Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

ROHO MKONONI - 3

 





    Simulizi : Roho Mkononi

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Hali aliyoikuta kwa Fonga ilimfanya afikirie upya juu ya Isaya!!

    Akafikiria kumwendea bwana huyo ili amlilie katika shida yake, nafsi ilimwingia baridi sana kwa jaribio alilotaka kulifanya lakini angefanya nini iwapo mambo yanamuwia magumu kiasi hicho!!

    Akaishika simu yake aweze kumpigia Isaya!!

    Alisita mara kadhaa, akaghairi na kuamua tena zaidi ya mara tatu. Kisha akabofya na kuanza kusikiliza upande wa pili.

    Simu ikaita lakini haikupokelewa!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Alipojaribu kupiga tena mara simu yake ikaanza kuita akajikuta anapokea upesi akidhani ni Isaya.

    “Mambo bro Isaya!!” alisabahi..

    “Kituo cha polisi Magomeni Usalama….Joyce Keto. Unahitaji kituoni haraka iwezekanavyo!! Fika upesi bila kukosa, Asante. Ukifika mapokezi utakuta maelezo.”

    Simu ikakatwa!!

    Ebwana eee!! Joyce alitamani kukimbia, akatamani apae juu na apotee kabisa. Miguu ilikuwa inatetemeka kupita kawaida, mara mkoba mdogo aliokuwanao ukaanguka chini. Akahaha huku na kule katika kuuokota mara pikipiki zikapiga honi.

    Hofu hii ilikuwa kubwa zaidi, yaani anaitwa polisi? Kwa jinsi alivyokuwa anayaogopa mambo ya polisi leo hii anaitwa polisi haraka iwezekanavyo!! Weeee!

    MSHIKEMSHIKE!!!

    Joyce baada ya kutuliza akili kwa muda akaamua kuondoka muda huo huo kuelekea kituo cha polisi Magomeni.

    Njia nzima alikuwa analikumbuka onyo alilopewa la kutowashirikisha polisi juu ya taarifa na masharti aliyopewa, kwani kwa kufanya hivyo angeupoteza uhai wa Betty na yeye pia kujiweka katika mashaka ya hali ya juu.

    Joyce akitokea maeneo ya chuo kikuu, aliwasili Ubungo baada ya robo saa kisha akachukua basi lililompelekahadi Magomeni Usalama.

    Ndani ya dakika ishirini alikuwa akitazamana na kituo cha polisi. Kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam.

    Mawazo yake kila alivyotazama kituo cha polisi yalikuwa juu ya kufungwa jela, alivyofikiri kuhusu hili akaanza kutetemeka miguu na mikono huku moyoni akifanya majuto asijue anajutia nini.

    Macho ya askari wa kike yakatazamana naye mbele ya mzunguko wa mapokezi.

    “Nini shida!” aliulizwa

    Akajieleza juu ya kupokea simu ya kuhitajika kituoni pale. Alipojieleza zaidi na zaidi akaombwa ile namba ambayo ilimpigia. Wakati anataka kuitoa ile namba mara akaganda kama sanamu la kuchongwa.

    Macho yake yalikuwa yanatazamana na Isaya, alikuwa pamoja na polisi aliyevaa sare zake rasmi.

    Isaya alipomuona Joyce akanyoosha kidole kama anamwonyesha kitu yule afande. Hapa Joyce alitamani kukimbia lakini miguu ikawa mizito!!

    Yule askari akamkaribia Joyce na kumuuliza iwapo ni yeye aliyepokea ile simu, Joyce akakubali kuwa ni yeye. Akashikwa mkono na kuongozwa kuelekea mahali.

    Wakakifikia chumba fulani hivi, huko yakaendelea mahojiano juu ya wapi asili ya Betty na ni nani yake, na kuhusu namna alivyotekwa iwapo kuna taarifa yoyote anaweza kuwanayo.

    “Joyce, inavyoonekana kuna dalili kuwa unajualolote kuhusiana na jambo hili, maana kwa maelezo ya Isaya ni kwamba mlikuwanaye karibu lakini ghaflaakamvisha pete Betty ambaye n I rafiki yako, hivyo wivu wa kimapenzi ukakusababisha uchukue uamuzi wa kumteka Betty na kumfanya lolote ujualo. Na baada ya muda mrefu kupita leo Isaya akiwa chumba cha mahojiano ulimpigia simu, bila shaka ulitaka kumweleza kuwa Betty ametoweka wewe uchukue nafasi binti” alijieleza yule askari huku akimkazia macho Joyce.

    Joyce ambaye hakuna hata dakikamoja aliyojaribu kuizoea hali yam le ndani alifanya jitihada za kujitetea lakini kwa sababu ilikuwa mara yake ya kwanza kuhusisishwa katika kesi ya aina hii alijikuta akijiumauma tu!

    “Naapa afande, Betty ni rafiki yangu sana mimi, hakuna ubaya kati yangu mimi na yeye. Sijawahi kufikiri na sikuwahi kumfanyia hivyo!! Naapa kabisa afande.” Alijibu huku akitetemeka.

    “Lakini umewahi kuwa na wivu juu yake alipovishwa pete na Isaya.”

    “Hapana sijawahi afande, sijawahi hata siku moja.”

    “Mbona hukuhudhuria sherehe yake kama kweli hauna wivu, tena wivu mkubwa?” aliulizwa swali ambalo lilimchanganya sana. Alikosa cha kujibu akaanza kujiuma uma kucha zake.

    “Na inavyoonyesha wakati sherehe zikiendelea wewe hapo na ndugu zako mlikuwa katika mpango kabambe wa kumteka Betty na Isaya, mbinu yenu chafu ikatibuliwa ndipo mkajipanga tena. Ndo maana haukuwa katika sherehe wewe Joy. Unaona sasa ulivyokuwa muongo?” askari mpelelezi wa ile kesi akazidi kumbana maswali yenye ushahidi Joyce.

    Hapa sasa Joy akaona amekamatika, kweli hakuhudhuria sherehe na ni kweli muda ule aliutumia kufanya mtego wa kumzuia Isaya asifanye mapenzi na Betty ilimradi tu asiukwae Ukimwi.

    Mambo mengi kwa pamoja yakakizingira kichwa cha Joy. Akatamani sana kusema juu ya tukio la usiku ule, lakini bilakusema kuwa Betty ni muathirika basi hataaminika na atajiweka katika kitanzi mwenyewe, akatamani pia kusema juu ya ujumbe alioletewa usiku katika bahasha ya kaki, lakini akahofia kuwa Betty atauawa na yeye kujikuta matatani.

    Mkanganyiko huu wa aina yake ukamweka katika fumbo. Akakosa cha kujibu, jasho likaanza kumtoka.

    “Mtoto mzuri kama wewe unajihusisha katika utekaji nyara, kwani wanaume mbona wapo wengi tu akina sisi hapa hatujaoa mbona umng’ang’anie huyo Isaya. Tatizo lenu watoto wa chuo mnapagawa sana kusikia mtoto wa mbunge…haya nd’o hautoki tena hapa.” Alisema kwa kebehi yule askari.

    “Jamani afande mimi sijahusika na chochote, siwezi kumfanyia hivyo swahiba wangu siwezi mimi hata yeye akiletwa hapa sekunde hii hapa atausema ukweli lakini mimi sijui lolote afande, jamani afande mimi bado mwanafunzi nionee huruma mimi nakuomba.” Joyce alisihi, safari hii huku akibubujikwa na machozi. Afande yule hakujali, badala yake akachukua karatasi na kalamu.

    “Haya binti nyamaza, huu ni wakati wa kutoa maelezo yaliyonyooka sasa kuhusiana na utekwaji nyara wa rafiki yako.” Afande alimsihi, kisha akaanza kumuuliza maswali ya kawaida tofauti na yale ya awali ambayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kumtetemesha. Na hakika alitetemeka kweli!!

    Baada ya mahojiano Joyce pasi na kutarajia alishangaa akiingizwa katika karandinga ya polisi.

    Alitakiwa kuongoza njia kwenda mahali alipokuwa anaishi ili aweze kupekuliwa iwapo kuna ushahidi wowote wa kumuweka matatani.

    Moyo wa Joyce ukapasuka kwa hofu kuu! Akaduwaa kama vile anaangalia filamu ya kutisha ambapo anangoja tukio moja limalizike kisha lifuate jingine.

    Alikuwa amekumbuka juu ya ujumbe aliotumiwa katika bahasha ya kaki. Alitamani kumwagiza mtu yeyote yule akautoe kabla hawajafika pale lakini bahati mbaya simu yake ilikuwa imekamatwa na kuzimwa tayari ili asije kuharibu upelelezi wa kesi ile.

    Karandinga lilifunga breki kwa fujo katika maeneo ya Ubungo Kibangu ambapo ndipo aliishi Joyce na Betty katika nyumba ya chumba kimoja na sebule, huku sebule ikigeuzwa kuwa jiko.

    Askari takribani wanne walishuka kisha akatelemka Joyce, mrundikano wa watu kundi kwa kundi ukaanza kufuatilia tukio hili huku wengine wakijifanya wanajua tayari kinachoendelea.

    Joyce alikuwa katika fedheha kubwa ambayo hakuwahi kuitegemea hata siku moja, hakikalilikuwa jaribu ambalo alihisi lilikosea njia na kumkumba yeye.

    Mapenzi haya!! Alijisemea huku akimfikiria Isaya. Laiti kama asingekuwa yeye basi asingekuwa hapo alipo.

    Akatamani kumchukia lakini akakosa sababu ya kumchukia maana alimpenda mtu aisyejua kama anapendwa kwa dhati!!

    Chumba kikafunguliwa,baada ya mwenyekiti wa mtaa kutoa Baraka za ukaguzi huo. Joyce akaingia pamoja nao ndani iwapo watahitaji upekuzi zaidi aweze kuwasaidia.

    Hii haikuwa kesi ya kawaida!! Polisi walikuwa wamejikita vilivyo, wakapekua kila kona, lakini waliishia kupata picha za Joyce na Betty wakiwa katika furaha. Mara maua na kadi walizotumiana kama ishara ya upendo.

    Simu ya Joyce nayo ikapekuliwa lakini hapakuwa na ujumbe wowote hatarishi.

    Hatimaye wakafikia madaftari ya Joyce, daftari moja bada ya jingine. Sasa walikuwa wamelifikia daftari lililokuwa na ile bahasha, lilivyonyanyuliwa tu bahasha ikadondoka chini, askari akainamana kuikota. Joyce alitamani kufanya muujiza bahasha ile isifunguliwe lakini haikuwa hivyo bahasha iukafunguliwa.

    Karatasi ikatolewa.

    Nimekwisha!! alijisemea Joyce huku akiinama chini kungojea aibu ya mwaka ya kupigwa pingu na kisha kubambikiziwa kesi ya utekaji nyara.

    Karatasi ile ilikuwa imeandikwa maneno machache tofauti na awali. Polisi akasonya na kuitupa mbali, Joyce bado alikuwa ameinama akingoja maswali lakini hapakuwa na swali lolote.

    Polisi wakakiri kuwa hapakuwa na lolote la kuwasaidia kutoka kwa Joyce.

    “Tukikuhitaji wakati wowote tutakuita kituoni na ufike mara moja kwa wakati.” Askri mmoja alitoa amri hiyo, kisha akaongozanana wenzake wakatoka nje na kuliendea karandinga.

    Joyce akaketi huku akiwa haamini kabisa kama alikuwa ameachwa huru siku hiyo. Machozi yalikuwa yanamtoka na jasho jingi. Alikuwa akijiuliza ina maana hawakuelewa ujumbe katika ile bahasha, hapo akainuka ghafla na kuisaka tena ile bahasha.

    Huku akakutana na ile bahasha, ujumbe ukiwa pembeni lakini safari hii ulikuwa tofauti kabisa na ule wa awali.

    “MAMBO SHOSTI” ujumbe uliandikwa hivyo kwa herufi kubwa!!

    Joyce akachoka!!

    Majirani walikuwa mlangoni wakitaka kumuuliza nini kimetokea, akasimama kama anayetaka kuwasikiliza, akaufikia mlango akaufunga kisha akaingia chumbani kwake akajirusha kitandani.

    Tayari ilikuwa saa kumina moja jioni!!

    *****

    FONGA alishtushwa sana na habari za Joyce kuwa kituo cha polisi. Habari hizi alizipata mapema sana kupitia kwa Isaya ambaye alikuwa amemaliza kuhojiwa.

    Kwa uzoefu wake kidogo Fonga alitambua kuwa Joyce atatetemeshwa sana na kutishwa sana ili aseme hata asilolijua.

    Huruma ikamwingia na akawa kama anayemuona Joyce jinsi anavyohangaishwa na maswali ya polisi watukutu.

    Fonga akaamua kutumia nafasi hii!!

    Aliiona ya kipekee sana.

    Majira ya saa tatu usiku alikuwa katika nyumba ya kulala wageni maeneo ya Sinza, alikuwa ametulia tuli akijitahidi kuondoa uoga aliokuwanao.

    Baada ya nusu saa mlango ukagongwa.

    Akaufungua, Joyce akaingia ndani!!

    Akaketi katika mojawapo ya viti vilivyokuwa katika nyumba ile.

    Fonga alikuwa mwingi wa mawazo na aliyetazamika kama mtu mwenye uchungu sana. Macho yake yalipepesa huku na kule kabla hayajatua katika uso wa Joyce.

    Akainama chini na kuanza kutiririka maneno mfululizo ambayo yalikuwa mageni sana kwa Joyce.

    “Unajua Kidoti, huwa inafikia mahali kama mwanadamu inabidi useme tu inapobidi. Ni muda mrefu sana mimi nimefahamiana na wewe japo sio kwa ukaribu kama huu wa sasa. Joyce nimeguswa sana na tatizo lako, na nimesikitika zaidi na kufadhaika niliposikia umepelekwa polisi na kisha kuondoka na karandinga, mrembo kama wewe hakika haustahili hata kidogo. Ni kweli mimi ni maskini lakini hii haijalishi linapotokea tatizo kwa mtu ambaye unampenda. Nipo radhi kufanya jambo lolote jema hata kama linanigharimu kwa mtu nimpendaye, Joyce Kidoti mimi sina elimu labda nd’o maana nikajikuta nikishindwa kuwa imara na kukabiliana nawe wakati ukiwania mashindano ya urembo hapo chuoni, lakini sasa najihisi kama nakosa kabisa amani nikiendelea kujinyima haki hiyo. Huenda Mungu ametuunganisha tena kwa namna ya kipekee ili niweze kujieleza kuwa nakupenda sana. Na ninakuhitaji hakika, ulipokuwa jirani na Isaya sio siri nilikuwa naumia sana. Niliumia sana kwa sababu moja tu Isaya hana mapenzi ya kweli. Na hapo alipo anafanya kuwachezea tu wasichana na kuwaacha, wewe hukustahili kuchezewa hata kidogo, mimi ni jasiri na huwa sina mpango wowote na watoto wa kike zaidi ya kujikita katika kazi zangu uzijuazo lakini kwako Joy naweza kusema nimeshindwa kabisa.

    Sitaki niseme mengi katika hili tatizo huenda unaweza usinielewe kutokana na wakati tunaopitia kwa sasa ambapo Betty ametoweka. Basi nakuomba tu kwa muda huu utambue kuwa ile milioni tatu, imepatikana na kama kweli hao watekaji wana shida hiyo tu basi Betty watamuacha huru!! Haijalishi imenigharimu ama itanigharimu katika siku za usoni lakini nimeyafanya haya kwa msichana ambaye ninampenda kwa dhati” hapa akamaliza akamtazama Joy machoni.

    Akakutana na macho yanayong’ara kwa furaha kuu, Fonga akatambua kuwa amezipanga karata zake vizuri kabisa na sasa alitakiwa kufunga goli na mchezo uishie hapo.

    Joy akamrukia Fonga na kumkumbatia, alimkukumbatia kwa mambo mawili makuu kwa wakati huo, kwanza alikuwa ameongea maneno ambayo Joy aliwahi kuyasema wakati akijitoa kwa marehemu mwalimu Japhary na kisha kuukwaa Ukimwi, ‘Nipo tayari kufanya lolote kwa mtu ninayempenda’……pili alimkumbatia kwa sababu alikuwa kama malaika wa ukombozi.

    Hapa angeweza kumwonyesha Betty ni jinsi gani anamjali kwa kumwokoa kutoka katika mikono ya watu wabaya.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Furaha ikizidi sana hupunguza uwezo wa kufikiri!! Uchungu ukizidi vilevile huleta tatizo hilo hilo.

    Joyce akalala na Fonga hadi asubuhi.

    Alipotoka pale ndani alikuwa na milioni tatu kibindoni huku nyuma akimwacha Fonga akijiuliza ile ladha ya penzi alilolingoja kwa muda mrefu hatimaye ameipata.

    Watu wawili walikuwa wanaota kwa pamoja lakini ndoto mbili tofauti.

    Joyce akiota kumuokoa Joy kwa sababu pesa aliyoipata akiongezea na ile ya kwenye akaunti ya Betty basi jumla inafika milioni sita!!

    Fonga akaota ndoto ndogo tu lakini nzito, akaamua kuweka tena kichwani suala la kuoa. Kumuoa Kidoti.

    Baada ya muda mrefu wa kuachana na mapenzi baada ya tukio la mwenye pesa mmoja kumnyang’anya mpenzi wake aliyempenda hadharani kisha kumweka rumande kwa kesi asiyoijua, kesi iliyomfanya atumikie kifungo cha miezi tisa jela.

    Kitendo ambacho kilimfadhaisha Fonga na kukoma kabisa kujihusisha na mapenzi, sasa alikuwa amefika tena kwa Joyce Kidoti. Na kisha akatangaza ndoa katika nafsi yake.

    Hakika ilikuwa ndoto ndogo, lakini nzito sana!! Ilikuwa nzito kwa sababu hakujua kama kuna mambo mengine mazito yalikuwa yakiendelea chini ya pazia!!



    *****

    SAA nne asubuhi Kidoti allikuwa amejitawala katika chumba chake, hakutaka kukumbuka sana juu ya Fonga na nini kilichotokea, alichofikiri kwa wakati huo ni pesa aliyopata na katika namna ya kumwokoa Betty bila kutumia kivuli cha Isaya.

    Joy alijipa moyo kuwa penzi alilompa Fonga ilikuwa njia tu ya ukombozi na hapakuwa na jingine la ziada pale.

    Joy hakutulia sana chumbani kwake, akaitwaa kadi ya benki ya Betty, akajisogeza katika mashine ya kutoa pesa.

    Akatoa shilingi laki tano. Kiwango cha mwisho kabisa kutoa pesa katika mashine kwa kipindi hicho.

    Akatoa katika akaunti yake pia shilingi elfu hamsini!!

    Akarejea nyumbani, alipotulia akapiga simu katika ile namba iliyokuwa imemuonya kuwa apige simu akiwa ana pesa, vinginevyo asifanye thubutu yoyote ya kuwasiliana naye.

    Sasa Joy alikuwa na pesa kadhaa, akamtwangia simu bwana mwenye sauti nzito!!

    Simu ikaita kidogo kisha ikapokelewa.

    “Samahani kaka nimepata nusu hadi sasa lakini baada….” Kabla hajamaliza akaingiliwa kati na sauti ile.

    “Nitafute ukiwa na pesa kamili. Nakupa siku mbili tofauti na hapo sitakuwa na haja na pesa yako. Nakukumbusha. Ole wako uwashirikishe polisi!!” Kisha simu ikakatwa.

    Ama kwa hakika mtekaji huyo hakuwa na utani hata kidogo. Alinuia kabisa kufanya kitu kibaya kwa Betty.

    Joyce akabaki kuitazama tu simu yake akidhani itasema naye lolote!!

    Haikufanya jitihada zozote za kumfurahisha…..

    Taratibu akalegea bila kujizuia, kisha akaanza kutokwa na kilio cha chini chini kama mtoto mdogo anayelia huku akiwa amezibwa mdomo wake!!

    Hakufanya jitihada zozote za kuyafuta machozi yake!!

    Hakika alikuwa matatani!!

    Ule mzigo wa urafiki wa dhati ulikuwa unaanza kumuelemea haswa.

    Alipokumbuka kuwa anakaribia siku nne bila kuhudhuria vipindi darasani, akataharuki, akampigia simu kiongozi wa darasa kuulizia lolote lile linaloendelea.

    Akaambiwa kuwa asubuhi ya siku inayofuata kutakuwa na mtihani. Akatajiwa somo, akapagawa!!

    Lilikuwa somo gumu sana na muhimu katika kozi yake.

    Joyce akajikunyata baada ya kukata simu, akaanza kulia kama mtoto, akakumbuka kumlilia na mama yake aliyekufa miaka kadhaa nyuma.

    Alisikitisha kumtazama!!!!

    ****

    Mzee, Akunaay Zingo na mwanaye kipenzi, Isaya walikuwa katika mshangao mkubwa. Mshangao wa kujiuliza ni akina nani wale ambao walidiriki kumnyakua Betty kutoka mikononi mwa mwanaye na kisha kukaa kimya hadi dakika hiyo.

    Mzee Akunaay alikuwa ametoa maelezo polisi juu ya namba iliyowahi kumpigia simu na kumtahadharisha juu ya mpango kabambe wa kutekwa kwa wapenzi wawili, Isaya na Betty ambao walikuwa wametoka kuvikana pete za kujitambulisha kama wapenzi.

    Tatizo namba ile ilikuwa haipatikani tena!!

    Ikawa haina maana tena.

    Isaya alikuwa amepagawa zaidi kwa hilo tatizo. Cheo cha baba yake hakikusaidia lolote kuhusu upatikanaji wa Betty ambaye ni mchumba wake, na alitarajia kumuoa kabisa ili aweze kujiweka katika nafasi nzuri ya siasa za chuoni na pia kama shambulizi la uhakika kwa Joyce ambaye alimtosa na kuapa kuwa hampendi hata kidogo.

    Sasa alikuwa katika fumbo na kujiuliza ni nani yuko nyuma ya mambo haya. Lakini jibu halikuwa jepesi. Jeshi la polisi nalo lilikuwa halijapata mstakabali wowote maana kila penye dalili ya kuleta mwanga wa mafanikio, kiza kisichotarajiwa kilitanda.

    Huu ukawa mtihani mkubwa sana!!

    Mtihani mgumu kabisa kuwahi kuwafika!!

    Pesa na umaarufu zikakosa umaana.

    Mzee Akunaay akaamua kuhoji juu ya mahusiano yao yalipoanzia na ni wapi walikutana.

    “Unawafahamu wazee wake kwani?” Alimuuliza mwanaye huku akiwa amesimama akipiga hatua kwenda mbele na kurudi nyuma.

    “Tulikuwa hatujaenda bado.” Alijibu huku akiwa ameinama Isaya.

    “Kwa hiyo, hauwajui si nd’o hivyo!!” alikazia mzee Akunaay.

    Isaya hakujibu kitu.

    “Yaani Isaya mwanangu wewe na akili zako za kiutu uzima kweli unakwapua tu msichana barabarani haufuatilii hata wazazi wake, mji anaotoka, ghafla ghafla tu unamvika pete eti unataka kuoa. Hivi kilikusibu nini lakini mwanangu eeeh! Ulikuwaje Isaya ukafanya mambo ya kishenzi kama haya. Sasa sisi tutajuaje kama alikuwa ni mtu mbaya labda, sasa tazama amekuingiza katika matatizo tayari….mi si nilishasema watoto wa siku hizi mkishapata elimu kidogo mnajifanya kujua kila kitu. Mnajichagulia tu wqsichana wa kuoa, hakuna kuwasikiliza hata wazazi. Haya yapo wapi? Yapo wapi Isaya.” Alibwatuka mzee Akunaay huku akisahau kabisa kuwa ni yeye alikuwa akitamba katika kipaza sauti siku ya sherehe ya Isaya, kuwa mwanaye amechagua mke anayefaa sana.

    Na kama haitoshi ni yeye aliyelipia chumba kwa ajili ya mapumziko yao baada ya kuvikana pete.

    Sasa anamgeuka Isaya na kumwona kama mkurupukaji katika maamuzi. Maamuzi ya kujiingiza katika mahusiano na Betty.

    Binti ambaye mzee Akunaay alilalamika kuwa hakuwa akijulikana ni wapi anapotoka na wapi anaishi.

    Isaya alitaka kujibu tuhuma za mzee wake lakini akakumbuka kuwa yule alikuwa ni baba na alikuwa na haki ya kulalamika bila kukumbuka lolote lile.

    Na mtoto kwa mzazi hakui!!

    “Sasa nasema kama baba yako mzazi, kuanzia dakika hii sitaki ujihusishe na huyo binti. Apatikane ama asipatikane! Unanielewa Isaya, nasema hivi, apatikane ama asipatikane!! Sitaki kukusikia naye tena.” Alimaliza kwa amri, kisha akatoweka katika chumba ambacho alikuwa amechukua kwa hifadhi jijini Dar es salaam.

    Isaya akachanganyikiwa!!

    Lakini hakuwa na ujanja, mzee akapunguza makali katika kuwasisitiza askari juu ya umuhimu wa huyo mtu aliyepotea, na kufikia hapo Isaya bnaye akanywea! Akabaki kujipa imani kuwa ipo siku Betty atarejea.

    Huo ukawa mwisho wa kumsaka kwa kuwatumia askari.

    Akamfikiria mtu mwingine ama namna nyingine ya kumsaka Betty katika njia ambayo baba yake mzazi hataweza kuitambua.

    Akaumiza sana kichwa na kupata jibu!!

    Alipoachana na baba yake huku kila upande ukiwa umenuna. Isaya aliamua kupiga simu na kujaribu harakati nyingine.

    Hii ilikuwa ni masaa machache kabla hajaenda polisi kuandika maelezo yake ya ziada. Akaamua kumaliza kwanza jambo hili kwa kadri akili ilivyomtuma.

    Simu ikaanza kuita! Akatabasamu!!

    ******

    FONGA alikuwa katika chumba chake akiona kama miujiza juu ya filamu nzima ilivyochezeka katika namna ya kustaajabisha, ni kweli hakuwa na pesa za kutosha. Na alifadhaika sana kumwomba Joyce shilingi elfu mbili wakati alikuwa katika matatizo.

    Tatizo la kumwomba pesa halikumsumbua sana kichwa kwani hilo lilikuwa la kupita, akalipuuza.

    Kisha akakumbuka kuwa lipo la kudumu ambalo ni mapenzi. Hili lilimuumiza kichwa kwa mwaka na miezi kadhaa. Aliisikia kabisa nafsi yake ikimsukuma kumtamkia Joy kuwa anampenda, lakini akajikosoa kwa kujiuliza, ‘nitamwonyesha vipi kuwa nampenda bila kuwa na pesa?’…hiki kikawa kikwazo kwake.

    Akaingojea sana siku ya kupata pesa, hiyo siku haikufika mapema kama alivyotaraji. Hata siku Joy anamweleza juu ya shida ya shilingi milioni kadhaa alihisi fadhaa ikiishi naye kwa nukta kadhaa, aliamini kuwa kama angekuwa na pesa hiyo ilikuwa siku ya kumweleza Joy kuwa anampenda. Angempatia pesa kisha angemchombeza, aliamini kuwa asingeweza kukataa. Lakini hakuwa na pesa!

    Mara baada ya Joyce kutoweka, alijiendea nyumbani kwake akiwa na mawazo hayohayo. Alisikitika na kujutia sana kuikosa nafasi.

    Mara akapokea simu ambayo ilibadili kila kitu.

    Alikuwa ni Isaya! Isaya aliuhitaji sana msaada wake kiupelelezi kama itawezekana atambue ni nani amemteka Betty na wapi anaweza kupatikana.

    Kwa sababu ilikuwa dili ya kipelelezi Fonga akaomba apewe miliuoni tatu na nusu kama kianzia ili aweze kuunda majeshi yake vizuri kwa kazi.

    Kwa sababu Isaya alikuwa na shida sana, hakupingana naye. Akakubali kutanguliza milioni tatu na laki nane.

    Upesi Fonga akajiandaa na kwenda kukutana na Isaya.

    Akaikuta pesa tayari ipo katika bahasha!!

    Akajitia kuwa yu makini sana na kazi yake.

    Alikuwa amevaa miwani ya jua na koti kubwa ilhali jua lilikuwa linawaka. Alifanya haya ilimradi tu kumpagawisha Isaya na kumpumbaza kimawazo.

    Isaya akauvaa mkenge.

    Fonga akatia pesa kibindoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipotoka pale akampigia simu Joyce Kidoti kwamba wakutane lipo la muhimu la kujadiliwa!! Joyce ambaye alinusurika kulala rumande siku hiyo akakubali mara moja!

    Majira ya saa tatu usiku walikuwa nyumba ya kulala wageni.

    Pesa ya kuwalipa watu kwa ajili ya upelelezi, ikakabidhiwa kwa Joyce Keto Kidoti. Huku mfukoni akisalia na shilingi laki nane pekee.

    Ama kwa hakika, nguvu ya penzi ni mojawapo ya nguvu za ajabu zisizoonekana ulimwenguni. Mapenzi haya yalikuwa yameitafuna sasa akili ya Fonga.

    Pesa ilipotoka, penzi nalo likatolewa.

    Bwana Fonga akakiri kuwa alikuwa sahihi kabisa kusema, asingeweza kumpata Kidoti iwapo haipo pesa ya kutangaza nia hiyo.

    Cha kustaajabisha zaidi ni penzi la usiku ule, hakika lilikuwa maridjdhawa na sasa Fonga yupo kitandani kwake akiitafakari siku hiyo nzima ilivyoanza kwa tabu na kuisha kwa furaha iso’ kifani.

    Fonga akapiga funda kubwa la kahawa iliyoanza kupoa. Kisha akajikita katika wazo la ziada. Wazo kuhusu ile pesa aliyoitoa.

    Alitambua kuwa ile ilikuwa pesa ya kazi, lakini mapenzi yakaizidi nguvu kazi iliyokuwa mbele yake.

    Ghafla akashambuliwa na wazo la ghafla!

    Kama ile pesa ilitolewa kwa ajili ya kumpata Betty, basi hata ikiwa katika mikono ya Joy bado ilikuwa ni kwa ajili ya kumrejesha Betty.

    Hapa sasa Fonga akavamiwa na wazo kuwa anatakiwa kufanya kila namna Joy aweze kumshirikisha juu ya Betty na jinsi gani atazitumia pesa zile kuweza kumwokoa.

    Kwa kulijua hili, iwapo Betty atapatikana basi Fonga angeweza kumhadaa Isaya kuwa ni juhudi zake hadi hapo kumwokoa.

    Hili lilikuwa wazo sahihi kabisa. Wazo lisilokuwa na utata wa aina yoyote.

    Kisha akajikumbusha kuwa Joy anatakiwa kukolea haswa katika mapenzi ili aweze kudiriki kumsimulia juu ya Betty na mbinu ambazo anahitaji kuzitumia kumpata.

    Ni hapa Fonga alipokiri kuwa, anatakiwa kumtawala kiakili mtoto wa chuo kikuu, mlimbwende nambari wani. Joyce Keto.

    Fonga akajipa moyo kuwa elimu yake ya kidato cha nne itamwongoza vyema ikisaidiwa na elimu ya mtaani.

    Kitu cha kwanza kabisa alihitaji kujua kwa nini Betty ametekwa? Hili lingempa mwongozo mpana sana hadi kufahamu kwa nini Joyce adai milioni kadhaa kwa ajili ya kumwokoa?

    Na kwa nini alimtuma Fonga kumfuatilia siku ile ili asifanye mapenzi na Isaya?

    Swali hili lilimshtua sana Fonga. Siku yeye alipoagizwa kumfuatilia Betty nd’o siku hiyohiyo ambayo Betty alitekwa na kupotea moja kwa moja hadi wakati huo pakiwa hakuna taarifa yoyote.

    Lazima kuna kitu Joy anatambua hapa!! Na ili mambo yaende sawia, lazima awe name bega kwa bega kama mpenzi wake.

    Kwa kufanya hivyo nitazijua siri zote na kisha nitafaidi pesa ya Isaya!!

    Alijisemea Fonga huku akirusha miguu yake huku na kule kama kwamba jambo hilo ni dogo na litamalizika mara moja!!

    Laiti angejua kisa cha Betty kutoweka, laiti angeonyeshwa japo kwa sekunde kadhaa tu mchezo ambao anataka kuingia kuucheza.

    Basi angeghairisha mara moja na kuendelea na maisha yake ya kuunga-unga jijini Dar es salaam!!

    Lakini Mungu ni wa ajabu, hata sekunde moja ya mbele yako hujui nini kitatokea.

    Fonga mtoto wa Manzese, akajiingiza kichwakichwa mchezoni!!



     Asijue kuna nini kimejificha nyuma ya pazia!!

    *****

    Betty alijaribu kuangaza huku na kule huenda atapata walau picha ya eneo ambalo alikuwa, lakini bahati mbaya hakuwa mwenyeji wa kona nyingi za jiji hilo. Hakupata hata hisia ya mahali alipo. Na angeweza vipi kujipa uhakika kuwa yupo jijini wakati safari ya kutekwa kwake ilichukua zaidi ya masaa mawili. Huku akiwa amefungwa kitambaa usoni na bunduki shingoni iwapo ataleta usumbufu wowote ule. Kuna muda gari lilienda kwa mwendo kasi mkubwa na kuna muda lilipunguza mwendo, kuna muda lilipita barabara yenye mabonde na kuna muda barabara ilikuwa imenyooka. Betty alikuwa amepotezwa uelekeo kabisa, hadi alipofunguliwa tena kile kitambaa na kukutana na watu asiowajua!! Tofauti kabisa na wale waliomteka maeneoya Kinondoni wakijifanya kuwa wao ni askari polisi. Kuna sura zilionyesha ugaidi mkubwa na zilitisha kuzitazama, lakini nyingine zilikuwa sura zilizojaa upole. Betty alitarajia kukutana na maswali mazito ambayo atashindwa kuyajibu na hatimaye kupokea kipigo kutoka kwa majangili wale. Lakini kwa siku ya kwanza aliishia kuulizwa jina lake na historia yake kwa ufupi.

    Betty aliielezea kwa ufupi kweli, japo alikuwa anatetemeka!! Alielezea alipozaliwa na anapoishi kwa sasa, alikumbuka pia kutaja elimu yake kwa uchache. Siku zikaendelea kukatika asijue ni kipi kilichosababisha afanyiwe jambo lile. Betty akaona kukaa kimya haitakuwa na maana akaamua kuuliza.

    Alimuuliza mwanaume ambaye mara kwa mara alikuwa akimpelekea chakula katika chumba alichokuwa amehifadhiwa.

    “Dada, mimi sijui lolote kwa kweli yaani naishi kwa kanuni. Mimi wajibu wangu ni mambo ya usafi na chakula. Mengineyo sijui hata.” Alijibu kijana yule huku akijaribu kujitoa katika hatia. Jibu hili likamvuruga zaidi Betty. Akafikia maamuzi ya kumuuliza yeyote yule ambaye atakuja mbele yake.

    Huenda atamfikia muhusika na kupata jawabu. Kutekwa gani huku, hapigwi, hanyanyaswi wala hagombezwi na anakula chakula kizuri tena kwa wakati!! Aliisubiri hiyo siku ya kuonana na mtu mwingine tofauti na yule muhudumu lakini haikufika upesi kama alivyotarajia. Hadi wakati huu akijiuliza ni eneo gani la jiji la Dar es salaam anaweza kuwa yupo. Bado hakuwa na jibu la ni kwa nini amefichwa hapo? Bila kudaiwa chochote, bila kunyanyaswa!!!

    ****

    FONGA hakutaka kulaza damu, alijipa tahadhari kuwa alikuwa amechukua pesa ya Isaya tayari na hivyo kwa namna yoyote lazima afanye jambo la maana na busara ili aweze kuendelea kula pesa ya kijana huyo na pia aweze kuchuma pesa zaidi.

    Hakutaka kuchelewa zaidi, akafanya mawasiliano na Joyce Kidoti.

    Akitaka waonane. Joyce aliipokea simu hii kwa sauti iliyoonyesha kukata tamaa, Fonga alilitambua hilo lakini hakutaka kuuliza kupitia simu.

    Kidoti akamuelekeza nyumbani kwake, Fonga akaanza safari upesi, akipitia njia za mkato ambazo zingemwezesha kufika upesi. Majira ya saa tatu usiku alikuwa nyumbani kwa Joyce. Walizungumza kwa kina.

    Joyce akihitaji pesa nyingine ya ziada lakini kwa minajiri ya kuirejesha baada ya siku tano, Fonga naye akihitaji kujua juu ya Betty na ukombozi upi ulikuwa unahitajika aweze kuwa huru. Joyce, alitamani sana kumpa majibu yote kama yalivyo Fonga lakini lile onyo la kutomshirikisha mtu yeyote katika mpango huo ndio lilikifanya kinywa chake kuwa kizito kusema lolote.

    Akasita kumweleza Fonga juu ya masharti ya watekaji wale ambao hadi wakati huo hakuwa akiwafahamu kwa majina wala sura.

    “Joyce unatakiwa ujenge imani na mimi. Uniamini name nikuamini wewe nd’o tutaweza kulitatua tatizo hili, vinginevyo litakuwia gumu sana hakika. Niambie kama kuna watu Betty ana ubaya nao labda au aliwadhulumu…eeh!!” Fonga alisihi huku akipapasa bega la Joyce.

    Joyce akapinga kuwa hakuna lolote ambalo anajua kuhusu kutekwa kwa Betty lakini kuna watu anahitaji kuwapatia pesa washughulikie tatizo hilo.

    “Baada ya kuona mimi nakubabaisha si nd’o hivyo Joy.” Alisema katika namna ya kusuta Fonga.

    Joyce akainama chini asijue namna gani anakabiliana na hali ile. Kimya kikatanda kwa dakika kadhaa, kisha Joyce ambaye alipitiwa na mawazo mengi kwa muda akakiri katika nafsi yake kuwa alikuwa amefikwa na kama ni maji sasa yalikuwa ‘maji ya shingo’.

    Akaamua kutumia ule usemi wa liwalo na liwe. Akaamua kumshirikisha Fonga juu ya jambo hili, ili walau apunguze mzigo alionao kichwani mwake.

    “Fonga, sina budi kukueleza. Nakueleza kwa sababu nakuamini sana na ninajua utanisaidia, kama ulivyonitafutia pesa ile nyingi naamini hili halitakushinda, wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini hebu nikushirikishe…” alisita kuzungumza pale simu ya Fonga ilipotoa mlio wa kupokea ujumbe.

    “Aah endelea..” Fonga alitaka kuupuza na kumsikiliza Joyce, lakini Joyce alimpa ishara kuwa ausome kwanza ndipo aendelee.

    Fonga akatii, akaufungua ujumbe ule katika simu yake. Baada ya kuusoma huku akiwa anaukazia macho, hapakuwa na mazungumzo tena ndani ya chumba hicho. Mashaka yakatawala, hofu kila nukta. “Kuna nini kwani Fonga.” Aliuliza Joyce.

    “Nitakueleza…..we nielekeze mlango mwingine wa kutokea kama inawezekana.” Aliongea sauti ya kunong’ona huku jasho likimtoka.

    “Hakuna mlango zaidi ya huu!!” Joyce naye asiyejua nini kinatokea alimjibu Fonga. Maisha ya jela, hutanua akili sana.

    Mara nyingi mfungwa hubuni akili zaidi ya mwenzake ilimradi tu aweze kumtawala ama la aepuke kuonewa.

    Mfungwa si mbumbumbu!!

    Fonga aliyewahi kutumikia kifungo cha miezi tisa jela, alikuwa na mabaki ya umachachali wa jela. Alitazama huku na kule kisha akaona chuma ngumu ambayo ilikuwa imeegemezwa katika mlango. Akaitwaa na kukimbilia chumbani kwa Joy, Joy akamfuata nyuma huku akiwa ametaharuki sana. Akaingiza ile chuma katika nondo za dirisha la chumbani.

    “Wewe nyumba ya watu laki…..”

    “Shhhhh!!” Fonga alimnyamazisha, huku macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa mekundu sana, jasho likimtoka lakini hakuwa na uoga tena.

    Na kwa mara ya kwanza Joyce akatambua kuwa Fonga alikuwa mtu wa mazoezi, pale alipoishuhudia misuli yake wakati akitumia chuma kile kutanua dirisha. Nafasi ikapatikana, Fonga akamuamuru Joyce apitie dirishani, Joyce akauliza kwa nini. Fonga akamnasa kofi mgongoni nakishaakatumia amri!!

    Joyce akiwa ameduwaa Fonga alimbeba juu juu na kufanikiwa kumpitisha katika tundu lile.

    “Joyce,ni muda wa kuniamini mimi. Mimi tu! Joyce, kuna tatizo kubwa niamini nakusihi niamini mimi. Tumevamiwa na watu wabaya..” Fonga alimweleza kwa sauti ile ile ya kunong’ona.

    “Nimeacha hela jamani……pale mezani…” Joy alilalamika huku akipiga piga miguu chini kama anayekaribia kujikojolea. Fonga akaruka upesi, akakimbilia sebuleni. Akakwapua pochi ya Joyce. Akarejea tena chumbani na kupita katika tundu la dirisha lililotanuliwa. Alionekana ana mwili mkubwa lakini alitua kama paka!!! Bila vishindo!!

    Akamshika Joyce mkono , wakaanza kutoweka eneo lile. Hawakufika mbali sana, kikasikika kishindo.na umeme ukakatika katika nyumba aliyokuwa anaishi Joyce. Kabla hawajashangaa zaidi ukasikika mlio wa bunduki!!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Joyce akataka kupiga kelele, Fonga akawahi kumziba mdomo!!

    “Wangeniua hawa mabwege aisee!!!” alisema Fonga kwa masikitiko!! Joyce akabaki kuduwaa!!

    Safari yao ikaishia katikanyumba ya kulala wageni!!! Waliingia kama bibi na bwana!!

    Usiku ukawakuta wakiwa wamekumbatiana!!

    *****

    UMAARUFU ni jambo jema na baya kwa namna moja au nyingine. Umaarufu unaweza kukuletea matatizo na wakati mwingine kukuweka mbali na tatizo.

    Umaarufu mwa mtu husababisha jina lake kutamkwa na watu wengi, aidha kwa mazuri ama mabaya, kiurafiki ama kinafiki. Hivyo ndivyo jina la Fonga lilivyotajwa na watu mbalimbali.

    Fonga alikuwa maarufu haswa.

    Wengi walilifahamu jina tu bila kuifahamu sura na bado waliweza kumzungumzia kama waliwahi kumuona.

    Namba yake ya simu ilitapakaa na kuwafikia wengi, walioitaka huduma yake waliwasiliana naye. MALLE Stan, alikuwa mmoja kati ya watu waliowahi kusikia jina hilo na kuipata namba yake baadaye katika mazingira mengine. Alilisikia jina lake lilivyokuwa maarufu kisha siku aliyokutana naye akajikuta akifadhaika kukutana na mtu wa kawaida sana tofauti na jina lake.

    Ni siku hii aliyoamua kuchukua namba yake baada ya kuwa amefanya naye mazungumzo ya muda mrefu kama rafiki waliyekutana kwa dharula.

    Walikutana katika daladala, wakaketi siti moja. Fonga alipopigiwa simu na kujitambulisha, Malle akaanzisha urafiki akamuuliza iwapo ni yeye avumaye. Fonga hakuzungusha maneno kwa sababu alitambua fika kuwa alijulikana na wengi.

    Akakubali nakuendelea na stori za hapa na pale hadi kila mmoja alipofika mwisho wa safari.

    Usiku huu mnene wakiwa katika kutekeleza kazi waliyopewa na mkuu wao wa kazi. Analisikia tena jina hili la Fonga na sasa akiwa na namba yake ambayo wenzake hawakuwa nayo.

    Jina hili lilitajwa na wenzake watatu, likiwa jina geni kwao. Lakini kwake lilikuwa halina ugeni wowote. Akajiuliza je ni Fonga huyo huyo ama? Hapakuwa na sifa yoyote mbaya katika jina hili, na mbaya zaidi kumfahamu kabla ya tukio hilo kukamweka katika hatia ya kujiona akijihusisha katika mauaji ya mtu ambaye anamfahamu.

    Malle, hakuwa tayari na hakuwahi kuua mtu anayemfahamu walau kwa jina tu. Kwa matukio haya ili asiyakumbuke alikuwa tayari kuua asiowafahamu mia kuliko mmoja anayemfahamu. Hali hii iliathiri sana ubongo wake!!

    Alijua kuwa wakifanikiwa kuingia katika nyumba ile isiyokuwa na mlinzi basi hataweza tena kumtetea Fonga. Wakati ulikuwa ni ule.

    “Roho yake ipo mikononi mwangu!!” Malle alijisemea. Akachukua simu yake akautuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda katika namba ya Fonga!! Namba aliyopewa siku ile katika gari!!

    “Kama upo na Joyce, ondoka naye fasta. Kuna wajinga wanaitaka roho yako usiku huu kisha wanaondoka na Joyce. Fasta….” Ujumbe ukatumwa!!!

    Ni ujumbe huu uliomkurupua Fonga na kufanikiwa kutoroka asijue aliyemuokoa ni nani…. Malle akiungana na wenzake watatu waliivamia nyumba ile katika hali ya kishari shari kama walivyokubaliana. Malle hakuwa na imani kuwa ujumbe ule umesomwa na Fonga huyu anayetaka kuuawa usiku huu ama la!

    Lakini kitendo cha kuikuta nyumba tupu, kisha walipoingia chumbani wakakuta nondo imetanuliwa.

    Malle akakiri katika nafsi yake kuwa Fonga ni zaidi ya anavyomfikiria!!!

    Hakutarajia angekuwa mwepei kiasi hicho. Majambazi wengine nao wakakiri kuwa. Fonga alikuwa kiboko!!! Hawakujua kuwa mwenzao mmoja aliwazunguka. Wakatoweka baada ya dakika kumi za kutikisa mtaa!!

    Asubuhi na mapema walikuwa mbele ya meza ya kung’ara ya Mzee Beka.

    “Sijaona kichwa cha habari hata kimoja juu ya kifo chake!!” Beka aliunguruma huku akizunguka katika kiti chake. “….kapitia dirishani aisee…sijui kashtukaje tu” alijibu kiongozi wao.

    “Yeye nd’o ----- ama nyie aliyewatoroka? mnamuita …., yaani anapita na yule Malaya wake dirishani mnasema -----. Bastard!!!” aling’aka huku akitabasamu, vijana wale wakatambua kuwa amechukizwa na kilichotokea.

    Kila alipokasirika alikuwa akitabasamu. Hawakuwa na cha kujibu!!! “Sihitaji maelezo marefu zaidi. Sitanunua gazeti lolote hadi mtakaponiletea gazeti likizungumzia kifo cha Fonga!!” aliamrisha kisha akafanya ishara ya kuwafukuza vijana wale!!

    “Na sihitaji kukaa wiki nzima bila kusoma magazeti….” Alimalizia huku na wao wakimalizia kutoka nje ya ofisi ile. Beka akisema huwa anamaanisha!! Hilo walilitambua, kila mmoja akaondoka na lake kichwani akijaribu kutafakari ni namna gani watamridhisha Beka. Kasoro Malle tu!! Yeye aliwaza juu ya Fonga!!



    Asubuhi na mapema walikuwa mbele ya meza ya kung’ara ya Mzee Beka.

    “Sijaona kichwa cha habari hata kimoja juu ya kifo chake!!” Beka aliunguruma huku akizunguka katika kiti chake.

    “Bwege kapitia dirishani…sijui kashtukaje tu” alijibu kiongozi wao.

    “Yeye nd’o bwege ama nyie aliyewatoroka?mnamuita bwege, yaani anapita na yule Malaya wake dirishani mnasema bwege. Bastard!!!” aling’aka huku akitabasamu, vijana wale wakatambua kuwa amechukizwa na kilichotokea. Kila alipokasirika alikuwa akitabasamu.

    Hawakuwa na cha kujibu!!!

    “Sihitaji maelezo marefu zaidi. Sitanunua gazeti lolote hadi mtakaponiletea gazeti likizungumzia kifo cha Fonga!!” aliamrisha kisha akafanya ishara ya kuwafukuza vijana wale!!

    “Na sihitaji kukaa wiki nzima bila kusoma magazeti….” Alimalizia huku na wao wakimalizia kutoka nje ya ofisi ile.

    Beka akisema huwa anamaanisha!!

    Hilo walilitambua, kila mmoja akaondoka na lake kichwani. Kasoro Malle tu!!

    ****

    SAA nane usiku,si Joyce wala Fonga aliyekuwa amepata usingizi. Japo walipeana migongo na kila mmoja kutulia kana kwamba amesinzia.

    Joyce ndiye aliyekuwa na hofu zaidi. Mwanzo alijihisi yu salama sana na mtu ambaye alistahili kuonewa huruma alikuwa ni Betty pekee. Sasa mambo yamebadilika na yeye anahofu juu ya uhai wake.

    “Fonga….we Fonga!!” Joyce aliita huku akimtikisa Fonga.

    Fonga akageuka na kutazamana na Joyce.

    “Ni nini kimetokea, na ule mlipuko sijui risasi, kuna nini Fonga?” aliuliza Joyce.

    Fonga akachefuliwa na lile swali, lilikuwa la kitoto sana, Joyce alifahamu fika kuwa wote walikuwa katika kukimbia uliposikika ule mlio. Sasa kulikoni anamuuliza yeye. Alitaka kumjibu vibaya lakini akajionya kuwa Joyce anaweza kumfikiria vibaya. Isitoshe bado hajawa na uhakika kama penzi litachanua ama kusinyaa na kutoweka.

    “Tutazungumza asubuhi Kidoti. Kwa sasa lala!! Maana halipo jipya.” Alijibu kisha akampa tena mgongo..

    “Ah ah Fonga…nataka kujua sasa hivi.” Alilazimisha huku akimgeuza tena yule mwanaume.

    “Kidoti, nikikwambia unatafutwa uuwawe nd’o kipi sasa utafanya usiku huu.” Alisema kwa hamaki kidogo.

    Joyce akakodoa macho, akajutia kulazimisha kuelezwa jambo hilo usiku huo. Japokuwa alikuwa amelala kitanda kimoja na Fonga bado hakuhisi amani, akaamua kumkumbatia kabisa ili aamini kuwa wapo wote kitandani.

    Usingizi ulimpitia baadaye sana!!!

    ***

    UZURI wa chuo kikuu cha Dar es salaam ni uwingi wa wanafunzi. Unaweza kusoma miaka mitatu na ukamaliza masomo yako bila kufahamu wanafunzi wenzako.

    Baadhi ya masomo kuna wanafunzi hadi mia nane. Hivyo ni ngumu sana kumfahamu mwanafunzi mmoja mmoja. Vinginevyo uamue kabisa kumfahamu kwa matakwa binafsi.

    Hakuwahi kuvaa mavazi ya aina ile, lakini siku hii alilazimika kuyavaa. Nikabu!!

    Alikuwa akionekana macho yake tu na viganja vya mikono. Alikosa amani kabisa lakini alilazimika kuwa hivyo!!

    Miezi iliyobaki ili mwaka wa chuo uweze kumalizika ilikuwa mingi sana kutokana na hali halisi.

    Kwanza rafiki yake kipenzi hajulikani alipo, kabla hajakaa sawa anakutana na mwanaume anampatia pesa naye anampatia penzi.

    Hii haikuwa jibu!! Bado likaongezeka jingine la kuvamiwa nyumbani kwake akiwa na huyo mwanaume. Tukio hili la ajabu linamtatanisha na kumweka katika maswali.

    Akiwa hana ndugu wala rafiki, anaamua kumuamini Fonga. Mwanaume ambaye alimpa pesa kwa penzi kisha wakakumbanana tukio la ajabu.

    Akaamua kumsikiliza Fonga kwa atakalosema. Hakuwa na ujanja!!

    Hakuijua historia yake lakini akaamua kumuamini!!

    Sasa Fonga alikuwa amemuamuru awe anavaa Hijabu ambalo ataificha sura yake humo. Akapewa sharti la kutoitembelea tena nyumba yake iliyovamiwa usiku ule. Fonga alisema mengi ya muhimu!! Joyce akayasikiliza kwa makini moja baada ya jingine.

    Kisha akaambiwa neno la mwisho!! Naye akalikariri.

    “Mengineyo niachie mimi!! Betty anarudi na wewe chuo unamaliza”

    Joyce akatii. Kwani maji ya shingo tayari yashamfika.

    Sasa alikuwa darasani akifuatilia kipindi huku akijiuliza nini hatma yake.

    Alipishana na rafiki zake bila kuwasalimia.

    Jambo lililomtesa zaidi!!

    Joyce akahamia nyumbani kwa dada yake Fonga aitwaye Zubeda!!

    Zubeda akamtambua kama wifi yake!!

    Maisha yakaendelea!!!

    *****

    BEKA, mzee aliyefanikiwa kuzichuma sana pesa enzi za ujana wake alikuwa amekaa kitandani akitafakari mambo mengi sana kwa wakati mmoja.

    Ilikuwa ni siku ya tatu, kimya kikiwa kimetanda. Hakuna gazeti lililoletwa katika ofisi yake. Hiyo ilimaanisha kuwa Fonga alikuwa hai na Joyce bado alikuwa mtaani.

    Hii ilikuwa ni fedheha sana kwake, na alikosa imani na vijana wake wa kila siku ambao anawaamini kuwa hawawezi kumuangusha.

    Sasa walikuwa kimya!!

    Mzee huyu ambaye jina la Beka lilikuwa limetapakaa kuliko jina lake la kuzaliwa alikuwa akimtafakari Fonga kisha akamfikiria Joyce Kidoti. Akawaweka katika mzani na kuona Fonga anafanya uvunjaji wa haki za binadamu kuwa katika mahusiano na msichana yule. Beka aliamini kuwa hawaendani hata kidogo!!

    Sasa alikuwa anaitaka roho ya Fonga na akimtaka Joyce akiwa hai!! Lakini atampata vipi iwapo vijana wake machachali walikuwa wanaelekea kushindwa?

    Swali gumu kabisa lililokosa jawabu!!

    Akapiga kite cha hasira na kujitupa tena kitandani!!

    Kisha akachukua simu yake na kuwapigia vijana wake. Akitarajia majibu yoyote yenye uhai aliishia kuambiwa, Joyce hakuwahi tena kukanyaga nyumbani kwake, na Fonga hajulikani alipo.

    Kama hiyo haitoshi, Joyce haingii tena darasani!!

    “Mmejaribu kuangalia kama polisi wamemchukua kwa ajili ya upelelezi wao.” Aliuliza kwa upole.

    “Tumefuatilia kwa makini, polisi walikuja siku mbili tu kisha wakasema upelelezi unaendelea. Bila shaka hawakumpata.”

    “Una uhakika gani kwa kusema upelelezi unaendelea wanamaanisha hawakumpata?” aliuliza huku akicheka kwa dharau.

    “Niliwasiliana mapema na yule Mr. X Inspekta uliyeniunga…..”

    “Haya nimekuelewa…nadhani umeelewa sasa maana ya kukuunganisha naye. Umenifurahisha kwa hilo.” Alijibu Beka kwa utulivu!!

    Kisha akaendelea, “Jitahidini….hapana…hakikisheni wiki haimaliziki bila kumpata huyo mshenzi wa tabia.” Alimaliza na simu ikakatwa.

    Kichwa kilikuwa kinamchemka sana, hakuamini kuwa ni Fonga alikuwa amerejea tenakatika maisha yake!!

    Kwanini Fonga? Kwa nini? Alijiuliza mara mbilimbili huku akijisikia fedheha kuibughudhi akili yake kumfikiria kijana yule!!.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amenitafuta maksudi ama bahati mbaya mimi sitajali na sitajisumbua kumpa onyo….nataka kusoma gazeti kuwa Fonga amekufa…..tena kafa kinyama!!! Alisema kwa sauti ya juu huku akihaha kujirusharusha katika kitanda chake cha kifahari.

    Kabla ya kulala, alipiga simu mahali kuwa anajisikia hovyo na daktari amemzuia kufanya shughuli zozote, hivyo hataweza kuhudhuria mkutano wao walioupanga!!

    *****

    TAARIFA ya Joyce kuvamiwa ilisambaa kupitiamarafiki zake, walihaha kuupata ukweli juu ya wapi Joyce atakuwa amepelekwa.

    Ilionekana balaa sana hali hii ya mwanafunzi kutekwa. Tena mwanafunzi mwenyewe Joyce Kidoti. Msichana maarufu kabisa.

    Kila aliyemjua alipatwa na mafadhaiko.

    Polisi waliowahi kufika eneo la tukio walifanya mahojianona majirani, pia katika upekuzi wakafanikiwa kupata kitambulisho cha kupigia kura!!

    Joyce Kisaka!! Kilisomeka hivyo!!

    Siku iliyofuata wakaenda katika uongozi wa chuo kikuucha dar es salaam. Wakaelekezwa ofisi inayoshughulika na mambo ya wanafunzi, ‘Dean of student’. Huku wakamuulizia Joyce Kisaka.

    Mwanamama mratibu wa ofisi ile akasaka hilo jina na majibu yakawa ‘hakuna mwanafunzi aitwaye Joyce Kisaka’ katika orodha yake.

    Polisi wakashangaa, kwani kila aliyekuwa jirani nanyumba hiyo alitambua kuwa mkaaji wa nyumba ile alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu. Japo hawakujua ni mwaka wa ngapi.

    “Nilisikia wakisema anaitwa Kidoti sijui…” alisema polisi mmoja jina hilo maarufu.

    “Ahaaa!! Joyce Kidoti…..huyo sawa!!” alisema kwa furaha yule mwanamke huku akibofya kompyuta yake na kisha kuwaonyesha sura iliyopo katika jina la Joyce Keto.

    Sura ya Joyce Keto na Joyce Kisanga ilifanana. Kikubwa zaidikilichofananisha sura hizikilikuwa ni kidoti.

    Polisi wakajiuliza kwanini anatumia majina mawili tofauti.

    Hawakujua kuwa Joyce Keto ni jina la kununua tu na jina halisi ni Joyce wa Kisaka.

    “Huyu Joyce Keto unayemsema unamtambua uwepo wake chuoni?” askari mmoja alimbana swali yule mama asiyeisha kutabasamu.

    “Aaaah…..ok….hebu ngooja..” aliongea kwa kusita huku akibofya kompyuta yake.

    “Alright!! Joyce Keto ana ruhusa, alichukua siku ya jumatatu, siku nne zimepita sasa si leo nd’o ijumaa eeh.” Alisema yule mama. Kisha akaendelea, “Halafu alisema akifika Makambako atanipigia huyu mtoto jamani.” Alilalama.

    Polisi wakaduwaa, nyumba anayoishi ilivamiwa siku ya jumatano.

    Ina maana Joyce aliondoka siku mbili kabla? Kwa hiyo hajui kaqma amevamiwa? Haya yakawa maswali.

    “Hivi kwani nyie ni kina nani jamani eeh maana siwaelewi elewi.” Ghafla yule mama kutabasamu akaficha tabasamu lake sasa akawa makini, na kuwauliza wanaume wale.

    Wakajitambulisha kuwa ni askari, tabasamu likaendelea!!

    Polisi hawakuwa na jingine.

    Tukio la nyumba ile kuvamiwa likahesabiwa kama kesi ya kawaida tu ya ‘kuvunja na kuiba’.

    Cha msingi aliyehisiwa kujeruhiwa alikuwa hayupo siku ya tukio basi amani ikatawala tena!!

    Kwa akili hii ya kushikiwa na Fonga, Joyce alitikisa kichwa na kukiri kuwa Fonga alikuwa ‘Babu kubwa’. Kwanza katika mchezo huu alianza kwa kuwaondoa polisi mchezoni, wasijisumbue kumtafuta Joyce ambaye hakuwepo siku ya tukio.

    Pili alimtengenezea Joyce mazingira ya kutuliza akili yake, ili asije akafeli masomo yake ambapo mitihani ilikuwa imekaribia!!

    Huo ukawa mwisho wa Joyce kuhudhuria chuoni kwa amani huku akiwa na ruhusa maalumu. Ruhusa ambayo aliipata tarehe ya kufoji kwa kutoa pesa.

    Mama kutabasamu akaingiza katika pochi shilingi laki moja.

    Japo alitokwa kijasho kusikia Joyce anatafutwa na askari, lakini hakuthubutu kumkana kutokana makubaliano.

    Kwa kufanya hivyo angejipotezea pia kibarua chake alichosotea mpaka kukipata!!

    Mchezo ukaendelea vyema!!

    Fonga akazichanga karata!!

    Joy akaendelea kuishi na Zubeda maeneo ya Machimbo!!!

    ****

    ISAYA alikuwa mmoja kati ya wanachuo ambao si tu walikuwa wamechanganyikiwa bali walikuwa wanakaribia kurukwa na akili kabisa.

    Taarifa ya kupotea kwa Betty ikiwa haijatulia katika kichwa chake, mara anasikia Joyce Kidoti kavamiwa,jibu la kwanini kavamiwa nalo likiwa halina wa kujibu. Linatokea zito jingine kabisa kuwa siku anayovamiwa hakuwepo kwake.

    Uthibitisho zaidi ni kuwa alikuwa na ruhusa siku mbili kabla.

    Isaya akachanganywa sana na taarifa hii!! Akaiona kama ni ya kuundwa vile. Lakini nani wa kuiunda kisomi kiasi kile? Alishangaa.

    Hakika alitakiwa kuhisi hivyo maana. Siku ya jumatano kuna rafiki alimtembelea Joy kisha akampigia simu Isayana kumwambia kuwa ametoka kwa Betty muda mchache uliopita.

    Lakini katika kuvamiwa inasemekana Joyce hakuwepo.

    Hapana!! Joyce katekwa si bure hii!!

    Isaya alikataa kata kata yeye na nafsi yake.

    Katika kukataa huku akaamua kumpigia simu Fonga ili aweze kumpadili la kumfuatilia Joy huku akiendelea kuhakikisha Betty anapatikana.

    Akajaribu kupiga simuya Fonga!!

    Simu haipatikani!!!

    “Fonga naye kwa vimeo aaargh!”alilalamika, huku akijaribu tena na tena pasi na mafanikio.

    Isaya hakutaka kulazia damu hili jambo, kwa sababu alipajua nyumbani kwa Fongaakaamua kumfuata huko huko.

    Hakuwa na hofu na lolote kwa sababu alikuwa anatumia gari binafsi. Hata asingemkuta bado isingemgharimu chochote.

    Isaya akaenda peke yake nyumbani kwa Fonga.

    Akapita njia za mkato Mabibo, akaibukia Manzese.

    Nyumbani kwa Fonga hapakuwa na mtu.

    “Alikuwa hapa leo lakini akaondoka, hakusema anaenda wapi.” Kijana mmoja alimjibu Isaya.

    Gari lilipotoweka kijana yule akanakiri namba!!

    Huyu alikuwa ni kijana wa Fonga!!

    Kijana katika oparesheni yake ambayo alikuwa hajaipa jina.

    ****

    Wakati Isaya anafika nyumbani kwake. Yeye Fonga alikuwa njiani kuelekea Machimbo kuonana na Joyce. Kuna jambo muhimu ambalo Joyce alihitaji kujadili naye, hata Fonga naye alihitaji kumweleza Joyce juu ya maendeleo ya mchakato huo ambao kwa wakati huo ulikuwa mchakato wa kumrejesha Betty uraiani akiwa hai.

    Kama walitarajia kuonana kwao ni kwa ajili ya kujadili kuhusu Betty pekee basi hawakuwa sawa hata kidogo!!

    Ilizuka vita mpya,huenda ngumu kuliko ile ya awali ambayo Fonga alikuwa amejipanga kukabiliana nayo!!



    Wakati Isaya anafika nyumbani kwake. Yeye Fonga alikuwa njiani kuelekea Machimbo kuonana na Joyce. Kuna jambo muhimu ambalo Joyce alihitaji kujadili naye, hata Fonga naye alihitaji kumweleza Joyce juu ya maendeleo ya mchakato huo ambao kwa wakati huo ulikuwa mchakato wa kumrejesha Betty uraiani akiwa hai.

    Walikutana maeneo ya Buguruni. Fonga hakutaka kukutana naye nyumbani kwa dada yake kwa sababu kwa kufanya hivyo angeweza kuongeza tatizo juu ya tatizo. Tayari alishatambua kuwa kuna watu wabaya nyuma yake wanamfuatilia yeye na Joyce. Hakujua sababu lakini alichukua tahadhari mapema. Kama ilivyo ada akamwelekeza Joyce aina ya mavazi ambayo alitakiwa kuvaa.

    Naye akatii!! Katika mgahawa mmoja akaonekana msichana akiwa na baibui akizungumza na mwanaume!!

    Fonga na Joyce!! Mazungumzo haya yalihusiana na hatma ya maisha ya Joyce na muafaka wa Betty huko alipo. Fonga hakukurupuka kujibu badala yake akamuuliza swali.

    “Joy!! Unajua kuwa roho ya Betty ipo mikononi mwako?”

    “Una maana gani wakati wewe umenihakikishia kuwa nitarejea shuleni na Betty atapatikana?” aliuliza kwa hamaki kidogo.

    “Joyce!! Kuna jambo lolote ambalo unanificha labda kuhusiana na tukio hili, yaani lolote hata kama ni la kihisia wewe nieleze mimi na hapo nitajua wapi wa kuanzia sawa mamii” Fonga alisihi huku akiyatazama macho ya Joyce kutokea katika nikabu!!!

    “Mi kwa kweli sijui lolote kuhusiana na Betty, zaidi ya hayo yote niliyokwisha kueleza zamani.” Alijibu Joyce katika namna ya kukwazika na kukata tamaa.

    Fonga alimung’unya midomo yake huku akitikisa mguu wake wa kulia kama vile amegundua jambo tayari.

    Naam! Fonga alikuwa akijaribu kufikiri mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kusababisha Joyce na Betty wawe matatani. Mwanzoni alitupa karata yake katika mambo ya pesa lakini kwa mtazamo tu Joyce hakuwa na pesa, lakini alikuwa na urembo ambao ungeweza kumletea pesa nyingi tu. Alipofikiria jambo hili akajiuliza, kwanini hana pesa? Jibu sahihi kutokana na hisia zake likawa, amegoma kutumia urembo wake kujipatia pesa. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa amewakataa wanaume wengi sana wenye pesa zao, jambo hili huenda limewakasirisha na sasa wanalipiza kisasi. Sasa hawa wanaume ni akina nani? Akajiuliza kisha akamtazama tena Joyce.

    “Nani alikuwa mpenzi wako siku za nyuma? Hapa chuoni!”

    “Sijawahi kuwa na mpenzi mimi, mbona waniuliza maswali hayo jamani?” alifoka kidogo. Fonga hakujali.

    “Ina maana tangu uje hapa chuo hujajihusisha na mapenzi?”

    “He! Fonga unataka nikuchoree nd’o uamini ama maana nasema hunielewi.” Alikazia Joyce. Fonga hakutaka kuendelea kuhoji, akaamua kutupa karata nyingine ambayo Joyce bila kujua kuwa ni karata ileile kama ya awali alijikuta akiipokea vizuri.

    “Joyce, ujue tunahitaji pesa ya ziada katika jambo hili, kuna maadui wametuzunguka. Tunachokitafuta sasa sio tu kupatikana kwa Betty, bali tupo katika kuitafuta amani yetu pia.

    Maana kwa sasa hata serikali inaamini kuwa sisi ni waarifu, hakuna anayetuamini hata mmoja. Hivyo ni sisi tunatakiwa kutafuta kuaminiwa na turejee katika maisha yetu ya awali. Nikisema jambo hili lazima mimi na wewe tushirikiane namaanisha kuwa tusifichane lolote lile, nimekuamini nikaamua kukusaidia nawe niamini kama nikuaminivyo!!” alihitimisha Fonga.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakuelewa sana Fonga na ninajitahidi sana kuwa mkweli kwako. Hakuna jambo ambalo ninakuficha.” Alisisitiza Joyce kwa kujiamini. Fonga aliisoma akili yake na kugundua alikuwa ni mtu wa kukata tamaa upesi sana. Akatikisa kichwa kumsikitikia.

    “Ehe! Ulikuwa nawe una jambo gani la kunishirikisha.” Fonga aliuliza kivivu vivu.

    “Ahaa! Ni kuhusu kutafuta mtu mwenye nyadhifa serikali aweze kutusaidia katika jambo hili ama waonaje wewe.” Alisema Joyce.

    “Tunampata wapi mtu huyo sasa, na unajuaje kama mtu anayetukosesha amani naye ni wa huko serikalini? Huoni kama unataka kujikabidhi katika domo la mamba kiulaini.” Fonga alijibu kwa utulivu!! Maneno yakamuingia Joyce akilini. Akakiri tena kuwa Fonga alikuwa mtu wa aina yake, alikuwa na akili ya ziada.

    Uwezekano huo wa kupata mtu wa serikali ambaye atawasaidia ukafutwa rasmi. Wakaendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale kisha wakaagana. Fonga akizidi kumsisitiza Joyce kuwa amuachie mambo yote yeye na kila kitu kitaleta majibu ya uhakika.

    JOYCE alihangaika kuupata usingizi kwa siku ile, alikuwa ameichoka hali ile ya kukosa uhuru wake aliokuwa ameuzoea. Akafikiria sana na kuona kuwa

    Fonga hana lolote la kumsaidia zaidi ya kuzungusha maneno yenye ushawishi. Kitu ambacho Joyce hakukipinga ni kuwa Fonga alikuwa ana nia lakini huwezo hakuwa nao.

    Uwezo wa kupambana na adui asiyefahamika. Joy akaukumbuka usemi wa akili ya kushikiwa changanya na ya kwako, akaanza kulitafuta jibu la ni kwa namna gani anaweza kujiweka huru.

    Akafumba macho yake mara akakumbuka kisanga cha takribani mwaka mmoja uliopita. Kisanga ambacho hakutaka kukikumbuka katika maisha yake japo kiligoma kujifuta akatika akili yake siku zote licha ya kupitia mengineyo mengi. Hiki kilikuwa kisa ambacho aliamua kuishi nacho kwenye akili yake tu!! Hata rafiki yake wa damu kabisa Betty, hakuwahi kumshirikisha juu ya jambo hilo. Hakumshirikisha kwa sababu hakutaka kulikumbuka kamwe!!

    MISS CHUO KIKUU, 2007

    WAHKA wa kutawazwa kuwa mrembo wa chuo kikuu ulikuwa umempanda, sifa kemkem alizokuwa amemwagiwa zilimfanya azidi kupagawa na kutamani kuonyesha kuwa anaweza. Walikuwa warembo ishirini waliokuwa wakichuana vikali kuwania taji hilo. Jina lake lilitajwa midomoni mwa wadau wengi wa mambo ya urembo kama mshindi mtarajiwa. Jambo hilo lilimtia hamasa sana!

    Akamfikiria mpinzani wake mkuu aliyeitwa Monica, akatabasamu na kuifikiria siku ambayo atavikwa taji la urembo huku Monica akisimama pembeni kama mshindi wa pili. Monica nd’o alikuwa mpinzani wake haswaa!!

    Kambi ya Joyce Kidoti walimtegemea kijana Fonga kwa ajili ya kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka kambi pinzani, hivyo kuwawezesha kujipanga vyema wasitetereke. Siku nne kabla ya mpambano ndipo kikatokea kisanga hicho cha aina yake. Joyce alipokea simu kutoka kwa mwanaume aliyejiita Bernad Karama.

    Alijitambulisha kama jaji mwenye ushawishi na aliyepewa mamlaka zaidi katika shindano hilo la ulimbwende. Joyce alimuuliza iwapo anamuhitaji kwa mambo binafsi ama ni kwa shughuli hiyo iliyopo mbele yao. Bwana Karama akamweleza kuwa ni shughuli ya kiofisi zaidi na ilikuwa lazima waonane jioni hiyo hiyo. Joyce akakubali wito huku akijionya kuwa iwapo patakuwa na jingine la ziada basi atakataa.

    Akafunga safari hadi maeneo ya Changanyikeni, ni huku bwana Karama alikuwa amemuelekeza. Kwa sababu mshiriki alikuwa ni yeye basi hakulazimika kwenda na mtu mwingine. Majira ya saa moja usiku alikuwa nyumbani kwa Karama. Bwana huyu akamueleza kuwa amelishikilia taji la mrembo wa chuo kikuu, na ni yeye atakayeamua kumpatia aidha yeye Joyce ama kumpatia Monica. Joyce hakuelewa mara moja bwana yule anamaanisha nini. Lakini kadri alivyozidi kujipambanua ndipo walipolifikia lengo. Karama alikuwa anahitaji penzi la Joyce ili aweze kumpatia ushindi!! “Joyce, acha kuwa kamamtoto mdogo. Ni nani atakayejua kuwa jambo hili limetokea unadhani? Kumbuka kuwa unao mashabiki wengi sana huenda kuliko Monica lakini ni mimi nitakayetoa kura kuu ya mwisho.” Alisisitiza Karama huku akionekana kumaanisha alichokuwa akisema. Joyce alikuwa kimya akitafakari juu ya maneno ya Karama na kisha kujiuliza ataweza vipi kuzihimili kelele za mashabiki wa Monica iwapo atashindwa katika mchuano huo. Akafikiria mengi na kisha kujikuta katika mtego wa Karama. Mtego ambao aliamua kuubakisha kama siri yake ya maisha kwa sababu hakutaka kila mtu aujue udhaifu wake kutokana na kelele za mashabiki. Joyce akakubaliana na Karama usiku uleule. Wakati Karama akidhani kuwa Joyce ni msichana kama wasichana wengine wenye uzoefu katika mambo hayo mbele yake, alijikuta katika wakati mgumu wa kupambana na Joyce ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya mapenzi. Karama akaitoa bikra ya Joyce!! Maajabu!! Maajabu asilani!

    SIKU ya mpambano, jaji Karama alikumbwa na dharula hakuweza kuhudhuria mpambano huo wa kukata na shoka. Mchuano wa ulimbwende. Hali ya kutomuona Karama katika meza ya waamuzi ilimtia Joyce katika mashaka na kujikuta akikosa lile tabasamu lake halisi. Akakosa uchangamfu na mwisho wa mpambano. Monica akaamuriwa kuwa mshindi!! Joyce Kidoti akiikamata namba mbili kwa masikitiko makubwa. Hakumweleza mtu yeyote juu ya jambo lililotokea kati yake na Karama.

    Baada ya jumamoja ndipo usumbufu ulipoanza, Karama akarejea tena katika maisha yake. Sasa alikuwa akitaka kumuoa Joyce, jambo lililopingwa vikali na binti huyo. Alipinga haswa. Karama hakuchoka kubembeleza, alisisitiza kuwa yupo tayari kumtambulisha kwa wazazi wake na kisha kumchumbia kisha amuache akiwa anasoma. Lakini bado Joyce akuvutika na mwanaume huyo aliyemtoa usichana.

    Sasa Joyce amekwama, anakumbuka kuwa yule jaji Karama sasani mbunge. Ana heshima kubwa katika jamii, na kutokana na tatizo alilonalo anaamua kumtafuta ili aweze kumsaidia na amani iweze kurejea tena. Anaitafuta namba yake na kuipata kupitia watu kadhaa aliofahamiana nao. Anampigia simu na kujitambulisha, Karama anazungumza kwa shangwe sana na asiamini kile alichokuwa anakisikia. Wakapanga kukutana!! Joyce mwenye matatizo tena dhidi ya mbunge Karama Benard.

    ****

    FONGA alipokea simu kutoka kwa dada yake, Zubeda. Majira ya saa nne asubuhi. “Fonga, huyu mkeo ameondoka muda si mrefu hapa na hajaniaga bali amesema anawahi kurudi.” Dada mtu alimpa taarifa Fonga kama ambavyo alikuwa ameelekezwa kuwa iwapo ataondoka basi apewe taarifa upesi. Fonga akakurupuka kutoka kitandani, akajipongeza kwa machale yake sahihi. Fonga ambaye alikuwa nyumba ya jirani kabisa na mahali anapoishi dada yake alivaa shati lake na kisha akaingiza miguu yake katika makubadhi. Akanyata na kutoka nje akiwa ametinga kofia ya pama. Ilikuwa ngumu kumtambua, kwa mbali akamuona Joyce akitembea upesi upesi. Fonga akasikitika kisha akatabasamu, alikuwa anaufurahia mchezo ambao alikuwa anaenda kuucheza. Mchezo wa kufungiana tela!! Upesi akachumpa katika taksi ambayo alikuwa ameikodi kwa shughuli za hapa na pale hasahasa katika tukio zima la kumsaka mbaya wao. Akatazama kwa makini Joyce naye akiwa na baibui lake akijiweka katika taksi mojawapo. Ilipoanza kuondoka naye akaingiza gari barabarani na kuanza kumfuatilia yule binti mahali ambapo alikuwa anaelekea. Safari yao ikaishia katika hoteli ya ‘Rombo Green View’ iliyopo maeneo ya Sinza Legho. Fonga akaegesha gari yake na kisha kuingia katika hoteli hiyo na kujiweka katika kona moja matata ambayo hakuna ambaye angeweza kutambua alikuwa na jambo gani. “Niletee Safari mbili za baridi.” Alitoa oda kwa muhudumu. Wakati huo macho yake yapo kwa Joyce ambaye alikuwa akiangalia saa yake kila mara. Amenifurahisha sana kuvaa kama nilivyomwambia!! Fonga akajisemea huku akimtazama Joyce aliyekuwa hana habari kabisa. Mara baada ya dakika kadhaa lilifika kundi dogo la wanaume watatu. Wakaangaza huku na kule, Fonga naye akawatazama kwa jicho la wizi wizi. Waliporidhika mmoja wao akapiga simu. Na hapo likatokea tukio la kuogofya!! Akaingia mwanaume ambaye alikuwa nakila dalili ya maisha ya kifahari. Akapiga hatua moja baada ya nyingine na kuifikia meza aliyokuwa ameketi Joyce Kidoti. Bila shaka alikuwa ameelekezwa kwa njia ya simu tayari juu ya namna gani binti huyu alikuwa amevaa.

    Damu ya Fonga ni kama iliongeza mwendo kutokana na mapigo ya moyo kuongeza kasi yake. Macho yake yalikuwa yanatazamana na mwanaume ambaye alikuwa akimchukia kupita wote duniani!! Mwanaume katili aliyetia doa historia ya maisha yake. Mzee Beka!! Mwanaume aliyemtupa jela kwa miezi tisa bila kuwa na kosa. Mwanadamu mbaya asiyekuwa na huruma!! Fonga alitaka kuinuka na kumvagaa lakini akajionya kuwa mvumilivu na kutazama ni kipi kinaendelea baina ya wawili wale. Fonga alimtazama Beka huyu tofauti kabisa na yule wa zamani, huyu alikuwa nadhifu zaidi. Na alionekana kuimarika zaidi ya awali. Kwa mara ya kwanza Fonga anamuona Beka ambaye awali walipoonana alikuwa akiitwa Bernad Kamara, sasa alikuwa amelifupisha jina lake kamili na kulifanya kuwa moja!! Sasa anaitwa Beka!!!

    Wakati akijiuliza ni kipi afanye, mara alishtukia anaguswa begani. Alipogeuka akakutana na mwanaume akiwa ndani ya vazi la suti. Alikuwa akitabasamu na macho yake yalizibwa na miwani nyeusi ya jua. Kwa wepesi wa akili yake, akatambua kuwa kuna jambo. Alipokazia macho mikono ya yule bwana katika suti yake akaona umbo ambalo halikuwa geni vilevile machoni. Mtutu wa bunduki!!! “Habari bwana!!” yule mtu alimsabahi huku akimpa mkono. Fonga akastaajabu, kasha akkiri kuwa akiwa lelemama huo ni mwisho wa mchezo. Fonga akatambua kuwa alikuwa anakabiliana na mzee Beka kwa mara nyingine katika maisha yake. Mchezo wa kwanza alipoteza vibaya….na huu nao dalili ikaanza kuonekana awali…. Amejuaje uwepo wangu hapa!! Alijiuliza huku akiwa hajafanya maamuzi….. Jicho moja likamtazama Joy akishikwa shikwa bega na mzee Beka, jicho jingine likageuka na kukutana na kijana mwenye mtutu wa bunduki!!!

    Hatari!!!



    “Fonga Fonga Fonga rafiki yangu, usithubutu walau kukimbia ama kufanya vurugu ya aina yoyote, nyanyua macho yako tazama pembe ya kushoto na kulia.” Sauti ilimsihi, Fonga akatazama na kukutana na wanaume wawili, mmoja katika kila kona. Wote wakiwa na mawani nyeusi.

    “Wanakutazama wewe, ukifanya aina yoyote ya usumbufu hawatasita kukupasua kichwa chako kibovu mara moja!!

    Hivyo kuwa mtulivu bwana mdogo!!” aliendelea bwana yule huku akiiondoa miwani yake machoni. Wakatazamana ana kwa ana na Fonga mwenye hofu!!

    Bwana yule akamkazia macho Fonga kisha akamwambia maneno bila kutoa sauti katika namna ya kusisitiza.

    “Fonga, soma ujumbe katika simu yako!!” alimwambia bila kutoa sauti, hivyo Fonga alitakiwa kuusoma mdomo wake jinsi unavyocheza cheza. Kwa mara ya kwanza Fonga hakuelewa kitu lakini kwa mara ya pili Fonga ambaye alikuwa mtu wa kupenda kujua mengi alipokuwa gerezani alizikumbuka ishara mbalimbali zilizokuwa zikitumika gerezani hasahasa pale ambapo wafungwa wanafanya mawasiliano bila mnyampara kuwasikia ama kujua kinachoendelea. Wafungwa walizungumza kwa ishara za midomo na macho na walielewana sana!! Fonga akausoma mdomo na kuuelewa unamaanisha nini, lakini angeweza vipi kumuamini yule bwana asiyemjua? Pia alishangaa huyu bwana ameijuaje namba yake mpya upesi kiasi hicho hadi amsisitize kuusoma ujumbe katika simu yake? Huu sasa ukawa utata!! Fonga alikuwa katika fumbo asijue nini cha kufanya, lakini wazo la kukimbia alishalitoa akilini upesi.

    “Fonga, kama ulivyo nakusihi usimame kisha hatua za taratibu, moja baada ya nyingine fuata uelekeo ninaokuelekeza.” Sasa alitoa sauti. Fonga hakuleta ubishi, alisimama na kuanza kufuata alichokuwa anaelekezwa. Ni kama walikuwa marafiki tu lakini waliotofautiana kauli, hakuna mtu ambaye angeweza kushtukia jambo lililokuwa linaendelea baina yao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa nafasi nyingine muhimu ya Malle kumwokoa Fonga na kisha kumfahamu kiundani zaidi, macho ya vijana wa mzee Beka yalipomuona aliamua kuchukua jukumu la kumkamata upesiupesi. Alifanya maamuzi hayo ili aweze kumwokoa. Kabla hajamkabili alijaribu kumtumia ujumbe mfupi wa kumtahadharisha juu ya usalama wake, lakini ajabu hakumuona akijishughulisha kuitoa simu yake na kusoma ujumbe. Ni hapa alipoamua kumkabili na kwa usalama wake kwani alikuwa amevaa vinasa sauti ambavyo vilisafirisha kila alichokiongea na kuwafikia wenzake. Hivyo ilikuwa mtihani mwingine kumweleza Fonga juu ya jambo linalokaribia kumtokea. Malle, alipomweleza Fonga asimame na kufuata maelekezo yake alikuwa katika uelekeo wa kumtegesha Fonga mahali pasipokuwa na watu wengi ili kuwapa nafasi wenzake ambao walikuwa tayari kuua waweze kufyatua risasi na kummaliza Fonga!! Roho ilikuwa inamdunda sana kwa tukio ambalo alikuwa anakaribia kulishuhudia!! Nafsi ilimsuta. Akaukumbuka uchangamfu wa Fonga, akazikumbuka harakati zake ambazo zilimpa umaarufu. Akakikumbuka na kisa ambacho kinasababisha Fonga auwawe, kilikuwa kisa cha kiuonevu sana. Malle hakuwahi kushiriki katika mauaji ya kionevu kama yaliyopangwa kwa ajili ya Fonga!! Yaani Fonga huyu huyu aliwahi kusota miezi tisa jela na mingine mine rumande kabla ya hukumu.

    Kisa Monica!! Msichana ambaye alikuwa katika mapenzi na bwana Beka, kisha akaachana naye na kujihusisha na Fonga. Bila Fonga kutambua kuwa alikuwa ametoka kumwacha kibopa yule kwa mbwembwe zote. Fonga akajikuta matatani, akafungwa akijua amefungwa kionevu kabisa, angefanya nini wakati mwenye pesa alikuwa ameamua? Sasa Fonga akiwa mtaani tena anakumbwa na mkasa huyu, dhidi ya bwana Beka tena kisa tu bwana Beka anamtaka Joyce kinguvu na Joyce hamtaki!! Malle akauhesabu huu kama uonevu dhidi ya mtu mtaratibu sana akaamua kumpigania tena. Roho ya Fonga ilikuwa mikononi mwa Malle. Kwa akili ya upesi ya kuzaliwa, Malle alipoukaribia mlango alijifanya kupishana vibaya na muhudumu wa hoteli ile, mara wakagongana, kinasa sauti kidogo kilichokuwa sikioni kikadondoka. Akainama upesi kukichukua lakini hakufanya juhudi za kukirejesha sikioni, mawasiliano baina yao yakawa yamekatika. Tukio hili la kugongana na muhudumu lilionwa na wenzake kutoka pande zote za ukumbi ule. Hawakujua kuwa Malle amefanya yale maksudi!! Sasa aliweza kuongea bila wao kumsikia. “Fonga, sikiliza Beka ameagiza uuwawe, nipo upande wako. Ni mimi niliyekutumia ujumbe ulipokuwa na Joyce siku ile pale kwake hatimaye ukapitia dirishani, sasa sikia. Naomba ufanye jambo moja la kuwahadaa wale wenzangu. Akili yako ifanye kazi upesi sana, Fonga yaani upesi sana. Naamini utaweza, ukisikia nasema neno maliza, timua mbio. Haraka..uwashe simu yako nitawasiliana na wewe.” Alimaliza kuzungumza kwa sauti ya kawaida kisha akajiweka makini na kukivaa tena kinasa sauti. “Fonga utasimama hapo hadi nikuruhusu mimi kuondoka, na hautaondoka bila kunijibu maswali yangu!! Sina hofu kuhusu wapiti njia. Nitakisambaza kichwa chako na hautakuwa na nafasi nyingine ya kujutia ulichokifanya pumbavu mkubwa” Malle alibwatuka maneno yale kwa ghadhabu kuu. Fonga akawa katika mchanganyiko wa hofu na uoga.

    “Brother one, Brother two. MALIZA!!”

    Mlio wa bunduki haukusikika lakini hekaheza zilizushwa na mtapakao wa damu eneo lile, kila mmoja alihaha na kujiuliza nini kimetokea. Mabonge makubwa makubwa ya damu yalikuwa yameharibu hali ya hewa. Ulikuwa ni mshikemshike. Mwili wa mwanadamu ulikuwa umetulia tuli chini. Haukutamanika kuutazama hata kidogo. Ulikuwa ni mwili usiokuwa na kichwa. Yalikuwa mauzauza ya ghafla sana kutokea pale. Malle hakugeuka mara mbili kutazamana na maiti ya Fonga, matone ya damu katika nguo yake yalimaanisha kuwa Fonga alichelewa sana kukimbia.

    “Nilijaribu kadri ya uwezo wangu!!” alisema kimoyomoyo huku akitoweka eneo lile ambalo halikuwa salama tena. Malle akatokwa namachozi baada ya miaka mingi kupita. Tukio lile lilikuwa limemuumiza sana. Kuuwawa kwa mwanadamu kiuonevu. Tena mwanadamu ambaye wanafahamiana. Heka heka zile zilizoondoa amani katika eneo lile zilimfanya Beka pia aamue kuingia chumbani kwake. Aliongozana na Joyce Kidoti Keto.

    ****

    BEKA alikuwa katika shangwe kuu, alifurahia taarifa ya tetesi kuwa yule bwana aliyepigwa risasi maeneo ya Rombo Green View ni Fonga. Taarifa hii ya tetesi alipewa na kijana wake aendaye kwa jina la Malle.ni huyu ambaye alikuwa amemuweka Fonga katika mtegowa kufyatuliwa risasi na jukumu la kufyatua likibaki kwa wale vijana wengine. Sasa Beka alikuwa chumbani na Joyce. Alikuwa katika kutimiza lengo lake la pili. Kummiliki Joyce moja kwa moja hasahasa baada ya Fonga kuuwawa. Beka akiwa na furaha ileile mara simu yake iliita, alipoitazama ilikuwa ni namba mpya.

    “Bernad Kamara” sauti ilimuita upande wa pili, haikuwa sauti ngeni.

    “Naam, nani mwenzangu.” Aliitika katika sauti ya utulivu sana.

    “Muache huru binti huyo uliyenaye na kisha bila kushurutishwa mwache Betty huru. Kisha endelea na mambo yako bila tatizo.” Alisisitizwa kwa sauti iliyotangaza amani na humohumo ikitangaza vita. Maneno kutoka simu yalilifikia sikio la Joyce, akajikaza kama ambaye hajasikia neno lolote lakini asingeweza kujikaza zaidi.

    “Wewe ni nani na unanipigia simu ya kunipa vitisho vya kitoto.”

    “Hutakiwi kunifahamu Beka maana haitakusaidia lolote. Mwache Joyce bila kumfanya lolote muathirika wa Ukimwi mkubwa wewe, mwache huyo mtoto. Natambua kuwa ulimuua Monica kwa sababu angekutangaza kuwa ulimwambukiza Ukimwi, mwache Joyce asome…mwache Betty huru pia….kwani hao wamekukosea nini?” sauti ile iliendelea kuuliza.

    “Unasema nini mpumbavu wewe. Hivi unatambua mimi ni nani? Unatambua kuwa unazungumza na nani shenzi wewe.” Beka alitaharuki, yaliyosemwa yalikuwa na ukweli ndani yake. Huyu ni nani sasa ajuaye kuhusu yeye, huyu ni nani huyu?

    “Roho yako ipo mikononi mwangu dakika hii hapa. Lakini ipopia katika maamuzi yako. Sikutishi bwana Kamara Benard. Namaanisha kuwa, mwache huru binti huyo? Mwache mara moja na yule mwenzake mwache huru.”

    “Wewe ni nani kijana. Na nani amekupatia namba yangu ili upige simu kunichafua?”alihojihuku akiwa anatabasamu. Hasira ilikuwa imempanda.

    “Fonga wa Fonga, napiga simu kutoka kuzimu!!” akajitambulisha kisha simu ikakatwa!!! Beka alivyopiga haikuwa ikipatikana. Wacha wee!! Beka alihaha, mara avute shuka mara ashike laptop yake, mara achukue taulo. Joyce Keto akiwa katika nguo za kulalia alikuwa akimtazama kwa uoga mkubwa sana. “Joyce mpenzi …..eehh hivi umemsikia huyo mjinga?” aliuliza Beka huku akiwa anaona haya kumtazama Joyce machoni.

    “Amesemaje?” aliuliza kinafiki Joyce.

    “Achana naye ni mjinga mmoja tu anataka kunichafua” alijibu Beka huku akirejea tena kitandani bila kuwa amefanya walau moja ya jambo lolote alilonuia kufanya. Hali ilikuwa tete!!

    ****

    MIKONO ya Fonga ilikuwa inatetemeka sana wakati akiwa kandokando ya barabara ya Shekilango akitazama hekaheka za hapa na pale kuwatazama wananchi walivyokuwa wanalia na wengine wakiogopa kuutazama mwili usiokuwa na kichwa.

    “Kwa hiyo ningekufa vile ama!! Beka nilikukosea nini?” alijiuliza huku akikosa muhimili thabiti na asiamini kama yu hai tena.

    Ghafla akamkumbuka bwana ambaye alimwokoa kutoka katika mauti yale ya mara ya pili. Sasa alimuamini kupita maelezo na kuelewa kuwa bwana yule hakika alikuwa na kitu cha ziada. Fonga akalivua shati lake lililopata madoa kadhaa ya damu ya mwanadamu, akasalia na fulana yake isiyokuwa na mikono. Akajitupia garini na kuondoka zake huku akijiuliza Beka atamfanya nini Joyce. Lakini asingeweza kurejea tena eneo lile mpaka akili yake ipate utulivu kiasi fulani. Safari yake iliishia Manzese, huku hakuelekeakatika chumba chake. Bali alienda katika vyumba vingine walipoishi marafiki zake ambao alishirikiana katika mambo mengi. Ni huku alipoweza kufungua simu yake ambayo aliweka namba yake ya siku zote. Akakutana na jumbe mbili tofauti ambazo zilikuwa na maana kubwa sana kwake. Kwanza akakutanana ule ujumbe wa kumsihi atoweke eneo lile (Rombo Green view) kwani si salama, ujumbe huu haukuwa na maana tena. Lakini ujumbe wa pili ulikuwa na maana zaidi na ulimfanya awe na kiburi cha kuamini kuwa atamshinda mpinzani wake. Lakini alisikitika kuwa kijana aliyejisajili simu yake kwa jina la ‘Malemi Stanslaus’ aliamini kuwa yeye ni maiti, kwani ujumbe mwingine uliingia ukisema ‘NILIJARIBU KILA NIWEZAVYO R.I.P Fonga’. Fonga akatabasamu na hapo akaamua kujiita Fonga kutoka kuzimu!!

    Hata alivyompigia simu Beka na kumweleza juu ya maasi yake alikuwa akijiona kama mfu, na hakuhofia kuhusu kifo. Kama alitakiwa kufa kwa kupigwa risasi ya shingo, na sasa yu hai. Kuna lipi jingine la kuhofia. Hakuwa na lolote la ziada. Fonga akaingia katika chumba kimojawapo cha bafuna kujisafisha mwili wake, kisha akabadili nguo zake. Rafiki zake walikuwa wakimtazama kila mara wasiamini kama yu hai tena!! Maana kwa alichowasimulia ni kama filamu tu!! Filamu ya kutisha na kushangaza.

    ****

    Alichofanikiwa Joyce ni kumshawishi Beka kwa mara ya kwanza atumie kondomu, hilo alifanikiwa.lakini baada ya simu ile, mambo yakabadilika Beka akalazimisha wafanye mapenzi bila kinga, kisa tu alikuwa na mpango wa kumuoa siku za usoni hivyo hata akipata mimba si tatizo kwake. Joyce alikataa katakata huku akilia na kumzuia Beka.

    “Kwa hiyo hicho kiFonga chako nd’o huwa unakubali bila kondomu sivyo, sasa ni heri unichukie lakini hutoki humu ndani hivi hivi. Nasema hivi ama zangu ama zako maana ninapokubembeleza Joyce unaniona mimi kabisa. Umalaya wako alokufundisha mama yako sasa hapa umefikia kikomo bastard!!” Beka akapandwa na hasira na kujikuta akitokwa na maneno hayo mazito, huku akihaha kupambanana Joyce. Joyce alikuwa ni yuleyule aliyembwaga dada mkuu wa shule ya Kifanya mjini Njombe baada ya kujaribu kumnyanyasa na kisha akafikia mbalina kumtukania mama yake ambaye tayari ni marehemu. Beka naye akamtukania mama yake. Joyce akapandwa na hasira na hatimaye akamkabili. Akamrukia na kumshambulia kwa kucha zake huku akitweta kwa hasira. Beka hakutegemea shambulizi kutoka kwa mrembo yule, akajirusha kando lakini Joyce alikuwa mwepesi na tayari kwa lolote, pale unapomtukania mama yake. Joyce akamvagaa Beka na kufanikiwa kumtupa chini, hapa sasa ikajirudia ile filamu ya Joyce na dada mkuu wa shule ya Kifanya. Joyce aliyekuwa maridadi katika kufuga kucha ambazo zilipakawa hina na kuwa imara zaidi alianza kushambulia kwa kufinya uso wa mzee Beka. Mara amfinye kifuani. Beka akaanza kusota kwa maumivu, kabla hajakaa sawa Joyce akamdokoa machoni. Ebwana ee!! Beka akaanza kulia kama mtoto mdogo. Joyce akamwacha na kuruka kitandani aweze kuchukua nguo zake avae na kuondoka. Beka akasimama na kumuwahi huku akiona kwa kutumia jicho moja. Kosa alilofanya Beka ni kumkaba Joyce kabali kwa nyuma. Kabla kabali ile haijanoga. Joyce makucha alitumia tena makucha yake. Akaurusha mkono ukatua mahali sahihi alipokuwa anahitaji. Mkono ukakamata korodani za Beka, kisha kucha imara zikabinya huku zikifinya. Sio balaa hili??? Beka akalegeza ile kabali, akanyanyua miguu yake na kusimamia kucha!!

    Macho akayakodoa mpaka usawa wa mwisho. Hauhitaji kusimuliwa maumivu yanayotokana na shambulizi la namna ile. Beka hakuwa na ujanja. “Beka unataka kuniambukiza mimi ukimwi, unataka kuniua maksudi, kumbe ni wewe ulimuua Monica, kumbe ni wewe unamshikilia Betty. Beka wewe ni mnyama, mnyama kabisa hufai kuendelea kuishi hayawani wewe.” Joyce alikaripia huku akizidi kumbana.

    “Sasa ili tusiende mbali nakuomba usiniguse hadi nitakapotoka nje ya chumba hiki, vinginevyo nitakuua Beka. Nitakuua” alitisha Joyce, Beka akakubali. Joyce akavaa nguo zake huku akimtazama mzee yule iwapo atafanya lolote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Fungua mlango!!” aliamrisha Joyce. Beka akapiga hatua. Akaufikia mlango na kuufungua. Joyce akapiga hatua aweze kutoka nje, na hapa mambo yakambadilikia. Beka aliachia teke moja madhubuti likatua katika tumbo la Joyce Kidoti. Binti akarushwa nyuma na kutua kitandani. Beka akamuwahi tena na sasa akawa amemkalia kwa juu. Kipigo kitakatifu kikafuata!! Joyce alipokea ngumi nzitonzito kutoka kwa Beka.

    “Sasa na wewe unamfuata huyo Monica wako sawa eeeh!!” alisema Beka, wakati huo damu zikiwa zimeyachafua mashuka haswa. Joyce alikuwa hoi.

    “Yaani Monica ameniambukiza Ukimwi halafu mnasema mimi ndo nimemwambukiza sivyo,sasa nakuua ili ukamuulize yeye mwenyewe nini mkasa wa kifo chake sawa eeh.” Alizidi kuwaka. Beka alikuwa ameingiwa na roho ya kuua. Hakuwa na huruma zaidi. Mara mlango ukafunguliwa, ilikuwa kama kimakosa hivi, lakini hapakuwa na kosa lolote. Mara wakaingia wanaume wawili na mwanamke mmoja. Beka akakumbuka kuwa aliacha mlango wazi baada ya kufuata sharti la Joyce alipotaka amfungulie mlango aondoke.

    “Bernad Karama, mheshimiwa mbunge wa jimbo la madhambi una swali la nyongeza?” sauti ya kiume iliuliza. Sauti ambayo Beka alikuwa anaifahamu. Alipotazama vyema akakutana na mshtuko wa mwaka 2008. Alikuwa anatazamana na marehemu Fonga!!

    Alipokodoa macho, Fonga akatambua kuwa alikuwa akiuliza swali kuwa ‘si umekufa wewe?’ naye akalijibu.

    “Nimekufa lakini nimerejea kidogo tu kukuletea salamu zako kutoka kuzimu!!”

    “Fonga…” sauti ya mshangao kutoka kwa Joyce!!.

    “Beka kuzimu wanakuhitaji!! Ni hilo tu.” Alisema kwa hasira kiasi safari hii.

    Beka akapagawa!! Hakika alikuwa amekamatika. Wakati Beka akidhani kuwa mtu mwenye kumtia hofu ndani ya chumba kile ni Fonga peke yake, haikuwa hivyo!!

    Vichwa vitatu ndani ya chumba kile vilikuwa vimekamilika haswa! Alipojaribu kufurukuta, alijikuta akitua katika mikono ya mwanamama. Kilichomtokea hakukitegemea kutoka kwa mwanamke!!

    Meno mawili yakadondoka chini. Alipigwa kichwa kimoja tu na yule mwanamama ambaye alikuwa kimya na hata alipomtoa meno hayo bado alikuwa kimya kama vile sio yeye aliyempiga na kichwa. Beka akatua chini kama meno yake, sasa alikuwa amepiga magoti damu zikimtoka mdomoni.



    PIGO lililoyaondoa meno mawili ya muheshimiwa Beka, ni mpigaji pekee ambaye hakulishangaa lakini Fonga na mwenzake wakishirikiana na Joyce walilishangaa haswa. Pigo makini kutoka kwa mwanamke makini. Fonga aligutuka na kutambua kuwa kilichowaleta ndani ya chumba kilikuwa hakijakamilika, alichukua kitambaa na kumfuta Beka damu kisha akaamuamuru kusimama. Beka alijaribu lakini ni kama lile pigo zito lilimpa kizunguzungu sana. Akataka kuanguka mara akadakwa na yule mbaya wake aliyeyaondoa meno yake mawili.

    “Beka yaani hivi tu unataka kuanguka bosi.” Kwa mara ya kwanza yule mwanamke alizungumza. Beka akamgeukia, wakatazamana!! Beka akataka kusema neno lakini kinywa kikawa kizito!! Hakuweza kusema lolote lakini ni kama alikuwa akimtambua yule mwanamke!!

    *****

    MALLE aliona kwa mbali ujio wa watu watatu majira ya usiku katika hoteli ile ya Rombo Green View, alitikisa kichwa chake na kujisikitikia kuwa kazi ya kumlinda mwanadamu ni ngumu sana, hasa hasa mwanadamu muovu mwenye maadui wengi wanaomzunguka. Lakini hakuwa na jinsi maana bila kumtumikia Beka angekosa kula yake!! Sasa alipowaona wale watu, kwa nidhamu ya kazi yake haramu hakutakiwa kuwaamini hata kidogo. Japo kwa mtazamo walionekana kama wapangaji wa kawaida katika hoteli. Lakini wapangaji gani wanaongozana watatu kwa pamoja, wawili wanaume na mmoja mwanamke? Hili swali lilimvuta na kumfanya awape wenzake taarifa. Wakajisogeza mapokezi baada ya wageni wale watatu kutoweka. Wakiwa wanafahamika kama walinzi wa muheshimiwa, walipewa ushirikiano wahali ya juu sana. “Ni akina nani watu wale?” aliuliza Malle. “Ni polisi, wapo hapa katika kupeleleza tukio la mauaji yaliyotokea hapa jioni”alijibu kwa staha muhudumu wa kike. Malle hakuridhika kabisa na maelezo yale, kwani ni muda mfupi uliopita polisi wengine walikuwa eneo lile. Halafu polisi gani hawa wanaongozana wote watatu kwa pamoja? Si kawaida ya polisi hata kidogo kuongozana mithiri ya kumbikumbi wakiwa katika upelelezi. Hapana!! Alikata Malle katika kichwa chake, kisha akatoweka bila kusema neno. Akawaendea wenzake ambao walikuwa wakijiburudisha kwa bia kila mmoja akiwa na yake. Alijaribu kuwaeleza juu ya hofu yake kuwa kuna watu wabaya wameingia eneo lile. “Kwa hiyo unashauri nini Malle.” “Wenye jukumu la kulinda chumba chake bora wawe jirani na eneo hilo kwa tahadhari tu lakini. Si mnamjua mzee vizuri….”alijieleza Malle. “Tatizo lako Malle huwa muoga sana na unajifanya machale sana yaani.”alilalamika Rasi, mmoja kati ya vijana wa Beka. Ni yeye alikuwa zamu ya kulinda chumba cha Beka akiwa katika tabia zake za uzinzi. “Halafu si unajua bosi hapendi haya mambo ya kumsimamia mlango akiwa na Malaya wake?” Rasi aliendelea kujiwekea sababu kutokwenda kulinda chumba. “Rasi eeh! Uamuzi ni wako lakini usije ukasema sikukueleza.” Alimaliza Malle kisha akaondoka kuelekea nje kabisa ya hoteli ile. Rasi, akiwa amekasirika aliamua kutimiza wajibu. Akainywa bia iliyobakia katika chupa katika mfumo wa tarumbeta. “Oya Kenny, niangalizie hiyo simu akipiga Suzi mwambie nimetoka kisogo lakini anisubiri nakuja”alihitimisha . Kisha akatimua mbio kukiendea chumba cha Beka kilichokuwa ghorofani. Alipokifikia chumba akakiri kuwa Malle ni habari nyingine. Machale yake yanaishi!!! Alisikia vurugu ndani ya chumba, kulikuwa na majibizano ambayo hakuweza kuyasikia vizuri. Lakini palikuwa na lundo la watu katika chumba kile. Rasi akaiweka vyema bunduki yake!! Akajibanza mahali ili aweze kuona nini kitatokea. Alingoja hadi mlango ulipofunguliwa. Akamshuhudia bosi wake akisaidiwa kutembea, na ni kama alikuwa amejeruhiwa!! Rasi akabaki katika kigugumizi, afyatue risasi ama aendelee kuvuta subira. Simu yake alikuwa ameiacha katika meza aliyokuwa ameketi na mwenzake hivyo asingeweza kuomba msaada kiurahisi. Rasi alikuwa akijiuliza ni nani watu hawa, alihofia kuwakumba kwa kuhofia kuwa wanaweza kuwa askari hivyo kujikuta akimwingiza muheshimiwa katika matatizo mengine, kigugumizi hiki kilitoweka baada ya macho yake kutazamana na jambo la ajabu asilolitegemea. Jambo ambalo likimkuta mtu mwingine yoyote yule lazima ashtuke na huenda akapiga kelele kabisa. Lakini Rasi hakupiga kelele. Ni mwanadamu gani anaweza kutabasamu akikutana na mzimu wa mtu ambaye anamfahamu. Na mbaya zaidi ikiwa alishuhudia kwa macho yake kifo chake. Rasi alikuwa anatazama mzimu wa Fonga, kijana ambaye kifo chake kiliwapa ahueni na kufikia hatua ya kunywa pombe ili kujipongeza. Sasa anamtazama akiwa hai tena kama kweli yupo hai. Lakini alichoamini ni kwamba alikuwa akitazama mzimu ana kwa ana. Swali likamvamia kuwa ni kipi bora kupambana na mzimu wa Fonga na wenzake ama kuruhusu uoga na kisha bosi wake aendelee kusoteshwa na watu wale!! Kwa wakati huo hakuwa na wazo tena kuwa wale ni polisi. Alichoamini ni watekaji kama watekaji wengine. Rasi akaruka hatua kubwa nne bila kuruhusu vishindo. “Mikono juu wote. Simama hapo hapo bila kufanya vurugu zozote zile, la si hivyo napasua vichwa vyenu!!” sauti tulivu ya Rasi iliamrisha. Bunduki yake ndogo ikiwa inatazama visogo kadhaa. Nguvu zikarejea katika mwili wake. “That’s my boy Rasi.” Alijitutumua Beka, akazungumza huku akiruhusu damu zilizochanganyikana na udenda zimwagike chini. Fonga alihisi miguu ikimlegea, Joyce akatokwa na yowe dogo la hofu na mshtuko. Mark hakujua nini cha kufanya. Mbaya zaidi hakujua maadui walikuwa wangapi na wamejipanga vipi. Mark akajuta kumsaidia Fonga katika oparesheni hiyo Mambo yalikuwa yamewageukia!!! Mdomo wa bunduki ulikuwa tayari kutema risasi!! Fonga kwa jicho la kuibiaibia akakutana na bunduki ambayo iliua mtu jioni ile. Pia akakutana na macho yale yale yaliyomtazama kabla hayajafyatua risasi. Fonga akakiri kuwa ngoma ilikuwa imemshinda!!!

    ****

    UTOTONI lilionekana kuwa jambo la kawaida sana alipojichanganya na kucheza mpira wa miguu na wavulana, hakupendelea na wala hakuwahi kucheza michezo ya mdako ama baba na mama. Hili nalo halikuchukuliwa uzito wowote. Alipoanza shule, sketi pekee aliyokuwa akivaa ni ile ya shule. Nguo zake za kushindia zilikuwa suruali ama kaptula. Zote za kiume. Akiwa darasa la tano wakaanza kumtania ‘jike-dume’. Mwanzoni aliwavumilia, hakusema neno walipomtania. Lakini walipozidi kumtania akawabadilikia, alimkamata mvulana mmoja na kumfanya mfano. Kipigo alichokitoa kilimshangaza kila aliyeona. Hakuna aliyeamini kama yule aliyepokea kipigo kile alikuwa ni mvulana mkubwa tu na aliyetoa kipigo ni msichana. Ikabakia kuwa simulizi!! Utani ukakoma. Alipomaliza darasa la saba, wazazi wake walifariki katika kile kilichoitwa imani za kishirikina. Husna akabakia kuwa mpweke!! Tena yatima. Ukorofi wake ukamsababisha akose ndugu wa kuishi naye, na ile tabia yake ya kupenda kuwa mwanaume ikamsababisha akose mvuto. Hii ikawa safari ya Husna kuingia mtaani akijichanganya na watoto wa kiume katika kupigania maisha kama Chokoraa. Maisha ambayo alilazimika kuyamudu. Asingeyamudu ni wapi angekimbilia? Akiwa na miaka kumi na nane tu, alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na nusu baada ya kumpiga dada mmoja ambaye alikuwa akifanya naye kazi ya ‘ubaamedi’. Kosa lilikuwa lile lile kumuita ‘jike-dume’. Kipigo alichompa yule dada kilipelekea mimba yake kutoka. Mahakama ikamuuliza Husna kama angeweza kuilipa mimba ya miezi mitano, Husna akashindwa na kuambulia hukumu hiyo ya miezi kumi na nane Ni katika maisha ya ufungwa wake ndipo alipobatizwa jina la ngumi jiwe. Hii ilitokana na vichapo alivyokuwa akivitoa wakati akitumikia adhabu hiyo. Hakuna aliyemtetemesha binti huyo wa ajabu ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya ndondi wakati akiwa uraiani. Wanyampara wakamuita ‘ngumi jiwe’. Jina hili likamkaa. Aliporejea uraiani, wale wasichana aliokutana nao jela wakalileta jina lile mtaani. Husna Ngumi jiwe!! Baada ya kutoka jela alihaha kujiweka katika mstari, lakini kwa mara nyingine tena akaangukia katika ubaamedi. Ni huku ambapo alikutana na Mark B, kijana wa miaka ishirini na tano. Mtukutu anayejua nini maana ya utukutu, huyu akamuingiza Husna katika harakati za kusaka pesa kwa njia zisizokuwa halali. Kilichomsababisha Mark avutiwe na Husna ni ujasiri wa Husna na pia kamahilo halitoshi, Husna alikuwa na machale, kitu ambacho watu wachache walikuwa nacho. Kabla ya kumchukua alikuwa amempa mitihan ni mingi bila kujua kama alikuwa akmipewa mitihani. Mark akatambua kuwa Husna ni nguzo imara sana. Katika tukio la kwanza Husna hakushiriki ipasavyo, lakini hili la pili Husna ngumi jiwe amesambaratisha meno mawili ya mzee Beka ambaye aliwahi kumsumbua sana enzi hizo akiwa baamedi. Sasa sio baamedi tena!!

    Wakati Fonga akihaha na kukaribia kujikojolea, Joyce akiwa anatetereka na asijue ni kitu gani kinaendelea duniani, Mark ambaye naye alikuwa amenyanyua mikono juu alikuwanusu ana matumaini na nusu akiwa anaona dalili ya kufikia mwisho wa kufadhaisha. Lakini akiwa bado na utata akilini mwake, likatokea jambo ambalo alikuwa hatarajii.

    Husna ambaye aliwaruhusu wenzake watangulie nje ya chumba wakiwa na Beka, yeye aliendelea kupekua chumba kile bila kujuani kitu gani alikuwa akikagua. Lakini jibu alilipata baada ya kumaliza kupekua kitukisichojulikana. Alipotoka nje akakumbana na kijana mgeni akiwa ameielekeza bastola yake katika visogo vya Mark, Joyce na Fonga. Upesi alikivua kiatu chake kilichokuwa na kisigino kirefu. Akaanza kunyata, wakati akinyata mzee Beka naye alikuwa anageuka upande aliokuwepo. Hapa ukaibuka mchezo wa ujanja kuwahi. Husna hakurejea nyuma, alijionya kwa kauli ya. Adui mfuate!! Beka alikutanisha macho yake na kiwiliwili cha Monica. Kwa jinsi ambavyo alikuwa ametokwa damu hata hakuweza kuonekana kama alikuwa amekodoa macho, Beka alijaribu kunyanyua mkono wake ili aweze kumwonyesha Rasi hatari iliyokuwa nyuma yake lakini mkono ule haukunyanyuka badala yake akakosa muhimili na kupinduka chini. Husna akaitumia fursa hiyo kucheza utaalamu wa ajabu ambao ungeweza kuondoka na roho yake. Husna alitambua kuwa roho tatu zilikuwa mikononi mwake, na pia alikuwa na jukumu kubwa la kuikoa roho yake. Akakirusha kiatu pekee alichokuwa nacho mkononi katika upande wa mbele wa Rasi mlinzi wa Beka. Rasi naye akafanya makosa ya kijinga ya kuhadaika, akageuka ghafla kutazama ni wapi mlio huo ulipotokea. Husna akaruka upesi na sasa alikuwa amemfikia Rasi, hakumsubiri ageuke, akajivuta nyuma kwa nguvu kisha akafyatuka na kichwa kikali, kikatua katika kisogo cha Rasi, akakohoa kidogo kisha akalegea taratibu na kusalimiana na sakafu!! Kisha konde moja zito likatua katika uso wa Beka ambao ulikuwa umeanza kuchanua kwa tabasamu hafifu. Beka akapoteza fahamu rasmi!! Fonga, Mark na Joyce wakabaki kuduwaa wakimtazama Husna asiyekuwa na hofu wala mchecheto wa aina yoyote. “Twende zetu ama!” alisema Husna, na hapo kila mmoja akili ikasogeleana upya. Wakatambua kuwa wapo kazini. “Vipi huyu sasa?” Mark alimuuliza Husna. “Huu mzoga tu achana nao.” Alijibu huku akiukanyaga mwili wa Rasi na upesi wakatoweka eneo lile wakijiamini kabisa kwani tayari walijitambulisha kama askari mapokezi pale. Huku wakiuburuta mwili uliuopoteza fahamu wa muheshimiwa Beka, walifika mapokezi. Afande feki Mark alitoa shukrani kisha wakaanza kutoka nje na mzoga wao. Baada ya kumtoka Rasi kiwepesi, wakafikia himaya ya nje ambayo ilikuwa chini ya vijana wawili tu ambao walijifananisha na makomandoo wa kivita. Kenny (Rambo) na Malle!! Vijana wasiokubali kushindwa kirahisi, vijana wasioogopa kuua dakika yoyote ile. Silaha kali katika himaya yao na pia wakiona fahari kuwa kama walivyo. Kundi dogo la akina Fonga ambalo halikuwa limejipanga ki-silaha, likajikuta limecheza makosa mawili ambayo yaliubadili usiku huu kuwa usiku wa machozi na damu!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku nyuma Rasi alirejewa na fahamu, huku nje Malle na Rambo walikuwa moto wa kuotea mbali katika kitu kinachoitwa ulinzi wa nje. Rambo mtaalamu katika mashambulizi ya kutumia silaha. Huku upande mwingine Malle akiwa bingwa wa machale. Na kwa sababu alishachezwa machale mapema juu ya watu wale waliojitambulisha kama askari. Aliwangoja wakitoka aweze kuthibitisha utambulisho wao.



    ITAENDELEA
    Pseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog