Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

SALHAT - 2

 







    Simulizi : Salhat

    Sehemu Ya Pili (2)



    Baada ya muda Salhat na mama yake walikuwa wamesharudi eneo lingne walilolipata katikati ya msitu.



    "Salhat kwanzia sasa hivi nataka ukate mazoea na Johnny yeye ni binadamu na wewe ni jini Siku zote adui wa binadamu ni jini na adui wa jini ni binadamu.......hivyo kwa usalama wako nataka nikwambie binadamu siyo watu wa kuhaminik kama alivyokuwa baba yako nilimpenda lakini yeye hakunipenda mimi mwenyewe akampenda mwanamke mwingne wa kibinadamu na ndiye aliyenifanya hivi nilivyoleo mimi sikuwahi kuwa hivi hata baada ya kunifanya mimi hivi bado aliamua kumuuwa baba yako kwaajili ya kumiliki Mali na baba yako alikufa hata baada ya kummaliza baba yaki bado walianza kukufuatili wewe hadi Tukakutengenezea mchezo wa kifo na watu watambue ya kuwa umekufa nikawa nakuficha ndani kwaajili ya kukukwepesha na macho ya binadamu lakini sijui umetokeana wapi na Johnny Tafadhali kama unahitaji usalama wa maisha yko basi usijiingiz kwenye mahusiano na binadamu kwaamaana siyo sampuli yako!! Alizungumza maneno hayo Samia na kumuacha mwanaye katika dimbwi Kubwa la mawazo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakti Huo nao.

    Mr matata alirudi ndani ya nyumb yake na alishngaa baada ya kuona imebadilikwa kwa kiasi kikubwa hakukuwa na picha ya mjukuu wake yeye wala mkewe zaidi ya picha moja tu ya Naseeb.



    Alitoa amri moja tu na picha zote zilianza kutolewa na kuwekwa za Salhat pindi alipokuwa mdogo.



    Ghafla ilisikika sauti ya mtoto wa kike ikisema.



    "Nani kakuruhusu ushike picha yangu na utoe mahali nilipoiwek.????



    Aliitikia Mr matata.



    "Mimi mwenye nyumba ndiyo nimesema ifanywe hivyo kuna tatizo kwani!!!???.

    Alimuuliza Grace na kubaki wakitizamana machoni kwa macho haliyojaa tu chuki.



    "Mwenye nyumbaaaa!!!!! Alirudia neno lile Grace kwa mshangao na dharau kidogo. Hapo hapo Badra alitokea nyuma yake.



    "Mume wangu" aliita na kuanza kushuka ngazi haraka haraka kwaajili ya kwenda kumlaki ila alipokaribia kumfikia Mr matata alimnyooshea mkono wa kumaanisha asimsogelee karibu zaidi.



    "Mr matata!!! Aliita kwa upole.



    "Mume wangu nilikuwa nataka nije kukutizama lakini maswala ya kampuni yalinibana sana ila kwa kweli leo ndyo nilikuwa nimejiandaa nije kukuona mimi na Grace. Grace njoo msalimie baba alizungumza na kufanya macho ya Mr matata na Grace yakutane walitizamana kwa dakika kadhaa wote wakiwa kimya kabisa.



    "Sihitaji salamu yake" alizungumza Mr matata kisha akaanza kupanda ngazi huku akifuatwa na wakili wake nyuma.



    ***** ******** *****



    Salhat aliwaza sana usiku kucha na asubuhi alipata jibu la kumpa mama yake.



    "Mama!!!sawa nimekuelewa sitaweka tena mahusiano na Jay lakini na wewe nataka unihakikishie ya kuwa hutomdhuru Jay"



    "Nitafanya vile upendekezavyo Kama nawe utafuata masharti yangu niliyokupa"



    Hatimaye waliweka kiapo kwmba hataweka mahusiano na Jay na wala yeye hatomuumiza Jay kwa namna yoyote ile.



    ****** *******



    Jay alitoka zake bafuni akiwa anapiga miluzi yake huku anajifuts maji yake kichwani ila alishtuka baada ya kuhusi ya kuwa kuna mtu nyuma yake aligeuka na macho yake yaligongana na Salhat.



    "Salhat" aliita Jay na kumsogelea huku akimkumbatia.



    Salhat na yeye alinyoosha mikoni yake kisha akamkumbatia huku akitoa machozi.



    "Kwann unalia Salhat........aliuliza Jay huku akiwa anampangusa machozi........."mama mzima??? Alimuuliza.



    Salhat alitingisha kichwa ishara ya kuwa ndyo mzima.



    "Na wewe Je????



    Salhat alitingisha tena kichwa kama alivyofanya mwanzo.



    "Sasa kwanini unalia??? Aliuliza huku akimtizama.



    Salhat alijisogeza karibu naye na kulala kifuani mwake huku akimkumbatia zaidi.



    Jay alishindwa kuelewa ni kipi kimemkuta Salhat hivyo na yeye alimkumbatia huku akimpiga piga mgongoni kwa ishara ya kumtuliza asilie.



    Baada ya Salhat kukaa sawa Jay alibaki akimtizama sana usoni hadi kumfanya Salhat kutokuwa comfortable.



    "Jay usinitizame sana bhna hivyo" alizungumza baada ya uzalendo kumshinda.



    "Kwanini ulikuwa unalia???



    Salhat alipelekea juice yake mdomoni aliyokuwa amepewa na Jay huku akimtizama baada ya kupiga fundo moja aliishikilia mkononi na kuendelea kumtizama Jay ambaye macho yake hayakubanduka kwenye uso wa Salhat.



    Salhat aliinua tena glass na kutaka kupeleka mdomoni lakini Jay aliimnyang.anya glass kisha akaiweka chini na kumshika mikono yake miwili Salhat aliyeanza kukwepesha macho yake.......



    "Jay sitaweza kukwambia" alizungumza kimoyomoyo Salhat.



    "Na kwanini usiweze kuniambia??? Aliuliza Jay design kama aliyasikia maneno aliyoyazungumza Salhat.



    Salhat alishtuka na kumtizama.



    "Mbona maneno hayo nimeyazungumza ndani ya moyo wewe umeyasikiaje??? Aliuliza Salhat kwa kutahamaki.



    Jay alitabasamu na kumwambia hii ni siri yako.



    "Me huwa nasikiaga chochote kile mtu akikiongea hata kama ni mlio wa ndege na yuko mbali kiasi gani huwa nasikiaga na unajua ilianza lini hiyo........Siku ambayo nilikutana na wewe kijijini ndyo na mim nilianza kupatwa na ugonjwa huu" aliongea Jay kwa kumuelewesha zaidi Salhat.



    "Sasa nifanyaje, nitamwambiaje mama kwamba nimeshindwa?? Hapana sitaki Jay awe katika hali ya!!!!!.........



    "Salhat unazungumza sana vingi mpaka nashindwa kukuelewa wewe shida yako ni nini???! Aliuliza tena Jay.



    "Ntarudi" ndyo neno alilolisema Salhat na kupotelea.



    Salhat!!! Salhat!!!!, alibaki akiita tu lakini tayari mama yake alikwisha tambua mtoto wake yuko katika hali gani sasa.



    Alianza kukumbuka baadhi ya matukio Siku ambayo alikuwa akiwaza ampeleke Jay njee ya nchi kwaajili ya masomo zaidi lakini Jay alitokea na kumwambia sitaenda popte mimi.



    "Siku aliyokuwa jikoni huku akifikiria kuhusu Jay na Salhat kwa kuzungumza ya kuwa kama wataowana ukubwani basi familia yao itakuwa yenye furaha sana"

    Jay alitokea na kumwambia.



    "Naona unawaza juu yangu na Salhat!!!

    Na alipomuuliza umejuaje Jay alishtuka na kumwambia naamaanisha uso wako unaonyesha kwamba unatuwaza.



    "Sasa ni hichi kimempta mwanangu!! Alianza kujiuliza hapo hapo tukio la Salhat kupotea mbele ya macho yake lilijirudia kichwani mwake.



    "Na Salhat mbona kama........alizungumza na kukumbuka tukio la kupotea kwa Salhat.......hpana kwamba ni mchawi huyu mtoto alijiuliza na kunikuta kichwa kinamuuma.



    "Hapan lazima niende mahali kwaajili ya kuupata ufafanuzi zaidi. Aliongea na kukimbia chumbani kwake akabeba kipochi chake kisha akatoka ndani ya nyumba yake na kulipanda gari lake kisha akaondoka nalo.



    ***** ********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mr matata akiwa amekaa sebleni huku akitizama TV yake Grace alikuja na juice kisha akaiweka mezani.



    "Baba karibu juice alizungumza na kumsogezea karibu zaidi.



    Mr matata aliita.

    "Ashura.........Ashura!!!



    Ashura naye aliitika na akaja.



    "Uko jikoni!!! Aliuliza Mr matata.



    "Ndiyo baba"



    "Kama uko jikoni basi utakuwa unahisi kiu chukua hiyo juice unywe umalize.......



    "Hapana baba mimi sihisi kiu kabisa" alijibu Ashura na wakati Huo Bahati alikuwa akipita.



    "Bahati njooo"



    Bahati alijisogeza mpaka pale.



    "Ulikuwa njee ukipiga dawa mauwa amah kwa hakika umechoka sana na unahitaji kinywaji cha baridi.



    "Ndiyo baba ndyo maana breki yangu ya kwanza naelekea kwenye friji"



    "Chukua hiyo juice na unywe"



    "Ahsante aliongea na kuikimbilia ile glass ya juice Kisha akataka kuipeleka mdomoni alishtuka baada ya kukutana na jicho Kali LA Grace.



    "Hapana nilisahau mimi nitaenda kunywa tu maji yatanitosha........ Alizungumza Bahati.



    "Nimekwambia kunywa alizungumza kwa ukali sasa na kufanya Bahati aipeleke ile juice mdomoni na kuinywa yotee.



    Baada ya kumaliza alicheuwa na kushukuru kisha kaanza kuondoka na glass.



    "Hapana glass yangu wewe iache hapo hapo mezani kisha mkaendelee na kazi zenu" wote walitoa heshima kisha wakaondoka baada ya bahati kufanya vile alivyoagizwa.



    " nafikiri ungechukua sasa glass yako na kuondoka nayo na wakati mwingine ni vizuri kwa wewe kutambua ya kuwa mimi huwa natumia nini na nini situmii na utafanya hivyo kwa kumuuliza Ashura maana hata Huyo mama yako hajui mimi napendelea nini! Alizungumza na kuinuka kisha akaenda zake ndani.



    Grace aliipasua glass ile kwa hasira na kupiga kelele.



    "Mpumbavu kabisa pumbavu wewe unafikiri wewe ni nani mpaka unipelekeshe mimi namna hii sasa utakufa nakwambia utakufaaa tuuuuu!!!!!! Na huyu mpuuuzi bahati yuko wapi yuko wapi huyuuuuu!!!!!!!!!!!!!!! Alizungumza kwa kelele Kubwa sana na kwa wakti Huo Mr matata hakuwa ameenda mbali na pale hivyo kila alichokizungumza alikisikia alitabasamu tu na kucheka kisha akasema "sijui li toto la nani Hili likorofi sana alafu sasa la kike" hahahaah alutabasamu na kukuta Ashura akiwa anamtizama baada ya Ashura kugundua ya kuwa ameonekana basi aliondoka na kuingia jikoni ila wakati Huo wote Mr matata alimsindikiza kwa macho hadi alipopotelea na kulikuwa na siri nzito katikati yao hao wawili lakini hakuna mtu yoyote aliyeweza kuifahamu siri yao zaidi ya wao wenyewe.



    ******** **********



    Huku nako mama yake Jay akiwa anaelekea sehemu ambayo alihisi ni sahihi kufika gari lake liliharibika hivyo alishuka na kuanza kutembea kwa miguu kwani tayri alishakaribia kufika.



    Aliingia kwa mganga ambaye ndipo alipowahi kufika Mr matata.



    Mganga baada ya kumuona alitabasamu sana kisha akasema.



    "Hatimaye Siku yangu ya kifo changu imetimia leo.......kwani hii ndyi harufu ya mwisho ambayo nitainusa................................. Kilichokuleta hapa nakitambua lakini hakina mpinzani katikati yake kwani hao walizaliwa kwaajili ya kuwa pamoja hata mbingu na ardhi wanalitambua hilo na nivigumu kulitengua kwani tayri wamesha share kitu ambacho kingewafanya wasikutane.



    "Unamaanisha nini!!!!! Aliuliza mama yake Jay.



    "Busu na siyo busu tu wameshare Bali mpaka mate"



    "Mpaka mate............!!!!!!! Aliuliza kwa kutahamaki....



    "Ndyo namaanisha mpaka mate......lakini siyo unavyofikiria wewe walishare mate kwa kuchangia pipi moja hivyo ni vigumu kuwatenganisha na uwezo alionao mwanao ni kutokana na mate waliyoweza kushare. Alizungumza mganga yule.



    Na hapo hapo aliingia Samia akiwa katika umbo lake la kijini kisha akaketi.



    "Nilijua hata na wewe utakuja lakini kama nilivyosema ni vigumu sana kuwatenganisha watu hao wawili kwa njia yeyeto ile labda mtumie uwezo wa kibinadamu kwa kuwatenganisha"



    "Kivipi aliuliza Samia.



    "Kwamba hamjanielewa mcheze mchezo wowote wa kufanya wachukiane na kuachana wenyewe maana kwa nyie hamtaweza kuwatenganisha ila hata mkifanya hivyo watatengana kwa miaka michache tu ila watakutana tena hapo sasa itategemea kwa jinsi gani wataweza kukutana kwani wanaweza wakasababisha kheri au wakasababisha matatizo makubwa ambayo yatawapata mpaka nyie na kusababisha vifo vya watu wengi kwahiyo muangalie lipi la kheri." aliongea Mganga yule na hapo hapo alikohoa damu kisha akafariki.



    Walimuita lakini hakuweza kuitika hata kidogo.



    "Tafadhali tuambie unamaanisha nini ukisema watasababisha matatizo pindi watakapokutana tena!!!! Aliuliza mama yake Jay akitaka kujua zaidi lakini tayri alishachelewa kwani tayri mganga alishapoteza maisha.



    Hatimaye walikaa kwa kutulia baadye wenyewe wawili.



    "Vyovyote na iwe sihitaji mwanangu awe mahusiano na jini" alizungumza mama yake Jay.



    Samia alidondosha machozi na kuyakumbuka maneno ya mwanamke mmoja ambaye alimwambia sihitaji mwanangu awe na mahusiano na jini.

    Machozi yalimteremka na aliyafuta kisha akamgeukia mama yake Jay na kumwambia sawa tufanye vile utakavyo.



    "Sawa mimi nitakwambia...kipi cha kufanya alizungumza na kumuacha Samia eneo lile.



    ***** ******



    Grace akiwa ndani na mama yake huku wakitizamana tu.



    "Unanitizamia nini??? Aliuliza Badra .



    "Hamna" alijibu tu kwa ufupi na kutizama TV.



    Akiwa eneo lile aliuhisi upepo ambao aliamini ni wito wa kuelekea kwenye kambi yao na yeye alisimama kisha akaingia ndani kwaajili ya kuelekea kuleambako aliitwa.



    Baada ya kufika alimtizama mama yake aliyekuwa akimtizama kwa hasira sana.



    Huku akiwaangalia baadhi ya majini wenzake waliokuwa wako chini na kuvujia damu kwa adhabu waliyopewa.



    "Salamuu eeee malikia wa ukoo wetu wa Abandandi.".



    Kabla hajamalizia salamu yake alipigwa kibao na mama yake na kumfanya adondoke chini.



    Alishika shavu lake na kumtizama mama yake kwa hasira ila alirudi katika hali yake na kulishika shavu lake.



    "Yani wewe ni bure kabisa huna la kheri lolote uliloenda kulifanya huko dunia......Salhat bado yuko hai na haitoshi tayri ameshakutana na mtesi wetu sasa hivi tutakufa na ukoo wetu utafilia mbali kwann hufanyi vitu kwa umakini wewe!!!!



    "Malikia unamaanisha nini unaposema Salhat yuko hai!!! Aliuliza Badra kwa kushangaa"



    "Bora angekuwa yuko hai tu ingetosha lakini sasa nguvu zake zimeongezeka Mara dufu yani Mara nyingi zaidi" aliendelea kuongea malikia wa Abandandi.......



    Badra alitizamana na wasichana wale ambao alishghulika nao katika swala la kumuulia mbali Salhat.

    Baada ya muda waliweza kutambua ni kipi Siku ile walichezewa mchezo wa aina gani mpaka wakaamini ya kuwa Salhat amekufa.



    "Lakini mimi ikiwa Salhat Yuko hai lazima mmoja kati ya hawa alikufa kama hakufa Samia basi Sultan Shariphu amekufa na Hiyo ni faida kwetu" alizungumza Badra.



    "Unaongea kuhusu nini wewe??? Aliuliza mama yake.



    "Katika mkono wa Salhat kulikuwa na kinga ya majini na jini wa aina yoyote yule lazima kinga hiyo ingemuadhiri kwani ni yenye nguvu sana na kama hata kufa basi nguvu zake za kijini zitapotea na kubaki chache sana..........ni vizuri kama tutamuuliza Spy wetu wa kule katika ukoo wa Sultan tutizame kama Sultan au Samia yuko hai" aliongea na hapo hapo wazo lilimjia mam yake kisha akapotea kimazingara tu.



    ***** ******* ****



    Huku nako mchezo ulichezwa kwaajili ya kuwatenganisha Salhat pamoja na Jay Hili wachukiane kabisa kwani wazazi wao hawakutaka watoto wao wawe pamoja hata kidogo Siku hiyo Salhat alikuja na mama yake kwa kina Jay huku mama yake akimwaminisha ya kuwa yameshaisha Yale yote aliyoweza kuyazungumza juu yake yeye na Jay na wanaweza kuendelea kuwa marafiki tu.



    Siku hiyo ilikuwa furaha Kubwa sana kwa Jay na Salhat huku wakiamini ya kuwa maisha sasa yatakuwa mazuri tu. Lauh kama binadamu angeweza kutambua ni kipi kinaweza kutokea kwa dakika za mbele zijazo basi mama yake Jay na Salhat wangeacha kutengeneza hicho walichokuwa wanataka kukifanya.



    ****** ******



    Huku nako taarifa zilirudi katika koo ya Abandandi na wote walipewa taarifa ya kuwa Sultan Shariph alifariki na sasa anayekaa kama sultan ni Sayid akishirikiana na Samir ambao huwezo wao hauwezi kuwatisha hata kidogo.



    Malikia na wafuasi wake wa ukoo wa Abandandi walicheka sana kisha wakajiaminisha ya kuwa Sasa ukoo wao wataweza kuupanua kama watawashinda vita majini wale na wote wakawa chini yao.



    "Vipi kuhusu Samia na Salhat??? Aliuliza Badra



    "Samia nguvu zake zimezidi kupungua zaidi ukiachana na kwamba alilala na binadamu hivyo tutaweza kummaliza kirahisi na tukitaka kummaliza Salhat ni kwa kumtumia mama yake pamoja na Johnny tunaweza kuziteketeza nguvu zake kupitia watu hao wawili"

    Alitoa maelezo hayo malikia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa kufanyaje"



    "Usijali nitawaambia na leo jioni ndyo itakuwa Siku muhafaka wa sisi Kimsambaratishia Samia na Salhat na kazi Hii hata mimi nitajiunga nanyi" aliongea na kucheka kwa kebehi na zarau ya hali ya juu.



    ***** ******



    "Nafikiri mchezo wenyewe tuufanye jioni ya Siku ya leo" aliongea Mama yake Salhat na kuhafikiana na mama yake Jay.



    ***** ****** ****



    Upande mwingine nao Mr matata aliletewa picha ya Salhat akiwa katika umri wa miaka 7.



    "Ni kweli kafanana sana na bibi yake na wala hajabadilika kwa kiasi kikubwa sana" alizungumza na kuipapasa sura ya Salhat iliyokuwa kwenye picha kisha akaanza kukagua picha nyingne ambazo alimuona Johnny kwa kila picha.



    "Huyu Naye ni nani???? Aliuliza Mr matata.



    "Huyu ndye kijaa wa.mama ambaye anakaa Salhat sasa na mama yake" alizungumza kijana yule aliyeweza kuzilete picha.



    "K sawa hata hivyo siyo mbaya sana anafaa kuwa mkwe wangu" alizungumza na kucheka.



    "Bossi tunasubiria kauli yako.



    "Ahaa sawa......naona muda mzuri wa kwenda kumchukua ni leo jioni sitataka tena akae mbali na mimi na muulize yule mwenzko kama tayari ameshaandaa ile ndege kesho asubuhi sana nitaondoka na mjukuu wangu hapa Tanzania tuende tukaishi mbali kabisa.



    ***** ****** ****



    Haya hatimaye Siku ya Siku hiyo jioni ikafika huku bado ikiwa ni Siku ya tabasamu baina ya Jay na Salhat.



    "Salhat.......nahisi kuna kitu hakipo sawa kabisa kwamaana kama naona vitu vitu vya ajabu alafu sielewi" alizungumza Jay.



    "Vitu gani hivyo???



    "Kama vile mimi nakuchoma we kisu kisha naona maiti ya mama yako mama yangu na m babu ambaye simuelewi pia na watu ambao nao siwaelewi wakicheka kisha............ "



    "Jay unazungumza nini wewe......mama yangu wala mama yako hawawezi kufa mapema hiyo ni ndoto tu kama ndoto nyingne wala usifikirie sana"



    "Lakini Salhat haionekani kama ndoto kwasababu sijalala Bali natembea na ninaona kabisa hapa ndipo nitakapoku............"



    "Shshshshshshshshs najua huwezi kuniuwa mimi wala hakuna chochote kibaya kitakachoweza kutokea juu yangu wala juu yako wala juu ya mama zetu" alizungumza Salhat kwa kumtoa shaka Jay.



    Jay alimtizama sana Salhat.



    "Sitaki ufikirie hivyo nimeshakwambia kila kitu ni salama tafdhali nielewe hivy na unipe tabasamu lako"



    Jay alimtizama na kutabasamu.



    Lakini vile Jay alivyokuwa anaona ndicho kitakachoweza kutokea kwani Huo pia ni uwezo mwingne ambao aliweza kuzaliwa nao ila ungeweza kujitokeza tu pindi atakapokutana na Salhat ambaye ndyo watakaoweza kuwa wakombozi wa dunia nzima.



    ****** ****



    Hatimaye jioni ilifika iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na kila mmoja ambaye alikuwa na jambo lake juu ya Salhat.



    Wakati mama yake Jay akipita katika nyumba yake ghafla alidakwa na hata mama yake Salhat nayeye alidakwa na wtu asioweza kuwafahamu na wakati Huo Huo watu waliruka geti kwajili ya kuingia ndani na kufanikiwa huku Mr matata akiwa mmoja wao.



    Salhat na Jay nao walikuwa wakielekea ndani huku wakicheka bila kujua lolote lile.



    Lakini Jay alimuita Salhat ila Salhat aliendelea na safari.



    "Salhat aliita tena Jay.



    Salhat aligeuka na kumkuta Jay akiwa tayri ameshabadilika katka sura yake.



    "Kuna nini??" aliuliza Salhat



    "Sijisiki vizuri kabisa na sijui kwann!!! Aliendelea kuzungumza Jay.



    Salhat alipiga hatua za nyuma na kumfuata Jay.



    "Jay nimeshakwambia kila kitu ni salama sasa kwann unawaza sana achana na hivyo ambavyo wewe unaviona ni wasiwasi wako tu" alizungumza Salhat.



    "Sawa nimekuelewa"

    Jay alijitizama shingoni kisha akatoa cheni ambayo alipatiwa na Salhat kisha akamvisha na kumwambia.



    "Hii ni kinga yako hakuna chochote kibaya kitakachoweza kukutokea wewe" alizungumza na kutabasamu.



    Huku nako mama yake Jay aliachiliwa na alimuona mama yake Salhat ndiye aliyemshika.



    "Kwanini umefanya hivi!?????



    "Nataka tubadilishe mchezo hiki ni kisu unatakiwa unichome nacho cha tumbo!! Aliongea mama yake Salhat.



    "Lakini hatukupanga kufanya hivyo" aliongea mama yake Jay.



    "Usijali nataka tufanye hivyo Hili kuwatenganisha kabisa"



    "Je kisu hakitakudhuru???



    "Hapana hakiwezi wewe Fanya vile nitakavyo mimi kwasababu mimi ni jini na siwezi kufa kirahisi namna hiyo" aliongea Samia na kumpa mama yake Jay kisu kisha akamwambia tukutane sehemu ambayo tulipanga.



    Mama yake Jay alitingisha kichwa akimaanisha ni ishara ya ndyo na hapo hapo safari ilianza ya kuondoka eneo lile. Wakati akiondoka tu Samia aligeuka na kucheka wala hakuwa Samia Bali Badra ambaye alitizama pembeni ambako Samia alikuwa ameshikiliwa kijini.



    Wakati Huo nao Mr matata na genge lake la watu watatu walianza kumtafuta Salhat kwaajili ya kumchukua na kuondoka Naye.



    Wakati Huo nao Badra alijibadilisha na kuwa na umbo la mama yake Jay kisha akawafuata na kuwaambia ya kuwa.



    "Salhat embu nifuate alafu Jay ingia ndani ukaniletee maji ya kunywa kisha ujie kwa njia Hii haraka"



    Salhat aliongozana na Badra bila kumtambua ila alipomshika tu mkono wake na kumtizama aliiona sura ya Badra.



    Alitoa mkono wake na kumuuliza.



    "Wewe ni nani mbona siyo mama yake na Jay!!!!?? Alimuuliza Badra ambaye alishtuka na kumtizama Salhat.



    "Unakichaa nini embu twende huku mimi siyo mama yake na Jay sasa mimi ni mama yake nani?? Aliongea Badra kwa kumpotezea Salhat.



    "Hapana wewe siyo"



    "Haahahahahahahhaa alicheka sana Badra kisha akamwambia.



    "Ni kweli mimi siyo na sijui umenijuaje haraka namna hiyo unaonekana una nguvu kweli"



    "Yuko wapi mama yake Jay??? Aliuliza Salhat.



    "Badala ya kumuulizia mama yako unamuuliza mama wa mtu ambaye anakuulia mama yako......."



    "Unaongelea nini wewe??? Aliuliza kwa mshangao.



    "Tizama mimi ni mdogo wake mama yako nimekuja hapa kukusaidia wewe kwa vile mama yako maisha yake yapo hatarini na mama yake Jay ndye anataka kumuuwa Hili amridhi nguvu alizonazo"



    "Hapana wewe ni mwongo sana wewe ni mwongo" alizungumza Salhat na kuanza kuzunguka huku akiliita jina la mama yake Jay.



    Alipofika mbele alimuona mama yake na Jay akiwa ameshikilia kisu huku akimfuata mama yake ili amchome kisu kama walivyokubaliana.



    Wakati huo nao mama yake Salhat alikuwa akimuonyeshea ishara ya asifanye chochote kile bila kuongea na hii inatokana na kwamba tayri alishanyang.anywa nguvu kidogo za kijini alizokuwa amebaki Nazo na kukatwa ulimi hivyo ilikuwa vigumu kwa yeye kuongea.



    Mama yake Jay alimfuata na kufunga macho huku akimchoma kisu kile cha tumbo hapo hapo mama yake Salhat alidondoka chini na kuanza kumnyooshea mkono Mama yake Jay ila hazikupita dakika kadhaa mama yake Salhat alifariki palepale.



    Salhat alimfuata mama yake na kupiga magoti chani huku mama yake Jay akiwa hana wasiwasi wowote akijua ya kuwa ni game wanacheza.



    "Umemuuwa mama yangu????



    "Ndyo kwasababu nazitaka nguvu zake na hapo amekufa wala hata fufuka tena" alizungumza mama yake Jay kwa kujiamini bila ya kujua ya kuwa tayari ulikuwa msala.



    Alishangaa baada ya kuona damu zinamtoka mdomoni alienda na kupiga magoti kisha akamfunua mdomo alishtuka na kudondoka chini.



    "Ni nini Hii!!! Alianza kujiuliza mwenyewe.



    Salhat kwa hasira alizonazo alishindwa kuzicontrol nguvu zake za kijini alizonazo na kujikuta macho yamebadilika rangi pale pale alimtizama mama yake Kisha akachomoa kisu kilichomchoma mama yake na kuanza kumfuata wakati Huo nao Jay alishaanza kukata kona na kukaribia eneo lile.



    Salhat alimfuata hadi ukutani ambako hakukuwa na pa kwenda tena.



    "Salhat mwanangu mimi sijafanya hivyo Tafadhali zicontrol hasira zako"



    Salhat akuelewa kitu Bali alibaki kunguruma kama simba na alimchoma mama yake na Jay kisu wakati huo na Jay alishafika eneo lile na kuona tukio lile.



    "Salhat!!! Aliita Jay bila mafanikio na kelele hizo ziliwashtua wakina Mr Matata ndani.



    Johnny alifika lakini tayri ilikuwa ameshachelewa na wakati huo bado Salhat alikuwa na hasira zake. Jay alipomfuata alimsukuma mbali sana na kufanya adondokee sehemu ambayo na yeye aliamka hapo hapo Badra alitupa kisu bila Jay kujua na alikiona alianza kumfuata Salhat kwa hasira huku akiwa ameshikilia kisu mkononi mwake.



    Alipofika alichoma kisu ila Mr matata alijitokeza mbele yake na kufanya kisu kile kimpate alimshika Jay kisha akamshikika mkono wa Salhat na hapo hapo hasira za Salhat zilimpotea na kurudi katika hali yake ya kawaida.



    Mr matata na yeye hakusema neno Bali alidondoka hapo hapo Jay alikishika kile kisu na kukichomoa kisha akaanza kuitizama mikono yake ambayo ilimfanya akamchoma kisu Mr matata.



    Alitupa kisu chini kisha akamfuata mama yake ambaye wakati huo Badra alimuingilia kabla hajakata roho.



    "Usimuache mzima Salhat muuuwe........nasema muuuuwe....na kile......kisu ulichokiokota......alizungumza kwa shida kisha akakata roho papo hapo wakati huo Salhat alikuwa akimtizama Mr matata aliyeweza kuyakomboa maisha yake.



    Ghafla alihisi kisu amepigwa cha mgongo aligeuka nyuma tartibu kabisa na macho yake yaligongana naya Jay ambaye alidondoka chini kwa uwoga alionao kwa wakati huo.



    "Kisu alichochomwa Salhat kilikuwa kisu cha tofauti na visu vya kawaida kwani alianza kupukutika kiungo kimoja baada ya kingine na hapo ndipo Jay alipokwenda kumshika.



    "Salhat.......!!!!!!!!! Aliita Jay lakini tayri alishachelewa kwani tayari mwili wa Salhat ulianza kupukutika.



    Mwili wote uliishia mikononi mwa Jay na hapo hapo alishangaa kuwaona watu waliokuwa wakija na kuanza kumcheka alijitahidi kuziba masikio yake lakini haikusaidia kwani sauti zao Kali zilipenya mpaka katikati ya ngome ya masikio yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni baada ya mwili wa Salhat kupukutikia mikononi mwa Jay huku Jay akizisikia sauti za vicheko masikioni mwake.



    Hapo hapo watu wale walioweza kuja na Mr matata walitokea na wao walishtuka kisha kudondoka chini kwa sauti zile Kali.



    Walimchuku Jay kwa kumburuta huku wakiyaficha masikio yao kutokana na sauti zile Kali hatimaye walifanikiwa kumtoa kabisa njee ya sehemu ile ila wawili waliweza kudondoka kutokana na masikio yao kuanza kuvuja damu hata nao hawakuchukua muda mrefu wakafariki palepale.



    Alibaki kijana mmoja ambaye yeye ndye aliyeweza kutoa taarifa za wapi alipo Salhat.



    Alimbeba Jay ambaye kwa wakati huo na yeye masikio yalianza kumtoka damu na kumuingiza ndani ya gari kisha akaondoka naye eneo lile.



    Katika hali isiyokuwa ya kawaida eneo lile lilikuwa tulivu sana huku maiti zikiwa zimetapakaa ndani ya nyumba ile hapo hapo alitokea Sadick na Samir ambao waliweza kupata hisia hizo na kuja eneo lile wakiwa wamechakaa damu hiyo ni kutokana na vita vikali vilivyoweza kutokea ndani ya ngome yao na wao walifanikiwa kutoroka kwaajili ya kuja kuutizama usalama wa Samia na Salhat.



    Walipofika hawakuamini macho yao baada ya kukuta kile walichokiona.



    Walifanikiwa kumuona Samia lakini hawakuweza kumuona Salhat.



    "Yuko wapi Salhat?? Aliuliza Samir.



    "Salhat.....alianza kuita Sadicky lakini hakukuwa na mrejesho wowote ule..



    Samir alimshika Sadick kisha wakaanza kutumia nguvu zao za kichawi kwaajili ya kujua wapi alipo Salhat walianza kurudisha matukio nyuma kupitia ufahamu wao wa akili Hili waweze kutambua wapi alipo Salhat.





    Hatimaye waliweza kutambua ila zile kelele na wao ziliwaletea sana shida masikioni mwao na hata Samir alianza kutokwa na damu puani.



    "Samir!!! Aliita Sadick lakini Samir alimnyooshea mkono ya kuwa awe mtulivu tu kwani atarejea katika hali yake.



    Walifika mpka sehemu ambayo waliyaoma majivu ya Salhat.



    "Hichi kisu alichochomwa ndyo pekee kinachoweza kusambaratisha majini na kufanya wasirudi tena duniani" alizungumza Samir kwa kukitolea ufafanuzi kisu kile.



    alikitizama kile kisu kisha akasema "lakini kwa kumtoa jini mmoja sadaka kuna uwezekano wa Salhat kurudi duniani" aliongezea Sadick.



    "Lakini uwezekano huo ni mdogo sana bora kungalikuwa na mwili lakini amebaki majivu tu kwahiyo ni kazi ngumu sana kumrudisha tena duniani Salhat.



    "Sasa tufanyaje kwasababu hatuwezi kuuwacha ukoo wetu wa Sultan uteketee tu ikiwa tayri tulishaletewa mkombozi ambaye anauwezo mkubwa sana wa kusaidia ukoo wetu sasa tunawezaje kumpoteza katika wakati huu ambao na sisi tayri tumeshanyang.anyanywa ukoo wetu????? Alizungumza kwa hasira sana Sadicky.



    Samir alitizama bila kupata jibu na kuonekana kama mtu mwenye tamaa kwa wakti huo Vitone vya machozi yake vilikuwa vikidondokea katika majivu ya mwili wa Salhat na kuna mabadiliko yalianza kutokea bila wao wenyewe kujua.



    "Samir!!! Hatuwezi kukosa vyote......tulikuja kumtizama Salhat lakini ndo tayari sasa ameshafariki hatuna budi kurudi ili tukaupambanie koo wetu.



    Samir alisimama eneo lile kisha akajifuta machozi yake na kufanya yadondokee pale zaidi kisha akapotea yeye pamoja na Sadicky.



    Wakati huo nao katika majivu Yale yalianza kujikusanya sehemu moja na kuanza kuchora umbo la mtu kisha cheni ile ya ulinzi wa Salhat ikajisogeza na kukaa katika shingo ambayo ilijichora katika majivu Yale.



    ****** ****** ******



    Katikati ya kijiji kimoja kilichopo huko maeneo ya pwani mwa Tanzania watu wengi wa kijiji hicho waliweza kujishughulisha sana na shughuli za uvuvi na alikuwepo bwana mmoja ambaye aliweza kuishi na mkewe kwa takribani miaka 9 huku wakiwa hawajabahatika kabisa kupata mtoto katika maisha yao. Watu hao walikuwa ni Lillina na Joseph ambao waliweza kumsaidia Samia Mara ya kwanza katika kuokowa maisha ya Salhat.



    Usiku wa Siku hiyo Mr Joseph alikwenda katika shughuli zake za baharini huku akiwa ni mwingi wa mawazo yakuwa lini na yeye angeweza kupata mtu ambaye angeweza kulisimamia jina lake ila hata ambako yeye hatokuwepo duniani basi abaki japo mridhi wa jina lake japokuwa hana kitu.



    Akiwa katika dimbwi la mawazo alihisi amekanyaga kitu ambacho kilimfanya mguu wake ushtuke Alitoa haraka mguu wake huku akaimini ni nyoka na kujiandaa kupambana naye.



    Alishangaa baada ya kuona ni binti mdogo tu wa kike aliyeweza kujilaza maeneno Yale.



    Aliinama tartibu kisha kumgeuza Hili amtizame machoni kama angeweza kumfahamu lakini hakumjua alitizama kulia na kushoto kama kuna mtu yoyote aliyeweza kumuacha hapo lakini hakukuwa na mtu zaidi ya yeye na mawimbi tu ya bahari.



    Aliinama na kumtizama kama yuko hai au amekufa. Alishtuka baada ya kugundua ya kuwa yuko Hai. Alimbeba haraka haraka na kisha kumpeleka nyumbni kwake ambako hakukuwa mbali na eneo lile.



    Mkewe alimpokea na kumlaza kitandani kisha akaanza kumfunika na mablangeti kwani alionekana kutetemeka baridi Lillina aliwasha jiko na mkaa kisha akaweka karibu kabisa na kitanda huku akiendelea kufunika nyumba yake kwa mapazia.



    "Umemtolea wapi huyu mtoto??? Aliuliza Lillian.



    "Nilimkuta kule maeneo ya baharini akiwa amelala chali, ikabidi nimchukue kisha nimlete hapa kisha tumpatie Huduma muhimu. Alijielezea Joseph ambaye aliaminika sana kwa mkewe.



    "Ni mzuri sana eti!! Aliongea huku akimpapasa papasa usoni na hapo aliiona cheni shingoni mwa binti yule kisha akaitoa njee na kuanza kuitizama.



    "Kama vile Hii cheni Si ngeni machoni pangu" alizungumza Lillian akiendelea kuitizama kwa makini na nikweli haikuwa ngeni machoni pake kwani tayari alishamuonaga nayo Salhat baada ya kupatikana na babu yake Mr matata kisha kufanyiwa karama.



    ***** ****** ****



    Asubuhi ilifika na bado Salhat hakurejelea katika fahamu zake na hali hiyo ilianza kuwashtua Lillian na mmewe Joseph.



    "Joseph Je kama amekufa....na kama wazazi wake wanamtafuta........halafu hatujatoa taarifa sehemu yoyote ile....unajua utajiingiza katika matatizo makubwa sana wewe!!!



    "Sasa tufanyaje???!!



    "Usiku ukiingia tuendee tukamtupe huko huko baharini" alizungumza Lillian aliyeanza kuogopa.



    "Lakini ni.mtoto huyu tutamtupaje na sisi tunatufa mtoto kwa miak9 sasa yawezekana huyu ndye Mungu aliyeweza kutupatia kwa njia Hii" aliongea Joseph lakini haikusaidia kitu kwani usiku ulipofika hata yeye aliingiwa na mashaka na sasa alihafikiane na mkewe.



    Walienda wkamuwekea chini ya kibanda kimoja kilichokuwa karibu na ufukweni hapo na hapo Joseph alianza safari ya kuinuka na kufatiwa na mkewe ambaye alihisi ameshikwa mkono.



    Aligeuza macho yake na hapo alikutana na tabasamu mwanana la Salhat huku akiita.



    "Mama!!!.....





    Hiyo ilikuwa furaha Kubwa sana kwa Lillian baada ya kuitwa mama na Salhat.



    Alimshika Salhat ns kumkumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakimtoka na hiyo ilikuwa furaha kwa mumewe Joseph.



    ***** ****** ***



    Huku nako alionekana Johnny akiwa mwingi wa mawazo katika moja ya boti iliyokuwa ikielekea maeneo ya pwani huku akili yake yote ikiwaza Siku ile ambayo iliyabadilisha maisha yake yote na ndyo Siku ambayo aliweza kuwapoteza wale wote alioweza kuwapenda kutoka moyoni mwake.



    Mtu yule aliyeweza kumsaidia aliitwa Cojack muda wote alikuwa karibu naye huku akimfariji zaidi.



    "Unajua Mr matata alisema ya kuwa wewe ni furaha ya mjukuu wake Salhat hivyo hupaswi kuteseka ndo maana nilikusaidia kukutoa katika eneo lile lakini kutokana na kuwa wauwaji wote unawafahamu huna haja ya kuacha kulipiza kisasi juu yao ndomaana nimekusaidia nami nitasaidiana nawe katika kuwaangamizi wale majini wote"



    Johnny alitabasamu kisha akasema.



    "Sitohitaji msaada wowote tena wala kutoka kwa mtu yoyote yule nitajisaidia mwenyewe na kisasi changu nitakilipa mwenyewe na kwanzia leo natangaza vita Kubwa dhidi yao" aliongea huku akitetemeka kwa hasira alichukua kitabu chake na kuanza kufunua kurasa moja baada ya nyingine na humo ndani kote aliweza kuzichora picha za majini wote ambao walipelekea vifo vile alifunua kwa utaratibu kabisa na kwa kukremisha zaidi picha zile kichwani kwake.



    ***** ****** ****



    Salhat akiwa pembezoni mwa ufukweni huku akitizama alifanikiwa kuiona boti kwa mbali na boti hiyo ndipo alipokuwepo Johnny.



    Alijikuta akiendelea kuitizama boti ile huku akivutiwa na kijana yule ambaye alionekana akiwa anakuja katika ufukwe ule. Ghafla alisikia akiitwa Salhat.



    Basi alianza kukimbia na kuelekea sehemu ambayo jina lake lilitajwa. Kila alipokuwa akipiga hatua moja ndivyo ulivyoweza kuongezeka mwaka mmoja katika maisha yake.



    Hatimaye uliweza kuonekana mguu wa msichana ambaye sasa tayari umri wake ulikuwa umeenda, aliinama na kuokota kava la konokono kisha kulipuuliza kwa kuutoa mchanga ulioko ndani hatimaye sura yake iliweza kuonekana alikuwa msichana mwenye tabasamu nzuri sana na mwenye kupendeza machoni pa watu wengi.



    "Salhat!!! Mara ngapi nakwambia sipendi ukakae huko ufukweni watoto wenzko wa kike hukaa na mama zao nyumbni lakini wewe unamfuata tu baba yako" alizungumza Lillian ambaye kwa sasa umri umeenda.



    "Mama tayri nimeshafanya kazi zangu zote na sasa Si ndyo nikaenda ufukweni kwaajili ya kumsubiria baba kwani ameenda kuvuwa na wavuvi wengine" alijielezea Salhat.



    "Salhat sipendi kabisa tbia yako hiyo ya kumfuata fuata baba yako kila mahali ilihalli wewe ni mtoto wa kike, unastahiki kukaa nyumbani sasa na kutafuta mwanaume wa kukuchumbia" alizungumza Lillian.



    "Mama mimi siwezi kuolewa kisha nikakuacha wewe pamoja na baba mimi nimewazoea sana wewe siwezi kabisa kufanya hivyo, tutabaki wote hapahapa"



    "Hata mm nilipokuwa na umri wako nilisema hivyo hivyo lakini baadaye nilipokutana na baba yako nilisahau yote hayo.......nakuombea kwa Mungu ukapate mwanaume ambaye ataweza kuendana na akili zako kwamaana wewe umekaa kama mtoto" alizungumzia Lillian na kuanza safari ya kurejea nyumbani akiwa na mwanaye.



    "Mama yani wewe mimi kwanza nataka mwanaume ambaye atanizidi urefu kiasi......nywele ziwe nyeusi alafu zenye mawimbiwimbi flani hivi kichwani......mikono yake iwe imejazi japo kwa kiasi........

    Wakati akiwa anazungumzia maneno hayo alionekana kijana mmoja akiwa anashuka katika boti yake huku akiwa amebeba begi lake dogo tu na akiwa kifua wazi akiwa anaelekea upande ule alioko Salhat na mama yake Lillian.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Awe amekata kifuani hivi kama baba alafu macho yake yawe meusi mdomo wake uwe mpana kidogo pua yake ya kuchongeka............ Na napenda zaidi awe mtu ambaye yuko simple tu na pale anapokosea basi aweze kusema sorry". Akiwa anayazungumza maneno Yale kwa hisia nzito sana huku akigeuka nyuma alishtuka baada ya kupamia kifua cha mtu na kujikuta amemshika kifuani alipandisha macho yake juu na hapo hapo yaligongana na mwanamme ambaye alikuwa akizielezea sifa zake wakati Huo Huo.



    Mwanaume Huyo alimtizama bila kusema lolote kisha akamshika bega na kumsogeza pembeni huku akiendelea na safari zke.



    Salhat alibaki akiitizama sehemu ambayo alishikwa bega na mtu yule huku akiipapasa na kutabasamu huku akimtizama mtu yule kwa kufunga na kufumbua macho yake.

    Ghfla alipigwa kibao na mama yake.



    "Hivi huoni hata Aibu mimi nimo hapa na unamtizama mwanaume namna hiyo???.



    "Nani??? namtizama wapi??? Namshangaa anavyoshika shika watoto wa kike bila hata kuwa na Aibu!! Alizungumza na kuanza kuondoka baada ya kuhisi amepotezea kisha akaendelea kucheka na kutabasamu mbele ya safari yake.



    Siku iliyofuata alifika tena ufukweni na safari Hii alikuwa akitizama kulia na kushoto kama vile kuna mtu alikuwa akisubiria kumuona huku akitizama saa yake.



    "Unamsubiria nani????!!! Aliuliza Joseph.



    "Baba!!!!! Alishtuka kisha akampokea mzigo mdogo aliokuwa ameubeba.



    "Kuna mtu umeweka miadi naye??



    "Hapna ntaweka miadi na nani mimi nilikuwa nawasubiri wakina Sarah kama wangeweza kutkea nicheze nao lakini bado hawajaja!! Alizngumza.



    "Ila unajua Salhat umri ulionao wewe siyo wa kucheza tena mwanangu inabidi ujiweke kama msichana na mtu mzima sasa ambaye utasthili kuanza maisha Siku chache za mbeleni" alizungumza Joseph.



    "Nimeshasema mmi siolewi na mtu yoyote siwezi kukuacha wewe na mama wenyewe mimi nikaenda kukaa na mtu mwingne" alizungumza na kumshika baba yake mkono kama alivyoweza kutambua yeye na kuanza kuondoka naye katika eneo lile huku akiendelea kutizama nyuma kama angebahatika tena kumuona kijana yule ambaye alimvutia machoni pake.



    ***** *******



    Katika upande mwingine alionekana Grace na yeye akiwa na marafiki zake wawili wa kike wakiwa wanakuja na boti yao ndogo katika eneo lile kwajili ya kujivinjari tu.



    Walishuka katika boti yao hiyo na kuelekea kwenye hotel moja ambayo ilikuwa maarufu sana eneo lile. Walipishana na Grace na Salhat bila hata mmoja kumtambua mwenzke ila Salhat alipofika mbele kidogo alipata hisia ambazo zilimfanya ageuke nyuma na kumtizama Grace hapo macho yao yalikutana na kila mmoja alimtizama mwenzke na asijue kwanini amemtizama mwenzke ila hawakutilia maanani na kila mmoja aliendelea na safari zake.



    Grace alipofika hotelini tayari alikuta chumba ambacho alikiwekea order kikiwa na mtu. Sasa alianza kufoka kama siyo kumgombeza mtu ambaye alihusika na shughuli zile.



    "Nataka Huyo mtu aliyekodisha chumba hicho ahamishwe mimi siwezi kulala chumba kingine tofauti na hicho na wote mnatambua kuwa hicho chumba ni chakwangu



    "Lakini madam Grace hatuwezi kufanya hivyo kwani chumba kile tayari kimeshalipiwa tena kwa mwezi mzima"



    "Unaamaana gani unaposema huwezi muite manager wako maana sitaki kuzungumza na wewe" aliongea Grace na wakti Huo Huo manager alifika eneo lile.



    Kisha akamtaka radhi Grace na kumwomba achukue chumba cha pembeni yake kwani hakina tofauti kubwa sana na kile ambacho tayari kimechukuliwa.



    "Huyo ambaye yuko kwenye hicho chumba ndiyo ahame kwanini msifanye hivyo mimi nitaongezea pesa mara dufu"



    Wakiwa katika mzozano wa hap na pale aliyeweza kukodisha hicho chumba alikuwa akija na chombo chake ambacho huteleza nacho baharini . Aliwapita watu wote bila kuwasemesha na hapo alisikia jina lake likitajwa..



    "Proffesor J

    ohnny" aliita manager wa hoteli ile namfanya mtu yule ageuke na kumtizama.



    "Samahani nilikuwa nauliza kama kuna uwezekano..........."



    "Hapana hakuna uwezekano aliijibu short and clear kisha akapandaa juu.



    "Manager aliita Grace kwa sauti ya upole.



    "Ndyo madam Grace"



    "Umesema kuna chumba pembeni tu ya anapokaa professor???



    "Ndyo madam"



    "Nakitaka hicho chumba"



    Alizungumza huku akingata mdomo wake kimahaba zaidi.



    Wakti Huo nao Johnny alipanda mpka juu ya kile chumba anachoishi kisha akafungua dirisha kutizama kinachoendelea chini.



    "Grace lazima uingie kwenye mtego wangu alizungumza namna hiyo na akafunga dirisha lake ila alishtka baada ya kuhisi kaona kitu ambacho kimemshangaza kidgo alifungua tena dirisha lake na safari Hii macho yake aliweza kuyapeleka kwenye kibanda kidogo kilichokuwa hakipo mbali na ufukweni pale.



    baada ya Johnny kuona kitu ambacho kiliweza kumshangaza.



    Alichukua darubini yake na kutazama kwa karibu zaidi hap alikuwa Salhat akichezea mchnga kwa kutengeneza nyumba na wa toto wadogo wenye miaka 12 mpka 14.



    Alicheka tu na kuamua kuendelea na shughul zake nyingine huku akijisemea kimoyomoyo.



    "Sasa likubwa kiumbo lakini linacheza na watoto"



    Akiwa anatoka katika chumba chake kwaajili ya kuelekea kwenye bahari ili aendelee kuteleza zake alisikia akiitwa jina lake.



    "Proffers Johnny"!!! Ilikuwa Sauti ya mtoto wa kike na Huyo alikuwa ni Grace na yeye aliweza kuvalia mavazi ya kuelekea baharini huku akishika kile alichoshika Johnny kwaajili ya kuteleza baharini.



    Johnny alimtizama kwanzia juu mpaka chini bila kusema neno lolote lile.



    "Naona unaelekea baharini kwahiyo siyo vibaya kama tutaenda wote" alizungumza na kupitisha mkono wake katika mkono wa Johnny.

    Johnny Aliutoa mkono wa Grace kisha akaendelea mbele na safari zake.

    Wakati hayo yakiendelea rafiki zake Grace nawao walikuwa nyuma wakishuhudia tukio hilo na kukikuta wakicheka kwa siri Hili Grace asitambue na wao waliweza kuvalia mavazi Yale ikiwa ni amri ya Grace. Grace aliwatizama na wote walikaa kimya kisha wakaendelea na safari ya kumfuata Grace aliyekuwa akimfuata Johnny.



    ***** ****** ****



    Katika koo ya Abandandi ilikuwa koo yenye nguvu kuliko koo zote zile za kijini ni hiyo ni baada ya kuipiga na kuichukua koo ya Sultan iliyokuwa na nguvu kuliko koo zote na baada ya kufanya hivy basi wakachukua pia na koo nyingine za kijini na kuzimiliki wao huku Samir na Sadicky wakiwa katika kifungo kikali cha kijini kwani wao walikuwa wabishi na wakaidi kuliko majini wote pale.



    Malikia wa Abandandi aliweza kuwaongoza atakavyo yeye huku akimwaga damu nyingi za binadamu pamoja na majini wasiokuwa na hatia huku akiiona ni fahari sana na hatimaye alipata wazo sasa la kuweza pia kuiweka dunia chini yake kwani hakuna tena atakayeweza kumtishia kwa chochote kile.



    ****** *********



    Huko nako jijini Arusha maisha ya Badra yalikuwa maisha ya kawaida tu huku akiwa amejimilikisha nyumba Kubwa ya Mr matata baada ya kufariki na akiyafurahia maisha ya duniani zaidi kuliko ya kijini.

    Kila alichokuwa akitaka aliweza kukipata kwa muda muhafaka ambao angeutaka yeye na hiyo ilikuwa kero Kubwa sana kwa Ashura aliyekuwa akiishi ndani ya nyumba ile kwani alimchukia sana Badra na akiamini lazima analolote atakalokuwa amefanya juu ya kifo cha Mr matata, kwani Badra alihitaji Mali kuliko kitu chochote kile.



    ****** *********



    Ulikuwa ni usiku wenye mbalamwezi mkubwa sana ambao uliweza kumuulika dunia kwa kiasi kikubwa sana.

    Alionekana Salhat akiwa amekaa pembezoni kabisa mwa bahari huku akiwa anafikiri mambo ambayo alikuwa akiyajua na kuyafahamu mwenyewe sura yake ilibadilika kabisa kutoka katika sura yake ya kawaida na kuwa sura ambayo watu ambao walikuwa wakimfahamu wangeweza kustaajabu kwani hawakuweza kuionaga taswira hiyo usoni mwa Salhat.



    Akiwa eneo lile alipita Grace na marafiki zake wawili. Huku wakiwa wanapiga story ghafla alishtuka baada ya kukutana uso kwa uso na sura ya Salhat iliyoonekana haihitaji masihara hata kidogo.



    "We masikini kwanini umenitisha mimi namna Hii?? Aliuliza Grace huku akimtizama Salhat.



    "Unaniita mimi masikini......unanifahamu mimi ni nani wewe binti....... Unataka kufa sindiyo..... Alizungumza na kuendelea kumsogelea Grace ambaye alikuwa akirudi nyuma na marafiki zake kwa kuogopa.



    Salhat alichomoa kisu na kumuonyeshea Grace kisha akamchoma cha tumbo.



    Zilisikika kelele zilizofanya wale wote walioweza kujenga pembezoni mwa ufukweni waamke.



    Grace alijishika tumboni na kushngaa hamna damu.



    Salhat alikipandisha kisu chake juu kumbe kilikuwa cha kuingiza na kutoa. Aliangua kicheko kwa kumtizama Grace kisha kupashana mikono na mashoga zake wa kitoto kwa kusema ya kuwa yeye ni shida upande wa uigizaji.



    Watu walioweza kuamka tayari walishafika eneo lile na baada tu ya kumuona Salhat na Sarah walitambua tu lazima kuna kitu wamefanya.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Grace alimfuata Salhat aliyekuwa akicheka kwa kumcheka yeye na kumpiga kibao kimoja cha nguvu kilichofanya kicheko kile kiwe kikomo na kubaki hali ya mshangao.

    Wakati hayo yakiendelea Lillian alishafika eneo lile na kushuhudia Salhat akipigwa kibao.



    Katika kitu ambacho Lillian hataki mzaha nacho ni mtu kumliza Salhat au kumfanya Salhat aumie.



    Grace aliinua tena mkoni wake na kumpiga Salhat ambaye tripu hii alidondoka mpka chini kisha wakaanza kumchangia kwa mangumi na mateke hapo hapo aliingia Lillian na kumsukuma Grace ambaye alidondokea upande mwingine kabisa kisha akamtizama mwanaye Salhat ambaye alishaanza kuvimbia damu kwenye mwili wake kutokana na weupe alionao.



    Grace alisimama kwa hasira na kutaka kwenda kumpiga Lillian lakini alizuiliwa na Joseph ambaye alishafika eneo lile.



    "Mnawezaje kumpiga mtu mmoja nyie wote?? Aliuliza kwa kuwatizama.



    "Huyo ndiye aliyeanzaa upumbavu wake wa kunitishia mimi kunichoma kisu"



    "Hata kama kwani adhabu pekee uliyoona inafaa ni kumpiga anawazazi huyu ungekuja na utushtakie sisi tungechagua adhabu ya kumpa lakini siyo kumchangia watu watatu kwa Mara moja" aliongezea Joseph.



    "Nyie hamnitambui sasa nitawaonyesha madam Grace ni nani??? Alizungumza Grace kisha kuelekea hotelini ambako alikuwa amepanga.



    Nyumbani nako Mr Joseph alikuwa akimtizama Salhat ambaye alishindwa kummaliza na kujikuta anasunya tu.



    "Yani na wewe ndiyo unamuendelekea Lillian.....ungemuacha alale na hayo madonda alafu ungeona kama kesho angefanya Huo mchezo wake wa ajabu tena"



    "Muache yeye bado ni mtoto na kwanza alikuwa mwenyewe wale walikuwa watatu.... Hata kama amekosea hawakupaswa kumchangia wote watatu embu ona walivyomvimbisha" alizungumza Lillian aliyekuwa akimkanda na maji ya moto Salhat huku akimpuliza taratibu kabisa.



    ****** ********



    Kulikucha asubuhi na Jay aliamka katika chumba chake na kujikuta akishangaa chumba chake jinsi kilivyo kwani kilimwagia maganda ya mayai na mauchafu uchafu mengi sana ambayo alishindwa kuelewa yametoka wapi ndani kwake alichukua simu yake na kupigia wahudumu waje ndani kwake.



    Wakati Huo ilionekana mikoni miwili ikiwa inapasha kwa kujipongeza kwa kazi nzuri waliyokuwa wameifanya alikuwa ni Salhat na Sarah. Huku wakiwa wameshika ndoo matakataka waliyotoka kumwaga katka chumba cha Jay wakiamini ni chumba cha Grace na watamkomesha zaidi na zaidi.



    Na hiyo ndiyo ikawa tabia yao ya kila Siku basi Siku moja Jay akiwa anatizama na darubini yake akiwa katika chumba chake alifanikiwa kumuona Salhat akiwa anachota matakataka kutoka kwenye pipa la takataka na kuwekea katika ndoo ndogo akishirikiana na Sarah na baada ya hapo wakawa wanakuja uelekeo wa hotelini.



    'Mpuuuzi hivi ni huyu binti mkubwa ndiye anayeweza kuletafa uchafu kwenye chumba chngu sasa leo nitamkamata.



    Baada ya kufika usiku Salhat aliweka ngazi na kushikiwa na Sarah kisha akapanda na kuona kila Siku kumwagia dirishani haifai wacha akamwagie kabisa ndani ......basi akaingilia chumba kile kupitia dirishani. Na baada ya kuingia Johnny alitazama chini na kumuona Sarah ambaye baada ya kuona ameonekana alikimbia.



    "Sarah!!! Leta tochi Hili nisije kuparamia vitu vya watu huku ndani" aliongea Salhat.



    Johnny Alitoa tochi na kumpa.

    Alianza kumwaga kwa kusambaza pale sebleni huku akishangilia kabisa bila kujua ya kuwa ameonekana.



    "Sarah!!!!!!!.........natamani tungekuja na ndoo nyingine zikawa tatu kisha tukamwagia na chumbani anakolala....au wewe unasemaje twende tukachukue ndoo nyingne"



    "Itakuwa vizuri kama mtalisogeza na lile pipa kwa hapa ili msipate shida ya kwenda kuhamisha matakataka kule na kuleta hapa" ilizungumza Sauti ya Johnny na kumfanya Salhat ashtuke hapo hapo Johnny aliwasha taa na waligongana macho kwa macho.





    baada ya Jay kuwasha taa na kuonana uso kwa uso na Salhat.



    "Uuwwwhhh anataka kunibaka!! Alizungumza Salhat.



    "Nini!!!!! Aliirudia Johnny sentensi ile kwa mshangao na kumtazama Salhat ambaye hakuweza kushikika zaidi ya kupiga kelele alimwambia nyamaza lakini Salhat aliendelea kupiga kelele.

    Johnny alimrukia Salhat na kumshika kiuno kisha kumvutia karibu na mwili wake alafu akamfumba mdomo wake na kumwambia "nyamaza"



    Salhat alijikuta akishindwa tena kuzungumza kutokana na alikoshikwa na Jay. Alibaki akiw kimya na kumeza mafundo machache ya mate tu yaliyokuwa magumu kupita katika koo lake. Hapo hapo mlango wa chumba cha Jay uligongwa na wahudumu baada ya kelele za Salhat kusikika.

    Jay alimgeuza Salhat na kum bananisha ukutani huku akiwa amemshika mabega yote mawili na kumwambia.



    "Ole wako upige kelele au useme chochote tulia"



    Hapo hapo wahudumu waliingia.



    "Niwasaidie nini??? Alizungumza akiwa amemficha Salhat katika kordo moja mwenyewe.



    "Tumesikia kelele za nabakwa ndo maana tukaona tuje katika chumba hichi" Alitoa maelezo hayo mhudumu mmoja kati ya wale waliokuja kugonga mlango akiwa na baunsa mmoja.



    Wakati Huo Salhat alianza kunyata na kutaka kutoka taratibu lakini Jay alipitisha mkono wake kwenye tumbo la Salhat na kumgandamiza ukutani.



    Salhat alijikuta akipata kama siyo shida ambayo hakuwahi kuipata tangu azaliwe kwani Jay aliweza kulikamata tumbo lake dogo sawasawa kabisa na kufanya mkono wake uenee katika kitovu chake kidogo kilichoweza kuzama ndani ya tumbo lake.



    Baada ya muda wahudumu waliondoka kwa kuwa Jay aliwataka waondoke na waache kusema wamesikia Kelele za mtu aliyekuwa akisema anabakwa katika chumba chake.



    "Tuje tufanye usafi???? Alizungumza muhudumu baada ya kuona chumba cha Jay kimechafuliwa tena kwa Mara nyingine.



    "Hapana kwasasa nalala sitaki kelele mpka kesho asubuhi na Tafadhali naomba muende" alizungumza Jay.



    Wahudumu wale wawili walimtaka radhi Jay na kuondoka wakiwa na Muhudumu.



    "Lakini nimeisikia kama Sauti ya Salhat!! Alizungumza muhudumu yule kwa kumsemesha mwenzke.



    Jay alimtizama Salhat ambaye mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi na kufanya kifua chake kipande juu na kushuka kwa uwoga alioupata baada ya kushikwa.



    Jay alimtizama na kugundua alipomshika Salhat ndipo panapomfanya aheme namna hiyo.



    Alitabasamu kisha akalikamata tena vizuri tumbo la Salhat ambaye Alitoa mlio ulioweza kumshangaza hata Jay na kujikuta akimtizama sana machoni kwa sekunde kadhaa.



    Baada ya Jay kurejea katika hali yake Alitoa mkono wake katika tumbo la Salhat na kuanza kuukung.uta kung.uta kama vile alikuwa ameshika kitu kichafu.



    Salhat alibaki pale bado mapigo yake ya moyo yakiwa hayajarejea katika hali yake ya kawaida kabisa.



    "Ukimaliza uondoke!!! Alizungumza Jay kwa kigugumizi na kupanda ngazi harakaharaka kisha kurudi juu katika chumba chake cha kulalia.



    Alpofika alisogeza pazia lake kidogo na kumtazama Salhat ambaye bado alikuwa pale pale alipomuacha.

    Salhat aliinua mkono wake mmoja kushika tumbo lake ambalo lilikuwa limeshikwa na Jay.

    Alijipapasa hadi kitovuni kwake na wakati akifanya hivyo Jay aliutizama mkono uliomshika Salhat na kuuangalia tena na tena kisha kuurudisha chini huku akitabasamu.

    Hata yeye alijishtukia baada ya kujikuta anatabasamu.

    Kisha akajiuliza Jay htimaye leo umefanikiwa kucheka baada ya miaka 13 kupita. Aliporudi katika fahamu zake wala hakumuona tena Salhat ndani ya chumba chake Bali mlango tu ukiwa wazi hivyo kumaanisha alipita mlangoni.



    Alitoka ndani ya chumba chake na kukimbia harkaharaka kwaajili ya kumtizama.



    Salhat akiwa amelishika tumbo lake huku akiendlea kutembea kama mtu aliyepigwa bumbuwazi aliweza kuonekana na Grace ambaye alikuwa bado hajalala Bali alikuwa akijiandaa na kutaka kwenda katika chumba cha Jay.



    Akitizama alipotoka Salhat ni katika chumba cha Proffesor Jay.



    "Mbona ametoka katika chumba cha Jay wangu na kwanini anajishika tumboni kwake???? Alijiuliza Grace ila kabla hajajijibu alisikia harakati za viatu vingine vikitoka katika chumba cha Jay alijificha Hili aone ni nani Huyo.



    Alikuwa ni Jay alyekuwa akivaa vizuri nguo yake ya kulalia na kuufunga mkanda wake vizuri huku akimfuata Salhat kwa nyuma.



    "Kwanini????? Hapna haiwezekani???? Wanawezaje wakawa wamelala!!!! Hapan Professor Johnny ni wangu tena ni wangu pekee yangu Huyo masikini imekuwaje akatoka katika chumba cha mpenzi wangu???? Alijiuliza sana Grace na hapo Sauti na nabakwa alizosikia baadaa ya dakika7 kupita zilianza kujirudia.



    "Hapna.......hapana......haiwezani hata kidogo" alizungumza na kuamua kuunga msafara kwa kumfuata Johnny nyuma.



    Salhat akiendlea kupiga hatua zake za kinyonge kwa kwenda mbele wahudumu walishangaa Salhat ametoka wapi?.



    Mhudumu mmoja alitaka kwenda kumsemesha lakini Jay alimpa ishara ya amuache wala asimguse kisha akaacha ufunguo wa chumba chak Kaunta kwa kuwataka wakafanye usafi huku akisema



    "Huyu anaota huku anatembea kwahiyo mkimsemesha tu anakufa" aliwadanganya kinamna Hiyo na kuendelea kumfuata taratibu kabisa Salhat bila kujua ya kuwa hata yeye nyuma alikuwa akifuatiliwa na Grace.



    Akiendelea kumsindikiza Salhat kwa kumfuata nyuma alihisi kuna mtu nyuma yake hapo aligeuka na kumuona Grace ambaye alikuwa akitizama chini kwa muda Huo hivyo hakujua ya kuwa Jay alimuona.



    Baada ya Jay kugundua Grace yuko nyuma alitembea haraka haraka na kwenda kumbeba Salhat, huku akimwambia anatembea taratibu sana na yeye anataka kurudi katika chumba chake akalale.



    Nguo aliyoweza kuivaa Salhat ya juu ilikuwa nyepesi sana hivyo nguo yake ya ndani iliweza kuonekana "sidiria" wakati anabebwa Nguo hiyo ilijivuta juu kidogo na kufanya mkono wa Jay ushike kiuno cha Salhat na kuyakamata vyema mapaja yake.



    Lillian hakuweza kulala kabisa kwani hakumuona mwanaye ndani. Hatimaye aliweza kuona mtu akiwa amebebwa kwa mbali huku wakielekea eneo lile alilokuwapo.



    Baada ya kusogea karibu alimuona Salhat.

    Alimkimbilia na Jay alimshusha chini Salhat.



    "We mpuuzi ulikuwa wapi??? Alizungumza huku akimpiga kibao kilichomfanya Salhat azinduke katika mawazo aliyoweza kuwa nayo.



    "Mama!! Aliita Salhat.



    "Mpuuzi wewe unaona unawaletea watu shida......ya kukubeba na kukuleta mpka nyumbani Mara ngapi nakwambia sitaki ukakae ufukweni mwenyewe.......... Ahsanteh Sana'a kijana wangu Mungu akubariki"



    "Lakini mama hakuwa........... Kabla hajamalizia sentensi yake Salhat alimuwahi na kumbana mdomo huku akimkumbatia kama rafiki yake na kumwambia mama yake.



    "Huyu ni rafiki mwema sana amenisaidia sana kunitoa ufukweni hadi hapa nyumban......na sasa hivi anataka kuondoka alizungumza Salhat akimgeuza Johnny na kuanza kumsukuma kwa kumshika kiuno chake.



    "Kwaheri rafiki na ahsanteh sana...." Alizungumza huku akimfanya Jay aende mbali kabisa na nyumbani kwao.



    "Mpuuuzi huyu yani baada ya kumsaidia kote ananifukuza mimi.......ngoja nitamkomesha" aliongea Jay huku akipiga hatua za harakaharaka na kuelekea kwenye hotel yake kwaajili ya kujipumzisha.



    Huku nako Salhat alishikwa sikio na mama yake na kuanza kupigwa vibao.



    "Mshenzi we unafikiri unaweza kunidanganya mimi Huyo mpumbavu mwenzako Sarah ameniambia kila kitu kwanini unaleta shida hivi wewe???!!! Alizungumza Lillian.



    ******** **********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Palikucha Asubuhi na mapema Salhat aliweza kuamka mapema kama kawaida yake ila Asubuhi ya Siku hiyo ilikuwa ya tofauti kidogo na asubuhi zote.



    Aliamka na kukitazama kioo kikubwa kilichopo chumbani mwake ghafla alihisi kuna mkono umeshika tumbo lake.



    Alipiga kelele lakini alishtuka baada ya kugundua kuwa nimawazo yake tu alijipiga kichwa akatoka njee ya chumba chake ambako nguo yake ilipeperushwa na upepo kidogo na kufanya tumbo lake liwe wazi na kupigwa na upepo kidogo hap hapo alihisi kama ameshikwa tena tumboni kwake.



    Aliishusha nguo yake na kuendelea kutembea ila kila apigapo hatua bado alihisi anashikwa tena tumboni mwake hivyo akabaki akisema.



    "Usinishike tena tumbo langu we mkaka" alikuwa akijisemesha mwenyewe kwani hakukuwa na mtu tena pale.



    Wakati akifanya hayo aliweza kuonekana kupitia kwenye darubini aliyokuwa akiitazama Jay.



    Alibaki akicheka tu huku akitingisha kichwa chake alihisi kunamtu nyuma yake hivyo aligeuka na hapo alikutana macho kwa macho na Grace aliyekuwa amevalia tu night dress iliyoweza kuonyesha kila alichokivaa ndani. Grace alimuelekea moja kwa moja na kuanza kumpiga mabusu Jay alijitahidi kuzuia ila hali ilipomnogelea aliweza kudondosha ile darubini chini kisha akaanza kusaidiana na Grace katika kubadilishana ndimi zao.



    Wakati hayo yakiendelea alionekana Salhat akiwa njee ya geti lile huku akisema.



    "Lazima nimwambie mimi sipendi tabia yake kabisa ya kunifuata fuata kila saa" alizungumza huku akiingia ndani ya geti na kuendela kupanda ngazi kidgo.



    Huku nako mnogo uliendelea baina ya Jay na Grace na kufikia hatua ya Grace kutokuwa tena na night dress Bali nguo zake za ndani tu

    Wakati Huo nao Salhat wala hakubisha hodi Bali alifungua mlango moja kwa moja na hapo alistaajabu kwa alichoweza kukiona mbele ya macho yake......



    baada ya Grace kula kiapo cha kumuonyesha Salhat kwamba yeye ni nani.



    Usiku uliingia na Grace alikuwa pamoja na Jay wakizungumza kuhusu kuonana na mama yake.





    "Johnny, twende basi ukalale naona usiku umeingia" alizungumza Grace



    "Na wewe Je??? Aliuliza Johnny.



    "Me kuna mahali naenda Mara moja mama kaniagiza" alizungumza Grace na kumuacha Jay akielekea ndani.



    Baada ya Jay kuelekea ndani Grace alipiga simu kisha akasema



    "Kazi ianze" baada ya hapo alikata simu na kusema.



    "Unazubutu kushare na mimi mwanaume nimpendaye masikini kama wewe utanitambua sasa"



    ****** ******* ****



    Salhat akiwa katika pita pita zake za kwenda kumkopea baba yake usiku ghafla waliingia kundi la vijana watatu wakamkamata na kumvutisha Madawa ya usingizi hivyo kumfanya alale walimburuza kisha wakampeleka kwenye kijumba ambacho walimlaza kitandani na kuanza kumpiga picha kisha kumrarua nguo yake ya juu na kuendelea kumpiga picha baada ya kumaliza kumpiga picha walituma picha kwenye simu ya Jay na kumuelekeza mahali walipo.



    Jay alitoka mbio mbio na aligongana na Grace.



    "Unaelekea wapi Jay?? Aliuliza Grace



    "Na....na.....naelekea sehemu moja tu nimepigiwa simu na....watu wa kampuni hivy naenda" aliongea Jay na kuondoka zake.



    Grace alicheka tu na kuitizama simu yake ambayo picha ilikuwa ya Salhat akiwa na brazia pekee yake.



    "Ndo unaelekea huko siyo sasa tuone....... Alichukua simu akapiga kisha akasema.



    "Mbakeni hakikisheni hamu yenu inaishaa kabisa" alizungumza na kukata simu huku akizidi kucheka sana.



    ***** ****** *****



    "Bosi kasema tumbake" alizungumza na kuanza kuutazama mwili wa Salhat na kisha kuanza kuuchekea.



    "Alafu nasikiaga huyu binti ni bikra!! Aliongea mmoja na kuwatizama wenzake.



    "Ni kweli ni bikra na kwakuwa mimi ni bossi wenu basi nitaanza mimi" alizungumza mmoja wao na kuteremsha suruali yake.



    "Ohoooio kwahiyo mnafikiria tu kutoa bikra za wanawake ambao siyo wa kwenu...alafu wa kwenu awatoe nani??? Aliuliza Edrick aliyekuwa hapo pembeni akipuliza kisu chake na kulitazama Apple lake.



    Watu wale walishtuka na kumtizama Edrick aliyewatizama na kisha kutabasamu.



    "We....we....we ni nani????? Aliuliza mmoja kati ya wale baada ya kumuona Edrick.



    "Unataka kunifahamu mimi ni nani???! Mimi ni huyo mnayetaka kumbaka!!! Kwasababu damu aliyonayo yeye ndiyo damu niliyonayo mimi!!! Alizungumza Edrick na ghafla macho yake yalibadilika rangi watu wale walidondoka hapo hapo chini na kupotea katika mazingara ghafla alihisi kama kuna mtu anakuja maeneo Yale.

    Alijibadilisha na kuwa katika umbo la kawaida kabisa Jay alifungua mlango wa kile kibanda haraka sana. Alimkuta Salhat akiwa amelala kitandani.



    "We mwanamke ......we mwanamke....alijaribu kumuita huku akitaka kulikumbuka jina lake.



    Hapo hapo ndipo alipokumbuka jina la Salhat aliloitwa na Edrick.



    "Salhat" aliita jina lile na hapo aliweza kumkumbuka Salhat.



    Sauti ile ya Jay iliweza kupenya hadi kwenye ngome za Salhat na kumfanya jina la Salhat kujirudia rudia kichwani mwake na kama hiyo sauti aliweza kuikumbuka.



    Alifunua macho yake taratibu kabisa na hapo alikutana na sura ya Jay walitizama kwa sekunde kadhaa bila hata mmoja kumsemesha mwenzke.

    Hatimaye Jay alimshika na kumuuliza.



    "Uko salama wewe!!! Wapi umeumia??? Eeee!!! Hawajakufanya chochote??? Aliuliza maswali hayo kwa mfululizo.



    Salhat alikishika kichwa chake kisha akaanza kukumbuka vile alivyodakwa alijitizama mwili wake na kumwambia Jay

    "Usinisogeled wewe kwanini umenileta hapa???? Aliuliza Jay.



    "Me sijakuleta hapa bali nilitumiwa msg ya picha zako na mtu kisha.........aliacha kuongea baada ya kugundua ya kuwa ndani ya simu yake hakuna ujumbe wowote ule wala picha yoyote ile hata zile nmba hamna...



    Hapo hapo aliingia Edrick na kumpiga ngumi Johnny.



    Unataka kumfanya nini Salhat!!! Alizngumza na kumfuata Salhat

    Kisha kumuuliza kama yuko salama.



    "Me sijamfanya chochote mimi pia nilitumiwa msg na kuambiwa ya kuwa yuko hapa ndo nikaja" alijielezea Johnny.



    "Umetumiw msg ziko wapi wakati wewe ndye uliyenitumia mm msg za picha za Salhat ulizompiga na kuniambia nikichelew tu utamuuwa kwa kuwa unataka nikupe millions 20 na ndicho kilichokuleta hapa" alizungumza Edrick.



    "Mimi sijafanya hivyo" alijitetea Johnny



    "Leta simu yako aliongea na kuichukua simu ya Jay kisha akafungua upande wa msg na kumuonyesha Salhat kisha akafungua upande wa gallery na kumuonyesha picha zilizoweza kupigwa kwenye camera.



    Salhat alimtizama kwa hasira Jay ambaye alichukua simu yake na akabaki anashangaaa..



    "Imekuwake hiii hapana mimi sijafanya chochote mbona kwanini imekuwa hivi" alianza kujiuliza Jay.



    Salhat alisimama na kumpiga kibao kisha akatoka njee huku Edrick akimfuata.



    Edrick alitabasamu tu kwani kwa uwezo alionao anaweza kufanya chochote kile akitakacho.



    "Salhat huruhusiwi kujenga mahusiano na mwanaume yoyote isipokuwa yule uliyeweza kupangiwa kwaajili yako kwani ukifanya hivyo utaleta madhara makubwa sana hapa duniani kwa kumpenda mtu ambaye hukupangiwa kuwa naye kwaajili ya kuweza kuurudisha ukoo wa Sultan pamoja na kuilinda dunia kwa kile kitakachoweza kutokea kwa miaka ya mbeleni..........ni vumulie kidogo mpaka pale nitakapoweza kumtafuta yule ambaye alizaliwa kwaajili yako na we kwaajili yake kwani ndicho kilichonileta katika dunia hii" aliongea Edrick moyoni.



    Jay alirudi akiwa mnyonge sana na Grace alimuona akajua kazi imekwisha.



    "Jay imekuwaje mbona umenyong.onyea kwa kiasi kikubwa namna hiyo eti???? Aliuliza Grace kwa kumuinjoy.



    Hamna alijibu Jay kifupi na kupanda ngazi zake kisha kuelekea ndani ya chumba chake na kufunga mlango huku akifikiria ni kipi kimetokea mbona kama miujiza ambay hakuitegemea alichukua simu yake na kuiwasha tena kisha kutazama wala hakukuwa na picha yoyote tena kwenye gallery yake alipofungua upande wa SMS alistaajabu baad ya kuiona ile msg aliyotumiwa.



    "Kuna mpuuzi anacheza na mimi sasa hanitambui mimi ni nani eeeee!!! Grace na wewe ni Jini kama mama yako ila umeamua kunichezea mimi mchezo sasa utaanza kulipa wewe kabla ya mama yako alizungumza kwa hasira na kuuuma meno yake.



    Unafikiri Jay amepanga kufanya nini juu ya Grace.





    Baada ya Jay kuzungumza maneno Yale makali ya kutaka kumkomesha Grace kwamba yeye ni nani!!!



    Jay alikuwa na begi ambalo alilifungua na ndani kulikuwa na chupa moja Kubwa iliyokuwa na iliyoonekana kama kuna vitu ndani, alitoa kikamba kidogo sana kisha akakinyunyuzia dawa kidogo baada ya hapo alitabasamu tu na kuitizama ile chupa.



    "Imefika miaka mitatu sasa mko ndani tu ya chupa na bado kwa kile mlichoweza kunkfanyia bado sijaridhika mtakaa hapo mpaka nimlete mwenzenu kisha niwauwe wote kwa pamoja kama mlivyoweza kuiteketeza familia yangu kwa Mara moja" alizidi kuzungumza na kuitizama ile kamba.



    Chumba cha Grace kiliweza kuangaliana sawa sawa na chumba cha Edrick aliweza kuitegesha kamba ile ndogo nyembamba kupitia kitasa cha Edrick na cha Grace kisha akapita kwa kuinamaa na kuondoka eneo lile.



    Grace akiwa anakuja mbio mbio kwaajili ya kuelekea chumbani kwake Jay alisimama katika kordo moja kwaajili ya kutizama matokeo ya kile alichoweza kukifanya. Grace alifika kisha akafungua mlango wake kwa kuigusa kle kmba ndogo ila kabla hajaufungua vizuri alikuja muhudumu na kumwambia ya kuwa kuna mtu kapiga simu kupitia simu ya hotel na anahitajika.



    Hivyo kamba ile haikuweza kukatika alirudishia mlango wake na kutoka zake wakati akiondoka nako Edrick alikuwa akzipanda ngazi kadhaa kwaajili ya kufika kordon na kuelekea kwenye chumba chake.



    "Inamaana Grace siyo Jini kama yeye siyo sasa ni nani aliyoweza kunifanyia mimi vituko kama hivyo alizungumza huku akimtizama Edrick ambaye alibakiza hatua chache tu kabla ya kufika kwenye chumba chake. Jay aligeuka taratibu kabisa na kuanza kuondoka eneo lile.

    Edrick alifika na kushika kitasa chake hapo hapo zilisikika kelele zilizoweza kumshtua Jay na kumfanya ageuke.



    Edrick alitoa simu yake iliyokuwa ikiiunguruma kwa mlio wa simba na kutabasamu Jay aligeuka na kuondoka zake.



    Edrick aliweza kuumia mkono wake wa kulia na ulikuwa ukitoa moshi kwani uliweza kuungua sana.



    Aliingia ndani ya chumba chake na kujibadilisha katika umbo lake la kijini kisha akapotea na kuelekea baharini ambako aliweza kuudumbuliza mkono wake kwenye maji ya bahari alipiga kelele sana ni kutokana na maumivu aliyoweza kuyapata baada ya kuishika kamba ile iliyoweza kupakwa dawa na Jay bila kutambua.



    **** ***** ****



    "Haloo mama!!!!! Alipokea Grace simu.



    "Ndyo nitakuja naye kesho sawa......mama......sawa.....tutawahi ila naomba usifanye chochote kitu mpaka pale tutakapoweza kufika tafadhali mama yang.........ndyo umeniahidi ya kuwa hutaondoka mpaka tuje .....sawa ahsanteh mama nakupendaa alikata simu na kutabasamu sana.



    "Johnny" hilo ndilo jina aliloweza kulitamka baada ya kumaliza kuzungumza na simu.



    Alikimbia na kupanda ngazi haraka haraka kwaajili ya kuelekea chumba cha Johnny.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***** *******



    Baada ya Edrick kutuliza kidonda chake alichoweza kukipata baada ya kushika ile kamba alichukua bandage na kuanza kujizungushia mkononi mwake huku akiyafikiria haya.



    "Nani huyo ambaye ameweza kutambua ya kuwa mimi ni Jini??? Na mpaka akaja akaniwekea mtego katika chumba changu ni Jini gani huyo!???? Alijiuliza lakini alicheka na kusema.



    "Hapana hawezi kuwa Jini hata kidogo.......Jini hawezi kuishika dawa ile....huyu ni binadamu tu....sasa ni mpuuzi gani huyoo!!! Alizungumza kwa hasira na kupiga meza ngumu hadi kupasuka huku macho yake yakibadilika rangi kuonyesha wazi kabisa ya kuwa amechukia kwa kiasi gani.



    **** ****** ****



    Salhat akiwa nyumbani kwao uku akiwa anafikiria mmbo ambayo alikuwa akidhani Jay ndy kamfanyia.



    "Kwanini alitaka kunibaka?? Inamaana kulala na Grace haikutosha mpaka atake tena kulala na mimi?? Kwanini mbona anaonekana ni mtu wa tofauti na vile alivyoweza kuvifanya".



    Ghafla alishituliwa na kuzinduliwa kwenye mawazo yake baada ya kushikwa begani.



    "Unawaza nini??? Lilikuwa ni swali lililoweza kutoka kwa mama yake Lillian.



    "Hamna" alijibu Salhat na kusogea ili kumuachia mama yake sehemu kwaajili ya kukaa.



    "Utanambiaje hauna ilihali mimi nakuona upo kwenye mawazo mazito namna hiyo..??? Aliuliza na kukaa



    "Hamna kweli aliendelea kusisitiza Salhat.



    Lillian alimshika mwanaye Salhat mkono na kumgeuza kisha kumtizama usoni.



    "Unamuwaza Johnny??? Aliuliza Lillian.



    Salhat alitizama chini bila kutoa jibu Mama yake alitabasamu na kumshika uso wake kisha kumuinua.



    "Unamuwazo Johnny sindiyo????



    Alitingisha kichwa.



    "Kafanyaje???? Aliuliza Lillian



    Salhat alimtizama mama yake na kuanza kumuelezea.



    **** **** *****



    Asubuhi kulikucha na Jay aliinua darubini yake kisha akataka kutizama nyumba ya akina Salhat. Alisita kidogo pale alipokumbuka kibao alichopigwa na Salhat. Alitizama mabegi yake kisha akatizama darubini yake...aliinua na kutizama kwa wakina Salhat alishtuka baada ya kuiona sura ya Salhat karibu na yeye alishtuka na hapo Salhat alimwambia.



    "Nishike mkono nisidondoke"



    Johnny alimpa mkono Salhat na kumvutia ndani.



    Baada ya kuingia ndani Johnny alienda akafunga mlango .



    "Salhat" aliita na kumkumbatia Salhat hali ile ilimfanya Salhat akodoe macho macho na baadaye akaachia tabasamu kisha akamkumbatia na yeye.



    Ghafla mlango uligongwa na wote walishtuka.



    "Johnny mume wangu fungua mlango" ilikuwa sauti ya Grace.



    Salhat alimtizama Johnny na Johnny alibaki akimtizama.



    Jay alibaki katika wakati mgumu kwasababu hakutaka Salhat aondoke lakini pia hakutaka Salhat aondoke.



    Salhat akimtizama tu na kuanza kuelekea dirishani kwaajili ya kurudi alipotoka ila Jay alimfuata na kumshika mkono.



    "Unaweza ukajificha hapahapa ndani kwa dakika kadhaaa bado hujanmbia kile kilichokuleta?? Aliongea Jay na kuanza kumvuta Salhat kisha akamuingiza chumbani kwake na kutoka kwenda kumfungulia mlango Grace.



    "Mbona umechukua muda mrefu hivyo kunifungulia mlango?? Aliuliza Grace.



    "Nilikuwa chumbani nikimaliza kujiandaa" alidanganya Jay.



    "Umeshamaliza kujiandaa???



    "Ndyo"



    "Sawa twende tutaondoka na meli yangu niliyoikodisha kwaajili ya kumuwahi mama" alizungumza Grace na kubeba begi dogo la Jay.



    "Ammhhh sawa" Jay alitizama juu na aliona mlango wake ukiwa umefunguliwa kidogo aliamini Salhat anayaona yote Yale ambayo yanaendelea pale chini.



    "Nafikiri nimesahau simu yangu chumbni ngoja niifuate" aliongea na kuanza kupanda vingazi kadhaa ila aligeuka baada ya kuitwa na Grace.



    "Johnny!! simu yako hii hapa" alizungumza na kumfanya Jay asimame pale pale.



    "Ahaaa kumbe iko hapo chini.....basi ngoja nikachukue notebook yangu" alijibu Jay na kujaribu kupanda ngazi nyingine.



    "Sifikiri kama ni adabu kwa mimi kubaki kusimama hapa wakati mume wangu anahitaji kutafuta kitu......ngoja nipande mimi nikakuletee notebook yako".



    Grace alianza kumfuata Jay.



    "Hapana wala haina shida twende tu tutachelewa" alizungumza Jay na kumshika Grace mkono ambye alimshika mikono yote miwili na kumgeuza.



    "Johnny najua ya kuwa huwezi kunipenda kwa Mara moja Bali nakuhakikishia nitakupa upendo ulio bora kuliko wanawake wote hapa duniani.....na"



    "Grace amini ya kuwa mimi nakupenda wewe na wewe tu siwezi kumpenda mwanamke mwingne tofauti na ww ndiyo maana sina nia yoyote mbya na wewe.. Nataka niendee kwenu nikajitambulishe" alizungumza Jay kwa sauti ya upole.



    "Hata mimi naamini ya kuwa unanipenda Mimi tu ila kuna wanawake wengine hawaelewi eti kwamba wewe unanipenda mimi na huwezi kumpenda msichana mwingne tofauti na mimi ndyo maana mimi sipendi kabisa nikiona msichana anakufuata fuata naweza hata kumuuwa mtu me sipendi kabisa" alizungumza Grace na kuanza kujiliza.

    Jay alimfuta machozi na kumtabasamia.



    "Waache wao wafikiri vile ambavyo wanafikiri"





    "Me naamini moyo wako ni wa tofauti na wanaume wengine ndiyo maana humsaidia kila ambaye anaingia kwenye matatizo basi mtu akiona hivyo anafikiri ya kuwa unampenda" aliendelea kujieezea Grace akiendelea kumfafanua zaidi Jay.



    Wakati wakizungumza haya yote Salhat aliweza kuyasikia machozi yalimtoka na kujiona ya kuwa yeye ni waajabu sana anawezaje kumpenda mtu kutokana na kwamba alimsaidia...kumbe alimsaidia kwa kuwa ni kanuni yake wala siyo kwamba anampenda na hilo alidhibitisha baada ya kusikia ya kuwa Johnny anaenda kujitambulisha kwa kina Grace.



    Wakati huo nao Johnny alikuwa akitizama mlangoni ambako alibakiza ngazi chache tu kufika kwenye chumba chake.



    "Johnny mume wangu naamini ya kuwa. Utakuwa mwaminifu kwangu"



    .

    "Usijali kuhusu hilo wewe twende" alimshika na kuanza kumvuta Grace chini.



    "Unataka nikuamini ya kuwa huwezi kuwa msaliti kwangu basi nibusu" alizungumza na Salhat alishtuka akiwa ndani kisha akayarudisha macho yake mlangoni.



    Jay alimtizama Grace na alijua kabisa ya kuwa Grace anafanya hivyo kwasababu anajua Salhat Yuko ndani.



    Jay alitabasamu na kutaka kumpiga busu la pajani lakini Grace alimlazimishia mdomo na kuanza kuromance naye.



    Jay akiwa katika hali ile huku Grace akiendelea kumromance Jay alifungua macho yake ambayo yalikutana ana kwa ana na sura ya Salhat iliyojaa huzuni.



    Jay alimtoa Grace na kumwambia nafikiri imetosha sasa tunaweza tukaenda.

    Jay alichukua begi lake na kufungua mlango kisha akatoka njee akiwa amemuacha Grace ambaye aligeuka nyuma design kama anamtizama Salhat kisha akatabasamu na kuondoka zake.



    Salhat alitoka chumbani akiwa amejaa machozi na kauli ambazo zilitamkwa na Grace zikiendelea kujirudia kichwani mwake.

    Alianza kutabasamu na kucheka hapo hapo kisha akamalizia kilio chenyewe.



    Jay alipofika kwenye meli alitupa begi lake na kuingia katika chumba kilichopo ndani ya ile meli alikishika kichwa chake na kuanza kukivuta vuta nywele zake huku akipiga meli ile kwa hasira sana................!!



    ******* ******* ***



    Hatimaye Siku ilienda wiki zikakatika na ukaanza kuelekea mwezi sasa Salhat aliendelea na maisha yake ya kila Siku huku akiiendeleza tabia yake ya kucheza na Sarah pamoja na kumsubiria baba yake usiku wa manane mawazo ya Jay yalishamtoka kabisa lakini alikuwa na hofu kuhusu Edrick kwani alipotea katika mazingira asiyoweza kuyaelewa ndani ya chumba chake.



    Ilikuwa usiku mmoja ambako alikuwa baharini akimsubiria baba yake ambaye alianza kutokeza kwa mbali na wavuvi wengine. Siku hiyo baba Yake alipita na mvuvi mwenzake mmoja.



    "Binti yako amekuwa kweli hata kijana wangu amekuwa unaonaje tukianza kuunganisha undugu" alizungumza mzee yule.



    "Binti yangu huyu matatizo yake nayaelewa mimi na mama yake hivyo sitopenda kuwapa familia ngingne mizigo mizito huyu nitakaa naye hapa hapa" aliongea Mr Joseph ambaye tayri binti yake alishafka eneo lile.



    Alimpokea baba yake ila ghafla simu yake iliita.



    "Haloo mama"



    "Wahi kurudi nyumbani Leo kuna kitu kizuri nimegundua juu yako" alizungumza Lillian na kukata simu.



    Kisha akachukua Gazeti moja ambalo alikuwapo Salhat akiwa mdogo na cheni ambyo anayo mpaka sasa....aliinua picha mbili moja ilikuwa ya Mr matata pamoja na mama yake Salhat yani Samia.



    "Hivi ni kweli baada ya kuishi miaka mingi Leo ndiyo nakuja kugundua ya kuwa ile cheni iliyoko shingoni kumbe ni ya mwanao Samia yule ambaye tuliweza kumsaidia Mara ya kwanza kabida tukiwa arusha na Leo tena tumemkuza na kumlea" aliongea na kutabasamu huku akiuliza.



    "Kwani ni kipi kimekukuta Samia....na kwanini Salhat....hapana itakuwa ulimuweka Salhat kwa kuwa uligundua Joseph atamchukua na atakuwa mahali salama" aliendelea kuzungumza huku machozi yakimtoka.



    "Mama amenipigia ananiambia niwahi"



    Mzee yule mwingine alihisachi kama anatafuta kitu



    "Unatafuta nini mzee mwenzangu??? Aliuliza Mr Joseph.



    "Nafikiri nimeacha kiko changu kwenye mtumbwi" alizungumza mzee yule.



    "Salhat embu nenda kamchukulie mimi nakutizama"



    "Ndyo baba Salhat aliondoka na kuelekea kwenye mtumbwi hatimaye aliweza kukipata kile kiko na kuanza kurejea baada ya kutoka kweye Giza alishangaa baada ya kutokumuona baba yake wala yule mzee.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbona baba alisema atanitizamia??? Alizungumza na kuendelea kupiga hatua za mbele baada ya kusogea karibu zaidi alifanikiwa kuona mtu akiwa amelala chini.



    "Nani wewe????......wewe nani!???? Alizungumza Salhat akiendelea kupiga hatua za kwenda mbele.



    Hatimaye kiko kilimdondoka baada ya kuhisi aliyeweza kumuona ni baba yake.



    "Baba!!! Aliita kwa sauti ya juu na kuelekea mahali alipo.



    Alikuwa Mr huku akiwa amechomwa kisu cha tumboni damu nyingi zikimtoka na akiwa hana tena uhai.



    Baba!!! Baba!!!! Baba!!!!!! Salhat alikitizama kile kisu kisha akakishika kwajili yakukichomoa ila wakati akifanya hivyo alikuwa akipigwa picha bila yeye mwenyewe kujijua.



    Alimchomoa kisu ila bado haikusaidia.



    "Ndyo lazima twende kwa mama mama anatambua dawa nyingi sana za kumponyesha mtu Salhat alianza kumburuta baba yake mdogo mdogo na kila alipokuwa akimburuta damu nyingi zilizidi sambaa na alikuwa akipigwa picha alimburuta hadi kufika karibu na kwao ambako palikuwa na miti miti mingi kidogo kama alishangaa baada ya kuhisi kuna mwanga mkali unatoka ndani ya nyumba yao aliendelea kumburuza na alipofkla karbu aliona nyumba yao ikiwaka moto.



    "Hapana hapana....... Alizungumza na kuutupa mwili wa baba yake chini kisha kuanza kukimbilia kwenye nyumba yao.



    Moto tayri ulikuwa mkali hivyo kila alipojitahidi kuingia alishindwa na hatimaye alisimama kwa kugeuka na kutizama sehemu ambayo aliuacha mwili wa baba yake alipigwa picha tena akiwa anatoka na kuelekea alipo baba yake.



    Hakufika mbali alizimia na alipozunduka alikuwa hospitalini alipojaribu kuamka Alishangaa baada ya kuona pingu mikononi mwake.



    Ghafla waliingia askari watatu na mmoja alijitambulisha kwa jina la Akram



    "Miss Salhat uko chini ya ulinzi kwa kosa la kuhusika na kifo cha wazazi wako wote wawili"



    Salhat alishtuka na kutizama .



    "Nani kauwa nani ???? Aliuliza Salhat.





    Salhat alishtuka sana baada ya kukutana na habari hizo na kipa alipojaribu kukumbuka kipi kilitokea alishindwa kwani kumbukumbu zake hazikuweza kuja.



    Hatimaye alifikishwa katika chumba cha mahojiano baada ya hali yake kutengamaa kila alichoulizwa alijibu ya kuwa hakumbuki chochote kile hivyo alirudishwa tena hospitalini na hata dactari alieleza ya kuwa hali yake siyo nzuri kiafya. Hivyo alirudishwa mahabusi na kesi yake ilisimama hadi pale hali yake itakapokuwa nzuri ndyo kesi ipelekwe mahakamani.



    Aliingia katika mahabusu ambayo tayari kulikuwa na wafungwa wengine 5 katika hao wafungwa alikuwepo mmoja ambaye alikuwa mbabe wa hapo.



    Alipofika tu mbabe yule alisimama kisha akamfuata kwani Salhat alikuwa amekaa kona huku akijikunyata.



    "We binti mrembo mrembo.....unakuja tu na kujikunyata ni kwmba huwaoni wakubwa zako uje kuwasalimia? Aliuliza huku akianza kumsodola kichwani.



    "Alafu we mtoto wa mama kweli mlaini laini......alafu unadhubutu kufanya vitu vya aibu, unawezaje kumuuwa baba na mama yako??



    "Hata kama sina kumbukumbu yoyote ila siwezi kuwauwa wazazi wangu" alijibu Salhat huku machozi yakimtoka.



    "Ahaaa kumbe na wewe unakuwaga na sauti eeee tena unanijibisha mimi wewe kahaba" aliongea na kuanza kumpiga Salhat ambaye hakuweza hata kupiga kelele zaidi ya kumtizama tu. Haikuwa Mara yake ya kwanza kupigwa na mtu huyo hivyo ililuwa kama mazoea.



    Maisha yake yaliendelea kuharibika zaidi na zaidi akiwa gerezani huku kila Siku akiambulia vipigo ambavyo vilimfanya vimpotezee uzuri wake na aonekane mtu wa ajabu kati ya watu wote pale gerezani.

    Kila Mara Akram alipata shida juu yake kwani kila amuonapo tayri alikuwa ameongezewa ngeu usoni mwake.



    "Wewe binti inamaana katika ya watu wote walioko hapa mahabusu wewe ndye ambaye huna nguvu za kupigana na wenzako?? Aliuliza kwani kila Siku ilibidi aitwe dactari wa kumtibu.



    Salhat alimtizama bila kumjibu kitu na hii ndyo ilikuwa tabia yake mpya...baada ya kumaliza kutibiwa alirudi gerezani kisha akajitenga kama kawaida yake hata usiku unapofika inakuwa ni vigumu kwa yeye kulala huwa yuko macho akiwatizama wenzake ambao walikuwa wamelala.



    Hatimaye ilipita miezi 6 Salhat akiwa gerezani alibadilika sana mwili na hata sura yake ila bado aliendelea kuonewa.



    Usiku huo alilala na kumbukumbu zake zilianza mrejea taratibu akiwa usingizini alikurupuka na kupiga kelele gerezani hali hiyo iliwafanya wale waliokuwa wamelala naye na wao washtuke.



    "Hapna mbona ni mimi.....nimewezaje kuwauwa wazazi wangu hapana....hapana....hapana....aliendelea kupiga kelele na askari wa zamu waliingia na kumtoa njee kisha kumpeleka kwenye chumba cha adhabu na kuanza kumpa adhabu kwani aliambiwa anyamaze ila bado alishindwa kabisa.



    Asubuhi kulikucha na IGP Akram alishafika polisi pale alishtuka baada ya kupata ujumbe wa kuwa Salhat anataka kumuona.

    Wakiwa mezani na Salhat.



    "Nahitaji kesi ipelekwe mahakamani kwani mimi ndyo muuwaji" alizungumza na hatimaye kuamka na kuondoka eneo lile.



    "Hivi huyu binti hizo akili ni zake au kuna mtu anamsaidia kuziendesha ila kwa kuwa amekubali basi faili lake lipelekwe mahakamani" aliongea na kuondoka zake huku akimfikiria sana Salhat.



    IGP Akram alielekea hadi hospitalini akiwa na mauwa hiyo ni ishara ya kuwa yuko na mgonjwa wake katika hospital ile.



    Alifila katika chumba namba 87 na kufungua mlango hapo alionekana mtu aliyekuwa akipumulia mashine na mirija mingi ikiwa imetapakaa mwilini wake hii.



    Alitenga uwa pembeni kisha akasogeza kiti na kukaa karibu na mgonjwa yule huku akiinua mkono wa mgonjwa yule na kuushika.



    "Baba" aliita jina hilo na kutabasamu.



    Huyu alikuwa mtoto wa IGP Saidi ambaye aliweza kupambana katika kumpata Salhat lakini alishindwa na mwishoni haikujulikana kipi kimemkuta baada ya kuwa alikuwa akifuatilia kifo cha Mr matata basi alikutwa ametupwa karibu na nyumba yake akiwa katika hali hiyo na ni takribami miaka 14. Akiwa hajigusi wala aongei chochote.



    ***** ****** *****



    Kesi ilipelekwa mahakamani na vizibitisho vya picha pia viliweza kuletwa mahakamani hii ni kutoka na IGP Akram kutumiwa picha hizo na mtu ambaye hata yeye hakumfahamu ni nani.



    Kesi ilisomwa na hatimaye ulifika muda wa Salhat kujielezea na yeye alisema.



    "Nimewauwa...wote wazazi wangu... Nimewauwa mimi alizungumza huku machozi yakimtoka" na kwa sauti ya upole na huruma ambayo kila aliyekuwepo mahakamani pale alibaki akimsikitikia.



    Hakimu aliuliza huna chochote cha kujitetea.



    "Nilikuwa naomba nipewe adhabu ya kifo kwani ndyo itakayonifaa ili nisiendelee kuchelewa kuipata adhbu yangu Motoni" aliongea Salhat na kufanya watu wote waliokuwa ndani ya mahakama kumshangaa.



    Hata hakimu na yeye alibaki akimshangaa hadi IGP Akram na yeye alimshangaa.



    "Hakimu naweza kumtetea"



    "Sihitaji mtetezi aliongea Salhat na kumtazama Akram kisha akarudisha macho yake kwa hakimu.



    "Naomba hukumu yangu ikubaliwe" aliongea na kurudisha macho yake kwa Akram ambay alibaki akitingisha kichwa.



    Hakimu aliinama na kuandika kwa dakika 3 kisha akasema.



    "Ninaomba mtuhumiwa huyu apelekwe hospitali ya vichaa kwanza mpaka pale hali yake itakapotengamaa ndiyo kesi yake iletwe mahakamani.



    "Nimesema mimi siyo kichaa nipeni kifungo changu cha kuuwawa kwanini mnataka mimi nienddlee kuishi ilihali nimeshawauwa wazazi wangu..... Salhat alimkimbilia hakimu na kuanza kumvuta na hiyo ilikuwa patashika hapo mahakamani alikuja askari mmoja na kumpiga kitako cha bunduki cha tumbo hivyo kumfanya adondoke chini na kumuachia hakimu huku akisema "tafadhli nipe adhabu ya kifo....tafadhali...... Askari huyo aliinua tena Kitako cha bunduki kwaajili ya kumpiga ila IGP Akram alimzuia na kumfuata Salhat kisha akambeba na kutoka naye njee ambako alipigwa picha nyingi sana kabla hajafikia gari lake la polisi.



    Alikaa karibu kabisa na Salhat huku akimfunga pingu kwa mbele na kumtizama kwa hasira na huruma ya hali ya juu.

    Askari walioweza kumleta Salhat na wao waliingia ndani kwaajili ya kumrudisha tena mahabusu kisha kufanya mawasiliano na hospital ya vichaa kwaajili ya kuja kumchukua na kumpeleka huko.



    Ndani ya gari askari wote walkuwa kimya huku wakimtizama Salhat ambaye na yeye aliwatizama ila macho yake sana sana yalitizamana na ya IGP Akram.



    Ghafla IGP alianza kuona mabadiliko katika mwili wa Salhat.



    "Vipi unajisikia vibaya mbona jasho linakutoka?? Aliuliza IGP huku akimtizama Salhat ambaye hakuwa ameweka sura ya utani kabisa.



    Kila dakika zilivyozidi kwenda ndivyo mwili wa Salhat ulivyozidi kuonekana ya kuwa unaisha nguvu.



    "Unashida gani wewe??? Aliuliza IGP na kusimama kisha kuanza kumtazama Salhat ambaye alikuwa akicheka kwa kumcheka.



    IGP Akram alishtuka na kuifichua mikono ya Salhat ambayo aliificha katikati ya mapaja yake. Alikuta nguo ikiwa imejaa damu. Alipoitoa hiyo nguo ndipo alishtuka kwani tayri Salhat alishajikata katika mishipa yake yote miwili mikubwa ya kutolea damu.



    "IGP alichana nguo ya Salhat vipisi viwili na kuagiza gari ipelekwe hospitalini haraka sana huku yeye akimfunga Salhat juu ya mkono ili damu zisiendelee kutoka nyingi"



    "Hivi unafikiri utaweza alizungumza Salhat kwa shida huku akijitahidi kutoyafumba macho yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Huwezi kunisaidia tena kwani mimi ndyo nakufa" alizungumza Salhat na hapo hapo alidondokea kifuani kwa IGP Akram.



    "Salhta.......salhat...... Fasta ongezaaaaa spidiiii" akiongea huku akiendelea kukaza pale alipokuwa amefunga.



    Hatimaye kiliwekwa king.ora cha polisi juu na watu sasa walianza kupisha njia.



    ***** ***** ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog