Search This Blog

Sunday 19 June 2022

AJIRA TOKA KUZIMU - 3

 





    Simulizi : Ajira Kutoka Kuzimu

    Sehemu Ya Tatu (3)



     Brenda Brebre aliyetegemea kuwa Tembo atamsindikiza na kumwacha barabarani alishangaa safari inaenda hadi Mlimani City. Tembo akaegesha gari lake.

    “Kumbe na wewe ulikuwa unakuja huku?.” Brebre alimuuliza Tembo. Tembo akaachia tabasamu kabla ya kujibu, “Hapana nimefanya hivi kwa sababu yako Bre. Naamini hakuna kinachoharibika”

    Brenda akajisikia ufahari mkubwa sana kufikishwa pale Mlimani city na gari binafsi. Alijua lazima watu watamkodolea jicho. Ni kweli magari yapo mengi Mlimani city na ya kifahari lakini wapo wanaokuja kwa miguu, pikipiki ama bajaji, hawa ndio Brenda aliwafikiria jinsi watakavyomshangaa.

    Na alipenda sana kutazamwa na watu… kimoyomoyo akajipongeza kwa kuvaa nguo nzuri na kupendeza.

    Tembo alikuwa makini katika mahesabu yake. Kile kitendo cha kujibiwa majibu ya ajabuajabu na Mamamia kilikuwa kinamsumbua kichwa hakutaka kuzichanga karata zake vibaya kwa Brenda. Huku akaamua kuwa mtulivu na kwenda kwa hatua za kunyatia. Huku kichwani akiamini kuwa simba mwenda pole…….

    Bado kile kithembe cha Brenda kilikuwa kinampa mshawasha.

    Wakaingia ndani. Kwanza wakaanza kung’arisha macho wakitazama wapi pa kuanzia. Tembo akawa mtulivu akimtazama Brenda.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Brenda akaanza kuelekea mashariki, Tembo akafuata. Mara wakaingia katika mlango mmoja, humo ndani wakakutana na Vitabu mbalimbali, Brenda akawa anavitazama bei bila kuulizia.

    Tembo akamshtukia kuwa alikuwa akiogopa zile bei.

    Kosa kubwa sana kumwonyesha Munyama Mukubwa kama Tembo udhaifu wako ilihali ana pesa ambazo anaamini kuwa ni kamba ya kuvutia vitamu vingi vya duniani!!

    “Unapenda sana kusoma vitabu eeh!!.”

    “Yaani sana, napenda novels na kuwatch movies.” Brenda akatupia kiswanglish matata.

    “Tena kama riwaya za huyu nani hu…Hadley Chase, dah!” alizidi kutiririka.

    Tembo akatumia muda kidogo akaziona hizo riwaya alizozitamani Brenda.

    Elfu kumi na nane kitu gani kwa Tembo mwenye ajira bab kubwa isiyotoa jasho sana. Tembo akachomoa kitabu akalipia.

    Wakatoka hapo. Sasa wakaifikia Supermarket. Mara Brenda aseme natamani marashi yale, Tembo analipia, mara ile poda, Tembo analipia. Kama mchezo wa kuigiza vile.

    He!! Hiyo thabuni jamani!!!! Tembo analipia usiwe na wasiwasi.

    “Huo mthwaki umenivutia jamani..”… Tembo atalipa!!

    “Hathani angalia ile thimu. Mh!! Kuna thimu kali jamani.” Alijisemesha Brenda. Tembo akagundua kuwa anatakiwa kununua.

    Kosa kubwa sana!!!

    “Unaipenda eeh!!” Tembo akamuuliza.

    Brenda hakujibu. Akajidai hakusikia. Tembo hakuuliza tena.

    Kila alichokitaka Brenda sasa alikuwa amenunuliwa.

    Wakatoka nje!! Haoo Garini.

    Safari ya kumrudisha Brenda nyumbani.

    “Dah!! Brenda una haraka sana.”

    “Kwanini umeniulidha hivyo?.”

    “We nijibu kama una haraka sana.”

    “Thio kivile.” Brenda akatoa jibu ambalo Tembo alilitamani na sasa lilikuwa limetoka.

    “Safi sana twende tukale, nimekumbuka hatujala bado.”

    “Mhhh!! Jamani weweee!! Haya twende wapi huko.” Aliuliza

    “Twende hapa wapi hii ya Kinondoni hii inaitwaje.”

    “Best Bite…whaaooo!! Napenda chipth dhao wale.” Mama kithembe alijibu kwa furaha. Wakati huu alimuangukia Tembo begani.

    Ndege anajileta mwenyewe!!! Tembo aliwaza kisha akakanyaga mafuta.



    Huduma ilikuwa lazima ichelewe, Brenda alikuwa ametoa oda ya maana kama vile ile pesa angelipia yeye. Tembo akawaza juu ya kukomolewa, akamwona Brenda anataka kumkomoa.

    Akajichekea nafsini huku akimpa pole kimoyomoyo kwani kiama chake kilikuwa kinakuja.

    Wakati huo Brenda alikuwa haishi kubugia Ice cream za bei ghali. Tembo alikuwa ametulizana na juisi yake katika glasi kubwa.

    Ilikuwa juisi ya ‘water mellon’. Mnyama hana wasiwasi kuhusu pesa huku akiamini pesa ni kamba tu ya kuvutia vitu vizuri vizuri.

    Kuna vizuri gani zaidi ya wanawake?? Tembo akacheka huku akilifurahia jina lake na hilo jingine la utani. Munyama Mukubwa kamba fedha!!

    Chakula kikafika. Brenda kama vile alikuwa ametoka mfungoni kwa jinsi alivyoshambulia kile chakula. Tembo alikuwa anamchora tu.

    Walipomaliza kula, Tembo akagusia kuhusu kwenda kuangalia sinema.

    Mlemle Brenda akanasa. Alikuwa mlevi wa sinema.

    Quality Center!! Hapa ndipo walipokuwa majira ya saa tatu usiku.

    Waliingia kama mtu na mwenza wake. Wakalipia tiketi wakajichukulia nafasi zao. Walidumu kwa muda wa nusu saa Tembo akitafuta namna ya kufunga goli lake.

    “Unafahamu Vampaya wewe.” Tembo alimuuliza Brenda.

    Akili ya Brenda ikatoka katika filamu.

    “Yeah!! Nafahamu halafu nadhipenda hidho filamu, lakini da Lulu anaogopa kweli.”

    “Lulu ndo nani?.” Tembo aliuliza.

    “Dada Mamamia jamani.”

    “Aaah!! Ok nimekumbuka anaitwa Lulu.”

    “Sikia sasa unaikumbuka ile simu kule. Mlimani city.”

    “Yeah!! iPhone.”

    “Tukacheze mchezo ukinishinda nakununulia.”

    Moyo wa Brenda ukapasuka kwa matamanio. Akajaribu kuificha hofu yake. Lakini Tembo aligundua akajifanya hajagundua.

    “Mchezo gani.”

    “Wa mavampaya. Si hauogopi wewe.”

    “Siogopi ndio. Twende.”

    Wakasimama wakatoka ukumbini. Wakaelekea lilipo jumba kwa ajili ya madude hayo ya kutisha ambayo yapo katika mfumo wa 3D, unavaa miwani maalumu kisha unaingia katika chumba hicho kwa ajili ya kutazamana na madudu haya.

    Msomaji teknolojia ya 3D inamwezesha mtazamaji kuwa kama yupo ndani ya tukio. Kama ni mpira unachezwa basi nawe utajiona upo kiwanjani kama ni vita nawe utajihisi vitani. Na kama ni haya mavampaya basi utaliona kama linakukabili.

    Brenda alikuwa hajawahi kuingia katika chumba hiki pale Quality Center.

    Ambaye hataogopa ndio atakuwa amemshinda mwenzake!!!

    Hiyo ndio ilikuwa amri ya mchezo huo.

    Laiti kama Brenda angeijua janja ya Tembo angebaki zake kwenye sinema. Lakini maskini binti kithembe hakujua lolote.

    Hali ikaanza kuwa tete Brenda akawa anaogopa waziwazi baada ya kuwa na miwani usoni, mavampaya yakaanza kumtisha.

    Harufu ya kifo!!! Waziwazi.

    Wapi akimbilie kuepuka kifo hiki.

    Tembo pekee ndiye alikuwa msaada wake.

    Brenda akamkumbatia Tembo, ni hicho Tembo alikuwa anasubiri. Yeye hakuwa anaogopa chochote kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kuingia katika chumba hicho.

    Tembo akampokea Brenda kifuani.

    Mchomo wa matiti yaliyosimama imara ukapenya katika kifua cha Tembo.

    Akasisimka sana!!

    Bado Brenda aliendelea kuhema juu juu huku akiendelea kumkumbatia Tembo.

    Tembo akiwa na akili zake za kuzimu. Akafanya kitendo kingine cha ghafla. Akapenyeza mikono yake ikakutana na kigauni ambacho kilipangana na kitovu aidha kibaki nje ama kifunikwe. Kitovu kikashinda. Kikachomoza nje. Mara mkono ukagusa kitu kingine.

    Huyu mwenye kithembe naye alikuwa na kicheni chembamba kiunoni.

    Tembo mkorofi!! Akashuka zaidi…zaidi…zaidi tena…

    Akakutana na joto lenye ladha tamu kupita zote duniani!!!! Achana na hili joto la Dar linalokera… hilo joto la huko ni la aina yake!!

    Ni mikono pekee iliyofaidi lakini mwili mzima ulisisimka kama vile na wenyewe ulikuwa katika lile joto ambalo watu wenye maadili wanaliita joto la SIRINI.

    Brenda alikuwa msafi haswaa Tembo na mkono wake wa kuume walikiri jambo hilo.

    Kilichomchekesha Tembo ni uoga wa Brenda.

    Yaani anatetemeka hadi huku!! Hii mbona hatari. Vidole vilizungumza.

    Maskini Brenda hakugundua kama Tembo ametia mkono wake katika sehemu maalumu kama zile. Alikuwa katika uoga.

    Hata walipotoka nje tena huku akiwa bado katika taharuki hakujua kama kuna wakati mkono huu ambao sasa unaendesha gari ulimpapasa kwa uhuru mkubwa bila yeye kupiga kelele zozote.

    Kwa Tembo ulikuwa ni ushindi. Ushindi mkubwa.

    Brenda mdogo wake Mamamia akarudishwa hadi nyumbani.

    Noti nyekundu na nyingine zenye kifaru zilichanganyikana kubeba thamani ya shilingi laki mbili na nusu, zote katika himaya ya umiliki wa Brenda.

    Brenda alidhani kuwa Tembo amekosea lakini haikuwa hivyo. Pesa zile alikuwa amepewa.

    Brenda akazipokea bila kujua ni kazi gani hasa amefanya inayostahili malipo yale. Kisha akapewa tunda aina ya Apple ambalo hakumbuki Tembo alilinunua muda gani lakini hilo halikumshangaza.

    “Mpelekee Mamamia hilo, usimwambie nani amempa ila nitampigia simu. Namfanyia kama sapraizi.” Tembo alimwambia Brenda huku akimkabidhi. Brenda akapokea kisha akaachia tabasamu mwanana. Akamkumbatia Tembo wakaagana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa Brenda ilikuwa siku ya kipekee sana ya kufanya matanuzi kisha akapokea ujira mzuri kabisa.

    “Kuna wakaka wengine wathtaarabu jamani, angekuwa mwingine tayari keshanitongodha.” Alijisemea Brenda kwa sauti ya chini wakati Tembo akigeuza gari kisha akatokomea.

    Laiti kama Brenda angekuwa anaifahamu walau historia moja tu ya Hassan Tembo Munyama mkubwa. Asingediriki kupokea mali zile pamoja na lile tunda.

    Lakini hakujua lolote maskini binti kithembe!!

    Sasa alitakiwa kumpatia lile tunda dada yake aitwaye Lulu au maarufu kama Mamamia. Hajui Tembo kama aliaibishwa mchana na dada yake, hajui kama Tembo anakitamani kiuno cha Mamamia mbacho huzunguka na kupagawisha mashabiki jukwaani. Sasa Tembo alikitaka kino hicho kitandani.



     ****

    Brenda aliingia ndani na kumkuta Mamamia amejibweteka sebuleni akifuatilia tamthilia za kifilipino ambazo tangu utotoni alikuwa mfuasi mkubwa sana.

    Brenda akanyata na kufika akamfumba macho dada yake huyu. Mamamia akabahatisha akawa amepatia. Brenda akamwachia.

    “Ulikuwa umeenda kukiuza wapi?.” Mamamia alimuuliza kwa utani. Brenda akacheka!!

    Akiwa katika kuzubaa kuangalia ile tamthilia, Mamamia akamkwapua lile Apple. Brenda kiutani utani akajifanya kuligombania japo hakumaanisha. Mwisho wa siku akamwambia kuwa lile Apple ni halali yake alikuwa amepewa na mtu amletee. Mamamia alisita kutafuna kipande cha Apple alichokuwa amekitupia mdomoni.

    “Mtu? Nani huyo?” alihoji.

    “We kula kwani mpaka umjue.” Alijibu Brenda. Mamamia akajua ni janja ya nyani mleta Apple alikuwa huyohuyo mdogo wake, akaendelea kutafuna bila wasiwasi. Sasa Apple lilikuwa limebakia kipande kidogo.

    “Amekupa Hathani hilo tunda.we jishaue tu hapo.”

    “Hassan..Hassan ndo nani?.” Aliuliza Mamamia.

    Yule rafiki yako aliyekuja kukutafuta hapa asubuhi.

    “He!! Mazito. Umekutana naye wapi tena? Maana hata sura yake siikumbuki. Ninachokumbuka ni chaufupi kile dah!! Halafu ni mwandishi wa habari sijui….” Aliuliza kwa namna ya utafiti Mamamia. Brenda akafikiria kwa muda kabla ya kujibu.

    “Huko Mlimani city.” Alidanganya.

    “Anajidanganya kununua Apple ndo Lulu nitajua kuwa napendwa au. Yaani anachekesha yule mtoto jamani, sasa mimi ananipeleka wapi yule” Alisema Mamamia kwa sauti ya chini. Alitaka kulitupa lile Apple lakini bahati mbaya kipande kikubwa tayari kilikuwa kimepenya. Akaamua kulimalizia lote. Ladha yake ilikuwa ya kawaida kama ma-Apple mengine.

    Hakutilia shaka.

    Wenzake wanahonga pesa, magari na nyumba yeye analeta mapenzi ya ma-Apple hapa!!! Alilaani Mamamia huku akimwona kuwa Hassan Tembo amepitwa na wakati na hayo mapenzi yake anatakiwa ayapeleke kijijini.

    “Ma-apple siku hizi hadi yanauzwa kwa mafungu sokoni.. ye bado anadhani ni tunda la mapenzi… hovyoooo!!” akazidi kuponda Mamamia.

    Lakini ka-Apple katamu hako!!! Alikiri Mamamia huku akiachia tabasamu. Brenda hakujua lolote linaloendelea kichwani mwa dada yake.

    Saa sita usiku kila mmoja alimuaga mwenzake usingizi ulikuwa umechukua hatamu!!

    Kila mmoja akaenda chumbani mwake.

    ***

    USIKU WA BALAA!!!



    Simu yake ilimwongoza kujua kuwa ilikuwa ni saa tisa na dakika kadhaa usiku. Alidhani kuwa amebanwa na mkojo. Akasimama uchi wa mnyama kama ilivyokawaida yake kutolala na nguo. Akajikongoja kuelekea chooni. Choo kilikuwa nje lakini si mbali kutoka hapo mlango wa chumba chake.

    Sasa aliweka kanga kiunoni!!! Alikifikia choo. Akachuchumaa akitegemea mkojo utatoka. Wapi!!! Haukutoka.

    Akasubiri tena labda utatoka.

    Bado vilevile.

    Akasimama atoke chooni. Akagundua kumbe hakuwa amebannwa na mkojo bali jambo jingine lisiloelezeka. Mamamia alikuwa ana hamu!!! Ndio alikuwa ana hamu kubwa. Hamu ya mwanaume.

    Hamu ya mwanaume? Alijiuliza. Lakini hata ndoto ya namna hiyo hakuwa ameiota.

    Akajaribu kufikiria kuwa huenda amemuota mpenzi wake. Hakuna kitu kama hicho. Hakuwa ameota ndoto yoyote inayohusisha mapenzi ama kitendo chochote kinachohusiana na ngono.

    Sasa alikuwa kitandani uchi tena kama kawaida.

    Mara akafumba macho yake na kujenga picha ya mwanaume sasa. Akajikita katika mapenzi ya hisia. Akavuta kumbukumbu mara kadhaa alizowahi kufanya mapenzi. Wapi hakuna lolote lililosaidia.

    Akagalagala kitandani. Alikuwa peke yake.

    Ghafla wazo likamjia. Akanyata na kanga moja hadi sebuleni akafungua kabati akatoka na kitu kwenye kibahasha kidogo. Kitu hicho kilikuwa kimefichwa hapo kabla.

    Akarejea chumbani kwake akawasha luninga kisha akawasha na redio. Akaweka miziki kwenye redio kisha kwenye luninga akaweka santuli (VCD) ilikuwa ni kama vile inafuatisha muziki wa kwenye redio ulivyotoka lakini ghafla….

    Ghafla zikawa picha. Picha za watu wazima warembo kwa watanashati. Walikuwa uchi bila aibu.

    Ilikuwa filamu ya ngono. Mamamia alikuwa uchi sasa. Alitumbua macho huku akijivutia hisia kuwa yeye ndiye yule mwanamke anayeonekana kwenye filamu akiwa na mwanaume.

    Akajifaragua huku na kule huenda akakidhi haja za nafsi yake!!

    Wapi!!! Haikusaidia kitu. Mamamia alikuwa bado na hamu!!! Hamu ya kitu halisi.

    Sasa ni nini hiki? Alijiuliza. Akawa anachukia sasa kumwona yule mwanamke akijiliza bila sababu tena machoni pakavu kabisa.

    Bwege kweli hili linaigiza kumbe!!!! Alihamaki Mamamia.



    Akazima luninga. Redio ikabaki kupiga miziki yake isiyokuwa na msikilizaji.

    Mamamia akajaribu kujilaza. Akawaza kumweleza mdogo wake kilichomsibu usiku huo, ausikilize ushauri wake. Alipomfikiria Brenda, mara akazidi kutetemeka zile hisia zikapanda maradufu. Akajaribu kujisuguasugua akawa anapata haueni.

    Nini hichi jamani!!!! Au ugonjwa? Alijiuliza tena. Sasa aliwasha taa ya ndani. Akajitazama, kweli haikuwa ndoto.

    Alikuwa katika hali mbaya sana. Lakini hiyo hamu sasa haikueleweka ni ya nini.

    Mh!! Ngoja ngoja huumiza matumbo. Alisema Mamamia Mango, mtaalamu wa kukata viuno jukwaani. Akaitwaa simu yake akabonyeza namba kadhaa akapiga.

    ****



    Simu yake iliyoita ilimshangaza sana kwani ulikuwa usiku mnene. Hakuwa amesinzia hata kidogo. Alikuwa yu macho akijishangaa. Mwanzo alicheka kidogo kwa alichowaza lakini sasa kilizidi kumsumbua.

    Alikuwa amebakiwa na chupi yake tu iliyo katika mfumo wa bikini. Hakulala na hiyo bikini pekee, lakini alikuwa ameshasaulasaula akatoa kisidiria, mara nguo ya kulalia. Sasa akabaki na kichupi hiki cha ajabu kuliko chupi zote duniani.

    Ndio kichupi cha ajabu!! Kichupi gani kile.

    Vimikanda viwili, mara nyuma hakifuniki. To hell!!!

    “Thatha nini tena hichi jameniii.” Binti kithembe akawa analalamika. Huku akishangaa kama zoba.

    Huyu alikuwa Brenda. Hassan Tembo alimbatiza jina zuri tu la BreBre. Alikuwa akijishangaa anavyokuwa.hali aliyokuwanayo hakuweza kuielezea. Eti alihisi mpapaso fulani hivi. Haukufanana na wa yule mpenzi wake wa siku zote. Lakini huu ulikuwa wa kitofauti.

    Thatha!! Thatha!!...au…thatha eeeeh!! Aliendelea kutema kithembe. Mara simu ikaita.

    Mh!! Nani tena anapiga thimu uthiku!! Alijiuliza kama chizi vile.

    He!! Dada naye thatha anathemaje!! Alijiuliza.

    Akapokea.

    “Njoo chumbani kwangu.” Aliambiwa. Hakuuliza swali akaenda.

    Alivaa kanga pekee, ndani kibikini kikaendelea kutawala.

    Akafika bila kugonga hodi akaingia. Mamamia alikuwa uchi

    “Dada nawe sa uthiku hivi unasemaje.”

    “Njoo ukae hapa Brenda.”

    Brenda akasogea akakaa. Mamamia alikuwa katika hali inayozidi kuwa ngumu.

    “Hebu nisuguesugue huku sijui nimekuwaje. Muwasho si muwasho yaani hee!! ” Alimpa maelekezo.

    Brenda akasita lakini bila kujua aliutoa wapi ujasiri. Akaupeleka mkono akaanza kumsugua.

    Maajabu ya dunia!!! Mamamia akaanza kunung’unika kimahaba. Kama yule mwanamke aliyekuwa katika filamu ile ya ngonoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maajabu mengine tena. Brenda naye akaipenda ile sauti.

    Kilichofuata. Akazidi kusugua kwa juhudi zote. Mamamia naye akazidi kulia kwa sauti kubwa.

    Hao hao hao wakaendelea!! Mamamia akamdaka Brenda akamkumbatia.

    Hii ndio hamu haswaaaa!!! Aliyokuwanayo Mamamia. Na hiki ndio kilikuwa kinamuwasha Brenda kule chumbani.

    Tupa kule filamu za ngono, weka mbali wapenzi wao. Hapa walipokuwa ndio palikuwa penyewe.

    Mamamia alipagawa na mikuno hiyo. Na ni kama alipoteza fahamu baada ya wawili hawa kukutanisha midomo yao.

    Mamamia akawa bize akihangaisha kiuno chake!!! Brenda naye taabani juu ya mwili wa dada yake.

    Yaani ungewaona ungedhani watu wa maana na wanafanya kitu cha maana!!! Kumbe buree wote walikuwa wasichana.

    Wewe unabisha kwa sababu haukuwaona tulia mimi nakusimulia ilivyokuwa.

    Hali ya hatari!!! Kila mmoja hataki kumwachia mwenzake. Mamamia aliporidhika hakukumbuka kusema asante alipotelea katika dimbwi la usingizi. Brenda fahamu zikamrudia vyema. Alikuwa katika mwili wa dada yake. Akajirusha pembeni, kale kabikini hakakuwepo mwilini. Na hata alipokatazama chini kalikuwa kamechanika.

    Nani kakachana thatha, thaa ngapi? Lilikuwa swali aliojiuliza

    Mamamia alikuwa uchi!!! Miujiza mingine mikubwa tu kupata kutokea katika jumba lile.

    Mashuka yalikuwa yamevurugika sana.

    Kuja kuitazama mikono yake mh!!

    Nini kimetokea? Akajiuliza.

    Mbio mbio, akakimbilia chumbani kwake. Kabla hajafika chumbani kwake akafunga breki njiani akarudi mbio tena hadi chumbani kwa Mamamia akachukua kibikini chake kilichochanika.

    Mbioo!! Chumbani kwake akiwa uchi wa mnyama.

    Mitikisiko iliyotokea maeneo ya nyuma ya mwili wake. Hiyo siwezi kusimulia. Maana haisimliki.

    Brenda alitumbua macho mbele ya kioo kilichokuwa chumbani mwake… alijitazama na kujiuliza ni kitu gani kile kimetokea. Amefanya nini na dada yake!!!

    Ilistaajabisha haswa!! Lakini alikiri kuwa alifurahia ile hali…

    Lakini na dada yake??? Dada yake tumbo moja??

    Tena walipigana na mabusu!!!

    Alipofikia hapa akatimua mbio hadi chooni, akajilazimisha kutapika… hakutapika…

    Lile Apple la Tembo lililoliwa na Mamamia, ule mpapaso maridhawa katika mwili wa Brenda kule Quality Center ukawa umezua balaa la aina yake.

    Balaa kwa ndugu wa damu moja!!!



     Hali ya hatari!!! Kila mmoja hataki kumwachia mwenzake. Mamamia aliporidhika hakukumbuka kusema asante aliupotelea katika dimbwi la usingizi. Brenda fahamu zikamrudia vyema. Alikuwa katika mwili wa dada yake. Akajirusha pembeni, kale kabikini hakakuwepo mwilini. Na hata alipokatazama chini kalikuwa kamechanika.

    Nani kakachana, saa ngapi? Lilikuwa swali.

    Mamamia alikuwa uchi!!! Miujiza mingine mikubwa tu kupata kutokea katika jumba lile.

    Mashuka yalikuwa yamevurugika sana.

    Kuja kuitazama mikono yake mh!!

    Nini kimetokea? Akajiuliza.

    Mbio mbio, akakimbilia chumbani kwake. Kabla hajafika chumbani kwake akarudi mbio tena hadi chumbani kwa Mamamia akachukua kibikini chake kilichochanika.

    Mbioo!! Chumbani kwake.

    Mitikisiko iliyotokea maeneo ya nyuma ya mwili wake. Hiyo siwezi kusimulia.



    ****



    Siku ya kwanza kila mtu alichenga asiweze kukutana na mwenzake. Mamamia alidamka alfajiri na kuondoka kwenda ajuapo yeye, Brenda naye akidhani Mamamia yupo ndani alinyata na kutoweka majira ya saa moja asubuhi kwenda katika kona za hapa na pale.

    Siku ya pili hivyo hivyo kila mmoja akijaribu kumkwepa mwenzake kwa aibu ya tukio lililotokea usiku ule chumbani.

    Siku ya tatu wakajikuta tena katika hoteli moja maarufu wakiwa kama mume na mke. Alikuwa ni Mamamia tena aliyempigia simu Brenda na kumwomba afike pale Hotelini, akitumia uongo kuwa kuna jambo zito anahitaji wazungumze….

    Alipofika hapakuwa na maongezi, macho yao yakazungumza na mwishowe wakajikuta katika nchi nyingine kabisa ya burudani.

    Brenda na Mamamia. Mtu na dada yake.

    Siku hii palikucha wakiwa wote. Hakuna aliyeweza kuizungumzia hali hii. Ndio ilikuwa ya ajabu sana lakini uajabu huo uliwafanya wafurahie sana.

    Waliongozana wakatoka kila mtu akachukua taimu zake.

    Kamchezo kakanoga. Sasa hata mchana walikuwa wanakutana faragha wanacheza kwa raha zao.

    Mwishowe Mamamia akawa anamwita Brenda honey, naye Brenda akambatiza Mamamia jina la Sweetie.



    Kwa kuwa walikuwa watoto wa kike kwao kuitana hayo majina jambo la kawaida sana. Wasichana wangapi wanaitana ‘mpenzi’ na siku zinaenda. Ama ni wangapi wanashikana viuno hadharani wenye macho hatusubiri kuambiwa tazama.

    Kwa wanaume thubutu hata kuitana ‘DEAR’…patachimbika mbona. Kwa hiyo hata kwa Mamamia na Brenda lilichukuliwa kama suala la kawaida tu.

    Kwanza ni mtu na dada yake. Nani atajali hata wakitaniana mke na mume. Hakuna aliyejali hata kidogo…..



    BALAA LATAPAKAA!!



    Alianza Brenda visa kwa mpenzi wake, mara leo hataki kupokea simu yake, mara wakikutana hataki hata wapigane mabusu motomoto yale waliyoyazoea zamani, na mbaya zaidi hakuwa tayari kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake. Alikuwa anadanganya kuwa yupo siku zake za hatari, akiambiwa kuwa watatumia kinga akaruka maili mia nne na kusema akitumia kondomu huwa anawashwa.. hivyo hayupo tayari kutumia kinga hiyo.

    Bwana akachoshwa na visa hivi!!

    Na siku akibahatika kumwingilia kimwili basi ilikuwa kama karaha kwa Brenda, hakupata ladha yoyote ile.

    Wakati zamani alikuwa akihisi mpenzi wake ananukia sana, sasa akawa anasikia harufu ya kikwapa na wakibusiana alihisi mpenzi wake ananuka kinywa!!! Kaazi kwelikweli….

    Akajaribu kulivumilia hili, lakini akagundua pia mpenzi wake huyo amekuwa mzito sana…. Badala ya kufurahi sasa akaona kuwa anachoshwa bure!!!

    Akaapa kuwa atafanya kila namna waachane!! Furaha yake yote ilikuwa kwa Mamamia!!

    Bahati nzuri mpenzi wake alikuwa na wasichana wengine. Hivyo aliitumia nafasi hiyo kuachana rasmi na Brenda baada ya visa kuzidi. Brenda akabakia na mpenzi mmoja tu. Mamamia na moyo wake ukawa na amani.



    Kwa Mamamia naye yalikuwa hayahaya ya Brenda. Ladha ya mpenzi wake ikapungua. Mwisho akamtamkia waziwazi kuwa hawezi kuendelea naye tena.

    Mbaba wa watu akachanganyikiwa. Hakuamini ameachwa. Alikuwa akijisifia sana kwa kuwa na mahusiano na msichana mwenye jina kubwa mjini kama Mamamia Mango.

    Na alikuwa amejiandaa kumuoa siku moja.

    Ndoto zikaishia pale. Mamamia alimaanisha alichokuwa amekisema. Hakuwa na sababu za moja kwa moja za kumwacha yule bwana lakini neno lake lilikuwa limesimama hivyo!!

    Naye akabaki na mpenzi mmoja. Brenda.

    “Baby I love you.” Brenda alimwambia Mamamia siku moja wakiwa chumbani wamekumbatiana

    Hakika walikuwa wamepagawa.



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TEMBO AREJEA KAZINI!!



    Hassan Tembo alikuwa amemaliza kilikizo chake kifupi alichokuwa amejipatia. Aliamua kwenda kupumzika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Tembo alijihifadhi Tanga.

    Sasa alikuwa anarejea jijini Dar es salaam.

    Ni wiki tatu zilikuwa zimepita tangu aende Tanga.

    Majira ya saa sita mchana alipaki gari yake. Nyumbani kwake. Mbagala kwa Mama Tembo.

    Aliingia ndani kuisanifu nyumba yake. Kisha akajikubali kwa uvumilivu wake. Siku zaidi ya kumi na nne bila kuwa na mwanamke.

    “Dah!! Nimevumilia aithee!!” Tembo akasema kisha akashtuka kuwa alikuwa amepitiwa na kithembe. Akatabasamu

    Kithembe!!! Akashangaa. Mara akamkumbuka Brenda.

    Upesi akapandwa na midadi yake. Akakumbuka kale ka cheni alikokaona kiunoni. Akanyanyua simu akampigia.

    Wakajuliana hali kisha wakakubaliana kukutana kwa ajili ya chakula cha jioni.

    Hotel Travertine, Magomeni. Hapa ndipo walikutanika.

    Brenda alikuwa amependeza sana huku akiwa na furaha tele.

    Alikuwa anapenda sana ofa huyu dada!!

    Na kwa Tembo alikuwa amefika. Hakujua nini maana ya hasara.

    Wakati wanapata chakula. Macho yao yaligongana. Tembo akiwa anajiandaa kung’ata pande la kuku. Brenda akiwa anapeleka Uma iliyokuwa na kipande cha nyama ndogo. Wote wakasita wakakaziana macho. Kisha kwa pamoja wakacheka.

    Tembo akaachia kile kicheko chake cha kipekee. Maalumu kwa watoto wa kike.

    “Jamani umecheka kama Kanumba jamani. Nimemmith Kanumba ” Brenda akamwambia Tembo. Mnyama mkubwa akacheka tena bila kutarajia.

    Brenda akaendelea kufurahia.

    “Rest in Peace brother…..” Tembo akajisemea na Brenda akajibu ‘Amen’



    Akiwa katika kufurahia, Brenda ambaye alikuwa amepoteza kabisa ladha ya kuwa na mwanaume akahisi kitu. Zile hisia zinazompanda akiwa na Mamamia kitandani, sasa zilikuwa hapa alipo. Alitamani kitu!!

    Yes!! Alitamani kitu kilekile ambacho Mamamia huwa anamtimizia…… lakini mbona ..mbona kama Tembo anamvutia….

    Hicho kitu huenda ni Tembo anacho.



    Macho ya Brenda yalivyobadilika kutoka Brenda Brebre na kuwa Brenda mahaba. Tembo alikiona kitendo hicho.

    Tayari kaelekea kibra huyu!!! Alijisemea Tembo huku akiachia tabasamu jingine mwanana.

    Kwa hiyo!! Yupo tayari kwa kuchinjwa.

    Tembo akawaza hayo. Kilichofuata sasa ni kuchukua chumba na jinsi gani ya kumuingiza ndani.

    Mchezo mdogo sana kwa Tembo!! Akaaga kidogo.

    Akachukua chumba palepale upesi kisha akacheza mchezo wa kimataifa, mchezo ambao msichana wa kawaida kuchomoka anahitaji kufungwa hirizi kubwa kiunoni tena hirizi inayopumua na chanjo kama laki nane mwilini.



     BAADA ya kuchukua chumba huku akiamini si jambo jepesi kumwambia msichana aingie chumbani naye akaingia. Na alijiwekea tahadhari hiyo kwa sababu tayari aligundua kuwa familia ya akina Mamamia ni ya tofauti kiasi chake asije akakurupuka kichwakichwa akaukosea mchezo wake aliouanza vyema kuanzia sehemu ya kwanza.

    Brebre hakujua kama Tembo amechukua chumba tayari.. na ni jambo hilo ambalo Tembo alitaka iwe.

    Akarejea kuketi alipokuwa Brenda wakaendelea kutafuna chakula.

    “Brenda,,” Tembo akamuita… kama kawaida akamkazia macho zaidi yaleyale ya kupagawisha mabinti. Brenda mapigo ya moyo juu juu akaitika na sauti haikutoka.

    “Mbona kama haupo sawa…”

    “Kwanini Hathani…mi nipo thawa mbona…” alijibu huku akilazimisha tabasamu.

    Tembo akataka kuzungumza jambo, mara simu yake ikaita… akapunga mkono kumtaka radhi Brenda kisha akapokea.

    Akasogea kand na kuzungumza kwa takribani dakika tano. Neno alilolisikia Brenda ni moja tu. Tembo aliitaja hoteli ambayo walikuwepo….

    Travertine!!



    “Dah!! Brenda naomba unisaidie jambo moja… jambo moja tu tafadhali..”

    “Ni nini jamani..”

    “Kuna mtu anahitaji nimkopeshe kiasi fulani cha pesa, lakini marafiki zangu nikiwapa pesa hawarudishi. Sasa nimemweleza kuwa mimi sina pesa lakini kuna mahali naweza kumchukulia. Sasa wewe jifanye ndo mwenye hizo pesa unaniazima mimi halafu na mimi9 namuazima yeye… hapo lazima atanilipa….”

    “Mh!! Jamani Hathani mbona wanipoa mtihani mwendhio…”

    “Dah! Kama hautaweza basi ngoja niangalie namna nyingine…..”

    “Mh! Ushanuna jamani.. mi natania tu, haya nifundishe kidogo…” Brenda akaingia kule ambapo Tembo anahitaji.

    Hasan Tembo, Munyama mukubwa kamba fedha… akatabasamu kisha akamueleza kwa ufupi Brenda. Akafikia alipopahitaji.

    “Kwa kuwa ni pesa nyingi hatuwezi kupeana huku nje… jumla anataka milioni nne, wewe nitakupa milioni nne na nusu. Utahesabu nne halafu hiyo laki tano itakuwa ya kwako sawa!!”

    Ile kusikia pesa nyingi kama hiyo halali yake Brenda hakukumbuka hata kuuliza juu ya ulazima wa kujifungia chumbani ili waweze kumkabidhi yule mtu pesa. Kama msukule akaongoza njia kulekea chumbani…..

    Kichwani akiwaza kumiliki laki tano upesi upesi!!!

    Mlango ukafungwa!! Tembo akajipekua na kutoa kitita!!

    “Hebu zihesabu hizi ni ngapi..”

    Brenda akapokea….. akajikita katika kuhesabu. Hili lilikuwa kosa la jinai….

    Zile pesa badala ya kunukia kibenkibenki zikawa zinatoa harufu ya marashi ya Mamamia.

    Matamanio ya kuwa na Mamamia yakaanza kumpanda Brenda. Akajaribu kujizuia lakini hakuweza… mwishowe akakoma kuzihesabu zile pesa.

    Tembo akafanya tabasamu lake kama kawaida kisha akatumia fursa ile kutimiza kile alichokipanga katika kichwa chake!!

    “Brenda….” Akamuita kwa sauti yenye kitetemeshi cha amri fulani hivi. Brenda akamkazia macho tu.

    “Una maamuzi ya aina mbili hadi sasa…. Wewe kwanza na kisha dada yako…”

    Brenda akashtuka kusikia vile.

    “Maamuzi gani tena jamani…..”

    “Kuna mtu aliwapiga picha tena sio picha moja ni picha nyingi tu…”

    “Picha? Picha gani?”

    “Brenda… hujui kuhusu picha tena…. Si picha wewe na dada yako….”

    “Ndio mimi na dada thatha picha dhipi….”

    “Mkiwa mnafanya mapenzi…” Tembo akajibu!!

    Hamu zote zikamwisha Brenda ghafla…. Akatamani kujizika lakini hakuweza. Akatumbua macho..

    Tembo akatoa kile kicheko chake lakini safari hii hakikumvutia Brenda…

    “Nani amekwambia Hathani eeh nani? Na alitupiga picha nani?” alihoji Brenda huku hofu ikionekana wazi machoni pake.

    “Mi mwenyewe sijui hata nimeziona kuna mtu anazo nikaziiba….”

    “Zipo wapi kaka..”

    “Unataka kuona mlivyokuwa uchi mmekumbatiana..” maneno yalimtoka Tembo asijue ni wapi ameyapata…. Hakujua yu katika ulimwengu gani.

    Brenda alichoka!!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lakini hilo bado sio tatizo…. Tunaweza kulimaliza iwapo tutashirikiana….”

    “Kiaje thatha na wakati kuna picha tumepigwa..eeh aibu hii jamani weeee!!”

    “Picha ninazo mimi….. mmoja kati yenu anatakiwa kuzifuata mahali…”

    “Kama unazo hapa naziomba Hathani ama hata kama ni kwako twende..”

    “Ni picha za kikubwa sana anatakiwa kuzifuata mkubwa … kwani wewe na Mamamia nani mkubwa?”

    Brenda akashusha pumzi ndefu kabla ya kujibu kwa sauti iliyokata tamaa “MAMAMIA”

    “Basi ni yeye anayetakiwa kuzifuata….” Tembo alijibu huku akitabasamu.

    “Mh! Mamamia alikukaba aisee.. ila na wewe ni balaa yaani mwee! Ulimpagawisha hadi akapoteza fahamu. Doh! Hata mpiga picha naye alikuwa jasiri looh!” Tembo alijisemesha maneno yaliyomkera sana Brenda akajihisi kuabishwa sana na ilikuwa ni sawa na kuvuliwa nguo hadharani.

    “Hathani nitakupa chochote utakachotaka tafadhali kama kweli unadho hizo picha nipatie nami nikupatie chochote….” Brenda akajaribu karata yake ya mwisho.

    “Ni kweli BreBre nitakupatia iwapo tu utanipatia Mamamia….. hata hivyo kwa leo bado na wewe itabidi tu nikuondoe hofu..”

    “Uniondoe hofu? Kiaje labda….”

    “Sitahitaji pesa zozote kutoka kwenu kwa sababu hamuwezi kunipa nikitaka. Namuhitaji Mamamia azifuate picha zenu… ahaa kuhusu hofu ngoja nije nikunong’oneze …” Tembo akamsogelea Brenda… Brenda akamzuia kwa mikono yake.

    “Hutaki kujua ama unataka kujua…” Tembo akahoji kibabe… Brenda akawa mdogo akamruhusu Tembo amnong’oneze.

    Hili lilikuwa kosa la jinai!!!

    “Sitawaaibisha iwapo mtatii nitakachoomba!!” alinong’ona Tembo katika sikio la Brenda.

    He! Sasa hiki nd’o cha kuninong’onedha!!! Alijiuliza Brenda huku akipigwa na butwaa!!

    Wakati huohuo kidole chake kimoja kikijaribu kulikuna sikio lake, lakini huu mkono wa kidole haukutosha labda… Brenda akazidi kujikuna…..

    Huo muwasho haukuwa wa kawaida, ulikuwa ule muwasho ambao hukunwa na ulimi wa Mamamia wawapo wawili….. sasa muwasho sikioni umekuja akiwa peke yake?? No! hakuwa peke yake… mbele yake alikuwa ni Tembo.

    “Mimi nataka kwenda Hathani, sijisikii vizuri…” Brenda akamuaga Tembo huku akijaribu kusimama…. Lakini hakuweza miguu haikuwa na nguvu na alitambua haswa kuwa alikuwa anamuhitaji Mamamia eneo lile.

    Tembo hakulaza damu!!

    Brenda alikuwa anahofia kuaibika njia nzima atakayokuwa anatembea kwenda nyumbani…. Alipojitambua kuwa ana hofu… ni hapo akakumbuka kuwa Tembo aliahidi kumtoa Hofu….

    Naam!! Ilikuwa kama alivyodhani… Tembo akamdama na kutumbukiza ulimi katika sikio lile lililokuwa linawasha!!

    Ebwana eeh!! Brenda akatokwa na yowe kubwa… upesi Tembo akaiendea luninga akawasha na kuweka sauti ya juu kabisa.

    Yaliyoendelea yakabaki kuwa siri yao!!

    Lakini Tembo alimtoa hofu Brenda kwa asilimia zote!!

    Lakini huu ukawa mwanzo wa mkasa!!

    Brenda akiwa njiani kurudi nyumbani akawa anapima ladha ya tembo na ile ya Mamamia….. ladha ya Tembo ilikuwa baabkubwa zaidi. Lakini huyu Tembo anahitaji Mamamia nd’o afuate zile picha….

    Wivu!! Wivu ukamwandama Brenda ambaye alihitaji kuipata tena ile ladha ya kipekee… ladha ya Mnyama mkubwa!!!

    Tembo!!

    Akafikiria namna gani anaweza kumuhujumu Mamamia ili huyo wa kuitwa Hassan Tembo aweze kuwa mpenzi wake moja kwa moja.

    “Kwandha akiwa mpendhi wangu na hidho picha atadhichachana!!” Brenda alijisemea huku akitabasamu na kujipa matumaini yote kuwa ataibuka mshindi katika hili.



    ****



    MAMAMIA alijiona mjinga baada ya kutokwa machozi kwa muda mrefu.

    Hakika, kilio hakikuwa tiba juu ya haya ambayo alikuwa ameelezwa na mdogo wake juu ya picha za uchi zinazoshikiliwa na Hassan.

    Alipomkumbuka Hassan Tembo na kiumbo chake kidogo akajisikia aibu kujishusha kwake na kufuata maelekezo juu ya picha hizo. Lakini angefanya nini iwapo picha zingesambaa na heshima yake kuporomoka.

    MAMAMIA akaamua rasmi kulipigania suala hili kabla halijafika pabaya. Akachukua namba ya simu ya Tembo na kumpigia kwa ajili ya mazungumzo.

    Akategemea kuwa Tembo atamwomba penzi!!

    Haikuwa hivyo, badala yake akapewa miadi ya kukutana sehemu ya wazi kabisa kwa ajili ya kuchukua zile picha kama kweli zipo!!



    Mamamia akiwa anajijaza imani kali kuwa Tembo akiwa mwanaume kama wanaume wengine atauingia mkenge na kutamanika kingono. Akaamua kumvalia mavazi ambayo moja kati ya wanaume mia moja anaweza kukwepa kutamanika. Brenda akajisikia vibaya sana kumwona dada yake akiwa amevaa vile.. aliamini kwa kila namna Tembo ataingia mkenge!!

    Roho ilimuuma!!!



    SIKU IKAFIKA!!!!



    MAENEO ya Mbezi ya Kimara kwa Msuguli. Mamamia akiwa ameegesha gari yake mahali na Tembo naye akiwa ameegesha GX 100 yake. Wote walikuwa wakitazamana baada ya Tembo kumweleza Mamamia juu ya nini kinatakiwa ili azipate zile picha….

    Mamamia hakuamini kabisa kama kweli yawezekana sharti likawa dogo kiasi kile!

    Yaani kumsindikiza tu hadi nyumbani kwake na hata ndani siingii!!

    Jambo jepesi sana. Mamamia akakubali, Tembo akatabasamu kisha akaingia garini na kuanza kuongoza njia kuelekea bagala. Mamamia akifuata kwa nyuma.



    WALIIFIKIA nyumba ambayo Tembo alikuwa anaishi, Mamamia akamtazama Tembo na kujisikia vibaya sana. Tembo alikuwa mfupi kuliko yeye…… katika maisha yake aliwahi kuapa kuwa kamwe hatakuja kuingia katika mahusiano aidha na mwanaume ambaye amemzidi umri ama ambaye yeye amemzidi urefu.

    Sasa yupo na Tembo na anahisi amemzidi vitu vyote hivyo, umri na urefu!!

    Aibu gani hii!! Kiapo kikayeyuka. Sasa tembo alikuwa na sauti, akisema twende ni kwenda akisema hakuna ni hakuna!! Na sasa wameifikia nyumba ya Tembo. Amri ikatolewa.

    Ingia ndani!!

    Mamamia Mango hakuwa na ujanja. Akaingia ndani lakini kichwani akikumbuka mipango yake vyema iwapo Tembo atahitaji kufanya naye mapenziu. Na bila shaka ni hilo lilikuwa linafuata maana mwanaume kumwingiza msichanan chumbani kwake bila sababu kuu usikuusiku ni kukaribisha majaribu.

    Mamamia akaficha ghadhabu yake yote juu ya Tembo, akajifanya kutabasamu kila dakika huku akijifanya kuifurahia hali ya mle ndani.

    Awali alidhani huenda Tembo ni kakijana tu kazugaji hakana hili wala lile ila zile picha tu nd’o zinampa kiburi.

    “Hata hapa sio kwake wala nini!!” Mamamia akajisemea katika nafsi yake akiamini kuwa Tembo hana uwezo wa kuishi nyumba kubwa kama ile peke yake. Lakini hakuwa Tembo aliyempa jibu, macho yake yakakutana na picha ya Tembo ukutani. Picha kubwa kabisa iliyopachikwa imara ukutani.

    “Mh! Ananizuga huyu ameachiwa tu geto na wenyewe!!” bado Mamamia hakutaka kuamini moja kwa moja kuwa Tembo ana mafanikio makubwa vile kumzidi yeye.

    Alipogeuza macho kutoka katika ile picha akaanza kuzithaminisha samani za mle ndani, runinga bapa kubwa ilisheheni ukutani, sofa za bei ghali, zulia zito haswa, akazidi kuangaza zaidi na zaidi na mwishowe akakiri kuwa kama kweli Tembo anaimiliki nyumba ile basi heshima kwake.

    Mamamia akaanza kusahau kama alisema kuwa ka-Tembo ni kaqfupi na kadogodogo hakamfai. Wazo jipya likaibuka kichwani mwake. Akafikiria kumrubuni Tembo ili auingie mkenge kama kweli anazo zile picha basi ampatie ama azitie moto kwa heshima ya penzi.

    “Kwanza alikuwa ananitaka huyu tangu zamani…” Mamamia akajisemea huku akijiweka tayari kuingia kazini.

    “Halafu mbona kama Napata hisia naye jamani…” alizidi kujiuliza…..

    “Mamamia…karibu!!” hatimaye Tembo aliyekuwa ameingia chumbani alirejea na kumkaribisha Mamamia tena.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni wakati huo ambao Tembo hajajiandaa kufanya alichotaka kwa Mamamia likatokea jambo.

    Mamamia akijua kabisa kuwa lile zulia ni zito sana akapiga hatua mbili mbele akijifanya kukosa umakini akajikwaa na kuanguka chini.

    Yowe likamtoka!!

    Tembo akagutuka na kutimua mbio. Akamfikia pale alipokuwa, akainama ili aweze kumsaidia.

    Huyu sasa alikuwa Tembo halisi ambaye hayupo katika ajira!! Akamshika Mamamia.

    Binti mkata viuno akatabasamu katika nafsi na kujipongeza juu ya mtego wake kunasa.

    Akauvaa ujasiri na kisha akapitisha mikono yake yenye kucha ndefu kiasi, akamshika Tembo kidogo ya kiuno chake kisha akambinya kitaalamu, Tembo akaungana naye zuliani. Ili asiseme neno Mamamia hakutaka kumziba Tembo kwa kutumia mikono, majambazi ndo huziba watu kwa mikono.

    Dawa ya moto ni moto na hata dawa ya mdomo ni mdomo!!

    Mamamia akauwahi mdomo wa Tembo kwa kutumbukiza ulimi wake kule. Tembo aliyekuwa anahitaji kuzungumza akashangaa anabadili zoezi na kuanza kumung’unya ulimi ule aliotupiwa na Mamamia.

    Mamamia hakuhitaji kupoteza walau pointi moja katika zoezi hili, mkono mmoja ukasafiri hadi katika masikio ya Tembo, kidole kidogo cha mwisho kikazama sikioni.

    Sasa Mamamia alimwachia Tembo mdomo aweze kusema.

    Kwedli alisema lakini alisema maneno yasiyoeleweka. Wakati anasema hayo Mamamia aliendelea na shughuli nyingine.

    Baada ya dakika nne…..

    Tembo alikuwa kama alivyozaliwa. Mnaya mkubwa kamba fedha kwa mara ya kwanza katika ajira yake anakutana na mwanamke wa maajabu!!

    Mamamia!!!

    Wanaume ndo huwabeba wanawake na kuwapeleka chumbani!! Lakini Mamamia akaionyesha tofauti ambayo wengi hawaijui.

    Akamnyanyua Tembo na kumweka mgongoni….. kama vile mtoto mdogo Tembo akiwa uchi wa mnyama akasalimu amri….

    Mamamia akababia na kukipata chumba cha Tembo!!! Hakuwa na papara hata kidogo, shetani kapata mjanja wake!!

    Badala ya kumrusha kitandani kisha na yeye kujirusha hapo jambo ambalo Tembo alilitegemea, Mamamia akamrusha Tembo kisha yeye akatoka nje mbiombio na baada ya sekunde kadhaa akarejea akiwa na chupa ya asali aliyoitoa sebuleni kwa Tembo.

    Tembo hajui hili wala lile akapigwa bao jingine la kisigino!!

    Mamamia akamwagia asali kiasi mgongoni kisha akaanza kuilamba akiitapoakaza huku na kule. Nani wa kujali kuwa yale mashuka yanachafuka??

    Hakuna hata mmoja!!!

    Baada ya hapo Tembo akasafirishwa kwenda katika dunia nyingine. Ile ladha aliyokuwa anaiota siku nyingi sana sasa alikuwa anaipata hapa.

    Kiuno kisichokuwa na mfupa!!!

    Baada ya nusu saa Mamamia akiwa anampelekesha Tembo hatimaye alianza kumhoji maswali. Tembo akaanza kujibu kwa fujo hata ambayo hajaulizwa…..

    Hakujua kama anajibu ama hajibu!!

    Mamamia hakujali akaendelea na yake!!

    Baada ya saa moja na nusu!!! Tembo alikuwa hoi kivyake na Mamamia hoi kivyake.

    Walikuwa wamesinzia!!!

    Majira ya saa nane usiku Tembo anakurupuka usingizini anamwamsha Mamamia na kumweleza jambo moja zito.

    “Nakupenda Mamamia!!!” ajabu na kweli!!!!

    Mamamia akatabasamu kisha akambusu Tembo midomoni, halafu wakajifunika shuka tena ikawa zu ya kitanda kuhangaika kwa mara nyingine.

    Awamu ya pili tena Mamamia akawa mshindi. Kuhusu picha Tembo akamweleza Mia kuwa hazikuwepo na asitarajie madhara yoyote yale.

    Kwa shughuli aliyofanya usiku uliopita Mamamia alitarajia ushindi tu….

    Na kweli ulikuwa ushindi, lakini ushindi ulioleta balaa.



    ****



    BRENDA alikuwa akiumiza kichwa chake na kujiuliza anaanza vipi kuingia katika milki ya Tembo, akajiuliza dada yake naye akifanya mapenzi na kijana yule itakuwaje kama akinogewa?

    Usiku ulizidi kwenda hadi kunakuchwa bado Mamamia alikuwa hajarudi. Wivu ukamshambulia sana Brenda lakini hakuwa na namna akajiapiza kuwa iwapo Tembo atawapatia hizo picha basi huo nd’o utakuwa wakati muafaka wa kumrubuni Tembo hadi awe mpenzi wake wa kudumu.

    Hakujua kama Mamamia naye alikuwa na mawazo kama yake. Majira ya saa tano asubuhi Mamamia alirejea nyumbani akiwa na furaha tele!!

    Akamweleza Brenda kuwa picha zilikuwa kwenye kompyuta na zote wamezifuta!!

    Brenda akafurahia huku akijiahidi kumsaka Tembo kwa hali na mali.



    ****



    TEMBO hakujua kama anaishi kwa kanuni, kanuni ambazo hazikuandikwa mahali zaidi ya ndoto ile ya siku ya kwanza kuingia katika ulimwengu huu wa mauzauza. Tembo alikuwa anajiuliza sana ni kwanini akishafanya zinaa na msichana mmoja hataki wala hajisikii tena kufanya naye kwa mara nyingine.

    Hakujua kama hiyo nd’o ajira!!

    Lakini kwa Mamamia ilikuwa tofauti, usiku ule ulikuwa wa maajabu sana…. Akautamani ujitokeze tena.

    Clara, Lucy Kezi, Maria, Rehema, Brenda na wengineo wengi hakuwahi kuwaza kuzini nao tena….. lakini ladha ya Mamamia akaitamani tena.

    Baada ya juma moja akaamua kumtafuta….

    Wakapanga kukutana nyumba za kulala wageni!!

    Mamamia akakubaliana na Tembo, wakati huo wakiitana ‘mpenzi’.

    “Yaani ikiwezekana mi namuoa huyuhuyu kwani nini….” Tembo alijisemea siku hiyo. Na akatarajia kusema na Mamamia juu ya jambo hilo la ndoa.

    “Mh….ile asali ile…. Mh! Ule ulimi looh na vile viuno walah simwachii hivihivi yule mi naweka ndani, kwanza ninaishi nyumba kubwa nina pesa…. Yaani naona ndoa ileeee watu Temboooo Temboooo!!!” Hassan Tembo alikuwa anazungumza peke yake katika gari….

    Alichukulia wepesi jambo lile lakini hakujua ugumu wake!!!

    Na labda ule ukawa usiku ambao hakutaka kuusahau kamwe!!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog