IMEANDIKWA NA : AMANI KIZUGUTO
*********************************************************************************
Simulizi : Mwanamke Mwenye Kovu Jeusi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Nakumbuka vizuri ilikuwa siku ya jumapili ambayo kama ilivyoada kwangu huwa sikosi kwenda
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kanisani hasa misa ya kwanza kwani huwa napenda sana kusali misa ya kwanza ili baadaye niweze
kuendelea na mambo yangu mengine,siku hiyo niliamka asubuhi na mapema kutoka pale nyumbani
kwangu mnazi mmoja karibia na ofisi za chama cha mapinduzi za mkoa wa Dar-es-salaam na
kuelekea kanisani pale saint.alban posta taratibu kwa miguu kwani gari yangu ilikuwa imeharibika
wiki ya pili sasa na isitoshe pale nyumbani kwangu mpaka pale posta hapakuwa mbali sana kiasi cha
kama dakika 20 tu hasa kwa kijana kama mimi ambaye damu ilikuwa bado inachemka.niliingia pale
kanisani nikiwa sijachelewa sana misa ilikuwa imeanza kama dakika 7 hivi nakumbuka sana somo la
siku hiyo alilolitoa padri Kiaka lilikuwa linahusu umuhimu wa kuombea siku yako ya kufa kwani
haina siku wala saa.
Misa ilipoisha mida ya saa 3 asubuhi niliona nijivute mpaka mitaa ya upanga pale nyuma ya diamond
jubilee mwendo wa pole pole nikamuone rafiki yangu Martin ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi
mwenzangu. Sikutaka hata kumtaarifu kwenye simu kwani simu yangu haikuwa na pesa pia nilijua
kwa kuwa tuliahidiana jana kwamba kesho nikitoka kanisani nitaenda kwake basi haina shaka
nitamkuta tu kwani pia Martin huwa sio mzururaji sana hasa mida ya asubuhi kama haendi
kazini.Wakati naingia ndani kwa rafiki yangu kipenzi Martin nakumbuka ilikuwa ni mida ya saa 4
asubuhi mlangoni nilipishana na mdada wa makamo mweusi kiasi ambaye nakumbuka vizuri alikuwa
amevalia dela la rangi ya kijani kibichi likiwa linamichirizi ya rangi ya zambarau na kwa ndani
alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeusi huku kichwani akiwa amejifunga mtandio mweusi
kufunika nywele zake nilimsalimia aliitikia haraka haraka huku akikwepesha sura yake na huku
akionyesha ni mtu aliyekuwa na shauku ya kuondoka lile eneo haraka sana, mimi hata sikumjali
nilijua atakuwa ni mmoja kati ya wasichana ambao alikuwa na uhusiano nao bwana Martin kwa
kuwa rafiki yangu Martin alikuwa ni mtu aliyependa sana wasichana,nilifika mpaka pale alipokuwa
amepanga Martin ilikuwa ni nyumba ya uwani akiwa amepanga chumba na sebule huku nyumba ya
mbele kukiwa hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa amepanga kwa maelezo yake ile nyumba ya mbele
kulikuwa na mpangaji lakini amehama na sasa mwenye nyumba alikuwa yupo akiifanyia
marekebisho tayari kwa kuingia mpangaji mwingine. Ile nimefika tu mlangoni nikakuta mlango upo
wazi kitu ambacho kikawaida sio busara kuingia nyumba ya mtu bila kugonga basi nikajivuta pale
mlangoni na kuanza kuugonga ule mlango hallow Martin hallow niligonga kama dakika tano bila
kupata jibu lolote kutoka mule ndani ilinibidi nishangae kidogo kwa maana hata kama angekuwa
msalani ni lazima angesikia ile sauti yangu na kwa nini akae kimya sikuamini kama alikuwa amelala
wakati nimepishana na Yule dada anatoka chumbani kwake muda si mrefu,ikanibidi niingie tu ndani
kama hayupo atanikuta mule mule nikimsubili, mungu wangu sikuamini nilipoingia pale sebuleni
kwake nilikutana na michirizi ya damu kutoka pale sebuleni kuelekea chumbani kwake mh ikanibidi
nipitilize haraka moja kwa moja kule chumbani kwake ile kuingia tu nikakutana na mwili wa Martin
akinikodelea macho huku ukiwa umekakamaa huku pia ukiwa umegandana na damu na alama
kubwa ya kisu kwenye shingo yake,nilimkimbila pale alipokuwa amelazwa na kumuangalia mungu
wangu alikuwa tayari ameshakufa,nilifikiria pale haraka haraka ni kipi nifanye nikaanza kuitafuta
simu yake mule ndani mpaka nikaipata nikawapigia simu polisi na kuwaeleza lile tukio sikutaka
nijihusishe moja kwa moja na lile tukio ndio maana niliamua kutumia simu yake pia simu yangu
nilikuwa bado sijaweka vocha kisha nikaanza kutoka nje kabla sijatoka nje ya chumba chake macho
yangu yakatua kwenye meza ndogo iliyokuwa mule chumbani kwake mara nikakutana na karatasi
imeandikwa kwa Wino Mwekundu
“NILIYEMUUWA NI MIMI MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI” shiti moyo ulijikuta
unasisimuka na kuanza kudunda dunda kwani lile jina si mara ya kwanza kwangu kukutana nalo hasa
kwenye kazi zangu,mungu wangu huyu mwanamke amemuuwa tena na Martin? Martini
amemfanyaje tena huyu mwanamke hatari kama amemuuwa na Martin basi na mimi siku zangu
haziko mbali hapana inabidi nimzibiti kwa kila hali nilijikuta nimekaa naangalia ile karatasi
aliyoandika huku nikiutazama na mwili wake pale chini kwa muda wa dakika kadhaa mpaka machozi
yakaanza kunitiririka kwa mbali,nilishitushwa na kelele zilizotoka nje nikahisi polisi watakuwa tayari
wameshafika pale basi nikaona haina haja ya kuondoka tena nikachukuwa shuka pale na kuanza
kuufunika ule mwili hallow inspector vipi tayari umeshafika? Habari umeipataje? Ilikuwa ni sauti ya
bwana Gerald mmoja wa ma afisa upelelezi pale makao makuu, ndio mimi niliyewapigia simu
nilimjibu kwa mkato huku nikimsaidia kutoa vifaa vya kuchukulia finger print pamoja na camera
digital ya kipelelezi kupiga picha mule chumbani kwa ajili ya kupata nyayo zake na alama zingine za
Yule muuwaji,mkuu wangu wa kazi pia inspector Thomas na yeye pia alikuwa ni mmoja ya watu
waliokuwa wamefika pale kwa ajili ya kushuhudia lile tukio wakati kina inspector Gerald
wakiendelea kukusanya baadhi ya kumbukumbu mule ndani bosi wangu aliniita nje alipiga simu
hospitali ya taifa ya muhimbili kuwajulisha kuhusu lile tukio kisha akaanza kuniuliza maswali kadhaa
kuhusu lile tukio aliniuliza kwanza nilijuaje kama Martin amekutwa na lile tukio nikamjibu mimi
mwenyewe imetokea tu kama bahati kwani tulikuwa tumepanga kukutana naye siku ya leo nikitoka
kanisani ili tuelekee bagamoyo kusherekea siku ya mchumba wake ya kuzaliwa,ndio na mbona hili
tukio tumejulishwa kupitia simu yake aliendelea kunihoji, ni mimi ndiyo nilitumia simu yake
kuwajulisha kwani simu yangu haina pesa kabisa, je huyo muuwaji unamjua au unaweza kuwa
unamhisi nani? Ni MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI bosi wangu alijikuta anashituka ohh
wewe umejuaje? Aliniuliza kwa shauku kubwa ya kutaka kujua nimefahamu vipi aliyefanya lile tukio
ni mwanamke mwenye kovu jeusi nikamwambia kuwa kama kawaida yake ameacha note juu ya
meza mule chumbani mwa Martin ameandika kwa wino mwekundu, basi bosi wangu alinituma
nikamletee ile karatasi aliyoiacha huyo mwanamke mwenye kovu jeusi,basi nilienda na kutoka nayo
pale nje na kumpa aiangalie, aliiangalia kwa muda wa kama dakika 2 hivi halafu akaludisha macho
kwangu na mimi muda ule nilikuwa pia nimemetolea macho basi tukajikuta tumetoleana wote
macho,hivi hakuna anayemjua huyu muuwaji? Kwa maana sasahivi amezidisha haya mauaji
alianzisha tena mazungumzo,
simjui ila uwezo wa kumpata upo kwa nini asipatikane kwa maana tukimchekea tutajikuta na sisi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wote anatuondoa wakati nazunguma haya tayari gari ya kubebea wagonjwa kutoka muhimbili
hospitali ilikuwa tayari imeshafika pale nyumbani kwa marehemu Martin tayari kwa kuchukua ule
mwili kuupeleka hospitali ili ufanyiwe pia uchunguzi mwingine wa kitabibu .Wale manesi walishuka
kutoka ndani ya ya ile gari ya kubebea wagonjwa na kuingia mule ndani tayari kwa kuuchukuwa ule
mwili kwa ajili ya kuupeleka hospitali.
*************************************
Baada ya mwili kuondolewa pale nyumba ambayo Martin alikuwa amepanga kwenda hosptali kwa
ajili ya uchunguzi zaidi bosi wetu inspekta Thomas alituita wafanyakazi wote pamoja na askari kanzu
ambao tulikuwa pale kwenye lile tukio,ndio nimewaita hapa tuzungumze kidogo nazani mmeona
tukio lililotokea leo,hii hi fedheha sana kwa jeshi la polisi, huyu mwanamke haiwezekani tumshindwe
kiasi hiki mwanzo alikuwa anawauwa watu wengine lakini sasahivi ameingia mpaka kwenye jeshi
letu lapolisi, hapa maswali ya kujiuliza haraka haraka ni kwamba huyu mwanamke amejuaje kama
Martin ndio alikuwa anajukumu la kufuatilia hili faili lake? Inamaana kuna watu ndani ya ofisi yetu
watakuwa wanampa siri huyu mwanamke bosi alianza kuzungumza huku akionyesha kwenye sura
yake wazi kwamba kile kitendo kilikuwa kimemuumiza sana.
Basi taratibu mkuu haya tutaenda kuyazungumza ofisini mkuu maana hapa tulipo hatuwezi kujua
inawezekana akawa bado yupo au ameweka hata vinasa sauti maana inaonekana huyu mtu ni hatari
sana ,ilikuwa ni sauti ya Jamira mmoja wa askari shupavu sana tuliokuwa nao pale kituo cha kati
kwenye jeshi letu la polisi, ilionekana bosi aliafiki ule ushauri aliopewa na Jamira kwani baada ya
hapo alituambia ya kwamba tunaweza kwenda huku akimwabia Gerald ahakikishe baadaye
wanakutana ofisini kwake.
*******************************
Habari ya kifo cha kutatanisha cha Martin kila mmoja pale ofisini kilimhudhunisha sana kwani
Martin alikuwa mmoja ya vijana wachapakazi sana pale ofisini hadi siku umauti yanamkuta
nakumbuka yeye ndio alikuwa mtu anayefuatilia faili la huyu mtu aliyekuwa akijiita MWANAMKE
MWENYE KOVU JEUSI sasa tena na yeye kuuliwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina hilo kila mtu
alishituka sana.
Basi baada ya uchunguzi wa kitabibu hospitali ya taifa Muhimbili kukamilika ilibidi zianze taratibu za
kusafirisha mwili wa marehemu. Tuliusafirisha mwili wake mpaka wilayani Bunda ambapo ndipo
palikuwa nyumbani kwa wazazi wake. Na mimi ni mmoja ya watu tuliochaguliwa na bosi wangu
kusindikiza maiti ya marehemu nadhani hili lilitokana na ukaribu wangu baina ya mimi na Martin.
mazishi yake yalifanyika huko kwao kwenye kijiji kilichojulikana kwa jina la Kasunguti,kwa mimi
ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika mkoa wa Mara toka nizaliwe mara nyingi safari zangu
nyingi nilikuwa naishia mkoa wa Mwanza tu. Nakumbuka siku ile tulipoingia nyumbani kwa wazazi
wake tulikuta umati wa watu wengi sana, wazazi wake walikuwa hawaamini kama mtoto wao
amefariki mpaka pale walipoliona jeneza likishuka kutoka kwenye gari iliyokuwa imebeba ile maiti
ya Martin. Mama yake alikuwa akilia huku akilalamika ya kwamba Martini ndio alikuwa mtoto
tegemewa kwani alikuwa anawasomesha wadogo zake watatu sasa sijui watafanyaje. Sikuamini siku
ile kama ilikuwa ndio siku ya mwisho kuuona mwili wa rafiki yangu kipenzi Martin.
******************************
Ilikuwa imepita wiki moja baada ya kurudi kutoka Bunda kumzika Maritin nakumbuka siku hiyo
nilikuwa nipo ofisini nikijaribu kupitia faili moja lililokuwa linamhusu jambazi mmoja ambaye mpaka
siku ile ilikuwa bado sijamjua ni nani ila nilikuwa nimeshafanikiwa kupata baadhi ya nyaraka
muhimu kuhusu huyo mtuhumiwa mara ofisini kwangu akaingia Gerald, tuliongea mambo mbalimbali
kisha akaniambia ya kwamba lile faili la mwanamke mwenye kovu jeusi alikuwa amekabidhiwa yeye
na ameambiwa ndani ya wiki tatu ahakikishe tayari mtuhumiwa ameshajulikana na kukamatwa,
nilimwambia ajitahidi na awe makini sana kwani huyo mtu anaonekana hatari sana,akasema hakuna
shida kwani yeye kama iliyo ada siku zote huwa yupo makini. Alijaribu kuniomba ushauri pakuanzia
kumfuatilia Yule mtuhumiwa nilimshauri aanzie kwanza kupitia lile faili alilokabiziwa ili ajue ni wapi
Martin aliishia nadhani mpaka hapo atakuwa na nafasi nzuri ya kujua wapi pa kuanzia, tulizungmza
nae sana mambo yetu mengine nakumbuka sana siku hiyo mpaka muda wa kutoka kazini saa 9
arasili.
*******************************************
Basi kama iliyo ada ya majukumu ya kikazi Gerald alianza kuifuatilia ile kesi ya Mwanamke mwenye
kovu jeusi maana aliambiwa ndani ya wiki tatu awe tayari ameshajua kila kitu kuhusu huyo muuaji
wa kutisha ikiwezekana pia awe tayari ameshatia ndani ya mikono ya sheria, alianza kwanza kwenda
kufanya mahojiano na mwanadada mmoja ambaye alikuta jina na mahali alipokuwa anaishi pamoja
na sehemu aliyokuwa akifanyia kazi kwenye faili aliloliacha marehemu Martin huyo dada alikuwa
anafanya kazi benki ya taifa ya biashara makao makuu pale alijulikana kwa jina la Zainabu Athuman
akiwa mmoja wa maafisa mikopo pale makao makuu. Basi siku hiyo asubuhi na mapema Gerald
alidamkia pale benki kwani alihofia kwamba akichelewa Yule dada anaweza asimkute kwani mara
nyingi huwa anazunguka sehemu mbalimbali hasa kwenye maofisi kutoa elimu kuhusu mambo ya
mikopo. Ofisi ilipofunguliwa tu Gerald alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kuingia mule ndani ya
jingo la benki moja kwa moja mpaka mpaka mapokezi,”samahani naweza kuonana na Zainabu
Athuman?” ilikuwa ni sauti ya Gerald akimuuliza mmoja wa wahudumu pale meza ya
mapokezi,samahani una ahadi naye? Mdada mmoja wa pale mapokezi alimuuliza, hapana sina ahadi
naye ila ninashida naye. Ya kiofisi au ya binafsi? Ya kiofisi, ilibidi Gerald adanganye kidogo ili apate
nafasi tu ya kuonana naye,kuepuka usumbufu ambao huwa hauna maana uliojaa katika ofisi nyingi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hapa Tanzani ok sawa nenda gorofa ya kwanza mkono wa kulia utakuta ofisi imeandikwa ofisi ya
afisa mikopo ndio hapo hapo,Gerald alishukuru na kupanda ngazi kuelekea kuonana na Zainabu.
alipofika pale mlangoni, alikuta mlango ukiwa wazi na kwa ndani alimuona Zainabu akipanga mafaili
yake vizuri juu ya meza mule ofisini, Gerald akamuuliza,samahani naweza kuingia? Ndio hakuna
shida wewe pita Zainabu alimjibu Gerald huku akikaa kwenye kiti chake na kuanza kukizungusha
pale kwenye kiti kushoto kulia, Gerald aliingia na kukaa kwenye kiti cha wageni kisha na kumtazama
Zainabu hivi kama dakika 2 mpaka Zainabu akamshitua kaka vipi nakusikiliza wewe maana nataka
kuondoka hapa, alimwambia Gerald huku akimshusha chini juu chini juu,
Basi Gerald alianza kujitambulisha, kisha akatoa na kitambulisho chake halafu akamueleza nia ya
yeye kuwa pale ofisini muda ule,Zainabu alionekana kuishiwa nguvu kisha akaanza kumwelezea
Gerald ya kwamba mbona tayari alishakuja mwenzako na nilimueleza kila kitu lakini? Ndio hilo
nalijua lakini mimi imekuja ili kupata uhakika zaidi kuhusu hili jambo,Gerald alizungumza kwa
umakini huku akimkazia macho kuongeza msisitizo, hivyo basi na maswali kidogo naomba nikuulize
ili nipate majibu ya kuridhisha kutoka kwako. Unamfahamu vipi huyu mwanamke anayejiita eti
anakovu jeusi? Kiukweli simfahamu huyu mwanamke ila nachojua ni kwamba alikuwa na uhusiano
na mdogo wangu mpendwa Rashid,hapo hapo Gerald alimkatisha, huyo Rashid yupo wapi?
Alishafariki, maskini Zainabu aliendelea kuongea huku akionekana kama ni mtu aliyekumbuka mbali
sana. Unaweza ukaendelea, Gerald alimwambia, ndio huyu mdada simfahamu vizuri ila naweza
kusema kuwa alikuwa na uhusiano na mdogo wangu ambaye baadaye alikuja kufa kifo cha
kutatanisha kule bahari beach,mimi huyu mwanamke nimewahi kumuona mara mbili na hata hapa
pia nikimuona namkumbuka ilaaah ilaah ilaah alianza kusita kuendelea kuongea Zainabu, ila nini?
Wewe usiogope sema yote sawa maana hapo utakuwa umelisaidia sana jeshi la polisi.unajua Napata
tabu sana kwani huyu mwanamke ni wa ajabu sana kwanza aliacha ujumbe wa karatasi kwenye
mfuko wa marehemu mdogo wangu Rashidi pia na hata hapa ofisini wiki mbili baada ya kifo cha
mdogo wangu alikuja na kusema ya kwamba nikithubutu kumtaja jina lake basi kabla yeye
hajakamtwa mimi nitakuwa sipo duniani na pia kwa yoyote nitakayemtajia jina lake akijua pia lazima
atamuondoa duniani, ndio maana nakuwa na hofu ya kumzungumzia kwani pia mdogo wangu
Maimuna alikaidi huo ujumbe hapa napozungumza wiki ya pili sasa tumetoka kwenye msiba wake
hivyo mimi siwezi kuzungumza zaidi ya hapo samahani sana alimalizia Zainabu huku machozi
yakimtiririka ..
Gerald alibakia asijue la kufanya kwani wakati anaendelea kumbembeleza Zainabu amwambie
kuhusu Yule mwanamke aliyejiita mwenye kovu jeusi alisikia mlango wa ofisi ya Zainabu ukigongwa
kuashiria kuna mtu alikuwa anahitaji kuingia.
Basi pale pale Gerald alimuaga na kuondoka huku akimuahidi ya kwamba ataludi tena siku
nyingine,Zainabu hakumjibu kitu zaidi ya kujifuta machozi na kujiandaa kuzungumza na Yule mgeni
aliyekuwa pale mlangoni. Gerald alitoka mule kwa kasi ya ajabu huku yule mtu aliyekuwa anahitaji
kuingia mule ofisini akimshangaa mpaka nje kisha akaelekea kwenye sehemu ya maegesho ya magari
tayari kwa ajili ya kuchukua gari lake kuondoka basi Gerald akufungua gari lake na kuingia wakati
anataka kukaa kwenye siti akahisi kama amekalia kitu kigumu kilicho chini ya kava la siti ya kiti cha
gari ikabidi ainuke ili aangalie ni kitu gani hicho kwani gari ni ya kwake na ndio aliyokuja nayo pale
basi ikambidi ainue lile kava la siti ya gari alikuta kuna bahasha ya kazi ikabidi ashangae ni nani
aliyeiweka pale akaichukua na kuiangalia kujua inahusu nini, kuifungua akakuta kuna barua
imeandikwa kwenye karatasi ngumu yenye rangi nyekundu maandishi yakiwa ya rangi nyeusi,
maandishi yenyewe yalikuwa yanasema ifuatavyo
Ndugu Gerald najua ni wewe ndio uliyepewa jukumu la kunifuatilia mimi ila nakuomba utambue ya
kwamba mimi ni mtu hatari na hilo utaamini ukifika nyumbani kwako ni mimi “MWANAMKE
MWENYE KOVU JEUSI”
Gerald aliisoma ile karatasi zaidi ya mara 5 huku akiangalia kila upande kuona kama atamuona Yule
mwanamke hakufanikiwa alizidi kuchanganyikiwa pale huku akijiuliza huyu mwanamke amejuaje
kama mimi leo asubuhi nitakuwepo hapa? Nani amemwambia wakati hakuna hata mtu mmoja
aliyemwambia kuwa leo ataenda pale, pili Yule mwanamke aliweza vipi kupitisha ile bahasha mpaka
pale chini ya lile kava la siti ya gari lake,wakati alifunga na ufunguo,alijikuta akishangaa mpaka akaja
kushituliwa na mlinzi wa lile eneo la kuegeshea magari, “kaka samahani mbona gari umeliweka
vibaya wengine wanashindwa kuegesha magari yao”.ilikuwa ni sauti ya Yule dada aliyekuwa
anakusanya ushuru wa kuegesha magari,ilimbidi Gerald aombe radhi kisha akaondoa gari lake
kuelekea ofisi kwake aliendesha gari huku kichwani akiwa na mawazo, amakweli huyu mwanamke ni
hatari kwa staili hii inanibidi niongeze umakini.
******************************
Wakati Gerald yupo ofisini akiendela na kazi mara akipigiwa simu na jirani yake ya kwamba
anahitajika mapema sana yumbani kwake kwani kunatatizo ilemetokea,kusikia hivyo Gerald
alichanganyikiwa kwani alihisi Yule mwanamke mwenye kovu jeusi atakuwa ameshafika kwake na
kufanya jambo lisilo jema,
Naomba unisindikize kwangu samahani sana,Gerald alimuomba Siwah amsindikize nyumbani kwake,
Siwah alishangaa sana kwani kwa muda ule iliwapasa kuwa kazini, samahani bwana nisindikize kuna
dharura nimepigiwa simu hivyo sina budi kuwahi nyumbani alizidi kusisitiza huku akichukua simu
yake na kujaribu kumpigia mpenzi wake Furaha ambaye walikuwa wakiishi wote japo walikuwa
hawajafunga ndoa, alipiga simu zaidi ya mara tatu iliita bila kupokelewa,Gerald alijihisi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuchanganyikiwa, Siwah tafadhari twende nyumbani kwangu nahisi si salama, aliomshika mkono
Siwah na kumvuta nje waelekee kwenye gari tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea kwake. Wakati
wapo ndani ya gari wakielekea nyumbani kwa Gerald ndipo alipoanza kumuelzea kisa kizima
alichokutana nacho siku ile asubuhi toka alipoenda kazini kwa dada Zainabu maongezi yao yote
yalivyokuwa na mwisho alimueleza jinsi ile bahasha aliyoikuta china ya siti ya gari lake.Siwah
alishangaa sana kusikia yale maneno “sikia ndugu yangu huyu mwanamke ni hatari sana hata Martini
alikuwa analeta masihara nayeye umeona yaliyomkuta?” inabidi umakini uongezeke mara dufu
katika kufuatilia hili swala kwani bosi amekupa siku ngapi? Alimalizia Siwah kwa kumuuliza Gerald
huku wakiwa wamekaribia kabisa nyumbani kwake. Amenipa wiki tatu na sasa ni siku ya 4 hata
sijapata pa kuanzia wewe acha tu kama ni kazi basi hii imetia fola.
Walifika nyumbani kwa Gerald na kukuta watu wakiwa wamejaa sana ukizingatia ile nyumba
walikuwa wamepanga watu kawa wa 5 hivi, majirani pia wa nyumba za jirani pia walikuwa
wamekusanyika pale uwani kwenye ile nyumba. Waliposhuka kwenye gari wale watu walimtazama
kwa sura ya hudhuni sana Gerald kisha jirani yake mmoja akamuambia afadhali umekuja jirani hali
ya hapa nyumbani ni mbaya sana,Gerald aliona wanachokiongea hata hakieleweki moja kwa moja
akaelekea upande wa pili ambapo ndipo alipokuwa amepanga yeye, “sasa unaenda wapi bwana
mbona unakuwa kama sio mwelewa hebu subili kwanza hapa tuwasikilize tujue tatizo nini” ilikuwa
sauti ya Siwah huku akimshika shati Gerald asiondoke. Ilimbidi ahairishe kuondoka pale kwa
kufuata ushauri wa rafiki yake na kusimama kuwasikiliza kujua tatizo ni nini, samahani sana jirani
hapa nyumbani hali sio nzuri mida ya saa 5 hivi alikuja mdada mmoja akiwa amejifunika vitenge
akiwa na gari aina ya Toyota surf, alipofika hapo getini alipiga honi sana akatoka shemeji kwenda
kufungua ile kufika tu na kufungua lile geti, mbona wajiuma uma wewe nambie sema usiogope kama
wamemuuwa au vipi Gerald alidakia haraka haraka akongea kwa sauti iliyojaaa wasiwasi na shauku
ya kutaka kujua ni nini kimetokea, hapana siwezi kusema moja kwa moja wamemuuwa ila baada ya
kufungua tu geti Yule dada alishuka akiwa ameshikilia bunduki na kumuelekezea walekee ndani
kwako ndipo pale tulipokupigia simu, inamaana bado wapo ndani? Alidakiwa Siwah kumuuliza swali
Yule jirani aliyekuwa akihadithia pale, hapana waliingia ndani baada kama ya dakika 5 alitoka naye
na kumpakia kwenye gari huku wakiwa wamebeba baadhi ya makaratasi,shiiti ngoja kwanza hebu
twende ndani Gerald alimwambia Siwah hukua akitoa pisto yake ndogo na kutangulia, mbona una
haraka sana Gerald hata hawajamaliza kutuelezea wewe umeshaanza kukimbilia ndani haya hebu
endeleeni kunielezea mim,i Siwah aliwaambia wale majirani.
Gerald kuingia ndani alikuta vitu vimefumuliwa fumiliwa na kuchambuliwa sana huku kwenye kabati
za chumbani kwake zikiwa zimepekuliwa na baadhi ya karatasi zikiwa zimepekuliwa na zingine
zikionyesha wazi zimechukuliwa kuangalia pembeni mwa kitanda akaziona simu za mpenzi wake
zikiwa kwenye kabati dogo la vipidozi mule chumbani, akakuta kuna missed call nyingi na za kwake
zikiwepo pia, basi Gerald akachukua zile simu na kuziweka kwenye mfuko wake wa suruali wakati
anataka kutoka kuelekea sebuleni kuangalia juu ya mlango ule wa kuingia chumbani kwake
akakutana na maandishi yaliyoandikiwa kwa marker pen nyekundu MWANAMKE MWENYE
KOVU JEUSI LEO AMEKUTEMBELEA CHUMBANI KWAKO..
*******************************
Gerald baada ya kuona yale maandishi yalimchanganya sana pale pale alijihisi kuchanganyikiwa
ikawa mara atoke aelekee sebuleni mara aludi chumbani mara aingie chooni, haiwezekani huu ni
usanii wa hali ya juu huyu mtu amejuaje kama mimi naishi hapa, mtoto wa watu pia ameondoka naye
mimi nitawajibu vipi ndugu zake hapana huu ni usanii nafanyiwa wakati anaendelea kuzunguka mle
ndani peke yake huku akiongea mara Siwah akingia mule ndani akiwa ameshika kiatu kimoja cha
kike mkononi,kaka huyo mwanamke hatari amedondosha kiatu kimoja hiki hapa kinaweza kutusaidia
katika upelelezo wetu,mbona hueleweki Siwah alimuuliza Gerald baada ya kumuona amekaa kwenye
kochi sebuleni kwake huku akizungumza peke yakena kurusha rusha ngumi na mikono hovyo,Siwah
alimsongele kwenye kochi Gerald na kuanza kuzungumza naye kwa upole sana, Gerald alimulezea
kila kitu huku akimumbia aende chumbani kwake juu ya mlango akasome kilichoandikwa, wakati
wanaendelea kuzungumza mara simu ya mpenzi wake ikaita mfukoni Gerald aliitoa na kuipokea tu
mara akasikia sauti nzuri ya kike, samahani sana mimi naitwa Candra,Gerald alimjibu upande wa pili
samani mwenye simu hayupo, ndio hilo nalijua mwenye simu nipi naye kwangu hapa mimi naye
zungumza naitwa Candra au ukipenda niite wanamke wenye kovu jeusi nipo kwenye haraki za
kulifuta hili kovu langu jeusi unanisikia lakini? Alizungumza Yule mwanamke ambaye kwa sauti yake
ilikuwa ni ngumu sana kuamini kwamba ni yeye ndio aliyekuwa akifanya vile vituko, ndio nakusikia
Gerald alijibu kwa upole ndio sasa hebu sikiliza kwanza hii sauti alimwambia huku akimsogezea sauti
ambayo ilikuwa ikitoka kwenye kama redio Fulani hivi, Gerald alisika sauti yamaongezi baina yake
yeye na bosi wake siki alipokuwa akikabidhiwa lile faili, kisha akasikia na sauti ya maongezi baina
yake yeye na Zainabu siku ile asubuhi alipoenda ofisini kwake kwa ajili ya kumhoji,
mwisho Gerald alichoka kabisa aliposikia sauti ya mazungumo yake yeye na wale majirani wake
pale nje na maongezi yake yeye na Siwah ambayo yalikuwa hayana hata dakika 10 mule
ndani,Gerald alijikuta akichoka kabisa pale juu ya lile kochi.unanisika kwa makini sasa nakuomba
ujitoe kufuatilia hili jambo nakupa siku tatu kama unataka mpenzi wako aendee kuwa hai ilimalizia
ile sauti na kukata simu,Gerald akaichuka simu ili aangalie ile namba ainpigie kwa simu yake ajalibu
kuzungumza na mpenzi wake ajue kaka yu hai kuangalia kwenye received call hakuiona
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
namba,aliitafuta ile namba wapi hakuiona hata kidogo,Siwaha siwah hii kali huyu mwanke kila jambo
nalofanya analijua sasa ndio nini mbona hii kazi inazidi kuwa ngumu hivi? Gerald alimhadithia kila
kitu alichokisika kwenye ile simu.kaka inabidi siku yakesho asubuhi uombe kikao na bosi wetu
umueleze kila kitu bwana maana haiwezekani huyu mtu atuzidi maarifa kiasi hiki hapana hapana hiyo
haikubaliki hizo ni dharau sana
****************************
Baada ya kikao kilichokuwa takribani dakika 50 kati ya mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar-es-salaam
na ma afisa wapelelezi waandamizi kuhusu jinsi ya kumdhibiti Yule mwanamke mwenye kovu jeusi
kama yeye alivyopenda kujiita, mkuu wa upelelezi aliwaongeza watu wawili washirikiane na Gerald
akatika kumtafuta Yule mwanamke mwenye kovu jeusi kati ya watu waliongezwa Siwah pia likuwa
ni mmoja wapo na dada mmoja aliyejulikana kwa jina la inspekta Amina, baada tu ya kikao kuisha
wote walitawanyika kila mmoja akieleka mahali pa kuanza kumtafuta Yule mwanamke,
Mimi niliondoka moja kwa moja mpaka makao makuu ya mamalaka ya mawasiliano huku Gerald
akielekea kule benki ya taifa ya biashara kwenda kumuhoji tena dada Zainabu wakati Amina akibaki
pale pale ofisini akijalibu kupitia lile faili la Yule dada. Nilipofikia pale ofisi za mamalaka ya
mawasiliano nilijitambulisha na kuingia moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya injinia upande wa
mawasiliano ya simu nilifika pale huku nikiwa na simu ya Furaha mpenzi wa Gerald
aliyetekwa,ambayo aliitumia jana kumpigia Gerald, nilipofika mule ndani nilimkata kaka mmoja
ambaye alionekana ni mtu asiye na utani hata kidogo wala asiyependa masihara, haya kaka nambie
unashida gani? Na nani amekuruhusu kuja mpaka huku ofisini kwangu? Kwa maana shida zote za
wateja na malalamiko yanasikilizwa japo chini? Jamaa aliongea kwa sauti iliyojaa kejeli na dharau
sana,
Samahani sana kaka kwa kukuingilia kwenye ofisi yako huku ukiwa na kazi nyingi za kufanya, ahaa
acha maneno mengi bwana eleza shida yako nijue kama inanihusu ama vipi? Yule jamaa alinikatisha,
sawa kuna nambo moja imenipigia simu jana usiku sasa nilikwa nahitaji msaada jinsi ya kumtambua
huyo mtu mwenye iyo namba na anapatikana wapi,nilianza kumeleza Yule injinia. Sasa hiyo shida
ndio ya kuileta hapa? Mbona watanzania mnakuwa sio waelewa kabisa? Kwani amekutukana? Na
sisi hapa sheria zinasema ya kwama haturuhusiwi kutoa taarifa yoyote ile bila barua ya polisi na pia
hizo taarifa inabidi waje kuzichua polisi wenyewe sio mtu binafsi sijui unanipata kaka? Jamaa
alinieleza huku akiwa bize na kompyuta iliyokuwa juu ya meza yake pale ofisini.
Sikutaka kuendelea kuzungumza naye sana nilitoa kitambulisho changu na kukambidhi akitazame
alikipokea akakitazama kama sekunde 25 kisha mwenye akawa mpole, samahani sana afisa, hamna
shida nilinjibu, samahani sana unajua humu huwa kuna watu wengine wanakuja bila sababu za maana
mtu ameona meseji kwenye simu ya mpenzi wake basi huyo anakuja hapa au anaenda kwenye
kampuni za simu ajue ni nani yupo wapi samahani sana kiongozi, Yule injinia alizidi kujitetea huku
akiacha kuchezea kompyuta yake na kukaa kunisikiliza kwa makini. Ndio kaka hebu tuzungumze
sasa kaka hebu nambie tatizo nini? Kaka jifunze kuheshimu wa tu sio vizuri hivyo inamaana kama
mimi nisingekuwa afisa wa polisi ungeendela na majibu yako utumbo? Hata shida yangu
usingeisikiliza si ndio? Hapana kaka samahani sana watu ni wasumbufu sana kaka kama
nilivyokuambia niwie radhi kaka sikutaka kuendelea kujibishana nae Niliitoa ile simu ya furha na
kumuonyesha kuwa siku ya jana kuna simu iliingia lakini baada ya kumaliza tu kuongea nayo
haijabaki kwenye call list, aliichukua ile simu nay eye kuikagua hakuiona pia, kisha akainambia
nimtajie namba ya simu ya furaha, nilimtajia aliingiza kwenye computer yake na kuangalia, pia
hakuona ile simu kwenye data base zao, kaka nimeshagundua kitu kwani aliyewapigia simu
amezungumza nini? Sikutaka kumueleza kila kitu ila nilimuambia tu ya kwamba huyo mtu aliyepiga
simu ni mtuhumiwa na tunamtafuta, hapo hapo alidakia ah sawa nimeshamgundua…!!
Nilidakia hapo hapo, umeshamjua huyu mwanamke anayetusumbua? Bora hii zoezi liishe maana
tumeshachoka sasa, nilijikuta namtamkia huku akinitazama machoni na pia akinisikiliza maneno
niliyokuwa namuambia,hapana simaanishi namjua huyo mtu namanisha nishamgundua huyu mtu njia
aliyotumia kupiga mpaka namba yake isionekane, nilijikuta nachoka kabisa kwa maaana nilijua zoezi
linaweza kuwa limefika mwisho kumbe wapi, haya hebu nambie endelea nilijikuta nazungumza
kivivu na kwa nafsi ya kukata tama, huyu mtu atakuwa amekaa sana Columbia na brazili aliendelea
kuniambia, huko ndio huu kchezo upo pia atakuwa na utaaalamu sana na compyuta hapa hata
tufanyaje namba yake hatuwezi kuipata kirahisi maana alichokifanya hapa ni kuingilia kwenye
syteam ya wave transformation katika satellite yetu kuna code atakuwa ametumia kufanya
hivyo.niliishiwa nguvu kabisa, sasa tutaipataje kuipata nilimuuliza, hapo ndipo kazi ilipo kuipata iyo
namba ni kipindi tu pale itakapokuwa inazungumza ndipo hapa itasoma lakini baada ya hapo huwa
inafutika hii huwa inatumiwa sana na wauza madawa ya kulevya Brazil na Columbia kwa lengo la
kuwezesha shughuri zao pia huwa inatumiwa na watekaji wa watu huko chile ambapo kuna magenge
ya wahuni huwateka watoto wa matajiri na kuwapigia simu wazazi wao watoe pesa lasiivyo
watawauwa watotot wao hivyo huwa wanatumia hii system ili kuepuka kukamatwa,
Jamaa alizidi kuleta hadithi na maneno mengi mpaka akajikuta ametoka nje ya mada, kaka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nakuelewa sasa unajua nini lengo hapa ni moja tu jinsi ya kumkamata huyu mwalifu sasa
tunafanyaje? Tatizo ni kwamba naweza kutegesha hapa ikiita nijue lakini akibadili laini tu hapa
inakuwa kazi nyingine sipati kitu ila nakuahidi hili jambo nitalifanyia kazi kwa nguvu zote naomba
unipe siku tatu samahani sana tuwasiliane ijumaa aliniambia Yule injinia basi tuliagania huku
tukibadilishana naye namba za simu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment