Search This Blog

Monday, 20 June 2022

SITAISAHAU FACEBOOK - 3

    https://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/11/sitaisahau-facebook.html
    Simulizi : Sitaisahau Facebook
    Sehemu Ya Tatu (3)

    Taarifa ile kila mmoja kati yangu na huyo rafiki yangu tulipokea kimshtuko. Hasahasa mimi. Nilijiuliza kwa nini? Sikupata jibu.Maisha yakaendelea!!Hapakuwa na mauzauza tena. Na kizuri zaidi hatimaye mama alizinduka kutoka katika usingizi ule wa kifo. Suzi akajivutia kwake kwamba ni maombi yamemwamsha, mimi sikuwa na lolote la kusema.Mama hakuwa na kumbukumbu yoyote ile, alibaki kushangaa shangaa tu. Kwetu ilikuwa siku ya furaha sana. furaha iliyopitiliza. Sasa mama aliweza kula peke yake na hakuhitaji msaada tena. Walau furaha yangu ikarejea huku nikisahau kuhusu imani za kishirikina na kuamini mama alikuwa katika ugonjwa wa kawaida tu!!Sasa vipi kuhusu John na ile ndoto niliyoiota? Nilijiuliza. Maana mama alikuwa amezinduka lakini John bado hakuonekana. Chuo kilishindwa kusema lolote maana mwanafunzi wa chuo kikuu anachukuliwa kama mtu mzima hakuna anayemlinda, hakuna uzio uliowekwa kumzuia asitoke, hivyo maisha ya mwanafunzi wa chuo yapo mikononi mwa msomaji mwenyewe. Chuo kitasema nini kuhusu kutoweka kwa John!! Ajabu ni kwamba hakutoweka katika mazingira yoyote yanayoelezeka bali ni ghafla tu akagundulika kuwa hayupo chuoNami nikaichukulia ile taarifa kama ilivyo. Kwanza upendo wangu kwa John ulikuwa umepoa sana. nilikuwa nimeanza kuhisi kuwa huyu si mtu mzuri kwangu.****(Mimba ya maajabu)Baada ya siku tatu. Mama akiandamana na dada yangu Suzi walirejea Makambako. Kama kawaida pesa ilikuwepo. Kwa nini sasa mama yangu asipate jambo la kukumbukwa maishani. Na Suzi naye apate la kujitambia kwa walokole wenzake. Nikawapandisha ndege. Sasa nikabaki kuishi peke yangu tena!! Sikuwa na uoga mkubwa japo sikumruhusu rafiki yangu huyu kuondoka. Tukaendelea kuishi wote.Usiku huu ambao mama yangu alikuwa ametoweka nilikumbwa na hisia ama jambo la ajabu katika mwili wangu.Kichwa kilikuwa kinauma, nilijaribu kumeza dawa lakini hazikunisaidia sana zaidi ya kuniweka katika majaribu ya kupitiwa na usingizi.“Maria!! Mi nalala shosti.” Nilimwambia rafiki yangu. Aliyekuwa amejikita katika kuangalia filamu. Hivyo hakuitilia maanani sana taarifa yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mguu na njia nikakivamia kitanda nikaanza kuutafuta usingizi. Mara hizo hisia za kuumwa kichwa zikatoweka. Nikawa katika hisia nyingine zinazokera. Nikaanza kumkumbuka sana John . nikaukumbuka usiku ule mimi na yeye katika hoteli ya kifahari. Nikakumbuka pia jinsi nilivyoanza kuishi naye kama mchumba wangu. Mara nikayakumbuka mapenzi yake.Ni hapa sasa nikaanza kuhangaika!! Nilikuwa namuhitaji John.Nilikuwa nahitaji awe nami kitandani!! Lakini hakuwepo.Nilitaka kujilazimisha kuamka niweze kukabiliana na hisia hizi lakini sikuweza. Nikahisi macho mazito sana!!Mara likawa giza nene!! Kisha ndani ya sekunde kadhaa nikajihisi kama nina mikono ya ziada najipapasa. Mh!! Nikataka kufumbua macho bado yalikuwa mazito.*****Nilikuwa nimejilaza na kanga niliyokuwa nimeivaa wakati naandaa chakula. Ile mikono ya ziada nikawa naisikia kabisa ikiiondoa bila idhini ya akili yangu!! Nikajilazimisha kuamka. Sikuweza. Sasa nilikuwa sina nguo mwilini.Kisha ile hali ya kumkumbuka John ikazidi. Nikawa katika kuhitaji huduma fulani hivi ambayo ni John pekee aliweza kunitimizia.Penzi……..Sikuchukua muda mrefu nikapata kile ninachokitamani. Lakini lilikuwa kama gogo limeniangukia kifuani. Nikaanza kupalangana kulitoa. Pumzi zikazidi kuniishia lile gogo halikutoka kifuani kwangu.Sijui kama zilikuwa dalili za kufa ama vipi.Jamani nakufaaa! Nilipiga mayowe. Sijui kama sauti ilikuwa inatoka ama la! Hofu ya kifo ikanitawala.“He!! We naye unalala uchi? Kulikoni leo?” Niliisikia sauti ikiniuliza. Nikadhani bado nina lile gogo kifuani. Nikanyanyuka kwa nguvu sana. Maria alikuwa akitazamana nami uso kwa uso. Alinishangaa nami nikamshangaa.“Unaota wewe!”“Kwani kuna nini?” Nilimuuliza huku nikijishangaa kweli nipo kitandani, uchi kabisa. Halikuwepo lile gogo pale kitandani.Wasiwasi ukatanda!“Kweli ni ndoto..ndoto mbaya.” Nilimuunga mkono Maria.****Haikuwa ndoto kama nilivyodhani na kujiaminisha kuwa ile kanga ilitoka bahati mbaya katika mwili wangu. Kichefuchefu na kukosa hamu ya kula vikaanza kuniandama, mara niwe nataka vyakula vichachu, mara nikivipata navichukia. Ile hali ikanifanya nihisi ninakaribia kuugua ama nina ugonjwa tayari. Mtu menye pesa kama mimi kwa nini niugue niendelee kukaa ndani wakati kuna hospitali zinaweza kunihudumia vyema.Majuma matatu baada ya hali ile nikafikia uamuzi wa kwenda hospitali.Sikumshirikisha Maria kwa sababu nilihisi ni jambo la kawaida sana. Nikajikokota hadi hospitali. Daktari akanipokea nikamueleza kila dalili inayonifanya nijihisi aidha nina malaria ama ugonjwa mwingine wowote ule. Sikuwaza hata kwa mbali majibu aliyoyatoa daktari.Mimba!!! Una mimba Isabela, yalikuwa majibuSijui kama akili iliniruka name nikaruka nikamkunja daktari ama ni mizimu ilifanya hivyo. Sijui!!Daktari akatapatapa akanitoa na kunituliza. Huku akisisitiza kuwa ninayo mimba. Na majibu hayo yapo sahihi. Alikuwa ameghadhabika kiasi.Maajabu haya!! Nimeipatia wapi hiyo mimba.Mimi ni muelimishaji wa mambo ya kimapenzi na mahusiano na jinsi ya kujilinda na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotegemewa. Sasa nina mimba ya maajabu!! Anayeelimisha ameibeba…..Nimshirikishe Maria? Nilijiuliza. Nikasita. Maria alikuwa mropokaji sana angeweza kunisambazia habari hiyo na heshima yangu ikashuka. Sikuwa tayari kuabika mbele ya maelfu ya wanafunzi anaoniheshimu sana.Nikimueleza mama atanilaani!! Maana alikuwa akiniamini sana, bora basi angekuwepo John ningesema ni ya kwake.Sasa hapa namsingizia nani?Hapana sina mimba mimi!! Nilijikataa penye ukweli.Nikaenda hospitali nyingine. Jibu lilikuwa MIMBA.Akili ikahama, na nikaanza kuamini kumbe ule mtihani wa mama kupoteza fahamu ulikuwa mdogo sana. kumbe tatizo likikukumba wewe ndio utaugundua uzito wake.Nikimbilie wapi Isabela mimi!!! Nilitaharuki.Hisia zangu zikaenda kwenye lile gogo usiku ule. Nikajiona nimedhalilishwa kupewa mimba na gogo.Tena ndotoni!! Chumbani kwangu.Eeh!! Mungu nionee huruma mja wako. Nilikumbuka kumshirikisha sasa Mungu. Baada ya miezi kadhaa ya raha bila kufanya ibada.*****Dada yangu Suzi. Alikuwa ni mlokole lakini licha ya hayo yote alikuwa jasiri katika kutunza siri. Hili lilifahamika kwetu sote tangu tukiwa wadogo. Alitunza siri nyingi sana kifuani mwake. Siri za baba, siri za mama, zote alizibeba bila kuzitoa. Ama kwa hakika alikuwa mtu wa kipekee mwenye kifua haswa.Nikamuona mlokole huyu ni mtu sahihi katika kumueleza linalonisibu.Nikampigia simu tukapanga wakati tulivu kabisa wa kuzungumza.Tukapendekeza iwe usiku. Mumewe akiwa ameingia kazini.Usiku ukafika nikampigia simu.Baada ya salamu za hapa na pale nikautua mzigo.“Dada, yaliyonikuta ni makubwa mdogo wako…” nilianza kumuelezea mkasa ulivyokuwa huku nikisita kumshirikisha ukweli kuwa kuna ndoto ikiambatana na hisia ilinishika na nikahisi nafanya mapenzi ndotoni. Nilihofia ataleta ushauri wa kwenda kwa wachungaji feki kuombewa. Sikutaka kabisa kusikia mambo yake ya kilokole.Nilipomaliza ukawa wakati wake kunishauri ama kusema lolote.Kwa sauti tulivu tena iliyojaa unyenyekevu Suzi alianza kunieleza neno kwa neno.Sasa nikaanza kutetemeka alipoyatamka haya. Nikaketi chini, mapigo ya moyo yakaongezeka.Nikatamani nife kwa muda. Kisha nikakumbuka kuwa nilikuwa naogopa kufa!!! Nikalipuuzia wazo hilo.Wasiwasi ukazidi. Lakini Suzi alikuwa akiusema ukweli aliouficha moyoni kwa muda mrefu.Suzi aliongea huku akitia msisitizo kwa aliyokuwa anayasema.Ilikuwa ni historia ambayo sikuwahi kuisikia kamwe lakini sasa Suzi alikuwa ananifumbua macho. Uhusiano wa matukio alivyoupangilia ulinitia katika mashaka.Wakati nampigia simu wazo langu kuu lilikuwa kuitoa ile mimba ambayo hata sikuwa na uelewa imeingia vipi katika mwili wangu. Nikamdanganya kuwa mpenzi wangu amenipachika lakini hatukuwa na mpango wa kupata mtoto katika kipindi hicho.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Bela, Bela..usije ukathubutu kuitoa hiyo mimba!!! Usithubutu!!” alinikanya Suzi, hapo ni baada ya kunieleza kuwa kila msichana aliyethubutu kutoa mimba katika ukoo wetu alipoteza kizazi ama uhai.Maneno hayo yaliambatana na mifano kadhaa ya ndugu zangu ambao hadi leo hii wanalilia watoto. Umri unakwenda na hakuna dalili ya mimba. Wengine wanaachika na kuolewa tena lakini hakuna mabadiliko. Wanabaki kuwa wapweke na kumshushia lawama Mungu. Kumbe kuna siri mioyoni mwao. Mimba zilizotolewa!!Anti Rozi, mamdogo Sikujua, hao ni baadhi ya ndugu zangu waliokuwa wakinyanyasika katika ndoa zao kwa kuwa hawazai. Na kama na mimi ningethubutu basi ningekuwa katika mkondo huo.Maneno hayo makali kutoka kwa bingwa wa kutunza siri yakanichoma haswaa.Hapana!! Sipo tayari kudhalilishwa katika ndoa. Nilikiri.Kwa maongezi yale kati yangu na dada Suzi ilimaanisha kuwa sikutakiwa kuitoa ile mimba! Mimba ya gogo! Isabela niende kuzaa gogo. Hapana!Sasa ni kipi natakiwa kufanya hapa? Nilijiuliza bila kupata majibu. Ugumba sikuutaka na hata kuzaa na gogo n’do sikutaka kabisa kusikia.Suzi akaniaga nikakata simu!!Hofu kuu ilinitawala baada ya kuwa peke yangu tena. Bado nilikuwa nimeishikilia simu na nilikuwa natetemeka sana. Ni kama dunia ilikuwa imenigeukia na kunizomea baada ya kuwa imenivua nguo zote. Niliamini kuwa dunia ilikuwa inanionea. Haikuwa inanitendea haki hata kidogo. Kwa nini mimi kila siku, kwa nini wengine wanacheka, kilio kwangu tu kila siku? Mungu alikuwa ana upendeleo ama?Nililitazama tumbo langu dogo kisha nikafumba macho na kujenga picha jinsi litakavyokuwa siku za usoni. Tumbo kubwa kabisa na kila mmoja ataliona. Aibu kubwa! Halafu pia nitachekesha kiasi fulani, nilivyokuwa cha ufupi halafu na tumbo kubwa?? Fedheha.Kama hiyo haitoshi itafikia kipindi nitaugulia uchungu na hatimaye nitajifungua. Mtoto wa nani huyu? Nilijiuliza bila kupata jawabu sahihi. Sikutaka kujipatia jibu la gogo.Mawazo yakaniumiza kichwa nikameza dawa za kutuliza maumivu. Nikasinzia!Asubuhi nikashtuka kutoka usingizini. Tatizo lilelile haikuwa ndoto, nilikuwa na mimba. Nikawaza na kuwazua bado hapakupatikana jibu sahihi. Nikajaribu kupuuzia lakini suala hili liliniumiza kichwa.Sasa nikakumbuka kuwa nilikuwa na pesa za kutosha katika akaunti yangu. Sasa kwa nini niendelee kuhangaika kiasi hiki. Ina maana pesa haiwezi kutatua tatizo hili.Nikafikiria kugawana pesa zangu na mganga mwingine wa jadi. Lakini huyu sikutaka awe anatokea hapa Tanzania. Nilihitaji mgangamwingine kabisa kutoka nje ya nchi.Sikumshirikisha Maria, maana angegundua kuwa nina mimba. Hili nililiepuka sana.Kimya kimya nikampata mganga. Alijitambulisha kuwa anatokea Naijeria. Huyu alikuwa ananifaa.Nikamfungia safari! Alikuwa amejiundia ofisi yake nje kidogo ya jiji la Mwanza, maeneo ya Shamaliwa kata ya Igoma. Nililitazama tumbo langu dogo kisha nikafumba macho na kujenga picha jinsi litakavyokuwa siku za usoni. Tumbo kubwa kabisa na kila mmoja ataliona. Aibu kubwa! Halafu pia nitachekesha kiasi fulani, nilivyokuwa cha ufupi halafu na tumbo kubwa?? Fedheha.Kama hiyo haitoshi itafikia kipindi nitaugulia uchungu na hatimaye nitajifungua. Mtoto wa nani huyu? Nilijiuliza bila kupata jawabu sahihi. Sikutaka kujipatia jibu la gogo.Mawazo yakaniumiza kichwa nikameza dawa za kutuliza maumivu. Nikasinzia!Asubuhi nikashtuka kutoka usingizini. Tatizo lilelile haikuwa ndoto, nilikuwa na mimba. Nikawaza na kuwazua bado hapakupatikana jibu sahihi. Nikajaribu kupuuzia lakini suala hili liliniumiza kichwa.Sasa nikakumbuka kuwa nilikuwa na pesa za kutosha katika akaunti yangu. Sasa kwa nini niendelee kuhangaika kiasi hiki. Ina maana pesa haiwezi kutatua tatizo hili.Nikafikiria kugawana pesa zangu na mganga mwingine wa jadi. Lakini huyu sikutaka awe anatokea hapa Tanzania. Nilihitaji mgangamwingine kabisa kutoka nje ya nchi.Sikumshirikisha Maria, maana angegundua kuwa nina mimba. Hili nililiepuka sana.Kimya kimya nikampata mganga. Alijitambulisha kuwa anatokea Naijeria. Huyu alikuwa ananifaa.Nikamfungia safari! Alikuwa amejiundia ofisi yake nje kidogo ya jiji la Mwanza, maeneo ya Shamaliwa kata ya Igoma.Nyumba yake ilikuwa nzuri sana, tofauti na wale waganga waliotangulia ambao walikuwa wakiishi katika vibanda vya nyasi huku wakiwa mabingwa wa kuomba kuku na mbuzi kama njia ya kutibu tatizo.Huyu alikuwa katika nyumba nzuri sana. Huenda na tiba yake ilikuwa nzuri.Nilipokelewa vyema na kuandikisha jina langu getini. Nikafikishwa ofisini kwake. Na penyewe palivutia sana.Alikuwa anaye mkarimani wa kumsaidia kuweza kuwasiliana na wateja wasiojua kiingereza. Mimi sikuhitaji mfasiri nilikuwa najua kiingereza hivyo tulizungumza moja kwa moja.Alinisikiliza kwa makini, miwani yake machoni. Kisha akaanza naye kunipa maelekezo.Alitoa maelekezo mengi. Mwisho akaniambia nirejee usiku wa saa mbili aweze kunipatia tiba. Wakati huo ilikuwa saa kumi na moja jioni.Saa mbili nilikuwa kwa mganga tena. Sasa alinipeleka mahali anapotolea tiba.“Una mimba ya jini..jini la hatari..na ukilitoa kwa njia ya kuzaa.UTAKUFA! hakika UTAKUFA!” Alizungumza kwa msisitizo. Nikatetemeka kusikia suala la kufa.“Hongera umewahi sana..bado halijakomaa. Sasa unatakiwa ulitoe sasa hivi. Linatakiwa kutoka.”“Nitoe!.” Nilijikuta najibu huku ninatetemeka. Akacheka.“Vua nguo zako zote.” Alitoa maelekezo.Nikasita, akacheka tena. Kisha akanitazama.“Toa nguo zako!!.” Aliamuru kwa kiingereza chake chenye lafudhi ya Afrika magharibi. Alikuwa mweusi tii.Nikasalimu amri, mtaalamu huyu ndiye aliyekuwa ameshika mpini nami mikono yangu kwenye makali. Yeye mshindi.Nikasaula moja baada ya nyingine. Nikaacha chupi. Akakoroma huku akitetemeka. Nikaiondoa na hiyo iliyobaki. Sasa nijizibe wapi? Juu ama chini nikakosa maamuzi.Nikabaki katika mfadhaiko!.“Lala hapo kitandani!” aliamuru. Nikajilaza kitanda cha futi sita kwa sita chenye shuka jeupe kabisa.Mara taa ikazimwa. Giza likatawala. Kimya nacho kikatanda. Sauti ya mganga pekee akiunguruma kwa sauti ya chini ndiyo ilisikika. Mimi hofu tupu!Mara kitandani tukawa wawili. Mikono ikinipapasa. Tiba gani hii! Nilishangaa lakini sikuuliza.Katika hali isiyokuwa ya kawaida nikapatwa na kiu kikali sana ghafla. Kiu kilichokausha koo langu kabisa.“Thirsty (kiu)….” Nilinong’ona, mganga hakujibu. Nikajaribu tena kunong’ona sauti haikutoka. Lakini sikuwa katika uhitaji wa maji ya kunywa. Kuna kitu cha ziada nilikuwa nahitaji, sijui ni kitu gani sijui!! Lakini nilikuwa nahitaji.Mikono niliendelea kunipapasa. Sasa hakuwa anaunguruma tena lakini alikuwa anahema juu juu sana. Huku napapaswa huku nahisi kiu cha ajabu.Mara yule mganga akafika kifuani akaendelea kunishambulia. Kuja kutanabai alikuwa yu uchi! Hofu ya kubakwa ikanikumba. Nikajaribu kupiga kelele. Sauti haikutoka. Nikajaribu kumsukuma, alikuwa mzito kupita kiasi. Alikuwa na uzito kama lile gogo la usiku ule. Gogo lililonitia mimba. Kiu kikanifadhaisha na sasa sikuweza kujizuia zaidi nilitakiwa kupata kinywaji. Lakini sio maji wala soda.Mganga akazidi kunikumbatia. Nikafanya jaribio la kumn’gata ili asitimize kitendo chake cha kunibaka. Maajabu!! Ile ladha ya chumvichumvi la jasho ikanipendeza, nikaitamani na nikazidi kumng’ata, damu! Damu ikaanza kumtoka, sikutaka hata tone moja linipite kando. Alijirusha rusha lakini sikubanduka. Hadi pale kiu kiliponiisha.Wakati kiu kinaisha na yeye alikuwa ametulia tuli!Nimekunywa damu!! Nilighafirika. Nikasimama wima huku nikiwa siamini kabisa kilichotokea pale ndani. Nikatapatapa katika giza mara nikabonyeza bila kutarajia kitufe. Taa ikawaka!Macho yangu ana kwa ana na dude kubwa jeusi. Asili yake Naijeria likiwa limetulia kitandani. Shuka nyeupe sana bila hata tone la damu.Dude lile lilikuwa uchi wa mnyama. Lilitia kinyaa kulitazama maungo yake.Nikajifuta midomo nikaitazama. Hapakuwa na damu!! Na sikuwa na kiu tena. Kumbukumbu za kumshambulia yule mganga wa jadi zilikuwepo akilini na pia tukio la kumnyonya shingoni lilikuwa linaishi katika akili yangu. Sasa mbona hakuna damu. Mbona mashuka hayajachafuka.Nikavaa nguo zangu huku nikiziona dalili za kufa mbele yangu.Nikamtikisa yule daktari pale kitandani. Hakuamka. Na alidumu hivyo hadi nilipotoka. Hatua kwa hatua. Hadi nikatoka nje, hofu ikiwa inaniadhibu.Sikusimama sana barabarani nikapata taksi.“Nyegezi kona.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Nyegezi?” aliniuliza. Nikakubali.Akawasha gari tukaondoka. Sikutaka kuzungumza lolote. Nilikuwa najiuliza ni kipi kinanitokea mfululizo kiasi hicho.Simu yangu ikaita. Nikaitoa nikiamini ni Maria. Hakuwa yeye alikuwa Dokta Davis.Nikachelewa kupokea. Ikawa imekatika.Nikategemea atapiga tena! Hakupiga badala yake akatuma ujumbe.,“Nakutakia usiku mwema!”Sikumjibu.****Amani ikatoweka kabisa moyoni mwangu. Sikuyafurahia maisha yangu ya chuo. Sikuifurahia tena kazi niliyopewa na dokta Davis na kampuni yake.Nikiwa nimejaribu kwa waganga na kushindwa kupata msaada wowote. Na sikuwa nikiamini sana ulokole na imani za uponyaji sasa niliamua LIWALO NA LIWE. Nitailea mimba yangu hadi nitakapojifungua.Lakini nitakuwa na amani sana iwapo sitakuwa nachangamana na makundi ya watu. Na ili nisichangamane basi nilitakiwa kuiachia kazi niliyokuwa nimeipata. Kazi yenye kipato kizuri kabisa.Nikatokwa na machozi nilipofikiria kuandika barua ya kuacha kazi!! Roho iliniuma sana.“Na chozi langu likuangukie wewe uliyeniletea makwazo haya!!” nilitamka hayo wakati naweka nukta ya mwisho ya barua ile ya kumweleza Davis na kampuni yangu nia ya kuachana na kazi yao.Sikuweza kuwaelezea kuwa nilikuwa na mimba. Niliwaambia shule imenibana sana na utendaji wangu kimasomo ulikuwa umeshuka sana.Nikaituma kwa njia ya barua pepe kwenda kwa Dokta Davis.Barua ikawa imefika!Nikayasubiri majibu.Zile milioni milioni ziliniuma sana kuziacha ziende mbali nami.Lakini sikuwa na ujanja.Laana na zitue kwa mbaya wangu!!****Zilipita siku nne, kila siku nilikuwa napitia barua pepe yangu kutazama kama kuna majibu yoyote kutoka kwa Dokta Davis lakini mambo yalikuwa tofauti Davis hakupiga simu wala hakujibu ujumbe niliomtumia. Nilijiuliza je? Nimpigie simu ama niendelee kuvuta subira. Hali hiyo ya kungoja sana ikanitia mashaka, kumpigia simu pia nikasita kwa kukumbwa na maswali mengi. Kama hajaisoma ile e-mail itakuwaje? Na kama ameisoma pia nilitegemea maswali mchanganyiko ambayo yangeweza kunitia katika majaribu ya kumweleza Davis juu ya ile mimba ya kimaajabu! Jambo ambalo sikutaka kabisa litokee.Nikaendelea kuwa kimya!Siku zikasonga mbele. Amani finyu moyoni! Maria sasa akawa kama ndugu yangu, tuliendelea kuishi wote.*****Zilipokatika siku saba za kuikamilisha wiki moja, ustahimilivu ukanishinda, mateso ya nafsi yakanikita. Ujasiri ukaikimbia subira.Nikaamua kujaribu kupeleleza, kwanini? Davis hadi sasa hajasema neno.Sijui kwanini nilikuwa namuogopa Davis kwa kipindi hicho. Lakini sikuweza kumpigia simu.Nifanyeje? Nilijiuliza!Facebook! Jina hilo likanivamia kama jinamizi linalotisha lakini lenye msaada.Kwanini naogopa? Nilijiuliza.Ilikuwa saa moja usiku, nikiwa kitandani. Mkononi glasi ya juisi, kompyuta yangu ndogo ikiwa inamalizia hatua za kuwaka. Ilipomaliza, nikaingia katika mtandao. Tangu nitingwe na kazi niliyopewa na kampuni ya Dokta Davis na matatizo yaliyokuja baadaye nilikuwa nimeususa kabisa mtandao wa kijamii wa facebook, kwanza jina langu tayari lilikuwa kubwa pale chuoni hivyo nilikuwa napata usumbufu mtandaoni, pili sikuwa na muda kuingia kule mara kwa mara. Lakini siku hii nililazimika kuingia mtandaoni.Nia kubwa ikiwa kutazama akaunti ya Dokta, ni lini mara ya mwisho kuandika kitu mtandaoni. Kama ningejua hilo ningeweza kuhusisha hofu yangu ya kwamba aidha kuna jambo baya limemkumba Davis.Mdomo ukabaki wazi, nikapumbazwa na picha iliyokuwa katika akaunti yangu! Nikaitazama kwa makini! Haikuwa ndoto! Alikuwa yeye! Sasa ni lini ameiweka hapa? Nilijiuliza!Nikataka kumuita Maria, nikagundua hatakuwa na la kunisaidia. Kwanza ye mwenyewe hana hulka na mtandao huu!Nikabaki kuishangaa picha ya John! Alikuwa anatabasamu!John alizipata wapi namba zangu za siri za akaunti yangu ya facebook? Nilijiuliza bila kupata majibu.Mh! Au hii picha niliweka mwenyewe? Lini sasa? Nikajiuliza.Kwa hili sikushtuka sana. Nikajipa moyo kuwa huenda niliwahi kuiweka hii picha ya John bila kujitambua kutokana na kukolea katika penzi. Penzi la John ambaye hadi wakati huu hakuwa akifahamika ni wapi alipo. Nikiwa nimeamua kumpuuzia John na hiyo picha sasa nikaamua kuendelea na kile kilichonifanya niingie mtandaoni.Nikataka kuifungua akaunti ya Dokta Davis niweze kuikagua.Hata kabla sijaanza kuikagua akaunti ya Dotka, nikakutana na kitu kingine cha kushangaza, hapa sasa nilijikuta naitupa laptop na kuruka mbali nayo kama nimepigwa shoti ya umeme. Ama nimeona kitu cha kushtua sana.Ilikuwa picha nyingine, hii ilikuwa ina ujumbe juu yake 'In love with the guy!' marafiki zangu walikuwa wameishambulia kwa maoni, wengi wao wakisifia picha hiyo, huyu kwenye picha naye alikuwa anatabasamu, tofauti ya picha hizi ni kwamba John alikuwa amevaa fulana yake, lakini huyu mwingine alikuwa kifua wazi.Kwa mtazamo wangu hii picha ilikuwa picha mbovu, isiyokuwa na mvuto. Hasa hasa kwangu ambaye hadi kumsifia mvulana amependeza lazima nichunguze vitu vingi, sasa kati ya hizo sifa huyu hakuwanayo hata moja.Huyu hakuwa mwingine alikuwa ni yule mganga wa kinaijeria. Kamwe nisingeweza kumsahau maana nilimuona kwenye mwanga huku lile tukio la kujaribu kunibaka kisha akatulia tuli kitandani na lenyewe lilikuwa limenasa katika kichwa changu.Tatizo!!Bado nilikuwa wima natetemeka huku nikiiogopa ile laptop.Nani ameingia kwenye akaunti yangu na kufanya haya?Ujanja wa mtu muoga ni kukimbia shari. Palepale nikaitumia kanuni ile. Nikatimua mbio nikapishana na Maria alikuwa amekamata glasi iliyokuwa na juisi nikamsukuama yeye na glasi yake.Yeye akawahi kujizuia lakini glasi ikasambaratika vipande. Nikamsikia akitoa yowe la hofu!Maria, Maria njoo!! Nilimuita wakati huo tayari nikiwa sebuleni.Maria kwa hofu akanifuata. Nikamkumbatia. Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu sana. Lakini yangu yalikuwa juu zaidi. Kila mmoja alikuwa katika kuogopa.Sikuweza kuzungumza chochote. Nikamvuta Maria tukaelekea chumbani. Nia yangu kumueleza kila kitu kilichonisibu hadi nikatimua mbio. Tulifika chumbani, ajabu Maria alikuwa anatetemeka kuliko mimi muhusika.Tulitulia kitandani, nikaisogeza laptop nikaanza kumuelekeza Maria, kile nilichokiona. Hasahasa picha ya yule mganga. Lakini sikumweleza lolote juu ya mimi kumfahamu.“Jamani Bela…wame’HACK’ akaunti yako..mbona haka kamchezo ka kawaida tu!.” Alinieleza.Ni kweli jambo hilo nilikuwa nalifahamu. Lakini huyu mganga amejuaje kuwa mimi naitwa Isabela hapa facebook? Nilijiuliza.Ok! Kama ni kweli ameingilia akaunti yangu na kunidhalilisha hivi. Naapa atakiona cha mtemakuni. Nilimuapia Maria. Wakati huo sikumbuki kuwa palikuwa pia na picha ya John.****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sikuwa katika utani. Nilikuwa nimekerwa na kitendo cha yule mganga kunifanyia huu upumbavu. Kesho yake pesa ikaongea nikawapa pesa nzuri maaskari. Nikawapa na ushahidi. Ndani ya Defender kwenda kumkamata yule mganga. Lile jaribio la kutaka kunibaka lilikuwa moja kati ya mambo yaliyonitia hasira.Niliikumbuka vyema njia na tulifika bila usumbufu.“Mzee alitutoka. Ni wiki sasa imekatika.” Mke wa mganga alitueleza kwa huzuni kuu. Moyo ukawa wa moto ghafla. Mganga amekufa!! Mbona tarehe ya ile picha na kifo cha huyu mganga vinashangaza sasa. Tarehe aliyoweka ile picha tayari alikuwa marehemu.Ewe! Mwenyezi Mungu nichukue mimi Isabela, dunia imenishinda!!! Nilisali kimoyomoyo. Mauzauza yalikuwa yamenizidi nguvu.Nilirejea nyumbani nikiwa mwingi wa mawazo. Sikumueleza lolote Maria. Nilimpita akiwa anajisomea. Zaidi ya salamu sikusema neno. Moja kwa moja chumbani nikajinyoosha kitandani nikaanza kulia.Nikiwa bado sijasinzia vizuri. Simu yangu iliita. Alikuwa ni rafiki yake na John.Kidogo nisipokee. Lakini alipopiga tena na tena nikaamua kupokea.“Mambo vipi shemu?”“Poa!” nilimjibu kwa kujilazimisha.“Sijakuelewa kabisa shem! Una matatizo gani?” aliniuliza.“Kwa nini mbona niko poa sema nimechoka tu.”“Umechoka ndo unaandika mambo gani sasa haya kwenye facebook?” alizungumza kwa hasira kidogo. Nikakaa kitako, usingizi hakuna tena!!!“Nimeandika nini kwani eeh!! Hebu ngoja.” Nikamkatia simu.Haraka haraka nikafungua simu yangu sehemu ya mtandao. Jasho lilikuwa linanitiririka. Sijui ni kipi kilikuwa kimeandikwa. Na ni nani ameandika kama ambaye ameiingilia akaunti yangu tayari alikuwa ni marehemu.“1986-201..REST IN PEACE ISABELLA” Ilisomeka hivyo katika akaunti yangu.Karibia kila mtu alikuwa anauliza kulikoni nimeandika hivyo.Lakini bora ningekuwa nimeandika mimi! Mimi hata sijaandika. Nikaanza kulia nikajigalagaza kitandani, nikavua nguo zangu. Nikavuruga nywele zangu. Nikalia kama mtoto.“Nimekukosea nini Mungu wangu eeeh!! Nimekosa nini sasa!!” nililaumu sana, uchungu ukanikaba kooni. Ukasafiri hadi moyoni, ukanisurubu kila upande. Suluba nisiyoelewa chanzo chake. Suluba kamilifu.Naelekea kuchnganyikiwa? Nilijiuliza. Lakini nikajicheka. Tangu lini mwendawazimu anautambua wazimu wake? Huenda mimi ni kichaa tayari.Munkari ya kusoma ikapotea na mitihani ilikuwa karibu kabisa.Liwalo na liwe!!Nilitamani sasa kwenda kwa viongozi wa kiroho waweze kunishauri na kuniombea kama inawezekana lakini tatizo lilikuwa katika kuwaeleza kuanzia mwanzo. Zile ndoto za John anaua na mengine yote. Niliogopa kuaibika.Nikakaa kimya na siri yangu, mateso pia yakabaki kuwa yangu!!!Nilipowaza mitihani, wazo la kuwa nina mimba pia likajileta pia katika orodha.(Sharti gumu!!)Ule ujumbe ulioonekana katika akaunti yangu, ulinishtua sana. Sasa sikuwa na ujanja tena nikafikia hatua ya kukubali kuwa yamenishinda na ninatakiwa kumshirikisha mtu mzigo huu.Kitu cha kwanza niliiondoa akaunti yangu ya facebook katika matumizi ‘deactivation’. Sikuhitaji tena kuwa katika mtandao huo. Baada ya hatua hiyo nikaandika barua ya kuomba ruhusa ya kutofanya mitihani hiyo iliyokuwa mbele yangu pale chuoni.Kwa kuwa nilikuwa nafahamika sikupata usumbufu nikapewa ruhusa hiyo upesi. Nikaamua kufunga safari kuelekea nyumbani. Lengo kuu likiwa kumueleza mama kila kitu kilichonitokea na kutishia uhai wangu. Sikuwa na ujanja mwingine.Usiku nilikuwa nimetingwa katika kujiandaa. Ni Maria pekee ambaye nilimueleza kuwa nitasafiri, na wakati huo alikuwa akinisaidia kufungasha mabegi yangu. Tayari kwa siku inayofuata.Ilikuwa saa sita kasoro dakika kadhaa. Nilitulia nikamtazama Maria na yeye akanitazama mimi. Kisha kila mmoja akageuka na kutilia maanani kile kinachosikika. Mlango ulikuwa unagongwa.Hakika ni palepale katika nyumba yangu niliyokuwa naishi.Nani huyu muda huu? Nilimuuliza Maria kana kwamba yeye alikuwa anamfahamu aliyepo mlangoni. Maria hakuwa na cha kunijibu.Nikiwa nimemshika mkono Maria tuliufikia malango, tukaulizia ni nani? Hakujibu. Tukauliza tena!! Kimyaa!!Kila mmoja akamshikia mwenzake kwa nguvu sana!!Ghafla mlango ukabamizwa kwa nguvu sana.Mungu wangu!! Watakuwa majambazi! Nilihisi.Kabla sijajua nini cha kufanya, mlango ulisukumwa bila kutoa kelele ukafunguka. Waaa!!Ghafla pakawa giza. Nikasukumwa kando na mikono ya baridi sana. Nikajaribu kupiga kelele sauti haikutoka. Nikajaribu tena sikuweza kabisa. Kisha nikasikia mlio mkubwa. Kisha kama gunia la mahindi kitu kikatua chini huku kikipiga kelele. Ilikuwa sauti ya Maria.Kama vile haitoshi nikashikwa tena na yule mtu mwenye mikono ya baridi. Akaanza kuniburuza. Moja kwa moja hadi chumbani kwangu.Akaninyanyua akanitupa kitandani.Nikajaribu tena kupiga kelele sauti haikutoka.Mara taa ikawashwa!! Chumba kikang’ara.Ana kwa ana na mtu ninayemfahamu!!Ni yule niliyemuandikia barua ya kuomba kuacha kazi!!Dokta Davis mbele yangu!!Dokta wa maajabu.Alikuwa amevalia suti nyeupe. Na hakuwa akitabasamu!!Nikajaribu kuzungumza, sikuweza!! Akacheka, nikamsikia.“Isabela……” aliponiita, nikajaribu kuitika sauti ikatoka.Maajabu haya!!“Milioni thelathini, mama yako mzazi, ama wewe!” alinieleza kwa utaratibu.Sikumuelewa. Nadhani hata yeye aliitambua hali hiyo.“Ni hivi..hadi sasa umetumia shilingi hizo…sasa unatakiwa kabla sijaweka saini yangu katika barua yako kuhalalisha wewe kuacha kazi nahitaji ufanye maamuzi. Nakupa wiki moja tu!! Uwe umerejesha pesa hizo, ama mama yako akae mbali nawe maisha yako yote na mwisho ni uchaguzi ujitoe wewe kwa usiku mmoja!!”“Usiku mmoja?” nilijiuliza. Ikawa tena kama ananisikia.“Usiku mmoja wewe na mimi na kisha nitakuacha huru na uamuzi wako wa kuamua kuacha kazi. Ole wako umueleze mtu…nitachukua maamuzi ambayo hautaamini”Sikuamini kama maneno hayo yanatoka kinywani mwa mtu huyu. Na ameweza vipi kufika Tanzania bila kunieleza. Mbaya zaidi amekuja nyumbani kwangu usiku mnene.Kabla sijamjibu lolote. Alizima taa. Kisha nikasikia mlango unafungwa. Nikaendelea kutulia kama nilivyo huku naogopa.Nilidhani yupo jirani na eneo lile. Sikuthubutu kusimama. Baada ya dakika kadhaa nikasikia hatua zikijongea kuja katika mlango wa chumba changu.Anarudi! Niliwaza nikaendelea kutulia. Jasho likilowanisha shuka zangu.Taa ikawashwa. Kwa ncha za macho nikamtazama aliyepo mbele yangu. Alikuwa ni Maria. Uso wake ukiwa umevimba.“Bela…nimeanguka mwenzako.” Alianza kunieleza. Nikageuka kumtazama huku nikipatwa na hisia za kumwogopa.“Mh!! Mbona hivyo Bela. Kimekusibu nini?” aliniuliza.Sikuwa na cha kumjibu. Nilibaki kushangaa. Maana niliamini na yeye amemuona dokta Davis lakini hakuonekana kujua lolote.Nilitamani sana kumueleza lakini hofu ya onyo la Dokta ilinitawala. Maria akanisogelea akanikumbatia. Nikahesabu alama kadhaa za vidole katika shavu lake. Huenda kabla ya kuanguka alipigwa kofi.Siku iliyofuata nilitakiwa kusafiri. Maria aliwahi sana kuniamsha lakini sikuwa na uwezo tena wa kusafiri. Onyo la Davis kuwa iwapo nitamwambia mtu yeyote atafanya anachojua.Niliunda sababu kadhaa nikafanikiwa kumshawishi Maria kuachana na safari hiyo. Alishangaa lakini hakuwa na jinsi maana msafiri nilikuwa ni mimi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Siku ya pili hiyo zikasalia siku tano Dokta afanye yake aliyoyaahidi.Bado sikuwa nimepata jibu sahihi la kumpa. Milioni alizonitajia kwa kweli sikuwa nazo hata nusu yake. Kumuondoa mama yangu katika uso wa dunia ni jambo ambalo sikutaka kulisikia.Kulala na mimi usiku mzima. Lilikuwa ni sawa na tukio la kubakwa kwa hiari. Udhalilishaji!!Nikajilaani kumuamini sana Davis. Majuto yakaninyanyasa.Bila kumuaga Maria, niliamua kutoweka pale nyumbani kwangu na kwenda kupanga katika nyumba ya kulala wageni. Maeneo ya Igoma.Nilizima simu yangu! Siku zikazidi kukatika na sasa ilikuwa imesalia siku moja ya mimi kutamka jibu langu.Nikaiwasha simu yangu!! Nikaitafuta namba ya Davis. Nikafungua sehemu ya ujumbe nikamtumia.USIKU MMOJA MIMI NA WEWE. Nitakueleza wapi nipo uje!!Ujumbe ukapokelewa! Lakini haukujibiwa!!****Siku ya tukio ikafika!! Nilikuwa najaribu kumpigia simu Dokta huyu wa maajabu nimuelekeze wapi nipo lakini simu yake haikuwa inapatikana. Nilijaribu tena na tena bado hali ilikuwa ileile.Hofu ikanitawala! Huenda Davis ameamua kufanya anachojua yeye. Vipi kama ameamua kumtokomeza mama yangu!! Nilianza kulia baada ya kufikiria hayo.Nikiwa katika kulia simu ya chumbani ilianza kuita.Nikaitazama kisha nikaipokea.“Kuna mgeni wako..”“Mgeni?”“Anaitwa Davis.” Sauti ya muhudumu ilinijibu.Kulisikia jina hilo tu. Nikakurupuka kutoka kitandani bila kujua ni wapi ninakimbilia. Nilikuwa naogopa sana jambo ambalo lilikuwa linakuja mbele yangu. Kufanya mapenzi bila hiari na kiumbe cha ajabu sana.Haya yote niliyataka mwenyewe!! Sasa nikaanza kuhisi kuwa Davis hakuwa mtu mzuri kwangu!!Davis ni MCHAWI!!!Naenda kufanya mapenzi na mchawi!!Ghafla nikaijiwa na kumbukumbuku za chapa ya shetani 666, niulipokumbuka hili nikakumbuka na mshahara wangu ulikuwa una hizi namba, hata simu ya Osmani nayo ina 666, Davis aliwahi kunitumia nauli nayo ilikuwa na 666 na sasa nipo katika chumba namba 66 namsubiri huyu mfalme wa 666Hapana! Hapana! Niliipinga nafsi yangu. Na sasa nilikuwa nimeamua kumkimbia mchawi huyu. Kuikimbia chapa ya shetani!!!Nikawa najiandaa kukimbiaNilipokishika kitasa ili kuufungua nitoke nikakumbwa na kihoro! Mlango ukafunguka kama vile ulikuwa katika kungojea amri yangu!!Niliamini kabisa si muhudumu anayeweza kuingia katika chumba cha mteja bila ruhusa. Kwa hiyo kama sio muhudumu basi angekuwa Dokta.Hakika. Alikuwa ni yeye! Nikatazamana naye ana kwa ana, akapiga hatua mbili akawa ameingia vyema ndani ya chumba. Akaufunga mlango.Alitaka kuongea jambo lakini mlango ukagongwa tena, akasita kisha akaufungua! Alikuwa muhudumu."Barcadi, na Sprite!" aliagiza Davis bila kutoa malipo ya awali. Vinywaji alivyoagiza nilijua fika ni kwa ajili yangu na yeye!Mlango ukafungwa tena.Sasa aliufunga na funguo kisha akaziacha pale mlangoni zikining'inia.Mimi nilikuwa wima mkoba begani nikitetemeka.Davis akaliendea kochi kubwa hapo chumbani akaketi. Kisha kwa ishara akaniita!Naitwa na shetani! Nilihamaki. Nikasita kwenda."Hautaki?" aliuliza, sikumjibu!. Akaitwaa simu yake kubwa ya kisasa."Tabasamu kidogo nikupige picha Bela?" alinishawishi. Sikushawishika.Alipochoka kunichekesha nisiyecheka akatoweka na kwenda bafuni. Nikabaki chumbani peke yangu! Hapo likanivamia ghafla wazo la kutoroka! Funguo zilikuwa mlangoni! Kwanini nisikimbie? Nilijiuliza. Hapo sasa ndipo nikagundua kwanini sina ubavu wa kukimbia. Huyu bwana alikuwa anahodhi maisha ya mama yangu! Mwalimu Nchimbi.Nilipotambua hilo nikafadhaika. Nikakiendea kitanda nikajitupa, nikautupa na mkoba wangu!Ilikuwa lazima nifanye mapenzi na Davis ili kuokoa maisha yake.Nilifadhaika bila kujua nini la kufanya. Mlango wa maliwatoni ukafunguliwa. Kichwa kilikuwa kizito hata kunyanyuka kushuhudia ni kimbwanga gani kipya atakizua Dokta huyu!Akajikoholesha kama anayerekebisha koo. Nikaijua nia yake! Nikanyanyua kidogo! Macho wazi!! Yowe la uoga likanitoka kwa nilichokiona.Hili lilikuwa kubwa kupita yote!Kilichokuwa mbele yangu ni kiumbe kile kile kinachoitwa Davis.Lakini sasa hakuwa na nguo. Maungo yake yote yakawa yananidhihaki, japo alikuwa mweusi tii. Lakini ule mwanga pale ndani uliniwezesha kutambua kuwa alikuwa amelowana damu katika viungo vyake vya uzazi, na hiyo damu ilikuwa mbichi na ni kama ilikuwa inaendelea kumtoka lakini ajabu haikuwa inadondoka katika marumaru!Hapa sasa nilimsahau kwa muda mwalimu Nchimbi, nikauacha mkoba nikakimbilia mlangoni.Ajabu! Ule funguo haukuwepo tena mahala pake! Dokta akacheka sana huku akinifuata kwa hatua ndogo ndogo!Nilitegemea huenda nitapoteza fahamu. Lakini hiyo haikutokea niliendelea kushuhudia kiumbe huyu akinifuata.Alipochoka kunichekesha nisiyecheka akatoweka na kwenda bafuni. Nikabaki chumbani peke yangu! Hapo likanivamia ghafla wazo la kutoroka! Funguo zilikuwa mlangoni! Kwanini nisikimbie? Nilijiuliza. Hapo sasa ndipo nikagundua kwanini sina ubavu wa kukimbia. Huyu bwana alikuwa anahodhi maisha ya mama yangu! Mwalimu Nchimbi.Nilipotambua hilo nikafadhaika. Nikakiendea kitanda nikajitupa, nikautupa na mkoba wangu!Ilikuwa lazima nifanye mapenzi na Davis ili kuokoa maisha yake.Nilifadhaika bila kujua nini la kufanya. Mlango wa maliwatoni ukafunguliwa. Kichwa kilikuwa kizito hata kunyanyuka kushuhudia ni kimbwanga gani kipya atakizua Dokta huyu!Akajikoholesha kama anayerekebisha koo. Nikaijua nia yake! Nikanyanyua kidogo! Macho wazi!! Yowe la uoga likanitoka kwa nilichokiona.Hili lilikuwa kubwa kupita yote!Kilichokuwa mbele yangu ni kiumbe kile kile kinachoitwa Davis.Lakini sasa hakuwa na nguo. Maungo yake yote yakawa yananidhihaki, japo alikuwa mweusi tii. Lakini ule mwanga pale ndani uliniwezesha kutambua kuwa alikuwa amelowana damu katika viungo vyake vya uzazi, na hiyo damu ilikuwa mbichi na ni kama ilikuwa inaendelea kumtoka lakini ajabu haikuwa inadondoka katika marumaru!Hapa sasa nilimsahau kwa muda mwalimu Nchimbi, nikauacha mkoba nikakimbilia mlangoni.Ajabu! Ule funguo haukuwepo tena mahala pake! Dokta akacheka sana huku akinifuata kwa hatua ndogo ndogo!Nilitegemea huenda nitapoteza fahamu. Lakini hiyo haikutokea niliendelea kushuhudia kiumbe huyu akinifuata.Nikawa narudi kinyumenyume hadi nikafika mwisho. Davis akazidi kunisogelea. Sasa alikuwa amenifikia!Akanishika mkono! Kiganja chake kilikuwa cha baridi sana!! Akanitazama usoni, nami nikamtazama. Akaniachia kisha akasonya kwa dharau. Akakiendea kitanda akajirusha pale!Bado mashuka hayakuchafuliwa na damu mbichi.Hakika sikuwa tayari kufanya mapenzi na kiumbe kile cha ajabu!! Niliapa!Muwasho ulianza kama wa kawaida tu katika chuchu yangu moja, nikajikuna, muwasho ukapita.Mara ile chuchu ya pili nayo ikawasha nikaikuna ikatulia.Sasa zikawa zinawasha zote kwa pamoja, muwasho usiofanana na ule wa kumwagiwa upupu. Huu ulikuwa wa tofauti. Nikatazama kitandani yule Dokta alikuwa amesinzia. Nikaitoa Sidiria yangu ili nijikune vizuri. Nikabaki bila nguo kwa juu. Nikafanya jitihada za kujikuna!! Ile hali ya kujikuna ikautwaa uoga wangu nikahamia katika hisia za raha! Raha ya kujipapasa! Mazito!Ni heri ningekuwa na mikono mitatu huenda ningeweza kuipinga hali hii. Maana sasa kati kati ya mapaja muwasho ukazaliwa. Niache wapi? Nikune wapi? Nikajiuliza.Raha ikawa karaha!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nikaanza kulia huku nagalagala chini. Nilijikunja na kujikukunjua bila mafanikio! Nilihitaji msaada wa hali ya juu! Msaada wa kukunwa!Mara kama ameshtuka ndotoni yule kiumbe pale kitandani aligutuka. Akasimama akanitazama kisha akachuchumaa. Akanisogelea karibu zaidi. Sikuwa na nguvu mwilini.Hakuwa na nguo nami sikuwa na nguo!Kama vile alijua ninapowashwa! Akaanza kunikuna kwa namna ya kupapasa! Nikahisi raha ya kipekee ambayo sijawahi kuipata duniani. Bila kujitambua nikamkumbatia Dokta Davis.Akaendelea kunikuna! Sasa nilikuwa hoi.Fanya unalotaka! Ndivyo ningeweza kusema kama angeniuliza.Lakini hakuniuliza!Nikajikuta katika ulimwengu wa mahaba mazito! Kama kukunwa hakika nilipata mkunaji!Muwasho ukatoweka kabisa. Jasho mwili mzima.Nikapitiwa na usingizi kutokana na uchovu.*****Saa kumi na moja alfajiri hapakuwa na Dokta wala nguo zake pale ndani. Nilikuwa peke yangu.Maumivu kifuani kama niliegemezewa gogo! Maumivu haya yakanikumbusha ndoto za kuota nazini na gogo!Nikashtuka! Mbio mbio bafuni nikatapika!Kumbukumbu ya kufanya mapenzi na Davis usiku uliopita ilinijia kichwani!Yupo wapi sasa shetani yule? Nilijiuliza.Ile hali ya maungo ya Davis kuwa na damu ilinisisimua na kujiona kuwa sina thamani tena ulimwenguni.Kama sina thamani, bora nife! Niliamua!Nitakufa vipi sasa? Hilo likawa swali la kujiuliza. Nikayakumbuka maneno ya dada Suzi. Kuhusu utoaji mimba na madhara yake!Nikafikia maamuzi ya kutoa mimba! Kisha nitajua nini cha kufanya!Wakati natoka pale chumbani na kupita mapokezi nilikumbana na swali, "mwenzako bado yupo? Maana tunataka kufanya usafi". Mwenzangu? Mwenzangu nani? Wanamaamisha Dokta Davis. Sikuwajibu nikajongea na kupotea eneo lile.Nikaamua kurejea nyumbani kwangu. Tayari nilikuwa na taarifa kuwa mama anaendelea vizuri kiafya!Tumbo! Tumbo! Tumbo lilianza ghafla kuniuma, upande wa kushoto!! Nililalamika sana, dereva wa teksi akaegesha pembeni akaniuliza kulikoni.“Nipeleke hopitali!! Nipeleke nitakulipa” nilimsihi huku nikizidi kuugulia.Kama nilivyoomba akaendesha hadi hospitali iliyokuwa jirani. Alikuwa ni kati ya masalia ya watu wakarimu waliobaki hapa duniani. Aliwahi kuwaita manesi. Japo walichelewa lakini walikuwa kunibeba kutoka ndani ya gari lile.Moja kwa moja nikakimbizwa wodi ya wanawake!!Nikapatiwa huduma ya kwanza!!Baada ya muda damu ikaanza kunitoka!! Nilikuwa nimeingia katika siku zangu ama? Nilijiuliza bila kupata majibu!! Mjamzito naingia katika siku zangu!!Kadri damu ilivyokuwa inavuja ndivyo maumivu yalizidi kupungua na hatimaye kuisha kabisa.Majibu ya daktari yalikuwa kwamba. Ni tatizo la kawaida tu kwa mwanamke kuumwa tumbo akiwa anaingia katika siku zake. Lakini mimi nilikuwa mjamzito sasa!! Au mimba imetoka. Sikutaka kuondoka na dukuduku. Nilimvuta daktari tukazungumza kinagaubaga.Akafikia hatua ya kunipima ujauzito!!Hakuchukua muda mrefu akarejea. Alikuwa hajachangamka na ni kama alikuwa na jambo anahitaji kunieleza.“Ina miezi miwili sasa!!.” Aliniambia katika namna ya mshangao.“Ni maajabu wewe kuingia katika siku zako!!” aliendelea. Mimi nikiwa msikilizaji.“Kwa hiyo ni nini Dokta.”“Rudi baada ya siku saba. Kama ikiendelea hivyo. Ama la basi utakuwa mshtuko tu.” Alimaliza.Nikaondoka zangu huku nikiitazama dunia jinsi inavyonizomea.****Maria hakushangazwa na hali yangu ya kuvuja damu!! Aliamini ni kawaida tu kwa msichana. Hakujua kama nina mimba!!Siri nikabaki nayo. Mimi na daktari!!Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu….damu zinaendelea kuvuja tena bila kukoma!!!! Kazi ikawa ipo kwangu kila mara kubadili nguo zangu.Siku ya nne, ya tano….bado tatizo likawa lile lile. Mateso sasa!!! Mimba gani hii!!!Sikuingoja siku ya saba ifike. Nikarejea hospitali.Daktari alinipokea vizuri. Nikampa kwa siri kiasi fulani cha pesa ili aweze kunihudumia kwa upendeleo.“Hadi leo bado damu inakutoka?” alishangaa daktari. Nikamthibitishia kuwa bado zinatoka tena mfululizo.Akakuna kichwa chake chenye mvi nyingi kasha akahamia kidevuni. Na penyewe akajikuna kwa muda.“Hebu njoo…” akanipeleka katika chumba kingine. Akanipima tena mimba.Daktari akashtuka!!!“Kwa mara ya kwanza katika miaka yangu 20 ya kazi!!!” alihamaki.“Nini? Nini dokta.” Niliuliza.“Wiki iliyopita ilikuwa na miezi mingapi vile.”“Miwili ulisema.”“Sasa imefikaje miezi sita leo???” aliniuliza. Nikahisi kuzizima. Nikakaa chini!!!Daktari naye alikuwa ana hofu!!****Ni kama daktari alikuwa haamini ambacho amekiona, katika mwili wangu na alichokuwa akifanya pale ni kunitoa tu katika hofu. Mabadiliko ya mimba yangu yalimfanya achanganyikiwe.Tulirejea katika chumba chake cha ofisi. Mazungumzo yaliyokuwepo ni juu ya kuitoa mimba ile.Daktari alikataa kata kata akidai kuwa mimba ikifikisha miezi sita na msichana akijaribu kuitoa basi lazima atapatwa na matatizo na kuna uwezekano wa kufa.Maelekezo ya daktari yaliyoambatanishwa na neno KUFA yalinipa ahueni ya nafsi kwa sababu nilikuwa nataka kufa. Sikuwa na ujasiri wa kujiua na hakika nilikuwa naogopa kufa.Lakini kufa kwa namna anayoitaja daktari hata hakunipa hofu badala yake nikavutika na kumsihi anisaidie kuitoa ile mimba.Mazungumzo yalikosa kabisa muafaka. Daktari yule alikuwa mbishi sana hakutaka kushiriki katika utoaji mimba huu. Nilipoona daktari huyu amekuwa na msimamo sana niliamua kutumia njia fulani ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Nikaangusha mezani shilingi laki mbili. Akazikataa, nikaaga nikatoka. Niliporejea niliziongeza zikafika laki nne.Daktari akazikodolea macho, kisha akatazama kushoto na kulia.“Umekuja na nani?” akaniuliza.“Mwenyewe!” nikamjibu. Akatazama tena kushoto na kulia kisha akazikwapua zile pesa akazizamisha katika sehemu zake za siri. Nikakwepesha macho.Akanifanyia ishara ya mkono. Nikamfuata hadi katika chumba kilichokuwa na harufu kali ya madawa. Akakifunga na funguo tukabaki wawili tu! Kimya.Daktari alikuwa na hofu. Nililitambua hilo. Sikutaka kuuliza chochote.“Toa nguo zote.” Aliniamuru. Kauli yake ikanikumbusha kauli ya yule Mnaijeria aliyetaka kunibaka kwa kujifanya ananifanyia tiba ya asili. Huyu sasa alikuwa daktari, nikaamua kucheza pata potea. Kwanza nilikuwa natokwa damu. Sidhani kama angeweza kujaribu kunibaka.Nikaziondoa zote, wakati huo yeye alikuwa amejikita katika kuchanganya madawa yake ambayo sikuelewa kazi yake ni ipi. Nikabaki kumsubiri.Njoo hapa!! Aliniamuru huku akinielekezea kitandani.Geuka hivi!! Nataka kukuchochoma sindano. Nikageuka huku nikiwa katika uoga. Kifo! Nilikuwa naogopa kufa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nikahisi kitu cha baridi kikinipapasa. Nikauma meno yangu kungoja uchungu wa sindano. Nilingoja huo uchungu lakini hamna nilichohisi.“Acha kujikaza wewe sindano itakatikia ndani.” Alinigombeza daktari. Nikashangaa hizo lawama zinatoka wapi wakati mimi hata sijajibana. Alipoona simjibu kitu akanichapa kibao. Nikashtuka.“Mkubwa hivyo unaogopa sindano alaa!!” alinigombeza. Sikumjibu!!Nikatega tena aweze kunichoma!! Hali ikawa vile vile.“Sasa mimi nakuchoma hivyo hivyo.” Alichukua maamuzi yake binafsi.Nikageuka. Nikayasubiri maumivu!!Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.Kisha nikamfuata hadi ofisini!“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”“Wenzangu? Wapi”“Mnaomtumikia”“Nani?” nilihoji kwa hofu.“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.“Daktari sijui lolote mbona.”“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.Kisha nikamfuata hadi ofisini!“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”“Wenzangu? Wapi”“Mnaomtumikia”“Nani?” nilihoji kwa hofu.“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.“Daktari sijui lolote mbona.”“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.“Ndio maana nimejishangaa sana, iweje leo nikubali kuchukua rushwa, nikubali kutoa mimba msichana. Ama kweli kila mwenye alama hii hatakataliwa na dunia kwa lolote.” Daktari alinong’ona kama anasema mwenyewe vile. Nilisikia kila kitu.Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa!“Nitakusaidia.” Alinyanyua uso daktari akanieleza huku akinitazama vyema usoni.Nilifarijika sana kusikia maneno yale. Kisha akaendelea, “Lakini uwe mkweli kwa kila kitu. Ukijaribu tu kuficha lolote lile. Nasema ukijaribu kuficha lolote lile. Wewe, marafiki na ukoo wako wote utatokomea. Mimi nakueleza haya kama mzee wako, katika kipindi changu cha miaka ishirini ya udaktari nakutana na matukio mengi. Lakini hili ni la tatu katika maisha yangu. Wenzako wawili, mmoja miaka saba imepita na mwingine mwaka juzi, nilitaka kuwasaidia lakini wakaleta ujanja ujanja. Tuliwazika!! Aah!! Hatukuwazika insearch labda niseme tuliyafukia mabaki yao.” Alimaliza kunielezea kisha akashusha pumzi kali sana.Macho yangu nilihisi kama yanajilazimisha kutazama mbele. Machozi yalikuwa yamezidi. Mapigo ya moyo yalikuwa juu, sasa nikaanza kuamini niliyokuwa nayatazama katika filamu za kinaijeria. Kumbe uchawi upo? Hakika uchawi upo!!“Kesho njoo!!” alinipa ahadi hiyo.“Kwa hiyo sitatokwa damu tena?” niliuliza swali la kijinga.“Kwani mimi ndiye niliyekuwekea” Daktari naye akanipa jibu la kijinga kama nilivyotegemea.“Usimwambie mtu yeyote kuhusu maongezi haya.” alinionyaNikaaga! Kiguu na njia hadi nikaipata taksi.Njia nzima nilikuwa nawaza na kuwazua. Zile ndoto zangu za kumjengea mama nyumba nzuri, wadogo zangu kusoma shule za kimataifa, mimi kuwa maarufu zaidi chuoni, ndoto za kwamba nataka kuwa mtakatifu! Zote zilikuwa zimekufa. Sasa nilikuwa nahangahika huku na huko huku nikisurubika na mateso ya nafsi.Swali likajengeka katika kichwa changu. Dokta Davis linizuia nisimueleze mtu kuhusu mambo haya. Sasa daktari ananisihi nisifiche kitu. Hapa sasa nimuamini nani? Nilijiuliza.“Kata kushoto!!” nilimuelekeza dereva.Mawazo yangu yakawa yameishia hapo.Maria aliniona kuanzia mbali. Akanikimbilia, akafika akanikumbatia.“Da Bela jamani. Mbona mnyonge hivyo!.”“Nimemkumbuka sana John.” Nilidanganya, huku siri kubwa nikiwa nayo mwenyewe.Maria akaniongoza hadi ndani. Nikajibweteka kwenye sofa sebuleni. Maria akaniletea maji ya matunda niliyokuwa nayapenda, nikayagida kwa fujo kisha nikagundua kuwa nilikuwa na njaa. Chakula kilikuwa tayari!! Maria akanihudumia. Sasa niliweza kupumzika!! Sikutaka kwenda chumbani. Nililala sebuleni.Kila baada ya masaa kadhaa nilikuwa naamka na kubadilisha pedi na nguo ya ndani kisha kuoga. Hali hii japo ilikuwa haijatimiza hata mwezi kwangu ilikuwa mateso makubwa. Sasa sikuweza kwenda kwa marafiki wala nisingeweza kwenda. Nilijihisi ninanuka, japo Maria hakuwa ameniambia hata siku moja lakini nilijijua mwenyewew kuwa sikuwa kawaida hata kidogo.Siku hii ikamaliza bila tatizo!!(Mateso ya 666)Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi sana kuamka. Badala ya kumuomba Mungu anijalie uzima na aniepushe na matatizo haya mimi niliwekeza imani yangu yote iliyosalia kwa daktari yule ambaye hadi sasa sikuwa namfahamu jina lake.Saa nne kamili asubuhi. Nilikuwa katika mlango wa kuingia ofisini kwake. Japo kulikuwa na watu kadhaa waliohitaji kuonana naye. Mimi nilipewa kipaumbele, nikawapita nikaingia ndani.Ahaaa!! Binti! Vipi kwema? Alinichangamkia sana. Nikamjibu salamu yake. Nikakaa kitako kumsikiliza.“Ngoja niwaondoe hawa watu hapo nje. Wewe nitakupigia simu uje mahali.” Alininong’oneza. Nikamuelewa nikampatia namba yangu ya simu kisha nikaaga.****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sikuchoka kusubiria. Japo alichukua muda sana. Baada ya masaa mawili na nusu. Aliniita odisini kwake. Nikaenda upesi nikamkuta akiwa pamoja na mwanaume ambaye laiti kama ningekutana naye wakati ule ambao nilikuwa na jeuri ya pesa sidhani kama alikuwa na hadhi ya kupokea salamu yangu. Nilimsalimia kwa kuwa tu alikuwa pamoja na daktari.Nilipomsalimia badala ya kunijibu, akanikonyeza!! Nikataka kusonya nikasita.Kwa ncha za macho yangu nikamtazama mwanaume huyu, kuanzia mavazi yalivyochoka, amechakaa nywele zake na hata ngozi ilikuwa imepauka. Nikaamini hata akili yake haiku sawa. Nilipokumbuka jambo hili la akili kutokuwa sawasawa nikaamini atakuwa ni mgonjwa wa akili. Na daktari huyu alikuwa katika kumpa tiba. Kimoyomoyo nikamsamehe kwa kosa la jinai alilofanya la kunikonyeza.“Binti..kama nilivyokueleza jana!! Usisite kuusema ukweli wote. Ukificha haitakusaidia kitu zaidi ya kuuangamiza ukoo wako wote.” Alinieleza kwa utulivu. Yule tahira akacheka.“Sawa daktari.” Nilimjibu. Tahira akacheka tena!! Akaanza kunikera.“R.I.P mtu wako niliyekwambia ndio huyu.” Sasa daktari hakuwa akizungumza na mimi, bali alikuwa akisemezana na yule tahira. Nikashtushwa na hali ile, ina maana ananikabidhi mimi kwa yule chizi au alikuwa anamtania. Niliomba iwe hivyo lakini haikuwa. Alimaanisha.Sasa tahira akanivagaa akanishika mikono. Nikajitoa mikononi mwake akacheka!!“Nenda naye ofisini kwake huyo akakupe maelekezo. Anaitwa R.I.P”“Na yeye anaitwa nani.” Yule mtu niliyedhani ni tahira sasa aliuliza.“Jitambulishe binti.” Tahira alinieleza huku akinishika makalio. Kidogo nimtukane. Nikasita baada ya kuona daktari hakushtushwa na jambo hilo.Nitafanya nini sasa!! Nikaanza kufuata uelekeo alionipeleka. Mara kwa mara alikuwa anacheka. Tulipishana na watu wengi lakini hakuna aliyemshangaa. Huyu sio tahira!! Nililazimika kuaminiMlango ukafunguliwa nikaingia ndani!! Ofisi yake ilikuwa na hewa nzito sana ya madawa lakini yeye aliifurahia.Karibu ukae…aaah!! Usikae kwanza hebu njoo huku.” Akanivuta kwa nguvu, nikamfuata. Akafungua kabati moja kwa fujo.Mungu wangu!! Maiti!! Nikaruka pembeni, akacheka!!“Binti hawa nao walikuwa wajing wajinga tazama….njoo..njoo” akaniita. Nikasogea.Akavuta kabati jingine likafunguka.Maiti ya mwanamke. Akamgeuza. Alikuwa na alama ya 666 katika makalio yake. Maiti huyu nilikiri kuwa kabla ya kuwa hivi alikuwa mrembo sana.Sijui nini kilimuua maskini!!Akanipeleka katika kabati jingine akavuta tena. Akatoka mtoto mdogo. Hana kichwa na y eye ana alama ya 666..R.I.P kazi yake ilikuwa kucheka tu kama tahira. Wakati mimi nilikuwa katika hofu kuu.Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa. Maiti karibia tano zilikuwa pamoja nasi, waziwazi. Amani ikatoweka moyoni.“Na wewe ukificha neno lolote tu!! Utakufa na vizazi vyote vitakavyofuata.” Aliongea bila kucheka sasa.Nilikuwa natetemeka.“Hata huyo uliyemkalia na yeye nadhani ni walewale..hebu funua.”“Wapi?” nilimuuliza, likiwa neno langu la kwanza hapo ndani.Akanionyesha kwa kidole. Ni pale nilipokuwa nimekaa. Nikafunua nikiwa natetemeka.“Mamaaa!!” nikapiga kelele. Kumbe nilikuwa nimekaa juu ya maiti. R.I.P akacheka sana!!Zile dharau zangu zikawa zimeishia hapa!! Nikamuheshimu!!!R.I.P hakujali kama nilikuwa nimeshtuka ama la! Aliendelea kuongeaongea huku akiwatukana matusi mazito ya nguoni wale maiti kama vile wanamsikia. Hakika alifanana na mtu aliyerukwa akili. Kuishi na maiti napo kazi sana huenda ndo maana amechanganyikiwa.“Ulisema unaitwa nani vile.”“Naitwa Isabela.”“He!! Unaitwa Isabela, yupo mwenzako humu hebu njoo umuone.” Akanivuta kwa kutumia nguvu sana hadi mkono ukashtuka. Yeye hakujali hayo. Akanivuta vuta hadi tukafikia kabati jingine. Nikajiandaa kushuhudia maluweluwe mengine.“Hili nalo lilikuwa linakula nini sijui likanenepa hivi. Majitu mengine mapumbavu sana ujue. Heri yako wewe haujanenepa sana.” Alizungumza peke yake.Akatumia mikono miwili akavuta. Likatoka bonge la mwanamke. R.I.P akaanza kucheka, kicheko kikubwa hadi akatoa machozi.“Anaitwa Isabela huyu, mpumbavu sana huyu alienda kunenepeana huko. Amewasumbua sana siku ya kumleta humu ndani. Kuna vindugu vyake, vyembamba hivyo basi likawa linawaponyoka. Linaanguka puu!!”alisimulia huku anacheka. Mimi sikuwa namuelewa.Kisha tukarejea tena mahali tulipokuwa nikalazimika kukaa juu ya lile jokofu la kuhifadhia maiti.“Au nimlete Isabela make nae, Isabela bonge.” Aliniuliza. Mimi nikawa namshangaa. Yaani alikuwa kama mpumbavu fulani.“Isabela….umewahi kufa wewe?” aliniuliza.Swali gani sasa hili la kijinga!! Nikawaza.“Bado”“Mwenzako niliwahi kufa. Na wewe una hamu ya kufa.”He!! Umewahi kufa….kivipi.”“Kwani mtu akifa anakuwaje?” aliniuliza, sikujibu.Akaendelea, “hebu tuachane na hayo..msichana mdogo kama wewe ukifa sio vizuri ujue.”“Kama ukiwa makini hautakufa. Tena wewe hautakufa, nitakusaidia usife sawa!!”“Sawa!!” nilijibu kwa nidhamu kubwa.“Njoo huku…”Nikamfuata hadi mahali patulivu kabisa. Sasa hii ilikuwa ofisi kweli. R.I.P akanipokea. Akaniacha ofisini kwa muda, kisha akaingia tena baada ya dakika kadhaa.Hakuwa yule tahira, hakuwa mchafum,chafu kama nilivyokueleza mwanzoni. Huyu alikuwa na hadhi ya yule mvulana ninayemuhitaji. Alikuwa mtanashati.Hakuwa akicheka hovyo! Alikuwa makini na mtaratibu.Roho Iliyo Potea (R.I.P). Alianza kwa kujitambulisha jina lake halisi. Kisha akaniupongeza sana kwa ujasiri wangu hadi kufika hapo.Akajieleza kwa ufupi maisha yake ya utafutaji huku na kule hadi alipojikuta akitafuta kwa njia za mashetani. Ni katika maelezo haya alinieleza juu ya namba 666. Nilishangazwa sana na maelezo yake lakini nilipiga moyo konde nikiamini tiba ipo.Baadaye akanieleza jinsi alivyojitoa katika harakati hizo za kumtumikia shetani. Haikuwa njia rahisi. Aliwapoteza ndugu zake kadhaa lakini mwisho akawa amejikomboa.Hiyo chapa uliyopigwa lazima ifutwe! Ni njia hiyo tu ya kukukomboa kutoka ufalme huo.Nilikuwa makini nikimsikiliza.!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog