Simulizi : Bomu La Karafuu
Sehemu Ya Nne (4)
13 - Mbaroni
Ingawa kitendo cha kuwatia mbaroni wale maafisa wanne kilikuwa cha mafanikio makubwa, bado hali ilibakia tete. Suala kwamba Pei bado alikuwa mikononi mwa wale waendesha magendo halikuwa zuri na ilibidi kuwekwa mikakati ya kwenda kumwokoa na pia kuwatia mbaroni wale waliomteka.
“A5, nakupongeza kwa kazi nzuri hadi hapa tulipofikia, lakini bado ipo kazi kubwa zaidi mbele yetu,“ huyo alikuwa KK.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nashukuru Mkuu, nami pia bado sijaridhika hadi tujue Pei ana hali gani huko aliko, na ndio maana nikaomba huyu Mkurugenzi Swadif tubaki naye,“ BeBe alijibu.
“Mnhuu, A5, nadhani nafahamu ni kwa nini umetaka tubaki naye, lakini hebu eleza mwenyewe fikra zako.“ MB alimuuliza.
“Mkuu, nimeona tuwe naye kwa muda kwa vile yeye anayo mengi ya kutueleza kuhusu huko aliko Pei, kwani naamini kwa ukaribu alionao na hawa jamaa, kwa vyovyote atakuwa ameshafika kule waliko kisiwani Chumbe,“ BeBe alijibu.
“Upo sahihi kabisa A5, fikra zako zimelingana na nilichokuwa nikikifikiria, huyu ndugu kwa vyovyote atakuwa anafahamu ni wapi wamekwenda kisiwani Chumbe,“ MB alisema.
“Ndiyo Mkuu, na si hivyo tu, kwa vile ameshafika huko, basi atatueleza hali ya mazingira ya huko yalivyo, ikiwa ni pamoja na ulinzi uliopo. Hii ni muhimu kwetu kwa ajili ya kupanga vyema mashambulizi,“ BeBe alisema.
“Sawa kabisa A5, nami pia nilipata wazo kwamba huyu bwana anaweza kutupa taarifa zaidi kuhusu hawa jamaa zake waendesha magendo. Ndugu Swadif, umeelewa tunachohitaji kukifahamu?“ KK alimuuliza.
Kwanza Mkurugenzi Swadif alisita, akawa kama asiyetaka kujibu, lakini bila shaka alihisi kuwa hakuwa na pakukwepea, ikabidi aseme ukweli.
“Nimeelewa, nitawapa taarifa mnayohitaji juu ya walikokwenda kule Chumbe.“
“Vyema, basi twende hatua kwa hatua. A5, tuongoze. Ni kipi hasa ungependa kujua kuhusu huko Chumbe?“ KK alimuuliza BeBe.
“Asante Mkuu. Ndugu Swadif, tafadhali jibu maswali yangu kama nitakavyoyauliza. Kwanza tufahamishe, kutoka Chumbe bandarini hadi huko waliko kuna umbali gani?“
“Ni kama kilomita ishirini na nane.“
“Huko waliko ni makazi ya nani, au ni kwa nani?“
“Ni makazi ya Bwana Mudrick, ambaye ndiye kiongozi wao.“
“Ni makazi tu au ndiko pia kituo kikuu cha uendeshaji wa magendo haya ya karafuu?“
Mkurugenzi Swadif alisita kidogo, kisha akajibu: “Si makazi tu, huko....“
Alisita tena, ikabidi KK aingilie kati kwa ukali kidogo.
“Ndugu Swadif, usitupotezee muda, kumbuka hivi sasa na wewe ungekuwa rumande pamoja na wenzio. Jibu ulichoulizwa.“
Mkurugenzi Swadif alimeza funda la mate, kisha akasema: “Sawa, kama nilivyosema kule Chumbe yapo makazi ya Bwana Mudrick, lakini si makazi tu, ndiko pia kuliko na maghala yao.“
“Maghala ya kuhifadhi nini, karafuu?“ BeBe aliendelea na usaili.
“Ndiyo, ni maghala makubwa na ndiko usafirishaji wa karafuu kwenda nje unakofanyika.“
MB na BeBe walimtupia macho KK, ambaye naye aliwatazama akatikisa kichwa kuashiria hilo lilikuwa geni kwake.
“Usafirishaji huo unafanyikaje?“
“Kwa maboti, usiku sana. Ni kwamba zinakuwapo meli za mizigo ambazo hutia nanga mbali na ufukweni, upande wa pili wa kisiwa, na si upande wa bandari ndogo ya Chumbe. Maboti maalum ya hawa jamaa hubeba marobota ya karafuu na kuyapeleka kwenye meli nyakati hizo za usiku.“
“Karafuu hiyo ya magendo wanaipataje?“
Mkurugenzi Swadif alisita tena kwa sekunde kadhaa, kisha akashusha pumzi na kusema:
“Ni mfumo ambao wameuanzisha, ambapo yapo makampuni maalum yananunua karafuu hizo kwa magendo kutoka kwa wakulima na huu mtandao wa Bwana Mudrick unanunua karafuu hizo na kutafuta masoko yasiyo rasmi nje ya nchi.“
“Kwa hiyo ofisi yako ambayo ndiyo yenye dhamana kubwa kwa taifa mnalifahamu hilo, lakini kwa tamaa za kujishibisha binafsi mnafumbia macho na kushiriki kwenye magendo hayo?“ Huyo alikuwa ni KK, kwa sauti kali ya kufoka.
Mkurugenzi Swadif hakujibu, alibaki amejiinamia.
Baada ya kuwapo kimya kidogo pale ndani, BeBe alimuuliza KK:
“Naweza kuendelea, Mkuu?“
“Samahani, ndiyo, endelea A5,“ KK alimjibu.
“Ok, Ndugu Swadif, kuhusu ulinzi huko kwa Bwana Mudrick, kuna ulinzi wa aina gani?“
Mkurugenzi Swadif alimeza tena funda la mate, na safari hii sauti yake ilionekana kupwaya, mfano wa mtu aliyeonyesha kukata tamaa.
“Kuna mageti mawili kwa upande wakuingilia kutokea bandari ndogo ya Chumbe, na kuna mageti matatu kwa upande wa kuingilia kutokea pwani ya upande wa pili. Mageti yote hayo yanalindwa na walinzi wenye silaha za moto, bunduki.“
“Katika kila lindo wanakuwapo walinzi wangapi?“
“Kwa siku ambazo nimewahi kwenda huko, nimeona kuwa kwa mchana kila geti linakuwa na walinzi wawili, lakini usiku idadi hiyo huongezwa mara dufu. Na kwa upande ule wa pili ambako ndiko yanakopita magari ya kupeleka maroborota ya karafuu kwenye maboti, siku ya shughuli ya usafirishaji kunakuwa na ulinzi mkubwa zaidi ambao kwa kweli ziwezi kuuelezea kwa uhakika.“
“Na kwa upande wa eneo la nyumba na kuzunguka nyumba ulinzi ukoje?“
“Kwa kweli ulinzi ni mkali sana. Wapo vijana wengi ambao wanaunda kikosi cha ulinzi cha Bwana Mudrick, hata sifahamu amewatoa wapi na silaha amezitoa wapi. Lakini ni kikosi kikubwa na wanaelekea wamepitia mafunzo ya kutosha.“
“Wanatumia njia yoyote ya mawasiliano wanapokuwa kwenye lindo?“
“Ndiyo, kuna mawasiliano ya redio maalum ambayo inawaunganisha, na kama ujuavyo pia kuna simu za mikononi.“
“Mageti yao yanafungwa na kufunguliwa kwa njia gani? Wanatumia njia za kisasa za umeme au ni mageti ya kawaida ya kufuli na funguo?“
“Mageti ya mwanzo yote ni ya kawaida, ambayo hutumia makomeo na makufuli, lakini mageti ambayo ni ya kuingilia eneo la nyumba pande zote mbili yanatumia umeme.“
“Ndugu Swadif, umeshawahi kwenda na mwanamke huko nyumbani kwa Bwana Mudrick, Chumbe?“
Lilikuwa ni swali la kushitukiza sana kutoka kwa BeBe, hata MB na KK walimtupia macho yaliyokuwa na maswali, lakini yeye alionekana ametulia tuli akisubiri jibu. Kwa upande wa Mkurugenzi Swadif lile swali hakulitegemea kabisa, na ilichukuwa sekunde kadhaa kwa kulitafakari na kulijibu.
“Mnh, kwa nini unaniuliza swali hilo?“
“Nafahamu kwa nini nimeuliza. Tafadhali nijibu.“
“Mmm, ndiyo, niliwahi kufanya hivyo, mara kadhaa.“
“Mara hizo kadhaa, ulikwenda na mwanamke huyohuyo mmoja au wanawake tofauti.“
Mara hii pia Mkurgenzi Swadif alisita akawa anamwangalia BeBe, ambaye naye alimwangalia kwa macho yasiyopepesa akisubiri jibu.
“Mnhuu, aaa, ilikuwa ni wanawake tofauti.“
“Vyema, basi safari hii, leo, utakwenda huko ukiwa pamoja nami.“
Mkurugenzi Swadif alikurupuka kutoka kwenye sofa, akasimama wima kwa kasi ya ajabu, akionyesha dhahiri kuwa matamshi ya BeBe yalimshitua.
“Unasemaje? Hapana, hiyo....hapana, hiyo si rahisi, haiwezekani,“ Mkurugenzi Swadif aling’aka huku akitupatupa mikono hewani kusisitiza mtafaruku uliompata.
MB, KK na BeBe walitupiana macho ambayo yaliuliza maswali na pia kutoa majibu, lakini aliyetamka akasikika ni BeBe.
“Ndugu Mkurugenzi, hakuna lisilowezekana, na hili nililosema linawezekana. Mimi na wewe leo tunakwenda Chumbe kushiriki kwenye shughuli za mwaka koga, na safari hiyo itatufikisha nyumbani kwa Bwana Mudrick.“
MB na KK walitupiana macho, kisha KK akasema: “Hee, A5, ni kweli leo Chumbe kuna sherehe za mwaka koga, na kwa hakika ni usiku wenye wasaa mzuri wa kufanya mashambulizi nyumbani kwa Bwana Mudrick. Habari hii ya mwaka koga umeijuaje A5?“
“Mkuu, nimeisikia kutoka kwa dereva wa gari la kukodi ambalo nimekuwa nikilitumia kwa mchana huu wa leo. Nashauri Mkurugenzi Swadif ampigie simu Bwana Mudrick na amweleza kwamba atakwenda Chumbe kwenye sherehe hizo jioni hii, na amfahamishe kwamba hatakuwa peke yake.“
“Sawa...sawa A5, simu za mkononi za Mkurugenzi ninazo, tulizizima. Ndugu Swadif, tafadhali mpigie Bwana Mudrick na umueleze kama alivyosema partner wako wa leo kwenye sherehe hizo za mwaka koga,“ KK alimwagiza Mkurugenzi Swadif huku akimpa moja ya simu zake.
“Lakinii, jamani mimi ... aah, sihitaji partner, nina mke na siwezi kuonekana hadharani na mwanamke mwingine.“
“Ndugu Swadif, hakuna cha lakini. Wewe unahitaji kujikwamua kwenye janga hili na kuepusha aibu kubwa ambayo itakupata pamoja na familia yako. Narudia tena, ushirikiano wako hadi mwisho wa sakata hili ndio utakaopunguza makali ya kisu ambacho kinaelekea kukukata,“ MB alisema kwa sauti yake ambayo wakati wote ilikuwa tulivu.
“Ndugu Mkurugenzi, ondoa hofu, mimi sitakuwa nawe hadharani. Huko kwa Bwana Mudrick yupo yule mgeni wenu, na unanipeleka nikamstareheshe kama ulivyowapeleka wanawake wengine. Wewe usku huu hutakuwa na shughuli yoyote nzito zaidi ya kuhakikisha kuwa tunapita kwenye mageti yote mawili. Mambo yatakayoendelea baada ya hapo utaniachia mwenyewe,“ BeBe alimweleza.
MB na KK walimtupia macho BeBe ambaye hata hivyo macho yake yalikuwa kwa Mkurugenzi Swadif. Ilikuwa dhahiri kuwa BeBe alikuwa na mpango madhubuti akilini mwake kuhusu kitakachofanyika mara afikapo Chumbe kwa Bwana Mudrick. Si MB wala KK aliuliza lolote.
Mkurugenzi Swadif hakuwa na ujanja, alipokea ile simu kutoka kwa KK, akaiwasha kisha akabonyeza vitufe kadhaa, simu ilipoita na kupokelewa akaongea, huku akiwa ameiweka kwenye spika ili MB, KK, na BeBe nao wasikilize mazungumzo yao.
“Hallo, Bwana Mudrick, habari za tangu asubuhi?“
“Nzuri tu Sheikh Swadif, mbona ulikuwa hupatikani kwenye simu yako ya mkononi?“
“Aaa nilitingwa kidogo kwenye mkutano wizarani, unajua tena kule simu zinazimwa tukiwa ukumbini.“
“Niliongea na sekritari wako akanambia upo mkutanoni, mambo yamekwenda sawa?“
“Ndiyo, mambo yamekwenda salama na jamaa zetu wamefurahi.“
“Vipi, kuna tatizo lolote kwako?“
“Hapana usiwe na wasiwasi, hakuna tatizo, ila nimepiga kukufahamisha kuwa jioni hii nitakuja Chumbe kwa ajili ya sherehe za mwaka koga.“CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Karibu sana Sheikh, tena mimi nimepata mwaliko rasmi kama mmoja wa wageni maalum.“
“Anhaa, hiyo ni habari njema, basi vizuri huenda na mimi nikapewa heshima kupitia mgongo wako.“
“Aaah, hata wewe mkurugenzi, nafasi yako ipo Sheikh. Vipi, utafika kwangu kwanza?“
“Ndiyo, nilipanga kufanya hivyo ili nitokee huko kwako pamoja nawe.“
“Unakaribishwa, nitawaarifu vijana. Vipi utakuwa na mgeni kwa ajili ya mgeni wetu, maana yeye hatakwenda kwenye sherehe?“
“Aaah, hilo ni wazo zuri, bila shaka nitamletea mtu wa kumliwaza.“
“Mie nakupendea hapo Sheikh, na najua uchaguzi wako ulivyo mzuri. Basi nitamwarifu juu ya hilo?“
“Aaah, hapana shaka, nitamletea chombo hata wewe utaona wivu.“
“Akifurahi yeye itakuwa ni furaha kwetu sote. Vipi mkeo atakuruhusu kuja kwenye sherehe bila yeye?“
“Bahati nzuri hivi sasa yeye na watoto wapo bara kwa shughuli ya arusi ya yule mdogo wetu.“
“Ooh, imekuwa kheri kubwa. Basi tutaonana jioni. Tena kuna jambo moja nikufahamishe Sheikh. Huku kwangu tunaye kijana ambaye asubuhi tulipokuwa tukitoka hapo ofisini kwako alikuwa akitufuatilia.“
“Alikuwa akiwafuatilia, mbona sikuelewi.“
“Usitishike, tulimuwekea mtego akanasa, hivi sasa yupo taabani. Tumetumia mbinu zote lakini kakataa kusema lolote. Vijana walitaka kummaliza nikawazuia.“
“Hee, kwa hiyo bado yupo hai?....Sasa mnakusudia kumfanya nini?“
“Tumempa muda wa kurudisha fahamu na kupata nguvu kidogo halafu mbinu mpya na mbaya zaidi zitatumika, asiposema katumwa na nani basi, itakuwa ndio mwisho wake.“
“Aaah, unajua haya mauaji nayo yakizidi...“
“Sheikh, hakuna anayependa kupoteza roho ya mtu, lakini ikibidi kufanya hivyo inafanyika, maana ukimwacha aishi pia ni tatizo.“
“Naelewa Bwana Mudrick, lakini yakizidi...“
“Tatizo lako Sheikh una moyo laini sana. Kwenye shughuli hizi inabidi uwe na moyo mgumu kidogo, la sivyo mambo hayawezi kwenda.“
“Sawa, hayo nawaachia wenyewe, lakini ikiwezekana mwacheni aende zake.“
“Teh teh teh, tumwachie ili akawaeleze waliomtuma kuhusu shughuli zetu! Hilo tuliache, je huko kwako ni salama kabisa, hakuna tukio lolote lisilo la kawaida?“
“Mnh, hapana kwangu hakuna tukio lolote linalotia wasiwasi.“
“Vizuri, lakini uwe mwangalifu, inawezekana huyu hakuwa peke yake.“
“Sawa..Basi vyema tutaonana hiyo jioni.“
“Aaah, Sheikh, karibu ningesahau. Ni kwamba usiku huu tutatumia hali ya sherehe ya mwaka koga kutoa sehemu ya shehena ya karafuu kwenda kwa jamaa zetu wa nje.“
“Anhaa, ni kweli ni usiku mzuri kwa shughuli hiyo, sasa utajigawaje?“
“Hilo si tatizo, vijana wa kazi wapo.“
“Aaah, sawa, najua unao vijana makini, na yule mgeni wenu vipi?“
“Yupo hapa nyumbani, ataondoka na huo mzigo. Ndio maana nikasema uje na mgeni ili awe naye hadi atakapoondoka.“
“Anhaa, nimekuelewa, na muda wa shughuli utakuwa wa kawaida?“
“Ndiyo, nyakati zetu ni zilezile, lakini yawezekana leo tukawahi kidogo, maana hata wavuvi siku ya sherehe kama hii hurudi mapema majumbani, na wengine hawaendi kabisa.“
‘Basi vizuri Bwana Mudrick, tutaongea zaidi nitakapofika huko.“
Mkurugenzi Swadif alikata simu na akaikabidhi tena kwa KK, ambaye aliichukuwa akaizima kisha akaitia mfukoni mwa suruali yake.
“Vizuri sana Ndugu Swadif, kwa hakika umetoa msaada mkubwa hadi sasa, na hasa kwenye mazungumzo hayo ya simu. Siwezi kuahidi lolote kubwa, lakini tutajitahidi kuona unafaidika kwa namna moja au nyingine kutokana na ushirikiano huu unaotupa,“ KK alimweleza Mkurugenzi Swadif.
“Ni kweli, hata mimi nakupongeza sana kwa ushirikiano huu unaoutoa, ingawa bado kuna kazi kubwa zaidi mbele yetu na utahitajika kutoa ushirikiano mkubwa zaidi. Nami pia nakuahidi kuwa jitihada zitafanyika kuona ni jinsi gani tunaweza kukusaidia huko mbele,“ MB naye alimpoza Mkurugenzi Swadif.
“Wakuu, naona muda unakwenda, ningeomba twende faragha, tumuache Ndugu Swadif ili tukazungumzie masuala mengine,“ BeBe alisema.
“Sawa A5, waite vijana wawili hapo nje waje wakae na Ndugu Swadif,“ MB alimwagiza BeBe.
“Ni kweli, hata mimi nakupongeza sana kwa ushirikiano huu unaoutoa, ingawa bado kuna kazi kubwa zaidi mbele yetu na utahitajika kutoa ushirikiano mkubwa zaidi. Nami pia nakuahidi kuwa jitihada zitafanyika kuona ni jinsi gani tunaweza kukusaidia huko mbele,“ MB naye alimpoza Mkurugenzi Swadif.
“Wakuu, naona muda unakwenda, ningeomba twende faragha, tumuache Ndugu Swadif ili tukazungumzie masuala mengine,“ BeBe alisema.
“Sawa A5, waite vijana wawili hapo nje waje wakae na Ndugu Swadif,“ MB alimwagiza BeBe.
14 – Mipango
Baada ya kuhakikisha kuwa Mkurugenzi Swadif alikuwa chini ya ulinzi madhubuti pale sebuleni, MB, KK na BeBe walihamia kule kwenye chumba cha kulala, wakawa na kikao.
“Angalao tumepata matumaini kuwa Pei bado yu hai, kama alichokisema huyo aitwaye Mudrick ni cha kweli,“ MB alianzisha maongezi.
“Ni kweli, inatia matumaini, na kwa jinsi alivyosema yule bwana inaelekea kuna ukweli ndani yake,“ KK alisema.
“Wakuu, mimi naamini kuwa Pei bado yupo hai, lakini kama tulivyosikia kutoka kwa huyo Mudrick, mwenzetu atakuwa katika hali mbaya sana, na tusipoweza kumwokoa leo basi tutampoteza,“ BeBe alisema.
“Upo sahihi A5, kwa vyovyote vile jitihada leo zifanyike aokolewe. Je, umeshafikiria kipi cha kufanya?“ MB alimuuliza.
“Mkuu, unakumbuka siku ya kwanza kabisa tulipokutana hapa nilikwambia kuwa usijeshangaa ukasikia nimeolewa huku Unguja. Basi leo ndiyo siku ya kupata mchumba,“ BeBe alijibu huku akitabasamu.
“Enhee, tueleza, mkakati huo ukoje?“ KK alimuuliza, naye pia akiwa na tabasamu.
“Kama nilivyosema muda mfupi uliopita, nitakwenda huko chini ya kivuli cha Ndugu Swadif, na hii imerahisishwa sana kwamba nitakuwa ni mgeni wa kumliwaza mgeni wao. Hii ina maana kuwa nitabaki naye wakati wao wakienda kwenye mwaka koga. Nadhani sina haja ya kueleza kitakachotokea nikibaki na mgeni huyo huko nyumbani kwa Mudrick,“ BeBe alisema.
“Nina kuelewa, lakini fahamu kuwa kama alivyotueleza Ndugu Swadif huko kuna ulinzi mkubwa, je unadhani peke yako utaweza kuwadhibiti?“ KK aliuliza.
“Sitakuwa peke yangu. Dereva wa gari ambayo ninaitumia ni askari mstaafu, na ndiye atakayeendesha gari ya Bwana Swadif. Anaonekana ni mtu jasiri na anaweza kutumia silaha. Nadhani tukijipanga vizuri tutawadhibiti hadi msaada utakapotufikia,“ BeBe alijibu.
“Nadhani A5 yupo sahihi. Hii ni siku yao pia ya kusafirisha karafuu, kwa hiyo ulinzi wao utagawanyika, na bila shaka watauelekeza zaidi katika ile njia ya kupitisha marobota ya karafuu. Ikiwa A5 na huyo dereva wataweza kumwokoa Pei naye akawa katika hali ya kuongeza nguvu, basi yatapatikana mafanikio tunayotarajia,“ MB alisema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vyema, na nafikiri tutapanga vizuri MB, itabidi tuwe na mashambulizi kutokea upande wa pili ambapo tutazuia usafirishaji wa karafuu usiku huu,“ KK alisema.
“Naam, hilo ni muhimu sana, itakuwa ni kuzuia usafirishaji wa karafuu na pia kuwatia mbaroni wahusika. Itakuwa kazi ngumu, lakini lazima ifanyike,“ MB alisisitiza.
“Mkakati uliopo ni kutumia kikosi cha wanamaji. Unajua MB, pwani ile ya upande wa pili wa Chumbe siku zote hizi tumekuwa tukiamini inatumika kwa mashua za wavuvi, lakini kumbe ndiyo njia kuu ya kupitisha magendo!“ KK alieleza.
“Kibaya zaidi ni kwamba baadhi ya viongozi ndani ya SIAFU na idara zingine za umma wamekuwa wakilijua hilo lakini wakaficha. Huu sasa ndio mwisho wao,“ MB alisema.
“A5, utaendelea na mkakati wako, na huu upande wa pili ni kwamba askari watatokea pwani kuelekea nyumbani kwa huyo Mudrick. Kitachofanyika ni kwamba magari yao yatakayokuwa yakisafirisha karafuu yatakamatwa moja baada ya lingine yakiwa njiani kuelekea pwani. Nia ni kwamba baadhi ya askari wawe wamefika nyumba kwa Mudrick mapema ili kukupeni msaada,“ KK alielezea.
“Sawa Wakuu, ni mkakati mzuri, nadhani tukiwa makini tutafanikiwa. Na nitaomba tuwe na mawasiliano ya redio wakati wote na kikosi kitachokuwa kazini ili kuweza kuwa na mafanikio mazuri zaidi,“ BeBe alishauri.
“Nakubaliana nawe A5, na kwa bahati nzuri hivi karibuni SIAFU tulipokea radio za kisasa na za masafa marefu kutoka rafiki zetu wa Korea. Tutazitumia katika zoezi hili la leo,“ KK alisema.
“Kuna jambo moja A5, bado natatizika kuhusu huyu Swadif, asije akakugeuka mtakapofika huko kwa huyo Mudrick?“ MB aliuliza.
“Hilo nimelifikiria Mkuu, na nimepata ufumbuzi wake. Sitakwenda naye hadi huko kwa Mudrick, bali ataishia Chumbe, ambapo ataendelea kuwa chini ya ulinzi,“ BeBe alijibu.
“Utawezaje kuingia peke yako huko kwa Mudrick?“ KK naye aliuliza.
“Tayari Mudrick anafahamu kuwa yupo mwanamke atakayepelekwa na Swadif kwa ajili ya huyo mgeni wao. Kwa hiyo tukifika Chumbe, Swadif atampigia Mudrick kutoa udhuru kwamba atamsubiri huko kwenye viwanja vya mwakakoga, na kwamba dereva wake anampeleka huyo mwanamke nyumbani kwa Mudrick. Hivyo ndivyo ninavyofikiria, au mnaonaje?“
“Mmm, sina hakika na atakavyoichukulia huyo Mudrick, lakini naona ni njia nzuri,“ KK alisema.
“Aaa, nadhani ni wazo zuri, hasa kwa vile tayari Mudrick anajua kuwa kuna mgeni atakayepelekwa huko, na kwa vile hamfahamu A5, sidhani kama atashtuka. Wasiwasi wangu ni huyo dereva utakayekwenda naye, je kama wakimshtukia kuwa siye waliyezoea kumuona na Mudrick?“ MB aliuliza.
“Ni kweli Mkuu, hilo linaweza kuwa tatizo, lakini hatuna njia nyingine. Jambo ambalo halitawapa wasiwasi ni kwamba gari tutakalotumia ni analotumia Swadif,“ BeBe alieleza.
“Sawa, mimi nadhani tuendelee na mkakati huo,“ MB alisema.
“Ndiyo, tutakwenda hivyo na mimi pamoja na MB tutakuwepo Chumbe kwenye mwakakoga, lengo letu ni kuhakikisha kuwa Mudrick hatuponyoki,“ KK aliongeza.
Basi hadi mpango mzima wa mashambulizi ulipokamilika pale hotelini tayari ilishakuwa saa kumi na moja za jioni. BeBe alipata fursa ndogo tu ya kwenda kuonana na shogake, Zamoradi kule Michenzani. Alimweleza hali halisi ya mambo yalivyokuwa, japo si kwa undani sana, na akamfahamisha kuwa jioni ile angekwenda Chumbe kuendeleza mapambano.
“Looh, dunia hii, wajua Beli tangu nimfahamu yule Barshid moyo wangu haukuwa mtulivu, na hata aliposema ataka kunioa nilikubali tu kwa kuona amenigharamia kwa kiasi fulani hivi. Lakini kwa hakika nilikuwa na mashaka sana naye,“ Zamoradi alimweleza shogake.
“Ndivyo ilivyo Zamo, chui aweza kuvaa ngozi ya kondoo ukampotea, lakini hayo sasa yatakwisha. Leo usiku tutapambana nao, na sijui nini kitatokea,“ BeBe alisema.
“Mie sina la zaidi ila naomba uwe mwangalifu maana hao utakaopambana nao wanaroho za kinyama,“ Zamoradi alisema.
“Ni kweli, nitakuwa mwangalifu na naamini tutawamudu,“ BeBe alisema.
Waliagana kwenye majira ya saa moja usiku ambapo BeBe aliungana na MB, KK, na maafisa wengine wa SIAFU, ikiwa pia walikuwa naye Mkurugenzi Swadif. Jioni ile Mkurugenzi huyo alipelekwa nyumbani kwake akiwa chini ya ulinzi, ambako alichukuwa gari lake binafsi aina ya Toyota Landcuriser V8. Ilibidi wachukue gari hiyo kwa vile alisema ndiyo aliyokuwa akiitumia wakati alipokuwa katika shughuli zake za binafsi, ikiwa ni pamoja na safari zake zilizopita kwenda Chumbe kwa Bwana Mudrick.
Gari hiyo ya Mkurugenzi Swadif ilikuwa ikiendeshwa na Dereva Kaku, ambaye gari yake aliiacha nyumbani kwake baada ya kuombwa na BeBe aendeshe ile nyingine. Ndani ya gari hiyo alikuwemo BeBe, Mkurugenzi Swadif na vijana wawili kutoka SIAFU, ambao walichukuliwa mahsusi kwa ajili ya kumdhibiti Mkurugenzi Swadif. MB na KK walikuwa ndani ya gari lingine, la SIAFU, ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva wa kikosi hicho.
Msafara wao ulifika pwani majira ya saa moja na nusu hivi na wakakuta kivuko kikiwa ndio kinatia nanga kutoka Chumbe. Kwa kawaida, kivuko hicho humaliza safari zake kila siku saa kumi na mbili jioni, lakini kwa usiku ule ambapo ulikuwa usiku wa mwakakoga, kivuko kiliruhusiwa kufanya safari zake hadi saa sita usiku ili kuwezesha wageni waliotokea Zanzibar mjini na kwingineko waweze kurejea makwao.
Safari ya kivuko kuelekea Chumbe ilianza saa mbili na robo, ambapo magari waliyokuwemo BeBe, wakuu wake na waliofuatana nao yalibahatika kuwa ya mwanzo kuingia kwenye kivuko. Ulikuwa ni mwendo wa nusu saa tu kwa kivuko hicho hadi kufika pwani ya Chumbe, na walipofika tu walikuta shamra shamra zimeanza kisiwani humo kwa mirindimo ya ngoma, mazeze na nyimbo zilizosikika kutoka uwanja wa sherehe za mwakakoga, ambao haukuwa mbali sana na bandari ndogo ya Chumbe.
Mara tu baada ya kutoka kwenye kivuko wakiwa tayari ndani ya magari yao, walikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha polisi cha Chumbe. Yalishafanyika mawasiliano ambapo chumba maalum kilikwishatengwa kwa ajili yao. MB, KK, BeBe na Mkurugenzi Swadif waliingia kwenye chumba hicho ambacho kilikuwa na meza moja ndogo na viti vipatavyo sita. Baada ya wote kukaa kwenye viti, KK alimpa Mkurugenzi Swadif simu yake.
“Mpigie huyo jamaa yako Mudrick, mwambie hutaweza kwenda kwake, yeye aje akukute huku kwenye uwanja wa sherehe, na umfahamishe kwamba dereva wako atanipeleka kwake kwa ajili ya huyo mgeni wenu,“ BeBe alimweleza.
“Aaa, hiyo haitawezekana, sijawahi kwenda kwa Bwana Mudrick nikiwa na dereva, hatakubali,“ Mkurugenzi Swadif alisema.
“Hilo la kukubali au kutokubali tutalisikia, wewe mpigie na umweleze nilichokueleza,“ BeBe alisema.
“Sasaa..., mmh, nitampa sababu gani ya mimi kutokwenda huko? Hawezi kunielewa, hii haijatokea hata mara moja,“ Mkurugenzi Swadif alizidi kuweka pingamizi.
“Mpigie, mweleze kwamba atakukuta hapa, na sababu ni kwamba umekutana na baadhi ya viongozi ambao wamekutaka uwe pamoja nao,“ BeBe alimweleza.
Wakati malumbano hayo yakiendelea kati ya BeBe na Mkurugenzi Swadif, wakuu wake walikuwa kimya wakiwasikiliza. Hatimaye Mkurugenzi Swadif alipiga simu na ilipopokelewa akaiweka kwenye spika, na mazungumzo yakawa:
“Assallaam Alleikum Bwana Mudrick.“
“Wa-alleikum salaam, vipi bwana mbona umetuweka muda mwingi na sherehe zitakuwa zimeanza hivi sasa, kulikoni.“
“Aaah, sheikh wangu wee, wajua tena mambo ya uongozi. Nimefika hapa Chumbe nikajikuta nimo ndani ya msafara wa baadhi ya viongozi wa Serikali, basi nimelazimika kuwa nao na tayari tumekwishaketi. Niwie radhi sana sheikh, lakini kuja huko itakuwa vigumu.“CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Amaa, vipi tena Sheikh Swadif, mimi nilishamwahidi mgeni wetu kuwa atapoza moyo kabla ya safari yake, sasa, looh, mbona umeniangusha!“
“La hasha, sijakuangusha sheikh, hilo nimelitimiza, wala usitie shaka. Dereva wangu atamleta na gari yangu, kisha atamsubiri hukohuko, na......“
“Sheikh Swadif, dereva wako unamwamini, anapajua huku?“
“Namwamini wala usiwe na wasiwasi. Huko kwako hajafika lakini nimemwelekeza vizuri, atafika tu, la muhimu ni kuwapa taarifa walinzi ili wasiwasumbue.“
“Sawa sheikh, basi Inshallah, tutaonana baadaye.“
“Vyema, tutaongea zaidi utakapokuja.“
Baada ya mazungumzo hayo kati ya Mkurugenzi Swadif na Bwana Mudrick, MB, KK na BeBe walitikisatikisa vichwa kuashiria kuridhishwa kwao na hali ilivyokuwa.
“Safi sana Ndugu Swadif, katika hali hii unazidi kujiweka katika mazingira mazuri ya angalao kupunguza makali ya msukosuko uliopo mbele yako. Bado ahadi yetu ni kukusaidia kwa kadri tutakavyoweza,“ KK alisema.
Kilichofuatia ni kwamba Mkurugenzi Swadif aliwekwa chumba cha mahabusu pale pale kwenye kituo cha Polisi cha Chumbe, na aliwekwa chumba cha peke yake. Aliilalamikia sana hali hiyo, lakini malalamiko yake hayakumsaidia.
“Itabidi ukae hapa hadi tutakapokamilisha kilichotuleta huku Chumbe, mengine yatajulikana kesho tutakaporudi Unguja,“ KK alimweleza Mkurugenzi Swadif, ambaye alikuwa amenywea huku akionyesha wazi kukata tamaa kabisa.
Baada ya mazungumzo hayo kati ya Mkurugenzi Swadif na Bwana Mudrick, MB, KK na BeBe walitikisatikisa vichwa kuashiria kuridhishwa kwao na hali ilivyokuwa.
“Safi sana Ndugu Swadif, katika hali hii unazidi kujiweka katika mazingira mazuri ya angalao kupunguza makali ya msukosuko uliopo mbele yako. Bado ahadi yetu ni kukusaidia kwa kadri tutakavyoweza,“ KK alisema.
Kilichofuatia ni kwamba Mkurugenzi Swadif aliwekwa chumba cha mahabusu pale pale kwenye kituo cha Polisi cha Chumbe, na aliwekwa chumba cha peke yake. Aliilalamikia sana hali hiyo, lakini malalamiko yake hayakumsaidia.
“Itabidi ukae hapa hadi tutakapokamilisha kilichotuleta huku Chumbe, mengine yatajulikana kesho tutakaporudi Unguja,“ KK alimweleza Mkurugenzi Swadif, ambaye alikuwa amenywea huku akionyesha wazi kukata tamaa kabisa.
15 – Mwakakoga
Kutokana na maelekezo mazuri waliyopewa na Mkurugenzi Swadif, ambaye pia aliwachorea ramani ya njia ya kupita, BeBe na Dereva Kaku walifika kwenye lango la kwanza la kuingilia nyumbani kwa Bwana Mudrick yapata saa mbili na robo hivi usiku.
Ilikuwa dhahiri kuwa lile gari la Mkurugenzi Swadif lilifahamika vizuri kule kwa Bwana Mudrick, maana walinzi waliokuwepo zamu wakati ule walipoliona tu walifungua lile lango. Hata hivyo, walinzi hao walimwashiria dereva aliegeshe gari hilo pembeni mara tu baada ya kupita kwenye geti. Walilipekuwa gari bila kuwauliza lolote waliokuwemo, zaidi ya kuwasalimia. Bila shaka walinzi wale walishapata maelekezo kutoka kwa wakubwa wao kuwa wageni hao walikuwa wakitegemewa nyumbani kwa Bwana Mudrick.
Baada ya ukaguzi huo, waliruhusiwa kuendelea na safari yao, na BeBe alipata fursa ya kupata picha halisi ya ulinzi ulivyo pale kwenye lango la mwanzo. Aliona wakati wanaondoka kuwa mmoja wa wale walinzi aliongea kwa redio, bila shaka kuwaarifu waliokuwepo huko walikokuwa wakielekea kuwa walishapita pale langoni.
Walifika lango la pili baada ya mwendo wa kama robo saa hivi, nako pia walifunguliwa na kuruhusiwa kupita, safari hii pia waliamriwa kuegesha gari pembeni na upekuzi ukafanyika. Jambo ambalo lilimfurahisha BeBe ni kwamba upekuzi wao uliishia kwenye gari tu, hawakupekuwa mkoba aliokuwa nao au kuwakagua yeye na Dereva Kaku. Wangefanya hivyo bila shaka hali ingekuwa tofauti kwa vile mkoba wake ulikuwa na zana muhimu za kazi, na pia Dereva Kaku alikuwa na bastola na zana nyingine.
Baada ya upekuzi waliruhusiwa kwenda hadi walipofika kwenye jumba la Bwana Mudrick, ambako walinzi wanne waliokuwa na silaha walionekana wakiwa wamesimama katika maeneo tofauti mbele ya jumba hilo. Walipofika mbele ya mlango wa jumba hilo, Dereva Kaku alisimamisha gari, BeBe akatoka akiwa amebeba mkoba wake, mlinzi mmoja akamwashiria aelekee kwenye mlango. Dereva Kaku alipewa maelekezo kuwa akaegeshe gari lake kwenye banda la kuegeshea magari, ambako kwa wakati huo kulikuwa na magari mawili tu yaliyokuwa yameegeshwa.
BeBe aliingia ndani ya lile jumba, na mguu wake ulipovuka kizingiti unyayo ulikutana na zulia nene la katani. Ulikuwa ni ukumbi mkubwa uliopambwa na taa nyingi zilizoning’inia kutoka darini. Mle ndani mlikuwa na masofa kama seti tatu hivi za rangi tofauti, na pembeni upande wa kulia kulikuwa na meza kubwa ya chakula, ilikuwa ni ya viti nane.
Kwa wakati ule pale ukumbini alikuwepo yule mgeni ambaye BeBe na Pei walimpekuwa kule Hoteli ya Ufukoni, ambaye pasi yake ya kusafiria ilionyesha kuwa jina lake ni Seidati Mohanei. Pamoja naye pale ndani alikuwepo mtu mwingine mwanamume wa umri usiopungua miaka hamsini, ambaye BeBe alifahamu baadaye kuwa alikuwa ndiye Bwana Mudrick.
Aliyemkaribisha BeBe alikuwa ni Bwana Mudrick, ambaye alisimama na kumuashiria akae kwenye sofa ambalo lilikuwa karibu na lile alilokuwa ameketi Bwana Seidati.
“Karibu, karibu binti. Bila shaka umetokea kwa Bwana Swadif?“
“Asante, Assallaam Alleikum...ndiyo nimetokea kwa Bwana Swadif.“
“Wa-alleikum salaam, karibu sana. Yeye umemwacha wapi?“
“Yupo Chumbe, viwanja vya sherehe ya mwakakoga.“
“Sawa, karibu sana. Mimi najulikana kwa jina la Mzee Mudrick, na huyu ni mgeni wetu, Bwana Seidati. Nitawaacha hapa nyumbani hadi nitakaporudi kutoka huko kwenye sherehe, bila shaka umeongea na Bwana Swadif kuhusu kuja kwako huku?“
“Ndiyo, nimeongea naye, waweza kutuacha tu, hakuna tatizo.“
“Vyema, Bwana Seidati, huyu binti utakuwa naye hadi muda wa safari yako. Nitakupigia simu baadaye ili kujua mambo yanakwendaje. Binti, unaitwa nani?“
“Naitwa Zamzam.“
“Aaah, jina zuri sana hilo. Haya, Zamzam nakuacha na mgeni wetu, usiwe na wasiwasi, jisikie upo nyumbani. Mengine tutaongea nitakaporudi, bila shaka tutakuwa pamoja na Bwana Swadif.“
“Sawa, asante.“
Bwana Mudrick na Bwana Seidat walitoka pamoja pale ukumbini wakamwacha BeBe peke yake. Katika muda ule wa kama dakika tatu hivi, BeBe alipata nafasi ya kuungalia vizuri ule ukumbi na vilivyokuwamo. Kila kitu kilichokuwamo mle ndani kilikuwa cha thamani kubwa, na ilikuwa dhahiri kuwa ni vitu vilivyonunuliwa nje ya nchi. Kwa mtizamo wa haraka haraka, BeBe alihisi kuwa huenda vitu vile vikawa ni vya kutoka Dubai, au hata nchi za ulaya.
“Magendo...washenzi hawa wanajitajirisha, wakulima wanaishi maisha duni, na Serikali inakosa mapato..“ BeBe alijesemesha kimoyomoyo.
Wakati BeBe akiwa katika fikara hizo, Bwana Seidat aliingia pale ukumbini akitokea nje kumsindikiza Bwana Mudrick. Bwana Seidat hakukaa kwenye sofa bali alisimama karibu na BeBe, akamnyooshea mikono yote miwili na kusema:CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Njoo Bi. Zamzam, nina safari ndefu leo nahitaji kupumzika, twende zetu juu.“
BeBe alisimama, akamruhusu Bwana Seidat amzungushie mkono mmoja kiunoni na kumtomasa, kisha akamwongoza hadi kwenye ngazi, wakapanda ghorofani. Walipofika juu waliingia chumba kimoja kilichokuwa upande wa kulia. Kilikuwa ni chumba kikubwa kilichokuwa na kitanda kimoja kikubwa, yaweza kuwa cha futi saba kwa saba. Ilikuwa ni vile vitanda vinavyoitwa vya mede, ambavyo hunakshiwa kama desturi ya watu wa mwambao ilivyo.
Mle ndani pia kulikuwa na jokofu dogo na meza moja ya ukubwa wa wastani iliyokuwa na chupa ya chai na vikombe kadhaa vya kawaida na vya kahawa. Bwana Seidat alimkalisha BeBe kitandani, naye pia akaketi karibu naye.
“Je, Bi. Zamzam, ungependa kinywaji chochote?“
“Hapana, asante.“
“Basi vyema, nadhani bora tupumzike.“
“Sawa, lakini naomba niingie maliwatoni kidogo.“
“Bila shaka, bibie, ni mlango ule pale.“
Wakati wote ule, BeBe alikuwa bado amejitanda ushungi. Aliinuka, akachukuwa na mkoba wake akatembea kwa mwendo wa pole kuelekea kulikokuwa na maliwato. Huku nyuma alimwacha Bwana Seidat akimkodolea macho na mwili ukimsisimka.
BeBe aliingia maliwatoni akafunga mlango. Haraka-haraka alivua ule ushungi pamoja na gauni la dira alilokuwa amevaa, akatoa kutoka kwenye mkoba wake kaptura nyeusi ya mpira, ambayo alipovaa ilimbana barabara kiunoni na mapajani. Kwa upande wa juu, kifuani alikuwa amevaa sidiria nyeusi, na shingoni alikuwa na mkufu mwembamba wa dhahabu. Masikioni na mikononi hakuwa na hereni wala bangili.
Kutoka kwenye mkoba huo alitoa pia bastola ndogo aina ya Beston, ambayo aliikagua kisha akairejesha ndani ya mkoba. Alitoa kanga moja akaivaa, kisha akajifukiza uturi uliokuwa kwenye kijichupa kidogo cha rangi nyekundu. Alitoa kinasa sauti kidogo kilichokuwa mfano wa kibweta cha kuwekea sigara, akakiwasha na kukirekebisha kisizime hadi ufike muda wa dakika 60 au saa nzima.
Alirejesha na avipanga vizuri vitu vilivyokuwemo kwenye ule mkoba, akajitazama kwenye kioo, kisha akafungua mlango akatoka. Alitembea kwa mwendo wa taratibu wa kunyumbulika hadi pale kitandani. Aliuweka ule mkoba juu ya meza ndogo iliyokuwepo pembeni mwa kitanda, kisha akapanda kitandani.
Wakati huo Bwana Seidat alikuwa kalala chali pale kitandani akiwa amevaa chupi aina ya boksa. Ilikuwa dhahiri kuwa alikuwa akisubiri kwa hamu ujio wa BeBe, aliyemjua kwa jina la Zamzam, maana alipopanda tu pale kitandani, Bwana Seidat aligeuka akampokea kwa kumkumbatia na kumvutia kwake.
BeBe naye hakufanya hiana, alikubali kuvutwa huko akajiachia akumbatiwe. Bwana Seidat alianza kumtomasa BeBe hapa na pale na bibie hakutoa pingamizi, lakini ilipofikia hatua ya bwana yule kutaka kushusha ile kaptura huku akionyesha dhahiri kuwa alishapata moto, BeBe alimshika mkono.
“Mbona una haraka hivyo, Bwana Seidat, hata hatujafahamiana vizuri?“
Kwa sauti iliyopwaya na iliyokuwa na mtetemo, Bwana Seidat alisema: “Aaah, wajua tena, nimetoka kwangu siku nyingi, nina hamu kubwa, nawe ni mwanamke mzuri mno. Waonaje twende kwanza kishapo tutaongea?“
Bwana Seidat alisema hayo huku akiendelea na jitihada za kumvua BeBe ile kaptura, lakini kwa vile ilikuwa imembana mno, ilikuwa si kazi rahisi.
“Mnh, usiwe na mchecheto, kila jambo lataka maandalizi Bwana Seidat, mbona hujaniandaa. Kwani wewe umetokea wapi mwenzangu?“
“Nimetokea Ngazija, lakini nimezaliwa na kukulia Unguja. Tafadhali, naomba niruhusu basi japo ni....“
“Utafanya utakavyo, nimekuja huku kwa ajili yako, lakini kwanza niandae, eeh mpenzi,“ BeBe alisema, akawa anazichezea nywele za kifuani za Bwana Seidat kwa mkono wake wa kulia, huku akiwa amejiegemeza kwa kiwiko cha mkono wa kushoto.
Ilibidi Bwana Seidat asalimu amri, na hali ikawa ni ya kutomasana hapa na pale na huku maongezi yakiendelea. Hata hivyo, maongezi yaliendelea kwa BeBe kuuliza maswali ambayo kama Bwana Seidat angekuwa makini angefahamu kuwa hayakuwa maswali ya kawaida ya watu ambao walikuwa katika hali ya malividavi.
Katika hali ambayo BeBe alimpumbaza kabisa Bwana Seidat kwa mambo aliyokuwa akimfanyia, aliweza kupata taarifa muhimu sana kuhusu shughuli ya biashara ya magendo ya karafuu. Bila kujua, Bwana Seidat alielezea kuwa shughuli yao ilikuwa ni ya sindiketi iliyohusisha watu wengi. Aliwataja washirika wake wa Unguja, ambao baadhi BeBe alishawajua na walishatiwa mbaroni. Lakini aliwataja pia wengine ambao walikuwa watu wenye majina makubwa na vyeo vikubwa katika taasisi mbalimbali za umma.
BeBe aliweza pia kupata taarifa za jinsi usafirishaji wa karafuu za magendo ulivyokuwa ukifanyika na kule zilikokuwa zikipelekwa kuuzwa. Alielezwa pia mipango ya usiko ule ilivyopangwa, akafahamu kuwa tayari karafuu zilikwishapakiwa kwenye malori kwa ajili ya safari ya kuelekea pwani ambako zingevushwa kwa maboti kupelekwa melini. Alifurahi kusikia kuwa wale vijana wawili, Barshid na mwenzake walikuwa wamekwenda pwani na msafara wa malori ili pia kwenda kuhakikisha maboti yapo tayari kwa kazi ya usiku ule.
Hii ya mwisho ilikuwa taarifa nzuri kwa BeBe, kwani ilikuwa na maana kuwa ulinzi uliokuwa umebaki pale kwenye lile jumba haukuwa wa kutisha sana kwa wakati ule. Baada ya kupata taarifa alizozihitaji, BeBe alijifanya kama na yeye kakolea, akajilegeza na kumbusu Bwana Seidat kwenye paji la uso, akaushusha mkono wake kutoka kwenye kifua na kuushusha taratibu huku akimkuna tumboni hadi kufikia kwenye winda wa bukta aliyokuwa ameivaa.
Bwana Seidat alikuwa akitoa mhemo ambao hauelezeki, lakini ilikuwa dhahiri kuwa sasa ilikuwa ni asilimia mia moja asingeweza kuvumilia. Hilo BeBe alilijuwa, basi ndio akazidisha machezo, na kama unavyojua, yasemekana Tanga ndiko kulikoanzia mapenzi, kwa hakika hali ilikuwa mbaya kwa Bwana Seidat.
“Mpenzi, sasa nipo tayari, je unao mpira wa kinga?“ BeBe alimuuliza Bwana Seidat kwa sauti ya kusinzia huku akimbusu tena kwenye paji la uso.
“Aah, sina kondomu, lakini ya nini, kwani hujiamini, au huniamini?“ Bwana Seidat alisema, huku akiwa anavua bukta kwa mikono ambayo ilikosa utulivu.
“Suala sio kuaminiana, bali wajua hatufahamiani na kufanya ngono uzembe ni hatari,“ BeBe alisema akiwa bado anamtomasa kifuani na tumboni.
“Mmm, usijali, tafadhali njoo mwenzio niko vibaya sana,“ Bwana Seidat alisema huku akijaribu kumgeuza BeBe alalie mgongo.
“Fanya subira mpenzi, nilijua hili lingetokea, nimechukua tahadhari, nimekuja nazo kondomu, ngoja nichukue kwenye mkoba wangu,“ BeBe alisema, akajinasua kutoka mikono ya Bwana Seidat.
Aliteremka kutoka kitandani. Akiwa amempa kisogo Bwana Seidat, BeBe alifungua ule mkoba akatoa ile bastola, kisha akageuka kwa haraka huku akiwa amemlenga.
“Kwa usalama wako, tulia tuli Bwana Seidat. Nisingependa kukua au kukujeruhi, lakini ukifanya fyoko sitasita kufanya hivyo.“
“Lakinii...mbona...“ Bwana Seidat alimaka huku akinyoosha mikono yake mbele kama vile anayejaribu kujikinga asipatwe na risasi.
“Hakuna cha lakini, shuka taratibu kutoka hapo kitandani, mikono yako ukiwa umeinyoosha juu, geuka, angalia kitanda....“
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bi. Zamzam...mbona...sikuelewi!“
“Wala hutanielewa. Upo chini ya ulinzi, na kwa taarifa yako, hao jamaa zako Mudrick na Swadif nao pia hivi sasa wameshatiwa mbaroni...usigeuke, piga magoti..“
Wakati Bwana Seidat akiwa katika hali ya kutaka kupiga magoti, BeBe alimpiga kichwani sehemu ya kichogoni kwa kutumia chuma kifupi lakini kizito, kilichokuwa kimeviringishwa nguo. Bwana Seidat alitoa mguno mdogo wa maumivu akaanguka kama gunia tupu, akawa amepoteza fahamu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment