Simulizi : Niliua Kwa Kukusudia
Sehemu Ya Nne (4)
PAMOJA na kwamba ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuona bastola ana kwa ana, hali ile ilinishtua sana. Nishtuka kwa mengi, kwanza sikuwahi kuwaza au kufikiria kuwa yule Mwarabu alikuwa akimiliki silaha ya aina hiyo.Nikabaki nimetoa macho mithili ya mjusi aliyekuwa amebanwa na mlango. Huku mwili ukinitetemeka, nilijikaza na kumuamkia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Shikamoo bosi.""Marahaba," aliitikia huku akiendelea kuifuta ile bastola na kuigeuza mara kwa mara. Hakuonekana kabisa kujali uwepo wangu ofisini kwake.
Kila mara, uoga wangu ulizidi kuongezeka. Hali hiyo ilichangiwa na kumuona akiwa katika uso wa hasira sana. Hakika niliogopa kuliko maelezo."Vipi, mbona unashtuka na kuonesha woga kiasi hicho?" aliniuliza na kunisogelea kitendo kilichozidisha woga maradufu moyoni mwangu. Bila kutarajia nikaanza kutetemeka."Hii inaitwa bastola aina ya Beretta, inanisaidia kujilinda kwa mambo mengi sana," akasema na kuisogeza karibu yangu. Ilitisha kwa kuitazama tu. Akazidi kunisogelea, aliponifikia akanishika begani kwa kutumia mkono mmoja. Hapo nikazidi kujawa na hofu kubwa. Kijasho chembamba kikawa kinanichuruzika."Usiogope, hii ni silaha ya kawaida sana, ukitaka kuitumia unafanya hivi," alianza kunielekeza namna ya kuitumia.Akanifundisha kila kitu. Nikajikuta nikivutiwa na jinsi ya kuitumia ile bastola. Ghafla hofu na woga wa awali ulianza kunitoka. Sijui ni kwa nini lakini huenda ni kutokana na lugha laini ambayo alikuwa akiitumia huyo Mwarabu yaani bosi Elhakimu.Baada ya maelekezo yake, nikamweleza shida yangu ambapo tofauti kabisa na matarajio yangu, alikubali kirahisi mno kunisaidia kiasi cha pesa kilichohitajika kukamilisha upangaji wa chumba.Akarudi kwenye kiti chake. Taratibu akafungua droo iliyokuwa chini kabisa ya meza yake. Akaiweka ile bastola kisha akanitazama usoni huku akitabasamu.Alinitazama sana usoni hali ambayo ilinifanya nione aibu na kuishia kuinama na kuanza kupikicha vidole vyangu.Akachukua kalamu na kikaratasi kidogo na kuanza kuandika maandishi ambayo sikuyaelewa kutokana na umbali uliokuwepo kati yetu."Sikiliza Tunu, mimi siwezi kukukopesha pesa ila nimeamua kukusaidia, sawa binti mzuri?" akasema na kunifanya nishtuke tena. Kilichonishtua si kitendo cha kunisaidia ila ni ile kauli ya kuniita binti mzuri. Kwa jinsi ambavyo nilikuwa nikiheshimiana na huyo Mwarabu, tena akiwa bosi wangu, hakuwahi kuniita jina kama hilo tofauti na Tunu.Akachukua simu yake ya mezani na kupiga namba fulani. Muda mfupi baadaye, aliingia msichana mrefu mwembamba, mweupe na mchangamfu sana.
"Tunu," aliniita yule bosi."Bee," nikaitika na kumtamza usoni.
"Huyu ni mhasibu wetu, anaitwa Zulekha, naomba uongozane naye ili akupatie hiyo pesa ambayo naamini itasaidia mahitaji yako."Licha ya kutomtajia bosi ni kiasi gani cha pesa nilichohitaji, nilishangaa akisema kuwa anaamini kitasaidia kukidhi mahitaji yangu. Nikaongozana na yule mhasibu hadi ofisini kwake.
Wakati tunaondoka, yule bosi Mwarabu akaniambia nipitie tena ofisini kwake kuna maagizo aliyotaka kunipa.Tulipofika ofisini kwa mhasibu huyo, alichukua bahasha na kuanza kunihesabia pesa alizoagizwa na bosi anipatie. Akanikabidhi kisha nikaondoka. Nilipofika nje, nikaanza kuzihesabu zile pesa ambazo zilikuwa ni shilingi laki mbili na nusu. Sikuamini hata kidogo. Kwa mbali nikaanza kumuona yule Mwarabu kama mkombozi wangu maishani. Niliamini hata kitendo chake cha kunigonga na gari kule Chalinze, ulikuwa ni mpango wa Mungu."Nimeamini kila jambo hutokea kwa makusudi, kumbe huyu Mwarabu kunigonga na gari ulikuwa ni mpango mkubwa wa Mungu, ahsante Mola wangu," nilijikuta nikitamka maneno hayo.
Baada ya kuzihesabu, nikazirudisha kwenye bahasha kisha nikaelekea ofisini kwa bosi ili nikamsikilize tena alichoniitia. Moyoni nilijawa na furaha ya ajabu mno.Kila aliyeniona kwa wakati huo, aliweza kung'amua kwa haraka sana furaha niliyokuwa nayo. Hakika nilifurahi, nashindwa hata kuelezea ni furaha ya kiwango gani.
Nikafungua mlango wa bosi na kumkuta akizungumza na simu. Alipomaliza alinigeukia akiwa na uso wa huzuni.Usinione nina uso wa huzuni hivi, nina habari kutoka kwa yule mdogo wangu, zinamhusu mdogo wako," akasema na kunikazia macho kauli iliyonifanya nishtuke kwa nguvu.
Kauli ya bosi ilinifanya nikae vyema kwenye kiti na kuanza kumsikiliza kwa umakini mkubwa kuliko ule wa awali. Kengele ya hatari ilikuwa imeshaanza kugonga kichwani mwangu. Nikahisi huenda mdogo wangu Inana amepatwa na janga lingine, jambo ambalo hakika sikuwa tayari kulisikia kabisa."Mdogo wako anaendelea vizuri, ila kuna mambo yangu ya kibiashara hayajakaa sawa ndiyo maana unaona niko katika hali hii," alisema na kunikazia macho.Nilishusha pumzi kwa nguvu. Angalau nikawa na ahueni kwani nilikuwa nimeshaanza kuchanganyikiwa. Nilimpenda sana mdogo wangu. Baada ya kuniambia hivyo, tuliagana ambapo niliondoka nikiwa na furaha ya kupewa ile pesa. Haraka sana nikaenda kuonana na yule mama mwenye nyumba ambayo nilitakiwa nihamie. Nikakamilisha taratibu zote muhimu zilizokuwa zikihitajika.Siku hiyohiyo nilienda kununua godoro na kuliweka ndani. Nikanunua na baadhi ya vitu muhimu kama jiko na vyombo vya kutekea na kuhifadhia maji pamoja na karai la kufulia nguo.
Kwa kuwa sikuwa nimemuaga shangazi, nikapanda gari hadi Buguruni kumuaga shangazi. Licha ya kuonekana kunichoka, shangazi alishituka sana nilipomueleza juu ya suala la kuhama na kuanza kujitegemea."Sasa maisha ya kujitegemea utayaweza kweli Tunu? Au umepata bwana wa kukuoa na hutaki kunieleza ukweli?"
"Hapana shangazi, nimeamua kujitegemea."
"Mbona hukuniambia mapema?""Nilikuwa nakamilisha taratibu zote muhimu shangazi, hata hivyo sioni kama kuna kosa," nikazidi kujieleza kwa shangazi.
"Hata hivyo, kuhusu sijui mwanaume, sina hata wa dawa shangazi," nikaongeza na kumfanya shangazi abaki kimya na kunitazama kwa macho ya kuibia kwa chini.Baada ya mazungumzo hayo mafupi, nilimuaga. Nikaingia ndani na kuchukua vitu vyangu muhimu ikiwemo nguo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaondoka nikiwa na furaha hadi kwenye kituo cha mabasi ya kuelekea Mwananyamala. Nilifika majira ya saa mbili na nusu na kufikia nyumbani kwa kuwa hapakuwa mbali na kituo cha mabasi. Niliingia ndani nikiwa mwenye furaha isiyokuwa na kifani.Kwa mara ya kwanza maishani nilikuwa naanza kulala kwenye nyumba ambayo nitakuwa naigharamia kwa pesa na jasho langu. Nikaweka sawa godoro langu na kulala. Nililala kwa usingizi wa pono. Nilishituka ikiwa ni asubuhi na kushangaa kuwa nilikuwa nimelala na nguo.
"Mmh! Hiki chote ni kiherehere cha makazi mapya," nilijisemea moyoni huku nikitabasamu.Nikatoka nje nikiwa na ndoo ambapo niliteka maji na kwenda bafuni kuoga. Nikajiandaa kwenda kazini. Nikafunga mlango huku nikiimba nyimbo za kaswida. Hakika furaha niliyokuwa nayo haielezeki.
Nikaondoka hadi kazini. Nilifika na kubadili nguo na kuvaa za kazi, nikaanza kuwajibika kama kawaida.Nikiwa naendelea na kazi, kwa mbali nilimuona meneja akija upande wangu. Moyo ulinilipuka na kuongeza bidii ya kazi. Alipofika bila hata kunijulia hali alinitaarifu kuwa bosi yule Mwarabu alikuwa akiniita ofisini kwake.Nikajiuliza maswali kadhaa, kikaanza kujihoji juu ya tabia ya bosi kuniiita ofisini kwake mara kwa mara. Hata hivyo, sikwenda mbali zaidi kimawazo kutokana na jinsi ambavyo bosi huyo nilikuwa nikimuamini.
Nikaenda hadi ofisini kwake na kumkuta akiongea na simu. Aliponiona kwa mbali alininyooshea ishara ya kunitaka kutoingia kwanza na kuashiria kuwa alikuwa na mazungumzo ya faragha ambayo hayakuhitaji uwepo wa mtu yeyote zaidi yake.Nikarudi hadi ofisini kwa katibu muhtasi na kukaa kwenye kochi la wageni. Baada ya nusu saa, simu ya mapokezi ilipigwa na baada ya kuongea, yule dada alinipa maelekezo kuwa bosi alikuwa akinihitaji sasa.Nikanyanyuka na kuelekea ofisini kwake. Nilipofika alinikaribisha kwa furaha na tabasamu la bashasha. Na mimi nikajikuta nikiachia tabasamu bila kujizuia."Leo naomba twende pamoja matembezi ya jioni kwa ajili ya chakula cha jioni kama hutajali," bosi aliniambia akiwa ananiangalia kwa mkazo bila hata kupepesa macho.
Kutokana na kitendo cha kumuamini kupita kiasi, nilimkubalia kwa haraka bila hata kuonesha wasiwasi wa aina yoyote.Jioni ya siku hiyo, tulikuwa kwenye ufukwe wa Coco.
"Sikukuita huku kwa bahati mbaya, kuna jambo nataka nikuambie," alisema bosi na kusimama.
KITENDO cha bosi kusimama baada ya kuniambia kuwa kuna jambo alitaka kunieleza, kilinishtua na kunifanya nibaki kimya huku nikimtazama kwa macho ya woga. Sikuwa na hisia juu ya nini alitaka kunieleza.
"Kama kuna mahali nitakukosea, basi nitaomba msamaha wako lakini nadhani nitakuwa sahihi," alisema bosi na kuendelea kuzungukazunguka mahali alipokuwa amesimama.
Muda kidogo, aliketi na kuendelea na mazungumzo yake.
"Kwanza kabla ya kuendelea, ngoja tuagize vinywaji kwani huwa unapendelea kinywaji gani?"
"Maji yanatosha sana," nikamjibu kwa mkato.
"Tunu bwana, yaani nyumbani unywe maji, hata sehemu kama hizi?"
"Basi ngoja ninywe juisi bosi," nikamjibu na kumwangalia usoni.
"Kuna kinywaji kinaitwa Redd's, hakika kitakufaa."
"Lakini sikifahamu bosi, kwani siyo pombe?"
"Hakina kilevi, ila kinachangamsha tu," alinijibu na kuachia tabasamu.
"Sawa," nikakubali kwa haraka. Sijui ni nini? Maana nilikuwa namuamini sana bosi kwa kila jambo aliloniambia kiasi kwamba sikuwa na uwezo wa kupinga jambo lolote aliloniambia.
Mhudumu aliitwa na kuagizwa vinywaji vyote. Baada ya kurejea, alikuwa amebeba kisado kilichojaa. Akaweka chupa tatu za Redd's kwa upande wangu na kwa bosi. Kinywaji cha bosi kilikuwa tofauti kabisa na cha kwangu.
Kwanza chupa zangu zilikuwa za kopo zikiwa na rangi nyekundu na maandishi ubavuni. Lakini kinywaji cha bosi kilikuwa ni chupa ndefu ambayo ubavuni ilikuwa imeandikwa Grants.
"Naomba utuitie mtu wa jikoni tafadhali," bosi alimuagiza yule mhudumu na kutuacha tukiendelea na mazungumzo yetu. Moyoni nilikuwa na hamu na shauku kubwa ya kujua ni kitu gani hasa ambacho bosi alikuwa amepanga kuzungumza na mimi hadi kuamua kunitoa kwa matembezi ya jioni ikiwemo kuninunulia chakula cha usiku.
Bosi alinifungulia chupa yangu na kunitaka nionje ili nione ladha yake.
Taratibu nilichukua Redd's iliyokuwa imefunguliwa na kuanza kuimimina taratibu kinywani. Hakika ilikuwa nzuri, nilifurahia ladha yake yenye utamu wa kuburudisha mdomoni.
Sasa nikawa nakunywa bila uoga wowote huku mazungumzo yakizidi kunoga.
"Huo ndiyo ukweli wa moyo wangu Tunu, nakupenda nakukuhitaji sana, sawa?"
"Hapana bosi, hakika siwezi kuwa na uhusiano na wewe, lakini pia siyo wewe tu, umri wangu wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yeyote bado haujafika," niliendelea kutoa kauli zenye upinzani hali iliyosababisha kuanza kumkera bosi Elhakimu kwani alianza kubadilika kuanzia machoni, sura na hata mazungumzo yake kwani alianza kutoa maneno kwa ukali na kejeli kidogo.
Wakati namalizia chupa ya kwanza, ghafla nilianza kuhisi hali ambayo sikuwahi kuwa nayo. Nikawa naona vitu kwa taswira mbilimbili. Kuna wakati nikawa namuona bosi kama mtu wa kawaida tu. Uwezo wa kuzungumza ukawa unaongezeka na kuanza kucheka hata pale ambapo hapakuhitajika kufanya hivyo.
Licha ya kusikia hali hiyo lakini sikuwa tayari kukubaliana na ombi la bosi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mimi. Moyoni nilijiapiza kuweka msimamo usiotetereka.
"Au labda unaona kama sikufai?" alihoji bosi Elhakimu huku akipeleka kinywani kwa fujo chupa yake ya Grants.
Tukiwa tunaendelea na mazungumzo, mhudumu wa jikoni alikuja na vyakula alivyokuwa ameagizwa ambavyo ilikuwa ni mbuzi wa kukaangwa na ugali sahani mbili, kachumbari pembeni na pilipili kwa mbali. Kabla ya kuweka mezani, harufu ya mbuzi ilitawala na kutufanya sote tuwe na hamasa ya kuikabili ipasavyo.
Mhudumu alitunawisha na kutukaribisha kwa heshima na taratibu zote ambazo mteja husitahili kupewa wakati wa kupewa huduma. Tukaanza kula huku bosi akiendelea na ajenda yake ya kunishawishi nikubali kuingia naye kwenye uhusiano wa kimapenzi jambo ambalo sikuwa tayari hata kidogo kukubaliana nalo.
Tulipomaliza kula, tayari nilikuwa nimeshabadilika, nilikuwa nazungumza bila kupumzika, maneno yakatawala.
Baadaye macho yalianza kuwa mazito. Usingizi ukaanza kuninyemelea na kujikuta nikiinamia kwenye mapaja yangu na kuanza kusinzia.
Nilishtuka baaada ya kuguswa na kitu kisichokuwa cha kawaida mwilini mwangu. Nikafumbua macho kwa tabu. Sikuamini nilichokishuhudia. Ghafla ulevi ukaniisha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikuwa ndani ya gari kwa upande wa nyuma. Bosi alikuwa amevua suruali yake na kukomea magotini, ambapo sasa alikuwa amebaki kama alivyozaliwa. Mkono wake wa kuume ulikuwa ukijaribu kunivua sketi niliyokuwa nimevaa.
Nikajitutumua kwa kumsukuma japo sikuwa na nguvu sawia kutokana na ile hali ya ulevi.
Bosi alipoona kuwa nilijaribu kuleta kipingamizi, sasa alitaka kwa nguvu kutimiza alichokuwa amedhamiria dhidi yangu. Alikuwa akinibaka. Sikuwa tayari hata kidogo kufanyiwa kitendo kama kile bila ridhaa yangu. Nikawa naizuia mikono ya bosi Elhakimu aliyekuwa akiendelea kunivua kwa nguvu.
Purukushani iliendelea ndani ya gari huku nikijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyesikia kutokana na milango ya gari lile la kifahari kuwa imefungwa, vioo vyake vilikuwa vyeusi ambavyo kwa kisasa huitwa tintedi. Nikawa najaribu kumuondoa bosi maungoni mwangu lakini sikufanikiwa kutokana na kuzidiwa nguvu.
Hatimaye nikaamua kumuacha yule Mwarabu ambaye kwa wakati huo sikuwa nikimhesabu kama bosi tena kutokana na kitendo cha udhalilishaji alichokuwa akinifanyia kwa wakati huo. Katika maisha yangu sikuwahi kusikia maumivu makali kama hayo.
Maumbile makubwa ya yule Mwarabu yaliniumiza. Maumivu yalikuwa ni makali, hayasimuliki na kumbuka kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingiliwa na mwanaume, tena kwa nguvu na bila ridhaa yangu, yaani nilikuwa nabakwa! Inauma mno, hadi sasa kila nikikumbuka juu ya tukio hilo, machozi hunitiririka.
Bila huruma huku akitoa sauti ya kuashiria kufurahishwa na kitendo kile, Mwarabu huyo aliendelea kutoa sauti ya miguno. Licha ya kulia kwa nguvu na maumivu, Elhakimu hakujali, kwa takriban saa moja na nusu aliendelea kuniingilia kwa nguvu nyingi kadiri alivyoweza.
Baada ya kumaliza kunitendea unyama huo, Elhakimu alivaa na kuniacha nyuma ya gari nikiwa nimelala, nilijaribu kuinuka lakini nikashindwa, nikatupa macho sehemu zangu za siri, machozi yalinitiririka, nilikuwa nimeharibika vibaya mno. Ghafla nikiwa katika hali ile, macho yalianza kuona giza kwa mbali, nikasikia yule Mwarabu akiwasha gari, nikawa nasikia kizunguzungu cha ajabu huku giza likizidi kutanda machoni na kizunguzungu kikazidi kunisumbua, baada ya hapo sikujua kilichoendelea.
*****
Majira ya saa kumi na moja alfajiri, fahamu zilianza kunirejea taratibu. Nikafumbua macho na kuanza kuangaza huku na kule. Nilikuwa ndani ya chumba kilichokuwa na vitanda vingi sana. Nilipojaribu kunyanyuka, nilishindwa kutokana na mikono yangu kubanwa na kitu ambacho kwa haraka sikukijua.
Nikaangaza macho vizuri na kugundua nilikuwa hospitali nikiwa nimelazwa, kwa haraka sikuweza kukumbuka nilifikaje mahali pale na kwa nini nilikuwa nimelazwa. Kumbukumbu za matukio yote ya jana yake zilianza kumiminika kichwani mithili ya filamu ya Kihindi ambapo kila kitu kilikuwa kikipita kichwani.
Katika kukumbuka, ndipo tukio la yule Mwarabu kunibaka likauvamia kwa kasi ubongo wangu. Maumivu yalirejea upya na kuanza kulia. Nilipojaribu kujitingisha, maumivu yalikuwa makali kuliko neno lenyewe!
Mikononi nilikuwa na dripu za maji. Nikaanza kulia kwa nguvu huku nikitaja majina ya wazazi wangu. Ulimwengu ulikuwa umenigeuka sasa, maisha yalikuwa yakinielemea, najaribu kujihangaikia lakini shetani anazidi kuweka kucha zake katika kila njia ninayojaribu kuipita.
Nilianza kulia taratibu, lakini kadiri kumbukumbu za tukio la kubakwa zilivyozidi kuongezeka, ndivyo sauti ya kilio ilizidi kuongezeka ndani ya wodi na kujikuta nikigeuka kero kwa wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa!
"Dokta, dokta, doktaaa," nikazidi kuita huku nikilia kwa nguvu. Mchanganyiko wa maumivu na uchungu wa kubakwa na mtu niliyemuamini kama Elhakimu, ulizidi kunifanya niione dunia kama jehanamu.
Muda mfupi baadaye, alikuja daktari kwa mwendo wa haraka hadi nilipokuwa nimelazwa na kuniinamia huku akiniangali kwa hofu kubwa.
"Mungu ni mkubwa, uliletwa hapa ukiwa hujitambui kabisa," alisema yule dokta na kunifanya nianze kukumbuka ni nani aliyelileta mahali pale.
"Nani alinileta dokta?" nikajikuta nikimuuliza kwa sauti ya kwikwi ikisindikizwa na machozi yaliyosababishwa na maumivu makali niliyokuwa nayo.
Wakati dokta akijiandaa kunijibu, ghafla mlango ulifunguliwa na kutokea mtu ambaye wote tulibaki tumemuangalia kwa mshangao!
Alikuwa mwanamke ambaye kwa kumwangalia mara moja, ni lazima ukubaliane na akili yako kuwa hakuwa na akili timamu. Alikuwa amevalia matambara yaliyochanika na kuchakaa sana. Hakika alionesha kila dalili ya kuwa mlemavu wa akili.
Katika hali ya kushangaza, alikuja moja kwa moja hadi kitandani nilipokuwa nimelazwa. Alimsabahi kwanza dokta kisha kunigeukia na kunikazia macho huku akishindwa kusema neno.
Habari za kwako, unaendeleaje? Hatimaye alivunja ukimya kwa salamu hiyo.
Salama, nashukuru Mungu kwa kweli, nilimjibu lakini sikuacha kumshangaa kutokana na hali aliyokuwa nayo. Mimi na yule daktari tulisitisha mazungumzo kwa muda na kusubiri kuona nini alikusudia kufanya yule mwanamke.
Pole sana kwa yaliyokukuta jana, ulikuwa na hali mbaya mno, alisema yule mwanamke na kupiga magoti kitandani kwangu huku machozi yakianza kumlengalenga. Nilibaki nikimshangaa kwani sikuwahi kuonana naye hata siku moja na nikawa najiuliza maswali mengi lakini kubwa ni alinijuaje na nani alimwambia kuwa nilikuwa na hali mbaya siku iliyopita!
Nilishapoa, lakini wewe ni nani maana sina uhakika kama tunafahamiana? nikamjibu na kumtupia swali ambalo niliamini jibu lake lingenitoa gizani kujua yule mwanamke alikuwa nani hasa na alinijuaje.
Hata hivyo, moyo ulinienda mbio sana kwani sikutaka mtu yeyote tofauti na madaktari ajue kuwa nilikuwa nimeingiliwa na mwanaume bila idhini yangu. Binafsi niliamini kitendo cha kubakwa ni udhalilishaji mbaya kuliko wowote katika maisha ya mwanamke.
Mimi ni msamaria mwema niliyekuokota jana mtaroni usiku wa manane ukiwa hujitambui na damu nyingi zikikububujika kama maji ya bomba. Ulikuwa umepoteza fahamu, alisema yule mwanamke.
Uchungu nilioupata kutokana na maelezo yake ulikuwa wa kiwango cha juu mno. Hasira na chuki dhidi ya yule Mwarabu vilinijaa.
Kumbe alinibaka na kunitupa mtaroni? nilijikuta nikitamka maneno hayo kwa sauti ya juu bila kujali uwepo wa wagonjwa wengine waliokuwemo mle wodini.
Mwanamke ambaye awali nilikuwa nikimhesabu kama mwendawazimu sasa aligeuka shujaa kwangu. Ndiye aliyeniokoa na hali mbaya niliyokuwa nayo baada ya kubakwa na bosi Elhakimu, mtu ambaye nilimuamini na kumheshimu kama mwajiri wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kumbukumbu mbaya ya jinsi nilivyobakwa ikaanza kujirudia upya akilini mwangu. Kufikia hapo, moyo wangu ukatengeneza chuki isiyosimulika dhidi ya wanaume wote duniani hasa yule Mwarabu aliyejivika ngozi ya kondoo ilihali ni mbwamwitu. Sikumtofautisha na wanyama wa mwituni.
Pole sana, mimi huwa nalala kwenye mtaro huo kwa kuwa sina makazi maalum, ugumu wa maisha ndiyo ulionifikisha hapo, ufukara huu huwafanya watu wengi wadhani mimi ni mwehu, jambo ambalo si kweli, akaendelea kusema yule mwanamke.
Kuna gari la kifahari lilisimama mtaroni hapo, akashuka mwanaume wa Kiarabu na kuanza kuangaza huku na kule, muda mfupi baadaye akafungua mlango wa gari na kutoa mzigo.
Awali nilidhani ni mzigo kumbe ulikuwa wewe, akakutupa mtaroni na kuingia kwenye gari lake haraka sana na kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Nilipokusogelea, ulikuwa hujitambui na damu zilikuwa zikikuvuja kwa wingi, nikaita watu na kwa pamoja tukakuleta hapa hospitalini, alisimulia yule mwanamke huku uso wake ukiwa umechakazwa na machozi ya huruma.
Pamoja na maadili ya taaluma yake, kukutana na matatizo mbalimbali na makubwa ya wagonjwa wengi, yule daktari ambaye kwa jina alikuwa amejitambulisha kama Dokta Masalu alishindwa kuyazuia machozi wakati yule mwanamke alipokuwa akisimulia jinsi alivyoniokota.
Ilionesha kuwa yeye hakuwepo wakati nafikishwa pale hospitalini. Nilimuona akionesha hisia za machungu na maumivu makali.
Basi ngoja nikuchome sindano kwanza, nikupe dawa fulani ndipo tuendelee na tiba nyingine, alisema Dokta Masalu na kumtaka yule mwanamke atupe muda kwani hata hivyo, muda wa kuangalia wagonjwa ulikuwa umepita kwa asubuhi ile.
Yule mwanamke aliondoka na kuahidi kurudi mchana kunijulia hali. Wakati anaondoka, macho yangu yaliganda kwake na kumuona kama shujaa wa kipekee maishani mwangu kwa wakati huo.
Bila huyu mwanamke ningefia mtaroni mimi, nilijikuta nikitamka maneno hayo huku machozi yakinitoka na kulowanisha mashuka.
Kuna jambo nitakueleza nikirudi, ila inabidi uwe na kifua, alisema yule mwanamke na kufungua mlango huku akiubamiza kwa nguvu.
Mimi na yule daktari tulibaki tukitazamana kwa mshangao. Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kilichosikika masikioni mwetu muda mfupi uliopita. Hapohapo nikakumbuka msemo wa mama yangu ambao alikuwa akinieleza mara kwa mara enzi za uhai wake.
"Mwanangu siku zote za maisha yako usithubutu kumdharau mtu yeyote kwa sababu ya mwonekano wake."
Kweli, maneno ya mama yalikuwa yamedhihirika kwani mwanamke ambaye hapo awali nilimuona kama mwendawazimu sasa aligeuka lulu na mwenye thamani kubwa sana maishani mwangu. Asingekuwa yeye huenda hadi wakati huo ningelikuwa marehemu kutokana na maelezo yake kuwa wakati akiniokota nilikuwa
nikivuja damu nyingi sana kupitia sehemu zangu za siri baada ya kubakwa vibaya na yule Mwarabu.
Moyoni nikazidi kujiapiza kulipa kisasi kwa Mwarabu huyo, japo sikujua nitatumia njia gani kwani alikuwa ni mtu mwenye pesa na utajiri mkubwa mno kiasi cha kuogopeka hata kwa baadhi ya viongozi wa serikalini na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali.
"Haki. Ndiyo, haki pekee ndiyo itaniokoa katika hili, nitafungua mashitaka dhidi yake, kwani mama aliwahi kuniambia kuwa hakuna aliye juu ya sheria hivyo pamoja na pesa zake ni lazima sheria ichukue mkondo wake dhidi ya Mwarabu huyu," nikajiwazia na kujipa matumaini makubwa moyoni mwangu.
Jioni ya siku hiyo, wakati nikimalizia kula, yule mwanamke aliyekuja asubuhi na kunieleza kuwa ndiye aliyeniokota, alirudi na kuanza kunisimulia historia ya maisha yake.
Alinisimulia jinsi ambavyo aliwahi kuishi maisha ya kitajiri na kifahari huko nyuma, lakini kwa sababu ya kuwaamini wanaume ndiyo maana kwa wakati huo alikuwa akiishi kama mnyama mwituni ili hali alikuwa binadamu ndani ya nchi yake huru.
Akasimulia jinsi alivyozaliwa na kukulia kwenye utajiri mkubwa wa wazazi wake, jinsi alivyosoma shule za kimataifa tangu msingi hadi ngazi ya vyuo mbalimbali. Katika mazungumzo yake, nilishangaa aliponiambia kuwa kwa wakati huo alikuwa ni msomi wa shahada ya udhamili (Master Degree) katika masuala ya sayansi na utafiti.
Nilizidi kubaki mdomo wazi aliponieleza mashirika aliyowahi kufanya kazi duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Uholanzi.
"Mapenzi, mapenzi ndiyo yamenifikisha hapa nilipo, leo nalala jalalani, nakula kwa kuombaomba kwenye migahawa na kuonekana kama mwendawazimu, kisa ni mapenzi," akazidi kunisimulia yule mwanamke na kunifanya niendelee kumshangaa kwa kila sentensi aliyoitamka.
Sikupata picha ni pigo gani alilipata kupitia mapenzi kwani kukulia kwenye familia tajiri, kusoma hadi ngazi hiyo ya juu kabisa kielimu na kufanya kazi nchi kubwa kama alizozitaja na leo hii kuonekana kama mwehu asiyekuwa na makazi maalum kulinishangaza sana, hakika lilikuwa pigo kubwa katika maisha yake.
Akaniambia jinsi ambavyo alikutana na mwanaume wake aliyekuwa Mtanzani nchini Uingereza na kuanzisha naye uhusiano. Akasema walipendana na kuaminiana kupita kiasi na kufikia hatua ya kurudi nchini Tanzania kwa utambulisho na maandalizi ya kuoana.
Yule mwanaume alimshawishi kuacha kazi na kuja kuishi nchini Tanzania ambapo mali na utajiri wote aliokuwa nao aliuandikisha kwa jina la mwanaume huyo, akasema siku chache baada ya kufunga ndoa akiwa amemkabidhi kila kitu mumewe, manyanyaso yalianza kujitokeza na kufikia hatua ya kumfukuza nyumbani
walipokuwa wakiishi. Kutokana na hali hiyo kuusumbua ubongo wake, alilazimika kujiiingiza kwenye matumizi mabaya ya pombe hali iliyosababisha kuathirika kisaikolojia.
Ilikuwa ni sumulizi ndefu na ya kusisimua iliyonitia uchungu mkubwa mno moyoni mwangu. Hasira dhidi ya CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wanaume ikazidi kupanda maradufu na kujikuta nikizidi kujiapiza kisasi kikubwa baada ya kupona ingawa hakika sikuwa najua ni njia ipi rahisi ambayo ningeweza kuitumia tofauti na kutegemea sheria kuniokoa katika janga hilo.
Siku zilikatika hatimaye nikapata nafuu na kwenda kufungua mashitaka kituo cha polisi. Huko nilienda na vipimo vyote muhimu kutoka hospitalini na maelezo ya daktari ambayo niliyaambatanisha kwa pamoja.
Kwa ushahidi niliokuwanao niliamini Elhakimu angepatikana na hatia, angenilipa fidia kwa kitendo alichonifanyia na kufungwa jela miaka thelathini ili iwe fundisho kwa wanaume wenye tabia kama yake.
Pale kituoni nilimkuta mkuu wa kituo, nikamweleza shida yangu lakini baada ya kumtajia kuwa mhusika alikuwa Elhakimu yule Mwarabu alishituka na kutamka maneno yaliyonifanya niishiwe nguvu.
likiri wazi kuwa kama kweli mhusika alikuwa ni Elhakimu, ilikuwa ni vigumu mno kumtia hatiani kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo kwa baadhi ya viongozi wakubwa serikalini. Nguvu iliyotokana na ushawishi wa fedha aliyokuwa nayo.
Mara nyingi kila alipokuwa akifanya maovu, hakusita kumwaga fedha chafu na kuwahonga viongozi. Katika hali ya kushangaza, mkuu wa kituo alikuwa mkali na kunigeuzia kibao kwa madai kuwa huenda natumiwa na wabaya wa Elhakimu ili kumchafulia jina, kauli ambayo ilinikata maini na kunifanya nimuangalie yule mkuu wa kituo kwa jicho kali na la chuki.
"Wewe binti wewe, usitake kuhatarisha maisha yako kwa pesa ndogo na za kijinga ulizohongwa na maadui wa Elhakimu wanaotaka kumharibia sifa nzuri ya jina lake," alisema yule mkuu wa kituo kwa sauti ya ukali na kufoka huku akinikazia macho yake mekundu.
"Hapana afande, hakika Elhakimu amenibaka, tena akanitupa mtaroni baada ya kunifanyia unyama huo, naomba unisaidie ili haki itendeke na kumfikisha mbele ya sheria, naomba baba yangu," nilisema kwa sauti iliyochanganyika huruma na hasira, hakika chuki niliyokuwa nayo dhidi ya Elhakimu haikuwa na mfano wa kusimulika hata kwa chembe.
"Ushahidi wa kuwa umebakwa na Elhakimu uko wapi," aliniuliza huku akinisogelea mahali nilipokuwa nimesimama karibu kabisa na meza ya mapokezi ya kituo hicho kidogo cha polisi.
"Kama ulivyoona vipimo vya daktari hivi hapa," nikamjibu na kumyooshea kwa vidole vipimo na maelezo ya daktari aliyokuwa ameyashikilia mkononi.
"Sawa, haya ni maelezo tu nataka ushahidi kwamba aliyekubaka ni Elhakimu."
"Lakini baba, nimekuja kuripoti jinsi nilivyobakwa, pia nikakutajia mhusika sasa mbona ninageuka mtuhumiwa kwa kunihojiwa rundo la maswali magumu namna hii?" nilijikuta nikitamka maneno hayo mazito mbele ya mkuu huyo wa kituo huku nikijishangaa mwenyewe kwa ujasiri mkubwa nilioutumia.
"Kwa hiyo unanifundisha kazi siyo," akahoji tena kwa kufoka.
"Sasa sikiliza, kwa leo nafungua maelezo yako kwenye kitabu cha kutoa taarifa, yaani Reporting Book (RB)," alisema na kuchukua daftari kubwa lilikokuwa na maandishi makubwa ya rangi ya bluu kwa juu.
Kwa muda wa dakika saba, alikuwa akiandika kitu ambacho sikukijua, alipomaliza aliniangalia huku akiwa kimya.
"Haya, sasa anza kueleza upya huku nikiandika maelezo yako kwenye daftari hili."
Nikaanza kusimulia jinsi ambavyo nilikutana na Elhakimu, alivyonigonga hadi kuanza kufanya kazi hotelini kwake, nikasimulia hadi siku hiyo ya tukio ambapo alinialika kwa chakula cha jioni na kunieleza nia yake ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mimi.
Pia, nikaeleza namna ambavyo nilimkatalia kwa msimamo wa hali ya juu, hata tulivyoanza kunywa pombe mimi Redd's na yeye Grants.
Kila nilichokuwa nikieleza, yule mkuu wa kituo alikuwa akiandika na kunitazama usoni kila mwisho wa sentensi.
Baada ya maelezo, yule afande aliniambia niende nyumbani ambapo alinitaka kurudi kesho yake kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria. Akaahidi kunikutanisha na Elhakimu.
Sikujua nia na lengo la yeye kunikutanisha na Elhakimu ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mtuhumiwa wa ubakaji.
"Sasa huyu ana maana gani, kwa nini asikamatwe huyo Elhakimu ili ajibu mbele ya mahakama?" niliwaza huku nikiondoka kituoni hapo.
"Sikiliza wewe binti, hakikisha kuwa kila ulichokisema kina ukweli na uhakika halisi, huyu mtu si wa mchezo," alisema yule afande lakini sikujibu chochote zaidi ya kumkazia macho na kuanza kuondoaka kituoni hapo.
Moyoni niliamini kuwa yule afande alikuwa ni miongoni mwa watumishi wa serikali waliokuwa wakimuogopa na kumhusudu Elhakimu kutokana na jeuri ya fedha aliyokuwa nayo, ndiyo maana alikuwa akitoa kauli mbaya na chungu za kunikatisha tamaa kabisa.
Wakati nakata kona ya kuelekea nyumbani kwangu, ghafla lilikuja gari moja la kifahari jeusi lililokuwa na vioo vyeusi visivyoonesha ndani na kupaki karibu kabisa na miguu yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment