Simulizi : Mwanamke Mwenye Kovu Jeusi
Sehemu Ya Nne (4)
Niliingia mule kwenye ile ofisi na kumkuta Yule mhariri ambaye alikuwa kijana wa makamo tu kama
mimi, tulisalimiana kisha nikamwambia ya kwamba nilikuwa nahitaji maelezo ilikuwaje mpaka
wakaniweka kwenye habari mbele kwenye gazeti lao bila hata ya mimi kuniuluza, alionekana kujaa
wasiwasi na woga hasa baada ya kuona mimi nilikuwa serious huku nikiwa sicheki ili kuonyesha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
msisitizo
Alianza kuniambia ya kwamba zile habari pamoja na picha wao walitumiwa na mwandishi mmoja
kwa njia ya barua pepe aliyejitambulisha kwa jina la “ mwanamke mwenye kovu jeusi”.
Niliguna kisha nikamwambia aendelee kunipasha, aliendelea kuniambia ya kwamba Yule mwandishi
wa habari aliwatumia ile habari huku akiwa ameambatanisha na namba yake ya simu basi wao
walichokifanya ni kumpigia simu na kumuuliza ili kupata uhakika zaidi ambapo aliwambia ni kweli
kabisa, nilimkatisha kisha nikamuuliza “ je ile ilikuwa ni mara ya ngapi kwa yule mwanamke
kuwapatia habari”
Aliniambia ya kwamba ilikuwa ni mara ya kwanza nay a kuwa Yule dada ni mwandishi wa habari za
uchunguzi ndivyo yeye alivyodai ndio maana hata jina lake hakutaka lifahamike. Nilisononeka sana
baada ya kusikia vile nilijua Yule mwanamke amefanikiwa kunivuruga kabisa kuanzia kwenye jamii
hadi kazini kwangu.enhe unaweza labda kuniambia huyo mwanamke mmeshawahi kufanya nae kazi
labda na pia yupo vipi mounekano wake? Halafu anakaa wapi? Nilijikuta namuuliza maswali
mfululizo bila hata ya kusubili nijibiwe, Yule mhariri alijiua fika jilikuwa nimepaniki kwani alianza
kunishusha hasira zangu kwa maneno yaliyojaa samahani na utetezi mwingi ili nisimchukulie hatua
yoyote , tulijaribu kupiga ile namba aliyokuwa nayo ya Yule mwanamke lakini haikupatikana, baada
ya kumaliza kupiga ile simu nilimwambia Yule mhariri awe makini na kazi yake kama miiko ya kazi
yao imewashinda basi aachane na hiyo kazi akatafute kazi nyingine. Niliondoka pale ofisini huku
hasira zikiwa zimenijaa sana kifuani kwani mpaka pale Yule mwanamke alikuwa amefanikiwa vizuri
sana kunipotezea mwelekeo alionekana Yule mwanamke alikuwa ni mtu mjanja sana huku akiwa ni
mtu mwenye mbinu mbalimbali ili aweze kufanikisha malengo yake.
Kule kusimamishwa kazi kwa muda usiojulikana kusema kweli kulinichanganya sana nilijaribu
kuwasiliana na Amina na Gerald ili wanieleze ni kipi kilikuwa kinaendelea, lakini wote walionekana
kama vile walikuwa wakinikwepa, nilijihisi mnyonge sana kwa kutengwa kwa sababu zisizo na
maana nilijua watakuwa wameamliwa vile na mkuu wetu wa kazi eti kwa lengo labda siri zisivuje
kwani walidai mimi nilikuwa na uhusiano na Yule mwanamke mwenye kovu jeusi. Nilikaa wiki nzima
nyumbani bila hata ya kwenda popote nikisubilia labda nitaitwa kazini lakini ilikuwa tofauti mwisho
nikaamua ni bora niende nyumbani Tanga nikapumzike na kusalimia wazazi kwani kuendelea kukaa
Dar es salaam nilikuwa nazidi ku kuweka matatani maisha yangu bila ya sababu za maana.
Basi siku iliyofuata nilianza safari ya kuelekea nyumbani kwetu Tanga ambapo nilipanga niende
nikapumzike angalau kwa muda wa wiki nzima kupumzisha akili huku nikiwa nasubili hatima yangu
kazini nilondoka mida ya saa 6 hivi kwani Tanga sio mbali sana tena kwa mimi ambaye nilikuwa
natumia usafiri wangu binafsi isingeweza kuchukua zaidi ya saa 4 kufika Tanga mjini maeneo ya
chumbageni ambapo ndipo wazazi wangu walipokuwa wakiishi niliwachukulia wazazi wangu zawadi
ndogo ndogo kwa maana ingekuwa ni aibu kwenda nyumbani nikiwa sina hata zawadi ya
kuwapelekea wazee kwani ilikuwa imepita zaida ya miezi ita bila ya mimi kwenda Tanga kwani mara
ya mwisho nakumbuka ilikuwa kwenye msiba wa mtoto wa mama yangu mdog ambapo napo nilienda
lakini sikukaa sana kwani ofisini nilipewa likizo ya siku mbili hivyo basi nilienda kuzika na kuludi tu.
Nilianza safari yangu taratibu sana kwani nilijua hiki kipande cha Dar es salaam mpaka chalinze
huwa kinakuwa na magari mengi sana hivyo sikutaka kwenda mwendo wa kasi bure nisije kupata
ajali ya bila kujitakia wakati naendelea kuendesha gari iliingia meseji kwenye simu yangu lakini
sikutaka kuisoma kwanza kwani nikiwa naendesha gari hasa kwenye barabara kubwa kama ile
morogoro road huwa sipeni kabisa kusoma meseji au kabisa hata kuwasiliana na mtu yoyote na simu
ili kujiepusha na ajali zisizo na ulazima niliendelea na safari yangu huku nikiwa naskiliza nyimbo ya
zilipendwa ya otto jazz ambao siku hizi wanaitwa msondo ngoma wosia kwa watoto, kwani ule
wimbo mara zote ulikuwa ukinikumba enzi za zamani wakati baba yangu bado anafanya kazi katika
mashamba ya mkonge kule hale muda mwingi alikuwa akiludi toka kazini basi alikuwa anawasha
redio yake ya kanda kisha anauweka ule wimbo na kuniita mimi niusikilze,basi kwa kuwa nilikuwa
naelekea nyumbani kila nilivyokuwa nausikiliza ulikuwa ukizidi kunipa hamu ya kufika nyumbani.
Nilipofika chalinze nilipaki gari njiani kwa ajili ya kununua bidhaa zingine za kwenda nazo nyumbani,
wakati wale wafanya biashara wakiniwekea zile bidhaa kwenye gari ndipo nilipokumbuka ya
kwamba kuna kipindi kuna ujumbe wa meseji uliingia kwenye simu yangu ya mkononi nilikuta ni
ujumbe wa meseji kutoka kwa Yule mwanamke mweye kovu jeusi kama kawaida yake lakini akidai
ya kwamba mpaka mimi ndio nilikuwa hatari katika kumfuatilia hivyo amejitahidi kunidhibiti kama
niliendelea tena basi atanitoa uhai,niliguna huku nikiwa na hasira sana huku nikijiapiza nitakapoludi
Dar-es-salaam nitaanza kumtafuta mwenyewe kwa siri nilitangaza kisasi nay eye mpaka nimpate
kama ni uhai basi na mimi anitoe niliwasha gari nakuendelea na safari yangu taratibu sana.
*******************************
Nyumbani niliwaelezea kisa chote ambapo walinionea huruma sana kisha mama akaniambia inanibidi
niwe makini sana na watu wa mule ofisini kwani inawezekana kabisa tukawa tunachezeana mchezo
kwa sabau ya wivu na kuona jinsi labda nilivyokuwa makini sana katika kazi zangu.sikiliza
mwanangu katika hizi ofisi watu hawapendani kabisa bora utambue hilo huwezi jua itakuwa labda
wametumia kigezo hicho ili kukuondoa ofisini alinieleza mama yangu huku tukiwa tumekaa
varandani jioni tukinywa chai kwani nyumbani kwetu tulipenda sana kunywa chai jioni pamoja na
chapatti mihogo,bagia,na nyama ya kusaga,basi pale mama alinihusia mambo mengi sana moja wapo
likiwa ni kuoa kwani umri ulikuwa unanitupa mkono sana, alivyozungumza vile nilimkumbuka sana
Jamila mwanamke shupavu ambaye tulikuwa tukifanya nae kazi lakini ilikuwa muda sasa akiwa
masomoni akiwa ameenda kuoneza ujuzi wa elimu yake, nilimkumbuka kwa sababu alikuwa
mwanamke mzuri sana mwaminifu mwenye heshima huku akiwa ni mtu aliyenijali sana japo kila
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilipomuomba tuanzishe uhusiano alikuwa akikataa bila ya sababu za muhimu eti ya kwamba
alikuwa akinionea huruma.
Usiku ule nilijaribu kumuandikia barua pepe kwani ndio nji niliyokuwa naitumia kuwasiliana naye
huku nikimpa mkasa mzima ulionikuta,nililala siku hiyo usiku sana kwani kwani muda mwingi
niliutumia kuwa kwenye net huku nikifungua kurasa mbalimbali kusoma njia mbalimbali za
kiitellejensia zilizokuwa zinatolewa kwa njia ya mtandao nilijikuta nikijifunza njia mbalimbali za jinsi
ya kuchunguza na kufuatilia uhalifu ambazo kwangu niliona zingenisaidia sana .
Kesho yake baada ya kumaliza mizunguko ya hapa na pale huku nikipita sehemu mbalimbali kuona
jinsi mkoa wangu wa Tanga ulivyokuwa umebadilika kwani sikuwa nimepata kwa muda
mrefu,nilizunguka sana kwa kutumia gari yangu huku nikiwa na mdogo wangu wa kiume William,
Jioni nilimwambia sio mbaya kama tukielekea raskazoni ambapo ndipo palikuwa na beach nzuri
twende tukapunge upepo maana pia sehemu zile nilikuwa na muda sana sijapata kuhudhuria kwani
kwa Dar-es-salaam muda mwingi nilikuwa nakuwa bize sana kaziBasi tuliona kuingia katika beach za
Kiswahili isingekuwa vizuri sana hivyo basi tukaona ni bora tuingie Mkonge hotel ambapo pale
tulikuwa tukipigwa na upepo moja kwa moja wa bahari huku tukiziona meli zilizokuwa zikiingia na
kutoka katika banadri ya tanga tulikaa pale huku mdogo wangu yeye akiwa anatumia kilevi ila mimi
sikutaka kunywa kwani akili yangu ilikuwa bado haijakaa sawa tuliendela kukaa pale huku nikitumia
muda ule kumshauri mdogo wangu kwani nilipata malalamiko kutoka kwa mama kuhusu baadhi ya
mienendo yake wakati tunaendelea na mazungumzonilitaka kumpigia simu mama kumjulisha ya
kwamba chakula cha jioni wasituhesabu kwani tungeweza kuchelewa ndipo nilikumbuka ya kwamba
nilisahau simu yangu moja niliisahau kwenye gari, nilimpa ufunguo wa gari yangu mdogo wangu na
kumwambia aende kunichukulia simu yangu. Aliondoka pale tulipokuwa lakini baada ya kama dakika
saba nilimuona akitokea kwenye kona huku akiwa analudi kasi sana pale nilipokuwa huku akiwa
ananiita jina langu kuashiria kabisa hapakuwa salama.
Nilishituka na kumfuata ili tukutane nae njiani, alikuja kasi sana na aliponifikia alinishika huku
akihema na kunielekeza tutoke nje haraka sana pombe zote ilionekana zilikuwa zimeshamtoka
kichwani, kaka kaka Mary nimekutana nae akitoka kweny gari yako, alizungumza huku akiwa
anathema sana kiasi kwamba amneno yalikuwa yanatoka huku yakiwa yamekatika katika sana
mpaka maneno mengine nikawa siwezi kuyasikia tulitoka nje mpaka kwenye parking ambapo tulikuta
gari langu mlango wa mbele ukiwa wazi , mdogo wangu alianza kunieleza ya kwamba wakati anatoka
nje alikutana na Mary akiwa kama vile anapekuwa kwenye lile gari langu na baada ya kumuona
anatoka alichomoka haraka haraka sana na kuondoka huku akiwa ameondoka na simu yangu,
nilimsikiliza kwa makini sana kisha nikamuuliza wewe unamjua huyo mtu? Alinjibu huku akili ikianza
kumludi sawa baada ya zile pombe alizokuwa amekunywa kuanza kumuisha kichwani, ndio namjua
japo sio sana kuna siku alinipigia simu na kukutana nae pale capchino ambapo ambapo tulizungumza
nae mambo mbali mbali ya biashara. Mh niliguna baada ya kusikia mambo ya biashara kisha
nikamwambia aendelee kunielezea, alidai ya kwamba Yule mwanamke ni mfanya biashara akiwa
anajihusisha na biashara ya kuuza milungi akiitoa nchini Kenya hivyo basi alikuwa anataka nimsaidie
kumkutanisha na wewe ili iwe rahisi kwake yeye kuwa anaiingiza Dar-es-salaam, sikuweza kupata
muunganiko kati ya biashara na mimi gari yangu kusachiwa kisha kuondoka na simu yangu, niliingia
ndani ya ili gari nakaiangalia angalia ndipo nilipokuja kugundua ya kwamba kumbe alikuwa ameweka
kinasa sauti kidogo sana mbele ya gari kwenye ubao ulioshikilia kioo nahisi baada ya kumuona
mdogo wangu alikurupuka ndio maana hakuweza hata kukiweka vizuri kile kinasa sauti, hapo hapo
akili yangu iligutuka na kujua atakuwa tu Yule mwanaharamu, sasa nilianza kujiuliza je alijuaje kama
mimi nimeenda nyumbani? Hapo ndipo palianza kunitatiza nilimpa pesa ya kulipia vinywaji mdogo
wangu na kisha kumuambia ya kwamba yeye aende akalipe kisha aje tuelekee zetu nyumbani kwani
siku yangu nilihisi ilikuwa imeshaharibika tayari.
Tuliondoka pale mkonge hotel huku akili yangu ikiwa imezidi kuvurugika nilijihisi kama maisha
yangu yanazidi kuwa hatarini hivyo nilikuwa nahitajika kuchukua hatua za tahadhari mapema
sana.wakati tunakaribia kmitaa ya makataba mdogo wangu alinionyesha kwa mbali Yule mwanamke
huku akiwa amevaa hijabu kabeba na mkoba akiteremka kuelekea bondeni ambapo palikuwa na
barabara ya kuingia bandarini basi na sisi tuliongeza mwendo na kwenda kushika njia ya kuingia
bandarini tulifika pale bandarini ambapo palikuwa na harakati sana kwani kulikuwa na meli ya
mizigo iliyokuwa inapakia sementi nilishika kwenye gari na kuwauliza wale walinzi wa bandari, kama
wamemuona mdada mmoja akiingia mule walinijibu ndio Yule dada alikuwa akielekea shelisheli na
ile meli ya sementi mume wake ndio alikuwa amechukua ule mzigo. Nilishangaa sana kusikia vile,
mara kwa ndani nikamuona Yule mwanamke akiwa anazunguka mule ndani alipotuona tupo getni
alijifanya kama kushituka vile ahalafu akaongeza mwendo kuelekea kwenye gati palipokuwa
pamepaki ile meli ya mizigo na mimi niliona wale askari wa bandari walikuwa wananichelewesha
wakati mbaya wangu namuona kwa mbele akipotea kwenye macho yangu nilitoa kitambulisho
changu haraka haraka kisha nikamuachia mdogo wangu ufunguo wa gari kisha na mimi nikazama
mule bandarini niliingia mule moja kwa moja mpaka kwenye ile meli na kuanza kumsaka huku
nikiwa na tahadhari kubwa sana. Niliendelea kumsaka mule bila mafanikio mpaka mida ya saa 4
usiku huku nikiwa nasaidiwa na baadhi ya askari wa bandari, mwisho meli ilimaliza kupakia mizigo
na kuanza kupiga honi kuahiria kwamba ilikuwa tayari kwa safari, sikuwa na jinsi zaidi ya kujikatia
tama na kuanza kutoka nje wakati meli inaanza taratibu kuacha ardhi na kuelea baharini kwa muda
kama dakika ishirini hivi huku nikiwa nimejisimamia nikiwa sina la kufanya ndipo nilipomuona kwa
mbali Yule mwanamke kwenye ile meli ya mizigo akipanda ngazi kutokea chini akieleka juu roho
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
ilinimua sana kwani kwa pale nisingeweza kumpata tena nilitoka mule bandarini nikiwa sina jinsi tena
mungu wangu huyu adui kweli kama kucheza na akili yangu basi amefanikiwa sana tu,
*****************************
Kwa kuwa nilikuwa bado nipo likizo niliamua kufanya maamuzi magumu ya kwenda shelisheli kwani
nilijua Yule mwanamke kule patakuwa ndipo panamakazi yake kwani nakumbuka hata mule pangoni
katika zile hati za kusafiria tulizozikamata moja ilikuwa ikimtambulisha kama ni mtu wa visiwa vya
shelisheli basi nilijua inaweza kuwa kweli kwa maana nilikusudia kumsaka mahala popote kwani
salama yangu ilikuwa ni yeye kukamatwa kwani sasa ilibainika ya kwamba mimi pia nilikuwa
nahusika na Yule mwanamke sasa ilinibidi kutumia juhudi zangu binafsi ili niweze kuwathibitishia ya
kwamba sio mimi pale kazini walinisimamisha tu kutokana na chuki zao binafsi.siku ile ile asubuhi
niliwaaga nyumbani kuwa niludi Dar-es-salaam kulikuwa na dharura imetokea kumbe upande wa pili
nilikuwa nataka niende nikafanye utaratibu ili ikiwezekana siku ile ile niweze kupata visa ya visiwa
vya sheli sheli ili jioni yake nianze safari ya kuelekea kule kwani nilijua kama nikiweza kupata usafiri
wa ndege nilikuwa na uhakika kabisa wa kuiwahi ile meli kabla haijafika hivyo basi ningeweza
kumuona Yule mwanamke pindi ile meli ikiwa inashusha mizigo.nilifika Dar-es-salaam mida ya saa 5
asubuhi ambapo nilipitiliza mpaka kwenye ofisi za ubalozi wa shelisheli nchini niliingia pale na
kukutana na afisa mmoja katika ule ubalozi nilimueleza ya kwamba nilikuwa naenda mapumziko
mwezi mmoja, nashukuru kati ya nchi ambazo zilikuwa na uhusiano mzuri na Tanzania na ambazo
hazikuwa na taratibu ngumu sana sisi kwenda Shelisheli nilogongewa pale visa yangu kisha moja kwa
moja nikaelekea ofisi za afrifight agent ambazo zlikuwa ni ofisi za mawakala wa tiketi za ndege,
niliwauliza wahudumu wa pale waliangalia kwenye computer kisha waliijibu ya kwamba kwa siku ile
kulikuwa na Kenya airways ambapo ilikuwa inanipasa niende mpaka Nairobi kisha niunge na ndege
nyingine.ya shirika lile lile mpaka shelisheli basi baada kumaliza ile booking ya ile ndege ambayo
walisema ilikuwa inaondoka saa kumi na moja jioni, basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea nyumbani
kwangu kwenda kupaki gari langu kisha nichukue taxi iweze kuniwahisha uwanja wandege kwani
muda uliokuwa umebakia ulikuwa ni mdogo sana kwani pale ilikuwa tayari imeshafika saa 8 na robo.
Hivyo ilinipasa kuongeza mwendo.
**************************************
Nilifika kwangu na kuchukua tu nguo zangu chache sana nikaziweka kwenye begi lagu dogo, laptop
yangu, viatu na raba pea moja kisha nikachukua na atm yangu ya Barclays bank kwani sikutaka
kubeba hela nyingi ule ulikuwa ni utaratibu wa kizamani sana ndio niliona hivyo nilichukua ile ya
Barclays ili nikifika kule niweze tu kupata huduma kupitia visa card na master card nilikuwa nipo
simple sana kiasi kwamba kama mtuangeniona asingezania kama nilikuwa na safiri.
Nilimaliza kupaki vitu vyangu huku muda ukiwa umeenda sana kisha nilitoka nje na kuchukua taxi
kwani pale nyumba niliyokuwa naishi kwa nje kulikuwa na tax nyingi sana zilizokuwa zinapaki
nilipanda kwenye taxi moja kisha na kumuambia dereva anikimbize uwanja wa ndege kwani muda
ulikuwa ni saa tisa kasoro kama dakika kumi hivi dereva alitoka kwa mwendo mzuri sana huku
akijaribu kupita sehemu zingine kwenye panya road ilimradi tu tuwahi kufika tulipofika stesheni
tulikutana na foleni kubwa sana kwani trafiki pale alikuwa amkasirika kisa deriva daladala mmoja
alimwambia kwa nin alikuwa akivuta magari ya upande mmoja tu?basi kwa hasira ule upande
akaamua kuuacha kabisa kuruhusu magari kupita kwa muda wa zaidi ya saa sasa niliangalia pale
ilikuwa tayari imeshafika saa kumi na robo. Mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka kwani ndege
ilikuwa inaondoka saa kumii na moja kamili na muda wa kufika ilikuwa na saa moja kabla basi pale
pale nikaampa Yule dereva taxi elfu kumi kisha mimi nikashuka zangu nakupanda boda bodaili niwee
kuwahi ndege kwani ilikuwaimefika kwenye saa kumi na dakika ishirini hivi.
Yule dereva wa boda boda aliniondoa kwa kasi ya ajabu sana pale tazara huku akijitahidi kuvuka
magari kwani yalikuwa mengi sana kutokana na ile foleni iliyosababishwa na yule trafiki pale kwenye
mataa, nilifika uwanjani ilikuwa saa kumi na moja kasoro dakika ishirini, niliruka kwenye pikipiki
kisha nikamkabidhi yule dereva wa boda boda kiasi cha shilingi elfu tano sikutaka hata kuulizui
chenji kwani juda ulikuwa umeenda sana ,nilikimbia kama mtu aliyekuwa anakimbia hatari Fulani
hivi nilifika mahali palipokuwa na wale wakaguzi walitazama tiketi yangu huku begi langu likipita
mahala pa ukaguzi nilipita haraka na kuelekea kwenye line namba moja kwani ndipo ndege
niliyokuwa nasafiri nayo ndipo ilikuwa imepaki ikijiandaa kupaa niliikimbilia ndege huku nikipiga
kelele za wanisubili kwani jamaa walikuwa wanataka kufunga mlango sasa.Nashukuru sana mungu
nilifanikiwa kuingia kwenye ndege japo kwa kuchelewa sana nilikaa kwenye seat huku ndege ikianza
kuiacha ardhi taratibu.
*****************************
Nilifika visiwa vya shelisheli mida ya saa 7 usiku kwani tulichelewa sana uwanja wa ndege wa Jomo
Kenyatta Nairobi nchini Kenya, kwani ndege nyingine tulikuwa tukiisubili kutokea Egpty ilichelewa
sana, nilishuka pale uwanja wa ndege wa visiwa vya shelisheli uliokuwa ukijulikana kwa jina la
aeropor intertanional de seyc pointe larue, uliopo kwenye mji mkuu wao unaojulikana kwa jina la
Victoria basi nilienda mpaka mapokezi ambapo nilitoa hati yangu ya kusafiria yule dada wa pale
uhamiaji aliikagua ambapo aliona nilikuwa nimeingia mule kama mtalii kisha akaigonga mhuri na
kuniruhusu kuengia huku upande wa pili begi langu nalo pia likipita kwenye mkanda wa kukagua
mizigo ambapo pia hawakuona kitu. Nilipitia katika duka la kubadilisha fedha lililokuwa pale pale
uwanja wa ndege ambapo nilibadili pesa zangu chache nilizokuwa nazo kutoka kwenye shilingi
kwenda kwenye rupee kwani pale shelisheli walikuwa wanatumia rupee kisha nilitoka njen a kukuta
taxi nyingi zikiwa zimepaki zikisubili abiria wanaoshuka kutoka kwenye ndege
Nilimuomba yule dereva wa taxi anipeleke kwenye hoteli ambayo haikuwa na gharama kubwa sana
ili niweze kuzimudu kwa muda wote nitakaokuwa mule kwani sikuwa na kiasi kikubwa sana cha pesa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na pia ile safari nilikuwa nimejigharamikia mimi mwenyewe kwa pesa yangu ya mfukoni, aliniskiliza
kwa makini kwani nchi ile watu walikuwa wanatumia lugha mbili kiingereza na kifaransa sasa yule
dereva ilionekana yeye alikuwa anajua sana kifaransa kuliko kiingereza kwani hata kunijibu kwake
kulikuwa kwa wasiwasi japo alikuwa mchangamfu sana tulianza safari ya kutoka pale uwanja wa
ndege na kuelekea kwenye hoteli ambayo ndio nilikuwa naenda kufikia iliyojulikana kwa jina la
silhouette island hotels, moja ya hotel yenye hadhi nzuri huku ikiwa na bei ya kumudu kwa mtu
yoyote yule huku ikiwa jirani na bandari kwani nilimdanganya ya kwamba mimi nilikuwa ni
mfanyabiashara nilikuwa nasubili meli yamgu iwasili niweze kupakua mizigo, basi usiku ule niliweza
kuuona ule mji wa Victoria kiukweli ulikuwa ni mji mzuri sana huku kuna sehemu kukiwa na mifereji
kutoka baharini na kuingia ardhini huku sehemu zingine kukiwa na madaraja tuliyotumia kuvuka
kutoka kisiwa kimoja kwenda kingine yani ile nchi sikuwahi kuona ilikuwa nchi yenye visiwa vingi
vidogo vidogo sana vingine vikiwa vimeungana vingine vikiwa vimeachana na kutenganishwa na
mfereji mdogo wa maji ya bahari.
Nilimlipa yule dereva wa taxi pesa yake kisha mimi nikajivuta na kuingia kwenye ile hoteli nilikuta
vyumba bado vikiwepo nilichukua chumba ambacho kilikuwa kipo juu ambapo nilikuwa na uwezo
wa kuona shughuri zote zilizokuwa zinaendelea katika bandari yao ya pale Victoria nilifurahi sana
kwani nilijua ya kwamba kupitia pale ningeweza kuifuatilia ile meli ambayo nilikuwa na uhakika siku
ile asubuhi lazima ingewasili tu pale bandarini.
*******************************
Kesho asubuhi na mapema baada ya kumaliza kunywa chain a kuosha mwili wangu niliamua sasa
kuianza ile kazi moja kwa moja ya kumsaka yule mwanamke nilivaa kofia za wapanda farasi kisha
nikaweka na miwani usoni ili kiasi kwamba isiwe rahisi kwa mtu kunitambua kirahisi kwa maana
nilijua yule mtu ni hatari nisipokuwa makini itakuwa tatizo ukizingatia hata sikuwa nimeaga mtu
yoyote nilitoka nje na kuanza kutembea taratibu kuelekea kule palipukuwa na bandari yao nilifika
pale mapokezi na kujifanya naulizia kama kulikuwa na meli yoyote iliyokuwa inatikea Tanzania
kama ilikuwa imeshafika kwani kulikuwa na mzigo wangu yule dada wa pale mapokezi wa bandari
alinitazama sana kisha akaguna na kunijibu ya kwamba mbona wao wanavyojua meli iliyokuwa
imeenda kubeba simenti Tanzania ilikuwa imekodiwa yote na mkodishaji alikuwa ni serikali ya pale
shelisheli na ilikuwa imeende kubeba simenti kwa ajili ya kutekereza mpango wao wa kujenga
nyumba za bei nafuu kwa wananchi wa shelisheli, nilijikuta Napata kigugumizi kisha nikamwambia
ya kwamba niliwamomba na mimi nipakie mzigo wangu wa machungwa kwa makubaliano
maaalumu, yule dada alisema lile ni tatizo kwani kwa nchi yao pale itahesabika kama rushwa hivyo
lazima yule msimamzi wa ile meli atakuwa hatianika kwani atakuwa amevunjwa sheria za nchi
niliona yule dada maneno yakiwa mengi ndipo nikaamua kumwambia “ sawa basi nimekuelwea ila
nachokuomba hapa ni kunijulisha tu lini hiyo meli inaingia lini hayo mengine itajulikana nikifika”
alinijibu inaingia leo mchana kwani ilipita pia Mombasa kupakia sementi zingine kutoka kiwanda cha
East Africa Portland cement,hivyo basi itanipasa kugeuka pale mchana kuanzia mida ya saa tisa hivi,
Nilianza kuondoka pale huku nikiwa na wasiwasi baada ya kusika ile meli imepitia Mombasa kwani
nilijua moja kwa moja inawezekana yule mwanamke akawa ameshukia Mombasa, nilianza kujiuliza
maswali mengi sana kuhusu yule mwanmake na ile meli uhusiano wao baada ya kuambiwa ya
kwamba ilikuwa imekodiwa na serikali ya shelisheli, au inawezekana yule mwanamke atakuwa na
uhusiano na kati ya nahodha au baharia katika ile meli ndio swali nililojiuliza kichwani,ok sawa yote
yatajulikana ngoja kwanza hiyo meli ifike ndipo nitajua kipi cha kufanya, nilijirudisha katika ile hoteli
niliyokuwa nimefikia ili niweze kupata chakula cha mchana kisha nikae dirishani kuangalia iyo meli
kuona pindi itakapoanza kuingia, nilimazlia kula kisha nikasogelea computer iliyokuwa ipo mule
chumbani kwangu mahususi kwa ajili ya wateja kisha nikaiwasha na kuanza kufungua mitandao
mbalimbali ya kitanzania ili niweze kitambua ni kipi kilikuwa kinaendelea nyumbani nilifungua barua
pepe yangu ambapo nilikuta kuna ujumbe mbalimbali kutoka kwa rafiki zangu mbalimbali huku pia
na kipenzi change Jamila akiwa amenijibu na kunijulisha ya kwamba baada ya wiki atakuwa
ameshaludi nchini huku akiniambia alikuwa ameshamaliza mafunzo yake kule marekani huku akinipa
pole sana kutokana na masahibu yaliyonikuta na kuniomba ni bora niache kujishughurisha na
kumfuatilia yule mwanamke mwisho na mimi nisije kupotea duniani bure wakati yeye akiwa bado
ananihitaji, nilijitahidi kumjibu vizuri huku nikijitahidi kupangua zile hoja zake kwa njia tofauti
kwamba hata kama yule mwanamke nikiachana naye ila kwa yale mauaji yake ya kutisha siku moja
angeweza kuniua kama sio mimi basi hata yeye pia kwani alikuwa akifanya mauaji hovyo na hata
bila ya kutoa sababu za msingi wala kusema ni kipi alichokuwa kikitaka.
Baada ya kumaliza kumjibu barua pepe Jamila ndipo nilipofungua mtandaa wa kijamii wa Darhotwire
sikuamini nilipokutana na picha ya mwanaume aliyelala hku damu zikimtoka sehemu mbalimbali na
pia kukiwa na alama nyeusi ikiwa imeziba sehemu zake nyeti huku kukiwa na kichwa cha habari
“afisa wa polisi afanyiwa mauaji ya kutisha” akatwa na kisu nyeti zake sehemu za siri mwili ulianza
kusisimka nakujihisi kupata kibaridi Fulani hivi cha woga baada ya kungalia picha ile kwani ilikuwa
ni picha ya mkuu wangu wa kazi inspekta Thomas.
*******************************
Mwili ulinisisimka sana nikajihisi kuishiwa nguvu huku machozi yakiwa yananitoka kwani nilijua kifo
cha mkuu wangu wa kazi na hivi nilikuwa nipo kwenye mgogoro nay eye basi ungeniweka matatani
kabisa kwani tulikuwa tupo kwenye mgogoro na yeye kabla ya kifo chake sasa kitendo cha yeye kufa
tena kifo cha kutatanisha ilimaanisha kabisa ningehisiwa ni mimi nimefanya vile ili kuwakomoa au
kuonyesha ya kwamba sio mimi japo wamenisimamisha kazi lakini bado mbona mauaji yanatokea,
mwili ulinisismka sana nilijikuta nashindwa kuendelea kuisoma ile habari nakuludi na kukaa kwenye
kochi lililokuwa mule kwenye chumba change na kuanza kufikiria ni kipi cha kufanya, baada ya
kuwaza kwa muda kidogo niliona ngoja nijikaze kiume nilitoa kijitabu change kidogo ambacho
kilikuwa kimejaa namba za watu mbalimbali kisha nikaangalia namba ya Gerald na kuamua
kumpigia, simu iliita sana bila hata ya kupokelewa mpaka nikajikuta nakata tama ya kwamba labda
atakuwa yupo msibani na yupo kwenye taratibu za mazishi, niliacha kuipiga ile namba na kuamia
namba ya Amina nayo iliita pia bila kupokelewa nahisi wote waliogopa kuipokea baada ya kuona ni
namba ngeni halafu ilikuwa sio namba ya ndani ya nchi basi nilijikuta nakaa tu bila ya kujua ni lipi la
kufanya kwani watu wote niliokuwa nawategema kupata habari kutoka kwao ndio hivyo tena simu
walikuwa hawpokei tena basi wakati najiandaa kutoka mule chumbani niludi kule bandarini ili
kwenda kuangalia kama ile meli itakuwa tayari imeshawasili, mara simu ya mule chumbani kwangu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ndipi ilipoanza kuita kwanza nilihisi labda watakuwa ni wale wahudumu wa mule labda kuna jambo
wanataka kuniambia au kulikuwa na mtu yoyote alikuwa ananitafuta,lakini baada ya kuipokea ile
namba mambo yalikuwa ndivyo sivyo kwani yule aliyekuwa amepiga simu alianza kwa kucheka sana
tena kwa kicheko cha dharau sana,nilikuta nashituka kwani sauti nilihisi kama naijua ila ni sauti
amabyo nilikuwa sijaisika muda mrefu sana, ile sauti y kike iliniambia ya kwamba nilikuwa najifanya
mjanja wakati mimi ni mpumbavu sana, kuwa alinitega ili niondoke nchini ili yeye huku aendeleze
mipango yake, aliniambia kuwa na Gerald alikuwa tayri ameshamteka anasubili siku yoyte aamue
amfanye lolote, mwili ulisisimka na mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi sana, kwani nilijua
kwamba pale pia nilikuwa nimuzwa na yule mwanamke, niliikata simu kwa hasira kisha na kuangalia
ile namba iliyokuwa imetumika kupiga nilikuta ni namba ya Gerald, nilizidi kuishiwa nguvu kwani
nilijua ni kweli basi Gerald atakuwa ametekwa nayule mwanamke, nilijiona kama ni mpelelezi
niliyekuwa situmii akili kwa kuuzwa kijinga kule Tanga mpaka nikakurupuka na kufunga safari
mpaka kule visiwani huku mtuhumiwa nikiwa nimemuacha nchini, nilijjishangaaa sana lakini nikaona
sio mbaya lazima nihakikisha nafanya uchunguzi kwanza kwenye ile meli nikisha jihkikisha ndipo
niweze ondoka kule shelisheli.
Nilifika pale bandarini na kukuta meli ile ikiwa imeshafika huku wakisema ya kwamba itaanza
kupakuwa mzigo kesho yake basi nilikaa sehemu na kuvizia kuona wafanyakzi wa ile meli pindi
watakapopita basi mmoja wao nimuite niweze kuzungumza nae maneno mawili matatu. Nilijua
ningeweza kupata kitu basi baada ya kukata tama kama baada ya saa zima ndipo nilipoona watu
nilijua kabisa walikuwa wafanyakazi wa ile meli nilimuona mmoja ambaye alikuwa na rangi ya
kiafrika zaidi tofauti na wale wengine ambao rangi zao zilikuwa ni mchanganyiko, alikuwa amevalia
overolly la rangi ya blue huku akiwa ameshika begi lake la nguo mkononi, baaada ya kumuita
kwanza alisita kisha ila nahisi baada yak union kwamba mimi ni mwafika mwenzake alikuja bila
wasiwasi huku akiona kama mtu aliyekuwa na haraka sana, nilimsalimu kiingereza, alinijibu huku
akiniuliza mimi ni mtu wa wapi nilijitambulisha kwamba ni mtanzania ambaye nilikuwa nipo mule
visiwani kwenye utalii, alinichangamkia sana baada ya kusika hivyo aliniambia kwamba yeye
alikuwa ni mmadagaska ila kutokana na kazi yake ya ubaharia ilimuwezesha kwenda sehemu
mbalimbali ndani ya Afrika tulianza kuondoka naye yae maeneo huku tukuwa tunazugumza taratibu,
aliniambia ya kwamba yeye kazunguka nchi nyingi lakini Tanzania ni wakarimu sana kuwa walikuwa
Tanzania siku nne zilizopita, nilizidi kufurahi baada ya kuona mimi na yeye tumeanza kuelewana vile
kwani ingenirahisishia mimi shughuri yangu ya kujua yule mwanamke ilikuwaje mpaka akapanda
kwenye ile meli na yuppo wapi kwani kwa muda wote niokuwa pale langoni ikuweza kumuona
akishuka pia nakumbuka alinipigia simu kupitia namba ya Gerald ya kwamba alikuwa ameniuza mimi
niondoke ili yeye aweze kutimiza mipango yake mingine, yule kaka maybe baadaye nilikuja
kugundua kwamba alikuwa naitwa Frednando aliendela kunuambia kuwa pamoja nayote ila
wanawake wa Tanzania walikuwa wajanja sana, nilihisi kama aliuwa anataka kuja kwenye mada
niliyokuwa naitaka, “kwa nini?” nilijikuta namuuliza haraka haraka sana, kuna mwanmake mmoja
rafiki yangu alimpata Tanga juzi lakini walipofika Mombasa yule mwanamke aliwatoroka bila ya wao
kujua huku akiwa amebeba kiasi kikubwa sana cha pesa kutoka kwenye ile meli. Ambazo zilikuwa za
nahodha nilijifanya nasononeka kisha nikamuuliza kwani alimjuaje? Aliniambia ya kwamba yule
mwanamke walikuta naye chichi club walipoenda siku moja kabla hawajondoka,huku akinimabia ya
kwamba wakati anatoroka alidondosha pochi yake ambayo walifanikwa kukuta baadhi ya vitu vyake,
nilimuuliza ni wapi tunaweza kuupaa hoa mzigo, alinitazama kisha akawa kama anajaribu kunijibu
kwa lugha ya Kiswahili lakini kilionekana kumshinda kabisa,kisha ndipo akaniambia tu kwa lugha ya
kiingereza kwamba vipi umetumwa au kakupigia simu ulifuatilie nini? Nilicheka kinafiki ili kupoteza
lengo kwani yule kaka alianza kuinyesha kama kuchoka hivyo basi nikaona kama nisipokuwa mjanja
basi sitojua lile begi lipo wapi, alinimbia ya kwamba hana uhakika ila anahisi litakuwa tu mule
kwenye meli, kwani lilikuwa na vitu vya kike kike tu, tuliendelea kuzungumza mpaka tukafika
barabarani ambapo yeye alipanda taxi na kuelekea hoteli ambayo ndio huwa wanafikia, nilipia
hesabu ni vipi nitaweza kuingia kwenye ile meli bila ya kuonkena, basi pale pale wazo likanijia
namimi nikakodi taxi na kuingia mjini kwenye maduka.
Jioni ile nilivaa overlloy la blue na viatu vigumu chini nikawa kama vile mmoja wa mabaharia nilifika
getini pale bandarini na kujifanya kama na mimi nilikuwa baharia wa ile meli huku nikijifanya ya
kwamba nimesahau ndani baadhi ya vitu vyangu ikiwemo hati yangu walinitazama kisha yule dada
niliyemkuta mchana akanitazama kama vile alikuwa anafananisha kitu hivi, aliniuliza jina nikamtajia
la yule jamaa yangu niliyekuana naye pale, walilitazama kwenye daftari la mabaharia walioshuka
kisha akaniruhusu, sikuamini kwani mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kasi sana, niliondoka pale
getini kwa kasi ya ajabu sana huku nikiwa naogopa hata kuangalia nyumna,niliingia kwenye ilemeli
ambapo nilikuta shughuri ya upakiaji ikiwa bado inaendelea,wale wapakuaji hawakuwa na muda hata
na mimi nilisogea mpaka kwenye mlango wa kuelekea kwenye chumba cha nahodha nilijaribisha
kuufungua nikakuta upo wazi, basi nikaingia huku nikitazama kila upande kama naonekana nilianza
kufanya upekuzi haraka haraka sana mara kwenye kabati kwa juu nikaona mkoba mweusi wa kike
basi nikajihakikishia kuwa ndio wenyewe niliuchukua na kuanza kuuweka kwenye mfuko mweusi
niliokuwa nimeingia nao. Wakati namalizia kuuweka mara nikasikia vishindo na sauti ya watu
wakielekea mule kwenye kile chumba nilichukuwamo..
Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio sana wale watu walizidi kusogea kwenye kile cumba huku
wakiwa wanazungumza kifaransa, niliinuka na kuanza lutafuta mahali pa kujificha kwani niljua kama
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walikuwa ni baadhi ya wale ma baharia wangenitambua kuwa sio mwenzao hivyo ningekuwa
matatani sana, nililisogeza kabati mule chumbani na kupenya kwa chini ambapo palikuwa na uvungu
mkubwa tu kiasi kwamba kama wangeingia isingekuwa rahisi kwa wao kuniona, nilikaa mule kwa
takiribani zaidi ya dakika kumi na tan bila ya mtu kuingia huku zile sauti zikionekana zikizidi
kupotelezea, nilishusha pumzi kisha nikatoka mule uvunguni na kuanza kuangalia njia sasa ya kutoka
nje kwani muda ulkuwa umeenda sana.
**************************
Baada ya kuingia chumbani kwangu pale hotelini cha kwanza kabisa nilikuwa na hamu ya kujua je ni
kipi kilichokuwepo ndani ya lile begi. Nililifungua lile begi na kukuta kuna vitu vya kike tu kama
nguo za ndani, marashi, sabuni, na mapambo mengine, roho iliniuma sana kwani nilijiona kama
nimepoteza muda wangu na kujiweka hatarini bila ya sababu ya maana, nililitupa lile begi chini kwa
hasira sana, nililipo anguka chini ndipo nikaona kama kuna vitu vikitoka kwenye zipu ya pembeni,
basi nililiinua haraka tena lile begi kisha na kuanza klikagua tena kumbe lilikuwa na zipu ya pembeni
niliifungua haraka haraka sana, nilikutana na kijiabu kikiwa na namba mbalimbali za simu baada ya
kuanza kuzipia moja baada ya nyingine nilikuta namba karibia za wafanyakazi wote wa pale ofisini
zikiwepo, nilishituka sana baada ya kuona hivyo, niliendelea kufunua kile kjitabu nikakutana na
sehemu ambapo alikuwa ameandika kumbukumbu zake mbali mbali kila jambo na tukio nilishangaa
sana baada yakukuta karibia kila tukio alilokuwa akifanya likiwa lipo kwenye kile kijitabu, mpaka
tukio la mwisho ambalo lilikuwa ni kuonana na mimi kule Tanga, niliendelea kukikagua kile kitabu
mwisho nilikuta na majina ya watu mbalimbali ambao walikuwa kwenyempango wake wa
kuwaondoa duniani ambapo kulikuwa na mlolongo waa majina mbalimbali,nilishangaa baada ya
kukta pia jina la marehemu bosi wangu huku jina la mwisho likiwa ni mkuu msaidizi wa idara ya
mafunzo katika chuo cha mafunzo ya upolisi, mwili ulinisisimka sana kwani kwani kile kitabu
kilikuwa kinaelezea kila mtu na sehemu anayoishi, vitu anavyopendelea na jinsi ya kumuondoa
duniani, nilijikuta nashindwa kuendelea kukisoma kile kitabu na kukiweka pembeni kwani kilikuwa
siri nyingi sana za yule mwanamke,
Niliendelea na kukagua kwenye ile zipu ya pembeni ambapo pia nilikutana na nailony eyes za bandia
pamoja na sura tatu za bandia, nilikuta na hati ya kusafiria ikimuonyesha kama ni raia wa shelisheli
huku pia kukiwa na funguo ambazo zilionyesha kwamba zilikuwa za nyumba yake kwani kwenye
key holder yake zilikuwa zinaonyesha kila ufunguo na mlango wake, nilijikuta nafurahi huku nikijua
sasa kumbe ile safari yangu haikuwa ya bure kabisa nikajikuta sasa naanza kuvipanga vile vitu vizuri
huku nikiviamisha kutoka kwenye begi lake kwenda kwenye begi langu vile nilivyohisi ni vya maana.
Nilimaliza na kuanza kulikung’uta lile begi Wakati naendelea na lile zoezi mara nikasikia kitu
kigumu kikianguka chini baada ya kukiangalia vizuri ilikuwa ni simu ya mkononi huku ikiwa
imeviringishwa na pedi kiasi kwamba isingekuwa rahisi kuonekana, niliichukua ile simu aina ya htc
na kujaribisha kuiwasha lakini lionekana kutokuwa na chaji, nikaona sio mbaya nitatafuta chahi yake
niichaji iliniweze kujua ni kipi kimehifadhiwa mule ndani, mpaka pale nilikuwa na matumani sana ya
kuweza kumtambua yule mwanamke kutokana na vile baadhi ya vitu nilivyoweza kuvipata siku ilea
ma kweli mtembea bure si sawa na mkaa bure.
**********************************
Nilifika Dar es salaam salama kabisa nilitoka mule uwanja wa ndege mpaka barabarani kisha
nikapanda zangu daladala kama vile nilikuwa ni mtu niliyekuwa katika mihangaiko yangu ya kila siku
nilishuka mnazi mmoja kisha na kuelekea nyumbani kwangu, ambapo nilikuta papo kama ilivyokuwa
nimepaacha tofauti na mwanzo nilivyokuwa nimefikiria kwamba nitakuta pamekaguliwa ila haikuwa
hivyo basi jambo kwanza niliwasha simu zangu na kangalia ni nani walikuwa wamenitafuta kwa
kipindi kile chote ambacho sikuwepo, uliingia ujumbe wa meseji mbalimbali huku pia na namba za
simu ambazo zilionekana kunitafuta kwa ule muda ambao sikuwepo, nilijaribu kuzipia nyingi
zileonyesha tu zilikuwa zikinijulisha kuhusu msiba wa mkuu wetu wa kazi, sikuzijali sana kwani kama
taarifa nilikuwa tayari naijua hivyo basi sikuona kama ni kitu kigeni sana.
Baada ya kumaliza kuosha mwili wangu naa kubadili nguo basi moja kwa moja nilitoka nje nikaingia
mitaa ya nyuma ili nijirabu kutafuta chaji ya ile simu ili niweze kujua kulikuwa na nini niliingia
maduka ya simu ya kariakoo muda ule ule wa jioni kwani navyojua mara nyingi yale maduka huwa
ikifika jiona mara zote vitu huwa vinashuka bei kwani kuwa mwingine unakuta hajauza siku nzima
hivyo hawezi kukataa pesa, basi baada ya kupita pita kwenye yale maduka mengi hayakuwa na chaji
ya ile simu mpaka mwisho kabisa nilienda kuipata kwenye duka moja ambalo lilikuwa kwenye
uchochoro mmoja uliokuwa ukitokea mtaa wa Swahili nipo nilikuta mhindi mmoja akiwa nayo basi
sikutaka sana kubishana nae sana kwenye bei nilimpatia pesa yake kisha nikaondoka zangu haraka
sana kuludi nyumani kwani sikutaka nionekane sana kwani nilihofia kukutana na mtu yoyote ambaye
nilikuwa namjua, basi baada yakuichaji ile simu na kuiwasha nikakkuta na password, nilijua tu yule
mwanamke atakuwa amefanya vile ili isiwe rahisi watu kujua je ni kipi kilikuwapo mule ndani, basi
nika download programmer ya kiuwa ile password kwenye computer yangu ili niweze kujua mule
ndani kulikuwa kuna nini niliiwasha kwa shauku kubwa sana ya kutaka kujua kilichokuwepo mule
ndani, moja kwa moja niliaanza nu sehemu ya ujumbe mfupi ambapo pale sikuweza kukutana kitu
chochote cha maana,sikupajali,nikaingia kwenye faili liliokuwa na picha na video, pale niliweza
kukutana na picha za matukio mbali mbali pia niliweza kuuta baadhi ya picha za msichana mmoja
akiwa amepiga kwenye nyumba moja hivi basi nilihisi moja kwa moja atakuwa ni yeye, niliachana na
mahali pa picha nikijua kwa zile nilizokuwa nimeziona zinatosha kuweka kumtambua basi nikaamua
kuhamia kwenye upande wa barua pepe kwenye ile simu yake, wakati nanaendelea na ile shughuli
mara mlango wangu nikasikia ukigongwa kwa nguvu sana niliamka taraibu na kwenda kufuungua,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mwili ulinyon’gonyea nilipokutana na baadhi ya wafanyakazi wenzangu wakiniambia ya kwamba
nilikuwa natafutwa sana naitajika makao makuu kwa ajili ya mahojiano.
****************************************
Niliguna baada ya kusikia vile nilijua moja kwa moja nilikuwa nahisiwa kuhusika na kifo cha
mkubwa wangu wa kazi,niliwaomba dakika kadhaa niweze kujiandaa kwani nilikuwa nipo kifua wazi
huku nikiwa nimevaa suruali ya kulalia tu, waliniambia hukuna tatizo, nilijua ingekuwa ngumu kwa
mimi kunipeleka kama watu wengine kwani baadhi yao pale nilikuwa nawazidi cheo ofisini, basi
niingia ndani na kujiandaa kisha nikabeba na baadhi ya vitu kwenye mkoba wangu na kutoka kwa
ajiliya kuanza safari ya kuelekea makao makuu muda ule ule wa jioni kwa ajili ya mahojiano kama
wao walivyokuwa wamenambia, niliinia kwenye ile discover ya polisi na kuanza kuelekea makao
makuu.mule ndani ya gari wale wafanyakazi wenzangu walionekana kama ni watu waliokuwa
wakinihofia sana kwani hata mazungumzo na mimi walkuwa wanazungumza kwa kusita sit asana
hasa baadhi ya maswali ambayo nilikuwa nahitako ufafanuzi wao na ushirikiano wao. Nilijua tu
itakuwa ni sumu iliyokuwa imesabazwa kuwa mimi nilikuwa nikishirikiana na yule muuaji katika
kufanya yale matukio,kitu ambacho mimi kilinishangaza sana kwani sikuona ushirikiano baina ya
mimi na yule mwanamkepia sikuona umuhimu wake ule wa kuuwa watu hovyo basi sikuwa na jinsi
nianza kujiona kama mpweke Fulani hivi na mtu ambaye nilikuwa ninategwa na jamii bila ya sababu
zisizo na maana, sikuwa na jinsi niona njia ya kulitatua lile tatizo ni moj tu nalo ni kuhakikisha yule
mwanamke namkamata na kumfiksiha mbele yao hiyo ndio itakuwa njia yangu mimi kujosha kwani
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
tofauti na pale bado jamii na wafanyakazi wenzangu watahisi ni mimi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment