Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MACHO YA BUNDI - 5

 





    Simulizi : Macho Ya Bundi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Nakumbuka kabla ya kuondoka Padri Kalo alichungulia ndani ya gari na kuniona nikiwa najinyonganyonga kwa maumivu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama nendeni kwa amani, Mungu atawatangulia na malaika wake wako pamoja na wewe, usiwe na wasiwasi."

    Mume wangu alizidisha kasi ya gari nikamuambia apunguze mwendo, tulifika katika Hospitali ya Mkomaindo salama, nikapokelewa.

    Kilichonishangaza ni kumuona bundi mwingine akiwa juu kabisa ya paa la hospitali hiyo. Macho yake yalikuwa yanang'aa. Niliingizwa hospitalini huku moyo ukienda mbio.

    Haikuchukua muda nilijifungua mtoto wa kiume. Alikuwa na afya njema na baada ya dakika chache mume wangu aliitwa akamuona mwanaye.

    Tulifurahi sana.

    Tulirudi nyumbani tukiwa na furaha isiyo kifani.

    Nilikaa na mwanangu nyumbani, siku ya kliniki ilipofika nikampeleka.

    Wakati naingia hospitali moyo ulidunda paa kwani nilimuona bundi akiwa amesimama kwenye dirisha la mlango ambao nilitakiwa kupita ili niingie hospitali.

    Moyo wangu ulidunda sana kwani bundi huyo hakuwa na uoga na sisi kwani mume wangu alijaribu kumfukuza lakini hakuondoka.

    Sikuvumilia ilibidi nimuite nesi ambaye nilikuwa nimemzoea na nikaamua kumuuliza kwamba kwa nini kila nikienda pale, nilimuona ndege huyo akiwa amesimama dirishani au juu ya paa?

    "Usiwe na wasiwasi hawa bundi hapa ni makazi yao. Wapo hapa baada ya kuhama kutoka Mlimani Mkomaindo ule palee. Wanafuata vyakula," alisema nesi na kuniondoa wasiwasi.

    Niliporudi nyumbani nilitafakari jibu la nesi hivyo nilimuambia kijana wangu wa kazi atafute kwenye miti iliyozunguka nyumba yetu kama kuna kiota chochote cha bundi baada ya muda alikuja na jibu.

    "Mama ule mti mkubwa pale kuna viota vingi sana vya bundi ndiyo maana usiku huwa wengi karibu na nyumba yetu."

    Hapo niliondoa shaka kwamba bundi wote ninaowaona karibu na nyumba yetu kuwa ni wa kishirikina. Nilijua ni wa kawaida tu.

    ***

    Mtoto wa Pili alikuwa ameshakuwa mkubwa na mume wangu akaniambia kuwa atakwenda kijijini kwa Pili akafanye uamuzi mzito.

    "Uamuzi gani tena mume wangu?"

    "Nataka kwenda kwa Mei kumtangazia kuwa namuacha mtoto wake Pili."

    "Hapana usifanye hivyo, Pili siyo mbaya, ubaya anao mama yake ambaye mimi ni rafiki yangu."

    "No. Nitamuacha kwa ahadi kwamba atarudi darasani na mtoto wake tutamlea sisi. Pili nitamhudumia kila kitu mpaka amalize masomo yake, kisha achukue hamsini zake."

    Nilifikiri na kumshauri kwamba kabla ya kufanya uamuzi huo, ajadiliane kwanza na yeye Pili kujua kama atapenda kurudi shuleni au la.

    Mume wangu aliamua kumuita Pili pale nyumbani kwetu. Wakawa wanazungumza:

    "Pili nimekuita kwa jambo moja. Nilitaka urudi darasani na mtoto utuachie tumleee sisi, unasemaje kuhusu hilo?"

    "Ni ghafla sana natakiwa kutafakari."

    "Utafakari nini? Nenda shule mama." Niliingilia.



    Pili aliniangalia na akatafakari kwa dakika kama mbili hivi kisha akasema anakubaliana na ushauri huo.

    Mume wangu alimtafutia shule nje ya nchi na akasoma huko hadi alipomaliza chuo kikuu.

    Mei naye maisha yalimshinda akawa anataka kuja kwangu lakini akawa anashindwa jinsi ya kuniingia.

    Baadaye alimtumia Padri Kalo ambaye alifika nyumbani kwangu akiwa na ujumbe.

    “Rafiki yako Mei alikuja kanisani na kuniomba nije kwako nimuombee radhi kwa yote aliyokufanyia na Mungu alisema tuwe tunasameheana, naomba umsamehe,” alisema Padri Kalo.

    Nilimuambia padri kwamba mimi sina ugomvi na Mei kwa sababu yeye ndiye aliyenichokoza mimi kwa hiyo sina cha kumsamehe kwa sababu sikuwa na kinyongo naye na mimi ndiye niliyemshauri mtoto wake Pili aende kusoma.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya maelezo yangu padri hakukaa sana nyumbani kwangu aliaga na kusema atafikisha ujumbe kwa Mei.

    Siku mbili baadaye Mei alikuja kwangu na tulizungumza mengi. Nilimueleza kasoro zake na kwamba asifanye hivyo tena siyo kwangu bali kwa mtu mwingine yeyote.

    Baada ya mazungumzo aliniambia hana nauli, niliingia chumbani nikampa shilingi 200,000 huku nikimshauri kuwa akaanzishe biashara ndogondogo hata kama ni za kuuza karanga na ubuyu.

    Nilipata habari baadaye kwamba Mei aliamua kuhamia kijijini kwetu Mtandi kuishi baada ya kuona hana jinsi.

    Nilisahau kumfahamisha mume wangu kwamba Padri Kalo alitupatanisha na Mei aliyekuja nyumbani na kutokwa machozi. Mimi sikumuona kwa sababu aliishia nje ya geti na ilitokana na maelekezo ya mume wangu kwa mlinzi wetu kwamba akija Mei asifunguliwe geti na kuruhusiwa kuingia ndani.

    Nilijua baadaye baada ya mlinzi kuja na kunipa taarifa. Alinipa taarifa baada ya kumuona akizungumza na mtu ambaye nilikuwa simuoni kutokana na geti kutofunguliwa.

    Nilipomuona yule mlinzi katulia kwenye kibanda chake ndani ya ua wetu, nilichukua kiwiko cha simu na kumpigia.

    “Nimekuona unazungumza na mtu hapo getini, ni nani huyo?”

    “Si yule mwehu. Eti anataka kuingia kwa nguvu nikamwambia asithubutu kwani nitampasua.”

    “Mwehu yupi?” nilimuuliza makusudi kwa sababu yule kijana alikuwa akimchukia Mei pengine kuliko mimi.

    “Mama si yule mama yake Pili? Nimempasulia ukweli kwamba mtoto yupo kwa baba yake, mwanaye kaachwa na anasomeshwa sasa yeye anafuata nini hapa?”

    Nilimuambia mlinzi kwamba amefanya vema lakini sasa nalegeza kamba kwamba akija asimtimue, aniambie.

    Hazikupita siku nyingi Mei alikuja tena nyumbani na mlinzi kama nilivyomuagiza akanipigia simu.

    “Mama yule ju….” alishindwa kumalizia bila shaka kwa kuwa alikuwanaye karibu lakini nilijua alitaka kusema ****.

    “Mpe ruhusa apite.”

    Nilimuona Mei akiingia huku akiwa amejiinamia. Ile anakaa tu kwenye kochi mume wangu naye akawa anaingia. Alipomkuta alihamaki.

    “Nani kakuruhusu kuingia humu ndani si nilikupiga marufuku kufika hapa, hivi unanitafutia nini Mei?”



    Nilimuona Mei akiingia huku akiwa amejiinamia. Ile anakaa tu kwenye kochi mume wangu naye akawa anaingia. Alipomkuta alihamaki.

    "Nani kakuruhusu kuingia? Mei nilikupiga marufuku."



    Niliingilia kati na kumueleza mume wangu kuwa Padri Kalo katusuluhisha..

    "Nisamehe mume wangu. Nilimruhusu mlinzi amruhusu Mei kuingia hasa baada ya kupatanishwa na Padri Kalo, nilikueleza mume wangu. Tumsamehe tafadhali."

    Wakati wote Mei alikuwa akibubujikwa na machozi ambayo alikuwa akiyafuta kwa upande wa kanga.

    "Unalia nini rafiki yangu?" nilimuuliza.

    "Nisamehe sana rafiki yangu."

    "Nikusamehe nini?"

    "Nimegundua ubaya wangu niliowafanyia."

    "Upi?"

    Alianza kunieleza jinsi alivyotaka kunitibulia ili niachane na mume wangu, alivyokwenda kwa waganga ili kuturoga kwa nia ya kusambaratisha ndoa yetu.

    Alikiri pia kwamba alikwenda kwa waganga kufunga kizazi changu lakini alipoona nimepata ujauzito na kujifungua, akagundua kuwa alikuwa akidanganywa na yule mganga wake.

    Ilikuwa ni simulizi ya kusisimua kwa sababu aliyekuwa akifanya hayo alikuwa ni rafiki yangu mkubwa ambaye hata kuolewa kwangu zaidi ya miaka minane nilimshirikisha kwa asilimia mia moja.

    Aliniambia kuwa kila wakati alikuwa akimuambia Pili amuambie mume wangu kuwa mimi nina wanaume, natembea nao nje ya ndoa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini pia nakumbuka kuwa hata mimi alikuwa akinieleza (Mei) kuwa mume wangu alikuwa na wanaume wengi wa nje, hali iliyosababisha tugombane sana na mume wangu na nikawa nasusa kulala katika chumba chetu.

    Kususa huko kulisababisha mume wangu ampate Pili mtoto wa Mei na niligundua hilo siku mume wangu aliponipa taarifa ya kumuoa Pili kimila.

    "Mume wangu, Mei mimi ni rafiki yangu na wala sina kinyongo na aliyonifanyia. Nampenda na nitazidi kumpenda. Tumsamehe na mimi nimeshamsamehe, shetani alimpitia."

    Tulikumbatiana na Mei na tukawa wote tunatoka machozi. Nilimuambia wasiwasi wangu kuhusu macho ya bundi, nyumbani na hospitali ambako nilikuwa nakutananao kwamba kumbe wala siyo wa kichawi.

    Simu iliita ilikuwa inatoka kwa Pili. Niliipokea, nilipigwa na butwaa baada ya Pili kuniambia kwamba kuanzia sasa yeye siyo aliyekuwa mke wenzake bali mimi ni mama yake.

    "Najua mama alifanya ubaya kwako na ndiye aliyenilazimisha nitembee na mumeo nikapata mimba. Naomba umsamehe," alisema Pili.

    Nilimuambia kuwa nimeshamsamehe na hivi nipo naye hapa nyumbani. Pili japokuwa alikuwa mbali na sisi hukohuko Ulaya alisika akisema Wawoo kwa furaha.

    Naye akasema alipiga simu kwanza kwangu kabla hata ya kumpigia mama yake mzazi na mume wangu ambaye amemuacha na kumsomesha.

    Anasema ananiona kama mama yake na siyo mke mwenza, akasema kusudio lake la pili ni kutaka kuniarifu kwamba amepata mchumba hivyo anataka baraka zangu na anataka ndoa hiyo ifungwe hukohuko Ulaya anakosoma.

    Nilimuambia anipigie baada ya dakika kumi ili niwaambie mama yake na mume wangu.

    Baada ya kukata simu wenzangu wote wakawa wananishangaa kwani nilirukaruka kushangilia.

    "Salome naona una jambo kubwa, ulikuwa unazungumza na nani?" Mume wangu aliniuliza.



    Niliwaambia kila kitu alichoniambia Pili kuhusiana na alivyopata mchumba na kuniomba nimsamehe yeye na mama yake. Habari ya kuchumbiwa ilitufanya sote watatu tukawa na furaha.

    Mimi nilikuwa na furaha zaidi kwa sababu nilijua kuwa ibilisi hataweza tena kumkumba mume wangu na kufunga safari kwenda Uingereza kumfuata Pili ambaye ni mume wa mtu.

    Lakini pia nilifurahi kwa kuwa kumbe hata Pili alikuwa na mawazo kama yangu ya kumsamehe mama yake aliyesababisha ufa mkubwa katika ndoa yangu na uhusiano wetu na mama yake.

    ***

    Baada ya siku chache Pili alituletea tiketi mimi na mama yake na siku ilipowadia tulisafi na kufika London, Uingereza.

    Pili alitutambulisha kwa mchumba wake kwamba mimi ni mama yake mdogo na mlezi na Mei ni mama yake mzazi.

    Siku ya kufungwa ndoa iliwadia na shughuli hiyo ilipangwa kufanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Duniani la Canterbury jijini London.

    Ratiba ilikwenda kama ilivyopangwa na Pili akafunga ndoa na mchumba wake Muingereza anayeitwa Philip Jackson.

    Baada ya ndoa sherehe ilihamishiwa katika Ukumbi wa City Hall uliopo Mtaa wa Queen’s Walk katikati ya London.

    Mshereheshaji ukumbini wakati wa sherehe hiyo nzito akawa anasema maharusi wameunda kitu kinaitwa dabo P yaani Pili na Philip.

    Mimi nilitambulishwa kama mama yake mdogo ambaye nimefuatana na mama yake mzazi.

    Sherehe ilikuwa kubwa watu walikula na kunywa na tulishangiliwa sana na wazazi wa upande wa Philip.

    Baada ya sherehe tulipata muda wa kuzungumza na Pili nami nilimuambia kila kitu cha moyoni mwangu kuhusiana na vituko walivyokuwa wananifanyia.

    “Uzuri ni kwamba nilikuwa siwaombei mabaya kwa Mungu, nilikuwa nikimuomba muumba awape mwanga muuone ubaya, kwanza mjue kwamba mnachonifanyia ni katazo kwake na pili awape maono ya kuweza kufanikisha maisha yenu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kha! Mama una roho nzuri sana na sitaweza kukusahahu,” alisema Pili huku akifuta machozi.

    “Nakumbuka kama ni dhambi basi ni moja tu ambayo nilikuwa naifanya kwenu. Kila wakati nilikuwa namuona bundi, macho yake yakiwa mekundu na nikawa nahisi kwamba nyinyi mlinitumia bundi ili anidhuru,” niliwaambia.

    “Sasa ukaamini vipi kwamba hatuhusiki?” aliuliza Pili.

    Nilipokwenda hospitali nako nikakutana na bundi na macho yake mekundu. Nesi wa pale akaniambia kuwa ni ndege wa kawaida ambao wamehama kutoka Mlima Mkomaindo na kuja pale hospitali kufuata mabaki ya chakula na nyumbani pia wana viota kwenye miti mikubwa nyuma ya nyumba yetu.”

    ***

    Siku ya kurejea nyumbani Tanzania iliwadia na mume wa Pili alinipa zawadi ya gari na Mei naye akapewa gari kama langu yote aina ya Ford.

    Tulirudi Bongo tukiwa na furaha na hadi sasa Mei na mimi ni marafiki wakubwa, sasa tumekuwa kama ndugu.

    Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Blog