Search This Blog

Sunday 19 June 2022

MCHEZA FILAMU ZA NGONO - 4

 





    Simulizi : Mcheza Filamu Za Ngono 
    Sehemu Ya Nne (4)





    Vyombo vingi vya habari nchini Marekani vilikuwa vikitangaza kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa kati ya mwanamke ambaye alikuwa maarufu duniani katika



    uigizaji wa filamu za ngono, Katie pamoja na mwanaume kutoka nchini Tanzania, Gibson.

    Kila mtu ambaye aikuwa akiziangalia taarifa zile katika vyombo mbalimbali vya habari hakuonekana kushtuka sana kutokana na kufahamu kwamba kuna siku

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kitu kama kile kingetokea kutokana na Katie kuwa miongoni mwa watu ambao waikuwa wakiigiza filamu za ngono duniani.

    Kila kitu kilionekana kubadilika sana katika maisha ya Katie, mwanaume ambaye alikuwa akimheshimu sana, Gibson kwa wakati huo hakuwa pamojanae. Katie



    akawa mwanamke wa kulia tu, kila siku alikuwa akijifungia chumbani kwake na kulia kupita kawaida.

    Moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Kuna wakati alikuwa akijuta sababu zilizompelekea kuolewa na mwaname ambaye wala hakuwa amekaa nae



    sana katika mahusiano huku wakati mwingine akijuta sababu ambazo zilimpelekea kutokumwambia Gibson ukweli juu ya kazi ambayo alikuwa akiifanya ya



    uigizaji wa filamu za ngono.

    Alijua ni lazima kungekuwa na sababu moja kubwa ambayo ilimfanya Gibson kuamua kufanya uamuzi wa namna ile kwani alijua kwamba Gibson hakuwa na



    lengo la kumuacha kwa wakati ule kutokana na sababu kubwa ya kumruhusu kwa moyo mmoja kuendelea kuigiza filamu za ngono.

    Wasiwasi ukaanza kumuingia Katie kwamba kulikuwa na mtu ambaye alikuwa nyuma ya mpango ule wote, alichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kupeleleza.



    Kazi ya upelelezi ilikuwa kubwa sana kitu ambacho kikamfanya kuwaita vijana maalumu kwa ajili ya kuifanya kazi ile.

    Vijana waliifanya kazi ile kwa moyo mmoja, waliangaika kila sehemu lakini mwisho wa siku hawakupata kitu. Katie akaonekana kuchanganyikiwa,



    alichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kuyafuatilia maisha ya Gibson tu.

    Alijua fika kwamba Gibson alikuwa akielewa kila kitu juu ya sababu ambazo zilimfanya kutaka ndoa ivunjwe kwa haraka sana, umuhimu wa kumuuliza Gibson



    ulikuwa ukionekana kufaa kwa asilimia zaidi ya mia moja.

    Katie akaanza kugundua vitu fulani, kwanza akaanza kujiuliza juu ya siku ile ambayo Gibson alikuwa ametekwa na kisha kumwambia kwamba alikuwa



    amewatoroka watekaji. Swali ambalo lilikuwa kichwani mwa Katie ni kwa namna gani Gibson alikuwa ameweza kupigana na watekaji hata bila kujeruhiwa



    katika sehemu yoyote ya mwili wake na wakati watekaji wale walikuwa na bunduki?

    Katie akaanza kuingiwa na wasiwasi, akaanza kujua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kiliendelea na aliamini kwamba kitu hicho ndicho ambacho kilimfanya



    Gibson kutaka kuachana nae na kuuvunja mkataba wa ndoa ambao walikuwa wameusaini.

    “There’s something (Kuna kitu)” Katie alisema.

    Wazo jingine likaingia kichwani mwa Katie, akaanza kugundua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Tanzania ambacho hicho nacho



    kilikuwa kimechangia kwa asilimia kubwa kwa Gibson kuamua kufanya vile.

    Katie akaanza kugundua kwamba kulikuwa na uwezekano Gibson alikuwa na mpenzi nchini Tanzania ambaye alikuwa ameishika akili yake kupita kawaida na



    ndio maana alitaka kuachana nae ili aeze kurudi nchini Tanzania na kuendelea na maisha yake.

    Alichokifanya kwa wakati huo ni kuwatuma vijana wake nchini Tanzania kwa ajili ya kuufanya upelelezi ambao kwake aliuona kumletea majibu yote. Alihitaji



    kila kitu kifanyike huku akiwaelekeza kwamba ilikuwa ni lazima kwao kufikia katika mbuga ya Mikumi ili kupata ukweli juu ya kila kitu kuhusiana na Gibson.

    “Nitawagawia kila kitu, ninachokitaka kutoka kwenu watatu ni kunipa kila kitu nitakachotaka kukifahamu” Katie aliwaambia vijana wake watatu ambao



    walikuwa wakijiandaa kuja nchini Tanzania.

    “Sawa! Hautakiwi kuhofia kitu chochote. Kuna kingine?” Reuben aliuliza.

    “Ndio! Kama anaishi na mwanamke, inatakiwa mmuue kama kisasi changu” Katie aliwaambia.

    “Sawa! Kingine bosi”

    “Ni hivyo tu” Katie alisema.

    Alichokifanya kwa wakati huo ni kuwagawia vijana wale kiasi cha dola milioni moja kwa ajili ya kuja nchini Tanzania huku fedha nyingine akiwatumia pale



    ambapo wangekuwa wanazihitaji wakati watakapokuwa nchini Tanzania.

    Harakati za kutafuta viza zikaanza mahali hapo, wala hawakupata tabu kutokana na kuelezea katika ubalozi wa Tanzania kwamba walikuwa wakitaka kuja nchini



    Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii tu. Mara baada ya kupata viza, wakakata tiketi za ndege na siku iliyofuata kuanza safari ya kuja nchini Tanzania kufanya kile



    ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika tu.

    ****

    Reuben, Filbert na Andrew walikuwa ndani ya ndege ya Gulf Airlines wakielekea nchini Tanzania. Muda wote walikuwa wakiongea mambo mbalimbali ambayo



    walitakiwa kuyafanya nchini Tanzania, ramani kubwa ya nchi ya Tanzania ilikuwa mikononi mwao kwa kuwa walikuwa wakihitaji msaada mkubwa sana wa



    kufika kule walipoelekezwa bila kumuuliza mtu yeyote yule.

    Ndege ilichukua masaa zaidi ya ishirini na ndipo ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere. Walipofika hapo, hawakutaka kukaa



    sana, walichokifanya ni kukata tiketi ya ndege ya kuelekea Morogoro huku lengo lao likiwa ni kufika katika mbuga ya Mikumi na moja kwa moja kuelekea



    katika hoteli iitwayo Mikumi National Park ambako huko ndipo wangeanza kumuulizia mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Gibson Lyimo.

    Safari ya kwenda mkoani Morogoro ikaanza kwa kutumia ndege ya Precious na baada ya saa moja kuingia mkoani Morogoro ambako wakaanza kuyafuata



    magari ya kuelekea katika mbuga hiyo na kisha kuanza safari. Kila mmoja akilini mwake alikuwa akifikiria lake tu, mtu ambaye walitakiwa kumuua hakuwa



    huyo Gibson bali mtu ambaye alitakiwa kuuawa alikuwa mwanamke ambaye alikuwa akiishi nae katika kipindi hicho.

    Walipofika katika hoteli hiyo iliyokuwa mbugani, wakachukua vyumba na kutulia huku upelelezi ukifanyika chini kwa chini. Walikaa katika hoteli hiyo kwa



    muda wa siku mbili na ndipo walipoamua kumuulizia Gibson kupitia kwa mkurugenzi wa hoteli hiyo.

    “Mnamuuizia Gibson! Huyo mtu aliacha kazi kipindi kirefu cha nyuma. Kwa sasa hivi ni miongoni mwa watu wenye fedha nyingi sana hapa nchini” Mkurugenzi



    wa hoteli hiyo, Massawe aliwaambia.

    “Kwa hiyo hatuwezi kupafahamu anapokaa?” Reuben aliuliza.

    “Anakaa Dar es Salaam. Labda kama mnataka kulipia ili mfanyakazi wangu awapelekea huko mpaka nyumbani kwake” Massawe aliwaambia.

    Reuben na wenzake hawakuwa na jinsi, kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kumfahamu mwanamke ambaye alikuwa akiishi na Gibson na



    kisha kufanya kile ambacho walikuwa wameagizwa, walichokifanya ni kumlipa mkurugenzi na kisha kupewa kijana mmoja ambaye walianza safari nae ya



    kuelekea Dar es Salaam.

    Njiani hawakukaa kimya, mara kwa mara walikuwa wakimuuliza maswali mbalimbali kijana yule ambaye walikuwa nae kama namna mojawapo ya kuchunguza



    zaidi na kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na jiji la Dar es Salaam ambalo walikuwa njiani kuelekea uko.

    Walipofika Dar es Salaam, moja kwa moja wakakodi teksi mbili ambazo ziliwapeleka mpaka hotelini na kisha Reuben peke yake kutoka na kuelekea uko



    alipokuwa akiishi Gibson huku akiongozana na yule kijana.

    “Do you see that house? (Unaiona nyumba ile?)” Kijana yule alimuuliza Reuben huku akimuonyeshea nyumba aliyokuwa akiishi Gibson.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Please! Stop the car (Tafadhali! Simamisha gari)” Reuben alimwambia dereva ambaye alisimamisha gari lile.

    “Thank you for your help (Asante kwa msaada wako)” Reuben alimwambia kijana yule huku akimtaka dereva kuwarudisha hotelini.

    “So, why dont you want to meet him? (Kwa hiyo kwa nini hautaki kuonana nae?)” Kijana yule alimuuliza Reuben.

    “I wanted to know the place (Nilitaka kupafahamu)”Reuben alimwambia.

    ****

    Mchakato bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida, walihitaji kufanya mambo yao kwa haraka haraka hata kabla wiki haijakatika na kuwakutia ndani ya jiji la Dar



    es Salaam. Kitu ambacho walikuwa wakikitaka katika kipindi hicho kilikuwa ni bunduki tu.

    Hawakutaka kumuua mke wa Gibson kwa kutumia silaha yoyote zaidi ya bunduki, wakaanza kuangalia uwezekano wa kupata bunduki lakini kila



    walivyoangalia, hawakuona dalili ya kuweza kuipata aina ya silaha hiyo.

    Hawakutaka kujiuliza maswali mengi sana, wakaona kwamba hata mikono yao ilikuwa na nguvu sana kukabiliana na huyo mtu tena alikuwa mwanamke, kwao



    alionekana kutokuwa na usumbufu wowote ule. Wakajipanga upya, ilikuwa ni lazima utekaji ufanyike, tena kwa haraka sana.

    Hawakujiuliza sana kuhusiana na usafiri ambao wangeutumia siku hiyo, teksi ya kukodi ndio ambayo ingetumika katika kufanya safari zao za huku na kule.



    Walichokifanya mara baada ya kuweka majadiliano ya muda mrefu, wakachukua ramani ambayo ilikuwa katika begi na kisha kuanza kuiangalia kwa makini.

    Wakaanza kupanga kila kitu kwamba mara baada ya kumaliza kufanya kazi ambayo ilikuwa imewaleta nchini Tanzania basi ilikuwa ni lazima kuondoka kuelekea



    nchini Kenya tena kwa gari kwa kupitia njia ya Tanga, njia ambayo ingewafanya kutokea Mombasa na kisha huko kupanda ndege na kurudi nchini Marekani.

    Kwao, kazi hiyo wala haikuonekana kuwa ngumu hata kidogo, waliona kwamba ingeweza kufanyika ndani ya masaa machache hata kabla ya kumtaarifu Katie na



    kumwambia kwamba kazi aliyokuwa amewatuma ilikuwa imefanyika, tena kwa mafanikio makubwa bila kuwa na tatizo hata moja.

    Walipanga mambo mengi sana, walichokuwa wameanza kukifanya ni kuanza kwenda katika mtaa aliokuwa akiishi Gibson na kisha kuangalia mandhari yote.



    Hawakuona kama kungekuwa na ugumu sana, mitaani huko wala hakukuwa na kamera kama ilivyokuwa katika mitaa mingi jijini New York ambayo ilikuwa



    ikikaliwa na matajiri, mpaka hapo, tayari wakaiona kazi hiyo ya kumteka Prisca kuwa nyepesi sana.

    Muda mwingi walikuwa wakishinda ndani ya chumba cha hoteli huku mishemishe yao ikiendelea kama kawaida, kila kitu ambacho walikuwa wakikipanga



    kilionekana kutokufaa, hivyo walikifuta na kuanza kupanga tena.

    “I will be a doctor (Nitakuwa daktari)” Reuben aliwaambia wenzake.

    “Ok! We will be your assistants (Sawa! Tutakuwa wasaidizi wako)” Filbert alimwambia Reuben.

    Mpango ambao walikuwa wameufikia kwa wakati huo ilikuwa ni lazima wajifanye madaktari ambao walikuwa wametoka nchini Marekani kuja nchini Tanzania



    kwa ajili ya kuwatibia watoto na kuwapa chanjo ambayo ingekuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa mbalimbali hasa katika kipindi cha ukuaji.

    Wote walikuwa wamekwishajua kwamba Gibson alikuwa akiishi na mwanamke ambaye alikuwa na mtoto mdogo hivyo kama wangetumia njia hiyo ingekuwa ni



    rahisi kwao kumpata mwanamke huyo na kisha kutoroka nae kuelekea porini na kumuulia huko huko mbele ya safari kabla ya kuanza safari ya kuelea nchini



    Marekani.

    Mpango ulikuwa umekwishapita, walichokifanya siku hiyo ni kwenda kwenye kituo kikubwa cha upokeaji na usambazaji madawa, MSD (Medical Store



    Departiment) na kisha kuanza kujitambulisha kama madaktari wakubwa ambao walikuwa wametoka nchini Marekani kwa nia ya kuja hapa kwa ajili ya



    kuwafanyia tiba watoto.

    Wasimamizi hawakuonekana kufahamu kitu chochote kile, mbaya zaidi wala hawakuomba hata vitambulisho kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kutolewa kwa



    kila aliyekuwa na nia ya kuomba vitambulisho vyao hasa katika ngazi za chini.

    Kila mtu ambaye alikuwa akipewa fedha, alikuwa akiwaruhusu kufanya mambo mengine ambayo wala hayakutakiwa kufanywa kwa mtu yeyote ambaye



    hakuonyesha kitambulisho cha kumjulisha kama alikuwa daktari.

    “Madawa hayatoki mpaka nivione vitambulisho vyao” Mkuu wa usambazaji madawa katika kitengo hicho, mzee Samweli alimwambia msaidizi wake.

    “Ila mkuu inab.....”

    “Nimesema hakuna. Kama wao ni madaktari iliwabidi waje na madawa yao kama watu wengine wanavyofanya. Wanakuja huku halafu dawa wanategemea



    kwetu, hauoni kama huu ni ujinga?” Mzee Samweli aliuliza.

    “Kama ukiangalia, unaweza kusema ni ujinga, ila naomba ujifikirie mkuu, ni mara ngapi tumekuwa na vitu hapa nchini halafu tukashindwa kuvitumia? Wape



    nafasi waokoe roho za watoto wetu” Mrisho alimwambia mzee Samweli.

    “Sasa wao wameigia ndani ya nchi yao kama nani? Mbona hatujasikia taarifa za ujio wao?” Mzee Samweli aliuliza.

    “Wamesema kwamba walipokuja hapa hawakuja kama madaktari bali walikuja kama watalii mkuu” Msaidizi, Mrisho alimwambia Samweli.

    “Kumbe ni watalii! Sasa utalii na udaktari unaingiliana vipi hapo?” Mzee Samweli aliuliza.

    “Wao ni madaktari ambao wamekuja huku kwa ajili ya kufanya utalii kama sehemu ya mapumziko yao ya likizo. Walipofika hapa, wamesikitishwa na hali



    waliyoikuta hasa kwa watoto. Kwa hiyo sasa, wameamua kuuvua utalii na kuuweka pembeni na kisha kuuvaa udaktari wao na kuingia kazini huku wakiwa na



    lengo moja tu, kuwanusuru watoto wetu ambao wapo katika matatizo makubwa hasa katika kipindi cha ukuaji” Mrisho alielezea kwa kirefu.

    “Hebu waite kwanza niwaone” Mzee Samweli alimwambia Mrisho ambaye aliwaita Reuben na wenzake ndani ya chumba kile.

    Mazungumzo yakaanza upya ndani ya chumba kile. Reuben na wenzake walikuwa wamevaa nyuso za bandia, nyuso ambazo zilikuwa zikionyesha kwamba



    walikuwa na uhitaji wa kuwasaidia watoto wa Kitanzania ambao walikuwa wakikua huku wakishambuliwa na magonjwa mbalimbali.

    Japokuwa walikuwa wakiongea mengi na kukubalika lakini wakaona kwamba kulikuwa na kitu cha ziada ambacho kilitakiwa kufanyika zaidi, umwagaji wa



    fedha ndani ya ofisi hiyo. Hawakutaka kuchelewa, walianza kujiumauma mwisho wa siku noti za dola mia moja zikawekwa mezani. Kwa haraka haraka mzee



    Samweli akazichukua na kuanza kuziangalia, zilikuwa noti za dola mia moja zilizokuwa kumi.

    Kiasi cha dola elfu moja kilionekana kuwa kiasi kikubwa hasa kwa mtanzania kama mzee Samweli ambaye maisha yake yalikuwa yakitegemea sana mshahara wa



    kawaida. Wala hakutaka kujiuliza kama alitakiwa kuzichukua au kuziacha, alichokifanya ni kuziingiza mfukoni.

    “Mrisho, hebu wapeleke stoo na kisha wape watakachokihitaji” Mzee Samweli alimwambia Mrisho ambaye alifanya kama alivyoambiwa.

    Kwa Mtanzania, fedha ndio ilikuwa kila kitu, uwepo wa fedha ulikuwa na nafasi kubwa ya kubadilisha mambo mengi ambayo wala yasingeweza kubadilishwa.



    Fedha ikaonekana kuwa kila kitu, fedha hizo hizo ndizo ambazo zilikuwa zikiwafanya Reuben na wenzake kupelekwa katika stoo ya madawa ambako huko



    wakachagua madawa wanayoyataka na kisha kuondoka.

    Kazi ilikuwa imebaki moja tu, kwanza ilibidi kwenda katika serikali ya mtaa wa Masaki na kuelezea kile ambacho kilikuwa kimewaleta mahali pale, walipofika



    huko, walimwaga kiasi kidogo cha fedha na wakaruhusiwa kufanya kazi zao katika mtaa huo.

    Hawakuishia hapo, napo wakaenda mpaka katika hospitali ya Halmashauri iliyokuwepo Masaki na kisha kuongea na uongozi wa hospitali ambao ulionekana



    kuwa na furaha kupita kawaida, Reuben, Filbert na Endrew wakakaribishwa kuanza kufanya kazi katika hospitali hiyo.

    Matangazo yakaanza kufanyika mitaani kwamba kulikuwa na chanjo ambayo ilikuwa ikitolewa kwa watoto waliokuwa chini ya miaka mitano na hivyo wazazi



    wao walitakiwa kuwapeleka watoto wao wao wenyewe kutokana na kutakiwa kuulizwa maswali mengi kuhusiana na watoto, chanjo hiyo ilitakiwa kufanyika



    siku inayofuatia.

    “Nitampeleka Genuine huko huko kesho asubuhi” Prisca alimwambia mumewe, Gibson.

    “Ni vizuri sana. Usimwache mfanyakazi ampeleke, si umesikia kwamba ni mzazi mwenyewe ndiye anayetakiwa kumpeleka?”

    “Nimesikia mume wangu. Nitampeleka tu. Si wamesema mwisho jioni? Nitahakikisha nampeleka hata saa kumi” Prisca alimwambia Gibson.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana mpenzi. Nenda uko hata asubuhi. Usikawie, hauwezi kujua wingi wa watu. Wahi zako asubuhi tu” Gibson alimwambia Prisca.

    “Sawa. Usijali mume wangu” Prisca aliitikia na kulala huku akiwa na hamu ya kumpeleka mtoto wake akapatiwe chanjo ya kumkinga na magonjwa mbalimbali



    katika kipindi chake cha ukuaji.



    Gibson alikuwa amekaa ofisini mwake huku akiendelea kufanya kazi zake kama kawaida. Kwa wakati huo, akili yake alikuwa ameituliza kwa mke wake tu,



    hakutaka kumfikiria Katie wala kitu chochote ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake pamoja na Katie.

    Alikuwa amekwishaomba msamaha kwa mke wake kwa hiyo wala hakutaka kumkasirisha tena na wala hakutaka kutembea nje ya ndoa. Moyo wake ulikuwa



    ukimpenda mke wake zaidi ya kitu chochote kile katika maisha yake.

    Mtoto wao, Genuine alikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao, alimpenda sana mtoto wake na kumthamini sana. Mara kwa mara alikuwa akitamani kuwa karibu



    nae, kila alipokuwa akimwangalia Genuine, alikuwa akiona umuhimu wa kumpenda zaidi mke wake, Prisca.

    Gibson aliendelea kufanya kazi zake kama kawaida. Ilipofika saa nne asubuhi, akaanza kujisikia hali ya tofauti moyoni mwake. Moyo ukaanza kujaa majonzi



    huku ukiwa mzito. Hali hiyo haikuonekana kuwa ya kawaida moyoni mwake, akaacha kufanya kila kitu na kutulia.

    Hali haikuonekana kubadilika, bado alikuwa akiendelea kuihisi hali ile ile. Amani moyoni mwake ikatoweka, alichokifanya kwa wakati huo ni kuichukua simu



    yake na kuanza kuangalia baadhi ya namba, alipoona ameridhika, akampigia simu mke wake.

    “Umefikia wapi?” Gibson alimuuliza Prisca.

    “Kuhusu nini mpenzi?”

    “Kumpeleka mtoto hospitalini”

    “Ndio najiandaa mpenzi. Nilikuwa nikimnywesha uji kwanza”

    “Sawa. Nisubiri nakuja”

    “Vipi kuhusu kazi?”

    “Hakuna tatizo mpenzi. Moyo wangu umekuwa mzito sana kubaki ofisini, amani imenitoweka kabisa moyoni” Gibson alimwambia Prisca.

    “Mmmh! Sasa tatizo nini?”

    “Bado sijajua. Nisubiri nije huko huko. Nitataka kuwa karibu na familia yangu” Gibson alimwambia Prisca.

    “Sawa. Nakusubiri mpenzi” Prisca alijibu na kisha kukata simu.

    Gibson hakutaka kuendelea kubaki ndani ya ifisi ile, alichokifanya ni kutoka na kisha kuanza kuelekea sehemu ya magari na kuchukua gari lake na kuanza



    kuelekea nyumbani kwake. Hali ya moyo wake wala haikubadilika kabisa, ilikuwa vile vile. Mawazo yalikuwa yakimsonga kichwani mwake, hakujua ni kitu gani



    ambacho kilikuwa kikitaka kutokea ambacho mpaka katika wakati huo kilikuwa kimemkosesha amani kabisa.

    “Kuna nini tena? Mbona najisikia hivi moyoni?” Gibson alikuwa akijiuliza mara kwa mara lakini hakupata jibu lolote lile.

    Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali ile ilivyozidi zaidi na zaidi, alikuwa akiendesha gari lake lakini akili yake ilikuwa ikifikiria mambo



    mengi kwa wakati huo. Alikuwa akizifikiria biashara zake kwa kuona kwamba labda kungekuwa na kitu kingetokea au aliona dalili fulani lakini kila alipokuwa



    akijzifikiria, hakuona jambo lolote lile baya.

    Alifika nyumbani baada ya dakika kumi, kitu cha kwanza ni kuelekea chumbani kwake, alipokuta mke wake, akamkumbatia kwa furaha. Akaendelea kumuelezea



    mke wake juu ya hali ambayo alikuwa nayo moyoni, Prisca ndiye mtu pekee ambaye alikuwa akimtoa wasiwasi moyoni mwake.

    “Usijali mume wangu. Kila kitu kitakuwa salama tu na wala halitotokea jambo lolote lile baya” Prisca alimwambia Gibson.

    “Una uhakika?”

    “Yeah! Hatutakiwi kuogopa kitu chochote kile mpenzi” Prisca alimuondoa wasiwasi Gibson.

    “Ok! Twende huko hospitalini. Leo sitaki kukaa mbali nanyi kabisa. Ninyi ndio kila kitu kwangu” Gibson alimwambia Prisca.

    Alipomaliza kujiandaa, Prisca na Gibson wakaanza kuelekea garini na kisha kuanza safari ya kuelekea katika hospitali hapo Masaki. Walitumia dakika chache



    sana wakawa wamekwishafika katika hospitali ile ambapo Prisca akaelekea kujiandikisha na kurudi benchini kwa mumewe.

    “Vipi?”

    “Nimejiandikisha tu”

    “Kwa hiyo inabidi usubiri hapa kama wenzako?”

    “Ndio”

    “Sawa”

    Waliendelea kukaa katika lile benchi huku wanawake wengine wakiendelea kufika mahali pale pamoja na watoto wao. Baada ya dakika thelathini, zamu ya Prisca



    ikafika na kuingia ndani ya chumba kile kwa ajili ya kuhudumiwa huku Gibson akimsubiria benchini.

    Dakika ziliendelea kusonga mbele lakini Prisca hakutoka nje ya chumba kile jambo ambalo lilionekana kumtia wasiwasi Gibson na kuwakasirisha wanawake



    wengie ambao walionekana kuwa na haraka. Gibson akaendelea kuwa mvumilivu, nusu saa ya kwanza ikapita, saa moja likatimia lakini Prisca hakuweza kutoka



    ndani ya chumba kile.

    Gibson akaonekana kushikwa na wasiwasi, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya chumba kile mpaka mke wake kucheleweshwa kutoka



    namna ile na wakati wanawake wengine walikuwa wakitumia dakika tano hadi kumi.

    Gideon akasimama na kuanza kuusogelea mlango ule na kisha kutaka kuufungua, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani. Tayari Gibson akazidi kushikwa na



    wasiwasi zaidi, alicokifanya ni kuwasiliana na ofisi ya dokta mkuu ambaye akafika mahali hapo haraka sana.

    Wote wakajaribu kufungua mlango lakini wala haukufunguka. Kila mmoja alibaki kuwa na maswali juu ya kitu ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya chumba



    kile.

    “Ngoja nipitie mlango wa nyuma” Dokta kuu, Kimaro alimwambia Gibson.

    “Kuna mlango wa nyuma?” Gibson aliuliza.

    “Ndio”

    Gibson hakutaka kumuacha daktari aende peke yake, alichokifanya ni kwenda pamoja nae. Walipofika nyuma, mlango ulikuwa umefungwa lakini walipojaribu



    kuufungua, ulifunguka. Kila mtu akapigwa na mshangao, ndani ya chumba kile hakukuwa na mtu yeyote yule jambo ambalo lilionekana kumshtua kila mtu.

    “Hawapo. Mungu wangu! Mke wangu na mtoto wangu!” Gibson alisema kwa mshtuko.

    *****

    Huduma za kuwahudumia watoto zilikuwa zikiendelea kama kawaida hu wakiwa wamekabidhiwa chumba ambacho kilikuwa na mlango wa nyuma ambao



    ulionekana kuwa kama mlango wa tahadhari. Japokuwa mlango huo ulikuwa haujafunguliwa kwa muda wa miaka mitatu lakini Reuben akahitaji mlango huo



    ufunguliwe.

    Hakukuwa na daktari ambaye alileta ubishi wowote ule, mlango ukafunguliwa. Saa nne asubuhi, huduma ya chanjo kwa watoto ikaanza, wanawake wengi



    walikuwa wamewaleta watoto wao kwa ajili ya kufanyiwa chanjo. Walichokifanya Reuben, Filbert na Andrew ni kuwaandikisha wanawake ambao walikuwa



    wakiwaleta watoto wao pamoja na majina ya wanaume ambao walikuwa wamezaa nao.

    Hiyo ndio ilionekana kuwa nafasi pekee ambayo ingewafanya wao kumjua mwanamke ambaye angekuja mahali hapo na kuona kwamba huyu alikuwa mke wa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Gibson. Wanawake walizidi kumiminika hospitalini hapo pamoja na watoto wao ambako moja kwa moja wakajiandikisha



    majina yao.

    “Is she here? (Yupo hapa?)” Reuben alimuuliza Filbert ambaye alikuwa akiendelea kuandikisha majina.

    “Nope. She ain’t here (Hapana. Hayupo hapa)” Filbert alijibu.

    Bado wanawake walikuwa wakiendelea zaidi na zaidi kujiandikisha katika kupata huduma za watoto wao kupatiwa chanjo katika hospitali ile kutoka kwa



    wazungu ambao walionekana kuja kutoa msaaada bila kufahamu lengo ambalo lilikuwa limewaleta mahali pale na kujifanya kutoa huduma hiyo.

    Dakika ziliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo Prisca alipokuja kujiandikisha. Filbert akaonekana kushtuka, hakuamini kwamba hatimae walikuwa



    wamempata mtu ambaye walikuwa wakimsubiria kwa kipindi kirefu. Alichokifanya ni kusimama na kuelekea ndani ya chumba kile cha tiba huku lengo lake



    likiwa ni kuongea na wenzake.

    “She is here (Yupo hapa)” Filbert aliwaambia.

    “Are you sure? (Una uhakika?)

    “100% (Asilimia mia moja)”

    Reuben hakuonekana kuamini, alichokifanya ni kuufungua mlango huku akijifanya kuwaangalia wanawake ambao walikuwa wamekusanyika katika mabenchi.



    Wanawake zaidi ya ishirini walikuwa wamekaa kwenye mabenchi yale huku mwanaume akiwa mmoja tu, Gibson.

    “There she is (Yule pale)” Fibert alimwambia Reuben.

    Tabasamu pana likaonekana usoni mwa Gibson, tayari alikuwa ameyaona mafanikia makubwa mbele yao, kitendo cha Prisca kufika mahali pale kilionekana



    kumfurahisha kupita kawaida. Alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba yule ndiye alikuwa mke wa mtu ambaye walikuwa wakimsubiria mahali hapo



    kutokana na Gibson mwenyewe kuonekana pembeni yake.

    Walichokifanya ni kuendelea kutoa huduma kama kawaida yao. Waliandaa kila kitu, gari ambalo walikuja nalo tayari walikuwa wamekwishalipeleka nyuma ya



    chumba kile ili lisiwape usumbufu wowote wakati wa kutoka katika hospitali hiyo.

    Wanawake waliendelea kuingia na kutoka mpaka pale zamu ya Prisca ilipowadia. Akasimama huku akiwa amembeba mtoto wake, genuine na kuingia ndani ya



    chumba kile huku mume wake, Gibson akiwa amemuacha benchini.

    Kitu alichokifanya Reuben wakati Prisca ameingia ndani ni kumchukua mtoto wake, Daniel na kisha kumvutisha Prisca kitambaa kilichokuwa na dawa ya



    usingizi, wala hazikupita hata sekunde kumi, Prisca akapitiwa na usingizi mzito.

    Hakukuwa na muda wa kuchelewa mahali hapo, walichokifanya ni kumbeba Prisca pamoja na mtoto wake na kisha kuanza kuelekea nae nje ambako



    wakawaingiza ndani ya gari. Kila kitendo ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akikiona kutokana na lile gari kupakiwa



    nyumba kabisa ya chumba kile, mahali ambapo si watu wengi walikuwa wakifika mara kwa mara.

    “What next? (Nini kinafuata?)” Andrew aliuliza.

    “Lets get out of here (Tuondokeni mahali hapa)” Reuben aliwaambia na kisha Andrew kuwasha gari lile.

    Andrew hakutaka kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kwa kuogopa kushtukiwa, alichokifanya ni kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu na kutoka nje ya



    hospitali ile huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye alikuwa akifahamu kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali pale.

    Safari ambayo walikuwa wameipanga kwa wakati huo ilikuwa ni kuondoka na kuelekea Tanga ambako huko wangeumuua Prisca porini na kuunganisha safari



    yao kuelekea Mombasa na kisha kuelekea Nairobi ambako wangepanda ndege na kuelekea nchini Marekani huku wakiwa wamekwishakamilisha kila kitu



    walichokuwa wameambiwa wakamilishe nchini Tanzania.



    Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, kutokumkuta mtu yeyote ndani ya chumba kile kuliwachanganya zaidi. Gibson hakuonekana kuamini kile ambacho



    alikuwa akikiona, hakuamini kama mke wake, Prisca pamoja na mtoto wake, Genuine hakuwa ndani ya chumba kile. Kila mmoja alikuwa akijiuliza mahali



    ambapo walikuwepo watu hao lakini hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na jibu.

    Kitu walichokifanya ambacho kilikuwa ni cha haraka sana ni kuwasiliana na polisi na kisha kuwaelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Ni ndani ya



    dakika kumi, mapolisi wa kituo cha Masaki wakafika mahali hapo huku wakiongozana na polisi wa kituo cha Oysterbay.

    Dokta akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea hospitalini hapo kuhusiana na wazungu hao ambao walikuwa wamefika mahali hapo kama



    madaktari ambao walifika mahali hapo kwa ajili ya kutoa chanjo kwa watoto wadogo walio chini ya miaka mitano.

    “Unasema walitoka wapi?” Gibson aliuliza.

    “Nchini Marekani” Dokta alijibu.

    Tayari Gibson akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi mahali hapo, kichwa chake kikawa kama kimekwishahisi kitu fulani ambacho kilikuwa kimeendelea mahali



    hapo. Gibson akaondoka na kwenda kukaa pembeni kabisa ya polisi wale huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.

    “Vipi?” Dokta alimuuliza mara baada ya kumuona akiwa ameelekea kule pembeni.

    “Mke wangu na mtoto wangu”

    “Usijali. Tumekwishatoa taarifa polisi, wanalifanyia kazi” Dokta alimwambia Gibson.

    Polisi hawakutaka kulala, mtu ambaye alikuwa akilalamika kwamba mke wake na mtoto wake walikuwa wametekwa na watu kutoka nchini Marekani na ambao



    walijifanya kama madaktari walikuwa wakimfahamu sana. Gibson alikuwa ni tajiri mkubwa nchini Tanzania ambaye alikuwa akisaidia watu mbalimbali nchini



    hasa wale ambao walikuwa na matatizo mbalimbali.

    Ni ndani ya dakika arobaini, waandishi wa habari wakafika mahali hapo na kuanza kupewa maelezo juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea. Muda wote Gibson



    hakuwa muongeaji, alikuwa kimya huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.

    “Ni Katie. Huyu atakuwa Katie tu” Gibson alijisemea.

    Mawasiliano yakaanza kufanyika, tayari polisi walikwishajua kwamba watekaji hao bado wangekuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam tu. Simu zikaanza kupigwa



    sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ulinzi huku aina ya gari lile ambalo walikuwa wameondoka nalo likiwa linatolewa taarifa kwa kila aliyeambiwa



    japokuwa namba zake hawakuwa wakizifahamu.

    Walichokiona kwa wakati huo, walijua fika kwamba watu hao walikuwa na uwezekano wa kuondoka kuelekea Bagamoyo, Barabara ya Morogoro au ile ya



    kwenda Mtwara. Kitu walichoona kuwa cha maana ni kuwasiliana na polisi wote ambao walikuwa katika sehemu hizo na kuwaambia kwamba ulinzi na upekuzi



    wa magari ulikuwa ukihitajika kufanyika tena kwa haraka sana.

    Vyombo vya habari hasa televisheni na redio vikaanza kutangaza kile ambacho kilikuwa kimetokea, kila mtu akaonekana kushangaa, taarifa ile ilionekana



    kuwashtua kupita kawaida. Kila mtu akalaani kitendo kile ambacho kilikuwa kimetokea, utekaji ulionekana kuwa kitu kigeni sana kutokea nchini Tanzania.

    “Watekaji ni lazima wakamatwe na mateka ni lazima wapatikane wakiwa hai” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi, Oswald aliwaambia waandishi wa habari huku



    mapolisi wakiwa wamekwishaanza kazi yao.

    ****



    Taarifa ile ilikuwa ikiendelea kusambazwa kama kawaida na ilivuma kwa kasi hata zaidi ya upepo. Kila mtu ambaye alikuwa akisikia alionekana kutokuelewa ni



    kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea mpaka Prisca na mtoto wake kutekwa manyara.

    Polisi wakaanza kuzunguka ndani ya jiji la Dar es Salaam huku lengo lao likiwa ni kulitafuta gari lile ambalo lilikuwa linaendeshwa na watekaji wale. Kila kona,



    polisi walikuwa wakizunguka zunguka, watu ambao walikuwa wakisafiri kwa kutumia ndege, safari zilikuwa zimesimamishwa kwa muda, msako ulikuwa



    ukiendelea kila kona.

    Kwa wakati huo, Gibson pamoja na dokta mkuu wa hospitali ya Masaki, dokta Philip walikuwa wamekwishafikishwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya



    maelezo zaidi. Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo yake juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea.

    “Ina maana hamna uhakika kwamba watu hao walikuwa madaktari?” Manase ambaye alikuwa polisi aliyehusika zaidi kwenye kuhoji watu alimuuliza dokta



    Philip.

    “Sikuwa na uhakika lakini kila nilipoona vibari vyote walivyokuwa navyo, niliridhika nao na wala sikutaka kuhoji maswali zaidi” Dokta Philip alijibu.

    “Kwa hiyo walikuwa na vibali vyote?”

    “Ndio”

    Manase hakutaka kuendelea kubaki ndani ya chumba kile, akawaacha na kisha kuelekea nje ambako huko akaanza kuongea na polisi wengine, simu zikaanza



    kupigwa sehemu mbalimbali na kisha kurudi tena ndani ya chumba kile.

    Hadi kufikia wakati huo, hali ilionekana kuwachanganya kupita kawaida. Ni kweli walikuwa na uhakika kwamba watu wale hawakuwa madaktari lakini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    walivipata wapi vibali ambavyo viliwaonyesha kwamba wao walikuwa madaktari?

    Kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza lilionekana kuwachanganya kupita kawaida, kwao, watu hao wakaonekana kujiandaa kupita kawaida katika kufanya kila



    kitu ambacho walikuwa wamepanga kukifanya kwa wakati huo.

    “Unahisi kitu chochote kile?” Manase alimuuliza Gibson.

    “Ndio”

    “Kitu gani?”

    “Kuna mtu amehusika katika tukio hili”

    “Mtu gani?”

    “Kuna mwanamke mmoja amehusika”

    “Mwanamke yupi?”

    “Katie”

    “Ndiye nani huyo?”

    “Mcheza filamu za ngono aishiye nchini Marekani”

    Manase na dokta Phillip wakaonekana kushtuka, jibu ambalo alilitoa Gibson likaonekana kuwashangaza sana. Hawakujua ni kwa nini Gibson aliwaamba



    maneno yale, hawakujua kama Gibson alikuwa na uhakika juu ya kile ambacho alikuwa amekisema au la.

    “Unatuchanganya. Ndiye nani huyo?” Manase aliendelea kuuliza.

    “Mcheza filamu za ngono” Gibson alijibu.

    Hapo ndipo Gibson alipoanza kuelezea kila kitu kilichotokea katika maisha yake huku akizungumzia kwa undani kila kitu ambacho alikuwa amekifanya pamoja



    na Katie. Kila mmoja alikuwa makini akimsikiliza, mpaka anamaliza, kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba Katie alikuwa amehusika katika mchezo mzima.

    “Amehusika katika hili” Manase alimwambia Gibson.

    Manase akatoka ndaniya chumba kile na kisha kuanza kuongea na wenzake kuhusiana na kila kitu ambacho alikuwa ameambiwa na Gibson. Taarifa zikaanza



    kutolewa sehemu mbalimbali ila kitu kikubwa ambacho kilikuwa kikihitajika kwa wakati huo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba watekaji wale wanakamatwa na



    hatimae kumtaja mhusika aliyewatuma kufanya utekaji ule.

    “Kuna tetesi zozote?”

    “Ndio. Watu wa Chalinze walisema kwamba waliliona gari hilo likipita kwa kasi”

    “Kuelekea wapi?”

    “Kama si Kilimanjaro, basi itakuwa Tanga”

    “Sawa sawa. Wapigieni simu polisi wa Segera na kuwaambia kwamba inawapasa kuangalia kwa makini magari yote yatakayopita huku sisi tukianza safari



    kwenda huko” Manase aliwaambia na kisha kutoka nje ya ofisi ile pamoja na Gibson na dokta Manase na kisha kuanza kuelekea Segera ambako walijua fika



    kwamba watekaji wale wasingeweza kuvuka salama bila kukamatwa.

    “Chochote kitakachotokea kwa familia yangu. Nitawaua wote waliohusika” Gibson alisema huku akionekana kuwa na hasira.

    ****

    Mara baada ya kutoka katika hospitali ya Masaki moja kwa moja safari ya kuelekea Tanga ikaanza huku wakiwa wamekwishajikamilisha kwa kila kitu. Andrew



    ambaye alikuwa katika usukani akiliendesha gari lile wala hakutaka wachukue muda mwingi kuchelewa njiani, kila alipoona kwamba hakukuwa na magari



    mengi barabarani, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi.

    Prisca bado alikuwa amelala usingizi mzito huku mtoto wake, Genuine akiwa analia kupita kawaida kiasi ambacho akaanza kuonekana kuwa kero kwa watekaji



    wote ambao walikuwa ndani ya gari lile. Kadri Genuine alivyokuwa akizidi kulia na ndivyo ambavyo kelele zile zilionekana kuwa kero zaidi.

    Hawakujua ni kitu gani ambacho walikuwa wakitakiwa kukifanya kwa wakati huo, vichwani mwao kulikuwa kukifikiriwa vitu viwili tu, ilikuwa ni lazima



    wamtupe mtoto huyo barabarani au kama walikuwa wakitaka kwenda nae basi ilikuwa ni lazima kufanya kitu ambacho kingemfanya mtoto yule kutokulia kwa



    sauti kubwa kama ilivyokuwa.

    “What should we do? (Tunatakiwa tufanye nini sasa?)” Filbert aliuliza.

    “Open the window (Fungua dirisha)” Reuben alimwambia Filbert.

    “What for? (Ili iweje?)” Filbert aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “I want to do something (Nataka kufanya kitu)” Reuben alimwambia Filbert.

    “This is crazy Reuben, dont dare to do what you want to do (Huu ni upuuzi Reuben, usithubutu kufanya hicho unachotaka kukifanya)” Filbert alimwambia



    Reuben.

    “I have to do this Fil. If I ain’t do this, then, we are going to die (Inanibidi nifanye hiki Fil. Kama sitofanya hivi, tunakwenda kufa)” Reuben alimwambia Filbert.

    Mtafaruku bado ulikuwa ukiendelea ndani ya gari huku Andrew akiwa bize kuendesha gari kwa kasi. Kitu ambacho alikuwa akikitaka Reuben kilikuwa ni



    kumtupa mtoto Genuine dirishani huku gari likiwa kwenye mwendo ule wa kasi lakini Filbert hakutaka kuona kitu hicho kikitokea.

    Walikuwa wamekwishafika Kimara, sehemu ambayo magari mengi yalikuwa barabarani huku hata idadi kubwa ya watu ikiwa pembezoni mwa barabara. Kitu



    alichokuwa akikitaka Filbert ni kumtupa Genuine katika eneo ambalo halikuwa na wakazi wengi kwani kama wangefanya vile mahali pale basi ilikuwa ni lazima



    kugundulika tu.

    Safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akilitilia mashaka gari lile ambali bado lilikuwa likiendelea na safari ya



    kuelekea Tanga. Kutokana na mwendo wao kuwa mkali, walichukua dakika arobaini wakawa wamekwishafika Chalinze.

    “Twende kulia” Reuben alimwambia Andrew ambaye akakata kulia. Ramani ambayo walikuwa nayo mikononi mwao ndio ambayo ilikuwa ikiwaongoza katika



    kila njia ambayo walikuwa wakienda kwa wakati huo. Lengo lao kubwa kwa wakati huo lilikuwa ni kufika Tanga ambapo huko wangeonganisha mpaka



    Mombasa na kuelekea Nairobi na kisha kuchukua ndege na kurudi nchini Marekani hasa mara baada ya kukamilisha kumuua Prisca.

    Walitembea na gari lao kwa muda wa dakika thelathini, wakaanza kufika katika maeneo mengi ambayo hayakuwa na makazi, maeneo ambayo yalikuwa na miti



    mingi sehemu zilizoonekana kuwa kama pori. Hapo ndipo makubaliano yale yakafikiwa muafaka, walitakiwa kumtupa Genuine kupitia dirishani huku gari



    likiwa katika mwendo ule ule wa kasi.

    Huku wakiwa wamekwishakubaliana kitu cha kufanya, ghafla Prisca akaamka kutoka katika usingizi na kuanza kushangaa mahali ambapo alipokuwa. Fahamu



    zilivyomjia vizuri, akaonekana kukumbuka kila kitu.

    Kitu cha kwanza akaanza kumtafuta mtoto wake, tayari alikuwa katika mikono ya Reuben ambaye alikuwa akijiandaa kumtupa nje Genuine kupitia katika dirisha



    lile huku Filbert akiwa amekwishafungua dirisha.

    Hata kabla Prisca hakuongea kitu chochote kile, Reuben alikifanya kitu kimoja tu, akamtupa Genuine nje kupitia dirisha huku gari likiwa katika mwendo mkali



    wa kilometa 120 kwa saa. Kilichosikika ni sauti ya Genuine tu ambaye akajigonga katika miti kadhaa, damu zikatapakaa katika kila mti aliojiginga na kuwa



    mwisho wake.

    Lilikuwa ni tukio kubwa na baya katika macho ya Prisca, hakuamini kile ambacho alikuwa amekiona kwa wakati ule. Akapiga uy owe mmoja tu, akajikuta



    akipoteza fahamu, tukio ambalo alikuwa amelishuhudia kutupwa kwa mtoto wake lilionekana kumshtua, kumuumiza kupita kawaida.

    Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuonekana kujali, kitu ambacho walikuwa wakikitaka mahali hapo ni kufika Tanga ambapo wangeonganisha mpaka



    Mombasa, ila kabla ya kufika Mombasa, ilibidi wamuue Prisca na kisha kuendelea na safari ya kuingia Mombasa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna tatizo mbele yetu” Andrew aliwaambia huku wakiwa wamekaribia kufika Segera, njia panda ya kuendea Kilimanjaro na Tanga.

    “Kuna nini?”

    “Kuna magari mengi yanaonekana kusimamishwa, nafikiri kuna kitu kinaendelea” Filbert alijibu.

    “Tumia mpango B” Reuben alimwambia Andrew huku akiangalia ramani aliyokuwa ameishika.

    “Usijali. Nimekusikia kiongozi” Andrew aliitikia.

    ****

    Mpango B ukafanyika mahali hapo, Andrew akakata kona kulia na kuingia kichakani. Mwendo ulikuwa ni wa kasi sana, katika kipindi hicho tayari walikuwa



    wamekwishashikwa na wasiwasi kwamba polisi walikuwa wamekwishagundua na hivyo walikuwa katika kila njia kuhakikisha wanakamatwa.

    Bado Andrew alikuwa akiendesha gari kwa kasi, katika kipindi hicho walidhamiria kuingia mkoani Tanga ambako wangeanza kuelekea Zigaya ambako wala



    hakukuwa mbali sana kuingia Mombasa nchini Kenya.

    Kila mtu aklini mwake alikuwa akifikiria lake kwa wakati huo, ni kweli kwamba walikuwa wakitamani sana kufika nchini Kenya ambako huko wangechukua



    ndege na kuelekea nchini Marekani lakini uwepo wa Prisca ndani ya gari uliwafanya kuchanganyikiwa.

    Lengo kubwa hasa ambalo lilikuwa limewaleta nchini Tanzania lilikuwa ni kumuua Prisca lakini cha kushangaza, mpaka muda huo hawakuwa wamekamilisha



    kile kilichokuwa kimewaleta nchini Tanzania japokuwa Prisca walikuwa nae.

    Safari ilikuwa ikiendelea zaidi huku ramani ambayo walikuwa nayo ndio ambayo ilikuwa ikiwasaidia katika kuwaongoza kule ambako walikuwa wakiendelea



    kwenda mbele. Kwanza kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo kilikuwa ni kuingia Tanga mjini ambako wangeongeza mafuta kwenye gari lao na



    kisha kuendelea na safari yao kama kawaida.

    Masaa mawili yakakatika huku wakiwa bado wakitembea porini na ndipo wakaamua kuingia barabarani. Hapo, Andrew akaongeza mwendo zaidi, walijiona



    kuwa nyuma ya muda, walikuwa wakitaka kufika haraka iwezekanavyo ili kazi yao izidi kuwa nyepesi zaidi.

    Wakaingia Tanga mjini saa sita kasoro mchana na moja kwa moja kuanza kuelekea katika kituo cha mafuta kwa ajili ya kuongeza mafuta kabla ya kuendelea na



    safari yao zaidi. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na wasiwasi wowote ule, wakazi wengi wa Tanga hawakuonekana kulitilia umakini tangazo ambalo lilikuwa



    limetolewa katika vyombo mbalimbali vya habari juu ya utekaji ambao ulifanyika jijini Dar es Salaam.

    “Lets make hurry (Tufanyeni haraka)” Filbert aliwaambia.

    “Dont worry. We are safe in here (Usihofu. Hapa tupo salama)” Reuben alimwambia Filbert huku akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule.

    “There is no more peace. I have seen the news on the television about us (Hakuna amani hapa. Nimeona habari kwenye runinga kuhusu sisi)” Filbert aliwaambia.

    “Thats not true. When did you learn to undrestand Swahili language? (Hiyo si kweli. Umejifunza lini lugha ya Kiswahili?)” Reuben aliuliza huku uso wake



    ukiwa na tabasamu.

    “I saw Gibson on the television, then tell me what do you think is goin on (Nimemuona Gibson runingani, aya niambie unafikiri nini kinaendelea?)” Filbert



    alikuwa akijitahidi kuelezea kila kitu ambacho alikuwa amekiona kwenye televisheni lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kumuamini, wote



    walimuona Filbert kuwa mtu muoga sana.

    Kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kula chakula hata kabla safari yao haijaendelea zaidi na zaidi. Wakaenda hotelini na kuingia ndani, wakala



    chakula na kisha kuendelea na safari yao.

    Muda wote huo, Prisca alikuwa amepoteza fahamu, mshtuko mkubwa ambao alikuwa amekutana nao ulikuwa ulimfanya kuwa katika usingizi mzito mpaka



    katika kipindi hicho. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kujali, kupoteza fahamu kwa Prisca kulionekana kuwa nafuu kwao kwa kuamini kwamba hakukuwa



    na usumbufu wowote kwa wakati huo ndani ya gari.

    Wakaanza kushika barabara ya kuelekea Mombasa, daladala nyingi zilikuwepo njiani, idadi ya watu ilikuwa kubwa barabarani huku kila sehemu kukionekana



    kuwa na uchangamfu mkubwa. Kitu ambacho walikuwa wamekifanya kwa wakati huo, waliandaa fedha za kutosha kwa kuamini kwamba kama wangefika



    mpakani, wasingeruhusiwa kuvuka ila kwa kutumia dola ambazo walikuwa nazo, wala kusingekuwa na tatizo lolote lile.

    Safari iliendelea mbele zaidi na zaidi, tayari walikuwa wamekamilisha asilimia themanini ya kazi ambayo walikuwa nayo na zilibakia asilimia ishirini tu, za



    kuingia Mombasa, kusafiri mpaka Nairobi na kisha kuchukua ndege na kurudi nchini Marekani huku wakiwa na ushindi mkubwa mioyoni mwao kitu ambacho



    kingekuwa furaha kubwa kwa Katie ambaye alikuwa amewatuma nchini Tanzania.

    “Tufanyeni kitu kimoja” Filbert aliwaambia.

    “Kitu gani?” Reuben aliuliza.

    “Tumuueni huyu mwanamke kabla hatujaingia nchini Kenya. Yaani namaanisha kabla hatujafika mpakani”

    “Wazo lako zuri. Nafikiri umeona kwamba anaweza kutuletea matatizo hapo mpakani”

    “Hilo ndilo nililolifikiria” Filbert aliwaambia.

    Wazo ambalo lilitolewa na Filbert likaonekana kufaa sana, walichokifanya kwa wakati huo ni kukata kona na kisha kuanza kuingia porini, sehemu ambayo



    wangeweza kumuua Prisca huko na kisha kuendelea na safari yao ya kuelekea mpakani.

    Ghafla, Prisca akarudiwa na fahamu, akabaki akimwangalia kila mtu ndani ya gari lile. Kwa mara ya kwanza hakuonekana kukumbuka kitu chochote kile ila



    baada ya sekunde kadhaa, akakumbuka mambo mengi, likiwepo lile la kutupwa kwa mtoto wake, Genuine.

    Prisca akaanza kulia, akamvamia Reuben kwa lengo la kupambana nae kwa kile kitendo cha kumtupa mtoto wake nje ya gari na wakati gari hilo lilikuwa kwenye



    mwendo wa kasi. Reuben akafanikiwa kumdhibiti Prisca ambaye akalazwa kitini huku akiwa amekandamizwa na kiganya cha Reuben.

    Walipofika porini zaidi, gari likasimamishwa na kisha Reuben kumtoa Prisca nje ya gari huku akiwa amemshika shingoni. Prisca alikuwa akilia kama mtoto,



    akili yake kwa wakati huo ilikuwa kama imechanganyikiwa, hakumpenda Reuben hata kidogo, alikuwa akimchukia kupita kawaida.

    “Niachieeeeee....niachieeee” Prisca alikuwa akipiga kelele lakini Reuben hakuweza kumuachia.

    Kila kitu kwa wakati huo kikaonekana kuwa na amani, mazingira yalionekana kumridhisha kila mtu. Kitendo kilichokuwa kikitakiwa kufanyika mahali hapo



    kilikuwa ni kumuua Prisca na kisha kuondoka kuelekea mpakani.

    Alichokifanya Reuben kwa wakati huo ni kuanza kumkaba roba kali Prisca. Prisca akabaki akitoa milio ya tofauti tofauti huku akijitahidi kutaka kuitoa mikono



    ya Reuben shingoni mwake lakini wala hakuweza kufanikiwa hata kidogo. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Reuben alivyomkaba zaidi



    na zaidi.

    Ghafla, Prisca akaanza kuona kizunguzungu huku giza la mbali likianza kuonekana mbele yake. Tayari kwa wakati huo alikuwa amebakisha muda mchache sana



    wa kuwa hai, muda ambao wala haukuzidi hata dakika mbili. Giza lile alilolkuwa akiliona kwa mbali likaanza kumsogelea zaidi na zaidi, baada ya hapo,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akayafumba macho yake huku akihisi mtoa roho akiwa amekwishamfikia kwa ajili ya kuichukua roho yake.



    Je nini kitaendelea mahali hapo?

    Je Prisca amekufa?

    Je watekaji watakamatwa?



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog