Simulizi : Mwanamke Mwenye Kovu Jeusi
Sehemu Ya Pili (2)
Nilitoka kwenye zile ofisi za mamlaka ya mawasiliano na kuingia kwenye gari yangu ndogo tayari
kulekea ofisini ili kujua pia wenzangu ni kipi wamekipata maana tuliahidiana ya kwamba saa 6 wote
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
watatu mimi Gerald na Amina tuwe ofisini tufanye kakikao kadogo kujua ni kipi cha kufanya,
niliendesha gari yangu taratibu huku nikwa nazungumza na simu nakumbuka nilipofika pale
magomeni kulikuwa na foleni kubwa sana kwani msafara wa rais wetu ulikuwa unapita basi
nilipungumzamwendo na kuendelea kuzungumza na simu huku nikiwa nimeshusha kioo cha gari
yangu kwani air condition yangu ilikuwa imeharibika mara ikaja pikipiki aina ya baja kwa nyuma
kwenye ile foleni ya magari ikiendeshwa na mtu mmoja ambaye alikuwa amevalia helment ya blue
kichwani akiwa amevalia utazani ni mtu aliyekuwa anaenda safari ya mbali sana kwani kwenye
mikono na miguu alikuwa amevaa plastiki za kuzuia michubuko ile pikipiki ilikuja mpaka usawa wa
gari yangu kisha Yule mwendesha pikipiki akanitazama kwa sura ya tabasamu hapo ndipo
nilipogundua ya kwamba ni mwanamke akanisalimia kaka habari, nilimuitikia kwa kichwa kwani
nilikuwa nazungumza na simu bado, mara akatupia bahasha mule ndani kwenye gari yangu halafu
huyo akaondoka kwa mwendo wa kasi nilishituka nikajikuta nawepa pembeni simu yangu na
kuiangalia ile bahasha huku nikimtazama na Yule mwanamke kwenye kioo cha gari yangu kwa mbele
akiondoka bila hata kusimama pale kwenye mataa kiasi kwamba mpaka akasababisha ajali maeneo
yale kati ya daladala nagari moja lililokuwa limebeba maji ya kunywa ya uhai ambalo lilionekana
lilikuwa ni gari la kusambaza maji sehemu mbalimbali hapa mjini.
Niliitazama ile bahasha kwa wasiwasi sana kwa juu ilikuwa imeandikwa jina langu halisi, huyu mtu
amelijuaje jina langu halisi? Hii ni hatari potelea mbali nikaichukua ile bahasha na kuichana kujua
mule ndani kuna nini, nilkuta kuna ujumbe uliokuwa umeandikwa kwa rangi nyekundu uliokuwa
ukisomeka
Dear Siwah Erique
mimi naitwa Mwanamke mwenye kovu jeusi kwa leo nilikuwa nakusalimia tu na kukuambia ya
kwamba karibu sana kwenye himaya yangu nitaludi tena kukusalimia vizuri baaadaye kazi njema.
Nilipousoma ule ujumbe nilishangaa sana kisha nikajikuta nacheka mwenyewe,amakweli mimi ni
mjinga yani nashindwa kumkamata mtuhumiwa mbele yangu kweli kazi ipo mwaka huu sawa na aje
tu mimi hata simuogopi hata kidogo. Upande wetu uliruhusiwa na trafiki nikaondoa gari yangu
taratibu kuelekea stesheni ambapo ndipo ofisi zete zilipokuwa.
Niliwakuwa wenzangu wameshafikia wakinisubili mimi, tuliingia kwenye ofisi ya Amina kwa ajili ya
kufanya kakikao kadogo cha watu watatu, alianza Gerald kuzungumza ya kwamba hakumkuta
Zainabu kazini siku ile kwa taarifa aliyoikuta ni kwamba alikuwa mgonjwa, alipoomba namba yake
ya simu alimpigia ambapo alipokea mdada mmoja aliyejitambulisha kama mdogo wake ambaye
alisema ya kwamba Zainabu jana aliludi toka kazini akiwa hajisikii vizuri wakampeleka hospitali
ambapo yupo hoi wodi ya wagonjwa mahututi alizidi kuleza Gerald ya kwamba allipofika pale
muhimbili na kujitambulisha aliambiwa ya kwamba kuwa Yule mwanamke jana imeonekana alipigwa
na kamera ya mionzi ambayo ndio imekausha damu yake na pale alipo uhakika wa kupona ni mdogo
sana.
Basi baada ya kueleza hayo na mimi nilieleza ya kwangu toka pale ofisi za mamlaka ya mawasiliano
mpaka kule barabarani nilipotupiwa ile bahasha na Yule mwanamke mwenye gari yangu kisha
tukaanza kujadili jinsi ya kupambana na Yule mwanamke, Amina alitueleza ya kwamba Yule
mwanamke tu ndio atakuwa amempiga hiyo mionzi Zainabu, hivyo basi inabidi tuongeze umakini,
tulijadiliana na kufikia mahitimishoa ya kwamaba ni lazima kesho asubuhi tuanza kumsaka, kaka hili
zoezi ni gumu ten asana tututa,tafutia wapi? Hata pa kuanzia hatupajuai kila anayegusa anga zake
anaondoka duniani hapa nilipo mimi sina hata raha kwa maana sijui hata mtoto wa watu Furaha
anaendeleaje.Gerald alilaamika tulikubaliana tukaanze kumsaka mitaaa ya mbezi beach ambapo
ilisemekana kuwa alikuwa akiishi na mdogo wake Zainabu kabla hajafa, tulielewane tukajaribu kwa
siki nzima ya kesho kwenda kufanya upelelezi upande wa kule.
Wakati tumemaliza kujadiliana mara simu ya Gerald ikaita kuangalia alishangaa kuona namba yake
simu ndio ilikuw ikimpigia, jamani nashangaa hapa simi inaita namba inayoonekana kwenye screen ni
namba ya ngu what is this? Mimi hata kuipokea naiogopa alisema huku akiiweka wenye meza pale
ofisini mara Siwah akaichukua na kuipokea haraka haraka enhe nani mwenzangu? Ni mimi
mwanamke mwenye kovu jeusi sauti iliongea upande wa pili huku ukiacha isikike sauti Siwah
aliiweka simu loudspeaker ili wasikie wote, walishangaaa sana kusikia yale mazungumzo yao ambayo
yalikuwa hayana hata dakika 2 yakizungumzwa kupitia ile simu yakiwa yemerekodiwa mwisho wa
yale maongezi Yule dada alisema ya kwamba nilikuambia ujitoe kufuatilia hili jambo lakini
inaonekana wewe sio mwelewa si ndio? Sasa nakusubili kwako ile sauti ya kike ilizungumza kisha
ikakata simu. Gerald alijihisi kuogopa sana pale pale wakaanza kujadili hivi huyu mwanamke
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
inakujae haya mazungumzo yetu tunayazungumza hapa hapa na anayapata hapa hapa? Kwa staili hii
hatufanyi lolote sasa nilijikuta nazungumza kwa ukali kidogo, usikasilike hapa ni kujua haya
maongezi anayapataje?
hebu tusachi kwanza humu ndani Amina alizungumza huku akianza kuangalia kila mahali kuona
kama kuna kinasa sauti chochote…!
****************************
Amina aliangalia kila mahali bila kuona kinasa sauti chochote huku mimi na Gerald tukiwa tu
najaribu kujadili kuhusu hatima ya Yule mwanamke mwenye kovu jeus,i basi wakaafikiana ya
kwamba kwa usalama zaidi wa Gerald ni bora siku hiyo asiende kulala kwake kwa maana siku zote
mambo aliyoyazungumza Yule mwanamke yalikuwa yanatokea, waliagana nakuelekea nyumbani
kwa Siwah kwa ajili ya kulala.
**************************
Kesho yake asubuhi na mapema baada ya kuwasili ofisini mimi Gerald na Amina tulipewa askari
kanzu watano wa ziada kwa ajili ya kuelekea maeneo ya mbezi beach kujaribu kumtafuta mwanamke
mwenye kovu jeusi, tuliaacha wote gari zetu pale kwenye maegesho ya magari ya kazini na kuchukua
gari zingine kabisa za kazini lakini zenye namba za kiraia ambazo huwa tunazitumia kwenye shughuri
zetu mbali mbali maalumu ambazo hatukupenda kujulikana, tulichukua gari tatu moja nikiwa nayo
mimi na dereva nyingine Amina na nyingine Gerald akiwa na askari kanzu mmoja, bai tulienda moja
kwa moja kufika mbele tukagawana majukumu, mimi nitakuwa napita kwenye ma ofisi mbali
mbali,Gerald kwenye nyumba za wageni na nahotel huku Amina tukimpa kazi ya kupeleleza
ufukweni
,nilipita kwenye viwanda na ofisi mbalimbali nikijitambulisha kisha na kuomba list ya wafanyakazi na
picha zao ambapo nilikuwa najaribu kuangalia baadhi ya wafanyakazi na kuwahoji kidogo na
wengine kuwaahidi ya kwamba nitawatafuta wakati natoka kwenye kiwanda cha kutengeneza dawa
za mswaki na mafuta ya mwili mara nikasikia ile simu ya Furaha mchumba wa Gerald ikiita kwani
mpaka kipindi hicho ilikuwa bado nonayo mimi toka juzi tulipotoka nyumbani kwa Gerald kuangalia
kumbe ilikuwa ni meeji imeingia ikisomeka ya kwamba niliwaambia mjitoe kujihusisha na kunifuatilia
mimi sasa subilini majibu baada ya masaa kadhaa,kuangalia kama kawaida namba ya aliyetuma
haikuonekana nikajua tu atakuwa Yule dada mwanaharamu tunayemtafuta, nilitafakari nikaona
nikiwajulisha wenzangu nitawaondoa kwenye morali ya kufanya kazi, nikaona si mbaya nitawajulisha
baadaye tukikutana,wakati nikiendelea kutafakari mara simu yangu ya mkononi ikaaita kuangalia
kumbe alikuwa ni Yule injia wa pale mamalaka ya mawasiliano, “Ndio injinia nakusikiliza, sasa
kakaleo asubuhi niliitegesha hiyo namba hivyo nimefanikiwa kuipata namba ya simu ya huyo mtu
anayewasumbua na pia inaonyesha muda huu anapatikana mitaa ya bahari beach inspekta, alimalizia
kuniambia yule injinia wa mamlaka ya mawasiliano. Sawa kaka basi naomba unitumi hiyo namba
yake ili tuanze kumtafuta kwa maana tupo mitaa ya karibia na hapo unaposema alipo sasahivi,
nilimjulisha Yule injiniaalinielewa na baada ya kama dakika 2 alinitumia data zote ile namba ya simu
jina lililotumika kuisajili ile laini na umbali ambapo ilionekana Yule mwanamke yupo kutokea kwenye
mnara wa simu, nilimjibu kwa kumshukuru kisha nikawapigia simu Gerald na Amina kuwaambia ya
kwamba tukutane karibia na hayo maeneo si chini ya nusu saa kwa ajili ya kuhakikisha tunamtia
nguvuni Yule mwanamke, basi tulijongea pale lile eneo ambalo lilikuwa kando kabisa mwa bahari ya
hindi, mimi nikiwa wa kwanza kufika, tulipofika lile eneo niliwambia vijana wangu niliokuwa
nimeongozana nao kuwa makini kwani tupo kwenye eneo hatari sana,tulikaa pembeni kidogo
kwenye mwamba Fulani uliokuwa pale ukingoni mwa bahari tukiwa tukiwasubiri kina Gerald pamoja
na Amina, mara nao walifika lile eneo bila kukawia kila mmoja akitokea upande wake,alipofika lile
eneo Amina aliliangalia kisha akaniambia kwa sauti ya majonzi, “maeneo hay ndipo tulipoikuta maiti
ya marehemu Yule mdogo wake na Yule dada anayefanya kazi benki” kisha akaendelea nahisi huyu
mtu atakuwa yupo haya haya maeneo,mwili ulinisisimka sana kusikia vile kwani kumbe nilikuwa
kwenye eneo hatari ambapo muda wowote umauti unaweza kutukuta, haya hakuna muda wa
kupoteza hapa cha msingi tuanze kumsaka haya maeneo kwa maana nimeambiwa ya kwamba yupo
maeneo haya haya, nilianza kuwaambia ili tuanze kuwajibika huku kila mmoja wetu nikimwambia
achukue tahadhari, tulipnaga mikakati pale na kungalia asili ya lile eneo kiukweli kulikuwa na watu
kwa mbali ndani ya bahari wakiendele na shughuli zao za uvuvi hasa mida ile nazani walikuwa
wakikagua tu zana zao za uvuvi kwa ajili ya maandalizi ya uvuvi siku ile usiku, lile eneo lilikuwa
tulivu sana kwani kwa muda wa takribani kumi tulizokaa pale tukipanga mipango yetu mbalimbali
hapakuonekana mtu wa aina yoyote kupita lile eneo, kweli haya yatakuwa ni maficho yake lakini
katika mazingira haya mbona kuna wavuvi tu? Sioni nyumba wala mwatairi ya magari, wala sasa
anaishi vipi? Gerald alijikuta akutuambia pale, au inawezekana huyo injinia wa mamlaka ya
mawasiliano nchini amenunuliwa au ni huyo mwanamke pia amefanya utundu wake kwenye simu ili
kutupoteza jama maana hili eneo huyo mtu ataishi wapi? Aliendelea kusisitiza Gerald, ndio
inawezekana huyu mwanamke itakuwa alianza kushituka au alihisi kuwa tumekaribia kumpata ndio
akafanya hivi, haiwezekani hili eneo halina mtu bwana Amina pia alendelea kusisitiza.
Ilinibidi niwashushe munkari kidogo ili tuweze kuelewana, sawa jamani yote yanawezekana hapa cha
msingi ni tufanye yafuatayo tutawanyike kutokea hapa kuelekea sehemu mbali mbali kama yupo
maeneo haya tutampata sawa na kama hayupo basi tuendelee na zoezi letu
Tulitawanyika pande zote huku tukiambina kwa yoyote atakayohisi au kumuona basi atujulishe
mapema sana iwezekanavyo, tuliendelea na lile zoezi la kumtafuta mara kwa umbali kama wa mita
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
70 nilimuona mwanamke akiwa chini amelala kwenye mchanga ule wa kando kando ya bahari huku
akiwa kama ni mtu asiyekuwa na nguvu akiomba msaada alionekana kama ni mtu ambaye kuna
jambo baya lilikuwa limemkuta ,basi pale pale nilimuamrisha mmoja wa wale askari kanzu niliokuwa
nimefuatana nao awajulishea kina Gerald na Amina wote wafanye kuja upande ule tuliokuwepo huku
sisi tukizidi kumsogelea lakini kwa tahadhari kubwa sana kwani tulijua fika atakuwa ni mwanamke
mwenye kovu jeusi ameamua kutumia ile mbinu baada ya kuona tayari tumeshagundua makazi yake,
nilimuambia Yule askari kanzu atoe maelekezo waje upande ule ila wafanye kama vile kuzunguka
kwani wote tukielekea upande mmoja anaweza kutuzidi ujanja kwani wote tulikuwa hatujui alikuwa
na silaha gani pale..!!
Tuliendelea kumsogelea Yule dada kwa tahadhari kubwa sana huku kila mmoja wetu akiwa ameweka
silaha yake tayari kwa lolote litakalotokea,tulizidi kumsogelea Yule dada moaka zikabakia kama mita
kumi hivi huku tukiwa tumemzunguka, pande zote dada Yule alionekana wazi akiwa hana nguvu hata
kidogo kwani likuwa akijaribu kujivuta lakini alishindwa, Gerald ambaye alikuwa upande wa kulia
tukiwa tunaangaliana mara nikasikia Gerald akitamka kwa nguvu, my god mpenzi wangu Furaha
jamani muacheni mpenzi wangu alizidi kusema kwa sauti ya juu Gerald, basi tuliacha kumuelekezea
silaha Yule dada wote kisha tukamskimbilia kwa kasi Yule dada.
Tulipofika tulimkuta hali yake ikiwa si nzuri kwani alikuwa anaonekana ni mtu aliyechoka sana huku
akiwa kama vile amekimbia mateso Fulani,ohh mpenzi wangu jamani kumbe alikueleta huku
alizungumza Gerald huku machozi yakiwa yakimtiririka,bila kupoteza muda nilinyayua simua yangu
ya mkononi na kuwapigia simu hospital ya taifa ya mwanayamala ili waje na gari la kubebea
wagonjwa waje kumchukua kwani hali yake ilikuwa ni mbaya sana,Gerald alikuwa akijaribu
kumsemesha lakina Furaha hakuwa hata na nguvu ya kuzungumza alikuwa akijaribu kuonyesha kwa
ishara na macho pande wa kaskazini ambapo sisi wote tulipojaribu kupaangalia hatukuona
kitu.tuliamua kufanya maamuzi ya haraka haraka kwa kuwa tuliona pale muda unaenda na kwa
foleni ya jijini ingewezekana akatufia mikononi wakati tukiwa na usafiri hivyo tuliamua kusogea na
gari tuliyokuwa naye ili tukutane nao barabarani
*********************************
Tulimfikisha hospitali ya mwananyamala huku hali yake ikiwa bado si nzuri wauguzi na madakatari
walimpeleka wodini na kumutundika na dripu za kumuongezea nguvu kwani ilionekana fika alikuwa
hajapata cjakula kwa zile siku mbili alizokuwa kwa Yule mateka,sisi tulitoka nje na kukaa kusubili
ripoti ya madaktari watuambie alikuwa anaendeleaje tulikaa pale kwa muda wa takiribani saa 2 ndipo
muuguzi akatoka nje na kutuambia kwa muda ule tungeweza kuingia ndani na kwenda kumsalimia
tuliingia kwa ukweli tulimkuta akiendelea vizuri sana japo aliweza kuzunguma maneno mawili ma
tatu japo kwa shida shida sana tuliwashukuru ma daktari na kuwataka sisi tuende huku tukiahidi
kuludi kesho yake kwa ajili ya kumchukua mahojiano kuhusiana na mwanamke mwenye kovu
jeusi..!! mimi na Amina pamoja na wale askari kanzu wengine tuliondoka huku tukimuacha Gerald
akiwasubili ndugu zake na Furaha waje wamuone kisha na yeye aende kujipumzisha.
*****************************
Niliamka asubuhi na mapema kama kawaida yangu baada ya kufanya mazoezi ya viungo asubuhi
kwa kufuatiliza kipindi cha mazoezi cha kituo cha hbari cha terevisheni cha ITV nilienda kujoga na
kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kazini, nilifika ofisini asubuhi na mapema baada ya kusaini kitabu
cha mahudhurio nilielekea moja kwa moja ofisini kwangu nilishika faili la ile kesi ya huyu
mwanamke aliyejiita mwenye kovu jeusi na kuanza kulipitia hatu kwa hatua huku nikijaribu kunote
baadhi ya vitu amabvyo nilihisi ya kwamba vitakuwa vya muhimu kwa siku hiyo kabla sijaelekea
hospitali kwenda kumuona Furaha.niliendelea kufanya ule uchambuzi kwa kama dakika 20 hivi
ndipo alipoingia Amina ofisini kwangu kunijulia hali na kuniambia ya kwamba kama nipo tayari basi
tutoke wote tuelekee hosptali ya mwananyamala kwenda kumjulia hali mgonjwa ikiwezekana na
tufanye nae mahojiano kidogo kisha sisi tuendelee na majukumu mengine,nilimuelewa Amina tulitoka
wote ambapo tulielekea mwanayamala hospital tukiwa na usafiri wangu binafsi ambapo tulipitia
kwenye mgahawa mmoja mitaa ya kinondoni kwa ajili ya kupata kifungua kimywa kwanza kisha
ndio tuendelee na safari yetu. Wakati tupo pale tunakunywa chai kwa pembeni yetu alikuwepo dada
mmoja ambaye alikuwa kama mtu aliyekuwa hajiamini kabisa huku akiwa yupo makini akifuatilia
maongezi yetu, ila sisi ahtukumjali mpaka pale tulipokuja kutoka nje kuendelea na safari ndipo
ujumbe wa meseji ulipoingia kwenye simu yangu ya mkononi kwanza sikutaka kuusoma kwani ni
vibaya kuendesha gari huku ukiwa unasoma meseji au unazungumza na simu. Tulifika hospitali
ambapo tulimkuta Gerald akiwa tayari ameshafikaakiwa nje ya wodi huku akiwa na na dada yake na
Furaha sura ya Gerald ilionekana ikiwa ni yenye tabasamu bashasha, karibuni sana jamani
alizungumza dada yake na Furaha kwa rafudhi ya kihehe ambaye baadaye nilikuja kugundua ya
kwamba alikuwa akiitwa Witness,tuliingia wodini ambapo tilikuta daktari na nesi wakijaribu
kuangalia maendeleo ya afya yake “samahani daktari tunaweza kumchukuwa mahojiano kidogo?
nilimuuliza daktari baada ya kuona tayari wameshamaliza kumungalia maendeleo ya afya yake, ndio
ila mpaka kwa sasa hali bado haijamludi sawa hivyo basi inabidi mumulize taratibu hasa itakuwa
vizuri kama huyu mpenzi( wake huku akimshika shati Gerald na kumvuta mbele yetu) yeye ndio
kama akifanya hiyo kazi alizungumza Daktari, basi Gerald alikaa kwenye kitanda na kumvuta mpenzi
wake Furaha na kumlalia kwenye mapaja kisha akaanza kumuuliza maswali madogo madogo huku
akimnywesha uji ili azidi kupata nguvu. Furaha alijaribu kutuelezea japo kwa shida sana kwamba
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule dada hakuwahi kumuona kabla ila kwa sasa akimuona atamkumbuka alijaribu kutueleza ya
kwamba anamakao yake kwenye yumba moja iliyopo kando mwa bahari mitaa ya mbezi
beach.wakati mazungumzo yanaendelea ghafra aliingia nesi akiwa amevalia sare ya nguo za kinesi na
kutuomba tumpishe kidogo kuna dawa anataka kumpa mgonjwa Yule nesi alionekana akiwa na
wasiwasi Fulani hivi, basi bila ya hiyana tulimpisha wote tukatoka nje alichomoa sindano na
kumchoma Furaha kisha akaondoka zake baada ya kama dakika 5 hivi na sisi ndipo tulipoludi wodini
ile kufika tu, tukakuta hali ya Furaha imebadilika tena asaivi imekuwa mbaya zaida hata ya jana
tulivyomleta pale hospitali palepale Witness akatoka nje haraka na kwenda kumuita nesi kwenye
chumba chao nesi alikuja na kustaajabu, vipi tena hapa imekuaje? Alianza kusema jamani jamani
mpenzi wangu mmemfanyaje yani mmemchoma sindano baada ya dakika tano tu amekuwa zezeta?
Alizungumza Gerald kwa machungu machozi yakimtiririka hapana sio sisi alianza kuruka nesi mbona
sisi tulishapita mida na dakitari yalianza pale mabishano kati ya Witness, Gerald na Yule nesi,mimi
niliona ya kwamba tukiendeleza yale mabishano wakati hali ya mgonjwa inazidi kuwa mbaya sio
vizuri basi pale pale nikatoa simu ili niwapigie muhimbili wajiandae kumpokea mgonjwa mahututi
ikiwa kama order kutoka kituo cha polisi, wakati naitoa ile simu ndipo nikakumbua ya kwamba kuna
msejeji iliingia kipindi tumetoka kunywa chai pale kinondoni halafu sikuisoma kipindi tunakunywa
chai kwanza nlitaka kuiacha lakini nikaona sio mbaya ngoja niisome mungu wangu sikuamini ule
ujumbe niliousoma kwenye ile simu yangu….!!!
Ujumbe ulikuwa umekuja kwa namba isiyofahamika ukisema ya kwamba “najua mnaenda
kumchukua mahojiano Furaha ila haitawezekana mwanamke mwenye kovu jeusi” mwili
ulinisisimuka kwani nilijua ya kwamba basi atakuwa ni yeye aliyejifanya nesi pale hospitali na
kumchoma sindano ile Furaha ili kupoteza ushahidi,mungu wangu tatizo la kutokumjua sura huyu
mtu ndio kunasababisha haya yote haiwezekani mtuhumiwa anatukimbia hapa hapa, nilijikuta
nasema kwa sauti ya chini chini huku nikisubili kuzungumza na simu upande wa pili,baada ya
kumaliza kuwataarifu hospitali ya muhimbili furaha aliingizwa kwenye gari ya wagonjwa tayari kwa
ajili ya kupelekwa muhimbili, huku mimi Amina na Geral tukitoka nje kwa ajili ya kushauriana kipi
hasa cha kufanya ambapo Gerald alikuwa kama amechanganyikiwa vile kutokana na lile tukio,ilibidi
niwaeleze kila kitu kuhusu ule ujumbe nilioupata kutoka kwenye namba isiyojulikana, hivyo basi
niliwaomba tusilaumiane bali tuwe makini na tumuombe tu mwenyezi mungu Furaha afifariki kwani
yeye ndio atakayeweza kutusaidia ile kazi ya kumkamata Yule mtuhumiwa hatari anayefanya mauaji
ya hovyo kila siku pale jijini.
Tulimaliza kupanga baadhi ya mikakati kisha na sisi tukajipakia kwenye gari kwenda hospitali ya
taifa ya muhimbili kwenda kuona ni kipi kilikuwa kinaendelea kule. Ki ukweli tulikuta hali ya
mgonjwa ikizidi kuwa mbaya tena mbaya sana kwani japo kuwa alikuwa amelazwa kwenye wodi ya
wagonjwa mahututi lakini pia walituamba hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakiende taratibu
sana kwa mwendo wa kusua sua sana hivyo tumuombe sana mwenyezi mungu kauli ile ilizidi
kumchangaya Gerald na sisi pia kwani pale ndio ilikuwa mahali ambapo tuliona panafaa kupata
habari zote tulizokuwa tunazihitaji basi tuliona hakuna jinsi zaidi ya kumuomba mwenyezi mungu tu
amsaidie lakini wakati bado tunaendelea kushauriana mara akatoka Witness ambaye alikuwa ni dada
wa Furaha alitoka nje akija pale tulipokuwa tumekaa huku akilia sana pale pale indicator ikanigonga
kichwani ya kwamba Furaha atakuwa tayari ameshatutoka, basi Gerald baada ya kusikia hivyo
alianza kulia sana pale pale ilibidi tufanye zoezi la kumuondoa Gerald na Witness pale hospitali.
*************************************
Baada ya kumaliza msiba wa mpenzi wake na Gerald nakumbuka vizuri sana Gerald alipewa likizo
ya mwezi ofisi hivyo basi zoezi la kuendelea kumsaka Yule mwanaharamu aliyejiita mwanamke
mwenye mkono wa bandia lilibakia mikononi mwangu na Amina huku mkuu wetu kazini akizidi
kulalamika kabisa kwa nini tunashindwa kumtia kizuizini wakati kuna wahalifu wengi zaidi yak wake
ambao tuliweza kuwazibidi tena kirahisi tu sana, nilimhakikishia mkuu wetu wa kazi atupe muda
zaidi kwani Yule dada alionekana ni mjanja sana hivyo tusipokuwa makini anaweza kutumaliza wote
hadi yeye, mkuu japo alikuwa ni muelewa ila alikuwa ni mtu mwenye papara sana alitaka kila jambo
limalizike kwa muda aliotaka bila hata kuangalia uzito wa jambo lenyewe na aina ya watu au mtu
tuliyekuwa tukikabiliana naye. Basi tulimaliza maongezi na mkuu wetu huku tukitoka ofisini mimi
nilimwambia Amina ya kwamba naelekea nyumbani kwa Gerald maana aliniomba siku ile nimsindike
makaburini kwenda kuangalia kaburi la mpenzi wake, basi tulikubaliana vizuri yeye Amina huku
nikiwa nimemuagiza aelekee kule maeneo ya mbezi beach karibia na tulipomkuta marehemu Furaha
akajaribu kama kufanya uchunguzi kwa njia yoyote ile kwani angeweza kuambulia lolote, kwa
sababu ni mtu wa pili sasa anakutwa mitaa ya kule kwani hata mdogo wake na Zainabu Yule mdada
aliyekuwa akifanya kazi benki ya biashara mwili mwa maehemu mdogo wake ulikutwa maeneo
yaleyale,basi tulikubaliana akaniahidi nisijali ataenda na atahakikisha anakuwa makini sana,
alichukua baadhi ya camera za cctv akaziweka kwenye begi lake baadhi ya vinasa sauti pamoja na
nyaraka zingine ndogondogo kwa ajili ya kwenda nazo kulepamoja na bastola moja ili ikiwezekana
zile kamera akazifunge mahali ziwe zinachukuwa matukio yote ya mahali pale, pia alichukua kile
kiatu ambacho tulikihisi ni cha Yule mwanaharamu ambacho tulikikuta kule nyumbani kwa Gerald
siku ile ambapo alikidondosha pindi alipoenda kumteka marehemu Furaha. Baada ya hapo tuliondoka
wote kwa pamoja nikimpa lifti na kwenda kumucha mwenge kisha mimi nikaelekea zangu nyumbani
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwa bwana Gerald kwenda kumchukua ili tuelekee makaburi ya kinondoni kwenda kutembelea
kaburi la mpenzi wake furaha ambaye kutokana na maelezo ya madaktari tuliamni ya kwamba
atakuwa amekufa kwa kuchomwa sindano ya sumu ili kuficha ushaidi na Yule mwanamke aliyejiita
eti anakovu jeusi. Bai nilifika nyumbani kwa rafiki yangu Gerald nikamkuta akiwa tayari
ameshajiandaa akiwa amevalia t-shirt nyeupe yenye picha ya marehemu Furaha mbele ya
kifua,suruali nyeupe huku pia akiwa amejifunga kitambaa cha rangi yeupe mkononi sikujua alikuwa
akimaanisha nini.
Tuliondoka taratibu kutokanna nafoleni ya jijini mpaka mida ya yaa 5 asubuhi tukawa tumeshafika
tayari makaburini, basi tulipofika kwanza tulitafuta mahali tukapaki gari kisha tukaelekea kwenye
kaburi lile ambapo baada ya kufika Geral alisali juu ya lile kaburi kisha akawa kama vile anafanya
usafi na kupanga mashada juu ya lile kaburi, wakati anaendelea nilisikia sauti ya mlinzi wa pale
makaburini akiniita kwa mbali huku akionyesha ishara ya kwamba gari langu nilikuwa nimelipaki
vibaya kuna mtu ambaye tulikuta gari yake imepaki pale aina ya escudo rangi ya kijani alidai alikuwa
anataka kulitoa gari lake basi sikuwa na jinsi zaidi ya kumwambia Gerald anisubili naludi baada ya
kama dakika 5 nilifika na kulitoa gari kisha nikampisha Yule mtu ambaye alikuwa anatoka mule na
gari lake wakati naludi kwa mbali nilimuona Gerald akiwa amepiga magoti akisali huku akiwa
amepiga magoti na mwanamke mkmoja jirani yake nahisi alikuwa hajamuona kwanza sasa nilianza
kujiuliza Yule atakuwa ni nani? Maana tulienda watu wawili tu na Gerald hakunambia kama alikuwa
amemuambia mtu yoyote wakutane pale,baada ya Gerald kufngua macho alishituka sana kisha
nikawasikia kwa mbali kama wakiwa wanazozana na Yule mwanamke basi na mimi nikaongeza
mwendo kuwahi lile eneo kwa maana niliona kama vile mazozano yamezidi na sio vizuri kwa mtu
kama yeye kwani ule ulikuwa muda mzuri sana kwake kutuliza akili Yule mwanamke aliponiona
nakuja kwa kasi kwanza alishituka kisha akachoma kama kifaa Fulani chenye insha nyembamba kwa
mbele akamlushia nacho Geral mkononi kisha huyo akakimbia zake kwa kuluka ukuta upande wapili
nilifika na kumkuta Gerald akiwa tayari amesha kichomoa kile kifaa lakini mkono wake ukiwa kama
unavimba vile nilimuuliza Yule ni nani na kwa nini imekuwa vile?
Alinijibu ya kwamba Yule mwanamke ni Yule mwanaharamu ambaye ndio tulikuwa tukimtafuta na
pale anadai alikuwa ananisubili kwa hamu sana na siku yangu ilikuwa imefika huku akisisitizaya
kwamba kama tukitaka kuwa salama basi tuachane na ule mpango wetu wa kumfuatilia..!! nafsi
ilishangaa sana palepale nilijikuta nakosa mpaka raha inamaana nani kamuambia sisi muda ule
tungekuwa pale?na amejiamini vipi mpaka kutufuata mpaka pale? Je kwanini alimfuata Gerald pindi
mimi nilipoenda kuondoa gari kwenye parking ili aipite? Nilianza kuhisi sasa ya kwamba Yule
mwanamke hakuwa peke yake walikuwa wengi waliokuwa wanafanya ule michezo huku
wakishirikiana pia nilijiuliza Na kile alichomchoma nacho Gerald mkononi ni nini? Kwa maana
mkono ulikuwa kivimba tu..!! japo alikuwa ameshakichomoa je angekuwa bado ingekuwa aje…?
*******************************************
Nilimuambia Gerald tuondoke haraka kwani mahali pale palikuwa sio salama tena hatukujua Yule
mdada alikuwa amejipangaje kama aliweza kuja hadi pale makaburini na kuweza kutufanyia ule
ushenzi basi tusingeweza kujua alikuwa amejiandaje basi tulielekea kwenye gari nakuondoka zetu
huku tukipitia hospitali ya regency kwenda kunda kuangalia ule mkono Gerald alikuwa amechomwa
na nini? Basi tulipofika hospitali daktari alitueleza ya kwamba kile kitu kilichomchoma Gerald
kilikuwa na sumu kali sana kwanza Yule daktari wa kihindi alianza kutuangalia kwa wasiwasi sana
huku akishindwa hata kutuelezea akidai ya kwamba kwa kuwa tayari wameshampa dawa basi
inatosha, baada ya kumsisitizia ndipo akajaribu kutafafanulia kuhusu ile sumu ya kwamba ile ni sumu
hatari sana na inapatikana nchi ya vietnamu ambayo unapichomwa nayo usipokichomoa hicho kitu
ulichochomwa nacho ndani ya dakika kama kumi basi uwezekano wa kuendelea kuishi unakuwa
haupo kabisa,Yule daktari alisema yeye sio mzoefu sana ila anachokijua ni kwamba ile sumu huwa
wanaitumia huko nchini Vietnam kwenye mapigano yao ya jadi ambapo watu huwa wanaiweka
kwenye silaha zao za jadi. Tulijikuta mimi na Gerald tukistaajabu sana na kisha kuangaliana bila ya
kujua ni vipi imekua vile na ile sumu imeingiaje nchini.
Basi tulimshukuru sana daktari kwa matibabu yake kisha tukaondoka zetu ambapo tulipitia fast food
kupata chakula cha mchana kisha nikamludisha Gerald mpaka nyumbani kwake na mimi nikaelekea
nyumbani kwangu sikutaka hata kuludi kazini tena kwani nilihisi ya kwamba muda ulikuwa umeisha
na isitoshe ni bora niwahi nyumbani nikapumzike nifanye usafi kwani ni mara chache sana huwa
Napata muda wa kufanya usafi ukizingatia nilikuwa naishi mwenyewe.
*************************************
Nilifika nyumbani kwangu nakumbuka ilikuwa kama mida ya saa kumi na moja jioni, baada ya kufika
nikaona nitoe nguo nifanye usafi, ila wakati hata sijatoa nguo nje mara ukaingia ujumbe wa simu
kutoka kwa Amina ukunitaka tukutane mwenge yeye akiwa anatokea mbezi beach,kuna jambo la
muhimu sana nilinyanyua simu na kumpigia Amina lakini simu ilikatwa nilijaribu tena vile vile
ikakatwa mara ikaingia meseji tena samahani jpo mazingira mabaya boss wewe fanya hivyo, basi
sikuwa na jinsi zaidi kuvaa nguo za jioni kisha kupanda gari yangu na kwenda mwenge kuwahi
kuonana na Amina, nilitumia kama muda wa saa moja na nusu mpaka kufika lile eneo nilipaki gari
yangu pale mbele kidogo mwa benki ya efatha kisha nikachukua simu yangu na kumpigia Amina
ambaye baada ya kupokea aliniambia ya kwamba mbona yeye hakuniambia lolote na wala hajatuma
meseji yoyote isitoshe yeye alikuwa bado yupo kule mbezi beach akiendelea na uchunguzi, nilikata
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ile simu kisha nikashangaa hii imekaaje? Inamaana kuna mtu alitumia simu ya Amina kuwasiliana na
mimi au meseji zilijituma zenyewe nilifungua simu yangu upande wa meseji kisha na kuangalia kama
zile meseji kweli zilikuwa zimetumwa na Amina au nilikosea nilikuta ni kweli zilikuwa zinaonyesha
zimetoka kwa Amina, basi sikuwa na jinsi akili ilinicheza haraka haraka nikajua tu atakuwa Yule
mwanaharamu anatuchezea akili tu hakuna jingine pale pale niligeuza gari kwa kasi ya ajabu na
kuanza safari ya kuludi nyumbani kwangu.
Nilipofika nyumbani kwangu hali niliyoikuta haikuwa ya kawaida nilikuta tofauti sana, nilikuta vitu
vimechambuliwa hovyo hovyo huku ikionyesha dhahiri mule ndani palikuwa pamepekuliwa sana
nilipoingia ndani chumbani kwangu pia baadhi ya nyaraka zangu sikuzikuta hazikuepo, lakini
kilichonishangaza ni jinsi milango yangu nilivyoikuta kwani niliikuta kama nilivyokuwa
nimeiacha,akili ilinicheza nikajua tu Yule mwanaharamu atakuwa amepita kwangu,mungu wangu
yani inamaana mpaka sasa sisi watu wa usalama tunaanza kuishi kwa woga kisa mhalifu? Hii si sawa
haina maana ya kuwa wanausalama sasa haiwezekani huyu dada maisha yangu na mimi ayaweke
hatarini? Na kwa nini hasemi anachokitaka? Na pia huyu mtu anajiamini nini? Na anaweza vipi
kutuchezea akili kiasi hiki? Na kwanini kila mtu anayejua anajua siri kuhusu yeye au kumfuatilia
lazima amuondoe duniani? Hii haiwezekani hata kidogo, kwanza kajuaje kama naishi hapa? Nahisi
kuna mtu atakuwa anampa baadhi ya data pale ofisini kama ikiendelea hivi itabidi mimi nijitoe tu
katika kufuatilia hii kesi kwa maana sijawahi kukutana na kesi ngumu kama hii.
Huyu mtu hana huruma hata kidogo kamuuwa kikatili mchumba wa Gerald mchana wa leo tena
kataka kumuuwa Gerald? Sasa kama uwezo wake ni huu sizani kama atashindwa kumfuata Gerald
hata nyumbani kwake kumtoa na kumtoa uhai, nilijikuta natafakari mwenyewe huku nimekaa juu ya
kitanda changu huku nikitazama jinsi chumba changu kilivyokuwa kimenyambulika,kwa kusachiwa,
nilijikuta machozi yakianza kunitiririka taratibu pale juu ya kitanda kila nilipojaribu kuoanisha
matukio kuhusu Yule mwanaharamu, haiwezekani yani afisa upelelezi kabisa wa jeshi la polisi naishi
kwa wasiwasi hivi hii haina maana kabisa nilijikuta najisemea kila muda maneno yale mpaka usingizi
ukanipitia pale pale juu ya kitanda.
Nilikuja kushituka mida ya saa 8 usiku baada ya kuhisi kama kulikuwa na watu wakipita pita nje ya
kile chumba changu,nilijiweka sawa juu ya kitanda kisha nikashika bastola yangu kwa ajili ya jambo
lolote kama lingeweza kutokea, niliinuka na kuanza kuangalia kila upande kama kuna usalama au
vipi, nilizunguka mpaka sebuleni kisha nikachungulia na dirishani nikajihakikishia palikuwa salama
ndipo nilipogundua tu ya kwamba kilichokuwa kinanitesa ni woga.hivi huyu mwanamke inakuwa
anatuzidi maarifa?atakuwa mwanamke mmoja kweli? Au watakuwa ni kundi la watu maana siamini
kama mwanmake mmoja anaweza kuwa na ujasiri wa hivi..!hii itakuwa ni ngumu sana sasa hapa
najitoa mhanga ngoja nilivagae hiliswala kwa muda wa wiki 2 likinishinda namwambia mkuu
kwamba basi nimenyoosha mikono. Maana kwa sasa anamuwinda tena Gerald sasa sijui anahisi
marehemu Furaha kuna vitu alimwambia Gerald? Yani hii ni mbaya na aibu kwa jeshi letu yani
watoto wa mjini wapelelezi wazima tunazidiwa mbinu kweli hii ni mbaya sana.
*************************************
Asubuhi kama kawaida yangu niliamka na kufanya mazoezi ya viungo vya mwili kisha nikajiandaa
kwa ajili ya kuelekea ofisini kwenda kulipoti kisha kundelea na majukumu mengine.nilipofika ofisini
nakumbuka vizuri sana siku ile nilimkuta Amina akiwa tayari ameshafika tuliingia ofisini kwangu
kisha akaanza kunihadithia kuhusu jana yake alivyokuwa kule mbezi alipoenda kumfuatilia huyu
mwanaharamu,kaka yangu zile kamera nilizifunga kisha mimi nikaenda kukaa mahala kwa mbali
kidogo ambapo kulikuwa na mama lishe huku nikiwa nalaptop yangu nikifuatilia kila kitu
kilichokuwa kikiendelea pale, alisimama kuzungumza Amina huku akivuta pumzi kwa juu.huku mimi
nikimtazama usoni kwa umakini na macho yangu yaliyokuwa yamekata tama.ndio nakusikiliza
nilimwambia,huku nikimuona akitoa laptop yake na kuanza kunionyesha baadhi ya matukio,
nilimuona mwanamke aliyekuwa amevalia suruali ya blue poolneck la rangi ya kaki miwani mieusi
akitokea mhali pasipojulikana maana palikuwa kama kuna mfuniko Fulani hivi mahali pale nahisi
alikuwa kama ametoka kwenye pango Fulani hivi kisha akaenda moja kwa moja mpaka kwenye zile
kamera na kuzichukua zote,shiit huyu mwanamke alijuaje kama umefunga kamera hayo maeneo?
Inamaana huyu mwanamke anaakili kuliko sisi nilimwambia aludishe ludishe nyuma pale alipokuwa
akitoka na kuigandisha sura yake ambapo tuliipiga picha afadhali huyu mwanamke hapa ndipo
yatakuwa makazi yake. Mitaa hii nilianza kumwambia Amina ila kinachonishangaza ni jinsi kila
jambo tunalopanga anakuwa analijua hapo ndipo panapo nitatiza na kisha nikamuhadithia jinsi jana
mimi na Gerald yaliyotukuta kule makaburini na jioni alivyonichezea akili kisha akaingia nyumbani
kwangu na kufanya ukaguzi na kuondoka na baadhi ya nyaraka basi tulimaliza mazungumzo pale na
Amina kwa kuahidiana ya kwamba inabidi tujipange tukafanye uvamizi tukiwa na askari kwa
kutosha lie eneo, tuliagana na Amina huku akiwa anatoka nje ya ofisi yangu huku akiniachia laptop
yake ili niendelee kumuangalia kwa umakini Yule mwanamke katika zile crip mara nikasikia simu ya
mezani pale ofisini kwangu ikiita nikanyayua waya kupokea ile simu upande wa pili kulikuwa na
sauti ya kike ambapo ilianza kuzungumza bila kupumzika kwa maneno makali.
********************************
Nilitulia tulii nikimsikiliza Yule mwanamke ambaye alikuwa akitoa vitisho sana hasa kuhusu
kumfuatilia kwangu akijitambulisha kwamba yeye ndio mwanamke mwenye kovu jeusi, na ya
kwamba kila kitu alikuwa anakijua, tunachokifanya kwani mtandao wake ulikuwa ni mkubwa sana,
alizungumza kwa vitisho sana, nilitulia kimya nikimsikiliza kwa makini mpaka alipomaliza kuongea,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ndipo nilipomuuliza sawa dada umemaliza? Hakunijibu zaidi ya kukata simu tu, nilijaribu kuangalia
tena namba ya simu aliyonipigia kwenye simu yangu lakini sikuikuta hata nikajua itakuwa kama
kawaida yake huyu mwanamke atakuwa ametumia private namba ili tusiweze kumtambua kwani
namba yake ilikuwa hata haisomi kwenye mitandao ya simu, basi niliendele kuiangalia ile picha yake
pale kwenye laptop huku nikiigandisha ili kuiangalia kwa umakini zaidi, nilipojilizia na ile picha
nilimpigia simu Amina aje ofisini kwangu huku akiwa na nyaraka mbalimbali zote zilizohusu Yule
mwanamke baada ya dakika 5 Amina aliingia huku akiwa amebeba nyaraka zote wakati anaingia
mule ofisini kwangu mara Amina alijikwaa yale mafaili na vitu vingine vyote alivyokuwa amebeba
vikadondoka chini,mungu wangu nusura ajipigize kidevu kwenye meza iliyokuwa pale ofisini kwangu
bahati nzuri aliwahi kuweka mkono pale mezani, nilimpa pole huku nikisimama na kwenda kumsaidia
kuokota yale mafaili na vitu vingine ambavyo alikuwa amevibeba na kuja navyo mule ofisini kwangu
wakati nakusanya vitu pale chini nikakiona kiatu cha kike kile ambacho tulikichukua nyumbani kwa
Gerald siku marehemu Furaha alipoenda kutekwa nyara na Yule mwanamke haramu kama mimi
nilivyopenda kumuita ambacho tulisadiki kitakuwa ni kiatu cha Yule mwanaharamu, nilipokiinua kile
kiatu pale chini mara kwenye kisigino nikaona kama kumetikisika hivi halafu kukawa kama kuna vitu
vinacheza cheza kwa ndani nilipokibinua na kukitoa kile kisigino mungu wangu mule ndani ya kile
kiatu niliona kuna vifaa Fulani hivi vya mawasiliano, japo mimi sikuwa mtaaramu sana wa mambo ya
erectronics ila niliweza kuona kuna kama kipaza sauti kidogo hivi, huku kikiwa kimeambatanishwa
na vitu vingine vikiwa vimewekwa kwa ustadi mkubwa mule kwenye kile kisigino cha kile
kiatu,nilijikuta naacha hata kuendelea kukusanya vitu vingine na kuludi kwenye kiti changu huku
Amina akinitazama sana akiwa hajui ni kipi kilikuwa kinaendelea,nilimuonyesha vile vinasa sauti
alishangaa sana pia na yeye, kumbe ndio maana kila siku tunakuwa tunalaumiana ya kwamba huyu
mwanamke siri zetu anakuwa anazipata wapi kumbe hiki kiatu ndio tukiwa tunazungumza yeye
anazipata habari zote moja kwa moja mungu wangu, alizungumza Amina kwa sauti ya upole ila
iliyojaa udadisi sana huku akitazama kile kiatu na kuitoa ile microphone na kuwa kama anaichezea
chezea vile mipango yake sasa mwisho wake umefika, nilimtazama kisha nikamuambia sikia hicho
kiatu kitoe kwanza nje ndipo tuanze mazungumzo kwani hadi hapa tunapozungumza maongezi
anayasikia huyu mwendawazimu, Amina alitii kile nilichomuambia akakitoa kile kiatu nje kisha
akaludi mule ofisini kwangu tukaendelea na maongezi.
Kwetu tuliona ni hatua kubwa sana kwani mpaka pale tulikuwa tumefanikiwa kupata mkanda wa
video uliokuwa na picha ya Yule mwanamke japo haonekani vizuri sana, lakini pia tulikuwa
tumefanikiwa kugundua kifaa alichokuwa akikitumia kunasa mazungumzo yetu ambayo kuna kipindi
mpaka sisi wenyewe ilikuwa inatuchanganya mpaka tukawa tunahisi wenyewe tunasalitiana,
tulipanga usiku ule ule kwenda kuweka kambi mitaa ile huku tukiwa na kikosi cha kutosha
kuhakikisha Yule mtuhumiwa tunamtia kifungoni siku ile kwani karibia mambo yote muhimu
tulikuwa tumefanikiwa kupata basi nilitoka pale ofisini kwangu huku nikiwa nimemuacha Amina
mule ndani na kwenda ofisi ya mkuu wetu wa kazi kwa ajili ya kumuambia maazimio tuliyokuwa
tumefikia ili ikiwezekana aweze kutupatia vitendea kazi vya kutosha pamoja na wasaidizi wa kwena
nao kwenye operesheni ya usiku ,mkuu wetu alituelewa akadai pia na yeye atashiriki katika ile
operesheni siku ile akiwa kama msimamizi mkuu pia akasema tusiende wengi twende watu wa nne
tu, tunatosha kumdhibiti, sikuwa na la kumpinga, nilijua pia ya kwamba mkuu na yeye alitaka
akashiriki kwa minajili ya kujijengea umaarufu hasa kama tukifanikiwa kumkamata kwani kazi yote
itaonekana kama aliifanya yeye ili aweze kujenga sifa nzuri ikibidi apandishwe hata cheo kwani
mabosi wengi wa upelelezi huwa hapo hivyo wanapenda sana wao kupata sifa za mwishoni
mwishoni, basi tulikubaliana pale na inspekta Thomas ambaye ndio alikuwa mkuu wetu wa kazi
kwamba itabidi mida ya saa kumi tuanze safari ya kuelekea huko,basi tulitawayika kila mmoja
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akiendelea na shughuri zake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment