Simulizi : Mwanamke Mwenye Kovu Jeusi
Sehemu Ya Tatu (3)
****************************************
Mida ya saa 9 tulianza kujiandaa kwa ajili ya ile oparesheni tunayoenda kuifanya, tulichukua bastola
kila mtu yake huku tukiwa na risasi za ziada za kutosha kwa kila mmoja kisha tukachukua kamera,
zile picha tulizozipata kutoka kwenye ile kamera, intelligence auto mobile call, kisha kila mmoja wetu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akavaa na kifaa cha kuzuia risasi kifuani, halafu mkuu wetu wa kazi pamoja na Amina walivaa
miwani ambazo zilikuwa zina uwezo wa kuvuta picha umbali wa mita mia mbili. Baada kujihakikisha
tupo tayari tulichukua moja ya gari zilizopo pale kituoni ambayo ilikuwa na namba za kiraia ili isiwe
rahisi kugundulika. Tulianza safari yetu taratibu huku tukiwa tunapiga story tu zingine dereva akiwa
ni mmoja wa wafanyakazi wenzetu pale ofisini aliyejulikana kwa jina la Salimu, ni moja kati ya vijana
ambao mkuu wetu aliwapenda sana kuwatumia katika shughuri ambazo nay eye alikuwa anahusika
tulienda taratibu sana kama vile tukiwa hatuna haraka yoyote huku mkuu wetu akisema ya kwamba
sipati picha jinsi vichwa vya habari kesho au keshokutwa vitakavyokuwa vinapamba na hili tukio,
sijui wataandikaje MUUWAJI AKAMATWA,MUUWAJI AULIWA, POLISI WAFANIKIWA
KUMZIBITI MUUWAJI HATARI, mimi nilikaa kimya tu na kumungalia maana nilijua wazi shughuli
iliyopo mbele yetu si ndogo kutokana na jinsi Yule mwanamke alivyokuwa mjanja na mwepesi wa
kucheza na akili zetu pia nilihofia ya kwamba huwenda alikuwa na habari kuwa tulikuwa tunaenda
hivyo lazima atakuwa amejipanga kwa mawili iwe kukabiliana na sisi au kukimbia, basi tulifika
mpaka kwenye hilo eneo na kupaki gari yetu mbali kidogo ili isiwe rahisi kufanikiwa kuonekana
kisha tukashuka na kupanga ni jinsi gani tutelekea lile eneo mkuu wetu wa kazi akasema eti mimi na
Amina ndio tutangulie halafu wenyewe watakuja kwa nyuma huku wakiwa kama wanafanya kujenga
duara Fulani,nilijua tu Yule mkuu alitaka kama ni jambo baya litukute sisi halafu yeye aepuke sikuwa
na jinsi zaidi ya kutangulia kwani kwa sheria zetu za kazi huwezi kumbishia mkuu wako wa kazi kwa
kila atakalolisema, basi tulitangulia mimi na Amina huku mimi ndio nikiwa kwa mbele zaidi, wakati
tunzazidi kukalibia lile eneo mara kwa mbali nikaona mwanamke akiwa amevalia suruali ya kaki na
juu t-shirt ya rangi ya kijivu akitokea upande wa pili na kuelekea sehemu ambapo palikuwa kama
kuna mwamba Fulani, Yule dada alikuwa makini sana huku akiangalia upande huu mara ule, alipofika
pale akabinua kama jiwe Fulani kisha akazama ndani,atakuwa ndio yeye leo mwisho wake umefika
sijui anatoka wapi nilimwambia Amina huku nikikimbia kwa kasi sana mpaka pale, ambapo nilikuta
lile jiwe likiwa limefunikwa sikupoteza muda pale pale akili ikanituma haraka haraka nikamjulisha
mkuu wa kazi kupitia zile intelligence mobile phones nilizokuwa nimevaa kwamba Yule mwanamke
tumeshamuona alipoingia hivyo basi aongeze kasi waje kwa maana anaweza kutuzidia, sikutaka hata
kusikia jibu lake pale pale nilifungua lile jiwe huku Amina akiwa ameshafika lile eneo, nilihangaika
kwa muda wa kama dakika 2 hivi ndipo nilipofanikiwa kulitoa lile jiwe sikuamini nilichokiona mule
ndani kwani kulikuwa na ngazi zilizokuwa zinateremka kuelekea chini huku kukiwa na mwanga
hafifu, niligeuka nyuma kumuangalia Amina vipi upo fiti nilimuuliza akanijibu kwa kuonyesha ishara
ya dole gumba kwamba yupo sawa, niliangalia kwa mbali nikamuona mkuu wetu akiwa na Salimu
nao wakija lile eneo pale pale nilimuonyesha ishara ya tuzame chini Amina, kisha mimi nikaanza
kushuka zile ngazi.
******************************************
Nilishuka huku nikiwa na tahadhari kubwa sana kwani sikujua Yule adui yetu alikuwa yupo mahala
gani na pia alikuwa na silaha gani na isitoshe sikuwa na pafahamu vizuri mule pangoni,basi kila hatua
niliyozidi kupiga na mwanga ndivyo ulizidi kuongezeka nilipiga hatua kushuka chini huku kwa nyuma
nikimuona Amina akiwa ananifuata kwa ukaribu kabisa, pia nilisikia na vishindo vya kina inspekta
Thomas na Yule Salim na wao ndio walikuwa wamefika na kuanza kushuka zile ngazi wakitufuata,
nilishuka zile ngazi mpaka chini kabisa aithee lilikuwa ni handaki kubwa sana lile kwani kumaliza tu
zile ngazi nilitumia zaidi ya dakika tano nilipofika chini kabisa sikuamini kwani nilijihisi kama vile
nilikuwa nipo sebuleni kwa mtu palikuwa mahali pa pana kabisa pale huku kukiwa na baadhi ya vitu
palikuwa pamechimbwa vizuri kiasi kwamba sikuweza kudhania kama nilikuwa pangoni, palikuwa na
vitu muhimu ambavyo huwa vinakuwepo sebuleni kama makochi, television meza na kadhalika yani
kwa ufupi ilikuwa ni sebule iliyokuwa imekamilika,sikutaka kuendelea kushangaa pale sebuleni
kwani nilijua linaweza kuwa kosa na Yule adui akatukuta pale na kututeketeza wote kwani tulikuwa
tupo kwenye himaya yake hivyo hatukujua alikuwa yupo upande gani.
Nilimsubili Amina na yeye akafika pale kisha na mkuu wetu akafika tukaangalia kisha tukapeana
ishara tutawanyike kwenye ile nyumba iliyokuwa chini ya ardhi tulitawanyika sisi watatu huku mkuu
wetu wa kazi yeye akiwa amebakia pale sebuleni, basi mimi nilielekea upande wa kushoto ambapo
nilikutana na kama chumba Fulani hivi nilipoingia nilikutana na geti la chuma ila likiwa wazi ambapo
ilinibidi niingie kwa uangalifu sana, baada ya kuchungulia ndipo nilipogundua ya kwamba mule ndipo
palikuwa selo ya Yule mwanamke kwani kulikuwa na majeraha ya damu damu sana mule huku
kukiwa na vifaa vya kutesea watu kama shoti za umeme na vingine, nilizidi kushangaa ila sikutaka
kupoteza muda tena nikachumpa upande wa pili nikajikuta nimetokea mahali ambapo nilihisi ndipo
palikuwa chumbani kwake kwa maana palikuwa pazuri ajabu huku kukiwa na mapambo na vifaa
vya kisasa kabisa kama computer, air condition na vingine, nilijiuliza mule chini umeme Yule
mwanamke aliupata wapi? Kwa maana palikuwa kama mchana, nilijaribu kupaangalia pia
nikajihakikisha hapakuwa na mtu nikatoka haraka nikashika korido nyingine nikakuta mahali ni kama
pa wazi Fulani hivi huku pakiwa na njia kubwa iliyokuwa ikielekea mahali ambapo palikuwa na
mwanga zaidi nilizidi kuufuata ule mwanga mwisho nilijikuta nimetokea sehemu ambapo palikuwa na
maji maji yaliyokuwa yamejenga kama mkondo Fulani hivi ukiwa umeingia kwenye kama mwamba
Fulani pembezoni mwa bahari, wakati natoka ili niweze kupakagua vizuri nikaona boat moja ndogo
ikitoka pale na kuelekea baharini umbali wa kama mita mia mbili toka nilipokuwa nimesimama,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mungu wangu atakuwa ndio yeye huyu ametukimbia, nilijikuta nasema kwa sauti ya juu huku
nikilaani, kugeuka kwa nyuma nikamuona Salimu na Amina nao kumbe walikuwa wameshafika pale,
ndipo Salim alipoanza kutuambia ya kwamba yeye ndio alikuwa akimfukuzia alimuona mara ya
kwanza kwa mbele kwenye kona moja akitokomea huku akiwa amebeba mkoba Fulani hivi na begi
ambapo begi lilimzidi uzito hivyo basi aliliacha chini alimkimbiza kwa kuhusi kwamba atamkuta,
hatukuwa na jinsi tena ikatubidi tuanze kuludi sebuleni tumsikilize mkuu wetu atasemaje, tuliludi
huku tukiwa tumelipitia lile begi alilokuwa amelidondosha na kisha kuludi pale sebuleni, kwa kweli
wote tulishangaa jinsi ile nyumba ya chini ya mwanga iliyokuwa kwani kama mtu ungebebwa na
kuwekwa tu pale katu usingehisi chochote kama upo kwenye nyumba iliyopo chini ya ardhi. Tuliludi
pale sebuleni ambapo tulimkuta mkuu wetu yeye akiwa amekaa hana hata wasiwasi, tulimueleza ya
kwamba tayari tumeshamkosa, akasema sawa sasa inabidi tufanye upekuzi mule ndani ili kujua kama
kuna vitu vyoyote ili tuweze kuondoka navyo tulisimama na kuanza kuelekea chumbani kwake
kwanza wakati tunakaribia kuingia mule chumbani mara umeme ukakatika ghafla, mungu wangu
Amina alijihisi woga akanishika mkono na kuning’ang’ania
mule ndani palikuwa giza sana kiasi kwamba hatukuweza hata kuonana sisi kwa sisi na hatukuwa na
mwelekeo wowote ule tena ilitubidi tusimamekwa dakika kadhaa ili tuweze kulizoea kwanza giza
kisha ndipo tujue la kufanya, akili ikanicheza haraka haraka nikatoa simu yangu mfukoni ambayo
ilikuwa na tochi kwa mbele nikaiwasha ile tochi ili angalau tuweze kufanikiwa kutoka mule ndani,
ilibidi tuailishe kwanza zoezi la kuendelea kusachi mule ndani tukaona njia sahihi ni kutoka nje
kwanza kwani hatukujua Yule mtu alikuwa amezima vipi ule umeme na isitoshe pia ingewezekana
akawa ametegehsa hata mabomu mwisho wake tukajikuta wote tunalipuka mule tulianza kutoka nje
kwa tahadhari kubwa sana, tuliporudi mpaka pale sebuleni mara tukasikia sauti ya mtu akizungumza
huku ikiwa na kama mwangwi Fulani hivi, mmeanzisha mapambano sasa sioni hata mmoja wenu
ambaye atakaepona sasa, tuligeuka ili kungalia wapi sauti ilikuwa inatokea mara simu yangu ilipigwa
na kitu ikadondoka chini, sikuaimi kile kitendo kwani kama ilikuwa risasi yenyewe ilitoka bila kelele
yoyote na mlengaji akionekana akiwa na shabaha sana,paligeuka tena mule ndani kuwa giza huku
wote tukiwa tumekumbatiana kwa hofu, nilianza kusikia sauti ya mkuu wetu wa kazi kwa chini chini
akiboboja, nilimfunga mdomo asije kuharibu kila kitu, Yule mwanamke alizidi kuzungumza huku sauti
yake ikiwa kama vile inajirudua rudia “haya kama nyie wanaume kweli tokeni basi tuone leo mwisho
wenu umefika” nilizidi kuchanganyikiwa kiukweli toka nizaliwe sikuwahi kukutana na wakati mgumu
kama siku ile, ilibidi tuwe wapole tu pale kwanza
nilishangaa huyu mwanamkwe si ameondoka na boat sasa ilekuaje tena awepo mule mule ndani
kipindi kile?na kwa nini alihindwa kutuuwa kama kweli alikuwa anatuona Au huyu mwanamke ni jini
nini? Halafu tutachukuaje hatua wakati yeye hatujui amejificha upande gani kwani yeye tu ndio
nilihisi alikuwa anatuona wakati sisi hatukujua alikuwa sehemu gani. Tulikaa pale kwa muda wa zaidi
ya saa tano huku tukiwa hatuna jinsi ya kufanya kwa kuhofia usalama wetu,mpaka baadaye sana
sikumbuki ilikuwa ni saa ngapi ila nahisi ilikuwa ni usiku sana ndipo simu ya mkuu wetu ilipoita na
kuitoa mfukoni tena bila woga na kuanza kuzungumza nahisi ilikuwa ni simu ya mke wake kutokana
na mazungumzo waliokuwa wakizungumza huku akiwa analalamika mbona alikuwa kimya sana siku
nzima bila ya kumpa taarifa yoyote , baada ya kumaliza kuzungumza na ile simu mkuu wetu aliwasha
tochi ya simu yake bila woga alimulika chini pale tulipokuwa tumesimama kwa kuhofia kumulika
pengine kwa kuhisi Yule mwanaharamu angeweza hata kutupa adhabu yoyote ile au kutuuwa pia
kwa maana Yule mwanamke ki ukweli alikuwa katiri sana,kwa pale chini alipomulika niliweza kuiona
simu yangu nikainama na kuichukua wakati naichukua ndipo kwa pembeni yake niliweza kukiona
kama kichuma Fulani chembamba kilichoipiga ile simu mpaka ikaanguka, mimi nilijua ni risasi kumbe
ilikuwa tofauti niliwasha simu yangu na kumulika juu kwa woga woga ndipo nilipoona kumbe kule
juu kulikuwa na vyuma vingi sana hivyo basi kile kipisi kitakuwa kilikuwa kimeanguka tu pia
niliweza kuona vi spika vidogo vikiwa vimewekwa kwenye kona juu kabisa ambavyo ndivyo
nilivyokuja kugundua alikuwa anatumia kutolea ile sauti
nilipata moyo wa ujasiri ghafla tena kwani nilijua sasa sio risasi kama nilivyokuwa nimedhania
mwanzo, niliwambia wenzangu kwa sauti ya kuwanong’oneza ya kwamba inatubidi tutoke mule bila
kuhofia chochote liwalo na liwe,kwani Yule mwanmke alikuwa natuchezea akili tu kwa kutumia
teknolojia hata hakuwepo tulikubalina wote kwa pamoja kisha tukaanza kutafuta njia yakutokea kwa
kutumia tochi ya simu yangu na ya mkuu tulifika mpaka pale sebuleni kisha tukaziona zile ngazi za
kupanda kutoka, pale mwanga hafifu wa nje tulianza kuuona kwani muda ule ilikuwa ni usiku sana
hivyo isingewezekana kuwa na mwanga sana.
**********************************
Tulifanikiwa kutoka nje ilikuwa yapata kama mida ya saa sita hivi usiku pale nje kando kando mwa
bahari palikuwa pametulia sana hakukuwa na pirika pirika zaidi ya kuona kwa mbali boti za wavuvi
zikieleka kando kando mwa bahari baada ya kumaliza shughuli za uvuvi, tulijiangalia kama wote
tulikuwa tupo salama, tulijihakikisha wote tupo salama huku Salim akiwa amefanikiwa kutoka na lile
begi liliokuwa na vitu mbalimbali vya mwanamke mwenye kovu jeusi,tulielekea hadi mahala
tulipokuwa tumepaki usafiri wetu tuliokuwa tumekuja nao,tulilikuta gari likiwa vile vile kama
tulivyokuwa tumeliacha.
****************************
Nilifika kwangu pakiwa pamepambazuka kabisa mida ya saa kumi na moja hivi, basi kwa kuwa
nilikuwa nimechoka na huku usingizi ukiwa umenishika sana niliingia ndani moja kwa moja
chumbani na kulala,bila hata ya kubadili nguo nilizokuwa nimezivaa.
Nilikuja kushituka mida ya saa nne asubuhi baada ya simu yangu kuita ambapo baada ya kuangalia
nilikuta kuna missed call zaidi ya tano, niliangalia simu ilikuwa inatoka kwa Gerald, nilimpigia
ambapo aliniambia Yule mwanamke mwenye kovu jeusi jana usiku alimpigia simu na kumuambia
ajiandae kwani zamu yake ilikuwa imefika kisha baada ya yeye nitafuata mimi, nilicheka kidogo
kisha nikamuambia “sikiliza ndugu yangu huyu mwanamke anatapatapa tu hana lolote kwani mpaka
sasa tumeshafanikiwa kuzibiti uwezo wake wa kupata taarifa zetu kitu ambacho ni kikubwa na kizuri
zaidi halafu pia tumefanikiwa kuyagundua makazi yake ya ajabu yaliyo kwenye pango” nilizidi
kumuhadithia jinsi usiku wa jana yake ilivyokuwa na kila kitu mpaka tulivyofanikiwa kutoka ndipo
Gerald nay eye pia akanambia ya kwamba basi Yule mwanamke atakuwa ni hatari sana kayajuaje
yale makazi kwani kwa upeo wake na kumbukumbu yake ndogo ni kwamba ile ilikuwa ni moja ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
sehemu ambazo zilikuwa makazi ya waarabu enzi za ukoloni ambapo wakoloni walitumia kama
sehemu za kujificha na ikiwezekana kutoroka pindi mambo yalivyokuwa hovyo, kisha Gerald
akanambia ya kwamba mbona hata michoro ya mahala pale yapo mule ofisini na pale panajulikana
kama pameshafungwa na Yule mwanamke pale sijui alipajuaje.tuliongea mengi huku akiniambia ya
kwamba mkono wake ulikuwa ukiendelea vizuri nilimwambia ni vizuri basin a kama nikipata muda
kesho jioni yake nitaenda kumsalimia.
Nilijiinua pale kitandani kisha kuelekea jikoni kwa ajili ya kupasha maziwa kidogo ninywe kisha
niendelee na majukumu mengine kabla ya kujiandaa ili nielekee kazini maana tulipanga tukutane
mida ya saa tisa,
Wakati naingia jikoni chini ya mlango wangu niliona kuna vitu vilikuwa vimetegeshwa huku vikiwa
vimefunikwa na karpet niliviangalia ndipo nilipokuja kugundua kuwa vilikuwa ni vinasa sauti
nilivichomoa pale nikaviweka sebuleni kwa minajri ya kwamba nitavipitia niende navyo ofisini kwani
nilijua ya kwamba vilikuwa tu vimewekwa na Yule mwanamke mwenye kovu jeusi na swali langu
kubwa lilikuwa ni wapi Yule mwanamke alikuwa anavitoa vile vifaa kwani vingine kwa jinsi
vilivyokuwa advanced vingine teknolojia yake hata hapa nchini ilikuwa haijafika kweli mtu
tuliyekuwa tunapambana naye hakuwa mtu wa mchezo hata kidogo.
*********************************
Tulikuwa kwenye ofisi ya mkuu wetu inspekta Thomas tukiwa wanne mimi inspekta Thomas Amina
na Salim, mkuu wetu inspekta Thomas alipandisha juu lile begi tulilolitoa janausiku kule kwenye ile
nyumba ya maficho ya Yule mwanaharamu alianza kulifungualile begi na kutoa vitu vilivyomo mule
ndani, alitoa pesa ambazo zilikuwa kwa juu juu tu pale ndani ya begi ambazo zilikuwa ni pesa za
kimarekani zaidi ya dola elfu mbili kisha kwa chini kulikuwa na sura za bandia zaidi ya kumi na mbili
huku tatu zikiwa ni za kike kisha kulikuwa na kopo Fulani ambali baada ya kulisomoa tuligundua
kulikuwa na sumu hatari sana, nahisi ndiyo aliyotumia kumchoma nayo Gerald kule makaburini,pia
kulikuwa na note book moja ambayo mkuu aliitoa alipojaribu kuiwasha kulikuwa na password, humu
kuna siri kubwa sana inaonekana haiwezekani ifungwa na password ambazo zipo moja kwa moja
kwenye system, alilalama bosi, huku akimsogezea Salimu ajalibu kuifungua, pia tulikuta palikuwa na
passport sita mbili zikiwa za Tanzania huku zikiwa na sura tofauti, na majina tofatu, moja ikiwa ya
Kenya, moja ya Africa kusini, moja ikimuonyesha kama ni raia wa visiwa vya shelisheli humu ya
mwisho ikimuonmyesha kama ni raia wa brazil,mh mh mh aithe huyu mwanamke ni hatari yani hivi
vitu vyote jamani lakini mwisho wake umeshafika,alizungumz Amina huku mwili ukiwa
unamsisimka, chini kabisa ya lile begi kulikuwa na faili ambalo ndani yake kulikuwa na makaratasi
mengi mengi sana, nililichukua na kuanza kuchambua zile karatasi nilikuta mkataba wa Yule
mwanamke wa nyumba ya kupanga nchini Victoria sherisheri, ambapo palionekana ndio palikuwa ni
makazi yake, hapo nilivuta picha na kukumbuka usiku ule aliotukimbia pale na ile boat nahisi ndio
alikuwa anaelekea huko, pia nilikuta mkataba mwingine ukimuonyesha kama mpangaji kwenye
nyumba moja iliyokuwepo mikocheni,pia kulikuwa na karatsi ambazo zilionyesha akiwa na akounti
katika benki ya taifa ya biashara, baada ya kuona karatasi hii pia nikavuta picha za Yule mkaa
marehemu ambaye dada yake ni mfanyakazi wa benki ya biashara pale makuu Zainabu,tena
nilishituka sana kwani mara ya mwisho taarifa nilizozipata ni kwamba Yule dada alikuwa hoi hospitali
ya taifa muhimbili akiumwa sana, mungu wangu nikitoka hapa leo itabidi nijaribu kwenda kumuona
huyu dada sio vizuri nahisi pia atakuwa na siri nzito sana kuhusu huyu mwanamke,nilijikuta najisema
mwenyewe huku tukiendekea kuchambua vitu mbalimbali ndani ya lilebegi,
kwenye zipu ya pembeni ya lile begi Salim alikuta kuna simu aina ya nokia3350 ambapo baada ya
kuiwasha ndipo alipogundua ya kwamba hakukuwa na laini ile wenye ile sumu kulikuwa na meseji
mbalimbali zingine zikioneka zimetoka nje ya nchi na kilichotushangaza zaidi na kutuchanganya
kuna baadhi ya meseji tulizikuta mule zilionyesha kwamba Yule mwanamke alikuwa kama anapewa
maeleko tu ya kufanya kwa malipo huku mtu aliyekuwa akimuelekeza ikionekana kama alikuwa ni
mtu mmoja mkubwa serikalini kwani alimuambia asiwe na tatizo lolote likitokea yeye atamsaidia,
wote tulishangaa, mkuu wetu alichukua simu yake na kujaribu kuipiga ile namba ya simu lakini
haikuita aliambiwa namba aliyopiga haikuwepo, tuliona jambo la msingi ni kuikaihifadhi kisha
tutaenda tume ya mawasiliano kwenda kuulizia wataweza kutusaidia zaidi,tulichambua sana mule na
kuhakikisha kila kilichokuwepo tumekiona ilipofika mida ya saa kumi na moja mkuu wetu alisema
twende tukale kisha mapema kisha tukiludi tumalizie ile kazi kwani yeye alikuwa na njaa sana mimi
nilimjulisha ya kwamba nilikuwa nimeshiba kwani nilikuwa nimetoka kula si muda kabala sijaja
kazini lakini mkuu wetu akasema si shida twende nitakunywa hata kinywaji chochote kwani sio
vizuri nikibakia peke yangu mule ndani, katika kazi kuna muda wa kupumzika alinambia, basi sikuwa
na kipingamizi zaidi kwa maana ningeonekana kama vile nimekataa ofa yake basi tulitoka kuelekea
kwenye mgahawa ambao haukuwa mbali sana pale ofisini huku vile vitu tukiwa tumeviacha mule
ofisini kwa mkuu wetu.
*************************************
Tuliporudi kutoka kula ilitushangaza sana baada ya kukuta ofisi ya mkuu wetu ikiwa wazi wakati
tuliacha pakiwa pamefungwa,baada ya kuingia mule ofisini mule mungu wangu hatukuamini baada
ya kukuta vile vitu vyote vikiwa havipo…..!!!
*****************
Bosi wetu alihamaki kukuta mule ofisini kwake palikuwa peupe ilihali mlango tuliacha akiwa
ameufunga, huku mlango ukiwa umeludishiwa vile vile, tulihamaki sana kutokana na ile hali
“Sasa huu utakuwa ni utoto sasa na haya ni zaidi ya matusi” alisema bosi kuhu akiwa amejaa
ghazabu sana ilibidi tuanze kumshusha zile ghazabu ili tuanza kufuatilia ili kujua ni kipi kilichojiri,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya mkuu wetu kuwa mpole nilitoka nje na kumuita dada aliyekuwa pale kaunta ili kumchuma
maelezo atuambie ni kipi kilichojiri,alikuja huku akionyesha wazi hakuna alilokuwa analifahamu,
baada ya kuingia mule ndani mkuu alianza kumuuliza ya kwamba ni nani aliyeingia mule ndani, kwa
kipindi kile kifupi ambacho sisi tulinda kula? Alionekana kama ni mtu aliyekwa akijaribu kuvuta
kumbukumbu kisha akatuambia ya kwamba alipita pale mapokezi mdada ambaye alikuwa amevalia
sare za kiaskari, na sura yake sio ngeni sana machoni pake, lakini hakumbuki ni nani kwa maana
muda ule kulikuwa na askari wengi sana waliokuwa wamekuja kutoka depo, na muda ule walikuwa
tayari wameshatawayika kwenda kwenye ma lindo sehemu mbalimbali baada ya kumaliza gwaride la
saa 12 pale ofisini, tulimsikiliza kwa makini kisha mkuu wetu akampigia simu mkuu msaidizi wa kituo
huku akimuomba amletee majina ya watu wote waliohudhuria paredi la saa 12 alikuwa na shida nayo
sana,basi Yule OCS hakusita alikuja nayo mle ofisini kuhu akionyesha ya kwamba ndio alikuwa
akiondoka kazini, aliniuliza kama kuna tatizo lolote,mkuu wetu alimjibu ndio kuna vitu vimepotea
mule ofisini kwake katika muda mchache ambao tulikuwa tumetoka kwenda kula sasa kutokana na
taarifa za askari aliyepo mapokezi anadai ya kwamba kuna mwanamke ndio alikuja humu kati ya
wale waliokuwa kwenye paredi lile la jioni.
Basi walikubaliana ya kwamba itabidi kesho asubuhi na mapema watakapoludi kurepoti kabla ya
kwenda kwenye makazi yao basi lifanyike paredi la ugunduzi ambalo latafanywa ka kusaidiwa na
Yule mwanamke wa pale mapokezi, tulitawanyika pale huku mkuu wangu akinisisitizia mimi kesho
niwahi mapema sana kwa sababu toka pale mnazi mmoja nilipokuwa nimepanga mpaka stesheni
hapakuwa mbali sana hivyo itanibidi niwahi ili kufanya lile zoezi. Sikuwa na kipingamizi katika lile
tulikubaliana nao kisha kila mmoja wetu akitawanyika
**********************************
Nilifika kwangu usiku ule mida ya saa mbili usiku baada ya kuoga nilivaa nguo mahususi kwa ajili ya
kulalia kisha nikwa nimekaa naangalia taarifa ya habari, mara simu yangu ikaita alikuwa ni Amina
akinijulisha ya kwamba alikua anaomba kama inawezekana nimsaidie kumpeleka kwake sinza mori
kwani alikuwa na vitu vingi halafu alikuwa amekaa zaidi ya saa toka nilipomuacha pale stendeni ya
vidaladala stesheni bila ya gari yoyote kuja, niliona si mbaya kwani Amina alikuwa ni mmoja ya
wadada niliokuwa nao karibu sana pale kazini yeye pamoja na Jamila ambaye Jamila ni mdada
niliyekuwa nampenda sana toka nilipomjua kwani alikuwa ni mkimya sana huku akiwa ni mtu
asiyekuwa na makuu sema kwa kipindi kila Jamila alikuwa ameenda nchini marekani kwenye course
ya social intelligence kwa takiribani miezi mitatu, muda mwingine nilikuwa namkumbuka sana Jamila
kwani achilia mbali na kumpenda ila alikuwa ni mchapakazi na huku akili yake ikiwa nyepesi sana
katika kuchambua mambo.
Nilimkuta pale stesheni Amina na kumchukua na gari yangu ili kumuwahisha kwakeambapo alikuwa
akiishi peke yake kwa maana nay eye pia aliniambia atajitahidi kesho kuwahi hata kwa kutumia taxi
wani alikuwa hajafanikiwa kununua gari, ili tuje tusaidiane katika lile paredi la utambuzi, basi
tulienda taratibu kutakana na foleni huku tukipiga story mbali mbali tulifika kwake ilikuwa ni mida
ya saa 4 hivi usiku basi wakati tumepaki gari nje tuliona taa za ndani kwake zikiwa zimeweka,Amina
alishituka na kuniambia ya kwamba yeye pindi alipoondoka alicha taa amezizima, wakati tunajishauri
mara kwa ndani kupitia dirishani tuliweza kumuona mtu kwa mbali ambaye baada ya kuona gari
imesimama nay eye alichokifanya ni kuzima taa mule ndani hivyo basi tukakosa ujanja wa kuingia
ndani kwa maana tusingeweza kuingia ndani wakati mtu Yule amezima taa na hatukujua ni nani na
alikuwa na silaha gani.
Tulishauriana pale huku tukiwa hatuna la kufanya hatukutaka kuita watu kwanza tulijua tu atakuwa
ni mwanamke mwenye kovu jeusi atakuwa ameingia kutegesha vinasa sauti vyake au kufanya
upekuzi kama ilivyokuwa ada yake. Lakini kitu kilichotushangaza ni jinsi alivyoweza kucheza na
muda kwani mara zote kila alipoenda sisi hatukuwepo sasa tulijiuliza kwa siku ile alijuje kama Amina
atachelewa kazini. Tulijadiliana pale kwa zaidi ya saa zima kwani yle mtu alikuwa kama akitufanya
watoto akiwasha simu na kuzima mara ya chumbani mara ya jikoni mara ya sebuleni ili mradi tu
kutuchanganya kisha nikamwambia Amina liwalo na liwe nikamuomba bastola yake kisha
nikachungua fungua na kuanza kuingia mule ndani, nilifungua mlango na kuwasha taa pale sebuleni
sikuweza kumuona mtu, palikuwa pametulia tulii, nilijaribu kutazama tena kwenye korido sikuweza
kumuona mtu, nilielekea jikoni wakati natokea tu nikaona mlango wa kule jikoni uliokuwa ukitoka
nje pia ukifunguliwa na mtu akitoka kwa kasi ya ajabu akikimbia kulekea barabarani basin a mimi
sikutaka kupoteza muda nilitoka nje ambapo aliniona nikija kwa kasi kumbe alikuwa makuja na piki
piki akawa ameipaki nyuma ya ile nyumba aliponiona nakuija kwa kasi alishindwa hata kuipanda ile
pikipiki na kuanza kukimbia kwa miguu akielekea barabarani, sikutaka kumuacha nilianza na mimi
kumkimbiza huku nikimjulisha Amina kwa sauti sina hakuka kama alinisikia nilimkimbiza alishika
barabara akawa kama anaelekea sinza parestina alikuwa na mbio za ajabu zijawahi kuona, nilizidi
kumfuata kwa kasi ya ajabu huku bastola ikiwa tayari tayari mkononi na kwa muda mule barabara
ilikuwa imeshakuwa nyeupe kwani watu wengi walikuwa maeshalala ilikuwasaa sita hivi inaelekea
saa saba usiku, basi Yule mtu alipofika sinza makaburini alisimama kidogo na kuningalia kama
nilikuwa bado namfuata aliponiona nilikuwa bado namfuata akakimbilia ndani ya makaburi, namimi
sikutaka kujifikiria nilipofika pale na mimi nikaingia mule makaburini, sikuweza kumuona tena mule
kila upande nilipoangalia hakuonekana, basi nikasimama mule makaburini kwa muda wa kama
sekunde tano huku mapigo ya moyo yakianza kuongezeka nikasogea mbele kama hatua nane hivi
palikuwa na kaburi kubwa ambalo lilikuwa limejengwa kifahari sana na likiwa limeinuka juu ambalo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lilikuwa chini ya mti mkubwa wa mkuyu, nilimuangalia kama alikwa labda amejificha pale mbele ya
lile kaburi lakini sikumuona, nilijikuta nakata tamaa na kuona potelea mbali haikuwa siku yake
kumkamata basi nikageuka ili niludi kwa Amina niende zangu nikalale,mungu wangu kila nilipojaribu
kupiga hatua nilihisi kama kuna kitu kinanivuta kwa nyuma,nilisimama nikajua kama ni Yule mtu basi
atazungumza kitu au atafanya jambo lolote,nilisubili kwa muda wa zaidi ya dakika 5 bila kusikia wala
kuhisi lolote nikajaribu kupiga hatua tena niondoke lakini wapi nilijikuta navutwa tena. Mwili ulianza
kusisimka kwa maana sehemu yenyewe niliyokuwa ni makaburini palikuwa panatisha na ni usiku
nilianza kujisemesha pale ili kama ni Yule mtu basi anijibu lakini wapi palikuwa kimya sana,huku
upepo tu ukivuma kwa mbali,nilijaribu tena kupiga hatua kusogea mbele lakini wapi bado nilivutwa
hapo hapo nikajua mwisho wangu umefika tayari…..!!
*******************************
Nilijitahidi kukauka pale kwa takribani robo saa bila kufanya lolote ili niweze kuona kipi kingefuata
lakini hali ilizidi kuwa tofauti kwani muda ulivyokuwa unaenda ndivyo na mimi woga ulivyozidi
kuniingia, “sasa si unidfanye lolote wewe uliyenishika jamani mbona wanifanyia hivyo” nilijikuta
nazungumza kwa sauti iliyojaa utetemeshi sana, kila nilivyojaribu kuongea kwa nyuma nilihisi kama
sauti ya viumbe wa ajabu amabo walikuwa wanazungumza ,mungu wangu haya yatakuwa mashetani
sasa yamenishika sio bure, nilijikuta najisema mwenyewe moyoni, haiwezekani akawa mtu haya
yatakuwa ni mashetani tu ni hivi nimekuja hapa makaburini mida hii ni saa saba inanenda saa 8
mungu wangu au itakuwa ni mizimu tu ya mtu mmoja wapo hapa makaburini, sasa sijui nitafanyaje
mimi hapa?
mara kwa mbali sana niliweza kuona watu wakiingia mule makaburini mvulana mmoja na msichana
wakiwa wanakuja mitaa ile niliokuwa mimi nilijua tu atakuwa jamaa ameopoa mwanamke anayejiuza
mitaa ile kwani ile ni moja ya sehemu ambapo huwa kuna wasichana wengi wanaofanya biashara ya
kuuza mili yao,pale pale nikajua itakuwa ni pona yangu labda ile mizimu iliyokuwa imenishikiria
nyuma itaniachia,nikaanza kunyoosha mkono juu ili wanione, mungu wangu baada ya kuniona
walikimbia sana huku wakipiga kelele basi namimi nilizidi kushituka huku mapigo yangu ya moyo
yakizidi kwenda mbio, ooh watakuwa wameyaona haya mamizimu yaliyonishika huku nyuma,
mungu wangu leo nimepatikana sio bure, au huyu mwanamke mwenye kovu jeusi atakuwa ni mzimu
nini? Kwanini alikimbilia humu? Na kwa nini namtafuta haonekani jamani,
ilinibidi nisimame pale potelea mbali litakalokuja kutokea na litokee pia huku muda ukizidi kwenda
kila nilipotaka kugeuka nyuma moyo ulikuwa unasita kwa kufohia sura yangu kukuta uso kwa uso na
mizimu, kwani kwa mila za kwetu mtu ukiona sura za mizimu huo ni mkosi kubwa sana katika
maisha. Nilikaa pale huku usingizi ukiwa unaninyemelea sana muda mwingine nilikuwa najihisi
kusinzia mara nashituka na kuendelea kusimama sawa.
Ilipofika mida ya saa 9 hivi nilijaribu kugeuka nyuma kwa minajili ya kwamba litakalokuwa na liwe
niligeuza shingo yangu pole pole sana kuangalia kule nyume kulipokuwa na lile li mti la mbuyu
likubwa bahati nzuri sikuweza kuona kitu chochote, nikageuka mbele na kutaka kuondoka sasa lakini
wapi bado nilijikuta nikiwa navutwa pale pale machozi yalianza kunitoka taratibu na kujua mwisho
wangu ulikuwa umefika tayari maana ile mizimu itakuwa imekasirika kwa mimi kugekuka nyuma na
kuangalia sura zao, niliendelea pale kusimama nakumbuka sikuwahi kusimama kwa kiasi kile zaidi ya
miaka mitano toka nilipotoka kambini, kwa siku ile kwangu ilikuwa ni azabu tosha huku nikijiapiza
kabisa ya kwamba kama nikiweza kunusurika pale itanibidi niombe kujitoa katika kufuatilia ile kesi
kwani majaribu niliyokuwa nakutana nayo na jinsi utata uliokuwa ikijitokeza kila siku ulikuwa
unanchanganya sana.
Nilisimama pale mpaka mida ya saa kumi na moja na robo hivi bila kukosea ndipo moyo wa jasiri
ulipoanza kuniludia tena baada ya kuona tayari pameanza kukucha na jua kutokeza ikanibidi nigeuke
nyuma tena ili kuiangalia ile mizimu ikiwezekana niiombe msamaha kwani muda waliokuwa
wameniweka pale ilikuwa ni adhabu tosha sana upande wangu basi niligeuka taratibu tena
nyuma,sikuweza hata kufanikiwa kuona jambo lolote wala mtu yoyte kula ntuma zaidi ya ndege tu
waliokuwa wapo juu ya ule mti wa mbuyu huku wakiwa wanalia lia kuashiria ya kwamba palikuwa
pamekucha sasa,nilishusha pumzi chini kisha na mapigo yangu ya moyo yakaanza kuludi sawa,kwa
maana wakati nageuka tena mapigo yalikuwa yanenda kasi sana.
Basi baada ya kujihakikishia pale hapakuwa na kitu chochote wala sura ya mzimuwala umbo kwa
mara ya pili tena nikajaribu kutaka kuondoka tena lakini bado nikajihisi navutwa,kuangalia ndipo
nilipokuja kugundua ya kwamba kumbe kuna kipande cha nondo kilichokuwa kimetokeza kwa
pembeni baada ya kaburi kujengewa kumbe ndicho kilikuwa kimechoma kwenye ile suruali yangu ya
kulalia kwa chini na kusababisha nijihisi kama vile nimeshikwa navutwa.nilijichoma pale huku
nikijilaumu kwa woga wangu wote umenifanya nilale makaburini bila ya sababu za msingi.
Niltoka pale makaburini haraka haraka ilikuwa yapata kama mida ya saa kumi na moja hivi
nikaelekea moja kwa moja mpaka nyumabani kwa Amina ambapo nilikuta akiwa na wasiwasi sana
hhuku akinieleza muda wote ule alikuwa hana amani moyoni kwani ilimbidi ampigie mpaka mkuu
wetu simu kumjulisha kuhusu lile tukio, sikutaka kukaa sana kwani nilikuwa na usingizi sana
kutokana na kulala makaburini kwa kujitakia, kisha nilimuhadithia tukio zima kwa nini ilitokea
mpaka mimi nikalakla mule makaburini, alinionea huruma sana huku akiniomba nimsamehe kwani
bila ya yeye kumsindikiza kwake haya yote yasingetokea.
Nilimuambia hakuna shida kwani ile ilikuwa ni kama ajali kazini kisha nikamsisitizia tuondoke naye
muda ule ili mimi niende kwangu nikalale yeye aelekee kazini kwa ajili ya kwenda kufanya lile zoezi
la utambuzi kwani jana amri ilitolewa watu wasitawanyike mpaka lilezoezi liwe limekamilika. Hivyo
basi nilimsisitiza akalifanye lile zoezi kwa uangalifa sana akishirikiana na Yule dada ambaye alikuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mapokezi pia pale pale tilimpigia simu mkuu wetu na kamanda wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni
kumuelezea hali halisi hivyo kama kuna hatua walikuwa wamepanga kuzichua basi waziache mara
moja.
**********************************
Nakumbuka siku ile nililala fofofo sana kwa ajili ya kulala makaburini bila ya kujitakia,ilikuwa
kuamshwa saa kumi na simu ya Gerald iliyokuwa imeita zaidi ya nusu saa sasa niliipokea huku
nikiongea kwa uchovu uchovu sana, aliniuliza wapi nilipokuwa nilimjibu nipo nyumbani kwangu
ndipo kuna kitu kama alikuwa anataka kunielezea kuwa nitafute gazeti jioni ya leo haraka
sana.nilishituka nikajua itakuwa wamefanikiwa kumzibiti Yule mwanamke mwenye kovu jeusi Au
ameuliwa wakati akili sasa inatoka kwenye usingizi ili niweze kumuuliza vizuri kwani kulikuwa kuna
habari gani zaidi hadi anipigie simu na kuongea kwa msisitizo vile mara simu yangu ikakata chaji na
mtaani umeme ulikuwa umekatika….!!!
*********************************
Nililaumu sana juu ya ule ukiritimba uliokuwa ukifanywa na shirika letu la umeme kwani kwa mtu
kama mimi kukata vile umeme walikuwa wananiathiri sana sababu nilikuwa na vifaa vingi sana
ambavyo vilikuwa vikihitaji umeme,mungu wangu sasa hapa nafanyaje? Nilijiuliza nikaona hakuna
jinsi zaidi ya kutoka nje na kwenda kuangalia hilo gazeti lilikuwa na habari gani kwani sikuwa na
uhakika umeme ungerudi muda gani. Basi nilienda bafuni kwanza kuoga kisha nikavaa track suti
zangu ambazo nilikuwa napendelea kuzivaa sana mida ya jioni kisha nikatoka zangu nje huku
mkononi nikiwa nimeshika shilingi elfu moja kwa ajili ya kununulia hilo gazeti nilitoka nje na kushika
barabara mpaka pale mahakama ya mwanzo ya mnazi mmoja ambapo ndipo palikuwa na vibanda
vya kuuzia magazeti nilifika na kuanza kuangalia vichwa vya habari pale vya magazeti huku muuza
magazeti akinitazama kwa umakini sana huku akitazama na gazeti alilokuwa amelishika kama vile
akifananisha kitu hivi
Sikuamini baada ya kuliona lile gazeti ambalo Gerald aliniambia kama nimeliona macho yalinitoka
sana baada ya kuona kichwa cha habari “AFISA WA POLISI AMEFUMWA MAKABURINI
AKIWANGA USIKU WA MANANE” huku juu ya lile gazeti kukiwa na picha zangu tatu zimepigwa
nikiwa natoka makaburini, muyo wangu ulinyong’onyea ghafla nikajihisi mnyonge sana nililichomoa
lile gazeti na kumpa Yule muuza magazeti pesa yake kisha mimi nikaanza kuludi zangu kwangu,
nililikunja lile gazeti mkononi kwa kuwa nilipanga nitaenda kulisomea nyumbani.
********************************
Niliwaza sana kuhusu ile habari kuwa pale juu ya lile gazeti kwanza nilihisi iliwekwa kwa dhumuni la
kunichafua kwani habari yenyewe ilikuwa inadai ya kwamba nilienda kuwanga eti ili nifanikiwe
kumtoa bosi wangu ili mimi niweze kushika ile nafasi huku wakiwa wamepamba na maneno mengi
tu ya uongo roho iliniuma sana kwani nilikuwa kwenye wakati mgumu sana kwanza tayari walikuwa
wameshaanza kunifitinisha na mkuu wangu wa kazi halafu pia ingeweza kusababisha
nikatolewakatika kitengo cha upelelezi kwani sasa kila mahala ningepita watu wangekuwa wananijua
hivyo basi ingeniwia vigumu san katika utendaji wangu wa kazi,nilifikiria lile gazeti la udaku
ambalolilikuwa linatoka kila siku jioni walijuaje kama mimi nilikuwa makaburini mpaka wakanivizia
na kunipiga zile picha, niliona tofauti na mazingira ya kazi yangu kuwa ngumu lakini pia jamii sijui
itanichukuliaje katika lile jambo, hadi kunakipindi nikaanza kujilaumu kwa nini nilikubali
kumsindikiza Amina usiku ule kwake kwani haya yote yasingetokea nilijipa moyo konde kwani
nilijua mimi ni mwanaume jambo lile nikilitilia akilini sana lingeweza kuniathiri hata nishindwe
kufanya mambo mengine niliamua vyovyote itakavyokuwa nitapambana na lolote litakalojitokeza.
Siku inayofuata sikuweza kwenda kazini kwani niliona ni bora kupumzika kwanza ili kuepuka
maneno na pole ambazo ningekutana nazo kutokana na ilie tukio huku siku nzima nikishinda kwa
dada yangu maeneo yak awe.
Kesho yake niliamka asubuhi na mapema sana ili kuwahi kazini kujua ni kipi kilichojiri kwani siku ile
nzima simu yangu haikuwa na chaji hivyo sikuweza kupata majibu kutoka kwa Amina kuhusu lile
zoezi la utambuzi kama lilikuwa limefanikiwa, nilitaka nikapate majibu kisha nielekee kwenye ofisi
za lile gazeti ili kujua ilikuwaje mpaka wakaniandika vile. Wakati naingia ofisini pale wakati napanda
ngazi nilishangaa sana baada ya kuona kila mfanyakazi akinitolea macho huku wakijaribu kama
kunikwepa hivi roho iliniuma sana baada ya kukutana na dada mmoja pale kazini na kumsalimia kwa
kumpa mkono akakataa kupokea mkono wangu na wakati naondoka nikasikia akizungumza ya
kwamba nilikuwa na dawa hivyo basi kwa atakayeshikana mkono na mimi dawa aliyopewa na
mganga eti itamuingia.
Roho iliniuma sana kwa lile tukio nilifika mapokezi ambapo nilisaini kisha kuelekea ofisini kwangu
ambapo Yule dada wa mapokezi pia alikuwa akinitazama kwa wasiwasi. Nilianza kufanya shughuli
mbali mbali mule ofisini kwangu baada ya kama nusu saa simu ya mezani ya mule ofisini iliita
ambapo niliambiwa nilikuwa nahitajika katika ofisi ya kamanda mkuu wa mkoa ambaye yeye ndio
alikuwa mkuu wetu kwa mkoa mzima wa Dar-es-salaam upande wa polisi usalama barabarani na
upelelezi, moyo ulishituka kwani haikuwa kawaida yake kukutana na watu ambao tulikuwa chini ya
upelelzi kwani mambo yote alikuwa akitoa maagizo kwa mkuu wetu wa upelelezi wa mkoa inspketa
Thomas, nilijiinua pale kitini na kutoka na kisha kuanza kupanda ngazi kuelekea floo ya mwisho
ambapo ndipo zilikuwepo ofisi zake niliingia mbapo nilimkuta kama mtu aliyekuwa akinisubiri kwa
hamu sana, alianza kuneleza kwa sauti iliyojaa jazba sana kwamba mimi ni mshirikina sana toka
zamani nawachezea wenzangu pale ofisini kwamba kila jambo lina mwanzo na mwisho “ si unaona
sasa mpaka magazeti yamekuona” enhe hii ni fedheha sana katika jeshi letu hatuwezi kuvumilia hii
hali, aliendelea kuzungumza bila kituo wala kunipa nafasi ya mimi kumjibu, hii haiwezekani hapa
umeenda kinyume na tofauti zetu za kazi haiwezekani kabisa aliendelea kusisitiza,huku akiniambia
kwa aibu zangu kutokana na lile tukio ndio maana hata jana sikuweza kwenda kazini, nilikaa kimya
ambapo alizungumza mengi sana kwamba mimi navujisha pia siri kwa mwanamke mwenye kovu
jeusi ndio maana inakuwa ngumu sana kumkamata “usibishe kuna barua pepe zenu mlizokuwa
mkitumia kuwasiliana nae na simu zenu tumezipata usizani huyo mwanamke wako mnamfuatilia nyie
tu mpo vikosi vingi sana” kisha akaniambia ya kwamba kuanzia muda ule nimeshushwa cheo changu
cha afisa upelelezi msaidizi wa mkoa kwa muda usoijulikana nilijaribu kumuelezea hali halisi jinsi
ilivyokuwa kule makaburini ya kwamba hata kama wanataka kuamini basi wamuulize Amina lakini
hakuonekana hata kunisikiliza, sikia bwana Siwah hili ni agizo kutoka kwa kamishina wa polisi idara
wa upelelezi makao makuu mimi hapa nilipo natimiza amri ya mkuu wangu tu, alisisitizia huku
akinipa na barua na kuonyesha kama ni mtu aliyekuwa akitaka kutoka mule ofisini.
Sikutaka kubishana naye sana kwani nilijua tu ningeweza kupandisha hasira zangu tu, nilitoka mule
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ofisini huku roho yangu ikiwa inaniuma sana baada ya kusikia eti mimi nauhusiano na mwanamke
mwenye kovu jeusi yani juhudi zote nilizozionyesha leo imekuwa vile? Sikuwa na jinsi niliona
wameamua kutumia tu sababu zisizo na msingi ilimradi tu wanitoe kafara. Basi nilitoka pale ofisini na
kuelekea mitaa ya gerezani ambapo ndipo zilipokuwa ofisi zalile gazeti la la jioni leo ambalo ndilo
lilikuwa limeichapa ile habari iliyokuwa inanihusu mimi,nilifika pale mapokezi ambapo nilikutana na
dada mmoja wa pale mapokezi nilimuomba kuonana na mhariri wa lile gazeti, Yule dada alianza
kunijibu majibu ambayo sikuridhika nayo mara mhariri hajaja, oh hawezi kuonana na wewe kwa
muda huu wa asubuhi aliongea mengi nikaona yote hayana maana kisha nikatoa kitambulisho change
nikakiweka pale juu ya meza, alikiangalisha huku pia akinitazama na mimi usoni kisha akasema “oh
kumbe ndio wewe” nilihisi alikuwa tayari ameshajua tu kilichonipeleka pale ni kuhusiana na ile
habari ya juzi kwenye gazeti lao basi alimpigia simu Yule mhariri kisha akanijulisha ya kwamba
naweza kwenda huku akisimama na kunielekeza mahali ambapo ofisi yake ilipokuwa ndani ya lile
jingo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment