Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

KISU CHENYE MPINI MWEKUNDU - 4

 





    Simulizi : Kisu Chenye Mpini Mwekundu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Moja ya furaha iliyokuwa inarindima katika kichwa cha sajenti wa jeshi la wananchi Frank kilindo ni barua ya likizo iliyokuwa pale mezani kwake. Ilikuwa ni likizo ya miezi mitatu. Alikuwa amepanga kuutumia muda wake wa likizo nyumbani kwao Mahenge. Hakuweza kufikiria kama kuna kitu kingekatisha furaha ile. Akiwa kwenye mawazo hayo ya furaha ghafla, simu yake ya kiganjani ikaanza kuita. Akaitoa ile simu mfukoni kisha akaangalia mpigaji ni nani. Ilikuwa namba mpya akaamua kupokea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hallow unaongea na sajenti kilindo hapa nani mwenzangu.”

    “Naitwa mwalimu Mateka ni mwalimu hapa zanaki” Ilijibu sauti upande wa pili kisha ikaendelea.

    “Kuna taarifa kuhusu mwanao Vick, tumempima ameonekana ana ujauzito wa miezi miwili.”

    “Uhfuuu.” akashusha pumzi sajenti.

    Akatoka ofisini huku furaha yake yote ikimezwa na hasira. Akaingia kwenye gari lake na kuliondoa kwa kasi kuelekea nyumbani. Njia nzima alikuwa anasonya kwa hasira huku akitamani kukutana na Vick amrarue.



    Alipofika nyumbani akafunguliwa geti na mkewe.

    “Vipi baba Vick, mbona hivyo?” Aliuliza mkewe baada ya kuona jinsi numewe alivyobadilika.

    “Naomba maji baridi.” Hakutaka kujibu swali la mkewe. Baada ya kunywa maji akaongea bila kumtazama mkewe. Alikuwa kama anayeongea na mtu amabye anamuona peke yake.

    “Yaani nahangaika ili mwanangu asome leo anakuja kuniletea mimba.”

    “Nini?” Mama yake alipatwa na mshituko.

    “Mwanao Vick ana mimba ya miezi miwili nimepigiwa simu kutoka shuleni kwao.”

    “Paaaa.” Chupa ya chai iliyokuwa mkononi ilimtoka mama Vick kwa mshituko alioupata.

    Akakaa kwenye kiti na kushika tama. Furaha ya likizo ilikuwa imeyeyuka. Hakuna aliyefurahia tena safari yao ya Mahenge.

    Muda wa kumsubiri Vick ili amalize hasira zake kwa kipigo atakachompa ulikuwa mrefu mno. Alishauweka mezani ule mkanda wa jeshi tayari kwa kipigo. Hasira kali ilirindima kwenye nafsi yake.

    Masaa yalizidi kuyoyoma Vick hakutokea nyumbani. Subira ikamshinda Sajenti. Akaamua kumfuatilia hukohuko shuleni. Jua lilikua linaanza kuwaaga wakazi wa Dar. Haikuwa kawaida ya Vick kurudi usiku lakini muelekeo ulionyesha kuwa angerudi usiku. Licha ya uchungu kwa kitendo kilichofanywa na mwanae bado mama Vick alikuwa na wasi wasi na hatua itakayochukuliwa na mumewe. Alijua jinsi gani mumewe anakuwa mtu hatari akiwa na hasira. Aliogopa sana kuwa anaweza kumuua mwanawe lakini aliogopa zaidi kumzuia kwani kitendo hicho kingemfanya aone kuwa walikuwa na ushirikiano pia aliogopa kugeuziwa kibao na kupata kipigo cha paka mwizi. Akaamua kutulia na kumwacha mumewe afanye atakalo.



    * * *

    Baada ya kupata matokeo Vick aliondoka shuleni akiwa kama aliyechananyikiwa. Alikuwa anajiuliza nini atamwambia baba yake kwani alishapewa barua ya kufukuzwa shule. Kila aina ya uongo aliofikiria kutunga alijua wazi kuwa usingekubalika mbele ya baba yake. Kilichomtia hofu zaidi ni uwezekano wa baba yake kupata taarifa kutoka shuleni moja kwa moja. Akaona hana sababu ya kuongopa isipokuwa asubiri aone majaliwa yake yatakuwaje. Hakutaka kwenda nyumbani moja kwa moja akaamua kupitia kwa Beda. Hakukuta mtu. Kwa kuwa alijua pale walipoficha funguo akachukua na kufungua mlango kisha akajilaza kwenye jamvi lililochoka pale sebuleni. Akashikwa na usingizi akalala.



    Saa kumi na mbili na nusu akaamshwa na Beda ambaye aliingia ndani na kushangaa baada ya kumuona Vick akiwa amelala pale.

    “Vipi Vick kulikoni?” Aliuliza Beda. Akaamka akafuta macho kwa mkono wake wa kuume.

    “Kuna matatizo Beda.” Alianza kuongea huku akitazama chini.

    “Kuna nini?”

    “Nimefukuzwa shule.”

    “Umefanya kosa gani?”

    “Nina ujauzito wa miezi miwili Beda.”

    Kwanza alihisi tumbo likianza kuunguruma kisha akakaa pale kwenye jamvi.

    “Una mimba?” Aliuliza Beda kwa mshangao. Ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa.

    Vick akaanza kulia. Ni wazi hakuna mtu aliyemuogopa zaidi ya baba yake. Alikuwa anajiuliza ni hatua gani itachukuliwa baada ya kufukuzwa shule.



    * * *

    Sajenti Frank Kilindo aliamua kurejea nyumbani baada ya kugundua kuwa hasira zilikuwa zinamwendesha vibaya. Ni hasira tu zilizokuwa zinamchanganya hata akashindwa kuvuta subira na kumsubiri Vick.

    Saa 1.32 Vick akawasili nyumbani. Alijitahidi kuficha kilio na huzuni yake. Alipofika sebuleni akamkuta baba yake akiwa amekaa mkao ambao haukumpa shida kuutafsiri kuwa ameshapata taarifa. Huku akitetemeka akakatisha pale sebuleni hadi chumbani kwake bila kumsalimia baba yake kama alivyozoea. Baba yake naye akajifanya kama hajamuona.

    Baada ya dakika chache Vick akajisalimisha pale sebuleni kwani alijua kitendo cha kubaki chumbani kingemfanya baba yake amfuate jambo ambalo lingekuwa hatari zaidi kwake.

    “Habari za shule mwanangu.”Alisalimia sajenti. Anaigiza? Alijiuliza Vick.

    “Nzuri shikamoo baba.”

    “Marhaba vipi habari za shule.”

    “Nzuri.” Alijibu Vick huku akijua wazi kabisa kuwa maswali yote hayo yalikuwa ni mtego tu. Asingeweza kudanganyika kabisa kuwa baba yake alimsalimia katika hali ya kawaida.

    “Mwanangu, najua kabisa kuwa una uja uzito.” Aliongea kwa sauti tulivu ambayo ilimshangaza hata Vick. Baada ya kupiga chafya akaendelea.

    “Nilikuwa nimekuandalia adhabu kali sana, nafikiri unauona huo mkanda hapo mezani. Nimefikiria muda mrefu nimeona hakuna sababu ya kukuadhibu kiasi hicho kwani ni kosa lako la kwanza hivyo jiandae jumatatu twende hospitali tukaitoe hiyo mimba.” Aliongea sajenti kwa sauti tulivu ambayo ilimshangaza hata mkewe ambaye alikaa karibu na dirisha ili kuweza kujua nini kitatokea.

    “Unaweza kwenda.” Vick akaondoka kurudi chumbani huku akiwa haamini kabisa kilichotokea.

    * * *

    Jumatatu ilimkuta vick akiwa kwenye zahanati ya Sakina ambayo iko Tandika sokoni. Zahanati hii ilikuwa na kitu cha ziada kwa Vick. Asingeweza kusahau jinsi mwanafunzi mwenzao Hawa alivyopoteza maisha baada ya kujaribu kutoa mimba katika hospitali hiihii. Ilikuwa ni baada ya kupata sifa kuwa kuna daktari nzuri wa kukatisha uhai wa watoto ambao bado hawajauona mwanga wa dunia hii. Wazo likapita kichwani mwake, kwanini atoe mimba? Mama yake alikuwa ameingia chumba cha daktari. Jinsi mikasi na vyombo vya hospitali vilivyokuwa vinagongana vilimtia hofu sana.

    Hakutaka kumsubiri mama yake, aliamua kuondoka akiwa na uamuzi wa kutotoa mimba. Alishaamua kuwa liwalo na liwe. Wakati mama yake akiongea na daktari juu ya gharama za shughuli ile vick alikuwa anapiga hatua kuelekea kituo cha daladala pale Tandika. Akakatisha pale kituo cha polisi akatokea barabarani. Huku akigongana na watu kutokana na msongamano aliendelea kutembea kasi. Mara kadhaa alilazimika kupokea matusi kutoka kwa wanawake wenzake ambao aligongana nao wakati wa kupishana. Wanaume ni watu wa ajabu, hali ile ya kugongana na wanawake kwao ilikuwa ni faraja ingawa nao walichukia pale walipogongana na wanaume wenzao.

    Aliyapuuza macho ya watu waliokuwa wanamshangaa kwa haraka aliyokuwa nayo. Akafika kituo cha daladala zinazoelekea Mbagala. Akaingia kwenye daladala lililokuwa linakaribia kujaza abiria.

    Siku ya tukio alipata msamaha . Itakuwaje leo baba yake atakapopewa taarifa za kukimbia kwa daktari. Ni kweli inaweza kutokea miujiza kama ya siku ile? Mkanda wa jeshi ulikuwa mezani lakini ghafla sajenti yule wa jeshi la wananchi akabadili mawazo. Kwa upole kabisa akampa nafasi mwanawe. Ilikuwa ni nafasi ngumu ambayo ilimuathiri Vick kifikra. Kwanza alikuwa anatakiwa kuua kiumbe asiyekuwa na hatia, pili alikuwa anahatarisha maisha yake. Hakuwa tayari kufanya lolote kati ya hayo, Ujasiri ulikuwa mkubwa kwenye nafsi yake. Alijiandaa kukabiliana na kipigo, alijiandaa kuabiliana na lawama za aina yoyote.

    Alikuwa siti ya dirishani huku akiangalia nje. Alikuwa anaangalia nje lakini fikra zake zilikuwa zimeondoa uwezo wa macho. Hakuweza kuona chochote kule nje. Macho yake yaliona vitu tofauti na vitu halisi vilivyokuwa mbele ya macho yake. Aliweza kumuona baba yake akiwa na ule mkanda wa jeshi, aliweza kumuona Beda akimbembeleza na kumliwaza baada ya kupigwa kwa mkanda ule. Pia aliweza kumuona mama yake akimtafuta pale ‘Dispensary’ bila mafanikio. Haiwezekani huu ni uuaji. Aliwaza.

    Saa 6.30 aliwasili Mbagala. Akaanza kutembea kwa miguu huku akiwa hajitambui vema kutokana na mawazo. Baada ya dakika kadhaa akafika nyumbani . Moja kwa moja akaelekea chumbani kwake ambako alijilaza kitandani na kuyaelekeza macho yake juu.

    Alilishika tumbo lake, bado lilikuwa dogo halikuwa na dalili yoyote ya kuonyesha kuwa ni mja mzito. Baada ya mawazo ya muda mrefu akapitiwa na usingizi.

    Akashtushwa na vishindo vya mtu aliyekuwa anagonga mlango kwa nguvu. Alijua tu. Hakuwa mwingine zaidi ya baba yake. Akaamka pale kitandani na moja kwa moja akaenda kufungua mlango.

    Akakutana na sura ile ya simba aliyejeruhiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vick sitaki nikupige kwa hasira nilizo nazo naomba uondoke humu ndani najua utanipa kesi ya mauaji. Pia nataka ujue kuanzia leo mimi sio baba yako, nenda ukamtafute baba yako huko aliko.” Ilikuwa ni hotuba fupi nzito iliyobeba ujumbe wa kutisha. Aende wapi? Alijiuliza.

    “Nakupa masaa mawili ya kukaa humu ndani, nikirudi huku ninakoenda nisikukute.” Alifoka Sajenti.

    * * *



    Sajenti Frank kilindo alikuwa anajiandaa kwenda kumchukua mkewe na mwanawe ambaye alimuacha pale zahanati Tandika. Huku akijipongeza kwa kuweza kudhibiti hasira yake kwa mwanae Sasa alijua mwanae ataendelea na masomo baada ya kutoa mimba.



    Aliendesha gari taratibu kuelekea Zahanati. Alipofika akamkuta mkewe akiwa katika simanzi. “Vipi?” Swali fupi lenye maana kubwa.

    “Katoroka.”

    “What?” Kimya.

    “Ingia kwenye gari twende.” Ilikuwa amri.

    “Hatusubiri?”

    “Sina mtoto nisubiri nini?” Ukimya ukatawala baada ya kauli hiyo huku kila mmoja akitafakari tukio lililofanywa na Vick.

    Alipofika nyumbani hakuwa na hatua nyingine zaidi ya kumfukuza na kumkana mwanae. Mama Vick alisikia uchungu sana lakini aliogopa kutia neno lolote kwani lingemgharimu.

    Baada ya baba yake kuondoka Vick alikusanya vitu vyake kama alivyoamrishwa na baba yake hatimaye akaondoka. Wakati anaondoka akageuka na kuiangalia nyumba ile ambayo amekulia yeye na kaka zake watatu ambao wote wameajiriwa na jeshi la wananchi. Yeye ndiye mtoto wa mwisho bado alikuwa mwanafunzi wa sekondari. Ndoto zake zimeishia hapo. Huku akiwa na mizigo yake hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya nyumbani kwa Beda.

    Alipofika akashangaa kuwakuta Beda na mama yake wakiwa katika hali ya simanzi. Akashangaa kuona wana nyuso zilizojaa woga.

    Baada ya kusalimiana akakaa huku akijiandaa kusimulia kile kilichomtokea. Ajabu. Hakuna aliyeshangazwa na ujio wake. Hili lilimshangaza zaidi.

    “Mwanangu Vick.’ Alianza mama Vick huku akionekana kusita kidogo kwa alichokusudia kuongea kisha akaendelea. “Taarifa zako zote tunazo baba yako alikuja hapa akatoa vitisho vizito na kaapa kama tutathubutu kukupokea basi kifo itakuwa halali yetu sote.”

    Vick alishtushwa na kauli hiyo akajikuta akikosa nguvu akalala pale kwenye jamvi.

    Kilio kilichoambatana na kwikwi kikaanza kumtoka Vick. Mama Beda naye akashindwa kuvumilia akaingia ndani huku akilia. Asingeweza kuusahau moyo wa huruma ulioonyeshwa na Vick. Vick ni kama mwanae, pamoja na ujinga walioufanya alijua ni utoto wa kutofikiria nini kitatokea mbele ya safari. Kama si vitisho vya baba yake alikuwa tayari kumtunza na kumuhudumia. Afanyeje? Aliwaza. Akaendelea kulia huku kila alilolifikiria akiliona kuwa zito upande wake. Kiio kilikuwa kimetawala nyumba hii. Beda naye alikuwa analia kwa matatizo yaliyokuwa yanamkuta Vick yeye akiwa sababisho.

    “Beda naomba uniwekee hili begi kubwa ndani.” Aliongea Vick huku akijifuta machozi. Alionekana kama aliyepata wazo jipya. Beda alipotoka ndani hakumkuta Vick. Hakushtuka kwa sababu alihisi kuwa huenda hayuko mbali. Lakini alishtuka baada ya kuona masaa yanakatika



     Mama Beda naye akashindwa kuvumilia akaingia ndani huku akilia. Asingeweza kuusahau moyo wa huruma ulioonyeshwa na Vick. Vick ni kama mwanae, pamoja na ujinga walioufanya alijua ni utoto wa kutofikiria nini kitatokea mbele ya safari. Kama si vitisho vya baba yake alikuwa tayari kumtunza na kumuhudumia. Afanyeje? Aliwaza. Akaendelea kulia huku kila alilolifikiria akiliona kuwa zito upande wake. Kiio kilikuwa kimetawala nyumba hii. Beda naye alikuwa analia kwa matatizo yaliyokuwa yanamkuta Vick yeye akiwa sababisho.

    “Beda naomba uniwekee hili begi kubwa ndani.” Aliongea Vick huku akijifuta machozi. Alionekana kama aliyepata wazo jipya. Beda alipotoka ndani hakumkuta Vick. Hakushtuka kwa sababu alihisi kuwa huenda hayuko mbali. Lakini alishtuka baada ya kuona masaa yanakatika.

    Jua lilishaanza kupoteza nuru yake. Bado Vick aliendelea kutembea. Alitembea hadi kiza kilipoingia. Hakujua wapi anaelekea. Ingawa kwa kufuata ramani ya nchi alikuwa ameshauacha mkoa wa Dar es salaam na kuingia mkoa wa Pwani. Hatimaye aliiacha ardhi ambayo ilikuwa na majumba. Akaingia maeneo ambayo hakuiona nyumba yoyote zaidi ya barabara ile ya lami. Magari mengi yalikuwa yanapita kwa kasi eneo lile. Hakupenda jinsi magari yalivyokuwa yanammulika kwa taa zake. Alijua wazi wako madereva wenye roho nzuri ambao watasimama na kutaka kumpa msaada ambao hakuuhitaji wakati huo. Akaamua kuacha barabara kuu inayoelekea wilaya ya Mkuranga na mikoa ya kusini akaingia msituni. Alianza kwenye mashamba hatimaye akaingia kwenye msitu kamili. Hofu na mashaka na mateso yalitawala katika safari yake. Alishaamua kufia huko msituni. Alitembea mpaka akachoka. Akaamua kulala chini ya mti mkubwa. Saa nane usiku akashtuka ghafla kutoka usingizini. Alipoangalia vizuri akagundua kile kilichokuwa mbele yake. Ajabu. Ingawa kulikuwa na giza nyoka yule mkubwa aling’aa na kuweza kuonekana. Alikuwa anajiburuza taratibu kuelekea kule aliko Vick. Alimtambua vizuri nyoka huyu. Ingawa alikuwa hajawahi kumuona lakini alibaini moja kwa moja kuwa ni chatu. Alitamani sana kufa lakini kamwe hakutamani kifo hicho kitokane na chatu. Alitetemeka lakini akawa mtulivu akisubiri kifo chake. Alimfikiria sana yule aliyekuwa tumboni. Hakujua itakuwaje. masikini nakufa na mwanangu hata dunia hajaiona. Aliwaza Vick huku akianza kutokwa na machozi.



    *****



    Nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam walisimama vijana wenye nyuso zilizojaa wasiwasi. Miongoni mwao alikuwa ni Beda Sanga. Huyu alikuwa miongoni mwa vijana waliomaliza kidato cha sita ambao wamebahatika kuitwa kwenye usaili wa kujiunga na jeshi la Polisi. Pengine huyu ndiye mtu aliyekuwa na hofu zaidi, kichwani mwake yalipita mambo mengi zaidi. Kubwa zaidi ilikuwa ni ile fikra ya kulipa fadhila alizofanyiwa na mama yake. Alikumbuka jinsi mama yake alivyopata tabu kwenye malezi yake. Miongoni mwa vitu ambavyo vilimuhuzunisha ni kifo cha Vick. Kilichomsikitisha zaidi ni aina ya kifo chake. Vick alitoweka Ghafla kwenye macho yake. Dakika, saa…… hatimaye miaka Vick hajaonekana. Mama Beda alimlilia sana licha ya vitisho kutoka kwa baba mzazi wa vick kuwa iwapo atathubutu kmpokea basi angewaua wote watatu. Vick kachukua hatua ya kutoroka. Hatimaye hakujulikana wapi aliko. Baada ya miaka mitatu kupita kila mtu akapitisha kwenye fikra zake kuwa Vick ni marehemu. Amejiua, ameuwawa au ame…. hakuna aliyeweza kufumbua fumbo hilo. Jambo la ajabu baba yake hakujisughulisha tena na jambo lolote kuhusu Vick kwake ukurasa ulikuwa umefungwa ingawa alipata lawama kubwa kutoka kwa ndugu na jamaa hakujali.

    “Beda Sanga….” Alishtushwa na sauti iliyokuwa inaita ndani.

    “Nipo.” Aliitika kwa sauti huku akijitahidi kutembea kwa ukakamavu kuelekea ndani. Alitembea mwendo ambao alidhani ungewashawishi wasimamizi wa usaili kumchagua.

    Akasimama mbele ya meza ile ile iliyozungukwa na watu waliokuwa ‘siriasi’ kiasi cha kumtia hofu mtu wa kawaida.

    “Kwanini unataka kuwa Polisi?” Alihoji mmoja. Aina gani hii ya maswali. Alijiuliza Beda.

    “Nataka kulitumikia Taifa langu.” Alijibu na kukaa kimya.

    “Huwezi kulitumikia taifa kwa njia nyingine tofauti?” Aliuliza mwingine.

    “Naweza.” Alijibu kwa mkato huku akimwangalia yule aliyekuwa katikati jinsi alivyokuwa anakagua vyeti vyake.

    “Kwanini usilitumikie Taifa kwa njia nyingine.” Aliendelea kuuliza

    “Kwa sababu huu ni kama mgawanyo wa kazi hivyo mimi nimechagua huku.”

    “Kwa hiyo lengo lako ni kuitumikia nchi tu.”

    “Si hivyo tu nahitaji pia mshahara ambao utaweza kunifanya niendeshe maisha yangu ya awaida.”

    “Unasema maisha ya kawaida unaweza kufafanua ni maisha gani si ya kawaida?”

    “Ndiyo. Ni maisha ya anasa na………..” Hakumaliza akakatishwa na swali lililoulizwa na yule aliyekuwa anakagua vyeti vyake.

    “Kwanini umeghushi vyeti vya Elimu ya Sekondari.”

    “Sijaghushi ni vyeti halisi.” Alijibu Beda kwa kujiamini.

    “Haya nenda.” Aliamrishwa.

    Akaondoka huku akiwa hana uhakika nini kitatokea.



    * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa kama ndoto. Beda hakuamini siku aliyoripoti makao makuu ya jeshi la Polisi akiwa askari aliyehitimu vema mafunzo hayo. Alianza kazi yake kwa ufanisi mkubwa jambo lililosababisha athaminiwe na kupewa majukumu mengi zaidi. Aliamua kumuhamisha mama yake kule Mbagala wakahamia maeneo ya Ubungo. Hakuipenda nyumba ya Mbagala kwa sababu ilimpa kumbukumbu mbaya katika maisha yake. Ndipo alipoamua kwenda kutafuta chumba maeneo mengine.

    Siku moja Beda alikuwa kwenye mizunguko ya kawaida pale Kariakoo. Ndipo akakutana na kitu ambacho kilimshtua.

    Ombaomba. Hakuwa ombaomba wa kawaida. Alimwangalia kwa makini akajikuta moyo wake ukienda mbio. Pumzi zikaanza kupanda na kushuka haraka haraka. Akaamua kuondoka eneo lile harakaharaka. Ni mzuka au sadifa? Alijiuliza huku akiwa amesimama kwenye makutano ya mtaa wa Swahili na Sikukuu. Akakaa pale kama dakika kumi bila kujua afanye nini. Ndipo alipoamua kupiga moyo konde na kurudi tena nyuma. Huku anatetemeka akaita.

    “Vick.”

    “Bee.” Yule ombaomba aliitika na kuzidi kumtisha Beda. Ni yeye. Kama alikuwa Vick kweli basi kidogo alionyesha kumsahau Beda. “Naomba shilingi mia baba mwanangu ana njaa si unamuona.” Aliongea yule mwanamke ombaomba huku akimuonyesha Beda kwa kidole mtoto aliyekuwa ameegemea ukuta. Beda akamuona yule mtoto, alikuwa na miaka kati ya sita na minane. Mungu wangu. Alishtuka Beda baada ya kumuona kiumbe aliyefanana na mama yake mzazi akiwa kwenye kundi la ombaomba. Machozi yakaanza kumtoka.

    “Vick unanikumbuka?” Aliuliza Beda. Hapo Vick akamtazama vizuri aliyekuwa anaongea naye.

    “Beda.” Alishtuka Vick na kumkazia macho Beda kwa mshangao. Wakakumbatiana huku wakiendelea kulia. Kilio chao kilivuta hisia za ombaomba wengine na wapita njia ambao walitaka kufahamu kulikoni Kijana yule mtanashati akumbatiane na ombaomba tena kubwa zaidi wakikipamba kitendo kile kwa kilio. Wengi walisimama wakisubiri kusimuliwa. Hakutokea wa kusimulia mkasa ule. Ili mradi kila mmoja aligeuka na kumuuliza jirani yake. Jibu halikupatikana na watu hawakuondoka walizidi kujaa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wapita njia wenye haraka.

    “Twende.” Aliamrisha Beda baada ya kuona watu wanazidi kuongezeka.

    Wakatembea hadi kituo cha teksi cha sikukuu.

    “Nipeleke Ubungo maziwa.” Alisikika Beda huku akiingia kwenye teksi.

    Beda alikuwa amepanga vyumba viwili na sebule. Baada ya kumlipa dereva wa ile teksi wakateremka na kuingia ndani. Mama Beda ambaye alikuwa nje hakujishughulisha sana na wageni wale kwani alishazoea kupata wageni wengi toka mwanawe alipoajiriwa na jeshi la polisi. Maisha yake yalibadilika unafuu ulikuwepo. Angalau alianza kuonja ladha ya elimu ya mwanae.

    “Karibu Vick.”

    “Ahsante.”

    Aliitikia Vick. Vick mchovu sio yule aliyetoroka kwa baba yake wakati anang’aa. Nyuma alifuatiwa na binti aliyevaa kanga na kuifunga shingoni kama mtoto wa kijijini. Alikuwa na kila dalili ya umaskini.

    “Huyu ni nani?” Aliuliza Beda huku akimkazia macho yule binti wa miaka sita au saba.

    “Ni mwanao Beda huoni jinsi alivyofanana na mama yako?”

    Beda akainamisha kichwa chini kwa uchungu. Hakuwa na sababu ya kukataa, yule mtoto alifanana kila kitu na mama yake mzazi. Yule mtoto alionyesha utulivu mkubwa sana. Kwanza alijua kuwa ameletwa pale kuja kusaidiwa tu. Haikumuingia akilini kuwa yule aliyeko mbele yake ni baba yake mzazi. Asingeweza kuamini kabisa na pengine ni kitu ambacho hakuwahi kukifikiria. Alijua kuna watu walistahili maisha fulani lakini sio yeye. Alijiweka katika kundi ambalo aliona ni halali kuishi maisha ya kuomba.

    “Mama, mama.” Aliita Beda baada ya kuinua kichwa chake.

    Mama yake akaja. Akakaa kwenye kiti pembeni kidogo na pale alipokaa Vick na mwanae.

    “Unamfahamu huyu.” Aliuliza huku akimuonyesha yule binti mdogo. Mama yake alimtazama kwa makini yule binti kisha akashituka. Hii sura si ngeni nilimuona wapi? Alijiuliza mama Beda. Kuna kitu kikamshangaza katika uso wa yule binti mdogo. Kulikuwa na alama ndogo nyeusi ambayo aliifahamu sana. Aliiona wapi? Alishituka alipokuja kubaini kuwa sura anayoiangalia haikuwa na tofauti na sura mbili anazozifahamu sana. Sura ya kwanza ni ya marehemu mama yake mzazi na sura ya pili ni ya kwake mwenyewe. Mungu wangu kama najitazama kwenye kioo nani huyu?

    Akamgeukia Beda na kumtazama kama mtu anayetaka majibu ya maswali ambayo yanapita kichwani mwake.

    “Unamfahamu?” Beda alirudia swali lake.

    “Simfahamu lakini kwa kuwa hujawahi kumuona bibi yako basi mtazame huyu mtoto.” Aliongea mama Beda huku mshangao ukiwa haujafutika usoni kwake.

    “Na huyu mama yake unamfahamu?” Akamkazia macho mgeni yule dhaifu, mchafu. Hakukumbuka alimuona wapi.

    “Simfahamu.”

    Alijibu kwa mkato.

    “Huyu ndiye ambaye umelitunza begi lake karibu miaka sita sasa.”

    “Begi?”

    “Ndiyo hakuna mtu alituachia begi lake miaka sita au saba iliyopita?”

    “Mungu wangu, Vick.” Alishituka mama Beda.

    Hakuweza kuvumilia mbele ya miujiza ile, akajikuta akiangua kilio kikubwa.



    **Amakweli ni MUUJIZA………



    Na huyu mama yake unamfahamu?” Akamkazia macho mgeni yule dhaifu, mchafu. Hakukumbuka alimuona wapi.

    “Simfahamu.”

    Alijibu kwa mkato.

    “Huyu ndiye ambaye umelitunza begi lake karibu miaka sita sasa.”

    “Begi?”

    “Ndiyo hakuna mtu alituachia begi lake miaka sita au saba iliyopita?”

    “Mungu wangu, Vick.” Alishituka mama Beda.

    Hakuweza kuvumilia mbele ya miujiza ile, akajikuta akiangua kilio kikubwa. Majirani wakaanza kukusanyika wakiwa na wasiwasi huenda kuna msiba. Beda alijitahidi kuwarudisha na kuwaambia hakuna tatizo ni mambo ya kifamilia tu. Majirani wabishi walisimama madirishani kutaka kujua kulikoni. Kwa kutambua hilo hawakuanza mapema kuongea juu ya jambo hilo. Beda alikuwa na hamu kubwa kutaka kujua Vick alipotelea wapi mpaka leo anarudi mikononi mwake akiwa na mtoto yule. Hakutaka kuuliza hilo mapema kabla hajahakikisha kuwa hakuna mtu asiyehusika atakayenasa mazungumzo yale.

    “Mtoto anaitwa nani.”

    “Anaitwa Veronica.” Alijibu Vick kwa mkato.

    Mama Beda huku machozi yakimtoka akamchukua Vero na kumpakata. Vero alishangaa kwani alikuwa hajawahi kupata mapenzi zaidi ya yale ya mama yake mzazi. Alikumbuka maisha ya mateso aliyoishi kwenye mitaa mbalimbali ya kariakoo. Baadhi ya maeneo walitukanwa pia kuna wakati waliambiwa wanafanya makusudi. Alikumbuka pia jinsi walivyopigwa makofi na baadhi ya wenye maduka. Nani huyu ambaye leo anathubutu kumkumbatia kwa hisia kali za mapenzi ya kweli kama yale aliyoyapata kutoka kwa mama yake? Ni nani huyu ambaye hajali hata haya mavazi yangu yenye harufu mbaya?

    Kulikuwa na utulivu mkubwa. Akachungulia dirishani, hakukuwa na mtu tena. Akafungua friji akatoa Soda. Moja akampa Vero nyingine akampa mama yake Vero. Shauku aliyokuwa nayo isingemfanya asubiri muda zaidi kujua kile alichohitaji kutoka kwa Vick.

    “Please naomba unieleze nini kilitokea. Anzia siku uliyotoroka mpaka kufikia leo.”

    Vick akainua kichwa juu.



    * * *



    “Ng’aa, nng’aa, nng’aa.” Saa 6.00 sauti ya mtoto mchanga ilisikika kutoka ndani ya nyumba ndogo ya nyasi. Kibatari chenye mwanga hafifu kiliwasaidia wakunga wa jadi kumsaidia Vick kujifungua salama. Mwanga wa kibatari ulizidi kufifia, mabibi wale wenye kila dalili za umaskini walitazamana wakashindwa kujua nini wafanye. Bibi mmoja akatoka nje, akachukua kuni na kuja nazo ndani. Akaziweka kwenye jiko lile la mafiga. Baada ya kuhangaika kwa dakika tano moto ukawaka. Mwanga ule ukaumeza mwanga wa kibatari. Baada ya dakika chache wakaja kina mama wengine kutoka nyumba za jirani. Kila mmoja akafanya kazi aliyoona inafaa ili kumsaidia mzazi. Vick alishukuru sana baada ya kupata ushirikiano nzuri kutoka kwa wanakijiji.

    Pamoja na umasikini waliokuwa nao alibaini kuwa ni watu wenye mapenzi ya kweli. Alikumbuka jinsi alivyookotwa msituni na kisha kutunzwa katika kijiji hiki cha Jaribu mpakani kilichopo katika mkoa wa Pwani. Asingeweza kusahau jinsi alivyonusurika kumezwa na chatu. Alijiuliza jinsi chatu yule alivyoweza kupita karibu yake bila kujishughulisha nae. Alikuwa ameshiba? Alijiuliza Vick. Lakini alikuwa amesikia simulizi mbalimbali kuwa chatu akishiba hukaa sehemu moja mpaka shibe yake iishe. Hakuwa na uhakika na simulizi hizo kwani wote walioongea hakukuwa na mtaalamu wa mambo ya viumbe.

    Baada ya chatu kumsogelea zaidi Vick alipoteza fahamu.



    ****

    Siku ya pili ilimkuta mama Tatu akitafuta kuni kule porini, ndipo alipomuona Vick akiwa amepoteza fahamu. Alikimbia hadi kijijini ambako alitoa taarifa juu ya kuonekana kwa binti yule. Wanakijiji kadhaa wakashirikiana kumbeba hadi kijijini ambako alipewa huduma za awali hadi aliporudiwa na fahamu. Akawaeleza mkasa wake wote bila kusahau dhamira yake ya kujiua. Wanakijiji walisikitika sana wakampokea na kuanza kuishi naye.

    Miezi ya kujifungua ikafika. Akajifungua mtoto wa kike ambaye alipewa jina la Veronika. Siku, saa na hatimaye miaka ikakatika Vick akaamua kurudi kwa baba yake kuomba msamaha. Wanakijiji wakamchangia nauli. Si mbali sana kutoka kijijini Jaribu mpakani hadi Dar es salaam.

    Aliwasili Dar akiwa na Vero ambaye alishakuwa mkubwa. Miaka sita aliyokaa kijijini haikuweza kumsahaulisha mazingira ya Dar. Akafika pale kweye nyumba yao. Akakuta nyumba mbili kubwa zikiwa jirani na nyumba yao. Nyumba hizi zilikuwa zimejengwa eneo ambalo lilikuwa na nyumba ndogo ndogo.

    Aligonga geti huku akiwa na hamu kubwa ya kumuona mama yake. Alishangaa kuona akitoka mtu tofauti kabisa na familia yao.

    “Habari yako.”

    “Nzuri shikamoo mama.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Marhaba nikusaidie nini.”

    “Naweza kumuona mzee Kilindo?”

    “Yule mzee mwanajeshi?”

    “Ndiyo.”

    “He.Ina maana huna habari kuwa yule mzee alikufa yeye na mkewe kutokana na ajali ya gari iliyotokea mwaka juzi?” Alijibu yule mama. Lilikuwa ni pigo kubwa kwake.

    Akaondoka akiwa na huzuni kubwa. Aliijua vema historia ya baba yake ambaye hakuwa mtanzania. Aliingia hapa nchini kiujanja ujanja na hatimaye kujipatia ajira katika jeshi la wananchi kwa njia alizozijua mwenyewe. Mama yake alikuwa mtu wa Mahenge ambako hajawahi kufika. Hakuwa na mahusiano mazuri na kaka zake ambao hawakuwa wa mama mmoja.

    Akaamua kuondoka na kwenda nyumbani kwa Beda. Akiwa na matumaini makubwa ya kupata masaada huko alipigwa na butwaa baada ya kukuta nyumba hiyo ikiwa gofu.

    Hakuwa na njia nyingine zaidi ya kuingia mtaani na kuwa ombaomba. Maisha yalikuwa magumu sana. Ni kipindi ambacho kilikuwa na mateso makubwa zaidi ya kipindi chochote katika maisha yake. Alidhalilika akadharaulika.

    Hakuamini alipojikuta tena kwenye mikono ya Beda. Ukawa mwanzo wa maisha mapya. Furaha ikarejea tena kwenye nafsi yake.



    ****



    Kutokana na juhudi kubwa na ujasiri wa aina yake Beda alijikuta akipandishwa vyeo na hatimaye kuwa Inspekta. Fedha haikuwa tatizo tena. Alinunua nyumba kinondoni baada ya kupata mkopo mnono kutoka moja ya benki za hapa nchini.

    Jumatatu moja Inspekta Beda alikuwa katika semina ya maafisa wa jeshi la polisi. Semina hiyo ilikuwa nzuri kwa sababu ilidhaminiwa na moja ya makampuni makubwa ya simu. Baada ya semina kwisha ulifika muda wa kujipongeza.

    “Aaah. Afande onja kidogo hii bia.” Alibembeleza Inspekta Makenzi.

    “Mh. Chungu afande.’ alilalamika Inspekta Beda baada ya kujaribu kumeza funda moja la bia ile.

    “Jaribu tena utazoea tu.”

    “Kwa hiyo unataka nizoee ulevi.”

    “Acha hizo afande. We hutaki kuvumbua dhahabu.”

    Inspekta akacheka huku akijimiminia funda lingine. Hatimaye akamaliza chupa nzima ya bia ile. Semina iliisha kila mmoja akarudi kwenye kituo chake cha kazi.

    Siku iliyofuata mara baada ya kazi akaenda maeneo ya Manzese. Akatafuta sehemu ambayo ilikuwa tulivu kidogo.

    “Naomba bia baridi.”

    “Bia gani boss.”

    “Naomba yoyote ambayo si kali sana.” Alijibu huku akiona aibu kwa kutojua majina ya bia.

    Alikumbuka kuwa bia hizi hutangazwa redioni mara kwa mara lakini alisikia kuwa hutofautiana ukali.

    Alijimiminia kinywaji kile, akaanza kunywa taratibu mpaka alipomaliza chupa ya kwanza hatimaye akaagiza ya pili.

    Ile ya pili hakumaliza akainuka pale kwenye kiti baada ya kuhakikisha amelipa kiasi anachodaiwa. Akachukua teksi iliyompeleka nyumbani kwake Kinondoni. Saa 6.32 aliwasili nyumbani kwake.

    “Vipi dear mbona umechelewa sana?” Aliuliza Vick.

    “Si unajua majukumu yetu ya kazi.”

    “Na hiyo pombe mlikuwa mnakunywa kazini?”

    Hakuwa na jibu. Akaingia bafuni kwenda kuoga kisha akatoka na kukaa mezani. Vick alimuangalia Beda bila kuongea lolote.

    “Mh.” Aliguna bila kuongea neno lolote kisha akaingia chumbani kwenda kulala.

    “Vipi mtoto alienda shule leo?” Aliuliza Beda baada ya kuingia chumbani.

    “Alienda walimu wake wanamsifia sana wanasema ni mwepesi wa kuelewa.”

    Baada ya hapo wote wakawa kimya.



    * * *



    Ulikuwa ni mwezi wa nne toka Inspekta Beda aanze kuwa mnywaji wa pombe mara nyingi aligombana na mkewe. Maelewano yalianza kupungua nyumbani siku nyingine aligombana na mama yake ambaye hakupenda kabisa tabia hiyo mpya ya ulevi.



    Siku moja Ispekta Beda alikuwa amejipumzisha kwenye baa moja iliyoko maeneo ya Majumba sita. Akiwa hapo aliagiza pombe kama kawaida yake. Mara akaingia mwanamke ambaye alienda kukaa kwenye meza moja na Beda. Baada ya kuagiza vinywaji alivyohitaji akaanzisha mazungumzo na Beda.

    “Kaka unaonekana una mawazo mengi sana.”

    “Ah. Hapana labda ndo’ nilivyo.” Wote wakacheka kisha wakaendelea na maongezi mengine. Muda wa saa nzima waliokaa pale uliwatosha Beda na yule mama kuanzisha uhusiano. Maongeza yalikuwa motomoto huku yakisindikizwa na muziki ndani ya ile baa.

    Mwisho wa yote wakakubaliana kwenda kulala gesti.

    “Una mke.” Aliuliza yule mwanamke huku akiwa amelaza kichwa chake katika kifua cha Inspekta Beda.

    “Ndiyo.” Alijibu kwa mkato akionekana kukerwa na swali hilo.

    “Unajua kwa nini nakuuliza……” Aliongea huku akionyesha wazi kukolewa na kilevi.

    “Nataka tufanye mapenzi ya heshima ambayo hayatamfanya mkeo abaini jambo lolote.’

    “Poa.” Alijibu Inspekta huku akitembeza mkono wake katika mwili wa yule mwanamke.

    Inspekta alionekana kulewa kweli kweli kwa mapenzi ya yule mama. Siku moja tu. Lilikuwa jambo la ajabu kwa mtu aliyemtambua vizuri Inspekta Beda jinsi alivyotekwa na kuweza kubadilishwa na pombe kwa muda mfupi namna ile hata akawa hana maamuzi sahihi.

    Asubuhi ilimkuta Inspekta akiwa amelala na yule mwanamke. Aliamka akavaa nguo zake tayari kwa safari ya nyumbani.

    “Unaenda wapi tena dear si uliniambia kuwa leo utakuwa Off.” Aliuliza yule mwanamke. Sauti yake laini ikamfanya Inspekta arudi tena kitandani. Akashangaa ni saa ngapi alimwambia kuwa atakuwa off. Ni kweli alikuwa Off lakini hakukumbuka kutoa kauli hiyo. Kweli pombe si chai. Aliwaza huku akihisi kuongea mengi ambayo hakutakiwa kuongea na mwanamke yule aiyekutana naye kwa mara ya kwanza.

    “Beda.” Aliita yule mwanamke.

    “Hivi kweli unanipenda?”

    “Nakupenda sana.” Alijibu Beda huku kiasi fulani akishangazwa na swali lile kwani ni pombe tu ndio zimewafanya wajumuike pale kitandani.

    “Nitahakikisha vipi kuwa unanipenda?”

    “Labda ulitaka nikuthibitishie vipi?” Aliuliza Beda huku kiasi fulani akilisanifu na kulisifia moyoni mwake umbo la yule mwanamke.

    “Nataka unioe.”

    Beda akashusha pumzi bila kuongea lolote.

    “Usijali lakini kwanza inabidi nipate mbinu nzuri ya kumuondoa mke wangu.” Akaongea baada ya kukaa kimya dakika kadhaa, huku akishangaa jinsi siku moja ilivyotosha kumfanya awe dhaifu kwa mwanamke aliyeokotana naye baa. Akashangaa zaidi baada ya kugundua kuwa alikuwa na dhamira ya dhati ya kumuondoa mkewe Vick pale nyumbani.



    Siku ya tatu Vick alikuwa hajamtia Beda machoni. Mabadiliko haya ya Beda hayakumuudhi Vick tu, bali hata mama yake alichukia. Saa 1.36 Usiku Beda alifika nyumbani. Hakuzungumza na yeyote akaacha fedha za matumizi mezani kisha akaondoka huku akiwa na kimkoba ambacho aliweka sare zake za kazi. Vick alianza kulia. Kilikuwa kilio kipya mtu ambaye amempigania maisha yake yote leo anamgeuka? Alijiuliza huku akisikia uchungu. Mama yake Beda alikuwa anajitahidi kumbembeleza Vick. Vero hakuelewa kitu, umri wake mdogo ulimuwezesha kutafsiri baadhi ya mambo huku mengine yakiwa kama fumbo kwake.

    Maisha yalibadilika. Hakuna alichokosa, lakini mumewe hakuonekana nyumbani. Alihuzunika kwa kukosa mapenzi ya mume wake. Mapenzi haya aliyoyapigania miaka na miaka leo yamegeuka shubiri. Alilia kwa nguvu zake zote, kilio hakikusaidia kitu. Alihuzunika lakini bado huzuni yake haikuwa suluhisho la matatizo yake Mwisho akaamua kukaa kimya ili aone matokeo yake.

    Upande wa pili Inspekta Beda alikuwa amezama kwenye penzi jipya la Mwanamke yule ambaye kiumri alikaribiana na mama yake mzazi. Hakukuwa na uwiano wa umri kati yao. Yule mama alikuwa na watoto watatu. Lucy, Koku na Fredi.

    “Hivi unaonaje tukihamia kwenye nyumba yako kule Kinondoni?” Aliuliza mama Lucy.

    “Utaweza kukaa na mke mwenzio?” Aliuliza Inspekta Beda.

    “Hakuna tatizo kuliko kukaa huku kwenye nyumba ya kupanga nimechoka maneno na masimango.”

    “Mh. Sawa lakini ngoja kwanza nijadiliane na mke mwenzio.” Alijibu Inspekta Beda.

    Mama Lucy alifurahi moyoni mwake huku akiwa na dhamira ya kumteka kabisa Beda.

    “Hivi unafikiri atakubali?” Aliuliza mama Lucy.

    “Sina uhakika lakini wacha nijaribu.”

    “Inaelekea unampenda sana mkeo.”

    “Si kwamba nampenda ni yeye ndio kajipendekeza kwangu nilimsaidia kutoka kwenye kundi la ombaomba nikamhurumia nikaamua nimuoe.”

    “Kwani yule mtoto si wako?”

    “Ni wa kwangu nilimpa ujauzito kabla hajawa ombaomba.”

    “Kwani ilikuwaje mpaka akawa ombaomba.”

    “Tuache hizo stori dear kwani kwa sasa hazina maana.” Aliongea hivyo huku akiwa amesimama tena na kujiandaa kuondoka.

    Baada ya kuondoka kwa mama Lucy akaenda moja kwa moja nyumbani kwake ambako alikutana na mkewe na kumweleza mpango mzima.

    “Vick mpenzi nina neno nataka kuongea na wewe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ongea tu mume wangu.”

    “Nataka ujue wazi kuwa nakupenda lakini pamoja na hilo nimeamua nikuletee dada yako hapa nyumbai.”

    “Dada yangu yupi?.” Aliuliza Vick huku akionyesha wazi kushangazwa na kauli hiyo.

    “Namaanisha kuwa nataka kumleta mwanamke mwenzio hapa nyumbani.”

    “Mh. Ndio maana ukatanguliza maneno ya kunilaghai mara nakupenda sijui hivi na vile……sawa lakini kumbuka tulikotoka Beda.”

    “Najua tumetoka mbali lakini lazima ujue maisha ni safari na hii ni sehemu ya safari.”

    “Kwa hiyo ikiwa safari unaweza kulifanya lolote linalokufurahisha huku ukiwakera wenzio?”

    “Sio hivyo mpenzi najua unahisi kuwa sitafanya usawa. Naomba uelewe wazi kuwa nitakujali na kukuthamini.”

    “Ndio najua utanithamini kwani dalili si nimeanza kuziona, umelala nje siku tatu bila taarifa nafikiri ndio thamani unayoikusudia.”

    Inspekta akainamisha kichwa kwa hasira.

    Vick akaenda kwa mama Beda na kumsimulia mawazo ya mwanawe. Mama Beda huku akiwa mwenye hasira aliamua kumwita mwanawe na kumkalisha.

    “Mwanangu Beda, naomba ukae unisikilize…”Aliongea mama Beda mbele ya mwanae na Vick.

    “Hii dunia mwanangu…..”

    “Ongea basi mama si unanichanganya tu. Hii dunia kuna asiyeijua?” Alikuja juu Beda bila kujua anayeongea naye ni mama yake.

    “Mwanangu mimi mama yako hutakiwi kunijibu hivyo.”

    “Kama unaongea upuuzi lazima nikujibu vibaya lazima ujue kuwa wewe ni mama yangu una mipaka yako najua sana Vick kakusimulia kila kitu na hayo ni maamuzi yangu kama hataki huyo Vick aondoke aniachie nyumba yangu hajachangia hata shilingi.” Aliongea Inspekta Beda kwa hasira.

    “Mwanangu mbona umebadilika.”

    “Mama, kama umechoka kukaa hapa ndani na wewe ondoka, sikujua kama mama yangu ni mkorofi kiasi hiki kumbe ndio maana ulikuwa uligombana na majirani kipindi kile na inawezekana kuna ukweli wewe ndio umesababisha kifo cha baba yangu.”

    “Mwanangu maneno gani hayo unaniambia?” Aliuliza mama Beda huku akianza kutokwa machozi. Bila kujali Beda akaendelea kumshushia mvua ya maneno yaliyomtia uchungu.

    Mama Beda akashindwa kuvumilia maneno yalikuwa makali sana. Akaanza kulia huku akirudiwa na kumbukumbu za kipindi cha maisha magumu alichomlea Beda. Ikawa zamu ya Vick kumbembeleza mama Beda. Beda alikuwa amebadilika sana.



    * * *

    “Vipi dear umefanikisha.” Aliuliza Mama Lucy huku akimrembulia macho Beda.

    “Amekataa tena hata mama amekataa.” Alijibu Beda huku akikuna kichwa.

    “Kina mama si watu wa kuwasikiliza sana kwani umri wao unawafanya wawe hivyo.”

    “Nimemfokea sana nimemwambia aache kuingilia mambo yangu.”

    “Wewe ndio mwanaume bwana, askari unatakiwa kuwa mkakamavu hata nyumbani kwako.” Aliendelea kusisitiza Mama Lucy.

    “Kwa hiyo tujiandae kuhamia huko?”

    “Eeh. Weka kila kitu sawa siku ikifika tunakuja kukusanya na kupeleka nyumbani.” Alisisitiza Beda huku akionyesha wazi kufurahia.

    “Ndiyo maana nakupenda ooh, kumbe unanijali mpenzi.” Aliongea mama Lucy huku akimkumbatia na kumpiga busu la kinafiki Beda.

    “Nisubiri mpenzi natoka kidogo.” Alisikika mama Lucy huku akitoka mle chumbani.

    Akaenda moja kwa moja chumbani kwa Lucy na Koku, wote wawili walikuwa wanasoma shule ya sekondari ya Jangwani. Watoto wa mama Lucy wote watatu walikuwa wa baba tofauti huku kukiwa hakuna uhakika kuhusu baba wa watoto wale. Isingeweza kusahaulika jinsi mama Lucy alivyogonganisha wanaume wawili huku kila mmoja akifahamu kuwa yeye ndiye baba wa Lucy, baada ya kufahamiana wale wanaume hawakuwa na sababu ya kugombana kila mmoja akaingia njia yake huku wakimwachia mama Lucy jukumu la kumlea mwanae peke yake.

    Ni huyu mama Lucy ambaye kwa tamaa yake ya fedha alithubutu kumuua baba wa kifungua mimba wake Fredi kwa matumaini ya kurithi mali zake, hakuamini pale alipowaona ndugu wakija na kuuza nyumba baada ya kufuatilia ikabainika kuwa ile nyumba haikuwa ya mumewe ilikuwa ni ya mama yake mdogo mumewe, akakosa vyote.

    Huyu ndiye mama Lucy ambaye historia yake imejaa machafu huku mikono yake ikiwa na damu ya baba Fredi. Mtoto wake wa mwisho alikuwa hajulikani kabisa baba yake. Aibu.

    “Lucy…lucy…” Aliita mama Lucy alipofika mlangoni.

    “Bee mama.” Aliitika Lucy huku akishtushwa na ujio huo wa mama yake kwani ilikuwa saa nane usiku. Lucy akasogea mlangoni na kuanza kuongea na mama yake.

    “Mwanangu hili bwege limekubali kunihamishia nyumbani kwake, kesho mwambieni kaka yenu arudishe chumba kwani tumepata sehemu ya kula.” Lucy akatabasamu huku akipeana mkono na mama yake.

    “Poa mama.” Alisikika Lucy huku akirudi chumbani.



    * * *



    Baada ya mwezi mmoja Vick alianza kuhisi dalili za uja uzito. Hali hiyo ilimsumbua sana kwani hakupata mapenzi yaliyotakiwa kutoka kwa mumewe. Ni siku hii ambayo ilikuwa pigo lisiloweza kusahaulika katika maisha ya Vick. Akiwa amekaa barazani na mama Beda Akaliona lori kubwa likifika pale nyumbani kwao. Inspekta Beda aliteremka akiongozana na mwanamke mweupe.

    “Mama Vero. Nafikiri nilikueleza mapema kuwa kuna mwenzako anakuja hapa….” Vero hakuweza kumaliza kusikiliza ile kauli akaangua kilio kikubwa ambacho hata hivyo kwa Beda ilikuwa kama kumpigia mbuzi gitaa. Mama Beda hakuongea kitu aliogopa sana matusi ya mwanae. Akawa anatazama kila linalotendeka kwa uchungu mkubwa. Vyombo vya Vick vikahamishwa na kuwekwa chumba cha uani. Ilikuwa ni dharau kubwa kabisa. Hata Vero alilia akaambulia makofi mawili matatu kutoka kwa baba yake.

    Furaha ilipotea kabisa ndani ya familia hii baada ya kuhamia mwanamke huyu ambaye alionekana wazi kuwa mshari.

    Kadri miezi ilivyozidi kusonga mbele ndivyo mama Beda alivyoendelea kukosa uvumilivu. Alianza kupata upya mateso ambayo alishayasahau. Kila alipokumbuka shida alizozipata ili mwanae asome machozi yalimtoka. Hali yake kiafya ikaanza kubadilika. Mara kwa mara alisumbuliwa na tatizo la kifua na malaria. Beda hakuwa na muda wa kujua afya ya mama yake wala Vick ambaye alikuwa mjamzito.

    Siku za kujifungua zikafika. Vick akajifungua salama mtoto wa kike ambaye aliitwa Sara. Bado Beda hakuonyesha mapenzi yoyote. Mara nyingi aliacha fedha za matumizi bila hata kumuona mtoto.

    Watoto wa yule mama wakahamia pale nyumbani kwa Beda. Toka wahamie wale watoto chuki ikazidi. Ajabu. Beda akaonyesha mapenzi makubwa kwa wale watoto kuliko Vero ambaye ni mtoto wake wa kumzaa.



    * * *



    Ingawa alikuwa mdogo lakini alikuwa na uwezo wa kuelewa mambo. Vero alikuwa akiliona kila lililokuwa linatendeka. Mara nyingi wale watoto watatu walipenda kukaa faragha na mama yao. Hali hii ilisababisha Vero aanze mtindo wa kuwavizia na kuwasikiliza kwa siri walichokuwa wananong’ona. Mara nyingi alikuwa anamfikishia mama yake. Mengi yalikuwa ni maneno mabaya na ya kashfa.

    Mama Beda alishachoka mazingira ya pale akanong’ona kitu na Vick kisha akabeba mizigo yake akaondoka pale nyumbani. Hali yake ya kiafya haikuwa nzuri lakini alilazimika kuondoka. Akaenda alikokujua yeye na Vick ambaye alimuaga. Alishindwa kwa sababu alikuwa anafanyiwa vitimbi vya chini chini na mwanamke aliyemleta Beda. Kilichomkera zaidi ni kuhisi kudhalilika kwani kiumri alihisi kutotofautiana sana na yule mwanamke. Labda tofauti ni mfumo wa kulazimisha ujana kwa kutumia vipodozi ndio uliomfanya mama Lucy aonekane kama msichana.



    Ajabu. Kuondoka kwa mama yake bado hakukumzindua Beda. Mara nyingi alifurahia maisha na mama Lucy kwa vinywaji na starehe mbalimbali. Ilikuwa ni kawaida yake kwenda kwenye baa maarufu na sehemu nyinginezo zilizosifika kwa starehe.

    Siku moja Vero alipita karibu na chumba alichokuwa analala Koku na Lucy akawasikia wakinong’ona na mama yao.

    “Kwa hiyo itakuwaje?”Alisikia sauti ya Koku ikiuliza.

    “Tumemwagiza Fred akanunue ile sumu kisha tutamwekea yule mama, tukizubaa atatuzidi kete.”

    “Eee. Dunia yenyewe tunatakiwa kuchangamka tukilaza damu yule mama atatusumbua baadaye si unaona anazidi kuongeza vitoto hapa.” Alilalamika Lucy.

    Kauli ile ilimchanganya kidogo Vero lakini kutokana na utoto akajikuta akiipuuza.

    Siku zikakatika, hatimaye ikafika ile siku mbaya kuliko zote. Mama Vero alikuwa anaoga bafuni. Aliporudi akafunua ndoo yake ya maji ya kunywa. Alipokunywa tu akaanza kuhisi tofauti. Hali ilikuwa mbaya. Inspekta Beda alipofika bado hakumjali. Kama alivyofanya mama Beda, naye akaamua kuondoka pale ndani. Akatoroka na mwanae Vero na Sara ambaye alikuwa na umri wa miezi miwili tu. Lakini wakati anatoroka alikuwa anasumbuliwa na tumbo ambalo alihisi kuwa ni sumu baada ya kudokezwa na Vero wakati tukio limeshatokea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog