Search This Blog

Sunday 19 June 2022

WANAWAKE NI WAUAJI ?! - 5

 







    Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?!

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Leo kuna kitu kimoja tu, kilinichanganya kuhusu mke wangu."

    alionekana Kamishna Shebby akiongea na Cj4 kwenye sehemu yao maalum waliyokuwa wanakutana kwa mazungumzo pasi na mtu yeyote kuona.

    "Kitu gani hiko?"

    aliuliza Cj4

    "Kwenye mazungumzo yake nikiwa kama askali mzoefu sasa niligundua kuna kitu ananificha kinachonihusu kabisa"

    "Mh! hebu nipe nukuu yake."

    "Alianza maongezi akiwa makini na kunimaanishia kuwa niamini kama ananipenda, lakini alivyoendelea alinambia kuwa ila anaona hastahiri mimi kumpenda vile na nilipomuuliza sababu akanambia ana wasiwasi kwa vile ninavyompenda kuwa sitompenda hivyo siku zote. Nilipomuuliza kwanini ana wasiwasi huo ndipo akanambia kuwa anahisi kuna siku nitakuja kumchukia sana na hata kumuua.... Dah! hapa ndipo nilipochoka na kuhisi lazima kuna kitu tu. Hawezi kuanzisha mada yenye maneno makali kama yale yaani mimi Nimuue mke wangu mwenyewe?"

    aliongea Shebby wakati huo Cj4 alikuwa anmsikiliza kwa umakini mkubwa.



    "kwa hiyo hukumuuliza kwanini amefika mbali hivyo?"

    "Nilimuuliza kiongozi."

    "Akasemaje"

    "aagh! jibu lake nililiitikia tu lakini halikuwa na ukweli wowote nilijua tu ni Zuga"

    "sawa aliemaje?"

    aliuliza Cj4 lakini wakati Shebby anataka kujibu mara simu yake ambayo ilikuwa na line ile ya nyumbani tu ndipo ilipoita na kuipokea ambapo sauti ya upande wa pili ilimfanya abadilike ghafra uso.

    "Vipi Shebby?"

    "Kumekucha Mkuu Mr X ameamua kuivamia nyumba yetu alfajiri hii kule kwa mzee."

    aliongea Shebby ndipo mkuku alikimbilia kwenye gari pamoja na Cj4 ili kuwahi nyumbani kwao ambako ilionesha wazi kuna matatizo mazito.



    "Nani huyo kapiga simu?"

    aliuliza kwa sauti nCj4 wakati huo Shebby aligeuza gari kwa fujo na kugonga mti upande wa nyuma kabla hajatia gea ya mbele na kukanyaga mafuta kwa fujo bila kujali kishindo cha nyuma alipogonga kumetokea madhala kiasi gani.

    "Nani kakupigia Shebby?"

    aliuliza tena Cj4 huku akibamiza dashboard kwa kofi kali baada ya kuona Shebby yupo kimya huku akili yake ikiwa mbali sana.

    "Ni mfanya kazi... Ni dada wa kazi kiongozi... aaagh! anaongea huku analia na nilisikia sauti za vitu vikiongwa gongwa..."

    aliongea kwa pupa Shebby wakati huo barabara waliyokuwa wanapita mbele yake kulikuwa na kijiforeni kilichomfanya ahamie bara bara ya pili huku akivipana vile vizuizi vidogo vya barabara na kusababisha gari iruke ruke na kutaka kudondoka pasi nae kujali kuwa anaingia upande usiomruhusu ambao haukuwa na magari mengi na wala hakupunguza mwendo Shebby aliendelea kukanyaga mafuta huku akizikwepa kwepa gari zilizokuwa zinakuja mbele yake.



    Kelele za honi zilisikika kwa fujo kama zile kelele za mavuvuzela katiaka kombe la dunia kule south pindi Shebby alipokuwa anakosana kosana kugongana na gari nyengine zilizokuwa zinakuja mbele yake na hiyo yote ilikuwa kutaka kuwahi nyumbani kuzuia matatizo yaliyokuwa yanatokea muda ule akihofia mr X asiwadhuru watu wote wa familia yake hususani baba na mamaake pamoja na mkwewe ambae ni Hussein bubu.

    "Cj4 ushauri wako safari hii umeniponza. Aaaagh! umeona kumuacha Hussein bubu nyumbani matatizo yanatokea na kuwaumiza watu wasiohusika kabisaaaaa aaah! ona tunawaponza watu wengi zaidi? Ni bora tungemueka sehemu ya kumlinda wakati tukimsaka Mr X."

    alilalama Kamishna Shebby huku machozi yakimtoka wakati kichwa chake kilipotengeneza mazingira ya nyumbani na kuona jinsi wazazi wake wanavyoumizwa na watu wa Mr X.

    Wakati Kamishna Shebby akilalama Cj4 yeye alikaa kimya na kuvuta picha na kuona lazima Hussein ndie aliyeanzisha kasheshe huko baada ya kugundua kitu kuhusu Mr X, na si wala kwamba kuna mtu zaidi kavamia ile nyumba na kusababisha mauaji.



    Gari iliiingia mkuku na kugonga geti hadi walinzi walistuka mno na hapo Kamishna Shebby alipiga teke mlango mdogo wa geti baada ya kushuka kwenye gari huku akiwa ameikamatia bastora ndogo mkononi na kustaajabu kukuta walinzi wakiwa wamejificha kwaajili ya kupambana na uvamizi waliotaraji kutokea na wao kushangaa kuona ni Kamishna Shebby.

    Tofauti ya Shebby kwa upande wa Cj4 yeye hakuingilia pale getini zaidi alizunguka eneo la nyuma ya ukuta na kurudi nyuma kutafuta speed ya kukimbia kidogo kabla hajaruka beki kavu tatu zilizompeleka moja kwa moja hadi ndani ya fance sehemu kulipokuwa na bustani ya kupumzika na bwawa kubwa la kuogolea na ajabu zaidi Cj4 alijipanga kwa vita akiwa mikono mitupu.



    * * * *

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Zaaainaab.. Zaiiiiinaaaab.. Zainaaaaaabuuuu leo na wewe lazima ulipe damu ya mwanangu."

    aliongea Hussein bubu huku akipiga hatua kumsogelea mama Shebby kwa hasira pale chini alipokuwa anasote huku akilia kwa uchungu.

    "Hapaanaaaa, hapaaanaa .. aaah! Haaapaana Mume wanguu."

    alijitahidi kutoa sauti mama Shebby japo hakufanikiwa kuitoa kwa nguvu kama vile alivyoilazimisha ila ilitosha kusikiwa na Hussein.

    "Mume wako? Mume wakoo!! hahahaha Mume wako unaemlilia huyu Shetani mtoa roho za watu? hahahaa nakusafirisha sasa hivi umfate huko aliko ila kwanza nataka unijibu swali moja Zai... KWANINI ULINIGEUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MWANANGU NA KUNIHARIBIA MAISHA YANGU YOTE???"

    Aliuliza Hussein kwa hasira iliyokuwa inamfanya hadi atetemeke mwili mzima pindi alipokuwa amemfikia mama Shebby ambae ni kweli kabisa ndie Zai wake yule yule.

    "Hapana Hussein, hapana sikujua kabisa kama yangekuja kutokea mazito kiasi hiki wala sikuweza kuyafanya yasiendelee kutokea aaahggggg nimejiponzajeeee mieeeee."

    aliongea kwa uchungu Zai na kuendelea wakati huo Hussein alikuwa anazidi kutetema kwa hasira akingojea jibu la Zai kabla hajaanza na yeye kumponda ponda kichwa chake kwa kile chuma kilichotapakaa damu.



    "Hussein, unastahiri kabisaaaaa kufanya haya Mume wanguuu......."

    "STOOOOOP. Nihadithie kwanini na wala usinite Mume wangu. Utafanya nikuue kabla hata sijasikiliza jibu lako."

    alimkatisha kwa hasira na kumpelekea Kofi moja kali lililomfanya Zai kupasuka lipsi ya mdomo baada ya kujing'ata kwa kupigiza kichwa pale kwenye ngazi.

    "sawaaaa... sawaaa .. sawa..aaaghhhhh, wala sikumwambia Mr X akuue, wala sikupanga mwanangu azushiwe kuuliwa nawe pamoja na mimi mwenyewe, wala sikuyajua hayo yoteee Hussein. Naomba uniaminiiiii... Ila tatizo wewe hukuwa Mume wangu wa Kwanza kunioa na kunilipia mahali japo ulikuwa mwanaume wa kwanza kuniingiza katika ulimwengu wa mapenzi.

    Sikuona jinsi gani ya kukwambia ukweli hadi unielewe na kuniruhusu nikaishi kwa mume wangu. Hussein najua leoo upo sahihi na mimi ndie niliekuwa nastahiki kulipa nafsi za hao wote.. Lakini unadhani ningefanyajeee? huyo Mr X ndie mume wangu kabisa wa kwanza aliyejulikana hadi na wazazi wangu..... wewe umemjua bibi tu Hussein lakini mimi nilikujua muda mrefu kabla hatujahamia Arusha.



    Na ahadi yako ya utotoni hasa vile ulivyonambia kama utani naona leo inakuwa kweli aaaaaaaah!! Nataka ujue kabla hujaniua kuwa mimi ni KINOGE rafiki ako wa utotoni ZUNGU."

    aliongea kwa uchungu zaidi Zai na kumshangaza tena Hussein baada ya kutajiwa kwa mara ya pili jina la Zungu na kukumbuka siku aliyokubaliwa kuwa na mahusiano na Zai alimwita jina hilo lakini alijikuta anachoka zaidi na kushangaa baada ya kujua kitu ambacho hakuwahi kukijua kumbe Zai ni Kinoge msichana waliyependana mno toka watoto na mara ya mwisho walipoteana wakiwa darasa la tatu.

    "Haaa, KINOGE??!!"

    Alitahayuri akiwa bado na hasira Hussein na ndipo kichwani mwake ilipokuja taswira na picha ile ya Kinoge pindi walipokuwa watoto.





    ..............................

    ZUNGU => Kinoge Ona huyu ndio mtoto wetu, huyu ndio mimi hapo na huyu wewe harafu huyu aliyelala hapa adui nimekufuma nae anataka kuninyang'anya nimempiga nimemuua sasa nakupiga na wewe hapo hahaha nakuacha unalia harafu nam beba mwanangu tunaondoka hukoooo.

    KINOGE => hahaha Zungu bwana, sasa kama wewe baba na mimi mama unafikiri adui atatoka wapi? tutakuwa tunapendana kama baba angu na mama angu si eti eeh?

    ZUNGU => haya ila mi nitampenda sana mwanangu kama baba alivyokuwa ananambia kuwa mimi ndie ndugu yake na sio mamaangu kwani ana ndugu zake. Na wewe utakuwa na ndugu zako na mimi ndugu yangu mwananguuu.

    KINOGE => Jamani Zungu, utakuwa unanipiga?

    ZUNGU => Akuuu, ila nikikukuta na adui nitampiga hadi afe na wewe nitakupiga kibao kimoja tu..

    ^^^^^^

    (<<<>>>) ^^^^ (<<<>>>)

    .....................



    Yalikuwa ni mawazo ya Hussein bubu pindi alipokumbuka mara ya mwisho kuongea na Kinoge siku hiyo majira ya jioni walipokuwa wanacheza mchezo wa kibaba baba huku akiwa ametengeneza watu wa kufinyanga kwa udongo na Kinoge alikuwa anapikapika kwenye vifuu.

    Maneno ambayo aliwahi kuyaongea kitoto toto katika michezo ya watoto leo hii yamekuwa na ushabihiano mkubwa sana na kilichokuwa kinatokea japo hakuwahi kuwaza, kuhisi wala kujua kama Zai ndie rafiki ake wa utotoni yule aliyekuwa akimwita mchumbaake kabla ya wazazi wake kuhama na hakujua walihamia wapi na hata alipokua mkubwa ilifika wakati Hussein alisahau kabisa habari za Kinoge.



    Lakini mbali na hayo yote bado msimamo wa Hussein ulibaki palepale, alishadhamiria kumuua na Zai na alikuwa anasubiri jibu moja tu lenye sababu za msingi kwani yote yale aliyokuwa anazungumza Zai ilikuwa kama anazunguka tu.

    "Uwee Kinogeee uwe Zaaiii nataka kujua kwanini ulifanya yote yale na kuwa tayari kuimwaga damu ya mwanangu kinyama namna ile hata kichwa chake nisikionee?? Wee ni mwanamke wa aina gani!!??? Lazima leo Ufe na hii si kwa niaba yangu tuu, bali ni kwa niaba na damu ya mwanangu mliyeniekea viganja vyake mfukoni ili mkanifunge vizuri Wanyama Mbwa wakubwa nyiee... Hii ni kwaajili ya damu ya mwangu Mwin she heeeeeee...."

    aliongea kwa uchungu Hussein na kukikamatia vizuri kile chuma huku akiwa kanyoosha mikono yake juu kwa niaba ya kuanza kumshushia kisago mama Shebby au Zainabu au kwa jina la utoto Kinoge.

    Lakini akiwa kakamata kile chuma akinyanyua mikono kabla hajakishusha kichwani mwa Zai, ndipo alipopiga ukelele wa kukanusha kile alichokisema na kukiamini Hussein.

    "HAPANAAAA, SIJAWAHI KUUA DAMU YANGU."

    Kauli hii ilimfanya kwanza Hussein asite na kumuuliza Zai.

    "Unamaana Gani? Nini kilitokea juu ya Mwanangu?!!"

    "Hakuna kibaya chochote kilichompata mwanetu Mwinshehe... Mwanao mzimaaaa na ni rafiki ako mkubwa tuuu..."

    "NINI? Unamaanisha nani? Kamishna??"

    "hiiiiihiiii Nisameeeeheeee .. Ni kweliiiii Kamishna Shebby ndie mtoto wetu yuleyule Mwinshehe hiiiiigggr ... Eeee Munguuuu wanguuuuuuu"

    Aliongea mama Shebby na kumzidisha machungu na taharuki Hussein aliebaki katumbua macho huku akiwa haamini kile anachokisikia masikioni mwake.

    "NINI???!"

    "Ndio hivyoooo aaah!! kweli mimi ni mkosaaaaji lakini Shaaban ndie mwnetu yule yule Mwinshehe na hata ile alama bado anayo pale nyuma ya shingo karibu na bega japooo aaaagh haaataa Mwin-chaaande umemuuua bila kutambuaa ukweli huuuuuuu"

    kilio cha mama Shebby sambamba na maneno yake kilizidi kumkasilisha Hussein bubu ambae alizidi kutetemeka kwa hasira kuhu machozi yakimtoka na kuchirizika mashavuni huku yakisukuma damu iliyomgandia Hussein ambayo ilimrukia pindi alipokuwa anamuua mzee Mwinchande Mr. X.

    "Ina maaaaanaaa Zaii.. aaah UmeniekaaUchiiii umenitukanisha vya Kutoshaaaa!!!!! HaaH! siamini mimiii Zainab?? Kinoge?? Mwanamke wa ndoto zangu leo acha maneno yangu yatimieeee"

    aliongea kwa uchungu sana Hussein huku akizidi kunyanyua juu kile chuma na kukaza mikono.

    "Wanawake ni Wauaji... Aaaagh! Wanawake ni Wauaji nyinyiii... Ona kwa sababu yako watu wangapi wamekufa Zai..Ona ulivyonitukanishaaa... Onaa sasaa wanangu mwenyewe nimewaoza mwenyeweeeeee!!! haaaaaaaa...

    siwezi kumlaumu Asha wala Shebby iiiiiihhh Umenitukanajeeee!!? Kinogeee Hustahiri kabisa kubaki hai.. Hustahiri kabisa kuishi Zaiiii hata ninavyokuua leo sipaswi kuhukumiwa kwa hilo kwani hukumu yangu ya kukuua ilishapitishwa na kuitumikia miaka mingi sanaaaaaaa Zai kuishi sasa HUSTAHIRIIII"

    Aliongea kwa hasira sana Hussein na sasa alikuwa anataka kushusha kile chuma kichwani mwa Zai ambae alijua sasa mwisho wake umewadia na hakuwa na ujanja wa kumkimbia Hussein bubu pale zaidi ya kufumba macho kusubiri kusikia chuma kikitua kichwani mwake na kusambaratisha fahamu zake zote kabla ya kuiacha dunia na kwenda kwenye makazi ambayo hajui yakoje.

    Lakini kabla Hussein bubu hajashusha kile chuma kichwani kwa aliekuwa mkewe miaka hiyo bi Zainab ndpo ghafraaaaaaaaaaa mvunjiko wa kioo cha dirisha ulisikika sambamba na mtu aliyevaa mavazi ya polisi magereza mwenye cheo kikubwa alieonekana akiingia kwa mtindo wa kuruka huku mikononi akiwa kakamata mguu wa kuku (bastora ndogo) kishupavu kabisa na pindi alipoangukia tu mule ndani sekunde ileile kwa mbali alipomuona Hussein bubu akiwa anataka kumuua mamaake mzazi huku kushoto kwake akiuona mwili wa babaake mzazi ukiwa umepasuliwa vibaya sehemu za kichwa, nae palepale akiwa kakunja goti mguu mmoja alipiga kelele za uchungu huku akimfatulia risasi yule mtu aliemsimamia mamaake akitaka kumshushia vyuma vya kichwa na alimtambua kabisa kuwa yule ni nani ila aliamini kuwa amechanganyikiwa.

    "HUSSEEEEENIIII BUUBUUUUU"

    Alipiga ukelele Kamishna Shebby huku akiachia risasi mfurulizo kumuelekezea Hussein lakini sekunde ile ile kwa style ya ajabu kabisa alistukia kiatu kikubwa aina ya buti kikitua mikononi mwake Kamishna Shebby na kumshuhudia mwanaume wa shoka Cj4 akitokea upande ule wa juu kwenye ngazi na si kwa kushuka ngazi bali ni kwa kuruka nje ya ngazi na kutua pale alipokuwa anadondoka Hussein bubu na kumdaka kimaajabu na kubimbilika nae hadi maeneo ya mlango wa jikoni ambapo Cj4 aliingia na Hussein bubu na kujibanza nae nyuma ya Friza la kuekea nyama jikoni.

    "aaaaaghrrr Na-kuuu-ku-mbuu-uu-k-kk-kaa raf--f-fiki--ang-gu"

    aliongea kwa shida Hussein bubu mara macho yake yalipokutana na macho ya Cj4 aliekuwa kampakata nyuma ya lile friza lililokuwa karibu na mlango wa kuingilia jikoni.

    "Polee rafiki angu mimi nipo hapa. Utapona tu"

    "We-ni-As--ss-sskari?"

    "Kweli rafiki angu mimi naitwa Cj4 ni askali niliyetumwa na serikali kwaajili ya kujua ukweli wako uliomfanya Shebby ashambuliwe kule Mkuyuni ila sasa kila kitu kipo sawa rafikiangu jikazee"

    aliongea harakaharaka Cj4 huku akimuangalia kwa huruma Hussein bubu ambae damu zilianza kumvuja mdomoni na hata nyengine kuchuruzika kwenye mikono ya Cj4 na kugundua kuwa kuna risasi zilimpata Hussein mgongoni na kujilaumu Cj4 moyoni kuwa alichelewa kumuokoa Hussein.



    "Cj4 kama umeungana na huyo Muuaji wa familia yangu tambua na wewe ni adui yangu sasaaaaa.. Aaaaaaggggggghh"

    aliongea kwa hasira Shebby pindi alipoinuka na kuiokota bastora yake pale ilipodondokea na kuanza kuelekea kule jikoni alibimbilikia Cj4 na Hussein bubu.

    "Mwananguuuuuu Shebbyyyyy usimuuue Husseeeeein ni babaaakoooo"

    alipiga ukelele Zai ambae ni mamaake Kamishna Shebby ili kumzuia mwanae kutoendelea kufanya kile alichokifanya muda mfupi uliopita baada ya kufatua risasi mfurulizo zilizomfanya abaki kainama huku akiziba masikio na macho kwa uoga.

    "Shebiii mwananguuuuu nisikilizeeeee"

    alizidi kupiga kelele Zai lakini Shebby hakujali wala kusikia maneno ya mamaake kwa hasira alizokuwa nazo kwa kuhisi pia huenda na mamaake alikuwa kachanganyikiwa kwani anawezaje kumtetea mtu aliyekuwa anataka kumuua muda si mrefu? na tayari kamuua hadi mumewe? aliona wazi mamaake kachanganyikiwa na alikuwa tayari kupambana na Cj4 ambae alionekana kumtetea Hussein bubu.

    ("Huyu sasa anazidi upuuzi, acha kwanza nimfunze kuwa wanaume wanapokuwa kazini hutanguliza umakini mbele na si upendo.")

    ilikuwa ni sauti ndani ya moyo wa Cj4 huku akimtoa mapajani mwake Hussein bubu pindi aliposikia vishindo vya hatua za minyato vya Shebby vikiwa vimekaribia pale mlango wa jikoni.



    "Shebby mwanangu mimi Sijachanganyikiwaaaa wala huyooo unaetaaka kumuua hajaachanganyikiwaaaa... Nataka Ujue mimi ndie Zainab mke wa Hussein na wewe ndie mtoto wake aliyesingiziwaa kamuuaa na huyooo unayejuaa babaako ndie MR X.."

    kauli hii ya mama Shebby aliyokuwa anaiongea kwa sauti ya uchungu sana na maumivu ndiyo iliyomfanya Shebby asiamame ghfra na kujikuta hadi ile bastora iliyokuwa mkononi mwake ikimdondoka chini kwa mshtuko mkubwa na kugeuka kumtazama mamaake aliekuwa anasota kumfata pale aliposimama mlango wa kuingilia jikoni.

    "Mwananguuu Shebby, Hussein ndie babaako kweli kabisaaa. Ni kweli kabisaaa kweli sisi wanawakeee ni wauajiii aaaaaaaaaghhhh Nisamehe mwananguuuu"

    aliongea huku akilia Zai akiwa amekamata miguu ya Shebby aliejikuta anashindwa kuongea lolote zaidi ya kuchezesha midomo tu kwa mtetemo ambao ulikuwa haukujulikana kama ni hasira au maumivu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maneno yale pia yalisikiwa vizuri sana na Cj4 na hata Hussein mwenyewe aliekuwa anahangaika na roho yake huku kila alivyojitahidi kuongea ndivyo damu zilipozidi kumvuja mdomoni na kubaki anaongea na Cj4 kwa kumtazama tu na alifanya hivyo hata pale Cj4 alipotaka kumlaza chini kwa kujiandaa kumuadhibu Shebby, Hussein bubu alimtazama kwa jicho lile la kumzuia asifanye hivyo.

    "MAMAA !!! Ina maana...."

    alitaka kusema kitu Shebby na kujikuta akishindwa ndipo alipokimbilia ndani mule jikoni kumuangalia Hussein bubu na kumkuta akiwa kashikiliwa na Cj4.

    "Amini hivyo Shebby ukweli huyu ndie babaako."

    alikazia Cj4 pindi Shebby alipoingia ghafra na hapo Hussein alijikuta kama anapata nguvu tena mara baada ya macho yake kukutana na uso wa Shebby na kumuashiria asogee pale na ainame.

    Kwa mwendo wa 'sielewi' na taharuki nyingi alisogea Shebby na ajabu alipoinama tu Hussein aliweza kumuinamisha zaidi na kumuingiza mkono begani mwake kupitia ile kora ya shati ya Shebby na hapo mkono wa Hussein ulikutana na uhisio wa alama kama ile ya lengelenge mtu kaungua ama viuvimbe vyeusi vinavyowatoka watu (sunzua) kikiwa kwa urefu kuelekea maeneo ya begani.

    Shebby alistuka na kutaka kuutoa mkono wa Hussein lakini Cj4 alimzuia aache na baada ya Hussein kuridhika aliutoa ule mkono huku akiwa katabasamu hali iliyowashangaza na hata mamaake Shebby nae aliingia kule jikoni kwa mtindo ule ule wa kusota mithili ya mlemavu huku akiwa bado analia huku akimsisitizia Shebby kuwa yule ndie babaake.

    "ww-wa-ww-waa-aa-n-.."

    alibabaika kusema Hussein na kujikaza kumwambia Shebby na Cj4 pale kwa mara nyengine na wote wakiwa wametaharuki Hussein bubu akarudia tena.

    "uwwwan-aa-ang-uu Wa-na-wa-ke ni- Wa---u-aj-i."

    na hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Hussein bubu na kuaga rasmi dunia akiwa mikononi mwa Cj4 huku pembeni yake alikaa mwanae ambae ni Shebby na kwa mbele mlangoni alionekana Zainab mamaake Shebby.

    "BAABAAA"

    Aliita kwa nguvu Shebby na kujipiga piga kichwa kwa majuto kwani alijua fika risasi zilizofatuliwa kwa mikono yake mwenyewe Shebby ndio zilizosababisha umauti wa mtu ambae alikuwa hajui kwanini moyo ulimsukuma mno kumsaidia na leo hii anajua akiwa amemuua kwa mkono wake akijua anamtetea mtusahihi kumbe sivyo.

    Lakini toka hivyo Shebby alisimama na kutoamini kama yule ni babaake na yule ndie Mr X na wazo hili lilipomjia alikumbuka kauli ya yule marehemu Mnyungunyungu kuwa mr X ana alama usoni nahapo alijikuta anaingiwa roho mbaya nusu chizi Shebby alirudi pale ilipokuwa maiti ya mtu aliyeamini siku zote ni babaake na kuanza kumpekua usoni ambapo alikuwa na mdevu nyingi na katika hali ambayo hakuitaraji ni kweli aligundua alama ya X iliyokuwa usawa wa chini ya kidevu karibu na koromeo na hapo ndipo alipoanza kuamini sasa kuwa kweli yule mtu aliyedhani babaake alikuwa ndie mr X na jina X lilitokana na ile alama yake ambayo huwezi kuiona kwa kumtazama tu, lakini alijiuliza kwanini yamekuwa yote yale? ndipo hapo kwa uchungu mno Shebby alianza kulia huku akimuuliza swali mamaake kwanini imetokea yote hayo.

    "Maaaaaa Why? kwanini mama yamekuwa yote hayaa? aaaaghh"

    Maumivu aliyokuwa nayo Shebby hayapaswi hata kusimuliwa kwa jinsi alivyokuwa anaumia huku akifikiria kwanza kamuoa dadaake, pili kamuua babaake wa kweli, tatu ni kwanini mamaake aliishi na siri iliyokuwa inapoteza roho za watu kila siku???

    "Mwanangu Shebby ni kweli sistahiri kabisa kuishiii aaaaah! leo nimejifunza wakati tayari ni too late, ila naamini mwanangu mimi ndio chanzo cha yote hayaa... Eee Mungu naomba unipe tu hukumu inayostahiki juu yangu ..... Shabaan mwanangu vyovyote utachoamua unisamehe ama usinisamehe lakini ukweli mimi ndie chanzoooo aaaaaaaah! Ama Kweli sisi Wanwake ni Wauaji."





    CHANZO



    ( MIAKA 50 NYUMA )

    .................................

    ...............



    Ilionekana familia moja ya bwana na bibi Juma wakiwa katika kupanga panga vitu vyao husasi mabegi na kadhalika huku vijana wengine watatu walionekana kubeba viti, mbao za kitanda sambamba na magodoro wakipeleka nje na kupakia kwenye gari moja aina ya Canter iliyopaki karibu kabisa na ile nyumba ikionesha dhahiri bwana na bibi Juma walikuwa wanahama sehemu ile na kuhamia sehemu nyengine kwenye makazi mapya.



    Wakati heka heka za kuhama zikiwa zinaendelea, upande wa pili kulipokuwa na nyumba inayotazamana na ile ambayo walikuwa wanaishi bwana na bibi Juma alionekana kijana mdogo wa kiume mwenye umri usiopungua miaka 12 akiwa amekaa mlangoni ameshika tama huku akiwa na huzuni kubwa wakati anaishuhudia familia ile ikihama pale mtaani kwao.

    Moyo ulimuuma sana yule mtoto ambae alikuwa maarufu pale mtaani kwa watoto wenzie kwa jina la Zungu japo jina lake halisi halikuwa hilo.

    Kilichokuwa kinamuumiza zaidi si kuhama kwa bwana na bibi Juma bali ni kuondoka pamoja na mtoto wao mdogo wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 8 ambae alikuwa ni rafiki ake mkubwa sana shule na mtaani walicheza wote na mara nyingi walipenda kujiita baba na mama.

    "Kinoge mbona humuagi rafiki ako Zungu si unamuona alivyopooza"

    aliongea bwana Juma kumuambia mwanae yule wa kike ambae nae alionesha kutoipenda kabisa ile safari na alijisikia moyo kumuuma hata kumuaga kwa mdomo rafiki ake zaidi ya kumuangalia kwa jicho huruma na kumnyooshea mkono wa kwaheri pindi alipokuwa anapandishwa ndani ya gari ile mara baada ya kila kitu kumalizika kupakiwa.

    ("wewe ndie rafiki niliekuzoea, leo hii unaondoka na kuniacha mwenyewe. Najua huko utapata rafiki mwengine utayecheza nae kama mimi kibaba baba lakini jua kama nikimuona nitamuua kwa kua atakuwa tayari adui yangu.")

    aliwaza maneno mazito sana yule mtoto Zungu pindi alipoishuhudia gari ile ikiondoka eneo lile la mtaani kwao na kumuachia msiba mzito wa upweke moyoni mwake.





    "Hussein mwanangu, usiwe mnyonge hivyo. Ndugu yako nipo hapa si nishakwambia...? mimi ndio ndugu yako babaa"

    ilikuwa ni sauti ya mwanaume mtu mzima iliyosikika nyuma ya mlango alipokaa mtoto Zungu ambae jina lake halisi alikuwa anaitwa Hussein.

    Sauti ile ilimfanya Hussein ageuke huku machozi yaliyojazana machoni muda mrefu alipokuwa anawaangalia kina Kinoge wakihama bila kupepesa macho, yalianza sasa kutiririka mashavuni mwake na kumtazama kwa uchungu yule mtu aliyemsemesha.

    "baba, babaa unajua inauma sana. sasa wewe umewezaje kukaa mwenyewe na kuvumilia bila kulia pindi mama alipoondoka?"

    aliuliza mtoto Hussein na kumfanya yule mtu ambae alikuwa ni babaake mzazi amnyanyue pale na kumkumbatia kwa nguvu huku akimsihi atulize kwanza moyo kwa kumshikashika kichwa akizichezea nyele zake ndogo za kipilipili huku mkono mwengine akimpigapiga mgongoni.

    "Mwanangu Hussein, mbona ni rahisi sana baba...! ni rahisi mwanangu twende ndani nikakuhadithie"

    aliongea babaake Hussein na kumchukua mwanae mpaka chumbani kuwapisha wapangaji wengine waendelee na shughuli zao mida ile pale ukumbini waliposimama jilani na mlango wa kutokea.



    "Mwanangu mamaako amekuacha ungali una miaka mitano lakini japo nilimkumbuka ila haikuwa sababu ya kunifanya niwe mnyonge na kukosa kabisa furaha. Unajua kwanini?"

    alianzisha maongezi babaake Hussein pindi walipokua wamekaa kitandani pale chumbani kwao.

    "hapana baba, sijui"

    "Kwa sababu wewe ulikuwepo, unajua kwanini uwepo wako ulikuwa sababu ya mimi kukosa huzuni na kuwa na furaha mbali ya kuwa mamaako hakuwepo tena?"

    "Hapana baba sijui."

    "Kwa sababu wewe ndie ndugu yangu na yule alikuwa mke wangu na ndio maana ameolewa tena na mwanaume mwengine na hata huko anaweza kuondoka tena na kuolewa pengine."

    "aaah, sasa baba na mimi mama sio ndugu yangu?"

    "Hapana mwanangu, wewe ni zaidi ya ndugu yako kwa sababu wewe ni mwanae na yeye ni mamaako unapaswa kumuheshimu na kumtembelea mara kwa mara."

    "sawa baba, kwa hiyo Kinoge sipaswi kumlilia kwa kua sio ndogo yangu na huko aendako anaweza kupata rafiki kama mimi na wakihama tena atamuacha na kwenda kupata rafiki mwengine ikawa hivyohivyo eeeh.."

    "Ni kweli kabisa mwanangu, hutakiwi kumuweka sana moyoni mwanamke mwengine zaidi ya mamaako mzazi ambae hawezi kuondoka na kukuacha moja kwa moja hata uwe uweje, ila hawa wengine mwanangu usiwaamini kabisa na kuwaeka sana moyoni kwani wataweza kukusababishia maumivu na mateso makubwa pindi watapogeuka na kwenda kwengine."

    "sawa baba"

    "Ndio hivyo mwanangu hupaswi kuumia mimi nipo na hata kama nisipokuwepo amini wa kukusaidia kweli ni mwanaume mwenzako japo wanawake ndio wanaoonekana kuwa na mioyo mepesi ya kusaidia lakini bado msaada wa ukweli upo kwa mwanaume baba. haya nyamaza wewe ni mmwanaume shika hela hii kanunue chapati uje tunywe chai"

    "Asante baba nimeelewa, nami nakuahidi sitoumia tena kwa sababu ya Kinoge"

    aliongea Hussein na kufuta machozi baada ya kuchukua pesa kwenda kununua hivyo vitafunwa huku akimuacha na tabasamu zito babaake.



    * * * * *



    Safari yao iliwachukua masaa mengi garini siku hiyo tokea asubuhi ile walipoliacha jiji la Dar na kuingia jijini Arusha majira ya saa moja usiku ambapo safari bado iliendelea mpaka kwenye vijiji vya mbali na Arusha mjini na huko ndiko kulikokuwa na makazi mapya ambayo walihamia familia ya bwana na bibi Juma pamoja na mtoto wao kipenzi aliyeitwa Kinoge.

    "haaa! mamaa ndio tumefika hapaa!!?"

    aliuliza kwa mshtuko Kinoge pindi alipoyaangalia mazingira waliyofikia kwa nje ambapo muda huo wale vijana waliopakia vitu kule jijini walikuwa wanavishusha wakipewa maelekezo pa kuviingiza na bibi mmoja ambae ndie alikuwa mwenyeji wao aliyewapokea.

    "Kinoge kwani wee unapaonaje si pazuri tuu.. tena huku kuna maembe na machungwa kibaoo unayopenda furaaaahi basii."

    mama alijaribu kumliwaza mwanae ambae sasa alikuwa tayari kakunja uso kutokana na kuchukizwa na mazingira yale ya kijijini.

    Aliangalia kwanza hakukuwa na umeme, hakukuwa na barabara nzuri, nyumba zilikuwa zipo mbalimbali hali iliyomuumiza Kinoge na kuona ni afadhali wangemuacha jijini Dar na rafiki ake Zungu asingekuwa mpweke kuliko kuletwa pale ambapo aliamini hata marafiki wa kucheza nao kama Zungu hawakuwepo.

    "iiihhhhhhyyaaaaaaaaaa.. sipaaatakiii mimiiii... Nirudiisheeeni kwa Zunguuuuu"

    alianza kulia kwa sauti Kinoge na mamaake kujitahidi kumnyamazisha wakati huo babaake alikuwa anasombelea vitu na kuvipanga kwenye ile nyumba pamoja na wale vijana.



    Baada ya shuguli zote za uhamiaji kukamilika na ile gari waliyokuja nayo kuanza safari kuelekea mjini na hatimae sasa Kinoge aliamini kuwa kweli wamefika na hasa pale alipokuja babaake na kumwambia.

    "Mwanangu Kinoge, maisha ni mlima leo unapanda kesho unashuka harafu maisha ni popote usiangalie mazingira kwanza ukayakimbia unafikiri hata kule mjini kulikuwa vile? kule napo kulikuwa kama huku.. Watu wakahamia na kupasafisha wakaishi na kupatengeneza hadi leo umepaona vile. Basi hata huku napo kutakuwa kama vile endapo tutakaa na kupatengeneza. Haya twende ndani ukasalimiane na bibi eeeh"

    Maneno ya babaake ndio yaliyompa nguvu Kinoge na kupiga moyo konde kuwa tayari kuanza maisha mapya.



    Bwana Juma ambae ni baba mzazi wa Kinoge yeye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi na wakati huo alikuwa amepata uhamisho wa huko Arusha ambapo aliuomba yeye mwenyewe ili apate nafasi ya kurudi nyumbani kwa mamaake ambae alikuwa mzee na alihitaji uangalizi wake na kwa kuwa miaka mingi aliipoteza Dar mpaka anazaliwa Kinoge na kufikia umri ule alikuwa hajawahi kufika pale kijijini lakini sasa hawakuwa na budi wote kwa pamoja walihamishia makazi kijijini kabisa.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kinoge kupotezana na Zungu.



    Maisha ya pale kijijini yalikuwa magumu sana kwa Kinoge na si ugumu wa kula au kuvaa bali ni ugumu wa kuchangamka na marafiki.

    Hakukuwa na watoto wengi kama ilivyokuwa Dar na mambo yao yaliendeeshwa kimira sana tofauti na Dar walivyokuwa wanaishi kizungu na kujiachia sana.

    Na hata alipoamishwa shuleni bado mambo yalikuwa magumu na alikosa kabisa marafiki wazuri walioendana na rafiki ake aliyemuacha Dar ambae alikuwa amemzoea kwa jina la Zungu.



    Upweke uliendelea kwa Kinoge miezi mitatu zaidi kabla ya siku moja ambapo alishuhudia ugeni wa watu kadhaa nyumbani kwao walioeka kikao na wazazi wake kwa muda mrefu huku yeye akiwa amekaa nje na mtoto wa kiume aliyekuja na wale wazee ambae yeye alionekana mkubwa kuliko Kinoge na kuliko hata rafiki ake wa Dar Zungu.

    "Eti wewe unaitwa nani?"

    Kinoge alimuuliza rafiki ake yule mpya waliekuwa wanacheza wote pale nje.

    "Naitwa Mwin-Chaa-nde umeona mjina wangu huoo!!!? wewe jee?"

    alijibu yule mtoto na kumuuliza tena Kinoge swali

    "Mi naitwa Kinoge."

    "KINOGE!!!?"

    "Eeeh"

    "hahahahahahaaaaaaaaaaaa"

    "sasa mbona unanicheka?!"

    "Una jina la Kishaaaambaa Duh!.. Kinoge??!"

    alicheka sana na kustaajabu yule mtoto wa kiume aliyejitambulisha jina la Mwinchande na kulicheka jina la Kinoge kabla wazazi wake hawajatoka mara baada ya kumaliza kikao mule ndani na kuagana nae huku Kinoge akiwa amekasirika kwa kuchekwa na Mwinchande juu ya jina lake.



    Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kinoge kukutana na Mwinchande ambae nae alihamishiwa shule ile aliyokuwa amepelekwa lakini tofauti Mwinchande alikuwa darasa la sita huku Kinoge ambae awali alikuwa anaingia darasa la tatu ila alianzishwa tena la pili kutokana na kuwaishwa sana shule.

    Mazoea yao yaliyoambatana na utani ndio ikawa sababu Kinoge kutaka kubadilishiwa jina na wazazi wake ambao awali walijua ni mambo ya utoto lakini walipoona mtoto wao anang'ang'ana sana na kukosa furaha na amani shuleni na mtaani ndipo alipofika la tatu walifanya masahisho ya jina Shuleni na kumwita jina la Zainab.

    Jina ambalo lilitolewa na bibiake, mama wa babaake waliekuwa wanaishi nae pale kijijini.



    Kuanzia siku hiyo Kinoge alifurahi sana na kulitangaza kila sehemu jina lake jipya huku akiwa hataki kabisa mtu amwite jina la Kinoge.

    Safari hii alimtambia rafiki ake yule ambae hakujua wanakoishi lakini ilikuwa kawaida kila baada ya siku mbili wazazi wake walikuwa wanakuja kukutana na wazazi wa Zai kuzungumza na katika hali ya kushangaza siku hiyo Zai alishangaa kuona wazazi wa rafiki ake wakija kwao huku mikononi wakiwa wameshika kamba zilizokuwa zinawavuta Ng'ombe wawili wakubwa na kuwaingiza katika zizi moja la miba lililokuwa awali kwaajili ya mbuzina kuwachanganya wale ng'ombe.

    Awali ya yote Zai alikuwa hajui nini Kinaendelea kwani mifugo ilizidi kuletwa taratibu na hatimae baada ya mwaka mmoja lilijengwa zizi kubwa lililokuwa na Ng'ombe sita sambamba na mbuzi wanane wote wakiwa wameletwa na wale wazazi wa yule rafiki ake wanaetaniana taniana aliyeitwa Mwinchande ambae mwaka huo ndio alikuwa yupo darasa la saba huku Zai akiwa darasa la tatu.



    Kumbe nyuma ya pazia kilichokuwa kinaendelea na ambacho kimeongelewa na wazazi wa pande zile mbili ni juu ya kuwaunganisha watoto wao ili watapokuwa wakubwa waishi pamoja.

    Na hivyo wazazi wa Mwinchande walikuwa wanalipia kabisa mahali ya mtoto wa bwana Juma ambae ni Zai ili awe mke halali wa mtoto wao wa kiume ambae ni Mwinchande.

    Habari ile ambayo kumbe hata Mwinchande alikuwa anaijua na pindi alipokuwa anamwita Zai mke wangu nae Zai akimwita Mwinchande mume wangu akihisi ni utani tu bila kujua kuwa tayari kuna ukweli ndani yake hadi siku moja alipoitwa na wazazi wake na kumwambia kuwa anapaswa awaheshimu sana wale watu aliokuwa anawaona wanakuja na Ng'ombe pale nyumbani kwani wamelipia gharama za yeye kuja kuishi na Mwinchande baadae pindi atapomaliza masomo yake.

    Ilikuwa ni kawaida kimila kipindi hiko kuwaoza watoto wangali wadogo japo serikali ilipiga marufuku suala hilo na kuwapa adhbu kali kisheria wale waliobainika kuwaoza mabint zao wangali watoto lakini pia ilikuwa ngumu kuwagundua kama ilivyokuwa kwa Zai na Mwinchande ambao wazazi wao waliwahimiza kuhusu shule.



    Baada ya shughuli za kimila kukamilika kipindi hiko Mwinchande alimaliza darasa la saba na Zai ndio alikuwa anaendea darasa la Nne waliunganishwa kwa kufungishwa ndoa ya siri nyakati za usiku na kuanzia siku hiyo kila mmoja alipewa nasaha na kuonywa na wazee kuwa asije kuthubutu kumtaka mtu mwengine wa kuishi nae hapo baadae kwani tayari wao ni mke na mume na watapokuwa wakubwa hawataoana tena bali wataishi pamoja na kuanzia siku hiyo jukumu la huduma za Zai lilisimamiwa na wazazi wa Mwinchande.



    * * * * *



    Mikosi ilianza kumkumba Hussein miezi michache baada ya kumpoteza kwa kuhama rafiki ake kipenzi aliyekuwa akitaniana nae kama mkewe na hatimae babaake kipenzi ambae ndie aliamini rafiki wa ukweli nae alifariki dunia.



    lilikuwa ni zaidi ya pigo kwa mtoto Hussein japo ndugu wengi walitaka kumchukua lakini hatimae aliondoka na mamaake ambae nae haikupita miezi mitatu alifariki ghafra na kuzidi kuongeza pengo la uyatima moyoni mwa Hussein na hapo ndipo alipochukuliwa kulelewa na mjombaake kaka wa mamaake lakini bado hakuwa tena na furaha kwa kuwapoteza wazazi wake mfurulizo namna ile pia aliumizwa mno na maneno ya watu yaliyokuwa yanasemwa mitaani kuwa wale wazazi wake wote walikuwa na virus vya Ukimwi na ndio ilikuwa chanzo cha kuachana kwao miaka mitano iliyopita.

    Aliumia sana Hussein kwa kuwa tayari alikuwa darasa la nne na mambo ya Ukimwi walishaanza kufundishwa tokea darasa la tatu na alijua kuwa ni ugonjwa m baya na wa aibu mtu kukutwa nao kwa hiyo wanaohadithia wazazi wake walikuwa na ugonjwa huo aliwachukia sana na kuwaona ni watu wabaya upande wake.



    Maisha na kwa Mjomba hayakuwa ya kudumu sana baada ya kuchukuliwa na babaake mkubwa aliyekuwa mganga wa kienyeji lakini huko nako alikaa muda mchache kabla shangazi yake kumchukua baaaaasi ilimradi Hussein alikua kwa kulelewa kama mpira wa kona mpaka ile siku alipowashangaza watu kwa kusema anataka aishi mwenyewe kwenye nyumba ya kupanga.



    Maisha yalienda ilimradi siku zinaenda na Hussein alisoma kwa Shida mpaka anamaliza darasa la saba hapo ndipo alipoanza kuhangaika mitaani kufanya kazi mbalimbali ili mradi mkono uende kinywani na hakuchoka kujituma.

    Muda wote alipenda kujichanganya na watafutaji wenzake huku akiwa na ndoto siku moja maisha ataweza kuyamudu nae kujenga nyumba kutimiza mawazo ya babaake ambae mpaka anafariki hakuweza kuwa na nyumba japo alitamani kufanya hivyo.



    Wahenga walisema 'Mungu hamtupi Mja wake' na ndivyo ilivyokuwa kwa Hussein miaka sita baada ya kuhitimu darasa la saba alibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ambayo iliweza kumlipa pesa zilizomuwezesha kuyamudu sasa maisha yake na kuheshimiwa hata na baadhi ya ndugu zake kwa juhudi alizozionesha na hapo sasa alianza kuyafurahia maisha.



    Kipindi hiko alikuwa ana umri wa miaka 21 na hapo ndipo alipoanzisha mahusiano na msichana mrembo aliyeitwa Mariam huku akiwa kasahau mambo mengi ya utoto akiwemo yule rafiki ake wa utotoni aliyeitwa Kinoge.

    Mapenzi yake na Mariam yalikuwa mazuri mwanzoni lakini baadae kidudumtu kiliingia mara baada ya mwaka mmoja wa mahusiano yao pindi alipokuwa anaangalia kipindi cha YA WALIMWENGU kupitia Becker TV ambapo kulikuwa na mada ambayo msimuliaji alilaani kuwa Wanawake ni Wauaji.

    Mada hiyo ndio iliyompotezea muda Hussein na kusahau juu ya ahadi ya kukutana na mpenzi wake yule ambae tayari karibu robo tatu ya ndugu zake walishamjua.

    Ugomvi wao wa ghafra uliosababishwa na kile kipindi mara baada ya Mariam kufika pale kwa mchumbaake na kukuta muda mwingi akiwa bussy na tv kuliko yeye na zaidi alichefuliwa na kile kipindi hali iliyomfanya Mariam aondoke kwa hasira na katika kumtafuta kwake Hussein kwa mara ya kwanza ndipo alipoyaelewa maneno ya kile kipindi mara baada ya kuchezea kichapo cha aibu ndani ya fukwe za coco pindi alipomfumania Mariam akiwa na mwanaume mwengine na hapo ndipo alipoapa kutopenda tena, lakini mapenzi yana nguvu sana na hii ilidhihiri mwaka mmoja baadae baada ya maisha ya kibachela walipopata safari ya kikazi Arusha huko ndipo alipokutana na msichana ambae awali alitokea kumuota kabla hawajaonana kweli akiwa na rafiki ake.

    Msichana huyo ndie Zai kama alivyoota lakini hakuwahi kufikiria kama Zai yule ndie Kinoge rafiki ake wa utotoni.



    * * * * *



    Kwa upande wa maisha ya Zai mara baada ya kuozeshwa kimila akiwa bado mtoto maneno ya wazee na wazazi wake yalimjengea hofu ya kuja kukiuka kuwa hajaolewa au kuwa na mwanaume mwengine.

    Na kwa hali ile ilibidi ampende zaidi Mwinchande na hasa mara baada ya wazazi wake kufariki kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea Arusha mjini na hatimae Zai alibaki yatima pindi akiwa darasa la sita wakati huo Mwinchande alikuwa kidato cha tatu akisomea Arusha mjini na ilikuwa kila mwisho wa wiki alirudi kijijini na kuleta zawadi mbalimbali kwa mkewe ambae nae sasa alikuwa anaelewa nini maana na aliamini kuwa Mwinchande ndie mumewe na hana uwezo wa kupinga hilo.

    Alisahau kabisa habari za Hussein ama Zungu kama alivyopenda kumwita mwenyewe na aliridhia ndani ya moyo wake pindi atapomaliza masomo kuishi na Mwinchande kama ilivyo mipango kwani alikuwa tayari ni mumewe.

    Lakini kipindi cha kiangazi watu wakiwa katika kuandaa mashamba bahati mbaya lilitokea janga la moto pale kijijini.

    Moto ulioacha misiba ya kihistoria na huzuni kubwa kwa wanakijiji mara baada ya nyumba nyingi kuungua na mifugo ikiwemo nyumba ya kina Mwinchande ambapo msiba mzito ulitokea mara baada ya wazazi kushindwa kujinusuru na kuteketea huku Mwinchande pekee ndie akisalimika halikadhalika kwa kina Zai napo bibi pamoja na mjukuu wote walifanikiwa kutoka salama japo nyumba yao na zizi vyote viliungua.



    Ulikuwa ni zaidi ya msiba kilio kila kona serikali na manispaa ya jiji la Arusha waliwasaidia wahanga wa moto na kuwatengea eneo kulekule kijijini.

    Kwa upande wa Mwinchande alikuja Shangazi yake aliekuwa anaishi jijini Dar na kujitolea kuondoka nae kumuendeleza kielimu Huko japo shangazi alijua kuwa tayari mwanae ana mke aliyeozeshwa kimila lakini alipuuzia na kuona ni mila potofu na ndio sababu ya kumuacha Zai aendelee kusoma pale kijijini na hata siku Mwinchande anaondka na Shangazi ake mara baada ya kumaliza misiba bibi alimpa moyo mjukuu wake Zai kwa kumwambia asiwe na wasiwasi mumewe anaenda kutengeneza maisha yao na atarudi kumchukua.



    Lakini mambo yalizidi kwenda kombo baada ya miaka kuzidi kupita toka kuondoka kwa Mwinchande na shangazi yake huku maisha pale kijijini yakizidi kuwa magumu mpaka pale alipomaliza darasa la saba na kujikuta akikaa zaidi ya miaka miwili mbele bila kuuona uso wa mumewe hadi siku moja alipokuwa katika mizunguko Arusha kipindi hiko alikuwa na umri wa miaka 17 alistuka pindi alipoitwa jina na mtu asiyemfahamu japo kwa mbali sura yake haikuwa ngeni ila alificha.

    Hakujua mwnzo kama yule ndie Zungu wake kipindi cha utoto na Zungu hakujua kuwa yule ndie Kinoge wake wa utoto na kwa bahati mbaya hayo majina yalikuwa yashakufa kwao wote. Zungu alifahamika zaidi kwa jina la Hussein ambalo Kinoge alikuwa hajalizoea na Kinoge pia alifahamika kwa jina la Zainab ambalo Zungu hakuwahi kulisikia kabisaaaaa.



    Baada ya kukutana na yule kijana ambae hakutaka kumwambia jina lake alilijua vipi wakati hawajawahi onana Zai aliondoka huku akiwa na namba ya simu ya yule kijana ambae alimsihi na kumwambia atapompigia ndipo atamwambia amelijuaje jina lake.

    Na kutokana akilini mwa Zai kuhisi kama kuna taswira ilikuwa inamjia juu ya yule kijana hakusita sana kuichukua ile namba huku akiwa nae anaumiza kichwa pindi alipoondoka kufikiria wapi aliwahi kumuona yule mtu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini kwa bahati mbaya alipofika nyumbani alisahau kabisa ile namba mara alipoiweka kwenye begi na yote ilichochewa na mawazo mengine aliyokuwa nayo juu ya mumewe Mwinchande kwani licha ya uzuri aliobarikiwa Zai lakini bado aliweza kujidhibiti na kujitunza kwa wanaume mbalimbali akikwepa vishawishi akiamini yeye ni mke wa mtu lakini huyo mumewe amekuwa mpotevua na miaka ikawa inazidi kupogoma.



    * * * * *



    Walionekana vijana wapya wa polisi wakiwa wanapangiwa maeneo baada ya kuhitimu mafunzo ya pili ya jeshi la polisi na kuajiliwa kuwa askali rasmi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Kila mtu alifurahi pindi majina yalipokuwa yanatajwa na mahala husika ambapo miongoni mwa majina ya wale askari wapya lilisikika jina la Mwinchande na mahala alipopangiwa ambapo ilikuwa ni mkoa wa Pwani Kibaha.

    Alikuwa ndie yeye Mwinchande mume wa Zai mara baada ya kusoma mpaka kidato cha sita na kwenda kujiunga na jeshi la polisi baada ya kufanyiwa mpango na shangazi yake.



    Nyota ilikuwa upande wake Mwinchande toka ajiunge na jeshi la polisi kwani baada ya mwaka mmoja zilitokea nafasi adhimu ya vijana watano waliohitajika kwenda israil kuchukua mafunzo mapya yaliyokuwa yanatolewa jinsi ya kupambana na waharifu wanaotumia akili nyingi tofauti na zile mbinu zilizokuwa zinatumiwa na nchi nyingi za kiafrika hususani Tanzania walichofundishwa ni jinsi ya kumdhibiti na kupambana na muharifu kwa utumia nguvu zaidi na silaha inapobidi.

    Nafasi ilikuwa imetolewa kila nchi askari watano na kwa bahati nchi ya Tanzania miongoni mwa askari wengi walioomba hiyo nafasi, mwisho wa siku majina matano yalivyotoka na jina la Mwinchande lilikuwa miongoni mwa Askari wanaohitajika kwenda huko Israel ambapo kozi nzima ilikuwa ni ya miaka miwili.



    Na huo ndio ukawa mwanzo wa Mwinchande kuvuka mipaka ya nchi na kuzidi kutanua milango yake ya kufikiri na kujengeka fikra pana huku moyoni mwake akimkumbuka mke aliyeozeshwa na wazazi wake na mara zote Mwinchande aliamini yule ndie mkewe na hatoolewa na mwengine kwa kuwa wao hawakuachana.

    Na kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia Zai moyoni na kumpenda aliamini atamkuta tu hata kama atakaa zaidi ya miaka mitano huko Israel na hii ilimpa moyo kutokana kabla hajaondoka alimpa maagizo rafiki ake aliyekuwa mganga wa kienyeji ambae alifahamiana nae mara baada ya kuugua ghafra kipindi akiwa mgeni pale pwani na kuonekana matatizo yaliyomkumba yalikuwa ni ya kienyeji baada ya watu washirikina kumjaribu na hapo ndipo alipopewa msaada na mkuu wake wa kituo ambae alikuwa ni Inspector Cyplian kwa kumpeleka kwa mtaalam wa mitishamba na ramli aliyesifika ambae alikuwa anapatikana katika kijiji cha Hakipo kilichokuwa maeneo ya Kibamba pembezoni kabisa mwa jiji la Dar.

    Hapo ndipo urafiki wa Mwinchande na Mganga yule ambae alifahamika kwa jina maarufu la Mnyungunyungu ulianza baada ya kuwa anamtembelea mara kwa mara na hata zilipotokea zile nafasi alimlilia Mnyungunyungu aangalie uwezekano wa kulifanya jina lake ling'ae na liwe miongoni mwa majina yatayochaguliwa kwenda kwenye hiyo kozi.

    Na kweli jina lake lilipotoka Mwinchande alizidi kuamini kuwa Mnyungunyungu kweli ni kiboko na ndio kikawa chanzo kabla hajaondoka alimuhadithia kila kitu kuhusu mkewe aliyeozeshwa angali shule na alimuomba Mnyungunyungu afanye dawa ambayo itamuwezesha pindi atapoonana na yule mkewe asije kubadilika yaani ampende vilevile kama zamani hata kama kuna mwanaume atakuwa kashaingilia kati kipindi yeye hayupo.

    Na hili ndilo lililomuaminisha Mwinchande ambapo pia alimuomba shangazi yake kama atapata muda aende akamchukue mkewe kule kijijini japo alijua kwa Shangazi yake kufanya vile itakuwa ngumu kutokana yeye hakuipenda kabisa ile mila iliyotumiwa.

    Na baada ya wiki kadhaa toka uteuzi ule ufanyike hatimae ndipo Mwinchande alipoungana na wenzake kwa safari hiyo ya nchini Israel kwaajili ya hayo mafunzo maalum.



    * * * * *



    Siku zilikatika kwa upande wa Zai maisha ya kusubiri yalizidi kumchosha lakini bibi ndie alikuwa mstari wa mbele kumsihi na kumpa moyo kuwa mumewe atarudi tu kwani ile ni mira na haivunjiki kamwe.

    "Bibi mi sidhani kama kweli Mwinchande atarudi kunichukua wakati huko mjini nasikia kuna wanawake wengi wazuri kama nini.."

    "Hapana mjukuu wangu Zainab Mwinchande ni wako, yule ni mume wako.. Atarudi tu kukufata wee subiri mjukuu wangu, kikubwa ni kuzidi kujisitiri na kusali kila siku.. Usiache kabisa kusali na kumuomba Mungu yeye ndie mjuzi."

    alisisitiza sana bibi Zai mara Zai alipokuwa anahoji juu ya suala lile la kurejea tena kwa Mwinchande.



    Lakini baada ya muda tena ndipo ilipokuja barua pale kijijini iliyotokea jijini Dar ikimtaka Zainab afanye safari ya kwenda huko ambapo anaishi mumewe.

    Na barua iliandikwa na shangazi wa Mwinchande mara baada ya kuona Mwinchande akimuulizia sana juu ya kumfata huyo mkewe ambae yeye hakumpenda kabisa wala kumuhitaji kwani alihisi kile kilichofanyika ni dhulma tu kuwachagulia watoto wanaume/wanawake wa kuishi nao.

    Lakini aliona kwa kuwa Mwinchande mwenyewe king'ang'anizi, aliamua kutuma tu hiyo barua kama ataweza huyo bint aende kama atashindwa basi na ndani ya barua pia kulikuwa na namba yake ya simu.



    Moyo wa furaha ulimripuka sana Zai baada ya kupata ile barua na kufanya mawasiliano na shangazi mtu.

    Nahapo sasa ilibaki kazi ya kufuafua na kujiandaa kwenda Dar es salaam jiji ambalo aliondoka akiwa bado mtoto na toka miaka hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kurejea tena jijini.

    Lakini wakati akipekuapekua ndipo alipokiona kile kikaratasi chenye namba za simu za yule kijana aliyewahi kutana nae siku moja na hapo ndipo alipokumbuka kumpigia akiwa na shauku ya kujua alimjuaje? kwani upande wake alishindwa kabisa kumkumbuka vizuri.

    Mara baada ya simu kupokelewa na Zai kujitambulisha alimuuliza tena lile swali huku akimuomba amwambie walipoona na hadi kumfahamu kwani hawatoweza kukutana tena kutokana na safari yake ya jijini Dar.

    Lakini alishangaa baada ya yule kijana nae kumwambia kua yuko huko huko Dar na pindi atapofika basi wataonana na atamwambia alimjuaje.



    Alisafiri salama usalimini toka Arusha hadi katika jiji la Raha na Karaha na alipofika ubungo alipokelewa na Shangazi yake Mwinchande na kufika nae Kinondoni ambapo ndipo walipokuwa wanaishi.

    Wiki moja baadae Zai alifanya mawasiliano na kukutana na Hussein maeneo ya stendi Mkwajuni baada ya kumuacha shangazi yake akiwa amelala mchana ule lakini alipofika kuongea na Hussein nia na madhumuni kujua alimjuaje juaje alishangazwa na majibu ya Hussein eti kuwa alimuota ndotoni.

    Akilini mwake Zai alihisi hawa ndio wale wanaume aliowasikia wapenda ngono na kumtaka kila msichana mzuri na hivyo alimkataa kabisa palepale na kumsisitizia kuwa yeye kilichomleta Dar ni masomo na si vinginevyo, jambo ambalo moyoni mwake alijua si kweli lakini hakuona umuhimu kumwambia vile kutokana na jinsi yeye mwenyewe alivyo.



    Aliporudi ndipo kwa mara ya kwanza alianza kuigundua roho mbaya aliyokuwa nayo Shangazi ake Mwinchande mara baada ya kumkuta ameamka.

    "Hee! yaani wewe huna hata mwezi tayari ushavijua hadi vichochoro vya kukuniwa?... Wewe ni bint wa aina gani unafanywa hadi mchana huu tena ugenini..? haya utanambia ulipokuwa wapi na umalaya wako usije kuniulia mwanangu.."

    alibwata shangazi na kuanza kumpiga Zai na ufagio uliokuwa pale ukumbini kama mtoto mdogo.



    Maisha yalienda kwa mtindo huo pale nyumbani na kipindi hiko chote hakuwahi kupata nafasi ya kuzungumza na mumewe ambae ni Mwinchande aliyekuwa huko Israel ktk mafunzo maalum na hadi unakatika mwezi tayari Zai maisha ya pale kwa Shangazi yalimkifu mno na hadi kufikia kukubali moyoni mwake kuachana na Mwinchande ili apate mwanaume mwengine ambae kidogo kwao kunaweza kuwa na amani kuliko maisha ya pale kwa shangazi vile anavyofanyiwa mara kwa mara na kupewa maneno ya kashfa na kejeli asijue wapi zinapotokea huku akiambiwa kuwa asije akamuua Mwinchande kutokana na tabia yake ya umalaya ambao hakuujua kabisa na ukweli hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote tokea kuzaliwa kwake.

    Hali ile ilimfanya siku moja amkumbuke Hussein na kutamani kumfahamu zaidi.

    Lakini aliwaogopa sana wanaume Zai hali hiyo ilimfanya kabla hajampigia Hussein simu alipiga kijijini kwao Arusha kwa Ustaadh mmoja aliyekuwa na utaalam mkubwa wa kusaidia watu kupitia Marohani (Majini) na ndie huyo aliyemfundisha yeye Qur'an.

    Mara alipompigia simu simu na kuongea nae kwa kujiiba siku moja majira ya usiku ndipo alipomuelezea juu ya kijana aliyekutana nae toka Arusha na kwa mara ya pili Dar ambae alimwambia kuwa eti jina lake aliliota, hivyo alikuwa anataka Ustaadh kupitia marohani yake wajaribu kumtazama huyo kijana kama ni mwanaume mzuri au ni wale wahuni wenye tamaa na ndipo hapo Ustadh yule alipofanya mambo yake baada ya kutaka jina la huyo kijana na vile alivyo ndipo baada ya dakika kadhaa Ustadh alianza kuzungumza lakini safari hii kwa sauti tofauti na ya awali na Zainab aligundua kuwa sasa anayezungumza nae ni Jini.

    [["Zainab, huyo Kijana ni mwanaume mzuri sana kwako kuliko huyo unayeamini mumeo kwa sasa. Japo nae anakupenda...! lakini si mume bora kwako kama huyo Hussein.

    Pia labda tukwambie kitu huyo Hussein ndie mumeo ambae Allah amekuandikia uwe nae na kupata familia na ukumbuke mwenye kumiliki Ndoto nini Mwenyezi Mungu pekee... Amemuonesha Hussein wewe ni nani sasa baada ya kutojua kuwa ulibadilishwa jina.. Yaani ina maana kama hujui yule Hussein ndie yule yule rafiki ako wa utotoni uliyemjua kwa jina la Zungu. Na inaonesha wazi Mungu ndie anayewakutanisha nyinyi ili muungane muwe kitu kimoja na amini kabisa kulingana na nyota zenu zilizong'aa pamoja tangia wadogo kuwa matatimiza ndoto zenu kama mkiwa pamoja. Hussein ana ndoto ya kujenga nyumba na kama akikuoa hautopita muda mrefu atajenga kweli na wewe una ndoto ya maisha ya furaha na watoto wawili wa kwanza awe wa kiume na wa pili wa kike, na kama utaolewa na Hussein kwa mapenzi yake Mungu utapata ila kama haitakuwa hivyo basi niyi nyote hamtotimiza ndoto zenu pia utengano wenu wowote ule unaweza kuleta madhara ama dholuba kubwa, tena Dholuba kubwa sana litaloponza hata nafsi za watu wasio na hatia..... Kumbuka haya Zainabu jua kama hutokuwa muwazi na kumwambia Hussein kuwa uliwahi kuolewa kimira basi jua utakuwa bado unatengeneza dhoruba kubwa zaidi kwa jinsi nyota za huyu mumeo zinavyoonyesha. Muombe sana Mungu Zai usiufiche ukweli ingali bado mapema.

    waaadhaa Salaaam.."]]

    Ndivyo alivyomaliza yule Jini aliyeongea na Zainab kupitia Ustadh na maneno yake yalimfanya Zainab apigwe bumbuwazi baada ya kusikia kuwa kumbe yule kijana ndie yule Zungu wake wa utoto.

    Alijikuta anatabasam na kumshukuru Mungu kumkutanisha tena na Zungu japo alijua kuwa Zungu hamkumbuki na hakutaka amkumbushe kwani alijua angesababisha maswali kuwa mengi mwisho wa siku akayajua mabo ambayo hakutaka ayajue.

    Na hapo ndipo alipompigia simu Hussein na kumuomba amuelekeze anapoishi ili aweze kwenda mwenyewe wakaongee kirefu zaidi juu ya kile alichokizungumza awali.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * * *



    ("Wanaume ni watu waongo kweli, yani Mwinchande kumuamini kote leo hii ameondoka ameniacha nimekuja kukaa na shangazi na hata muda wa kuongea na mimi hana?! sasa hat huyu lazima nimpe masharti kabambe nisiamini moja kwa moja kwa sababu eti nimeambiwa na kiumbe mwenye uwezo wa kuona zaidi yangu.. Lazima nimpe mtihani")

    Yalikuwa ni mawazo akilini mwa Zai siku aliyokuwa anaenda kukutana na Hussein na kweli baada ya mazungumzo yao alimpa masharti magumu sana matatu ambayo yote Hussein alikubaliana nayo na kumshangaza sana Zai aliyejikuta furaha inamzidi na kumkumbatia Hussein huku akijisahau na kumwita jina la Zungu ambalo lilistua masikio ya Hussein lakini mwishoe alipuuzia tu japo kuna muda alitamani kumuuliza amelijuaje lile jina lakini kutokana na kuwehuka ghafra kwa vile alivyokubaliwa huku akiwa kaekwa kwenye mabano ya mtihani ambao kwa upande wake aliamini lazima ataufauru kwani aliweza kukaa mwaka mzima kabla hajaonana na Zai baada ya kuachana na mchumbaake wa awali Mariam ambae kumbe alikuwa na mimba changa siku wanaachana na hakulijua hilo hadi kipindi hiko anakubaliana kuwa wapenzi na Zai tayari upande wa pili Mariam alishajifungua katoto ka kike.



    Lakini baada ya miezi kadhaa Mwinchande alirejea Tanzania kwa dharula maalum mara baada ya wenzao wawili kufariki katika mazoezi maalum ambayo hayakuekwa wazi huku yeye Mwinchande akibaki na alama ya kuchomwa na kitu cha ncha kali maeneo ya shavu ambayo alama ile iliyojichora herufi ya X haikuekwa wazi nini hasa kilichopelekea zaidi ya yeye mwenyewe kukiri kuwa aliumia kwenye hayo mafunzo na wenzake wawili wote walikufa kwa bahati mbaya kwenye hayohayo mafunzo.

    Na mara baada ya Mwinchande kurudi na kumkuta mkewe wa mila alifurahi mno japo hakupata muda wa kukaa nae na kuzungumza mipango kutokana na kupewa wiki moja tu na Taifa ili watapomaliza kuistili miili ya wenzao basi na wao warejee wakamalizie hiyo kozi ambayo ilijumuisha askali kutoka nchi mbalimbali.

    Lakini kuna jambo ambalo Mwinchande aliliona la muhimu sana lililomfanya siku mbili kabla ya safari ya kurudi Israel aliomba ruhusa ya uongo ya masaa sita ambayo aliyatumia kurudi nyumbani na kumchukua mkewe hadi kwa rafiki ake yule mganga aliyeitwa Mnyungunyungu nia na madhumuni ikiwa ni kumuonesha live huyo mkewe aliyewahi kumuongelea japo Zai hakuelewa kitu na nia ya pili ilikuwa ni yeye mwenyewe kufanyiwa dawa itayomuwezesha kufuzu vizuri kwenye hayo mafunzo na hapo ndipo Manyungunyungu alipomfanyia kitu maalum na kuipitisha dawa aliyoiita 'Kauzibe' kuwa itamfanya awe mtu asiyeonekana iwe kwenye vita au matatizo yatayomfanya atafutwe na kadhalika na alimwambia pia ile dawa ua 'kauzibe ' itaweza kudumu mwilini mwake kwa miaka thelathini, jambo ambalo Mwinchande alilifurahia mno. na kumpa zawadi kubwa ya fedha taslimu Manyungunyungu kabla ya kuondoka na mkewe na kumrudisha nyumbani nae kurudi kambini kureport na baada ya siku mbili walirudi tena Israel



    Siku zilienda haraka na baada ya kuondoka Mwinchande kama kawaida huku mateso na manyanyaso yalirudi na kuzidi kwa Zai pale alipoishi na yule Shangazi, ikafika muda Zai akiwa anaongea na yule Ustaadh kwa njia ya simu alikuwa hadi analia jambo lililomfanya Ustaadh aende kumshawishi bibiake Zai kuwa akubaliane nae wamruhusu mjukuu wake kuondoka tu pale na kuja na huyo mwanaume aitwae Hussein ambae Ustaadh alimuhakikishia yule bibi kuwa huyo ni mwanaume bora kuliko wanavyofikiria.

    Na kutokana na kuheshimika sana kwa yule Ustaadh pale kijijini ndipo bibiake Zai alipokubali bint ake ampeleke huyo mwanaume kule kijijini wamuozeshe tu akaishi maisha ya amani na upendo kuliko pale alipokuwa anateseka na kunyanyaswa bila sababu ya msingi.

    Na hayo yote yalitimia baada ya mwaka ambapo Zai aliamua kumfanyia Suprise Hussein na kuamua kuubatilisha ule uongo wake wa awali pindi aliposema kuwa alikuja Dar kwaajili ya masomo na badala ya kumwambia ukweli kama alivyopewa yale maagizo na yule jini wa Ustaadh. alijikuta Zai akiuvua uongo ule wa shule na kujivisha uongo mwengine kuwa alikuja kwaajili ya kazi zandani na yote yale alifanya vile kwaakili zake kuwa Hussein ndio atamuelewa na kumpokea kuliko angesema kuwa aliolewa basi asingeaminiwa na angeachwa kwenye mataa.

    Kumbe hakujua kabisa Zainab kama uongo wake alioendelea kuufuga kwa maslahi ya muda ule... ulikuwa unatengeneza hasara kubwa ya baadae.



    Baada ya Zai kuhamia kwa Hussein na kumhakikishia kuwa yeye alikuwa bado bikra hasa mara baada ya Hussein kutaka kulazimisha wafanye mapenzi usiku, safari ya kwenda kijijini kwao ilipangwa ndani ya wiki hiyo ambapo katika hali ya kupagawa na penzi la msichana mrembo Zai, Hussein alijikuta anakubali na kupanga safari hiyo bila kuwasiliana na ndugu zake na mwishoe waliondoka wawili tu mpaka kule kijijini Arusha ambapo Ustadh yule yule ndie alihusika kuwafungisha Ndoa hiyo iliyomshangaza hata Hussein mwenyewe baada ya kutajiwa mahali ndogo sana kiasi aliona kama ndoto kumuoa msichana mrembo na mwenye tabia za kipekee kama Zai kwa pesa ile.

    Lakini ukweli ulibaki vile Hussein alimuoa Zai kabla ya kufanyiwa sherehe ndogo ya kimila usiku wake na kulala pamoja kwa mara ya kwanza aliweza kumuingiza katika ulimwengu wa kiutu uzima Zai mara baada ya kumtoa bikra kulekule shamba na kumbe kulikuwa na mabibi maalum wa mila waliokuwa wanasikilizia kujua mjukuu wao wa kike alijitunza kiasi gani lakini waliposikia ukelele walijua hapo ndio penyewe na kuangusha kicheko kilichowajulisha ndani Zai na Hussein kuwa kuna watu walikuwa wnawachungulia.



    Hawakukaa sana pale kijijini baada ya ndoa ya ghafra iliyohudhuliwa na watu wachache mno, ndipo Hussein alipomchukua mkewe kurejea jijini Dar na kuwataarifu habari zile ndugu zake kwa njia ya simu ambao wengi walimlaumu kwa kuoa pasi na kuwaarifu mapema na ndipo mjombaake Hussein alipomuandalia tafrija fupi ya kumpongeza ambayo alimwambia atapofika tu afikie pale kumtambulisha mkewe kwani na ndugu wengine watakuwepo pamoja.

    Na ndivyo ilivyokuwa baada ya Hussein na Zai kuwasili jijini Dar walifikia kwa mjomba ambapo baadhi ya ndugu wa Hussein walikuwepo kumpongeza na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao mapya wanayoenda kuyaanza.

    Lakini katika utambulisho mmoja wa ndugu wa karibu kabisa wa Hussein upande wa babaake ambae alikuwa ni mkubwa kuzaliwa aliyejishughulisha na mambo ya tiba asilia au uganga alimshangaa mno mara baada ya kumuona bibi harusi na kubaki na maswali mengi kichwani mwake asijue aanzie wapi kuongea na mwanae juu ya mkewe ambae alionesha kuwa anampenda kupita kiasi.

    Hakuwa mwengine huyo ndugu bali ni Mnyungunyungu ambae hata Zai alipoiona sura ya mganga Mnyungunyungu alistuka moyoni mwake lakini alijitahidi kuficha ili watu wasigundue chochote juu yake zaidi ya yule mganga Mnyungunyungu kuzidi kumuangalia kwa taharuki.

    Hali ile Hussein hakuipenda na hata kesho yake Mnyungunyungu alipojaribu kumpa maneno ya kumfanya amuulize kulikoni juu ya mkewe lakini Hussein ndio kwanza alimkingia kifua mkewe na hakutaka kusikia chochote kibaya kikihisiwa wala kusemwa juu ya mkewe kwani kitendo tu cha kumkuta Zai bikra akiwa na umri ule tena mwenye uzuri wa ajabu kuanzia sura mpaka umbo na bado kaweza kujilinda na vishawishi kutoka kwa wanaume mbalimbali..!? Hakika bikra ya Zainab ilikuwa silaha tosha ya uaminifu kwa Hussein asitake kusikia maneno eti Zai alishawahi kuwa na mwanaume tena ingekuwa kichekesho kabisa kwake kama angesikia eti huyo uliyemuoa ameshaolewa muda mrefu.

    Halkadhalika yote na yote Hussein na Zainab waliweza kuanza maisha yao mapya kama mke na mume rasmi.





    Siku zilienda baada ya Hussein na Zainab kufunga ndoa na kama alivyotabiri yule jini aliyeongea nae Zai kupitia Ustadh wake kuwa pindi atapoolewa na Hussein basi ndoto zao zitatimia pamoja kutokana na nyota zao zinavyosoma, na ndivyo ilivyokuwa kwani baada ya mwaka mmoja tu waliweza kupata pesa iliyowawezesha kuknunua kiwanja huko Kigamboni.

    Upendo wao ulikuwa unazidi kuimalika siku baada ya siku kila wanavyoonana yaani walipendeza mno.

    Kwa kiasi kikubwa Zai aliweza kuifanya tabia ya Hussein izidi kuwa nzuri na kuwashangaza hadi rafiki zake hasa alipoanza kusali.

    Hali hii iliongeza amani na furaha wala hakuna aliyewaza kati yao kama ipo siku watakuja kunyoosheana walau vidole lakini kumbe bado ile siri aliyokuwa anaifuga Zai ilikuwa inazidi kulimong'onyoa shina la mti wa wapendanao pasi na yeyote kujua wala kuhisi.



    Baada ya mwaka mmoja ndipo shughuli za usimamizi wa ujenzi zilianza huku Zai akiwa ndie msimamizi mkuu kutokana na Hussein kubanwa na mambo ya kazi na kutaka kumuonesha mkewe jinsi gani anamuamini.

    Lakini siku baada ya siku kadri nyumba kule ilivyozidi kusogea na kuanza kufika usawa wa madirisha, siku moja Zai majira ya jioni alipokuwa yupo kwenye Pantoni amesimama alistushwa na sauti ya mtu mmoja akimwita kwa jina lake kutokea kwenye gari moja kubwa ya Maofisa wa polisi na alipogeuza macho kumtazama aliyemwita hakuamini kabisa pindi alipomuona askari aliyevaa sare yenye vyeo vingi huku akiwa na wenzake wawili kwenye ile gari na hakuwa mwengine yule polisi bali ni Mwinchande.

    Moyo ulimripuka sana Zai pindi alipomuona Mwinchande na hofu pia ilianza kutanda kwenye ubongo wake na kushindwa kujua jinsi ya kumtoka toka hasa alipomuona akifungua mlango wa ile gari na kushuka kumfata pale aliposimama.

    "Kweli Mungu muacheni aitwe Mungu aaaaah! ni zaidi ya miezi mitatu toka nimerejea nakutafuta wewe tu mke wangu kila kona hadi Arusha sikuoni... Dah! lakini leo hatimae Mungu kanionesha. Najivunia sana mke wangu Zainab, habari za siku..?"

    aliongea kwa furaha Mwinchande mara baada ya kufika pale aliposimama Zai amba alitamani ayeyuke kwa jinsi moyo ulivyokuwa unamuenda mbio akishindwa atunge uongo gani ili iwe rahisi na salama kwake kumuepuka Mwinchande kwani tayari pia yeye ni mke wa Hussein tena wameoana kila mmoja akiwa na akili timamu mbele ya Sheikh tofauti na wao waliozesha ozeshwa tu kiila na walikuwa wote hawajui kitu kuhusu Ndoa, hasa Zai kwani ndie alikuwa mdogo sana.

    Lakini alishindwa kujua aongee neno gani la kueleweka mbele ya Mwinchande muda ule? na huo ndio ulikuwa mtihani kichwani mwake kipindi hiko Pantoni ilikuwa inaegesha upande wa Posta.



    "Zai mbona unaonekana kujifikiria mke wangu! twende basi tutaongea vizuri."

    aling'ang'aniza Mwinchande mara baada ya kuona Zai amejibu ile salamu kinyonge na alipoombwa waingie kwenye gari alionekana kusita huku akifikiria kitu.

    Alichowazia zaidi ni vipi akubali aondoke na Mwinchande wakati tayari kuna Hussein anamsubiri nyumbani?

    Aliamua kutunga uongo ili amuepuke Mwinchande siku hiyo lakini bado uongo wa Zai haukuwa na nguvu mbele ya Mwinchande.

    "Nakuomba mume wangu nakuomba sana, mimi ni wako na Mungu ametukutanisha tena ila hebu angalia ni ghafra sana tumekutana ni muhimu uniache kwanza niende kwa huyu mama, harafu nikishaaga na kuweka mambo sawa basi Kesho tutakutana mume wanguuu"

    alizidi kuomba Zai na safari hii kidogo Mwinchande alilegeza uzi.

    "sawa basi kwa kuwa kesho jioni tutakuwa na safari inabidi unitafute mapema asubuhi nitakuelekeza wapi nilipo tuweke mipangon ya maisha yetu sawa mke wangu."

    aliongea Mwinchande na kumkabidhi namba za simu Zai sambamba na Elfu hamsini za nauli ya daladala hiyo kesho na hapo ndipo alipofaulu Zai kumkwepa Mwinchande siku hiyo lakini alijua kuwa kesho ana kibalua chengine kigumu jinsi ya kuondoka hiyo asubuhi kukutana na Mwinchande.

    Moyo wake ulijikuta unakuwa na hofu kila anapomfikiria Mwinchande kuliko Hussein na ikumbukwe hiyo yote ni kwa sababu ya dawa aliyotengenezewa Mwinchande juu yake Zainab.



    Na kweli siku ya pili yake aliwasiliana na Mwinchande kwa siri na kukutana nae maeneo ya hoteli ya Kilimanjaro.

    Kabla hajatoka Zai alifanya utundu wa kuchanganya ndimu (...) kuji(........) kwenye(...........) mwishoe alifanikiwa kujitengenezea bikra ya uongo ili iwe silaha yake kwa mumewe Mwinchande kwani alijua lazima watapokutana atataka ahakikishe kama kweli hajamsariti na kulingana na mila za kwao mwanamke aliyekuwa si bikra hafai kuolewa na ndio kigezo cha wazee wengi kuwaoza mabint zao mapema ili wasije watia aibu hapo baadae.



    Na kweli alichokifikiria Zai ndicho kilichotokea kwani pindi tu Mwinchande alipokuwa na Zai chumbani alianza kumdadisi.

    "Mke wangu wewe ni mzuri sana tena sana, hivi hujashawishika kweli?!!"

    aliuliza Mwinchande huku akimshika sehemu za paja Zai aliyekuwa anajifanya bado mtoto.

    "Aiii, Jamaani ina maana huniamini? Mi bado nipo kama ulivyoaniacha mume wangu nimejilinda sana kukusubiri."

    alijibu kwa kudeka Zai na kuzidi kumpa matamanio Mwinchande.

    "Kweli?!"

    "Kweli mume wangu."

    "Basi acha nihakikishe kabla sijasafiri leo."

    aliongea Mwinchande huku akizidi kumpapasa Zai

    "aaagh, jamaaani mi naogopaaa."

    alizidi kudanganya Zai na kumfanya Mwinchande aanze kutumia nguvu ambapo ukweli walisumbuana sana huku Zai akibana miguu na kurusha mateke lakini kutokana na mbinu alizokuwa nazo Mwinchande ukijumlisha na hamu ya tunda, mwishowe alifauru kumsongomeka dungio lake alilolijaza mate ya kutosha ili iwe rahisi kumuingilia na ndipo Zai alipopiga kelele ndani ya kile chumba kama amekanyaga mwiba kwenye kidonda cha unyayoni na kumfanya Mwinchande achomoe taratibu gunguso lake ambalo lilibahatika kuingia kidogo na kutokana na hamu iliyochochewa na usumbufu alioupata alijikuta Mwinchande akifika kilele palepale alipoanza kulirudisha nyuma kwaajili ya kulichomoa

    "Ooooooooghh Shiit.."

    Aliugulia kwa mautamu Mwinchande pindi alipokuwa anajitua mzigo wa nye* na alipoitoa kabisa aliamini kwa kuona kweli damu zimetapakaa kwenye dunguaji lake na kufurahia moyoni kwa kuweza kumtoa katika utoto mkewe yeye mwenyewe hali iliyomfanya aamini kweli Zai ni mwanamke wa kipekee.



    Kazi ilibaki kum bembeleza Zai aliyekuwa analalamika kuhisi maumivu makali sehemu zake huku akilaani mapenzi kumbe yanaumiza vile na kuzidi kuziteka hisia za Mwinchande kuamini kuwa kweli Zai alikuwa mtoto sana.

    Ilibidi Mwinchande amuachie kiasi kikubwa cha pesa Zai na kumtaka afanye mpango wa kurudi Arusha ili akamchukue rasmi kwa utaratibu na baraka za bibi waweze kuwa pamoja.

    Nae Zai alikubali kabisa na akilini aliona mchezo aliouanzisha anaweza kuumaliza bila tatizo japo aliuanzisha bila kujua ataumalizaje.



    * * * * *

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zilienda kwa mara ya kwanza Zai aliweza kumsariti mumewe Hussein bila kuwaza kama itafika siku atamfanyia hivyo Hussein.

    Na siku ambayo Zai anakutana na Mwinchande pale hotelini alikuwa tayari ana Mimba changa ya wiki tatu hali iliyomfanya baada ya kupita wiki ambapo ndio alikuwa anaingia mwezini alishangaa kuona amepitiliza na kuamua kwenda kupima kimya kimya kwanza akiwa na kigezo kikubwa cha kutoka nyumbani ni kwenda kuangalia ujenzi kigamboni.

    Alipima na kugundulika kuwa na mimba ya Mwezi mmoja na alipopiga mahesabu aligundua kwa asilimia zote mia mimba ni ya mumewe Hussein lakini aliwaza itakuwaje Mwinchande atapokuja kugundua kuwa yeye ni mjamzito?

    Na je atawezaje kuishi na wanaume wawili kwa wakati mmoja?

    ("Aaagh! Mungu atanisaidia siwezi kutoa hii Mimba, Mwinchande hatoweza kugundua kitu namvutia pumzi wiki tatu namwambia ninavyojisikia na Hussein ananiamini sana nitamuomba ruhusa ya kwenda kijijini nikafanyiwe dawa ili Mimba ikue salama na nitatumia muda huo kukutana na Mwinchande ili aniamini zaidi tutafika kwa bibi... aaagh, nitampanga tu bibi atanielewa... Nikishampelekea sukari na mkate hatokuwa na neno na uzee ule. Mchezo mdogo tu mwishoe nitajua yupi bora nimfate. mh! ila wananishanganya.. lakini acha nitumie akili za ziada za kuzaliwa naamini kila kiru kitakuwa sawa.")

    Aliwaza na kujiambia akilini mwake Zainab mara baada ya kujigundua ni mja mzito.



    Mbali ya kuwa mcha Mungu wa kusali, mwenye kupenda kujisitiri, mkwepa vishawishi, mpole, mtaratibu, ana roho nzuri, mkalimu.... lakini bado alisahau kuwa yeye ni mwanamke na Mungu amemuumba kuwa mtu wa pili Duniani baada ya mwanaume.

    Alijisahau kuwa upeo wake wa kufikiri na utendaji hasa juu ya maswala yajayo umewekewa ukumbi finyu tofauti na mwanaume.

    Alisahau kuwa mwanamke ubongo wake hucharge taratibu sana kuliko mwanaume hasa katika maamuzi ya haraka na magumu.

    Laiti angejua maamuzi aliyokuwa anayafanya siku ile aliyokutana na Mwinchande yangekuja kuleta balaa kubwa baadae, basi angekubali alaumiwe mwenyewe tu siku ile na aachwe na Mwinchande kwa maneno ya kashfa ambayo yangemuumiza kwa siku kadhaa lakini baadae maisha yangeendelea na kila kitu kingebaki hadithi.

    Lakini aliogopa lawama Zai.

    Aliogopa kuonekana mwanamke aliyekosa uvumilivu na kumsariti mtu ambae tayari alikuwa mumewe, pia aliona kama ataenda kinyume na Mwinchande anaweza kuwa ameenda kinyume na matakwa ya wazazi wake.

    Lakini alisahau kujiuliza, mbona alishamsariti Mwinchande na kuolewa na Hussein? na mbona sasa amemsariti na Hussein? japo alijiona yuko sawa kwa upeo wake lakini Zainab hakuwa sawa kabisa na kadri siku zilivyozidi kwenda mbele alijikuta anazidi kutengeneza bomu hatari zaidi ya Nyuklia asilojua hata jinsi ya kulitegua.



    * * * *



    Akiwa safarini Mwinchande ambae alikuwa anamuendeesha Kamanda mkuu mpya wa Jeshi la polisi nchini ambae pia aliwahi kuwa mkuu wake wa kituo alichoanzia kazi pale Kibaha mkoa wa Pwani aliyeitwa Cyprian Ng'umbilwa.

    Tabia za Cyprian kupenda sana wanawake zilikuwa zinamkera sana Mwinchande lakini alishindwa jinsi ya kufanya na hata hiyo safari waliyokuwa wanasafiri siku hiyo majira ya jioni wakienda jijini Arusha haikuwa kwa niaba ya kazi ama ziara yoyote zaidi alikuwa anampeleka kwa kimada wake tuu.

    Na hiyo ilikuwa ni safari ya tatu ya kuunganisha juu kwa juu mara baada ya kutokea Mwanza, Shinyanga kulipokuwa na kikao maalum cha makamanda wa polisi na sasa badala ya kurudi Dar Cyplian aliamuru msafara wote utangulie na yeye kuondoka na Kiraia na Mwinchande ambae alikuwa anaaminiwa sana kutokana na uwezo alioupata huko Israel na alipewa jukumu la kumuendeesha Kamanda mkuu wa jeshi na kufundisha makamanda mbinu maalum za nadharia alizozipata huko Israel japo yeye alikuwa zaidi kwa kujua na vitendo.

    Mawazo yake zaidi Mwinchande yalikuwa kwa Zai ambae siku hiyo mapema alimpigia simu kumjuza kuwa yeye ni mjamzito na alinasa hiyo mimba siku ileile ya kwanza walipokutana vilevile keshokutwa yake alikuwa anarudi rasmi Arusha.

    Mwinchande alifurahi awali akijua wakiunganisha Dar mapema angemuwahi mkewe lakini kitendo cha mkuu wake kilimfanya aendeeeshe gari huku akiwa na hasira sana moyoni mwake lakini ilikuwa ngumu mno kubaini usoni mwake.



    Baada ya siku mbili za utumwa jijini Arusha siku hiyo ambayo Mwinchande mapema aliwasiliana na mkewe aliyemuelekeza kuwa yuko safarini na hiyo siku ndipo ilipotakiwa sasa kurejea na Kamanda Cyplian jijini Dar lakini Mwinchande aliweza kufanya ujanja ujanja hadi wakachelewa na Zai alipofika stand na kumpigia simu Mwinchande aliyeenda na gari akiwa na bosi wake wakati wakiwa tayari kuondoka na hapo ndipo macho ya Cyprian yalipoiona sura nzuri ya Zainab na kujikuta anaapa nafsini mwake kumpata pasi na kujua ni mke wa Mwinchande.



    "Yule mwanamke uliyesimama nae pale ni nani?"

    aliuliza Cyprian baada ya Mwinchande kurudi garini.

    "Aliwahi kuwa mwanafunzi mwenzangu."

    "Basi vizuri naomba ufanye chini juu nimpate, hakika nitaoa kabisa hahaaaa"

    aliongea huku akicheka Cyprian bila kujua anatonesha kidonda kisichoguswa na hapo ndipo kukaanza tatizo mara baada ya Cyprian kuamua kushuka mwenyewe kumfata Zai kuongea nae ambae alikuwa amesimama akingojea gari ya kwenda kijijini kwao ifike mara baada ya kuongea na Mwinchande.

    ("Huyu mkuu ananitaka ubaya sasa... Anatafuta kifo")

    aliongea moyoni kwa hasira Mwinchande pindi alipokuwa anamuangalia Cyprian akimsemesha Zai na baada ya muda alishangaa kuona Zai ameamua kuchukua taxi kuondoka baada ya kuona ushawishi wa Cyprian unazidi.

    "sasa Mwinchande yule bint inaonekana amekuzoea sana wewe na mimi hafahamu kama ni mtu mkubwa hivyo hakikisha tukifika Dar unafanya utaratibu wa gharama yoyote nimpate."

    "sawa mkuu."

    alijibu Mwinchande na kuwasha gari kuondoka eneo lile huku moyoni akijiapiza endapo kama mkuu wake akiekea mkazo suala lile anaweza hata kumuua.

    Alishindwa kumwambia kuwa yule mkewe kwa kuwa hakukuwahi kuwa statement yoyote toka anapokelewa kuwa ana mke na yule alikuwa ndie mkuu wake toka anakuwa polisi hivyo alimjua vizuri japo hakuijua siri yake na Zai.



    Baada ya siku kadhaa kupita Mwinchande alipoona usumbufu unazidi kwa bosi wake siku hiyo aliamua kumchana ukweli bila kujali ukuu wake wala nini.

    "Sikia kiongozi, ujue nimekuvumilia sana lakini naona bado unakazania sasa nataka ujue yule mwanamke nina mipango nae tayari."

    aliwaka Mwinchande hadi Cyprian alishangaa na hapo walijikuta wanatengeneza bifu la kijinga na Cyprian alikosa ujanja jinsi ya kumuadhibu Mwinchande zaidi alimtafutia safari kimakusudi kupitia wazili wa mambo ya ndani na kulichomeka jina la Mwinchande awe miongoni mwa maafsa wataoenda kwenye kozi nyengine ya ngazi ya juu ya kipolisi nchini India, lakini nia na madhumuni ya Cyprian ni kumkomoa Mwinchande wakose wote akisahau kuwa upande mwengine anamtengenezea nafasi ya kuheshimika zaidi.



    * * * * *



    Kwa upande wa Hussein hakuona kazi wala ajizi kumuacha mkewe aliyempenda na kumuamini vilivyo kuwa aende Arusha kwao kwa safari ya mwezi mmoja kutengenezewa dawa juu ya mimba aliyokuwa nayo kwa kuhofia mambo ya wanga na wachawi.



    Hakuwahi kuwaza wala kufikiria kama kuna mchezo wowote unachezwa nyuma ya pazia na hata Zai alipofika kijijini alimlewesha maneno bibiiake na kwa bahati mbaya yule Ustaadh alikuta amefariki ambae alifikiria kuongea nae ampe msaada wa kusolve tatizo lake alilolianzisha na hivyo baada ya kumkosa tena Ostaadh wake yule hakutaka tena mtu mwengine ajue suala lake nakutokana na bibi kuwa mzee sana alikosa amri kwa kile alichokuwa anamwambia mjukuu wake hasa kutokana na bibi kuanza kupoteza kumbukumbu kutokana na kuzeeka sana.



    Baada ya mwezi ndipo Zai kweli alirudi kuishi na mume wake kipindi hiko Mwinchande walipata tena safari ya India ambapo jina lake lilichomekwa na Cypian kwaajili ya kumkomesha tu asifanikiwe kumpata yule bint bila kujua kuwa tayari alikuwa me wa Mwinchande kimila.



    Miezi ilisonga na hatimae kwa mara nyengine Hussein alisafiri na Zai mpaka kijijini kwao na kumuacha kipindi akiwa na mimba ya miezi sita nae kurudi katika mihangaiko yake ya kujiandaa kwani alijua anakwenda kuwa baba siku si nyingi.

    Lakini baada ya miezi tisa kutimu hadi Zai anajifungua kule kijijini Mwinchande ndie aliyekuwa wa kwanza kufika mara baada ya kutoroka mara moja India na kurudi Arusha ambako alikaa kijijinisiku mbili kwa shauku ya kumuona tu mtoto aliyeamini ni wake na yeye alikuwa mwanaume wa kwanza kumbeba mtoto yule huku akiwa na furaha mno.

    "haaaaaa... babaangu amezaliwa.Babaangu amezaliwaa huyu ni Shaaban.. huyu ni Shaaban"

    alizunguka na kufurahi Mwinchande huku akiwa amekibeba katoto kale kachanga na kumpa jina la Shaaban.





    Hila iliyofanyika ni kwamba Hussein alicheleweshwa kupewa habari za kujifungua Zai kwa kuhofia asije kugongana na Mwinchande ukawa mtihani kwake.

    Hakufikiria kuwa hata yale yaliyofanyika bado kuna mtihani na mdudu m baya aliyekuwa anazidi kumfuga.

    Hata hivyo Hussein alishindwa kusafiri kutokana na kuyumba kiuchumi na kuamua kuwangojea ubungo baada ya miezi miwili tokea Zai ajifungue na kweli hatimae Zai alirejea akiwa na mtoto wake wa kiume na kumfurahisha sana Hussein pindi alipomuona mwanae na kumkumbatia huku akifurahi.

    Zainabu alijisikia fahari kuwatengenezea furaha wanaume wawili kwa wakati mmoja huku moyoni akijiona amecheza kama pele.

    "Oooooooh! babaangu huyoooo aaaah.. Huyu Mwinshehe kabisaaa aaammm.. Mwanangu Mwinshehee."

    alifurahi sana Hussein na kuingia ndani ya Taxi pamoja na mkewe ambae alikuwa ana siri kubwa sana juu ya mtoto yule ambae tayari ana baba wawili kwa wakati mmoja.

    Tena kila mwanaume akijinasibu na kumfurahia mtoto yule akimpa jina la babaake kwa heshima kubwa.

    Kwa pamoja Mwinchande na Hussein wote walimuamini sana Zainabu kutokana na kumuona ni mwanamke wa kipekee sana kitabia na uzuri hivyo walimuamini wote kupita kiasi bila kujua kinachoendelea kichwani mwake na kusahau kuwa Zainabu hata aweje ila bado ni Mwanamke na mwalimu mkuu wake ni Kipofu.



    Matatizo yalianza baada ya Mwinchande kurudi tena nchini ambapo kutokana na kufuzu kwake kwa alama za juu jeshi la polisi lilimtunuku vyeo zaidi na heshima yake kuongezeka mpaka kuwa kamanda mkuu msaidizi wa polisi nchini.

    Lakini muda mfupi baada ya uteuzi na kupata heshima kubwa katika jeshi la polisi Mwinchande shauku yake ilihamia kwenda Arusha kumchukua mkewe Zainabu na mwanawe Shaaban.

    Na hapo ndipo kisanga kilipoanza kubumbuluka mara baada ya kutofanikiwa kumkuta mkewe kijijini na bibi kukosa maneno yenye kueleweka hali iliyomfanya Mwinchande machale kumcheza na kuanza kufanya utafiti kwa watu wa kijijini waliomjua Zai.



    Waswahili wanasema kuwa 'mtu atakunyima chakula si neno' na ndivyo ilivyokuwa mara baada ya Mwinchande kufanya utafiti wa siku mbili tu na kupata tetesi kuhusu Hussein japo hakujua kama alimuoa ila wambea walimwambia kuwa walimuona huyo mwanaume pale kwa bibi na wakatoa tetesi kuhusu jijini walipokuwa wanaishi hali iliyozidi kumpa mwanga na kumrahisishia Mwinchande jinsi ya kumnasa huyo mwanaume ambae aliona kuwa ni m baya wake kupita maeleazo, haiwezekani amtoroshe mkewe na mtoto.

    Na ndipo baada ya kurudi Dar aliongea na vijana wake wa polisi waliobobea kwenye upelelezi na kuwakabidhi picha za mkewe Zai wamtafute kimya kimya maeneo yale ya jiji aliyopata maelekezo kule kijijini na ndipo zoezi la kumsaka Zai na kumpeleleza kwa siri lilifanikiwa na kuanza kumpeleleza mwanaume aliekuwa anaishi nae na kupata habari zake zote muhimu na hapo ndipo Mwinchande aliamua kumuandikia barua la onyo Hussein tena aliamua atumie mbinu ya jina litalomuweka kwenye mabano ili kama atakiuka aweze kumfanyia unyambisi bila shida.

    Na katika kulifikiria jina ambalo litakuwa maalum kwake siku hiyo akiwa chumbani kwake usiku akijiangalia kwenye kioo ndipo lilipomjia wazo mara baada ya kuiona ile alama ya X chini kidogo ya shavu lake na kuona jina kivuli litalofaa kwake ni MR X.

    Ila kabla hajafanya hayo yote alimtafuta Zai ambae alikuwa na line ya siri aliyoitumia kuwasiliana na Mwinchande kwa njia ya sams lakini Hussein hakuwahi kugundua uwepo wa hiyo line.

    ("Haiwezekani kabisaaa..! Dah! Yaani Zai asinisariti muda wote huo aje anisariti leo hii? tena akiwa na mtoto mdogo? hapa kuna mchezo tu na huenda huyo jamaa akawa mchawi na kama hii ripoti a vijana kudai kuwa ana udugu na Mnyungunyungu basi hii itakuwa dawa tu si bure")

    Aliwaza sana Mwinchande na kuanza kuandika mwseji nzito kwenda kwa Zainab.

    Baada ya Zai kupata ujumbe toka kwa Mwinchande wa kumuonya kuhusu usariti wake, aliamua kujitetea na kudai hata yeye hajui ilivyokuwa kuwa na hapo alizidi kumtia hasira Mwinchande aliyeamini kuwa hiyo njia iliyotumiwa si kosa la Zai bali ni uchawi wa Hussein na madawa.

    Na hapo ndipo barua ya onyo ilipotumwa kwa Hussein na kupewa siku saba ahakikishe amemrudisha yule mwanamke kijijini kwao Arusha.



    Ni ujanja na akili nyingi uliotumiwa na askali mpelelezi mmoja kumkabidhi Hussein ile barua ambayo ilipofika kwa Zai tu, alikanusha mdomoni na kujifanya hajui kitu lakini moyoni alijua kila kitu kuwa ile barua ilimuhusu yeye na mtu aliyejitambulisha kuwa Mr X ni mumewe wa kimila anayeitwa Mwinchande.

    Kwa upeo wake Zai alijitahidi kujiiba na kuwasiliana na Mwinchande akimsihi asilipe ubaya wowote kwa yule mwanaume aliyemlaghai kichawi na kumtorosha wala wasifikie habari ya kumpiga na kumuua.

    Suala lile la Zai awali Mwinchande aliligomea kwani alichohitaji yeye Hussein auawe kabisa.. Lakini kutokana na ombi la hisia kali tena za kiuungu na dini alilokuwa analiwasilisha Zai mara kwa mara ndipo lilimkubalisha Mwinchande na kumwambia Zai kuwa hatomuua tena Hussein kwa mikono yake.



    * * * *



    "Inspector wewe utaongoza hawa macoplo kwenda kuchukua zile maiti za ajali ambazo bado hawajatokea ndugu wa kuzichukua, kuna ya mama na mtoto aliyekatika kichwa mfanye haraka sasa."

    ilikuwa ni mipango nyeti ya Mwinchande katika mtego alioudhamiria mara baada ya kupokea sms kutoka kwa Zai kuwa wanaelekea kule kwa baba yao mkubwa Manyungunyungu na wakati huo Mwinchande alikuwa katika hospitali ya Tumbi kulipoletwa maiti nyingi zilizotokana na ajali mbaya ya basi maeneo yale ya kibaha.

    Alichokifanya Mwinchande harakaharaka na kutokana kuwa na makazi pia pale Kibaha aliondoka yeye na rafiki ake mmoja aliyempata kwa kumpa msaada wa matibabu ya mwanae na katika kuishi alipenda kumfundisha uninja na ndie aliyempa siri kidogo kuhusu yeye japo zilikuwa za uongo lakini rafikiake yule alimuamini mno hasa kwa msaada aliouonesha kwake kwa kumsaidia mwanae ambae alijua angekufa hivyo hata na yeye kumsaidia kwenye ile kazi aliona ni haki kabisa.

    Hakuwa mwengine bali ni Ally ambae Mwinchande alipenda kumwita seven seven kutokana na kujuana nae siku ya tarehe 7 mwezi wa 7 hivyo akwa anamwita jina la Ally77. Na hapo ndipo walipochukua mavazi yao ya kazi (Kininja) ambayo waliyaweka kwa pembeni ya gari muda wanatoka na kuwahi Kibamba walipoiacha gari na kutembea kwa miguu karibu na ile jia panda walipochepuka na kuyavaa sasa mavazi ya Kininja na kupita njia za msitu mpaka sehemu moja waliyoona panafaa kutimiza lengo.

    "tega upande ule mi natega upande huu, vijana wangu wanakuja taratibu na maiti. Nishampanga mke wangu akifika eneo hili atachutama kukojoa na hapo mimi nitatoka kumnyang'anya mtoto huyu mpuuzi kwani lazima amshike yeye na wewe utatoka nyuma yake na hilo gongo hakikisha unampiga maeneo yale niliyokuelekeza."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alitoa agizo Mwinchande na kueka mipango sawa.



    Na ndivyo ilivyokuja kuwa mpaka Hussein anakuja kukamatwa na kusingiziwa kesi ya mauaji baada ya kuzimia pale chini punde alipopigwa na Ally77 ndipo muda zile maiti zilifikishwa na nguo alizovaa Shaaban alivalishwa yule maiti mtoto na kusogezwa pale kichakani huku mpelelezi mmoja akiwa maeneo karibu ya kijiji akingoja amri ya kwenda kuwaibua wananchi wenye hasira kali.

    Zai alilia sana kwani alijua Hussein angeachwa tu pale na kuamka kujikuta pekeake lakini hakujua kama kuna mpango mwengine wa Mwinchande juu ya kumuua Hussein japo si kwa mkono wake lakini aliamini kisheria lazima atanyongwa.



    Na hatimae Hussein alianza maisha ya jela na Mwinchande pamoja na Zai walianza maisha yao mapya katika jumba kubwa la kifahari ambalo ndani yake kulikuwa na chumba maalum kilichotengenezwa kwaajili ya mawasiliano maalum aliyokuwa nayasuka Mwinchande ili siku moja nchi isije kugundua kile alichokifanya na aliapa kuilinda siri yake mpaka mwisho wa maisha yake na kutokana na mbinu nyingi alizozipata Israel na India aliiendeleaza mission zake na kukichimba kizazi cha Hussein hasa mara baada ya kumuona bint mmoja aliyekuwa na mtoto wa kike akilia kule mahakamani na kudai kuwa yule mtoto ni wa Hussein na alikuwa na barua yake ambayo askali aliyeipokea aliitwa na Mwinchande mwenyewe ambapo aliifungua na kuisoma ile barua ndipo aliporuhusu ipelekwe huko gerezani kwa muhusika nae akaanza kufanya mipango ya kumueka katika anga zake mtoto wa Hussein aliyeitwa Asha.



    Na hiko ndio kilikuwa CHANZO cha Mwinchande kugeuka kuwa mtu m baya na muuaji kwa kila anayeona anahatarisha siri zake.



    "Mwananguuuuuuuu Shaaaabaani mimi ndie mkosaaaajiii iiiiiih Najuutaa leeeeooooo aaaaaaaaaaaaaagh iiiiiiiiiiiiiih

    Ona sasaa watuu niliowapeendaaa, watuu waliojitahidi kunionesha kila aina ya upendoooo, waliniaminiiii lakini leo nimewauaaaaa.... aaaaaah!! Mwanangu Shebby wewee si muuuajii wala babaako Hussein si muuajii hata Mr X piaaaaa. kwaani yoooote hayaa chanzo ni mimiii japo sijamuuaa mtuu kwa mkono wanguuuuuu... Lakini mimi ndie muuajii...Ooooooooooh eeeeeeeeeeeeh"

    aliendelea kulia kwa uchungu sana Zainab mara alipokuwa anawasimulia chanzo cha matatizo Kamishna Shaaban na Cj4 aliyekuwa ameipakata maiti ya Hussein bubu huku wote machozi yakiwatoka baada ya kujua chanzo kizima.

    "Maamaa, maamaa, mama ina maana Asha ni dadaangu? Mama!!! umeacha nimuoe dadaangu?!! aaaaagh."

    aliumia zaidi Shaaban na alijua kuwa Asha hajui chochote kinachoendelea pale lakini kumbe Asha alishatumiwa ujumbe mfupi na Cj4 kumtaka kufika pale kwa kina Shebby haraka kutoa msaada kwani uvamizi umetokea.

    Cj4 alifanya vile makusudi tu ili awaoneshe uwezo wa Asha ulivyo na kweli mara ghaaaaaaaaafraaaaa wakiwa wametahayuri wote ndipo walipomshuhudia mtu akiingia kwa style ya salakasi za ajabu kupitia dirisha lile alilovunja Shebby pindi akiingia na mara baada ya kuingia yule mtu na kutua mbele yao wote walishangaa kumuona ni mwanamke aliyezuia uso kwa nikabu nyeusi huku akiwa kavaa track suit juu na chini mikononi akiwa na visu vidogo zaidi ya vinane alivyovishika kimaajabu kwenye pachu pachu ya vidole vya mkono na kumfanya Shebby atake kuiwahi bastora yake lakini Cj4 alimkata ngwala punde tu alipotaka kuinuka na kumwambia.

    "Huwezi ua tena kwa wasio na hatia mbele ya Cj4. Yule ni dadaako mke wako adui wa adui yako na yeye ndie Lady Ninja Asha."

    maneno yale yalimfanya Shebby ataharuki zaidi hasa pale Asha alipodondosha vile visu chini na kupiga magoti akilia kwa uchungu kwa kubainika na kuona kile kilichokuwa mbele yake huku akifungua nikabu yake na kwa mara ya kwanza akawa dhahiri shahiri mbele yao kwa kuwahakikishia asemacho Cj4 na hapo hata Shebby alijikuta anapoteza fahamu kwa taharuki.



    <<<< MIAKA 15 BAADAE >>>>

    ^^^^^^^^^^^^

    * * *

    ^^



    Ni katika makaburi ya Makanya Dar es Salaam wanaonekana watu wawili wakiwa wote wamevaa nguo nyeusi mmoja akiwa ni mtu mzima na mwengine mtoto wa miaka isiyozidi 14 wakiwa wamepiga magoti mbele ya makaburi yaliyojengewa kwa mtindo wa kufanana baada ya kuyasafishia na walionekana walifika pale kwa muda mrefu sana na kulikuwa na hadithi ndefu aliyokuwa anaisimulia yule Mkubwa kwa yule mtoto huku akimuonesha onesha makaburi yale.



    "Hadithi hii imeniuma sana baba Cj4 aaah!! Mungu wasamehe ndugu zangu wote, kwa hiyo nini kilitokea sasa baada ya baba kujua kumbe mama alikuwa Ninja mara aliporudiwa fahamu?"

    aliuliza yule mtoto.

    "Baada ya babaako Kamishna Shebby kuzinduka ilikuwa tayari kashachelewa mara baada ya bibi ako kuzidiwa ghafra kwa presha iliyomshuka pindi alipogundua kumbe mumewe babu yako Mr X alikuwa amemtumia mamaako zaidi ya alivyojua yeye, kwani bibiako alijua kama mumewe anamtumia Asha lakini si kwa mauaji bali ni kumueka tu karibu ili amfiche kama yeye ni mtu m baya dhidi ya babaake ambae ndie babu yako mzazi Hussein.

    Ilibidi sasa mamaako amuwahi kakaake ambae pia ni babaako pale chini pindi alipozinduka lakini nae alichelewa hata mimi pia nilichelewa kumuwahi kutokana na kumuweka chini babu yako Hussein aliyekuwa kashakufa na kumuwahi bibi yako Zai kwa kumpa msaada bila kujua nyuma yangu Shebby amezinduka na kwa kuchanganyikiwa kwa kile akionacho alishindwa kujizuia na kuiokota tena bastora yake na hapo nilisikia tu mlio wa risasi sambamba na kelele za mamaako Asha na nilipogeuka hakuwa Asha aliyepigwa risasi bali ni Shebby mwenyewe alijipasua kichwa na kusambaratika ubongo palepale.."

    alipofika hapa kidogo alisita na kwa mara ya kwanza Cj4 chozi lilimdondoka hadhalani toka afuzu mafunzo ya Ukomando Cuba zaidi ya miaka 20 iliyopita.

    "Mwanangu Hussein, sikumbuki lini ilikuwa mara ya mwisho kutoa chozi kwani hata kipindi yale yote yanatokea sikudondosha chozi. Zaidi nilisimama kiume kukabiliana nayo kwani ilibidi nimuache bibiako Zainab niliyeona wazi kuwa yupo katika hatua za kumalizikia baada ya presha kushuka sana na kushuhudia mwanae akijimaliza na hapo ilibidi niluke kishujaa kumuwahi mamaako Asha ambae nae alikuwa anataka ajimalize kwa bastora ile ile aliyojimalizia babaako.

    Jinsi nilivyoruka sikuwahi kufundishwa wala kudhani kama nina uwezo wa kuluka vile, lakini ndivyo ilivyokuwa niliweza kumuwahi mamaako na kumuokoa mbele ya kifo alichokuwa anajitengenezea mwenyewe na nilichokifanya niliubetua mshipa wake mdogo wa fahamu uliokuwa nyuma ya sikio na kumzimisha.

    Hapo ndipo nilipoweza kuwasiliana na mkuu wangu wa majeshi na kumpa taarifa zote kabla sijaondoka eneo lile huku nikiwa nimem beba mamaako ambae sikujua kumbe tayari tumboni ulikuwapo wewe."

    Story ya Cj4 ilimuuma sana yule mtoto lakini alionesha alikuwa jasiri sana na mwenye moyo wa uvumilivu kwani alikuwa anatokwa machozi lakini aliweza kusikiliza kwa umakini na kuuliza maswali muhimu.

    "Kwa hiyo baba Cj ilikuwaje sasa ulipoondoka na mama hasa pale fahamu zilipomrudia?"

    "Mwanangu Hussein, mamaako kwanza alichelewa sana kupata fahamu hadi nilianza kuhofu lakini alipopata fahamu nilikuwa nae kwenye kambi maalum ya kijeshi ambapo ndipo nilipoelekea mara baada ya kutoka pale kwenye ile nyumba.

    Niliongea nae na kumpanga kwa maneno ya kishujaa na mbinu maalum ambazo utakutana nazo pindi utapokuwa kama mimi hapo baadae, nikikutazama naona wazi utakuwa zaidi ya mimi.

    Basi mamaako japo ilikuwa ngumu kuelewa lakini tuliweza kumdhibiti ndani ya kambi ile iliyokuwa haijulikani kabisa na watu wengi hadi kwa wanajeshi wengi wenye vyeo vya chini.

    Japo alikuwa ni wa kuzimia mara kwa mara lakini hatimae aliweza kutulia taratibu kadri siku zilivyozidi kwenda hadi tulipomgundua kuwa alikuwa na mima baada ya kumfanyia vipimo vya utrasound pindi tulipoona tumbo linazidi kuwa kubwa na kugundua uwepo wako.

    Sikuweza kuhudhulia mazishi ya babaako, bibiako, babu ako na babu ako mlezi wa babaako Mr X ambao wote walizikwa kwa pamoja hapa kama unavyoona makaburi yao yalivyofatana kwa sababu ya kuwa karibu na mamaako na kumliwaza japo niliweza kuyashuhudia baadae kupitia rekodi kamili ya ule mkanda tulioutazama tena sote jana usiku.

    Serikali ndio waliolizima suala lile baada ya taarifa za ripoti yangu kamili kufika kwa muheshiwa Rais."

    "sawa baba, sasa mama nae alikufa kufa vipi?"

    "Mamaako kilichomuua ni sumu iliyokuwa mwilini mwake iliyokuwa ikimtafuna muda mrefu.

    Sumu hiyo ilitokana na kile kisu cha kininja alichochomwa na Tyga siku ile usiku... Kwa hiyo siku aliyokuwa anajifungua ndio siku aliyofariki pindi alipokuwa anakupush kwa nguvu kumbe alikuwa anajimalizia baada ya sumu kushambulia sana maeneo ya uti wa mgongo na mbavu.

    Mamaako alikufa kishujaa kwa kuwa aliweza kuvumilia hadi akafanikisha kumzaa Shujaa mpya ambae ni wewe mwanangu Hussein niliyeamua kukupa jina hili la babu yako ambae pia alikufa mikononi mwangu lakini kupitia wewe nikaona kama amezaliwa tena mikononi mwangu.

    Na hivyo ndivyo ilivyokuwa Hussein wewe ulikuwa chini ya usimamizi wangu wala hukuwa na ndugu yeyote zaidi yangu.... Simama sasa nataka nikuulize nami maswali yangu."

    aliongea Cj4 na kusimama sambamba na mtoto Hussein ambae ndie alikuwa mtoto halali wa Marehemu Dokta Asha au Lady Ninja na Marehemu Kamishna Shebby.



    "Ulivyoelewa historia yako asili yake na matatizo yote chanzo ni nini?"

    "MWANAMKE"

    alijibu Hussein bila hata kusita.

    "Vizuri na je, ulivyosoma historia ya ushujaa wa Samson dhidi ya Wafiristi hadi siri zake zikabainika na kukamatwa kupata mateso makali hadi alipoomba nguvu kumrudia na kufa pamoja na mamia ya watu je nae kilichomponza hasa chanzo ni nini?"

    "MWANAMKE"

    alijibu tena Hussein.

    "Vizuri sana, na vipi kuhusu asili ya dhambi ya baba etu Adam kusariti ahadi aliyopewa na mungu na kushawishika kula lile tunda, kihistoria ulivyosoma shetani alimtumia nani kumshawishi kiurahisi Adam."

    "MWANAMKE"

    "Ni kweli mwanangu Hussein na hivi unajua kwanini Wanawake ni wengi kuliko Wanaume?"

    "hapana baba Cj4, sijui."

    "Basi ni kwasababu mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na alikuwa mtoto wa Adam aliyepigana na ndugu yake sababu ikiwa ni mwanamke. na hapo ndipo uwiano wa namba ulipozidi.

    Kwa hiyo kwa uelewa wa kawaida kabisa umeona kumbe hata mtu wa kwanza kufa chanzo ilikuwa nini?"

    "MWANAMKE baba Mh!!"

    "Huo ndio ukweli ambao alikuwa anamaanisha babu yako wala si uchizi.. hivi unajua chanzo cha mimi kukuhadithia hadithi ya maisha ya asili ulipotokea chanzo ni nini?"

    "Ndio baba chanzo ni Halima mtoto wa baba Kanali Suma mara baada ya kusababisha nimepigana na kumuumiza Amos mtoto wa Luten Frenk."

    alijibu kwa upole Hussein.

    "sawa kwa hiyo Halima ni nani?"

    "ni mwanamke baba"

    "kwa hiyo chanzo cha kukuhadithia ukweli huu na kukuonesha video ya mazishi mpaka sasa tupo hapa chanzo ni.....?"

    "MWANAMKE"

    "Ndio, sasa umejifunza nini hapa."

    "Naapa baba Cj4 mbele za Mungu, mbele ya makabuli haya ya ndugu zangu kuwa nitakuwa makini makini sana na Wanawake kamwe sintokuwa mzembe wa kuwaaamini kwa asilimia zote kwa kuwa Wanamke wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili."

    aliapa kwa nguvu na sauti ya kumaanisha Hussein.

    "sawa unadhani kwanini umeapa hivyo? hivi kiapo chako uko sahihi kweli?"

    "Naamini baba Cj4 nipo sahihi, na ili nikuaminishe nipo sahihi kusema kuwa 'wanawake wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili' nataka nikuulize swali."

    "Uliza tu mwanangu."

    "Je ni dini gani kati ya ukristo na uislam pamoja na matawi yake inasema Mungu alituma manabii na mitume wanawake kwaajili ya kuwaogoza na kuwaokoa watu?"

    "Mh!! HAKUNA mwanangu wala sijawahi kusikia."

    "unadhani Mungu ana upendeleo kwa wanaume?"

    "Hapana, ila ninachojua Mungu alimuumba mwanamke kwa sababu ya kumtuliza na kumliwaza mwanaume."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kwa hiyo hapo baba ndipo kwenye 'ulemavu na dhaifu wa asili ya mwanamke' japo wenyewe hawataki na naamini mwanamke asiyekubali kuwa dhaifu mbele ya mwanaume naamini ni muuaji na mwanamke asiyekubali kuwa ana ulemavu wa upeo basi atajiamulia vitu kama bibi Zai na faida yake ataiona mwishoni na atakuwa muuaji tu."

    aliongea kwa uchungu Hussein na Cj4 alishangaa kuona maneno ya Hussein mtoto yanashabiana na nukuu za marehemu Hussein mkubwa na kuamua amkumbatie kwa nguvu pindi alipoona anazidi kuongea huku akilia na kumsihi sasa inatosha waondoke.

    "Basi mwanangu basi mwanangu tuondoke sasa ila zingatia haya na ufanye utafiti na uwaokoe wanaume wengi wasiojua hili pamoja na kuwaelimisha wanawake wakubali udhaifu wao ili matatizo zaidi yasiendelee kutokea na kabla hujaongea nao wala kuwasimulia waulize kwanza je, WANAWAKE NI WAUAJI..!? sikiliza na uhesabu majibu yao kisha uwasimulie story hii na ikiwezekana uiandike kabisa na uitolee Kitabu ili wengi wakipate na mara utapomaliza kuwasimulia/kuandika waulize tena kwa mshangao swali lilelile la mwanzo kuwa WANAWAKE NI WAUAJI..!? uone tena majibu yao."



    _________________________

    ____________

    * MWISHO *

0 comments:

Post a Comment

Blog