Simulizi : Usinibanie
Sehemu Ya Tatu (3)
NIKAONA ni jambo la hatari kumruhusu mpinzani akutawale
mchezoni. Mwanamume nikaanza kupiga ’kaunta ataki’ au kwa
lugha fasaha mashambulizi ya kushtukiza. Nikawa namgusa zile
sehemu zitakazomfanya apoteze kasi yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilianza kumtoa kitambaa cha kichwani alichokitumia
kuzistiri nywele zake, nikaanza kuzichezea nywele zake
taratibu nikimpiga busu masikioni na kushuka taratibu hadi
shingoni. Nikamuona akianza kuhema kama mgonjwa wa pumu.
Tausi alianza kuhema kwa shida akitetemeka, nikajua sasa
nimeudhibiti mchezo. Nikamlaza pole pole kitandani.
"Nakupenda sana Hoza" aliniambia akihema.
Nilimwangalia kwa makini, hakuonyesha masihara akitamka maneno yale. Mambo yote toka tuliache gari pale mbele ya benki yalituchukua takribani dakika kumi na tano, nikaona kuwa
bado naweza kulifanya nilitakalo kwa muda uliobakia.
Nikajipa tena dakika tano za ’shoo gemu’.
"No, no Hoza!" Tausi alisema akinizuia kwa mikono kuendelea
na pilika zangu za kimuvi muvi. Nikaweka kituo na
kumwangalia usoni nikimshangaa. Nilimshangaa kwa kuwa yeye ndiye aliyeanzisha pambano kwa pasi zake za haraka haraka iweje sasa asimamishe pambano!
"Vipi mpenzi!" Nilimropokea neno mpenzi kiasi cha kumfanya
atabasamu kabla ya kuniambia sababu ya kunizuia vile tena
wakati nalikaribia lango.
Alinieleza sababu ya msingi ambayo ilinifanya nikatulia kwanza kabla ya kuamua kumkumbatia kwa nguvu pale kitandani,
bila kusemezana chochote.
Mkanganyiko wa mawazo ulitawala kichwa changu, wakati
mwingine nilijiona mwenye bahati ila wakati mwingine
nilijiona nina bahati mbaya. "Huyu mtoto atanitia uchizi
mimi!" Nilijisemea moyoni.
Ghafla akakurupuka na kunitaka tujiandae kutoka tusije
kushtukiwa na dereva pamoja na yule binti mtumishi wa ndani.
Pamoja na kuwa hatukumalizia tulichokianza, tulitoka nafsi
zetu zikiwa shwari kabisa.
Burudani tuliyoifanya ilikonga moyo wa kila mmoja wetu.
Tausi, yaani we acha tu! Mtoto alinipa burudani ya uhakika,
yaani kama ni timu ya mpira leo ilikuwa ni mechi ya Arsenal
na Barcelona.
Ngoma ilikuwa inagongwa moja moja huku tukiachiana nafasi ya kuonyesha vipaji binafsi. "Mi hata ng’ombe mia nalipa kwa
ajili ya Tausi" nilijikuta nikijisemea wakati nikimwangalia
anavyojitengeneza kwenye kioo. "Tausi" Nilijikuta nikimuita
Tausi "Abe mpenzi wangu!"
Nikaanza kumweleza kilicho moyoni mwangu, nilimweleza kwa
sauti ya kutulia. Nilimwambia.
"Nikisema sijawahi kupenda kabla, nitakuwa nakudanganya
lakini ukweli ni kuwa sijawahi kuwa na penzi tamu kama hili. Tausi, hakuna maneno ambayo yanaweza kutafsiri ninavyojihisi
moyoni mwangu kwa penzi hili. Nakiri nakupenda sana!"
Nilipomaliza kumwambia maneno hayo, niliyaona machozi
yakitoka machoni pake. Aliinuka na kunikumbatia, "We ndio
mwanamume wa maisha yangu, Hoza. Ila naomba nikuulize kitu!"
Nilidakia kumruhusu aniulize, akaniuliza kama nitamweleza
ukweli wa atakayoniuliza. Nikaahidi kujibu ukweli tupu.
"Umeoa?" Nikamjibu hapana. Akaendelea kuniuliza maswali
mengi ya kiuhusiano na yote nikamjibu ukweli mtupu. Swala la
mwisho aliloniambia ndilo lilinibabaisha kuliko yote aliyoniuliza.
"Unaonekana una ufahamu mkubwa kuliko kazi
unayoifanya nitatafuta siku unipe historia yako ya maisha."
Kimtindo nilijuta kuyaanzisha maongezi yale, nilijikuta
nimejiweka katika mazingira magumu sana endapo angenihoji
kweli.
Tukaanza safari ya kurudi garini kupitia njia ile ile,
nikamuuliza aliijuaje, akaniambia kuna mtu alimhadithia kuwa
ametapeliwa katika jengo la Ushirika. Niliishia kucheka
kabla ya kujiweka katika hali ya kuwa tena mfanyakazi na
bosi wake.
Tukarudi ndani ya gari, nikimcheka ujinga yule dereva
aliyekuwa akiniona kimbelembele. Nikamuona akiangalia saa
kibwegebwege.
Usiku ule nilijilaza nitandani nikiwazia maneno aliyokuwa
akiniambia Tausi, Tausi hajawahi kufanya ngono katika maisha
yake. Alikuwa bikira!
Na siku ile ilikuwa ndio nimuingize katika ulimwengu
mwingine. tatizo likawa ni namna atakavyoonekana akitembea
wakati anarudi! Dah ingekuwa bonge la noma! Halafu ishu
kubwa aliyokuwa akiiogopa ni tabia ya mama yake kumkagua
kila akiwa anarudi baada ya kutoka. Hupenda kumwangalia na
kumhoji sana.
Mtihani nilioupata ni kuwa natakiwa kuifanyia shughuli hiyo
chumbani kwake kwa njia ile ile ambayo huwa ninaitumia
kumbinjukia. Baada ya siku kama kumi za mawasiliano ya simu,
niliamua kujitoa kimasomaso siku moja kuivamia ngome ya Mzee Nurdin ili nitimize kazi iliyobakia, kuufaidi uroda wa
Tausi. Nikajiweka tayari kwa ajili mashambulizi.
Giza lilipoingia tu, nikatoka polepole na kunyata taratibu
kuelekea nyumba kubwa. Kwanza nikaenda mpaka dirishani
kumpigia chabo. Nikam’bamba akiwa katoka kuoga, alikuwa
akijifuta maji. Moyoni niliamini kuwa alikuwa akijiandaa
kunipokea.
Hali hiyo ilinipa ujasiri wa hali ya juu, nikazunguka fasta
na nikaanza kupanda bomba kuelekea juu ya nyumba ya Mzee
Nurdin ili niitumie njia ile ile kuingilia ndani. Kufika juu
nikakutana uso kwa uso na walinzi wawili wanaopasha misuli
moto.
Mmoja akashtuka, "mwizi!" Akaja kwa kasi kuja kunifuata
katika kigiza kile akinipelekea ngumi kama nne za kasi
ambazo moja ilinipunyua na moja ikanipata vizuri haswa huku
mbili nikizikwepa.
Kabla sijajiweka vizuri nilijikuta nikichapwa teke moja kali
sana nikayumba na kutaka kudondoka chini. Nikarudi kwa kasi
na kulidaka bomba, nikajiselelesha hadi chini. Natua tu
chini, na yule mlinzi akawa ametua tayari kwa kuniendelezea
kichapo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikajua hapa nikilegea tu nitajikuta mikononi mwa Mzee
Nurdin na kila kitu kitakuwa kimeharibika. Nikaamua kukomaa
naye, akarusha tena ngumi mbili, nikaziona. Nikampelekea
teke moja la tumbo, akaguna na kuinama chini, nikampiga
kifuti cha uso akainuka na kutoa mlio kama mbwa aliyepigwa
jiwe.
Nikajikuta nimedandiwa shingoni na mlinzi mwingine,
nikampiga ugokoni kwa kisigino kwa haraka nikamuongeza
kiwiko ambacho kilimpata vyema kwenye chembe. Nikamsikia
akiugulia na kuiachia mithili ya aliyepigwa na shoti ya
umeme.
Yule mwingine tayari alikuwa amesogea huku amekinga ngumi
utafikiri yuko ulingoni. Nilicheza nao kwa takribani dakika
tatu hivi nikitumia mapigo makali sana na kuwaacha wakiwa
hoi wanagalagala kwa maumivu.
Nikakimbia kwa kasi na kurudi kibandani kwangu, nikamtumia
ujumbe Tausi kuwa sitaenda nimepatwa na dharura. Najihisi
kichwa kinaniuma sana, akanipa pole tukalala.
Niliogopa kumwambia kilichotokea kwa kuwa kingemshtua na
kuzidisha mashaka kuhusu ukweli juu yangu. Asubuhi hali
ilikuwa shwari sana, wakati nafagia nikapita karibu na wale
walinzi wa usiku uliopita.
Walikuwa wakipakana dawa za kuchua misuli. "Ngumi za yule
babu zinauma sana!" Nikawa nachekea tumboni. Waliniona kama babu kutokana na nilivyovaa usiku ule, nilivaa suruali fupi
kama za wale jamaa wenye msimamo mkali wa kidini na nusu
kanzu. Kichwani nilijifunga kitambaa kama kilemba. Vyote
hivyo vilikuwa ni vyeusi!
Lengo lilikuwa ni kuuondoa kabisa muonekano ambao ingekuwa rahisi kunishuku endapo ningefumwa na kukimbia. Sikuwahi kufikiria kabla kama ningeingia kwenye mapambano. Na cha kustajaabisha ni kuwa, wale walinzi hawakutoa taarifa ya uvamizi ule. Nahisi waliogopa kuonekana wazembe na kuharibu kibarua. Ila nilijua kuwa ulinzi ungeimarishwa.
Wakati nimejipumzisha baada ya kazi, nikapokea ujumbe toka
kwa Tausi, ’jitahidi leo, baada ya leo itabidi usubiri siku
za hatari zipite na kabla hazijaisha nitakuwa safirini.’
Sikutaka kufikiri kuhusu hiyo safari anayoisema japo kujua
tu anapoenda, akili yangu ilikuwa kwenye kulifanikisha zoezi
la kuingia chumbani kwa Tausi. Kumuingiza katika ulimwengu
wa mapenzi ndiyo kitu pekee kilichobakia kichwani mwangu,
nilikuwa nikipanga na kupangua njia za kutumia. Mwisho
kichwa kilichoka nikapitiwa na usingizi.
Baada ya saa kadhaa kupita, nilishtuka, usingizi wangu
haukuwa mzuri kwa kusema ukweli. Nilikuwa naota vitu vya
hovyo hovyo tu ambavyo havieleweki.
Saa hazigandi, usiku ukawadia wakati kichwani sikuwa na
mpango wowote wa kupenya na kuingia chumbani kwa Tausi.
Kidogo meseji ya Tausi iliingia, alikuwa akiulizia kama
nitaenda ama la.
Meseji ile ilinihamasisha na hatimaye kupata njia. Nikamjibu
ndio nakuja. Nikajiandaa mwanamume, nikatoka. Nikaenda
lilipopaki gari la kununulia mahitaji ya ndani, nikatoa
kiasi fulani cha petroli na kukiweka kwenye chupa yangu.
Nikaiziba na karatasi nililolifinyanga. Nikatambaa hadi karibu na getini, nikikodolewa macho na mbwa ambao nadhani walikuwa wakinishangaa wasijue nilichokuwa
nakifanya. Nilipokaribia getini nikaliwasha lile karatasi na
kuirushia ile chupa nyuma ya kibanda cha walinzi.
Nikarudi mbio hadi nyuma ya nyumba kubwa, ghafla ukasikika
mlio mkubwa sana. Lilikuwa ni bomu la petroli. Nilisikia
vishindo vya walinzi wakikimbia huku na kule, nikapanda juu
haraka kupitia bomba, nikamuona mlinzi wa juu akiwa
anatumbulia macho getini.
Nikaingia kwa haraka kupitia ngazini hadi ndani kwenye chumba kidogo kile cha giza. Nikaenda kwenye swichi kubwa ya umeme na kuizima, kisha nikachubua nyaya na kuzikutanisha. Giza likatawala.
Nikatembea kwa haraka, nikauchokonoa mlango ule mdogo ambao huwa ninautumia kuingia eneo la vyumba. Nikaingia na kwa kasi nikazama chumbani kwa Tausi. Wakati huo wote sikuwahi kufikiria kuwa nitatokaje ndani ya jumba hilo la Mzee
Nurdin.
Nje nilimsikia mlinzi akitangaza kuwa kila mtu atulie alipo
hadi atakapotangaza tena. Ndani nilimkuta Tausi anatweta kwa
woga, nikawahi kumkumbatia nikijitambulisha ili asije
akapiga kelele. Akanikumbatia kwa nguvu akiniuliza kuwa ni
nini kimetokea.
Nikamjibu kuwa sikuona kitu labda ni hitilafu ya umeme.
Tukabaki tumekumbatiana huku tumesimama, nikamchukua
taratibu na kumpeleka kitandani. Tukawa tumejilaza kitandani
bila kuongea chochote wala kufanya chochote, nilijua kuwa
Tausi bado hakuwa tayari kuhamia katika ulimwengu wa mahaba.
Baada ya takribani dakika arobaini hivi, wakawasili polisi
kadhaa na mafundi umeme. Kila kitu kikarekebishwa hali ikawa
shwari, mlinzi akathibitisha.
"Twende tukaoge" nilimnong’oneza Tausi bila kujali kuwa
alikuwa ameshaoga ama la lakini ilikuwa ndio njia ya
kumuondoa hofu na kuirudisha akili yake mchezoni.
Niliinuka kwa haraka, nikimwacha akijiinua taratibu.
Nikamsaidia kunyanyuka kabla sijambeba ghafla na kumpeleka
kwenye bafu ambalo limo humo humo ndani ya chumba chake.
Nikazitoa nguo zangu kama niliyepagawa.
Tausi akawa akiniangalia kwa wizi wizi huku akiona aibu,
nikaanza kumtoa nguo zake taratibu. Nikamkumbatia na
kulifungulia bomba la mvua wakati tayari nimerekebisha
mchanganyiko uliotoa maji ya uvuguvugu.
Nilikuwa nikimsugua kwa kugusa zile pointi muhimu ambapo
nilikuwa pale mahsusi kwa ajili hiyo. Tulipomaliza kuoga
alikuwa hoi, nikamfuta taratibu na kujifuta mwenyewe.
Nikamnyanyua kumrudisha kitandani.
Tausi alikuwa mpole sana mithili ya ngamia aliyepigwa dua na
kulala akisubiri kisu kipite shingoni, niliendelea
kumchokoza na kumhamasisha. Naye akijibu kwa kutoa
ushirikiano unaostahili.
**********
Ilikuwa yapata saa saba za usiku tuliporudi bafuni kuoga.
Ilionekana dhahiri kuwa Tausi hakutaka niondoke usiku ule,
muda wote alikuwa kaniganda.
Tulirudi kulala kitandani lakini pamoja na kuifanya shughuli
iliyonipeleka pale kwa ufanisi wa hali ya juu, akili yangu
yote ilikuwa juu ya namna ntakayofanya ili niweze kutoka
katika jumba lile bila kushtukiwa.
"Saa kumi na mbili walinzi wanabadilishana, utatoka muda
huo" alisema Tausi huku akipandisha kifua chake juu ya kifua
changu. Baada ya muda Tausi alikuwa amelala fofofo kifuani
kwangu kwa kudeka, lakini sikuwa hata na lepe la usingizi.
Nilishindwa kuelewa ni nini Tausi anachonitakia mtoto wa
mwanamke mwenzake. Kutokana na uchovu nilionao baadaye
nilijikuta na mimi nikipitiwa na usingizi.
Tulikuja kushtuka saa mbili kasoro dakika chache, ilibidi
aanze kutoka Tausi ili aangalie hali ilivyo. Kote kulikuwa
kumejaa wafanyakazi na walinzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na tayari kulikuwa na wengine ambao walikuwa tayari kwa
ajili ya kukifanyia usafi chumba cha Tausi. Tausi akarudi
ndani tulibaki tunaangaliana tusijue la kufanya.
"Tutafanyaje Hoza?" Aliniuliza Tausi akiwa na hofu.
Nilimfuata aliposimama, nikamkumbatia kwa nguvu kumtoa hofu. Nilijua kuwa hata nikiogopa isingesaidia kitu sana sana
ningepoteza uwezo wa kufikiri. "Nitatoka tu, usihofu"
nilimwambia nikimvutia kitandani na kulianzisha tena.
"Wee Hoza, huogopi?" aliniuliza akiwa kakosa raha. Nami
sikumjibu bali niliendelea kumlegeza viungo na kumpagawisha.
Tukawa tumejilaza kitandani, ’nikimkuza’.
Baada ya kumalisha shughuli pevu ya kumlea Tausi, tukawa
kitandani tukipumzika. Nikaanza kumweleza Tausi. "Leo
itanibidi niondoke, niache kazi." Tausi alishtuka sana na
kuniangalia.
"Kwa nini?"
"Hadi sasa watakuwa wamekwishagundua kuwa sipo, na sitaweza kuelezea nilipokuwa. Kwa hiyo sina budi
kutoroka!" Machozi yalianza kumtoka Tausi, mwisho akaanza
kulia akinikumbatia kwa nguvu.
"Utaishije Hoza mpenzi wangu bila kazi, isitoshe ni lazima
baba atakusaka ili kujua ulipokimbilia. Atakuumiza au
atakuweka ndani" aliongea kwa uchungu Tausi. Nilimhakikishia
Tausi kuwa nitakuwa poa tu.
Nilijaribu kucheza na akili yake nikafanikiwa kumfanya
aniamini. Akanifungia kwenye kabati kubwa la nguo lililo
ukutani kisha yeye akatoka kuelekea sebuleni kwao. Nikasikia
watumishi wakiingia kufanya usafi, huku wakimteta kuwa
amechelewa sana kutoka huku wakichunguza ili kujua
kilichomchelewesha.
Bahati nzuri mashuka yote yaliyotumika tuliyaficha, alikuwa
anataka ayafue mwenyewe kwa kuwa yalikuwa na siri kubwa.
Watumishi walimaliza wakaondoka na umbeya wao. Mara Tausi
akaingia, akaufunga mlango wake na kunitoa mule kabatini.
"Njoo tule" Alikuwa kabeba msosi wa maana! Baada ya
kuhifadhi ile menyu tumboni, tukarudi kitandani na kulala
huku tukipiga stori na kupanga namna tutakavyokuwa
tukiwasiliana baada ya mimi kutoka pale.
Giza lilipoingia alinipa cheni yake ya dhahabu na simu yake,
mi nikamuachia ile Nokia ya jeneza (3310). Nikaanza safari
yangu ya kutoka. Kufika kwenye chumba cha giza nikaanza
kupandisha ngazi taratibu kuelekea juu, kwa tahadhari.
Ghafla nikahisi nimewekewa kitu cha baridi kichwani, nikajua
ni bunduki! "Tulia hivyo ulivyo!" ilisikika sauti nzito.
Niliongozwa kupanda juu huku mtutu ukiwa kichwani. Ilibidi
nijifanye mwoga sana, nikawa nalia nikiomboleza kuwa
wasiniue mi sio mwizi.
Nilifanya hivyo ili nitakapohojiwa iwe rahisi kwao kuamini
kuwa nasema ukweli hata kama ningewadanganya. Nilipofika juu nikakalishwa chini, wakaongezeka walinzi wengine wawili.
Wakati huo kote kulikuwa shwari, ni mbwa tu waliokuwa
wakizungukazunguka.
"We ni nani na unatafuta nini humu?" Kabla sijajibu mlinzi
mmoja akanimulika na tochi usoni, nikafumba macho kuzuia
mwanga mkali wa tochi usiniumize. "Kha! We mgosi! Hoza!"
Kimya kilitawala kwa sekunde chache, yule aliyeniwekea mtutu
wa bunduki akautoa kichwani kwangu. Wote wakazunguka na
kusimama mbele yangu. Walinihoji pale kwa zaidi ya dakika
kumi, ilibidi niwaambie ukweli kuwa nilienda kum’binjukia
Tausi.
Nilijua bila kuwaeleza vile yangefumuka mambo kuhusiana na
upekuzi nilioufanya ofisini kwa Mzee Nurdin. Hakuna
aliyeamini kama ni kweli nilikuwa kwa Tausi hadi pale
nilipompigia Tausi na kumweleza kuwa nimekamatwa na walinzi
na wanataka kunipeleka kwa Mzee Nurdin.
Kimsingi nilichomwambia Tausi ndicho nilichoelekezwa na
walinzi niseme. Alichosema Tausi ni kuwa nimpe mlinzi
mmojawapo aongee naye. Alichosema na yule mlinzi ni siri yao
lakini kilichofanyika toka pale ni kwamba nilipelekwa hadi
kibandani kwangu, nikachukua vitu vyangu vya muhimu.
Baada ya hapo nilisindikizwa hadi nje ya geti kubwa na
kuruhusiwa kuondoka. Nijani wale walinzi walikuwa wakinisifu
japo kwa kutumia maneno ya kuudhi. Eti waliniambia mimi ni
mchawi, nimemloga mtoto wa bosi wao hadi akaingia laini.
Nilikereka kwa namna walivyonishusha kiwango lakini sikutia
neno, niliona ni heri nusu shari. Unajua nikiamuaga
kujifanya bwege hadi utanichukia, lakini ili mradi ubwege
huo uwe ni kwa faida yangu.
Nilipofika mbali na pale kwa Mzee Nurdin, ilinibidi nitoe
taarifa kwa mkuu kuhusu lililotokea lakini sikumwambia kuwa
niliuzamia uroda wa Tausi, nilimdanganya kuwa niliingia
kuendelea na uchunguzi wangu.
Kikubwa kilichonisukuma kutoa taarifa usiku ule ni usafiri,
sikuwa na namna yeyote ya kufika nyumbani usiku ule. Mkuu
akanitumia gari lakini aliniamuru kwamba niripoti ofisini
kwake usiku ule ule kwa ajili ya majadiliano zaidi.
Kwa sauti aliyokuwa akiiongea mkuu nilijua wazi kuwa
kitawaka, ila kwa kulinganisha na uroda nilioupata kwa Tausi
sikuwa na wasiwasi wowote. Nilichukulia poa tu, kama mbwai
mbwai!
Njia nzima nilikuwa nikiwasiliana na Tausi, alionekana
ameridhika sana na mapenzi niliyompa na alikuwa na matarajio
makubwa sana kutokana na uhusiano tulioanzisha. Ila kuna
kitu kimoja kilikuwa kinanitatiza kuhusiana na mapenzi
nilioyaanzisha na Tausi, nitamwambiaje kuwa mimi ni
mpelelezi?
Mara zote nilijisikia kumweleza kutokana na maongezi yake
ambayo yalinisisitiza nijiendeleze kielimu ili nipate kazi
nzuri tuweze kuishi maisha ya raha.
Katika kipindi kile cha takribani miezi mitano kasoro
nilichokuwa kwa Mzee Nurdin niligundua vitu vingi sana
kutokana na mienendo ya ingia toka ya baadhi ya watumishi wa
serikali wasio waaminifu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikubwa kilichokuwa kikiniweka ni kujua ni lini wangefanya
biashara yao ili nitoe taarifa wakamatwe, nilikuwa hasa
naivizia biashara ya kusafirisha binadamu.
Usiku ule nilikaa na mkuu hadi kunakucha tukijadili mambo
mbali mbali kuhusiana na uchunguzi wangu. Baada ya
kuridhika, mkuu akaniruhusu kupumzika kwa siku tatu tu.
Nikarudi nyumbani kwangu kwa mara ya kwanza baada ya karibia miezi mitano.
Nyumba yangu iko maeneo ya Boko, haiko mbali sana na bahari
ya Hindi. Niliingia na kujitupa kitandani ili kupunguza
uchovu wa kazi na wa kulala sehemu mbovu kwa miezi.
Jioni ya siku hiyo baada ya kupumzika na kurekebisha masuala
mbalimbali ya nyumbani, niliinua simu na kumpigia Tausi ili
nimjulie hali. Simu ya Tausi haikuwa ikipatikana.
Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio huku nikiijaribu tena
mara kadhaa bila mafanikio. Kichwa kikaanza kuniuma! Sio
siri, Tausi nilimpenda toka moyoni, nilimpenda haswa na hilo
hata mwenyewe alilijua.
Hadi naamka asubuhi siku ya pili, simu ya Tausi bado ilikuwa
haipatikani. Nikaanza kufikiria namna ya kuwasiliana na
Tausi, sikuweza kuvumilia kabisa ukimya ule. Lazima niende,
lazima nionane na Tausi au nipate habari zake kwa hali
yeyote.
Siku mbili za kutowasiliana na Tausi zilikuwa ni ngumu sana
kwangu. Nilifikiria kumkamata msichana wangu yeyote wa
zamani anitoe mawazo lakini katika mademu wangu wote
niliowafikiria hakuna aliyekaribia kiwango cha kunitoa
mawazo ya Tausi.
Giza lilipoingia nilivaa suti yangu nyeusi, ndani nilivaa
fulana ya bluu bahari na kichwani nilivaa pama kubwa jeusi
lililoficha kidogo uso huku macho nikiyaficha na miwani.
Nikakachukua kagari kangu keusi aina ya Toyota Starlet na
kutoka pale kwa mwendo wa kasi.
Akili yangu yote ilikuwa ni kuhusu Tausi, nikawa
nimeshapanga cha kufanya. Baada ya muda mchache nikawa
nakaribia geti la nyumbani kwa Mzee Nurdin, niliongeza sauti
ya muziki katika gari.
Kutokana na muziki kuwa mzito, gari lenyewe lilikuwa
linatikisika. Niliongeza spidi na kuingia kwa kasi katika
geti ambalo lilikuwa limeachwa wazi na walinzi.
Nikalisimamisha karibu kabisa na lango la nyumba kubwa.
Nikafungua mlango wa gari na kutoka bila kuufunga.
Kutahamaki walinzi wakawa wamenizunguka na silaha mkononi,
nikaanza kutukana kwa kutumia lugha za Kifaransa na
Kiingereza.
Nilikuwa nikitukana huku nikiangalia lango la nyumba kubwa,
hakuna mlinzi aliyejaribu kunijibu chochote kwa kuwa
hawakuwa wakielewa nilichokuwa nakizungumza.
Katika uhalisia, kwa kitendo hicho nilichokuwa nikikifanya
pale ni tiketi ya kufukuzwa kazi moja kwa moja na
kufunguliwa kesi kwa mujibu sheria za jeshi. Lakini
sikufikiria chochote, akili yangu ilikuwa kwa penzi la
Tausi.
Nilikuwa nikidai nimemfuata mdogo wangu Hoza ambaye
amechukuliwa kijijini na kuletwa kutumikishwa kazi kwa Mzee
Nurdin. Nadhani walinzi walichokuwa wakisikia ni jina tu la
Hoza.
Ilibidi atoke Mzee Nurdin mwenyewe ambaye ndiye anayejua
Kiingereza kwa ufasaha. Nikabadilisha na kuanza kuongea
kifaransa tupu, nilijua kuwa hawatakuwa na ujanja zaidi ya
kumtoa Tausi.
Katika kipindi nilichokaa niligundua kuwa Tausi anakifahamu
Kifaransa vizuri mno kutokana na kusomea nchi zinazotumia
lugha ya Kifaransa.
Muda mfupi kidogo Tausi akaitwa, kitu cha kwanza
nilichokigundua kwa Tausi ni kwamba, alikuwa akiniangalia
sana kifuani. Nikagundua kosa nililolifanya, nilivaa mkufu
alionipa Tausi.
Nikamwambia kuwa awaambie kuwa mimi ni kaka yake Hoza,
nimerudi toka ughaibuni na kukuta kuwa mdogo wangu
amechukuliwa kutumikishwa kazi.
Tausi akawa anawatafsiria huku macho yake yakinichunguza
kupita kiasi. Tausi aliniambia kuwa Hoza katoroka, ila
alivyoufikisha ujumbe huo alikuwa kama anayenitega. "Kama
Hoza sio wewe, Hoza alitoroka."
Moyo ukaanza kwenda kasi, nikamuuliza kama kuna ajuaye
kifaransa pale, akanijibu hakuna. Ila aliniambia kuwa
anahisi Mzee Nurdin anasikia juu juu ila hataki kujionyesha
kama anajua. Nikaamua liwalo na liwe, nikamchana laivu.
"Mbona simu yako haipatikani?" nilimuuliza swali ambalo
lilimfanya atake kuanguka kwa mshtuko.
"Ni wewe?" Nilihisi kitu kutokana na mtazamo wa Mzee Nurdin.
Baadae nililijua kosa langu, unajua nilipofika pale mara ya
kwanza nilikuwa na mzuka, nilikuwa napayuka hovyo hovyo,
lakini alipotoka Tausi nilipigwa ganzi.
Ujasiri wangu wote ulitoweka, nilijisikia kama nimrukie,
nimkumbatie na kummiminia mibusu isiyo idadi. Nilikuwa
nimemmisi haswa mpenzi wangu Tausi. Kingine kilichonifanya
niache kupayuka ni ukweli kuwa nilikuwa nikijaribu
kumwangalia kwa umakini kama yuko salama, ukimya wake
ulinitisha sana.
Sijui nikuhadithieje ili upate picha ya urembo wa Tausi,
huyu binti amenifanya mtumwa ndani ya moyo wangu. Alikuwa
amevaa gauni refu na pana huku amejifunika kichwani, lakini
haikutosha kuufunika urembo wake uliokithiri. Nilijikuta
nakwama kuendelea kuigiza.
Nilipomtupia jicho Mzee Nurdin, nilihisi kuwa aliwapa ishara
fulani walinzi wake. Mlio wa hatari ukalia kichwani mwangu,
hasa pale walinzi hao walipotawanyika.
Tausi akarudia tena kuniuliza swali lake, "Ni wewe?"
Sikumjibu kwa kuwa sikuweza kumdanganya, bali nikamwambia
kuwa nitarudi siku nyingine kupata habari za Hoza. Ukweli ni
kwamba nilikuwa najichanganya changanya katika kauli zangu
ila kikubwa naamini kuwa Tausi alishajua kuwa ni mimi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila nilijishebedua kumwomba kuwa anipe taarifa yeyote
atakayoipata kuhusu Hoza, nikajifanya kusema kuwa hata kama
atakuwa amekufa wasisite kunijuza. Nikamtajia namba yangu
kwa kuirudia rudia ili hata kama karatasi litakaloandikiwa
namba yangu likibaki kwa Mzee Nurdin, Tausi naye awe
kaikariri kichwani mwake.
Wasiwasi wa kuwa Tausi ni mzima wa afya au la ulinitoka, ila
nikawa ukaonegezeka wasiwasi mwingine. Kanimwaga? Kama Tausi ni mzima, ni nini kilichokuwa kikimfanya asinipigie? Na kama
kungekuwa na bifu kati yake na wazazi wake mbona sikuona
dalili yeyote alipoitwa na Mzee Nurdin.
Kwa kuwa namba hiyo ni rahisi sana kukaririka, nilikuwa na
uhakika kuwa Tausi ataikariri. Kazi ilikuwa ni kushika namba
ya kuanzia ya mtandao tu. Sikutaka kuaga, nikaingia ndani ya
gari langu na kuligeuza kwa fujo.
Kufika getini nikalikuta geti limefungwa. Kila nilipopiga
honi hakukuwa na dalili za kufunguliwa, nikajua kuwa
nimekwisha.
Nilianza kujilaumu kwa kuwa mtumwa wa penzi la Tausi, nikawa
nikiwaza ni nini kingetokea endapo taarifa zingemfikia mkuu.
Heshima yangu yote ingepotea achilia mbali kupoteza kazi na
kufukunguliwa mashitaka.
Nilianza kuingiwa na ubaridi, kutahamaki nikaliona difenda
la polisi likiingia kwa kasi. Wakati halijasimama vizuri
wakashuka vijana wakazi kama watano hivi, wote wakiwa na
silaha. Nikajua hapa tena kumekucha, akili yangu ikaanza
kwenda spidi japo haikuwa ikiweza kufikiria jambo lolote kwa
sekunde kadhaa.
Nikaanza kupata picha ya magazeti ya kesho yake ambavyo
yangeripoti tukio hilo. ’Mzee Nurdin anusurika kuuawa,
Jambazi lamiminiwa risasi na polisi’ Nikaanza kusisimkwa
mwili, nikawa namuona mkuu anavyoipokea taarifa hiyo.
Nikajiona kweli nimebugi stepu kwenda pale, nikajua tayari
’nimeingia choo cha kike’.
Kabla sijashangaa vizuri likaingia gari jingine la polisi
likiwa na msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Kutahamaki
gari langu likawa limezungukwa likiwa chini ya ulinzi.
Kwanza nilifikiria nikubali kukamatwa halafu nikifika
kituoni nijitambulishe lakini kutokana na mawasiliano
yaliyokuwa yakifanyika nikahisi hatari. Wangeweza
kunimiminia risasi kisha wakanisingizia ujambazi, nikapiga
akili ya haraka haraka nikapata wazo.
Nikaitoa simu yangu kumtafuta Omar, huyu Omar ni rafiki
yangu mkubwa na tulikuwa wote mafunzoni ila yeye amepangiwa
kuwa katika misafara ya rais.
Mimi na Omar huwa tunasaidiana sana katika vimeo hasa
ambavyo hatutaki wakubwa wetu wajue japo mwenzangu amenizidi kwa viskendo vya hapa na pale. Wakati huo yule bosi wa
upelelezi alikuwa akiongea na Tausi na Mzee Nurdin huku gari
langu likiwa limewekwa chini ya ulinzi na vijana wa kazi.
Walipomaliza maongezi yao akaja liliposimama gari langu na
kunionyesha ishara ya kushuka kwa kuwa nilikuwa nimejifungia
garini. Sikuteremka wala kujibu lolote, mijamaa ikawa
inalizunguka zunguka tu gari langu. Zilipita takribani
dakika tano wakiwa wanajadiliana namna ya kufanya.
Kimsingi wasingepata maelezo ya kutoa endapo wangenimiminia
risasi mule ndani ya gari lakini endapo ningetoka wangekuwa
na mengi ya kusema na kuandika.
Ghafla ulionekana mwanga mkali wa taa za magari kisha
ulisikika mlio wa magari matatu yanayoongozana. Yakasimama
nje ya geti.
Zilikuwa benzi mbili nyeusi zenye namba za ikulu, walinzi
wakazifungulia huku wale polisi wakibaki wameshangaa. Kule
barazani pia nilimuona Mzee Nurdin na mlinzi wake mmoja
wamepigwa na butwaa.
Akateremka Omar, nikashusha pumzi ndefu. Msaidizi wa mkuu wa
upelelezi wa mkoa akamsogelea na kutoa heshima. Wakati huo
kwenye kila benz walitoka watu watatu watatu waliovalia suti
nadhifu, jumla wakawa tisa, na Omar alikuwa wa kumi.
Polisi wote wakaamuriwa kukaa mbali na gari langu, sijui
Omar alimwambia nini yule bosi wa polisi bali baada ya
kuongea kidogo ndipo amri ile ilitolewa. Nikatoka ndani ya
gari, Omar na wenzake wakanipa heshima.
Nikachekea moyoni, na kwa haraka haraka nikajua ilikuwa ni
namna ya kuwatishia zaidi wakina Mzee Nurdin kuhusu wadhifa
wangu.
Nikawapa mikono na kurudi ndani ya gari langu, nikafungulia
muziki kwa sauti kubwa kama kawaida. Nyumbani kwa Mzee
Nurdin kukageuka kuwa kama ukumbi wa disko kwa muda kabla
sijapandisha vioo tena.
Omar akarudi ndani ya gari na wenzake wakamfuata na kuingia
kila mtu kwenye gari alilotokea, likaanza kuondoka la kwanza
kisha nikawasha gari langu na kulifuata. Nyuma lilifuatia
gari alilopanda Omar, na jingine likamalizia nikaacha
mshangao mkubwa nyumbani kwa Mzee Nurdin.Ila bado nilikuwa
na mawazo kuhusu Tausi.
Tuliongozana kwa umbali fulani kisha tukaachana huku Omar
akitaka kujua chanzo cha yote yaliyonitokea, ila ’nikampotezea’.
Nikamwambia ningemhadithia siku nyingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila nilikuja kumhadithia mkasa mzima wa kumfukuzia Tausi
japo uongo ulikuwa ni mwingi zaidi, sikumwambia kama vile
hasa ilivyo na kazi niliyopewa na mkuu, nilimdanganya kuwa
nilionana naye nje ya nchi.
Baada ya siku moja tu toka niokolewe na kina Omar nyumbani
kwa Mzee Nurdin nikapokea simu toka kwa Tausi. "Halo..Jhe
mapele Tausi!" alimaanisha kuwa naitwa Tausi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment