Search This Blog

Sunday 19 June 2022

NILIUA KWA KUKUSUDIA - 5

 





    Simulizi : Niliua Kwa Kukusudia

    Sehemu Ya Tano (5)



    Nilishituka na kusogea pembeni kidogo ambapo nilianza kuchungulia kwa umakini ili kujua ni nani aliyekuwa ndani ya gari hilo.

    Nikiwa naendelea kusumbua ubongo wangu juu ya hilo, ghafla niliona kioo cha upande wa dereva kikianza kushuka taratibu, nikatoa macho nikiwa na hamu ya kujua ni nani aliyekuwa ndani. Bila kutarajia alishuka yule mdogo wake na Elhakimu aliyekuwa akiishi na mdogo wangu Inana. "Habari za kwako?" alinisabahi huku akionesha uso wa uchangamfu wa hali ya juu. Sikumjibu kwa furaha kama siku zote, hali iliyomlazimu ashuke haraka ndani ya gari na kuja hadi nilipokuwa nimesimama. Akaanza kuniangalia kuanzia miguuni hadi utosini mwa kichwa na kushusha tena macho taratibu huku akionesha dalili zote za kunishangaa. "Vipi Tunu, kulikoni?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana, niko sawa na mdogo wangu anaendeleaje?"

    "Anaendelea salama, lakini ni kama una tatizo, naweza kukusaidia tafadhali!"

    "Aah, hapana lakini naomba ukifika nyumbani umwambie kuwa namhitaji aje kwangu, sawa?"

    "Sawa lakini chukua hii kama nauli maana jua linaanza kuwa la utosi sasa," alisema Ashraf ndipo nikagundua wazi kwamba hakuwa akijua unyama alionitendea kaka yake Elhakimu.
    Akaingiza mkono mfukoni na kutoa pochi lake la kutunzia fedha, haraka akatumbukiza mkono na kutoa noti nyekundu kama tano hivi.

    Baada ya kunipa akarejea kwenye gari lake akaondoka huku akiniacha nikiwa nimesimama wima.

    Japo hapakuwa mbali sana na mahali nilipokuwa nikiishi, Ashraf hakulijua hilo, nikajikongoja kuelekea nyumbani kwangu.
    Maumivu yalikuwa ni makali ambapo licha ya kupewa dawa nyingi zikiwemo zile za kuzuia maambukizi lakini niliendelea kupata maumivu makali sehemu zangu za siri na kiunoni.

    Kadiri maumivu yalivyozidi kushamiri kila nilipokuwa nikipiga hatua, ndivyo chuki dhidi ya Elhakimu zikazidi kunipanda, kwa mara ya kwanza maishani mwangu nikatamani kulipiza kisasi kwa kuua!
    Yalikuwa ni mawazo mabaya mno kwa mtoto wa kike tena binti mdogo kama mimi kuyawaza, lakini sikuwa na jinsi, hakika nikajikuta nikidhamiria kuua japo hadi wakati huu sikujua nitaua kwa njia gani.

    "Lakini kwani lazima uue, hakuna njia nyingine ya kulipiza kisasi tofauti na kuua," nilisikia sauti ikijirudia nafsini mwangu. Nikazidi kubaki njia panda.
    Wakati nausogelea mlango, ghafla sauti ya marehemu mama yangu ikaanza kusikika moyoni.

    "Hakika usilipize baya kwa baya, siku zote epuka maisha ya visasi kwa wakukoseao, kamwe usilipe kisasi kwa yoyote akutendeaye kosa, hata kama ni kubwa namna gani," ilikuwa ni sauti ya mama ikijirudia kwa kasi ya umeme, maneno ambayo alipenda kuniambia mara kwa mara enzi za uhai wake.
    "Hapana mama, kwa hili utanisamehe, siwezi kuacha kulipiza kisasi kwa mtu kama Elhakimu, hapana mama, nisamehe mama yangu popote ulipo, lazima nilipe uovu huu, tena kwa sasa natamani kuua, nisamehe mama, hata Allah anisamehe kwa hili. "Kwani si uliamua kutegemea sheria, subiri akamatwe na haki yako itapatikana ndipo sheria ichukue mkondo wake, kuliko hiyo hatua mbaya ya kuua unayotaka kuichukua," sauti nafsini mwangu ikazidi kuchukua nafasi kubwa. Nilikuwa katika wakati mgumu na mbaya mno. Kwa hapa naomba niweke wazi kitu kimoja kabla sijaendelea na simulizi hii ya kuumiza.

    Maumivi juu ya tukio hilo la kubakwa na Elhakimu yalikuwa ni mara mbili, mosi alikuwa amenivunjia malengo yangu ambayo nilikuwa nimejiwekea kuwa ni lazima mume wangu aikute heshima yake ya ndoa. Lazima awe wa kwanza kukipasua kikombe changu, sasa ndoto na malengo hayo yalikuwa yamefutwa na Elhakimu. Hakika nilimchukia kuliko kiumbe chochote kinachoishi chini ya jua.
    Pili, sikuwahi kufikiri kama kuna siku nitadhalilishwa kama alivyonitendea Elhakimu, hakika moyo wangu ulikuwa umejawa na maumivu makali yasiyosimulika kwa maneno wala maandishi. Mateso, maumivu, simanzi, huzuni na masononeko yalikuwa ni sehemu ya maisha yangu kwa wakati huo, hakika sikujua ni kwa nini Elhakimu ambaye nilimheshimu na kumchukulia kama mzazi wangu alifikia hatua ya kunifanyia unyama ule bila ya chembe ya huruma. "Lazima niue," nilijikuta nikitamka maneno hayo kwa sauti ya juu.



    Nilitamka maneno hayo nikiwa katika lindi la mawazo. Sikuona kabisa thamani ya kuwepo kwangu chini ya jua. Moyoni nikajiona ni kiumbe mwenye bahati mbaya kuliko viumbe vyote vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu.



    Taratibu nikajilaza kitandani na kuendelea kuwaza juu ya maisha yangu, hadi wakati huo sikujua nini hatima yangu hapa duniani. Nikaendelea kulia kwa maumivu hadi nilipopitiwa na usingizi. Jioni nilienda bafuni na baada ya kuoga nikabadili nguo na kuandaa chakula.

    Kabla ya kulala nilikunywa dawa nilizoandikiwa na daktari za kuondoa maumivu na kuzuia maambukizi zaidi. Baada ya kunywa dawa, nilimshukuru Mungu kwa kunilinda na kunipitisha salama kutwa nzima ya siku hiyo. Ingawa niliamini Mungu aliruhusu majanga yote hayo yaendelee kunizonga maishani mwangu, bado sikukata tamaa ya kumuomba kila siku na kila wakati kama marehemu mama yangu alivyokuwa akituagiza kila mara kuwa kumtegemea Mungu ni chanzo cha maarifa na ndiye nguzo muhimu maishani.

    Nilichutama na kupiga magoti ambapo nilianza kuomba dua kwa Mungu ya kumtaka anilinde na malimwengu wakati wa usingizi. Nilipomaliza kuomba, nilivua nguo zote na kubakiza ya ndani tu. Nikapanda kitandani na kuchukua shuka langu zito. Kabla sijajifunika, nilipata wazo la kujikagua sehemu zangu za siri, bado kulikuwa na bandeji ambazo daktari alikuwa amenifunga pamoja na dawa. Machozi yakanitoka mfululizo, machungu niliyokuwa nayo yakaongezeka maradufu.

    Haraka nikakurupuka kitandani na kukaa kitako huku nikiwa nimeshika shuka langu mkononi. Licha ya kupulizwa na kijiupepo cha feni, jasho jembamba la hasira lilikuwa nikinitoka! Hakika nilikuwa na hasira isiyoweza kusimulika kwa urahisi.

    Niliendelea kukaa kitandani nikiwaza na kuwazua mambo kadha wa kadha. Mawazoni nilimuona Elhakimu amesimama mbele yangu. Hasira zikazidi kunipanda na kutaka kufanya jambo ambalo hakika sikuwahi kuliwaza maishani mwangu. Kuua!

    Lakini yalikuwa ni mawazo tu ambayo hayakuwa na ukweli wowote. Moyoni nilitamani iwe kweli ili niweze kulipiza kisasi cha maumivu niliyokuwa nayo dhidi ya Elhakimu.

    Nikaamua kujilaza na kujifunika kwa shuka gubigubi hadi kichwani. Sikupata usingizi kwa haraka kwani mawazo mengi yalikuwa yakikinzana ubongoni mwangu. Sikujua nililala saa ngapi kwa usiku huo lakini nilishtuka na kudamka tayari ikiwa ni saa mbili kasoro robo asubuhi.

    Nikakumbuka kuwa nilitakiwa kufika kituo cha polisi kwa ajili ya mwendelezo wa kesi yangu dhidi ya Elhakimu. Moyoni nikapuuzia baada ya kukumbuka yale maneno ya kukatisha tamaa ambayo niliambiwa na yule mkuu wa kituo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini nikaamua kwenda kujua nini kitajiri ingawa moyoni nilikwishaanza kukata tamaa na kupunguza matumaini ya kumtia nguvuni Elhakimu. Maisha yakuwa yamenielemea sana.

    Nikaamka kivivu na kwenda moja kwa moja kuchota maji na kuingia bafuni kwa ajili ya usafi. Nikabadili nguo na kuandaa chai pamoja na kitafunwa. Nilipomaliza kunywa chai, nikameza dawa na kuanza safari ya kuelekea kituoni.

    Njiani nilitembea kwa mwendo wa taratibu licha ya maumivu kupungua lakini sikuweza kujiachia. Wakati mwingine nililazimika kupumzika ili kupunguza maumivu.

    Maumivu yalipopungua nikaendelea na safari lakini kabla ya kufika kituoni, nilishtuka nikiguswa begani na nilipogeuka alikuwa ni mdogo wangu Inana. Furaha ikanijia kwa kasi na kusalimiana na Inana kwa kukumbatiana. Nikamuomba tukae mahali ili nimsimulie yaliyojiri kati yangu na Elhakimu.

    "Bosi aliniambia kuwa mlikutana lakini ukiwa na hali isiyokuwa ya kawaida, kulikoni Tunu?" Inana alifungua uwanja wa mazungumzo kabla sijaanza kumjuza kisa changu.

    "Ni kweli Inana, sikuwa sawa kwani nina matatizo makubwa mno mdogo wangu."

    "Matatizo gani tena dada yangu jamani?" Inana aliuliza huku akinikazia macho kwa shauku kubwa ya kutaka kujua kilichonisibu.

    "Elhakimu alinibaka na kunitupa mtaroni."

    "Unasemaje wewe?" Inana aliuliza huku machozi yakitengeneza mifereji machoni mwake.




    Kufumba na kufumbua machozi yakaanza kumtiririka Inana. Nilipoona hivyo, machungu yakanishika nami nikajikuta nikianza kulia. Tulilia kwa uchungu mkubwa huku tukimuuliza Mungu kulikoni aendelee kuruhusu matatizo yazidi kutuandama.

    "Kwa nini sisi Mungu, kwa nini jamani?" Inana alilia huku akitamka maneno hayo.

    "Hapana usiseme hivyo Inana, huenda Mungu ana mpango wake kwetu," nilimtia moyo mdogo wangu Inana huku nikiendelea kulia kwa uchungu na maumivu makali yasiyokuwa na kipimo wala kusimulika kwa namna yoyote ile.



    Moyoni niliendelea kuwachukia mno wanaume. Nikaona si viumbe wema hata kidogo. Wakati tukiendelea kulia, ghafla kuna jambo lilinishitua mno na kujikuta nikisitisha kidogo kulia. Kilichonishitua ni kiwango cha kulia alichokuwa akikionesha Inana. Kwani alilia kwa sauti kubwa na kwa muda mrefu mno. Hakika alionesha uchungu mwingi kuliko hata mimi ambaye nilikuwa nimekumbwa na tatizo hilo.

    Ikabidi ninyamaze na kuanza kumbembeleza kwa kumtaka aache kulia kwani kama ni kubakwa tayari nilishabakwa. Na kwa wakati huo nilikuwa nikielekea polisi kudai haki yangu.

    "Hapana dada, kuna jambo limeniuma zaidi," alianza kusimulia Inana kwa sauti ya kitetemeshi iliyoambatana na kwikwi ya hasira.

    "Jambo gani tena Inana zaidi ya hili la kwangu la kubakwa na Elhakimu?," nilimuuliza nikitaka kujua ni jambo gani lililomuumiza zaidi Inana kama alivyokuwa akidai.

    "Samahani kwa kuwa nilikuficha dada, hata mimi huyo Elhakimu alinibaka nyumbani kwa mdogo wake ninapofanya kazi."

    Nilikuwa kama niko ndotoni. Maneno ya Inana nikayachukulia kama ndoto ndefu ambayo kwa hakika niliamini kama ingekoma muda si mrefu na kubaki katika hali yangu ya kihalisia.

    "Ni kweli kabisa dada, Bosi wako Elhakimu alinibaka mwezi mmoja uliopita sasa, lakini niliogopa kukuambia kwani ni jambo la aibu na udhalilishaji wa hali ya juu mno," alisema Inana huku nikizidi kumshangaa kwani sikuwa tayari kabisa kuyaamini maneno yake.

    Kabla sijasonga mbele na simulizi hii, hapa naomba niweke wazi jambo moja muhimu sana.Ukweli ni kwamba hadi sasa nikiwa nasimulia hivi, sijawahi kuisahau siku hiyo kwani ilibadili kabisa mfumo mzima wa maisha yangu. Moyoni nikaanza kujiona kama nimebadilika na kuwa na roho chafu ya kinyama. Nilianza kuhisi harufu ya damu ikinukia kutoka kila pande ya dunia na ulimwengu kwa ujumla.

    Basi ngoja niendelee. Inana akanisimulia mkasa mzima kwa jinsi alivyobakwa na Elhakimu kabla hajanibaka mimi. Akasema siku ya tukio Elhakimu alienda nyumbani kwa mdogo wake aitwaye Ashraf mahali ambako mdogo wangu alikuwa akifanya kazi. Kama utakumbuka ni Elhakimu ndiye alinipa wazo la kumtafutia mfanyakazi Ashraf na kulazimika kumfuata Inana huko Chalinze nilikokuwa nimemuacha akihangaika na vibarua vya kujitafutia riziki.

    Haya ngoja niendelee. Inana alisema kuwa siku hiyo alikuwa peke yake nyumbani ndipo Elhakimu akafika na kuanza kuzungumza naye. Katika mazungumzo yao, Inana alikuwa akishangaa kuona Elhakimu akimsogelea kila sekunde iliyokuwa ikiondoka.

    Inana akaendele kusimulia kuwa, Elhakimu alianza kumshika pasipo ridhaa yake na kuanza kumvua nguo kwa nguvu huku akimwambia maneno ya kimapenzi. Pamoja na kukataa huku akitoa upinzani mkubwa wa kujinasua mikononi mwake, Elhakimua alizidi kutumia nguvu nyingi na hatimaye kufanikisha kumvua nguo zote na kuanza kumwingilia mwilini bila huruma!

    Akaweka wazi kuwa, baada ya tukio hilo Elhakimu aliondoka na kumuacha akiwa hajitambui na damu nyingi zikimtoka lakini alipozinduka na kukuta hakuna mtu, aliamua kujikanda kwa kutumia majani ya mtapei yalitokuwa nyuma ya nyumba hiyo ambapo aliyachemsha. Hata alipokuja bosi wake hakuthubutu kumweleza chochote.

    Akaendelea kuishi kwa taabu na kujifichaficha hadi alipopona kabisa.

    Hadi Inana anamalizia kusimulia mkasa huo wa kubakwa na Elhakimu, sikumbuki vyema machozi yalikuwa yamefika wapi kwani hata macho yalikuwa hayawezi kufumbua vizuri kutokana na kuzidiwa na wingi wa machozi. Haraka nikajikuta nikigairi kwenda kituo cha polisi kuendelea na kesi na kujikuta nikiamua kuchukua uamuzi hatari mno.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Ulikuwa ni uamuzi wa kuua! Kwa dhati kabisa nilikuwa nimedhamiria kuua. Ndiyo, kumuua Elhakimu. Moyo wangu ulijawa na chuki kali mno dhidi yake na hakika sikuona adhabu au kisasi kingine alichostahili mwanaume huyo zaidi ya kifo.



    Nikamwambia Inana turudi nyumbani kwani nahitaji zaidi muda wa kupumzika. Akili yangu ikawa inawaza ni kwa jinsi gani nitaweza kuikamilisha kazi iliyokuwa mbele yangu. Kazi ya kumwaga damu. Damu ya Elhakimu.



    Tulirudi na Inana hadi nyumbani kwangu. Tulipofika nikajilaza kitandani kwangu huku machozi yakinitiririka kimyakimya. Hata Inana alikuwa akilia japo awamu hii si kwa sauti ya juu kama alivyoanza mwanzo. Tulikuwa katika wakati mgumu mno maishani. Maumivu na mateso yalishakuwa sehemu kubwa ya maisha yetu na kamwe hatukuona kama kuna siku tutakuja kupata faraja na kuyafurahia maisha kama wengine.



    "Dada, mimi naamini haya ni majaribu na mapito ya muda tu. Kwa sasa Tunapita kwenye tabu na mateso lakini yote ni kwa sababu Mungu ana mpango maalum na sisi," alisema Inana huku akiniangalia machoni kwa uso uliomaanisha kile alichokuwa akikisema.

    Kauli yake ikanifanya ninyamaze. Inana alikuwa akizungumza kwa busara na hekima ya hali ya juu mno ukilinganisha na umri aliokuwa nao.



    "Kwani baada ya tukio la kukubaka uliendelea kufanya kazi hotelini kwake?" Inana aliniuliza.

    "Hapana, tangu siku hiyo sijarudi tena hotelini kwake na sitaki kabisa, kama ni kufa na njaa nitakufa lakini kwa sasa ninachofikiria ni kumwaga damu yake."

    "Haaa! Wewe dada Tunu wewe!" Inana alihamaki kwani sikuwahi kumtamkia kuwa nilikuwa na mpango wa kumuua Elhakimu.

    "Mbona unashtuka sana Inana?"

    "Si ulivyosema kuwa unatamani kumwaga damu ya Elhakimu."

    "Ndiyo, lazima nimuue huyu mwanaharamu."

    "Siyo vizuri dada," Inana alianza kunisihi nisiendelee na mpango wa kuua.

    Pamoja na jitihada zote za Inana, hakuweza kufanikisha kuondoa mpango uliokuwa umeota mizizi moyoni mwangu kwa wakati huo. Moyo wangu ungefurahi endapo nigeona damu ya Elhakimu ikimwagika kupitia mikononi mwangu.

    Inana alikaa nyumbani kwangu hadi jioni ambapo aliondoka na kuniacha nikiwa nimejilaza. Akasema angerudi baada ya siku mbili ili kuja kunijulia hali japo na yeye alikuwa hajapona sana.

    ****

    Majuma machache baadaye, hali yangu ilikuwa imeimarika kwa kiwango cha kuridhisha. Moyoni nilikuwa bado na maumivu makali mno dhidi ya kitendo cha kinyama nilichofanyiwa na Elhakimu.

    "Lazima nitimize nilichodhamiria, lazima kesho nimwage damu ya Elhakimu," nilikuwa nikiwaza usiku huo wakati nikiwa kitandani nikiusaka usingizi kwa nguvu. Mpango wa kuondoa roho ya Elhakimu sasa ulikuwa unaelekea kutimia.



    Nililala hadi asubuhi ambapo nilijiandaa kwa kuoga. Nikavaa nguo nzuri. Nilipita sokoni ambapo nilinunua kisu kikali, kirefu na chenye ncha kali sana huku kikimeremeta. Nikakiweka kwenye mfuko maalum na kukibeba kwa uangalifu wa hali ya juu.



    Nikatembea hadi mahali walipokuwa wakipaki bodaboda. Nikakodisha mojawapo na kumwambia mwendeshaji anipeleke Mikocheni, mahali alipokuwa akiishi Elhakimu. Moyoni nilikuwa nikiwaza mambo ambayo hakika yalikuwa yakimchukiza Mungu kwa kiwango cha juu mno.



    Njiani nilikuwa nikimhimiza mara kwa mara dereva bodaboda aongeze mwendo kwani nilikuwa na haraka isiyokuwa na kifani. Mahali palipokuwa na msongamano mwingi na foleni ndefu ya magari na pikipiki, nilichukia mno.



    Tulipofika, nikamlipa bodaboda ujira wake. Akaondoka nami nikatembea hadi nyumbani kwa Elhakimu. Kwa kuwa haikuwa mara yangu ya kwanza kufika, mlinzi wake hakunitilia shaka. Aliponiruhusu nikaenda moja kwa moja hadi sebuleni na kumkuta Elhakimu akiwa amekaa kwenye kochi huku akisinzia.



    Mbele yake kulikuwa na meza ndogo ambayo kwa juu kulikuwa na bastola ambayo aliwahi kunionesha ofisini kwake. Nikiwa na hasira kali huku mikono na midomo ikinitetemeka, niliichukua ile bastola na kumwangalizia Elhakimu. Nikaanza kuhesabu moja, mbili hadi tatu.




    ila kusita nikammiminia kwa hasira risasi kadhaa mwilini mwake. Risasi ya kwanza nilihakikisha inapenya na kuharibu sehemu zake za siri kama adhabu ya kuzitumia sehemu hizo vibaya kutunyanyasa kijinsia mimi na mdogo wangu Inana. Risasi ya pili nilihakikisha inatua katika paji la uso wake nikilenga kuuadabisha ubongo wake kwa kuthubutu kuwaza kutubaka. Baada ya kutekeleza unyama huo, ghafla hasira zangu ziliyeyuka.



    Nikaanza kuingiwa na hofu kuu kutokana na mauaji niliyoyafanya ambayo sikuwahi kuyafikiria. Kuna wakati nikiwa nimeishika ile bastola baada ya kumpiga risasi mbili, nilihisi nimefanya maamuzi sahihi hasa baada ya kukumbuka unyama alionifanyia lakini baada ya muda tena nikajiwa na mawazo kwamba nimechukua uamuzi mbaya ambao utaniharibia kabisa maisha yangu. "Potelea mbali," nilijikuta nikitamka maneno hayo na kuitupa ile bastola chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kuangalia chini, nilitoka kwa kukimbia kuelekea nje ya nyumba ya Elhakimu ambaye kwa wakati huo nilikuwa na uhakika kuwa tayari ni mmoja kati ya wafu waliopokelewa kuzimu siku hiyo. Kabla sijafika mlangoni, nilijikuta nikiwekwa chini ya ulinzi na askari polisi wakiongozwa na yule mlinzi wa Elhakimu ambaye nilikuwa na uhakika alisikia milio ya risasi wakati namuua bosi wake hivyo kuamua kuniitia polisi.



    Kutokana na idadi ya polisi waliofika, sikuwa na ujanja, nilikuwa mpole nikijua fika kuwa hakuna cha kunifanya niwe huru kutokana na tukio lile la mauaji. Siku hiyo kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilipelekwa kituo cha polisi kama mtuhumiwa, mikononi mwangu nikiwa na pingu huku askari wakiwa pembeni na nyuma yangu, wawili wakiwa wameshikilia bastola.



    Baada ya kufika kituoni nilichukuliwa maelezo kuhusiana na tukio hilo ambapo nilikataa katakata kuwa sikuua jambo ambalo liliwachukiza polisi wale waliokuwa na uhakika kuwa nilihusika kwa asilimia mia moja na mauaji ya Elhakimu. Bila kupoteza muda waliniingiza ndani ya selo nikiwa navuja jasho huku nikionekana kama niliyechanganyikiwa.



    Nililala mpaka siku iliyofuata ambapo mdogo wangu Inana alikuja kuniona na kuniletea chakula. Sikuwahi kumuona Inana akiwa katika hali hiyo kabla kwani uso wake ulikuwa mwekundu ajabu. Macho yake yalikuwa na rangi ya manjano kuonyonesha kwamba alilia kwa muda mrefu kabla ya machozi kukauka.



    "Dada, hata siamini! Siyo wewe wamekusingizia tu. Wewe siyo muuaji dada, niamini haya nisemayo," aliniambia mdogo wangu Inana huku akiangua kilio kikubwa palepale kituoni. Bila kujali kwa pamoja tukaanza kulia wote huku nafsi yangu ikinisuta kwa maneno ya mdogo wangu ambaye kwa wakati huo hakuamini kabisa kama ningeweza kufanya unyama ule.



    Kilio chetu kilibadilika na kuanza kuwakera mahabusu wenzangu, ikabidi polisi wamtake mdogo wangu aondoke mara moja kituoni hapo jambo ambalo alilifanya japo kwa uzito. Siku moja kabla ya kesi yangu kutajwa, kaka mmoja aliyejitambulisha kama wakili wangu alikuja kunitembelea gerezani na kunitaka nimsimulie kila kitu kilichotokea na uhusika wangu katika mauaji ya Elhakimu.



    Kwa kuwa nafsi yangu ilikuwa imeanza kujutia yote niliyoyafanya, nikamuelezea mwanzo hadi mwisho bila kuficha jambo lolote ili yeye ajue kama ni kunisaidia, ananisaidiaje. "Pole sana kwa yaliyokukuta, lakini naomba nikuambie kwamba, usije ukathubutu kukubali kuwa umeua na kusimulia ukweli wote huo mbele ya



    hakimu," aliniambia wakili huyo kwa msisitizo na kuahidi kuwa atatumia taaluma yake ya sheria kuhakikisha kuwa siingii hatiani.

    "Sawa kaka," nilimjibu wakili huyo, tukaagana na kurudishwa selo. Nikiwa mle selo watuhumiwa wenzangu walikuwa na shauku ya kujua nilikuwa nimefanya kosa gani hadi kufikishwa pale kituoni huku nikiwa binti mdogo. Mmoja wao ambaye alionekana alikuwa na cheo mle selo, aliniita na kuniuliza nilifanya kosa gani lililonifanya niwe pale




    We binti kwani umefanya kosa gani?" aliniuliza mama huyo huku wafungwa wengine wakinisogelea kwa shauku ya kutaka kujua kilichonikuta mpaka nikawa pale.

    "Nimeua!" nilijikuta nikisema maneno hayo kwa kukaza meno, lakini kilichonishangaza ni kitendo cha kila mmoja kuanza kucheka kwa dharau wakiamini kuwa kwa muonekano wangu nisingeweza kuua hata panya sembuse kuua mtu!



    Kwa vicheko vile, moyo wangu ulizidi kupata simanzi. Nilitambua fika kuwa kweli sikupaswa kuwa mahali pale, tena kama muuaji kwa kuwa hata muonekano wa sura yangu ulikuwa ni wa upole mno.

    Niliinamisha uso wangu kwa muda kidogo kisha nikainua macho yangu na kuanza kuwasimulia bila kuficha mkasa mzima uliosababisha mimi kuua.

    Nilipomaliza kusimulia kila mmoja alinionea huruma na kuniunga mkono kwa kitendo nilichokifanya japo wengine walipinga na kusema kuwa nilifanya jambo hilo kwa kukurupuka na kuwa ningelijutia baadaye.

    "Ndiyo hivyo tena umeshakuwa mfungwa, sasa ndo umepata nini? Binti mdogo umejiharibia maisha yako yote kwa hasira za mkizi.



    "

    Tulaleni jamani kila siku stori mpya leo huyu kesho atakuja mwingine utasikia kamuua mume wake kisa mali," alisema mfungwa mmoja kati ya wafungwa wale walionizunguka kisha kila mmoja akatawanyika na kwenda kulala kwenye kigunia chake alichokitandika sakafuni.

    Yule mfungwa aliyeonekana kuwa na cheo zaidi pale ndani alinitupia kipande cha gunia na kunionesha kisehemu cha kulala pale sakafuni. Huwezi amini kwa jumla tulikuwa kama watu kumi na sita hivi sote tukiwa tumelala chini tena kwa kubanana sana kiasi kwamba ukilala upande mmoja basi ni huohuo mpaka asubuhi.



    Usiku mzima nilikesha nikifikiria juu ya hatima yangu kwa kuwa hata kama nitakwepa adhabu ya kunyongwa hadi kufa, basi sitaepuka kifungo cha maisha.

    ***

    Kwa kuwa uchunguzi wa kesi yangu ulimalizika mapema, siku chache tu zilizofuatia mimi na mahabusu wachache niliowakuta gerezani, tulipandishwa kwenye gari la magereza na kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yetu na wengine kusikiliza hukumu zao.

    Njiani niliwaza mambo mengi sana hadi kichwa kikaniuma. Ukweli ni kwamba japokuwa nilimuua Elhakim, lakini bado kila nilipofumba macho nikijitahidi kufuta kumbukumbu ya ile siku aliyonibaka, nilishindwa kabisa.

    Kuna wakati nilihisi huenda adhabu ya kifo niliyompa Elhakimu ilikuwa haitoshi hata kidogo. Nikajiapiza kuwa hata kama nitafungwa lakini nilitaka kesi yangu iwe somo kwa wanaume wote wenye tabia kama za Elhakim, nikaona ni vyema nisikanushe mashitaka yangu kama nilivyoambiwa na wakili wangu.

    Dhamira yangu ilinituma kukubali kuwa niliua.

    Gari letu lilipofika mahakamani tulishushwa harakaharaka na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba maalum huku mmoja baada ya mwingine alikuwa akiitwa na kesi yake kusikilizwa.

    Tukiwa katika chumba hicho tuliweza kusikia sauti za wenzetu wachache wakifurahi na ndugu zao kwa kuachiwa huru baada ya hukumu huku mara kadhaa tukisikia vilio ambavyo mara moja tulitambua kuwa kuna mwenzetu alihukumiwa jambo ambalo lilinitia woga.



    "

    Tunu Ramadhani!" liliitwa jina langu na askari mmoja wa kike ambaye alikuja kufungua chumba tulichokuwemo na kunifungua pingu kisha kunipeleka kwenye chumba cha mahakama kila kona nikiwa nimezungukwa na askari.

    Nikiwa kizimbani niliweza kumuona mdogo wangu Inana ambaye machozi yalikuwa yakimtiririka kama mvua. Kwa upande mwingine niliwaona ndugu wa Elhakim walioonesha chuki ya wazi juu yangu jambo ambalo lilizidi kunitia hofu. Kwa kifupi, chumba cha mahakama kilikuwa kimejaa watu wengi sana ambao wote walivutika kujua nini hatima yangu.

    Nikiwa nimezama katika ulimwengu wa majuto, sikuwa na nafasi ya kutazama kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Nilijikuta nikishtuliwa na wakili wangu aliyenitaka nisimame ili jaji aingie mahakamani jambo ambalo nililifanya.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kupoteza muda, jaji alichukua faili langu na kulisoma kwa muda kisha akaniuliza huku akinitazama kupitia sehemu ya juu ya miwani yake aliyoishusha mpaka puani.

    "Tunu, mnamo tarehe 2, Machi ulimuua kwa bastola bwana Elhakim, unakubali au unakataa?"

    Niliinua macho yangu na kumtazama wakili wangu ambaye kwa wakati huo alikuwa akiniminyia jicho kunikumbusha nikatae kwa kusema sikuua ili kesi iaharishwe kama tulivyopanga jana yake.

    Tofauti na tulivyokubaliana, nilijikuta nikikubali huku machozi yakinitoka kwa hofu na aibu kiasi kwamba nilishindwa hata kumtazama mdogo wangu.

    "Nakubali," nilipomaliza kusema hivyo ghafla nilishuhudia mdogo wangu akidondoka kama gunia palepale alipokaa, lakini kabla jaji hajachukua hatua yoyote msichana mmoja alisimama.

    "Hapana jaji huyo hakuhusika na mauaji yoyote, mimi ndiye niliyemuua Elhakim," alisema msichana huyo kwa kujiamini huku akisogelea kizimba.


     Nikiwa gerezani, nilijiuliza yule msichana aliyeamua kujitwika kesi yangu alitokea wapi na lengo lake lilikuwa ni nini? Sikupata majibu.



    SIKU hiyo ilikuwa ndefu sana kwangu kwa sababu kila nilipojitahidi kuyafumba macho ili kuutafuta usingizi nilishindwa.



    Bado sehemu ndogo ya moyo wangu haikufurahia hata kidogo na wazo la mimi kutokuwa mtu pekee niliyemuua Elhakim. Nadhani hiyo ilitokana na kisasi kikubwa nilichokuwa nacho kwa muda mrefu dhidi ya Elhakim aliyetubaka mimi na mdogo wangu.

    Siku iliyofuata kabla ya kupandishwa kizimbani, wakili wangu alinifuata kwa ukali akijaribu



    kunionya hasa baada kutofuata ushauri wake alionipa kuwa nisikubali mbele ya Jaji Athumani kuwa nilimuua Elhakim.



    "Una bahati sana! Kama asingekuwa yule msichana usingeniona tena nikikusaidia katika kesi yako," alisema wakili wangu kwa ukali, akaendelea: Ripoti ya vidhibiti na uchunguzi wa maiti ya Elhakim (postmortem) imetoka leo asubuhi.



    Nilipewa ruhusa maalumu ya kuvipitia, unajua nini nilichokigundua?" Wakili wangu aliniuliza swali ambalo nilijua halikuwa lazima kulijibu japo nilikuwa nikitamani kujua nini alichokiona.



    "Umegundua nini?"

    "Ripoti ya alama za vidole katika ile bastola zinaendana kwa asilimia mia moja na vyako. Pia bastola ile ilionekana kutumika dakika chache mara baada ya wewe kukamatwa hivyo kwa mambo hayo mawili wewe ndiye mtuhumiwa namba moja. Siamini hata kidogo kama yule dada aliyejiita muuaji, aliua."



    Kabla sijazungumza chochote, karani mmoja wa mahakama alikuja mpaka nje ya chumba nilichowekwa akiwa na askari wa mahakama na kututaarifu kuwa muda wa kesi yangu ulikuwa umewadia.



    Wakili wangu aliondoka mara moja na mimi nilichukuliwa na askari yule na kupelekwa moja kwa moja hadi kwenye chumba cha mahakama nikisubiri hatma yangu.

    Tofauti na siku nyingine, siku hiyo niliweza kumuona mke wa Elhakim ambaye ni mtu pekee aliyeongezeka katika orodha ya ndugu wa Elhakim waliofika hapo.



    Kwa upande mwingine nilimuona mdogo wangu akiwa ameketi viti vya mbali akinitazama kwa huruma dada yake nikiwa kizimbani.

    Kama kawaida, kesi ikaanza kusikilizwa.



    Maswali yakaulizwa; upande huu ukiulenga upande ule na upande ule ukiulenga upande huu, hatimaye ilifika zamu ya Jamila, yule msichana aliyedai kumuua Elhakim kupanda kizimbani na kueleza mbele ya mahakama jinsi gani alikuwa akihusika na kifo cha Elhakim.



    Kwa kujiamini, Jamila alisimama kwenye kizimba kile na kuanza kuelezea:

    "Kama nilivyosema jana, jina langu ni Jamila Msuya. Mimi ndiye muuaji wa Elhakim. Mnamo mwezi Julai, mwaka juzi, nikiwa mkoani Iringa, dada mmoja alikuja nyumbani kwetu akisema kuwa anamtafutia rafiki yake aishiye Dar mfanyakazi wa ndani.



    "Kwa kuwa sikuwa na shughuli yoyote ya kuniingizia kipato, niliamua kumwambia dada huyo kuwa ningependa kwenda Dar kuifanya kazi hiyo.



    "Baada ya kuwaaga wazazi wangu na taratibu zote kukamilika, nilisafiri na yule dada hadi hapa Dar. Sikujua hata kidogo kuwa nyumba ambayo ningefikia ingekuwa ni ya Elhakim, laiti kama ningelijua hilo hata nisingethubutu kuikubali kazi hiyo.



    "Nikiwa nyumbani kwa Elhakim, siku za kwanza nilifanya kazi kwa furaha na niliishi vizuri sana na mkewe pamoja na ndugu zake ambao wengi wao wapo hapa mahakamani leo hii.



    "Nilianza kujua tabia mbaya za Elhakim, siku chache baada ya mkewe niliyezoea kumuita dada kusafiri. Kwa mara ya kwanza nilishangaa kumuona Elhakim akiwa na mazoea ya kuingia ghafla chumbani kwangu.



    "Mara nyingine alikuja akiwa na nguo za kulalia na kama hiyo haitoshi alikuwa akitaka kulala na mimi kwa kunilazimisha, jambo ambalo nilikataa na kuamua kutoka chumbani na kuwa nalala sebuleni ambako aliogopa kunifuata kwa kuwa watoto wake wangemsikia kama tu ningepiga kelele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nafahamu kuwa marehemu hasemwi kwa ubaya lakini siyo kwa Elhakim ambaye kila siku alikuwa akibuni njia ya kuninasa katika mtego wake. Hakujali hata pale nilipotishia kumwambia mkewe.



    "Nikiwa katika maisha hayo ya kupambana, siku moja baada ya mlo wa mchana nilihisi kupoteza nguvu zangu jambo nililokuja kulifahamu baadaye kuwa aliniwekea dawa za kulevya katika maji ya kunywa kwani kabla sijapoteza fahamu nilimuona Elhakim akinibeba na kunipeleka chumbani kwake.



    "Nikiwa sina nguvu hata ya kuniwezesha kunyanyua midomo yangu kupiga makelele kuomba msaada, Elhakim alinivua nguo zangu zote na kuniacha kama nilivyozaliwa kisha akaniingilia kimwili na mbaya zaidi aliniingilia hadi kinyume na maumbile.



    "Kwa kuwa nilikuwa na uchungu sana, nilipoteza fahamu na kuzinduka siku iliyofuata ambapo mwili wote ulikuwa ukiniuma. Nilipomfuata na kumueleza kwa nini alinifanyia kitendo kile, alinidhihaki na kunitaka niondoke nyumbani kwake.



    "Kwa kweli, kwa siku hiyo sikuweza kufanya jambo lolote zaidi ya kuondoka nyumbani kwake, nikiapa kuwa lazima siku moja nitamshikisha adabu kwa kitendo alichonifanyia," alisema Jamila huku macho yaliyojaa ujasiri mkubwa yakianza kulengwalengwa machozi.

      




    Sikuwa na wazo lingine muda huo, nilimchukua mwanangu nikidhamiria kuondoka haraka mahali hapo, lakini kabla sijafika mbali nilikiona chakula kikiwa mezani. Kwa jinsi kilivyokuwa kimewekwa nilitambua kwa vyovyote Elhakim alikuwa akijiandaa kula.




    Akili yangu ilifanya kazi kwa kasi. Kwa kuwa sikuwa mgeni wa nyumba ile, haraka niliingia chumba cha stoo na kuchukua sumu ya panya katika moja ya masanduku ambayo niliyakumbuka vyema.

    Kwa bahati nzuri niliiona, nikaichukua kisha nilienda moja kwa moja nakuichanganya sumu ile kwa wingi katika chai ya Elhakim. Sekunde chache baada ya kufanya hivyo nilimsikia Elhakim akizungumza na simu akitokea jikoni, nikaondoka haraka mezani hapo na kwenda kukaa kwenye sofa nikijifanya namnyonyesha mwanangu.

    Bila kushtuka Elhakim aliketi mezani na kula chakula chake huku akishushia na ile chai niliyoijaza sumu. Sikumsumbua mpaka nilipohakikisha kuwa amemaliza kunywa ile chai.
    Kama kawaida yake aliponiona tu aligeuka mbogo na kunifukuza nyumbani kwake kwa ukali tena kwa wakati huo alikimbilia ndani na kuichukua bastola yake akitishia kuniua.

    “Kwa kuwa niliogopa, niliamua kuondoka zangu na mlinzi wake aliniona nikitoka na bosi wake akirudi ndani salama salimini. Nilirudi baada ya dakika chache nikimsihi mlinzi wake aniruhusu niingie ndani lakini alinikatalia. Lengo langu wakati huo halikuwa kuingia ndani kweli, bali kuhakikisha kama nimeshammaliza.


    “Kwa macho ya uwongo nilimsihi sana mlinzi yule angalau aniitie Elhakim mwenyewe aje nje nizungumze naye. Baada ya kumuomba sana yule mlinzi alinionea huruma na kuamua kwenda kuniitia bosi wake.



    Nakumbuka alinijibu kwamba, bosi wake alionekana amechoka sana kwani alimkuta amelala bila hata kumalizia chakula chake pale mezani, hivyo hawezi kumsumbua kwa ajili yangu.


    “Kwa maelezo hayo nilitambua kuwa tayari ile sumu ilikwishafanya kazi yake. Niliondoka zangu nikishangilia ushindi mkubwa. Sikujua nini kilichokuwa kikiendelea humo ndani, lakini nilikuwa na uhakika kuwa Elhakim ameshakufa muda mchache baada ya mimi kuondoka.


    “Siku mbili baadaye nilisikia kuwa kuna msichana amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua Elhakim. Hiyo ndiyo ikawa mara yangu ya kwanza kuingia mahakamani na kukutana na kesi hii. Kwa nilivyosikiliza niligundua kuwa mtu anayeshtakiwa yaani huyu dada hapa (huku akininyooshea mimi) aliipiga risasi maiti ya Elhakim lakini siyo Elhakim. Elhakim nilimuua mimi,” alimaliza Jamila.


    Kwa maelezo yale, miguu yangu iliisha nguvu nikajikuta nikikaa chini kama mzigo. Nilipopata nguvu nilijitahidi kuvuta kumbukumbu zangu vizuri. Kweli siku ile nilipofika nilimkuta Elhakim akiwa amelala sikumuangalia kama alikuwa mzima au la. Bila kuchelewa nikammiminia risasi papohapo, hivyo kwa maelezo yale ya Jamila huenda kweli Elhakim hakuwa kama nilivyofikiria awali, hakuwa amelala bali alikuwa amekufa.


    Baadaye nilirudishwa gerezani huku wakili wangu aliyekuwa akinitembelea gerezani karibia kila siku, akinieleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu kesi yangu. Kwanza aliniambia kuwa mwili wa Elhakim ulikuwa umefukuliwa ili kufanyiwa uchunguzi tena. Matokeo yalionesha kuwa kweli Elhakim alikuwa amefariki dunia kutokana na sumu kabla hajapigwa risasi, hivyo niliambiwa ningeweza kuachiwa huru maramoja kuanzia siku hiyo.
    ***



    Siku chache baada ya kutoka gerezani nilisikia kuwa Jamila amefungwa na anatumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuua kwa kukusudia, bila shaka hiyo ndiyo adhabu ambayo ingenikuta mimi.


    Baada ya miaka miwili nikiwa katika matembezi yangu ya kawaida nilimuona Jamila akiingia ndani ya nyumba moja nzuri sana karibu kabisa na nyumba niliyokuwa nikiishi mimi.
    Sikuamini kabisa kwa kuwa nilijua Jamila alikuwa gerezani, akitumikia kifungo cha maisha.



    Nilijaribu kumfuata na kumuulizia ndani ya nyumba ile lakini walisema kuwa hakukuwa na mtu kama huyo.



    Sijui kama waliniambia ukweli au waliniongopea, lakini nilikuwa na uhakika kuwa niliyemuona alikuwa ni Jamila kwa kuwa sikuweza kabisa kuisahau sura yake na haiba yake ya ujasiri.


    Nikaamua kuyaacha mambo hayo kwa kuwa tayari nilikuwa nimeshaanza maisha mapya na kuhusu Elhakim, nilikuwa nimeshamsahau, au labda ningemkumbuka sana kama mwanangu angefanana naye, lakini namshukuru Mungu aliniepushia hilo, mwanangu alikuwa amefanana kila kitu na mimi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO
    '' THE END''



      

0 comments:

Post a Comment

Blog