kikuu bahati mbaya.

    Licha ya jamii kumchukulia katika namna mbili zinazoweza kuwa zinamfanya kuwa kama alivyo na kulitendea haki jina lake la 'baba mchungaji'. Hali ilikuwa tofauti juma hili ,baba mchungaji kama alivyozoeleka jumapili kwake ni siku ya mapumziko kimasomo lakini kimatendo ya uzima hakuwa na kawaida ya kupumzika, alikuwa akitoka asubuhi basi anarudi jioni kabisa. Hakika alikuwa anajiweka mbali na mambo ya kidunia.

    Utaratibu huu ulikuwa mgumu sana kwa wanafunzi wengine, lakini yeye aliumudu na kuutawala.

    Hakuna mwanafunzi wa SAUT aliyeishi maeneo ya Nyamalango ambaye hakumjua ‘baba mchungaji’

    Alikuwa mtu wa watu!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    JUMAPILI hii ikaja na mambo yake mazito….

    Joshua alikuwa amevaa bukta yake nyepesi kabisa ya kulalia, alikuwa anaelekea katika kutimiza jambo ambalo kwake ni siri kubwa. Siri ambayhajawahi kuivujisha kw a mtu mwingine.

    Siri ya Joshua kuwapuuzia wasichana na kisha kuonekana mbele za watu kuwa ni mtu mwenye msimamo.

    Joshua alikuwa anaelekea bafuni ili aweze kujichua (masturbation).

    Hii nd’o ilikuwa kinga yake kila alivyokuwa anapata hyamu na msichana, mchezo huu alijifunzia akiwa Seminari na aliuendeleza hadi chuoni.



    Kabla hajalifikia bafu, mara mlango wa chumba chake ukafungulia, aliyeingia alikuwa ni jirani yake wa chumba cha pili.



    Clara alivamia chumba chake asubuhi ya siku hiyo. Alikuwa na kanga moja huku akionekana kama amelewa vile lakini harufu ya pombe haikutawala hata chembe hapo ndani, alikuwa kama anayekata roho lakini Israeli akawa bize na mambo mengine hakujishughulisha na roho hii.

    Clara alimvamia Joshua bila kuongea lolote, wakati huo Joshua alikuwa amevalia pensi laini ya kulalia pekee. Alipokumbatiwa lile joto kutoka katika matiti yaliyojaa ya Clara likapenya katika kifua chake ki-pensi kikaongezeka ukubwa kwa kwenda mbele ghafla, alitamani kumsukuma Clara pembeni. Ndio mikono ilitaka kumsukuma lakini mara mkono wa kulia ukausaliti ule wa kushoto, wakati mkono wa kushoto ukisukuma wa kulia ukamkumbatia Clara. Mkono wa kushoto ukakumbwa na wivu wa ghafla ukaamua kufanya makubwa zaidi ya ule mkono wa kulia hii yote ni kulipiza machungu, ukarudi kwa kasi ukakamata titi moja la upande wa kushoto wa Clara ukaminya, sasa ikawa vita ule mkono wa kulia ukakasirika sana kuona kitendo hicho ukavamia lile titi lililosalia na upweke huku likitamani kutendwa kama lile la kushoto. Lile titi likiwa katika hali hiyo likajikuta nalo linaminywa. Mminyo wa kipekee!!!! hakuna wivu tena mikono ikawa na amani na matiti hayakuwa na wivu tena. Muwasho ukapata mkunaji.

    Baba mchungaji!!



    Punde wakawa kitandani, Joshua alishaufunga mlango kitambo, Clara akiwa kama amezimia vile lakini akitoa sauti za chini chini zilizoyafurahisha masikio ya Joshua, basi na ye Joshua akaendelea na juhudi za kumzindua Clara, si kwa kummwagia maji wala kumpepea lakini ni kama mchezo ulivyoanza basi kila kiungo kikawa katika harakati zake!!!!!



    Baada ya jitihada za muda mrefu hatimaye Clara alizinduka, badala ya wawili hawa kufurahia maajabu haya wote wakawa wakioneana aibu. Clara akakimbilia chumbani kwake akimuacha Joshua nyuma!!

    Muwasho wa maajabu ulikuwa umepata mkunaji mbadala!!

    Mtumishi wa Mungu Joshua a.k.a ‘baba mchungaji’



    Iliwagharimu siku tatu kuizoea hali ile. Lakini katika namna wasioitegemea, hali ile ikajirudia tena jumapili Iliyofuata hivyo Joshua hakwenda kanisani, na hata Clara pia.

    Mchezo huu sasa ukamnogea baba mchungaji akawa anafurahia kutoa huduma hii tena kwa njia za mafanikio kinyume na kumhubiria mtu aokoke. U-baba mchungaji ukakaa kando sasa akawa BABA MTENDAJI, kanisa likakaa pembeni na halikuwa na thamani tena, kila jumapili Clara anapata muwasho mkali, aliyekuwa baba mchungaji, Joshua Joseph akawa mkunaji wa siri.

    Na alikuwa anakuna kweli!!!

    Zile hasira za kuukosa mchezo huu tangu akiwa mdogo kutokana na vitisho vya wazazi na walezi sasa alikuwa akizimalizia kwa Clara tena katika namna ya MARA NNE KWA MWEZI. Upweke ulioje kwa zile sabuni zilizokuwa zikimfariji Joshua, zikabaki katika ukiwa hazikuwa na maana tena kwa Joshua. Joshua alikuwa amepata sabuni iliyomtosheleza.

    wawili hawa hawakushangazwa na hali hii kujitoka siku za jumapili tu!! Hawakujua kuwa kuna ajira wamepewa, ajira kutoka kuzimu!!

    Laiti wawili hawa wangejua wanayemtumikia na malipo yake??!!

    CLARA kila jumapili anawashwa na mkunaji amelisahau kanisa… kila jumapili lazima AKUNE!!

    *****



    TEMBO KAZINI TENA



    Tembo alikuwa anaanza kuipoteza kumbukumbu ya ladha ya kipekee ya Clara wa Mwanza. Sasa alikuwa ameangukia katika mikono mingine tena mikono mikubwa!!! mikubwa zaidi ya ile iliyopita.

    Bado alikuwa katika mtandao huu wa kijamii wa facebook. Biashara zake za samaki pale feri zilizidi kuchanganya, mapato kutoa matumizi majibu yakawa faida kubwa zaidi ya awali. Tembo alikuwa akicheka kila siku alipokuwa akiletewa mahesabu mezani. Hakika maisha yalikuwa yanaanza kwenda kama alivyowahi kuota!!!!!

    Maisha bora sana.



    Lucy Kezi, mwanamama mwenye umri wa miaka arobaini, lakini ni kama hakuupenda sana uzee uliokuwa ukimfuata kwa kasi, alijaribu kupambana nao na kwa kiasi fulani alikuwa ameweza, kwani kwa jicho la haraka haraka alikuwa amepungua kama miaka kumi na kuwa nayo thelethini pekee. Siku hii alikuwa katika gari yake ndogo aina ya Lexus, alikuwa akiendesha taratibu huku akisikiliza miziki laini. Yalikuwa majira ya saa kumi na moja na wala hakuwa na hofu yoyote ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani mume wake alikuwa amesafiri kikazi kwenda China, lengo la safari hii lilikuwa kukutana na kijana machachari kijana ambaye anapamba kava la mbele la kitabu chetu, nani mwingine kama sio Hassan Tembo.

    Dhumuni kuu lilikuwa kununua kitabu ambacho Tembo alimwambia mtandaoni kuwa amekitoa tayari kitabu cha "Misumari kumi ya moto katika mapenzi", mama huyu alivutiwa sana na uandishi wa Hassan na kwa jinsi alivyokuwa anaandika ni kama aliyasomea mambo hayo. Kingine kilichomvutia mama huyu kuhitaji kukutana na Hassan ni machache waliyochat katika mtandao na Hassan kumwambia kuwa hana mpenzi lakini hata hivyo hapendi kuwa katika mahusiano na wanawake waliomzidi umri. Katika mtandao Hassan alikuwa akimwita Lucy mama na yeye Lucy akijibu mwanangu.

    Salamu za shkamoo zilijibiwa marahaba na mama huyu.



    Sasa leo hii alikuwa anakutana na mtoto wake huyu, mtoto wa mtandaoni, mtoto mwenye kipaji cha utunzi. Mtoto ambaye aliyajua mapenzi nje ndani kumpita yeye na miaka yake arobaini. Lucy sio kwamba tu alizidi kushangazwa na kipaji cha Tembo lakini alihisi kuwa huenda kijana huyu anadanganya umri, labda ana miaka zaidi ya ishirini na tano aliyomtajia.

    Maana mambo aliyokuwa anayaandika na kuinua hisia za mashabiki, tofauti kabisa na umri wake!!



    Sasa alikuwa anaenda kuhakikisha kila kitu. Lucy hakuwa na wazo lolote juu ya uwezekano wa Hassan kuwa anaiba maneno hayo na kuyatafsiri, hakujua kama Hassan huyu kuna kazi ameagizwa afanye katika nchi ya bluu. Lucy hakujua lolote na sasa alikuwa maeneo ya Kimara kituo cha kona ni hapa waliahidiana kukutana na Hassan Tembo kisha waangalie ni wapi watakwenda kwa ajili ya mazungumzo zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "0653**1640" Lucy Kezi akazibonyeza namba alizonakiri kutoka katika mtandao, zilikuwa ni namba za Hassan Tembo. Mara upande wa pili simu ikaanza kuita!!!!!

     Simu iliita mara tatu kisha ikapokelewa, alikuwa ni Hassan Tembo aliyeipokea.

    “Mambo Hassan, Lucy mie nishafika hivyo hapa Kimara Kona”

    “Ahaa!! Haya mamangu nakuja sasa hivi” Tembo alijibu kwa heshima zote. Kisha akakata simu. Lucy aliweka gari pembezoni kabisa mwa barabara ambapo palikuwa salama bila usumbufu kwa wengine kisha akajilaza katika kiti chake akimsubiri Hassan aweze kuja.

    Baada ya dakika kumi Hassan alikuwa tayari amefika baada ya kuelekezwa kidogo akaiona gari akakata simu na kuiendea.

    Akataka kukaa siti ya nyuma Lucy akamlazimisha akakaa mbele.

    “Shkamoo aunt!!”

    “Mzima wewe!!!” Lucy akaikwepa heshima ya ‘shkamoo’ kijanja. Tembo akaligundua hilo lakini hakutaka kujiuliza chochote kile aliamini kuwa ni hali ya kawaida.

    “Za huko kwenu Hassan”

    “Nzuri tu mama tunaendelea na maisha”

    “Wazazi wazima huko??”

    “Aaah!! Wazima tu hawajambo!!” alijibu kwa nidhamu kubwa Tembo

    Kimya kilitanda kwa muda, Lucy akiwa makini kabisa na kuendesha gari kuelekea mahali ambako Tembo hakuwa akielewa hata hivyo jambo hilo halikumtia uoga wowote ule. Na hakujua ni kwanini alikuwa akijiamini kiasi kile.

    Mitaa ilizidi kuachwa na sasa walilifikia geti, kubwa jeusi, Lucy akapandisha vioo juu wakati gari linaingia ndani hadi lilipofika eneo la kupaki.

    “Karibu Hassan hapa nyumbani kwangu nisamehe kwa kukuleta bila taarifa mpandwa” Lucy Kezi, alimwambia Tembo kwa upole sana.



    He!! Mara hii nishakuwa mpendwa!!! Alijiuliza Tembo huku akijibu, “Usijali mamangu!!” Lucy alimwongoza Hassan wakaingia ndani, ilikuwa mara ya kwanza Hassan kufika eneo maridadi kama hili. Yeye alizoea kuwapeleka wasichana maeneo ya gharama lakini leo ni yeye alikuwa ameletwa eneo la namna ya kipekee.

    “Mh!! Huyu hapa sina ujanja nitamwanzaje sasa. Huyu sio type yangu huyu” alijiuliza Hassan huku akiitafakari gharama iliyotumika kuitengenezea sebule ile akakosa majibu. Sebule ilikuwa na kila kitu kinachoifanya kuwa sebule.

    Ilikuwa sebule ambayo mgonjwa wa homa kutoka uswazi akifika pale, homa inakoma kwa dakika mbili ili aweze kuishangaa sebule ile.



    Watu wana pesa duniani!!! Tembo alikiri.



    Baada ya muda Lucy Kezi alirejea akiwa na kijikaratasi,.

    “Utakunywa nini my dia” aliuliza kwa utulivu kama anamuuliza baba mwenye nyumba. Tembo akasita kujibu.

    “Kuna sweet wine, Amarula, bia na juisi ya embe” aliulizwa Tembo huku Lucy akisoma kile kikaratasi

    “We nichagulie tu mama!!!” alijibu kiaibuaibu.

    “Mh!! Haya nakuletea sweet wine inalewesha kidogo, lakini katika namna ya kuchangamsha. ”

    “Usijali mama asante kwa uchaguzi huo, nikilewa unanibeba hadi kwa mama Tembo nyumbani”



    Baada ya nusu saa Hassan alikuwa amemaliza glasi ya kwanza, kweli ile wine iliyotengenezwa kwa tunda la Rozella ilikuwa ya kipekee ukiinywa hujui kama unalewa yaani unaifurahia tu!!! Unafurahi unafurahi hatimaye unalewa huku ukifurahi.

    Kuhusu kulewa!! Huenda hiyo ilikuwa si kwa Hassan Tembo bali kwa wale wazembe wazembe kama mume wa Lucy ambaye walikuwa hawajafunga ndoa bado aliyeitwa Isaya, huyu alikuwa amezidiwa sana na ulokole, alikuwa akipitiwa na kunywa vilevi basi alikuwa anageuka kituko, Rose Mhando yeye, Bahati Bukuku shangazi yake, Upendo Nkone binamu, Jenipher Mgendi dada yake tena tumbo moja, Seleman Mukubwa pacha wake, yaani kila nyimbo alikuwa anaziimba kwa juhudi kubwa, bila kupangilia mashairi vizuri. Na hapo ni baada ya kubwia walau glasi moja tu. Baada ya hapo anakuwa hoi analala fofofo, lile wazo la mkewe kuwa baada ya kulewa anaweza kuwa mjanja na kumlidhisha kitandani linatoweka anabaki kujisugua sugua bila mpango.

    Siku akiwa hajalewa ndo hataki kusikia juu ya suala la kufanya ,mapenzi. Shahada ya uchumi aliyochukua ilikuwa imemuathiri hakupenda kupoteza muda.

    Sasa kwa Hassan baada ya kuwa amefuta glasi nne za wine kwa mbaali akakisikia kichwa kikihama huku na huko, mara likaja wazo, wazo la kishetani wazo la kuifanya kazi yake kazi inayomwingizia mshahara. Ajira kutoka kuzimu!!!!!

    Akiwa hajui kama ameajiriwa.



    Hasan Tembo akiwa anajidai amelewa alikuwa akimtazama Lucy kwa uchu, yale maziwa makubwa yaliyokuwa yakitunzwa vyema yakawa yanamwita lakini akaogopa kwenda.

    “Hassan kwanza kitabu changu???” Lucy Kezi, akaulizia. Tembo akajidai kushtuka, “Ahaa!! Dah!! Yaani inabidi nikusimulie kwa kweli yaani ile hamu ya kuonana na wewe nimekisahau mezani nisamehe sana” alidanganya Hassan, Lucy akajifanya amenuna, Tembo akamwomba msamaha yakaisha.

    “Haya sasa nisimulie walau sindano moja tu ama mbili”

    “Usijali mamangu….sasa mimi sauti sina itabidi usogee karibu nikusimulie kisha niondoke zangu mie”

    “Sasa unawahi wapi..baba yako hayupo mpaka wiki ijayo ameenda China huko” majibu hayo ukijumlisha na pombe kichwani yakampa ujasiri Tembo, akajiapiza kuwa lazima atimize azma

    Bila kusita Lucy ambaye naye alikuwa anabwia Ndovu baridi, alijisogeza na kukaa karibu na Hassan, alipoketi akaunyanyua mguu wa kuume ukaukalia wa kushoto.

    Paja jeupe nje!!!!! Hassan akachungulia, akalitamani, akameza mate ya tamaa.



    “Sindano ya kwanza hii ni ubunifu, wapenzi wanatakiwa kuwa wabunifu sana ili kuulinda uhusiano wao, kitanda ama chumba ni sehemu ya kuheshimu sana, kule chumbani mwanamke anatakiwa kuhakikisha anamvutia mpenzi wake na mwanaume vile vile anatakiwa kujishughulisha ipasavyo, sio lazima kutumia nguvu nyingi sana, maandalizi muhimu sana, mikono ifanye kazi yake, ulimi pia ulitangaze penzi kwa kupapasa sikio la mwenza, midomo isiachane, hakuna haja ya maneno mengi, sakafuni, bafuni pote ni haki yenu wapenzi. Mwanaume ajishushe na kuwa kama mtoto anyonye maziwa yanayomtazama kwa huruma wakati mwanamama yupo kifua wazi………” Tembo akasita kidogo akamtazama Lucy, macho yake yalikuwa yamelegea, alikuwa kama asiyesikia lolote lile, alikuwa kama zezeta. Lucy alikuwa amesafiri nchi ya mbali tayari.

    “Golden chance!!!!” alijiambia Tembo, kisha akamshtua Lucy, wakati huu akijidai amelewa zaidi.

    “Usingizi!!!” alilalamika kilevilevi, Lucy kuja kushtuka Tembo alikuwa amelala kwenye kochi akiwa anakoroma.

    “Hassan!! Hassan!!” aliita Lucy, Tembo akasikia lakini hakujibu. Lucy akamsogelea na kumnyanyua aweze kumpeleka chumbani, Tembo akatumia nafasi hiyo akawa amemshika Lucy Kezi maziwa kimakosa, Lucy akaanza kuhema juu juu, Tembo akafanya tabasamu la dhihaka bila Lucy kumwona.



    Lucy alibaki akiwa amemkumbatia Hassan huku akiamini alikuwa amezimika tayari kutokana na ulevi, Hassan naye akazidi kuyabinya maziwa ya yule mwanamama, ile mihemko ikageuka kilio, yule mlevi aliyekuwa amebebwa akageuka mbebaji.

    Nani afanye safari ndefu ya kwenda chumbani huku akiwa amebeba zigo zito namna ile, kwani sebule ina kasoro gani. Punde Hassan akawa baba mwenye nyumba.



    Isaya!!! Isaya!! Isaya!!....ndio jina lililokuwa likimtoka Lucy lakini aliyekuwa mbele yake hakuwa Isaya bali Hassan. Jina hilo halikumkera Hassan kwani na yeye alikuwa mpitaji!!! Somo alilolitoa pale, machozi aliyomwaga Lucy Kezi, miguno na vilio lilikuwa somo lililoeleweka!!!!.

    Baadaye wakahamia chumbani, yale maneno aliyokuwa akimsimulia kwa mdomo sasa yakawa katika vitendo.

    “Hassan nataka uwe mume wangu!!!” Lucy alijikuta akimtamkia Hassan alfajiri baada ya kipengele walichoishia usiku uliopita.

    Hassan akacheka kimoyomoyo, kisha akajisemea “He!! Miaka 45 kwa miaka 25, huyu mwendawazimu kweli hajui kama ana kesi ya ubakaji hapa…”



    Lucy akadhani amepata bwana wa kumtuliza kila anapokuwa katika haja, akamtegemea Tembo kwa asilimia mia awe mume wake wa siri. Lakini hiyo ilikuwa ndoto. Tembo akawa anamkwepa kila siku, Lucy akajiuliza na kupata majibu. Tembo ni kijana, basi vijana ni wengi. Lucy akaingia rasmi katika kumsaliti mume wake kwa kutembea kimapenzi na vijana wa umri wa kuwazaa, utamu ukamzidia sasa ikawa tabia.

    Lucy akawa mfuasi wa dini ya Tembo, Lucy akaanza kumtumikia Tembo kwa kufanya uzinzi na vijana wadogo!!!

    Tembo naye alikuwa akimtumikia mtu bila yeye kujua!!!

    AJIRA TOKA KUZIMU!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********



    HEKAHEKA COCO BEACH



    “Mambo vipi dada!!!” Tembo alimsalimia binti aliyekuwa jirani na ufukwe wa Coco jijini Dar es salaam. Alikuwa amevaa kinguo cha kuogelea kilichomchora umbo lake lote kwa uzuri.

    “Poa!!” alijibu bila kumwangalia Hassan. Lakini Hassan alipata fursa ya kipekee kuvitazama vishimo vilivyojiunda kimaksudi katika mashavu ya dada huyu!! Baada ya kuijibu ile salamu yule dada bila kumjali Hassan akaanza kutembea katika maji yale mafupi yaliyofunika miguu yake kidogo tu. Tembo aligeuka na kuanza kumsindikiza kwa macho, alikuwa anatikisika nyuma bila kumaanisha kumtamanisha Hassan, huyu binti alikuwani mrembo haswaa. Tembo alikiri hilo, huku akijisogeza na kukaa katika mchanga laini pembezoni mwa bahari.

    Alijaribu kumpoteza yule binti katika akili yake, lakini hakufanikiwa, baadaye alimwona jinsi alivyokuwa anahangaika kujaribu kucheza na maji. Tembo akaongeza umakini.

    Ajabu!!!! Binti yule hakuwa akijua kuogelea!!!!!. Kama vile Tembo amewekewa injini ndogo katika miguu yake alitimua mbio kuelekea mahali alipopajua yeye.

    “Amekwisha huyu na atajuta kuja katika ufukwe huu!!!” alijiapiza Tembo huku akizidi kukimbia!!!!!



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog