Simulizi : Binti Kipofu
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unashida gni wewe?? Aliuliza mtu yule baada ya kurukiwa na Jimmy.
" Kuna nini hapa" aliuliza Vanessa akijitengenezea nguo yake ya juu.
"Madam Vanessa aliita Jimmy na kumtazama mtu yule aliyekuwa chini yake baada ya kumpiga na kumfanya damu izidi kulowa zaidi.
" umemfanyaje mpishi wa watu?? Aliuliza Vanessa na kumtoa juu Jimmy.
"Ammmhhh ammmhhh nilidhni........ Alishindwa kumalizia kuzungumza.
" Nilikuja njee baada ya kugundua kuwa uliacha cheni yako mezani wakati ukiniambia nikutengenezee nyama ya design gani?? Alizungumza mpishi yule.
"Wewe ni nani na kwanini umempiga mtu huyu?? Aliuliza Vanessa akiwa tayari ameshamsahau Jimmy.
" eeeeeehhhhh Jimmy alibaki akiitikia tu.
Huku akimtizama Vannesa aliyekuwa akimtizama kwa makini kama vile anamfananisha na nani.
**** ***** ****
"Sidhni kama huku tuendako ni sahihi" alizungumza Patrick na kukaa chini.
Hapo hapo simu ya Vikram iliita.
"Rickson umeshampata?? Aliuliza Dr Kim.
" hapana nimesha zunguka maeneo yote ya karibu na hapo pia nimezunguka sehemu zote wanazouza vinywaji pia sihampata unajua nashindwa hata kufikiria kwamba yuko wapi kichwa kinaniuma sana mpaka nashindwa fikiri. Alizungumza Vikram aliyeonekana kuchangangikiwa.
"Hawajampata bado?? Aliuliza yule mlevi.
" bossi wangu ni mtu ambaye yuko makini sana katika mawazo yake kama atatulia lakini akishakuwa na presha anashindwa kabisa kufikiri. Alizungumza Dr Kim akimtizama yule mlevi.
"Wewe ukilewaga huwaga unaenda wapi?? Aliuliza Dr Kim.
" kama nmekunywa kwaajili ya mtu lazima nimfuate kwa unywaji wa yule msichana mwenye gauni jekundu kuna mtu amemkera leo kwahiyo lazima amfuate" alizungumza mlevi Vikram liweza kumsikia.
"Nani kamkera Tropina leo??
" unaaliza nani kamkera wakati ni wewe na yule mwanamke wako" alizungumza Patrick na kumtazama Vikram.
"Mwanamk wangu aliuliza Vikram kwa mshangao.
Baada ya muda alionekana Vikram na Patrick wakiwa ndani ya gari na kuelekea nyumbani kwa Vikram.
Hapo hapo simu ya iliita na alikuwa ni mama yake na Alice .
" mama"Kuna mwanamk amekuja hapa na amelewa sana anagonga mlango wako kwa nguvu na akisema utoke na mwanamke wako ndani."
"Mama nisaidie kumuingiza ndani kwako na usimuache akaenda popote" aliomba Vikram.
"Sawa" alijibu mama yake na Alice.
**** *** *****
"Mbona signals yake iko nyumbani kwetu?? Alijiuliza Alice aliyekuwa akishangaa.
" mpuuzi mkubwa huyu amemfuata Vikram wangu.... Kwakuwa anamali anafikiri ataweza kumchukua Vikram kutoka kwangu...... Sitakuruhusu sasa kaa hapo hapo uone nitakacho kufanyia.
Alitafuta jina la Adrian kwenye simu yake na hatimaye alipiga simu.
**** **** ****
"Kaa kwanza kwenye kochi Vikram anakuja muda si mrefu. Alizungumza mama yake Alice akijaribu kumtuliza Tropina aliyekuwa akihitaji kutoka njee.
" najua yuko ndani na yule mwanamke wake hataki tu kunifungulia mimi mlango...... Najua yuko ndani na mwanamke mwingine. Alizungumza huku akiangulia kilio.
"Vikram hanaga mwanamke mbona wewe ndiyo mwanamke wa kwanza nakuona ukija kwake" alizungumza mama Alice.
"Yupo alikuja jioni hii na walilala wote pamoja wewe hukuwepo ndo maana unaongea hivyo. Alisema Tropina.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" mimi ni kama mama yake Vikram namtambua vizuri kabisa Vikram siyo kama hao vijana wengine wa mtaani....na msichana anayeingia kwa Vikram tena mara moja moja ni binti wangu wa kike ambaye anamchumba wake. Alizungumza mama Alice.
"Ni kwli?? Mbona sasa nilimuona akitoka na taulo?? Aliuliza Tropina.
" naamini Vikram hana mwanamk mwingine tulia kwanza hapa nikakubandikie chai wakati Vikram anakuja" alizungumza mama Alice na kumshika mikono ghafla Tropina alipiga kelele kwani mikono yake ilikuwa imelowa damu baada ya kuweza kulitoa tofali lile katka choo kwaajili ya kutoroka.
"Mbona umeumia hivyo?? Aliuliza mama Alice.
" Ngoja nikakuletee dawa kwaajili ya kukupaka alizungumza na kumuacha Tropina ndani ambaye aliweza kutoka tena njee na kwenda kugonga chumba cha Vikram wakati akifanya hivyo ilionekana mikono yenye kamba nyembamba ikimsogelea karibu kabisa na mwili wake na kutaka kumuulia mbali. Wakati huo nao Vikram bado alikuwa barabarani akiendesha gari kwa kasi Kubwa sana.
Huku nako alionekana Adrian akiishika mikono yake kwa nguvu huku akisema
"Hii ndiyo plan yangu ya mwisho nikishindwa bac sitamuuwa tena wala sitahitaji hizi mali tena"
********
*******************
"Samahani" alizungumza Vikram na kutoa simu yake mfukoni alipoona ni jina la Alice alimtizama Tropina ambaye aliamua kutoka kitandani.
"Usiogope kupokea simu yake pokea umwambie uko njiani unaenda kwake" alizungumza Tropina na kuelekea kwenye kabati lake la nguo kwaajili ya kutoa taulo na kujikausha maji.
Vikram alibaki akiitizama simu yake na kumtazama Tropina.
Alitabasamu na kumfuata Tropina nyuma.
"Pinah.......me sina mahusiano naye yoyote yale na unaposema kuwa mimi nimelala na mwanamke mwingine tofauti na wewe hapana sijawahi kulalaga na mwanamk yoyote yule katika dunia hii isipokuwa mmoja'
" nani huyo?? Aliuliza Tropina na kumkazia macho Vikram ambaye alitabasamu.
Alimshika nywele ghafla simu yake iliita tena.
Tropina alimsukuma na kutaka kuondoka zake Ila Vikram aliwahi kumshika mkono na kumvuta karibu na kifua chake.
Alikata simu ile mbele yake na hatimaye aliizima kabisa huku akimuonyeshea Tropina kuwa ameizima baada ya kufanya hivyo aliirushia kwenye kochi na kumshika Tropina kiunoni kwa mikono yake yote miwili.
"Unajua ni mwanamk gani huyo ambaye.............." Kabla hajamalizia kuongea Tropina alimjibu.
"Wala sitaki kumjua" alizungumza na kutaka kujitoa mikononi mwa Vikram ambaye alimng.ang.ania barabara.
"Kwanini unakuwa na uwivu hivyo eti? Aliuliza Vikram na kumtazama Tropina machoni.
" Uwivu wa nini?? Aliuliza Tropina akiwa anamtizama Vikram machoni.
"Mwanamk mwenyewe ni wewe. ....nataka uwe mwanamk wa kwanza kulala na mimi" alizungumza Vikram.
"Kwahiyo niwe wa kwanza tu?? Aliuliza Tropina.
" hapana utakuwa wa kwanza na wa mwisho" alizungumza Vikram na kutabasamu.
Ghafla simu ya mezani iliita.
"Ni nani huyo?? Aliuliza Vikram.
"Ngoja nikapokee alafu nitajibu swali lako" alisema Pina na kutoka mikononi mwa Vikram.
"Halo" alizungumza Tropina lakini hakukuwa na majibu yoyote yale.
"Kwanini kapokea huyu kipofu?? Alizungumza kwa hasira Alice aliyekuwa akiona kila kinachotokea.
" haloo" aliendelea kuita Tropina na Vikram alikuja nyuma yake akimbusu sehemu za shingoni pamoja na kumpapasa.
"Vi...cky...subiri" alizungumza Tropina kwa sauti laini iliyoweza kupenya masikioni mwa Alice aliyekuwa akifa kwa wivu juu ya mume wa mwenzke pasina yeye mwenyew kutambua hilo.
Vikram aliendelea kumbusu na hatimaye Tropina aliamua kukata simu baada ya kuona mtu haongei na tayri Vikram ameshamzidi ujanja kwa kuweza kumlegeza mwili wake wote.
"Vicky aligeuka na kumuita.
Vikram alimbeba kwa kumshika sehemu ya kiuno na kumkalisha katika meza ile ya iliyokuwa simu.
Alitabasamu akimtizama Tropina aliyekuwa kafunga macho yake yote akisubiri kitu kutoka kwa Rickson.
Ghafla upepo mkali uliweza kuingia ndani na kufanya baadhi ya vitu vidondoke Tropina alienda kufunga dirisha la upande wa kushoto huku naye Vikram akienda kufunga dirisha la upande wa kulia ambapo camera iliweza kutegeshwa alipopita aliweza kuiona camera ile iliyokuwa juu ya kitabu kimoja.
Alijua kabisa ya kuwa wanaonekana hivyo baada ya kufunga dirisha alijifanya amejikwaa na kudondokea baadhi ya vitabu ikiwepo na kile chenye camera kwa kuvigusa na mkono wake na kuvifanya viendee chini.
" Rick uko salama? Aliuliza Tropina na kumfuata Vikram ambaye alipoinuka aliweza kuiona ile camera ikiwa chini na kuikanyaga kanyaga kwa design ambayo ingekuwa vigumu hata Tropina kusikia kama kuna kitu kimeweza kukanyagwa.
"Ni nini hii?? Alibaki akilalama tu Alice huku akigusa gusa laptop akiwa haamini kama camera haifanyi kazi tena na Vikram yupo na Tropina chumba kimoja.
" nimesema sikubali........lazima atalipa kwa hili alizungumza Alice huku akitupa tupa vitu vilivyokuwa mezani hapo.
"Wewe ni kwanini unatupa tupa vitu hivyo?? Aliuliza Danielle na kumtazama Alice aliyekuwa akihema kwa hasira sana.
" ni nini hapa ?? Aliuliza Calvin baada ya yeye kuwasili.
**** ***** ******
Vanessa alikuwa akielekea mlangoni kwa Tropina baada tu ya kukucha lakini ghafla aliitwa na Diana.
"Ni nini shida?? Aliuliza Vanessa.
" Madam Tropina amelala bado"
"Sindiyo nataka niende nikamtizame ameamkaje alizungumza Vanessa.
" ameamka vizuri tu alijibu Diana.
"Kuna shida gni mbona hutaki niingie kwa Tropina? Aliuliza Vanessa.
" hapana lakini amelala ungemuacha tu' alijibu Diana.
"Sawa " alijibu Vanessa akielekea kwenye chumba cha Vikram.
"Hata yeye amelala" alisema Diana.
Vanessa alimgeukia na kumtizama Diana kisha akatazama mlango wa Tropina na mlango wa Vikram alafu akarudia kumtizama Diana tena aliyekuwa akitabasamu huku akimtizama.
"Chai tayari tushuke chini ukanywe. alizungumza Diana na kumfuata Vanessa kisha kumkokota kwa kumshusha kwenye ngazi Vanessa alibaki akikitizama chumba cha Tropina kwa wasiwasi.
" ameondoka" alisema Vikram na kupumua huku akimtizama Tropina aliyekuwa kitandani akiwa amejiziba na shuka katika sehemu zake za kifua.
"Twende bafuni tukaoge" alizungumza Vikram na kumfuata Tropina.
"Tuoge wote.........!!!! Aliuliza kwa kutahamaki Tropina.
" eheeeee mbona umeshtuka hivyo........ndiyo twende tukaoge wote" alizungumza na kumsogelea kwa karibu zaidi Tropina aliyekuwa akirudi rudi nyuma.
"Tangulia nakuja alisema Tropina
Vikram alicheka kisha akakaa kitandani.
" eti unaogopa nini labda?? Aliuliza Vikram.
"Hamna"
"Haya kama Hamna twende tukaoge alizungumza Vikram na kumshika mkono Tropina kwa kumuinua.
" Ricky..........aliita Tropina kivivu.
" yes my Queen " aliitikia Vikram na kumfanya Tropina akose cha kuongea zaidi ya kumtizama tu Vikram.
"Pinah..... Nataka ujue ya kuwa nakupenda....nakupenda sana...sana....sana....sana...sana.....hadi naumwa yani" alizungumza na kumbusu Tropina mdomoni.
"Me too hubby, nakupenda sana sana sana sana sana sana sna mpaka naumwa" alijibu Tropina na kutabasamu
Walicheka wote kwa pamoja na Vikram alimuinua Tropina na kumwambia.
"Kwa kuwa tunaenda kuoga toa shuka basi" alizungumza Vikram na kuanza kuchomoa shuka kifuani mwa Tropina ambaye alifunga macho yake kwa mikono yake.
"Pinah....unaogopa nini eti?? Aliuliza Vikram na kucheka zaidi akifungua shuka huku akimtizama Tropina macho yake kwa chini.
" nakuchungulia hivyo" alisema Vikram akimtizima Tropina.
"Bwana aaaahh alisema Tropina huku akipiga piga miguu yake chini kwa aibu.
" basi twende bafuni hivyo hivyo alizungumza na kumbeba mzima mzima Tropina kisha kuingia naye bafuni.
Upande wa njee wa nyumba hiyo liliweza kuingia gari kwa kasi sana na aliteremka Alice akiwa amejaa hasira.
********
************
********************
Ni baada ya Adrian kutamka jina la Rickson mbele ya Alice.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
'Mbona umeshtuka hivyo unamfahamu?? Aliuliza Adrian.
Hapo hapo Alice alikumbuka ya kuwa kuna siku alimuuliza Mr Harlan kwanini Danielle aende akaishi kwa kina Tropina.
Mr Harlan hakumjibu kitu zaidi ya kusema wafanye vile anavyosema na yeye akapewa nafac ya kuelekea kwenye kampuni anayoifanyia kazi Adrian.
Alitabasamu baada ya kugundua hilo.
"Sasa kama anamwanaume wake Rickson kwanini anamtaka tena Vikram wangu?? Aliuliza Alice.
Adrian alipandisha mabega ishara ya kuwa hafahamu.
" Sawa tumtumie huyo Winnie" alizungumza Alice na kutabasamu.
***** ****** ******
"Siku ile ilikuwaje mlivyoenda kumuokowa Tropina?? Aliuliza Danielle.
" Siku gani?? Aliuliza Calvin.
Danielle alimtizama Calvin na kuelewa ya kuwa hafahamu chochote kitu.
Calvin alimtizama na kumwambia.
"Mbona unanisoma akili yangu wewe?? Aliuliza Calvin.
***** **** ****
Tropina alikuwa ndani kwake ghafla simu yake iliita na namba ilikuwa ni ngeni.
" haloo.............. Unataka nini wewe mwanamke?? Aliuliza Tropina na hapo hapo aliingia Vikram.
Vikram alivua koti lake na kumsogelea karibu Tropina huku akimpiga busu sehemu za shingoni na kumkumbatia kumbatia.
"Ni nani huyo?? Aliuliza Vikram.
" Mke mwenzangu alijibu Tropina na kumpa simu Vikram huku akitaka kuondoka Vikram alimvuta na kumuweka karibu na kifua chake kisha akamgeuza na kufanya macho yake yaangalie kule anapoangalia Vikram.
Pinah aliona boksi lekundu likiwa ndani ya chumba chake.
Vikram alimpa ishara alifuata.
"Haloo" alizungumza Vikram akiwa ameibana sauti yake.
"Rickson!! Aliita Winnie kwa mshtuko.
" Winnie hili ni onyo la mwisho nakupatia, usije ukampigia mke wangu Tropina kwa chochote kile na kama utaendelea kunisumbua mke wangu......unaelewa kipi kitamkuta Baba yako...ile kesi yake nitaifufua upya na utaifanya familia yako ikose furaha. Sasa angalia kipi ni kizuri ukose furaha ww mwenyewe au uwakoseshe furaha familia yako nzima" baada kumaliza kuzungumza hivyo alikata simu. Kisha akageuka akiongea kwa sauti ya kawaida na ya juu kabisa.
"Nashukuru kwa kunielewa kuwa nampenda Tropina wangu sna sana sana sana sana mpaka naumwa" baada ya kuzungumza kikawaida hivyo alikata simu na kumfuata Tropina aliyekuwa akitabasamu na kutizama kipi kilichokuwa ndani ya boksi.
Vikram alimfuata na kukaa nyuma yake huku akimbusu shingoni.
"Ricky.......niachie bhna alizungumza kwa sauti ya utaratibu na kugeuka nyuma ambako macho yake yaligongana na macho ya Rickson yaliyokuwa yakihitaji kitu fulani kutoka kwake.
Walitizamana taratibu kabisa na hatimaye waliweza kusogeleana kwa ukaribu zaidi na Vikram alimbusu mdomoni Tropina mara moja na kumtazama.
" my Queen (malikia wangu)."
Abee.
"Pinah.....unajua nakupenda sana mpaka nashindwa kujielewa yani ukikaa mbali tu na mimi nahisi kuumwa kila nikikaa karibu na wewe najisikia tu nikuguse kila mahali katika mwili wako....sijui nikwambie nini ili ujue jinsi gani ninavyokupenda" alizungumza Vikram aliyeonekana kufa na kuoza juu ya tropina aliyekuwa akiachia Tabasamu.
"Ni Sawa tu ukiwa karibu na mimi fanya chochote kile ukipendacho kwani mwili wangu ni halali yako" alizungumza Tropina na kumtazama Vikram ambaye macho yake tayari yalishaweza kulegea na midomo yake aliyokuwa akiing.ata tu.
Tropina alifungua tai ya Vikram na kuanza kufungua kifungo kimoja kimoja cha shati alilokuwa amevaa Vikram huku akimpiga busu sehemu yak ya kifua kila alipokuwa akifungua kifungo kimoja.
Alipomaliza kufungua shati lote alipitisha mikono yake yenye kucha ndefu katika kifua cha Vikram huku akimbusu na kuelekea mpaka kwenye suruali ya Vikram.
Alifungua bakoli kwenye mkanda wa Vikram na kuanza kuuvuta taratibu tu wakati huo wote Vikram alikuwa kimya akimtizama Tropina aliyekuwa akihangaika na mwili wake.
Alipomaliza kuutoa mkanda wote alimtizama Vikram na kupeleka kinywa chake katika pua ya Vikram kisha akaing .ata kidogo tu kwa mahaba na kuupitisha ulimi wake katika sikio la Vikram huku mkono wake ukifungua zipu ya suruali ya Vikram aliyekuwa akihema kwa sauti ya juu.
Vikram alimshika Tropina kwa mikono yake yote miwili kwa nguvu na kumtupia kitandani kisha akamtizama kwa sekunde chache na kumfuata kitandani kwa kasi ya 4G.
*** my dear's ya huko hayatuhusu tuendeleni na stori maana masikio hapo yamewasimama kweli******
Winnie alipokuwa akizungumza hakuzungumza mwenyewe bali Adrian na Alice walikuwa pale.
"Huyu kipofu anawezaje kuwachukua wanaume wote wawili yeye tu kam ana Rickson wke kwanini amchukue na Vikram wangu!! Alibweka Alice kwa hasira sana.
"Ni kweli kwamba Rickson ni furaha yangu lkini mimi siyo furaha ya Rickson na yote kwa yote familia yangu ni kitu cha kipekee kabisa katika maisha yangu sitaweza kuishi kwa furaha mimi wakati huo Baba yangu anasotea gerezani kwahiyo nimeamua kuachana na hayo yote na nitaondo katika nchi hii alizungumza Winnie kisha akasimama na kumuacha Alice na Adrian.
" anaenda wapi huyu?? Aliuliza Adrian na kutaka kumfuata.
"Mwache huyo huyo tutatumia maisha yake kumchafulia jina Tropina" alisema Alice akimtizama Winnie aliyekuwa akipanda gari lake na kuondoka.
****** **** *****
Kwa upande wa Tropina na Vikram walikuwa wamemaliza kufanya yao na wakiwa kitandani huku Vikram akiwa amelala kifuani kwa Tropina.
Na akifunua shuka
"Unataka nini aliuliza Tropina.
" nataka kunyonya" alijibu Vikram akicheka.
"Mjinga sana wewe mwanaume mshenzi wewe alizungumza Tropina na kukitoa kichwa cha Vikram kifuani kwake.
Vikram alimtizama Tropina na kutabasamu zaidi huku akimbusu na kumlaza Tropina kifuani kwake.
" my Queen " aliita Vikram.
"Yes"
"Kwanini ujaniulizaga swali lolote juu ya jina la Vikram nililipatiwa wapi pia hajawahi kuniulizaga nilikuwa wapi miaka yote vipi kuhusu Baba yangu hajawahi pia........."
"Rickson sitaki nikuforce wewe uniambie chochote juu ya maisha yako nahitaji uniambie wewe mwenyewe kwa kupenda kwako kwani naamini kila yote hayo uliweza kuyafanya kwasababu unayo sababu maalumu ya kufanya hivyo" alizungumza Tropina na kumfanya Rickson adondoshe machozi.
"Kwnini unalia sasa aliuliza Tropina na kumfuata machozi Vikram"
"Pinah siku nikipata muda nitakwambia kila kitu kuhusu maisha yangu mimi pia nashukuru kwa kuniamini mimi" alizungumza Vikram na kumkumbatia Tropina zaidi.
Hapo hapo simu ya Tropina iliita.
"Unataka kufanya nini?? Aliuliza Vikram ambaye alimuona Tropina akitaka kuamka kitandani pale.
" simu yangu inaita Ricky" alizungumza Tropina na kujitahidi kuamka tena.
"Hakuna kupokea simu laza kichwa chako hapa hapa" alisema Vikram na kumkumbatia vizuri Tropina aliyejisogeza na yeye kumkumbatia vizuri Vikram.
Simu hiyo alikuwa akipiga Winnie laiti angelipokea basi ingemsaidia kitu.
**** **** ****
Vanessa alienda shuleni kwa kina Larry. Alipofika alikaa katika chumba cha wageni ghafla Alisikia kelele za watoto wa shule wakiwa wanakuja kwenye chumba kile.
"Miss Queen huyu amekuja walizungumza na kuingia kwa fujo ndani. Walitulia tuli baada ya kumuona Vanessa.
" Madam Vanessa shikamo walisalima wote na kutoka njee ambako walikutana na Larry.
Larry alicheka na kutabasamu
"Leo amewakata break za kiherehere eeee" alizungumza Larry na kujitengenezea vizuri nguo zake kisha akaingia ndani ya chumba hicho akiwa serious.
"Si nilikwambia usije siku ya leo bila taarifa" alizungumza Larry na ghafla Alisikia sauti ya ikimjibu.
"Ulimwambia nani asije bila taarifa"
Alishtuka na kumtazama alikuwa ni mama yake.
"Vanessa!! Aliita kwa mshangao.
" Ni nani huyo uliyemwambia asije bil taarifa?? Aliuliza tena Vanessa.
"Hamna mtu kwani wewe unafikiri ni nan?? Kwanza kwnini na wewe umekuja hapa? Aliuliza Larry.
Vanessa alitoa begi aliloweza kuja nalo na kuliweka mezani.
" nilipitia super market jana nikakununulia pizza baada ya kujitengeneza pmoja na sandwich ndo nimekuletea leo.
"Sawa ahsante unaweza ukaenda" alichukua begi na kuanza kuondoka.
"Maajabu sana ya leo wala huniombi hela ya matumizi kabisa alafu kwanini unaniharakisha niondoke?? Aliuliza Vanessa ghafla ilisikika sauti ya kike nyuma ikiita jina.
" Larry " alijitokeza Queen.
Mungu wangu alisema Larry na kugeuka kumtizama mama yake.
Queen alimsogelea mpaka karibu na kumpatia kipochi alichoweza kuja nacho.
"Nimekutengenezea nyama ya kuku nyingi nyingi nyingi na chipsi alafu nimeweka na pilipili kidogo nikanunua na kinywaji cha baridi kabisa"
Kuna nini leo mbona hunisemeshi aliuliza Queen na kutazama mbele.
"Ni nani wako yule?? Aliuliza baada ya kumuona Vanessa.
Larry alishindwa kuelewa na afanye nini na kumwambia Queen.
"Mama"
"Mama!!?? Aliuliza Queen kwa mshangao na kumtazama Vanessa.
"Yani mama yako?? Aliuliza Queen.
Larry alitikisa kichwa ishara ya ndyo na kumfanya Queen ashtuke.
Vanessa alisimama na ghafla simu yake iliita.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halo.
Hapo hapo simu ya Queen naye iliita
'Halo"
Wote walishtuka baada ya kuzisikia taarifa walizoweza kuzipata kupitia simu zao za mikononi.
"Tropina!!! Aliita kwa mshangao Vanessa.
Na Queen na yeye alisikika akisema.
" Winnie !!!
Larry alibaki akiwashngaa wote wawili.
"Amekufa" alisema Queen na kukaa chini.
"Unamaanisha nini unaposema Tropina ameuwa?? Aliuliza Vanessa ambaye kipochi chake kilimdondoka.
Ni baada ya Queen na Vanessa kupokea simu ambazo ziliwafanya wachanganyikiwe.
"Kipi kimetokea" aliuliza Larry akimfuata Queen aliyeweza kudondoka chini.
Queen alibaki akimtizama tu Larry ambaye alishindwa kuelewa kipi kimetokea.
"Vanessa ni nini shida?? Aliuliza Larry akishindwa kuelewa kipi kimetokea.
Hapo hapo aliingia Obama.
" ninataarifa mbaya juu yako alizungumza Obama.
"Kipi kimetokea? Aliuliza Larry.
" Inabidi uendee nyumbani kwasababu Tropina
Anahusishwa na mauaji ya kumuuwa winnie namaanisha Dada yake Queen.
Larry baada ya kusikia maneno Yale alijikuta miguu imemuishia nguvu na hawezi kabisa hata kuchuchumaa.
Vanessa alikata simu yake na kuanza kutembea lakini hakupiga hatua nyingi na aliweza kujikwaa.
Obama aliwahi kumshika kisha akamtoa njee.
Larry alimuinua Queen ambaye alikuwa ameduwaa tu na kuanza kumtembeza taratibu alimpeleka hadi kwenye gari ambalo aliweza kujaa nalo. Larry alimtizama tu bila kusema neno lolote lile.
"Tafadhali mpeleke nyumbani na uhakikishe anafika salama. Alizungumza Larry akimwambia dereva wa Queen kisha akamtizama Queen na kuufunga mlango wa gari kisha akaelekea katika gari aliloweza kuja nalo Vanessa na kupanda.
*** **** *** ***
Tropina akiwa katika kituo cha polisi katika chumba cha mahojiano huku George akiwa mbele yake.
"Kwanini umemuuwa Winnie??
" Sijamuuwa mtu yoyote Mimi alizungumza Tropina huku akizipuliza kucha zake na kutabasamu.
"Unamfahamu Winnie?? Aliuliza George.
"Kidogo tu alizungumza Tropina kwa kuonyesha kidole chake.
" Unamfahamu kivipi??
"Alikuwa mke mwenzangu kwa Rickson. Alijibu Tropina.
"Rickson?? Aliuliza kwa mshangao George.
"Yap unamfahamu ?? Mbona umeshtuka hivyo?? Aliuliza Tropina akimtizama kwa makini George.
George alimtizama tu na kuamua kutoka katika kile chumba.
" anashida gani huyu........wewe officer nahitaji kuondoka katika hiki chumba sipendi kabisa kukaa hapa mimi ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha.
Aliingia Vanessa na Larry wakiwa na wakili au mwanasheria Josephat.
"Nimekuja kumuwekea bili mteja wangu Tropina Livingstone katika kesi ambayo hausiki na polisi hamna vizibitisho vya kutosha" alizungumza josephat na kutoa barua kisha akampatia George.
Aliingia Vikram na wakili.
"Vanessa, Tropina yuko wapi?? Nimemleta wakili yeye ni mzuri sasa katika upande wa utetezi.
" Tayari ameshaenda ndani wakili wa familia ndo tunasubiria majibu hapa kama ataweza kuachiwa au lah! Alizungumza Vanessa huku akiisokota mikono yake.
Baada ya dakika tano kupita wakiwa njee chumba cha mahojiano kilifunguliwa na alitoka Tropina.
"Kuna shida gani mbona mmejazana hapa na kikesi chenyewe ni kidogo sana aliuliza Tropina akiwatizama.
" Uko salama aliuliza vikram na kumsogelea kwa ukaribu.
"Niko salama Mimi" alijibu Tropina na kutabasamu.
Vikram alimkumbatia Tropina huku akimpiga piga mgongoni.
Vanessa na yeye alimfuata na kumkumbatia.
"Mnahangaika na mtu ambaye amesema yuko salama?? Aliuliza Larry na kugeuka zake nyuma huku akiongoza njia ya kuondoka.
" Kaone hako" alizungumza Tropina na kutabasamu baada ya kumuona mdogo wake.
*** *** *** ***
"Sasa ni nani atakuwa amemtengenezea kesi Tropina au ni Mr Harlan?? Aliuliza Dr Kim.
" Harlan hamfahamu Winnie inamaana mtu aliyefanya hivi anajua kabisa ya kuwa Pinah hapatani na Winnie ndo maana akaamua kufanya hivyo " alizungumza Rickson.
"Suluhu ni tufahamu kwanini amefanya hivyo lazima iwepo sababu ya kufanya hivyo" alizungumza Jimmy.
"Kim, uliweza kumpta yule jamaa aliyetusaidia tukampata Tropina siku ile pale hotelini??
"Hapana" alijibu Dr Kim.
"Tungempata yeye angeweza kutusaidia zaidi, ulifanya ujinga ulipomuacha mwenyewe" alilalama Rickson.
"Lakini Mimi nilikuwa nikimuwekea umakini mpaka pale ulipopiga simu na kuniambia nije kumsaidia Tropina kwa haraka ndo nikamuacha"
"Huu siyo muda wa kulaumiana ni tuntakiw tufahamu nani kaweza kufanya hivyo kama siyo Mr Harlan basi ni upande wa Tropina tunatakiwa tufahamu nani adui wa Tropina" alizungumza Jimmy na kuwafanya wote wamtazame.
Hapo hapo aliingia Obama.
"Jamani tupate msosi kwanza kabla ya kufikiria hilo jambo.
*** *** *** ***
Tropina aliweza kuletewa faili zima lililokuwa na details zote juu ya kifo cha Winnie na Diana.
"Naanza kusoma" alizungumza Diana
"Majira ya saa tatu asubuhi ya Leo tar 1/11/20011 kituo cha polisi walipokea simu iliyopigwa kutoka kwa Winnie Bariki akilalamika na kupiga kelele za kuita Tropina Tropina kisha ikasikika kelele kubwa na hapo ndipo polisi walipoweza kwenda na kukuta maiti ndani pamoja na hereni moja ambayo inasemekana ni ya kwako. Alizungumza Diana.
" ohooo kwahiyo ushahidi walio nao ni kutajwa jina langu pamoja na hereni moja mjinga gani huyo mpuuzi anafikiri kwa ushahidi wa kitoto hivyo anaweza kunifunga Mimi" alizungumza Tropina na kucheka.
"Sawa unaweza ukaenda alisema Tropina na kusimama alipokuwa amekaa kisha akaichukua red wine yake na kuweka mdomoni.
Baada ya Diana kuondoka na kuacha file lile mezani Tropina alilichukua na kulifungua.
Baada ya kufungua picha ya juu ilikuwa ya Winnie akitabasamu.
Alipofungua karatasi lingine hapo ilikuwa picha ya marehemu Winnie. Alipoitazama ilikuwa imejaa damu huku akiwa amepigwa zaidi sehemu ya kichwa.
Tropina alimtizama kwa makini na kutaka kugundua ni kitu gani ambacho kiliweza kutumika kumuulia Winnie.
" Hichi nichuma kizito tena ambacho kitakuwa na uwezo wa kilo 5 na atakuwa amempiga mara tatu kichwani kwasababu alama ya kwanza ni ya kwenye paji la uso ya pili ilipiga karibu na paji la uso pia alafu ya tatu ilipiga hapa uchogoni sasa ushahidi ambao haujaonekana ni hicho chuma lazima kiwe na fingerprints za muuwaji huyo kikipatikana hicho kitaweza kunisaidia.....pia kwanini alinitaja jina langu sina adui yoyote tofauti na Adrian alizungumza Tropina na kuendelea kutizama picha ile.
Wakati huo nao George alikuwa akitizama picha ya Winnie.
"Hapa kilichoweza kutumika kumpigia ni Chuma ambacho hakitakuwa na ujazo zaidi ya kilo tano pia kwa kutizama kichwa chake amepigwa Mara tatu kwani alama hizo zinaonyesha.....
Tropina siyo mwanamke mwepesi wa kumpata kama kweli ni yeye kahusika na mauaji kwasababu ana degree ya sheria hatuwezi kumpata kirahisi rahisi lakini cha kufanya tupate kitu kilichoweza kumpiga.
Thobias alimtaza George na kumwambia.
" lakini atawezaje kumuuwa mtu ambaye anamacho yake yote mawili....hapo ndo nashangaa Tropina ni kipofu alafu akamuuwa mtu ambaye anamacho mawili lakini hana scratch sehemu hata moja ya mwili wake? Aliuliza thobias na kumfanya George afikirie kidogo kisha akamtizama Tobias na kumwambia Inabidi tuende kwenye eneo la tukio tena lazima kuwe na ushahid tulioweza kuuacha.
**** **** ***** ****
"Lakini Pinah ni vizuri kama tutaweka wakili" alizungumza Vikram aliyekuwa na Tropina.
"Usijali ni kesi ndogo sana wala sihitaji wakili wa aina yoyote yule" alizungumza Tropina akimshika mikono Vikram.
"Lakini!!!!
" Shshshshsh.............Tropina alimnyamazisha Vikram kwa kumpiga busu la mdomo.
"Hodi!!! Aligonga Larry na kuingia ndani.
" Narudi shule mimi kwasababu umeshasema ya kuwa kesi ni ndogo" alizungumza Larry na kuanza kuondoka.
"Bwashe" aliita Vikram na kumbusu Tropina shavuni kisha kumfuata Larry.
"Nakupeleka shule" alizungumza na kumshika Larry mkono kisha kutoka naye njee.
***** ***** *****
"Umekuwa kimya sana na siyo kawaida yako kama unatatizo niambie Mimi ni bwashe wako nitakusaidia" alizungumza Vikram.
Larry hakuwa akisema kitu zaidi ya kufikiria ni jinsi gani ataweza kuzungumza na Queen.
"Unajua........au ........yani mimi.............au acha tu" alizungumza Larry na kutizama njee ya kioo cha gari.
"Ni kuhusu Queen?? Aliuliza Vikram.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Larry alimtizama na kutingisha kichwa.
" Unataka ukamuone?? Aliuliza Vikram.
"Nataka kujua anaendeleaje tu kwasababu siwezi kwenda kuzungumza naye kabisa ikiwa Tropina ndo anashutumiwa kumuuwa dada yake. Alizungumza Larry kwa huzuni.
" Sawa nitakupeleka ila itabidi tuende usiku kidogo kwani ikitokea tutaonekana onea lil e unaelewa kipi kitatokea" alizungumza Vikram.
"Sasa muda bado mwingi sana tunafanyaje sasa hivi? Aliuliza Larry.
" Nataka nikakutambulishe kwa mtu ambaye ukiwa shuleni shida zako zote utamwambia yeye na yeye atakutatulia kama pia utahitaji kuzungumza na mimi utamtumia yeye "
"Sawa"
"Larry... Unaamini ya kuwa Dada yako atakuwa ameuwa Winnie?? Aliuliza Vikram.
"Namfahamu vizuri sana Dada yangu hawezi kufanya hivyo hata kama ana anaonekana mbaya sana machoni pa watu wengi" alizungumza Larry
*** **** *****
"Najua atakana kuwa yeye hajamuuwa lakini kipo kitu kingine ambacho kitamfanya ashindwe kujitetea zaidi maana anajifanya smart sana" alizungumza Alice.
"Tropina ana degree ya sheria siyo kirahisi kumtengenezea kesi" alizungumza Adrian akimtizama Alice.
"Chuma hichi ndicho kilichoweza kumuondoa uhai Winnie kinachohitajika ni alama za vidole za Tropina"
"Tropina siyo mjinga akishike eti hivi we unamjua yule kipofu?? Aliuliza Adrian.
" usijali yeye ni kipofu tu hawezi kufanya chochote kunizidi akili Mimi alizungumza Alice na kucheka.
"Chuma hichi atakishika mwenyewe akitaka kuniuwa Mimi" alizungumza Alice.
"Kukuuwaje?? Aliuliza Adrian.
"Tulia nitakuonyesha kwanini naitwa Veronica" alizungumza Alice na kutabasamu.
Ni baada ya Alice kuapa na kusema ya kuwa Tropina lazima afungwe.
**** *** **** ****
Tropina akiwa chumbani kwake msg iliingia kwenye simu yake na ilikuwa ni msg kutoka katika namba ya Vikram.
"Waoooo Vicky amenipa appointment niende nyumbani kwake alizungumza Tropina na kutabasamu.
Huku nako Vikram alikuwa akiingia katika nyumba ya kina Winnie kwa kuiba.
Hpo hapo msg iliingia aliiwahi simu na kuisoma ilikuwa ni msg ya Tropina.
"Njoo chumbani kwangu.
Vikram alitabasamu na kumwambia Larry.
Me nitakuacha hapa na Obama baada ya kuwaingiza ndani nataka nirudi nyumbani. Alizungumza Vikram na kuendelea kuonyesha njia.
Alice baada ya kutuma msg zote mbili alitabasamu na kuzungumza
"Sasa ndo tunaanza game Tropina kuwa makini unafikiri unaweza kuwadanganya wote kwamba wewe ni kipofu shukrani kwa mama yangu kwani amenirahisishia njia rahisi sana ya kukulia mbali huko gerezani.
Alikumbuka Alice mchana wa siku hiyo alimuona mama yake akiwa mwingi wa mawazo huku akijaribu kutafakari jambo.
" Alice"
"Abee" aliitika Alice.
"Hivi yule Tropina ni kipofu kweli???
" Ndiyo ni kipofu kwanini umeniuliza?? Aliuliza Alice.
"Siku ile mchana alipohisi we umelala na kaka yako Vikram nilipishana naye na ufunguo ulidondoka ule ulioniambia nikauchongeshe chaajabu aliinama na kuokota kisha akanipa. Bado unafikiri ya kuwa ni kipofu tu??
Alice alitabasamu baada ya kukumbuka maneno hayo.
" hawezi kuwa kipofu kwani asingeweza kujibu msg niliyoweza kumtumia kupitia laini hii ya Vikram niliyoichongesha kwa gharama kubwa sana.
**** ***** *****
Tropina aliweza kufika katika nyumba ya Vikram na moja kwa moja aliushika tu mlango ulifunguka alikuta ndani pamepambwa vizuri na vinywaji vikiwa juu ya meza pamoja na chakula.
Tropina alituma msg ya "Nimefika" na msg hiyo ilienda moja kwa moja hadi kwa Vikram aliyekuwa ndani ya gari.
"Niko njiani nakuja" alituma msg Vikram na ilienda kwa Tropina.
Wakati huo Alice aliingia chumbani kwa Tropina kwa Siri sana ila wakati anaingia Danielle aliweza kumuona lakini kutokana na giza hakuwa na uhakika kama aliyewza kumuona ni Alice.
"Hawezi kuja hapa tena akaingia chumbani kwa Tropina hawezi" alijishauri hivyo Danielle na kuelekea kwenye chumba chake.
Vikram alifika chumbani na alikuta kumepambwa vizuri sana taa iliweza kuzimwa na ilibaki tu mishumaa iliyokuwa na mwanga hafifu sana ambayo isingeweza kuwa rahisi kwa Vikram kujua ya kuwa alioko ndani siyo Tropina.
"My Queen" aliita Vikram kwa utaratibu sana huku akijitahidi kumtafuta Tropina yuko wapi.
Ghafla alishtukia amefungwa kitambaa machoni mwake na hiyo ikamfanya asitambue ni nani.
Simu yake iliita na Alice aliitoa mfukoni kisha akatizama na kugundua ni Tropina anapiga alikata simu na akaamua kuizima kabisa kisha akaichukua simu yake na kuiweka upande wa record na kuirushia kitandani kisha akamfuatisha Vikram ambaye hakuwa anaelewa kipi kimetokea.
Alianza kumvua koti na kuanza kufungua vifungo vya shati.
"Tropina ni nini hii Leo mbona umenifumba macho?? Aliuliza Vikram kwa kushangaa na kutaka kutoa kitambaa machoni lakini Alice alimshika mkono na kuutoa baada ya hapo alivua nguo gauni la kulalia la Tropina aliloweza kulichukua.
Kwa upande wa pili Tropina alikuwa ndani ya chumba cha Vikram huku akijaribu kupiga simu lakini haikupatikana.
Mishumaa iliyokuwa ndani ilishaanza kufifia mwanga wake na Tropina tayari alishakunywa wine karibia na kuisha.
Alitoka njee akitizama kulia na kushoto kama Vikram ataweza kutokea lakini bado hakukuwa na mtu kutizama saa yake tayari ilishakaribia saa 5 usiku.
Mama yake Alice alitoka njee baada ya kusikia mlango umefunguliwa.
" We ni nani?? Aliuliza mama yake Alice.
Tropina aligeuka na kumpa heshima.
"Mama shikamo"
..ahaaa Tropina aliita mama yake Alice na kumfuata.
"Unaendeleaje?? Aliuliza Tropina.
" Naendeaje kivipi?? Aliuliza mama yake Alice.
"Namaanisha kuwa kama unaendelea vizuri Alice alisema unaumwa" alizungumza Tropina.
"Mimi naumwa hapana mbona me wala sijaumwa siku hizi za karibuni" alizungumza mama yake Alice na kumfanya Tropina awaze kidogo tu.
**** ***** *****
Vikram akiwa amefungwa macho na baada ya kumaliza shughuli yao alizungumza.
"Tropina siku ya Leo umekuwa wa tofauti sana" alizungumza Vicky na kutabasamu.
"Nimekuwaje wa tofauti Vikram aliuliza Alice kwa sauti ya chini iliyomfanya Vikram ashtuke na kutoa kitambaa machoni.
" Alice aliita kwa mshtuko na kutoka kitandani.
Huku akichukua nguo yake na kuivaa .
"Wewe mbwaaa unafanya nini hapa ndani?? Aliuliza Vikram.
" Mbona unakuwa mkali ghafla na tulikuwa tukifurahishana dakika chache zilizopita eti" aliuliza Alice na kusimama akiwa uchi.
"Hivi wewe kichwa chako kinafanya kazi kweli eti Alice umefanya nini nakuuliza yko wapi Tropina?? Aliuliza Vikram.
Alice aliinama na kuchukua nguo ya kulalia ya Tropina kisha akaivaa.
" Tuongelee kwanza kuhusu Mimi na wewe na usiku huu mzuri wa kuvutia siyo habari ya Tropina alisema Alice akimsogelea na kumshika Mkono.
Vikram alimpiga kibao na kutafuta simu yake mahali ilipo aliikuta imezimwa aliiwasha na kumtazama kwa hasira Alice.
Aliichukua simu yake na ku play audio alivyokuwa akinung.unika Vikram na yeye wakati wakifanya mapenzi.
"Wewe umefanyaje leta hiyo simu hapa"
"Ukitaka audio hii isimfikie Huyo mwanamke wako Inabidi ufanye vile nitakavyokuamuru Mimi ukifanya tofauti na hivyo unaelewa kipi kitatokea.
Alisema Alice akimtizama Vikram.
" Unataka nini?? Aliuliza Vikram.
"Tufanye tena" alizungumza Alice na kumsogelea karibu Alice.
"We mbwaaa" aliita Vicky kwa hasira sana hadi Alice aliogopa na kurudi nyuma saa hiyo hiyo mlango uligongwa na Vanessa.
"Rickson kila kitu kipo salama?? Aliuliza Vanessa.
Vicky alimtizama Alice ambaye alifahamu kabisa kuwa Vikram amechukia kwa alichomwambia.
Alipiga hatua za mbele na kuufikia mlango kisha akaufungua mlango kidogo tu.
" Mama tuko salama ni kidogo tu tumepishana lakini tuko salama " alizungumza Vicky akitizama chini hapo hapo simu iliita ya Vanessa.
Akamtizama Vikram.
"Mbona Tropina sasa ananipigia" aliuliza Vanessa.
Eeeeeeeehhhhh aliitika Vikram kwa uwoga na kumpokonya simu Vanessa.
Kisha akatizama ndani na kuzungumza.
"Pinah mbona unampigia mama simu tutayamaliza acha kumsumbua mama alisema Vikram na kukata simu ya Tropina kisha akafunga mlango.
" Vaa nguo zako na uondoke hapa" alisema Vikram na kwenda kuvuta shuka lililokuwa kitandani na kuzima mishumaa yote baada ya Alice kuvua nguo aliyokuwa ameivaa ya Tropina Vikram aliichukua na kuichanganya sehemu moja pamoja na Yale mashuka kisha akayaweka kwenye Dustin.
Simu iliita tena alitizama Alice kwa muda kisha akaipokea.
"Halo"
"Vikram uko wapi?? Nimeogopa sana eti nilivyopiga simu yako ikiwa haipatikani.. Kwanini sasa haujaja mpaka masaa yamepita hivi. Nimekusubiria sana eti? alizungumza Tropina kwa furaha.
" nisubiri hapo hapo nakuja" baada ya kuzungumza hivyo alikata simu na kumtazama Alice.
"Yuko wapi Tropina?? Aliuliza.
" Nyumbani kwako alijibu Alice.
Vikram alianza kuondoka.
"Vikram nimekwambia uniwekee umakini Mimi na ukienda kinyume na Mimi nitamuelezea mwanamke wako jinsi gani nilivyolala na mwanaum wake tena katika kitanda chake" alizungumza Alice.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Uuchunge huo mdomo wako usije ukafupisha siku zako za kuishi duniani.....usihitaji kunifahamu kiundani Mimi ni nani kwamaana siku utakayonifahamu Ndiyo siku utakayomfahamu Israel" alizungumza Vikram na kumtazama Alice kwa macho makali sana kisha akatoka.
Alice alirusha mto uliokuwa karibu na yeye katika mlango aliowezalioweza kuipitia Vikram.
***** ****** ******
"Vikram" aliita Tropina na kumkimbilia baada ya kumuona.
Vikram aliitoa mikono ya Tropina na kumpa heshima mama yake Alice kisha akatangulia ndani.
"Anashida gani huyu?? Alijiuliza Tropina na kumfuata ndani.
Alimkuta Vikram akiwa amekaa kwenye kochi. Alikaa karibu na yeye lakini Vikram alimuacha na kwenda kitandani kisha akajilaza.
Tropina alisimama na kumfuata kisha akakaa chini.
" Vicky nimekosea nini mbona umekuwa hivyo ghafla?? Aliuliza Tropina na kumfanya Vikram ageukie upande mwingine.
"Sasa nimefanyaje mbona hauongei na Mimi niambie basi nimefanyaje ili nikutake radhi au umechukia kwa kuwa nilimpigia mama simu nikakuulizia.........basi samahani....kama ndo hilo lililokukera lakini nilitaka kujua tu kama uko nyumbani Ricky ili na Mimi nije nyumbani Ricky!! Aliita Tropina na kutaka kumgusa ila Vikram alisogea zaidi.
Tropina alijikuta ameishiwa na maneno na kujikuta akisimama.
" Mimi naenda nyumbani pale utakapotaka kuniambia nimekukosea nini basi utanipigia simu nikutake radhi " alizungumza Tropina na kuanza kupiga hatua za kivivu kwaajili ya kuondoka.
"Pinah" aliita Vikram na kukaa kitandani.
"Abee" aliitila Pinah kwa furaha na kugeuka nyuma.
"Unaweza ukalala hapa hapa mpaka kesho?? Aliuliza Vikram.
" Ndiyo " alijibu pinah na kurudi karibu kabisa na Vikram.
"Utalala kitandani......Mimi nitalala kwenye kochi" alizungumza na kutoka kitandani.
"Sawa" alijibu Tropina kinyonge na kuelekea kitandani kisha akalala.
Vikram akiwa kwenye kochi aliweza kumuona Pinah akifuta machozi yake.
"Pinah......sihitaji ushike jasho la mwanamke mwingine katika mwili wangu.......mpaka kesho nitakuelezea kila kitu nisamehe kwa Leo. Alizungumza Vikram akimtizama Tropina kitandani.
Wakati huo Alice alikuwa njee na aliweza kusikiliza vyotr vilivyoweza kuzungumzwa.
" Najua kesho utataka kumwambia ila nakuhakikishia kabla hujamwambia nitaanza kumwambia Mimi"
Alice alicheka huku akiwa ameshikilia mfuko wenye nguo ndani.
Kulikucha asubuhi na Tropina alikuwa wa mwisho kuamka alitoka ndani kwa kupiga hatua za kivivu na kuelekea njee. Alitizama njee kote lakini hakukuwa na mtu yoyote tofauti na yeye.
Ghafla aliweza kumuona Alice akiwa ametoka katika nyumba yao na kujinyosha huku akiwa na gauni la kulalia.
Tropina alimtizama tu bila kuweka neno lolote lile na Alice alisogea zaidi na pale alipo Tropina.
"Mambo"
'Pouwa"
"Mume wetu yuko wapi?? Aliuliza Alice akijinyoosha.
Tropina alimtizama bila kumjibu kitu chochote.
" Samahani namaanisha Vikram yuko wapi?? Alirudia swali lile Alice.
"We anakuhusu nini?? Aliuliza Tropina.
" hata hivyo asubuhi na mchana huwa hanihusu ila usiku ananihusu zaidi"
"Unaongea nini wewe?? Aliuliza Tropina na kumsogelea kwa ukaribu zaidi.
" Hahahaha nakutania tu.....Jana mama alinambia ulimsubiria sana Vikram na alikuja usiku zaidi hivi hauna mashaka kwanini alichelewa kurudi!? Aliuliza Alice.
"Hayo ni maswala yangu na Tropina wewe hayakuhusu" alizungumza Vicky aliyekuwa tayari kafika eneo lile.
"Hey sweet" aliita Vikram akiwa amejawa na Tabasamu mwanana usoni kwake. Alimsogelea Tropina na kumpiga busu la mdomo kwa sekunde kumi....kisha akamtazama na kumbusu tena.
Baada ya hapo alimtizama Alice na kumcheka Alice ambaye alikuwa amejawa na hasira.
"Pinah..............Si unajua nikikukosa ndani ya masaa machache tu kitandani naumwa......tunaweza tukaenda sasa" alisema na kumshika kiuno Tropina kiuno kisha kuelekea naye ndani.
"Kwahiyo baada ya kwenda kusafisha ndo umekuja kumzuga boya wako" alisema Alice akijidai anaongea na simu aliyokuwa ameiweka masikioni.
"Kuwa makini sana maana naamini Huyo mjinga hawezi kuelewa mchezo wetu na tutaendelea kuucheza kila siku" Alice aliondoka zake.
"Imekuwaje mbona umesimama?? Aliuliza Tropina.
Wakati huo Vikram aligeuka nyuma na kumtizama Alice aliyekuwa amevalia gauni la kulalia tu.
" Kuna shida gani?? Aliuliza Tropina tena kwa Mara nyingine.
Vickam aliutoa Mkono wake kiunoni mwa Tropina na kuelekea ndani.
Hapo hapo honi ya gari ilisikika na alishuka Vanessa.
"Kama mlikuwa mnaondoka nyumbani na kuja huku kwanini msinijulishe?? Aliuliza Vanessa.
"Kivipi?? Aliuliza Tropina aliyekuwa hafahamu kitu.
" Jana niliwasikia mlipokuwa mkigombana,
"Mama" aliita Vicky na kutoka njee ya chumba chake.
"Nimeamka asubuhi nyumbani nikiwatafuta na nimewakosa ndomaana nikaona nije huku mnaendeleaje? Aliuliza Vanessa.
"Jana hatukuwa na ugomvi wowote ule bali nilikuwa sijisikii vizuri Ndiyo nikamwambia Tropina abaki hapa hapa alafu Leo tutakuja nyumbani" alizungumza Vikram na kumfanya Tropina asielewe chochote kile.
"Ni sawa kama mko salama" alisema Vanessa na kutoa miwani yake machoni.
"Me nawaacha naelekea ofisini kwanza kwasababu Kuna matatizo kidogo yametokea nasikia wawekezaji wanataka kutoa hisa zao katika kampuni ya madini kutokana na kesi inayokukabili hivyo nahitaji kwenda kuzungumza nao. Alisema Vanessa.
" Kwani share zao zote zipo asilimia ngapi?? Aliuliza Tropina.
"Kama sikosei ni 37? nyingine zote zilizobaki ni share yangu yakwako pamoja na Larry. Alizungumza Vanessa.
"Jamani ngoja Mimi niwahi"
"Tutaenda wote" alisema Tropina na kumfuata mama yake.
"Pinah....nahitaji tuzungumze alisema Vicky na kumshika Mkono.
" Hapana siyo kwasasa hivi alisema Tropina na kuutoa Mkono wa Vikram.
"Pinah....ni kitu cha muhimu sana nahitaji kukwambia Jana usiku........."
"Vikram nitarudi Alisema Pinah na kuondoka na mama yake.
Baada ya kuondoka Alice alitoka njee na kupiga makofi.
"Unafikiri kumwambia kwamba Jana ulilala na mwanamke mwingine chumbani kwake" alizungumza Alice na kumsogelea kwa karibu zaidi.
"Usijaribu kufanya hivyo kwasababu utajiharibia mwenyewe na utajuta kufanya hivyo" alisem Alice.
"Nitamwambia nakuapia kwa hilo na Tropina wangu ni muelewa sana lazima atanielewa alafu wewe sasa utajuta kitakacho kukuta" alizungumza Vikram na kutabasamu.
Alice aliiwasha simu yake kisha akamtumia kitu Vikram na kumwambia.
"Tuone kama utaweza kumwambia ya kuwa Mimi nilikulazimisha kufanya nawe mapenzi...wakati inaonyesha ya kuwa wewe Ndiye uliyeweza kunipatia gauni la Tropina la kulalia.
" lakini sikukupa nilikunyang.anya na kulitupa kwenye Dustin na tayari nimeshalichoma moto" alizungumza Vikram baada ya kuona picha aliyotumiwa na Alice.
"Lakini picha haina uwezo wa kuongea hilo na hapo inaonyesha ya kuwa wewe ndiye uliyenipa gauni lake....na pia tayari ameshaona nimelivaa" alisema Alice na kucheka.
Vicky alipotizama kwenye picha na gauni alilolivaa Alice yote yalikuwa sare.
"Kwanini umefanya hivyo wewe?? Aliuliza Vicky na kutaka kwenda kumpiga kibao.
"Ukitaka nisikuharibie ndoa yako inabidi utendee yale niyatakayo na ukienda kinyume na nitakavyokuamuru basi utaona kipi kitafuata.......na kitu kingine tegemewa kuitwa baba kwani Jana ilikuwa siku yangu ya hatari"
Vikram alishika kichwa chake na kuvuruga nywele zake. Alipiga piga mateke makopo yaliyokuwa na mauwa kwa hasira sana.
****** ***** *****
Katika kikao cha board member wa kampuni ya madini iliyoenda kwa jina la
" Precious Mineral Company " alifika Tropina pamoja na mama yake walioweza kuhudhuria katika kikao hicho ni watu ambao walikuwa na share katika kampuni hiyo baada tu ya kumuona Tropina wote walikuwa kimya.
"Idadi yenu?? Aliuliza Tropina baada ya kufika na kukaa katika kiti cha mbele.
Secretary wa kampuni hiyo alitaja idadi ya watu wale.
" 22 madam Tropina"
"Idadi ya hisa walizonazo katika hii kampuni?? Aliuliza tena Tropina.
" 37%" alijibu secretary.
"Nikigawanya kwa idadi yenu moja moja inabaki 10% ambayo wachache wenu mtakuwa na % 3, 2 na wengi mkiwa na % 1.......Sasa sijaona cha kubabaisha hapa ni nini ikiwa sisi tuna hisa za 64% kama mnahitaji kutoa hisa zenu mnaweza mkaondoa na hakuna fidia yoyote ile itakayoweza kutolewa juu yenu kwasababu mmetaka wenyewe.. ............. Secretary" aliita Tropina.
"Ndiyo madam Tropina"
"Katowe pesa katika account yangu nafikiri hisa zao haziwezi kuzidi million 70 na kila mmoja katika hisa yake moja utamkata million 3 kama kufidia usumbufu katika hii kampuni" alimaliza kuongea na kuanza kuondoka.
"basi mimi sitatoa tena hisa zangu Nina asilimia 3 sitatoa alizungumza mmoja kati ya wale walioweza kuhudhuria katika kikao kile.
" Nina %1 sitaitoa tena "
"Hata mimi"
"Na Mimi"
"Na Mimi pia"
Wote waliweza kukubali kutoweza kutoa hisa zao katika kampuni hiyo na hatimaye Tropina aliondoka katika chumba kile cha mkutano huku Vanessa akimfuata njee pamoja na secretary.
Mmoja wao alisimama na kutupa karatasi zilizokuwa mbele yake.
"Mshenzi huyu kipofu mdogo hivyo anatupelekesha sisi jinsi atakavyo"
"Lakini hatuna cha kufanya kwasababu share moja ni kama million 5 sasa akikata tena million3 tunabaki na nini?? Aliuliza mmoja wao na kusimama kisha akaondoka katika chumba kile wengine nao waliweza kumfuata nyuma.
" Huyu binti nitamuonyesha siwezi kumsamehe kwahili" alisema mzee yule ambaye makamo yake kidogo yalienda.
**** ******** *****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Vickam hajaja nyumbani?? Aliuliza Tropina baada ya kufika nyumbani.
" Yupo chumbani" alisema Danielle baada ya kuulizwa swali hilo.
Aliingia chumbani na kumkuta Vicky akiwa amejipumzisha kwenye kochi.
"Baby" aliita Tropina na kwenda kumbusu Vicky
"Eee nmbie mambo yameendaje?
" Vizuri tu nimeyamaliza" alisema Tropina
"Na Mbona huna furaha tena kama nilivyokuacha?? Aliuliza Tropina.
" Hamna niko sawa " alijibu Vicky na kumvuta Tropina kwenye kochi kisha akamlaza juu ya mwili wake na kumkumbatia.
"Unauhakika lakini ya kuwa kila kitu kipo salama?? Aliuliza Tropina.
" Huniamini mumeo kwani?? Aliuliza Vikram.
"Nakuamini sana ila uumebadilika kwanzia usiku wa Jana ulivyonitumia msg niende kwako halafu ukufika ulirudi usiku na hukutaka nikuguse kabisa.......alafu mama alisema Jana usiku" alitaka kuzungumza zaidi lakini maneno yalimuisha baada ya kuona kitu pembeni ya kitanda chake.
Alimka pale na kuinama katika kitanda aliweza kutoa Mkono wake na Mkono huo ulitoka akiwa na sidiria.
Vikram alisimama kutoka kwenye kochi na kumtazama Tropina aliyerudisha macho makali katika sura yake.
***** ***** *****
Katika upande mwingine walionekana watu tisa wakiwa wamekaa katika chumba kimoja huku wakijadiliana swala la Tropina kuiendesha kampuni kwa kuforce na kutowaogopa kabisa.
"Baba yake hakuwa mjinga kama alivyo yeye...mshenzi sana huyo binti" alisema mzee mmoja.
"Natamani ata angekufa kwenye ile ajali angebaki tu baba yake" alizungumza mwingine
"Mmmhhhhhh huyo hata angekuwa marehemu ni balaa angeweza kututokea mpaka kwenye ndoto" alisema mwingine na kufanya wacheke.
"Embu acheni ujinga na tuwaze tutafanya nini ili kumuondoa huyu mtoto katika kampuni hiyo hata kama ni ya baba yake na wao Ndiyo wanamiliki hisa nyingi kutuzidi" aliendelea kuzungumza mzee yule ambaye alionekana kutamani kuwa kiongozi wa kampuni ile jina lake walimuita
Mzee Mpalila.
"Mmmmhhhhh sidhani kama itawezekana kweli yule ni kipofu tu lakini anatupelela mbio hivyo....akipata macho mawili yule ni hatari" alizungumza mzee mwingine.
"Jamani tena akigundua ya kuwa tumemuweka kikao nakwambia hata hizo hisa tutanyang.anywa zote. Alisema mmoja wao.
" Alafu hiyo kesi kweli kauwa?? Aliuliza mmoja.
"Hana hata dalili za kuuwa yule"
Yaliendelea mabishano ya hapa na pale na mwishowe maongezi yao yaliweza kuingiliwa na sauti ya kike.
"Naweza nikawaisaidia na mkamuweka kiongozi mpya katika kampuni hiyo ya Precious mineral limited.
Wote waligeuka na kumtizama Alice aliyewaachia Tabasamu mwanana katika uso wake.
" We ni nani??? Aliuliza mzee Mpalila.
Unafikiri kipi kitatokea baada ya Tropina kupata sidiria katika chumba chake.
"We ni nani?? Aliuliza Mr Mpalila.
" Naitwa Alice Mimi ni mke wa Vikram ambaye Tropina amemchukua kutoka kwangu kutokana na pesa alizonazo mume wangu anapata shida sana juu yake.
"Tutaaminije hilo??
Alice alifungua kipochi chake na kutoa simu yake kisha akaigusa mahali na kumpatia mzee mmoja ambaye aliitizama akamtizama na yeye kisha akampatia mwenzake, wa mwisho kutazama hiyo picha alikuwa Mr mpalila.
" huyu kijana namuonaga na yule kipofu ndo mume wako?? Aliuliza.
"Ndiyo ila Vikram hawezi kufanya chochote kwani Tropina ameapa kumuumiza mtoto niliyeweza kumbeba tumboni kama atamshtaki Tafadhali tusaidiane kwa pamoja kumuondoa kabisa katika njee ya dunia hii na tumpeleke gerezani" alizungumza Alice
"Sasa Unataka sisi tukusaidiaje?? Aliuliza Mr mpalila
Alice alicheka kichinichini baada ya kuona ya kuwa ameeleweka.
**** **** *****
"Hii ya nani?? Aliuliza Tropina.
" ammmhhhh........Pinah unajua..... hiyo ni ya..............."
Alizungumza kwa kigugumizi sana Vikram.
"Yanani?? Aliuliza pinah akimsogelea kwa ukaribu zaidi Vikram.
" aaaaaaaaaammnnnmnhhhhhh .......hiyo ni ya........ Actually............nataka kukwambia kwamba....... "
"Kitu kidogo tu hivyo unashindwa kuongea na unaona aibu kuniambia utafikiri unaivaa wewe...... Ila sijui kama itanienea inaonekana kubwa kidogo ila haina shida nitaibana kwa vichupio vya nyuma....santeh Vicky ila kipindi kingine usiwe unaninunulia nguo za ndani" Alisema Tropina akijaribu sidiria ile.
"Eeeeeehhhhhhhheeee" Vicky alishngaa baada ya kuona Tropina anasema amemnunulia.
"Nashukuru alafu nimebakiwa siku Tatu kabla ya kwenda mahakamani kwahiyo Kuna vitu kidogo nahitaji kuvikusanya eneo la tukio kabla ya kwenda mahakamani.
Hapo hapo simu ya Tropina iliita.
" yes hallo..... Sawa.......nakuja" alikata simu kisha akaichukua sidiria ile na kuiweka kabatini mwake.
Vicky narudi alisema Tropina na kuondoka.
"Pinah"
"Abee"
Vicky alifikiria kidogo kisha akatabasamu tu na kumwambia.
"Kuwa makini alafu uwahi kurudi nyumbani na kama utahitaji msaada basi usisite kuniambia"
"Sawa.....Love u" alisema Tropina na kuondoka bila kusubiria jibu lolote lile kutoka kwa Vikram.
Vikram alielekea mpaka kwenye kabati la Tropina na kulifungua aliitoa ile sidiria na kuitupa chini kisha kuikanyaga kanyaga na kwenda kuitupa kwenye dustbini.
"Huyu mshenzi Alice huyu??? Aliongea kwa jazba na kutoka njee ya chumba kile.
***** **** ****
" madam hili ndilo eneo la tukio ambalo Winnie aliweza kuuwawa hapa" alikuwa Danielle akitoa taarifa.
"Hakuna kitu chochote ulichobahatika kukipata?? Aliuliza Tropina.
" hakuna" alijibu Danielle na kusimama aligeuka nyuma na kutoa kitu mfukoni mwake alikuwa ameweka cheni iliyoweza kuoneka ikiwa na damu.
Alitoka njee na kumuacha Tropina ndani.
***** *** *****
"Haloo Adrian game linaanza sasa fanya kama nilivyoweza kukuelekeza" alizungumza Alice na kukata simu.
"Sawa ngoja tuone hapa atatokaje tena Tropina" alisema Adrian na kufunga kamba zake za viatu kisha akatoka njee ya chumba chake.
****** ******
Tropina akiwa anarudi kutoka katika eneo lile huku akimtizama Danielle aliyeeonekana na yeye kumtazama kupitia side mirrow iliyoko mbele ya gari.
"Danielle" aliita pinah.
"Ndyo madam pinah"
"Kwahiyo hujaona chochote kabisa ambacho ni kama ushahidi katika eneo lile?? Aliuliza Tropina.
" hapana "
"Lakini inaonekana unamashaka makubwa sana means Kuna chochote unachokijua kama hujaona chochote. Alizungumza Tropina na kumtizama Danielle.
" actually Mimi naona siyo kipofu na kunamtu ameniframe katika hiyo kesi sijajua ni nani na Kuna kitu gani anahitaji zaidi kutoka kwangu...... Danielle naweza nikawa naonekana mkorofi sana lakini siwezi kuwa naonekana muuwaji alizungumza Tropina na kutabasamu.
"Sijawahi kumuita mama yngu mama namuitaga Vanessa tu tokea kifo ch baba yngu kwani nilikuwa nikijisikia vibaya sana kumuona anatembea na mwanaum ambaye aliniulia baba yngu...... Bila kujali ya kuwa mama yngu anajisikiaje pale anapolala na mwanaum ambaye ameweza kumuulia mumewe na kufanya watoto wake wawe yatima na yeye kuwa mjane...........muda mwingi huwa nakaaga na kumtizama mama yangu naamini ya kuwa hakuna aliyewahi kuteseka katika dunia hii kama mama yangu sitaki kuwa mzigo tena juu yake kwa hii kesi inayonikabili mama anapata shida katika makampuni yake na watu wanataka kutoa hisa zao katika kampuni sasa mama yangu anapata shida sana kupambana kwaajili yangu kwaajili ya kampuni alizoacha marehemu baba yngu kupambana na mwanaum aliyeweza kumuulia mume wake.......mpaka namuonea huruma..
.lakini kwasasa namshukuru Mungu kwa kuwa ametokea Vikram katika maisha yetu na anaweza kumsaidia mama kwa kiasi kikubwa sana.....nampenda sana Vikram kwasababu ni mwanaum wa pekee sana"
Baada ya kuzungumza hayo yote Tropina aliyafuta machozi yak na kuzungumza.
"Nimewezaje kukwambia siri zangu zote hizo na kulia mbele yako"
"Unajisikia vizuri?? aliuliza Danielle
" Ndiyo" alijibu Tropina akimalizia kuyafuta machozi yake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Danielle alisimamisha gari.
'Mbona umesimamisha gari?? Aliuliza Tropina.
"Madam...." Aliita Danielle na kuingiza Mkono wake mfukoni kwaajili ya kutoa ile cheni na kumpatia Tropina ila kabla hajatoa Pinah aliondoka zake ndani ya gari.
Aliirudishia cheni yake mfukoni kisha na yeye akatoka ndani ya gari. Alitizama alipotizama Tropina na alimuona Vikram akiwa amekaa huku akiwa kama vile anamsubiria mtu.
Pinah alitaka kwenda ila aliamua kumpigia simu kabla ya kwenda.
"Vikram niko...................."
"Tropina nipo kwenye kikao cha muhimu ntakupigia nikitoka" Vikram alikata simu bila kujua ya kuwa Tropina alikuwa nyuma yake..
Hapo hapo alikuja Alice na kumbusu Vicky mdomoni kisha akaketi kwenye kito cha pembeni.
Vikram alimshika mkono Alice kwa nguvu na kuuweka mezani kisha akamsogelea kwa ukaribu zaidi na kumwambia
"Iwe Mara ya mwanzo na mwisho kunisogelea tena kwa ukaribu zaidi na kunibusu"
Kwa alipokuwa amekaa Tropina aliweza kuona ya kuwa Vikram alikuwa akimbusu Alice kwani Alice alimshika Vicky sehemu ya kichwa pindi alipokuwa amemsogelea.
Tropina aliingia ndani ya gari na Danielle ndiye aliyebaki akishngaa huku akijiuliza yule amuonaye ni Veronica au anamfananisha na watu wengine.
Aliingia ndani ya gari akiwa anajiuliza alimtizama Tropina nyuma na kwa Mara ya kwanza kabisa aliweza kumuona akiwa anamtizama mahali bila kupepesa macho.
Alijifunga mkanda na kumtazama Tropina kama amejifunga mkanda alipomtizama aligundua kuwa hajajifunga.
"Madam naendesha gari Tafadhali funga mkanda" alisema Danielle lakini Tropina hakuongea chochote kile.
Alijisogeza na kumsaidia kufunga mkanda kisha akawasha gari na kuliondoa eneo lile.
Alice alicheka baada ya kuona Tropina ameondoka.
"Mimi nakusemesha wewe unajifanya uko busy na mambo mengine" alizungumza Vikram na kusimama.
"Nafikiri umeweza kunielewa nilichokwambia" alizungumza Vikram na kwenda kupanda gari lake huku akimpigia Tropina.
"Unaenda eeeeee sasa utakutana nacho huko" alizungumza Alice na kucheka huku akiwasha simu yake na kutuma msg.
Vikram aliweza kufika nyumbani na kutoa begi ambalo amekuja nalo aliweza kutoa nguo ya ndani nyingine aliyoweza kununua baada ya Tropina kudhania nguo ya Alice ni Vikram aliyeweza kumletea.
Aliitoa nguo design ile ile kisha akatoa label iliyokuwa katika sidiria hiyo.
Aliiweka sehemu tofauti na ile aliyoweza kuiweka Tropina Mara ya kwanza.
"Yuko wapi Pinah?? Alijiuliza na kuchukua simu yake kisha kumpigia.
Simu iliita hadi ikakata bila kupokelewa
" Kuna shida gani mbona hapokei simu? Alijiuliza huku akipiga tena simu.
Alikumbuka kuwa Kuna kitu alitaka kuambiwa na Tropina lakini alimkatisha baada ya kumuona Alice alikumbuka pia ya kuwa wakati anaondoka alisema anaelekea sehemu ambayo angeweza kupata ushahidi.
Alipiga simu tena kwa Dr Kim.
"Kim"
"Yes boss"
"Unaweza kuniambia mahali alipo Pinah kwasasa? Aliuliza Vikram
"Ndiyo ngoja nikutumie location ya mahali alipo" Alisema Kim na kukata simu.
Vikram aliiwasha simu yake baada ya msg kuingia.
"Anafanyaje huko ufukweni?? Alijiuliza Vicky na kutoka njee ya chumba.
**** ***** *****
" umefanya vile nilivyoweza kukuagiza?? Aliuliza Adrian.
"Ndiyo nimefanya kama ulivyoweza kuniagiza" alizungumza Daud.
"Vizuri"
Adrian alishika simu yake na kumpigia Alice.
"Kazi uliyonipa nimemaliza sasa ni muda wa kufanya kazi yako" alizungumza Adrian na kukata simu.
Alice alitabasamu kisha akasema mchezo halisi utaanza kesho sasa kwamaana kesho kutwa utaenda mahakamani.
"Halo Mr mpalila, Ndiyo ni Alice anaongea Tafadhali naomba ufanye kama vile tulivyoweza kukubaliana....... Ndiyo nimekuelewa sawa ahsante"
**** ***** *****
Vanessa akiwa barabarani gari lake liliweza kugongwa kwa nyuma baada ya kufika eneo la taa za barabarani alishika kichwa chake na kuzungumza.
"Nani huyo ambaye haoni saa12 hii aliuliza Vanessa na mtumishi wake alitoka njee ya gari.
Baada ya Vanessa kuona mtumishi wake amechukua muda mrefu na yeye aliamua kutoka njee.
Hapo ndipo alipokutana na Mr mpalila.
" unashida gani wewe mzee mpaka ugonge gari langu?? Aliuliza Vanessa.
"Siyo mimi niliyekuwa nikiendesha" alijibu Mr mpalila na kutabasamu.
Katika upande wa dereva kilishuka kiatu cha kike chekundu na hatimaye aliweza kushuka kabisa.
"Hey Vanessa!! Alisema Alice aliyeteremka kwenye gari la Mr mpalila.
" Huyo anafanya nini huko??
"Ahaaa huyo ni partner wangu katika biashara kwasasa na anaweza kunisaidia kwa kiasi kikubwa na kuniwezesha mimi nipate kile nitakacho"
"Nikwambie kitu kile unachokohitaji katika maisha ya binti yangu huwezi kukipata labda nikiwa marehemu Mimi ndo utaweza kumchukua mume wa binti yangu"
Alice alicheka baada ya kusikia maneno hayo kwa Vanessa. Alimsogelea kwa ukaribu zaidi kisha akamkumbushia maneno ambayo aliuliza siku ile alipokuwa chumbani kwa Tropina.
Vanessa alimshangaa na kujikuta anamuuliza.
"Wewe ulikuwa wapi??
"Inamaana hata huitambui sauti ya binti yko alafu unajiita mama" aliuliza Alice na kutabasamu.
"Mr mpalila embu tuendelee na safari yetu.........ohhhhhhoooo nimesahau aliingia ndani ya gari na kutoa kipochi chake kisha akatoa pesa na kumtupia Vanessa chini kisha akamwambia
" itakusaidia kutengeneza hilo gari sehemu iliyoweza kuvunjika na chenchi itakayobaki utamnunulia matunda Vikram ili azidi kuwa mzuri kitandani "
"Huyu malaya anamwambia nani hivyo?? Aliuliza Vanessa na kumfuata kisha akampiga kibao na kuanza kumpiga kwa kumnyongorota nywele hapo hapo waandishi wa habari waliweza kutokea na kuanza kupiga picha tukio lile. Calvini alijitahidi kuzuia na Jimmy naye aliweza kutokea pale kisha akamchukua Vanessa akampandisha ndani ya gari lake na kumuondoa eneo lile.
"Mpigie huyo bossi wako mpigie na umwambie akutane na Mimi sasa hivi" alizungumza Vanessa kwa ukali sana na Jimmy aliichukua simu yake kisha kumpigia Rickson.
****** ****** ******
"Ni nini hichi kimetokea?? Alijiuliza Larry baada ya kuingia mtandaoni na kukuta kashfa nyingi zikiwa zinamuongelea mama yake.
" Inavyoonekan mama yako bondia sana mpaka anapigana na visichana vidogo" aliuliza mwanafunzi mwenzake Larry aliyekuwa mpinzani wa Larry mkubwa sana jina lake walimuuita Collin yeye alikuwa mtoto wa tajiri maarufu tu aliyekuwa akipambana na Vanessa katika upande wa biashara za magari.
Larry alimtizama bila kusema neno lolote lile kisha akatoka njee na kumuacha Collins ndani ya darasa.
**** ***** *****
"Aaaaahhhh imekuwaje tena simu imezima chaji na Pinah hayuko tena huku ufukweni usiku sasa umeingia atakuwa wapi?? Aliendelea kujiuliza Vikram.
***** **** ****
" madam nikupeleke wapi?? Aliuliza Danielle.
"Nipeleke katika hotel yoyote ile nahitaji kupumzika huko sihitaji kwend nyumbani Leo pia utakuja kunichukua asubuhi na mapema alafu usimpe taarifa mtu yoyote yule mahali ulipoweza kuniacha"
Alijibu Tropina na kujilaza zake.
"Nimekuelewa madam.
***** **** *****
" Kipi kinaendelea huko katika familia ya Tropina mbona kama kuna matukio yasiyoweza kueleweka aliuliza Mr Harlan alikimuuliza mtumishi wake.
"Sijapata taarifa zozote kutoka kwa Veronica labda nimpigie" alisema mtumishi na kuchukua simu.
"Hapana usimpigie embu mpigie kijana wangu Harman" alitoa kauli hiyo Harlan na simu iliweza kupigwa.
***** ****** *****
"Nakuuliza nini hiki unakifanya Alice......sijakulelea katika misingi hiyo mimi.......ulivyo sasa si kama ulivyokuwa mwanzo na si kama nilivyoweza kukupokea miaka mitatu iliyoweza kupita......hata kama Mimi siyo mama yako mzazi unawezaje kufanya hivyo eee" alizungumza mama yake Alice akimgombeza Alice.
"Lakini mama"
"Hakuna cha lakini Unafikiri ya kuwa sijui ulilala na Vicky..... Hivi unawezaje kulala na mwanaum ambaye ni wamtu tena katika chumba cha mke wake halali wa ndoa??? Eeeeeehhhhhhhheeee alafu unaona haitoshi Leo tena unamshtaki mama wa mwanamke uliyeweza kutumia chumba chake na mume wake eti kwa kosa la kukuvamia na kukupiga na ninauhakika huo ugomvi uliutaka wewe Ndiyo maana waandishi wa habari walikuwa eneo lile"
"Unajua wewe mwanamke unakiherehere sana na ndicho kitakachokufanya upoteze maisha kama binti yako"
"Nini??? Aliuliza mwanamke ambaye tuliweza kumfahamu mwanzo kama mama yake na Alice.
" Hivi Unafikiri binti yako alikufa kwa ajali.....hahahaha hapana siyo ajali ile Mimi Ndiyo niliyoweza kukata break za gari lake kisha nikamuachia aendee kituo cha polisi........ Kwasababu alifahamu Siri yangu ambayo ilikuwa ni nzito sana na nisingeipenda mtu yoyote aifahamu lakini yeye na kiherehere chake aliweza kuifahamu"
"Hivi umewezaje.....
Umewezaje kumuuwa mtoto Wang ambaye ni wa pekee na Ndiyo huyo huyo niliyekuwa naye katika maisha yangu yote unajua niliteseka kiasi gani kumpata huyo binti yangu wewe aliuliza huku akimsukuma sukuma.
" sitaacha uharibu tena maisha ya mtu mwingine nitaenda kukureport polisi" alisema mama yake Alice na kusimama kisha akaanza kuelekea mlangoni.
"Hicho ndo kitu ambacho hukiwezi" alisema Alice na alipogeuka tu nyuma Alice alimpiga na chungu kidogo cha kichwa kilichopo mezani na kumfanya azimie hapo hapo aliisikia sauti ya mtu ikisema.
"Mama Alice ndyo ninarudi nyumbani mume wako alizungumza baba yake Alice na kuufungua mlango.
" Kipi kimetokea mbona kimya sana" alijiuliza na kumkuta mke wake akiwa chini na damu zikimtoka katika paji lake la uso.
"Kimetokea nini?? Aliuliza baba yake Alice na kujitahidi kumuinua mke wake aliyekuwa akitizama nyuma yake.
"Unatizama nini aliuliza na kugeuka nyuma na hapo ndipo macho yake yalipoweza kugongana na Alice.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Alice mkubwa kipi kimemtokea mama yako?? Aliuliza.
"Baba Alice umekuja wakati mbaya alizungumza hivyo na kumpiga na kibobo kingine cha uwa alichokuwa amekiweka nyuma yake.
Ghafla alidondoka chini na kuanza kuhangaika hangaika.
" nini shida alijiuliza Alice na kuanza kurudi nyuma.
Mapovu yaliweza kumtoka mdomoni na hatimaye aliacha kuweweseka.
"Ni nini hichi kimetokea alijiuliza Alice akiwa haamini kipi kimetokea.
Wakati huo wote mama yule aliweza kuyashuhudia yote na hakuwa na nguvu za kupiga kelele wala kumsogelea mumewe.
Baada ya muda alionekana Alice akiwa ndani ya kimsitu kidogo na akiwa anaburuta kitu alichokihifadhi katika saflet na kukitupia ndani ya shimo aliloweza kulichimba. Alifukia na kuhakikisha ya kuwa amesambaza pale na hakuna mtu yoyote yule atakayeweza kuona utofauti wa eneo hilo na maeneo mengine.
" Tropina hata hili ni kosa lako ni wewe uliyeweza kumuuwa baba yake na Alice siyo Mimi wewe ndo chanzo" alizungumza huku akiwaa amekaa juu ya kaburi lile baada ya kumaliza kazi yake ile.
Aliweza kurudi nyumbani na kuanza kusafisha zile damu ila wakati akifanya hivyo Kuna mtu dirishani alimuona akifanya tukio hilo la kusafisha damu zile.
"Inawezekanaje Veronica akafanya jambo la namna hii?? Alijiuliza Danielle aliyeweza kushuhudia tukio la Veronica kumuuwa baba Alice.
Aliushika ile cheni na alikumbuka ya kuwa cheni ile yeye aliweza kuinunua na kumpatia Veronica na kilichoweza kumleta hapo ni kumuuliza imekuwaje cheni aliyoweza kumpatia yeye iwe katika eneo la tukio aliloweza kuuwawa Winnie.
Alirudi nyumbani akiwa amenyong.onyea sana.
"unamatatizo gani wewe mbona umepowa hivyo?? Aliuliza Calvin huku akimfuata Danielle nyuma.
Danielle aliingia mpaka ndani ya chumba chake na kufunga mlango.
" kwanini ananifungia mlango ? Alijiuliza Calvin na kuanza kumgongea hapo hapo simu yake iliita na alikuwa ni Mr Harlan.
"Yes boss"
***** ****** *****
Vanessa aliweza kutolewa katika kituo cha polisi baada ya mwanasheria Josephat kufika hapo.
Alipotoka njee alikutana na Larry.
"We mbona uko huku?? Aliuliza Vanessa na Larry alimtizama bila kusema neno lolote lile alitoka njee na hapo alipishana na George ambaye alimgonga na kumfanya adondoshe makaratasi kisha kumpita bila kusema neno lolote lile.
Vanessa na yeye alimtaka radhi kwa ishara ya kichwa kisha akamtaka Jimmy mtumishi wake ayaokote.
Vikram alirudi nyumbani baada ya kumkosa Tropina na kuamini ya kuwa atakuwa nyumbani pia baada ya kupata taarifa za Vanessa.
" Vanessa kaja?? Alimuuliza Diana.
"Hapana"
"Tropina na yeye???
" hapana "
"Ameenda wapi mbona hapokei simu yangu alijiuliza kisha akatoa simu yake mfukoni.
" aaaaahhhh nilisahau ya kuwa imezima chaji" alizungumza na kumpa Diana simu yake akamsaidie kuchajisha.
Aliingia Vanessa na baada ya kumuona Vikram alimfuata na kumpiga kofi kwa hasira.
"Unawezaje?? Unawezaje kulala na mwanamke mwingine ndani ya chumba cha Tropina???
Kila mtu aliyeweza kuyasikia maneno Yale aliweza kushangaa.
" Nini???
"Nini???
"Vanessa unasema??? Aliuliza Larry kwa mshangao.
" Diana nenda na ukatoe takataka zote za huyu ndani msaliti ndani ya chumba cha mtoto wangu na utupe njee njeee kabisa ya nyumba hii". Alizungumza Vanessa.
"Lakini mama......"
"Usiniguse nilikuamini sana lakini siyo kwa kitendo cha kumleta mwanamke mwingine na kulala naye katika chumba cha binti yngu Tafadhali ondoka na talaka nitaiandaa" alisema Vanessa na kupanda zake katika chumba chake.
Larry alimsogelea kwa ukaribu zaidi kisha akamuuliza kwa sauti ya utaratibu.
"Bwashe, mama anachokizungumza ni ukweli, kamba umeleta mwanamke mwingine katika chumba cha Dada yangu na kulala naye???
" Larry "
"Tafadhali jibu swali langu" alizungumza Larry kwa hasira na machozi yakimtoka.
"Ndyo lakini............"
"Katoe viti vyake njee Diana fanya haraka" alitoa sauti kali na kumfanya Diana apande haraka haraka na kwenda kutoa vitu vyake njee.
Larry alipanda na kuelekea katika chumba chake.
Obama ndiye aliyebaki akimtizama Vikram.
"Obama naamini ya kuwa huamini hilo"
"Ndyo nilikuwa siamini lakini baada ya wewe kukubali nimeamini sasa......nafikiri mkataba wangu na wewe umeisha narudi kwetu" Obama alitoa heshima ya mwisho kumpatia Vikram na kuondoka zake.
"Alice nitakusamehe kwa yote lakini siyo kwahili" alizungumza Vicky na hapo hapo simu ya mezani iliita alienda kuipokea.
"Hakuna hata mtu mmoja anayekuamini sasa rudi tu kwangu na Mimi nitakupokea" alizungumza Alice aliyekuwa akimuona Vikram kupitia laptop yake ndogo.
"Alice naapa kwa jina la Mungu nitakuuuwa"
"Aaaaahhhh umenitisha sana Rickson.... Baada ya kutamka jina hilo alianza kucheka na kumfanya Vikram ashangae amejuaje ya kuwa yeye ni Rickson.
Ni baada ya Alice kupiga simu na kucheka huku akitaja jina la Rickson.
"Unashangaa nimekujuaje ya kuwa wewe ni Rickson sindiyo....sasa fanya upuuzi wowote na uone kitakachoweza kutokea hiyo familia ambayo unajifanya unaipenda sana.
Alikata simu yake.
" Huyu mshenzi anazungumza nini.... Alice...Alice... Alice " aliita Vikram lakini simu tayari ilishakatika.
"Lazima uje kwangu huna pa kwenda Rickson nimekukamatia hapo" alicheka baada ya kumuona Rickson anatoka katika nyumba ile.
"Sawa nakusubiria nyumbani kwetu" alisema na kumtazama mbele yake mama Alice.
Aliichukua picha ya binti mmoja kisha akasema.
"Alice Mimi sijaifanya chochote familia yako yote hayo ni makosa ya yako wewe kunikaribisha kwenu....na kunifanya mimi nikutane na mwanaum mzuri kama Vikram nakushukuru kwahilo hata hivyo jina lako nitalitumia vizuri sana ahsanteh kwa kunipa nafasi ya kulitumia jina lako" alisimama na kusema nafikiri hapa ni mahali salama hakuna mtu yoyote yule atakayeweza kujua ya kuwa uko hapa.
**** ***** *****
Larry akiwa chumbani kwake aliweza kuyakumbuka matendo yote aliyowahi kuyafanya na Vikram.
"Hivi anawezaje?? Anawezaje kumfanyia hivyo Dada yangu??? Alijiuliza na kuanza kurusha kila kitu alichoweza kupewa na Vikram katika chumba chake.
Kwa upande wa Vanessa na yeye alibaki akimpigia Tropina aliyekuwa hapokei simu.
" yuko wapi huyu mwanamke alijiuliza akikata na kuendelea kupiga simu.
*** **** *** ****
Huku nako Vicky aliweza kuelekea mpaka alipo Alice katika nyumba ambayo aliwezaga kumpeleka huko wakati akigonga mlango alikuwa akipigwa picha bila yeye mwenyewe kutambua.
Mlango ulipofunguliwa aliweza kumrukia Alice shingoni na kuanza kumnyonga huku akimwambia "kufa, nakwambia kufa, unawezaje kuja kuharibu kila nilichoweza kukitengeneza katika miaka mingi hivyo??
****** ****** ******
Kulikucha asubuhi na Tropina aliweza kutoka katika hotel ile lakini alishangaa baada ya kuona kila anapopita watu wanamtizama na kuteta jambo.
Aliwatizama bila kusema jambo lolote na kuchukua simu yake kisha kumpigia Daniel.
Simu haikuweza kupokelewa hivyo aliamua kumpigia Tobias.
" Njoo nichukue nipo katika hotel ya grand view palace hotel" alipomaliza alikata simu na kuelekea mgahawani bado watu waliendelea kumtizama.
"Nachukia kutizamwa Mimi alizungumza na kupiga hatua za kuelekea mbele zaidi.
Baada ya muda Tobias aliwasili.
Alimfungulia mlango na alipanda ndani ya gari.
" hawa watu wanashida gani Leo kwanini wananiangalia alijiuliza na hapo aliweza kumuona Tobias akimtizama.
"Kuna shida gani?
" Madam Kuna matatizo yametokea"
"Matatizo gani?? Aliuliza Tropina.
***** ***** ****
"Nani huyo alienda kuyapokea hayo magari bandarini?? Aliuliza Vanessa akiwa anatoka katika chumba chake.
" Madhara gani yameweza kutokea.......watu tisa??? Aliuliza Vanessa.
"Sawa nipo njiani nakuja" alikata simu na hapo hapo simu iliita tena.
"Unasemaje tena........ Nini??? Wawekezaji wanataka kutoa hisa zao pamoja na fidia.....subiri nakuja" alikata simu
"Tropina yuko wapi jamani?? Alijiuliza Vanessa na kupiga simu.
Katika kampuni ya Magari anayomiliki Vanessa walionekana watu wakiwa wengi njee huku walinzi wakijitahidi kuwazuia wasiingie ndani. Hapo hapo liliweza kuuingia gari na alishuka Tropina. Watu wale walianza kumkimbilia na walinzi wakijitahidi kumuwekea ulinzi ili asiguswe alinyoosha Mkono wake juu na watu wote walinyamaza.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Haina haja ya kuniwekea ulinzi alafu nione huyo anayetaka kunigusa Mimi ni nani?? Alitoa kauli hiyo Tropina na kuvaa miwani yake kisha akaanza kukatiza katikati ya wale watu walioweza kumpisha baada ya kuyasikia maneno Yake.
"Niitieni huyo Adrian alitoa kauli hiyo na kukaa katika ofisi ya mama yake.
" bado hajaja kazini" alizungumza secretary.
"Sawa andaa kikao cha wawekezaji wote ndani ya saa4 kamili wote wawe hapa" alitoa amri hiyo na kusimama kisha kutoka katika ofisi hiyo huku Tobias akiwa nyuma yake.
Alipita mpaka sehemu yaliyokuwa wamekaa wawekezaji baada ya kufika hapo aliwatizama kisha akacheka kidogo na kuondoka.
"Unaona dhauri za huyu kipofu!!! Unaona?? Aliuliza mzee mmoja.
Wakati huo huko njee pembeni kabisa ya watu wale waliokuwa wakiandamana huku wakisem kampuni ile ifungwe.
" amekuja Tropina na amezungumza ya kuwa yoyote atakayehitaji kumgusa amguse alafu aone kitakachotokea.
"Huyo kipofu ndo kasema hivyo?? Aliuliza Alice.
" ndyo"
Alice aliitupa simu yake chini kwa hasira.
"Huyu mbwaa huyu kwanini anaharibu mipango yangu alijiuliza Alice.
***** ***** ******
"Wanasema kwamba magari hayo yaliweza kuingia Jana saa 7 mchana na mpaka usiku yakawa yameuzwa magari ya sampuli hiyo9 na Ndiyo yote yameweza kufumuka matairi na watu kadhaa wameweza kuumia lakini hakuna aliyeweza kupoteza maisha hata mmoja" alitoa maelezo hayo Jimmy akimpa Vikram.
"Ndni ya saa7 mpaka saa12 ni masaa 4 haiwezekani ndani ya masaa hayo yaweze kuuzwa magari 9 tena ya sampuli moja na magari yote hayo hayakukidhi viwango"
"Hapo hata mimi nahisi Kuna kitu"
"Nani alisign karatasi za kupokea huo mzigo? Aliuliza Vicky
" bado sijajua"
"Sasa kwnini unaleta information nusu nusu" aligomba Vikram.
"Samahani bossi"
"Eti mbona najaribu kumtafuta Obama lakini simpati? Aliuliza Kim.
" amerudi nyumbani " alisema Vikram akiwatiza.
"Wapi?? Aliuliza Kim.
"Amerudi south Africa" alijibu Vikram huku akiwatizama kwa macho ya huzuni.
***** **** *****
Vanessa aliweza kuwasili katika kikao hicho cha saa4 kamili akiwa na Tropina pamoja na Larry walioweza kuja kwa pamoja. Pinah alivaa shati nyepesi ambayo iliweza kumuonyesha nguo yake ya juu ya ndani aliyoweza kuivaa.
Aliingia katika kikao hicho na aliweza kupishana na Alice aliyekuwa amekaa na wawekezaji wa kampuni ile.
Wote waliingia ndani kisha wakakaa Tropina aliweza kumsindikiza kwa macho hadi kwenye kiti.
"Sijui uko hapa kwa niaba ya nani? Aliuliza Tropina.
Alice alitoa barua kisha akamptia wa mbele yake ambaye na yeye aliweza kuipass mpaka ikamfikia Tropina ambaye baada ya kuisoma alitabasamu na kumtizama.
"Inavyoonekana unanifahamu vizuri sana mpaka ukapata ufahamu wa kuwa nimeshapona macho"
Wawekezaji waliobaki waliweza kushangaa na kuulizana.
"Anaongea nini huyu?? Aliuliza Alice na kucheka.
" secretary " aliita Tropina na kutoa ishara iliyomfanya secretary aanze kugawa karatasi alizoweza kuziandaa.
"Magari hayo yaliweza kuingia Jana saa 7 mchana na mpaka kufikia saa12 yaliweza kuuzwa magari 9 nani jambo la ajabu na lakushangaza sana kwani yaliingia magari sampuli Tatu lakini iliweza kuuzika sampuli moja...nilipoweza kufuatilia Bandarini nimegundua ya kuwa magari hayo yalifika salama yakiwa hayana shida yoyote kwani yaliweza kukaguliwa bandarini na uzito wake ulikuwa ni sahihi kabisa ila baada ya kufika katika kampuni yetu na kupimwa uzito tena wa magari hayo yalionyesha kupungua na bila kujali manager wenu alimruhusu Vanessa asign pasina kumpa taarifa zozote zile....kitu kingine baada ya kuligundua hili aliyeweza kwenda kupokea mzigo bandarini ameweza kutowek na bado tuko mbioni kumpata.....ila pia kutoroka kwake haiwezi kuwa changamoto kubwa sana kwani Mimi kama wakili wa kampuni hiyo ninayo haki ya kuweza kuwakamata wale wote walioweza kuja kuyanunua magari haya kwani nilipofuatulia background zao hawana uwezo wa kumudu wa kuyanunua magari hayo. Hivyo basi nataka kumalizia kwa kusema kama kuna mpuuzi yoyote aliyediriki kuucheza mchezo huo mchafu wa kuliharibia jina kampuni hii basi atalipia kwa kuupoteza muda wangu wa kumpata yeye pia kwa kuiharibia sifa kampuni hii. Alimaliza kuzungumza Tropina na kumtazama Alice na Adrian kisha akatabasamu na kutoka pale alipoweza kusimama.
"Sisi tunahitaji kutoa hisa zetu hatutaki kujua kipi kimetokea" alizungumza Alice.
"Ahaaaa kutoa hisa zenu.... Alizungumza na kumsogelea kwa ukaribu zaidi.
" secretary angalia Mr mpalila anahisa kiasi kipi katika hii kampuni ya Magari.
"7 madam Tropina"
"Sawa uza hisa zangu 7 na umpatie huyu pesa zake aendee zitabaki hisa ngapi baada ya kutoa hizo saba??
" zitabaki 50" alijibu secretary.
"Sawa fanya hivyo na hisa hizo utakata katika hisa za manager siyo za director kwamaana yeye ndiye aliyeweza kumruhusu director a sign bila kupitia na kuhakikisha kila kitu kipo sawa.
" madam manager ana hisa 6 tu hivyo itapelea hisa moja" alijibu secretary.
"Nitakupatia account namba yake na ukatoe pesa bank kwaajili ya kufidi hiyo hisa moja" baada ya kumaliza mazungumzo hayo alitoka njee na kuwaacha ndani.
"Nafikiri tumemaliza vizuri sasa Kuna anayehitaji kutoa hisa zake tena? Aliuliza Larry.
Wote walikaa kimya na kumtizama tu.
" natumaini hakuna hivyo endeleeni kupambana alisema Larry na kuondoka wakati huo Vanessa alimtizama Alice na kucheka aliipangusa miwani yake vizuri kisha akaiweka machoni na kumuaga kwa nyuma Alice.
"Uliniambia kila kitu kitakuwa sawa mbona sasa mambo yamegeuka?? Aliuliza Adrian.
" Huyu Tropina ni mjanja sana na hiyo sheria aliyoweza kuisoma Ndiyo inayompatia kiburi...kesho ni anahitajika mahakamani na kama sitaweza kutafuta njia nyingine kesho Tropina anaweza akakana na kuweza kuachiliwa huru. Na kwahilo sitaruhusu litokee" alikula kiapo Alice kwa hasira na sura ya Tropina ikipita katika kichwa chake
"Tobias....nataka uniletee taarifa zote za huyo Alice ikiwezekani ata wakati anazaliwa nataka kujua alitoka kwa miguu au alianza kichwa" alizungumza Tropina baada ya kuingia ndani ya gari.
Wakati huo wote Vanessa alikuwa akitabasamu tu ila baada ya kutizama mbele ya macho yake aliacha kutabasamu.
Alikuwa ni Vikram aliyekuwa mbele ya macho yake akiwa na Jimmy aliyefungua na kumlango wa gari kwa ishara ya Vanessa aingie ndani ya gari.
Vanessa alimtizama bila kusema neno kisha akamuamrisha Danielle aende nyumbani na Larry. Alielekea kwenye gari lile.
Baada ya dakika 30 kupita.
"Nitaaminije?? Aliuliza Vanessa.
" Mama unajua nampenda Pinah nisingeweza kufanya chochote kile cha kumuumiza lakini sina cha kufanya zaidi ya kufanya vile anavyotaka hiyo Ndiyo njia pekee ya kuwasaidia ninyi nyote. Alizungumza Vikram.
"Huyo Alice ulimtolea wapi na wewe?? Aliuliza Vanessa.
" hata mimi sijui ametokeaje katika maisha yangu" alijibu Vicky.
"Usijali lakini Tropina hajui chochote kama uliweza lala naye katika chumba chake unaweza ukaenda kumwambia mwenyewe kabla taarifa hizi hazijamfikia kupitia mtu mwingine Tropina ni muelewa naamini atakuelewa, vipi kuhusu wewe uko salama sasa? Aliuliza Vanessa akimtizama kwa huruma Vikram
Aliyeweza kutingisha kichwa huku machozi yakimtoka.
Vanessa alimshika na kumfuta machozi huku akimpiga piga mgongoni.
***** ***** *****
" Historia yake kidogo inanitatanisha alizungumza Tropina baada ya kuletewa file nzima lenye stori ya Alice.
"Nahitaji kwenda kuzungumza na mama yake Kuna kitu sijakielewa hapa" alisema na kumrudishia file Tobias.
Huku nako alionekana Daniel akiwa na Alice.
"Kwanini unafanya vitu vya namna hii eti...unawezaje ukauwa watu ambao wameweza kukulelea wewe kama mtoto wao kwaajili tu ya mwanaume ambaye hana hata mapenzi na wewe?? Aliuliza Danielle.
" sijauwa mtu Mimi yule kipofu ndo amekwambia Mimi nimeuwa.......alafu unasemaje watu nilioweza kulelewa nao?? Aliuliza kwa mshangao.
"Veronica unaweza ukawadanganya wote lakini huwezi kunidanganya Mimi nilikuona ukideki damu katika nyumba yenu na hiyo haikutosha pia hii cheni Mimi Ndiyo nilikununulia wewe imekuwaje damu ya Winnie ikawa katika hii cheni unahusika katika kifo cha Winnie"
"Daniel!!!
" hivi unajua hii cheni nikiipeleka polisi kipi kitatokea juu yako, kazi yetu na kumtafuta Rickson lakini siyo kuwauwa watu wasioweza kuwa na hatia unafikiri Mr Harlan akisikia hivyo atafanya nini juu yako ??
"Daniel na ninafuraha ya kuwa wewe Ndiyo uliyoweza kuipata...hiyo cheni Tropina alininyang.anya na nilikuwa najua tu lazima ataipeleka huko katika eneo la tukio ili Mimi nichukue zambi zake......."
"Veronica sitaki uwongo nimekuona Mimi mwenyewe ukifanya mauaji alafu unaniambia Tropina"
"Ndyo Mimi Ndiyo nimemuuwa Unataka je sasa, kupeleka ushahidi polisi ili nifungwe peleka peleka sasa rafiki gani wewe.....unawezaje kuniuza Mimi kwaajili ya mwanamke ambaye hata hakutambui wewe kama mtu wa dhamani katika maisha yake....... Katika dunia hii hakuna mtu anayeweza kusimama kwaajili yangu na kupambana kwa yangu watu wote wanamtetea mtu ambaye yeye ndiye sababu ya mm kuwa hivi leo" Alice alizungumza huku akitupa tupa vitu Hatimaye aliona kisu na kuamua kukifuata.
"Bora Mimi nife ili nisiendelea kuona marafiki zangu wote wa karibu wananisaliti Mimi alianza kushusha kisu katika mwili wake ila Danielle alimuwahi na kutupa kisu mbali na huku na kumkumbatia.
" usifanye hivyo Veronica nitajitahidi kukusaidia kubeba makosa yako na nitayalipa Mimi" alizungumza Danielle akimpiga piga mgongoni wakati huo Alice alikuwa akitabasamu na kufuta chozi moja lililoweza kutoka katika jicho lake moja.
"Nashukuru kwa kuwa umeamua mwenyewe kunisaidia basi utanisaidia kitu kimoja"
Alizungumza Alice.
"Kitu gani hicho??
" nitakwambia muda ukifika" alijibu Alice na kutoka katika mwili wa Daniel kisha Kuondoka zake
Aliweza kucheka kwa mbele kwani tayari alishaichukua cheni ile kutoka kwa Daniel bila Danielle kufahamu.
***** ****** ******
Tropina aliweza kufika katika nyumba ya kina Alice aligonga bila mafanikio na wakati akigonga mlango uliweza kujifungua hivyo aliingia ndani kwa utaratibu kabisa.
"Mama Alice......Mimi Tropina....... Haloo
......samahani Kuna mtu yoyote ndani aliita Tropina na kuendelea kutembea hapo hapo alikanyaga kitu na kukifanya kipasuke.
Alitoa mguu wake na kukitazama ilikuwa ni kioo cha saa kilichoweza kupasuka.
Wakati anakishika kioo hicho alihisi Kuna kitu kiko tofauti pale ndani baada ya kusikia kishindo kidogo katika chumba kilichokuwa mbele ya macho yake. Alisimama na kukiacha kile kioo pale kisha kuanza kupiga hatua za kuelekea katika kile chumba. Ghafla alimuona paka akitoka katika kile chumba aliamini ya kuwa ni kishindo cha paka lakini haikuwa kweli alikuwa ni mama yake Alice aliyekuwa amefungwa vizuri sana katika kile chumba na kumfanya kutokutoa sauti yoyote wala kujigeuza geuza. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alirudi pale na kuanza kukagua kagua kwa kushika shika baadhi ya vitu ambavyo viliweza kumvutia.
Alifika mpaka katika kile kibobo cha uwa kilichoweza kumpiga baba yake na Alice na kutaka kukigusa alipeleka Mkono wake hadi karibu kabisa na pale na hapo hapo simu yake iliweza kuita hivyo ikamfanya asiweze kukishika tena kikopo kile.
" haloo"
"Niko kwa kina Alice unashida gani na mimi?? Aliuliza Tropina akionyesha kuvimba kwa hasira.
" Sina muda mwingi wa kukaa hapa nitaondoka sasa hivi hivi.....
Sawa itategemea na wewe mwenyewe kama utaweza nikuta" alizungumza na kukata simu.
Baada ya kukata simu alitabasamu.
"At least ata umenipigia simu..... Najua utakuja kuniomba tu samahani na sitakusamehe kirahisi hivyo Vicky.
" waoooo ni nani huyo?? Aliuliza Tropina na kuelekea katika picha moja aliyoweza kuiona ilikuwa ni picha ya Alice au mtoto halisi wa nyumba ile.
"Huyu ni nani?? Aliuliza na kumtazama kwa makini zaidi.
Hapo hapo alisikia sauti nyuma yake.
" unatafuta nini huku?? Alikuwa Alice.
"Najiuliza huyu ni nani?? Alafu mama yako yuko wapi Kuna maswali nataka kumuuliza. Alizungumza Tropina kwa kujiamini.
Veronica alitizama chumba ambacho aliweza kumuweka mama yake na Alice na kuamini ya kuwa Tropina hakumuona.
Alirudisha chombo alichoweza kukibeba akitaka kumpigia nacho Tropina akiamini ya kuwa Tropina hajamuona.
" unashida gani wewe mbona unamashaka mashaka?? Aliuliza Tropina akitizama chumba ambacho Alice aliweza kukitizama kisha akamtizama tena Alice.
Veronica alimsogelea na kuchukua ile picha kwa nguvu kutoka kwa Tropina.
"Unashida gani wewe?? Aliuliza Tropina akimtizama Alice.
Hpo hapo alisiikia akiitwa na Vikram.
Vikram alifungua mlango na hapo aliweza kukutana na Alice macho kwa macho na kufanya furaha yote aliyoweza kuja nayo imuisha.
Tropina alimtizama na kumtazama Alice.
" Ahaaaa umeshtuka baada ya kutuone wanawake wako wote wawili tuko ndani sindiyo" alizungumza Tropina
"U namaanisha nini?? Aliuliza Vikram huku akimtiza Alice aliyekuwa kavimba kwa hasira.
Tropina alianza kupiga hatua za kuondoka katika nyumba ile. Alipofika karibu na Vikram alimtizama kisha akampush na kutoka njee.
Vicky aligeuka na kutaka kuondoka.
"Inavyoonekana hutaki kabisa kunielewa nilichokwambia hivi unafikiri sitaweza kufanya kile nilichoweza kukwambia Unataka kuona maiti ya Larry..... Sasa endelea" alizungumza Alice na kupiga simu.
"Alice samahani alizungumza Vikram na kumsogelea kwa ukaribu zaidi.
"Sitarudia tena" alisema Vikram na kupiga magoti.
Wakati huo aliingia Tropina ndani..
"Eti unafanya nini hapo?? Aliuliza Tropina na kumuinua Vikram alimchukua na kumtoa njee
Kisha akamrudia Alice.
" Vikram ni mwanaum wangu Mimi..namaanisha hivi Vikram ni mume wangu Mimi, sasa usitake kujua ya kuwa huwa nawachukiaga kiasi gani wanawake wanaotembea na wanaume ambao siyo wa kwao alizungumza alafu baada ya kumaliza alimtizama na kumwambia.
"Mama yako akija umwambie nataka kumuuliza maswali kadhaa juu yko na swali la kwanza litakuwa ni hili je wakati anakuzaa ulitanguliza kichwa au miguu kuingia duniani?? Alipomaliza alimtizama kwa hasira sana Alice kisha akatoka njee na kumshika Vikram Mkono kisha akampandisha ndani ya gari na kuelekea kuendesha.
" Tobias rudi nyumbani na gari......nitachelewa kurudi nyumbani na kama Kuna chochote kitatokea basi utanitaarifu" Tropina aliwasha gari na kuondoka zake.
Akiwa ndani ya gari alimtizama Vikram aliyeeonekana kama kutokuwa katika ufahamu wake.
"Mama.....alizungumza Vikram na kumtazama Tropina.
" Mama.......nani...?? Aliuliza Tropina.
"Nataka kuzungumza na Vanessa naomba simu yako alizungumza Vikram na Tropina alimpa simu.
Vikram aliushika kwa kutetemeka na simu ilimdondoka.
" unashida gani wewe?? Aliuliza Tropina na kusimamisha gari kisha akaokota simu na kumpigia vanesa kisha kumpatia simu Vikram.
Vikram alikuwa akihangaika kufungua mlango wa gari.
Tropina alimtolea lock kisha akamfungulia mlango alianza kutembea barabarani na kukoswa koswa na magari.
"Anashida gani huyu ??? Aliuliza Tropina na kutoka ndani ya gari kisha kumfuata Rickson.
Alisimama mpaka magari yalipoweza kupita yote alielekea katika upande aliokuwa Vikram.
Alikuwa amekaa chini huku akitizama sehemu moja tu.
" Mama.....aliita Tropina lakini Vanessa hakumjibu kitu.
"Ni nini kinaendelea aliuliza Tropina na hapo hapo simu yake iliita tena.
" Vanesa Kuna shida gani mbona siwaelewi" aliuliza Tropina
"Mlete Vikram Nyumbani" alisema Vanessa na kukata simu.
"Ni nini hik?? Aliuliza Tropina na kumzindua Vikram kwa kumpiga piga usoni.
" huyu mbwaa kamfanya nini Vikram..?? Aliuliza Tropina kwa hasira.
Baada ya muda alionekana Vikram akiwa amejilaza chumbani kwa Tropina huku akiwa amefunikwa na shuka na kutetemeka kwa hofu.
"Mama Kuna shida gani?? Aliuliza Tropina.
" Huyu Alice huyu sitamuacha hai naapa anatakaje kucheza na maisha ya mtoto wangu? Aliuliza Vanessa na kupiga simu.
"Nimesema hivi muuuwe huyo Alice kama ni dhambi acha ziwe juu yngu muuwe na maiti yake ilitwe hapa" alizungumza Vanessa na kukata simu.
"Madam Vanessa"aliita Diana kwa sauti ya juu na mshtuko.
" Nini??? Aliuliza Vanessa.
"Larry.... Larry"
"Kipi kimemtokea?? Aliuliza Vanessa.
" Chumbani kwake" alizungumza Diana na Tropina alikimbilia chumbani kwa Larry huku Vanessa akimfuata nyuma.
Chumba chake kilikuwa kimevurugwa na dirisha lilikuwa wazi huku kitambaa kimoja cheupe kikiwa chini.
Vanessa alikifuata na kukichukua.
"Usikinuse alisema Tropina lakini tayari alishachelewa kuzungumza Vanessa.
" ni nini hii aliuliza Vanessa na hapo hapo alidondoka.
"Madam Vanessa aliita Diana na kumkamata kabla hajafika chini.
Hapo hapo simu yake iliita.
" Vanesa unafikiri utaweza kuniuwa Mimi kirahisi hivyo..... Sasa fanya haraka uje katika godown ile aliyoweza kufa Winnie kwaajili ya kuuchukuwa mwili wa mtoto wako baada ya mwili wa Winnie kuchukuliwa.
Alikata simu bila kujua ya kuwa aliyepokea simu ni Tropina.
Tropina alirudi mpaka chumbani kwake na kuchukua bastola yake kisha akamtizama Vikram aliyekuwa bado akitetemeka na macho yake yakiwa yamefungwa.
"Vikram naenda kumaliza matatizo yote" alisema na kumpiga busu la paji la uso.
Wakati akitoka njee ya nyumba Alice alimuona.
"Waoooo ikawaje unakuja wewe......hata hivyo harakisha ili game iishe leo" alizungumza na kutoa bastola yake kisha kuikock.
Baada ya Alice kuzungumza hivyo alimtaka Daudi aondoke eneo lile kisha akatoa ishara kwa vijana wengine wawili waende na kumtoa Larry katika kiroba walichoweza kumuweka.
Larry alitolewa akiwa bado hajapata fahamu kabisa.
"Tumfanyaje?? Aliuliza kijana mmoja.
" Mpaka hapo kazi yenu imeisha mnaweza mkaenda ila ondokeni na hicho kiroba alisema Alice na waliweza kufanya vile alivyoweza kuelekezwa na kuondoka zao.
Hapo Alice aliichukua simu yake na kupiga kituo cha polisi.
"Haloo.....halo..... Kituo cha polisi.....natoa taarifa za mauwaji hapa mtaa wa........nyumba nambari 43 nimemuona muuwaji na ananifukuza.....aaaaahhhh" alipiga kelele na kukata simu kisha kuanza kucheka.
Kwa kelele zile ziliweza kumshtua Larry na kuanza kujishika kichwani.
"Tajiri mdogo mbona umechukuwa muda mrefu hivyo kuzinduka aliuliza Alice na kucheka.
" Nani wewe?? Aliuliza Larry na kumtizama Alice akiwa anavuta kumbukumbu amemuona wapi.
"We secretary wake Adrian kwanini niko hapa......ahaaaa huyo mpuuzi Adrian amekutuma unikamate?? Aliuliza Larry
Alice alitikisa kichwa ishara ya hapana.
Larry alijisachi mfukoni mwake lakini hakuwa na simu.
" Embu nipe simu nimpigie Danielle alete gari"
"Danielle.....
Yule pale" alinyoosha Mkono mahali alipo Daniele hapo.
Larry alishtuka kwani ulikuwa ni mwili wa Danielle na siyo Danielle mwenye uhai tena pembeni yake pia ulikuwa mwili wa Mr Harlan.
Daniel aliita Larry na kumkimbilia pale alipo huku akimshika na kumuamsha bado alikuwa hajamalizikia kukata roho.
Daniel aliingiza Mkono wake mfukoni kwa tabu sana na kutoa kifuko cheupe kisha akampatia Larry kisiri bila Alice kuona na kumpa ishara ya asogee kwenye masikio yake kisha akamnong.oneza neno
"Mpe....mpe.....ma....da......m......tro.........." Kabla hajamaliza kuzungumza alipigwa risasi ya kichwa na kumfanya afie hapo hapo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unakuwa na roho ngumu kama ya paka Ricskon unatakiwa ufe haraka bhna" alizungumza na kuipuliza bastola yake huku akimtizama Larry.
"Kwnni umemuuwa?? Kwanini umemuuwa??
" Nani....Mimi au Tropina me Sijamuuwa yoyote yule ni dada yako ndo kahusika na haya yote" alisema Alice na kucheka.
***** ***** *****
Wakati huo nao Calvin alikuwa akiipiga simu ya Danielle lakini haikuwa ikipatikana.
" anashida gani huyu Daniele mbona aliniambia ataenda kukutana na Alice kisha atawahi kurudi tueleke wote club sasa imekuwaje tena na simu kazima?? Alijiuliza na kuendelea kupiga lakini majibu yalikuwa ni Yale Yale.
**** **** ***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment