Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

KAFA NA UTAMU WAKE - 5

 





    Simulizi : Kafa Na Utamu Wake

    Sehemu Ya Tano (5)







    D Rose akiwa nje ya Mapokezi ya hotel ya Fiesta Zone, Daftari la kusajili wageni likiiwa mkononi akitazama kitu na kuandika andika katika kitabu chake.

    "Kwa siku huwa mnaweza kupokea wateja wangapi?" Swali toka kwa D Rose lilienda kwa Muhudumu wa mapokezi wa Hoteli ile. "Mh inategemea mara nyingine wateja 30 mpaka 50" D Rose anaandika katika kile kitabu kisha anamuangalia yule muhudumu.

    "Huwa mali za wateja za thamani kama fedha mnahifanyi nyie au wanahifadhi wenyewe?" Swali jingine kutoka kwa Mwandishi wa Habari na Mtangaji wa kituo cha Radio cha Sweet Fm mwanadada D Rose lilimfikia muhudumu yule. Wakati anajiandaa kujibu swali lile mara unasikika mlio mkubwa wa Risasi ndani ya Hotel ile..........!

    "PAaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah"



    ***************** *********************

    Sasa Endelea.......................



    Wingi wa watu wakiwa wamekaa katika mabenchi wakisubiri kupata huduma, katika vyumba vilivyojipanga kwa namba vitanda vilivyopangana huku kukiwa na watu wawili mpaka watatu katika vitanda hivyo, Sura za uchovu na Mirija ikiwa imetoka katika chupa za plastiki ikipitisha maji na damu kuingia katika mishipa wa watu waliolala katika vitanda hivyo. Wauguzi wakiwa bize kutoa huduma kwa wgonjwa wale. Ni katika hospitali ya wilaya ya Temeke, Mgonjwa mmoja anaingizwa akiwa kalegea na kuwekwa kitanda kimoja na mama mtu mzima, majibu ya vipimo kutoka kwa mgonjwa yule yanamshtua daktari ni ugonjwa wa kipindupindu umeikumba wilaya ya Temeke ikiwa mgonjwa wa kwanza toka Temeke Mikoroshini akiwa amelele juu ya kitanda kile akiwa hoi.



    Askari wa jiji wakiwa katika harakati za kuzuia vyanzo vya maambukizi ya ugonjwa ule, wakiwa wameongozana na ma bwana afya wa wilaya katika operesheni ya mtaa kwa mtaa kufunga magenge yote yanayouza vyakula. Usafi ndicho kitu pekee kilichokuwa kikitafutwa ili kuwanusuru wananchi wasiathirike kwa ugonjwa wa kipindupindu. Ndani ya banda kubwa la Mama Janila wateja wakiwa wamekaa kwa mafungu katika mabenchi huku sahani zikiwa juu ya meza kila mmoja akipata kile kitakachoitokomeza njaa. Macho yake ya mviringo yakiwa yamepambwa na nyusi zilizokolea rangi nyeusi, Midomo yake mipana yenye lipsi za rangi nyeusi akiwa na pua pana, Shingo nyembamba iliyogawanywa na pingilipingili ikiwa imebeba shanga nyembamba yenye rangi nyeusi nyekundu na kijani, huku kifuani akiwa kabeba embe changa zilizochomoza kama ncha ya mshale na kufanya blauzi yake aliyovaa kuinuka na kutengeneza kama bastola mbili zinazomsubiri adui, Kiuno chake kilichokaa vyema na kutengeneza alama ya namba nane ndicho kilichopelekea kuumbwa kwa miguu yenye ukubwa wa chupa ya bia na kukamilisha wasifu wa mtoto wa kizaramo Janila. Akiwa makini kuhakikisha kila mteja anapata huduma anayostahili kwa wakati ule ndani ya banda la chakula la mama yake lililopo Tandika Gereji. Sahani iliyoshehena wali wa maharagwe ikiwa mkononi huku akitembea taratibu kuelekea alipokaa mteja ghafla anakutana na buti la Askari wa jiji linalotoa moja kwa moja kwenye sahani ya ule wali na kuhamaki tayari uko chini huku rungu la mgambo likishuka katika mgongo wa Janila, Yowe la nguvu lililotoka kwa binti yule likazalisha taharuki kutoka kwa Mama yake.



    ************** *******************



    Mlio wa risasi ulimshtua D Rose na kutupa macho upande wa pili, Kimya kikawa kimetawala wateja waliokuwa wamekaa tayari walikuwa wametawanyika kila mmoja akitafuta njia ya kuokoa roho yake, Shauku ya kutaka kujua kinachoendelea kule Mlio wa risasi ulipotokea ilimuandama na tamaa ya kuwa mmoja wa watu wa mwanzo kupata habari ile ilikuwa ishamkamata. Tayari mguu wa kushoto ulikuwa ushanyanyuka na kuruhusu kuhusu mguu wa kulia kuubeba mwili ili kuweza kupiga hatua kuelekea kwenye ngazi. Meneja wa Hoteli ile akiwa na mwendo wa kasi alimpita d rose na kupanda zile ngazi kuelekea kule D Rose anapopawaza, Kitendo kile cha Meneja wa hotel kumpita kilimuongezea D Rose nguvu na kujikuta akiongeza mwendo na kuwa sambamba na Yule meneja.



    Mwanaume aliyekamata Bastola vyema akiwa mbele ya mlango uliokuwa wazi kwa kuchanwa vipandevipande kwa risasi alikuwa akiongea kwa sauti kali.

    "Nimesema Toka nje mwenyewe Malaya wewe"

    Sauti ya mzee mutamegwa iliongeza hofu kwa Mkewe aliyekuwa amesimama pembeni ya ukuta wa bafu lililo ndani ya ile hoteli huku Jorome akiwa keshaingia chini ya uvungu wa kitanda.

    Roho ya kikatili na mafunzo aliyopata mama mutamegwa katika jeshi la wananchi kabla ya kustaafu ilichukua nafasi na kutambaa kama nyoka mpaka kwenye pochi yake na kutoa bastola yake na kuishika vyema. Mguu wa kulia wa mumewe ukawa unajiandaa kuingia ndani ya kile Chumba Risasi moja toka kwenye bunduki aliyoshika mama Mutamegwa iligawanyisha kipande cha mlango kilichobaki ikasababisha Hofu na mshikemshike kati ya Mzee Motamegwa pamoja na D Rose na Meneja waliokuwa wamefika eneo lile kila mmoja akijificha katika kona yake, Akiwa uchi bila kujisitiri mwili mkubwa wa mama Mutamegwa ulijitokeza nje huku akiwa kakamata bastola yake vyema.



    "Nasema weka chini bastola yako" Mutamegwa alitoa sauti huku akiwa kajificha, "Siweki" Sauti ya kikakamavu kutoka kwa mama yule ilitoa jibu lililomaanisha anachokizungumza. "Kumbe ndio tabia yako hii" Mutamegwa alimlaumu mke wake. "Wewe kwani unafanya nini huku kama sio umalaya?" Mama mutamegwa alijibu huku kaikamata bastola yake vyema macho yake yakiwa yanamtazama mume wake vyema. Filamu ile ilimvutia sana D Rose akawa anapiga picha kwa kutumia kamera yake ndogo huku tape recorder ikiwa inafanya kazi ya kudaka kila kinachoongelewa. "Mimi nimechelewa kufika nikaja pumzika hapa. Chumba cha pili kwenye mlango ulio wazi akajitokeza mwanamke aliyevaa Taulo huku akishangaa kinachoendelea akamsogelea Mzee Mutamegwa. "Vipi mpenzi" Risasi moja kutoka kwenye Bastola ya mama yule ikapasua katikati ya mguu wa Nance na kuzalisha kilio kikubwa kilichomshtua Mzee Mutamegwa na kutupa Bastola yake na kuanza kutimua mbio kutoka nje, Akiwa kavaa suruali huku kifua kikiwa wazi Tayari alikuwa nje ya uvungu wa kitanda kwa kasi ya ajabu alitoka nje akikimbia na kukutana na Miale ya picha kutoka katika kamera Ya D Rose, Jorome akashuka ngazi kwa mwendo wa kasi.



    *************** ******************

    Penzi alilopewa Nima binti wa kimasai lilimchanganya mpaka kuamua kutoondoka ndani ya jiji la Bongo mpaka atakapompata Jorome, Aliyemtoroka pale hotelini na kumuacha mwenyewe. Tayari alikuwa keshamaliza kila kona ya jiji akimtafuta Jorome bila mafanikio, Ikiwa ni Asubuhi Nima akiwa na Abby Boy kijana maarufu ndani ya jiji la Dar es Salaam, Umaarufu wake ulimfanya aishi ndani ya jiji hilo kwa starehe sana. Umuulizie nani Abby Boy asimjue! Utake nini yeye asikufanikishie, Kwa ujira wa laki Tono Abby Boy akiwa ndani ya Gari yake aina ya Toyota GX100 walikuwa wakielekea Machimbo Yombo kumuonyesha Nima sehemu anayoishi Jorome.



    Gari aina ya Land Cruiser LX likiwa limepaki mbele ya nyumba anayoishi Jorome huku Mama mwenye weusi wa kung'aa akiwa kasimama na mzee wa makamo wakionekana wanajadili kitu, Tayari Abby Boy alikuwa keshapaki gari pembeni ya ile gari na kuruhusu milango kufunguka Nima akawa wakwanza kushuka na akafuatiwa na Abby Boy, Kwa mbwembwe Abby boy akamsogelea Yule mama na kumuuliza.

    "Samahani jamani namuulizia jamaa mmoja anakaa kwenye hichi kijumba" Yule mzee alimuangalia Abby Boy na kutoa jibu lililomchanganya. "Kafa"

    "Kafaaaaaa" Abby Boy alirudia lile jibu likatua moja kwa moja kwa Nima na kupelekea kusogea mpaka pale. "Eti nini!" Nima alijikuta akiuliza lile bila kuamini.

    "Kwani wewe ni nani yake" Yule mzee alimuuliza Nima swali ambalo Abby Boy alilijibu kwa kujiamini. "Huyu ni Dada yake kaja kumtafuta" Jibu la Abby Boy lilimfurahisha yule mama na kumuangalia nima kwa Tabasamu. "Ooh wewe ni dada yake na Jorome?" Nima alijibu kwa kujiamini zaidi. "Ndio"

    "Sawa naomba tuongee kidogo kama hutojali, Tunaweza ongelea kwenye Gari?" Nima alimuangalia Abby Boy akampa ishara anataka kulipwa ujira wake mkono ukaingia kwenye pochi kubwa iliyo kwapana na kutoa burunguti la pesa akampa Abby Boy na kuondoka, Nima akafungua mlango wa mbele wa lile gari na kukaa akimuangalia yule mama aliyejaa mbele kwenye Usukani wa lile Gari.



    *************** ******************

    Akiwa katika mwendo wa kasi Jorome anashuka ngazi anapishana na watu wengi waliokaa kwa kujificha katika eneo la kupumzika la hoteli ile, Karibu na Geti la kutokea Macho ya Serena yanagongana na Sura ya Jorome bila kuamini anamuangalia Jorome mara mbilimbili huku akiwa na hofu, Picha ya hadithi aliyokuwa anasoma tayari ilikuwa imehamia mbele ya macho yake. Mwanaume aliyelala na Bibi Lizbeth miezi kadhaa iliyopita na kumalizwa kwa kidonge cha sumu kali aina ya Trixomic alikua mbele yake, Ni mwanaume aliyemliza Bibi Lizbeth. Akiwa kapigwa na butwaa Asijue cha kufanya Jorome alimpita na kutokomea nje ya hoteli ile.

    Serena akikimbia aliingia mpaka mapokezi mwa ile hoteli na kukutana na D Rose akiwa kafika mbele ya mapokezi akiita muhudumu bila mafanikio. Mwanamke aliyelowa damu akiwa anashushwa huku hajitambui alisababisha Serena apigwe na mshangao.

    "Sory can i help you please" {Samahani naweza kuwasaidia} Sauti ya muhudumu iliwashtua Serena na D Rose waliokuwa wakimuangalia Nance akipelekwa nje ya Hoteli ile kwa msaada wa wahudumu na Meneja. "Samahani naweja kufahamu majina ya wapangaji wa chumba namba 78 na 79?" D Rose alimuuliza muhudumu huku Kitabu chake cha kuandikia kikiwa mkononi tayari kwa kuandika jibu atakalopatiwa. Muhudumu akafungua kitabu cha kujisajili na kuangalia kwa makini. "Namba sabini na nane yupo Nance na Mr. Mutamegwa na namba 79 yupo Mrs Mutamegwa na Jorome" D Rose na Serena kwa Mshtuko wakajikuta wakitamka kwa pamoja "JOROMEEEEEEE!!!"



    *********** *******************



    Akimuangalia Nima kwa Tabasamu yule mama akakaa vizuri na kuanza kuzungumza, Samahani mimi naitwa Madame NeriaLwanko sijui unaitwa nani tafadhali?" Nima akiweka koo lake vizuri "Naitwa Nima" Alijibu kwa kifupi. "Mmh sawa umesema wewe ni ndugu ya Jorome" Mdame Neria aliuliza swali lingine kwa kiswahili kibovu. "Ndio kwani vipi?" Jibu lililoambatana na swali lilizaliwa katika midomo ya binti wa kimasai. "OOh usijali, Kwa ufupi, Mimi nampenda sana your brother nataka awe mume wakwangu" Jibu lile liliamsha hasira ndani ya nafsi ya binti yule sauti ya subira ilivutana na haraka za shari, Tabasamu feki likaupamba uso wa Nima, Kikohozi cha mfululizo alichotoa Nima kilimvuta Madame Neria kusogea karibu na Nima na kumpiga piga mgongoni kosa ambalo liliunganisha pigo kali katika eneo la kupitishia hewa safi na kutolea hewa chafu katika shingo yake lililosababisha Madame Neria Kulala kimya na kusubiri Maziko yake katika nyumba ya Milele. Kabla Nima hajamuweka vizuri Madame Neria Mara yule mzee anagonga kioo cha mlango aliokaa Madame Neria huku akionyesha ishara kama kamuona Jorome akija.

     **********************

    Ghadhabu zikamkaba, Shetani wa shari alikuwa keshamteka, Kisu kikali kilichokuwa juu ya sinia lililo juu ya ndoo ya maji kilikuwa kimekaa barabara katika kiganja chake cha mkono. Fundo kubwa lililofungwa vyema katika kiuno chake ili kuweza kuifanya kanga aliyovaa imsitiri vyema kwa kutweta alikuwa tayari kamfikia Askari wa Jiji, Pigo la kushtukiza kutoka kwa Askari aliye pembeni lilitua vyema katika mgongo wake na kujikuta yupo juu ya vyombo huku akitweta kwa maumivu.

    "Funga pingu peleka hao peleka kule kwenye gari"

    Sauti ya mkuu wa wagambo mzee mwenye kitambi ilivuma kama upepo na kupokewa na utekelezaji haraka tayari Mama mtu mzima mwenye Mimba kubwa akiwa na Binti yake Janila walikuwa yake walikuwa wameshafungwa pingu na safari ya kuelekea katika gari la polisi ishaanza. Tayari kwa kufunguliwa kesi ya kukaidi Amri ya Jiji kwa kutojihusisha na ufanyaji wa biashara ya chakula katika maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.



    Baada ya kifo cha mumewe yule Kanali wa jeshi aliyetolewa roho na mwanamke katili aliyezama katika penzi la Jorome mwanadada Chaurembo, Hali ya kimaisha ya Mary stela iliyumba na kupelekea kurudi nyumbani kwao Tandika na kuanza maisha mapya, Akiwa na binti yake Janila aliyemzaa miaka 18 walianza maisha mapya katika chumba kimoja cha hali ya chini. Ndugu wa Mumewe walimfukuza na kuhodhi mali zao zote walizochuma na mumewe. Akiba kidogo ya fedha aliyokuwa nayo ndiyo iliyotumika kufungua Banda la kuuzia chakula katika eneo la Temeke Gereji, Idadi kubwa ya wateja wake ilikuwa ni vijana waliokuwa wakija pale kumzengea binti yake Janila. Tangazo la kufungwa kwa mabanda ya kuuzia chakula katika wilaya ya Temeke liliingia katika sikio la kulia la mama Janila na kutokea sikio la kushoto. Sasa ukaidi wa Amri ya manispaa tayari ulikuwa umeshamuingiza Mama Janila au Mary Stela katika hatiha, Tena akiwa mshtakiwa wa Jamuhuri, Machozi huku mlango wa gereza ukimchekea yeye na binti yake ukimsonga katika akili yake.

    "Kaa chini hapo"

    Ni sauti ya Amri toka kwa askari waliomkuta katika kituo cha kati, Kwa hofu Janila na mama yake wakakaa kwa kujikusanya pamoja, Yule askari akichukua daftari kubwa na kalamu akaanza kuandika andika juu yake.

    "We mama unaitwa nani? " Sauti ya amri toka kwa askari polisi asiye na mzaha.

    "Naitwa Mary stela" Mama Janila akajibu kinyonge, Askari akaendelea kuandika.

    "Na wewe unaitwa nani" Swali kama lile la awali likahamia kwa Janila.

    "Naitwa Janila Chacha Marwa" Janila alijibu huku kainama chini, Yule askari aliacha kuandika akamuangalia janila kwa mshangao,

    "Baba yako ni Askari?"

    Swali lilimtoka Yule askari lililojibiwa kikamilifu na Janila.

    "Hapana ni kanali wa Jeshi."

    Yule askari akaweka kitabu pembeni na kusimama huku akiangalia huku na kule,

    "Sasa mbona hamtoi maelezo mapema mnataka leta problem hapa, Haya ondokeni msije tuletea balaa. Bila kuamini kama jibu lile la Janila limewatenganisha na mlango wa Gereza kama wanakimbizwa na simba katika msitu mkubwa walikuwa wakikatisha katikati ya mitaa na kutokomea.



    *************** **************

    Macho yake yalikutana barabara na Jorome akiwa kwenye Tax huku akiwa kifua wazi, Mshtuko aliopata ulimsababisha kupatwa na kigugumizi, tax ikiwa mbele ya nyumba mlango wa chumba cha jorome, kama mshale jorome akaingia ndani kwake. Maamuzi ya kutoa Taarifa kwa mama anayemtafuta Jorome yalikuwa sahihi kwa wakati huo katika akili ya Mzee ndungai, Hofu juu ya mgongaji wa dirisha la mlango wa gari ilimtanda Nima na kufanya akili yake kufanya kazi zaidi ya kawaida, Kwa haraka Nima akashuka na kuzunguka kule alipo mgongaji.

    "Jorome kaja na Tax ile kaingia ndani?" Kauli ya mzee ndungai ilipokewa kwa furaha na Nima furaha iliyozalisha noti tano za shilingi elfu kumi katika kutoka katika mikono ya nima kwenda kwa mzee ndungai kama shukrani. Mzee Ndungai Akiondoka huku akishukuru ndiyo ilikuwa nafuu kwa Nima na kurudi katika gari huku macho yake yote mawili na akili vilikuwa vikiangalia katika mlango wa Chumba cha Jorome. Jorome kwa mwendo wa kasi alirudi katika gari huku akivaa shati harakaharaka, Tayari nima alikuwa upande wa dereva na Madame Neria alikuwa keshalala kwenye siti ya nyuma ya lile gari. Muungurumo wa injini wa lile gari ulianza kuchanganya akifuatilia Tax iliyombeba Jorome. Hatua kumi toka alipo ilipo Tax ya iliyombeba Jorome Mzee wa makamo Balozi wa Mtaa anaoishi Jorome alikua kainama akizungumza na mtu aliyekaa siti ya mbele ya ile tax na kisha Tax ikaendelea na safari.



    Askari waliokuwa wakifanya ukaguzi wa stika za ushuru wa huduma ya zimamoto katika eneo la Tandika Relini ndio uliombadilisha muelekeo Nima, Wazo la kukatiza njia ya vumbi inayotokea Tazara ndilo lilikuwa sahihi kwake ili kuwakwepa wale askari, Maiti aliyokuwa nayo katika Gari lilie ndiyo ilikuwa kikwazo kwake, Mbele ya macho yake Tax iliyombeba Jorome ilikuwa ikipotea huku akisonya kwa hasira.



    **************** ***************



    Kutajwa jina la Jorome eneo lile ilikuwa kama Mshtuko na ajabu katika masikio ya Serena, Mawazo ya mzimu aliouona muda mfupi uliopita yalianza kujifuta na kushangazwa na kitendo cha jorome kuwa hai, Dawa ya Trixomic aliyowekewa kwenye maji na Giant ilikuwa haijaudhuru uhai wa Jorome, Machozi ya Bibi Lizbeth aliyolia yalimfanya Serena kuondoka kwa kasi kuelekea katika chumba chake kufanya kitu muhimu kitakachoongeza furaha ya Bosi wake Bibi Lizbeth, Kitita cha fedha alichokuwa akiwaza kama ahsante kutoka kwa bibi yule kilimuongezea kasi ya kuufikia mlango wa chumba chake na kufanya kile kinachowezekana kwa wakati huo,



    D Rose akiwa haamini kauli iliyotolewa na Muhudumu, Jina la Jorome lilikuwa sahihi ila nafsi yake ilipingana na sura aliyokutana nayo muda mchache uliopita, Kauli ya Trovina iliyomaanisha ubaya wa sura ya Jorome ilimpa nafasi kubwa ya kukubali Mtu aliyeutoa usichana wake na aliyekuwa anahangaika kumtafuta muda wote ndie yule aliyesababisha varangati kubwa pale hotelini, Maamuzi ya kutoitoa habari ile ili kuilinda heshima ya Jorome yalikuwa na nafasi kubwa kwa wakati huo, Kwa unyonge akaelekea palipo na mlango huku akijiapiza kumtafuta Jorome na tayari alikua na pakuanzia jina la Yombo Machimbo lililoandikwa kwenye kitabu cha mapokezi kama eneo analoishi jorome ndilo lilimpa mwanga kamili.



    ***************** *****************

    Mabishano kati ya Jorome na Meneja wa Swiss Cash yalizidi kupamba moto, Hofu ya kumpatia Jorome fedha zote kwa mkupuo bila kupitia katika benki nyingine ilikuwa imemtanda Meneja wa benki ile, Kutokana na Mvutano uliopo kati ya Jorome na Meneja walifikia muafaka Jorome apatiwe pesa zake na kuamua atakwenda kuziweka wapi, Mbele ya sanduku kubwa la chuma Tayari pesa zilikuwa zikipakuliwa na kuwekwa katika kiroba kikuukuu na Jorome alikua tayari na shilingi milioni mianane za kitanzania katika Mfuko huo. Moja kwa moja katika Tax aliyokuja nayo kiroba kikilala katika buti na Tax ikang'oa gina na kuondoka kuelekea upande wa magharibi wa benki ile.



    Tayari ni sa kumi na moja jioni Jorome akiwa na kiroba chake moja kwa moja mpaka kwenye banda la chakula na kukaa wali maharwe ulikuwa mezani kwa haraka akaanza kula ili kuipooza njaa yake. Msichana mwenye uzuri wa kipekee akiwa kavaa nguo zisizoendana na uzuri wake akiwa kashika bakuli kubwa tayari mbele ya muuzaji akipakuliwa wali katika bakuli lile na kulipa kisha akatoka. Kwa haraka Jorome akiwa kabeba kiroba chake alianza kumfuatilia yule msichana kwa nyuma. Sauti ya kusimamishwa kutoka kwa Jorome ilippokewa na msichana Yule na kkukutana macho kwa macho na sura mbaya Jorome.

    "Samahani wewe ni mwenyeji wa huku" Jorome aliuliza swali la kizushi.

    "Ndio kwani vipi?" Jibu lililokerwa na swali la kiumbe wa ajabu aliyesimama mbele yake lilimtoka yule binti.

    "Samahani tena natafuta nyumba ya wageni ya bei nafuu, Ukinionyesha nitakulipa vizuri" Jorome akazidi kupangilia maneno kwa binti yule.

    "Kaka nina haraka na mimi sijui nyumba za wageni huku" Yule binti alijibu kisha akaanza kuondoka, Jorome akimfuata akili yake ikifanya kazi ya ziada tayari burrunguti la pesa lilikua katika mkono wake mpana huku akimuita yule binti.

    "Dada..! Nisaidie Tafadhali" Jorome alizidi kubembeleza, Kwa hasira Yule msichana akageuka kabla hajasema neno macho yake yakatua katika kiasi kikubwa cha fedha kilicho mkononi kwa Jorome pesa zile zilizochanganya ubongo wa msichana yule na kujikuta akiachia tabasamu pana.

    "Unasemaje mpendwa?" Jibu la yule msichana lilimfurahisha Jorome na kujikuta keshasogea karibu na yule binti. "Chukua hizi fedha ni advance tu na ukinionyesha sehemu salama ninayoweza kulala nitakuongeza nyingine kama hizo"

    Yule msichana akipokea zile pesa kwa woga na kutazama pande zote akazisunda katika nguo yake ya ndani. "Mmmh twende huku" Yule msichana alitoa jibu lililomfurahisha Jorome na kuanza kumfuata Yule msichana wakikatiza katika vichochoro kadhaa.

    "Unaitwa nani sasa yangu?" Swali la ufahamu toka wka jorome llilienda moja kwa moja kwa Yule Msichana.

    "Naitwa Janila Chacha Marwa."



    **************







    Huku akihema kwa kasi tayari alikua mbele ya mlango wa chumba chake, Mokono ukinyonga kitasa cha mlango na kujaribu kufungua bila mafanikio, Kwa fujo akaanza kugonga mlango sauti za mtu akitembea ndani na kisha funguo kulalamika kelele zilizosababisha mlango kufunguliwa sura ya Mpenzi wake Scotch ilikuwa na Maswali, "What is Wrong?" {Kuna tatizo gani?} Scotch alimuuliza Serena huku serena akimpita na kwenda mojakwamoja kwenye begi lake na kutoa computer Mpakato aina ya apple na kuiwasha haraka haraka, Scotch akimsogelea karibu yake huku akishamshangaa Serena, "What is going on?" {Nini kinaendelea?} Scotch alimuuliza Serena huku Serena akihangaika kuingiza Modem ya intaneti katika ile komputa. "Just Cool.." {Kuwa mpole} Tayari neno skype lilikuwa katika ukurasa wa kutafutia mtandao, Akiweka headphone masikioni kusikiliza kitu kutoka katika headphone ile. "Rexs pedroe Lizbeth Suprix" {Nina suprise kubwa sana Madame Lizbeth} Serena alianza kuongea huku akikaa vizuri, Sauti ndogo iliyosikika kutoka kwenye zile headphone ilimfanya serena atoe tabasamu. "Trox lodet Suprix?" {Ni Suprise gani tena} "Loct medinc greav sobrif" {Niahidi zawadi utakayonipa} Serena alijibu kwa tabasamu. "Ansel, ansel metros frisdre medomegrix" {Kuwa mpole kuwa mpole, Je unataka nikujengee hekalu au nikupe pesa} Kauli ile kutoka kwa bibi Lizbeth ilimuongezea Serena Furaha na kumtazama Scotch kisha akaendelea kuongea huku bibi Lizbeth aliwa anaonekana kwenye kioo cha ile komputa. "Covanta lombul mubaaa le pex nedod lovix sesil" {Nimemuona yule kijana aliyekupa penzi huku Afrika} Serena alitoa maelezo kwa kujiamini. "Sontel Souzes, Namibia, Eritrea netes lovix mubaa Tanzania" {Ni wa nchi gani ni yule bwege wa Afrika ya kusini, Namibia au Yule kichaa wa Eritrea au unamzungumzia yule marehemu aliyenipa penzi la Ajabu wa Tanzania} Bibi Lizbeth alijibu kwa shauku. "Litied nesubr netes Tanzania" {Ni yule Marehemu wa Tanzania} Bibi Lizbeth alipatwa na Mshtuko kwa jibu lile. "Serena nes droek sobe sobe karegth" {Serena fanya unaloweza nikija nimkute naandaa Safari ya kuja huko} Bibi Lizbetha alijibu kisha mawasiliano yakakatika Serena kwa Furaha akamkumbatia Mpenzi wake Scotch.



    ************* **************

    Kitita cha pesa kilichokuwa katika mikono yake kiliihamisha akili yake kabisa, Matatizo waliyokuwa nayo sasa anauona mwisho wake, Kauli ya kuongezewa fedha zaidi ya zile ilimfanya aongeze mwendo na safari iliishia Stereo Guest House nadani ya chumba kipana chenye bafu na choo ndani. Akiwa kasimama huku akimuangalia kiumbe wa ajabu aliye mbele yake. "Jalia una umri gani" Jorome alimuuliza yule binti, "Miaka ishirini sasa" Jalia alijibu huku akiangalia chini, Jorome alifungua kile kiroba na kutoa Burunguti la pesa. "Jalia huu mfuko umejaa pesa nataka nikupe wote"Jorome alizungumza kwa sauti ya upole, Kauli ile ilizidi kumchanganya Jalia harufu ya pesa ilimuathiri na ubaya wa sura ya Jorome ukatoweka na kumuona kama Mwanamitindo mwenye mvuto wa kipekee. "Mmh Kwanini Unipe zote?" Jalia aliuliza swali la mtego. "Nataka unizalie mtoto mmoja tu..." Kauli ya Jorome ilimzindua Jalia kutoka katika Mawazo na kupatwa na mshangao. "Hapana kaka yangu haiwezekani" Ni jibu lisilo na mzaha kutoka kwa Jalia.

    "Sawa usijali wacha nikutoe" Kitita cha pesa kilicho katika mikono ya Jorome kilirudi katika ule mfuko, Tamaa ya Fedha ikamuandama Jalia, Miguu ikashindwa kwenda, Maisha mazuri akayaona kupitia ule mfuko wa fedha pale chini, Kidole Gumba cha mguu wa kushoto kikawa kinachora chora sakafu ya kile chumba. Mikono migumu ya Jorome ikawa ishaanza kutembea katika mwili wa mtotombichi Jalia, Joto la mapenzi likamuathiri Jalia, Mzuka wa kikurya na kizaramo vikampanda Wakajikuta wako kitandani Jalia akiwa mtupu huku Jorome akicheza na shanga Moja aliyovaa Jalia kiunoni.



    ************ ***************

    Jorome ndilo jina lililozidi kuumiza kichwa chake, Hitaji la kuonja utamu alioupata kwa mara ya kwanza lilizidi kuisonga nafsi yake, Maamuzi yaliyojijenga katika serikali ya ubongo wake ya kupambana na mtu yeyote atakayesogelea penzi la Jorome yalikuwa ni maamuzi sahihhi kwa wakati huo, Tukiolililomkuta ndani ya Hoteli ya Sunlight, Kitendo cha kuzidiwa nguvu na mwanamke mwenzake kilimfedhehesha sana, Moshi mwingi wa bangi ukiwa umesambaa ndani ua chumba alichokaa, Bastola yake ilikua mkononi huku akikagua risasi mojamoja na kuweka katika sehemu maalumu ya kuweka risasi katika bastola ile, Akafunga Kiwambo cha kuzuia sauti, Bastola ilikuwa imekaa vyema katika kiuno chake na tayari kwa kwenda katika mapambano ya kupigania penzi la Jorome.



    Chaurembo akiwa mita chache na nyumba anayoishi Jorome, Macho yake yot mawili yakitazama mlango wa Jorome uliokuwa umefungwa, Harufu ya damu ya mwanamke yeyote atakayesogelea mlango ule ndio ilikua ikiandama katika pua za Chaurembo. Vita tena vita vikali ni vita vya kuhakikisha anammiliki Jorome bila kupata upinzani wa aina yeyote, Uwezo wake wa kulenga shabaha ndio pekee aliojivunia na kujihakikishia ushindi kwa kummaliza kila atakayesogelea penzi lake kwa Jorome.



    ********* ************

    Akili ya ziada ilibidi itumike ili kupata angalau wasaa wa kukaa na Jorome na kisha kumueleza hisia zake. Kumwambia kiasi gani anampenda, Mapambano ya shari aliona si wakati wake tena kwa maana upande huo ulimshinda, Wazo la kumtafuta Rafiki yake ambaye ni askari mkakamavu mwenye uwezo wa kumtisha mtu na kufuata maamuzi yake ndilo lilikuwa sahihi muda huo, Alichowaza kichwani kwake ni kumkamata Jorome kwa Tuhuma za kuhusika katika Tukio lililotokea Fiesta Zone na kabla hajafikishwa kituoni atokee na kumsaidia aliona mbinu hiyo itamsaidia kumsogeza Jorome karibu yake. Tayari mipango ilikuwa ishapangwa kati yake na Rafiki yake Ambaye ni Askari polisi aitwaye Hidaya na kazi ilikuwa inatakiwa kuanza maramoja.



    Akiwa kavalia Suruali ya khaki yenye mifuko mikubwa miguuni na raba, huku Tisheti nyeusi ikiwa imefunika eneo la juu la mwili wake, Miwani ya jua ikiwa inamsaidia kukinga jua la Macho yake, Hidaya alikuwa mita chache na Mlango wa chumba cha Jorome huku akizidi kuusogelea.



    Kiumbe kilichokuwa kinasogea katika mlango wa Jorome kilimzidisha hasira Chaurembo, Wivu tena wivu wa mapenzi ukamuandama, Pembeni ya ukuta katika uchochoro Chaurembo alikua kakaa vizuri huku bastola yake ikisubiri kile kiumbe kiuguse mlango wa Jorome ili iweze kuruhusu Risasi kutenganisha uhai na Mauti katika mwili wa kile kiumbe, Kitendo cha kugusa mlango wa Chumba cha Jorome kiliambatana na Sauti ya kusonya Toka kwa Chaurembo na Kidole kikivuta kitufe cha kufyatulia Risasi katika bastola yake.



    ************ **********

    Askari wakiwa wamezunguka gari aina ya Land cruiser lililotelekezwa porini huku kukiwa na mwili wa mwanamke ulioharibika vibaya, Mawasiliano yalikuwa yakifanyika kwa njai ya simu za upepo, Kwa kusaidiana na wasamaria wema wa eneo lile mwili ule ulitolewa katika gari lile, Vitambukisho vyake vilitanabaisha ni mfanyakazi wa Bank ya Swiss Cash, Neria Lwanko ambaye ni Raia wa Rwanda, Gari iliyokuja kwa kasi na kupaki kisha wakashuka watu zaidi ya wanne katika lile gari walikuwa ni viongozi wa bank ya Swiss Cash, Waliutambua Mwili wa Madame Neria huku wakiwa na sura za majonzi, Kifaa maalumu cha kuongozea magari GPS kiliwashwa na kuangalia gari lilikuwa wapi mara ya Mwisho, Yombo machimbo ndio sehemu iliyoonekana kama eneo ambalo Gari lilikuwepo mara ya Mwisho.



    Sauti ya muungurumo mkali wa injini huku tairi za Gari zikilalamika kwa kusuguana na lami tayari askari wapatao wanne wakiwa na silaha za moto walikuwa kwenye gari tayari safari ya kuelekea, Machimbo yombo kwenda kutafuta chanzo cha mauaji yale na kukabiliana na chochote watakachokutana nacho.



    ********** *





    "Subiri kwaaanza..aaaaa"

    Sauti iliyojaaa mahaba ilitoka katika kinywa cha mtoto mbichi wa kizaramo mwenye mchanganyiko wa damu ya kikurya, Ni mtoto wa mwanajeshi aliyelelewa zaidi kwa bib yake mzaa mama, Ufundi wa kumchanganya mwanaume aliopata unyagoni wakati anavunja ungo chini ya kungwi wake Bibi nyambaso, Akilegeza kiuno chake na milio ya kimahaba iliyopelekea Jogoo wa Jorome aliyefungiwa vyema kutaaka kuvunja kibanda na kutoka nje ili aweze kupanda mtungi wa mtoto mzuri Janila. Ombi la Janila lilipokewa na Jorome kwa shingo upande akiwa kasimama pembeni huku suruali yake eneo la mbele pakicheza kama kuna kitu kinataka kutoka nje kwa hasira, Janila huku kalegeza macho akamsogelea Jorome na kupeleka mkono mpaka mbele ya suruali ya Jorome na kumshika huku akipapasa taratibu eneo lile.

    "Leo siko salama"

    Janila alitoa sauti ya kubembeleza iliyopokewa kwa kwa shingo upande na Jorome.



    Mazoea ya Jorome kuwaridhisha wanawake yalimsababisha asione kitu cha tofauti kutoka kwa wanawake wote aliowahi kulala nao, Mapenzi ya dhati yakaanza kuchipua taratibu na kujikuta anampenda kwa Dhati Janila, Utundu aliofanyiwa na Janila ulimteka akili na kuanza kuwaza kummfanya Janila kuwa mke wa Maisha yake. Wakiwa ndani ya Tax nje ya nyumba wanayoishi Janila Tabasamu na ahadi kem kem vilichukua nafasi na Janila kushuka kwenye gari akiwa na kiasi kikubwa cha pesa.



    ************** ****************

    Furaha ilizidi pale aliposikia sauti laini toka kwa Muhudumu wa ndege ya Fly Emirate ya kuwapa taarifa kuwa wamekwishafika nchini Tanzania na Abiria wafunge mikanda Tayari kwa ndege kutua katika uwanja wa kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam, Akifunga mkanda kisha akafunga jarida la Matangazo liitwalo DAR na kuliweka katika mfuko wa siti. Akalaza kwichwa chake huku akitabasamu. Ndege ya Fly Emirate ilikuwa imetua na Abiria walikuwa wanashuka mmoja baada ya mmoja.



    Serena akiwa na Scotch nje ya uwanja wa ndege eneo la kupokelea wageni huku macho yao yakiwa makini kushuhudia mtu muhimu wanaemsubiri atokeze, Bibi Lizbeth akiwa anasukuma Toroli lenye begi lake kubwa alitokeza na kutengeneza Tabasamu pana lililopokewa na Serena huku wakikumbatiana kwa furaha.

    "Li trozee gecsof lov" {Umekua mrembo sana mpenzi} Bibi Lizbeth alimwambia Serena. Serena akatabasamu na kumsaidia Bibi Lizbeth begi na kuingia kwenye Tax wakaondoka.



    ************** ****************



    D Rose akiwa kasimama mbali na nyumba ya Jorome akiwa kajificha macho yake yakiangalia tukio zima huku akisubiri Hidaya atoke na Jorome na kukamilisha kazi ya kumfanya Jorome awe wake, Wakati Dayana anakaribia Mlango wa Jorome shngo ya D Rose na akili vikahama na kuhamia kwa msichana aliyejificha katika uchochoro huku akiwa na silaha mkononi, Sura yake haikuwa ngeni machoni pake kwa mwendo wa kunyata akajikuta yupo nyuma ya Chaurembo, Wakati chaurembo anajiandaa kufyatua kitufe cha Kuruhusu risasi itoke katika bastola yake hapo ndipo D Rose alipomuita jina lake.

    "Chaurembo"

    Kuitwa kwa jina lake kulimfanya ayumbishe mkono tayari risasi ilikua imekwisha ruhusiwa kutoka na kukutana na ukuta wa chumba ch jirani ya Jorome sauti kubwa ya risasi kukutana na ukuta ilimshtua Hidaya na kujirusha pembeni kulingana na mafunzo aliyopata huku bastola yake ikiwa tayari kwa mashambulizi,Kikumbo kikubwa kutoka kwa Chaurembo kilimkuta D Rose na kujikuta tayari yuko chini huku silaha yake ikiwa tayari kwa mashambulizi, Milio ya risasi kutoka katika bastola ya Hidaya ilimchanganya D Rose na kujificha katika Mtaro.



    Kutokana na umaahiri wa mapambano na shabaha ya kulenga vitu vilivyo mbali aliokuwa nao Chaurembo risasi moja tu iliweza kuzima jitihada za Hidaya akawa yuko chini akiugulia maumivu ya mkono wake uliochanwa vibaya kwa risasi, Huku akishuhudia Chaurembo akipotelea mbele ya macho yake.



    Milio ya Risasi ndiyo ilifanya dereva wa gari lililowabeba askari kuongeza mwendo huku Askari wakiweka silaha zao vizuri, Walipofika eneo la mtaa anaoishi Jorome sehemu gari lilipokua mara ya mwisho kulingana na majibu ya GPS tayari askari walikua chini na Bunduki zao zikimuangalia Hidaya. Kwa shida na maumivu kitambulisho chake kilikua mkononi kikimtambulisha kama Askari polisi. Maelezo ya kukutana na Jambazi wakati akiwa kazini na kumjeruhi kwa risasi yalitosha kuunganisha tukio lile na tukio la mauaji ya Madame Neria. Hidaya akabebwa na kukimbizwa hospitali huku askari wengine wakifanya uchunguzi katika eneo lile.



    ************ ****************

    Ikiwa ni siku ya pili tokea Jalia aonje penzi la Jorome, Alikua amekufa na kuoza katika penzi la kijana huyo mwenye sura mbaya na ya kutisha. Akiwa kalala juu ya kifua cha jorome ndani ya chumba chenye giza wakiwa wamelala juu ya kiroba chenye pesa ndani Jalia alikua akideka kama mtoto.

    "Nataka nikakutambulishe kwa mama yangu"

    Jalia alimwambia Jorome huku akimpapasa kifuani, Jorome akitikisa kichwa kwa ishara ya kukubalina na kile Jalia alichosema kilimfanya Jalia kuanza kumbusu Jorome Mfululizo na Kuamsha hisia za Mahaba katika mwili wa Jorome. Taratibu walianza kuzama katika sayari nyingine huku lugha za maneno zikipotea na kuzaliwa lugha za mihemo na sauti za kuvuta utamu, Ufundi wa Jalia katika kukata kiuno huku akihakikisha anampatia Jorome kile kinachostahili kwa wakti ule ulimfanya Jorome kuongeza ufundi na kuzaliwa kilio cha hali ya juu huku Jalia akishukuru kwa kile anachokipata toka kwa Jorome.



    Giza nene lililofunika anga na kutengeneza safari ya kuelekea siku mpya haikumtisha tena Jalia, Ukali wa mama yake haukua kitu tena kwake alifurahia wasaa wa kuwa na mwanaume anayemtendea haki katika chakula cha jioni huku akiisifia bufee ya Jorome iliyoshehena chakula kitamu na ambacho hakikinaishi.

    "Nataka unipe kila saa"

    Jalia akijikuta akimwambia Jorome kutokana na kile alichokipata kutoka kwa Mtaalamu Jorome.



    ************** ******************



    Akiwa katika ofisi yake kalamu ikiwa mdomoni File la kesi ya mauaji likiwa mezani kwake Nisha mpelelezi maarufu asiyeshindwa na kitu alikua akitafakari huku akioanisha matukio mawili tofauti yaliyounganishwa katika tukio moja, Tukio la kuuawa kwa Afisa wa Bank ya Swiss Cash na Tukio la kupigwa risasi kwa Afande Hidaya katika eneo ambalo linasadikiwa marehemu Neria alikuwa mara ya mwisho na mwanamke aliyekutana naye pale ndiye aliondoka nae na mwishowe kukutwa ameuawa.

    "Hii haiwezekani kuna kitu hapa" Nisha alisimama na kuwekalile file katika kabati la kuhifadhia file na kutoka moja kwa moja mpaka kwenye kijiwe cha Tax.

    "Nipeleke Machimbo"

    Dereva tax akawasha gari na safari ya kuelekea machimbo ikaanza, Kila alichokiona njiani Nisha alikua akikiangalia kwa makini, Mazingira ya eneo lile hayakumvutia na kuamini kuwa Majambazi yanaweza kwenda kufanya uhalifu kule na kuacha kwenda sehemu kama mbezi au msasani tena kwa kutumia silaha, Akiwa kasimama mbele ya ukuta wa chumba cha jirani na Jorome huku akiangalia alama ya risasi macho ya nisha yakageuka na kugundua Sehemu mfyatuaji wa Risasi alipokua amesimama, Akaenda mpaka eneo alilotumia kujificha Chaurembo. Kipisi cha sigara kilichokua pale chini kilichokanyagwa kwa kiatu chenye ncha kama cha kike kilimvutia na kukiokota akakitizama kwa muda kisha akasogelea duka lililo hatua chache na pale.

    "Mambo" Nisha alimsalimia muuza duka

    "Poa tuu" Jibu lililotolewa kwa lafudhi ya kichaga lilimfurahisha Nisha na kugundua Muuzaji ni mchaga na kama si wa kibosho basi atakuwa wa Rombo Mkuu.

    "Samahani kuna sigara"

    "Ndio zipo" Yule muuza duka alijibu huku akiwa anafunga sukari katika mifuko midogo ya nailoni.

    "Naomba moja" Nisha alitoa pesa na kupatiwa sigara kisha akasogea pembeni na kuivunja ile sigara akabakiwa na kipisi akalinganisha na kile kipisi alichookota. Kisha akatikisa kichwa kama amegundua kitu, Akarudi pale dukani.

    "Katika maisha yako ulishawahi kumuona Msichana Mrembo akivuta sigara"

    Nisha aliuliza swali la kushtukiza kwa Muuza duka.

    "Sijawahi kabla ila juzi ile palipotokea milio ya bunduki alikuja Mdada mrembo hapa akanunua sigara na kuvuta"

    Nisha alifurahiwa na Jibu la muuza duka na kuanza kuona mwanga wa urahisi wa kazi yake.

    "Du alikuaje huyo Dada?"

    "Mweupe hivi na ni mwembamba ila anaalama kama kakatwa na kitu hapa karibu na jicho la kushoto" Jibu la muuza Duka lilimaliza kila kitu katika upelelezi wake. Mawazo ya kwenda kumalizia kwa Muandishi wa habari aliyeripoti tukio lile kama alikua wakati wa tukio ndio lilikua chaguzi lake la mwisho kabla ya kumsaka na kumtia mbaroni muhalifu.



    Tax ilikua imesimama nje ya Jengo la Radio ya Sweet Fm, Nisha kwa mwendo wa Taratibu akapanda ngazi na kupishana na D Rose njiani, Sauti ya D Rose akiwa anaongea na simu ilimfanya akasimama na kugeuka kisha akamuita.

    "Samahani Dada"

    D Rose akatoa simu sikioni na kuangalia kule alipoitwa.

    "Natumai wewe ni D Rose!"

    "Ndiyo bila shaka" D Rose alijibu kwa kujiamini, Kwa tabasamu N isha akatoa kitambulisho na kumuonyesha D Rose.

    "Naweza ongea nawe kutokana na habari uliyoiripoti juzi ile ya kule yombo"

    D Rose kwa kujiamini zaidi akakubali na wakaenda nje wakaingia kwenye Gari na kuanza kuzungumza.

    "Mh Sory hivi ulipataje habari ya lile tukio?"

    D Rose akikaa vizuri kujiandaa kujibu lile swali macho yake yakagongana na kioo cha nje cha lile gari akakutana na sura ya Chaurembo ikiwa inakuja bila wasiwasi kufuata ile barabara gari ilipopaki. D Rose akashusha pumzi na kuongea kwa sauti ya Chini sana.

    "Muuaji huyo anapita yupo nyuma ya hii Gari"

    Kupitia miwani nyeusi aliyovaa Nisha yenye uwezo wa kuona kilicho nyuma yake pasipo kugeuza kichwa macho yake yalitua katika paji la Uso la Chaurembo na kukutana na Alama juu ya jicho lake ni ileile aliyoambiwa na Muuza Duka huku Chaurembo akivuta sigara. Bastola yake ikiwa tayari mkononi huku kamshika D Rose na kujificha nae huku akimsukuma ashuke kwenye Gari.



    ****************



    Macho yakiwa kwenye saa kubwa iliyo ukutani Mshale wa Sekunde ukiwa unatembea taratibu kuizunguka mishale miwili iliyokuwa kama imesimama kulingana na haraka ya mtazamaji, Muda ulikua hauendi kabisa huku usiku ukiwa bado mbichi, Ilikua imekwishatimia saa nane na nusu usiku na yalisalia takribani saa sita ili kutimia saa mbili na nusu asubuhi muda ambao aliahidiwa atapelekwa kwa yule anayemuwaza kila mara. Akijinyonga nyonga pale kitandani huku akijishika maziwa yake malaini yaliyokaa kwa muda mrefu pale kifuani kwake, Akitazama dari la kile chumba lililopambwa kwa rangi nzuri ya Pinki huku likiwa limebeba kawa nzito yenye kung'ara iliyobeba taa nyingi ndogondogo zinazotoa mwanga hafifu na kuzidi kupendezesha kile chumba. Akilegeza macho yake kama msichana wa miaka 20 huku akijilamba midomo yake iliyogeuka kuwa na rangi nyekundu kwa kuzoeshwa kupakwa rangi nyekundu ya midomo kwa muda mrefu. Tamaa ya kufanya ngono ilikuwa inamuwaka na kumfanya atamani kitu alichopewa miezi kadhaa iliyopita akipate tena kwa muda ule ila shida ilikuwa ni jinsi ya kumuona huyo muhusika ili ampe kile anachohitaji. Pesa zake na umaarufu wake haukuweza kumsaidia chochote kwa wakati huo alikua ndani ya chumba chake peke yake huku akimtegemea mtu mmoja tu amkutanishe na mwanaume aliyempa penzi ambalo hakuwahi kulipata katika maisha yake yote.



    Akiwa anahesabu mbao za zilizobeba paa la chumba chake, Juu ya kitanda kidogo chenye Godoro lililozeeka alikuwa akitamani asubuhi ifike mapema ili aweze kufanya biashara ambayo itatengeneza maisha yake. Mawazo yalizama na kujikuta yupo katika chumba chenye thamani ambacho hakuwahi kukifikiria kama yeye atakuwa mmiliki wa chumba kama kile. Sofa seti iliyokaa vyema juu ya zulia la rangi ya hudhurungi, Meza nzuri ya kioo iliyopambwa kwa ua zuri lenye naksi naksi za rangi ya Dhahabu huku mbele yake kukiwa na Tv pana aina ya Sumsung Plasma, Mkononi akiwa kashika glass ndefu yenye wine huku kavaa nguo nadhifu na kutengeneza tabasamu lililofanya mchoro wa herufi O uliozunguka katika mustachi wake mpaka na kuungana na ndevu za kidevuni. Mlio wa jogoo wa saa kumi ndio ulimshtua Dullah Bonge na kujikuta bado yupo katika chumba chake kile kile kilicho Tandale kwa Mtogole. Ni dili la kumpeleka Bibi Lizbeth mahali anapoishi Jorome huku akiwa amehaidiwa zaidi ya shilingi milioni kumi kwa kazi hiyo ambayo haihitaji cheti.



    *********** **************



    Maumivu makali katika Tumbo lake ndiyo yalimfanya aache kazi aliyokuwa akifanya kwa wakati huo na kuamua kurudi nyumbani kupumzika, Safari za mara kwa mara za kwenda chooni zilimkera na kuamua kutumia ndoo yake ambayo hutumia kuwekea maji ya kupigia mswaki kujisaidia. Kila muda uliipozidi kusogea ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya na kupelekea kupoteza nguvu. Sauti ya kusukumwa kwa mlango na sura ya Jalia kuingia ndani ndicho kilimfanya kujikaza na kuketi vizuri pale kwenye kiroba anachotumia kulalia.

    "Mpenzi vipi nimekumiss nimekuja unitibu"

    Jalia alimsemesha Jorome huku akivua nguo na kuzitupa pembeni bila kujali vumbi lililopo pale ndani. Jorome akilazimisha Tabasamu

    "Usijali ila kuna kitu nataka unisaidie kufanya kwanza"

    Jorome alimjibu Jalia na Kupelekea Jalia kusitisha zoezi lake na kusubiri hicho alichotakiwa kufanya, Jorome akainuka kwa kujikaza akatoa kile kiroba alicholalia.

    "Chukua huu mfuko naomba kanihifadhie huu mzigo kwenu"

    Alimpa jalia kile kiroba chenye fedha anachotumia kulalia.

    "Kwani kuna nini humo! Si tufanye kwanza halafu nitaondoka nao" Jalia alijibu huku akilegeza macho.

    "Hapana mpenzi peleka kwanza ndo uje" Jorome alimjibu Jalia jibu lililopelekea Jalia kuvaa nguo zake na kuchukua ule mfuko na kuondoka akiwa hajaridhika kwa kunyimwa kile alichokitegemea kutoka kwa Jorome kwa wakati ule.



    ************ ******************

    D Rose akiwa mbele huku nyuma yake kwa tahadhari mwanadada Nisha akiwa kakamata silaha yake vyema, Chaurembo bila kutegemea alijikuta mikono yake ikiwa juu kusalimu amri tayaari mdomo wa bastola ulikua ukigusana na mbavu zake, Bila ubishi akaingia kwenye Tax na safari ya kuelekea kusikojulikana ikaanza.



    Ndani ya chumba kidogo mwanamke asiye na mzaha anapokua kazini akiwa kasimama mbele ya chaurembo aliyeketi katika kiti, Maelezo ya Chaurembo ya kupigania Penzi ambalo ni la kijana aliyemtambulisha kama mume wake na kueleza Uvamizi wa Afande Hidaya katika Penzi lake uliopelekea kumjeruhi kwa Risasi katika mkono wake, Maelezo yale yalimvutia sana Nisha na kugundua kuna jambo la ziada katika Tukio lile, Ndio Chaurembo ni mtuhumiwa ila si muuaji wa Madame Neria kwa hiyo kuna muuaji. Inamaana muuaji atakua ni Afande Hidaya? Ni maswali yaliyozidi kusonga ubongo wake na kushindwa kupata jibu. Maamuzi ya kwenda kwa Jorome akiwa na Chaurembo ndiyo yalikuwa maamuzi sahihi kwa wakati huo.

    Kama mwanajeshi anavyoambiwa abebe kilichochake kwa ajili ya safari ya kwenda vitani ndivyo Nisha alivyombeba Chaurembo mpaka kwenye Difenda lilyopaki nje na safari ya kuelekea kwa Jorome ikaanza.



    ********** ************

    Kumkosa Jorome lilikuwa kosa kubwa sana kwake, Fedha aliyokuwa akimiliki baba yake na mamlaka aliyokuwa nayo katika kuitumia yalimfanya kujiona kama ni mwenye haki ya kufanya chochote chini ya hili jua pasipo kushindwa. Akiwa kasimama mbele ya kioo kikumbwa mtupu bila nguo akijitizama uzuri wa umbo lake, Chupi nyekundu aina ya G String ilipanda Taratibu kwa msaada wa mikono yake na kufunika eneo muhimu tu huku mkanda mwembamba ukipita katikati ya makalio yake, Sidiria ya rangi ya ile chupi iliziba vyema chuchu zake ndogo zilizochomoza kama embe bolipo na kutengeneza muonekano wa Mwanamke mwenye hadhi ya kuwa na kijana mtanashati na mwenye Fedha zake. Alipojitazama na kuridhika kwa nguo za chumbani alizovisha mwili wake ndipo alipoanza kuvaa nguo za hadharani. Jeans ya Rangi ya kibuluu iliyochanwa chanwa katika eneo la mbele la mapaja huku top nyeupe ikiziba eneo la juu na viatu vyeupe vikiziba vyema miguu yake, Pochi ilikwishakaa kwapani na harufu ya Marashi aina ya Passionate ilikua ikiburudisha pua za kila aliyepishana nae wakati akielekea katika kituo cha Tax.

    "Nipeleke Yombo Machimbo"

    Ni sauti laini ya Nima iliyotua kwa Dereva tax

    "Elfu ishirini sister"

    Dereva Tax alijibu huku akiingiza funguo wa gari katika sehemu ya kuwashia Gari

    ""Usijali twende, Ukiniwahisha nitakulipa zaidi"

    Tayari Gari lilikua likiitafuta Barabara ya kuelekea Wilaya ya Temeke.



    ********** ***********

    Kiasi kikubwa cha Fedha alichokuta katika begi la Jalia kilimshtua sana na kujikuta akikaa juu ya ndoo iliyo pembeni na eneo lilipo begi la nguo la binti yake, Ni zaidi ya milioni mbili zilikua ndani ya begi lile kukiwa na simu ya Bei ghali aina ya Sonyericson Experia II, Kidole kikibonyeza kitufe cha kuwashia ile simu mlio mdogo ukatotoka katika ile simu ukiambatana na Mwanga kisha simu ikawaka macho yake yakatua katika kioo kilichojaa Picha kubwa ya Mwanaume aliyekua akimtafuta kwa muda mrefu, Si mwingine ni Muhusika wa ujauzito alioubeba, Ndiye chanzo cha Kifo cha Mume wake na ndiye Mwanaume pekee aliyempa penzi la dhati.

    "Joromeeeee" Ni sauti iliyotoka kwa sauti na kukutana na masikio ya Jalia aliyekuwa tayari kafika mlangoni katika harakati za kuingia ndani. Kutajwa kwa jina la Jorome kulimfanya Jalia kusita kuingia ndani na kusimama mlangoni, Kivuli cha mtu pale mlangoni kilimfanya Mama yake kugeuka na kumuona Jalia kupitia upenyo wa mlango na kwa hasira akamuita.

    "We malaya kuja hapaaaa" Mary Stela aliita kwa hasira huku akisogelea Mlango. Jalia kwa woga akaingia huku kakubatia ule mfuko bila kujua una nini ndani.

    "Hizi pesa na simu umepata wapi?"

    Ni swali gumu sana kwa Jalia kwa wakati huo ila lilikuwa rahisi sana kujibika mbele ya Mama yake.

    "Niliokota Jana usiku" Jibu kutoka kwa Jalia lilikunjua mikunjo iliyokuwa imejijenga katika Sura ya Mary Stela na kumsogelea Binti yake.

    "Huo mfuko una nini?" Swali jingine lisilokua na jibu lilimyumbisha jalia na kukosa pa kuegemea na kujikuta kashikwa na kigugumizi kikali kilichopelekea Mama yake kumpokonya ule mfuko na macho yake kutua kwenye shehena ya Fedha zilizomshtua Jalia. Mawazo ya siku ya kwanza alipokutana na Jorome yalimrudia Jalia na kukumbuka ule mfuko huku akijilaumu kwa kosa alilofanya la kutoufungua ule mfuko kabla hajafika nyumbani.

    "Wewe umetoa wapi hizi Fedha?" Swali lenye mshangao lilikutana na Jalia ambapo lilizaa jibu lililorudisha hasira za Mary Stela upya.

    "Nimepewa na Jorome"

    "Umepewa na Joromeee! Jorome yupi? Huyu picha yake ipo kwenye hii simu? We mtoto umeanza lini umalaya?" Maswali mfululizo yalimtoka Mary Stela. Mfuko wa pesa ukiwa chini Tayari mkono mkakamavu umemkamata Jalia

    "Sasa nipeleke kwa huyo Jorome" Ni Amri ilitoka kwa Mama yake, Kwa wakati huo alikua akihitajika Jorome tu na si fedha.



    *********** **********

    Foleni kubwa ya Magari ndiyo ilimkera Dullah Bonge, Akiwa kakaa kwenye Daladala inayotokea Gongo La mboto huku akiwa mwenye mawazo, Hadithi za Dereva bila kuonyesha jitihada za kutafuta njia mbadala kama madereva wengine wanavyofanya ilipelekea Dullah Bonge kushuka katika ile daladala na kuchukua pikipiki maarufu kama Bodaboda na safari ya Kuelekea Hotel ya Fiesta Zone ikaanza, Baada ya dakika Thelathini alikua mbele ya wazungu watatu ambao ni Bibi Lizbeth, Serena na mpenzi wake Scotch, Tatizo la kutokujua lugha yeyote zaidi ya kiswahili na kimanyema lillimfanya Dullah Bonge kutoa ishara tu wakaingia kwenye Tax na Safari ya kuelekea Yombo Machimbo anapoishi Jorome ikaanza, Kichwani kwa Bibi Lizbeth kulikuwa kunamuwaza Jorome tu, Mamuzi ya kuondoka na Jorome kwenda nae Uswiss na kufunga nae ndoa ndiyo yalikua yakimsonga na alitamani Gari ipae na ajikute yupo mbele ya Jorome. Kila mmoja katika ile Gari alikua na mawazo Serena alikua akiwaza Zawadi atakayopatiwa na Bibi Lizbeth kwa kua anafahamu ni kiasi gani Bibi huyo akiwa na Furaha anavyotoa Fedha, Kwa upande wa Dullah Bonge alikua Tayari keshauaga umasikini huku akitathmini thamani ya ile tax aliyopanda na kuona hana hadhi ya kutembelea Gari kama ile, Alikua akihesabu magari waliyoyapita na kufanya Tathmini ni gari gani zuri atanunua ili aweze kuwapanga warembo wa Jiji la Dar es Salaam, abasamu pana likachukua nafasi kwa kijana wa Kimanyema Dullah Bonge.



    *********** ********

    Kimya kilichotawala katika ile nyumba kilimpa wasiwasi mkubwa na kuzidisha kasi ya kugonga mlango wa chumba kimoja bila majibu, Akitazama huku na huko kutazama kama kuna mtu wa kumuuliza bila mafanikio kulisababisha aendeleze jitihada za kugonga mlango ule. Akiwa kakata tamaa na kuamua kuondoka Mara Tax ikasimama karibu na nyumba ile akashuka msichana mrembo binti wa kimasai Nima na kusogelea kule ilipo ile nyumba aliyosimama, Hofu ilimtanda D Rose na kupapasa kilipo kitambulisho chake cha kazi na kukishika vyema.

    "Samahani dada wewe ni Mwenyeji hapa" Swali kutoka kw Nima lilimuondoa hofu D Rose.

    "Hapana mimi mwenyewe ni Mgeni"

    Kelele za Jalia akilia kutokaka na kipigo cha mama yake kiliwashtua na kugeuka kutazama kule sauti inapotokea, Mara Gari aina ya Difenda ikasimama na Nisha akashuka akiwa kamkamata Vyema Chaurembo, Macho ya Nisha yakatua kwa Chaurembo na kuona Tatizo lililo mbele yake, Akiwa anataka kuondoka sauti ya Chaurembo ikamsimamisha.

    "Unakimbia nini sasa wewe muuaji" Chaurembo aliamua kuutua mzigo w Tuhuma na kumbebesha Nisha pasipo kujua kama yeye ndiye muhusika halisi. Nisha kwa haraka bastola yake ikiwa tayari imemkaa vyema mkononi ilikua ikimuangalia Nima.

    Ilikua kama filamu mbele ya chumba cha Jorome, Jalia akiwa analia mama yake alimsukuma huku akifoka kama mbogo.

    "Nionyeshe huyo Jorome yuko wapi"

    Kutajwa jina la Jorome kulihamsha hisia za mauaji katika kichwa cha Nima na Chaurembo.

    "We unamuulizia Jorome wa Nini?" Nima aliuliza kwa hasira swali lililotua vyema katika masikio ya Mary Stela.

    "Jorome ni mume wangu na ndo mwenye huu mzigo" Mary Stela alijibu kwa kujiamini.

    "Mume wakooo?" Jalia alihamaki nakutengeneza mabishano makubwa eneo lile.

    Kelele zile zilizimwa na Gari iliyopaki eneo lile kwa kasi kisha mwanaume mwenye mwili mkubwa aliyeshika bastola vyema huku kamuelekezea mwanamke mnene si mwingine ni Mama Mutamegwa akiwa na mumewe.

    "Nionyeshe huyo Jorome aliyekupa hiyo mimbaaaaa"

    Mzee Mutamegwa aliongea huku akitetemeka na sauti yake isiyo na mzaha. Matukio mfululizo yalisababisha Nisha kuomba msaada kituo kikuu na Gari ya polisi iliyo na Askari wa kutosha wenye silaha ikawasili na kutawanya watu waliojaa eneo lile. Mzee mutamegwa alikua chini ya ulinzi huku wahusika wengine katika lile tukio wakiwa wamekalishwa chini.

    Mlango wa Jorome ukagongwa kwa muda mrefu bila kufunguliwa maamuzi kutoka kwa mkuu wa polisi akiwa na Mwenyekiti wa mtaa wakaamua mlango uvunjwe, Baada ya mlango kuvunjwa askari wakaingia huku silaha zikiwa tayari kwa Jambo lolote. Mwanaume akiwa kavaa jeans nyeusi miguu ikiwa juu ya kiroba na mwili ukiwa ardhini alikua kalala kimya. Kwa Tahadhari askari akasogea na kufungua dirisha Mwanga ukakikumba kile chumba Mkono wa askari ukagusa kifua cha Jorome kupima mapigo ya moyo.



    Wingi wa watu eneo lile ulimshtua Dullah Bonge na kujenga tabasamu la uongo huku akiwaashiria wale wazungu washuke katika Gari huku akimuashiria bibi Lizbeth nyumba anayoishi Jorome, Bibi Lizbeth akakimbilia katikati ya wale watu huku akijipenyeza kuelekea katika nyumba anayoishi Jorome, Macho yake yakatua katika machela juu yake kalala mtu aliyeonekana amekwishafariki muda mrefu sana. Bibi Lizbeth kama kichaa akakimbilia na kuzuia ile machela huku akilia. "He iis Dead" Ni sauti ya Askari iliyoamsha kilio kikubwa kilichopokewa na wanawame waliokuwa eneo lile.



    Msiba msiba msaibaaaaa, Ni msiba mkubwa wa Jorome aliyekufa kwa ugonjwa wa Kipindupindu, Kwa huzuni akitembea kwa upole huku machozi yakilowanisha mashavu yake D Rose alikua akikumbuka utamu aliopatiwa na Jorome na wakati huo alikua keshanyamaza mileleeee.



    Napenda kushukuru wale wote waliokua wakifuatilia hadithi hii



    *********** MWISHO *****************







0 comments:

Post a Comment

Blog