Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

WANAWAKE NI WAUAJI ?! - 1

 







    IMEANDIKWA NA : MTOTO WA BECKER ( HUSSEIN BAKARI )



    *********************************************************************************



    Simulizi : Wanawake Ni Wauaji ?!

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa kunipa pumzi na afya njema hadi leo hii niko hai japo niko tofauti sana na awali hadi wasionijua wakiniona hii leo wanadhani nilizaliwa hivi… La hasha! Ila leo nitawaambia ukweli wa yote yaliyonisibu na yanayowasibu wanaume wengi kila siku ktk dunia hii ya leo. Nakumbuka babu aliwahi kunambia na kunisihi niwe makini sana na wanaake pindi nitapokuwa mkubwa na alinifundisha niwasome na niwaelewe wanaake ni watu wa aina gani, lakini sikuwahi kuamini maneno yake hadi yalipokuja kunisibu haya na ndipo nilipokumbuka na kuelewa maneno ya babu.



    Aaaaagh! Wanawake ni mama zetu na ni pambo la dunia na ndio maana mungu aliwaumba ili watufariji na watulee lakini ukweli bado unabaki kuwa wanawake ni watu hatari sana kwetu wanaume. Hebu tukumbuke hata kwenye hadithi za watu wa kale kwenye vitabu vya dini tukianzia mwanzo kabisa wa dunia enzi za Adam na Hawa/Eva. Adam alitii kila kitu ktk mamlaka aliyopewa na mungu lakini mwishoe anakuja kumkosea mungu kwa kutenda dhambi aliyoponzwa na mkewe Hawa baada ya kushawishiwa na Shetani, Eeeh, amini usiamini shetani ni vigumu sana kumuingia mwanaume hivyo anamtumia mwanamke kama alivyomtumia Hawa kwenda kumlubuni mwanaume kama alivyolubuniwa Adam na kujikuta mwanaume anaumia kwaajili ya upendo na kumuamini sana mwanamke pasi na kuelewa kiundani udhaifu mkubwa wa mwanake mwenyewe.



    Tuachane na Adam, tukumbuke Samsoni mtu mwenye nguvu sana aliyewapa tabu sana Wafilisti enzi hizo lakini mwishoe anakuja kukamatwa na kupata mateso makali baada ya kulubuniwa na Delila aliyetumiwa na Wafirist kubaini siri za nguvu za Samsoni. Eee, Samsoni nae akaponzwa kwaajili ya mwanamke na si yeye wala Adam tu tukumbuke hata mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na sababu ya kifo chake kilitokana na Mwanamke!! EE ni wanaume wengi mno wameponzeka kwaajili ya wanaake na mmoja wao ni mimi na ndio maana leo hii nasema WANAAKE NI WAUAJI. Najua wengi mtanielewa vibaya hususani wanaake lakini naomba msizime t.v zenu ili mnielewe vizuri kwanini hasa nimekazania kusema Wanaake ni Wauaji…. Hii ni asili iliyoanza toka kwa mwanamke wa kwanza kabisa kuumbwa na bado ipo na itakuwepo na itawaumiza wanaume wengi sana wasiokuwa makini na ndio maana hata mungu hakuwahi kushusha nabii wa Kike. Wanaake ni wadhaifu wasiokubali udhaifu wao na ndio maana nawaita Wauaji..



    Achilia mbali vitabu vya dini tukija kwenye maisha yetu ya kila siku lini ulishawahi kusikia Mwanaume katupa katoto kachanga? Naamini kama mimba wangekuwa wanabeba wanaume usingesikia neno Kutoa Mimba. Hivi ushawahi kujiuliza mwanamke ana moyo wa namna gani?!! au Unadanganywa na maumbile yake na sauti raini unajisahau na unaacha kuwa makini nae? hivi hujui kwamba Simba Dume ana muungurumo mkubwa sana lakini Jike ndie jasiri wa kuua..?

    huo ni mfano tu lakini nataka unielewe na uwe makini kwanini nasema WANAAKE NI WAUAJI..."""""



    Ilikuwa ni sauti kutoka kwenye luninga kutoka kwa bwana mmoja mlemavu wa macho na miguu akiongea ktk kipindi cha YA WALIMWENGU LIVE kilichokuwa kinarushwa kupitia kituo cha BEKATV kila siku za Jumaapili asubuhi na marudio yake Jumaamosi jioni.



    Nilikaa kwenye sofa huku nikiwa nimeshikilia kikombe cha chai, kwa umakini mkubwa macho na masikio niliyaelekezea kwenye TV huku nikichukua rimoti na kuzidisha sauti kwa lengo la kumsikia yakinifu yule bwana kwani mada yake ilinistua na kunigusa sana hali iliyochochea niwe na shauku kubwa ya kusikiliza hiyo story yake ili nielewe vizuri kwanini anasema wanaake wote ni wauaji....!!!??



    Nilitulia na kujikuta nashindwa hata kupeleka chai mdomoni na kubaki nimeshikilia kikombe nikimsikiliza kwa makini pindi yule bwana alipokuwa anazungumza ambapo aliendelea kwa kusema….



    “Nakumbuka miaka kumi iliyopita nilikuwa na maisha mazuri kabisa nay a furaha mimi na mke wangu kipenzi baada ya kufunga ndoa, ki ukweli nilimpenda sana mke wangu nae alionesha mapenzi hasa na kunisahaulisha maumivu niliyopata kutoka kwa mke wangu wa kwanza tuliyeachana muda mfupi tuu baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu na kuanza visa vilivyosababisha nimuache aishi maisha aliyotaka yeye na ndipo baada ya miezi kadhaa nilipompata huyu mwanamke wangu mwengine aliyeonesha kuwa na vigezo vyote nilivyohitaji na mwaka mmoja tu katika mahisiano yetu tuliamua kufunga ndoa kabisa.

    Kiukweli mke wangu nilijivunia uzuri aliokuwa nao upole wake na tabia ya kupenda ibada na mara nyingi alinibadilisha kwa maneno matamu na kunisihi niache kunywa pombe na kweli ilifika kipindi niliacha pombe na taratiibu nilipunguza kabisa kuvuta sigara kutoka pakiti moja kwa siku hadi ikafika mahali siku nzima nikavuta sigara mbili tu, hali iliyofanya hadi walionijua kunishangaa na kumsifu sana mke wangu na ndipo name nilizidisha moyo wa kumpenda na kumpa uhuru wa kila kitu kwani nilimuamini mno…”



    Alinyamaza Yule bwana kasha aliendelea…….



    “Kila nilichofanya nilihakikisha lazima mke wangu ajue na nilisikiliza sana na kufata ushauli wake kuliko mtu mwengine akisema nisifanye kitu frani name nilitii akisema nifanye name nilitii hiyo yote nilifanya nikiamini namjenga na kumuonesha kiasi gani namthimini bila kujua kua kuna ugonjwa m baya nilikuwa naufuga.. Awali sikuona tofauti yoyote wala kuhisi kama kuna kitu nakosea zaidi nilianza kusikia minong’ono kutoka kwa majirani na baadhi ya ndugu zangu kuwa napelekeshwa na nimetawaliwa na mwanamke, kiukweli nilichukizwa na habari zile na kugombana na baadhi ya ndugu zangu waliomsema vibaya mke wangu nikiamini fika wanataka watugombanishe na wananionea wivu kwa kupata mke wa namna ile kwani maisha yetu yalizidi kunyooka siku hadi siku.

    Aaaaaagh.. kuna muda huwa nahisi kama ndoto vilee kwani sikujua kabisa kumbe kuna bomu nalitengeneza mwenyewe ambapo baadae litapolipuka litaniletea madhala makubwa na kama si kuniua basi litanipa ulemavu wa kudumu kama ilivyotokea baadae…. Aaaagh, mke wangu!!!...”



    Alivyozidi kuongea Yule bwana ndivyo nami nilivyozidi kutulia kumsikiliza kwa makini huku nikibofya bofya rimoti kuongeza sauti mara kwa mara utafikiri nina ubovu wa masikio. Nilimuangalia kwa jicho la shauku ya kujua yaliyomsibu kwani alitia huruma pia alionesha kuna mazito yalimkumba hadi kusababishiwa ulemavu ule.

    Lakini kabla sijafaidi vizuri hadithi ya Yule bwana ghafra umeme ulikatika na kila kitu kuzimika.



    “Aaaagh, kum*m*ake Tanesco bwana kama maboya!!!”

    Nilinyanyuka kwa hasira na kuzima Switch ya TV na kuwasha switch ya taa ili umeme utaporudi tuu taa inijulishe mapema.



    Wakati huo ile chai ilikuwa ya baridi kabisaa na sikuambulia kunywa hata chembe ndipo nilipoenda kuimwaga na kurudisha kikombe na muda huo nilikumbuka kuwa nimeacha simu ndani kwenye chaji na isitoshe tulikuwa na miadi ya kukutana na mchumbaangu Mariam au Mamu kama nilivyozoea kumwitaga.

    Nilikuta simu ikiwa na missed call tisa msg nne na nilipofungua zote zilikuwa toka kwa mamu.

    Nilizisoma zile msg ambapo mojawapo iliandikwa hivi…



    MBONA HUPOKEI SIMU WALA HUJIBU MSG ZANGU? KAMA UPO NA MALAYA WAKO SI UNAMBIE TU NISIJE..!!



    “hahaa Wanaake bwana..”

    Nilijisemea moyoni na kuingia sehemu ya ujumbe kui reply ile msg lakini kabla sijabonyeza Send mlango uligongwa na nilipoenda kufungua alikuwa ni Mamu kipenzi change ambapo nilifurahi kumuona nilimkumbatia na kum busu japo alionesha wazi kuwa kanuna kisha aliingia na kunipita bila kusema chochote na kwenda kukaa Sebureni.

    Nilibaini kuwa amenuna kutokana na kutopokea simu yake na nilijua sasa nina wajibu wa kum bembeleza nimuweke sawa .

    “Unakunywa nini bebi..”



    “Sitaki kunywa chochote niache..”



    Jiubu lake lilizidi kunihakikishia kuwa nina kibarua ka kubembeleza mtu mzima sasa lakini kabla sijafanya hayo yote mara taa ya sebureni iliwaka na ndipo nilipokumbuka kuwasha TV kwanza niendelee na kile kipindi huku moyoni nikiwa na shauku na mamu nae amsikie Yule bwana juu ya story yake na kuwatuhumu kuwa Wanaake wote ni Wauaji.



    Mada ya Yule bwana hasa kauli yake ya kuwa wanaake wote ni wauaji ilimchukiza sana Mamu na kuamua kuzima TV kwa hasira.



    “Aaag! Wee vipi?”

    “Vipi nini!!?”

    “Si uache tuangalie sasa unazimia nini..!!”

    “Hivi Hussein kwa akili zako timamu unaona hiki kitu anachokizungumza huyu mpuuzi ni sahihi!!”

    “Kitu gani..”

    “Kusema wanaake ni wauaji..”

    “..Mh! hapo kumjaji moja kwa moja itakuwa ngumu, sasa nitamjaji vipi wakati hata story yenyewe sijaisikia!! anaweza kuwa sahihi au si sahihi inategemea na point zake mwenyewe.”

    ..”Hivi nyinyi wanaume mpoje!!!”



    Aliwaka Mamu kwa sauti ya juu na kusimama huku akinitazama kwa hasira kutokana na majibu yangu.



    “Hivi mnatuchukuliaje sisi wanaake eeh!!?”

    “Kivipi baby.. mbona tunawakiana sasa.”

    “Sio Nawakaa.. ila nakwambia ukweli acha kuwa na mitazamo ya kijinga au ndio kashakulisha ujinga huyo mpuuzi mwenzio…! Kwa hiyo na mimi muuaji si ndio, au unanionaje!!”

    “Hapana baby sijamaanisha hivyo..”

    “kumbe unanionaje..”

    “Unaweza kuwa muuaji au si muuaji inategemea tuu..”

    “Aahaa.. kwa hiyo hadi mamaako aliyekuzaa Muuaji, dada zako wauaji, shangazi zakoo si ndio..!”

    “Sasa mamu hayo matusi..”

    “Matusi nini.. si Wanaake ni Wauaji!!! We vipi.. Hebu nipishe huko nisije nikakuua buree..”



    Alichukua mkoba wake pale kwenye sofa kwa hasira Mamu alielekea mlango wa kutokea ulipo na kutoka huku akiubamiza kwa nguvu ule mlango.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aaagh!! Sasa huo mlango umekukosea nini..”



    Nilibaki nimetahayuri pale kwenye kiti huku nikiwa nimechanganyikiwa kwa jinsi Mamu alivyonibadilikia huku nikijilaumu upande mwengine kwa kusababisha mpenzi wangu kuwa na hasira mara tatu zaidi alivyoingia.



    Niliuendea mlango na kuokota funguo zilizodoka pindi ulipobamizwa na Mamu kasha nilirudi na kujitupa kwenye sofa huku akili yangu ikiwa haipo sawa niliiwasha tena TV safari hii nikiwa sina mzuka kabisa wa kuangalia kile kipindi ambacho ndio kilikuwa kinaishia lakini kuna maneno ya mwishoni ya Yule bwana yalipenya vizuri masikioni mwangu na kukistua kichwa change kidogo pindi aliposema…..



    “Najua wanaake wengi wataobahatika kunisikiliza na kunitazama watanichukia na kuona nimewadhalilisha na kuwatusi.

    Na mimi sitoshangaa wala kuogopa hilo kwa sababu najua kuwa wanaake tayari wana ulemavu wa asili ambao mungu aliwaumba nao kwa dhumuni la kuwa wasaidizi na wafariji kwa wanaume tu. Mwanaume hajaumbwa kwaajili ya mwanamke ila mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume na ndio maana tunaambiwa kuwa mwanamke ametoka ubavuni kwa mwanaume. Lakini udhaifu wao ndio unafanya tuone mpaka leo hii wanaake wakitaka kushindana na wanaume nah ii kutokana na kuwa mwanamke ni rafiki mkubwa wa shetani anayetumiwa ktk kuiharibu dunia na hata baadhi ya wasomi wa dini wanatwambia wanaake wengi sana wataingia motoni.



    Mungu ameweka mifano mingi sana ya wazi kuwakumbusha wanaake kuwa mwanaume ni kiongozi na anapaswa kunyenyekewa na mwanamke japo kwa akili mbovu za wanaake wengi wanaona kufanya hivyo ni ujinga kwani hata wao wanaweza kufanya wanayofanya wanaake.. ha ha haa yaani hata mifano ya wanyama hawaioni!! Wazee waliosema Wanaake mwalimu wao kipofu walikuwa na maana kubwa sana ambayo sasa wengi hawaizingatii.



    Cha mwisho nakukumbusha wewe mwanaume unayenitazama hususani wewe uliegombana na Mkeo au mpenzi wako hivi punde chanzo kikiwa hiki kipindi na hii mada yangu… Nataka ujue kwamba uko katika wakati mgumu sana na huyo mwanamke.. tena nakusihi uwe makini nae sana.. Ukipuuza siku moja yanaweza kukukuta kama yaliyonikuta mimi hata kama hautakuwa na ulemavu wa viungo kama mimi. Kuweni makini na wanaake wanaume wenzangu..”



    Nilishtuka kwa maneno yale na kuhisi kama naambiwa mimi moja kwa moja.



    Muda mfupi baada ya kile kipindi kuisha nikiwa nimeketi huku kichwa changu kikiwa na mawazo kibao nikijiuliza mwenyewe nishike yapi niache yapi huku nikikumbuka na kauli za Mchumbaangu kipenzi.

    Nikiwa nimeduwaa nikifikiria jinsi ya kusorve tatizo langu ili nimueke sawa mamu mara msg iliingia kwenye simu yangu,

    Nilipoichukua kuifungua alikuwa ni Mariam.



    Msg ilisomeka hivi…

    “”” Hussen nashukuru sana kwa matusi yako ya kuwa eti mi ni muuaji haina shida ila kama ulikuwa hunitaki na ulikuwa unatafutia sababu ungenambia mapema tuu kuliko kupoteza muda wangu.. Nashukuru sana nakutakia Maisha Mema..”””



    Sio siri msg ya Mamu ilinichanganya sana kwani sikutaraji kabisa kama kile kipindi kinaweza kusababisha yote yale,

    Niliisoma mara mbili mbili ile msg na kuamua kumpigia mpenzi wangu Mamu lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

    Sikuchoka niliendelea kupiga lakini bado haikupokelewa na mara nyengine ilikatwa na mwishoe nikawa nasikia sauti ya huduma kwa wateja wakinambia kuwa namba ninayopiga inatumika.



    Niliachana na simu na kuingia bafuni kuoga niliporejea chumbani nikatupia pamba kama kawaida yangu.

    Eeeh.. kupendeza ilikuwa kawaida kwangu kutokana na jinsi nilivyojua kupangilia mavazi hadi watu wengi kitaani wakawa wananita bitozi, si unajua tena uswahilini kila chocho unayokata ukiwa umejitupia sana watu macho kodooo.



    Nilirejea sebureni baada ya kujiridhisha kwa nguo nilizovaa siku hiyo na kabla sijatoka nilipiga tena simu ya Mamu lakini jibu lilikuwa lile lile kwamba namba ninayopiga ipo bize.



    Sikuwa na jinsi ilibidi nitoke na kuchukua bodaboda kuelekea kwa kina Mariam nikiwa na nia na madhumuni ya kwenda kuomba msamaha ili mapenzi yetu yaendelee kwani nilimpenda sana na nilijua kama nisingeenda muda huo basi ingebidi nisubiri hadi wiki ijayo kwani nisingepata nafasi kutokana na kuwa kazini muda mwingi na kuchelewa kurejea.



    Baada ya mwendo wa dakika kumi tulifika maeneo ya kina mam na kumlipa ujira wake yule dogo aliyenileta nami moja kwa moja nikaanza kuongoza njia ya kwa kina Mamu huku nikiwazia jinsi ya kuanza.



    “Karibu baba.”

    Nilikaribishwa na mamaake niliyemkuta akiwa nje amekaa kwenye kolido ya nyumba yao akiwa anasukwa na mwanae mwengine wa kike mdogoake Mamu.

    “Asante mama shkamoo”

    “Marahaba baba za huko”

    “Safi tu mama sijui nyinyi”

    “Sisi ka unavyotuona tunamshukuru mungu enhee mbona hivyo baba kwema!”

    “hehee.. Kwema tu mama”

    Nilijibalaguza kwa kujichekesha baada ya kuhisi huenda mama Mamu kashastukia mchezo nikiwazia kwa kurudi Mariam mapema vile na ujio wangu pia lakini nilikuja kushangaa baada ya mama Mamu kuniuliza swali ambalo nilikuta nashindwa kulielewa na kuuliza tena badala ya kujibu mithili ya mtu mwenye matatizo ya masikio.



    “Unasemaje mama!!?”

    “Nimekuuliza mwenzio yuko wapi..? maana alituaga anakuja huko kwako muda mrefu tu aliondoka hapa sasa umenishangaza nawewe umekuja muda huu ukiwa pekeako, ndio maana nimekuuliza kwema?”



    Nilijikuta nashusha pumzi kwanza mara baada ya kusikia na kubaini kuwa Mamu hajafika kwao tangia muda ule alipoondoka kwangu.



    “Vipi baba mbona huongei..! unatutisha wenzako”

    Ilikuwa ni sauti iliyonizindua kwenye dimbwi la mawazo ya ghafra nilipokuwa nafikiria alipoenda Mamu muda wote ule hajafika kwao.

    Niliogopa kimtindo kwa kuhisi kama kitampata kitu kibaya huko basi namimi nitahusika kwa kiasi kikubwa pia nilivyoelewa kuwa Mamu atakuwa kachanganyikiwa sana na anaweza kujifanyia hata kitu kibaya mwenyewe kutokana na kujua kiasi gani ananipenda na mara nyingi hakutaka nimuudhi kabisa.



    “Hah, ni hivi mama kweli Mamu alikuja lakini hakukaa sana akadai kuwa kuna vitu amesahau so, nimsubiri kuwa anarudi nyumbani kuchukua hivyo vitu na atakuja tena, sasa nimekaa na nilipoona anachelewa sana ndipo nikaamua kuja huku kwa lengo la kumfata yeye.

    Sasa ulivyoniuliza ndio mana nimeshangaa ina maana hujamuona huku kurudi..!”

    “Hee!! We babaa eeh ina maana awe karudi afu mi nikudanganye! Mwanangu hajarudi na si mzurulaji hebu usitufiche baba nambie umemuacha wapi mwenzio au nini kimetokea huko kwenu..?”

    “Hakuna chochote mama”

    “sasa mbona hueleweki eleweki simu unayo kwanini hukumpigia kujua alipo hadi unakuja kumuulizia”

    “Okeeey, samahani mama nimekumbuka alinambia kabla ya kuja huku kuna sehemu kwa shogaake angepitia kule mwenge. Tena ngoja nimfate huko kabisa nahisi hajatoka”

    Ilinibidi kudanganya na kuongea maneno ya matumaini hasa mala baada ya kumuona yule mama akizidi kubadilika.



    Kiukweli nilitambua fika kuwa Mariam anapendwa sana na mamaake muda mrefu tuu na ukizingatia yule mama alikuwa na watoto wawili tu wote wa kike na babayao alifariki muda mrefu sana hivyo hata jinsi alivyowalea wanae walikuwa si watu wa kutokatoka ovyo wala kuzurula hivyo kitendo cha kusikia mwanae hayupo kwangu kilianza kumpa presha kidogo nami nikatumia akili ya ziada kumpunguza na kumkwepa kwa kujidai naenda Mwenge kwa huyo shogaake Mamu.



    “Baba naomba utavyorejea uje na mwanangu tafadhali, kwanza kisheria na kidini bado hujakabidhiwa. Asilale hukoo”

    Aliongea yule mama kipindi hiko nilikuwa nimesimama na kuaga kisha niliondoka kuelekea stendi ya daladala nikiwa na mawazo tele mara mbili na niliyokuja nayo.



    * * * * *



    Safari yangu ilinipeleka mpaka pande za fukwe za coco na lengo halikuwa kuogelea wala kufanya mazoezi bali ni kupunguza angalau robo mawazo yaliyoandama kichwani mwangu siku hiyo na kufikiria ni heri tusingekutana tu siku hiyo na Mamu kwani mipango yote ya kufurahi pamoja wikiendi ile iliyeyuka ghafra kama machoci ya samaki kwenye maji.



    Niliwazia nitamwambia nini yule mama endapo Mariam asingeonekana siku hiyo kabisa.

    Niliwaza pia ina maana Mamu anaweza akajifanyia tukio hata la kunywa sumu kwa kajiugomvi kale tuu! Na kama akifanya hivyo nini kitanikuta baadae..! si ndio itakuwa basi tena.



    Niliwaza mambo mengi sana na kuchukua tena simu kupiga nmba ya Mamu lakini bado jibu likawa lilelile ndipo nilipogundua sasa Mamu atakuwa kanireject.

    Nilijisonyea moyoni na kuemtumia msg nikimsihi na kumuomba popote alipo basi arudi nyumbani haraka wanamtafuta.

    Japo nilituma zaidi ya meseji tano lakini hakuna hata moja iliyojibiwa.



    Nikiwa bado nimekaa juu ya jiwe moja nikining’iniza miguu huku nikiirusharusha na kuangalia watu mbalimbali waliofurika week end ile wakiogelea na kufurahia maisha.

    Nikiwa nimeangaza huku na kule moyo wangu uliripuka ghafra nilipomuona bint mmoja akiwa kavaa kipensi chepesi kifupi kilichom bana bara bara huku akiacha sehemu kubwa za mwili wake nje ambapo kifuani alijisitiri na kisidiria kidogo cha kamba kutokana na udogo wa matiti yake.

    Kilichonistua zaidi si umbo lake tuu na mavazi yake bali nilipouona uso wake vizuri akiwa kashikwa kiuno na baunsa mmoja ambae kushoto kwake alishika pila kubwa la kuogelea.

    Hakuwa mwengine yule bint bali kipenzi changu Mariam akiwa na yule njemba wakielekea majini huku wakionesha nyuso za furaha.

    Nilijikuta mwili unatetemeka kwa hasira na midomo kunicheza cheza huku macho yakiwa hayaamini kile kilichokuwa kinaonekana.



    "Shiiiiiitttttt!!!!!!...?!~!!"



    Niliruka pale juu ya jiwe na kujikuta nakanyaga maji licha ya kuwa nilivaa raba na suruali yangu ya jeans lakini sikujali wala kufikilia hilo nilitembea haraka kule alipokuwa kipenzi changu Mamu na yule boya na kabla hawajafika kwenye kina cha kuogelea niliwakuta na kulianziasha palepale.



    “Mamu hapa unafanya nini na huyu ni nani..!?”

    “Hii we kaka vipi.. Eti baby unamjua huyu!!?”

    Alijibu kwa taharuki Mariam huku akimuangalia yule baunsa na kujisogeza jirani zaidi na kujifanya hanijui kabisaaa. Moyo ulinichoma na kujikuta naongea huku midomo ikinicheza cheza kwa hasira na kutoamini kama yule ndie Mamu ninayemjua mimi au kivuli chake.

    “Mamu !!? hivi umepatwa na nini lakini..!”

    “Hivi baby unamuelewa huyu..”

    Aliongea Mamu kauli iliyonichoma zaidi ya msumali uliopigiliwa katikati ya kidonda na kubaki natazamana na yule baunsa huku nae akionesha kunishangaa na kukereka

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oyaa mwana, usitupotezee muda katika starehe zetu hebu jikatae haraka kabla cjakufanya kitu mbaya sasa hivi, tena usinihamshie wazimu oooohoooo Tokaa Bwegeee..”

    Aliongea yule baunsa na kunisukuma lakini nami sikukubali japo sikuwa baunsa wala kuwahi kucheza mchezo wa ngumi nilijikuta namsukuma na mimi.

    “afu nawewe kum* tu usinizingue hizo nyama tu hata kwenye sambusa za kichina zipo. Hunitishi wala nini.”

    Nilibwatuka baada ya kumpush yule njemba lakini hamadi!! Nilistukia napigwa ngumi kali ya meno iliyonipeleka moja kwa moja chini na niliponyanyuka ili nikabiliane nae alinibamiza na lile pila usoni hadi nikaona cheche za moto mbele yangu na nafsi yangu kutamani watu waje kutugombezea lakini tofauti na ubaya wa watu wa Dar ndio kwanza walikusanyana na kuzunguka eneo lile kutazama video ya bure huku kipenzi changu Mamu ndio kwanza hakuonesha kujali chochote.



    ‘’’’PWAATCHAAA’’’’



    Kelele za maji zilisikika pindi nilipodondoshwa kwa mara ya pili na kuloana mwili mzima na mengine kuniingia puani na mdomoni.

    Kilichonisikitisha zaidi ulinzi eneo la fukwe naweza kusema kama haukuwepo kabisa kwa raia zaidi askari wachache walikuwepo eneo la nyuma za fukwe wakilinda magari yaliyopack huku wengine wakiwa maeneo yale ya ndani ya kumbi na kujisahau kama raia wa nje hasa akina sisi wa hali ya chini pia tunahitaji kulindwa hasa linapotokea kasheshe la uonevu kama lililonikumba mda ule.



    Nilipiga hesabu za harakaharaka na kuona kama nitazembea zaidi naweza kufa kwani Yule baunsa alinichachamalia hasa baada ya kuona watu wanamshangilia.

    Nilinyanyuka kwa mbwembwe huku nikijifanya nami namtafuta nimpachinge zangu ndipo ghafra kwa kwa kasi ya kope niliinama sambamba na kutoa ukelele wa hatari na kumrushia maji usoni Yule baunsa na alipozubaa tu sekunde zilezile nilipenya kwenye ukuta wa watu na kukimbia eneo lile huku watu wakizomea huku wengine wakicheka hali ya kuwa mwenzao nilizidiwa bila hata kunionea huruma na kwa mbali kipindi nakimbia nilisikia kicheko cha sauti ya juu toka kwa mpenzi wangu Mamu huku nae akinizomea pia.

    Daaah!! ktk siku nilizowahi kujisikia vibaya na kupatwa aibu kubwa na sitoweza kuzisahau na hii pia ni mojawapo, kwani nilijisikia vibaya sana na sikumbuki vizuri speed niliyotoka nayo kama yule baunsa alinifukuzia ama laa, lakini nilichokuja kukumbuka vizuri zaidi ni pale nikiwa ndani ya daladala mara baada ya kustuliwa na sauti ya dada mmoja.



    “Wee kaka vipi! Simama vizuri unaniroweshaa…!!”

    Sauti hii ilinifanya nijibane zaidi mlangoni aliposimama konda

    Huku abiria wengi wakinishangaa kwa jinsi nilivyoonekana kwani siku hiyo jua lilikuwa kali sana nami nililowa chapachapa tena nikiwa nimepiga pamba za nguvu na raba kali.



    Ilinibidi nishuke tu kituo cha mbele kwa aibu na kuanza kupiga hatua mdogo mdogo na njia nzima kila niliyepishana nae aligeuka kunishangaa si mkubwa wala mtoto yaani niligeuka bonge la kituko cha siku kila nilipopita.

    Nilizama geto na kubadili zile nguo na nilipojitazama kwenye kioo ndipo nilipobaini kuwa nilikuwa na uvimbe (nundu) kwenye paji la uso pia mdomo wangu wa chini ulipasuka kidogo na kulikuwa na vidamu vimegandia sehemu ya kidevu.

    Nilijisonyea mwenyewe na kumlaani Mariam kwa alichonifanyia huku nikimshukuru Mwenyezi mungu kwa kuniokoa kwenye mikono ya baunsa yule na muda uleule nilikumbuka kuifuta kabisa namba yake kwani nafsi yangu tayari iliingia kinyongo na sikutamani kuja kuonana nae kamwe..!! Lakini nilipotazama mifukoni kutafuta simu nayo sikuiona hata wallet yangu nayo haikuwepo ndipo nilipobaini kuwa nilividondosha navyo kwenye hekaheka ile na kukumbuka kuwa hata kwenye daladala nauli sikulipa wala konda hakunidai hata nilivyoshuka kule njiani.

    Nilishusha pumzi na kumshukuru tena mungu na kuwazia hata nitaponunua simu sitokuja kuleinew line wala sitomtafuta tena Mariamu kivyovyote.



    * * * * *



    Ilipita wiki nzima nikiwa mnyonge sana kuanzia kazini mpaka mitaani sikuwa na shauku hata ya kutaka kujua maendeleo ya mamu niliamua kujieka bussy na mambo mengine huku upande wa pili moyoni nilikubaliana na maneno ya yule bwana kuwa inawezekana kuwa kweli wanaake ni wauaji.

    Niliwazia endapo yule baunsa angenizimisha ama kuniua yote ingekuwa kwa sababu ya Mamu… pia niliwaza kuwa ina maana mamu alidhamilia muda mwingi kufanya vile ama alifanya kama kulipa kisasi kwa maneno yangu? Lakini ikawaje iwe mapema vile tena siku ileile.

    Nilichoka na kuendelea kumlaani licha ya kuwa ukweli nilimpenda sana.



    Miezi ilipita na hatimae ilikatika miezi nane nikiwa sijawahi kuwa na mahusiano mengine yoyote wala kukutana kimwili na mwanamke yeyote.

    Na katika siku hizo tulipata safari kikazi mkoani Arusha na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Arusha.

    Jiji la Arusha lilikuwa tofauti sana na Dar kuanzia hali ya hewa hadi tabia za watu, sio siri ktk kipindi kifupi nilijikuta nalipenda sana jiji lile.

    Nakumbuka siku moja usiku nikiwa nimelala niliota ndoto kuna sehemu tumeenda kufanya kazi muda wa mapumziko mchana tulizunguka eneo moja ambapo nilikutana na msichana mrembo sana na katika maongezi nilipomuuliza jina alinambia kuwa anaitwa Zai.

    Nilishtuka usingizini na kufikilia sana ile ndoto na siku mbili baadae nilishangazwa na taarifa kuwa inatakiwa tufike eneo ambalo nililiota na tulipofanya kazi ilipofika mida ya chakula na mapumziko ya mchana nilishangaa tulikuwa tunazunguka maeneo yenye mandhali ileile kama niliyoiota na kilichokuja kunishangaza zaidi na zaidi nikiwa na mshikaji wangu tunatembea tulipishana na msichana mrembo sana na tuliangaliana huku sura yake ikiwa haina tofauti kabisa na yule niliyemuota na chaajabu zaidi nilijikuta namwita jina lile nililoliota kwa mara tatu mfululizo hadi rafiki angu niliekuwa nae alinishangaa



    "Zaiii, Zaaii.. Zainaab.."



    “Oya unamjua au unaropoka tu..”

    Aliniuliza rafiki angu pindi nae alipogeuka na kuona yule binti kasimama nami bila kusita nikaamua kumfuata.

    “mambo Zai..”

    Nilimsalimia.

    “Poa, ila mi mbona sikukumbuki na sidhani kama tuliwahi kuonana!!?”

    “ni kweli unaweza kuwa sahihi kwa upande mwengine miili yetu haijawahi kuonana ila nafsi zetu ziliwahi..”

    “kivipi mbona sikuelewi.”

    “Utanielewa tu, kama hautajali chukua namba zangu hizi tuwasiliane zaidi”

    Niliongea na kumkabidhi kikadi changu cha mawasiliano huku nae akikipokea kwa mshangao akiwa haelewi tulikutana vipi nami sikungoja maswali zaidi niliondoka na kumkimbilia rafiki yangu ambae alibaki ameduwaa muda wote niliposimama na yule mrembo.







    “mwanangu mbona sikusomi!!”

    “hahahaaa hamnaaa utanisomaa tuu.”

    “heee! Hayaa, sema mtoto mkali kishenzi, umemjuaje, ?”

    “nitakwambia tuu usiogopee”

    Nilimzuga mshkaji japo bado alionesha hajaridhika na majibu yangu lakini kwa upande wangu kichwani nilijiuliza sana imekuaje nimeota ndoto na imetokea vilevile..!!

    Nilihisi ujinga kama nitamwambia mshkaji eti nimemuota yule dem nilijiua asingeniamini kabisa kwani ni nadra sana mtu kumuota mtu asiyemjua akamtajia mpaka jina harafu siku si nyingi wakakutana tena kiukweli na ikawa vilevile.



    Tulirudi kuendelea na kazi na chaajabu siku zilipita sikupigiwa simu na Zai wala kupata sms yake na kwakuwa sikuchukua namba yake iliniwia vigumu kumtafuta na hata tulipotembelea tena yale maeneo sikuwahi kumuona hadi muda wa kuwepo Arusha ulipoisha na safari ya kurejea Dar ilijili na kukusanya vitu vyetu na kurudi rasmi jijini DSM.



    * * * * * * *



    Ilipita miezi minne sawa na mwaka mmoja tangu niachane na Mariam na nilikuwa nimehama kabisa lile eneo nililokuwa nakaa awali na nilipanga sehemu nyengine mbali kabisa pembezoni mwa jiji.

    Siku hiyo nilipotoka kuoga baada ya kurudi kazini nilikuta simu ikimalizia kuita na nilipocheki namba ilikuwa ngeni na kulikuwa na missed calls nne . Nikiwa bado nina taulo niliamua kuipiga ile namba huku nikiwa nimesimama najiangalia kwenye kioo cha dressing table na haikuchukua muda kuita sana upande wa pili mara ilipokelewa na sauti raini ya kumtoa nyoka pangoni ilisikika.

    ‘’’Hallow, samahani naitwa Zai nipo hapa Arusha uliwahi nipa hii namba siku moja japo ni muda kidogo ulipita nilikuwa na matatizo nilisahau kukupigia.. nadhani naongea na mtu sahihi..”

    Sio siri nywele zote zilinisisimka

    kusikia sauti ya mrembo ambae niliwahi kumuota na kukutana nae nilipokuwa Arusha kikazi na nilishakata tamaa ya kuonana nae tena lakini ikawa ajabu leo kanitafuta baada ya kimya kingi kupita.

    Kwa kutoamini kwangu nilijikuta namjibu harakaharaka.

    “kweli kabisa ni mimi Hussein hapa upo wapi Zai..”

    “Mi niko Arusha na leo asubuhi nilipokiwa napangapanga nguo zangu kwaajili ya safari kesho ndio nikaikuta namba hii kwenye begi langu moja niliihifadhi na nilishasahau lakini nilipoiona tu ndo nikakukumbuka hivyo nimeona vyema nikuage pia unikumbushe umenijuaje au kama unaweza tuonane leo maana umenitia shauku sana ya kujua umenijuaje”

    “Oooooh, unasafiri kesho.. wapi sasa”

    “naenda Dar”

    “Dar!!! Haha mungu mkubwa mi mwenyewe niko Dar kule nilikuwa kikazi tu”



    Nilimjuza Zai na tukaongea mengi sana juu ya safari yake ambapo alinambia kuwa ndio mara yake ya kwanza kuja jijini DsM na safari yake ni kwaajili ya masomo ya elimu ya juu na angefikia kwa shangazi yake huko Kinondoni japo alinilazimisha nimwambie tulionana wapi lakini nilimzuga kuwa tutapoonana nitamkumbusha.

    Na kweli baada ya Zai kufika jijini na ilipofika wiki moja siku ya jumapili ilibidi nizuke pande za Kino kuonana nae kwani alidai asingeweza kutoka hivyo angenisubiri stend tuongee kwa dakika japo tano, nami sikuremba nilijisongesha pande zile nilipofika stend na kweli nilipompigia alikuja.

    Moyoni nilifurahi japo kichwani sikuamini kama yule mrembo wa ndoto leo niko nae kwa mara ya pili na bila mbwembwe nyingi nilijikuta namwambia ukweli kuwa hatukuwahi kuonana lakini niliposema nafsi zetu ziliwahi kuonana nilimaanisha kuwa niliwahi kumuota na akanitajia mpaka jina.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hahahahahaaa usinichekeshe bwanaa hebu nambie kweli”

    Alicheka na kwa mara ya kwanza nilimshuhudia vizuri kiasi gani alivyokuwa mrembo hadi nashindwa kuelezea.

    “kweli Zai na ndivyo ilivyokuwa ila mi nahitaji tuwe karibu zaidi ya hapa”

    “kivipi..”

    “namaanisha tuwe na mahusiano ya ndani kabisa na endapo utakuwa radhi niko tayari kukuoa hata kesho Zai kwani naamini wewe ni mwanamke niliyeelekezwa na mungu moja kwa moja kwenye maono”

    Niliongea kwa herufi kubwa lakini maneno yangu safari hii hayakumfurahisha Zai na kujikuta ananiaga huku akinambia kuwa anachelewa kwao pia akinisisitiza kama ndio haja na nia ya kumtafuta kumbe ilikuwa na lengo lile basi nisahau kabisa haitakuja tokea.

    Nilijaribu kumzuia ili anisikilize zaidi lakini Zai hakusimama na aliondoka nami ikabidi nigeuze huku nikijilaumu upande wa pili kwa kuwahi kumwambia vile kabla hata sijamueka karibu zaidi.



    * * * * *

    Baada ya wiki mbili ikiwa kila siku nilimtumia msg asubuhi Umeamkaje mchana Umeshindaje na ile ya usiku mwema lakini hata moja haikuwa kujibiwa na Zai zaidi ya ujumbe uliorudi kuwa msg imepokelewa.

    Sikuchoka nilimtumia msg mbalimbali za vituko na vichekesho bila kuacha zile za kuomba msamaha tena nikimsihi kama kumwambia kwangu vile ndio ilikuwa kosa basi anisamehe sitonyanyua tena mdomo wangu juu ya mada ile ila tu asinikasilikie.. lakini pia hakujibu.



    Baada ya muda nilianza kukata tamaa lakini nakumbuka siku moja ijumaa majira ya usiku nilipokea msg iliyotoka kwa Zai ambayo aliandika kuwa anahitaji kuonana na mimi kwa mara nyengine lakini safari hii alihitaji aje ninapoishi. Sikuamini nilipoisoma nami kwa haraka nilimuelekeza na kumuahidi kuwa asubuhi angenikuta stend japo nilijua kuwa kesho yake pia nilihitajika kazini lakini nilijikuta naua kazi na baada ya kumaliza kuchart na Zai nilituma msg ya msiba kazini na kuwambia kuwa nisingefika kesho nitasafiri kwenda msibani Mwanza.



    Kesho yake kama ndoto majira ya saa tatu asubuhi Zai alinipigia kuwa yuko njiani nami nilifika stend mapema na kweli mtoto alishuka huku akiwa kavaa gauni lefu na mtandio tulisalimiana na kumuomba tufike tukaongelee nyubani japo awali alidengua lakini mwishoe alikubali na taratibu tulianza kuifata njia ya getto huku moyoni nikiwa siamini kabisa na swali pekee lililoniumiza kwa muda huo ni kwamba ndio nimekubaliwa ombi langu au kuna lengine tena …! Lakini kuna muda nilijiuliza kaswali kengine ka uzushi kuwa hivi huyu bint Zainabu ni binaadam wa kawaida au isije kuwa ni jini linanifanyia mchezo..!!

    Nilimuangalia pindi tunaingia ghetto na kukaa kimagutumagutu sebureni mara baada ya kumuhudumia kinywaji alichohitaji na kufungua maongezi lakini ajabu nilishangazwa zaidi na kile alichokuwa anaongea Zai siku hiyo na kubaki na bumbuwazi zito sana na kutoamini nisikiacho Daaah!!... Unajua alisemaje..?



    Zai alinsema hivi..

    “Kiukweli kwanza naomba nisamehe kwa kutopokea simu yako wala kujibu msg zako, lakini nilikuwa nafikilia sana swala lako kwani sijawahi kuwa na mwanaume japo nakutana na majaribu ya kutongozwa mara kwa mara na huku Dar nilichofata ni masomo tu na ndivyo nilivyoapa ila sijui inakuaje nakufikiliaga na leo nimeamua kuja ili nikuhakikishie kuwa nimekubali lakini kwa masharti matatu..”



    Aliongea na kunyamaza nami nikatumia nafasi ile kumeza mate na kukaa vizuri.



    “sharti la kwanza naomba tusikutane kimwili mpaka utaponioa..."

    Aliongea huku akinikazia macho nami nikatikisa kichwa juu chini juu kwa ishara ya kukubali na kumruhusu aendelee hilo sharti lengine.

    "Lapili nipe mda nisome usinipigie simu ovyo hadi nikutafute mimi na kila mwezi tuonane mara moja tu tena maongezi yetu yasichukue zaidi ya nusu saa"

    Aliniangalia huku mi nikiwa tuli namsikiliza akaendelea.

    "Na la mwisho uniapie kuwa hutokutana kimwili na mwanamke yeyote hadi utaponioa..”

    Alimalizia Zai huku akinikazia macho nami nikayatafakari harakaharaka yale masharti na kwajinsi nilivyotokea kumpenda sana Zai nilijikuta nakubali haraka huku nikijinadi…

    “Ondoa shaka kabisa mke wangu mtarajiwa niko tayari kufata masharti yote hayo na nakuapia sitokuja kuvunja hata moja niamini..”

    Alinyanyuka Zai na kunikumbatia lakini chaajabu nilipomtazama machoni nilishangaa kuona anatokwa machozi.

    “Vipi mbona unalia tena”

    “hamna ni mapenzi tu.. Nakupenda sana Zungu”

    Nilishangaa Zai aliponiita jina la Zungu kwani lilikuwa ni jina langu la utani enzi niko shule ya msingi sasa sikujua kalijuaje wala sikumbuki kama niliwahi mtajia mtu jina hilo na mbona ni miaka mingi mno hata kazini hakukuwa na mtu aliyenijua kwa jina hilo hata mwenyewe nilishalisahau.. Nilitaka kumuuliza lakini nilijikuta napotezea na kusahau hadi pale aliponiaga na kumsindikiza awahi kwao huku moyoni mwangu nikiwa na furaha iliyopitiliza.



    Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa ukurasa wa kitabu changu kipya chenye kava zuuuurii la mapenzi ya dhati lililonakshiwa kila aina ya mvuto na kumpendeza yeyote akionacho kitabu hiko na kutamani kukisoma bila kujua kuwa ndani yake kuna kurasa zenye maandishi mazuuuuuri mno ila yana Misamiati migumu sana yenye tafsiri mbaya sana sana sana na za kuumiza. Daaah!! laiti ningejua nisingeendelea kusoma misamiati hii na kuipuuza bila kujua maana yake. Na Laiti ningefunua kwanza nyuma ya kitabu kujua tafsiri yake nadhani kitabu changu ningekisoma kwa tahadhali na umakini mkubwa ama nisingekinunua kabisaaa lakini Mwe!! Tafsiri niliyoikuta kwenye kurasa ya mwisho imekuwa matokeo tu ya haya niyaonayo baada ya dhalau yangu ya kutosoma hata dibaji na kukimbilia kusoma nisiyoelewa maana kiundani nikifurahia kwa kukodolea macho picha za michoro mizuri kwenye zile kurasa bila kujua siri na maana yake na nilipomaliza kufunua kurasa ya mwisho kulipofafanuliwa maana nikawa nishachelewa sanaaaaa Daaah!! Aaaaaaaaagh… amini usiamini baabaaa aaaaaaaa WANAAKE NI WAUAJI.



    *<>* *<>* *<>*



    Naam, mpenzi msomaji hiyo ilikuwa ni hadithi ndefu iliyojaa maumivu iliyokuwa inasimuliwa na bwana mmoja wa umli zaidi ya miaka hamsini aliyeitwa Hussein akionekana amekaa pembezoni mwa fukwe nzuri ya Sun rise huku pembeni yake alionekana ameketi kijana mmoja wa umli usiozidi miaka ishirini na saba akiwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa, huku wote wakiwa wamevalia suti kali sana.

    Lakini alipofikia pale Hussein alinyamaza na uso wake ulibaki ukiwa unatililikwa na machozi na Ghafra kilisikika kilio cha kwikwi kutoka kwa bwana yule (Hussein) na ndipo sasa kazi ikawa kwa yule kijana waliokuwa sambamba pale fukwe kuanza kum bembeleza na kumtuliza.



    * * * *

    <<<---->

    (MIAKA 8 NYUMA)

    HATUA ZA

    > SHAABAN MWINCHANDE <

    ----------------------------------

    -------------------------------



    Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia ya mzee Mwinchande kufatia kuhitimu elimu ya juu kwa kijana wao mpendwa mtoto wao pekee Shaaban.

    Baada ya sherehe za kumpongeza kuisha siku hiyo Shaaban alikaa na mzee wake kwa niaba ya mazungumzo juu ya hatua itayofata kuhusu elimu aliyoipata huko Nairobi Kenya alipokaa zaidi ya miaka mitatu kimasomo.



    “Mwanangu nimefurahi umefauru vizuri na umerejea salama lakini sikufurahishwa na kile ulichoenda kujifunza na laiti ningejua mapema sikufichi nisingegharamia pesa zote zile sababu najua ulichojifunza hakitokusaidia hapa nchini kwetu labda ungekuwa ulaya.”

    “kwanini baba ila mi ndio nilitokea kupenda tena sijui kwanini nilipenda ghafra hivyo kwani hata kabla sijajiunga na chuo sikuwazia kama ningeenda kusomea saikology na maisha ya viumbe”



    Aliongea na kujitetea Shaaban lakini msimamo na alichokuwa anaongea mzee Mwinchande kilibaki palepale na alimuhakikishia kama atang’ang’ana na elimu hiyo basi asubirie kuendelea kukaa nyumbani na kutafuta kazi.



    Na kweli baada ya kikao kile siku zilienda Shaaban alizunguka huku na kule kutafuta kazi juu ya kile alichokisomea lakini ikawa vilevile kama alivyoambiwa na babaake na hatimae mwaka ukakatika bila kufanikiwa lakini hakukata tama aliamua kurudi chuo kuendelea zaidi lakini miaka miwili baadae aliporudi bado hali ikawa vilevile hakuna kazi hata alipofungua ofisi yake kibongobongo bado ilikuwa bure tu.

    Ugomvi mkubwa uliokuwepo kwa babaake ukawa palepale kuwa Elimu ya Saikology na mahusiano ya maisha ya viumbe hususan kibongobongo na Afrika mashariki pia ilionekana haina umuhimu sana japo watu wengi walionekana kuwa na matatizo hayo bila wao wenyewe kujijua.



    Na kweli safari hii Shaaban baada ya kuona kuwa hakukuwa na dalili yoyote ya faida ya alichosomea hatimae sasa aliamua kumuomba msamaha babaake na kumtaka amsaidie ushauli pia cha kufanya kwani kiukweli alichokisomea ni kikubwa na muhimu lakini hakina faida upande wa kipato imekuwa kama kazi ya kujitolea tu na kwa kipindi hiko chote aliweza kuwasaidia watu mbalimbali mashuleni na kwenye semina lakini bado hakukuwa na chamaana alichokivuna zaidi ya kupigiwa makofi ya hapa na pale, kula misosi ya semina na kuendelea kuishi nyumbani tu akitegemea wazazi huku na umli nao unasogea.



    “Sikia mwanangu mi nilikuwa nakuangalia kwanza nilijua tu ungerudi kwenye mawazo yangu .. sasa usijali elimu unayo vyeti unavyo nataka ulithi kazi yangu wiki ijayo nitakupeleka makao makuu, kwani mwezi ujao ndio usaili unaanza .. usijali naamini pia huko utapata nafasi ya kuitumia kazi yako kwani kuna mengi sana kwa wafungwa”

    Aliongea mzee Mwinchande na safari hii Shaaban hakuwa na pingamizi japo awali hakutaka kabisa kuja kuwa askali magereza kazi aliyoifanya babaake kwa miaka 35 na kipindi hiko Alishastaafu.



    Siku zilienda na kweli shaaban alijiunga na jeshi la magereza na kwenda mafunzoni miezi sita baadae akawa askali magereza na kutokana na juhudi na elimu yake haikuchukua muda mrefu mbele alijikuta anapandishwa vyeo na hatimae kuwa Kamishna kwa miaka minne tu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwaka mmoja baadae akiwa kamishna alihamishwa na kupelekwa kwenye gereza moja lililohusisha wafungwa wa makosa mazito mazito mara baada ya mkuu wa gereza lile kuugua na kufa ghafra na huko ndipo alipokutana na story ya mfungwa aliyekuwa pale kwa zaidi ya miaka ishirini na tano akijizolea umaaarufu jera kwa jina la Babu bubu alilotungwa na wafungwa wenzake kutokana na kuwapo gerezani kwa muda mwingi na kituko kikubwa alichokuwanacho ni kutopenda kuzungumza wala kujichanganya na wenzake na muda mwingi anapotulia hutumia kuandika maneno ya ajabu ajabu na hata kwenye kuta za jera alitumia mawe kusugua na kuandika japo alishaadhibiwa sana na kuteswa juu ya swala hilo lakini hakukoma kwa miaka yote ile yalikuwa ni mazoea yake na aliharibu kuta nyingi kwa michoro yake na maneno ya ajabu kama mtu aliyechanganyikiwa na alihukumiwa pale kifungo cha maisha kilichotokana na kesi iliyomkabili ya mauaji mara baada ya kuwakatakata viungo familia yake mwenyewe kwa imani iliyosadikika kuwa ya kishirikina, na ni kwa dhumuni la kujipatia utajiri kwa njia ya mkato, na hata hivyo kutokana na serekali kutoamini nguvu za giza na kutolidhika na ushahidi huo pekee ndipo ulipofanyika ushahidi wa kisayansi kwa kufanyiwa vipimo huenda alirukwa na akili lakini alipochunguzwa na kufanyiwa vipimo zaidi vya kitaalamu bado majibu yalionesha kwamba hakuwa na tatizo lolote la akili hivyo alifanya yote kimakusudi na ndipo hukumu ilipotoka na haikuruhusiwa rufaa yoyote kwa mfungwa yule.



    Kilichomshangaza zaidi Kamishna Shaaban ni baada ya kufatilia michoro ya huyo mfungwa kwa umakini kabisa ambae kiumli alikuwa kama babaake na alipoichunguza zaidi kwa uyakinifu aligundua kuna maneno ndani yake yaliyosomeka ‘’’WANAAKE NI WAUAJI’’’

    Na huu ndio ukawa mwanzo wa Kamishna Shaaban kumtafiti na kumchunguza huyo mfungwa akianzia historia ya mafaili yake hadi kuhukumiwa na kuletwa pale huku moyoni Shaaban akiapa lazima atafute jinsi ya kuongea na huyo mtu kwani maneno yake yalionesha yana siri nzito na maana kubwa kwenye maisha yake.



    Kazi ilikuwa ni nzito kuyatafuta mafaili yale ya zamani yakiwa yametengwa sehemu maalum na kwa kuwa Shaaban alikuwa ni Kamishna na mkuu wa gereza lile kwa muda mara baada ya mkuu wa gereza wa awali kufariki ghafra naye kuletwa pale kukaimu tu mpaka jeshi litapomchagua mkuu mpya rasmi, hivyo alitumia wadhfa aliokuwa nao kuwaagiza askali walioshughulika na utunzaji wa kumbukumbu na mafairi ya wafungwa na kuwaagiza watafute faili la Hussein Muhondogwa aliyefungwa pale kwa zaidi ya miaka 25 na watapolipata wamletee mara moja.



    Na kweli baada ya siku kadhaa faili lilipatikana na maelezo yalionesha kuwa mtuhumiwa yule aliyejulikana kwa jina la Hussein alihukumiwa pale kwa kosa la kuwaua kwa kuwakatakata viungo mkewe na mwanae ambae alikuwa mtoto mdogo wa kiume wa umli wa miezi isiyozidi sita ikiwa ni familia yake aliyokuwa anaishi nayo na imeonekana kuwa mtuhumiwa alidhamiria kufanya hilo tukio kwa imani ya kishirikina kuwa angekuwa tajiri baadae na ndio sababu kabla ya tukio alipanga nao safari ya mbali huko kijijini ili kufanikisha zoezi hilo kirahisi na katika hali ya kupoteza ushahidi ilibidi akubali kupigwa na watu alioshilikiana nao na kujitia kuzimia kwa kuidanganya serikali kuwa walivamiwa.

    Hukumu yake ilionesha kuwa alifungwa kifungo cha maisha sambamba na kazi ngumu.



    Baada ya kusoma yote yale Kamishna Shaaban kwa kutumia uwezo wake binafsi na uzoefu aliokuwa nao ndipo alipoanza kazi ya kumfatilia Hussein au babu bubu kwa njia ya kuwaagiza baadhi ya askali wa chini waliokuwa wanawasimamia zaidi wafungwa.

    “Hakikisha Coplo unampiga picha kwa kila akifanyacho na uwe unanirekodia nyendo zake zote huko site, sawa..”

    “Sawa mkuu”

    Yalikuwa ni moja ya maagizo kutoka kwa Kamishna Shaaban kwenda kwa coplo mmoja kati ya askali waliowasimamia kina Hussein huko walipokuwa wanaendaga kuvunja mawe (kokoto)

    .

    Kama kawaida yake Hussein alipokuwa huko hakutaka story na yeyote zaidi ya kufanya kazi kwa nguvu sana licha ya umli wake kuwa ni mtu mzima lakini bado mwili wake ulikuwa na nguvu huku uso wake muda wote ukionesha ni mtu mwenye mawazo mengi sana na ikawa kawaida saa nyengine atabasam na kujichekea mwenyewe tena kwa sauti kubwa na anapofanya hivyo ndipo anapoongeaga maneno yake ya ajabu ajabu na mwishoe alisema Wanaake Ni Wauajiiii..



    Wafungwa wenzake walishamzoea na walichukulia kawaida kwani hata walipojaribu kumuuliza kwa kuongea nae alikuwa ni zaidi ya bubu na hakutaka kabisa kuzungumzia hilo kwani alijijua maisha yake ndio yameishia pale.

    Lakini zile rekodi na picha zilipomfikia Kamishna Shaaban toka kwa vijana wake mbalimbali aliowapandikiza kumfatilia mfungwa yule zilizidi kumpa picha ktk halmashauli yake ya kichwa hususani ktk kitengo cha utafiti na akaona kuna umuhimu mkubwa wa kuongea na huyo mfungwa ndipo siku moja majira ya saa mbili usiku waliingia maaskali kumi kule ktk vyumba vya wafungwa na kumchukua Hussein mkuku mkuku huku wakiwa wamemfunika kitambaa usoni na kumpiga pingu huku Hussein akiwa hajui kwanini imekuwa hivyo na wapi wanampeleka ndipo alijaribu kuwafanyia fujo na kujikuta anapigwa kitako cha bundukio kichogoni mwake na kupoteza fahamu.

    Anakuja kustuka Hussein baada ya kumwagiwa maji usoni na kujikuta amekalishwa kwenye kiti na mbele yake alikaa mtu ambae hakumfahamu ikizingatiwa hakuvaa sare zozote.



    Alikuwa ni Kamishna Shebby na baada ya kukutana na Hussein pale aliwaamuru vijana wamfungue pingu kwanza japo awali kidogo wale askali walisita kutokana na kumjua Hussein ni mtu hatari kutokana na mwili mkubwa alioutengeneza huko huko jera kwa kufanya kazi ngumu mfululizo na alionekana mfungwa wa ajabu kadri siku zilivyozidi kwenda mbele hakuwahi kuwa na rafiki jera wala mazoea na mtu hivyo waliona si salama kumuacha aongee na muheshimiwa wao akiwa hajadhibitiwa walau mikono lakini cha ajabu Kamishna Shebby aling'ang'ania na kusisitiza wampe uhuru wamfungue na wampeleke akaoge kwanza.

    Baada ya hapo huku askali wakiwa wanamshangaa pia kamishna wao hasa pale alipokaa nae meza kuu ya chakula mtuhumiwa yule na kuamuru kula pamoja hali iliyomshangaza hata Hussein mwenyewe kwani hakukumbuka mara yake ya mwisho ilikuwa lini kula chakula kizuri kama kile na hakuwahi kukiona toka amehukumiwa pale.



    Baadae kwa uzoefu mkubwa na waajabu aliokuwa nao kwenye kuisoma saikology ya mtu Kamishna Shaaban alianza kumchombwezachombweza kwa maneno Hussein na kumuonesha heshima kubwa hasa kwa kumtunuku jina la 'baba' ambalo Hussein ktk maisha yake hadi kipindi hiko akiwa na miaka hamsini na kitu hajawahi kuitwa baba. Alisikia faraja kidogo moyoni Hussein licha ya kuificha machoni lakini alistaajabishwa zaidi na tabia na ukalimu aliyoonyeshwa na kijana yule ambae bado alikuwa mgeni machoni mwake kutokana na kuwafahamu watu wengi pale Gerezani.



    Kamishna Shaaban nae hakuwa na papala zaidi aliamua kumtembeza tembeza eneo lile la mjengo ambapo Hussein licha ya kuwepo pale kwa muda mrefu lakini hakuwahi kufika maeneo yale na hakupaelewa vizuri japo alijua ilikuwa ni ndani ya maeneo ya gereza lile.

    Tena huku wakiwa wawili tu baada ya kuwasihi walinzi wasimzongezonge pindi anapokuwa na mfungwa yule Kamishna Shaaban au Shebby aliongea mada tofauti tofauti akimsimulia mfungwa yule ambae muda mwingi alikuwa ni mtu wa kukaa kimya tu na baadae aliwaruhusu askali kumrudisha tena walipomtoa.

    Siku hiyo Hussein hakulala zaidi ya kufikilia juu ya yule kijana na muda wote huo hakujua kama yule ndie Kamishna mpya aliyeletwa pale.



    Hali ile iliendelea sasa ikawa mazoea kila inapofika week end jioni bila ghasia wala kufichwa Hussein aliongozana na askari waliokuwa wanakuja kumchukua na kwenda kukutana na Kamishna Shebby na kujumuika kwa chakula pamoja na kuangalia tv na kubadilishana mawazo ya hapa na pale japo kwa upande wa Hussein hakupenda kabisa kuongea kutokana na kuamini hana zaidi alichokibakisha duniani zaidi ya kungojea siku yake ya kufia gerezani tu, lakini maneno ya Shebby na hali aliyokuwa anamuonesha kila siku za wiki heshima na unyenyekevu aliokuwa anamfanyia ndipo taratiiibu zilianza kubadilisha imani na hisia za Hussein na kuanza kuona maisha ni kawaida tu na kupunguza vituko vyake japo mara nyingi alikuwa mkali na kutopenda kuulizwa swali juu ya kile alichokuwa anaropokaga na kuandika kuwa Wanaake ni Wauaji.



    Lakini pia Kamishna Shaaban (shebby) hakuchoka na alitumia mbinu mbalimbali m badala na ndipo siku hiyo alimtoa eneo tofauti kabisa Hussein tena kwa siri iliyojulikana na askali wachache wakubwa baada ya kuagiza ziletwe suti mbili kali na moja wapo alivalishwa Hussein huku nae akivaa yake na hata magari yalipotoka Askali wengi hadi wa getini hawakujua kama kuna mfungwa mmoja anatoka na kamishna zaidi walidhani ni kiongozi mwengine tu wa jeshi.

    Na ndipo msafara wa gari mbili ambapo moja ikiwa na walinzi maalum waliovaa kiraia pia kwa dhumuni la kumpa ulinzi kamishna anapokuwa nje pia ya gereza na ndipo Kamishna Shaaban alipomuamuru dereva wake kuwa aongoze msafara ule kuelekea maeneo ya viwanja vya Sun rise beach.



    Walipofika Sunrise beach na kutokana na mazingira yale yalimfanya Hussein akumbuke mambo mengi hasa mara baada ya kuliona jua la nje na wanawake mbali mbali wakiogelea huku wakikumbatiana na waume zao wakifurahia maisha.

    Mboni za Hussein zilistaajabishwa na jiji jinsi lilivyokuwa kubwa huku kila kitu kikiwa katika mitindo tofauti kidogo aliyoiacha kabla ya kwenda jera na aliona wanawake wengi sana pande zile kuliko wanaume na hilo alilibaini mara baada ya kila mwanaume aliyemtazama kuona alizungukwa na mwanamke zaidi ya mmoja. aliwatazama sana wale wanawake na ghafra aliangua kicheko cha ajabu sanaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ha ha ha ha aaa HAHAHAHAAAAA .."

    Alicheka Hussein kwa sauti ya juu na kumfanya Shebby amuulize kulikoni, lakini alichojibu Hussein Babu bubu kilimshtua hadi muhudumu wa kike aliekuwa kakaa meza ya jirani ukiachilia mbali wale walinzi wengine.



    "Wanawakeeee... wanawakeeee .. wanawaaaake wazuuuri sana mwananguu ukiwatazama kwa nje tu, ila kwa ndani ni wabaya sanaaaa tena saaanaaaa na ni WAUAJI wakubwaaaa.. ha ha ha hahaaa.."

    Aliongea kwa mara ya kwanza na kuendelea kucheka Hussein na ndipo Kamishna shebby alipobonyeza kitufe cha record ktk simu yake kwani alijua sasa ule wakati alioutafuta na kuusubiri kwa muda mrefu sasa umetimu, hivyo alimuuliza na kumpekecha kujua kulikoni zaidi kilichokuwa nyuma ya pazia kwa bwana yule? na kweli taratiiiibu ndipo Hussein alijikuta kwa mara ya kwanza akianza kufunguka na kusimulia historia yake na chanzo cha yeye kuja kufikia vile. Na alianzia kukumbuka na kusimulia kwa kuanzia siku ile aliyokuwa anaangalia kile kipindi cha ya walimwengu kutoka BECKER TV na hadithi yake ndio ilianzia pale.



    Baada ya kusimulia yote yale hadi alipofikia pale alipojuana na Zai msichana mrembo aliyemuota na kukutana nae hadi alipomshangaza kwa kumtaja kwa jina lake la utani la utotoni na jinsi mapenzi yao yalivyochanua ghafra na kupendana kuliko kifani licha ya kupewa masharti magumu matatu.

    Lakini alipofikia hapo ndipo Hussein alipoanza kulia sana na Kamishna Shaaban kuanza kumfariji na kumsihi kwa maneno matamu kuwa asihofie sana aendelee kumsimulia tu ili aielewe kauli yake ya kuamini kuwa Wanaake Ni Wauaji.



    *<>* *<>* *<>*

    <EnDeLeA>

    _______

    Kum bembeleza mtu mzima ilikuwa si kazi ndogo pia muda nao ulienda sana na kutokana baadhi ya watu kuanza kutega masikio kujua kulikoni hasa walipoona kuna mtumzima mmoja alietinga suti kali ya heshima anatokwa machozi hivyo kama unavyojua ukimuona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo na kwa kukwepa kujaza watu ndipo Kamishna Shebby sambamba na vijana wake waliamua kuondoka haraka na kurejea gerezani na baadae baada ya kurudishwa kwenye chumba cha siri na kuvalishwa nguo zake za gerezani aliamuru Hussein ahamishwe toka sero za awali na kupelekwa sero za v.i.p ambako walifungwa watu wenye pesa na viongozi wakubwa.



    Ndipo siku nyengine ilikuwa saa sita za usiku Babu bubu (Hussein) alichukuliwa kama kawaida na kupelekwa kwenye chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na masofa mazuri huku kamera mbalimbali zilitegwa na kamishna Shebby pasi na kujua yeyote kwenye chumba kile ndani ya makao ya Kamishna gerezani pale ndipo Hussein alijikuta akiendelea kuhadithia ile story ambayo aliapa awali kuwa ingebaki kuwa siri moyoni mwake.



    * * * * * *

    .......

    < MASWAHIBU >

    (MIAKA 29 ILIYOPITA)

    <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>



    Kiukweli japo masharti aliyonipa Zai yalikuwa magumu sana lakini kutokana na upendo wa ajabu niliokuwa nao nilijikuta navumilia na kusubiri na taratibu miezi ikasonga na nikaanza kuisoma tabia nzuri na ya kipekee aliyokuwa nayo Zai.

    Kwanza alipenda dini alikuwa muislam safi sana pili alikuwa ana akili za kipekee mno na zaidi ya yote alijiheshimu tofauti na wasichana wengi niliowajua.



    Siku zilisonga na hatimae mwaka mmoja ulikatika na siku hiyo Zai alinipigia simu tena kuwa anakuja getto nami nikafanya usafi harakaharaka na alipofika siku hiyo nilishangaa jinsi alivyokuja huku akiwa na begi kubwa la nguo na zaidi ni mada aliyokuja nayo nikajikuta nabaki mdomo wazi pale aliposema.



    “Hussein amini mimi ni wako na sasa nimekuwa wako rasmi. Najua huna kipato kikubwa lakini una uwezo wa kunioa hata kesho, ukweli mi huku sikuja kusoma wala sina ndugu zaidi nilikuja kufanya kazi za ndani tu kwa mama mmoja wa kichaga aliyekuja kuniomba kwetu ila samahani nilikudanganya awali na kukupa masharti yote yale kwa lengo la kukujua vizuri ili uniimanishe kama umenipenda kweli au umenitamani na wanaume wote walionitongoza na kuning’ang’ania niliwakubalia wote na kuwapa masharti hayo matatu na woote walijitahidi kuvumilia lakini walishindwa baadae na hakuna hata aliyefika miezi sita lakini wewe umekuwa wa ajabu kwangu na naamini ndie mume bora kwangu… naomba unipokee kwani kule nimeondoka rasmi kutokana na manyanyaso na tabia za pale nyumbani.”



    Nilibaki namuangalia Zai kile alichokuwa anakisema huku nikifikilia kichwani mwangu nimkubalie harakaharaka vile au kuna uongo anauendeleza tu kwani baadhi ya mambo ya Zai yalinistaajabisha kidogo hasa kuniamini na kunambia mi ni waajabu ilihali tulikuwa hatukai wote lakini kiukmweli toka niachane na Mamu sikuwahi kufanya ngono hadi dakika ile.

    Na ukichochea upendo niliokuwa nao na uzuri wa Zai nilijikuta namkubalia na kupanga nae safari siku tatu zijazo twende huko kijijini kwao Arusha.



    Ulipotimu usiku kwa mara ya kwanza baada ya Zai kusali alipanda kitandani na kulala pamoja na mimi huku akiwa kava gagulo na kiblauz alinibusu na kunambia kuwa nisitamani wala ntusifanye ngono hadi siku tutayofunga ndoa na kuninong’oneza kuwa yeye ni bikra pia.

    Moyoni sikuamini hata kidogo alichosema Zai kwani alikuwa mrembo mno si rahisi kudumu na bikra hadi umli ule… niliona kuwa sasa nadanganywa na ktk umli wangu wote ule nilikuwa sijawahi kukutana na mwanamke bikra.



    Usiku huo usingizi haukuja kabisa kila mara nilimuangalia Zai alivyolala umbo lake zuri lilivyojichora namba nane nilijikuta paipu yake inasimama na nyege za mwaka zikisisimua mwili wangu baada ya taswira za pepo chafu kutawala hisia zangu nilijikuta najisogeza karibu kabisa na Zai na kuanza kumpapasa kiuno na taratibu nilianza kupeleka mkono ndani ya gagulo lake na kukutana na kufuri lake lililoficha sehemu zake za utamu na kujikuta mate yakinijaa mdomoni kama fisi mwenye njaa aliyekutana na mzoga mbele yake.



    Niliendelea kumpapasa taratibu nikiwa makini kabisa ili nisimstue usingizini na hatimae mkono wangu hususani vidole vyangu vile vya kati viliweza kupenya katika pachupachu ya chupi na kukutana na kajoto ka ajabu kutokea kwenye mashine ambayo sikuamini kama kweli ni mpya kabisa na haijawahi kutumiwa hapo kabla.

    Katika hali nisiyoitarajia nililazimisha kwa ustadi mkubwa kupenyeza kidole changu kile ambacho ukimnyooshea mtu lazima mgombane,

    Sikuamini pindi nilipoona kila dariri kuwa ni kweli ile mashine ilikuwa mpya na nilipolazimisha kupenyeza kidole kwa kuvisukuma vile vijinyama vilivyoziba njia Zai aliruka na kushtuka kwa sauti ya juu name kuutoa mkono haraka na kujigeuzia pembeni kwa speed ya hali ya juu.



    “Hussein baby kwanini unataka kunifanyia hivyo?... tuseme huniamini nilivyokwambia!!? Mimi ni bikra kweli sijawahi kuguswa na mwanamme yeyote na niwewe pekee niliyekuamini na nahitaji uwe mume wangu wa ndoa ndio itakuwa raha siku utayonifungulia njia hii ya starehe ya wapendanao… baby najua una hisia lakini naomba vumilia tuu honey”

    Maneno ya Zai yaliweza kumrusha ibilisi aliyenishika ghafra na kujikuta Napata moyo na nguvu na kumkumbatia huku nikimuomba samahani na kumuahidi sitamgusa tena mpaka tutapooana.

    “So sorry baby.. sitorudia tena ni shetani tu alinipitia nikataka kukujaribu ili nihakikishe but sitorudia tena mpaka siku tutapohalalisha ..”



    Niliongea maneno haya kwa busara ya hali ya juu nae Zai bila kinyongo aliniitika kwa kichwa na kunibusu kisha tukalala na sikumgusa tena hadi kulipokucha na mishe mishe ziliendelea hususani kwenda kukata tiketi kwajili ya safari huko kwao na siku mbili baadae niliaga tena kazizni ambapo nilipewa likizo ya wiki moja kwaajili ya kumaliza msiba niliodanganya awali na kutumia fulsa hiyo kusafiri na Zai mpaka jijini Arusha ambapo tulipanda tena gari lililotupeleka vijiji vya ndani ndani kabisa.



    Tulipokelewa vizuri pia bibiake Zai alikuwa mcheshi mno baada ya kufika alituandalia chakula cha asili na katika jambo ambalo sikulitarajia ni mara baada ya Yule bibi kuelewa kila kitu kuhusu mimi na Zai na hata kabla sijajitambulisha Yule bibi alinitajia kila kitu na kunambia bintie hakumficha chochote awali kuhusu mimi na tayari wajomba zake waliujua ujio wetu na wiki hiyo hiyo watatufungisha ndoa ili tuwe mke na mume rasmi.



    Sikuwa na kiasi kikubwa cha pesa lakini nilishangaa kusikia mahali tutalipana wenyewe zaidi nilitakiwa kutoa elfu hamsini tu kwaajili ya mila zao.

    Nilishangaa sana kumpata mke haraka vile tena kwa bei chee namna ile sikuamini kabisa na baada ya ndoa usiku wake tulitengewa chumba maalum kwaajili ya kulala na ndio ikawa mwanzo sasa wa kujilia lile tunda ambapo purukushani ilikuwa kubwa sana kwani zai alibana miguu na kuogopa sana nami nilikuwa jasiri wa kumkamata na kumdhibiti hatimae niliweza kumsongomeka msumari japo haukuingia wote na kwa shida sana Zai alipiga kelele mno za maumivu na chaa ajabu alipopiga zile kelele nilisikia sauti ya vigeregere nje ndipo nilipogundua kuwa kulikuwa na watu walikuwa wanatusikilizia.



    Tulikaa siku saba kabla hatujarudi Dar ambapo tulifungashiwa zawadi kibao kwaajili ya kwenda nazo na nilipokuwa njiani niliwasiliana na ndugu zangu baadhi ambao walikuwa wananisubiri kwa hamu kubwa huku wengi wakiwa wamenilalamikia kwa kitendo cha kwenda kuoa pasi na kuwataarifu mapema.

    Safari yetu ilifikia kwa Mjomba kakaake na marehem mama kwakuwa sikuwa na wazazi kipindi hiko na tuliwakuta baadhi ya ndugu na kutupokea vizuri tu na kuanza kuwatambulisha mke wangu lakini chaajabu kipindi nawatambulisha nilipofika kwa baba mkubwa ambae alikuwa ni mganga wa kienyeji aliposhikana mikono na Yule bint alimuangalia sana hadi Zai alionesha kusikia aibu na jicho la ba mkubwa kidogo lilinishangaza hata mimi.

    Nilipomuangalia zaidi mke wangu alikuwa kainamisha kichwa chini huku baba akiwa bado kamkazia macho na kugeuza shingo kisha kunitazama kwa mshangao hali iliyoanza kidogo kunipa wasiwasi.



    Lakini nilijibaraguza na kukenua meno kwa kucheka kidogo huku nikijiiminisha kuwa hali aliyoonesha baba huenda ilikuwa ya masihara na kautani kidogo nikiamini alishangaa kuona nimewezaje kung'oa kifaa kama kile.

    Nakumbuka baada ya pongezi na zawadi mbalimbali ambapo napo kulikuwa na sherehe ndogo kwa niaba yangu, usiku uliingia tukalala lakini asubuhi na mapema nilipoamka na kutoka nje nilikutana na Ba mkubwa ndipo aliponiita na kunivutia pembeni.

    “Pole sana kwa safari mwanangu”

    “asante baba.. vipi kwema”

    “kwema, ila naomba nikuulize swali”

    “lipi baba”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hivi huyu bint kabla hujenda kuoa ulishawahi kuishi nae japo mwezi mmoja au miwili?”

    Swali la ba mkubwa kidogo lilinibabaisha kujibu na kujikuta nauliza swali badala ya kujibu



    “kwani vipi baba..”

    “hapana .. nimekuuliza tu mwanangu maana hukutwambia mapema kama unaishi na mtu baada ya yule Mariam aliyekuwa anakuja kwako mara kwa mara pia hukutwambia kama mliachana na umepata mchumba mwengine, lakini pia mwanangu kwanini hukumjulisha ndugu yeyote kama ungekuwa na safari ya kwenda kuoa..? tena mkoa wa mbali kabisa eeh..! hii imenitisha kidogo. ni afadhali ungeoa mtu wa nyumbani mwanangu sidhani kama huyu bint ni chaguo lako sahihi kabisa.”

    Maneno ya baba yalininyima raha kidogo kwa kuona kama wananisimanga zaidi ili hali nilishaomba radhi hapo kabla na kauli yake ya kuwa afadhali ningeoa mtu wa nyumbani kidogo ilinichefua kwa kuona sasa wanataka kuanza kumnyanyapaa mke wangu nimpendae mapema ile.

    Uso wangu kidogo ulibadilika sambamba na sauti pindi nilipomjibu tena ba mkubwa na kumwambia

    “daah! Kiukweli ndio maana niliwaomba msamaha mapema tu baba kuwa nilipitiwa, lakini mimi ni mtu mzima na jua zuri na baya hivyo mkae mkijua namtambua vizuri sana mke wangu na sikukurupuka kumuoa ni chaguo langu sahihi kabisa.”

    “Basi vizuri Mwanangu kama unamtambua vizuri, ila kumbuka Mpotea njia mara nyingi si Muulizaji”



    Aliongea ba mkubwa na kuingia ndani na kuniacha nimesimama pale nje nikitafakari kidogo maneno yake na methali zake za mafumbo huku nikifikilia picha ya jana yake alivyoonana na mke wangu Zai na jinsi alivyomuangalia, nilijikuta najisonyea mwenyewe na kumpumbaza ba mkubwa moyoni kuwa kumbe bado ana akili za kizamani kabisa na mila potofu za kuchaguliana mke.



    Nilipuuzia huku nikijichekesha kupotezea hasira iliyoanza kuubadilisha uso wangu na kurudisha tabasamu bandia ili mtu mwengine asinigundue asubuhi ile japo moyoni nilichefuka kidogo kisha nikaamua kurudi chumbani na baada ya sherehe kuisha siku hiyohiyo niliaga kwa ajili ya kuondoka japo awali mjomba tulikubaliana kuwa tungekaa siku tatu lakini nilieka visingizio kaza wa kaza hasa kuhusu kazini mpaka wakanielewa japo moyoni sababu kubwa ya kutaka kuondoka mapema ile ni baada ya kutibuliwa na ba mkubwa.



    Na ndipo tulisindikizwa mpaka kule nilipokuwa naishi na baadhi ya ndugu waliotoka kijijini kwa kina Zai ili kupafahamu tulipoishi na waligeuza asubuhi hiyo na kutuacha wenyewe pale ndani na baadhi ya ndugu wa palepale mjini.

    Baada ya nasaha mbalimbali hatimae kila mtu akaondoka na maisha mapya kabisa baina yangu na Zai yakaanza rasmi na yalinoga siku hadi siku.

    Siku zote nilimshukuru mungu kwa kupata mke bora na mwema kama yule lakini ujinga mkubwa niliofanya ni kupuuzia swali na maneno ya Ba mkubwa yaani Laiti ningeyatilia maanani japo kidogo maneno ya ba mkubwa nadhani yasingenikuta yoote haya baadae… loh!! Kweli muda mwengine wanaume ujasiri wetu unatuponzaga kwani katika miaka miwili tu ya ndoa yetu ilitosha kabisa kuamini na kukumbuka maneno pia ya yule mlemavu wa kile kipindi kilichorushwa na kituo cha Becker TV nilichoangalia miaka mitano iliyopita hadi kupelekea kugombana na mchumbaangu wa awali kwa sababu tu ya ile mada na kauli ya msimuliaji kuwa Wanaake ni Wauaji.



    Ni ngumu kunielewa harakaharaka lakini usijali utanielewa tu.

    Ukweli mke wangu alikuwa mtu wa kufatilia ibada sana, alinisihi na kuniasa mara nyingi huku akinionya kwa upole mara kwa mara na kunisomea hadithi mbalimbali kuhusu watu waliomuasi mungu karne hizo na adhabu walizozipata.

    Taratiibu nilijikuta nami nikianza kufatilia ibada na ndipo maendeleo yetu yalizidi kuwa mazuri na tulinunua kiwanja huko kigamboni na kuanza kujenga huku mke wangu akiwa msimamizi mkuu.

    Mwaka mmoja baadae ikiwa ni miaka mitatu baada ya ndoa yetu nakumbuka siku hiyo majira ya jioni nikiwa ndani ya daladala nikitokea kazini kama kawaida nikiwa nimesimama na kutokana na wingi wa watu waliokuwa wanahitaji huduma ya usafiri jioni ile wakitokea makazini na mashuleni tulijikuta tukiwa tumebanana mno ndani ya daladala ile.



    Nakumbuka vizuri tukiwa kwenye foleni kuna mtu alienisalimia akiwa amesimama nyuma yangu na niliitikia pasi na kugeuka kumtazama japo sauti yake sikuifahamu lakini alionesha kunifahamu zaidi kutokana na kunisalimia kwa kunitaja na jina, aliongea nami kwa sauti ya chini na kunambia ana ujumbe wangu.

    Nilishindwa kumuelewa hali iliyonifanya nijalibu kujigeuza sasa nitazamane nae lakini kutokana na m banano wa watu nilishindwa kufanya hivyo hadi nilipoona napenyezewa bahasha ndogo kwa juu nami nikaipokea japo sikuelewa ni barua ya nini na inatoka wapi lakini nilijipa imani watu watapopungua mbele nitaongea nae huyo mtu ili anieleweshe zaidi na kilichomo ndani ya bahasha ile japo nilielewa kuwa ni barua lakini sikujua inatoka wapi na ni kwa dhumuni gani.



    Gari ilisogea na kweli kituo cha mbele watu wengi walipungua ndipo nikapata nafasi ya kugeuka na kumtafuta yule aliyeniongelesha na kunikabidhi barua lakini cha ajabu kila niliyemtupia macho kuhisi ndie alibaki nae kunikodolea na kunishangaa tu na kujieka bussy na mambo yake,

    Nilihisi na kujilidhisha huenda akawa kashuka pale kituoni gari iliposimama lakini nilijiuliza kwanini hata hajaniambia kama anashuka? Niliachana nae na kuendelea na yangu huku nikiwa na shauku ya kufika haraka nyumbani niweze kusoma kile kilichoandikwa ndani ya ile barua.



    Nilifika nyumbani na kupokelewa vizuri na kipenzi changu kama kawaida na kumnyanyua mwanangu kipenzi ambae alikuwa anakaa chini kipindi hiko kwani tayari mungu alitubariki mtoto mmoja wa kiume na niliipenda na kuijali sana familia yangu.

    Mara baada ya mke wangu kipenzi kuniekea maji bafuni na nilipomaliza kuoga nilitoka kuja sebureni kwa ajili ya kupata msosi lakini niliikumbuka ile barua na kurudi chumbani na kuichukua kwa shauku ya kuisoma kujua dhumuni lake ndipo nilipotulia sebureni nikiwa nasubiri msosi kipindi hiko mke wangu alikuwa busy jikoni ananipakulia ndipo nikaanza kuisoma barua ile ambayo nje haikuwa na anuani yoyote lakini kadri nilivyozidi kuisoma ndivyo mapigo yangu ya moyo yalivyozidi kuongezeka.

    aaaagh! Kamishna babaaaa.....

    Naikumbuka vizuri ile barua iliandikwa hivi.,………………..



    ……………………………………………………………………………………………..

    NDUGU,

    POLE NA MAJUKUMU NA HONGERA KWA KUISHI NA MWANAMKE MZURI NA KUJIMILIKISHA MTOTO.

    NISINGEPENDA KUONGEA ZAIDI ILA NIA NA MADHUMUNI YA KUKUANDIKIA HII BARUA NI KUKUONYA NA KUKUTAHADHARISHA JUU YA MKE WANGU UNAYEISHI NAE.

    SIKUWA HAPA JIJINI KWA MUDA MREFU KIDOGO LAKINI NIMEPATA HABARI ZOTE JUU YA JANJA YAKO ULIYOTUMIA HADI KUITEKA NA KUILAGHAI FAMILIA YANGU.

    SASA KWA USALAMA WAKO NAKUPA SIKU SABA TU.

    ANZA KUHESABU KUANZIA KESHO UMRUDISHE HUYO MWANAMKE KWAO ARUSHA NA HUO NDIO UTAKUWA USALAMA WAKO.

    ZAIDI YA HAPO UTAJITAFUTIA MATATIZO MAKUBWA YATAYOKUFANYA UJUTE MILELE NAMI NISINGEPENDA YAKUKUTE MAJUTO.

    AHSANTE.

    WAKO….. MR. X



    ………………………………………………………………………………………………



    Nilishindwa kuielewa ile barua licha ya kuirudia kuisoma zaidi ya mara tatu na mke wangu alinishangaa pindi aliponitengea chakula na kubaki nimeduwaa tu na barua ile huku uso wangu nao ulishaanza kubadilika ghafra hali iliyomfanya anisogelee na kuniuliza kwa upole nami sikumjibu zaidi ya kumpa ile barua ambapo aliisoma nae alianza kushangaa na kuonesha wazi hakuielewa kabisa hasa aliponiuliza kuwa ile barua ya nani?

    Nilimjibu nimepewa mimi ni yangu na inanihusu mimi na yeye.

    Aliniuliza tena imetoka wapi, hapo ndipo niliposhindwa kuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kuitaka ile barua na kuisoma tena lakini sikuambua chochote zaidi ya mke wangu kuniapia na kunisihi kuwa ule ni ujinga wenye uongo wa kutupwa wala haumlengi yeye inawezekana muhusika amekosea.

    Nilikubaliana na mke wangu lakini pia nilijiuliza mbona amepataja Arusha? ilihali kweli mke wangu nimemuolea huko?

    Na atasemaje yule ni mke wake wakati nimemuoa takribani miaka mitatu? Na kwa maelezo ya ile barua niligundua kuwa mwandishi alimaanisha kuwa nilimchukua yule mwanamke akiwa ana mtoto mdogo…

    hahahaha hapo nilijikuta nikicheka mwenyewe moyoni kwani mke wangu nilimuoa akiwa m bichi kabisaaaa na bikra yake na alikuwa hajawahi kuguswa wala kujihusisha tendo na mtu yeyote zaidi yangu hadi anapata ujauzito na kurudi kwao kwa miezi minne ya mwisho walipomuhitaji akaugulie huko na baadae alijifungua salama mtoto wa kiume na niliwaacha mpaka mtoto alipotimiza miezi miwili ndipo nilipowafata kuwachukua na kuendelea na maisha.

    Niliamini wazi hiyo barua imekosewa tena si kidogo na nilitamani sana kumuona yule aliyenipa ile barua.



    Lakini swali lililonishangaza tena mbona yule mtu alinitaja kwa jina langu kabisa akionesha kunifahamu kabla ya kunipa ile barua?

    Hapo nilikosa jibu kamili lakini niliamua kupotezea na siku zilienda ambapo zilipita siku nne tangu nipate ile barua ndipo siku nyengine tena nikiwa kwenye daradara safari hii nilipata siti sikuwa nimesimama kama siku ile na wala watu hawakuwa wengi sana kutokana na kuwahi kutoka kazini siku hiyo ndipo nikiwa ndani ya ile daradara mara simu yangu iliita na nilipoitoa mfukoni kuangalia aliyekuwa ananipigia ilionesha ilikuwa namba ngeni machoni mwangu ndipo nikaipokea kujua nani aliyekuwa ananipigia lakini nilipopokea tu kabla sijasema 'hallow' nilianza kuisikia sauti ya aliyenipigia ikinikumbusha kuwa zimebaki siku tatu na kuniasa nisije kupuuza nilichoambiwa kwenye ile barua kisha simu ilikatwa.



    “HALOOW!! NANI WEWE??”

    Nilipayuka kwa sauti ya juu hadi nikawastua abilia wenzangu na kunishangaa ambapo nilionesha kuchanganyikiwa kwa hasira na ndipo nilipojaribu kuipiga ile namba lakini cha ajabu haikupatikana kabisa hata niliporudia zaidi ya mara tano ndipo nilipoamua kutuma msg lakini nayo haikuleta majibu kama imefika.



    Nikiwa nimepagawa ndani ya daradara nikitafakari cha kufanya mara simu iliita tena kwa mara nyengine na nilipoiangalia namba nayo ilikuwa ngeni lakini ilikuwa tofauti na ile niliyopigiwa muda mfupi na mtu nisiyemfahamu.

    Nilishusha pumzi na kuipokea kwa sauti ya upole lakini nilijikuta nastaajabu nilipoisikia sauti ya aliyenipigia ilikuwa tofauti na ya yule wa mwanzo lakini mada ilikuwa ileile hasa aliponambia.

    “Usipanick ndugu yangu na kuwastua watu kwenye daladala ila nakupenda sana ndio maana nakusihi na kukukumbusha kuwa zimebaki siku tatu na hujatekeleza maagizo ya kwenye barua nakusihi tafadhali fanya hima sasa kwa usalama wako’’’

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilibaki nimeganda safari hii pasi na kujibu chochote hadi simu ilipokatika nilibaki nimeduwaa huku kichwa kikijawa mawazo lukuki nikihisi sasa kuna uwezekano wa kile nilichodhalau kikawa na ukweli ndani yake lakini ni ukweli upi huo kama sio udanganyifu na kutaka kuporwa mke wangu kinguvu?

    Niliangaza kona zote ndani ya gari ile nikihisi waliokuwa wananifanyia kale kamchezo huenda niko nao ndani ya gari ile lakini sikuambulia chochote zaidi ya watu nao kunishangaa tu kwa kuchanganyikiwa kwangu.

    Nilijisikia aibu sana kwa mara nyengine nikikumbuka aibu iliyonipata kipinde kile baada ya kupigwa na baunsa niliyemfumania na mchumbaangu Mariam.



    Gari ilifikia kituoni na taratiiiibu nilishuka na kuelekea nyumbani ambapo siku hiyo mke wangu alinigundua kuwa siko sawa tangia aliponipokea nje na kuingia ndani ambapo nilijibwaga kitandani bila kuzungumza chochote.

    Haikuwa kawaida yangu kurudi bila kumkumbatia mke wangu na kumnyanyua mwanangu kwa furaha huku nikimchekesha chekesha na kucheza nae na ndipo kwa mshtuko mke wangu aliniuliza kulikoni lakini nilizuga kwa kudanganya kuwa naumwa na alipohoji kuhusu kwenda hospitali nilidanganya kuwa nishakunywa dawa za maralia kazini na ningependa kupumzika muda huo.

    Nililala kitandani huku mke wangu akiwa pembeni akinifariji sambamba na mwanangu aliekuwa akinichezea chezea mikono.

    Moyo uliniuma sana na kumlaani shetani aliyekuwa ananiandama kutaka kuisambaratisha familia yangu.



    Nilifikilia kupiga simu polisi na kutoa taarifa zile lakini kabla sijafanya hivyo nilinijia wazo la kumtafuta babaangu mkubwa ambae alikuwa mganga wa kienyeji na moyo ulinisukuma kumtafuta yeye moja kwa moja pasi na mtu mwengine kutokana na lile tukio lililojili miaka mitatu iliyopita na maneno yake ya mafumbo aliyoniambia nilihisi huenda kuna kitu ambacho alikijua mapema kuhusu mke wangu.



    Safari hii sikutaka kumwambia ukweli moja kwa moja mke wangu juu ya kilichonikuta tena nikihofia kumtisha pia nilijipa mda wa kutafakari kitu cha busara cha kufanya na akili bado ilinituma moja kwa moja niwasiliane na ba mkubwa tu nimuhadithie kila kitu huenda yeye akawa na msaada mzuri wa kiushauli na cha kufanya.

    Takriban siku mbili nilishindwa kwenda kazini na nilipopata nafasi ya kuwa pekeangu baada ya mke wangu kuniaga kuwa anaenda bombani kuchota maji ndipo nilimpigia simu ba mkubwa na kumuelekeza yaliyojili ambapo hakuonesha kushangaa sana wala kustushwa na habari zile ila alinionya nisithubutu kutoa taarifa polisi wala kwa mtu yeyote kwanza kabla sijaonana nae na aliniomba na kunisihi sana nifanye hima niende kwake haraka ikiwezekana kesho au jioni ya siku hiyo ambapo kwa mujibu wa ile barua ndio ilikuwa siku ya saba.

    Nami sikutaka kuremba japo nilijua safari ya kwa bamkubwa ilikuwa mbali kando kando ya mkoa wa pwani mpakani mwa dare s salaam lakini niliona niondoke na familia yangu jioni ile ile kwa kuhofia tusije kuvamiwa usiku bure na watu wa huyo Mr.X kwani namba yangu tu ya simu waliijua sembuse nilipokuwa naishi?



    Mke wangu aliporudi kuchota maji nilimsihi ajiandae kwa safari haraka ambapo nae alishangaa mno lakini hakupinga hivyo tulijiandaa pamoja na lisaa limoja baadae tayari tulikuwa tupo safarini kuelekea kwa ba mkubwa.

    Moyo wangu kidogo ulianza kupata amani na kupata shauku ya kuonana na ba mkubwa kwani alisaidia na kuaminika na watu wengi mno hivyo niliamini kama tatizo letu kuna nguvu za giza ndani yake basi litakuwa limeisha kabisa kwani ba mkubwa nae alikuwa ni nooooowmaa ktk maswala ya kwechekweche na tunguli.



    Saa tatu kasoro usiku tulishuka eneo husika na kuchepuka kukifata kibarabara chembamba kilichoelekea huko alipopatikana ba mkubwa ambapo kulikuwa na umbali wa kilometa kama mbili kukifikia hiko kijiji.

    Kwa kuwa ulikuwa usiku na giza lilishaingia huku kukiwa na kijimbaramwezi kwa mbali ilibidi tutumie tochi kumulikia na njia nzima kulikuwa kimya sana.



    Nakumbuka baada ya mwendo kidogo tukiwa tumebakiza kama kilometa moja na nusu kufika mke wangu aliniomba ajisaidie haja ndogo kwani alibanwa mno na asingeweza kuendelea mbele nami nilimuonya ajisaidie palepale njiani asiingie polini kwani kuna wadudu wengi kwenye majani na ndipo nilipompokea mtoto na kusimama kumsubiria.



    Nikiwa nimesimama mke wangu anajisaidia ghafra nilisikia chakala chakala na nilipogeuka nilishangaa kumuona mtu aliyevaa kininja akininyang’anya mtoto kwa nguvu na kabla sijafanya lolote kujitetea mara kwa nyuma nilipigwa na kitu kizito bila kumuona aliyenipiga na kujikuta naanguka chini huku kwa mbali nilisikia ukulele wa mke wangu kipenzi Zai akisema.





    ‘’’’’’Jamaaniii iiiinatoshaaaaa Nilishawaaambiaa msimuuueeee..’’’



    Sitoweza kuisahau kamwe kauli ile ya Mke wangu Zai.. Zai wangu kipenziii msichana wa ndoto yangu niliyeamini nimeoneshwa na Mungu lakini leo hii anatoa kauli iliyoniaminisha na kuniumiza moyo wangu kupelekea kupoteza fahamu pindi nilipoanguka baada ya kugundua kuwa kumbe mchezo wooooooootee nae alihusika na aliujua vizuuuuri. looh!

    Ama kweli adui wako mkubwa ni mtu wako wa karibu na Udhaniae ndie sie ila sie ndie.

    Nilijihisi nakaribia kufa huku nikijiuliza kumbe Zai aliishiii kwa kuniigiziaa?!! aaaaaghh!!!!!… Ni vigumu sana kuaminilll! lakini Chunga sana baaabaa Kamishnaaa usiombe kabisa yakukute kama yaliyonikutaaaa.

    Siku hiyo ndio kwa mala ya kwanza niliikubali thabiti ile kauli kuwa Wanaake ni Wauaji, nami nakazia kabisa leo hadi siku ya kufa kwangu nitasema kuwa WANAAKE NI WAUAJIIIIII.



    *<>* *<>* *<>*



    Kilifuata tena kilio cha sauti ya juu na kwikwi kutoka kwa Hussein na kazi ikabaki kwa Kamishna Shaaban Mwinchande kum bembeleza na kumtuliza ili apate kuelewa na kubaini kilichoendelea ktk hadithi yake baada ya kurudiwa na fahamu.

    Safari hii sasa hata Kamishna Shaaban mwenyewe alijikuta nae machozi yakim bubujika kwa jinsi alivyokuwa anasikiliza kisa kile cha Hussein na zaidi alipomtazama uso wake wa kiutuuzima uliokuwa unatiririkwa machozi kama mtoto kadri alipokuwa anasimulia na alionesha dhahili kuwa ana ghadhabu kubwa juu ya wanaake kwani ktk hadithi yake ile hadi muda huo ilibeba maumivu tu na mateso yote ameyapata sababu ya mwanamke aliyempenda na pia kwa uzoefu wake wa kusoma saikology za watu Kamishna shebby alizidi kumuamini na kubaini kuwa kweli mfungwa yule alionewa na hakuwahi fanya ubaya wowote.

    Lakini maswali bado yalibaki kichwani mwa Kamishna Shebby na alitaka kujua zaidi ilikuaje hadi kukawa na uthibitisho wa maiti hizo mbili ya mkewe na mtoto? na iweje huyo Zai mke wa Hussein afahamiane na hao watu na kueka mbinu kisha wamgeuke pia na wamuue sambamba na mtoto? ilikuwaje kuwaje hapo... na huyo Mr. X ni nani kwa mujibu wa barua ya kutatanisha aliyoipata Hussein.

    Japo alikuwa mtaalamu sana Shaaban na alijaliwa ubongo mwepesi ktk kufikiri na kufumbua jambo lakini kwa maswali yale yaliyosumbuka kichwa chake muda ule juu ya hadithi ya Hussein hakuweza kupata majibu ya haraka zaidi ya kumsihi mfungwa wake (Hussein) ajikaze ili aendelee kumsimulia kilichotokea baada ya kurudiwa na fahamu mpaka kukamatwa na kuhukumiwa.



    Siku hiyo Hussein japo maumivu yalikuwa mazito mno moyoni mwake kwa kukumbuka mapito yaliyoinyamazisha ndoto zake na kujikuta anazeekea jera akisubiri kifo tu lakini alijitahidi na alipania kuwa aweke kila kitu wazi kwa kijana yule ambae awali hakutambua kama ndio kamishna lakini sasa alijua na hakuwa na jinsi zaidi ya kumuelezea kila kitu hasa baada ya kugundua ni askali kiongozi mwenye moyo wa kipekee sana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku akifuta mafua baada ya kimya cha zaidi ya dakika arobaini Hussein aliendelea kusimulia ilivyokuwa mara baada ya kupigwa na kitu kile kichwani hali iliyompelekea kuanguka na kupoteza fahamu.



    *<>* *<>* *<>*

    ..........





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog