Search This Blog

Sunday 19 June 2022

MKANDA WA SIRI - 2

 







    Simulizi : Mkanda Wa Siri

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jijini Dar es salaam. Peter Kissali (Mwendawazimu) alikuwa kashauwa mtu, na kumwacha mlemle ndani ya gari. Sasa alikuwa Ubungo akiendelea na uendawazimu wake. Alikuwa anataka kufanya kitu kwanza kisha nd'o aende Zanzibar. Ilikuwa ukimwona utaamini kweli alikuwa Mwendawazimu. Alikuwa amevaa suruali ndefu ya kitambaa iliyochanikachanika na kuchafuka sana, mguu wa kulia wa suruali aliyovaa ulikuwa mrefu hadi katika vidole vya mguu ule, wakati mguu wa kushoto ulikuwa mfupi usioweza kufunika hata paja lake tu. Mgongoni alikuwa na kifurushi kikubwa cha kilichotengenezwa kwa kitambaa chakavu chenye matambara na makorokocho mengi sana ndani yake. Alikuwa amekining'iniza mgongoni na kukishika kwa mkono wa kushoto, mkono ukiwa umepita katika bega lake la kulia na kukishika hiko kifurushi kwa nyuma. Hakuwa amevaa nguo yoyote juu, alikuwa tumbo wazi. Huku tumbo lake likiwa na michirizi mingi meusi, ya grisi ama lami, hakuwa na viatu miguuni na mkono wa kulia akiwa ameshika fimbo ndefu ya kuwachapa watu watakaomkaribia. Kuanzia nywele, sura, mavazi na jinsi akivyotembea. Alikuwa anamuaminisha kila mtu amtazamaye kwamba yeye alikuwa Mwendawazimu!



    Ni wiki sasa Mwendawazimu huyo alikuwa akirandaranda katika stendi hiyo ya mabasi ya kwenda mikoani, Ubungo. Watu walimchukulia kama Mwendawazimu wa kawaida. Aliyechanganywa na bangi ama kurogwa. Walimdharau tu...... Kumbe Mwendawazimu alikuwa anasubiri kitu pale Ubungo, na leo alianza kuuheshimu uamuzi wake wa kukaa pale Ubungo kwa wiki mzima na kusubiri. Fikra zake zilikuwa sahihi. Alimuona Martin pale, na alianza kumfatilia Martin kuanzia pale. Mvua na foleni vilikuwa upande wake. Alienda sambamba na ile foleni hadi Magomeni. Yeye akitembea kwa miguu, Martin akitembea kwa gari. Haikuwa kazi ngumu kutokana na foleni ile. Foleni ilivyokuwa kubwa zaidi Magomeni yeye alitangulia kwa miguu hadi Jangwani. Ndipo alipokutana tena na gari la Martin na kuingia kimyakimya. Ingawa alikuwa ametorokwa na Martin kwa mtindo wa kufungiwa ndani ya gari lakini sasa alikuwa na amani moyoni. Kwa kuwa alikuwa ametuma salamu tayari. Ndani ya gari ya Martin aliacha maiti!

    Na sasa alikuwa amerudi tena Ubungo. Akisubiri kitu kingine muhimu sana kwake kabla ya kwenda Zanzibar katika ‘OMS’ kama simu toka kwa Malolo ilivyomtaka.



    Kule Zanzibar, hadi saa tisa alfajiri Zanzibar bado hali ilikuwa ileile. Wajuaji walikuwa bado wanawindana. Lakini kitu ambacho hata wenyewe walikuwa hawakijui, wote shabaha yao ilikuwa ni moja. Malkia alikuwa anawawinda wakina Martin, wakina Martin walikuwa wanamuwinda Malolo. Kwamaana hiyo Malolo ndiye alikuwa shabaha yao kuu wote, uelekeo wa Malolo ndio uliokuwa unaamua uelekeo wa wengine wote. Malolo pamoja na jitihada zake zote lakini hakuwaona kabisa wakina Martin. Saa zaidi ya sita alihangaika pale nje. Aliambulia patupu...Safari hii giza lilikuwa upande wa kina Martin. Namna jinsi ya walivyojificha ukichanganya na giza ilikuwa ngumu sana kuwaona. Malolo aliamua kurejea tena ndani ya viwanja vya Maisala. Alikuta bado maiti na wahanga wa ajari walikuwa wanaletwa katika viwanja vile. Pembeni ya maiti kulikuwa na mkusanyiko wa watu. Wakiwa wamezunguka kwa mtindo wa duara. Wakishangaa kitu...Malolo nae akavutika kwenda kushangaa pamoja nao. Lilikuwa duara kubwa kiasi, wake kwa waume wakiwa wamezunguka na kutengeneza duara hilo. Malolo hakuwa mrefu sana, Ilimpasa atumie nguvu kidogo hadi kufika sehemu ambayo ingemuwezesha kuona kilichokuwa kinaendelea katikati ya duara. Kabla hata hajaona alibahatika kusikia, alisikia neno moja likirudiwa mara kadhaa.



    "Mkanda wa siri, mkanda wa siri, mkanda wa siri........."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti toka kwa msichana aliyekuwa katikati ya duara.



    "Etiiii!" Ukelele wa fadhaa ulimtoka. Alifadhaika!



    Sasa alitumia nguvu zaidi ili kufika mbele, kuona ni kitu gani hiko. Alipekenyua watu kwa fadhaa. Na alifika. Alimuona msichana mmoja akigalagala chini huku akisema neno mkanda wa siri mara kwa mara! Msichana akiwa anavuja damu kichwani! Watu badala ya kumsaidia, walikuwa wanamshangaa. Iliwachukua kama dakika tatu wakina Martin nao waliwasili eneo lile. Martin alikuwa mrefu zaidi. Wala hakusumbuka kwenda mbele ya watu waliozunguka duara lile. Alimuona kwa macho na kumsikia kwa sauti, kwa wakati mmoja. Alimtambua...



    "Binunu!" Martin aliita kwa sauti kubwa yenye hamaniko ndani yake. Baadhi ya watu waliacha kumuangalia yule msichana akiyelia pale chini na kumuangalia kijana aliyeita kwa nguvu. Waliiona sura ya kijana yule ilivyotaharuki! Akiwa upande wa pili wa duara lile, Malkia nae aliushuhudia mstuko na taharuki aliyoipata yule kijana, miongoni mwa vijana akiowafatilia. Akajua lipo jambo la muhimu kwa yule dada akiyegaragara vumbini pale chini. Akawa makini zaidi. Kuufatilia mchezo. Malkia alistuka zaidi aliposikia neno toka kwa yule msichana.



    'Mkanda wa siri' Akaziamini hisia zake, akajua sasa kumekucha!



    Ghafla...Martin na Malolo walifika pamoja pale chini alipolala Binunu. Wote wakidai ndugu yao. Watu waliwashangaa! Wakatazamana usoni. Hasira, chuki na visasi viliwasilishwa kwa ustadi mkubwa katika nyuso zao, katika macho yao. Kila mmoja alitaka kufanya alichojisikia, lakini haikuwezekana, kulikuwa na watu wengi sana, Malkia alikuwa mtulivu zaidi. Hakutaka kuendeshwa na hisia kama Malolo. Siku zote yeye alikuwa anapiga hesabu kabla ya kuchukua maamuzi. Hesabu zake zilimwambia muda bado. Aliendelea kuusoma mchezo. Richard nae alikuwa mithili ya Malkia, hakuingia kichwakichwa katikati ya duara! Aliusoma mchezo kwanza. Aliona muhimu yeye kubaki, huku akimlinda Martin. Wakati Malkia alikuwa na kazi mbili, kumwangalia Martin pale katikati ya duara na kumwangalia Richard pale alipokuwa amesimama. Richard alikuwa na kazi moja tu....kumwangalia Malolo katikati ya duara.



    Pale katikati ya duara ilikuwa kasheshe, Binunu alikuwa anagombaniwa na watu wawili mithili ya mpira wa kona. Wakati Martin akisema ni dada yake. Malolo akisema ni mke wake. Watu walibaki wakiwashangaa. Kwa vipi mtu na shemeji yake wasifahamiane? Ghafla... Richard alidondoka pale alipokuwa amesimama.

    Kikazuka kizazaa kipya.

    Watu wakaanza kumzunguka na Richard. Sasa yakatengenezwa maduara mawili. Wale waliokuwa katika duara alilolala Richard walikuwa hawajui nini kimempata kijana yule. Bora wale waliokuwa katika duara alilolala Binunu, walikuwa wanaelewa kilichompata Binunu ila walikuwa hawajui maana ya maneno akiyoyatamka.

    'Mkanda wa siri'

    Martin nae aligeuka nyuma, alipigwa na butwaa kugundua kuwa mshirika wake Richard nae alikuwa ameanguka. Sasa akabaki njia panda. Abaki kwa Binunu ama aende kwa Richard. Baada ya kuwaza kwa sekunde zisizozidi kumi Martin alikuwa ameshaamua tayari. Alikwenda pale alipolala Richard, huku akimwacha Binunu katika mikono ya Malolo. Pale chini Richard alikuwa anagombania hewa. Akivuta pumzi kwa shida sana. Martin alienda kwa kasi na kupiga magoti pale alipokuwa kalala Richard. Aliweka sikio lake la kulia upande wa kushoto wa kifua cha Richard. Alikuwa anasikiliza mapigo yake ya moyo. Richard alikuwa anapumua, lakini kwa mbali sana. Alitumia sekunde thelathini tu kusikiliza mapigo ya moyo ya Richard. Ghafla likatokea tukio lililomshangaza kila mtu, Martin nae hakuinuka pale kifuani kwa Richard. Alimlalia Richard akiwa hajitambui, nae aliishiwa pumzi, nae alipoteza fahamu, nae alikuwa anagombea hewa! Unaweza ukadhani ni maigizo lakini amini ilitokea kweli katikati ya viwanja vya Maisala!





    Martin nae aligeuka nyuma, alipigwa na butwaa kugundua kuwa mshirika wake Richard nae alikuwa ameanguka. Sasa akabaki njia panda. Abaki kwa Binunu ama aende kwa Richard. Baada ya kuwaza kwa sekunde zisizozidi kumi Martin alikuwa ameshaamua tayari. Alikwenda pale alipolala Richard, huku akimwacha Binunu katika mikono ya Malolo. Pale chini Richard alikuwa anagombania hewa. Akivuta pumzi kwa shida sana. Martin alienda kwa kasi na kupiga magoti pale alipokuwa kalala Richard. Aliweka sikio lake la kulia upande wa kushoto wa kifua cha Richard. Alikuwa anasikiliza mapigo yake ya moyo. Richard alikuwa anapumua, lakini kwa mbali sana. Alitumia sekunde thelathini tu kusikiliza mapigo ya moyo ya Richard. Ghafla likatokea tukio lililomshangaza kila mtu, Martin nae hakuinuka pale kifuani kwa Richard. Alimlalia Richard akiwa hajitambui, nae aliishiwa pumzi, nae alipoteza fahamu, nae alikuwa anagombea hewa! Unaweza ukadhani ni maigizo lakini amini ilitokea kweli katikati ya viwanja vya Maisala!



    Saa 05:28 P.M

    Malolo na Malkia walikuwa katika kasri ya Chifu. Wakiwa na mateka wao, Binunu! Ni Malkia ndiye aliyewadondosha wale wanaume wawili kirahisi sana. Kama kina Martin walikuwa wanajiona wajuaji basi Malkia alikuwa mjuaji zaidi yao, Malkia alikuwa ni moto wa kuotea mbali. Ni dawa aina ya Rox ndio iliyowalaza kina Martin kijinga namna ile. Walilaliana na walikuwa na saa tatu mbele za kulala.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walipokuwa pale katika mzunguko wa kumzunguka Binunu, Malkia alifikiria cha kufanya, alimsogelea Richard kimyakimya na kwa usiri mkubwa alimnusisha sumu ya Rox kwa kutumia mtandio wake, alifanya kama amekosea na kumpitishia usoni ule mtandio. Richard alidumu akiwa amesimama wima kwa sekunde tano tu. Sumu ya Rox ilifanya kazi yake, sumu inayolaza haraka zaidi mara baada ya mtu kuinusa. Sekunde ya sita ilipotimu ndipo Richard aliishiwa nguvu na kuanguka chini kama mzoga. Martin nae alifanya kosa la kiufundi, kumkaribia namna ile Richard, eti kumwangalia kama Martin anapumua lilikuwa kosa, nae ilimpata harufu ya sumu ya Rox. Nae alilala chini na kwa mujibu wa sumu ile alikuwa na saa tatu mbele za kulala. Watu walichanganyikiwa katika uwanja wa Maisala. Hakuna aliyethubutu kuwasogelea wakina Martin. Sasa walimuacha Binunu na kuwashangaa wale wanaume waliolaliana kwa mbali. Hapo ndipo Malkia na Malolo walipopata nafasi ya kuondoka na Binunu. Aliyekuwa anaimba tu njia mzima ' mkanda wa siri.....mkanda wa siri!



    Saa 9:04 P.M

    Ndani ya kasri ilikuwa mauzi, au tunaweza ita ni vichekesho. Saa nne sasa zilikuwa zimepita hakuna lolote la maana. Kila wanachomuuliza Binunu jibu lake lilikuwa moja tu....... 'mkanda wa siri'

    Kule ndani, chumbani kwa Chifu nako kulikuwa tafrani. Chifu alikuwa anazunguka chumba chake huku akiongea mwenyewe ....akivyoongea havieleweki!



    Muda huohuo...katika hospitali ya Mnazimmoja, hali ilikuwa tete. Saa moja ilikuwa imepita tangu Martin na Richard waamke. Walipishana dakika tano tu kuamka. Alianza kuamka Richard, na Martin akafata. Aliyeanza kulala, alianza kuamka...nao waliamka na neno moja tu.. 'Binunu'.

    Saa zima walilitaja jina la Binunu tu bila kukoma. Na hospitali nako hali ilikuwa tete!



    Muda huohuo katika stendi ya magari ya kwenda mikoani ya Ubungo, kulikuwa na kasheshe. Peter Mwendawazimu alikuwa katika windo, alikuwa anamfatilia kijana mmoja wa kizungu. Kijana huyo alikuwa ameshuka punde tu katika basi ya kisasa ya Sumry akitokea Morogoro. Alivyofika Ubungo yule Mzungu alishangaashangaa kwa muda na kukodi teksi. Mwendawazimu nae alikuwa juu ya pikipiki akila sahani moja na mzungu yule. Alichokuwa anakifuata. Alikuwa anakijua yeye mwenyewe! Lakini alichokiacha Ubungo ni mishangao na maswali. Mwendawazimu juu ya pikipiki? Kalitoa wapi? Anaenda wapi? Hivi kweli ni Mwendawazimu yule? Au kapona? Yalikuwa maswali lakini hakukuwa na wa kuyajibu.



    Ndani ya teksi kulikuwa na watu wawili tu. Kijana mmoja mrefu aliyevaa suruali nyeusi na shati jeupe, chini akiwa amevaa viatu vyeusi aina ya moka. Nywele zake alizikata ndogondogo, vijana wamjini huita ungaunga, huyo ndiye alikaa upande wenye sukani wa gari ile, alikuwa Dereva teksi. Pembeni yake alikaa kijana wa kizungu aliyevaa suruali aina ya timberland na T-shirt nyeusi, huku akiwa amevaa raba kali nyeupe zenye nembo ya Nike... kichwani nywele zake ndefu alikuwa amezikusanya pamoja na kuzifunga kwa nyuma kama fungu la mchicha... kijana alikuwa amekaa siti ya mbele, upande wa kushoto wa dereva. Kijana wa kizungu alikuwa katika sura iliyosawajika haswa. Yenye kujaa mawazo na fikra tele. Ilikuwa ukimwangalia sura tu ilikuwa inawakilisha matatizo kadhaa aliyokuwa nayo. Dereva teksi alikuwa kimya, makini na usukani huku akimwangalia abiria wake mara chachechache kwa kutumia kioo cha kati. Dereva aliiona sura ya Mzungu yule ilivyo katika tafakuri nzito, hakumsemesha. Alikuwa anatekeleza kazi yake ya kumpeleka mteja wake katika hoteli ya Grand Villa, Kijitonyama, hoteli aliyoombwa kupelekwa na abiria wake wa kizungu mara tu alipoingia mle ndani ya gari.



    Zanzibar; saa 10:00 A.M

    Hali katika kasri ilikuwa kama ilivyokuwa awali. Ingawa sasa maamuzi yalikuwa yameshapita. Waliamua kumpigia Dokta wa familia ili aje kuingalia hali ya mgonjwa wao. Nusu saa baadae Dokta wa familia ya Chifu aliwasili. Na moja kwa moja alikutanishwa na mgonjwa. Dokta alimuuliza maswali kadhaa ili kuitambua hali ya mgonjwa wake. Lakini jibu toka kwa kila swali lilikuwa ni moja tu.....Mkanda wa siri. Dokta Dickson aliomba kuondoka na yule mgonjwa. Kwenda nae katika hospitali yake. Kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Ombi lake lilipitishwa na wote. Binunu alipakizwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser. Mali ya Dokta Dickson, huku pembeni akiambatana na Malolo kwa ajili ya kwenda kumfanyia uchunguzi mgonjwa yule wa kike. Njia nzima yalikuwa makelele tu toka kwa Binunu...mkanda wa siri, mkanda wa siri, mkanda wa siri.......



    Dar esSalaam Saa 1:54 P.M

    Range Rover Vogue ya Martin bado ilikuwa bandarini. Hakuna mtu yeyote aliyedadisi uwepo wa gari ile pale. Hata kugundua kama gari ile haikuwa na kioo kimoja hawakujua. Vijana wa bandarini halikuwastaajabisha Range Rover kuwepo pale saa kadhaa ila kuliwastaajabisha kutoonekana kwa Mansour pale Bandarini kwa saa kadhaa. Haikuwahi kutokea Mansour kupotea bandarini saa nyingi namna ile. Walijaribu kumpigia simu, simu yake haikuwa inapatikana. Kitu ambacho walikuwa hawakifahamu, simu ya Mansour alikuwa nayo Mwendawazimu. Mwendawazimu aliua mtu ndani ya Range Rover Vogue na kuondoka na kitu. Simu ya Mansour ndio iliyomjulisha Mwendawazimu ujio wa mzungu yule aliyekuwa anamfatilia. Martin alimtumia Mansour meseji kuwa akamsaidie kumpokea mgeni wake Ubungo na kumpeleka hotelini. Gari amuachie mtu yeyote ailinde kwa muda. Na hiyo ndio sababu ya Mwendawazimu kurudi tena Ubungo kumfata mzungu yule kisha nd'o aende Zanzibar....Hakuwa na haraka ya kwenda Zanzibar kwenye ‘OMS’ wakati Dar es salaam kulikuwa na muendelezo wa ‘OMS;

    ‘ pia.



    Yule mzungu alifika hadi hoteli ya kisasa ya Grand villa. Mapokezi alikutana na wahudumu wawili wa hoteli wakiwa wamevaa sare. Wote wakiwa wamevaa mashati meupe pamoja na tai nyeusi na kwa chini walikuwa wamevaa sketi fupi za bluu.



    "Habari zenu kina na na na dada" Yule mzungu alisalimia kwa kiswahili fasaha.



    "Nzuri karibu sana Grand villa hoteli, naitwa Irene Paul na huyu mwenzangu anaitwa Paulina Kennedy" Dada mmoja kati ya wale wawili aliitikia kwa bashasha tele, na kujitambulisha huku yule mwengine aliyetambulishwa kwa jina la Paulina akitoa tabasamu mwanana lililoruhusu mwanya wake kuonekana.



    "Na na na naataka chumba...lakini kabla ya yote nihakikishieni hali ya usalama katika hoteli yenu" yule mzungu aliongea baada ya kuwaangalia kwa muda kama wa sekunde hamsini wale wahudumu.



    "Chumba umepata kaka hata ukitaka vyumba vipo..., kuhusu hali ya usalama..... hoteli yetu ina usalama mzuri zaidi ya hoteli yoyote hapa jijini. Tuna walinzi wanne wenye silaha kama ulivyowaona pale getini. Kuna walinzi wengine kadhaa ndani ya hoteli wanaozunguka kila mahala. Ninaposema walinzi namaanisha walinzi kweli, waliofunzwa kwa kazi ya ulinzi, ushawahi kusikia chochote kuhusu Ultimate security? pia tuna camera za ulinzi zinazoonesha kila mahala ndani ya hoteli. Aina za ulinzi wetu mwengine ni siri, ila amini Grand villa ni sehemu salama, halijawahi kutokea tukio lolote la kihalifu hapa na hatutegemei.....never ever!"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nimeridhika na na na maneno yako...nataka room na na mna restaurant hapa?"



    "Ndio, ni ule upande uliosikia sauti ya muziki wakati unaingia, wateja wetu wanakula na kunywa huku wakiburudika na live band"



    "Ok, nice ..."



    "Unaitwa nani mteja wetu"



    "Na na na naitwa Michael, Michael Zulender" Mzungu alisema bila wasiwasi.



    Na baada ya kukamilisha utaratibu wote alipatiwa chumba. Paulina ndio alikuwa na jukumu la kumpeleka. Alimsaidia kubeba begi la mzungu na kuelekea chumba namba 208. Na sasa Michael alikuwa ndani ya chumba namba 208 katika ghorofa ya tatu katika hoteli hiyo.

    Paulina alirejea.

    Walipoonana tu na Irene wote walicheka, na Paulina akasema na na na na....na Irene nae akadakia na na na...walikuwa wanamuiga yule mzungu. Na tangu siku hiyo wakampachika yule mzungu jina la Mr Na na na.



    Kwa upande wa Mwendawazimu, yeye alikuwa nje ya hoteli ya hoteli ya Grand villa. Akiliwinda windo lake.



    Zanzibar moto, Dar es salaam moto...





    Huko Zanzibar katika hospitali binafsi ya Dokta Dickson iitwayo Samaritan Private Hospital ndani ya chumba cha daktari Dickson kulikuwa na watu wawili tu. Yeye na Binunu. Malolo alibaki nje akilinda usalama wa kina Binunu. Kabla hajampima kitu chochote Daktari alianza na kichwa cha Binunu, ambacho sasa kilikuwa kimeganda damu kavu upande wa kisogoni. Kwa kumkagua tu aligundua mbonyeo pamoja na jeraha kubwa nyuma ya kichwa cha Binunu. Tayari Dokta Dickson alishaligundua tatizo la Binunu litakuwa limeanzia hapo. Alimfanyia uchunguzi kuthibitisha tu. Na kweli jibu lilikuwa lilelile. Ubongo wa nyuma wa Binunu ulikuwa umechanganyika na damu!

    Saa mbili baadae Dokta Dickson akiwa amesafisha kidonda cha Binunu na kumfunga bandeji iliyoenea kichwa chote, Binunu na Malolo walirejea tena katika kasri ya Chifu. Walikutana na Malkia sebuleni akiwa kashika tama.



    "Eeeh nipe ripoti ya uchunguzi wako Dokta......" Malkia aliuliza pindi tu walipoingia kabla hata kina Dokta Dickson hawajakaa.



    "Malkia.....huyu dada ana tatizo. Tena tatizo kubwa sana. Ubongo wake wa nyuma umechanganyika na damu!"



    "Haaaa" Malkia alimaka.



    "Nashangaa kwanini huyu dada yuko hai hadi sasahivi, unamkumbuka yule msanii mkubwa wa filamu Tanzania...."



    "Steven Marashi' Malolo alidakia.



    "Naam Malolo ....alikuwa anaitwa Steven Marashi, alipatwa na tatizo namna hii baada ya kusukumwa na mpenzi wake chumbani, hakuomba hata maji aiseee Steven alifariki palepale!..Kwa upande wa huyu dada inaonesha amegongwa na kitu kizito kwa nyuma, wengi hufa hapohapo wapatapo tatizo kama hili kama ilivyokuwa kwa Steven Marashi! Hapo ndipo naposhangazwa huyu dada kuendelea kupumua mpaka dakika hii" Dokta Dickson alieleza kwa kirefu.



    "Blood swine we dokta inamaana ukitaka huyu dada afe!" Malkia aliwaka kwa jazba.



    "Hapana Malkia..sijamaanisha hivyo..." Dokta Dickson alinywea.



    " Ninachotaka kujua toka kwako Dokta ni kimoja tu, huyu dada atapona...haponi? Sitaki siasa.." Malkia aliuliza kwa sauti kubwa.



    "Mh mh mh aah aah tuseme ni Fifty fifty aisee" Dokta Dickson alijibu akiwa amekata tamaa.



    "Fifty fifty ndio nini wewe Daktari? Nd'o umefunzwa kutibu wagonjwa kwa mtindo wa fifty fifty...nakuamini sana Dokta Dickson hujawahi kuniangusha kila nilipokutumia, sasa fanya juu chini apone huyu mgonjwa. Ana jambo la muhimu sana huyu" Malkia alieleza kwa sauti yake ya ukali.



    "Nimefanya kazi nyingi sana na wewe, sijawahi kukuangusha hata siku moja pia sijawahi kukudanganya, sio siwezi kukudanganya wewe tu, siwezi kumdanganya mteja wangu yeyote yule, mimi kwangu nyeupe ni nyeupe, nyeusi ni nyeusi, siwezi kusema nyeupe wakati ni nyeusi au kusema nyeusi wakati ni nyeupe. Ukweli ni kwamba huyu dada kaumia sana tena kaumia sehemu mbaya sana, ingawa nakuahidi nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida, ila siyo rahisi as u think Malkia, anaweza akapona ila akapoteza kumbukumbu zake zote, kurejewa na kumbukumbu zake inategemea na kudra tu za Mwenyezi Mungu..."



    "Doktaaaaa....kazi ya daktari kutibu pekee sio kutabiri. Familia imeajiri daktari sio Mtabiri...muhimu huyu dada asiye na jina ni kupona, kupona ina maana pamoja na kurejewa na kumbukumbu zake, mimi nina shida na hizo kumbukumbu sio huu mwili! Eti kudra za Mwenyezi Mungu, naona umekuwa shekhe sasa badala ya taaluma yako ya udaktari..."



    "Malkia hivi uliisikia ile ishu ya Steven Marashi...si nilikwambia yaliyomkuta Marashi, sasa huyu binti kapatwa na madhila tena makubwa zaidi ya yaliyompata Steven Marashi, mimi nakwambia bila uwepo wa Mungu tungekuwa tunaongea story nyingine kabisa"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sijawahi kumuona Dokta mpumbavu kama wewe...usifananishe hii ishu na ya Steven Marashi, Mwigizaji aliyekufa kizembe kwa sababu za kizembe, tena kauawa na mwanamke mzembe! hivi kwa akili yako...mwanaume wa shoka kama Malolo anaanzaje kusukumwa na yule binti sijui anaitwaaaa nani...Ruby sijui kale kabinti kaigizaji nacho, eti kamsukume jibaba kama Steven Marashi kisha afe! Kwa ule mwili wa Steven Marashi kweli?..."



    "Usiseme hivyo Malkia, amini kuna mstari mwembamba sana kati ya uhai na kifo! Na hakuna kifo cha kizembe.....Lakini tuache sababu zilizofanya Steven Marashi afe..labda ilikuwa ni njia ya kulianika lile penzi la siri lijulikane hadharani, hebu tuongelee namna Steven Marashi alivyopata ile athari kichwani..sehemu ya nyuma ya kichwa ni sehemu laini na hatari sana..."



    "Toka nje Dokta!" Malkia alimkatisha Dokta Dickson.



    "Malkia, kumbuka tumefanya mangapi pamoja mpaka leo hii unafikia hatua ya kunifukuza kama mbwa? Kumbuka nimewasaidia mambo mangapi mazito na ya siri wewe na Chifu. Leo hii kusema ukweli ndo unifu...."



    "Umeshindwa kazi Dokta! nitatafuta namna ya huyu dada asiye na jina kupona, naamini anaweza kupona bila uwepo wa mtu anayejiita Dokta Dickson!"



    Dokta Dickson hakutia neno tena, alitoka nje akiwa amefura kwa hasira. Huku nyuma Malkia alitukana tusi zito la nguoni. Huku akirusha mkono wake uliokunjwa ngumi hewani. Hakika ngoma ilikuwa nzito!

    Wakati majadiliano yale yaliyoishia kwenye ugomvi mkubwa yakiendelea....Binunu alikuwa amekaa chini katika zulia pale sebuleni. Akiwa ametulia huku akichorachora kwa kidole chake cha mwisho cha mkono wake wa kushoto ukutani. Akiwa hana habari kabisa juu ya kilichokuwa kinaongelewa pale sebuleni. Yeye alikuwa makini na mchoro wake. Malolo yeye alikuwa amesimama, mwanzoni alikuwa anawasikiliza kina Malkia, lakini sasa alikuwa makini akiungalia ule mchoro ukiochorwa na Binunu pale ukutani, hakuwa anasikia kabisa kilichokuwa kinajadiliwa pale ukumbini. Hakusikia chochote wakati taaluma na hasira zilipokuwa zinabishana pale ukumbini.



    Upande wa hali za kina Martin sasa zilikuwa nzuri. Walikuwa wamerejea katika hali zao za kawaida. Wakivuta hewa kama kawaida. Hakuna aliyeelewa nini kilichowatokea. Walienda katika viwanja vya Maisala wenyewe kwa hiari yao lakini walipelekwa hospitali na wasamaria wema bila hiari yao, wakiwa hawajitambui. Na sasa waliruhusiwa kutoka hospitali. Njiani walijadiliana kwa kina juu ya chanzo cha hali ile iliyowatokea.



    "Hivi ni kitu gani kilitokea pale Maisala?" Richard alikuwa anamuuliza Martin kwa sauti yenye uchovu kana kwamba Martin alikuwa ameshuhudia kila kitu.



    "Yaani hata mimi sielewi Rich....ila nahisi itakuwa tulivutishwa sumu iliyotufanya tupoteze fahamu" Martin alijibu huku akiweka wazi dukuduku lake.



    "Inavyoonesha yule jamaa tuliyekuwa tunamfatilia hakuwa peke yake, alikuwa na mwenzake ama wenzake, bila shaka wakati sisi tunamfatilia nasi pia tulikuwa tunafatiliwa bila kujua..na huyo mwenzake au wenzake ndipo walipofanikiwa kutupaka au kutunusisha sumu kwa siri...na ndipo tukapoteza fahamu!"



    "Nami naamini hivyo lakini kwa namna gani sasa inawezekana hiyo Rich, kwanini tulale wawili tu uwanja mzima tena kukiwa na umati wa watu..je wale wengine hiyo sumu ilikuwa haiwadhuru ama?"



    "Hapo hata mimi napatwa na mashaka makubwa sana.."



    "Unajua tumefanya makosa makubwa sana yaani..Tumempoteza Binunu, tumempoteza yule jamaa..na kosa kubwa zaidi ya yote tumepoteza mkanda, yaani mkanda hauko mikononi mwetu!" Richard aliongea kwa kulalama.



    "Ila tusijilaumu sana, twende Maisala, sehemu tulikopoteza fahamu zetu ndipo sehemu tunapoweza pata sababu ya kupoteza fahamu zetu.."



    "Daah sawa twe'nzetu"



    Wakiwa njiani Richard alianzisha mjadala mpya.



    "Hivi vipi Brown amewasili Bongo kutokea Moro?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nilimpa kazi ya kwenda kumpokea yule mshkaji wetu wa bandarini, yule Mansour, lakini sijawasiliana nae bado"



    "Nice kaka, usimpigie kwanza, ngoja tulimalize hili kwanza...maana Brown akisikia mkanda umepotea........"



    "Patachimbika haki ya Mungu!"



    Walipofika katika viwanja vya Maisala walikuta bado kuna umati mkubwa sana wa watu. Kina Martin safari hii walikuwa makini kupita kawaida, lakini pamoja na umakini wao na kujitahidi kutafuta sana lakini hawakufanikiwa kumuona Binunu wala yule jamaa. Walijaribu kuulizia kwa watu pale uwanjani, hawakupata lolote la maana, kila mtu alijibu sijui...sijui...sijui. Walichanganyikiwa walikuwa wamewapoteza watu wale muhimu sana...watu ambao wangeweza kuwa ni jibu juu ya mahali ulipo mkanda wa siri. Walitoka nje ya viwanja vya Maisala. Nje waliiona gari yao iliyokuwepo mahali palepale walipoiacha kabla ya kupotelewa na fahamu zao. Bila kusemashana maneno yoyote wala kudadisi waliingia ndani ya gari. Wakakaa. Richard alikuwa amekaa katika kiti cha dereva, na Martin alikaa katika kiti cha upande wa kulia, kiti cha abiria. Dakika zipatazo tatu walikuwa macho....na kuongea.



    "Unakumbuka katika ‘OPS’ kule Arusha siku ile tuli--vyo--ingia ka-mbi--ni kwa wa-le jam....." Martin hakumalizia kusema alichotaka kusema. Mdomo wake ulikuwa mzito ghafla! Hali ilibadirika mle ndani ya gari, sasa majamaa walikuwa wanashindana na macho yao, macho yanataka kufumba kilazima, wao wanataka kufumbua kilazima. Ilikuwa tafrani!



    'Ni nini hii Martin lakini....' Richard alijiona anasema kwa nguvu, lakini sauti haikufika hata katika sikio lake mwenyewe. Aliishia kutoa madenda tu, sauti ile ilisikiwa na ubongo wake tu. Kujua kama alikuwa anataka kuongea labda ni yale madenda yaliodondokea katika kava ya sukani ya gari, mdomo nao ulikuwa mzito! Haukuthubutu kutoa hata neno moja nje. Mashindano kati ya ubongo wao uliokuwa hautaki kuruhusu macho kufumba na macho yakiyotaka kujifumba uliendelea. Siku zote ubongo ndio huamrisha macho kufumba au kufumbua. Lakini leo macho hayakufata amri ya ile ya ubongo. Wakati ubongo ukitaka macho yasijifumbe, macho yalikuwa yanalazimisha kujifumba.



    Balaa!



    Upande wa hali za kina Martin sasa zilikuwa nzuri. Walikuwa wamerejea katika hali zao za kawaida. Wakivuta hewa kama kawaida. Hakuna aliyeelewa nini kilichowatokea. Walienda katika viwanja vya Maisala wenyewe kwa hiari yao lakini walipelekwa hospitali na wasamaria wema bila hiari yao, wakiwa hawajitambui. Na sasa waliruhusiwa kutoka hospitali. Njiani walijadiliana kwa kina juu ya chanzo cha hali ile iliyowatokea.



    "Hivi ni kitu gani kilitokea pale Maisala?" Richard alikuwa anamuuliza Martin kwa sauti yenye uchovu kana kwamba Martin alikuwa ameshuhudia kila kitu.



    "Yaani hata mimi sielewi Rich....ila nahisi itakuwa tulivutishwa sumu iliyotufanya tupoteze fahamu" Martin alijibu huku akiweka wazi dukuduku lake.



    "Inavyoonesha yule jamaa tuliyekuwa tunamfatilia hakuwa peke yake, alikuwa na mwenzake ama wenzake, bila shaka wakati sisi tunamfatilia nasi pia tulikuwa tunafatiliwa bila kujua..na huyo mwenzake au wenzake ndipo walipofanikiwa kutupaka au kutunusisha sumu kwa siri...na ndipo tukapoteza fahamu!"



    "Nami naamini hivyo lakini kwa namna gani sasa inawezekana hiyo Rich, kwanini tulale wawili tu uwanja mzima tena kukiwa na umati wa watu..je wale wengine hiyo sumu ilikuwa haiwadhuru ama?"



    "Hapo hata mimi napatwa na mashaka makubwa sana.."



    "Unajua tumefanya makosa makubwa sana yaani..Tumempoteza Binunu, tumempoteza yule jamaa..na kosa kubwa zaidi ya yote tumepoteza mkanda, yaani mkanda hauko mikononi mwetu!" Richard aliongea kwa kulalama.



    "Ila tusijilaumu sana, twende Maisala, sehemu tulikopoteza fahamu zetu ndipo sehemu tunapoweza pata sababu ya kupoteza fahamu zetu.."



    "Daah sawa twe'nzetu"



    Wakiwa njiani Richard alianzisha mjadala mpya.



    "Hivi vipi Brown amewasili Bongo kutokea Moro?"



    "Nilimpa kazi ya kwenda kumpokea yule mshkaji wetu wa bandarini, yule Mansour, lakini sijawasiliana nae bado"



    "Nice kaka, usimpigie kwanza, ngoja tulimalize hili kwanza...maana Brown akisikia mkanda umepotea........"



    "Patachimbika haki ya Mungu!"



    Walipofika katika viwanja vya Maisala walikuta bado kuna umati mkubwa sana wa watu. Kina Martin safari hii walikuwa makini kupita kawaida, lakini pamoja na umakini wao na kujitahidi kutafuta sana lakini hawakufanikiwa kumuona Binunu wala yule jamaa. Walijaribu kuulizia kwa watu pale uwanjani, hawakupata lolote la maana, kila mtu alijibu sijui...sijui...sijui. Walichanganyikiwa walikuwa wamewapoteza watu wale muhimu sana...watu ambao wangeweza kuwa ni jibu juu ya mahali ulipo mkanda wa siri. Walitoka nje ya viwanja vya Maisala. Nje waliiona gari yao iliyokuwepo mahali palepale walipoiacha kabla ya kupotelewa na fahamu zao. Bila kusemashana maneno yoyote wala kudadisi waliingia ndani ya gari. Wakakaa. Richard alikuwa amekaa katika kiti cha dereva, na Martin alikaa katika kiti cha upande wa kulia, kiti cha abiria. Dakika zipatazo tatu walikuwa macho....na kuongea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unakumbuka katika ‘OPS’ kule Arusha siku ile tuli--vyo--ingia ka-mbi--ni kwa wa-le jam....." Martin hakumalizia kusema alichotaka kusema. Mdomo wake ulikuwa mzito ghafla! Hali ilibadirika mle ndani ya gari, sasa majamaa walikuwa wanashindana na macho yao, macho yanataka kufumba kilazima, wao wanataka kufumbua kilazima. Ilikuwa tafrani!



    'Ni nini hii Martin lakini....' Richard alijiona anasema kwa nguvu, lakini sauti haikufika hata katika sikio lake mwenyewe. Aliishia kutoa madenda tu, sauti ile ilisikiwa na ubongo wake tu. Kujua kama alikuwa anataka kuongea labda ni yale madenda yaliodondokea katika kava ya sukani ya gari, mdomo nao ulikuwa mzito! Haukuthubutu kutoa hata neno moja nje. Mashindano kati ya ubongo wao uliokuwa hautaki kuruhusu macho kufumba na macho yakiyotaka kujifumba uliendelea. Siku zote ubongo ndio huamrisha macho kufumba au kufumbua. Lakini leo macho hayakufata amri ya ile ya ubongo. Wakati ubongo ukitaka macho yasijifumbe, macho yalikuwa yanalazimisha kujifumba. Balaa!

    Mpambano ule ulidumu kwa muda takribani wa dakika moja tu, na macho yakaibuka mshindi kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Majamaa walilala usingizi mzito sana. Richard alikuwa kalalia sukani. Martin alikuwa kalalia kiti cha abiria. Kilichowalaza..... kwa maana ya chanzo cha mpambano ule, hakikujulikana!



    Saa 6:09 P.M

    Bandarini, Dar es salaam hali ilikuwa ya wasiwasi sana. Watu wengi walikuwa wameizunguka Range Rover Vogue moja ambayo ilianza kutoa harufu kali. Walivyoichunguza vizuri Range Rover ile waligundua kuwa kioo cha nyuma kilikuwa kimevunjika ama kimevunjwa. Hofu ya kuwa kuna kitu kibaya ndani ya ile gari ikawavaa. Haraka haraka Polisi wakapigiwa simu. Na nusu saa baadae Polisi walifika mahali pale kwa Land Rover yao nyeupe. Askari watano na bunduki zao aina ya SMG mkononi walishuka kabla hata ile Land Rover haijasimama vizuri. Polisi watatu walikuwa wanalizunguka lile gari. Huku bunduki zao zikiwa zimetangulizwa mbele, askari wawili ndio walikuwa wanaisogelea ile Range Rover kwa tahadhari kubwa. Polisi mmoja akiwa kavaa sare safi za jeshi la Polisi na kifimbo cheusi mkononi, na bunduki yake ikiwa inaning'inia begani huku yule mwengine akiwa nae amevaa sare za jeshi la Polisi lakini hakuwa na kifimbo kama yule mwenzake huku bunduki yake ilikuwa imara mkononi akiielekeza katika ile gari, waliisogelea kwa tahadhari kubwa sana. Njiani walikutana na upinzani wa harufu mbaya sana toka ndani ya Range Rover kila walivyokuwa wanaikaribia. Wakasimama kwa pamoja, wakavaa viziba pua vyeupe vilivyokuwa vinaning'inia shingoni mwao. Wakaendelea kupiga hatua kuelekea kwenye harufu kali baada ya kuridhika kuwa waliziziba vizuri pua zao. Askari yule asiye na kifimbo cheusi alifika pale dirishani. Akajipekua mfukoni na kutoa 'gloves' mbili, akazivaa katika mikono yake. Yule askari mwenye kifimbo cheusi akaitoa bunduki yake begani, akaishika imara mkononi. Akiielekeza mdomo wa bunduki garini. Alikuwa tayari kwa lolote! Askari asiyekuwa na kifimbo cheusi aliining'iniza bunduki yake begani. Sasa mikono yake yote ilikuwa huru. Akapeleka mkono wake wa kulia mlangoni, akijaribu kuuvuta mlango wa mbele wa dereva. Haukufunguka. Akapata wazo la kuchungulia ndani ya gari kupitia dirishani. Wazo ambalo alilipitisha katika halmashauri ya kichwa chake. Akitaka kufanya uamuzi sawa na alioufanya kijana Mansour na kupelekea kifo chake! Alivyotaka kuingiza tu, mwenzie akampa onyo.



    "Hatari hiyo Afande hujui ndani kuna nini!" Yule askari asiye na fimbo nyeusi akarudisha kichwa chake kwa haraka! Askari wakarudi nyuma kidogo, ili kupata nafasi ya kufikiria namna mzuri ya kuufungua ule mlango wa gari.



    "Funguo Malaya" Askari aliyeshika kifumbo cheusi alisema kwa kunong'ona, na sauti ile ilisikiwa vizuri na yule askari mwengine. Na alitekeleza.

    Askari asiye na kifimbo cheusi akaenda haraka haraka kwenye gari yao iliyopaki kama meta thelathini kutokea pale kwenye Range Rover, huku yule askari mwenye kifimbo cheusi akibaki pale karibu na gari, yu imara na bunduki yake mkononi, masikio na macho yake yakiwa makini kuliko kawaida, yakisubiri mtikisiko wowote ule toka ndani ya ile gari autungue. Dakika moja baadae, askari asiye na kifimbo alirudi tena kwa mwendo wake uleule wa haraka, akiwa na funguo ndogo mkononi. Alienda moja kwa moja hadi katika mlango wa mbele wa Range Rover. Akiwa makini pasi na kawaida, huku yule askari mwenzie akimlinda kwa kutumia ile bunduki yake. Na midomo mengine ya bunduki tatu, za wale askari wengine zikiwa zimeelekezwa katika ile gari. Wananchi wakiwa umbali wa kama mita mia moja wakiwa makini, wanataka kuwa mashuhuda wa tukio lile. Askari asiye na kifimbo akapenyeza ile funguo malaya katika lile tundu la kupitisha funguo. Aliutekenya kidogo tu, mlango wa Range Rover Vogue ulifunguka! Pamoja na kile kiziba pua lakini ilipenya, alikaribishwa na harufu kali sana, askari asiye na kifimbo cheusi ambaye ndiye aliufungua mlango wa ile Range Rover alitanguliza mdomo wa SMG mbele huku mwili wake ukiwa nyuma. Tayari kuishambulia hatari yoyote atakayokutana nayo ndani ya Range Rover. Haikuwa kama walivyofikiria, hakukutana na hatari yoyote ya kuwashambulia, alikutana na hatari isiyoshambulia, maiti ya binadamu ikiwa imevimba vibaya sana, huku ikiwa imezungukwa na inzi wa kutosha! Kizungumkuti!



    "Kuna maiti tu humu afande!" Askari asiye na kifimbo alimtaarifu mwenzio kwa sauti iliyotokea puani (nasal sound), hii ni kutokana na kile kiziba pua alichokitumia kuzibia pua yake.



    "Hakuna kitu kingine chochote cha hatari?" Askari mwenye kifimbo cheusi nae aliuliza.



    "Hapana afande, ni maiti tu"



    Taratibu za kiusalama zikafuatwa. Na mwili wa wa ile maiti iliyokuwa imeanza kuharibika ukatolewa ndani ya gari. Vijana wa Bandarini walikuwa umbali wa mita mia moja tokea pale Range Rover Vogue ilipo, lakini waliona. Wengi wa vijana wale waliropokwa kwa sauti kali wakati mwili wa jamaa ukitolewa ndani ya gari.



    "Mansoouuur!"



    Maiti ya Mansour ikabebwa msobemsobe na kupelekwa hospitali. Na mara moja upelelezi wa sababu ya mauaji ya Mansour ulianza. Askari waliokabidhiwa upelelezi wa kifo kile cha kutatanisha ni walewale, askari mwenye kifimbo cheusi na mwenzie, askari asiye na kifimbo cheusi. Hatua ya kwanza walioichukua ni kuitafuta kadi ya gari. Lengo ni kumpata mmiliki wa gari ile. Walishaelezwa na vijana wa bandarini kwamba Mansour hakuwa na gari, kwa maana hiyo aliuwawa na kutelekezwa ndani ya gari. Kwanini auwawe? Ile gari ni ya nani? Je kuna uhusiano kati ya mwenye gari na ile maiti? Ili kuyajibu maswali hayo na mengine kadhaa yaliyowazunguka kichwani mwa askari wale. Askari wakaamini ili wajue chanzo cha mauaji au mtu anayejua lolote kuhusu mauaji ya mtu yule ni kumtafuta mmiliki wa ile gari. Lazima atawapa mwanga wa kitu gani kilichotokea. Hawakupata shida. Nakala ya kadi ya gari waliikuta mlemle ndani ya gari!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmiliki wa ile gari tulioikuta maiti anaitwa Martin Nguzu" Askari asiye na kifimbo alisema wakiwa ofisini. Huku mkononi akiwa ameshikilia nakala ya kadi ya gari.



    "Martin Nguzu! Sio jina geni katika masikio yangu...nimelisikia wapi hiviiii?" Askari mwenye kifimbo aliuliza huku akikuna kichwa kujaribu kuvuta kumbukumbu.



    "Mimi sijawahi kulisikia hili jina kwa kweli" askari asiye na kifimbo cheusi alisema.



    "Hebu tuangalie katika database yetu ya wahalifu, kama tutalikuta hilo jina...ila jina lake si geni kabisa katika masikio yangu....Martin Nguzu..."



    "Sawa Afande. Ngoja tuwasiliane na Mtunza kumbukumbu za Wahalifu tuone kama ataliona hilo jina?



    " Nusu saa baadae majibu toka kwa Mtunza kumbukumbu za Wahalifu yalikuwa mezani kwao. Hakukuwa na mtu mwenye jina hilo katika orodha ndefu ya wahalifu waliokamatwa na walio katika orodha ya kutafutwa katika jeshi la Polisi nchini Tanzania.



    "Itabidi twende TRA kupata maelezo zaidi ya mtu huyu...kwa kuwa hii gari imesajiliwa haitotupa shida sana" Askari mwenye kifimbo alitoa wazo.



    "Sawa Afande, hakika kule tutapata mambo mengi muhimu kuhusu huyu mtu aitwaye Martin Nguzu"



    Nje ya viwanja vya Maisala.....Zanzibar Martin na Richard walikuwa wamelala fofofo ndani ya gari. Hawakuwa wanajitambua kabisa, hawakujua jinsi hatari ikivyojitengeneza huko Dar es salaam kwa kasi kubwa sana ili isafiri na kwenda kumvaa Martin Zanzibar. Sumu aina ya Rox iliyokuwemo ndani ya gari lao iliwalaza kwa mara ya pili. Kumbe kabla Malkia hajaingia katika viwanja vya Maisala alianza kupulizia Rox ndani ya gari ile, kisha ndipo alienda ndani ya viwanja vya Maisala. Alifanya hivyo makusudi. Endapo angewakosa kuwapulizia ile sumu kule ndani ya uwanja, basi waje kukutana nayo ndani ya gari yao. Na Malkia alifanikiwa kwa asilimia mia...Rox iliwapata ndani, Rox imewapata nje...walikuwa na saa tatu zingine za kulala, huku kina Malkia wakiendelea na harakati za kutafuta hatma ya mkanda wa siri. Hivi vilikuwa vita vya akili, vilivyokuwa vinahitaji watu wenye akili kuvicheza, na Malkia alikuwa mwanamke wa kipemba aliyejaaliwa akili hizo, akili za VITA. Na ndomana Chifu mwenye akili aliamua kumuoa Malkia mwenye akili, kwakuwa Chifu siku zote alikuwa mtu wa vita na alikuwa anajua ya kwamba vita vyahitaji akili sana!



    Sasa kwanini asimuoe mtu mwenye akili?



    ***



    Askari mwenye kifimbo cheusi na askari asiye na kifimbo cheusi waliwasili katika makao makuu ya ofisi za TRA. Baada ya kufuata taratibu zote za kiofisi maaskari walipewa anuani ya mmiliki wa ile Range Rover Vogue, Martin Hisia, pamoja na namba yake ya simu. Askari walitoka nje na kuingia ndani ya gari yao, wakiwa na matumaini tele ya kufumbua utata wa kifo kile cha kitata. Askari mwenye kifimbo cheusi ndiye aliyechukua jukumu la kuipiga ile namba ya Martin.



    Simu ya Martin iliita, ikakata, akaipiga tena, ikaitaa weee mpaka ikakata, akapiga tena matokeo yakawa yaleyale, akapiga tena na tena, lakini simu ya askari mwenye kifimbo cheusi haikupokelewa.



    "Jamaa hapokei simu.." Askari mwenye kifimbo cheusi alisema huku akimwangalia mwenzake.



    "Labda yupo mbali na simu, lakini la msingi namba yake inapatikana, anaweza kutupigia yeye atakapoikuta 'missed calls' katika simu yake, asipopiga tutampigia baada ya muda kidogo" Askari asiye na kifimbo cheusi alishauri.



    "Ahaa wazo zuri, twende kwanza kituoni tuisubirie simu ya jamaa, tukiona kimya twende moja kwa moja nyumbani kwake"



    "Sawa afande"



    Waling'oa gari yao na kurejea kituoni.



    Nje ya viwanja vya Maisala.....Zanzibar Martin na Richard walikuwa wamelala fofofo ndani ya gari. Hawakuwa wanajitambua kabisa, hawakujua jinsi hatari ikivyojitengeneza huko Dar es salaam kwa kasi kubwa sana ili isafiri na kwenda kumvaa Martin Zanzibar. Sumu aina ya Rox iliyokuwemo ndani ya gari lao iliwalaza kwa mara ya pili. Kumbe kabla Malkia hajaingia katika viwanja vya Maisala alianza kupulizia Rox ndani ya gari ile, kisha ndipo alienda ndani ya viwanja vya Maisala. Alifanya hivyo makusudi. Endapo angewakosa kuwapulizia ile sumu kule ndani ya uwanja, basi waje kukutana nayo ndani ya gari yao. Na Malkia alifanikiwa kwa asilimia mia...Rox iliwapata ndani, Rox imewapata nje...walikuwa na saa tatu zingine za kulala, huku kina Malkia wakiendelea na harakati za kutafuta hatma ya mkanda wa siri. Hivi vilikuwa vita vya akili, vilivyokuwa vinahitaji watu wenye akili kuvicheza, na Malkia alikuwa mwanamke wa kipemba aliyejaaliwa akili hizo, akili za VITA. Na ndomana Chifu mwenye akili aliamua kumuoa Malkia mwenye akili, kwakuwa Chifu siku zote alikuwa mtu wa vita na alikuwa anajua ya kwamba vita vyahitaji akili sana!



    Sasa kwanini asimuoe mtu mwenye akili?



    Askari mwenye kifimbo cheusi na askari asiye na kifimbo cheusi waliwasili katika makao makuu ya ofisi za TRA. Baada ya kufuata taratibu zote za kiofisi maaskari walipewa anuani ya mmiliki wa ile Range Rover Vogue, Martin Nguzu, pamoja na namba yake ya simu. Askari walitoka nje na kuingia ndani ya gari yao, wakiwa na matumaini tele ya kufumbua utata wa kifo kile cha kitata. Askari mwenye kifimbo cheusi ndiye aliyechukua jukumu la kuipiga ile namba ya Martin.



    Simu ya Martin iliita, ikakata, akaipiga tena, ikaitaa weee mpaka ikakata, akapiga tena matokeo yakawa yaleyale, akapiga tena na tena, lakini simu ya askari mwenye kifimbo cheusi haikupokelewa.



    "Jamaa hapokei simu.." Askari mwenye kifimbo cheusi alisema huku akimwangalia mwenzake.



    "Labda yupo mbali na simu, lakini la msingi namba yake inapatikana, anaweza kutupigia yeye atakapoikuta 'missed call' katika simu yake, asipopiga tutampigia baada ya muda kidogo" Askari asiye na kifimbo cheusi alishauri. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Ahaa wazo zuri, twende kwanza kituoni tuisubirie simu ya jamaa, tukiona kimya twende moja kwa moja nyumbani kwake"



    "Sawa afande"



    Waling'oa gari yao na kurejea kituoni.



    Saa 6:07 P.M

    Kijitonyama Katika viunga vya hoteli ya Grand villa hali ilikuwa tulivu sana. Watu wengi walikuwa katika Mgahawa safi wa hoteli hiyo wakipata makulaji pamoja na vinywaji huku wakisikiliza muziki murua toka kwa bendi ikiyoburudisha mbele ya ule Mgahawa. Brown ambaye pale hotelini alijitambulisha kama Michael Zulender alikuwa chumba namba 208. Nae kwa muda mrefu akiwa mle chumbani alikuwa amejaribu kuipiga namba ya Martin mara kadhaa lakini hakukuwa na majibu. Simu Iliita tu bila kupokelewa. Alikaa katika sofa mle chumbani mwake akitafakari hali ile, iweje leo Martin asiipokee simu yake. Vinyweleo vya mkono wake wa kushoto vilimsisimka, alistuka. Mara zote hali kama hiyo humkuta pale tu anapoikaribiana na hatari. Akaviamini kama siku zote anavyoviamini vinyweleo vile, na havikuwahi kumuangusha hata siku moja. Sasa akaanza kuchukua tahadhari kwa kila anachokifanya. Brown alikaa sofani akitafakari hadi saa moja ya usiku. Ndipo alipohisi njaa. Alikumbuka kuwa alikuwa hajala tangu alivyokula asubuhi Morogoro. Alienda bafuni akajimwagia maji haraka haraka, alirudi chumbani kwake na kuvaa jeans nyeusi na jezi ya timu ya Taifa ya Congo, chini alivaa viatu vya wazi. Alitoka nje ya chumba chake.



    Akiwa kwa nje Mwendawazimu alikuwa anatafuta namna sahihi ya kumkabili yule Mzungu, aliyepata taarifa zake kupitia simu ya yule jamaa aliyemuua kule bandarini. Mwendawazimu alitamani kwenda kuvamia katika chumba alichopanga yule Mzungu na kutafuta kitu ambacho alihisi tu kuwa yule mzungu anacho bila ya kuwa na uhakika. Lakini tatizo lilikuwa kupita pale getini kwa jinsi alivyo asingeruhusiwa hata chembe na walinzi kuingia ndani ya hoteli ile ya kifahari. Na hakukuwa na sehemu nyingine ya kupita kuingia katika hoteli ile zaidi ya pale getini. Mwendawazimu aliamua 'kupotea' kwa muda kwa kutumia ile pikipiki yake!



    Brown alifungua mlango wa chumba chake na kutoka nje. Alisimama nje ya mlango wake, alitumia kama dakika moja kuchezea kila kitasa cha mlango, aliporidhika aliifata lifti na kuiamuru imshushe chini. Baada ya dakika tatu lifti ilisimama. Alifungua mlango wa lifti na kutokea palepale mahali alipoingilia awali. Alitembea taratibu hadi mapokezi, alipofika pale mapokezi aliwakuta wale wahudumu wawili waliompatia chumba muda mfupi uliopita. Walipomuona, Irene Paul na Paulina Kennedy waliangaliana kisha wakatabasamu. Walitaka kuongea lakini Brown ambaye alijiandikisha pale kama Michael, ambao kwa wahudumu wale alipachikwa jina la Mr Na na na alikuwa ameshafika mbele yao. Aliwapungia mkono huku akitabasamu, nao walitabasamu kwa pamoja. Akatoka nje ya hoteli. Irene na Paulina wakagongesha mikono ya kwa furaha.



    "Mr Na na na...." Walijikuta wakisema kwa pamoja.



    "Tumesahau kumwambia aache funguo..." Irene alisema.



    "Anaenda mgahawani tu Mr Na na na" Paulina alijibu bila wasiwasi.



    Brown alifika nje ya Mgahawa wa hoteli ile, Grand villa Restaurent, maandishi yakiwa yanawakawaka na kubadirika rangi, mara yawe ya bluu, mara mekundu, mara njano, ilikuwa ni taswira nzuri ya kuitazama. Brown aliingia ndani ya Mgahawa, alikuta kuna watu wengi sana, toka katika mataifa mbalimbali duniani, wakila na kunywa huku wakiangalia muziki ukiopigwa mbele ya Mgahawa ule. Brown alichagua meza iliyokuwa katikati ya Mgahawa. Akakaa. Haraka haraka Mhudumu alimkimbilia.



    "Welcome Grand Villa hotel" Mhudumu wa kike alisema huku akimwangalia Brown kwa bashasha zote.



    "Ahsante sana" Brown alijibu kwa Kiswahili ingawa alikaribishwa kwa Kiingereza.



    "Sijui nikusaidie nini ndugu mteja?" Mhudumu nae aliamua kuuliza kwa kiswahili.



    "Ugali kwa nyama choma na na na maji makubwa ya Kilimanjaro" Brown aliagiza.



    "Ugali wa kawaida ama wa dona, na nyama ya mnyama gani wataka?"



    "Ugali wa dona na nyama choma ya mbuzi" Brown alijibu.



    Haraka haraka Mhudumu aliondoka, baada ya dakika zisizozidi tano alirejea na sahani kubwa mkononi, huku maji akiwa ameyaweka kwenye trei lenye rangi ya bluu. Baada ya chakula kuwekwa mezani na kukaribishwa, Brown alishukuru na kuanza kula taratibu.



    Zilipita takribani dakika kumi tu tangu Brown aanze kula kile chakula. Mgeni mwingine aliingia pale Mgahawani. Alikuwa ni kijana wa makamo aliyevaa suti safi nyeusi na shati jeupe ndani ya kote, huku chini akiwa amevaa viatu vyeusi vilivyochongoka kwa mbele, viatu maarufu kama mkuki moyoni. Kijana alitembea taratibu huku akizungusha funguo yake kwa kutumia kidole chake cha mwisho, bila shaka ilikuwa funguo ya gari. Kijana akapita karibu kabisa na ile meza ya mzungu.

    Na hapo ndipo alipoiona.

    Brown aliweka funguo ya chumba chake juu ya meza ya chakula. Yule kijana aliiona vizuri sana namba ya chumba alichofikia yule Mzungu....



    "Chumba namba 208" Alisema kimoyomoyo huku tabasamu jepesi likichanua usoni mwake.



    Kijana alipitiliza pale Mgahawani baada ya kukiona alichohitaji kukiona, namba ya chumba alichopanga yule Mzungu. Tokea pale kijana moja kwa moja alielekea upande kulikokuwa na mlango wa ile hoteli. Kijana alidhani atapita kirahisi pale mapokezi na kuelekea ndani ya hoteli ya Grand villa lakini haikuwa hivyo...kila mteja wa hoteli ile ilikuwa ni lazima apitie mapokezi ili kuchukua funguo ya chumba chake, na ilikuwa hupewi hivi hivi tu, ilikuwa ni lazima wathibitishe kwamba ni kweli chumba chako, baada ya kujibu maswali kadhaa toka kwa kina Irene na Paulina ndipo unakabidhiwa funguo ya chumba chako. Na kama wewe ni mgeni na umemfata mwenyeji wako hotelini, ilikuwa lazima utoe maelezo ya kutosha kwa Irene na Paulina, kisha simu ya mezani ipigwe kwa mwenyeji, atakapothibitisha kuwa ni kweli ana mgeni ndipo utapelekwa chumbani kwa mwenyeji wako. Kwa kujiamini kijana alifika hadi mapokezi. Maswali matatu tu toka kwa Irene, kijana akaona hawezi kuingia kwa namna aliyofiikiria awali. Akabadirisha mbinu.



    "Aaah tuache hayo, nahitaji chumba....." Kijana alisema akiwa amebabaika kidogo.



    "Kama vyumba vipo kaka" Paulina alijibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikambidi jamaa apange chumba kilazima. Na zikamtoka shilingi laki moja kwa ajili ya huduma hiyo. Akapatiwa na Mhudumu wa kumuongoza hadi chumbani, alikuwa ni Paulina. Waliifata ile lifti, Paulina alibonyaza namba kadhaa kisha wakaingia, na lifti ilianza kupanda juu. Wakafika floo ya tatu ya hoteli ile, wakawa wanapita huku wakiangalia mlango wa chumba kimoja baada ya kingine. Wakakifikia chumba namba 208, Kijana akauangalia kwa mshangao mlango wa kile chumba. Paulina aliuona mshangao wa kijana yule aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Chomwingo. Lakini hakutilia maanani sana, Paulina alienda hadi katika mlango wa chumba namba 215, akasimama. Akatoa funguo katika pochi yake na kuufungua ule mlango. Mlango ukafunguka. Walikuwa wanatazamana na chumba safi na kizuri cha hoteli ya Grand villa. Baada ya makabidhiano na kumuelekeza hili na lile, Paulina aliondoka, jamaa akabaki peke yake ndani. Ilimchukua dakika saba tu tangu Mhudumu kuondoka, jamaa nae alitoka, alisimama nje ya mlango wake, akaangalia kulia, kisha akaangalia kushoto, korido ilikuwa tupu, hakuna mtu. Jamaa alielekea upande wa kulia, upande alikuona mlango wenye namba 208....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog